26
yaweza kusonga kwenye Soka ZANZIBAR Bakhressa apania uwekezaji Zanzibar ZANZIBAR DAIMA ONLINE JARIDA LA KILA MZANZIBARI www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013 ZANZIBAR DAIMA ONLINE Septemba /Oktoba 2013

Zanzibar Daima Online Na. 04

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Zanzibar Daima Online Na. 04

yaweza kusonga kwenye Soka

ZANZIBAR

Bakhressaapaniauwekezaji

Zanzibar

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N ESeptemba /Oktoba 2013

Page 2: Zanzibar Daima Online Na. 04

PAGE

2

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

3

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

2

Yaliyomo

16 18 22

1206

SAID SALIM BAKHRESSABilionea wa Kizanzibari anayeurejesha utajiri kwao

TINDIKALI ZANZIBAR

NCHI IMEKALIA BOMUUtitiri wa vijana wasio ajira waongezeka

WARAKA KUTOKA BONNUmuhali watuumiza Wazanzibari

HATUJAACHA KUSEMAMabunge mawili ya Muungano

Graphics

Designer

(Hassan)www.zanzibarimage.com

HKDesigner

MHARIRI MKUUAhmed Rajab

Email: [email protected]

MHARIRI MSAIDIZIMohammed Ghassani

Email: [email protected]

MHARIRI MSANIFUHassan M Khamis

Email: [email protected]

COMMUNICATION MANAGERHassan M Khamis

WAANDISHIJabir Idrissa

Email: [email protected]

Othman MirajiEmail: [email protected]

Hamza RijalEmail: [email protected]

Salim Said SalimEmail: [email protected]

Ally SalehEmail: [email protected]

WASAMBAZAJImzalendo.net

zanzibardaima.netzanzibardaima/facebook

MATANGAZOHassan M Khamis

Simu: +44 7588550153Email: [email protected]

WASIALIANA [email protected]

JARIDA HILI HUCHAPISHWA NAZanzibar Daima Collective

233 Convent WaySouthallUB2 5UH

Nonnstr. 2553119 Bonn

Germany

www.zanzibardaima.net

Zanzibar Daima Online

Timu Yetu

Zanzibar Daima Online Toleo 04 03

28 38 42Inafaa na ni muhimu matamshi ya Kamishna Mussa yafafanuliwe na yaelezewe katika usuli mwema la sivyo yanaweza kuwa na hasa-ra kubwa kwa Zanzibar, kwa sisi wenyewe kujiimbia nyimbo mbaya kuwa kumbe Al-Shabaab wamewe-za kufika Zanzibar

Mkristo akifa Zanzibar, Waislamu wanahudhuria mazikoni, na vivyo afapo Mwislamu. Wakristo wangapi Zanzibar wamekufa mikononi mwa Waislamu na Waislamu wakasi-mamia maziko yao kanisani mpaka wanashushwa makaburini

Haji Gora Haji ni mtu wa kisiwa cha Tumbatu, kaskazini magharibi karibu na Unguja. Tumbatu ina magofu ambayo, pamoja na Unguja Ukuu, ni ya zamani kuliko popote pengine huko Zanzibar,

Page 3: Zanzibar Daima Online Na. 04

Hamna shaka yoy-ote kwamba walio-washambulia watu

Unguja kwa kuwamwagia tindikali kwa kipindi cha karibu mwaka sasa wame-fanikiwa. Hawakufanikiwa kwa moja. Wamefanikiwa kwa mawili. Kwanza, kwa kuwadhuru waliowalenga.[Angalia Uk. 12] Pili, kwa kuidhuru Zanzibar.

Washambulizi hao wa-meidhuru Zanzibar kwa sababu hawakuwamwagia tindikali waliowalenga tu bali pia wameimwagia tin-dikali Zanzibar yetu. Waki-taka, wasitake hiyo ndiyo athari walioiacha baada ya kuwamwagia tindikali hao waliowamwagia. Ndio maana tukaiona sura ya Zanzibar mbele ya ulimwen-gu ghafla imebadilika.

Mashambulizi hayo ya-meifanya Zanzibar isawijike. Wajihi wake unachusha. Umejaa majaraha na mak-ovu. Umefujika, umecha-fuka, umevurugika. Hau-tamaniki tena. Kwa hakika, unatisha khasa.

Hivyo ndivyo baadhi ya walimwengu wanavyoiona Zanzibar siku hizi. Kuna wenye kuiogopa, hawataki

tena kuja kututembelea. Ingawa watalii bado wangali wakiendelea kuvizuru visiwa vyetu kwa mkururo, sekta ya utalii imepata mtikisiko kidogo kwa sababu kuna baadhi ya watalii kutoka nje ya Bara la Afrika waliovunja safari zao za kuja Zanzibar baada ya matukio ya kari-buni ya mashambulizi ya tindikali.

Pengine hiyo ndiyo iliyoku-wa dhamiri ya washam-bulizi; kuukata miguu utalii visiwani mwetu. Na tukiyas-ema haya tusieleweke viba-ya, kwamba labda tunazililia pesa mbili tatu zinazotu-tiririkia kutoka sekta hiyo. Tunachokililia ni kupoteza sharafu yetu na sifa yetu ya jadi ya kuwa watu wavumil-ivu, wapenda amani na we-nye kuheshimu dini na imani za wengine. Tunachokililia ni jinsi mashambulizi hayo yalivyotumiwa kuuchafua na kuutia madoa Uislamu pamoja na ustaarabu wetu.

Ni wazi kwamba serikali imeshindwa kufanya kam-peni yoyote ile ya kuwaam-sha watu kuhusu madhara ya mashambulizi kama haya kwa uchumi wetu na kwa jamii kwa jumla. Kwa hivyo, Zanzibar Daima Online ime-

jitwika dhima ya kuanzisha kampeni ya kutanabahisha-na Wazanzibari sote kuhusu madhara ya kujihujumu wenyewe kwa mashambu-lizi yasioingia akilini. Ni matumaini yetu kwamba asasi za kiraia, vyombo vya habari vya Serikali na vina-vyomilikiwa binafsi, walimu maskulini na katika ma-drasa, wazee majumbani, mashekhe misikitini, vijana katika baraza zao, duru zao na vikao vyao pamoja na wadau wengine wataziunga

mkono juhudi za kuzinduana kuhusu uovu huu. Kaulimbiu yetu ni nyepesi: Tusiimwagie tindikali Zanzibar.

Vyombo vya habari vina dhamana ya kuwae-limisha wananchi kuhusu madhara na hasara inayopata nchi yetu kutokana na masham-bulizi kama haya. Vinapaswa pia kuwashini-kiza viongozi wetu wachukue hatua zinazo-hitajika kuzuia pasizuke tena mashambulizi kama haya katika jamii yetu. Jengine ambalo vyombo vya habari vinaweza kufanya ni kuihimiza Serikali ifanye kampeni yake ya kulisafisha jina jema la Zanzibar.

Sambamba na kampeni hii tunatoa wito kwetu sote katika jamii tuwe macho ku-waangalia wote wale ambao kwa vitendo vyao wataifanya Zanzibar iwe na jina baya.Hili si jukumu la mtu mmoja, la kikundi ki-moja, wala la chama kimoja. Hili ni jukumu letu sote. Lazima tuhakikishe kwamba juu ya mata-tizo yote tuliyo nayo tunaendesha shughuli zetu na harakati zetu zote kwa njia za amani. Lazima tuhakikishe kwamba tunaishi katika mazingira ya usalama na utulivu. Lazima tuhakikishe kwamba tunaujenga Umoja wetu na Mshikamano wetu juu ya misingi ya amani.

Usiimwagie tindikali ZanzibarNa Ahmed Rajab

TAHRIRI

PAGE

4

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

5

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

4

Page 4: Zanzibar Daima Online Na. 04

Jarida la kibiashara linalo-heshimika duniani, Forbes, linamtaja kama tajiri mkub-

wa kabisa wa Tanzania na kumuweka kwenye nafasi ya 30 kati ya matajiri wakubwa kabisa barani Afrika. Mtandao mashuhuri wa Wikipedia un-amtaja kama tajiri aliyekwea ngazi mwenyewe kuelekea kilele cha mafanikio.

Jina lake ni Said Salim Awadh Bakhressa, Mzanzibari ali-yezaliwa mwaka 1949 na aliyejipatia sifa kama ‘mwa-naviwanda’ katika eneo hili.

Miongoni mwa kampuni zilizomo kwenye mtandao wake ni Azam Marine na Kili-manjaro Fast Ferries za usafiri wa majini, ambayo meneja wake, Hussein Mohamed Said, anasema haijafikia ki-wango hasa cha mafanikio inachotaka kukiona katika hu-duma za usafirishaji abiria na mizigo kwa njia ya baharini.

“Tunakusudia kuweka nguvu Pemba na Tanga. Unajua kule Mkoani (Pemba), Ban-darini vyombo vinafunga gati kwenye ukuta badala ya gati nzuri. Tunataka tufunge gati kama tunavyofunga hapa Dar es Salaam na kama tunavyo-funga pale nyumbani Zanzi-bar,” anasema.

Hussein maarufu kwa jina la Meneja Hussein, anasema Azam Marine pamoja na Kili-manjaro Fast Ferries, wame-

kusudia kubadilisha sura nzima ya usafirishaji abiria kwa njia ya bahari kutokea Zanzibar hadi Dar es Salaam na Zanzibar hadi Tanga kupi-tia Pemba.

Baada ya kutokuonekana akielekeza nguvu za uwekez-aji kwenye ardhi ya kwao, kwa siku za karibuni, Bakhressa ameshuhudiwa akifanya mengi visiwani Zanzibar yanayoashiria dhamira hiyo.

Katika kufanikisha dhamira yao hiyo, Meneja Hussein anasema: “Hatufanyi biashara leo kwa ajili ya leo. Hapana. Biashara hii ukiingia un-abaki huko mpaka ufe na kile unachopata kama faida kina-rudi kuimarisha miundombinu na maslahi ya wafanyakazi waliochangia mafanikio.”

Ndani ya kauli yake hiyo, ana-onesha upande wa Bandari ya Dar es Salaam, pembeni mwa ofisi kuu za kampuni hiyo am-bako mahojiano na mwandi-shi wa Zanzibar Daima Online yalifanyika.

Meneja Hussein anaulizwa sababu za uwekezaji mkubwa kufanywa kipindi hichi. “Tuli-kusudia muda mrefu kuweke-za, lakini vikwazo vilikuwa vingi.”

Anakumbusha maneno ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mo-hamed Shein ambaye alipoz-indua eneo jipya na la kisasa

la abiria kwenye Bandari ya mjini Zanzibar miezi miwili iliyopita, alisema pale anapo-tokea mwekezaji akataka kuwekeza fedha zake asisum-buliwe, asaidiwe.

Wengine wanadhani, ukimya wa Bakhressa visiwani Zan-zibar ulimaanisha hakuwa akifanya kitu kikubwa, ingawa inakumbukwa kwamba siku zote amekuwa mstari wa mbele, lakini chini kwa chini, kusaidia hapa na pale.Yumkini kwa sababu ya ku-tokupendelea kwake kujitoke-za binafsi kwenye vyombo vya habari, ndio maana si mengi sana yanayojuilikana kuhusu jitihada hizo na hata za maisha binafsi ya Said Bakhressa.Lakini mtandao maarufu wa Wikipedia unasema Bakhressa alilazimika kua-cha masomo akiwa na umri wa miaka 14 tu, alipojiingiza kwenye biashara ya kuuza urojo, chakula maarufu kina-chouzwa visiwani Zanzibar nyakati za jioni na sasa un-amtaja kuwa kigezo cha watu waliokwea ngazi za mafanikio ya kiuchumi kwa jitihada zake mwenyewe.Biashara yake ya kuuza chakula katika mitaa ya Dar es Salaam katika miaka ya 1970, ilikuja ikamuibua kuwa mmiliki wa himaya kubwa ya biashara ndani ya miongo mi-tatu baada ya hapo. Himaya yake imejichawanya kuanzia

HABARI KUU

Na Jabir Idrissa

SAID SALIM BAKHRESSA

PAGE

6

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

7

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

6

Sasa Bakhressa aijenga Zanzibar

Page 5: Zanzibar Daima Online Na. 04

kwenye vyakula na vinywaji hadi usafiri wa baharini na viwanda vya kusindikia nafaka na maziwa, na hivi karibuni mradi mkubwa wa vyombo vya habari, akianzia na televisheni ya Azam TV. Timu machachari ya mpira wa miguu nchini Tanzania, Azam FC, inamilikiwa na makampuni haya.Dk. Shein anayesemekana kuongoza mwenyewe msu-kumo wa Serikali katika ku-fanikisha dhamira ya Azam Marine ya kuwekeza eneo hilo, alisema ameshangazwa na mitizamo dhaifu ya wa-tendaji wa taasisi za kusaidia wawekezaji kutumia fursa za kuwekeza.

“Mtu anakuja na pesa zake, anataka kuwekeza eneo fulani, mnamsumbua weee mpaka anachoka anaondoka. Hatuwezi kwenda namna hiyo mjuwe mwenye pesa ana sehemu nyingi za ku-tumia pesa zake. Badilikeni viongozi nyie. Muwe wepesi wa kumsaidia mtu kama huyu bila ya kukiuka tara-tibu,” Dk. Shein alisema.

Tunaambiwa kumbe Azam Marine walikuwa na ma-jadiliano siku nyingi na Seri-kali ya Mapinduzi Zanzibar yaliyohusu kuruhusiwa ku-jenga eneo la kisasa la abiria bandarini lakini woga na urasimu uliwakwamisha.

“Tulikuwa na ndoto hii zamani. Tukafanya ma-zungumzo mara nyingi na viongozi wa serikali lakini kila tulipomaliza hatuku-ona maendeleo ya mambo

tuliyokubaliana. Tukaamua kuacha lakini tukiumia sana kwa sababu kila mtu anajua hali ya bandarini ilivyokuwa mbaya,” anasema Meneja Hussein.

Bila ya kuficha, anakiri hali hiyo ilitokea wakati wa Serikali ya Awamu ya Sita (SAS), chini ya Amani Abeid Karume.

“Rais hakuwa tatizo. Tatizo ilikuwa watendaji wizarani na kule Bandari. Unakuta wanaogopa hata kufanya majadiliano. Tunashukuru safari hii tumepata ushirikia-no mzuri ndio maana unaona kazi imefanyika. Wamebadi-lika kama alivyowahimiza Dk. Shein.”

Anakiri hakukuwa na zabuni lakini anahoji kwani kuna

mtu alikwenda kuomba ku-wekeza akakataliwa? “Sisi ndio tulipata wazo baada ya kuona hali inavyo-zidi kuwa mbaya. Tukaenda serikalini kujieleza. Tukataka ruhusa hatimaye tukasaidi-wa kutekeleza azma yetu.”

Kupitia uwekezaji wa Azam Marine na Kilimanjaro Fast Ferries, kumejengwa eneo la kisasa la abiria banda-rini Zanzibar ambako watu wapatao 600 wanakaa wakati wakisubiri kusafiri.

Meneja Hussein hapendi kutaja kwa uhakika thamani ya uwekezaji huo. “Tumetu-mia kama shilingi bilioni mbili hivi.” Kwa upande wa eneo la abiria bandarini Dar es Sa-laam, ametaja gharama nusu ya hizo.

Anasema wamewekeza pia kwa sababu wamegundua nini abiria wanakitaka. Abiria wanataka kusafiri kwa raha. Wanataka kuona mandhari wakiwa ndani ya boti, wen-gine wakiwa nje wamekaa, mbele au nyuma ya chombo.

