22
1 ZANZIBAR DAIMA ONLINE COLLECTIVE I TOLEO NAMBARI 08 DISEMBA 2013 Unaweza ku”scan codes hizi kukupeleka kwenye Mtandao wetu 43 Kurasa zimepangwa na HK DESIGNER Zanzibar Daima ONLINE DPP ANA KIBARUA KIGUMU KWA UAMSHO Kesi hiyo inawahusu masheikh 11 ambao wanasota gerezani 04

Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Jarida la kila Mzanzibari

Citation preview

Page 1: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

1

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

ZANZIBAR DAIMA ONLINE COLLECTIVE I TOLEO NAMBARI 08 DISEMBA 2013 Unaweza ku”scan codes hizi kukupeleka kwenye Mtandao wetu

43Kurasa zimepangwa naHK DESIGNER

Zanzibar Daima O N L I N E

DPP ANA KIBARUA KIGUMU KWA UAMSHOKesi hiyo inawahusu masheikh 11 ambao wanasota gerezani

04

Page 2: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

Zanzibar Daima Online

MHARIRI MKUUAhmed Rajab

Email: [email protected]

MHARIRI MSAIDIZIMohammed Ghassani

Email: [email protected]

MHARIRI MSANIFUHassan M Khamis

Email: [email protected]

MSIMAMIZI WA MAWASILIANOHassan M Khamis

WAANDISHIJabir Idrissa

Email: [email protected]

Othman MirajiEmail: [email protected]

Hamza RijalEmail: [email protected]

Mohamed AbdulrahmanEmail: [email protected]

Ally SalehEmail: [email protected]

WASAMBAZAJImzalendo.net

zanzibardaima.netzanzibardaima/facebook

MATANGAZOHassan M Khamis

Simu: +44 7588550153Email: [email protected]

WASIALIANA [email protected]

JARIDA HILI HUCHAPISHWA NAZanzibar Daima Collective

233 Convent WaySouthallUB2 5UH

Nonnstr. 2553119 Bonn

Germany

www.zanzibardaima.net

Timu Yetu

2

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

3

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

06 10

04 AHMED RAJAB Tunapaswa kuwasikiliza vijana wa leo

06 JABIR IDRISSA DPP anakabiliwa na kibarua kizito cha kuwabana UAMSHO

10 IBRAHIM HUSSEIN Muungano, Zanzibar na Watumwa Wawili

12 MOHAMMED ABDULRAHMAN Kwa la CHADEMA Vyama havichekani

16 ALLY SALEH Tusipime Maendeleo kwa Miradi ya Ujenzi

20JABIR IDRISSA Wazanzibari na hamu kubwa ya kujua ni kitu gani kimo ndani ya Rasimu mpya

18 DESIGNERS SPECTACULAR Lublium modiena, publibu nulescit, noviri prisIgno

24 MOHAMMED GHASSANI Sisi ni kizazi cha waliopundua na waliopinduliwa

28 FARREL JUNIOR Zanzibar inataka Muungano wa Heshima, Haki na Usawa

BURUDANI

30 TUFUNGUE KITABU Vuta N’kuvute kielelezo cha Uandishi wa Kizanzibari

34 HEKAYA ZA ZANZIBAR Meza fupa

38 LADHA YA BETI Nitabaki Zenjibari

39 LADHA YA BETI Lingekuwa la kujua

40MICHEZO Challange Cup: Mashujaa wa Zanzibar washindwa kabla ya Mashindano kuanza

12 16

20 24

YALIOMO>

Page 3: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

• Uchambuzi wa kina kutoka wa

waandishi wenye uzoefu

• Kwenye jarida hili Makala za uhakika

• Taarifa sahihi na sio za udaku

• Hakuna upendeleo, ni jarida lenye

kuandika habari za Zanzibar kwa asilimia 100.

Jiandikishe kwa kupitia ukurasa wetu wa Zanzibar Daima Collective kupitia mtandano wa kijamii wa Facebook.

ANUANI YETU NI

www.zanzibardaima.net

[email protected]

Jisajili kwenye “inbox” yetu ya Zanzibar Daima Online Collective kupata nakala

yako kwenye “email” yako

4

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

5

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

TUNAPASWA TUWASIKILIZE

HUU ni wakati muwafaka kwetu Wazan-zibari kutafakari. Tuyatafakari yaliyopita,

tuyatathmini na tujipangie yajayo. Tarehe 10 mwezi huu ilitimu miaka 50 tangu visiwa vyetu vipewe uhuru wake na Mwingereza. Tarehe 12 mwezi ujao itatimu miaka 50 tangu Mapin-duzi yaliyoing’oa kwenye madaraka Serikali ya kwanza ya Zanzibar huru iliyodumu kwa muda wa mwezi mmoja na siku mbili.

Matukio yote hayo mawili ni matukio makubwa katika historia yetu.

Tunavyoambiwa ni kwamba Zanzibar haijawahi kuwa koloni la Uingereza lakini tangu mwaka 1890 visiwa hivi vyetu vilikuwa chini ya himaya ya Uingereza mpaka tarehe 10 Desemba, 1963. Unaweza kuitafsiri hali hiyo kuwa labda Zanzibar ilikuwa dola huru ambalo Uingereza ikilihami.

Ukweli wa mambo unaonyesha hali nyingine. Ukweli huo unaonyesha kwamba tafauti baina ya kuwa koloni na kuwa himaya ilikuwa ndogo mno kama unyoya wa paka. Kwa kila hali Zanzibar ilikuwa ikitawaliwa kikoloni na Uingereza na ndio maana Sultan wa Zanzibar hakuwa na nguvu za kiutawala. Madaraka yote alikuwa nayo Balozi wa Uingereza aliyekuwa Zanzibar akiiwakilisha Serikali ya Uingereza. Hivyo, mtawala halisi wa Zanzibar alikuwa Mngereza.

Hii ndiyo sababu ya kwa nini wananchi wa Zan-zibar walisimama kidete kuupinga utawala wa Kiingereza na kudai uhuru wao. Mwamko wao wa kisiasa ulizidi kuhamasishwa na matukio yaliyo-zuka kwingine duniani baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Matukio hayo yalikuwa pamoja na hatua ya waza-lendo wa Indonesia ya kujitangazia uhuru mwaka 1945 na vuguvugu la kudai uhuru wa Bara Hindi (siku hizo Pakistan ilikuwa bado haijajiengua ku-toka Bara Hindi na hivyo hata hapajakuwepo Paki-stan ya Mashariki, ambayo baadaye nayo ilijitenga kwa nguvu na kuwa Bangladesh.)

Bila ya shaka mavuguvugu mengine ya kupigania uhuru yaliokuwa yakivuma kwingineko Afrika nayo pia yaliwahamasisha wazalendo wa Kizan-zibari waudai uhuru wa visiwa vyetu. Wazalendo hao wa Kizanzibari nao walianza kuwa na mavu-guvugu ambayo baadaye yaligeuka na kua vyama

kamili vya kisiasa vilivyosajiliwa rasmi na Serikali ya kikoloni.

Vikubwa miongoni mwa vyama hivyo vilikuwa vyama vya Afro-Shirazi Party (AS), Zanzibar Na-tionalist Party (ZNP), Zanzibar and Pemba Peo-ple’s Party (ZPPP) na Umma Party. Vilikuwepo pia vyama vingine vidogodogo kama vile Zanzibar Communist Party na Haki za Binadamu.

Vyama vyote hivyo viliudai uhuru wa Zanzibar. Hakuna hata kimoja kilichoiambia Uingereza isitoe uhuru. Kweli, kwa muda ASP kilikuwa na kaulimbiu ya ‘zuia’, ya kuitaka Uingereza iakhirishe tarehe ya kutolewa uhuru. Lakini kampeni hiyo ilidumu kwa muda tu na haikumaanisha kwamba kimsingi ASP ikipinga uhuru. Ndio maana uli-potolewa uhuru kiongozi wa ASP Sheikh Abeid Amani Karume aliukaribisha uhuru huo. Na alitoa hotuba iliyostahili kutolewa na kiongozi wa ha-dhi yake. Hakuiambia Uingereza kuwa hatuutaki uhuru endeleeni kututawala.

Bila ya shaka kuna waliohisi kwamba uhuru ulika-bidhiwa mikono siyo. Na hiyo ndiyo moja ya sa-babu za Mapinduzi ya Januari, 1964. Wazanzibari wa kizazi cha leo wanasema kwamba hawataki matukio hayo mawili ya Uhuru na Mapinduzi yaigawe jamii yetu. Wanasema kwamba wao ni “kizazi cha waliopindua na waliopinduliwa”. Wa-nachosisitiza ni mambo mawili. La kwanza, kuwa na umoja na la pili, kujifunza kutoka historia yetu ili tusiweze tena kutawaliwa. Hayo ndio maudhui ya makala ya Mohamed Khelef katika toleo hili. Ni hoja nzito na yenye nguvu ambayo sote tunapas-

wa tuisikize

Na Ahmed Rajab

TAHARIRI

>

Page 4: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

6

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

7

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

KIBARUA KIPEVU CHAMKABILI DPP KUWABANA UAMSHO

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar inacho kibarua kigumu cha kusuka au kunyoa kuhusiana na kesi yake dhidi ya masheikh wa Jumuiya ya

Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMUIKI) iliowapeleka mahakamani.

Kesi hiyo inawahusu masheikh 11 ambao wanasota gerezani kwa zaidi ya mwaka sasa wakikabiliwa na tuhuma za kuhatarisha usalama na kuharibu mali.

Masheikh hao wakiongozwa na Amir wao Sheikh Farid Ahmed Hadi, mkazi wa Mbuyuni mjini Zanzibar mwenye umri wa miaka 41, wana kesi mbili mahkamani wakidaiwa kuvunja Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwa-ka 1968 inayosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kesi nyingine ipo mbele ya hakimu wa wilaya kwenye Mahkama ya Mwa-nakwerekwe, mjini Zanzibar ambayo watuhumiwa walifanikiwa kupata dhamana lakini wakazuiwa kutoka rumande kwa amri ya Mkurugenzi wa Mashitaka wa Zanzibar (DPP), Ibrahim Mzee..

Masheikh wengine walio ndani ni Mselem bin Ali Mselem (52) wa Kwam-tipura, Mussa Juma Mussa (47) wa Makadara, Azzan Khalid Hamdan (48) wa Mfenesini, Suleiman Juma Suleiman (66) wa Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakar Suleiman (39) wa Tomondo, Ghalib Ahmada Juma (39) wa Mwanakwerekwe, Abdalla Said Ali (48) wa Misufini na Majaliwa Fikirini Majaliwa wa Magomeni.

Sheikh Farid Hadi

Viongozi wa UAMSHO, kutoka kushoto Sheikh Azzan Khalid, Sheikh Msellem Ali, Sheik Farid

>

Na Jabir Idrissa Zanzibar

Page 5: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

Wanakabiliwa na mashitaka matatu kwa pamoja ya kuharibu mali, kufanya uchochezi kwa kushawishi na kuhamasisha fujo, na kula njama ya kutenda kosa.

Sheikh Azzan ana shitaka moja zaidi la peke yake la kutoa ma-neno ya matusi kwa Kamishna wa Polisi Zanzibar yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Makosa hayo ambayo wote wameyakana, wanadaiwa kuy-atenda katika maeneo tafauti ndani ya Manispaa ya Mji wa Zanzibar, kati ya Oktoba 17, 18 na 19 mwaka jana. Wako gerezani kutokana na kuzuiwa kwa dhamana yao kwa kibali cha DPP Mzee.

Baada ya kesi zao kutajwa na kutajwa tena na tena, mojawapo iliyofika Mahkama ya Rufaa Tan-zania, jijini Dar es Salaam, kwa rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka wa Zanzibar, in-aanza kusikilizwa wiki hii na Jaji Mkuu Omar Othman Makungu.

Taarifa za ndani ya serikali na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashi-taka wa Zanzibar , zinasema kazi ngumu kwa Mkurugenzi huyo ndiyo inaanza sasa anapotakiwa kuwasilisha mashahidi.

“Sasa ndio kazi hasa inaanza. Unajua kesi hii baada ya kupig-wa danadana na serikali, im-efikia mahali pagumu kwa DPP kutoa ushahidi utaoiridhisha mahkama ili hatimaye watuhu-miwa wakutwe wanayo kesi ya kujibu.

“Tunaona wanavyohangaika kuingia katika hatua hii. Haraka-

ti nyingi kwelikweli, lakini ngoja muda ufike tuone wame-jiandaaje,” chanzo cha habari kimeliambia jarida la Zanzibar Daima Online.

Chanzo chetu kingine cha habari ni cha ndani ya Polisi am-bako inasemekana kwa wiki kad-haa askari wa upelelezi wame-kuwa wakiitwa na kujasirishwa watoe ushahidi mahkamani.

