48
USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, TANZANIA Utafiti uliofanywa na kitengo cha Haki za Jinsia cha Oxfam nchini Tanzania Desemba 2015

USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

USHIRIKI WA WANAWAKEKATIKA UCHAGUZI WA 2015,

TANZANIA

Utafiti uliofanywa na kitengo chaHaki za Jinsia cha Oxfam

nchini Tanzania

Desemba 2015

Page 2: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

MtafitiProfesa Ruth Meena

© OXFAM, 2015

Page 3: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

3

YALIYOMO

VIFUPISHO ....................................................................................... 5

SURA YA KWANZA .................................................................. 6

MUKTADHA NA MALENGO YA UTAFITI ................................................. 7

1.1 Utangulizi ..................................................................................... 7

1.2 Kwa nini Oxfam imelenga wanawake? ........................................... 7

1.3. Malengo Ya Utafiti ........................................................................ 8

1.4. Mbinu zilizotumika Katika Utafiti Huu ............................................ 8

SURA YA PILI .......................................................................... 10

UCHAMBUZI WA MAKALA KUHUSU USHIRIKI WA WANANAKE

KATIKA UCHAGUZI .............................................................................. 11

2.1 Utangulizi .................................................................................... 11

2.2. Mfumo wa Uchaguzi na Usawa wa Jinsia (Electoral Regime) ............ 11

2.3 Utaratibu wa Uteuzi na Usawa wa Jinsia (Candidate nomination

Procedures) ................................................................................... 11

2.4 Mila, Desturi na Taratibu Zinavyoathiri Usawa wa Jinsia Katika

Uchaguzi ..................................................................................... 14

SURA YA TATU ........................................................................ 16

MATOKEO YA UTAFITI .......................................................................... 17

3.1 Utangulizi .................................................................................... 17

3.2 Wajibu wa Vyama vya siasa katika Ushiriki wa Wanawake Katika

Uchaguzi ..................................................................................... 17

3.3. Wajibu wa Tume ya Uchaguzi Katika Kuwezesha Ushiriki wa

Wanawake Katika Uchaguzi .......................................................... 19

3.4 Jukumu la Msajili wa vyama vya Siasa Katika Kuwezesha Ushiriki

wa Wanawake Katika Uchaguzi ..................................................... 21

3.5 Jukumu la Taasisi Ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Katika

Kuwezesha Ushiriki wa Wanawake Katika Uchaguzi ....................... 22

Page 4: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

4

3.6 Jukumu La Watendaji wa Serikali za Mitaa katika Kusimamia Haki

za Wanawake Katika Uchaguzi ...................................................... 24

3.7 Simulizi za wagombea wanawake katika uchaguzi mkuu 2015,

Tanzania ...................................................................................... 25

3.7.1 Nancy Mrikaria (Aliyekuwa Mgombea Ubunge, Jimbo la

Temeke, Dar es Salaam) ..................................................... 25

3.7.2 Mh. Angeline Mabula (Mbunge wa Jimbo la Ilemela,

Mwanza na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na

Maendeleo ya Makazi) ...................................................... 28

3.7.3 Magreth Mashenene (Aliyekuwa Mgombea Udiwani,

Kata ya Shishani, Magu, Mwanza) ..................................... 31

3.7.4 Khadija Msawira (Aliyekuwa Mgombea Udiwani, Kata ya

Makurumla, Kinondoni, Dar es Salaam) .............................. 33

3.7.5 Mh. Safia Mkama (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela,

Mwanza) .......................................................................... 35

3.7.6 Anna Elisha Mghwira (aliyekuwa mgombea Urais wa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) .................................. 37

SURA YA NNE ........................................................................ 41

MAJUMUISHO ........................................................................ 42

Page 5: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

5

ACT Alliance for Change and Transparency

CCM Chama Cha Mapinduzi

CEDAW The Convention on the Elimination of all Forms of

Discrimination Against Women

CEMOT Coalition for Election Monitoring and Observation in

Tanzania

CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo

CHAUMA Chama Cha Ukombozi wa Umma

FOS Fahamu Ongea Sikilizwa

KKKT Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania

PPT Progressive Party of Tanzania

SADC Southern African Development Community

TAKUKURU Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa

TAMWA Tanzania Media Women’s Association

TGNP Tanzania Gender Networking Programme

TLP Tanzania Labour Party

UKAWA Umoja wa Katiba ya Wananchi

UNDHR Universal Declaration of Human Rights

UNGA United Nations General Assembly

UNSC United Nations Security Council

UWT Umoja wa Wanawake Tanzania

VIFUPISHO

Page 6: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

SURA YAKWANZA

Page 7: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

7

1.1. UtanguliziUtafiti huu ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Fahamu Ongea Sikilizwa awamu ya pili (FoSII). Mradi huu ulitekelezwa katika mikoa 9 ya Tanzania Bara na Visiwani. Madhumuni ya Mradi huu ni kuchangia katika kuwezesha uchaguzi wa mwaka 2015 uwe huru na wa haki ambao raia wote hususani wale walioko pembezoni ikiwa ni pamoja na wanawake na vijana waweze kushiriki katika kupiga kura, kuonyesha nia ya kuwania nafasi za uwakilishi, na kama wagombea wa nafasi husika. Mradi huu ulitekelezwa na Oxfam chini ya usimamizi wa kitengo cha Haki za Jinsia (Gender Justice Program) kwa kupitia wabia wake katika mikoa husika. Mradi huu uliwalenga wanawake.

1.2. Kwa nini Oxfam imelenga wanawake? Wanawake ni wadau muhimu katika shughuli zote za kisiasa na maendeleo ya jamii zote. Idadi yao kama wapiga kura, wanachama wa vyama vya siasa na kama wazalishaji wanaoendeleza kizazi ni kubwa na haiwezi kupuuzwa. Vilevile haki za wanawake za kushiriki katika uchaguzi kama wapiga kura na wanaowania nafasi za uongozi zimebainishwa katika mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda na katika sheria na katiba ya nchi. Baadhi ya hiyo Mikataba ni pamoja na Tamko la Kimataifa Kuhusu Haki za Binadamu (UDHR: 1948). Vifungu vya 2 na 21 vinatamka kwamba binadamu wote wana haki sawa za kisiasa bila kubaguliwa kwa njia yoyote ikiwa ni pamoja na ubaguzi wa jinsia. Baraza la Umoja wa Mataifa lilisisitiza haki za wanawake za kisiasa katika mkataba wake wa Haki za Wanawake za Kisiasa (UNGA) uliopitishwa mwaka 1952. Haki hizi zilisisitizwa zaidi kwenye Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Raia na za Kisiasa (ICCPR: 1966). Mkataba huu ulifuatwa na Mkataba wa Kutokomeza Ubaguzi wa Aina yoyote dhidi ya Wanawake (CEDAW: 1979), ambao uliweka mkazo haki za kushiriki na haki za kutobaguliwa. Matamko mengine ni pamoja na Mapendekezo ya Baraza la Usalama (UNSC: 2000), Mpango Kazi wa Beijing (1995), Malengo ya Millenia ya Maendeleo (Lengo la 3), pamoja na Malengo Endelevu ya Millenium.

Katika ngazi ya kikanda kuna Mkataba wa Ziada wa Haki za Wanawake (2003) wa AU, Tamko la SADC la Jinsia na Maendeleo (2008) na Mkataba wa Nyongeza Kuhusu Haki za Wanawake (1995).

MUKTADHA NA MALENGO YA UTAFITI

Page 8: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

8

Vilevile, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) pamoja na Mapendekezo ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2014/15) zimebainisha haki za wanawake za kushiriki katika maamuzi ikiwa ni pamoja na ushiriki wao katika uchaguzi kama wapiga kura na wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi. Sera ya Maendeleo Ya Wanawake na Jinsia (2000) inakiri kwamba “Wanawake hawajitokezi kiasi cha kutosha kugombea nafasi za uongozi na kwa jumla hawashiriki katika maamuzi katika ngazi mbalimbali kuanzia familia hadi taifa.” Lengo la sera ni kuweka mazingira yatakayoboresha hali hii.

1.3. Malengo Ya UtafitiLengo lilikuwa ni kupata taarifa za kuwezesha Oxfam kuimarisha na kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha elimu ya uraia ili kuwezesha wanawake washiriki kikamilifu kama wapiga kura, wagombea na wasimamizi katika mchakato wote wa uchaguzi.

Malengo mahususia) Kuongeza hamasa ya Watanzania katika kuelewa vipingamizi

vinavyozuia wanawake kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi.

b) Kutumia taarifa itokanayo na utafiti katika kuwahamasisha wadau wote wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, Tume ya Uchaguzi, msajili wa Vyama vya siasa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na asasi zisizo za kiserikali kubuni mbinu mbadala za kuwezesha ushiriki wa wanawake katika uchaguzi wa haki na huru.

c) Kutoa mrejesho wa matokeo ya mafunzo ya mradi wa Fahamu, Ongea, Sikilizwa II.

1.4. Mbinu zilizotumika Katika Utafiti HuuUtafiti huu ulitumia vyanzo viwili vya kupata taarifa. Chanzo cha kwanza ni uchambuzi wa makala mbalimbali zilizoandikwa na wanazuoni na watafiti katika eneo hili. Chanzo hiki kilitupa picha ya nini kinachojulikana na mielekeo mbalimbali ya chambuzi. Mbinu ya Pili ni njia ya simulizi na mahojiano, kwanza na wadau wakuu wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, Tume ya Uchaguzi, viongozi wa vyama vitatu, TAKUKURU, pamoja

Page 9: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

9

na watendaji kutoka serikali za mitaa. Mahojiano na wadau hawa yalitupa picha ya tafsiri ya wadau husika kuhusu majukumu yao katika kuwezesha usawa wa jinsia katika mchakato wa uchaguzi.

