9
UFA WA UTEKELEZAJI WA SERA YA UWEZESHAJI NA USHIRIKISHWAJI KATIKA TASNIA YA UZIDUAJI KWENYE MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Ni Jeneza la Uchumi wa Viwanda? Na: Prof Handley Mpoki Mafwenga Simba Ph.D (Finance), MSc (Finance), MBA (Mg.Eco), LLM (Taxation), PGDTM, LLB, ADTM [Mchambuzi wa Sera za Uchumi, Bajeti na Kodi] Tunaweza kujiuliza Watanzania; Kwanini tunahitaji Uwezeshaji na Ushirikishwaji? Kuna mambo matatu ya kuangalia (1) Kufuatilia Ukamilishaji wa Miradi; ambapo Uwezeshaji na Ushirikishwaji ni Mkakati wa Kutiliwa Maanani katika ukamilishaji wa Miradi inayowekezwa nchini. Wawekezaji wenye Miradi kwenye Sekta ya Mafuta na Gesi wanapaswa kuheshimu Uwezeshaji na Ushirikishwaji kuwa ni Thamani Kubwa katika kupendekeza miradi itakayowekezwa nchini kwenye mafuta na gesi; aidha Uwezeshaji na Ushirikishwaji ukihusishwa kwenye Tathmini za miradi itawawezesha Wawekezaji hao; ikiwa ni pamoja na kupata faida ya ushindani kwenye Asasi za Ubia wakati zikihitaji leseni kwa kupewa leseni kwa urahisi na pia kusaidia zaidi wakati wa majadiliano ya Mikataba na nchi yetu. (2) Kusaidia Biashara au Malengo ya Sera za Umma; ambapo Kanuni za Uwezeshaji na Ushirikishwaji kama vile, Utoaji taarifa, unapaswa kuzingatiwa wakati ambapo husaidia sana biashara na malengo ya sera za umma kuundwa vyema. Kila Mpango Mkakati wa Uwezeshaji na Ushirikishwaji unapaswa kuwa na Viashiria sahihi vinavyoruhusu kampuni kupima utekelezaji wa miradi yake dhidi ya malengo. Kukusanya takwimu sahihi pia kunasaidia kukidhi mahitaji ya utoaji taarifa; na (3) Kuwepo kwa Matumaini; ambapo kutokana na mazingira ya ushindani unaosababisha kushuka kwa uzalishaji (kwa sababu mafuta ni rasilimali inayokwisha baada ya kuvunwa) ukilinganisha na kukua kwa uuzaji wa rasilimali za nishati; kampuni katika Sekta ya Mafuta na Gesi zinakabiliwa na matumaini makubwa kuwa uzalishaji wa mafuta na gesi utapunguza kwa kiasi kikubwa athari mbaya za kiuchumi, kijamii na kisiasa, na itakuwa ni chanzo kikubwa cha kodi, mrabaha na kuwa moja ya nguzo ya kutekeleza Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT

UFA WA UTEKELEZAJI WA SERA YA UWEZESHAJI NA USHIRIKISHWAJI KATIKA

TASNIA YA UZIDUAJI KWENYE MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Ni Jeneza la

Uchumi wa Viwanda?

Na: Prof Handley Mpoki Mafwenga Simba Ph.D (Finance), MSc (Finance), MBA (Mg.Eco), LLM (Taxation), PGDTM, LLB, ADTM

[Mchambuzi wa Sera za Uchumi, Bajeti na Kodi]

