271
1 25 MEI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE ________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Thelathini na Nne - Tarehe 25 Mei, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Randama za Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka 2013/ 2014. HOJA ZA SERIKALI Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2013/2014 Wizara ya Nishati na Madini (Majadiliano yanaendelea) SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea pale tulipoachia siku ile. Sasa nitamwita Mheshimiwa Devotha Likokola, atafautiwa na Mheshimiwa Josephine Chagula, Mheshimiwa Sylvester Kasulumbayi, Mheshimiwa Hasnain Mohamed Murji, Mheshimiwa Lucy Mayenga, Mheshimiwa Abdul Mteketa, Mheshimiwa Ezekiel Maige, Mheshimiwa

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

  • Upload
    others

  • View
    8

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

1

25 MEI, 2013

BUNGE LA TANZANIA________

MAJADILIANO YA BUNGE________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Thelathini na Nne - Tarehe 25 Mei, 2013

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:-

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI:

Randama za Makadirio ya Matumizi ya Wizara yaArdhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka 2013/2014.

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2013/2014Wizara ya Nishati na Madini

(Majadiliano yanaendelea)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea paletulipoachia siku ile. Sasa nitamwita Mheshimiwa DevothaLikokola, atafautiwa na Mheshimiwa Josephine Chagula,Mheshimiwa Sylvester Kasulumbayi, Mheshimiwa HasnainMohamed Murji, Mheshimiwa Lucy Mayenga, MheshimiwaAbdul Mteketa, Mheshimiwa Ezekiel Maige, Mheshimiwa

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

2

25 MEI, 2013

James Lembeli, Mheshimiwa Raya Ibrahim Khamis naMheshimiwa Brig. Gen. Hassan Ngwilizi. Kwanza niishie hapohalafu tutaendelea baadaye. Mheshimiwa Likokola!

MHE. DEVOTHA M. LIKOKOLA: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuchangia Wizara hii.Kwanza kabisa, niungane na Wabunge wenzangu, kuungamkono hoja ya Wizara ya Nishati na Madini. Ninashukuru sanana ninaipongeza Wizara hasa Mheshimiwa Waziri na NaibuMawaziri, kwa kazi nzuri wanayoifanya, lakini pia wamewezakutengeneza timu nzuri sasa Wizarani kwa ajili ya kuendelezamasuala ya Nishati na Madini katika nchi yetu. Ili maendeleoya nchi yoyote yaweze kufikiwa, yanahitaji rasilimali watu,lakini pia yanahitaji rasiliamli fedha.

Mheshimiwa Spika, suala la rasil imali watu,tunashukuru Wizara imejipanga vizuri, imetengeneza taasisinzuri, ambazo zinaweza kuleta mafanikio makubwa yamageuzi katika masuala ya nishati katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, suala ambalo ninatakatuliongelee leo kwa kina ni la rasilimali fedha. Wabunge naWananchi wote wa nchi hii, kwa mwaka huu tuna ajendamoja kubwa ya umeme vijijini. Hakuna Mbunge ambayehataki vijiji vyake vipate umeme na hakuna Diwani ambayehataki vijiji vyake vipate umeme. Serikali yetu imefanya jambozuri, imetengeneza Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Mheshimiwa Spika, ninaomba Mwongozo kwako ilituweze kuhakikisha kuwa, REA inapata fedha za kutosha naumeme vijijini uende wa kutosha; tutoe hoja gani? Ni suala lakusikitisha sana, leo Watanzania wengi wako vijijini, asilimia80 wako vijijini na watu hawa hawana umeme, Kamatiiliiomba REA ifanye makadirio ili umeme vijijini uweze kwendawangehitaji kiasi gani. Wametoa takwimu zao kwambawanahitaji shilingi bilioni 800 na sisi ndiyo tuna wajibu wakugawa bajeti ya nchi hii, leo tunawapa bilioni 150, bilioni650 atazitoa nani?

Leo ninaomba sisi Wabunge kama kweli tuna wajibu

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

3

25 MEI, 2013

wa kupitisha bajeti ya nchi hii vizuri ili Wananchi wanufaike,tutoe hoja gani i l i umeme vij i j ini uweze kwenda.Hatutakubaliana na hoja yoyote ambayo itaendana naWizara hii bila kuongeza pesa za REA. REA waongezewe pesa,umeme vijijini uweze kwenda. Mheshimiwa Waziri, ametamkahapa, bajeti yake ina takwimu na figure; hizo takwimu nafigure kama hazina pesa zina maana gani? Lazima tuwewakweli na hapa tuliuliza Wabunge tunataka pesa za REAzitoke wapi? Tuliishauri Serikali; kuna hela za mawasiliano, kunahela za mafuta, kwa nini hela hizi haziendi REA?

Mheshimiwa Spika, ninaomba Mheshimiwa Waziriatakapojibu, atueleze kinagaubaga kwamba kwa nini REAinaendelea kupata fungu dogo na inaendeleakuwachanganya Wataalamu wa REA, hawawezi kufanyakazi nzuri bila kupata fedha za kutosha? Wana nia nzuri, wanamoyo safi, lakini kulingana na ufinyu wa bajeti wanayopata,wanashindwa kuendeleza umeme vijijini.

Ninaomba nizungumzie umeme wa kutokaMakambako kwenda Songea. Ajenda hii ya umeme wakutoka Makambako kwenda Songea ni ya miaka mingi tanguwengine hatujawa Wabunge, tangu wengine hatujazaliwaumeme wa Makambako – Songea, Mtwara Corridor tunasikiahabari hizi. Lakini kila siku kwenye Bajeti ya Serikali tunasikiaooh kuna Mtwara Corridor kuna umeme wa Makambako –Songea; mbona hautekelezeki?

Bajeti hii pia umeme wa Mkambako – Songeaimewekwa lakini sisi tunataka utekelezaji. Safari hiininakuomba Mheshimiwa Spika, kwa sababu na weweumeme huu utakugusa katika Jimbo lako la Njombe,tuungane mkono Wabunge wa Ruvuma na Wabunge waNjombe, kuhakikisha kuwa kipaumbele ni Mradi huu waUmeme wa Makambako – Songea. Wananchi wa Songeawanapata shida sana, suala la umeme limekuwa ni kerokubwa.

Mheshimiwa Spika, Umeme Vijijini; Wilaya ya Nyasaambako kuna Bandari kubwa ya Mbamba Bay, hakuna

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

4

25 MEI, 2013

umeme. Ninawaomba REA mfanye kila linalowezekana, ileBandari haiwezi kufanya kazi vizuri kama hakuna umeme.

Mheshimiwa Spika, hapa Bungeni tunasikiakinagaubaga Mikoa mingine vijiji vyao vina umeme na ni vijijivingi watu tumefanya mahesabu kuna Mikoa mingine vijiji30, vijiji 20, vijiji 60, lakini Mkoa wa Ruvuma ni vijiji viwili tu. Mkoamzima wa Ruvuma ni Peramiho umeme umeenda namasuala ya Chipole. Nawapongeza sana wale Masista, bilaule Mradi wa Masista Chipole tungekuwa Mkoa wa Ruvumakatika vijiji vyetu ni Kijiji cha Peramiho tu ndicho kingepataumeme; kweli hii ni haki?

Mheshimiwa Spika, ninaomba nikuulize hii ni haki;Mkoa wa Ruvuma ambao ndiyo wazalishaji wakubwa wachakula kwa nchi hii, wanalisha nchi hii; umeme hakunakatika vijiji vyao vyote; kweli jamani siyo vizuri! MheshimiwaWaziri, ninakuomba ajenda ya Mkoa wa Ruvuma ni lazimauipe kipaumbele, kwa sababu haiwezekani, Mkoa waRuvuma ni watu ambao wamejikita katika uzalishaji naimekuwa bahati mimi kuwepo katika Kamati hii, tumekwendakutembelea vijiji vingine umeme umeenda Wananchihawawezi kuunganisha, hawana uwezo. Mkoa wa Ruvuma,Wananchi wake wana uwezo, pelekeni umeme Wananchiwataweka, wataunganisha katika nyumba zao kwa sababuwale Wananchi ni wazalishaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninaomba nizungumzie masualamazima ya Vij i j i vya Mkoa wa Ruvuma, ambavyowakipelekewa umeme kwa haraka wangeweza kusaidikasana. Wilaya ya Tunduru, umeme uko pale katikati kidogo tu,lakini tunahitaji uende maeneo mbalimbali. Tuna suala zimala makaa ya mawe ya Ngaka; pale pana matatizo, Serikaliiliahidi kuwalipa fidia watu, lakini wengine walilipwa kidogona wengine hawakulipwa, imesababisha mpaka tarehe 30mwezi wa nne mradi ule ulifungwa kwa muda. Serikaliimeahidi mpaka tarehe 15 mwezi wa sita wale watuwatakuwa wameshalipwa. Ninaomba Serikali msifanyemchezo katika hilo, hatutaki machafuko yatokee katika nchiyetu.

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

5

25 MEI, 2013

Ninashukuru sana kwa umeme wa Namtumbo;umeme umewaka lakini umewaka pale Namtumbo tuKindakindaki na tunafurahi sana Wananchi wa Namtumbokuwasha umeme pale, lakini tunataka umeme uendeNamabengo, uende Suluti, uende vijiji vingine vya Litola, vijijimbalimbali mpaka Lumecha, mpaka Songea. PaleNamtumbo sasa hivi ni rasilimali ya Taifa, ninyi wenyewemnajua Namatumbo kuna nini; kwa hiyo, kama umemehauingii, itakuwa ni tatizo kubwa sana.

Mheshimiwa Spika, kuna Miradi ya Solar, ninaiombaWizara ieleze kinagaubaga ili mashule yetu yaweze kupatawatoto. Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringawaliungua kwa ajili ya umeme wa kusomea. Kwa nini mashuleyetu yasiwekwe solar mpaka tupoteze watoto? Umeme wasolar ungeweza kuwasaidia watoto waweze kusoma katikamabweni yao.

Mheshimiwa Spika, ninaomba Miradi mingine tuipekipaumbele ili tuweze kuendeleza gurudumu letu la masualaya Nishati mbele. Kama kweli tunataka maendeleo ya nchihii, bila kuwekeza katika umeme hakuna uchumi. Wananchiwanazalisha wanashindwa ku-process, wanauza malighafi,wanashindwa kuweka viwanda vidogovidogo; kwa ninihatuelewi? Mbona ni mahesabu ya kawaida kabisakwamba, huo uchumi hata tukiwaambia walime vipi kamahawa-process hawawezi kunufaika; mbona ni mahesabumadogo madogo haiwezekani.

Mheshimiwa Spika, ninaomba nikimaliza kuongeahapa, unipe Mwongozo nitoe hoja gani REA waongezewepesa ili umeme vijijini uweze kupatikana na Wabungewenzangu ni nani hataki umeme kwenye vijiji vyake? Nakama tunataka si tunapitisha bajeti hapa, basi tuazimie REAipate pesa, hakuna Mbunge ambaye hataki umeme kwake.Haina maana, tunapitisha bajeti halafu tunaacha umemekwenye viji j i vyetu hatupati, haiwezekani, Wabungewenzangu tuungane, leo ni leo, REA wapate pesa, umemevijijini uende. (Kicheko/Makofi)

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

6

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, ninaomba nizungumzie suala lawachimbaji wadogowadogo. Wizara imefanya kazi nzurikuwaunganisha wachimbaji wadogowadogo na tunaombakazi hiyo isiishie hapo, wale wachimbaji wadogowadogopamoja na matatizo yote, wana matatizo ya mitaji. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante.

MHE. DEVOTHA M. LIKOKOLA: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Umekataa halafu unaunga mkonohoja! (Kicheko)

SPIKA: Sasa Mheshimiwa Josephine Chagulla!

MHE. JOSEPHINE T. CHAGULLA: Mheshimiwa Spika,ninakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili na mimi niweze kutoamchango wangu katika Hotuba iliyoko mbele yetu ya Wizaraya Nishati na Madini. Ninaanza na kuunga mkono hoja kwaasilimia mia moja ili Waziri akaendelee na kazi nzuri aliyoianza.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, siyo siri, wote tumeshuhudia nimuda mfupi sana tumeona mabadiliko makubwa katikaWizara hii; kwa hiyo, tunawapongeza sana na tunawaombawaendelee na kazi hiyo na Mwenyezi Mungu, atawaongoza.Tunawaomba kasi waliyoanza nayo waendelee kuwa nayo.

Niende kwenye hoja yangu; Mkoa wa Geita nimiongoni mwa Mikoa mipya, ambayo imeanzishwa hivikaribuni. Wananchi wa Mkoa wa Geita wanahitaji umemekatika majumba yao, wanahitaji umeme katika shule zao zasekondari na za msingi, wanahitaji umeme makanisani nakatika vijiji vyao. Ni haki ya kila Mtanzania kupata umeme.Ninaomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa kujibu hojaza Wabunge, awajibu Wananchi wa Mkoa wa Geita kuwa

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

7

25 MEI, 2013

ni lini Serikali itawapa umeme Wananchi wa Mkoa wa Geitapamoja na Wilaya zake za Bukombe, Mbogwe, Chato naNyang’hwale?

Mheshimiwa Spika, umeme ni maendeleo, bilaumeme hatuwezi kuendelea, ninawaomba sana tena sana,Serikali iwaone Wananchi hawa, kwa sababu ni Mkoa mpyawaweze kupata umeme ili Mkoa wao uweze kuendeleamapema. (Makofi)

Ninakuja kwenye madini, Mkoa wa Geita ni Mkoaambao una madini mengi sana na tuna wachimbaji wengisana. Kinachotushangaza na kutusikitisha sisi Wananchi waMkoa wa Geita, ni pale wachimbaji wetu wadogowadogowanapoanzisha sehemu zao za kuchimba madini, Serikaliinawaondoa na kuwapa wawekezaji; hii siyo sahihi. (Makofi)

Unapowaondoa wachimbaji wadogo hawa maeneoyale ni mashamba yao, ni sehemu zao za kuweza kujikimu,tunaiomba Serikali iwasaidie wachimbaji wadogo hawawapate ruzuku, wapate mitaji, wapate leseni ili na waowaweze kuendesha maisha yao katika maeneo yale.Nikisema hivi sina maana kuwa hatutaki wawekezaji Geita,wawekezaji tunawapenda sana, lakini na wenyeji naowaangaliwe kwa jicho la huruma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,ninaomba niwaombe Wananchi wa Mtwara, wakwe zangu,watulie, Serikali imesikia kilio chao waache kuuana hovyo,wasubiri matunda mazuri, Serikali ina mpango mzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hivyo, ninaungamkono hoja. (Makofi)

MHE. EZEKIA D. WENJE: Mheshimiwa Spika, ninashukurusana kwa kunipa nafasi. Ninaomba nianze kwa kuzungumziamisamaha ya kodi na upotevu wa mapato ya Taifayanayotokana na Wizara hii. Kuna ripoti moja inaitwa TheAfrican Department of IFM Report ya mwaka 2006 na kunasehemu hapa ninaomba ninukuu kidogo inasema: “All the

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

8

25 MEI, 2013

evidence suggest that the disadvantages of tax incentivesvastly outweigh the advantages.” Kwa tafsiri ya kawaida nikwamba, hasara na athari zinazotokana na misamaha yakodi ni mikubwa sana kuliko faida zinazopatikana namisamaha ya kodi na kuna sehemu kidogo pia inasema: “Taxincentives are not an important factor in attracting foreigninvestment.”

Mheshimiwa Spika, baada ya nukuu hizo, hata janatulikuwa tunazungumza hapa kuhusu tax incentives, lakiniSerikali haichukulii hili jambo serious. Katika Ripoti ya IFM yamwaka 2006 kuna takwimu inasema, katika kipindi cha miakamiatano iliyopita export inayotokana na madini; kwa mfano,dhahabu, imeongezeka kutoka five thousand million USDollars mpaka 1.5 billion US Dollars, lakini mapato ya Serikaliya Tanzania yamebaki kwenye wastani wa one hundredmillion US Dollars, kwa sababu ya misamaha ya kodi, yaanihundred million ndiyo imebaki average pale pale. Pamojana kwamba, mapato yameongezeka kwa sababu yaongezeko la thamani ya dhahabu katika soko, lakini averageimebaki pale pale kwa sababu ya misamaha mingi ya kodi.Ripoti ndiyo inasema.

Mheshimiwa Spika, wametoa mfano na ninaombanimpe Mheshimiwa Waziri; kwa mfano, kwenye fuel levy pekeyake, exemption inayotokana na fuel levy uki-refer kwenyeRipoti ya Bomani inasema kwamba, mwaka 2006/2007 hasarazilizopatikana kwa upotevu wa mapato ilikuwa ni Shilingi zaKitanzania 39.8 bilioni, mwaka 2007/2008 imeongezekakwenda Shilingi za Kitanzania 59 bilioni, mpaka mwaka 2011mwishoni makampuni yanayochimba dhahabu nchi hiiyalikuwa yanaidai Serikali kwenye 275 million US Dollars kamafidia ya ile exemption wanayopewa.

Meshimiwa Spika, hii ni hasara kubwa sana. Hoja yamsingi ninayotaka kuijenga hapa ni kwamba, kuna Ripotininayo hapa inaitwa Enhancing Revenue Collection inTanzania, hawa watu wamefanya study inasema moja yaswali kubwa walilouliza ni kwamba; kuna mechanisms zipiambazo Serikali inatumia kufanya control. Kwa mfano,

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

9

25 MEI, 2013

wanauliza na hili swali ninakuuliza Meshimiwa Waziri;tunapotoa kwa mfano misahama ile fuel levy; ni controlmechanism ipi tuliyonayo in place inayohakikisha kwambamafuta ambayo wanatumia wanaochimba, inaenda kwaajili ya hiyo kazi tu ya uchimbaji?

Zipo ripoti za siri zinasema kwamba, hata mafutatunayotoa misamaha, kuna wengine wanaenda kuuza tenahaiendi kwenye intended use. Wanasema hata mashineambayo tunatoa misamaha inayokuja kwenye migodi, kunazingine zinakuja tunauza tena.

Kwa hiyo, ninachotaka kujua kutoka Serikalini nicontrol mechanism ipi ipo in place inayohakikisha kwamba,kama misamaha tunatoa inaenda kwenye ile intended usepeke yake il i kupunguza hasara inayopatikana kwamisamaha hii tunayotoa?

Mheshimiwa Spika, kitu kingine kinachonishangazasana na Mheshimiwa Waziri utueleze; je, kama Serikali tunaouwezo wa kujua kwamba Geita Gold Mine kwa mfano kwamwaka wamechimba dhahabu kiasi gani na wamesafirishakiasi gani. Kama wanavyo viwanja vya ndege kwenye migodina ndege inaweza ikaja pale ikaruka direct ikaenda hadiNairobi. Je, tuna Ofisi ya TRA pale? Kama Sheria ya Madiniya 2008, contract inasema huwezi ukafanya snap checkkwenye migodi, lazima umwambie investor, yaani umpe ripotiya awali kabla hujaenda hata kufanya snap check; what isthe control mechanism?

Mheshimiwa Spika, ninachohoji ni kwamba, viwanjavya ndege vinavyokuwepo kwenye maeneo ya mining ni vyakufanyia nini? Je, tuna Ofisi ya TRA pale? Tuna ofisi yaImmigration kwenye viwanja vya ndege? Kuna taarifa sahihikwamba, ndege inaweza ikaruka kutoka Gold Mine ikaendadirect Nairobi; what is the control mechanism?

Je, Mheshimiwa Waziri unaweza ukaliambia Taifakwamba kwa siku moja; kwa mfano, Nyamongo Gold Minekule Tarime wanapata dhahabu kiasi gani? What is is the

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

10

25 MEI, 2013

control mechanism humu, yaani ni kwamba, taarifaunayopata Mheshimiwa Waziri unategemea taarifawanayotoa wao kwa hisani yao, sisi hatuna controlmechanism ya kujua kwamba what is realy happening in dailybasis?

Mheshimiwa Spika, kinachonishangaza sana, hataaudit iliyofanyika kwa mara ya kwanza ya Tanzania Mining(TMA) mwaka 2010, yenyewe pia imegundua kuwa kunamatatizo. Kwa mfano, kuna matatizo kwenye hayamakampuni makubwa duniani kote, kuna study na researchimesema kwamba, maeneo mengi wanadanganya. Sasakama maeneo mengi wanadanganya na sisi hatuna controlsystem ya kutosha na ndiyo maana hata hii Audit ya kwanzaya mwaka 2010, ilibaini kwamba, kuna maeneo mengi wana-over estimate mpaka cost of operation ili ije i-affect kamakuna kodi yoyote wanatakiwa walipe.

Sheria yenu mbovu ya Mining Act kuna sehemuinasema they can actually carry unlimited loss forward.Kwamba, mwaka huu wanaweza wakafanya kazi wakasemawamepata hasara, mwaka kesho wakipata faida ile hasarawaliyoipata mwaka huu inakuwa carried foward. Kwa hiyo,definetely Serikali bado haiwezi ikapata chochote. Hiyo sheriambovu ya Mining Act, 2008, pamoja na marekebisho yakeyaliyofanyika mwaka 2010.

Mheshimiwa Spika, kinachoshangaza zaidi nikwamba, kama Kabanga Nickel, naambiwa utafiti ulianzatoka tunapata Uhuru mpaka leo; hivi sisi hatushtuki! Mtuanafanya utafiti kutoka Uhuru mpaka leo; anafanya utafitigani kutoka Uhuru mpaka leo hatushtuki?

Mheshimiwa Spika, naomba nizungumzie habari yaumeme. Juzi hapa nilimwuliza Mheshimiwa Waziri ndani yaBunge, nikamwambia ni kweli kwamba, TANESCOwanachukua pesa za watu, fedha nyingi kweli, mtu anaendaana-apply umeme analipa, anakaa mpaka miezi sita.Mwanza kuna kesi nyingi sana, Kata ya Mkolani, Bugarika,Ilemela, Maina, watu wamelipia umeme toka mwezi wa nane

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

11

25 MEI, 2013

mwaka jana, wengine wamelipia umeme toka mwaka janamwezi wa kumi na mbili, hawajaunganishiwa mpaka leo. Sikuile niliwahoji hapa huu utaratibu wa TANESCO kukopa fedhakwa Wananchi na kufanyia biashara utakoma lini?

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, mtu anaenda benkianakopa fedha au anaenda kwa mtu anachukua pesa iliaweke umeme aunganishe afanye biashara, labda awekemashine asage arudishe pesa. Sasa kama mtu anakopa pesaanaenda ku-apply umeme TANESCO inachukua mpaka miezisita hajafungiwa umeme; huu utaratibu ni upi?

Mheshimiwa Spika, mwaka jana Mheshimiwa Waziriulitueleza hapa wakati tunashughulikia tatizo la TANESCO,alituambia na katika Hotuba yake, ukurasa wa 29, nafikiri kunasehemu ametoa takwimu ya bei ya nguzo ya umeme.

Mheshimiwa Waziri alituambia kwamba, watu waTANESCO walikuwa wanachukua nguzo Iringa wanapelekasijui Mombasa wanagonga muhuri wanarudisha inaonekanakama imetoka South Africa. Wakati kipindi hicho takwimuzako zinaonesha nguzo za Tanzania ni za gharama ya juukuliko nguzo zinazotoka nje; je, ulilidanganya Bunge? Kwasababu logically haiji akilini kama bei ya nguzo Tanzania ipojuu. Sasa mtu atachukuaje tena halafu hizo hizo ndiyozisafirishwe zirudishwe tena kwamba zimetoka South Africawakati logically takwimu zako na wewe unakiri kwambanguzo za Tanzania zipo bei ya juu!

Mheshimiwa Spika, ningependa tupate tamko laSerikali kwamba, tabia ya TANESCO kuchukua fedha zaWananchi wanakaa nazo itakoma lini na wale Wananchi waMwanza walioomba umeme toka mwezi wa sita mwaka janampaka leo hawajapewa umeme wataunganishiwa lini? Sikuhiyo, Naibu Waziri aliniambia kwamba, amepiga simuTANESCO Mwanza lakini mpaka leo hawajaunganishiwaumeme.

Mheshimiwa Spika, napenda nimweleze Waziri,akienda kama Marekani, ukinywa hata soda ukahudumiwa

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

12

25 MEI, 2013

kwenye baa, unalipa tip ya ten percent iko kwenye sheria.Sasa sisi tunashindwaje kuweka serious policy iwe sheria interms of percentage? Hata siku ile tukiwa Pius Msekwa kunaMbunge aliwashauri, kwa sababu ukiangalia hata hii Ripotihawa jamaa wanasema, ukilinganisha mabilioni ya fedhaambazo haya makampuni yanapata kutoka kwenyemachimbo yetu na ukilinganisha na vyoo wanavyokujakujenga kwenye shule na mabwawa wanayotuchimbia …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante, muda umeisha. Sasa ninamwitaMheshimiwa Ngeleja, atafuatiwa na Mheshimiwa LucyMayenga na wengine nitawataja baadaye.

MHE. WILLIAM M. NGELEJA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Namshukuru Mwenyezi Mungu na mimi kupatafursa ya kuchangia katika Wizara hii. Naomba nianze kwakuunga mkono hoja hii kwa asilimia mia moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo tunajadili Wizara ya Nishati naMadini, lakini kimsingi sisi Wabunge wa Chama cha Mapinduzini sehemu ya utekelezaji wa ahadi ambazo tulizitoa baadaya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Kwa hiyo, kwa dhatikabisa na kwa mujibu wa taratibu ambazo tumejiwekeakama nchi, ni wajibu wetu sisi kuipitisha mipango ambayotuliwaahidi Watanzania ili hatimaye kufikia malengo ambayotumeyakusudia.

Mheshimiwa Spika, Mpango huu wa Bajeti umeelezamambo mengi sana na ni jambo dhahiri kwamba, kwamwendo huu tunaokwenda nao, mambo yanayosemwakatika Sekta ya Nishati na Madini ni dhahiri kwamba, mpangowa kuifanya nchi yetu iwe na uchumi wa kati ifikapo mwaka2025 upo wazi kabisa. Ndiyo maana bila mashaka yoyote,naunga mkono hoja hii na bajeti hii na pia napendaniwatangazie Wanasengerema kwamba, katika mambomazuri ambayo Wizara imeyasema hasa masuala ya umemeambayo yamekuwa yakiipasua nchi kwa muda mrefu sana.

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

13

25 MEI, 2013

Wanasengerema wanafaidika na mambo mengi, vijiji vingivitapata huduma ya umeme, wakiwemo Wananchi wa Kijijicha Ibondo ambapo hivi karibuni tutakuwa tunafanyauchaguzi wa marudio kumpata Mheshimiwa Diwani.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana wakati Wizara yaNishati na Madini inawasilisha bajeti yake, lakini kabla yahapo ilitanguliwa na Wizara ya Fedha, tulihabarishwakwamba, hali ya Uchumi wa Tanzania na kwa kupindi kilekwa kuangalia kigezo cha mfumuko kwa bei, tulikuwa karibiaasilimia 20, tulikuwa kwenye asilimia kumi na nane na pointikadhaa kama siyo kumi na tisa ya asilimia ya mfumko wabei. Tuliambiwa kwamba, mambo ambayo yalikuwayamesababisha mfumko kwa kiwango kile ilikuwa kwanzabei ya chakula, lakini pia bei ama gharama za uzalishaji waumeme. Sasa hivi tunavyoongea, kiwango cha mfumko wabei kimeshuka hadi chini ya asilimia kumi, maana yake nikwamba, Serikali ya CCM kama ilivyotuahidi mwaka jana,imetimiza wajibu wake kwa Watanzania kuwaletea nafuu yakimaisha kwa kuwapunguzia mfumko wa bei, kwa kuhakikishakwamba mgawo wa umeme unadhibitiwa na hatimayetunajionesha katika hali halisi ilivyo leo. (Makofi)

Kwa hili naipongeza sana Serikali na tunaona ukisomaHotuba ya Waizri katika ukurasa wa 12, Serikali kwa dhatiimeamua kutoa bilioni 402, ukijumlisha na mkopo ambaowameupata kutoka taasisi za kifedha wa zaidi ya bilioni yamia moja ili kudhibiti mgawo wa umeme. Hili ni jambo jema,ni jambo ambalo tunatakiwa tuipongeze Serikali kwamaamuzi haya. Tumpongeze sana Mheshimiwa Waziri waFedha kwa kuliona hilo, kwa sababu mgawo wa umemekama tungeendelea na juhudi zetu za kutolisaidia Shirika laUmeme TANESCO, kutoisaidia Wizara hii, leo maisha yaWatanzania yangekuwa katika hali mbaya sana. Ndiyomaana tunasimama hapa kifua mbele kwa dhati,kuipongeza Serikali kwa mipango hii ambayo imeileta, kwajuhudi ambazo Serikali imechukua, masuala menginetutayajadili baadaye. Bila juhudi hizo, leo Watanzaniatungekuwa tunaumia sana na pengine hali isingekuwa hivi

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

14

25 MEI, 2013

kama tunavyoongea. Kwa hiyo, tunaipa mkono wa pongeziSerikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumekuwa tukihabarishwa naSerikali kupitia Wizara hii na hata Wizara zingine kwamba,mpango wa Serikali ifikapo mwaka 2015, wa kigezo chauzalishaji wa umeme ni lazima tuwe na megawatizisizopungua 3000. Tunaona miradi iliyotajwa katika Hotubaya Waziri inakidhi na kujibu utashi na matarajio yaWatanzania. Tuna sababu gani ya kutoiunga hoja hii mkono?Kwa sababu miradi ambayo inatekelezwa sasa ambayoutekelezaji wake umeanza miaka kadhaa, kwa hakikainatupeleka zaidi ya kuzalisha megawati 3000. Miradi yausafirishaji imesemwa pamoja na usambazaji.

Mheshimiwa Spika, yapo mengi ambayoyamefanyika katika Wizara hii, ambayo tunahitaji kuipongezaSerikali; mojawapo ya mambo ambayo yamefanywa vizurisana na Wizara hii ni pamoja na kudhibiti biashara ya mafutaTanzania. Kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati,(EWURA), tumeona utekelezaji wa uagizaji wa mafuta kwapamoja na hata lile zoezi la kuweka vinasaba, imeisaidia sananchi yetu kupunguza kiwango cha uchakachuaji wa mafuta.Pia imewezesha Serikali kupata mapato na kupata takwimusahihi kwa mapato ambayo vinginevyo ilikuwa ngumu sanana kulikuwa na mianya mingi ya wafanyabiashara wasiokuwawaaminifu kuikosesha Serikali mapato. Kwa hiyo, tuna kilasababu ya kuipongeza Serikali kwa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukisoma Hotuba ya Kambi Rasmiya Upinzani, kuna mahali wanamtaja Katibu Mkuu wa Chamacha Mapinduzi, Mheshimiwa Kinana, wakisema kwamba, kwasababu wakati fulani alihusishwa kuwa mmojawapo waWakurugenzi wa kampuni iliyokuwa inaitwa Artumas, ambayobaadaye ilinunuliwa na Kampuni ya Wentworth, wanatumiakigezo hicho kuanza kujaribu kumpaka matope Katibu Mkuuwa Chama cha Mapinduzi. Mazoea haya ni jambo bayasana, tunahitaji kulikemea kwa dhati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo zipo taasisi ambazo

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

15

25 MEI, 2013

zinaongoza kuchangia mapato ya kodi kwa uchumi wa Taifa,ikiwemo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na SerengetiBreweries. Makampuni haya miongoni mwa Viongozi wakekatika usimamizi wa taasisi hizi ni Watanzania. Waziri MkuuMstaafu, Mheshimiwa Cleopa David Msuya ni Mwenyekiti waTBL, hapo inapokuwa imefikia hatua hiyo ujue kwambaWatanzania tumefikia hatua ya kujivunia, tunaaminika,makampuni yamesajiliwa katika masoko ya hisa za Dunia.Mpaka kufikia nafasi ya kuaminiwa katika kiwango hiki, siyorahisi sana; kwa hiyo, najaribu kuwashauri wenzangukwamba, tunapokuwa tunawataja hawa watu, tunawatajetu kwa sababu ya siasa zetu. Yapo maeneo ambayotunaweza kwenda kuchakachua na kwenye maeneo yamajukwaa, lakini tunapokuwa katika jumba hili takatifuambalo tunachangia baada ya kusoma dua na kumwombaMungu kwamba atuongoze katika mjadala huu, ninatarajiakwamba, wenzangu pia wawe na umakini wa hali ya juu,kutojaribu kutumia jumba lako Tukufu kuwapaka matopeWatendaji wa Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kinana kuwammojawapo wa Wajumbe wa Kampuni iliyokuwa inaitwaArtumas haikuwa dhambi, ndiyo maana leo tunajivuniaushiriki na imani ambayo makampuni ya nje yamewapawazee wetu kama Mheshimiwa David Msuya na akina MzeeBomani, Mzee Ufuluki kwenye Kampuni ya Geita Gold Mine,wapo wengi, akina Mzee Mengi.

Mheshimiwa Spika, jambo hili ni la hatari sana, kwasababu siasa bila uchumi haiwezi kwenda. Mimi nina uzoefuwa kutosha, kauli zetu za kisiasa zimekuwa zikichoma nazinaogopesha wawekezaji katika nchi hii hata wale wa ndani.Mwaka 2009, baada ya mitambo ya Dowans, Serikalikushindikana kuinunua tena kwa bei ya kutupa ya dola milioni59.7, niliitisha kikao na Shirikisho la Wafanyabiashara Tanzania(CTI), akina Mzee Mengi na akina Mzee Chande na MzeeMosha, nikawashauri kwa sababu Serikali na TANESCOtumeshindwa kununua mtambo huu, ninaomba ninyimuunganishe nguvu zenu mwanzishe kampuni kubwa,mnunue mtambo huu kwa bei ya kutupa ambayo

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

16

25 MEI, 2013

ingetusaidia kuzalisha umeme. Walichoniambia Waziri wakatihuo, hoja yako tunaiona lakini siasa zenu zinatutisha.

Mheshimiwa Spika, siasa kama hizi za kuwashambuliaWatanzania ambao wanaaminiwa, wanasimama na sisiinakuwa kigezo cha kujivunia, ni hatari kwa Taifa hili, ni lazimatuzikemee. Mtambo ule ule tuliokataa kununua Watanzaniaumenunuliwa na Wamarekani kwa zaidi ya dola milioni miamoja. Tumeutumia mtambo ule, umetusaidia kupunguzamgawo wa umeme, tunautumia kwa muda mrefu na tunalipacapacity charge. Ingekuwa ni Watanzania wamenunua bilakutishwa na kauli kama hizi, leo Watanzania tungekuwatunanufaika sana. Haya ni mambo ya hatari. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama Taifa tunapita katika halingumu, tupo kwenye trial moment, ninawaombaWatanzania, Wadau wote na hasa Viongozi wa makundiyenye ushawishi mkubwa wakiwemo Viongozi wa Dinitushirikiane. Mambo haya makubwa ambayo Taifatunayafanya sasa ndiyo msingi wa kutuondoa katika umaskiniambao Taifa letu limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu.Naomba Viongozi wote wa Dini na Viongozi wa Kisiasa,tushirikiane kusaidiana na juhudi za Serikali kutekelezamipango ambayo itatutoa hapa na kutusogeza hatua mbelezaidi. Sisi kama Taifa, tuache tofuati zetu za kidini na za kisiasana hata tofauti za kimitazamo, kwa sababu mamboyaliyotajwa katika Hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini nikielelezo tosha cha dhamira ya kweli ya Serikali ya Chamacha Mapinduzi; kututoa hapa tulipo na kutusogeza hatuanyingine.

Ninaomba sana Watanzania watuelewe,tunapokuwa hapa sisi kama Chama Tawala, tunatekelezawajibu wetu, lakini nao kwa sababu baada ya Uchaguzi Mkuuuliopita na ndivyo inavyokuwa katika nchi inayoongozwa nademokrasia, wenzetu wana dhamira ya dhati ya kutung’oamadarakani, siyo kwa risasi lakini kwa sababu ya mabishanona kujaribu kutudhoofisha kwa kadiri watakavyoweza. Kwahiyo, Watanzania wafahamu kwamba, zipo kauli zinatolewahapa lengo ni sisi kung’olewa madarakani.

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

17

Ndiyo maana tunaposimama hapa tunaunga mkonomipango ya Serikali yetu kwa sababu ndiyo iliyotuaminishakwa Watanzania wakatuchagua kwenye uchaguzi uliopita.Tutaendelea kuwaambia Watanzania kwamba sisitunasimamia uchumi na maendeleo ya Taifa hili. (Makofi)

Hatutaogopa kusema ukweli kwa sababu Taifa hili nila kwetu sote. Lakini na nyinyi mtaendelea na kazi yenu kwakadri mtakavyoona fursa ambazo zinawezekana, mtasema,lakini nasi tutajibu mapigo kwa nia ya kujenga Taifa letu kwasababu hili ndilo Taifa ambalo Watanzania tunajivunia. UsioneMataifa makubwa yanakuja hapa kushirikiana na sisi, ni kwasababu tuna rasilimali, tunaaminika na tuna uwezo wa kuwana impact katika dunia ya leo. Lakini kwa siasa ambazozinasemwa, hatuwezi kufika huko. Chama cha Mapinduzitutasimama imara. Twendeni tukashindane kwenye siasa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukawaambie, barabarazinajengwa, mgao unadhibitiwa, miradi ya umemeinasambazwa na inaongezewa fedha. Mtakayokuwanayo,myaseme pembeni... (Makofi/Kicheko)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante. Muda umekwisha. Namwita Lucy T.Mayenga, atafuatiwa na Mheshimiwa Abdul Mteketa.

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza kabisa, nianze kwakutamka kwamba naunga mkono hoja kwa asilimia miamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama wenzanguwalivyozungumza hapo awali, nianze kwa kuipongeza Wizarahii. Nampongeza sana Waziri wa Nishati na Madini -Mheshimiwa Prof. Mhongo pamoja na Katibu Mkuu - BwanaAliakim Maswi pamoja na Watendaji wake wote wa Wizara

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

18

hii. Kazi mnayoifanya ni kubwa sana, endeleeni na kazi hii,mmeisafisha Wizara kwa kiwango cha juu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, labda tu mimi ni-declare interestkwamba mimi ni mmoja kati ya waumini ambao ninaaminikatika principal ya Kimarekani ya fire and hire. Mtu kamahatekelezaji wajibu wake lazima aondoke! Watendaji, kamani Wahasibu wa Wizara hii, kama ni watu ambao wanafanyakazi katika Wizara hii ambao wanaonekana kwambawahafai, ambao wanaonekana kwamba wanaihujumu nchiyetu wanatakiwa waondoke, waingie wengine wapya.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, umeme ni uchumi. Nchi yetu tukokatika matatizo ya aina mbalimbali. Lakini kitu pekeeambacho kitatusaidia kuweza kukabiliana na hali hii yamatatizo mbalimbali ya kiuchumi ambayo tunakabiliananayo ni suala moja kubwa sana nalo ni upatikanaji waumeme katika maeneo ya vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya MheshimiwaWaziri, amezungumzia kuhusu upatikanaji wa umeme vijijini.Niungane tu pamoja na wenzangu tangu majadiliano hayayameanza kuhusu kutoa pesa REA. Lakini labda tu nimsaidieMheshimiwa Waziri; sisi tunalalamika REA ipewe pesa, nayehana budi kutafuta support ya kwetu sisi ili tumuunge mkono.Serikali kwa ujumla wake iweze kuangalia uwezekano wakupata pesa. Lakini yeye lengo analo. Cha msingi tu,tuangalie pesa hii tutaipata kutoka wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa takwimu,imeonekana umeme uki-stabilize, inflation inashuka. Mwaka2012 kuanzia Septemba mpaka Desemba na mpaka Februarimwaka huu inflation ilifika kiwango cha asilimia 19.3, almostasilimia 20. Lakini baadaye kuanzia Aprili mwaka huu mpakahivi sasa imeshuka imefikia asilimia tisa. Ni kiwango ambachoinaonesha kwamba umeme ukifika vijijini, hali za maisha yetuna hali ya Tanzania na uchumi wetu itaboreka kwa kiwangokikubwa sana. (Makofi)

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

19

Mheshimiwa Spika, lakini katika hili, REA wamepewaShilingi bilioni 150, wanahitaji Shilingi bilioni 881 kutekelezamiradi katika kipindi cha miaka miwilli kukamilisha miradi yao.Lakini kwa kipindi cha mwaka huu mmoja wanahitaji Shilingibilioni 450.

Mheshimiwa Spika, sisi kama Wabunge, ni lazimatuangalie njia za kuweza kuhakikisha Serikali inapata pesa iliREA iweze kuongezewa pesa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mahitaji katika maeneo ya vijijiniyanaongezeka. Kwa mfano, kwa mujibu wa takwimu kwamwaka 2012/2013 mahitaji yalikuwa ni Megawatts 851.35.Lakini mwaka 2011 ilikuwa ni Megawatts 820, hii ni kutokanana maendeleo ya miradi mingi vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niko hapa na MheshimiwaMbunge mwenzangu, Mheshimiwa Hamoud - Mbunge waKibaha Vijijini. Yeye alikuwa ananiambia hapa kwambamiradi kule kwake Chalinze, Magindu na Lukenge, mradiumeanza kuanzia mwaka 2009 lakini mpaka sasa hivihaujakamilika. Hii miradi ambayo imeshaanza huko vijijiniikamilike. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini solution, mimi ambalonaliona katika hili, ni lazima tuwe na utaratibu wa kuangaliaSerikali inasimamiaje mapato yake, lazima sasa ufike wakatiwa kutokuoneana aibu, lazima sasa ufike wakati wakuwajibishana kwa haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais Obama anakujaTanzania. Hii kwanza inaonesha kwamba Taifa letulinathaminiwa, linaheshimiwa na bado Serikali yetu hii yaChama cha Mapinduzi ni Serikali ambayo bado hata hayaMataifa makubwa, bado yana imani na sisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hata kwa wale ambaowanaanza kujipa labda matumaini na zile ndoto za mchanakwamba labda tunaondoka mwaka 2015 wasahau. Kwasababu haya Mataifa makubwa, kiongozi mkubwa kama

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

20

Obama hawezi kuja kwenye Taifa ambalo anajua kwambaRais wa hii nchi anaondoka baada ya miaka miwili au Serikaliya hii nchi inaondoka baada ya miaka miwili ijayo. Kwa hiyo,nawaombeni tu msahau, kwa kifupi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niipongeze Wizara hii kwa launchile ya round four ya utafutaji wa gesi. Hii ni hatua ya msingisana kwa sababu kwa kipindi kirefu sana launching hizizimekuwa zikifanywa Houston na London. Kwa hiyo, kwakufanyika hapa Tanzania, tunatangaza Taifa letu. Lakininapenda kuwaambia wenzangu kwamba haya manenomengine ambayo yanasemwa na baadhi yetu sisi Wabungena hasa hawa wenzetu wa upande wa pili, haya mambo yakusema hii launching ikifanyika, utafutaji huu ukifanyika, basina vibali vinatoka hapo hapo, siyo kweli. Utafiti huuunafanyika mpaka kukamilika ni miaka 10 au 11. Sasa kamainachukua miaka 11 mpaka kuja kukamilika, yasipoanza sasahivi, itakuwa ni muda mrefu sana.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba sana, sisi kamaWabunge, tusione haya majukwa na hizi microphone, basitunakaa tunafurahia tu, ukiona hivi na haya makofi yanazidikuwa mengi na nini, tujue kabisa kwamba baadhi ya manenoambayo tunayasema tunapotosha Watanzania wenzetu.Launching hii ikishafanyika, baada ya miaka 11 ndiyomasuala ya vibali yaanza kufanyika. Hii Serikali siyo kwambani Serikali ambayo imelala tu, kwamba mambo yatakuwayanafanyika kiholela holela tu, siyo namna hiyo. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi naomba kuipongeza Serikali,kwamba kwa kufanya hivi tumetangaza Taifa letu kwakiwango cha juu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala lingine, nayo nitaarifa iliyopo katika nchi yetu kuhusu upotevu mkubwa sanawa madini katika nchi yetu. Upotevu wa rasilimali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lipo tatizo kubwa sana ambalomimi naliona katika nchi yetu. Nalo ni kutokuwepo na

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

21

Ministerial Inter-connection katika nchi yetu. Kwa nini nasemanamna hiyo? Tunapokaa tunasema kwamba Wizara fulani,kwa mfano, Wizara ya Nishati na Madini, inasimamia nishati,inasimamia madini. Lazima Serikali yote kwa ujumla wake,tujipange na tuangaliane: Je, tuko pamoja? Kwa sababutusipoangalia, tunaweza kujikuta tunakaa; Wizara mojainakuwa iko strict inasimamia principals kwamba sisitumesema hatutaki madini yasafirishwe nje kwa wizi. Lakinikuna watu wengine ambao wanawajibika na masuala hayoya usimamizi, let us say Polisi, au watu wengine wa TRA. Walewatu wasipotekeleza wajibu wao hatuwezi kufika paleambapo tunapataka.

Nitolee mfano, tarehe 8 Desemba, 2012 Bwana FungJung, huyu ni Mchina; alikuwa anapita katika kiwanja chandege cha KIA akiwa na madini ya Tanzanite, madini ya vitoyenye thamani kubwa sana. Wizara ya Nishati na MadiniTMAA wakamkamata yule mtu. Baada ya kumkamata yulemtu, wakamkabidhi Polisi pamoja na watu wa TRA, watu waForodha.

Mheshimiwa Spika, baada ya kumfikisha kule, hiyonilikuwa ni tarehe 8 Desemba, 2012. Baada ya siku hiyokumkabidhi kule; akaa, aka-lobby, akaongea na Polisi naalikamatwa na mtu mmoja anaitwa Tumaini Makwesa paleKIA. Baada ya kumaliza pale, siku iliyofuata yule mtu ambayealikuwa na Hati namba G24938191 alitoroka kupitia kiwanjacha ndege cha Kimataifa cha Dar es Salaam. Ina maanakwamba aliachiwa.

Mheshimiwa Spika, ninaomba Wizara hii, ninaombaWizara ya Mambo ya Ndani na kama siyo leo nitawezakusikika kwa leo, nitakuja kurudia siku nyingine. Naomba watuwote waliohusika na kumwachia Mchina huyu ambayealikuwa anasafirisha madini, ambayo yalikuwa yana thamanikubwa sana ya billions of money kuachiwa na badala yake,yule Bwana Tumaini Makwesa anaendelea kusumbuliwa.

Naomba huyu mtu asiondoke pale! Kwa sababuanaonekana kwamba huyu mtu ni mzalendo, tuko naye,

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

22

anaumia na tatizo hili la utoroshwaji wa madini katika nchiyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa zilizopokatika nchi yetu, tani 20 za dhahabu katika nchi yetu ambazozinazalishwa, ni tani mbili tu ndiyo zinapita katika mkondorasmi ambao unafaa. Tani 18 zinapotea tu kiholela, Tunaibiwapesa nyingi sana! Pesa nyingi sana zinapotea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Nilimwita Mheshimiwa AbdulMteketa, atafuatiliwa na Mheshimiwa Lolencia Bukwimba,halafu nitaendelea tena. (Makofi)

MHE. ABDUL R. MTEKETA: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa nafasi hii. Kwanza napenda kumshukuruMwenyezi Mungu kwa kusema “Shika Neno, Tenda Neno.”(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii mia kwamia. Pili, napenda kuipongeza sana Wizara, Waziri na hasaNaibu Waziri Mheshimiwa Simbachawene ambaye anakuwamsikifu na mchapakazi na mwadilifu. Kitu ambacho natakakusema ni kwamba Tanzania yetu ina utulivu mkubwa sana,na Tanzania yetu inasifika kote. Lakini leo hii Tanzania inatakakuharibika.

Mheshimiwa Spika, toka zamani Tanzania, watu woteni waungwana. Chakula chetu tukipata, tuna-share, tunakulapamoja. Leo hii tunaonekana Watanzania tunaanza kuwawachoyo kwa kusema hiki change, hiki chako. Hicho kitutunaomba tukifute kabisa! Kuna watu wanakaa wananukuukauli ya Baba wa Taifa, wakisema Baba wa Taifa amesemahivi, amesema hivi. Lakini ni hao hao wanakwenda kinyume,wanawachonganisha watu, wanaanza kuleta fujo katika nchiyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa naomba kabisa watu wanamna hiyo wasitumie jina la Baba wa Taifa kuharibu jina

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

23

lake bure. Kwa sababu Baba wa Taifa hajasema hata sikumoja tugombane au tutengane. Wote tuwe kitu kimoja.Naomba kabisa hicho kitu kiachwe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili mimi nataka kujikita hasa katikaJimbo langu. Kwanza, napenda sana kuipongeza Wizarakatika miradi ya umeme ambayo miradi itakayotekelezwakwa ruzuku kutoka Mfuko wa Nishati Vijijini mwaka huu namwaka kesho 2014 ambapo katika Wilaya ya Kilomberonimepata Chita, Ikule, Mkangawago, Mchombe, Njage,Idete, Mofu, Namawala, Mbingu, Mgeta, Gereza la Idete naKisawasawa. Nawapongeza sana kwa kunisaidia kwasababu sisi kwanza katika Jimbo la Kilombero tuna gridi mbiliza umeme na sisi miaka yote tunalinda tu nguzo kutoka Kihansimpaka kuja Kidatu. Tunalinda tu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunaomba kwambamlivyotuangalia, tunawashukuruni sana na tunawapahongera nyingi kwamba Kilombero mmeikumbuka namtekeleze, siyo kwamba imeandikwa tu isitekelezwe. (Makofi)

Vile vile tuna tatizo kubwa sana Ifakara. Niliongea naMheshimiwa Waziri, kwamba Ifakara kila wakati umemeunazimika. Ukizimika, ikija mvua kidogo, umeme umezimika.Ukija upepo, umeme unazimika na ukizimika unachukua wikimoja au wiki mbili au siku tano. Sasa hatuelewi sababu ni ninihasa. Tunaomba sana, Meneja wa kule tunaongea nayelakini majibu yake hayaturidhishi. Tunaomba Wizara iangaliekwa nini Mji wa Kilombero umeme kila saa unazimika. Umemeni kitu cha maana sana katika jamii, na sisi kwetu kule kunamalori mengi ambayo inabeba mizigo kutoka Mbingu kuletaIfakara. Zinakatatika spring; zikikatika spring wakitaka kwendakuunga umeme hakuna kwa siku tatu au siku nne. Hiyo nidhahama kubwa sana ambayo tunaipata. Tunaomba kabisaWizara iangalie suala hilo kwamba sisi tunapata taabuKilombero hasa Ifakara umeme hakuna, hakuna hakuna!

Mheshimiwa Spika, wawekezaji pale ni wengi, kunawatu wana mashine za kusaga, watu wana maduka yastationery na vitu vingine vingi. Vile vile kama mlivyopanga

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

24

kuweka umeme Mbingu, Mbingu tunashukuru sana, umemeuje haraka kwa sababu kuna matunda mengi sana. Watuwanaweza kuweka mashine ya processing wakatengenezakila aina ya matunda katika makopo na katika vitu vingine.

Mheshimiwa Spika, sina mengi ya kusema, ila natakakutoa shukrani sana kwa Wizara kwa kunikumbuka na naungamkono hoja mia kwa mia. (Makofi)

SPIKA: Ahsante kwa kuniazima muda. MheshimiwaLolesia Bukwimba, atafuatiwa na Mheshimiwa Rweikiza.

MHE. LOLESIA J. M. BUKWIMBA: Ahsante sanaMheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi ili na mimi niwezekuchangia katika Wizara hii ya Nishati na Madini. Wizara hii nimuhimu sana kwangu hasa kwa wananchi wa Jimbo laBusanda na Geita kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, nianze kwakumshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kusikiliza kilio chawananchi wa Geita kwa upande wa fidia ambaowamechukuliwa maeneo yao na GGM na vile vile kwa hatuaambayo Mheshimiwa Waziri wa Ardhi aliyofikia. Namwombatu Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, ahadi yake ya kwambabaada ya Bunge atatembelea Geita ili kuweza kusuluhishamigogoro hii na kuweza kuhakikisha kwamba wananchi waGeita wanalipwa fidia zao. Namwomba Mheshimiwa Waziriahakikishe kwamba anatimiza ahadi hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nianze na mambo ya madini.Kama jinsi ambavyo nimesema, mimi ni mdau mkubwa sanakatika shughuli za madini. Katika Mkoa wetu wa Geita kwakweli Mungu ametubariki kama ambavyo huwa nasemakwamba tunayo madini ya kutosha ya dhahabu, na tunawachimbaji wadogo wadogo ambao wanajishughulisha nashughuli za uchimbaji. Uchumi wa Mkoa ule unainuliwa zaidina shughuli za uchimbaji wa madini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wachimbaji wa madini wanazochangamoto nyingi sana. Cha kwanza, hawana mitaji, lakini

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

25

vile vile hawana elimu ya kutosha kuhusiana na namna nzuriya kuchimba madini haya. Kwa hiyo, naomba tu kwambakwa vile katika Sera ya Taifa ya mwaka 2009 ya Madiniimesema wazi kabisa kwamba Serikali ni wajibu wakekuhakikisha kwamba inawezesha wananchi wake kuchimbamadini haya na kuweza kunufaika vizuri zaidi, kwa hiyo,naiomba Serikali kwamba Sera hii itafasiriwe sasa ili wananchiwaweze kunufaika na sera hii ya Madini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu katika suala la madini,wananchi wetu wanahitaji mitaji kama jinsi ambavyowakulima kwa mfano katika upande wa Kusini kuna hiiSAGCOT ambayo inawawezesha wakulima, wanapewaruzuku. Kwa hiyo, hata katika madini vile vile naomba Serikaliiwekeze kwa wachimbaji wadogo. Maana wachimbajiwadogo wakiwezeshwa, nina hakika kwamba kipato chaokitaweza kuongezeka na hivyo kuweza kuchangia katikapato la Taifa letu, na hapo tutaweza kufikia malengo yamilenia. Kwa sababu hatuwezi kufikia malengo ya millenniapale ambapo tunawaacha wananchi wetu wakishindwakunufaika kutokana na raslimali zao ambazo Munguamewajalia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba kwamba,Serikali kwa hatua ya kutoa maeneo kwa aji l i yakuwawezesha, tayari imekwishatoa maeneo katika baadhiya maeneo kule kama Rwamgasa. Lakini vile vile nimeonakatika ramani ambayo ametupa Mheshimiwa Waziri, ramaniile imeonesha pia hata Nyarugusu ni eneo limetengwa kwaajili ya wachimbaji wadogo. Naomba sasa Serikali ihakikishewananchi hawa wanapewa hilo eneo, maana kimekuwa nikilio chao cha muda mrefu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini vilevile kule Kaseme, Sobora,ni eneo ambalo ni muhimu, wananchi wanahitaji wapewemaeneo hayo waweze kunufaika kwa ajili ya uchimbajimadini. Vikundi vingi sana vya uchimbaji wa madinivimejiunga katika eneo la Jimbo la Busanda na ni vikundikama 100 hivi vyenye watu zaidi ya 1,000. Kwa hiyo, naombaSerikali kwa kweli iwekeze kwa wananchi hawa, ili kuweza

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

26

kupata ajira. Watu wengi wataweza kujiajiri kutokana nashughuli hizi za uchimbaji wa madini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika suala hilo hilo la madini, nivyema sasa Serikali ikaanzisha kuweza kuwawezeshawachimbaji wadogo kuweza kuongeza thamani ya madinikwa sababu, bila ya kuongeza thamani ya madini,haiwezekani kabisa kupata faida kutokana na shughuli zauchimbaji.

Kwa hiyo, Serikali, iwawezeshe wananchi hawa,ianzishe Vituo kwa ajili ya uongezaji wa thamani, iwezekuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kuwawezeshawachimbaji hawa, ili madini wanayoyapata wawezekuyaongeza thamani. Kama ni hereni za dhahabu, watuwavutiwe basi hata kuja Geita; kuwepo na kituo maalum kwaajili ya kuuzia madini haya, ili wananchi waweze kufaidika;na mikufu mizuri mizuri kwa ajili ya akina mama. Kwa hiyo,naomba Serikali iangalie namna ya kuwawezesha wananchihawa kuongeza thamani ya madini, hasa katika Mkoa waGeita, ambako ndiko ni Mji wa dhahabu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie pia masuala yahuduma katika maeneo haya. Wote tunatambua kwambamaeneo ya uchimbaji wa madini kuna population kubwasana. Watu wengi wanavutiwa na shughuli za uchimbaji wamadini. Kwa hiyo, unakuta kwamba, huduma za kijamiiambazo Serikali inatoa, zinakuwa hazitoshi. Kwa mfano, paleNyarugusu, kuna watu wengi sana, kwa hiyo basi, wanahitajihuduma za jamii. Haiwezekani mkapeleka dawa sawasawana Kijiji kingine.

Kwa hiyo, naomba tu kwamba Serikali iangaliesehemu hizi za madini kwamba, iweze kuongeza hudumakulingana na idadi ya watu. Kwa mfano, huduma za afya,vilevile barabara, kwa sababu magari yanapita kwa wingisana na uzito mkubwa. Serikali, ikijenga barabara baada yamuda mfupi inaharibika. Kwa hiyo, naomba tu kweli Serikaliituangalie zaidi katika maeneo kama haya. (Makofi)

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

27

Mheshimiwa Spika, halafu sambamba na hilo, miakamiwili iliyopita GGM walikuwa wameanza kufanya utafitikuhusiana na barabara ya kutoka Geita kwenda Kakora kwaajili ya kuiwekea lami.

Kwa hiyo, ningependa kujua kwamba wamefikiahatua gani kuweza kujenga lami barabara hii, barabara yaGeita kupitia Bukoli kwenda Kahama. Naomba kwa kweliwatu wa mgodini waweze kujitahidi kuiwekea lami barabarahii maana magari yanapita kwa wingi, yanaleta vumbi kubwana kuleta athari kwa wananchi walioko kandokando yabarabara hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile kuna baadhi ya sehemuambazo zimepitiwa na bomba la maji la GGM. Kwa mfano,Kijiji kile cha Chigunga kule Salagurwa, kwa kweli, bombalinapita pale, lakini wananchi wale hawana maji. Kwa hiyo,naiomba Serikali pia iangalie uwezekano mzuri wa kuwasaidiawananchi ambao wanaishi karibu na rasilimali hizi ambazowatu wa GGM wanatumia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa umeme,nichukue nafasi hii kuishukuru sana Serikali, kama jinsiambavyo tunasema kwamba, unapofanyiwa mambo mazurini vizuri ukashukuru. Kwa hiyo, mimi nashukuru sana kwaumeme wa MCC, japokuwa bado haujawaka, lakini wikiiliyopita Mheshimiwa Waziri, alinaihidi kwamba kufikiaSeptemba, wananchi wataanza kufaidika na umeme huukwa sababu, utakuwa umewaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu umeme huu nimuhimu sana kwa ajili ya uchumi wetu, hasa katika Wilayaya Geita na Mkoa Mpya wa Geita, naiomba Serikali kwambaumeme huu unapopita katika maeneo ya Kijiji fulani penyeShule za Sekondari zote, Serikali ihakikishe inaweka umemehuu katika Vituo vyote vya Afya. Kwa mfano, pale Bukoli, Kituocha Afya Bukoli kiwekewe umeme, Shule ya Sekondari Bukoliiwekewe umeme, vilevile Shule ya Sekondari ya Rwamgasaiwekewe umeme, Kituo cha Afya cha Genge Kumi piakiwekewe. (Makofi)

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

28

Mheshimiwa Spika, vilevile kuna baadhi ya sehemumuhimu kabisa ambapo kuna huduma ambazo zinatolewakwa ajili ya wananchi wengi, kwa mfano, Gereza lile laButundwe. Ninashukuru kwamba Serikali katika bajeti yamwaka huu kupitia umeme wa REA, tayari imeweka bajeti.Nilikuwa naomba utekelezaji ili wananchi waweze kunufaikana huduma hii ya umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda kusema tu kwamba paleKatoro, kwa mfano shule ya Sekondari ya Katoro, haina nguzoza kwa ajili ya kuwekewa umeme. Naiomba tu Serikaliihakikishe shule hii ya Sekondari wapate huduma ya umeme.

Vilevile kuna biashara pale, kuna shughuli ndogondogo, viwanda vidogo vidogo vya kukoboa mpunga paleKatoro, pamoja na pale kona ya kuelekea Nyamigota,naiomba Serikali ihakikishe kwamba wananchi hawa wotewanapata umeme wa kutosha ili tuanze kunufaika sasa naumeme huu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile niwaombe watumbalimbali, wawekezaji, waje Geita sasa kuwekeza maanatunapata umeme wa uhakika. Ni umeme wa Gridi ya Taifana tunajivunia kwamba, kuanzia mwezi wa Tisa, nina uhakikakwamba, sasa wawekezaji tunawakaribisha waje kuwekezakatika Mkoa Mpya wa Geita, maana tutakuwa na umemewa uhakika kabisa wa Gridi ya Taifa.

Halafu, vilevile kule tuna matunda. Kwa hiyo,niwaombe tu kwa kweli, mje mwekeze katika viwandambalimbali vya matunda ili kuwawezesha wananchi waGeita kupata ajira ndogo ndogo kwa maana hakika Serikaliimetuona katika hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache, napendakusema kwamba, nashukuru sana kwa kunipa nafasi naninaunga mkono hoja, nikiamini kwamba Serikali, sasainakwenda kuyafanyia kazi haya yote ambayonimeyazungumzia hapa.

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

29

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja, ahsantesana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa namwita Mheshimiwa Rweikiza,atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt. Mbassa.

MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Spika, ahsante.Nami niseme kwamba, naunga mkono Hoja kwa asilimia miamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii pia kuwapapole wananchi wa Bukoba ambao hivi karibuni walikumbwana maafa ya mvua kali na upepo mkali na kupoteza mazaomengi sana na nyumba zaidi ya 200 zimeporomoka na mvua,na mtoto mmoja kule Kasule Kata ya Kisogo amefarikikutokana na mafuriko hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nijikite kwenye umeme na hasaUmeme Vijijini. Nitumie nafasi hii kuishukuru sana Wizara nahasa Wakala wa Umeme Vijijini, (REA). Namshukuru Dkt.Mwakalesa na timu yake kwa kazi nzuri anayoifanya.Anafanya kazi nzuri sana kupeleka umeme vijijini, sehemunyingi za vijijini zimepata umeme, na hii ni kazi nzuri ya Serikaliya CCM, hasa kupitia REA. Lakini hawa watu wanafanya kazikwa mafanikio makubwa, lakini kwa mazingira magumu;Hawana pesa za kutosha. Wanapeleka umeme wakiwahawana hela ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa nafasi hii namshukuruMheshimiwa Waziri, kwamba siku anawasilisha Bajeti yakealisema kuna watu ambao hawakutoa hata senti tano, lakiniwanajitapa kwamba wao ndio wamepeleka umeme Vijijini.Hali hii iko Bukoba. Kule Bukoba tuna mradi mmoja mkubwauliokamilika wa Ikimba Area, unakuta umeme unawaka vijijizaidi ya 50. Kuna mtu kule anasema yeye ndio amepelekaumeme, kwamba yeye kwa fedha zake ndio amepelekaumeme kule. Anasema kwamba yeye amepeleka umemekwa fedha zake, na siyo Serikali.

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

30

Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Wazirikwa kusema kwamba, kuna watu wa namna hiyo, nakwamba ule mpango aliousema wa kupeleka Mawaziri,Naibu Waziri, kwenda kufungua miradi hii, aanzie Bukoba, iliwawaeleze wananchi kwamba ni kazi ya Serikali ya CCM,siyo kazi ya mtu binafsi yule anayejitapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa kwenye mradi huo kunasehemu chache zimerukwa, kama pale Ilango, paleKaibanja, kuna sehemu pale Katoma; juu kuna waya zaumeme, chini watu hawana umeme. Sasa naomba jitihadaziongezeke kusudi wapate umeme. Pale Bujugo, Kata nzimaimezungukwa; baada ya mradi huu kukamilika, kote kunaumeme. Mashariki kuna umeme, Kaskazini kuna umeme,Kusini, kila mahali kuna umeme isipokuwa Kata hii imerukwa,imekuwa kama kisiwa na yenyewe iangaliwe ipewe umeme.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye orodha tuliyopewa hapa,kuna vijiji vingi ambavyo vimeorodheshwa hapa vya BukobaVijijini ambavyo vitapata umeme, naomba nivisome. Vijiji vyaBugabo, Kagabiro, Buhendagabo, Kagya, Kishanje, Rubafu,Ibosa, Mwizi, Izimbya, Kyaitoke, Kasikizi, Ibwero, Mugajwale,Makongola, Kanyabuguru, Kanyabuhoro, Kitoro, Kalego,Nyakaka, Kyampisi na Kangabusaro. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa ni jitihada nzuri lakini ninawasiwasi, kwa sababu najua kwamba, REA hawana pesa zakutosha. Miradi ambayo iko REA inasubiri kutekelezwa inahitajiShilingi bilioni 881, hela waliyonayo mwaka huu kwenye Bajetikwenye Book hili kubwa, ni Shilingi bilioni 150, haifiki hata robo;ni hela ndogo sana. Kwa hiyo, nina wasiwasi kwamba hatamiradi hii huenda isitekelezwe kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa mimi nina pendekezo ambalonataka nilitoe. Nawashukuru Wizara walishafanya ubunifumwaka 2011 na mwaka 2012 na REA. Wakaja na pendekezokwamba kwenye simu za mkononi kuwe na tozo ya Sh. 4/=kwa dakika. Hela hii iende REA, ipeleke umeme vijijini. Wakatihuo ilikuwa Sh. 4/= kwa dakika, wakati kupiga simu kwa dakika

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

31

moja ilikuwa ni Sh. 150/= mpaka Sh. 200/=. Gharama ilikuwakubwa, wakapendekeza Sh. 4/= tu kwa dakika. Leo simuzimeshuka bei baada ya kuingia kwenye Mkongo wa Taifa,ni Sh. 30/= mpaka Sh. 40/= kwa dakika. Kwa hiyo, naomba hiiSh. 4/= ianze mara moja, iingie kwenye simu za mkononi, tozohii ianze ili pesa hii ipatikane iende REA isaidie kupelekaumeme vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2012 kama mradi huuungeanza, REA ingepata Shilingi bilioni 123. Zingesaidia sanakupunguza pengo la pesa na kupeleka umeme vijijini. Lakininasikia kwamba Wizara ya Mawasiliano inazuia mpango huuusitekelezeke. Sasa sijui kama ni kweli! Naomba MheshimiwaWaziri aeleze, kwa nini mpango huu hauanzi? Leo gharamaya simu imeshuka kutoka Sh. 150/= mpaka Sh. 200/= kwadakika hadi Sh. 30/=. Kwa hiyo, hata wananchi hawatasikiauchungu kama itaongezwa kwenye simu hii Sh. 4/= auSh. 5/=, hata ikiwa Sh. 10/=, itakuwa nafuu sana kupataumeme vijijini. Huu ni mpango mzuri ambao utasaidia vijijikupata umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, bila umeme huwezi kufanya kazina simu, na minara ile inatumia umeme. Simu hizi huwezikutumia bila kuzi-charge na umeme. Kwa hiyo, ni jamboambalo linategemeana. Napendekeza kwamba, mpangohuu uanze, Sh. 4/= zitozwe au Sh. 5/= au hata Sh. 10/= kwenyekila dakika ili REA ipate pesa ya kutengeneza miradi yakeiliyonayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivi leo TANROAD inatozaSh. 250/= kwa lita ya mafuta, dizeli na petroli, Sh. 250/= tu! Siunaona kazi wanayofanya! Nchi nzima wanajenga barabaraza lami, Mikoa inaunganika kwa Sh. 250/= tu kwa lita moja.Wameomba waongezewe Sh. 150/= ziwe Sh. 400/=, miminasema hapana. Isiende Sh. 150/= kule, iende REA angalauSh. 100/=, iongezwe REA, ndani ya mwaka mmoja mpakamiwili, itapatikana Shilingi bilioni 800 na miradi hii itakamilika.Tutapata umeme vijijini na miradi mingi itaweza kukamilishwana vijiji vitapata umeme. (Makofi)

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

32

Mheshimiwa Spika, mchango wangu ni huo.Nakushukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Sasa namwita Mheshimiwa Dkt.Mbassa, atafuatiwa na Mheshimiwa Maige na MheshimiwaLembeli ajiandae.

MHE. DKT. ANTHONY G. MBASSA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi, ili na mimi niweze kuchangiahoja iliyoko mbele yetu. Labda kabla sijaanza mchangowangu naomba nieleze machache. Ni kweli kabisa kazi yetukama Wabunge ni kuisimamia Serikali na kuishauri paleinapowezekana na kuweza kueleza yale mabovu ambayoyanajitokeza, ili kusudi tuondokane na hali ambayo ni mbovu.

Mheshimiwa Spika, tunapoeleza mambo ya ufisadiKambi ya Upinzani, siyo kwamba tunakuwa tunayafurahia,hapana. Tunataka yakomeshwe na yasirudiwe. Lakiniimekuwa wazo kwamba kila tukiongea kitu, inaonekanatunarudia kitu kile kile. Tunaeleza ukweli uliopo na namshukuruMheshimiwa Lucy kwa yale aliyoyasema. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kumekuwa na kauli kwamba,sisi tuna-quote kauli za Baba wa Taifa; ni kweli kabisa kamatungezifuata kauli za Baba huyu, Taifa hili lisingekuwa mahalihapa hata siku moja. Sasa kwa anayetenda mazuri lazimatumsifie na kwa aliyetenda mabaya, lazima tueleze ili kusudituondokane na uchafu huu unaoendelea katika nchi yetu.Ni kweli, Baba wa Taifa, alikuwa mwadilifu na ndiyo maanakatika shughuli zake zote hakuwahi kuvaa sare ya Chamachochote, lakini watu wanaovaa sare, ndio haowanaoturudisha nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nirudi nichangie sasa yaliyokoJimboni kwangu. Jimbo langu la Biharamulo Magharibi, nikati ya sehemu ambako tatizo la umeme ni kubwa sana. Kiliochetu kimekuwa cha muda mrefu na tumekuwa tukilielezahili mara kwa mara, lakini ni kutokana na sababu kwamba,tuna generator mbili ambazo zimechoka, tunazitumiagenerator hizi pamoja na wenzetu wa Chato, kwa ndugu

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

33

yangu Mheshimiwa Dkt. Pombe John Magufuli, ambapo sasaumeme wa mgawo umekuwa ni jambo la kuzoeleka.

Mheshimiwa Spika, lakini inasikitisha kwamba juzi katihapa, Naibu Waziri wa Nishati na Madini - MheshimiwaSimbachawene akijibu maswali, alisema kuna generatoszinateremshwa Biharamulo na Ngara. Kwa kweli nilisikitikasana, jambo ambalo siyo kweli; lakini nilifikiri labda ulikuwa nimpango huu ambao umeelezwa katika kitabu cha Hotubaya Mheshimiwa Waziri, ukurasa wa 10 kwamba kuna mashinetatu ambazo zinakuja kwa ajili ya Biharamulo, Mpanda naNgara.

Mheshimiwa Spika, umeme ni kila kitu. Leo hii uzalishajiwetu ungekuwa juu sana, vijana wengi wangejiajiri, lakinikama hawana nishati ya umeme hawawezi kufanya lolotelile. Ni wazi kabisa kwamba watu walioko pembezoniwanaweza kusema wameachwa kwa sababu, gridi ya Taifahaipiti kule. Sasa juhudi hizi zinapofanyika, zifanyike ikijulikanakwamba watu wanahitaji umeme na wanahitaji umeme wakweli na siyo mambo mengine. Naomba mradi huu ambaowanasema upembuzi yakinifu umeshafanyika, utekelezajiwake ndiyo bado haujafanyika; utekelezaji wake unaotajwakatika mwaka huu 2013/2014 tunaomba tupate japo maeneoya jumla, lakini tupate time frame, unaanza lini na unakamilikalini? Watu wa Biharamulo wanahitaji umeme na siyovinginevyo.

Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na miradi mingiambayo imekuwa ikitajwa ya umeme. Kwa mfano, kunamradi nilishawahi kuusikia wa Masaka kupitia Karagwekwenda mpaka Rusumo, uunganishwe na umeme wa majiambao ulikuwa unapaswa uanzie pale Rusumo kuja mpakapale Nyakanazi. Lakini katika Kitabu cha Mheshimiwa Waziri,katika hotuba yake nimejaribu kupitia, wala siioni sehemuyoyote hata ambako suala hili linatajwa kwa urefu na upanawake. Sasa linapoongelewa suala zima la kubadilisha umemewa gridi kutoka kV 220 kwenda mpaka kV 400, sijui kama ndiyomradi huu unaoongelewa. Naomba Mheshimiwa Waziri,anapokuja kutoa maelezo, basi atueleze kama ndiyo mradi

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

34

huu, tuweze kujua Wana-Biharamulo tutakuwa katika haligani?

Mheshimiwa Spika, lakini jambo lingine linalosikitishani suala zima la gharama za ufungaji wa umeme majumbanimwa watu. Gharama hizi zimeendelea kuwa juu sana nazinatakiwa zilipwe kwa mkupuo mmoja, kiasi kwamba, watuwengine hawawezi. Kwa nini kusiwepo na utaratibu kwambawatu wafungiwe umeme na wawe wanalipa taratibuwanapokwenda kununua umeme?