Mwisho tulipata simulizi kutoka kwa wanawake walioshiriki katika kinyang’anyiro cha uchaguzi kama wagombea katika nafasi ya urais na ubunge wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, na waliowania nafasi za uwakilishi wa mabaraza ya Kata au miji. Simulizi hizi zilitupa shuhuda kuhusu fursa zilizopo zenye kuwezesha pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo wanaposhiriki kama wagobea wanawake wa nafasi mbalimbali za uchaguzi.

Page 10: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

10

SURA YAPILI

Page 11: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

11

2.1. UtanguliziKatika sura hii, tunatoa kwa muhtasari chambuzi zilizoandikwa kuhusu ushiriki wa wanawake katika uchaguzi. Uchambuzi huu unajikita zaidi kwenye maeneo makuu matatu; eneo la kwanza ni uchambuzi kuhusu mifumo ya uchaguzi inavyoathiri ushiriki wa wanawake katika uchaguzi. Pili makala hii inachambua mifumo mbalimbali ya uteuzi wa wanawake inayotumiwa na vyama vya siasa ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika uchaguzi. Mwisho makala inachambua mila na desturi zinazoongozwa na mfumo dume zinavyoweka vizingiti katika kuleta usawa wa jinsia.

2.2. Mfumo wa Uchaguzi na Usawa wa Jinsia (Electoral Regime)Wanazuoni wengine wanabaini kwamba mfumo wa uchaguzi unaotumiwa unaathiri sana utekelezaji wa uchaguzi shirikishi hususani ushiriki wa wanawake. Kuna aina tatu za mifumo ya uchaguzi nazo ni; mfumo wa uwiano shirikishi (proportional representation) wa pili ni ule unaoruhusu mshindi mmoja kupita (majority rule) na wa tatu ni ule unaochanganya mifumo hii miwili. Mfumo wa uwiano shirikishi unatoa fursa kwa vyama vya siasa kutoa orodha ya wagombea wake wote, kwa kuzingatia dhana ya ushiriki wa makundi. Mfumo huu hutumika huko Afrika ya Kusini. Mfumo wa pili ni ule unaotoa mgombea mmoja na anayepata kura nyingi zaidi, anakuwa mshindi. Mfumo huu unaompa mtu au chama uwezo wa kunyakua madaraka yote pale kinapopata kura nyingi hautoi mwanya mkubwa kwa ushiriki wa makundi mengi kama wanawake, vijana na watu wenye changamoto mbalimbali. Huu ndio utaratibu tunaotumia hapa kwetu Tanzania. Mfumo wa tatu unachanganya mifumo yote miwili. Mfumo huu hutumika huko Rwanda.

2.3. Utaratibu wa Uteuzi na Usawa wa Jinsia (Candidate nomination Procedures)Utaratibu unaotumiwa na vyama vya siasa katika kuteua wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi wakati wa uchaguzi unaathiri sana matokeo ya uchaguzi hususani uwakilishi wa wanawake. Kuna aina tatu za uteuzi wa wagombea nafasi za uongozi zinazotumiwa na vyama vya siasa wakati wa uchaguzi ili kuwezesha ushiriki mkubwa wa wanawake katika nafasi za uongozi. Mifumo hiyo ya uteuzi ni kama ifuatavyo: uwiano wa wagombea uliobainishwa kisheria (legislated

UCHAMBUZI WA MAKALA KUHUSU USHIRIKIWA WANANAKE KATIKA UCHAGUZI

Page 12: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

12

candidate quotas), viti maluum vya uwakilishi vilivyobainishwa kisheria (legislated special reserve seat) na uteuzi wa hiari unaotumiwa na vyama vya siasa (Voluntary Party Quotas). Ifahamike kuwa njia hizi tatu hutofautiana kiumadhubuti katika kuhakikisha ushiriki wa makundi yaliyosahaulika katika nafasi za uongozi ndani ya vyama na hata katika chaguzi mbalimbali za kidola.

2.3.1. Mfumo wa uwiano unaokubalika Kisheria (Legislated candidate quotas)

Mfumo huu huainishwa na sheria za nchi. Aidha katiba au sheria za uchaguzi zinabainisha kiwango cha chini cha wagombea kutoka jinsi moja kinachohitajika kutoka vyama vya siasa wanapopendekeza majina ya wanaowania viti vya uwakilishi

2.3.2. Mfumo wa Viti Maalum vilivyobainishwa kisheria (Legislated quotas or special seats for women) Zipo nchi chache sana zenye sheria ya kutenga viti maalum kwa ajili ya uwakilishi wa wanawake. Takwimu za IDEA (2014) zilibaini kwamba kulikuweko na nchi 36 tu duniani zenye sheria ya kuweka viti maalum kwa ajili ya wanawake. Njia mbalimbali hutumika kwenye kuwapata wabunge wanawake wa viti maalum. Kuna nchi zilizotenga majimbo maalum kwa ajili ya kuchagua wanawake tu. Kwa mfano Rwanda ina majimbo ya uchaguzi 24 (electoral colleges) yaliyotengwa kwa ajili ya wagombea wanawake tu. Vilevile India katika ngazi ya mitaa kuna majimbo yanayotengwa wakati wa uchaguzi kwa ajili ya wagombea wanawake tu. Huko Morocco kumetengwa orodha ya viti 60 vya wanawake wakati Mauritenea ina viti 20 vilivyotengwa kwa ajili ya wanawake tu.

2.3.3. Mfumo wa hiari wa kuleta uwiano (Voluntary Party Quotas)Mfumo huu unatokana na maamuzi ya hiari ya chama kubaini kiwango cha uwakilishi wa jinsi moja katika uteuzi. Mfumo huu wa hiari ulianza kutumiwa na chama cha Social Demokrat cha Sweden kutokana na shinikizo la wanachama wanawake waliodai mabadiliko ya uteuzi ndani ya chama yatakayoweka

Page 13: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

13

mazingira wezeshi ili kuongeza idadi ya wanawake watakaoteuliwa na vyama na hatimaye kuwezeshwa na vyama kushinda.

2.3.4 Ni Mfumo Upi Ulio Bora Kwenye Kuleta Usawa wa Jinsia? Mifumo yote mitatu ina faida na changamoto zake. Mfumo wowote ule unaweza kuboresha ongezeko la usawa wa jinsia kutegemeana na muktadha na hali halisi ya mfumo wa siasa ya nchi. Kwa mfano, mfumo wa viti Maalum kama tunaotumia Tanzania, una faida na changamoto zake. Pale ambapo mazingira siyo wezeshi na vyama haviko tayari kuleta mabadiliko ya hiari, viti maalum vinahakikisha ushiriki wa wanawake na makundi mengine katika vyombo vya uwakilishi. Changamoto kubwa ya mfumo huu ni kupata uhalali (legitimacy) ya uwakilishi. Vilevile mfumo huweza ukatumika kama njia ya kuwaondoa wanawake na makundi mengine katika siasa za ushindani wakati wa uchaguzi, jambo linalojionesha hapa Tanzania.

Tatizo jingine la mfumo huu ni kutokuweka taratibu zilizo wazi kuhusu vigezo vinavyotumika kuchuja wale wote wenye kuonesha nia ya kugombea nafasi katika uchaguzi. Kwa mfano hapa Tanzania, kila chama hutumia taratibu walizojipangia kuteua wajumbe wa viti maalum. Wabunge hawa hawapigiwi kura kitaifa na baya zaidi hawapewi hadhi sawa na wabunge wa majimbo na hubaguliwa katika kufikia na kutumia rasilimali za ubunge.

Mfumo wa viti maalum, sharti uende sambamba na mabadiliko katika uwanja wa uchaguzi ili hatimaye wanawake na makundi ya pembezoni yaweze kushiriki katika kuchaguliwa na wapiga kura wote.

Mfumo wa uwiano wa wagombea uliobainishwa kisheria Mfumo kuweka au kufuata utaratibu wa kuwezesha ushiriki sawa wa wanawake na makundi mengine una faida na changamoto zake. Kwanza kabisa vyama vingi vilivyojikita katika misingi na imani ya mfumo dume, ni vigumu sana

Page 14: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

14

kukubali mabadiliko kwa hiari endapo wanaharakati ndani ya vyama hawana nguvu ya kushinikiza mabadiliko yatakayokubalika na wanachama hususani viongozi. Kwa vile nchi nyingi zimeafiki mikataba ya kimataifa na kikanda yenye kuwajibisha ushiriki wa wanawake na makundi mengine katika kuwania nafasi za uongozi, basi pale ambapo kuna upinzani sharti sheria ivibane vyama kuzingatia mikataba ya kimataifa na katiba za nchi. Shinikizo la kisheria linapozaa matunda mazuri katika kuboresha ushiriki na hatimaye sera na maendeleo ya nchi pamoja na kuleta tija kwa vyama vya siasa, hatimaye mfumo linganifu utakubalika na kutekelezwa kwa hiari. Changamoto ya mfumo unaoshinikizwa na sheria ni kipindi cha mpito kinachohitaji ufuatiliaji wa karibu na utumiaji wa rasilimali nyingi kwa ajili yakukaza ufuatiliaji. Changamoto kubwa ni utekelezaji wake, hasa katika mazingira yenye upinzani mkubwa.

Mfumo wa hiari wa kuwezesha uwiano sawa wa uteuzi wa wagombea ni mzuri pale ambapo dhana ya usawa wa jinsia imekubalika kama msingi wa kuongoza shughuli za vyama. Mfumo huu hauhitaji rasilimali ya kukaza ufuatiliaji. Hata hivyo kwa mazingira yenye upinzani, hauna nguvu madhubuti kwani hutegemea sana utashi wa kisiasa na utayari wa chama kuleta mabadiliko katika kuimarisha demokrasia ndani na nje ya vyama.

