180
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA SABA Kikao cha Pili – Tarehe 6 Novemba, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. ASIA MINJA – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya mwaka 2018. NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Kipindi cha mwaka 2016/2017 hadi robo ya kwanza 2019/ 2020. NAIBU SPIKA: Ahsante. Katibu.

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

  • Upload
    others

  • View
    2

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA

____________

MAJADILIANO YA BUNGE

___________

MKUTANO WA KUMI NA SABA

Kikao cha Pili – Tarehe 6 Novemba, 2019

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu.

NDG. ASIA MINJA – KATIBU MEZANI:

HATI ZA KUWASILISHA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:-

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU:

Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya mwaka 2018.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO:

Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwaKipindi cha mwaka 2016/2017 hadi robo ya kwanza 2019/2020.

NAIBU SPIKA: Ahsante. Katibu.

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

NDG. ASIA MINJA – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

NAIBU SPIKA: Tutaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu,Mheshimiwa Mashimba Ndaki sasa aulize swali kwa niabaya Mheshimiwa Makame Mashaka Foum.

Na. 14

Sheria Na.9 ya 2010 ya Watu Wenye Ulemavu

MHE. MASHIMBA M. NDAKI (K.n.y. MHE. MAKAMEMASHAKA FOUM) aliuliza:-

Sheria Na.9 ya mwaka 2010 ya Watu wenye Ulemavuimeainisha haki za msingi za Watu wenye Ulemavu ikiwa nipamoja na haki ya ukalimani katika maeneo ya utoajihuduma kama vile hospitali, taarifa ya habari, shuleni nk:-

Je, Serikali inachukua hatua gani ili kuharakishautekelezaji wa sheria hii?

NAIBU SPIKA: Majibu, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi yaWaziri Mkuu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, WATU WENYEWALEMAVU (MHE. STELLA IKUPA ALEX) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu,naomba kujibu swali la Mheshimiwa Makame Mashaka Foum,Mbunge wa Kijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Watu wenyeUlemavu Na.9 ya mwaka 2010, imeweka misingi yaupatikanaji wa haki kwa watu wenye ulemavu ikiwepo hakiya upatikanaji wa habari kwa kundi la viziwi kupitiawakalimani katika sehemu mbalimbali ikiwemo hospitali,shuleni pamoja na vyombo vya habari yaani luninga.

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea najitihada za kuweka mikakati ya kuwa na wakalimani wakutosha wa lugha ya alama kwa kuanzisha programu yamafunzo ya lugha ya alama katika Chuo Kikuu cha Dar esSalaam kupitia Mradi wa LAT (Lugha ya Alama Tanzania).Chuo kimeandaa mwongozo wa mwaka 2019 wa majaribioya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu(KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa darasala awali, la kwanza na la pili. Aidha, imeandaliwa kamusi yalugha ya alama na machapisho mbalimbali yanayotoamwongozo wa namna ya kujifunza lugha hiyo kwa lengo lakuongeza wakalimani.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuendeleza kundikubwa la wakalimani na watumiaji wa lugha ya alama,Serikali imechukua hatua ya kutumia lugha ya alama kamalugha ya kufundishia na kujifunzia shuleni. Aidha, kufundishalugha ya alama kama somo mojawapo katika shule na vyuo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia hotuba yaMheshimiwa Waziri Mkuu katika kilele cha Wiki ya Viziwiiliyofanyika katika Manispaa ya Iringa alitoa maagizo kwavyuo vya elimu ya juu na kati kuweka mtaala ambaoutawezesha wahitimu kusoma lugha ya alama kama somola lazima katika masomo yao (compulsory subject). Aidha,Mheshimiwa Waziri Mkuu aliagiza vyombo vyote vya habarikuwa na wakalimani wa lugha ya alama katika vipindi vyaluninga zao.

MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana. Kwa kuwa sasa lugha ya alama inatumikakwenye chombo kimoja tu cha TBC lakini TV stations zinginehazina ikiwa ni pamoja na TV station ya hapa Bungeni. Je,Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba TV stationskaribu zote zina wakalimani na watafsiri wa lugha ya alama?(Makofi)

NAIBU SPIKA: Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, majibu.

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nipongeze piamaswali ambayo yamejibiwa na Naibu Waziri lakini kamaambavyo swali limeulizwa kwamba sisi kama Serikali tunampango gani katika kuhakikisha kwamba vyombo vyotevinatoa huduma ya ukalimani kwa watu ambao wana tatizola ulemavu, sisi kama Serikali ambao tumekuwa tukisimamiamasuala mazima ya habari, kwa upande wa TBC ni wazikwamba tumeboresha na sasa hivi tuna wakalimani zaidi yawanne na vipengele vyote muhimu ikiwepo taarifa ya habarina vipindi maalum, wakalimani wa lugha za alamawamekuwa wakitoa hizo tafsiri. Ni takwa la kisheria kuwa nawakalimani na sisi kama Wizara ambayo tunasimamiamasuala ya habari tumekuwa tukisisitiza kwamba vyombovyote vya habari vikiwepo vyombo vya umma pamoja nabinafsi vihakikishe kwamba vinakuwa na wakalimani walugha za alama.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nitumie nafasi hiikutoa wito kwa wamiliki wote wa vyombo vya habarikuhakikisha kwamba wanatekeleza takwa hilo la kisheria kwakuwa na wakalimani wa lugha za alama. Nashukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ritta Kabati.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niulize swali dogo lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa watu wenyeulemavu wamekuwa wakipata shida sana wanapokwendakutibiwa katika hospitali zetu kwani kumekuwa hakunamawasiliano kati ya daktari na mtu mwenye ulemavu kwasababu ya daktari kutojua lugha za watu wenye ulemavu.Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba wanawekamkalimani kati ya daktari na mtu mwenye ulemavu ili awezekutibiwa kile ambacho anatakiwa kutibiwa?

NAIBU SPIKA: Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Watuwenye Ulemavu, majibu.

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, WATU WENYEULEMAVU (MHE. STELLA IKUPA ALEX): Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ritta Kabati, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa suala ambaloameliuliza Mheshimiwa Mbunge kama ambavyo nimejibukwenye jibu langu la msingi kwamba tuna upungufu wawakalimani wa lugha ya alama. Wizara ya Afya ilishatoamaelekezo kwamba kwa kuwa sasa hivi tunajiandaa natunawaandaa wakalimani wa lugha za alama basi watuwenye ulemavu wanapoenda hospitali waruhusiwe kwendana watu ambao wanawaamini ili mawasiliano yawezekufanyika vizuri kati ya mtu mwenye ulemavu na daktari amana mtu anayemhudumia.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ally Saleh, swali lanyongeza.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Kwa kuwa kitu chema kinaanza nyumbani basinapenda kumuuliza Mheshimiwa Waziri kwa nini lugha yaalama haianzii hapa Bungeni pale juu tukawa na mkalimanimaana hii haioneshi kwamba kweli tunataka mabadiliko kwasababu Bunge lilitakiwa liwe mfano? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Watuwenye Ulemavu, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, WATU WENYEULEMAVU (MHE. STELLA IKUPA ALEX): Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ally Saleh,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ndani ya Bunge hili laJamhuri ya Muungano wa Tanzania wapo wakalimani walugha ya alama wawili. Hata sasa hivi tunavyozungumza hayayanayoendelea hapa yanatafsiriwa kwa lugha ya alama.Ahsante.

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Khadija Nassir.

MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Kwa kuwa Tanzania ni nchi wanachama waUN na tuliridhia na kusaini Mkataba wa Haki za Walemavu.Je, ni lini Serikali itakuwa tayari kupeleka Ripoti ya Utekelezajiwa Haki za Binadamu UN ili sasa tuweze kuona way forwardya wenzetu ambao wana ulemavu? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Watuwenye Ulemavu, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, WATU WENYEULEMAVU (MHE. STELLA IKUPA ALEX): Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa KhadijaNassir, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ni kweli iliridhia Mkataba huu waKimataifa na inatambua kwamba iko haja sasa ya kupelekaUN Ripoti ya Utekelezaji wa Masuala ya Watu wenye Ulemavu.Ripoti hii inaandaliwa, ipo kwenye hatua za mwisho na karibiaitawasilishwa. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Tunaendelea na swali la MheshimiwaAnne Kilango Malecela, Mbunge wa Kuteuliwa.

Na. 15

Mwaka 2019 Kuwa Mwaka wa Uwekezaji Tanzania

MHE. ANNE K. MALECELA aliuliza:-

Tarehe 8 Machi, 2019, Mheshimiwa Rais Dkt. JohnMagufuli, alipokuwa Ikulu kwenye dhifa ya Mabaloziwanaowakilisha nchi mbalimbali Duniani aliutamka mwaka2019 kuwa ni mwaka wa uwekezaji: -

Je, Serikali imejipangaje katika kutekeleza tamko hilomuhimu sana?

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi yaWaziri Mkuu (Uwekezaji), majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (UWEKEZAJI)alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu napenda kujibu swali la Mheshimwa Anne KilangoMalecela, Mbunge wa Kuteuliwa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendeleakutekeleza mipango na mikakati mbalimbali inayolengakuhakikisha tamko la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, ali lolitoa katika dhifa yaWaheshimiwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapaTanzania, la mwaka 2019 kuwa Mwaka wa UwekezajiTanzania, linatekelezwa ipasavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kutekeleza tamkohilo, Ofisi ya Waziri Mkuu imeanza kufanya mapitio ya Seraya Uwekezaji ya mwaka 1996 pamoja na Sheria ya Uwekezajiya mwaka 1997 ili kuweka misingi imara ya kuboreshamazingira ya uwekezaji yatakayoendana na hali ya sasa yakiuchumi duniani.

Aidha, Serikali imeongeza mkazo katika kuimarishamiundombinu wezeshi ya kiuchumi ikiwa ni pamoja naupatikanaji wa nishati ya uhakika na ya bei nafuu, maji,mawasiliano, ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji ya reli,barabara, madaraja, anga, vivuko na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile, Serikali imeendeleakutekeleza Mpango Kazi wa Kuboresha Mifumo ya Udhibitiwa Biashara (Blueprint Action Plan) ambapo hadi sasa Serikaliimeweza kufuta na kuboresha tozo na ada 54 zilizoonekanani kero kwa wawekezaji na wafanyabiashara kupitia bajetiya mwaka 2019/2020. Hatua nyingine ni pamoja na kuondoamigongano na muingiliano wa majukumu miongoni mwaMamlaka za Udhibiti kama vile Shirika la Viwango Tanzaniana Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba.

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kutangaza fursa zauwekezaji zilizopo mikoani vilevile Ofisi ya Waziri Mkuu kupitiaKituo chetu cha Uwekezaji (TIC) imeendelea kushirikiana naOfisi za Mikoa kuandaa makongamano ya uwekezajiyanayonadi vizuri fursa za uwekezaji mikoani. Kwa mwakahuu 2019 kwa mikoa ambayo tayari imeshafanyamakongamano hayo ni takribani mikoa 9 na kwa sasatunaendelea na maandalizi katika Mkoa wa Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, Serikali imejidhatitikuhakikisha changamoto zinazokabili wawekezaji nchinizinapatiwa ufumbuzi kupitia mikutano ya mashauriano katiya Serikali na sekta binafsi katika ngazi za Mikoa na katikasekta mbalimbali. Kwa sasa tumeshafanya mikutano hiyokatika Mikoa ya Arusha, Ruvuma, Lindi na Mtwara.

Aidha, Serikali inaendelea kuvutia uwekezaji kutokanje kwa kutekeleza ipasavyo diplomasia ya uchumi kupitiaBalozi zetu za nje pamoja na kufanya mikutano ya kimkakatina wawekezaji wa nje waliowekeza nchini ili kuvutia uwekezajizaidi na kufanya mashauriano nao.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Anne Kilango Malecela,swali la nyongeza.

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kupata jibu kwamba Serikali inashughulikia sualahili lakini naomba kuuliza swali moja tu la nyongeza, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Tanzania ni nchimojawapo katika nchi 4 za Afrika ambazo zinalima pambaambayo ni organic. Naomba Serikali iniambie ina mikakatigani ya kuwaalika wawekezaji katika zao hili la pamba nchiniili wafungue viwanda hapa nchini kuliko ambavyo tunauzapamba ghafi ambapo tunapata hasara sana? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi yaWaziri Mkuu (Uwekezaji), majibu.

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (UWEKEZAJI):Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la MheshimiwaAnne Kilango Malecela, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nimpongezekwa namna ambavyo amekuwa akisimama imara katikakuhakikisha kwamba zao letu la pamba linaongezewathamani ili badala ya kuuza zaidi ya asilimia 70 ya pambayetu ghafi basi kwa kiasi kikubwa tunaweza kuiongezeathamani hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa kama Serikalitunayo mikakati ya muda mfupi, wa kati pamoja na mudamrefu. Mfano ukiangalia katika nchi zingine kama Bangladeshna Ethiopia kwa upande wa Afrika ambazo zimefanikiwaunaangalia kuna mnyororo wa thamani, wapo ambaowameanzia katika utengenezaji wa nyuzi, mfano kamaBangladesh na Ethiopia wao wameanzia katika mnyororo wamwisho kabisa wa kutengeneza mavazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia katika masualaya mtaji, mfano mwekezaji mmoja tu ambaye anatengenezamavazi anaweza akaajiri mpaka watu 20,000 lakini wakatihuohuo mtaji wake anaoutumia inaweza ikawa ni dola milioni3 mpaka milioni 4. Wakati ukianzia katika ngazi labda ya nyuzipamoja na vitambaa inaweza ikakugharimu zaidi ya dolamilioni 10 au zaidi na wakati huohuo ajira pia inakuwa sionyingi sana. Kwa hiyo, kama Serikali tunatambua umuhimuwa mnyororo mzima wa thamani, tunachokifanya kwa sasani kuangalia sasa twende vipi, twende na hatua zote kwaupande huo wa mnyororo au tujikite zaidi kama ambavyowenzetu wa Ethiopia wamefanya na ukizingatia kwambahata hawazalishi pamba nyingi zaidi hai kama ambavyotunafanya Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, nisema tu kwamba kwanzanaendelea kuwapongeza wakulima wote wa pamba nanaendelea kutoa rai kubwa waone ni kwa namna ganiwanaboresha ubora wa pamba yenyewe wanayoizalishakupitia kilimo. Ukiangalia katika uzalishaji wenyewe wa mavazi

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

pamoja na nguo zetu kwa kiasi kikubwa zinahitaji kuwa naconsistency katika mnyororo mzima. Haiwezekani leo ukawana ubora wa aina hii halafu kesho una ubora mwingine. Kwahiyo, niendelee kutoa rai kwa Maafisa wetu wa Uganiwaendelee kutoa elimu kwa wakulima wetu wa pambakuhakikisha kwamba katika uzalishaji wa pambawanayoizalisha basi kuona kwamba inaendelea kuwa naubora unaotakiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ukiangalia hatakatika viwanda vyetu, pamba inayozalishwa ni takribani tani300,000 mpaka 400,000 kwa mwaka. Katika msimu wa mwakahuu kwa makadirio ya Wizara ya Kilimo ni kuweza kupatatakribani tani 450,000 lakini ukiangalia uwezo wa viwandavyetu takribani 54 ni kuweza kuzalisha zaidi ya tani 786,000.Kwa hiyo, bado tuna upungufu ni lazima yote haya uzalishajipamoja na kuboresha uwekezaji viweze kwenda sambamba.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo ni sualazima la mitaji. Ukiangalia katika sekta nzima ya uzalishaji wanguo na mavazi, viwanda vinahitaji mitaji mikubwa sana. Sihilo tu, wapo ambao wamefanikiwa kama kina JamboSpinning lakini wamejikuta wameshindwa kuendelea nauzalishaji. Hii ni kutokana na sababu kwanza mtaji ni mkubwalakini akifanikiwa kuweka mtaji bado mazingira siyo wezeshisana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunachokifanyakama Serikali sasa hivi ni kuangalia sekta ndogo hii ya nguona mavazi kupitia Mkakati wetu ule wa Nguo na Mavazi wamwaka 2016 – 2020 kuweza kuona ni kwa namna gani sasatutaweza kuweka vivutio maalum. Kwenye hili siwezi kusematutaweka vivutio vya aina gani kwa kuwa tutatunga sheriapamoja, Mungu akijaalia nadhani muda si mrefu tutakuja naMuswada wa Sheria ya Uwekezaji ili tuweze kuangalia katikazile sekta ndogo mbalimbali, ni sekta zipi ndogo ambazokama nchi tunaziwekea kipaumbele tukitambua kwambandizo zinaajiri watu wengi lakini tukitambua kwamba inakuwana mnyororo mkubwa wa thamani.

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, napendakumpongeza sana Mheshimiwa Kilango na WaheshimiwaWabunge wote ambao wamekuwa wakifuatilia sanauzalishaji wa pamba lakini zaidi uongezaji wa pamba namatumizi yake. Nakushukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mariam Kisangi, swali lanyongeza.

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya kuuliza swali langukwanza kwa ruhusa yako napenda nimpongeze sanaMheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano waTanzania na Serikali yake kwa kutuletea ndege mpya ainaya Dreamliner Na.787 ambayo imefanya ndege zetu sasakuwa saba (7). Sambamba na hilo, pia uboreshaji wamiundombinu ya barabara na madaraja katika Jiji la Dar esSalaam. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema manenohayo, sasa naomba niulize swali langu la nyongeza, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali imejipanga vipikatika kuhakikisha inaleta wawekezaji wengi na kuendelezamiradi mingi ya uwekezaji kwenye Jiji la Dar es Salaam katikamaeneo ya Kigamboni ambayo yana ardhi ya kutosha, Ilalamaeneo ya Chanika lakini pia Kinondoni katika maeneo yaMabwepande? Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Angellah Kairuki, Waziri waNchi, Ofisi ya Waziri ya Mkuu, Uwekezaji, majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kujibu swalila Mheshimiwa Mariam Kisangi, Mbunge wa Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nisemekwamba tunashukuru kwa niaba ya Serikali na kwa niaba yaMheshimiwa Rais kwa pongezi alizozitoa kwa jitihada ambazoMheshimiwa Rais amezifanya mpaka sasa katika kuhakikishakwamba tunaongeza miundombinu ya usafirishaji lakinivilevile miundombinu mingine kama vile ya mawasilianopamoja na ya ujenzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa maeneoya uwekezaji nipende tu kumhakikishia Mheshimiwa MariamKisangi kwamba kupitia Wizara Ardhi tayari maeneo yauwekezaji yameshatengwa kwa Dar es Salaam Kigambonina tutaendelea kufanya hivyo katika maeneo mengine yaMkoa wa Dar es Salaam na tutaona ni kwa namna ganitunaendelea kuhakikisha kwamba tunapeleka Wawekezajikatika maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano kwa Kigambonitulishapata Wawekezaji hao wanaojenga Mradi huu waNyerere Hydro, wamekuwa wana nia ya kujenga Industrialpacks pamoja na vyuo vya kiufundi na tayaritumeshawapeleka Kigamboni waweze kuangalia na endapowataridhika na maeneo hayo, basi kwa hakika watawezakuwekeza kwa upande wa Kigamboni.

Pia niendelee kumuhakikishia pia MheshimiwaMbunge wapo Wawekezaji wengine katika viwanda vyanguo kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara watakuja tarehe8 Novemba, kutoka Italy na kwenyewe pia tutafanya hivyokuona ni kwa namna gani tunawapeleka wakaangalie nakuendelea kuwashawishi ili waweze kuwekeza katika maeneohayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee niendee kutoa raikwa Wizara ya Ardhi pamoja na Mamlaka zetu zaHalmashauri kuendelea kutenga maeneo ya uwekezajiambayo yana miundombinu wezeshi ili na sisi iwe kazi rahisikuvutia uwekezaji, lakini wanapokuja basi wapate maeneoambayo ni tayari ambayo watatumia muda mfupi katikakuanzisha uwekezaji wao, nakushukuru.

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Raphael Chegeni, swalila nyongeza.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri sana yaMheshimiwa Waziri wa Uwekezaji naomba nijikite kwenyesuala la Mheshimiwa Anne Kilango Malecela kuhusiana nasuala la pamba.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli mnyororo wathamani katika suala la pamba cotton to cloth unapaswakufanyiwa mkakati mahsusi kwa kumwezesha mkulima awezekupata thamani ya kile anachokifanya, lakini swali langu nikwamba wakulima wa pamba ambao mwaka hadi mwakawamekuwa wakifanya kazi ya kulima pamba wanakuwawanapata hasara; kwa mfano leo hii wakulima wa Mkoa waSimiyu na hasa Wilaya ya Busega wameuza pamba tokamwezi wa Tano mpaka leo hawajalipwa fedha yao? SasaMheshimiwa Waziri haoni kwamba hii ni ku-discouragewakulima wasiweze kufanya kilimo kizuri zaidi na nini tamkola Serikali juu ya hili? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo,majibu.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. HUSSEIN M. BASHE):Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la MheshimiwaRaphael Chegeni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nikiri kwamba baadhi yawakulima wa pamba hawajalipwa fedha zao, pambamwaka huu mpaka sasa hivi jumla ya bilioni mia nne kumi nasaba zimeshalipwa kwa wakulima wa nchi nzima. Wakulimaambao hawajalipwa wanadai bilioni hamsini kufikia sasa hivina sababu ya msingi ni nini? Ni kwa sababu lazima tufahamukwamba pamba asilimia zaidi ya 80 inakwenda nje ya nchi,wanunuzi wetu wanakabiliwa na mtikisiko wa bei ambaoumewakabili katika soko la dunia na sisi kama nchi tulitoamaelekezo ya bei ya kununulia kama Serikali. Haya yalikuwamaamuzi ya Serikali kwa ajili ya kumlinda mkulima asipate

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

hasara, lakini Serikali imefanya intervention kuongea nafinancial institutions zote na kuweza kuwasaidia namna ganiya kupunguza interests kwa wanunuzi ili waweze kwendasokoni kununua bei ya pamba kwa Sh.1,200.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimuhakikishieMheshimiwa Mbunge, siku ya tarehe 14 tutakutana na Kamatiya wanunuzi wote makampuni yote yanayonunua ilikuangalia flow ya fedha inavyokwenda, lakini pamba yoteil iyokuwa kwa wakulima imeshakusanywa, sasa hivikilichobaki mkononi mwao ni tani 5,000 tu, ambayo tunaaminimpaka mwisho wa mwezi huu itakuwa imekwishaondokamikononi mwa wakulima na msimu unapoanza tarehe 15tunaamini wakulima wote pamba yao itakuwa imeondoka.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili la intervention yabei Serikali tunajitahidi kupunguza gharama kuanzia msimuhuu unaokuja na hatutoingilia kupanga bei, bei itakuwadetermined na soko na sisi jukumu letu kama Serikali itakuwakuhakikisha mkulima hatopata hasara. Tutatafuta njia zingineza kumlinda mkulima kuliko kumwathiri mnunuzi. Hii ndiyohatua ambayo tunachukua kama Serikali. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaendeleana Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.Mheshimiwa George Malima Lubeleje, Mbunge waMpwapwa, sasa aulize swali lake. (Makofi)

Na. 16

Ujenzi wa Soko Jipya - Mpwapwa

MHE. GEORGE M. LUBELEJE aliuliza:-

Soko la Mji wa Mpwapwa, ni dogo, limechakaa nahalifanani kabisa na hadhi ya Mji wa Mpwapwa ambao idadiya watu ni zaidi ya laki moja?

Je, Serikali ina mpango gani wa kusaidia ujenzi wasoko jipya na la kisasa katika mji huo?

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa niabaya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa, naomba kujibu swali la Mheshimiwa George MalimaLubeleje, Mbunge wa Mpwapwa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya yaMpwapwa inafahamu changamoto ya udogo wa soko laMji Mpwapwa na imekwishaandaa mikakati ya kujenga sokohilo la kisasa linaloendana na hadhi ya idadi ya watu katikaeneo hilo. Halmashauri imetenga eneo katika Kiwanja Na.61 Kitalu B Mazae chenye ukubwa wa mita za mraba 15,000kilichopo katika Kata ya Mazae.

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri inaendeleakuandaa Andiko la Mradi pamoja na kufanya usanifu ili iwezekuwasilisha andiko hilo Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa na hatimaye Wizara ya Fedha na Mipangokupitia utaratibu wa Miradi Mikakati, vilevile Halmashauriinaendelea na mazungumzo na uongozi wa Mradi wa LocalInvestmest Climate ili kupata fedha za ujenzi wa soko.Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa George Malima Lubeleje,swali la nyongeza.

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spika,pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninamaswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwaSerikali ilichukua vyanzo vingi vya mapato katika Halmashaurizetu, kwa hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa hainamapato ya kutosha ya kuweza kujenga soko; je, kwa niniSerikali isitoe fedha kwa ajili ya kujenga soko la Mpwapwakama vile inavyotoa fedha kujenga majengo mengine kamavile Vituo vya Afya na majengo mengine?

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa miminiliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Serikali zaMitaa na kwa kuwa jukumu la Mikopo ya Serikali za Mitaa nikukopesha Halmashauri ili ziweze kujenga masoko, kujengaVituo vya Mabasi; je, huo mpango umeishia wapi? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) MheshimiwaNaibu Spika, ahsante. Naomba nijibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa George Malima Lubeleje, kwapamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kweli kwambakuna vyanzo vingine vilichukuliwa na Serikali Kuu kutokaSerikali za Mitaa kwa maana ya Halmashauri, lakini hizi fedhaambazo zilichukuliwa kuletwa Serikali Kuu, kwa maana MfukoMkuu wa Serikali ni fedha ambazo zinatumika kujenga miradimikubwa ya Kitaifa ambayo inanufaisha maeneo yote yanchi. Zingeachwa kama ilivyokuwa maana yake kunaHalmashauri zingine zingepata miradi zingine zingekosamiradi, kitendo cha kupelekwa Hazina maana yake fedhahizi zinasimamiwa na Serikali na inapeleka miradi mikubwaambayo kila Mtanzania mahali popote alipo wananufaika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niliweke sawajambo hilo, lakini jibu langu la swali la pili ni kwamba, ni kwelikwa sasa kuna miradi ambayo Halmashauri Kuu inapewafedha kutoka pengine kwa Wafadhili wa nje, kadri mudaulivyokuwa unaenda miradi hii ilikuwa unapanga mipangoambayo huna uhakika nayo. Sasa Serikali imeleta MpangoMkakati ambayo ina uhakika hata mikopo kutoka Mfuko waSerikali za Mitaa ilikuwa ni fedha ambayo ina riba na wakatimwingine haina uhakika sana na kuna Halmashauri zinginezimekopa fedha zinadaiwa mpaka leo hawajawahikurejesha.

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

Mheshimiwa Naibu Spika, Kwa hiyo Serikaliaimetengeneza Mkakati pamoja na Wizara ya Fedha, fedhazipo Halmashauri inaandika andiko na Mheshimiwa Mbungeni Mjumbe katika Halmashauri yake vikao vya Kamati yaFedha wanaainisha mradi ambao wanadhani wao utakuwani mkakati wao kupata fedha nyingi, wanaleta Tawala zaMikoa na Serikali za Mitaa unaenda Hazina unapitiwa naWataalam, wakipata fedha hizo wataanzisha mradi mkubwakama hilo soko Mbunge alivyosema hiyo, hiyo fedhaikipatikana watafanya miradi ambayo wana uhakika nayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, yako maeneo juzi nilikuwaManispaa ya Moshi, wana Mradi wa zaidi ya shilingi bilioniishirini na nane, Jiji la Dar es Salaam wana bilioni hamsini nanane, maeneo mengine bilioni kumi na sita, kumi na saba,kumi na nane, kwa hiyo fedha zipo Mheshimiwa Mbunge naHalmashauri husika waandae Andiko la Kimkakati, tufanyetathmini wapate fedha wajenge mradi ambao utapatafedha za uhakika ili waweze kufanya miradi ya maendeleokatika eneo lao. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Qulwi Qambalo, swali lanyongeza.

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Mji wa Karatu ni Mji wa Kitalii na ni mji ambaounakua kwa kasi sana, lakini bahati mbaya mji huo hadi wasasa hauna soko la uhakika, Halmashauri kwa kutumiamapato yake ya ndani imeanza ujenzi wa soko la kisasa, je,Serikali lini itaunga mkono jitihada hizo za Halmashauri yaKaratu?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) MheshimiwaNaibu Spika, nakushukuru. Naomba nijibu swali moja lanyongeza la Mheshimiwa Qambalo Mbunge wa Karatu kamaifuatavyo:-

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwenyejibu langu la msingi ni kwamba Halmashauri zote hiziWakurugenzi wameelekezwa, wameitwa DodomaWakurugenzi wote nchi nzima, Waweka Hazina, MaafisaMipango wakapewa utaratibu, Serikali inachofanya kamasoko lenu mnadhani kwamba linakidhi viwango walete kamanilivyosema andiko ili fedha zitolewe waweze kufanya kazi,wanakopeshwa fedha, wanawekeza, wanasimamiawenyewe, wanaanza kurejesha kidogo kidogo. Hiyo ni fedhaambayo ina uhakika tofauti na kuahidiwa bilioni kumi halafuhaiji au unapata bilioni moja. Fedha za Miradi ya Kimkakatizipo, walete andiko tupitie, wapate fedha wasimamie naMheshimiwa Mbunge awepo ili wapate fedha ya uhakikana soko lisimame wapeleke huduma na kupata mapatomema ya kujenga Halmashauri yao.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu, swali lanyongeza.

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Kama ulivyo Mji waMpwapwa kuna Mji wa biashara unaitwa Endasak Wilayaya Hanang ni mahali ambapo wanahitaji soko kama hilowanalolihitaji Mpwapwa, naomba kujua kwa MheshimiwaWaziri ni nini kitakachofanyika kushirikiana na Halmashauriyetu pale tujenge soko kwa sababu imezungukwa navitunguu saumu, vitunguu maji, makabichi na nini na hakunasoko, Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) MheshimiwaNaibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi yaRais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, naomba nijibu swalila nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu, Mbunge waHanang kama ifuatavyo:-

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

Naomba majibu haya pia yaende kwa WaheshimiwaWabunge wote ambao wana maswali yanafanana na hayo;maelekezo ni kwamba Wakurugenzi na Wataalam wetukatika Halmashauri wameelekezwa, hii ni fursa tunaombawaitumie. kila Halmashauri inaangalia fursa ya kibiasharailiyopo, kuna wengine wameandika Miradi ya Kimkakatikujenga masoko, wengine wamependekeza kujenga stendina miradi mbalimbali kama hiyo na wale ambaowamefanikiwa tunavyozungumza fedha wamepewawanaendelea na ujenzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo MheshimiwaMbunge na Waheshimiwa wengine wote Halmashauri zotewalete maandiko katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa pamoja na Hazina tutapitia, fursa iliyopo waitumie,fedha hizi zipo pale, isipokuwa wale ambao walileta mkakatiwakapewa fedha na fedha zile hawakuzitumia, maelekezoyametoka vinginevyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, waandike haraka andikolao, washirikishe Wataalam wao, Waheshimiwa Wabungewashiriki, fedha zipo waanzishe miradi ya kimkakati tupatefedha za uhakika ili kukamilisha miradi ya maendeleo yawananchi na kuondoa kero katika maeneo yetu. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana swali la Mheshimiwa Salome Wycliffe Makamba, Mbungewa Viti Maalum, swali lake litaulizwa kwa niaba naMheshimiwa Sophia Mwakagenda.

Na. 17

Walimu wa Shule za Sekondari KuhamishiwaShule za Msingi

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA (K.n.y MHE. SALOMEW. MAKAMBA) aliuliza:-

Je, kuna sababu gani za kitaalam zinazosababishaWalimu wa Shule za Sekondari kuhamishwa Shule za Msingi

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

wakati ufaulu kwa Shule za Sekondari kwa masomo ya sanaaupo duni?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,naomba kujibu swali la Mheshimiwa Salome WycliffeMakamba, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilihamisha baadhiya walimu waliokuwa wanafundisha shule za sekondarikwenda kufundisha shule za msingi katika mwaka wa fedha2017/2018 ambapo walimu 8,693 walihamishwa. Walimu haowalihamishwa kutokakana na ziada ya Walimu wa masomoya sanaa waliokuwepo katika shule za sekondari za Serikalinchini ambapo wakati huo shule za msingi za Serikalizilionekana kuwa na upungufu mkubwa wa Walimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kitaalam Walimu wote washule za msingi na sekondari wameandaliwa na wanamfanano katika maeneo ya mbinu za kufundisha, yakisaikolojia na malezi na makuzi ya watoto wetu. Maeneohayo ambayo kimsingi ni muhimu kwa kila Mwalimu nahufundishwa katika ngazi zote za vyuo vinavyotoa taalumaya Ualimu nchini.

Naomba pia nilifahamishe Bunge lako Tukufu kuwa,suala la ufaulu duni husababishwa na sababu mbalimbalizikiwemo za kimazingira, ushiriki wa wazazi na jamii katikamchakato mzima wa ufundishaji na ujifunzaji kwa watoto.Hivyo, wingi wa Walimu pekee hautoshi kumfanyamwanafunzi afanye vizuri katika mtihani wake. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, swalila nyongeza.

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante. Serikali haioni kwamba imewavuruga Walimuwa sekondari ambao wamesomea kufundisha watu wa rikaya sekondari na kuwapeleka katika elimu ya msingi, haionikwamba imewachanganya na imeshusha morari ya utendajikazi zao? Hilo ni swali la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Serikali haioniumuhimu wa kuajiri Walimu ambao wako mtaanihawajaajiriwa kwa kukosa ajira kwa muda mrefu, kwa niniwasiwaajiri Walimu hawa wakaenda kufundisha shule zamsingi katika ngazi ambayo wao wameisomea? Ahsante.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya RaisTawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaNaibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Mwakagenda kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanzaanazungumza kwamba tunashusha morari, siyo ya kweli, hayoyalikuwa ni mapokeo tu, sisi wengine Walimu tunafahamukwanza mzigo wa kufundisha sekondari na shule ya msingiunatofautiana, ni heavy duty sekondari kuliko shule ya msingi,ile inawaelekeza kwamba watu walipopelekwa palehatukuwa na maandalizi mazuri, watu wakapokea tofauti,lakini waliopokea vizuri wameendelea kufundisha nahakukuwa na shida.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kupanga Mwalimuafundishe shule ya msingi au shule ya sekondari siyo kushushamorari yake, hili tu nimesema kulikuwa na upungufu mkubwa,kama Serikali, kama una watu zaidi ya 11,000 wakowanafundisha vipindi vichache sana kwa siku na kuna Walimukatika shule ya msingi wanafundisha vipindi vingi, ilikuwa nibusara kutumika kuwapeleka kule kufundisha, lakinitumeshachukua hatua, tuliwaelekeza Maafisa Elimu wa

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

Mikoa na Halmashauri zetu, wakakaa wakazungumza naowanaendelea kufanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la ajira, ni kwelikwamba tuna upungufu mkubwa wa Walimu katika shule zamsingi na sekondari, lakini juzi hapa tumeajiri Walimu 4,500,tumeomba kibali cha Walimu 22,000 hasa masomo ya shuleza msingi, masomo ya fizikia na hisabati katika maeneo hayo.Kwa hiyo, kadri Serikali itakapopata uwezo ndivyo inawezakuajiri, huwezi kuajiri tu kwamba kuna Walimu mtaani,hapana, lazima uajiri Walimu lakini wapate stahiki zao nauwezo wa kuwalipa kila mwisho wa mwezi pamoja namahitaji mengine. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana swali la Mheshimiwa Kabwe Ruyagwa Zitto, Mbunge waKigoma Mjini.

Na. 18

Fedha za Elimu Zinazotumwa Moja kwa Moja Mashuleni

MHE. KABWE Z. R. ZITTO aliuliza:-

Katika kutekeleza mpango wa kutuma fedha za elimumoja kwa moja mashuleni Serikali hutuma shilingi bilioni 18kila mwezi kwenye akaunti za shule nchini kwa mujibu wamaelezo ya viongozi kwa umma?

(a) Je, Serikali imeshatuma kiasi gani cha fedha katiya Januari – Desemba, 2016, 2017 na 2018 kwenda kwenyeshule nchini?

(b) Je, Serikali imefanya ukaguzi wa matumizi ya fedhahizo na kama zilizotoka Hazina zilifika kwenye shule husika;Je, Serikali ipo tayari kuleta Bungeni Ripoti za Ukaguzi huo?

(c) Kama Serikali haijafanya ukaguzi huo; Je, ipo tayarikuagiza ukaguzi maalum utakaofanywa na CAG na kuwekaTaarifa ya Ukaguzi huo?

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba yaWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali zaMitaa, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kabwe RuyagwaZitto, Mbunge wa Kigoma Mjini, lenye sehemu (a), (b) na (c),kwa pamoja kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, katika kutekelezaMpango wa Elimu msingi Bila Malipo kuanzia Januari, 2016hadi Disemba, 2018 jumla ya Sh.798,170,400,005.04zimetolewa na Serikali na kutumwa moja kwa moja shuleni.Fedha hizo zimejumuisha chakula kwa wanafunzi, fidia yaada, uendeshaji wa shule, posho ya madaraka kwa Wakuuwa Shule na Walimu Wakuu na Maafisa Elimu wa Kata. Fedhahizi zinajumuisha pia fedha zinazokwenda Baraza la Mitihanikwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya Kitaifa kwa ngazi husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika utaratibu wakawaida wa ukaguzi wa fedha za Serikali, Mkaguzi na MdhibitiMkuu wa Hesabu za Serikali hufanya ukaguzi katika Wizara,Taasisi, Mashirika ya Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaakila mwaka. Kwa kuwa, fedha za Elimu Msingi Bila Malipo nisehemu ya fedha zinazotumwa katika Mamlaka za Serikaliza Mitaa na kwa kuwa fedha hizo hutengwa kwenye bajetikila mwaka wa fedha, ni dhahiri kuwa fedha hizo hukaguliwana CAG pale anapofanya ukaguzi kwenye mamlaka husika.Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kabwe Ruyagwa Zitto, swalila nyongeza.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika,Bunge lako Tukufu kila mwaka linatenga jumla ya shilingi elfu10 kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi. Katika fedha hizoshilingi elfu sita zinapaswa kwenda moja kwa moja kwenye

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

mashule na shilingi elfu nne zinakwenda TAMISEMI kwa ajiliya ununuzi wa vitabu, lakini Serikali inafahamu kwamba katikampango wa GEP, Serikali ilipata zaidi ya shilingi bilioni 45 kwaajili ya kununua vitabu, na kwa jumla ya idadi ya wanafunziwaliopo nchini wa shule za msingi, kuna zaidi ya shilingi bilioni144 zilipaswa zinunue vitabu na shule hazina vitabu na kunavitabu ambavyo viliondolewa, Serikali….

NAIBU SPIKA: Uliza swali.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika,Serikali haioni kwamba, ni muafaka sasa kufanya ukaguzimaalum ili kuweza kutambua jumla ya fedha hizi shilingi bilioni190 zimetumika namna gani?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, katika uchunguziuliofanywa kwenye jumla ya halmashauri za wilaya 12 hapanchini, katika shilingi elfu sita inayopaswa kwenda kwenyemashule kwa kila mtoto, fedha inayofika, kwenye hii sampleya wilaya 12 ni shilingi elfu 4200 tu. Serikali haioni haja yakufanya ukaguzi maalum ili kuweza kufahamu hii shilingi 1200ambayo haifiki kwenye shule inakwenda wapi?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, swali lakwanza ni la kitakwimu, una uhuru wa kulijibu kama unalo,lakini swali la pili, majibu!

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaNaibu Spika, kwanza si kweli kwamba TAMISEMI tunanunuavitabu, tumegawana kazi, suala la vitabu na kiwango chakena ubora wake linafanywa na Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia. Kwa kuwa ameuliza swali la kitakwimu naMheshimiwa Naibu Waziri mwenzangu yupo hapa, basiunaweza ona namna ya kutenda hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini suala la kujibu hapani kwamba, Mheshimiwa Zitto, anasema halmashaurizimekaguliwa, sisi kama Serikali hatuna taarifa ambayoanaizungumzia hapa Mheshimiwa Zitto, kwamba fedha

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

hazifiki katika shule zetu, na Mheshimiwa Zitto Kabwe, bahatinzuri kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya LAAC,Halmashauri ya Kigoma Ujiji ambayo ni Halmashauri yachama chake cha ACT, ndiyo halmashauri ambayo imekuwana hati chafu miaka minne mfululizo, lakini vilevile miradi yaelimu iliyopo pale, ina hali mbaya kweli kweli. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kama kunahalmashauri imekaguliwa tuna takwimu za kutosha nihalmashauri ya Mheshimiwa Mbunge. Jibu ni kwamba,hakuna taarifa ambazo anazitoa, siyo za kweli, hakunaukaguzi uliofanyika mahususi na hakuna malalamiko ambayoyameletwa kwamba Serikali tufanye ukaguzi maalum,tukipata taarifa hizo na maombi hayo, Serikali itachukuahatua kufanya ukaguzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukaguzi wa fedha ya elimuna miradi ya Serikali inafanyika kila wakati, kuna Kamati zaBunge, imeenda TAMISEMI, imeenda watu wa Ustawi waJamii wamekagua na taarifa zipo. Kila wakati tunachukuahatua kabla ya bajeti na baada ya bajeti hii ya Serikali.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, swali lamwanzo ambalo linahitaji takwimu, utampatia takwimuMheshimiwa Zitto Kabwe. Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia majibu!

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Zitto kasema kwambafedha za Global Partners for Education dola milioni 46zinatumika kwa ajili ya vitabu. Naomba nimfahamishekwamba, fedha hizo zinatumika kwa ajili ya kuendeleza sektaya elimu kwa ujumla na siyo specific kwa ajili ya vitabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia naombanimhakikishie kwamba, fedha zote ambazo zinakwendakwenye vitabu, zimeenda kwenye Taasisi yetu ya Elimu na

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

kwa sasa tumefikia sehemu ambayo karibia vitabu vyotevinapatikana. Kuna vitabu ambavyo tunaendeleakuvichapisha lakini kwa sehemu kubwa vitabu vinapatikanasasa isipokuwa kama kuna changamoto kwenye halmashaurimoja moja, inakuwa ni kesi ambayo ni specific lakini kwaujumla kwa sasa tumeshaondokana na shida ya vitabu,tulichapisha vitabu vipya na tena vitabu ambavyo havinamakosa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini zaidi, ninawezanikakutana na Mheshimiwa Zitto nimueleweshe zaidi kwasababu takwimu yeye ndiyo kaja nazo ambazo ziyo takwimuza Serikali, kwa hiyo, akitaka ufahamu zaidi anawezaakakutana na mimi nikamfahamisha.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri TAMISEMI, swalila kwanza linalohusu takwimu limeshajibiwa na MheshimiwaNaibu Waziri wa Elimu. Mheshimiwa James Mbatia, swali lanyongeza!

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana, katika kuibadilisha dunia, ku-transform dunia,kigezo cha elimu kimepewa kipaumbele namba nne nakigezo cha elimu bora. Je, fedha hizi zaidi ya bilioni 900ambazo zimekwenda kwenye shule zetu, kigezo cha kupimazimefanikisha kwa kiasi gani ubora wa elimu na viashiria vyakevyote ukoje!