“Ndio maana tunatengene-zesha boti kwa kuzingatia mahitaji hayo ya wasafiri. Tunamwita mchoraji na ku-muelekeza chombo kiwe vipi. Wapi pakae viti vya abiria, vingapi; wapi pakae vyoo, vyoo viwe vya kubonyeza au kuvuta.

“Designer wetu kutoka Aus-tralia alikuja tukampeleka mpaka Pemba na Tanga ku-ona mwenyewe. Ameangalia ukubwa wa bahari, nguvu za mawimbi. Wapi makubwa,

wapi madogo. Anatafiti namna ya kujenga chombo kitakachokuwa salama. Hapo inakuwa kazi rahisi kutu-jengea chombo kinachofaa mazingira ya watu wetu,” anasema.

Meneja Hussein anatoa kisa cha mama ambaye licha ya kulipa tiketi za daraja la juu, amekataa kukaa panapohi-tajika. Aliamua kukaa chini, watoto wake wakakaa nje wapunge upepo. Pale kwe-nye viti vya VIP ameweka tu mabegi yake, yeye amekaa apendako.

Anachoeleza hapa, abiria wengi wanapenda kukaa nje zaidi kuliko ndani ya boti wakati wa safari. Hata watalii, hawapendi kukaa ndani ya boti. Wanataka ku-ona kila kitu kizuri kwa karibu

huku wakipiga picha.

“Haya yametusu-kuma kubuni mfumo mpya wa kupata vyombo vya kisasa. Ni tofauti na ilivyo kwa wenzetu. Kwe-tu ni joto si baridi kama Ulaya,” anas-ema Meneja Hus-sein kuhusu nini hasa kinavutia wao kupata vyombo vya kisasa.

Alipoulizwa ni kwa nini wanadhani muhimu kujua ma-hitaji ya watu wa-naosafiri, anasema “Kwanza tumeamua kumvuta mtu aje kutumia usafiri huu kwenda Zanzibar, Pemba na baadaye

Tanga. Tunataka ile picha hal-isi ya nchi yetu aipate kupitia safari yake. Lazima umpum-baze mtu kwa kumuonesha kizuri unachoweza kumpa-tia. Zamani ilikuwa vigumu. Hatukufanikiwa kuwavuta watu.”

Meneja Hussein anasema leo, wasafiri wengi wa Zan-zibar kutokea Dar es Salaam wanatumia boti. Hata alipo-banwa kufafanua kwa vile kwa boti mtu anatumia muda zaidi kuliko ndege, anasema:

“Tupo katikati ya jiji. Mtu akifika akiwahi chombo cha muda huo anaondoka. Hii ni kitu cha dakika 15. Akitumia saa mbili baharini anaona mambo mengi, anapata ku-ona mandhari, anaiona nchi kutoka baharini.

“Sasa inachukua saa moja na zaidi kufika Airport. Tena unatakiwa kuripoti saa mbili kabla ya muda wa kusafiri. Ukifika uwanja wa ndege Zanzibar, utafute gari ya kukupeleka mjini. Huku uki-shuka tu boti, upo mjini. Hii ndiyo tafauti kubwa ya safari hii moja kwa njia mbili.”

Anasema kwa baharini, abiria ana uchaguzi saa moja asu-buhi, saa 3.30 asubuhi. Saa 6 mpaka 7 mchana. Na chom-bo cha mwisho ni saa 9.45. Chombo kikiondoka, una saa mbili umefika uendako. Hii ndiyo njia nzuri kabisa kwa anayetaka kwenda Zanzibar na Pemba.

“Asiyejua utamu wa kwenda Zanzibar kwa boti, aulize wageni na watalii. Wao

Afisi ya Uhamiaji bandarini Zanzibar, seheme ya jengo jipya lilojengwa na Said Bakhressa

PAGE

8

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

9

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

8

HABARI KUU

Page 6: Zanzibar Daima Online Na. 04

wakisafiri hawatulii, kila dakika wanapiga picha. Wanaona mambo ya ajabu baharini kwa karibu na kwa mbali kutokea kwenye boti.

“Hiyo tisa, waangalie boti inapokaribia kufika Zanzibar. Wana-ona mambo kwa karibu zaidi basi kila mmoja anashughulika kupiga picha. Na hizi ndio raha wanazozitaka ambazo kwao haziko.”

Meneja Hussein anasema ushindani hauwasumbui kwa sa-babu wao wanatoa huduma zinazomvutia kila mtu.”Ushindani upo lakini sisi tunajua abiria wanachokitaka. Tuna vyombo vizuri vya kisasa.

, lakini si kampuni pekee kwenye mtandao wa makampuni unaomilikiwa na mfanyabiashara huyu wa Kizanzibari, Said Bakhressa, ambaye kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia, yeye mwenyewe ndiye kiini cha mafanikio yote hayo ya makampuni yake, kupitia dira yake na stadi zake binafsi za ujasiriamali na usimamizi wa mi-radi anayoianzisha.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes la mwaka 2012, utajiri wa Bakhressa ni sawa na dola milioni 520 na yumo kwenye oro-dha ya matajiri wakubwa kabisa 40 barani Afrika. Nchi jirani ya Tanzania, kama vile Rwanda, zinategemea unga unaozalishwa na viwanda vya Bakhressa ambapo hupokea tani 120,000 za unga wa ngano na mahindi kwa mwaka, kiwango kinachopun-guza makali ya kupanda bei za vyakula kwenye nchi ambayo asimilia 52 ya familia zake hazina uhakika wa kupata chakula chao. Kwa mujibu wa Mkakati wa Usaidizi wa Nchi uliobuniwa na Benki ya Dunia, hili ni jambo lenye manufaa sana. Vile vile, miradi ya Bakhressa nchini Rwanda inatarajiwa kuunda nafasi za ajira na kusaidia mapato ya nchi hiyo yatokanayo na kodi ya makampuni.Nchini Tanzania, Bara na Zanzibar, makampuni ya Bakhressa yameajiri watu wapatao 2,000 na yanatajwa kuwa makam-puni makubwa kabisa kumilikiwa na kuendeshwa na mzawa kwa asilimia 100. Jina lake la Azam ni alama ya mtengenezaji mkubwa wa chokoleti na malai nchini Tanzania.

Kampuni yake ya vinywaji, zikiwemo sharubati, soda na maji, ina uwezo wa kuzalisha tani za ujazo 2,100 kwa siku na mwaka 2011 iliuza bidhaa zenye thamani ya dola milioni 800. Kitengo chake cha usafiri wa majini, Azam Marine, kinatoa usafiri wa hadhi ya kitalii ndani ya Tanzania. Nje ya miradi ya kibiashara, Bakhressa anajihusisha na miradi ya kijamii kama vile mradi wa kupunguza athari za ugonjwa wa malaria kwa wafanyakazi wake na kuzuwia kusambaa kwa maradhi kwenye maeneo yake ya kazi. Matokeo yake, kampuni yake hutumia dola 3400 tu kwa mwezi kwa ajili ya matibabu ya malaria kinyume na dola 10,000 za kuwatibu waajiriwa wake wanaouguwa. Wafanyakazi wake waliacha kutumia madawa aina ya Fansi-dar na kutumia madawa mchanganyiko, ambapo makampuni mengine nchini Tanzania yanatajwa kuungana na Bakhressa Group katika kampeni ya kupambana na malaria kwenye eneo la Afrika ya Mashariki na Kati. Hata wakaazi wengine nchini Tanzania wanaofanya kazi nje ya kampuni za Bakhressa wa-nafaidika na vita vya kupambana na malaria vya kampuni hiyo barani Afrika.

BOTI MV KILIMANJARO INAYOSAFIRI BAINA YA DAR ES SALAAM, UNGUJA NA PEMBA

PAGE

10

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

11

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

10

HABARI KUU

Page 7: Zanzibar Daima Online Na. 04

Zanzibar ‘inapomwagiwa’ tindikali

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akimpa pole Sheha wa Shehia ya Tomondo, Unguja, Mohamed Omar Said (Ki-devu), aliyeshambuliwa wa tindikali na watu wasiojuilikana mwezi Mei 2013

NGURUMO LA MKAMANDUME

Na Mohammed Ghassani

Mtazamo wangu ni kwamba kuendelea kwa mashambulizi kama haya ni kiele-lezo cha uwezo mdogo wa jeshi la polisi kiintelijensia na kitaalamu, kwani licha ya kuwa ni la Muungano, Zanzibar jeshi hili limezoea kutumikia siasa tu.

Mtazamo ni neno dogo la-kini kubwa. Udogo wake umo kwenye wepesi katika ma-zungumzo ya kawaida. Kwa mfano, unapohitalifiana na mwenzio huwa mwepesi wa kusema: “Lakini huo ni mtaza-mo wako tu. Mimi sijakusudia hivyo!” Nalo likabaki kuwa

hivyo – mtazamo sio ukweli wa mambo.

Ukubwa wake upo kwenye uhalisia, kwani mtazamo ni namna unavyolitazama jam-bo kwa jicho la ndani na sio la nje tu. Waswahili waliposema “jicho si mboni” walipatia kwa

mengi, kwani namna unavyo-litazama jambo kuna maana kubwa kwa mwelekeo wa ku-liendeleza jambo hilo na hati-maye matokeo yake.

Tafsiri yako ya mtazamo hu-zaa tabia zako, matendo yako na hata maelezo yako juu ya

jambo hilo. Kwa ujumla, nam-na unavyolitazama jambo kwa jicho la ndani, ndivyo pia unavyolipokea kwa mikono ya ndani.

La mashambulizi ya tindikali visiwani Zanzibar nalo lin-aangukia kwenye mitazamo kwa: ikiwa si kwa wayafanyao na wafanyiwao, basi angalau kwetu sisi tuyatafsiriyo. Ndio maana ndani yake kuna mi-tazamo mingi tafauti kutoka kwa watu wengi tafauti.

Kundi moja la watu linay-atazama mashambulizi haya kwa mtazamo wa kidini. Ni-taliita “tindidini”. Hawa wa-nasema mashambulizi haya yanafanywa na Waislamu wa Kizanzibari wenye chuki dhidi ya dini nyengine, hasa Ukristo.

Kanisa, vyombo vya habari vya ndani na nje na, kwa hakika, hata vyombo vya dola vime-kokotwa na mtazamo huu.

Kwa sababu ya mtazamo huo, hivi sasa polisi ya Zanzibar imetoa ile ninayoiita “kadi ya mwaliko” kwa kundi la kigaidi la al-Shabaab, kupitia kauli ya Kamanda Mussa Ali kwamba eti miongoni mwa walioka-matwa mwishoni mwa wiki wakiwa na tindikali, wamo waliosema walikuwa njiani kwenda Somalia kuwasaidia al-Shabaab.

Tindikali haijawahi kuwa mbinu ya makundi ya kigaidi kokote duniani. Kimsingi wa-pambanaji wao wanaamini juu ya kupambana kwa kujitoa mhanga, yaani kuitumia miili yao kama silaha kuwadhuru wengine. Lakini kusema haya hakuondoshi ukweli kwamba

mwelekeo, tabia, matendo na maelezo ya kundi hili la “wa-natindidini” yamo ndani ya duara hilo la dini.

Kuna mtazamo mwengine un-aosema kwamba mashambu-lizi haya ni uhalifu wa kawaida unaotokana na visasi vya ama kitaasisi, unyumba na au bi-ashara. Kwao ni sadfa tu kuwa miongoni mwa waliolengwa ni viongozi wa kidini, Sheikh Suleiman Soraga na Padri An-selm Mwang’amba.

Ndio maana huko nyuma ku-likuwa pia na Mkurugenzi wa Manispaa, ambaye si kiongozi wa dini. Ndio maana kuna pia wasichana wadogo wa Kiin-gereza, ambao hawakuwapo Zanzibar kwa sababu za kidini. Wenye mtazamo huu huse-ma hata viongozi wa Kikristo waliokumbwa na masham-bulizi haya na mengine ni Wakatoliki tu. Mwelekeo, ta-bia na maelezo ya kundi hili yamo kwenye duara la kwam-ba hii ni “kazi ya ndani”.

Mtazamo wa tatu ni wa hu-juma dhidi ya Zanzibar. Huu una mbeya mbili – kisiasa na kiuchumi. Kisiasa, wanasema inayolengwa hapa ni, kwanza, Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na pili ni ajenda ya Zanzibar kuelekea mamlaka kamili.

Kwa kuwa kwa mara ya kwan-za Wazanzibari wameweza kupaza sauti zao kudai nafasi kubwa ndani ya Muungano, jambo ambalo linaonekana “kuwezeshwa” na mfumo wa serikali uliopo, basi njama zi-nafanyika kuikwamisha seri-kali na, hivyo, hatimaye kui-kwamisha ajenda hiyo.

Kiuchumi, “wanahujuma”, wanasema unaokusudiwa kuhujumiwa hapa ni utalii, ambao ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Zanzibar. Wa-geni hawatavutiwa na pahala ambapo mashambulizi kama haya yanafanyika. Sekta ya utalii itaporomoka na serikali itashindwa kupokea mapato yatokayo nao.

Wazanzibari wenzangu wen-gi wanaamini nadharia hii ya “hujuma”. Kwa jicho la ndani ndivyo wayaonavyo masham-bulizi haya na kwa mikono ya ndani ndivyo wayapokeavyo. Mwelekeo, tabia na maelezo yao yamo ndani ya duara hilo la hujuma.

Lakini mimi nataka nitafau-tiane nao juu ya nani anatuhu-jumu. Nayatazama matukio haya kupitia jicho la uweze-kano wa visasi au uhalifu mwengine na sio hujuma kwa nchi wala serikali yetu ya Umoja wa Kitaifa. Naamini kila tukio linajitegemea.

Mashambulizi ya tindikali Zanzibar si mageni. Yaliku-wapo hata kabla ya kuundwa serikali hii ya sasa. Nakum-buka mikasa ya huko nyuma iliyoambatana na ‘siasa’ za kuripuliwa mabomu ya petroli kwenye taasisi za umma au nyumba za mawaziri kila uki-karibia au ukimalizika ucha-guzi. Lakini mengi ya mabomu hayo yaliishia kuharibu ma-banda ya kuku au milango tu.

Na hata uchunguzi ulipo-fanywa na wataalamu kutoka Bara, uliishia kwenye ripoti zilizofichwa hadi leo, pengine kwa kuwa vidole vya usha-hidi vilielekea kule ambako

PAGE

12

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

13

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

12

Page 8: Zanzibar Daima Online Na. 04

NGURUMO LA MKAMANDUME

‘wakubwa’ wasingelitaka vielekee, au kwa kuwa haukuwa uchunguzi jambo.

Mtazamo wangu ni kwamba kuendelea kwa mashambulizi kama haya ni kiele-lezo cha uwezo mdogo wa jeshi la polisi kiintelijensia na kitaalamu, kwani licha ya kuwa ni la Muungano, Zanzibar jeshi hili limezoea kutumikia siasa tu.

Mtazamo wangu ni kwamba tunajihuju-mu wenyewe kwa kuwa na jeshi la polisi lenye kiwango tulichonacho.

Wala pasisemwe kwamba hii ni taasisi ya Muungano na sisi hatuna dhima yetu katika, kwa mfano, askari wangapi na wenye uwezo gani wawepo Zanzibar. Tunayo dhima hiyo.

Ni sisi tunaopeleka majina ya nani na nani waingie Chuo cha Polisi Moshi. Asil-imia kubwa ya hao hurudi kufanya kazi

nyumbani. Lakini ni nani hao tunaowapeleka Moshi na wana sifa gani kielimu?