2.4. Mila, Desturi na Taratibu Zinavyoathiri Usawa wa Jinsia Katika UchaguziWapo wanazuoni wengi wanaodai kwamba, mwendelezo wa tamaduni zinazowabagua wanawake katika uongozi zinaendelezwa katika mataifa mengi. Mfumo huu unaanza kwenye kaya kwa njia ya malezi. Mtoto wa kiume ana thamani tofauti, ana wajibu tofauti na stahiki tofauti za ufikiaji wa rasilimali za kaya kwenye suala la mirathi. Mfumo huu huendelezwa na jamii kwa njia ya mgawanyo wa kazi na thamani ya utu na huimarishwa kwenye shule kwa njia ya mitaala yenye viashiria vinavyojenga dhana ya uwezo tofauti wa mwanamke na mwanaume. Na mwisho huhalalishwa na sheria zinazoruhusu vipengele vya ubaguzi kwa msingi wa jinsi na jinsia. Mfumo huu

Page 15: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

15

ndio unazaa matunda yanayoongoza taratibu za vyama, katika kuteua, katika kutoa rasilimali na hatimaye katika kuamua nafasi za uongozi katika taifa. Utamaduni huu ndio chanzo cha harakati zote za ukombozi wa mwanamke. Utamaduni huu ambao haumthamini mwanamke umesababisha vikwazo vingine kama vile kukosa rasilimali ya kampeni, ukatili dhidi ya wanawake wakati wa uchaguzi na ubaguzi wakati wa kuchuja wagombea.

Page 16: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

16

SURA YATATU

Page 17: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

17

3.1. Utangulizi Sura hii inatoa muhtasari wa matokeo ya utafiti. Kwanza tutatoa muhtasari wa mambo yatokanayo na majadiliano na wadau wa uchaguzi, ikifuatiwa na simulizi za wanawake waliogombea ili kupata uzoefu wao wa ushiriki aidha wakashinda au wakashindwa.

3.2. Wajibu wa Vyama vya siasa katika Ushiriki wa Wanawake Katika Uchaguzi

3.2.1 UtanguliziVyama vya siasa katika mfumo wa Demokrasia ya vyama vingi ni taasisi muhimu ya kujenga, kulea na kuimarisha kada la viongozi wa kisiasa. Vilevile vyama vya siasa ni nguzo kuu ya utawala bora kwa mantiki ya kuwajibisha serikali iliyoko madarakani kuzingatia utawala wa sheria, haki na uwazi. Utawala wa sheria unajengeka tu pale ambapo kila raia, mwanamke kwa mwanaume, wa makundi na tabaka zote wanapewa fursa sawa mbele ya sheria. Vyama vya siasa vinapopewa dhamana ya kuingia katika vyombo vya uwakilishi vinahusika katika utunzi wa sheria na sera za nchi. Hii inamaanisha kwamba vyama hivi vina nguvu ya kuleta mabadiliko katika mifumo kandamizi kwa kutunga sheria zitakazobatilisha sheria kandamizi ikiwa ni pamoja na sheria zinazohalalisha ukandamizaji wa kijinsia.

3.2.2 Yatokanayo na Majadiliano• Utafiti ulibaini kwamba, licha ya ukweli kuwa wanawake

wamekuwa nguzo kuu ya kujenga vyama, ushiriki wao katika uongozi wa vyama vyao umekuwa finyu katika mfumo mkuu wa maamuzi ndani ya vyama kama wenye viti kitaifa, kimkoa na wilaya, wajumbe wa halmashauri kuu, kamati kuu, makatibu wakuu, na nafasi nyingine za utendaji ndani ya vyama husika.

• Vyama vyote vilivyoshiriki kwenye utafiti huu vilikiri kwambahavina sera ya jinsia lakini masuala ya jinsia yamebainishwa katika machapisho mbalimbali ya vyama ikiwa ni pamoja na katiba zao, na Ilani za vyama za uchaguzi.

• Vyama husika vina ‘matawi’ ya wanawake yanayohusika namasuala ya wanawake.

• Vyama vilivyoshiriki katika utafiti huu vina utaratibu wenyemlolongo mrefu wa uteuzi wa wagombea ikiwa ni pamoja na

MATOKEO YA UTAFITI

Page 18: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

18

wanawake wenye kugombea viti maalum. Ingawaje mlolongo huu unahusisha ngazi za chini kwenye kura za maoni, ngazi za juu zina maamuzi ya mwisho, ya kutengua au kuafiki mapendekezo ya maamuzi ya ngazi za chini.

• Vyama husika havijachukua hatua mahususi ya kuelimishawanachama wao kuhusu haki za wanawake.

• Kigezokimojawapokinachotumiwanavyamakatikauteuziwawagombea wa nafasi za uchaguzi wa ngazi zozote ni uwezekano wa kuchagulika na kushinda.

• Vilevilemgombeashartiaonyeshekwambaatawezakugharamiakwa kiasi kikubwa gharama za uchaguzi.

3.2.3 Changamoto Vyama husika havina mfumo wa hiari wa kuwezesha kufikia usawa wa jinsia katika uteuzi wa wagombea.

Mfumo unaotumika kuchuja wanawake wenye nia ya kuwania nafasi hauko rafiki kwa wanawake, na vigezo vinavyotumika vinaashiria kumchuja mwanamke hata pale ambapo amepita kwenye kura za maoni katika ngazi za awali kutokana na mfumo dume unaoongoza fikra za viongozi wa chama. Jambo hili hukatisha tamaa wanawake wengine wenye kutamani kuwania nafasi za uwwakilishi.

3.2.4 Nini Kifanyike Sheria ya Vyama vya Siasa ibadilishwe ili iwajibishe vyama vya siasa kuzingatia misingi ya usawa wa jinsia katika uteuzi wa wanaowania kugombea nafasi za uwakilishi.

Page 19: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

19

3.3. Wajibu wa Tume ya Uchaguzi Katika Kuwezesha Ushiriki wa Wanawake Katika Uchaguzi

3.3.1. UtanguliziUchambuzi huu ulijikita katika kubainisha majukumu ya Tume Ya Uchaguzi kisheria na jinsi Tume Ya Uchaguzi inavyotafsiri majukumu yake kwa mrengo wa jinsia. Tume ya Uchaguzi imeundwa kwa mujibu wa katiba Ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania (1997) Ibara 74(1). Tume ya Uchaguzi ina mamlaka ya kisheria ya kusimamia na kutoa miongozo inayoelekeza matumizi ya rasilimali za uchaguzi zitumike kwa ulinganifu, ikiwa ni pamoja na muda wa kujinadi katika vyombo vya habari vya umma na maadii ya uchaguzi yanayoongozwa na msingi wa kutokubagua. Baadhi ya Majukumu ya Tume ya Uchaguzi ni:

• Kusimamianakuratibushughulizotezamchakatowauchaguziwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano, Wabunge wa Bunge La Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, pamoja na madiwani wa mabaraza ya halmashauri za vijijini na mijini.

• Kuhakikimipakayamajimboyauchaguziiliyaendanenaongezekola watu.

• KutoaElimuyaUraianawapigakura.

3.3.2 Yaliyojitokeza kwenye MajadilianoTume ya Uchaguzi haina sera ya jinsia wala mpango wenye mikakati ya kuwezesha wanawake kushiriki katika uchaguzi kwa kuzingatia misingi ya usawa.

Katika mahojiano, utafiti ulibaini kwamba shughuli nyingi za Tume zinaweza kuingiza masuala ya jinsia na uzingatiaji wa haki za wanawake.

3.3.3 Changamoto:Kimuundo Tume ya Uchaguzi ina makamishina saba tu ambao ni wateule wa Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania. Uwezo wa rasilimali watu wa Tume ya Uchaguzi ni changamoto katika utekelezaji wa shughuli zake. Tume ya uchaguzi ina makamishina saba tu na secretariat ndogo. Haina ofisi mikoani na hivyo inakuwa vigumu kusimamia misingi ya usawa wa jinsia na kufuatilia uvunjwaji

Page 20: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

20

wa sheria na kanuni za uchaguzi. Kutokuwepo sera au miongozo inayowajibisha Tume kuingiza masuala ya jinsia katika utendaji kazi wake ni changamoto.

3.3.4 Nini kifanyike• Kwenye kupanga mpango wa kusimamia mchakato wote wa

uchaguzi Tume ingaliweza kuingiza masuala ya jinsia kama sehemu ya mpango kazi wa Tume.

• Kwenye kutoa elimu yawapiga kurana yauraia,Tume inawezakuingiza masuala ya haki za wanawake kama sehemu ya kuelimisha umma wa Tanzania kuhusu haki za wanawake.

• Watendaji wa Tume wapewe mafunzo na taaluma ya kuingizamasuala ya jinsia na haki za wanawake katika mipango yake.