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais(TAMISEMI) majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kwamba tumepeleka fedha zaidi yashilingi bilioni 900 kama nilivyosema kwenye jibu langu lamsingi la swali la Mheshimiwa Zitto, na Mheshimiwa Mbungeanataka kujua vigezo vya kuonyesha kwamba elimuimeboreka ni kwa kiwango gani.

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, fedha hiiinafanya mambo mengi sana ikiwepo ni pamoja nauendeshaji wa shule, usimamizi wa elimu Tanzania umeimarikasana. Tumenunua pikipiki katika Waratibu Elimu wa kata zotenchini, sasa wanaweza ku-move kutoka shule moja kwendanyingine, maana yake ni kwamba hata utoro rejarejaumepungua shuleni, kiwango cha watoto kupata mimba nakuchukua hatua, tuna kesi mbalimbali mahakamani nabaadhi ya watu ambao wametuhumiwa kuwapa wasichanawetu mimba wameshafikishwa mahakamani na wenginewamefungwa, kesi ziko katika hatua mbalimbali. Hiyo ni kwasababu fedha hiyo imekwenda, imepeleka vifaa vyautendaji, pikipiki na imewezesha.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo la pil i,tumejenga hosteli maeneo mbalimbali, kitendo ambachokimepunguza watoto wa kike wengi sasa wanakaa katikashule zetu na utaangalia matokeo mbalimbali, darasa lasaba, form four na form six, kiwango cha ufaulu cha watotowa kike kimeongezeka sana. Tumejenga mabweni na hostelimaeneo mbalimbali, watoto wa kike wengi wanakaa katikamaeneo ya shule na usimamizi wao umekuwa ni mzuri zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini elimu msingi bilamalipo, sasa hivi tunapozungumza, vijana wetu wa kidatocha nne wanafanya mitihani. Mwaka 2018 wanafunzi ambaowalisajiliwa, watahiniwa wa kufanya mitihani, walikuwa427,000, mwaka huu ni 485,866, maana yake ni ongezeko lawanafunzi ambao wameingia kidato cha nne zaidi ya asilimia1.37, huu ni ufaulu mkubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vijana wengi waTanzania maskini ambao walikuwa hawana uwezo wakusoma wa kike na wakiume, wengine walifanya kazi zahouse girl, wengine walikuwa makuli kwenye masoko,walikuwa wapiga debe, ninapozungumza hapa, vijanawengi kitendo cha Mheshimiwa Rais, Dkt. John PombeMagufuli kuondoa ada katika masomo yao, watoto wengiwapo mashuleni, hata wananchi ambao wanataka ma-

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

house girls wanapata shida sana kuwapata, vijana,wasichana wengi wanasoma.

Mheshimiwa Naibu Spika, hayo ni kwa uchache, lakiniMheshimiwa Mbatia ni kweli kwamba, yeye anafahamu, hatamatokeo ya form six yameongezeka, elimu ya high schoolimekuwa ni kubwa sana, kwa sababu ya fedha hizi ambazozimekwenda kuimarisha huduma. Ndiyo maana, hatawananchi ambao walitoa nguvu zao kuchangia kujengamaboma, tumepeleka fedha zaidi ya bilioni 29, angaliahalmshauri zote nchini ili tumalize maboma, watoto wetuwaendelee kukaa katika madarasa ambayo yapo sawa nawapate matundu ya vyoo. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Goodluck Asaph Mlinga,swali la nyongeza!

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana, kumekuwa na matumizi ya hovyo kabisakatika halmashauri zetu na kupelekea halmashauri hizokupata hati chafu. Kwa mfano, Halmashauri ya Wilaya yaUlanga imepata hati chafu kwa mwaka mmoja, mimi najionakama natembea bila nguo, lakini halmashauri kamaalivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri, Halmashauri ya Ujijiambayo inaongozwa na ACT anapotoka Mheshimiwa ZittoZuberi Kabwe, miaka minne mfululizo imepata hati chafuwakati yeye akishinda twitter na instagram. Je, Serikali inampango gani wa kuzifuta halmashauri hizi? (Kicheko)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais(TAMISEMI) majibu!

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kwamba, kwanza nimpongezeMheshimiwa Mbunge wa Ulanga, alikuwa anasema manenomengi sana hapa Bungeni wakati mwingine akaonekanakwamba ni kituko, lakini naomba niwahakikishieWaheshimiwa Wabunge, kauli ya Mheshimiwa Mbunge waUlanga imetusaidia sana TAMISEMI na watu wengi

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

wamewajibishwa katika halamshauri ile na uchunguzimahususi umefanyika tukagundua kuwa ni kweli kwambawatumishi wetu wamwekuwa wabadhilifu, fedha nyingizililiwa, kama alivyokuwa analalamika.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nimhakikishieMheshimiwa Mbunge ni kwamba, ni kweli, Kamati ya Bungeya LAAC wapo, Mwenyekiti yupo hapa na Wajumbe wenzakewanafamu. CAG alipopitia baadhi ya halmashauri, hata miminilishangaa, halmashauri mbili, wamepoteza fedha zaidi yashilingi bilioni kumi na kitu, lakini Halmashauri ya Kigoma Ujiji,halmashauri hii imekuwa na hati chafu mfululizo miaka minne,lakini tulipowahoji viongozi wa pale, wakatuambia viongoziwetu wa kisiasa, wanaingilia mpaka manunuzi ya kisheria,mpaka tenda ambazo zinagawanywa pale Kigoma Ujiji,wanapewa kwa itikadi za kivyama, hizi ni taarifa rasmi zaBunge, ninazozitoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tumetoamaelekezo, ni kweli kwamba, ile halmashauri ikiendeleakupata hati chafu ya tano na itapewa ukaguzi mahususi, kunauwezekano mkubwa Mheshimiwa Zitto halmashauri yakokufutwa kwa sababu husimamii vizuri, na wewe ni mtaalamwa mahesabu. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaendeleana Ofisi ya Rais, (Utumishi na Utawala Bora), MheshimiwaOmary Ahmad Badwel, Mbunge wa Bahi, sasa aulize swalilake.

Na. 19

Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

MHE. OMARY A. BADWEL aliuliza:-

Kwa muda mrefu sasa baadhi ya wananchiwamekuwa wakinufaika na mradi wa TASAF ambao kwa kiasiumekuwa ukifanya vizuri, aidha mradi huu umefika vijiji

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

vichache tu na vijiji vingine bado havijafikiwa na Serikali iliahidikuwa vijiji vyote vitanufaika na mradi huu.

(a) Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi yake ya mradi waTASAF kufikia vijiji vyote nchi nzima?

(b) Kumekuwa na utaratibu wa baadhi ya viongozikukata fedha za walengwa wa TASAF moja kwa moja kwakuwakatia bima, michango mbali mbali ya vijiji na kadhalikabila ridhaa yao. Je, Serikali inatoa kauli gani katika jambohilo?

NAIBU SPIKA: Mhehimiwa Waziri, Ofisi ya Rais, Utumishina Utawala Bora majibu!

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHIWA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma naUtawala Bora), naomba kujibu swali la Mheshimiwa OmaryAhmad Badwel Mbunge wa Bahi lenye maswali mawili kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mpango wa Kunusuru KayaMaskini ulipoanza mwaka 2013 uwezo wa fedha uliokuwepoulitosheleza kufikia Vijiji/Mtaa/Shehia 9,986 ikiwa ni asilimia 70ya Vijiji/Mitaa/Shehia zote nchini. Vijiji/Mitaa/Shehia ambavyohavijafikiwa ni 6,858.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeshakamilishahatua zote za maandalizi ya Kipindi cha Pili cha Mpango huuwa Kunusuru Kaya Maskini ambacho kinatarajia kuanzautekelezaji mwishoni mwa mwaka huu 2019 baada ya Serikalikupata fedha. Kipindi cha Pili ya Mpango wa Kunusuru KayaMaskini kitatekelezwa kwenye Halmashauri zote 185 zaTanzania Bara na Wilaya zote za Zanzibar katika Vijiji/Mitaana Shehia zote ikiwa ni pamoja na kufika kwenye Vijiji/Mitaa/Shehia 6,858 ambavyo bado havijafikiwa.

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe ufafanuzikuhusu matumizi ya fedha za walengwa wa Mpango waKunusuru Kaya Maskini. Fedha hizi ambazo ni ruzukuzinatolewa ili kaya iweze kugharamia mahitaji ya msingi kamachakula, gharama za elimu na afya na kuwekeza kwa ajiliya kuanzisha miradi ya kuongeza kipato. Hivyo, ni maamuziya kaya husika kupanga matumizi ya fedha hizi ili mradihaziendi kwenye matumizi ambayo hayaisaidii kayakujikwamua na umaskini.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika baadhi ya maeneo,viongozi wa vijiji wanalazimisha kukatwa kwa ruzuku zawalengwa ili kukatiwa bima ya afya au kulipia michangombalimbali. Hii si sawa na haikubaliki. Napenda kusisitiza, lakinivilevile niagize, kwamba walengwa wasikatwe fedha zaomoja kwa moja bali walipwe stahiki zao na iwapo kunamichango inayotakiwa kama ni kwa ajili ya shughuli zamaendeleo ya kijiji basi michango hii itozwe kwa wananchiwote wa kijiji husika na siyo kukata moja kwa moja kutokafedha za walengwa wa TASAF peke yao. Nimalizie kwakusisitiza kwamba viongozi wote waliokuwa wanatoa amriya kukata fedha za walengwa wa TASAF moja kwa moja bilaridhaa ya walengwa hao, waache kufanya hivyo mara moja,kwa kuwa huu siyo utaratibu na wala siyo sahihi na vinginevyowatachukuliwa hatua kali za kisheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilieleze Bunge lako Tukufukwamba, baadhi ya halamshauri zilishawahi kufanya hivyona Wakurugenzi waliagizwa warudishe fedha hizo na tayariwamesharudisha. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Omary Ahmad Badwel,swali la nyongeza!

MHE. OMARY A. BADWEL: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawilimadogo ya nyongeza. Pamoja namajibu mazuri sana yaMheshimiwa Naibu Waziri na ninampongeza kwa kazi nzuri,nilikuwa na maswali madogo mawili.

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwakatika miradi ya TASAF Awamu ya I na TASAF Awamu ya II,ulikowepo pia utekelezaji wa miradi ya miundombinu kamaujenzi wa barabara, ujenzi wa madarasa, miundombinu yamaji, utoaji wa fedha kwa ajili ya VIKOBA na miradi minginembalimbali, zikiwemo zahanati. Lakini baadaye katika TASAFthree, TASAF Awamu ya II miradi hiyo kwa kiwango kikubwailiondolewa, ama ilikuwepo kwa kiasi kidogo au haikuwepokabisa.

Sasa je, katika huu mpango wa awamu ya pili waTASAF inayofuata sasa miradi hii itahusika katika utekelezajikatika vijiji vyetua mbapo ilikuwa imetoa faida kubwa sanakatika sekta mbalimbali? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali la pili, kwa kuwaAwamu hii ya III ya ugawaji wa fedha kwa walengwawalikuwa wanakwenda kugawa fedha moja kwa moja kwawalengwa kwa maana hizi kaya maskini, lakini ilijitokeza piauwepo wa kaya hewa, jambo ambalo lilisababisha fedhahizi za Serikali kwenda mahali ambapo kwa watu hawakuwawaaminifu na hivyo kutokufikia malengo yaliyokusudiwa.

Je, katika awamu hii ya pili ya ugawaji wa mradi huuwa fedha za TASAF Serikali imejipangaje kuhakikisha kwambahakutokei tena walengwa hewa ili fedha hizi ambazozimepangwa na Serikali kupelekwa huko ziweze kupelekwahuko ziweze kufanya kazi iliyokusudiwa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Utumishi naUtawala Bora, majibu!

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHIWA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza na yeye ninampongeza akiwa mmoja wapo wa watuma-champion mahiri katika kufuatilia walengwa wetu wakaya maskini kupitia mpango wetu wa TASAF.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimjibuMheshimiwa Mbunge kabisa kwamba, mpango wa kunusuru

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

kaya maskini, ni kweli awamu ya kwanza ulihusisha sanamiundombinu, na ninaomba niliambie Bunge lako Tukufukwamba, katika awamu yetu hii ya tatu kipindi cha kwanza,ambacho kinaisha mwezi huu na kipindi cha pili ambachokinaanza mwezi ujao wa 12 mwaka 2019, tutaendelea nampango wa miundombinu lakini tutajikita zaidi katika publicworks, kwa maana ya kwamba, zile ajira kwa muda, kwa walewalengwa ambao wanatokana na kaya maskini sana iliwaweze kufanya kazi, waweze kupata ujira na ajira katikakuwawezesha maisha yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili, anasema Serikalitumejipangaje katika awamu ya tatu, Awamu ya II niliambieBunge lako Tukufu kwamba tumejipanga, Serikali ya awamuya tano, kuhakikisha kwamba walengwa wote kuanzia sasahivi tutakuwa tunawaendea kwa kutumia njia za kidijitali kwamaana ya GPS, tutakuwa tunapiga picha kwenye kayahusika, lakini tayari tumeshafanya pilot project areas katikaMtwara DC, katika Halmashauri ya Nanyamba, lakini hatakule Siha na changamoto tulizozipata kule, ndizo ambazozitatufanya tuboreshe katika maeneo mengine ambayotutafika katika sehemu yetu hii ya pili inayoanza mwezi ujao.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile naombaniliambie Bunge lako Tukufu kwamba pia tutakuwatunawalipa walengwa kwa njia za kielektroniki, vilevile VIKOBAna tayari tumeshaweka mpango mkakati mwingine,kuhakikisha kwamba tutakuwa na wale wanaofuzu, kwamaana ya graduation, tutakuwa tunawapatia mafunzo natunawaunganisha na taasisi za kifedha na hii yote ili kuwezakuwa na multiply effects. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Fatma Toufiq, swali lanyongeza!

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.Kwa kuwa wanufaika wengi wa TASAF ni wazee wasiojiwezana wanatoka katika maeneo ya pembezoni na inapofikiasiku ya kupokea mafao, huwa wanafika pale katika maeneo

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

ya vijiji kwa kutumia usafiri na usafiri huo wanalipia zile fedhaza mafao. Je, Serikali haioni umefikia wakati wa kubaini wazeehawa wasiojiweza na kuweza kuwapelekea zile fedha katikamaeneo yao?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Utumishi naUtawala Bora, majibu kwa kifupi!

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHIWA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika,hapa wakati najibu maswali yangu ya msingi na ya nyongezaya Mheshimiwa Badwel nimesema, mkakati mmoja wapo waSerikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha tunaboresha,kwamba tutakuwa tunawalipa walengwa wote kwa njia zakielektroniki kwa maana ya kwamba tumegundua kwambawalengwa wengine walikuwa wanakatwa fedha zao bilaridhaa yao na wengine walikuwa wanadhurumiwa, ndiyomaana katika kuboresha, tumeamua kwamba tutakuwatunawalipa kwa njia ya kielektroniki. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hawa Subira Mwaifunga,swali la nyongeza!

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi, kumekuwa na utaratibumbovu kwa baadhi ya viongozi wanaogawa fedha hizi,wakitumia itikadi za kisiasa, ikiwepo ukiwa mwanachama wachama fulani, unaweza ukapewa fedha hizo, lakini ukiwamwanachama wa chama kingine hupewi fedha hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningeomba Serikali itoetamko fedha hizi wanaotakiwa kupewa ni watu wa ainagani? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Utumishi naUtawala Bora, majibu.

NAIBU WAZIRI WA OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa NaibuSpika, Serikali ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli haina

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

ubaguzi. Ni Serikali ya Watanzania wote. Naomba niliambieBunge lako Tukufu kwamba pesa hizi zinazotokana naMpango wetu wa TASAF ni kwa walengwa wotewanaotokana na zile kaya masikini sana na hakuna ubaguziwowote. Nitoe rai na agizo kwamba yeyote atakayeletaubaguzi katika kuhakikisha kwamba walengwawanaotokana na mpango huu wa kunusuru kaya masikiniwanasaidiwa, watoe taarifa na watachukuliwa hatua kaliza kisheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa AngelinaAdam Malembeka, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swalilake.

Na. 20

Elimu Juu ya Majanga ya Moto

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA aliuliza:-

Majanga ya moto yamekuwa yakitokea mara kwamara hasa Viwandani, Majumbani na katika majengo yaSerikali:-

(a) Je, Serikali ina mkakati gani wa kutoa mafunzokwa Wafanyakazi na wananchi juu ya mbinu za kujihami nakujiokoa katika majanga ya moto?

(b) Je, Serikali imejipangaje katika kutoa mafunzokatika maeneo ya kazi na wananchi juu ya matumizi yamitungi ya kuzima moto (Fire Extinguishers)?

(c) Je, Serikali ina mpango gani wa kukagua mitungihiyo kama bado inafaa kwa matumizi au imeshapita mudawake wa kutumika?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, naomba kujibu swali laMheshimiwa Angelina Adam Malembeka, Mbunge wa VitiMaalum Mkoa wa Kaskazini Unguja, lenye sehemu (a), (b)na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Jeshi laZimamoto na Uokoaji linaendelea kutoa mafunzo ya mbinuza kujihami na jinsi ya kujiokoa katika majanga ya motokwenye maeneo ya kazi na wananchi kwa ujumla. Elimu dhidiya kinga na tahadhari ya moto imeendelea kutolewa katikamaeneo mbalimbali nchini ikiwemo maeneo yenyemikusanyiko ya watu kama vile masoko, Shule za Sekondarina Msingi, Vyuo, Makanisani na Misikitini kupitia vyombombalimbali vya habari vikiwemo magazeti, radio natelevisheni.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Jeshi laZimamoto na Uokoaji limejipanga vyema kutoa mafunzokwenye maeneo ya kazi na wananchi juu ya matumizi yamitungi ya kuzimia moto kwa kuanzisha kampeni mbalimbalikama vile “Ninacho, Ninajua Kukitumia,” “Mlango kwaMlango” na “Nyumba Salama” zenye lengo la kuhamasishawatu kuwa na vizimia moto na kujua kuvitumia katika maeneoya makazi, viwanda, maeneo ya vyombo vya usafiri nausafirishaji, majumbani, maeneo ya biashara na katikamikusanyiko mikubwa ya watu. Aidha, wananchiwanaendelea kupatiwa elimu na mafunzo juu ya mifumo yoteya kuzima kuzima katika majengo na maeneo mbalimbali ilikuepusha majanga ya moto.

(c) Mheshimiwa Naibu Spika, Ukaguzi wa tahadharina kinga dhidi ya moto kwa mujibu wa Kanuni za Jeshi laZimamoto na Uokoaji umeendelea kufanyika sambasambana ukaguzi wa mitungi ya kuzima moto na kumshauri mtumiajijuu ya ubora wa mtungi na kumshauri mmiliki ipasavyo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Angelina Malembeka, swalila nyongeza.

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA: MheshimiwaNaibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuulizamaswali ya nyongeza. Kwanza nimpongeze Naibu Waziri kwamajibu mazuri ambayo yanaonesha kabisa Serikali ina nianzuri ya kusaidia wananchi wake. Kwa niaba ya wanawakewa Mkoa wa Kaskazini Unguja nilikuwa nina maswali mawiliya kuongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nilitaka kujua: Je,huduma ya uokoaji na kuzima moto kuna gharama zozoteambazo mhudumiwa anatakiwa alipe?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili: Je, kamagharama hizo zipo, ni utaratibu gani unatakiwa ufanywe ilialiyepatiwa huduma aweze kulipa bila kuwa na taharuki?Maana kipindi kile anakuwa amechanganyikiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mamboya Ndani ya Nchi, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kwa dhati kabisanimpongeze sana Mheshimiwa Malembeka kwa kazi nzuriambayo anayoifanya katika Mkoa wake wa Kaskazini. Kwakweli anawatendea haki wapiga kura wake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, nikijibu maswali yakepamoja, kwanza huduma za kuzima moto ni za bure, hakunagharama. Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria ya Jeshi la Uokoajina Zimamoto ya mwaka 2007 Sura ya 427, inaeleza kwambaJeshi la Zima Moto na Uokoaji lina Mamlaka ya kuweza kutoaleseni kwa makampuni binafsi kutoa huduma hizo ikiwemohuduma ya kuzima moto pamoja na vifaa.

Mheshimia Naibu Spika, kwa hiyo, makampuni hayandiyo ambayo yanaingia mikataba na Taasisi binafsi na ndiyoyanakubaliana malipo, lakini kwa maana ya huduma hizi zazimamoto ni bure.

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na utaratibuambao unatumika, unapiga namba 114 na kikosi chetukinafika pale haraka iwezekanavyo kutoa huduma hizo bilamalipo yoyote. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Wizara ya Nishati. Mheshimiwa Mussa Bakari Mbarouk,Mbunge wa Tanga Mjini, sasa aulize swali lake.

Na. 21

REA III Kupitia Perry Urban – Tanga

MHE. MUSSA BAKARI MBAROUK aliuliza:-

Tanzania ina jumla ya Majiji sita likiwemo Jiji la Tanga;katika Majiji hayo kuna maeneo ambayo yako nje ya Jijiambayo ni Mitaa, Vitongoji na Vijiji (Perry Urban); Kitengo chaPerry Urban kimekabidhiwa jukumu la kusambaza umeme waREA III katika Majiji:-

Je, ni lini Perry Urban itaanza kusambaza umemekatika Jiji la Tanga?

WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Mussa Bakari Mbarouk, Mbunge wa Tanga Mjini,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala waNishati Vijijini (REA) inaendelea na utekelezaji wa miradi yaumeme iliyopo katika vijiji, vitongoji na maeneo mbalimbalikandokando ya miji na vijiji yaani Perry Urban. Awamu yakwanza ya utelelezaji wa mradi huu umeanza katika Mkoawa Dar es Salaam na Mkoa Pwani na kwa upande wa Dares Salaam katika Wilaya ya Kigamboni. Utekelezaji wa mradihuu utakamilika mwezi Aprili, 2020. Baada ya kukamilika kwamradi huu, Serikali itaanza kutekeleza mradi huu katika Mikoayote nchini.

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Jiji la Tanga Serikaliimekamilisha upembuzi yakinifu na kubainisha kuwa miradiwa kupeleka umeme maeneo ambayo yako kandokandoya Jiji la Tanga unahusisha ujenzi wa njia ya msongo wakilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 15, ufungaji wa transfoma15 kati ya hizo transfoma 4 ni za KVA 200, transfoma sita zaKVA 100 na 5 za KVA 50.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi ya Perry Urban katikaJiji la Tanga pia utahusisha ujenzi wa njia ya Msongo wakilovoti 11 yenye urefu wa kilomita 48.8, ufungaji transfoma35; na kati ya hizo transfoma nane ni za 200KVA, 20 za 100KVAna saba za KVA 50. Kazi nyingine ni kuvuta laini ndogo ya kV0.4 yenye urefu wa Kilomita 200. Wateja wa awaliwatakaonufaika na mradi huu katika Jiji la Tanga ni 5,125ambao wanatarajiwa kupata umeme katika maeneo hayo.Utekelezaji wa mradi huu utaanza mwezi Julai, 2020 nakukamilika mwezi Machi, 2021. Gharama za mradi huo nishilingi bilioni 7.5

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mussa Mbarouk swali lanyongeza.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri lakinipamekuwa na malalamiko katika yale maeneo ambayoyameshapelekewa transfoma za Kilovolt 50. Je, tatizo hili kwanini linajirudia tena? Kuna baadhi ya maeneo yametajwakwamba katika transifoma 35, transifoma saba za KV 50halafu kuna transifoma nyingine nne. Kwa nini tusipeleke zileambazo ni za kuanzia KV 100?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili katikataarifa hii haikuainisha baadhi ya maeneo ambayo ndiyohasa yaliyokusudiwa. Kwa mfano, kwenye Kata ya Kirare kinamaeneo ya Mapojoni, Mtambuuni, Msakangoto, Kiromberelakini kwenye Kata ya Mzizima kuna maeneo ya Kihongwe,Rubawa, Mleni, kwenye kata ya Kiomoni kuna maeneo yaPande Muheza, Pande Masaini, Pande Mpirani, Kata yaMarungu kuna Mkembe, Geza Ndani na Geza Barabarani;

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

Pongwe kuna maeneo ya Pikinangwe; na Kata ya Mawenikuna Machembe, Mtakuja na Mwisho wa Shamba: Je,maeneo haya sasa hususan noyo yamo katika huu mradi nalini hasa yataanza kufanyiwa huu uwekezaji wa REA III?(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nishati, majibu.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanzani kweli yako maeneo ambayo tulikuwa tukipeleka transfomaza KV 50 na nyingine 100 na 200 na kuendelea, lakini maeneotunayopeleka KV 50 inategemea pia na uwekezaji na ainaya wateja. Ziko faida nyingi sana za kupeleka transfomandogo ndogo katika baadhi ya maeneo na hasa katikakukabiliana na uharibifu wa mitambo inapotokea dharura.Kunapokuwa na transfoma za 50 nyingi, kwa hiyo,kunapokuwa na dharura ya kuharibika transifoma moja,wateja wengine wanaendelea kupata umeme bila matatizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hasara za kuwa natransifoma moja kubwa, ni kwamba ikishaharibika watejawengi wanakosa umeme, lakini tumelichukua ombi laMheshimiwa Mbunge tutaendelea kusambaza transifoma zakila aina kukabiliana na hali hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na swali lake lapili katika Jiji la Tanga tunayo maeneo 12 yatakayopelekewaumeme wa Perry Urban ikiwemo kama alivyotaja maeneoyake, lakini yako maeneo ya Chongoleani, Mabwakweni,Majani Mapana na maeneo mengine mpaka 12 nautekelezaji unaanza Julai mwakani na kukamilika mweziDesemba, 2021. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea na swali laMheshimiwa Benardetha Kasabago Mushashu, Mbunge waViti Maalum, swali lake litaulizwa kwa niaba na MheshimiwaHalima Bulembo.

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

Na. 22

Hitaji la Umeme wa REA – Kagera

MHE. HALIMA A. BULEMBO (K.n.y. MHE. BENARDETHAK. MUSHASHU) aliuliza:-

Mkoa wa Kagera una vijiji 134 ambavyo havijafikiwana umeme wa REA; Biharamulo Vijiji 29, Bukoba Vijiji 9,Karagwe Vijiiji 8, Kyerwa Vijiji 31, Misenyi Vijiji 5, Muleba Vijiji 25na Ngara Vijiji 27:-

(a) Je, ni lini Serikali itapeleka umeme wa REA katikaVijiji hivyo?

(b) Umeme wa REA ulifika kwenye vijiji vingi lakinihaukusambazwa: Je, mradi wa ujazilizi utaanza lini MkoaniKagera ili wananchi waliorukwa wapatiwe umeme?

WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Bernadetha Kasabago Mushashu lililoulizwa naMheshimiwa Halima Bulembo, lenye sehemu (a) na (b) kwapamoja kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakalawa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi kabambe wakupeleka umeme katika vijiji vyote nchini kufikia mweziDesemba, 2021. Kwa sasa Mkandarasi Nakuroi anaendeleana kazi ambapo kufikia mwezi Oktoba, 2019 viji j i 82vimewashwa umeme katika Mkoa wa Kagera na kazi yauunganishaji wa wateja inaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, vijiji vyote vitakavyosaliakatika Mkoa wa Kagera vitapatiwa umeme kupitia mradi waREA awamu ya pili, unaozunguka kuanza sasa ambaoutakamilika mwezi Januari, 2020. Pia kukamilika kwa mradihuu mwezi Desemba, 2021 kutapeleka umeme katika

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

maeneo yote katika Mkoa wa Kagera pamoja na Vitongojivyake.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa ujazilizi awamuya pili (Densification IIA) utatekelezwa katika Mikoa tisa nautaanza kutekelezwa kuanzia mwezi Novemba, 2019 hadimwezi Juni, 2020. Mradi wa ujazilizi katika Mkoa wa Kagerautaanza kutekelezwa kupitia mradi wa ujazilizi awamu ya IIB(Densification IIB) utakaoanza kutekelezwa kuanzia mweziJulai, 2020 na kukamilika mwezi Machi, 2021. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Halima Abdallah Bulembo,swali la nyongeza.

MHE. HALIMA A. BULEMBO: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Kwanza kabisa naomba nimpongezeMheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri kabisa, lakini ninamaswali mawili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza Mkoa wa Kagerasiyo vijiji peke yake ambavyo havijapata umeme wa REA.Kumekuwa na Taasisi kubwa kama shule na Vituo vya Afyaambavyo bado havijapata umeme wa REA na kupelekeakushindwa kutoa huduma zinazotakiwa kwa wakati. Je,Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha taasisi hizi zinapataumeme? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, wananchiwa Mkoa wa Kagera wamekuwa wakikumbwa na kadhiaya kulipishwa nguzo za umeme. Serikali au Wizarainazungumziaje kadhia hii inayowakuta wananchi wa Mkoawa Kagera? Nakushukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nishati, majibu.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa HalimaBulembo anapofuatilia masuala ya umeme katika Mkoa waKagera. Nampongeza sana na kweli kazi kubwa imeonekana

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

kutokana na jitihada zake hasa kwa kupitia vijana. Hongerasana Mheshimiwa Mbunge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa nijielekezekatika masuala yake mawili ya nyongeza. Swali la kwanzaanataka kujua kuhusiana na upelekaji wa umeme katikataasisi za Umma. Naomba nitoe maelekezo kwa Halmashaurizetu na Waheshimiwa Madiwani wanaonisikiliza. Ni kweliSerikali imekuwa ikipeleka umeme katika maeneo yote hasavijijini lakini baadhi ya taasisi zimekuwa hazilipiwi na wamilikiwa taasisi hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawaomba sana wamilikiwanaohusika walipie gharama ya 27,000 ili taasisi zotezipelekewe umeme. Maelekezo na mwelekeo wa Serikali nikuhakikisha taasisi zote zinapelekewa umeme. NakupongezaMheshimiwa Halima Bulembo kwa sababu katika Mkoa waKagera hadi sasa taasisi 897 zimepelekewa umeme na hii nijitihada kubwa. Naomba maeneo mengine ambayohayajapelekewa umeme, wanaohusika waendelee kulipia.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunazungumzia taasisitukiwa na maana ya shule, Vituo vya Afya, Zahanati, Misikiti,masoko na hata kama kungekuwa na maeneo madogo yaviwanda. Kwa hiyo, nitoe sana ombi kwa WaheshimiwaWabunge kupitia kwa Madiwani na Wenyeviti waHalmashauri tupeleke kwa kulipa shilingi 27,000/= katika Taasisiza Umma.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na swali la pilikuhusu kulipishwa nguzo; ni kweli zipo changamoto katikabaadhi ya maeneo, yapo maeneo bado Wakandarasi naMameneja wa TANESCO wanaendeleza kutoza nguzowateja. Naomba nitoe tamko kali sana kupitia Bunge lakoTukufu kwamba ni marufuku kutoza nguzo kwa wateja wote;iwe Mkandarasi awe Meneja wa TANESCO, awe Injinia, aweKibarua wake ni marufuku kulipiza mteja nguzo. Hii ni kwasababu Serikali imegharamia kwa asilimia 100.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabunge,muda wetu umekimbia, kwa hiyo, tunaendelea na Wizaraya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Mheshimiwa SilvestryFrancis Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini, sasa aulize swali lake.

Na. 23

Barabara ya Njia Nane Kutoka Ubungo Hadi Kibaha

MHE. SILVESTRY F. KOKA aliuliza:-

Serikali inajenga njia ya barabara nane kutokaUbungo hadi Kibaha:-

Je, barabara hiyo inaishia eneo gani la Mji wa Kibaha?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(ELIAS J. KWANDIKWA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, naomba kujibu swali laMheshimiwa Silvestry Francis Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara yaUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ipo katika utekelezaji wamiradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara na madaraja nchiniikiwemo mradi wa upanuzi wa barabara kuu ya Morogorosehemu ya Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani. Mradihuu unahusisha upanuzi wa barabara kutoka njia mbili zazamani mpaka njia nane hadi njia 12 katika baadhi yamaeneo pamoja na ujenzi wa madaraja ya Kibamba, Kiluvya,Mpiji na Mlonganzila Overpass.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Serikali ipo katikautekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi huu kuanziaKimara na kuishia Kibaha Maili Moja mbele ya mizani ya

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

zamani takribani mita 150 kutoka mizani ilipo. Barabara hiiinayopanuliwa ina jumla ya kilometa 19.2. Lengo la mradihuu ni kupunguza msongamano mkubwa wa magariyanayopita katika barabara hiyo ambayo yanazidi magari50,000 kwa siku ikizingatiwa kuwa Jiji la Dar es Salaam ni kitovucha biashara hapa nchini na kuna bandari inayotumiwa nanchi jirani za Malawi, Zambia, Burundi, Rwanda, Uganda naJamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi EstimConstruction Co. Ltd wa hapa nchini kwa gharama ya Shilingibilioni 140.45 na kusimamiwa na Kitengo cha Usimamizi waWakala wa Barabara Tanzania (TANROADS EngineeringConsulting Unit – TECU). Utekelezaji wa mradi huuunagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania kwa asilimia 100. Hadi sasa utekelezaji umefikiaasilimia 48 na mradi umepangwa kukamilika mwezi Januari,2021.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Silvestry Francis Koka swalila nyongeza.

MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Kwa kweli nichukue nafasi hii kwa niaba yawananchi wa Kibaha kumpongeza sana Mheshimiwa Raispamoja na Serikali yake kwa kazi nzuri ya ujenzi wa darajalile la Ubungo, lakini vilevile barabara hii kubwa ambayo kwasasa itaishia Kibaha na itaokoa gharama kubwa zamsongamano wa magari kutoka Mjini Dar es Salaam kujaPwani. Pamoja na pongezi hizo kubwa, ninayo maswali mawiliya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii ambayo nikilometa 19.2 inaishia kidogo tu baada ya mizani ya zamanipale Kibaha. Maana yake ni kwamba ile trafic ya magariyote ambayo yatakuwa yanakwenda mikoani yatakuja kwakasi na yataishia pale ambapo ni almost katikati ya mji wetumdogo wa Kibaha. Kwa maana hiyo ni kwamba Mji wetuwa Kibaha magari yatakuwa mengi na hakika utakuwaumesimama wananchi wa Kibaha hawataweza kufanya

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

shughuli zao za kiuchumi katika mji ule kwa sababu ni mdogona magari yatakuwa mengi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kikao chetu cha RegionalRoad Board tuliomba barabara hii angalau iongezewempaka pale Kwa Mathias ili sasa iweze kuhudumia Mji ulewa Kibaha na kuleta maana njema zaidi ya maendeleokatika mji wetu. Vilevile kama tutamwongezea mkandarasihuyu aliyepo kazini gharama zitapungua kwa maanahakutakuwa na mobilization hata process za tenda. Je,Serikali ina mpango gani sasa kukubaliana na ombi letu ilibarabara hii iweze kuleta manufaa zaidi katika mji wetu waKibaha?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili barabara KwaMathias hadi Msangani ambayo inakwenda mpaka MakaoMakuu ya Land Force tumejenga mita 400 za lami nabarabara ya TAMCO kwenda Mapinga inaendeleakujengwa kilometa 4 na wananchi hawajapata fidia. Je,Serikali ina mpango gani kukamilisha barabara hizi nakuhakikisha wananchi wanapata fidia? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Koka,Mbunge wa Kibaha Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, nizipokee pongezinyingi alizotoa Mheshimiwa Koka lakini pia nimpongeze sanakwa juhudi anazofanya kwa kushirikiana na Mkoa wa Pwanikuhusu maendeleo mbalimbali ya Jimbo lake.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanzaanazungumzia juu ya kuendelea na ujenzi wa barabara hiikutoka eneo ambalo tunaishia kwa maana ya Maili Mojakwenda mpaka Kwa Mathias. Kama nilivyojibu katika jibulangu la msingi ni kwamba ujenzi wa kilomita 19.2 ni awamu

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

ya kwanza. Kwa hiyo, tutaendelea na awamu zingine kadritunapopata pesa kwa maana ya kuendelea na ujenzikwenye eneo hili kupita Picha ya Ndege - Kwa Mathias -Mlandizi – Chalinze. Kwa hiyo, nimtoe hofu tu tumejipangavizuri na Serikali tunafahamu kwamba baada ya upanuzi huowa barabara kwa kweli tutaleta magari mengi sana kwaupande wa Kibaha na maeneo haya Mlandizi kwa maanahiyo tutakuwa tumehamishia foleni kwenye maeneo haya.Kwa hiyo, tumejipanga vizuri kwamba tutakuja na awamuzingine ili tuweze kutatua na kuendelea kufanya maboreshomakubwa ya ujenzi wa barabara.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia amezungumziabarabara ile ya Kwa Mathias kwenda Msangani na barabaraya kutoka TAMCO kwenda Mapinga ambayo ni kilometa 24na tumeshapata wakandarasi kuanza ujenzi katika maeneohaya. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba sualala fidia tunalishughulikia kwa sababu ni utaratibu na kanunikwamba kabla mkandarasi hajaanza kazi fidia zitakuwazimelipwa. Tunafanya jitihada za kuwasiliana na wenzetuWizara ya Fedha ili tuweze kulipa fidia. Pia niwahakikishie tuwananchi wa maeneo haya waondoe hofu tumejipangakuwafanyia maboresho ya barabara zao lakini pia tutawalipastahili zao za fidia kama ilivyo kulingana na taratibu zetu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Josephine JohnsonGenzabuke, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake.

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante. Kwanza kabisa, kabla ya kuuliza swali langu,naomba uniruhusu niwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwakunifariji wakati wa kipindi kigumu nilipoondokewa na babayangu. Nawashukuru sana kwa mapenzi yao naninawashukuru wananchi wa Mkoa wa Kigoma. (Makofi)

Na. 24

Tatizo la Mawasiliano ya Simu – Kigoma

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:-

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

Maeneo ya mipakani katika Wilaya za Kakonko,Kibondo, Kigoma Vijijini, Buhigwe na Kasulu yanakabiliwa natatizo la mawasiliano ya simu kutokana na kukosekana kwaminara ya simu:-

Je, ni lini Serikali itajenga minara ya simu katikamaeneo ambayo hayana minara Mkoani Kigoma ili kuondoatatizo la mawasiliano kwa Wananchi?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, napenda kujibu swali laMheshimiwa Josephine Johnson Gezabuke, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko waMawasiliano kwa Wote mwezi Julai 2019, ilitangaza zabunikwa ajili ya kufikisha huduma za mawasiliano katika kata 521zenye vijiji 1,222 nchini. Zabuni hii ilifunguliwa Oktoba, 2019na baada ya tathmini yake maeneo yaliyopata wazabuninchi nzima na maeneo mbalimbali ni kama yafuatavyo:-

(i) Kwa upande Wilaya ya Kakonko, nikizungumziaMkoa wa Kigoma kata zil izopata miradi ni Kata zaNyamtukuza na Rugenge, Kijiji cha Kasongati;

(ii) Katika Wilaya ya Kigoma Vijijini, ilikuwa ni Kata yaZiwani ikijumuisha Vijiji vya Kalalangabo na Kigalye;

(iii) Katika Wilaya ya Buhigwe, tulikuwa na Kata yaMugera, Kijiji cha Katundu; na

(iv) Katika Wilaya ya Kasulu, ilikuwa Kata ya Kitangana Kijiji cha Kitanga.

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maeneo yaliyopatawazabuni, utekelezaji utaanza mapema mwezi wa Desemba,2019.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Upande wa Wilaya yaKibondo, Kampuni ya Simu ya Viettel (Halotel) itajenga mnaraili kufikisha huduma za mawasiliano katika Kijiji cha Kibuyeambapo wanatarajiwa kuanza mwisho wa mwezi Desemba,2019.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Josephine Genzabuke,swali la nyongeza.

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibumazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali moja lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Wilaya hizonilizozitaja, vipo vijiji ambavyo ukipiga simu mawasilianounayoyapata ni ya nchi jirani ya Burundi siyo Tanzania. Kwamfano, katika Wilaya ya Kakonko ipo Kata ya Mgunzu, kipoKijiji cha Kigra na Chulazo ambavyo mawasiliano yake ni yashida. Hata katika wilaya nilizozitaja viko vijiji ambavyohavikuweza kutajwa kwenye jibu la Waziri ambavyomawasiliano yake bado ya wasiwasi. Je, Serikali iko tayarikuendelea kuhamasisha makampuni kujenga minara katikamaeneo hayo ili wananchi waweze kupata mawasiliano yauhakikika?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kujibu swali moja la nyongeza MheshimiwaJosephine Gezabuke, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote kwanzanimpongeze sana Mheshimiwa Josephine Gezabuke kwa jinsi

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

anavyopambana kuhakikisha kwamba wananchi katikamaeneo mbalimbali hasa ya Mkoa wa Kigoma na maeneomengine ambayo yapo mpakani ya nchi yetu yanapatamawasiliano ya uhakika bila muingiliano kutoka nchi nyingineza jirani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwa kujibu swali lake,Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)tumeendelea kuwasiliana na nchi jirani ili sheria iliyowekwakutokana na Mkataba wa East Africa Communication uweunaweza kutekelezwa vizuri. Utaratibu unataka mnara wamawasiliano uwekwe kilometa 5 toka eneo la mpaka kwakila nchi i l i wananchi wanaohusika waweze kupatamawasiliano kutoka nchi husika lakini kuna maeneo ambayokwa nchi za wenzetu wamekiuka utaratibu huo. Katika kikaokinachotegemewa kukaa mwezi Februari, 2020 tunategemeaEast African Communication wata-resolve suala hilo kwasababu kuanzia Julai limekuwa likijadiliwa ili kuhakikishawananchi ambao wanapaswa kupata mawasiliano ya nchihusika wanaendelea kupata bila kuingiliana na watuwengine. Hilo linahusu vilevile na muingiliano wa masuala yaredio. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Wizara ya Viwanda na Biashara, Mheshimiwa DeogratiasFrancis Ngalawa, Mbunge wa Ludewa, sasa aulize swali lake.

Na. 25

Fidia kwa Wananchi waliopisha Miradi yaMchuchuma na Liganga

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA aliuliza:-

Kumekuwa na uhakiki wa mara kwa mara wamaeneo ya watu waliopisha miradi ya Mchuchuma naLiganga:-

Je, ni lini wananchi hao waliopisha na kutoa maeneoyao watalipwa fidia?

