5
HISTORIA YANGU Mimi naitwa Elimina Rajabu ni mzaliwa wa Tanga wilaya ya Korogwe kijiji cha Kwamkole kata ya Magunga Msambiazi. Ni mtoto wa nne katika familia yetu. Kuna kaka wawili na dada wawili. Nilisoma Shule ya Msingi Mlimani katika wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha. Baada ya kumaliza elimu ya msingi nilichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari ya wasichana Kondoa wilaya ya Kondoa mkoa wa Dodoma. Nilihitimu elimu ya sekondari mwaka 2002 na kufanikiwa kujiunga na chuo cha ualimu Euckenford kilichopo mkoani Tanga. Baada ya kuhitimu mafunzo ya ualimu nilipangiwa mkoa wa Kilimanjaro wilaya ya Moshi Vijijini, kijiji cha Rauya, Kata ya Marangu Mashariki, Shule ya Msingi Rauya. Nilianza kufundisha kama mwalimu tarajali kwa mwaka mmoja na kupatiwa ajira rasmi baada ya kumaliza mwaka wa mafunzo. Nimebahatika kupata watoto wawili wakiume na wakike.Mtoto wa kiume yupo darasa la pili na wa kike yupo awali. Nikiwa kazini niliomba kusoma na nikabahatika kupata kujiendeleza na stashahada ya Elimu ya kawaida ya Elimu ya Msingi kwa miaka miwili. Nilipangiwa chuo cha ualimu Marangu kilichopo Moshi

pmeelahomelibrary.files.wordpress.com · Web viewHivyo nikifika shuleni nitawafundisha walimu wenzangu katika kulitulia jedwali la kutahini kwani litawaonyesha ni nyanja zipi watapima

  • Upload
    others

  • View
    0

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: pmeelahomelibrary.files.wordpress.com · Web viewHivyo nikifika shuleni nitawafundisha walimu wenzangu katika kulitulia jedwali la kutahini kwani litawaonyesha ni nyanja zipi watapima

HISTORIA YANGUMimi naitwa Elimina Rajabu ni mzaliwa wa Tanga wilaya ya Korogwe kijiji cha Kwamkole

kata ya Magunga Msambiazi. Ni mtoto wa nne katika familia yetu. Kuna kaka wawili na dada wawili.

Nilisoma Shule ya Msingi Mlimani katika wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha. Baada ya kumaliza

elimu ya msingi nilichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari ya wasichana Kondoa wilaya ya Kondoa

mkoa wa Dodoma.

Nilihitimu elimu ya sekondari mwaka 2002 na kufanikiwa kujiunga na chuo cha ualimu

Euckenford kilichopo mkoani Tanga. Baada ya kuhitimu mafunzo ya ualimu nilipangiwa mkoa wa

Kilimanjaro wilaya ya Moshi Vijijini, kijiji cha Rauya, Kata ya Marangu Mashariki, Shule ya Msingi

Rauya. Nilianza kufundisha kama mwalimu tarajali kwa mwaka mmoja na kupatiwa ajira rasmi baada

ya kumaliza mwaka wa mafunzo.

Nimebahatika kupata watoto wawili wakiume na wakike.Mtoto wa kiume yupo darasa la pili na

wa kike yupo awali.

Nikiwa kazini niliomba kusoma na nikabahatika kupata kujiendeleza na stashahada ya Elimu ya

kawaida ya Elimu ya Msingi kwa miaka miwili. Nilipangiwa chuo cha ualimu Marangu kilichopo

Moshi Vijijini mkoa wa Kilimanjaro ambapo mpaka sasa nipo chuoni naendelea na masomo.