Mheshimiwa Spika, hili lingesaidia sana na lingefanyawatu wengi sana waweze kupata nishati hii adimu, iwezekuwasaidia katika shughuli zao. Leo hii kuna baadhi yawanavijiji inafika mahali mpaka wanachanga pesa zao;wanakwenda kwa Meneja wa TANESCO kuomba wafungiwe,lakini inakuwa ni vigumu. Wanarudishwa kwamba,wakaandae mihutasari, wakaandae sijui vitu gani, vituambavyo wakati vimeshafanyika lakini inashindikana kutoamaamuzi. Wizara hii ina mpango gani? Mameneja hawawanawasaidiaje wananchi hawa ambao wanahitaji kupatanishati hii, angalau hata kile kidogo kilichopo kiwezekuwasaidia? Naomba Waziri anapokuja, atusaidie katika hilo.

Mheshimiwa Spika, lakini pamoja na hayo, ukurasawa 23 katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri, ameongeleasuala zima la usambazaji wa mradi wa umeme vijijini, REA.Ninashukuru kwa vijiji alivyovitaja. Vijiji vile viko karibia 12, lakinivijiji vile ukiangalia viko kwenye mwelekeo ambao pamojana hayo, kuna vijiji ambavyo vingeweza kupata.

Ukiangalia mradi unaotoka pale kabindi kuja RunaziCentre kuja Katahoka, Nyamahanga, Ntungamo, Kibale,Nyambale mpaka Lusahunga. Vilevile wangeweza kuchukuavijiji vinavyopitia katika Kata ya jirani kiasi kwamba watu hawawangeweza kupata umeme. Mfano, kuna Kata yaNyantakala, Nyantakala pale ni barabarani kabisa. Wakovijana wamejiajiri wenyewe, wajasiriamali, viko vikundimbalimbali vya ujasiriamali ambavyo laiti kama wangewezakupata umeme huu, vingeweza kuwasaidia.

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

35

Mheshimiwa Spika, jirani hapo kuna Kata ya Nemba,kuna shule za Sekondari ziko pale, kuna Vituo vya Afya vikopale, Zahanati wanahitaji umeme huu, lakini vijiji hivivimeachwa. Kwa kweli, naomba katika mradi huu uwezekuangalia maeneo hayo kwa ukaribu sana ili kusudi watuhawa nao waweze kujikwambua katika maisha yao ya kilaleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kitu kinginekinachonishangaza, leo hii watu wote tunahitaji huu mradiwa REA na mradi wa umeme vijijini ambako ndiyo 80% yawananchi wetu wanaishi hawana umeme. Ukiangalia bajetiya mwaka 2012, iliyotengwa, fedha zilizokuwa zimepangwakwenda REA ni 13% tu imekwenda. Fedha hizi nyinginezimekwenda wapi? Kama zimepelekwa TANESCO, ni juhudigani zinafanyika kusaidia hawa REA nao wapate fedha yakutosheleza waweze kupeleka umeme vijijini? Tunapaswatupate jibu la makini hapa.

Mheshimiwa Spika, lakini naomba niongee sualalingine kuhusu Sekta ya Madini. Katika ukurasa wa 56 wahotuba ya Mheshimiwa Waziri, ametaja migodi ambayoitafungwa mwishoni mwa mwaka huu ikiwa ni pamoja namgodi wa Tulawaka na Mgodi wa Golden Pride Nzegaambayo inategemea kuchukuliwa na mwekezaji wa katiambaye ni STAMICO.

Mheshimiwa Spika, jambo hili limeshapangwa najambo hili linapaswa liangaliwe. Mgodi huu unapofungwa,kuna huduma za jamii ambazo zilikuwa zinapaswa kufanywana migodi hii, zimetekelezwa kwa kiasi gani? Au hawawawekezaji basi wanafunga wanaondoka wanaachakukamilisha miradi hii ambayo walikuwa wameahidi kwenyejamii, na hapa ndiyo tunapozua migogoro na jamii iliyopo.

Mheshimiwa Spika, kuna wafanyakazi waliokuwawakifanya kazi katika migodi hii. Je, wakati hawa wanaelekeakufunga, stahili zao zimeshaanza kuangaliwa? Au ndiyo hawawanaondoka tena tunaanza kushikana uchawi, kwambaKampuni imeondoka, imekuja Kampuni nyingine? Naomba

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

36

tafadhali kabla hawajakamilisha miradi yao, wahakikishewafanyakazi wao maslahi yao yameandaliwa vizuri namikataba yao ieleweke.

Mheshimiwa Spika, lakini jambo lingine ni ajira kwahawa watu wanaokuja kuanza uwekezaji. Tunaomba ajirazitengwe na ziwekwe kwa wazawa wa maeneo hayo. Siyowatu wanakuja kuanzisha migodi pale lakini wanakuja nawatu wao tayari wamekwishaajiri. Hili suala linafanya vijanawetu wanakuwa demoralized na kwa kweli wanajenga hisiana chuki kubwa sana. Watoe ajira kwa vijana waliokomaeneo yale, sawa najua kuna stadi na ujuzi mbalimbaliunaohitajika, lakini kwa kazi ndogo ndogo, wachukuliwe watuwa maeneo ya pale wafanye kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine, ni jinsi gani STAMICOimejipanga kuendeleza wachimbaji wadogo wadogo nakuwapatia maeneo ya kufanyia kazi? Jambo hili limekuwa nitatizo kubwa sana, tumeliongelea hapa mara nyingi, lakinikila siku tunapata jibu la kwamba Serikali inajipanga,tunajaribu, tupo katika mchakato. Huo mchakato utakwishalini?

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante, nashukuru. Sasa namwitaMheshimiwa Ezekiel Maige, atafuatiwa na MheshimiwaJames Lembeli na Mheshimiwa Brig. Gen. Hassan Ngwiliziajiandae.

MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Naomba nianze kwakumshauri Mheshimiwa Waziri. Mwaka 2012 nilimshauriMheshimiwa Naibu Waziri, nadhani sasa ni vizuri nikamshauriMheshimiwa Waziri mwenyewe. Naomba Mheshimiwa Wazirinimrejeshe kwenye maandiko matakatifu kwenye kile kitabucha Mithali aya ya 20, mstari ule wa tisa, unasema kwamba:“Mashauri ya moyoni ni kama kilindi, lakini mtu mwenyeufahamu atayateka.” (Kicheko)

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

37

Mheshimiwa Spika, namwomba sana MheshimiwaWaziri, ushauri huu ninaompa, ninampa sio mimi tu, lakini piaaelewe ninaongozwa na Roho Mtakatifu aliyenipelekakuyasema hayo. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nimwambie jambo lakwanza kabisa kwamba muda wa kutoa ahadiumekwishapita. Tulitoa ahadi mwaka 2010 tukataja vijijivitakavyopata nini. Tulitaja vijiji vitakavyopata umeme, tulitajavijiji vitakavyopata maji tukapigiwa kura. Mwaka 2012tulipewa orodha na ramani na mwaka huu tumepewaorodha na ramani.

Mwaka 2012 tulipewa orodha na ramani ikionyeshavij i j i vya Wilaya ya Kahama kwa Jimbo la Msalalavitakavyopata umeme kupitia REA vilikuwa vijiji sita na vijijivitakavyopata umeme kupitia Electricity Five vilikuwa ni vijijivinne, jumla ni vijiji kumi. Mpaka hivi sasa vijiji vyote kumihavijapata umeme. Tulichotegemea leo, tungekujakuambiwa katika vijiji kumi, vijiji vitatu tumefika hapa, vijiji vinnetunakwenda hivi. Kwa hiyo, wale wananchi walinipigia jananikawaambia nimepewa tena ramani. Wakaniambiakwamba, mshauri Mheshimiwa Waziri asiendelee kutoaramani, atoe umeme. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, nil itaka nimwambiekwamba kumekuwa na matatizo makubwa ya umemekwenye Mji wa Kahama kwa muda mrefu pamoja na Mijimidogo ya Kagongwa na Isaka. Matatizo haya yanatokanana uchakavu wa njia ya umeme inayotokea Ibadakuli kujakahama. Tumekwishaomba sana na ndugu yangu, kakayangu, Mheshimiwa Lembeli, imekuwa ni kilio chake cha sikunyingi sana kwamba Mji wa Kahama uunganishiwe umemekutoka Buzwagi. Kilio hiki kiliishawasilishwa na mpaka sasa hivihakuna kilichofanyika wala hakuna indication yoyote kwenyebajeti. Naomba Mheshimiwa Waziri alizingatie sana hilo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ushauri wa pili, ujumbe kutokaMtwara; mimi nilivyopokea na kuelewa ni kwamba wananchi

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

38

wa Tanzania hivi sasa wanachokisema ni kwamba rasilimalihizi tuzigawane kwa kutambua maeneo ambayozinapatikana. Niseme tu kwamba sidhani kama wananchiwa Mtwara au sehemu nyingine wanasema rasilimali yoteibaki kule. Nilikuwa kwenye Tume ya Bomani, tulizunguka nchinzima zenye madini, wananchi wanasema tugawanemrabaha. Hii siyo mara ya kwanza au siyo kitu kinachofanyikakatika sisi kuanza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye Idara ya wanyamapori,tunafanya hivyo. Tunasema 25% ya mapato yanayotokanana uwindaji wa kitalii yabaki kwenye vijiji, inafanyika hivyo.Kwenye madini mbona inakuwa kwamba Taifalitagawanyika? Kenya wanafanya hivyo, percentage fulaniya rasilimali wamepitisha juzi kwenye Katiba yao, inabaki pale.Ghana wanafanya hivyo, India wanafanya hivyo, Afrika Kusiniwanafanya hivyo na bado Mataifa yale yapo nayameendelea kuwa strong. Tunasema, tunaomba rasilimalihizi tubakishe kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye Tume ya Bomanitulipendekeza 40% ibaki kwenye maeneo madiniyanapopatikana, 60% iende kwa Watanzania wote. Kwa hiyo,naomba sana, hatumaanishi kwamba madini haya yabakipale yalipo, hapana. Kiasi fulani kibaki pale. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimweleze tu Mheshimiwa Wazirikwamba, Wasukuma kwa mfano, sio wapole kamainavyodhaniwa, na sio wajinga kama inavyodhaniwa wakatimwingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wasukuma ni wavumilivu. Lakinihawapendi kabisa kuiona Shinyanga iko hivyo, Mwadui ikopale ikijenga South Africa Johannesburg; hawapendi kuonaTulawaka iko pale inafungwa inaiacha Biharamulo ile,ikajenga Toronto; hawapendi kuona Golden Pride inafungwaikiiacha Nzega iko vile ikajenga Australia; kadhalikahawapendi kuiona Kahama ikibaki vile, Bulyanhulu ikijengaSouth Africa, ikijenga Toronto, ikijenga London. Tunaombatueleweshwe na ninaomba Mheshimiwa Waziri aelewe

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

39

kwamba vitu vya namna hii vinawa-provoke wananchi navinatuletea matatizo makubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kutokana na hii messageya Mtwara, nimshauri Mheshimiwa Waziri, mkubali kupokeana kukubali kuwa na mjadala mpana kuhusu namna ya ku-share rasilimali za nchi. Tulisema mwaka 2012 na mwaka 2011kwamba tusiwafanye wananchi wa maeneo ambayorasilimali zinapatikana wakaona ni balaa kuwa na rasilimalizile. Rasilimali hizi ni Baraka, ni kweli rasilimali ni zetu wote,lakini population ya Kahama sasa hivi ni kubwa mara kumiya vile ilivyokuwa kabla ya madini kugunduliwa. Maishayamepanda, bei ya mkate ambayo tulikuwa tunanunualabda kwa Sh. 200/= sasa hivi imeongezeka several times kwasababu ya kuongezeka kwa population iliyotokana namadini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hii athari inabebwa nawananchi wa Kahama, haibebwi na Watanzania wote. Ndiyomaana tunasema tunahitaji tutazamwe kwa jicho la kipekeena hatumaanishi kabisa kwamba madini yote yabakiKahama, gesi yote ibaki Mtwara. Tunaomba, kamailivyopendekezwa kwenye Tume ya Bomani. Kamahamuiamini, mliipa fedha, tukazunguka dunia nzima, tukajana ushauri huo. Kama bado hamwamini, zungukeni tenamwaulize Watanzania, mnasemaje kuhusu usimamizi namatumizi ya rasilimali hizi? Tusi-command kwamba wanatakahivi, tunataka hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, matatizo ya Kahama, Service Levy;Kahama tuna sheria ya Serikali za Mitaa Sura namba 290 yamwaka 1982 inaruhusu Halmashauri kukusanya ushuru wahuduma. Katika Mkataba MDA uliosainiwa ulivunja Sheria ilekwa kusema kwamba itakuwa inalipa kitu kinachoitwaConsolidated Local Fees kwa Dola 200,000. Tatizo lililoko nikwamba 0.3% ambayo ndiyo ushuru halali wa huduma, nimkubwa kuliko Dola 200, 000 na Waziri aliyesaini Mkatabaule hakuwa na mamlaka ya kuvunja Sheria iliyopitishwa naBunge hili. Kwa hiyo, tunawasilisha na tulikwishakusematarehe 8 mwezi wa Tano Mheshimiwa Leticia Nyerere aliuliza

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

40

swali na mimi nikasema naomba mwongozo; hatujalipwaService Levy Kahama. Tulicholipwa ni local fees kwa mujibuwa MDA ya Bulyanhulu na Buzwagi iliyosainiwa na Wizara.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya ServiceLevy iliyopitishwa na Serikali za Mitaa au iliyopitishwa na Bungehili, hakuna kilicholipwa na tunadai Dola za Kimarekani milioni12.15. Tukilipwa fedha hizi ninaamini kabisa Kahamahaitakuwa na vumbi kama ilivyo sasa, Kahama haitakuwana mashimo na hatutachangisha wananchi kujenga zahanatiwakati dhahabu yao ipo, service levy yao ipo, Sheriailishapitishwa, mtu mmoja anakwenda anasaini mkataba.Kwa hiyo nilikuwa naomba suala hilo tuweze kuliona. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho, nizungumzie matatizoya wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu, wana matatizomakubwa sana. Kwanza, kuna ubaguzi katika mishahara.Watanzania wanaofanya kazi sawa sawa na Wazunguwanalipwa wastani wa Sh. 800,000/= wakati Wazunguwanalipwa zaidi ya Shilingi milioni 12 kwa kazi zinazofanana.Nimeshamwambia Mheshimiwa Waziri wa Kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili wanaumia sana katikamazingira yao ya kazi, wanaendesha malori yasiyo na spring,wanavunjika disk za migongo, wapo Dar es Salaam, kunaHotel inaitwa Durban wako wafanyakazi 42 as we speakwana matatizo ya afya. Tunaomba sana wafanyakazi walewatazamwe na hasa Wizara ya Kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni suala la wachimbajiwadogo. Nimesikia orodha, Kahama haimo wakati ndiyoyenye madini sawasawa na Geita, sawasawa na maeneomengine. Nashindwa kujiuliza, hivi kweli pressure yaWachimbaji wadogo Kibaha inalingana na Kahama?Mnatenga eneo la wachimbaji wadogo Kibaha mnaachaKahama? Sheria tulipitisha mwaka 2010 tukasema maeneoyatakuwa chini ya Waziri baada ya leseni ku-expire ili Waziriaweze kutoa kwa wachimbaji wadogo. Kwa hiyo, tulikuwatunaomba sana hii lugha ya kwamba mnaendeleakujadiliana na wawekezaji ili waangalie maeneo yanayobaki;

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

41

yaani wenyewe waangalie wachague wanachukua firigisi,wanachukua mapaja halafu sisi wanatuachia vipapatio?Hapana! (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante Mheshimiwa.

MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Spika, naombakusema kwamba nitapenda sana kuunga mkono baada yakusikia majibu hapa. (Kicheko/Makofi)

SPIKA: Hiyo juu yako. Sasa namwita MheshimiwaLembeli atafuatiwa na Mheshimiwa Brigedia Generali HassanNgwilizi, atafuatiwa na Mheshimiwa Hamad Ali Hamad naMheshimiwa Gosbert Blandes ajiandae.

MHE. JAMES D. LEMBELI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, naombakwa moyo wa dhati kabisa kuunga mkono yale yote ambayoMheshimiwa Maige - Mbunge wa jimbo la Msalala,ameyazungumza kwa niaba ya wananchi wa Wilaya yaKahama. Nami sitarudia mengi aliyoyazungumza, badalayake nitazungumza yale ambayo hakupata fursa yakuyazungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tangu mwaka 2006 nilipoingiandani ya Bunge hili, kila mwaka na bila kuchoka, nimekuwanikichangia hotuba ya bajeti ya Wizara hii ambayo ni muhimusana kwa uchumi wa nchi na ustawi wa Taifa na wananchiwetu. Kwa nini nimefanya hivyo? Kwa sababu Jimbo laKahama na Wilaya ya Kahama ina kero nyingi zinazohusianana aidha Sekta ya Nishati au Sekta ya Madini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikianza na madini, nilishawahikusema ndani ya Bunge hili Tukufu na ndugu yangu,Mheshimiwa Maige amerudia hii leo. Kama Mbunge usiombehata siku moja eneo lako lipatikane na madini. Ni balaa, nikero kubwa, sio tu kwa Mbunge lakini pia kwa wananchi

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

42

wanaoishi katika eneo hilo. Kero ya kwanza, wananchikutokusaminiwa kabisa na wawekezaji, wakati mwinginehata Serikali inawatelekeza pale wanapodai fidia zao.Wananchi wengi waliokuwa wakiishi katika maeneo yamigodi ya Bulyanhulu, Buzwagi waliondolewa katika maeneohayo bila kusaminiwa kama wao sio wananchi wa Taifa hilina sasa wanahangaika kama mbuzi ambao hawanamwenyewe na Serikali ipo.

Mheshimiwa Spika, lakini pia, pale ambapowachimbaji wadogo wakij itafutia maslahi yao,wanapogundua na kuanza kuchimba katika maeneoambayo Wilaya ya Kahama kwa mfano, yote imeshagawiwakwa wawekezaji kufanya utafiti wa madini na wanapokutwawakichimba katika maeneo hayo, basi ni balaa lingine;wanafukuzwa, wanateswa, wanakamatwa na Polisi kanakwamba wao sio Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mambo haya hayastahili kabisa,hayafai, hata mbele ya Mungu ni dhambi. Sasa swali, kwanini Serikali inafumbia macho matatizo kama haya?Nitapenda kumsikia Mheshimiwa Waziri wakati akihitimisha,anajibu maswali haya ambayo nimeyazungumza hapa.

Mheshimiwa Spika, lakini tofauti na miaka mingineyote katika sekta ya madini, safari hii na leo kwa namna yakipekee kabisa napenda niipongeze Serikali, nipongezeuongozi wa African Barrick na uongozi wa mgodi wa Buzwagipale Kahama mjini. Baada ya miaka mingi ya kilio kwambawananchi wa Mji wa Kahama na Vitongoji vinavyozunguka,hawaoni manufaa kabisa ya mgodi wa Buzwagi, sasaangalau wameanza kuona mwanga. Nami ninaaminipengine Roho Mtakatifu amewashukia na sasa kwa mara yakwanza mwaka huu mgodi wa Buzwagi utajenga barabaraya lami ya kilomita tano katika Mji wa Kahama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii ilikuwa ni ndoto ya wananchiwa Mji wa Kahama kwa miaka yote, nami naomba uongoziwa African Barrick na mgodi wa Buzwagi na Serikali, hizikilomita tano zisiwe danganya toto. Mwaka ujao wajenge

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

43

barabara nyingine za kilomita tano na mwaka unaofuata2015 barabara nyingine kilomita tano za lami ili Mji waKahama kweli uwe Gold town kama ilivyo Johannesburg.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, mnyonge mnyongeni, haki yakempeni, hapa African Barrick, Buzwagi, ninawapongeza kwaniaba ya wananchi wa Wilaya na Jimbo la Kahama. Lakiniisiishie tu hapo, waendeleze kasi ya kuchangia huduma kwawananchi. Ninatambua mchango wao hivi sasa, wamejengaKituo cha Afya pale Mwendakulima, wamejenga Ofisi ya KataMwendakulima, wamejenga Shule ya Sekondari Kidato chaTano na Sita Mwendakulima wanaendelea kulipa Shilingimilioni 60 kwa Kijiji cha Mwime. Naomba Shilingi milioni 60 nimakubaliano ya miaka kumi iliyopita wakati bei ya dhahabuilikuwa chini. Leo bei ya dhahabu imepanda, nauomba sanauongozi na Serikali iwasaidie wana-Mwime, kiwango hichocha Shilingi milioni 60 kiongezwe kulingana na bei ya dhahabukatika Soko la Dunia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini yapo mambo mengineambayo wanastahil i kuyafanya. Maji katika vij i j ivinavyozunguka mgodi huu wa Buzwagi; haiwezekani waowaendelee kumwagilia maji barabara kule ndani, lakini kijijikilichoko mita 100 hakina maji. Maji yapelekwe kijiji chaMwendakulima, Kijiji cha Mwime na Kijiji cha Chapulwa.

Mheshimiwa Spika, sasa niongelee kuhusu nishati.Umeme katika Wilaya ya Kahama na Mji wa Kahama ni kerona ni dhihaka. Pamoja na kwamba Wilaya hii inajulikanakwamba imeunganishwa na grid ya Taifa, ukweli ni kwambani uongo. Ni kiini macho. Mji wa Kahama umeme wake ninguzo tu, hauwaki kama inavyotakiwa! Mgao wa umeme nikila siku, tofauti na maeneo mengine yote hapa nchini.Tunachoambiwa ni nguzo za umeme, uchakavu wamiundombinu kutoka kule Shinyanga kuja Kahama.

Mheshimiwa Spika, tangu nimeingia Bunge hili, kilaWaziri anapojibu, anasema uchakavu wa miundombinu. Sasakilomita 150, urekebishaji wa mtandao ule uchukue miaka

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

44

sita! Mimi sikubali! Leo nataka nisikie kutoka kwa MheshimiwaWaziri, anasema nini? Mgao wa umeme Mji wa Kahamautakwisha lini?

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mhongoalipochukua Wizara hii ndani ya Bunge hili alizungumza, tenakwa kauli nzito na kwa kujiamini akisema kwamba mgao sasamwisho. Sasa wananchi wa Mji wa Kahama kila siku mgao,ana neno la kuwaambia wananchi wa Kahama?

Mheshimiwa Spika, watu wa Kahama wanatakaumeme. Pale Buzwagi ni jambo la kusikitisisha sana, kanakwamba nchi hii ina Mji wa London na wengine Kahama.Pale Buzwagi tangu wamewasha umeme kwenye mgodi ulehaujawahi kuzimika hata siku moja. Lakini Kijijini na Mji waKahama ulioko kilometa tatu, nne kila siku kuna mgao waumeme. Tumesema ule umeme unaowaka kila siku paleBuzwagi kwa nini hauwashi Kahama? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama alivyosema ndugu yanguMheshimiwa Maige, kweli leo nilikuwa na hamu sana yakuunga mkono hoja hii. Lakini kwa suala hili, nitaunga mkonohoja hii, pale tu ambapo Mheshimiwa Waziri atasema nakwa uhakika, kwa nini umeme unaowaka Buzwagi hauwakiMji wa Kahama? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, namaliza. Mnyonge mnyongeni,haki yake mpeni. Kwa mara ya kwanza, nasema Serikaliinapeleka umeme katika vijiji vilivyopo kwenye Jimbo laKahama.

Ndugu yangu Mheshimiwa Maige amezungumziaJimbo la Msalala, nami sitaki kusikia hii ndoto tunayoambiwakwenye makaratasi haya ambayo yameletwa hapa kwambwebwe kwamba umeme vijijini utakwenda, lakini bajetihaioani na maneno yaliyopo hapa! Lakini kwa sababu kwamara ya kwanza wananchi katika vijiji vya Jimbo la Kahamana wao wamekumbukwa, wameingizwa kwenye mradi huuwa upelekaji wa umeme vijijini, napenda niishukuru Serikalina niipongeze. Vijiji ambavyo vimezungumzwa hapa katika

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

45

Jimbo la Kahama, ni pamoja na Nyandekwa, Seke,Bukondamoyo, Wigehe, Mbulu, Kisuke na kule Bulungwaninakotoka mimi anakoishi mama yangu. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa maneno haya, naombanisipoteze muda wako mwingi, lakini pamoja na pongezi hizi,nasita kuunga mkono hoja hii. Kama alivyosema ndugu yanguMheshimiwa Maige na mimi nitasubiri mpaka paleMheshimiwa Waziri atakapokuwa anahitimisha na kamaatatoa maelezo nitakayoridhika nayo na kwa hakikawananchi wa Kahama, nitaunga mkono hoja. Ahsante sana.(Makofi)

SPIKA: Wala hujanipa muda wa akiba! Sasa namwitaMheshimiwa Brig. Gen. Hassan Ngwilizi, atafuatiwa naMheshimiwa Hamad Ali Hamad na Mheshimiwa GosbertBlandes ajiandae.

MHE. BRIG. GEN. HASSAN A. NGWILIZI: MheshimiwaSpika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Nianze nakuunga mkono kauli ya Mheshimiwa Rais kuhusu rasilimali zaTaifa, kwamba rasilimali za Taifa ni mali ya Watanzania wote.Hiyo ni kauli ambayo haihitaji mjadala, ni kauli ambayoinahitaji kuungwa mkono na Bunge hili. (Makofi)

Vilevile naunga mkono hatua za Serikali za kuhakikishakwamba ulinzi, usalama na utulivu katika maeneo yale yoteambayo yametokea rapsha unadumishwa. Hilo ni jukumu lamsingi la Serikali yoyote ile. Kwa wale wote ambao wanafikiriakuleta chokochoko, wajue kwamba nchi hii inavyo vyombovya dola. Yakitokea yatakayowatokea, wasilaumu vyombovya dola, wala wasije wakailaumu Serikali, wajilaumu waowenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitoe angalizo hapa, kwambamatukio haya, sasa hivi Watanzania tumeanza kuzoeakwamba tunapenda kuhadithiana; lilitokea hili na fulanikavunjwa mguu na sijui fulani kafanywa nini! Hili lilikuwa nijukumu la Serikali kuzuia, siyo kungojea mpaka yatokee.(Makofi)

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

46

Mheshimiwa Spika, kazi ya kuripoti matukio ni kazi yaWaandishi wa Habari, na kazi ya Serikali ni kuzuia mambohaya yasitokee. Ndiyo maana vipo vyombo vya dola na kaziyao ni hiyo ya kuhakikisha inawadhibiti wale wote ambao niwakorofi ambao wanavunja sheria na kanuni za nchi hii. Hilolinatakiwa lifanywe na vyombo vya dola bila kujali mtu anacheo gani, anatokea wapi na ana imani gani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hilo nilidhani ni jambo la msingi lakuunga mkono kauli ya Mheshimiwa Rais kwani yeye ndioRais wa nchi hii na yeye ndio Amiri Jeshi Mkuu. Anavyovyombo vya kuhakikisha kwamba matarajio ya wananchiyanatimizwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, sasanikubaliane na Mheshimiwa Waziri kwamba, umeme niuchumi, umeme ni maendeleo, lakini naomba kuongezeazaidi, kwamba sasa hivi umeme ni haki ya Binadamu. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Sawa! (Makofi)

MHE. BRIG. GEN. HASSAN A. NGWILIZI: MheshimiwaSpika, tuondokane na dhana ya umeme kama suala labiashara tu. Sasa hivi umeme unahitajika na kila Mtanzaniakama ambavyo anahitaji dawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nianze kuiuliza Serikali,simwulizi Mheshimiwa Waziri kwa sababu naamini kwambaMheshimiwa Waziri nia yake ni nzuri. Naiuliza Serikali na katikahili naomba niipongeze sana Kamati ya Nishati na Madini.Azimio la Bunge lile la mwaka 2012, tuliloazimia hapa,kwamba tozo ya Sh. 5/= kwa kila dakika ya maongezi ya simukwenda REA, kutenga Shilingi bilioni 300 kwa ajili ya matumiziya umeme vijijini, kutoka katika Shilingi bilioni 600 ambazo nikiasi kil ichookolewa kutokana na uamuzi wa Serikalikulinganisha kodi za mafuta ya taa na dizeli: Kwa nini Serikaliimeshindwa kutekeleza hili Azimio la Bunge? Kwa sababuinaelekea Bunge tunatoa maelekezo hapa, tunaazimiahapa, lakini Serikali haitaki kutekeleza hilo. (Makofi)

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

47

Mheshimiwa Spika, sasa naomba nitoe changamotohapa, kwamba Mheshimiwa Waziri wa Fedha atakapokujakutoa bajeti yake ya Serikali, atupe jibu kuhusiana na Azimiola Bunge hili. Kwa sababu kama Bunge linaazimia na Serikaliinaamua kupuuza, maana yake ni kwamba Serikali imeamuakutosikiliza Bunge. Kama Serikali imeamua kutosikiliza Bunge,maana yake ni kwamba hata hii bajeti hapa tunayokaakuzungumza haina maana. Tunapitisha bajeti hapa ambayohaitakwenda kutekelezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala la nguzo zaumeme. Nguzo za umeme bado ni kero. Mwananchiakitakaka kuunganishiwa umeme anaambiwa ni lazima alipienguzo, lakini akishalipia nguzo ile, ni mali ya TANESCO. Hilonamwomba Mheshimiwa Waziri akija kujibu hoja zaWaheshimiwa Wabunge atoe maelezo hapa; hivi kunajustification gani ya mwananchi kutakiwa kulipia nguzo yaumeme ambayo hawezi kuuita ni ya kwake, inaitwa ni yaShirika la TANESCO? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile wote tunataka umemeuwake nyumbani kwake. Kila Mtanzania anataka hilo, ndiyomaana nikasema umeme ni haki ya binadamu. Lakini vilevile Miji yetu ina barabara hazina taa! Hivi sasa ukiangalianchi zote zinazotuzunguka, iwe ni Msumbiji, Malawi, Zambia,Kongo sina hakika, Rwanda, Burundi, Kenya, Ugandabarabara zao zina taa. Sisi Tanzania tunahitaji formula ya ainagani kuhakikisha taa za barabarani zinakuwepo katika mijiyetu?

Mheshimiwa Spika, ni aibu, unaruka na ndege kutokakatika nchi hizo, ukishaingia eneo la Tanzania, ukishakutahuoni Miji, hiki ni kielelezo kwamba sisi tumeshindwa kuwashataa katika nchi yetu.

Hata hivyo, Mkoloni alikuwa na utaratibu mzuri tukwamba kila ambaye anatumia umeme anatozwa senti;wakati ule nadhani ilikuwa senti mbili kwa ajili ya kuchangiakuwasha taa za barabarani. Hali ile iliendelea mpaka miakaya 1970. Hii ni kwa nini tumeiacha? Kazi yetu sasa hivi ni

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

48

kusema, Halmashauri zinazohusika, sijui ziwashe taa.Halmsahauri hizo fedha zinatoa wapi? Kwa nini tusichangiefedha kila mteja anapochangia? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naishukuru Wizara kwambakulingana na ramani zile, sasa umeme katika Jimbo la Mlaloutaendelezwa kutoka Viti kuelekea Manolo, Kibaoni, Pelei,Rangwi, Makose, na hatimaye utakwenda Sunga,Mamboleo, mpaka Mtae. Hiyo ni katika awamu ya kwanza,kwa sababu kila kitu lazima kiwe na mahali pa kuanzia. KatikaJimbo la Mlalo siyo Vijiji hivyo tu, tunayo Tarafa nzima yaUwumba haina umeme hata kidogo. Tuna Kata kama Shumena Mbalamo hazina umeme. Kwa hiyo, nategemea kwambakatika awamu ya pili ya REA umeme utafika kule.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi tunazungumza kwambatunawapelekea Watanzania umeme. Taa, sawa. Hata hivyo,tunazungumzia suala la uhifadhi wa mazingira. Kamahatujazungumzia Watanzania watapika vipi kwa kutumia kwaumeme, tujue kwamba mazingira yetu, misi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana. Sasa namwita MheshimiwaHamad Ali Hamad, atafuatiwa na Mheshimiwa GosbertBegumisa Blandes.

Waheshimiwa Wabunge, kwanza, naombatushauriane. Yaani vurugu iliyopo hapa haijapata kutokea.Kila mtu hapa anasema nataka kuchangia, natakakuchangia, lakini limit ya time tuliyokubaliana jana ipo. Hivisasa nikimaliza na Mheshimiwa Blandes, nadhani ndiyomwisho.

Sasa mna uamuzi, Jumamosi mnaweza kukaa mpakasaa 12.00, lakini lazima itolewe hoja. Kama haitolewi hoja yakuongeza muda, mimi nitaendelea kwa muda tuliopanga.

WABUNGE FULANI: Ndiyo! (Makofi)

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

49

SPIKA: Sana sana huwezi kuongeza zaidi ya saa moja,kama mnataka mtoe hoja. Mheshimiwa Waziri wa Nchiunaweza kutoa hoja kwamba tuongeze saa moja zaidi? Atoehoja kama mnataka kuongeza na kama hamtaki basi.(Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (SERA,URATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa Spika, jana tulitoa hojakwamba leo tutakuwa na Bunge mpaka saa 8.00. Kwa hiyo,kwa ridhaa ya Waheshimiwa Wabunge, naomba Bunge lakolikubali angalau tuongeze muda mpaka saa 9.00 alasiri leo.Naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika,naafiki.

SPIKA: Ahsante kwa kuunga mkono. Hoja imeungwamkono. Alichosema Mheshimiwa Waziri ni kwamba, kwamujibu wa marekebisho yaliyofanywa jana, kikao hikikingekwisha saa nane. Lakini sasa kwa kweli hapa nina vurugusiyo kidogo. Hata hivyo, saa moja maana yake tutaongezawatu sita, haidhuru, siyo mbaya.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Bunge liliridhia hoja ya kuongeza muda waBunge likae mpaka saa 9.00 jioni)

SPIKA: Sasa nimwite Mheshimiwa Hamad Ali Hamadatafuatiwa na Mheshimiwa Gosbert Blandes.

MHE. HAMAD ALI HAMAD: Mheshimiwa Spika, ahsante.Nami nashukuru kwa kupata nafasi hii. Mkutano wa WachumiDuniani uliofanyika Marekani walikubaliana kwamba, nchizote zenye rasilimali kama madini, gesi na nyingine, zinaingiakwenye migogoro ya wenyewe kwa wenyewe kwa sababuya mgawano mbaya wa rasilimali.

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

50

Mheshimiwa Spika, uchimbaji wa madini ya dhahabuTanzania. Tanzania kwa muda mrefu sasa tumekuwatukichimba madini haya ya dhahabu na kwa kweli ni tatizola uelewa. Serikali lazima ibebe dhamana hii ya kwambaimekuwa ikitoa taarifa zisizokuwa pana kwa Watanzania kiasikwamba wananchi walio wengi hawaelewi.

Mheshimiwa Spika, Mtanzania yeyote, awe Mbungeau mwananchi wa kawaida akizungumza suala la dhahabuanajua ni rasilimali yenye thamani kubwa kweli kweli.

Mheshimiwa Spika, kwa muda wote huo ambaotumekuwa tukichimba dhahabu Tanzania, nina wasiwasikwamba hata Waheshimiwa Wabunge humu ndani pamojana wananchi wenyewe hawaelewi dhahabu hii inachangiakiasi gani katika pato la Taifa.

Mheshimiwa Spika, Wabunge pia ni mashahidi, kilaMbunge anayetoka katika Wilaya na Viji j i ambavyovinachimba dhahabu anaonesha kwamba dhahabu hiihaifaidishi katika maeneo wanayotoka wao na wananchiwao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie mahusiano kati yawachimbaji na wananchi wetu. Katika maeneo yanayotokadhahabu, wananchi ambao wamezunguka maeneo yamachimbo ya dhahabu, wamekuwa wao na wachimbajiambao ndio tunawaita wawekezaji wakiangalia kwa jichola uadui, na wamekuwa wakipeana majina ya kiuadui kamavile wananchi kuwaita wachimbaji makaburu, wanyonyaji,wezi na kadhalika. Lakini hata Wawekezaji nao wamekuwawakiwaita wazalendo kwa majina ya wachimbaji haramu,wavamizi, majambazi na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, imekuwa ni kawaida kusikia kwakipindi kirefu sasa ama wananchi wanauawa katika maeneohayo, au wana ugomvi na walinzi katika maeneo yamachimbo, Polisi na hata wawekezaji wenyewe katikamigodi. Kwa mfano, maeneo ya Mererani, Mwadui, Buzwagi,North Mara, Isanga, na maeneo mengine. (Makofi)

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

51

Mheshimiwa Spika, wananchi hawa wanaelewakwamba madini haya yanayotoka kwenye maeneo yaoyana thamani kubwa ambayo haiwafaidishi wao. Kwakuzingatia hilo ndiyo maana wameamua kwa namna yoyotesasa na wao waone kwamba kuna haja ya kufaidika narasilimali zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali ilikuwa ina wajibu wakuzingatia kwamba angalau yale maeneo yanayochimbwadhahabu, basi kuwe na angalau kiasi fulani kibaki katikamaeneo yale kama mrahaba wao. Jambo hili lingewezakuwapunguzia manung’uniko. Lakini katika maeneo hayo,wananchi wamebaki na matatizo; magonjwa mbalimbali,barabara zao ni chafu, hawana maji, hawana Zahanati nahawana majengo ya madarasa.

Mheshimiwa Spika, hivi ndiyo vipimo na vigezo vyawananchi kuona kwamba wanafaidikaje na rasilimalizinazotoka kwao. Serikali inasema kwamba rasilimaliinapopatikana popote ni mali ya Watanzania wote, ni kweli.Lakini Watanzania hawaelewi hiyo, wanachoelewa nikwamba eneo lao linatoka rasilimali yenye thamani, kwa hiyo,na wao wanaangalia kufaidika. Ndiyo maana tunasemakwamba maeneo yale, basi yapewe, yaangaliwe kwa jichola huruma.

Mheshimiwa Spika, hata wale vijana wetu waKitanzania wanaofanya kazi kwenye machimbo,wanaambulia maradhi mbalimbali yanayotokana nakemikali zinazotumika kwenye maeneo yale ya machimbo,wanapata magonjwa yasiyotibika, lakini bado hawaangaliwikwa jicho la huruma hata kwa wale wawekezaji wanapoonakwamba hawa watu wameathirika wakachukua namna yakuweza kuwafikiria.

Mheshimiwa Spika, Tanzania tumegundua gesi, inatiashaka kwamba tunaweza tukawa na petroli vilevile, lakininaomba niseme kwamba jambo hili na tumwombe MwenyeziMungu sote kwa pamoja ainusuru nchi yetu isije ikaelekeahuko kwenye nchi nyingine walikoelekea. Ajalie iwe ni neema

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

52

kwa Watanzania na isije ikageuka kuwa dhahama kwetu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, watu wa Mtwara na Lindi niWatanzania ambao wanaishi Tanzania, wanajifunza kwakuona na kusikia katika maeneo mengie ambayo rasilimalihizi zinapatikana. Wamejifunza kwamba, kwenye maeneomengi ya machimbo nchini kwetu wananchi wamebakidhoofulhali, hawana matumaini, hawaangaliwi kwa jicho lahuruma. (Makofi)

Sasa mimi naomba niishauri Serikali kwamba badotuna nafasi ya kwenda kuzungumza na watu wa Mtwarajambo la busara, na hili naomba Serikali tusione kwambatutakuwa tumefanya jambo baya. Hakuna ambalohalizungumziki. Watu wanafika kuuana nchi nyingine nawanakaa kwenye meza wanaelewana, wanaishi. (Makofi)

Suala linaloendelea sasa hivi Mtwara, niwapongezeWanajeshi wetu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzaniawamekuwa wakiwasaidia wananchi kuwaelekeza nakuwapa matumaini ya usalama wao, kiasi kwambawameamua kutoka mafichoni na wamekuja katika makaziyao. Lakini kuna taarifa zisizokuwa nzuri kwamba Jeshi la Polisi,badala ya kulinda raia na mali zao, wanafanya udokozi.Jambo hili siyo zuri kwa Jeshi la Polisi, na ni sura mbaya.Naomba niwashauri kwamba wawe walinzi wa raia na malizao na waachane na mtindo huo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia niiombe Serikali kwamba,kwa kuwa sasa tunaelekea kwenye Sheria, Sera…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ah, nasikitika ni kengele ya pili.

MHE. HAMAD ALI HAMAD: Nakushukuru.

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

53

SPIKA: Ahsante sana. Namwita Mheshimiwa GosbetBlandes, Mheshimiwa Shah, halafu atakuja Mheshimiwa Arfi.Hawa ndio walikuwa bado.

MHE. GOSBERT B. BLANDES: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi. Naomba nianze kwa kusemanaunga mkono hoja hii kwa asilimia 100. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri na timu yako tuna imani kubwasana na ninyi, naomba mwendelee kuchapa kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nianze kwanza na Mgodi waNICKEL wa Kabanga, ambao uko Wilayani Ngara Mkoa waKagera, kwenye Jimbo la Mheshimiwa Ntukamazina. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, huu ni mgodi wa siku nyingiambao utaifaidisha nchi hii kwa kiasi kikubwa sana. Nilitakanifahamu mikakati ya Serikali, Mheshimiwa Waziri atuambie,ni lini mgodi huu wa Kabanga wa NICKEL utaanza ili Taifaliweze kufaidika kama ambavyo ni matarajio ya watu wengi?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, zimekuwepo ahadi nyingine hapaBungeni za Waheshimiwa Wabunge mbalimbali, mojawapoya ahadi hizo, ni ahadi ya Mheshimiwa Nyambari Nyangwine- Mbunge wa Tarime, kuhusiana na mradi wa kupelekaumeme vijijini, kwenye Kata zake mbalimbali ikiwemo Kataya Bumera, Susuni, Nyandoto, Gorong’a, Nyarukoba,Bungurere, Kangariani, Geta Gasembe, Komaswa, Ibaso,Kigongo, na kadhalika. (Makofi)

Mheshimiwa Nyambari amekuwa ananyong’onyeasana, anataka kujua umeme utakwenda lini katika maeneohayo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini tuna mgodi wetu wa NorthMara ambao uko Mkoa wa Mara. Wamiliki wa mgodi huuwaliahidi tena mbele ya Mkuu wa Mkoa na viongozi wetuwa kiserikali kujenga barabara inayotoka Nyamwagakwenda Nyamongo, hadi Mto Mara kwa kiwango cha lami.

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

54

Wananchi wa Tarime walitaka kujua, hawa watu wa mgodihuu ni lini watajenga barabara hii kwa kiwango cha lami?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda kutambua juhudi nyingisana na za makusudi ambazo Waziri na timu yake wanafanyakatika kupeleka umeme vijijini. Kwanza nawapongeza sana,na mimi nawahurumia, pamoja na kwamba mmetoa orodhahii ya vijiji, lakini nawahurumia, nia mnayo, lakini hamna fedha.REA hawana fedha.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2012, wakati wa bajeti2012/2013, tulipanga tozo ya Sh. 5/=, kutoka kila simu yamkononi kwa kuchangia Mfuko wa Umeme Bijijini. Bunge hilitulipanga kwamba fedha hizo ziende REA, na REA wawezekupeleka umeme. Orodha ya vijiji vyote ambavyo tunavyohapa, hakuna hata kijiji kimoja ambacho Serikali imeanza.Sasa mwaka wa fedha umekwisha, tulitegemea kwamba,mimi ninayo barua ambayo ilikuwa inasema mradi huuutatekelezwa katika mwaka wa fedha ule uliokwisha. Sasaleo Wizara haijaanza ni kwa sababu gani? Fedha hizihazijapelekwa kwenye Wizara baadaye zikaenda kwenyemfuko wa umeme vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lazima ifike mahali tuwe serious!Bunge linapoamua mambo fulani, mambo yake, huyo mtuasiyetaka kutekeleza tuletewe hapa, na Mheshimiwa Waziriusiwe mnyonge, sisi Bunge kama tumeamua, mtu hajaletafedha hizo, ulete taarifa hizo hapa, na sisi tufanye maamuziya busara na magumu kwa haraka sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile tulisema kwamba zitengwefedha kiasi cha Shilingi bilioni 300, zipelekwe katika Mfuko waUmeme Vijijini, fedha hizo ilikuwa zikusanywe kutoka kwenyemafuta ya Taa. Tulifanya maamuzi magumu hapa kwa ajiliya Taifa letu. Mpaka hivi ninavyozungumza, taarifa ambazoninazo hakuna hata Shilingi moja ambayo imepelekwa katikaMfuko huo wa Umeme Vijijini. Mimi nilitaka nijue, huyo ni naniambaye anapinga maamuzi ya Bunge hili? Kama mtuanapinga, kwa nini tunasimama hapa kufanya maamuzi?

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

55

Nataka Mheshimiwa Waziri, najua pengine hatakuwa na jibukatika hili. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tutakapofika katika Wizaraya Fedha, mimi nataka katika hili tulisimamie kwa nguvu zote,tuhakikishe tunajua fedha hizi, Shilingi bilioni 300 ziko wapi nakwa nini hazijaenda REA kwa ajili ya kupeleka umeme vijijinikwa wananchi wetu?

Mheshimiwa Spika, mimi natoka Wilaya ya KaragweMkoa wa Kagera, inapakana na Wilaya ya Kyerwa. Mwaka2012 tulizungumzia kupeleka fedha katika mradi wa umemewa Hydro huko Mrongo, na tulitegemea kwamba shughulihii iwe imeanza, na mradi wa Mrongo wa umeme (MrongoWater Falls), tulitegemea ulete changamoto katika kujengaviwanda, migodi ya Tin, lakini pia tulitegemea fedha hizizisambaze umeme katika Wilaya za Ngara, Biharamuro,Muleba, Bukoba Viji j ini, Ngara na sehemu nyingine.Tulitegemea mradi huu wa Mrongo uweze kuchangia kuletachangamoto katika kukua kwa uchumi katika Mkoa waKagera. siyo hapo tu, pia hata Pangani, tunao mradi waWater Falls Pangani, Water Falls Rusumo na sehemu nyingine.Pengine nilitaka nifahamu, Serikali imejipangaje katika miradihii ya Hydro katika nchi yetu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda kumpongezaMheshimiwa Waziri na timu yake na REA kwa ujumla,wameendelea kutuhabarisha habari ya mkakati wa kupelekaumeme vijijini. Mimi nashukuru vijiji vya Jimbo la Karagwenaviona humu, na wengine msishangae vijiji vya Karagwevinaonekana vingi, lakini kwa sababu ya utitiri wa ukaribukaribu, utakuta ni 0.5 Kilomita, 0.4 Kilomita, lakini napendakusema kwamba, nimewapelekea wananchi wa Jimbo laKaragwe orodha hii, nimetoa photocopy kwa kila kijiji, kwakila Mwenyekiti wa Kitongoji, na kila Mwenyekiti wa Kijiji. Kwakweli wote wamefurahi na wanashukuru na wanaipongezaSerikali kwa mkakati huo. Nimewaambia Serikali imeniahidikwamba mradi huu utatekelezwa kabla ya mwisho wamwaka 2014, utakuwa umekwisha na mkandarasi atakuwaameondoka. (Makofi)

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

56

Mheshimiwa Spika, sasa nilikuwa naangalia Bajetiiliyopangwa kwa ajili ya miradi hii, nimeona zimepangwaShilingi bilioni 153, wakati zinatakiwa Shilingi bilioni 881.Ninaanza kuwa na wasiwasi, inawezekana nikawanimejichongea kwa wananchi wangu kuwapa habari njemahizi, ambazo pengine hazitatekelezeka. Nikiangalia kwaharaka haraka, hizi Shilingi bilioni 153, ambako kuna upungufuwa mabilioni kadhaa, kama hizi Shil ingi bil ioni 881hazitapatikana, REA wakabaki na Shilingi bilioni 153, mradihuu wa kupeleka umeme vijijini kwa vijiji hivi tu vichacheutachukua siyo chini ya miaka sita mpaka saba, nainawezekana humu ndani akawa hakuna Mbunge hatammoja wa kukumbushia Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nilikuwa napendekeza, nianjema sana ya Serikali, nia njema ya Kamati ya Nishati yakupendekeza tozo la Sh. 100/= kwenye mafuta. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, naomba tukubaliane tozoya Sh. 100/= kwenye lita moja ya mafuta, fedha hizo ziendekwenye Mfuko wa Umeme Vijijini, tukubaliane kwa pamoja.Kama mtu huyu hapeleki fedha, mumlete hapa sisitumuwajibishe haraka iwezekanavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini tukubaliane tozo nyingine yaShilingi tano mpaka kumi katika kila dakika ya simu yamkononi. Tukubaliane fedha hizi ziende kwenye Mfuko waUmeme Vijijini. Katika hili Mheshimiwa Waziri tunaomba uweunatuletea taarifa angalau ya kila quarter kwamba mfukohuu umepokea Shilingi ngapi kutoka Serikani? Kama hawaleti,sisi tuchukue hatua za haraka sana, kwa sababu tukikaampaka mwaka uishe ni matatizo kwetu. Kwa hiyo, nikuombesana Mheshimiwa Waziri, tupe taarifa na sisi tujue cha kufanyakwa yule ambaye anakaidi agizo la Bunge.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwa kupelekamradi wa umeme katika Jimbo la Karagwe, katika vijiji vyaBisheshe, Nyaishozi hadi Ihembe. Najua kwamba kunaaddendum two inakuja, wananchi wananiuliza inakuja lini,pengine Mheshimiwa Waziri ni vizuri ukanijulisha hilo. Lakini

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

57

sambamba na hilo, tuliambiwa kwamba kuna fidia yawananchi ambao waliharibiwa mazao yao kwa kuruhusumradi huu kupita. Tuliambiwa kuna Shilingi milioni 200 zikomahali fulani. Siyo kwamba tunadai, sisi tunapenda sanamaendeleo. Lakini kwa kuwa tuliambiwa, tulipewa taarifahizo, tungetaka kujua kwamba fedha hizo ziko wapi, nazitalipwa lini?

Mheshimiwa Spika, kwa leo kwa kweli niwashukuru,niwapongeze, Mheshimiwa Professor tuna imani na wewe,Katibu Mkuu - Maswi, watu wa REA, TPDC, wote tunawaamini,lakini tatizo ni fedha. Waheshimiwa Wabunge tujifunge katikaBajeti tuhakikishe kwamba suala la umeme vijijini linapatiwaufumbuzi, fedha zinapatikana, na yule aliyekatalia Shilingibilioni 300, tulizopitisha hapa, kabla hatujamaliza Bunge hilitunataka tufahamu ni nani na ziko wapi na tunataka ziendezianze kazi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naungamkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa namwita Mheshimiwa Arifi,atafuatiwa na Mheshimwa Charles Mwijage, MheshimiwaBeartrice Shellukindo atafikiwa, Bwana Ussi atafikiwa,Mheshimiwa Ole- Sendika atafikiwa na Mheshimiwa“Buyogera atafikiwa.

MHE. ABDULKARIM E. H. SHAH: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa fursa hii niweze kuchangia mimi kupitiaWizara hii ya Nishati na Madini. Kwanza kabisa na mimi sinabudi kuungana na Waheshimiwa Wabunge wote kwakumpongeza Mheshimwa Waziri, Manaibu, Katibu Mkuu natimu yako yote ya wataalam, lakini bila ya kumsahauMkugenzi Mkuu wa REA kwa jitihada zake zote anavyojitahidikuhakikisha kwamba umeme unafika vijijini. Pia nisimsahaukwa Mafia, nimshukuru kwa pekee Ndugu Mramba - KaimuMkurugenzi Mkuu wa TANESCO. Kwetu sisi Mafia ni muhimuna tunamshukuru na kumpongeza na kumtakia kila la herina ninafikiri Serikali itakuona ikuthibitishe. (Makofi)

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

58

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri alivyoanza tuhotuba yake, alianza kusema neno kwamba umeme niuchumi, umeme ni maendeleo. Nakubaliana naye kabisa nanasema na sisi wana-Mafia tumepokea, na tutapokeaendapo hiyo kauli yako ikiwa ni thabiti. Naamini kwa umriuliokuwa nao, huwezi ukakaa hapa, ukasimama ukalihutubiaBunge hili, ukawahutubia Watanzania na dunia nzimaikakuona kwamba hapa unatulaghai. Siyo rahisi! Naaminikauli yako itakuwa thabiti, kwa maana ya kupitia umri nayale ambayo wewe unayategemea.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono maelezo yaWaheshimiwa Wabunge wenzangu, kama MheshimiwaBlandes alivyosema, kwamba lile tozo tulilosema la asilimiatano la muda wa maongezi wa simu, limekwenda wapi?Tunataka tupate maelezo kamili na ili tuweze kuchukuahatua. Isiwe hatua anachukuliwa mtu mwingine, lakini kunamtu anayezuia maendeleo katika nchi yetu kwa ubinafsiwake tu akaamua kulizuia na kuweza kuleta matatizo na kerokwa wananchi ambao wanaadhibika kule vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nianze. Baada yakuishukuru Serikali, naomba nitumie fursa hii kuishukuru Taasisiya Mafia Island Development Foundation (MIDF). Naombani-declare interest kwamba mimi pia ni member wa hiyopamoja na wenzangu katika kuona kwamba jambo lakupeleka umeme vijijini, nafahamu Wizara inafahamu, nakama haifahamu imwulize Mkurugenzi Mkuu wa REA - NduguMwakahesya, sisi MIDF tumechangia Shilingi milioni 500kuweza kuharakisha mradi huu kuja katika vijiji vya Wilayayetu ya Mafia. (Makofi)

Tumehangaika, tumejitahidi, tumeweza kupataufadhili wa Shilingi milioni 500. Sasa naomba mradi huu kwaMafia usije ukawa tena unatubabaisha. Tumechangia nguvuzetu, Wamafia tumechangia. Hatukusubiri mpaka nyinyiSerikali peke yake, asil imia 100 kwa 100 mlete. Sisitumechangia Shilingi milioni 500, ikiwa asilimia mbili, asilimiatano, ikiwa asilimia 10, lakini uchungu tulionao tumeuonyeshakwa kuweka nguvu yetu. Lakini pia nitumie fursa hii

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

59

kuwashukuru viongozi wangu wa MIDF kwa jitihada zao zoteza kuhakikisha kwamba wameweza kutafuta fedha nakuweza kuchangia mambo haya, na mambo ni mengi sanaya kimaendeleo ambayo yanaletwa kupitia MIDF.

Mheshimiwa Spika, Mafia leo tunatumia mitambo yakuzalisha umeme ya mafuta ya diseli. Nilikuwa naomba,nimeleta ushauri wa kimaandishi, lakini nataka niseme tukidogo kwamba mafuta yale, mashine zile mbili zinazozalishaKilowatts 800, 900, sasa hivi mmeweza kutuongezea, kutuleteamashine nyingine mbili zi l izotoka Njombe na sasazimeshafungwa, tunategemea zianze kufanya kazi. Zikifanyakazi kwa maana Mafia tutapata umeme wa Megawatts mbili.Lakini tupime kwenye gharama.

Mheshimiwa Spika, mashine mbili zile za mwanzo,kabla ya mbili zilizoletwa, gharama yake kwa mwakazinatumia mafuta lita 1,286,000. Kwa gharama ya bei ya leoya mafuta au kwa hesabu tuliyopiga, kila lita moja inafikathamani ya Sh. 2,500/=.

Kwa jumla kwa mwaka kwa mashine zile mbili, Serikaliinatumia bilioni 3.235 kwa mwaka kwa kuendesha mitambomiwili inayozalisha Kilowatts 900. Mashine hizi hazitoshelezi,ndiyo maana mkaona umuhimu baada ya kumwambiaMheshimiwa Rais na Rais akalichukua, na ninafikiri utekelezajiwake mmeuonesha. Mmeleta mashine mbili nyingine zenyeuwezo wa kuzalisha kilowatts 600, 600, kwa maanaukichanganya 600, 600, inakuwa 1,200 na zile 900 itakuwakama 2,100.

Mheshimiwa Waziri, sasa hebu liangalieni, ukichukuahizi ukijumuisha kwa mashine nne, gharama za matumizi kwamwaka ni zaidi ya Shilingi bilioni 3.29. Matumizi haya ya mafutakwa mitambo hii miwili, ukija ukichanganya kwa kipindi chamiaka 25 na natoa mfano wa miaka 25 kwa sababunimepata taarifa, nimesoma vijarida kupitia jarida mojalinalotoka Wizara ya Nishati ya Zanzibar kwamba imetumiaShilingi bilioni 111, sawa na Norwegian Krone milioni 400 kulazaumeme cable ile ya Baharini kutoka Pemba hadi Tanga.

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

60

Sasa ukichukua gharama hiyo na kule urefu wake ni kilomita72. Wakati Naibu Waziri alipokuwa Mheshimiwa AdamMalima, alitoa mawazo kwamba kwa nini tusivushe umemekutoka Rufiji, Nyamisati kuja mpaka Mafia kwa kulaza cable.Pale umbali wake ni kilomita 35, 36 mpaka 37, haiwezi kuzidihapo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuangalia gharama hizi,tunaweza tukatumia shilingi bilioni 50 au 55 kwa kulaza cablekuja Mafia pamoja na mitambo yake yote na kulipa fidialakini kama tukisema tutumie mashine hizi nne za mafuta yadizeli, tutatumia zaidi ya shilingi bilioni 164.67. Kwa hiyo,tutaokoa mabilioni ya fedha na zitaweza kusaidia wananchiwengine au shughuli nyingine za kimaendeleo katika nchiyetu hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba sana Mheshimiwa Wazirialipokee hili, alichunguze na waangalie uwezekano wakuweza kudhamiria kulaza cable hii ni gharama ndogo tenaya miaka 30 gurantee kulala baharini. Kwa hesabu niliyokupamafuta yasipande bei kwa miaka 25, kitu ambachohakiwezekani. Kwa hiyo, tutaharibu mazingira yetu kwamafuta yale na sasa hivi kuna mitambo mingine inayotumiabiomass ya kukata miti, sijui wataalam tulifikiria nini lakininachosema hii ndiyo solution peke ya kuweza kupata umemewa uhakika kwa Mafia. Tukipata umeme huu, basi Mafiainaweza ikawa Mini-Singapore katika East and Central Afrika.Ni kisiwa ambacho kinaweza kikaleta tija katika nchi yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba sana, nitumie fursa hii,kumwomba Mheshimiwa Waziri, vij i j i vyangu 23tuliokuchangia nguvu zetu, usitutupe mkono. Katika maombiyetu ya kwanza wakati wanaanda study ile walitaja vijiji 13lakini tumeongezea hivi vijiji, naomba sana, vijiji ambavyohavikuorodheshwa na nil iandika barua maalum,nikamkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa REA kumwambiakwamba vile vijiji vilivyosahauliwa viweze kuingizwa katikahii program na waweze kupata umeme.

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

61

Mheshimiwa Spika, sina mengi ya kusema upande waumeme, nikutakie kheri lakini tunataka tumjue nani yulealiyezuia hii pesa wewe usipewe tuliyokuwa tumeipitisha hapaBungeni na kuitolea maamuzi mazito, kwamba shilingi tanoya muda wa maongezi ya simu zije kuchangia REAzimekwenda wapi? Hilo nataka kulijua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho, nizungumzie kuhusundugu zetu wa Mtwara. Niwaombe sana, mengiyamezungumzwa, busara nyingi …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Haya ahsante. Sasa nitamwita MheshimiwaSaid Arfi, atafuatiwa na Mheshimiwa Charles Mwijage,Mheshimiwa Beatrice Shelukindo, Mheshimiwa JeromeBwanausi, Mheshimiwa Christopher Ole-Sendeka naMheshimwia Agripina Buyogera.

MHE. SAID A. ARFI: Mheshimiwa Spika, nikushukurusana kwa kunipa nafasi hii lakini ninapaswa nimshukuru sanaMwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha kwa kunipa afyana kuweza kusimama hapa.

Mheshimiwa Spika, tupo katika kipindi cha majaribu.Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi, alipomteuamja wake Nabii Suleiman, akampa ufalme na mali lakini NabiiSuleiman akamwomba Mwenyezi Mungu amjalie hekima.Pamoja na kuwa na ufalme na mali, Nabii Suleiman alionaamepungukiwa kama atakuwa hana hekima. Hekimaimendikwa hulijenga Taifa. Ni matumaini yangu katika hayaambayo yanajiri katika Taifa letu sasa, hekima itatamalaki ilikuweze kuwepo amani na upendo miongoni mwaWatanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa namna yoyote ile, kwaunyenyekevu napenda kuiomba Serikali na kuishauri sababundiyo wajibu wa Mbunge kuishauri Serikali, wawashirikishewananchi katika masuala yanayohusu maisha na

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

62

mustakabali na maendeleo yao ili waweze kuepukamisuguano isiyokuwa na lazima. Rasilimali ambazo MwenyeziMungu ametupa, ni kwa ajili ya manufaa na maslahi yaWatanzania wote. Ni elimu ya kutosha kama ingekuwepona ushirikishwaji uliokuwa mpana, tusingefika hapa tulipofikalakini bado nina matumaini makubwa sana kwamba hekimana busara itatamalaki ili tuweze kufikia mahali pazuri. Kadritunavyochelewa katika kulifikia na kulitanzua tatizo hili,ndivyo tunavyorudi nyuma katika kupiga hatua zamaendeleo. Kwa sababu majirani zetu Msumbiji sasa hiviwanakwenda kwa kasi. Hatua zozote za kuturudisha nyumatusiende katika malengo tunayokusudia, tunaweza piatukachelewa kufika katika hilo soko tunalotarajia kwenda.Kwa unyenyekevu niwaombe Watanzania wenzanguwaweze kuona na kutanguliza maslahi ya Taifa letu nakudumisha amani na upendo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo,nizungumzie sasa wachimbaji wadogowadogo. Wasemajiwaliotangulia wamezungumzia maeneo yao, nami sina budinizungumzie Mpanda kama eneo moja ambalo limekuwana wachimbaji wadogowadogo kwa takriban zaidi ya miaka40. Cha ajabu, katika maeneo na mahekta zilizokuwazimetengwa, maeneo ambayo yana migogoro yawachimbaji wadogowadogo hayakuguswa kabisa,yametizamwa maeneo mapya kama yale ya Kibaha naIlagala, mkaacha Kahama na Mpanda ambako kunamatatizo makubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wachimbaji hawawadogowadogo wamekuwa pale na familia zaowakiendesha maisha yao, wakitegemea kufanya kazi hizolakini cha ajabu maeneo yao wamepewa wale wanaojiitakwamba ni wachimbaji wakubwa. Matapeli wachache nabaadhi ya waliokuwa viongozi, wamehodhi maeneo hayona muda ulipokwisha, wamebadilisha jina la Kampuni nawanaendelea kuhodhi. Hali hii haiwezi kuvumilika na wakatimwingine inasababisha wananchi kufikia kuchukua hatuakama hizo wanazozichukua sasa huko Buhemba. Ni lazimaWizara ikae na wachimbaji hawa wadogowadogo walioko

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

63

Mpanda, Kahama, Buhemba, waweze kwanza kutanzuamigogoro iliyoko sasa kabla ya kufikiria kuanza kuchukuahatua zingine. Wanavyoendelea kuwapuuza hawawachimbaji wadogowadogo, ndivyo wanavyozidisha chukidhidi ya Serikali, chuki dhidi ya viongozi, kwa sababu hawajalina kuwaondolea kero zao.

Mheshimiwa Spika, badala ya kuwasaidia hawawachimbaji wadogo kilichotokea ni kwamba Wizaraimeamua kupandisha ada na tozo mbalimbali za leseni ilihawa Watanzania maskini wasiokuwa na uwezo wasiwezekumiliki maeneo hayo ya kuchimba madini. Jambo hili si jemasana. Niiombe Wizara ijaribu kuangalia kama ina nia njemana kuwasaidia Watanzania maskini, viwango vinavyotozwaviangaliwe view ni vile ambavyo Watanzania wanawezakuvimudu.

Mheshimiwa Spika, Wizara imechukua hatua yakupunguza gharama za kuingiza umeme huko Kusini kutokagharama ya shilingi laki moja na kidogo mpaka shilingi elfutisini na tisa, kwa kuwa na vigezo fulanifulani ambavyowalivitazama kutokana na hali za maisha za wakazi wamaeneo hayo lakini hali ya Watanzania inafanana. Kamammeamua kupunguza gharama za kuingiza umeme kutokaSh.160,000/= mpaka Sh.99,000/=, ziwe kwa nchi nzima. Kwakufanya usawa huo mtakuwa mmelisaidia sana Taifa hili ililiweze kufikia malengo yanayokusudiwa. Vinginevyo kuwekatabaka, eneo moja linapunguziwa, eneo linginelinapandishiwa, bado mtaleta manung’uniko na kelele kwawananchi.

Mheshimiwa Spika, wametengeneza mpango wakuwasaidia mikopo hawa wachimbaji wadogowadogo.Katika bajeti iliyopita ya mwaka 2012/2013 zilitengwa shilingibil ioni 8.9 lakini mpaka sasa hivi hakuna mchimbajimdogomdogo hata mmoja ambaye amepata mkopo huokutoka na urasimu, mchakato na mambo kadha wa kadha.Mikopo hii inategemewa itaanza kutolewa mwezi Julai, 2013,tena kupitia Benki ya TIB ambayo iko Dar es Salaam.Unamsaidiaje mchimbaji mdogomdogo wa Mpanda ili

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

64

aweze kupata mkopo kupitia TBI Dar es Salaam. Hili ni tatizolingine ambalo kwa kweli bado linatusumbua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la umeme,nimesoma katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri, Mpandailikuwa miongoni mwa ile awamu ya kwanza ya Kibondo,Kasulu na Mpanda kupata generator mbili mbili za umemetena ikiwa ni ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania bado hazijafika. Sasa imeingizwa katika mpangowa Ngara, Biharamulo na Mpanda wa kupata generatormoja. Nataka kuelewa ni kwa nini tumetoka kwenye mbilina kuja kwenye moja na kwa nini mpaka sasa haijafika?Pamoja na kwamba pengine Mheshimiwa Waziri, ulimi tuuliteleza akasema kwamba hivi sasa ninapozungumza nanyinyi, hizo generator zinateremshwa huko Ngara,Baharamulo na Mpanda ambapo si kweli, generator hizohazijafika. Naomba sana kupata maelezo juu ya eneo hilo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni mradi wa Malagarasi.Kanda ya Magharibi haijaunganishwa katika grid ya Taifakwa maana ya Mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa nasehemu kubwa ya Mkoa wa Kagera. Hakuna mkakati wanguvu na wa makusudi na tegemeo kubwa ilikuwa ni mradiwa Malagarasi ambao umesuasua kwa sababu mbalimbalilakini kwa sababu sasa kuna compact three, tulikuwatunataka tujue ni lini sasa mradi huu wa Malagarasi utaanza.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni kwa nini NDC ilipoingia katikamikataba na makampuni haya ya Kichana ya kuchimbamakaa ya mawe, upande mmoja wana hisa asilimia 30 naupande mwingie wana hisa asilimia 20? Je, Wizara hainampango mahsusi kwamba mikataba tunayoingia basitutakuwa na hisa ya kiwango Fulani? Ni matakwa tu, nimakubaliano tu, hata tukiwa na hisa 10 zinatosha? Ni kigezogani kinachotumika hapa iwe 30 na hapa iwe 20? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho napenda kujua mipangoya rasilimali zilizopo Liganga na Mchuchuma. Imeelezwa

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

65

habari za kufua umeme lakini chuma hakuna maelezoyoyote. Kuna mkakati gani sasa wa kuona kwamba rasilimaliya chuma inalisaidia Taifa hili?

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Mbunge ahsante sana. Sasanamwita Mheshimiwa Charles Mwijage na MheshimiwaBeatrice Shellukindo ajiandae.

MHE. CHARLES J.P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipatia nafasi na nianze ku-declareinterest kwamba mimi ni mdau wa sekta hii sana. Ninafanyakazi za ushauri na Mungu akinijalia katika miaka mwili aumitatu ijayo nitakuwa operator. Napenda nikiri kuwa mimini Mwenyekiti wa Chama anayesimamia sekta hii.

Mheshimiwa Spika, nitoe utangulizi au niwasaidiawatu wa Serikali, shilingi bilioni 300 zinazongumzwa zilifikiwavipi? Tulipofanya maamuzi yale, unaweza kuyaita vyovyote,Serikali ilikuwa imeshindwa kudhibiti uchakachuaji wamafuta, vitendo viovu ambavyo vilivyoiingiza hasara nchihii. Makadirio ya kitaalam, mimi ni mtaalam wa sekta hii,Taifa lilikuwa linapoteza Sh.50,000,000,000/= kwa mwezi namwaka mmoja una miezi 12, ukizidisha miezi 12 naSh.50,000,000,000/= unapata Sh.600,000,000,000/=. Baada yamafanikio ya kudhibiti tatizo hili, busara ikalituma Bungekusema basi, mafanikio ya kudhibiti uchakachuajiSh.300,000,000,000/= wapewe wananchi ambao waliumizwa.Kwa hiyo, mtalaam wa Serikali atakayekuja kubisha, abishekwa kuanzia Sh.50,000,000,000/= kwa mwezi na abishekwamba mwaka wa Kitanzania hauna miezi 12. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kumpongezaWaziri, kwa namna alivyokuja na mpango wa umeme lakinimimi niende kwa Mtemi Chenge, Mjumbe wa Kamati kuwezakuchangia pamoja na Wabunge wenzangu namna ganituweze kupata pesa za kumpa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni wazi Serikali imehangaika

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

66

kutafuta rasilimali. Rais wa nchi hii amezunguka dunia nzimaakitafuta rasilimali za kujenga barabara na umeme,waliobeza wamebeza lakini sisi busara za kwetu zinasema,“entukuru egarukoa nyamgarura.” Unapomtembelea mtu nayeye akikutembelea, ukimpelekea zawadi anakuleteazawadi. Kwa hiyo, waliombeza Rais wangu wanaokujakumtembelea wanamletea zawadi. Rais wa China aliletazawadi, kama hamkuona, angalia bomba litajengwa.Mheshimiwa Barack Obama, Rais wa Marekani, atakuja nazawadi, Power for Africa na Power for Africa, inazinduliwaTanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba nashabikiakupewa lakini busara inanituma kwamba sisi kamaWatanzania tukibebwa lazima tujikaze. Wakati umefikaWatanzania tujitahidi kwa pamoja na sisi tuwe tayari kutoa,tupunguze matumizi yetu tuweze kutoa. Naungana naWajumbe na Kamati yangu iliyosema kwamba tutoeSh.100/= kwa kila lita ya mafuta tutumiayo kusudi kuchangiamfuko wa REA, tutaweza kupata Sh.250,000,000,000/=.Kumbe makampuni ya simu yalikuwa yakitu-charge Sh.130/=mpaka Sh.150/=, sasa wamekuwa na busara, wamerudimpaka Sh.30/=. Tufanye maamuzi, tutenge Sh.20/= tuwezekukusanya Sh.250,000,000,000/= kwa mwaka tuiweke kwenyeumeme. (Makofi)

Mheshmiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa Nishati naMadini, natambua uwezo wako wa Kimataifa wakuzunguuka dunia nzima kuomba lakini unapokwendakuomba chakula basi na sisi tukusanye kuni nyumbani.Huwezi kwenda kuomba chakula, ukarudi ukaomba na kuni.Lazima na sisi kama Taifa tusimame tuchangie chochotekusudi uwe na uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, manufaa ya tozo. Mamlaka yaREA, itakapokuwa na tozo ya uhakika katika mafuta na simu,itakuwa na uhakika wa Sh.500,000,000,000/= kwa kila mwaka.Inaweza kumweka mkandarasi site bila kujua kama pesaitakuja kwenye bajeti au haitakuja. (Makofi)

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

67

Mheshimiwa Spika, mimi nimewaona Wabugnewenzangu kila mtu ana haraka. Mimi nina haraka sana,hakuna kijiji katika Jimbo langu kitakubali kwamba kisipateumeme. Ninamshukuru Mheshimiwa Rweikiza,amewatangazia ndugu zangu wa Makongora kwambaumeme unakuja. Namshukuru sana ndugu yangu huyu.Napenda umeme uende Bulembo, Luanda, Kyanshenge,Lwigembe, katika sehemu hizi zote kwenye ramani ile hazipo.Mimi ile ramani ninaipenda sana tena ina rangi nzuri lakininikiipelekea Jimboni watu wa Lwigembe, Bulembo,Kyanshenge, Ruanda wasipoiona hawatanielewa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nimejenga hoja kwambatuweke tozo na Wabunge wote wameshakubali, walikuwawananiita nje wakaniambia, Waziri mnaelewana mwambiesisi tumekubali tozo. Sasa Wizara ya Fedha, sisi tumekubaliwenyewe, mtu akikukinga kichwa mnyoe, kwa nini usimnyoe,tumekubali sisi kwa niaba ya wananchi wetu. Wananchi waKafunjo wanataka kuchangia umeme, msichange,tutachanga Taifa zima, twende kama Taifa, Taifa ni mojatuchange. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie kuhusu wachimbajiwadogo. Wachimbaji wadogo wengi wana mapungufu.Ninajenga hoja kwamba Chuo cha Madini cha Dodomakiimarishwe, kijitegemee, kiwe kama vyuo vingine imara.Kisiwe Idara ya Wizara, wapange mipango yao lakinimipango ninayoitaka ni mipango ile ambayo mwanafunzianapoingia katika chuo ajue kwamba hatapewa kazi ilaanapotoka pale anakwenda kujiajir i. Kwa sababutumejenga utamaduni wa kutoa mikopo, walewatakaokuwa wamepata mafunzo ya chuo, ndani ya chuoau kwenye site, wawe watu wa kwanza wa kupewa mikopohiyo.