“Haitazamiwi kama watakuwa na mashahidi wasiokuwa askari polisi. Tunawaona baadhi ya raia wanaingia ofisi ya upele-lezi lakini sijasikia kama wapo watakaopandishwa kizimbani kutoa ushahidi,” kilisema chanzo hicho.

Jarida hili lilipouliza iweje wako-sekane raia wa kutoa ushahidi ilhali matukio ya fujo wakati ule yalitendeka mitaani na kush-uhudiwa na wananchi mbal-imbali, chanzo hicho kilisema “nadhani wanahofia migogoro ya mitaani.”

Siku zote wanafalsafa wanapo-zungumzia dhana ya utawala wa sheria katika nchi zenye demokrasia changa, husema kuwa kesi ya jinai inapofikia hatua ya kusikilizwa ndipo uta-baini ushujaa wa serikali iliyoko madarakani.

Hata baadhi ya majaji wenye ujasiri, mara nyingi hutamka kauli kama hii kuhusu usikili-zwaji wa kesi za jinai, hasahasa wakati wa kusoma hukumu za kesi.

Aliwahi kueleza haya jaji aliyesikiliza kesi ya maofisa wa

polisi walioshitakiwa kwa ku-tuhumiwa kuwaua wafanyabi-ashara wa madini wa Mahenge, mkoani Morogoro, pamoja na dereva wa jijini Dar es Salaam, aliposema hapakuwa na usha-hidi wa kuwatia hatiani watuhu-miwa.

Alisema upande wa mash-taka ulishindwa kutoa ushahidi madhubuti, au ulitoa ushahidi dhaifu usio na nguvu za kisheria. Akitangaza kuwaachia watuhu-miwa wote kwa sababu hiyo ya kukosekana ushahidi, jaji alisema anataka serikali imsake ofisa wa polisi aliyejulikana ku-tenda mauaji hayo ili apelekwe mahkamani.

Kulingana na ushahidi uli-otolewa mahkamani na zaidi ya mashahidi kumi, ilionekana yule askari aliyekuwa na bun-duki wakati wa tukio, na kuify-atua na kuua wafanyabiashara waliotajwa, hakukamatwa na kupelekwa mahkamani, bali waliopelekwa hawakuhusika maana hakukuwa na ushahidi uliowabana.

Hata katika hukumu ya kesi iliyomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanza-nia, Sheikh Ponda Issa Ponda, Hakimu Nongwa, alisema kesi ikishafunguliwa kazi inayobaki mbele yake ni kuwasilishwa ushahidi wa nguvu kuishawishi mahkama kuwapata na hatia washitakiwa.

“Hapa nataka kuieleza ofisi inay-osimamia ushahidi, kwamba kazi inabaki kwao kuleta ushahidi imara utakaoiridhisha mahkama kuwapata na hatia washitakiwa.

Siyo wanaleta kesi hapa halafu wanaingia mafichoni wakitu-mainia mahkama iwafunge washitakiwa. Hii mahkama inafuata sheria,” alisema Hakimu Nongwa.

Katika kesi hiyo ya tuhuma za uchochezi na wizi wa malighafi za kampuni ya Agritanza ze-nye thamani ya Sh. Milioni 59, Sheikh Ponda alihukumiwa ki-fungo cha nje cha mwaka mmoja baada ya kukaa gerezani karibu mwaka mzima.

Alikutwa na hatia ya kuingia kwa jinai kwenye kiwanja cha Chang’ombe Markaz, kina-chodaiwa kumilikiwa na kam-puni hiyo ya Agritanza na amba-cho utata wake wa umiliki ndio sababu kukamatwa kwa Sheikh Ponda na Waislamu wengine.

“Mahkama inawaachia huru washitakiwa wengine 49 baada ya kukosa kuwatia hatiani kwa makosa matano yote waliyoku-wa wakishtakiwa nayo. Sababu ya kuwaachia ni upande wa Jamhuri kushindwa kuleta usha-hidi wa kuishawishi mahkama iwaone wana hatia na kwamba upelelezi uliofanywa na Jeshi la Polisi katika kesi hiyo ni dhaifu na kwamba mahkama haiwezi kumfunga mtu kwa ushahidi wa hisia tu,” alisema Hakimu Non-gwa.

Sheikh Ponda na wenzake 49 kwa mara ya kwanza walifik-ishwa mahkamani Oktoba 18, mwaka jana, muda unaofanana na walipokamatwa masheikh wa Uamsho. Walikamatwa wakati kukiwa na harakati nyingi za viongozi wa taasisi za Kiislamu

kupigania haki za Waislamu zikiwemo za kikatiba.

“Hali kama hii inaweza ku-wakuta serikali wakati wa usikilizaji wa kesi. Mashitaka waliyowafungulia masheikh ni mazito yanayohitaji ushahidi uliotimia na sio wa kubahatisha. Hichi ndo kitu muhimu kina-chotarajiwa kutoka kwa DPP,” amesema mtumishi ndani ya Ofisi ya Wizara ya Katiba na Sheria ya Zanzibar.

Mwanasheria mmoja wa Zanzi-bar aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, amesema shtaka la kuhatarisha usalama ni gumu kulithibitisha ambapo mwendesha mashitaka atatakiwa kueleza kwa ufasaha namna wale anaowatuhumu walivyohusika kuhatarisha usalama.

Masheikh wa Uamsho wa-likamatwa katikati ya mwezi Oktoba mwaka jana mara tu Sheikh Farid alipoibuka baada ya kutoonekana kwa siku tatu mfululizo.

Kuibuka kwake kulizusha mjada-la mkali huku viongozi wenzake wa Kiislamu wakishinikiza Jeshi la Polisi litoe taarifa kwa kuwa hicho ndicho chombo mah-susi cha nchi chenye jukumu la kusimamia na kuwahakikishia raia ulinzi na usalama wao na wa mali zao.

Hata hivyo, badala yake Polisi , walimtaka Sheikh Farid afike kituoni na kueleza alikokuwa.

Viongozi wakuu wa Polisi wa-likanusha tuhuma kwamba

Sheikh Farid alitekwa na wa-nausalama na kufichwa kusiko-julikana, isipokuwa wanasema alijificha makusudi ili kuisingizia uovu serikali.

Sheikh Farid aliitika wito wa Kamishna wa Polisi Zanzibar (ZCP), Mussa Ali Mussa kuripoti Makao Makuu ya Polisi yaliyo Mwembemadema, ambako alihojiwa.

Hakupewa dhamana, badala yake waliendelea kumshikilia hadi walipompeleka mahakam-ani kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwa nia ya kuzusha tafrani kati ya wananchi na seri-kali yao.

Kutoka hapo, Polisi wakawa wanamwita sheikh mmoja baada ya mwengine na waliwaita hata watumishi wa ofisi ya Uamsho.

Sheikh Azzan amekuwa nje kwa dhamana tangu mwezi uliopita baada ya kuruhusiwa na Mahka-ma Kuu kusafiri nchini India kwa ajili ya matibabu. Amekuwa akiumwa figo ambazo zimeota vijiwe, hali iliyomzidia akiwa gereza la Kiinua Miguu, Kilimani, mjini Zanzibar.

Uamsho ni taasisi kama taasisi nyingine za Kiislamu zinazo-fanya kazi kwa mujibu wa sheria baada ya kusajiliwa rasmi. Kwa sehemu kubwa Uamsho ilisaid-iwa na Ofisi wakilishi ya Uba-lozi wa Marekani iliyopo mjini Zanzibar, katika kupata vifaa na samani za ofisi yake iliyopo mtaa wa Mkunazini, na kuiwezesha

kusajiliwa mwaka 2003

8

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

9

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

Page 6: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

mkoloni wa Kireno aliyekuwa ka-tili laisalkiasi.

Ni bahati mbaya kwamba, miaka zaidi ya 150 baada ya kumshinda mkoloni wa Kireno, walikuja Wao-mani wengine, chini ya Sultan Said al-Busaid, kuja kuweka himaya ya utawala.

Hii ni bahati mbaya iliyoikumba Zanzibar na ambayo ilijirejea tena baada ya mwaka 1964 pale baadhi ya Wazanzibari walipokwenda ku-waomba msaada watu wa Tangan-yika kuipindua serikali iliyoundwa baada ya uchaguzi wa 1963. Baa-da ya Mapinduzi hayo ya Januari 1964, Watanganyika nao waka-bakia na kuitawala Zanzibar hadi sasa, miaka 50.

Kama ambavyo kuna Waomani waliouawa wakati wa kumwondoa mkoloni wa Kireno na kuukomboa upwa wa Afrika ya Mashariki, kuna pia Watanganyika waliopoteza maisha yao wakati wa Mapinduzi ya 1964 kwa ajili ya kuiondoa seri-kali na ufalme kwa wakati mmoja.

Hilo linasema kwamba mahusiano baina ya Mzanzibari na Muomani hayawezi kudhalilishwa kama vile ambavyo haifai kuyadhalilisha ma-husiano kati Mzanzibari na Mtan-ganyika.

Lakini vile vile halisemi kwamba Zanzibar haipaswi kuwa huru inay-otawaliwa na watu wake wenyewe – kando ya ushawishi wa Kiomani na wa Kitanganyika. Wala halisemi kwamba mtu hawezi kuwa Mzan-zibari kwa kuwa ana asili ya Kio-mani au ya Kitanganyika.

Hapana. Ukiangalia na kutafakari kauli za wanasiasa katika madai ya usultani, utumwa, utwana, ubwa-na, uarabu na uungwana ndani ya siasa za Tanzania, utakuta hakuna pengine popote maneno yanapo-

tumika isipokuwa kwenye vinywa vya viongozi wanaotumiwa ku-pandikiza fitna, majungu, ubaguzi na chuki dhidi ya wale wanaojiita Wazanzibari.

Viongozi hawa wanatumiwa ku-haribu mahusiano yaliyopo baina ya makabila mbalimbali kwenye nchi na pia baina ya nchi na wa-tawala wa zamani. Lakini hilo lina-fanyika kwa upande wa Zanzibar tu, tena dhidi ya Waarabu na wa-tawala wa Kiomani tu.

Sio Tanganyika, ambayo chini ya utawala wa Kijerumani na baa-daye wa Kiingereza, watu wake waliteswa, kufungwa jela na ku-jengeshwa njia za reli kwa mijeledi, huku wengi wao wakifa kutokana na mateso na madhila waliyoyapa-ta. Huko kila mwaka husherehek-ewa uhuru wa tarehe 9 Desem-ba, lakini hatukuwahi kumsikia Mwalimu Julius Nyerere wala waliomfuatia kwenye utawala ku-walaani au kuyakumbusha yale waliyoyatenda Wajerumani na baadaye Waingereza wakati wali-poitawala Tanganyika.

Nimalizie kwa hoja kwamba un-apolinganisha madhara ya bi-ashara ya watumwa na biashara ya kuuza nchi, basi ya kuuza nchi ni mbaya zaidi, maana inachuku-wa kila kitu. Hii inawafanya wote waliomo ndani ya nchi iliyouzwa kuwa watumwa, wakitafautiana baina yao kwa kutumia ule mfano wa Mtumwa wa Nyumbani na Mtumwa wa Mitaani kama ulivyo-tolewa na Malcom X, mwanaha-rakati wa haki za weusi nchini Marekani.

Mtumwa wa Nyumbani anaishi katika nyumba na bwana wake. Anavaa na anakula vizuri zaidi kul-inganisha na wa Mtaani kwa kuwa yeye hula na kuvaa makombo ya bwana wake. Analala humo humo

ndani ya nyumba ya bwana wake ingawa yeye hulala sakafuni. Huyu humpenda bwana wake kuliko hata huyo bwana anavyojipenda mwenyewe.

Mtumwa huyu hudiriki hata kuji-tolea maisha yake ili kulinda nyum-ba ya bwana wake tena kwa moyo mkubwa kuliko hata huyo bwana mwenyewe. Kama bwana wake akisema: “Tuna nyumba nzuri hapa“, basi mtumwa huyu atarukia haraka “Kweli bosi tuna nyumba nzuri.” Kila wakati ambapo bosi hutumia sisi na yeye hatosita kutu-mia neno hilo.

Kama nyumba ya bwana imeshika moto, Mtumwa wa Nyumbani ana-kimbilia zaidi kuuzima moto kuliko hata mwenye nyumba mwenyewe. Kama bwana akiumwa, utamkuta mtumwa wake anaumia zaidi ku-liko bwana mwenyewe, maana kila wakati hujifanya kumtambua bosi wake zaidi ya bwana wake anavyo-jitambua mwenyewe.

