2
Ubia Mkakati wa Zao la Mpunga Muhtasari Mpunga (Oryza sativa) ni zao muhimu la pili kwa chakula nchini Tanzania baada ya zao la mahindi. Takwimu halisia zinaonyesha kuwa inakadiriwa tani za ujazo milioni 2.2 za mpunga huzalishwa nchini, hii inaifanya Tanzania kuwa nchi inayozalisha mpunga kwa wingi katika ukanda ikiwa ni wastani wa tani 2.2 kwa hekta (NRDS-II, 2019). Zaidi ya asilimia 70 ya mpunga unaozalishwa nchini hutoka mikoa sita ya Shinyanga, Tabora, Mwanza, Mbeya, Rukwa and Morogoro. Mikoa mingine ni Songwe, Katavi, Arusha, Kilimanjaro, Kigoma, Manyara, Iringa, Mara na Tanga. Inakadiriwa kuwa asilimia 20 ya wakulima nchini Tanzania wanajishugulisha na uzalishaji wa mpunga (FAO, 2015). Wakulima wadogo hulima mpunga kwa kutegemea mvua katika maeneo ya uwanda wa chini. Baadhi ya wakulima wadogo hupanda na kumwagilia mashamba yao ya mpunga chini ya skimu za umwagiliaji wakitumia njia asilia au skimu zilizoendelezwa kwa kiwango cha wastani. Mashamba makubwa yanategemea kilimo cha umwagiliaji lakini kilimo biashara cha uzalishaji mkubwa katika mashamba makubwa sio jambo linalofanyika maeneo mengi hapa nchini bali hufanywa na makampuni machache katika mikoa ya Mbeya, Morogoro na Pwani ambapo skimu za umwagiliaji zimebinafishwa kwa makampuni binafsi (FAO, 2015). Aina kuu za mbegu za mpunga zinazozalishwa nchini ni Kilombero, Supa, Zambia, Kyela Ndefu na Saro 5. Mpunga aina ya Saro 5 (TXD 306) ndiyo mbegu pekee iliyoboreshwa na kuzalishwa kwa wingi nchini Tanzania. Wadau Muhimu katika Ubia wa Zao la Mpunga Sekta ya Umma, Sekta Binafsi, Washirika wa kimaendeleo, Vyama vya Wakulima na Asasi za Kiraia Mpango wa Kukuza Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) Ni ubia kati ya sekta ya umma na binafsi unaolenga kuchochea uwekezaji unaowajibika kwenye kilimo biashara katika ukanda wa kusini nchini Tanzania. mapinduzi katika kilimo kwenye Nyanda za Juu za Kusini mwa Tanzania. Programu hii hasa inalenga kuendeleza wakulima wadogo kusudi shughuli za uzalishaji kwenye mlolongo / mnyororo wa thamani zilete faida inayotarajiwa. Kituo cha SAGCOT kinafanya kazi kama dalali wa ubia na kitovu cha habari kwa wabia wa SAGCOT katika kuwezesha uwekezeshaji kwenye minyororo ya thamani inayoshirikisha jamii na kuzingatia uhifadhi endelevu wa mazingira. Kituo cha SAGCOT kinakuza na kuwezesha ubia mkakati ili kuimarisha mbinu shirikishi na kuboresha ushirika uliopo miongoni mwa wadau muhimu ndani na nje ya minyororo ya thamani iliyopewa vipaumbele. Nini kinasababisha ubia wa zao la mpunga kuwa ubia mkakati ? Mtiririko wa bidhaa zinazotokana na mnyororo wa thamani wa mpunga huanzia kwenye pembejeo mpaka mlaji wa mwisho/sokoni ikiungana na sekta ya viwanda vya utengenezaji wa chakula cha mifugo na kisha sekta ya nishati. Bidhaa za mwisho ziingiazo sokoni ni mchele kwa matumizi ya binadamu wakati pumba laini za mpunga ni bidhaa muhimu kwa viwanda vya kutengeneza chakula cha mifugo. Pumba ngumu za mpunga hutumika kama chanzo mbadala cha nishati katika Ukanda wa SAGCOT hususan kuchomea matofali ya udongo na pia nishati muhimu kwenye mitambo ya viwandani kama vile Kiwanda cha Sementi cha Lafarge Holcim kilichopo Mbeya. Hakuna takwimu au rekodi sahihi inayoonyesha ni kiasi gani cha ujazo wa pumba ngumu za mpunga kinatumika kama chanzo mbadala cha nishati lakini kutokana na mlundikano wa pumba ngumu unaoshuhudiwa kwenye vinu vya kuchakata mpunga inaashiria kuwa pumba ngumu za mpunga hazitumiki kikamilifu kama chanzo mbadala cha nishati. Mpunga unaotoka kwenye ukanda wa SAGCOT umekuwa ni sehemu ya bidhaa muhimu ya biashara kati ya Tanzania na nchi jirani. Kwa sasa hivi mchele kutoka Tanzania huuzwa zaidi kwenye nchi za Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mchele kutoka kongani za Mbarali, Ihemi na Kilombero pia huuzwa kwenye soko la ndani ya nchi ambapo mkoa wa Dar es salaam unabakia kuwa ndio soko kubwa ukifuatiwa na na mikoa ya Tanga na Arusha. Kuimarika kwa usalama wa chakula na hali ya maisha katika kaya. Ubia wa Mpunga unalenga kuongeza mara mbili tija na kuongeza mara tatu faida ya kifedha kwa wakulima wa mpunga kuanzia tani 2.1 mpaka tani 5 kwa hekta katika ukanda wa SAGCOT. Ndoto ya Ubia wa Mpunga ni kufikia uwezo wa kidunia wa uzalishaji wa tani 13 kwa hekta. Kutafuta masuluhisho ya kudumu katika mnyororo wa thamani. Ubia wa Mpunga ulianzishwa kimkakati ili kujumisha wadau kutoka kila eneo linalohusisha mnyororo huu na watendaji kutoka maeneo yote yanayozalisha mpunga katika ukanda wa SAGCOT kama vile wilaya za Mbarali na Kyela mkoani Mbeya, wilaya za Momba na Ileje mkoani Songwe na wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Ubia Mkakati wa Zao la Mpungasagcot.co.tz/wp-content/uploads/2020/08/SAGCOT-Brochure-Mchele.pdfProject, walichangia katika maandalizi ya Hadidu za Rejea na Mpango kazi wa Ubia Mkakati