Taaluma ya kompyuta inatufundisha kanuni ya GIGO - yaani Garbage In, Gar-bage Out. Tukipanda michongoma, tuta-vuna chongoma. Askari polisi waliopata kazi kwa mirengo yao ya kisiasa wana-jua tu kutumikia mirengo hiyo na siyo taaluma ya upolisi.

Hawa hawataweza kuwalinda wenyeji na wageni na mali zao. Wataweza tu kuulinda mfumo wa kisiasa uliowapa ajira zao.

Hata hivyo, ukweli ni kwamba katika mashambulizi haya ni Zanzibar inayo-mwagiwa tindikali. Ni Zanzibar inayo-tendewa uhalifu huu kama nchi na kama taifa.

Nalaani vikali kitendo cha kumwagiwa tindikali kwa Padri Joseph Mwang’amba kilichotokea mchana wa siku ya Ijumaa

ya tarehe 13 Septemba 2013 huko Mlandege, Zanzibar. Kwa kweli ni kitendo cha kinyama kisichoendana na mila na desturi zetu za Ki-zanzibari zinazofuata misingi na mafundisho ya dini yetu ya Kiislam na ni kitendo cha uvunjifu wa haki yake ya kuishi kwa salama na amani bila bughudha yoyote.

Kuna mengi ya kujadiliana juu ya masuala kama haya yenye kuhatarisha mustakbali wa amani yetu na maisha yetu kwa ujumla. Nakubaliana na baadhi ya wenzangu wenye mtazamo wa kuwa wengi wa polisi wetu inavyoonekana huwa wanasainiwa na ku-pelekwa masomoni bila ya kuangaliwa ama kupimwa viwango vyao vya kielimu, bali kwa kujuana ama kwa ushawishi wa kisiasa. Hivyo utendaji wao wa kazi tunauona kuwa si wa kuridhisha kabisa kila siku zikienda.

Tuje kwenye hili tatizo la kumwagiwa tindikali. Ni lazima tuangalie kila aina za uwezekano juu ya tatizo hili, kwanini limekuwa linatokea mara kwa mara hususan siku za hivi karibuni huko nyumbani Zanzibar?

Wako watakaoshuku kuwa inawezekana ikawa ni hujuma dhidi ya Wazanzibari wa-onekane ni watu wenye ubaguzi wa kidini hasa katika kipindi hichi cha kudai mamlaka kamili ya Zanzibar, ili wasipate kuungwa mkono na mataifa ya Magharibi juu ya lengo lao hilo.

Inawezekana ni mipango ya kundi la watu fu-lani wenye malengo fulani tusiyoyatambuwa

ambao wanatutumia ujumbe, lakini tunash-indwa kuufahamu. Inawezekana ni wahalifu waliozoeleka wakiwa kwenye shughuli zao za kihalifu. Inawezekana ni watu wanaojuana wenye visasi vya siku nyingi, wanalipiziana.

La kufanya ni kuliimarisha jeshi letu la polisi kwa kulipatia vitendea kazi vya kisasa na mafunzo imara na ya mara kwa mara kwenye utaalamu wa kisasa wa kisayansi na kiinteli-jensia ili kuweza kufanya kazi zao vyema.

Vile vile, kuhimiza ushirikiano mzuri ulio wa kuaminiana na usio na vitisho baina ya polisi na raia wa kawaida katika jamii yetu. Jeshi la polisi nalo liache upendeleo wa kutumikia chama tawala na badala yake lifanye kazi zake bila upendeleo kwa kuzingatia haki na usawa ndani ya jamii ili wananchi warejeshe imani kwa jeshi hilo na wawe tayari kushiriki-ana nalo katika kuzuia vitendo vya kihalifu na pia kuwafichua wahalifu wanapofanya viten-do vya kihalifu.

Kwa kweli tukiweza kufanya hayo, basi tut-aweza kupiga hatua nzuri na za kuridhisha sio kama ilivyo hivi sasa kwani jeshi letu la polisi limekosa imani ya wananchi na hivi sasa linaonekana halifanyi kazi zake kwa ufanisi wa kutosha na kuridhisha kwani vitendo vya kihalifu na kinyama kama kumwagiana tindi kali vinazidi kuongezeka na watenda uhalifu huo wamekuwa wagumu kupatikana na ku-fikishwa kwenye vyombo vya sheria. Lazima tutafakari ama sivyo tutaishia pabaya.

Mimi,Haji Jingo

WASEMAVYO WANAFACEBOOK

Padri Anselm Mwang’amba wa Kanisa Katoliki Zanzibar alishambuliwa kwa tin-dikali na watu wasiojulikana wiki iliyopita Mjini Unguja.

PAGE

14

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

15

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

14

Page 9: Zanzibar Daima Online Na. 04

Nchi yetu imekalia bomuWARAKA MAALUM

Na Mustafa Sharif

Vijana wa nchi hii kama vijana wengine kwen-gineko duniani wame-

kuwa wakipuuzwa na kuim-biwa nyimbo ambayo sasa wameshaanza kuchoka kuisikia.

Kila nikikaa na kutafakari na-ona vijana wengi miongoni mwetu huchoshwa na hali ya kutokuwa na ajira au njia za kuweza kujipatia kipato na kuendeleza maisha yao na familia zao.

Kubwa linalonitisha mimi ni hili suala la kuona utitiri wa vijana ambao hawana ajira wakiwa wamezagaa mitaani bila ya kuwa na la kufanya wala mwelekeo mahsusi wa maisha yao ya sasa na baa-daye.

Hali si shuwari kiasi cha kwamba tukiacha wale am-bao walikosa au walikataa fursa ya kujitafutia elimu na hivyo kukosa vigezo vya ku-weza kuajiriwa imefika hadi wale ambao wameweza ku-soma na kufikia viwango vya juu vya elimu nao huwawia vigumu kuweza kupata ajira hata katika zile fani ambazo wana utaalamu nazo.

Bila ya shaka ni kweli kwam-ba kwa sasa hali ya kiuchumi ni duni nchini kwetu na seri-kali yetu haiwezi kumua-jiri kila kijana ambaye yuko tayari kupatiwa ajira, lakini kuna mengi mengine am-bayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kukuza tatizo hili la ukosefu wa ajira.

Msemo wa kiingereza wa “it does not matter who you know but what you know” kwa maana ya kwamba haijali-shi nani unayemjua bali nini unachokijua umegeuzwa

sasa na imekuwa “it does not matter what you know but who you know” yaani haijali-shi unachokijua bali nani un-ayemjua kwani fursa za ajira zimekuwa zikitolewa kwa kujuana tu, watu wanapeana kazi kimjomba mjomba na hizo kazi zenyewe zinafany-wa kimjomba mjomba. Wale wenye utaalamu na wa-naostahiki kupewa hizi na-fasi hakuna anayewauliza au hata wakiulizwa kitu kidogo nacho kitembee.

Serikali na jamii kwa ujumla

zimekuwa zikilaumiwa kwa kutofanya juhudi za maksudi za kutoa fursa ambazo zi-naweza kuwapatia vijana wengi ajira na kuwaondoa mtaani ili wasije wakaleta majanga kwao na kwa taifa kwa jumla.

Elimu yetu iitwayo ya bure ni bure kwa maana haina thamani na sio tu kwamba haipatikani kwa pesa. Elimu wanayopatiwa vijana wetu imekuwa haiwawezeshi ku-wapa ujuzi ambao wanawe-za kuutumia katika ushinda-ni wa soko la ajira au kuweza

kuwajengea uwezo wa kubuni njia za kujiajiri we-nyewe na hatimaye kuondo-kana na tatizo la ukosefu wa ajira.

Vijana wamekuwa miaka mingi madarasani bila ya ku-fundishwa mbinu mbadala za kuweza kujiajiri na kuajiri-wa katika sekta mbali mbali za kiuchumi.

Tunapokosa kupanga mi-pango madhubuti ya namna gani tunaweza kuwapatia shughuli za kujishughuli-sha vijana wetu, tunaandaa

mazingira ya kuwafanya waripuke siku ustaha-milivu utakapowashinda. Likitokea hilo sijui kama tutakuwa na uwezo wa kuwazuia maana wataku-wa wengi na wenye ha-sira, waliokata tamaa na wasiosikia tena maneno tunayowaambia sasa ya kuwapoza na kuwatuliza.

Mifano mengi tumeiona ya jinsi vijana walivyoripu-ka kuanzia Tunisia, Libya, Misri na kwengineko du-niani. Mengi miongoni mwa haya yametokana na vijana kukosa imani na viongozi wao ya kwamba hawapo kwa ajili ya kusi-

mamia maslahi yao na ku-watengenezea fursa za kuishi maisha bora, hivyo inapofika wakati huona bora litote ili ijulikane mbichi na mbivu.

Siombi tufike huko ila nina-chokiomba ni kwa viongozi wetu waweze kuliona hili la vijana kukosa ajira kama ni bomu la masaa au kijanga cha moto kinachochezewa kwenye mafuta na kutafuta njia ya kuyaepusha makub-wa yasitokee.

PAGE

16

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

17

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

16

Page 10: Zanzibar Daima Online Na. 04

Umuhali unatuumiza WazanzibariWARAKA KUTOKA BONN

Wazanzibari tunalitu-mia sana neno Mhali au wengine Muhali.

Huenda kwa vile tunafun-gamana sana, kivitendo, na maana ya neno hilo ambayo ni: jambo lilisowezekana au shida kulifanya kwa vile athari zake zitakuwa si nzu-ri, linaweza kuleta ugomvi, kutoelewana au bughudha baina ya watu (Kamusi ya Kiswahili sanifu ya TUKI).

Umuhali umekuwa sasa sehemu ya utamaduni wetu. Badala ya kuwa mazoea ma-baya tumeugeuza ati kuwa ni maadili bora ya kuigwa, ati ni kufanyiana hisani. Kuna hatari ya umuhali kuwa

karibu na nuksani kwa maendeleo yetu sote, kwa-ni umejipenyeza pia hata katika mfumo wa namna tunavyoendesha masuala ya kiutawala.

Wajerumani wana neno moja — „Unangemessen“ — lenye maana karibu sawa na muhali, japokuwa wao wanao kidogo na wanaupiga vita. Wao huzungumia kama vile „kutumia vibaya nafasi au cheo chako na kupinda kanuni zilizowekwa ili ujipa-tie faida ya kitu, umaarufu, heshima na kupendwa na watu, licha ya kwamba athari zake ni mbaya kwa maslahi

jNiliwahi kuhudhuria mazishi Unguja. Ilipomalizika sala ya maiti msikitini niliingiwa na shauku kutaka kulisindiki-za jeneza hadi makaburini, Mwanakwerekwe. Hakuja-kuweko teksi ya kunipeleka. Watu hapo waliniambia sina haja ya „kupoteza“ pesa kwa teksi. Niliongozwa hadi kati-ka moja ya magari ya serikali yaliowaleta watu mazikoni. Lilikuwa lori, nilipanda, na pamoja na magari mengine yaliongozana hadi makabu-rini. Kurejea nilifikishwa hadi mlangoni nyumbani. Nilimuuliza dereva kiasi gani malipo ya usafiri. Alinijibu: „Wacha nishai Mzee. Hii si

Na Othman Miraji

daladala; hii ni gari ya serikali na wewe ni serikali, ni mali yako.“

Hivyo ndivyo ilivyo na kuna watu wanaoona bora mambo yabakie vivyohivyo. Hiyo ni hisani tunayofanyiana, tunapeana faraja kwa namna hiyo. Mfanya kazi wa serikali au wa taasisi ya umma huko Zanzibar, pale anapofiwa anaomba na anapatiwa gari ya serikali, dereva na petro-li bila kulipia, ili iwachukue watu wake kwenda mazikoni na kuwarejesha. Gharama za mafuta na kuchakaa kwa

gari inabeba serikali.

Nilijiuliza bima inakuwaje kwa abiria waliojazana po-moni ndani ya gari ya serikali pale, Mwenyezi Mungu ae-pushe, inatokea ajali? Sijapa-ta jibu. Na kwa nini mterem-ko huo anaupata mtumishi

wa serikali au wa taasisi ya umma tu, na si raia mwengi-ne? Hapo nahisi inakosekana haki. Niliambiwa hisani kama hiyo inawapa motisha wafa-nya kazi. Kweli?

Hamna kanuni za kazi zi-nazotaja kwamba mkuu wa

Biashara ya holela holela imekuwa sehemu ya maisha ya Wazanzibari licha ya miaka kadhaa ya historia ya biashara ndogondogo na kubwakubwa ya visiwa hivi vya Bahari ya Hindi. Uholela na umuhali unayarudisha nyuma maisha kwa kiasi kikubwa bila ya watu kujijua.

PAGE

18

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

19

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

18

Page 11: Zanzibar Daima Online Na. 04

idara ya serikali anaweza kutoa nafuu na ureda huo kwa wafanya kazi wake. Bosi wa idara pamoja mchunguzi wa hesabu wote wanafumbia macho jambo hilo, wanataka waonekane wazuri mbele ya wenziwao. Umuhali.

Mimi sipingi kufanyiana hisani na kupeana faraja wakati wa dhiki, hasa katika msiba. Ni utu, ubinadamu, lakini si kwa mgongo wa hazina ya pamoja ya serikali, tena kuwafariji kifedha pia watu ambao kwa vyovyote, kutokana na uluwa na uwe-zo wao wanazimudu kwa urahisi gharama za mazishi. Kama kufariji basi wafanya kazi wenzake wamsaidie mfiwa kwa kuchangia kuto-ka mifukoni mwao.

Hili si suala la kutojali ma-saibu ya wenzako, lakini ni kwamba mwishowe sote, kama nchi, tunaharibikiwa. Nchi nyingi duniani hazifanyi hivyo na pia mashirika ya kimataifa yalioko hapohapo Zanzibar hayafanyi hivyo. Ni suala la uchumi, hasa kwa nchi inayopata taabu kila mwaka kusawazisha bajeti yake.

Waziri mmoja wa serikali ya Muungano, Mzanzibari, ali-nipa hadithi kwamba waziri mwenzake wa kutoka Uje-rumani alimtembelea ofi-sini kwake, Dar es Salaam. Baada ya mazungumzo yao, waziri wa Kijerumani aliom-ba apatiwe simu ili azun-gumze na mkewe Bonn.

Alizungumza kwa muda wa dakika tano. Mjerumani baadaye aliomba aambiwe kiasi gani iligharimu kupiga ile simu ili alipe. Waziri wetu akamwambia mwenzake asifanye hivyo, yeye alikuwa mgeni wake, na zaidi simu ni ya serikali.

Mwaka uliofuata waziri wetu wa Kitanzania alifanya ziara ya kulipizia mjini Bonn.

Baada ya mazungumzo na mwenyeji wake ofisini, naye aliomba simu azungumze na mkewe Tanzania. Alipa-tiwa simu na akazungumza dakika 20. Dakika chache baadaye waziri wa Kijeru-mani akamuomba sekretari wake amletee waziri wetu bili inayoonesha muda aliozungumza na nambari iliopigwa. Gharama ni mark za Kijerumani 140. Ndugu yangu waziri alilipa.