Mtumwa wa Mitaani anapomtem-belea mwenzake wa ndani kumua-sa watoroke, anamkuta Mtumwa wa Nyumbani anamuangalia kwa jicho la mshangao na kusema: “He! Una wazimu? Una maana gani una-vyosema tutoroke? Wapi nitakaa katika nyumba nzuri kama hii? Wapi nitavaa nguo nzuri kuliko hizi? Wapi nitakula kizuri kuliko hiki?“

Huyo ndiye Mtumwa wa Nyum-bani, ambaye bado tunaye humu ndani ya visiwa vyetu hivi sasa. Anaipenda nyumba ya bwana wake (Muungano) kuliko ana-vyoipenda yake (nchi yake ya Zanzibar). Na kama mwenzake akija kumshauri kuondoka kwenye nyumba hiyo, humuuliza kwa ukali: “Unamaanisha nini kusema tutoke katika Muungano? Muungano huu ni mzuri wa Waafrika“

10

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

11

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

Muungano,Zanzibar na watumwa wawili

Na Ibrahim Hussein Makala Maalum

MAKALA ya Mohamed Seif Khatib kwenye gazeti moja

la kila Jumapili lililotoka tarehe 13 Januari mwaka huu, ilibeba kichwa cha habari kisemacho “Si Njozi“, ikijenga hoja ya unyama na ubaya uliofanywa na gengi la ukoo wa kinyonyaji la watu wa Oman.

Mwandishi anaelezea namna Oman ilivyowanyonya Wazanzi-bari na kuwadhalilisha wenyeji wa visiwa hivi, huku akishadidia kwamba baya zaidi kuliko yote ni ile biashara ya kuuza watu, yaani biashara ya utumwa.

Lengo hasa la mwandishi lilikuwa ni kuwafahamisha vijana wa leo, kwani walikuwa hawajui wala kuy-aona yaliyotokea nyuma, si njozi. Ndio maana anawauliza vijana hao ikiwa wanajuwa kuwa wapo watu wakiitwa watumwa, watwana na masuria?

Kujaribu kukumbusha mambo ya Waomani na usultani, utumwa na Uarabu katika milenia mpya ni ubutu wa mawazo ya siasa au ufinyu wa dhamira ya historia ya mambo hayo.

Mtu anaweza akajiuliza, inaku-waje mwandishi huyu, ambaye ni kiongozi na mwanasiasa aliyeshika nafasi kadhaa kubwa serikalini, akaweza kuandika mambo am-bayo yanaweza kuleta chuki baina ya watu wa Visiwa hivi ambao wengi wao wamechanganya damu na watu wa Oman tokea zamani?

Si dhamira ya makala haya kusema kwamba utawala wa Kiomani visi-wani Zanzibar ulikuwa wa malaika wasiofanya uovu. Hapana, lakini mantiki inatulazimisha kuandika mambo kwa mizani.

Unapomuelezea kijana wa leo maovu ya utawala huo, basi pia

unapaswa kumueleza na mema yake – kama unataka kuyaona – na kama hutaki kuyaona, basi angalau kumuelezea kwamba utawala huo ulioitwa wa Kiomani ulikuwa na msingi, asili, na mjengeko gani.

Lakini pia ni busara zaidi kutengan-isha baina ya Waomani watawala, kwa maana ya ukoo wa Busaidi na wenzao, na Waarabu wengine walioingia kwenye upwa wa Afrika ya Mashariki karne kadhaa kabla ya hata majilio ya utawala wa Ki-busaidi, na hata ambao walikuja baada ya hapo, lakini hawakuwa kabisa sehemu ya utawala.

Ama mimi nibakie huko huko kwenye hao watawala na uovu na wema wao kwa Visiwa hivi. Wao-mani kama watawala hawakujileta wenyewe kwenye upwa wa Afrika ya Mashariki, bali waliitwa na we-nyeji wa eneo hilo katika karne ya 16 kuwasaidia kupambana na

>

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akimvisha nishani ya utumishi uliotukuka Bwana Mohammed Seif Khatib

Page 7: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

MIAKA iliyopita baada ya kuru-di mfumo wa vyama vingi nchini Kenya   mwanzoni mwa miaka ya 1990, misukosuko ilianzia ndani ya chama tawala cha KANU chini ya uongozi wa Rais mstaafu Da-niel Arap Moi. Chanzo kilikuwa ni kuhojiwa na wanasiasa vijana kwa uamuzi wake wa kutaka mrithi wa kiti chake awe Uhuru Kenyatta.

Wanasiasa hao walitaka mgom-bea apatikane kwa njia ya uchagu-zi wa kidemokrasi ndani ya chama. Kundi lililopinga mkakati wa Moi,“ liliongozwa na wanasiasa mahiri, Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na William Ruto na kujienguwa kwao na kuunda chama cha Libe-ral Party baadaye kulifungua njia ya kuibuka vyama vyengine.

Yaliofuata baadaye ni marefu,laki-ni la kusisimua na kuwashangaza Watanzania ulikuwa ule mtindo wa wanasiasa kuhama kutoka upande mmoja kwenda mwengi-

ne na hasa wanapokosa nafasi ya uongozi.

Miaka  ya karibuni  yale yaliokuwa yakitushangaza kuhusu Kenya ya-mevisibu vyama vyetu vya kisiasa Tanzania. Wingu lililotanda hivi karibuni, ni uamuzi wa Kamati kuu ya Chama kikuwa cha upin-zani Chadema kuwavua nyadhifa zao viongozi wawili Zitto Zuberi Kabwe, aliyekuwa Naibu Kati-bu Mkuu, na mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo.

Walishutumiwa kula njama za kukivuruga chama. Matukio haya yamesababisha gumzo kubwa li-naloendelea sio tu miongoni mwa wanachama na wapenzi wa Cha-dema bali hata wa vyama vyengi-ne na wale wasio na vyama. Kub-wa katika kadhia hii ni suala zima la demokrasia.

Kilichowachongea kina Zitto ni

ule unaoitwa waraka wa siri wa kukihujumu chama. Waraka huu unasemekana ulikuwa na mkakati wa kundi hilo kujipanga kwa ucha-guzi wa chama 2014 pale uongo-zi wa sasa utakapomaliza muda wake.

Inasemekana wahusika wamekiri kuwa waliandaa kitu kama hicho, lakini mtu unajiuliza kuna ubaya gani kwa sababu makundi katika vyama ni sehemu ya karata za ki-siasa. Hivi ni kusema kuwa upin-zani ndani ya chama cha kisiasa ni jambo la kawaida, huibua hoja za kujadiliwa ili kuweka msingi wa makubaliano na hiyo ndiyo demo-krasia na kinyume cha hayo si kin-gine bali ni udikteta.

Kwetu si mapya

 Mtikisiko ndani ya Chadema unaotajwa kuwa mzito tangu kil-ipoundwa miaka 20 iliopita hata hivyo si kitu kipya katika siasa za

Tanzania. Haya yametokea takri-ban katika vyama vyote.

Ndani ya chama cha CCM,tuta-kumbuka jinsi Rais wa awamu ya pili wa Zanzibar Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi alipolazimishwa na kamati kuu ya CCM, chini ya Mwalimu Julius Nyerere, kujivua vyeo vyote 1984 kutokana na kile kilichoelezwa ni „ kuchafuka hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar,“ alipohoji mfumo wa Muungano. Kuna kadhia pia ya kufukuzwa CCM, Maalim Seif Shariff Hamad, na kundi lake la watu sita.

Baadaye ul-i p o a n z a m f u m o w a

KWA LA CHADEMAVYAMA HAVICHEKANI

Na Mohamed Abdulrahman Nionavyo12

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

13

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

Page 8: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

vyama vingi    wimbi   likakikum-ba chama   cha NCCR-Mageuzi kilicholeta msisimko na kukitia homa CCM wakati wa uchaguzi wa 1995. Chama hiki kilichokuwa kikiongozwa na Augostino Mre-ma aliyejitoa CCM kiliandamwa na mgogoro na uchaguzi uliofua-ta kikaporomoka kikipoteza hata idadi ya wabunge. Kilifufuka baa-da ya uchaguzi wa 2010.Kuen-guliwa wanasiasa kadhaa katika kura za maoni wakati wa kutafuta wagombea kwa uchaguzi chama-ni au kitaifa ni mtindo  wa  takri-ban vyama vyote vyenye uwaki-lishi bungeni. Kuna sababu  mbali mbali zilizotajwa iki-wemo ya  uki-ukaji wa maadili na mwongozo wa chama.

Lakini  kumekuweko na  matukio ya kutengwa  na hata kufukuzwa kwa  sababu tu wamediriki kupin-ga au kuhoji utendaji wa viongozi wa ngazi ya juu.

Baadhi ya hao walikimbilia vyama vingine vikawasimamisha kwenye uchaguzi na wakashinda. Mfano mmoja katika  CCM ni kuondo-lewa jina la baadhi ya wagombea walioshinda katika kura za maoni katika majimbo yao, dharuba ili-omkumba  John Shibuda aliyeji-unga na Chadema na  ikamsima-misha katika jimbo lake  la Maswa magharibi Mkoa wa Shinyanga na akashinda. Pamoja na hayo hata huko Chadema nako ukosoaji wake umemponza mara kadhaa, kiasi cha kuambiwa anakisaliti chama kwa manufaa ya CCM ali-kotoka.

Walio Zanzibar hawana tafauti.

Vyama vikubwa ambavyo vina mvutano Zanzibar na bara ni CCM na CUF, ingawa Cha-dema kinabakia kuwa cha-ma kikubwa na kiongozi wa upinzani katika Bun-ge la Muungano. Janga ninalolizungumzia ha-likuwabakisha CCM na CUF visiwani.

Chama Cha Wananchi (CUF) Ki-liingia kwenye mgogoro na baad-hi ya watendaji wake akiwemo mbunge wa jimbo la Wawi Pemba, Hamad Rashid Mohamed , waka-ti aliyekuwa kiongozi wa Umoja

wa vijana „ Blue Guards“ Said Miraji alipotangaza kujitoa na kuanzisha chama chake De-mocratic Alliance. Hamadi alifukuzwa na kwenda maha-

kamani.

Mahakama iliamuru utaratibu haukufuatwa na kuwa aendelee kuwa mbunge. Hamadi anaen-delea kuwa bungeni lakini CUF hamtambuwi kuwa ni mwanacha-ma wao.

 

Agosti mwaka huu,CCM Zanzi-bar nayo  ilimfukuza mwanasiasa  anayeinukia  Zanzibar  Mansur  Yussuf Himidi kwa sababu ya  msimamo wake kuhusu  Muunga-no akiunga mkono muungano wa mkataba, kinyume na  msimamo wa chama chake. 

Ni dhahiri  yaliyomsibu Himidi aliyepoteza  kiti chake cha Kiem-be samaki yalitokana na  shinikizo la wahafidhina Zanzibar walio-kuwa na sababu zao za binafsi, kwani kuna viongozi kadhaa kati-ka CCM pande zote mbili za  Mu-ungano  wenye misimamo tafauti na chama katika suala hilo na ha-wakuathirika hata kidogo. Kiroja cha mambo Mwenyekiti  Jakaya Kikwete alitamka kuwa   kila mtu

ana uhuru wa kuuzungumza Mu-ungano katika kipindi hiki

ambapo Tanzania imo katika mchakato wa

Katiba mpya.

 

Wanasiasa wengi wanaonekana kuwa

na uwoga unaotokana na  hofu ya kuhatarisha ma-

silahi yao. Hali hii itaendelea hadi pale utaratibu mzima wa  demo-krasia utakapokuwa nguzo  katika maamuzi ndani ya vyama vyote vya  kisiasa. Kama viongozi wana nia ya dhati ya kujenga demokra-sia basi  hapana budi paweko na  utaratibu wa kutumia njia za kide-mokrasia kufikia uamuzi katika masuala yanayohusika na muhi-mu ni kuwepo na uwazi na kuvu-miliana. Kinyume chake  vyama vitaendelea kuidumaza demokra-sia vikiendelea kuimba nyimbo hiyo na kucheza udikteta.

Yanayoendelea Chadema yana-weza kuwa na athari si kwake tu lakini kwa jukwaa zima  la siasa nchini Tanzania Kwa ujumla   la Zitto na Dr Kitila ni muendele-zo tu wa  visa na matukio ya kila wakati ndani ya vyama. Viongo-zi  hawana budi kufahamu vyama si mali ya mtu zaidi ya wanacha-ma na kama lilivyo taifa kwa raia wake, wanachama ndiyo wenye mamlaka ya vyama na ndiyo waa-muzi. Takriban vyama vyote vina wanasiasa vijana wenye mvu-to   na kama si mkubwa   basi wa kiasi fulani kwa wapiga kura.  

Pana wajibu mkubwa wa kuwalea vijana hawa pamoja na kutele-za  baadhi  ya wakati, kwani ni rasilimali kama viongozi  wa siku zijazo. Hili lisiangaliwe kwa ma-tazamo wa itikadi za kichama bali

masilahi ya  taifa

14

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

15

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

MATANGAZO YA BIASHARANunua nafasi hii kuweka matangazo yako ya vifaa uuzavyo kama mfano wa hapa chini

JINA LA BIDHAA

Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

JINA LA BIDHAA

Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

JINA LA BIDHAA

Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

JINA LA BIDHAA

Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

JINA LA BIDHAA

Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

JINA LA BIDHAA

Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

JINA LA BIDHAA

Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

JINA LA BIDHAA

Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

JINA LA BIDHAA

Na Maneno yasiozidi kumi ya kutoa wasifu wa bidhaa yako.