• Kama washauri na wadau wakuu katika utungwaji wa sheriaTume ya Uchaguzi ishauri na itoe mapendekezo ya maboresho na/au kuleta mabadiliko ya sheria za uchaguzi ili zizingatie mrengo wa jinsia. Vifungu vinavyohitaji maboresho/mabadiliko ni pamoja na:

a. Sheria au vifungu vya sheria ya matumizi ya fedha za uchaguzi, kubainisha viwango vyenye kuendana na uhalisia wa hali halisi ya Mtanzania wa kawaida. Aidha sheria ibainishe kikomo cha matumizi ya uchaguzi kinachobebeka na mwanamke.

b. Kupendekeza kuwepo kwa fungu maalum la kuwezesha wanawake katika kuchangia gharama za kampeni. Kuwajibisha vyama kufuata misingi ya uwazi na linganifu katika kutumia rasilimali za chama wakati wa uchaguzi.

c. Kupendekeza maboresho na kusisitiza mkazo wa sheria inayohusu matumizi ya vyombo ya habari vya umma kufikiwa na wagombea wote. Kupendekeza vipindi maalum kwa wagombea wanawake kutoka vyama vyote kama hatua ya makusudi ya kusawazisha uwanja wa ushindani kwa wanawake.

d. Kusisitiza mkazo wa sheria na miongozo ya maadili ya wanaowania nafasi za uwakilishi kwa njia ya kupiga marufuku matumizi ya lugha na vitendo vyovyote venye kudhalilisha mgombea yoyote hususani wanawake.

Page 21: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

21

e. Kupendekeza mfumo wa kutoa malalamiko ulio rafiki kwa makundi yote hususan wanawake wanaponyimwa haki kutokana na kukataa rushwa ya ngono.

3.4 Jukumu la Msajili wa vyama vya Siasa Katika Kuwezesha Ushiriki wa Wanawake Katika Uchaguzi

3.4.1 Utangulizi Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya siasa (Sura ya 258) Msajili wa Vyama vya siasa ana wajibu wa kusimamia vyama ili viendeshe shughuli zake kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya siasa. Utafiti ulijikita katika kuchunguza ni kwa kiasi gani ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inawajibisha vyama vizingatie vipengele vya sheria vinavyokataza ubaguzi wa aina yoyote wakati wa mchakato wa uchaguzi. Vilevile utafiti ulidadisi kama Msajili ameweza kutafsiri majukumu na wajibu wake kwa mrengo wa jinsia.

3.4.2 Yatokanayo na Majadiliano Ofisi ya Msajili ya Vyama vya Siasa ina uelewa wa kina wa jukumu lake katika kusimamia vyama kuzingatia usawa wa jinsia katika uchaguzi. Hii imejihidhirisha katika mambo yafuatayo;

• Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa iko kwenye mchakato wakukamilisha sera ya Jinsia itakayotumika kwenye kuongoza utendaji wa kazi zake za kusimamia vyama vya siasa.

• Maafisawotewaofisihiiwameshapatiwamafunzoyajinsia.• Ofisiimetayarishamiongozoyauchaguziyenyekuwajibishavyama

vya siasa kuzingatia misingi ya usawa wa jinsia katika uteuzi wa wagombea katika nafasi mbalimbali za uwakilishi

• Ofisiyamsajiliinakitengokinachoshughulikiamasualayajinsia.• Ofisiimetoamapendekezoyamabadilikoyasheriayauchaguziili

kuwajibisha vyama vyote vya siasa vitumie utaratibu ulio wazi na wenye kuzingatia usawa wa jinsia wakati wanapoteua wagombea wao wa nafasi mbalimbali za uchaguzi.

Page 22: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

22

3.4.3 Changamoto• Miongozoiliyotayarishwahaikutumikamwakahuuwauchaguzi

kwa sababu sheria ya Vyama haikubadilishwa ili kuwezesha matumizi yake.

• Vyama vya siasa havijaonesha nia na ya kuleta mabadilikoyatakayoweka taratibu zilizo wazi, zenye kuzingatia usawa wa jinsia.

• Vilevilevyamavyasiasahavijaonahasarawanazopatazitokanazona kutoshirikisha wanawake katika ngazi ya maamuzi ndani na nje ya vyama vyao kama kwa mfano; kushindwa kutumia rasilimali watu ya wanachama katika kuboresha sera, kushindwa kuingiza mawazo mbadala ya kuimarisha vyama, kupoteza mvuto wa wanachama wanawake wenye uwezo wa kujenga vyama vyao na kushindwa kufaidi kikamilifu matumizi ya vipaji vya wanawake katika maeneo mbalimbali ya vyama.

• JamiikubwayaWatanzaniainaongozwanamfumodumewenyekujikita kwenye imani ya uongozi wa mwanaume.

3.4.4 Nini Kifanyike• Sheria yaVyama vya siasa ibadilishwe na kuboreshwa ili iingize

mapendekezo ya kuwajibisha vyama kuzingatia misingi ya usawa wa jinsia.

• Kuendeleza na kuimarisha elimu kwa umma kuhusu haki zawanawake na faida ya mfumo wa uchaguzi shirikishi.

• Kuendeleza jitihadazakujengeawanawakeuwezo iliwaendeleekutetea na kudai haki zao za ushiriki katika nyanja ya siasa.

3.5 Jukumu la Taasisi Ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Katika Kuwezesha Ushiriki wa Wanawake Katika Uchaguzi

3.5.1 Utangulizi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Kupambana na Rushwa (Sheria Namba 11, 2007). Sheria hii inafafanua majukumu ya Taasisi hii kama ifuatavyo: i. Kuchunguza na kushauri taasisi za umma na binafsi ili kubaini

kuwepo au dalili za kuwepo viashiria vya rushwa.ii. Kushauri taasisi za umma na binafsi mbinu za kuzuia rushwa,

pamoja na rushwa ya ngono.

Page 23: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

23

iii. Kupeleleza tuhuma za rushwa na kuchukua hatua stahiki za kisheria.

Kwenye eneo hili, utafiti ulidadisi kama taasisi hii imeweza kutafsiri majukumu yake kwa kuzingatia mrengo wa jinsia na kama kuna shughuli mahususi zinazolenga kuzuia au kuchunguza rushwa zinazotokana na tofauti za jinsia kama rushwa ya ngono wakati wa uchaguzi.

3.5.2 Yatokanayo na Majadiliano • TAKUKURU haina sera ya jinsiawalamikakati ya kushughulikia

rushwa zinazotokana na tofauti za kijinsia.• WatendajiwaTAKUKURUhawajapatiwamafunzoyakuwawezesha

kuingiza masuala ya jinsia katika utendaji kazi wao.• TAKUKURU haijaletewa wala haijachunguza kuwepo kwa

malalamiko kuhusu vitendo vya rushwa ya ngono wakati wa uchaguzi. Hii ni pamoja na ukweli kwamba wachunguzi wa uchaguzi CEMOT, na washiriki katika mafunzo ya uwezeshaji ya wanawake kama ULINGO na TGNP walibaini kuwepo kwa vitendo vya kunyimwa haki kwa baadhi ya wanawake walioonyesha nia ya kuteuliwa kwa ajili ya kukataa rushwa ya ngono.

3.5.3 ChangamotoTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa haijajijengea uwezo wa kutambua tofauti za jinsia zinavyoathiri rushwa wakati wote hususani wakati wa uchaguzi.

3.5.4 Nini Kifanyike • Taasisi ijenge uwezowa Kitaaluma kwenyemasuala ya jinsia ili

iweze kuingiza masuala ya jinsia katika utendaji wake wa kuzuia na kupambana na rushwa.

• Taasisi iwe na kitengomaalum cha kushughulikia, kupambana,kuelimisha na kuzuia rushwa ya ngono wakati wa uchaguzi na katika maeneo mengine katika sekta za umma na binafsi.

• Wanawakewapewenyenzo za kupambanana vitendo vyovyotevya rushwa vinavyowadhalilisha.

Page 24: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

24

3.6 Jukumu La Watendaji wa Serikali za Mitaa katika Kusimamia Haki za Wanawake Katika Uchaguzi

3.6.1 UtanguliziKatika eneo hili utafiti ulichunguza jinsi watendaji katika ngazi hii wanavyotafsiri jukumu lao katika kuwezesha wanawake washiriki katika uchaguzi. Vilevile utafiti ulipata maoni ya watendaji kuhusu matokeo ya mafunzo ya Oxfam hususani kwenye kuyaelewa majukumu yao kwenye kuwezesha ushiriki wa wanawake katika uchaguzi.

3.6.2 Yatokanayo na majadiliano • Watendaji wengi katika ngazi hii hawana uelewa wa kutosha

kuhusu jukumu lao katika kuwezesha ushiriki wa wanawake katika uchaguzi.

• Kadahiiniwalinziwaamanikatikamaeneoyao.Hivyohuhusikamoja kwa moja katika kusimamia amani wakati wa uchaguzi.

• Watendajihawahusimamiataratibunasheriazauchaguzizikiwanipamoja na taratibu na miongozo kuhusu jinsi watakavyowezesha wanawake wenye uja uzito, wanaonyonyesha na wenye ulemavu wakati wa kujiandikisha na wakati wa kupiga kura.

• MafunzoyaOxfamyaliwafunuamachokwenyekutambuawajibuwao na haki za wanawake.

3.6.3 ChangamotoWatendaji wengi katika ngazi hii hawana ustadi wa kuingiza masuala ya jinsia katika shughuli za uchaguzi.

3.6.4 Nini Kifanyike Kuwe na programu maalum kwa watendaji wa ngazi hii kuhusu haki za wanawake kwa ujumla na katika uchaguzi.

Page 25: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

25

3.7 Simulizi za wagombea wanawake katika uchaguzi mkuu 2015, Tanzania

3.7.1 Nancy Mrikaria (Aliyekuwa Mgombea Ubunge, Jimbo la Temeke, Dar es Salaam)

Nancy anakiri kuwa wazazi wake hasa baba yake alikuwa na mchango mkubwa katika kumhamasisha siyo tu kufanya vyema katika masomo yake shuleni, lakini pia kujenga uwezo wa kujiamini. Kwa hili la kujiamini, ndiyo ulikuwa msingi mkuu katika maisha yake. Sababu nyingine ya mafanikio yake ilikuwa shule alizosoma na walimu wake. Katika shule za msingi na sekondari, Nancy alichaguliwa kuongoza nafasi mbalimbali kwenye ngazi za darasa na shule.

