177
1 19 JUNI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Hamsini na Mbili – Tarehe 19 Juni, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Ifuatayo Iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za Chuo Kikuu cha Ardhi kwa Mwaka 2011/2012 (Ardhi University Annual Report and Audited Financial Statements for the Financial Year 2011/2012). MASWALI NA MAJIBU Na. 421 Haki ya Kupiga Kura MHE. YUSUF HAJI KHAMIS aliuliza:- Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa haki mwananchi kuchagua au kutochaguliwa katika madaraka ya Ubunge au Urais:- Je, ni Sheria ipi inawanyima haki wananchi wa

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

  • Upload
    others

  • View
    0

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

1

19 JUNI, 2013

BUNGE LA TANZANIA________________

MAJADILIANO YA BUNGE___________________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Hamsini na Mbili – Tarehe 19 Juni, 2013

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati Ifuatayo Iliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:

Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za ChuoKikuu cha Ardhi kwa Mwaka 2011/2012 (Ardhi UniversityAnnual Report and Audited Financial Statements for theFinancial Year 2011/2012).

MASWALI NA MAJIBU

Na. 421

Haki ya Kupiga Kura

MHE. YUSUF HAJI KHAMIS aliuliza:-

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampahaki mwananchi kuchagua au kutochaguliwa katikamadaraka ya Ubunge au Urais:-

Je, ni Sheria ipi inawanyima haki wananchi wa

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

2

19 JUNI, 2013

Tanzania Visiwani kwenye Majimbo yao kupewa haki ya kuramoja tu ya kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania na kumnyima haki ya kumchagua Mbunge kwakura za Muungano?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBUNA BUNGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa WaziriMkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yusuf Haji Khamis,Mbunge wa Nungwi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nakubaliana na MheshimiwaMbunge kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 21 ya Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kila Raiaanayo haki ya kuchagua ama kuchaguliwa katika madarakaya Ubunge au Urais.

Mheshimiwa Spika, aidha, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,Sura ya 343 (12) (a), inaainisha utaratibu wa uandikishaji wawapiga kura Tanzania Zanzibar. Kifungu hiki kinafafanua wazikuhusu wanaostahili kuandikishwa na kushiriki katika kupigakura za kumchagua Rais au Wabunge kwa Tanzania Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Taifa yaUchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzihuwaandikisha wale tu ambao hawakuandikishwa kwenyeDaftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Taifa yaUchaguzi ya Zanzibar, hivyo kuwa na haki ya kumpigia kuraRais wa Jamhuri ya Muungano na sio kwa Wawakilishi katikaBunge la Muungano.

Mheshimiwa Spika, katika mazingira hayo, Kisheria niwazi kwamba, kuna baadhi ya Watanzania waishio Zanzibarwanapoteza haki ya msingi ya kuwachagua Wabunge waJamhuri ya Muungano.

Mheshimiwa Spika, ni matarajio ya Serikali kwamba,kasoro hii ya Kisheria pamoja na nyinginezo zitarekebishwakatika mchakato unaoendelea wa kuandika Katiba Mpya

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

3

19 JUNI, 2013

ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo basi,namwomba Mheshimiwa Mbunge na wengineo wavutesubira hadi zoezi hil i muhimu kwenu, l itakapokuwalimekamilika.

MHE. YUSUF HAJI KHAMIS: Mheshimiwa Spika, ahsante.Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, lakini ninaswali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Sheria hii ipo kwaTanzania nzima, lakini ilionesha kuwabagua watu waliopoUnguja, Pemba wamechagua Mbunge na Rais wa Jamhuriya Muungano, kwa sababu zipi za msingi, nataka kujua?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBUNA BUNGE): Mheshimiwa Spika, swali hili nimeshawahi kulijibuhapa. Tatizo ni Sheria ya Zanzibar na sifa za Mpiga Kura waZanzibar ndizo zinazotatiza kwa sababu, mtuanayeandikishwa kule lazima awe ameshaishi kwa kipindifulani. Pia sifa za mtu anayestahili kupiga kura kwa Zanzibaryenyewe zilizoainishwa na Sheria ya Zanzibar, zimetajwa naTume ya Uchaguzi ya Zanzibar, inasimamia jambo hilo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kutokana namkanganyiko huo ndio nilisema na nasema tena kwamba,inakuwa vigumu sana kwa Tume ya Uchaguzi ya Barakusimamia jambo hili kwa sababu, yule Mzanzibari anayeishiZanzibar, anaishi kwa Sheria ya Zanzibar, ndio maana hilijambo limetokea, lakini na sisi tumeliona.

Mheshimiwa Spika, ni gumu kulifanya, kwa sababuyako mengi ya namna hii ambayo tunafikiri utaratibu huuwa Katiba mpya unaweza ukarekebisha, ili angalau tuwetuna uelewa mmoja na utaratibu mmoja ambao tunawezakuutumia.

SPIKA: Naomba tuendelee na swali linalofuata kwasababu sikumwona mtu mwingine. Mheshimiwa Dkt. AntonyMbassa, kwa niaba yake Mheshimiwa Rajab MbaroukMohammed!

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

4

19 JUNI, 2013

Na. 422

Biharamulo Kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED (K.n.y. DKT.ANTONY G. MBASSA) aliuliza:-

Je, ni lini mchakato wa kutangaza Mamlaka ya MjiMdogo wa Biharamulo utakamilika?

NAIBU WAZIRI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZAMITAA (TAMISEMI) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa WaziriMkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. AnthonyGervas Mbassa, Mbunge wa Biharamulo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Tangazo lakeNamba 355 la tarehe 17 Septemba, 2004, chini ya Sheria zaSerikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya mwaka 1982,ilitangaza nia ya kuanzisha Mamlaka ya Mji Mdogo waBiharamulo. Aidha, katika kipindi hicho hicho Serikali,ilitangaza kuigawa Wilaya ya Biharamulo ili kuanzisha Wilayaya Chato, ambapo mwaka 2005 mchakato wa kuigawaWilaya hiyo ulikamilika.

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa 2007, Halmashauriya Wilaya ya Biharamulo ilianza kutekeleza azma ya kuundaMamlaka ya Mji Mdogo wa Biharamulo, kwa kuanza kupimaeneo la kiutawala la Mamlaka hiyo. Mchakato huo ulihusishaupanuzi wa eneo la kiutawala kwa kuanzisha Kata mpyambili, ili kuafanya idadi ya Kata kuwa tano. Mchakato huuwa kuanzisha Kata ulikamilika mwaka 2010.

Mheshimiwa Spika, Vikao vya kujadili uanzishwaji waMamlaka ya Mji Mdogo wa Biharamulo, vilianza mwaka 2010na tayari agenda hiyo imejadiliwa na kuridhiwa na Vikaovyote vya Kisheria vya Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo.Aidha, Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC),ambacho kimepangwa kukutana mwezi Novemba, 2013,

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

5

19 JUNI, 2013

kitajadili agenda hiyo na mapendekezo ya Kikao hichoyatawasilishwa kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali zaMitaa kwa hatua zaidi.

Mheshimiwa Spika, nawaomba WaheshimiwaWabunge, washirikiane na uongozi wa Mkoa wa Kagera ilikuharakisha mchakato wa uanzishaji wa Mamlaka ya MjiMdogo wa Biharamulo.

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED: MheshimiwaSpika, kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, nchi yetuimeongezeka katika maeneo makubwa ya kiutawala namgawo wa Kata na Halmashauri umeongezeka. Kwa hiyo,moja kwa moja ni kwamba, hata mgawanyo wa rasilimalifedha ambazo zinapelekwa katika Halmashauri zetu, sasainabidi uangaliwe upya.

Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali, kupitia Wizarahusika, itatoa mwongozo maalum wa Idadi za Kata katikakila Halmashauri ili hizi Halmashauri ziwe na uwiano katikaidadi hizi za Kata na ziweze kupata mgawo wakekisawasawa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, mchakato wa kupataKata au Halmashauri unakuwa ni mrefu sana kupitia Serikalini.Je, Serikali, haioni kwamba, sasa iko haja ya kuanzishamchakato mwingine mpya ambao utarahisisha maombiyanayotoka katika Halmashauri yakafanyiwa kazi haraka?

NAIBU WAZIRI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZAMITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, kwa niaba yaMheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la nyongezala Mheshimiwa Rajab Mbarouk Mohammed, Mwenyekiti waKamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, yako mambo mawili ameyasemahapa, kama nitakuwa nimejichanganya, basi nitaelimishwa.La kwanza, hil i la rasil imali kwa maana ya fedhazinazokwenda na vigezo vinavyotumika. Hata ukichukua uleMfuko unaoitwa Constituency Development Catalyst Fund

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

6

19 JUNI, 2013

umesema kwamba, cha kwanza, unaangalia idadi ya watu,25% inakwenda kule, unasema wote tunapigwa flat, aliyetokaUrambo, aliyetoka Siha, aliyetoka wapi, popote ulipotokaatakupiga hiyo 25%.

Pili, atakwenda ataangalia kiwango cha umaskini natatu kuna mambo mengi ambayo anayaangalia kule,miundombinu na vitu vingine vya namna hiyo. Hiyo ninahakika na yeye mwenyewe ndio maana nimemtaja kwanafasi yake kama Mwenyekiti wa Local Authorities AccountsCommittee.

Mheshimiwa Spika, formula hii na wenyewe watu wafedha wako hapa wanafahamu, ni formula ambayo ina-apply kote mpaka kule kwako Njombe, ndio hiyo hiyotunayoitumia.

Mheshimiwa Spika, sasa la pili anakwenda kwenyesuala la Kata kwamba, zinakuwa ngapi na vitu vingine vyanamna hiyo. Hizi Kata tunazozizungumza hapa, ukiangaliatunakozungumzia, kule Chato, wakati walipogawana pale,wale waliobaki kule Biharamulo, walipotaka kuundaMamlaka ya Mji Mdogo pale walihitaji uwe na Kata tano.Nina hakika hata akisimama Moses Machali, atauliza hilo swalihapa kwamba, ni kwa nini sasa ile Mamlaka yake haijafikiahatua hiyo?

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwa kifupi kwamba,hawa jamaa wanaozungumzwa hapa, wanaoelezwa hapawa Mamlaka hii ya Mji Mdogo wa Biharamulo, wamefika lakimoja na moja. Wao wanatakiwa wawe na watu 10,000 tu,yaani hawa wameshavuka kile kwango.

Mheshimiwa Spika, ndio maana nimemwambia hivi,kilichobakia hapa, ingekuwa kama Regional ConsultativeCommittee, ingekuwa haijakaa kwa sababu, zinakaa marambili tu kwa mwaka na watakaa tena mwezi Novemba. Hilijambo analozungumza Mheshimiwa Rajab, litakuwa taken

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

7

19 JUNI, 2013

into account na namwomba radhi kama kuna mahaliambapo nimejichanganya, basi tunaweza kukutana tukakaavizuri, ili tuweze kuzungumzia hilo.

Mheshimiwa Spika, hili analozungumza la pili lakwamba, huu mlolongo ni mrefu; huwezi ukaenda Kasulu paleau ukaenda Siha, ukagawanya eneo la watu bilakuwahusisha wenyewe wanaohusika. Kwa dhana ya D by Dhuwezi, huwezi kuvunja Kijiji hapa mpaka Mkutano Mkuu waKijiji ukutane, useme tuko tayari kuvunja Kijiji hiki kiwe Vijiji viwili.Nenda kasome Ibara ya 145 ya Katiba ya Nchi, nendakasome na Ibara ya 146 ya Katiba ya Nchi, inatambuaMamlaka hizi ninazozisema hapa. Nenda kasome SheriaNamba Saba na Sheria Namba Nane, Cap 207 na 208ambazo zinatambua kuwepo kwa Mamlaka za Serikali zaMitaa kwa maana ya D by D.

Mheshimiwa Spika, huwezi ukauacha utaratibu huuukagawa nchi hapa baada ya hapo, kama ni Wilayautakwenda kwa Rais wa Nchi, kama ni Kata utakwenda kwaWaziri Mkuu; hizi nyingine huku chini zote zinapitia hapa,zinaishia hapo, ndio utaratibu uliopo.

Mheshimiwa Spika, lakini kama Mheshimiwa Rajabuanafikiri kwamba, kuna namna nyingine nzuri ya kuondoahuu urasimu nilioueleza hapa, basi, tunaweza tukakaatukajadili, tutamshauri Mheshimiwa Waziri Mkuu, ambayendiye mwenye dhamana ya kugawa na Mheshimiwa Rais,anayegawa Tarafa, Wilaya pamoja na Mikoa katika nchi kwaujumla.

SPIKA: Mheshimiwa Machali hebu uliza swali tukusikie.(Kicheko)

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa fursa nimuulize swali moja dogo.Eneo linaloitwa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, halitakiwikumegwa lipelekwe eneo lingine kimipaka, ni hilo ambalolinaunda Jimbo la Kasulu Mjini, ambalo lina Kata zipatazonane.

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

8

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, lakini kwa mujibu wa taarifa yaSerikali, imeonesha kwamba, Halmashauri ya Mji wa Kasulu,haiwezi ikaanza sasa mpaka baada ya uchaguzi wa mwaka2015, lakini ukienda, Ilemela imeanza ina Kata tisa. Sihaanakotoka Mheshimiwa Waziri Halmashauri ile ilianza ikiwana Kata tano.

Mheshimiwa Spika, ningependa kupata sababu zaSerikali, ambazo zimesababisha kwamba, sasa Halmashauriya Mji wa Kasulu, isianze? Kwa sababu, kama maeneomengine yameanza yakiwa na Kata chache na hiiHalmashauri ya Mji wa Kasulu, nayo ina Kata ambazozinafanana na nyingine kuzidi hata baadhi ya ambazozilianza.

Mheshimiwa Spika, ni nini Kauli ya Serikali? Kwa niniisifikirie upya uamuzi wake, Halmashauri hii ya Mji wa Kasuluikaanza sasa?

SPIKA: Haya, ndio hilo swali ulikuwa unalijua? Naombasasa ujibu. (Kicheko)

NAIBU WAZIRI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZAMITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, kila mtu anafahamukabisa kwamba, tulijua hizi Mamlaka zote zingekuwaMamlaka za Miji, ikiwemo Mamlaka ya Mji wa Kasulu. Ndivyotulivyoelewa kwa Nzega, ndivyo tulivyoelewa kwa Masasi nakwa maeneo mengine.

Mheshimiwa Spika, zile Kata za kwake ambazozinatamkwa kule wakati zinatamkwa hizo Kata, zilikuwahazijaingizwa sasa katika hiyo Mamlaka Mpya ambayotunaizungumzia. Ziko pale na anafahamu kwamba, ziko palezinatamkwa, lakini zilikuwa hazijaingia; kuingiza Kata mlendani maana yake ni kwamba, una Kata, una Diwani wake,una Ward Development Committee na kila kitu.

Mheshimiwa Spika, tumezungumza na MheshimiwaMachali sana, hivi anavyozungumza hapa ni kwamba,anataka na wananchi wa kwake kule Kasulu wajue kwamba,

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

9

19 JUNI, 2013

Mbunge anafuatilia jambo hili. Nampongeza sana kwajambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Katapale, tuziondoe, ujue implications zake ni kwenda kuundatena hii Mamlaka na kwenda kuitisha Uchaguzi mwinginempya ambao utaku-affect hata wewe mwenyewe, kamauko tayari. Lakini nasema hivi wame-qualify na kila kitukimemalizika, wala hakuna tatizo lolote. Nataka niseme tu nisuala la kuvuta subira.

Mheshimiwa Spika, sasa kuna kitu amekisema hapana Mheshimiwa Spika wa zamani anafahamu jambo hili,Mheshimiwa Sitta. Anasema unajua bwana hata Sihailipoanza pale, kwanza nataka nisahihishe hapo, Kata zilizokopale sio nne, ni Kata 12 zilizoko pale na Madiwani waliokopale ni 17. Najua humu ndani akifanya hizo hesabu atazionapale, lakini yale yote yalikuwa determined kabla ya kuanzishahizo Mamlaka, ambacho ndicho kina-miss katika Mamlakaile anayoizungumzia ya Kasulu.

SPIKA: Jamani mmeshapata lecture ya Kata, sasatwende Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, MheshimiwaDavid Silinde atauliza hilo swali, kwa niaba yake MheshimiwaFelix Mkosamali Agent. (Kicheko)

Na. 423

Viwango vya Michango ya Hiari

MHE. FELIX F. MKOSAMALI (K.n.y. MHE. DAVID E.SILINDE) aliuliza:-

Michango ya Sekondari Majimboni ni hiari kwawananchi kuchangia ili kuendeleza elimu katika maeneoyao:-

(a) Je, ni nani mwenye jukumu la kupangakiwango cha michango hiyo?

(b) Je, ni hatua zipi atachukuliwa mwananchiendapo atashindwa?

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

10

19 JUNI, 2013

(c) Je, viwango vya michango ya hiarivinafanana kwa nchi nzima?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDIalijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa MboziMagharibi, lenye sehemu (a), (b) na (c), kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Waraka waElimu, Namba Nane (8) wa Mwaka 2011, Serikali inaelekezajukumu la kuchangia maendeleo ya elimu kwa wanajamiiwote, chini ya utaratibu au uratibu na udhibiti wa Kamati yaShule kwa Shule za Msingi na Bodi za Shule kwa Shule zaSekondari na pia Bodi za Vyuo kwa Vyuo vya Ualimu, baadaya kupata kipata Kibali cha Kuchangisha Michango hiyokutoka katika Halmashauri husika.

(b) Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Uongozi waShule, Bodi ya Shule ya Sekondari na Wanajamii ndiowanaohusika kupanga viwango vya michango na kuombaKibali cha Kuchangisha kutoka katika Halmashauri zao, haohao ndio wanaoweza kuamua kwa pamoja hatua zakuchukua dhidi ya wananchi wanaoshindwa kuchangiamichango hiyo.

(c) Mheshimiwa Spika, michango ya hiyari yakuendeleza elimu katika shule inategemea mahitaji ya shule,kibali cha kuchangisha na uwezo wa wachangiaji katikaHalmashauri husika, hivyo viwango vya michango havifananikati ya shule moja na nyingine. Kwa mantiki hii, viwango vyamichango ya hiyari kwa wananchi kuchangia ili kuendelezaelimu katika maeneo yao, havifanani kwa nchi nzima.

MHE. FELIX F. MKOSAMALI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa, Wizarandio iliyotoa Mwongozo wa uchangishaji na sasa hivi kuna

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

11

19 JUNI, 2013

watu wanaweka michango kiholela, ovyo ovyo, kwa niniWizara isiingilie kati ikaweka vigezo vya kuanzisha hiimichango? Kwa sababu, kuna watu wanaanzisha Bodi,zinakaa miaka 20 mpaka 30, hazibadilishwi kwa sababu yamaslahi ya hawa Wakuu wa Shule, kwa nini Serikali, isiingiliekati suala hili?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, elimu ni moja ya vigezovya haki za binadamu. Sasa watoto wanaposhindwa kulipaada, wamekuwa wanafukuzwa shuleni muda wa masomo.Serikali, inasemaje kuhusu kuwafukuza watoto muda wa shulewakati wao hawana uwezo wa kutafuta ada hizo?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, anachosema Mheshimiwa Mkosamalihapa siyo kweli, Serikali tayari ina Waraka. Kama nilivyosemakwenye jibu langu la msingi, upo Waraka wa Elimu namba(8) wa mwaka 2011 wa kukithiri kwa michango mashuleni nahuo Waraka ni huu hapa, kama Mheshimiwa Mkosamali hananingeomba nimtolee photocopy nimpe.

Mheshimiwa Spika, lakini hayo mambo mengineyanayofanyika mashuleni, ni namna tu ya Wakuu wa Shulewanavyotelekeza Waraka huu na Waheshimiwa Wabungemnapofanya ziara kwenye shule mnaweza mkathibisha hayo.Lakini sisi kama Mawaziri au watu wa Wizara ya Elimu tunapitakwenye mashule tunaendelea kuwaambia wananchi nakuwaelimisha juu ya michango mashuleni.

Mheshimiwa Spika, lakini ipo vile vile michangoambayo ilikatazwa na hapa lazima niiseme; michango yakuandikisha wanafunzi darasa la kwanza ama kidato chakwanza haipo, barua za utambulisho wa wanafunziwanaofaulu darasa la saba kwenda Sekondari, barua zoteza wanafunzi kuitwa kujiunga na shule za Sekondari au Vyuona fomu za kujiunga na kidato cha kwanza katika shule zisizoza Serikali.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nawaombaWaheshimiwa Wabunge tushirikiane kwa pamoja, kwa

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

12

19 JUNI, 2013

sababu hili suala ni kubwa na Waheshimiwa Wabunge wotemtakapokuwa mnakwenda huko, tupeane tu taarifa,ukinipigia simu hata mimi kwa shule husika, huwa nakuja maramoja na naweza kuchukua hatua zinazostahili.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kuhusu Bodi za Shulekwamba, labda zinakaa muda mrefu, upo utaratibu naWaraka kwamba, miaka mitatu mitatu Bodi ile ina-expireinachaguliwa Bodi nyingine. Sasa baadhi ya wajumbewanakuwa ni wajumbe ambao kidogo wanawezawakaisaidia shule, kwa hiyo unakuta Mwalimu Mkuu au jamiiinamrudisha mtu kwa wakati mwingine au mara tatu, lakinikikomo angalau ni mara tatu, lakini mara ya pili anaruhusiwakuwa mjumbe wa Bodi tena.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, kuna lile swali mojalile la watoto wanaofukuzwa shule.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, watoto wanaofukuzwa kwa sababu yamichango, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingikwamba, Halmashauri husika katika Wilaya husika yenyeweama Kata ama shule na jamii kwa ujumla, ndiyo wanaojuapale kwamba huyu mtoto anayefukuzwa hana michangokabisa aidha, ni yatima au ana uwezo, lakini tulishapigamarufuku kwamba, watoto wasifukuzwe shule kwa sababuya michango, kwa sababu michango inabidi Kamati yaWazazi ikae ili Mwenyekiti wa Shule au Mwenyekiti wa Bodiawatangazie wazazi michango hii na jinsi inavyowezakutolewa utaratibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (SERA,URATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa Spika, naomba kutoanyongeza ya majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri ambayeameelezea michango inayohusiana na kibali kinachotolewana Wizara ya Elimu. Lakini katika maeneo yetu kunamichango ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ambayo huwainapitishwa na vikao mbalimbali vya Serikali za Vijiji au WardC; michango ile ikishapitishwa na Ward C inakuwa ni jukumula wazazi kuchangia kwa mujibu wa makubaliano.

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

13

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, michango hiianayozungumzia Mheshimiwa Naibu Waziri ni michango ileambayo inahusisha vitendea kazi katika shule, lakinimichango ya maendeleo kwa ajili ya miundombinu ya elimu,inapopitishwa na vikao halali inakuwa ni lazima kilamwananchi mwenye uwezo wa kuchangia achangie kwamujibu wa Sheria.

Mheshimiwa Spika, vile vile Halmashauri fulani fulanihuwa zinatunga bylaws zao (Sheria ndogo) kwa ajili yamichango. Sasa zikiwa na by laws hizo ni lazima kuchangia.Nilitaka niweke sawa haya mambo mawili yaeleweke iliisionekane kwamba kuna michango haramu na michangoisiyo halali. Michango hii mingine ya maendeleo ambayoimepitia utaratibu wa vikao hivi, ni halali.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Spika, imebainikakwamba, kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa wakiwemoWabunge mfano, Mbunge wa Singida Mashariki,amehamasisha wananchi wake wakatae kuchangiamichango yote ya maendeleo katika Jimbo lake. Kuliachiajambo hili kuendelea ni kuwashawishi na Majimbo menginewaige mfano huo mbaya. Je, Serikali inatoa kauli ganikukemea vitendo kama hivi ambavyo vinadumazamaendeleo ya nchi yetu? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, anachosema Mheshimiwa haji hapa nikweli kabisa, kuna baadhi ya Waheshimiwa Wabunge hataMheshimiwa David Silinde na yeye huko Mbozi, hataangekuwepo hapa ningemwambia hilo na yeye alishawahikupiga marufuku wananchi wake wa Tunduma pale wakawahawakuchangia michango.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alipofanya ziaramwaka juzi ilileta matatizo kidogo hata kwenye mkutano wahadhara. Lakini tulikwenda tukafanya ziara pale,tukawaelimisha wananchi wa Tunduma na wakachangia.Sasa hivi angalau wamejenga hata madarasa sita kwaSekondari na wototo wao wamekuwa enrolled pale.

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

14

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, hili la Mheshimiwa Mbunge waSingida na Wabunge wengine ambao kwa kweliwanahamasisha wananchi wasitoe michango, Serikaliinalilaani kabisa, kama alivyosema Mheshimiwa Waziri waNchi, Mheshimiwa Lukuvi ipo michango ambayo ni halalikabisa RCC ama Ward C ama DCC, wanakaa kwenye vikaovyao halali, wanapitisha kwamba michango hii itakuwa nihalali.

Mheshimiwa Spika, michango hiyo ni kama ulinzi washule kwa mfano, kujenga uzio au vyoo, ziara za kimasomo,chakula cha mchana cha wanafunzi, kulipia ankara za majiau umeme na mitihani ya masomo kama mock na kadhalikakwa form two na form four na miundombinu kama alivyosemaMheshimiwa Lukuvi, ni michango halali, vikao vinakuwavimekaa vya kisheria ngazi ya Kata, ngazi za Wilaya hatangazi ya Mkoa wanapitisha.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Waheshimiwa Wabungemnaokataza wananchi michango, suala hili kwa kweli kamaSerikali hatuwezi kulinyamazia, lazima tuhamasishane naWaheshimiwa Wabunge wote mnanisikia humu kwamba,tuendelee kuwaelimisha wananchi juu ya michango hii.(Makofi)

SPIKA: Ahsanteni. Naomba tuendelee limekuwa namchango mkubwa hili swali, sasa twende Wizara ya UjenziMheshimiwa Freeman Aikael Mbowe kwa niaba yakeMheshimiwa Mwenyekiti mwingine wa Chama cha NCCRMageuzi, Engineer Mbatia.

Na. 424

Barabara za Lami Wilayani Hai

MHE. JAMES F. MBATIA (K.n.y. MHE. FREEMAN A.MBOWE) aliuliza:-

Mbali na barabara kuu itokayo Dar es Salaam

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

15

19 JUNI, 2013

kwenda Nairobi kupitia Moshi na Arusha ambayo hukatizaJimboni Hai:-

(a) Je, ni barabara ngapi za urefu ganizimejengwa kwa kiwango cha lami katika Jimbo la Hai kwakipindi cha miaka 30 iliyopita?

(b) Je, ni vigezo gani vya kiuchumi, kitaalam,kimazingira na kisiasa hutumika kuchagua Wilayazinazojengewa barabara kwa kiwango cha lami?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziriwa Ujenzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa FreemanAikael Mbowe, Mbunge wa Hai, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inasimamia kilomita35,000 ambazo ni barabara kuu na za Mikoa na madaraja4,880 katika nchi nzima. Kwa mantiki hiyo, Wizara yanguhaihusiki na barabara za Majimbo au barabara za Wilaya(District Roads). Aidha, ukiacha barabara kuu itokayo Dar esSalaam kwenda Nairobi, Jimbo la Hai lina barabara za Mkoazenye jumla ya kilomita 40, zinazohudumiwa na Wakala waBarabara (TANROADS) ambazo ni Kwasadala – Kware –Lemira, kilomita 15; Kilimanjaro Machine Tools – Machame,kilomita 15; Bomang’ombe – Sanya Juu, kilomita 10.

Mheshimiwa Spika, kati ya ya hizo barabara zenyeurefu wa kilomita 25 ni za lamo ambazo ni KilimanjaroMachine Tools – Machame na Bomang’ombe kwenda SanyaJuu. Aidha, barabara ya Wilaya ya Kwasadala – Masamakilomita 12.5, inaendelea kujengwa kwa kiwango cha lamiikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Mheshimiwa Dkt. JakayaMrisho Kikwete. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaaliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010. Hadisasa jumla ya kilomita saba zimekamilika kujengwa kwakiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, vigezo zinavyotumika katika

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

16

19 JUNI, 2013

kuchagua barabara za kujengwa kwa kiwango cha lami nipamoja na uwepo wa fedha, idadi ya magari yanayotumiabarabara kwa siku, uwepo wa huduma za jamii kama vilehospitali kubwa, umuhimu katika kuunganisha eneo husikana maeneo mengine na idadi ya watu pamoja na shughulina fursa za uzalishaji zilizopo pamoja na Sheria Na. 13 yamwaka 2007. Aidha, lengo ni kuendeleza barabara kuu naza Mikoa yote, hatua kwa hatua jinsi uwezo unavyoruhusu.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Spika, nashukurusana. Kwa kuwa barabara alizouliza Mheshimiwa Mboweinayotoka Moshi Mjini kwenda Arusha ijulikanayo kama TheGreat North Road toka Cairo, Misri mpaka Cape Town Afrikaya Kusini ni barabara ya tangu wakati wa Mkoloni nabarabara ya Kilimanjaro Machine Tools – Machame Kilomita15 imejengwa mwaka 1952. Je, Serikali imewekeza kwa kiasigani kwa kuwa barabara hizi nyingine ziko mlimani,kuhakikisha mifereji ya kuondoa maji barabarani na kufanyaroutine maintenance kwenye barabara hizi za kihistoria katikanchi yetu? Hilo ni swali la kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa barabarahizi zinatumika na magari makubwa ambayo axle load yakeinaharibu barabara na kupitisha mizigo mikubwa. Je, Serikaliimejipanga namna gani kuwekeza zaidi kwenye reli yakwenda Kaskazini, reli ya kati ili mizigo mikubwa ipitishwekwenye njia ya reli badala ya kuzunguka kwenye barabarahizi ambazo zinagharimu Taifa hili fedha nyingi?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kwanzakabisa nikupongeze Mbatia kwa swali zuri na kuwakumbushaWatanzania kwamba, mipango ambayo tunayo sasa hivitumeweka Mfuko wa Barabara, kazi yake kubwa ni kufanyamatengenezo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hiyo routinemaintenance anayozungumzia Mheshimiwa Mbatia ndiyokazi ya ile fedha, kwa hiyo fedha za Mfuko wa Barabara

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

17

19 JUNI, 2013

zitahakikisha barabara hizi ambazo tumezitengeneza kwakiwango cha lami zinaendelea kuwa katika hali nzuri, kwahiyo, tutazitengeneza mara kwa mara.

Mheshimiwa Spika, suala la axle load, kwa maanaya standard ya barabara ili ziweze kudumu kwa muda mrefu,ushauri wake kwamba, tuwekeze zaidi kwenye reli ni ushaurimzuri na tumeuchukua. Sasa hivi ndiyo tumeamua kwamba,tuanze kwanza kuimarisha reli ya kati, iweze kuchukua mizigomingi zaidi kuliko hii mizigo yote kwenda kwenye barabarahii ya kati.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ili barabara hizi ziwezekudumu, lazima tuwekeze zaidi kwenye reli na tutachukuapia upande wa Kaskazini kutoka Tanga kwenda Moshi ilimizigo iweze kusafirishwa kwa reli. Kwa hiyo, Serikali itawekezazaidi kwenye reli kusudi barabara zetu ziweze kudumu.

SPIKA: Ahsante. Sikumwona mtu mwingine, hamwezikusimama baada, mnatakiwa msimame kabla muonekane,halafu niwaite. Tunaendelea, Mheshimiwa Pindi HazaraChana swali linalofuata, kwa niaba yake Mheshimiwa KapteniKomba.

Na. 425

Kivuko Katika Mto Ruhuhu

MHE. JOHN D. KOMBA (K.n.y. MHE. PINDI H. CHANA)aliuliza:-

Kivuko cha Mto Ruhuhu kimeondolewa injini namamlaka husika, hivyo kivuko kutokufanya kazi:-

(a) Je, ni lini injini hiyo itarudishwa ili kivuko kianzetena kufanya kazi?

(b) Je, Serikali ina mpango gani wa kujengadaraja kwenye Mto Ruhuhu?

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

18

19 JUNI, 2013

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziriwa Ujenzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Pindi HazaraChana, Mbunge Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b), kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu swali namba 90lililoulizwa na Mheshimiwa Captain John Komba tarehe 8Februari, 2012, injini ya kivuko cha Mto Ruhuhu iliyokuwaimeazimwa kwenda kufungwa kwenye Kivuko cha Kilomberoilirudishwa na kufungwa kwenye kivuko cha Mto Ruhuhutarehe 9 Januari, 2012. Injini hiyo ilihamishiwa katika Kivukocha Kilombero kwa muda kutokana na dharura ya kuharibikakwa injini ya Kivuko cha Kilombero.

Mheshimiwa Spika, aidha injini ya Kivuko cha Ruhuhuiliazimwa wakati kivuko hicho hakifanyi kazi kwa kuwa Kivukocha Ruhuhu hakifanyi kazi wakati maji yamepungua au majiyamejaa sana. Kwa sababu hii Kivuko hiki hufanya kazi kwamiezi mitatu au minne tu kwa mwaka kati ya mwezi Aprili naAgosti.

Mheshimiwa Spika, Serikali imepanga kujenga darajalitakalojumuisha bwawa (Bridge Cam Dam) kama mradimmoja katika Mto Ruhuhu ili pamoja na kutumika kamadaraja, bwawa litumike kwa shughuli za umwagiliaji katikabonde la Mto Ruhuhu eneo la Lituhi upande wa Mkoa waRuvuma na Kipingu kwa upande wa Mkoa wa Njombe.

Serikali inaendelea na maandalizi ya kufanyaupembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kujengadaraja bwawa la kumwagilia na tayari hadidu za rejea kwaajili ya kumpata Mhandisi Mshauri kwa kufanya usanifuzimekamilika.

Mheshimiwa Spika, mradi huu utahusisha Wizara yaUjenzi, Wizara ya Maji, Wizara ya Kilimo, Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi yaMakamu wa Rais, Mazingira.

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19

19 JUNI, 2013

MHE. JOHN D. KOMBA: Mheshimiwa Spika, ninamaswali mawili ya nyongeza. Upembuzi yakinifu, usanifu nimaneno ambayo yamesikika mara nyingi sana tangu miakamitano iliyopita katika jambo hili la kuweka daraja katika mtohuo. Je, hii lugha itakwisha lini?

Mheshimiwa Spika, namba mbili, hivi kweli Serikali inahuruma na watu wale walioko eneo hilo?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kwanzakabisa naomba Mheshimiwa Komba asikate tamaa namaneno ninayosema ya upembuzi yakinifu. Daraja lile ililiweze kudumu kwa muda unaotarajiwa ni vizuri tukafanyakazi hii kwa mpangilio unaotakiwa.

Tufanye usanifu wa kina, halafu tuweze kuitishakandarasi tuweze kujenga daraja lile na tayari hata Raisameshasisitiza kwamba, tuanze upembuzi yakinifu harakaiwezekanavyo. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbungekwamba, kazi hiyo itafanyika haraka iwezekanavyo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu huruma ya Serikali, kwakweli ipo, kwanza kile kivuko kilikuwa kinachukua tani saba,Serikali ikabidi inunue kivuko kingine kinachochukua mpakatani 50. Tatizo lililoko pale ni maji. Maji yakipungua kile kivukohakiwezi kufanya kazi na maji yakizidi pia kile kivuko kwasababu ni kikubwa hakiwezi kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, kwa huruma ambayo Serikali yaChama cha Mapinduzi inayo, ndiyo maana tumeonatugharamie kujenga daraja ambalo litafanya kazi zote,kupitisha magari pamoja na umwagiliaji. Kwa hiyo, naombaMheshimiwa Komba pamoja na wananchi wa kule Mbingawatuvumile, Serikali itatatua tatizo hilo.

SPIKA: Ahsante. Sikumwona mtu mwingine kabla yahapo na tunaendelea na Wizara ya Nishati na Madini,Mheshimiwa Abdulsalaam Amer, kwa niaba yake ataulizaswali hilo Mheshimiwa Nassir.

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

20

19 JUNI, 2013

Na. 426

Kupeleka Umeme Katika Vijiji

MHE. YUSUPH A. NASSIR (K.n.y. MHE. ABDULSALAAM S.AMER) aliuliza:-

Je, Serikali itapeleka lini umeme katika Vijiji vyaZoumbe, Lumbe, Kipekenya, Ulaya Mbuyuni, Ulaya Kibaoni,Nakala na Mhenda?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishatina Madini, napenda kujibu swali la Mheshimiwa AbdulsalaamSeleman Amer, kama ifutavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Vijiji vya Zoumbe,Lumbe, Kipekenya, Ulaya Mbuyuni, Ulaya Kibaoni, Makalana Mhenda bado havijapatiwa umeme. Hata hivyo, Serikalikupitia Shirika la Umeme inatarajia kufanya tathmini kwenyevijiji hivi katika mwaka wa fedha 2013/2014 ili kuanisha kiasicha fedha kinachohitajika.

Mheshimiwa Spika, tathmini hii ikikamilika itaiwezeshaSerikali kutafuta fedha za utekelezaji kutoka kwenye vyanzombalimbali ukiwemo Mfuko wa Nishati Vijijini kwa ajili yakuvipelekea umeme vijiji hivyo.

MHE. YUSUPH A. NASSIR: Mheshimiwa Spika, nashukurunina swali moja tu la nyongeza. Kwa kuwa ratiba iliyotolewana REA ya mchanganuo wa miradi katika Jimbo hili la Mikumihaikutaja vijiji husika, je, Mheshimiwa Waziri anatuambiajekuhusiana na utaratibu mzima wa kupata fedha ili miradi yaumeme kwenye vijiji hivi iweze kutimia?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba vijijivilivyotajwa na Mheshimiwa Mbunge katika swali hili havimo

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

21

19 JUNI, 2013

katika REA phase II, lakini awamu hii ya pili ya miradi ya REAsiyo ndiyo mwisho wa miradi ya REA. Sasa hivi tuko katikamchakato wa kuandaa awamu ya tatu, kwa hiyo,nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika awamu ya tatu vijijihivi vitakuwemo.

Mheshimiwa Spika, aidha, nipende kutambulisha naniwaeleze wananchi wa Jimbo la Mikumi kwamba baadhiya vijiji ambavyo vimo ni pamoja na Kijiji cha Malolo,Wazaganza na vijiji vingine ambavyo vitapatiwa umemekatika awamu hii.

