8
1 Sikika Ushiriki wa jamii katika Mpango wa Utoaji Huduma za Afya wa Wilaya

Ushiriki wa jamii katikaMpango wa Utoaji Hudumaza Afya wa Wilaya

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Ushiriki wa jamii katika Mpango wa Utoaji Huduma za Afya wa Wilaya

Citation preview

Page 1: Ushiriki wa jamii katikaMpango wa Utoaji Hudumaza Afya wa Wilaya

1Sikika

Ushiriki wa jamii katika Mpango wa Utoaji Huduma

za Afya wa Wilaya

Page 2: Ushiriki wa jamii katikaMpango wa Utoaji Hudumaza Afya wa Wilaya

2 3

UtanguliziKipeperushi hiki kimeandaliwa na Sikika (zamani Youth Action Volun-teers, YAV) kwa lengo la kuelimisha wananchi juu ya dhana ya ushiriki wa jamii katika Mipango ya Afya na umuhimu wake ili kuimarisha ubora wa maisha na ustawi wa jamii na kuchochea uwazi na uwajibikaji ambavyo ni misingi mikuu ya utawala bora wa kidemokrasia.

Sikika ni shirika lisilo la kiserikali linalochochea upatikanaji wa huduma za afya zenye uwiano, viwango vya ubora unaokubalika, gharama nafuu na zilizo endelevu. Kwa kuimarisha ushiriki wa jamii na kukuza uwazi na uwajibikaji katika kupanga, kutekeleza na kusimamia mikakati ya afya ndani ya mifumo ya afya ya Wilaya

Ushiriki wa JamiiNi utaratibu uliotokana na sera ya serikali kutoa nafasi kwa jamii kuchukua majukumu zaidi kwa maendeleo yao katika kufanya maamuzi kuchagua mradi wa jamii, kupanga, kutekeleza, kutawala, kudhibiti na kuongoza ili kuleta maendeleo.

Mpango Kabambe wa Afya wa Wilaya (CCHP) ni nini?Ni mpango kazi wa mwaka unaoandaliwa wilayani kuongoza utoaji wa huduma bora za afya na kuelezea rasilimali zote zilizopo katika wilaya husika, zikiwemo rasilimali watu. Hujumuisha vyanzo vyote vya fedha katika Halmashauri, shughuli za watoa huduma wote bila kujali umiliki na kuangalia matatizo ya jamii. Hulenga hasa kudhibiti magonjwa makuu katika jamii na matatizo mengine ya kiafya.

Ni nani anayeandaa Mpango huu?Halmashauri kwa kushirikiana na Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) hushiriki kuandaa mpango huu. Baraza la Madiwani la Halmashauri wanahusika kupitisha Bajeti na MIpango ya Afya ya Wilaya.

Nafasi ya wananchi Kushiriki katika Mipango ya AfyaMaandalizi ya mipango ya afya huanzia mwishoni mwa mwezi Novemba kila mwaka na kukamilika ndani ya wiki ya pili ya Juni. Wananchi wamepewa nafasi pekee ya kushiriki katika mpango wa afya kwa kuainisha vipaumbele/mahitaji yao ya afya katikati ya mwezi

Page 3: Ushiriki wa jamii katikaMpango wa Utoaji Hudumaza Afya wa Wilaya

2 3

Desemba kila mwaka. Vipaumbele vya wananchi vitakusanywa kupitia mikutano ya wananchi na kupelekwa katika kamati za afya za vituo vya huduma. Vipaumbele hivi vitawekwa pamoja na vipaumbele vya watoa huduma katika vituo vya huduma na kuwasilishwa kwa Timu ya Usimamizi wa Afya ya Halmashauri na kupitishwa katika kila hatua ya utayarishaji wa mpango ili kuleta ufanisi bora katika kuboresha miundo na huduma ya afya katika maeneo ya jamii na vituo vya huduma na hatimaye kukidhi malengo ya Taifa ya 2025 na yale ya Milenia 2015.

Kwanini mwananchi ushiriki katika Mpango Kabambe wa Afya wa Wilaya?

• Kukupa mamlaka ya kuamua kulingana na mahitaji yako hivyo kumiliki huduma zitolewazo kwa jamii.

• Kuwawezesha wananchi kutambua matatizo yanayowazunguka na kuweza kuyatatua kwa kutumia nguvu zao wenyewe.

• Kutoa nafasi na uwezo kwa mwananchi kuleta mabadiliko katika sera na huduma zitolewazo katika ngazi zote za vituo vya huduma.