Mheshimiwa Spika, huwezi kumpa mtu mkopo wacompressor wakati hajawahi kuitumia, ataogopa kuvaamask, Mheshimiwa Profesa unayajua haya. Kwa hiyo,tunajenga hoja, kwamba Chuo cha Madini ukubali kiondoke.Ukichkure. Mtoto hata kama ukimpenda vipi, ukifika wakati

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

68

wa kuacha kunyonya, muachishe ziwa. Chuo cha Madini,kiache kitembee ukiangalie kwa mbali. Ni kwa kuwezeshaChuo cha Madini, wananchi watashiriki kwenye kuchimbana wakichimba watapata pato na wakipata pato wakalipeushuru na wakilipa ushuru baki wanapeleka nyumbani, ndipomtakapoweza kuona tangamano la faida ya madini. Huwezikuona faida ya madini kwa kuyaangalia. Hatayangelichimbwa jikoni mwako lazima ushiriki. Unashiriki vipi?Kwa kuchimba au kwa kuwa mgavi wa kupeleka chakula.Tusibaki kuwa watazamaji katika shughuli ambayo MwenyeziMungu aliiweka mlangoni mwetu.

Mheshimiwa Spika, nitakuwa ninadanganyanisipozungumzia Kampuni ya Mafuta ya Taifa. Hofu namashaka ya Watanzania walio wengi kuhusu sekta ya mafutani kwa sababu hawashiriki na wataalamu wa masoko waUnilever walisema ukitaka uhondo wa ngoma uingie ucheze.Sasa kama mafuta yana faida kubwa, napenda kuuliza,kigugumizi cha Serikali kwa muda wote kuanzisha Kampuniya Mafuta ni nini? Nimuulize Waziri ambaye ni msomialiyebobea katika nishati, kuna hasara kuanzisha Kampuniya Kitaifa au hatuna Mameneja? Azaliwe nani aje aweMkurugenzi ya Kitaifa?

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais aliwahi kusemakwamba Tanzania tunayo location advantage na miminiwaambie ni mtaalamu katika sekta hii, nchi zilizotuzungukazinakuwa na busara ya moyo yaani peace of mind kamazitafanya biashara na kampuni ambayo ina dhamana yakitaifa. Kampuni za Kongo, Rwanda na Burundi zikiagizamafuta kupitia National Oil Company, zinakuwa na peaceof mind, tunasubiri nini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haihitajiki mtaji kwani mteja wakowa kwanza ni Halmashauri, mteja wa pili ni mashirika yaumma. Imefika wakati kwamba wale watakaojitokeza zaidikujenga nchi hii tuwawezeshe, upendeleo wa kuwaambiakampuni ya kitaifa i-supply mafuta katika mambo ambayotuna interest, siyo kificho wala siyo uonevu, inafanyika hivyoMarekani na huko China na nilikuwepo juzi nimeona kwamboni zangu mwenyewe.

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

69

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala la wawekezajina nitawapa mfano mdogo. Mwezi Desemba rafiki yangualikwenda nyumbani na gari aina ya Toyota Noah, mdogowake mdogo kabisa akamwambia Kaka umekuwa fisadi,akamuuliza kwa nini, akamwambia umenunua gari la Noah.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda niwashauri Watanzaniawenzangu kwamba huwezi kupambana na umaskiniukiogopa utajiri. Kama kuna mtu ni fisadi mumpelekeMahakamani ili wimbo wa fisadi uishe. Ninyi mnaowaitawenzenu mafisadi kwa sababu wanatembelea Noah,mnataka watembelee tumbo? Kama mtu ni fisadi,anahujumu, mtafute Wanasheria ili mumpeleke Mahakamanimambo yaishe, Noah ni ufisadi? Kwa hiyo, ndugu zangumambo ya kusema mafisadi yafike mwisho.

Mheshimiwa Spika, nirudie kwa niaba ya Kamatikuizungumzia TANESCO. TANESCO wanafanya kazi kubwalakini wamebanwa mbele na nyuma, wana hali ngumu,wananunua umeme ghali na wanauuza rahisi. Waziritumekushauri katika Kamati uwaangalie watu hawa,huenda upungufu wao unatokea hapo.

Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii kumpongezaMeneja wa TANESCO Muleba kwa kazi nzuri anayofanya yakusambaza umeme katika Wilaya ya Muleba. Wananchiwangu wamefikia hatua ya kutaka kuchanga ili kufikishaumeme.

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. CHARLES J.P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika,naomba niunge mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante. Sasa namwita MheshimiwaBeatrice Shellukindo na Mheshimiwa Jerome Bwanausa,Mheshimiwa Christopher Ole-Sendeka na MheshimiwaBuyogera wajiandae.

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

70

MHE. BEATRICE M. SHELLUKINDO: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi. Kwa kweli ningesikitika sanakwa sababu nilikuwa na salamu za kutoka Kilindi.

Mheshimiwa Spika, inasemekana kwambausiposhukuru kwa machache na makubwa huwezi kuyapata.Kwa niaba ya wananchi wa Kil indi ambao ndiyonawawakilisha hapa, nichukue fursa hii kwanza kabisakumshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini,nimshukuru sana pia Naibu Waziri wa Madini, Kamishna waMadini, Katibu Mkuu na wengine wote, kwa jinsi walivyowezakushughulikia mgogoro ambao ulikuwa sasa unaingiakwenye sura tofauti ambayo kwa kweli ilikuwa inatuzuiakufanya maendeleo zaidi ya kuzungumzia mgogoro mmoja.Mgogoro huu ulikuwa katika eneo ambalo li l ikuwalimetengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo yaani eneotengefu. Katika eneo hili walikuwa wamepewa watu waAshanti ubia lakini leseni yao ilikuwa inapita kwenye maeneoya vijiji vinne. Vijiji hivi vinne havikupewa haki yao mpakahawa wakubwa niliowataja walipoweza kusimama kidetena kutoa maamuzi na hakika sasa tunashukuru. Vilevilenimeombwa sana kumshukuru Mheshimiwa Ngeleja kwawakati wake, Mheshimiwa Malima na Mheshimiwa Kafumuwakiwa pale wao ndiyo walianza mchakato ambao sasatumehitimisha, tumekuwa huru sasa na nafurahi kusema palejuu kwenye gallery kuna wananchi wametoka katika vijijihivyo vya Msamvu, Kikunde na Ludewa ambao wamekujakushiriki siku ya leo na kuleta salamu za shukrani kubwa sana.Kwa hiyo, kwa niaba ya wananchi wangu nasema ahsantenisana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini vilevile tumeahidiwa janana Mheshimiwa Waziri kwamba tarehe 3/6 wanakwendawatafiti kutoka Wizara ya Madini Geological Survey, watafikakule katika eneo husika ili kutathmini ukubwa wa eneo namali iliyopo na kutoa maelekezo nini kifanyike. Kwa hiyo,tunaendelea kumshukuru sana Profesa Mduma. Vileviletumeahidiwa na Naibu Waziri wa Madini, MheshimiwaMaselle kwamba mafunzo yatakwenda mara moja kwawatu wale ambao ni zaidi ya vijiji 12 na kwa sababu Kilindi

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

71

kila sehemu ni madini kwa hiyo kote kule wameahidikwamba watatupa mafunzo kwa hiyo tunaendeleakushukuru. Tumeambiwa tukishajiunga kwa taratibu ambazotutaelekezwa na wataalamu basi watu wetu wataweza piakupata mikopo pamoja na maelekezo ya jinsi ya kutumiamaeneo hayo kwa njia ya usahihi. Kipekee kwa niaba yawananchi wangu, naomba niseme ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, la pili, niseme namshukuru sanaNaibu Waziri, Mheshimiwa Simbachawene. MheshimiwaSimbachawene pamoja na Mr. Mwakahesya wa REA. Hawanao wametusaidia sana, ni kweli tulipata umeme kipindi chamwaka 2010 lakini wameendelea kuwa bega kwa bega nasisi na kusikia kilio chetu kila tulipokuwa tunakipeleka kwao,kwa hiyo, nashukuru.

Mheshimiwa Spika, niendelee tu kusema kwambapamoja na shukrani, kuna mambo machache ambayo nilazima niyasemee. La kwanza kabisa, tunashukuru kwambatumepewa umeme katika awamu hii ya mwaka 2013/2014katika vijiji vinne, Gairo ambayo tunapakana nao ambapondipo umeme utapita imepewa vijiji sita. Tumekaa namwenzangu Mheshimiwa Shabiby tukaangalia vijiji vingine,wengine wana vijiji mpaka 50, 60 au 69 lakini sisi tumepewakidogo ambapo kwa kweli umeme ndiyo kwanza umeanzakungia katika Wilaya zetu. Kwa hiyo, naomba tu nilisemeehilo.

Mheshimiwa Spika, lakini zaidi ya hapo, katika Wilayaya Kilindi, vile vijiji vitatu ambavyo vimetajwa, Kijiji chaMswaki, Mgera na Kwamaligwa, tayari umeme umepita pale.Mwaka 2011 niliuliza kwa nini umeme umepita lakinitransformer haziwekwi watu wakanufaika na umeme?Nikaambiwa transformer hazikuwepo lakini zikifikatutawekewa. Mwaka 2012 nikauliza swali hilohilonikaambiwa sasa zimefika lakini zile nguzo fupi za distributionhakuna. Sasa niulize, hii ni miradi mipya au tunakwendakukamilisha kazi ya awali? Kama ni kukamilisha kazi ya awalibasi naomba vijiji vitatu katika Wilaya ya Kilindi, kati ya vijiji102, vijiji 86 havina umeme wala hawajawahi kusikia,

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

72

naomba basi vile vijiji vitatu ambavyo tayari umeme ulipitani kukamilisha tu kuweka transformers, basi vijiji hivi viongezwelakini niseme tu nashukuru.

Mheshimiwa Spika, vilevile umeme Kilindi mudamwingi sana umekatika, sisi tupo kwenye constant mgawo,mgawo hauishi, mara transformer imeungua, mara nguzozimeanguka yaani hatumalizi wiki tukiwa na umeme wakudumu. Naomba sana Mheshimiwa Waziri, suala hilinimelifikisha mara kadhaa kwenye ofisi yetu ambayo ikoHandeni vilevile nimelifikisha hata Tanga, lakini inaelekeatatizo ni kubwa zaidi. Naomba sana tuweze kusaidiwa kwaupande huu.

Mheshimiwa Spika, ofisi ya Madini Wilaya ya Kilindi nimwaka wa nne huu tunaomba tuwe na Ofisi ya Madini. Robotatu kama siyo yote ya Wilaya ya Kilindi ni Madini matupuambayo tumeyatambua na ambayo hayajatambuliwa yaaniyanayoendelea kutambuliwa. Tunaomba Ofisi ya Madinikwani kwenda Handeni kilomita 132 ni mbali na hatausimamizi unakuwa ni mgumu na ndiyo maana hata watuwetu hawawezi kupata elimu ya madini. Naomba sana Ofisiya Madini, sasa jamani mlisema tuwape chumba, chumbakipo, njooni mfunge vifaa, tupeni wataalamu MheshimiwaWaziri ili na sisi tuweze kufanya kazi na kuona tunanufaikavipi kwa kushirikiana nao ili tuweze kuona Wilaya yetuinanufaika vipi na madini hayo.

Mheshimiwa Spika, toka tarehe 27/7/2012, Serikaliilipandisha gharama kwa kiwango cha juu na gharama hizini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa hizi leseni za utafutaji madinikutoka dola 100 mpaka 300, kodi ya mwaka dola 40 mpaka100 kwa kila kilomita ya mraba ambayo hii kwa kweli ni fedhakubwa mno. Sasa kodi hizi zimekuwa ni kubwa, tumeendeleakupokea malalamiko mengi sana ambapo wananchi wakawaida ambao wamethubutu kuingia kwenye shughuli hii,kwa kweli wanashindwa kuzimudu. Sasa mimi naomba kwasababu kuna taarifa kwamba wengi sasa wanasema bwana

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

73

tumeshindwa inabidi tuachie, mimi naomba kweli suala hilisasa liangaliwe kwa upya ili kuhakikisha kwamba hatuathiriuchumi wetu na hawa Watanzania ambao wamekuwawakifanya kazi hiyo.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa wachimbajiwadogowadogo kama wa Kilindi ambao kwanza hawanaelimu lakini pili wanachimba na nyundo na sululu, wanamazingira duni na hata hayo madini yenyewe mpakawayapata madeni ni makubwa. Kulikuwa hakuna kulipia adaya maombi ya leseni ndogo lakini sasa hivi wanatozwaSh.50,000/=. Ada ya kutayarisha leseni kutoka Sh.20,000/=imekwenda kuwa Sh.50,000/=, ada ya mwaka ya lesenikwenye vito, almasi na dhahabu ni Sh.20,000/= hadi Sh.80,000/=, madini mengine kutoka Sh.10,000/= mpaka Sh.50,000/=,jamani hawa wananchi wanashindwa. Kuna dhanainayosema kwamba watu hawapendi kulipa kodi lakinitumefanya tathmini ya kuona kwa nini hawataki kulipa kodi?Kwa sababu mwananchi wa Kilindi anachukua muda mrefukuchimba anakuja kupata gramu mbili lakini akiziuzaanakuwa na madeni kuzidi ile gharama na hao wenginehali kadhalika.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli mimi naomba pamojana kwamba sheria ya mwaka 2010, kifungu 112 inamruhusuWaziri na Ofisi yake kuweza kubadilisha hivi viwango vya tozolakini palepale nimeona kuna kipengele cha tatu mbali nakusema kwamba ni lazima washauriane na Waziri wa Fedhana Kamishna na kadhalika labda hayo aliyafanya, anasemaatashauriana na wadau wa sekta ya madini pamoja nawachimbaji wadogo, sasa hawa hawakuhusishwa. Miminaomba ili tusiwaathiri, nia ni njema, Serikali inahitaji kupatamapato, tunakubali kabisa nia ya Waziri najua ilikuwa ninjema lakini basi tufanye utafiti tuone kweli tunachokifanyani sahihi kwamba kitawasaidia hawa watu au ndiyotunawaondoa kwenye sekta hii?

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nisichukuemuda mrefu, lengo langu kubwa lilikuwa kusemea hayomambo mawili ya msingi sana ambayo nimeona kwa leo,

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

74

nikirudia tena kuwashukuru kwa niaba ya wananchi waKilindi. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Nimwite Mheshimiwa JeromeBwanausi atafuatiwa na Mheshimiwa Mnyaa halafuMheshimiwa Christopher Ole-Sendeka.

MHE. JEROME D. BWANAUSI: Mheshimiwa Spika,kwanza nichukue nafasi hii kukushuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuchangia kwenyeWizara hii kwa kuungana na Wabunge wenzangu wotewanaosema REA kupatiwa fedha za kutosha kwa ajili yakupeleka umeme vijijini ni jambo muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini nitoe masikitiko yangukuhusiana na Jimbo langu la Lulindi. Kwa kweli huyu mgeniREA wananchi wa Lulindi wanamsikia tu, naomba sanaWizara ihakikishe katika awamu hii vijiji vilivyopo katika Jimbola Lulindi ambavyo havikupata awamu ya kwanza kabisa,viweze kupewa nafasi ili wale wananchi wa Kata za Chiwata,Mpindimbi, Nanjota, Mbuyuni, Namalenga, Navila pamojana Chikolopola waweze kupata umeme katika maeneo yaoikiwa ni pamoja na Mchaulu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ningeweza pia kumsemeaMheshimiwa Dkt. Kikwembe ambaye Wilaya yake ya Mlele,Inyonge inafanana na Jimbo la Lulindi, Kata zake zotehazijapata umeme nadhani ni vizuri nazo zikaweza kupatanafasi ya kupata umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna suala hili la ofa iliyotolewakwa Mikoa ya Lindi na Mtwara ya Sh.99,000/=. Mimi naishauriSerikali kupitia Wizara kwamba ofa hii isiwe ya vipindi vyamiezi sitasita, ni vizuri sasa ikatangazwa kwamba ofa hii ipoya kudumu kwa sababu tangu tutoe ofa hii wananchi wengihawajanufaika kwa sababu upatikanaji wa vifaa kupitiaTANESCO umekuwa ni wa kusuasua sana, kwa hiyo, ni vizurihii ofa iwe ni ya kudumu.

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

75

Mheshimiwa Spika, lakini jambo lingine ambalonataka kulielezea ni juu ya kukatikakatika kwa umeme katikaMikoa ya Mtwara na Lindi. Suala hili sasa limekuwa ni tatizosugu. Bbahati nzuri sana Mikoa ya Lindi na Mtwara kwa sasahaitumii gridi ya Taifa na tunao umeme wa kutumia gesiMtwara lakini upo upungufu ikiwa ni pamoja na nguzo lakinikuna vifaa ambavyo TANESCO wanadai kwambavinasambabisha umeme huu kukatikakatika. Kwa hiyo,namwomba sana Waziri atakapokuwa anahitimisha hotubayake, ajaribu kuwaeleza wananchi wa Mikoa ya Mtwara naLindi hili tatizo la kukatikakatika kwa umeme litamalizika lini?

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni suala laupatikanaji wa vifaa kwa mfano mita za Luku, kwa kweli nitatizo kubwa sana. Maeneo mengi nchini ikiwa ni pamojana Mikoa ya Kusini tumeanza kuwekewa Luku lakini unakutakwamba kila wananchi wanapotaka kwenda kuomba, kwakweli upatikanaji wake umekuwa ni wa kusuasua sana. Nivizuri niishauri Serikali kupitia Wizara kuhakikisha jambo hililinafanyiwa marekebisho.

Mheshimiwa Spika, nije kwenye suala la uwekaji waviwanda katika maeneo ya Mikoa ya Lindi na Mtwara. Miminaishauri Wizara kwamba ni vizuri ikatoa maelezo thabiti juuya namna gani itakavyoweza kuweka vivutio vitakavyofanyawawekezaji wa viwanda wavutike kwenda kuwekeza katikaMikoa ya Lindi na Mtwara. Moja ya pendekezo ambalonapendekeza kwa Wizara ni kwamba ni vizuri bei ya GesiMtwara na Lindi iwe tofauti na maeneo mengine ili kuvutiawawekezaji waone ni nafuu zaidi kwenda kuweka viwandakatika Mikoa hiii badala ya kuweka katika maeneo mengineambayo gesi itapelekwa.

Mheshimiwa Spika, lakini jambo lingine muhimu sanani upatikanaji wa ardhi Mtwara kwa ajili ya wawekezaji, napokusiwe na urasimu ili wawekezaji waweze kuona kwambani vizuri wawekeze viwanda vyao pale.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo nashaurikuhusiana na maeneo haya ni suala la mafunzo. Suala la

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

76

mafunzo katika maeneo haya kuanzia kwenye ngazi yaVitongoji, Vijiji, Mitaa pamoja na Wilaya na Mkoa kwa ujumlani jambo muhimu sana. Naiomba sana Wizara wala wakatimwingine isione kwamba inapoteza fedha kwa ajili yakufanya jambo hili bali jambo hili ni muhimu hasa ukizingatiakwamba sekta ya gesi katika nchi yetu ni jambo geni sana.Kwa hiyo, elimu inabidi itolewe vya kutosha ili wananchiwaweze kunufaika kuielewa vizuri.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ni suala la kupewakipaumbele kwa wananchi wa Mikoa hii hasa vijana kuingiakwenye mafunzo ya sekta ya gesi, madini na petroli. Badoutaratibu uliopo sasa nadhani unapaswa uboreshwe kwasababu hata matangazo yanayotolewa sidhani kamayanafika mpaka kwenye ngazi ya Vijiji na Kata kwambakunahitajika vijana. Kwa hiyo, kama kweli tumedhamiriakuwasaidia vijana hawa, ni lazima matangazo haya yawewazi na yatangaziwe Mtwara na Lindi siyo Dar es Salaam iliwananchi waweze kupata unafuu wa kupata taarifa nakuweza kushiriki kikamilifu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kweli mambo haya mengiambayo yanazungumzwa na niwathibitishie wananchi waMikoa ya Lindi na Mtwara kwamba Kamati ya Nishati naMadini chini ya uongozi wa Mheshimiwa Mwenyekiti VictorMwambalaswa inafanya utaratibu wa kuhakikisha kwambainayatembelea maeneo hayo yote na kuweza kupata fursaya kuzungumza na wananchi ili waweze kutoa dukudukuzao na kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali ambayoyanatokana na hali iliyopo kule. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ni muhimusana na napenda kuishauri Serikali ni juu ya makampuniambayo yanapata nafasi ya kwenda kutoa huduma katikamaeneo haya ya Mtwara na Lindi. Hivi sasa hata wafagizina mamesenja wanatoka Dar es Salaam na maeneomengine. Pamoja na kwamba tender zinatangazwa lakinini vizuri wakati mwingine Serikali ikatoa maelekezo kwahawa wanaoandaa hizi tender kwamba wale wanaoshindawahakikishe baadhi ya kada ambazo si za kitaalamu zaidi

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

77

ziweze kutoa fursa kwa wananchi wa maeneo haya iliwaweze kupata ajira i l i waondokane na matatizoyanayowakabili.

Mheshimiwa Spika, nilitaka pia nizungumzie suala lakutoa vipaumbele vya walau mikopo midogomidogo kwawananchi wa Mikoa hii. Kwa sasa ni kweli kabisa nyanya,nyama na kadhalika havitoki kwenye Mikoa labda kwasababu upatikanaji wa bidhaa hii si wa kutosheleza kwamahitaji ambayo yanatolewa. Sasa kama wananchihawakupewa fursa ya kupewa mikopo kwa ajili ya ufugajina kilimo, hata tukiwahamasisha kwamba walime ili wapatesoko bado watakuwa katika mazingira magumu sana. Kwahiyo, ni vizuri Serikali iangalie uwezekano wa kuwapavipambele vya mikopo wananchi hawa ili wapate fursa yakuweza kuchangia na kushiriki katika kunufaika na masokoyanayotokana na maeneo haya kutokana na upatikanajihuu wa gesi katika maeneo haya.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana na sasa nimwite MheshimiwaEngineer Mnyaa na Mheshimiwa Ole-Sendeka na wa mwishoni Mheshimiwa Buyogera.

MHE. ENG. MOHAMED HABIB JUMA MNYAA:Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, mimi sitazungumzia gesi Mtwarabaada ya Profesa Lipumba kuongea jana na Waandishi waHabari na nafikiri maelezo yake yake kwenye mtandao.Vilevile tunategemea busara ya Bunge lako ambapowananchi wa Mtwara bado wanaamini Wabunge wao.

Mheshimiwa Spika, mimi nitajikita katika hotuba yaWaziri juu ya kitu ambacho kipo ukurasa wa 58, kwa ufupikinaitwa TEITI - Tanzania Extractive Industry TransparencyInitiatives au kwa Kiswahili Mpango wa Uhamasishaji waUwazi katika Mapato ya Madini, Gesiasilia na Mafuta.

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

78

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kusema kwamba, nilazima nilishukuru Bunge lako Tukufu kwa vipindi au utaratibutunaoita wa kuwajengea uwezo Wabunge au capacitybuilding ambapo mimi pia nilibahatika wakati wa Bunge laTisa kuhudhuria semina mbalimbali zinazohusiana na TanzaniaResource Watch, FNF na hii TEITI iliyokuwa based Oslo. Nishukurukwamba mambo haya sasa yameleta matunda kwa Jamhurina mbio zetu za kutaka kiundwe chombo kama hiki katikaTanzania na kijiunge na jumuiya ya Kimataifa zimefanikiwana mwaka 2007 Tanzania ilifanikiwa kujiunga na sasa hivituna Tanzania Extractive Industry.

Mheshimiwa Spika, hatua hii imeleta manufaa kwanibaada ya kuundwa tu kwa chombo hiki, Wizara hii ya Nishatina Madini ilikitumia na waliweza kupata Hart Nurse Limited,ni Chartered Accountants (UK) pamoja na BDO ya East Africa.Katika ripoti yao ya kwanza ya reconciliation wakagunduamadudu makubwa kwamba Tanzania tunaibiwa kupitiamakampuni yanayowekeza katika rasilimali za madini. Ripotiile iliweza kugundua kiasi cha shilingi bilioni 254.9 ambazoSerikali ilikuwa haijalipwa kutoka kampuni ya TPCC. Bahatinzuri baada ya kugundulika, tarehe 16 Julai, 2012, fedha hizizimeweza kulipwa Serikalini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile katika ripoti hiyowaligundua kwamba kuna dola milioni 18 pamoja na shilingiza Kitanzania milioni 657, pia kuna Sh.24,115,000,000/- ambazozinatokana na royalties na kodi mbalimbali kama vile PayAs You Earn (PAYE) ambapo ilionekana discrepancieskwamba Serikali imekosa mapato hayo.

Mheshimiwa Spika, baada ya kutokea matatizo hayo,CAG akaingilia kati katika ile reconciliation report na baadayeakagundua kwamba, hata kama si zile dola za Marekanimilioni 18, ni kweli ziko fedha shilingi bilioni 2.1 mapatoambayo hayaonekani kama yalilipwa na kuingia Serikalini.Kwa hiyo, fedha hizi zikatakiwa zilipwe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka Mheshimiwa Wazirianijulishe au alijulisha Bunge hili, je, hizi fedha zilizogunduliwa

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

79

na CAG sasa zimeishalipwa au bado? Kama hazijalipwa, nikwa nini? Kama hazijalipwa katika muda wote huo inamaana pia tunaweza tukagundua jambo lingine katikamfumo wetu wa TEITI Tanzania, inawezekana bado hakunasheria ambayo ina- enforce utendaji kazi wa TEITI ili paleupungufu unapojitokeza kwamba wale wanaotakiwa kulipawalipe na iwepo sheria inayowabana. Ningeomba Wizarailichukulie hatua jambo hili na iwepo sheria maalum ya TEITIambayo itayabana yale makampuni ambayo hayajalipanayo sasa yalipe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna ripoti ya pili ambayo ili-covermuda wa kuanzia Julai, 2009 mpaka Juni, 2010. Ripoti hii piaikaendelea kugundua madudu ya ubadhirifu au upotevu wafedha na mara hii wakagundua kuna shilingi bilioni 727.2ambazo pia zilikuwa ni mapato ya Serikali na hazijalipwa.Kati ya fedha hizo, shilingi milioni 543.7 zinatokana na kodimbalimbali. Katika hii ripoti ya pili pamoja na addendumyake, yakagundulika mambo mengine makubwa kwamba,kuna matatizo baina ya GGM na TRA kuhusiana na shilingibilioni 35 ambazo hazionekani. Sasa kukawa kuna kurushianampira; GGM wakawa wanasema wameishalipa TRA na TRAwanasema fedha hizo hazionekani.

Mheshimiwa Spika, hili limeleta mzozo mkubwa, lakinila ajabu ni kwamba, hawa watuhumiwa wawili GGM naTRA, tarehe 18 Desemba, 2012, TRA inaiandikia TEITI, baruaNa. TRA/HQ/DIA/1.1 ikieleza kwamba zile fedha shilingi bilioni35 ambazo zilikuwa hazionekani wameshaziona na ilikuwani double payment ya VAT na kodi nyingine, kwa hiyo, ni kweliGGM wameilipa TRA. Sasa jambo hili kidogo linashangaza;watuhumiwa wawili wanakubaliana, yule aliyekuwaanamwambia mwenzake kwamba nimekupa fedha na huyuanasema fedha hazijaonekana na hawa BDO East Africawakagundua fedha hizi hazijalipwa, sasa TRA anasemanimeishaziona, mahesabu yalikuwa yamekaa vibaya, nidouble payment, hii kidogo inatia wasiwasi. Naiomba ofisiya CAG waingilie kati jambo hili waone nini kinaendelea,kwa sababu kama wewe ni mtuhumiwa huwezi kusemafedha nimeiona na kweli umenilipa wakati chartered

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

80

accountants waliopewa kazi hiyo waligundua matatizohayo. Kwa hiyo, tunaiomba ofisi ya CAG kupitia kwako iingiliekati suala hili na tujue haswa fedha hizi zimepotelea wapi.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, mpango huu ambao unafanyikaTEITI usiishie katika kuchunguza fedha zinazolipwa namakampuni makubwa, bali mpango huu wa uhamasishajiwa uwazi kuhusu matumizi na rasilimali za madini, unahitajikuchunguza hata fedha inayolipwa Serikalini ionekaneinatumiwa vipi, inawasaidia wananchi kwa namna gani naimelisaidia vipi taifa katika nyanja nyingine mbalimbali?

Mheshimiwa Spika, kuna utaratibu ambapo ripotimbalimbali zinaletwa Bungeni, lakini bado ripoti za TEITIhatuzipati hapa Bungeni. Tungeshauri kupitia ofisi yako ripotihizi nazo ziletwe hapa kwa sababu zina mambo mengiambayo yatawawezesha Wabunge kujua zaidi na kupataufafanuzi kuhusu ripoti hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa harakaharaka nije katikaukurasa wa 34 wa hotuba ya Mheshimiwa Waziri, alianza kwakueleza kwamba, bajeti yake hii si ya porojo, bali ni yatarakimu. Sasa katika ukurasa ule kuna habari ya zile MW 400Mtwara pamoja na Kv 220, fedha hii mbona hatuioni katikabajeti yake? (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Haya ahsante. Sasa nimwite msemaji mwingine,Mheshimiwa Christopher Ole - Sendeka na tutamalizia naMheshimiwa Agripina Buyogera.

MHE. CHRISTOPHER O. OLE - SENDEKA: MheshimiwaSpika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia Wizarahii muhimu ya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Spika, amani ya Tanzania, ni tunuisiyostahili wala isiyopaswa iruhusiwe kuchezewa na yeyote

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

81

yule, wakati wowote ule na kwa sababu yoyote ile.Natambua yanaweza kuwepo mahitaji na madai ya hakilakini ni vizuri yakaombwa au kudaiwa kwa njia stahili bilakuvuruga amani na umoja wa Kitaifa. Kwa sababu hiyonampongeza sana Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete, kwamaelekezo aliyoyatoa ambayo yanastahili kuungwa mkonona Watanzania wote bila kujali itikadi wala dini yoyote ile.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawasihi sana wenzangu waMtwara waendelee kuieleza Serikali madai yao na naisihi sanaSerikali yetu iendelee kuona umuhimu wa kusikiliza matatizoya wananchi wa Mtwara, maana wale ni watu wazima nawana akili zao, hawawezi wakapiga kelele bila kuwa nasababu ya msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, natambua sana umuhimu wasekta ya gesi katika kuleta mapinduzi makubwa kwenye sektaya nishati. Kama kuna mzigo mkubwa unaobebwa naSerikali yetu kupitia TANESCO, ni kuendelea na mitamboinayotumia mafuta mazito lakini zaidi mitambo ya kukodi.Ukienda kwenye taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini yasasa na Kamati zilizopita, tuliomba sana Serikali iwekezekwenye sekta hiyo ili kuhakikisha tunapata mitambo yetuwenyewe ili tuepukane na gharama tunazopata kutokanana mitambo ya watu binafsi. Napenda kuona sambambana mradi wa kuvuta umeme kutoka Mtwara kuja Dar esSalaam, nione mkakati wa dhati wa kuhakikisha mitamboitakayokuja kuzalisha umeme Dar es Salaam na Mtwara niya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na siyo yawatu binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukiendelea kutumia mitambo yakokodi, tutaleta gesi Mtwara, tutapeleka gesi Tanga,tutapeleka gesi popote, lakini kama tunapeleka kwamitambo ya watu binafsi tutaendelea kuumia. Taarifa yaWaziri inathibitisha kwamba, tunatumia zaidi ya shilingi bilionitano ambazo ni zaidi ya dola za Marekani bilioni moja kwamwaka, ambazo ni sawa na shilingi trilioni 1.6. Kwa hiyo,kama tutaendelea na mitambo hii ya kukodi maana yake ni

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

82

kwamba, tutakuwa hatujamsaidia Mtanzania wa kawaida.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninatambua jitihada na dhamiranjema ya Waziri Muhongo katika kuhakikisha kwamba mzigohuu unapungua, lakini ninataka nimshauri Profesa Muhongokwamba siku zote asikubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Nivizuri akawa shahidi, akathibitisha, akawa Thomaso, asijekuingizwa mjini kama alivyoingizwa mwaka jana wakati wabajeti iliyopita. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka jana Mheshimiwa Wazirialiliambia Bunge hili kwamba kulikuwa na nguzo zinatolewaIringa zinakwenda Mombasa, zinakwenda Afrika ya Kusinikisha zinarudi hapa nchini kwa bei ghali na ni deal ya watuwachache. Mheshimiwa Waziri amesema compliance yashilingi bilioni 16 tuliyohoji kuhusu ununuaji wa mafuta ya PUMAambao haukuzingatia Sheria ya Manunuzi, nikahoji kwenyeKamati ya Nishati na Madini na amezungumzia habari yamisumari. Nataka nilihakikishie Bunge lako hili kwamba kaulizake hizo zimethibitishwa na ripoti ya Controller and AuditorGeneral kwa kutumia kampuni ya Ernest & Youngi l iyothibitisha kwamba hoja zile Mheshimiwa Wazirializoletewa na wasaidizi wake na yeye kuzitamka Bungeni niza uongo kwa kiwango ambacho hakiwezi kuonewa haya.

Mheshimiwa Spika, naomba nithibitishe, ripoti hii hapaya Ernest & Young na nitaiweka Mezani ili kama kuna mtuanabisha, kuthibitisha wazi kwamba, kauli ya Wazirialiyoambiwa na wataalam wake ni ya uongo. Tena naitamkavizuri na akitaka aende kwenye ukurasa wa 79 wa ripoti hiyokwa upande wa nguzo, ukurasa wa 211 na aendee kwenyeukurasa wa nane (8) kwa upande wa shilingi bilioni 16ambazo Maswi alizitumia bila kushirikisha Bodi ya Zabuni yaWizara, wala kushirikisha Bodi ya Zabuni ya TANESCO. Ripotiya CAG iliyokaguliwa na kampuni ya Ernest & Young ipokwenye Bodi yake ya TANESCO, imefungiwa na haitakiwikutolewa hadharani kwa sababu Katibu Mkuu wakeanahusika. Leo tena Mheshimiwa Waziri anaingizwa mjini kwamara ya pili katika sekta ya madini.

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

83

Mheshimiwa Spika, tulipitisha Sheria hapa ya Madinitukasema vito vichimbwe na Watanzania kwa asilimia 100.Tukasema leseni itolewe kwa Mtanzania na yeye aombekumleta mgeni, kama anahitaji teknolojia au mtaji zaidi, kwaushauri wa Bodi ya Ushauri wa Madini. Kana kwamba hiyosheria hawakuisoma wataalam wako, Kamishna juzi ametoaleseni kinyume cha sheria. Nazungumza kinyume cha sheriana nitatamani na nitaleta maelezo hapa kwa sababu dakika10 hazitoshi. Kwanza sheria iko hivi, leseni imetolewa kwaSTAMICO ikishirikiana na Tanzanite One Mining Ltd, wakatiambapo ninazo certificates zao hizi hapa, wamebadilishamajina mara kadhaa kwenda Richland kutoka TanzaniteOne. Nataka nimwambie Mheshimiwa Waziri nitampanyaraka hizi ili athibitishe kwamba hata hicho walichoingiamkataba huenda hakiishi kwa mujibu wa uhalali wa kisheria.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimesema hili na waangalie piasuala la Buhemba. Hakuna sababu ya baba kugombana nawatoto wake, wapeni wachimbaji wadogo maeneo fulanipale Buhemba. Mtasema STAMICO, leo mnaleta STAMICOpale Mererani, mtaletaje STAMICO Mererani? Ni sawasawana mama kunogewa na uji wa watoto akaunywa yeyebadala ya kuwapa watoto.

Mheshimiwa Spika, nataka Mheshimiwa Waziri anipemajibu, hii ni nakala ya gazeti la Mwananchi la tarehe 26Oktoba, mwaka 2010, ambapo Mheshimiwa Kikwete,alipokuwa Olkesemet alisema, mara baada ya leseni yaTanzanite One kwisha nitawagawia wachimbaji wadogo.Mheshimiwa Rais Kikwete amesema, Mheshimiwa Waziriasome gazeti hilo na nitaweka Mezani kama anahitajimaana ninaona anatikisa kichwa.

Mheshimiwa Spika, nataka nikuhakikishie jambomoja, anasema hivi mgombea urais kwa tiketi ya CCM,Jakaya Kikwete, amewahakikishia wakazi wa Wilaya yaSimanjiro, Mkoani Manyara kuwa wachimbaji wadogowatapatiwa maeneo kwenye mgodi wa madini waTanzanite One mara leseni ya kampuni hiyo itakapomaliza

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

84

muda wake. Hii ni kauli ya Rais Kikwete, Wizara inakwendakinyume na kauli ya Rais! Nataka kujua Rais ni Muhongo auDkt. Jakaya Mrisho Kikwete? Kama kauli ya Rais haiheshimiwi,nathibitisha magazeti ya tarehe 26 Oktoba 2010 someni, lakiniukitaka hata mikanda ya video, waulize wasaidizi wa Raiswakwambie. Nilimwambia Mheshimiwa Waziri, tatizo lakeni kwamba hawataki kusikiliza hili, lakini zaidi msiingizemwamvuli huo mnajua kuna mgogoro. Tume ya Bomani,Tume ya Jenerali Mboma ilisema baada ya leseni ya kampunikubwa kwisha wapewe wachimbaji wadogo, leo mnailetaSTAMICO, STAMICO inakwenda kwenye strategic minerals,wapelekeni kwenye urani. Leo hata kwenye urani yenyewebado hamjawapa, mnaendelea kuzungumza, hata ushauriwa Bodi yenyewe ilisema kwamba, msitoe leseni mpaka paleambapo wawekezaji wale watakapoweza kutoa ile freecarried ya shares zile kwenye kampuni ya STAMICO. Hilo nalobado halijakaa vizuri.

Mheshimiwa Spika, nalisema hili kwa sababu tunakazi ya umeme wa REA vijijini. Waheshimiwa Wabunge wotemnajifurahisha hapa, kama hamjatatua tatizo la uhamishajiwa fedha kutoka kwenye REA kwenda kwenye mitambo yakukodi ya watu binafsi, hamwezi mkapata fedha za umemevijijini. Vijiji vilivyoorodheshwa pale, leo mimi ni faraja ….

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Muda umeisha.

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: MheshimiwaSpika, sitaunga mkono hoja mpaka hapo itakapopatamaelezo stahiki. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Buyogera!

MHE. AGRIPINA Z. BUYOGERA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ili na mimi niwezekutimiza wajibu wangu wa Kikatiba wa kuwasemeawananchi wa Jimbo langu la Kasulu Vijijini.

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

85

Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba kwanzaniishukuru Kamati ya Uongozi ya Bunge, inayoongozwa nawewe kama Mwenyekiti, kwa kuahirisha Bunge kwa mudawa siku mbili ili tuweze kupata utulivu wa kutosha kulinganana tatizo kubwa lililokuwa limetokea kule Mtwara.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, naombaniungane na Wabunge wote wanaosema REA iongezewefedha. Kwa kuwa mimi ni Mbunge wa Vijijini, ninaunga mkonokwa asilimia mia moja, Serikali isikie na ihakikishe inatafutafedha za kuwapatia REA ili wananchi tunaotoka vijijini tuwezekupata umeme.

Mheshimiwa Spika, nikiwa naendelea na REA,naomba niwashukuru na kuwapongeza kwa kazi nzuriambayo wanaendelea kuifanya vij i j ini. Nimekuwanikilalamika humu Bungeni tangu nimeingia kwamba, Jimbola Kasulu Vijijini lenye kata 19 hakuna kijiji hata kimojaambacho kina umeme, lakini kwa kupitia REA angalauwameweza kupeleka umeme kwenye zahanati ambaponafikiri wataweza kufikisha umeme wa solar kwenye zahanatizote za Jimbo la Kasulu Vijijini na vituo vya afya. Niombezoezi hili linalofanyika huko wajitahidi kufikisha hizo solarkwenye shule za sekondari katika jimbo la Kasulu Vijijini ilivijana wetu waweze nao kuiona dunia mpya baada ya uhuruwa miaka 50.

Mheshimiwa Spika, katika salamu hizo njema kwaJimbo la Kasulu Vijijini, ninaomba niungane na WaheshimiwaWabunge wenzangu waliotaja vijiji vilivyopata neema yakuingizwa kwenye ramani ya Mheshimiwa Waziri na miminivitaje ili na wananchi wangu huko waanze kujiandaa. Kijijicha kwanza ni Nyachenda, cha pili ni Nyakintonto, cha tatuMakele, cha nne Mvugwe, Nyamidaho, Nyumbigwa, LungweMpya, Titye, Nyenge, Kasengezi, Lusesa na Kwaga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, huu ni mwanzo mzuri, Waswahiliwanasema asiyeshukuru kwa kidogo hata kikubwa hawezikushukuru. Mimi ni mungwana, naomba nishukuru, lakininashukuru kabla umeme haujawaka, shukrani zangu

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

86

naomba zisipotee bure. Tafadhali mhakikishe umemeumewaka katika vijiji nilivyovitaja ili kuwapa matumainiwananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini kwamba hata vijijivilivyobaki vina uhakika wa kupata umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niende kwenye madini. NashukuruMheshimiwa Naibu Waziri wa Madini amewahi kutembeleaKasulu na alipotembelea Kasulu, alitembelea kijiji cha Makere,aliongea na vijana wachimbaji wa chokaa. Pale kunamgogoro ambao kwa akili za kawaida sioni kwa ninimgogoro ule unaendelea. Wizara ya Nishati na Madiniimewapa leseni watu wachimbe chokaa lakini Wizara yaMaliasili na Utalii na Wizara ya Mazingira wanawakimbizakila siku wanasema kwamba wasichimbe hawaitambuileseni. Sasa mimi ninashindwa kuelewa Serikali ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania ni moja inayoongozwa naMheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Baraza laMawaziri ni moja, iweje Wizara hii inatoa leseni halafu Wizaranyingine inaenda kuwakimbiza Watanzania kama wakimbizi?Naomba suala hili Mheshimiwa Waziri muwasiliane na Wizaranyingine muweze kulitatua.

Mheshimiwa Spika, huu utaratibu wa kulimbikizamatatizo madogo madogo na kuyaacha yakawamakubwa, Wabunge tunakuja hapa kutimiza wajibu wetuwa Kikatiba, lakini viongozi hamtaki kutusikia, haya ndiyomambo ambayo mnayalimbikiza na baadaye yanaletamatatizo makubwa bila ya sababu ya msingi. Ukienda Kasulupale Jimbo la Kasulu Vijijini mimi ndiyo ninayemsaidiaMheshimiwa Rais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri yaMuungano. Mheshimiwa Rais amepigiwa kura pale na miminimepigiwa kura na wananchi wale. Kwa hiyo, kilio chao niwajibu wangu mimi kukifikisha hapa Bungeni. Sasa kamaninakifikisha hapa Bungeni ili kumsaidia Mheshimiwa Rais sikuakitembelea kule asihojiwe maswali yasiyokuwa na maananyie hamtaki kunisikia. Naomba hili walichukue na tatizo lawachimbaji wadogo wa Makere litatuliwe. Naomba nisisitizemsikubali kabisa kupambana na Majimbo yanayoongozwana akinamama, ni hatari, kwa sababu hakuna mwanamumeyeyote aliyepo duniani ambaye hajazaliwa na mwanamke.

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

87

Sasa usifike mahali ukanikasirisha, nikikasirika hata mama yakoaliyekuzaa atakasirika, awepo au awepo kaburini. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, ninaongea maneno haya kwauchungu kwa sababu tangu nimeingia Bungeni ninaililiaMakere. Chokaa iliyopo kijiji cha Makere inatumika tanguwakati wa mkoloni. Majengo yote wanayoishi viongozi waSerikali katika Mkoa wa Kigoma tangu enzi za mkoloniyamejengwa kwa chokaa inayochimbwa Makere. Iwejetusiwaandalie mazingira mazuri hawa wananchi wa kijiji kilena wao wakanufaika, wakajidai kupata maisha bora kwenyenchi yao kama mnavyozungumza.

Mheshimiwa Spika, la pili na nadhani ni la mwisho.Naomba Wizara iandae wataalam waende kutembelea kijijicha Nyenge. Kule kuna madini ambapo wananchi kulewanayachimba kwa kienyeji na wanauza kwa bei ya kutupashilingi 3,000 mpaka 5,000. Mheshimiwa Naibu Waziri hizitaarifa unazo, ninaomba ulifanyie kazi. Kwanza, itasaidiapato la Taifa, lakini pia itasaidia kuwaondolea umaskini.Juzi nimezungumza hapa, nikasema wananchi wa Mkoa waKigoma hatuna sababu yoyote ya kuitwa maskini kwasababu tuna utajiri wa kutosha. Sasa wakati umefikamtuandalie wataalam waende wakafanye utafiti, waangaliemadini yanayopatikana katika kijiji cha Nyenge ili yawezekuwasaidia wananchi kule, lakini pia yasaidie kuongeza patola Taifa.

Mheshimiwa Spika, bila kupoteza muda, nimesemaninawasilisha hoja za wapiga kura wangu na nimefikishaujumbe, ninashukuru. Ninaomba majibu kwa maslahi ya Taifa,ahsanteni. (Makofi)

MICHANGO YA MAANDISHI

MHE. ALBERT O. NTABALIBA: Mheshimiwa Spika,naomba nipongeze juhudi kubwa inayofanywa naMheshimiwa Waziri na Manaibu Mawaziri katika Wizara hii,kwa kweli wanafanya kazi nzuri.

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

88

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja hii.Mchango wangu katika Wizara hii ni mfupi kama ufuatao:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, REA. Katika mipangoiliyopo ya kupeleka umeme katika Jimbo la Manyovu/Wilayampya ya Buhigwe, tunaomba nasi tupewe kipaumbele kwanitumeachwa na sekta mbalimbali kwa muda mrefu. Ombilangu ni kwamba Wizara hii tunaimani nayo nanimewaaminisha wananchi wangu kwamba kwa team hiiya watendaji itafanya. Vijiji vya Manyovu vimesubiri umemekwa muda mrefu sana na ni vizuri mipango hii itekelezwe.Je, ni lini mradi huu utakamilika?

Mheshimiwa Spika, kuhusu solar; niipongeze sanaSerikali kwa kuweka umeme wa jua katika zahanati zetu nabaadhi ya shule za sekondari na masoko yaliyoezekwa.Tunaomba kuwekewa umeme kwenye shule za sekondari kwashule ambazo zimebaki mfano shule za sekondari zote zaTarafa ya Muyama, zahanati ya Mlela Mission/Buhigwe nashule ya sekondari ya Janda na nyingine ambazohazijawekwa.

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Spika, napendakutumia nafasi hii kwa njia ya maandishi kuwapongeza Waziriwa Nishati na Madini, Mheshimiwa Sospeter Muhongo (Mb),Naibu Waziri Mheshimiwa George Simbachawene (Mb), NaibuWaziri Stephen Maselle (Mb), Katibu Mkuu pamoja naWatendaji wote walioshiriki kuandaa bajeti hii nzuri yenyemwelekeo wa kuinua uchumi wa Watanzania kupitia madinina nishati mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, Serikali kukomesha tabia zawanasiasa wanaopotosha wachimbaji wadogowadogo.Inasikitisha sana ninapoona baadhi ya wanasiasawakiwapotosha wachimbaji wadogo huko kwenye migodikupuuza sheria za nchi. Naiomba Serikali kufuatilia tabia zabaadhi ya wanasiasa wanaojiingiza kupotosha wachimbajiwadogo ili kujua wanafanya hivyo kwa maslahi ya nani nakwa sababu gani, hawajui sheria au wanafanya hivyo kwamakusudi. Nitafarijika sana endapo Waziri atalieleza hiliwakati wa majumuisho.

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

89

Mheshimiwa Spika, vilevile ninaipongeza Wizara kwakuendelea kutoa semina mbalimbali kwa lengo la Wabungekuendelea kupata uelewa. Naomba semina hizi zitolewe kilamara il i kukuza uelewa wa wanasiasa, wachimbajiwadogowadogo na wananchi kwa ujumla. Nitafurahikupata kauli ya Serikali wakati wa kuhitimisha bajeti.

Mheshimiwa Spika, Serikali kutenga maeneo yawachimbaji wadogo. Utaratibu wa kuwapatia wachimbajiwadogowadogo maeneo yao ya kuchimba kabla ya kutoaleseni kwa wachimbaji wengine ni muhimu sana. Kwa kuwakumekuwa na migogoro ya wachimbaji wenye leseni nawachimbaji wadogo wadogo, naiomba Serikali kufuatiliakwa karibu maeneo yote yenye migogoro na kuimaliza ilikuzuia matatizo makubwa yanayoweza kujitokeza. Naombamaelezo ya Serikali yatolewe wakati wa majumuisho.

Mheshimiwa Spika, mgogoro wa wachimbajiwadogo na mchimbaji mwenye leseni Mgodi wa Mgongo –Shelui – Iramba. Naiomba Serikali kufuatilia mgogoro huuambao umesababisha mgodi kufungiwa. Mimi naonakulikuwa na uchochezi wa baadhi ya viongozi. Kwa kuwawachimbaji wadogo sasa inaelekea wanajutia, naombakazi ya kuunganisha wachimbaji wadogo na mwenye leseniufanyike, wameshaonja joto ya jiwe.

Mheshimiwa Spika, maombi ya umeme kupitiaumeme vijijini. Napenda kutuma maombi Serikali kupelekaumeme kutoka Shelui kwenda Mtoa, Msai, Tyeme, Mtekentena Urughu pia kupeleka umeme kutoka Shelui hadi Mgongo,Sekenke, Ntwike, Mingela, Tulya, Doromoni na Kidani. Nasubirimajibu mazuri ya Waziri maana Wilaya hii ya Iramba badoina vijiji vingi sana ambavyo havina umeme.

Mheshimiwa Spika, mwisho, namalizia kwa kuungamkono hoja hii, Mungu awatangulie, utekelezaji wa bajetiuende vema.

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Spika, naungamkono hoja hii mia kwa mia.

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

90

Mheshimiwa Spika, ombi muhimu kwa Wilaya yanguni kusambaza umeme katika Mji wa Namanyere maanampaka sasa ni asilimia 30 tu ya wananchi wa Mji waNamanyere ndio wanaopata huduma ya umeme.

Mheshimiwa Spika, kupeleka umeme katika Mji waKirando na Swaila. Maombi ya kupeleka umeme Kirando naSwaila yako kwenye mpango wa REA. Nashukuru sana tenasana maana Engineer Msofe wa REA amenieleza mpangowa kupeleka umeme Kirando na Swaila katika Wilaya yaNkasi umo katika mpango wa REA awamu hii ya pili. Kwahiyo, ombi langu ni kupewa kipaumbele tu kwa huo mpangowa kupeleka umeme pia katika vijiji vya Londikazi, Miyombo,Mashete, Mtega Mwai na Paramawe.

Mheshimiwa Spika, Wizara ione kuwa umeme kufikakatika Mji wa Kirando ni ukombozi kwa wavuvi wa samakina dagaa, yaani wakazi wote wa mwambao wa ziwawanategemea sana uvuvi wa samaki aina ya migebuka nahakuna hifadhi, huwa wanaoza na kufukiwa na kuendelezaumaskini kwa wavuvi wa ziwa Tanganyika. Umeme utakuwaukombozi wao kwa vile wataweza kuhifadhi migebuka.Nashukuru kwa umeme kufika Namanyere na vijiji vyotebarabarani.

Mheshimiwa Spika, katika mji wa Namanyere sehemumuhimu ambazo umeme haujafika ni pamoja na shule nneza sekondari, shule nne za msingi, eneo la viwanda vidogona visima vya maji vinne ambavyo vilikwishaunganishwa naumeme wakati tunatumia generator ili wananchi wapatemaji kwa urahisi na nafuu.

MHE. HAMAD ALI HAMAD: Mheshimiwa Spika, kikaocha wachumi duniani kilichofanyika Marekani miaka miwiliiliyopita, walikubaliana kwamba nchi nyingi zenye rasilimali(madini na gesi) na kadhalika zinaingia katika migogoro(vita) vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na mgawanombaya wa rasilimali hizo.

Mheshimiwa Spika, Tanzania tumeanza uchimbaji wa

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

91

dhahabu na madini mengine kwa muda mrefu sasa na badokuna malalamiko makubwa kwa wananchi walio katika yalemaeneo yaliyozunguka migodi na pia kuna kutokuelewanakati ya wananchi na wachimbaji (wawekezaji) kwa kiasi chahata kupeana majina ya kiuadui kutokana na hasira zakukosa maslahi stahiki kama vile wenyeji huwaita wawekezajikwa majina ya makaburu, wanyonyaji, wezi na kadhalikalakini pia wawekezaji huwaita wananchi kwa majina yawachimbaji haramu, wavamizi, majambazi na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, kwa kipindi kirefu sasa tumezoeakusikia ama watu wameuawa au kuna vurugu kati yawananchi waliozunguka maeneo ya migodi na walinzi, polisina au wawekezaji wenyewe katika migodi ya Mererani,Mwadui, Buzwagi, North Mara, Isanga na kadhalika. Hii sidalili nzuri kwa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, kwa nchi za Afrika, Algeria ndionchi ya kwanza inayotoa gesi kwa wingi na inachangiaasilimia 3% ya pato la Taifa lakini pia inapunguza tatizo laajira kwa 10%. Tanzania tumegundua gesi na pia inasadikikakwamba tunaweza tukawa pia na mafuta ya petroli.

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Mtwara na Lindi niWatanzania na wamejifunza kutoka katika yale maeneoambayo yanatoa madini (dhahabu) kwa muda mrefu nandio maana nao walichachamaa vile. Naiomba Serikali ijena sheria na kanuni zitakazoonesha au kutoa matumaini kwaWatanzania inayoonesha ni kwa kiasi gani gesi hii itaongezapato la Taifa, lakini pia ni vipi itaweza kujibu tatizo sugu laajira kwa Watanzania.

Mheshimiwa Spika, naomba nitoe angalizo na pianiishauri Serikali kwamba, tusipokuwa waangalifu juu ya gesihii, Taifa linaweza likaingia katika matatizo makubwa natukajikuta kwamba badala ya neema imekuwa kama laanakwa Taifa. Kwa pamoja tumwombe Mwenyezi Mungu ajaalieiwe ni neema na isijekuwa laana.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha, ahsante.

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

92

MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMAZINA: MheshimiwaSpika, nianze kwa kumpongeza Waziri, Mheshimiwa ProfesaSospeter Muhongo kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuletamatumaini kwa wananchi ili wafaidike na rasilimali zao. Pianiwapongeze Naibu Mawaziri kwa kumshauri vizuriMheshimiwa Waziri. Bila kumsahau Katibu Mkuu Eliakim Maswi,kwa umahiri na uadilifu wake. Pia nawapongeza timu yoteya wataalam.

Mheshimiwa Spika, sekta ya nishati na madini ni sektamuhimu sana kwa maendeleo ya uchumi wetu na ni mojaya vipaumbele vya kutuvusha katika jangwa na kufikia nchiya ahadi, nchi yenye uchumi wa kati. Bila umemeuliosambazwa nchi nzima hakuna maendeleo, lazimawananchi wafaidike na madini yetu. Madini yaliyoko ardhinini mali ya Watanzania wote. Nickel ya Kabanga iliyoko Ngarasiyo mali ya watu wa Ngara ni mali ya Watanzania. Ni upuuzikuwaendekeza wananchi wa Mtwara na Lindi kwamba gesini yao. Bomba la gesi Mtwara Dar es Salaam ni lazima.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2001 Tanzania ilikuwa naumeme mwingi kuliko Kenya na Uganda. Sasa hivi Kenyainatuzidi sana. Kenya inazalisha MW 1,400, Tanzania inazalishaMW 700 na Uganda inazalisha MW 400. Utafiti nilioufanyaunaonyesha kwamba Kenya wanatuzidi kwa sababuwalikuwa wepesi wa kutekeleza wazo lililoanzishwa na PSRCla kutenganisha Generation, Transimission na Distribution.

Mheshimiwa Spika, Makaa ya Mawe ya Mchuchumana Ngaka yatazalisha umeme mwingi. Basi umeme huouwekwe kwenye National grid ili Wilaya zote ikiwemo Wilayaya Ngara waweze kupata umeme wa grid.

Mheshimiwa Spika, Ngara ni Wilaya yenye madinimengi ambayo hayajachimbwa. Hii inatokana na taarifailiyoachwa na Wajerumani. Ngara imejaa Nickel na dhahabu.Madini haya yafanyiwe utafiti.

Mheshimiwa Spika, Mgodi wa Kabanga Nickelumekuwa sasa ni hadithi. Hadithi hii imekuwepo tangu

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

93

miaka ya 1970. Wawekezaji wamekuwawakibadilikabadilika. Tunaambiwa kwamba mgodi huu niwa pili duniani katika utajiri wa deposits baada ya ule waCanada. Wakati tumeanza kuamini kwamba sasa wataanzakuchimba, mwekezaji mmoja Barrick Gold ameamuakujiondoa. Anatafuta mwekezaji mwingine wa kununua hisazake ambazo ni 50%. Mwekezaji wa pili ni Extrata.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa sijaona dalili za Serikalikuwa serious na mgodi huu. Mheshimiwa William Ngelejaalipokuwa Waziri aliwahi kuutembelea mradi huu.Mheshimiwa Waziri nakukaribisha uutembelee mgodi huu iliwananchi wawe na imani kwamba Serikali iko serious.

Mheshimiwa Spika, Nickel itakayochimbwa kwenyemgodi wa Kabanga – Ngara inangojewa kwa hamu iliichanganywe na chuma cha Liganga kupata chuma chapua. Kabanga Nickel inahitaji vibali kutoka Wizara hii kamaLeseni ya uchimbaji, Kibali cha Mazingira (EIA), MDA.Naiomba Wizara iharakishe vibali hivyo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu umeme wa REA – Rulenge.Naomba nitoe shukrani za pekee kwa uongozi wa REA nahasa Dkt. Lutengano Mwakahesya na Msaidizi wake Eng.Msofe kwa kazi nzuri wanayoifanya. Watendaji hawa niwachapakazi na ni waadilifu sana. REA imeshatengenezatransformer ya Rulenge bado kuweka line. Nina imanikwamba nguzo zitaanza kuwekwa kuanzia Djuokuligwa hadiRulenge mwezi wa saba kama nilivyoahidiwa. NaiombaWizara izidi kuiongezea REA bajeti kwa sababu watendajiwake ni waadilifu sana.

Mheshimiwa Spika, kuhusu umeme wa Orio – Holland,mpaka sasa Wizara haiko wazi ni lini mradi wa umeme waOrio kwa Wilaya za Ngara, Biharamulo na Mpanda utaanzakutekelezwa. Naiomba Wizara ianze kutekeleza mradi huukwa kuweka generator mbili kwenye kituo cha TANESCONgara ili umeme usambazwe kwenye vijiji vya Mugoma,Benaco, Rusumo, Kabaheshi, Nyamahwa na Kashinga.

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

94

Mheshimiwa Spika, kuhusu umeme wa solar, naiombaWizara ifikirie mpango wa kuweka umeme wa solar katikashule za sekondari na vituo vya afya katika Wilaya ya Ngara.

Mheshimiwa Spika, kuhusu umeme wa Rusumo.Naiomba Wizara iharakishe mchakato wa umeme wamaporomoko ya Rusumo kwa kushirikiana na nchi za Rwandana Burundi.

MHE. LUCY P. OWENYA: Mheshimiwa Spika, kwa ajiliya maendeleo vijijini, Serikali ilipunguza bei ya nguzo nakuunganisha umeme ili kila mtu aweze kupata umeme. Chakusikitisha haswa TANESCO Moshi unakuta watu wanaendakwa ajil i ya kulipia nguzo lakini wakifika pale ofisiniwanaambiwa hakuna form za kujaza na wale waliobahatikakulipia na kupata form hawaunganishiwi umeme ule kwakisingizio vifaa hakuna kama nguzo, wire, mita, luku, hii nimbaya sana kushikilia fedha za watu kwa muda mrefuwakati wangeweza kutumia fedha hizo kwa ajili ya mambomengine? Je, ni sababu zipi zinapelekea TANESCO Moshikutopelekewa vifaa kutoka Makao Makuu ya TANESCO nakupelekea wananchi kupata usumbufu wa hali ya juu?

Mheshimiwa Spika, Bunge la Novemba 2012,nilimuuliza Waziri swali hapa Bungeni kuhusu nguzo zilizopochini kwa zaidi ya miaka miwili kule katika Jimbo la Hai, Kataya Machame Kaskazini na Hai Mjini. Mpaka sasa hivi nguzozile bado hazijasimamishwa na mvua zinazoendelea sijuizitakuwa kwenye hali gani? Utakuta tunalalamika TANESCOipo kwenye hali mbaya kifedha, je, kwa kuziacha nguzo hizosi upotevu wa fedha za umma na kuwakandamizawananchi?

Mheshimiwa Spika, TANESCO wamekuwa waki-printbill za wenye mita kuanzia tarehe 18 – 19 ya kila mwezi lakiniikifikia tarehe 25 -27 ya mwezi kwa wale ambao hawajalipaTANESCO wanawakatia umeme wateja hawa. Huu niunyanyasaji ukizingatia watumishi wengi unakutahawajapata mishahara. Nashauri TANESCO wa-print bill hizomwisho wa mwezi tu utakuta watumishi wameshapatamishahara.

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

95

Mheshimiwa Spika, Moshi Vijijini, Old – Moshi, Uru,Kibosho, Mbokomu, Mabogini ni kama hakuna umeme ikifikajioni na watu wote wakishawasha umeme hauwaki kabisa,ni mdogo sana, inabidi watu watumie mishumaa auvibatari? Ni lini wananchi wa Moshi Vijijini watapata umemewa uhakika? Waziri anasema umeme ndio uchumi, kwa halihii kuna maendeleo?

Mheshimiwa Spika, Shirika linaidai Serikali na Taasisizake Sh.83,773,824,632, ni lini fedha hizi zitalipwa? Ni rahisikuwakatia umeme wananchi wasiolipa Sh.10,000 lakiniwadaiwa sugu hawakatiwi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu madini, wawekezaji wengiwanakuja Tanzania kutafiti ni wapi madini yanawezakupatikana hata wengine kuondoka na michanga kwakisingizio cha utafutaji lakini tukumbuke wakoloni hawakwenye maktaba zao tayari wanajua kila eneo la nchi hiimadini ya aina gani yanapatikana wapi. Mfano gesiilishagunduliwa siku nyingi sasa, kwa nini watu hawawasamehewe kodi za mafuta wakati tayari ilishajulikanamadini yapo wapi.

Mheshimiwa Spika, je, hii gesi iliyogundulika tunayoSera ya Gesi? Serikali inajua hatuna Sheria ya Gesi lakiniwanasema watatumia Sheria ya Mafuta ya 1980. Je, sheriahii inakidhi mahitaji ya sasa? Je, pakitokea kutokuelewanakati ya Kampuni na nchi, kesi hiyo ni lazima ikafanyikie nje yanchi na mikataba hii itakuwa ni ya muda gani?

Mheshimiwa Spika, pamekuwepo na malalamikokwa wawekezaji wa ndani hawatendewi haki katika ulipajiwa leseni, huwa hawashirikishwi na inachukua mudakuwalipa fidia pindi eneo linapokabidhiwa kwa wawekezaji.

Mheshimiwa Spika, madini yote ya vito yanatakiwayamilikiwe na wazawa. Je, madini ya Tanzanite ni kwa kiasigani Watanzania wanamiliki madini haya?

Mheshimiwa Spika, je, mchakato wa kuanzisha

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

96

kiwanda cha kukata veto pale Kilimanjaro InternationalAirport umefikia wapi?

Mheshimiwa Spika, uchangiaji wa sekta ya madinikwa pato la Taifa ni 3.5%, asilimia hii ni ndogo sanaukilinganisha na aina ya madini yanayopatikana nchini.Tunapoteza fedha nyingi sana kwa kutoku-process madinihaya hapa nchini.

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa Spika,nianze kwa kuipongeza Wizara kwa kazi nzuri wanayoifanyakusambaza umeme nchi nzima. Niwapongeze kwakukamilisha mradi wa MCC Wilayani Misungwi. Vilevilenishukuru kwa niaba ya wananchi wa Misungwi kwa mradiwa Benki ya Afrika katika maeneo ya Wilaya ya Misungwi. Nimatarajio yangu kwamba mradi huu utatekelezwa kwamuda uliopangwana kuwapatia wananchi nishati hiimuhimu kama ilivyotarajiwa.

Mheshimiwa Spika, vilevile niombe Wizara kupitia REAiongeze kasi ya kutekeleza mradi wake katika Wilaya yaMisungwi kwani maeneo husika viongozi mbalimbaliwameahidi kwamba umeme utakuwa umepatikana kablaya mwaka 2015. Vilevile wataalam walipita katika maeneohayo na wananchi kuweza kujiandaa kwa kufunga nyayaza umeme kwenye nyumba zao kitu ambacho kinasababishamalalamiko kwamba wamedanganywa na kuwasababishiahasara. Naiomba Wizara kupitia REA kuongeza kasi yautekelezaji wa mradi huu ili kupunguza manung’uniko kutokakwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja 100%.

MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Spika, kwanzanaipongeza sana Wizara hii kwa kazi kubwa inayofanyakatika maeneo yake makuu mawili ya nishati na madini. Hatahivyo, napenda kuchangia kidogo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ahadi za Mheshimiwa Rais kuhusuumeme. Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

97

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika nyakatimbalimbali na maeneo mbalimbali Mbozi ikiwemo aliwekaahadi za utekelezaji wa miradi ya umeme. Ili kuendeleza imaniya Watanzania kwa Rais, Chama cha Mapinduzi na Serikali,nashauri Wizara hii itekeleze ahadi zote zilizowekwa na Raiskuhusu usambazaji wa umeme. Kwa Wilaya ya MboziMheshimiwa Rais aliahidi kupeleka umeme Tarafa ya Itakana katika Kituo cha Afya cha Itaka. Ni matumaini yangukwamba ahadi hii ya Rais itatekelezwa katika mwaka huuwa fedha 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji miradi ya umemekatika vijiji vinavyopitiwa na Gridi ya Taifa ya umeme – Mbozi.Mwaka 2009 niliiandikia REA barua kuhusu kupeleka umemekatika vijiji vya Nanyala, Senjele, Ivwanga na Old Vwawa.Katika majibu yake REA ilikubali kuvipatia vijiji hivyo umemekwa kuweka ‘transformer’ hata hivyo tangu wakati huo(mwaka 2009) hakuna kitu kilichofanyika. Hata hivyo, hivikaribuni niliongea na viongozi wa REA ambao kimsingi, baadaya kuwakumbusha kuhusu ahadi yao sasa wamekubalikuvipatia vijiji hivyo umeme. Ni matumaini yangu kwambaREA watakuwa waaminifu kwa kutekeleza ahadi yao yamuda mrefu sana kama tulivyokubaliana.

Mheshimiwa Spika, aidha, naiomba REA ifikisheumeme katika Kituo cha Afya cha Isanza. Naomba piaikumbukwe kwamba moja ya madhumuni ya kupelekaumeme Isanza ilikuwa ni Kituo cha Afya. Bahati mbaya sanaumeme huo umefika Isanza, lakini siyo Kituo cha Afya Isana.Umbali uliobaki kufikisha umeme Kituo cha Afya cha Isanzani kama kilometa 1½ hivi.

Mheshimiwa Spika, nilishafanya mazungumzo naviongozi wa REA kuhusu kufikisha umeme katika kituo chaafya Isanza. Kimsingi REA walikubali kufikisha umeme katikaKituo cha Afya kwa kumtumia mkandarasi aliyejenga mradihuo. Mkandarasi bado hajakabidhi mradi huo. Naomba REAwahakikishe ahadi hiyo inatekelezwa.

Mheshimiwa Spika, ili kuongeza kasi ya kusambaza

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

98

umeme vij i j ini, nashauri Serikali ihakikishe pesa zotezinazoidhinishwa kwa REA zinatolewa zote na kwa wakati.Vinginevyo ahadi/lengo la Serikali la kusambaza umemevijijini kufikia asilimia 30 hadi mwaka 2015 itakuwa ndoto.

Mheshimiwa Spika, utafiti wa makaa ya maweMagamba – Mbozi. Iko kampuni ambayo inajihusisha nautafiti wa makaa ya mawe katika eneo nililolitaja hapo juu.Utafiti huo umechukua muda mrefu sana zaidi ya miaka sabasasa. Wananchi wa maeneo hayo pamoja na viongozihawajui kinachoendelea hadi sasa. Kampuni hiyo imekuwaikisomba makaa ya mawe mengi sana kwa maelezokwamba ni katika mchakato wa utafiti. Tunaomba Serikaliitueleze ni lini utafiti huo utakamilika na nini faida ya makaahayo kwa uchumi wa maeneo hayo. Maana kilichoendeleani uharibifu wa barabara zetu kunakofanywa na kampunihusika kupitisha magari yake ambayo ni mazito sana.

Mheshimiwa Spika, kuhusu makaa ya mawe Kiwira.Kwa nyakati tofauti aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini,Ndugu Ngeleja na Waziri wa sasa Profesa Muhongo waliahidikwamba mradi huo ungeanza kazi mapema sana. Hadi leohaijulikani kinachoendelea. Sasa nataka kujua ni lini mradiwa Makaa ya Mawe Kiwira yatafunguliwa na kuanzauzalishaji na hivyo kuongeza uzalishaji wa umeme nchini?

Mheshimiwa Spika, naunga mkono na nawasilisha.

MHE. FATUMA A. MIKIDADI: Mheshimiwa Spika,kutokana na adha au changamoto tunazozipata Lindi naMtwara za kupigwa viongozi, kuchomewa nyumba moto,maandamano ya wananchi, kunyanyaswa kwa viongoziwakiwemo Wabunge na Madiwani wa Lindi na Mtwara,tunaiomba Serikali kuanza uwekezaji wa viwanda mbalimbaliMikoa ya Lindi na Mtwara kabla ya kuendeleza miradimingine. Viwanda kwanza kwa kutumia gas iliyopo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu gesi asilia Tanzania, Serikaliiandae Sera ya Gesi asilia haraka iwezekanavyo ili kuondoachangamoto zilizopo za gesi Lindi na Mtwara.

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

99

Mheshimiwa Spika, madini yaliyopo Wilaya zaNachingwea, Ruangwa, Liwale, Lindi ambayo yanachimbwabila utaratibu. Serikali ianzishe utaratibu rasmi wa uchimbajihuo ili wachimbaji wadogowadogo waweze kufaidika napia Halmashauri za Wilaya ziweze kupata mrabaha.

Mheshimiwa Spika, mradi wa Mchuchuma na Ligangaunaendeleaje? Naomba tupate taarifa.

MHE. SHAFFIN A. SUMAR: Mheshimiwa Spika, Wizaraya Nishati ni moyo wa Tanzania kimaendeleo. Nchi zotezilizoendelea duniani ziliwekeza sana kwenye umeme, sasasisi Tanzania kama tusivyowekeza vya kutosha kwenye sualala umeme basi lengo letu la 2015 kuwa nchi yenye pato lakati haitowezekana.

Mheshimiwa Spika, mwaka wa fedha 2011/2012,tulipendekeza kuongeza bei ya mafuta ya taa na ongezekola fedha ilikubaliwa Bungeni kupelekwa REA lakini hadi leofedha hizo hazijapelekwa REA na mwaka jana 2012/2013niliuliza katika mchango wangu kipindi cha Bajeti lakinisijajibiwa.

Mheshimiwa Spika, TANESCO, Shirika hili linahitajiuwekezaji mkubwa ukizingatia kwamba linajiendesha kwahasara. Serikali iwekeze hasa katika kununua mashine zakufua umeme kwa kutumia gesi asilia na ziwe mali yaTANESCO kwa 100% ili kupunguza utegemezi mkubwa wakununua umeme kwenye makampuni ya nje. Tanzaniatumejaliwa lakini sisi (Serikali) haijali. Tumejaliwa upepo, maji,jua, joto ardhi, gesi asili ambapo vyote vinaweza kusaidiakuzalisha umeme.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2012/2013, katikamchango wangu Bungeni nilisema ili kuokoa mazingira,TANESCO waanze kutumia nguzo za concrete badala yanguzo zilizopo za kusambaza umeme. Nguzo za concretezina maisha marefu zaidi kuliko nguzo za miti zilizopo,ambazo ni aghali na adimu kupatikana.

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

100

Mheshimiwa Spika, kuhusu uranium, Serikali sasa ianzekufikiria kutumia uranium kwenye kuzalisha umeme.

Mheshimiwa Spika, kuhusu gesi asilia, gesi hii ni maliya Taifa, ni bora wenzetu wa Mtwara waelimishwe vyakutosha, vurugu zinazoendelea ni uchochezi wa nguvu zakutoka nje ili sisi tuendelee kumalizana na hao wageniwanufaike kama jinsi ambavyo imekuwa ikifanyika nchinyingine duniani.