MHE. DKT. PUDENSIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaSpika, ahsante kwa kunipatia nafasi nami kuweza kuuliza swalila nyongeza. Kwa kuwa mazingira ya Mikumi yanafananakabisa na mazingira ya Wilaya mpya ya Mlele. Je, ni lini Serikaliitapeleka umeme katika Kata ya Ilunde, Nsekwa, Mwese,Katuma na Mpanda Ndogo?

SPIKA: Aah Mheshimiwa! Haya hebu jaribu kujibu, swalijipya hilo, jibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, katika miradi ya REAphase II, Wilaya karibu zote zimepatiwa vijiji vichachevichache. Naomba tuwasiliane baada ya hapa, tuwezekuona hivi alivyovitaja kama vimo katika orodha hii.

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika,nashukuru sana kwa kunipa nafasi. Serikali imetekeleza vilivyoahadi ya Mheshimiwa Jakaya Kikwete ya kupeleka umemeMjini Namanyere, lakini njiani kote umeme haujasambaa,umepita na kudondoka nyumba mbili au tatu, lakini sasawananchi wanauliza ni lini umeme huu utaenea katikamaeneo yote ya vijiji kwa sababu wanauhitaji, wanauonaunapita na kudondoka katika nyumba mbili, tatu kuondoka?Naomba majibu ya Serikali.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

22

19 JUNI, 2013

umeme ulipokwenda katika Wilaya ya Namanyere na Nkasi,umepita katika baadhi ya maeneo na baadhi ya maeneobado. Niseme tu hili litakuwa ni zoezi la kudumu, kwa sababuhata kama tutasema tunapeleka umeme vijijini, haiwezekanitukapeleka vijiji vyote kwa mara moja, kwa sababu makaziyatakuwa yanaongezeka na watu wanaongezeka, kwa hiyo,ni jambo linaloendelea, siyo kwamba litakoma mara moja.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba, tutaendelea kusambazaumeme kadri tunavyopata fedha, lakini kadri ya maombi yawananchi, hata Dar es Salaam yenyewe, Dodoma na Mikoamingine yote, si kweli kwamba wananchi wote katika Mikoahiyo mijini wana umeme. Kwa hiyo, usambazaji utakwendakadri ambavyo tunapata fedha na kadri ambavyo wananchiwanahitaji.

SPIKA: Naomba tuendelee na swali linalofuata,Mheshimiwa John Chiligati!

Na. 427

Utafiti wa Madini ya Urani Manyoni

MHE. KAPT. JOHN Z.CHILIGATI aliuliza:-

Kampuni ya URANEX imeanza utafiti wa Madini yaUrani kwenye Vijiji mbalimbali Wilayani Manyoni na kuwapawananchi hofu kubwa kuhusu zoezi hilo:-

(a) Je, Serikali itachukua hatua ganikuwaondolea wananchi hofu waliyonayo kuhusu usalamawao na hatma ya mashamba yao endapo yatachukuliwana mwekezaji huyo?

(b) Je, hadi sasa utafiti huo umeonesha matokeogani?

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

23

19 JUNI, 2013

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. STEPHENJ. MASELE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishatina Madini, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kapteni JohnChiligati, Mbunge wa Manyoni, lenye sehemu (a) na (b) kamaifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, Sera ya Madini ya mwaka2009 na Sheria ya Madini ya mwaka 2010 zinatumika katikakusimamia shughuli za utafutaji wa Madini ya Urani nchini.Kanuni maalum (The Mining (Radioactive Minerals)Regulations, 2010) zimetungwa chini ya Sheria ya Madini yamwaka 2010 kwa ajili hiyo.

Kanuni na Sheria zote zilizotungwa na zinazoendeleakutungwa zinahusiana na usimamizi wa Madini hayo ya Uranina zinalenga kuzingatia Miongozo, Taratibu za Shirika laKimataifa la Nguvu za Atomu (IAEA) za Usimamizi wa Madinihayo na zinahakikisha kuwa uchimbaji (exposing of uraniumare on the surface) hauleti madhara au athari kwa watu namazingira.

Mheshimiwa Spika, wananchi wa vijiji mbalimbali vyaWilaya ya Manyoni, wasiwe na hofu yoyote kuhusu utafiti waMadini ya Urani unaoendelea kufanywa na URANEX, kwanikampuni hii inafanya shughuli zake kwa mujibu wa Sheria naKanuni nilizoziainisha.

Kampuni hiyo inaendelea na utafiti wa kimaabarawenye nia ya kutaka kuanza uchimbaji wa Urani katika eneohilo. Ikiwa URANEX itahitaji sehemu ya ardhi ya wananchi,wenye ardhi katika eneo hilo watahusishwa na watapatafidia stahiki pamoja na kuhamishwa na kujengewa makazimapya kwa gharama ya kampuni hiyo.

(b) Mheshimiwa Spika, hadi sasa Kampuni yaURANEX imegundua takribani Ratili milioni 29 za mashapo yaurani katika eneo la Manyoni. Pamoja na kwamba kiwangohicho cha mashapo kinatosha kuanzisha uchimbaji, Kampuni

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

24

19 JUNI, 2013

hiyo inaendelea kufanya utafiti wa kimaabara na ubora wakutenganisha urani katika mashapo hayo yenye udongo wamfinyanzi kwa wingi. Mara zoezi hilo litakapokamilika naufanisi wa kampuni hiyo itaanza taratibu za kuanza uchimbajiwa madini hayo.

MHE. KAPT. JOHN Z.CHILIGATI: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja dogola nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hivi sasa kuna Asasi zaKiraia (NGOs) zinapita katika maeneo ya Wilaya ya Manyonina ya Bahi, zikisambaza upotofu na chuki kwa wananchi dhidiya shughuli hii ya madini haya. Je, Serikali kwanza inajuaharakati za Wanaharakati hao na kama inajua, inatoa tamkogani kukomesha harakati hizo?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. STEPHENJ. MASELE): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba na sisitunatambua kwamba, kuna harakati mbalimbali zawanaharakati kueleza ama kupotosha wananchi kuhusianana uchimbaji wa urani, lakini kama nilivyoeleza kwenye swalila msingi kwamba, shughuli hizi za uchimbaji wa uranizinafanywa kwa taratibu zote za Kimataifa zinazosimamiauchimbaji wa urani, chini ya Shirika la Nguvu za Atomi la Dunia.

Wanaharakati hawa wanafanya pia shughuli hizipengine kwa maslahi fulani kutoka kwa hawawanaowafadhili kufanya shughuli hizo.

Waheshimiwa Wabunge, ningependa tu nisemekwamba, madini ya urani ni madini ya kimkakati. Kwa hiyo,dunia, Mataifa makubwa pia yanayatazama madini hayakwamba, yanazalishwa wapi, yanakwenda wapi nayanatumikaje. Kwa hiyo, wale walioyapata, ambaohawakuyapata pia hawafurahii kuona yameshikiliwa namakampuni ya nchi ambazo pengine wanasigana kisiasa zakidunia.

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

25

19 JUNI, 2013

Kwa hiyo, shughuli za wanaharakati wetu pia lazimawatambue anayepiga ngoma hiyo anamaanisha nini na sisitusidandie tu kucheza ngoma ambayo mpigaji hatujuianamaanisha nini. Kwa hiyo, niseme tu Serikali tunasimamiana tunazingatia taratibu zote za uchimbaji wa urani.

Mheshimiwa Spika, madini haya yapo kila siku tunaishinayo na hatujapata taarifa ya kuambiwa kwamba, kunamadhara yametokea katika eneo la Bahi ama Manyoni, amamaeneo ya Mkuju ambako tuna shughuli hizi za urani, lakininamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutaendeleakusimamia kuhakikisha Sheria hazivunjwi na taratibu zotezinazingatiwa.

MHE. VITA R.M. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kwakuwa mradi wa urani pia tumebahatika na sisi Wilaya yaNamtumbo tuna mradi wa Mkuju na taratibu za utoaji wavibali vya mazingira umeshakamilika, Wizara ya Nishati naMadini mmeshatoa Leseni, lakini sasa hivi mpo katikamajadiliano ya Mkataba (MDAs). Sasa je, ni lini mtamalizamajadiliano hayo ili mradi huo uweze kuanza na watu waNamtumbo waweze kuona manufaa ya mradi huo?

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwa kifupi,muda umekwenda.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. STEPHENJ. MASELE): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba,tumekamilisha zoezi la kutoa Leseni na katika eneo lamkataba, kuna maeneo ambayo tulikuwa hatukubalianinayo kama Serikali kwa maslahi ya nchi hasa kwenyemaeneo ya kodi (withholding tax) katika interest na service,Serikali tumeshatoa msimamo wetu jana na tumeshapelekataarifa hiyo kwa kampuni inayohusika.

Sasa offer iko mezani, either wanaichukua auwanaiacha, lakini sisi kama Serikali tumeshaweka msimamowetu na position yetu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge,

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

26

19 JUNI, 2013

nikuombe tu kwa maslahi ya wananchi wa Namtumbo,kuangalia upande wa pili wa ile kampuni kama ile positionyetu wataichukua au wataiacha. Ahsante.

MHE. ENG. HAMAD YUSSUF MASAUNI: MheshimiwaSpika, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza swali lanyongeza. Swali langu ni kwamba, wakati wa uhamisho waumiliki wa mradi huu kutoka kwenye Kampuni MANTRASinasemekana Serikali ilipoteza kiwango kikubwa sana chakodi, je, hatua gani imefikia kupitia TRA kuweza kuzipatafedha hizi?

SPIKA: Unadhani umeelewa, sisi hatujaelewa.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. STEPHENJ. MASELE): Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kwambaMANTRA Tanzania Limited, ndiyo iliyouza hisa zake kwakampuni ya MANTRA ya Australia na Kampuni ya MANTRA yaAustralia iliuza kwa Kampuni ya Kirusi ya ARMZ kwa one billiondollar na Serikali ilidai kuwa imesitahili kupata malipo yacapital gain tax.

Mheshimiwa Spika, sasa kesi ile iko Mahakamani nainasimamiwa na TRA na siyo Wizara ya Nishati na Madini kwasababu ni kesi inayohusiana na mambo ya kodi ambayokimsingi TRA ndiyo yeye mandate ya kusimamia.

Kwa hiyo, nisingeweza kutoa details kwa sasa kwasababu shauri hili liko Mahakamani na linaendelea huko kwamujibu wa taratibu za Sheria za Kodi.

SPIKA: Muda umekwenda, twende Wizara ya Ulinzi naJeshi la Kujenga Taifa.

Mheshimiwa Maryam Salum Msabaha atauliza swalihilo, kwa niaba yake Afande mwingine Mheshimiwa EsterBulaya atauliza swali hilo.

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

27

19 JUNI, 2013

Na. 428

Mgogoro Kati ya Kambi ya Bavuai naWananchi wa Mpendae

MHE. ESTER A. BULAYA (K.n.y. MHE. MARYAM SALUMMSABAHA) aliuliza:-

Kumekuwepo na mgogoro wasiku nyingi kati yaKambi ya JKT ya Bavuai, Zanzibar na wakazi wa Mpendaewalio maeneo ya Kaburi Kikombe na Migombani kwawananchi kuchukuliwa maeneo yao na mpaka leohawajapata ufumbuzi:-

(a) Je, Serikali inawaambiaje wakazi wanaoishikatika maeneo yanayopakana na Kambi ya Jeshi?

(b) Serikali haioni kwamba inaingia kwenyemigogoro baina ya Wanajeshi na wananchi?

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Maryam Msabaha, Mbunge wa Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, napenda kumfahamishaMheshimiwa Maryam Msabaha kuwa, katika mwaka huu wafedha 2013/2014, Jeshi la Wananchi wa Tanzania lina mpangowa kupima mipaka ya Kambi ya Bavuai ambayo inamgogoro na wananchi wa Mpendae.

Iwapo katika upimaji huo wa mipaka itabainika kuwaJeshi la Wananchi wa Tanzania limechukua maeneo yawananchi, basi wananchi hao watalipwa fidia stahiki, lakiniiwapo itabainika kuwa wananchi nao wamechukua maeneoya Jeshi, basi wananchi hao watatakiwa kuondoka kwenyemaeneo hayo.

(b) Mheshimiwa Spika, Serikali haina sababu

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

28

19 JUNI, 2013

yoyote ya kuwa na mgogoro na wananchi wakeinayowahudumia. Kama nilivyosema awali, Wizara yangu inampango wa kupima maeneo yote ya Kambi ya Bavuai ilikuweka wazi mipaka ya Kambi hiyo na hatimaye kuepukamigogoro hiyo.

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, namshukuruMheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri.

Mheshimiwa Spika, migogoro ya mipaka pia ipo naTanzania Bara na hasa katika Kata ya Kunduchi, Jimbo laKawe na najua Serikali ilikuwa inashughulikia suala zima lauwekaji mipaka, nataka kujua, wamefikia wapi ili kutatuamgogoro wa Kata ya Kunduchi.

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwenye Kambinyingi za Jeshi, zimekuwa zikiongozwa na akinababa, lakiniwapo akinamama wanajeshi ambao wanavyeo ambavyovinafaa na wenyewe kuongoza kwenye Kambi hizo. Sasa je,Mheshimiwa Waziri huoni kwamba kuna haja sasa kwenyehivi Vikosi vingine vya Jeshi, akinamama wapate nafasi yakuongoza?

SPIKA: Ili wapime mipaka. Ni swali jipya kabisa, lakininaomba ujibu tu.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna maeneo mbalimbali yenyemigogoro na kama nil ivyosema wakati nil ipokuwanikiwasilisha bajeti ya Wizara yangu, kuna migogoro kama80 hivi ukiwemo mgogoro wa Kunduchi, lakini kwa taarifaniliyo nayo na bahati nzuri nimezungumza na MheshimiwaMbunge wa Kawe, suala hili limefika katika hatua nzuri sanaya utekelezaji. Tunayo ahadi mimi na yeye baada yakumaliza Bunge hili Tukufu tupate nafasi sasa ya kwendakuangalia utekelezaji wa upimaji wa mipaka hiyo katikaKambi hiyo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la akinamama, najuakwamba wapo akinamama, wana nafasi nzuri tu ya uongozi

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

29

19 JUNI, 2013

katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Bahati mbaya sana,tunapotafuta kiongozi katika Jeshi, tunatafuta Mwanajeshiama mwanamke au mwanamume kwa kuzingatia sifa.

Mheshimiwa Spika, sasa pale tutakapoona kwambamwanamama anazo sifa zinazostahiki hatutakuwa na hiyanahata kidogo ya kumpa nafasi hiyo anayostahiki. Kamamwana baba anazo sifa ya kushika nafasi fulani na yeyehatutamfanyia hiyana kwa sababu ati ni mwanamme.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tumekuwa tukiendeleakutenda haki kwa kadri hali inavyoruhusu. NamhakikishiaMheshimiwa Mbunge kwamba tutaendelea kutekeleza nakuhakikisha kwamba tunawatendea haki wanaume nawanawake katika utumishi wa Jeshi la Wananchi waTanzania.

MHE. AMINA ABDALLAH AMOUR: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja lanyongeza. Nini ufumbuzi wa kudumu wa migogoro ya ardhikati ya JWTZ na wananchi?

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inachukua hatua tatu ilikuhakikisha kwamba tunapunguza au hatimaye kumalizakabisa migogoro kati ya wananchi na Jeshi la Wananchi waTanzania.

Hatua ya kwanza, tumeamua kuyapima maeneo yaJeshi hasa yale yenye migogoro, likiwemo lile eneo la Kambiya Bavuai na maeneo mengine ili kuainisha mipaka kati yaJeshi na Wananchi.

Pil i, kuwalipa wananchi ambao maeneo yaoyamechukuliwa na Jeshi kwa ajili ya shughuli za ulinzi.

Tatu, kuendelea kuwaelimisha wananchi naowaheshimu na wathamini maeneo ambayo yanamilikiwa naJeshi kwa sababu Jeshi la Wananchi wa Tanzania lipo kwaajili ya shughuli za ulinzi wa nchi yetu.

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

30

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, najua wananchi wanayatamanisana maeneo ambayo yanamilikiwa na Jeshi kwa ajili yashughuli za maendeleo, lakini ni kweli vile vile kwamba, Jeshilinahitaji maeneo hayo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi nausalama wa nchi yetu.

MHE. MWIGULU L.N. MADELU: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Kwanza nimwombe Mheshimiwa Waziriatakapokuwa anashughulikia migogoro akumbuke na Kambiya JKT Msange kule Tabora na yenyewe iko kwenye mgogoro.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia niseme kwamba, kwa kuwamigogoro hii mingi inatokana na uhaba wa maeneo yaaniardhi kwenye Kambi ambazo zimekuwa katikati ya miji. Je,kwenye ufumbuzi wa kudumu, kwa nini Mheshimiwa Waziriasilete Kambi zingine kwenye maeneo ambayo yapo tukama Iramba kule na eneo lilishakubalika, lipo, halinamgogoro ili kuyaacha maeneo ya mjini ambako ardhiimekuwa kwa matumizi ya binadamu wengine?

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Spika, nimekubali kwamba Kambi ya JKT paleMsange ina tatizo la mgogoro wa ardhi. Kama nilivyosema,tutafanya kila linalowezekana kushughulikia suala hilo.

Mheshimiwa Spika, suala la kuhamisha Kambi za Jeshila Wananchi wa Tanzania kutoka maeneo ya mjini kwendamaeneo ya vijijini, nasema kwamba, Jeshi la Wananchi waTanzania limewekwa katika maeneo haya, hasa katikamaeneo ambayo ni nyeti na yana umuhimu sana katikashughuli za ulinzi.

Mheshimiwa Spika, litakuwa ni jambo la ajabu sana,Jeshi unaliondoa katika eneo la mjini kama kwamba hatunadhima ya kuwalinda wananchi waliko kwenye maeneo yamjini. Nasema tu, ushauri tumeupokea, lakini ni jambo ambalotunapaswa kulizingatia, kwa sababu umefanyika utaalamsana wa kitaalam ili kujua kwa nini Kambi inawekwa kwenyemaeneo mahususi.

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

31

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, pamoja na ombi hilo, tutalifanyiakazi na kutoa uamuzi, nadhani kwamba uamuzi huo utakuwawa busara na wa hekima.

SPIKA: Tuendelee na Wizara ya Kilimo, Chakula naUshirika. Mheshimiwa Donald Max atauliza swali hilo!

Na. 429

Kufufua Kiwanda cha Ushirika Geita

MHE. DONALD K. MAX aliuliza:-

Geita ni Mkoa mpya na una kiwanda kimoja chaUshirika pamoja na maghala kadhaa ya kuhifadhia bidhaana nafaka:-

Je, Serikali haioni umuhimu wa kukabidhi mali hizo zaushirika ili Mkoa mpya wa Geita uweke mikakati ya kufufuakiwanda hicho ili kuongeza ajira kwa wananchi na kuongezapato la Taifa pamoja na kuwapa moyo wakulima wa zao lapamba ambalo liko katika hali mbaya?

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA (K.n.y.WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Donald Kelvin Max, Mbunge wa Geita, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mkoa mpya wa Geita unaViwanda vitatu vya Kuchambua Pamba, vilivyoko Kasamwa,Chato na Masumbe, ambavyo vimelalamikiwa na VyamaVikuu vya Ushirika vya Nyanza Cooperative Union (1984)Limited- NCU, Shinyanga Region Cooperative Union (1984)Limited- SHIRECU na Biharamulo Cooperative Union (1996)Limited ambavyo viko katka Mikoa mitatu ya Mwanza,Shinyanga na Kagera.

Mheshimiwa Spika, Jineri (Kiwanda) cha Kasamwa ni

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

32

19 JUNI, 2013

mali ya Wanaushirika wa Geita kupitia Nyanza CooperativeUnion (1984) Limited. Aidha, Vyama vya Ushirika vya msingivilivyopo Mkoa wa Geita ni vyama wanachama ndani yaNyanza Cooperative Union (1984) Limited, ambavyovilichangia, vimewekeza rasilimali zao ikiwa ni pamoja namitaji na katika shughuli za uzalishaji mali ikiwemo ujenzi waKiwanda cha Kasamwa na hivyo Kiwanda cha Kasamwabado ni mali vya Wanaushirika wa Geita.

Mheshimiwa Spika, mali za kudumu za Vyama Vikuuvya Ushirika zilizoko kwenye eneo la utawala wa Mkoa waGeita zinaweza kuendelea kuwa za Wanaushirika kwautaratibu wa Vyama Vikuu vyenye mali za kudumu kuwauziaWanaushirika walioko katika Mkoa wa Geita Hisa. Aidha,Wanaushirika waliokuwa wanahudumiwa na NyanzaCooperative Union (1984) Limited, Shinyanga RegionCooperative Union (1984) Limited- SHIRECU na KageraCooperative Union-KACU, pamoja na BiharamuloCooperative Union (1996) Limited-BCU ambao kwa matakwayao walijitoa kwenye Vyama Vikuu vya Ushirika, kwa mujibuwa Kifungu cha 96 cha Sheria ya Vyama vya Ushirika yaMwaka 2003, watalazimika kugawana mali na madeniyaliyopo, hivyo kuanzisha Chama cha Ushirika kipya kikirithimali za madeni yaliyopo.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mali za Kiwanda chaKaswamwa zipo chini ya ushirika, Serikali haiwezi kukabidhimali hizo za Ushirika kwa uongozi wa Mkoa mpya wa Geitakwani Wanaushirika wenyewe ambao ndio wamiliki lazimawashirikishwe kutoa uamuzi kuhusu mali hizo ikiwa ni pamojana kutafuta mbia mwenza au mwekezaji.

MHE. DONALD K. MAX: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Hapa swali langu nafikiri halikueleweka vizuri, kwasababu siyo nia yetu sisi kwamba hii mali ya Wanaushirikaipewe Serikali. Tunachosema ni kwamba, NyanzaCooperative Union, pamoja na SHIRECU pamoja naBiharamulo Cooperative, hivi Viwanda vyote vya Pamba sasa

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

33

19 JUNI, 2013

hivi, asilimia 90 viko ICU, sisi tunavitazama tu, hii ni miakakaribu miaka 15 hivi viwanda havifanyi kazi watu wanang’oavipuri wanakwenda kuuza kama scrapper.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka kujua Serikaliinakuja na mkakati gani, tutakaa tunavitazama tu vimekaa.Kwa sababu hivi viwanda ndivyo vilivyowasomesha Babuzetu, Baba zetu na hata sisi. Nataka kujua Serikali inakuja namkakati gani, hata vile vya nguo, Tabora Textile, MwanzaTextile, vyote vimelala. Tunataka kujua Serikali ina mikakatigani? (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri, tena sawa sawa Waziri waViwanda, hata kama ni ya Kilimo lakini ni ya Viwanda.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA (K.n.y.WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Mheshimiwa Spika,ni kweli kama anavyosema kwamba, Vyama Vikuu vikongwe,kama vile Nyanza na Mwanza kile cha National CooperativeUnion, pamoja na Biharamulo ni vyama vikongwe ambavyokwa sasa hivi viko ICU. Lakini kwa vile anasema kwamba,kuna Kiwanda cha Kuchambua Pamba cha Kasamwaambacho kipo Geita na halafu suala la kuomba kwambaChama cha Ushirika kiundwe Geita wakati Kaswamwa ikoGeita na Kaswamwa iko chini ya Nyanza Cooperative Union.

Mheshimiwa Spika, Kiwanda hiki cha Kasamwakilijengwa mwaka 1959 na sasa hivi nacho kinafanya kazi vizurisiyo vibaya sana. Lakini kuundwa ushirika wa Geita kwa sasahivi itakuwa ni vigumu. Ombi hili limefanywa na Mkuu waMkoa ambaye amemwandikia Mrajisi wa Vyama vya Ushirikaili aweze kuunda Ushirika mpya kwa Geita, ukiachana naVyama Vikuu hivi kama nilivyosema vya Nyanza, Mwanza nakule Kagera.

Mheshimiwa Spika, shida ni kwamba, Wanaushirikawa Kasamwa ndiyo wamiliki wakuu, lazima washirikishwekama kuna kuunda Ushirika mpya na kwa sababu nimesemakwamba Kasamwa yenyewe ipo chini ya Nyanza. KuuaNyanza au kuanzishwa kwa Kasamwa ni lazima Wanaushirika

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

34

19 JUNI, 2013

wa Kasamwa ambao ndio wamiliki washirikishwe. Iko sheriaya vyama vya ushirika ambayo inatawala, kwa hiyo kama nikuuawa kwa Vyama vile Vikuu vitatu na kuanzisha chamakingine kipya, au kubakiza kile cha Kasamwa ambacho kipoGeita na kina Washirika wa Geita, Sheria iliyopo lazimaichukue mkondo wake.

SPIKA: Tatizo la Viwanda vyote vilivyosimama, ndichotunachotaka kusikia. Naomba nimpe Waziri wa Viwanda naBiashara, pengine.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaSpika, pamoja na majibu mazuri yaliyotolewa na MheshimiwaNaibu Waziri, napenda kuongezea majibu ya swali laMheshimiwa Max, kama hivi ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tunaelewa kwamba hivi sasabaadhi ya Viwanda hasa vya Pamba, vingi havifanyi kazi.Lakini mkakati tunaouchukua sasa hivi, tayaritumekwishawasiliana na Kampuni moja kubwa tu kutokaJapan, ambayo inaitwa Nitori ambao wao wana nia yakuwekeza katika eneo la kutengeneza nguo na kuzalishaPamba yenyewe.

Mheshimiwa Spika, tayari Kampuni hiiimekwishatembelea mikoa kadhaa pamoja na Shinyanga.Wamekwishafika maeneo ya Geita, kitu wanachokifanyasasa ni kuzungumza na wahusika wa Ginneries hizi ili kuona niuwezekano gani kama wanaweza kuingia ubia na kufanyakazi kuhakikisha kwamba Viwanda hivi vinafanya kazi. Kwahiyo Kampuni hiyo ya Nitori tumeshakaribisha na tayariimeshaonesha interest ya kuendeleza viwanda hivi. (Makofi)

SPIKA: Nadhani Mawaziri wote mnataka mjibu. Haya,Waziri wa Nchi.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA URATIBUNA BUNGE): Mheshimiwa Spika, nataka kutoa taarifakwamba, Waheshimiwa Wabunge watakumbuka kuwa,tumeshasoma mara ya Kwanza Muswada wa Sheria mpya

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

35

19 JUNI, 2013

ya Ushirika. Naomba Waheshimiwa Wabunge waisome,Sheria ile, kwa sababu katika Bunge lijalo tutaipitisha, ndiyoitatoa kasoro zote ambazo Mheshimiwa Max ameulizazinazotokana na Sheria.

Mheshimiwa Spika, tunajua uko udhaifu mkubwa sanaambao umesababisha vyama hivi vingi vya Ushirika kufilisika,SHIRECU, Nyanza na vingine. Kwa hiyo, nawaomba sanamarekebisho yote ya Sheria hii mpya ya Ushirika inayokujatujizatiti vizuri hii ndiyo itakayotoa majibu ya kwamba vyamavya sasa vinaundwa namna gani na mali zake zinakwendamahali gani.

Mheshimiwa Spika, la pili, juu ya mali zilizokwishauzwaambazo hazifanyi kazi, tulishawahi kusema hapa, pamoja namajibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri wa Viwanda, Serikaliimeshafanya tathmini ya mali zote, viwanda na mashirika yoteyaliyouzwa, ili kubaini hali yake na namna ya kufanya, yaaniCHC imekwishapendekeza hatua za kuchukua.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa taarifa hiyo iko Serikalinina wakati wowote Serikali itatoa taarifa baada ya kuipitia,mambo gani yafanyike kulingana na mapendekezo ya CHC,kwa Shirika na Kampuni moja moja iliyokwishauzwa ili viwezekufufuliwa na viweze kufanya kazi. (Makofi)

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NAURATIBU): Mheshimiwa Spika, nataka kutoa ufafanuzi tu juuya Sheria ya Ushirika. Kwamba iwapo wanachama wa Geitawanataka kuunda Chama chao cha Ushirika na kwa sababukuunda Ushirika ni hiari, uko utaratibu hata kwa sheria ya sasaambao unawawezesha kutumia mikutano mikuu ya Vyamavya Ushirika ambavyo wanachama wa Geita ni wanachamaili kuweza kufikia maamuzi ya kama wanaweza kuundaushirika nje ya Nyanza Cooperative Union au SHIRECU.

Mheshimiwa Spika, lakini vile vile mali za Vyama vilezina matatizo kwa sasa kwa sababu nyingine zimewekezwa,kwa hiyo, hata kama wakiunda ushirika wa Geita sasa,

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

36

19 JUNI, 2013

watapata matatizo ya kupata mgao wa mali za vile vyama,mpaka migogoro inayohusiana na mali hizo itakapokuwaimetatuliwa.

SPIKA: Ahsante. Tuendelee na swali lililobaki la Wizaraya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, swali hilo litaulizwana Mheshimiwa John Mnyika, kwa niaba yake MheshimiwaMurtaza Mangungu.

Na. 430

Sera ya Taifa ya Vijana na Mkatabawa Vijana wa Afrika

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU (K.n.y. JOHN J.MNYIKA) aliuliza:-

Utekelezaji wa haraka wa Sera ya Taifa na Mkatabawa Vijana wa Afrika ni hatua muhimu katika kuboreshamaisha ya vijana na kuchangia katika maendeleo ya nchi:-

(a) Je, ni lini Serikali itawezesha kukamilishwa kwamchakato wa uundaji wa Baraza la Vijana la Taifa?

(b) Je, ni hatua gani imefikiwa katika kuanzishaBenki ya Vijana Tanzania ili kurahisisha mfumo wa Vijanakupata Mikopo na mitaji ili kuweza kujiajiri;

(c) Je, l ini Sheria itatungwa ya kuwezeshautekelezaji wa malengo ya msingi ya Sera ya Taifa ya Vijanana Mkataba wa Vijana wa Afrika?

NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NAMICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, napenda kujibu swali laMheshimiwa John John Mnyika, lenye sehemu (a) (b) na (c),kama ifuatavyo:-

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

37

19 JUNI, 2013

(a) Mheshimiwa Spika, mchakato wa uanzishajiwa Baraza la Vijana unaendelea vizuri. Hadi sasa Warakakwa Baraza la Mawaziri kuomba kutunga Sheria ya kuanzishaBaraza la Vijana umekwishajadiliwa katika ngazi ya MakatibuWakuu na baadaye kupelekwa kwenye Baraza la Mawazirikwa maelekezo zaidi. Mara uamuzi wa Baraza la Mawaziriukitolewa hatua ya kuandaa Muswada itaendelea.

(b) Mheshimiwa Spika, hatua iliyofikiwa katikakuanzisha Benki ya Vijana ni kwamba hadi sasa mchakatowa kumpata Mshauri Mwelekezi upo katika hatua za mwisho.Mara Mshauri Mwelekezi akipatikana atafanya upembuziyakinifu na kutoa ushauri wa kitaalam ambao utazingatiwakatika kuanzisha Benki ya Vijana endelevu.

(c) Mheshimiwa Spika, kwa sasa Waraka waBaraza la Mawaziri wa kuomba kutungwa Sheria yautekelezaji wa Mkataba wa Vijana wa Afrika unaandaliwa,pindi utakapokamilika utapelekwa kwenye ngazi za juu zaSerikali kwa utekelezaji ikiwa ni pamoja na kuandaa Muswadawa Sheria.

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika,nashukuru. Napenda kujua, kikubwa ambacho tunazingatiahili suala litachukua muda gani yaani tuwe na timeframe,isije akawa mpaka wanafikia kuwa wazee huu mchakato naupembuzi haujakamilika. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, swali lingine, pamoja na vijanakuwezeshwa na kuweza kupata namna ya kuweza kujikimu,lipo suala la Utaifa kwa Vijana. Zipo jitihada kubwa ambazozimeoneshwa na Dkt. Mengi ambaye anamiliki Radio Onena Clouds FM inayomilikiwa na Joseph Kusaga, kuhamasishaUtaifa, uzalendo kwa vijana. Sasa Serikali inatoa tamko gani,kwa vyombo vingine vya habari kuiga mfano huu mzuri wakuhamasisha vijana kuelewa nini maana ya uzalendo naUtaifa wao?

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri unaombwa ujibu.Wakizeeka, vijana wengine wanakuja. (Kicheko)

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

38

19 JUNI, 2013

NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NAMICHEZO: Mheshimiwa Spika, kama tulivyosema katikamjadala wetu wakati tunawasilisha Bajeti hapa, tulisemakwamba jambo hili l imechukua muda mrefu. Lakinitumefanya jit ihada, mpaka sasa tayari suala hil ilimeshajadiliwa katika Kikao cha Makatibu Wakuu nalimekwenda kwenye Baraza la Mawaziri.

Mheshimiwa Spika, muda wowote utakapokuwaumekamilika, sisi tutaleta Muswada huu hapa utungiwesheria, lakini pia nilishaahidi kwamba mimi mwenyewe nimdau katika suala hili la vijana toka lilipoanza.

Mheshimiwa Spika, la pil i, nakubaliana naMheshimiwa Mangungu, namna ambavyo vyombo vyahabari vinaendelea kuelimisha vijana na suala zima la Utaifa.Nataka kusema kwamba, katika Mkataba huu wa Afrika waVijana, unaeleza nchi wanachama wajibu wao kwa vijana,lakini na wajibu wa vijana kuhakikisha kwamba wanatii sheriana kulinda nchi yao na jamii kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, nakubaliana naye na navitakavyombo vya Habari vyote na kuwataka vijana kuonakwamba, wanadumisha amani na kuwa na maadili memana kujenga utaifa katika Taifa letu la Tanzania. (Makofi)

Na. 431

Wananchi Kuibiwa kwa Ujazo wa Lumbesa

MHE. MCHUNGAJI LUCKSON N. MWANJALE aliuliza:-

Wananchi wanapouza mazao yao kama vile mahindi,viazi na kadhalika hutakiwa kupima kwenye lumbesa ambaoni ujazo mara mbili zaidi ya ujazo wa kawaida.

Je, Serikali inatoa tamko gani juu ya wizi huounaofanywa na wafanyabiashara kwa wananchi?

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

39

19 JUNI, 2013

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Viwandana Biashara, napenda kujibu swali la Mheshimiwa MchungajiLuckson Ndaga Mwanjale kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kupitia Bunge lakoTukufu kusema kwamba, ni dhamira ya Serikali kuhakikishawafanyabiashara wanatumia vipimo vil ivyo halaliwanaponunua mazao kutoka kwa wakulima. Niseme hapana niwaeleze wafanyabiashara na wakulima wote kuwa,hakuna sheria inayosema kuwa wakulima wanapouza mazaoyao eti wanatakiwa kupima kwenye lumbesa. Huu niudanganyifu na kuwadhulumu wakulima.

Mheshimiwa Spika, nawaagiza wafanyabishara kotenchi, kuacha mara moja mtindo wa kuwalazimisha wakulimakutumia vipimo vya Lumbesa wanapouza mazao yao na vilevile wakulima wasishurutishwe kutumia lumbesa. Hatua kalizitachukuliwa dhidi ya wafanyabiashara wote watakaokiukaagizo hili.

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Vipimo Na. 20 ya mwaka1984 ikisomwa pamoja na Tangazo la Serikali na 16 la tarehe8 Februari, 2008 inaeleza bayana matumizi ya mizani sahihikatika kufanya biashara, vipimo vya Lumbesa ni vipimo batilina haviruhusiwi kisheria kutumika katika kufanya biashara.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imefanyamarekebisho ya Sheria Mama (The Weight and Measures Act,1984) na kuwa (Legal and Metrology Act) kwa lengo lakuongeza usimamizi, udhibiti na adhabu kali dhidi yawafanyabiashara watakaokiuka sheria hii. Mapendekezo yamabadiliko ya Sheria hii yamepelekwa katika Baraza laMawaziri kwa kuridhia na baadaye kuletwa mbele ya Bungelako Tukufu.

MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE: MheshimiwaSpika, nashukuru kwa majibu ya Serikali. Kwa kuwa suala hilila lumbesa, limejitokeza hapa katika Bunge lako Tukufu zaidi

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

40

19 JUNI, 2013

ya mara tatu na majibu karibu ni yale yale. Sasa sijajua nazoezi la kudhibiti lumbesa bado haliendelei limekwama,nauliza je, Serikali ina mkakati gani mpya kabisa, ambao kwakweli utafanya zoezi liweze kufanikiwa?

Mheshimiwa Spika, maagizo hayo wamepewawafanyabishara, lakini kwa nini Wakuu wa Mikoa na Wakuuwa Wilaya wasipewe maagizo haya ili waweze kusimamiazoezi hili?

SPIKA: Nami naunga mkono suala hilo, ninalo tatizokubwa kabisa la lumbesa kwangu. Mheshimiwa Naibu Waziri,tunaomba majibu ya kuridhisha. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:Mheshimiwa Spika, suala la lumbesa lina wabia wengi,kusema kweli linapaswa likomeshwe kabisa ili suala hiilidhibitiwe mikoa yote nchini na liishe kabisa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la kwanza, lakwamba mkakati gani ambao Serikali inafanya ili kukomeshakabisa lumbesa, labda niseme kwamba, sasa hivi kulikuwana tatizo la sheria iliyokuwepo, ilikuwa inatoa adhabu ndogosana. Kama mnavyofahamu ilikuwa inatoza Sh. 10,000/= kwamfanyabiashara yeyote ambaye alikuwa anakiuka sheria hii.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hili limekuwa ni tatizona limetunyima meno sisi watu wa Serikali hasa Wizara katikakutoa adhabu kati. Kwa hiyo, mfanyabiashara akitozwa Sh.10,000/= alikuwa anaona ni kitu kidogo, hivyo aliendeleakuvunja sheria hii.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kutokana na tatizo hili,ndiyo maana nikasema kwamba, Serikali inabuni auimeanzisha sheria hii mpya ambayo itatoa adhabu kali sanakwa wafanyabiashara ambao watakuwa wanakiuka sheriahii.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, mapendekezoambayo tumeyapeleka kwenye Baraza la Mawaziri ni

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

41

19 JUNI, 2013

kwamba, kosa la kwanza liwe na adhabu kali, kiasi cha shilingimilioni 100 au miaka mitatu jela au vyote kwa pamoja. Kamautaendelea kufanya kosa, kosa la pili, litakuwa na adhabukali vile vile ya shilingi milioni 200 pamoja na miaka saba (7)au vyote kwa pamoja. Hiyo nafikiri itasaidia sana katikakukomesha suala hili la lumbesa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, la kusemakwamba tushirikishe viongozi wengine wa Mkoa na hataWilaya. Kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi yakwamba, Sheria hii mpya tayari imeshajaribu kuwaunganishaWakuu wote wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya ikiwa ni pamojana Viongozi wengine wa Halmashauri zote, ikiwemoManispaa na Majiji, Viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongojji iliwaweze kushirikishwa katika suala hili.