Page 9: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

TUSIPIME MAENDELEO KWA MIRADI YA UJENZI

KUANZIA sasa na kwa mwezi mmoja ujao Zanzibar

itakuwa na “fete” ya Mapinduzi. Hizi ni sherehe za kuadhimisha miaka 50 tokea kuondoshwa kwa Sultan wa Zanzibar au kwa lugha sahihi zaidi kupinduliwa Ufalme au Mfalme am-baye alikuwa mtawala wa Zanzibar.

Mapinduzi hayo yalifanywa mwezi mmoja tu baada ya Zanzibar kupata uhuru wake kutoka kwa Waingereza ambao ndio waliokuwa na mamlaka halisi ya Zanzibar na sio Mfalme.

Uhuru huo wa Desemba 10, 1963 umekuwa hoja kubwa ya kisiasa na hata kiitikadi na umeigawa Zanzibar lakini vyovyote iwavyo kwa uhuru huo Zanzibar ilipata kiti chake, na hata kukikalia, katika Umoja wa Mataifa.

Zanzibar imefanya sherehe nyingi za kuadhimisha Mapinduzi na hii ya Januari 12, 2014 itakuwa ni ya 50. Na kila baada ya miaka 10 zimeku-wa zikifanywa sherehe kubwa kwa kufurahia kuingia muongo mpya na

Na Ally Saleh Barza ya Jumbamaro

16

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

17

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

>

Page 10: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

kusonga mbele kwa nchi.

Mara nyingi pia sherehe hizo zimekuwa zikitumika kupima hatua za maendeleo zinazopigwa. Mara zote hatua hizo za maende-leo zinapimwa kwa kuangalia idadi ya nyumba zilizojengwa na serikali, au hospitali, barabara au viwanda vilivyojengwa. Hapo ndipo kipimo chetu cha kusonga mbele huwekewa alama.

Kwa hivyo kila sherehe ya mwaka mmoja, muongo mmoja na sasa miaka 50 tunapima maendeleo yetu kwa kutizama tumejenga nini, kikubwa gani, wapi na kad-halika. Kwa fikra zangu kwa muda wote tumekuwa tukipima sivyo.

Kwanza, kwa sababu mara nyingi miradi kama hiyo haiwi ni matak-wa ya wananchi kwa sababu hawaulizwi wala hawashauriwi na kwa hivyo kama tutarudi nyuma kutizama miradi hiyo basi pengine tunaweza kuona kuwa

mingi yao ama imekufa, haiku-songa mbele au imewekwa kando na wananchi.

Pili, miradi hii hutumia fedha ny-ingi na tunaweza kusema kjuwa wakati wa ujenzi huwa ni wakati wa manufaa kwa wengi serika-lini maana ununuzi wa vifaa vya ujenzi huo hauna udhibiti mad-hubuti na kwa hivyo inawezekana kinachopatikana hakiakisi tha-mani halisi ya fedha.

Miradi ni muhimu lakini si vyema kutumika kuwa ni kipimo pe-kee cha maendeleo hasa iwapo miradi hiyo hutumika kuwa ni sehemu ya sherehe. Tumeona hili linavyokosa kina pale kwa mfano Mwenge wa Uhuru ulipotumika kwa dhana hiyo hiyo na wananchi kulikataa hilo.

Swali langu katika hili ni vipi wananchi au Wazanzibari wa-nashiriki katika sherehe hizi mbali ya kuhudhuria sherehe

zinazosimamiwa na viongozi za kufungua au kuzindua miradi ka-tika maeneo yao, miradi ambayo wao hawakuulizwa lakini imeota maeneo yao au imeshushwa kama Manna na Salwa.

Ni vipi umma au mwananchi mmoja mmoja atapewa au amepewa nafasi ya yeye kutoa tathmini yake ya Mapinduzi toka yalipoanza hadi leo ili aweze kweli kueleza ni vipi amefaidika, wapi amepunjwa na kwa hivyo ni kitu gani anataka miaka 50 ijayo.

Ningependa kujua wakati tuk-isherehekea mbali ya kujipima kwa majengo na miradi tunapima vipi hisia, hamasa na mapenzi ya kizalendo ya wananchi wetu tukielekea miaka mengine 50 ya Mapinduzi ambayo ni migumu na yenye majaribu zaidi.

Tumeanza 1964 tukiwa na utawala wa Kimapinduzi na wa chama kimoja, imefika wakati

tukarejelea kuwa na vyama vingi japo shingo upande mwaka 1992 lakini hakuna dalili kuwa mfumo wa vyama vingi utaondoka tena hapa kwetu.

Na pia kwa upande mwengine tu-lianza kuwa na Serikali ya Muun-gano hapo mwaka 1964 ukiwa na Serikali mbili. Serikali hizo ni ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndani yake imo na imekuwemo Serikali ya Tanganyika, mfumo ambao umeleta changamoto nyingi.

Wakati tukiadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi mfumo huo wa Serikali mbili ndani ya Muungano hauelekei tena kuwa na sababu, mashiko wala hoja na kwa hivyo kuna uwezekano wa Muungano sasa kuwa wa Serikali tatu.

Pia kumekuwa na mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa nchi baada ya viongozi na vyama

vya siasa kuchoka na magomvi na hivyo kuamua kukubali kuwa Zanzibar iendeshwe kwa mfumo wa muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Tumekuwa na kizazi cha pili sasa cha mapinduzi na tunaelekea kuwa na kizazi cha tatu na kwa hivyo kuna zaidi ya nusu ya Wa-zanzibari ambao hawakuyaona kabisa Mapinduzi hayo na kwa hivyo kiungo chao na Mapinduzi hayo ni taarifa wanazozipata na fursa yao ya kusoma.

Kwa hivyo ni fikra zangu kuwa sherehe hizo hazitanoga kwa kufungua na kufunga miradi tu. Itakuwa ni kosa kubwa kutochu-kua bidii yoyote ya kuhimiza na kuchapuza mijadala mbali mbali ya watu wa umri na fikra tafauti.

Kuna haja ya sauti za watu kusikika ili watoa mawazo yao, waeleze hisia zao, watamke vipa-umbele vyao, waeleze wanata-

kaje kutawaliwa, kama ni vijana waeleze matarajio yao, waseme wanataka nini ndani ya Muunga-no na iwapo kutakuwa na mab-adiliko ya muundo wa Muungano pia wajue wataongozwaje katika zama mpya.

Miaka 50 imepita ni zama nzima, na sasa zama mpya zinaanza. Si vyema, si sahihi na si halisi kuingia katika zama mpya bila ya watu kujitizama upya. Ni kwa kujitizama ndipo watapojiona  na watasema wanatakaje Zanzibar yao iwe.

Wenye sauti ya kusema wanaita-ka Zanzibar ielekee wapi, kwa kasi gani na kwa faida ya nani. Wao ni wenye nchi na Serikali haina njia isipokuwa kuwasikiliza, la sivyo sherehe zitaishia kuwa

sherehe tu

19

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

18

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

Page 11: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba, alieleza mbele ya hadhara ya watu walioshuhudia akitangaza rasimu ya awali ya Katiba kwenye viwanja vya Karimjee, mjini Dar es Salaam, kwamba waliotaka serikali ya mkataba ni wengi na walikuwa na hoja nzito.Sawasawa kabisa. Wazanzibari walio wengi wanatarajia rasimu itakayotoka wakati wowote kuan-zia wiki ijayo, itatambua mahitaji yao hayo ya kuletewa mfumo wa Muungano wa Mkataba.Tume ilishakengeuka kilio hichi cha kupatikana Muungano wa Mka-taba, lakini Wazanzibari hawataki kuamini hata chembe kuwa tume itabadilisha msimamo iliouridhia kwa kueleza katika rasimu ya awali kuwa mfumo wa serikali tatu ndani ya Jamhuri ya Muungano haukwe-peki.

Nasema kwa ufasaha kuwa wana-chokitaka pasipokuwa na Muun-gano wa mkataba, angalau rasimu ijayo iridhie kwamba Katiba ita-kayopelekwa mbele ya wananchi kwa ajili ya uamuzi, itakuwa ni ile inayotandika msingi wa kuwepo kwa serikali ya Tanganyika, baada ya zile mbili wanazoishi nazo.Kwa maana hiyo basi, ni matara-jio ya Wazanzibari kuwa Tume haitafinya macho kwa kutimiza ahadi yao hiyo, hata kama wana-tume wanajua kwa asilimia zote watakorofishana na wakuu wa CCM.Chama hichi kinachoshika dola tangu uhuru, viongozi wake wame-jitia pamba na kutaka kung’ang’ania mfumo wa serikali mbili, kama vile wamethibitisha utaleta maajabu ya kuuinua uchumi wa Zanzibar un-aoaminika unaathiriwa na chusha

za mifumo ya kodi ya Muungano.Kujitegemea na kupata mamlaka ya kujenga uchumi wake kwa mipango yake yenyewe, ndio hasa kilio cha Zanzibar kwa sasa, kama ilivyo kwa muda wote tangu pale ilipo-dhihirika kuwa nchi hii imekuwa inatumikia minyororo inayoinyima fursa za kustawisha uchumi na hivyo kunufaisha watu wake.CCM waliazimia kuwa wanachama wao wajadili rasimu ile ya awali iliyotolewa Juni 03 mwaka huu na watoe maoni yao wanataka mfumo gani. Hata hivyo, wakati uongozi wa juu ulitoa uhuru kwa wanachama, ulichapisha mwongozo unaoe-lekeza kuwalazimisha kuabudu mfumo wa serikali mbili.Waziwazi viongozi wakuu wa CCM wamepita nchi nzima wakihimiza wanachama wao na kuwalaghai wa-nanchi wengine kutambua ulazima

WAZANZIBARI wana hamu kubwa ya kujua ni nini hasa kimo ndani ya rasimu ya mwisho ya Katiba ya Jam-huri ya Muungano wa Tanzania.

Wanataka kufahamu wamewekwa wapi katika Katiba ijayo? Hawa wanajiuliza kwani hadhi yao itakuwa vipi ifikapo Aprili mwaka 2014, muda uliotajwa kuwa Katiba itakuwa imepatikana?Sasa wanajiuliza rasimu itatambua kilio chao cha kutaka mabadiliko ya mfumo wa Muungano au itakuja na

mfumo uleule unaotakiwa kwa udi na uvumba na Chama Cha Mapinduzi (CCM)?Kila Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipopita na kukusanya maoni ya

wananchi Unguja na Pemba, ilikuta sauti ya mabadiliko ya mfumo imeshtadi. Hata wenyewe wajumbe wa Tume walikiri uk-

weli huu.

>

MATARAJIO YA WAZANZIBARI KATIKA

RASIMU YA PILI

Caption

Mikusanyiko mbali mbali ya Wazanzibari katika kudai Katiba mpya

Na Jabir Idrissa Kauli ya Mwinyi Mkuu

21

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

20

BOXED CREATIVE MAGAZINE TEMPLATE 03>

WWW.YOURDOMAIN.COM ISSUE 03 - WINTER 2012>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

Page 12: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

wa kuwepo mfumo huo uliopitwa na wakati.Wamesema mfumo wa serikali tatu utaongeza gharama, lakini wameshindwa kueleza kama mfu-mo wanaoapia kubaki umesaidia vipi kukuza uchumi wa Zanzibar na kuipatia mamlaka ya kufanya mambo inayoona yanawafaa watu wake.Wazanzibari wanaamini wanayo haki ya kutaka mabadiliko ya mfu-mo wa Muungano, kwa kuwa kwa muda mrefu wamenyimwa haki ya kiutu kuujadili Muungano ingawa waliambiwa kuwa ni “Muungano wao.”Hakuna anayeamini kuwa kikwazo kikubwa cha kukubaliwa mfumo wa serikali tatu au Muungano wa mka-taba utakayoipa Zanzibar mamlaka yake kamili ya kujiamulia ipendacho na kujiongoza itakako, ni gharama

kubwa.Suala hili limefafanuliwa vya kuto-sha na Tume ya Mabadiliko ya Kat-iba. Wamekuta gharama zinaweza kukidhiwa na nchi washirika kwa kila moja kusabilia ushuru wa bid-haa zinazoingizwa nchini. Serikali ya shirikisho itapata trilioni kadhaa za fedha za kujiendesha.Lakini hiyo haitoshi. Mbona vion-gozi wa CCM hawajaeleza namna watakavyoziba mianya ya kifisadi inayochangia kupoteza mapato mengi kila mwaka na kuinyima serikali uwezo wa kukidhi bajeti ya maendeleo hadi kutegemea wa-hisani? Mbona hawajasema watau-komesha vipi ufisadi?Kinachoonekana ni kwa viongozi wa CCM kuzama ndani ya tope zito la ufisadi kwa kuwa hata chama chao wamekifutika makwapani mwa mafisadi. Hili ni dhahiri hata

Mwenyekiti wao, Rais Jakaya Kikwete anakiri chama kimeishiwa pumzi kwa ufisadi katika uchaguzi wao.Wanapodai mamlaka kamili, Wa-zanzibari wanataka masuala ya fedha na sarafu, mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, uhamiaji na uraia yabaki kwenye himaya za nchi washirika wa Muungano.Ninachelea kuwa iwapo Tume ya Mabadiliko ya Katiba itakuja na rasimu isiyowapa matumaini Wa-zanzibari, na wakajiridhisha kuwa wamebezwa, watakuja kutoa sauti yao kwa nguvu kubwa kwenye Kura ya Maoni.Je, wakifikishwa hapo, yupo wa ku-jibu swali la kwamba hasara kubwa itaanguka kwao au itawajia wata-wala wanaodhani wana hatimiliki

ya nchi?