Tunaweza kujiuliza Watanzania; Kwanini tunahitaji Uwezeshaji na Ushirikishwaji? Kuna mambo matatu ya kuangalia (1) Kufuatilia Ukamilishaji wa Miradi; ambapo Uwezeshaji na Ushirikishwaji ni Mkakati wa Kutiliwa Maanani katika ukamilishaji wa Miradi inayowekezwa nchini. Wawekezaji wenye Miradi kwenye Sekta ya Mafuta na Gesi wanapaswa kuheshimu Uwezeshaji na Ushirikishwaji kuwa ni Thamani Kubwa katika kupendekeza miradi itakayowekezwa nchini kwenye mafuta na gesi; aidha Uwezeshaji na Ushirikishwaji ukihusishwa kwenye Tathmini za miradi itawawezesha Wawekezaji hao; ikiwa ni pamoja na kupata faida ya ushindani kwenye Asasi za Ubia wakati zikihitaji leseni kwa kupewa leseni kwa urahisi na pia kusaidia zaidi wakati wa majadiliano ya Mikataba na nchi yetu.

(2) Kusaidia Biashara au Malengo ya Sera za Umma; ambapo Kanuni za Uwezeshaji na Ushirikishwaji kama vile, Utoaji taarifa, unapaswa kuzingatiwa wakati ambapo husaidia sana biashara na malengo ya sera za umma kuundwa vyema. Kila Mpango Mkakati wa Uwezeshaji na Ushirikishwaji unapaswa kuwa na Viashiria sahihi vinavyoruhusu kampuni kupima utekelezaji wa miradi yake dhidi ya malengo. Kukusanya takwimu sahihi pia kunasaidia kukidhi mahitaji ya utoaji taarifa; na (3) Kuwepo kwa Matumaini; ambapo kutokana na mazingira ya ushindani unaosababisha kushuka kwa uzalishaji (kwa sababu mafuta ni rasilimali inayokwisha baada ya kuvunwa) ukilinganisha na kukua kwa uuzaji wa rasilimali za nishati; kampuni katika Sekta ya Mafuta na Gesi zinakabiliwa na matumaini makubwa kuwa uzalishaji wa mafuta na gesi utapunguza kwa kiasi kikubwa athari mbaya za kiuchumi, kijamii na kisiasa, na itakuwa ni chanzo kikubwa cha kodi, mrabaha na kuwa moja ya nguzo ya kutekeleza Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

Page 2: UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT

Wananchi wa ndani ya nchi ikiwa ni pamoja na wanaozunguka maeneo ya utafiti na uchimbaji hawaepukiki kuwa na matumaini makubwa juu ya miradi iliyokaribu nao. Hii ni kwa vile Uwezeshaji na Ushirikishwaji unaongezeka thamani kwenye Mnyororo wa Thamani wa Tasnia ya Uziduaji na huzalisha Uchumi shirikishi na endelevu kupitia kwenye mseto wa Uchumi na nafasi za ajira. Mfano; Jamii ya watu wa Mtwara baada ya kusikia upatikanaji wa mafuta na gesi walikuwa na matumaini makubwa ya kuondokana na wimbi la Umaskini kwa kuwa na matumaini ya kushirikishwa na kuwezeshwa kwenye sekta hiyo.

Picha Na 1: Jamii Inayozunguka Maeneo ya Rasilimali za Mafuta na Gesi Wanapokuwa na Matumaini Makubwa

Uwezeshaji na Ushirikishwaji unapaswa kufuatiliwa na kusimamiwa kwa karibu ili rasilimali zetu ziende sambamba na uchumi wa Viwanda. Katika hilo, Vifungu Na 220 na Na 221 vya Sheria ya Petroli Na 21 ya Mwaka, 2015; Wenye Mikataba na Wakandarasi wa Kati wanalazimika kuwasilisha Taarifa juu ya Utekelezaji wa Ajira zao, Mafunzo na Manunuzi na Programu ya Kuendeleza Wauzaji wa ndani, ikiwa ni pamoja na hatua zilizotekelezwa na wenye Leseni kuziba mianya ya Mafunzo iliyobainika kwenye Mamlaka za Udhibiti. Wenye leseni wanao wajibu wa kutoa taarifa juu ya Programu za Manunuzi ya Wakandarasi wa Kati. Hii inasaidia kulinda ongezeko la thamani kwenye Uwezeshaji na Ushirikishwaji ili Ongezeko