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwandana Biashara, majibu.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waViwanda na Biashara, napenda kujibu swali la MheshimiwaDeogratias Francis Ngalawa, Mbunge wa Ludewa, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nikiri nakumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa jinsi alivyo makinikatika kuwakilisha wananchi wake katika mradi huu muhimuhapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo tumekuwatukijibu mara kwa mara, Serikali imeendelea kujipangakutekeleza miradi ya kimkakati awamu kwa awamusambamba na kuandaa wataalam wenye ujuzi wa kutoshakatika kuendeleza miradi hiyo kwa tija.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kutekeleza mradi huumuhimu wa Chuma cha Liganga chenye ujazo wa takribanitani milioni 126 na makaa ya mawe tani milioni 428 ikiwa nipamoja na kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha eneo lamradi, Serikali imeendelea kutafuta fedha ili kukamilisha ulipajihuo wa fidia. Nikuahidi Mheshimiwa Mbunge, Serikaliitatekeleza ahadi hiyo mara pale hali ya kifedhaitakaporuhusu ikizingatiwa kuwa kwa sasa iko katikamajukumu mengine muhimu yanayofanana na hayoyakiwemo ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mwl. Nyerere, ujenziwa Vituo vya Afya pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwauwekezaji wenye tija unaohusisha kufanya tafiti stahiki.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Deogratias FrancisNgalawa, swali la nyongeza.

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali yanyongeza.

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanzaa, suala lakuanza Miradi ya Liganga na Mchuchuma nimekuwanikiliuliza mara nyingi katika Bunge lako na nimekuwa nikiulizamfulizo miaka yote. Kwa hiyo, kuhusu fidia imekuwa nisintofahamu kubwa kwa wananchi wa maeneo ambayomiradi hii inatakiwa kufanyika. Je, kwa nini sasa Serikali isioneumuhimu wa wananchi hao kuendelea kuyatumia maeneohayo mpaka hapo itakapokuwa tayari kulipa fidia hizo?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, imekuwaikiwekwa bajeti miaka miwili mfululizo sasa juu ya ulipaji wafidia. Kwa nini Serikali isilipe fidia wakati inaweka kwenyebajeti zake? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwandana Biashara, majibu.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali yanyongeza ya Mheshimiwa Deogratias Ngalawa, kamaifuatavyo:-

Katika suala la wananchi kuendelea kutumia maeneohayo mimi kwa mtazamo wangu naweza nikasema kwambawanaweza kuendelea kutumia katika misingi ya kilimo nashughuli zile ambazo hazitakuwa na uwekezaji mkubwa ilikuhakikisha kwamba wanaweza kupata tija inayotokana namatumizi hayo lakini masuala ya ujenzi au kuwekeza kwagharama kubwa zaidi na kwa sababu tayari tathminiimeshafanyika ni vema wasifanye hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili kuhusu bajeti imekuwaikitengwa lakini haipatikani, kama nilivyosema hapo awalikwamba kutenga bajeti ni namba moja lakini upatikanaji wafedha unategemeana na makusanyo yetu lakini pia matumizikutegemeana na mahitaji na vipaumbele tunavyojiwekea.Sasa tumeona badala ya kulipa fidia wakati mradi huuhauendelezwi kwa sasa ni vema hela zikaelekezwa kwenyeyale maeneo ambayo tayari miradi inatekelezwa ili sasa

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

miradi hiyo iendelee kuwezesha kuzalisha fedha nyingi zaidizitakazowezesha kukamilisha hata hiyo miradi mingine yakimkakati.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, ili tusipatewakati mgumu, wananchi wanaruhusiwa kufanya shughulizao kwenye maeneo hayo? Kwenye jibu lako la swali lanyongeza la swali la kwanza, je, wanaruhusiwa sasa kwendakulima na kufanya shughuli nyingine ukiacha hizo za ujenzi?

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:Mheshimiwa Naibu Spika, imekuwa ni kawaida kwa masualaya kilimo hata maeneo ambayo yana uwekezaji ulimaji wakawaida huwa upo tu.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Nadhani MheshimiwaMbunge amesikia atawapelekea majibu watu wake.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na swali laMheshimiwa Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Chumbuni,swali lake litaulizwa kwa niaba na Mheshimiwa Jaku.

Na. 26

Bidhaa za Zanzibar kuwekewa Vikwazo Tanzania Bara

MHE. JAKU HASHIM AYUOB (K.n.y. MHE. USSI SALUMPONDEZA) aliuliza:-

Kumekuwa na malalamiko ya bidhaa zinazozalishwaZanzibar kupata vikwazo kuingia katika Soko la TanzaniaBara:-

(a) Je, Serikali imechukua hatua gani kuondoa tatizohilo katika kulinda misingi ya Muungano hasa baada yamaziwa na sukari kuwekewa vikwazo zaidi?

(b) Je, Zanzibar inaweza vipi kutumia Soko la Jumuiyaya Afrika Mashariki wakati soko la ndani bado bidhaazinazozalishwa zinawekewa vikwazo?

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwandana Biashara, majibu.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waViwanda na Biashara, napenda kujibu swali la MheshimiwaUssi Pondeza Mbunge wa Chumbuni, lenye sehemu (a) na(b) kwa pamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania imeweka utaratibu mahsusi wakushughulikia changamoto zisizo za Muungano zikiwemo zakibiashara ili kuimarisha Muungano wetu. Utaratibu huohuendeshwa kwa kutumia vikao vya ushirikiano wa kisektaambapo Ofisi ya Makamu wa Rais imetoa mwongozo kwasekta za pande mbili za Muungano kujadili changamotokupitia vikao kuanzia ngazi ya Wataalam, Makatibu Wakuuna Mawaziri na kushauri mamlaka za maamuzi. Utaratibu huounazingatia pia kutekeleza matakwa ya Katiba ya Jamhuriya Muungano ya mwaka 1977 katika kuimarisha Muunganowetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, chini ya utaratibu huo, Sektaya Viwanda na Biashara kwa nyakati tofauti imekuwaikipokea, kujadili na kutafutia ufumbuzi changamoto zabiashara zilizoibuliwa kutoka pande zote mbili za Muungano.Baadhi ya bidhaa zilizowahi kushughulikiwa chini ya utaratibuhuo ni pamoja na kuku, sukari, maziwa na bidhaa nyinginezo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia utaratibu huo, mwaka2019 Wizara ya Viwanda na Biashara (SMT) na Wizara yaBiashara na Viwanda (SMZ) kwa pamoja zilipewa maagizoya kushughulikia malalamiko kuhusu suala la sukari kutokaZanzibar kuingia Tanzania Bara. Wizara hizo ziliunda Timu yaPamoja ya Wataalam ambao walichambua suala hilo nakuwasilisha taarifa yake kwa Viongozi wa Wizara hizo mweziSeptemba, 2019 kwa hatua zinazofuata. Hivi sasa suala hilolinafanyiwa kazi kupitia ngazi zilizobainishwa ili hatimaye

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

maamuzi yaweze kufanyika. Hivyo, namuomba MheshimiwaMbunge aendelee kuwa na subira katika suala hilo na yaleyanayofanana nalo yanayoendelea kushughulikiwa ili kupatasuluhu ya kudumu, yenye tija na maslahi mapana kwa pandezote mbili za Muungano.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, nichukue fursa hiikumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa jitihada anazofanyakufuatilia kwa karibu na kushauri namna ya kuboresha nakuimarisha masuala yanayohusu biashara kati ya pande hizimbili za Muungano.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Jaku, swali la nyongeza.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa NaibuWaziri, subira ina mipaka yake, nisubiri hadi lini maana hatakuna wimbo umeimbwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, je, ni linimtairuhusu Zanzibar kujiunga moja kwa moja katika soko laJumuiya la Afrika Mashariki kwa nchi zile za Uganda, Burundina Rwanda kwa vile soko la Tanzania Bara limefungwa kabisa,Zanzibar hairuhusiwi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa vile Jamhuriya Muungano ndiyo yenye nguvu katika sekta ya fedha, seraza kodi na ndiyo mhimili mkubwa wa uendesha wa biasharana nchi. Je, hamuoni mnaendelea kuikandamiza Zanzibarkiuchumi kwa vile bidhaa za Tanzania Bara zinaingia Zanzibarbila vikwazo kwa maana kwamba saa 24 milango iko wazina zinapokelewa na kupigiwa salute? Je, lini mtaondoshapingamizi hilo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwandana Biashara, majibu.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali yanyongeza, kama ifuatavyo:-

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza hapoawali masuala yanayohusu Muungano wa nchi yetu hii nimuhimu na sensitive na ndiyo maana yamewekewa utaratibumaalumu wa namna ya kujadiliana. Kwa hiyo, niseme tukwamba hayo yote ambayo yanaonekana yanahitajikufanyiwa maboresho mbalimbali ni vema yakajadiliwakupitia vikao hivyo ambavyo tumeona ni muhimu sana navimekuwa vikifanya kazi nzuri sana katika kutatuachangamoto za Muungano.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Wizara ya Kilimo, Mheshimiwa Dunstan Luka Kitandula,Mbunge wa Mkinga, swali lake litaulizwa kwa niaba naMheshimiwa Timotheo Mnzava

Na. 27

Mbegu Bora ya Viungo vya Vyakula

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA (K.n.y. MHE. DUNSTAN L.KITANDULA) aliuliza:-

Kata za Kigongoi, Mhinduro na Bosha Wilayani Mkingazinalima kwa wingi viungo vya chakula kama vile hiliki,mdalasini, pilipili manga na karafuu:-

Je, Serikali ipo tayari kuwawezesha Wakulima haokupata mbegu bora ili waweze kuongeza uzalishaji wa mazaoyao?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo,majibu.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. HUSSEIN M. BASHE):Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo,napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dunstan Luka Kitandula,Mbunge wa Mkinga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimuwa kuwekeza katika mazao mbalimbali ya kilimo yakiwemo

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

mazao ya viungo ambayo mahitaji yake yanaendeleakuongezeka ndani na nje ya nchi. Kwa kutambua umuhimuhuo, Serikali kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI)imeanza kufanya utafiti wa kupata mbegu bora za mazaoya viungo na mazao mengine ya bustani aina ya horticultureili kuongeza uzalishaji na tija.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara yaKilimo inapitia Sera ya Kilimo ya Mwaka 2013 ambapo sektandogo ya mazao ya bustani ni miongoni mwa maeneomuhimu yanayozingatiwa. Vilevile, kutokana na umuhimu wamazao hayo, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo itafanya kikaocha wadau wa mazao hayo tarehe 8 Novemba, 2019 ilikuandaa Mkakati wa Miaka Mitano wa Kuendeleza Mazaoya Bustani. Mkakati huo unalenga kuongeza uzalishaji, uborawa mazao na kuimarisha mifumo ya masoko ya mazao hayo.Aidha, mkakati huo utakuwa ni sehemu ya utekelezaji waDira ya Maendeleo ya Taifa unaolenga Taifa letu kufikiauchumi wa kati mwaka 2025.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hatua hizo,Serikali inaendelea kutoa elimu ya kilimo bora cha mazao yaviungo na mazao mengine; uhifadhi, usindikaji na masokokwa kushirikiana na Sekta Binafsi kikiwemo Chama chaWadau wa Mazao ya Viungo Tanzania (Tanzania SpicesAssociation – TASPA), Sustainable Agriculture Tanzania (SAT)na vyama vingine vya wakulima.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Timotheo Mnzava, swali lanyongeza.

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Kabla sijauliza maswali ya nyongeza, niruhusuniendelee kuwapa pole wananchi wa Jimbo langu laKorogwe Vijijini na Mkoa mzima wa Tanga kwa mafurikomakubwa yaliyotupata siku chache zilizopita. Tunaendeleakutumaini juhudi ya Serikali kurejesha miundombinu yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuriya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali madogo mawili

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

ya nyongeza. Swali la kwanza; moja ya sababu ya nchitunazoshindana nazo kwenye soko la mazao ya viungo namazao ya bustani kufanya vizuri ni wao kuwa na mamlakaza kusimamia mazao haya. Je, ni lini Serikali yetu itaonaumuhimu wa kuanzisha Mamlaka ya Kusimamia Mazao yaViungo na Mazao ya Biashara?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; wananchi waTarafa ya Bungu, Wilaya ya Korogwe, ni wakulima wakubwana wazuri sana wa mazao ya viungo na zao la chai, lakinitumekuwa na changamoto kubwa sana ya bei kwenye zaola chai. Je, ni upi mkakati mahususi wa Serikali wa kuhakikishakwamba wanaboresha bei ya zao la chai ili kuwezakuwaletea tija wananchi na wakulima wa zao la chai nchini?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo,majibu.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. HUSSEIN M. BASHE):Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Mnzava kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza napenda kutumianafasi hii kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge pamoja naWaheshimiwa Wabunge na Watanzania wote kwambaWizara ya Kilimo inafahamu umuhimu wa kuanzishwa kwataasisi itakayosimamia mazao ya horticulture na mazao yaviungo. Hivi sasa tunapitia mfumo na muundo wa Wizarakupunguza idadi ya bodi na kuanzisha mamlaka chacheambazo hazitazidi tatu, mojawapo ikiwa ni Mamlaka yaMaendeleo ya Mazao ya Horticulture.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mwenyezi Mungu akijaaliahivi karibuni Bunge hili litapokea sheria ambayo itaoneshamabadiliko ya muundo wa taasisi mbalimbali ndani ya Wizaraya Kilimo ili kuipa sekta hii nafasi inayostahili kwa sababu nisubsector ndogo katika Sekta ya Kilimo inayokua kwakiwango kikubwa sana na inahitaji attention inayostahili. Kwahiyo nimtoe hofu kwamba tuko katika hatua za awali na kabla

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

ya kufika Bunge lijalo la Bajeti tutakuwa tumeshaanzishaMamlaka ya Mazao ya Horticulture.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la chai; ni kwelikama Serikali hatua tunazochukua mojawapo sasa hivi tukokatika hatua za mwisho za kuanzisha a primary market katikaeneo la Dar es Salaam ili tuwe na mnada wa kwetu hapaTanzania. Tumesha-earmark eneo na sasa hivi tuko katikahatua za awali kutengeneza utaratibu ili chai yetu badalaya kwenda kuuziwa katika soko la Mombasa sasa ianzekuuziwa katika soko la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tutatumia mfumo waTMX ili kuwaruhusu wanunuzi duniani waweze ku-bid.Mchakato huu unawahusisha Sekta Binafsi ambaowamewekeza katika chai ili kuhakikisha kwamba zao la chailinapata soko na bei ya uhakika. Kwa hiyo WaheshimiwaWabunge tunaamini kwamba ndani ya muda mfupitutaanzisha soko la kwetu ndani ya Tanzania na chai yetuitauziwa hapa na itapunguza gharama na kumpatia mkulimabei nzuri.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Leah Komanya.

MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Katika Mkoa wa Simiyu tayari mbegu za pambazimeshaanza kusambazwa na kupata mbegu za pamba kwawakulima mpaka uzinunue. Wapo baadhi ya wakulima badohawajalipwa pamba na wanunuzi; je, Serikali inawasaidiajeili wakulima hao waweze kupata mbegu za pamba?

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo,majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. HUSSEIN M. BASHE):Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua tatizo hilo alilolisemaMheshimiwa Leah Komanya, ni kweli kampuni binafsi naningeomba kupitia Bunge Watanzania wote wakaelewa;

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

walionunua pamba sio Serikali ya Jamhuri ya Muungano,walionunua pamba ni kampuni binafsi za Watanzania, lakinitunafahamu kwamba Watanzania wote hawajalipwawanaodai kampuni hizi. Mpaka sasa wameshalipa bilioni 417,wakulima wanadai bilioni 50. Tarehe 14 tutakutana nawanunuzi ili kulitatua tatizo la wao kumalizia kulipa kwawakulima ili wakulima waweze kupata fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hilo vilevilemakampuni yaliyopewa haki ya kusambaza mbegu borakatika maeneo ya wakulima wa pamba nao tutakutana naoili kutengeneza utaratibu ambao hautowalazimisha wakulimawanaodai kulazimishwa kulipia mbegu ya pamba.Tutatengeneza utaratibu ambao utamfanya mkulima kamaanaidai kampuni kampuni hiyo impe mbegu wakati anamlipaatakata gharama yake ya mbegu alizompatia. Kwa hiyotarehe 14 tutamaliza tatizo hili na hili halitakuwa tatizo tenamuda mfupi ujao.

NAIBU SPIKA: Tunaendelea na swali la MheshimiwaMbaraka Kitwana Dau, Mbunge wa Mafia, swali lakelitaulizwa kwa niaba na Mheshimiwa Zaynab Matitu Vulu.

Na. 28

Kushuka kwa Bei ya Nazi Nchini

MHE. ZAYNAB M. VULU (K.n.y. MHE. MBARAKA K. DAU)aliuliza: -

Bei ya zao la nazi imekuwa ikishuka kwa kasi kubwakatika miezi ya hivi karibuni: -

(a) Je, ni zipi sababu za kushuka kwa bei ya zao hilo?

(b) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuokoa zao hilo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo,majibu.

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA)alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waKilimo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbaraka KitwanaDau, Mbunge wa Mafia, lenye sehemu (a) na (b) kwapamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, sababu za kushuka kwa beiya zao la nazi ni pamoja na:-

Uwepo wa wanunuzi wachache wa nazi na hivyokutokuwepo kwa bei ya ushindani ikilinganishwa na misimuiliyopita; kupanda kwa gharama za usafirishaji wa nazi kutokaSh.2,800 miaka mitatu iliyopita na kufikia Sh.5,500 kwa gunialenye nazi 200 mwaka 2019; kupungua kwa wanunuziwakubwa wa viwanda vya mafuta ya nazi na bidhaa zake;kuongezeka kwa matumizi ya bidhaa mbadala za nazi kamavile mafuta ya kula ya mawese toka nje ya nchi na matumiziya mafuta ya kupaka yasiyotokana na nazi; kushuka kwathamani ya shilingi dhidi ya dola na kushuka kwa mfumukowa bei toka asilimia 11 kwa mwaka 2006 mpaka asilimia nnemwaka 2018/2019; kushuka kwa uzalishaji wa nazi nchinikutokana na magonjwa na mabadiliko ya tabia ya nchiambayo yamesababisha kupungua kwa uzalishaji wa nazina kutowavutia wawekezaji wa ndani na nje kwa sekta yaviwanda vya kuchakata nazi kutokana na hofu ya kukosamalighafi ya kutosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kushirikiana nawadau wa maendeleo inafanya jitihada za kuongezawawekezaji katika zao la nazi kwa lengo la kumpatia mkulimasoko la uhakika na bei nzuri. Jitihada hizo ni pamoja na kutoaelimu katika mnyororo wa thamani wa zao la nazi ikiwa nipamoja na kuwapatia wakulima mashine za kukamuamafuta ya nazi. Hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2019,Vikundi vya Wajasiriamali vya Tujitegemee na Kaza Moyovimepatiwa mashine zenye uwezo wa kukamua mafuta yanazi lita 400 kwa siku ambapo lita moja huuzwa kati yaSh.8,000 hadi Sh.10,000.

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali inaendeleakutafuta masoko ya mazao yote ya kilimo likiwemo zao lanazi kwa kuwaunganisha wakulima na wanunuzi kupitiavikundi na vyama vya ushirika. Vilevile, Serikali inaendeleakuweka miundombinu ya usafiri kwa kuunda kivukokitakachowezesha kuwaunganisha wananchi wa Mafia nasehemu zingine kwa usafiri kutoka Mafia hadi Nyamisati,Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti na hivyo kuwawezeshawakulima wa Mafia kusafiri na mizigo yao pamoja na nazikwenda Dar es Salaam ambapo watauza kwa bei nzuri katikamasoko makubwa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zaynabu Matitu Vulu, swalila nyongeza.

MHE. ZAYNAB M. VULU: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa NaibuWaziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa Serikaliimebaini kwamba kuna tatizo la soko; na kwa kuwa Serikaliimebaini kuna uhaba wa zao lenyewe na watumiaji. Je,Serikali haioni sasa kuna haja ya kuweka mkakati madhubutiwa kuwatafutia wakulima hawa soko la nje wawezekusafirisha nazi zao kwenda nje ya nchi kwani hapa Tanzaniakwa mujibu wa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziriinaonekana kwamba soko limepungua? Pia wangewezakutoa elimu ya kutosha watu wakajua matumizi na thamaniya zao la nazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; bila shaka NaibuWaziri anajua thamani ya zao la nazi, zao la nazi lina thamanikubwa sana. Kwanza mti wenyewe unatumika kama mbao,unatumika kwa kutengenezea furniture, mti wenyewe unatoanazi, nazi inatoa tui ambalo linapikiwa, nazi ina maji ambayoyanatumika kwa afya zetu; nazi machicha yake yanatumikakwa ajili ya kutengenezea kashata na vitu vingine, lakini piamnazi huohuo unatoa makuti ambayo yana thamani katikautalii wetu wa hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati huo huo mnazi huohuo unatoa kitu kinaitwa kitale, kitale kina thamani kubwa

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

sana watu wa afya wanaweza wakajua na watu wa Pwaniwanaweza wakaelewa thamani ya kitu kinachoitwa kitale.Sasa ni lini Serikali itaweka mkakati wa kuhakikisha zao hili lanazi halipotei nchini kwetu kwa kurudisha vituo vya utafitivilivyokuwa Dar es Salaam, Mafia, Bagamoyo na Lindi iliwakulima wale wasiweze kupoteza thamani ya zao la nazi?Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo,majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Zaynabu Matitu Vulu, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanzaanataka kujua mikakati ya Serikali kutafuta soko la nazi njeya nchi; ni kweli kwamba kama Serikali tuna mikakatimbalimbali lakini tufahamu kwamba matatizo makubwa yasoko la nazi sio bei, tatizo kubwa ni kipato kidogowanachopata wakulima wa nazi na kipato hicho kinawezakuongezeka kutokana na bei kubwa au tija kuongezeka aukuongeza uzalishaji, lakini pia kupunguza gharama zauzalishaji wakulima hao wa nazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Serikali mojaambalo ndiyo tumeanzisha vituo vya utafiti hivi 16,kimojawapo ni Kituo chetu Cha Utafiti cha pale Mikocheniambacho kimepewa mahususi kwa ajili ya utafiti wa zao lanazi. Lengo ni kuja kupunguza gharama za uzalishaji, lakinikupata mbegu bora zinazoweza kuhimili ukame namagonjwa kwa ajili ya kuongeza tija na uzalishaji kwawakulima wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili anatakakujua ni lini Serikali tutaanza kurudisha vile vituo vyetu vyautafiti kama zamani. Kama nilivyosema katika majibu yetuya msingi, kwanza zamani hatukuwa na vituo vile vya utafiti

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

zaidi ya hiki cha Mikocheni, tulikuwa na vituo vya kuzalishamiche ya minazi na baadaye kuisambaza kwa wakulima.

Mheshimiwa Naibu Spika, huo utaratibu mpaka sasahivi tunao, tunacho kule Zambezi Bagamoyo, tunacho paleMkuranga na tutaendelea kufungua vituo hivyo Mafia nasehemu zingine kwa wakulima wakubwa wa nazi, lakini hasabaada ya kupata taarifa za utafiti kutoka kwenye kituo chetuhiki cha TARI pale Mikocheni ambacho tumewapa mahususikwa ajili ya kufanya utafiti wa zao la nazi ili kuja sasa na mbeguambayo inahimili ukame na magonjwa tuachane na mbeguyetu ile fupi tuliyoletewa kutoka nje ambapo kule ni nchiambazo ni za baridi, haiwezi kuhimili kutokana na hali ya jotona hali ya mazingira ya nchini kwetu. Kwa hiyo, nitoe witokwa wakulima wote; sasa hivi tunasisitiza tutumie mbegu yetuile ya asili ya East African Tall ambayo inahimili ukame, jotona mazingira yetu.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tumalizie swaliletu la mwisho, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa;Mheshimiwa Maryam Salum Msabaha, Mbunge wa VitiMaalum, sasa aulize swali lake.

Na. 29

Kuliwezesha Shirika la Mzinga

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA aliuliza:-

Shirika la Mzinga limekuwa likifanya kazi zake kwaweledi na uaminifu mkubwa lakini lina changamoto za vifaakama vile mashine za ramani:-

Je, kwa mwaka 2019/2020 Serikali ilitenga kiasi ganicha fedha kwa ajili ya Shirika hilo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa, majibu.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA alijibu:-

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Maryam Salum Msabaha, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mwaka wa Fedha2019/2020, Shirika la Mzinga limetengewa jumla ya shilingi2,000,000,000.00 kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha shirikalinatekeleza majukumu yake kwa ufanisi, shirika limeanzakutekeleza Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2017/2018 –2021/2022) ambao unakusudia kupanua wigo wa uzalishajiwa mazao ya kijeshi. Aidha, shirika limepanga kuanzishakiwanda cha kutengeneza baruti kwa ajili ya matumizi yasiyoya kivita (civil explosives) na kupanua mradi wa kutengenezamashine ndogo ndogo zitakazowezesha wajasiriamalikuongeza thamani ya mazao ya kilimo na misitu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Maryam Msabaha, swali lanyongeza.

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante. Naomba nimuulize Mheshimiwa Wazirimaswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza, shirikalimekuwa likipata tenda kutoka ndani ya Serikali na limekuwalikifanya kazi hizi kwa weledi mkubwa sana. Je, Serikali inamikakati gani kuhakikisha shirika linalipwa kwa wakati ili hatazile changamoto ndogondogo wanapopata zile hela kwawakati wapate kuzitatua wenyewe?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; miundombinuya haya mashirika, hiki Kikosi cha Mizinga kwenye makambimengi ni chakavu na si rafiki sana na ni siku nyingi. Sasa Serikaliina mikakati gani ya kutenga fedha na kuangalia hiki kitengokwa sababu hiki kitengo ni kwa kazi maalum na kinafanyakazi kwa ujasiri na kwa weledi mkubwa. Je, Serikali na Wizaraya Fedha ina mkakati gani kuhakikisha kwamba kilekinachotengwa kwa ajili ya kitengo hiki kinapelekwa ili kutoahizi changamoto ambazo zipo katika Kikosi hiki cha Mizingakatika hili Shirika la Mzinga? Ahsante.

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa, majibu.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Maryam Msabaha kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu malipo kwa kaziambazo shirika linafanya za Serikali naweza nikamuelezaMheshimiwa Mbunge kwamba malipo hayo yanafanyika. Hivikaribuni Shirika la Ujenzi la Mzinga limepata kazi kadhaaikiwemo ujenzi wa ofisi za Serikali hapa Dodoma, lakini katikabaadhi ya halmashauri pia wamekuwa wakipata kazi. Kwataarifa nilizokuwa nazo ni kwamba malipo yanafanyika nafedha hizo zinawasaidia kuboresha mambomadogomadogo katika shirika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu miundombinu yashirika lenyewe; ni kweli kwamba kwa kiwango kikubwamiundombinu pale katika Shirika la Mzinga imechakaa, ni yamuda mrefu na ndiyo maana kama nilivyosema katika jibulangu la msingi ni kwamba sasa wametengeneza mpangomkakati ambao kwa kiwango kikubwa ukipata fedhautaweza kushughulikia yote haya ikiwemo kuboreshamiundombinu, lakini kuleta wataalam waliobobea katika fanihizo na kuwa na mtaji wa kuweza kuendeleza shirika hili. Nimatumaini yetu kwamba mpango mkakati huo utapitishwana Serikali ili shirika liweze kupata fedha na kuweza kuboreshamiundombinu yake.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tumefikamwisho wa kipindi chetu cha maswali na majibu. Nitaletakwenu matangazo tuliyonayo.

Waheshimiwa Wabunge, tumefika mwisho wa kipindichetu cha maswali na majibu, nitaleta kwenu matangazotuliyonayo Kwanza ni tangazo la wageni waliopo Bungenisiku ya leo. Tutaanza na wageni waliopo Jukwaa laMheshimiwa Spika, na hawa ni wageni wa Mheshimiwa Spika.

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

Wa kwanza ni ndugu Faustine Martine Kasike ambaye niKamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, karibu sana. Karibusana, karibu sana Kamishna wa Magereza. (Makofi)

Pia, tunaye ndugu Mgongoro Jonathan ambaye nimwandishi wa vitabu, karibu sana. Tunao pia wageni kutokaChama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania na Shirika laKaragwe Community Based Rehabilitation Programwakiongozwa na Katibu wao ndugu Mussa Kabimba. Karibunisana, karibuni sana. Tunao pia wageni kutoka Shirika lisilo lakiserikali la Tangible Initiatives for Local DevelopmentTanzania, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo nduguChristina Kamili, karibuni sana.

Waheshimiwa Wabunge tunao pia wagenimbalimbali wa Waheshimiwa Wabunge na tutaanza nawageni wa Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, wageni 26ambao ni Wachungaji wa Makanisa ya Kipentekoste kutokaTukuyu, Mkoa wa Mbeya wakiongozwa na Mwenyekiti waoMchungaji John Mwakapugi. Karibuni sana, karibuni sana.(Makofi)

Tunao pia wageni wanne (4) wa Mheshimiwa JumaHamad Omar ambao ni familia yake kutoka Zanzibarwakiongozwa na mke wake ndugu Zamda Mnete. Karibusana, karibu sana, karibuni sana. (Makofi)

Zamda Mnete ndio yupi kati yenu! Ndiyo wifi yetu huyojamani, karibu sana. Wengine shemeji yao, naona wanaumewalikuwa wanaona wametengwa kidogo hivi!

Tunao pia wageni wawili (2) wa Mheshimiwa MaftahaNachuma ambao ni viongozi wa wafanya biashara kutokaMkoa wa Mtwara, na hawa ni ndugu Abilahi Shilingi na nduguTwaha Ngozoma, karibu sana. (Makofi)

Tunao pia wageni 12 wa Mheshimiwa Balozi AdadiRajab ambao ni Viongozi wa Chama cha Kutetea AbiriaTanzania (CHAKUWA), wakiongozwa na Mwenyekiti Taifa

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

ndugu Hassan Mchanjama. Karibuni sana, karibuni sana.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge tuonao pia wageni ambaowamekuja kwa ajili ya mafunzo, nao ni wanachuo 40 kutokaChuo cha Uhasibu Arusha ambao wameongozwa na Raiswa Chuo hicho ndugu Laurent Wilson, karibuni sana (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge hao ndiyo wageni tulionaoBungeni siku ya leo, lakini pia lipo tangazo kutoka Idara yaUtawala na Rasilimali watu. Waheshimiwa Wabungemnatangaziwa kwamba Wabunge ambao ni Mabalozi waUsalama Barabarani kwamba, TAWLA wameandaa seminaya kuwajengea uwezo juu ya athari za kiafya na kiuchumizinazosababishwa na ajali za barabarani. Semina hiyoitafanyika Nashera Hotel, Dodoma kuanzia Saa 07:30 mchanampaka Saa 10:30 jioni leo tarehe 06 Novemba, 2019. Orodhaya Wabunge ambao ndiyo wanaoalikwa huko itakuwaLango A la kuingilia hapa Bungeni.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge majina yaWabunge wanaoalikwa huko yapo Lango A yakaangaliwehuko. Kama hukualikwa basi nadhani sasa wapo wahusikawenyewe wanaotakiwa kwenda huko, usije ukajikutaunarudishiwa mlangoni.

Pia, lipo tangazo la Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mt.Thomas More hapa Bungeni, Mheshimiwa Shally Raymond,anawatangazia Waheshimiwa Wabunge wote kuwa siku yaleo kutakuwa na Ibada ya Misa ya Wakristo Wakatoliki saasaba mchana mara baada ya kuahirisha Shughuli za Bunge.Waheshimiwa Wabunge wote na wageni wote mliokoBungeni mnaalikwa katika misa hiyo ambayo itafanyikaJengo la Pius Msekwa, ghorofa ya pili.

Waheshimiwa Wabunge hayo ndiyo matangazotuliyokuwa nayo siku ya leo tutaendelea na ratiba yetu.Katibu!

MHE. ANATROPIA K. THEONEST: Mwongozo.

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Hoja ya kuahirishamjadala wa Bunge unaoendelea.

MHE: ANATROPIA K. THEONEST: Mwongozo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwakajoka.

HOJA YA KUAHIRISHA BUNGE

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru kwa kupata nafasi hii ili niweze kutoamwongozo wangu kwenye suala la dharura ili Shughuli zaBunge ziweze kuahirishwa tuweze kujadili jambo la dharurakatika Bunge letu. Kutokana na jambo ambalo janaMheshimiwa Waziri wa TAMISEMI ametoa ufafanuzi kwambakutokana na malalamiko ya mchakato wa uchaguzi ambaounaendelea sasa hivi wa Serikali za Mitaa kwamba jana naleo iwe ni siku ya kupeleka pingamizi ya wale wote ambaowalikuwa wameondolewa kwenye mchakato huo. Lakini chakushangaza ni kwamba mpaka sasa hivi Watendaji tokaasubuhi hakuna ofisi yoyote iliyofunguliwa, ofisi zote zawasimamizi wa uchaguzi zimefungwa na hakunakinachoendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa wananchi wanatakakupata kauli ya Serikali, hivi taarifa aliyoitoa MheshimiwaWaziri jana ni kwamba Wasimamizi wa Uchaguzi katikamaeneo yote na Wasimamizi Wasaidizi wamegoma kauli ilekwamba hawawezi kutekeleza na jambo hili halitafanyikakama ambavyo amezungumza na nini kifanyike? Kwasababu tunaona ni jinsi gani ambavyo kuna dhamira ovu yakuvuruga uchaguzi na kuvuruga amani na mshikamano waTaifa hili kwa sababu ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunataka tupateufafanuzi pia kutokana na jambo hili ili ikiwezekana Bungelako lijadili, kwa idhini yako Bunge lijadili jambo hili la dharurana lina maslahi mapana ya Taifa, lakini pia linawezakusababisha mvutano mkubwa, lakini pia na uvunjifu waamani katika Taifa hili. Tunashangaa sana kwanini jambo hili

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

Serikali inalifumbia macho na lisiichukulie kama ni jambo lamsingi. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Anatropia.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. ANATROPIA R. THEONEST: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru. Nasimama kwa Kanuni ya 47 sitaisoma,lakini suala ninaloongelea hata gazeti la Mwananchiwameandika, “Wapinzani walia kila kona Chaguzi za Serikaliya Mitaa”. Tunataka ufafanuzi, kuna mambo yamefanyikahuko kwenye mchakato wa kurudisha fomu wa Serikali yaMitaa ambao wakati mwingine ukiyafikiria unashindwakuelewa dhamira. Eti mgombea anaenguliwa kwa madaikwamba Chama cha CHADEMA, Chama ACT Wazalendo,Chama cha CUF, NCCR na vyama vingine kwambahavijasajiliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunataka ufafanuzi,tunataka tusikie kauli ya Serikali; Je, nini dhamira yake? Nidhamira ya Serikali kuona nchi inajaa machafuko kwakuminya haki za wananchi kufanya uchaguzi? Au, na kamadhamira yake ni kulinda amani, itangaze mchakatouangaliwe upya kwa maana ya watendaji ambaowamewaondoa wagombea kwa hila, kwa kasorondogondogo, lakini kwa kuonesha kwamba walikuwa nalengo la kupitisha wagombea wa CCM bila kupingwa. Watoekauli, watoe maagizo kwamba huo mchakato batili urejeweupya na tupate haki zetu. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Maftaha.

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kunipa nafasi. Jana nilisimama kwaKanuni ya 69(1), na leo naomba nisimame tena kusimamiahoja yangu ambayo nili-raise jana kwamba mjadala waBunge unaoendelea kujadili Mpango wa Maendeleo wamwaka 2020/2021 uahirishwe kwa sababu ya suala hiliambalo naenda kulizungumza.

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

Mheshimiwa Naibu Spika, jana nilisema kwambauchaguzi huu ambao Wapinzani wameenguliwa nchi nzima,maeneo yote ya ngome za Chama cha Wananchi - CUF,CHADEMA, NCCR, ACT, Wapinzani wote wameenguliwa. Hivisasa ninavyozungumza kuna taharuki kubwa sana hukomitaani, wananchi wanatupigia simu sana kama viongozi wavyama vya siasa wanatuuliza tufanye nini. Tunawaambiatulieni, tulieni, tulieni, kwa hiyo, kuna taharuki sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa sisi Bungetunajadili Mpango wa Maendeleo na hakuna maendeleobila amani, duniani kutakuwa na maendeleo bila amani.Nilikuwa naomba kutoa hoja katika Bunge lako tukufukwamba liweze kujadili hili suala tuweze kujadili amani yaWatanzania kwa kufuata demokrasia ya vyama vingi. Hivisasa kama unavyoona wapinzani walivyoenguliwa wote janatulielezwa kwamba tulete vielelezo hapa, leo nimekuja navielelezo ninavyo kibao hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba tuwasilishemezani Wabunge nitoe hoja ya kujadili suala hili kwa sababuni suala muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu hili,vinginevyo nchi haitakuwa sawa sawa. Hatuwezi kamaWabunge kujadili maendeleo hapa wakati huko hali haikusawa sawa. Naomba kutoa hoja Waheshimiwa Wabunge,naomba mniunge mkono Waheshimiwa Wabunge ili tuwezekujadili hili suala. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Naomba mkae, Mheshimiwa Musukuma.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana. Nilikuwa naomba mwongozo wako kwaKanuni ya 68(7) kwenye swali Na. 18 lililoulizwa na MheshimiwaZitto wakati Serikali ikitoa majibu na swali la nyongezalililoulizwa na Mheshimiwa Mlinga imeeleza vizuri tu kwambaHalmashauri ya Ujiji imepata hati chafu kwa miaka minne.Nimekuwa Mwenyekiti wa Halmashari, upo mwongozounaotuelekeza kwamba Halmashauri inapopata hati chafumara tatu inatakiwa kufutwa na kuwa kwenye usimamizimkali. Pia imeelezwa na Mheshimiwa Waziri kwamba, moja

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

ya sababu inayosababisha kupata hati chafu kwenyehalmashauri hiyo ni pamoja na mvutano wa WaheshimiwaMadiwani na Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilitaka kufahamu, kamatumeshaingia hasara miaka minne, tunaenda mwaka watano tunajua kabisa tunaenda kudumbukia kulekule. Ni ninihatua ya Serikali kutekeleza Waraka wa kuifuta Halmashauriya Ujiji ili iweze kuwa kwenye uangalizi wa Kamati?

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijajibumambo ambayo yameelezwa na Wabunge hapa. Kunawageni wa Mheshimiwa Spika ambao wameingia sasa hivihapa Bungeni, na mmoja ni Mheshimiwa Balozi wa Canadanchini Tanzania, Bi. Pamela O’Donnell. (Makofi)

Honorable Pamela, can you stand up! Karibu sana,karibu sana. (Makofi)

Pia, tunaye Bi. Sandra Rossiter ambaye ni CouncilorPolitical Economic and Public Affairs, naye anatoka Ubaloziwa Canada, karibuni sana. (Makofi)

Tunaye pia mgani wa Mheshimiwa Joyce Sokombiambaye ni Hilda Newton, karibu sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge amesimama MheshimiwaFrank Mwakajoka akiomba mwongozo halafu akatoamaelezo kwamba ni jambo la dhararu ambayo wotemmeyasikia. Ameeleza mambo kwa kirefu yanayohusuUchaguzi wa Serikali za Mitaa na jambo ambalo alilitoleaufafanuzi Mheshimiwa Jafo. Pia, amesimama MheshimiwaAnatropia Theonest Rwehikila kuhusu jambo linalofanana nahilo, yeye akisema anasimama kwa mujibu wa Kanuni ya 47kwamba ni jambo la dharura na tulijadili. Wakati huohuoamesimama Mheshimiwa Maftaha Nachuma, yeyeamesimama kwa mujibu wa Kanuni ya 69 akiomba Bungeliahirishe jambo linalofanywa sasa ili tuweze kujadili hilohilojambo linalohusu uchaguzi.

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

Waheshimiwa Wabunge jambo hili lilianza kujitokezaBungeni jana na Mheshimiwa Spika alitoa maelezo kwambaaletewe vielelezo kuhusu mambo aliyokuwa akiyazungumzaMheshimiwa Maftaha. Mheshimiwa Maftaha wakati huohuoanasema ameleta vielelezo vya kuonesha yale yaliyotokeahuko. Kwa hiyo, haya mambo matatu yote yaliyozungumzwakwa kuwa yanazungumzia jambo moja, na wote wamekirikwamba Mheshimiwa Jofo alitoa maelekezo jana ambayoyanafanyiwa kazi jana, leo na kesho, maana yake Serikaliimeshaanza kuchukua hatua juu ya mambo ambayoyanalalamikiwa humu ndani. (Makofi)

Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge hatuwezi sisi humundani ambao hata hivyo vielelezo hatuna sote kushiriki huumjadala. Na kwa kuwa Serikali imeshatoa maelekezo nandicho kilichokuwa kinaombwa hapa, maelekezo na kauliya Serikali imekwisha kusikika, na kwa kuwa leo ni sehemu yahizo siku ambazo Serikali inalifanyia kazi jambo hilo Serikaliinaendelea na utaratibu wake. Kwa mujibu wa Kanuni zetu,sote tunafahamu jambo ambalo linakuwa kwenye utaratibuhuo Bunge haliwezi kuingia hapo kufanya kazi. Kanuni ya 47ambayo inazungumzia udharura wa jambo ni pamoja na hilojambo kushindwa kufanyiwa kazi katika utaratibu wakawaida.

Nimeombwa pia mwongozo na Mheshimiwa JosephKasheku Musukuma kuhusu Halmashauri ya Ujiji kupata hatichafu mara nne mfululizo au kwa miaka minne mfululizo, naameelekea kwenye majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziriambaye ameeleza jambo hilo kwamba limefanyiwa utafitiama ukaguzi na inaonesha kwamba hati chafu wotetunafahamu zinatolewa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabuza Serikali. Kwa hiyo maana yake ni jambo lililodhahiri.

Lakini kwenye kuuliza swali kama Serikali ina mpangogani kuhusu kufuta hiyo halmashauri, nadhani Naibu Waziriameeleza vizuri hapo akij ibu swali kwamba waowanaendelea na utaratibu wao na si Bunge linalofutahalmashauri ni Serikali. Kwa hiyo, Serikali inaendelea nautaratibu wake ikiwa ni hiyo halmashauri haitabadilika ikipata

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

chafu mara tano mfululizo. Kwa hiyo, tunataka kuaminikwamba, kwa kuwa hilo jambo limezungumzwa hapa ndaniwanaohusika katika kuingilia michakato ya manunuzi hukoKigoma kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri,tunaamini kwamba watajirekebisha na watafanya mamboyatakuwa mazuri kuliko kusubiri mpaka wafutwe na Serikalikama ambavyo wametoa majibu hapa.

Kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge kwa yoteyaliyokuwa wamesimama Waheshimiwa Wabunge majibuyake ni hayo, lingine tunasubiri Serikali imalize mchakato wakelakini pia hilo la Ujiji limeshatolewa majibu hapa kwa hiyotutaendelea na ratiba yetu.

Katibu!

NDG. LAWRANCE MAKIGI – KATIBU MEZANI:

KAMATI YA MIPANGO

NAIBU SPIKA: Kamati ya Mipango!

MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae. WaheshimiwaWajumbe wa Kamati tutaendelea na uchangiaji kamatulivyoanza jana na kwa mujibu wa utaratibu wetu wakikanuni nimeletewa majina hapa ya wachangiaji kutokavyama wawakilishi Bungeni. Tutaanza na Mheshimiwa SalimTurky atafuatiwa na Mheshimiwa Sophia Mwakagenda,Mheshimiwa Victor Kilasile Mwambalaswa ajiandae.