Aidha, alichaguliwa katika ngazi mbalimbali za uongozi ikiwamo kwenye kanisa alilokuwa akisali na jamii iliyokuwa ikimzunguka. Yote hayo yalichangia kumjenga uwezo wa uongozi.

Lakini pia sifa hizi za uongozi zimeimarishwa zaidi kwa mafunzo mbalimbali aliyohudhuria yakiwamo yale yaliyoandaliwa na taasisi za kiraia za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na taasisi isiyo ya kiserikali ULINGO. Lakini pia, Nancy alijihusisha na mijadala mbalimbali iliyotayarishwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi. Uzoefu wake akiwa mjumbe wa lilikokuwa Bunge la Katiba, ambalo lilikua na wajibu wa kuandika Rasimu ya Katiba Mpya, umechangia kwa kiasi kikubwa ari ya kupigania haki za wanawake.

Nancy alianza safari yake ya uongozi ndani ya chama chake cha Tanzania Labour Party (TLP) akiwa Katibu wa Wilaya ya Temeke mwaka 2000, na kati ya mwaka 2002/2003 akawa Katibu wa Mkoa wa Dar es Salaam wa Umoja wa Wanawake wa TLP. Mwaka 2011, alipanda ngazi na kuwa Naibu Katibu Mkuu wa TLP. Safari haikuishia hapo. Mwaka huu akachaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa TLP. Mafanikio yote hayo yamemwezesha kupiga hatua na kujijenga kisiasa.

Page 26: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

26

Matokeo ya mafunzo ya FOS Awamu ya Pili Nancy anasema mafunzo hayo yalimpatia fursa ya “kubadilishana uzoefu na maarifa kati ya rika mbalimbali”. Nancy anatoa maoni kuwa mafunzo shirikishi yenye kuwaleta pamoja washiriki kama hayo ya FOS ya Awamu ya Pili yalikuwa na msaada mkubwa kwa washiriki wote yaani wale waliokuwa na uzoefu mkubwa na waliokua na uzoefu mdogo. Kwa wale washiriki vijana au waliokuwa wagombea nafasi mbalimbali kwa mara ya kwanza ilikuwa ni fursa ya kujifunza kutokata tamaa kwani ilishuhudiwa kuwapo kwa washiriki ambao huko nyuma walikua wagombea wa uchaguzi wakashindwa kwa sababu mbalimbali lakini hawakukata tamaa. Nancy anasema mafunzo yalikuwa mazuri kwa sababu yalikuwa shirikishi na yalihusu mchakato mzima wa uchaguzi. Mafunzo yalianza na wapiga kura, kuelekea kwa wagombea na hatimaye wagombea washindi wa vyama husika. Mwisho, kulikuwa na madarasa ya majumuisho ambayo yaliwaleta pamoja wagombea ambao hawakufanikiwa kushinda uchaguzi katika ngazi mbalimbali na wale ambao walishinda nafasi hizo ili kubadilishana uzoefu na kujitathmini kama wagombea wanawake.

ChangamotoChangamoto pekee katika mradi huo iliyojitokeza ni kuwa mafunzo yalianza yakiwa yamechelewa kidogo wakati vyama vya siasa vilikua vimeshawachuja wagombea wake wa nafasi mbalimbali na wakati huo wagombea hao walishaanza matayarisho yao ya kuanza kampeni husika.

Nancy anaeleza zaidi kuwa moja ya changamoto kuu ilikuwa ni hali ya kisiasa. “Demokrasia shirikishi ya vyama vingi bado haijaweza kukumbatiwa kama tamaduni ya kisiasa nchini hasa kwa chama tawala na pia kutoka kwa washindani wa kiume,” anasema Nancy. Ushindani ulikua mkali na pesa ilikua kigezo muhimu kushinda uchaguzi.

Anasema: “Kwa ujumla nimetumia kama Sh2 milioni kutoka mfukoni kwangu na baadhi ya marafiki walinichangia.” Lakini kiwango hiki ni kama mzaha: “Kiwango cha chini cha gharama za kuendesha kampeni kwa mkutano mmoja ni wastani wa kama Sh300,000. Kwa maana hiyo, ningeweza kuandaa mikutano kama sita tu kwa fedha niliyokuwa nayo. Kuna gharama nyinginezo kama vile vifaa, matangazo, usafiri,

Page 27: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

27

posho kwa timu yako ya kampeni na mahitaji yako binafsi.”

Kwa Nancy, suala kubwa hapa sio kukosa stadi sahihi na ujuzi wa kuendesha kampeni na kushindana katika uchaguzi, bali gharama za uchaguzi na hapa anadokeza umuhimu wa ruzuku kutoka serikalini hasa kwa vyama vidogo akisema mafunzo pekee bila msaada wa fedha haitakua na tija inayotegemewa kwa wagombea wanawake hasa wale wanaotoka katika vyama vidogo au wale wanaoingia katika kuwania uongozi wa kisiasa kwa mara ya kwanza.

Nini KifanyikeMipango ya kuwajengea uwezo wagombea wanawake ianze mapema kabla ya muda wa kampeni. Mwisho wa kipindi cha uchaguzi ndiyo pia uwe mwanzo wa kipindi kingine kama hicho. Kuna haja ya kuwa na mikakati ya muda mrefu kwenye mipango ya mafunzo ya aina hii ambayo pia inawalenga wanawake vijana. Pia, juhudi na mipango ya pamoja inahitajika kutoka kwa washirika wa maendeleo na vyama vya kijamii ili kuhakikisha kuwa hakuna mwingiliano wa mipango inayofanana na pia kuhakikisha kuwa tija inapatikana kwa kiwango cha hali ya juu.

Mfuko wa kuwasaidia wanawake watakaonyesha nia na uwezo wa kusimama kwenye uchaguzi uanzishwe. Michango kwa kadri ya uwezo kutoka kwa watu binafsi ambayo itaweka vigezo kwa wenye sifa kupata ufadhili wa ruzuku husika ianzishwe. Mwisho kuimarisha vuguvugu la wanawake likisaidiwa na mifumo na sera za kisheria ili kuwa na usawa wa ushindani katika siasa kwa jinsia zote ni wa umuhimu wa kipekee.

Page 28: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

28

3.7.2 Mh. Angeline Mabula (Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Mwanza na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi)

Angeline anatoka katika familia ya wanasiasa. Babu yake alikuwa chifu wakati baba yake alikuwa ni diwani na pia Mkuu wa Wilaya. Angeline anasema: “Historia hii bila shaka imekuwa na ushawishi katika safari yangu ya kisiasa.” Lakini mafanikio yake bila shaka yaliwezeshwa kwa kiasi

kikubwa na wazazi wake ambao walimtia moyo katika masomo na uwezo wa kujiamini.

Mbali ya historia yake hiyo ambayo ilimpa mwanga wa kisiasa, Angeline anasema: ‘‘Nina hulka ya kupenda kufanya kazi na jamiikatika ngazi za chini’’. Fursa yake ya kwanza kufanya kazi na jamii ilikuwa wakati alipofanya kazi na shirika la misaada la kimataifa Caritas akiwa mhasibu na mratibu wa Jinsia na Maendeleo. Anasema alisukumwa na kuguswa baada ya kushuhudia kiwango cha umaskini katika jamii na kugundua kuwa ni kwa namna gani sehemu ndogo ya msaada wenye ubunifu unavyoweza kuwezesha jamii hizi kujiendesha na kujikwamua.

Ni wakati huo alipoamua kuacha kazi yake ya kitaaluma na kujiunga na siasa mwaka 2000 alipojitosa kuwania nafasi ya udiwani na kushinda. Baadaye alionekana anafaa na kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mkuu wa Wilaya. “Hii ilikuwa fursa muhimu kufanya kazi na watu kwa ukaribu na kusimamia rasilimali zao kwa maendeleo yao,” anasema.

Lakini Angeline hakukaa muda mrefu kwenye nafasi hii, alitaka kuendelea mbele kwenye nafasi za juu za utawala na uamuzi ili kupaza sauti yake na kusaidia kusukuma mbele maendeleo ya watu. Mwaka 2010 alitaka kuingia bungeni kupitia viti maalum lakini kwa

Page 29: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

29

sababu kadhaa, hakufanikiwa azma yake hiyo. Lakini mwaka huu, alijaribu tena bahati yake kupitia siasa za ushindani wa uchaguzi wa kuchaguliwa kupitia jimbo na kufanikiwa kushinda. Pia, ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Sababu zilizochangia mafanikio ya Angeline

Haiba binafsiKinachoakisi mafanikio yake ni ari yake ya kutaka kuleta mabadiliko katika jamii na kutokukata tamaa. Sifa hii imekuwa ni kichocheo na wakati mwingine kumwezesha kuvumilia kutukanwa na washindani wake wa kisiasa. Hata hivyo, anasema uungwaji mkono kutoka kwa wanawake wenzake, marafiki zake na hata watu ambao hakuwajuwa kwa ujumla ulichochea ari yake katika harakati hizi. Jambo hili lilichochea ari yake katika harakati hizi. “Wanawake wenzangu walikua nami wakati wote. Wakati mwingine wapinzani wangu waliamua kuwa na mapambano ya kunikashifu binafsi na mbinu nyingine zisizo za kistaaarabu,” anasema. Angeline ni mwanasiasa mwenye haiba ya kipekee na mwenye uhusiano mzuri na watu na sifa hizi zilichangia kufifisha mashambulizi ya kisiasa kutoka kwa washindani wake.