Page 3: UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT

hilo liwe ni sehemu ya Mnyororo wa thamani wa Uchumi wa Viwanda tunaoutarajia. Aidha, jukumu hilo limebainishwa katika Ibara ya 21 (f) ya Mkataba wa Uzalishaji na Ugawanaji Faida (MPSA wa Mwaka 2013) ambao unawataka Wakandarasi kuwasilisha Mpango wa Mwaka wa Uwezeshaji na Ushirikishwaji, ambao unapaswa kuwasilishwa na Programu ya Mwaka ya Kazi na Bajeti kwa ajili ya Shughuli zinazohusiana na Petroli.

Maendeleo ya Nguzo Viwanda ni Mhimili mkubwa wa Kukuza Ongezeko la Uwezeshaji na Ushirikishwaji. Hii itategemea Zaidi uwepo wa Uwazi na Utawala Bora katika Myororo wa Uwezeshaji na Ushirikishwaji. Wakandarasi wanapaswa kufuatiliwa kwa karibu kupitia kwenye Taarifa zao zilizo wazi na kuhakikiwa na Mtaalamu Huru. Kwa mujibu wa Ibara ya 21(g) ya Mkataba wa Uzalishaji na Ugawanaji Faida (MPSA, wa Mwaka 2013) Mkandarasi analazimika kuwasilisha Taarifa ya Mwaka ambayo itahakikiwa na Mtaalamu Huru mwenye Ujuzi na inatakiwa kujumuisha maelezo ya shughuli za Mkandarasi; mbali na Majukumu ya Ugawanaji Faida ya Uzalishaji na ya Kibajeti ndani ya Mkataba na athari zake kwenye Uwezeshaji na Ushirikishwaji na Umuhimu wake katika Kuongeza thamani ya ndani ya nchi.

Mikataba ya Utafiti na Uchimbaji wa mafuta na gesi ni eneo lenye utata katika dhana ya Kuwawezesha na Kuwashirikisha Watanzania. Hata hivyo, Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) linapaswa kutekeleza kwa ufanisi utekelezaji wa vifungu vya sheria za Uwezeshaji na Ushirikishwaji ndani ya Mikataba. Hii itawezesha raia wa Tanzania kuweza kushiriki kikamilifu na kufaidika na fursa katika sekta ya mafuta na gesi kama vile ajira na uzalishaji wa bidhaa na huduma katika Tasnia ya Uziduaji. Ugawanaji wa Faida hutokana na Jumla ya Uzalishaji, ambao pia hutoa Mrabaha wa asilimia 5% nje ya Bahari Kuu na asilimia 12.5% ndani ya Bahari Kuu. Ukomo wa Marejesho ya gharama kwa Tanzania ni kati ya asilimia 60% na asimilia 70%. Ukomo huu hutumika pale tu ambapo hakuna Uchimbaji wa pamoja baada ya mgao wa marejesho ya gharama za Mkataba kwa mujibu wa Ibara ya 10 (f) (iii) ya Mkataba wa Uzalishaji na Ugawanaji Faida (MPSA, wa Mwaka, 2008). Baada ya marejesho ya gharama anayojirejeshea Mkandarasi ndipo hupatikana faida inayogawiwa kati ya Mkandarasi na TPDC kwa utaratibu wa kupunguza Mgao kwa kiwango cha Uzalishaji. Faida hiyo hutozwa asilimia 30% ya Kodi ya Mapato; na Pato baada ya tozo hutozwa kodi ya zuio kwa asilimia 10% ambayo ni Gawio na Riba (Kama ilivyooneshwa katika Picha Na 2).