Bila ya kutegemea kuuza bidhaa zako kupitia mtu wa kati [Dalali] Tangaza biashara yako moja moja kwetu

Jarida letu inasomwa karibu nchi 87 ulimwenguni, China, UK, Russia, USA, UAE, Oman, Dubai, Tanganyika, Kenya na sehemu nyengine.

Unakila sababu ya kutangazia kwetu.

LOGO YAKOwww.tunauza.com

Tangaza biashara kupitiaZANZIBAR DAIMA ONLINEBei ni nafuu...

• Ukiwa na Nyumba• Kiwanja• Gari• Bidhaa za dukani • hata mtandao wako

Tangazia bidhaa zako Bure kwa toleo moja na nusu bei kwa toleo jengine

Wasiliana nasi kupitia anuani hiziZanzibar Daima Collective

TEL +44 7588 550 153

WEBSITE www.zanzibardaima.net ZANZIBAR DAIMA ONLINE

Siku zote wasiliana nasi kwa matangazo yako ya aina yoyote, nasi tutafanya kazi vyema nawe

Lete picha za Bidhaa zako

Pamoja na maelekezo yako

22

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

23

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

Chagua nafasiJee unataka ukurasa mzima ama nusu?

Una kila sababu ya kutangaza na Zanzibar Daima Online. Jarida la mtandaoni lisomwalo karibu na nchi 80 duniani.

35% TUMEPUNGUZA

WASILIANA NASI

OFFER MAALUMU TOLEO LIJALO

TANGAZIA BIASHARA YAKObei nafuu na pia tutakupa offer ya matoleo mawili bure!

ANUANI ZETU ZIPO KWENYE UKURASA 23

Page 13: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

WAKATI Mapinduzi yanafanyika tarehe 12 Januari 1964, baba yangu (Mungu amrehemu) alikuwa ndio kwanza ame-

wasili kisiwani Unguja akitokea Bara, ambako alikuwa ameishi kwa takribani miaka mitano mtawalia.

Katika pirikapirika za Mapinduzi hayo, siku ya Jumatatu akakamatwa na watu wenye silaha ku-tokea Bara akiwa mitaa ya Kikwajuni. Jambo la kwanza aliloulizwa lilikuwa ni jina lake.

“Naitwaga Massanja!“ Ndilo lililokuwa jibu lake. Lakini rangi yake ya kahawia na nywele zake laini zikamsaliti ingawa alikuwa kweli na lafudhi ya Kimasanjamasanja.

Hakupigwa sana, lakini alifikishwa kwenye kam-bi ya Raha Leo na pale usuhuba wake wa utotoni na Salim Ghafir, nao pia ukamsaliti, maana al-ipomuona tu akainuka na kuanza kulia: “Khelef nawe umeletwa huku!?“

Baada ya rabsharabsha za Mapinduzi ku-tulia, baba yangu alirudi kwao Pemba. Akaanzisha maisha yake, akiwa kiongozi si tu wa ukoo wake wa Ghassani, bali pia baadaye akaja akawa balozi wa nyumba kumi kumi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wakati mimi nakua, niliikuta bendera ya CCM ikipepea kwenye paa la makuti la nyumba yetu.

Hata tarehe yan-gu halisi ya ku-

zaliwa ilibadilishwa kutoka mwezi Janu-

ari na kuwa 5 Februari 1977.

Baba yangu hakuwa se-hemu ya waliopindua.

Hakuwahi kuwa muumini wa Afro-Shirazi (ASP) wala wa

Umma Party. Ukoo mzima wa baba yangu ulikuwa wanachama

wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP ama Hizbu). Lakini mazingira

yaliyomkuza yalikuwa ya ustahamil-ivu wa kisiasa.

Katika Zama za Siasa, alikuwa na rafiki yake mkubwa, Bwana Mo-hammed Fakih wa Kangani Mkoani (Mungu amrehemu), ambaye ukoo wake mzima ulikuwa ASP. Wakati wa msimu wa karafuu, baba alion-doka na aila yake kwenda kupiga kambi kwenye familia ya Bwana Mohammed Fakih Mkoani kwa aji-li ya biashara ya mikate ya Ajemi, ambayo ni urithi wa ukoo wetu.

Lakini wiki nzima kabla ya aila ya baba kuwasili Mkoani, wazee wa Bwana Mohammed (Mungu awarehemu) walikuwa wakitoa tangazo kwamba muda wote am-

bao “Khelef atakuwepo, hakuna kutajwa siasa za vyama.“ Na ndi-vyo ilivyokuwa pia wakati familia ya Bwana Mohamed ilipokuwa ikitembelea kwetu Pandani.

Sisemi kwamba hakukuwa na visa vya karaha na kukomoana kati ya

wafuasi wa kambi hizo mbili kwen-gineko visiwani Zanzibar. Nina-chosema ni kuwa zaidi ya asilimia 70 ya Wazanzibari wa leo ni wale waliozaliwa na kuishi baada ya Uh-uru wa Desemba 1963 na Mapin-duzi ya 1964. Miongoni mwao pia, muna idadi isiyo ndogo ambayo pande mbili za wazazi zimetokea kwenye mitazamo tafauti ya kisia-sa, panapohusika dhana hizo mbili za Uhuru na Mapinduzi.

Nadhani familia ya Rais Mstaafu Amani Karume ina hadithi ya ku-sisimua zaidi katika hili, kwani mke wake, Bi Shadya, anatokana na ki-zazi cha waasisi wa siasa za utaifa

>

Nadhani familia ya Rais Mstaafu Amani Karume ina hadith ya kusisimua zaidi katika hili, kwani mke wake, Bi Shadya anaotkana na kizazi cha waasisi wa siasa za utaifa wa Zanzibar, huku Amani akiwa mtoto wa Rais wa kwanza wa Zanzibar

Sisi ni kizazi cha waliopinduana waliopinduliwa

Wakati mimi nakua, nilikuta bendera ya CCM ikipepea kwenye paa la makuti la nyumba yetu

Na Mohammed Ghassani Ngurumo la Mkama Ndume

24

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

25

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

Page 14: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

za Zanzibar, huku Amani mwenyewe akiwa mtoto wa Rais wa Kwanza wa baada ya Mapinduzi.

Wapo wengi pia ambao ni matokeo ya mchang-anyiko sio tu wa wa-zazi wenye mitazamo tafauti ya kisiasa, bali pia mchanganyiko wa visiwa viwili vikuu vya Unguja na Pemba na pia mchang-anyiko wa pande mbili za Muungano, yaani Zanzi-bar na Tanganyika.

Kuna wengine pia am-bao waliinukia wakiwa wafuasi wa kambi moja

ya kisiasa lakini wame-badilika sasa na kuwa waumini wa mtazamo mwengine wa kisiasa. Vyama vikuu vya siasa vya Zanzibar hivi sasa sio tena kielelezo cha Zanzi-bar ya miaka 50 iliyopita nyuma.

Kuna ambao walikuwa wafuasi wa ASP na Umma Party, lakini ama wao we-nyewe au watoto wao wamekuwa leo wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF). Kuna ambao wa-natoka kwenye mizizi ya Hizbu na Zanzibar and Pemba People’s Party

(ZPPP), lakini hivi leo ndio wafuasi namba moja wa CCM. Baraka Mu-hammed Shamte ni kada mkubwa wa CCM akiwa ndiye mtoto wa kwanza wa muasisi wa ZPPP na Waziri Mkuu wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Mu-hammad Shamte (Mungu amrehemu).

Kuna pia wasiokuwa na chama chochote cha sia-sa, na ambao kwao siasa za vyama hazina nafasi katika maisha yao. Wote hawa ndio sehemu ya sisi leo. Sisi Wazanzibari.Binafsi nimeishi kwenye

visiwa vyote viwili vikuu vya Zanzibar. Maisha yangu ya kifamilia pia ni mchanganyiko wa visiwa hivi na mitazamo hiyo ya kisiasa. Ndani ya familia yangu mnatembea damu za walioupokea Uhuru wa 1963 pale Maisara, siku hizo ukiitwa Uwanja wa Coopers na waliokuja kuupindua Uhuru huo Jumamosi, tarehe 12 Januari 1964. Kuna am-bao walikuwa viongozi na watumishi wa umma kabla ya Mapinduzi na ambao walikuwa hivyo hivyo baada ya 1964. Zote hizo ni pande zangu.

Na zote hizo ni historia zangu.

Na wala si peke yangu mwenye pande hizo. Tuko wengi jumla yetu, maana kila taifa lina his-toria yake, mazuri na ma-baya, kupanda na kush-uka. Lakini mwisho wa yote, kila taifa hupaswa kusimama kama taifa, likiitukuza historia yake na wakati huo huo liki-jifunza kwa matukio na matokeo ya historia hiyo kwa minajili ya kusonga mbele.

Wakati tukiadhimisha

nusu karne ya Uhuru na Mapinduzi ya Zanzibar, hatupaswi hata kidogo sisi kizazi cha sasa kuy-achukulia matukio hayo ya kihistoria kama msin-gi wa kutugawa. Hatuna sababu ya kuwapa fursa wazee ambao dunia yao inawalizikia, kuturith-isha dunia ya matatizo na migogoro kwa msingi wa historia ya kabla na baada ya Uhuru na Map-induzi.

Sisemi kwamba hatuna chochote cha kujifunza kwao, lakini nasisitiza kwamba tuchukue ma-

zuri kutoka kwao na tu-waachie wafe na mabaya yao. Moja ya mabaya hayo ni kosa walilolif-anya wote wawili wakati huo, ambapo upande wa Hizbu/ZPPP wakajisa-hau kwamba Zanzibar ni ya wote na kupatwa na kiburi cha madaraka na uluwa, huku upande wa ASP/Umma Party ukijio-na kwamba wao tu ndio wenye haki ya kuitawala Zanzibar kwa msingi wa “wingi wa watu“. Wote hawakutaka kujua kuwa Zanzibar ni yetu sote.Matokeo yake, pande zote mbili, ama kwa ku-

jua ama kutokujua, zili-changia kuja kuifanya historia ya kutawaliwa kwa Zanzibar kuwa refu zaidi. Hilo halimaanishi kwamba pande hizi mbili hazikuifanyia mema yoy-ote nchi yao.

Hapana. Zilifanya mengi. Lakini sisi wa leo, tu-napaswa kuyatumia mafunzo haya ya kihisto-ria kupunguza urefu wa nchi yetu kutawaliwa. Si

vyenginevyo

26

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

27

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

Rais wa Jamhuri za Tanzania, Jakaya Mrisho akishuhudia moja wa utiaji mikataba baina ya Oman na Zanzibar kwenye ziara ilifanyika hivi karibuni huko Oman

Page 15: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

28

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

29

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

> NATUANGALIE namna ya kuufanya mfu-mo wa Muungano uwe bora ili uwe na nguvu za kisheria, uhalali kwa wa-nanchi na pia maendeleo yaliyokusudiwa katika uundwaji wake.

Kwa sasa mfumo wa seri-kali mbili kuelekea moja umefeli na kuundeleza ni kuendeleza makosa yalioleta chuki, fitna na ukiritimba mkubwa wa maendeleo nchini. Sina haja ya kurejea his-toria ya Muungano huu au uasisi wake kwa saba-bu ya mazonge mengi yanazouzonga mfumo mzima wa Muungano kuanzia uundwaji wake na miaka karibu 50 ya uhai wake.

Ila tutatazama namna ya kuufanya uwe bora na kuhakikisha mfumo ujao utajenga utamaduni wa kuaminiana, kufahami-ana na kurejesha hes-hima iliokuwa kama ni lengo la kuungana hasa kwa namna ya Wazan-zibari waliowengi wal-ivyoufahamu muundo

huu na kuamini kama ndio maudhui makuu ya uundwaji wake.