MHE. RACHEL M. ROBERT: Mheshimiwa Spika, nchi yetuimezungukwa na madini lakini pia kuna maeneo wananchiwanalala juu ya madini. Tatizo ni vipi rasil imali hiiitawanufaisha Watanzania wote. Badala ya kuongeza kipatotumekuwa tukiongeza migogoro katika maeneo ambayoyana madini.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali iangalie upyasuala la wachimbaji wadogowadogo aidha kwa kuwapamaeneo yao wenyewe na si kuwaacha kama yatima, kwanina wao kama madini yao yakikusanywa vizuri yanawezakuliongezea pato Taifa. TMAA wamekuwa wakijishughulishana migodi mikubwa mikubwa na kuwaacha wachimbajiwadogo wakiamua wao wafanyeje kuhusu madiniwanayopata na wengi wao wamekuwa wakidhulumiwa nawafanyabiashara wajanja.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana Serikali ilisemainatarajia kuanzisha au kukamilisha taratibu za mfuko rasmiwa kuwaendeleza wachimbaji wadogo wadogo. Ninaombasasa jibu la Serikali, ni lini sasa mfuko huu utakamilishwa iliwachimbaji hawa waweze kupatiwa mikopo na nyenzo/vifaa vya kuchimbia vya kisasa il i wajikwamue nawaondokane na uchimbaji wa kienyeji ambao ni hatari kwaafya zao?

Mheshimiwa Spika, bado kuna migogoro katikamaeneo yenye madini ambapo wachimbajiwadogowadogo aidha wao kwa wao au na wachimbajiwakubwa wakiwemo watafiti wa madini, wamekuwa

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

101

wakigombana mara kwa mara. Tatizo ninaloliona mimi nikuwa Serikali iangalie upya utaratibu wa kutoa leseni za utafitikutokea Makao Makuu ya Wizara, kwani watendajiwamekuwa wakigawa maeneo ya utafiti huku wamekaakwenye computer zao bila kujua kuwa tayari eneowalilogawa lina wananchi ambao pengine tayariwameshaanza nao shughuli za uchimbaji. Naiomba Serikaliiangalie uwezekano wa kuhamisha kitengo cha utoaji leseniza utafiti kwenda Mikoani ambapo ni rahisi sasa kwa Afisakufika eneo husika kabla ya kutoa leseni kwa mtafiti.

Mheshimiwa Spika, lakini pia kuna tatizo la watafitikupewa leseni mbili yaani ya kuchimba na hapo hapoanatafiti na kama si hivyo basi wanapofanya utafiti wenginewanachimba kabisa madini. Hili hapa ni tatizo, naiombaSerikali iangalie tena kwa kukagua maeneo yenye leseni zautafiti ili kuona kama kweli hakuna uchimbaji unaofanyika.

Mheshimiwa Spika, pamoja na Serikali kuweza kuokoakiasi kikubwa cha madini yaliyokuwa yanasafirishwa nje kwawizi, bado inahitaji kuongeza nguvu za ziada ili kuziba mianyaambayo inasababisha wizi huu ufanyike kwenye viwanjavyetu vya ndege. Tumeona ni jinsi gani Taifa linapotezamapato yake kutokana na watumishi wasio waadilifu.

Mheshimiwa Spika, kuna tatizo sugu sana la migodimikubwa kutolipa “service levy” kwenye Manispaa husikakulingana na mikataba yao lakini Serikali hailioni hili na bilaMbunge wa eneo husika kufuatilia migodi hii haishtuki nawala haitoi “service levy” hiyo. Ninaomba kuuliza tozo hizoni hisani au ziko kwenye mikataba? Kama zipo kwenyemikataba yao kwa nini sasa mpaka wafuatiliwe ndio walipetozo hizo?

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na malalamiko mengisana kutoka kwa wafanyakazi wazawa waliopo migodini,wamekuwa wakidhalilishwa sana, sijui kama Serikali hainataarifa kuhusu unyanyasaji wa Watanzania unaofanywakatika migodi nchini. Nina taarifa kuhusu Mgodi wa Mwaduini moja ya migodi ambayo inanyanyasa na kudhalilisha

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

102

Watanzania. Kama Serikali inaona na inasikia, kwa nini basiisikemee vitendo hivi vinavyofanyika katika migodi yetu yaaniwaje wachukue rasilimali zetu lakini bado watunyanyase?Mie nasema si haki hata kidogo. Ninaomba Serikali ione sasakuna haja ya kutembelea migodi yote na kuongea nawafanyakazi ili wasikie vilio vyao ikishirikiana na Wizara yaKazi na Ajira.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa nizungumzie nishati.Kumekuwa na changamoto kubwa sana katika maeneomengi ya kukatikakatika kwa umeme mara kwa mara haliambayo inaleta kero sana na hofu kubwa kwa wananchi.Wapo wanaodiriki kuhoji kama ni mgao au ni hitilafu tu.Naomba Serikali kupitia Wizara ije na majibu, je, tatizo ni ninihasa linalofanya umeme ukatikekatike katika maeneo mengibila hata taarifa?

Mheshimiwa Spika, kumekuwa kukiendelea namatukio ya hujuma ya miundombinu ya umeme zikiwemonyaya, pamoja na mafuta ya transfoma, hivyo kusababishamaeneo husika kukosa umeme. Pamoja na kukosa umeme,Shirika la Umeme linapata hasara kubwa sana kutokana nahujuma hizo. Naomba sasa pamoja na baadhi yawatuhumiwa kukamatwa na kufikishwa Mahakamani,adhabu kali sana zichukuliwe ili iwe fundisho kwa wananchiwote ambao wamekuwa wakilihujumu shirika hili.

Mheshimiwa Spika, bado kumekuwa na tatizo laupatikanaji wa mita za luku katika maeneo mengi.Ninaomba zoezi la uunganishwaji wa umeme katika maeneouende sambamba na upatikanaji wa mita za luku. Aidha,imeonekana nguzo za umeme bado ni tatizo hasa maeneoyaliyoko pembezoni. Kuna haja sasa ya Serikali kuhakikishanguzo zinapatikana kila Mkoa lakini hata bei yake iwe nafuuili idadi kubwa ya wanaoomba kuunganishiwa umemewaweze kupata umeme kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, pamoja na changamoto zotezinazoikabili TANESCO, naiomba Serikali iliangalie Shirika hilikwa macho manne (4) ili liweze kufanya kazi kwa ufanisi

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

103

kabisa na kuwachukulia hatua Maafisa wake ambao kwanjia moja au nyingine wanalisababishia Taifa hasara.

Mheshimiwa Spika, Wakala wa Nishati Vijijini (REA)ina lengo zuri sana la kupeleka huduma za nishati bora vijijinikwa lengo la 30% ifikapo 2015, nilitaka kujua ni vijiji vingapiambavyo viko katika lengo hilo katika Mkoa wa Shinyanga?

Mheshimiwa Spika, baada ya kuchangia haya,naomba kuwasilisha.

MHE. ALI KHAMIS SEIF: Mheshimiwa Spika, ukiangaliahotuba ya Waziri, ukurasa wa 78, aya 147, imezungumzia vyakutosha kuhusu uwezo wa rasilimali watu kwa kuwapelekaWatanzania nchi mbalimbali kwa maneno. Wakowatakaokwenda kusoma Brazil, China na Uingereza. Mpakasasa suala la mafuta ni la muungano na hata elimu ya juu nimuungano, katika wanafunzi hao wanaokwenda kusomanchi za nje, ni wanafunzi wangapi wanatoka Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa kuna mawazoyanayotofautiana juu ya hali ya TANESCO. Wako wanaofikiriakuwa TANESCO ipunguziwe majukumu. Mimi navyohisimajukumu ya TANESCO si tatizo bali ni changamotozinazolikabili shirika hil i, ndio tatizo kubwa. Iwapochangamoto zitaondoshwa basi Shirika linaweza kupigahatua kubwa ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, changamoto moja kubwainayolikabili Shirika hilo ni bei ya umeme. TANESCO inauziwaSh.495/= mpaka Sh.808/= kwa unit moja, wao wanauza kwaSh.198/= kwa unit moja. Katika hali hiyo, hata TANESCOikipunguziwa majukumu basi utendaji wake utakuwa haunaufanisi. Pia changamoto nyingine ni madeni ya Shirikawanayoidai Serikali na taasisi nyingine zinazohusiana naSerikali.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa nchi yetu imeshavumbuatakribani futi za ujazo trilioni 41.7 za gesi asilia. Hii ni neemakubwa kwa nchi yetu kama nchi yetu itatumia vizuri mali hii,

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

104

vinginevyo kama fursa hii haitatumiwa vizuri inaweza gesihii ikaleta maafa makubwa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na faida nyingizitazopatikana kwa kupata gesi asilia, faida moja ni kupatagesi ya kupikia katika nyumba zetu. Hili ninaliona katikakulinda mazingira ya nchi yetu linachukua nafasi ya pekee.Iwapo wananchi hawatakuwa na uwezo wa kuwezakutumia gesi hii kwa kupikia basi tuelewe nchi yetu itakabiliwana janga kubwa la uharibifu wa mazingira kwa ukataji wamisitu yetu kwa ajili ya utengenezaji wa mkaa. Ili gesi hii iletemanufaa ya kimazingira, ni lazima bei ya gesi ya kupikia iwerahisi kuliko kutumia mkaa. Hapo ndipo wananchi watawezakuhama kutumia mkaa na kutumia gesi. Naomba Serikaliinieleze watachukua hatua gani ili kuhakikisha kuwa bei yagesi ya kupikia itakuwa ni rahisi kuliko mkaa.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, kwanzanaanza kuiunga mkono hoja na kuipongeza Wizara kwa kazinzuri ambazo zimeshafanyika na zitakazofanywa.

Mheshimiwa Spika, pia naipongeza Serikali kwakusimamia na kutimiza ahadi zake baadhi kama vile uletajiwa umeme katika Jimbo la Nyang’hwale, nguzo na nyayazinaendelea kusambazwa. Je, ni lini sasa kazi hiyo itakamilikana umeme kuwashwa?

Mheshimiwa Spika, napenda kuipongeza Wizara kwakufuta leseni 161 za utafiti wa madini na moja moja yauchimbaji. Je, katika leseni hizo zilizofutwa na eneo la Wilayaya Nyang’hwale zimo? Kama zipo ni maeneo gani? Kamahakuna je, Wizara ina mpango gani wa kuwatengea maeneowachimbaji wadogowadogo Wilaya ya Nyang’hwalesababu maeneo mengi ya Nyang’hwale yana madini ainaya dhahabu.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kupata ufafanuzi wamalipo ya mgodi wa Bulyang’hulu yaani (service levy) kwa

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

105

Halmashauri ya Wilaya ya Kahama maana ni haki yao. Je, nilini sasa Wilaya ya Nyang’hwale itaanza kulipwa? Sababuuchimbaji wa mgodi huo unaelekea Jimbo la Nyang’hwalena madhara mengi kujitokeza kama milipuko na kupasukabaadhi ya nyumba na ardhi na uharibifu wa mazingira.

Mheshimiwa Spika, napenda kupata ufafanuzi kuhusuni namna gani Wizara imejipanga kuwasaidia wachenjuajikupatikana kwa chemical aina ya (cyanide) kwa bei nafuusababu hivi sasa inapatikana kwa njia ya panya tena kwabei kubwa sana. Wachenjuaji wote wanasubiri majibu yaWaziri kwa hamu sana kusikia Wizara yao inawasaidiaje kwasababu nao wanachangia pato la Taifa.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. AMOS G. MAKALLA: Mheshimiwa Spika, naombakuchangia hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini nikijikitakatika mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kuchelewa utekelezaji mradi waumeme vijijini kupitia REA. Nilianza kwa kuandika barua yamaombi mwaka 2011 kuomba kupeleka umeme vijiji vyaKidudwe, Kunke, Lusanga Ng’ambo, Kisala, Mgudeni, Makuyuna kata za Doma, Melela, Kanga na Kibati. Nilikubaliwamaombi yangu kwa barua, nimeshaandika barua mbili kwaWaziri, Profesa Muhongo na zote ameniahidi mradi huuutatekelezwa. Mwaka jana bajeti 2012/2013, zilitengwa fedhalakini mpaka sasa hakuna kinachotekelezwa. Nashukurutena mwaka huu 2013/2014, vijiji hivyo na kata hizo zipo katikampango wa kupelekwa umeme. Naomba sana REA itekelezemaombi yangu.

Mheshimiwa Spika, mradi wa MCC. Naomba Wizaraikamilishe miradi ya MCC ikiwepo kupeleka umeme (Mgeta,Mbogo, Sokoine, Dihombo, Mji Mpya (Madizini) na kitongojicha Mtakuja, kijiji cha Dakawa.

Mheshimiwa Spika, maombi ya kupeleka umeme Kijijicha Msufini, Mlaguzi, Dibamba, Lukenge, Mlumbilo na Lungo.

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

106

Naomba Wizara ipokee maombi ya kupeleka umeme katikavijiji nilivyovitaja. Nilishaandika barua kwa Meneja TANESCOMkoa ya kuomba vijiji hivyo kupelekewa umeme kutokanana mahitaji muhimu kwa sasa.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja, naombanijibiwe.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, umemevijijini. Umuhimu wa upatikanaji wa umeme vijijini ni haki yakila Mtanzania. Hata hivyo, asilimia 80 ya Watanzaniawanaishi vijijini huko ambako hawana matumaini ya kupataumeme kutokana na gharama kubwa za kufungiwa umeme,malipo makubwa yenye makato lukuki kila mwezi, uhabawa umeme wenyewe na changamoto ya kutofungiwaumeme kwa wakati na kadhalika. Kwa kuwa matatizo hayoyameendelea kuwa kikwazo cha wananchi wengi kukosaumeme jambo ambalo ni haki yao, je:-

(a) Ni kwa nini wananchi waliomaliza kufanyawiring katika nyumba zao inawachukua muda mrefukuwashiwa umeme?

(b) Je, ni kwa kiasi gani Wizara inahakikisha nguzoza umeme zinapatikana katika ofisi za TANESCO Wilayani iliwananchi wapate umeme?

(c) Wananchi ambao wanatumia umemewanakatwa fedha nyingi kila wanaponunua umeme mwishowa mwezi, kwa nini wananchi hawa wanapata gharamakubwa kila mwisho wa mwezi pindi wanaponunua umeme?

(d) Je, ni kwa nini wananchi walio maeneoambayo nguzo za umeme zimefika hawajawashiwa umemempaka leo, ikiwa ni Wilaya ya Karatu – Kata ya Endamarariek.

(e) Je, ni lini sasa umeme utapelekwa katika Kataza Mang’ola na Mbulumbulu Wilayani Karatu? Je, katikampango ujao wa REA 2013/2014, kata hizo zipo katika orodhaya kupata umeme?

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

107

(f) Gharama za kufungiwa umeme zimeendeleakuwa kubwa hivyo kuwanyima wananchi hao haki ya kupataumeme. Je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza gharamahizi ili kuwafanya wananchi kumudu gharama hizo?

Mheshimiwa Spika, nawasilisha.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati naMadini.

Mheshimiwa Spika, Wizara hii ndio roho inayosukumadamu iliyojaa virutubisho vya uchumi wa Taifa la Tanzania.Nishati ya umeme ulimwenguni kote imekuwa ni chimbukola mapinduzi ya viwanda.

Mheshimiwa Spika, kwa bahati nzuri, MwenyenziMungu ametujalia kuwa na vyanzo vingi vya uzalishaji waumeme ikiwemo maji, gesi, jua, joto ardhi, upepo, makaaya mawe. Vyanzo hivi vya uzalishaji wa umeme vinaiwekanchi yetu katika nafasi nzuri sana ya kuwa mzalishaji mkubwawa umeme na kwa vyovyote vile baada ya muda mchacheujao, Tanzania itakuwa na uwezo wa kuwa na umeme waziada ambao unaweza kuuzwa hata nchi jirani hasa katikanchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa vyovyote vile iwavyo,upatikanaji umeme wa gharama nafuu utavutia uwekezajikatika sekta ya viwanda na hivyo kuchochea ukuaji wauchumi wa nchi yetu. Kuwepo kwa umeme wa uhakikakutachochea uwekezaji wa viwanda vya kuongeza thamanikwa mazao ya kilimo na hivyo kuboresha tija kwa wakulimawa nchi hii. Ni imani yangu kuwa zao la pamba ambalolimekuwa linakumbwa na tatizo la kupanda na kushuka kwabei, kwa kuwepo kwa umeme wa uhakika kutachocheanguvu zaidi kuelekezwa katika uwekezaji katika viwanda vyanguo ambazo zitauzwa ndani ya nchi na hata nje ya nchi nahivyo kuingiza fedha za kigeni na hivyo kuchangia ukuaji wauchumi wa nchi yetu na kupandisha hata bei ya zao lapamba.

Mheshimiwa Spika, aidha, naipongeza Serikali kupitia

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

108

Wizara hii ya Nishati na Madini kwa kuendelea na mpangowake wa kuipatia Wilaya yangu ya Mbogwe huduma yauhakika ya umeme kupitia mradi wa Electricity Vunaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nakutekelezwa na mkandarasi wa ujenzi M/S Eitel Networks TEAB kutoka Sweden na kwamba utekelezaji wa mradi huuunatarajiwa kuanza mwezi ujao wa Juni, hongera sana.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Wakala waUmeme Vijijini REA, Mbogwe tunanufaika pia katika mwakahuu wa fedha na vijiji vya Bwendamwizo, Bwendanseko,Nambubi, Ilolangulu, Bugalagala, Kashelo na Lulembela.Nachoomba hapa ni Serikali kuongeza fedha zaidi REA iliasilimia kubwa ya Watanzania ambao wanaishi vijijiniwapate umeme. Naiomba Serikali iongeze fedha il iWatanzania wengi zaidi wapate huduma hii. Kusambazaumeme vijijini kutasaidia sana kukuza uchumi na kuokoauharibifu wa mazingira kupitia ukataji hovyo na miti kwalengo la kupata mkaa.

Mheshimiwa Spika, sekta ya madini ina mchangomkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Taifa letu. Hata hivyo,zipo changamoto nyingi hasa katika sekta ya wachimbajiwadogo na jinsi Wizara kwa niaba ya Serikali kuona ni jinsigani Serikali itakavyomiliki angalau asilimia hamsini 50% katikamigodi ya madini na sekta ya gesi.

Mheshimiwa Spika, Wilayani Mbogwe kuna taarifa zauwepo wa madini ya dhahabu katika maeneo ya Bukandwe,Lugunga, Shenda, Nyakafuru na kadhalika. Naiomba Wizaraione ni kwa namna gani itakavyowasaidia wachimbajiwadogo wa maeneo tajwa hapo juu.

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla naipongeza Wizaraya Nishati na Madini kwa kuja na bajeti ambayo ina lengo lakuiweka nchi yetu katika nafasi ya mataifa yanayokuzauchumi kwa kasi kubwa.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

109

MHE. HAMOUD ABUU JUMAA: Mheshimiwa Spika,napenda kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha nami nisememachache juu ya bajeti hii ya Wizara ya Nishati na Madini yamwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, napenda kumpongezaMheshimiwa Waziri kwa kazi ngumu anayoifanya nakuhakikisha usimamizi wa sheria katika sekta ya madiniunasimamiwa vizuri. Bajeti hii imelenga kutekeleza Ilani yaChama cha Mapinduzi lakini changamoto bado ni nyingisana katika sekta hii, inabidi ifanyike kazi ya ziada ili wananchiwaridhike na utendaji wa sekta hii ya nishati na madini.

Mheshimiwa Spika, katika eneo kubwalinalolalamikiwa sana na wananchi ni sekta ya umeme. Kilakukicha umeme umekuwa tatizo kubwa kwa wananchi.Napenda kuipongeza Serikali kwanza kwa kupunguza adaya kuunganisha umeme ambayo hapo awali ilikuwa ni kerokubwa kwa wananchi na hata kuleta mianya ya rushwa kwabaadhi ya wafanyakazi wa TANESCO. Tatizo la kukatikakatikakwa umeme limekuwa la kudumu, bado halijapatiwaufumbuzi, mpaka karne hii imekuwa ni aibu kwa Taifa letukuwa na migao ya umeme isiyokuwa rasmi na kukatikakatikaovyo kwa umeme kusikokuwa na taarifa yoyote kwawatumiaji. Hali hii inaonyesha kama hatutaki kubadilika,kujifunza kutoka kwa wenzetu mbinu walizotumia kuepukanana adha hii. Ikumbukwe umeme ni kila kitu, bila umeme,maofisini kazi zinazorota, mahospitalini wagonjwahuhatarisha maisha yao, viwanda havitazalisha, amauzalishaji utapungua na kushusha uchumi wa nchi. Naombatutilie mkazo katika hilo ili tuondokane na matatizo haya nahata ikionekana njia hii ya uzalishaji umeme wetu ndio tatizobasi zifanyike juhudi za makusudi kupata njia mbadala. Leohii tumesikia TANESCO imeshindwa rufani ya kesi iliyokuwainapinga kuilipa kampuni ya DOWANS, kwa maana hiyoDOWANS inatakiwa ilipwe. Naishauri Serikali kuliangalia hilikwani TANESCO haina uwezo wa kulipa hizo fedhavinginevyo mzigo huu watatupiwa wananchi katika njia yakupandishiwa bei ya umeme na kugeuka kuwa mzigo kwao,kwa hili Serikali haina budi kuchukua hatua.

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

110

Mheshimiwa Spika, sekta ya madini imekuwaikilalamikiwa sana hapa nchini, zaidi mikataba tunayoingiana hawa wawekezaji ambao mwisho wa siku naaminiwanatunyonya tu. Kuna baadhi ya maeneo kuna migogoromingi sana kati ya wananchi na hawa wawekezaji, lakiniSerikali imeonekana kuwalinda ama kuwabeba hawawawekezaji ili hali wananchi wanauawa kwa kupigwa risasina wawekezaji hao.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali irekebishe hiiSheria ya Madini ili itunufaishe wazawa kwani mikatabatunayoingia ni ya muda mrefu na haitunufaishi kitu wazawa.Pia Serikali iwafuatilie hawa wawekezaji kuhusu utekelezajiwa ahadi walizokubaliana kwenye hiyo mikataba kwaniimegundulika utekelezaji wake kwa jamii umekuwa mdogomno. Vilevile usimamizi wa madini yapatikanayo hapa nchiniuongezwe kwani inasemekana kuna madini hutoroshwa bilaSerikali kujua na kupoteza fedha nyingi.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali kufuta misamahaya kodi kwa wawekezaji hawa pale wanapokuja kuwekezakatika sekta ya madini kwani hatuna budi kuringia urithi wetutuliopewa na Mwenyezi Mungu, kwani madini yanajitangazayenyewe na hakuna uhitaji wa kumbembeleza mwekezajikwenye sekta hiyo. Ikumbukwe madini hayaozi hatayakiachwa milele vizazi vijavyo vitakuja kufaidika nayo lakinisi kwa hali hii ya kuingia kwenye mikataba mibovu nakupoteza rasilimali zetu kwa wageni.

Mheshimiwa Spika, kuna tatizo la watumishiwanaofanya kazi katika sekta hii ya madini kupatwa namatatizo makubwa ya kiafya baada ya kutumia vifaaambavyo vina madhara na baadaye kutokupata msaadawowote kutoka kwa waajiri wao. Naiomba Serikalikuboresha sheria ili kuwabana wawekezaji hawa ili kuwalindawananchi wetu wanaopata athari hizo na mwisho kufikiakufariki dunia.

Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia, napendakukumbushia kilio cha wananchi wa Jimbo la Kibaha Vijijini,

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

111

matatizo ya umeme bado ni kero na kutokujua hatma yakeni lini. Mheshimiwa Rais alitoa ahadi ya kutatua tatizo hili nakupeleka umeme Kata ya Ruvu. Ufuatiliaji wa utekelezaji waahadi hii ulishaanza kwa Waziri wa Nishati na Madini kufanyaziara katika Jimbo hili na akaona ukubwa wa tatizo. Napendakujua ni hatua zipi zimefikiwa na nini kinaendelea katikautekelezaji wa ahadi ya Mheshimiwa Rais ya kupeleka umemekatika Kata ya Ruvu. Kwani kupeleka umeme katika Kata yaRuvu kutasaidia kuleta maendeleo ya haraka na kupandishauchumi wa wakazi wa Jimbo la Kibaha Vijijini.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, naombakuwapongeza Waziri na Naibu Mawaziri wa Nishati naMadini, Katibu Mkuu na Maafisa wote wa Wizara hii kwa kazikubwa na nzuri wanayoifanya ya kuandaa, kujenga nakusimamia rasilimali ya nishati na madini kwa ajili yakuendeleza uchumi wa nchi yetu Tanzania. Ushauri wangu,Serikali iendelee kutumia juhudi na maarifa waliyonayowatumishi wazalendo ya wanaosimamia sekta hii ili tuijengenchi yetu.

Mheshimiwa Spika, umeme, sisi wananchi wa Wilayaya Namtumbo tunaishukuru Serikali kwa kuwa sikivu,niliposhauri na kuiomba kutuwekea umeme wa generatorwakati tunasubiri mradi wa umeme wa Gridi Makambako –Songea 220KV. Leo Namtumbo Mjini umeme unawaka lakinikuna changamoto yake. Tulipokubaliana umeme uwekwesehemu zipi, Makao Makuu ya Wilaya Namtumbo, walipofikawataalam, Wahandisi Umeme na Mipango, tulikubalianaumeme utawekwa pia katika Hospitali ya Wilaya, lakini nguzoza umeme hazikufika hospitalini, zimeishia katika maeneoya nyumba za wananchi tu, ni umbali ambao hauzidi kilomitamoja. Naiomba Serikali kupitia (REA) watuongezee fedha zadistribution line ili umeme ufike pia Hospitali ya Wilaya nakukamilisha lengo tulilokusudiwa na wananchi, wagonjwawapate huduma stahiki katika Hospitali hiyo ya Wilaya.

Mheshimiwa Spika, naomba kutumia fursa hii kwa

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

112

hatua zilizofikiwa za utekelezaji wa mradi wa umeme wa220KV Makambako – Songea, Namtumbo ikiwa mojawapoya Wilaya zitakazofaidika. Tunachowaomba, kwa mujibu wataarifa mliyotusambazia wadau watakaofaidika na mradihuu na ratiba ya mradi utakavyoanza na sisi tuwahamasisheau tuwa-sensitive wananchi waliopo na wale ambao njiaya umeme itapita kwenye maeneo yao, waweze kutoaushirikiano kama Serikali mlivyoomba. Sasa sisi sensitizationtutakayoifanya ni pamoja na kuwaambia kazi hiyo itaanzalini na tunategemea pia kukamilika lini ili waweze kupishamapema kwa maana ya kuacha kulima au kuyatumiamaeneo hayo ambapo njia ya umeme itapita. NachoiombaSerikali, mradi ufuate ratiba mliyotueleza katika taarifamlizotusambazia. Sisi ni wanasiasa tunapoenda kuwaelezawananchi wanaamini tuyasemayo, sasa kama bado mnafikirimradi hautaanza kama mlivyotueleza, tuelezeni mapemakabla hatujaanza kazi hiyo ili isije kutufanya tusieleweke nakuanza kazi ya kuelezea kwa nini mradi haujaanza baadaya kutumia muda mwingi wa sensitization kwa wahusika iliwatupe ushirikiano. Pia anapoacha kuitumia ardhi yake,mwananchi wa kijijini maana yake ni kwamba anapunguzaeneo lililokuwa linampatia pato lake. Hivyo anatakiwa aonekazi iliyomfanya aiachie ardhi yake inatekelezwa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu madini, kumekuwa natetesi kuwa kuna baadhi ya wawekezaji wakubwa wa njena baadhi ya taasisi wanapinga chinichini na wazi miradimikubwa ya maendeleo yetu ya uchimbaji gesi na urani. Je,Serikali inasema nini kuhusu tetesi hizo na kuhakikisha miradihiyo inatekelezwa kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchiyetu na kukamilisha lengo letu la kuja kuwasaidia wananchimaendeleo yao kiuchumi na kukuza pato la uchumi wa nchiyetu?

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa pia kumekuwa na tishiola usalama wa miradi yetu, nashauri tutumie vyombo vyetuvya ulinzi na usalama kulinda miradi hii. Tusikubali hata kidogokuruhusu makampuni ya ulinzi ya nje ya-control ulinzi wamiradi yetu mikubwa. Kama ikibidi ushirikiano wa ki-teknolojiabasi Head of command lazima viwe vyombo vyetu vya ulinzi

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

113

na usalama. Hapa tutajihakikishia mambo matatu, moja,pato litakalopatikana kutokana na kazi hiyo, pili, uhakikawa ulinzi wa mali zetu bila kuhujumiwa na tatu, kamatutashirikiana na kampuni za nje vijana wetu watapataknowledge ya teknolojia ya ulinzi wa kisasa katika miradimikubwa.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. AHMED M. SHABIBY: Mheshimiwa Spika, napendanami kuwa mmoja wa wachangiaji katika Wizara hii. Naanzakuchangia kwa maandishi lakini pia kwa vile nimeombakuchangia kwa kuongea, nikipata nafasi nitayaongea haya.

Mheshimiwa Spika, sina shaka na utendaji wa Wizarahii kwa sasa kwa maana ya viongozi wa juu Wizarani nanaipongeza Wizara hii na hotuba ya Waziri.

Mheshimiwa Spika, nachotaka kuanza nacho nimiradi ya umeme ya REA Awamu ya Kwanza ambapo katikaWilaya ya Gairo tulipewa Kata za Rubeho, Kibedya naChakwale. Kama majibu ya Waziri ya tarehe 7/5/2013 katikaswali langu namba 158.

Mheshimiwa Spika, hatua zilizofika ni upimaji wa njiana kuweka alama kwa asilimia 100 lakini mpaka sasa badohakuna kazi yoyote au (Mkandarasi) anayeendelea na kazihiyo kwa muda mrefu toka kazi ya upimaji imalizike. Hofuyangu ni kwa vile upimaji huu ni wa muda mrefu na sehemuzilizopimwa ni mashamba ya watu. Kuchelewesha mradi huukutasababisha wananchi waendelee na shughuli zao katikamaeneo yaliyopimwa kama ujenzi na kusababisha kerozingine kujitokeza kwa vile hawakupewa taarifa. Kwamaana hiyo, nashauri mradi huu uanze mapema kutoa aukuzuia kero zozote ambazo zinaweza kujitokeza katika bajetiya mwaka2013 – 2014.

Mheshimiwa Spika, miradi itakayotekelezwa na REAkatika Wilaya ya Gairo, vijiji saba tu ndio vya Wilaya ya Gairo,vijiji sita sio vya Wilaya ya Gairo. Kama Kiegea na Mtumbatu

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

114

ni Wilaya ya Kilosa na Kikunde, Kwa Maligwe, Mswaki, Mgela– ni Wilaya ya Kilindi. Vijiji vya Gairo ni Madege, Nguyami,Idibo, Italagwe, Makuyu Kinyolisi na Iyogwe. Kwa masikitikosana Wilaya ya Gairo ina watu wengi sana kwenye vijiji vyakena watu wanaojituma na wana uwezo wa kuweka umemekatika nyumba zao na viwanda vidogovidogo vya usagajina ukamuaji mafuta. Cha ajabu mpaka leo ni Gairo Mjini tundio pana umeme pamoja na hayo bado Gairo hiyohiyoinapatiwa vijiji saba tu katika bajeti hii ya 2013/2014ukilinganisha na Bunda vijiji 69 ndani ya nchi moja. SielewiREA inafanyaje utafiti wake, hapa napata mashaka. Naombaangalau uwiano sehemu zilizosahaulika miaka mingi tokauhuru uzingatiwe.

Mheshimiwa Spika, maoni yangu katika vij i j ivilivyopendekezwa kupatiwa umeme viongezwe vijiji vyaLeshata na Kitaita, vipate umeme kutoka katika Kijiji chaIdibo ambacho kimo kwenye bajeti hii na umbali wake nikilometa sita tu kutoka Idibo.

Mheshimiwa Spika, umeme unaoenda Chakwaleupelekwe katika vijiji vya Tabu Hotel na Ihenje, umbali wakeni kilometa nne tu.

Mheshimiwa Spika, umeme wa Gairo Ukwamaniuende vijiji vya Majawanga, Luhwaji, Mkalama, Meshugi naumbali wake ni kilometa saba tu.

Mheshimiwa Spika, ni ajabu katika ukanda wa tambalalekatika Tarafa ya Nongwe, Kata ya Chanjale inayopakanana Wilaya ya Mpwapwa. Vijiji vyote vya Mpwapwa vimokatika bajeti hii wakati vinapakana kwa kilometa mbili navijiji vya Jimbo la Gairo mfano, Mlembule, kijiji cha Mpwapwakinapata umeme wakati cha jirani kwa kilometa moja nanusu kijiji cha Kumbulu, Wilaya ya Gairo hakimo. Kingine,Mwenzele (Mpwapwa) mpaka Mavisi na Chanjale (Gairo)kilometa kumi (10) havimo, inaleta picha mbaya sana kwavijiji hivi na hata kiwilaya, kisiasa na kirasilimali za nchi.

Mheshimiwa Spika, mwisho naomba nieleweke,

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

115

sitopenda kupinga bajeti hii kwa mwaka huu. Naombasehemu nilizozitaja zifanyiwe kazi.

MHE. CELINA O. KOMBANI: Mheshimiwa Spika,naomba kuwapongeza Wizara ya Nishati na Madini, kwaHotuba nzuri, yenye Facts & Figures kwa upande wa Jimbo laUlanga Mashariki. Tunawashukuru sana REA (Umeme Vijijini),kwa kazi nzuri ambayo wameifanya katika Mradi wa Umemewa Mahenge hadi Mwaya. Umeme huo umeanzia MahengeMjini na kupitia Vijiji vya Mzelezi, Ruaha, Chirombora hadiMwaya. Wakandarasi walifanya kazi hiyo kwa kasi nakusimamisha nguzo na nyaya katika mtandao wote.

Mheshimiwa Spika, ombi kwa Wizara; naomba Mradiukamilike kwa sababu umeme haujawaka wakati nyaya nanguzo zimekamilika miezi saba iliyopita. Naomba Mradi huosasa utoke Kata ya Mwaya kwenda Kata ya Mbuga ambakoni Makao Makuu ya Mbuga ya Selous, ambayo ina wawindajiwengi wanaongeza Pato la Taifa.

Mheshimiwa Spika, naomba Mradi huo pia utoke Kataya Mwaya kwenda Kata ya Ilonga na Ketaketa. Nitashukurusana ombi hili likikubaliwa.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Spika, kwanini umeme uishie Kibaoni na Usevya tu usifike Kata zaMiginga, Muze, Mtowisa, Milepa, Ilemba, Kaoze naKilyamatundu?

Mheshimiwa Spika, Serikali iliahidi kufikisha umeme Kijijicha Sakalilo kwa nia ya kufunga mashine za kukoboampunga ili Wananchi wauze mchele badala ya kuuzampunga na vilevile kuna Skimu ya Umwagiliaji; ni lini umemeutafika?

Mheshimiwa Spika, ni l ini Mto Nzovwe ambaoulishafanyiwa utafiti kuwa una uwezo wa kutoa megawatinane na zaidi Serikali itafanyia kazi lini? Pia Mto Mombamegawati kumi?

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

116

Mheshimiwa Spika, kwa nini umeme uishieKamsamba uache kufikishwa Kilyamatundu wakati umbaliuliopo ni kama mita mia moja? Huu ni ubaguzi naombamajibu?

Mheshimiwa Spika, Ukanda wa Ziwa Rukwa woteunahitajika kuwa na umeme kwani ni ukanda wa uzalishaji.Mawaziri tembeleeni Ukanda huu mwone fursa zilizopo.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri ni tegemeoletu sote; atutendee haki nasi.

MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE: MheshimiwaSpika, nampongeza Mheshimiwa Prof. Muhongo na NaibuMawaziri na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,kwa kazi yao nzuri ambayo imeliletea Taifa maendeleo yaaina yake.

Mheshimiwa Spika, nina mambo kadhaa ambayonataka nichangie katika hoja ya Wizara hii:-

Mheshimiwa Spika, mpango mzuri wa kusambazaumeme vij i j ini ni mpango wa pekee kabisa ambaoumekusudia kuboresha maisha ya Wananchi vijijini, lakiniMradi huu unakumbwa na tatizo la kutengewa fedhakidogo. Hata kama zinatengwa na kuwekwa katika bajeti,lakini Wizara ya Fedha inashindwa kutoa fedha zotezilizowekwa kwenye bajeti na hivyo kuifanya Miradi yoteiliyokusudiwa kutekelezwa kushindwa. Hali hii huwakatishatamaa Wananchi ambao tumekuwa tukiwaahidi tukiwaMajimboni.

Mheshimiwa Spika, tatizo l ingine ambalolinakwamisha Wananchi wa vijijini kupewa huduma hii yaumeme ni uchache wa transformer zinazoletwa.

Mheshimiwa Spika, mimi kwangu Mbeya Vijijini kunavijiji vingi ambavyo umeme mkubwa unapita katika vijiji hivyolakini Wananchi wanashindwa kupewa huduma hiyo kwasababu transformer hazipo. Aidha, mfano wa vijiji hivyo ni

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

117

Lwanjilo, Ihango, Nsongwi Juu, Shibolya, Tembela, Iyela,Nyara, Ikoho Sekondari, Iyela Sekondari, Hatwelo na vinginevingi. Je, Serikali ina mpango gani wa kuvipatia vijiji hivyohuduma hiyo?

Mheshimiwa Spika, Kijiji cha Nsongwi Juu kinapakanana Ituha Mbeya Mjini ambako majirani zao wanapataumeme wa MCC. Je, Kijiji hiki hakiwezi kuunganishiwaumeme huo wa MCC?

Mheshimiwa Spika, naipongeza kazi nzuri inayofanywana Wakala wa Umeme Vijijini (REA). Kwa kuwa sekondarinyingi za kata ziko vijijini; kwa nini Serikali isiwe na mpangomaalum wa kupeleka umeme katika shule za kata? MbeyaVijijini ina shule za kata ambazo zipo karibu kabisa na mapitioya umeme. Mfano wa shule hizo ni Nsongwi Juu Sekondari,Igale, Isato, Mshewe, Ihango, Ikoho Sekondari, Shibolya,Mwakipesile, Ikukwa na zingine nyingi. Ili kupeleka elimu yaTEKNOHAMA katika shule hizo ni vizuri pia zingefikiriwa katikampango maalum wa kupeleka huduma hiyo. Walimu wengipamoja na Waganga walioko vijijini, hawatakimbia wataishivijijini.

Mheshimiwa Spika, tulielezwa katika Bunge lako Tukufukuwa, vyanzo vingine vya mapato ya REA ni kutoza fedhakwenye simu. Je, huo mpango ukoje; Wananchi wanajuakwamba kila mtu akipiga simu fedha kiasi zinakatwa kwaajili ya umeme vijijini? Tulipoelezwa katika Bunge lakotuliwaeleza Wananchi hivyo. Naomba Waziri atuelezeamekwama wapi?

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali kutafiti au kupatachanzo kingine cha mapato kwa ajili ya kuiwezesha REAwaweze kusambaza umeme kwa haraka vijijini. Kutegemeafedha za wafadhili tutakwama, angalia Miradi ya Maji, nayokwa kutegemea fedha za wafadhili haitekelezwi karibumiaka kumi sasa. Bila shaka Waziri atatoa majibu yenyematumaini.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

118

MHE. DKT. TITUS M. KAMANI: Mheshimiwa Spika,kwanza, nampongeza Mheshimiwa Waziri na Timu yake, kwamaandalizi ya Hotuba nzuri, inayoleta matumaini mapyakatika Sekta ya Nishati na Madini Nchini. Kwa kuwa Sektaya Nishati ipo katika Mpango wa Serikali wa Big Results Now,tunaomba fedha ya kutosha ipatikane kwa utekelezaji waMiradi yote iliyowekwa na pia uwepo usimamizi madhubutizaidi ili iweze kukamilika kwa wakati. Kukamilika kwa Miradihiyo kutasaidia sana kuondoa umaskini wa watu wetukutokana na matumizi ya nishati ya umeme na pia kupunguzauharibifu wa mazingira.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, napenda kuhojimambo machache kama ifuatavyo:-

Kitaifa kunakuwa na kusuasua sana kwa Miradiinayotekelezwa na Kampuni ya Symbion na inaonekanakuwa Serikali haina meno ya kuwahoji wala kuwachukuliahatua. Sasa Wananchi waelewe nini kuhusu Miradi hiyoukiwemo Mradi wa siku nyingi katika Jimbo la Busega waNyashimo – Kabita – Nyamikoma – Kalemela. Baadhi yanguzo zilisimikwa tangu Aprili mwaka 2012 hadi leo hakunakinachoendelea zaidi. Wananchi wanahitaji kufahamuhatima ya Mradi huu ambao unapita katika vijiji muhimu vyauchumi.

Viwanda vya pamba katika Mkoa wa Simiyuvimekuwa vikitozwa malipo ya umeme kwa miezi mitatuzaidi baada ya kufunga msimu wa kusindika pamba kamaKVA charges ambazo ni asilimia 75 ya gharama ya matumiziya kila mwezi. Hivi gharama hii ni ya kazi gani wakatimitambo huwa imezimwa? Kimsingi, gharama hii huwainawaongezea mzigo mkubwa wasindikaji wa pamba nakuwarudisha nyuma kiuchumi. Mara kadhaa wasindikajiwameleta malalamiko kuhusu suala hili lakini wanapewaahadi zisizotekelezwa. Gharama hii inatufanya tuhisi kuwani mradi wa kifisadi unaosimamiwa na watu fulani maalumndani ya TANESCO. Nahitaji ufafanuzi zaidi kuhusu hili nakimsingi tunataka mtindo huu ukomeshwe. Ninadhamiriakuondoa shilingi kwenye mshahara wa Waziri iwapo sualahili halitapata ufumbuzi.

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

119

Mheshimiwa Spika, viwanda vya pamba vingivilivyoko Wilaya za Busega na Bariadi havina umeme wauhakika, kwa sababu umeme kutoka Shinyanga ni mdogona hukatika mara kwa mara. Kulikuwa na maelezo yakuvipatia umeme viwanda hivi kutokea Bunda ambapotransformer ilipelekwa Arusha kutengenezwa ili ije isaidiekuimarisha uzalishaji wa umeme wa Bunda. Hata hivyo,mashine hiyo bado haijafungwa. Matokeo yake, kwaviwanda ambavyo vimeunganishwa na umeme wa Bunda,inapofika msimu wa kusindika pamba huwa umemeunakatwa kuja Bariadi ili viwanda vya pamba vya Bundavijitosheleze kwanza. Hali hii husababisha hasara kubwa kwakukaa na pamba bila kuisindika kwa muda mrefu vikisubiriviwanda vya Bunda vimalize. Kwa nini Serikali hailipatii uzitowa kutosha suala hili linalochangia kudidimiza Wananchikiuchumi?

Mheshimiwa Spika, kuna wakati nilimwandikia baruaMheshimiwa Waziri kuhusiana na Miradi ya Umeme WilayaniBusega: Lamadi – Mkula – Mwanangi – Badugu – Busami hadiKasolo na ule wa Nyashimo – Nyamatembe – Shigala – Busega– Igalukilo – Malili – Ngunga – Ngasamo. Majibu niliyopatayalikuwa na matumaini sana, lakini hadi sasa bado hakunakinachoendelea. Miradi hii ipo katika hatua kadhaa zautekelezaji lakini kwa nini sasa kisifanyike kitu kamilikikakamilika? Nitaomba sana hata kwenye taasisi kama shulena zahanati ambapo miradi hii inapitia nazo zipate umeme.

Mheshimiwa Spika, ni lini kwa hakika Mradi wa Mgodiwa Dutwa – Ngasamo utaanza uzalishaji? Wananchiwamesubiri sana kujua maendeleo ya mgodi il i naowajipange jinsi ya kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo.

Je, ni lini TANESCO itawalipa taasisi ya fedhailiyogharimia ujenzi wa njia ya umeme kutoka Mwanangi hadiKiwanda cha Pamba cha Alliance katika Kijiji cha Kasoli?Baada ya kufanikisha ujenzi huo, sasa imekuwa ni usumbufumkubwa kudai fedha hiyo kutoka TANESCO.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

120

MHE. ANNA MARYSTELLA J. MALLAC: MheshimiwaSpika, naomba nianze moja kwa moja kuchangia katikaWizara hii ya Nishati na Madini na nijikite katika suala lamadini.

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Madini ni Sekta muhimusana, inayoinua maisha ya watu na hasa vijana kiuchumikatika nchi hii. Kumekuwa na ugumu wa upatikanaji waleseni za uchimbaji hasa kwa wachimbaji wadogowadogowamekuwa wakihangaika na kunyanyasika sana. Kwanza,hawana maeneo ya kufanyia shughuli zao za uchimbaji.Wanafanya shughuli za uchimbaji bila leseni kwaniwamekuwa wakisumbuka namna ya kupata leseni.

Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya Mwaka 2012/2013,Hotuba ya Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana, aliongeleajuu ya upatikanaji na utoaji wa leseni za uchimbaji pamojana kuendeleza uchimbaji mdogomdogo, ukurasa wa 97/98na Serikali iliainisha maeneo yatakayotengwa kwa ajili yauchimbaji mdogo, lakini mpaka sasa Wananchi badowanahangaika. Mfano, mzuri ni wachimbajiwadogowadogo wa dhahabu Wilaya ya Mpanda.

Mheshimiwa Spika, wachimbaji hao wananyonywakwa kuwa wanachimba kwenye maeneo ya watu na kwamasharti magumu, kwamba wanapochimba lazimawamuuzie mwenye eneo.

Mheshimiwa Spika, namwomba Mheshimiwa Wazirimwenye dhamana atakapohitimisha bajeti yake, awaelezeWatanzania na wachimbaji wadogowadogo ni l iniwatapata uhuru wa masoko ya madini wanayochimba? Nani lini watapata leseni na kupewa maeneo maalum iliwaendeshe shughuli zao?

Mheshimiwa Spika, pia wachimbaji wakubwa wamadini wanaotoka nje ya nchi na wanaopewa leseni yakuchimba kama vile Wachina, Waturuki na kadhalika,wamekuwa wakiwanyanyasa Watanzania kwa kuwafanyishakazi kwa ujira mdogo na Wananchi wanakosa pakulalamikia.

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

121

Mheshimiwa Spika, ninamwomba Waziri mwenyedhamana, alitolee tamko suala hili ili Wananchi wasiendeleekunyanyasika ndani ya nchi yao.

Mheshimiwa Spika, nije kwenye suala la nishati, sualaambalo maisha ya Watanzaia walio wengi huendeshwakutegemea nishati tofauti.

Mheshimiwa Spika, nikianzia na nishati ya umeme, kazizilizopangwa kutekelezwa kwa bajeti ya 2012/2013 kamaHotuba ya Bajeti ya Mheshimiwa Waziri mwenye dhamanaukurasa 75 na 76 inavyosema; lengo ni kuongeza uwezo wakufua umeme na ujenzi wa njia za kusafirisha na kusambazaumeme makao makuu na vijiji.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa malalamiko kwaSerikali kwamba, Mkoa mpya wa Katavi tumesahaulika sana,kwani mpaka sasa tunatumia jenereta chakavu nazilizochoka. Tunamwomba Mheshimiwa Waziri atuelezekuwa ni lini Mkoa wa Katavi tutaunganishwa na umeme waGridi ya Taifa ili kupata uhakika wa umeme au ni lini tutapatajenereta mpya ili kuepuka adha ya umeme?

Mheshimiwa Spika, katika Mkoa mpya wa Katavikuna Wilaya mpya ya Mlele ambayo ni muunganiko waTarafa mbili kubwa ambazo ni Mpimbwe na Inyonga.Namwomba Mheshimiwa Waziri atupe macho katika Wilayahii ili Wananchi waweze kupata nishati ya umeme. Pia kunaTarafa nyingine kama Mwese na Karema, tunaomba Serikaliifikishe umeme katika Tarafa hizi ambazo zipo mpakani mwaTanzania na Nchi Jirani za Congo, kuimarisha ulinzi nakuchochea maendeleo kibiashara.

Mheshimiwa Spika, nawasilisha.

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, Wizaraya Nishati na Madini imejitahidi sana katika kutekelezaMipango ya Serikali. Jambo kubwa ambalo ninawapongezani kumudu kusimamia TANESCO kwa kuondoa mgao mbayawa giza ambalo lililikabili Taifa letu. Pamoja na changamotoza miundombinu lakini wamejitahidi sana.

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

122

Mheshimiwa Spika, pongezi za kipekee kwa Serikalikuboresha umeme katika Jiji la Dar es Salaam. NikiwaMbunge wa Mkoa, natoa shukrani nyingi kwa Serikali yaChama cha Mapinduzi, kwa mipango yao mizuri yakuboresha Jiji.

Mheshimiwa Spika, kwa upekee, natoa shukurani kwaWizara kunijengea uwezo kwa mafunzo katika nchimbalimbali ambayo ndani ya mafunzo nimegunduayafuatayo:-

Kumbe Serikali yangu (Wizara) mnayo mipango mizuriya Kimataifa ikiwemo ya uboreshaji miundombinu ya umemekatika Miji Mikuu.

Mheshimiwa Spika, nashauri endeleeni hivyo pamojana changamoto za ukosefu wa fedha za kutosha, lakini juhudizenu zinatia moyo. Umeme katika Wilaya ya Temekeumeshafika Kimbiji, sasa ufike Kata ya Pemba Mnazi.

Wilaya ya Ilala nashukuru Serikali imepeleka umemempaka kwa waathirika wa mabomu, naomba wanakijijiwaliopo njiani ulimopita umeme nao wapewe umemewashushiwe transformer.

Wilaya ya Kinondoni kuna matatizo ya kukatika katikaumeme maeneo ya Sinza, Kijitonyama, Mwenge na sehemunyinginezo, tuangalie tatizo bado halieleweki vizuri kwaWananchi.

Mheshimiwa Spika, katika kujengewa uwezo,nimeona Nchini Bangkok jinsi gani wana-control matumiziya umeme. Unapotumia vyombo vya umeme mfano air-condition hata ukiweka high speed inarudi kwenye matumiziya kawaida tu. Hali hiyo inasaidia katika ku-balancematumizi ya umeme kila Mwananchi aweze kufaidika nahuduma hiyo. Nashauri tuangalie kwa undani tuone kamainaweza kusaidia.

Mheshimiwa Spika, Tanzania tunatumia sana umeme

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

123

wa jua lakini katika sehemu kubwa ya watumiaji kila mmojaanakuwa na panel yake. Katika uboreshaji umeme vijijini nibora Serikali ikaweka utaratibu wa kupata Kituo cha Umemewa Solar na kuingiza katika Gridi ya Taifa kisha ukagawiwakwa Wananchi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi kubwa zaSerikali kuendeleza upatikanaji wa umeme, lakini nyumbazinajengwa siku hadi siku Jijini Dar es Salaam mpakamaghorofa yanaanguka. Je, kuna mawasiliano baina yawajengaji na TANESCO?

Nashauri Serikali isimamie majengo; vinginevyo,TANESCO watalaumiwa kila siku kwa tatizo la umeme kumbena sisi Wananchi tuna makosa kwa kujenga bila utaratibukwenda kinyume na mipango au bajeti za Serikali. TANESCOwashirikishwe kwenye Kamati za Mipango Miji zinazotoa vibalivya ujenzi waweze kutambua mahitaji yao mapema.

Mheshimiwa Spika, TANESCO inapata hasara kwakununua umeme wa gharama kubwa na kuuza kwagharama ndogo. Pamoja na juhudi kubwa za kupata gesiasilia iweze kuzalisha umeme wa bei nafuu. Tukiweza kubadilimuundo wa uendeshaji wa TANESCO na tukaleta fedha,tunaweza kulipia umeme kwa tariff tofauti ya mijini na vijijini,kulingana na maeneo; mfano, Osterbay na Masaki, beitofauti na Mbagala na Manzese. Mbona hata kodi zaviwanja na rent za nyumba zinatofautiana kulingana namaeneo?

Mheshimiwa Spika, ushauri uzingatiwe, Uongozi waWizara; Mheshimiwa Waziri, Naibu Mawaziri na Katibu Mkuu,waendelee kuchapa kazi kama wanavyofanya;tutawakumbuka, hongereni sana tuko nyuma yenu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. ABIA M. NYABAKARI: Mheshimiwa Spika, ilikuwezesha ufungaji wa mashine za kukoboa mpungawakulima wauze mchele badala ya mpunga na kukuzakipato chao; je, ni lini umeme utafikishwa Sakalilo?

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

124

Mheshimiwa Spika, Wananchi wa Mkoa wa Rukwawamekuwa wakitambuliwa na Serikali kama wakulima stadina wavuvi wa samaki. Pamoja na hayo yote, Serikaliinaonesha kutojali maendeleo yao. Sasa tunataka kujua nilini maendeleo ya umeme yataboreshwa Mkoa wa Rukwaukiacha Laela na Kasanga ambapo tuliahidiwa umeme waREA?

Mheshimiwa Spika, tunaomba sasa na sisi watu waRukwa mtuone tu binadamu na Watanzania wenzenu,tunaohitaji kuishi kwa kukifurahia Chama cha Mapinduzi naSerikali yake.

Mheshimiwa Spika, ni kwa nini katika Mkoa wa Rukwamaendeleo ya uwekaji umeme yanaonesha kutojali Mkoawetu na kutufanya tuendelee kuonekana kama sisi hatukoTanzania, wakati ukipita Mikoa mingine utaona kama kwelini Tanzania?

Mheshimiwa Spika, kuna tatizo gani katika Mkoa waRukwa ukilinganisha na Mkoa mpya wa Katavi ambao sasaunamelemeta kwa umeme hadi Vijiji vya Usevya vina umemeau katika Mkoa wa Rukwa hatuna wataalam wanaowezakusimamia umeme kama utaongezwa katika maeneomengine?

Mheshimiwa Spika, maendeleo ya Mkoa wa Rukwayanaonesha kuzorota kwa sababu ya Miji midogo kukosaumeme na hii inasababisha Serikali kuwa na ubinafsi kwawakubwa wenzao kupewa upendeleo wa pekee kufuatanana nafasi walizo nazo Serikalini.

Mheshimiwa Spika, katika jambo hili la kutojaliwanyonge litajionesha tu hata upande wa umeme wa REA,Mkoa wa Rukwa kuwa wa mwisho japokuwa tuna watumishimahiri TANESCO na wenye bidii na kazi na ujuzi pia.

Mheshimiwa Spika, jambo ninalosema hapa, naombakatika suala la umeme wa REA na sisi tupewe kipaumbele.Siyo hivyo tu, inasikitisha kuona Wananchi walio wengi Mkoa

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

125

wa Rukwa, Wilaya ya Kalambo Vijijini na Jimbo la Kwela hatavijiji vya jirani ya Mkoa – SBA Mjini na Wilaya Nkasi, hawanahuduma ya umeme. Mnajua kabisa umeme ni maendeleo,ajira, starehe, huduma, biashara, ni kinga ya uharibifu wamazingira na pia ni ustaarabu.

Mheshimiwa Spika, hivyo, kutowafikishia umemeWananchi wa Rukwa ni kuwadumaza kimaendeleo, nikuwafunga speed governor ya maendeleo yao.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Sumbawanga Vijijinikutokuwa na umeme hata kijiji kimoja wala Wilaya yenyeweni Wilaya ya muda mrefu, ina vyanzo vingi, makaa ya mawena vyanzo vingi vya Maporomoko ya mito na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, kuchelewa kufikisha umeme MjiMdogo wa Laela kushusha katika vijiji vya njiani katika Kataza Kaengesa, Mpanda Muungano, Sandulula, Mpui,Kalambanzite na Lusaka; je, ni lini sasa Wananchi wategemeekupata umeme huo na hata Ukanda wa Ziwa Rukwa?

Mheshimiwa Spika, umuhimu wa umeme katikamaeneo haya ni utayari wa watu, ujenzi wa nyumba bora,sekondari nane, vituo vya afya vinane na zahanati 40. Uchumikwa Wananchi, wauze mchele badala ya mpunga, wauzejuice na unga badala ya mahindi.

Mheshimiwa Spika, Viongozi au Mawaziri wazungukemaeneo yote ya Mkoa wa Rukwa, siyo kupendelea baadhiya Mikoa fulani ili kuona fursa zilizopo katika maeneo yote yanchi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, kwania ya maandishi, nichangie Bajeti ya Wizara ya Nishati naMadini. Nishati na hasa mafuta jamii ya petrol kwa uchumina usalama wa nchi ni kama damu kwenye mwili wabinadamu.

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

126

Mheshimiwa Spika, mchango wa kwanza ni hali yaongezeko la watu wanaotegemea au hata kufuatiliashughuli za tasnia ya madini ili kukidhi kiu hii na hasakupunguza malalamiko ya Wananchi. Nashauri Chuo chaMadini Dodoma kibadilishwe muundo wake na kisukwe upya.Ijengwe taasisi itakayosimama yenyewe badala ya mfumowa sasa inapoendeshwa kama Idara ya Wizara ya Madini.Chini ya muundo mpya, chuo kiajiri wakufunzi na walimuwa kutosha. Miundombinu iandaliwe kwa kupokeawanafunzi wengi kwa wakati mmoja. Yawepo mafunzo yamuda mrefu (miaka minne), muda wa kati na muda mfupi(majuma mawili - mtatu). Lengo hapa ni kuwa Chuokiwekwe katika hali ya kuwafundisha vijana na kwendakujiajiri katika Sekta ya Madini. Pia wale ambao tayari wapokatika shughuli kwa mtindo wa mafunzo mafupi, wafuatwehuko na kupewa ujuzi wa shughuli. Kupitia Chuo hiki, sikuzijazo, mikopo kwa wachimbaji wadogo wadogo itolewekwa kada ya watu ambao uwezo wao unafahamika.

Mheshimiwa Spika, mchango wa pili ni tasnia yamafuta jamii ya petrol, yaani down stream activities. Itoshekusema, Serikali haijaisimamia vizuri Sekta hii na mamboyanaonekana yanakwenda vizuri kwa sababu daima Munguyuko nasi, uendeshaji wa uagizaji wa mafuta kwa wingi unaupungufu. Chombo – PIC, muundo wa au uendeshaji wakesiyo sawa, narudia tena kuionya Serikali utendaji wa Chombohiki unaweza kupelekea kushitakiwa na kuibebesha nchiadhabu kubwa katika mamilioni ya Dola za Kimarekani.Rejea mawasilino ya matishio toka kwa wagavi kwenda PIC.

Nilitegemea baada ya kutoa tahadhari ya kwanzaJulai, 2012, Serikali ingejiangalia na kuweka mambo sawa.Hii ni pamoja na mipangilio isiyo sawa, ambayo ilipelekeavipindi fulani nchi kukaribia kukosa mafuta na ujanja wakubadili lay can unatoa faida kwa wagavi. Kitaalamu, binafsinasikitika wakati vyombo vinavyohusika, Serikali ikiwemoNchi, inaposhindwa kupata faida ya kushusha premium MR–LR, kama ilivyoahidiwa. Nashauri kuwa, Serikali ilisimamiehili, kinyume chake inaweza kuchukuliwa kuwa ni uzembeau makusudi.

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

127

Mheshimiwa Spika, upungufu mwingine katikausambazaji wa mafuta, Serikali inashindwa kuona kuwa vituosalama vya mafuta vimerundikana mijini tu na kwenye njiakuu. Wilaya za pembezoni na vijijini, mafuta yanauzwakwenye vibuyu, ndoo za plastic na viloba vya rambo. Udhibitiunaelekeza macho sehemu moja! Msingi wa utawala wamafuta kwa uchumi, usalama na ustawi wa nchi niavailability, quality & affordability of product with maximumsafety. Mafuta jamii ya petrol kwenye mfuko wa plastichakuna ubora na usalama. Hii haihitaji mshauri toka Canadaau Ujerumani. Tunapaswa kuwa na vituo kwa ngazi zotetatu; petrol service station, petrol station na kebsite. Kampunizote za mafuta zidhibitiwe kwa kuwa na vituo mijini mpakavijijini na asiyekubali aelezwe, huo ndiyo udhibiti. Kanuni yakupanga bei yaweza tunzwa kutoa motisha.

Mheshimiwa Spika, hoja ya tatu ni Kampuni ya Mafutaya Kitaifa. Faida kubwa ya Taifa letu kuwa na kampuni yaaina hii ni kutuondoa hofu na mashaka, lakini pia kutoa fursaya kujifunza. Ipo hali ya kutokujua miongoni mwa jamiiwakiwemo wasimamiaji wa sekta, kwa sababu moja tu kuwana ujuzi usiokuwa na uzoefu wa kutenda. Matokeo yake nihofu na mtu kuishia kuhesabu faida ya pale ambapohukuwekeza mtaji. Kampuni ya Kitaifa itawezesha mkonowa Serikali kushiriki katika shughuli na kuwa na uhalisia wamambo yanavyokwenda, yaani kuondoa hofu na mashaka.Inapotokea fursa na faida kupindukia, pato hilo linakwendaSerikalini. Sielewi king‘ang‘anizi cha kuanzisha kampuni hiikinatokea wapi?

Tunayo faida ya nchi jirani ambazo zitakuwa naamani ya moyo kuendesha shughuli na kampuni ya Serikali.Tunazo Halmashauri za Wilaya na Taasisi za Serikali ambazozitageuka wateja wa kwanza. Kampuni ya Kitaifa itakuwatayari kufungua kituo kila pembe ya nchi hii kwani ni ya Kitaifa,kampuni binafsi hata ikilazimishwa itakuwa inaonewa tu.Nashauri hoja itafutiwe muda na kuongelewa kwa kina ilitupeane uzoefu wa wenzetu.

Mheshimiwa Spika, hoja ya nne ni umeme. Kigezo

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

128

cha kupima maendeleo ya Taifa lolote ni pamoja na matumiziya umeme. Hata hivyo, kipimo hicho kitakuwa na upungufuiwapo umeme huo utakuwa unaishia na kutumika kwa wingikatika migodi na viwanda.

Mheshimiwa Spika, nashauri kuendeleza miradi yakupeleka umeme vijijini kwa wingi, kwa faida zilizo dhahiri.Ipo mitambo midogo ya kukausha nafaka (drier), ambapomaharagwe yaliyovunwa saa nne asubuhi baada ya saa tatuyamekaushwa na tayari yanakwenda sokoni. Tunapotezamazao mengi katika hatua hii ya uzalishaji. Ufugaji wa samakikatika mabwawa unahitaji mitambo ya kuongeza oxygen.Mitambo hii inahitaji umeme na pale inapotumika tija nimara sita. Hii ni kwa kutaja mifano michache inayowezakulipandisha hadhi Taifa letu, kwa kufanya vizuri kile kilichokatika uwezo wetu.

Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu huo, hapajuu hoja yangu ni kuwa, jitihada zifanyike kukamilisha MradiKabambe II katika kipindi cha mwaka mmoja. Hoja ya tozoya shilingi 100 katika kila lita ya mafuta; diesel na petrol, upoumuhimu wa kuweka kiwango katika simu za kiganjani ilitupate angalau shilingi bilioni 150 kwa mwaka.

Mheshimiwa Spika, muhimu kwa Watanzania kamaTaifa ni kuelewa kuwa, misaada tunayopewa, Serikalizinazotupatia mikopo hiyo, hutoza kodi Wananchi wake.Uzuri wa Miradi ya REA ni kuwa tozo zinaweza kupewa mudakikomo, tuweke tozo miaka miwili au mitatu tukusanye trilionimbili, tujenge miundombinu mambo yaishe. Naiona taswiraya Tanzania mpya pale ambapo shule zote zinapokuwazimepata umeme ukiambatana na mtandao wa simu.

Mheshimiwa Spika, hoja ya tano ni rasilimali gasi asiliana mafuta jamii ya petrol yachimbwayo. Historia ya shughulihii, yenye gharama kubwa, inahusisha imani kwa walewaliomwacha Mungu wakati unapotafuta rasilimali yenyethamani kubwa kama hii na hasa unapotumia gharamakubwa hapana budi kuomba.

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

129

Mheshimiwa Spika, kama nilivyowahi kusema katikaBunge lako Tukufu, imani yangu inanituma kuwa, ipo sikumimi nikiwa Mbunge bado na Rais wa Nchi akiwaMheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, tutasherehekea Bungeniuvumbuzi wa mafuta mengi tu. Imani yangu inanituma piakuwa, waasisi wa tasnia ya utafutaji wa mafuta kamahawataalikwa katika jukwaa la Spika na kutambuliwa, juhudizetu zitachelewa zaidi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na maelezo mengi hojahapa ni kulenga kwenda pamoja kama Taifa hasatunapofanikiwa kuhusisha rasilimali iliyotumika hapo mwanzona kuleta mafanikio kwa ajili ya kuazima uzoefu, lakini piakuwaenzi. Tunapofikiria kuanzisha Kampuni au Idara ya TPDCya kwenda kuchimba mafuta au gesi ni busara wastaafuwenye nguvu bado wakarudi na kufanya kazi kwa mkataba.

Inasikitisha mfanyakazi aliyeshiriki zoezi gumu la hatuaza mwanzo, asishiriki katika hatua za kuona matunda. Kundihili nashauri lihamasishwe kuanzisha kampuni na vijana tokavyuoni katika kushiriki shughuli nyingine zitokanazo na tasniaza gasi asilia. Kundi hili ambalo nategemea kuona Serikaliikilitumia kuelimisha jamii juu ya gasi asilia na mafuta badalaya makundi ya waviziaji wanaojitokeza kwa sasa.

Mheshimiwa Spika, tusingoje hao wastaafu waombetuwafuate. Kimsingi, Serikali iwafuate. Katika mazingiraambapo wahamasishaji wanadai Wananchi waruhusiwekuchota gasi kwa ndoo au basi walipwe dola 2,000 kwa kilajuma, ni nafuu kuangalia matumizi ya kundi hili ambalokufikisha miaka 60 kumewatoa ofisini.

Mheshimiwa Spika, gasi asilia Mikoa ya Lindi naMtwara, Gazeti la Raia Mwema, toleo la tarehe 16 Januari,2013 lilikuwa na makala yangu juu ya rasilimali hii. Makalahii imesambazwa kwa watu wengi, ikiwemo WatendajiWaandamizi wa Serikali. Gasi asilia ina faida kwa Taifa namahali inapochimbwa. Huo ndiyo mchango wangu.

Mheshimiwa Spika, Rasimu ya Sera ya Gasi Asilia

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

130

tuliyopewa ni ya downstream, lakini wawekezaji wakubwawanaotia hofu inaanzia upstream. Pamoja na hali hiyo,nashauri Sera itamke kwenye specific objective yafuatayo:-

- Pato la gasi asil ia l itawekezwa kwenyeshughuli za asili za Watanzania ili wazalishe kwa tija kubwana wasitegemee gasi asilia (wasibweteke); na

- Pato la gasi asilia litawekezwa kwenye elimuya Wananchi ili kuwapa ujuzi wa kujitegemea.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa Spika,kuna malalamiko kutoka kwa Wananchi ambaowanazungukwa na migodi ya madini. Wananchi haohawanufaiki na migodi hiyo. Wawekezaji wengi ambaowamezunguka migodi, wamekuwa hawatimizi ahadi zaoambazo wamekuwa wakizitoa kwa Wananchi. Kwa mfano,kuwajengea Wananchi shule, zahanati na visima vya majisafi; ahadi hizi wamekuwa hawazitimizi kwa wakatimwafaka. Wamekuwa wakijinufaisha wao wenyewe(wawekezaji). Je, ni lini Serikali itahakikisha inawadhibitiwawekezaji waliowekeza kwenye migodi ya Madini ilikuhakikisha wanatekeleza ahadi za maendeleo walizozitoakwa Wananchi?

Mheshimiwa Spika, hawa wawekezaji katika migodi;kwa mfano, Mgodi wa Geita (Geita Gold Mine); katikati yahuu mgodi kuna uwanja mkubwa wa ndege, ambao ndegezinaruka na kutua usiku na mchana kwa ajili ya ubebaji wadhahabu kupeleka nje ya nchi. Je, Serikali ina udhibiti ganikuhakikisha dhahabu haitoroshwi kwenda nje ya nchi?

Je, Serikali ina udhibiti gani kuhakikisha kila dhahabuinayotoka pale kwenye Mgodi wa Geita inalipiwa kodi?

Kumekuwa na tabia ya kufichwa kwa mikatabamikubwa mikubwa inayofanywa baina ya Serikali nawawekezaji wakubwa wakubwa na kuwafanya Wananchi

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

131

wawe na maswali ya kujiuliza, kwa nini mikataba hiyo ifichwekama haina matatizo. Je, ni lini Serikali itakuwa inawekamikataba wazi ili kuwaondolea wasiwasi Wananchi?

Mheshimiwa Spika, gesi asilia inaleta matatizo katikaMkoa ilikogunduliwa gesi hiyo. Mkoa huo umekuwa haunaamani na kabla gesi hii haijachimbwa, Wananchi wa Mkoahuo ni lazima wapatiwe elimu ya kutosha na Serikali. VilevileSerikali iwanufaishe Wananchi wa Mkoa huo kabla gesihaijasafirishwa kwenda Mikoa mingine.

Mheshimiwa Spika, kwenye Mkoa huo pajengwekiwanda cha kusafishia gesi ili kutoa ajira kwa Wananchi waMkoa huo na kuepusha migogoro baina ya Serikali naWananchi.

Mheshimiwa Spika, ni takribani miaka 52 tangu tupateUhuru, lakini cha kushangaza vijiji vingi havijapata umemena vilivyokuwa na umeme, umeme wake ni wa kusuasua.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali itenge bajeti yakutosha ili Wananchi wa vijijini wapate kunufaika na umeme.

MHE. PROF. ANNA K. TIBAIJUKA: Mheshimiwa Spika,ninampongeza Mheshimiwa Waziri Prof. Muhongo, Manaibuwake na Katibu Mkuu, kwa kazi yao nzuri, pamoja na ugumuwake.

Mheshimiwa Spika, teknolojia ya kisasa katika nyanjazote inahitaji nishati ya aina moja au nyingine. Kwa hiyo,umuhimu wa sekta hii katika uchumi wetu haina mjadala.Tatizo linakuwa ufinyu wa bajeti. Ninashauri tutambuekwamba, Sekta ya Nishati tukielekeza ndani yake italipayenyewe. Tutazalisha zaidi.

Wilaya ya Muleba ina wakulima, wafugaji na wavuvi.Wakiwa na umeme katika vijiji na nyumba, watawezakuzalisha zaidi; ni jambo linalohitaji kuangaliwa na REA kwaumakini. Visiwa vya Mazinga na Ikuza ndiyo wazalishaji wasamaki, lakini wengi huharibika au kulazimika kukaushwa na

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

132

kupungua thamani, kwa sababu hakuna umeme. REAwafanye jitihada maalum kupeleka umeme katika Visiwahivi. Aidha, REA watambue Kata za Muleba ambazozimeomba kwa muda mrefu lakini hadi leo hawajapataumeme. TANESCO imekuwa ikitoa vikwazo mbalimbali,ninaomba sasa kati ya TANESCO na REA, suala hili na ahadiza Mheshimiwa Rais zitekelezwe.

Mheshimiwa Spika, kero kubwa iliyoenea katikamaeneo ya madini na migodi ni Wananchi kutopewa fidiastahiki. Ninaomba Wizara ya Madini ishirikiane na Wizara yaArdhi, kutekeleza sheria ambazo ziko wazi katika suala hili.Anayepewa Mining Rights, huwezi kuanza kuchimba kablahujafidia na kuwahamisha (reseltle), wakazi wa paleinapohitajika. Haikubaliki kwamba, sheria hii inavunjwa.Mheshimiwa Waziri ana mkakati gani juu ya tatizo hili katikaMikoa ya Madini?

Mheshimiwa Spika, tunampongeza MheshimiwaWaziri kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo, lakini kodiiliyowekwa kwenye PML ni kubwa na wengi hawamudu.Mheshimiwa Waziri anafuatilia madeni ili STAMICO iwezekuwasaidia vyema zaidi.

Mheshimiwa Spika, ninapongeza na kuunga mkonohoja hii.

MHE. MATHIAS M. CHIKAWE: Mheshimiwa Spika,kwanza kabisa, naunga mkono hoja ya Waziri wa Nishati naMadini.

Mheshimiwa Spika, naomba kuzungumzia hoja mojatu; umeme katika Vijiji vya Nachingwea. Mwaka janaMheshimiwa Waziri alitoa orodha ya vij i j i ambavyovingepatiwa umeme. Orodha hiyo haina tofauti na orodhaya mwaka huu; yaani ni kusema kuwa, kwa mwaka janahakuna hata kijiji kimoja kilichopatiwa umeme.

Mheshimiwa Spika, naomba mwaka huu umeme huoupatikane kama ilivyopangwa. Aidha, vijiji viongezwe ili

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

133

angalu vijiji vile vikubwa vyenye miradi ya uzalishaji vipatiweumeme. Vijiji vya Mnero, Lionja na Marambo, viongezwekatika orodha hii. Umeme uliopo unapita karibu sana navijiji hivi. Gharama haitakuwa kubwa sana.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kuzungumziamgogoro mkubwa uliopo katika Kijiji cha Ikungu na NtakaHill, baina ya wachimbaji wadogo wadogo wenyewe kwawenyewe na wachimbaji wakubwa na wachimbaji wadogowadogo. Mgogoro huu ni wa siku nyingi na Maafisa waMadini wa Kanda wameshindwa kuutatua kwa sababuwenyewe wana maslahi katika sehemu hizo. Aidha, kilawakati wachimbaji wadogo wanapogundua madini,wakienda kuomba leseni wanaambiwa kuwa sehemu hiyotayari imeshachukuliwa. Mara nyingi hii siyo kweli bali walemaafisa wakishapata taarifa hizo, huwa wanawapa lesenindugu zao na hii huzalisha migogoro ambayo haina sababuza msingi. Waziri achukue hatua dhidi ya maafisa hawawasiotimiza wajibu wao.