Page 4: UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT

Ibara ya 24 (b) ya Mkataba wa Uzalishaji na Ugawanaji Faida (MPSA wa Mwaka, 2004) unaipa TPDC haki ya kufanya ukaguzi wa taarifa za hesabu kwa Kampuni za Kimataifa za Mafuta kwa kuhakiki gharama zilizowasilishwa na Kampuni hizo kama gharama hizo wanastahili kujirejeshea au la. Kiambatanisho D cha Mkataba wa Mwaka, 2004 kinaitaka TPDC kuhakiki marejesho ya gharama za utafiti ndani ya miaka miwili baada ya mwaka wa kuanza kufanya shughuli zinazohusiana na Petroli. Hii ni kabla ya kipindi cha Mwaka Mmoja wa kipindi ambacho Wakandarasi kama walipa kodi wanapaswa kukadiriwa kodi zao na ni kipindi cha kabla ya Miaka Mitatu wanayopaswa kuhifadhi rekodi za hesabu zao kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato Sura ya 332.

Iwapo TPDC haitaweza kuhakiki marejesho ya gharama, ina maana Kampuni hizo za Mafuta za Kimataifa zitainyima Tanzania manufaa yanayoweza kupatikana kwenye sekta hiyo. Ikiwa ni pamoja na thamani halisi ambayo ingepatikana Kwenye mnyororo wa Uchumi wa Viwanda. Uhakiki wa marejesho ya gharama hizo una lengo la kuipatia Tanzania manufaa ya hali ya juu ambayo yanategemewa kupatikana katika faida inayopatikana kwenye mafuta na gesi baada ya Kuondoa gharama za uwekezaji uliyofanywa na Kampuni hizo wakati wa Utafiti. Hata hivyo, kwa sasa hakuna Sera, Kanuni, na Mwongozo ambao unaweza kusaidia na kushinikiza utekelezaji wa Uhakiki wa gharama za kurejeshwa. Ili kuziba mwanya huo, Muundo wa Utumishi wa TPDC unapaswa kuelezea kuhusu Uhakiki wa gharama za marejesho na kubainisha kazi zinazostahili kufanywa. Hii ni pamoja na kubainisha hatua za kuhakikisha kuwa Uhakiki wa gharama za marejesho zinazotumika na Kampuni za Kimataifa za Mafuta unafanywa kwa muda unaostahili kwa mujibu wa Mikataba ya Uzalishaji na Ugawanaji Faida (PSAs). Kunapaswa kuwepo pia na mfumo wa Usimamizi na Tathmini kwa ajili ya mapitio na maboresho ya kazi za Uhakiki wa gharama za marejesho; aidha, Wizara ya Nishati na Madini inapaswa kufuatilia Uhakiki huo. Aidha, Maafisa Dawati wa TPDC wanapaswa kuwa na Majukumu ya Kazi yanayohusisha Uwezeshaji na Ushirikishwaji. Wana Sayansi wa Jiolojia waliobobea kwenye shughuli za Utafiti na Uchimbaji wanapaswa kupewa uwezo unaoweza kupanua wigo wa elimu yao Zaidi kuhusisha Uwezeshaji na Ushirikishwaji kwenye Sekta ya Mafuta na Gesi. Uhakiki wa gharama zilizotumika na Kampuni za Mafuta za Kimataifa unafanywa na Kurugenzi ya Ukaguzi wa Ndani ya TPDC kuanzia Mwaka 2008, ikiwa ni pamoja na shughuli zake muhimu za ukaguzi wa ndani na mifumo ya kudhibiti ikiwa ni pamoja na gharama za TPDC.

Page 5: UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT

Picha Na 2: Mgawanyo wa Faida Kwa Mujibu wa Mikataba na Mapato ya Serikali Kwenye Sekta Ya Mafuta