Waziri wa Kijerumani haja-taka umuhali, alinisimulia waziri wetu. Alifanya kazi yake kama inavyotakiwa. Waziri huyo alimwambia mwenzake wa Tanzania: „Nyinyi serikali zenu Afrika ni maskini, lakini zinatumia kitajiri; sisi zetu ni tajiri, tunalazimika na tuko tayari kuishi kimaskini, inapohita-jika.“

Aliyekuwa Rais wa Uje-

rumani, Christian Wulff, alijiuzulu mwaka jana kuto-kana na mbinyo wa umma na uchunguzi uliofanywa na mwendesha mashtaka wa serikali akituhumiwa kwamba marafiki zake, wafanya biashara, wa-limpa mkopo wa kununua nyumba na kugharamia safari zake za likizo. Hayo huenda, kisheria, yasione-kane kuwa ni uhalifu, lakini kwa Wajerumani yanatoa

harufu kwamba hisani hiyo aliofanyiwa rais hiyo huen-da baadaye akailipia kwa kutumia cheo chake. Ni aibu na fedheha kwa mkuu wa nchi kufadhaliwa na kuiku-bali hisani kama hiyo akiwa madarakani.

Novemba Mosi mwaka huu rais huyohuyo mstaafu ata-fikishwa mahakamani kwa mashtaka kwamba mwaka 2008 alilipiwa (mwenyewe anadai alikuwa hajui) na rafiki yake, mfanya bias-hara, gharama ya euro 719 kwa makazi katika hoteli na kula chakula. Takrima nayo pia, kwa Wajerumani, mara nyingi honekana ni hongo, rushwa, hasa inapomhusu mheshimiwa aliyomo seri-kalini. Hamna muhali hata kwa rais wa nchi.

Nahisi uchapaji kazi kati-ka utumishi wa serikali na mashirika ya umma uko chini kwa sababu ya um-uhali wa maafisa kukubali mibinyo iliozoeleka kijamii, kutoa umbele kwa jamaa zao - mto wa shangazi na mjomba - japokuwa wako watu wengine wanaoweza kufanya kazi vizuri zaidi. Kuna ubadhirifu mkubwa wa mali za umma kutokana na umuhali.Tuwe majasiri wa kutumia maneno kama vile SINA, SITAKI, SIWEZI badala ya kudanganya-na kwa maneno kama vile NITAJARIBU, NITAANGALI au NITAONA ambayo yana-tufanya mwishowe tuwe watumwa wa umuhali.

Licha ya kuwa picha hii ya Ndagoni, Pemba, kuonyesha taswira ya umaskini lakini penye nidhamu ya ufua-taji mambo ipasavyo, kijiji kama hichi kinaweza kuwa alama ya utajiri wa watu na utamaduni wao.

WARAKA KUTOKA BONN

PAGE

20

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

21

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

20

Page 12: Zanzibar Daima Online Na. 04

MKEKA WA MWANA WA MWANA

Hatujawahi kuacha kusema

Lazima tuuheshimu mchango mkubwa sana wa viongozi wa Zanzibar waliopita kwa hatua ya Tume ya Mabadi-liko ya Katiba inayoongozwa

na Jaji Mstaafu Joseph Warioba ya kupendekeza muundo wa Muun-gano wa Serikali Tatu. Iwapo hili ndilo hatimaye litakuwa chaguo la wananchi kwenye kura ya maoni ama la, ukweli utabaki kwamba Wazanzibari kwa mara nyengine tena walipuliza zumari na walio Mrima wakaicheza.

Ukimwacha Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, ambaye alilazimishwa ku-jiuzulu nyadhifa zake zote serikalini na chamani na mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya uwenyekiti wa Mwalimu Julius Nyerere, kwa sababu tu ya kuite-tea Zanzibar ndani ya Muungano, hakuna utawala wa awamu yoyote

ya baadaye visiwani Zanzibar ulio-acha kufanya uwezalo kupigania haki ya nchi hii – japo kwa njia za kimya kimya zaidi.

Katika awamu ya tatu na ya nne, kwa mfano, Serikali ya Zanzibar ili-fanya juhudi za kusawazisha kaso-ro za Muungano (baadaye zimekuja kupewa jina la kero) kupitia vikao vya pamoja baina yake na Serikali ya Mungano.

Katika awamu ya tano, Serikali ili-chukua hatua nyingi zaidi kuliko awamu yoyote kabla yake kuyas-hughulikia matatizo ya Muungano. Ilifika hadi hata Rais wa awamu hiyo, Dk. Salmin Amour Juma, aki-onekana kama mbogo aliyejeruhi-wa machoni mwa uongozi wa Bara.

Salmin hakuwa akificha hisia zake za kutoridhishwa na namna Muun-gano ulivyokuwa ukiendeshwa. Msimamo wake ulikuwa wazi ka-tika kudai marekebisho kwenye maeneo kadhaa, hasa masuala ya uchumi, orodha ya mambo ya Muungano na suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Awamu ya sita nayo pia inajulikana wazi kwa msimamo wake juu ya suala la nishati ya mafuta na utam-bulisho wa nchi ya Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano. Mara tu baada ya Rais Amani Karume ku-ingia madarakani, aliunda kamati ya wataalamu ambayo ilichambua kasoro za Muungano na kupende-keza mambo ya kupunguzwa au kuongezwa pamoja na utaratibu

Na Riziki Omar

wa kuendesha masuala ya Muungano kisera, kiutawala na katika kutunga sheria za Muungano huo.

Pendekezo moja mahsusi la kamati hiyo na ambalo linaonekana kuakisi-ka kwenye Rasimu ya Katiba Mpya ni lile la Bunge la Tanzania kuwa na mabaraza mawili, yaani Baraza la Chini (Lower House) la kushughulikia mambo ya Tanganyika tu na ambamo Zanzibar haitokuwa na wajumbe na Baraza la Juu (Upper House) ambalo litashughulikia mambo ya Muungano

tu na lenye uwakilishi sawa baina ya Tanganyika na Zanzibar.

Kwa hivyo, kama mtu anafuatilia uk-weli, atakuta mambo mawili: kwanza, Wazanzibari na viongozi wao ndio waliojenga taswira ya mabadiliko ya Katiba yajayo kwa kuwa, na hili ndilo la pili, hawakuwahi kukaa kimya pa-napohusika hatima ya nchi yao ndani ya Muungano.

Hili ni jawabu kwa wale wanaouliza walikuwa wapi Wazanzibari siku zote

hizo wanapodai nchi yao imekuwa ikichukuliwa dhiraa kwa dhiraa bila ya ridhaa yao na ikawa leo ndo wa-nalalamika. Jawabu ni kwamba kwa muda wa takriban miaka 50 ya Muun-gano, siasa za Serikali ya Muungano juu ya Zanzibar zimewanyima Wa-zanzibari fursa ya kuziondosha kero za Muungano.

Ndio maana leo hii wengine tunashan-gaa kuwaona viongozi wa CCM wa Zanzibar, kuwa hata baada ya mi-hanga yote ambayo Wazanzibari wa-

Rais wa Awamu ya Sita wa Zanzibar, Amani Karume, ambaye serikali yake ilipendekeza kuwa na mabunge mawili ya Muungano.

PAGE

22

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

23

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

22

Page 13: Zanzibar Daima Online Na. 04

meitoa, bado wanathubutu kung’ang’ania kile kile amba-cho serikali yao, katika awamu mbalimbali, imekikataa.

Ni vipi leo viongozi wa CCM ya Kisiwandui wakawa wa-napingana na ukweli kwamba hawajawahi kusikilizwa hata siku moja juu ya namna Muun-gano huu unavyopaswa kue-ndeshwa na wanang’ang’ania kuyapinga mapendekezo ya Rasimu ya Katiba, kwa kuwa tu wanadhani yatahatarisha kuwepo kwao madarakani? Hawasomi, hawajifunzi jiti-hada ambazo Zanzibar ilija-ribu kuzichukua huko nyuma lakini ikaangukia kwa pua na kwamba sasa umefika wakati wa kulimaliza jambo hili dumu daima?

Kwa mfano, baina ya mwa-ka 1990 na 2003, Serikali ya Zanzibar peke yake ilishaunda kamati 12 za kutatua kero za Muungano: Kamati ya Baraza la Mapinduzi (Kamati ya Am-ina) ya 1992, Kamati ya Rais ya Kupambana na Kasoro za Muungano (Kamati ya Sham-huna) ya 1997, Kamati ya Rais ya Kuchambua Ripoti ya Jaji Ki-sanga (Kamati ya Salim Juma Othman), Kamati ya Kuandaa Mapendekezo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Juu ya Kero za Muungano (Kamati ya Ramia) ya 2000, Kamati ya Baraza la Mapinduzi Juu ya Sera ya Mambo ya Nje, Ka-mati ya Rais ya Wataalamu Juu ya Kero za Muungano ya 2001, Kamati ya Baraza la Mapinduzi ya Jumuiya ya Af-rika Mashariki, Kamati ya Ma-futa, Kamati ya Madeni Baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muun-

gano wa Tanzania, Kamati ya Suala la Exclusive Economic Zone (EEZ), Kamati ya Masu-ala ya Fedha na Benki Kuu na Kamati ya Rais ya Masuala ya Simu (1996 – 1999).

Mbali na kamati hizo, SMZ na SMT zilishafanya vikao vya pamoja visivyopungua 80 katika ngazi mbali mbali, ili kuzungumzia kero za Muun-

gano. Vile vile serikali hizo mbili mwaka 1994 ziliomba msaada wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ili kuz-ishauri kuhusiana na Benki Kuu, mgawano wa misaada na uhusiano wa kifedha.

Licha ya kamati na vikao vyote hivyo, Muungano huu umeen-delea kukabiliwa na matatizo yale yale yaliyoundiwa kamati

na au yaliyowekewa vikao. Kero zilizozun-gumziwa mwaka 1984 katika vikao vya pamoja ndizo hizo hizo zilizozungumzwa katika ripoti ya Shelukindo ya 1992 na ka-tika mwafaka baina ya SMT na SMZ wa mwaka 1994 na kuzungumzwa tena katika kamati ya wataalamu ya SMZ ya 2001.

Wakuu wa CCM/Kisiwandui wanaopingana na matakwa mapana ya Wazanzibari, wa-napaswa kujiuliza ni kwa nini juhudi zote hizo zimeshindwa?

Jibu ni kuwa, Muungano huu una kasoro za kimaumbile na za kuzaliwa nazo. Unakosa uwiano na uadilifu baina ya pande mbili zinazouunda. Umetawaliwa na sahau au dharau kwamba Tanganyika na Zanzibar zina mamlaka sawa kwenye Muungano huu na sio kwamba upande mmoja una nguvu zaidi kuliko mwengine.

Basi hata hili hawalioni? Wakiliona hawali-semi? Walionao wakalisema, wanawafuku-za na kuwatungia majina mabaya mabaya. Tuwaeleweje wenzetu hawa?

Rais wa Awamu ya Tano ya Zanzibar, Dk. Salmin Amour, ambaye naye alikuwa akichukuliwa na Bara kama kiongozi asiyesemezeka lilipohusika suala la nafasi ya Zanzibar kwenye Muungano.

MKEKA WA MWANA WA MWANA

PAGE

24

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

25

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

24

Page 14: Zanzibar Daima Online Na. 04

Hii ndio tindikali ipaswayo kupigwa vita

Mashambulizi ya tindikali yanafasiriwa kama kitendo cha kurusha tindikali au kemikali yoyote inayofanana nayo

kwenye mwili wa mtu kwa lengo la kuuhari-bu mwili huo, kumtesa au kumuua mtu huyo. Kwa fasili yake, itafahamika wazi kwamba mashambulizi haya ni uhalifu mkubwa na wa-naoufanya ni wahalifu wasiovumilika.Mara nyingi wahalifu hawa huwarushia wa-lengwa wao tindikali usoni, wakaunguza na kuziharibu ngozi na baadhi ya wakati maji hayo ya kemikali huzama hadi kwenye ngozi.Tindikali maarufu zinazotumika ni pamoja na salfuriki, naitriki na haidrokloriki, ambazo visi-wani Zanzibar – kama ilivyo kwengineko du-niani – zinapatikana kirahisi zikiwa katika mi-undo tafauti. Huwa kama maji kwenye betri za magari, kemikali kwenye viwanda vya kienyeji vya sabuni na vipodozi majumbani au hifadhi ya madawa kwenye maabara.Kwa hivyo, ni sahihi kusema Zanzibar inaishi ndani ya duara la “silaha hizi za kemikali”, am-bazo ni rahisi kuangukia mikononi mwa watu

wabaya wanaozitumia dhidi ya wenzao kwa njia za kikatili kama ambavyo imekuwa iki-shuhudiwa.Kwa mujibu wa watafiti, nchi ambazo zime-athiriwa sana na mashambulizi haya ni pamo-ja na Bangladesh, India, Pakistan, Cambodia, Vietnam, Laos, Hong Kong, China, Uingereza, Kenya, Afrika ya Kusini, Uganda, Afghanistan, Iran na Ethiopia. Hata hivyo, ni nadra kwa waathirika wa mashambulizi haya kupoteza maisha kwa sa-babu ya mashambulizi yenyewe. Kwa mujibu wa Wakfu wa Wahanga wa Tindikali ya Paki-stan, idadi kubwa ya walengwa hao huendelea kuishi muda mrefu baada ya kushambuliwa.Lakini ukweli ni kuwa wanakabiliwa na chan-gamoto za kimwili zinazohitaji operesheni ny-ingi na za muda mrefu na pia za kisaikolojia ambazo nazo zinahitaji msaada mkubwa wa ushauri kutoka kwa watu wa karibu na jamii kwa ujumla katika kila hatua ya kupona kwao kimwili.Kwa upande wa matibabu, madaktari humshu-

ghulikia mgonjwa kwa mujibu wa kiwango, aina ya tindikali iliyotumika na pia urefu wa muda baina ya pale mwathirika aliposhambuliwa na kuwa amepata huduma ya mwanzo ya kuosh-wa kwa maji au tindikali hiyo kuyeyushwa kwa viyeyushaji vyake.Mtaalamu mmoja wa kemia ameiambia Zan-zibar Daima Online kwamba baadhi ya tindikali kama vile salfuriki ni sawa na moto ulioko kwe-nye hali ya kimiminika, kwa hivyo mtu anapom-wagiwa ni kama aliyemwagiwa moto mwilini mwake. Kwa haraka sana, tindikali huweza kuila ngozi, sehemu ya mafuta kwenye ngozi hiyo na katika baadhi ya matukio, huweza ku-zama hadi kwenye mifupa. Nyusi na midomo inaweza kuharibiwa kabisa na pua na masikio kuathirika vibaya. Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia, tafiti zimeonesha kuwa madhara yafuatayo yame-wahi kuwakumba walengwa wa mashambulizi haya:

· Fuvu la kichwa kuharibiwa na nywele ku-potea kabisa

· Mkano wa sikio kuharibiwa na kusababi-sha uziwi

· Kope huungua kabisa na kuyawacha macho yakiwa wazi na makavu na hivyo kupelekea upofu

· Mkano wa pua kuharibiwa na hivyo pua yenyewe kuondoka kabisa

· Mdomo kutanuka na kusinyaa na kuy-aweka meno nje na hivyo kusababisha ugumu wa kuzungumza na kula

· Kuharibiwa kwa mfumo wa kuingia na kutoa hewa mwilini kwani viungo kama pua na mdomo ambavyo vinahusika huwa vimeathirika.