Mheshimiwa Spika, katika sheria hii mpya kutakuwepona vituo vya mauzo ya mazao yaani Trading and ServicesCentre vitakavyotumika kwa ajili ya kuwawezesha wakulimawote kupeleka mazao yao katika eneo moja, ambapo zoezila ukaguzi na uhakiki wa vipimo kwa mujibu wa Sherialitafanyika. (Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tumetumia mudamwingi sana ambao siyo wa maswali.

Napenda kusema kwamba, tunaye ProfesaNderakindo Perpetua Kessy ambaye ni Mbunge wa Bungewa Afrika ya Mashariki kwa upande wa Tanzania, yuko hapakututembelea, karibu sana. Nadhani tutapata muda wakuongea naye. (Makofi)

Halafu nina shughuli za kazi. Makamu Mwenyekitiwa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge,Mheshimiwa Captain Mstaafu John Chiligati, anaombaniwatangazie Wajumbe wa Kamati hiyo kwamba, leo saa7.00 mchana kutakuwa na kikao cha Kamati katika UkumbiNa. 219. Hivyo basi, Wajumbe wa Kamati ya Maadili wawetayari kuhudhuria.

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

42

19 JUNI, 2013

MBUNGE FULANI: Mwongozo.

SPIKA: Mwongozo hauna tatizo utauliza badaye.

HOJA ZA SERIKALI

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2012/2013 Pamojana Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka 2013/2014na Makadirio y Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2013/2014

(Majadiliano yanaendelea)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge wafuatao ndiyowataanza kuchangia hii hoja. Mheshimiwa Engineer HamadYusuf Masauni, Mheshimiwa Jenista J. Mhagama,Mheshimiwa Susan Kiwanga, hayupo; Mheshimiwa SylvesterMabumba, Mheshimiwa Beatrice M. Shellukindo, MheshimiwaKhatib Said Haji. Sasa namwita Mheshimiwa Engineer HamadMasauni.

MHE. ENG. HAMAD YUSSUF MASAUNI: MheshimiwaSpika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuwa mtu wa kwanzakuchangia leo.

Mheshimiwa Spika, katika bajeti yetu ya Serikali yamwaka huu, mimi binafsi sina pingamizi na vipaumbele hasakwa kuwa suala la umeme ni moja katika vipaumbele.

Mheshimiwa Spika, kitendo cha kuongeza bajetikwenye sekta ya umeme kutoka shilingi bilioni elfu moja mianne na kitu kutoka shilingi mia saba na themanini na kitu hiyomwaka jana ni jambo ambalo linapaswa kupongezwa.Tukiamini kwamba sekta ya umeme ni muhimu na athari zakesote tunazijua, leo hii kutokuwepo kwa mgawo wa umemekumesaidia sana kuweza kupunguza inflation ambayo ilikuwainawaathiri sana wananchi wa kawaida katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, lakini pia katika eneo la umemevijijini, nipongeze jitihada za kuongeza bajeti katika eneo hilo

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

43

19 JUNI, 2013

na sasa hivi tumefikia 21% ya wananchi ambao wanapataumeme Tanzania kutoka 10% kwa takribani si zaidi ya miaka10 toka kuanzishwa kwa Mfuko huu wa REA. Kwa hiyo, nijambo jema sana kuongeza fedha hizo.

Mheshimiwa Spika, lakini tatizo langu kubwa lipokatika masuala mawili makubwa yaani utekelezaji na udhibiti.Inasikitisha sana na inauma sana kwamba sisi Wabunge waZanzibar kila siku tukichangia humu katika bajeti maneno nihayo hayo, kulalamika, kero na mambo ambayo hayaishi.

Mheshimiwa Spika, inatupa mashaka sana hasakuhusiana na watendaji wa Wizara hii ya Fedha, leo hii Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar imepitisha bajeti yale ikitegemeakama ulivyo utaratibu wa GBS ama mgao wa fedha zawafadhili kwa 4.5% kama il ivyopangwa. Lakini hivitunavyozungumza matatizo haya ya kila kukicha mpakaJanuari mwaka 2013 GBS iliyolipwa ni shilingi milioni 20 pekeyake.

Mheshimiwa Spika, si hivyo tu, lakini katika eneolinguine, payee ambayo miaka iliyopita tumekuwa tukiipigiakelele hapa Bungeni, tumekuwa tukizungumza na tukiahidiwakwamba hili jambo litapatiwa ufumbuzi, lakini mpakatunavyozungumza payee ya kuanzia mwezi Februari, Machina Aprili bado haijalipwa na wala haina dalili ya kulipwa.Mheshimiwa Waziri ni lazima atueleze ni kwa nini hii haijalipwa,lakini siyo kutueleza tu bali tunataka payee ya miezi mitatuilipwe na matatizo haya yasijitokeze tena.

Mheshimiwa Spika, leo hii tunawapa watu midomotu, watu ambao hawaitakii mema nchi hii, watu ambaohawautakii mema mustakabali wa Muungano wetu kupatavisababu vya kuweza kuathiri Muungano wetu kwa mamboambayo yapo ndani ya uwezo wetu na mambo ambayohayaonekani ni kwa nini yanafanyika hapa.

Mheshimiwa Spika, kama sheria ipo na utaratibuunaeleweka ni kwa nini sasa watendaji hawa wanakuwa nakiburi kiasi hicho? Itoshe kwamba, fedha hizi zilipwe lakini na

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

44

19 JUNI, 2013

watendaji hawa wachukuliwe hatua ili liwe fundisho kwawengine ambao wanachangia katika kuzoroteshamustakabali wa Muungano wetu.

Mheshimiwa Spika, lakini jambo lingine ambalonataka nizungumze katika eneo hili hili la utekelezaji wa bajetina eneo hili hili ambalo Zanzibar imekuwa ni muathirikamkubwa. Katika utekelezaji wa bajeti hii, ni lazima Serikali iwena mipango ambayo inatekelezeka na niipongeze Serikalikwa kufanya hivyo, lakini kama hatujasimamia nahatujawajibika, matatizo haya hayatakwisha.

Mheshimiwa Spika, lakini katika eneo la pil ilililozungumzwa ni eneo la udhibiti, Tanzania ama nchi yetuinapoteza fedha nyingi sana katika bandari, nipongeze juhudiambazo zimechukuliwa mpaka sasa hivi na Serikali kufanyaudhibiti wa baadhi ya maeneo.

Mheshimiwa Spika, lakini hiyo haitoshi, taarifa ambayoimetolewa na Tanzania Economic Update inaoneshakwamba nchi yetu kupitia bandari moja tu ya Dar es Salaampeke yake inapoteza dola za Kimarekani bilioni 1.8 kwamwaka, ambayo hiyo ni sawa na 7% ya pato la Taifa. Lakinipia inapoteza kodi kupitia TPA kwa wastani unaokadiriwadola za Kimarekani milioni 157, ukiachilia mbali athari ambazozinatokea kwa nchi jirani ambazo zinatumia bandari hiikusafirisha mizigo yake.

Mheshimiwa Spika, hali hii haivumiliki hata kidogo.Haiwezekani leo Serikali inapanga bajeti ya kuwakamuawananchi kulipa kodi, lakini wakati huo huo kuna maeneoambayo yanavujisha kodi na yanaendelea kuachiwa.Niseme kwamba kuna jitihada zinahitajika kuongezwa katikakuhakikisha kwamba udhibiti wa mapato ya nchi hii katikamaeneo mbalimbali unaimarishwa. Eneo moja ambalolinasikitisha na linahitaji kuangaliwa zaidi na zaidi ni kuongezajitihada ni eneo la bandari.

Mheshimiwa Spika, leo hii utafiti unaonesha kwamba,inachukua takribani siku kumi kwa meli kupanga foleni kutua

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

45

19 JUNI, 2013

mzigo wake bandarini, lakini siku kumi nyingine kwa ajili yakuupakua mzigo ule mpaka uweze kusafirishwa wakatiInternational Standards inahitaji mizigo hii iwe inatolewa kwamuda wa siku mbili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kana kwamba hiyo haitoshi,nchi yetu ipo katika ushindani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,leo hii wenzetu wa Kenya, bandari yao ya Mombasa ambaowameanzisha mfumo mpya ambao unaitwa National SingWindow ambao utasaidia kuimarisha na ku- improveefficiency katika bandari yao, lakini wao inachukua nusu sikutu kwa meli kufikia bandarini na takribani siku tatu mpakanne pekee.

Mheshimiwa Spika, sasa tukiangalia tofauti hii nikubwa mno. Kwa hiyo, nahisi kwamba, suluhisho la matatizoya ufanisi katika eneo hili la usafirishaji halipo katika uwezo,tuna bandari za kutosha kabisa, leo hii uamuzi wa kujengabandari Bagamoyo sioni kama una haraka hivyo. Tatizolililopo ni ufanisi duni uliopo katika bandari zetu, tuna bandariya Zanzibar, Mtwara, Tanga na kadhalika, hizi zingewezakabisa kuimarishwa na kuwa na uwezo wa kuhimili ufanisikatika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, lakini suala lingine ni suala larushwa iliyokithiri katika mifumo ya kodi ya nchi yetu na hasakatika hili eneo la bandari. Inakisiwa kwamba takribani dolala Kimarekani 13,000 hutumika kwa ajili ya rushwa tu. Sasaniseme kwamba, kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba,Wabunge wengi wamechangia wamelizungumzia kwa hisiakali sana hili.

Mheshimiwa Spika, wapo wengine ambao walikuwakila siku wanazungumzia kwamba suala la rushwa limekuwani wimbo wa Taifa, kila siku tumekuwa tukizungumza tu lakinihatua madhubuti bado hazijachukuliwa. Kuna haja ya Serikalikuhakikisha kwamba fedha hizi ambazo zimetengwazinatumika katika kuhakikisha kwamba ufanisi unapatikanakwa maana ya kuimarisha miundombinu na teknolojia katikabandari, lakini kuhakikisha kwamba suala la rushwa

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

46

19 JUNI, 2013

linafanyiwa kazi ipasavyo na hatua kali zinachukuliwa kwawale wote ambao wataonekana kwamba wanapokea amakutoa rushwa.

Mheshimiwa Spika, ni imani yangu kwamba, maeneohayo yakiangaliwa kwa undani zaidi na kupewa msukumowa kipekee, basi nchi yetu itaweza kuhakikisha kwambainaimarisha ufanisi na hatimaye kodi inaweza kukusanywana kutumika inavyotakiwa.

Mheshimiwa Spika, niseme kwamba, j it ihadazilizotumika za kuongeza kodi katika baadhi ya maeneombalimbali ni jitihada ambazo zinatia moyo ingawa maeneoyamekuwa hayo hayo kila siku. Kwa hiyo, kuna haja ya Serikalikuwa wabunifu zaidi katika kuona kwamba inaongeza kodi.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, eneo moja la kodikatika maeneo ya mazao, hili kwa kweli si jambo la busarasana, kwa sababu unapoongeza kodi katika maeneo yamazao, maana yake unapeleka mzigo ule kwa wananchiwa kawaida ambao hatma yake inachangia katikakuongeza ugumu wa maisha, lakini pia kuongeza mfumukowa bei katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niseme kwamba kwaujumla bajeti yetu hii haijakaa vizuri...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wamzungumzaji)

MHE. ENG. HAMAD YUSSUF MASAUNI: MheshimiwaSpika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hiyo. (Makofi)

SPIKA: Ahsante, nashukuru, Mheshimiwa JenistaMhagama atafuatiwa na Mheshimiwa Rajab MbaroukMohammed. Kama hayupo atatengewa baadaye.

MHE. JENISTA J. MHAGAMA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana. Kwanza kabisa naomba nichukue nafasi

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

47

19 JUNI, 2013

hii nikipongeze sana Chama cha Mapinduzi kwa ushindimkubwa ambao umepatikana katika chaguzi ndogo za Kataambazo zimefanyika muda si mrefu uliopita. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hiyo ni dalili kwamba, badoWatanzania wana imani na Chama cha Mapinduzi na wanaimani na Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Naombanichukue nafasi hii kuwapongeza wale wote walioamuakuchagua Madiwani wa Chama cha Mapinduzi kwa sababuwamechagua chaguo la maendeleo. Nawapongeza sana!(Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, naomba nikupongeze sanawewe mwenyewe, kwa mara ya kwanza Bunge letulimeweka historia. Limeweka historia ya kuunda mfumo mpyawa bajeti ambao ni mfumo wa mashauriano kati ya Bungeambao ni wawakilishi wa wananchi na Serikali ambayo niwasimamizi wa shughuli za maendeleo na hatimaye leotunaona kwamba mfumo huu mpya umeweza kutufikishamahali pazuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni ushahidi wa kutosha kwaWatanzania na wale wote waliokuwa wanabeza kwamba,Bunge hili halipo makini, lakini naomba niseme kwa mara yakwanza tumewathibitishia kwamba, tupo makini,tumejipanga sawasawa kwa maslahi ya Watanzania zaidina hii imejidhihirisha kwa kwa kazi tulizozifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bajeti imetufanyia kazinzuri sana kwa kushirikiana na Serikali na tumeona hapa,naomba niwaambie Watanzania, wakati tunaendelea nabajeti, tuligundua mambo mengi ya kimsingi ambayoWatanzania kupitia Serikali yao ya Chama cha Mapinduziwalitakiwa wayapate.

Mheshimiwa Spika, tuliomba fedha ziongezwekwenye bajeti ya Maji zimeongezwa, tuliomba fedhaziongezwe kwenye Mifugo zimeongezwa, tuliomba fedhaziongezwe kwenye bajeti ya Kilimo ili wananchi wawezekupata pembejeo na ruzuku zimeongezwa, tuliomba fedha

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

48

19 JUNI, 2013

ziongezwe kwa ajili ya maendeleo ya akinamama katika nchiya Tanzania zimeongezwa, tuliomba fedha ziongezwe kwaajili ya Vijana imeongezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia tuliomba fedha ziongezwekwa ajili ya Miundombinu ya mawasiliano zimeongezwa,tuliomba fedha ziongezwe kwa ajili ya madawa kwawananchi wa Tanzania zimeongezwa, tumeomba fedha kwaajili ya umeme vijijini vikiwemo vijiji vyangu vya Jimbo laPeramiho fedha zimeongezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa haya ni machache, yapomambo mengi, wananchi wa Jimbo la Peramiho nisubirini,baada ya Bunge hili nitakuja kuwaeleza moja baada yalinguine, nini mmepata katika bajeti hii shirikishi ya Serikali.Serikali ya Chama cha Mapinduzi iendelee kudumu naiendelee kuwa sikivu kama hivyo nilivyosema na kuwa kwakufanya hivyo, mnaokoa maisha ya Watanzania wengi nakuwaletea maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nijikite sasa pia katika maeneokadha wa kadha katika bajeti hii. Eneo la kwanza, kipindihiki ambacho kwa sababu bado tunaendelea na mashaurina Serikali kuhusiana na haya ambayo Serikali imetuletea naKamati ya Bajeti inayoongozwa na Mtemi Chengeimetuletea, naomba nirudie kusema, Mheshimiwa Chengeatakapokaa na Serikali kodi hii iliyoongezwa kwenye mafutana hasa petrol na diesel ikaondolewe na kama siyokuondolewa yote ikapunguzwe kwa kiasi kikubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapozungumzia suala lamfumuko wa bei, base ya mfumuko wa bei ni mafuta. Leotunategemea mafuta kama ni chanzo cha kila kitu, mitamboyote ya kuzalishia mazao, mitambo yote ya viwandani,usafirishaji na usafiri vyote vinategemea mafuta. Kwakuongeza tozo hiyo, tutakwenda kuwatesa sana wananchiwa Tanzania na hasa wale ambao wako vijijini. Nashauri sanakatika eneo hilo kwa kweli kuna umuhimu wa kwendakuangalia upya.

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

49

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, sambamba na ile kodiiliyoongezwa kwenye ngano, hiyo nayo tukaitazame. Hofuyangu akinamama wengi na hasa wafanyabiasharawadogo wadogo wanategemea biashara hizi za bidhaazinazotokana na unga wa ngano. Akinamama lishe na Mamantilie wengi sana mpaka vijijini wanategemea unga wangano, ndiyo kitega uchumi chao kikubwa. Nadhani tunaumuhimu wa kuangalia pia eneo hilo kwa kiasi cha kutosha.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono kufuta kodikwenye huduma ya Bajaji itasaidia, lakini nafikiri kunaumuhimu wa kutazama, tunapofuta hiki tunafanya kitu ganikingine ili kuweza kuongeza mapato katika kodi zetu?Tulishaunda Tume ambayo ilifanya uchunguzi wa kiasi chakutosha kupitia Bunge lako kuangalia vyanzo vingine.

Mheshimiwa Spika, niungane mkono na Wabungewaliosema, hivi kweli Serikali mmeshachukua karibu yalemawazo yote ya vyanzo vyote vya mapato ambavyovinaweza kuongeza angalau kufidia huko tunakoshaurituondoe kuwakandamiza Watanzania kwenye kulipa kodi?

Mheshimiwa Spika, Wabunge wenzanguwamezungumza kuhusu suala la uvuvi katika maji marefu. Hivitunapata kigugumizi gani kusimamia mapato yanayotokanana uvuvi ndani ya bahari? Naomba tuone namna ganitunaweza kufanya, bahari kuu uvuvi haramu unaendelea,nchi nyingine zinajitajirisha kwa kiasi kikubwa, tungewezakupata mapato ya kutosha na hizi kodi mbili au tatu ambazotumeziongeza, tunafikiri zitawaumiza wananchi, tungewezakuachana nazo tukategemea uvuvi kutoka bahari kuu.

Mheshimiwa Spika, naomba sana kipindi hiki chamashauriano kwa sababu haijajitokeza kwenye Serikali. Hebutuone tunawakamataje wale wavuvi kwenye bahari kuuwaongeze mapato kwenye Serikali yetu ili tuweze kuendeleambele.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie pia kwa ujumla wakesuala moja ambalo ni la msingi sana sijui tunalitazama namna

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

50

19 JUNI, 2013

gani. Ongezeko la idadi ya Watanzania kwa mtazamo wanguhaliendani sambamba na ongezeko la uchumi katika nchiyetu. Idadi ya Watanzania inaongezeka kwa kasi kubwa,lakini ongezeko la uchumi wa nchi yetu haviendi sambamba.

Mheshimiwa Spika, sasa tukifanya hivyo nafikiri lipotatizo mahali fulani kwenye mipango yetu. Narudia kusemakwamba, tunapokuja kwenye mipango, ina maana kwenyeutaratibu wetu wa kuangalia vipaumbele, nadhani kunamahali tuna matatizo, kuna mahali hatujakaa salama, ikohaja kabisa ya Tume ya Mipango kuona nini kifanyike.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini ipo sekta ambayotumeisahau sana na tunaidharau ambayo ingewezakuchangia sana kukua kwa uchumi kwa kiasi kikubwa sana.Sekta hii siyo nyingine zaidi ya sekta isiyo rasmi ambayoinaweza kuunganisha wafanyabiashara wadogo wadogokwa kiasi kikubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la uchumi na maendeleoya uchumi, haliwezi kuacha kuendana sambamba na sualala ajira katika nchi yoyote. Utengenezaji wa ajira utakwendasambamba na ongezeko la uchumi. Ukiangalia kwenye bajetiyetu mwaka huu fedha nyingi inakwenda kulipia mishahara,lakini mishahara hiyo ina tija kiasi gani katika kuletamaendeleo ya nchi yetu ya Tanzania? Wapo watuwanalipwa mishahara hawana kazi wanazozifanya zenye tijakuleta maendeleo kwenye nchi yetu. Sasa nadhani tuitumiesekta hii isiyo rasmi katika kukuza uchumi.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa nasoma nikagunduakwamba, kwa mfano wenzetu wa Zimbabwe mwaka 1997kupitia hii sekta isiyo rasmi, uchumi wa nchi yao ulichangiwana sekta hiyo kwa 40% mpaka 45%, walifanya nini? Kwasababu unapochukua sekta isiyo rasmi, ina maana kwanza,unakwenda kufanya kazi ya kuhamasisha uchumi mdogomdogo vijijini. Pili, unakwenda kukuza teknolojia vijijini.

Mheshimiwa Spika, tatu unakwenda kutengeneza

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

51

19 JUNI, 2013

masoko na nne unakwenda kutengeneza mzunguko wafedha wa kutosha katika maeneo ya vijijini ambapo asilimiakubwa ya Watanzania wako huko na tunajua maendeleoya nchi za Ulaya yalitokana na viwanda vidogo vidogo nateknolojia.

Mheshimiwa Spika, sasa kama tutaweza kuwekakipaumbele kwa sekta hii isiyokuwa rasmi ikawakuta vijanahuko, kwanza, tutawafanya wasihame kwenda mijini lakinimbili tutawatengenezea viwanda vidogo vidogo kule vijijini.Tukiweka pesa ya kutosha huko tutatengeneza masoko yakudumu ya biashara zao.

Mheshimiwa Spika, tatu tutatengeneza mzungukomzuri wa fedha kule vijijini na hivyo ukuaji wa uchumiutaendana na ukuaji wa idadi ya Watanzania, lakiniutakwenda kutatua tatizo la umaskini unaowagusaWatanzania moja kwa moja kule Vijijini. Tunalalamika hapauchumi unakua, lakini umaskini haufanyi haupungui walahauondoki! Haya ndiyo matatizo ambayo nafikiri tunatakiwakuyatazama.

Mheshimiwa Spika, tumetenga fedha kwenye Mfukowa Vijana, sasa Mfuko huu tuwaombe wenzetu wa Serikaliwanapoongeza hiyo fedha, tutazame namna ya kukuzateknolojia na ajira vijijini kwa vijana.

Mheshimiwa Spika, tumetenga fedha za akinamama,nashauri tuzipeleke vijijini tukatatue hilo tatizo la ajira, lakinipia tukatengeneze teknolojia za kukuza uchumi kule ambazozitasaidia kuondoa umaskini wa Watanzania kule vijijini. Hivyoukuaji wetu wa uchumi utakwenda sambamba kwa maanaya kipato kuongezeka na hali za Watanzania, umaskiniunaondoka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nafikiri bado tuna kaziya kutosha ya kujitathmini upya kuangalia mfumo wavipaumbele vyetu...

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

52

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja nanawatakia heri Serikali katika kutimiza majukumu hayo.(Makofi)

SPIKA: Ahsante. Namwita Mheshimiwa Rajab MbaroukMohammed, atafuatiwa na Mheshimiwa Sylvester MaselleMabumba na Mheshimiwa Beatrice Shellukindo ajiandae.

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED: MheshimiwaSpika, nakushukuru kwa kunipa muda huu wa dakika 10 ili namimi niweze kutoa mawazo yangu katika bajeti hii kuu yaSerikali.

Mheshimiwa Spika, nataka nianze na ukurasa wa 64wa hotuba ya Waziri kuhusiana na suala zima la ukusanyajiwa kodi. Tunalalamika kuhusiana na suala zima la misamahaya kodi. Katika ukurasa huu Waziri anaelezea kwamba,msamaha wa ushuru wa forodha utaendelea kutolewakwenye vifaa mbalimbali vilivyotumika katika kutoa hudumaya utalii. Moja katika maeneo ambayo hatufanyi vizuri katikanchi yetu katika kukusanya kodi ni sehemu ya utalii.

Mheshimiwa Spika, ni dhambi kubwa kusamehe ainayoyote ya kodi ama ya VAT, ushuru au tozo la aina yoyotekatika sekta ya utalii. Hivi sasa katika nchi yetu watalii wengiwanaokuja hapa wanakuwa wameshalipa kila kitu huko njehata vitanda. Kwa kweli ni lazima Serikali ikae makini naiandae mpango mkakati mpya mwingine wa kuhakikishawanadhibiti mapato au tozo hizi kutoka katika vyanzo hivivya utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 71 MheshimiwaWaziri anazungumzia suala la kuongeza ushuru wa bidhaawa asilimia 14.5 kwenye huduma zote za simu. Fedha hizianasema asilimia 2.5 zitatumika kugharamia elimu hapanchini. Nakubaliana naye na nampongeza, ila nataka nitoetahadhari na hasa kutokana na uzoefu ambao tumeupatahuko nyuma, uzoefu wa fedha za rada.

Mheshimiwa Spika, fedha za rada zilikuwa ni za

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

53

19 JUNI, 2013

Muungano, lakini matokeo yake fedha zile zikabadilishwanadharia na kupelekwa kuhudumia shule za msingi. Kituambacho kilijulikana dhahiri kwamba, unapopeleka katikashule za msingi Zanzibar haiwezi kupata pato lake pale kwasababu elimu ile ya msingi si ya Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa tunataka Waziri alifafanue hilina aliweke vizuri, simu tunatumia Watanzania sote, hizi asilimia2.5 Wazanzibari wao watapata nini? Tunaomba hili liwekwekatika hali nzuri ili ieleweke mgawanyo wake utakuwaje.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala la vipaumbele.Tumeona vipaumbele vyetu hasa suala la miundombinu,nakubaliana nacho lakini uwanja wa miundombinu nimpana. Nataka nichukue mfano mmoja wa kule Kigomakatika eneo la Katosho. Katika mpango, Serikali imesemakwamba pale imekusudia kuweka bandari kavu.

Mheshimiwa Spika, tatizo linalokuja pale ni kwamba,sasa hivi Halmashauri ya Kigoma inawanyanyasa nakuwasumbua wananchi wale wa Katosho. Lile eneo laKatosho kwa ajili ya bandari kavu lilipimwa tangu mwaka1964, lakini leo hii wamekwenda kuweka mipaka mipyaambayo wanaingia hata katika nyumba ambazo ziko palekwa muda mrefu. Hili linaleta usumbufu kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaiomba Serikali, palewanapozungumzia suala la vipaumbele hasa katika maeneokama haya ya wananchi, hebu wajaribu kuangalia aukuepuka kusababisha mkanganyiko na wananchi kwani hiiinaleta shida.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi wananchi wa Katoshohawazikani, Mheshimiwa Dkt Chizeba hili analifahamu,atusaidie tuondoe lile tatizo pale Katosho. Mipaka ilikuwepotangu mwaka 1964 na bado iko, lakini leo wamekwendakuweka mipaka mipya wanaingia mpaka kwenye maeneoya wananchi, hii hali ikoje?

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

54

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, bado kuna eneo kubwa ukitokapale ambalo ni pori tu liko wazi, kwa nini hawa wananchiwanyanyasike sasa hivi wakati ambapo hiyo reli yenyewebado Serikali haijawa nayo. Hiyo bandari yenyewe ndiyohivyo hivyo meli hakuna, leo mnaanza kusumbua wananchiwa Katosho bure! Serikali ione huruma katika hili ili walewananchi kwa kweli wasisumbuke. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Fedha iliyofanyiwamarekebisho mwaka 2008 ambayo inampa madaraka Waziriwa Fedha kukopa pamoja na ile Sheria ya PPP ya mwaka2012 zinakinzana. Mkinzano huu wa sheria hizi unasababishasasa baadhi ya Halmashauri zetu kupata matatizo na sasahivi umesababisha urasimu kiasi kwamba, ule mtindo wamwanzo wa Halmashauri zinapotaka kukopa inabidi sasazirudi tena kwa Waziri wa Fedha. Kwa kweli hapa kunakuwana urasimu.

Mheshimiwa Spika, mfano mzuri ni Halmashauri yaMpanda wameleta maombi yao muda mrefu tu ya kutakakukopeshwa fedha kwa ajili ya mipango yao ya maendeleo.Halmashauri ya Kilwa walitaka kujenga stendi paleNangurukuru, mpaka leo hawajapewa majibu.

Mheshimiwa Spika, hebu Mheshimiwa Waziri azioneehuruma hizi Halmashauri zetu, wana mipango mizuri,wameibua mambo yao, wanahitaji kukopa fedha, waowenyewe wanajua namna gani ya kuzilipa. Hebu wasaidieni,hii hali ya kuwazungusha sana inakuwa siyo vizuri. Tumekubalihapa mfumo wa D by D tuwaachie waweze kufanya kazi,wanapokuja na matatizo yao wasaidieni kwa haraka.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala la matumizimakubwa ya Serikali na hapa nataka nizungumzie suala laTANESCO. Sasa hivi TANESCO haiwezi kuwekeza, hili ni sualaambalo liko wazi kwamba sababu kubwa ya TANESCOkushindwa kuwekeza ni mzigo mkubwa wa madeni ilionaoambapo sasa hivi inadaiwa takribani shilingi bilioni mia nnena kitu.

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

55

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, kwa kweli si rahisi kwa TANESCOkuweza kujiendesha au kuwekeza. Tunaiomba Serikali kamaambavyo imefanya kwa STAMICO na ATCL kwa kuyachukuamadeni yao, hebu ichukue madeni ya TANESCO ili Shirika hililiweze kujiendesha au kuwekeza.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi TANESCO wanapewatakribani shilingi bilioni tano kwa siku kwa ajili ya kununuamafuta mazito ya kuendeshea mitambo. Mnawapa fivebillion kwa siku ambapo kwa mwaka ni takribani 1.9 trilioni.Hizi fedha kwanza tunauliza zinatoka wapi? Ni fungu ganiambalo liliidhinishwa mkaweza kutoa fedha hizi everydaykupeleka five billion TANESCO? Tunaomba majibu ya Waziriwakati wa kuhitimisha.

Mheshimiwa Spika, mbali na hivyo ni kwamba, fedhahizi vile vile ni mbali ya zile shilingi billion 27 ambazo mnazitoakwa ajili ya capacity charges na energy charges. Jananilimsikiliza Mheshimiwa Waziri wa Fedha anasema kwamba,sasa hivi tunaingia katika mikopo na mkopo alioupata janawa kujenga flyovers anasema ni mkopo poa.

Mheshimiwa Spika, hili neno poa liliwahi kuzungumzwahumu ndani ya Bunge na Mheshimiwa Naibu Waziri mmoja,wakati huo alikuwa back bencher na tafsiri yake akaita niparalysis of analysis. Sasa hebu iangalieni TANESCO kwaupana wake, ili hii poa mnayoizunguza isiwe ni paralysis ofanalysis. Tunaliomba sana hilo kwenu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie thamani ya shilingi.Thamani ya shilingi yetu bado inaendelea kuporomoka sikuhadi siku na hii ni kwamba wataalam wa Wizara ya Fedhapamoja na Waziri mwenyewe ama Naibu Mawaziri wenyewe,bado hawajajikita na kuwa makini katika suala zima lakudhibiti mzunguko wa fedha nchini. Nina shaka kwambahivi sasa nikimuuliza Mheshimiwa Waziri ni fedha ngapi zikokatika mitandao ya simu au mikononi, sidhani kama atakuwaanaweza kupata jibu la haraka. Kwa hiyo, hii tunayoita moneycirculation inaonekana bado udhibiti wake ni mbovu.

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

56

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, ni vizuri sasa Wizara ije na mpangona mkakati maalum unaoonesha ni namna gani sasa hivitunadhibiti fedha zetu ili shilingi yetu isiendelee kuporomoka.

Mheshimiwa Spika, tatizo lingine kubwa ni suala zimala commodity exchange. Mfumo wa commodity exchangeuna matatizo, uangalieni upya. Hii inasababishwa na sualazima la kuuza bidhaa zetu nje ya nchi. Wanunuzi wakubwawa bidhaa zetu nje ya nchi ni matajiri wa humu humu ndani,wananunua kwa fedha zetu za ndani wanakwenda kuuzanje wao kwa fedha za kigeni. Matokeo yao hawa matajiriwanachokileta hapa ni baiskeli, sijui vyandarua, mambomadogo madogo ambayo kwa kweli yanapoingia hapanchini hayalipishwi ushuru. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hili suala hebu liangalienivizuri, tutakapoweza kutoa bidhaa zetu nyingi kuuzawenyewe nje, tutaingiza fedha za kigeni na hapa thamaniya shilingi yetu itaweza kuwa stable. Sasa hivi thamani yashilingi yetu haiko stable. Tunaomba hilo Mheshimiwa Waziriwa Fedha alizingatie. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala la deni la Taifa.Ukuaji wa deni la Taifa kwa kweli ni wa kasi mno kiasi kwambasasa hivi unahatarisha hata usalama wetu. Ikiwa leo hii mtotowangu wa mwisho Manahali mwenye mwaka mmojaanadaiwa shilingi laki tano na ushee kutokana na deni hili latrilioni 23.7…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Mheshimiwa hiyo ni kengele ya pili. Naombanimwite Mheshimiwa Sylvester Mabumba, atafuatiwa naMheshimiwa Ester Bulaya na Mheshimiwa Khatibu Said Hajipia ajiandae.

MHE: SYLVESTER MASSELE MABUMBA: MheshimiwaSpika, awali ya yote nikushukuru kwa kunipa nafasi hii, lakini

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

57

19 JUNI, 2013

pia nikupongeze kwa ubunifu ambao umeuleta katika kujadilibajeti ukianzia na bajeti ndogo na sasa bajeti kuu ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, pia nikipongeze Chama chaMapinduzi kwa kuzoa viti vingi sana vya Udiwani. Huu niushindi wa kimbunga kwamba katika viti 22 tumepata viti 16.Pongezi kubwa kwa Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba sasa nijielekeze kwenyehotuba hii. Taifa letu linatekeleza Mpango wa MKUKUTA II wakuondoa umaskini Tanzania, lakini lengo la MKUKUTA nikuhakikisha Watanzania hawa wanaondokana na umaskiniifikapo mwaka wa 2025.

Mheshimiwa Spika, hofu yangu ni kwamba, benki hiziambazo zinakopesha wananchi hapa Tanzania badozinatoza riba kubwa sana ambazo haziwezi kutusaidiakuondokana na umaskini. Mkopaji anapaswa alipe riba yaasilimia 15 mpaka 18, lakini yeye akiwekeza fedha zakekwenye benki anapata faida ya asilimia nne au tano. Sasakwa namna hii benki zinawaibia Watanzania, zinafanyaujambazi mkubwa sana. Naiomba Wizara ya Fedha na Serikaliyetu izielekeze benki kushusha riba ili kweli kama tunatakatufikie malengo ya MKUKUTA tuweze kuona manufaa kwaWatanzania.

Mheshimiwa Spika, eneo la pili, nataka nizungumziepia hotuba ya Waziri anapoelezea nia ya kutoza kodi kwa ileSheria ya Fedha Na. 147. Hivi karibuni Waheshimiwa Wabungetulikuwa na semina hapa ya kampuni ya vinywaji, TanzaniaDistillers Company Limited.

Mheshimiwa Spika, wameeleza mbele yetu kwamba,wao wanalipa kodi Serikalini, ukiziangalia kodi za aina zotezinazofikia kwa mwezi shilingi bilioni 6.9 ambazo ni karibushilingi bilioni saba (7). Hata hivyo Serikali yetu haizilindikampuni hizi kwani zinapata changamoto sana. Kwa mfano,kampuni hizi zinapopeleka bidhaa zao nchi jirani ya Kenya,kule wanakumbana na vikwazo vya jinsi ya kupata soko.

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

58

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, sasa ningependa Serikali yetuilinde kampuni hizi kwani kama kampuni inalipa takribanishilingi bilioni saba (7) kwa mwezi, ni kwa nini Serikaliinashindwa kulinda kampuni kama hizi ili ziweze kuendeleakuchangia zaidi pengine ya shilingi bilioni saba (7)?

Mheshimiwa Spika, wanaeleza kwambawanapopeleka bidhaa kule Kenya, kule Serikali imewekautaratibu inawaambia sijui chupa za ujazo wa mililita 205hazitakiwi wakati Watanzania ndizo ambazowanatengeneza, lakini bidhaa za Kenya zina soko Tanzania.Sasa kwa nini bidhaa kama hizo kutoka nchi ya nje hapakwetu hazizuiliwi ili kulinda kampuni zetu ziweze kuendeleakulipa kodi nzuri?

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kwamba, uliundaTume ya kuishauri Serikali vyanzo vipya vya mapato, chaajabu ni kwamba kwenye pendekezo la Mheshimiwa Waziriamejikita kwenye maeneo yale yale, kuongeza ushurukwenye mafuta, vinywaji, sigara, ambavyo ni traditional.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa nini Mheshimiwa Wazirianataka kuumiza watu wetu? Unapoongeza kodi kwenyemafuta hata ile anayosema kwamba mfumuko wa beiutashuka, hauwezi kushuka kwa sababu kuna kitu kinaitwacost pool inflation ambayo inalazimishwa kutokana nagharama za usafiri. Unapandisha kodi ya dizeli, petrol halafuunasema unataka kuwa na inflation ya single digit ya asilimiasita (6%) unaipata wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nadhani Serikali ikae chiniishirikiane na Kamati yako, mapendekezo ambayoyaliangaliwa na Tume yako uliyoiunda, basi Serikali iyatumie.Haiwezekani kila siku kodi iongezwe kwenye mambo yale yaleya vinywaji na nini, Watanzania wakiokoka inakuwaje?Utapata kodi wapi? Siku zote tunaambiwa sigara zinamadhara katika afya zetu, je wakiacha kuvuta sigara Taifalitakwenda kweli? (Makofi)

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

59

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali sasa ikae na ofisiyako ya Bunge, iangalie na iweze kuangalia vyanzo vinginena siyo hivi vya kila siku ambavyo ni traditional.