MHE. SALIM HASSAN TURKY: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Sina budi kumshukuru Mwenyezi MunguSubhana wa Taallah kwa kutujalia sisi tulioko humu wazimawa afya. Nachukua fursa hii kumpongeza sana Waziri wetuwa Mipango kwa kweli mpango aliouleta ni mzuri sana namadhubuti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuendelea na safarihii pia nataka nimpongeze sana Mwenyekiti wetu wa Chamacha Mapinduzi ambaye ndiyo Rais wa nchi hii, Mheshimiwa

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayotufanyia yakutaka kuhakikisha kwamba Tanzania tunaingia katikauchumi wa kati. Sitaki kutafuna maneno, wakati MheshimiwaRais anaingia madarakani na alipotoa matamko yake yalekwa kweli nilipigwa na butwaa nikasema hivi kweli mambohaya yanawezekana kwa kipindi hiki kifupi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ameweza kuthibitisha namimi nachukua fursa hii kumpigia salute kabisa kwamba, kwakweli anatupeleka kwenye maendeleo makubwa sana japonjia ni ngumu lakini dalili njema zimeshaanza kuonekana.Katika hilo wakati akiwa kama Waziri alikuwa akipiga kelelesana hapa kutaka madaraja yale ya ubungo pamoja naairport lakini nashukuru alipoingia madarakani tu alihakikishadaraja lile la pale njia ya airport TAZARA linasimama laMfugale mara moja na limesimama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli kwa sisi ambaotunatoka Zanzibar kuja Dar es Salaam na Dar es SalaamZanzibar, kwa kweli njia sasa hivi imekuwa ni ya muda mfupisana. Kwa hiyo, hizi nia ambazo amezipanga, MwenyeziMungu azibariki na amjalie afya njema. Kwa walewanaomtakia mabaya Mwenyezi Mungu amwepushe nayo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na-declare interest kwambani mfanyabiashara pamoja na viwanda, kwa hiyo, madaambazo nitaongelea ni hizo na nitaanza na viwanda. Juzimoja tulirushiwa clip nzuri sana ya viwanda kutoka Ethiopia.Kwa kweli ukitaka kujifundisha jambo lolote, tushindane kwamazuri. Katika Afrika yetu hii, Ethiopia ndiyo inaonekanakwamba ni nchi moja iliyojizatiti kweli kweli kutokana naumasikini na kuendelea mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, walichokifanya wao kamaSerikali, wametafuta wawekezaji wakaingia nao ubia,wakajenga eneo kubwa sana la viwanda. Wamejenga eneohilo na kuwakaribisha wawekezaji. Kwa hiyo, mwekezajianapokuja nchini, hahangaiki tena kwenda kutafutamaeneo ya kuwekeza, kuanza kutafuta umeme na maji. Hayo

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

yote yamepitwa na wakati katika dunia hii tunayokwendanayo. Kwa hiyo, inatakiwa katika eneo hilo sasa hivi Serikalina labda Mheshimiwa Waziri wa Fedha akija katika mipangoyake atueleze kwamba amejipanga vipi? Kwa sababu eneohilo linafanya kazi vizuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hata katikakurejesha pesa kwake kwa mradi ule, wao watazame zaidikwamba ile miradi inapokuja nchini, wananchi wetu wapateajira. Kwa mfano tu leo, Tanzania tuko nyuma sana katikaviwanda vya nguo. Tuna pamba ambapo leo MheshimiwaWaziri ametoa tamko hapa nimemsikia kwamba pambainayotakiwa kwa viwanda vyetu ni nyingi kuliko tunayozalisha.Kwa hiyo, tayari zile kelele za watu wa maziwa kule kupigakelele hilo jambo naona limeshapata ufumbuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, i l i tutoke hapa,tunafanyaje? Nakumbuka Mheshimiwa Waziri Mwijagealipokuwa hapa alisema kwamba anataka kila mtu aweanazalisha na kushona nguo. Vita vikubwa vya kushona nguoTanzania ni kuruhusu mtumba. Mitumba inadumaza viwandavya nguo. Kama hatutajipanga vizuri, naamini kwamba kunanguo ambazo tunanunua China zinauzwa rahisi sana. Je,zikishonwa na pamba yetu wenyewe hapa Tanzania bilakusafirishwa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kuna haja yamakusudi kujipanga kuhakikisha kwamba hilo eneo laviwanda linasimamiwa kwa nguvu zote na ile kodi ikawekwandogo sana ili wananchi waweze kunufaika na ajira namapato ya Serikali yatakuwa makubwa sana kwa kupitiahuduma mbalimbali katika eneo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, mwanzowa kipindi hiki cha tano tulikuwa tunasimama hapa Bungenina kupiga kelele, nami wakati ule nilikuwa niko katika Kamatiya Viwanda na Biashara, tulifanya ziara bandarini natukasema kwamba sasa hivi watu wote wamekimbia bandariyetu kutokana na tozo zilizopangwa kwa wakati ule; mamboya VAT na nini yaliyowekwa pale.

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana ziara ile ilizaamatunda; Waziri na Serikali ambayo ni sikivu walionaupungufu wakajirekebisha. Sasa hivi naweza kusemakwamba Bandari ya Dar es Salaam imechangamka mia kwamia. Nampongeza sana Mkurugenzi Mtendaji wa TPA kwakazi kubwa anayofanya pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli mwaka ule wakwanza watu waliyachukua magari yale ya kusafirishamakontena wakapeleka nchi jirani. Hivi ninavyoongea naBunge hili, kuna upungufu mkubwa sana wa magari yakusafirisha container katika Bandari yetu ya Dar es Salaam,kwamba biashara imekubali Bandari ya Dar es Salaam.Naipongeza sana Serikali yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili biashara hiyo iwe nzurizaidi, Serikali imejipanga kwa kujenga bandari kavumbalimbali. Serikali hiyo hiyo ilitoa tamko kwamba zile ICDza watu binafsi zote ambazo ziko katika mji wetu wa Dar esSalaam zihame ziende katika umbali wa kilometa 35 nje yaDar es Salaam ili kuondoa msongamano wa magari. Hilo nijambo jema sana ambalo limepangwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta binafsi iko tayarikujenga ICD mbalimbali nje ya Dar es Salaam. Serikaliinapanga bandari kavu sehemu mbalimbali, ni jambo jemasana, lakini naomba sana TPA, hao watu wanaotaka kujengaICD nje ya Dar es Salaam, walipoenda kuwaomba kwambawaweke wakaambiwa kwamba tutawapa ruhusa ya miakamiwili, baada ya hapo, kama Serikali ikiwa imeshajipanga,basi itakuwa wamefeli wao. Hilo jambo limewatisha privatesector.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ajili hiyo, naiomba sanaSerikali yangu itazame uwezekano kwa sababu sasa hivitunachoongelea hapa kwamba Bandari ya Dar es Salaaminazidi kujengwa na ninaamini muda siyo mrefu nchi jirani zotemizigo yao itakuwa ikipitishiwa hapa na hasa reli itakapoanza.Kwa hiyo, makontena yatakuwa ni mengi mno. Nafikiri Serikalihaina haja ya kuwa na hofu na private sector, hawa ni

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

partners wetu, twende nao sambamba watatusaidia kamawanavyotusaidia sasa hivi. Sasa hivi mizigo tena imejaa katikaICD za private kwa sababu mzigo umeshakuwa mwingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, bora Serikali ikatoatamko kuhakikisha kwamba tunapanga mipango mizuri yakwenda pamoja. Tusitanguliane private na GovernmentSector ni partners, tutembee pamoja tutashinda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi natokea Zanzibar nasiku zote napendelea sana Zanzibar na Bara tuwe ndugu wakupendana na kushirikiana na tusiwe washindni. I latunapoingia katika uchumi, tunaona kuna ushindani mkubwasana. Ushindani gani?

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Turky, muda wakoumekwisha. Kengele ya pili imeshagonga. Ahsante sana.(Makofi)

Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, atafuatiwa naMheshimiwa Victor Kilasile Mwambalaswa na MheshimiwaProf. Norman Sigalla ajiandae.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niwezekuchangia Mpango huu wa Maendeleo katika Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2018, nilisimamahapa na nikaongea na Mheshimiwa Waziri Dkt. Mpangokumwambia kwamba mipango tunayoipanga kama Taifana Bunge likaridhia na tukapitisha, ni vyema Serikali ikasikiayale ambayo tumeyashauri na kuyatendea kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ina zaidi ya asilimia70 ya wananchi ambao ni wakulima. Cha kushangaza, bajetiiliyopita tulipata shilingi bilioni 100 iende kwenye kilimo ili iwezekusaidia shughuli mbalimbali ikiwemo utafiti, shughuli za kilimo

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

na mambo mbalimbali ya Wizara husika. Napenda kusikitikakwamba imetoka shilingi bilioni mbili peke yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumzia kilimo niuti wa mgongo, kwa sababu najua kauli hii haijatenguliwatoka tumepata uhuru wa Taifa hili; leo hii ambapo wakulimani wengi huko vijijini na hususan wanawake tunaowawakilisha,kama hujapeleka pesa unakuwa hujawatendea haki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili ufanikiwe katika viwanda,tunasema kwamba sasa hivi tunaenda kwenye viwanda vyakati kama Taifa. Usipowekeza kwenye kilimo, ambapo kilimondiyo kinatoa malighafi kwa viwanda hivi, unakuwa badounafanya siasa kwenye mambo ya makini ya Taifa hili.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika asilimia 100 ya bajetiambayo Bunge lako Tukufu lilipitisha, asilimia 98 ya gawio lafedha Mheshimiwa Dkt. Mpango haikupelekwa. Ninaombatunapopanga vitu na Bunge lako likaridhia, Serikali na Wizaraiweze kuachia fedha kwa ajili ya watu hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maafisa Ugani ni wachache.Kwa mfano, nikichukua tu kwenye Wilaya ya Rungwe,wasimamizi wa kilimo wako wachache, hawawezi kufikiawakulima wote. Tuna Chuo cha Uyole Mbeya; Chuo kilekinasaidia utafiti. Huwezi kuwa na kilimo kisichokuwa na Utafiti.Tunataka kujua ni ng’ombe gani bora wenye mbegu borakwa ajili ya kilimo? Utawezaje kujua pasipo utafiti?

Mheshimiwa Mwenyekiti, chuo kile takribani miakamitatu sasa hakijapelekewa fedha za maendeleo, unawezajekuwasaidia wasomi hawa ambao wanasimamia raslimali zaTaifa na ni washauri wa kundi kubwa la wakulima? Hawanafedha. Naomba Wizara yako Mheshimiwa Dkt. Mpangoiliangalie suala hili kwa umakini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumzia pembejeo.Tumekuwa na kilio kikubwa sana juu ya pembejeo. Leo hiikuna mbegu za aina mbalimbali na nyingine hazioti,

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

wakulima wanalalamika. Tumesema Maafisa Ugani ambaowangetusaidia, leo hii ajira ya kuwaleta na kutuongozea kulevijijini hawapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tujipange nabahati mbaya sana tumebaki na mwaka mmoja kama siyomiezi sita i l i tuweze kumaliza mipango tuliyokuwatumejiwekea. Naomba tafadhali tusimame kwa yaletunayoyasema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii tunapozungumziambolea, kuna sehemu nyingi sana; sehemu za Mbarali nasehemu nyingine mbalimbali ambazo mimi nawakilisha,mbolea inaenda kwa kuchelewa. Wakati mwingineMawakala mnaowapa wamekuwa hawawatendei hakiwakulima jinsi ambavyo ilipaswa wafanye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niache hapo, niendekwenye suala la elimu. Taifa lolote likitaka kukandamiza watuwake linaweka elimu kuwa ni ya hali ya chini. Usipowekezakwenye elimu, umeandaa jeshi la watu wajinga ambaowatakuwa rahisi sana kupotea. Elimu kwa bajeti yamaendeleo iliyopita tuliweka shilingi bilioni 249. Sasamnasema elimu bure, elimu isiyokuwa na malipo. Ni kweliukitamka shilingi bilioni 200 kwa mwananchi wa kawaidaanaona ni fedha nyingi, lakini ukienda kwa Mwalimu wa Shuleya Sekondari kwa mfano, anakwambia amepewa shilingi200,000/= Capitation. Shilingi 200,000/= anunue chaki, alipemlinzi na vitu kama hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri tunahitaji kuwekezazaidi. Tunaposema bure, nafikiri bora turudishe kamatulivyokuwa mwanzo, kwa sababu wananchi walijitoleawakatusaidia, watoto wote walikula chakula cha mchana.Ukisema bure, kuna wazazi wengine wamegomba kutoamichango kwa sababu Serikali imesema elimu ni bure.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni nyumba za walimu.Hiki ni kilio kikubwa sana. Walimu wengi wamepanga,wanakaa mbali na maeneo ya shule. Mishahara

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

haijaongezeka. Mheshimiwa Waziri, hebu tuwatazamewalimu, maabara na vitu kama hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matundu ya vyoo ni tatizohususani kwa watoto wa kike. Nazungumzia suala la bajeti.Tunapopitisha pesa, mashirika mengi, Wizara nyingi zinapatarobo ya mapato inayostahili kupata. Sasa inakuwa kama vile;aidha mtuambie Serikali haina hela, lakini Serikali ya Awamuya Tano inasema ina hela nyingi. Sasa bajeti ya shilingi bilioni100, unapata shilingi bilioni mbili. Tunaomba maelekezo yakina, kwa nini Bunge linapitisha halafu fedha inayotokainakuwa kidogo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni deni la Taifa.Mwaka 2018 nilizungumza juu ya deni la Taifa. Tumevuka sasazaidi ya shilingi trilioni 50. Naomba, na nilisema mwaka 2018pia, tusikope pesa. Tulete sheria humu Bungeni Serikali isikopempaka Bunge liwe limeridhia. Hii tabia ya kukopa pesa hatujuitunalipaje, deni la Taifa limekuwa kubwa na mnasema ni denihimilivu na mna lugha zetu za kisomi, lakini mwisho wa sikuwanaolipa madeni haya ni watoto ambao leo hawajazaliwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua Mheshimiwa Dkt.Mpango ni msomi, naomba asimamie hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni mifugo na uvuviambayo ndiyo imeajiri sekta ya watu wengi. Kwenye uvuvitulitoa shilingi bilioni nne ya maendeleo, tunarudi pale palekwamba ni asilimia tatu ya fedha ndiyo iliyotoka. Tuna maziwamakubwa; Ziwa Nyasa, Ziwa Victori na Ziwa Tanganyika,kama Taifa tusipojipanga juu ya kutumia maziwa haya kuletamaendeleo kwa vijana wetu, nafikiri tutakuwatunajidanganya. Unafanyaje maendeleo pasipokuwawezesha?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna maendeleo bilademokrasia. Ndugu zangu wameongea habari yademokrasia. Leo hii tunapanga mipango lakini kwa njia yafigisu mmewaengua watendaji ambao ndio waleta

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

maendeleo. Mnaendeleaje? Tukae chini kama Taifa, tuacheuwoga, tufaanye kazi kama team. Leo hii mmeumiza watuwengi nafsi zao na kujiandikisha wameona ni kitu chakupoteza muda. Tunaomba demokrasia ichukue nafasi yake.Wengine wameumizwa na wengine wako ndani. Hivi ni watugani wajinga wasioona? Kwa sababu mwisho wa siku, watuwanaishi na watu kule chini. Mmetupa watu ambao sisihatujawachagua, tunapangaje maendeleo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, demokrasia ni tunda la haki.Pasipo haki, amani haiwepo. Naomba tusimame na hilo,tuwasimamie Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya,naunga mkono Kambi Rasmi ya Upinzani. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Mpango nilitarajiahapo ungepiga meza, hoja yako imeungwa mkono naMheshimiwa Sophia Mwakagenda.

Waheshimiwa Wabunge, hoja huwa ni moja tu ndiyoambayo inajadiliwa hapa. Hayo mengine ni maoni, kwa hiyohuwezi kuunga mkono maoni.

Mheshimiwa Victor Kilasile Mwambalaswa,Mheshimiwa Profesa Norman Sigalla, atafuatiwa naMheshimiwa Balozi Adadi Rajab.

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili naminichangie kwenye hoja il iyopo mbele yetu ambayoimewasil ishwa na Mheshimiwa Waziri wa Fedha.Nampongeza sana, amewasilisha vizuri sana utekelezaji waMpango wa mwaka 2018/2019 na Mapendekezo ya 2021.Hongera sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kwenye uso wadunia wanadamu tuko zaidi ya bilioni saba; na kadri miakainavyosogea kwenda mbele, wanadamu tutazidikuongezeka sana. Wanafalsafa wanasema, vitu ambavyo

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

vitakuwa adimu sana miaka ijayo kwa kuanzia ni viwili; majina chakula. Kwa hiyo, wanaendelea Wanafalsafawanasema, mtu anayetaka kuwa tajiri miaka 20 ijayo, aingiekwenye kilimo leo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naipongeza sanaSerikali kwa kuweka kipaumbele kwenye uchumi waviwanda. Naipongeza sana. Naomba kwa kuwa Tanzaniatuna ardhi kubwa sana na nzuri sana, tuna mito na mabonde,naomba tuupe kipaumbele sana uchumi wa viwandakwenye kilimo. Tuige mfano wa kile kiwanda cha sukariambacho kitajengwa hapo Morogoro. Tuige, tuwe na uchumiwa viwanda kupitia kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna vyuo vya kilimo vingisana. Tuna Chuo Kikuu cha Kilimo SUA ambacho kinawataalam wabobezi wengi sana ambao wanaheshimikaAfrika na dunia nzima. Afrika ya Kusini wanawapenda sanawataalam wanaostaafu kutoka hapa SUA. Naomba Serikaliiwatumie wataalam hawa. Tuwachukue, tuwafungie ndani,watupe Blueprint ya namna gani tutatumia ardhi yetu hiituweze kupata mazao ya kilimo na kuweka viwanda vyakuchakata mazao yetu. Naiomba sana Wizara ya Kilimo,Wizara ya Uwekezaji, Wizara ya Viwanda, Wizara ya Fedhatuwatumie sana hawa wataalam wetu wa Chuo Kikuu chaSUA waweze kutupa Blueprint ya namna ya kutumia ardhina maji yetu tuliyonayo tuweze kujikomboa kwa viwandakuanzia kwenye kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwenyezi Mungu tenaametupa neema ya bandari. Naipongeza sana Serikali, sasahivi Serikali inaboresha Bandari ya Dar es Salaam, Mtwara naTanga. Bandari zetu hizi zinahudumia nchi karibu nane autisa za Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Zambia, Zimbabwe,Malawi na zinginezo. Kwa hiyo, naomba uboreshaji huutunaokwenda nao ulenge kushindana na bandari zingineambazo ziko kwenye ukanda wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, umeona nchi jirani hapa juziimeona Bandari ya Dar es Salaam inaboreshwa na mizigo

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

mingi inapitia Bandari ya Dar es Salaam wakapunguza ushurukwenye mafuta ili tuweze kushindana. Kwa hiyo, naombauboreshaji huu wa bandari uendane na kujipanga sawasawakwa kushindana na nchi ambazo tuanshindana nazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niliona mwaka au miakamiwili iliyopita Bandari ya Dar es Salaam TPA waliweka ofisiyake kwenye nchi jirani ya Congo, jambo zuri sana. Hiiinasaidia kufanya marketing ya shughuli zetu. Naomba hiiiendelee kwa nchi nyingine zote ambazo tunazihudumiakibandari, tuweke ofisi zetu kule ili tuweze kuwahudumia,tuweze kushindana na wenzetu ambao tunashindana katikaeneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona vilevile kwenyempango, Serikali inaendeleza ujenzi wa reli ya kati (StandardGauge), inaendeleza kuboresha reli iliyopo ya meter gaugena vilevile ina mpango wa kuanza kujenga Standard Gaugeya kutoka Dar es Salaam kwenda Mtwara na kutoka Tangakwenda Arusha mpaka Musoma, ni jambo zuri sana hilo. HiiStandard Gauge ya reli ya kati mwisho wa mwaka huuitakamilika kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro nainaanza Morogoro kuja Makutupora na itaendelea hukompaka Tabora – Mwanza – Kigoma. Wenzetu nchi jirani yaRwanda imeingia kwenye bandwagon hii, imeamua nayokutafuta njia za kujenga kutoka Kigali kuja mpaka Isaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali sasa tui-entice Burundi nayo iingie kwenye mpango huu ili na waowajenge kutoka Msongati kuja mpaka Uvinza halafu wajengekutoka Msongati – Uvira kwenye nchi ya Congo. Hii reli yaSGR ili ilete faida kubwa kwa nchi yetu inahitaji kusafirishamizigo zaidi ya tani milioni 20 kwa mwaka. Sasa tusipoitumianchi ya Congo, itakuwa ni hasara. Kwa hiyo, naomba Serikalituwa-engage Burundi nao waweze kutafuta fedha wajengekutoka Msongati mpaka Uvinza na kutoka Msongati kwendaUvira katika nchi ya Congo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuboresha hiiSGR na meter gauge, ipo hii reli ya TAZARA ambayo yenyewe

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

ni cape gauge. Naomba ili tuweze kuitumia vizuri bandariyetu tuiboreshe reli hii ya TAZARA na katika kuiboresha hiiinahitaji tu kuiwekea umeme ili treni ziende kwa kasi. Naombatuiboreshe reli hii na vilevile Serikali iwe na mpango wakujenga Bandari Kavu pale Inyara ambapo tumekuwatunaiongelea mara kwa mara. Bandari kavu ikiwepo Inyaraunaweza kujenga reli ya mchepuko kutoka pale Inyaraikaenda mpaka Lake Nyasa tukatumia vizuri meli ambazoSerikali imezinunua kusafirisha mizigo kutoka Bandari ya Dares Salaam kwenda Malawi na Msumbiji. Kwa hiyo, naombareli ya TAZARA na yenyewe iwemo katika mpango huu wakutumia reli zetu na uchumi wetu wa jiografia kuweza kujileteamaendeleo hapa Tanzania na kuwahudumia jirani zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yangu yalikuwa hayomachache, naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa ProfesaNorman Sigalla atafuatiwa na Mheshimiwa Balozi AdadiRajabu, Mheshimiwa Dkt. Diodorus Kamala ajiandae.

MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwakumpongeza Waziri pamoja na Naibu Waziri kwa Mpangomzuri waliouleta. Hawa ni rafiki zangu na wameleta Mpangomzuri sana, nawapongeza sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, nampongezasana Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi kubwana nzuri ambayo imemfanya apate sifa Afrika na dunia nzimaya kuekeleza na kusimamia mipango ya maendeleo yetuwenyewe kwa fedha zetu wenyewe. Mipango ya ujenzi wabandari, viwanja vya ndege, maji Mtwara na mipango mingimizuri inayofanywa na Rais wetu, inampa sifa na heshimiaduniani kote. Mungu ambariki sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie kidogo maeneomachache. Unapoongelea kukuza Pato la Taifa ni vizuri

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

kuangalia katika sura mbili. Sura ya kwanza ni ile inayomgusamtu mwenyewe mmoja mmoja, fedha inayomgusa mtummoja mmoja. Kwa hiyo, naomba sana kwenye eneo hili,benki zetu hizi za kilimo kama Tanzania Investment Banktuweke riba ndogo sana kwa wakopaji wanaomaanishakwenda kuwekeza kwenye kilimo angalau asilimia 10 lakinisio 17 au 19, haifai kwa sababu ni kilimo. Kwa hiyo, naombasana wawekezaji wa kilimo wanapokwenda kukopa TanzaniaInvestment Bank wakope kwa asilimia angalau 10. Tukifanyahivyo basi tutaona maparachichi yakipandwa kwa wingi kulekwetu Makete, Rungwe na kila sehemu yatapandwakwa wingi kwa sababu ukopaji utakuwa umerahisishwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni dhahabuyetu. Kwa sisi wachimbaji wadogo wa dhahabu ni vizuri sanaGeological Survey Institute inayoongozwa na Profesa Mrumaikapewa fedha kwenda kufanya explosion test ili tuwe nauokaji wa dhahabu tunayoijua kiwango chake. GeologicalSurvey Institute inayongozwa na Profesa Mruma ipewe fedhaili kwenda kufanya kazi hizo za kuhakiki kiwango cha dhahabukilichopo kwenye ardhi kwa kila mchimbaji wa dhahbumdogo mdogo. Tukifanya hivyo, tutasaidia wananchi waliowengi kupata dhahabu yao na fedha zao kwa wingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni upande waelimu. Kwa mfano, shule za msingi Makete ni wastani wawalimu watatu kila shule sasa wanafunzi hao watasomaje?Naomba sana Wizara ipeleke walimu wa sekondari kwamshahara wa sekondari wakafundishe shule za msingi, walewaliomaliza wapelekwe shule za msingi kwa mshahara wasekondari. Wanachotaka wao ni fedha (mshahara),wapelekwe kwa mshahara wa sekondari lakini wafundisheshule za msingi. Shule za msingi orientation yake ni ndogo,figisu figisu na michanganuo ya kusema kwamba ufanye hivi,ufanye hivi, wanapewa elimu ya mwezi mmoja,wanahamasika halafu tunajenga shule zetu vizuri kwa sababusasa hivi ni tatizo kubwa sana kwa shule za msingi za elimuwilayani Makete. Walimu watatu ndiyo wastani wa walimukwa shule zangu, hali ni mbaya sana.

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo, nihitimishekwa kusema kwamba kama mipango yote hii tukiifanya,upande wa elimu tukawapeleka walimu wengi katika shuleza msingi, upande wa kilimo tukawapa wakulima mikopo yaasilimia ndogo, asilimia 10 kwa mfano, Upande wa dhahabutukapeleka fedha Geological Survey kwa Profesa Mrumaakaweza kuhakika kiwango cha dhahabu kila sehemu basitutakuwa tumesaidia kukuza uchumi wa nchi hii. Nafahamukwamba Geological Survey team walikuwa wameshapewafedha kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, sasa hivi hazipo lakiniwalikuwa wameshapewa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwishonizungumzie kuhusu ujenzi wa reli. Ujenzi wa reli ni jambomuhimu sana lakini naomba sana, reli ninayoikazia hapa niya Uvinza - Msongati, kwa sababu Msongati kuna chuma tanizaidi ya 3,000,000. Watazamaji wote wa reli hii wanafikiriakwamba ile reli itakuwa inameza chuma kile kwa kusombachuma kile ili tonnage yetu iwe ya maana. Tonnageinayopelekwa Mwanza na Bakhresa ambaye ndiye mpelekajimkubwa, akipeleka mara moja tu Uganda tonnage yakeyote itakuwa imeisha, meli imeenda mara moja inakuwaimeisha lakini tonnage ambayo ni ya uhakika ni ya Msongatikwa sababu pale pana chuma na tayari tunao mkatabawalioingia Mawaziri waliopita wa Burundi na Tanzania wa jinsiya kushirikiana na DRC-Congo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mungu awabariki sana,ahsante sana, naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Balozi AdadiRajab, atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt. Diodurus Kamala,Mheshimiwa Masoud Abdallah Salim ajiandae.

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru sana kupata nafasi hii ya kuchangiaMpango huu wa Taifa ambao ni muhimu sana. Kabla sijaanzanapenda kutoa pole kwa wananchi wa Muheza kwamafuriko ambayo wameyapata pamoja na Mkoa mzima wa

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

Tanga na kuwahakikishia kwamba Serikali inashughulikiamatatizo yao na athari zote ili kurudi kwenye hali ya kawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana WaziriDkt. Mpango kwa kutuletea Mpango mzuri na ambao hataukiuona unaona kweli uko kwenye mwelekeo mzuri. Mimisitakwenda kwenye takwimu ambapo naona tunakwendavizuri kwenye ukuzaji wa uchumi ambao kwa sasa tukokwenye asilimia 7.2 na tunategemea 2020/2021 tufikie asilimia10 na hata mfumuko wa bei uko vizuri tu kwenye asilimia 3.Kwa hiyo, nitajikita kwenye miradi ambayo imeanza nainaendelea kutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kil imolimezungumzwa kwa bidii sana na wachangiaji wengi lakinina mimi napenda kuongeza kwamba tunategemea kwenyeMpango huu ambao utakuja basi suala hili lipewe umuhimuwa kipekee. Tunaamini kabisa kwamba kilimo ambachoWatanzania wengi wanafanya na kinatoa ajira karibu asilimia65 tunategemea kwamba kitatuinua. Ni suala la kuwekamipango vizuri kuhakikisha kwamba suala la umwagiliajilinapewa kipaumbele, suala la uanzishwaji wa mabwawalinapewa kipaumbele na naamini kabisa kwamba tukiwekafedha nyingi kwenye kilimo basi tutaweza kuendelea kwaharaka sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pamoja na mambohayo, kuna masuala mengine ambayo yako kwenye kilimokwa mfano suala la chai. Nimefarijika sana hapa nilipomsikiaNaibu Waziri asubuhi akisema kwamba wana mpango wakuanzisha mnada hapa nchini na kuondokana na suala lamnada wa Mombasa. Suala hilo sisi Muheza limetuathiri sanakwa sababu kampuni kubwa ambayo inalima chai paleinapeleka chai yake kwenye mnada Mombasa na Mombasawananunua na wanafanya packaging na kurudisha tenakuuza hapa hapa nchini. Suala hili kiuchumi kwakwelilinatuathiri sana na ni vizuri liangaliwe kwa uhakika na umakinikabisa ili tuanzishe mnada wetu hapa tuondokane nakupeleka haya mambo Mombasa. Vivyo hivyo ni vizuri piakuangalia mazao mengine na kuanzisha hasa mazao ya

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

viungo na mazao ya machungwa ili tuweze kuwa na beielekezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Kitengo cha TMXambacho Kamati ya Bajeti ilitembelea, kitengo hiki ni kizurisana ambapo kikitumika vizuri basi Serikali inaweza ikawa namazao mengi elekezi kwa bidhaa nyingi sana. Naombakabisa Mheshimiwa Waziri Kitengo hiki kitumike ipasavyo.Tulikwenda pale lakini tumeona kwamba kitengo hikihakitumiki kama inavyopaswa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile limeongelewa sualala uvuvi, Bandari ya Uvuvi ni muhimu sana. Bandari hiiilianzishwa kwenye bajeti iliyopita na ilitengewa fedha,nakumbuka mwaka 2017 kuna fedha ambazo zilitengwalakini haijapewa umuhimu wake. Tunaamini kabisa kwambatukifungua Bandari ya Uvuvi basi tutakuwa tumefika mbalisana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la PPPambalo nimekuwa nikiliongelea kila mara na naamini kabisajuhudi ambazo zinafanywa na Serikali sasa hivi, miradi hiimikubwa yote, SGR, ndege, umeme kwenye Bwawa laNyerere naamini kabisa haya yangeoana na PPP sasa hivihapa Tanzania tungekuwa tuna-boom. Kwa hiyo, naaminikabisa kwamba tumepitisha sheria hapa mwaka jana lakinimpaka sasa hivi hatujaona utekelezaji wake. MheshimiwaWaziri tumekuwa tukisisitiza na naomba kusisitiza kwambatangaza hiyo miradi ambayo tumeichagua. Tuliiona hapamiradi kumi ambayo bajeti iliyopita mlitusomea, tafadhaliitangazwe ili watu wajitokeze na kama hawatajitokeza tuonetuna tatizo gani lakini ni suala ambalo linatakiwa lipeweumuhimu mkubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ATCL tumepita,nashukuru ndege zimefika lakini cha msingi hapa nikuhakikisha kwamba tunaboresha na tunaanzisha routenyingi zenye tija ili kuweza kuleta watalii na wawekezaji hpanchi kwetu. Tunataka Airport ya Dar es Salaam iwe hub,tuhakikishe kwamba hii Terminal III ambayo ipo inatumika

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

kikamilifu. Sasa Terminal III bado ndege ziko chache lakinitunaamini kabisa kwamba wanaohusika watafanya juhudikuweza kushughulikia na kuhakikisha kwamba Airport yetuinakuwa changamfu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la bandari ni muhimusana. Uboreshaji wa bandari umekuwa mzuri, Bandari ya Dares Salaam inaboreshwa vizuri, vilevile ya Tanga na Mtwara.Nimefarijika sana kwamba sasa hivi Bandari ya Tangainachimbwa ili kuweza kupata kina kikubwa na naaminibaada ya kazi hiyo kukamilika basi meli kubwa zitaweza kutuapale badala ya kwenda kutua Mombasa ambapo ilikuwazinatua kule na baadaye zinaweza kuletwa hapa nchini. Kwahiyo, suala hili ni la kupongezwa na tunaomba kabisamuendelee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa bajetinilizungumzia kiwanda kimoja kikubwa sana ambachokinatarajiwa kujengwa na Wachina kule Tanga Hengia.Kiwanda hiki cha saruji tunategemea kitakuwa kikubwa nakuleta ajira kati ya 4,000 mpaka 8,000. Kiwanda hikitunategemea kitoe tani karibu milioni saba kwa mwaka lakininilipopita mara ya mwisho Tanga sioni chochote ambachokinafanyika naambiwa tu mazungumzo bado yanaendeleakuweza kuwaruhusu Wachina hawa waweze kuweka hikikiwanda. Kiwanda hiki ni kikubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapopata wawekezajikama hawa inabidi na sisi tuchangamke wasijewakatupokonya. Kwa hiyo, naamini kabisa wakati wawinding up na nashukuru Waziri wa Uwekezaji yupo hapawatupe msimamo kiwanda hiki kimefikia wapi. HawaWachina wanazunguka karibu miaka miwili hapa na vibalimara hiki mara kile, mara incentives sasa tunaomba tupateuhakika nini kinaendelea. Huyu ni mwekezaji mkubwa natunaamini kwamba atakapoweka kiwanda kile basi mamboyatakuwa vizuri sana siyo kwa nchi hii tu bali hata kwa Mkoawa Tanga mambo yata-boom.

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo natakakulizungumzia, la mwisho ni suala la Soko la Hisa pale Dar esSalaam (Dar es Salaan Stock Exchange) tulifika pale lakinisoko hili limeonekana limeduwaa kidogo haliko very activena tunaona haliko very active kwa sababu watu wengihawajaliorodhesha, nataka Mheshimiwa Waziri ahakikishekwamba Sheria i l ishapitisha mashirika yote haya yacommunication kwamba wajiandikishe kwenye soko la hisa,lakini mpaka sasa hivi ni Vodacom tu ambao wamejiandisha,sasa haya mashirika mengine ya simu kwa ninihayajajiandikisha? Nataka Waziri akija hapa aeleze ili tuwezekujua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ni kwamba Soko la Hisala Dar es Salam lilikuwa linachangamshwa sana na hayamashirika ya kijamii. Sasa baada ya kuunganisha hayamashirika ya kijamii, tangu uunganisho huo umefanyika, shirikahili letu la sasa hivi halijajiandika tena pale wala halijapelekakununua hisa wala kuuza hisa. Tunaomba shirika hili ambalolimejumuisha mashirika yote ya kijamii basi lijiandikishe ili liwezekufanya lile soko la hisa liweze kuwa very active, baada yakusema hayo nakushukuru sana na naunga mkono mpangohuu. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Dkt. DiodorusKamala atafuatiwa na Mheshimiwa Masoud Abdallah Salim,Mheshimiwa Andrew John Chenge ajiandae.

MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana. Kwanza naomba nianze kwakusema kwamba naunga mkono hoja iliyo mbele yetu.Naunga mkono hoja kwa sababu mbalimbali na nitazitajachache. Hoja iliyo mbele yetu imeeleza vizuri katikaparagraph ya kwanza kwamba tunatarajia kuandaaMpango wa Maendeleo wa Tatu wa Miaka Mitano kwasababu sasa tunamalizia huu tunaoutekeleza kwa sasa. Sasakilichonivutia zaidi kuunga mkono hoja hii ni kwamba dhimainayotarajiwa katika mpango wa tatu utakaoandaliwaambao inabidi sasa katika mapendekezo tunayoyapitishaleo tuanze sasa kuweka mambo ya msingi yatakayotusaidia

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

kuwa na mpango mzuri wa miaka mitano mingine; na dhimahiyo inasema kama ilivyobainishwa katika paragraph yakwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuongeza mauzo nje nauwezo wa ushindani Kikanda na Kimataifa. Hili ni jambo jemana dhima hiyo itatusaidia kwa sababu tunapokamilisha huumpango wa miaka mitano ambao tulijielekeza katika kujengaTanzania ya viwanda, sasa tukielekea sasa kuongezampango wa tatu ukijikita kwenye kuongeza mauzo nje nauwezo wa ushindani Kikanda na Kimataifa itakuwa ni jambojema. Kuna mambo ya msingi ambayo itabidi yawepokwenye mpango wetu wa mapendekezo sijayaona naningependa Mheshimiwa Waziri baadaye angalie ni jinsi ganianaweza akachukua mapendekezo hayonitakayoyapendekeza kuwa sehemu ya mpango wetututakaoupokea na kuupitisha katika Bunge hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ambaloni muhimu sana kama tukitaka kujenga, kuongeza uwezo wamauzo ya nje na kujenga ushindani lazima tuanze kwakujenga ushindani wa ndani. Kwa nini ushindani wa ndani nimuhimu? Ni muhimu kwa sababu huwezi ukauza nje, huweziukajenga uwezo wa ushindani kama hujajenga uwezomkubwa wa ushindani wa ndani, nitatumia mfano mmojatu, mfano wa wine, uzalishaji wa wine; ukiangalia Sekta yaWine kidunia kwa mfano ukiangalia Italy wao wanazalishachupa za wine bilioni sita. Tanzania ukichukua kwa makadirioya juu kabisa tunazalisha chupa za wine laki mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ukiwa unazalishachupa za wine laki mbili, ukitaka kujenga uwezo wa ushindanikwamba tuwezeshe sasa wine yetu iweze kushindana hatandani ya Afrika Mashariki, basi lazima tuanze kujengaushindani wa ndani kwanza. Sasa kujenga ushindani wandani wa wine peke yake ukiangalia kwa mfano winetulizonazo hapa Dodoma ukiangalia chupa sitataja aina yawine na kampuni kwa sababu unaweza ukajikuta labdakampuni ukiitaja kwamba haifanyi vizuri inaweza isijisikie vizuri,kwa hiyo sitataja.

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, ukiangalia hizichupa utakuta kuna nyingine ina lebo ambayo ni water proofhapa hapa Dodoma, lakini utakuta wine nyingine ina leboambayo mvua ikinyesha hiyo lebo inaloana hapo hapo. Sasanamna hiyo, ukiangalia Sekta ya Wine tu kwa hapa Dodomani kwamba, ukisema unataka kusaidia wine iweze kushindanamaana yake uangalie je unawezeshaje hii Sekta ya Wine kwamfano, kuwawezesha kupata lebo ambazo zinawezazikajenga ushindani, lakini kwa kuanzia lazima ujengeushindani wa ndani wakishindana ndani ndiyo unawezaukapata mtu wa kuweza kushindani nje kwenda kwenye sokola nje. Kwa hiyo huo ni mfano mmoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mfano mwinginemdogo, kuhusu soko la kahawa la ndani na soko la pambala ndani, lazima tujenge ushindani wa ndani, kwa mfano,kwenye kahawa ushindani wa ndani maana yake ni nini?Lazima tuangalie katika mpango huu tunaokuja naotuangalie nini tunaweza tukafanya kujenga ushindani wandani wa ununuzi wa mazao yetu, kushindana ndani. Kwamfano, mkulima wa kahawa yeye anapenda akiuza kahawayake apate fedha yake pale pale. Natambua kuna hii dhanakwamba hela itapitia kwenye akaunti, watu wafungueakaunti, lakini mkulima anaangalia, yeye kama anazalishakilo 10 au 20, unapomwambia utalipwa kupitia benkianakushangaa kwa sababu anaona gharama ya kufuatiliahiyo hela ni kubwa kuliko kile ambacho atakuwa anakifuatilia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo kuna uwezekanowa kuweka mazingira ya ushindani ndani. Kwa hiyo ili tufanyehivyo mkulima huyu angependa awezeshwe aweze kuzalishakwa tija, akiweza kuzalisha kwa tija utaweza kujengaushindani. Kwa hiyo, ushauri wangu ni kwamba katikamapendekezo haya sijaona vizuri inavyoweka mazingira yakujenga ushindani wa ndani kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambaloningependa nilizungumzie kwa haraka haraka ili kujengaushindani tunahitaji mkulima kumwezesha kwa mfano, kupataviuatilifu. Mheshimiwa Waziri anafahamu kwamba Wizara

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

yake walitenga bilioni kumi nafahamu, lakini baada yakutenga bilioni kumi LC ikafunguliwa pale BOT, Kampuni yaTFC ikapewa jukumu la kuagiza hiyo viuatilifu. Viuatilifu hivyompaka ninavyozungumza hivi sasa viko pale bandarini, bilionikumi zimetoka lakini viuatilifu mpaka sasa hivi vinaozeabandarini na bilioni kumi zimetumika. Sasa mambo ya namnahiyo hayajengi ushindani, kwa nini? Kwa sababu hivyoviuatilifu vikitoka bandarini vimekuja havijatoka bandarinimaana yake tunaendelea kumkwamishwa mkulima na hilosiyo lengo letu. Kwa hiyo Mheshimiwa labda atapokuwaanatoa ufafanuzi nitaomba atueleze hizo bilioni kumi alizotoana mpaka sasa hivyo viuatilifu viko pale bandarini vimelalapale ni jitihada zipi ambazo amezichukua za makusudi, fedhaalitoa lakini viuatilifu vinaozea pale bandarini mambo yanamna hiyo hayatusaidii kujenga ushindani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ningependakuzungumzia kwa ufupi kwenye kujenga ushindani kuhusukilimo. Natambua pale tuna Mkulazi one na Mkulazi two, lakiniukisoma kwenye mapitio ya utekelezaji kwenye vitabualivyotupa Mheshimiwa Waziri, ukisoma pale huoni kamakuna kitu kinachoendelea kwenye Mkulazi one na Mkulazitwo kuhusu uzalishaji wa miwa. Ukisoma pale unaambiwaekari 3,500 zimelimwa na ekari 750 zimepandwa. Sasaunajiuliza kama umelima 3,500 umepanda 750 maana baadaya miezi sita na zile ulizolima zitakuwa zimeshaharibika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi unapolima miwahalafu kiwanda hakijajengwa wala mitambo haijaja, baadaya miezi 12 miwa iko tayari kiwanda hakipo, maana yakehiyo miwa huwezi kuitumia tena. Ningeshauri kwa kweliMheshimiwa Waziri umefika wakati Serikali ikajiondoa masualaya kujenga viwanda badala yake iachie Private Sector. HapaTanzania tuna viwanda ambavyo vinafanya vizuri sana katikasukari sitaki kutaja ni kipi, lakini ni vizuri tungeiachia PrivateSector ikafanya hivyo na hii Mifuko ya Hifadhi tuiachieiendelee na shughuli zake za mambo ya hifadhi, kwa sababukwa kuendelea kuiambia Mifuko ya Hifadhi ifanye shughuliza uzalishaji wa miwa tunajenga mazingira ambayo hayanatija.