Hayo ni matokeo ya mashambulizi ya tindikali kimwili, lakini kama tulivyosema matatizo zaidi huwa kisaikolojia, kwani utafiti unaonyesha kuwa waathirika wengi wa mashambulizi haya hukabiliwa na maradhi ya mfadhaiko, wasiwasi na wengine hata hupoteza akili zao moja kwa moja, kwani taswira ya maumbile yao mapya huwa inawaandama kama jinamizi.Katika hili, huhitajika msaada wa ziada kutoka kwa familia, marafiki na jamii kwa ujumla ili kumuonyesha mwathirika wa mashambulizi

haya kwamba maisha yanaweza kuwa mazuri tena hata kama mwili au sehemu ya mwili huo imepata ulemavu wa kudumu.Mashambulizi kama haya mara nyingi huwa-fanya walioathirika kubakia kuwa wategemezi wa familia zao kwa muda wote uliobakia wa maisha yao. Inapotokea kwamba wao waliku-wa ndio wanaoihudumia familia hiyo, basi hilo huiingiza familia nzima kwenye ‘uathirika’. Kazi nyengine ambazo waathirika walikuwa wakizifanya kabla ya kushambuliwa zilikuwa zikitegemea sura zao, na inapotokea kwamba hawawezi tena kurudi kwenye kazi hizo, lazima kuwe na mpango maalum wa kijamii na kitaifa kuwarudishia maisha yao ya kawaida.Katika baadhi ya mikasa hii, familia zimeporo-moka au kuvunjika kabisa. Kwa mfano nchini Uganda asilimia 25 ya waume wenye wake walioathiriwa, waliwaacha wake zao, ingawa ni asilimia 3 tu ya wanawake waliowakimbia waume zao waliomwagiwa tindikali. Na kwengineko, wahanga wa mashambulizi haya ambao hawajaoa au kuolewa, wamejikuta wakipoteza kabisa matumaini ya kuanzisha fa-milia zao wenyewe, maana ni shida kuwapata wenza wanaowakubali kama walivyo wakiwa na miili iliyoharibiwa.Tafiti zimeonyesha kwamba kuna njia kadhaa za kukabiliana na mashambulizi haya hatari na ya kikatili duniani. Nchi kama Bangladesh, am-bako mashambulizi haya yamekuwa yakipun-gua, mafanikio yake yametokana na marekebi-sho makubwa kwenye mifumo ya kisheria. Hata hivyo, haja kubwa pia ipo kwenye uanzish-waji wa taasisi zisizo za serikali katika kujenga uwelewa wa umma kwa tatizo hili na pia ku-wasaidia walioathirika kurudi kwenye mai-sha ya kawaida. Kama ulivyo uhalifu mwen-gine wowote, huwa hasa umetayarishwa na jamii husika, wahalifu wakabakia na kazi ya kuutekeleza tu. Mashambulizi ya tindikali pia yanaingia kwenye kundi hilo. Jamii isiyo na mwamko wa kutosha kuhusu tindikali huwa inajitayarishia yenyewe uhalifu wa kemikali hizo. Hili ndilo linalofanya pawe na hoja na haja ya kuwa vuguvugu la wananchi kupingana na mashambulizi haya ya kinyama.

This is caption text for this

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akimjuulia hali Sheikh Fadhil Soraga katika Hospitali ya Muhimbini mwishoni mwa mwaka jana

Na Mwandishi Maalum

MAKALA MAALUM

PAGE

26

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

27

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

26

Page 15: Zanzibar Daima Online Na. 04

BARZA YA JUMBA MARO

Wimbo mbaya wa magazeti ya Bara

Waswahili tunajua sote msemo maaru-fu wa Wimbo Mbaya

Hachombezewi Mtoto. Kwa mila na utamaduni wetu mzazi atajiepusha kwa kila hali kuimba wimbo aina hiyo ambao unaweza kumpeleka au kumuelekeza mtoto paba-ya.

Lakini hii haiwazui watu wengine wasimwimbie wim-bo mbaya mtoto wako. Na miongoni mwa watu wengine ni pamoja na ndugu zako kama ilivyotokea hivi karibuni kwa magazeti ya Tanzania Bara kuchapisha makala ye-nye kuiimbia nyimbo mbaya sana Zanzibar.

Kisingizio chao cha kuchapi-sha ni kuwa makala hayo yamepatikana kutoka kwe-nye mashirika ya habari ya

kimataifa, au yameandik-wa baada ya uchunguzi wa waandishi wao. Lakini kwa fikra zangu waha-riri wanapaswa kuwa na nadhari kuwa makala yatokayo nje yanayoeleza kuwa kuna mvutano na uhasama wa kidini na wenye mnaso wa Ki-Alqa’ida au wa Ki-Al-Sha-baab, hayawezi kutumiwa tu hivi hivi.

Kwa itakavyokuwa na kwa kipimo chochote kile Mhariri wa gazeti lolote

lile la Bara anapaswa kuwa anaijua Zanzibar. Mbali na hayo alipaswa pia kufanya juhudi kuyatia makala hayo katika mizania na kwa hivyo yawe yametumika pia kwa faida ya Zanzibar, ambayo ni sehemu ya taifa hili.

Upotoshaji mkubwa ulio-fanywa katika makala kama hayo, au hata maoni ya Wa-hariri yasiojenga, unaidhalili-sha Zanzibar. Lakini upo-toshwaji mkubwa ni ule wa Mhariri kukubali makala hayo yachapishwe katika gazeti lake akijua kuwa yanau-kashifu upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, yaani Zanzibar.

Kwa kuyakubali makala hayo Mhariri anakuwa anakubali kuwa hali iko mbaya sana Zanzibar kwa sababu ya matukio ya watu kumwagiwa tindikali na kwa sababu za kidini wakati waliotiwa tindi-

kali ni pamoja na Waislamu akiwemo Sheikh Fadhil Sora-ga. Na wakati Tanzania Bara nako tindikali inatumika, na ambako pia risasi, mabomu sio vitu vigeni, tena vyereje kwa Zanzibar iwe mwao?

Kama hisia za kuwepo kwa mtafaruku wa kidini ni kwa sababu ya kupata nguvu Uamsho, Mhariri wa gaze-ti anapaswa kujua kuwa jumuiya ya Uamsho imepata nguvu si kwa ajili ya mtizamo wa kidini ila ni kwa sababu ya

kudai haki za Wazanzibari. Na haya Bara si mageni pia.

Mhariri anajua hilo kwa sa-babu Uamsho imesajiliwa, imefanya kazi nyingi za ki-jamii lakini jina lake limeingia dosari katika kipindi hiki cha

mchakato wa Katiba kwa ku-dai Zanzibar ipate haki zake kamili ndani ya Jamhuri ya Muungano. Kamwe Uamsho haijasema kuwa inataka Zan-zibar ijitenge wala Zanzibar iwe dola ya Kiislamu.

Na Ally Saleh

Kamishna wa polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa

PAGE

28

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

29

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

28

Page 16: Zanzibar Daima Online Na. 04

BARZA YA JUMBA MARO

Kinachonisikitisha zaidi ni ku-ona Serikali ya Zanzibar ime-kaa kimya, burdan wa sururi, haya yakifanyika na yakifany-wa na ndugu zao wa damu. Haiwezekani wala haikhalis kabisa kwa Serikali ya Zanzibar kulinyamazia suala kama hili.

Naamini ingekuwa jambo hilo limefanywa na gazeti la Zan-zibar Leo kuchapisha makala yanayoipaka matope Serikali ya Muungano basi Serikali hiyo in-gekuwa imeshafanya vishindo dhidi ya Zanzibar.

Kama ningepewa fursa ya kuishauri Serikali ya Zanzibar katika hili, basi inatosha ku-waambia kuwa wawasiliane moja kwa moja na wenzao wa Tanzania Bara juu ya hujma hii.

Lakini wakati nyimbo mbaya ikiimbwa upande wa pili wa bahari, hata humu ndani pia mwenzetu mmoja, Kamishna Mussa Ali Mussa, naye ame-chukua tarumbeta akipaza nyimbo kama hiyo, anapiga zumari ndani ya nyumba yake.

Katika kipindi hiki cha mtikisiko wa masham-bulizi ya tindikali, ambayo wengi tunayalaani kwa nguvu zote kuwa ni ya kinyama na yasi-ovumilika, Kamishna Mussa ametoka had-harani mnasaba na hilo akisema kuwa kuna wapiganaji wa Al-Shabaab waliokamatwa wanaotaka kwenda kupigana Somalia.

Hili ni suala zito.Sijui kama Kamishna Mussa alitaka kuy-aunganisha mashambulizi hayo ya tindikali na kundi hilo, lakini mantiki ya kawaida ime-kataa kwa sababu mashambulizi hayo hayana mwelekeo wa ki Al-Shabab kwa aina ya silaha na pia kulenga mtu mmoja mmoja, na zaidi pia

kulenga Wakristo.

Al-Shabab hutumia silaha, tena za maanga-mizi, tena hulenga maeneo ya kistratajia na zaidi hukusudia kutia hasara kubwa ya mali au maisha.

Pili, nyimbo hiyo mbaya ya Kamishna Mussa ina mwangi mkubwa. Je, alitaka kusema kuna vikundi vya siri (cells) vya Al-Shabab hapa Zanzibar na kama vipo waliopatikana ni wach-ache tu kati yao, na kama wapo wengine kwa nini akatoa taarifa hizo hadharani wakati bado hawajatiwa mbaroni?

Ingawa kuna Wazanzibari waliowahi kuhusika na matukio ya kigaidi, hatujawahi kusikia bado kama kuna vikundi vyovyote vya siri humu ndani, na kutangaza kama Al-Shabaab wamepita tu, maana yake ni kuiogopesha na

kuipelekea Zanzibar itengwe bilashi.

Inafaa na ni muhimu matamshi ya Kamishna Mussa yafafanuliwe na yaelezewe katika usuli mwema la sivyo yanaweza kuwa na hasara kubwa kwa Zanzibar, kwa sisi we-nyewe kujiimbia nyimbo mbaya kuwa kumbe Al-Shabaab wameweza kufika Zanzibar.

Ugumu bila ya shaka utakuja tunapotaka kujipapatua kwa sababu ya kauli ambayo pengine ilipaswa kuzuiwa au kufanyiwa utafiti zaidi. Katika mazingira kama hayo

humkumbuka mjomba yangu Faisal Mbamba aliyewahi kuniusia, “Bora kujikwaa dole uta-tia chokaa, kuliko kujikwaa ulimi.”

Nataraji uungwana wa Kamishna Mussa, pamoja na cheo chake ni muhimu kwa maslahi ya Zanzibar, maana nchi itaendelea kuwepo na kwa vyovyote vile Uislamu hapa kwetu hautaweza kufutika, ila Uislamu wa siasa kali hatuutaki wala hatuukaribishi, na tusitoe dhana kwa wengine kuwa una nafasi.

UJUMBE KWA KAMISHNA MUSSANataraji uungwana wa Kamishna Mus-sa, pamoja na cheo chake ni muhimu kwa maslahi ya Zanzibar, maana nchi itaendelea kuwepo na kwa vyovyote vile Uislamu hapa kwetu hautaweza kufutika, ila Uislamu wa siasa kali hatu-utaki wala hatuukaribishi, na tusitoe dhana kwa wengine kuwa una nafasi.

PAGE

30

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

31

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

30

Page 17: Zanzibar Daima Online Na. 04

Wanasiasa ni wana-siasa. Na wa kwetu si tafauti sana na

wa kwengine. Wana khulka moja, sifa moja na tabia moja. Aghalabu huukimbia ukweli.

Lau wangaliweza ku-kaa pamoja wakajadili-ana mambo kiungwana. Wakaujadili ukweli. Lakini tumekwishazoea kuwaona wakizozana, wakitukanana. Wakiukimbia ukweli.

Wengine huwatukana wen-zao kwa kistaarabu. Wen-gine huwa hawana adabu. Lakini wote wamezoea kutukana. Ndio maana kuna wengi miongoni mwetu tunaoziona siasa kuwa ni chafu.

Na wapo wanasiasa ambao kwa vitendo vyao na kauli zao hujifanya wenyewe wawe wachafu.

Sina azma ya kutaja majina. Nikifanya hivyo nitawapa umuhimu wasioustahili hao wahuni wa kisiasa. Sote tunawajuwa. Na wao we-nyewe wanajijuwa. Wa-nazipa siasa jina baya. Hilo pengine hawalijui.

Pengine makosa si yao peke yao; pengine sisi pia ni wakosa. Ni wakosa kwa sababu hao wanasiasa wetu pengine wanaamini kwam-

ba tunachokitaraji kutoka kwao ni kuyasikia matusi yao.

Labda wanavyofikiri ni kuwa kazi yao ni ya kuuchekesha umma na kwamba kila wakiwatukana mahasimu zao, na mara nyingine hata wenzao, sisi hufurahi.

Kwa nini wasifikiri hivyo ikiwa sisi wenyewe tu-nawapigia makofi na wa-nawake wanawapigia vigelegele?

Halafu kuna zile nguvu maalum wanazohisi kuwa wanazipata wanapokuwa wamesimama juu ya majuk-waa wakipayuka mbele ya vipaza sauti.

Hapo ndipo wanapokoroga mambo. Hapo ndipo wa-napokuwa wevi. Huyaiba maneno kwa kuyatumia vibaya. Wanapotosha maana ya maneno; wanay-apinda maana na kuyafanya maneno si tu yasiwe na maana yake asilia bali hata hufika hadi ya kuyafanya maneno yasiwe na maana yoyote.

Sisi tunaowasikiliza huwa hatuna la kufanya ila kudu-waa. Hiyo ni moja ya hila zao. Ni moja kati ya mika-kati yao ya kutufanya tuzibe midomo yetu, tunyamaze, kwani huwa hatujui tuseme

nini.

Mbinu hiyo ni moja ya silaha za wanasiasa. Na ni silaha za hatari.

Wanasiasa hutuziba mi-domo yetu, hutufanya tun-yamaze, pale wanapoanza kutoa shtuma za kibinafsi dhidi ya wanasiasa maha-simu zao.

Tuchukue mfano wa wa-nasiasa fulani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa-naposimama jukwaani na kuwashtumu Wazanzibari wenye kutaka muundo wa Muungano ubadilike uwe wa Mkataba au wa Serikali Tatu kuwa wana lengo la kuuvunja Muungano. Au kuwa wanataka kuurejesha usultani.

Japokuwa hao wanasiasa wa CCM wanatambua we-nyewe kwamba wayas-emayo si ya kweli, wana-chodhamiria khasa kufanya ni kuwachimba wale wenye kutetea muundo wa Muun-gano ugeuzwe na Zanzibar iwe na mamlaka yake ka-mili. Wanataka watu wa-siwaamini tena hao wenye kuipigania Zanzibar.

Kwa hakika, tukichunguza kwa makini tutaona kwam-ba hotuba za wanasiasa zina malengo kadha wa kadha; na kati ya hayo lengo

moja tu lilitakiwa liwe ni la kusema ukweli.

Juu ya yote hayo kwa kawaida sisi tusio wana-siasa huwatarajia viongozi wetu wa kisiasa wawe waa-minifu, waadilifu na wenye kusema kweli.

Kwa kuwaziba mdomo wa-nanchi wanasiasa wanaku-wa wanawapokonya uwezo wao wa kusema, wa kuhoji na wa kujizatiti. Wanawa-fanya wasiweze kusema.

Kuna njia nyingine wanayo-tumia wanasiasa kuwan-yamazisha watu. Huwan-yamazisha kwa kuwanyima msamiati wa kueleza madai yao.

Hebu tuchukue tena mfano wa CCM/Zanzibar. Wa-nasiasa wake wamezoea

kuyatumia maneno fu-lani na kuyafanya kuwa kama yake yenyewe kana kwamba vile vyama vingine havina uhalali wa kuyatumia maneno hayo. Kuna mifano mingi ya maneno hayo lakini yanayonijia haraka kichwani ni ‘uzalendo’ , ‘mapinduzi’, ‘maadui wa nchi’, ‘wapinga maendeleo’ na ‘wenye nchi’.