Wizara ya Nishati na Madini inapaswa kuandaa Mipango kuhakikisha kuwa Watanzania wanaajiriwa na Kampuni za Mafuta za Kimataifa ikiwa ni pamoja na Wakandarasi wa kati kwa hali ya juu inayokidhi mahitaji kama ilivyobainishwa kwenye Mikataba. Hii inapaswa kuwekwa kwenye Mpango Mkakati ili kuonesha shughuli zote za Kujenga Uwezo kwa Watanzania ili waweze kupata fursa ya kuajiriwa na Kampuni za Mafuta za Kimataifa na Wakandarasi wa Kati. Kwa upande mwingine Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TPDC ambaye ni mmiliki wa Leseni wanapaswa kufuatilia kwa karibu shughuli za Wakandarasi wa Kati kuhakikisha kuwa Watanzania wanaajiriwa. Na hii itawezekana tu pale ambapo TPDC wana Mikataba na Wakandarasi hao ili Shirika hilo liwajibike moja kwa moja kufuatilia badala ya kuziachia Kampuni za Mafuta za Kimataifa kufanya ufuatiliaji huo.

Kunapaswa kuwepo na uratibu wa wazi na Mkakati wa mwasiliano kati ya Wizara ya Nishati na Madini na TPDC kuhusu Uwezeshaji na Ushirikishwaji. Wizara ya

Page 6: UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT

Nishati na Madini ndiyo Taasisi inayoongoza Sekta ya Mafuta na Gesi, hivyo inalo jukumu la kuratibu na kuwasiliana na Wadau wengine katika Tasnia ya Uziduaji katika masuala yanayohitaji mahusiano baina yao. TPDC inapaswa kuandaa mfumo wa Ufuatiliaji na Uhakiki kwa ajili ya kufanya marejeo ya shughuli ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Kampuni za Mafuta za Kimataifa kwa ajili ya matakwa yanayohusiana na Uwezeshaji na Ushirikishwaji. Aidha, Kurugenzi inayohusiana na Bahari Kuu ya TPDC inao wajibu wa kufuatilia utekelezaji wa Mikataba ya Mafuta kwavile TPDC pia ni mmiliki wa Leseni. Idara hii inayo Mipango Kazi ya kufuatilia kuhusu Uwezeshaji na Ushirikishwaji na hii ni pamoja na Bajeti za Kampuni za Mafuta za Kimataifa. Kurugenzi hii pia inafanya kazi kama hizi kwa upande wa Mikataba.

Kuna Changamoto Zinazoweza kujitokeza katika kutekeleza Sera ya Uwezeshaji na Ushirikishwaji ya Mwaka, 2014 ambazo ni; (1) Ukosefu wa Uwezo wa Raslimali Watu na Ujuzi wa Elimu; ambayo ina mitazamo miwili (i) Mitazamo kwa Nchi zinazoendelea; Ukosefu wa Ujuzi unazuia kuwajumuisha wafanyakazi wa ndani yaani Watazania kwenye Tasnia ya Uziduaji na kuendeleza Viwanda Msingi unaohitajika kusambaza manufaa ya Sekta ya Mafuta na Gesi kwenda kwenye sekta zingine; (ii) Mtazamo kwa Kampuni za Uchimbaji; Ukosefu wa ujuzi unaweza kusababisha ucheleweshaji wa miradi mipya, kuongeza gharama na hata kudhoofisha malengo ya Uwezeshaji na Ushirikishwaji. Ni Bahati kuwa pamoja na mambo mengine, mnamo Mwezi Mei, 2015 Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ilitoa Rasimu ya Mkakati kwenye Asasi ya Afrika inayojishughulisha na Maliasili (African Natural Resources Center) iliyoanzishwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Mwaka, 2013 kuhakikisha kunakuwepo na Programu ya Ujenzi wa Uwezo kwa nchi Wananchama wa Benki hiyo. Maeneo kama Maji, Misitu, Ardhi, Uvuvi, Mafuta, Gesi na Madini ndiyo yaliyoangaliwa changamoto zake. Tatizo kubwa la Sera ya Uwezeshaji na Ushirikishwaji ni kuwa; uwepo wa Ujuzi wa watu wa ndani ya nchi mara nyingi huwa nyuma ya mahitaji ya Tasnia yenyewe. Kampuni nyingi za mafuta na gesi zimekuwa zikitumia hali hii ya kuchelewa kwa Ujuzi kuwa kisingizio cha kutotekeleza Sera hiyo.