Mheshimiwa Spika, vile vile kila anayesimama hapaanaisifu TRA, mimi nataka kutofautiana kidogo, TRAwanachezea akili zetu, tunasema wanakusanya mapatokupindukia, siyo kweli. Leo hii baadhi ya maafisa walio wengindiyo wanawasha hasira kwa Watanzania kuichukia CCM,baada ya mwaka mmoja au miwili unamkuta amelimbikizamali nyingi sana. Amepata wapi na ana mshahara upi?Naomba Tume iundwe kuwachunguza wote ambao wanamali nyingi watwambie wamezipataje? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna maafisa wengi sana wa TRAambao siyo waadilifu. Halafu sielewi, TRA toka ilipoundwa,watu wameanza kazi pale mpaka hii leo wanazeeka as ifhakuna sehemu nyingine ya kuwapeleka. Kwa nini Serikalihaiwahamishi hawa? Haiwezekani ikawa wewe kwa kuwandiyo umesomea mambo ya finance ukae pale TRA siku zote.Hapana! Naomba Serikali iliangalie hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hawa wanakiwashia chamachetu hasira dhidi ya wananchi kwa sababu wamejilimbikiziamali nyingi sana. Harufu ya umaskini hawaijui hawa.Mtanzania hata mkate wa shilingi 100 anashindwa kuununua,lakini unamkuta mtu anasema kwanza yeye hawezi kulamkate bila siagi, ni jeuri gani hiyo?

Mheshimiwa Spika, naomba pia nizungumzie kuhusudeni la Taifa. Kwanza niipongeze Serikali yetu kwa kujengaimani na matumaini makubwa kwa nchi wahisani namashirika yanayotusaidia. Ombi langu hapo ni kwamba,misaada hii tunayoipata basi itumike kutatua kero halisi zaWatanzania hasa katika sekta ya elimu, maji, miundombinuya reli, barabara na bandari.

Mheshimiwa Spika, kama tunapata misaada namikopo hii. Mikopo hii lazima itumike kwa tija, misaada hiilazima iwe na tija, Tanzania leo hii kusini mwa jangwa la

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

60

19 JUNI, 2013

Sahara ndiyo nchi inayopokea misaada mingi sanaukilinganisha na nchi majirani, lakini ndiyo iliyokuwa nyumakimaendeleo kwa nini?

Mheshimiwa Spika, madeni haya tunayoyapata yawena tija hata kama yatakuwa ni makubwa kiasi gani?Tunapowaonesha nini tumetumia misaada na mikopo hiyo,basi naamini wananchi hawatakuwa na maswali wala hofuna namna Serikali yetu inavyotenda. Lakini kama misaadana mikopo tunayoipata haina tija, huwezi kuona utekelezajiwake, basi nina hakika tutakuwa na kazi sana mwaka 2015.

Mheshimiwa Spika, nataka pia nizungumze kuhusumakusanyo ya mapato yasiyokuwa ya kodi, ukusanyaji wakehauridhishi. Ametwambia ali-target kukusanya bilioni 644.6,lakini mwisho mpaka alipotoa taarifa hii aliweza kukusanyabilioni 357 ambayo ni chini ya lengo lao. Sababu alizozielezahapa ni kwamba, uwezo wa mdogo wa kukusanya kodi, sijuivifaa duni, baadhi ya mashirika na wakala hawachangiisawasawa. Sasa analiambia Bunge ili limsaidie kufanya kazihizi?

Mheshimiwa Spika, nadhani yeye alikuwa anapaswakutuambia hapa kwamba, kwa sababu wamekusanyakidogo, Serikali imejipanga kufanya hivi, kuwashughulikiaipasavyo hawa ambao wamesababisha isifikie lengo lake.Kwa sababu sisi si kazi yetu hapa Wabunge kwenda kujengauwezo wa wataalam kukusanya mapato haya yasiyokuwaya kodi. Lakini pia si kazi ya Wabunge kutoa vifaa ili kujengamifumo imara, ni kazi ya Serikali. Atwambie amejipanga vipikufanya mambo hayo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini anapotwambiaamekusanya kidogo kwa sababu imekuwa hivi, mimi kidogo,mtani wangu namheshimu sana, basi wasaidizi wakewamsaidie. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda pia nizungumzie taarifaya Mheshimiwa Waziri kwamba, wanapandisha kodi ya

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

61

19 JUNI, 2013

magari yanayozidi miaka kumi na huku tunaamini kwambaTanzania ni nchi maskini na hili jambo halina ubishi.

Mheshimiwa Spika, ni Watanzania wangapiwataweza ku-afford magari mapya? Naomba Serikali ifikirieupya jambo hili jamani! Humu Wabunge tumepewa pesa,tulio wengi tulinunua magari used , hakuna Mbungealiyenunua gari ya kiwandani na gari leo hii siyo anasa.Naishauri Serikali yangu ifikirie sana uamuzi huu kwa sababuhatutaweza kumudu.

(Hapa Kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MHE: SYLVESTER MASSELE MABUMBA: MheshimiwaSpika, naunga mkono hoja ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa nimwite Mheshimiwa EsterBulaya, Mheshimiwa Khatib Said Haji, Mheshimiwa SalehAhmed Pamba na Mheshimiwa John Paul Lwanji ajiandae.

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi na pia kwa dhamira ya dhatikabisa nikupongeze kwa kuunda Kamati ya Bajeti kwasababu itachangia kuhakikisha Bunge linakuwa imara nakuisimamia Serikali ipasavyo.

Mheshimiwa Spika, lakini pia usipoweza kushukuru kwakidogo, hutoweza kushukuru hata ukipewa kikubwa. Mimikama Mbunge wa Vijana naishukuru Serikali kwa kutengabilioni tatu kuweka katika Mfuko wa Vijana. Wabunge vijanakilikuwa ni kilio chetu, huu mwaka wa tatu mfululizo kwasababu Mfuko wa Vijana ulikuwa haupewi fedha za kutosha.Kwa hiyo, naishukuru sana Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini niweke angalizo tu, kutengafedha ni jambo lingine na usimamizi wa fedha na kuhakikishazinawafikia walengwa ni jambo lingine. Sasa niiombe Serikaliyangu, isipokuwa makini, tutazijutia fedha hizi kupotea kama

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

62

19 JUNI, 2013

ambavyo zilipotea fedha za mabilioni ya JK kwa kutokwendakwa walengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa Mifuko hii ya Vijana tunajuakabisa itakwenda kusimamiwa kwenye level ya Halmashaurina kwenye Halmashauri kumekuwa na urasimu mkubwasana. Watu wengine wanawaweka huko watoto wawajomba zao na wa shangazi zao ambao hawana utaalamwowote na ambao hawana biashara zozote na kuwapa hizofedha na mwisho wa siku fedha hazirudi, hazizunguki na walahaziwasaidii vijana wengi. Kwa hiyo, ninachokiomba kuwena usimamizi wa kutosha katika fedha hizi.

Mheshimiwa Spika, lakini ningependa kuzungumziasuala nzima la ongezeko la tozo ya petrol. Nilichangiakwenye Wizara ya Uchukuzi, nikazungumzia ongezeko la naulina nikatetea sana kwamba nauli inapoongezekawanaoumia ni wananchi wa kawaida. Leo tunakwendakuongeza tozo ya petroli, Mheshimiwa Jenista Mhagamaamezungumzia pale. Watakaoendelea kuumia ni wananchihawa wa kawaida.

Mheshimiwa Spika, wamiliki wa vyombo vya usafiriwataongeza tena nauli. Kwa hiyo, hapa tunazalishaongezeko tena lingine la nauli na kuwaongezea mzigoWatanzania ambao wengi wao wanashindwa kumudu hatamilo mitatu kwa siku. Sasa naiomba Serikali iangalie vizuri sualahili.

Mheshimiwa Spika, hali ni ngumu ya maishatunazungumzia hapa sijui uchumi umepanda, tunazungumziaongezeko la uchumi, lakini tukiangalia asilia uchumi waMtanzania mmoja mmoja bado ni duni, bado Watanzaniani maskini na hasa wanaoishi vijijini. Leo hii tunakwendakuwaongezea mzigo kwa kupandisha tozo ya petrol, kwakweli hatuwatendei haki Watanzania.

Mheshimiwa Spika, lakini niipongeze Serikali kwakuondoa kodi ya bodaboda, lakini naomba waliangalie kwakina kwa sababu vijana wengi, vijana wenzangu hawamiliki

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

63

19 JUNI, 2013

hizi bodaboda wala hizi pikipiki. Mwisho wa sikuanayekwenda kufaidi ni mmiliki na wala siyo mwendeshaji.

Mheshimiwa Spika, sasa ningependa kuishauri Serikaliiangalie kwa kina, kuboresha suala hili ili wale vijana wenyewewaweze kunufaika na kuondolewa kwa hii tozo yabodaboda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia wenzanguwamezungumzia suala nzima la magari na mimi naungananao. Ni kweli kwamba, siyo Watanzania wote wana uwezowa kununua magari mapya. Hapa tunazungumziaWatanzania hawa ambao ni wafanyakazi wanaopatamishahara midogo, anadunduliza kipato chake, anajinyima,aweze kupata usafiri utakaomwezesha kuwahi ofisini, leo hiitunaweka kikwazo.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabungewamezungumzia hapa na mimi nikiwa mmojawapo sikuwana uwezo wa kununua gari jipya mbali na kupata mkopo.Hatuwatendei haki wafanyakazi ambao na wenyewewanataka kutoka kwenye kutembea kwa mguu wawezekumiliki magari, hawatakuwa na uwezo wa kununua garijipya.

Mheshimiwa Spika, tunaona urasimu uliokuwepobandarini pale, lakini tunaendelea kuwaongezea mzigowafanyakazi, huku tunawapunguzia kodi na hukutunaendelea kuwaongezea kodi kwa mgongo mwingine.Naomba Serikali pia iliangalie hiki kwa kina.

Mheshimiwa Spika, niipongeze Serikali kwa kuongezabajeti trilioni 18, sina tatizo nalo. Pia niipongeze kwa kuongezafedha kwenye baadhi ya Wizara. Lakini naiomba sana Serikali,kuongeza fedha ni jambo lingine na kuhakikisha fedha hizizinakwenda katika miradi na lenyewe ni jambo lingine.

Mheshimiwa Spika, mwaka juzi tuliongeza fedhakatika Wizara ya Uchukuzi, lakini Wabunge watakubalianana mimi je, hizo fedha zilitoka? Mwaka jana tuliongeza fedha

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

64

19 JUNI, 2013

kwenye bajeti ya umeme, lakini hizo fedha hazikutoka. Sasasi vyema Wabunge tukaendelea kuimba wimbo ule ule kilamwaka, tukapewa majibu yale yale na utekelezaji ule ule,hatutakuwa tunawatendea haki Watanzania.

Mheshimiwa Spika, hii ni kutokana na fedha zamaendeleo kutegemea wahisani na Mheshimiwa Chengealisema kama kuna wahisani ambao tunaona wanatu-letdown tuangalie vyanzo vingine, tuangalie wadau wenginewa maendeleo. Wengine hao wanataka kutumia mgongohuu wa kuahidi kutupa hela, lakini hawatupi na kuhakikishamambo hayaendi, mwisho Serikali yetu iendelee kuchukiwana wananchi.

Mheshimiwa Spika, niiombe Serikali kama kila sikutunategemea watu ambao hawatupi fedha kwa mudaunaotakiwa, tuanze sasa na sisi kama Taifa kuona uwezekanowa asilimia 80 ya bajeti ya nchi itokane na vyanzo vyetuwenyewe. Hili linawezekana kama tutahakikisha tunaminyamianya ya watu kukwepa kodi. Majirani zetu wa Kenya leohii asilimia 80 ya bajeti yao ni fedha zao za ndani. Siyo wahisaniwote wanatupenda na wengine kama mnavyojuahawapendi kuendelea kuona Tanzania hii yenye neemainaendelea kuwa na amani na utulivu.

Mheshimiwa Spika, sasa naiomba Serikali yanguiangalie suala hili kwa kina. Mambo ya kuwa tunaendeleakutenga fedha, halafu tunapata majibu yale yale, ooh,wahisani hawajaleta, sisi Wabunge humu ndani tumechoka.Kusanyeni kodi, zibeni mianya ya rushwa, tuhakikishetunaongeza mapato na tuwe na uwezo wa kuhakikisha bajetitunayotenga, tunaitenga kwa fedha zetu wenyewe za ndani.

Mheshimiwa Spika, siyo kila siku tunataja figure trilioni18, kumi na ngapi, fedha za nje kiasi Fulani, halafu haziji,hatulitendei haki Taifa hili. Uwezo wa kukusanya mapatotunao. Wale wote ambao wanakwepa kodi wafikishwekwenye vyombo vya sheria na tuminye mianya yote ambayoinatoa mianya ya watu kukwepa kodi.

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

65

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, naomba nizungumze mradi wamaji wa Bunda. Leo hii ukienda hospitali ya DDH utakutanana akinamama wodini wana maji kwenye ndoo za lita 20 na10, hospitali! Mradi huu umeanza muda mrefu na kutokamilikakwa mradi huu kunawachonganisha Wabunge na wananchi.Wananchi wa Bunda wamechoka kunywa maji machafu nawenyewe ni Watanzania, wanahitaji maji safi na salama.

Mheshimiwa Spika, hapa nilisema pia, kuna baadhiya Wakandarasi hawazitendei haki tender ambazowanapewa na mpaka tunashangaa kwa nini wanaendeleakupewa. Mkandarasi anakwenda site baada ya kuonaviongozi wa kisiasa, haiwezekani!

Mheshimiwa Spika, sasa tujue wanapewa pesa auhawapewi au wanashindwa kutimiza majukumu yao.Tunaomba sana, wananchi wa Bunda wanaomba mradi wamaji ule ukamilike. Tuliambiwa ungekamilika mwaka janamwezi Julai, lakini mpaka leo hata asilimia 30 ya mradihaujakamilika. Imechimbwa mitaro mpaka imetitia tena.Mabomba yanarundikwa kule wakisikia labda Mbungeanakwenda au Waziri anakwenda, lakini hakunakinachoendelea.

Mheshimiwa Spika, tunaomba mradi wa majiukamilike haraka, operation zinakwama kwa kukosa maji,akinamama wanakwenda hospitali wakiwa wamebeba majikwa sababu hospitalini hakuna huduma ya maji, wananchiwa Bunda wamechoka wanataka maji safi na salama.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru na naunga mkonohoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa nimwite Mheshimiwa Khatib SaidHaji na Mheshimiwa Saleh Pamba, Mheshimiwa Paul Lwanjina Mheshimiwa Riziki Omar Juma wajiandae.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsantenami kwa kunipa nafasi ya kuwa mmoja miongoni mwawanaochangia hotuba hii muhimu.

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

66

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, nami naomba nianze kwa kutoapongezi kubwa sana kwa Chama cha Wananchi (CUF)kushinda uchaguzi wa Jimbo la Chambani, Pemba nakuwashinda CCM na washirika wao akiwemo ADC. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia mimi siyo mchoyo,nawapongeza CCM kwa ushindi wa viti vya Udiwaniambavyo wameendelea kuchukua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Chama changu cha wananchi(CUF) kiliniteua kuwa mshiriki wa uchaguzi wa Udiwani katikaKata ya Handeni ambako tuligalagazwa na CCM katikauchaguzi ule.

Mheshimiwa Spika, lakini nimejifunza jambo kwamba,si lazima ushinde hata ukishindwa Mpinzani makini hutoamkono kwa ahsante kwa aliyekushinda. Lakini katika mojanililojifunza kule Muheza ilipofika saa sita mchana, nilikutanana Mheshimiwa Mbunge mwenzangu wa Tarime NyambariChacha Nyangwine akaniambia kwa kheri, naondoka zangu.Nikamwuliza unakwenda wapi na uchaguzi unaendelea.Akaniambia CCM tumeshashinda, tayari tumeshindaMheshimiwa Mbunge, mimi nafunga machungwa, naondokaMuheza.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nilichojifunza pale nikwamba, tutaiangalia hii teknolojia mnayoitumia wenzetu waCCM ya kuweza kujua mmeshinda kabla hata uchaguzihaujamalizika.

SPIKA: Wewe hujui Maji Marefu yupo kule! (Kicheko)

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante.Sasa nianze mchango wangu kwa kusema kwamba,nimeridhika sana na usikivu angalau ambao umeanzakuoneshwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi katikamaeneo haya nitakayoyataja. Nimeridhika kwa kuondoakodi ya bodaboda kwa vijana wetu wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, pia naipongeza Serikali leo kwa

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

67

19 JUNI, 2013

kusikiliza kilio cha Wabunge cha kuondoa mtindo wa directrelease katika bandari zetu. Jambo hili katika bajeti ya Wizaraya Fedha mwaka uliopita akiwa Waziri Mkulo nililisema hapa,Serikali inapoteza mabilioni ya shilingi kwa kuruhusu mtindowa kuamini wafanyabiashara wakubwa kwa mtindo wakutoa mizigo bila kukaguliwa bandarini.

Mheshimiwa Spika, nililisema hili nikijua, kwa sababuMheshimiwa Waziri anakaa karibu sana na Rais, lakini sisitunakaa karibu sana na wananchi. Tunajua wananchiwanazungumza nini na tulijua kuna matatizo gani kuruhusukuendelea kutumika kwa mtindo ule wa direct release. Lakinimwaka jana yalipuuzwa kwa sababu labda waliokuwawakitetea jambo lile tulionekana ni Wapinzani.

Mheshimiwa Spika, naomba wenzetu, wakatitunapoleta mawazo yetu ya maana ya kusaidia nchi hii katikaukusanyaji hasa wa kodi wayasikilize na wayatekeleze.Wapinzani wapuuzi, wapuuzeni, lakini Wapinzani makiniwasikilizeni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili lingesikilizwa mwaka jana, leotungeokoa mabilioni ya shilingi za Watanzania ambazozil ikuwa zikipotea kwa mtindo huu direct release .Tunaposema, nasema tena, tunaposema msichukulie kilaMpinzani analosema halina maana, angalieni na mwangaliekwa uzito muone mambo yenye maana myachukue.

Mheshimiwa Spika, alikuwepo mwimbaji mmojamaarufu, muasisi wa Taarabu kule Zanzibar sasa hivi nimarehemu, alikuwa anaitwa Siti binti Saad, huyu mamaalikuwa mbaya wa sura sana, lakini alikuwa na sauti nzuriajabu. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, katika kumponda wapinzani wakewaliwahi kumtolea mashairi yaliyosema hivi. Nataka weweuyasikilize, ni mazuri, walimwambia; Siti binti Saad umekuwamtu lini, ulitoka kwenu na kaniki mbili chini, kama siyo hiyosauti wewe ungekula nini? Siti binti Sad aliwajibu; si hoja

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

68

19 JUNI, 2013

uzuri wa sura jamali, utukufu wa kabila na wingi wa mali,hasara ya mtu kukosa akili. Kwa hiyo, wanayoyasema wenyeakili yafuateni na myazingatie. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwa hilo nanaamini hakuna haja ya kuwapandishia Watanzania kodi yamafuta kwa sababu pato litakalopatikana kwa ukwepajimkubwa wa kodi ulitokana na njia hii, unatosha kufidia pengohilo. Mabilioni ya shilingi yaliyokuwa yanakwepwa na matajiriwakubwa kwa mtindo huo wa utoaji wa mizigo inatoshakufidia pengo hilo.

Mheshimiwa Spika, hakuna haja ya kuongezea kodiya mafuta wala kodi ya simu kwa watumiaji wa kawaida,hiyo fedha itafidiwa na hapo. Msituulize hapa, hata huyokipofu ukimkabidhi mkia wa paka hakuulizi makalio yake yakowapi? Atajua tu na ni kipofu. seuze wewe mwenye macho,unauliza makalio ya paka yako wapi wakati mkia umeushika,kodi ipo haijakusanywa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, nataka niseme na si hapo tu, kunakilio kikubwa sana cha wananchi wetu hasa wa vijijini,wanatozwa kodi ya mkaa gunia moja sh. 8,000, guniaanalokwenda kuliuza mjini sh. 25,000 anatozwa sh. 8,000.Ukipiga hesabu mwananchi huyo kama atapeleka magunia30 kwa mwezi, analipa kodi 480,000/= akienda kwa mwakani milioni 5,700,000/=. Mwenye lori lile hafikii kulipia Serikali kodihiyo analipa mtu wa kawaida.

Mheshimiwa Spika, leo mzee wangu ametoka kuleTanga Vyeru, Monga, Kichalikani anapofika na gunia lake lamkaa analipishwa fedha hiyo. Kwa kweli tunawanyonya natunawaumiza wananchi wetu. Tuangalieni hizo kodizinazokandamiza watu wetu, mtu anayeilipa Serikali5,700,000/= hata akiumwa anapokwenda hospitalianaambiwa anunue hata kidonge cha panadol, hii siyo haki,tuangalieni.

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

69

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, nitakwenda moja kwa mojakwenye kero za Muungano. Nampongeza Mheshimiwa PindiHazara Chana, jana aligusia suala la kero za Muungano.Kumekuwa na vikao vya Waziri Mkuu na Makamu wa Raiswa Zanzibar kila mwaka kujadili kero za Muungano na mojakati ya kero hiyo na napenda kuisema sana ni Watanzaniakutoka Visiwani, wanapoingia na magari yao kwa ajili yamatumizi yao Tanzania Bara. Kumekuwa na usumbufu nahali isiyokuwa ya kawaida na hili ukilizungumza unaambiwalimo katika kero ya Muungano. Sisi hatutaki methali hii yakero ya Muungano, inayowaumiza Wananchi, hicho siyo kitucha kujivunia. Wenzetu wamesema na sisi tunasema, hapanina fomu hii ya TRA ambayo imebatizwa jina la C32 (CustomRegulation 136 Section Two), ambayo hii inawaruhusu watuwote wanaotoka katika East and Central Africa, nchi zaCOMESA, zote kuingia na magari yao hapa wakatumia kwamtindo na kuna sehemu tu hapa unapigiwa muhuri wakuingia na muhuri wa kutoka pasipo na vikwazo vyovyote.

Kwa Zanzibar au kwa Watanzania wanaotokaZanzibar, haliwi hilo na nimekuwa nikifuatilia jambo hili, maraya mwisho nimeletewa jibu hili. Mimi ni Mjumbe wa Kamatiya Uchumi, Viwanda na Biashara, niliuliza swali hili katikamoja ya vikao na Kamishna wa TRA, akasema jambo hilohajui kama liko kama Mzanzibari anapoingia na gari lakepale Dar es Salaam kutaka kutumia mwenyewe anakutanana kikwazo hicho. Nataka nisome leo jibu ambalonimeletewa officially na Watanzania walisikie, mwonenamna gani ambavyo yanatumika mambo mengine katikakuzorotesha hata huo Muungano wenyewe na kwa hilikama tunafikia hapa, basi hakuna ubaya watu kuchukiaMuungano, kwa sababu kero za Muungano zimezidi.

Mheshimiwa Spika, jibu nililoletewa ni hili linasema:“Mtu yeyote anayetoka nje ya Tanzania kwa ajili ya kufanyamakazi ya muda ndani ya nchi wakiwemo wa Jumuiya yaAfrika Mashariki, SADC, anaruhusiwa kuingiza gari kwa ajiliya matumizi yake wakati akiwa nchini kwa mashartiyafuatayo: Anatakiwa kulipa ada ya Dola 20 za Kimarekanina kutumia gari hilo kwenye barabara za Tanzania. Niruke

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

70

19 JUNI, 2013

kwa sababu ni mengi, lakini naenda kwa mtu anayetokaZanzibar sasa. Mtu anayeingiza gari lake kutoka Zanzibarhatakiwi kuacha taarifa zilizotajwa hapo juu, badala yakemtu huyo anaagiza gari ambalo lina namba ya usajili waZanzibar kuweka dhamana benki au fedha taslimu ambazoni sawa na tofauti ya kiasi ambacho atatakiwa alipe.”

Mheshimiwa Spika, hii paragraph ni ndefu lakinikifungu cha mwisho kinasema: “Hata hivyo, suala lakuwezesha magari yaliyosajiliwa Zanzibar kuweza kutumikaBara, l ipo katika orodha ya kero za Muungano nalinatafutiwa ufumbuzi wa kudumu. Toka sijafika kwenyeBunge hili, miaka 20 kero hii inatafutiwa ufumbuzi! Hii nifedheha, kumchukua Waziri Mkuu wa Nchi, Makamu waRais wa Zanzibar, wakakaa kujadili eti suala dogo la kerokwa sababu ya gari kutoka Zanzibar kutumika Bara. Sisi niWatanzania, leo hii kila Mtanzania anadaiwa shilingi 500,000hapa hawapo Warundi wala Wanyarwanda; kwa nini?

SPIKA: Kengele ya pili hii. Hiyo document uliyosomainatoka wapi?

MHE. KHATIB SAID HAJI: Inatoka kwa Wizara yaFedha, majibu ya hoja za Waheshimiwa Wabunge.

SPIKA: Inatoka ndani?

MHE. KHATIB SAID HAJI: Haitoki hapa ndani inatokahuko kwenye Kamati yangu?

SPIKA: Sawa ni Bunge hilo. Haya ahsante nadhaniwamesikia. Mheshimiwa Saleh Pamba, atafuatiwa naMheshimiwa Lwanji, atafuatiwa na Mheshimiwa Riziki OmarJuma, atafuatiwa na Mheshimiwa Devota Likokola,Mheshimiwa Barwany ajiandae na Mheshimiwa Dkt.Christine Ishengoma.

MHE. SALEH A. PAMBA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii na mimi niweze kuchangiakatika hoja iliyoko mbele yetu. Awali ya yote, napenda

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

71

19 JUNI, 2013

nichukue nafasi hii kuipongeza Wizara ya Fedha, Waziri,Naibu Waziri na Watendaji wote, kwa kutuletea bajeti hiiambayo inatupa mwelekeo wa kule ambako tunaelekea.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo natakakulizungumzia, nataka nikupongeze wewe binafsi, umeachalegacy kubwa sana kwa kuleta utaratibu huu wa BudgetCycle mpya. Haipo katika maeneo yetu, sisi na Ugandana Rwanda ndiyo ambao tunayo Budget Cycle ya aina hii.

Mheshimiwa Spika, zipo changamoto, lazimatukubali kwamba, katika jambo jipya lolote unalolileta,lazima litakuwa na changamoto. Tunaiomba Serikali kwayale ambayo yamejitokeza katika kipindi hiki, ambayo nichangamoto katika utayarishaji wa bajeti, wachukue kamachangamoto za kuweza kuzifanyia kazi. Hakuna jambojipya ambalo litaanza bila ya kuwa na changamotombalimbali, lakini nakupongeza sana, umefanya kazi nzurisana kwa nchi yetu na jina lako litabaki katika historia;hongera sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi ni Mjumbe wa Kamati yaBajeti, kwa hiyo, lazima ni-declare interest kwamba, nikokatika Kamati ile. Napenda pia nikupongeze sana kwakuanzisha Kamati hii ya Budget Scrutiny, kwa sababuinasaidiana na Serikali. Kamati hii imekuwepo katikakuiongoza Serikali kwenye maeneo ambayo imeshindwakuyaona. Kamati ya Bajeti imefanikiwa sana katikakuongeza bajeti ya karibu shilingi bilioni 513. Fedha za majishilingi bilioni 184.5 hazikuwepo, fedha za umeme shilingi bilioni153 hazikuwepo, fedha za mabehewa hazikuwepo, lakinikatika ushirikiano uliokuwepo kati ya Kamati ya Bajeti naSerikali, kwa kukaa pamoja kwa sababu wote tunafanyakazi moja, fedha hizo zimepatikana na sasa nina uhakikakabisa fedha hizo zitaweza kwenda kuwaletea Wananchimaendeleo.

Mheshimiwa Spika, katika Jimbo langu la Pangani,tutapata Miradi mipya ya Maji katika maeneo yaKigurusimba, Mikocheni, Mzambarauni, Masaika, Stahaku,

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

72

19 JUNI, 2013

acha miradi mingine ambayo inaendelea. Tutapata mradimkubwa wa umeme wa karibu shilingi milioni 800 kutokanana fedha hizi ambazo zimeongezwa. Napenda nichukuenafasi hii, kuishukuru sana Serikali kwa hatua hii ambayowameichukua. Suala la kutenga bajeti ni moja, suala lakuwa na miradi ni suala mojawapo, lakini suala la usimamizina utekelezaji wa miradi ni suala lingine. Ninaiomba Serikalikwamba, katika fedha hizi ambazo zimetengwa kwa ajiliya maendeleo na kwa ajili ya miradi mbalimbali ziletwe,zipelekwe na zilindwe. Kulindwa maana yake fedha zamiradi ziwe ring-fenced, zisiende katika matumizi mengineambayo yanajitokeza; hapo ndipo tutaweza kupiga hatua.

Mheshimiwa Spika, naomba niende haraka harakakwenye Sera ya Mapato. Katika Sera ya Mapato na katikaBajeti ya Waziri wa Fedha, mara nyingi tumekuwa tukiendakatika maeneo yaleyale; sigara, vinywaji, juice, vinywajivikali, mvinyo na kadhalika na pay as you earn. Sasa lazimatufike mahali tuondokane na maeneo kama hayo. Lazimatuwe na miradi mikubwa, tuachane na kutoza kodi kwenyemaeneo ambayo ni traditional. Sasa tunafanya nini? Kunamaeneo ambayo lazima tuyafanyie kazi na tuyawekeemkakati, maeneo ambayo tunaita mega projects, miradimikubwa mikubwa ambayo ita-stimulate uchumi. Kwamfano, miradi inayohusiana na madini ya uranium, madinimakubwa, madini ya viwandani kama nickel, madini kamaChuma cha Liganga na Mchuchuma, mambo kama gesi,maeneo ya mafuta haya ni maeneo ambayo Serikali lazimaiweke mkakati maalum na iweke vivutio maalum ili kuwezakuhakikisha kwamba, maeneo haya yanachangia nayatachangia katika uchumi.

Nitatoa mfano, nchi ya Mozambique ilikuwa namatatizo lakini waliamua kuingia katika mradi mmojamkubwa kabisa na Kampuni ya Japani inaitwa Mitsubishi.Waliamua wakajenga kiwanda cha kuyeyusha aluminium.Huu ni mradi mkubwa, ndiyo miradi ambayo tunaita megaprojects, miradi ambayo inafufua uchumi kwa haraka. Huumradi unaitwa Mozambique Aluminium, ulipojengwamwaka 2000 pale Msumbiji matokeo yake yalikuwa nini?

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

73

19 JUNI, 2013

Matokeo yake ni kwamba, walitoa ajira ya watu 3,000 maramoja. Waliweza kutumia umeme megawati zaidi ya 50 paleKiwandani na vilevile Pato la Taifa la Mozambique, uchumiwa Mozambique ulikua kwa asilimia tano mara moja. Kwahiyo, haya ni maeneo ambayo lazima Serikali yetu iyafanyiekazi. Maeneo ya viwanda vikubwa, maeneo ya viwandamkakati, hayo naiomba Serikali na nimeona miradi mingiiliyomo humu nayo inatuelekeza huko; kwa upande waSerikali nasema hongera sana.

Mheshimiwa Spika, nataka nizungumzie suala laMiradi ya Public Private Sector (PPP). Miradi hii tusikae nayokwenye madawati. Fedha zipo nje, kwa hiyo, lazimatwende nje kutafuta fedha za kusukuma Miradi ya PPP.Twende Uchina, Marekani, Ulaya, twende na Marekani yaKusini ili tuweze kuhakikisha Miradi hii yote nayo inapatawawekezaji, tusikae nayo peke yetu kwa sababu hukondiko ambako kuna fedha.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nataka nizungumziemasuala mawili muhimu sana. Suala la kwanza ni la nidhamuya matumizi. Serikali tutapitisha bajeti ya shilingi trilioni 18.2.Serikali inayo madaraka ya kubadilisha vifungu hapa napale, lakini ndani ya Serikali wana utaratibu wa kusemakwamba, wanayo Action Plan. Kwa hiyo, as long as waohawatabadilisha, ile figure haitabadilika, wanawezawakatumia fedha hizo. Tunachoiomba Serikali ni kwamba,lazima waufuate ule mkakati wao wa Action Plan. Kwasababu ukizitoa fedha katika fungu moja ukazitumia zikazidi,maana yake ni kwamba, maeneo mengine yaliyoko katikaMpango Mkakati wako hayatafanyiwa kazi. Kwa hiyo,tunahitaji nidhamu ya matumizi kuhakikisha kwamba, fedhazinatumika katika maeneo yale tu ambayo yamepangwa,maeneo mengine ambayo hayajapangwa, basi fedha hizozisubiri bajeti nyingine.

Pamoja na kwamba, Waziri wa Fedha anayomadaraka ndani ya vifungu vyake vya bajeti kwakuyabadilisha hapa na pale, lakini tunafikiri kwamba, mahaliambapo tunatakiwa tuendelee, lazima tuhakikishe

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

74

19 JUNI, 2013

tunakuwa na discipline, tunakuwa na financial disciplinekuhakikisha kwamba, fedha iliyopangwa ndiyo ileileinayotumika hata ndani ya kifungu hicho hicho haizidi nahapo ndipo ambapo tutaweza kusonga mbele.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo natakakulizungumzia ambalo naliona ni la msingi kabisa na hotubazote mbili zimelizungumzia, Hotuba ya Waziri wa Fedhapamoja na Hotuba ya Waziri wa Mipango, ambalo sijaonamkakati wa Serikali wa kuweza kulitekeleza. Haya yotetunayozungumzia ...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Naona kengele ya pili.

MHE. SALEH A. PAMBA: Mheshimiwa Spika, naungamkono hoja, asilimia kwa mia. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Lwanji, atafuatiwa naMheshimiwa Riziki Omar Juma na Mheshimiwa DevothaLikokola ajiandae.

MHE. JOHN P. LWANJI: Mheshimiwa Spika, ahsantekwa kunipa nafasi na mimi nichangie bajeti hii. Nachukuanafasi hii, kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Fedha, kwakuwasilisha bajeti nzuri na yenye mwelekeo. Wakatianahitimisha labda nimnukuu alisema: “Mheshimiwa Spika,yote niliyoyasema yanawezekana iwapo kila mmoja wetuna Wananchi kwa ujumla, tutatimiza wajibu wetu kila mmojakwa nafasi yake kwa kushiriki na kuwajibika kikamilifu katikakutekeleza sera na mipango tuliyojiwekea.”

Mheshimiwa Spika, maneno haya ni muhimu na nimazito na sisi kwa upande wetu Wabunge, nadhanitumeshiriki na tumetoa michango yetu toka mwezi waMachi kwenye Kamati, tumekuja hapa miezi yote hiitumekaa hapa nadhani tumetoa michango ambayoitaisaidia Serikali kusimamia mapato hayo

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

75

19 JUNI, 2013

yatakayokusanywa na matumizi yake. Tuna tatizo hilo lauwajibikaji, lakini sisi tunamrudishia tena Waziri asimamienyumba yake hiyo, hayo mapato yatakapopatikanayaweze kusimamiwa vizuri.

Mheshimiwa Spika, tatizo tunalo nchi hii la rushwa,kitu kidogo, vitu kama hivi na tatizo hili limekithiri miakanenda rudi. Fedha zinakusanywa lakini katika matumizi,CAG na vyombo vingine vinatoa taarifa mbaya kwambamatumizi hayasimamiwi vizuri. Sasa ningeliomba safari hiibasi tufanye kweli, tusimamie fedha hizi za umma ziwezekutufanyia kazi ambazo tumefanya.

Mheshimiwa Spika, Rais wa Liberia, Mama Ellen SirleafJohnson, nadhani aliposhika madaraka alipofika tu maraya kwanza aliangalia Wizara ya Fedha, alikuta uozo. Kitualichokifanya, aliwaondoa wote pale, akakodisha watukutoka nje wakashika hiyo Wizara ili Serikali iweze kuwa namapato ya kutosha pamoja na nidhamu ya matumizi,alifanya hivyo. Sasa miaka ijayo, nafikiri haya ni mawazoyangu, tusione aibu basi kwa sababu tutakuwatumeshindwa tusione aibu ya kuweza ku-outsource autupate wataalamu katika Wizara hii kutoka nje ili wawezekusimamia maana sisi hatuwezi. Utaratibu huuinavyoonekana kwa sisi ndugu, jamaa, marafiki na nini,tunaoneana aibu. Mheshimiwa Keissy hapa alisemakwamba, wanyongwe, hata tukiwanyonga haiwezekanishughuli itakwenda hivyo. Mimi naona suala hapa ni lautaalamu, ni la usimamizi wa kina kuhakikisha kwamba,fedha za umma zinatumika kama zilivyolengwa na sivinginevyo.

Mheshimiwa Spika, Marehemu Meresi Zenawi,aliyekuwa Rais wa Ethiopia; Nchi ya Ethiopia inategemeasana pilipili kama zao kuu la biashara, linapeleka nchi zaKiarabu na nini, lakini mwaka mmoja walipata shidawafanyabiashara walihoji sana zao hili wakanunua kwawingi wakahodhi wakaficha, sasa uchumi wa nchi ukawaunalegalega kwa sababu zao hil i ni muhimu kwao,walichofanya, walifanya operesheni maalum kabisa.

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

76

19 JUNI, 2013

Operesheni maalum ya makusudi, wakaingia katikamaduka yao wakakuta wafanyabiashara kadhaa wengiwamehodhi zao hili. Kwa hiyo, alichofanya yule alikuwa niMwanajeshi, alituma maaskari wake wakaendawakakamatwa wale watu waliokuwa wamehodhi nabidhaa zao zikawekwa nje pale, kilichofuata ziliwekwa nguzokila nyumba kwa huyo mtu, akafungwa pale basi wakalashaba wote na nidhamu ilirudi. Sisi mambo hayo sidhanikama tunaweza tukayafanya.

Mheshimiwa Spika, mimi nafikir i kitu muhimutunachoweza kufanya, tuone kama mama yule wa Liberiaalivyofanya, kama Wizara ya Fedha haitengamai basituombe msaada watu hawa waje watusaidie twende naWizara nyingine kama inaonekana pale pameimarikatwende na Wizara nyingine, basi tuwaweke watu weupehawa watusaidie, maana inaonekana bila ya hao watuweupe hatuwezi kuendelea mbele, hatuwezi kusongambele katika mipango yetu. Kwa hiyo, ninashauri kwamba,Wizara isimamie mapato hayo.

Mwaka jana tumeambiwa kwamba, fedha zawahisani nyingi hazikuletwa na ni kisingizio wanasema unajuafedha za kigeni hazikuja, lakini ukweli wenyewe ni kwamba,taarifa hatupeleki kwa wakati maana hizi fedha kila quoterlazima ziwe na taarifa. Tumeambiwa kwamba, baadhi yamaeneo taarifa hazikukamilika, sasa watatoaje fedha hawawatu kama taarifa hazikukamilika; hawawezi. Kama taarifahakuna na hii imeanzia kule juu katika taarifa hizi mpakachini, mpaka hata kwenye Halmashauri na kwenye Serikaliza Vijiji, taarifa za fedha na mapato hatusomi na hatupelekikwa wakati.