Namna maneno hayo yana-vyotumiwa na chama hicho ni aina ya propaganda na daima katika siasa tunaona jinsi propaganda inavyob-adili thamani ya maneno na kushusha hadhi yao.

Nchini mwetu ambapo vyombo vya habari vya serikali vinatoa propaganda ni rahisi kuona jinsi kutoa-miniana na uwongo ulivyo-shamiri. Kwa hivyo, hata ikiwa watu wa jamii fulani

wanaweza kupokea habari za kuaminika, kwa kupitia kwa mfano, mtandao wa intaneti, hao watu daima huwa hawaziamini. Kuwa-ziba midomo wananchi ni aina moja ya propaganda. Kwa hivyo, katika kuwan-yamazisha watu, kuwafanya wasiweze kusema, wan-yamaze tu, wanasiasa wa-nakuwa wanamwomdoshea mtu au kundi la watu uwezo wa kuwasiliana na wengine.

Lakini nafikiri kwamba kwa mazingira yetu ya kisiasa yalivyo siku hizi Zanzibar – ambapo tuna shauku kubwa ya kuuimarisha Umoja na Mshikamano wetu — ni muhimu tuzingatie hatari za kuitumia vibaya lugha na hatari za kuipotosha kwa faida ya wanasiasa wenye kuyafikiria maslahi yao tu.

Jinsi wanasiasa wetu wanavyotuziba midomoKALAMUYA BIN RAJAB

Na Ahmed Rajab

Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi wakishagiria moja ya hotuba ya viongozi wao.

PAGE

32

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

33

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

32

Page 18: Zanzibar Daima Online Na. 04

Kamishna Mussa hakufikiri ili atende

Kama kuna jambo ambalo nililichukia tokea siku ya kwanza

tu lilipotajwa kuhusiana na mpango wa kudhibiti ugaidi duniani, basi ilikuwa ni uamuzi wa Marekani kushinikiza mataifa ya dunia kutunga sheria inayohusu kampeni yake ya kupam-bana na ugaidi.

Hili jambo lilinikera kwa kiwango kikubwa. Sababu ni moja tu: huwa sipendi amri za Marekani kwa ma-taifa maskini kama haya yetu ya barani Afrika. Siku zote nimekuwa nikiamini kuwa amri za taifa hili lenye nguvu kubwa za kiuchumi na kijeshi, kwa nchi zetu, huwa hazizingatii maslahi ya kweli ya nchi zetu.

Kwa hulka yangu, sipendi udhalimu, nachukia utawala wa kibabe, napinga unyan-yasaji na udhalilishaji bin-adamu kwa namna yoyote ile. Inapotokea hayo nisi-yoyapenda, yale ninayoya-chukia na ninayoyapinga, yanatendwa juu ya watu dhalili kihali na wale wanao-hitaji msaada sana ili ku-ondokana na udhalilifu huo na kuwa wanaopata matu-maini badala yake, nakuwa nachomwa zaidi.

Sasa kwa kuwa sipendi sera za mabavu, maonevu na udhalilishaji binadamu hasa wanyonge, na kwa kujua kwamba Marekani ni taifa mshiriki mkuu wa matendo hayo mabaya kutokana na kampeni inazoziendesha kwa visingizio vya kupam-

bana na ugaidi katika nchi mbalimbali, nilikerwa nilipo-sikia Marekani inashinikiza mataifa mengine kutunga sheria ya ugaidi.

Nilijua ukumbatiaji wa shini-kizo lile utaleta madhara makubwa kwa nchi zetu na watu wake. Kwanza kwa taifa tu kutunga sheria inayotokana na inayofuata misingi iliyoshawishiwa na taifa lenye nguvu, peke yake ni sawa na taifa hilo kuku-bali utumwa.

Si uongo, sheria nyingi zilizotungwa na nchi za

Kiafrika, achilia mbali za mabara ya Asia na Amerika ya Kusini, zimezusha ma-lalamiko mengi. Zilitungwa kwa njia ya zimamoto, kwa hivyo hazikuwa bayana; zilikosa utashi wa kukubalika na kwa kweli, zililalamikiwa na kupingwa.

Hali hiyo inaweza kutafsirika kuwa na maana ifuatayo: sheria zilizoshinikizwa kwe-tu, zimeleta matatizo katika nchi zetu. Ina maana sheria hizi hazikutuletea tija iliyoku-sudiwa bali zaidi, zimejenga nguvu kwa utawala kukan-damiza watu wake.

Watu katika nchi ambako sheria-shinikizo zilitungwa wameumizwa na wangali wanaendelea kuumizwa. Utasikia mtu kavamiwa nyumbani kwake, kapeku-liwa, akutwe au asikutwe na kilichokuwa kinatafutwa katika upekuzi, anawekwa kizuizini. Haelezwi hayo yanafanywa kwa sababu gani.

Wala mtu huyo haelezwi kama kuna tuhuma anazo-kabiliwa nazo ili atumie haki yake ya kujitetea. Katika kutumikia sheria-shinikizo, wapo watu waliouliwa kwa kupigwa risasi. Wapo wengi

wamejeruhiwa kwa risasi. Mtu kwa hisia tu kwamba labda fulani ana-husika na ubaya huu au ule, kama ni ubaya kweli, anapigwa risasi.

Moja ya kifungu katika sheria-shini-kizo za kupambana na ugaidi zilizoan-dikwa Marekani na kuenezwa mabara yote duniani kwa ushawishi wao, ni

kile kinachoruhusu mtu ku-wekwa kizuizini – wenyewe wanaita kitendo hiki kwa jina zuri la “kumhifadhi.”

Eti mtu “anahifadhiwa” asikochagua kwa namna yoyote ile kwa muda usioju-likana. Ndio maana wengine tuliamini mapema kwamba katika kampeni ya kupamba-na na ugaidi iliyoanzishwa na Marekani baada ya masham-bulio mawili ndani ya nchi yake, mwaka 2001 – Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi (Pentagon), Washington, na Kituo cha Kimataifa cha Biashara (WTC), New York, ilikuwa ni kueneza chuki

KAULI YA MWINYI MKUU

Na Jabir Idrissa

PAGE

34

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

35

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

34

Page 19: Zanzibar Daima Online Na. 04

dhidi yao wenyewe duniani kote.

Uenezaji wa chuki umetokea kwa sababu kwa wale wa-naoumizwa na kampeni hiyo, kupitia zile sheria-shinikizo, wanachokiona si kingine isipokuwa kunyanyaswa na kud-halilishwa na wasimamiaji wa sheria ya ugaidi.Na kwa sababu wanaoumizwa kwa kunyanyaswa na kud-halilishwa pamoja na kujeruhiwa na au kuuliwa, wanajua kuwa yote hayo yanatokana na shinikizo za Marekani. Kwa hivyo walimwengu wanajua kwa sababu ya shida za Marekani, wao wanaumizwa.

Sasa, inasikitisha kukuta Zanzibar ina mtendaji wa taasisi muhimu ya dola anayejifakharisha kwa kutamka kuwa wamekamata watu wanaoshirikiana na makundi ya Al Qaeda na Al-Shabaab. Inaonekana Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, hata haelewi madhara ya kutoa matamshi kama hayo.

Ni bahati mbaya sana kuwa ofisa wa ngazi ya juu katika Jeshi la Polisi kama yeye, haelewi madhara ya alichoki-fanya mwanzoni mwa wiki hii alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia uchunguzi wa tukio la kumwagiwa tindikali Padri Joseph Anselmo Mwang’amba.

Hivi ni kweli hajui kuwa kutamka hivyo ni kushawishi Marekani na washirika wake waamini kuwa Zanzibar ina-fuga watenda ugaidi? Hajui kuwa ukishatajwa unafuga

watenda ugaidi nchini kwako unakaribisha maaskari wa mataifa hayo kuja kuchunguza? Hajui yote haya? Ndiyo nikasema ni “bahati mbaya sana” kama hajui.

Uchunguzi wa kuangalia kama kweli Zanzibar inafuga au kuhifadhi watenda ugaidi, kwa kufahamu au kwa ku-tofahamu, hufanywa na matokeo yake mara nyingi ni kuigharimu nchi na watu wake. Labda Kamishna Mussa hafuatilii yale yanayotokea kwenye nchi zinazotajwa kwa hilo.

Dunia inashuhudia namna nchi zinazotajwa kutumika kwa ajili ya kuhifadhi watenda ugaidi zinavyokumbwa na mata-tizo ya kiusalama kila siku. Ikipita wiki bila ya kutokea tati-zo hakika mnamshukuru Mola aliyewaumba. Ni shughuli pevu.

Kamishna Mussa laiti kama angefuatilia yanayotokea Afghanistan, Pakistan, Yemen, Irak, Libya, Somalia na Ke-nya, angefikiri mara mbili kabla ya kufikiria kupanga kutoka mbele ya waandishi wa habari na kusema “Zanzibar kuna watu wanatumiwa na makundi ya Al-Qaida na Al-Sha-baab.”

Simbishii Kamishna Mussa ila nataka kumtanabahisha kuwa alichokifanya ni kitu kibaya na kitaigharimu Zanzibar, nchi ambayo tayari imesingiziwa majanga mengi yakiwemo yaliyosababishwa na ulegevu wake yeye kama mkuu wa

polisi na Serikali kwa jumla.Ni nani walioingilia mikutano ya Jumuiya ya Uamsho na kuiletea nchi fadhaa kubwa mbele ya macho ya kima-taifa? Ni nani waliofanikisha mpango wa kuwanyamazi-sha masheikh kwa kuwakamata na kuwatia gerezani kwa karibu mwaka sasa wakati hawajahukumiwa kwa lolote baya?

Ni nani aliye mas’uul wa kadhia zinazowakuta watoto na familia za masheikh hawa katika kipindi ambacho baba, wajomba na walezi wao wanahilikika gerezani pasina kut-hibitishwa kuwa wametenda kosa lolote?

Jeshi la Polisi ndilo lililoanzisha mchezo mbaya wa kucho-chea wafuasi wa Uamsho kujilinda na kulinda viongozi wao. Kabla ya mchezo mbaya huo wa Polisi, Uamsho wali-shafanya mikutano yapata 100 kote Unguja na Pemba na hakuna aliyeguswa.Ilikuaje mikutano ya wakati kazi kubwa ishafanywa ikumbwe na vurugu? Inasikitisha kuwa watendaji kama Ka-mishna Mussa wanaona yale yaliyotokea nchini ni madogo kwa hivyo ni bora kutafuta makubwa zaidi.Na iwapo Kamishna Mussa anadhani hilo ni sahihi, na alichokisimamia ni haki, basi asubiri mguso mbaya kwa Zanzibar kufuatia matamshi yake ya kuwa ina watu wa-naoshirikiana na makundi maovu ya Al-Qaida na AlSha-baab.

KAULI YA MWINYI MKUU

SOMA JARIDA LA ZANZIBAR DAIMA ONLINE KILA WIKI MBILI

PAGE

36

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

37

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

36

Page 20: Zanzibar Daima Online Na. 04

Zanzibar sio limbukeni wa uvumilivu wa kidini

Zanzibar imekumbwa na matukio ya mfululizo ya kihalifu. Hilo halina sha-

ka. Miongoni mwa matukio hayo yamewalenga viongozi wa kidini. Hilo ni kweli. Ma-tukio haya hayakubaliki ku-fanywa wala hayavumiliki. Nalo pia ni sahihi. Matukio haya yana mkono wa kidini na au chuki dhidi ya wageni. Hilo si kweli.

Napinga kuhusishwa ma-tukio haya na dini kwa saba-bu kadhaa. Moja ni historia na uzoefu wa nchi yetu wa kuishi karne na dahari kwa uvumilivu mkubwa wa kidini na kimadhehebu, Mji Mkon-gwe wa Zanzibar ukiwa ni ushahidi unaotosha.

Katika mji huu uliojengwa kwenye karne ya 18 kuna misikiti 52 ya Waislamu wa madhehebu za Sunni, Ibadhi na Shi’a, mahekalu matatu ya Wahindu (Shree Sana-tan Mandir, Hekalu la Arya Samaj na la Jain Derasa) na makanisa mawili: moja la Kianglikana na jengine la Kikatoliki.

Kanisa la Kianglikana lililo Mkunazini lipo karibu kabisa na Msikiti Jibril [jina sahihi Msikiti Jibrin]. Adhana iki-adhiniwa Jibril inaingia moja kwa moja kwenye madhaba-hu ya Kanisa na makengele ya Kanisa yanaingia moja kwa moja kwenye kibla cha Jibril. Na hilo limekuwapo kwa miaka nenda miaka rudi.

Kanisa la Kikatoliki la Minara Miwili nalo liko karibu sana na Masjid Istiqama, ambao ni msikiti wa Ibadhi.

Msikiti wa Shi’a Ithnaash-eri wa Hamamni upo karibu kabisa na Msikiti wa Iba-dhi kwa nyuma na kusho-to kwake umegandana na Msikiti wa Shi’a Bohora wa Zenabhai. Halikadhalika ma-hekalu ya Wahindu yaliopo Mji Mkongwe yamezunguk-wa na misikiti ya Waislamu.

Misikiti ya Sunni imejengwa na Shi’a na Ibadhi na kwe-nye misikiti ya Sunni wanas-wali Shi’a na Ibadhi, huku Sunni nao wakiswali kwenye misikiti ya Shi’a na Ibadhi.

Ardhi ya kujengea makanisa

na mahekalu ni za Waislamu na wafalme wa Zanzibar waliwapa ardhi hizo Wakris-to na Wahindu wajengee nyumba zao za ibada.

Katika historia ya karibuni hapa Zanzibar, kuna Mkristo ambaye aliichana Qur’an, la-kini Waislamu hawakulipiza kisasi kwa kuchana Biblia. Kwa hakika, kuna familia ambazo wengine ni Waisl-amu na wengine ni Wakristo, au ambazo wengine ni Sunni na wengine ni Ibadhi au Shi’a.

Mkristo akifa Zanzibar, Wais-lamu wanahudhuria maziko-ni, na vivyo afapo Mwislamu. Wakristo wangapi Zanzibar wamekufa mikononi mwa Waislamu na Waislamu wakasimamia maziko yao kanisani mpaka wanashush-wa makaburini?

Wahindu wao wakifa wana-

chomana, kitendo ambacho ni kinyume na dini ya Kiisl-amu, lakini bado pande hizo mbili hushirikiana katika msiba na hufika mpaka wa-napochomana Wahindu au wanapozikana Waislamu.

Wakristo wenye asili ya Zan-zibar huvaa mabuibui na mi-tandio na kanga. Na huwa pia wanahudhuria kanisani wakiwa wamejitanda kan-ga na mitandio. Ukiwaona masokoni, maskulini, vyuoni na kadhalika huwezi kumjua nani Mkristo nani Mwislamu. Hatutofautishwi na mavazi yetu.

Ramadhani ikifika tunaa-likana futari bila ya kujali dini au madhehebu zetu. Siku za Sikukuu hushirikiana pamoja pia. Tunapelekeana vyakula na Wakristo wao ikifika Pas-aka na Krismasi wanatuletea vyakula na tunaalikana kati-

ka kumbi mbali mbali. Katika Viwanja vya kusherehekea Idd huwakuta Wahindu na Wakristo kwa pamoja wa-nasherehekea Idd na Waisl-amu.

