2
BULLETIN ambapo mkoa wa Kagera umeweza kuleta Skau wapatao 186 na mkoa wa Kilimanjaro 125 hii ni kwa mujibu wa Kamishna wa Skau wa Mkoa huo. Akielezea sababu zilizopelekea wao kuweza kuleta Skau wengi zaidi Padri Prochesus Mtungi ambaye pia ni Kamishna wa Skau mkoa wa Kagera alisema kuwa na ushirikiano mzuri na umoja walionao ka ya viongozi wa Skau wa Skau mkoani Kagera kwa usimamizi mzuri wa watoto na vijana mashuleni. Hongera Mama Afrika kaka kum- bukumbu ya siku ya kuzaliwa kwako. Rashidi (kushoto) na Helena (kulia) (kibaha- Pwani) wakiwa Skau Pr- Lab studio kwa mahojiano. Picha na: Sassi Salim na Fransco Nyoni JeWajua siri ya Skauti Kutoka Mbeya na Pikipiki hadi Dodoma..?

ULLETIN - scout.org Special... · ULLETIN ambapo mkoa wa Kagera umeweza kuleta Skauti wapatao 186 na mkoa wa Kilimanjaro 125 hii ni kwa mujibu wa Kamishna wa Skauti wa Mkoa huo

  • Upload
    others

  • View
    11

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

BULLETIN

ambapo mkoa wa Kagera umeweza kuleta Skauti wapatao 186 na mkoa wa

Kilimanjaro 125 hii ni kwa mujibu wa Kamishna wa Skauti wa Mkoa huo.

Akielezea sababu zilizopelekea wao kuweza kuleta Skauti wengi zaidi Padri

Prochesus Mtungi ambaye pia ni Kamishna wa Skauti mkoa wa Kagera

alisema kuwa na ushirikiano mzuri na umoja walionao kati ya viongozi wa

Skauti wa Skauti mkoani Kagera kwa usimamizi mzuri wa watoto na vijana

mashuleni.

Hongera Mama Afrika katika kum-

bukumbu ya siku ya kuzaliwa

kwako.

Rashidi (kushoto) na Helena (kulia)

(kibaha- Pwani) wakiwa Skauti Pr-

Lab studio kwa mahojiano.

Picha na: Sassi Salim na Fransco

Nyoni

Je…

Wajua siri ya Skauti

Kutoka Mbeya na Pikipiki hadi

Dodoma..?

Skauti PR Lab wakiweka

mabango mjini Dodoma.

Samina Rajab na Devina Adosi

SKAUTI WAMIMINIKA DODOMA

Skauti Morogoro na Mbeya

waweka historia

Kagera watiafora

Katika hali ya kufurahisha na ku-

washangaza wengi Skauti wameamua

kuweka historia ya aina yake hapa Tan-

zania ambayo haijawahi kutokea. Skauti

hao ambao wamedhaminiwa na Mkuu

wa Morogoro pamoja na SAT

(SUSTAINABLE AGRICULTURE TANZANIA)

hawakusita kuonyesha furaha yao na

shahuku waliyonayo ya kutaka kuanza

na kumaliza safari yao ili lengo lao la

Ujasiri liweze kutimia na kuweka historia

ya kipekee ambayo haijawahi kutokea

katika Skauti hapa nchini.

Akizungumza na Pr Lab Tanzania

kiongozi wa watembea kwa miguu

kutoka Morogoro hadi Dodoma Rova

Aloyce Zengwe ambaye pia ni askari

wa jeshi la ukoaji na zimamoto Tanza-

nia alisema kuwa ujumbe ambao wal-

ikabidhiwa na Dkt. Steven Kabwe

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kupitia

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa

Tanzania ni kupiga vita mimba za

utotoni,kupambana na kuzuia rush-

wa,kupambana na madawa ya

kulevya,kutoa elimu ya kilimo endele-

vu kilimo ambacho hakitumii dawa

wala mbolea zenye kemikali na kutoa

elimu juu ya kuwafichua wahalifu.

Naye Rova Allen J. Mpande alisema

kuwa” Kila kitu kinahitaji uthubu-

tu,huwezi kufanya jambo bila kuthubu-

tu,hii sherehe ya Skauti wote,hivyo

tunapaswakufanya yale yanayoweze-

kana kufanywa kwa wakati huu ili jamii

na Tanzania nzima ijue kuwa

tunaazimisha miaka 100 ya Skauti”

Skauti hawa wamefika Dodoma

tarehe 21 mwezi Julai 2017 na

wametembea umbali wa kilomita

264.4.

Wakati huo huo ndugu Nsubili Solo-

mon Kibopile kiongozi wa Skauti St.

Mary International Mbeya na Kaimu

naibu kamishna wa Skauti Mkoa wa

Mbeya. Aliamua kutumia usafiri wa

pikipiki kutoka wilaya ya Kyela Mkoa

wa Mbeya hadi Dodoma iwe moja ya

historia na kuweka kumbukumbu hasa

wakati huu wa kuadhimisha miaka 100

ya Skauti Tanzania. Changamoto am-

bazo amekutana nazo njiani ni pamoja

na kuwa baadhi ya madereva wengine

hawapo makini barabarani, wakati wa

usiku kulikuwa na tatizo kidogo hasa

kwenye maeneo ambayo yana

mashimo, ama madereva wengine

kuwasha taa na kuweka mwanga

mkali wakati wa usiku ama mwanga

mdogo sana. Umbali aliotumia kutoka

Kyela hadi Mbeya ni kilomita 124,

Mbeya hadi Iringa kilomita 340 na

Iringa hadi Dodoma ni kilomita 260

jumla ametumia kilomita 724.

Tusiwe waoga tuwe wajasiri kama

alivyotembea yeye mchana na usiku

na kuweza kutoa huduma mbali mbali

njiani, pia wasiokuwa Skauti wajiunge

na Skauti kwani ndugu Kibopile ana

amini Skauti imemjengea ujasiri na

uthubutu huu. Aliondoka Kyela tarehe

20 Julai 2017 na kufika Dodoma

tarehe 21 Julai 2017 saa kumi nambili

jioni. Katika safari hiyo aliongozana na

Skauti mwingine anayejulikana kwa

jina la Ayubu. Skauti wengine wakuto-

ka Mbeya wanakuja kwa basi na wa-

tawasili siku ya tarehe 22 julai 2017

(mapema leo).

Wakati huo huo Skauti kutoka Mkoa

wa Kagera na Kilimanjaro wametiafora

kwa kuleta Skauti wengi Zaidi ukilin-

ganisha na Skauti wa mikoa mingine,

PR LAB

UKIWA NA HABARI ZA

SKAUTI, TAFADHARI WASILI-

ANA NA KITENGO CHA MA-

HUSIANO NA UMMA (PR

LAB) SKAUTI TANZANIA

+255-789-012-364

TUMA HABARI NA PICHA ZA

MATUKIO YA SKAUTI PO-

POTE TANZANIA.

tanzaniascout.org