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaposema tunajengaTanzania ya viwanda lazima tuweke mazingira mazuri yakuwa na mikopo ya uhakika, natambua tunayo TIB lakiniukiiangalia unakuta kwamba hii Tanzania Investment Bankuwezo wake ni mdogo, lakini tunayo mabenki mengi hukoya nje ya nchi ambayo yako tayari kuja Tanzania kuwekeza.Nadhani katika Mpango huu wa Maendeleo ujao tungewekavivutio vya kuwezesha kuvutia investment banks kuja hapaTanzania kuwekeza na kwa kufanya hivyo tutasaidia kuwekamazingira mazuri ya kuendelea kujenga Tanzania ya viwandana pia kujipanga vizuri katika kutekeleza ule mpango wa tatututakaouandaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia katika taarifatuliyopewa ya utekelezaji wa mpango wa maendeleouliopita, utaona kwamba tulitenga bilioni 123.9 kwa ajili yakilimo, lakini zilizotoka ni bilioni 56.5 ambazo ni sawasawa naasilimia 45.46. Pamoja na kutenga fedha kidogo na tukatoakidogo, lakini kilimo ndicho kimechangia kwa asilimia kubwakwenye pato la Taifa, kimechangia asilimia 28.6. Hii maanayake ni nini? Maana yake ni kwamba tukitenga fedha nyingizaidi kwenye kilimo tunaweza tukapata matokeo makubwazaidi na uchumi wa nchi unaweza ukanufaika zaidi, hiyo ndiyomaana yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama hivyo ndivyoil ivyo, nimejaribu kusoma kwenye mapendekezo yaMwongozo, sioni popote ambapo mapendekezoyametolewa moja kwa moja kuagiza sekta mbalimbali,kuagiza Idara mbalimbali, kuagiza halmashauri zetu ilikutenga fedha za kutosha kuelekea kwenye kilimo, sioniikijitokeza moja kwa moja. Kwa hiyo katika mpango wetulingekuwa ni jambo jema kama jambo hilo lingeangaliwa nalikajitokeza moja kwa moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine ambayoningependa niongelee kabla muda wangu haujakwisha,tunayo East Africa Master Railway Network natambuakwamba tunazungumza hii SGR tunaendelea kuijenga nijambo jema, natambua kwamba itatoka Isaka itaenda Kigari,

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

lakini ningeshauri ikifika maeneo ya Runzewe au Biharamuloi-branch pale ielekee Kagera, ikifika Kagera ielekee Kampala,ikifika Kampala ielekee South Sudan. Tukifanya hivyotutakuwa tumejenga uchumi nzuri kwa nchi yetu, piatutawezesha hata Mkoa wa Kagera kuuandaa kushiriki katikauchumi shindani na kuongeza mauzo yetu ya nje ya nchi natufikie hata viwanda vyetu mbalimbali vilivyo katika Mkoawa Kagera viweze kuibuka na kufanya vizuri zaidi...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa, muda wakoumekwisha. Mheshimiwa Masoud Abdallah Salim, atafuatiwana Mheshimiwa Andrew John Chenge, Mheshimiwa DavidErnest Silinde, ajiandae.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: MheshimiwaMwenyekiti, awali ya yote nimshukuru Mwenyezi MunguSubhanahu Wataala aliyetujalia uzima na afya njema yakuweza kuchangia mapendekezo ya mpango huu tulionaoleo mbele yetu. Nianze na mwenendo wa viashiria vyaumaskini kama ambavyo wenyewe waliotuletea Madaktariwetu mabingwa kama hivi vifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, walituambia kwamba,mapato na matumizi ya Kaya binafsi yamepungua naumaskini umepungua kutoka asilimia 9.7 hadi asilimia 8.0kutoka mwaka 2011 – 2017. Kwa hivyo umaskini unaelekeaumepungua kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, najiuliza umaskinihuu uliopungua ni kwa kiasi gani wameangalia Watanzaniahawa wanakula milo mingapi, mwaka 2011 walikuwawanakula milo mingapi, 2012, 2013, 2014, 2015, 2016 na 2017kama wanatembea kweli vij i j ini na kama wataalamhawawadanganyi umaskini hata kipindi hicho haujapunguana haujapungua kwa sababu bei za bidhaa zimekuwazikipanda. Mwaka 2011 debe la mahindi lilikuwa Sh.5,000mpaka 6,000; debe la mahindi mwaka 2017 lilikuwa Sh.12,000,sasa debe la mahindi limefika Sh.18,000 na kuendelea,wanasema umaskini umepungua.

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukija kwenye unga wasembe wenyewe, mwaka 2011 bei yake ilikuwa ni ndogokwenye Sh.700, 800 hadi 1,000 leo 2019 bei ya unga wa sembeni aibu imefika hivi sasa hadi Sh.1,500, umasikini umepungua!Jamani wataalam wetu madaktari hebu tuambieni ukweli,waliowaambia maneno haya, utaalam huu ni akina nanihata mtuambie hivi maana sisi wengine si Madaktari kamanyie, ni watu wa kawaida tu, ni Walimu tu wa shule zasekondari, lakini tunataka watuambie kupungua kwaumaskini huu na kupanda kwa bei; sukari, 2011 kama kwelikutoka asilimia 9.7 hadi asilimia 8.0 bei ya sukari mwaka 2011,2012, 2013 na sasa waangalie 2017 sikuambii hivi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, wanasemakwamba mfumuko wa bei kwanza kutoka Januari 2019 hadiSeptemba 2019 umetoka kwenye asilimia 2.3 hadi asilimia3.2, wao wenyewe wamekiri kama kuna mfumuko wa bei,si jui madaktari wetu wanatuambia nini ningeombaniwashauri; kwamba bado hali ya umaskini nchini kwetuunaongezeka, wanaokula milo mitatu sasa wamepungua,kunakuwa na pasi ndefu, sasa wanasema ni pasi ndefu,wanakunywa tu chai mchana wakitoka hapo usiku kidogo,basi wanalala. Hiyo ndiyo hali halisi ilivyo, tembeeni vijijinimuone hiyo ndiyo hali ya umaskini ulivyo msidanganywe nawataalam wanaoleta kwenye makaratasi, twende kwenyeuhalisia mtembee vijijini muone shughuli, ni kizaa zaa, mwakahuu!

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamezungumza kwenyeumaskini ule mwingine wa kipato, kwamba nao umaskini wakipato umepungua hapa ni sawa na utaalam wao, lakinihasa waangalie hasa na hali ya umaskini inavyoongezekakwenye Jiji la biashara tuje Dar es Salaam ambapo ndiyolinaitwa Jiji la biashara, ukienda pale Kariakoo madukayamefungwa, mpango huu hauna jibu, hauna jibu, hautoitija yoyote kuonesha mkakati gani ambapo wataboreshamaisha ya wafanyabiashara katika Jiji la biashara la Dar esSalam, maduka pale Kariakoo yamefungwa, mpango huuhauoneshi jambo lolote, hakuna mpango hakuna mpangilio.Watuambie wana mpango gani au wana mpangilio gani

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

wa kufufua Jiji la kibiashara la Dar es Salam. Shughuli ipo kweli!Watuambie madaktari wetu sisi ni wadogo sana kwao, waowamesoma zaidi sisi ndiyo hivyo tena, watuambie madaktarihawasomeki, hawaeleweki waliowandikia sijui ni akina nani,shauri yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, kwenyeukurasa huu wa 43 wamezungumza habari ya utawala bora.Hasa utawala bora umo kwenye Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, kuna Tume ya Haki za Binadamuna Utawala Bora, Ibara ya 29 na 30 yaani majukumu yake.Sasa wamezungumzia moja kwenye utawala bora, mkakatiwa Serikali kuhamia Dodoma, kwani utawala bora ni hilo tu?Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema ukienda kwenyeIbara ya 3(1) inazungumzia Tanzania ni nchi ya kidemokrasiayenye kufuata mfumo wa vyama vingi na ni nchi ya kijamaa.Ibara ya 5(1) inazungumzia haki ya kupiga kura yaanikuchagua na kuchaguliwa hawajagusa kitu hawa Madaktari,kule kwetu wanasema tawileni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hali ya kawaida,katika hili la kupiga kura kuchagua na kuchaguliwa,tunaelekea kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa demokrasiaimeminywa, demokrasia imepuuzwa, leo ni malalamiko kilakona, vyombo vya habari kila kona ndani na nje ya nchikwamba hali ya demokrasia Tanzania imeminywa,wagombea wote wa Upinzani wameondolewa, matatizoyamekuwa ni makubwa na kwangu mimi kama mdau waulinzi na usalama ambaye napenda amani na utulivu wakweli naona hicho ni kiashiria kibaya cha ulinzi na usalamalazima niseme kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani watu kufanyamadudu yao waliyoyafanya ukaondoa wagombea waUpinzani kwenye demokrasia ya mfumo wa vyama vingi, ikondani ya Katiba, leo ukasema na sisi tunataka amani nautulivu. Jamani, Madaktari Serikali nzima inisikie, MheshimiwaJafo kasema kwamba watu waendelee kupeleka pingamizihapa na pale, imeelezwa na Mheshimiwa Mbunge mmojahapa, kwamba hao wanaopelekewa wamekimbia hawapo.

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

Huu ni mfumo wa vyama vingi, kama hamtaki mfumo wavyama vingi, futeni vyama vingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu najiuliza mamboambayo kila siku ninyi mko kwenye redio masaa 24,mmefanya hiki, mmefanya hiki, anakuja Polepole anasema,mko peke yenu siku saba tu ambazo ni kampeni, waacheniwatu wachague na kuchaguliwa, raha ya kushinda nikushindana, msiende peke yenu muone mambo mengimliyokwishafanya mnatutangazia wananchi watapima, lakinitunakwenda kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, ni aibuna fedheha kubwa ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe Serikali MheshimiwaJafo katoa tamko lake lakini pamoja na hayo hebu jamaniangalieni hili, warudisheni hawa wagombea nchi hii twendekwenye amani na utulivu wa kweli lakini kilio kila kona hawani binadamu. Kumbe viashiria hivi vinavyofanywa najiuliza je,Serikali ya kijiji ndio inataka amani itoweke? Ni Serikali zakwenye kata au za kwenye wilaya au kuna baraza ganinajiuliza mimi mwenyewe binafsi kwa sababu unapowanyimafursa watu kuchagua na kuchaguliwa hili ni tatizo ni kiashiriakibaya kwenye amani na utulivu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe MheshimiwaWaziri wanaohusika na vyombo vya ulinzi na usalamawaliomo ndani na nje ya humu ndani niwaombe sana sualahili si la kulifumbia macho ni lazima wahakikishe kwambawatoe tamko la wagombea hawa wa upinzani kurejeshakugombea, nchi hii twenda vizuri tuko katika mfumo wavyama vingi. Ama kama sikio la kufa halisikii dawa shauri yenumimi nishasema na kwa sababu lugha yangu hii naizungumzamnaifahamu vizuri ni Kiswahili cha kawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hayanirudie tena kwa sababu mimi binafsi ni mdau mkubwa waulinzi na usalama, ukataka usitake huwezi kuzungumzamasuala ya ulinzi na usalama humu ndani Bungeni usimtajeMasoud. Kwa hiyo, lazima niseme kwamba dawa mfumo wa

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

vyama vingi tuangalie viashiria ambavyo vinaweza kuletatatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie mzungumzaji hukuniko peke yangu dakika zangu mlizonipa hizo nimeongea nawenzangu kwamba niendelee na shughuli, nashukuru hayasawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie mpango huu piahautojibu hamna chochote mtazungumzia habari ya jibu lamilioni 50 kila kijiji umaskini utapungua wapi. Serikali iliahidikwamba mtatoa bilioni 50 kwa kila kijiji hamna kitu, mpangohauna jibu lolote kama kweli mnataka kukuza uchumi nakupunguza umaskini mpango hauna jibu lolote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mnaposema milioni 50kwa kila kijiji mwaka wanne huu si mngetuacha tu tukaendakwenye vijiji tukawaambia wananchi hiyo ndio hali kumbemnaogopa kweli mfumo wa vyama vingi, shughuli ipo mwakahuu, hakuna jibu milioni 50 kila kijiji imekufa hivi hivi waziwazi.Madaktari mngekuja mtuambie milioni 50 kila kijiji uko wapimpango bado mnao? Mpango huu hauonyeshi mkakati wakuboresha maendeleo ya wafanyakazi, mishahara yawafanyakazi annual increment nyongeza hata ya kila mwakanayo ni tatizo shaghalabagala mwaka! Mtuambie madaktarinini mmekusudia mnataka kuipeleka wapi Tanzania? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uzuri bahari kuu humuhakuna mpangilio maalum deep sea fishing ambao dunianikote tuna bahari ya kutosha, deep sea fishing humu mtuelezeukubwa wake mna maelezo kidogo tu. Uvuvi wa bahari kuuuko wapi watu wanakuja hapa na meli zao wanachukuasamaki wanakwenda kuuza, sisi katika hali kama hiyotuangalie mkakati wa kuboresha uvuvi wa bahari kuu, lakiniMheshimiwa Mpango huu haoneshi madaktari mtuambie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie na suala zima lakilimo mmegusia sehemu ndogo ya uhitaji wa masoko lakinikatika mwaka uliopita wakulima wa mbaazi waliathirika sanahadi leo wakulima wa mbaazi wana wasiwasi kupata soko

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

la uhakika kwa sababu walikuwa wanalalamika wakauza kiloya mbaazi shilingi 200 mpaka 300 mtuambie mkakati waSerikali wa kuboresha soko la uhakika la wakulima wa mbaaziuko wapi, mpango unaonesha mtuambie na hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Wazirianaangalia kwelikweli kumekucha kweli katika mkakati huumimi nafikiri mtupe majibu mazuri. Kwa sisi wengine mwezihuu unaitwa mwezi wa mfungo sita mwezi ambao MtumeMuhammad Sallallahu alayhi wa sallam tupo wataratibuwapole tukimaliza hii tena uko mbele lakini tunataka Serikaliitoe majibu sahihi ituambie mkakati madhubuti na endelevuwa kuboresha masoko ya uhakika ya mazao ya kulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hayo machachekwa sababu nilibamizwa na mambo mengine hapa nisemehayo yanatosha lakini nisisitize suala zima la utawala boralifanyiwe kazi isiwe bora utawala. Kama tunataka utawalabora twende kwenye utawala bora kama unataka borautawala endeleeni kwa sababu mna nguvu. Narudia tenakusema kama kuna utawala bora kama mlivyoandikaukurasa 43 twendeni kwenye utawala bora tuwe na chaguziya mfumo wa vyama vingi watu wachague wachaguliwe,kama mnataka bora utawala endeleeni kwa sababu mnanguvu. Lakini hii ina athari kubwa utawala bora nyie mnatakabora utawala, tatizo ni nini kuna hofu ya nini nyie ni watuwazima humu ndani katika Bunge hili upande huu wa upinzanihuu mimi ndio mtu mzima wao na ukiona mtu mzima analiakuna jambo. Kama mnataka kusikia sikieni kama hamsikiishauri yenu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, asanteni sana nashukuru(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Waheshimiwa Wabungetukumbuke tu kwamba huu mpango ni sehemu ya ulempango wa miaka mitano ambao Bunge hili lilishaupitishalikajadili wakatoa mawazo. Kwa hiyo, ni vizuri tujikite pale ilitusifikiri kwamba huu mpango kwa namna yoyote ileunaweza kutoka kwenye kile ambacho Bunge tulishasema

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

kule nyuma. Kwa hiyo, ni vizuri tuwe nayo yote miwili tuwetunatazama ni mambo gani yameshakwisha na yepi tunaonakwamba ni muhimu yaendelee kuwepo humo ndio kazi yetu.

Waheshimiwa Wabunge nilikuwa nimeshamtajaMheshimiwa Andrew John Chenge atafatiwa na MheshimiwaDavid Ernest Silinde, Mheshimiwa Dkt. Lemomo Kiruswaajiandae

MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekitinikushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii niweze kuchangiakidogo kuhusiana na mapendekezo ya mpango wamaendeleo ya Taifa kwa mwaka 2020/2021 ambao ndioutakuwa umefika ukomo wa kipindi cha miaka mitano kwahuu mpango wa pili ambao tumeanza kuutekeleza tangu2016/2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sanaMheshimiwa Waziri wa Fedha na timu yake kwa kutuleteamapendekezo haya na wewe umesema sasa hivi vizuri sanahuu ni mwendelezo katika utekelezaji wa mpango wa pili wamaendeleo ya Taifa ambao tumeingia sasa huu mwaka wanne. Ni kweli lazima tu-take stock na ndio maana Serikaliinakuja hapa na mapendekezo haya. Sisi kama wadau kamasehemu ya uongozi wa Taifa hili ambao tumeaminiwa nawatanzania wema katika nyumba yao hii tuweze kuonanamna ya kuboresha, kuishauri Serikali ndio kazi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwashukuru sanaWaheshimiwa Wabunge waliotangulia katika kuchangiatuisaidie Serikali maana nikilalamika nikishamaliza kulalamikakwani itakuwa imesaidia? Saidia kuonyesha njia, miminadhani tukienda hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza sana Serikali yaAwamu ya Tano kwa haya makubwa inayoyafanya sasaunaweza usione muunganiko wa moja kwa moja kwamaendeleo ya mwananchi mmoja mmoja kwa Bwawa laNyerere la kufua umeme. SGR inayojengwa hata ndege hizizinazonunuliwa lakini nawaambieni miradi hii itakapokamilika

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

suala tunalosema la tija, ufanisi kwenye viwanda vyetu,umeme ndio kichocheo kikubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia reli hii ambayonitaisemea sasa hivi reli ya kati ndio kiini ni injini ya ukuaji wauchumi wa mataifa yote na ndege hizi utalii watanzaniaMwenyezi Mungu ametujalia kitu ambacho lazima tuendeleekukinufaika, tunufaike nacho sasa na kesho na kesho kutwa.Pesa hiyo ndio inayoenda kusaidia kuboresha huduma zajamii kama afya, maji yote haya ambayo tunayaongelea kwafaida ya watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sitaki kuchukua mudamwingi kwa hilo lakini sisi kazi yetu tuishauri Serikali katikamaeneo ambayo tunadhani tunaweza tukafanya vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na hili la kilimo,limesemwa vizuri sana kwenye taarifa ya waziri aliyowasilisha;niseme pia ni Mjumbe wa Kamati ya Bajeti tumeyasema sanalakini nashukuru taarifa ya Kamati ya Bajeti. WaheshimiwaWabunge isomeni lakini tumeongea sana na Serikali kwenyekamati kusaidia haya mawazo na sisi tunabaliana na wengimnaosema kwenye kilimo, kwenye uvuvi, kwenye mifugohuko tukiweza kuboresha hayo maana ndio sekta ambazoukinyanyua hizo ndio zinaunganisha na zinachochea ukuajiwa sekta nyingine ifanywe vizuri kwenye kilimo nasema kilimocha Tanzania kama tutafanikiwa kikuwe kwa kasi asilimia sitana tukawa persisted kwa kipindi kirefu miaka 10, 20 utaonamchango wake kwa Pato la Taifa tulikuwa kubwa sana nandio itabeba wananchi wengi kuwaondoa katika lindi laumasikini, mipango ndio hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimia naomba sana katikavipaumbele vya mwaka kesho tuweke intervention kubwatupeleke kwenye kilimo pia kwenye mifugo, kwenye uvuviionekane kwenye bajeti yetu kwenye sekta hizo kupitiampango huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naelewa Serikali maanatunamaliza mpango huu wa pili mwakani ndio tutakuwa

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

Bunge litakuwa karibu linakaribia kuvunjwa lakini Tanania ipoitaendelea kuwepo wananchi wa Tanzania watakuwepo naSerikali itaendelea kuwepo na Bunge la Tanzania litaendeleakuwepo, kwa hiyo watakaorejea tunataka tuje tuoneangalau ifanyike tathimini ya kipindi tuone mpango wa piliwa miaka mitano ambao tulikuwa tumemaliza kuutekelezakipindi hicho tunapoenda kwenye mpango wa tatu wamaendeleo ya Taifa letu tuone ni nini ambacho tumefanikiwasana, nini maeneo gani hatukufanikiwa sana, nini kifanyike ilitunapoenda kwenye mpango huo wa tatu na wa mwishotuwe kweli confidence.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza sana Serikalihata katika hatua hii kwa sababu kupanga mwalimu alikuwaanatukumbusha kupanga ni kuchagua tungekuwa narasilimali nyingi ambayo unaweza kutekeleza yote haya kwawakati mmoja tungeweza kufanya hivyo lakini hatuna lazimakile kidogo ambacho tumekubaliana kukifanya tukifanye kwaufanisi na ndio maana mimi nasema naelewa baadhi yetutungependa tuone mambo tunasema haya ni mengi mnotuliyoyabeba, lakini utafanyaje Tanzania hii nchi ni kubwatuna wananchi milioni karibu 53,000,000 lazima uende hivyounaumia hapa kidogo lakini huko mbele wengine panaendavizri, ukifanya stock nzima unasema Tanzania inasonga mbele.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa reli concernyangu iko kwenye taarifa ya bajeti kama ripoti ya taarifa yabajeti Kamati ya Bajeti tunafanya vizuri tumetumia pesa yandani jasho la Watanzania kutoka Dar es Salaam mpakaMorogoro heshima kubwa kwa nchi hii heshima ehee!Tujivunie wananchi pesa ya ndani tumekopa kutokaMorogoro kuja Makutupora ndio lakini ni mkopo wetu waWatanzania. Na tunajiandaa sasa tutafute pesa nyinginekutoka Makutupora kwenda Tabora, kwenda Isaka, kwendaMwanza na baadae kwenda Tabora, kwenda Kigoma,Uvinza Msongati tutatoka Kaliuwa, Mpanda tuende mpakaKalema, ndio mipango yetu hii kalema kwenye LakeTanganyika tuna mipango tunaiona Tanzania na majirani.(Makofi)

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nini concern yetu nandio imo kwenye taarifa ni kwamba tunachukua mikopo hiibahati mbaya ni ya muda mfupi, masharti yake ingependezakama tungeshambulia reli hii, ujenzi wa reli hii kwa wakatimmoja kwa sababu tunajua pesa hizi kwa kupata mkopowa muda mrefu itakuwa ni ngumu sana lakini tukiwezavipande hivi tukavishambulia kwa wakati mmoja tutakuwatumekamilisha ujenzi wa reli hii na matawi yake muhimuharaka sana na ndio tutaona faida, ndio ushauri wetu huokwa Serikali. Naelewa misaada imepungua sana, mikopo yamasharti nafuu imepungua sana, eneo ambalo tunawezatukapiga hodi na nadhani tumekaa vizuri ni kwenye exportcredits iwe ni ya Waingereza ya Wafaransa ya Wajerumaniangalau ukipata mkopo ule mpaka miaka 21 window hiyoipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri naiombaSerikali tuangalie option hizo tutafanya vizuri na kwenye relinasema reli hii tuikamilishe naomba sana Serikali reli hii yaKati tuikamilishe na ningependa sana ndoto aliyonayoMheshimiwa Rais Dkt. Magufuli aikamilishe reli hii wakati wauongozi wake heshima kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho tuna miradimikubwa kwanza nipongeze kazi nzuri ya Dar es SalaamBandari Port Gati moja mpaka namba 7 ile kazi inaenda vizuri,tunapanua lango pale kuingilia kazi nzuri. Mtwara inaendavizuri sana is the natural Port Mtwara is the deep sea Portehee nashukuru sana Magati yale yanaongezeka. Tanga yasasa na sawa tunawekeza kwenda toka mita depth ya mita4 kwenda 15 lakini Mwambani ndio yenyewe TangaMwambani ndio kwenyewe eehe tuangalie huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini narudia kama kwaBagamoyo tumeona muwekezaji huyo hafai haimaanishikwamba mradi wa Bandari ya Bagamoyo haufai hapana,tutafute muwekezaji mwingine ambaye ataendana namatakwa yetu ili bandari ya Bagamoyo ijengwe ndiomatumaini ya Taifa hili Dar es Salaam pamoja na maboreshoyanayoendelea hatutaweza kupata meli zile kubwa za tani

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

kuanzia 50,600 yale yanaitwa ports kwanama yale hayawezikuingia kwenye lango la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho naomba Liganga naMchuchuma tukamilishe mazungumzo kama imeshindikanana muwekezaji huyo tutafute mwingine lakini hii taarifa hiikila mwaka tunarudi nayo mpaka tunataka kumaliza miakamitano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua muda wangu ndiohuo lakini mimi naipongeza sana Serikali Mheshimiwa Waziriwa Fedha na timu yako hongereni sana tuwaunge mkononajua changamoto ni mapato tuwasaidie ni maeneo yapitunadhani tunaweza tukaongeza to argument mapato yaSerikali ya ndani hasa mapato ya ndani ya kodi ya siyo yakodi mnaona tangu tuanze matumizi ya ufanisi wa electroniki,mapato yanaongezeka ya kodi lakini pia na yasiyo ya kodi.Nadhani likisimamiwa vizuri tutaweza kupanda kutokakwenye trilioni 1.2 ambao tumegota kidogo sasa na tukawezakuongeza mapato yetu. Tuangalie maeneo mengineameyasema vizuri Mheshimiwa Masoud eeh! Bahari ya Hinditutumie, blue economy ya Tanzania hiyo hiyo tuichukue vizuritufanye mambo makubwa, inawezekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, umenipa heshimaumenivumilia mchango wangu ni huo tuhimize tufanyemaamuzi ya haraka katika maeneo ya vipaumbele ambayotumejiwekea sisi wenyewe nakushukuru sana ubarikiwe sana.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Masoudalikuwa anasikiliza kwa makini sana kwa hiyo, nikaona ngojaumalize Mheshimiwa Chenge. Mheshimiwa David ErnestSilinde tutamalizia na Mheshimiwa Dkt. Lemomo Kiluswa.

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana ambaye ndio Mwenyekiti wetu wa kikao kwasiku ya leo, kunipa fursa kujadili mapendekezo ya mpangowa maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2020/2021.

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikiliza michango mingina mingi ni mizuri. Kwa sababu mpango wetu huu ni wamwisho, mimi nitajielekeza kwenye Kitabu cha Mpango waTaifa wa Miaka Mitano ambacho Bunge lako Tukufu lilipitishana miradi ambayo mpaka sasa haijatekelezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka wa 2016 tulipokuwatunajadili kitabu hiki kuna miradi ya kielelezo ambayo sisi kamaTaifa tulipanga itekelezwe. Katika miradi ya kielelezo, ipoambayo tumefanikiwa kwa kiwango fulani na ipo ambayotumeiondoa kabisa na Serikali inashindwa kuleta majibu yamsingi kulieleza Bunge lako Tukufu kwa nini tumeshindwakuitekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi Na.1, ukisoma ukurasawa 83, miradi ya kielelezo inayohusiana na Kanda zaMaendeleo, kuna ujenzi wa Bandari Mpya ya Bagamoyo,amezungumza Mheshimiwa Mtemi Chenge hapa. Nikwamba bandari hii, lile eneo lote lilikuwa lina uwezo wakuongeza ajira zile zisizo rasmi na kufikia 100,000. Sasa hebufikiria leo katika nchi ambayo wananchi wanalalamikahakuna ajira, hii bandari ambayo ilipaswa iwe tayariimetekelezwa, tangu mpango wa pili tumeanza kuuandika,mpaka leo hakuna majibu ya kutosha, Serikali inashindwakutueleza ni kwa nini jambo hili linashindwa kutekelezeka?

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu ni uanzishajiwa Kituo cha Biashara na Huduma Kurasini. Hii ipo kwenyeMpango ukurasa huo huo wa 83(e). Jambo hili mpaka leohalipo popote na Serikali imelipa fidia lile eneo, limekaa palehalina kazi yoyote. Maana yake tulipitisha Mpango ambaotumeshindwa kuutekeleza na leo Serikali haijatoa majibu.Mradi huu vilevile ulikuwa unaongeza ajira ambazo zinafikiawalau zile zisizo za moja kwa moja pale, zaidi ya 100,000zingeweza kupatikana kwa mradi huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uanzishwaji wa Mji wa KilimoMkulazi. Tuliandika kwenye Mpango huu wa Miaka Mitanona mpaka leo tunakwenda kwenye mpango wetu wamwisho, huwezi kuona Serikali inakuja kutoa maelezo, huo

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

mradi wetu wa ujenzi wa Mji wa Kilimo wa Mkulazi mpakasasa tumefikia wapi na matokeo yake ni nini kulingana nampango tulivyoupitisha?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi mwingine tulioupitishakwenye Mpango ambao mpaka sasa hivi haujatekelezwa niuanzishaji wa viwanda vya vipuri na kuunda magari. Hii ipokwenye kitabu hiki cha Mpango wetu ukurasa wa 84. Mpakaleo huo mradi haujatekelezwa, hakuna viwanda vya vipurivya kutengeneza magari hapa ambavyo vimeanzishwa;wala viwanda vya kuunda magari ambayo tulikuwatunahitaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ya uchimbaji wamakaa ya mawe ya Liganga na Mchuchuma, hii imekuwastory. Mimi tangu nasoma sekondari miaka ya 1990 mpakanimeingia Bungeni, sasa nafanana na akina MheshimiwaMkuchika sasa hivi, bado story ni ile ile ya Liganga naMchuchuma. Mheshimiwa Mtemi Chenge amezungumza,tunashindwa kuingia mikataba ambayo inaeleweka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliweka malengo sisi kamaTaifa letu; malengo na viashiria kwa ajili ya utulivu wa kufanyabiashara katika Taifa letu. Kwa mfano, mwaka 2015/2016urahisi wa kufanya biashara Tanzania ilikuwa katika nafasiya 139 kati ya nchi 189 na malengo tuliyoweka katika mpangotulisema inapofika mwaka 2020/2021 tuwe katika nafasi ya100. Yapo kwenye vitabu hivi, lakini unapozungumzia leo, nchiyetu iko nafasi ya 144. Lengo lilikuwa nafasi ya 100, lakinimpaka sasa tuko wa 144 kati ya nchi 190. Ni malengotuliyojiwekea ambayo mpaka leo katika huu Mpangohayajateklezwa. Sasa unaweza…

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (UWEKEZAJI):Taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Silinde kuna Taarifa.

Mheshimiwa Angella Kairuki.

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

T A A R I F A

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (UWEKEZAJI):Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo anapotosha. Ukiangaliakwenye nafasi ambayo Tanzania kwa sasa tumeishikilia kwaripoti iliyotoka mwezi wa Kumi, tumetoka nafasi ya 144kwenda nafasi ya 141. Nami nilitarajia angeweza kupongezakwa sababu, ukiangalia siyo nchi nyingi ambazo zimewezakupata mafanikio hayo; na hii ni hatua katika kuelekea katikamaboresho makubwa kwa ajili ya kuweza kuboresha nafasiya Tanzania katika tathmini hii ya Benki ya Dunia. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Silinde, unaipokea Taarifahiyo?

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa hiyo Taarifa. Labda nimweleze tu. Ndiyomaana nimezungumzia Mpango. Mpango wetu tulisematunavyozungumza leo, tuwe nafasi ya 100. Uko nafasi ya 141.Au unataka tukupongeze wakati Mpango huu tumeandikasisi wenyewe? Issue ni malengo. Tumesema mwisho wamwaka utafanya mtihani utapata marks 90, umepata 54,unataka upongezwe. Wewe uko ume-under score. Sijui kamaumenielewa! (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ndiyo upungufu wakutokukubaliana na hali halisi. Mwaka 2010 Tanzania ndiyoilikuwa katika nafasi bora kabisa ambayo yumewahi kufikia.Mwaka 2010 tulikuwa nafasi ya 125 ya urahisi wa kufanyabiashara katika nchi 189. Kwa hiyo, tumerudi nyuma, hatuwezikujipongeza katika vitu ambavyo hatujafanya vizuri sana. Kwahiyo, nasi haya tumeyatoa ili Serikali iweze kuyafanyia kazi,sio ku-counter attack tu kila kitu, hamwezi kufanikiwa katikahicho kitu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenyemapendekezo yangu ya Mpango, nini ambacho Serikali sasainapaswa kukifanya ili kuhakikisha baadhi ya mambowanaweza kuyafanya.

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo namba moja kamaTaifa ambalo tunapaswa sana kuliwekea mkazo ni kutumianafasi yetu ya kijiografia kuhakikisha tunatumia huu ukandawetu, kwa maana sisi kama Tanzania tunazungukwa na nchizaidi ya nane. Hizi nchi ndiyo tunapaswa kuzifanyia biasharakuliko hizi porojo ambazo tumekuwa tukifanya hivi sasa. Hiyondiyo namba moja. Nilitegemea kwenye Mpango, Serikaliingekuja na Mpango huu unaokuja watueleze ni namna ganitutafanya biashara na nchi zote zinazotuzunguka kwakutumia Tanzania kama sehemu ambayo ndiyo itakuwa kituokikuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nilikuwa nasoma ripotiya wiki iliyopita, Kenya peke yake kwa kutumia bandari yaotu wamesema wamepunguza asilimia 50 ya ushuru kwawafanyabiashara wote watakaotumia Bandari ya Mombasa.Hao Kenya, yaani wameshaweka incentives ya kuhakikishawanatunyang’anya hata hizi biashara tunazofanya na nchinyingine. Sasa Serikali na Mheshimiwa Dkt. Mpango hapa,nataka aieleze nchi kwamba nasi tunafanya nini kuvutia hizinchi wanachama zinazotuzunguka kuhakikisha tunapatafaida ya kuwa katika nafasi bora kabisa katika…

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Silinde kuna Taarifa.Mheshimiwa Eng. Isack Kamwelwe.

T A A R I F A

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumpa Taarifamzungumzaji kuhusiana na uwongo ambao umetembeakwamba Bandari ya Mombasa imepunguza ushuru kwaasilimia 50. Jambo hilo halipo, ilikuwa ni uwongo, uchochezitu wa wafanyabiashara. Bei iko pale pale kule Mombasa.Dar es Salaam ndiyo tunaendelea kupunguza bei ili tuwe nameli nyingi na ndiyo maana sasa hivi zinaanza kuingia meli

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

kubwa za mita mpaka 300 zinazobeba ma-container mpaka5,000. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Silinde unaipokea Taarifahiyo?

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Mwenyekiti,bahati nzuri huwa tukizungumza tunapowapa data huwawanaelewa na wanafuatilia na huwa hawayatolei majibumpaka tuwakumbushe humu ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yangu hapa nikuhakikisha tunatumia nafasi, geographical positionadvantage tuliyonayo kuhakikisha tunafanya kuwa incentivesya ku-promote biashara kushirikiana na nchi nyingine. Hiyondiyo hoja yangu kubwa. Hata kama Mheshimiwa Wazirihapa anasema ni speculation, lakini hiyo haiondoi mantikiya kwa nini watu wamepeleka hizo speculations Kenyabadala ya kuzileta hapa Tanzania, kwamba kwa kufanyabiashara hapa Tanzania, maana yake unaweza ukapata hizobenefits na kuondoa hiyo migogoro inayoendelea? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, tuwe wakweli. Nchi yetu kwa sasa bado tunashindwa kuwekeza katikamifumo ya PPP. Hii tumeieleza muda mrefu sana, naminitaieleza kwa kifupi sana. Mheshimiwa Mtemi hapaamejaribu kuzungumzia, lakini sisi nchi yetu tukiruhusu PPPninaamini mambo mengi makubwa yanaweza kufanikiwakuliko tunavyofanya sasa hivi. Nami ninachokitaka hapa, PPPielekezwe kwenye miundombinu na wala siyo kitu kingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi unapoleta sekta binafsiikashirikiana na Serikali, ikajenga barabara kutoka Dar esSalaam mpaka Morogoro, Dar Express Way, muundombinuukakaa pale, ile sifa inakwenda kwa Serikali, haiendi kwenyesekta binafsi kwa kujenga ile barabara. Ukichukua hela hizohizo, kwa mfano reli tumeigawanya maeneo mengi, fedhahizi hizi ukachukua PPP ukajenga reli, faida ya ile reliinakwenda kwa wananchi na wala siyo kwa ile sekta binafsi.

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kifupi sana, ukiangaliawenzetu wa Malaysia walipokuwa wanaanza huu mfumo waPPP, katika phase ya kwanza waliingia mikataba ya hovyoambavyo na wao wenyewe wanakiri, lakini pamoja nakwamba walifanya mikataba ya hovyo wakasema phase yapili walirekebisha phase ya kwanza. Sasa sisi hapa kamauling’atwa na nyoka zamani, unasema sasa hiyo njia sisihatutaki kuelekea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hoja yangu kwaSerikali katika huu Mpango, tujikite kuwekeza kwenye PPPkatika miradi ya miundombinu. Ukijenga reli hapa hakunamwekezaji ataondokanayo, mtu akijenga barabara hapahata akiingia hasara hakuna mtu ataondokanayo, lakini kitupekee ambacho nisingekubaliananacho, PPP isifanyikekwenye masuala ya service only. Yaani kwenye upande wahuduma, nchi ijitegemee yenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kwa sababu sasa hivituna ndege, tunataka tuone sasa katika Mpango wetu hapa,service industry tunaiwekeza kwa kiwango gani katika nchiyetu? Tufanye kama wanavyofanya wenzetu wa Rwandapale, yaani wana Conference Tourism, wana Business Tourism.Sasa hivi dunia nzima iwe ni vikao vya FIFA, iwe ni vikao vyaMabunge ya Afrika, iwe ni vikao vya Mabunge ya Dunia, wotewanakwenda Rwanda kuwekeza kwa sababu wanaona ka-nchi kao ni kadogo, hawana rasilimali za kutosha kwa hiyo,wana-promote watu kwenda Rwanda kufanya mikutano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, shirika lao landege linapata faida, lakini na nchi vilevile inapata mapatokwa sababu, watu wengi wanakwenda pale. Sasa hayondiyo mambo ambayo tulitegemea Mpango wetu uwekeze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kidogo tu cha mwisho,tumenunua Dreamliner mbili ambazo nafikiri ninyi wenyewemmeziona. Tusingependa kuziona zinakaa pale, tunatakatuone kwenye Mpango hapa route za Kimataifa. Routekubwa ziwe zinaainisha kama ambavyo wale wotewanaopanda ndege kwenda Kimataifa ukisoma vile vitabu

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

vyao vinakuonesha destination ambazo wanatarajiakwenda, destination za sasa. Sasa na haya tuyaone hapa iliwalau hizi ndege zisiwe hasara kwa Taifa, badala yake ziletefaida. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Dkt. LemomoKiruswa.

MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ili nami niweze kuchangiakatika hoja iliyoko mbele yetu ya Mpango wa Taifa kwaMwaka wa 2020/2021.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeangalia kwenyeMpango na nimetazama baadhi ya maeneo mahususi kamamaeneo ya vipaumbele na hasa nikavutiwa na mirdimikubwa ya kielelezo, ni mingi, lakini napenda kutaja umemewa maji wa Nyerere National Park, reli ya standard gauge,Shirika la Ndege kuimarishwa, bomba la mafuta, gesi asiliana huu mradi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya mabadilikoya tabianchi ambayo sasa hivi yanasababisha kuweko kwaupungufu mkubwa wa rasilimali ya nishati mbadala kamakuni na uhalisia wa kuhitaji uhifadhi mazingira na haja ya sisikupiga marufuku ukataji wa mkaa hovyo, napenda kuishauriSerikali kwamba, hii miradi miwili mikubwa ya nishati mbadala,gesi asilia pamoja makaa ya mawe ingepewa kipaumbelekikubwa kabisa. Serikali ingefanya kila liwezekanalo hatakama ni kukopa fedha hii miradi itekelezwe kwa kasiWatanzania waanze kubadilika sasa na kutumia gesi kwawingi zaidi na makaa ya mawe ili tuondokane na athari zakuharibu mazingira, kuchangia katika hali mbaya ambayotayari tunayo inayoletwa na mabadiliko ya tabianchi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipengele kinginenilipoangalia ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda,nimeguswa sana kutaka kusemea maeneo mawili; eneo lakilimo cha mazao na mifugo na eneo la wanyamapori. Kwa

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

upande wa kilimo cha mazao, katika karne hii ya 21 tuliyopokwa kweli matamanio yangu ni kuona Tanzania ikiondokanana kutegemea kilimo cha jembe la mkono na jembe lakukokotwa na wanyama. Tuondokane sasa katika hiyosayansi ya karne zilizopita tuwekeze na Serikali ifanye kilaliwezekanalo katika kilimo cha kisasa zaidi kinachotegemeamatrekta na power tillers.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuishauri Serikaliwaanze tena kama zamani nilipokuwa mdogo, kuna wakatimatrekta ya vijiji yalikuwa yanatolewa. Wapeleke matrektavijijini hata wakopeshwe vijiji matrekta na power tillers tuwezeku-phase out kilimo cha jembe la mkono na jembe lakukokotwa na wanyama ili kilimo chetu kiweze kuwa na tijazaidi tuzalishe kwa wingi zaidi. Sambamba na hilo, Serikaliiwekeze kwa kila hali katika kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika sekta ya mifugonimeona kwamba kuna mipango mizuri inayowekwa yakuongeza tija, masoko, uzalishaji, maeneo ya malisho, lakininaomba suala la maji lizingatiwe. Asilimia kubwa ya mifugoambayo ndiyo inabeba uchumi wa wafugaji katika nchi hiini mifugo ya asili ambayo mingi ndiyo ambayo inaiingiziaSerikali mapato kwa mifugo inayouzwa ndani na nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sekta hii ya mifugo,naishauri Serikali kwamba, waangalie katika zile nyanda zamalisho za wafugaji, waweke kabisa nguvu katika kuwekamaji; maji ya mabwawa, visima virefu, sambamba nakuhakikisha masoko yetu ambayo nimeona wamewekamkazo kwamba, kuna uboreshaji wa masoko na viwandavya kuchakata nyama na bidhaa za mifugo, masoko yetuyahakikiwe yaweze kutoa bei yenye tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi mifugo mingi yanchi yetu inapelekwa nchi za jirani na hasa Kenya. Endapotutakuja kutengeneza viwanda, tusipokuwa na mkakati wakuweka bei inayofanana na ile ambayo wenzetuwanaopeleka mifugo Kenya wanaipata, tutaendelea

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

kupoteza mazao ya mifugo kwa sababu wafanyabiasharawa mifugo wataendelea kutamani kupeleka nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali itendeeSekta ya Mifugo kama kile kinachofanyika kwenye Sekta yaMazao ya nafaka kama korosho, kahawa na chai, wawewanawekewa bei elekezi ambayo ninaamini huwainatengenezwa kitaalam kwa kuangalia hali halisi ya bei zamazao hayo katika Soko la Dunia. Mifugo pia ifanyie hivyo ilimfugaji aweze naye kupata bei ambayo inamvutia, apendekuuza kwenye masoko ya ndani na apate faida ambayoataipata tu popote atakapokwenda na asiwe na hamu yakutaka kupeleka mifugo nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nilikuwa nimeangaliakatika suala la kufungamanisha uchumi na maendeleo yawatu, nikatamani sana nitoe maoni kwa Serikali na ninaombaniishauri Serikali kwenye suala la ardhi. Ardhi ndiyo mama yetusisi wote, ndiyo chimbuko la kila kitu; na ardhi ya Tanzaniahaiongezeki, sisi tu binadamu ndio tunaongezeka na viumbewengine walioko katika hii ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali itilie mkazosana suala la upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhikuhakikisha kwamba tunawasomesha wataalam wa kutosha,tunawekeza katika kuweka vifaa vya kutosha na kuhakikishakwamba hii ardhi inapangwa na ipangwe mapema kuepukaadha tunayopata ya makazi holela na migogoro ya ardhiisiyoisha. Hii itatusaidia sana kuondokana na migogoro nakatika kuhakikisha kwamba Watanzania wa kesho watakutaardhi i l iyopangiliwa na ambayo matumizi yakeyameshabainishwa na tutaondokana na adha kubwatuliyonayo kwa sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa suala la wanyamapori,kwa kuwa naona muda wangu umeisha, nilikuwa naombakwa sababu wanyamapori wameongezeka baada yauhifadhi kuimarika, Serikali sasa iwekeze katika kuwekapackages, mafungu yenye kuvutia ya kufidia au kutoa vifutamachozi na vifuta jasho vitakavyowafanya Watanzania

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

waendelee kuthamini rasilimali yawanyamapori tuliyonayo.Hilo likifanyika, uhifadhi wa wanyama utaweza kuwaguaranteed. Kwa sababu sasa hivi mgongano wawanyamapori na binadamu unazidi kwa sababu wanyamawamehifadhiwa na sisi pia tunaongezeka; na suluhisho la hiloni kuwafanya wananchi wawe wavumilivu kwa kuwapamafao mazuri kutokana na hifadhi ya wanyamapori.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayomachache, napenda kusema kwamba naunga Mpangomkono na ninaipongeza Serikali yangu kwa kazi kubwainayoendelea kufanya katika kutekeleza Mpango wetu waMiaka Mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipanafasi hii. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana.