Changamoto ya pili ni Miundombinu Mibovu: Miundombinu dhaifu inazuia upanuzi wa Viwanda Msingi katika uzalishaji. Huduma za jamii kama vile barabara, reli na usafiri wa ndege, mawasiliano, usambazaji wa umeme na maji unajenga mazingira ambayo yanawezesha biashara kuendelea na kuleta tija kwa ujumla. Uhaba wa Miundombinu hiyo ya Jamii ya msingi hapa Tanzania unazuia uhusiano wa Maendeleo kati ya Tasnia ya Uziduaji na Sekta zingine za Uchumi. Changamoto

Page 7: UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT

ya tatu ni Udhaifu wa Viwanda Msingi na Ujenzi wake Thabiti; Tasnia ya Uziduaji inapaswa kujikita katika uwezo wa ndani uliopo kwenye Viwanda vya uzalishaji bidhaa na huduma. Hata hivyo, katika nchi nyingi Viwanda Msingi ni dhaifu, ni mdogo, una teknolojia dhaifu, ufadhili wa fedha na taarifa dhaifu, na hivyo hauna ushindani katika mazingira ya Tasnia ya Kimataifa. Serikali ina vitu viwili inaweza kutumia katika kuhakikisha kuwa Mafuta, na gesi zinachangia Kukuza Viwanda Msingi. (1) Mrabaha na Ukusanyaji wa Mapato ya Kodi. Hii ni kwavile, faida ya mafuta na gesi ni sehemu ya Wigo wa Kodi ambao unaipa Serikali mapato yanayowekezwa kwenye miundombinu na miradi mingine inayoweza kusaidia kuendeleza na kupanua Viwanda Msingi. (2) Uwezeshaji na Ushirikishwaji ambapo Mkakati huu unapewa kipaumbele kwa Watanzania na Kampuni za ndani ya nchi. Serikali inahitaji eneo hili liwe kubwa katika Manunuzi ya bidhaa na huduma kwenye soko huria. Kuweka upendeleo kama vile bei za chini kwa wazalishaji wa ndani wakati wa kutoa zabuni.

Aidha kuna Changamoto ya Nne ambayo ni Utawala Mbovu na Mazingira ya Biashara Duni; Nchi zenye maliasili nyingi zinakosa mazingira wezeshi kuinua ujenzi wa biashara za ndani. Uwezeshaji na Ushirikishwaji ukifanywa vizuri unasaidia Kukuza Maendeleo ya Viwanda kupitia kwenye hatua ya mpito yenye Uchumi mdogo kwenda kwenye Uchumi jumuishi katika Uchumi wa Kimataifa. Matokeo ya Uwekezaji kutoka nje ambao ni mtapakao wa matokeo ya Uchumi unaweza kusababisha Viwanda vya ndani kukua na kujifunza kwa kuingia kwenye ushindani wa kimataifa na kwenye viwango vya kimataifa. Hata hivyo, rushwa inaharibu heshima ya biashara katika nchi na inazifanya Kampuni za kigeni kuvunja Sheria za nchi. Mfano; huko Angola, Watumishi wa Umma wanapata faida kubwa kutoka kwenye Sera ya Uwezeshaji na Ushirikishwaji ambayo inazitaka Kampuni za kigeni kuwa na Ubia na Kampuni za Wazawa katika kupata leseni. Kuna ushahidi zaidi kuwa Kampuni za Mafuta za kigeni zinawalipa ada kubwa Watumishi wa Umma wa Angola na Wasomi katika fani ya Uchumi kuunda Kampuni zinazokuwa mstari wa mbele kupata leseni huku zikikosa uwezo wa kitaalamu na kifedha kufanya shughuli za mafuta. Viongozi Wakubwa wa Serikali ya Angola ndiyo wanadhibiti na kumiliki Hisa za Kampuni zilizo kwenye Ubia. Ukweli ni kuwa Ukosefu wa Muundo wa Uhusiano na Uwezo mdogo wa Kitaasisi na ukosefu wa Utawala bora ni tatizo kubwa linalozuia Sera ya Uwezeshaji na Ushirikishwaji kuleta Maendeleo halisi ya Uchumi Barani Afrika.