MHE. JUMA S. NKAMIA: Mheshimiwa Spika, naombaSerikali inisaidie nijue ni lini Wilaya mpya ya Chemba MkoaniDodoma itapata umeme?

Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka jana,inayomalizika Juni mwaka huu, Serikali ilitenga fedha kwaajili ya kupeleka umeme, tathmini tayari imeshafanyikakilichobaki sasa ni kupeleka nguzo tu.

Mheshimiwa Spika, pili, Kijiji cha Tandala chenye idadikubwa ya watu, nyumba nzuri na barabara ya TANROADkitapewa umeme lini? Umeme upo kilomita nne tu jamani,jitahidini basi wapate umeme.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

MHE. AMINA ABDALLAH AMOUR: Mheshimiwa Spika,umeme ni nyenzo muhimu katika maisha ya binadamu, lakinila kusikitisha baada ya miaka 50 ya Uhuru, bado upatikanajiwa umeme ni mdogo sana hasa vij i j ini. Kwa kuwa

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

134

Mheshimiwa Waziri amesema kwenye Hotuba yake kwamba,atasambaza umeme vijijini na mjini, basi tunataka tuone kwavitendo na siyo kwa maneno.

Mheshimiwa Spika, usambazaji wa umeme hapanchini unachukua muda mrefu kutokana na sababu nyingikama vile gharama za usambazaji umeme kuwa kubwa,ughali wa nguzo za umeme, pamoja na watendaji wabovuwa Wizara hii. Naiomba Serikali ilione hili na ilipatie ufumbuzi.

Mheshimiwa Spika, Watanzania walifurahi sana kwaupatikanaji wa gasi Mkoani Mtwara na Lindi. Furaha ileimekwishatoweka baada ya kuona jambo zuri kama hilolimeleta chuki, uhasama, fujo na uchonganishi katika nchiyetu. Baadhi ya watu ambao hawaitakii mema nchi yetu,wameanza kupotosha Wananchi na kusababisha mauwajina uharibifu wa mali.

Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Rais,kwa Hotuba yake aliyosema wahusika wakamatwe bila kujalini nani. Naamini kuwa, ujumbe umefika na wahusika wakusaka wahalifu wafanye kazi hiyo mara moja na ni lazimawatuhumiwa wote wapatikane na wafikishwe mahakamani.

Mheshimiwa Spika, nataka kuiuliza Serikali; kwa kuwafujo hizi ziliwahi kutokea mwaka jana; je, hatua ganizilichukuliwa kwa wale waliofanya fujo na kusababisha vifona uharibifu mali nyingi zikiwemo za Wabunge?

MHE. MTUTURA A. MTUTURA: Mheshimiwa Spika,naomba majibu kutoka kwa Mheshimiwa Waziri, kwamaswali yafuatayo:-

(i) Tunduru itapata umeme wa uhakika wa Gridiya Taifa kutokea wapi; Namtumbo au Masasi?

(ii) Umeme huo utafikishwa Tunduru lini?

(iii) Hivi mnajua kwamba Wananchi wa Tundurutumechoka kuona umeme ukisambazwa kwenye vijiji vya

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

135

Wilaya za wenzetu huku sisi tukiwa tunaendelea kutumiavibatari?

(iv) Mnafahamu kuwa binadamu huwa anafikiakiwango cha mwisho cha kuvumilia na kusubiri?

Mheshimiwa Spika, Bajeti ijayo tunataka majibu kwavitendo na si maneno tena.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

MHE. PROF. PETER M. MSOLLA: Mheshimiwa Spika,awali ya yote, napenda kumpongeza Waziri, Naibu Mawazirina Katibu Mkuu, kwa kuwasilisha Hotuba nzuri Bungeni nayenye kutoa matumaini makubwa kwa maendeleo ya nchiiwapo yaliyomo yatatekelezwa.

Mheshimiwa Spika, aidha, napenda kuwapongezazaidi kwa kutoa vielelezo vingi vya utekelezaji wa upelekajiumeme vijijini na maeneo mbalimbali ya utafutaji nauchimbaji mafuta au gesi asilia na madini sawia.

Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hizo,nasikitishwa na ucheleweshaji wa upelekaji umeme vijijini.Kwa mfano, umeme ulivutwa kutoka Tagamenta – Iringahadi Kidabaga Wilayani Kilolo tangu mwaka 2009 naulizinduliwa na Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 27 Oktoba,2009. Inasikitisha kuona vijiji mbalimbali kama vile Kilolokibaoni, Luganga, Ilamba na Shule za Sekondari zaUdzungwa, Maria – Consolata na Dabaga, hazijafikishiwaumeme.

Mheshimiwa Spika, aidha, mwaka 2011 umemeulivutwa kutoka Ilula hadi Ruaha – Mbuyuni, Wilayani Kilolo.Inasikitisha kuona kwamba, umeme huo haujashushwakatika Shule ya Sekondari ya Lukosi na Vijiji vya Kidika naMsosa; hivyo, kupunguza kasi ya maendeleo katika Wilaya

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

136

ya Kilolo. Je, ni lini hasa umeme sasa utafikishwa katikamaeneo hayo?

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Spika, kwaupande wa Miradi ya Umeme katika Jiji la Dar es Salaam,ikiwa ni sehemu ya mapitio ya utekelezaji kwa mwaka 2012/2013, Wizara ya Nishati na Madini, inipatie majibu juu ya hatuailizochukua kupitia maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani yatarehe 27 Julai, 2012 na michango yangu ya maandishi tarehe27 Julai na 28 Julai, 2012. Pia nipewe majibu juu ya hatuaambazo Wizara ya Nishati na Madini kupitia kabrasha lenyebarua za muda mrefu za Wananchi kwenda kwa TANESCOza matatizo ya umeme katika maeneo yao, ambayonilikabidhi kwa Wizara wakati ilipoitisha mkutano na ziarana Viongozi wa Jiji la Dar es Salaam kuhusu Miradi ya Umeme.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Nishati na Madiniitambue kuwa, kwa upande wa Jimbo la Ubungo, yapomaeneo ambayo nguzo zinaanza kuwekwa. Hata hivyo,kumekuwa na uhaba wa vifaa mbalimbali kama nyaya navifaa vingine. Hii ni kwa sababu mfumo wa ununuzi wa vifaaambao unaratibiwa na TANESCO Makao Makuu, unahusishakupeleka katika Mikoa na kwenye Miradi, vifaa vichachebadala ya kupeleka vifaa vyote vinavyohitajika (CompletePackage). Katika kuhakikisha kwamba, vifaa vinapatikana,Wizara iweke mkazo katika miradi ya maeneo yafuatayoambayo ilipangiwa fedha miaka ya nyuma, lakini utekelezajiwake haujakamilika mpaka hivi sasa: Malamba mawili,Msingwa, Msikiti kwa Mtoro, Msakuzi Loperanya kwa Bibi, kwaMasista Hondogo, Kibwegere Mloganzila, Goba Kulangwana Goba Matosa Darajani.

Mheshimiwa Spika, aidha, katika Mwaka wa Fedha2013/2014, Wizara tofauti na miaka iliyotangulia, itekeleze kwawakati miradi ya kusambaza umeme maeneo ya pembezoni,ikiwemo katika maeneo ya Msumi. Hatua kama hizozichukuliwe kuhusu maeneo ya Miradi ya Maji inayohitajiumeme; mfano, katika Kata ya King’ongo.

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

137

Mheshimiwa Spika, Wizara itoe maelezo juu yasababu za kutokamilisha mchakato wa kulipa fidia kwaWananchi walio eneo la karibu ya mitambo ya umeme,maeneo ya Ubungo, Kibo na Kisiwani, pamoja na bajetikutengwa katika mwaka 2012/2013. Aidha, Wizara naTANESCO, wamshirikishe Mbunge katika makubalianoyanayofikiwa na Manispaa ya Kinondoni kuhusu tathmini yafidia kwa Wananchi wa maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, naomba kupata pia majibukuhusu hatua ambazo Wizara ya Nishati na Madiniimechukua juu ya mapendekezo nil iyotoa kuhusumiundombinu ya usambazaji na matumizi ya gesi asilia katikaJiji la Dar es Salaam. Aidha, Wizara ishirikiane na Wakala waVipimo (WMA), katika kuhakikisha Wananchi wanapatathamani halisi ya fedha (value for money) ya gesi ya mitungina EWURA iongeze ufanisi katika udhibiti wa fedha.

Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo yaliyomokatika Hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini, katikamajumuisho, ni muhimu Waziri akatoa maelezo ya ziadakuhusu masuala yafuatayo:-

Uchimbaji wa madini ya urani: Sababu za Wazirikutoa leseni ya Kampuni ya Mantra kwa ajili ya uchimbajiwa madini hayo katika eneo la Mkuju River, Namtumbo, bilakuzingatia maoni tuliyotoa mwaka 2011/2012 na bila kujalikwamba hatua hiyo ingeweza kutumika kuibana Kampunihiyo kulipa kodi inayodaiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA).Aidha, Wizara ipitie Kanuni (Regulation), ambayo ilitungwana Wizara ya Nishati na Madini mwaka 2010 na Kanuni zamwaka 2011, kubaini mgongano wa kimajukumu baina yaWizara na chombo chenye dhamana ya masuala ya mionziya kiatomiki hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, Wizara izingatie kuwa chombo hikindicho kimepewa mamlaka pia na vyombo vya kimataifa,kuhakikisha usalama katika uchimbaji na usafirishaji wamadini hayo na pia kuepusha madini hayo kuuzwa kwa nchizenye mipango ya kuandaa silaha za nyuklia.

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

138

Mheshimiwa Spika, kuhusu Tanzanite; Wizara yaNishati na Madini itoe maelezo ya sababu za kwenda kinyumena ahadi za Mheshimiwa Rais Kikwete za mwaka 2005 na2010 katika eneo la Mererani, ambapo aliahidi leseni yaKampuni ya AFGEM/Tanzanite One, ikifika ukomo eneo hilolingetolewa kwa wachimbaji wadogo ama umiliki wawazawa kwa ujumla. Uamuzi wa Wizara ya Nishati na Madinikupitia STAMICO kuingia ubia na kuwa na hisa asilimia 50kwa 50, hauendani na ahadi zilizotolewa na Rais. Aidha,Wizara na STAMICO kwa pamoja hawakuzingatia baadhiya masuala muhimu kwa mujibu wa nyaraka za makubalianoyaliyofikiwa mpaka hivi sasa.

Mheshimiwa Spika, Wizara iweke wazi makubalianohayo yaliyofikiwa na hatua zinazochukuliwa kurekebishakasoro zilizopo.

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Madini (MRI); Wizara yaNishati na Madini ieleze hatua ilizochukua kutekelezamapendekezo tuliyotoa mwaka 2011 kuhusu Chuo husika.Mwaka 2011 tulipendekeza kuanzishwe Chuo Kikuu chaMafuta na Gesi Mtwara, Serikali ikakubali. Hata hivyo, sualahilo halikuwa kwenye utekelezaji mwaka 2012/2013 na halikokwenye Bajeti ya 2013/2014. Hivyo, kwa kuanzia katika mwaka2013/2014; Chuo cha Madini kianzishe Kampasi (Campus)Mtwara.

Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara iweke wazi Ripotiya Kamati iliyoundwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri yaChuo cha Madini (MRI), Profesa Mruma, kufuatia malalamikoya Wananchuo. Pia Waziri wa Nishati na Madini aeleze hatuazilizochukuliwa kufuatia barua iliyoandikwa kwake nawananchuo mwanzoni mwa mwaka 2013, yenye madai juuya matumizi mabaya ya fedha na madaraka yenye atharikwa Wananchuo na Umma kwa ujumla.

MHE. ABDALLA HAJI ALI: Mheshimiwa Spika, awali yayote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, muweza wamambo yote. Aidha, nakupongeza Mheshimiwa Spika, kwauongozi wako wa busara na hekima kubwa juu ya Bungelako Tukufu.

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

139

Mheshimiwa Spika, napenda kwa ufupi sana,nizungumzie mambo makubwa yanayoikabili nchi yetu kwasasa, nalo ni kuhusu vurugu za Mtwara zinazohusishwa nagesi asilia iliyogunduliwa huko Mtwara.

Mheshimiwa Spika, jambo hili Serikali isilichukulie urahisihata kidogo, kwani tayari limekwisha gharimu maisha yawatu na mali zao.

Mheshimiwa Spika, mambo mawili napenda kuishauriSerikali, kama yatafanywa huenda yataisaidia Serikali nakuondokana na vurugu za Mtwara na mfano wa hizo katikasehemu nyingine ambazo zinaweza kutokea.

Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza ni kwamba,watu waelimishwe juu ya rasilimali za nchi kwamba, popotepatokeapo maliasili nchini ni ya Watanzania wote. Kinyumena ufahamu wa watu wengine kwamba, kilichoonekanaMtwara ni cha Mtwara pekee. Elimu hii watu hawana nandiyo wengi wakadhani kwamba, wanaporwa rasilimali yaona Serikali ili ikatumike sehemu nyingine. Naishauri Serikali itoeelimu kiasi cha kutosha hadi watu waondokane na fikramgando kwamba kitokeacho kwao ni cha kwao tu.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kwamba,naishauri Serikali ikae na Wananchi wa Mtwara, iwasikilizewanataka nini juu ya suala zima la rasilimali ya gesi. Serikaliifahamu kwamba, suala la vurugu za Mtwara kwa kiasi fulanilinapigiwa debe kisiasa, lakini kwa nia njema ya Serikali juuya Wananchi wake, nashauri kwamba, Wananchi wa Mtwarawasipuuzwe. Vyombo mbalimbali vitumiwe kufanyamazungumzo na Wananchi hawa na ili nchi itulie, basiWananchi washirikishwe katika mazungumzo wasemewanataka nini juu ya rasilimali hii na Serikali isiwe kaidi katikahili na iwape matumaini mazuri kiasi kwamba tuondokanena balaa ya fujo ambayo haina tija yoyote katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali kwa maranyingine tena, ijaribu kutumia mbinu shirikishi kwa maslahiya nchi.

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

140

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, kwakifupi kabisa, napenda kuchangia maeneo makuu matatu:-

Tathmini zinazofanywa kwa ajili ya Wananchi kupishashughuli za mgodi, zoezi hili kwa sasa limegubikwa na rushwana dhuluma kubwa sana. Wananchi wanafanyiwa mambokama vile siyo watanzania. Zamani tathmini ilikuwa ikifanywabaina ya Mgodi na Wananchi, ambapo Barrick walikuwawakitoa fidia ya dola 25,000 kwa heka na hii ilikuwa pamojana fidia nyingine kadiri itakavyompendeza Barrick. Sasa hiviUongozi wa Wilaya pamoja na Mkoa kwa maana ya TaskForce ambapo huenda kwenye tasnia bila hata taarifa,kuweka alama na wakati mwingine huvunja nyumba na malizingine. Vilevile hudai walipwe fedha kati ya shilingi 100,000na 300,000 au wengine huombwa watoe sehemu ya maeneoyao.

Mheshimiwa Spika, ombi la Wananchi wa Nyamongona hasa Kijiji cha Nyakunguru ni kufanyiwa tathmini na Mgodi.Kwa maana Serikali isitwae ardhi kwa niaba ya Mgodi. Hiisiyo haki kwani hutia mwanya wa ukandamizaji; iwenegotiation kati ya mthaminiwa na mgodi. Pia kwa mujibuwa Mining Act, inatakikana Mgodi uwape makazi mbadalawale wote wanaohamishwa sambamba na kuwapa fedha;hivyo, naomba Wizara yako pamoja na Wizara ya Ardhikustopisha zoezi la Task Force mara moja, kwani sasa hali nitete.

Mheshimiwa Spika, pili ni kuhusu wachimbaji wadogowadogo. Mwaka 2011 yalipotokea mauaji ya wananchiwatano, Mawaziri wa Nishati, Mahusiano na Uwekezaji,walienda kuongea na Wananchi na kuwaahidi kuwa,watatenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogowadogo, ikiwa ni moja ya utatuzi wa Wananchi kwendakuokota mawe kwenye vifusi, kwani kabla ya uwekezaji naubinafsishaji, Wananchi wale walitegemea mgodi ule kamachanzo muhimu cha fedha, hamna shughuli za ufugaji walakilimo kule. Serikali ilituahidi kutenga maeneo, kutoa elimupamoja na vifaa na mtaji kwa Wananchi, vilevile Mgodi waBarrick walikuwa tayari kuwapa na kuwezesha artsan miners,

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

141

lakini Barrick wapo tayari na wanasema Serikali ndiyowanachelewesha.

Mheshimiwa Spika, vilevile tulishauri juu ya kuwekwamaeneo muhimu kwa ajili ya kumwaga vifusi ili Wananchiwaweze kwenda kuokota left-over. Vilevile vifusi na kokotovingetumika katika kujenga nyumba za kudumu au kujazakwenye barabara. Tunaomba sana haya yazingatiwe.

Mheshimiwa Spika, mwisho ni juu ya Askari wa Jeshila Polisi kutumika kulinda Mgodi. Hili ni jambo lisilokubalikana mwaka jana aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani yaNchi alisema, kuanzia mwaka ule polisi hawaruhusiwi kulindaMgodi. Hadi leo polisi bado wapo na wameendelea kuuwaraia. Wao ndiyo wachonga deal, wakikosa wao wanafukuzaWananchi kwenye vifusi na hata kuwapiga risasi. Serikali piaisiruhusu Mgodi kufanya kazi wakati bado Wananchi wapo,hii siyo halali na hupelekea athari kubwa.

MHE. NIMROD E. MKONO: Mheshimiwa Spika,Wananchi waishio Buhemba wanaishi kwa tabu sana.Wawekezaji mbalimbali wamekuwa wakija Buhembakuchimba dhahabu tangu enzi za Ukoloni hadi enzi zaMEREMETA. Wawekezaji hao wamepora mali zote pale nakuacha Wananchi bila barabara, shule, zahanati, maji nakadhalika.

La aibu kabisa, hata baada ya Waziri Mstaafu kutumaMawaziri watatu; Mheshimiwa Wasira, Mheshimiwa IbrahimMsabaha na Mheshimiwa Profesa Mwandyosa, kuona halimbaya ya Butiama, Serikali imeitelekeza Buhemba. Hivi sasaBuhemba is an environmental disaster, a national disaster.Dhahabu yote iliyochimbwa hapa hakuna fedha zozotezilizolipwa kwa kuboresha huduma za jamii. Badala yake,majitaka yaliyokuwa yapo kwenye mashimo ya kuosheamawe kwa kutumia cynide yameachwa ovyo na mvuazinaponyesha husambaza uchafu wote kwenye vyanzo vyotevya maji wanayokunywa Wakazi wa Buhemba. Cynide nisumu, Serikali imewaacha Wananchi wanywe maji hayo.

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

142

Ng’ombe na mbuzi wanakufa, Wananchi wanaishi kwa hofuna Serikali imekaa kimya.

Mheshimiwa Spika, niliomba Serikali ilete STAMICOkurithi MEREMETA. STAMICO wamefika bila kuwa na mtaji wakutosha. Wametegemea wabia wenzao ambao naambiwawao pia hawataki kuwekeza katika uboreshaji wa mazingira.Mheshimiwa Profesa Mhongo, amesikika akiwaambiawapiga kura wangu kwamba, hatafika Buhemba kamwe.Mimi pia naambiwa sina haki ya kuzungumza humu Bungenimaana niko conflicted. Conflicted eti kwa kuwa nimekuwanikililia Serikali ilete STAMICO, Chombo cha Serikali kiwasaidieWananchi wangu wapate huduma bora Buhemba. Mimi sinabiashara yoyote ninayofanya Buhemba, badala yakenaombaomba marafiki na jamii watusaidie ujenzi wahuduma mbalimbali kama vile shule, zahanati, barabara,maji na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, Wananchi wa Butiama hawaishikama Watanzania wenzao, Wananchi hawa hawanamaisha bora na hawako huru. Juzi Wizara ya Nishati naMadini imekwenda Buhemba na kutoa amri ya kuwafukuzawachimbaji wadogo wadogo, sasa kuna vurugu kubwa.Hakuna usalama tena Buhemba. Nataka kujua ni liniMheshimiwa Waziri Mkuu au Mheshimiwa Rais ikiwezekana,watafika Buhemba na kutuliza hali tete iliyopo Buhemba?

Mheshimiwa Spika, bila kupata kauli ya Serikali kuhusuhali hii, sitaunga mkono hoja hii.

MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA: Mheshimiwa Spika,maeneo mengi nchini yaliyopatikana na madini, badala yakuwa na furaha imekuwa ni kilio na kusaga meno. Mfanomdogo ni katika Mkoa wa Singida, maeneo ya Mang’onyi,Sumbaru, Londoni na kadhalika; kumekuwa na kilio nakusaga meno baada ya maeneo hayo kugundulika kuwayana dhahabu.

Kampuni ya Shanta Mining i l ipewa uhalali wakuchimba dhahabu baada ya wachimbaji wadogo wadogo

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

143

kufukuzwa na Wananchi wengi kunyang’anywa mashambana makazi yao ili kupisha mwekezaji huyu. Mpaka leo kunakilio na watu bado wanalalamikia fidia zao. Nilitaka Serikaliiangalie umuhimu wa kuyainua kimaisha maeneo yenyerasilimali hizi za madini kwa kuwapa vipaumbele vya hudumabora za kijamii kama shule, hospitali, barabara, maji nakadhalika ili nao wafaidike na ambavyo Mwenyezi Munguamewajalia.

Mheshimiwa Spika, suala la wachimbaji wadogowadogo limekuwa ni kero nchi nzima hasa kwa kutokupewauwezo na maeneo yanayoeleweka ili nao wafaidike na malizilizopo kwenye maeneo yao. Wachimbaji wadogo wadogowamekuwa wakinyanyaswa wa wawekezaji wakubwa kanakwamba wao hawana haki ya kunufaika na mali na madiniyaliyopo. Serikali kama ilivyokwishaanza kuonesha nia yakuwajali, basi isiachie hapa ila mkazo mkubwa uwepokuwasaidia hawa Watanzania ambao wanatakiwakunufaika na mali zilizopo nchini.

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Singida Kaskazini(Singida), katika Kijiji cha Khanoda, lilipata bahati yakuwekewa nguzo za umeme katika Kijiji hicho tangu mwaka2002; lakini kwa masikitiko makubwa, mpaka sasa hakunatransformer iliyowekwa na mpaka ninapoandika mchangohuu, nguzo mbili zimeshaanguka! Hii ni hasara kubwa sana,kwa sababu nguzo hizi ni ghali na kabla ya kuanza kufanyakazi yake, tayari zimeshaanguka. Je, Serikali itakamilisha linikufunga transformer katika Kijij i hiki na kuwapelekeaWananchi hawa umeme? Suala hili ni la muda mrefu sanana limeshaongelewa sana Wizarani, naitaka Serikali inipemajibu kwa hilo.

Mheshimiwa Spika, ushauri kwa Serikali; ifike mahalisasa nchi yetu itumie vizuri rasilimali za madini, mafuta nagasi asilia katika kuwanufaisha Wananchi wa Tanzaniaipasavyo. Ni aibu kwa nchi hii kuwa maskini na ombaombakwa nchi za wenzetu ilihali tuna mali za kutosha. Lazima sasatuepushe vita kwa kuingia mikataba isiyo na tija kwa nchibali kwa wachache wenye roho ya ubinafsi hawatufai katika

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

144

nchi yetu ni wasaliti. Tujifunze toka Afrika Kusini, nchi ambayoinaongoza kwa kutoa dhahabu, i l ipoamua kuwapawawekezaji eneo la Egol lililokuwa limesheheni dhahabu,baada ya kuchimba dhahabu hiyo wawekezaji waliujengaMji huo ambao ni wa kisasa sana na wakauita ‘Egol the placeof Gold’ kama kumbukumbu ya dhahabu iliyokuwepo pale.

Afrika Kusini hawakuachiwa mashimo na vifusi vyavumbi kama ilivyo Nyarugusu, bali Mji mzuri wa kupendeza.Kwa nini sisi Tanzania tusiige yale mazuri wanayofanya jiranizetu na badala yake tunauza mali zote kwa wageni bilamrejesho unaolingana? Ni wakati wa Taifa kufanya maamuzimagumu sasa na si kesho!

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. ELIZABETH N. BATENGA: Mheshimiwa Spika,Hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini ni nzuri na yenyeufafanuzi. Inaonesha mipango ni mizuri, lakini utekelezajiutakwama kwa kutokuwa na fedha ya kutosha. NaombaSerikali ikubali kukusanya fedha kwenye mafuta na simu kamaBunge lilivyokwisha kuishauri.

Mheshimiwa Spika, tangu tusikie mradi wa kuzalishaumeme kwenye maporomoko ya Rusumo ni muda mrefusana. Je, ni lini hasa utaanza? Umeme huo ungewezakusambazwa na kuleta maendeleo katika Wilaya za Ngarana Biharamulo.

Mheshimiwa Spika, kuna tatizo au uhaba wa nguzoza umeme Mkoani Kagera (TANESCO). Nguzo zinazalishwahapa hapa nchini sasa tatizo linakujaje? Naomba majibukatika haya yote.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. DKT. ANTONY G. MBASSA: Mheshimiwa Spika,nianze kwa kuelekeza mchango huu kwenye suala zima laMradi wa Umeme Vijijini (REA). Hakika asilimia 80 ya wananchiwanaishi vijijini sehemu ambazo uzalishaji hakika ukipewa

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

145

msukumo wa nishati ya umeme utakuwa wa hali ya juu sana.Hakika wafanyabiashara wadogo kwa wakubwa wanahitajinishati hii muhimu sana kwa ajili ya uzalishaji na uchocheziwa shuguli za maendeleo. Katika mradi huu kuna vijijiambavyo vimewekwa kwenye mradi huu JimboniBiharamulo Magharibi ambavyo ni Kabindi, Runazi, Rwagati,Katohoka, Nyamahanga, Ntungamo, Kibale, Nyambale,Lusahunga, Nyakahura na Nyakanazi, lakini pamoja namaeneo hayo kuainishwa bado yapo maeneo mengiambayo mradi huu wa REA unapaswa kuharakishwa sana.

Mheshimiwa Spika, kuna Kata ya Nyabusozi pale kunaCentre kubwa ya Isambara, Nyabusozi yenyewe, Nyabusozisekondari, Mwanga zahanati, Kabangani, Kata ya Nembahususan Nemba sekondari, Nemba centre, Kisenga,Kazilambwa, Kata ya Nyantakala; Nyantakala centre,Iyengamulito, Nyantekara sekondari, Mgera, Mtunduni mpakaNyakanazi, hakika maeneo haya yote niliyoyataja yanamakundi mengi ya vijana wanawake na makundi mbalimbaliya jamii ambayo kweli kama yangepata umeme huu waREA hakika tungepunguza umaskini ambao unazidi kukithirikatika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, kuna tatizo la wananchi kuombakuunganishiwa umeme, lakini mamlaka zinazohusikakuwanyima wananchi fursa hiyo. Hakika kuna maeneoambayo kuna nguzo zinazipita na wananchi wana ushuhudiaumeme kwenye waya ukipita na wao wakibaki gizani.Hakika hii si sahihi hata kidogo, TANESCO kupuuza nguvu zawananchi. Pale wanapopeleka maombi wanaambiwawapeleke mihtasari kitu ambacho tayari wamekwishafanya,lakini hakika hata wakipewa bado hakuna utekelezaji.Naomba mamlaka zinazohusika zifikirie wananchi hawa kiliochao.

Mheshimiwa Spika, niombe suala hili la umemelifanyiwe kazi haraka sana ili kuweza kuchochea maendeleoya wananchi na hakika umeme ndio nguzo ya uchumi wetu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja zote

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

146

zilizoainishwa kwenye hotuba ya Kambi ya Upinzani ambayohakika imeainisha mianya yote ya ubadhirifu baina yamikataba mibovu. Upotoshwaji na uporwaji wa madini yetukatika migodi yetu. Hakika maendeleo hayana itikadi, hayanachama na wala hayawezi kuwa ya mtu mmoja mmoja tu,bali yanategemea nguvu ya pamoja. Ni imani yangu kamawote tutasimamia nguvu ya pamoja tutafanikisha adhmahii ya kupata kile tunachokihitaji kutokana na rasilimalitulizonazo. Zawadi ya Watanzania wote toka kwa MwenyeziMungu.

MHE. HERBERT J. MNTANGI: Mheshimiwa Spika,nawapongeza Mheshimiwa Waziri, Manaibu wake, KatibuMkuu na viongozi wa Taasisi chini ya Wizara ya Nishati naMadini.

Mheshimiwa Spika, naishauri Wizara kusimamia diraya TANESCO ili ifanikiwe.

Mheshimiwa Spika, pili, Wizara na TANESCO wawekedhamira ya kweli kuondolea Taifa mzigo wa gharama zakampuni za umeme na dharura IPTL AGGREKO na Symbion.Jitihada zilizofanyika kuwezesha Aggreko kupunguzagharama za Capacity charge kwa asilimia 34% ni mfanomzuri.

Mheshimiwa Spika, tatu, napongeza jitihada zakuongeza uzalishaji kwa miradi mipya ya Mwanza mw 60;Kinyerezi (1+2) mw 390; Somanga fungu mw 320; Mchuchumamw 660; Makaa ya mawe Ngaka mw 400; makaa ya maweKiwira mw 20; Murongo na Kikagati mw sita; Mtwara –Symbion mw 400; jumla mw 2,386.

Mheshimiwa Spika, ni vema mradi wa MtwaraSymbion 400 mw ukapewa kipaumbele na kuwatambulishahivyo wananchi wa Mtwara ikiwepo ziada ya miradi ya REA,huko Masasi, Nanyumbu, Newala na Tandahimba na piamiradi chini ya Mfuko wa Umeme Vijijini (REA).

Mheshimiwa Spika, maombi nil iyopitisha REA,

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

147

nimeomba na narudia kuomba umeme kwa vijiji vinnevifuatavyo:-

(a) Kiwanda; hapa kipo Chuo cha Maendeleo yaUfundi, Zahanati na Nyumba za Walimu na Daktari namabweni ya wanafunzi.

(b) Tongwe; i l i kufikisha umeme Kiwanda,umeme upo sasa Kijiji cha Bombani; hivyo ukitoka Bombanilazima upite Tongwe ili kufika Kiwanda.

(c) Tingeni; hapa upo uchaguzi wa Diwani,baada ya aliyekuwepo kufariki. TANESCO Muhezawalishapima na kufanya makadirio ila hawajathibitishakuingizwa katika mpango wa 2013/2014. Umeme kwendaTingeni unaweza kutoka Muheza Mjini, Kata ya Kwamkabaraau kutoka Kerenge, Kijiji ambacho kipo ndani ya Kata hiyoya Tingeni.

(d) Kwakifua; hapa ni Makao Makuu ya Kata yaKwakifua na ipo zahanati na nyumba za Walimu shule yamsingi Kwakifua.

Mheshimiwa Spika, kauli ya Wizara ya Nishati naMadini, Bungeni 2012/2013, mara kwa mara imetolewa kaulikwamba, pale waya za umeme zikipita juu ya eneo la kijijikuelekea kijiji cha mbele ya kijiji au kitongoji hicho umemeutashushwa ili kijiji hicho kipate umeme. Kwa maelezo hayo,naomba muiagize TANESCO Muheza kuteremsha umemekwenye kijiji na kitongoji cha Mabungu.

Mheshimiwa Spika, nguzo na waya za umemezimepita hapa Mabungu, sasa miaka 18 imepita wakatiumeme ukipelekwa katika Kijiji cha Misozwe. NilisaidiaTANESCO miaka hiyo 18 iliyopita kuwezesha umeme kufikaMisozwe bila gharama yoyote ya fidia na wananchi walishirikikusaidia kazi ya kuchimba mashimo kwa ajili ya nguzo zaumeme, pamoja na jitihada hizo kwa miaka 18 TANESCOhaikuwezesha kusogeza umeme hata kwa kitongoji kimojacha ziada! Hata nilipoomba umeme usogezwe kwa nguzo

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

148

nne tu kuingizwa katika nyumba ya Mapadre ndani ya Kijijicha Kwemingoji ambapo ndio ulipoishia umeme waMisozwe, nimetakiwa kulipia gharama zote kuwezeshaumeme kufikishwa hapo! Nashukuru leo kwa mpango waREA vijiji ndani ya Kijiji cha Misozwe vimekubaliwa katikaorodha iliyopo na kuondoa kero hiyo ya miaka mingi (Vijijivya Matogoro, Amtakae na Soweto) ila kimebaki Kijiji kimojacha Kisinga”

Mheshimiwa Spika, mwisho, natoa ushauri wa ziadaufuatao; mchango katika Mfuko wa Umeme Vijijini uongezwena kuongeza usimamiaji wa matumizi ya fedha hizo nakuhakikisha makusanyo yanasimamiwa vizuri na kuingizwakatika mfuko kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, REA (Rural Energy Authority),chombo hiki ni mamlaka ya umeme vijijini hivyo sio busarakuendelea kuwa kitengo ndani ya TANESCO. REA iwe chombohuru na kiutawala katika kujiendesha, hii itasaidia kuwa nachombo cha pili muhimu katika usambazaji wa umemevijijini.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. HAMAD ALI HAMAD: Mheshimiwa Spika,nimechangia kwa kusema, lakini hili sikulifikia kwa sababuya muda.

Mheshimiwa Spika, naomba niishauri Serikali kupitiaWizara kwamba, kwa kuwa Watanzania wanaonekanawamekata tamaa na manufaa yatokanayo na rasilimali zao.Hivyo basi, Wizara ije na sera itakayowapa matumainiWatanzania wote popote walipo.

Mheshimiwa Spika, mambo matatu sera ioneshe seraigawe pato lote litokanalo na madini kwa ujumla kamaifuatavyo:

(a) Sehemu moja iwe inakwenda kulipa madeniili kuliondolea Taifa na vizazi vijavyo mzigo wa madeni;

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

149

(b) Sehemu nyingine ioneshwe kwamba,inakwenda kujenga miundombinu ya barabara, maji, reli,shule, zahanati na kadhalika; na

(c) Sehemu nyingine hii igawanywe kwaWatanzania wote kuanzia aliyezaliwa leo hadi yule wa miaka100.

Mheshimiwa Spika, huo ndio ushauri wangu kwaSerikali yangu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, nashukuru na naombakuwasilisha.

MHE. CLARA D. MWATUKA: Mheshimiwa Spika,napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Waziri na NaibuWaziri kwa kazi yao ambayo kweli ni nzuri.

Mheshimiwa Spika, napenda nitoe machache kamataarifa na maombi kwa Serikali kuhusiana na hali ilivyo nainavyoendelea Mtwara. Taarifa za uhakika ninazopata nikwamba, wananchi madai yao ni kwamba, wanatakaviwanda vijengwe kwanza ili wawe na imani ya kweli, ndipoyale ya kupeleka Kinyerezi yafanyike. Hofu yao ni palewanapoona unaharakishwa utaratibu wa kusafirisha kablaya kiwanda, isije ikawa ya Songosongo.

Mheshimiwa Spika, amini usiamini fujo kubwazinafanywa na Polisi, hawa Polisi imezoeleka mahali pengipenye matatizo, wao huwachokoza wananchi ili wafanyefujo ili wao wafaidike. Huwa wanavunja maduka na kubebamali, juzi Polisi walishukiwa na askari wakiwa na majokovu(friji) nne, walinyang’anywa na kupeleka kwenye Kambi yaJeshi. Pamoja na hayo wao huwa wanavunja nyumba nakuwakamata watu usiku na kuwapiga wanawake.Mabwana kupelekwa kituoni wakiona kitu kizuri mle ndaniwao wanachukua.

Mheshimiwa Spika, watu waliovunjiwa nyumba zao,vibanda vya biashara hivi sasa wanahangaika na watoto

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

150

kwa kukosa chakula na kadhalika. Ieleweke wananchi, waondio wadai wasingeweza kujiumiza wenyewe (kujivunjiamajumba).

Mheshimiwa Spika, pamoja na yote, Serikali isilalieupande mmoja wa kuwa waletao fujo ni Wapinzani, walewote kule sio Wapinzani, CCM wapo na ndio wengi. HaoWapinzani wana nguvu gani ya kuweza kuwashawishi vigogoau makada wa CCM wakakubali kurubuniwa? Tafadhalisana wapiganapo ndovu ziumiazo ni nyasi.

Mheshimiwa Spika, kwa kawaida mzazianapomwona mtoto analia, humhoji analilia nini. Ikibidikumpatia kama kipo na kama hakipo humtuliza kwa lughanzuri ili anyamaze na sio kushika bakora na kumchapa,matokeo yake kitakachotokea pale kinaweza kikawakibaya. Kumbuka lahaula haitangulii. Serikali iliangalie hili kwamapana hasara zinazopatikana ni kazi ya Serikali kugharamiamatengenezo. Vile vile nchi inapoteza sifa yake ya amanina utulivu.

Mheshimiwa Spika, hali iliyopo hadi hivi usiku nilikuwanaongea na mwanangu wakati na majira ya saa tatu,niliisikia milio miwili ya mabomu. Asubuhi hii nikaambiwalilisikika la tatu. Ikumbukwe kwamba ushauri mwingineunaotolewa na baadhi ya viongozi kwa Serikali unachocheamambo kuzidi kuwa mabaya. Hivyo, naiomba Serikali ikaechini na kutafakari kwa kina ili amani ipatikane.

Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia kwamachache juu ya suala la umeme vijijini. Shule nyingi zasekondari za Kata zipo vijijini ambako hakuna umeme, humomashuleni mna mahitaji makubwa hasa kwa somo la sayansi.Somo hili linatakiwa vitendo hasa kwenye somo la kemiakaribu shule nyingi wanafunzi hawapati na matokeo yakewanafeli mtihani. Hivyo, Serikali ione umuhimu wa kupelekaumeme ili kuwasaidia wanafunzi kupata somo hilo la sayansi.

Mheshimiwa Spika, katika vijiji vile ambavyo hakunaumeme, kuna vituo vya afya na zahanati pia. Pamoja na

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

151

sehemu zingine kuweka generator kunakuwa na ukosefu wamafuta na shughuli zingine za uendeshaji wa kazi kukwama.Vile vile pale palipopelekwa solar kama mvua zinanyeshamfululizo na kupelekea ukosekanaji wa mwanga wa juanako huleta matatizo pia. Hivyo umuhimu wa umeme nimkubwa.

Mheshimiwa Spika, umeme ni kila kitu, shughuli nyingiza uzalishaji wa uchumi zikikosa umeme hakuna maendeleo.Hivyo, naiomba Serikali izingatie sana juu ya upatikanaji waumeme, sio mijini tu bali na vijijini. Maana katika kufanyahivyo kutasaidia utunzaji wa mazingira pia kukatwa mitihovyo kwa ajili ya mkaa kutakoma au kutapungua.

Mheshimiwa Spika, ahsante na naunga mkono hoja.

MHE. HAROUB MUHAMMED SHAMIS: MheshimiwaSpika, awali ya yote, namshukuru Mwenyezi Mungu(Subhanah Wataala) kwa neema na rehema zake nyingikwangu, familia yangu na Taifa kwa jumla.

Mheshimiwa Spika, kila alichokiumbwa MwenyeziMungu (Subhanah Wataala) katika ulimwengu huu ni kwamadhumuni ya kumnufaisha mwanadamu. Kila alichopewamwanadamu kama afya, elimu umasikini au utajiri ni mtihanikwake. Ni wajibu wa mwanadamu huyo kutumia akili yake,elimu yake, busara yake na hata ushauri ili aitumie vizuri neemaaliyopewa. Nchi yetu imejaliwa rasilimali nyingi na zenyethamani sana, hivyo basi ni wajibu wa Serikali kuzisimamiavizuri rasilimali hizi ili zilete neema kwa nchi yetu na isiwekinyume chake! Naiomba Serikali iendane na ushauri ilidhahabu, almasi na hata gesi zinufaishe nchi kama dhahabuilivyonufaisha Afrika ya Kusini hadi Mji wa Egoli ukaitwa theplace of gold kama Oman ilivyonufaika na mafuta, Abudhabina nchi nyingi za Middle East!

Mheshimiwa Spika, naiomba na kuisihi Serikali yetu iwewazi katika mikataba ya Madini na Gas ili kuondoa fitina nawasiwasi uliotanda katika nchi. Nguvu sio suluhisho lamatatizo la kuendeleza rasilimali zetu.

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

152

Mheshimiwa Spika, tusipoziba ufa sasa tutashindwakujenga ukuta baadaye wakati ni huu! Ni bora lawama kulikofedheha. Tukiogopa kulaumiwa hivi sasa kwa kurekebishamikataba na Sera ya Gesi na madini tutapata fedhehabaadaye ya kuendelea kuwa maskini bila msaidizi.Wanaochota rasilimali zetu sasa watakuwa wa mwanzokutucheka na kutukejeli kuwa ni wapumbavu.

Mheshimiwa Spika, nakushuru sana inawezekana,timiza wajibu wako, Mungu ibariki Tanzania na mali zake.

MHE. MOZA ABEDI SAIDY: Mheshimiwa Spika,niungane na watanzania wenzangu kuwapa pole wale wotewaliopoteza ndugu na jamaa zao waliopoteza maishakwenye migodi na hasa huko Mererani, Arusha.

Mheshimiwa Spika, napinga kauli ya kubezana ndaniya Bunge hili kwani kila mtu anayo fursa ya kuongea na kutoamawazo yake na mchango wake na ukathaminiwa kamamchango kwa Serikali au kuishauri na hata kuikosoa Serikalihasa upande wetu Wapinzani imekuwa kila kitu kwetuhakifai, inavyoonekana kwa wenzetu wa utawala, jamboambalo linaleta mtafaruku kila mara hapa Bungeni.Naomba mambo haya si mazuri, Serikali ikubali kukosolewana ikubali kupokea mawazo ya upande wa pili.

Mheshimiwa Spika, nianze na mchango wangu wamadini; madini ni uchumi, madini ni utamaduni wa rasilimali,lakini madini hayalimwi useme yataota tena kama mimea,ukiyachimba na kuyatoa hayarudi tena. Sekta hii ni mchangomkubwa katika uchumi wa Taifa.

Mheshimiwa Spika, katika sekta hii ya madiniimepoteza ndugu zetu kwa kufia kwenye machimbo bilakuwepo uangalizi wa uchimbaji hasa wachimbaji wadogowadogo hata wengine kukosa kifuta machozi wanapopatamadhara. Swali Mheshimiwa Waziri naomba kwenyemajumuisho yake aelezeo nini hatima ya vijana wetuwanaojiajiri kwenye migodi pindi wamalizapo kuchimba aukuachishwa na hata kufa, Serikali inawasimamiaje?

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

153

Mheshimiwa Spika, madini yapo sehemu kubwa yaTanzania, Serikali mbona inaachia uchumi huu unatowekabila vipaumbele vinavyosemekana, maeneo husikahavikamilishwi kama makubaliano yalivyo? Nini tatizo lawawekezaji hao je, ni elimu gani itolewayo na Serikali hasakwa wale wanaovumbua madini hayo wananufaikaje?Kwani tunaona matatizo yapo kwa waendesha migodi hiyokutokuwathamini Watanzania wanaowaajiri, naishauriSerikali ipitie mikataba upya na iangalie mikataba yawaajiriwa kwenye migodi iko sahihi?

Mheshimiwa Spika, nimalizie, sekta hii bado haijakaavizuri, kwa kiasi kidogo ifanye marekebisho ili uchumi wetuhuu usiwe mateso kwa Watanzania na wafukie yale mashimokama kuna makubaliano haya na udongo usitoke kwendakwingine kokote na wananchi wapewe fursa ya kutafuta rizikindogo ndogo pembeni mwa migodi ili waweze kujikimukimaisha kwani ndiyo rasilimali zao, wasinyanyasike hasa hukoGeita na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, bajeti ya Wizara hii ni ndogohaikidhi mahitaji na Maafisa Madini wa Kanda na wasiwena upendeleo na watekeleze kazi zao ipasavyo. Hivyo,sitoiunga mkono hoja hii kwani ina upungufu mwingi ikiwepona bajeti yenyewe.

Mheshimiwa Spika, nichangie tena Wizara yaTANESCO Wizara hii imepata bajeti ya kutosha, lakini badoina mapato mengi, mengine ni kuwakandamiza wananchihasa kwenye nguzo limbikizo lisilojulikana makosa yaongezeko la bilioni na kutoainisha mteja kwa makundi nakuwatoza bili kubwa kuliko matumizi.

Mheshimiwa Spika, Wizara imepanga makundi yamatumizi kwa makundi mbalimbali ikiwemo kundi lamatumizi madogo ya nyumbani wastani wa kwhr 50, angaliamatumizi haya yamepewa ruzuku na shirika. Sasa mtejaatajuaje hiki ni kiwango chake halali, mbona hailingani natozo yake nini tatizo? Pia shirika wakati linafunga umemekwa mteja huwa hawaambii au hayo huja tu.

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

154

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri ana uhakikana meneja wa Shirika kasomea utawala au ni injinia katikasehemu zake zote za mashirika yaliyopo, naomba ufuatiliehilo ili kuepuka malimbikizo na kulipiza wananchi bili kubwa,kuliko hitaji na kuwaambia walipe tu watakuja fidiwa auComputer ndiyo imesema hivyo.

Mheshimiwa Spika, kutokana na rasilimali za asilizilizokuwepo nchini ambazo ni vyanzo vya asili vya nishativikiwemo gasi maji ya mito na kadhalika mtumiaji wa umemewa Tanzania analipa bili kubwa.

Mheshimiwa Spika, bei kubwa ya umeme; hudumahii pamoja na bei zake zinadumaza ukuaji wa uchumi waTanzania, naiomba Serikali itoe agizo kwa TANESCO iwezekurekebisha bili za umeme kufuatana na makundi, nawekamfano huo.

Mheshimiwa Spika, DI watumiaji wadogo kiwangocha 0 - 50 ni ndogo angalau watoke mpaka unit 0 -100, wanafunzi wanashindwa kujisomea wakati wa usiku.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na malalamiko yapower fact ambapo mtumiaji analipa mara mbili yagharama hasa kwa wachomeleaji wa pembejeo za kilimo,moja eneo la mrijo chini ya Wilaya ya Chemba sasa EWURAipitie bei hizo na kurekebisha umeme kama ilivyo.

Mheshimiwa Spika, kuna maeneo kuna nguzo natransfoma, lakini hakuna umeme katika Kata ya Dalai, Serikaliinasemaje kuwapa umeme wananchi hao na mnara huowa simu upo pale Pilui? Ina maana minara miwili yote ipohapo Pilui mafuta ya taa hayapatikani na yana gharamakubwa sana.

MHE. DUSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Spika,naomba nianze kwa kuunga mkono bajeti ya Wizara hii,nikitambua kuwa umeme ni muhimu.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuunga mkono bajeti

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

155

ya Nishati na Madini ni ukweli usiopingika kuwa fedhatulizotenga hazitatuwezesha kufikia malengo tuliyojiwekeahususan katika kupeleka umeme vijijini.

Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu sasa suala laumeme vijijini limekuwa likipata fursa ya kuzungumziwa sana,lakini kwa bahati mbaya sana uungwaji mkono huu umekosavitendo thabiti. Hali hii inaweza kuthibitishwa na upuuziajiau kutokutekelezwa kwa uamuzi wa Bunge wa kupeleka REAfedha za tozo la mafuta ya taa, ili fedha hizo ziweze kutumikakupeleka umeme vijijini. Hali hii ni sawa na kosa tulilolifanyakatika miaka ya 1970 tulipositisha uanzishwaji wa Tanzaniarural electrification company (TARECO). Uamuzi ule ulidumazakasi yetu ya kupeleka umeme vijijini.

Mheshimiwa Spika, wananchi wa vijijini wanasubirihuduma ya umeme kutokana na ukweli kuwa, tumewaahidikwa muda mrefu. Mafanikio tuliyoyapata katika ujenzi wazahanati na shule katika Vijiji na Kata lazima yaendesambamba na upatikanaji wa huduma ya umeme. Wananchiwa Mkinga katika Viji j i vya Daluni, Gombero, Vuga,Mapatano, Bwiti, Manga, Bosha, Mhimbiro na Mwakijembe,wamesubiri kwa muda mrefu sana kwa bahati mbaya lichaya ahadi za mara kwa mara kwa mwaka huu vijiji vitatu tundio vimejitokeza kwenye orodha tofauti na miaka iliyopita,wananchi hawatatuelewa katika hili.

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaSpika, napenda kuchangia katika haya yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, katika mikataba inayosainiwahapa nchini kuna component ya mafunzo kwa Watanzania.Mchango huo ni kati ya dola laki moja mpaka dola laki mbili.Je, ni Watanzania wangapi wamekwishapata fursa hizo zamafunzo na ni wa kada zipi?

Mheshimiwa Spika, kuhusu wachimbaji wadogo kwaniaba ya wana Katavi, napenda kuiomba Serikali iwapatiewananchi na wachimbaji wadogo wadogo maeneowaliyoomba na si kuwapa maeneo mapya ambayo

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

156

hawayafahamu, kwa mfano, wana Mpanda wameombamaeneo haya yafuatayo:-

(i) Ibindi.(ii) Kampuni.(iii) Kakese.(iv) Kasinde.(v) Singililwa.

Mheshimiwa Spika, pia maeneo ambayo kampuni yaGBA ya Kirusi ina maeneo ambayo haiyafanyii kazi. Hivyobasi, maeneo hayo ni vema wakapewa wananchi amawachimbaji wadogo wadogo wa Mpanda wa maeneoyaliyopo pembezoni ya kampuni hiyo ya GBA.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. DKT. DALALY PETER KAFUMU: Mheshimiwa Spika,wakati nachangia kwa maneno niliipongeza sana Wizarakatika kutekeleza mabadiliko ya sera za uchumizinazohamasisha na kukuza uwekezaji nchini. Zilizoanzishwamiaka ya 1990, sera hizi zililenga kuzifanya Sekta za Nishatina Madini kuwa mhimili mkubwa na injini ya uchumi wa nchi.Nilisema lazima tuhakikishe sekta hizi zinafungamanishwa nasekta nyingine za uchumi ili kuwafanya wananchi wengiwashiriki katika uwekezaji huu na kupata manufaa zaidikulingana na Sera ya Nishati ya mwaka 2003 na Sera ya Madiniya mwaka 2009, sasa naomba kuchangia kwa maandishikutoa ushauri kadhaa kwa Serikali.

Mheshimiwa Spika, nishati; wananchi wa Vijiji vya Kataza Mbutu, Mwamashimba na Igunga waliopitiwa na laini yaumeme wa gridi inayotoka Singida hadi Shinyanga walipewafidia hivi karibuni. Fedha zilipelekwa na wananchi wakalipwafedha taslimu. Kuna malalamiko mengi kuwa baadhi yawananchi walilipwa fidia kwa kupunjwa, wengine walilipwazaidi na wengine hawakulipwa kabisa. Suala hil inimelishughulikia kwa kushirikiana na DC na kulifikishaTANESCO, nao wakaahidi kulishughulikia. NamwombaMheshimiwa Waziri atoe maelekezo stahiki kwa uongozi wa

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

157

TANESCO ili malipo haya yapitiwe upya na malipo kufanyikakadri ya haki ya kila mwananchi.

Mheshimiwa Spika, naishukuru Wizara kwa kuletamiradi ya umeme vijijini ambapo Vijiji vya Kata za Itunduru,Igurubi, Itumba na Mbutu zitapatiwa umeme kutoka kwenyeMfuko wa REA naiomba Serikali iharakishe utekelezaji wamiradi hii ili wananchi wa maeneo haya watambue kwamba,Serikali yao ya CCM inawajali.

Mheshimiwa Spika, madini; katika usimamizi wa sektaya madini jambo kubwa ni kuhakikisha uwekezaji wa ndanina nje unasaidiwa kukua na kuleta manufaa makubwa kwawananchi wa Tanzania. Katika kufanya hivyo, kumekuwepomchanganyiko na mwingiliano wa majukumu ya taasisi naidara za Serikali, jambo ambalo limeanza kuidumaza Sektaya Madini. Mwingiliano huu umewasumbua sana wawekezaji,lakini pia umeifanya Serikali itumie fedha nyingi sana kufanyajambo lile lile.

Mheshimiwa Spika, msimamizi Mkuu wa sekta yamadini ni Kamishina wa Madini kwa mamlaka aliyopewachini ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010 na kanuni zakeakisaidiwa na makamishina wa Madini Wasaidizi wa Kandanane nchini; Mkaguzi Mkuu wa migodi na Makamishina waMadini Wasaidizi watano waliopo Makao Makuu ya Wizarawanaoshughulikia Ukaguzi wa Migodi; matumizi ya Baruti;uchumi na biashara; uongezaji thamani ya madini utoaji waleseni na usimamizi wa uchimbaji mdogo. Lakini ukiangaliahotuba ya Mheshimiwa Waziri inaonekana dhahiri kuwaWakala wa Ukaguzi wa Madini. Tanzania Mineral AuditAgency (TMAA) imechukua kazi na mamlaka ya Kamishnawa madini. Baadhi ya mifano ya mwingiliano huo inaelezwahapa.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, kazi ya kukusanyamaduhuli kutoka kwenye madini yote yakiwemo madini yaujenzi ni ya Kamishna wa Madini kwa kutumia ofisi zaMakamishna Wasaidizi wa Kanda na Maafisa Wakazi waliopomikoani katika Kanda nane za utawala wa Wizara. Lakini

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

158

ukiangalia ukurasa wa 69 wa hotuba, kifungu cha 131inaonekana wazi kuwa TMAA imechukua kazi ya ukusanyajiwa maduhuli kinyume cha sheria. Maafisa Madiniwanaopaswa kufanya kazi hii kwa Sheria ya Madini ya mwaka2010 wanafanya nini?

Mheshimiwa Spika, ukiangalia tena ukurasa wa 70,kifungu cha 133, TMAA sasa imeweka madawati ya kukaguausafirishaji wa madini kwenda nje, kazi ambayo kwa Sheriaya Madini ya mwaka 2010, inapaswa kufanywa na KamishnaMsaidizi wa Uchumi na Biashara ya Madini. Pamoja na Ofisiza Makamishna wa Madini Wasaidizi waliopo karibu namaeneo ya mipakani na Viwanja vya Ndege vya Kimataifa.Hivi kumetokea nini kiasi kwamba, Wakala ulioundwa kwania njema ya kushughulikia ukaguzi wa migodi kwa ajili yaudhibiti yaani auditing. Sasa Wakala unafanya kazi zausimamizi yaani inspection kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.Ukusanyaji wa maduhuli na biashara ya madini. Hii siyo sawani ku-duplicate shughuli za Serikali na kuzifanya kuwa nagharama kubwa.

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 71, kifungu 134kinaonesha dhahiri kuwa TMAA inafanya kazi ambazozingeweza kufanya na NEMC wakisaidiwa na Kitengo chaMazingira cha Wizara ya Nishati na Madini na Ofisi ya MkaguziMkuu wa Migodi kwa ufanisi. Kulingana na Sheria yaMazingira ya mwaka 2004 na Sheria ya Madini ya mwaka2010.

Mheshimiwa Spika, pia ukiangalia maelezo ya ukurasawa 68 hadi 69, vifungu namba 129 na 130 vinaonesha kanakwamba mafanikio ya ulipaji wa kodi ya mapato (corporatetax) yanatokana na tathmini ya kodi kwenye migodiyametokana na kazi ya TMAA pekee. Lakini kwa uhalisia wajambo hili TRA inao mchango mkubwa zaidi na ni kazi yaTRA kwa sheria ya TRA kufanya kazi za ukaguzi wa uwekezajikwa lengo la kutathimini kodi. Hapa tena TMAA inafanyakazi ya taasisi nyingine kinyume cha sheria.

Mheshimiwa Spika, ukiongea na wawekezaji na

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

159

wadau wa sekta ya madini wanalalamika sana kuwaukaguzi wa jambo lile lile unaofanywa kwenye migodi nataasisi zaidi ya moja linawapotezea muda, ni gharamakubwa sana kwao. Kiashiria hiki siyo kizuri kwa mustakabaliwa kuinua uwekezaji nchini.

Mheshimiwa Spika, pamoja na haya yote, nimesomapia mapendekezo ya Kamati ya Nishati na Madiniinayopendekeza TMAA iwe Mamlaka, inaonekana Kamatihaijaelimishwa vema juu ya kazi na majukumu ya TMAA.

Mheshimiwa Spika, haiwezekani kuwepo kwaMamlaka ya Madini na pia Idara ya Madini, itakuwa nikutengeneza Taasisi mbili zenye kazi sawa. Taifa changalinalotaabika kujaribu kujenga uchumi wake halipaswikutumia rasilimali nyingi kiasi hicho kufanya kazi zinazofanana.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2007 Kamati ya Bomaniilipendekeza kuwa Idara ya Madini ibadilishwe na kuwamamlaka ili kuipa nguvu ya kuweza kufanya kazi zake kwaufanisi. Idara hiyo yenye mamlaka na madaraka ya kisheriakusimamia Sekta ya Madini iwe na uwezo wa kitaasisi,kirasilimali watu na fedha na kiteknolojia kama ambavyonchi ya Ghana ilivyobadili Idara ya Madini kuwa Mamlakahuru iitwayo Mineral Commision of Ghana.

Mheshimiwa Spika, Serikali wakati inatekeleza baadhiya mapendekezo ya Kamati ya Bomani ilisema uundwaji wamamlaka usubiri wakati muafaka. Kwa nini sasatunazungumzia TMAA badala ya Idara ya Madini?

Mheshimiwa Spika, nchi zingine kama Australia, AfrikaKusini, Canada, Botswana na nyingine nyingi zimeimarishaIdara za Madini zinazofanya kazi za ukaguzi na usimamiziwa migodi kwa ufanisi mkubwa. Marekani inayo idarainayojitegemea inayoitwa Mineral Bureau. Idara hizi na taasisikatika nchi hizi hufanya kazi zote za usimamizi wa Sekta yaMadini, lakini shughuli za ukaguzi wa uwekezaji (shughuliambazo zil itengwa zifanywe na TMAA hapa kwetu,hufanywa na mamlaka za mapato za nchi hizo. Nchi hizo

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

160

zimeimarisha Mamlaka za Mapato kuweza kukagua nakusimamia masuala ya uwekezaji katika sekta ya madini ilikodi stahiki zilipwe.

Mheshimiwa Spika, tuliunda TMAA kufanya kazi zaukaguzi wa madini (Auditing) kazi ambazo hazitoshelezikulingana na ukubwa wa taasisi tuliyounda matokeo yakeTMAA ikaanza kujichukulia kazi za taasisi zingine. Viongoziwa Wizara wamefunikwa na kukosa kujua ukweli na hivyokuamini kuwa TMAA ni taasisi yenye faida kubwa kwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, kwa uzoefu wangu wa kuwaMsimamizi wa Sekta ya Madini kwa miaka sita suala hililinaidumaza sekta ya madini na pengine laweza kuiua kabisa,na hasa pale ambapo TMAA inajionesha kama kwamba,imegundua wizi mkubwa katika migodi na kutangaza kwaumma hali inayoweza kuondosha wawekezaji wengi sananchini. Serikali inao wajibu wa kushughulikia ukiukwaji washeria kwa hekima. Badala ya kutangaza uovu huo kwaumma.

Mheshimiwa Spika, chimbuko la kuundwa kwa TMAAlinatokana na baadhi ya viongozi wa Serikali hususani Wizaraya fedha na Benki kuu wakati huo katika miaka ya 2003waliunda kampuni binafsi iitwayo Alex Stewart AssayersGovernment Business Corporation (ASAGBC) ili kufanya kaziya kukagua uwekezaji na uzalishaji wa migodi. Kampuni hiyoil ifanya kazi hadi mwaka 2007 ambapo wananchiwalilalamika kuwa kampuni hiyo ilikuwa inaiibia Serikali kwakufanya kazi ya ukaguzi kwa bajeti kubwa (takriban shilingibilioni 13 kwa mwaka) inayokaribia bajeti ya TMAA ya karibiashilingi bilioni 10.

Mheshimiwa Spika, nikiwa Kamishna wa Madininilimshauri Waziri wa Nishati na Madini wakati ule kuwakampuni hiyo iondolewe na uwezo na utaalam ilioujengauwekwe chini ya Idara ya Madini kwa muda ili Serikali itafakarinamna bora ya kukagua uwekezaji katika sekta ya madinikwa kujifunza kutokana na uzoefu wa nchi zingine. Kitengocha Gold Audit Program (GAP) kikaundwa chini ya Idara ya

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

161

Madini. Kitengo hiki kilipata fedha nyingi kuendeleza ukaguzihuo ilipofika wakati wa kutafakari hatima yake baadhi yaviongozi wa Wizara bila kuzingatia maslahi mapana ya Taifawaliendesha mchakato wa haraka sana kuunda TMAA,mchakato uliharakishwa kiasi kwamba, kazi za TMAAzikaorodheshwa nyingi zikiwa ni zile zile za TRA, NEMC naIdara ya Madini.

Mheshimiwa Spika, maoni ya TRA, NEMC na Idara yaMadini yalikuwa ni kwamba, kutakuwa na mwingiliano wamajukumu, hayakuzingatiwa na Serikali ikaaminishwa kuwahili ni jambo zuri sana. Nilishauri tufanye mchakato wenyetija kwa kuwasiliana na wadau muhimu wa Sekta za Nishatina Madini na wataalam wa kodi na financial naenvironmental auditing kutoka TRA na Controller and AuditorGeneral (CAG) na Baraza la Utunzaji na Uhifadhi wa Mazingira(NEMC,) ushauri huo haukukubalika na matokeo yake mwaka2009 TMAA ilianzishwa.

Mheshimiwa Spika, wengi pia walishauri GAP iwesehemu inayojitegemea chini ya TRA ili kufanya kazi zaauditing kwa ajili ya kuhakikisha Makampuni ya Madini naMafuta hayakwepi kodi. Wengine walipendekeza GAP iwesehemu chini ya CAG ili kufanya auditing kwa ajili kuhakikishamapato yatokanayo na kodi yanapatikana ipasavyo. Ushaurihuu haukuzingatiwa na TMAA ikaundwa tena kwa harakasana.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa TMAA iliundwa kufanyakazi za ukaguzi unaofanana na ule wa TRA, CAG na NEMCna kwa kuwa kazi hizo hazikuweza kutosheleza au ku-justifyuwepo wake harakati za kujitanua na kuchukua kazi za Idaraya Madini zilianza na sasa kazi nyingi za Wizara ya Nishati naMadini zinazohusu sekta ya madini zinaonekana kufanywana TMAA bila kuzingatia Sheria ya Madini ya mwaka 2010.

Mheshimiwa Spika, inashangaza kabisa kuona kuwasuala la TMAA limeonekana kuwa na mafanikio sana nakuisahau kabisa Idara ya Madini. Nimeshuhudia TMAAikifadhili shughuli za Idara ya Madini kwa vile idara hiyo

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

162

haipewi fedha za kutosha kulingana na wingi wa rasilimaliwatu. Miundombinu na shughuli zake. Kwa mfano, kwenyebajeti ya 2013/2014, ofisi zote za Kanda nane zenye ofisi 22mikoani na watumishi zaidi ya 260 zimepewa shilingi milioni10.25 na TMAA inapewa fedha kiasi cha shilingi bilioni 9.5zisizolingana na uwingi wa watumishi wake wasiozidi 30 namiundombinu yake, hivi kuna taabu gani kuzitengea fedhaza kutosha Ofisi za Kanda za Madini chini ya Kamishna waMadini zikafanya kazi zote hizi.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu nikiwa Kamishnawa Madini haukuzingatiwa, mwaka jana pia nikiwa Mbungeniliandika suala hili mara kadhaa, lakini hakuna aliyeonekanakulitilia maanani. Nimeamua kuandika haya tena kwa kirefukuishauri Wizara ifanye mapitio mapya ya majukumu ya TMAAna umuhimu wake kwa kushauriana na wadau wa Sekta yaMadini ili kuhakikisha kuwa ujuzi uliojengwa na TMAAunawekwa mahali muafaka ili kazi za TMAA zilete thamaniyake ya kifedha, value for money.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali itoe nafasi yakujadiliana na wadau juu ya mwingiliano huu ili kuondoamatumizi mabaya ya fedha za Serikali kwa kuwa na Taasisinyingi zinazofanya shughuli ile ile. Wadau wa sekta ya madinini pamoja na mamlaka za Serikali za TRA, CAG na NEMCwakihusishwa wawekezaji chini ya Tanzania Chamber ofMinerals and Energy (TCME), ni jambo jema pia kuiwezeshaIdara ya Madini yenye Ofisi nchini kote kuweza kufanya kazizake kulingana na Sheria ya Madini ya mwaka 2010 badalaya TMAA.

Mheshimiwa Spika, kuiacha hali hii ya sasa yamwingiliano mkubwa wa majukumu ambayo siasainaonekana kutawala kutaendelea kudumaza sekta yamadini. Naishauri Wizara ilishughulikie suala hili kwa umuhimuwake ili kukuza uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Madininchini. Kama ushauri huu bado utaangukia kwenye masikioziwi, natarajia kuleta Muswada binafsi Bungeni ili suala hililieleweke kwa Wabunge wote na Serikali ishauriwe ipasavyokwa manufaa ya nchi na Watanzania.

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

163

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na naunga mkonohoja kwa asilimia mia moja.

MHE. SYLVESTER MASSELE MABUMBA: MheshimiwaSpika, nampongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Mawaziri naWatendaji wote wa Wizara hii kwa kazi nzuri na ngumuwanayoifanya.

Mheshimiwa Spika, katika masuala yote ya utafutaji,uchimbaji wa madini hapa nchini naiomba Serikali iwe makinikatika mikataba inayoingia na Makampuni mbalimbali. Sikuzote jitahidini kuiweka Tanzania mbele katika mikataba hiyo.Aidha, wachimbaji wadogo wawezeshwe na wapewe kilaaina ya msaada.

Mheshimiwa Spika, katika sekta ya gesi, naiombaSerikali ili kuondoa hofu ambayo inawaingia wananchisehemu mbalimbali hapa nchini mikataba iwekwe wazi,manufaa yatakayopatikana yaelezwe kwa uwazi, mapatoya nchi yetu yatokanayo na gesi yawekwe wazi na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, katika kusambanza umeme kwawananchi vijijini (REA) iwezeshwe, ikiwezekana wananchiwote wanaotumia simu za mikononi wawe wanachangiaasilimia fulani kutoka kwenye matumizi ya simu zao zamkononi.

MHE. KHATIBU SAID HAJI: Mheshimiwa Spika, kwaheshima na taadhima na mimi kuwa miongoni mwawachangiaji katika Hotuba ya bajeti hii muhimu ya Wizaraya Nishati na ya Madini na moja kwa moja naanzakuzungumzia sula la gesi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na Mwenyezi Mungukatujaalia neema hii muhimu, ni vizuri tukajenga mshikamanona kuepuka chuki na fitina ambazo zimeanza kijitokeza katikanchi yetu. Hivyo, ni wajibu wa Serikali kuwapatia elimu yakutosha wananchi ambao wamezungukwa na rasilimali hizi.

Mheshimiwa Spika, ni wajibu kutolewa na

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

164

kufahamishwa wanachi kwamba rasilimali za Tanzania nikwa ajili ya Tanzania na haijatokea duniani kote kwa nchiyoyote ambayo rasilimali ya eneo moja inatumika kwa eneohilo tu.

Mheshimiwa Spika, imeanza kujitokeza huko Mtwarasasa hivi, Mheshimiwa Spika naiomba Serikali ikae na isichokekuwapa maelezo juu ya umuhimu wa wananchi kukabilianana uamuzi wa Serikali na kujenga bomba la gesi kutokaMtwara kuja Dar es Salaam kwa maendeleo ya Taifa na piawana Mtwara kwa ujumla na kuwaondolea hofu iliyotandakwamba, kujengwa kwa bomba hilo ni uhamishaji kwaujumla wake, jambo ambalo litawaacha wao mikonomitupu.

Mheshimiwa Spika, pia naiomba Serikali ifanyeuchunguzi kwa umakini ili kuwapata wale wote waliojifichanyuma ya mgongo wa gesi na kufadhili ghasia kwa ajili yamalengo yao mbalimbali, aidha, iwe ya kisiasa au kibiashara.

Mheshimiwa Spika, uzoefu unatuonesha kwamba,kuna watu ambao hawaitakii mema nchi yetu na hawaridhikikuona amani ya nchi yetu hii iendelee kuimarika, hivyo,wamekaa tayari kujipenyeza katika eneo lolote ambalowataona wanafanikiwa kutimiza nia zao mbaya. Hivyo,naiomba Serikali iwe makini zaidi kukabiliana na hali yoyoteinayojitokeza na kudhibiti amani ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, naanza nakuunga mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, yapo mambo ambayo naombakupata ufafanuzi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu madini ya vito; Sheria yaUmiliki wa Migodi inasema Madini ya Vito imilikiwe nawazawa kwa 50% au zaidi. Leseni itolewe kwa mzawa namwekezaji anaingia ubia 50%.

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

165

Mheshiwa Spika, jambo hili ni jema sana, naipongezaSerikali kwa hilo. Lakini Serikali imepandisha sana ada na tozoza leseni kwa wamiliki wazawa na pia hata kwa wachimbajiwadogo. Hii inaleta adha kubwa sana badala ya kumsaidiainamuumiza na kushindwa kutimiza azma waliyojiwekea kwaajili ya wazawa.

Mheshimiwa Spika, ni vigezo gani vinatumika kwaupandishaji tozo hilo kwa sababu zimepandishwa zaidi yaasilimia mia moja.

Mheshimiwa Spika, ada za mwaka na ada zakuhamisha leseni za ufuatiliaji madini, zimepandishwa sanakatika Sekta ya Madini nchini Tanzania ukilinganisha na nchinyingine.

Mheshimiwa Spika, nitoe mfano wa ada na tozo zaleseni kwa wachimbaji wadogo:-

(i) Ada ya maombi kutoka 0.00 mpaka 50000.

(ii) Ada ya kutayarisha leseni kutoka 20,000 – 50,000/=.

(iii) Ada ya mwaka ya leseni.

- Madini ya vito, almasi na dhahabukutoka 20,000-80,000/=.

- Madini mengine 10,000/= mpaka50,000/=.

Mheshimiwa Spika, matokeo ya upandishaji huu,wachimbaji wengi wadogo, wameshindwa kulipia leseni zaona kunyang’anywa na wenye pesa. Badala ya kuwasaidiawananchi wadogo kufanya tathmini ya mazingira naupembuzi yakinifu ili wachimbaji wadogo wapate andikona kuweza kukopa Benki inawapandiswa ada na tozo.

Mheshimiwa Spika, naomba Waziri wa Nishati na

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

166

Madini anao uwezo na mamlaka ya kuandaa kanuni zaMadini zinazorekebisha viwango vya tozo na ada za lesenimbalimbali kwenye Sekta ya Madini kulingana na Sheria yaMadini ya mwaka 2010 (kifungu 112) ada hizi ziangaliwe upya.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Umeme Vijijini; naiombaSerikali iongeze juhudi kwa ajili ya kuhakikisha vijiji vinapataumeme, pia Serikali imewekwa kuhakikisha vijiji vingivinafikiwa? Mkakati wa Serikali katika kuhakikisha kuwa Shulezote zisizokuwa na umeme zinapatiwa? Sababu hili ni tatizokubwa sana, ni vema ukaandaliwa mpango mkakati wakuhakikisha Shule zote za Sekondari zenye maabarazinapatiwa umeme. Pia hata Makambi mengi ya Jeshihayana umeme, ipo haja ya Serikali pia kuweka mkakati huo.Pia bila kusahau vituo vya afya, wananchi wengiwanapoteza maisha.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. SALEH A. PAMBA: Mheshimiwa Spika, nampahongera sana Mheshimiwa Waziri kwa hotuba nzuri yenyekuonesha mwelekeo. Nimeona mipango mizuri ifuatayo:-

(1) Kinyerezi II na Kinyerezi III. Miradi hii isimamiwevizuri ili kuongeza capacity ya umeme wetu kufikia 350 Mw.

(2) Bomba la gesi lisimamiwe vizuri ili tuwezekupata gesi ya kutosha kuendesha Turbine hizo za Kinyerezi,lakini gesi hii isiwe ya kuchoma kwa kushirikiana na Wizaraya Viwanda kufufua na kuongeza Viwanda vinavyotumiagesi, kama plastiki na kadhalika Jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri a- speed upmatumizi ya gesi majumbani ili umeme uende viwandani.

(3) Hydro scheme; umeme wa maji ni nafuu,angalia miradi ambayo ilikuwepo, lakini haijatekelezwa.Anzeni kufikiria miradi Ruhudji, Stiglers George na maeneomengine. Wizara iweke mkakati.

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

167

(4) Gesi pipeline; extend the pipeline to Tanga andKenya as well. We can earn foreign exchange by selling thegas to Kenya.