  • Upload
    others

  • View
    1

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Ubia Mkakati wa Zao la Mpungasagcot.co.tz/wp-content/uploads/2020/08/SAGCOT-Brochure-Mchele.pdfProject, walichangia katika maandalizi ya Hadidu za Rejea na Mpango kazi wa Ubia Mkakati

Ubia Mkakati wa Zao la Mpunga

MuhtasariMpunga (Oryza sativa) ni zao muhimu la pili kwa chakula nchini Tanzania baada ya zao la mahindi. Takwimu halisia zinaonyesha kuwa inakadiriwa tani za ujazo milioni 2.2 za mpunga huzalishwa nchini, hii inaifanya Tanzania kuwa nchi inayozalisha mpunga kwa wingi katika ukanda ikiwa ni wastani wa tani 2.2 kwa hekta (NRDS-II, 2019). Zaidi ya asilimia 70 ya mpunga unaozalishwa nchini hutoka mikoa sita ya Shinyanga, Tabora, Mwanza, Mbeya, Rukwa and Morogoro. Mikoa mingine ni Songwe, Katavi, Arusha, Kilimanjaro, Kigoma, Manyara, Iringa, Mara na Tanga. Inakadiriwa kuwa asilimia 20 ya wakulima nchini Tanzania wanajishugulisha na uzalishaji wa mpunga (FAO, 2015). Wakulima wadogo hulima mpunga kwa kutegemea mvua katika maeneo ya uwanda wa chini. Baadhi ya wakulima wadogo hupanda na kumwagilia mashamba yao ya mpunga chini ya skimu za umwagiliaji wakitumia njia asilia au skimu zilizoendelezwa kwa kiwango cha wastani. Mashamba makubwa yanategemea kilimo cha umwagiliaji lakini kilimo biashara cha uzalishaji mkubwa katika mashamba makubwa sio jambo linalofanyika maeneo mengi hapa nchini bali hufanywa na makampuni machache katika mikoa ya Mbeya, Morogoro na Pwani ambapo skimu za umwagiliaji zimebinafishwa kwa makampuni binafsi (FAO, 2015). Aina kuu za mbegu za mpunga zinazozalishwa nchini ni Kilombero, Supa, Zambia, Kyela Ndefu na Saro 5. Mpunga aina ya Saro 5 (TXD 306) ndiyo mbegu pekee iliyoboreshwa na kuzalishwa kwa wingi nchini Tanzania.