Waheshimiwa Wabunge, niwataje Wabungetutakaoanzanao mchana. Mheshimiwa Dkt. RaphaelChegeni, Mheshimiwa Edward Mwalongo, Mheshimiwa LuciaMlowe, Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere, MheshimiwaMendrad Kigola, Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa,Mheshimiwa Dkt. Rashid Chuachua na wengine tutaendeleakuwataja kadiri mjadala wetu utakavyoendelea.

Bunge linarejea.

(Bunge lilirudia)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nasitishashughuli za Bunge mpaka Saa 11.00 jioni leo.

(Saa 7.02 mchana, Bunge lilisitishwa hadi Saa 11.00 jioni)

(Saa 11.00 Jioni Bunge lilirudia)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu.

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

NDG. LAWRENCE MAKIGI – KATIBU MEZANI:

KAMATI YA MIPANGO

(Majadiliano yanaendelea)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae.

Waheshimiwa Wabunge, tutaendelea namajadiliano, baadhi ya Waheshimiwa Wabunge nilikuwanimetaja majina yao, tutaanza na Mheshimiwa Lucia Mloe,atafuatiwa na Mheshimiwa Mwalongo.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangiakatika hoja iliyopo mbele yetu. Awali ya yote niunge mkonohotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie mamboyafuatayo. Jambo la kwanza ni bajeti isiyotosheleza.Kumekuwa na tatizo kubwa la upelekaji wa bajeti zamaendeleo karibu kila mwaka, maeneo mengine imekuwainapelekwa pungufu au haipelekwi kabisa. Kwa mfano,Wizara ya Kilimo katika mwaka wa fedha 2016/2017 pesa zamaendeleo kiasi cha shil ingi bil ioni 100.25, zi l ikuwazimetengwa lakini hadi kufikia mwaka 2017 zilizotolewazilikuwa shilingi bilioni 2.2 tu sawa na asilimia 2.2.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tumeona katikamwaka 2017/2018, Wizara hii iliidhinishiwa na Bunge pesa zamaendeleo shilingi bilioni 100.2 lakini hadi kufikia mwezi Machini shilingi bilioni 16.5 tu zilikuwa zimetolewa sawa na asilimia11. Tukija katika mwaka wa fedha 2018/2019 fedhailiyotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika sekta yakilimo ilikuwa shilingi bilioni 98.119 lakini fedha iliyotolewailikuwa ni shilingi bilioni 41 sawa na asilimia 42.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tumeona huu mtiririkowote wa bajeti ya miradi ya maendeleo kwa jinsi ambavyoimekuwa ikisuasua na kwamba haipelekwi kwa wakati au

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

inapelekwa pungufu hata pungufu ya asilimia 50. Napendakuishauri Serikali kutokana na tatizo hilo la kutoweza kupelekabajeti za kutosha kwenye miradi ya maendeleo aukutopeleka kabisa ni vema basi Serikali ikaona namna ganitunawekeza au tunaweka mazingira wezeshi au mazuri kwawawekezaji ili waweze kutusaidia katika miradi mbalimbaliya maendeleo kama maji, miundombinu na miradi mingine.Hii ingeisaidia sana Serikali angalau kutokuwa na mapengomakubwa kama ilivyo sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba niongeleesuala la miradi ya maji. Miradi ya maji imekuwa ni tatizo nchinzima katika utekelezaji wake. Kwanza miradi mingi imekuwaikiripotiwa imekamilika lakini kwa uhalisia haifanyi kazi nawakandarasi wamekuwa tatizo. Naishauri Serikali na Wizaraya Fedha tuone namna gani pesa zinazokuwa zimetengwazipelekwe kwa wakandarasi kwa wakati unaotakiwa lakiniwakati huo huo tuwapime hawa wakandarasi maanawakandarasi wengine siyo waadilifu kabisa. Inapogundulikakwamba hawa wakandarasi siyo waadilifu basi watolewemara moja wasilelewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia suala la maji limekuwani tatizo hata maeneo yale ambayo yana vyanzo vya majivingi tu vya kutosha. Naiomba Serikali tuone namna yakuwapata wataalamu wanaokuwa wabunifu katika miradimbalimbali ya maji. Nitoe mfano tu katika Mkoa wa Njombe,ule mji umezungukwa na maji lakini pale Njombe Mjini hakunamaji na tuna wataalamu, kwa nini hao wataalamu wasiwena ubunifu na kutumia njia nyingine kuhakikisha majiyanaingia pale mjini ukiacha vijijini au ukiacha maeneomengine ambayo yana ukame. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia suala la maji katikanchi yetu tumeona kipindi cha mvua kunakuwa kuna majimengi sana na mafuriko. Hivi hatuwezi kupata wataalamuambao wanaweza wakatuelekeza namna kuvuna haya majina kuweza kuyatumia wakati wa ukame? Naishauri sanaSerikali tuone namna gani tunaweza kuelekeza nguvu zetukwenye vitu tulivyonavyo kwa sababu haya maji ya mvua

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

tunakuwa nayo na hata sasa hivi kuna maeneo mvuazinanyesha sana lakini haya maji hayavunwi mwisho wa sikumaeneo haya yanakujakuwa makame lakini wakati huo huokulikuwa kuna mvua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni watumishi.Suala la watumishi kwa kweli ni changamoto kubwa.Naiomba Serikali ione namna gani angalau kipindikilichobakia maana toka tumeingia mwaka 2015 hadi sasawatumishi hawajapandishiwa mishahara angalau hata yakudanganyishia tu. Watumishi wako katika hali ngumu sana.Nikitoa mfano wa walimu hata nyumba wanazokaa zinatiahuruma. Kwa mfano, sasa hivi kuna shule ambazozinakarabatiwa vizuri sana lakini nyumba za walimu hakuna.Sasa hata kama shule zimekarabatiwa vizuri walimuwanaweza kwenda kufundisha lakini kama wao hawananyumba nzuri bado haitasaidia. Niombe Wizara ya Fedhatuone namna gani tunawasaidia hawa watumishi hasawalimu kuwajengea nyumba kama tulivokarabati shule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni madini.Naomba kuongelea suala la madini Mchuchuma na Ligangaumekuwa wimbo wa taifa. Tumekuwa tukiongea juu yaLiganga na Mchuchuma, tulifikiri kufikia kipindi hiki tungekuwatayari tumeshaanza kufaidika na mradi ule. Ule mradiungekuwa na faida kubwa sana kwa Taifa letu, haya mambotunayohangaika nayo sasa hivi ya pesa pengine ingekuwani msaada mkubwa sana mradi ule. Naiomba Serikali kwakweli ichukue hatua ya haraka kutekeleza ule mradi waLiganga na Mchuchuma kusudi uweze kusaidia kuinuauchumi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni barabara.Maeneo mengi barabara zimetengenezwa lakini menginekwa kweli ni tatizo, barabara zimeanza kutengenezwa mudamrefu lakini hadi sasa hazijaisha. Mfano katika Mkoa waNjombe barabara inayounganisha Ludewa na Njombe Mjinimaana ya Itoni –Ludewa, barabara ile kwa kweli ni tatizo,kama ingefanikiwa kwisha ingekuwa msaada mkubwa sana.Hadi sasa hivi ni asilimia 30 tu na tunaambiwa kwamba

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

mpaka mwakani inatakiwa iwe imekamilika. Sasa najiulizakama mpaka sasa hivi imetekelezeka asilimia 30, je, mwakaniinaweza kumalizika kwa hizo asilimia 70 zilizobaki? NiiombeSerikali mtusaidie fedha kwa ajili ya kukamilishia ile barabara.Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Nilikuwa nimemtajaMheshimiwa Edward Franz Mwalongo, atafuatiwa naMheshimiwa Daimu Iddi Mpakate, Mheshimiwa Peter Msigwaajiandae.

MHE. EDWARD F. MWALONGO: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nimshukurusana Mwenyezi Mungu kwa kutujalia zawadi ya uzima.Nitumie fursa hii kwanza kuwapongeza sana MheshimiwaWaziri wa Fedha na Wizara yake na watendaji wote waWizara ya Fedha. Pia niwashukuru na kuwapongeza sanaSerikali yetu chini ya Rais wetu John Pombe Magufuli nawatendaji wote, tumefanya kazi vizuri kwa pamoja katikaMpango uliopita na matokeo yameonekana na sasatunaenda kujadili mpango kwa ajili ya mwaka wa fedhaunaofuata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na suala la kilimo.Kilimo ndiyo uti wa mgongo wa nchi yetu na Waziri katikakitabu chake ameeleza kwamba mafanikio ya kilimoyamekwenda zaidi ya asilimia 100 lakini kusema kweli nijambo la kusikitisha sana. Kilimo hiki ambacho kimetufikishahapa tulipo kwamba nchi ina chakula cha kutosha nakimekwenda zaidi ya asilimia 100 si kilimo kile ambachokimezalisha kwa nafasi ambayo tunasema ni sahihi, nikwamba watu wamefyeka sana misitu, wamepanua sanamashamba lakini mashamba yenyewe tija kwa eka iko chinisana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini hali iko namna hii?Hali iko namna hii kwa sababu, moja, udongo wa nchi yetuhaujapimwa. Wananchi wanatibu udongo kwa maana ya

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

kutia mbolea ya kukuzia mazao yao lakini hawajui kama hitajila udongo ni nini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini mbili wananchi hawahawana Maafisa Ugani. Wizara ya Kilimo kama sikosei kunakipindi haikuajiri Mabwana Shamba zaidi ya miaka 10.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni zana zakufanyia kazi. Tumeshuhudia makampuni mbalimbali yamatrekta mengine ya umma yameleta matreka katika nchiyetu matrekta yale mabovu, yamewatia hasara wananchi.Haiwezekani trekta unalimia msimu mmoja halafu inakufa.Tunashuhudia kabisa matrekta ya siku za nyuma yamekuwaimara na yamekuwa yakisaidia sana katika kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe tunapokwendakuandaa Mpango mwingine, tujipange vizuri tuhakikishekwamba tunapata Maafisa Ugani wa kutosha katika maeneoyetu ya kilimo ili kusudi wananchi wapate wataalamu wakutosha. Ni jambo muhimu sana wakulima wapatewataalamu wa kutosha tujipange tupime udongo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona kwenye kitabuinaeleza kwamba kutakuwa na upimaji wa matabaka yaudongo basi hilo jambo lifanyike kwa sababu litaendakuwasaidia wakulima. Mafanikio yake tuyaone kwambawakulima sasa watumie eneo dogo halafu wazalishe zaidilakini wanafyeka sana misitu na wanapanua sanamashamba ili kusudi wapate mazao mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kwa taasisizinazoleta vitendea kazi kama matrekta naomba Serikaliiangalie. Kama kweli tunataka kuinua kilimo na kusaidiawakulima tuhakikishe kwamba zana za kilimo zinazoletwakwenye nchi yetu ni imara na zinaweza zikawasaidiawananchi kwa muda mrefu kuliko sasa leo hii ni kilio, madeniwaliyokopeshwa wananchi kwa ajili ya yale matrektahayalipiki, taasisi zilizoleta matrekta zinalia hasara, mabenkiyanalia hasara lakini matrekta ni mabovu. Huu ndiyo ukweliwenyewe, yale matrekta ni mabovu. Najua nayasema haya

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

kuna watu watachukia lakini wacha wachukie tu, matrektayale ni mabovu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala lamasoko. Tutakapokuwa tumewawezesha wakulima tujitahidikuongeza masoko. Leo hii tunazungumza habari ya soko laCongo lakini tunalenga upande mmoja zaidi upande wakusafirisha mizigo tu lakini tukumbuke kabisa kwamba mazaoya kilimo vilevile yana soko Congo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mikoa ya Nyanda za JuuKusini tunaomba sana ile bandari ikamilike. Mtakapokuwamnapanga mipango hiyo sasa tunawashauri mkamilishebandari ile na iweze kufanya kazi vizuri kusudi tuanze kupelekamazao Congo. Siku mzigo wa Congo utakapokuwa haupo,mazao yetu ya kilimo yatakwenda Congo na kwa idadi yawatu ina maana wao ni wengi kuliko sisi kwa hiyo ina maanawanahitaji kula kuliko sisi ni soko mojawapo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine niMchuchuma na Liganga. Mchuchuma na Liganga hataukiangalia kwenye Hansard za Bunge sidhani kama kunakipindi cha Bunge kiliwahi kupita bila kuongelea Mchuchumana Liganga. Hebu sasa Serikali ifanye maamuzi ambayoyataifanya Mchuchuma na Liganga iweze kufanya kazi.Mmesema mmetenga fedha kwa ajili ya kulipa fidia kwawananchi lakini vilevile mnasema mnataka kulipa fidiasehemu ya kupitisha njia ya umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukumbuke umemeutakuwa ni zao la Mchuchuma ili uende Liganga lakini kunabarabara zinazokwenda kule, iko barabara ya Itoni - Mandampaka leo tunasema kilometa 30 tunapanga mpango wamaendeleo hapa naomba basi tukamilishe hii barabarakuanzia Itoni - Manda barabara ikamilike. Tunachoambiwakila siku ni kwamba ile barabara ni ndefu sana ya zege nchinzima hakuna barabara ndefu kama ile, haiwezi kutusaidiakama hii barabara haijaanzia Itoni.

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe sasa kama tunatakakufanya uwezeshaji migodi ile iweze kufanya kazi basitujipange tuweze kutengeneza na barabara iweze kufikamaeneo yale. Imekuwa ni bahati mbaya sana wataalamuwetu wanapopanga mipango unasikitika kuona kwambawanaweza wakapanga kujenga, nichukulie mfano mmojatu pale Njombe wamejenga Mahakama ya Mkoa lakini mradiule ulikuwa ni wa kujenga Mahakama tu hakuna hatabarabara kuifikia hiyo Mahakama yenyewe. Mkandarasianapita porini mpaka kuifikia hiyo Mahakama yenyewe, hataitakapokuwa imekamilika hakuna fungu la kutengenezeabarabara. Kwa hiyo, nafikiri tunapopanga mipangotuhakikishe kwamba kama tunajenga mradi kamaMahakama basi na mipango yake ya kujenga barabarakuifikia Mahakama hiyo iwepo kusudi itakapokuwaimekamilika iweze kusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana nasema hataMchuchuma, tunaiendea Mchuchuma tutakapokuwatunakamilisha kumpata huyo mbia ambaye atashiriki katikakuchimba madini haya basi aikute na barabara iko tayarilakini barabara hii ni barabara ya kiuchumi itasaidia sanakuhakikisha kwamba Mkoa wa Njombe unazidi kuleta uchumiwa kutosha ndani ya nchi. Huu ni mkoa unaozalisha chakulakwa wingi na itasaidia wananchi kufanya kazi zao vizuri lakinindiyo maendeleo yenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo linginekwenye suala la barabara ambalo napenda kuishauri Serikalini kwamba tunaposema tunataka barabara za kuunganishamikoa kwanza tujiulize tunaunganisha huo mkoa na mkoa ilitupitishe kitu gani? Wakati mwingine tunaunganishabarabara mkoa na mkoa kwa wiki linapita gari moja tu lakinitumeacha barabara inayounga wilaya na wilaya nainapitisha mazao ya kutosha, inachangia uchumi wa nchi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani mtizamo huotuuangalie upya kwamba tunajenga barabara ambazozitapitisha mazao, tuangalie zinapitisha nini. Tusijenge tu

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

barabara sababu tu watu wapite, waseme tu kwambatumeunganisha mkoa na mkoa, mmeunganisha so what, ilikifanyike nini? Itakuwa siyo msaada. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonapenda kuishauri Serikali ni suala la huduma za matibabuya UKIMWI. Leo hii asilimia kubwa sana ya fedha au ya dawawanazotumia waathirika wa UKIMWI ni za msaada. Tutambuemoja huu msaada iko siku utakuwa na ukomo, ni lazimakwenye mipango yetu tuhakikishe kwamba tunajiwekeautaratibu wa namna gani tutajimudu wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo la pekee kabisakwenye suala la UKIMWI liko suala la watoto waliojikutawamezaliwa na maambukizi ya UKIMWI, watoto hawa wanahali mbaya sana ya lishe. Kama Serikali kwenye mipango yetuambayo tunaenda kuipanga sasa kwa ajili ya bajeti ijayotulione hilo na tuhakikishe kwamba tunatenda kiwango kwaajili ya kusaidia watoto ambao wameathirika na UKIMWI kwasababu wamepata UKIMWI kutoka kwa wazazi wao. Watotohawa wanapokuwa shuleni l ishe ni duni sana nawanashindwa kusoma vizuri na magonjwa nyemeleziyanawasumbua sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutokuwa na bajeti yaSerikali kwenye jambo la kuhudumia watoto waliothirika naUKIMWI watoto hao wengi sana tunawapoteza. Leo hiiwagonjwa pekee waliobaki wanaumwa zaidi kutokana natatizo la UKIMWI ni watoto ambao wamejikuta wanamaambukizi kutokana na kuzaliwa na wazazi ambaowalikuwa na maambukizi.

Kwa hiyo, ni ushauri wangu kwa Serikali itakapokuwainapanga bajeti ihakikishe kwamba inaangalia kwa jicho lapekee kwamba tuwe na fedha ya kuweza kusaidia watotohawa ili kusudi waweze kupata huduma bora ya chakula iliafya zao ziweze kuimarika zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo nashukurusana kwa fursa. (Makofi)

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Daimu Iddi Mpakate atafuatiwa na MheshimiwaPeter Msigwa, Mheshimiwa Dkt. Raphael Chegeni ajiandae.

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi jioni hii kuchangia hojamahususi, naomba kwanza niunge mkono hoja hii. Pili,naomba niishukuru Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwakutimiza dhamira ya kuunganisha Mtwara na Mkoa waRuvuma kwa maana ya Mtwara Corridor kuhakikisha kipandekile cha Mbinga kwenda Nyasa kimeanza kujengwa kwakiwango cha lami.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, naombajambo hili haliwezi kukamilika kama hatutaweza kuzungumziasuala la reli ya kusini ambayo inaunganisha kati ya Mtwarana Mbambabay. Ukweli uzalishaji wa makaa ya maweNgaka, tunapozungumzia Mchuchuma na Liganga jambohili haliwezi kwenda sawasawa bila kuzungumzia suala la reliya kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali, nimeonakwenye maelezo ya Mheshimiwa Waziri lakini hayaletimatumaini kwa sababu wameendelea kutafuta wawekezajiwa reli hii lakini bado tunaona speed ya kuweza kuwekezakatika reli hii bado ni ndogo. Tunaomba, tunapofikiria sualala kujenga kiwanda cha Mchuchuma na Liganga iendesambamba na ujenzi wa reli ya kutoka Mtwara mpakaMbambabay ili kusukuma maendeleo katika ukanda wakusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara zetu kwa sasa hivikwa kweli zinaharibika sana, kwa mfano kuna malorimakubwa sana yanayobeba makaa ya mawe kutoka Ngakakwenda Dar es Salaam yanapita Songea – Tunduru –Lindi nakufika Dar es Salaam, lakini bado mengine yanapita Songea– Njombe mpaka Arusha. Jambo hili kidogo kama tungekuwatuna reli basi barabara hizi zingeweza kudumu kwa mudamrefu, ukiona barabara ya Songea – Njombe ina hali mbayasana, kama ni mgeni unaendesha barabara ile basi

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

utegemee kupata ajali wakati wowote kwa sababubarabara ile ina hali mbaya, inatokana na kwamba inabebamizigo mizito ya makaa ya mawe kutoka Ngaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, nilidhanikatika hotuba ya Mheshimiwa Waziri angeweza angalaukuingiza suala la ujenzi wa meli katika mwambao wa bahari.Kwa kweli barabara ya Mtwara – Lindi mpaka Dar es Salaamimeharibika sana; Dangote peke yake ana magari 600ambayo kila siku yanabeba simenti kupeleka Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, solution ya jambo hili ilikuwani Serikali angalau kuweka msisitizo wa kuwa na meli ya mizigokutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam ambayo ingewezakupunguza adha hii. Naomba Mheshimiwa Waziri aendekutoka Mtwara kuja Dar es Salaam ataona barabara ile jinsiilivyoharibika kwa hali ya juu, kitu ambacho kingewezakupunguzwa na usafirishaji wa simenti kwa kutumia meli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonaomba kulizungumzia ni suala la umeme vijijini. NaipongezaSerikali kwa jitihada kubwa inayoifanya. Pamoja na pongezihizi, umeme vijijini una dosari kidogo; baadhi ya maeneo vijijikwa kweli vina hali mbaya, umeme haujafika. Kwa mfano,kwenye Jimbo langu mpaka sasa nina vijiji vitano tu kati yavijiji 65, kwenye awamu hii nilipewa vijiji 23 lakini mkandarasibado hajaweza kufikisha hata vijiji nne, ukimuulizia ni suala languzo ambalo linasumbua. Jambo lingine ambalolinasumbua wanadai mkandarasi hajalipwa kwa muda mrefuanafanya kazi, invoice ime- raise lakini pesa badohajalipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, suala laumeme kwenye Halmashauri ambayo ina majimbo mawiliina shida kidogo, utakuta Halmashauri hiyo hiyo mwenzakoana vijiji 20 wewe una vijiji viwili. Jambo hili watu wa REAwanavyopanga mipango yao ya kupeleka umeme vijijini basiwaangalie maeneo ambayo yana Majimbo mawili, basiwaangalie maeneo hayo wawe wanagawa vijiji kadiriinavyowezekana.

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, tunapigakelele sana kwamba vijiji na vitongoji vyote vitakuwa naumeme lakini shida iliyokuwepo wakandarasi wanapewascope ndogo sana, ukiangalia high tension inaenda kilometa30 mpaka 40, katikati anavyopita kuna vitongoji ambavyohavijatajwa kwenye hiyo scope. Kwa hiyo, naomba sana kwaawamu ijayo basi waangalie scope wanayopewawakandarasi kwa ajili ya kusambaza umeme katika vitongojimbalimbali basi iongezwe angalau vile vitongoji vilivyo katikaline ile viweze kupata umeme kama ilivyokusudiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambaloningependa kuliongelea ni suala la kilimo, kama wenzanguwalivyoongea, kilimo ni uti wa mgongo lakini kilimo kwaupande wa kusini (upande wa korosho) tunategemea sanamfumo wa stakabadhi ghalani. Mfumo wa stakabadhighalani hauwezi kufanyika bila maghala, kuna maghala yaBodi ya Korosho yana muda mrefu sasa hivi ni mwaka watatu yalianza kujengwa lakini mpaka leo yale maghalahayajaweza kukamilika. Naomba Mheshimiwa Wazirialiangalie kwa jicho la huruma, tuna shida sana ya maghalakatika maeneo yetu hasa upande wa Tunduru hatuna ghalala kudumu ambalo lina uwezo wa kuhifadhi korosho kwawakati mmoja ili biashara ya mfumo wa stakabadhi ghalaniiweze kufanyika kama inavyofanyika kwa sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la maghala hataukiangalia kwenye vyama vya msingi kwa maana ya vijijini,maghala yao mengi ni mabovu, yanavuja, yanahatarishausalama na ubora wa mazao hasa korosho pamoja namazao mengine mpunga, mahindi, ufuta na kadhalika. Kwahiyo, naomba sana bajeti ijayo iangalie namna ya kusaidiaangalau ujenzi wa maghala katika vijiji mbalimbali ilikupunguza adha hii ambayo inawakumba wakulima wetukukosa mahali pa kuhifadhi mazao yetu ya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonapenda nilizungumzie ni suala la maji; maji ni uhai. Kunasiku moja nilicheka kidogo, Mheshimiwa Diwani mmojaalisema hivi tusipooga wote hapa wiki nzima tutakuwaje?

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

Jambo hili ni zito sana kwa sababu vijijini maeneo mengiukame umeathiri maji, maji yamekuwa ni tatizo. Naombaangalau tuweze kuhakikisha kwamba tunapata fedha nyingizinazoweza kuchimba visima angalau kila kijiji kipate visimavitano ama vinne, tujinyime kwa maana ya aina yoyote ilekwa sababu bila maji maisha kwa kweli yanakuwa nimagumu kwa sababu wote tunaishi kwa kutegemea majina magonjwa mengi yanapungua kama maji yatakuwepoya uhakika na usalama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sanapamoja na Waziri anayehusika basi waliangalie suala la majikatika maeneo mbalimbali ya vijiji vyetu kutilia mkazo ilikuhakikisha kwamba angalau asilimia ile ya maji iongezekeili wananchi waweze kupata maji salama ambayo ni yauhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ambalonapenda nilizungumzie ni suala la TARURA. TARURA kwa kweliwana kazi kubwa lakini kazi yao inakwamishwa kwa sababupesa wanayopewa ni kidogo ambayo haikidhi barabaraambazo tunazo/TARURA wanazimiliki. Ukichukulia mfanoWilaya ya Tunduru, ina kilometa 1,200 za barabara za vijijiniambazo zinamilikiwa na TARURA, lakini pesa wanayopewainaweza kutengeneza kilometa 100 mpaka 200 tu, sasa sijuitutachukua miaka mingapi kuzipitia barabara hizi mpakakumaliza maeneo yote. Kwa hiyo, naomba sana Serikaliwaangalie namna ambavyo wanaweza kuwaongezea pesaTARURA waweze kufanya kazi yao vizuri na wawezekuwahudumia wananchi kwa ajili ya kutengeneza barabarazetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho kabisa nisuala la afya. Naishukuru Serikali imefanya jambo jema lakuongeza vituo vya afya ambavyo vimeleta tija na matumainikwa wananchi wetu. Jambo hili linaenda sambamba naidadi ya watumishi, mimi Jimboni kwangu tuna vituo vya afyaviwili lakini kila kituo kina wafanyakazi sita/saba, jamboambalo linakwamisha juhudi hizi za kujenga vituo vya afyavipya na vizuri na utoaji wa huduma haulingani na hadhi ya

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

vituo vya afya ambavyo vipo kwa sasa. Kwa hiyo, naombaSerikali ifikirie suala la ajira la watumishi wa afya kuongeza ilikuhakikisha kwamba tunapunguza kero ya watumishi wa afyakatika zahanati zetu, vituo vya afya pamoja na hospitali zetuza Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho kabisa nisuala la watumishi upande wa elimu. Halmashauri yetu yaWilaya ya Tunduru ina zaidi ya shule 157, ina upungufu waWalimu zaidi ya asilimia 40 ambayo ni zaidi ya Walimu 600.Naomba Serikali iangalie namna pekee ya kuongeza idadiya Walimu hasa kwenye shule za msingi na sekondari ilikuhakikisha kwamba watoto wetu wanapata elimu iliyo borana ambayo inaweza kuwafanya waweze kuendelea vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipanafasi hii ya kuongea. Ahsante sana na naunga mkono hoja.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Nilikuwa nimemwitaMheshimiwa Peter Msigwa, atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt.Raphael Chegeni na Mheshimiwa Boniface Mwita Getereajiandae.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikushukuru kwa kunipa nafasi. Mheshimiwa Mpango, wakatianatuletea Mpango wa Miaka Mitano mara tu baada yaSerikali kuingia madarakani, mojawapo ya mambo ambayoSerikali i l ikuwa imetutangazia na kutuahidi kwambaitayafanya ni pamoja na masuala ya demokrasia na utawalabora ambayo yanapatikana katika ukurasa wa 111 katikakitabu hiki cha Mpango wa Miaka Mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mojawapo ya mamboambayo aliyasema alisema kuhakikisha usawa wa kiuchumi,demokrasia na uvumilivu wa kisiasa katika jamii. Ukomavuwa demokrasia na ushiriki wa wananchi utazidi kuimarishwakupitia, akaelekeza mambo gani yatapitia jinsi ganiitakavyoimarishwa. Mojawapo alisema kuwekeza zaidi katikakuboresha mfumo wa uchaguzi na kufanya kuwa wa kisasa

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

zaidi pamoja na kuzidi kupanua uhuru wa kujieleza, uwazi,upatikanaji wa habari; kuna mambo mengi sana alizungumzakatika mpango wa miaka mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunapozungumzatunakwenda kumaliza kipindi chetu kama Wabunge,Madiwani na kama Mheshimiwa Rais, lakini haya mamboyote ambayo Mheshimiwa Mpango alikuwa ameahidi katikampango, Serikali i l ituhakikishia kwamba itaimarishademokrasia tukianza moja baada ya jingine katika kipindicha miaka mitano, kila kitu hapa kimedorora. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna uwazi wa vyombovya habari, hakuna mfumo mzuri wa uchaguzi, hakunamfumo wa kidemokrasia. Mara tu tulipoingia Bungeni hapa,kitu cha kwanza tulizuiwa mikutano, tukazuiwa Bunge live.nataka nimuulize Mheshimiwa Mpango huko ndio kuimarishaambako alikuwa anatuambia wakati akituambia miakamitano? Kwa sababu wamezuia Bunge Live, wamezuiamikutano wakasema Wabunge sehemu tunazotokatutaruhusiwa kufanya mikutano na yenyewe wamezuia.Kibaya zaidi walisema wataimarisha chaguzi na hikitunachokiona sasa katika nchi yetu ya Tanzania ambachohakijawahi kutokea ni ishara tosha kwamba Serikali yenuhaina mpango wa kuimarisha demokrasia na chaguzi hurukatika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwa bahati mbayaMheshimiwa Jaffo hayupo hapa, kinachofanyika sasa hivikwenye Serikali za Mitaa kimsingi Chama cha Mapinduziwanakunywa sumu. You are just drinking poison, inawezekanaisiwaue leo lakini itawaua kidogo kidogo. Hamuwezikusimama hapa mka-claim kwamba ninyi ni ma-championand you don’t want to compete; victory inatokana naushindani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanajiitaje washindi nahawataki kushindana? Katiba yetu inasema kila baada yamiaka mitano tutapambana uwanjani na viongozi bora

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

wanapatikana baada ya ku-compete, hawatakicompetition, huo ni utawala bora wa aina gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tunapozungumza,Wenyeviti wa Mitaa wote karibu nchi nzima wamefunga ofisiwamekimbia, hawataki kupokea mapingamizi, watendajiwote wamekimbia kwenye ofisi za umma, tunasematunataka tuzungumzie utawala bora, hawapo wanakimbia...(Makofi)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa kuna taarifa kutokakwa Mheshimiwa Waitara.

T A A R I F A

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, naomba nimpe taarifa mchangiaji kwamba hilijambo limezungumzwa jana na leo. Mheshimiwa Spika janaalitoa maelekezo, leo wewe umetoa maelekezo na hapatunapozungumza Mheshimiwa Waziri hayupo hapa lakiniamekwenda Singida akakuta mambo sio kamawalivyozungumza humu ndani, ameenda Manyara;tumetuma maafisa wetu wamekwenda kule Moshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nampa taarifakwamba Mheshimiwa Msigwa tunayo kuanzia jana tarehe 5na tarehe 6 ya mapingamizi, tunayo tarehe 6, 7 mpaka 9 yaKamati ya Rufaa; maelekezo yaliyotolewa na Serikali nikwamba kuna mtu amelalamika kama inavyozungumzwawaandike barua za malalamiko na malalamiko yatafanyiwakazi, tunao muda mpaka tarehe 9. Kwa hiyo, usianue kwanzamatanga kabla msiba haujaisha. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa unaipokea taarifahiyo?

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,hii taarifa siipokei, inaonekana Mheshimiwa Waziri anatakakupotosha na hana information. Mimi kwenye Jimbo langunina mitaa 192, wameenguliwa watu 185, sasa hivi wapokwenye Ofisi za Kata zote zimefungwa; what are you talkingabout? Halafu mnataka kusema mnashinda, mnashindaje?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe mfano, wakatiwa segregation kule Marekani Malcom X anatoa hotubamoja naomba ukaisikilize, kulikuwa kuna field negro na housenegro. Humu ndani inawezekana wengine ni house negrohawajui tunacho-feel sisi ambao ni field negro kwenye field.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hamjui madhiratunayoyapata, kufanya siasa katika nchi hii imekuwa nicriminal, unahesabiwa kama ni mhalifu kufanya siasa ya nchihii wakati Katiba inanipa mamlaka/uhuru wa kujieleza(freedom of expression). Ninyi mmekuwa ni house negro kwasababu ni beneficiary wa mambo haya ndio maanahamuwezi kuyaona. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kuongea na wapiga kurawangu kwenye Jimbo langu na Wabunge wengi wenzanguwa upinzani ni uhalifu katika nchi hii. Tunaambiwa sisi lazimatuombe ridhaa ya kufanya mikutano, wengi wenu ninyi huwamnaenda kufanya mikutano huko wala hamuulizwi na mtuyeyote. Kwa hiyo, tunaongea mambo ambayo tuna-feel.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nchi hii mnasematushindane, Katiba inataka kila baada ya miaka mitanotushindane na nyie mnasema chama chenu kimeimarishwa;miaka minne hatujaongea, hatujafanya mkutano, Wenyevitiwa vyama vyetu hawajasafiri, mmesafiri ninyi peke yetu.Television mmezishika nyinyi peke yenu, unasema utawalabora; huo ndio utawala bora mnaotuambia hapa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, television, radio, mikutanoninyi, tunakuja kwenye mikutano seven days, you are running

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

away, halafu mnakuja hapa mnasema tunatengenezademokrasia, what kind of democracy is this? Mkifika uchaguzimnakimbia mnasema kuna democracy, what democracy isthis?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapokuja hapa kamatunataka tutengeneze nchi yetu tukubaliane kamatumeamua kufuta mfumo wa vyama vingi its well and good,mpo wengi, leteni Muswada wa Sheria hapa kwambatumefuta mfumo wa vyama vingi tutabanana hukohuko siitakuwa ni sheria, tutabanana hukohuko kwenye majimboyenu maana yake itakuwa ni sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katiba ya nchi yetu inatupauhuru kwamba, mtu ana mawazo tofauti na mwingine walahatugombani, wewe una mawazo yako na mimi ninamawazo yangu, tunashindana kwa hoja, baadaye tunaendakwa wananchi, huo uhuru uko wapi katika maelezo yaMheshimiwa Mpango aliyoandika hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye kitabu hicho hichoMheshimiwa Waziri amesema kuhikisha kuwepo kwamgawanyo wa madaraka na ufasaha wa mipaka baina yamihimili mitatu ya Serikali kwa kuimarisha uwezo wa taasisina rasilimali watu kwa kila mmoja kuwezesha ufanisi katikautekelezaji wa majukumu yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, democracy ilivyoanza,separation inahitaji balance, tunahitaji ku-balance, mhimiliunaojitegemea wenye mamlaka na nguvu.Tunapozungumza, nimezungumza hapa leo Bunge Livelilizimwa, huu ni mkutano wa wananchi wa Tanzania, tunakujakutunga/ tunapoingia Bungeni hapa tunapanga bajeti yawananchi milioni 50 waliotutuma tuje tuwatenge hela zaokatika bajeti hii, tunazungumzia kuhusu afya zao, kilimo, shulena afya zao, leo tunapozungumza Wabunge tuliotumwatunakuja hapa tupo gizani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu Kenya ambapoMheshimiwa Spika alikwenda, wao mpaka kamati zipo live.

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

Tunazungumza separation of powers, nguvu ya mhimili waBunge, hawa tunaowasemea mimi sijaja peke yangu na kilammoja hajaja peke yake, anawawakilisha watu wake.Tumekuja hapa ili wananchi wale waliotutuma wasikilizetunachosema, tunafanya gizani; hiyo ndio separation ofpower?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanasiasa tunashindamahakamani kwa kosa la kufanya siasa, sisi sio wezi,hatujavunja nyumba. Ninyi Serikali ya Chama cha Mapinduzimnapata wapi legitimacy ya kusema watu wasiwe wezikama nyie wenyewe mnaiba kura, where do you get that?Kama nyie wenyewe mna-rob kura mnapata wapi kwambawatu wasiibe mitihani, mnawaambia watoto wasiibe mitihanikama ninyi wenyewe hizi kura mnanyang’anya kwa nguvu,mnapata wapi kwamba watoto wasiibe mitihani? (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa NaibuSpika, kuhusu utaratibu.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika,where do you get that, where do you get that power?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU ENYE ULEMAVU: MheshimiwaNaibu Spika, kuhusu utaratibu.

MBUNGE FULANI: Wanatengeneza hao.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika,mnapata wapi hiyo nguvu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa. MheshimiwaJenista Mhagama, Utaratibu Kanuni.

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

Naibu Spika, ninaomba nitumie Kanuni ya 68 lakini naombaniende 68(1) lakini niende Kanuni ya 64(1) Kanuni ndogo ya(a) hiyo inakataza kabisa ndani ya Bunge mtu kutokutoataarifa ambazo hazina ukweli lakini nitakwenda mpakaKanuni ya 65. Naomba Mheshimiwa Mbunge kwa kweliasiendelee kulipotosha Bunge kwamba uwepo wetu sisi hapandani na uwepo wa Serikali yetu unatokana na vitendo vyawizi wa kura na ndivyo vinavyotufanya tuendelee kuwepomadarakani.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuhuma hii, ni tuhumakubwa na ni tuhuma ambayo sisi tunaojua Sheria na taratibuushindi wa mgombea yoyote unatawaliwa na Sheriatulizonazo, Sheria za uchaguzi Katiba ya Nchi yetu na hapandani ya Bunge tunatawaliwa na Kanuni katika kuyaelezahayo. Mgombea yoyote ambaye hajashinda ana uhuru wakwenda Mahakamani na kwenda kueleza Mahakamani nakule Mahakamani wanaweza wakatoa nafasi ya mgombeayoyote kuthibitisha ama kuweka wazi kile kinachomkera.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, si kweli nanadhani anataka kutudhalilisha anapotutuhumu sisi wote,Serikali nzima, Wawakilishi wote wa Wananchi na hasa kupitiaChama cha Mapinduzi kwamba uwepo wetu hapa ni uwepoambao si halali jambo hili si sahihi na anavunja Kanuni zaBunge. Kwa hiyo, tunamuomba sana Mheshimiwa Msigwaama afute kauli hizi ama ajielekeze katika mjadala bila yakuwa na tuhuma ambazo si za sahihi na hazina ukweli kwamujibu wa Sheria tulizonazo kwa mujibu wa Kanuni na kwamujibu wa Katiba.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge alikuwaakichangia Mheshimiwa Msigwa, ametoa maelezo marefuambayo Mheshimiwa Waziri wa Nchi amesimama kuhusuutaratibu akataja Kanuni ya 68 na akataja Kanuni iliyokuwaikivunjwa na Mheshimiwa Msigwa Kanuni ya 64(1)(a) ambayoKanuni ya 64 kwa ujumla wake inazungumzia mamboyasiyoruhusiwa Bungeni na (1)(a) inazungumzia kutokutoandani ya Bunge taarifa ambazo hazina ukweli.

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

Mheshimiwa Msigwa kwa muktadha wa Kanuni zetuukisoma hii kanuni ya 64 ukiizungumzia taarifa ambazo hazinaukweli itatupeleka kwenye Kanuni ya 63 inayozuia kusemauwongo Bungeni. Sasa kwa muktadha wa Kanuni hizo hizozinataka hizo taarifa kama hazina uwezo wa kuthibitishwabasi Mbunge apewe fursa ya kufuta hayo maneno yake iliaendelee kuchangia. Kwa hiyo, na wewe nitakupa hiyo fursaya kufuta hayo maneno yako halafu tutaangalia utaratibumwingine kama utakubali kufuta, utakuwa umefuta kamahukukubali maana yake nitasimama tena.

Mheshimiwa Msigwa!

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimezungumza suala hilo ukienda Ndarambo kule kwenyeJimbo la Silinde kura ziliibiwa kabisa mpaka tukaenda…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa, hapo unatakakueleza maelezo mengine, umepewa fursa ya kufuta kauliuliyokuwa ukizungumza, kama hukubali kufuta hiyo kauliuliyokuwa unasema, wewe sema ili nitoe maamuzi, umepewafursa ya kufuta kauli uliyokuwa ukizungumza kama hukubalikufuta unao ushahidi, wewe utasema, mimi nitaendelea nautaratibu wetu wa Kikanuni. (Kicheko)

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ushahidi wa kuibiwa kura tunao, ninao.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, WaheshimiwaWabunge kwa mujibu wa hizi Kanuni zetu na mambo ambayotunaweza kuzungumza humu ndani na sasa tunaelekeakukamilisha hili Bunge letu nataka kuamini kila mtu anaelewaKanuni zetu matakwa yake ni yapi?

Kwa kuwa Mheshimiwa Msigwa unao ushahidi wakuibiwa kura, na kwa kuwa huo ushahidi mimi hataungeniletea hapa sina uwezo wa kujua kama ni wa kweliama siyo utaenda kwenye Kamati ya Haki na Maadili iliukathibishe kule hiki ulichokisema hapa.

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

Kwa hiyo, kwa mchango wako wa sasa hayo manenoya kuibiwa hutarudia mpaka utakapoenda kuthibitisha kuleile Kamati italeta taarifa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: MheshimiwaMwenyekiti, sawa.