Page 8: UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT

Picha Na 3: Tarakibu (Model) Ya Uendelezaji Wa Uwezeshaji Na Ushirikishwaji Kwenye Tasnia Ya Uziduaji

Tarakibu katika Picha Na 3 inaonesha jinsi ambavyo mambo manne yaliyo nje ya Mchoro kama yakiingiliana yanaweza kuleta thamani Kwenye Tasnia ya Uziduaji nchini Tanzania. Maendeleo ya Uwezeshaji na Ushirikishwaji yameoneshwa katikati ya Mchoro. Sera za ndani ya Nchi zimejikita Kwenye sekta za Uchumi pamoja na Tasnia ya Uziduaji. Sera hizi zinajumuisha Sera za Umma na za Viwanda ambazo zinadumu pale tu palipo na Maendeleo ya Uchumi Endelevu; Kwa upande wa Miundombinu ya ndani ya Nchi masuala kama ya Teknolojia ya habari, mahitaji ya kampuni za ndani ya nchi, Viwango, na elimu katika Tasnia ya Uziduaji ni eneo muhimu sana; Mazingira ya ndani ya nchi ni jambo ambalo Sera zote za ndani, Uwezo wa ndani, Miundombinu ya ndani na mambo mengine yanahifadhika. Mfano mzuri ni Mazingira ya Uchumi Jumla ambayo ni muhimu kwa uwekezaji hasa ukiangalia masuala ya bei za ndani, masuala ya kubadilisha fedha za kigeni, riba n.k; Uwezo wa ndani ya Nchi unahusisha elimu, ujuzi na Maendeleo ya utaalamu, uhamishaji wa teknolojia, Utafiti, uzalishaji wa ndani na huduma zitolewazo na Kampuni za ndani ya Nchi; Aidha, kiwango cha Uwezeshaji na Ushirikishwaji kinategemea Zaidi Ubora wa mahusiano kati ya Masuala ya Kisiasa, Miundombinu, na Ukuaji wa Viwanda pamoja na athari zake. Uwezeshaji na Ushirikishwaji unahitaji mazingira na hali inayoweza kufikiwa kwa mafanikio. Kuna mambo matatu yanayofafanuliwa katika fasihi za utafiti; (1) Sera Sahihi (2) Muundo Sahihi na (3) Uwezo wa Tasnia ya ndani. Maeneo haya ndiyo yanayobebwa na Tarakibu (Model) Kwenye Picha Na 3.

Page 9: UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT

Nchi nyingi zilizoendelea, katika kipindi chao cha awali cha Maendeleo ya Viwanda, ziliweka hatua za kulinda Viwanda vyao ikiwa ni pamoja na Uwezeshaji na Ushirikishwaji, ambao unaweza kusaidia Maendeleo kwa Viwanda vya ndani dhaifu, kusaidia uhamishaji wa teknolojia, na hivyo kuziba mwanya mkubwa wa utofauti wa teknolojia kati ya nchi zinazoendelea na zilizoendelea. Uwezeshaji na Ushirikishwaji unaongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa ndani na unaleta ajira kwa sababu Viwanda vichanga vinahitaji kulindwa na nguvu ya soko dhidi ya Kampuni za Kimataifa; hivyo ufa unaojitokeza unahitaji kuzibwa kwa kuweka mahusiano ya kimaendeleo baina ya nchi hizo. Hakika kama kutakuwa na Ufa katika kutekeleza Sera ya Uwezeshaji na Ushirikishwaji ya Mwaka, 2014 itabaki kuwa Jeneza la Uchumi wa Viwanda.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA”