MONT NURSERY AND PRIMARY SCHOOLS LTD DARASA LA SABA...

Preview:

Citation preview

Ukurasa wa 1 ka� ya 7

DARASA LA SABA

01 KISWAHILI

Maelekezo

1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45)

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).

4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR na katika ukurasa wenye swali la 41 hadi 45

kwenye karatasi ya maswali.

5. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa

6. Weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililo sahihi kwa swali 1 – 40.

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi futa kivuli hicho kwa umakini

kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.

8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali la 1 – 40: na kalamu ya wino wa bluu

aumweusi kwa swali la 41 – 45.

9. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

MONT NURSERY AND PRIMARY SCHOOLS LTD

Ukurasa wa 2 kati ya 7

SEHEMU A: SARUFI (Alama 20)

Katika swali la 1 – 20 weka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu yako ya kujibia.

1. Neno lipi linakamilisha sentensi ifuatayo kwa usahihi? “Sikumkuta mwalimu _____ nilipotembelea

shuleni kwao.

A. yote B. wote C. yeyote

D.yoyote E. wowote.

2. Katika sentensi ifuatayo ni neno lipi limetumika kama kivumishi?

“Juzi mwalimu alivaa viatu vizuri”.

A. viatu B. alivaa C. vizuri

D. Juzi E. mwalimu.

3. Kipi ni kinyume cha neno “shuruti”

A. Radhi B. Lazima C. Sharti

D. Hiyari E. Haraka.

4. Katika sentensi ifuatayo neno linalokosekana ni lipi?

“Humo _____ alimopita mwanamichezo maarufu wakati anakwenda kwao”

A. Ndipo B. ndio C. ndiko

D. ndie E.ndimo.

5. Mtaalamu wa elimu ya nyota huitwaje?

A. Mpiga ramli B. Mshirikina C. Mtabiri

D. Mganga wa kienyeji E. Mnajimu.

6. Ili tupate mazao mengi ________ tulime kwa bidii.

A. ni budi B. kuna budi C. pawe na budi

D. hatuna budi E. pana budi.

7. Nyumba imeharibiwa na mvua; Sentensi hii ipo katika kauli ipi?

A. kutenda B. kutendewa C. kutendeana

D. kutendana E. kutendeana.

8. Kama Asha angalisoma kwa bidii _______-

A. angefaulu mtihani B. angelifaulu mtihani C. angalifaulu mtihani

D. angifaulu mtihani E. angelifaulisha mtihani.

9. Wewe ni mtoto mdogo. Neno wewe katika sentensi hii liko katika nafsi gani?

A. nafsi ya umoja B. nafsi ya kwanza C. nafsi ya tatu

D. nafsi ya wingi E. nafsi ya pili.

Ukurasa wa 3 kati ya 7

10. Mtoto mwema humsaidia mzazi wake.Neno “wake” katika sentensi hii ni nini?

A. kielezi B. nomino C. kivumishi

D. kitenzi E. kiunganishi.

11. Umoja wa sentensi “Njiwa hawa wanakunywa maji.” Ni upi?

A. Njiwa hii ina kunywa maji. B. Njiwa yule anakunywa maji C. Njiwa hili linakunywa maji

D. Njiwa huyu anakunywa maji E. Njiwa huyu imekunywa maji.

12. Mtu hodari asiyeogopa kwa neno moja huitwaje?

A. Mpiganaji B. Mpambanaji C. Jasiri

D. Jambazi E. Katili.

13. Masalale! Tumekwisha.Neno “masalale” limetumika kama nini?

A. Kiwakilishi B. Kihisishi C. Kiwakilishi

D. Nomino E. Kitenzi.

14. “Ingawa kulikuwa na nuru ya kutosha, tayari ilikwishatimia saa moja kamili”Neno“nuru”maana yake ni

A. taa B. mawingu C. giza

D. mwanga E. umeme.

15. “Asha na Amina wanapigana”.Neno “wanapigana” liko katika kauli ipi?