Sababu ni kuwa kume-tokea taswira za aina mbili za upokewaji wa Muungano: upande mmoja hususan ndani ya mamlaka ya Zanzibar wakiamini uwepo wa nchi ya Zanzibar kama ni muhimu sana na adhimu katika maamuzi yoyote ya uwepo wa Muungano huu wakati upande wa pili ukijijenga zaidi ka-tika safu za kuhakikisha Muungano huu utataf-siriwa kama ni wa nchi moja iliokamilika. Tuonavyo sisi Wazan-zibari tulio wengi ni

kwamba Zanzibar ni nchi iliokamilika na ku-jiendesha kwa misingi ya kimamlaka yanayoongo-zwa na ule uongozi mkuu wa ya Rais pamoja na serikali alioiunda baada ya kuridhiwa na uchagu-zi unaotegemewa kue-ndeshwa kwa misingi ya demokrasia. Katiba ya Zanzibar hu-susan baada ya mabadi-liko ya 2010 imeonye-sha kwa uwazi bila ya kuweweseka kwamba ni nchi kamili; na ikaenda mbali zaidi kuhakikisha mamlaka ya mkuu wa nchi hii hayatakuwa na kigugumizi kwa kuin-giliwa na nguvu nyen-gine ndani ya Muungano hasa baada ya kuhakiki-

sha kwamba ni Rais wa Zanzibar pekee mwenye madaraka na uwezo wa kuigawa Zanzibar katika mikoa bila ya ushauri wa yeyote kinyume na ilivy-okuwa awali.

Uthibitisho wa haya ni kura ya maoni ambayo hadi sasa inatazamwa kama ni mfano wa uch-aguzi pekee ulioendesh-wa kwa uwazi zaidi huku kundi la walipiga kura ‚ndio’ likibeba nguvu ya zaidi ya asilimia 66 ya wananchi walioikubali hiyo kura ya maoni.

Katika ilani ya CCM ya mwaka 2010 suala la ma-badiliko ya Katiba haliku-wemo. Wengi tunaamini

kwamba mabadiliko ya Katiba ya Muungano ya-mekuwa yakichochewa na mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ya 2010 hasa baada ya kuona kwamba Katiba mbili haziendani kimantiki hata kisheria. Na kwa vile katika kura ya maoni ya Zanzibar idadi kubwa ya wananchi walioipitisha hakukuwa na budi zaidi ya kuifanyia marekebisho Katiba ya Muungano ili iendane na sauti ya asilimia 66 ya Wazanzibari. Muundo ambao Jaji Mstaafu Joseph War-ioba na tume yake wal-ioupendekeza umeth-amini kauli ya wananchi kwamba ile dhana ya udogo wa sehemu ikawa ndio kigezo cha kuburura maoni yao iliondoshwa. Kwa vile msingi mkuu wa Muungano ni nchi mbili zilizoungana bila kujali ukubwa au idadi ya watu

wao, ni lazima mabadiliko yoyote yathamini maoni ya pande mbili huru ili paweze kupatikana mua-

faka baina yao na kuunda kitu kitachokubalika na wote. Ndio maana ukakuta hata maoni ya mamilioni ya Watanganyika wali-otamani serikali moja hayakuridhiwa kuwekwa katika Rasimu ya kwanza ya Katiba kwa sababu yalipingana na ya Wa-zanzibari hata wakiwa na idadi ndogo ya watu kul-inganisha na Bara.

Maoni yangu ni kwamba Jaji Warioba ametupa heshima tunayosta-hili Wazanzibari katika Muungano huu. Pia am-etupa matumaini kwam-ba mfumo ujao utaweza kuwa ni kielelezo kipya cha mabadiliko makubwa zaidi katika mfumo wa Muungano utaojengwa kwa misingi thabiti ya kuheshimiana, kuamini-ana, haki na usawa. Wengi tunaamini mfumo wowote wa Muungano katika ndoto ya Wa-zanzibari uendane na kauli mama ya Zanzibar kama ni nchi na yenye kujiendesha yenyewe ki-mamlaka.

Mifumo butu yenye tas-wira moja lakini lengo lililojificha haitakubaliwa katika ulimwengu wa sasa wa utandawazi hasa ukizingatia kwamba ari ya kuwa na mfumo wa Mkataba haukuasisiwa na chama chochote bali na wananchi wa kawaida ndani na nje ya visiwa hivi. Wao waliona mbali zaidi na walitaka ku-hakikisha mfumo ujao

hautakuwa na kigugumi-zi chochote juu ya uhalali wa kuwepo kwa taifa la Wazanzibari. Hili linawezekana hata ndani ya mfumo wa seri-kali mbili ikiwa yaliomo ndani ya Muungano yat-azingatia maoni ya wengi yalioweka wazi msimamo wa Zanzibar kama ni nchi yenye kila nyenzo ya kuji-tosheleza na kujiendesha yenyewe.

Jaji Warioba kafahamu maana kamili ya Muun-gano wa Mkataba na ndio maana akapende-keza rasimu ya mwanzo ya mfumo wa serikali tatu na ukakuta wengi waliopendekeza mfumo wa Mkataba hawakuwa na upinzani wa serikali tatu kwa sababu ya yali-yomo ndani ya rasimu hio iliopunguza mambo ya Muungano kutoka zai-di ya 30 hadi kufikia saba.

Ndio ukakuta wanama-geuzi wa kweli hawaz-ingatii jina la mfumo wa Muungano bali yaliyomo kwenye Muungano we-nyewe na kwa sasa ngu-vu zimeelekezwa katika kuyafuta yale yatayok-wenda kinyume na azma ya mamlaka kamili.Hoja zisizo na mashiko kama gharama za Muun-gano katika mfumo wa serikali tatu zenye ku-jitegemea zinaeleke-zwa zaidi kama khofu hususan kwa wazanzi-bari kama vile nchi hii haitaweza kujiendesha yenyewe wakati wahubi-ri hawa wanashindwa basi kuwaeleza watu kabla ya Muungano huu

Zanzibar inataka Muungano wa heshima, haki na usawa

Na Farrel Foum Jr. Zanzibar Tuitkayo

Miongoni mwa viongozi wakuu wa Tanzania, Waziri Mkuu Mizengo Pinda [kushoto] na Makamo wa Rais Mohammed Bilal

Waziri wa anaeshughulia Muungano Samia Suluhu [kulia]

Page 16: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

TANBIHIHii ni sehemu ya pili ya uhakiki ulioandikwa kwa lugha ya Kiingereza na FLAVIA AIELLO TRAORE kwa jina la INVESTIGATING TOPICS AND STYLE IN VUTA N’KUVUTE BY SHAFI ADAM SHAFI. Hapa tumeutafsiri kwa minajili ya kuwapa wasomaji wetu mtazamo wa wen-gine kwa fasihi ya Kizanzibari. Sasa endelea….

Tufungue Kitabu

> JAMBO la kufurahisha ni kuwa upinzani na

mapambano kwenye riwaya hii hayajumuishi vitendo vya kutumia nguvu dhidi ya binaadamu wengine, bali maandamano na mashambulizi dhidi ya alama ya nguvu za kikoloni (kama vile mikahawa iliyotengewa watu wa matabaka fulani tu), kusambaza kazi ambazo zinachukuliwa na serikali kuwa ni haramu na uanzishaji wa gazeti liitwalo Kimbunga.

Mambo yote haya yanaelezewa kwenye Vuta n’kuvute kama kipimo cha majaribu ya mapambano ya kusaka uhuru.

Hapa pia, kama ilivyo kwenye kazi

nyingi za Kizanzibari, tunaona uhusiano wa wazi baina ya jina na maudhi, ambao ishara yake inajidhihirisha wazi kwenye mtiririko wa visa unaomsaidia msomaji kuitafsiri riwaya katika muktadha wa kihistoria.

Katika Vuta n’kuvute, uhuru wa mawazo na kujieleza ni sehemu muhimu ya mapambano ya jumla, lakini baadhi ya wakati pande hizo mbili hukinzana. Kwa mfano, wakati mwengine mtu kusimamia haki yake kwenye mapenzi ni jambo la anasa linapolinganishwa na suala la ulinzi wa nchi, kama anavyoungama Denge katika ukurasa wa 145:

“Yasmin mimi najua kama unanipenda, na mimi nakupenda

vile vile, lakini kuna kitu kimoja napenda uelewe. Kuna mapenzi na wajibu wa mtu katika jamii. Kila mtu ana wajibu fulani katika jamii na mimi wajibu wangu mkubwa ni kufanya kila niwezalo kwa kushirikiana na wenzangu ambao wengine unawajua na wengine huwajui ili kuona kwamba nchi hii inakuwa huru. Hii ni kazi ngumu, ina matatizo mengi na inahitaji kujitolea muhanga na mimi ni miogoni mwa hao waliojitolea muhanga kufa, kupona, potelea mbali. Tupo wengi tuliojitolea namna hiyo, tena wengi sana, maelfu.”

Maisha ya Denge yametolewa muhanga kwa kile akiaminicho, ikiwemo kutengwa au kuishi uhamishoni, na Yasmin anapaswa

VUTA N’KUVUTE, KIELELEZO

CHA UANDISHI WA KIZANZIBARI

30

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

31

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

Page 17: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

kukubali majaaliwa yake ya upweke, na kushika njia akaenda zake.

Kwa mara nyengine, Yasmin anakabiliwa na upotoshaji wa kikabila. Makutano yake na Bukheti, aliyewahi kuwa jirani yake Mombasa, yanapingwa na familia zote mbili, zikionesha khofu na dharau zao kwake kama mkando.

Anadhalilishwa kwa kila aina ya maneno machafu, kama anavyoibuka na kutoa kauli kwenye ukurasa wa 254:

“Iko wapi heshima ya binadamu, ikiwa Muhindi anamwita Mswahili golo na Mswahili naye anamwita Muhindi ponjoro?”

Upatanishi uliofanywa na

marafiki wa zamani wa kifamilia na ambao ni watu wenye mwamko, unasaidia kuzitenga kando dharau hizo; na riwaya hiyo inamalizia kwenye muunganiko wa furaha, unaofunikwa na ghamu ya Yasmin.

Tukio la mwisho lenye kumuacha msomaji na athari kubwa kutoka riwaya hiyo linaelezewa kwa nyimbo ya Kihindi ambayo Yasmin aliisikiliza Mombasa, na kudimka peke yake kutuliza roho yake na pia kuiimba kwenye kundi la taarab kisiwani Unguja.

Daima Yasmin anauchukulia muziki kama kimbilio binafsi na beti za nyimbo hizo zinamkumbusha utamu na ukali wa uhuru.

Fani

Sasa natuangalie baadhi ya vipengele vya usimulizi wa riwaya hii ya Vuta n’kuvute, tukichunguza zaidi muundo wa hadithi yenyewe, mitindo na matumizi ya lugha.

Kama zilivyo kazi nyingi za Kizanzibari, kazi hii ina kiwango kikubwa cha kisanii, ikiwa imejengwa kwa kwa sura fupifupi kumi na nane, zinazokwendana na mjengeko wa matukio, mikasa, na mapigo yanayomfanya msomaji azidi kupata hamu ya kuisoma.

Kipengele cha wakati kwenye riwaya hii kwa jumla kimetumika vyema – ni nadra kukuta matukio yanayoelezewa kwa kurudi nyuma, kama lile la maisha ya Denge barani Ulaya.

Mtiririko wa visa unasimulia

hadithi mbalimbali za maisha ya wahusika wakuu, wakati mwengine zinazopishana na wakati mwengine kuoana. Matukio mengi ni muhimu sana kwa mjengeko mzima wa riwaya.

Ufundi huu wa uandishi unaipa riwaya sifa ya kuwa “riwaya ya masimulizi” bila ya kuondosha mantiki ya matukio kama lile la mazingira ya Roger na Salum kumtembelea Mwajuma na ugomvi uliozuka baina ya wanaume hao wawili.

Mwandishi amefanikiwa kwa ustadi mkubwa kuweka mizani baina ya mbinu za kuonesha (ambapo matukio huwa yanasimuliwa na wahusika) na ile ya kuelezea (ambapo matukio yanasimuliwa na msimulizi, yaani mwandishi mwenyewe).

Uwasilishaji wa msimulizi aliye wazi na aliyejificha ni miongoni mwa vipengele vya ubora kwenye kazi za fasihi, na katika riwaya hii tangu awali kabisa msimulizi huyo huonekana kwa sura zote mbili na katika viwango tafauti.

Kwa mfano, riwaya hii imejengwa kwa majibizano – ambapo msimulizi anakuwa haonekani kabisa – sio tu kwenye mazungumzo mafupi mafupi, lakini zaidi kwenye mistari mirefu ya kujenga hoja, lakini wakati mwengine majibizano haya huchukua nafasi muhimu sana katika kutoa taarifa kuhusu wahusika na au ujumbe muhimu, ambao mwandishi anauwasilisha kwa hadhira yake, kama dondoo zilizotajwa hapo juu za Denge na Pazi.