Watoto wetu wa Kiislamu tunawasomesha katika skuli za Kikristo zilizopo Zanzibar na wala Waislamu wa Zan-zibar hawajawahi kusema hawawapeleki watoto wao katika skuli za Kikristo. Kwa hakika, kuna mifano pia ya watoto wa Kikristo ambao wamesoma madrassa za Qur’an na watoto wenzao Wakiislamu.

Mitaani watoto wa dini ta-fauti wanacheza michezo yao pamoja bila ya kujali tafauti ya dini zao na wala watoto hawakatazwi na wa-zee wao wasicheze pamoja na watoto wa dini nyingine au madhehebu tafauti.

MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI

Uhindu,Ukristo, Uislamu na dini nyenginezo

zimekuwapo Zanzibar kwa miaka kadhaa

na hazijawahi kukwaruzana.

UVUMILIVU

Na Sujae Mkiji

PAGE

38

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

39

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

38

Page 21: Zanzibar Daima Online Na. 04

Rais Mstaafu Amani Abeid Karume aliwahi kumchagua Brigadia-Jenerali Adam Mwakanyuki kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Wizara ambayo chi-ni yake zipo Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar na ya Kadhi Mkuu wa Zan-zibar .

Na Waislamu walimheshimu na hakuna Mwislamu aliyemtaka Rais amuuzulu waziri huyo katika wizara hiyo inayoratibu mambo ya Waisl-amu.

Katika Sherehe za Kitaifa iwe za ki-serikali au za kidini hualikwa Wakuu wa kidini na wa kimadhehebu kuju-muika pamoja na viongozi wa kiseri-kali na wananchi mbali mbali.

Niliwahi kupeleka wageni wangu ku-

toka Italy kutembelea sehemu za ki-historia katika Mji Mkongwe na wali-nambia kuwa wao wametembea nchi nyingi duniani lakini hawajawahi ku-ona ustahamilivu mkubwa wa kidini kama uliopo Zanzibar na wanashan-gaa kuona watu wanafanya ibada zao bila ya kugombana.

Tunashangazwa sana kuona mafa-tani wanataka kutugombanisha na ndugu zetu wa Kikristo na wa dini ny-engine.

Pia inawezekana matukio haya ya watu kurushiwa tindikali ni visasi. Hatujui waliohujumiwa katika ma-tukio haya wamekosana nini na wen-zao.

Waislamu wa Zanzibar alivyomwagi-wa tindikali Sheikh wao hawajawash-

tumu Wakristo kuwa ndio waliofanya shambulio hilo lakini leo tunashangaa kuona ndugu zetu wa Kikristo wana-washtumu Waislamu kwa masham-bulio waliofanyiwa Mapadri.

Padri kamwagiwa tindikali na kasa-firishwa hapohapo, lakini Sheikh Az-zan Khalid yupo hospitali mahtuti na mpaka leo hajasafirishwa.

Baadhi ya Mabalozi waliokutana na Viongozi wa Uamsho wamepin-ga kuwa vuguvugu la Uamsho ni la magaidi.

Tuiache Zanzibar iendelee na safari yake na tusiyahusishe matukio haya ya kihalifu na safari ya Zanzibar ina-potaka kuelekea. Tusiifitinishe Zanzi-bar na dunia

MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI

Naomba nichukue fursa hii kukushukuru wewe mhariri mkuu pamoja

na waandishi wenzako wote kwa kuamua kuanzisha jarida hili mliloliita Zanzi-bar Daima Online. Mimi ni mmoja wa miongoni mwa Wazanzibari waliobahatika kuyasoma matoleo ya ma-jarida yote matatu yaliyopita na kusema kweli nimefu-rahishwa na makala mbali mbali nilizozisoma.

Tafadhali naomba upo-kee pongezi zangu kwa niaba ya waandishi wako wote wanaoendelea ku-tuelimisha katika makala zao mbali mbali za jarida hili lipatikanalo kwa kupitia njia ya mtandao. Tunakuwa tunasoma habari nyingi zinazoandikwa na magazeti ambayo mengi yanami-likiwa na vyombo vya habari vya Tanganyika. Mara ny-ingi wanapoandika habari kuhusu Zanzibar wanaan-dika watakavyo wao kwa

maslahi ya biashara yao. Mara nyingi habari huwa zi-naongezwa chumvi na mara nyengine zinaandikwa kwa kichukichuki hivi.

Inatia moyo na kufurahi-sha kuona kwamba kumbe tunao waandishi wetu ma-hiri kwenye tasnia hii ambao wanaweza kuandika habari na makala mbali mbali ze-nye kuleta matumaini kwa Mzanzibari. Habari ambazo zitawasaidia Wazanzibari na hasa vijana kuweza kue-

limika kuzikimbia siasa chuki zlilizopitwa na wakati na badala yake kujielimisha kutafuta njia mbali mbali za kuweza kuleta ukom-bozi wa kujiletea maendeleo yao na familia zao bila kusahau maendeleo ya nchi yao. Kuna matatizo mbali mbali yanayotukabili ambayo kwa kupitia njia hii ya habari watu wetu wanaweza kujifunza njia mbali mbali za kujikwamua na matatizo haya.

Ni matumaini yangu basi kuanzishwa kwa jarida hili kutakua ni njia mojawapo ya ku-weza kuendelea kutuelimisha Wazanzibari popote pale tulipo. Huu ni mwanzo mzuri. Ahsanteni tena kwa jitihada zenu za kue-ndelea kutumia taaluma yenu kuitumikia jamii.

Zanzibar Daima. Hamad London

Assalamu alaykum Mhariri wa Zanzibar Daima Online

BARUA ZA WASOMAJI

Alama za uvumilivu wa kidini Zanzibar

ZDO idumu

PAGE

40

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

41

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

40

Page 22: Zanzibar Daima Online Na. 04

TUFUNGUE KITABU

Sitiari za Mzee wa Kimbunga: Haji Gora (Sehemu ya Kwanza)

Tanbihi: Makala haya ambayo kwa mara ya mwanzo yalichapishwa kwa jina la “Tungo za Bwana Kimbunga: Haji Gora Haji” yameandikwa na mtaalamu wa lugha ya Kiswahili mzaliwa wa Uholanzi, PROFESA RIDDER H. SAMSOM, kuelezea kazi za kifasihi za gwiji wa sanaa ya ushairi katika zama hizi visiwani Zanzibar, Haji Gora Haji. Tunaichapisha tena hapa ikiwa imehaririwa kidogo kua-kisi wakati wa sasa.

HAJI GORA HAJI

Na jiwe linasitawi, panapo matumaini Jiwe lisilositawi, lisiloko aridhini Ah jiwe husitawi, hilo siyo jambo geni

Mauwaye yana rangi, tena nyingi naamini Ni kama mwezi sipingi, humwirika mawinguni Kama macho hizo rangi, ni yako wangu mwendani

Ni macho yenye madaha, kama fikira moyoni Huingiwa na furaha, ukiwepo muhisani Ulipo huona raha, kuhisi niko peponi

Rangi nyingi za mawimbi, yazukayo baharini Hwenda na kutowa vumbi, kwa upeo wa machoni Mpenzi kwako sitambi, sijiwezi taabani

Ah! jamani linastawi jiwe, bali ajabu sioni Lasitawi mno jiwe, husitawishwa na nini Lisilositawi jiwe, nini wake mtihani

Linanukiya upepo, unapasuwa puwani Miliyo yale ilipo, yapenya masikiyoni Maisha kimojawapo, kila siku furahani

Bwe bila wasi hufana, hufimisha tegemezi Huwanda hata kugina, ukalyona lijiezi Bwe halidumbu fana, pasipo mchinjigizi Hutaka tendelekezi, jibwe ndipo likafana

Rangi zakwe za mayuwa, si haba vezo pendezi Ja mwezi unaoyawa, ukamwilika arizi Hamba macho rangi huwa, jayako weye mpezi Huburudika mtima, tondole yangu hakona

Macho yano madaha, ja ya mtima simazi Huzangiwa ni furaha, hazicheleza pumuzi Ukawapo hona raha, mrembo mwenye mapozi Huburudika mtima, tondole yangu hakona

Rangi nyingi za mawimbi, yazukayo kibayazi Bahari inayo dumbi, kwa kusi na kaskazi

Ushairi ni mchezo. Mchezo wa maneno na hisia za watu. Katika makala haya nataka nieleze machache kuhusu tungo

za Mzee Haji Gora Haji anayejulikana pia kwa jina la ‘Mzee Kimbunga’ kutokana na jina la kitabu chake kilichopigwa chapa na kutolewa

1994. Nataka kutoa mifano michache ya sitiari anazozitumia, vipi zinavyohusiana na ‘fikra kuu hiyo inayoshikiliwa na kusisitizwa’ na yeye mwenyewe anatambulika kama mtu gani.

Utungo ufuatao, Jiwe Linasitawi, ameutunga mnamo mwaka 1997:

Kama kokwa za fenesi, zinapochomwa jikoni Ghasiya huja upesi, na kufika mitaani Kuona hata kuhisi, ni uhuru duniyani

Yavutiya vipepeo, vyenye kuruka angani Rangi nyingi zilo kwao, zinopendeza machoni Zaghilibu rangi zao, si kwa nani wala nani

Ndivyo linavyositawi, asiyejuwa ni nani Lisiloweza sitawi, marejeyo sikiyeni Ni huwa au haiwi, ilivyo nitajieni

Kwa hakika utungo huo aliotunga Mzee Haji katika bahari ya nyimbo unaonyesha hasa sio ubingwa wake tu, lakini pia mtindo wake na sauti yake. Nyimbo hii inatambulika kuwa imetungwa na Mzee Haji kwa sababu ya sitiari anayotumia yenye kiini cha mambo mawili kuhalifiana. Maana jiwe gani linaweza likastawi?

Arudhi ya nyimbo hii, mpigo wake, mdundo wake, mizani na vituo vyake pamoja na vina - hayo yote, jinsi alivyotumia, yanaonyesha kuwa hiyo ndiyo kazi yake Mzee Haji.

Sitiari nyengine anazoweka ni zile zinazoto-kana na mazingira yake huko Visiwani: mna mawingu na anga, mawimbi na bahmi; kuna

vumbi na upepo, mwezi na dunia, jikoni na mitaani; kuna madakha na ghilibu; matu-maini na mtihani na maisha.

Haji Gora Haji ni mtu wa kisiwa cha Tumbatu, kaskazini magharibi karibu na Unguja. Tum-batu ina magofu ambayo, pamoja na Unguja Ukuu, ni ya zamani kuliko popote pengine huko Zanzibar, yaani ya karne ya tisa. In-gawa lahaja za Kitumbatu na Kimakunduchi zinahitilafiana, kuna wasomi walioziainisha pamoja katika kikundi cha lahaja za kusini.

Kwa vile Mzee Haji ni Mtumbatu, anatunga kwa Kitumbatu vile vile. Kwa mfano utungo huo “Jiwe Linasitawi” aliutunga katika umbo la shairi kwa Kitumbatu ufuatavyo:

PAGE

42

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

43

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

42

Page 23: Zanzibar Daima Online Na. 04

Vikubwa vyakwe vitimbi, kingine sifananizi Kwa upeo usokoma, yanavyozuka kwayona

Ahi jamani hufima, tambuyani watambuzi Hufima mno hukona, kipata naliezi Bwe velyo lisipofana, huwa lina kizuwizi Huviya penye nakama, vepo halidumbu fana

Upepo linanukiya, puyani rihi ya fazi Miliyo yakwe yaliya, mashikiyo kuyahizi Maisha linaliliya, yasiwe na bumbuwazi Huviya penye nakama, vepo halidumbu fima

Hamba kongwa za fenesi, zikokwa hazitikizi Hasia huja upesi, wengine kwa sana razi Kona mpaka kuhisi, uhuru wa uwamuzi Huviya penye nakama, vepo haidumbu fima

Zavutiya vitunguja, virukavyo hata pazi Rangi kwao zizokuja, vezo nacho kivutizi Zahilibu kula mja, simwana wala mvyazi Hungi ni bumbuwazi, rangi hizo ukazona

Haji Gora Haji amezaliwa mwaka 1933 kijiji cha Kokoni huko Tumbatu. Alipokuwa na umri wa miaka mitano tu alichukuliwa na akakulia huko Mkunazini, mtaa wa katikati ya Zanzibar Mjini.

Hapo mjini alikuwa akisoma dini chuoni, lakini hakupata fursa ya kwenda skuli ya serikali maana ilimbidi aanze kufanya kazi akiwa bado mdogo. Akafundishwa na mjomba wake, Haji Mjumbe, uvuvi wa nyavu na baa-daye baba yake mdogo, Pandu Haji, alimpa ujuzi wa uvuvi wa madema.

Baba yake alikuwa baharia hodari na nahodha

wa majahazi yaliyopitia mwambao wote wa Afrika ya Mashariki. Naye Haji Gora mwe-nyewe tangu alipoanza kuvua, maisha yake yote hadi sasa yamehusiana na bahari akiwa mvuvi, baharia, mpagazi na mchukuzi banda-rini, msafirishaji wa karafuu na mwajiriwa wa kampuni ya Kichina huko Tanga aliyoitafutia majongoo ya ufukweni.

Alipokuwa na miaka 16 alijiunga na kikundi cha vijana kilichojiita ‘Ujinga Mwingi’ huko Tumbatu na kuanza kujihusisha na ngoma. Kama desturi ngoma za aina hii, hushindana kwa kutungiana mashairi na kuyaimba had-harani, kulumbana na kujibizana.

‘Ngekuwa mla hasara, ‘ngeoa kwa uzurio Hawa mja wa papara, hakona hakupendao Haikosapo busara, havutiwa uzurioLeo nakiri ‘ngeyuta, ngeoa kwa uzurio!

Nekumbuka ‘lipokona, mato yalipoangaza Malaika nekuona, wameta wanchichiza Hafikiri setaona, alokuzidi aziza Ningekiona cha moto, ‘ngekuoa kwa uzurio!

Akili libadilika, na moyo ukafatiza Matozi yebubujika, mtima wauumiza Henenda hajiapiza, ‘takuoa nikifanza Ela leo nakubali, ‘ngekuwa mla hasara!

Usia ulotolewa, wazazi walonifunza Mwanamke kuolewa, kwa tabia ni aziza Si sura wala si quwa, si ukoo unojuza ‘Ngewakana ningeyuta, mayuto ya milenia!

Basi lipokumbukia, wasia niloagizwa Nekaanza kukwambia, nawe kiona wavizwa Hasira ukatukua, na maneno yasofunzwa Ela ningelazimisha, leo ‘ngekuwa tabuni!

Dini mafunzo hubiri, kwa mchumba kumwegeza Mwili wake usitiri, na ngoma asijecheza Papo ugomvi shamiri, na matusi kichombezwa Wazazi walinipenda, ‘tawashukuru daima

Moyo ulipata tabu, kuyawacha yalopendwaHauasa sijesibu, kujidhuru sijetendwa Si bora kujisulubu, kwa mashaka yasoinda Leo unanipongeza, na raha wejionea!

Hawamba wangu mtima, hawamba nisijependa Huyu kwangu sio mwema, ni bora nimwache kwenda Nipate mwenye heshima, na dini anayependa Leo najishukuria, malengo yenfikiwa!

Baada kuusakama, mwisho moyo nikubali Ukinambia kwa wema, nitafute anojali Tena nioe kwa shima, nikae nae mithali Papo hajitafutia, mke nilonae sasa!

Sitara niitakayo, na heshima yangu nyumba Upole wa lisaniyo, akubali ya Muumba Tabia njema utuyo, “Hawaa” jina loumbwa Huyu ndie mke wangu, namshukuru Muumba!