Ukusanyaji wa rasilimali za kampeni “Kampeni ni gharama sana,” anasema Angeline. Anashauri zichukuliwe hatua za haraka kudhibiti hali hiyo ya gharama vinginevyo itakuwa vigumu sana kwa wanawake kumudu gharama za kampeni. Kwa kutambua hilo, Angeline alipanga bajeti ya uchaguzi mapema kutoka vyanzo vyake binafsi, marafiki na chama chake ambacho kilimsaidia vifaa vya matangazo. Kwa ujumla, anadokeza kwamba alitumia karibu Sh52 milioni. Kiasi hiki kilimwezesha angalau kukidhi gharama husika na anasisitiza kuwa hakujihusisha na vitendo vya kutoa rushwa kwa wapiga kura kama inavyodaiwa kukithiri kwa vitendo hivi kwenye uwanja wa siasa hasa wakati wa uchaguzi. Ujumbe wake kwa wapiga kura ulikuwa “Thamani ya kura yako au Sh5,000 kwa miaka mitano ijayo.” Anasema baadhi ya wapiga kura walielewa ujumbe wake lakini wenginewalimpuuzanakuitatimuyake‘timuyalofa’.

Page 30: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

30

Matokeo ya mafunzo ya FOS Awamu ya Pili Angeline hakushiriki mafunzo haya moja kwa moja. Wakati mafunzo yanaendelea alikuwa ametingwa na maandalizi ya kampeni yake lakini aliamua kutuma meneja wake wa kampeni ambaye alishiriki kikamilifu kwenye mafunzo hayo. Angeline alihudhuria sehemu ya mafunzo yaliyoandaliwa na Oxfam yaliyoangazia hatua na mchakato baada ya uchaguzi. Pia, alihudhuria baadhi ya mafunzo yaliyoendeshwa na taasisi ya Hansen Foundation. Kwa Angeline, mafunzo ya kujengewa uwezo kwa wanawake ni muhimu kuweza kufikia malengo yao. Stadi muhimu za mafunzo hayo ni kama vile mbinu za kukusanya fedha za kampeni na mbinu za mawasiliano ya umma ikiwamo namna bora ya kushirikiana na vyombo vya habari. Kwenye mafunzo hayo, alijifunza kuongeza mfumo wa mtandao wake wa kumuunga mkono ambao ni muhimu kwa wanawake katika siasa za ushindani.

Changamoto Anaona utamaduni hasi mbaya wa matusi na lugha za kudhalilisha wagombea wanawake unaashiria kuwajengea wanawake na vijana kwa ujumla hofu ya kuingia na kushiriki katika siasa za ushindani.

Suala la gharama za kampeni pia ni changamoto kubwa na linahitaji hatua za kulidhibiti.

Hatua za uwezeshaji kama elimu ya uraia haipo katika mipango ya muda mrefu na endelevu.

Nini Kifanyike? Anataka kuwepo usimamizi zaidi wa sheria ambazo zitazuia matendo ya udhalilishaji katika michakato ya uchaguzi na hasa lugha za udhalilishaji ya hadhi na utu wa wagombea. Anashauri pia mipango ya uwezeshaji ilenge kuwa ya muda mrefu na mwisho, vyama vya siasa vibuni vyanzo vya fedha kudhamini wagombea wanawake kwenye siasa hizi za ushindani.

Page 31: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

31

3.7.3 Magreth Mashenene (Aliyekuwa Mgombea Udiwani, Kata ya Shishani, Magu, Mwanza)

Nini kilimshawishi kuingia sisa za ushindani?Hii ni mara ya kwanza kwa Magreth kujaribu kuingia siasa za ushindani. Nia yake ya awali katika siasa ilikua kuingia katika baraza la madiwani na kutumia nafasi yake kushawishi uongezwaji wa bajeti katika sekta za afya, maji na miundo mbinu ya barabara, sekta ambazo ni changamoto kwa watu wanaoishi kwenye eneo lake kata ya Shishani, Wilaya ya Magu, Mwanza.

Magreth anasema wanawake wa sehemu hiyo ndiyo wamekuwa waathirika wakubwa kwa kukosekana huduma za maji, kutunza jamaa na familia wanapougua na pia kwenye uchukuzi wa mazao kutoka mashambani kwenda kwenye masoko.

Magreth pia alitiwa moyo kutokana na kufanya kazi za miradi mbalimbali inayolenga kuboresha maisha na hali ya wanawake ndani ya Kata yake ya Shishani. Pia, Jumuiya ya Wanawake ya Chama cha Mapinduzi (UWT) ilimtia moyo kugombea.

Gharama za kampeniKatika kuungwa mkono, Magreth anasema alikuwa na watu wengi nyuma yake wakiwemo marafiki, watoto wake wawili na pia chama chake kiliweza kumchangia Sh300,000. Kwa ujumla anasema alitumia Sh6 milioni kugharamia kampeni. Anasema kampeni za siasa nchini ni za gharama kubwa na ni changamoto kubwa kwa wagombea wanawake. Kwa sababu hiyo, anasema kuna haja ya kuwa na mikakati na mipango mingine ya kuwasaidia kutoka vyanzo mbalimbali.

Matokeo ya mafunzo ya FOS Awamu ya Pili “Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kupata mafunzo kama haya ya kunijengea uwezo”, anasema na kuongeza: “Yaliniwezesha kuwa na stadi muhimu ambazo zilinisaidia kama vile namna ya kuongea na kujieleza mbele ya hadhara, kutayarisha mikutano ya kampeni na aina za ujumbe mbalimbali za kampeni. Mbinu hizi za mafunzo zilimuongezea uwezo wa kujiamini.

Page 32: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

32

Aidha, mafunzo hayo yaliwawezesha kujifunza baadhi ya sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi pamoja na mikakati ya namna ya kushirikiana na vyombo vya habari.

Changamoto Moja ya changamoto anazoelezea Magreth ni baadhi ya mila na utamaduni za jamii zinazombagua mwanamke na kumdharau kijana wa kike mwenye nia na ndoto ya kuongoza. Jamii hizo bado zinamkandamiza na kuamini kuhusu nafasi duni ya mwanamke katika jamii. Wote, wanawake kwa wanaume, bado wana fikra potofu kuwa mwanaume ndiye anayefaa kuwa kiongozi na mwanamke yoyote anayethubutu kushindana na mwanaume hukumbana na matatizo mbalimbali ya ukatili yakiwemo matusi na mashambulizi.

Gharama za uchaguzi pia ni eneo lingine ambalo Magreth analiona kama changamoto kubwa. Chaguzi zimekuwa ni suala la gharama kubwa ambalo linatishia kuwasukuma wanawake nje ya ulingo wa siasa za uchaguzi za ushindani.

Nini kifanyikeElimu ya uraia lazima iendelee ikiwalenga zaidi jamii zenye kukumbatia mfumo dume. Vilevile, kuanzishwe mifuko maalumu ya fedha kuwasaidia wanawake wagombea hasa wale ambao wamejitosa kwa mara ya kwanza. Aidha, anataka kuwapo kwa mipango endelevu ya kujenga uwezo kwa wagombea wanawake.

Ansisitiza, desturi na mila zenye kukandamiza haki za mwanamke zibatilishwe. Pia, wanawake wasikate tamaa kugombea nafasi za uongozi katika Siasa.

Page 33: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

33

3.7.4 Khadija Msawira (Aliyekuwa Mgombea Udiwani, Kata ya Makurumla, Kinondoni, Dar es Salaam)

“Ningekuwa na rasilimali za kuniwezesha kuzunguka kata yangu yote hakika ningeshinda nafasi niliyoomba,” anasema Khadija kwa kujiamini. Ni kijana wa miaka 27 ambaye alihitimu masomo ya utawala wa biashara katika ngazi ya diploma na mwanachama wa chama cha CHAUMA. Baada ya kumaliza chuo, alitafuta kazi bila mafanikio na akachukua muda kutafakari hatima yake kujua hasa ni nini alitaka kufanya maishani. Hatimaye akagundua ana wito wa kutafuta nafasi za uongozi ili

asaidie kutoa mchango wake kwa jamii yake.

Alikuwa akishangazwa kuona uongozi uliokuwapo unashindwa kutatua changamoto zilizopo kwa kushirikisha jamii. Wakati akiwa na hamu hii ya kutafuta nafasi ya uongozi, hakuwa anajua ni kwa namna gani atafanikiwa katika azma yake hiyo ya kuwashawishi wapiga kura. Pia, alikabiliwa na hofu kubwa mbili; kwamba yeye ni mwanamke na ni kijana.

Alihofia kwamba jamii yake haitamtilia maanani kutokana na mila na desturi za kutukuza mfumo dume wenye kukandamiza jinsi ya kike na umri. Kwa hiyo anasema mafunzo hayo yalikuja kwa wakati muafaka.

Matokeo ya mafunzo ya FOS Awamu ya PiliKhadija anakiri kuwa mafunzo ya FOS Awamu ya Pili, yalimwezesha kujenga uwezo na stadi muhimu. Moja ya mbinu alizojifunza ni namna ya mawasiliano bora na umma, kutengeneza ujumbe sahihi kwa umma na namna ya kuzielewa na kuzielezea changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake. Zaidi ya mafunzo hayo, fursa ya kukutana na aliyekuwa mgombea mwenza wa Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ilimwongezea ari na kujiamini. Mama Samia aliwataka wanawake wote bila kujali vyama vyao kushirikiana katika harakati za kisiasa kuweza kuubomoa mfumo dume unaowanyima fursa sawa.

Page 34: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

34

“Kukutana na Mama Samia hakika kulichochea hamu yangu ya masuala ya siasa,” anasema Khadija. Khadija ambaye alimshinda mshindani wake wa kiume katika kura za maoni ndani ya chama chake kwa sababu ya uwezo wake wa kujieleza mbele ya wajumbe wa kamati ya mchujo.