Ndani ya riwaya hii, msomaji anagundua pia matumizi ya kauli zisizo za moja kwa moja, ambako maneno au mawazo yanasimuliwa na msimulizi lakini yakinasibishwa kwa ukaribu sana na mhusika, kama vile kwenye ukurasa wa 49 pale mwandishi anapoelezea namna Yasmin alivyomuona Denge kwa mara ya kwanza:

“Kwa Yasmin huyo alikuwa n’do Mwaftika wa kwanza kuambiwa ametoka Ulaya. Shilingi mbili za kununua ukanda wa kufungia suruali yake zinamshinda, na ile suruali isiyokuwa na pasi aliyovaa imezuiliwa kiunoni kwa tai labda aliyorudi nayo kutoka huko Ulaya, na hivyo viatu alivyovaa, karibu vidole vingine vinataka kuchungulia nje.”

Itaendelea....

Maalim Seif akizungumza na

kamishna mpya wa Polisi Zanzibar, Hamdani

Omar Makame > Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema licha ya

polisi kuwa na jukumu kubwa la kulinda usalama wa

raia na mali zao, jeshi hilo pia linapaswa kuwa mstari wa mbele katika utekelezaji na usimamizi wa sheria.

Akizungumza na Kamishna mpya wa Polisi wa Zanzibar, Hamdani Omar Makame, aliyekwenda ofisini kwake Migombani kumsalimia, Maalim Seif alilitaka jeshi hilo kuondosha muhali katika kusimamia utekelezaji wa sheria, ili kuona kwamba sheria zilizotungwa zinafuatwa na kuleta ufanisi katika jeshi hilo na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Kamishna Hamdani amemuhakikishia Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa atatekeleza majukumu yake ya kusimamia sheria, ili wananchi waendelee kuishi katika hali ya amani na usalama.

Aidha amesema jeshi la polisi kupitia kitengo chake cha “Intelijensia” kitaimarisha utafiti ili kupata taarifa za uhakika za kuweza kukabiliana na wahalifu na kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.

Ameongeza kuwa atatumia uzoefu alionao katika masuala ya teknolojia ya mawasiliano ili kuona kuwa kitengo hicho kinafanya kazi kwa uhakika na kuleta ufanisi uliokusudiwa.

Kamishna Hamdani amesema mafanikio aliyoyapata katika kipindi cha miaka 30 ndani ya jeshi la polisi, yametokana na mashirikiano aliyopata kutoka kwa viongozi na wananchi, na kuomba mashirikiano zaidi ili aweze kuyafikia matumaini na matarajio ya taifa katika ulinzi wa raia na mali zao

Polisi Z’bar yatakiwa kuwa adilifu

Chanzo, MKR1znz.wordpress.com

32

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

33

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

Page 18: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

> WALIPOFIKA ndani alianza kuchukuwa jina la mgonjwa na maelezo mafupi, baada ya hapo

alimchoma sindano ya kuondosha sumu ile lakini iliku-wa imeshaenea mwili mzima. Bi Tausi alijiona kuwa hawezi kuendelea kuishi, alimuomba daktari amruhusu Mwalimu Miftaha apite ndani kwani kulikuwa kitu aki-taka kumwambia. Daktari aliomba apewe yeye ule ujumbe aufikishe kwa Miftaha lakini Bi Tausi alikataa katakata, akidai kuwa ‘kuagiza n’maviza’

Mwalimu Miftaha aliruhusiwa apite ndani kumsikiliza Bi Tausi; naye Bi Tausi alimtaka daktari asubiri nje mara moja ili azungumze na Miftaha.

“ Mwanangu, ahsante, miye naishi kijiji cha Maukioni, nnakuja n’jini kutimiza utumwa wa shoga yangu aliyenileta huku, ni mzee sana tena wa miaka mingi, kutokana na hali yake, basi hawezi kuishi siku ny-ingi na… na…”Alikohoa na kuugua kwa maumivu na baadaye akaen-delea:

“Kanituma nintafutie kijana mwenye mapenzi na nchi hii ambaye ana dira nzuri ya maisha yake lakini sijamuona, nlikuwa narudi bila ya mafanikio na ndio maana baada ya kukuona weye nahisi unanifaa, nenda kwa huyu bibi ana kitu cha kukwambia, aitwa Bi Msiri”

Alikohoa na kuvuta pumzi yake ya mwisho na hapo ndi-

TANBIHIIlipoishia toleo lililopita: “Hakuna aliyemjali mgonjwa, kila mmoja ali-jishuhulisha na kazi zake, baadhi ya wauguzi walimtazama mgonjwa wa Miftaha kwa dharau bila ya kujali kuwa alikuwa katika hali mbaya kwani sumu ya nyoka ilikuwa inazidi kumuenea mwilini. Daktari wa zamu alikuwa amekaa nje anasoma kitabu cha riwaya. Miftaha alitoka hadi nje baada ya kuambiwa kuwa daktari wa zamu alikuwepo nje, alimkuta daktari amewacha kitabu na sasa anacheza karata na vijana wa mtaa. Ilimuuma sana kumuona daktari anacheza karata huku wag-onjwa wakiumia bila ya matibabu, alimsogelea daktari na kumwambia kuwa kuna mgonjwa yuko hali mbaya.....” Sasa endelea...

MEZAFUPAHekaya za ZanzibarNa Ally Hilal

34

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

35

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

Page 19: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

sana kwa kazi nyingi alizokuwa nazo, hili liliwakera wa-zazi, na kwa vile nilikosa bahati walizidi kulifanya hili kama kosa la jinai. Niliambiwa kuwa kuanzia wakati huo nitakuwa mfanyakazi wa ndani na yule mfanyakazi ali-fukuzwa nyumbani. Maisha yangu yalikuwa magumu pamoja na kuwa niliishi na wazee wangu tena hawaku-wa na maisha magumu. Baba yangu alikuwa waziri wa ardhi na majengo.

“Siku moja, nilitoka kuelekea mtoni kufua kama ilivy-okuwa kawaida yangu. Nilikusanyiwa nguo za nyumba nzima, sijawahi kulalamika hata siku moja, nilizifua nguo zote.

“Baada ya kumaliza nilirudi nyumbani na kumkuta mama yangu kwenye mlango wa jikoni akiwa ame-shafariki, alikuwa anavuja damu kichwani. Nilipoingia ndani niliwakuta ndugu zangu wawili wa miaka kumi na tano wameshafariki, hawa walikuwa pacha, nilichang-anyikiwa na kuanza kuita kwa sauti kubwa iliyojaa kitetemeshi. Hakuna aliyeitika, nililia sana, niliamua ku-ingia chumbani kwa baba ambako moyo wangu ulizidi kushituka nilipomkuta baba yangu amelala kitandani, kichwa chake kilikuwa kinaninginia chini na miguu iliku-wepo kitandani. Alikuwa amekatwa katwa mkono wake na kichwa chake kilivuja damu nyingi.

“Sikujua nifanye nini, nilikuwa na maswali mengi ya ku-jiuliza kuhusiana na aliyefanya mauji yale ya kutisha. Nilibaini baada ya kuokota kitambulisho chenye picha ya mtu. Kilikuwa ni kitambulisho cha afisa wa polisi kili-chokuwepo sakafuni, pia kilikuwepo kipochi mlangoni. Nilikifungua na kukuta makaratasi mengi, nilipojaribu kukifungua kikaratasi kimoja niliona kimeandikwa jina la afisa yule yule. Baada ya dakika mbili nikiwa nime-zubaa pasipokujua cha kufanya, nilisikia mvumo wa gari nje ya nyumba yetu. Nilijificha mvunguni mwa kitanda cha baba. Niliweza kuviona viatu vya buti nyeusi. Nili-tamani niione sura yake lakini sikuweza kuiona kwa wakati ule.

Nilisikia sauti mbili zikijinadi na kusema bila woga. “ Pochi yangu na kitambulisho hivi hapa”

Yule mwengine akajibu:

“ Mawaziri kama hawa tunafyeka sisi, hawatuy-umbishi, hivi unaijua sababu ya kuteketea kwa hili jamaa?”Aliuliza yule askari. “Najua, huyu juzi alisema kuwa raisi inabidi abadilike asiburuzwe na matakwa yake kwani yeye amewekwa na wananchi”

“Ah! Kumbe wewe wajua hivyo tu! Huna ujualo”

Walianza kubishana, niliroa jasho na miguu iliniteteme-ka huku masikio yangu yakisikiliza zile sauti.

“ Wewe hujui, huyu jamaa amepewa usimamizi wa ardhi, ameamua kuwatafuta wananchi wenye umi-liki halali wa eka zao na wengine amefanikiwa kuwarud-ishia eka zao za mashamba na hayo mengine yamefua-tia juu tu, na sasa wameamua kuuziba huu mdomo”

“Haya yote niliyasikia, nilifanya kuchungulia kidogo nikaweza kuziona sura zao. Alikuwa ni afisa wa polisi pamoja na waziri ambaye alikuwa anakuja sana nyum-bani, alikuwa ni rafiki wa karibu sana na baba yangu Ama kweli kikulacho kinguoni mwako, waziri huyu huyu ndiye aliyemuahidi baba kuwa hamu yake ni kuona fa-milia yetu na familia yao zinazidi kuungana kupitia ndoa za watoto wao, yaani mimi na mtoto wake waziri huyu.

“Baada ya muda walitoka nje na kuondoka. Nilijifungia chumba cha mabandani hadi usiku na nikaondoka. Nili-kuwa nikizisikia sauti za watu waliokuwa wakiingia na kutoka.

“Ilipofika usiku nilitoka na kuelekea chumba cha mare-hemu baba yangu, mwili wake ulikuwa umeshaondosh-wa, na hata miili ya mama na wadogo zangu haikuwepo tena. Iliniuma sana, nilichukuwa begi langu la nguo na kuondoka nikiwa sijui ninapokwenda. Waswahili wa-nasema “Kua uone mambo!”

Itaendelea

po alipoaga dunia.

Miftaha aliumia sana, alimwita daktari kumuangalia mgonjwa wake lakini alikuwa ameshapoteza maisha.Alirudi nyumbani kwao na kuchukuwa farasi wake, aliupakia mwili wa marehemu na kuupeleka kijiji cha Maukioni, alifika kjijini hapo saa mbili usiku. Aliwaulizia ndugu wa bibi yule na kuwapata. Baada ya kuwakabidhi maiti wao aliwaaeleza yote yaliyomkuta bibi yule halafu aliaga na kuahidi kurudi baada ya siku mbili.

Baada ya siku mbili, aliamua kwenda kijiji cha Maukioni pamoja na wenzake wawili, dada yake aliyeitwa Maimu-na na mwalimu mwenzake aliyeitwa Suheli.

Ilikuwa ni asubuhi mapema, vijana hawa walielekea kijijini kumtafuta Bi Msiri. Walikuwa na farasi wawili, mmoja alipanda Miftaha na Maimuna na mwengine ali-panda Suheli.Walifikia nyumbani kwa Bi Tausi ambaye alizikwa siku moja kabla, walikaa matangani kwa muda wa masaa mawili, walikaribishwa vizuri sana na wenyeji wao. Baada ya hapo waliomba wafahamishwe sehemu ali-yokuwa akiishi Bi Msiri. Kijana mmoja mdogo aliyeku-wa akianika nguo, alitakiwa awapeleke bondeni ilipoku-wepo nyumba ya bibi huyu.

Ilikuwa ni kibanda kidogo kilichoezekwa kwa makuti, baadhi ya sehemu kilizibwa kwa makuti, nje alikuwepo bibi anatwanga unga wa muhogo. Alikuwa amekaa kwe-nye gogo la mnazi, alivaa nguo zilizochakaa sana. Kanga yake iliandikwa “NIMESTAHAMILI TABU KUPATA SI AJABU”

Ujumbe huu ulimfanya Miftaha atabasamu peke yake, walisogea alipokuwepo Bi Msiri na kumsalimia. “ Shikamoo bibi”Bi Msiri alikuwa haoni vizuri lakini aliweza kusikia vi-zuri, aliwaitikia na kuwauliza maswali mengi.

“ Marahaba wanangu, sijawajua nnani nyiyee! Macho yenyewe yan’kwisha zake, sioni taaaa ule n’kono wangu.”

Miftaha alijitambulisha kwa kutoa mkasa wa Bi Tausi. Bi

Msiri alisikitika sana alipotajiwa shoga yake mpenzi ali-yepoteza maisha siku mbili tu zilizopita, aliwachangam-kia wageni wake baada ya kubaini kuwa ndio waliouleta mwili wa marehemu. Aliumia sana kwa sababu safari ya Bi Tausi kwenda mjini ilikuwa ni kutekeleza agizo lake Bi Msiri aliyemtaka akamtafutie mtu mwenye uchungu wa nchi yake, mzalendo wa kweli na si wa kinafiki. Baada ya kushindwa kutimiza lengo lake aliamua kurudi kijijini kwao na hapo ndipo yakamfika matatizo. Hiyo ndiyo ili-yokuwa sababu ya kifo chake. Bi Msiri aliwakaribisha chini ya mwembe na kuwa-tandikia mkeka. Bibi huyu alikuwa malenga mzuri sana, alizungumza maneno kwa ufupi sana lakini yalibeba maana nzito, Kiswahili chake kilimfurahisha sana Mifta-ha.