Sitaki tena mwengine, wa mtima kutibua Sitaki shoti niseme, niwambie wasojua Sitaki msijipime, kwangu ‘taka jirejea Nimesharidhika kwake, kwamwe mwengine simwebu!

Othman Ali Haji Zanzibar

Ningakuowa kwa Surayo

LADHA YA BETI

PAGE

44

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

45

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

44

Page 24: Zanzibar Daima Online Na. 04

NIONAVYO

Na Mohamed Abdul-RahmanMwanasiasa mwadilifu ni yule mwenye ujasiri wa kusema  kitu kisichowapen-deza wengine, ilimradi awe mkweli. Akikosoa awe ana-kosoa kwa kujenga na sio kubomoa na awe na moyo wa kueleza na kufichua had-harani tatizo linaloihusu jamii na kuipa jamii nafasi ya kuchangia katika kutafuta suluhisho.

Kwa bahati mbaya miongo-ni mwa wanasiasa tulionao katika Chama cha Mapin-duzi (CCM), chama chenye kutawala, kuna wasio na uja-siri huo. Huenda hawa waka-wa ndio wengi na wanapo-jitokeza baadhi ya wakati hadharani huwa zaidi ni ku-jitoa kimasomaso tu. Sababu kubwa labda inayowafanya wawe hivyo ni haja ya kuy-alinda masilahi yao binafsi.

Nimekuwa nikipitiapitia vi-dio za matukio ya kisiasa ya Zanzibar katika mtandao wa

YouTube na nikaziku-ta za mawaziri wawili wa Serikali ya Mapin-duzi Zanzibar (SMZ) w a k i u z u n g u m z a Muungano. Mawaziri hao walio-kuwa wakizungumza katika nyakati mbali mbali kuhusu kero za Muun-gano na jinsi Zanzibar ina-vyokandamizwa ni Waziri wa Fedha, Omar Yusuf Mzee,  aliyekuwa akizungumza katika semina ya Baraza la Wawakilishi. Mwengine ni Mwinyihaji Makame aliyeku-wa akitoa maoni katika Tume ya Katiba ya Jaji Joseph Wari-oba. Walioyaeleza yanatia unyonge, yanakereketa na  yanasikitisha. Yusuf Mzee alitaja kisa kili-chotokea wakati wa mku-tano wa Utalii Katika Nchi za Visiwa uliofanywa Mau-ritius. Ujumbe uliokwenda huko uliongozwa na Waziri

Ali Juma Shamhuna ambaye alilakiwa kama viongozi wa jumbe zote nyingine na ali-pewa heshima alizostahiki.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Yusuf Mzee, siku ya pili uli-wasili ujumbe wa Tanza-nia Bara na kuanzia wakati huo Mheshimiwa Shamhu-na alinyang’anywa gari na gari hilo akapewa Waziri wa Serikali ya Muungano na yeye Shamhuna akajiunga na wengine akiwa sehemu tu ya ujumbe.

Swali alilouliza Mzee lilikuwa “Tangu lini Bara ikawa nayo ni kisiwa?” Sijui kama Wa-ziri Shamhuna alimuuliza

mwenzake wa Bara swali hilo baada ya hayo kutokea. Manung’uniko ya Waziri Makame nayo yalihusiana na utiaji saini nyaraka mbili tafauti, waraka mmoja wa Muungano na  mwingine wa Zanzibar wakati wa ziara moja ya nchi za nje wakiwa katika ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa itifaki ilikuwa aanze Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe, na baa-daye yeye Makame kwa niaba ya Zanzibar.

Kiroja cha mambo ni kwamba Membe alizitia saini nyaraka

zote mbili. Kwa masikitiko Makame alisema alimuuliza Membe na akajibiwa “You have no instruments” ikiwa na maana Makame hakuwa na mamlaka (madaraka) ya kutia saini nyaraka iliyohusu Zanzibar.

Yeyote aliyeiona kanda hiyo na kuyasikia yaliyosemwa atakubaliana nami kuwa ya-likuwa mambo mazito na ye-nye kuhuzunisha.

Yaliyomkuta Makame ndiyo yaliyonisikitisha zaidi kwani alipokuwa akielezea yaliomsi-bu mbele ya Warioba aliyewa-hi kuwa Mwanasheria Mkuu na Waziri Mkuu wa Serikali ya

Muungano na Mzee Joseph Butiku, aliyekuwa karibu sana na Mwalimu Julius Nyerere alipokuwa Katibu Mkuu Ikulu, ilikuwa sawa na “mdogo kulalamika kwa mkubwa.”

Lakini huo ni upande mmo-ja wa kadhia yenyewe – upande wa namna Zanzibar inavyoonewa na mshirika mwenzake wa Muungano, Tanzania Bara.

Kuna upande mwengine wa suala hili – nao ni wetu wenyewe kama Wazanzi-bari na hasa zaidi viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kutusimamia na kutu-ongoza. Je, baada ya kad-hia zote mbili viongozi hao wahusika walifanya nini? Na laiti hakungekuweko na warsha na majukwaa ya ku-

weza kujieleza, wangekuwa na ubavu wa kuyazungumza hadharani?

Bila shaka waliyadhukuru kwa sababu palitolewa rukhsa na wakawa na fursa ya kutoa du-kuduku lao kadamnasi. Kwa kufanya hivyo, umma wa Wa-zanzibari umewaona walivyo washupavu kwa ajili ya nchi yao. Lakini je, ni kweli kwam-ba uthubutu huo wanao kwe-nye vikao vyao vya ndani, pale viongozi wa Bara kwa jina la Muungano wanapowakabili? Kama wanao, mbona hatuoni kinachobadilika? Nionavyo, majibu ya maswali haya

Lazima tujiangalie wenyewe

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Mwinyihaji Makame.

PAGE

46

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

47

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

46

Page 25: Zanzibar Daima Online Na. 04

yanahitajika sana ili wananchi wasiendelee kufanywa waamini kwamba uongozi wetu wa Zanzibar ni kielelezo cha udhaifu na unyonge mbele ya Bara. Uongozi unao-tishiwa kwa chui wa karatasi, ukaufyata mkia katikati ya mapaja.

Hofu iliyopo ni kwamba uongozi wa Zanzibar umekosa nia ya kweli na ujasiri wa kuitetea Zanzibar kwa uwazi bila ya woga au kificho. Huenda baadhi wakawa na maoni tafauti kwamba kuna mawaziri na wajumbe wa Baraza wasio katika kundi hilo, lakini ushahidi wa wazi ni kuwa ni wachache wenye ujasiri wa kina Mansoor Yusuf Himidi, Mwanasheria Mkuu Othman Masoud, Mkurugenzi wa Mashtaka Ibrahim Mzee au Mwakilishi Mohamed Raza.

Lau tungekuwa na hawa 10 kwenye safu ya juu ya uon-gozi, basi hadithi yetu ingelikuwa tafauti hivi leo.  Badala yake kinachoshuhudiwa huko juu ni woga, hofu na kutoana vikoa kwa pupa ya kunusuru masilahi binafsi, kwa jina la kulinda sera za chama. Kwa mfano tukichuku-lia kisa cha Mansoor kufukuzwa CCM, karibu nusu ya wa-jumbe wa Baraza la Mapinduzi kutoka CCM ni wajumbe wa Kamati Maalum ya chama hicho upande wa Zanzibar. Lakini ni wachache mno waliojitokeza kumtetea Man-soor. Kadhia nyengine ni mvutano uliozuka karibuni katika bunge la Muungano Dodoma kuhusu Rasimu ya Katiba na mizengwe iliyofanywa na chama kinachotawala kub-adilisha sehemu ya yaliomo ndani ya Rasimu hiyo.

Waliojitokeza kuitetea Zanzibar kwa kutoshirikishwa ni vyama vya upinzani CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi. Wabunge wa CCM Zanzibar akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Iddi, walilipa mgongo suala hilo na wa-likibariki kile kinacholalamikiwa na taasisi kadhaa huru nchini Tanzania kwamba ni ‘upotoshaji’.

Mansoor amewapa somo na mwangaza wenzake aloku-wa nao katika CCM kwa kuwakumbusha yafuatayo:

1. Mwanasiasa mwadilifu ni yule anayesimamia haki na ukweli daima. Hili limesisitizwa na mwongozo wa CCM yenyewe kwa maneno haya: “ Nitasema kweli daima fi-tina kwangu mwiko.” 2. Jukumu la mwanasiasa ni kuwaongoza waliomchagua kwa kutetea matakwa yao.

3. Vyama huja na kuondoka lakini taifa linabakia.

Wanalopaswa viongozi wa Zanzibar kulizingatia ni kwamba macho ya waliowachagua yanawamurika na ni misimamo yao ndiyo itakayowaweka wanapostahili ku-wekwa katika historia ya visiwa hivi.

Hapa siwazungumzi wanasiasa wa CCM pekee bali hata wale wa chama cha CUF wenye kufikiria matumbo yao tu.

Namkumbuka mzee wangu mmoja aliyeniambia kuwa siasa ya mwongo ni uwongo, ya fatani ni fitna na ya mk-weli ni ukweli, lakini huu ukweli unahitaji ujasiri.

NIONAVYO

UNAWEZA PIA KULISOMA ZANZIBAR DAIMA ONLINE KUPITIA MITANDAOYETU YA KIJAMII

FACEBOOK/ZANZIBARDAIMALTD

Waziri wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee.

PAGE

48

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

49

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

48

Page 26: Zanzibar Daima Online Na. 04

Zanzibar ina uwezo wa kusonga mbele kwenye soka

Na David Kambona

Jambo moja nataka niliseme wazi kabla ya kuendelea na makala

haya. Mimi si Mzanzibari, ni Mtanzania kutoka Bara lakini linapokuja suala la kimaendeleo huwa siangilii nina asili ya wapi, bali huwa ninaangalia bara ninalotoka.

Nchi yoyote ile kutoka Af-rika nitaiunga mkono. Huwa naamini mimi ni Mwafrika na ninawajibika kuwasaidia Waafrika wenzangu. Huo ndio msingi wa kuandika kwangu.

Tena mimi huwa nasikia raha nikiwa Zanzibar hasa Bwawani au Forodhani kwa sababu katika seh-emu hizi ukipita huwezi kusikia mindundo ya muziki kutoka nje ya Zanzibar au muziki wa Kimagharibi hasa nyakati za usiku. Lazima utasikia muziki maridhawa wa Taarab.

Kwa kweli ipo haja ya kuan-za kuthamini vya kwetu haya mimi natoka Bara tena Mnyasa wa Mbabay Kwambe kijiji alichozaliwa mmoja kati ya viongozi wa Tanzania Oscar Kambona lakini ninaweza kuyaona haya Zanzibar.

Wazanzibari wengi wame-

kuwa wapweke sana kwa kunyimwa haki yao ya kimsingi ya kutaka kut-ambuliwa na Shirikisho la kimataifa la Soka Duniani (Fifa) huku wakipata nafasi ya uangalizi kwa kutambu-liwa na shirikisho la soka Afrika, CAF, kupitia chama cha soka cha nchi hiyo, ZFA.

Zanzibar inaweza kuviondo-sha vizingiti hivyo kiurahisi tena bila ta kutumia nguvu. Katika uongozi wa ZFA yapo mengi sana ya kimsingi yanayotakiwa kwanza yafanywe kabla ya kwenda kujiunga na FIFA.

Kwanza ni kuondoa mi-vutano isiyokuwa na tija yoyote kwa viongozi wa ZFA toka Unguja na Pemba kukaa pamoja na kugawana mambo ya kitaasisi nusu kwa nusu bila kujali ukubwa wa kisiwa kimoja au kingine. Soka ni mchezo unao-pendwa zaidi Zanzibar na ulimwengu kwa ujumla kwa sasa visiwa vya Unguja na Pemba Vinatakiwa kuijenga ZFA kuwa taasisi inayot-ambulika ndani ya Zanzibar bila kujali uwepo wa TFF kwa Tanzania ambayo ndiyo taasisi inayotambuliwa na FIFA, CAF.

Kwa kuijenga ZFA itatakiwa kutazama mifumo mipya ya

uendeshaji soka ya vyama vingine duniani hasa katika suala la kikatiba. Hiyo ni sehemu iliyo muhimu katika sheria ya chama chochote kile cha soka duniani. Hili ni jambo linaloweza kufanywa hata katika muda wa miaka mitatu au mitano. Jambo la pili baada ya suala la kikatiba, ZFA itatakiwa kukaa na vilabu vyote vina-vyoshiriki ligi ya Zanzibar bila kujali daraja, ili vijadil-iane aina ya mfumo wa ligi na aina ya uendeshwaji ligi ya Zanzibar.

Wakati huo huo, vilabu kwa kushiriakina na wadau wa soka wa Zanzibar wata-tikiwa kutazama ni jinsi gani wanaweza kutengeneza miundombinu ya soka ya Zanzibar ili iweze kutoa wachezaji wenye uwezo na vipaji vikubwa.

Ikiwa sasa ambapo Zanzi-bar haina hata ‘academy’ na wachezaji wake wana uwezo wa kucheza kwenye vikosi vya timu za Bara, je kukiwa na shule za soka itakuaje?

Ukiwa na shule nne - mbili Unguja na mbili Pemba – na zikawa na usimamizi mzuri, katika muda wa miaka 10 ijayo lazima tutaona moja katika ya vilabu vya Zan-zibar vinashiriki katika ligi

ya Mabingwa wa Afrika kwa hatua ya robo fainali.

Tunaweza sema kuwa soka ya Zanzibar inahitaji mageuzi ya kimsingi kwa kuitazama tena upya soka. Ninaamini inawezekana. Hata kama watu wanasema Zanzibar haitambuliki, ipo siku wata-itambua kwa kufungwa na Zanzibar, kwani hata siku Zanzibar ilipotwaa kombe la Challenge ninaamini ya kuwa Afrika ya Mashariki ilitambu-lika. Haiwezekani nchi kama Cape Verde na nyengine ndogo za visiwa zishiriki mashindano ya mataifa ya Afrika, lakini Zanzibar ishindwe. Kwa hiyo natoa rai yangu kuwa tuanze sasa kuutazama mfumo

wetu na tuurekebishe.

Tujiulize, je unaendana na FiFA, CAF, CECAFA? Kinachotakiwa kwa Zanzi-bar ni kusimamisha mchezo mmoja kwanza kama zili-vyo kwa nchi nyingine am-bazo zimediriki kusimamisha mchezo mmoja. Mfano ni ri-adha kwa Kenya na Ethiopia.

Kwa maana hii lazima tufe kwanza ili tufanikiwe sehemu tunayotaka kwenda. Haita-kuwa jambo rahisi kutaka kutambulika Fifa kama mambo ya msingi katika mi-chezo hatutayawekea misingi imara. Kwa Zanzibar ambayo imepata kutambulika japo sio rasmi katika CAF ukifanya majumuisho unaweza kuona kabisa ya kuwa bado hatu-

jafika katika kiwango hata cha kufuzu duru ya pili ya mashindano ya kimataifa .

Endapo tutatengeneza mis-ingi katika taasisi kubwa ya kimichezo kama ZFA na pindi itakaposimama yenyewe ndipo vyama vingine vinawe-za kusimama kwa kufuata usimamizi wa ZAF.

Mfano kwa sasa ukitazama kimiundo mbinu ya michezo hata uwanja wa Mao Tse Tung hauridhishi katika vi-wango stahiki vya kimataifa. Je, utaitaka vipi Zanzibar itambuliwe na Fifa wakati mambo yetu hayajakaa sawa?

MICHEZO

Kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar

PAGE

50

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

51

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

50