MWENYEKITI: Nadhani tumeelewana vizuri, manenoya kuhusu kuibiwa kura utaenda uthibitishe kule kwenyeKamati.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninachosema tunapata wapi legitimacy kama sisi wenyewehatuwezi kuishi yale tunayoyasema, Mheshimiwa Mpangokwenye Mpango wako.

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Taarifa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,democracy…

MHE. DKT. GODWIN O MOLLEL: Taarifa …

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Democracy ni kitu cha msingi ambacho…

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Taarifa …

MBUNGE FULANI: Taarifa ya nini?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa kuna taarifa.Mheshimiwa Dkt. Mollel.

T A A R I F A

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: MheshimiwaMwenyekiti, kiongozi mwenzangu hapa anajaribukuzungumzia legitimacy ya kuzungumza mambo ya kiadilifuna kufanya mambo ya kiadilifu. Lakini yeye kwenye Kambiyake, kwa maana ya Chama cha Chadema Wabunge wote

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

sasa hizi wamegoma kuchangia chama kwa sababu yaMwenyekiti wao kuiba milioni mia sita akiwa yeye ni mbebamkoba, akiwa yeye ni mmoja wapo wa wabeba mkobakwenye wizi huo na hata ruzuku haionekani na siasa ndaniya chama chake, ndani ya chama chake haiwezekani kwasababu hakuna resources na watu wote wamegomakuchangia na kusaidia chama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa anasema hata huo wizialitumwa na Chama cha Mapinduzi ufanyike na kwendakununua hizo shamba Morogoro na vitu vingine ambavyo nivya kibadhirifu vilivyoumiza chama chake.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa unaipokea taarifahiyo?

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nil itegemea utasema naye athibitishe kwa sababuanatuhuma watu kwamba wameiba.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa unazifahamuKanuni ametoa taarifa, Kanuni inayohusu taarifa ni Kanuniya 68 na uzuri tumeletewa na Mheshimiwa Spika hapa hunahaja ya kubeba makaratasi, fungua Kanuni yako soma ya 68amesimama kuhusu taarifa, unaipokea taarifa hiyo?

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,siipokei, his house kneegrow anyway.

MWENYEKITI: Eeeh! Halafu Mheshimiwa Msigwa,unajua tangu mwanzo nilikuwa nimekuacha na weweunafahamu hayo maneno huko kwenye nchi unayoisemayana maanisha nini. Na wewe unasoma vizuri huwezi kuitaMbunge mwingine kama kneegrow, kama wewe unatakakujiita kneegrow ni suala lako wewe.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Haja-complain.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa…

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Haja-complain

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa…

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Ehehe! Hamnaaliyelalamika.

MWENYEKITI: Natoa maelezo kuhusu jambounalotakiwa kulifanya ndio ninacho…

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Haja-complain…

MWENYEKITI: Naomba ukae, naomba ukae. Siyo sualala yeye ku-complain kazi yangu mimi kusimamia utaratibuhakuna Mbunge anayeweza kuitwa kneegrow humu ndanihayupo.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kasema Mbowe mwizi, kasema Mbowe mwizi, kasemaMbowe mwizi, umenyamaza,

MBUNGE FULANI: Mwizi.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,si umenyamaza alivyosema Mbowe mwizi…

MWENYEKITI: Mheshimiwa, Mheshimiwa Msigwatusibishane, nimesema nakuelekeza utaratibu, kama unatakakuusikiliza, sikiliza usijibizane na mimi. Nasema hizi manenohayo kule yanakotumika yana maanisha kitu kibaya sana nawala hakuna mtu anataka kuitwa hayo maneno. Humu ndanihawezi kuitwa Mbunge mwingine hayo maneno kama mtuamelalamika, ama hajalalamika kazi yangu kusimamiautaratibu na nilikuwa nimekuacha tangu mwanzo ili umalizemchango wako halafu nije niseme mwisho ana maanishanini, sasa kwa kuwa unaendelea kuyasisitiza hakuna Mtuanayeitwa jina hilo humu ndani, naomba uendelee namchango wako. (Makofi)

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mheshimiwa Mpango ninachokisema kwenye kitabu chakoulituambia utasimamia democracy, tunaongea miakamitano sasa tunamaliza kipindi chetu democracy ya nchi hiisasa hivi iko ICU, uhuru wa Vyombo vya habari ni disaster,waandishi wa habari wamekamatwa, wengine wamepotea,wengine hawawezi kujieleza, vyombo vingine vimekamatwa,Wabunge hawawezi kufanya mikutano kwenye majimboyao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kubenea kwamfano miaka miwili hawezi kufanya Mkutano, MheshimiwaHalima hawezi kufanya Mkutano, Mheshimiwa Sugu hawezikufanya Mkutano, Wabunge tunakatazwa, hii ndiyodemocracy inayosema kwenye Mipango ya miaka yakomitano, na ulivyokuwa unazungumza Bajeti ya mwisho hapaulinukuu mpaka maneno ya Mungu, ukasema Munguatusaidie, ukanukuu na vifungu vya Biblia, halafu ukasemawananchi wakachague wagombea wa Serikali za Mitaawanaotokana na Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo huu uchaguzi ambaounasema wakachague huu wa kupora, wa kupora kwanguvu, katika nchi ya kidemokrasia, hebu vaeni vitu vyetunimesema mna hiari mko wengi, leteni Muswada hapakwamba tunafuta mfumo wa Vyama vingi tusijidhalilisheDuniani kwamba tuna democracy wakati hakunademocracy. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnaogopa, mnawekampira kwapani halafu mnashangilia, tumeshinda,tumeshinda… Unaweza kuwa champion bila kushindana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, the finishing line is for thewinners, you cannot be a winner without competition, ingizenimpira hapa, tuweke Wagombea wetu na ninyi muweke,tuone mziki wananchi wanamtaka nani. (Makofi)

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka mitano mmetuzuia,mmetuzuia muone tutakavyocheza mpira uwanjani, how doyou call you self that you’re a champions. Watu wa Turkey,Waturuki wanasema when the fish is rocking it is start fromthe head. Hizi zote vurugu za Watendaji wa Mitaa na nini, nimatatizo ya Wizara, ni matatizo ya Serikali yenyewe, hiki kiburicha kufunga Ofisi cha kufanya nini, msitudanganye, nikwamba mmeona huko nje hali ni mbaya mlisema tumekufa,hatujafa, we are still standing. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mnajiaminishamnaweza njooni uwanjani tucheze mpira, i l i hayouliyoyasema yathibitike tuweze kuendesha nchi nzuri ambayoMungu ametupa, tusidanganye hapa, nakushukuru sana.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Nilikuwa nimeshamtajaMheshimiwa Dkt. Raphael Chegeni atafuatiwa naMheshimiwa Boniphace Mwita Getere. MheshimiwaMendrad Kigola ajiandae.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana, napenda niungane na wenzanguwote kwanza kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri waFedha, Naibu Waziri wa Fedha, pamoja na timu yote ambayowameandaa Mpango huu vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yawezekana hapa tunaongea lugha ambayo haieleweki tu, lakini Watanzania sasawanaelewa, hata Mheshimiwa ambaye amemalizakuzungumza sasa hivi anasema kwamba eti kwamba tunauademokrasia, demokrasia ni historia katika nchi yoyote ile,Watanzania sasa hivi naomba niwapeleke kwa statistics.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuanzia mwaka 2015/2016Uwekezaji kwa wananchi ilikuwa ni zaidi ya trilioni 29.5 .

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2016/2017 ukafikatrilioni 48.5, 2017/2018 trilioni 55.17, na sasa hivi hadi Juni 2019ni trilioni 59. (Makofi)

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii maana yake nini,translation yake Mheshimiwa ambaye alikuwa anazungumzahapa ni kwamba Watanzania sasa wameanza kuelewademokrasia ni maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Watanzaniawameelewa kwamba kupitia maendeleo haya sasawalichagua Serikali halali ya chama cha halali na ndiyomaana sasa hivi hata wagombea wengi hawajajitokeza kwasababu hiyo. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Eehhe!

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: MheshimiwaMwenyekiti, unajua tuseme kitu ambacho Watanzaniawanataka, hatutaki maneno na porojo, tunataka translationya uchumi katika maisha ya Mtanzania, na sasa hivi nchiinavyokwenda chini Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufulindani ya miaka minne, tumeona mambo mengi yamefanyikana ndiyo watu walikuwa wanahitaji hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo, mnaposemakwamba hakuna demokrasia, jamani, hivi demokrasia maanayake nini? Demokrasia ni kwa ajili ya watu, ni kwa ajili ya watuna kwa mahitaji ya watu, sasa leo Watanzania wameridhikana maendeleo yanayoendelea sasa hivi hapa nchini,tumesema ujenzi wa misingi ya uchumi. (Makofi)

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MBUNGE FULANI: Taarifa ya nini wewe….

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Chegeni kuna taarifa.Mheshimiwa Frank Mwakajoka.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kumpa taarifa mzungumzaji anasemawananchi wameridhika na ndiyo maana hawajajitokeza,lakini tunataka tumkumbushe tu kwamba sisi tumesimamisha

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

vitongoji vyote, Mitaa yote na Vijiji vyote nchi nzima, lakinipia hatutaki demokrasia anayosema kama ile ambayowalikuwa wananyang’anyana matokea na MheshimiwaKamani. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji demokrasia yahaki ambayo Mtanzania anataka kwenda kupiga kura,ahsante. (Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Chegeni unaipokeataarifa hiyo?

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: MheshimiwaMwenyekiti, naona siipokei. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu nazungumziahapa ni maendeleo ya Watanzania. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba leo hii, kamaumewekeza kwa kiwango hicho, maana yake ni kwambaWatanzania walichokitamani wanakipata, leo ukizungumziasuala la maendeleo, tunazungumzia katika Mpango huukwamba lazima tujenge misingi ya uchumi wa viwanda,maana yake nini, maana yake kwamba tujielekezeWatanzania sasa kumboresha Mtanzania na aweze kufikiakiwango cha kujenga uchumi wa viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu tupunguze porojo namaneno, Watanzania tumeongea sana, miaka nenda rudi,lakini ndani ya minne, tumefanya mambo makubwa sana,ambayo kila mmoja ana historia nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ninyi Wabunge wote,pamoja na mimi tukienda Majimboni kwetu tunaonamiundombinu iliyopo, hii ya Afya, Elimu, Maji, Barabara navyote vile, ni kwa sababu gani kumekuwa na usimamizi mzuriwa utekelezaji wa Mipango ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa wananchiwanachagua nini, wanachagua maendeleo, hawachagui

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

maneno, Watanzania wanachagua maendeleo, sasamnapoanza kulalamika kwamba hakuna demokrasia,nawashangaa wakati mwingine, hebu muanzie nyumbanikwenu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi mna demokrasia gani?Kwa sababu katika baadhi ya vyama hapa hakunademokrasia ndani ya vyama vyenu, lakini hamlalamiki, sasaniseme kwamba hebu tuji-focus kwenye Mpango wamaendeleo ambao una tija zaidi kwa Watanzania.

MBUNGE FULANI: Una demokrasia!

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: MheshimiwaMwenyekiti, katika Mpango huu ukiangalia mwaka huu pekeyake wa fedha tumetenga asilimia 37 ya Bajeti yote kwashughuli za maendeleo, hao ni Watanzania wanataka hayo,leo umepanga trilioni 12.2 kwa ajili ya Miradi ya maendeleo,na hii ni kwa Watanzania wote bila kujali wa chama gani, namaendeleo hayana chama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tu-translate ndotoya Mheshimiwa Rais na hii naomba Watendaji na Wasaidiziwote, ndoto ya Mheshimiwa Rais kutokana na Watanzaniasasa wanapata maisha bora, wanapata maendeleo yakiuchumi, wanasonga mbele, haya yote utayafanya ikiwasisi sote tutaenda katika mwendo ule ambao MheshimiwaRais anautazama, na mimi niseme kwamba lazima tufikeWatanzania tujifunze tufanye namna hiyo, lakini vilevile Miradiya Mikakati ambayo leo Watanzania tunaifanya, tumeonaMiradi mbalimbali haijafanyika, lakini tumeanzisha Miradimikubwa ambayo hatukuwa nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa na Mashirika mengiya Umma, tuliweza, na mengine yalikufa, menginehayakufanya vizuri, leo hii kupitia Wizara ya fedha, kupitiaOfisi ya Msajili wa Hazina na Kamati ya Uwekezaji tumewekavigezo, KPI ili kusudi uweze kupima mwenendo wa kila Shirikana Taasisi ya Serikali aidha inatoa huduma au inafanya

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

biashara, na lengo lake ni kwamba tuongeze mapato katikamapato yasiyotokana na Kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini kabisa kwambaWatanzania tukiimba wimbo mmoja tutafika safari yetutunayoitaka, lakini tukienda kwa safari hii ambayo kila mmojaanataka aimbe anavyotaka mwenyewe tutashindwa kufika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu tuangalie, naombatuangalie kwamba tunapaswa tujenge kesho, kesho iliyo borakwa Watanzania, unaijengaje kesho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kuijenga kupitia Miradiambayo lazima Watanzania tuisimamie, lakini katika Mpangohuu naomba tu Mheshimiwa Waziri wa Fedha naombatujipange kidogo, hasa kwa Wakulima, Mkulima analima zaolake akijua kwamba akishavuna aweze kuuza, na ndiyomaana ya kuweka mnyororo wa thamani, lakini vilevilekumfanya Mkulima apate tija na Kilimo chake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Mkulima anapolima naningeomba sana liingie hili katika Mpango unaokuja, Mkulimaanapolima awe na hakika ya kupata bei ya mazao yake ilihii Mkulima imtie moyo wa kuweza kuzalisha zaidi na tuongezetija katika Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mkulima wa pambaameuza pamba toka mwezi wa tano mpaka leo hii hajalipwapesa yake, halafu unataka mwaka aanze kufanya Kilimo tenakwa ajili ya mwaka kesho, hii si dalili njema, ninaomba sanawasimamizi ndani ya Serikali lisimamieni hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua kuna suala la sokohuria lakini kama Serikali lazima itoe guarantee kwa Mkulimahuyu au mazao yote, iwe ni Pamba, Korosho, Katani, Chaina mazao mengine yote ili Mkulima apate tija kile ambachoanataka kukizalisha, lakini pili Viwanda hivi vitajiendelezanamna gani. Lazima na guarantee ya mazao yanayotokanana Kilimo chetu, lazima tufungamanishe sasa ukuaji wauchumi na maendeleo ya watu. (Makofi)

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo lazima tulifanyekwa nguvu zote kwamba sasa hivi Mtanzania yule yuleafungamanishwe na maendeleo ili aweze kupata maishaambayo tunayohitaji, leo hii mkulima tumemsaidia sanakumwekea miundombinu ya barabara, umeme, maji,upande wa afya, sekta ya afya, upande wa elimu, Serikaliinatoa fedha nyingi kila mwaka, lakini yote haya sasa lazimayasimamiwe vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuombe sana MheshimiwaWaziri wa Fedha, mwanzoni nilikuwa sikuelewi elewi, lakininimeanza kwamba sasa kumbe wewe ni msimamizi mzurisana wa raslimali za Watanzania na ni mzalendo, na hataKatibu Mkuu wako wa Fedha na Naibu wa Waziri wako kwelimnafanya ya kizalendo. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Mwambie shikamoo…

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: MheshimiwaMwenyekiti, na ninaambiwa hapa niseme shikamoo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri waFedha, nakwambia hapa niseme shikamoo MheshimiwaWaziri wa Fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumzia Ofisi ya Msajiliwa Hazina, endelea kuimarisha, inachangia pato lisilotokanana kodi zaidi ya shilingi trilioni moja sasa hivi kwa mwaka.Ninaomba iwe ni ofisi ambayo inapewa kila aina ya supportkusudi itekeleze majukumu yake inavyotakiwa.

Mheshmiwa Mwenyekiti, vilevile Taasisi za Serikali naMashirika ya Umma, yafuate misingi ambayo imewekwa nakufanya hivyo nina imani tutaweza kufufua uchumi wa nchiyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie kwakusema kwamba Watanzania tunaanza kumwelewaMheshimiwa Rais, tuendelee kumwelewa. Makandokandomengine haya, naomba Watanzania tupate fursa ya

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

kuyazunguza, lakini kama ni Mpango, tuuzungumzie Mpangokwa malengo na maslahi mapana ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana naninaunga mkono hoja hii. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Nilikuwa nimemwitaMheshimiwa Boniphace Mwita Getere, hayupo; MheshimiwaMendrad Kigola, atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt. RashidChuachua na Mheshimiwa Moshi Selemani Kakoso, ajiandae.

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa kunipa nafasi nami niweze kutoamchango wangu wa mapendekezo ya Mpango kwa mwaka2020/2021.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze na jambomoja ambalo ni la msingi sana, kutoa pongezi kwa Rais wetumpendwa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoamaelekezo kwa zile Halmashauri mpya kuhamia kwawananchi ili kutoa huduma kwa wananchi kwa ujirani sanana hatua hizo zimeshaanza kutekelezwa. Nampngeza sana,nami Halmashauri yangu imeshahama tayari na wanafanyakazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, nawapongezawananchi wa Jimbo la Mufindi Kusini kwa kujiandikisha kupigakura. Wananchi wamejiandikisha vizuri kabisa na uchaguziambao wenzangu wanaongelea wa kidemokrasia, nadhanikwenye Jimbo langu hakuna tatizo na tunakwenda vizurikabisa. Nawapongeza sana wananchi wa Jimbo langu laMufindi Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ni mapendekezo yaMpango, nami napenda nitoe mapendekezo yangu. Kwanzanampongeza sana Mheshimiwa Waziri, pamoja naMheshimiwa Naibu Waziri na wafanyakazi wote kwa kazi nzurisana. Wameandaa Mpango sana. Nimesoma Mpango wikinzima na bahati nzuri niko kwenye Kamati ya Bajeti, tulikuwatunajadili pamoja, hakuna kitu walichoacha, kila kitu

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

kimeandikwa vizuri na ukisoma vizuri, maana kuna utekelezajiwa miaka mitatu iliyopita na kuna mapendekezo ya Mpangokwa miaka inayokuja, wamefanya vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe mapendekezokwa TARURA. TARURA wanafanya kazi vizuri na ukiangalia tafsriya TARURA ni Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini; naukiangalia kazi zao wanavyofanya, kwa upande wa mijinina wenyewe wanajenga hata barabara za lami. Ukiendavijijini wanajenga barabara zile za kokoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia ile bajeti,tukisema tunawapa asilimia 30, fedha ile haitoshi. Sasa hivinchi nzima barabara zinazoangaliwa ni zile ambazo ziko chiniya TARURA. Wenzetu wa TANROADS walifanya kazi vizuri,kutekeleza ile sera ya kuungalisha barabara za mikoa namikoa na wilaya na wilaya. Walifanya kazi nzuri sana nabarabara nyingi sana zimejengwa. Ukiangalia Tanzania nzimasasa hivi barabara za mikoa na wilaya zinapitika vizuri, lakinituna tatizo kubwa kwa barabara za vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwenye Mpango huumpya, naiomba Serikali ijielekeze sana kuiangalia TARURAkuweza kuiongezea uwezo ili wafanye kazi vizuri sana natuhakikishe kwamba barabara za vijijini zile zinapitika vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, naipongezaSerikali kwa ujenzi wa hospitali katika wilaya 67. Ni jambo jemasana. Hizi hospitali zitasaidia sana wananchi na zimeendakasi. Sasa zile hospitali ambazo Serikali ilitoa fedha, nawezanikasema kwamba wameshafikia asilimia kuanzia 80 mpaka90 kwa kujenga, lakini wakimaliza tu kujenga, naiomba Serikaliitazame, zile hospitali zianze kutumika mara moja haraka sanaili value for money ionekane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukijenga hospitali zikakaamuda mrefu bila kutumika, itakuwa ni kazi bure. Kwa speedhiyo tuliyojenga, iende sambamba sasa na ununuzi wa vifaavya hospitali, kuwaandaa watumishi ili waweze kufanya kazikatika hospitali zile. Kuna hospitali nyingi sana tuna tatizo la

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

vifaa vya hospitali. Kwa mfano, hata pale Mjini Mafinga, tunatatizo moja la X-Ray, hospitali haina X-Ray.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hospitali mpya hizimaandalizi ya vifaa yawepo ili kuhakikisha tunapomalizamajengo yote, watumishi na vifaa viwepo ili hospitali ianzekufanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni mikopo kwawanafunzi wa elimu ya juu. Serikali mwaka huu mmefanyavizuri sana. Kila ukimwuliza mwanafunzi anasema nimepataasilimia 100, asilimia 80, asilimia 90, Serikali imefanya vizuri,mikopo imeongezeka sana kwa wanafunzi. Nilikuwa nasomahapa, hao wanafunzi wa mwaka wa kwanza karibu 41,000wameshapata mikopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe pendekezomoja, kuna wanafunzi ambao wako mwaka wa pili na watatu, kuna wengi walikosa mikopa na mwaka huuhawajaomba; sasa wameona wenzao wamepata mikopoambao wamekuja kwa mwaka huu na wale wa mwaka wapili na wa tatu wana vigezo vya kupata mkopo; sasakufuatana na bajeti ilikuwa kidogo, hawakupata mikopo.Naiomba Serikali, basi wale wa mwaka wa pili na wa tatuwaruhusiwe sasa, wafungue dirisha ili waombe na wenyeweili wale ambao walikopa waweze kukopeshwa tena. Kunawanafunzi wanapata taabu sana wa mwaka wa pili na watatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo nichangamoto hasa na tumejadili sana hata kwenye Kamatini kumiliki akaunti za benki. Wananchi, hasa kwenye vikundi,imetuletea shida sana kwenye vikundi. Unaweza ukaonakikundi kina akaunti au kijiji kina akaunti, sasa kwa sababuwanaweka fedha kwa msimu, akiwa na fedha ndiyoanakwenda kuweka, kama hawana fedha wanawezawakakaa hata miezi sita hawajaweka fedha. Kwa hiyo,akaunti yao inaonekana iko dormant. Sasa ikiwa dormant,wakipata fedha, wakitaka kwenda kuweka tena kwa mara

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

ya pili (hata kwenye Vyama vya Ushirika hili tumeliona),wanasema akaunti yako imefungwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni tatizo kubwa sana,naomba, Waziri wa Fedha, awaambie mabenki, mtu akiwekaakaunti yake, kwa nini ifungwe? Kwa sababu akianza processupya, anasema nenda kachukue barua kwa Mwenyekiti,nenda sijui kwa Mtendaji, anaanza process upya. Hiyoinawakatika tamaa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasi Wabunge kwa mfanohata kwenye Mfuko wetu wa Jimbo ukitaka kupeleka fedhakijijini kwa ajili ya maandalizi ya kununua vifaa kule kijijini,utasikia akaunti imefungwa. Kwa hiyo, unashindwa kupelekafedha. Wananchi kule kuji-organize kuanza upya processinachukua muda mrefu na vijiji vyetu viko mbali sana na benki.Sasa naomba Mheshimiwa Waziri atoe tamko kwamba benkivile kusema kwamba akaunti ziko dormant, hilo neno lisiwepo.Mtu ameonyesha ID number tu, akaunti inakuwa active;akiweka hata shilingi 10,000/= au shilingi 20,000/=, akauntiinakuwa active kwa sababu details zote zinakuwepo pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala lingine, Benki Kuuwalifanya kitu kizuri sana katika kupunguza riba kwa mabenki.Ile ilikuwa kwamba, wanapunguza riba kwa mabenki ilimabenki yale yaweze kukopesha wananchi. Tunajua kulekwa wananchi kuna wafanyabiashara wadogo,wafanyabiashara wakubwa na wafanyabiashara mtu mmojammoja. Sasa impact kwa wananchi bado haijaonekana,yaani ile juhudi ya Serikali kuwaambia kwamba wapunguzeriba kwa mabeki ili ilete impact kwa wananchi na wenyewewale mabenki ya biashara yapunguze kwa wananchi,hayajafanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, wananchi badowanalalamika, riba ni kubwa sana, kubwa sana. Sasa na hilonaomba Serikali ifuatilie ili kuondoa malalamiko hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo lingine,nimeona kwenye Mpango, umekaa vizuri kuhusu masuala ya

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

umeme vijijini. Serikali imefanya kazi vizuri sana. Hata kwenyevijiji vyangu vyote, upimaji, survey imeshafanyika, ingawakuna vijiji vingine bado kupeleka nguzo. Kuna sehemunyingine nguzo zimelala tu chini, wananchi wanalalamika.Naomba twende speed. Tumesema mwaka 2021 vijiji vyotevitakuwa vimepata umeme, vitongoji vyote vitakuwavimepata umeme. Sasa ile kasi tuliyokuwa tumeanza nayomwanzo iendelee, maana tunaona sasa Makandarasi kamawanafifia hivi, wananchi wanashindwa kuelewa vizuri.Tuwahamasishe wafanye kazi vizuri, kwa sababu Serikali inalengo zuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wanasema kwamba,kuna vijiji wanapita bila kupingwa kwenye uchaguzi. Kwa niniwasipite bila kupingwa kama wanaona umeme uko tayaripale? Wananchi wanachotaka ni huduma kwa wananchi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanaona mtandao wanamaji, wako wako site. Ingawa kuna chagamoto ya maji, lakiniwatu wako site, sasa mtu atapinga nini? Wanaona majengoya shule ambayo yalikuwa hayajaisha yanamalizika,wanaona Vituo vya Afya vinajengwa, Hospitali za Wilaya zipo;sasa mtu atalalamika nini? Barabara zinajengwa, sasautalalamika kitu gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, isipokuwa, tuishauri Serikalikuongeza speed ya kuhakikisha kwamba mazingira bora kwawananchi yanakuwepo kujenga hospitali, kujenga Vitu vyaAfya, kujenga Zahanati, barabara, umeme; tukiimarisha haya,ndiyo maisha bora kwa jamii tunayoyataka. Tukisemakupunguza umasikini, maana yake tunaangalia vitu kwa jamiivipo? Hospitali zipo? Madawa yapo? Hivi vitu vinafanyika.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maendeleo ni process, usijeukasema utafika siku moja, ukasema sasa tumetosheka kilakitu tunacho. Hata ukienda nchi za wenzetu zilizoendelea,barabara wanajenga mpaka leo. Hata ukienda paleUingereza, London penyewe pale mjini, barabara mpaka leo

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

hii wanajenga. Ukienda hata Marekani, barabara mpaka leohii wanajenga. Kwa hiyo, hii ni process ya muda mrefu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu muda wanguumeisha, naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa MoshiSelemani Kakoso, atafuatiwa na Martha Umbulla,Mheshimiwa Salum Rehani, ajiandae.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuwa miongoni mwawanaochangia Mpango. Awali ya yote naishukuru sanaSerikali, namshukuru Mheshimiwa Waziri na wasaidizi wakekwa kuleta Mpango mzuri ambao unaonyesha dira yamaendeleo yetu. Katika mpango huu yapo ambayoyametekelezwa na Serikali, kimsingi tunaipongeza sanaSerikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunampongeza MheshimiwaRais kwa jitihada kubwa sana ambazo amezifanya zakuboresha vitu vingi ambavyo amevileta katika nchi yetu.Kwenye Mpango amezungumzia suala la miundombinu.Tumeshuhudia Serikali ikiboresha eneo la miundombinu kwaujenzi wa barabara karibu nchi nzima. Haya ni maendeleomakubwa sana na unapotaka maendeleo, kwanza rahisishashughuli za kuwafikia wananchi, lakini bado Serikali tumeonaikitekeleza miradi mikubwa, wameboresha viwanja vyandege karibu 11 ambavyo tunategemea vitarahisha sanashughuli ya uchukuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, Serikaliimenunua ndege ili ziweze kukuza Sekta ya Utalii, lakini kutoahuduma kwa wananchi. Serikali bado imeendelea kuwaonawananchi hasa wale wa chini, imekuja na Mpango wakununua au kujenga meli mpya kwenye maziwa makuu; ZiwaVictoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa. Haya ni maendeleomakubwa sana. (Makofi)

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii Ziwa Victoria kunaujenzi wa meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kuchukuaabiria 1,200 na karibu tani 400 za mizigo. Eneo hili watakuwawamewasaidia sana wananchi wa kanda ya ziwa, ambaokwa kipindi kirefu walikuwa wana shida kubwa ya usafiri wamajini. Vile vile kuna ukarabati wa meli ya MV. Victoria, hayani maendeleo makubwa sana katika kipindi kifupi. Tunaonamipango ambayo iliwasilishwa na Serikali ikitekelezwa kwaharaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo, badokwenye hiyo hiyo Sekta ya Uchukuzi, Serikali imeamua kusaidiaau kupanua ujenzi wa bandari pale Dar es Salaam. Bandariyetu il ikuwa na uwezo mdogo, leo hii tunashuhudiamaendeleo makubwa sana ya upanuzi wa Bandari ya Dares Salaam na tumeshuhudia nchi yetu ikipokea sasa melikubwa ambazo zinatua kwenye bandari yetu na kupakuamizigo ambayo haikutegemewa huko nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado tuna Bandari ya kuleMtwara, imepanuliwa. Tunaamini eneo lile la Kusini nalolitakuwa katika huduma kubwa ya maendeleo katika nchiyetu. Bado kuna upanuzi wa Bandari ya Tanga, ambayo nayoipo katika Mpango. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo la Kanda yaZiwa Victoria, kuna ujenzi wa kivuko kikubwa karibu kilomitatatu kutoka Busisi ambacho kitatoa huduma kubwa sana kwawananchi. Maeneo haya ni Serikali inatekeleza kwa ajili yakusaidia wananchi kukuza uchumi wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaipongeza sana Serikali,lakini tumeona mapinduzi makubwa sana katika nchi yetu.Ili uweze kuendelea, tunahitaji miundombinu na nishati yaumeme. Mheshimiwa Rais kwa nia nzuri ameamua kujengabwawa kubwa la umeme katika Mto Rufiji; bwawa lilemaarufu kwa kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Hili litakuwani eneo ambalo litawasaidia wananchi wote katika nchi yetu.Ninaomba hizi jitihada tuziunge mkono na tuangalie maeneo

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

mengine ambayo yalisahaulika yaweze kupelekewa miradiya umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kilimo. Tukitakakuwasaidia wananchi walio wengi, baada ya Serikali kuwekamiundombinu, karibu maeneo yote, sasa Mheshimiwa Dkt.Mpango elekeza mawazo yako ukuze Sekta ya Kilimoambayo inawaguza wananchi wote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo hili natoaushauri, kwanza Serikali ianze kufikiria kutoa ruzuku kwenyemazao ya korosho, pamba, chai, tumbaku na yale mazaomakubwa ambayo yanatuletea fedha za kigeni kwa wingi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yeyote ile iliyoendeleainawasaidia sana wananchi hasa wakulima kuwezakushindana kwenye ushindani. Pale mazao yanapokuwayameanguka, lazima Serikali iweze kuwasaidia hawawananchi wapate nguvu, lakini wasiposaidiwa watakuwa namaeneo mabaya ambayo yatawafikisha kutokufanya kazina kuachana na hayo mazao ambayo yalikuwayakiwaingizia kipato. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie zao la pambaambalo linazalishwa wilayani kwangu. Zao la pambawananchi walilichukulia kwamba ni zao ambalo ni sasalingewatoa kwenye umasikini na wamezalisha kwa kiwangokikubwa na pamba nzuri, kuzidi hata ile iliyokuwa inazalishwaambako imetoka mbegu zake maeneo ya ukanda wa ziwa,lakini mpaka sasa wakulima bado hawajauza pamba, ikomajumbani kwao. Naomba eneo hili mkalifanyie kazi,mboreshe ili wananchi waweze kupata huduma inayostahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zao lingine ni tumbaku. Nchiyetu ilikuwa inapata fedha nyingi kupitia zao la tumbaku. Kwabahati mbaya sana mwaka huu yapo makampuni ambayoyalikuwa yananunua tumbaku kwenye nchi yetu kampunikama TLC lakini imeacha kununua zao hili. Tuna mikoa zaidiya 12 inayozalisha zao la Tumbaku ukiwemo na Mkoa wa

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

Kigoma ambapo Mheshimiwa Waziri ametoka wananchihawana mahali ambapo watauza tumbaku walizokuwawanazalisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashauri sasa Serikaliiangalie eneo la Kitengo cha Masoko, kwenye masoko badohamjapaangalia. Tunahamasisha kilimo lakini kuwatafutiawakulima masoko bado Serikali haiajawekeza kwa kiasi chakutosha. Niombe eneo hili nendeni mkalifanyie kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na kuboreshaeneo la masoko pia ni muhimu kuboresha mazao ya chakulaambapo mkiwasaidia hawa wakulima na mkawawekeamazingira mazuri ya masoko kilimo ni eneo ambalo litaajiriwananchi wengi na Serikali itakuwa inanufaika kupitiahuduma mbalimbali na kodi zitakazokuwa zinatokana naupatikanaji wa fedha. Tunaomba sana hapa Serikalimkapafanyie kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalotunapenda kushauri Serikali ni kwenye …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Muda umekwisha, ahsante sanaMheshimiwa.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Salum Rehani atafuatiwa na Mheshimiwa MirajiMtaturu, Mheshimiwa Engineer Gerson Lwenge ajiandae.

MHE. SALUM MWINYI REHANI: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii kuchangiakatika Mpango huu wa Taifa.

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuruMheshimiwa Waziri na Menejimenti yote ya Wizara kwa kuletahuu Mpango ambao tunataka tuone ni dira ambayo inawezaikatuondoa tulipo na kuelekea kwingine ambako tutakuwana taswira mpya ya kuifanya Tanzania hii iwe ni nchi yauchumi wa kati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi nataka nizungumziemaeneo yale ambayo tunayaita economic tools ambapotukiyatumia tunaweza kufikia kwenye huo uchumi wa katimbali na miundombinu na miradi ya kimkakati ambayoinatekelezwa na Taifa. Sina tatizo na miradi yote ya Serikaliiliyokuwa imeipanga ya kimkakati, ile miradi mikubwakwamba itakuwa ni sehemu ya kuifanya Taifa hili liwezekuelekea huko kwenye uchumi wa kati lakini napenda zaidiniishauri Serikali kwani kuna maeneo lazima tutoe lawamakwa kitu ambacho hakijafanyika ili Serikali wasikilize ushauriambapo utasaidia kutoka kuliko kuendelea kubaki kamatulivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa sekta yamifugo, Tanzania mbali ya kuwa ni nchi ya pili kwa mifugolakini bado sekta hii haijafanikiwa. Nimepitia Mpango huuhapa sijaona maeneo thabiti ambayo tunaweza kufaidikana mifugo lakini na fursa ya ufugaji hapa nchini. Kuchungatunakochunga hakutusaidii chochote hardly penginetunakwenda kwenye 2% or 3%. Tunataka tuone Wizara yaMifugo imejikita katika kuhakikisha kwamba inapeleka mfumowa artificial insemination vijijini ili kubadilisha aina ya ufugajikwanza, ili kubadilisha ng’ombe waliokuwepo kule ambaowana uwezo wa kutoa nusu lita na lita moja ya maziwa nawaende kuwa ng’ombe ambao wanatoa zaidi ya lita 20 nakuendelea, hilo linawezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo,tunataka kuona maziwa haya ambayo yanaweza kuzalishwandani ya nchi yanafaidisha nchi. Biashara ya maziwa wenzetuwa Zimbabwe ni sehemu ya uchumi wao mkubwa sana nakwa kipindi kile ilikuwa unachangia zaidi ya asilimia 12 lakinisisi Watanzania tumekuwa ni sehemu ya wanunuzi wakubwa

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

wa maziwa kutoka maeneo ya Zimbabwe na sehemunyingine wakati ndani ya nchi hapa tunaweza kuzalishamaziwa na kuuza na kuyatumia kwa matumizi yetu nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niiombe Serikali na Wizaraya Mipango tuwe na Mpango madhubuti na maalum wakuhakikisha kwamba tunaweza ku-handle maziwa ambayoyako zaidi ya lita milioni mbili kwa siku yanayozalishwayageuzwe kuwa bidhaa ambazo zinatumika katika maeneoyetu mbalimbali. Mimi niseme wazi nasikitika sana na mfumowa biashara ya kupokea maziwa mengi sana kutoka kwamajirani zetu kuingizwa ndani ya nchi kuliko maziwayanayozalishwa hapa nchini. Ni kitu gani ambachokinatushinda kuweza kuwa na viwanda ambavyo vinawezakuchakata maziwa ambayo yako hapa nchini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafahamu handling yake nigharama, sasa Serikali pamoja na miradi mikubwa ambayoinaifanya ielekeze nguvu sasa katika eneo hili ambapo rawmaterial yake ipo ndani ya nchi ya kutosha na tuache mfumohuu uliopo sasa. Nafikiri iwekwe kodi maalum kubwa yakudhibiti uingizwaji wa maziwa kutoka nje ili watu wawezekutumia maziwa yaliyoko hapa nchini. Mkiwauliza watu waMifugo, hata jana nilionana na Profesa Katibu Mkuu waWizara ya Mifugo bado anasema hakujawa na engagementya fedha ambazo zinakwenda kutengeneza mitamba yakutosha ambapo tutaisambaza katika maeneo yetumbalimbali na kubadilisha taswira ya ufugaji kuwa wa kisasazaidi kuliko kuendelea kuchunga ambapo tunasababishaugomvi wa wakulima na wafugaji uliokuwa hauna sababuwakati njia rahisi ya kutumia teknolojia ya kisasa ya ufugajiipo na hatujaitumia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, vilevile nilikuwanaangalia Mpango Mheshimiwa Dkt. Mpango kwa mara yatatu niseme kwamba bado hatujatumia bahari iliyokuwepondani ya nchi hii. Katika dunia hii watu wote wanatushangaa,Mheshimiwa Dkt. Mpango kinachoniuma zaidi nilipata fursaya kwenda Comoro kama miezi mitatu iliyopita. Comoro waokama kisiwa wameanza kufaidika na blue sea sisi kwetu bado.

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

Tuna suffer na 0.4 imekimbiza meli zote, tuna fursa ya kuifanyaSUMATRA iweze kukusanya karibu shilingi milioni 40 kwa kilameli iliyokuja kufanyiwa inspection ya kwenda kwenye uvuviwa bahari kuu na zaidi ya meli 200 hapa duniani zinatakakuja kuchukua leseni lakini kuna kikwazo hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile niombe Serikalibadala ya kuelekeza nguvu zaidi katika maeneo ya uwekezajiwa reli, umeme na uwekezaji mwingine wowote mkubwa i-engage pesa maalum kwa ajili ya blue sea. I will promiseBunge hili ndani ya miaka miwili break even ambayoitapatikana kutoka katika bahari hakuna sehemu yoyote yauchumi ambayo itaweza ku-compete. Fedha ziko nyingi naziko nje nje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii tunachosema hapademand inaendelea kuongezeka na kinachofanyika dunianitunatengenewa artificial fish siyo samaki halisi tunaoletewakwenye makontena hapa na Watanzania tunakula wakatituna bahari ya kutosha na bado tumeomba kuongezewaeneo la nautical miles 150 la nini sasa kama hatuwekezi?Kama tumeomba tuongezewe eneo basi tuiombe Serikaliiwekeze katika bahari ile tuoneshe kwamba na sisi tunayopotential ya kuitumia bahari hii iliyokuwepo hapa na Mungualiyotujalia tuweze kuleta mabadiliko chanya na tuendekwenye uchumi wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe sana kamawanavyoweza kufaidika watu wa Namibia kwa zaidi yaasilimia 11 ya uchumi wao GDP wanategemea samakiambao wanapenya tu katika mlango mmoja waMozambique Current kwenda katika eneo la Namibia nawanaweza kupata fedha ambazo zinaweza kuongezea GDPzaidi ya asilimia 11. South Africa pamoja na uchumi waomkubwa lakini 8% wanapata fedha kutoka bahari,tunachoshindwa Tanzania ni nini? Mimi nimeuona Mpangohalisi huu hapa lakini sijaona mkakati ambao tunaelekeakwenye bahari kuu na kuifanya nchi hii ni sehemu ya nchiambazo zinauza samaki nchi za nje. (Makofi)

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala zima la kilimo.Nchi hii tumejaliwa kuwa na maeneo mengi mengi ya kilimolakini pamoja na kuwepo na miradi ya SPDII ambayo mpakasasa hivi hatujaona uendelezwaji wake na kufanya kazi katikamaeneo ambayo yanaweza kuleta mabadiliko hayo chanya.Bado mwendo wake nauona unasuasua ingawaje mradi sasahivi umeshafikia miaka miwili. Ushauri wangu uko hapa, Serikaliinatakiwa iwekeze kwenye kilimo cha umwagiliaji maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile niombe Serikali kitukimoja, mfumo uliopo hivi sasa wa kujenga canal irrigationhautusaidii kitu, unakula fedha nyingi na unachukua mudakumalizika na wakandarasi ndiyo sehemu ambayowanaweza kupata pesa bila ya sababu.

Kwa ushauri wangu mimi tuzuie fedha zotezinazokwendwa kwenye canal irrigation ambapo tunawezatuka-save zaidi ya asilimia 70 kwa kutumia pipe irrigationambazo unaweza kuwekeza kwa muda mfupi tu. Wiki mbilitu unajenga zaidi ya hekta 200 au 100 kwa kutandikamabomba ukaweza kuhifadhi maji na akatumia maji ambayohayawezi kupotea. Tukitumia mfumo huo tuaweza ku-controlile wanaita Evapo-transpiration lakini vilevile contaminationya wadudu, maradhi, magugu na vitu vingine vyotetutaepuka. Hiyo ndiyo teknolojia tunayotaka twende nadunia huko ndiko iliko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kuendelea kujengamitaro kwa mawe na saruji ambayo baada ya mudawakandarasi wanapiga hiyo pesa na hakunakinachoendelea, niseme wazi kwamba huko sioni kama kunatija na hakuwezi kutufikisha. Tutumie njia rahisi ambapotutaweza kuzalisha na kuyatumia maji effectively kuliko hivisasa. Kwa hiyo, niiombe sana Serikali katika mipango yetuyote hizi billions of money zinazokwenda kwa ajili yakutengeneza canal za irrigation tuelekeze kwenye pipeirrigation ambacho ndicho kilimo cha kileo zaidi kuliko hukutunakokwenda.

MWENYEKITI: Muda wako umeisha Mheshimiwa.

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante, naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Nilikuwa nimeshamwitaMheshimiwa Miraji Mtaturu atafuatiwa na Mheshimiwa Eng.Gerson Lwenge, Mheshimiwa Justin Monko ajiandae.

MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikushukuru sana kwa kunipa nafasi ili na mimi niwezekuchangia katika hoja ambayo iko mezani. Kwa sababu leoitakuwa ni siku ya kwanza kuchangia naomba nimshukurusana Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi na uhai wa kuwezakuchangia hoja hii ambapo naishauri Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwanza kwakumpongeza sana Mheshimiwa Waziri pamoja na timu yakeya Wizara nzima, Naibu Waziri pamoja na Katibu Mkuu nawatendaji wote kwa kuandaa na kutuletea Mpango huuambao kwa kweli ni Mpango ambao umeendeleakutuonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kuwaleteaWatanzania maendeleo. Naomba nichukue nafasi hiikuwapongeza na naomba niseme tu kwamba tutaendeleakutoa ushauri ambao utakuwa na tija kwa ajili ya kuletamaendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwambaMpango wenyewe huu unakwenda kumalizia katika Mpangowa Miaka Mitano ninajua mambo mengi yako dhahiriambayo yameonekana yameshafanyika. Zaidi niseme tukwamba kuwa na Mpango ni jambo moja lakini kuusimamiana kuutekeleza ni jambo la pili. Kwa hiyo, sisi kwenye hilitunawapongeza kwa sababu tumekuwa na Mpango na sasatunaona namna ambavyo kwa muda huu unaendakumalizika mwaka wa tano mafanikio makubwa katikamaendeleo ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii kwa kwelikwa dhati kabisa kumpongeza sana Rais wetu, MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli kwa namna ambavyo ameoneshadhamira ya dhati katika kuhakikisha kwamba anawaletea

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

wananchi maendeleo. Najua kwamba utashi wake ndiyoambao unatupa hata jeuri au inaipa jeuri Serikali kuhakikishainafanya kazi vizuri kwa sababu tumekuwa tukipata fedhaya kuweza kutekeleza miradi hiyo. Tunaweza tukawa namipango mizuri sana isipowezeshwa itakuwa ni kazi bure naitakuwa inabaki kwenye vitabu kama ambavyo tumekuwatukiona baadhi ya maeneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba maeneomengi ambayo naweza kuyasema ni yale ambayo nasemakwamba tumeanza kuona dhamira ya Serikali katikakukusanya mapato. Unaweza ukawa na mpango mzuri lakiniukawa hauna fedha lakini ukiwa na mpango mzuri ikiwa nipamoja na kukusanya mapato inakusaidia wewe kuhakikishakwamba unatimiza malengo ambayo yako mbele yetu.Jambo kubwa ambalo ni vizuri tukalisema ni dhamira ile yakusimamia na kuzuia mianya yote ya kukwepa kodi katikanchi yetu. Siyo hivyo tu ni pamoja na kusimamia nakutokomeza kabisa rushwa katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika baadhi ya maeneoambayo tulikuwa tunateseka sana ni pale ambapo baadhiya watumishi ambao hawana dhamira njema wamekuwahawafanyi vizuri sana katika kusimamia mapato yetu. Kwenyehili, naomba niipongeze Serikali kwa namna ambavyoimesimamia na imeendelea kuongeza mapato katika nchiyetu yanayonifanya tuweze kutekeleza mipango ambaotunajipangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo yotenieleze sasa yale ambayo yanaonekana waziwazi. Tumeonanamna ambavyo tunaboresha sana miundombinu yabarabara ambayo kwa kweli imekuwa ndiyo nguzo kuu yauchumi wa nchi yetu. Niseme hapa katika mpango nimeonanamna ambavyo mwaka huu ambapo tunaelekea kwenyebajeti tutaenda kujikita katika kuongeza fedha ambazozinakwenda kuongeza uwezo wa kujenga barabara zetuikiwa ni barabara za lami na madaraja makubwa nakadhalika. Niombe tu kwamba haya ambayo yamepangwa

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

basi yawekwe vizuri kwa ajili ya kutoa fedha ili tuweze kuonamiradi hiyo inaweza kufanikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, si hivyo tumeona reli ya SGRinajengwa. Ni dhamira ya dhati tuliamua kama Taifa na leotunavyoona speed ni kubwa sana tuko zaidi ya asilimia 60 yautekelezaji wa mradi. Kwa hiyo, niseme tu kwamba hii nayoitakuwa ni kichocheo muhimu katika uchumi na usafirishajiwa mizigo ikiwa ni pamoja na kupunguza bei ya bidhaasokoni. Bei ya bidhaa ikipungua maana yake itamsaidiamwananchi wa kawaida kuweza kupunguza mfumuko wabei kwa sababu bei itakuwa chini katika usafirishaji wa mizigo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo yotehatutaacha kusema maneno machache kwenye sehemuya uboreshaji wa ununuzi wa ndege. Hili jambo tusipolisemana dhamira ya dhati ikaonekana maana wenginewamekuwa wakipotosha eti wanathaminisha ndegewanasema vingejengwa vituo vya afya kadhaa. Niseme tukama Taifa lazima tuamue nini cha kufanya, huwezi kusemaunaogopa kununua shati jipya kwa sababu huna utoshelevuwa kubadilisha kula mboga, huwezi kuogopa hilo, lazimauamue kwamba ndege zinazonunuliwa zinaenda kuongezauwezo wetu wa kuweza kuhudumia sekta ya utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wote tumekuwa tukiona natukilalamika na mimi nimekuwa nikiwaona WaheshimiwaWabunge wanasema ndani ya Bunge kwamba haiwezekaniwatalii washukie Kenya waletwe kwa magari kuja kwenyembuga zetu na baadaye warudi wakapandie Kenya kwashirika lingine la ndege. Leo tunapata ndege maana yaketuna uwezo sasa wa watalii wale wote kushuka kwenyeviwanja vyetu ndani ya nchi yetu na wanakwenda moja kwamoja kwenye utalii. Utalii ndiyo sekta ambayo inaongozakatika mapato katika nchi yetu. Kwa hiyo, tunapoboreshaShirika la Ndege maana yake moja kwa moja tunaiboreshahii sekta ya utalii ambayo ndiyo inaleta fedha nyingi ambapomwisho wa siku itajenga vituo vya afya, shule, itaboreshaelimu bure pamoja na mambo mengine. (Makofi)

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Taifa lazima tujivuniekwa sababu lazima nchi isonge mbele kwa kuwekeza kwenyemambo makubwa. Kwa hiyo, hatuwezi kuwa sisi wenyewetunafanya mambo makubwa lakini hatujui kama tunafanyamambo makubwa. Hii haitatujenga kama Taifa, Watanzaniatuipende nchi yetu kwa yale makubwa mazuritunayoyafanya. Tofauti ya vyama vya siasa isitufanyetuondoke kwenye reli, lazima tujivunie na sasa hivi tunaonaATCL wanafanya vizuri, Mheshimiwa Waziri anayehusika nasekta hii yupo pale kwa kweli kazi inafanyika vizuri na sisi kamaWaheshimiwa Wabunge ni lazima tuunge mkono juhudikubwa hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kueleza maelezohaya, kabla muda wangu haujaisha, nitoe manenomachache ya ushauri kwenye suala la kilimo. WaheshimiwaWabunge wengi wamesema, lakini naomba na mimi nielezekidogo, asilimia 80 ya wananchi wetu wanafanya kilimo.Kama kweli tutaweza kuwekeza kwa dhamira ya dhati katikakilimo itasaidia sana kutuongezea pato la Taifa lakini itasaidiauchumi wa mwananchi mdogo kule chini chini, wakati wakutegemea msimu wa mvua umepitwa na wakati, tuongezenguvu katika kilimo cha umwagiliaji na zaidi tuongeze uwezowetu wa kusimamia miradi hiyo na itoe matokeo, katikabaadhi ya maeneo tuweze kuvuna zaidi ya mara mbili ilitukipata mapato ya kutosha kwenye eneo hili itasaidia hatamapato ya ndani katika halmashauri zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halmashauri zetu nyingizinategemea mazao katika mapato, tukiwekeza kwenyekilimo naamini kabisa tutaenda kuongeza uwezo wawananchi wetu na kipato chao katika kaya. Kipato cha kayakikifanikiwa ndiyo tutasaidia kwenda kwenye huo uchumi wakati ambao tunausema kwa sababu tunaangalia natunatathimini namna ambavyo mwananchi anajipatiakipato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiondoka kwenye eneohilo, niende sasa kwenye eneo la pili la miundombinu.Tunaamini zile barabara kubwa zile trunk roads zinajengwa

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

kwa kiwango cha lami, lakini nieleze kidogo kwenyebarabara ambazo ziko chini ya TARURA. TARURA wamekuwawakitengewa fedha kidogo sana naamini wanataka kujengamadaraja, wanataka kuongeza uwezo wa ujengaji wabarabara zao, lakini fedha wanazopata ni ndogo sana hazinauwezo wa kututoa pale na ile dhamira ya kuanzisha hiiagency haitakuwepo kama hatutawapa fedha za kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niombe sanakwenye mpango huu naona imeguswa na imewekwa, lakininaona kabisa namna ambavyo mfano kama Wilaya ya Ikungipale, zipo barabara ndevu lakini nyingi hazijawahikutengenezwa, ni barabara za asili kama mapalio, naaminikabisa Mheshimiwa Waziri ananielewa ninavyoeeleza hayo,kwa sababu TARURA huwa wanaleta maombi yao nayamekuwa wakipata fedha kidogo sana, wakati ambapobarabara hizi zikijengwa zitasaidia kusogeza mbele suala lakuleta maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikimalizia kwenye eneo laumeme juhudi naziona ni nzuri sana, nipongeze sana Serikalikwa namna ambavyo wizara imeendelea kusimamiaupatikanaji wa umeme kwa kupitia miradi ya REA, tatizokubwa ambalo naliona lipo kwa wakandarasi, wakandarasiwamekuwa hawatekelezi miradi kulingana na mikataba yao,wakandarasi wengine wanalalamikiwa hata na wafanyakaziwao, hivyo inasababisha kufifisha juhudi za kuwapelekeawananchi umeme, kwenye eneo hili ni vizuri Serikali kupitiaWizara husika waweze kusaidia kuhakikisha kwambawananchi wanapatiwa umeme mapema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ndogoambayo ipo pia ni maeneo yale ambayo wanasemakwamba wanapelekewa umeme kwenye vij i j i lakiniwanapelekewa vijiji ambavyo viko pale pale centre, umemehauendi mpaka kwenye vitongoji. Inawezekana dhamira yaSerikali ni hiyo, lakini imekuwa tunavuka baadhi ya vitongoji,jambo hili linatuweka kwenye wakati mgumu ambapotunakosa majibu, wakati hamu ya wananchi ya kupataumeme ni ya hali ya juu. Baada ya maneno haya, naomba

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

tu niendelee kusema CCM hatujakataa kuingia uwanjani,tuko tayari, lakini naomba pia na wao wafuate mwongozouliowekwa ili waingie uwanjani wakiwa salama. Huwezikuingia uwanjani huna viatu wakati wenzako wanaingia naviatu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkonohoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa EngineerGerson Lwenge atafuatiwa na Mheshimiwa Justin Monki,Mheshimiwa Augustino Manyanda Masele ajiandae.

MHE. ENG. GERSON H. LWENGE: MheshimiwaMwenyekiti, nianze kwanza kwa kumpongeza sanaMheshimiwa Dkt. Mpango kwa hotuba yake nzuri na kwakuwasilisha Mpango mzuri ambao ni sehemu wa miakamitano ambao tulipitisha Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyonampongeza sana. Pia naomba nipongeze sana Serikali yaAwamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. JohnPombe Magufuli kwa kazi nzuri ambayo kila moja anaona.Kwabhiyo hata kama yupo anayebeza, anabeza kwasababu zake, lakini vitu vinavyofanyika vinaonekana waziwazi. Kwa hiyo niwapongezeni sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu nitajikitazaidi kwenye suala la miundombinu. Katika Mpango ambaoumewasilishwa, vipaumbele vimewekwa lakini katika hivivipaumbele kuna eneo la ujenzi wa barabara za lami na nchinzima tumeona barabara za lami zinajengwa, barabara zamkoa na barabara kuu zinazounganisha kati ya mkoa namkoa. Naomba sana kwamba ili kusudi barabara hizi ziwezekudumu ni lazima tuweke mkakati mzuri wa matengenezoyake, tuongeze bajeti ya matengenezo ya barabara hizi iliisiwe barabara inajengwa baada ya miaka miwili inafumuliwatena inajengwa nyingine. Ili tuweze kufikia maeneo yote yanch, tuwe na mkakati mzuri wa matengenezo. Kwa hiyo,naomba sana Serikali iongeze fedha kwenye fuel levy kwaajili ya kupeleka Wakala wa TANROADS na TARURA ilibarabara zetu ziweze kujengwa. Tumeanzisha TARURA

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

tukiamini kwamba TANROADS ilifanya kazi nzuri, lakini ilifanyakazi nzuri kwa sababu tuliweka fedha ya kutosha yamatengenezo, kwa hiyo tuweke nguvu sana kwenyematengenezo ya barabara zetu hizi ili ziwe sustained.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia naomba Mkoawetu wa Njombe ukumbukwe kwenye barabara kuu ambazoni muhimu ambazo hazijawekwa kujengwa kwa lami, kwamfano, kwa barabara inayotoka Njombe Makete ifike mpakaMbeya na barabara kutoka pale Ramadhani ifike mpakaLyai iunganishe na barabara kuu ya Tazam highway.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba sana katikampango huu tumeona kwamba kuna usambazaji wa umemevijijini na kazi nzuri sana inafanyika. Mwaka jana nimechangia,nilisema katika usambazaji wa umeme maeneo mengiambayo hata yameshajengewa miundombinu yamekuwasiyo sustained kwa sababu kwa muda mfupi unakuta nguzozimeanguka au transform zimeungua, lakini sababu kubwakwamba hatuweki bajeti kubwa ya matengeneo. Kwa hiyonaomba sana tuweke bajeti kubwa ya matengenezo katikamiundombinu ya umeme ili kwamba hivi vijiji vyote zaidi ya8,000 vimepata umeme, basi tufurahie kwambatumeshapata maendeleo unajua mambo ya miundombinuni kama mishipa ya damu ndiyo uhai wa mwili wamwanadamu, basi miundombinu hiyo tuliyoijenga kwenyeTaifa letu ni lazima iwe imewezeshwa sana hasa kwenye eneohili la matengenezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo natakanichangie ni suala la Mradi wa Liganga na Mchuchuma.Mwaka jana pia wengi wamechangia, mradi huutumeuzungumza miaka mingi toka mwaka wa kwanza waMpango huu tumezungumza Mradi wa Liganga naMchuchuma lakini mpaka leo hakuoneshi progress naaminikatika hii sehemu ya mwisho ya mpango huu tutaweka nguvukubwa, kama ni mradi wa kielelezo, kama ni mradi wakipaumbele tuone utekelezaji wake tusiishie kusikia badohatujalipwa hata fidia, sasa huu mradi kama kweli tumeamuakuujenga tuweke nguvu. Taifa lolote haliwezi kuendelea

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

kama hakuna chuma, chuma ndiyo malighafi mama yaviwanda na sisi ndiyo tunasema tunajenga uchumi waviwanda, kwa hiyo lazima tuweke nguvu katika kutekelezaMradi huu wa Liganga na mchuchuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo natakanilizungumzie, ni sekta ya afya. Ni kweli Rais wetu ameamuakwa nguvu kubwa kujenga vituo vya afya 352 na hospitali zawilaya 69, ni jambo jema mimi nampongeza sana. Naaminikabisa Taifa lolote lazima na watu wenye afya uwe nampango mzuri kwa ajili ya kuhakikisha Watanzania wanapatatiba iliyoboreka, kwa hiyo naomba sana awamu hii katikaMpango huu pia tuweke nguvu kujenga vituo vingi zaidi.Wananchi wetu katika maeneo mengi tuliwahamasisha,wamejenga zahanati kila kijiji na maeneo mengi kila katawamejenga vituo vya afya, lakini wamefika mahaliwamekwama, yale maboma yamebaki mpaka leo miakamitano, miaka sita, basi katika mpango huu naomba sanaSerikali iangalie namna ya kukamilisha hata angalau hizozahanati wananchi wamechangia waendelee kuwa naimani na Serikali ili angalau kila kijiji wawe wanaweza kupatahuduma ya msingi katika hili suala la afya. Pia huu mpangowa bima ya afya kwa wote, naomba uletwe haraka, ni jambomoja nzuri litakalowasaidia Watanzania kupata afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalotakakuongelea, ni suala la kujenga uwezo wa makandarasi wetundani najua miradi mingi inatekelezwa na makandarasi namiradi mikubwa mingi tunatoa kandarasi kwa makandarasikutoka nje. Tulianzisha Bodi ya Usajili wa Makandarasi ilituweze kuinua uwezo wa wakandarasi wetu. Ile bodi inakazi ya kusajili pia na kufuta, kama kuna wakandarasihawaendi sawasawa na maadili ya ukandarasi ile bodi inauwezo wa kufuta, kwa hiyo tusiogope kuwawezeshawakandarasi wetu kupata kazi. Suala kubwa ni kwamba kwasababu naamini kabisa wapo wakandarasi ambao wapodaraja la kwanza, kwa maana kwamba kazi yoyote ileinaweza hata ile Stiegler’s gorge lingeweza kujengwakujengwa na wakandarasi wetu wa daraja la kwanza,kinachohitajika ni kuwasimamia na kwamba pale ambapo

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

wakandarasi wamefanya kazi, wawe wanalipwa kwa wakati.Wengi wameshindwa kuendelea na kazi ya ukandarasi ni kwasababu Serikali imekuwa inachelewa kuwalipa kwa kaziambazo wamekuwa wamefanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kama anakaamiaka miwili, miaka mitatu hajalipwa baadaye tunaanzakusema yule mkandarasi ni mwizi kumbe hajalipwa, kwa hiyonaomba Serikali jambo hili ijaribu kuangalia ili wakandarasiwetu na kwa kweli tutafurahi sana kama kila kazi itafanywana wakandarasi wetu wa ndani. Nadhani hata ukiendaChina sehemu kubwa ya wakandarasi wanaofanya kazikwao kule ni wao wenyewe wa China, hakuna Watanzaniawanafanya kazi kule China. Sasa na sisi Taifa letu la uchumiwa viwanda lazima tufike mahali kazi zote zifanywe nawakandarasi wetu wa wazalendo ili tuwezeshe Mfuko huuutoke kutoka Serikalini uende kwa watu wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonataka kuongelea ni suala la kilimo. Ni kweli tunajengauchumi wa viwanda, lakini uchumi wa viwanda kamahatujainua kilimo, hautakuwa na manufaa kwa sababutunajenga reli sawa, lakini mazao ya kupitisha pale yatatokawapi. Kwa hiyo ni lazima tuwe na mkakati wa kutoshakuhakikisha kwamba kilimo chetu kinakua. Tuwe na pambaya kutosha ya kuitoa Mwanza kuleta bandarini na tukauzanje, tuwe na chai ya kutosha na mazao mengine ambayotumeweka ni ya kimkakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nafikiri jambolingine la kuangalia ni katika kuwezesha wakulima wetuwapate mbolea kwa wakati, lakini mbolea kwa bei elekeziambayo Serikali imeshaianzisha, naipongeza mpaka sasawanakwenda vizuri lakini nafikiri tufanye vizuri zaidi, tuangalieyale maeneo ambayo yalikuwa ni matatizo basi sasa hivituweze kuyaboresha ili wananchi wetu wapate mbolea kwawakati na mbegu ili kilimo hiki kiweze kukua. Pia tusaidiewakulima hawa kupata soko kama wenzangu walivyosema,soko limekuwa ni tatizo, mwaka juzi mahindi yalikuwayanauzwa kwa Sh.20,000 kwa gunia leo yanauzwa kwa

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

Sh.80,000 kwa gunia, napongeza sana hali hiyo. Hii inatokanana masuala ya tabia nchi, kwamba mikoa mingi haikuwezakupata mavuno ya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana tuwekenguvu katika kujenga miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji,hatutaweza kukuza kilimo kwa kutegemea mvua na miakahii nimeona mvua inapungua mwaka hadi mwaka. Kwa hiyo,niombe Serikali katika Mpango huu tuweke fedha za kutoshakwenye kilimo cha umwagiliaji, tumekuwa tunaweka fedhalakini hazitoki, naomba awamu hii ya mwisho wa Mpangohuu zitoke fedha za kutosha, tuone utekelezaji wa kilimo chaumwagiliaji, naamini kabisa ndiyo mkombozi mkubwa wakutufikisha katika uchumi wa viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi hii.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa JustinMonko, tutamalizia na Mheshimiwa Augustino ManyandaMasele.

MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nami nafasi ya kuweza kuchangiakatika mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifawa mwaka wa 2020/2021. Awali ya yote nimpongeze sanaMheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango, Naibu Waziripamoja na timu yote na niipongeze Serikali kwa ujumla wakeikiongozwa na Mheshimiwa Rais wetu Dkt. John PombeJoseph Magufuli kwa namna ambavyo imekuwa ikitekelezaMpango wa Maendeleo katika bajeti iliyopitia na bajeti hiiambayo inaendelea sasa ya mwaka 2019/2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona yako mafanikiomengi katika miradi mingi ya kielelezo ukiwepo Mradi waumeme wa Stiegler’s Gorge au bwawa la Mwalimu Nyerere,tumeona kwenye standard gauge, ununuzi wa ndege,uboreshaji wa miundombinu, lakini zaidi sana katika sekta yaafya tumeona juhudi kubwa sana za ujenzi wa hospitali za

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

wilaya, lakini na vituo vingi vya afya ambavyo kwa kwelivitakwenda kuboresha maisha ya wananchi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa zaidi pia tumeonamchango wa Serikali hii katika ukusanyaji wa mapato yaSerikali ambayo yameongezeka kwa kiasi kikubwa nainatusaidia sana sisi katika kutekeleza mipango, ukizingatiakwamba mipango mingi sasa ya Serikali tunaipanga kwakutumia fedha zetu za ndani. Mfano, katika mapendekezohaya ambayo yapo, katika fedha za mpango wa maendeleozaidi ya bilioni 12.6 za bajeti ya maendeleo zaidi ya trilion10.1 zitakuwa sasa zinatokana na fedha zetu za ndani. Kwahiyo tunaipongeza sana Serikali kwa juhudi kubwa ambayoimefanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nichangie katika sektambalimbali katika kuboresha Mpango wetu wa Maendeleowa mwaka 2020/2021, nikianzia na sekta ya afya, kamanilivyosema juhudi kubwa imefanyika katika Serikali hii yaAwamu ya Tano, lakini niombe sana katika Mpango huu kazitulioifanya kwa mfano kwenye vituo vya afya, pamoja nawingi wa vituo vya afya tulivyofanya ukilinganisha na idadiya Watanzania zaidi ya milioni 55 waliopo sasa, juhudi kubwabado inatakiwa katika eneo hili. Pia tujue kwamba bila kuwana afya njema hata kazi zetu na mipango yetu ya maendeleohaiwezi kutufikisha vizuri. Kwa hiyo niiombe sana Serikali naMheshimiwa Waziri waangalie namna ambavyo wataongezavituo vya afya. Ushauri wangu katika hili ni kwanza kukamilishamaboma ambayo yamekwishaanzishwa na wananchiwenyewe. Awamu zilizopita ikiwemo Awamu ya Nne yaMheshimiwa Kikwete tulianza, wananchi wamejitolea sanakatika ujenzi wa maboma ya vituo vya afya na mabomamengine kwenye sekta ya elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sekta ya afya, kwamfano katika jimbo langu, yapo boma katika Kata yetu yaNgimu lakini nyingine Makuro ambayo yamekaa kwa mudaya miaka 10, wananchi hawa wametoa nguvu zao, lakinimpaka leo maboma hayo hayajaweza kukamilika na kwakweli wananchi wamekuwa wamezidiwa na ukamilishaji wa

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

maeneo hayo kutokana na mipango mingi ambayotunawapelekea, ukizingatia kwamba kwa kila fedha zaSerikali zinazokwenda asilimia 20 ya nguvu za wananchiinahitajika huko. Kwa hiyo niombe sana Serikali ifanyempango wa makusudi kama ilivyofanya kwenye sekta yaelimu tuweze kukamilisha maboma haya ambayo yapokatika nchi nzima na wananchi walishajitolea katikakuyajenga ili kusudi tuweze kuboresha huduma za . Tunahitajiafya bora na hasa tunahitaji kuzuia vifo vya wa kina mamana watoto wakati wa kujifungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye sekta ya maji;sekta hii ni muhimu sana, kwa kweli tunao uwezo wa kufanyakila kitu, lakini tunaweza tukashindwa kuishi bila maji.Tumewekeza sana katika maeneo mengi, tumewekeza vizurikatika miundombinu, sasa hivi tunaendelea kuwekeza katikamiundombinu ya umeme, tunaendelea kuwekeza katikamaeneo mengine, lakini maji ambalo ni hitaji la msingi lamaisha ya binadamu kwa kweli bado tumekuwa na nguvukidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiangalia katika bajeti yamaji, imekuwa ni kidogo sana na haina uwezo wa kututoahapa tulipo. Tunajua Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatakaangalau kwa upande wa vijijini tufikie asilimia 85 mpakakufikia mwaka unaokuja. Sasa hivi tunaongelea chini yaasilimia 65, utaona kazi hiyo ni ngumu, kazi hiyo ni kubwa,kwa hiyo niombe sana, zitafutwe fedha za maji. Mwaka janatulikuja na ombi hapa la kuongeza shilingi 50, lakini ombi hilohalikukubaliwa na sisi hatupingani na hilo, lakini madhalivinaweza vikapatikana vyanzo vingine, suala la maji ni lamuhimu sana wewe mwenyewe ni shahidi, Mheshimiwa Raisalipotembea kila mahali alipokwenda ni maji, maji, maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la maji linawagusasana akinamama ambao ndio wazalishaji wakubwa nawanatumia muda mwingi sana kwenye kutafuta maji natunaona kwamba takwimu tunazokuwa nazo zinaweza zisiweza kweli kwa sababu tunadhani kwamba kisima kimojakinakwenda pale kama kinasema kinahudumia wananchi

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

250 au wananchi 500 au 600, hizo ndizo takwimu tunazokuwanazo, lakini utakuta wengine wapo zaidi ya mita 400 ambayondiyo sera yetu au Awamu hii ilikuwa imejiwekea, kusogezahuduma karibu na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niiombe sana Serikali,ukienda katika miradi ya vieleleze Sekta ya Maji sio sekta yamuhimu, sio sekta ya kipaumbele. Sasa hili halitupi sisi nafasiya kuweza kutenga fedha nyingi kwenye kuboreshamiundombinu ya maji. Niombe Mheshimiwa Waziri tulipekipaumbele cha kwanza kabisa sasa hivi kwenye bajetiinayokuja hii ya mwaka 2020/2021 ili tuweze kuwatua akinamama ndoo kichwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata walioko mijini badohawajapata maji ya kutosha, bado kumekuwa na urasimumkubwa. Ukiangalia hata katika Mkoa wa Dar es Salaamshida ya maji bado ni kubwa, katika majiji yote shida ya majibado ni kubwa. Kwa hiyo niombe sana Wizara hii iangalie naniombe sana Sekta ya Maji iwe ni moja ya sekta zakipaumbele katika Taifa letu. Tunaweza hata tukapunguzakwenye maeneo mengine; tunaweza tukaishi bila lami,tunaweza tukaishi bila miundombinu bora huko lakini hatunauwezo wa kuishi bila maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine lipo katika kilimo;Sekta ya Kilimo inaajiri zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania,wengi wao – asilimia 90 – wanatoka vijijini ambako mimi nimwakilishi wao, lakini pia wako wakulima ambao wanaishimijini. Bado mpango wa Serikali haujatenga fedha za kutoshakatika kuboresha Sekta ya Kilimo, bado tunahitaji kuongezafedha, tunahitaji kuongeza uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia katika mpangoambao umewasilishwa sasa, fedha nyingi zinazotegemewani hizi za mpango wa kuendeleza Sekta ya Kilimo ya Awamuya Pili (ASDP II). Fedha hizi hazitoshi. Fedha hizi zina maeneomaalum, yako mazao mengine ambayo hayawi-coveredkabisa kwenye mpango huu. Mpango huu wa ASDP II

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

wenyewe umelenga zaidi kwenye mazao yale ya kimkakatiambayo utakuta ni korosho, pamba, kahawa, chai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa yapo mazao mengineambayo kwa kweli yanahitaji yapewe kipaumbele; tunamazao ya mafuta kama ufuta, alizeti mchikichi, karanga namaeneo mengine. Haya yanahitaji kupewa kipaumbele kwasababu tunajua kwamba nchi yetu inatumia fedha nyingi,zaidi ya bilioni 410 katika kuagiza mafuta ya kula kila mwaka.Fedha hizi ni nyingi sana, tusipowekeza katika kilimo hatuwezikuwasaidia wananchi wetu. Huku ndiko wananchi wetu waliowengi tunakotoka sisi wote waliko. Kwa hiyo, niombe sanaSekta ya Kilimo ipewe umuhimu na kipaumbele cha kwanzapia ili kuweza kuboresha maisha ya wananchi wetu kule vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tukumbuke kwambanchi yetu sasa tunakwenda na tunakwenda kwenye uchumiwa kati ambao utaongozwa na uchumi wa viwanda.Viwanda hivi vitahitaji malighafi za kutoka mashambani,viwanda hivi vitahitaji malighafi za mifugo, viwanda hivivinahitaji malighafi kutoka kwenye uvuvi. Sasa tusipowekezakatika maeneo haya tutajikuta kwamba hatuwezi kufikiamalengo yetu vizuri na ndoto ya Mheshimiwa Rais wetu yakutufikisha uchumi wa kati 2025 haitaweza kutimia kwasababu ya uwekezaji mdogo katika Sekta ya Kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapozungumzia Sekta yaKil imo ni pamoja na mifugo vilevile. Tumeona zipochangamoto nyingi, na niipongeze sana Wizara ya Mifugo,sasa hivi wamekuja na utaratibu wa uhimilishaji wa mifugoambao unawasaidia wafugaji wetu kuwa na mazao borazaidi.

Kwa hiyo, niombe sana uwekezaji uongezwe katikasekta hizi ikiwa ni pamoja na Sekta ya Uvuvi. (Makofi)

MWENYEKITI: Kengele ya pili imegonga Mheshimiwa.

MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana, naunga mkono hoja.

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

MWENYEKITI: Ahsante sana, tutamalizia naMheshimiwa Augustino Manyanda Masele.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nianze kwanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai,na pili nikushukuru wewe kwa kunipatia nafasi ili na miminiweze kushiriki katika kuchangia hotuba ya Waziri wetumpendwa, Waziri wa Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwanza kwa kusemanaunga mkono hoja asilimia 100 kwa 100, na nianze kwakumpongeza Mheshimiwa Rais pamoja na Serikali yake yotekwa ujumla kwa utendaji wake mzuri wa kazi. Pili, nimpongezeMheshimiwa Waziri Dkt. Mpango, Naibu Waziri wake,Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, Katibu Mkuu na wataalammbalimbali wa Wizara hii kwa umahiri wao wa utekelezajiwa mipango yote ambayo tumeanza nayo ya miaka mitano.Hongereni sana kwa consistency ambayo mmekuwa nayo.Tumeanza na mpango wa mwaka wa kwanza, wa pili, watatu, sasa wa nne; utekelezaji wa mipango ya maendeleokatika sekta mbalimbali za vipaumbele hauna mashakaunatekelezwa kwa kiwango ambacho kinaridhisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa reli ya kisasa ukovizuri, ujenzi wa Bwawa la Umeme la Stiegler’s Gorge auBwawa la Mwalimu Nyerere unakwenda vizuri; upanuzi wabandari zetu unakwenda vizuri, ujenzi wa meli katika maziwamakuu; Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa mamboyanakwenda vizuri; ujenzi wa Daraja refu kabisa ambalolitakuja kuwa la kihistoria la Kigongo – Busisi mpangounakwenda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ununuzi wa ndege za kisasaumeendelea kutekelezwa vizuri; yote haya yamo katikamipango yetu ambayo tumeanza nayo tangu uongozi waSerikali ya Awamu ya Tano ulipoingia madarakani. Miradimbalimbali inatekelezwa, mpango wa elimu bila malipokuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nneunatekelezwa bila wasiwasi na Watanzania wanafurahia;uboreshaji wa huduma za afya na wenyewe unatekelezwa

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

na tunashukuru na ninaipongeza Serikali sana kwa sababuWatanzania sasa afya zao zinaimarika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema manenohaya napenda sasa niendelee kuchangia katika baadhi yamaeneo. Eneo mojawapo ambalo ninapenda kuchangia nikuhusiana na suala zima la ujenzi wa wilaya hizi mpya namikoa mipya. Wilaya yangu ya Mbogwe ni miongoni mwawilaya mpya; niipongeze sana Serikali kwa sababuimeendelea kufanya kazi zake vizuri inatupatia pesatunajenga makao makuu ya wilaya kwa maana yahalmashauri na ofisi za mkuu wa wilaya na tumepewa piapesa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali, naomba tu Serikaliiendelee kutupatia pesa ili tuweze kukamilisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nipende tu kuchukua nafasihii kuipongeza Serikali kwa uamuzi wake wa uhakika kabisana wa thabiti wa kuhamishia Makao Makuu ya Serikali hapaDodoma na ninaamini kabisa kila mmoja ni shuhuda kwambaofisi mbalimbali za Wizara mbalimbali zimejengwa kupitiamipango hiihii ya Serikali ambayo tunaendelea kuitekeleza.Niombe Serikali iendelee na mkakati wake sasa wa kumaliziaujenzi wa Uwanja wa Msalato ili kwamba Makao Makuu yetuya nchi yaweze kufikika kwa kufikia hata ndege na usafiri wakimataifa kutoka mataifa mbalimbali ya nje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii piakuipongeza Serikali kwa uamuzi wake wa kuyapandishamapori ya akiba kuwa hifadhi za Taifa; Mapori ya Kigosi, MtoUgala, Selous, Ibanda, Burigi Chato, mapori haya yanahitajisasa uwekezaji mkubwa. Tuiombe Serikali itenge pesa kwaajili ya ujenzi wa miundombinu katika mapori haya ili sasahuduma za utalii ziweze kufanyika kwa wepesi zaidi nauchangiaji wa Pato la Taifa kupitia hii Sekta ya Utali iwezekuonekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kilimoninapenda kuishauri Serikali iendelee kuwekeza katikaviwanda vya utengenezaji wa mbolea kwa sababuWatanzania walio wengi wanashiriki katika shughuli za kilimo,

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

na kwa maana hiyo tuiombe Serikali iwekeze zaidi katikakuvutia wawekezaji wa viwanda vya mbolea ili uzalishaji wamazao ya chakula na biashara uweze kuimarika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi ikijitosheleza kwachakula ninaamini kabisa hata ukuaji wake wa uchumiutakuwa ni wa uhakika zaidi kwa sababu wazalishaji maliwenyewe watakuwa wana nguvu za kutosha na kwa hakikawataweza kufanya uzalishaji katika sehemu mbalimbali zaSerikali na hata katika viwanda na maeneo mbalimbali yauzalishaji mali watafanya kwa uhakika zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe tena kuishauriSerikali sasa kuwekeza zaidi katika eneo la upimaji wa ardhi.Nchi yetu ina tatizo kubwa la ujengaji holela katika miji yetu,niombe kabisa Serikali ilipe kipaumbele suala zima la upimajiwa ardhi katika maeneo mbalimbali ya miji inayochipukiana miji mikubwa ambayo tayari tunayo katika nchi yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumzia habari yamaendeleo hatuwezi kuzungumza maendeleo bila kutajasuala zima la mawasiliano kwa njia ya barabara. NiombeSerikali iendelee kutoa pesa katika wakala mbalimbaliikiwemo TANROADS na TARURA ili ujenzi wa barabara za lamikuunganisha maeneo mbalimbali kwa maana ya mikoa namakao makuu ya wilaya uendelee kwenda kwa kasiinayokubalika. Pia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini nawenyewe ujengewe uwezo, vitafutwe vyanzo mbalimbali vyamapato ili kuweza kuisaidia wakala hii ambayo ni changa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaamini kabisa kwambaREA inafanya vizuri kwa sababu imekuwa na chanzo chauhakika cha tozo ya mafuta. Tumejikuta kwamba sasa hikichanzo kinausaidia sana Wakala wa Umeme Vijijini kuwezakufanya mageuzi makubwa sana ya upatikanaji wa umemekatika vijiji vyetu na kwa maana hiyo ninaamini kabisakwamba hata TARURA ikiwezekana kitafutwe chanzo kingine

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

ambacho kitauwezesha kuwa na pesa za uhakika za kuwezakutekeleza miradi yake kwa uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakala mwingine ni Wakalawa RUWASA ambao na wenyewe ni Wakala wa Maji Mijinina Vijijini. Wakala huu na wenyewe ni wakala ambao ndiyoumeanza, niiombe Serikali na yenyewe iendelee kuujengeauwezo wakala huu ili uweze kusambaza maji kwa uhakikakwa Watanzania ili waweze kupata maji safi na salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaamini kabisa kwambawatu wakipata maji safi na salama afya zao zitaimarika namagonjwa mbalimbali ambayo yanatokana na majiyanaweza yakazuilika tunaweza tukajikuta hata bajeti yamatumizi ya afya inaweza ikashuka kwa sababu kamatusipokuwa na wagonjwa wengi maana yake sasa hatamahitaji ya madawa yatapungua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema manenohao napenda kushukuru, ahsante sana kwa kunipata nafasina Mungu awabariki.

MWENYEKITI: Bunge linarejea.

(Bunge lilirudia)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae.

Kuna mambo mawili; moja ni tangazo, lingine ni lakukumbushana. Nitaanza na tangazo linatoka Ofisi ya Katibuwa Bunge; Waheshimiwa Wabunge mnatangaziwa kwambaofisi imeshaanza kupokea maswali kupitia njia ya kielektroniki.(Makofi)

Sasa wako Waheshimiwa Wabunge ambaowalituma nadhani kwa majaribio, yaani wakitaka kujuayanafika au hayafiki kwa hiyo waliandika mambo ambayokidogo mengine hayajakamilika lakini wametuma kwa hiyoOfisi imeniletea hapa ili niwaambie Waheshimiwa Wabungemlichotuma kimefika.

Page 178: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

Sasa kwa sababu tulielekezwa yale maswali waohawawezi kuyafuta kwenye mtandao wako wewe, inabidiuingie ufute kwa sababu la sivyo wataweka sasa kwenyeorodha kana kwamba kile ulichokuwa umetuma ndiyo swalilenyewe. Kwa hiyo, mnaombwa muingie ile sehemu yamaswali mfute yale maswali mliyokuwa mmetuma kwamajaribio kwa sababu kuna wengine wameandika Kichinahapa, wengine wameandika kabisa tunajaribu namna yakuwasilisha maswali, kwa hiyo, inabidi sasa ukafute.

Uzuri kule imeandikwa kabisa na ni nani anayetumakwa hiyo waliotuma Kichinachina na wenyewe wako hapa,waliotuma maswali ambayo yamekamilika lakini pengineinabidi wayatazame sasa vizuri ili liwe ni swali kamili pia wapo,orodha iko hapa. Kwa hiyo, mnaambiwa Ofisi ya Bungeimeshaanza kupokea na imeshapokea hata wale mliokuwamnajaribu kwa hiyo, mnaombwa muende sasa ile sehemuya maswali myafute kwa kuonesha kwamba hamkuwammekusudia yawe maswali kamili.

Lingine Waheshimiwa Wabunge la kukumbushana nimatakwa ya Kanuni yetu na namna ambavyo tumeletewahaya mapendekezo ili na sisi tushiriki kutengeneza huumpango wa Serikali. Lakini michango mingi tunayoitoahaikidhi Kanuni yetu ya 94 inachotutegemea Bunge tufanyesasa ili kutoa fursa kwa Serikali kwenda kutayarisha mpangoambao ndiyo utatoa mwongozo wa bajeti.

Tusipofanya hivyo mambo yale tunayotakiwakuzungumza sasa tutaanza kuzungumza wakati wa kujadilibajeti na mpango wa wakati huo, na wakati huo ndiyotunaanza kuona kama macho yamefunguka sana hivitunaona na vyanzo vingine vya mapato. Wakati wa kusemahayo kwa mujibu wa Kanuni yetu ya 94 ni sasa, ndichotunachotarajiwa kufanya.

Ukiisoma, uzuri sasa hivi huna haja ya kubeba kwahiyo iko humu; Kanuni ya 94 imesema kabisa mjadala wetuunatakiwa kujikita kwenye nini, na ukisoma 94(6) imeelezakabisa mjadala unatakiwa kuwa kwenye mambo ya jumla

Page 179: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

yanayohusu sera za kiuchumi na mambo kama hayo. Sisiwakati huu tunatakiwa kupendekeza vyanzo vya mapato;tunatakiwa kupendekeza vipaumbele. Serikali imeeleza yakwake na vipaumbele vyake, sisi tunasema nini? Na je, sisitunavyo vipaumbele tofauti? Na kama tunavyo sasa ndiyowakati wa kusema, na kama tunavyo vyanzo vya mapatovitakavyoisaidia Serikali kutimiza malengo yake ambayondiyo wameleta sasa mapendekezo tunatakiwa kusemasasa.

Kuja kusema baadaye ndiyo maana tunaanzakusema Serikali imegoma kutoa hata nukta, ni kwa sababutunasema wakati ambao sio. Serikali itaondoka hapa – hayayote tunayoongea ni kweli, kijiji chako hakina umeme ni sawa,Waziri wa Nishati atasikia, lakini Mheshimiwa Dkt. Mpangohicho anaandika pale lakini wala hatakitolea majibu hapakwa sababu sicho ambacho Kanuni zetu zinamtaka afanyekipindi hiki cha Bunge la mwezi wa kumi na wa kumi na moja.(Makofi)

Kwa hiyo, kanuni tunazo, wakati unaitwa jinakuchangia wewe pitia Kanuni yako ili ujipange unatakakuchangia kwenye hoja ipi kwa mujibu wa Kanuni zetu.Tukieleza kila mtu kwenye eneo lake, kila mtu sehemu yakeKanuni ya 94 haisemi, hayo tutakuja kuangalia MheshimiwaDkt. Mpango wakati huo yale tuliyomshauri sasawameyazingatia, wameyatazama?

Tusipowashauri yale aliyoyaleta yatakuja haya hayamwakani na wakati huo ndiyo tutaanza sasa ongeza 20 paleongeza 50 pale, ongeza sijui 100 pale, inakuwa wakati wetuwa kushauri kwenye hilo umepita na hauwezi kuilaumu Serikalikwamba sasa mbona haisikilizi kwa sababu wakati wetu wakushauri kuhusu mpango ni sasa kwa sababu Serikali imeletamapendekezo haina mpango bado, imeleta mapendekezo.

Tusome Kanuni yetu Waheshimiwa Wabunge, hilolilikuwa ni la kukumbushana kwa sababu siku tano zinakwishapunde na Mheshimiwa Dkt. Mpango atarudi nayo yale

Page 180: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE Kikao cha Pili – … 6 2019.pdf · ya kufundishia na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia Lugha ya Alama ya Tanzania kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

aliyotuletea na sisi tunatarajiwa kuyaboresha na kuangaliamambo mengine ambayo yeye pengine hajayagusa.

Baada ya kusema hayo Waheshimiwa Wabunge,naahirisha shughuli za Bunge mpaka kesho, tarehe 07Novemba, 2019, saa tatu asubuhi.

(Saa 1.22 Jioni Bunge liliahirishwa hadi Siku ya Alhamisi,Tarehe 7 Novemba, 2019 Saa Tatu Asubuhi)