A. Kutendeana B. Kutendwa C. Kutendana

D. Kutendewa E. Kutendea

16. Katika sentensi: “Mtoto anaendesha gari” herufi katika neno anaendesha inawakilisha kiambishi cha

aina ipi?

A. Rejeshi B. Wakati C. Tamati

D. Nafsi E. wakati.

17. Sentensi hii “Mama mdogo alikuwa analima shambani” ni aina ipi ya sentensi

A. Ambatano B. Changamano C. Sahili

D. Shurutia E. Sahili - shurutia.

18. Kitoto hiki kinacheza kitoto.Neno lililopigiwa mstari limetumika kama _______-

A. Kielelezi B. Kivumishi C. Nomino

D. Kielezi E. Kitenzi

19. Sikuweza kutambua ni nani amelala kitandani kwa sababu alijifunika shuka _______

A. Zama B. Nzima C. Lote

D. Zima E. Gubigubi.

Ukurasa wa 4 kati ya 7

20. Neno “BAKULI” lipo katika upatanisho wa ngeli ya aina gani?

A. U – YA B. I – IZI C. LI – YA

D. A – WA E. U – ZI

SEHEMU B: LUGHA YA KIFASIHI (Alama 10)

Katika swali la 21 – 30, weka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu yako ya kujibia.

21. Kunata ni_________

A. Kujisifu B. Kujikata C. Kuringa

D. Kuwa msafi E. Mrembo

22. Salumu anajikomba ina maana ya _________

A. Anajipenda B. Anajigamba C. Anajila

D. Anajipendekeza E. Anajishaua

23. Methali hii “Penye miti hakuna wajenzi” ni sawa na

A. Haraka haraka haina Baraka B. Mbio za sakafuni huishia ukingoni

C. Upele humwota asiye na kucha D. Akiba haiozi E. Ahadi ni deni

24. Babu huanika sembe usiku asubuhi huiondoa” kitendawili hiki jibu lake ni ______

A. nyota B. Mwezi C. Umande

D. Mvua E. Maji.

25. Methali hii “Kila mwamba ngoma, ngozi huvutia kwake” ina maana gani?

A. Ngoma ikilia sana upasuka B. Ngoma huwambwa kwa kutumia ngozi

C. Bandu bandu humaliza gogo C. Mtaka cha uvunguni sharti uiname

E. Kila mtenda jambo huvutia kwake.

26. Msemo “kubarizi” maana yake ni kukusanyika kwa ajili ya _________

A. Sherehe B. Chakula cha pamoja C. Mkutano

D. Mazungumzo ya kawaida E. Burudani.

27. Methali isemayo “Kila mtoto na koja lake” ina maana gani?

A. Kila binadamu ana mapungufu yake B. Kila mtoto ana matatizo yake

C. Kila mtoto ana mapungufu yake D. Kila binadamu ana tabia yake

E. Kila mtoto ana wazazi wake.

28. Tegua kitendawili kifuatacho “Nyumbani kwangu kuna jini mnywa maji.”

A. Mtungi B. Kata C. Kibatari

D. Kikombe E. Kinywa.

Ukurasa wa 5 kati ya 7

29. Wakulima wa korosho mkoani Mtwara wamepewa heko kwa kuzalisha korosho bora.

Msemo “wamepewa heko”hufanana na msemo gani kati ya hii ifuatayo?

A. Kupewa tunzo B. Kupewa pongezi C. Kupewa hawala

D. Kupewa heri E. Kupewa zawadi

30. Methali ipi kati ya hizi zifuatazo haifanani na zingine?

A. Mtegemea nundu haachi kunona B. Nazi haishindani na jiwe

C. Mlinzi wa kisima hafi kiu D. Anayekaa karibu na waridi hunukia

E. Mgaa gaa na upwa hali wali mkavu.

SEHEMU C: USHAIRI (Alama 06)

Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali 31 – 36 kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu lililo

sahihi katika fomu yako ya kujibia.