(5) Umeme Vij i j ini; this will stimulate ruraltransformation. Nashukuru kwa umeme wa Mkalamo –Mbulizaga, Jimbo la Pangani. Bado kuna Vijiji vya Choba,Kigumesimba na Kimang’a ambavyo havina umeme navyoviingie katika REA.

(6) Miradi mingine ya madini; malizeni suala laKabanga Nickel and other metals, shaba, chuma nakadhalika.

MHE. DKT. AUGUSTINE L. MREMA: Mheshimiwa Spika,naomba nimpongeze Waziri wa Nishati na Madini naManaibu wake kwa kazi nzuri, kazi kubwa wanayofanya.

Mheshimiwa Spika, naomba nimshukuru KaimuMkurugenzi Mkuu wa TANESCO anavyotatua matatizo yaumeme Vunjo. Transfoma zilipoungua katika Kata ya KilemaKusini, Kilema Kaskazini, Makuyuni na Kirua Vunjo Magharibialihangaika sana mpaka Transfoma zikapatikana.

Mheshimiwa Spika, pia naishukuru Wizara kwakutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha ufumbuzi wa umemekatika vijiji vya Lotima, Kata ya Himo, Makuyuni, Vijiji vya RauRiver, Ngasini, Oria na Kisangesangani, Kata ya Kahe.

Mheshimiwa Spika, kutokana na kupungua kwanguvu za umeme katika Jimbo la Vunjo, naishukuru Wizarakwa kufunga mitambo mipya katika Kijiji cha Makuyuni.Mitambo hiyo itasaidia kusambaza umeme katika Kata zoteza Jimbo la Vunjo. Ningependa kujua mradi wa Makuyuniutakamilika l ini i l i kuondoa kabisa tatizo la umemekukatikakatika Jimbo la Vunjo.

Mheshimiwa Spika, mwisho, namshukuru sanaMheshimiwa Muhongo Waziri wa Nishati na Madini kwa

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

168

kukubali kumpokea Bwana P.J. Mining wa Namibia na BwanaJac Lee, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo alifurahi sana.

Mheshimiwa Spika, Naomba kujua hatima yakampuni hiyo kama itashiriki katika uwekezaji wa gesi namafuta.

MHE. PROF. KULIKOYELA K. KAHIGI: Mheshimiwa Spika,Shule za Msingi na Sekondari katika Wilaya ya Bukombe,hazina umeme. Kutokuwepo umeme kunapunguza ufanisikatika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Serikali inampango gani wa kupeleka umeme katika Shule za Msingina Sekondari Bukombe? Aidha, hakuna umeme katika vituovya huduma za afya. Hali hii inasababisha huduma zisitolewekwa kiwango pungufu. Serikali ina mpango gani wa kupelekaumeme wa mionzi ya jua katika vituo hivyo ili kuinua viwangovya huduma?

Mheshimiwa Spika, kuhusu Miradi ya Umemeiliyopangwa katika Bajeti ya 2011/2012 ambayo haifahamikiitatekelezwa lini.

(1) Mheshimiwa Spika, Ukurasa wa 155; Miradi yaTaa za Mwanga Bora, Vijijini (Community Based Solar PowerTrading); Mradi huu ulipaswa kutekelezwa Chato, Biharamulo,Kahama na Bukombe, lakini hadi sasa hakuna dalil iutatekelezwa lini. Je, utaanza kutekelezwa lini?

(2) Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 117; TanzaniaAffordable Rural Electrification Plan (TAREP). Mradi huuulipaswa kutekelezwa Kibondo na Bukombe, lakini hadi sasahaujatekelezwa. Serikali inawaambia nini kuhusu Mradi huu?

Mheshimiwa Spika, kuhusu madini; kwanza kuna kiliocha wachimbaji wadogo cha kutokuwa na maeneo yauhakika ya kuchimba Madini na pia kutokuwa na zana stahikiza kuchimba. Serikali ina mipango gani ya kuwasaidiawachimbaji wadogo wa Bukombe? Jambo la pili linahusuMakampuni ya Utafiti wa Madini ya nje ambayo yamekuwa

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

169

yakifanya utafiti Bukombe, mathalani TANCAN, yapo maswalimawili kuhusiana na utafiti wa TANCAN.

(1) TANCAN imefikia hatua ipi katika utafiti wake?

(2) TANCAN inafanya utafiti kwenye Hifadhi. Je,ni Sheria ipi inaruhusu utafiti wa Madini ya Dhahabu katikaHifadhi hii? Ni athari zipi za kimazingira zitasababishwa naMgodi mkubwa wa dhahabu kama ukifunguliwa?

Mheshimiwa Spika, kuhusu masuala yanayohusianana Mgodi wa Ng’anzo. Wananchi wa Kijiji cha Ng’anzo, Kataya Ng’anzo wanalalamikia utaratibu uliotumika katikakuendeleza Mgodi wa Ng’anzo. Mgodi huo ulio katika eneola Shule ya Msingi, ulianza miaka iliyopita, lakini kwa kuwauko katika eneo la Shule ya Msingi (Mali ya Kijiji) Serikali Kuuilipendekeza Kijiji kianzishe ushirika na kisha kimtafutemwekezaji ili aihamishe Shule ya Msingi na kuendeleza Mgodihuo.

Mheshimiwa Spika, mambo yanayolalamikiwa nikama ifuatayo:-

(1) Ushirika ulioundwa haukufuata mchakatoshirikishi. Hakuna mkutano Mkuu wowote wa Kijiji ulioitishwa.Hakukuwa na uwazi wa aina yoyote na orodha ya wanaushirika imebaki ni siri.

(2) Mheshimiwa Spika, eneo li l i lotengwakuhamishia Shule ya Misingi halilingani na eneo la sasa la Shuleya Misingi. Eneo lililotengwa linadaiwa kuwa eka 20 wakatieneo la Shule ulipo Mgodi ni takribani eka 60.

(3) Mheshimiwa Spika, wana ushirikahawafahamiki wote, inadaiwa wapo wengi ambaowameingia kwa kutumia nafasi zao katika Uongozi waWilaya, lakini si wana Ng’anzo.

(4) Mkataba baina ya Ushirika na Mwekezajihauko wazi kuhusu Kijiji cha Ng’anzo kitanufaika kutokana

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

170

na Mgodi huo. Nashauri Serikali ichukue hatua za harakakurekebisha hali hii ambayo inaweza kuwa chimbuko lamgogoro usio na kikomo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu tatizo la leseni Na. 0014769(PML) ya Mkombozi Mining Cooperative Society Limited.Ushirika huu wa uchimbaji madini uliomba leseni ya uchimbajimahali paitwapo Kurugwete, Wilaya ya Biharamulo. Ilipataleseni Na. 0014769 ya 9 Juni, 2009, lakini eneo walilopewaCoordinate namba zake zilionesha kuwa liko Geita na siBiharamulo. Hakuna eneo linaloitwa Karugweta, Geita. Mimibinafsi nilipeleka barua yao kwa Kamishna wa Madini mnamomwaka 2011, lakini hadi sasa hakuna hatua yoyoteiliyochukuliwa. Nyaraka husika zimeambatishwa, nashauriSerikali itatue tatizo hili kwa sababu ni la muda mrefu.

MHE. REBECCA M. MNGODO: Mheshimiwa Spika,kuhusu Jiji la Dar es Salaam limeendelea kuwa na umemewa kukatikakatika mara kwa mara, wakazi wengi wa Dares Salaam wameharibikiwa na vifaa vyao vya ndani kamafriji, Microwaves na kadhalika, ingawa Wizara katika hotubayake inasema Transfoma mpya 15 zimefungwa Dar es Salaam,lakini ukweli ni kwamba, bado hali ya upatikanaji wa umememajumbani siyo wa kuridhisha. Nguvu zaidi ielekezwe Dar esSalaam ili kupunguza usumbufu mkubwa uliopo wa umemeusio constant.

Mheshimiwa Spika, utaratibu wa kupata umiliki wamaeneo ya ujenzi wa Viwanda (Industrial Park) kwa ajili yagesi huko Mtwara unaendelea, kwa maelezo ya hotuba yaMheshimiwa Waziri, ujenzi ambao utaongeza fursa za ajirakwa Watanzania.

Mheshimiwa Spika, je, ni viwanda vya aina gani navingapi vitakavyojengwa? Pia tutegemee ajira za aina ganikwa Watanzania? Tusiwe tukaishia kuwa wafagizi, wabebamizigo na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo wadogo wanchi yetu bado hawapati fovour kutoka Mamlaka husika,

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

171

wengi hawana leseni na hata wenye leseni ni wachachesana. Wizara iangalie jinsi ya kuwasaidia wananchi wadogowadogo kuwapatia maeneo na leseni bila kuwasumbua.

Mheshimiwa Spika, vijiji vingi hapa Tanzania vikogizani, Programu ya umeme vijijini (REA) itengewe fedha zakutosha ili kuendeleza umeme vijijini kwa kasi inayoridhisha.Wilayani Arumeru – Arusha kij i j i cha Mkoasenga,Ngarenanyuki, Kilinga na kadhalika, umeme upelekwe katikavijiji hivyo ili Watanzania/wananchi waishio maeneo hayowaweze kufaidika na hivyo wanawake kuondokana na adhakubwa waliyonayo ya ukosefu wa umeme.

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni Mheshimiwa Waziriwa Nishati na Madini, Sospeter Mwijarubu Muhongo, alisemandani ya Bunge lako Tukufu kwamba, wananchi wa Mtwarawataunganishwa umeme kwa bei nafuu, ukilinganisha nawananchi wengine wanaoishi katika maeneo yenye madini(almasi, dhahabu, tanzanite na kadhalika).

Mheshimiwa Spika, wananchi wanaoishi Mereranieneo lenye Madini ya Tanzanite, madini ambayo hayapatikanimahali pengine popote duniani ila hapa Mererani, Je, waowalipewa incentive gani? Je, Wizara haioni kwambakuwapendelea wananchi wa Mtwara kwa kuwaunganishaumeme kwa bei ya chini/nafuu ni kuleta maswali/manunguniko kwa Watanzania wenzao?

Mheshimiwa Spika, endapo sisi ni Taifa moja lenyeumoja, basi ni muhimu sana Watanzania wote wakanufaikana rasilimali zilizopo katika usawa bila kusema au kuruhusuwachache kunufaika kwa kigezo cha kuishi katika eneo lenyerasilimali fulani.

Mheshimiwa Spika, suala la production ya Gesiliangaliwe kwa umakini mkubwa, sera ya Gesi iandaliwe vizurina kwa haraka kwani ndio mwongozo wa jinsi ya kuendesha

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

172

shughuli zote zinazohusu suala la uchimbaji na usambazajiwa gesi.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. JITU V. SONI: Mheshimiwa Spika, naombanichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu na pianiipongeze Wizara ya Nishati na Madini kwa kuleta Bajetiyenye matumaini makubwa na hasa kwa wananchi waVijijini.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwa kuamuakufanya mapinduzi ya nishati bila kukatikakatika. Inaletamatumaini na kuboresha uzalishaji katika Viwanda. Naombanichangie kwa kushauri katika Wizara hii nyeti katika maeneomachache:-

(a) Mheshimiwa Spika, kuhusu Nishati; naombanishauri Serikali katika maeneo yote ambako kutakuwa naMiradi ya kupeleka umeme, izingatie maeneo yote yawananchi na maeneo yenye sifa au uwezo wa kiuchumi nahuduma kijamii gesi iachiwe. Huduma ya umeme ufuatemaeneo ya wananchi katika Miradi ya Babati kupitia REA.Nashauri mradi wa kupeleka umeme kutoka Bonga hadiBeseko ambao sasa unategewa kupita barabara kuu nahakuna vijiji maeneo hayo. Nashauri umeme ungepitia Tarafaya Gorowa katika Kata ya Ayazenda, Vijiji vya Ayasanda naEndanashan, Kata ya Gidai vijiji vya Endadimet na Kata yaBoay vijiji vya Gidefaboska kuelekea Bereko itakuwaimenufaisha Tarafa ya Gorowa ambayo kwa sasa hainakabisa nishati ya umeme na hapo baadaye Kata nne kupataumeme na vijiji 10 kunufaika. Ni Tarafa muhimu kama nishatikukosekana.

Mheshimiwa Spika, pia nashauri mradi wa umeme waKash – Endadosh uende hadi Hurui kama kilometa mbilimbele ambako kuna kijiji kikubwa na pia ni eneo ambapoRais Jakaya Mrisho Kikwete alitoa ahadi kufikisha hudumahiyo pamoja na maji na barabara ambao sasaunatekelezwa. Pia Mradi wa Babati (VETA) ufike katika eneo

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

173

ambalo tunajenga Chuo cha Ualimu na Mafunzo ya Kilimopamoja na Sekondari iliyoko jirani. Pia iende kilomita 2.5kuelekea Kijiji cha Mwinkatsi yenye makazi na huduma yajamii.

Mheshimiwa Spika, naomba pia nishauri kuwa mradiwa umeme unaotegemewa kwenda Magara kutokaShaurimoyo (shamba la Vicky Estate), nashauri umeme upiteKijiji cha Shaurimoyo na Kisangaji ambayo iko pembenikidogo na njia ya umeme kilomita 2.5 na mahali inapoishiasasa usogezwe mbele hadi Shule ya Sekondari na shamba laRift Wall kuelekea geti ya Iyambi katika hifadhi ya ZiwaManyara.

Mheshimiwa Spika, lingine katika upande wa nishati,naomba Serikali i j itahidi kuhakikisha maeneo yateyaliyopitiwa na umeme, umeme huo uteremshwe katika vijijihusika. Naomba pia Wizara kwa kupitia TANESCO iangaliesuala la kuanza kutumia nguzo za Saruji (Cement/Concreteblocks) mapema kupunguza uhaba wa nguzo za miti na piakupunguza uharibifu wa mazingira. Pia itaongeza ajira nanguzo hizo zinadumu kwa muda mrefu zaidi.

Mheshimiwa Spika, pia nashauri Wizara iangalie sualala kupata mikopo kutoka vikundi muhimu vya uzalishajiambako hakuna bajeti iliyopangwa kuendeleza mradi,kikundi kikope katika Taasisi za fedha na kulipa gharama zamradi na baadaye fedha hizo zirudishwe kwa makato katikabili za umeme. Pia Wizara iandae mpango wa kukopeshawananchi gharama za kuunganisha umeme na wawezekulipa kwa mkataba maalum.

Mheshimiwa Spika, nashauri pia Wizara iendeleekutoa elimu kwa umma juu ya matumizi sahihi ya umemena namna ya kupunguza matumizi mabaya ya nishati hiyo.Pia itoe elimu ya namna bora ya kupata nishati ya umemekwa njia mbadala mfano solar, biogas, upepo kwa maeneoyote nchini ambako hakuna uhakika wa kupata nishati hiyokwa kupitia gridi ya Taifa hivi karibuni.

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

174

Mheshimiwa Spika, Wizara iangalie namna ya kupatamradi wa uzalishaji wa nishati kwa kupitia solar kama nchiza Asia zinavyofanya, wanazalisha umeme mwingi kupitasolar kwa sasa, gharama ya uendeshaji kwa baadayeinapungua sana.

(b) Mheshimiwa Spika, katika Sekta ya Madininaomba nishauri kuwa kwani Sera na Sheria ya Usonaraiharakishwe. Itasaidia Sekta hiyo kukuwa na pia kuongezathamani na ajira. Pia kuboresha uthamini huo (Art andCraftmanship). Pia kushauri Serikali kuboresha kituo cha MadiniKanda ya Kaskazini (Arusha) kwa kuongeza vifaa vya mafunzovya kuchonga vito. Arusha inaweza kuwa kituo kikubwa chaVito Barani Afrika. Napongeza kupanga mipango mizurimliyoweka inayotarajiwa kuanza 2014/2015, lakini nashauriwakati tunaposubiri tuanze angalau na mashine 100 kwa sasaambayo haitagharimu Dola za Marekani laki mbili. Itaongezaajira, tutakuwa na waatalam wengi watakaotoka kwaawamu ambayo tukifika kipindi cha kituo kukamilika, basiwatakuwa wameshajifunza kiasi na watakuwa wanakujakujiboresha na kupata mafunzo ya muda mfupi tu kuongezataaluma kazi hii tusiachie Sekta binafsi tu. Serikali ichukuejukumu la kutoa mafunzo.

Mheshimiwa Spika, ahsante na naomba kuungamkono hoja kwa asilimia mia moja.

MHE. ABDULKARIM E.H. SHAH: Mheshimiwa Spika,kwanza naomba kabisa kuipongeza Serikali kwa maana yaWizara hii chini ya Mheshimiwa Waziri Prof. Muhongo naManaibu Waziri wake, Mheshimiwa Maselle na MheshimiwaSimbachawene. Bila ya kuwasahau Katibu Mkuu, Manaibuwake na Wakurugenzi, Mameneja na Vitendo vyote vilivyochini ya Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, Mafia ni Kisiwa na hivi sasa Kisiwahiki kipo katika kuinuka kwa kasi kimaendeleo. Naamini kamamiundombinu yake ikikamilika, kama Gati, Uwanja waNdege, barabara za ndani na kupitia REA umemeukishasambazwa vijijini, Mafia itakuwa ni sehemu nzuri ya

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

175

Kitalii na sehemu nzuri ya mapumziko. Umeme huu ukifikavijijini uchumi wa wananchi utakuwa kwa kiwango kikubwa.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa ushauri. Hivi sasamashine zinazotumika kule Mafia ni mbili zenye uwezo wakuzalisha Kilowatt 900. Mashine hizi hutumia mafuta ya Dizellita 3550 kwa siku. Hivyo kwa mwaka huu hutumia wastaniwa lita 1,286,250 ambazo gharama yake ni Sh.3,235,913,612.15 na ukijumlisha na lita 10,980 za mafuta yavikimisho (LUB OIL) zilizokuwa na gharama ya Sh. 57,513,323.40.Ukijumlisha gharama zote kwa mwaka ni Sh. 3,293,426,935.50.

Mheshimiwa Spika, uhai wa Kebo ya kuzamishabaharini ambayo ina uwezo wa kukaa baharini kwa zaidi yamiaka 25 mpaka 30, nafikiri ndiyo suluhisho pekee kwawananchi wa Mafia na pia itaipunguzia Serikali/Shirika laTANESCO gharama kubwa sana na hizo pesa zitawezakufanya shughuli nyingine katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ukichukua gharama zakuendeshea mitambo, hivyo tena sasa imeongezeka minginemiwili yenye uwezo wa kuzalisha Megawatt 1.2 (Kilowati1,280) kwa miaka 25 bila ya bei ya mafuta kupanda kwakipindi hicho. Naamini siyo kweli kuwa bei haipandi, ni lazimaipande. Gharama yake ni zaidi ya Sh. 164,671,346,776/= nawakati ukilaza Kebo hiyo sifikiri kama itazidi Shilibi bilioni 60.Naiomba sana Serikali ifikirie jambo hilo.

Mheshimiwa Spika, nimetoa mfano huo kupitia jaridala Zanzibar linalochapishwa na Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishatina Ardhi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambayo imesemakuwa imelaza Kebo hiyo kutoka Manyanyani, Tanga mpakaPemba kwa gharama ya Norwegian Krone milioni 400, sawana Shilingi zetu 111,712,910,400/= na gharama hii ni kwakilomita 72 kwa kila kitu mpaka umeme unaweka Pembakwa Mafia ni kilometa 36 tu toka Nyamisati Rufiji hadi Mafia,ndiyo maana naamini Shilingi bilioni 60 zinatosha kulaza Kebo.Naomba mlione hilo wataalam wetu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii kwaasilimia mia moja.

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

176

MHE. ENG. GERSON H. LWENGE: Mheshimiwa Spika,awali ya yote, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri, Prof.Muhungo pamoja na Manaibu Waziri kwa kazi safiwanazofanya katika kuongeza Wizara hii. Naomba kuungamkona hoja hii ambayo naamini utekelezaji wake utafikishanchi hii mahali tunapotarajia.

Mheshimiwa Spika, kuhusu TANESCO, Njombehawana umakini katika kufanya kazi zake. Zaidi ya miakamiwili sasa wamepeleka nguzo Shule za Sekondari za Igimana Wanike lakini mpaka leo kazi imesimama na ukiwauliza,hawakupi jibu la maana. Zaidi ya miaka 15 nguzo zipo karibuna Shule ya Sekondari ya Ilembula lakini hakuna wire walamwendelezo wowote wa mradi huo.

Mheshimiwa Spika, pia TANESCO Njombewanalalamikiwa na wananchi vijiji vya Mhaji, Mdandu,Ilembula ambao wamelipia kuingiziwa umeme lakini ni zaidiya miaka 2 hawajapewa umeme. Nimefuatilia na Ofisi zaTANESCO Njombe na Makambako lakini inaelekea kuna daliliya utapeli unaofanywa na baadhi ya wafanyakazi waTANESCO.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Kuna Wilayayangu ya Wapigangebe kwa kupitia REA, kuna baadhi yavijiji vimeorodheshwa. Naomba maelezo: Kwa nini vijijivingine havijaorodheswa kulingana na Tangazo la Zabunilililotangazwa gazetini na REA vikiwemo Mwilamba, Uhekule,Ujindile, Kijinte, Lyndebwe Lyanduki, Ujwala, Mungelege, ItemiUsuka, Wingilwa , Bonawamu na Kanawalenga?

Mheshimiwa Spika, katika kupeleka umeme Wilayampya, si jaona mpango wa kupeleka umeme eneolitakalojengwa Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging’ombepale Kijiji cha Igwachanya. Ni kweli Kijiji cha Igwachanya kinaumeme wa kiwango cha Kijiji lakini eneo la Makao Makuuyanajengwa, ni takribani kilometa moja ambapo patahitajikupelekewa umeme wa kiwango cha Makao Makuu yaWilaya ambapo patajengwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisiya Halmashauri pamoja na Ofisi nyingine za Serikali nanyumba za watumishi.

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

177

Mheshimiwa Spika, wananchi wangu wamegunduashaba maeneo ya Mtapa na wamejiunga kikundi,wamechimba shaba lakini hawajui soko waende wapi.Naomba Wizara hii itusaidie kutuelekeza soko, lakini piawatalaam wa madini wafike pale ili watoe utalaam namnaya kuendeleza uchimbaji huu wa shaba.

MHE. ZARINA S. MADABIDA: Mheshimiwa Spika, niukweli usiopingika kuwa umeme ni uchumi na uchumi nimaendeleo. Ni muhimu nchi ikaongeza upatikanaji waumeme.

Mheshimiwa Spika, Serikali ni lazima iangalie, pamojana upatikanaji wa umeme, bei ya umeme ipungue. Hii tundiyo itaweza kushusha gharama za bidhaa na watu wengiwaweze kuongeza thamani ya mazao na kuliongezea Taifamapato.

Mheshimiwa Spika, vifaa vya Solar vimekuwavinatozwa kodi kubwa sana na kufanya wananchi wengikushindwa kumudu manufaa ya upatikanaji umeme.Manufaa yake ni mengi sana hata kuonea tu (taa). Ni kwanini basi Serikali isiangalie jinsi ya kupunguza bei ya vifaa vyaSolar ili umeme huo wa Solar uweze kutumika majumbanikuonea, ili umeme wa vyanzo vingine utumike kwenyeviwanda vikubwa na vidogo na na kuongeza uzalishaji?Suala hili nalisema kwa mara ya pili maana mwaka 2012nilisema hili, lakini hakuna hatua iliyochukuliwa.

Mheshimiwa Spika, ili kutatua suala la umeme, nilazima liangaliwe kwa ujumla wake muda wa kuunganishaumeme.

Mheshimiwa Spika, TANESCO imezidiwa, ni vizuri sasaSerikali iangalie jinsi ya kuipunguzia majukumu TANESCO.Unalipa kutaka umeme, lakini inachukua muda mrefu kablaumeme haujaunganishwa.

Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo wadogowanaweza kuiongezea mapato Serikali iwapo Serikali

Page 178: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

178

ingewapa mikopo ili waweze kuzalisha kwa faida nakuchangia kodi kwa Serikali. Siyo hii tu, lakini pia ingewezakutoa ajira za moja kwa moja na hata zisizo ya moja kwamoja kwa kuongeza kipato cha wenye ajira na kuwezakununua bidhaa mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, naipongeza sana Serikali kwamsimamo wake wa kulinda maslahi ya Watanzania wotekwa ujumla kwenye masuala ya upatikanaji na utumiaji wagesi.

Mheshimiwa Spika, naomba nichukue nafasi hii piakuwapongeza sana Mheshimiwa Waziri, Manaibu wotewawili, Katibu Mkuu na Watendaji wote wa Wizara kwa kazinzuri sana wanayofanya, na kuwapa Watanzania imanikubwa sana na Wizara hii.

Naunga mkono hoja.

MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO: Mheshimiwa Spika,naipongeza Wizara kwa kazi nzuri wanayofanya. Wizara inachangamoto nyingi, lakini lazima tuzishinde. Umeme nimaendeleo, ni chombo cha kuleta maendeleo. Hivyo kuwana umeme majumbani ni haki na siyo anasa tena.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa usambazaji umemenchini unaonekana kupendelea sehemu fulani za nchi, zaidiMkoa wa Ruvuma, kwa mfano vijiji vyenye umeme havifikivitano. Huu ni Mkoa unaotoa chakula kwa nchi. Kule Mbingazao la Kahawa linachangia 1/3 ya kahawa ya arabika nchini.Lakini Wilaya ya Mbinga haina Kijiji chenye umeme mpakasasa. Pamoja na kuishukuru sana Serikali kwa kuweka umemekatika sehemu ya Mji wa Mbinga, natumai umemeutapelekwa sehemu zote za Mji za Kihahe, Mitarane, Lesakana Lesonga.

Mheshimiwa Spika, nashauri pia mpango wa kuwekaumeme vijiji idadi ya 10 mwaka wa fedha 2012/2014, naombakwa vile tunayo record II ya MCC Wilaya ya Mbinga ifikiriwekuwekwa katika Mradi huu ili Kata zifuatazo ziwe na vijiji vyake

Page 179: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

179

vipate umeme. Kata ya Ngima, Myangayanga, Luwaita,Mbuji, Langiro, Kipohilo, Ukate, Mpepai, Nyoni, Kitura, Kihangi,Mahuka, Namswee na Litumba Ndyosi.

Mheshimiwa Spika, naomba Wizara iweke nguvu naushirikiano katika mradi wa Umeme Ngaka.

Mheshimiwa Spika, tatizo la fidia kwa wananchi –Serikali kupita RC iliweka ahadi ya kulipa wananchi ifikapotarehe 15/6/2013. Naomba Serikali itimize ahadi yake,wananchi wamekuwa watulivu na tusiwabugudhi.

Mheshimiwa Spika, mazungumzo ya PPA kati yaTANCOAL na TANESCO sasa yaishe.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwapongezawawekezaji kwa nia yao ya kujenga mtambo wa kufuaumeme, lakini kama nchi hii, ina maslahi kwetu? Tunalo tatizola umeme tunataka umeme leo, siyo kesho. Kwa ninitunaachia suala hili mikononi mwa wageni? Je, Serikali kupitiaTANESCO/NDC, haiwezekani kupata fedha za ndani kujengamtambo huo na kuachana na capacity charges? NaombaSerikali ifanya review ya wazo hili bila kuathiri upatikanaji waumeme. TANESCO, wanatumia Shilingi bilioni 5.1 kwa siku.Je, hizi haziwezi kujenga mtambo huo?

Mheshimiwa Spika, ni kweli azma ni kufua umeme nakulisha grid ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, naomba fursa hii itumike kuletaumeme katika vijiji vya Wilaya ya Mbinga kwa kuanzia vijijivya Ntuduwaro na Ruanda. Kwa fursa hii naiomba REAizungumze na NDC/Tancoal na kuona uwezekano wakujenga mtambo mdogo wa MW 5 -10 ili umeme wakeutumike kuwaka katika vijiji vya Mbinga na vijiji vyote vyaMkoa wa Ruvuma.

MHE. MARGARETH A. MKANGA: Mheshimiwa Spika,naipongeza Wizara na Viongozi wake, Mheshimiwa Waziri,Manaibu Waziri wote wawili, Katibu Mkuu, Wakurugenzi wa

Page 180: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

180

Taasisi chini ya Wizara kwa kuonyesha dhamira ya dhati katikajitihada za kutaka kuondoa kwa kiasi kikubwa tatizo la nishatinchini baada ya muda siyo mrefu kuanzia sasa. Dhamira hiiimejionyesha kwenye hotuba ya Wizara na vipeperushivilivyogawiwa. Pongezi sana na mwendeleze dhamira hiikwa uwezo wa Mungu pia.

Mheshimiwa Spika, kazi zinazofanywa na REA ni nzurisana na kama nchi, yaelekea tukichelewa tu kuunda mfukohuu, kwa sababu kwa muda mfupi tangu uanzishwemafanikio yake yamekuwa ya kuridhisha.

Mheshimiwa Spika, la msingi REA wapewe fedha zaruzuku za kutosha ili waweze kusambaza umeme katika vijijivyote Tanzania ndani ya miaka michache ijayo. Zaidinimefarijika kupata maelezo kuhusu ufufuaji wa Shirika laSTAMICO hasa kwa dhamira mpya ya kuwa na hisa katikamiradi watakayoitekeleza nchini. Naunga mkono maoni yaKamati ya Kudumu ya Bunge inayohusika na Wizara hii kuhusuSTAMICO kukabidhiwa Mradi wa kufua Umeme wa Kiwira.Hivyo ni hatua nzuri kwa Serikali kumiliki rasilimali muhimukupitia Mashirika yake.

Hata hivyo, suala la malipo kwa wafanyakaziwaliokuwepo awali, malimbikizo ya mishahara na kadhalika.Lishughulikiwe kabla ya STAMICO kukabidhiwa ili Shirikalisianze kazi kwa matatizo.

Mheshimiwa Spika, ni mara ya kwanza kuona Wizarayoyote ikitenga fedha za maendeleo nyingi kwa asilimia 90%kwa ajili ya miradi yake. Nashauri mfumo huu iwe ndiyo diraya upangaji wa Bajeti katika Wizara zote ili kuleta mageuziya kiuchumi haraka badala bajeti zinapopangwa kwamatumizi almost ya anasa tu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu ujenzi wa bomba la gesitoka Mtwara, yaelekea baadhi ya wananchi wameamuakupinga tu utekelezaji wa mradi huu. Pamoja na elimu yoteiliyotolewa na Wizara, yafaa vyombo husika vifanyeuchunguzi wa kina il i kubaini sababu za upinzani

Page 181: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

181

unaoendelea. Inasikitisha kusikia kwamba hata hii leo vuruguzimetokea wakati Wizara ikiwasilisha hotuba yake Bungeni.Yawezekana kuwa ni hujuma yenye mizizi yake nje yaTanzania.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuchangia hayomachache, naunga mkono hoja na kuwatakia Wizara herikatika kutekeleza mikakati waliyojipangia.

MHE. SELEMANI S. JAFO: Mheshimiwa Spika,naipongeza Wizara kwa kazi kubwa inayoifanya juu yausambazaji wa umeme vijijini.

Mheshimiwa Spika, Wizara na Shirika la TANESCO kwaujumla imefanya juhudi kubwa kupeleka miundombinu yaumeme. Tatizo kubwa ni speed ndogo ya mkandarasiSIMBION, Transforma bado hazijawekwa kwa line ya Mlandizihadi Mzenga. Kwa line inayotoka Kisarawe Mjini hadi Msanga,Mkandarasi SIMBION amefanya kwa speed ya kinyonga.Naiomba Serikali iweke mkazo kwa mkandarasi ili umemeuwafikie wananchi.

Mheshimiwa Spika, katika Sekta ya Madini naiombaSerikali iwasaidie wafanyakazi wanaofanya kazi katikaMakampuni ya Madini. Kuna wafanyakazi wanasimamishwakazi na kisha wanawekwa katika orodha ya Black List.Mfanyakazi huyo hawezi kupata kazi kokote kwenye Kampuniya Madini yoyote. Naomba kauli ya Serikali: Je, ina mkakatigani wa kuzuia jambo hili ovu kwa wafanyakazi waTanzania? Pia kuna wafanyakazi wanaopatwa magonjwawakiwa kazini katika Makampuni ya Madini wanawatelekezabila huduma ya uhakika. Naomba kupata msimamo waSerikali katika hili.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali isiyumbe katikaujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara kwenda Dar esSalaam.

Naunga mkono hoja.

Page 182: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

182

MHE. ANGELLAH J. KAIRUKI: Mheshimiwa Spika,napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri,Waheshimiwa Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu, Makamishnawote na Wakuu wa Taasisi zilizoko chini ya Wizara hii ya Nishatina Madini.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Wizara kwa kuja nampango kabambe wa kuhakikisha Vituo vya Afya na Shulezote zinapata umeme. Ni jambo jema sana, kwani itasaidiasana kuleta ufanisi katika utoaji wa huduma, lakini piaitaboresha maisha na kuleta tija.

Naomba sana kwa niaba ya Wizara ya Katiba naSheria na Mahakama ya Tanzania, mtusaidie Mahakama zetunchini, kuanzia katika Vijiji vyetu hadi Mikoani (Mjini). Ngazizote nazo ziingizwe katika mpango huu muhimu, kwanihuwezi kuamini, ziko Mahakama nyingi nchini hazina umeme,hata Dar es Salaam zipo pia. Hii inatukwamisha sana katikamipango mbalimbali tuliyonayo ya kutumia TEHAMA katikauendeshaji wa mashauri Mahakamani. Uchapaji wa nakalaza hukumu kwa wahusika kwenye mashauri na washitakiwawengi inafika wakati wanashindwa kukata rufaa dhidi yamaamuzi ya Mahakama, kwani inabidi Mahakama za Wilayanzima zikachapwe nakala za hukumu na miendo yamashauri/kesi, katika Ofisi za Wilayani. Tunaomba sanamtusaidie katika azma hii itatusaidia sana na wananchiwatanufaika sana.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naungamkono hoja kwa asilimia mia moja.

MHE. ALIKO N. KIBONA: Mheshimiwa Spika, pongezikwa Wizara na Watendaji wote, hongera sana.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Kiwira Coal Mine, hali ikojesasa? Kwa 2013/2014?

Mheshimiwa Spika, Ileje ina vijiji 71. Kati ya hivyo, nivinne tu vina umeme. Je, miradi ya vijijini itaanza Ileje kwakuwa wanakwenda kusaga mahindi nchini Malawi? Umeme

Page 183: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

183

kutoka Ikuti Rungwe kwenda Ileje inapitia vijiji kadhaa kablaya kufika Itumba Makao Makuu kupitia Shikunga, Ibaba,kutokea Kijiji cha Powenda. Katikati ya Bwenda kuna Kataya Ngulilo; naomba ijumuishwe katika mpango. Aidha, katiya Sanga na Kalembo Kata ya Ngulugulu.

Mheshimiwa Spika, mwisho, mbele kidogo ya Ibaba,kuna Kata ya Itale na Nola. Naomba iongezwe.

MHE. ZABEIN M. MHITA: Mheshimiwa Spika, je, Serikaliinaweza kututhibitishia kuwa fedha ya kutekeleza miradiiliyopo kwenye REA II ipo? Na kuwa, vijiji kutoka Babatiambako kuna umeme kupitia vijiji vya Bereko hadi Kolompaka Kondoa vitapatiwa umeme hasa ikizingatiwa kuwaumeme unapita juu ya vijiji hivyo?

Naunga mkono hoja.

MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO: Mheshimiwa Spika,Wizara ya Nishati na Madini ni miongoni mwa Wizara ambayoni tegemeo kubwa linalokuza uchumi na kuongeza pato laTaifa litokanalo na vyanzo husika kama vile machimboyanayozalisha dhahabu, almasi, tanzanite, pamoja na mkaawa mawe, lakini vilevile vyanzo maji ambavyo vinazalishaumeme.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Tanzania siyomasikini. Hata hivyo, imepelekea Watanzania walio wengikuishi katika umasikini kutokana na kutotilia maanani maeneoya uzalishaji ambayo yangaliwezesha kuwapatia njiaWatanzania walio wengi. Ni wajibu wa Serikali sasakuhakikisha kwamba maeneo yote ya uzalishaji wa madininchini, wazawa wanapewa kipaumbele cha kuwapatiwavibali juu ya uchimbaji wa madini.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la uzalishaji waumeme, Tanzania bado halijaweza kutosheleza mahitaji yawananchi Mijini na Vijijini. Haya yote yanatokana na ubunifumdogo ambao ama wataalamu wetu wanao, auwamekosa uaminifu na uadilifu juu ya ukusanyaji wa mapato

Page 184: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

184

na njia mbadala ya namna ya kuwafikishia umemewananchi Mijini na Vijijini. Hata hivyo, Wizara ina wajibu wakuangalia uwezo wa viwango vya mapato ambayo kilaMtanzania anapata. Watanzania ni masikini, hivyo ni lazimatuangalie uwezo wao wa mapato.

Mheshimiwa Spika, umeme ni ukombozi, umeme niuchumi, umeme ni maendeleo endelevu. Hivyo, ni wajibuwa Serikali kuhakikisha kwamba Tanzania inazalisha umemewa kutosha na unawafikia Watanzania popote walipo, Mijinina Vijijini. Endapo suala la umeme litachukuliwa kuwa ni sualala haki ya msingi na haki ya ukombozi wa mwanadamu nakinyume chake, ichukuliwe kuwa ni kinyume cha haki zabinadamu.

Mheshimiwa Spika, suala zima la uchimbaji wa gesini suala ambalo litaweza kupunguza makali yatokanayo naupandaji holela wa bei za umeme nchini, hivyo Serikali inawajibu wa kutanzua migogoro na mizozo iliyojitokeza ilikuhakikisha kwamba suala hili limepatiwa ufumbuzi wa kufaaili uzalishaji wa gesi uweze kufanyika na hivyo kuwapatiaWatanzania walio wengi ajira, lakini na kuwaondolea ukaliwa maisha.

MHE. VINCENT J. NYERERE: Mheshimiwa Spika,kwanza, nitoe masikitiko yangu kwa yale yanayotokea Mkoawa Lindi na Mtwara.

Mheshimiwa Spika, napenda kutoa pole kwa wotewaliopatwa na majanga ya kuchomewa nyumba, magarina mali nyingine na hasa pole kwa familia za waliopotelewana wapendwa wao katika vurugu za Mtwara kwa namnamoja au nyingine, kwa ambao wamepoteza maisha.

Mheshimiwa Spika, nakubaliana kabisa na kaulimbalimbali za Serikali kuwa RasIlimali za nchi ni mali ya nchina siyo mali ya mtu mmoja mmoja au kikundi au Chamachochote cha kisiasa au cha kidini. Lakini ijulikane wazi piakwamba Serikali haipo Dar es Salaam peke yake, bali piaVijijini na Mijini hasa kule ambapo Rasilimali zinatoka.

Page 185: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

185

Mheshimiwa Spika, leo ukienda China utajifunzamengi sana kutokana na mgawanyo wa maendeleouliotapakaa maeneo yote, na siyo katika Miji Mikuu pekeyake. Hicho ndiyo kilio kikubwa kwa Wana-Mtwara na ndiyoujamaa aliojifunza Mwenyekiti wa Kwanza wa CCM naaliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano waTanzania - Mwalimu Julius K. Nyerere, alipanga kuyafanya hayohapa kwetu ila waliopo sasa wamepuuza.

Mheshimiwa Spika, tunaweza kutupia lawana baadhiya watu walisababisha vurugu na hili ni jambo rahisi sanasana kutamkika mdomoni, lakini tukasahau Chamakinachounda Serikali, sasa hakiaminiki tena, kwa kuwafumbiamacho wabadhirifu wa mali ya umma na kuachawajimilikishe mali kinyume cha utaratibu na kuwachukuliahatua kali maskini, huku matajiri wakiwa huru marawafanyapo uhalifu. Kumefanya Chama kinachotawala kuwana mporomoko wa kasi wa kutoaminiwa tena na wananchi.Ikumbukwe pia ahadi lukuki zilitolewa wakati wa kampeniza uchaguzi, imepelekea kabisa kutoaminika tena kwa kaulizitolewazo na Serikali.

Mheshimiwa Spika, ni vizuri Chama kinachoundaSerikali basi kiangalie upya namna nyingine kabisa ya kurudishaimani yake kwa umma ili kauli zake ziaminike.

Mheshimiwa Spika, leo tunachokishuhudia nimwendelezo wa kauli zisizoaminika tena toka Serikaliniambazo zimepelekea kabisa uvunjifu wa amani hukoMtwara, kwani ahadi nyingi sana zil itolewa na sasazimesahaulika na hiyo ndiyo imepelekea elimu na yoteyatolewayo juu ya gesi ya Mtwara, sasa imeonekana hainaukweli wowote. Hiyo ndiyo sababu kubwa ya vurugu na siyomaamuzi ya Wizara au hotuba ya Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Spika, napenda kutoa rai kwa Serikalikufanya tathmini ya kina kwa ahadi na kauli zake nakuzitekeleza kwa wakati ili kauli zijazo ziweze kuaminiwa nautekelezaji wake uwe wa ufanisi.

Page 186: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

186

Mheshimiwa Spika, yamekuwepo malalamiko yamuda mrefu sana kwa Watanzania kutosomewa mapatoya rasilimali na mchango wake katika kujenga Taifa.

Mheshimiwa Spika, ni vizuri sasa uwepo utaratibumzuri wa kusoma kila mwaka mapato ya madini na rasilimalinyingine za nchi na kueleza Watanzania fedha hizo zimefanyanini na hiyo itaondoa kama siyo tu kupunguza taharuki kwawananchi.

Mheshimiwa Spika, najua kama Wizara inayo nianjema ya kusaidia amani na kufanya madini na gesi ikiwemomafuta kuwa baraka badala ya laana, basi mawazo hayayatafanyiwa sana kazi na kupewa umuhimu.

Mheshimiwa Spika, ni vizuri kama tutaamua kwadhati kabisa kutoa punguzo kwenye uwekaji wa umemekwenye mashule yetu Vijijini, basi vijana wetu wataweza sanakusoma Sayansi vizuri na kuongeza muda wa ziada wakujisomea na kupata matoke mazuri ya kuwa nawanasayansi wazuri huko mbele ya safari.

Mheshimiwa Spika, linguine ni kuhusu umeme kwa njiaya mkopo. Nyumba ni kitu kisichohamishika na ni nyumbandiyo iwekwayo umeme.

Mheshimiwa Spika, napendekeza Wizara iwekeutaratibu wa kuwakopesha umeme (installation) na waowaweze kulipia polepole kila mwezi au kila wanapolipakwenye manunuzi ya Luku.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Benki ya NMB ipo karibuWilaya zote hapa Tanzania, basi ni vizuri sana Wizara ikaonani vyema kuwatumia wataalamu wao na jinsi gani ya kuwekamikataba vyema ili TANESCO waweze kuwapa watu wengizaidi kupata umeme na pia shirika liweze kujikusanyia mapatozaidi na kuweza kujiendesha kwa faida, kwani watumiajiwatakuwa wengi wanaolipa Ankara zao ambazo ndiyotegemeo la mapato la Shirika la Umeme la TANESCO.

Page 187: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

187

Mheshimiwa Spika, utaratibu huu najua utanufaishawengi na hasa wawekezaji wa viwanda vya kati na vidogoili tuweze kuwa na wawekezaji wengi ambao watavutiwana aina hii ya uwekaji umeme na kuongeza ajira, pato lamtu mmoja mmoja na pato la Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, itakuwa vigumu sana kuepukafujo migodini kama hatutatenga maeneo ya wachimbajiwadogo wadgo na ni vizuri sasa tukaweka sana utaratibuwa kuwatengea maeneo ili basi kuwanufaisha wananchihasa katika maeneo yanayozunguka mgodi.

MHE. FAITH M. MITAMBO: Mheshimiwa Spika, miminitaongelea kwanza Sekta ya Madini, wachimbaji wadogowadogo kutolipia leseni zao za kila mwaka; kuficha mapatohalisi ya dhahabu na madini mengine wanayopata ilikukwepa kodi; migogoro ya mipaka ya vitalu; utoaji wa lesenindogo ndogo kwenye maeneo ya leseni kubwa kubwa amaleseni za utafiti; viongozi na watendaji wa Sekta ya Madinihasa Ofisi za Kanda Mtwara kukiuka taratibu ambazo zikokwenye Sheria ya Madini ya mwaka 2010; na viongozi wangazi ya vijiji kutoa vibali na kuruhusu wachimbaji wadogowadogo kuchimba maeneo yenye leseni za Pl au PM.

Mheshimiwa Spika, kuhusu wachimbaji wadogowadogo kutolipa lesseni zao za mwaka; wachimbajiwadogo wadogo kutolipa leseni zao kwa wakati, ni tatizona kama Mheshimiwa Waziri alivyosema katika hotuba yake,wanalipunguzia Taifa mapato. Ushauri wangu ni kwambauwekwe muda maalum kwamba wachimbaji hawawadogo kama hawalipii leseni zao kufikia muda fulani, lesenizao zifutwe kama ambavyo sasa Serikali imefanya.Nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa kufuta leseni hizo,itasaidia sana kuleta discipline ya ulipiaji wa leseni zao kwamuda unaotakiwa.

Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo wadogo nikweli hawatoi takwimu halisi na za kweli kwa Serikali kuhusukiasi wanachopata kwa nia ya kukwepa kodi. Wilaya yaLiwale kuna machimbo mengi sana. Machimbo yaliyoko

Page 188: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

188

katika Kij i j i cha Kibutuka, wanayaita Kipelele Chini,yanakumbwa na hali hii. Wachimbaji wadogo wadogowamevamia eneo hilo na Wilaya inashindwa kupatatakwimu halisi ya mapato kutokana na wachimbaji hawa,walioko katika kijiji hiki.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali ichukue hatua zakutembelea na kufanya ukaguzi katika machimbo haya yaKubutuka kwa nia ya kufanya ukaguzi i l i kuona: Je,wachimbaji hawa wadogo wadogo wana hati miliki zakuchimba maeneo hayo? Je, wamefuata taratibu zote zaSheria za Madini za mwaka 2010? Je, mapato wanayopatawanaripoti wapi na wanalipa kodi wapi? Nina uhakikawachimbaji hawa ambao wengi wao ni kutoka nje ya Wilayaya Liwale, wanakiuka taratibu na Sheria ya Madini ya mwaka2010.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mgogoro ya mipaka yavitalu na utoaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo wadogokwenye maeneo ambayo tayari yana leseni ya PL ama leseniza uchimbaji PM; kuna migogoro tayari eneo la KibutukaLiwale ambapo wachimbaji wadogo wadogo wamevamiakwenye eneo hilo na kuendelea kuchimba. Nina mashakakama wachimbaji hawa wadogo wana lesseni za kuchimbaeneo hilo. Eneo hili tayari lina leseni kubwa za PL, lakiniwachimbaji hawa wadogo wadogo wanadai wamepataleseni za kuchimba kutoka Ofisi za Madini kanda ya Mtwara.

Mheshimiwa Spika, hivi inakuwaje wachimbajiwadogo wadogo hawa wanaruhusiwa kufanya shughuli zaoza uchimbaji kwenye maeneo ambayo tayari yana umilikina mmliki anayalipia? Wachimbaji hawa sasa wanalipiamaeneo hayohayo katika Ofisi zipi?

Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo wadogowamevamia kwenye maeneo ambayo tayari yana leseni zaPl, na kuendelea na shughuli zao ndani ya maeneo hayo kwakutumia Sheria ya Ardhi ya mwaka 2005. Viongozi wa Serikaliza Vijiji pia wanawaruhusu wachimbaji wadogo wadogo,kuchimba na kuwaruhusu kulipia ardhi katika Serikali ya Kijiji

Page 189: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

189

kwa kufuata Sheria ya Ardhi ya mwaka 2005. Viongozi waSerikali za Vijiji wameshindwa kutofautisha kati ya Sheria yaMadini ya mwaka 2010 na Sheria ya Ardhi ya mwaka 2005,na hivyo wanasababisha vurugu na mitafaruku isiyo na tijakwa Serikali.

Mheshimiwa Spika, naomba Wizara ya Nishati naMadini na hasa Ofisi za Madini Kanda ya Mtwara, ichukuehatua za haraka kufuatilia yanayoendelea katika eneo hili laKibutuka ili katika siku zijazo tatizo hili lisije likawa kubwa nakusababisha vurugu na migogoro isiyotarajiwa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu umeme wa gesi kuletwaWilaya ya Liwale; kwanza, nishukuru Wizara na hasa TANESCOkwa jitihada zilizofanywa za kuupatia mji wa Liwale umemewa uhakika, sasa hivi tuna umeme wa uhakika na kila mtumwenye kuhitaji umeme atapata.

Mheshimiwa Spika, pamoja na umeme huu ambaounazalishwa kwa kutumia generator, bado ninaendeleakuomba sana Serikali, Liwale tupatiwe umeme na gas, kwasababu umeme huu na generator ni ghali ukilinganisha naumeme wa gas kwa sababu generator hizi zinatumia kiasikikubwa sana cha mafuta kila mwezi.

Mheshimiwa Spika, katika Mkoa wa Lindi, ni Wilayaya Liwale pekee ndiyo iliyobakia kuunganishwa ama kupataumeme wa gas. Wilaya zote Mkoa wa Lindi zina umemeunaotokana na gas.

Mheshimiwa Spika, katika takwimu na data alizozitoaMheshimiwa Muhongo, ameiweka katika orodha yake Wilayaya Liwale ya 43, na kwamba amesema Wilaya ya Liwaleitaunganishwa katika umeme wa gas kutokea Ruangwa, nani Sera ya Wizara ya Madini na Nishati kwamba kila kijijiambacho umeme huo utapita, kitapata umeme. Wilaya yaLiwale tumewekwa kwenye Budget hii ya mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, ni matarajio yangu kwamba,Wilaya ya Liwale itaunganishwa kwenye umeme huu wa gas

Page 190: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

190

mwaka huu, na ikumbukwe pia kwamba imo kwenye ilaniya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010. Hata hivyo, umemewa gas utapunguza sana gharama za mafuta ambayo ninauhakika kiwango kikubwa sana cha mafuta ya kuendesheagenerators zilizopo kinatumika kila mwezi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa asilimiamia moja.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, Wizarahii ni muhimu sana katika ustawi wa Taifa letu. NaiombaSerikali itenge Bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuwezesha Wizarahii ili iweze kufanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Spika, gharama za umeme kupelekwakwa wahitaji ni kubwa sana. Ni muhimu Serikali ikaangaliaupya juu kupunguza gharama ambazo ni kubwa sanazainazomwathiri mwananchi wa kawaida mwenye kipatocha chini.

Mheshimiwa Spika, lingine ni kuhusu umeme wa vijijini(REA). Ili nchi iendelee, kunahitajika kupata umeme vijijiniambao utasaidia sana wananchi wa vijijini kukuza uchumiwao. Nilikuwa naishauri Serikali ihakikishe inaongeza fedhaza kutosha kuhakikisha Wakala wa Umeme Vijijini anakuwana pesa za kutosha ili aweze kusambaza umeme vijijini.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri aliahidi kutoahuduma za umeme katika vij i j i vya Kabungu,Mchakamchaka, Ifukutwa, Majalila (Mpanda ndogo).

Mheshimiwa Spika, naiomba sana Serikali ihakikisheinapeleka umeme katika maeneo haya. Kama Serikaliitapeleka umeme katika maeneo haya utatatua tatizo katikaTaasisi za Shule za Sekondari zilizo katika Kata ya Kabunguna Kata ya Mpanda ndogo.

Mheshimiwa Spika, suala la gesi ni lazima litoleweelimu ya kutosha kwa wananchi wa maeneo yanayotoa gesihasa Mikoa ya Mtwara na Lindi.

Page 191: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

191

Mheshimiwa Spika, gesi ni rasilimali ya nchi na siyomali za watu wa eneo fulani. Ni vyema Serikali iwaelimishewananchi kwa nguvu na kudhibiti wale wote wanaopotoshawananchi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. JUMA A. NJWAYO: Mheshimiwa Spika, napendakuchukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri na NaibuMawaziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote kwa kukabilianana changamoto mbalimbali. Nina maoni yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, mosi, natoa hongera sana kwaWizara hii kuongeza muda wa punguzo la kuunganishiwaumeme hadi Juni, 2014 kwa wananchi wa Mtwara na Lindiila tuhakikishe pia vitendea kazi na nyaraka muhimuzinapatikana kirahisi ili isitokee tena kulazimika wananchikuomba ongezeko la muda.

Mheshimiwa Spika, pili, Wizara ihakikishe miradi yaupelekaji umeme vij i j ini inatekelezwa kwa wakati.Kucheleweshwa kwa miradi kunakatisha tamaa na wakatimwingine kutoa mwanya kwa wachochezi kupenyeshauongo na taarifa zisizo rasmi.

Mheshimiwa Spika, tatu, napendekeza Serikali/Wizarahii kuwaelimisha Halmashauri zote nchini kuanza utaratibuwa kuweka Bajeti kila mwaka kwa ajili ya umeme angalaukijiji kimoja kila mwaka. Hii itasaidia sana kuongeza kiwangochetu cha umeme badala ya kungoja TANESCO/REA kutafutafedha kwa ajili ya umeme pekee. Ziko Halmashauri zenyemapato na uwezo wa kutosha kujiunganishia umeme,zikihamasishwa na kueleweshwa.

Mheshimiwa Spika, nne wakati umefika sasa kwendana kasi ya kuhakikisha TANESCO haifanyi kila kitu. TuanzisheTaasisi za kusambaza umeme. TANESCO izalishe tu ili kuletaurahisi wa utendaji.

Mheshimiwa Spika, tano, iwe marufuku kijiji chochote

Page 192: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

192

kurukwa au kutounganishwa na umeme inapotokea kunal ine imetengenezwa, kwani kuchomwa kwa nguzokunakotokea kwenye baadhi ya maeneo chanzo chake niwivu wa kuona wenzao wameteremshiwa Transforma nahivyo wao hawana.

Mheshimiwa Spika, sita, ule mchango unaokwendanje ya nchi pamoja na kuchakata madini kuangaliwe upya,kwani tunapoteza ajira nyingi.

Mheshimiwa Spika, mwisho, naunga mkono hoja.

MHE. SAIDI A. ARFI: Mheshimiwa Spika, naombakupata maelezo ya kina juu ya mambo mawili.

Mheshimiwa Spika, mosi, ni lini generators ambazotumekuwa tukiahidia ikiwa pamoja na Mheshimiwa Raiskusema jambo hilo. Je, ni lini sasa generator hizo zitapelekwaMpanda? Aidha, nataka kujua mpango wa matengenezoya generator zilizopo ambazo zinaharibika mara kwa mara.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, wachimbaji wadogowadogo ni wa muda mrefu, hauna ufumbuzi, matokeo yakemnapandisha ada ya viwanja na leseni ili Watanzaniamasikini washindwe na kuwapa wenye fedha na wageni.Eneo la mgogoro wa Mpanda ni eneo lao kuhodhiwa namatapeli na viongozi (waliokua) kumiliki eneo hilo ambalowameshindwa kuliendeleza na kulimiliki tena kwa jinalinguine, lakini ni watu wale wale.

Aidha, yapo madai na malalamiko juu ya Maafisawenu wa madini Mpanda kushirikiana kuuza maeneo aukujimilikisha maeneo potential, na wachimbaji wadogowadogo wapo tayari kuwataja na maeneo waliojimilikisha.Naitaka Wizara ishughulikie tatizo hili na kufuatilia.

MHE. YUSSUF HAJI KHAMIS: Mheshimiwa Spika, naanzakwa kumshukuru Mungu kwa neema ya uhai na afya njemanikiwa Bungeni. Nachukua fursa hii adhimu kuipongezaWizara kwa kazi nzuri kwa maslahi ya Taifa na watu wake.

Page 193: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

193

Nampongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na Manaibu wakewote wawili kwa kusimamia vizuri Wizara yao.

Mheshimiwa Spika, pamoja na nia nzuri ya Serikalikupandisha bei ya mafuta ya taa, ilingane na ile ya mafutaya diesel kwa ajili ya kuondoa uchakachuaji wa mafuta yadiesel, imeathiri kwa kiasi kikubwa wananchi walio wengihasa wale wa vijijini ambao ndio wahusika wakubwa wanishati hii ya mafuta ya taa.

Mheshimiwa Spika, ukweli ni kwamba wananchiwengi vijijini hawafaidiki na huduma muhimu ya umeme kwasababu mbalimbali ikiwemo kutokufika umeme sehemunyingi za nchi yetu, au uwezo wa wananchi kuwa mdogokimapato na kushindwa kuutumia kutokana na gharamazake kuwa kubwa. Kwa hiyo, wote hawa ni watumajiwakubwa wa mafuta ya taa.

Mheshimiwa Spika, athari kubwa ya uchafuzi wamazingira imekuwa kubwa sana kutokana na watu vijijinikutumia nishati mbadala ya kuni kwa bei kubwa ya mafutaya taa ambayo hawaimudu. Mimi naiomba Serikali, ile faidaya fedha ya mafuta ya taa ipelekwe REA kwa huduma yaumeme vijijini na kwa maslahi ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo wadgo wamadini wamekuwa na kil io cha muda mrefu kwakutotendewa haki katika sehemu mbalimbali za shughuli zakazi zao. Wanakosa elimu ya ufanisi kati shughuli za kazi zao,wanakosa fedha za kuwawezesha, wanakosa zana za kisasakatika uchimbaji, wanakosa soko endelevu la kuuza bidhaazao.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali iangalie kwamakini sana wachimbaji wadogo wadogo, wawezeshwekifedha, kielimu na nyanja zote muhimu katika shughuli zaowafanye kwa ufanisi.

MHE. AGRIPINA Z. BUYOGERA: Mheshimiwa Spika,kwanza napongeza kazi nzuri inayofanywa na REA. Imeanza

Page 194: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

194

kusambaza umeme katika Zahanati na Vituo vya Afya Jimbola Kasulu Vijijini. Niombe mpango huo huo upelekwe katikaShule zote za Sekondari.

Mheshimiwa Spika, pili, nahitaji majibu sahihi yakumaliza tatizo la wachimbaji wa chokaa Kijiji cha Makereambao walipewa leseni na Wizara, lakini watu wa Maliasilina Mazingira wanawazuia kuchimba madini ya chokaa.Mheshimia Naibu Waziri wa Madini analijua tatizo hilo vizurina niombe alitolee maelezo ili vijana wenzake wapatemaisha bora. Mbaya zaidi, chokaa imechimbwa tanguuongozi au utawala wa Mkoloni. Ni vyema wananchiwapewe elimu nzuri ili wanufaike na madini hayo.

Mheshimiwa Spika, mwisho, naomba wataalam wautafiti wa madini waende Kijiji cha Nyenge Wilayani KasuluJimbo la Kasulu Vijijini ili kubaini madini yanayopatikana hapokwa maslahi ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Spika, naombanichukue fursa hii nami nichangie katika Wizara hii muhimuya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Spika, naomba nianze kuchangia katikaeneo la umeme vijijini.

Mheshimiwa Spika, kama kuna jambo ambalolitabadili maisha ya wananchi wetu wa vij i j ini, nikuwapelekea nishati muhimu ya umeme.

Mheshimiwa Spika, tumekuwa na changamoto yamuda mrefu kwamba wakulima wetu hawapati tija katikashughuli zao za kilimo, na hali hii inatokana na ukwelikwamba wanapata bei ndogo ya mazao yao kwa kuwawanayauza yakiwa katika hali ghafi.

Mheshimiwa Spika, njia pekee ya kuwawezeshawananchi wetu kuongeza thamani ya mazao yao ili wapatebei nzuri na faida nzuri ni kuwapelekea huduma ya umeme.

Page 195: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

195

Mheshimiwa Spika, jambo lingine muhimu ambalotunatakiwa tufanye ni kuimarisha Shirika la Maendeleo yaPetrol (TPDC).

Mheshimiwa Spika, TPDC ndiyo shirika ambalolinaiwakilisha Serikali kama mbia katika mikataba yote yautafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi ambayoinafanywa na Makampuni makubwa yenye uwezo namaarifa ya hali ya juu.

Mheshimiwa Spika, ni lazima tuiwezeshe TPDC ili iwezekuwasimamia vizuri wawekezaji katika Sekta ya Gesi.

MHE. ENG. ATHUMAN R. MFUTAKAMBA: MheshimiwaSpika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

Mheshimiwa Spika, katika kitini cha mradi wa gesiasilia ya Songosongo ukurasa wa nne, Equality ShareholdersPreferred B TDFL $ 4 million 8%: Je, FMO $ 14.4 commonshare holding ni ngapi? Nimejumlisha:-

CDC 54% $ 38.6MFMO ?% $ 14.4MTDFL 8% $ 4.0MTPDC 29% $ 3.0MTANESCO 9% $ 1.0MJUMLA 100% $ 61.0M

Naomba ufafanuzi FMO share Equity $ 14.4M, lakini0%?!

Mheshimiwa Spika, naomba mrahaba wa kokotozinazochimbwa na RAHCO ya TRL tulipwe, kwani tangu reliijengwe mwaka 1905 mpaka 2013, hakuna mrahaba Kijiji chaTura. Wizara itusaidie tulipwe ili Tura ifanye miradi yamaendeleo. Mheshimiwa Simbachawene, Naibu Waziri waNishari na Madini alifika Tura na kuwaahidi wananchikwamba watalipwa. Walipwe sasa!

Page 196: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

196

Mheshimiwa Spika, umeme Jimbo la Igalula, Mbuyuni,Kinamagi, Kigwa ‘A’ na ‘B’, Igalula, Imalakaseko, Gowekona Nsololo; Vijiji hivi viko kwenye mpango wa REA. Ahadi hiikatika ilani ya Chama cha Mapinduzi ni tangu mwaka 2000,2005 na 2010. Naomba kabla ya mwaka 2015 umeme ujevijiji hivi na vingine vipewe kwa solar. Viko 50. Ahsante, Nimradi namba 109 kwenye ramani.

Mheshimiwa Spika, Panel ya Peer Report (Cape TownJuzi) ya Kofi Annan inasema mwaka 1998 – 2011 dhahabuiliyouzwa Tanzania ni US$ 11.3 billion. Serikali inapata U$ 450mhii inakuwaje? Mheshimiwa Waziri toa maelezo.

Mheshimiwa Spika, Vijiji vya Loya, Tura, Kizengi naMalongwe pamoja na Karangasi kuna Kimberlite pipes zaalmasi kutoka ukanda wa Singida na mgodi mmojaulifungwa wa Loya. Watafiti wako Mheshimiwa Waziriwafuatilie ili wana-Igalula wafaidike.

Mheshimiwa Spika, naomba mrejesho.

MHE. NYAMBARI C.M. NYANGWINE: MheshimiwaSpika, napenda kuchukua nafasi hii kuchangia Wizara yaNishati na Madini. Natoa pongezi kwa Watendaji wa Wizarahii kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mrahaba wa Halmashauriya Wilaya ya Tarime; naomba mgodi wa Bariadi North MaraWilayani Tarime ulipe Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kiasicha US$ 800,000 ambazo hazikulipwa toka mwaka 2002 –2005. Tafadhali nasisitiza hilo lizingatiwe.

Mheshimiwa Spika, mradi wa wachimbaji wadogowadogo ni muhimu ili kuepuka migongano isiyo ya lazima.Hivyo basi, naiomba Wizara iweke sera ya:-

(1) Kuwabaini wachimbaji wadogo wadogo hao niakina nani?

(2) Mahitaji yao muhimu ni yapi?

Page 197: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

197

(3) Ni wadogo kiasi gani?

Mheshimiwa Spika, kuhusu Mikataba ya Elimu, Afya,Maji, Umeme na Barabara, nashauri wawekezaji watimizeahadi zao kama walivyowekeana na wanavijiji.

Mheshimiwa Spika, nashauri mgodi wa Barrick NorthMara (Nyango) ulipe fidia halali kwa wananchi wa Tarime.

Mheshimiwa Spika, ni muhimu Wizara hii ishirikiane naWizara ya Mambo ya Ndani ili kukomesha mauaji ya raia yasiyoya lazima.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mahusiano mabaya yamwekezaji/wananchi; nashauri elimu itolewe ili kuwaelimishawananchi wanaozunguka migodi umuhimu wa uwekezaji.Pia wawekezaji watimize wajibu wao.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Tarime ina vijiji vingi sanavipatavyo 130. Naishauri REA kupeleka umeme katika Kataza Bumera, Susuni, Nyandoto, Gorong’a, Nyarukoba,Bungurere, Kangariani, Getagasembe, Komaswa, Gibaso,Masanga, Kegonga na vijiji vingine vyote.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Spika,pongezi Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na Watendaji wotekwa kuandaa hotuba hii na kuileta Bungeni.

Mheshimiwa Spika, umeme ni chachu kubwa sanakwa maendeleo na kuinua uchumi wa Taifa na wananchiwote. Idadi ya wananchi wanaotumia umeme vijijini badoni ndogo sana, inakatisha tamaa.

Mheshimiwa Spika, juhudi bado zinahitajikakuhakikisha programme ya REA inawezesha ili umemeuwafikie wananchi wengi wanaoishi Vijijini. Pesa/fungu la REAliongezwe kwa kutafuta fedha pahali popote hata kwamkopo ili miradi ya REA itekelezwe.

Page 198: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

198

Mheshimiwa Spika, Tanzania tunayo makaa ya mawehuko Kiwira, Ngaka, Mchuchuma, na kadhalika. Ipo miradiambayo imeanza uzalishaji wa makaa ya mawe, yanauzwanchi za nje. Ni kwa nini makaa hayo hayatumiki kwenyeviwanda vyetu hapa nchini? Ni kwa nini makaa hayahayatumiki kwa matumizi ya kupikia nyumbani?

Mheshimiwa Spika, vipo viwanda vinatumia kuni namagogo kama nishati. Watanzania zaidi ya 80% wanatumiamkaa na kuni. Nishati ya umeme ni ghali sana kupikia, mafutaya taa hayashikiki, gas bado ni ghali, wengi wanashindwakumudu.

Mheshimiwa Spika, mazingira yetu yapo hatarini,tutakuwa jangwa Taifa hili kama Serikali haitafuta nishatimbadala kwa matumzi ya kupikia.

Mheshimiwa Spika, gharama za malipo kwa mita zaLuku ni kubwa sana ukilinganisha na gharama za mita zakawaida. Serikali itoe maelezo ni kwa nini gharamazimepanda zaidi ya mara nne?

Mheshimiwa Spika, Kata ya Usingi Wilaya ya Kaliya inawakazi wengi sana na ni center ya biashara. Umeme wa eneohili wanatumia Alternator. Umeme ni dhaifu sana, wakatimwingine mashine za nafaka hazifanyi kazi. Serikali ipelekeumeme wa TANESCO.

Mheshimiwa Spika, mradi wa MCC maeneo menginchini ulichelewa kutekelezwa. TANESCO waliendelea na kaziyao ya kusambaza umeme maeneo mbalimbali, cha ajabuwataalam wa MCC walipokuja wanapita kule kule ambapotayari TANESCO wameshaweka umeme.

Mheshimiwa Spika, Serikali ni moja, ni muhimu kuwepona coordination kwenye utekelezaji wa kazi zake. Kwa kuwatayari TANESCO walishatumia rasilimali, nguvu na pesa nyingikusambaza umeme maeneo hayo, ni kwanini Serikali ambayotayari ina umeme mradi uhamie eneo la jirani ambalo halinaumeme? Haya siyo matumizi mabaya ya fedha za walipakodi?

Page 199: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

199

Mheshimiwa Spika, ni vigezo gani Serikali inatumiakupata uhakika wakati muafaka wa migodi ya madini kulipakodi ya mapato (corporate tax)? Ni nani anatafiti kujuakwamba mgodi umeanza kupata faida? Haiwezekanamgodi kama Bulyankulu, Buzwagi, North Mara, Mwaduiwanavuna madini kwa wingi kwa miaka yote hiyo! HawalipiCorporate Tax eti hawajapata faida! Hapa tunaibiwa!Tunaomba maelezo ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri amesemawameweka ukaguzi wa madini kwenye viwanja vya ndegekabla ya kusafirishwa kwenda nje kwenye baadhi ya viwanjavya ndege kwa mfano, KIA, DIA, na kadhalika na fedha nyingiimeokolewa.

Mheshimiwa Spika, ni utaratibu gani unatumikakuangalia kiasi cha madini yanayosafirishwa moja kwa mojakutoka kwenye viwanja vya ndege vilivyopo ndani ya migodimbalimbali ya madini?

Mheshimiwa Spika, katika ziara ya Mheshimiwa Raistarehe 09/01/2013 aliongea na wananchi wa Kata ya Usindi(W) Kaliua walipomsimamisha kwa vilio, wakaomba Kituocha Afya cha Usindi kipatiwe umeme. Mheshimiwa Raisaliahidi na kuagiza pale pale kituo kile kipatiwe umeme ndaniya muda mfupi. Naomba Serikali leo iwajibu wananchi ni liniahadi ile itatekelezwa?

MHE. SELEMANI S. BUNGARA: Mheshimiwa Spika,naanza kwa kuwapa pole wale wote waliokufa, kujeruhiwana kukamatwa katika vurugu iliyotokea Mkoa wa Mtwarana natambua kuwa haki ina thamani kubwa kuliko amanikwa maana pasipokuwa na haki hakuna amani.

Mheshimiwa Spika, pili, napenda kuishukuru Wizaraya Nishati na Madini kwa kusikia kilio cha muda mrefu chawafugaji wa Songosongo waliofiwa na mifugo yao kwakuwalipa waathirika wote. Hongera kwa hilo.

Mheshimiwa Spika, naanza kunukuu: “Mwongozo wa

Page 200: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

200

TANU 1971, Uchumi na maendeleo.” “Maendeleo ya nchihuletwa na watu “ukurasa wa 16.” kwetu sisi maendeleo yamaana ni yale yanayotuondolea kuonewa, kunyonywa,kunyanyaswa na mawazo ya kufungwa.

Mheshimiwa Spika, baada ya kunukuu Mwongozo waTANU 1971, napenda kuikumbusha Serikali kuwa sisi watu waMikoa ya Kusini tunahisi kuwa hatutendewi haki katikamambo mengi ya muhimu. Kwa lugha nyepesi tunaonewa.

Mheshimiwa Spika, mfano halisi, gesi ya Songo Songoimeanza kutumika mwaka 2004 na kuahidiwa kuwepokiwanda cha mbolea, kuwekewa umeme vijiji vinavyopitabomba la gesi, lakini mpaka leo vijiji vya Marendego, Miteya,Matundu na Manzese Somanga hakuna umeme. Hata huoushuru wa huduma 0.3 tumeanza kulipwa mwaka 2012.Miaka yote tulikuwa hatulipwi.

Mheshimiwa Spika, lakini cha kusikitisha zaidi, tangumwaka 2004 hakuna mpango wowote wa kuvipatia umemeVijiji vya Wilaya kama vile Mavuji, Kiwawa, Hoteltatu, Pande,Lilimalyao, Nanjirinji, Likawage, Mandawa, Miumba, Mtandi,Kirajeronje, na Mbwemkuru. Kwa kuwa mpaka leo hakunampango wowote wa kupatiwa umeme katika vijiji hivyo:Je, Serikali inasema nini kuhusu kupatiwa umeme katika vijijihivyo. Katika majumuisho yako Mheshimiwa Waziri napendaunipatie jibu la upatikanaji umeme katika vijiji hivyo; pia linitutapatiwa kiwanda cha mbolea KILMCO Kilwa?

Mheshimiwa Spika, sitaunga mkono hoja mpaka nijueni lini vijiji nilivyoviorodhesha hapo juu vitapata umeme nalini kiwanda cha mbolea kitajengwa?

Mheshimiwa Spika, mwisho, napenda kuitaka Serikaliifike Mtwara kuongea na wananchi wa Mtwara. KilichotokeaMtwara ni mambo waliyoyapata watu wa Kilwa. Watu waKilwa tumedanganywa na watu wa Mtwara wanajua kuwaKilwa hatukutimiziwa yale tuliyoahidiwa.

Mheshimiwa Spika, ombi letu tulipwe mrahaba katikagesi, ushuru wa huduma uongezwe, napendekeza 1.5%.

Page 201: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

201

MHE. KURUTHUM J. MCHUCHULI: Mheshimiwa Spika,napenda kuchukua fursa hii kuchangia machache katikaWizara hii muhimu katika kuinua uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, umeme wa gesi unaozalishwaSomanga Fungu unatumika katika Mikoa ya Lindi na Pwanihususan katika Wilaya ya Rufiji. Kumekuwepo na matatizoya kukatika kwa umeme mara kwa mara. Je, ni kwaniniumeme wa Somanga Fungu umekuwa ukikatika mara kwamara na kusababisha usumbufu na hasara kubwa kwawakazi wa Lindi na Rufiji wakati tunaelezwa kuwa gesiinayozalishwa ni nyingi kuliko inayotumika?

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa usambazaji waumeme vijijini kupitia REA unasuasua sana, kwa mfano katikaWilaya ya Rufiji takribani robo tatu ya vijiji ambavyovilitegemewa kupata umeme kupitia REA havijapatiwaumeme, mfano kijiji cha Mbunju, Mloka, na kadhalika. Je,tatizo ni nini?

Mheshimiwa Spika, napenda kupata ufafanuzi kutokakwa Mheshimiwa Waziri. Je, ni lini Kijiji/Mji mdogo wa Jaribumpakani (Rufiji) utapatiwa umeme?