************************

“Wanangu natakalitema fupa, nimelimeza likanikwama, hakuna anayejua lakini n’taka wajuvya nyiye, naamini mumetoka kwenye udongo wenye rutuba nzuri, inga-wa maji machafu huuathiri udongo wenu lakini naamini kuwa bado kuna michirizi ya maji safi ipitayo kwenye udongo huo, pia hewa safi kutokea pande za janibu ya kaskazini na kusini yake zaweza ipunguza sumu hii ya hatari.

“Nimeona kuwa kumeza fupa si suluhu ya kunifanya ni-siwe na njaa tena, wala si sababu ya kuwatia njaa mbwa wanaohaha huku na kule kwa kulitafuta fupa. Nataka mujuwe wanangu kuwa mimi nimekula chumvi sana. Hakuna anayejua hata mmoja kuwa mimi nimepindukia na kupindukia kuishi, nayajua hayo wasiyoyajua ma-babu wa babu zenu, katika wahenga na miye nimo na n’shahengeka. Nayajua hayo meusi yaitwayo meupe na meupe yaitwayo kijani. Umri wangu unapotea sasa, hebu tulieni niwajuvye.

“Nina miaka mia mbili, na nimeishi kijijiini hapa tangu baada ya baba yangu kuuwawa na familia yangu yote isipokuwa mimi.

“Mimi peke yangu nilisalimika, nilikosa bahati kwetu, wazazi wangu walinifanya kama mtoto waliyeniokota. Nyumbani kwetu alikuwepo mfanyakazi, nilimhurumia

36

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

37

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

Page 20: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

Siuki sina nendapo, pano ni pangu ngamani Nendapi we uonapo, nifikie kileleni Nasema mie sinapo, pengine kwa duniani Nitabaki Zinjibari, kwa nguvu zake Manani

Ingelikuwa nnapo, ningetoweka zamani Kitambo ngekuwa sipo, nishauka kiamboni Pa kwenda mie hapapo, pangu ni hapa shinani Nitabaki Zinjibari, kwa nguvu zake manani

Si dharuba ya upepo, unovuma baharini Wala si kwa mitetemeko, ivunjayo miambani Sitaseguka nilipo, kwa nguvu au amani Nitabaki Zinjibari, kwa nguvu zake Manani

Nimeshakula kiapo, siondoki asilani Hapa mie takuwepo, leo na kesho amini Nitakita papo hapo, hasa mwanitakiani Nitabaki Zinjibari, kwa nguvu zake Manani

Naapa sijaonapo, sawa na kwetu nyumbani Na kila nitembeapo, Unguja i akilini Kwa mfanowe haupo, Zenji ni nambari wani Nitabaki Zinjibari, kwa nguvu zake manani

Nawaaga mliopo, narudi zangu mwambani Wasia ni huo hapo, watoka mwangu moyoni Cha kukificha hakipo, Zenji ipo kifuani Nitabaki Zinjibari, kwa nguvu zake manani.

Mbarouk Sharif (Mnyonge wa Nyali), Waco, Texas Marekani

Nitabaki ZinjibariLaitani ningajuwa, hiyino ndio safariTiketi singenunuwa, kwanza ningajishauriKamwe singeliamuwa, chombo nikakiabiri

Lingekuwa la kujuwa, kwamba nendako ku mbaliAkiba ningachukuwa, mapeni na maakuliHaepuka kuishiwa, nisijafika mahali

Ningajuwa ningajuwa, njia ina majangiliMisafara huvamiwa, zikatwawa zote maliBunduki ninganunuwa, na upanga haamili

Halekuwa la kujuwa, kupita kwenye nadhariKwamba niliyoamua, yena ugumu safariKufumba na kufumbuwa, nedhani ningewasili

Bali madhali ya kuwa, nishaianza safariJapokuwa sikujuwa, ugumuwe na hatariKurudi havitakuwa, naiandama kwa ari

Lolote litalokuwa, njiani litalojiriNitalipiga kifuwa, nipambane kijasiriPindu nitalipinduwa, ama roho ihajiri

Kwa hapa nishapokuwa, siwazii kughairiKurudi nyuma si dawa, hivyo sitawa rijaliRijali akiamuwa, shoti itimu dhamiri

Mohammed Ghassani7 Desemba, 2013

Lingekuwa Lakujua

BETI BETILAD

HA

LAD

HA

YAYA

38

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

39

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

Page 21: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

KUANZIA tarehe 27 Novemba hadi 12 Disemba kila mwaka huwa kunafanyika mashindo ya Chalenji ambapo nchi za Afrika Mashariki na Kati huwa zinashiri-ki. Tanzania huwa inawakilishwa na timu mbili kutokana na tarati-bu za kitawala za nchi mbili amba-zo zimeungana lakini hujitegemea kwa baadhi ya mambo, yakiwemo ya michezo.

Moja kati ya timu iliyokuwa ik-ishiriki ni Zanzibar Heroes - Vi-jana wa Mzee Sheikh Karume Muasisi wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar - ambao walikuwa kundi moja na Sudan ya Kusini, Kenya na Rwanda. Timu hiyo iliishia kushinda mechi moja na kufung-wa mechi mbili.

Lakini jambo la msingi ni kujiuliza kwa nini mabingwa hawa wa mwa-ka 1995 wamechemka mapema?

Ikumbukwe mwaka jana wali-shika nafasi ya tatu wakiwafunga ndugu zao wa Bara lakini safari hii waliishia hatua ya makundi.

Moja kati ya sababu kubwa ya Zanzibar kushindwa safari hii na kubwa kuliko zote ni kuwa Zanzi-bar ilishashindwa tangu ilipotwaa nafasi ya Tatu mashindano yaliyo-pita baada ya wachezaji wa Zanzi-bar kugawana fedha. Jambo hilo liliwakera viongozi wa ZFA wakati chama kilipokuwa kikiongozwa na Ibrahim Amani Makungu. Mmoja kati ya wachezaji waliokumbwa na mkasa wa kufungiwa alikuwa nahodha wa klabu ya Dar es Sa-laam Young Africans ambaye safari hii hakuwemo kikosini. Wapo wachezaji wengine ambao hawakujumuishwa kikosini pia kama Agrey Moris ,Abdihalim Homoud,Twaha Mohammed japokuwa Nassor ‘Cholo’ Masoud

aliitwa.

Jambo la pili ambalo liliikosesha Zanzibar ushindi safari hii ilikosa kabisa kupata japo hata mechi ya kirafiki katika kujiandaa na mi-chuano hiyo japo ilijaribu kuomba mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya lakini ilikataliwa kwa kuibagua kuwa haitambuliwi na Fifa. Huu ulikuwa mwiba mkali kwa Zanzi-bar Heroes mwiba ulioanzishwa na Kim Poulsen, meneja wa timu ya taifa ya Tanzania. Zanzibar Heroes ilibakia kuwa yatima aliy-eachwa katika kina kirefu cha Ba-hari bila kupata msaada wowote na ndipo ilipoamua kucheza me-chi ya kirafiki na klabu ya ndani ya Zanzibar. Lakini kabla ya Zanzibar kukwea pipa kwenda nchini kenya baadhi ya wadau walianza kulala-mika kuhusu uteuzi uliofanywa na kocha Salum Bausi kwa kuchagua wachezaji wa upande mmoja wa

Unguja kitu ambacho kiliigawa tena Zanzibar Heroes na kuone-kana kuwa ni timu isiyo na usawa katika uteuzi. Ni dhahiri kuwa tayari Zanzibar Heroes ilishaain-gia katika msongo wa mawazo kwa wachezaji,kocha,pamoja na viongozi pasina kusahau mashabiki.

Zanzibar Heroes ambayo iliagwa na naibu waziri wa habari utama-duni na michezo Bihindi Hamad Khamis waliondoka huku wakia-hidiwa zawadi kem kem.Tuje kiwanjani Zanzibar He-roes ilifungua dimba na Sudan Kusini ambayo ndio mechi pekee w a l i o s h i n d a . Yawezekana ilikuwa ni k a m a b a -

CHALLENGE CUP 2013

Mashujaa wa Zanzibar walishindwa kabla mashindano kuanza

Na David Kambona Michezo

40

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

41

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >

Page 22: Zanzibar Daima Online Toleo la Nane

michuano hiyo. Zanzibar il-ishinda magoli mawili kwa moja mchezo ambao Zanzibar ilicheza lakini sio kwa kiwan-go ambacho wengi wetu tu-likitegemea. Jahazi la Zanzibar lilionekana linazama baada ya timu hiyo kukutana na Rwanda na baadaye Mwenyeji Kenya ambapo katika mechi zote mbili Zanzbar Heroes iliishia kupata vipigo.

Lakini kwa nini hasa timu yetu hii inafungwa au kwa nini ina-

fanya vibaya kwani hata Brazil huwa inafungwa. Sababu na-dhani ni mipangilio mibovu ya kiundeshaji. Tutazame mechi ya kirafiki Zanzibar ingeweza kuomba mechi ya kirafiki na nchi zifuatazo kama Somalia, Eritrea au hata timu za vijana za Uganda, Rwanda au hata Bu-rundi kwa sababu tayari Kenya walishaweka kizingiti cha kuwa Zanzibar haimo katika Fifa .

Ni wazi Zanibar ilikwisha shindwa kabla ya kukwea pipa

shida moja kuu ambayo inaiumiza Zanzibar hasa katika maende-leo ya kisoka ni kukosa uzalendo ,kutokuwa na uchungu ,kukata tamaa, na uwekezaji mbovu. Hadi kufika sasa bado hatujapata hasa aina ya mchezo wetu binafsi ki-wanjani. Kwa Zanzibar Heroes michuano pekee ya kimataifa ni mashindano ya Chalenji. Kama ingekuwa ipo katika uangalizi mzuri ndio timu ambayo ingechukua ubingwa wa mashindano haya mara nyingi zaidi kuliko timu nyingine yoyote kwani ndani ya miaka sita au saba ijayo nchi kama Kenya, Uganda na Rwanda sitashangaa kama zitaku-wa zinaleta timu za vijana katika mashindano haya kwa sababu tu-naona tayari baadhi ya wachezaji wao wameanza kupata nafasi za kucheza soka katika nchi za Ma-gharibi.

Lakini Zanzibar na Tanzania Bara bado hatujaweza kufanikiwa kwa hilo. Wachezaji wengi wa Zanzi-bar ukiwatazama wanapocheza katika timu ya taifa ya Zanzibar ni wachezaji ambao wanacheza soka wakiwa wana vipaji ambavyo havikuendelezwa na huu ndio umekuwa ugonjwa wa kudumu. Binafsi ningeona ZFA kuwa ina watu wa maana kama wataalian-galia suala hili kwa utimilifu baada ya mashindano haya kumalizika. Tungeanza mchakato wa kutafuta timu bora itakayoshiriki michua-no ya Chalenji mwakani kwa ku-wafuatilia wachezaji kwa ukaribu kwa sababu bado sijashawishika na uteuzi unaofanywa sasa katika Timu ya Zanzibar.

Je, ni kweli makocha wanafanya kazi wanavyositahili? Jukumu la timu ya taifa sio la kocha mmoja ni

la makocha wote wa Zanzibar na benchi la ufundi ni jambo la kitaifa sidhani kama kunakuwa na takwi-mu za kuwatazama kila baada ya mechi za ligi kujua uwezo, tabia, maana kuna mambo mengi ya kiufundi kujua faida na hasara za mchezaji za kila mchezaji.

Ninamaliza kwa kusema kama ha-tutazingatia mambo haya na tu-kiendelea kuchagua timu kiholela hatutoweza kufanya vizuri katika mashindano yoyote kwani mpira ni mchezo unaochezwa mchana kweupe. Hauchezwi kizani kana kwamba hatutaona makosa. Tu-tazame kwa nini tunajihujumu sisi wenyewe; kweli wanacheza wa-chezaji kumi na moja lakini waki-fungwa tumefungwa nchi nzima .Yatupasa kuwa na uchungu

TIMU YA TAIFA YA ZANZIBARWachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar wakifanya

mazoezi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kabla ya

kuondoka kwenda kushiriki mashindano ya Challenge

Cup 2013 huko Kenya

RAIS WA ZFA“Naelewa kila kitu kinacholikwamisha soka letu na

nazijua shida mlizonazo hivyo naomba mniamini

kuwa nitasimamia kanuni na katiba katika kuziondoa

na kwamba mjue wajumbe sote tutakuwa na hadhi

sawa na hakuna alie juu ya mwengine kikubwa ni

maelewano tu”

42

ZANZIBAR DAIMA ONLINE>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013>

43

TOLEO LA DISEMBA 2013 - JANUARI 2014 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 08 - DISEMBA 2013 >