Wadau Muhimu katika Ubia wa Zao la MpungaSekta ya Umma, Sekta Binafsi, Washirika wa kimaendeleo, Vyama vya Wakulima na Asasi za Kiraia

Mpango wa Kukuza Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT)Ni ubia kati ya sekta ya umma na binafsi unaolenga kuchochea uwekezaji unaowajibika kwenye kilimo biashara katika ukanda wa kusini nchini Tanzania. mapinduzi katika kilimo kwenye Nyanda za Juu za Kusini mwa Tanzania. Programu hii hasa inalenga kuendeleza wakulima wadogo kusudi shughuli za uzalishaji kwenye mlolongo / mnyororo wa thamani zilete faida inayotarajiwa.Kituo cha SAGCOT kinafanya kazi kama dalali wa ubia na kitovu cha habari kwa wabia wa SAGCOT katika kuwezesha uwekezeshaji kwenye minyororo ya thamani inayoshirikisha jamii na kuzingatia uhifadhi endelevu wa mazingira. Kituo cha SAGCOT kinakuza na kuwezesha ubia mkakati ili kuimarisha mbinu shirikishi na kuboresha ushirika uliopo miongoni mwa wadau muhimu ndani na nje ya minyororo ya thamani iliyopewa vipaumbele.

Nini kinasababisha ubia wa zao la mpunga kuwa ubia mkakati ?Mtiririko wa bidhaa zinazotokana na mnyororo wa thamani wa mpunga huanzia kwenye pembejeo mpaka mlaji wa mwisho/sokoni ikiungana na sekta ya viwanda vya utengenezaji wa chakula cha mifugo na kisha sekta ya nishati. Bidhaa za mwisho ziingiazo sokoni ni mchele kwa matumizi ya binadamu wakati pumba laini za mpunga ni bidhaa muhimu kwa viwanda vya kutengeneza chakula cha mifugo. Pumba ngumu za mpunga hutumika kama chanzo mbadala cha nishati katika Ukanda wa SAGCOT hususan kuchomea matofali ya udongo na pia nishati muhimu kwenye mitambo ya viwandani kama vile Kiwanda cha Sementi cha Lafarge Holcim kilichopo Mbeya. Hakuna takwimu au rekodi sahihi inayoonyesha ni kiasi gani cha ujazo wa pumba ngumu za mpunga kinatumika kama chanzo mbadala cha nishati lakini kutokana na mlundikano wa pumba ngumu unaoshuhudiwa kwenye vinu vya kuchakata mpunga inaashiria kuwa pumba ngumu za mpunga hazitumiki kikamilifu kama chanzo mbadala cha nishati. Mpunga unaotoka kwenye ukanda wa SAGCOT umekuwa ni sehemu ya bidhaa muhimu ya biashara kati ya Tanzania na nchi jirani. Kwa sasa hivi mchele kutoka Tanzania huuzwa zaidi kwenye nchi za Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mchele kutoka kongani za Mbarali, Ihemi na Kilombero pia huuzwa kwenye soko la ndani ya nchi ambapo mkoa wa Dar es salaam unabakia kuwa ndio soko kubwa ukifuatiwa na na mikoa ya Tanga na Arusha.