Mheshimiwa Spika, Ahsante.

MHE. BENEDICT N. OLE-NANGORO: Mheshimiwa Spika,nampongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu Mawaziri kwa kazinzuri wanayoifanya katika Sekta ya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Spika, katika sekta ya Madini nashauriuchafuzi wa mazingira udhibitiwe na Jumuiya zinazoishi jiranina machimbo ya madini zilindwe, afya zao na wao piawanufaike na madini yanayopatikana katika maeneo yao.

Mheshimiwa Spika, naomba katika mikataba yauzalishaji umeme haki itendeke. Mikataba itazamwe upyana irekebishwe ndani ya miezi sita. Mitambo isikodishwe tena.Katika programu ya “Big Results now” fedha za kutosha

Page 202: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

202

zitengewe na Serikali ya Tanzania inunue mitambo yake nahii itumike.

Mheshimiwa Spika, nashauri TANESCO igawanywe iweMamlaka ama Wakala tatu tofauti: (1) Power GenerationAgency; (2) Power Transmission Agency; na (3) Power Supply/Provision Agency.

(a) Agency namba 1, isimamie mabwawa namitambo inayozalisha umeme ikiwemo Bomba la mitamboya gesi;

(b) Agency namba 2, isimamie ujenzi wa lines zahigh tension, kwa mfano, usafirishaji wa umeme kutokakwenye mabwawa hadi Mijini na Vijijini; na

(c) Agency namba 3, kazi yake iwe ni kuwafungiawalaji umeme na kukusanya fedha za matumizi ya umeme.

Mheshimiwa Spika, kwa njia hii kutakuwepo na checkand balance.

Mheshimiwa Spika, umeme wa REA Kiteto utekelezeahadi ya kupeleka umeme katika kijiji cha Mbeli na Ndaleta.

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Spika, naungamkono hoja. Kwa kuwa nimetoa mchango wangu kwakuzungumza, naomba kuongeza jambo moja au mawilikama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba Serikaliisiwanyamazie viongozi wa kisiasa hasa WaheshimiwaWabunge ambao wanakubali kununuliwa na hivyo kujiingizakwenye malumbano yasiyo na msingi na Serikali. Serikali nahasa Wizara kamwe isiwaonee haya WaheshimiwaWabunge wa namna hii ambao baadhi pia wamekuwalicha ya kununuliwa tu, bali wamekuwa na maslahi binafsina watu hao au wafanyabiashara.

Mheshimiwa Spika, pili, ni kuhusu utekelezaji wa mradi

Page 203: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

203

wa umeme wa Chalinze – Magindu – Lukenge. Mradi huuumeanza mwaka 2010: Je, utakamilika lini? Naiomba Serikali/Wizara hii iangalie mradi huu kwa jicho la karibu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

SPIKA: Ahsante. Sasa nimwite Naibu Waziri,Mheshimiwa Simbachawene atafuatiwa na Naibu WaziriMassele kila mmoja anapewa dakika 20, Mheshimiwa Waziridakika 40.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, napenda kwanzanichukue nafasi hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwakunijalia afya na uhai.

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuwashukuru sanawachangiaji wote. Kwa kweli yaliyosemwa kuhusiana nasekta ya nishati ni mengi na karibu wachangiaji wotewaliozungumza na kuandika wamegusia suala la nishati.Nawashukuru sana.

Mheshimiwa Spika, naamini hawa waliopata bahatiya kusema na kuandika ni wachache, lakini wapo ambaohawakusema na hawakuandika lakini kwa hisia tu unaonanamna ambavyo nishati inachukua sura ya pekee katika nchiyetu. Sisi tutakuwa mstari wa mbele katika kuhakikishakwamba tunafikia katika malengo ya sisi viongozi lakini piamalengo ya wananchi wetu na Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kauli iliyotolewa naMheshimiwa William Ngeleja kwamba tusikatishwe tamaana kauli za kupinga mipango ya Serikali na kubeza kilakinachofanywa na Serikali. Mheshimiwa Ngeleja, kauli hii nikweli kwamba tunayo mipango mikubwa sana ya nishativijijini na inafanywa na kutekeleza na Serikali ya Chama chaMapinduzi iliyopewa dhamana na wananchi wa Tanzaniakatika kuhakikisha kwamba inapanga programu na mikakatimbalimbali ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.Tutafanya hivyo na sisi hatutakatishwa tamaa na tutakuwa

Page 204: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

204

bega kwa bega na yeyote anayependa maendeleo katikakuhakikisha kwamba maendeleo yanafikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna haja sasa ya kufanyaufunguzi wa miradi na Mheshimiwa Waziri ametuagiza mimina Naibu Waziri mwenzangu kwamba kila mradi uliofanyikalazima tuuzindue kuhakikishia kwamba Serikali inafanya kazi.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, zimetolewa hoja nyingi, moja katiya hoja zilizotolewa ni kuhusu ukamilishaji wa Sera na Sheriaya Gesi. Hili tunalitambua na ninawahakikishie wotewaliozungumzia suala hili akiwemo Mheshimiwa AndrewChenge, Mheshimiwa Hamad A. Hamad, MheshimiwaFatuma Makidadi na Mheshimiwa Deogratias Ntukamazinana wengine wengi waliozungumzia hoja hii, sisi tumejipanga,Sera ipo tayari, Waheshimiwa Wabunge mmetoa mawazoyenu na nina hakika kwamba ndani ya mwaka huu Seraitakamilika na pengine kati ya mwaka huu na mwanzonimwa mwaka unaokuja Sheria itakuwa tayari kwa sababuvitu hivi vilikuwa vinaandaliwa kwa pamoja. Kwa hiyo, msiwena mashaka kwamba zitatumika Sheria au Sera gani wakatiwa uuzaji wa vitalu vinavyotarajia kuuzwa. Hapa tumefanyakatika nia ya kutaka kuwahi kwa sababu tunashindana nawenzetu duniani, sisi hatuwezi tukalala hata tusizindue autusiitangazie dunia kwamba na sisi tuna vitalu na tunatarajiakuviuza, ndiyo dhamira, lakini Sheria na Sera ndizozitazotumika wakati huo mwakani mwezi Mei. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, limezungumzwa suala kwambakuzalisha umeme wa gesi, wapo Mheshimiwa Kombo KhamisKombo, Mheshimiwa Zarina Madabida, Mheshimiwa AnneKilango Malecela, Mheshimiwa Dkt. Antony Mbassa naWaheshimiwa Wabunge wengine wengi wamezungumziasuala la umuhimu wa kuzalisha umeme wa gesi ili tuwezekushusha gharama ya uzalishaji wa umeme. Nichukue nafasihii kueleza Bunge lako Tukufu lakini niwaeleze Watanzaniakwa ujumla. Leo umeme ambao tunauzalisha kwa kutumiama-generator haya yanayotumia mafuta mazito na mepesi,TANESCO inaununua kati ya senti za kimarekani 40 - 55 lakini

Page 205: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

205

endapo tutakuwa tunazalisha umeme wa kutumia gesi,tutaununua umeme huo kati ya senti 6 - 8 na kwa maanahiyo tutaokoa fedha nyingi sana. Kwa hiyo, niungane na wotewaliosema kwamba gharama zishushwe, hatuna namnawala muujiza wowote Serikali wa kushusha gharama zaumeme kama hatujaweza kusafirisha gesi ili tuweze kuzalishaumeme katika maeneo yote kuanzia Mtwara tutazalishamegawati 400 Mtwara na kuusambaza katika Mikoa yaSongea na Mkoa wa Lindi, lakini pia na Wilaya za jirani, lakinipia kuleta gesi hiyo ili kuweza kuzalisha umeme unaotumiagesi badala ya kutumia mafuta mazito na kuokoa helainayotumika kwa kila siku iendayo kwa Mungu shilingi bilioni5.5 kuzalisha umeme na badala yake tutatumia kiwangokidogo kuliko hicho. Kwa hiyo, hapa nadhani wala haihitajiuwe na Masters wala PhD kujua economics hizo namnazinavyokaa. Kwa hiyo, nikubaliane na wote walioitia moyoSerikali, tuendelea na suala la kuhakikisha kwamba gesiinakwenda kuzalisha umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini picha isiwe kwamba gesikazi yake ni kuzalisha umeme tu, gesi ina mazao menginemengi sana. Gesi yenyewe inatumika kwa kupikiamajumbani, gesi yenyewe inatumika kama nishati viwandani,gesi inatumika katika kuzalisha mbolea ya ammonia na vituvingine, ni vitu vingi sana vinavyoweza kutokana na gesi.Kwa hiyo, niseme tu kwamba hapa isizungumzwe gesi kamani kwa ajili ya kuzalisha umeme tu. Hapa nipende kujibu hojaya Mheshimiwa John Mnyika aliyesema kwamba gesiinayosambazwa Dar es Salaam ni ya kubeba kwenye mitungi.Sisi tunazungumzia gesi ya kusambazwa kwenye mabombaili watu wafungue majumbani, wanapikia gesi, ndichotunachokizungumza siyo kusambaza ile LPG inayosambazwa,hiyo ndiyo dhamira ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini lingine lililozungumzwa hapani suala la kwamba kujengewe mitambo ya kusafisha gesikule kule Mtwara. Tumekuwa tukisema hili mara nyingi natumesema sana, mitambo ya kusafisha gesi itajengwa hapogesi ilipogundulika, huna muujiza, huwezi kuisafirisha gesikabla hujaisafisha. Kwa hiyo, mitambo ya kusafisha gesi

Page 206: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

206

inajengwa Madimba Mtwara na treni nne zenye uwezo wakubeba cubic milioni fiti za ujazo 70, 70 na pia Songosongona kwenyewe hivyohivyo kutajengwa mitambo ya kusafisha.Kwa hiyo, ni kauli tu za watu wasiopenda kuelewa jambohili, sijui ni kwa makusudi au vipi ndiyo wanalirudia maranyingi, lakini sisi tunasema mtambo wa kusafisha gesiunajengwa Mtwara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ambalo limezungumzwahapa ni suala la elimu kuhusu manufaa ya gesi asilia kwajamii. Ni kweli sisi Wizara tumejitahidi kufanya hivyo natutaendelea kufanya hivyo lakini nichukue nafasi hiikuwaomba Waheshimiwa Wabunge na viongozi wote,wanasiasa na viongozi wote wa kijamii, elimu hii haiweziikatolewa na Wizara tu. Kama wewe umeelewa kazi yakona wewe ni kwenda kumwelewesha ambaye hajaelewa.Inashangaza unapomkuta aliyeelewa na naye anasemawatu hawaelewi, wewe uliyeelewa umefanya jitihada ganikatika kutoa hiyo elimu kwa wasioelewa? Kwa hiyo, hilijukumu ikipewa Wizara tu kwamba Profesa Muhongo naWizara yake ndiyo tufanye kazi hiyo, hatutaweza. Miminiwaombe sana, ambao mmeelewa waliopo ndani ya Bungena nje ya Bunge twende tukawaelimishe wenzetu ambaohawajaelewa ili tuweze kutunza amani ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, limezungumzwa suala la hapa laumeme katika Wilaya mpya 13. Niwahakikishie Wabungewote wenye Wilaya mpya 13 ikiwemo ya Chemba na Wilayazingine mpya zote, Buhigwe zote zilizotajwa, tupo katikamkakati na hii imewekwa katika miradi inayosimamiwa naTANESCO na REA na yote itagharamia karibu bajeti ya shilingibilioni 71 na fedha ipo katika hii iliyopo katika vitabu, itaanzakutekelezwa kwenye Wilaya hizo mpya ili na wenzetu twendesambamba tunapozungumzia usambazaji wa umeme vijijini.Kwa hiyo, niwatoe wasiwasi wote wanaotoka katika Wilayampya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini limezungumzwa suala lamaeneo mengine Mheshimiwa Mturura amelisema kwambaje, tuna mipango gani ya kuboresha umeme kwenye maeneo

Page 207: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

207

ambayo hayako-connected na gridi. Jamani, ni mpaka paletutakapokuwa na uwezo wa kuzalisha umeme na umemeambao kwa sasa ni wa haraka ndani ya miezi 18 ni wa gesi.Tukiwa na uwezo tukatia ndani ya gridi usambazaji huu nikazi nyepesi. Niseme tu kwamba kutokana na mradiutakaojengwa wa megawati 400 Mtwara, line ile itatoka palekupitia Wilaya hizo kwenda mpaka Songea, hatutaruka, kilatunapopitisha huo umeme na hapo tunashusha na kwa hiyomnaachana na ma-generator, huo ndiyo mpango waSerikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia limezungumziwa sualazima la ucheleweshwaji wa kuwaunganisha wateja na hililimesemwa na Wabunge wengi ambalo linafanywa naTANESCO. Nichukue nafasi hii kuwaomba sana, ni kwelikwamba tuliposhusha bei ya kuunganisha umeme kwenyemajumba, tuliposhusha toka mwezi Januari, 2013 mpaka leohii mwezi Mei, 2013, wateja karibu 90,000 wameombakuunganishiwa umeme na tumewaunganishia umemewateja zaidi ya 50,000, kuna wateja karibu 26,000 ambaohawajaunganishiwa umeme. Changamoto hiitumepambana nayo, sasa hivi vifaa vimeshuka na vifaavitaanza kusambazwa katika Mikoa yote na Wilaya zote, natuna hakika kwamba tutawasambazia umeme. Natoamwezi mmoja tu kwa Meneja wa TANESCO wa Mkoakuhakikisha kwamba wakipokea vifaa hivyo kila mtu mwenyebacklog ya wateja ambao wameomba ndani ya mwezi Junina Julai wawe wamekwisha wote kuunganishiwa umeme.Kwa sababu vifaa vipo na vimeingia, tunazo nguzo karibu65,000 ni nyingi sana na vifaa vingine vyote vipo msiwe nawasiwasi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa James Lembeliamezungumzia kuhusu umeme wa Kahama na kwambaoption ile ya kuunganisha na Buzwagi tunakubali na Serikaliimechukua hatua kali sana. Tumezungumza na Buzwagi,tumekubaliana kituo kile tunashirikiana sasa kiwe kikubwasana na sasa badala ya kutoka Ibadakuli sasa tutachukuliapale ili tusambaze umeme katika maeneo yale. Hiyo piahaitasaidia kitu kama haitaenda sambamba na ubadilishaji

Page 208: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

208

wa nguzo na vifaa vyote kutoka Shinyanga hadi Kahama.Lazima tubadilishe na hiyo ipo kwenye mpango naitatekelezwa katika mwaka 2014. Kwa hiyo, MheshimiwaJames Lembeli na Mheshimiwa rafiki yangu Ezekiel Maigemsiwe na wasiwasi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini nizungumzie suala laucheleweshaji wa miradi ya REA na miradi ya MCC. Hilolimesemwa na Mheshimiwa Selemani Jafo, Lucy Mayenga,Abuu Jumaa, Mbunge wa Kibaha Vijijini na WaheshimiwaWabunge na wengine wengi wamesema kwambaucheleweshaji huu tumekubaliana na Wakandarasi hawakwamba mwisho ni mwezi Septemba, kama mweziSeptemba, watakuwa hawajamaliza bora tuvunje hiyomikataba. Tumefanya hivyo kwa sababu ya complicationya utekelezaji wa miradi, inaweza ukute fidia ililipwa kwanjia hii, lakini unakuta mradi unatakiwa upite hapa, mnaanzanegotiation upya. Kwa hiyo, ucheleweshaji nao una sababunyingi tu. Kwa hiyo, niwaombe sana hadi mwezi Septemba,hakuna mradi wa MCC au REA Phase I utakaokuwahaujatekelezwa na itakuwa imekamilika na kukabidhiwa.Tumekubaliana kwa maandishi na Wakandarasi.

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ni kwamba Serikaliianzishe miradi katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.Tumezungumza miradi kwa maana ya viwanda,tumezungumza miradi kwa maana ya kuweka centre kwaajili ya biashara mbalimbali zinazotokana na mazaoyatokanayo na gesi na kwamba pale Mtwara na Lindi mpakasasa vipo viwanda. Pale Lindi kuna kiwanda cha sementitayari na sementi inapatikana pale na bei yake ni tofautikabisa na bei ya sementi huku kwingine. Pale Mtwara kunakiwanda cha Dangote, nimesikitika wakati huyu anayejengakiwanda hiki anashusha vifaa pale Mtwara wananchi haowanaosema kwamba lazima viwanda vijengwe, makontenakaribu zaidi ya 15 yanashushwa pale, Waziri wa Viwanda naBiashara anayapokea, wananchi wanazomea. Sasatunajiuliza wanajua wanataka nini? Wamesema wanatakaviwanda, jitihada ya Serikali ya kujenga viwanda inafanyika,watu wana-mobilize kuleta vifaa site, wananchi badala ya

Page 209: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

209

kufurahia wanazomea. Mimi ninasema hii elimu tujitahidiwote, isije ikawa wengine tunatoa elimu na wenginewanaharibu elimu inayotolewa. Sasa hapo lazima tuwemakini kuona ni nini hasa ambacho kipo kwa sababuviwanda vipo. Tumetenga eneo la industrial pack,tumekwenda mara chungu nzima. Mimi nimetumwa naWaziri wangu wangu, Mheshimiwa Mwakyembe,Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Kigodatumefanya pale hadharani, tumezungumza na vyombo vyahabari, wananchi wanaona, tunaongea na local mediawananchi wanaona. Kwa nini jamani elimu tunayotoawananchi wanaona kwa macho, ujenzi wa viwandaDangote, maeneo yaliyotengewa ya LNG bado inasemekanaelimu haifiki. Tujitahidi sote kutoa elimu. Mimi nakubali lakinitujitahidi sote kutoa hiyo elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu wananchi kushirikishwakatika uamuzi wa masuala ya huduma za jamii (cooperatesocial responsibility), hili tunalifanya, Mheshimiwa Anne Kilangoalil izungumzia, Mheshimiwa Khalfa Sulemain Khalifaamelizungumzia, ndiyo maana tumeiweka katika sera. Kwamfano, kwenye Sera ya Gesi tumesema cooperate socialresponsibility iwekwe katika sera maana yake itasemwa piakatika sheria, kwa hiyo, hili lisiwape mashaka. Katika sektaya gesi mikataba iliyopo ni mizuri na ni ya production sharingagreement, Serikali ikiwakilishwa na TPDC inaanza kupatakutoka siku ya kwanza uzalishaji unapoanza, siyo kamamikataba inayotumia formular ya concession. Hii yaproduction share agreement ni mikataba mizuri na maranyingi sana tumekuwa tukijaribu kwa kweli kupambana sanakatika kuitetea kwa sababu mabeberu wasingependa iwehivyo.

Mheshimiwa Spika, REA itengewe fedha za kutosha iliiweze kutekeleza miradi yake, hili limesemwa na watu wengi,Mheshimiwa Godfrey Zambi, Mheshimiwa Shaffin Sumar, rafikiyangu Mheshimiwa Gosbert Blandes, akiwemo MheshimiwaCharles Mwijage, sisi tunakubali. Sisi tunasema naMheshimiwa Waziri wangu atalisema hapa, katika shilingibilioni 881 tunazozihitaji katika kutekeleza miradi hii, tuanze

Page 210: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

210

hata kwa kupata shilingi bilioni 450, kazi itaanza na tutawezakutekeleza miradi kadri ambavyo tutaweza kwenda kwasababu miradi hii yote haiwezi ikatekelezwa siku moja ikaishasiku moja. Kwa hiyo, msiwe na mashaka, Serikali imekubalikilio chenu na wamesema na Kamati ile ya Bajeti imefanyakazi nzuri, naipongeza sana Kamati yako imetuweka vizurina tunakwenda vizuri, tutakubaliana na naamini Kamati ileni nzuri na itatusaidia sana.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine lililozungumzwahapa ni kuhusiana na suala zima la umeme vijijini kwa maanaya vijiji ambavyo vimeachwa, watu wengine hawajaridhika,havijakaa sawa, niwahakikishie Waheshimiwa Wabungeukiwepo na wewe mwenyewe Mheshimiwa Spika vile vijijivyako unavyovitaja, nimekaa nimeongea na wataalamwamenihakikishia kwamba hakuna jambo gumu. Kwasababu fedha zile zikiwepo, tukaanza kutekeleza mradi,adjustments zinawezekana kwa kushauriana na wadau naMbunge ndio mdau namba moja, leteni mawazo yenu,tutayazingatia na tutatekeleza mnavyotaka hata kwakuangalia vipaumbele mnavyovitaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Charles Mwijageamezungumzia umeme kwenye Kata zake, hii itakuwa veryspecific, lakini Mheshimiwa Mwijage nikuhakikishie mamboyako ni mazuri, unatusaidia sana Kamati kufanya kazi na sisitunakubaliana kabisa kwamba tutafanya kazi hiyo vizurikabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini amezungumzia Kampuni yaMafuta ya Taifa kama ndio mwarobaini na kwamba lazimaSerikali ya kisasa iwe inafanya biashara na ndio Serikali zawajanja wote duniani zinafanya biashara, sisi tusiseme tuSerikali isifanye biashara. Tunakubaliana, tunachukua wazohilo na tunalifanyia kazi na jitihada zipo na tuna hatuatulizozifikia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, TANESCO umeme wa ghali.TANESCO umeme ghali ni kwa sababu ya gharama zauzalishaji, ikiingia gesi unashuka na umeme utakuwa bei rahisi,

Page 211: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

211

hatuna njia yoyote ya haraka zaidi ya gesi ikiingia kuzalishaumeme tutaona gharama ya umeme inashuka na hivyohakuna tena tatizo katika hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu gesi kuleta neema kwawananchi, hili nimeshalizungumzia. Serikali ianze uwekezajiwa viwanda mbalimbali Mtwara, hili nimelizungumzia.Mheshimiwa Fatma Mikidadi, Serikali ihakikishe kuwa bombala gesi ya kutoka Mtwara/Dar es Salaam linajengwatumesema lazima lijengwe. Kwa hiyo, nasema wenzetuwatuelewe tu kwamba dhamira ni nzuri na watakuja kujutabaadaye kwamba kwa nini walikuwa wanacheleweshamaana manufaa ni ya watu wote bila kubagua anatokasehemu gani.

Mheshimiwa Spika, kupeleka umeme vijijini hililimezungumzwa na watu wengi na hili nimelizungumzia,upungufu wa bei tayari Mheshimiwa Madabida alisema nawengine walisema. Lini mradi wa Kiwira utafunguliwa, hilijambo linaendelea vizuri STAMICO tumewaweka paleMheshimiwa Godfrey Zambi na tumeshalipa fidia zote. Kwahiyo, sasa hivi mgodi wa Kiwira unamilikiwa na Serikali, kwahiyo, kwanza tulirejesha sasa ndio tuanze na shughuli hizozingine.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Hassan Ngwilizializungumzia kuhusu bei ya nguzo, nimesema katika sualahili kwamba TANESCO hawauzi nguzo, TANESCO wanawekaumeme kulingana na umbali wa mahali ambapo umemeunatakiwa kupelekwa. Kwa hiyo, niwaombe wenzangu waTANESCO hebu neno nguzo, nguzo liondoke kwenyemisamiati ya TANESCO, tuzungumzie umbali kama ni mita 60gharama yake ni hii, kama ni mita 120 gharama yake ni hii.Kwa sababu mita ndizo zinazosema waya kiasi gani, vikombekiasi gani, sasa ukianza kusema nguzo, mbona husemivikombe, mbona husemi waya tuondoke kwenye huomsamiati tuzungumzie umbali uliopo kati ya anayehitajikuwekewa umeme na umeme unapotoka.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Said Arfi, alizungumzia

Page 212: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

212

bei ya umeme iwe Sh.99,000/= maeneo yote, tutaendeleakulifikiria lakini tulishusha bei hapa na imeweza kuletamatokeo makubwa ambapo tumepata walioomba wengikuliko tulivyotarajia mpaka wengine tunashindwakuwahudumia, ingawa tunakubaliana tutawahudumia tundani ya miezi miwili tutahakikisha wote wamekwisha nchinzima, watu wawe wanaenda pale analipia siku hiyohiyokesho yake anawekewa umeme, ndicho tunachotaka.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, amezungumzia pia habari yajenereta za Mpanda, Biharamulo, Ngara, ni kweli, sikunilipokuwa najibu hapa swali, niombe radhi kwamba ulimiulitereza, jenereta ilikuwa inashushwa Ngara maeneo yaRulenge, sasa nilipojua ni Rulenge nika-generalise lakini ukwelini kwamba mradi huu utatekelezwa ndani ya mwaka huuwa fedha na tunahakikisha kwamba jenereta hizozinafungwa katika Wilaya za Mpanda, Biharamulo na Ngara.Suala la kwamba zilikuwa mbili sasa ni moja, ni moja kwasababu uwezo wake sasa ni mkubwa kuliko hizo mbili zaawali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini l ingine ambalolimezungumzwa ni mpango wa kuweka umeme wa solarkatika shule za sekondari na vituo vya afya. Hili tunalisemana nirudie kusema dhamira ya mradi wa REA ni kuboreshamaisha ya watu wa vijijini. Huwezi ukasema umeboreshamaisha kama hujapeleka umeme kwenye zahanati, shule zamsingi au sekondari na hujapeleka umeme kwenye kisimacha maji. Kwa hiyo, priorities za REA na mimi nataka nilisemehili, ni kwamba mnapoingiza umeme kwenye kijiji hakikishenikwanza umefika sehemu hizo ndio watu wengine wafuate.Haina maana kama tunafikisha umeme kwenye vijiwe watuwanacheza pale karata na pool, tunataka uende kwenyehuduma za jamii, kwa hiyo, hayo ndiyo malengo ya Serikali.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na naombakuunga mkono hoja. (Makofi)

Page 213: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

213

SPIKA: Ahsante sana. Sasa namwita Naibu Waziri,Mheshimiwa Maselle kwa dakika 20.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. STEPHENJ. MASELLE): Mheshimiwa Spika, awali ya yote na miminichukue muda mfupi sana kukushukuru wewe binafsi,napenda kutumia fursa hii pia kuwashukuru WaheshimiwaWabunge wote waliochangia hotuba ya Wizara ya Nishatina Madini kwa maandishi na kwa kuzungumza.

Mheshimiwa Spika, naomba nichukue nafasi hii pianiwashukuru Wakuu wa Nchi, Mheshimiwa Rais Jakaya MrishoKIkwete, Mheshimiwa Makamu wa Rais, Dkt. Gharib Bilal,Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu, kwa miongozombalimbali ambayo wamekuwa wakitupatia.

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuishukuru Kamati yaNishati na Madini kwa ushauri na michango waliyoitoa nanapenda pia kuishukuru Kambi Rasmi ya Upinzani kwa maoniyao.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo haya, napendakujibu hoja zil izotolewa na Waheshimiwa Wabungenikijielekeza zaidi kwenye hoja ya service levy ambayoimezungumzwa kwa uchungu sana na WaheshimiwaWabunge. Kwa haraka tu, kwa kuwataja majina MheshimiwaEzekiel Maige amezungumzia hili, Mheshimiwa Lembeli,Mheshimiwa Cecilia Paresso kule Karatu, Mheshimiwa Dkt.Hamisi Kigwangalla na Waheshimiwa wengine wote.Waheshimiwa Wabunge wote wanafahamu kwamba Bungelako mwaka 1982 lilitunga Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaaikizipa mamlaka Serikali za Mitaa kuanzia kwenye Mamlakaza Miji, Halmashauri za Miji mpaka vijiji kuweza kujikusanyiamapato ambayo yatatumika kwa shughuli mbalimbali zamaendeleo ya wananchi.

Mheshimiwa Spika, jukumu hili kimsingi ni la Serikaliza Mitaa lakini kwa kuwa baadhi ya wadau wanaohusikana kudaiwa kodi hizi ni makampuni ya madini, ni wazi

Page 214: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

214

kwamba Waheshimiwa Wabunge wana kila namna na hakiya kuuliza Wizara ya Madini inawasaidiaje kuhakikishakwamba wanapata fedha hizi. Mwaka jana tulianzakufuatilia kwa karibu sana eneo hili la madini na kuangalianamna gani makampuni ya migodi yamekiuka, nitumie lughaya kukwepa lakini hayakulipa service levy kwa mujibu washeria hii niliyoitaja kwenye Halmashauri mbalimbali nchini.Tulifanya hivyo kwa ushirikiano wa karibu sana na Wabungewa Nzega wakiongozwa na Mheshimiwa Dkt. HamisiKigwangalla na Mheshimiwa Selemani Zedi na Halmashaurinzima ya Nzega na tuliweza kufaulu kupata mapato hayazaidi ya shilingi bilioni 2.3 ambazo ziko kwenye Halmashauriya Nzega.

Mheshimiwa Spika, sasa kuna madai mengineambayo Halmashauri ya Nzega wanayo, mimi wito wanguni kwamba wafuate tu taratibu zilezile kwa sababu ni wajibuwao kudai. Sisi Wizara ya Nishati na Madini tutatoa ushirikianowote wa taarifa sahihi ambazo watazihitaji na tutatoa forumhiyo ili waweze kupata haki yao wanayostahili.

Mheshimiwa Spika, vivyo hivyo nitumie nafasi hiikumpongeza Mheshimiwa Ezekiel Maige na MheshimiwaJames Lembeli kwa kazi kubwa ambayo wameifanya piakwa kufuata njia ileile ya Halmashauri ya Nzega tumewezakwenye kikao ambacho tumekifanya tarehe 22 baina yaHalmashauri ya Kahama ikiongozwa na WaheshimiwaWabunge hawa pamoja na Mkurugenzi, mgodi wa Barrickumekiri kwamba kuna service levy haikulipwa kuanziamwaka 2001 mpaka 2005 kiasi cha jumla ya dola za Marekanimilioni moja, wamekiri watazilipa hizi kwenye Halmashauriya Kahama dola milioni moja lakini hivyo hivyo kwenyeHalmashauri ya Tarime watalipa kiasi cha dola laki sitaambazo ni za tangu mwaka 2001 mpaka 2005. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kuna madai mengineambayo Halmashauri ya Kahama imeyaleta na MheshimiwaMbunge ameyazungumza. Tulichofanya tumechukua

Page 215: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

215

takwimu zile ambazo kimsingi wamezitoa kwenye ofisi yanguna tumezipeleka rasmi kwenye migodi hii na wao waka-verifybaada ya hapo nitasimamia kikao hicho kuhakikishakwamba Halmashauri zote zinazodai service levy zinapatamapato yao kwa mujibu wa sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, service levy si tu kwa migodi,naomba nitoe wito kwa Halmashauri zote kwa sababuWaheshimiwa Wabunge pia ni Wajumbe wa Mabaraza yaMadiwani wahakikishe kwamba shughuli zinazofanyika kulekwenye sheria inasema kabisa “any corporate entities” zikocorporate entities nyingi zinafanya shughuli kwenyeHalmashauri zetu na zenyewe zina wajibu wa kulipa servicelevy kwa mujibu wa sheria ambayo ni 0.3% ya turnover.

Mheshimiwa Spika, sasa yako makubaliano baadhiya maeneo ambayo ndiyo yalikuwa msingi mkubwa wamalalamiko ya Mheshimiwa Maige kwamba mikatabailiyofungwa ilisema italipa dola laki mbili, lakini kwa hoja zamsingi na mazingira na mahitaji ya Halmashauri zetu na kasiya ukuaji wa miji yetu, tunashawishi migodi hii iweze kuridhiakulipa kwa mujibu wa sheria na waweze kuwalipaHalmashauri ya Kahama. Naomba niliweke wazi, Wizara yaNishati na Madini na Serikali kwa ujumla hatuwezi kuvumiliaukwepaji wowote wa kulipa kodi zinazostahili kwenyeHalmashauri na ndio maana tumesimamia kwa karibu nakwa nguvu zote kuhakikisha Halmashauri zetu zinapatamapato.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine napendanilizungumzie katika eneo hili ambalo Halmashauri zetuzimenufaika, Halmashauri ya Geita mwaka jana ilipata 1.4million dollar, fedha hizi wako kwenye mazungumzo yakukubaliana wajenge miradi ya kusambazia maji katika mjiwa Geita. Mradi mkubwa ambao unajengwa na mgodi waGGM wa kuyatoa maji Ziwa Victoria na kujenga reservoirambayo sasa hatua ya pili itakuwa ni kuyasambaza majikatika mji wa Geita. Kazi hiyo inaendelea na ni matumainiyetu mwisho wa mwaka huu kazi hiyo itakamilika.

Page 216: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

216

Mheshimiwa Spika, lakini Mheshimiwa James Lembeliamezungumza hapa ABG kwa mara ya kwanza inaanza sasakutekeleza miradi ya kujenga barabara. Itajenga kilomitatano katika Mji wa Kahama na hizi zote ni juhudi zaWaheshimiwa Wabunge hao kwa kushirikiana na Wizarakuhakikisha kwamba migodi hii inatambua sasa mchangowao katika jamii ambazo wanafanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivyohivyo katika Wilaya ya Tarimewameweza kujenga shule mbili ambazo zil ikuwazikilalamikiwa hapa na Waheshimiwa Wabunge wa Tarime,Mheshimiwa Nyambari Chacha Nyangwine pamoja naMheshimiwa Esther Matiko, shule hizo nina hakika sasa hivizitakuwa zimekamilika ama ziko kwenye hatua za mwishoza ukamilishaji. Wamejenga kituo cha afya nawamekarabati shule za msingi katika Wilaya ya Tarime nakuweka madawati mapya. Nzega pia wamepata shilingi 2.3billioni wanazifanyia nini, ni matumaini yetu kuwa fedha hizowalizozipata watazitumia vizuri kwa manufaa ya wananchiwote wa Nzega.

Mheshimiwa Spika, watu wengi wamezungumziamgawanyo wa rasilimali za nchi. Wote tunafahamu, kodimbalimbali zinazolipwa kutoka kwenye sekta ya madinilabda tu kwa uchache nizitaje, watu wengi wanaangaliamrabaha kama ndio kodi pekee lakini naomba nizitajekwamba Serikali inapata kodi nyingi ikiwemo corporate tax.Kuanzia mwaka 2005 mpaka sasa jumla ya shilingi bilioni 444zimelipwa Serikalini kama corporate tax, PAYE kuanziamwaka 1999 jumla ya shilingi bilioni 415 zimelipwa Serikalini,withholding tax zimelipwa shil ingi bil ioni 146, Skil lsDevelopment Levy jumla ya shilingi bilioni 90, VAT na kodizingine shilingi bilioni 117, sub total ya yote hii ni zaidi ya shilingitrilioni 1.2 lakini total ya jumla yote ni shilingi trilioni 1.6zimelipwa Serikalini.

Mheshimiwa Spika, mrabaha ni sehemu pia yamapato ambayo Serikali inayapokea kutoka kwenye

Page 217: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

217

uwezekaji huu wa madini. Mtakumbuka kwamba na hapanijibu tu hoja ya Mheshimiwa Mnyaa kwamba kuna 2.5 bilionikwenye ripoti ya CAG imeonesha kwamba hazikulipwaSerikalini. Mtakumbuka Sheria ya Madini i l ifanyiwamarekebisho mwaka 2010 ikaanza kazi Novemba, 2010.Baada ya kuanza kazi kipindi hicho toka Novemba 2010mpaka 2011, ndio kipindi ambacho Mheshimiwaanakizungumzia lakini migodi hii iliweza ku-migrate kutokakwenye 3% ambayo walikuwa wakilipa royalty kwendakwenye 4% ilipofika Mei 2012. Sasa kipindi cha mwaka 2010mpaka 2012, huu mwaka mmoja wa 2011, Serikali wakiwepowatangulizi wetu waliokuwepo ofisini Mheshimiwa Ngelejana Mheshimiwa Malima walianzisha kazi hii na Katibu MkuuBwana Maswi ya kujadiliana na migodi ku-migrate kutokakwenye 3% kwenda kwenye 4%. Sisi tulipofika pale tukawekamkazo kukamilisha kazi ile na kuanzia Mei Kampuni zikaanzakulipa 4% ya royalty na si tu kwamba wamelipa wanalipaunder protest. Kwa hiyo, hata sasa wanaendelea kulipa 4%na sisi kusema kweli tuliamua kufanya kwa makusudikwamba mapendekezo ya sheria ile yatekelezwe. Kwa hiyo,kwa kuwa mikataba waliyofunga MDAs zile zil ikuwazinatamka 3% na mabadiliko ya mkataba hayo ndiotunaendelea kuyajadili.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge wengiwanajiuliza mikataba hii tunai-review vipi? Katika hatua zaku-review mikataba hiyo na ndiyo hapo tulipofika kwenyeku-review eneo hili la royalty na kuwaambia kwa sheria zetuza sasa mnapaswa mlipe asilimia nne ya mapato yotemnayopata. Kwa hiyo, napenda kuliarifu Bunge lakokwamba migodi hii kuanzia Mei 2012 imekuwa ikilipa 4% yaroyalty na kiwango hiki tofauti ya asilimia tatu iliyokuwaikilipwa kwa mwaka jana tumeweza kukusanya shilingi bilioni30 kama nyongeza baada yaku-migrate kwenda kwenye 4%.

Mheshimiwa Spika, wengi wamezungumziaincentives, mtakumbuka kwamba pamoja na kuwa Wizaraya Nishati na Madini inasimamia sera pamoja na Sheria yaMadini, lakini inapokuja masuala ya majadiliano haya,maeneo ya kodi haya yaliwekwa makusudi na yanasimamiwa

Page 218: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

218

kikamilifu na Wizara ya Fedha na incentives hizi zilikuwa nisehemu ya package katika Sera yetu ya Uwekezaji kuangalianamna gani Serikali itashawishi wawekezaji kuja kuwekezakatika nchi yetu. Sasa kwa kuwa wawekezaji wanakuja naTanzania imejulikana kwamba ni kitovu na kituo chauwekezaji, Serikali itazingatia ushauri wa WaheshimiwaWabunge kuangalia katika incentives hizi kuzipunguza ilituweze kunufaika zaidi na mapato yanayotokana na madini.Kwa kufanya hivyo, wale ambao tunaendelea kufanyia kazimkataba wa MKUJU mnaweza kuona Serikali imekuwainachelewesha mkataba huu kwa sababu tunataka maeneoya kodi lazima Taifa linufaike zaidi na eneo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo,Waheshimiwa Wabunge wengi wamezungumzia akiwepoMheshimiwa Lolesia Bukwimba, Mheshimiwa Agripina ZaituniBuyogera, Mheshimiwa Charles Mwijage na MheshimiwaBeatrice Shellukindo. Serikali imeamua kwa makusudi kabisakuwatambua wachimbaji wadogo lakini naomba nikiri,ukiangalia taarifa mbalimbali zilizoko Wizarani, maeneo yanchi yetu mengi yalikuwa yameshikiliwa na leseni mbalimbali.Ukiangalia ramani karibu maeneo yote yamekuwa coveredna leseni. Sasa wachimbaji wadogo wanataka leseni Serikaliinaitoa wapi eneo la kuwapa. Mheshimiwa Arfiamezungumza hapa kwamba wameenda kutengewamaeneo mapya, ndiyo maana Wizara ikafikiria kwambatufanyeje ili tuweze ku-unlock nchi iwe wazi kwa baadhi yamaeneo ili tuweze kuyatoa kwa wachimbaji wadogo nandio msingi wa kuongeza pia hizi ada za leseni.

Mheshimiwa Spika, unakuta mtu mmoja anamilikileseni zaidi ya 200 peke yake, sasa mtu yule ameshikilia Wilayanzima, Wilaya hiyo ina wachimbaji wadogo na Serikaliinapaswa itoe leseni kwa wachimbaji wadogo, unatoa wapieneo hilo. Mfahamu kabisa leseni ni document ya kisheria,mwenye leseni ana haki zote za kisheria, ukimnyang’anyakwa nguvu atakushtaki. Kazi ambayo tunafanya ni kutafutamechanism ambayo hao wanaoshikilia maeneo makubwawashindwe kuyamudu wayaachie na tumefanya hivyo na

Page 219: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

219

matokeo yake ndio tumepata baadhi ya maeneo kwawachimbaji wadogo. Kwa hiyo, napenda hilo lieleweke kwanini tulikuwa tunafanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kwa maeneo ya Kahamaambayo kwa historia ni muda mrefu yamekuwa yakiaminikakuwa na madini pamoja na Kilindi, taarifa za madini zikokatika ofisi zetu za GST. Watu wengi wana access na taarifahizo. Kwa hiyo, wanakwenda kwenye maeneo ambayo nihot spot kwenda kukamata maeneo yale na bahati mbayasana wachimbaji wetu hawakufahamu hizi sheria kwambaanayewahi kupewa leseni ile ya utafiti ndio ana haki tayariya madini, ile minerals rights. Sasa wewe ambaye ulikuwaunachimba kwa sababu ni shamba la babu, shamba la bibi,maana yake huna mineral rights na hii iko wazi kabisa,mwenye kiosk hawezi kufanya biashara ya kiosk kama hanaleseni. Kwa hiyo, hata mwenye madini ni lazima akachukueleseni ili aweze kufanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Spika, kama Wizara tumeimarishaChama cha Wachimbaji Wadogo kote nchini, wana uongozikuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa mpaka Taifa tunayajadili hayakwa kina na tunatafuta ufumbuzi wa matatizo yao kwanamna ya kudumu. STAMICO ndiyo itakuwa inashughulikana wachimbaji wadogo na tunaendelea kuangalia modelmbalimbali ni namna gani tutakuwa na model ambayoitaiwezesha STAMICO kuweza kuwa na agent wa kununuadhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo na agent yuleaweze kulipa kodi na royalty na kodi zote kwa mujibu washeria ili aweze kuwa mkusanyaji wa mapato ya Serikali. Kwahiyo, tunaendelea kutafuta mbinu mbalimbali kuwezakuhakikisha kwamba wachimbaji wadogo naowanachangia pato la Taifa.

Mheshimiwa Spika, mambo ya mikopo, WaheshimiwaWabunge wamezungumzia uwepo wa TIB Dar es Salaam.Naomba niseme kwamba hakuna aliyetangaza TIB,tulitangaza zabuni ili tuweze kupata benki ambayo itawezakusimamia fedha hizi kwa wachimbaji wadogo. Mambo yamikopo ni taaluma na taaluma hii inasimamiwa na mabenki.Kwa hiyo, Serikali iliamua kwa makusudi kupeleka fedha hizi

Page 220: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

220

kwenye benki ili ziweze kusimamiwa kama ilivyo funds zingikekama Mfuko wa JK. Kwa hiyo, niseme tu kwamba mchakatowa zabuni ile unaendelea na unafanyika kwa uhuru na sisiWizara tunaendelea kusubiri matokeo ya zabuni hiyoatakayeshinda ndiye atakayekuwa na fedha hizo na kuwezakuwahudumia wachimbaji wadogo.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Lucy Mayengaamezungumzia utoroshwaji wa madini na nimwambieMheshimiwa Wenje amenukuu taarifa kutoka sijui kwenyetaasisi gani. Niseme kwamba sisi Tanzania kwa mujibu waSheria, 2009 Serikali iliunda hiki chombo cha TMAA. Baada yakuunda TMAA imefanya kazi nzuri sana, haya madeni yoteya nyuma tunayozungumza, TMAA ndiyo iliyoyaibua.

Mheshimiwa Mnyaa amezungumzia TEITI, TEITI ikokidunia kama EITI lakini Tanzania na sisi ni wanachama nainafanya kazi nzuri ya kukagua na kuhakikisha kwambakasoro zote zilizopo kwenye madini tunaweza kuzibaini nakuzitafutia suluhu hapohapo. Niseme tu kwamba bila kujuakasoro, huwezi kupata tiba ya tatizo. Serikali kupitia TMAAna Wizara ya Nishati na Madini tumeweka mitego mbalimbalikwenye airport zetu na sehemu mbalimbali za mipaka.Nataka niwahikikishe Waheshimiwa Wabunge hataWabunge wengine humu wamekamatwa na mitego yetuna wamenipigia simu kuniomba, Mheshimiwa vijana wakowamenishika hapa na madini, mimi nimenunua ya kuvaamwenyewe, naomba unisaidie nipite. Sasa ukiangalia kweliunakuta Mheshimiwa kanunua cheni zake za Tanzanite paleArusha anataka kuja Dar es Salaam. Nawaambia mwacheniMheshimiwa haendi kufanya biashara wala hafanyi biasharaya madini. Kwa hiyo, nataka kuwaonyesha tu kwambaSerikali iko makini na mitego ipo na kama unabisha ukitokahapa nenda airport chukua madini ficha, utashikwa. Haowote ambao wamekuwa wakikamatwa tangu tumewekamitego hii tumeweza kuokoa shilingi bilioni 13/- ambazozilikuwa zinatoroshwa. Kwa hiyo, kuna jitihada kubwa sanainafanyika kuhakikisha kwamba sekta hii inaendeleakuimarika na Serikali inapata mapato yake. (Makofi)

Page 221: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

221

Mheshimiwa Spika, viwanja hivi vya ndege, hata mimizamani nilikuwa nikifikiri kwamba Wazungu wale wanarukatu kule wanaondoka kwenda nje. Kuna regulations nyingisana ili ndege itoke nje ya nchi. Hakuna ndege inatoka tukwa kuwa imeruka inaweza kwenda popote. Ndege lazimaiongozwe kutokea chini. Kwa hiyo, ni fikra tu kwamba ndegeikitua uwanjani inaondoka. Ndugu zangu, viwanja vilevimewekwa kwa ajil i ya security. Una gold kilo kumiunaisarisha na gari kutoka Kahama kwenda Dar es Salaam?Haufiki. Kwa hiyo, viwanja vile vimewekwa kwa ajili ya securityya kuondoa mali ile kutoka sehemu ambayo imehusika navituo vile vyote vina TRA, kuna vyombo vyetu vya ulinzi nausalama pamoja na Wakaguzi wetu wa TMAA, wote wakopale kuhakikisha kila kinachozalishwa kinakuwa recorded nakodi inalipwa ipasavyo.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Ntukamazina naMheshimiwa Blandes wamezungumzia mradi wa KabangaNickel na Mheshimiwa Wenje alizungumza utafiti tangu miakaya 1970. Hii ni kazi ya kisayansi, huwezi kukopa fedha zakuendesha mradi wa mgodi wa zaidi ya dola bilioni laki tano,hauwezi ukapewa fedha kama huwezi kuonyesha mashapoya kile ambacho unaenda kukifanya. Kwa hiyo, kazi hiiimekuwa ikifanyika kwa muda mrefu kwa sababu inagharama kubwa na makampuni haya mengine yamekuwayanafil isika yanaachia njiani, mwingine ananunuaanaendelea lakini kwa taarifa tulizonazo sasa hatua zikomwishoni, wana-finalize hizo feasibility study na mradi uleutaanza. Kuna changamoto zaidi upande wa Serikali. Nickelni madini mazito, yanahitaji reli kuyasafirisha, yanahitajiumeme sio chini ya megawatt 40 kuendesha mgodi ule. Kwahiyo, kuna changamoto za kimiundombinu ambazo nazenyewe zimekuwa kama setback kwa ajili ya kutekelezamradi huu. Niwahakikishie kwamba timu yetu ya majadilianoya Serikali tayari imeshaanza kazi ya majadiliano na KabangaNickel kwa ajili ya mkataba na tutazingatia maslahi ya Taifaili mradi huu uweze kuanza kwa manufaa ya wananchi.

Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia nizungumzie CSR.

Page 222: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

222

Tunafanya jitihada kubwa kama Serikali kuhakikisha kwambamakampuni ya migodi yote, suala la CSR sio la hiari.Tunayashawishi kuwa na mfuko maalum ambao kila mwakamigodi hii itaweka fund kule kwa ajili ya huduma za jamii.Wote mtakumbuka kwamba uwepo wa mgodi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. STEPHENJ. MASELLE): Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkonohoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana.

Waheshimiwa Wabunge, nina matangazo kidogohapa. Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira,Mheshimiwa James Lembeli, anaomba niwatangazieWajumbe wa Kamati yake kwamba baada ya kuahirishakikao hiki watakuwa na kikao chao chumba namba 231.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mheshimiwa Margaret Sitta, anaomba niwatangazieWaheshimiwa Wabunge wote kuwa kesho tarehe 26 kuanziasaa nne asubuhi kutakuwa na semina kwa Wabunge woteitakayohusu Rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo. Semina hiiitafanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa. Wabunge mnatabia ya kuchelewa kufika, kwa hiyo mnakuta watu wakohalf way halafu mnakosa mwanzo.

Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mheshimiwa IddAzzan, anaomba niwatangazie Waheshimiwa Wabungewote kwamba leo hii jioni kutakuwa na mechi ya kirafikiri yampira wa pete kati ya timu ya Waheshimiwa Wabunge natimu ya vijana ya Dodoma. Mechi hizo zitachezwa katikauwanja wa Jamhuri Dodoma kuanzia saa kumi kamili jioni.

Page 223: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

223

Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge wote mnaalikwa kwendakuishangilia timu yenu.

Mheshimiwa mtoa hoja!

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika,awali ya yote, niwashukuru Wabunge mawazo yenu nimwanana, tumeyachukua na sisi tunachukua mawazo yapande zote mbili ya Wapinzani na ya CCM kama ni mazuri.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, napenda kama nilivyofanyamwaka uliopita, safari hii nimeleta wataalam wangu waTANESCO wa kila Kanda Tanzania. Hawa watakaa hapampaka Jumatano, saa mbili mpaka saa kumi na mbili kwenyeofisi yetu ya Madini ambayo iko nyuma ya Dodoma Hotel.Kwa kuwa muda ni mfupi, nawaomba WaheshimiwaWabunge, dukuduku nyingi hatutazijibu hapo lakini nendenipale. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile nimeleta Maafisa waKanda wa Madini wa Tanzania nzima, wako hapa naniliwaambia waje na orodha ya wachimbaji wadogokwenye Kanda zao zote na narudia kusisitiza, wachimbajiwadogo hawalipi kodi. Sasa kama mtu nauli ya kutoka Dares Salaam mpaka Morogoro ni Sh.20/- na yeye hajawahikusafiri kwenda Morogoro, ukiongeza ukaweka Sh.30/- anahaki gani ya kujadili nauli hiyo, hata kusafiri hajawahi kusafiri.Hao wote wanaotetea hizi kodi, mtagundua kuna baadhiyetu Watanzania wana maeneo karibu Wilaya nzima. Hakunamtu anayeongelea wachimbaji wadogo hapa, wengine nibiashara zao tu. Hiyo mkitaka tutaweza kuthibitisha kwakutaja makampuni na mtu na maeneo waliyonayo. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Wataje!

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Haitoshi hapa, kulewako wataalam wangu, nendeni kule.

Page 224: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

224

Mheshimiwa Spika, nilikuwa sipendi kuongelea hili laMererani lakini kwa sababu Mheshimiwa Rais ametajwainabidi nitoe ufafanuzi. Mheshimiwa Ole-Sendeka wapigakurawako Simanjiro wamekusikia lakini uliyosema yote si kweli.Tulikaa mimi na wewe Arusha ukarudia hili la MheshimiwaRais kutoa ahadi na bahati nzuri Mkuu wa Mkoa wa Simanjiroalikuwepo, nikamuuliza Mkuu wa Mkoa wa Simanjiroakaangalia kwenye daftari la ahadi…

SPIKA: Mkoa gani?

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Samahani Manyara,hakukuta ahadi ya Mheshimiwa Rais. Sasa ndugu zanguWatanzania Mheshimiwa Ole-Sendeka anataka tumsikilize,tukune kichwa hapa wakati Mkuu wa Mkoa wa Manyarahana hiyo ahadi. Isitoshe kwa kuwa nilikuwa naenda kwenyehicho kikao mimi mwenyewe nikampigia Mheshimiwa Raissimu, nikaongea naye, Mheshimiwa Rais akaniambiawasiniwekee maneno mdomoni mwangu, Rais hakutoa hiyoahadi. Sasa mimi nataka nimhakikishie Mheshimiwa Ole-Sendeka unayoyasema mimi msimamo wangu na wa Wizarani huohuo Rais hakutoa hiyo ahadi.

Mheshimiwa Spika, isitoshe basi ukaja kwangu unawazo Halmashauri ipewe hisa. Mimi nikasema sehemuambapo migodi ipo tukianza kila Halmashauri kuchukua hisandiyo kuigawa nchi. Je, Halmashauri zisizokuwa na madini?Nilikataa hilo wazo na Watanzania mnaonisikiliza hapa mnaimani na Halmashauri zenu kwa matumizi ya fedha?

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Ole-Sendeka akanijiana kikundi cha watu wanaanzisha ushirika. Miminikamwambia hivi mnaweza kuanzisha ushirika kwa ajili tuya Tanzanite hii? Kwa hiyo, ndugu zangu niachie hapohapo.(Kicheko/Makofi)

Page 225: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

225

KUHUSU UTARATIBU

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Kuhusu Utaratibu!

SPIKA: Tuko kwenye majumuisho utaratibuhauruhusiwi.

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Sasa ni uongo.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika,hili la Buhemba, ninaomba Mwenyekiti wa wachimbaji Mkoawa Mara na Mwenyekiti wa wachimbaji wa Buhembaambapo juzi nilikuwa naongea nao najaribu kuwatafutiaeneo. Ukweli wa sheria unasema, huwezi ukatoa leseni juuya leseni, hivyo ndiyo sheria inavyosema ndugu zanguWaheshimiwa Wabunge na Watanzania, hil i eneowamepewa STAMICO kisheria, wana leseni, sasa nitatoajileseni juu ya leseni? Badala yake nimejaribu kuwatafutia eneona nimetuma watu na nikasema natuma na ma-geologistwa Geological Survey kabla hilo eneo hawajapewa walewachimbaji wahakikishiwe kwamba kuna chochote kamaalivyosema Mheshimiwa Mama Shellukindo nilimwomba CEOwa Geological Survey na kweli tutampelekea ma-geologistkule. Haya mambo tunayoyangea hapa ndugu zangu hatakama humpendi mtu au hupendi ukweli si maneno ya porojoni ya uhakika. Kwa hiyo, hili la Buhemba nimewatuma kulewawatafutie na nikawauliza watu wa Buhemba kwani nyielazima mchimbe hapohapo au mko tayari kwenda Mkoamwingine? Wakasema hayo maeneo mliyotenga tuko tayarikwenda. Vilevile nimemwomba Mwenyekiti wa wachimbajiwa Mkoa wa Mara, namwomba na nadhani ananisikia naMwenyekiti wa wachimbaji wa Butiama waje kwangu ofisininiwaonyeshe kampuni ambazo zimekosa hilo eneo na sasalinataka kutuvuruga, watasoma wataniachia document.(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, nianze kwanza kwa hotuba ya

Page 226: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

226

Kambi ya Upinzani. Wametumia muda mwingi sanakuongelea juu ya Mwalimu Nyerere. Ndugu zangu Watanzaniamnaonisikia na wengine ambao sisi ni wanafunzi wazuritulimwelewa, Mwalimu maandiko yake yalikuwa ya sehemutatu. Kwanza, ilikuwa ubinadamu na utu, ndiyo maanalilitokea Azimio la Arusha. Mkienda Butiama nendeni kwenyeLibrary yake mtaona Mwalimu alivyokuwa anasoma. Sehemuya pili ilikuwa ni ujenzi wa Taifa. Ilikuwa ni utaifa na uzalendona sehemu ya tatu ilikuwa ni kusahihisha uongozi, hayaamekuja kuandika baadaye sana. Sasa kama wewe unatakakumwelewa Mwalimu vizuri, huwezi ukashika theluthi mojatu ya mwisho ya kusahihisha uongozi. Kwa hiyo, kama nimaksi kwa sababu ana sehemu tatu na wewe umejibutheluthi moja, una 33.3, wewe ni fail. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, vitu viwili muhimu kabisa kwaMwalimu na kwa umri wangu ambao tulikwenda sekondariulikuwa unakuta kwenye madarasa, kwenye mabweni yetu,Mwalimu anasisitiza kwa wale wenye bahati ya kupata hiielimu, those who have the privilege to receive education,hawa ni watu sawasawa na watu wanaopewa chakulakilichoko kwenye kijiji chenye njaa ili wale wapate nguvuwatembee, waendee mbali wakaleta chakula kwa wanakijijiwasiokuwa na chakula. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa Watanzania woteniwakumbushe, mtu aliyekula kile chakula akaenda hakurudiMwalimu alisema ni Mhaini, Traitor. Kwa hiyo, yoteyanayotokea sasa, kama wewe ulipata elimu, unaendaunawadanganya wanavijiji wewe ni Mhaini. Kama weweulipata elimu, unazunguka kwenye makampuni unakusanyafedha, wewe ni Mhaini. Kama wewe ulipata elimu,makampuni yako yakikosa kazi unaanza vurugu wewe niMhaini. Hiyo ndiyo statement ya kwanza ya Mwalimu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini shule niliyosoma mimi, MaraSecondari ilikuwa inaitwa Musoma College ilikuwa yaWamarekani, Neil Armstrong Apollo Mission 11 ilivyotua

Page 227: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

25 MEI, 2013

227

mwezini ilikuwa ni tarehe 21/7/1969, mimi nilikuwa form onena nilikuwa shule ya Wamarekani na walituletea filminamwonyesha Armstrong anatua mwezini na statementambayo Armstrong aliitoa ni hii hapa, “That’s one small stepfor man; one giant leap for mankind.” Hatua ndogo lakinimaendeleo kwa mwanadamu. Mwalimu alikuwa mjanjasana na sijui kama wengi wanasoma, mwaka huohuoalitueleza akasema, wengine wakienda mwezini sisi twendevijijini. Ndiyo maana Waheshimiwa Wabunge na Watanzaniawote mimi nimeleta bajeti ya kwenda vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mambo ya rasilimali kwambaMwalimu alisema zisitumike, ni uongo na makosa. Mwaka1969 ndiyo alianzisha Shirika la Mafuta la Petroli (TPDC). KamaMwalimu alitaka rasilimali zisitumike, kwa nini alianzisha shirikahili? Mwaka 1972 alianzisha Shirika la Madini la Taifa(STAMICO). Kwa hiyo, ndugu zangu ninaomba tuwewanafunzi wazuri wa Mwalimu na tujaribu kusoma vitabuvyake kwa undani zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hapohapo kwa kuwa tunaendavijijini ni suala la REA. Ndugu zangu bila umeme vijijini hakunamaendeleo. Dira yetu ya Maendeleo ya mwaka 2025itafanikiwa ikiwa wanavijiji watatumia umeme. Mambo yafedha tumeyasikia, sio ya kwangu peke yangu, ni ya Serikalinzima, hili jambo tutakwenda kulitafakari na ushauri wenutumeuchukua tunashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kwenye huohuo umemenataka niwaombe na nyie Waheshimiwa Wabunge mtusaidie.Sisi tuko hatua nyingi mbele sana, hatulali pale Wizarani.Tumepiga mahesabu ya kuweka umeme shule zote zaTanzania na zahanati na vituo vya afya vyote, tukafikia hesabuya kupata shilingi bilioni 2.2 USD. Kwa hiyo, sasa tusingoje tuSerikali, nawaomba nyie Wabunge kwa kuwa na nyie niMadiwani, muanze kwenye Halmashauri msikae tu kungojaSerikali, itatuchukua muda, kama tulivyofanya kwenye shule.

Page 228: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

228

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, REA wamepiga hesabu, kuwekaumeme kwenye shule yenye madarasa nane inahitaji milioni3.9, karibu milioni nne, kwa nini Halmashauri zetu zisije kuombaREA zina milioni nne mkononi, vijana wakawekewa umemena dispensary zetu zikawekewa umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vile vile tumepiga hesabu kuwekaumeme kwenye Zahanati na vituo vya Afya ni karibu milioni13. REA iko tayari kwa sababu ni ya Serikali, tafuteni hizo helanjooni Wizarani au nendeni moja kwa moja REA, kamawakikataa kuwawekea umeme msiwape posho kwa sababuwatakuwa wana posho ya Serikali, basi mtakuja kuniambia.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, hapo hapo tuna miradi mingiambayo itakuja, kwa mfano, MCC ndugu zangu tusijidharauprogram yetu ya umeme ni katika programs ambazozinaheshimika sasa hivi na ndiyo maana tumeshinda miradiya Marekani MCC one na MCC two na ndiyo maanaEuropean Union wamekuja hapa kufanya mazungumzo nasisi tuwe nao pamoja kwenye mambo ya umeme. Serikali yaMarekani focus yao/ushirikiano wao na sisi ni juu ya umeme.Kwa hiyo, ndugu zangu tutatumia njia zote, kuhakikishaumeme unawafikia wanavijiji (Makofi).

Mheshimiwa Spika, nije kwenye kutengeneza bajeti,ndugu yangu upande wa Kambi ya Upinzani bajeti za karnehii na karne inayokuja zina formular moja ndogo, lakini nzito.Economic prosperity in the 21 Century and beyond, equationhiyo inasema ni sayansi ukijumlisha teknolojia, ukijumlishaubunifu, unajumlisha mtaji, unajumlisha na rasilimali watu, theEconomic prosperity of the 21 Century equals; Science plusTechnology plus innovation, plus financial capital, plus HumanCapital. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuanzia hapa nawaombaWatanzania wanaonisikiliza, itakuwa ngumu menginemtasahau, nawaombeni mlipo mchukue kalamu na karatasi.

WABUNGE FULANI: Ahaa!

Page 229: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

229

25 MEI, 2013

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Watanzania waliokohuko nje, nyie Wabunge kama hampendi acheni, lakiniWatanzania kwa sababu haya ndiyo yatatoa mengi.

Ndugu zangu CHADEMA, nasema kwamba, mapatoyangu yote kwenye bajeti yangu, fedha za ndanizinazokwenda kwenye miradi ni 98%. Wewe ukija hapa kamaunatengeneza bajeti nzuri, ni lazima uje na tarakimuinayopingana na hii au inayokubaliana na hii siyo ya maneno.Nasema kuwa miradi ya maendeleo kwenye bajeti yoteitachukua 90% na mengineyo 10%.

Mheshimiwa Spika, ukiwakilisha bajeti ya kileocontemporary budgets ni lazima uje na tarakimuinayopingana na hiyo siyo maneno. Kwa maneno mengine,bajeti i l iyowasil ishwa hapa ya upande wa pil i, waowanasema kuwa Economic Prosperity kwa karne ya 21,nisikilize vizuri, ni sawasawa na porojo, unaongeza kesizisizokwisha, unajumlisha matusi, unajumlisha upotoshaji,halafu unajumlisha uchovu wa kitaaluma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ndugu zangunawaomba CHADEMA mkajifunze, hata wafadhili wenuwakawafundishe kutengeneza bajeti, nenda ukafuatilieMabunge yote, nenda Bunge la Marekani, Bunge laUingereza, bajeti wanakwenda na tarakimu zinazokinzana,siyo mwingine analeta tarakimu wewe unaleta porojo,haiwezekani! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nije uchumi wa Tanzania,hapo ndipo nilisema kuwa kuweni na kalamu ndugu zangu,ni lazima dira yetu ya maendeleo ya mwaka 2025 itufanyetuwe na uchumi shindani. Sasa nataka kuthibitisha kwa ninilazima tuwe na uchumi shindani na kwa nini sisi tulileta hiibajeti.

Mheshimiwa Spika, nachukua pato la mtu mmojammoja kwa baadhi ya nchi. Kwa mwaka jana, GDP percapital Tanzania sasa hivi ndio dola za Marekani 599 karibu

Page 230: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

230

25 MEI, 2013

600, Kenya ni 977, Uganda ni 589 na kwa kuwa wao mafutayakianza wataruka na kutuzidi sasa sisi tulishiriki katika harakatiza kuikomboa Afrika, sikiliza nchi ambazo tulizisaidia.

Mheshimiwa Spika, Zimbabwe GDP per capital ni 756,mbali ya vita yote wanatuzidi, Msumbiji GDP per capital ni650 wanatuzidi, South Afrika wamekuwa trained sehemunyingi, wao ndiyo wakubwa, ni dola 7507, Shelisheli wakatinilipokuwa Seychelles, Mheshimiwa Ngwilizi unaheshimikasana pale, mwingine alinitambulisha kuwa wewe ni Presidentwa Seychelles, wenyewe wana dola 11,226, Djibouti, Kisiwakidogo ni dola 1,523, wanatuzidi sisi. Kwa hiyo, ndugu zanguwa Vyama vyote nchi hii muda wa porojo na siasaumekwisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hivi tunaongelea uchumi namaendeleo na ndiyo maana ukinitajia hapa mlolongo wakesi ukategemea, nikafukue yale mafaili Wizarani, nadhanikuwa kwanza ni Mbunge wa kuteuliwa, nikapewa Uwaziri,nadhani hawakunituma pale kupekua mafaili. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa kwa sababu mtu una ushahidina vyombo vya dola vipo, nenda mbele kama alivyosemaMheshimiwa Mwijage kuwa vitu tuvimalize. Haliwezi kuwaTaifa, wewe unapata mtoto wako leo hii mpaka anamalizashule ya msingi unaongelea kitu hicho hicho, anaingia mpakaana-graduate unaongea kitu hicho hicho, hiyo ni stagnationya ajabu sana, stagnation of minds.

Mheshimiwa Spika, sisi tuna energy mix; umeme wetuutatokana na gesi, makaa ya mawe, hydro (maji), jua, upepo,joto ardhi pamoja na bio energies kama mabaki ya miwa.

Mheshimiwa Spika, sasa nataka kugusia mambo yabomba, ndiyo maana nilisema muwe na kalamu vizuri.Umeme ambao tunanunua sasa hivi na hii siyo siri, siyokwamba Serikali inaficha, mtu mwingine atasimama hapaatasema wamechukua hela wamepeleka TANESCO, sasaulitaka tubaki gizani?

Page 231: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

231

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, Economy gani inakufanya weweunazuia TANESCO isipewe fedha, hiyo ni primitive economy.Ni uchumi upi unafanya TANESCO isipewe fedha kuzalishaumeme. Ni vitu vya ajabu sana na sisi hatufichi, tunawapatiana ni fedha za walipa kodi na mnasikia kuwa Mheshimiwammoja alisema umeme ukiwepo inflation inashuka. Sasamwingine anasema tukae gizani. Sasa hawa ni baadhi yawale ambao labda wana biashara za majenereta aubiashara za mafuta, ni hawahawa. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuna kampuni saba ambazozinatuuzia umeme. Tuli- sign mkataba wa kujenga bombamwaka jana China, Septemba 2011. Tumepiga hesabu tokatuweke sahihi ya kujengewa bomba, Septemba 2011mpakatarehe 22 ambapo hapa wengine wanasema muwasikilize,mpaka tarehe 22 juzi tulivyoahirisha Bunge, mafutayaliyotumika ni pesa za Marekani milioni 596.49.

Mheshimiwa Spika, toka tuweke mkataba mwakajana Septemba mpaka juzi hapa ndugu zetu wanafanyamatatizo tarehe 22, katika mafuta tumetumia pesa zaMarekani milioni 596.49, ni sawasawa kwa fedha za kwetuTrilioni 940.66,

WABUNGE FULANI: Ni bilioni.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: No, no hizi ni milioni500 dola za Marekani, sasa Tanzania zinaingia kwenyematrilioni.

SPIKA: Haya sawa ni kiasi kikubwa.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika,mtatafuta exchange rate, hii ndiyo figure nilipiga anyway,lakini bado itakuwa ni zaidi ya hiyo, labda niongee kwa dola,hii conversion ina matatizo.

Mheshimiwa Spika, tumepiga kuanzia sasa hivi kuanziamwezi ujao, Juni bomba letu tumesema litakamilika Desembamwakani. Angalia mafuta tutakayotumia, ni fedha za

Page 232: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

232

25 MEI, 2013

Kimarekani Trilioni 1.44. Sasa ndugu zangu, Mwanasiasa mtuwa uchumi anayepinga bomba, unashangaa yeyeamesoma uchumi upi na ameusomea wapi?

Mheshimiwa Spika, sasa niwaambie vile vile umemewa maji ndiyo wa bei nafuu sana, lakini unahitaji fedha zaidi,umeme unit moja ni senti kati ya tatu mpaka tano, lakiniwenyewe ni capital intensive; umeme wa gesi ni kati ya sentisita mpaka senti nane, umeme wa makaa ya mawe ni katiya tano mpaka sita. Umeme wa mafuta Naibu Waziri alisemakuwa, ni senti 31 mpaka 55. Je, watu wako tayari kuachanana senti 55 warudi sita?

Mheshimiwa Spika, Kwa hiyo ndugu zangu njia pekeeya kukuza uchumi ni kuwa na hili bomba na hesabuzinaonesha hapa, hata ukila porojo bado hesabu zinakusutahizi kwamba, tutakuwa na vitu vizito sana.

Mheshimiwa Spika, wengine nadhani Kambi yaUpinzani ilisema mikataba ije hapa gharama hizo siyo za kweli.Tumekwenda vile vile ku- search bomba letu ni kilomita 542,ujenzi wa kilomita ni milioni 1.31.

WABUNGE FULANI: Ni shilingi au dola?

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Ni dola nimeonashilingi zina matatizo maana zinabadilika conversionzinabadilika. Halafu hii ni International Business we have toquote in Dollars. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa bomba kwa kilomita,halafu kwa kipenyo kwa milimita USD per millimeter ya kwetuni 1,426 ambalo wanasema la bei mbaya. Tukaenda Mabaramengine, hivi kweli tumedanganywa? Hawa wapigamaneno wanasema sijui tumeibiwa, sijui Wanasheriahawakuwepo.

Mheshimiwa Spika, tumekwenda bomba moja,Marekani wanayo mengi, la Texas tumechukua la umbali wakilomita 172.8. Wakati ujenzi wa kilomita moja sisi ni 1.31 milioni

Page 233: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

233

25 MEI, 2013

wao ni 1.61 milioni. Halafu ule ujenzi wa dola kwa kilomitakuendana na kipenyo, wao ni 1,759, sisi ni 1,426. TulivyotokaMarekani tukaenda Bara la Ulaya, tukachukua bombalililojengwa na Opel ya Ujerumani, kilomita 470.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa kilomita moja ni Dola zaMarekani milioni 2.98, la kwetu msisahau ndiyo maananilisema Watanzania wanaonisikiliza wachukue kalamu, lakwetu ni milioni 1.31, ukichukua kwa kipenyo hili la Ujerumanila kwetu ni Dola 1,426, wao ni Dola 2,124. Tukaingia Bara laAsia; kuna bomba linajengwa kati ya Iran na Pakstanilitakwisha mwakani na kwa kuwa bado linajengwa kwa hiyo,hawajakamilisha mahesabu.

Mheshimiwa Spika, wao kwa kilomita moja ni kati yaUSD in millions 1.35 mpaka 1.91. Halafu kwa kipenyo ni 1,427mpaka 1,784. Kwa hiyo, ndugu zangu WaheshimiwaWabunge na Watanzania wanaonisilikiliza, hawa wanaopigakelele kuwa tumedanganywa, tumefanya nini, ni walewaleambao walitumwa miradi yao haikushinda, sasawanatuchafua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mitambo ya kusafisha gesitulisema inabaki kule kule Lindi na Mtwara, hesabu za kujengamtambo wa kusafisha gesi Songo Songo - Lindi itachukuamilioni 151.74 Dola, nimesema niko kwenye Internationalcurrency sasa, USD milioni 151.74 na kule Mnazi Bay tutajengahuko huko.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mtu anayetiapropaganda kuwa gesi itasafirishwa na nini, ni vitu ambavyotumevieleza mara nyingi. Ya Mtwara itakuwa ni Dola zaKimarekani milioni 197.87. Kwa hiyo, ndugu zangu, huu niujenzi ambao unahitaji fedha. Je, ni sisi wenyewe hapaduniani tumeanza kuwa na haya mabomba?

Mheshimiwa Spika, nimechukua mabomba matatumarefu duniani kote; bomba la kwanza liko China na linaitwaNorth East Pipeline, linatokana Jiangjin mpaka Shanghai. Kwanini wamejenga bomba kutoka huko wakaleta kwenye

Page 234: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

234

25 MEI, 2013

Center ya uchumi Shanghai, si ndiyo center ya uchumi yaChina? Hii ni kilomita 8,656 kwa hiyo zetu za 542 ni kamamchezo, kilomita 8,656. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, bomba linalojengwa kati ya Boliviana Brazil bado ukiangalia uchumi wa Brazil na Bolivia, Baraziliko katika nane bora kiuchumi duniani sasa hivi, ni katika nchiiliyoingia kwenye matrilioni ya GDP. Kwa hiyo, bomba lakutoka Bolivia kwenda Brazil, kilomita 4,960, bado hapawametumia akili wanatoa bomba huku, wanapeleka kwenyeuchumi mkubwa na sisi hapa Tanzania kwa sasa hivi Dar esSalaam ndiyo inatumia nusu ya umeme wote tunaozalisha.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu ni lile la Ulaya ambalo ni lakilomita 4,172.8. Kwa hiyo, ndugu zangu uchumi wote dunianiwa gesi unakwenda na mabomba hakuna mahali kwenyegesi hakuna bomba, msidanganywe haipo duniani hapa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, Afrika labda sisi Tanzaniatunakosea, sehemu zingine Afrika wako makini. Mabombamawili yanayojengwa Afrika; moja linaitwa Trans-Saharanilinatoka Nigeria mpaka Algeria na kule unajua Algeria, Tunisiana Egypt wamejenga mabomba yanapita Mediteranian Seayanapeleka gesi Ulaya. Hayo yapo ni ya siku nyingi mengineyana miaka 20, 30 siyo mapya.