Mheshimiwa Spika, sasa hizi fedha; kwa mfano, bajetihii inasema kwamba, takribani shilingi trilioni nne tunatarajiakutoka kwa washirika wa maendeleo na wanaitadevelopment partners; sasa development partners hatamimi nashindwa kuelewa hili neon. Hivi huyo developmentpartner atakuwa na uhusiano gani na mtu maskini?

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

77

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, sisi tukubali tu kuwa waletewahisani. Wahisani wanatusaidia, lakini kama hatufuatimasharti yao tutafanyaje? Inabidi tufuate mashartiwaliyotuwekea ili waweze kutoa hela. Mimi nilikuwaninashauri Kamati yako hii ya Bajeti ipewe fursa kwamakusudi kabisa ya kutembelea Mabunge ya hizo nchi zawahisani. Juzi ametusomea Waziri wa Fedha hapa kuwa ninchi 19 zimetusaidia na taasisi tisa za Kimataifa. Kama pesazinasuasua, Kamati ya Bajeti haiwezi ikaishurutisha Serikalikuwa nendeni mkawaulize au mkafanye hivi. Kamati hii yaBajeti ipewe fursa ya kwenda kwenye Taasisi au Mabungeya nchi zinazohusika za wahisani wazungumze na wenzaojamani kuna tatizo gani kwa nini fedha hizi haziji kwa wakati.Kama wataambiwa tatizo liko kwenu basi na huku nakowafuatilie.

Mheshimiwa Spika, ninakupongeza kwa kuundaKamati hiyo, imetuonesha njia hapa kwa muda mfupi.Utaratibu huo uendelee, ninadhani itumike vizuri waendesambamba na Wizara hii, lakini kila mmoja a-play role yake.Sasa kama Wajerumani waliahidi; hivi kweli mmewekeanasahihi na kila kitu na ikatangazwa, mbona Japani pamojana matatizo yao yote waliyoyapata ya mwaka 2011, lakinihawakusitisha misaada kwa sababu they honor theircontract. Wajibu wao sasa kama zinasuasua basi hii Kamatiya Bajeti iruhusiwe itembelee hizo nchi, izungumze nawahisani kuwa nchi yenu imeweka mkataba na nchi yetu,lakini tunashindwa kuelewa ni kwa nini fedha haziji.Ninadhani hilo linaweza likatupa njia ya kuweza kupata hizifedha kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, niliomba Watendaji pamoja nakuwa wanahitajika kubanwa, lakini Serikali nayo ije namkakati wa kuweza kuwalipa Watumishi wa Serikali vizuri,kulingana na hali ya maisha ilivyo, labda hii nayo itasaidiahawa watu wasiweze kuangalia mianya mingine ya kutuibia.Kama unampa mtu jukumu la kusimamia fedha zaWananchi au hela za Serikali halafu mshahara wake nimdogo, lazima atatafuta njia zingine. Kwa hiyo,ninawaomba kwa makusudi kabisa kuwa, bajeti ijayo

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

78

19 JUNI, 2013

tuangalie pamoja na kuwa tunaongeza kidogokidogo,lakini maeneo ambayo tunaona ni muhimu, basi wawezekupata malipo ya kutosha kwa ajili ya maisha yao na kwaajili ya kuwaweka katika hali ya kuwafanya wasiwe natamaa.

Vipaumbele sita vya Kitaifa vilivyowekwa ninavionani vingi, tupunguze tubaki na vipaumbele vitatu. Nchi yaSweden, miaka ya 1950 ilijiwekea vipaumbele vitatu; elimu,halafu ikajiwekea control ...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante ya pili. Tukienda kuwauliza waleDonors sisi Bunge tutakuwa tunaingilia kazi ya Executive.Wabunge wa Bajeti watakwenda kujifunza katika nchiambazo zimefanikiwa vizuri zaidi. Sisi hatutafanya kazi yaExecutive, watafanya wenyewe. Mheshimiwa Riziki OmarJuma!

MHE. RIZIKI OMAR JUMA: Mheshimiwa spika,ninaomba nichukue nafasi hii, kumshukuru Mwenyezi Mungu,ambaye amenijalia uwezo wa kusimama hapa mbele yaBunge lako Tukufu, kuchangia hoja iliyoko mbele yetu.Nachukua nafasi hii kukupongeza wewe, kwa kazi nzuriunayofanya katika Kiti chako hicho katika kusimamia Bungehili. (Makofi)

Ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri naManaibu wake, pamoja na timu yake ya wataalamu, kwakujitahidi kufanya kazi ambayo tumewatuma. Ninaombaniseme kuwa, bado wanahitaji kufanya kazi ya ziada kwakutumia wataalamu wao ambao wanao il i tuwezekujikwamua hapa tulipo.

Ninaomba nianze na hoja ya utafiti. Utafiti katikabajeti hii umetengewa fedha ndogo sana. Nchi yoyotehaiwezi kwenda bila kuwa na utafiti wa kina na ndiyo maanaleo hii tunakuwa tukiongea humu ndani kila siku tunatafuta

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

79

19 JUNI, 2013

wapi ambapo tumejikwaa, lakini hatupajui, kumbehatufanyi utafiti wa kina ili kuweza kufikia malengo yetuambayo tumejipangia. Nchi yoyote bila utafiti hatuwezikufika mahala na ndiyo maana leo hii ki l imo chetukinaonekana kila siku ni kilimo ambacho hakina tija, kwasababu watafiti hatuwezi kuwatumia ipasavyo, kutokanana fedha ndogo ambayo tunawapangia. Nchi za wenzetuukienda jinsi wanavyozalisha utashangaa, ukiliona peralinakuvutia, ukiona embe unatamani kula, ukiliona chungwautalipenda.

Mheshimiwa Spika, ni kutokana na kwamba,wataalamu wao wanafanya utafiti wa kina na kuwezakufanya kilimo chao kwa utaalamu wa kutosha. Leo sisiwataalamu ninadhani tunao, lakini labda hatuwatumiiipasavyo, hatuna mbegu bora, hatuna mbolea bora naWananchi haziwafikii kwa wakati. Kwa hiyo, tunafikamahala tunabakia tunagwaya hapahapa, kilimo chetuhakina tija na mwisho wa siku tunafikia mahala Wananchiwetu wanaomba omba chakula, kwa sababu hakunachakula cha kutosha. Kila siku tunaomba chakula cha njaa,ni tatizo, ni kutokana na suala la utafiti. NinamwombaMheshimiwa Waziri wa Fedha, aangalie kwa kina suala hilila kuwatengea fedha za kutosha sehemu ya utafiti ili tuwezekufanya utafiti wa kina, mambo mengi hatuwezi kuyafanyabila ya kuwa na utafiti wa kutosha. (Makofi)

Ninaomba nije kwenye suala la kipaumbele;kipaumbele ni jambo muhimu sana na la msingi na kamahatujaamua tuweke kiupaumbele gani hasa ili tuwezekufika, tutakuwa na shida nyingi sana kila siku. Tuna fedhanyingi, ukitazama bajeti iliyotengwa safari hii ni trilioni 18,kama fedha hizi tungeziweka katika mgao mahususitukalenga kipaumbele gani hasa tunataka tukifanyie kazi,basi tunaweza kufanikiwa ndani ya kipindi cha miakamitatu. Kwa mfano, mwaka huu tungetenga fedha nyingitukazipeleka kwenye elimu na kwenye afya, sehemunyingine tukapeleka fedha kidogo; kwanza, tukubalikufunga mkanda, tukubali kujikita katika sehemu fulanituweze kuzalisha vizuri, basi tusingekuwa na tatizo. Kwa

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

80

19 JUNI, 2013

mfano, katika suala la elimu tuna tatizo la madawati, tunatatizo la vifaa, tuna tatizo la maabara, tuna tatizo la vifaavya maabara, walimu wanadai wana madeni yasiyokwisha,maandamano yasiyokwisha, hebu tujikite katika kitu fulaniili tujikwamuke hapa tulipo, mwaka ujao tufanye jambolingine.

Unajua sisi Waislam, tukifunga Ramadhani tunapikamuhogo, njugu, tambi, sijui mkate, sijui nini, mwisho wa sikuvyote huvili hivyo, kila mahali unatia mkono kidogo. Sasana sisi bajeti yetu tunaitumia kama futari, hatuwezi kufikamahala, tuchukue fungu kubwa tulielekeze mahala.Wenzetu China mwaka 1964 waliamua wakasema kuwaWachina wote wavae viatu, viwanda vikaagizwa,vikapewa uwezo, vikawezeshwa, suala la kuvaa viatulikatekelezwa. Wachina wote wakapewa viatu wakavaana wakapewa taaluma ya umuhimu wa kuvaa viatu nasisi Watanzania tukiamua tukajikita kwa kusema jambofulani lazima lifanywe, tutaweza kulifanya, tutaweza kabisahebu tuamue.

Mheshimiwa Spika, hatuwezi kutia mkono kila mahalatukasema tutafika, hatufiki, tutajenga barabara kilomitamoja, tutakwenda afya tumkomboe mzazi mmoja,tutakwenda elimu tulipe madeni walimu wawili wenginewanabaki, tutaendelea na mizozo na migogoro isiyokwisha.Tuchukue fungu tufanye jambo tuamue! Watanzaniatuwaambie tunataka kujikita katika elimu, mengine yotekwanza tunaweka pembeni, tutaweka fedha kidogokidogolakini sasa tunakwenda kwenye afya, ndani ya miaka mitatututakwamuka. Ninaamini tutakwamuka hapa tulipotutaondoka. Tuna miti mingi ambayo imejaa, tuwaelimisheWatanzania wapande miti halafu miti ya mbao ileHalmashauri ipewe kibali wakate miti ile ya mbao tuchongemadawati, tuchonge viti, tuwape wanavijiji tender wafanyehiyo kazi tueneze madawati shuleni, ili tuweze kupiga hatuahapa tulipo isiwe kila siku wanafunzi wetu wanakaa chini.Mtoto akirudi nyumbani suruali imechanika, anapindamagoti wakati wa kuandika, suruali imechanika magotini,imechanika matakoni, hatuwezi kwenda wakati miti ya

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

81

19 JUNI, 2013

mbao tunayo, Wananchi wapo wa kuweza kufanya kazi,lakini uamuzi hatujaamua. Waheshimiwa tutie nia natuamue, ninaomba tulifanyie kazi hilo.

Mheshimiwa Spika, nije kwenye suala la kuongezaushuru kwenye sigara, vinywaji na soda; hili halitusaidii,Mheshimiwa Waziri wa Fedha ni Mchumi na timu aliyonayoninadhani ni timu ya wataalamu mahususi, hebu tujiulizesiku Watanzania wakisema hatuvuti, hatunywi pombe,hatunywi soda, tutatoa wapi hizi fedha zingine? Hatuwezikutoa na mwisho magazeti huko siku nyingine yanatuambiasoda zina sumu, tunatishwa tishwa, kwa hiyo, wenginewanaamua kugoma kunywa soda na wengi wanapatasukari wanajikita sasa hivi wanasema hapana hakunakunywa soda tunakunywa maji tu. Kwa hiyo, itafika sikututashindwa vipaumbele vya kuongeza ushuru. NinaombaMheshimiwa Waziri, kwa uwezo wako ulio nao, ukae na timuyako ya wataalamu, tutafute vyanzo vya mapato vingine.Tuna madini ya kutosha, ninashangaa madiniyanachukuliwa. Mimi nina nyumba yangu ninakaa unanitoaunaniambia ninatakugawia hapo barazani ukae;inawezekanaje?

Haiwezekani, tuna fedha za kutosha, Watanzaniasiyo maskini ni matajiri, tuna uvuvi, bahari zimetuzunguka,tunaacha watu samaki wetu wanachukua, vyote hivyo nivyanzo vya mapato. Hebu tuvitumie vizuri, wataalamutunao timu, hiyo hapo mbele, mimi ninahisi ni timu yawataalamu, ifanye kazi ya ziada tuone namna ganitutapiga hatua.

Mheshimiwa Spika, suala la kuzuia kuingiza magariyenye umri wa miaka kumi; Watanzania ni maskini, hadi leoWatanzania ni maskini, lakini wote wanapenda kustarehe,hakuna asiyependa kustarehe. Ukizuia kuagiza magariyenye umri huo ni Watanzania wangapi wataweza kununuamagari mapya?

Mwenzangu mmoja amesema hapa yeye Mbungena hakununua gari jipya na siyo yeye tu na wengi humu

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

82

19 JUNI, 2013

ndani siyo wengi walio na magari mapya kabisa kwasababu uwezo wetu ni mdogo. Kwa hiyo, hili suala tulitafutieufumbuzi, tutawanyima Watanzania haki yao ya msingi.Gari siku hizi ni kitendea kazi muhimu sana, kinakuharakishiashughuli zako kabisa.

Mheshimiwa Spika, mtu akidunduliza akipata shilingizake milioni tatu, anakwenda kutafuta kigari kinamsaidiakumharakisha kazini, kinamsaidia kushughulika na harakatizake za kimaendeleo. Kwa hiyo, tusiwaondoe Watanzaniakatika matumaini ya ulimwengu huu wa kisasa. Ulimwenguhuu wa kisasa kila mtu anahitaji gari, anahitaji pikipiki,anahitaji vespa, kwa hiyo, tujitahidi tuliangalie kwa umakinihili suala jamani, ni gumu sana tunawatoa matumainiWatanzania wenzetu hawa ambao wanaishi maisha duni,tusiwakatishe tamaa. Mheshimiwa Waziri amesema kuwa,magari haya yanasababisha ajali, yanachafua mazingira,lakini je, amefanya utafiti kiasi gani na kuona kuwayanasababisha ajali; amefanya utafiti wa kina? Ndiyo paleniliposema kuwa hakuna utafiti.

Nije pia kwenye suala la kuongeza ushuru katikaunga wa ngano; anayepata athari siyo mfanyabiashara,hakuna mfanyabiashara anayekubali kupata hasara hatasiku moja; mwisho wa siku anayepata hasara ni mimi nawewe. Zaidi, tumwangalie Mtanzania aliye katika hali yachini kabisa, unga sasa hivi kilo moja ni shilingi 1500,keshokutwa utakuwa 2000, kwa hiyo ni tatizo. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana. Sasa nimwite MheshimiwaDevotha Likokola, Mheshimiwa Khalfan ajiandae,Mheshimiwa Dkt. Christine Ishengoma, Mheshimiwa MariaHewa na Mheshimiwa Kigwangala atakuwa wa mwishoasubuhi hii.

MHE. DEVOTHA M. LIKOKOLA: Mheshimiwa Spika,ninaungana na Wabunge wenzangu, kumshukuru sana

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

83

19 JUNI, 2013

Mwenyezi Mungu na kushukuru sana kwa ajili ya Bajeti hii.Ninawapongeza Wataalamu wa Wizara ya Fedha na waWizara ya Mipango na hasa Idara ya Mipango.

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo Wabunge wengiwamesema, umejenga historia ya nchi yetu, umewekaKamati ya Bajeti na inaweza kusaidia sana kuleta bajetiyenye manufaa kwa nchi yetu. Siyo tu umeleta Kamati yaBajeti, lakini umefanya kazi kubwa sana kuwasomeshaWabunge katika masuala haya ya bajeti, umewapelekaWabunge maeneo mbalimbali, umewapa mafunzo ya ainambalimbali yanayohusiana na bajeti; katika hil itunakupongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukianza na bajeti yetu, kwelibajeti yetu ni nzuri, lakini ina changamoto ni nyingi. Wananchiwetu wengi wanapokaa na kuisikiliza bajeti hii wanajiulizabajeti hii inawaletea matumaini gani? Kwa bajeti ya mwakahuu, ninapenda kuwaambia Wananchi ni bajeti yenyematumaini makubwa, kinachotakiwa ni Wananchikujipanga kuangalia vipaumbele vilivyopo na kuwezakushirikiana kutekeleza bajeti hii. Tukitaka bajeti yetuitekelezwe vizuri, bado tuna changamoto kubwa.Tunakusifu umeunda Kamati ya Bajeti, lakini tunatakakuiuliza Serikali ni lini italeta Sheria ya Bajeti, kwa sababukama tunataka bajeti itumike vizuri, basi tuwe na Sheria yaBajeti iweze kusimamia utekelezaji wa maazimio yoteambayo yanatolewa kwenye bajeti hiyo? Waziri amekuwaakiahidi mara nyingi kuwa ataleta Sheria ya Bajeti lakini hilibado halijatekelezwa. Tunaomba Sheria ya Bajeti iunganena nia nzuri uliyonayo ili bajeti yetu iwe inayotekelezeka.

Mheshimiwea Spika, tuna Mpango wa Taifa,ninaomba kuiambia Idara ya Mipango kuwa, Mpango huuni mzuri, lakini ninaomba Wananchi wengi waelezwe huuMpango, wengi hawaujui; na kama unapangwa bilakushirikisha Wananchi wengi ni ngumu sana Wananchiwakaona maeneo yao ya vipaumbele. Kama Wananchiwengi hawajashiriki katika kuviibua vipaumbele hivi, badokutakuwa na mgogoro katika kutekeleza, kwa sababu ni

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

84

19 JUNI, 2013

ngumu sana kutekeleza mpango ambao hujashiriki katikakuupanga. Ninaomba Wananchi waelekezwe Mpango huuwa Bajeti na Mpango wa Maendeleo wa Taifa.

Serikali ilianza kutekeleza masuala mazima ya bajetiya kijinsia, tunaomba katika mpango wadau mbalimbaliwashirikishwe ili utekelezaji wake uwe na manufaa kwa ainazote za watu walioko nchini. Tuna wanawake wengi sana,tunataka kujua ni namna gani wanawake wa nchi hiiwananufaika na bajeti hii; ni kwa asilimia ngapi vijana wanchi hii wananufaika na bajeti hii; na ni kwa kiasi gani wazeewa nchi hii wananufaika na bajeti hii? Tukiweza kujua kwatakwimu ni rahisi kila mmoja kuiona bajeti hii ni bajeti ambayoinaweza kuwasaidia watu wengi.

Mheshimiwa Spika, tuna kundi kubwa la walemavu,ni vizuri tukaainisha ni kwa namna gani walemavu katikanchi hii wananufaika na bajeti hii. Tusipoainisha hayamakundi maalumu, bado kutakuwa na manug’unikomakubwa katika jamii yetu. Ninajaribu kuangalia katikasuala zima la mapato ya nchi yetu, suala la mapato ni nyetina ninaomba maadam umeshaunda Kamati ya Bajeti, nivizuri Kamati hii ikajikita katika kuangalia mapato, maanabila mapato tutagawana nini? Tutakaa hapatunagombana mapato hayaonekani, kila mtuananung’unika hakuna mapato, hakuna mapato.

Mheshimiwa Spika, Mussa alikuwa anawapelekaWana wa Israel, walipofika Bahari ya Shamu wale Wanawa Israeli walikuwa wanalalamika, Mussa mwenyewealikuwa analia, lakini alimlilia Mwenyezi Mungu na MwenyeziMungu akamwuliza Mussa kwa nini unalia akasema sielewicha kufanya. Mwenyezi Mungu, alimwuliza Mussa una ninimkononi? Tumia ulichonacho, fimbo uliyonayo mkononi, pigamaji yatagawanyika na Wana wa Israeli watapita. Mimininaomba kuuliza Tanzania tuna nini mkononi? Lazimatujiulize Watanzania tuna nini mkononi? Tanzania hii ina watumilioni 44.9; kweli nchi hii tumeshindwa kutumia watu hawatupate maendeleo?

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

85

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, nchi hii ina vijana karibu inafikiaasilimia 60, kweli tumeshindwa kuwatumia vijana hawa ilitupate maendeleo? Kuna wanawake mahiri kweliwameshindwa kutumika? Kuna wazee, watu wenye uzoefu,wataalam wazuri, kweli tunashindwa kuwatumia na nchiyetu ikapata maendeleo? Tuangalie tulichonacho mkononi.

Mheshimiwa Spika, nchi hii ina ardhi, nchi hii ina madinimbona hatuoni mchango wa madini katika Pato la Taifa.Lazima tutumie tulichonacho, madini yako wapi jamani; nilazima tutumie madini yetu.

Mheshimiwa Spika, katika nchi nyingi sana bajeti zaoinaongoza kwa vile walivyonavyo. Nchi ya Botswanatunaambiwa madini waliyonayo yanasaidia kuongoza ilenchi; kwa nini isiwe Tanzania? Tunaambiwa Botswana wanaidadi ndogo tu ya ng’ombe, lakini inasaidia kukuza uchumiwa nchi ile, kwa nini isiwe Tanzania ina ng’ombe kila mahali?

Mheshimiwa Spika, mimi naona ajabu, tuna bahari,tuna mito, tuna maziwa, tuna gesi, jamani hivyo vituMwenyezi Mungu ameleta kwa aji l i ya Watanzania.Tukiendelea na mchezo wa kuingia mikataba isiyokuwa natija kwa Watanzania, Mwenyezi Mungu atatuangalia kwajicho baya na mimi ninaogopa.

Mheshimiwa Spika, ninaomba nizungumzie kuwa,kuna Wawekezaji Wakubwa, kuna Private Sector ambayoinatakiwa ikue katika nchi yetu, lakini je, tunawawezeshavipi? Wafanyabiashara wetu hatuwapi motisha, hatuwapimitaji, hatuwapi elimu; kwa nini? Private Sector isipokuanchi haikui. Kwa hivyo, ni lazima tuikuze Private Sector yetu.

Mheshimiwa Spika, ninaomba nizungumzie piamakampuni yanayofanya vizuri nchi hii. Ninashangaa Kitabucha Bajeti cha Waziri wa Fedha, anakazana kuwasifuwafadhili tu, ina maana nchi hii hakuna watu wanaofanyavizuri, hamna makampuni yanayolipa kodi vizuri, mbonahamyaleti hapa tukayasifu, kwa nini tuna mambo yakuangalia watu wa nje tu? Hii ni aibu kwa nchi yetu. Lazima

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

86

19 JUNI, 2013

tuseme katika nchi yetu makampuni haya yanafanya vizuri,yanalipa kodi vizuri na ni lazima tuyatambue kwa sababundiyo yatakayojenga uchumi endelevu.

Mheshimiwa Spika, naomba nizungumzie suala zimala Big Results Now. Nina ombi moja tu kwa Serikali, kamawanataka Big Results Now iende vizuri, wenzetu waMalyasia walianza kusomesha makundi ya watoto, walitoavijana wakawapeleka kusoma nchi mbalimbali na kwawingi, siyo hapa tunaambiwa sijui scholarship nane, mbili,mia, mia tano, elfu, ndiyo vijana wakirudi wakielewa yalemambo wataweza kujenga uchumi endelevu.

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Ruvuma, Barabara yaNamtumbo - Tunduru ishughulikiwe kwa mpango wadharura. Ile barabara ina hatari, watu wanapata tabu,tangu Uhuru mpaka sasa ile barabara ni ya hatari na nibarabara inayoshangaza. Siku moja nilikuwa naongea naMtaalam mmoja wa Wizara, akaniuliza hivi ni kweli ilebarabara haina lami mpaka leo! Nikamwambia ni kweli;akasema hapo Serikali haijawatendea haki. Big Results Nowkuna mtaalam anaitwa Dkt. Gwajima, yupo Wizara ya Afya,yule mama ana uwezo mkubwa na ni Daktari wa WilayaMkoa wa Singida, mchukueni yule anaweza kuleta BigResults Now, mpelekeni kule yule mama anaweza akafanyamambo makubwa na mapinduzi. Ameshafanya kwenyeWizara ya Afya, mchukueni kwenye Big Results Now na Idaraya Mipango ili aweze kusaidia.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Ahsante.(Makofi)

SPIKA: Yaani aende akajenge barabara? Miminilifikiri akasimamie afya siyo akajenge barabara, itakuwatatizo. (Kicheko)

Mheshimiwa Salum Khalfan, Mheshimiwa Dkt.Christina Ishengoma, Mheshimiwa Maria Ibeshi Hewa naMheshimiwa Dkt. Kigwangalla.

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

87

19 JUNI, 2013

MHE. SALUM K. BARWANY: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa fursa niweze kuchangia Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, nianze na ushauri mdogo tu kwaViongozi, Wabunge pamoja na Watanzania kwa ujumla.Uchumi imara kote Duniani hauwezi kupatikana kama nchihiyo au Wananchi wake hawatakuwa na amani, utulivu,ambao utawafanya pamoja kuzingatia ni namna gani nchiyao inaweza kuipeleka katika ustawi wa uchumi wao.

Mheshimiwa Spika, na kama nchi hizo hazitakuwana utawala wa sheria ili Wananchi wapate haki zao stahikina kama nchi hizo hazitakuwa na Utawala Bora kwa maanakwamba, Serikali itashughulikia kutoa huduma za jamii kamavile afya, elimu na mambo mengine, bado nchi hiyo itakuwandoto kwenda katika ustawi. Vilevile kama nchi haitakuwana demokrasia ya kweli, Wananchi wakapata Viongoziambao wanawaona wanafaa, hakutakuwa naujanjaujanja katika kuwapata Viongozi ambao wanawezakushika mamlaka ya dola, migogoro siku zote itakuwainaendelea katika nchi hizo na amani itakuwa haipo, mwishowake nchi hiyo bado itakuwa haiwezi kupata maendeleoya kutosha.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala zima la bajeti,ni kwa namna gani tunasema tumekuja katika Bunge hilikuja kupitisha Bajeti ya Serikali. Bajeti ipo kwa mujibu washeria, tupo hapa kupitisha bajeti kwa mujibu wa sheria,hatukuja hapa kama kitengo cha kisiasa, hapana. Tunawataalam wetu ambao tayari wanatushauri juu ya sualazima la kupitisha bajeti na sisi kama Wabunge, tuna wajibuwa kuhakikisha kwamba, tunaisimamia Serikali kutekelezawajibu wake katika kuifanya bajeti yetu ifikie malengo yake.

Mheshimiwa Spika, lakini hapa jambo la kusikitishani kwamba, tunapitisha bajeti leo, baada ya mwakammoja, mwaka wa Serikali unapoanza, Bajeti ya Serikaliinashindwa kufikia malengo yake. Tunapewa sababumbalimbali hapa; wahisani wameshindwa kutoa pesa kwawakati, makusanyo ya Serikali yamekuwa madogo, lakini

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

88

19 JUNI, 2013

uhalali wa kisheria wa kuwepo bajeti hii ukoje? Serikaliinapaswa kuwajibika kwa Wabunge kama tunavyowajibikakatika kuwasimamia. Pale tunapofikia mahali kwambabajeti imeshindwa kufikia malengo, sisi kama Wabunge tunawajibu gani kwa Serikali hiyo?

Mheshimiwa Spika, tunaambiwa hapa kwamba,bajeti ya 2012/2013 katika Wizara mbalimbali haikufikiamalengo yake. Tunaambiwa kuna asilimia 35, asilimia 40,Wizara zilikosa pesa, Halmashauri zetu hazikufikia malengoya bajeti, hili ni tatizo.

Mheshimiwa Spika, hata kama hapa tutaambiwatuna tri l ioni 23 katika bajeti hii, mwisho wa mwakatutaambiwa kwamba, pesa ambazo zimekwenda katikaWizara na Halmashauri mbalimbali ni asilimia 40 au 50 tu.Hatuwezi kufikia maendeleo yetu kama tunavyotarajia.

Mheshimiwa Spika, pia kuna jambo ambalo lipomuda mrefu bado halijafanyiwa kazi la kuhamisha mafunguya fedha kutoka Wizara moja kwenda katika Wizaranyingine bila idhini ya Bunge. Nimesema hapa kwamba, hiibajeti ipo kwa mujibu wa sheria, Bunge ndiyo limeidhinishakwamba kiasi hiki cha pesa kinakwenda katika eneo fulani,lakini kuna uzoefu uliopo sasa kwamba, tunawezatukahamisha mafungu ya pesa bila Bunge hili kuwa nataarifa. Inaonekana kama hili Bunge ni rubber stamp tu;kwamba, tunakuja ili ionekane bajeti hii imepitishwa naBunge, lakini mwisho wa siku Bunge hili bado halipati taarifajuu ya mabadiliko ya kibajeti ambayo yanafanywa naSerikali. Hili linaweza likatuletea tatizo.

Mheshimiwa Spika, tumeambiwa hapa tumeongezaeneo fulani fedha, tunakuwa tuna namba kubwa lakinimatokeo yake fedha hizi hazifiki katika miradi mbalimbaliambayo tunaitarajia.

Mheshimiwa Spika, sisi tunakuwa mabingwa wamikakati, ambayo imeshindwa. Tuna mikakati hapa zaidiya mitano, sita, tangu tunapata Uhuru, lakini mikakati hiyo

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

89

19 JUNI, 2013

yote siyo endelevu. Siyo mikakati ambayo tayari inatupamatumaini, Watanzania wamechoka na mipango hii.

Mheshimiwa Spika, leo tunasema mipango yote ipokwa mujibu wa Sera, lakini imebadilika, leo tuna mipangoipo kwa mujibu wa awamu siyo Sera za Chama, Sera zaNchi, Sera za Kitaifa. Mipango yote inakwenda kwa mujibuwa awamu zinazokaa madarakani.

Awamu ya Mkapa tulikuwa na Mtwara Corridor,hakuna maelezo ya Serikali juu ya Mtwara Corridor yakowapi leo, Mtwara Corridor imekwenda wapi? Utaratibuwake uliridhiwa na Bunge alipoondoka Mkapa katikamamlaka na Mawaziri wake, habari ya Mtwara Corridorhaipo, leo tunakuja na mpango mwingine huu ambao tayaritunao. Mimi naamini kabisa mpango huu baada ya Awamuhii ya Nne kuondoka atakayekuja na Serikali mpya atakujana mpango wake. Hatuna Mpango Maalum wa Kisera waKitaifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivyo, hatuwezi kufikia Malengoya Maendeleo kama bado hatujawa makini, ni lazima tuwena Sera za Kitaifa, ambazo awamu yoyote ambayo itakujamadarakani itakuja kuendeleza pale awamu nyingineilipoachia. Tuna uzoefu kwamba, kila awamu inayokujatayari inakuja na mpango mpya ambao bado hauwezikutuletea maendeleo. Tunasema tuna mipango isiyoendelevu na sisi ni mabingwa wa mikakati iliyoshindwa.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie kidogo eneo la watuwenye ulemavu. Bado Serikali inatoa ruzuku kwa makundimbalimbali ya watu wenye ulemavu katika Taifa letu, lakinibado ruzuku hiyo haitoshi, ni ruzuku ndogo kabisa, haiwezikuendesha vyama vya watu wenye ulemavu. Ceilingambayo inatolewa ni ile ile zaidi ya miaka kumi, mahitaji leoyameongezeka, walemavu wameongezeka, wapo wengikatika Taifa hili. Tunaitaka Serikali ihakikishe inaongeza ruzukukatika maeneo ya makundi ya watu wenye ulemavu ilituweze kufikia malengo yetu.

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

90

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, suala la formula ya mgawanyowa rasilimali katika Taifa letu bado ni utata na ndiyomanung’uniko mengi yapo ndani ya Taifa hili. Watu katikamaeneo wanalalamika, wanapiga kelele, huku maendeleohayapo, huku wamependelewa, kwa sababu hakunaformula maalum ambayo tayari inaelekeza kwambamgawo wa rasilimali katika Taifa letu ukoje.

Mheshimiwa Spika, katika Jimbo langu la Lindi Mjini,nimezungumza mara kadhaa na Waziri wa Fedha, ni namnagani sasa Manispaa ya Lindi imetoka katika Halmashauriya Mji. Tulikuwa tunapata ceiling ya milioni nane kablahatujawa na Halmashauri, tumeongezewa Kata tanokutoka Halmashauri ya Wilaya katika Majimbo ya Mchingana Mtama, lakini bado tunaendelea kupata ceiling ile ileya Halmashauri ya Mji, baada ya kuwa ndani ya Manispaaya Mji wa Lindi, tumeongezewa Kata tano zingine, badoSerikali imekuwa kiziwi, imekuwa kipofu juu ya hoja zaWananchi wa Lindi kwamba tayari Halmashauri ile imekujakisiasa tu, haikuwa na maana kwamba imeletwa Manispaakwa ajili ya maendeleo ya watu wake.

Mheshimiwa Spika, tunaitaka Serikali ihakikishemgawo wa bajeti uende sambamba. Mliahidi hapa katikaIlani ya Uchaguzi ya CCM kwamba, mtahakikisha mnatoakipaumbele katika maeneo ambayo bado yapo nyumakimaendeleo. Mlichukua kura nyingi kwa hoja hiyo, lakiniyote yale leo mmesahau kwamba mliahidi nini na ndiyo hayamatatizo ambayo leo yanajitokeza katika Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, bado kuna migogoro mingi, watuwamefikia mahali hawaiamini Serikali kwa kauli zake. Hivyo,hayo ndiyo mambo ya kuzingatia katika kuona kwamba ninamna gani tunaweza tukajenga uchumi imara ambaoWananchi watashirikishwa kikamilifu.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie pia suala la thamaniya bidhaa za kilimo. Bado inaonekana kabisa kwamba,kilimo hakioneshi kwamba kinaweza kikatoa mchangomkubwa wa maendeleo katika Taifa letu. Tunaendelea

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

91

19 JUNI, 2013

kuuza mazao yetu ya kilimo ghafi katika masoko ya nje,badala ya mazao hayo kuyafanyia process. Tuna viwandavya korosho kadhaa katika Mikoa ya Kusini ya Mtwara naLindi, lakini bado viwanda vile vimesimama tunaendeleakuuza korosho ghafi katika masoko ya nje. Tunanyima watuajira, hivyo ni wakati mwafaka tulitegemea kauli ije naufumbuzi wa tatizo ni namna gani sasa korosho, pamba,kahawa na vitu vingine ambavyo vinatokana na kilimovinafanyiwa process ili viwe na thamani katika kuboreshauchumi ndani ya Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa kwamba, kamahatujawa makini, hatujazingatia maendeleo ambayoyamepatikana katika nchi mbalimbali huko yameanziawapi. Walikaa hapo, wakakaa pamoja, wakaona tatizoletu la msingi ni nini. Tatizo ni elimu, ni afya, ni kilimo ni namnagani tunakwenda katika kutafuta ufumbuzi wa matatizoya nchi. Tunakurupuka tu leo katika kujenga uchumi wetu,hatuna uhakika tunakwenda katika jambo gani natunajiandaa kwa lipi.

Mheshimiwa Spika, tuna uhaba wa chakula katikanchi; nchi ina ardhi nzuri, ina mito, ina mabonde na ina watuwenye uwezo wa kufanya kazi, lakini unashangaaWatanzania leo wanalia na njaa na wanasema Taifa laolina njaa. Kuna nini hapa? Hatujawa na mpango madhubuti,hatujawa na mpango imara, hatujawa na mpangoendelevu, ambao unaweza kuwaondoa Watanzaniakatika umaskini uliokithiri.

Mheshimiwa Spika, tunalazimika sasa tuwe namjadala wa kitaifa katika nchi hii, hatuwezi kuwaachia watuwachache wafanye mipango ambayo imeshindwa kuletamaendeleo. Zaidi ya miaka hamsini leo, tumeachia kundimoja ambalo limeshindwa kuleta maendeleo katika Taifaletu. Wakati umefika sasa kama Taifa tukae pamoja,tutumie wataalam wetu, tuone tunatokaje katika umaskiniuliokithiri.

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

92

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, Watanzania wamechoka,Watanzania wana maisha magumu, Watanzania wanahitajimaendeleo. Nchi jirani zinazotuzunguka zimepiga hatuakubwa ya maendeleo sasa, sisi tunabaki nyuma kwa lipi?

Mheshimiwa Spika, Msumbiji tu hapa wamepigahatua kubwa, tumewasaidia kudai uhuru, wale wana miakathelathini tu tangu Uhuru wao lakini leo wanaishi vizuri katikaustawi wa Taifa lao.

Mheshimiwa Spika, kwa kusema hilo, nataka tukaetuone ni namna gani... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana. Sasa nimwite MheshimiwaChristina Ishengoma, Mheshimiwa Maria Ibeshi Hewa,Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla, Mheshimiwa Mangungu,huenda na Mheshimiwa Masoud Abdallah anawezaakafikiwa.

MHE. DKT. CHRISTINA G. ISHENGOMA: MheshimiwaSpika, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii ya kuongeakatika Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa pongezi kwakokwa kazi nzuri unayoifanya humu Bungeni kwa kuendeshavikao vizuri. Napenda pia kuwapa pongezi Mawaziriwanaohusika na bajeti hii na watu wote ambaowamehusika kuchambua na kutekeleza bajeti hii kuanziahuko kwenye Kata mpaka hapa tulipofikia Bungeni.

Mheshimiwa Spika, napenda kuongelea kuhusukupandisha ushuru wa petrol pamoja na diesel na mafutaya taa. Naomba sana iangaliwe kwa undani, ingawatumepunguza ushuru kwa vitu vingine na kodi, lakini hiiitaweza kuathiri mambo mengi hasa tukipandisha mafutaya petrol na diesel; itapandisha bei ya usafiri, itapandisha

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

93

19 JUNI, 2013

bei ya bidhaa mbalimbali, itapandisha bei ya vyakula. Kwahiyo, naomba sana hili jambo liangaliwe kwa undani.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mafuta ya taa,tunajua kuwa Wananchi wengi na hasa wa vij i j ini,wanatumia sana mafuta ya taa. Ningeomba sana naloliangaliwe vizuri, tusiathiri na kuleta mgongano kwaWananchi wetu ambao tunawapenda sana.