Changamoto

Gharama za kampeni Wakati Khadija anasesma alikuwa na uwezo na stadi zote muhimu kwa ajili ya kampeni, alishtuka pale alipogundua kuwa fedha alizokuwa nazo zilimalizikia kwenye uzinduzi wa kampeni zake. Alishindwa kutembelea kata yake yote na hivyo kuthibitisha kuwa harakati zake zimeishia ukingoni. Kugharamia kampeni ilikua ni changamoto kubwa. Khadija alijiwekea akiba ya Sh1.5 milioni huku familia yake na marafiki wakimchangia Sh2 milioni na chama kikichanga vifaa vikiwamo vipeperushi.

Ansema moja ya changamoto alizokumbana nazo ni kutakiwa kutoa rushwa ya ngono kwa baadhi ya wanaume aliyowaomba wamchangie ambayo aliikataa na kuipinga vikali aina hiyo ya udhalilishaji utu wa mwanamke.

Kukataa kwake, kulimgharimu. Hakufanikiwa kupata fedha alizohitaji sana hasa kutoka kwa wanaume ambao anasema baadhi yao walikua na uwezo wa kiuchumi wa kumsaidia.

Nini cha kufanya Mafunzo na mipango ya uwezeshaji yenye kuwalenga wanawake vijana ni vyema yawe endelevu, anashauri. Pia, anasema kuna umuhimu wa kuimarisha vuguvugu la wanawake na kuwahamasisha na kuwapa sapoti wanawake vijana wenye nia na uwezo wa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika siasa. Pia, anaeleza umuhimu wa vyama vidogo vikawezeshwa kifedha wakati wa uchaguzi ili waweze kumudu gharama za kampeni.

Page 35: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

35

3.7.5 Mh. Safia Mkama (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, Mwanza)

Safia alianza harakati zake za kisiasa kuanzia mwaka 2005 kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM (UWT) Kata ya Buswelu, Wilaya ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza. Mwaka 2013, alipanda ngazi na kuwa Mwenyekiti wa UWT Wilaya pia Mwenyekiti wa Tawi la Ilemela. Mwaka huu akawania kiti cha Udiwani kata ya Buswelu na kushinda.

Sababu zilizochangia katika safari yake ya kisiasa

Safia ana maoni kuwa wazazi wake walimjengea msingi imara wa safari yake hii kwa kumwezesha kupata elimu stahili. Nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya UWT zimemwezesha kumpeleka katika nafasi yake ya sasa ya Udiwani. Fursa kadhaa za mafunzo pia zimechangia yakiwemo mafunzo haya ya FOS Awamu ya Pili.

Matokeo ya mafunzo ya FOS ya Awamu ya PiliMh. Safia amehudhuria mafunzo mbalimbali yaliyoandaliwa na asasi za kijamii kabla ya ha haya ya FOS Awamu ya Pili. Baadhi yake ni yale yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na UWT.

Mafunzo ya FOS awamu ya Pili yamemwezesha kuwa na stadi muhimu katika uchaguzi. Kwa mfano mbinu za mawasiliano zilikua na usaidizi mkubwa katika kutengeneza mikakati ya mawasiliano na umma wakati wa kampeni. Pia, mbinu za kupata fedha za kampeni ni eneo jingine lililokuwa na faida kujifunza licha ya kuwa alikua na uzoefu katika shughuli nyingine za kukusanya fedha katika jamii kama vile harusi, misiba na hata zile za kidini. Pia, mafunzo hayo yalimwezesha kutambua uwezo wake wa kiuongozi. Mwisho, mitandao itokanayo na mikusanyiko ya washiriki wa mafunzo hayo, imemwezesha kupata nyenzo muhimu za kubadilishana uzoefu na kuimarisha nguvu za pamoja.

Page 36: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

36

ChangamotoVyama vya siasa havitengi fedha kuwasaidia wagombea wanawake kushiriki uchaguzi. Kwa mfano, ilibidi Safia atafute fedha mwenyewe kugharamia kampeni. Kwa kulijua hilo, alidunduliza akiba kwa kipindi cha miaka mitatu. Ilipofika muda wa kampeni, alihitaji fedha ya ziada kidogo kutoka kwa marafiki kwa kampeni ya gharama ya chini.

Anasema ikiwa wanawake watajipanga vyema na mapema, wanaweza kutumia kiasi kidogo cha fedha kwenye kampeni kuliko ilivyo kwa sasa kwa wanaume. Hata hivyo, anaona kuwa kampeni sio rafiki kwa wagombea wanawake akisema wanaothubutu kupambana na wanaume hukumbana na lugha za kashfa na udhalilishaji wa utu wao.

“Kuna dhana kuwa ni wanaume pekee ndiyo wanastahili fursa za kisiasa miongoni mwa wapiga kura,” anasema Safia na kuongeza: “Wanawake wanaothubutu kuchuana na wanaume wanahitaji ujasiri wa hali ya juu kuthibitisha uwezo wao.”

Mwisho, gharama za uchaguzi kwa wagombea, hususan wanawake ni changamoto kubwa. Tatizo hili lisipotafutiwa ufumbuzi litakuja kuwapa fursa wanaume na wanawake wachache tu wenye uwezo wa kiuchumi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi.

Nini kifanyikeKuwe na mafunzo mbalimbali na mipango ya uwezeshaji iwe endelevu. Pia, kuwepo mipango ya kuhamasisha umma kutambua namna wanawake wanaweza kuleta mchango muhimu kwenye Siasa.

Page 37: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

37

3.7.6 Anna Elisha Mghwira (aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)

Wakati wa Uchaguzi Mkuu 2015, Anna Elisha Mghwira alikuwa mwanamke pekee aliyegombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo.

Anna Mghwira ni nani? Anna alipokua mtoto alikabiliwa na maradhi ambayo hayakuweza kupatiwa ufumbuzi kwa wakati huo. Hali hiyo ilimfanya mtoto Anna kuchelewa kutembea na alitumia muda mwingi akiwa nyumbani. Kwa ujumla

alikuwa mtoto mkimya mno, isipokuwa Jumapili wakati sauti yake ya kuvutia iliposikika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) alilokuwa akihudhuria.

Anna alikuwa na kipaji cha ususi na stadi nyingine za kazi za mikono ambazo zilimwezesha kulipia karo ya shule kwa miaka miwili ya elimu ya sekondari. Baadhi ya bidhaa alizotengeneza ziliweza kuuzwa huko Amerika na mmoja wa waalimu wake na kumpatia kipato cha Dola za Kimarekani 1,200 kwa wakati huo.

Kazi hizi za mikono ziligeuka kuwa chanzo cha mapato ya kulipia ada na matumizi yake mengine. Baada ya baadhi ya wateja kutambua kipaji chake na waliamua si tu kununua bidhaa zake, bali walianza kuchangia karo yake ya shule mpaka sekondari ya Juu. “Wakati hali hii ikiwa ni baraka kwangu lakini ndio ikauwa kipaji changu cha kazi zangu za mikono na kunifanya niweze kuzingatia masomo yangu kikamilifu,” anasema.

Anna pia anajulikana kama mtu wa msimamo na mchapa kazi: “Muda wote wa maisha yangu ya shule nilihudumu katika kamati mbili; ya maadili na ile ya mapato. Tulikuwa na mawazo ya kibunifu wakati wote na mawazo ambayo yaliisaidia shule kukidhi mahitaji yake.” Mwanasiasa huyu shupavu anatoka pia katika familia yenye wanawake wenye msimamo imara. Bibi yake alikuwa mwanamke

Page 38: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

38

jasiri asiyekubali kuyumbishwa. Jambo la kusisimua kwa mujibu wa simulizi za baba yake ni kuwa, hata mama yake Anna (ambaye sasa ni marehemu) alikuwa na sifa na haiba kama ya bibi yake. Anasema kuwa alipata malezi ya kuwa mtu wa kujitegemea kimawazo na hili limechangia makuzi yake kama mwanasiasa. “Mzazi wetu alitufanya sisi wasichana tujisikie tuna thamani na wenye uwezo mkubwa wa kufikiri.” Malezi haya yalitufanya sisi watoto wa kike tusikubali kukandamizwa utu wetu na kubaguliwa kutokana na mawazo mgando katika jamii kuhusiana na hadhi, uwezo na thamani ya mtoto wa kike.”

Historia ya elimu Anna ni msomi wa shahada mbili, moja ya Theolojia na nyingine ya Sheria. Alianza masomo yake ya Sheria akiwa mwaka wa mwisho wa masomo ya Theolojia. Pia ni mhitimu wa Shahada ya Uzamili ya Sheria akibobea katika masuala ya Sheria za Kimataifa za Haki za Binadamu kutoka Chuo Kikuu cha Essex cha Uingereza. Amebobea na kufanya tafiti kwenye masuala ya haki za watoto, wakimbizi, wanawake, ardhi na mali asili.

Shauku kwenye siasa za uchaguzi Anna anapenda kufanya kazi na amehudumu katika nafasi mbalimbali za kanisa lake ndani na nje ya nchi. Akiwa bado mwanafunzi aliweza kutumikia kwenye bodi ya Elimu ya Theolojia ikiwa nafasi yake ya kwanza katika ngazi ya uamuzi, ikifuatiwa na nafasi katika Idara ya Wanawake wa Kanisa KKKT. Akiwa na nafasi hii alifurahia kazi yake ya kuhudumia wanawake na viongozi wao katika ngazi za mashina.