Mheshimiwa Spika, lakini hili Trans-Saharan inayotokaNigeria mpaka Algeria ni ya kilomita 4,128, wenzetu Waafrikawanajenga hilo. Mnigeria anajenga anataka kuuza gesiyake, lakini Mtanzania hutaki gesi yako uitumie kwenyeuchumi.

Mheshimiwa Spika, la pili, ni West African Gas pipeline,linatoka Nigeria linakwenda Benin linaingia Togo na mwishowake ni Ghana, kilomita 678. Kwa hiyo, ndugu zanguWabunge na Watanzania, niseme kwamba, bomba hili ndiyolitakuja kutoa umaskini nchini. Yeyote ukimsikia anapinga hilibomba, huyo siyo mwenzetu. Huyo atakuwa anawatumikia

Page 235: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

235

25 MEI, 2013

watu wengine au anatumikia makampuni mengine. Ndiyomaana nimewapatia hizi fedha za mafuta, mjue ni fedha kiasigani kama Taifa tutaingia hasara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, uchumi wa Taifa letu sasa hiviunakua kati ya asilimia sita mpaka asilimia saba, lakinitumeweka dira yetu ya maendeleo ambayo inasemakwamba, ifikapo mwaka 2025, tunataka kuwa nchi ya kipatocha kati (Middle income country). Sasa pale kuna layers tatu,kuna wale wa juu, wale pato lao la Taifa kwa mtu kwa siku nizaidi ya dola elfu kumi na mbili, wanakuja wa kati na wa chini.Chini kabisa ni kati ya dola 1250 mpaka 4800.

Mheshimiwa Spika, tuchukulie sisi tunakuwa wa chinikabisa hapo. Tuchukulie tunataka kwenda dola 3,000 na sasahivi pato letu ni dola 6,000, inabidi lazima tuzidishe mara tano.Inamaanisha uzalishaji wetu ni lazima uzidishwe mara tano.Inamaanisha umeme tunaoutumia sasa hivi ni lazimauzidishwe mara tano, ndiyo maana ya uchumi huo.

Mheshimiwa Spika, kama tukifika mwaka 2025, sisi ninchi ya kipato cha kati, hesabu zinaonesha ni lazima tuwena umeme siyo chini ya megawati 10,000, ndiyo maananiliwaambia tunatengeneza bajeti ya kwenda karne ya 22.Tunaanza sasa hivi kujitayarisha kutengeneza megawati10,000, lazima hizo megawati 10000 uanze sasa hivi.

Mheshimiwa Spika, huko tunakokwenda tukipatavyanzo vingine, kama vile katika makaa ya mawe tukapataumeme, hata umeme wa maji hatujasema kwambahatuutaki, ila hali ya sasa ya climate change inaoneshakwamba tusivuke nyuzi mbili, lakini huku Indian Ocean tayaritupo kwenye one degree Celsius na kuna sehemu zinginendani ya Tanzania wameshavuka nyuzi mbili. Kwa hiyo,hatusemi kwamba maji hatuyataki, lakini tunasema kwanzatutulie, tuendeleze vyanzo vingine, ili tutakapofika huko tuwena umeme ambao unaweza ukatufanya tukafika huko.

Mheshimiwa Spika, lakini kufika huko, nimesemauchumi wetu sasa hivi unakua kwa asilimia sita mpaka saba,

Page 236: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

236

25 MEI, 2013

tunapigana ili ifikapo mwaka 2015 uwe umeshafika asilimianane na huwezi ukafika huko bila umeme wa uhakika.Anayepinga tusiwe na umeme wa uhakika, siyo mwenzetuhuyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapokwenda kwenye nchi zakipato cha kati, sasa hivi GDP yetu ilikuwa 25, yaani pato lamwaka dola, naona shilingi zitakuwa nyingi kutamka, dola nirahisi kidogo. Kwa kuwa, pato letu sasa hivi limetoka dola zaKimarekani bilioni 23 kwenda mpaka bilioni 28, lakinitutakapofika mwaka 2025 kama kweli tunataka kufutaumaskini na kama kweli sisi ni nchi ya kipato cha kati, ni lazimapato letu la Taifa livuke dola bilioni mia moja. Kwa hiyo,namaanisha uchumi tulionao sasa hivi inabidi tuzidishe maranne, ndiyo dira yetu ya maendeleo iwe na maana kamatulivyokuwa tumekusudia.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hali hiyo, ndiyomaana sisi Wizara na Serikali tumeamua kulisuka upya Shirikala Umeme la Taifa. Hata kama una rafiki yako pale alikuwaanakupatia fedha siyo mambo ya ubinafsi haya ni mamboya Taifa. Kuisuka TANESCO haimaanishi tunamchukia mtu.TANESCO imeundwa mwaka 1964, lakini wazazi wa TANESCOwamekuwepo toka ukoloni mwaka 1931.

Ikiwa toka mwaka 1931, mwaka 1964 mpaka sasa hivi,ni asilimia 21 tu ya Watanzania wana umeme, tena ambaohautabiriki, umeme ambao tunagombana, umeme ambaokila mwaka mnafukuza Mawaziri, nadhani kama Taifa itakuwani vitu vya ajabu eti Taifa huo ndiyo mtindo wetu wakuendesha Serikali wa kila mwaka tunagombana, tunafukuza,nadhani ndiyo maana tumedhamiria kulisuka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, safari tumeianza tarehe 30 mwezihuu, Menejimenti na Bodi nimewaambia, hivi ninyi wenyewe,mkitaka TANESCO ibadilishwe mnataka iwe na sura ipi?Watanipatia ripoti yao na watalaam wangu Wizaraniwameshanipa ninayo.

Page 237: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

237

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, bahati nzuri tumetafuta hela AfricaDevelopment Bank na tumetia wenyewe terms of reference,tutapata document tatu. Lakini hatuwezi kulibadilisha Shirikaambalo lina madeni mengi, tumetafuta fedha World Bank,watatupatia jumla ya dola milioni mia tatu, (milioni mia miamara tatu). (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, tumekwenda AfricanDevelopment Bank, tumepata milioni mia mbili, zote hizo nidola. Kwa hiyo, Wabunge na Watanzania, hapatunapoongea ndiyo maana nasema siongei vitu vyamaneno, ni vya vitendo, ninazo dola milioni mia tanokuibadilisha TANESCO.

Mheshimiwa Spika, TPDC tunawaachia vitalu kulechini, mwingine anasema mmeacha kwa sababu yaWachina, nadhani ilikuwa kwenye speech, sasa na wewetuseme umetumwa na nani na Mwingereza? (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu hatuwezi kupatafaida kama TPDC haiwezi kufanya biashara ya kuchimba naya mafuta haiwezekani! (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nawaeleza Wabungekwamba, safari imeanza, tarehe 30 Mwezi huu watanipatiaripoti, Menejimenti na Bodi, Wizarani wameshanipa,tumepata grant za African Development Bank, siyo mkoponi grant ya ku-transform TANESCO na TPDC.

Mheshimiwa Spika, nimefika mwisho niseme tu watuwalioandika riwaya nyingi za mambo ya vifo walisemakwamba binadamu hafi na wengine wanaulizwa ukifautaenda wapi? Anasema nikifa sitakwenda mbali, nitakuwanimepumzika chumba jirani, lakini nawaangaliamnayoyafanya. Ndugu zangu Watanzania, Mwalimuanatuangalia, Karume anatuangalia, Kawawa anatuangaliana Sokoine anatuangalia. (Makofi)

Page 238: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

238

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, Sokoine alitoa msemo mmoja,alisema: “Kwenye nchi hii kuna watu hawajafanya kosalolote, hawajatufanyia baya lolote, lakini nao hawajawahikufanya zuri lolote, akasema watu hao hawafai”. Sasa kilaMtanzania anayenisikiliza ajipime mwenyewe. (Makofi/Kicheko).

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, Naafiki. (Makofi)

MHE. CHRISTOPHER O. OLE- SENDEKA: Mwongozo waSpika.

KAMATI YA MATUMIZI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 58 – Wizara ya Nishati na Madini

Kif. 1001 - Administration and Human Resources Management… … ..Sh. 8,505,134,000/=

MWENYEKITI: Ndiyo mshahara wa Waziri, mkiwa briefand nice mtapata nafasi wengi, Mheshimiwa Chenge!

MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii. Katika hatua hii tunapitiamafungu ya Wizara hii, nimesimama kujaribu kuiomba Kamatiyako ione umuhimu wa kusikiliza kauli na maombi yaWabunge wengi waliochangia katika hoja hii hasa kwenyeeneo la umeme vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosema mtoa hojamwenyewe na kama tunavyofahamu sote kwamba umemeni uchumi, umeme ni kichocheo cha maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najaribu kushawishi Kamatiyako kwamba, nilipochangia nilisema mahitaji ya REA kwa

Page 239: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

239

25 MEI, 2013

mwaka ujao wa fedha ni bilioni mia nne na hamsini.Tunafahamu uwezo wa bajeti yetu ndiyo huo, lakininilibahatika kuwa Mwenyekiti wa Kamati yako ya kutafutavyanzo vipya vya mapato, nashukuru pamoja na Wajumbewengine tulifanya kazi nzuri sana.

Mheshimiwa Spika, tunaamini yale mapendekezoyakichukuliwa na Serikali katika maeneo mawili, upande wasimu za mikononi ile miito tu kupiga simu. Tuiachie Serikalikuhusu viwango, hiyo ndiyo kazi ya Serikali, watakapoleta sisindiyo tunaweza kusema hapa jamani muongeze aumpunguze. Lakini ule msingi wa maeneo ambayo tunafikiriatunaweza tukapata pesa, tukapaleka kwenye REA, lakinitusisahau pia tupeleke kwenye Mfuko wa Mawasiliano Vijijini.Msingi kwenye eneo la simu, lakini pia katika miamala yakutuma na kupokea fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaamini pale tutapatapesa nyingi, tumepiga mahesabu tunajua. Kwa hiyo, nashauriSerikali waliangalie eneo hilo, kwa mahesabu tunawezatukapata very easily pesa ya kutosha kupeleka kwa Wakalawa Umeme Vijijini lakini pia kwa Mfuko wa Mawasiliano Vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalotunaliona na hapa napenda niwe muwazi kabisa kwamba,Serikali imewekeza sana kupitia Bunge hili katika ujenzi wabarabara. Mwaka 2007 nilipobahatika kuwa Waziri waMiundombinu, tuliongeza tozo ya mafuta kwa shilingi miambili. Hii imetufikisha hapa tulipo, lakini tunaamini kwambatunaweza pia tukaongeza tozo kwenye mafuta kwa kiwangoambacho kimesemwa, tuiachie Serikali. Naamini tukiendampaka 100 au 113 tupo sawa, kwa inflation.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tukichukua siyo yoteiende kwenye barabara, sehemu moja iende kwenyebarabara na sehemu nyingine iende kwenye REA, tutafikavizuri tu. Ahsante sana.(Makofi)

MHE. JAMES D. LEMBELI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa nafasi hii. Wakati nikichangia

Page 240: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

240

25 MEI, 2013

nilizungumzia kuhusu kero kubwa inayowapata wananchi waKahama na hususan wananchi wa Kahama Mjini kuhusukukatikatika kwa umeme kwa sababu ambazo zimekuwahaziridhishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nil isema kamahayatatolewa maelezo mazuri ya kuwafanya wananchi waKahama waelewe kwamba, Serikali ipo, sikuwa tayari kuungamkono hoja. Lakini kwa moyo wa dhati kabisa, majibuyaliyotolewa na Waziri na Serikali yanakidhi, kwa hiyo, naungamkono hoja. Ahsante sana.(Makofi)

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekitinashukuru. Mambo mengi sana yamezungumzwa juu ya faidanyingi na kubwa tunazotazamia kuzipata kutokana na utajirimkubwa wa Gesi Asilia iliyopatikana katika nchi yetu. Hiiinanikumbusha ahadi lukuki zilizotolewa wakati Sheria yaMadini ya mwaka 1998 inapitishwa kwenye Bunge hili. Ahadizilikuwa nyingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie sualahili na nipate majibu kutoka kwa Waziri Profesa Muhongo.Katika rasimu ya sera ya gesi asilia ambayo Wabungemmegawiwa kwenye ukurasa wa tisa, Serikali inasemakwamba, Sera hii ya Gesi Asilia inahusu shughuli za katikatina shughuli za chini katika mchakato mzima wa biashara yagesi. Kwa maana kwamba, ni shughuli za usambazaji nauchuuzi wa gesi. Sera hii inasema kwamba, shughuli zautafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa gesi zitaongozwa nasera nyingine itakayoandaliwa baadaye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni nini? Nikwamba, kuna mikataba zaidi ya 27 nafikiri ya utafutaji,uendelezaji na uchimbaji wa gesi ambayo Serikali imeingiana makampuni mbalimbali ya kigeni. Haya hayatakuwa chiniya hii sera ya gesi asilia, haya yapo chini ya utaratibu waSheria ya Mafuta ya mwaka 1980, pamoja na mikatabaambayo Serikali imeingia ile inaitwa Production SharingAgreements.

Page 241: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

241

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa la Mikatabaya aina hii Waheshimiwa Wabunge ni kwamba gharama zoteza utafutaji, uendelezaji na uzalishaji ambazo makampunihaya yanaingia zinaingizwa katika kitu kinaitwa kwenyemafuta kinaitwa costal oil kwenye gas kitakuwa cost gas.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni kwamba,wawekezaji hawa itabidi warudishe gharama zao zote hizoza utafutaji, uzalishaji uendelezaji na uzalishaji kablahawajaanza kutupatia sisi fedha. Sasa, kimsingi natakaMheshimiwa Waziri atuambie, hii mikataba ambayo tayariSerikali imeshaingia na watafutaji gas, iletwe Bungeni, tujuetumesaini kitu gani ambacho hakitafungwa na Sera hiiambayo Sera hii inasema hii mikataba haihusiki na hii gas.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, kwa mujibu wamikataba hiyo TPDC, Shirika la Mafuta linatakiwa lifanyeukaguzi, lifanye audit ya gharama zote za utafuta, uendelezajina uzalishaji wa gesi. Itakuwa vizuri Bunge lako Tukufu liletewetaarifa za ukaguzi za TPDC ambazo zimeshafanywa kwamakampuni ambayo tayari yamepewa mikataba hii iliWabunge waelewe, tayari hizo gharama ambazo inabidi zijeziondolewe katika mali yote itayopatikana ndiyo tuanzekuchangia kwenye kupata faida za huu utajiri mkubwaambao tunao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, isipofanyika hiyo,hatutakuwa tofauti na yaliyotokea kwenye Sekta ya Madiniambayo kwa takwimu za Waziri mwenyewe katika dola bilioni11 ambazo zimepatikana…

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaondoa shilingi nisemewazi.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Mawaziri naomba muwemnaandika. Nimwite Mheshimiwa Mangungu atafuatiwa naMheshimiwa Bungara. Mheshimiwa Mangungu!

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Kwanza nianze kwa kumshukuru

Page 242: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

242

25 MEI, 2013

sana Waziri wa Nishati na Madini na Katibu Mkuuu wa Wizaraya Nishati na Madini kwa kazi kubwa na ushirikiano waliotupakuhakikisha pesa zetu Wilaya ya Kilwa kutokana na uchimbajiule wa gas zinapatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niliyotaka kufahamu nikwamba, Serikali inatamka nini na inachukua hatua ganikuweza kuwafahamisha wananchi wa Mikoa ya Lindi naMtwara, ni jinsi gani ambavyo wananufaika au watakujakunufaika katika Sekta hii ya Gas na sekta nyingine mtambukakama vile Kilimo, Ufugaji pamoja na Uvuvi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana kwa kutokufanyikahili, ndio kunaleta matatizo na wananchi wanajichukuliasheria mkono kwa sababu wana wasiwasi kwamba uwekezajihuu utawanufaishaje. Hii inatupa wasiwasi maana tunawezatukakosa mwana na maji ya moto. Naomba ufafanuzi waSerikali.

MHE. SELEMANI S. BUNGARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Katika mchangowangu wa maandishi nimezungumzia habari ya Kiwanda chaMbolea kilichoahidiwa na Serikali kuhusu gas ya Songo Songo.Hii inamaanisha kwamba, Watanzania sasa hiviwanapoahidiwa jambo inabidi Serikali itekeleze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mliahidi Wilayaya Kilwa, wananchi wangu wanauliza ni lini Kiwanda chaMbolea kitajengwa Kilwa kutokana na gas ya Songo Songo?Tukiamini kwamba watu wa Songo Songo au watu wa Kilwa,tumeruhusu gas kuja Dar es Salaam. Tuliishtaki Serikali naSerikali mkatuambia tuondoe kesi Mahakamani ili gas ije Dares Salaam, kesi tukaondoa na mkatuahidi kwamba,mtajenga kiwanda cha mbolea na mpaka leo kiwanda hichohakijajengwa.

Je, Serikali inasema nini kuhusu jambo hili, kiwandacha mbolea kitajengwa lini? Haya ndiyo matatizo ambayoyanawapa wasiwasi watu wa Mtwara huko, kwamba

Page 243: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

243

25 MEI, 2013

mnapoahidi sivyo mnavyotenda. Je, Kilwa itapata linikiwanda cha mbolea kutokana na gas? Ahsante sana.(Makofi)

MHE. JOHN M. CHEYO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Nasimama kuunga mkono kabisa dhana yaWaheshimiwa Wabunge wengi ambao wamezungumzakwamba, pale palipo na rasilimali watu wa pale wafananefanane na hilo. Hili nalisema kwa sababu nilipokuwa nafanyaile biashara ya jumla ya Urais ndicho nilichosema 1995.(Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwamba ili watu wafananefanane na dhahabu, kwa hiyo nakubali. Lakini kwa rafikizangu, ndugu zangu, watani zangu wa Mtwara, kama kunawatu ambao ndiyo wangechangamkia kabisa bomba niwao. Kwa sababu wangechangamkia ile gas ichenjuliweMtwara na Waziri amesema hakuna njia yoyote, lazimaichenjuliwe Mtwara. Ukishaichenjua imekuwa mali na mahalisasa pa kuombea ni hapa, una kitu cha kuuza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikiwa haijachenjuliwa hunakitu cha kuuza na mahali pa kuuza hata ukiweka Kiwandacha Mbolea, wao wananunua iliyochenjuliwa, kiwanda chakufufua umeme wananunua gas iliyochenjuliwa. Soko likoDar es Salaam, wapelekee haraka watu wa Dar es Salaamwanunue upate pesa, ukipata pesa ndiyo unasema sasanimegee basi kidogo na mimi nifanane fanane kidogo nagas ambayo unayo. Naona kuwa lile ndiyo tungepigania,mambo mengine tunadanganywa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Mheshimiwa Wazirifigure moja kubwa ameizungumza ni ya umeme, one pointfive tri l l ion in a year. The tri l l ion moja kwa mwaka.Nimeangalia vitabu vyake vyote hapa, hii trilioni 1.5 iko wapikwenye kitabu chake na vitabu vingine sioni. Ndiyo kusemakila anapochukua pesa kupeleka TANESCO unakata REA,unakata na wengine, ndiyo unapeleka kule.

Page 244: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

244

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeshukuru MheshimiwaWaziri angesema hiyo 1.5 trillion jamani, hii ndiyo gharamana iko hapa. Kama hajawekewa kwenye kasma yake, basiatuambie fortunately name niko kwenye Kamati ya Bajeti,atuambie na ni lazima hii ionekane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ukiangalia hatakwenye Appendix I, hakuna transfer to TANESCO. Sasa hizozinatoka wapi? Kwa hiyo, ningependa hilo aliseme wazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hilo, helayote ambayo tutaikasimia kwa ajili ya REA, naomba iwe ringfenced isitumike mahali pengine. (Makofi)

MHE. DKT. AUGUSTINE L. MREMA: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Waziri waNishati na Madini kwa kazi nzuri, kazi kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, langu ni kutaka kumwungamkono Mheshimiwa Chenge aliloulizia kuhusu tufanye nini sisiWabunge katika kusambaza umeme vijijini. Naomba tufanyemaamuzi magumu, maamuzi ambayo yanawezayakatupatia fedha za kusambaza umeme vijijini. NafikiriaYarabi, hii kazi baadaye tutamlaumu Waziri, tutailaumuWizara, tutasema haifanyi kazi. Miezi mitatu tu iliyopita kuleVunjo, transformer nne ziliungua na nyingine zikaibiwa nawezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumehangaika sana naKaimu Mkurugenzi wa TANESCO namna ya kupata hizotransformer ilikuwa ni kazi ngumu sana hazipo, hazipatikani,ina maana hakukuwa na fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili kuna vijiji kule Vunjo kama10 ambavyo tayari tumechimba mashimo, nguzo za umemeziko chini, nyaya hakuna na hizo nguzo zimekaa zaidi yamiaka 10. Leo tukisema wasambaze umeme zile nguzowanakwenda kufanya nazo nini kama hatutafuti fedha zakutosha za kuwapa.

Page 245: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

245

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, kule Vunjo na Rombo sisimara nyingi umeme unakatika katika. Unakatika kwa sababuzile njia ambazo zinasafirisha umeme kwanza ni za zamani.Kwa hiyo, ina maana kwamba mvua zikinyesha nyingi,matawi yakianguka kwenye nyaya zile umeme unakatika,umeme unakuwa mdogo. Sasa tunafanyaje kusafirishaumeme huo wa Vunjo mpaka kwenda kule Rombo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninachotakakusema ni kwamba, kama tunataka kuinua maendeleo yawananchi vijijini hasa vijiji vyangu karibu vyote vya Vunjokutokana na maendeleo mliyokwishawaonyesha walewananchi wa Vunjo mambo ya barabara nzuri, mambomasoko, watu sasa wanataka umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninachotakakusema ni kwamba, naomba tufanye maamuzi kwenyeumeme, tuweke hela na kwenye mambo mengine tupatehela za kwenda vijijini. Ahsante sana.

MWENYEKITI: Ahsante Mzee. Suala la kutafuta fedhakatika maendeleo ambayo tumependekeza, nadhanimlifanyie kazi Serikali na Kamati ya Bajeti kwa sababu badotuna nafasi ya kuangalia.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Mheshimiwa Waziri katika majumuisho yakealisema kwamba, tumfikirie Mwalimu Nyerere na miminiungane naye kumfikiria Mwalimu Nyerere kwamba alisemaili nchi yetu iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozibora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa misingi hiyo hiyo yaMwalimu, mwaka jana, kwenye hatua hii ya Kamati, niliombaufafanuzi kwa Waziri kuhusu utekelezaji wa maamuzi yaBunge. Maamuzi ambayo kama yangetekelezwa tusingefikiahatua tuliyofikia. Mheshimiwa Waziri akijibu kuhusu hoja hiyoya kuhoji kuhusu utekelezaji wa Maazimio ya Bunge, akasema

Page 246: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

246

25 MEI, 2013

kwamba, yeye hafanyi kazi na vyombo vya habari walamagazeti. Nilikuwa nahoji kuhusu utekelezaji wa Maazimioya Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mwaka mmojaumepita na naamini Mheshimiwa Waziri alipata nafasi yakufikiria haya. Sasa ningependa kupata ufafanuzi kutokakwake. Kwa sababu watu wengi na hili ndiyo ametumia sanaMheshimiwa Waziri. Utekelezaji wa Maazimio ya Bungeanachukulia kama ni kufukua mambo ya zamani, anachukuani kama ya magazeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabungemambo haya yana uhusiano. Maazimio ya Richmondyalisema kwamba kuanzia baada ya Richmond, TanzaniaBunge liwe linashirikishwa kwenye maandalizi ya mikataba.Leo nchi inaingia kwenye migogoro ya mikataba ya gas,mikataba ya madini na mikataba mengine. Azimio hilihalijatekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maazimio ya Richmondyaliagizwa toka mwaka 2008 kufanyike uzalishaji mkubwa waumeme na megawatt 300 za Mtwara zikatajwa. Maazimiohaya hayajatekelezwa. Yakapitishwa maazimio mengine yagas asili, yakataka ushirikishwajii wa wananchi. Maazimio yotehaya hayajatekelezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukapitisha maazimio mengiya Bunge ambayo kama yangetekelezwa, tungepataufumbuzi na tukapitisha vile vile mwaka jana Bajeti, pesatumetenga za REA. Mwaka mzima umekwisha, pesazilizokwenda kwenye REA ni asilimia 13 tu za umeme vijijini.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ningependaMheshimiwa Waziri atoe ufafanuzi. Maana yake ametumiamaneno mengi sana ambayo mimi nayaona ni siasa chafutu siyo siasa safi ya kutumia asilimia, kuzipotosha na kila kitu.

Page 247: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

247

25 MEI, 2013

Kama tunatekeleza umeme vijijini kwa maana kupeleka pesakwa asilimia 13 tu, hivi kwa takwimu ya kawaida ni nanialiyeshindwa. Kwa asilimia 13 tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba MheshimiwaWaziri, atupe ufafanuzi, ni kwa nini maazimio ya Bunge mpakaleo hayajatekelezwa kwenye maeneo yote haya. (Makofi)

MWENYEKITI: Haya, tunaendelea. Maana yake leowote mnahutubia. Haya Mheshimiwa nilisema nani,Mheshimiwa Kayombo, atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt.Kikwembe.

MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO: MheshimiwaMwenyekiti nakushukuru. Mwaka 2006 wakati nikichangia,nilisema kwamba, kwa wakati mrefu ujao nchi hii uchumiwake utachangiwa zaidi na Mikoa ya Kusini na mimi natokaMkoa wa Ruvuma, niko katika Mtwara Corridor. Nasimamakwa ufahari kabisa kwamba Mungu ametujalia na rasilimalihizi ili kuchangia uchumi wa Taifa letu na ni wakati wa nduguwa Mikoa ya Kusini kuchangia Taifa hili. Hii ni fahari kubwasana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi letu ni kwa Serikali yetutu, kuona kwamba, wakati wananchi wako tayari kuchangiarasilimali hii kwa Taifa wanapewa haki zao za msingi. Katikabudget speech ya Mheshimiwa Waziri ameelezea mikakatiya umeme na umeme ambao ni mixed kwa maana yakwamba kutakuwa sasa na makaa ya mawe ambaounatokana na ule mradi wa Ngaka. Ule mkaa wa mawekule una mambo mengi sana. Yale majadiliano ya TANESCOyanavyochelewa, fidia za wananchi na umeme vijijini katikavile vijiji. Lakini hapa nataka tu kujielekeza katika hili la fidiakwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 30, ule mgodi Mkuuwa Mkoa aliufunga kwa sababu ya pressure ya wananchiya kudai tu fidia zao. Mgodi unaendelea, wale wananchiwanadai nyongeza ya fidia na wengine hajawalipwa kabisa.Hakuna juhudi zinaonekana kwamba wale wananchi

Page 248: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

248

25 MEI, 2013

watalipwa leo au kesho. Mpaka baada ya kufungwa mgodi,mpaka baada ya vurugu zile ndiyo Serikali inakuja na fix dateya tarehe 15 mwezi Juni, 2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa sababu huu mradiunachangia megawatt karibu 400 kwenye gridi ya Taifa,nataka tu Mheshimiwa Waziri awahakikishie wananchi walekwamba, huu mradi kweli utakuwepo. Maana yake bilakulipa hii fidia tarehe 15 utafungwa tena. Sasa sitaki tufikehapo na ikaonekana kwamba Mbunge anafanya vurugu nawananchi wakati Serikali ndiyo inakuwa chanzo. Je, fidiakwa wananchi kama ambavyo Sera inavyosema miradi hiiisiende mpaka pale ambapo fidia kamili kwa wananchiimetolewa, itafanyika katika mradi huu wa Ngaka ili tuwezekupata umeme na nina hakika utaweza kulisha Taifa letu,lakini pia nina hakika wale wananchi watapata umeme?Ahsante sana. (Makofi)

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi. Katika mchangowangu wa maandishi nilichangia suala la wachimbajiwadogo, kwamba, Serikali iangalie sasa na ifuate namnaambavyo wachimbaji wadogo wamekuwa wakiombamaeneo yao kwa shughuli zao za uchimbaji mdogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, katika Mkoa waKatavi nilipendekeza kwamba, pamoja na kwamba panaeneo jipya la Mihama limetolewa kule kwa ajili ya wachimbajiwadogo. Nil ipendekeza wachimbaji wadogo nawalishaandika barua kwa Wizara kwa namna ambavyowalipenda kupewa maeneo ya Ibindi, maeneo yaMagamba, maeneo ya Singililwa, maeneo ya KaseseKampuni na Kasinde. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia niliongelea sualala kampuni ya GBA ambayo ipo Mpanda kule maeneo yaKampuni na Kakesi kwamba, kuna eneo leseni yaoinawaruhusu kufanya kazi katika eneo fulani, lakini wana eneolingine la ziada ambalo hawalitumii. Nilipendekeza wapewewachimbaji wadogo katika eneo hilo.

Page 249: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

249

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nataka tu kuulizia je,Serikali ina mpango gani wa kununua mitambo yakeyenyewe ya kufulia umeme kupitia gas badala ya kusubirikutumia mitambo ambayo imekuwa ikiikodisha na hivyo kuwana gharama kubwa zaidi kutokana na ile capacity charges?Napendekeza wangenunua mitambo yao wenyewe yakufulia umeme, kwa sababu wanapokodisha inakuwa nagharama kubwa zaidi ya kiuendeshaji. (Makofi)

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi hii. Napenda tu kupataufafanuzi kutoka kwa Serikali. Tumejaliwa neema Tanzaniakuwa na makaa ya mawe katika maeneo mengi na kwenyehotuba ya Mheshimiwa Waziri hapa tumeona kwamba, kunamgodi wa makaa ya mawe Kiwira na kuna mgodi wa makaaya mawe Ngaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka tu kupata ufafanuzikwamba, kwenye mgodi wa makaa ya mawe wa Ngakakutokana na hotuba ya Mheshimiwa Waziri anasemakwamba tumeshaanza ku-export, tunauza nje na baadhi tanikama 121,685 zinauzwa ndani ya nchi. Ningependa kujua nikwa nini mpaka sasa hivi Watanzania wengi hawatumiimakaa ya mawe kama nishati ya kupikia nyumbani chakula?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia vipo viwanda ndani yanchi yetu ambao wanatumia kuni, wanatumia magogo,wakati tayari tunayo makaa ndani na mpaka tuna-exportnje. Sasa ningependa kujua mkakati wa Serikali wakuhakikisha kwamba, tunatumia makaa ya mawe ambayotayari tunayo na tumeshaanza kuuza nje.

Kwanza, viwanda vyetu vitumie makaa ya mawe,lakini pia Watanzania zaidi ya asilimia 80 ambao wanatumiamkaa waweze kutumia kwa ajili ya matumizi ya nyumbani ilikuepusha matumizi makubwa na uharibifu wa misitu ambaounaendelea ndani ya nchi yetu. Ahsante.

Page 250: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

250

25 MEI, 2013

MHE. DKT. HAMISI A. KIGWANGALA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Nianze kwa kumpongezaMheshimiwa Profesa Muhongo, kwa kutupa shule na hasakwa kumwelimisha Mheshimiwa John Mnyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasimama hapa nanitasema maneno kwa uchungu sana na naomba MwenyeziMungu, aniongoze. Ninayasema maneno haya kwa niabaya wananchi wa Nzega, ambao miaka 15 il iyopitawalinyang’anywa ardhi yao kupisha uwekezaji kwenye mgodiwa uchimbaji wa dhahabu wa Resolute, pale Nzega nampaka leo hii hawajalipwa fidia wala kifuta jasho, mbali naSera za nchi yetu zinavyoelekeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pil i, nasimamakuyasema hayo kwa niaba ya wananchi wa Nzega, ambaokwa miaka 15 wamekuwa wakiathirika na uwepo wa mgodiwa uchimbaji dhahabu pale Nzega. Nayasema hayo kwauchungu mkubwa nikitazamia kuona mgodi ukifungwa miezimichache ijayo wakati kukiwa hakuna rehabilitation bondambayo inapaswa kuwekwa, ili kutunza mazingira baada yamgodi ule kuondoka. Lakini pia nayasema hayo, tukiwatunadai bilioni nne na zaidi za ushuru wa huduma ambazohazijatolewa Kisheria, kwa mujibu wa Local GovernmentFinances Act ya mwaka 1982.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nayasema hayo niki-takestock ya mazungumzo ambayo tuliyafanya mwaka janabaina ya Serikali, Wawekezaji na sisi Wabunge na Madiwaniwawakilishi kutoka Nzega, ambapo tulikubaliana hayo yoteyatatekelezwa kabla mgodi haujafungwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kwamba,wananchi wa Nzega wamenituma. Kama Serikali, isipoingiliakati kama ilivyokuwa ahadi yake kwa kuwanyima kibali chakusafirisha dhahabu wachimbaji wa Resolute, ili wawezekutulipa na kutekeleza hayo yote, wananchi wa Nzegawamenituma niseme kwamba, hawatakuwa tayari mgodiule kuondoka bila sisi kulipwa fidia wala kulipwa ushuru wahuduma.

Page 251: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

251

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ili hayo yasitokee,Mheshimiwa Waziri, ananiambia nini kuhusu kutekelezamakubaliano yale ndani ya mwezi huu mmoja ama miwiliijayo, ili vurugu zisitokee Nzega? Naomba ufafanuzi na natoania ya kutoa Hoja ya Kuondoa Shilingi kwenye Mshahara waWaziri.

MHE. NIMROD E. MKONO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi hii na mimi nichangiemchango huu.

MWENYEKITI: Ni hoja moja, sio mchango tena, nijambo moja.

MHE. NIMROD E. MKONO: Mheshimiwa Mwenyekiti,katika hoja yangu ya msingi kimaandishi nilisema, tatizo laBuhemba limekuwa sugu kwa zaidi ya miaka 13, wakatiwananchi wangu wa Buhemba, wanaambiwa kuna Kampuniya Serikali ya MEREMETA inameremeta, inakuja pale itawapamaji, itawapa barabara nzuri, nilisimama hapa nikasemahawa ni wahuni, watatuibia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadaye, mudaulivyokwenda, hawa Makaburu walichimba dhahabu paleBuhemba, wakachukua kila kitu wakaondokanacho,wakakimbia. Eneo la Buhemba, walikuwa wanalimiliki pale,wao wa MEREMETA. MEREMETA ilipoondoka haikuaga, iliachama-cynide, madawa yale mabaya, yamemwagika hovyona watu wangu wote wa Buhemba na mifugo inakunywahiyo dawa mbaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka ya nyuma iliyopita,aliyekuwa Waziri Mkuu, nilimwomba akaone hali halisi yaBuhemba; alipeleka Mawaziri watatu akiwemo Waziri waNishati na Madini, Waziri wa Maji, pia Waziri Wassira, alikuwapale. Wakaenda wakaona pale ndani ya mgodi kuna dawa,kuna chemicals zinaitwa cynide yamemwagika hovyo;wakahoji je, ni safe kwa wananchi ama hapana?

Page 252: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

252

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakaambiwa na hawaMakaburu kwamba, mambo yako sawa. Mambo hayakuwasawa; mwaka hadi mwaka mifugo ikawa inakufa nabinadamu pia wanakufa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuwa napiga keleleBungeni hapa, tutafanyaje? Mpaka nikaomba tafadhali sanamtusaidie jinsi gani ya kuepuka, kuepusha tatizo kubwaambalo ni janga la Kitaifa hapa nchini, kuhusu Buhemba.Baadaye, wananchi wenye hasira wakaanza kugombanana hawa wa MEREMETA, MEREMETA wakatimka,wakaondoka bila kuaga, madawa bado yanazagaa pale,wananchi wanahangaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, palepale Buhemba, kunawachimbaji wadogo wadogo walikuwepo enzi hizo, tanguwakati wa Mkoloni mpaka leo. Walipoondoka, je, hawa watuwa STAMICO, ambao niliomba waje pale, walirithi assets naliabilities za MEREMETA ama hapana? Kama walirithi, je,watafanya hiyo...

MWENYEKITI: Muda umekwisha, dakika tano tayarizimekwisha. Mheshimiwa Ole-Sendeka?

MHE. CHRISTOPHER O. OLE–SENDEKA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona. Nilipokuwa nachangiana baada ya majibu ya kaka yangu Mheshimiwa Waziri,nil inukuu ahadi ya Mheshimiwa Rais, katika eneo lamachimbo ya tanzanite, Mererani. Waziri, akasema Mkuuwa Mkoa alimwambia ahadi hiyo hakuiona na ndio maanalabda pengine Wizara yake imefika mahali pa kuamua kutoaleseni hiyo na kuwaacha Wachimbaji Wadogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka tu niseme siwezikutumia jina la Rais vibaya. Naijua Kanuni ya 64 (1) (d),hairuhusu; nalisema jambo hili na kurudia kusema Dkt. JakayaMrisho Kikwete, tarehe 25 Oktoba, 2010, Orkesmet aliahidi.Mwaka 2005 alipoombwa na wananchi wa Mererani, paleMererani, alisema nipeni kwanza kura, tutahangaika na hayakwa mujibu wa Sheria, wakati huo Sheria hairuhusu. (Makofi)

Page 253: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

253

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, 2010 aliahidi na nitatoaushahidi kwako na kwa Waziri Mkuu na kwa Kamati yoyoteya Bunge kwamba, Rais, aliahidi kwamba, eneo hilo leseniya Tanzanite One itakapokwisha, ataligawa baada yakwamba, Sera tumebadilisha, sasa uchimbaji wa madini yavito ni kwa ajili ya Watanzania; hilo nitathibitisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nilimwambia Waziri,aepuke kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Sheria ya Madiniinasema bayana, wazi kabisa kwamba, kuna aina sita zaleseni na miongoni mwa leseni hizo ni pamoja na leseni yakuchimba Germstone, ni pamoja na leseni ya kuchimbaIndustrial Materials na leseni zingine. Huwezi kutoa leseni yaaina ya madini yanayoangukia kwenye leseni ya Germstone,leseni hiyo hiyo ukatoa idhini ya kuchimbwa kwa Marble naGrafite.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na ili kuthibitisha hili, hataMwanasheria wa Wizara ya Mheshimiwa Waziri, katika dokezolililoandikwa tarehe 12 Aprili, samahani nilipenya kwenye Ofisiyake mpaka nikahakikisha kwamba, ninazo nyaraka.Madokezo yote ya Wataalam yanakataa kwamba, huweziukatoa leseni kuruhusu leseni hiyo hiyo moja ichimbe madiniyasiyoangukia kwenye leseni hiyo, Wizara yake imefanya.Sasa nataka niombe hili, lakini sio hivyo tu, ukubwa wa eneola kuchimba madini ya vito kwa mujibu wa Sheria ni kilometamoja ya mraba. Offer iiliyotolewa, Notification of Grant,imetolewa ya kilometa 7.6 kinyume na Sheria ya Madini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimwambie tu Wazirikwamba, nataka maelezo juu ya eneo hili na kwa kweli,nakusudia kuondoa shilingi, ili kuhakikisha kwamba, maelezosahihi yanapatikana katika kuhakikisha kwamba, madini yavito yanachimbwa na Watanzania, bila kigugumizi.Nimhakikishie Naibu Waziri wake, ndiye alikuja tukashirikianawote, tukaazimia kuunda ushirika kati ya...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

Page 254: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

254

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema nataka maelezo,vinginevyo nitatoa shilingi.

MWENYEKITI: Haya. Waheshimiwa Wabunge, dakikazetu zinakuwa 25, nimeongeza mpaka zimefika karibu 35; sasanaomba muanze kujibu. Mnapojibu, mna-refer yule aliyetoahoja na isitoshe ninazo shilingi-shilingi nyingi hapo.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti, muulizaji wakwanza, alikuwa ni Mheshimiwa Chenge, ambaye alitoaushauri tu kwa Serikali, kuona namna ya kuweza kuongezamapato na sisi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya REA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili sisi tunalipokea Serikalini.Tutaona namna ya kuweza kufanya kwa ushirikiano naKamati yako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Mchangiaji mwinginealikuwa ni Mheshimiwa Lembeli, ambaye yeye kasemaameunga mkono baada ya kupata maelezo yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwingine alikuwa niMheshimiwa Tundu Lissu, ambaye amesema katika Rasimuya Sera, shughuli zinazozungumzwa ni zile za Mid Stream naDown Stream, lakini Up Stream haisemwi na inaelezwakwamba, tutakuwa na Sera Maalum kwa ajili hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu kubwa hapa ni kwasababu ya Industry hii ya gesi. Industry ya gesi na mafuta nikitu cha kitaalam sana na pengine kama majibu ya utaalamhuu ambao watu wanafanya mpaka Ph.D. yanatakiwakutolewa hapa, tutapata kazi kubwa kweli. Kwa sababu,najaribu kutafuta, wakati mwingine nikiulizwa, kwa sababuingawa si mtaalam wa sekta hiyo, lakini kwa kuwa ndiyo sektaninayoisimamia, najifunza kweli kweli, usiku na mchana nanaona tofauti iliyopo katika uelewa wa Sekta hii. Naona kunakazi kubwa, tutachukua muda mpaka tufikie wakati mzuri wakuelewana.

Page 255: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

255

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, Up Stream inazungumziauwekezaji mkubwa sana. Huwezi ukaiunganisha na MidStream na Down Stream kwa sababu, haya mambo ni tofautina ukichanganya hutapata vizuri zile hesabu zake. Sasa yeyeanasema kwamba, dhamira ya hii ni kwa sababu yaMikataba hii kwamba, inataka kuwa-favour wale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jibu ni hapana. NaombaMheshimiwa Tundu Lissu, tutachukua muda kidogokuelewana katika hili na pengine Ukumbi huu kwa muda huuhautoshi kueleweshana, maana inahitaji karibu saa nzimatukae tunajadiliana, i l i tuweze kuelewana kwa nini,tunakwnda katika msimamo huu wa kusema tutenganishehizi Sera mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia uwekezaji wake nitofauti. Anayefanya exploration ni mtu tofauti na anayekujakufanya hizi biashara ni mtu mwingine kabisa. Uwekezajiwake ni tofauti na aina ya business yake ni tofauti kwa hiyo,ndio sababu, tunafanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa juu ya kwamba, hii ainaya Regime au Modal ya Mikataba tunayoingia ya PSA(Production Sharing Agreement), akiwa anafanyacomparison na aina nyingine inayoitwa Concession.Concession ndio tunayotumia kwenye madini. Tofauti yaConcession na Production Sharing Agreement ni kwamba,kwenye Concession mnatakiwa, kwa maana ya Serikali naMwekezaji, kuchangia katika mtaji kabla hamjaanza kupatafaida; sasa unajiuliza sisi tunayo mitaji ya kuweza kuchangia?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndio maana sehemu kubwaya michango hatukutoa na ndio maana share zetu zikawazinaondoka. Pale tunazungumzia habari ya mgawanyo washare. Lakini kwenye Production Sharing Agreement nikwamba, mnagawana mapato ya uzalishaji na mnagawanakutoka siku ya kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Mikataba yetu,Mikataba ya Tanzania, Mikataba yetu toka siku ya kwanza

Page 256: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

256

25 MEI, 2013

watakapoanza. Mheshimiwa Tundu Lissu, anasema itabidiwarudishe kile walichowekeza, halafu ndio sisi tuanze kupata;si kweli. Utaratibu ni kwamba, from day one sisi tunakuwatuna asilimia za shares na wao wana za kwao. Sasa wakianzakuzalisha wanacheza na ile margin yao na sisi tunaendeleakuingiza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa tu ni kwamba,sisi katika Mikataba yetu yote ya uchimbaji wa gesi, hakunaambapo tunashuka chini ya 30% kutoka siku ya kwanza.Mikataba hii wala isiwe kwamba, ni kitu cha kutisha, walawatu wakasema kuna ufisadi. Ilishaletwa kwa Katibu waBunge, mkitaka tulete tena tutaleta, anayetaka kusomaafuate tu utaratibu wa Kibunge, Mikataba iko hapa hapakwa Katibu wa Bunge; hakuna siri katika jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niliona nichukue mudamwingi kulielezea hili, lakini Mheshimiwa Mangungu,amezungumzia suala la Lindi na Mtwara, ni jinsi ganiwatanufaika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, manufaa ya gesi hayaji bilakuanza na miundombinu. Ni mpaka uanze na miundombinundio uyaone manufaa. Vinginevyo tutabakia tunatakamanufaa, tunasema hatuyaoni. Nichukue nafasi hiikumwomba sana Mheshimiwa Mangungu, kama utulivuutatokea katika maeneo haya, wawekezaji wengi watakujakuwekeza na manufaa yataanza kuonekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, manufaa hayo ni pamojana ajira na biashara, kwa sababu, kama Industry hiiitaendelea vizuri katika Mikoa hiyo, ni dhahiri kwamba,biashara kubwa itakuwepo katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine kubwa hapani mgawanyo wa mapato. Katika Sheria yetu ya Fedha kwaSerikali za Mitaa, inasema kabisa kuna mgawanyo wa 0.3wa mapato, tena ni Gross. Sasa kama 0.3 unazungumzia gesitunayoizungumzia mabilioni ya fedha yatagawiwa kwamujibu wa Sheria ile, ni fedha nyingi. Pengine, ndio nasema,

Page 257: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

257

25 MEI, 2013

ukiisoma Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa vizuri, kunaKifungu kinachosema Waziri ana uwezo akagawanya yalemapato kadiri anavyoona inafaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hakuna ugomvimnaweza mkagawana hata katika Mkoa, mkagawanakatika Wilaya; maana kuna mivutano mingine inasema sisihatupati, wa Mtwara Mjini hatupati, wa Mtwara Vijini, si kweli.Sheria nimeisoma vizuri ya Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa,inasema Waziri anaweza akaamua atakavyoona inafaa,mwenye dhamana na Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, manufaa yapo nani makubwa. Ukiacha manufaa mengine ya viwanda na ajiraambayo yapo wazi na kila mtu anajua kwa hiyo, kukitokeautulivu, wananchi wataona manufaa hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Bungara,anasema ahadi ya Kiwanda cha Mbolea Kilwa. Wakatimwingine mambo haya unasikitika kidogo. MheshimiwaBungara, yeye ni Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo yaHalmashauri ya Wilaya ya Kilwa. Eneo walilokuwawametenga la Kilamko, yeye akiwa humo kwenyeHalmashauri hiyo, wameligawa viwanja, ambalo ndilo lilikuwaeneo la kujenga Kiwanda cha Mbolea. Sasa tena anakujahapa anasema, basi tutajitahidi tutafute eneo lingine, lakiniwako wawekezaji ambao wana nia na wameoneshadhamira ya kweli ya kutaka kuwekeza, tutawatafutia, lakinina ninyi mtusaidie kupata eneo, msigawe tena kama lilemliloligawa. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Cheyo,anasema palipo na rasilimali, wananchi wa pale ni lazimawafanane. Ni kweli, nakubaliana, lazima wafanane na ndiomaana kuna migawo hii. Kuna Corporate SocialResponsibilities, ambazo zinayataka haya makampuniyafanye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, safari hii katika Sera ya Gesi,tumesema Corporate Social Responsibility, ni wajibu kwa

Page 258: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

258

25 MEI, 2013

makampuni hayo, tumeweka kwenye Sera na tunatakiwaikitoka kwenye Sera, lazima iwekwe kwenye Sheria kwamba,wafanye kiasi gani. Kama ni kwa percent, basi hiyo CorporateSocial Responsibility, lazima tuione, iwe visible, kwa hiyo, siokama ile iliyokuwa kama hiyari hiyari hivi, tunataka ionekane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, wataanza kunukiakatika hali hiyo. Ukijumlisha na ile Service Levy, ukiweka namambo ya ajira, utaona wananukia tena watakuwawananukia kwelikweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine ambaloamelisema ni distribution, kwamba 1.5 trillion inayoonekanainatumika kwa mwaka kwa ajili ya kuendesha mitambo hiiambayo, kwa hakika mwaka jana ndio iliyofanya tukaendakuzalisha umeme badala ya kuendeleza kama wengiwalivyosema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niseme kwa wotekwamba, kwa kweli jamani, busara ya wakati huo ilitutakakwa hakika, huwezi ukaenda kusambaza umeme vijijini wakatihuo umeme wenyewe haupo. Huwezi kwenda kupelekaukatekeleze mradi Kijijini kupeleka umeme, wakati nchiinaingia gizani, viwanda vinakufa, uchumi unaanguka, weweunasema tusizalishe umeme, twende tupeleke umeme vijijini;kwa kweli, busara yetu ilikuwa hivyo, lakini tulifuata Kanunina Taratibu za Fedha za Serikali na kubadilisha matumizi yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, utaratibu huu niutaratibu wa Kiserikali. Kwa hivyo, pale tunapotaka kufanyamambo ambayo tunajua yana tija kwa maslahi yaWatanzania, lazima Serikali, iachiwe ifanye mambo yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nikubaliane kwamba,umesema huioni katika bajeti; ipo kwenye miradi yamaendeleo, tutakapofika kwenye Kitabu cha Maendeleo,utaona kiwango kile cha kuanzia, ambayo kwa kweli, fedhaile tumeitenga maalum kabisa kama mradi. Wakati ulehatukuwa na mradi wa namna hiyo, lakini sasa tuna mradi

Page 259: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

259

25 MEI, 2013

kwamba, mafuta sasa yatakayotakiwa kuendesha hayo ma-generator yanaonekana kwenye bajeti ya kwenye Kitabucha Bajeti yetu cha Miradi ya Maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mrema,amezungumzia kwamba, kuna nguzo zipo kule kwenye Jimbolake la Vunjo na Rombo na umeme sio wa uhakika. Kuhusunguzo hizo Mheshimiwa Mrema, nimewahi kujibu siku mojahapa, uliuliza swali la nyongeza; nikuhakikishie kwamba,tutajaribu kuona kama bado zina uimara na bado tunawezatukatekeleza mradi. Vinginevyo Mheshimiwa Mrema, tunampango mkubwa wa umeme vijijini na wewe hujaachwa,nikuhakikishie kwamba, tutashirikiana na tutaifanya hiyo kazivizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine nikwamba, umeme katika maeneo ya Mkoa wa Kilimanjarona maeneo ya baadhi ya Tanga na maeneo mengine Samena wapi, si wa uhakika sana kwa sababu ya uchakavu wamiundombinu. Tuna mradi mkubwa wa TEDAP ambaounatoka, pia upo katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu utakapotekelezwa, kwahakika utatusadia sana, kwa hiyo, huu mradiutakapotekelezwa na unaanza kutekelezwa kuanzia mwakahuu mwishoni, utaanza kutekelezwa na mwakani utakuwaumekwisha. Tatizo la umeme katika maeneo hayohalitakuwepo tena na umeme utakuwa wa uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mnyikaamezungumzia utekelezaji wa maazimio ya Bunge namikataba ya gesi. Nirudie kusema tu mikataba yote ya gesiipo kwa Katibu wa Bunge Mheshimiwa Mnyika, unawezaukaiona na kama una ushauri wako unaweza ukautoa, fursaunayo ni kufuata taratibu za kawaida na kwa hiyo hili lamikataba linakuwa limekwisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini suala la maazimio,suala la maazimio ni suala la Serikali na Bunge. Ukitaka hapatuseme kwa namna gani tumetekeleza maazimo ya Bunge,

Page 260: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

260

25 MEI, 2013

taarifa hii inahitaji muda wa kutosha na inahitaji mudamaalum. Nafikiri Spika anaweza akatenga muda maalumtukafanya hivyo, lakini kwa maana ya hapa, ukitakakukamata shilingi Mheshimiwa Mnyika hutaki tu nikupelekeeumeme kwenye maeneo yako ya Jimbo lako la Ubungo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kayomboamezungumzia, hili atalijibu mwenzangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kikwembeamesema kwa nini Serikali au TANESCO haijengimiundombinu ya kuzalisha. Mheshimiwa ukiangalia kwenyemiradi yetu ya maendeleo, kwenye kitabu chetu chamaendeleo tutakapofika, utaona tuna megawatt, KinyereziOne megawatt 150 na Kinyerezi Two megawatt 240.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii yote ni miradi ambayo niya TANESCO na fedha zake zimetengwa na miradi hiiitatekelezwa, lakini tutaenda kwa awamu. Tukimaliza hiitunakuja megawatt 300, kwa hiyo utaona tunalifanya hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia tunao uzalishaji wamradi wa umeme ambao lazima tushirikiane pia na sektabinafsi kwa mfano, kule Mtwara kama tulivyosema tunamegawatt 400 ambazo zitazalishwa pia pale, lakini piatutaunganisha Mtwara na Somangafungu na Mtwara naSongea. Hiyo yote inakaa kwenye mradi mmoja ambaotumeshaingia makubaliano na Symbion.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwahakikishiekabisa pengine huwezi kujua mradi huu unaweza ukakamilikamapema sana kwa sababu ya mikakati na mahusiano mazurituliyonayo na baadhi ya nchi marafiki wakiwepo Marekanikupitia MCC au vyovyote vile. Kwa hiyo, niwahakikishiekwamba, mradi utatekelezwa na wala msiwe na wasiwasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yale ambayo yalikuwayananihusu nimeyatolea ufafanuzi. Ahsante sana.

Page 261: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

261

25 MEI, 2013

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. STEPHENJ. MASELE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba name nijibuhoja zilizoelekezwa hapa. Nianze na hoja ya MheshimiwaSendeka kuhusu Mererani. Labda niseme masuala ya madiniyana uhusiano wa karibu sana na sheria. Hakuna maamuziyanafanyika kwenye madini bila kufuata Sheria ambazo zipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, Bungeliliazimia madini ya vito yachimbwe na Watanzania kwenyeSheria ya Madini ya mwaka 2010. Lakini Sheria hiyo hiyo yamadini ya 2010, kifungu namba 116, kinasema kwamba,kinaipa mamlaka Serikali kuhuisha leseni ya nyuma. Kwamfano, leseni ambazo zilitolewa wakati wa Sheria ya mwaka1998, zinaweza kuhuishwa kupitia kifungu hicho namba 116kama mwekezaji yule tayari alikuwa akiendelea kufanyashughuli zake wakati hiyo Sheria mpya imetungwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia katika Sheria hiyohiyo ya Madini ya 2010 kwenye eneo la vito, kifungu namba8(3), kinasema kwamba: “Madini ya vito yatachimbwa naWatanzania”, nakubaliana lakini kifungu namba 8(4) kinampamamlaka Waziri wa Nishati na Madini, pale anapoona inafaana kwa maombi maalum pale mradi ambao Mtanzaniaanadhani kwamba anahitaji msaada wa mwekezaji wakigeni kuweza kuchimba kwa teknolojia ambayo anadhanikwamba anahitaji msaada wa mwekezaji wa kigeni, Sheriainampa Mheshimiwa Waziri mamlaka hayo kupitia kifungucha 8(4) kuweza kuwapa leseni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, vifungu hivyovyote ndivyo vilivyotumika kujadili mkataba wa TanzaniteOne. Tanzanite One walikuwepo kabla ya Sheria ya 2010waliwekeza na walikuwa wakifanya kazi. Sheria imekujakutungwa, huwezi ukawafukuza ukawanyang’anya maanaile itakuwa ni nationalization, otherwise kama tunakubalianakwa Bunge hili tutaifishe migodi ile kinyume na Sheria hii jinsiilivyowekwa, basi nitaomba nijifunze kwa wataalam waSheria. (Makofi)

Page 262: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

262

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili la Buhemba MheshimiwaWaziri amelieleza vizuri sana kwenye maelezo yake. Ni kwelipalikuwa na historia ndefu sana nisingependa kuirudia.Kilichopo mbele yetu sasa STAMICO inamiliki leseni yaBuhemba na imeshapata mwekezaji kwa maana ya Mbiaambao watafanya kazi pamoja kwa taratibu ambazozilifuata taratibu zote za zabuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama kuna hojaza wananchi, kuna madai ya wananchi, yatahudumiwa paleSTAMICO itapoanza operation katika eneo la Buhemba kwataratibu kama tulizoziongea kwa wawekezaji wengine wauzalishaji. Pia Mheshimiwa Waziri amesema wale wananchiwa Buhemba anawatafutia eneo lao na amewaita kupitiaviongozi wao na ameshaagiza GST na taasisi zetu kuwatafutiamaeneo ambayo yatafaa na hili tunalifanya kwa nguvu sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Dkt.Kigwangalla amezungumzia fidia kwa wananchi wa Nzega.Katika Land Act ambayo Mheshimiwa mama Anna Tibaijukandiyo anasimamia Sera na Sheria za Ardhi inaeleza wazikwamba, kama kuna uwekezaji sehemu na kuna wananchiambao wanamiliki eneo lile kisheria, wana haki zote za kupatafidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hil i la Nzegalimepelekwa Mahakamani, kesi imekaa zaidi ya miaka sabana Mheshimiwa Tundu Lissu alikuwa Mwanasheria wa walewananchi waliokuwa pale, anazo taarifa vizuri ni kwa nini ilekesi walishindwa Mahakamani. Kwa misingi hiyo, kunahukumu zimeshatolewa na Mahakama kwamba wananchiwale hawakustahili kupata fidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichojaribu kukifanyamwaka jana tukishirikiana na Mheshimiwa Kigwangalla nikushawishi mgodi kwa njia zingine kwamba wananchi hawawameathirika kwa namna fulani baada ya uwekezaji huukuja, whether ni negative au positive.

Page 263: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

263

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo na wao katikarehabilitation lazima wafikiriwe kwamba ni sehemu ya jamiiambayo imeathirika. Kwa hiyo, wanapotenga rehabilitationfund wa-make sure kwamba, wanafanya consideration kwawananchi hawa, lakini kwa utaratibu tu ule wa fidia kisheriakesi hii ilikwenda Mahakamani na ilidumu miaka saba amanane na wananchi walishindwa kupitia kwa wanasheria wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia katika majadilianohayo hayo ambayo nampongeza tena MheshimiwaKigwangala, alifanya kazi kubwa na tumesaidiana,wamepata fedha 2.3 bilion kutokana na madeni ambayomgodi ule ulikiuka huko nyuma. Sasa kweli tulitumia vitishombalimbali ikiwemo kuwatishia, kuwanyima export permitsambayo kimsingi ni haki yao kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa misingi hiyo mgodihuu umeshafungwa hauzalishi, kama hauzalishi ina maanakama tulikuwa tunatumia gia au silaha ya export permitkuwanyima, sasa ile silaha haipo ina maana tunatakiwatutafute njia nyingine ya kuangalia hizi haki ambazoHalmashauri ya Nzega inazidai watazipata kwa njia ipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni jukumu la msingila Halmashauri kupitia Mbunge wao kuendelea kudai hakizao kutoka kwenye uwekezaji huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Sakaya,amezungumzia makaa ya mawe ya Ngaka. Makaa ya maweya Ngaka yanatumika kwenye viwanda vyetu vya ndani.Kiwanda cha Mbeya Cement kinatumia makaa ya mawehaya, Twiga Cement kule Wazo wanatumia, Tanga Cementwanatumia. Lakini kwa sababu location ya mgodi ule ipokaribu kabisa na mpaka wa Malawi, kampuni ile pia inamikataba ya kuuza katika kampuni za Malawi kule nawanafanya hivyo kwa taratibu zote za kisheria. Kwa hiyo hatu-export tu na sisi tunatumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda niunganishe hapohapo na Mheshimiwa Kikwembe aliuliza, nafikiri ni yeye

Page 264: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

264

25 MEI, 2013

mwenyewe Sakaya kwamba kwa nini tusiyatumie kupikia.Makaa ya mawe huwezi ukayapikia moja kwa moja labdauzalishe kwanza nishati, halafu ndiyo utumie nishati kupika.Kwa jinsi yalivyo na moto wake hizo sufuria mama, itakuwa ningumu sana kupikia moja kwa moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie MheshimiwaKikwembe amezungumzia wachimbaji wadogo. Suala ni lileli le maeneo yale yanamilikiwa kisheria maanawameshapewa leseni wale watu na Wizara ama Serikalihaiwezi kutoa leseni juu ya leseni. Kwa hiyo, njia pekee iliyoponi kwamba either mwenye leseni ile aridhie kuachia baadhiya maeneo yake. Kimsingi kisheria kama ni leseni ya utafitizile kubwa, anapomaliza muda wake wa kwanza miakaminne anatakiwa aachie eneo nusu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo yalewanapoyaachia tunawapa wachimbaji wadogo, lakinikama ule muda haujafika huwezi kutumia mabavukumnyang’anya mtu leseni yake, tuna kesi nyingiMahakamani, tunadaiwa pesa nyingi na tunalipa pesa nyingi.Tusingependa kuingia kwenye kesi zingine ambazo tunajuamwisho wake tunakwenda kushindwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachofanya sasa,maeneo yale ya Mpanda kweli yameshikiliwa na baadhi yawatu na tuna wa-engage kuwaomba ili waweze kuangaliakwamba kuna Watanzania wengine wanahitaji kuchimbamadini katika maeneo hayo. Kwa hiyo, watakaporidhia, basitutamega yale maeneo, tutatoa leseni kwenye vikundi vyawachimbaji wadogo kwenye maeneo ya Kata ya madini namaeneo mengine aliyoyazungumza kwenye ya magandana kadhalika. Eneo lile la ziada tulilowapatia ni kwa sababulil ikuwa liko wazi, halikuwa na leseni ndiyo maanatumeyatenga kwa ajili yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kayomboamezungumzia rasilimali za Taifa. Waheshimiwa Wabunge,huu wimbo wa rasilimali za Taifa kama revenue shared planni wimbo ambao kila mtu angependa kuuzungumza.

Page 265: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

265

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini leo fedha zotezinazotolewa kwenye Bodi ya Mikopo, fedha zotetunazogawana hapa kupitia Hazina ndiyo zinatokana namakusanyo mbalimbali ambayo Serikali inakusanya kutokakwenye vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo madini yaUsukumani. Kwa hiyo, madini ya Usukumani kodi zote zilikuwazinakwenda Mfuko Mkuu wa Hazina na ndiyo tulikuwatunagawana wote wa Pwani, wa Mtwara, wa Shinyanga nakadhalika tunagawana fedha hizo hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa misingi hiyo kama leotunataka sasa tuangalie namna gani kila mmoja aanzekuchukua mapato yake kuna njia mbili; njia ya kwanzaMbunge aandae Private Members Bill ailete Bungeni, Bungeliridhie tubadilishe Sheria zetu ili tuangalie kama Mrabahaama tozo ama Sheria, ama kodi zibaki kule, lakini kwa jinsizilivyo sasa hivi haiwezekani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutafuata mfumo ulivyo kwamujibu wa Sheria za Kodi na Sheria za Fedha. Kwa misingihiyo sasa Serikali imesikia, inaweza kupitia Ofisi yaMwanasheria wa Serikali ilete hoja hiyo Bungeni, sheriaibadilishwe, itungwe kama Wabunge wote na Watanzaniawatadhani kwamba, hoja hiyo itakuwa na maslahi kwa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini vinginevyo ni mjadalaambao unahitaji kabisa maamuzi mapana na si tu Waziri waNishati na Madini kuamua kuanzia leo loyalty ibaki Shinyanga,gesi nayo ibaki kule. Sisi hapa tunasimamia tu Sera na Sheriaya Madini, mambo ya kodi yanasimamiwa na Wizara yaFedha kupitia TRA na taratibu ziko wazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, fidia ya wananchi kuleNgaka, Serikali imeingilia kati kuhakikisha kwamba, wananchiwanapata haki yao. Nitoe wito tu kwa viongozi wenzetuMikoani, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Halmashauritusichukue maamuzi ya kufunga migodi hii bila kufanyaconsultations na Wizara kwa sababu kuna madharamakubwa ya kisheria.

Page 266: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

266

25 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, migodi i le imefungamikataba ya ku-supply, nimetaja viwanda hapa, viwandavile vikipungukiwa supply ya makaa ya mawe maana yakeuzalishaji unapungua, uzalishaji ukipungua maana yakekutakuwa na shortage ya simenti kwenye viwanda vyetu. Kwahiyo, kuna madhara makubwa sana ambayo yanawezakujitokeza ya kisheria kama mtu ataamua tu kufunga mgodibila kufuata taratibu ambazo zinatakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwaombeviongozi wenzetu kule tunatambua mchango wenu,tunatambua kazi yenu, lakini tuwaombe sana, tuwasilianekama kuna tatizo lolote la kiusalama, ama la madai ili tuwezekushauriana vizuri namna bora ya kufanya kabla ya kuchukuamaamuzi. Ahsante.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kwa mujibu wa Kanuniya 104 zimebakia dakika kumi tunaingia kwenye guillotine.

Kif. 1002 – Finance and Accounts… … … Sh. 1,909,224,000/=Kif. 1003 – Policy and Planning… … … … Sh. 1,715,299,000/=Kif. 1004 – Internal Audit Unit … … … … Sh. 948,080,000/=Kif. 1005 – Legal Service… … … … … … Sh. 1,952,138,000/=Kif. 1006 – Government Communication

Unit… … … … … … … … Sh. 1,404,320,000/=Kif. 1007 – Procurement Management

Unit… … … … … … … … Sh. 1,099,591,000/=Kif. 1008 – Environment Management

Unit… … … … … … … … … Sh. 578,227,000/=Kif. 1009 – Management Information

System… … … … … … … Sh. 1,987,018,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 267: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

267

25 MEI, 2013

Kif. 2001 – Minerals … … … … … … …Sh. 33,046,292,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi pamoja na marekebisho yake)

Kif. 2004 – Tanzania Diamond Sorting Agency (TANSORT… … … ... ..Sh. 1,941,404,000/=

Kif. 2005 – Eastern Zone… … … … ... ... Sh. 1,765,080,000/=Kif. 2006 – Western Zone… … … … ... ... Sh. 960,016,000/=Kif. 2007 – Lake Zone … … … … … … Sh. 1,610,893,000/=Kif. 2008 – Northern Zone… … … … ... ...Sh. 1,470,385,000/=Kif. 2009 – Southern Zone… … … … ... ... Sh. 999,771,000/=Kif. 2010 – Central Western Zone… ... ... Sh. 1,344,468,000/=Kif. 2011 – Central Zone… … … … … … Sh. 965,131,000/=Kif. 2012 – Southern Western Zone… … … Sh. 1,134,744,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 3001 – Energy and Petroleum… … Sh. 44,879,169,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi pamoja na marekebisho yake)

MIPANGO YA MAENDELEO

Fungu 58 – Wizara ya Nishati na Madini

Kif. 1003 – Policy and Planning… … … … … … ... Sh. 0/=Kif. 1008 – Environment Management Unit… … ... ... Sh. 0/=Kif. 2001 – Minerals… … … … … … … Sh. 45,240,000,000/=Kif. 2002 –Madini Institute… … … … … Sh. 1,220,000,000/=Kif. 2003 – Research and Laboratory

Services… … … … ... ... ... ... Sh. 1,000,000,000/=Kif. 3001 – Energy and Petroleum… … Sh. 944,752,745,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 268: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

268

25 MEI, 2013

(Bunge lilirudia)

T A A R I F A

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika,naomba kutoa taarifa kwamba, Bunge lako Tukufu limekaakama Kamati ya Matumizi na kuyapitia makadirio ya matumiziya fedha ya Wizara ya Nishati na Madini ya mwaka 2013/2014 na kuyapitisha pamoja na mabadiliko yake. Hivyo basi,naliomba Bunge lako Tukufu liyakubali makadirio haya.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika,naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madinikwa Mwaka 2013/2014 yalipitishwa na Bunge)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge naomba nichukuenafasi hii kwa niaba yenu kuwapongeza Waziri na Manaibuwake na Wataalam wote wa Wizara hiyo kwa kazi nzurimnayoendelea kufanya na mwendelee kufanya na kamamnavyoona suala la umeme, naamini ni suala ambalolinamgusa kila mtu katika kipindi hiki cha dunia. Kwa hiyo,nawatakieni heri, huu ni mwaka mmoja toka mmechukuakazi hiyo, sasa mwendelee kufanya vizuri zaidi katika miakaijayo.

MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!

SPIKA: Mheshimiwa nikisimama mimi naomba weweusisimame, ndiyo Kanuni inavyosema. Mimi nikisimama wewehuwezi kusimama na muda umekwisha, hakuna namna.

Waheshimiwa Wabunge, naomba nitoe taarifaifuatayo:-

Page 269: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

269

25 MEI, 2013

Waheshimiwa Wabunge, kama mnavyokumbuka,tarehe 31, Januari, 2013 kulitokea vurugu Mkoani Mtwarakutokana na mpango wa Serikali wa kujenga bomba kubwala kupeleka gesi Dar es Salaam kutoka Mtwara, ili kusaidiakupunguza tatizo kubwa la ukosefu wa umeme nchini.

Matumizi ya umeme wa maji yamekuwa tatizokutokana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi. Aidha, umeme wa mafuta ni ghali sana na ni mzigokwa Taifa ikilinganishwa na gesi asilia ambayo MwenyeziMungu ameipatia nchi yetu.

Pamoja na kwamba Waziri Mkuu alikwenda Mtwarakuwasikiliza wananchi na wadau mbalimbali wakati ule natukaamini kuwa mambo sasa yameeleweka. Bahati mbayasana tarehe 22 Mei, 2013 hali ya usalama ikawa mbaya katikaMkoa wa Mtwara baada tu ya Mheshimiwa Waziri wa Nishatina Madini kuwasilisha hotuba yake hali ambayo ilifanyaBunge kuahirisha shughuli zake ili Serikali itoe taarifa ya halihalisi ya usalama katika Mkoa wa Mtwara inavyoendelea.

Baada ya taarifa hiyo ya Serikali, Kamati ya Uongoziya Bunge ilikutana na kujadili hatua ambazo Bungelitachukua. Kamati ya Uongozi ya Bunge iliamua kuwa iundweKamati Maalum ili iende Mtwara na kuwasikiliza wananchikuhusu wasiwasi wao wa azma ya Serikali ya kujenga bombala gesi kwenda Dar es Salaam. Kamati ya Uongozi, iliagizakuwa katika mazingira ya utulivu na amani Kamati ikutanena wananchi mbalimbali na kuwasikiliza hoja zao.

Nawasihi wananchi wa Mtwara, Kamati itakapokujawawe watulivu, wawazi na huru kutoa mawazo yao bilawasiwasi wowote ule au mashaka. Kamati itapata nafasi yakutosha ya kukutana na wananchi, vikundi, taasisi hata nawatu binafsi. Kubwa tunaloomba sote ni amani, utulivu,upendo na maendeleo ya kila mmoja na jamii zetu na nchiyetu bila kubagua mtu, kabila, eneo, rangi wala Mkoa.

Page 270: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

270

25 MEI, 2013

Hivyo basi, kwa mujibu wa Kanuni ya tano ya Kanuniza Kudumu za Bunge, Toleo la mwaka 2013, naunda KamatiMaalum ambayo itakuwa na hadidu za rejea zifuatazo:-

Katika kutekeleza kazi hiyo naipa Kamati hiyo hadiduza rejea zifuatazo:-

(i) Kuchunguza chimbuko la mgogoro;

(ii) Kufuatilia hatua zilizochukuliwa na Serikalikutatua mgogoro huo;

(iii) Kukutana na wadau mbalimbali ili kupatamaoni yao kuhusu miradi ya gesi asilia; na

(iv) Kuangalia mambo mengine yoyote yenyeuhusiano na mgogoro huu.

Sasa Wajumbe ambao nimewateua ni hawawafuatao:-

Mheshimiwa Charles John Poul Mwijage, MheshimiwaSaid Amour Arfi, Mheshimiwa Dokta Dalali Peter Kafumu,Mheshimiwa Said Juma Nkumba, Mheshimiwa Cynthia HildaNgoye, Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, MheshimiwaEngineer Ramo Matala Makani, Mheshimiwa MuhammadAmour Chomboh, Mheshimiwa Cecilia Daniel Paresso,Mheshimiwa Rukia Kassim Ahmed, Mheshimiwa MariamNasoro Kisangi, Mheshimiwa Agripina Zaituni Buyogera,Mheshimiwa Selemani Said Jafo.

Mwenyekiti wao atakuwa Mheshimiwa Charles JohnPoul Mwijage. Hiyo ndiyo Kamati niliyounda, wataaanza kazikwanza kwa kuelewa mazingira yaliyo huku, mpakatutakapokuwa tunajua hali imetulia kule, ndiyo watakwenda,lakini wataanza kupata taarifa kwa vyombo ambavyovilihusika kwanza. Kwa hiyo, hii ndiyo Kamati tuliyonayo.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hivyo,nina tangazo moja tu, kesho nimesema kuna semina ya

Page 271: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461935604-HS-11-34-2013.pdf · Kuna mwaka hapa watoto wa Mkoa wa Iringa waliungua kwa

271

25 MEI, 2013

kuhusu Sera ya Elimu, makabrasha mnayo kwenye pigeonholes. Kwa hiyo, msije mkategemea mtapewa kule, yakokwenye pigeon holes waliwagawieni muda mrefumyachukue na myasome.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hivyo,naomba niwashukuru sana kwa kukubali kufanya kazi yaziada mpaka leo saa tisa hii, ikiwa ni weekend na tumewezakurudia kwenye ratiba yetu. Siku ya Jumatatu ni Wizara yaArdhi. Kwa hiyo, wanaohusika wote wajiandae.

Baada ya kusema hivyo, naahirisha kikao cha Bungempaka Jumatatu, saa tatu asubuhi.

(Saa 9.00 Alasiri Bunge liliahirishwa Mpaka Siku yaJumatatu, Tarehe 27 Mei, 2013 Saa tatu Asubuhi)