Mheshimiwa Spika, jambo ambalo ninaombakuliongelea tena ni kuongeza ushuru wa bidhaa hasazinazotokana na juisi. Tunajua kuwa, Tanzania sasa hivi tunamatatizo ya utapiamlo na upande wa vitamini ni matatizo.Akina mama hasa wajawazito, wanapata matatizo yaanaemia, upungufu wa damu kwa watoto. Kwa hiyo,ninaomba kwa sababu haya matunda yanazalishwa nchinikwetu, yasiongezwe ushuru wowote, ushuru wote utolewe.Juisi ni nzuri na hasa kwa manufaa ya akina mamawajawazito na watoto wadogo. Ninaomba ushuru utolewekabisa, ifanane na maji ambayo tumesema yanayozalishwakatika viwanda hayatakuwa na ushuru wowote. Naombahilo liangaliwe.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa uchambuziwa bajeti hii. Tangu tumeanza mpaka tulipo, imewezakushirikisha watu wengi, imeweza kushirikisha Wabunge vizurisana, tumeweza kuichambua na tumeweza hata kuongezafedha kwa Wizara zingine kama Maji, Kilimo na Maendeleoya Akina Mama na vitu vingine vyote ambavyotumesikilizwa na Kamati ya Bajeti na Wizara. Naishukuru sanana ninaipongeza sana Kamati ya Bajeti, kwa kazi nzuriiliyoifanya kwa kuweza kuongezea fedha kwa Wizarambalimbali ambazo tumeomba fedha na kukubalikuongezwa.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo naombakuliongelea ni kuhusu fedha, ni kweli tumeongea kwenyebajeti na fedha zimetengwa. Fedha zinazoenda kwenyeHalmashauri na kwenye mikoa ingawa siyo nyingi sana, lakini

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

94

19 JUNI, 2013

naomba sana ziende kwa wakati ziweze kufanya kazi hukovijijini.

Mheshimiwa Spika, Wananchi wengi zaidi ya asilimia70 wanaishi vijijini na wanapenda kuona maendeleo hukovijijini. Naomba hizo fedha zipelekwe kwa wakati, ziwezekufanya kazi ilivyo na zote kama zilivyotengwa zipelekwehivyo hivyo bila ya kupunguza au nini. Naamini Serikali yetusikivu inaweza, Serikali ya Chama cha Mapinduzi inaweza.Nitashukuru kama fedha zote zitapelekwa kama zilivyo.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ninaloombakuliongelea ni vipaumbele. Vipaumbele vya Taifa ni vizurisana. Naishukuru Serikali kwa kuweka hivi vipaumbele.Vipaumbele hivi vikitiliwa maanani, naamini Watanzaniawote wataweza kuona manufaa ya nchi yao na jinsiinavyowapenda. Nikianza na ukusanyaji wa mapato; kamakweli tutasimamia ukusanyaji wa mapato, pato letulitaweza kuongezeka na Wananchi wataweza kufaidiuchumi wao. Jambo muhimu ninaloliomba ni kuwa,tumeanza kukusanya mapato kwa kutumia electronic hasareceipt.

Mheshimiwa Spika, Wananchi wengi hawana elimuya kudai risiti mara wanaponunua bidhaa. Hii inarudishanyuma pato letu. Kwa hiyo, naomba elimu itolewe kupitiakwenye vyombo vya habari, kupitia kwenye vyombo vyovyote vinavyohusika na kupitia mahali popote pale, kusudiWananchi waweze kudai risiti mara wanaponunua bidhaazao kama nchi zingine zilizoendelea.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru ulinipelekaCanada, nil i j ionea mimi mwenyewe hata chakulaunachokula unatoa kodi inahesabiwa kwa pato. Kwa hiyo,wao wapo makini sana kutoa risiti zao. Naomba sanaWananchi wadai hizo risiti.

Mheshimiwa Spika, kwa kipaumbele cha kilimo,kama nilivyosema kuwa asilimia 70 ya Wananchi wanakaahuko vijijini na wanategemea kilimo. Jambo ninaloomba,

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

95

19 JUNI, 2013

fedha zilizotengwa kwa pembejeo zipelekwe kwa wakatikusudi kwa kutumia Wagani, Wananchi waweze kufaidikilimo chao. Kitu kingine ninachoomba, kufuatana namipango mbalimbali ya KILIMO KWANZA, SAGCOT, SmartPartnership, Big Results Now, zikisimamiwa vizuri, naaminiWananchi wetu wataweza kuona matunda ya kilimo nawataweza kufaidi matunda hayo pamoja na pato lao lakaya na nchi yetu litaweza kupanda.

Mheshimiwa Spika, kwa jambo hili la kilimo, naombasana tuwatumie Wataalam wetu wa SUA pamoja nawataalam wengine na watafiti wengine, kusudi tuwezekuleta mabadiliko kwa mara moja.

Mheshimiwa Spika, kitu kingine ni elimu hasa rasilimaliwatu kwa upande wa sayansi. Nyote ni mashahidi kuwa,wanafunzi wa siku hizi hawapendi sana kusoma masomoya sayansi. Nashauri kuwa, mpango au utaratibu wawataalam au walimu kupita mashuleni kushawishi wanafunzikuanzia hasa Form Two kuanza kuchukua masomo yasayansi, naomba uangaliwe. Kwa sababu wakishawishika,wataweza kuchukua hayo mafunzo ya sayansi na tutawezakupata rasilimali watu hasa kwa upande wa sayansi.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa nishati hasanishati ya viji j ini, nashukuru sana, hivi ninavyoongeaWananchi wengi na Wabunge wengi wamefurahi, helazimetengwa na zimeongezwa, kwa hiyo, Wananchi wengikwenye majimbo yetu wataweza kupata umeme. Hatakwangu kule Morogoro, naamini wataweza kupata umemena hivi ninavyoongea hata huko Ismani kwa siku hizi tatuwatapata umeme. Kwa hiyo, tunaishukuru Serikali kwakuliona suala hili la umeme. Pia kutokana na umeme,Wananchi wengi hasa wanawake wataweza nao kufaidikwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya usindikaji nanamna hii, tutaweza kukuza pato la Mwananchi na pia lanchi yetu.

Kwa upande wa miundombinu, barabara tunazionazinazidi kupendeza. Kwa upande wa reli, kwa upande wa

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

96

19 JUNI, 2013

viwanja vya ndege, hayo yote ni mambo mazuri ya Serikaliya Awamu ya Nne chini ya Mheshimiwa Dkt. Jakaya MrishoKikwete. Tunawashukuru Viongozi wetu wa Awamu ya Nne.

Kuhusu maji; maji safi na salama; ni muhimu sanakwa Wananchi. Sote tunajua kuwa Wananchi huko vijijiniwana matatizo sana ya maji, lakini kama hivi tumeombafedha tumeongezewa; tunashukuru sana kuona Wananchiwengi watapata maji na watazidi kupata maji safi nasalama. Akina mama waliokuwa wanapoteza muda waosaa 24 kutafuta maji, wataweza kufanya miradi mingine yamaendeleo.

Mheshimiwa Spika, naomba kuongelea kuhusumambo ya uchambuzi wa bajeti, nimeshaongea kuwanashukuru sana mpango ulikuwa mzuri. Tunakushukuru sanaMheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuchangia hayo machachena ninaamini hata vijana wataweza kujiajiri kwa sababuumeme utakuwa vijijini, maji yatakuwa vijijini na wataalamwengine wote watakuwa vijijini. Kwa hiyo, wataweza kujiajirihuko vijijini hawatapata muda wa kuja mjini kuranda randahovyo hovyo.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi hii.Ahsante sana na naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Sasa nimwite MheshimiwaMaria Ibeshi Hewa, atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt.Kigwangalla na Mheshimiwa Mangungu.

MHE. MARIA I. HEWA: Nakushukuru MheshimiwaSpika, kwa kunipa nafasi hii na mimi nitoe mchango wangukatika suala zima la bajeti ya kipindi hiki, bajeti ambayotumeianza na mabadiliko tofauti na tulivyokuwa tukizijadilibajeti za miaka iliyopita. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru pia kwa jinsiulivyokuwa jasiri, kwa kuunda Kamati ya Bajeti ambayoinaongozwa na Kiongozi mahiri kabisa, Mheshimiwa MtemiChenge, ambaye huwa anaongea kwa uhakika kwa kile

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

97

19 JUNI, 2013

kinachotoka kinywani mwake akiwa anasaidiwa na Kamatiyake hiyo ya Bajeti. Nakupongeza kabisa. (Makofi)

Pamoja na hayo, mfumo wetu huu tuliouanzisha kwasasa wa kuanza bajeti mwezi wa nne na kumaliza mweziwa sita, ninaamini tunaweza tukatoka mahala tulipo, kwasababu Wizara tunapozijadili mwanzo kwa kuwa na ceilingfulani baadaye mwishoni kunakuja kujitokeza fedha ambayoinakuwa ni kama vile albaki, ilikuwa ni 16 lakini tumekwendampaka 18. Hilo peke yake sasa inatupa mwanga wa kujuawapi vipaumbele vyetu ambavyo tumesuguana humukabla na kuvipa pesa, ambayo nadhani inauweka unafuuwa Wananchi wetu kujua Wabunge wamejadili nini kinagusakero zao katika utaratibu huu mpya tuliouanzisha.Ninaomba udumu kwa kweli, nadhani unatupeleka mahalapazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kabla sijazungumza menginiliyonayo, naomba nianze na ushuru ndani ya mafuta. Miminaweza nikasema okay mmeona kuna utaalam ndani wakuongeza ushuru kwenye mafuta ya petrol, dizeli na nini.Ombi langu futeni kuongeza ushuru kwenye mafuta ya taa.Naomba kabisa kwa sababu haya mafuta ndiyowanayotumia akina mama, bado vijijini wanapoendakujifungua, wanunua wenyewe. Kwa nini tufiche! (Makofi)

Sasa yanapopanda, yaani tunajiweka mahalipabaya. Msidhani kwamba huu umeme tunaouzungumzaumeme vijijini utakwenda kwa mwaka huu au mwaka keshondiyo tunamaliza shida za kuweka umeme kwenye vijijivyetu. Hapana, naomba hilo ni ombi rasmi nalileta kwakoMheshimiwa Waziri ufute ili akina mama waendelee kununuamafuta hayo kwa matatizo mbalimbali huko vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna kitu ambacho huwakinanichanganya kuhusu uzalishaji wa mali zetu viwandani.Viwanda vya nchini mwetu. Tunalalamika hatuna viwandavya kutosha. Tunazalisha mali kutokana na viwanda vyetu,lakini tunaagiza vitu kutoka nje kwa maana ya kufidiauzalishaji wetu tulionao pungufu. Nchi zetu jirani zina

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

98

19 JUNI, 2013

viwanda vya kutuzidi sisi, lakini wenzetu wanazalisha nabado wanaagiza vitu vingi kutoka huko nje na wanakujakuuza kwa bei ya chini. Sisi ambao tunaagiza pamoja naotunashindwa kuvinunua, badala yake tunakwendakununua kwa nchi jirani na kuuza tena kwa bei nafuu.

Sasa mimi huwa najiuliza ni nini; kama si sisi tunaushuru wa hali juu tusiotaka kujifunza hata kwa majirani zetuwanatoza ushuru wa namna gani ili twende sambambanao, Watanzania wasishawishike kwenda kununua vifaakwa nchi jirani. Tufanye utafiti wa kuona tutoze ushurunamna gani wa vifaa hivi na majirani zetu vifaa vyao vipochini kiasi cha kwamba, tunakimbilia kununua huko hatasimu. Simu za mikononi hivi wafanyabiashara wetu wadogowadogo wanakwenda kununua Kenya. Wanapeleka fedhazetu Kenya wanakuja kutuuzia humu tena kwa bei ya chinikidogo ukilinganisha na za kwetu humu. Simu inayonunuliwakwa shilingi 70,000 tunauza kwa laki na nusu. Hapo huwakuna nini? Hatutaki kujifunza kuona tunaishije na ushuruwa vifaa vyetu hivi ambavyo tunaagiza kutoka nje na walewenzetu wanatusababisha tunavinunua tunavileta.Tucheki ushuru wetu ukoje? Tupate majibu jamani. (Makofi)

Lingine ambalo ninapenda kuliongelea ni suala hilila bodaboda. Jamani watu wa bodaboda tusiwakatishetamaa. Tusiwakatishe kabisa tamaa kwamba bodabodani za matajiri. Sijui tufanye nini? Mtulie hivyo hivyo kabisa,msije mkaongeza, wale wanaosema ni za matajir iinawezekana wapo kweli matajiri ndiyo wanawapa hawawatoto hizo bodaboda. Isije ikawa kigezo sasa cha kusemazile ni za matajiri. Wamo pia wenye bodaboda zao ambaowanaishi nazo wamo kabisa.

Tatizo labda ni ule uchambuzi tu wangapi ambaowana bodaboda za matajiri. Wengine ambao nibodaboda za kwao, lakini msimamo ubaki pale pale.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni suala la ugawanyaji warasilimali hapa nchini. Rasilimali za maendeleo, rasilimali watu

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

99

19 JUNI, 2013

na ujuzi. Jamani Kanda ya Ziwa tuna Mikoa yapata sita,lakini hatuna Chuo Kikuu cha Umma. Miaka 50 ya Uhuru,tunazidiwa na Morogoro wana vyuo viwili vya Serikali, sisihata kimoja ndani ya Kanda. Tunalia walau tupate hatakiwanda cha cement nacho hakuna kimeanzishwakwingine. Barabara sisi mpaka tumekuwa wa mwishokuwekewa lami; jamani hivi tuna makosa gani Kanda yaZiwa? Kila kitu sisi wa mwisho. Tunayo ardhi ya kutoshakupata na sisi Chuo Kikuu cha Serikali. WasingekuwaWakatoliki hawa tungekuwa wageni wa nani? Ndiyowaliotujengea huko na bado wameendelea kufika hukoMtwara, wako Tabora, sijui wako wapi. Hawa ni private.(Makofi)

Sisi cha Serikali kiko wapi Kanda ya Ziwa? Haajamani, mnataka nishangae Kisukuma! Jamani tunaombaKanda ya Ziwa na sisi mtufikirie na walipa kodi wako huko.Kodi zetu zinakwenda wapi? Mnatuona sisi hatutakimaendeleo. Tunaomba, mmezungumzia hili, kipindi kijachotunaomba bajeti ijayo mtukumbuke katika hili. Ardhitunayo, Butiama kule, mimi sizungumzii wapi kijengwe, lakinitunataka Kanda ya Ziwa na sisi ni walipa kodi kule. (Makofi)

Mwisho, nasema Mheshimiwa Waziri, wewe ndiyeWaziri wa Fedha, sasa nakukumbusha tena na nilikwambiawakati fulani kuleta taarifa ya uendelezaji wa miradi. Fedhazetu zinapotoka zinafanya kazi gani quarterly au kwa mudawa miezi sita. Nadhani tukupe miezi sita, labda tutakwendavizuri ili tuwe tunajua fedha zinakotoka miradi imetekelezwakwa kipindi hicho. Hiyo ndiyo pekee tena Watanzaniatutaishi nao l ive kujua tumetaja hapa kitu halafukimetekelezwa. Hiyo ndiyo pekee tutaendana na nchi hiikujua hapa tumetamka fedha itoke, je, imetoka na kamaimetoka imekwenda wapi. Tuwe l ive na Wananchi.Tunataja miradi iliyoko huko katika maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Sasa nimwite msemajimwingine; Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla!

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

100

19 JUNI, 2013

MHE. DKT. HAMIS A. KIGWANGALLA: MheshimiwaSpika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Awali yayote, nitumie fursa hii, kumpongeza sana na kumkaribishaBungeni kaka yangu mpendwa, Dkt. Dalay Peter Kafumu,Mbunge wa Igunga, ambaye alichaguliwa kwa kura halalina Wananchi wa Igunga. Jimbo ambalo aliniachia kulileatoka aliponyang’anywa Ubunge wake na Mahakama.(Makofi)

Nitumie fursa hii kumpongeza sana na kumkaribishaBungeni, rafiki yangu Mheshimiwa Aeshi Hilary, Mbunge waSumbawanga Mjini, naye tena kwa kurejeshewa Ubungewake na Mahakama. Naamini Watanzania watakubalianana mimi kwamba, Mahakama sasa inatenda haki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya salamu hizo za awali,sasa naomba nijielekeze kwenye kuchangia hoja hii ya BajetiKuu ya Serikali iliyoko mbele yetu. Ninaomba niwekekumbukumbu sahihi kwamba, sitaunga mkono hoja hii kwasababu ambazo nitazisema. Kubwa zaidi, ikiwa ni kwamba,bajeti hii haitoi majawabu ya muda mrefu ya changamotoambazo zinalikabili Taifa letu. Changamoto hizi ni pamojana ajira kwa vijana, njaa na uhakika wa chakula, uharibifuwa mazingira, maradhi, lakini pia changamoto kubwa yamfumko wa bei kwenye bidhaa mbalimbali.

Pamoja na kutokujibu changamoto hizi ambazozinalikabili Taifa kwa sasa, Bajeti hii ni wazi kabisa iko pro-inflationary, kwa sababu inaongeza kiwango cha kodikwenye baadhi ya bidhaa ambazo kwa kiasi kikubwazinawagusa watu wa chini. Nitatoa mfano kwenye kodi yahuduma ya simu ambayo ni mawasiliano muhimu sanakatika uzalishaji, pia katika maisha ya kila siku ya Wananchi.Vilevile kodi kwenye mafuta kwa maana fuel in general,ambapo katika hali ya kawaida ukiongeza tu kodi kwenyemafuta, maana yake unaongeza gharama za usafiri nagharama za uzalishaji kwenye viwanda na hivyo bei zabidhaa mbalimbali kwenye soko zitapanda. Ninaombanitoe ushauri, wenzetu wa Wizara ya Fedha wajifikirie kwa

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

101

19 JUNI, 2013

mara nyingine tena, waweze kufanya marekebisho ambayoyataondoa taswira ya inflation kwenye bajeti hii.

Mheshimiwa Spika, nilisema sitaunga mkono hoja hiimpaka itakapotoa majawabu ya changamotozinazolikabili Taifa, ikiwa ni pamoja na ukweli kwamba, bajetihii haioni mbali sana, iko myopic in nature. Inaangalia kwakaribu tu, kwa mwaka mmoja tu, haingalii mbali zaidi kwakuwa haijielekezi kuwekeza kwenye sekta ambazozinawagusa watu wengi. Pia kwa kuwa haijielekezikuwekeza kwenye sekta ambazo zitakuza ajira ya watuwengi zaidi; na pia kwa haijielekezi kwenye sekta ambayoitapunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi na kujakwetu, ili kuweza ku-stabilise balance of payment accountsna hatimaye kupunguza mfumko wa bei na mwisho wa sikukukuza uchumi. Bajeti hii haielekezi ni namna gani tutakuzauzalishaji katika nchi yetu katika muda mfupi na katika mudamrefu na badala yake ni bajeti ya utekelezaji wa majukumuya Serikali kwa muda wa mwaka mmoja tu, mwisho.

Mheshimiwa Spika, nasema hivyo kwa sababutungetarajia bajeti ya karne hii iwekeze zaidi kwa watu;kwanza, kwa kupunguza zaidi kodi. Kwa wale Wataalamwa Uchumi wanafahamu zile reganomics, taxnomics nahata kigwanomics, ambazo zimekuwa named baada yajina langu, ambapo bajeti za aina hiyo zinalenga zaidikwenye kuwekeza kwa watu zaidi kuliko kwenye kuuachauchumi wa soko huria ujiendeshe kama unavyoenda, kwakufuata force za demand na supply, bila kuangalia ninamna gani tutawekeza kwenye sekta ambazo zitadurufuuchumi wetu kwa haraka zaidi, ili kupunguza umaskini nakuongeza ajira kwa Wananchi. Kwa mfano, kuwekezakwenye viwanda, kupunguza regulation kwenye sektambalimbali hususan kwenye private sector.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, kuongeza tax base,kupunguza tax kwa ujumla na kupunguza kodi kwa ujumlawake, lakini kuongeza wigo wa kodi kama ilivyofanyamwaka huu kwa kiasi fulani kidogo, lakini pia kuhakikishakuna tax equity, usawa kwenye kodi. Kwa mfano, leo hii

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

102

19 JUNI, 2013

mtu wa chini mwenye kioski, anatozwa kodi kubwa sanaukilinganisha na mtu ambaye amewekeza kwenye sektaya madini ama ya gesi au ya mafuta; jambo ambalohalikubaliki kwa kuwa haliweki usawa. Ndio maana nasemabajeti ya karne hii katika zama ambapo uchumi wetu niwa mchanganyiko, ambapo kuna ubepari umeingia kwenyeujamaa, ni lazima tutafute na tuweke misingi ya kuwekausawa kwenye kodi yetu, lakini pia usawa kwenyemgawanyo wa mapato yanayotokana na kodiwanayotozwa Wananchi.

Mheshimiwa Spika, bajeti hii haitoi Long Term Visionya kukua kwa uchumi wetu na ndiyo maana nimesemasiiungi mkono. Ninaomba pia niseme kwamba, leo hii tunafursa nyingi za kuweza kukuza uchumi wetu, ikiwa ni pamojana kuwekeza kwenye maeneo maalum ya kukuza ajira kwavijana, hususan wale ambao wanajiajiri kwenye sekta zakilimo na mifugo, ili waweze kuzalisha ajira nyingi zaidi napia waweze kupunguza importation ya goods. Leo hii nguozilizojaa kule kwenye maduka ya Kanda ya Ziwa zinatokeaKampala, madawa ya pembejeo hizi za kilimo yanatokeaNairobi; wakati huo sisi wenyewe tuna fursa ya kuweza ku-attract hivi viwanda vikaja kuzalishia hapa kwetu vika-supply kwenye nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie kutoamchango wangu kwa kuongelea jambo la amani na jinsiambavyo linaweza likasaidia kuwa chachu ya kukuzaUchumi wa Taifa letu. Tunaichezea amani, Viongozi waKisiasa wanasimama majukwaani, wanatoa kauli mbalimbaliambazo zinahatarisha amani, wanaachwa.

Mheshimiwa Spika, katika hali ambapo nchi yetuamani imekuwa so vulnerable, Kiongozi wa Kisiasaanasimama na kusema kwamba, yeye amewaonawaliolipua bomu kwenye mkutano wa hadhara. Inatiamashaka aliwaona wakati gani, kwa sababuninavyofahamu, Kiongozi ukiwa kwenye Mkutano unakuwambele, unakuwa jukwaa kuu na bomu halikupigwa jukwaakuu lilipigwa kwa nyuma. Sasa mtu ambaye anasema

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

103

19 JUNI, 2013

aliwaona wanaolipua mabomu, aliwaona wakati gani;alitumia kifaa gani; na kwa nini asiisaidie Polisi kuwezakudumisha amani? Badala yake anatoa kauli tata ambayoitatia mashaka na wasiwasi mkubwa kwa Wananchi, jamboambalo sidhani kama ni busara na ni la hekima kwa Kiongoziwa Kisiasa ambaye ana dhamana kwa Wananchi.

Mheshimiwa Spika, sisi Viongozi ni charismatic.Tunaaminiwa na Wananchi na kauli zetu zina madharamakubwa sana kwa Wananchi; aidha, madhara positiveama madhara hasi. Naomba sana sisi Viongozi wa Kisiasatuchunge ndimi zetu, tutoe kauli ambazo zitajenga nakudumisha amani, ili uchumi uweze kusonga mbele tuwezekufaidisha Wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, siasa ya karne hii haiwezi hatakidogo kuwa ni siasa ya vurugu, kuwa ni siasa yamapambano, kuwa ni siasa ya mapinduzi ya maandamano,ya vurugu, ya namna yoyote ile ambayo siyo ya amani. Siasaya leo hii ni uchumi. Tunajadili bajeti hapa, lakini sina hakikakama ndugu zangu Wana-Arusha, wanapata fursa yakusikil iza namna ambavyo tunajadili bajeti ambayoitawakomboa wao kiuchumi. Wapo katika hali ya mabomu,wapo katika hali ya mashaka, kazi haziendi kule Arusha;tunaomba sana sisi Viongozi wa Kisiasa, tujichungetuliongoze Taifa hili, tuweze kudumisha amani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ahsante sana.(Makofi)

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika enziya uhai wake aliojaliwa na Mungu, aliwahi kuandika Kitabukilichoitwa kwa jina la “Tanzania Itajengwa na WenyeMoyo”.

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kusema wale wenyemoyo ambao walitamkwa na Mwasisi wa Taifa hili, weweni mmojawapo. Kwa kipindi chote ambacho nimeingiakatika Bunge hili, nilikuwa ni miongoni mwa Wabunge ambao

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

104

19 JUNI, 2013

walikuwa wanapinga mfumo ule ambao tulikuwa tunaendanao kibajeti. Hii ilikuwa ni changamoto kubwa, lakini nisemetu kwamba, wewe ni mwanamke wa shoka, umewezakulisimamia hili na tumeweza kufanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukirudi katika bajeti ambayoimewasilishwa hapa na Waziri wa Mipango pamoja naMahusiano na Uratibu na Waziri wa Fedha, niseme tukwamba, mfumo wa bajeti bado una matatizo; kwanza,huu utaratibu wa kutoa vipaumbele. Serikali kwenyekutunga bajeti, kila Halmashauri, kila Mkoa wanapewaceiling, wao ndiyo ambao wanajua ni vitu gani vinaumuhimu kwa wakati huo, lakini inapokuja huku kwenyekuweka bajeti tayari inazuiwa wanasema kwamba, katikahili sisi tumeweka ceiling hii.

Mheshimiwa Spika, mnaweza mkawa mmetupangiasisi kutupa matrekta 100, lakini mahitaji yetu siyo matrekta100. Sasa naomba Serikali, ikubaliane na matakwa yaWataalam kutoka kwenye ngazi za Halmashauri na Mikoa,kwa vipaumbele ambavyo wanaviainisha kwa ajili yamaendeleo ya maeneo wanayoyaongoza. Hii itasaidiakukuza na kuharakisha maendeleo katika nchi yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninasema hivi kwa mfano,kwenye Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Mahusiano kuhusuhali ya uchumi, ameainisha hapa kwamba, kunamtawanyiko katika eneo la Mkoa wa Lindi ni 1/14; ndiyoeneo ambalo lina mtawanyiko mdogo kuliko maeneomengine yote. Sasa hivi mmeshawahi kujiuliza ni factor zipizinazosababisha watu wengi wasipende kuishi katika Mkoawa Lindi? Sababu, hakuna miundombinu ya kutosha.Tunapohitaji mahitaji ya zahanati, vituo vya afya na shule,tunaambiwa kwamba, pesa tulizozitenga safari hii ni kwaajili ya kukuza kilimo; sisi tumekuwa tukilima kabla hata hiinchi haijawahi kuitwa Tanganyika.

Mheshimiwa Spika, lingine ambalo limezungumzwahapa ni kuhusiana na inflation. Hii inflation, mimi ninaitafsiri

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

105

19 JUNI, 2013

siyo mfumko wa bei, Tanzania kuna bei ya mfumko; kwamaana kwamba, bidhaa zinapandishwa bei kiasi ambachohazihimiliki. Serikali kila mwaka inapanga kutoa excemptionkwa ajili ya bidhaa za chakula kuagiza nchini, lakini usimamiziwake unakuwa ni duni na hafifu. Mfano mzuri, mwaka janaambapo tulitoa vibali vya kuagiza sukari kutoka nje nikampuni moja tu ya Mohamed Enterprises, ilikubali kuuzabei ambayo ilitamkwa na Serikali ya shilingi 1,700, wenginewote sukari ilifikia mpaka shilingi 3,500. Tunatoa misamahaya kodi hii kumnufaisha nani? Sasa hili ni eneo ambalo lazimatuliangalie kwa umakini na tuangalie ni jinsi gani ambavyotunaweza kuweka mfumo mzuri wa kudhibiti mianya hii yauvujaji wa kodi.

Mheshimiwa Spika, katika eneo la mapato, Serikaliimezungumzia jinsi ambavyo imeweza kukabiliana na udhibitiwa uagizaji bidhaa na ukiukwaji wa kodi. Jambo mojaambalo najiuliza; wakati tunadai uhuru wa nchi hii, jambokubwa ambalo liliwahamasisha Wananchi walieleza kuhusuumuhimu wa kutokulipa kodi, tukipata uhuru wetuhatutalipa kodi. Sasa leo hii tumeshakuwa huru, tunahitajiWananchi washiriki kwenye kulipa kodi, ili tujenge uchumiwetu. Kwenye bidhaa zinazoagizwa nje, jambo la msingiambalo naiomba Serikali ifanye utafiti, wafanyabiasharahawajajenga utamaduni wa kuwa wakweli kulipa kodikama walivyo wafanyabiashara wa nchi nyingi nyingineDuniani; mmeshawahi kutafiti? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, bei ya bidhaa zinazoingia hapanchini zinatozwa ushuru kwa kutokulingana na thamani halisiya ununuzi. Sisi tunafuata viwango vya kimataifa, tunanunuavitu Asia huko, ambavyo quality yake haiwezi kuwa inaushindani katika World Market, ambapo na sisi ndiyotumetumia kama base yetu. Kwa hiyo, naomba tuwekekodi ambazo ziko reasonable i l i Wananchi wengi nawafanyabiashara wengi, waweze kushiriki na kukubali kulipakodi bila shuruti.

Mheshimiwa Spika, Deni la Taifa. Mwaka jana namwaka juzi, bajeti yetu tumekuwa tunalenga kulipa madeni

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

106

19 JUNI, 2013

ya ndani, lakini bado wadai wengi, wazabuni wengi,wanadai katika Idara mbalimbali za Serikali. Sijui ni sababuzipi zinazosababisha pesa zinatengwa, lakini bado madeniyanaendelea kuwepo. Hebu Serikali ichukue jitihada zamakusudi kuweza kufanya tathmini ya watu ambaowanadai kwa zabuni walizotoa, tuweze kujua uhalisia.

Mheshimiwa Spika, l ingine ambalo natakanilizungumzie, naipongeza sana Benki ya Stanbic, kwa jinsiambavyo imeweza kuisaidia Serikali, kwenye ile syndicateloan ambayo walifanya, ambapo tumeweza ku-raise600,000,000 dollars zitakazosaidia kukuza sekta nyingine,hasa umeme na barabara. Nilisoma gazeti moja wiki mbiliau tatu zilizopita, nimeona kwamba, Serikali imefanikiwakuweza kushawishi kupata sovereign bond za bilioni mbili.Naomba tu nii-caution Serikali, sovereign bonds zinamatatizo yake; matatizo ambayo nchi kama Ugiriki, Hispaniana Ureno wanayapata, yanatokana na hili. Kwa hiyo,tusikope pesa, tusiende tuka-raise funds huko nje kwa ajiliya matumizi ya kawaida. Tuwekeze katika miundombinuna tuwekeze katika maeneo ambayo yatakuwa na ustawikatika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho, katika sekta muhimuza Afya, Elimu, Jeshi, Polisi, lazima tuweke umuhimu sasa wakuwalipa mishahara ambayo inakidhi. Malalamiko katikasekta hizi muhimu yamekuwa mengi na ninaona tunawezatukaumiza uchumi wetu kama tusipoyazingatia nakuyaweka vizuri. Katika hili kumekuwa na malalamikomakubwa sana, hasa katika eneo ambalo ninaliwakilishapale Kilwa; Walimu na Watumishi wa Afya, wanakopeshwamikopo katika taasisi hizi za kifedha kwa interest kubwasana.

Mheshimiwa Spika, ninajiuliza ni kwa nini NMBambapo ndipo mishahara yao inapitia, isifanye kazi yakuwakopesha watumishi hawa? Mtaji wa Serikaliuliokuwepo ni kwa ajili ya kitu gani? Lazima tuangalienamna, kwa kuwa wale wanatumia mfumo huohuo wa ku-deduct pesa zao kila wanapolipwa mishahara kwa mwezi.

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

107

19 JUNI, 2013

Wanakopeshwa katika rate ya zaidi ya asilimia 30, hii nihatari, tuwaokoe watumishi na tuweze kuwapa nafasi nzuri.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho, mapatoyanayotokana na rasilimali za nchi yetu. NimemsikiaMheshimiwa Rais, amezungumza siyo chini ya mara mbili naMheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, aliwahikulizungumzia hili; ni lini Serikali itakuwa tayari kuanzishasovereign fund au heritage fund kwa ajili ya mapatoyanayotokana na gesi, uranium, pamoja na makaa yamawe? Kwa sababu, pesa hizi hatuwezi kuingiza kama nimatumizi ya kawaida, lazima itumike kwa ajili ya kuendelezaWananchi wetu na tuweze kuokoa uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, tunavyo viwanda vya koroshona hil i tunalielewa, tunaitaka sasa Serikali itusaidie.Tumekuwa na matatizo ya korosho, mwaka huu mmeonamatatizo sehemu mbalimbali. Viwanda ambavyowameshindwa kuviendeleza, basi Serikali ivirudishe ili tupatewawekezaji wengine au Serikali yenyewe iwekeze. Vilevilewale ambao wamepewa vile viwanda na wanao uwezowa kuviendesha, kwa nini Serikali inachelewa kutoa idhiniya hawa watu kukopesheka, kuwa na mitaji ya kuendeshahivi viwanda? Kuna tatizo kubwa sana la viwandakutokuwa na mitaji ya kutosha kuweza kujiendesha navilevile mitaji ya kuweza kununua korosho kutoka kwawakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na ninaombakuunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Kwa asubuhi hii, naona huyoalikuwa Msemaji wetu wa mwisho, naona dakika zimeisha.Tutakaporudi j ioni, watakaochangia ni MheshimiwaLivingstone Joseph Lusinde, Mheshimiwa Masoud AbdallahSalim, Mheshimiwa Idd Mohamed Azzan, MheshimiwaCapt. Chiligati, Mheshimiwa Abdulkarim Shah, MheshimiwaCynthia Ngoye, Mheshimiwa Omar Rashid Nundu,Mheshimiwa Ngeleja, Mheshimiwa Koka, Mheshimiwa Diana

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

108

19 JUNI, 2013

Mwatuka, Mheshimiwa Martha Umbula, MheshimiwaCharles John Mwijage na Mheshimiwa Kayombo. Ndiyo haona wengine watatajwa mchana.

Mimi sina matangazo mengine, naomba tusitisheshughuli za Bunge mpaka saa 11.00 jioni.

(Saa 6.55 mchana Bunge lilifungwa hadi saa 11.00 jioni)

(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia)

Hapa Mwenyekiti (Mhe. Jenista J. Mhagama) Alikalia Kiti

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana majadiliano ya hoja iliyoko mbele yetu na kwa mujibuwa utaratibu na kwa mujibu wa taarifa niliyoipokea kutokakwa Mheshimiwa Spika, wafuatao walishatajwa kuwawachangiaji wa mwanzo. Kwa hiyo, nitaanza kuwaita hawaambao Mheshimiwa Spika alishawaandaa kuchangiahotuba hii kwa jioni. I l ikuwa tuanze na MheshimiwaLivingstone Joseph Lusinde, naona hayuko ndani ya Ukumbiwa Bunge, basi nitamwita Mheshimiwa Masoud AbdallaSalim, Mheshimiwa Idd Mohamed Azzan ajiandae naMheshimiwa Capt. John Zefania Chiligati ajiandae.

MHE. MASOUD ABDALLA SALIM: MheshimiwaMwenyekiti, awali ya yote, namshukuru Mwenyezi Mungu,aliyenijalia uzima na afya njema hadi na mimi nachangiabajeti hii ya mwaka 2013/2014 na nikiwa mtu wa kwanzakwa jioni hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, natakaniikumbushe Serikali kwamba, nchi ya Rwanda ambayoilikuwa katika machafuko makubwa na vita vya wenyewekwa wenyewe, bajeti ya maendeleo mwaka huu ni asilimia50 na sisi ndipo hapo tulipo, tumepitwa na nchi ndogo kamaya Rwanda ambayo ilikuwa katika machufuko. Tunajifunzanini? Kazi kwetu sisi kama Watanzania.

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

109

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nianze sasakuchangia. Kwangu mimi nilikuwa najiuliza uko wapi mpangowa kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwenye Sektaya Uvuvi? Mwaka huu wa 2013/2014 Serikali imedhamiriana imepanga kuanzisha mashamba, vitalu na vituo sabavya kufuga samaki. Cha kushangaza, sehemu ambayoimetengwa katika kufuga samaki hao ni shilingi 217 milioni;najiuliza hivi ni kweli shilingi milioni 217 zinaweza kutosha kiasigani kuweza kufuga samaki katika vitalu hivyo au ni kutaniaTania?