Wanafunzi mashuleni, kuweni wenye nidhamu,

Masomo zingatieni, ulegevu uwe sumu,

Ya maana jifunzeni, kutokana na walimu,

Nidhamu kwa wanafunzi, ni msingi wa elimu.

Wengi hamjali, darasani kucheza tu,

Mafunzo ya maadili, mwayaona sio kitu,

Hamtaki kubadili,tabia hiyo ya kutu,

Nidhamu kwa mwanafunzi, ni msingi wa elimu.

MASWALI

31. Katika ubeti wa kwanza mshairi anaeleza kuwa ulegevu ni____

A. Unyonge B. Sumu C. Sugu

D. Huleta mafanikio E. Uwe mtaji.

32. Shairi hili lina jumla ya beti ngapi?

A. Tatu B. Mbili C. Nne

D. Moja E. Tano.

33. Vina vya kati na mwisho vya ubeti wa pili ni _______

A. nzi na mu B. ili na itu C. li na tu

D. li na tu E. mu na nzi.

34. Unafikiri tabia ya “kutu” inayoelezwa na mtunzi ina maana ya _______

A. Tabia nzuri B. Tabia ya unyonge C. Tabia ya majivuno

D. Tabia ya upendo E. Tabia mbaya.

Ukurasa wa 6 kati ya 7

35. Kichwa cha shairi hili kinachofaa ni _______

A. Nidhamu kwa wanafunzi B. Matatizo katika shule C. Wanafunzi na walimu

D. Ufundishaji shuleni E. Utoro wa wanafunzi

36. Mkarara katika shairi hili ni__________

A. Wanafunzi mashuleni B. Nidhamu kwa wanafunzi C. Tabia ya kutuwa elimu

D. Msingi wa elimu E. Nidhamu kwa wanafunzi ni msingi wa elimu.

SEHEMU D (Alama 04)

Umepewa insha yenye sentensi nne (4) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo katika swali la

37 – 40. Zipange sentensi hizo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A,B,C na D

.Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi katika fomu yako ya kujibia.

37. Hivyo mazoezi huleta afya, kwa hiyo ni muhimu kwa kila mmoja wetu kufanya mazoezi.

38. Mtu asiyefanya mazoezi anapata maradhi ya moyo;atanenepa kupita kiasi, kwa hiyo atapata ugonjwa

wa kuumwa mgongo na magoti.

39. Mazoezi ya viungo yanachangamsha misuli ya mwili, mifupa na ubongo.

40. Lakini mtu anayefanya mazoezi anaepuka magonjwa ya moyo na msukumo wa damu.

Ukurasa wa 7 ka� ya 7

SEHEMU E: UFAHAMU (Alama 10)

Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali 41 – 45 kwa kuandika jibu sahihi katika nafasi

iliyoachwa wazi.Tumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi.

Hakika majuto ni mjukuu.Leo najuta kwa kukataa kwenda shule.Nakumbuka hapo zamani wazazi wangu

waliposisitiza umuhimu wa elimu.Sikuamini kuwa elimu ni ufunguo wa maisha.Niliamini kuwa maisha ni

bahati.

Sasa nimekuwa mtu mzima.Mateso niyapatayo yananifanya niamini kuwa elimu ni ufunguo wa

maisha.Natamani siku zirudi nyuma ili nirudi shule, lakini haiwezekani asilani.Nimeyakubali mateso haya

japo leo inanibidi niwe mshauri wa walio shuleni.Pambaneni muipate elimu kwani itawatoa gizani katika

siku za usoni

MASWALI

41. Neno “asilani” kama lilivyotumika katika habari hii lina maana gani?__________________________ 42. Msimuliaji hakutaka shule kwani aliamini maisha ni nini?___________________________________ 43. Wazazi wa msimuliaji walisisitiza nini?___________________________________________________ 44. Msimuliaji anajuta kwa sababu alikosa nini?______________________________________________ 45. Msimuliaji ameamua kuwa nani? _______________________________________________________

Recommended