Fursa yake ya kwanza kujihusisha na siasa ni pale alipokuwa akifanya kazi na shirika la kimataifa la misaada la SNV Tanzania akiwa mshauri wa utawala na uongozi. Majukumu yake yalikuwa pamoja na kuimarisha ajenda ya demokrasia katika vyama vya siasa. “Hapo ndipo nilipoanza kuona changamoto na fursa za kuimarisha michakato ya kidemokrasia Tanzania,” anasema.

Baada ya kumalizika kwa mkataba wake SNV aliamua kujiunga na moja ya vyama vya upinzani, akatua CHADEMA ambako mwaka 2012, aliwania ubunge wa jimbo na pia katika Bunge la Afrika Mashariki.

Page 39: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

39

Lakini katika chaguzi zote hizo hakufanikiwa. Hata hivyo hakukata tamaa.

Itikadi ya Anna ni ujamaa wa kidemokrasia na anakosoa kuwa vyama vingi vya siasa Tanzania haviweki msisitizo kwenye itikadi inayowaongoza. Kutokana na kasoro hii, anasema aliamua kujiunga na chama cha ACT-WAZALENDO ambacho anasema kinajinasibu kwa itikadi yake ya ujamaa wa kidemokrasia. Mwaka huu, aliteuliwa na chama chake kuwania nafasi ya urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa mwanamke wa pili tangu Uhuru kugombea nafasi hiyo ya juu kabisa ya mamlaka ya uongozi wan chi wa kwanza wakiwa Anna Senkoro aliyefanya hivyo katika Uchaguzi Mkuu wa Desemba 2005 kwa tiketi ya PPT-Maendeleo.

Uzoefu wake wakati wa kampeni “Sikupanga kusimama nafasi ya Urais,” anadokeza na kuongeza: “Nilikua nimejitayarisha nafasi ya ubunge na safari hii nilikua na uhakika wa ushindi. Wakati chama kilipoamua kujiunga na mbio za Urais tulipendekeza majina kadhaa ambao hata hivyo, wote walikuja kukataa wito huo wakitoa sababu za kifamilia.” Ni desturi wakati chama kikielekea kupoteza mgombea urais, basi Mwenyekiti anachukua jukumu kuonyesha uongozi,” anasema na kuongeza kuwa, viongozi wenzake walimuhimiza kuchukua jukumu hilo. Mwanzo familia yake haikukubaliana na wazo lake lakini baadae waliweza kuridhia na kumuunga mkono.

Kampeni zilikua ngumu, anasema na kufafanua kuwa wakati kulikua na kambi kuu mbili zilizokuwa zikishambuliana vikali yeye, alijikita katika kushawishi wapiga kura juu ya sera za chama chake.

“Kamwe sikuwahi kuelekezewa mashambulizi ya kijinsia, matusi au kutishwa. Kampeni zangu zote zilipokelewa vizuri na kupata mrejesho chanya kutoka kwa jamii nilizotembelea, wanachama wa chama changu, familia yangu na marafiki. Ajabu hata hivyo hali hii haikuweza kuakisi kura nilizopata.”

Page 40: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

40

Changamoto Ukosefu wa rasilimali ilikua moja ya changamoto kubwa aliyokutana nayo. Kwa chama kichanga kama chake ilikua ni changamoto kujaribu kuuza sera kwa wapiga kura na kulazimika kusafiri katika kila kona ya nchi bila kupumzika. Anaongeza kuwa chama hakikua na hata nusu ya fedha iliyohitajika kukidhi bajeti ya kampeni na ilimlazimu kutumia fedha ya akiba aliyojiwekea na hata kukopa kutoka kwa marafiki na baadhi ya wana familia kukidhi mahitaji. Mwanasiasa huyu anasema alijikuta ametumia kiasi cha shilingi milioni 50 hadi pale kampeni zilipomalizika.

Anasema sehemu kubwa ya ghararama za uchaguzi nchini hujitokeza katika namna mbalimbali za rushwa akitoa mfano wa wapiga kura kutegemea wagombea kutoa rushwa ili wawape kura.

Gharama nyingine kubwa zinatokana na machapisha na vifaa vya kujitangaza. “Vyombo vya habari vilitoa mchango mkubwa lakini gharama zake ni mzigo mkubwa kwa wagombea,” anasema.

Nini kifanyikeAnna anapendekeza kuwe na mipango ya kiuchumi kwa wanawake ambayo itasaidia kuwaweka huru kutokana na utegemezi kiuchumi na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika siasa za ushindani.

Anashauri pia taasisi za kuwawezesha wanawake kuongeza jitihada za pamoja za kupigania haki na fursa sawa kwa kuandaa mipango endelevu na ya ubunifu ya kuwatambua na kuwaendeleza wanawake wenye uwezo na sifa za kiuongozi.

Kutafuta vyanzo vya mapato ni muhimu, anasema na kuongeza kuwa vyanzo vya nje vije kusaidia tu na visiwe vya kutegemewa zaidi kama ndivyo vyanzo vikuu katika uchaguzi.

Anasifu mpango wa tathmini ya uchaguzi ulioandaliwa na Oxfam akisema una manufaa makubwa kwani uliwajumuisha wagombea wanawake walioshinda na wale ambao hawakushinda uchaguzi kwa lengo la kubadilishana uzoefu. Anna anasema fursa hiyo ya kukutana na kubadilishana uzoefu kati ya wagombea ambao hawakufanikiwa kushinda na wenzao walioshinda, husaidia kujifunza na pia kufarijika kuwa wapo pamoja.

Page 41: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

41

SURA YANNE

Page 42: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

42

Sura hii inajumuisha mambo muhimu yaliyotokana na uchambuzi wa makala, mahojiano na wadau wa uchaguzi pamoja na simulizi za wanawake waliotoa shuhuda za ushiriki wao katika uchaguzi. Sura hii inajikita zaidi katika kutoa mapendekezo yatakayowalenga wadau wote wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na Oxfam, vyama vya siasa, Msajili wa Vyama vya Siasa, Tume ya Uchaguzi, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, asasi zisizo za kiserikali, serikali za mitaa, wanawake wenyewe na jamii kwa ujumla.

Oxfam iendeleze mradi wa FOSII na kuboresha mbinu zilizotumiwa kwani uligusa maeneo yote yanayoashiria kumwezesha mwanamke ashiriki katika mchakato wote wa uchaguzi kama mpiga kura, mtendaji katika mchakato wa uchaguzi, mwenye kuonesha nia ya kuwania, mgombea na hatimaye kama mshindi. Changamoto kubwa iliyojitokeza ni kutokuwa na mpango endelevu wa mafunzo haya ili yatolewe kwa muda mwafaka.

Mafunzo ya kuwezesha na kuwajengea wanawake uwezo wa kutambua vipaji vyao na kuwapa mbinu za kukabiliana na changamoto zilizoko kwenye mfumo wa uchaguzi yaimarishwe na yawekewe mipango endelevu na wadau wote wenye nia ya kuwajengea wanawake uwezo wa kushiriki katika uchaguzi. Mafunzo yalenge kundi kubwa la vijana wa kike wenye kuoneesha nia na wenye ndoto za kuingia kwenye siasa.

Kuna umuhimu wa kuchambua upya mfumo wa sheria ili kuondoa vipengele vyenye kuashiria kuacha mwanya wa ubaguzi wa jinsia, au kuimarisha vipengele vya kukazia ufuatiliaji. Tume ya Uchaguzi, msajili wa vyama vya siasa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa na asasi za kiraia, zitoe mapendekezo ya maeneo ya kuboresha kwa kuzingatia haki za wanawake, ili Bunge La Jamhuri ya Muungano iboreshe sheria zote za uchaguzi kwa kuzingatia mrengo wa jinsia.

Wadau wakuu wote wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na Tume ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama vya siasa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Serikali za Mitaa wajenge uwezo wa kutafsiri wajibu wao kwa mtazamo wa jinsia na kujijengea stadi za kuingiza masuala ya jinsia katika mipango kazi yao.

Gharama ya uchaguzi itazamwe upya na uwezekano wa kuanzisha mfuko maalum wa kuwezesha wanawake utazamwe.

MAJUMUISHO

Page 43: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

43

Mitandao na asasi za haki za wanawake ziimarishe nguvu za pamoja za kutetea haki ya ushiriki wa wanawake katika ngazi zote za maamuzi.

Azma ya kuleta usawa wa jinsia kwa 50/50 inahitaji mbinu na mikakati bunifu kwa wadau wote watetezi wa haki za wanawake. Mbinu na mikakati endelevu sharti zilenge mabadiliko kutoka ngazi ya familia, hususani kuwezesha jamii kutambua haki za mtoto wa kike na hasara zitokanazo na mfumo wa kumbagua katika ngazi hii ya awali. Wadau wa elimu na hususani wanaotayarisha mitaala, wawezeshwe kuingiza masuala ya haki za watoto wa kike katika ngazi zote za elimu. Hii ni pamoja na mafunzo ya ualimu, ili waalimu wawe na uelewa mpana jinsi ya kumwezesha mtoto wa kike kujitambua na mtoto wa kiume kuheshimu haki za mtoto wa kike. Elimu ya uraia ihamasishe jamii yote wa Kitanzania umuhimu wa haki za wanawake na hasara za mfumo wa ubaguzi wa kijinsia, katika uchumi, ustawi wa jamii na katika kujenga Tanzania yenye msingi mathubuti ya demokrasia shirikishi na yenye kuheshimu haki za binadamu.

Page 44: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

44

Page 45: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

45

Page 46: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

46

Page 47: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha
Page 48: USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA 2015, · PDF fileza Wanawake Katika Uchaguzi ... (Diwani, Kata ya Buswelu, Ilemela, ... kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha

KUTOKA KWA WATUWA MAREKANI

Kwa kufahamu zaidi kuhusu mradi huu tembelea

Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili wa