• Kuongeza ufanisi wa Serikali katika kuhakikisha kuwa nguvu kazi na rasilimali zilizopo zinatumika kikamilifu.

• Kuiwezesha serikali kuu na serikali za mitaa kutoa huduma kwa watu wengi na kwa gharama nafuu kutokana na michango na nguvukazi ya wananchi.

Page 4: Ushiriki wa jamii katikaMpango wa Utoaji Hudumaza Afya wa Wilaya

4 5

• Kuboresha usimamizi Kabambe katika utekelezaji wa maelekezo mbalimbali ya Serikali, sera na sheria za nchi.

• Kukuza utawala bora, uwazi, uwajibikaji na uadilifu kwa watoa huduma/viongozi kwa wananchi hivyo kuboresha huduma za afya.

Vyombo vinavyotoa mamlaka kwa jamii kushiriki katika kupanga, kutekeleza na kutathmini huduma ya afya katika vituo vya huduma na ngazi za juu.Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977• Kifungu cha 18.b kimeelezea haki ya mwananchi kutafuta, kupata na

kupashana taarifa bila kujali mipaka ya nchi.• Kifungu cha 18.d kimeendelea kusisitiza kuwa kila mwananchi ana haki

ya kupewa taarifa kwa wakati kuhusu matukio muhimu ya maisha na shughuli za wananchi na pia juu ya masuala mengine muhimu kwa jamii.

• Kifungu cha 21.1 kimeeleza haki ya mwananchi kushiriki katika masuala ya utawala ya nchi kupitia wawakilishi wao waliochaguliwa.

• Kifungu cha 21.2 kimeeleza haki na uhuru wa kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika kufanya maamuzi juu ya masuala yanayomhusu yeye na yanayohusu Taifa.

Sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 Kifungu (146.a)Sheria hii imeanzisha Halmashauri za Wilaya, Mamlaka za miji na Halmashauri za vijiji kama vyombo vitakavyosimamia utekelezaji wa shughuli zote za Serikali za mitaa. Sheria hii imehamisha mamlaka na rasilimali na imetoa majukumu kwa kila chombo ili kutoa nafasi kwa wananchi kushiriki katika kupanga, Kutekeleza na kutathmini miradi ya maendeleo katika maeneo yao. Kwa mfano ni wajibu wa halmashauri ya kijiji kuitisha mikutano ya kijiji kila baada ya miezi mitatu

Mpango wa nafasi na vikwazo katika MaendeleoHalmashauri za serikali za mitaa zina dhima ya kushirikisha wananchi katika kupanga mipango na utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kimaendeleo katika maeneo yao. Vilevile wanalo jukumu la kuangalia utawala wa sheria na kudumisha demokrasia ili kuleta maendeleo katika jamii.

Page 5: Ushiriki wa jamii katikaMpango wa Utoaji Hudumaza Afya wa Wilaya

4 5

Muongozo wa Mpango wa Afya wa Wilaya Muongozo huu unazipa Halmashauri jukumu la kushirikisha wananchi katika maamuzi, mipango na usimamizi wa utoaji wa huduma za afya kupitia wawakilishi wao katika Bodi na Kamati za Afya waliochaguliwa katika maeneo yao.

Sera ya Afya ya Taifa ya mwaka 2007 Imelenga kuimarisha ushiriki wa wananchi katika kupanga, kutekeleza na kusimamia huduma za afya kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa na kuweka msisitizo juu ya afya ya msingi.

Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM). Mkakati huu unalenga kuwezesha upatikanaji wa huduma muhimu za afya kwa wananchi wote kwa kuwashirikisha wananchi na sekta mbalimbali, kuimarisha uendeshaji na usimamizi wa huduma za afya. Serikali imelenga kuimarisha mfumo uliopo wa kuongeza umiliki na sauti ya wananchi katika utoaji wa huduma za afya na kuweka mazingira mazuri ya kuwezesha jamii kubuni njia na mikakati mbalimbali ya kuboresha afya zao na kutoa maelekezo kwa kamati za mamlaka za serikali za mitaa ili itekeleze na kusimamia huduma za afya ya msingi katika maeneo yao.

Wito wetu kwako…Ewe Kiongozi wa serikali ya Mtaa/kitongoji/kijiji,• Timiza wajibu wako wa kuitisha mikutano ya jamii kama

inavyoelekezwa katika miongozo ya TAMISEMI.• Andaa vipaumbele na mipango katika kuinua ubora wa huduma

kwa wananchi kama vile afya, elimu, maji, miundo mbinu, nishati na huduma nyingine muhimu kwa jamii.