Kuimarika kwa usalama wa chakula na hali ya maisha katika kaya.Ubia wa Mpunga unalenga kuongeza mara mbili tija na kuongeza mara tatu faida ya kifedha kwa wakulima wa mpunga kuanzia tani 2.1 mpaka tani 5 kwa hekta katika ukanda wa SAGCOT. Ndoto ya Ubia wa Mpunga ni kufikia uwezo wa kidunia wa uzalishaji wa tani 13 kwa hekta.

Kutafuta masuluhisho ya kudumu katika mnyororo wa thamani.Ubia wa Mpunga ulianzishwa kimkakati ili kujumisha wadau kutoka kila eneo linalohusisha mnyororo huu na watendaji kutoka maeneo yote yanayozalisha mpunga katika ukanda wa SAGCOT kama vile wilaya za Mbarali na Kyela mkoani Mbeya, wilaya za Momba na Ileje mkoani Songwe na wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Page 2: Ubia Mkakati wa Zao la Mpungasagcot.co.tz/wp-content/uploads/2020/08/SAGCOT-Brochure-Mchele.pdfProject, walichangia katika maandalizi ya Hadidu za Rejea na Mpango kazi wa Ubia Mkakati

Kuwakutanisha wabiaWabia 46 wakijumuisha wakulima wadogo, Sekta binafsi kama vile Yara, TARI, Mashamba na matrekta, LonAgro, Obo Investment, Raphael Group, Mtenda Kyela Rice, Mbeya Rice Company, Dick Lukala, NMB, CRDB; sekta ya umma kama Shirika la Viwango (TBS), Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Wizara ya Kilimo, Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Vyuo vya Utafiti wa Kilimo (TARI), taasisi kubwa kama Baraza la Mpunga (Rice Council of Tanzania), Baraza la Kilimo Tanzania (ACT), AMBERICO na Washirika wa Maendeleo wanaotoa fedha kwenye miradi kama USAID NAFAKA project, Kilimo Trust, NORAD TAPP2 Project, walichangia katika maandalizi ya Hadidu za Rejea na Mpango kazi wa Ubia Mkakati wa Zao la Mpunga.

Ubora wa mazao na manufaa kwa wakulima Umoja na Ushirikano wa Wabia umeweza kuwafikia idadi kubwa ya wakulima na kuwapatia mafunzo juu ya teknolojia mpya endelevu za kilimo, mbinu bora za kilimo ambazo zimeweza kuongeza ubora wa mchele unaozalishwa. Kwa mfano, Ushirika wa Wakulima wa Mpunga Mbeya (AMBERICO), umoja huu una idadi ya wakulima wa mpunga 15,000 waliofaidika na huduma zilizotolewa na Baraza la Kilimo nchini kupitia ufadhili wa TAPP 2, NMB, RAPHAEL Group, Kilimo Trust and YARA.

Kuonyesha athari chanya za kimazingira.Mfumo wa Kuimarisha Kilimo cha Zao la Mpunga (SRI) ulianzishwa nchini Tanzania mwaka 2009 na Mbia wa SAGCOT Kilombero Plantations Limited ikiwa ni mojawapo ya jitihada za kuongeza usalama wa chakula nchini. Mbinu za Mfumo wakuimarisha zao la Mpunga (SRI) zimeweza kuongeza uzalishaji kwa mkulima mdogo kutoka tani 3/hekta mpaka zaidi ya tani 5/hekta, na kufikia mwaka 2014 zimeweza kuongeza wastani wa uzalishaji wa mpunga mara tatu zaidi kwa familia 6,500 za wakulima wilayani Kilombero. .Mbinu za kuimarisha uzalishaji wa Zao la Mpunga (SRI) zimeongeza uzalishaji kwa zaidi ya asilimia (30%) huku matumizi ya maji yakiwa chini ya asilimia (40%) kulinganisha na pale mkulima atumiapo mbinu asilia za kilimo. Mbinu za SRI zimehakikisha kuwa na matumizi kidogo ya maji. Ni mbinu ya Kilimo hai kinachotumia miche michanga ya mpunga na kupandwa kwa nafasi 25sm kati ya mche moja na mwingine na pia unaweza kupalilia kwa kutumia vifaa maalum vinavyotumia mkono.Mkoani Mbeya, mbinu za kuimarisha zao la mpunga zimeongeza mara mbili uzalishaji wa zao la mpunga kwa hekta, kwa mfano skimu ya Madibira ambapo matumizi ya mbinu za SRI yameongea uzalishaji kufikia tani 9.3 kwa hekta kutoka tani 7.2 kwa hekta (utumiapo mbinu asilia za Kilimo). Katika skimu ya Uturo, mbinu za kuimarisha uzalishaji wa mpunga SRI umeongeza uzalishaji kufikia tani 13 kwa hekta kutoka tani 5.7 kwa hekta (utumiapo njia asilia za Kilimo) - Chuo Kikuu cha Cornell.