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba MheshimiwaWaziri hili aliangalie kwa makini sana. Huwezi kufuga samaki,ukaanzisha tatizo hili kubwa katika hali ya kuwakomboawavuvi ambao wengi ni maskini ukapeleka shilingi milioni217, ni kuwatania. Wavuvi ni masikni, lichukue, liangalie naandaa mazingira mengine ya kutafuta fedha ili uboreshenafasi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili, Tanzania kamanchi kubwa, Vietnam wenzetu wana mashamba ya kufugasamaki zaidi ya 100; najiuliza hivi sisi kama tunakwenda maranyingi huko nje na tunapata elimu ya kutosha; ni kwa ninibasi Mheshimiwa Waziri asiandae mazingira ya kufikiaangalau mashamba 50? Hili namwambia MheshimiwaWaziri, aliangalie kwa mapana yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2008 ukuaji wauchumi katika Sekta ya Uvuvi ilikuwa na asilimia tano, lakinimwaka 2012 ukuaji wa uchumi ilikuwa na asilimia 2.9 tu,tumeshuka. Hili ni jambo moja kubwa, tunapoweza kushukakatika sekta hii ambayo ni muhimu, basi kuna haja yakuangalia ni mipango gani iliyoweza kushusha asilimia hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niende kwenyeutalii. Tanzania ni nchi ya pili Duniani kwa kuwa na vivutiovingi vya utalii ikitanguliwa na Brazili. Kwa mujibu wa WorldEconomic Forum, mwaka 2011 Tanzania tulikuwa kwenyenafasi ya 110, mwaka 2012 tulikuwa kwenye nafasi ya 109,lakini wenzetu Kenya mwaka 2011 walikuwa kwenye nafasi

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

110

19 JUNI, 2013

ya 103, mwaka 2012 wenzetu Kenya walikuwa kwenye nafasiya 99 kwa kuingiza wageni wengi na kuingiza fedha nyingikwa ajili ya utalii. Mimi najiuliza tatizo nini kwetu; hivi badohatujifunzi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbaya zaidi, fedha zakutangazia utalii hazitolewi, kuna malalamiko makubwakwenye Balozi zetu hata pale ambapo wao tunawaambiawaandae mazingira ya Economic Diplomacy watafanyanini wakati fedha hatuwapi? Mabalozi wetu nchi za njewanalalamika sana kwamba hatuwapatii fedha hata zakufanya makongamano na warsha. Inakuwaje leo unasematunapanga mpango wa kuweza kuendeleza utalii?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni tatizo, lakini siyo hilotu, sisi hatuna ndege, wenzetu Kenya wana Kenya Airwaysmpaka Ulaya wanakwenda na kurudi, wanavutia. Ingawahiyo sisi hatuna ni tatizo; tumejifunza nini kwetu? Tunapigakelele siku zote, lakini Serikali bado naona haijachukuahatua madhubuti za kuweza kuiimarisha sekta hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa zaidi, hata zilefedha ambazo tuna maeneo, tuna watalii, hatuna udhibitiwa fedha. La kushangaza sana, jambo ambalo mimisilipendi hata kidogo, ukienda kule Millan Italy, wataliiwanaoondoka kule tumemuweka Mzungu mmoja ndiyoanayekusanya fedha, watalii wanakuja huku, baadayeanatupa anachotaka yeye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni tatizo, Millan Italy najina la mzungu mimi nalihifadhi, kwa sababu ninyi Serikalindiyo mlimuweka nyinyi mnaomjua; shauri yenu, tunapigakelele siku zote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye kilimo, tulikuwana kauli nyingi tu Siasa ni Kilimo, Kilimo Uti wa Mgongo, KILIMOKWANZA mwaka huu, lakini mpango wa Serikali wakuthaminisha mazao ya kilimo uko wapi. Bado siuoni,nilitarajia mtakuja na majibu kama ambavyo MheshimiwaWaziri wa Biashara na Viwanda alivyotuambia Bungeni

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

111

19 JUNI, 2013

hapa kwamba, bajeti inayokuja ya Serikali, Bajeti Kuu,itakuwa na mpango wa kufufua viwanda vilivyokufa ilikuboresha maisha ya Watanzania kuthaminisha mazao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia mpango wakufufua viwanda vil ivyokufa haupo na tulimwulizaMheshimiwa Waziri wa Biashara na Viwanda kwa wakatiule akasema, bajeti hii kuna mpango mahususi ambaoukifika tutaona vile viwanda vyote ambavyo Serikalimlivichukua mkawauzia Vigogo wa Serikali, baadayeutaratibu wa kuingia ubia na baadhi ya mashirika ya kijamiikuweza kuvifufua. Lakini ni aibu tupu, alituambiaMheshimiwa Waziri atawaita wale wote aliowapa viwandaili wakae pamoja waone namna gani ya kuweza kuboresha.Jamani kilo moja ya korosho safi ni shilingi 20,000, koroshoghafi haziwasaidii Wananchi wa Lindi na Mtwara. Umaskiniwa Lindi na Mtwara unachangiwa na Serikali, kwa sababumlipeana viwanda Vigogo wa Serikali na mmesemamtawaita lakini wapi maskini mnaogopana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikopa dola milioni 20kutoka nje mwaka 1970 mpaka 1980 kutoka Italia na Japani,tukasema kwamba mnajenga viwanda, lakini mnashindwakuwaita. Mlituambia mtawaita hamjawaita na naombamniambie Kiwanda cha Mtwara Mjini, Taasisi ya Fursa kwaWote ni Kigogo wa Serikali, mtu wa juu kabisa wa Serikalimmeshindwa kumwita mnaoneana aibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Newala One mmechukuaVigogo wa Serikali, kiwanda hiki mmepeana wenyewe kwawenyewe, hamjathubutu kuwaita; mlitudanganya Bungeni.Masasi ni ninyi wakubwa wa Serikali hamjawaita.Nachingwea nako ndiyo hasa kumeoza. Mtama ndiyokabisa. Tatizo nini Likombe, Lindi Mjini, Kibaha tatizo nini nakwa nini msiwaite Mheshimiwa? Thamani ya mazao iko wapi,leo uko wapi mpango wa kufufua SUNGURATEX umekufa,MBEYATEX, MUTEX, KILITEX, MWATEX, Morogoro Polytex, vyotevimekufa na mlituambia mna mpango madhubuti wakwenda kufufua viwanda ili kukuza uchumi na kuwapatia

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

112

19 JUNI, 2013

ajira Wananchi. Uko wapi mpango huo, mimi siuoni naonakizaazaa tu mwaka huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee, katikahili Wananchi wanalalamika Serikali imeshindwa kudhibitibidhaa bandia na bidhaa feki. Bidhaa feki ni nyingi,Wananchi wanaonunua mabati wanalalamika, baadhi yamabati hayana TBS, hayana muhuri wa TBS; tatizo nini?Nyaya za Umeme zinaharibu nyumba za watu, nyumbazinaungua, ukija kwenye mabati kuna viwanda kibao. Miminaomba uniambie kuna kiwanda cha Wachina Vingunguti,ndani yake kuna Kiwanda cha Korosho, Premium CashewNuts, kinajulikana kwa jina la Dragon Roofing Sheet; mabatihayana nembo ya TBS, yana migongo minne, unaponunuahupewi risiti na Mchina anakwambia wewe nenda bebatu ching chang, bei nafuu ninyi mnajua wenyewe mnakaatu Wananchi nyumba zinavuja shauri yenu. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwanda kingine kipoKurasini kule nyuma ya Chuo cha Diplomasia, nacho ni kwaajili ya kuunganisha aina ya pikipiki ya T-belta. Ukiingia getiniutakuta mtambo wa kutengeneza mabati, vilevile kunadada wa Kichina nipe risiti, beba tu bei nafuu; jamani,hamjui kweli ninyi au mnatuminyia minyia kibongo mbonahatuelewi!

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kwamba,tatizo kubwa lililopo hivi sasa ni rushwa. Udhibiti wa fedhaza umma haupo na hili ni eneo ambalo lilipigiwa kelele sana.Mwaka 2006 Serikali imepoteza bilioni 2.3, mwaka 2007tumepoteza bilioni 3.5, 2008 bilioni 3.1, 2009 bilioni 11.1, 2010bilioni 12.9; bilioni 33. Upotevu wa fedha za umma, ufisadiuliokithiri Tanzania, hiyo bilioni 33 ndiyo eneo hilo; tatizo nini?

Tunaposema hapa jamani ni kwa nini Serikalihaichukui hatua kwa wale wote waliobainika na ufisadi huu,tuko katika mchakato jamani. Wale wanyonge wa Mungu,wanaochukua vitu vidogo vidogo tu wanafungwa miakaminne, miaka mitano, wamejaa magerezani tunawasemea

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

113

19 JUNI, 2013

sisi wanyonge mbona hao matajiri wanaoonekanawanachukua mabilioni haya hawafungwi; tatizo nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi napata mashakamakubwa sana kwenye eneo hilo. Ikiwa Serikali inaruhusukuwaachia mafisadi wakubwa, lakini wale wadogo wadogowanabanwa, hili ni tatizo kubwa. Naiomba Serikali ikaemakini, ichukue hatua madhubuti na wale mafisadiwakubwa, mafisadi papa, wachukuliwe hatua zinazostahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. (Makofi)

MHE. IDDI M. AZZAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, naminakushukuru kwa kunipa nafasi jioni hii. Naungana nawenzangu kupongeza utaratibu ambao umetumika hivisasa wa bajeti yetu, kupitisha bajeti yetu hii. Zaidi,napongeza pale ambapo kulikuwa na upungufu kwenyebaadhi ya Wizara, kwa makusudi kabisa Serikali ilikubalikuongeza fedha na hasa kwenye suala la maji, ni tatizokubwa sana na lipo karibu nchi nzima. Mimi wa Dar esSalaam nimelifurahia sana, kwa sababu fedha ambazozimeongezwa, nina hakika Miradi ya Maji katika Jiji la Dares Salaam itakamilishwa kwa wakati, haitakuwa hadithitena, kwa sababu tatizo la maji lilikuwa ni kubwa sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa ambalotunalo kwenye bajeti hizi kila mwaka ni matumizi ya Serikali.Matumizi ya Serikali yamekuwa makubwa sana na hatabaadhi ya fedha za miradi ya maendeleo zinapokuwahazikupatikana, lakini fedha za matumizi ya kawaida hizolazima zipatikane, lakini kwenye miradi ya maendeleo hukufedha hazitapatikana, utaambiwa fedha hazijafika namambo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ningeomba sana hebutujaribu kuangalia matumizi ya Serikali ni jinsi gani tutawezakuyapunguza, kwa sababu matumizi yamekuwa makubwasana. Nitoe mfano tu miaka ya 80 wakati wa MwalimuNyerere na wakati huo Makatibu Wakuu wa Wizara

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

114

19 JUNI, 2013

walikuwa wanatumia magari madogo haya ya Saloon,Nissan Globatt na wakati huo kutoka mjini kuja Magomeniunatumia nusu saa, Jangwani barabara ilikuwa mbovu mno,lakini yalitumika magari hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa Serikali hii yaChama cha Mapinduzi, imejenga barabara takribani nchinzima kama anavyosema Mheshimiwa Magufuli, unawezakutoka Mtwara mpaka Bukoba kwa bajaji; lakini sasa ndiyotumeongeza kutumia magari makubwa ya kifahari, yenyethamani kubwa mno na siyo thamani tu ya kununua, lakinihata kulitengeneza hilo gari.

Fedha ambazo zinatumika kwenye matengenezo yamagari ni nyingi sana, lakini fedha zinazotumika kwenyeununuzi wa mafuta ni nyingi zaidi. Kwa hiyo, tuangalie nijinsi gani sasa tutaweza kupunguza matumizi kwa upandewa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeamua hapa kwambasasa magari ya CC 3000 yatumike, lakini CC 3000 ndiyounazungumzia Prado, ni magari hayo hayo ya thamanikubwa, yanatumia mafuta kwa wingi sana. Mimi ningeombasana, tuangalie uwezekano wa kurudi tena chini, wenzetuWakenya wameweza wanatumia magari ambayo hayazidiCC 2000 nafikiri na sisi pia tunaweza kufika huko. Twendetaratibu ili tuone ni nani anatumia gari ya CC 3000 na naniatumie gari la chini ya hapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani Waziri atumiegari la CC 3000, Mkuu wa Idara naye anatumie gari la CC3000, Rais anatumia VX, Mkurugenzi wa Halmashauri nayeVX hilo hilo; sasa huwezi kutofautisha, imekuwa kamakambale, baba ana masharubu na mtoto ana masharubuna mama ana masharubu. Kwa hiyo, lazima tuonetunakwendaje kwenye hilo. (Makofi)

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

115

19 JUNI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ambachoningeomba kukizungumzia ni suala la mfumko wa bei, mtaanibei ziko juu sana, vitu vina bei kubwa sana na hiiinasababishwa na wafanyabiashara kubanwa nawanabanwa kwenye maeneo mengi sana kununua bidhaahizi. Sasa anapobanwa yeye huko naye anakuja kuwabanaWananchi, mwisho wa siku anayeumia sana ni Mwananchiwa chini. Mfanyabiashara yeyote anayefanya biasharalazima aende benki akakope. Hebu sasa angalieni riba zakwenye mabenki na hakuna jitihada zozote za Serikalikuweka utaratibu kwamba hivi sasa jamani ukomo wa ribauwe ni kiasi fulani, asilimia fulani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini leo unakwendamahali kwenye mabenki, mikopo mpaka asilimia 24, asilimia22, sasa mfanyabiashara atachukua mkopo lakini mwishowa siku anakuja kumwumiza Mwananchi ndiye anayeumia.Kwa hiyo, tuweke utaratibu tu kwamba, jamani mabenkiyetu haya sasa asilimia 15 iwe ndiyo mwisho wa riba tusizidihapo.

Kinyume cha hivyo, tutakwenda kuwaumizaWananchi wetu, bajeti zitakuja lakini anayeumia sana niMwananchi wa chini. Kwa hiyo, tuone ni jinsi gani tunawezakumsaidia na ni karibuni tu mmesikia mabenkiyanavyotangaza faida, benki inatangaza kwa mwakainapata faida ya zaidi ya bilioni 50 au 60. Sasa jiulize bilioni50 au 60 anazozipata mwenye benki; ni kwamba,kawaumiza Wananchi, ndiyo maana yeye anapata faidakubwa kiasi hiki; ni faida kubwa kuliko inavyotarajiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba sana tuangaliehilo ili mambo yaende vizuri, Wananchi wetu wawezekupata unafuu wa vitu mbalimbali. Siyo hilo tu, kuna sualala matumizi ya fedha hizi za Kitanzania (Shilingi). Maeneomengi hivi sasa ukienda watu hawakwambii ulipe kwa shilingiwanakwambia ulipe kwa dola na hili limekuwa kubwa sanana ukienda kwenye maduka ya kubadilishia fedha wenyemaduka ndiyo wanaopanga fedha wauze kiasi gani siku

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

116

19 JUNI, 2013

hiyo. Hakuna utaratibu maalum ambao umewekwa naSerikali kwamba, shilingi yetu thamani yake ni hii, wenyemaduka ya kubadilishia fedha wasizidi kiwango hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenye maduka yakubadilisha fedha anaamua tu leo nibadilishe kwa shilingingapi na kesho nibadilishe kwa shilingi ngapi; na faidawanayoiweka wao ni kubwa sana tofauti na nchi nyingine.Kwa hiyo, naomba na hili nalo mliangalie ili kuwarahisishiaWananchi wetu waweze kupata unafuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni bidhaazisizokuwa na viwango. Tumeona ni juzi tu Dar es Salaamlilianguka ghorofa pale na uchunguzi unaendelea, lakiniunaweza ukaangalia tu nondo iliyotumika pale ina uborauliostahili. Twende kwenye simenti ambayo inatumika, nayoina ubora unaostahili. Siyo hilo tu, kaangalieni na matofaliyanayotengenezwa hivi sasa yana ubora au mradi tofalitu, kwa sababu unakwenda kuangalia tofali ni mchangamtupu.

Nakumbuka zamani Kiwanda cha Saruji Wazowalikuwa wanatengeneza matofali, lakini mfuko mmoja wasimenti wa kilo 50 utatoa matofali yasiyozidi 25, kati ya 18mpaka 25. Leo mfuko mmoja huo huo wa simenti unatoamatofali kati ya 40 mpaka 50. Kwa hiyo, tofali unalikutamchanga na tumekaa tunaachia majumbayanaporomoka. Ninafikiri na huko pia twende tukaangalieili tuhakikishe Wananchi wetu hawanunui bidhaa ambazosiyo imara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo bidhaa hizo za ujenzitu, yapo mambo mengi; kuna madawa na vyakulaambavyo vinaingizwa. Juzi tulikuwa na watu wa konyaginao wanaonesha jinsi pombe hizi zinavyoingizwa nchinikinyemela tu, hazina viwango, hazina TBS, hazina chochote,lakini zinaingizwa Wananchi wetu wanakunywa na nyingineni sumu.

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

117

Kwa hiyo, ni lazima tuhakikishe tunawalinda wananchi wetukwenye masuala ya vyakula, vinywaji na dawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ulinzi, tumeonaambayo yametokea hivi sasa, nimekuwa nikipigia kelele sikuzote juu ya nyumba za Askari. Leo tunavyozungumza, AskariMtwara walikuwa hawakai kwenye nyumba zao, nyumba zaowanazoishi zinachomwa moto, kwa sababu tu ya vuruguambayo imetokea. Kuondoa tatizo hili, ni lazima tuhakikishetunajenga nyumba za Askari. Sasa kwenye bajeti inayokujatuangalie umuhimu wa kujenga nyumba za Maaskari kwenyemakambi yao. Tusiruhusu Askari kuishi mtaani kwa sababuanashindwa kufanya kazi yake, kuna uwoga na mambombalimbali. Kwa hiyo, tuone jinsi gani tunawasaidia Askarikujenga nyumba kwenye line. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine, tumeondoa kodi yabodaboda, sawa, lakini unapoondoa kodi ya bodaboda,yule mwenye teksi unamweka wapi, kodi yake umepandishana ndiyo gari ambazo tunazitegemea. Wajawazitowatapanda teksi hawawezi kupanda bodaboda, lakiniumeondoa kodi ya bodaboda ambapo yeye kwa sikuanaingiza Sh.15,000 kwa tajiri na mimi ninazo, tena niseme tuninazo bodaboda na mmeondoa kodi na mimi nafurahia,lakini mnawaumiza wananchi, wangeweza na waokuchangia hata kidogo kwenye bajeti hii, lakinimmewaondolea kodi matokeo yake mnaendeleakuwaumiza wenye teksi ambazo ndizo zinazotakiwa na watuwengi wanapopata matatizo. Kwenye bodaboda huwezikumpakiza mzazi, lakini mmeziondolea bodaboda, mwenyeteksi mnazidi kumkandamiza, analipa kodi ya mapato, roadlicense, analipa kituo anachoegeshea pale anakatwa naHalmashauri, lakini mwenye bodaboda yuko huru tu nabaadhi ya wenye bodaboda hata leseni ya kuendesheahawana. Mimi naomba hivi sasa kwa sababu bajeti siyomsaafu, mwaka huu tumefanya hivyo, lakini mwakanituangalie jinsi gani tunafanya kuweza kutatua tatizo hilo.(Makofi)

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

118

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni mfanyabiashara naninaomba ni-declare na huwa naingiza mzigo kwa kontena.Kuna utaratibu ambao unatumika hivi sasa kwambaunapoingiza kontena nchini, unapotaka kwenda kuteremshaule mzigo, unatoka na lile kontena, ili utoke na kontenaunatakiwa uweke deposit ya dola na siyo shil ingi,wanakwambia ulipe dola 2,000, unaweka dola 2,000unashusha kontena mzigo wako, siku ya pili unarudishakontena, ukirudisha unafuata sasa ile dola 2,000 hawakupi,hiyo fedha hurudishiwi, huu ni wizi. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Barwany, naomba urudiulikotoka, unavunja utaratibu.

MHE. IDDI M. AZZAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, huu niwizi ambao unafanywa na makampuni haya, Maersk Line,Safmarine, Nyota Tanzania Limited, wao ndiyo wanafanyahivyo. Sasa hebu fikiria kontena 30 au 50 zinazotoka kwa siku,kila mmoja amelipa dola 2,000 ni shilingi ngapi hizo kwa siku,kwa mwezi ni ngapi na fedha hizo hazirudishwi, ukimdaianakwambia oooh, lete account number, aah mimi ninaakaunti ya dola ya nini, mimi sina akaunti ya dola, mimi ninaakaunti ya shilingi, nirudishieni shilingi basi, kwa sababunimekupa deposit dola 2,000 nirudishie hizo hawataki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninao ushahidi hapa, fedhazimelipwa tangu mwezi Oktoba, 2012, mpaka leo hawatakikurudisha hizo fedha na ni watu wengi wamefanyiwa hivyo,lakini Serikali wanalijua na hawachukui hatua. Watuwachache hao wanazidi kutuumiza, wanaumiza wananchiwetu kwa sababu ukinibana mimi mfanyabiashara na miminakwenda kuwabana wananchi, mwisho wa sikutunawaumiza wananchi. Ningeomba sana Serikali iliangaliehili na ichukue hatua zinazostahili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo,mimi niseme tu naunga mkono hoja hii, ahsante sana.(Makofi)

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

119

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Azzan.Sasa naomba nimwite Mheshimiwa John Zefania Chiligatianafuatiwa na Mheshimiwa Chacha Nyambari NyaribaNyagwine.

MHE. JOHN Z. CHILIGATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi nichangie bajeti iliyombele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, niseme kwambanaunga mkono bajeti hii na nitatoa sababu zangu baadaye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya matatizo makubwatuliyonayo hapa nchini sasa hivi, ni kuongezeka kwa kasi kwapengo kati ya walionacho na wasinacho, kati ya maskini namatajiri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haihitaji kuwa muumini waitikadi ya ujamaa kama mimi ili kuona athari za tatizo hiliambalo ninalolisema. Ni tatizo likiachwa likaendelea, kamahatua za kibajeti hazichukuliwi kulikabili tatizo hili, litazaa chukimiongoni mwetu, litazaa uhasama miongoni mwetu, litazaamapambano ya kitabaka kati ya makundi haya mawili,jambo ambalo litakuja kuvuruga umoja wetu na amani yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Watanzania wengihasa wafanyakazi wa kawaida na wakulima kule vijijini,mapato yao ni kidogo, wanashindwa hata kupata milomitatu kwa siku, baadhi ya wenzetu walionacho, tanguJumatatu mpaka Jumapili ni sherehe tu, tena za mamilioni,mara harusi, mara sendof, mara kipaimara, siku hizi hatamtoto akimaliza chekechea anakwenda darasa la kwanza,vilevile kuna sherehe ya mamilioni, Tanzania hiihii! Sina ugomvina matajiri, wala kutajirika si jambo baya, ili mradi kama utajirihuo mtu ameupata kwa njia halali, kafanya kazi halali,kafanya biashara halali, ametajirika, si tatizo. Tatizo letu nachangamoto yetu, ni kuwasaidia watu hawa wa chini kwakuwawezesha kupitia Wizara ya Mama Nagu na wenyewekuinua hali zao za maisha na bajeti ndiyo silaha yenyewe ya

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

120

kutufikisha huko. Chama kinachotawala, itikadi yake kubwani kusaidia wanyonge, ambao ni wakulima na wafanyakazi,sasa vitendo vyake lazima vionekane kwenye bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa bajeti ya mwaka huu,imejitahidi kidogo na ndiyo maana naiunga mkono kutazamamakundi haya, wakulima na wafanyakazi. Mfanyakazi wakawaida yule ambaye ni mwaminifu, hali rushwa,hadokoidokoi mali ya tajiri wake, hana mapato huyu, mapatoyake ni ule mshahara tu. Sasa mwaka huu kodi ya mshaharaimepunguzwa kwa kutoka asilimia 13 kwenda 12, ni isharanzuri ya huruma lakini mwakani hebu tuangalie vizuri eneohili, tuwapunguzie mzigo hawa wafanyakazi. Namna mojaya kumuongezea kipato mfanyakazi, ni kupunguza ile kodikwenye mshahara wake. Mwakani Waziri wa Fedha, hebushuka fika kwenye 10 hata tisa, ili huyu mfanyakazi tumpemotisha ya kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakulima vilevile bajeti hiiimewatazama na Serikali imesaidiwa na WaheshimiwaWabunge kuongeza bajeti kwa mfano ya kilimo, kumsaidiamkulima. Zile fedha zilizowekwa mwanzo, baada ya sisiWabunge kupiga kelele, Serikali imeongeza shilingi bilioni 21.Ni ishara nzuri, mwakani ongezeni zaidi ili wakulima tuwezekuwasaidia zaidi kuinua kilimo chao, mapata yao, ili pengokati ya hao matajiri walichonacho na hawa amabaohawana tulipunguze badala ya kuongezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ya mwaka huu vilevilesuala la maji hasa vijijini kule, wakulima vijijini kule, pamojana fedha za awali, zile shilingi bilioni karibu 760, Serikaliimekubali kuongeza zingine za nyongeza, shilingi bilioni 184,ni ishara nzuri kuwakumbuka hawa wakulima vijijini, ndiyomaana bajeti hii naiunga mkono. Kwa hiyo, vijiji vyangu, ilemiradi iliyokuwa imekwamakwama kule, Mpapa kule,Chelejeho, Kitinku, Maweni, Ngaiti, kwa bajeti ya mwaka huuwatakumbukwa. Kwa hiyo, lazima niiunge mkono bajeti hii,nikiikataa maana yake sitaki hawa wote wapate maji.(Makofi)

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

121

Mheshimiwa Mwenyekiti, vi levile bajeti hiiimewakumbuka wakulima vijijini hasa kwenye suala laumeme, Serikali hii, pamoja na fedha za awali ambazozilikuwa zimepangwa karibu shilingi bilioni 153, imeongezashilingi bilioni zingine 186 ili umeme ufike mpaka vijijini. Ndiyomaana naiunga mkobo bajeti hii, ni ishara nzuri na mwakaniSerikali hii ya Chama cha Mapinduzi, tuwakumbuke tenahawa wakulima na wafanyakazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo ambalo lipo, nikwamba je, hizi fedha ambazo tumeidhinisha, zitafika zote?Maana hapa tunaidhinisha karatasi tu, je zitafika zote. Sasaili zifike zote, ni lazima makusanyo ya Serikali yawe makubwa,kwa sababu tusipokusanya, hii bajeti itabaki kwenyemakaratasi, tatizo letu bado liko katika makusanyo. Tatizo lakwanza, Watanzania tulio wengi, mtazamo wetu kuhusu kodi,bado ni mtazamo hasi, bado ni mtazamo wa kukwepakwepakodi. Sasa tunataka Serikali ijenge barabara, iboreshe elimu,iboreshe huduma za afya, itafanyaje bila mapato! Tunatakahaki, lakini wajibu wetu wa kulipa kodi bado tuko nyuma sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naiomba Serikali,hebu tuanzishe hasa elimu ya uraia kuhusu wajibu wa raiakwa Serikali yake. Haki zetu tunafundisha sana lakini je wajibu?Kulipa kodi ni sehemu ya wajibu. Mtanzania yuko tayari hatakumsaidia yule ambaye anakwepa kodi. Unafika dukani,anakwambia shati hili ukitaka risiti Sh.20,000, bila risiti Sh.18,000,mwizi huyu. Sasa wewe unafurahi Sh.18,000, lakini amekwepakodi huyu ambayo ingeongeza huduma za elimu, maji,umeme, haya ni mambo ambayo naomba Serikali tuzidisheelimu ili Watanzania tujue kwamba kulipa kodi ni kuchangiamaendeleo yetu wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika mapato, kunabaadhi ya vianzio bado Mheshimiwa Waziri hujakusanya vyakutosha. Kwenye sekta ya mawasiliano, mawasiliano ni sektainayokua kwa asilimia 20, lakini kuchangia kwenye pato laTaifa ili hela na sisi itufikie huku mitaani, imechangia asilimiambili tu, ndizo fedha ambao zimeingia kwenye pato la Taifa,

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

122

asilimia 98 zimekwenda wapi? Hujakusanya MheshimiwaWaziri. Naomba sana tazama, kama kuna sheria inayokuzuiausikusanye ama taratibu, ama mikataba, tulitazame ili eneohili litoe mchango stahiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, madini, Mheshimwa Wazirihujakusanya ya kutosha, ni ng’ombe ana maziwa mengi,lakini hujakamua yote. Madini kwa mwaka jana ni sektaambayo imekua karibu kwa asilimia nane, lakini mchangowa madini kwenye pato la Taifa ni asilimia tatu tu. Hujakamuavya kutosha hapo Mheshimiwa Waziri wa Fedha, tunaombaukamue ili tupate fedha nyingi zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini liko eneo lingine laardhi, hili ndiyo hujakamua kabisa, kwa sababu huyu ning’ombe ana maziwa mengi, hujamkamua kabisaMheshimwia Waziri. Ardhi kule India, kwa miaka mingi ilikuwandiyo chanzo namba moja cha kukusanya mapato ya Serikaliya India, kwa miaka mingi sana. Mpaka ardhi ikawa chini yaWizara ya Fedha, kwa sababu ilikuwa ndiyo chanzo nambamoja kuingiza mapato. Walichofanya India, ardhi yotewaliipima, wakamilikisha. Sasa ukishapima ardhi ndiyoumeipa thamani, kwa hiyo, yule unayemmilikisha sasa utatozakodi, kama ardhi hujapima, hujamilikisha, huwezi ukatoza kodi.Kwa hiyo, wakatoza kodi kwa sababu walipima na yulealiyepata hati mil iki alinaitumia hati mil iki i le, sasaanakopesheka, anapata mitaji, anapata mikopo,wanazalisha, Serikali inakusanya kodi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa kwetu, hatujapimaardhi yetu, ndiyo maana hukusanyi chochote katika ardhi,ukiondoa eneo la maji, ardhi sasa ambayo haina maji, nikaribu squire kilometers 800,000. Sasa kuzipima hizo lazimakutumia picha za satellites. Sasa hivi tunanunua, mwaka juzitulikuwa tunapima kule Wilaya ya Bariadi na kule Babati,kununua picha ya satellites ili upime ile ardhi ni ya ghali, Wilayambili tu zilitugharimu karibu mabillioni, je, sasa Wilaya 159 sijuibilioni ngapi! Ndiyo maana mwaka 2010, Bungeni hapaSerikali ilileta wazo na likakubalika, tuwe na kituo chetu

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

123

wenyewe cha kupokea picha za satellites, badala yakununuanunua, sisi wenyewe tuwe na kituo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lile wazo lilikubalika, lakiniMheshimiwa Waziri wa Fedha, hujatoa fedha kwa ajili yakuanzisha hicho kituo cha kupokea picha za satellites natukasema hicho kituo kijengwe hapa Dodoma (UDOM), ilipicha za kupima ardhi yetu tuzipokee hapahapa na kile kituovilevile kitawasaidia wanafunzi wa UDOM wanaosomeamambo hayo ya picha za anga, sasa hivi picha hizitunazinunua nchi za nje. Mwakani Mheshimiwa Waziri,tunaomba zile fedha kwa ajili ya kuweka kituo cha kupokeapicha za satellites, kijengwe, ni kama shilingi bilioni 15 na sizote zitatolewa kwa mwaka mmoja, unazigawa, kwa sababukile kituo hakijengwi kwa mwaka mmoja. Kuna baadhi yavifaa, ukiagiza leo utakipata baada ya miezi tisa. Kwa hiyo,katika miaka miwili unaweza kabisa kuanzisha kile kituo,tukatenga fedha za kupima ardhi, tukapima ardhi yetu,tukaimilikisha, ili uweze kukusanya mapato ya kodi ya ardhi.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa kengele ya pili.

MHE. JOHN Z. CHILIGATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Sasa NamwitaMheshimiwa Chacha Nyambari Nyangwine atafuatiwa naMheshimiwa Hilda Ngoye.

MHE. NYAMBARI C. M. NYANGWINE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi hii ili niwezekuchangia bajeti ya Serikali kwa mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kusemakwamba nitaunga mkono bajeti hii kwa asilimia 100 na vilevilenitumie nafasi hii kuipongeza Serikali ya Chama chaMapinduzi kwa mambo mazuri ambayo inayafanya, hata

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

124

kama wenzetu hawaoni, lakini inafanya mambo mazuri sana,barabara na vitu vingine vingi tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee suala laamani katika nchi yetu. Suala la amani katika nchi yetu likomikononi mwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi na walewote ambao wanavuruga amani, mimi naomba Serikali yaChama cha Mapinduzi ichukue hatua za makusudikuhakikisha kabisa kwamba amani inakuwepo katika nchihii ya Tanzania. Hilo ni jambo la msingi na kila mmoja wetulazima tulisemee na tulikemee kwa hali na mali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwanza nianze kwakuipongeza Serikali kwa kunisaidia katika mambo fulani fulaniTarime, hasa katika suala la barabara na umeme. Kuna tatizokubwa la maji, Serikali kwa sababu imeongeza fedha na juzinimeona wanazindua mradi wa maji kule Tarime, naombahizo fedha kwa kweli ziende Tarime, zitatue tatizo la maji,mambo yote yatakuwa ni mazuri hasa upande wa suala laafya na la elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee Tume yaBei nchini Tanzania. Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Waziriwa Mipango msikilize suala hili, hapa Tanzania hatuna Tumeya Bei na hali hii imepelekea kila mmoja kujiuzia jinsianavyotaka yeye mwenyewe. Kalamu hii utakuta kwenyeduka fulani inauzwa Sh.500, ukitoka duka la jirani inauzwaSh.2,000, huu ni wizi na hii ndiyo inayoleta matabaka katikanchi yetu. Tunaomba kwa kweli Serikali iamue, maanakupanga ni kuchagua, wale walioondoa Tume ya Beiwakasema kila kitu huria, kwa kweli siyo huria kwa kila kitu,tunaumiza watu maskini, naomba tuanzishe Tume ya Beiambayo itadhibiti kila kitu katika nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitakuwa tofautikidogo na wale Wabunge ambao wanasema kwambaWatanzania wasilipe kodi, nchi yoyote ile haiwezi kuendeleakama mtu halipi kodi. Yeyote anayefanya biashara alipe kodi,nasisitiza alipe kodi ndiyo tutaendelea, kwa sababu katikanchi yoyote ile tunazoziona zilizoendelea watu walilipa kodi.

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

125

Nenda kwa mfano China, wanalipa kodi ya Serikali, kila mtuanajituma tu kuhakikisha kwamba analipa kodi bilakulazimishwa, lakini sisi hapa mara tunaondoa kodi kwabaadhi ya watu, tuwasamehe kidogo lakini walipe, hapondipo wataona uchungu, lakini tunaposema kwambatunawaondoa kabisa kila kitu burebure, haiwezekani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema kwamba kilammoja alipe kodi, hata kama ikiwezekana, hata kuna baadhiya madhehebu ambayo yanafanya biashara, ikiwezekanawalipe kodi, kwa sababu haiwezekani mtu akaanzishadhehebu siku moja, ya pili, ya tatu unamwona ametajirika,TRA mnafanya kazi gani? Walipe kodi, hapo ndipo tutawezakujenga nchi na nchi ikaendelea, lakini kama tutakuwatunasema kwamba tunawaonea watu kulipa kodi, sijuitutarithi nchi ya aina gani ambayo tutaendelea kuiongoza.Naombeni tuhakikishe kabisa kwamba kila mwenye uwezowa kufanya biashara na anayefanya biashara na alipe kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inaenda sambamba namisamaha ya kodi kwa wawekezaji. Mheshimiwa Waziriwawekezaji wananisikia, wawekezaji wanatunyonya,naomba muwawekee sera ya kulipa kodi, hawawezi wakajawakachuma katika nchi hii, wakaondoka, wakaifanya nchiya Tanzania kama shamba la bibi, hilo kwa kweli MheshimiwaWaziri nasema hatutakubaliana nalo. Watu walipe kodi, hiyoitawezekana kama sisi tutakuwa waaminifu na tutakuwawatiifu, hali kadhalika tutadumisha uzalendo katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la rushwa katikaHalmashauri zetu ndilo linaloturudisha nyuma, linarudishamaendeleo yanchi yetu nyuma. Mimi naamini kabisa fedhazinazokwenda katika Halmashauri zetu, tukizisimamia vizuri natukajiamini, wale wanaokula rushwa, tukawashikisha adabu,siyo kuwafukuza tu na muwafungulie mashtaka muwafunge,kwa kweli hii Tanzania itaendelea. Sasa kuna kuoneana aibu,mtu akichukua rushwa kwenye Halmashauri, katika manunuzi,tunawaonea aibu. Naombeni tuhakikishe tunapiga vitarushwa kwa hali na mali. Yeyote anayechukua rushwa, kama

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

126

mnawaonea huruma sana, basi wanyongwe, itakuwa niheshima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, TRA inashindwa kukusanyakodi na Mheshimiwa Waziri nakuomba usikilize hapa, maanamnasema kabisa kwamba TRA imekusanya kodi lakini ni watuwangapi wanaolipa kodi hapa Tanzania? Tunao Watanzaniawangapi? Watanzania tuko milioni 45 halafu leo hii tunasemakwamba tunakusanya shilingi bilioni 500 kwa mwezi. Mimininaishauri Serikali ihakikishe kabisa TRA inakusanya mapato.Kuna rushwa kuwa sana TRA. Kila Mbunge aliyechangia hapautasikia anasema TRA kuna rushwa, ni kwa nini msifanyemabadiliko makubwa sana TRA. Hata ikiwezekana kama nikuivunja muivunje na kuanzisha Kitengo kingine ambachokitakuwa na watu waadilifu ambao watakuwa tayari kuiteteanchi yetu.

Mheshmiwa Mwenyekiti, suala la maliasil i zi letulizonazo mfano utalii, madini, misitu bahari, mito maziwa,gesi, bandari, hata viwanja vya ndege na hata ndegezenyewe kama ikiwezekana tununue, itasaidia sana kuinuapato la uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ninaomba niulizeWaziri anayehusika na Mpango wa Taifa, naomba wataalamwetu watueleze kwa nini uchumi wa nchi yetu unakua lakiniWatanzania walio wengi ni maskini? Vilevile Waziri atuelezeni kwa nini nchi yetu ni maskini mpaka sasa hivi, tunatakamajibu sahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ninaomba Wazirianayehusika na Mpango wa Taifa wa Maendeleo atueleze,ni lini Serikali itajenga Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere kuleButiama. Maana toka tumepitisha bajeti ya mwaka 2011mpaka sasa hivi ni ahadi zinatolewa lakini utekelezaji hakuna.Tunaomba Mheshimiwa Waziri atujibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, naombakuwambia Watanzania kwamba tuache kulalamika, tufanyekazi. Zamani nilikuwa ninaona Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

127

Mikoa wanasisitiza kila mtu afanye kazi. Imeandikwa hatakwenye Biblia na Vitabu Vitakatifu kwamba asiyefanya kazina asilie lakini kwa sasa hivi tumejenga tabia mbaya ya kilamtu kukaa na kulalamika, hafanyi kazi anafikiri kwambaSerikali itamfanyia kazi. Kwa hilo, tunawaomba viongozi waSerikali, wale wote ambao wanawashawishi Watanzaniawasifanye kazi wachukuliwe hatua. Watanzania wafanyekazina kila mmoja atimize wajibu wake na hii Tanzania itabadilika.Watu hawafanyi kazi, muda mwingi ni kulewa tu tanguasubuhi, saa mbili asubuhi unakuta mtu amelewa, shambanihaendi, sasa wanafikiri Serikali itampelekea kila mtu hela?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli Watanzaniawenzangu tujenge tabia ya kufanya kazi na sana sanatusisitize kilimo. Kilimo bado ndio uti wa mgongo wa Taifaletu, lazima tuhakikishe Watanzania wanalima,wanajitosheleza kwa chakula, mambo mengine ndiyoyafuate. Tatizo sasa njaa ipo, watu hawafanyi kazi,wanategemea Serikali ipeleke chakula, kwa kweli kuendeleaitakuwa ni kazi kubwa sana. Mimi ninarudia kusema kwambaWatanzania, hata kama ni kuwalazimisha walazimishwe.Wenyeviti wa Vitongoji, Mabalozi, mpaka Wakuu wa Wilaya,wanafanyakazi gani? Hebu wahakikishe kwamba wakikutawatu wako vilabuni saa mbili asubuhi, kamata, weka ndanibaada ya hapo sheria itafuata na watu watafanya kazi nahii nchi itaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalize kwa kusemakwamba, nchi hii ni ya kwetu, tuna wajibu wa kuilinda kilammoja wetu. Yeyote yule ambaye anategemea kwambayeye ataweza akaingia au akasaka madaraka kwa kutumiavita, sisi vijana wa Watanzania tunasema kabisa kwambahatuwezi tukakubali. Kama ni demokrasia, nenda kauze serazako, ukiziuza barabarani ukashinda sawa lakini utegemeekwamba uingie kwa kutumia vita, kwa kushawishi watuwanafanya maandamano badala ya kukaa na kufanya kazi,ninasema kabisa kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduziifanye kazi na itemize wajibu wake kwa raia. (Makofi)

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

128

Mheshimiwa Mwenyekit, baada ya kuyasema hayo,naunga mkono bajeti hii kwa asilimia 100. (Makofi)

MWENYEKITI: Ninakushukuru sana MheshimiwaNyambari Nyangwine kwa mchango wako. Sasa namwitaMheshimiwa Cynthia Hilda Ngoye, atafuatiwa naMheshimiwa Omari Rashid Nundu na Mheshimiwa YahyaKassim Issa ajiandae.