• Simamia na chochea juhudi za wananchi katika kujiletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha katika Kupanga, kuamua na kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo afya.

• Simamia utekelezaji na uboreshaji wa sekta sambamba na sheria na miongozo mbalimbali.

• Fahamu vyanzo vya mapato na kusimamia matumizi sahihi ya mapato hayo ili kuzuia ubadhirifu wa rasilimali za umma.

Page 6: Ushiriki wa jamii katikaMpango wa Utoaji Hudumaza Afya wa Wilaya

6 7

Hamasisha wananchi kushiriki katika mikutano ya jamii…

Ewe mwananchi, tekeleza majukumu, haki na wajibu, wako wa kikatiba;

• Elewa fursa zote zilizopo za kushiriki katika maamuzi na mipango mbalimbali ikiwemo mipango ya huduma za afya na mpango wa marekebisho ya Serikali za mitaa na fuatilia pale inapopaswa.

• Shiriki katika maamuzi na mipango kwa kuhudhuria mikutano ya jamii katika vitongoji, vijiji na mitaa na hakikisha kuwa mikutano inafanyika kila baada ya miezi mitatu.

• Wasilisha matatizo/mahitaji yako ya afya kupitia wawakilishi wa jamii wa kamati ya afya ya kituo cha huduma kilichopo ndani ya eneo unaloishi na kwa mtoa huduma.

• Toa mawazo/maoni yako kupitia sanduku la maoni lililopo katika kituo cha huduma

• Tafuta taarifa mbalimbali za afya kama bajeti, mipango na utekelezaji wake, ripoti za fedha na kuzitumia taarifa hizo kushiriki katika kuboresha huduma zitolewazo kwa jamii.

• Pata taarifa ya bajeti ya mwaka, mapato na matumizi toka katika kituo husika.

Page 7: Ushiriki wa jamii katikaMpango wa Utoaji Hudumaza Afya wa Wilaya

6 7

“Suala la kupata taarifa ni haki ya msingi ya mwanadamu na kutumia taarifa kuleta mabadiliko na kukabiliana na changamoto ni kuimarisha demokrasia na utawala bora katika jamii…”

• Hoji au uliza pale unapoona bajeti na mipango haitekelezwi ipasavyo kupitia vikao au kwa kuwasiliana na mamlaka husika kama vile Mwenyekiti wa Serikali za mitaa, kamati ya afya ya kituo cha afya, Kamati ya maendeleo ya Kata au Mkurugenzi/Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ama Mganga mfawidhi wa kituo unachopatia huduma za afya.

Dai mikutano ili ubainishe mahitaji ya jamii yako na kupanga jinsi ya kuyatatua

Ewe Mwakilishi wa Jamii katika Bodi na Kamati za afya za vituo vya huduma, Kamati ya maendeleo ya kata…• Elewa nafasi yako kwa jamii na tekeleza wajibu wako• Shiriki kikamilifu katika mikutano ya bodi na kamati za afya kama

ilivyoelekezwa katika miongozo• Tafuta mawazo ya wananchi na kuyawasilisha katika Bodi/kamati ili

yaingizwe katika mpango wa kutolea huduma za afya• Toa mrejesho wa taarifa za maazimio na utekelezaji wake kwa jamii

yako

Page 8: Ushiriki wa jamii katikaMpango wa Utoaji Hudumaza Afya wa Wilaya

8

Tekeleza wajibu wako, shiriki katika mikutano ya jamii ili kuboresha huduma za afya.

Kwa pamoja Tunaweza!

Tuandikie kuhusu unavyoweza kuboresha huduma za afya katika jamii Yako kisha utume kwa anuani hapo chini:

........................................................................................................................

........................................................................................................................

........................................................................................................................

........................................................................................................................

........................................................................................................................

........................................................................................................................

........................................................................................................................

........................................................................................................................

........................................................................................................................

........................................................................................................................

........................................................................................................................

........................................................................................................................

........................................................................................................................

S.L.P 12183 Dar es Salaam, Simu: +255 22 2666355/57, nukushi (Fax): +255 22 2668015, Barua pepe: [email protected], Tovuti: www.sikika.or.tz.

Kinondoni. Barabara ya Tunisia, Mtaa wa Waverley, Ada Estate, Nyumba Na.69.

Sikika