Maisha ya chuo ni mazuri ila palipo na mazuri hapakosi changamoto mbalimbali. Uzuri wa

maisha ya chuo ni kwamba unakutana na watu kutoka sehemu mbalimbali. Pia watu hawa huwa na

tabia tofauti tofauti zilizo nzuri na mbaya. Tabia nzuri zilizonipendeza ni kushirikiana katika masomo

tukiwa kwenye vikundi na hata ndani ya darasa. Hapa chuoni tunafanya kazi za usafi wa mazingira ya

chuo na mabweni ambapo ndipo tunapolala. Kuna mabweni ya wavulana na wasichana. Mabweni yote

Page 2: pmeelahomelibrary.files.wordpress.com · Web viewHivyo nikifika shuleni nitawafundisha walimu wenzangu katika kulitulia jedwali la kutahini kwani litawaonyesha ni nyanja zipi watapima

yanamajina, hivyo watu hukaa kwenye mabweni kulingana na jinsi walivyopangiwa. Majina ya

mabweni ya wasichana ni Ukombozi, Mapinduzi, Usalama na Jitegemee. Mabweni ya wavulana ni

Ujamaa, Mwenge, Umoja, Jamhuri, Muungano na Azimio.

Tabia ambazo sikuzipendelea katika chuo ni baadhi ya wanachuo kutoka nje ya chuo bila kuwa

na sare za chuo na pia bila kuomba ruhusa. Kitendo hiki huwafanya wanachuo wanapokutana na

mwalimu wa chuo kuwakimbia au kuwakwepa na kujifanya kama hawajamuona. Tabia hii huwauzi

sana walimu. Pia kuna wanachuo ambao hunywa pombe na kulewa na wanapokuja mabwenini

huongea ovyo. Kitendo hiki huwauzi hata wanachuo wengine. Kuna wanachuo ambao hawapendi

kufanya usafi katika maeneo waliyopangiwa. Hii hupelekea viongozi wa wanachuo kuchukia kwani

hutolea nje kwa ajili ya kufuatilia wale ambao ni wazembe katika kufanya usafi. Tunaosoma wote ni

wanachuo tuliotoka kazini, kuna wanachuo ambao wanajituma kwa kufanya kazi kwa bidii ili

kuondokana na usumbufu wa kutolewa nje ya darasa wakati wa kipindi. Wanachuo wengi kwa sasa

wanafanya kazi wanazopangiwa kwa ushirikiano na kwa kujituma.

Masomo tunayosoma hapa chuoni ni ya kiswahili isipokuwa somo la kiingereza kwa mwaka wa

kwanza tulipoanza. Katika somo la kiingereza tulijifunza literature. Jaribio la kwanza katika somo hilo

lilikuwa la kuongea kiingereza. Kwa kweli ilithihirisha ni kwa jinsi gani wanachuo walivyo waoga

katika kuongea kiingereza. Nasema hivyo nikiwa na maana kwamba wanachuo waliogopa na wengine

walipata mshituko ambao hawakuweza kuongea. Kitendo hiki kiwafurahisha walimu kwani

waligundua kuwa walimu wa shule za msingi hawajui kiingereza na kutathimini kuwa kama walimu

hawa kiingereza kinawatesa je, kufundisha watoto shuleni inakuwaje? Hivyo walibaini kuwa

kiingereza katika shule za msingi ni tatizo.

Katika masomo tunayosoma tunasoma kwa mtindo wa semista. Kusoma kwa semista ni

Page 3: pmeelahomelibrary.files.wordpress.com · Web viewHivyo nikifika shuleni nitawafundisha walimu wenzangu katika kulitulia jedwali la kutahini kwani litawaonyesha ni nyanja zipi watapima

kwamba kile ulichokisoma semista ya kwanza hutarudia kukisoma katika semista ya pili. Usomaaji huu

ni mzuri kwani hubebi mzigo mkubwa wa masomo katika semista nyingine. Pia ukifaulu mitihani

unaendelea na semista inayofuata na kama ukifeli unapewa mitihani ya marudio ili uweze kuedelea na

semista inayofuata.

Nilichofurahia katika kujifunza kwangu ni katika kujifunza jedwali la kutahini kwani nilikuwa

silijui. Kwa sasa najua kuliandaa jedwali la kutahini na ninaweza kulitumia. Hivyo nikifika shuleni

nitawafundisha walimu wenzangu katika kulitulia jedwali la kutahini kwani litawaonyesha ni nyanja

zipi watapima na idadi ya maswali

Nimatarajio yangu nitasoma kwa bidii ili niweze kufaulu vizuri na kutumia elimu niliyoipata

katika tendo la ufundishaji na ujifunzaji niwapo shuleni. Pia kuwasaidia walimu wenzangu pale

wanapohitaji msaada wa namna ya ufundishaji.