Matokeo endelevu na shirikishiMbali ya kuwa ni zao la pili kwa chakula nchini Tanzania, zao la mpunga linatoa ajira angalau kwa wakulima 230,000 na ni chanzo cha nishati kwa mamilioni ya watu na wanyama (mifugo). Mpunga ustawi vyema kwenye mikoa yenye hali ya joto na mabonde yenye halijoto, maeneo ambayo kawaida huwa na idadi kubwa ya watu wanoishi (wakazi). Kwa hiyo basi uwekezaji katika mnyororo wa thamani kwenye zao la mpunga ni fursa pekee ya kusaidia mahitaji ya chakula kwa ongezeko kubwa la watu kote mjini na vijijini na kuchangia kwenye fursa za uzalishaji kipato kwa wakulima wa mpunga waishio vijijini.

Licha ya kuwa mpunga ni zao muhimu, lakini viwango vya tija ya uzalishaji bado viko nyuma ya wastani wa kidunia wa uzalishaji wa tani 8 kwa hekta, kwa mujubu wa takwimu za mamlaka ya serikali za mitaa. Lengo la Ubia wa Zao la Mpunga ni kuongezatija mara mbili na faida mara tatu kwa wakulima wanaoshiriki ndani ya ubia huu.

Changamoto muhimuKwa ujumla uzalishaji wa zao la mpunga kwa hekta nchini unaonyesha kuwa chini kwa tani 2.5 dhidi ya uzalishaji unaotakiwa wa tani 6.5 kwa hekta. Kushughulikia Changamoto zilizopo kutachochea ongezeko la tija katika uzalishaji na kuimarisha biashara ndani ya mnyororo wa thamani wa mpunga.

Uhaba wa upatikanaji wa mbegu bora za mpunga, Kiwango kidogo cha matumizi ya mbegu bora za mpunga, uhaba wa mahitaji muhimu ya awali kwa wakulima

Uzalishaji mdogo wenye tija kidogo, ukosefu wa skimu za umwagiliaji zinazojikita zaidi kwenye kilimo cha mpunga, matumizi madogo ya zana bora za kilimo cha zao la mpunga, Kilimo cha kujikimu badala ya Kilimo biashara, matumizi madogo na kutozingatia maelekezo ya matumizi sahihi ya mbolea

Mfumo wa soko uliokosa muundo kamili, Kutokuwa na uhakika katika uzalishaji wa umeme na mtandao duni wa barabara

Uratibu duni miongoni mwa watendaji, kuwepo kwa umoja dhaifu wa wakulima

Upatikanaji mdogo wa fedha kwa ajili ya uzalishaji kwenye kilimo

Kutotabirika kwa mazingira ya kibiashara

FURSA CHANGAMOTOKuongezeka kwa uzalishaji wa mbegu bora za Mpunga:

Kuongezeka kwa uzalishaji na tija kwa Zao la Mpunga

Kuimarika kwa Mfumo wa Soko

Kuimarika kwa ushirikiano miongoni mwa wanachama ndani ya Ubia Mkakati

Kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma za kifedha

Sera na Mazingiza Wezeshaji

Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia: SAGCOT Centre Limited Simu: +255 22 260 1024 +255 22 260 0146Gholofa ya 5, Jengo la Ikon Faxi: +255 22 260 2368Barabara ya Bains, Masaki S.L.P 80945 Barua Pepe: [email protected] es Salaam, Tanzania Tovuti: www.sagcot.co.tz