MHE. CYTHIA H. NGOYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Awali ya yote,naomba kuunga mkono hoja hii asilimia mia (100%). (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, naomba niipongezeSerikali kwa kukubali kuongeza fedha katika sekta zile muhimuambazo zinagusa wananchi. Zimetajwa kama kilimo, nishativijijini, maji na Kadhalika. Naomba tu niseme kwambanimejenga matumaini, maadam suala la nishati vijijinilimewekwa katika msisitizo mkubwa, naamini kabisa vile vijijivyetu vya kule Mkoani Mbeya, hususan Wilaya ya Rungweambavyo tumekuwa tukiviombea kila mwaka sasa vitapataumeme. Kama mjuavyo, Mkoa wa Mbeya ni mkubwa sanana unazalisha kwa kiwango cha juu sana, naamini sasa kwamazao ambayo yanalimwa kule yatapata nafasi yakusindikwa hukohuko vijijini na kuongezwa thamani nakusafirishwa nje ya nchi kwa kutumia uwanja ndege waMbeya wa Songwe, ambao umeanza kufanyakazi hivikaribuni, nashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ninaona kuna fedhakidogo ya barabara imeongezwa, naamini barabara ya lamiambayo tumekuwa tukiiombea fedha kila siku hapa yaKatumba, Rwangwa mpaka Tukuyu, sasa itajengwa. Haya nimatumiani yangu na ninawaombea sana wale Mawaziriwanaohusika wafanye kazi zao vizuri na tutawaonga mkonokwa asilimia mia (100%). (Makofi)

Mheshimwia Mwenyekiti, naomba sasa niende mojakwa moja nizungumzie hoja ambayo iko mbele yetu. Nianzena Sera ya Mapato. Nashukuru kwamba Serikali imepokea

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

129

mapendekezo ya Labs ya namna ya kuongeza mapato yaSerikali. Kuna pendekezo moja ambalo moja kwa mojaSerikali imekubali, nalo ni pendekezo la uvunaji wa vitalu vyamisitu kwa njia ya mnada. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi sina tatizo na hilo lakininachoamini hapa, ni kwamba tunachotazamia ni Serikaliipate fedha za kutosha. Kwa hiyo bidders wakubwa ambaowatatoa fedha nyingi ndiyo watakaofanikiwa. Vilevilenachokiona mimi bidders hawa ni wale ambao watakuwana uwezo mkubwa kifedha, kwa hiyo wata-bid kwa helanyingi, lakini nina uwoga wa aina mbili. Moja, hatutapatabidders ambao ni wananchi wa Tanzania wa kawaida. Haona mimi naamini kabisa watashindwa kwa sababu hililitakimbiliwa kwelikweli ninavyoona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watakuja hapa watu wenyehela zao wata-bid kwa viwango vikubwa sana nawatashinda na tutapata fedha, hiyo sina tatizo lakini mimihapa ninaona kuna jambo moja kubwa sana kwangu mimininavyoliona, ambalo linaweza likatokea na litatokea, kwasababu hawa wawekezaji watakuwa wameshapata misituya kuvuna, woga wangu ni kwamba suala la mazingira hapahalijatazamwa vizuri. Hawa watakuwa na interest ya kuvunamiti ili wapate fedha. Suala la mazingira they have noconcern na hilo kwa sababu wanachotaka ni fedha. Kwahiyo, ninaomba Serikali ituambie, itaweka utaratibu gani wakuhakikisha kwamba suala la mazingira pale, hii misitu yotehaiondelewi, tukaachiwa jangwa. Kwa sababu ni kweliwatavuna miti wataondoka, watakwenda zao lakini sisitutaachiwa jangwa halafu na sisi suala la mazingira linatuathirisana, tena sana. Ukame tumeshaanza kuuona, uhaba wamaji tunauona, uhaba wa chakula tunauona, je, Serikaliitaweka mikakati gani? Nachotazamia hapa lazima kuwepona sheria na kanuni ambazo zitasimamia uvunaji huo wamisitu kwa njia hiyo ambayo imewekwa na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili nalisema kwa msisitizo,kwa sababu hata uvunaji wa kawaida ambao siyo wa misituhii ambayo inasimamiwa na Maliasili, watu wanavuna miti

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

130

bila usimamizi wowote, wakiambiwa waende wakakate miti,wanakata wanavyotaka wao, hawajali miti midogo wala mitimikubwa. Hiki kizazi tunachokilea kinaenda wapi natunakiachia nini hapa Tanzania kama tunaangalia tu sualala fedha bila kuangalia huko tunakokwenda, tunafanya nini?Hapa tunagombana kila siku, kila mtu anadai maji kwa nguvukabisa, sina maji, sina maji au kwangu vimechimbwa visimahakuna maji yanayoonekana. Jawabu ndiyo hilo hakunamaji ni kweli tumeharibu mazingira kwelikweli. Hili miminimeliwekea woga huo lakini Waziri atakapokuwa anajibuatuambie Serikali kupitia Wizara inayohusika, itaweka mkakatigani wa kusimamia jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende moja kwa mojakwenye suala la Marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato,Sura ya 332. Wengi wamelizungumzia suala hili na mimininaomba nilizungumzie vilevile. Tumekuwa tukipatamalalamiko makubwa sana kutoka kawa wafanyakazi wakati, wafanyakazi wa chini, mishahara yao ni midogo kwasababu kodi inayokatwa ni kubwa. Sasa hapa leotunapunguza kiwango cha asilimia moja tu, kweli hii haiji.Naomba Serikali ilitaazame na mimi sitaki kuliachia hivihivikwamba Serikali ilitazame, mimi naenda moja kwa mojakushauri kwamba twende basi mpaka asilimia kumi (10%),tuanze nalo hilo ili hawa wafanyakazi wapate unafuu nawenyewe sasa tuwaambie ongezeni bidii ya kufanya kazikatika maeneo yenu, kwa sababu Serikali imewapenda,imewateremshia hata kodi ya mapato, wataongeza bidii yauzalishaji katika maoeneo yao kazi. Kwa hiyo, naomba Serikaliiende ikaliangalie hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua hapa nitaulizwa sasatunapata wapi fedha nyingine? Ni kweli swali hili ni la msingi,tunapata wapi fedha nyingine. Katika hotuba hizi zotezilizotelewa suala la Kilimo Kwanza na masuala ya SAGCOThayajapewa uzito unaotakiwa hata kidogo. Sasa tunahamiakwenye Labs, huku kwenye Kilimo Kwanza, kwenye SAGCOT,tuko a bit silent, hakuna herufi kubwa tunayoiweka ili kuwezakuzungumzia na kuona suala la kukuza uchumi katika masuala

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

131

haya. Vilevile kwenye SAGCOT ambako tunatazamiauzalishaji mkubwa wa chakula, tusihitaji kuagiza chakulakutoka nje, halizungumziwi sana lakini kuna mikakati gani yakuliwekea suala hili uzito ili kuongeza uchumi wa nchi, ilikuongeza uzalishaji wa chakula katika nchi hii, tumechokakuombaomba chakula kutoka nje. Chakula kutoka nje siyokitamu hata kidogo, chakula chetu hapa nchini ndiyo kizuri,chetu ni kizuri kwa sababu ni fresh lakini kile kimekaa miaka20 mpaka 25, unaletewa Mtanzania ndiyo ule, kweli ni hakihiyo kweli? SAGCOT ndiyo kimbilio letu. Nashauri kwa uzitomkubwa Serikali ije hapa na mipango thabiti ya kuinuamkakati huu wa SAGCOT. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha katika eneo hilihili lakilimo, hao vijana wetu kutoka Sokoine, bado hatujawatumiavizuri, ninasemea Sokoine peke yake, lakini kuna vyuo vingineambavyo ni vya Advance Diploma au Diploma auCertificate, bado tunasitasita namna ya kuwatumia. Hawandiyo wataalam watakaongeza uzalishaji wa kitaalam iliuzalishaji uwe mkubwa katika nchi hii na tuweze kuwa nafedha ya kutosha, both kiuchumi lakini vilevile tujitoshelezekwa chakula. Watalaam tunao, tunawalipia kiwangokikubwa cha fedha wengine miaka mitatu (3), wengine miezitisa (9), wengine miezi sita (6) lakini hatujawatumia vizuri. Tujehapa na mkakati. Serikali ituambie ni namna gani kuanziasasa hawa watu tutawa-diploy huko viji j ini, waendewatusaidie kwa nguvu moja ili nchi hii iweze kwenda mbele.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwakunipa nafasi hii, niliona haya machache niyachangie.Naunga mkono hoja hii kwa asilimia mia (100%). Ahsantesana. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukru sana Mheshimiwa CynthiaHilda Ngoye. Waheshimiwa Wabunge, sasa naomba nimwiteMheshimiwa Omar Rashid Nundu na Mheshimiwa YahyaKassim Issa ajiandae.

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

132

MHE. OMARI R. NUNDU: Mheshmiwa Mwenyekiti,ninakushukuru sana. Nianze kwa kuisifu safu ya Mawaziri waWizara ya Fedha, kwanza, kwa ushirikiano wao mkubwa nakazi kubwa wameifanya katika kipindi hiki kifupi. Uthibitishowa hayo ni kuwa watu wa Magaoni huko Tanga waliokuwawakidai fidia zao RAHCO, wamelipwa majuzi hivi. Barabaraya Horohoro imefunguliwa na wale waliokuwa wakidai fidianao wamelipwa. Sasa hivi mradi wa maji unaendelea kwenyevijiji vya Geza, Kirare, Mapojoni na Mgwisha. Pesa za Hospitaliza Wilaya zimetolewa, hospitali inajengwa, lakini naombaziongezwe ili imalizike upesi iwezekanavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumebakia malipo ya EPZ,sehemu ya Nema, ambapo sehemu hii iliunganishwa naKurasini, Bagamoyo na Kigoma, kama sehemu ambazozingelipiwa malipo mwaka huu 2013 kabla ya mwezi Junihaujafika. Naomba hili lifanyiwe bidii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika orodha ya vijijiambavyo vinapata umeme, pamoja na kuwa iliamuliwamwaka 2012, nguzo za umeme zinapopita vile vijiji vyoteambavyo viko katika mtiririko huo vipate umeme lakini badovijiji vya Wilaya ya Tanga, Bagamoyo, Kirare, Mapojoni,Mgwisha, Kisimatui, Mikweni, Mikocheni na vingine havijapataumeme. Nategemea hili litafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa pongezi kwa mfumohuu mpya wa bajeti. Nilisema hivyo nilipochangia Wizara yaFedha na ninarudia, mimi nikiuangalia ni kama speech yaGFK tarehe 15 Julai, 1960 ya New Frontier. Tuko kwenye NewFrontier, yeye aliishi kwenye Urais kwa siku 1,036 tu lakinimatokeo ya vision yake mpaka leo tunayaona yanaendelea.Sasa hii iwe ni New Frontier, twende huko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna vipaumbele. Katikavipaumbe hivi vilivyotajwa kimoja naona kinahusu Wizara hiimoja kwa moja, kile cha kuongeza mapato lakini niongezeeikiwa ni pamoja na kudhibiti matumizi. Sasa mimi ninatakanikiongelee hicho. Nchi yetu tumebahatika tunao wananchitakriban milioni 45 kwa sasa lakini wengi wa wananchi hawa

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

133

shughuli wanazofanya hazina tija, wanabangaiza tu,wanauza vitumbua, wanauza maandazi ili waweze kuishi,wanaendesha bodaboda.

Mheshimiwa Mwenyekiti nilipochangia kwenyeWizara ya Fedha nilizungungumzia suala la bodaboda,nikushukuru hapa kuwa ulielewa na umeondoa ada za leseniza bodaboda hizo, pamoja na pikipiki nyingine na bajaji.Lengo langu lilikuwa siyo hilo, lengo langu katika hii NewFrontier tunaibuaje walipa kodi wa uhakika hapa nchini,tunafanya nini kupata critical mass ya watu ambao watalipakodi? Unapomlipisha kodi hata iwe ndogo kiasi gani, mtuambaye biasahara anayoifanya kwanza ni ya hasara, nimatatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa niwashukuruWabunge wote ambao kwa njia moja au nyingine katikamichango yao wameunga mkono hatua ulizochukua kwakuondoa ada za leseni za bodaboda lakini kwa wale ambaohawajaelewa, labda nilieleze hili kinagaubaga kidogo.Ninalielezea hili kama mfano tu wa biashara nyingi ambazokutendwa kwao ni hasara tu. Watu inabidi wafanye ili wapatevihela vichache vya kuweza kuendeleza maisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukichukua ukurasa wa 67 wahotuba ya Waziri, amesema kwamba mapato ya jumlayasiyozidi shilingi milioni 2,040,000/= haya hayakatwi kodi.Ukigawanjya kwa siku 365, hicho ni kipato cha shilingi 5,500/= kwa siku. Kule Tanga ndiyo pesa ambazo mwenyebodaboda anapokea kutoka kwa dereva, Sh.5,500 kila sikulakini fedha hizi ndiyo hizohizo ambazo amortisation yabodaboda ile inatakiwa itokee, maintenance ya bodabodaiwe humo, kununua matairi ya bodaboda iwe humo,gharama ambazo zinafika karibu Sh.4,000/= anabaki naSh.1,000/=. Wale ambao wana shughuli nyingine wakibaki naSh.1,000/= kama hiyo kama ndiyo pesa za kujilipa walahawajafikiria kuweka kando pesa za kuweza kununuabodaboda nyingine ili biashara ikue, wataona kuwa biasharahii wanaweza kuifanya lakini wale ambao hawana kipatokingine haiwezekani. Fedha hizi kwa kiwango cha makusanyo

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

134

ya bodaboda kwa Tanga ni kuwa yule dereva anabaki naSh.6,000/=, kijana akibaki na Sh.6,000/= alipie chumba, alena aweke pesa za kujiendeleza, haiwezekani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimelifanyia uchunguzi sualahili na nimekaa na bodaboda karibu vikao vitatu kuongeanao. Kuna mtu hapa siku niliyochangia akasema kwambamimi nina bodaboda 15, sina bodaboda hata moja lakininina bodaboda 300 za vijana wangu Tanga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekaa nao,nimewafanyia hesabu, kuendesha bodaboda mojainagharimu zaidi ya shilingi milioni saba kwa mwaka, lakinikipato cha bodaboda Tanga cha Sh.16,000/= kwa siku niSh.5,600,000/=, kuna hasara hapo ya zaidi ya Sh.1,000,000/=.Narudia, bodaboda ni kitengo kinachojitegemea, kilabodaboda moja ikipata hasara hivyo ukiwa na kumi unahasara ya shilingi milioni kumi. Kwa hiyo, hii inaonyesha wazikuwa kama hawa wasiposamehewa kodi na inaonekanahapa mpaka ikifika shilingi milioni kumi ya mauzo kwa mwakainabidi wasamehewe kodi na wasiposamehewa kodi baadaya muda mfupi hizi bodaboda zote zitakuwa kwenye vijiwena biashara hiyo itakuwa imekufa. Kwa hiyo, naomba Wazirialiangalie suala hili. Mimi nimefanya utafiti huu na utafiti wawauza karanga pia, siku ile nilitaja hapa, lakini napendawengine wote waangalie ili mwisho wa siku tuibue watuambao kweli wanaweza kulipa kodi na wakaweza kuishi.Nasema hivyo kwa sababu, wapo watu ambao wanawezakulipa kodi lakini hawalipishwi kodi zinazostahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naona bado watuwanaoleta gari za utalii wanasamehewa kodi. Nimesemabiashara ya bodaboda sijafanya wala sitafanya lakini yadaladala nilijaribu mwaka 1998 nikiwa niko nje, nilinunuadaladala nne kutoka Simba Tours nawajua hata watuwenyewe, vika–operate pale Arusha maana mimi makaziyangu pia yapo Arusha. Nil ipovinunua Simba Toursnikaambiwa nilipe ushuru ambao wao hawakulipishwa lakinimimi nikalipishwa, tena wakauchukua wao ushuru ule halafuhawakuulipa, vidaladala vile vikasimamishwa njiani, biashara

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

135

ile niliiacha mapema sana. Nilijaribu viwili vingine Tangamambo hayohayo, zile biashara jamani watu wanaganganjaa ndiyo maana unakuta mtu anapostaafu akaendeshabodaboda kama hakuendesha mwenyewe baada ya mudabodaboda hakuna anapata shida.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Na yeye mwenyeweanakwisha.

MHE. OMARI R. NUNDU: Na yeye mwenyewe piaanakwisha kama anavyosema Mheshimiwa Ndassa, sasa hiloni lazima liangaliwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati tunafanya hivyo,watu wanaotoka nje kuja kuanzisha biashara hapawanapata mkopo benki na riba ile kubwa wanasamehewaushuru miaka mitano. Kwa hiyo, ile mambo ya riba ya benkihaiwa-affect kabisa wao. Tunafanya affirmative action kwawatu ambao siyo Watanzania, siyo sawa! Wote wanaokujakuanzisha biashara nilisema na ninarudia hapa kwetu kamawanakuja kujaribu watozwe tozo zile ambazo zinastahilikuwatoza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuaongelea hilo,siyo misamaha tu, hii mikataba tunayoingia lazima tuwewaangalifu sana. Wengi wamesema kuhusu bandari zetu namimi nilikuwa najaribu kukwepa sana kuongelea mambo yauchukuzi lakini inabidi wakati mwingine niliongelee, hasabandari ya Dar es Salaam. Tangu mwaka 2008 tulisematunajenga Gati 13 na 14. Wakajiingiza hawa CCCC tangumwanzo, wametuchelewesha kujenga Gati ile mpaka leo.Mwaka jana watu waliongea hapa mpaka walitoka mapovukuwa lazima Gati ile iwe imejengwa Juni, 2012 halafupakanyamaza kimya. Juzi hapa tunaambiwa wale CCCCkwa sababu PPRA waliwakataa basi tunawaacha kandotunapata mwekezaji mwingine anaitwa CHEC. Ukiendakwenye website ukisoma kuhusu CHEC inakwambia moja kwamoja kwamba hii ni subsidiary ya CCCC. Tena zipo tatu niCHEC, Bridge and Roads na CCCC yenyewe. Hii CHEC

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

136

ilianzishwa mwaka 1980 lakini mwaka 2005 ikajiunga na Bridgebaada ya Bridge kupata matatizo kule Phillipines kamaambayo yamepatikana hapa ndiyo waka-form CCCC naukweli ni kwamba hata ingepewa hii CCCC hii CHEC ndiyoambayo ingejenga kwa sababu inasema wazi hapa kuwaCHEC ndiyo International Operating Division of CCCC group,leo naona bado CCCC inapigiwa debe. Sasa PPRAwafanyaje? Waisimamishe na CHEC nayo? Ndiyo maanavitengo vyetu hivi wakati mwingine vinalalamika kuwahavipewi nguvu ya kufanya kazi tunavikatisha tama.Nitaangalia PPRA wata-react vipi kwenye jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanga tuna viwanda nakimoja ni kiwanda cha cement ambapo vipo kwingine pia.Mwaka juzi hapa tulipoomba tupewe idadi ya walipa kodiwazuri Tanzania viwanda vya cement vilikuwa ni vimojawapona hasa kile cha Tanga. Viwanda hivi sasa hivi vinazalishatani karibu milioni 3,700,000...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa, hiyo ni kengele ya pili.

MHE. OMARI R. NUNDU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana. WaheshimiwaWabunge, naomba sasa nimwite mchangiaji anayefuatiaambaye ni Mheshimiwa Yahya Kassim Issa atafuatiwa naMheshimiwa Silvestry Francis Koka na Mheshimiwa ZarinaMadabina ajiandae.

MHE. YAHYA KASSIM ISSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili na mimi niwezekuleta mawazo yangu katika Bunge hili. Kwanza, sina budikumshukuru Waziri pamoja na Manaibu Waziri wake wawilikutokana na jitihada wanazozifanza ili kufanikisha shughulizetu za bajeti. (Makofi)

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

137

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania tatizo kubwaambalo linatukabili ni ubinafsi na haya yote tunayozungumzahapa na mipango ambayo tunaipanga pasi na kuondoaubinafsi, hatuwezi kufanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta nyingi kwa waleambao tunawapa dhamana, kwa kweli hawatekelezi vizurikubwa anatazama maslahi yake ya baadaye. Kutokana nahali hiyo, hatuwezi kufanikisha kwa sababu hakuna sababuTanzania hadi leo kuwa tegemezi kwa misaada kutoka nchiza nje, hakuna sababu. Hii mimi binafsi, nilikuwa na rafiki yangummoja Mzungu, tulitembea sana katika sehemu mbalimbalina akaiangalia Tanzania, alishangaa sana kwamba mpakaleo sisi tunataka misaada kutoka nchi za nje yaani anahisikwamba rasilimali za kutuendesha tunazo lakini tatizo kubwalililotukabili na ambalo limetutawala ni ubinafsi. Katikauchukuaji wa hatua kwa wale ambao wanaokwendakinyume, tunakuwa wanagezi sana kuweza kuchukua hatuaambapo suala hili nalo linaturudisha nyuma yaani hapatunaendesha mambo yetu kiujamaa sana. Hali hii hatuwezikufika! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tuna wajibu wakufunga mkanda ili kuweza kufanikisha mambo yetu hayaambayo tunayapanga kwa sababu sasa hivi tunapangabajeti lakini mwisho wa mwaka hapa utasikia kwamba Wizarafulani fedha haikupata au imepata nusu yake. Tujiulize kwanini?

MBUNGE FULANI: Na hizo zilizopatikana zimetumikaje?

MHE. YAHYA KASSIM ISSA: Na hizo zilizopatikanahazikutumika vizuri na hapana hatua zozote zinazochukuliwa.Sasa hali kama hii tutakuwa bila shaka tunakula fedha zawananchi lakini hakuna litakalokwenda. Kwa hiyo,Watanzania tuna wajibu wa kujirekebisha, kasoro zetu tuwezekuziondoa hapo tunaweza kufika mahali pazuri. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Na kila mtu afanye kazi.

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

138

MHE. YAHYA KASSIM ISSA: Na kila mtu ana wajibu wakufanya kazi na hili ndiyo jambo ambalo Watanzaniatunakuwa na matatizo, ni wavivu. Ninyi mnakwenda nchimbalimbali nje ya nchi, hebu tuangalie wenzetu ni namnagani wanavyoendesha shughuli zao. Asubuhi utaona watuwanafanya kazi na mchana pia wanaingia wengine mpakajioni na wengine jioni mpaka usiku na mimi nilitegemea mezaza mbele huko mnakwenda nchi mbalimbali yalemnayoyapata kule mtayaleta huku ili kufanikisha lakinimatokeo yake hakuna! Hali hii hatuwezi kwenda! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijana tuna taratibu nyingiza kuwafanikisha, tuna ardhi ya kutosha, tuna bahari yakutosha lakini hakuna linalofanzikana, sasa lazima vijanatuwaweke pamoja kwani hizi ndiyo nguvukazi. Vijanatukiwaweka pamoja katika shughuli za uvuvi, kilimo nakadhalika, tunaweza kufanikiwa. Pasina kufanya hivyo si kweli,tutakuja hapa, tunaondoka lakini hakuna litakalokuwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kuna haja gani vibuakuletwa kutoka Afrika Kusini? Hawa ni samaki aina ya vibuakule kwetu tunawaita vibua, kuna haja gani ya kuleta vibuakutoka Afrika Kusini? Bahari tunayo ya kutosha, vijana wapowa kutosha, vyuo vya uvuvi vipo, lakini kwa nini iwe hivyo?Kwa nini tusijiandae tukasema kwamba sasa hivi tunatafutavyombo vinavyostahili ili kuweza kufanikisha mambo yetu,kwa nini tusifanye hivyo? Ndiyo maana Mzee akasema wakatihuo bado hata madini kuchimbwa kwa matatizo kama haya,sasa watakaofaidika ni wale wa nje. Wale wa nje hawawezikuja huku ila wana haja na wako katika uchumi, sasa waobila shaka watataka mapato, sasa ikiwa tunakwenda kamahivi hatuwezi kufanikisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais wetu wa kwanzaaliyefariki, Mwalimu Nyerere siyo ilikuwa kwamba wakati huomadini hayapo lakini aliona muda bado na haya ndiyomatatizo tunayoyapata, muda bado, tuna haraka na ndiyopale niliposema kwamba ubinafsi umetushika. Mfadhilianakuja wewe umepewa dhamana, unapanga naye,unazungumza naye, una hakika kwamba hisa fulani utapata,

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

139

kwa hiyo, unachukua kila njia kuhakikisha kwamba mahitajiyake mwekezaji yule yanakwenda kwa sababu na weweunapata chochote, hatufiki! Tukubali kwambatunawaongoza wananchi, tukubali kwamba tunawaongozawnaanchi na tunakuwa na dhima na tutakwenda kuulizwambele ya safari, tumewaongoza vipi watu wetu? Fedhandugu zanguni mtaziacha hapahapa duniani! (Makofi)

MBUNGE FULANI: Waambie!

MHE. YAHYA KASSIM ISSA: Hao wenzetu labda sisihatutumii masanduku lakini kweli ninyi mnatiliana pesa? Kwelimnatiliana mapesa kwamba katumie unakokwenda? Sasahammwogopi Mungu? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bodaboda, tunataka kutoaelimu, vijana wetu kweli tumejikubalisha, tumeondoa kila kitujuu ya bodaboda, lakini hebu tutazame namna ya vifovinavyotokea vya bodaboda. Wiki mbili Area C na Area D,vijana 20 wamepoteza maisha. Sasa hili suala inabiditulizingatie na wapo bodaboda wanaendesha hawana hataleseni. Sasa tuliangalie, je, haya mapato ndiyo yatakwendaikawa siku zote sisi tunatibu watu tu Muhimbili? Wapitunawapeleka, kweli tutafanikiwa? Lazima iwepo taalumamaalum kwa vijana wetu, sisi tuliangalia pamoja tu kwambatuna ajira lakini ajira ambayo kifo mbele ni ajira gani hiyo?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sasa tuhakikishekwamba vijana wetu wanapata taaluma ya kutosha naAskari wetu wahakikishe kwamba wanafanya kazi ya kutosha,waelimishwe kwa kanda maalum na kwa kila sehemu, tukifikahapo tunaweza kwenda vizuri. Gari zina speed zakezil izowekwa lakini bodaboda hakuna speed, vi janawanakwenda vibaya sana na akina mama ndiyo wateja waowakubwa, kabisa suala hili inabidi tulirekebishe, tukifanyahivyo nahisi tutafika mahali pazuri.

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

140

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kodi, vijana wengihapa wamesema kwamba tupunguze kodi, tutapunguza vipikodi na kodi ndiyo inayoleta uchumi wa nchi yetu?

MBUNGE FULANI: Bila kodi hatutakwenda.

MHE. YAHYA KASSIM ISSA: Bila kodi kweli tutakwenda?

MBUNGE FULANI: Hatutakwenda.

MHE. YAHYA KASSIM ISSA: Mtu anasimama hapaanasema vinywaji vipunguzwe, vinywaji ni kitu cha starehena huwezi kustarehe kama huna nafasi, mtu anastarehe kwakupata nafasi, mambo yamemnyookea.(Makofi)

MBUNGE FULANI: Starehe gharama.

MHE. YAHYA KASSIM ISSA: Na starehe ni gharama!Sasa masuala haya nahisi hapa si ya kuzungumza kama watuwazima. Mimi kama mngekuwa mnasema kwambatupunguze kodi kwenye tax ningekubali kwa sababu tax hivisasa kwa kweli zimetawaliwa sana na bodaboda, hawanakazi.

MBUNGE FULANI: Na bajaji.

MHE. YAHYA KASSIM ISSA: Wametawaliwa nabodaboda na bajaji, kwa hiyo hawana kazi. Kwa hiyo,tungesema hawa tuwapunguzie mzigo kwa sababu uchumiwao ni mdogo lakini vinywaji, vinywaji mwenzangu mamboyamekunyookea, mambo yako yamekwenda vizuri, pesaunazo mfukoni na nyingine zimebaki, ukitaka starehe nigharama! Ukitaka starehe ndugu yangu gharama,Mheshimiwa Mkuchika unajua hayo. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa kila mwaka tunakulahasara kutokana na mambo yetu ya barabara na hii nikutokana na tatizo la kutokuwa na reli sehemu husika. Mizigoinakuwa mikubwa na nchi yetu tunaijua tunaweka sehemuzile hata ikiwa mzigo mkubwa wakati mwingine unapitishwa.

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

141

Mtu akishapata chochote anamwambia nenda lakini hukubarabara zinaharibika. Sasa tuna wajibu wa kukuza njia zetuza reli ili kuweza kuondoa matatizo haya. Kkila mwakabarabara...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MHE. YAHYA KASSIM ISSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa YahyaKassim Issa kwa mchango wake na hasa kwa kusisitiza sualala starehe ni gharama lakini sasa sijui huo usisitizaji wako unamisingi ipi lakini tumepokea ujumbe huo.

Waheshimiwa Wabunge, nilisema atakayefuata niMheshimiwa Zarina Madabida atafuatiwa na MheshimiwaSilvestry Koka na Mheshimiwa Clara Mwatuka ajiandae.

MHE. ZARINA S. MADABIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ili na mimi nitoe mchango wangumdogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa na naombaniwapongeze Chama cha Mapinduzi kwa ushindi mzuri,hususani Temeke, Mianzini kwa kuchukua kata yetu kiulainipamoja na kwamba watu kutoka Kawe na Ubungowalikwenda kuchukua gesti na kulala hukohuko.Nawapongeza sana Mianzini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nimpongezesana Mheshimiwa Spika, kwa utaratibu huu mpya uliokujawa kujadili bajeti. Kwa kweli sasa hapa tunaongezea nyamalakini bajeti tumeijadili kwa kina. Niipongeze sana Serikali kwakuweza kukubali mapendekezo mengi sana ambayoyalitolewa na Waheshimiwa Wabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeisoma bajeti ni nzurisana, nampongeza Mheshimiwa Waziri na Manaibu wake

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

142

kwa kuweza kuandaa bajeti nzuri. Kusema kweli ile nyongezailiyofanywa itatoa tija nzuri ya umeme kwenye vijiji, maji,barabara Dar es Salaam na kote nchini, kwa hiyo,nawapongeza sana kwa hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo ninayomachache kidogo. Jambo la kwanza, ni ongezeko la kodikwenye petroli na dizeli. Pamoja na kwamba ongezeko hili nidogo, lakini unapoongeza kodi kwenye petrol na dizeliumeongeza karibu kila kitu. Unasema kwamba ni ndogo lakiniyale magari yanayobeba mizigo na abiria ni makubwa, kwahiyo, ni lazima kila kitu kitapanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba waliangalie upyasuala hili la ongezeko la kodi katika petroli. Nina hakika kabisakama watu wakijipanga vizuri katika kukusanya kodi, kunamahali ambapo tunaweza kufidia. Nimepeleka mchangomwingine wa maandishi ambao nimetoa mifano michachena Waheshimiwa Wabunge wengi wamezungumza kuhusuhilo. Naomba hilo liangaliwe sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu nyingine ambayonimeomba iangaliwe sana ni kurudisha VAT katika utalii. Utaliiunaingizia nchi hii pato la takribani dola bilioni 1.5 kwa mwakana pia inachangia kati ya asilimia 17 na 19 ya pato la nchiyetu, lakini tuna ushindani mkali sana kutoka nchi jirani.Ongezeko linaweza likafanywa lakini kuongeza ghaflainaweza ikatuletea matatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa wazo kwamba hatuaya kuondoa VAT isiwe ghafla, lakini waiangalie ni jinsi gani ileVAT itaathiri utalii wetu uki-compare na nchi nyingine. Kwanini nasema isiwe ghafla? Wenzetu wa Ulaya wanapotakakwenda kufanya utalii ambapo wanakuja huku Afrika, mtuanajiwekea fedha kidogo kidogo kwa mwaka mzima,anamlipa agent wa tours na wale wanakuwa wamefanyabooking ya mwaka mzima. Sasa unapoongeza VAT ghaflamaana yake unamwambia aende akamwambie yulemhusika aongeze, ukimwambia aongeze ni kamaunamwambia asije. Repercussion yake inaweza ikawa

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

143

mbaya sana. Kwa hiyo, naomba sana tuangalie jinsi ganikama ni kuongeza basi tuwape notice kisha tuongezebaadaye lakini siyo sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imewekavipaumbele tofauti ikiwa ni pamoja na barabara mbalimbali.Kusema kweli naishukuru sana Serikali kwa sababu mwakajana Dar es Salaam tumepata barabara nyingi sana na hiiyote ilikuwa ni katika kujaribu kuondoa msongamano Dar esSalaam. Hata hivyo, naomba nirudie tena na Serikali inisikilizekwa sababu barabara tulizofungua bila kufungua daraja laSalender, bado hatujafanya kazi nzuri kwa sababu wotetunaondoka huku kwenye barabara zilizofunguliwa nakwenda kukutana pale Salender Bridge na tunatumia saakadhaa kufika mjini na nguvu kazi kubwa sana inatumikapale. Maana yake wewe kama una kitabu au paperunasoma unaweza ukaimalizia palepale kabla hujavukaSalender Bridge. Kwa hiyo, naomba sana huku kwenye bajetiinawezekana haikuandikwa lakini Serikali itafute fedhamahsusi kwa ajili ya kulihudumia daraja la Salender Bridge.

MBUNGE FULANI: Ni Daraja la Salender siyo Daraja laSalender Bridge.

MHE. ZARINA S. MADABIDA: Ni daraja la Salender,naambiwa siyo Daraja la Salender Bridge, naongea Kiswahilina Kiingereza. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudi kidogo katika fedhaambazo zimetengwa kwa ajili ya benki ya akina mamapamoja na maendeleo yao, zile shilingi bilioni mbili (2)zilizoongezwa. Ukizitaja fedha hizi unaona ni nyingi sana lakinikusema kweli fedha hizo ni ndogo sana hasa ukitilia maananikwamba kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne au mitano,hizi fedha hazikutolewa. Sasa sielewi watakwenda kuzigawajefedha hizi kwenye Wilaya mpaka ziwatoshe wanawake?Niombe Serikali iangalie jinsi gani inavyoweza kuongezafedha hizi. (Makofi)

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

144

Mheshimiwa Mwenyekiti, si hizo tu, hata zile zaManispaa hatuzipati, Manispaa hawazitoi. Juzi kwenye bajetitulikuwa tunawaambia wakasema mtatusamehe lakini hiyofive percent mnazosema hatuna. Sasa tunafikiria kwambazile fedha za Manispaa zimepangwa five percent lakinihakuna, kwa hiyo hii shilingi bilioni mbili ndiyo wanawake wotewatakaa chini kuiangalia, ni kidogo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine la mwisho,kumekuwa na kubadilisha vipaumbele vya Halmashauri.Nazungumza hili kutokana na experience yangu kwenyeHalmashauri ya Kinondoni. Halmashauri inapeleka mipangoyake na maombi ya fedha. Sawa umeniambia sikupi shilingibilioni tano nakupa shilingi bilioni nne, ile shilingi bilioni nnepia unanipangia kwamba usiende kutengeneza barabaraya Kachube, nenda katengeneze barabara ya Masaki. Hilitunasema hapana! Mtuachie kama ni vipaumbele toa kwakipaumbele, sasa ukiishaniambia nisitekeleze kipaumbelechangu inamaanisha umenibadilishia na kile kipaumbeleambacho umenipa nikitekeleze. Sasa kwangu mimi kamaWilaya hicho ulichonipa wewe siyo kipaumbele. Hii ni keroambayo sisi pale Manispaa tunayo kwamba tumeombafedha kwa ajili ya kutekeleza kitu kingine, tumepangatutatengeneza barabara hii na hii, lakini inapokuja unapewabarabara ambayo kwako si kipaumbele, hiyo ni kero ambayonaomba Serikali iiangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine la mwisho kabisa niriba kubwa sana kwenye fedha za mikopo zinazotolewa hasaukienda kwenye microfinance. Ukienda kwenyemicrofinance mpaka unashangaa kwamba hivi huyuanayechukua anakwenda kufanya biashara gani ambayoatapata faida maana yake ukiweka cumulatively inafikampaka asil imia 48? Ndiyo maana utasikia huyukanyang’anywa TV, huyu sijui kitu gani, akina mamawanahangaika kwa ajili ya kupata mikopo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali naMheshimiwa Waziri suala hili waliangalie sana. Naibu Mawaziriwote ni wanawake wanajua jinsi wanawake

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

145

wanavyohangaika. Naomba sana rates za riba kwenyemicrofinances ziangaliwe ili kusudi ziwe realistic mtuanapokwenda kuchukua mkopo afanye biashara apate,lakini mtu anakwenda kuchukua mkopo halafu anashindwahata kulala nyumbani kwake kwa ajili ya kuogopa riba nakwamba akii-default vitu vyake vitakuja kuchukuliwa.Naomba sana Mheshimiwa Waziri aliangalie hilo sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naomba niipongeze tena Serikali na ninaunga mkono hoja.Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Zarina. Sasanitamwita Mheshimiwa Silvestry Francis Koka, atafuatiwa naMheshimiwa Clara Mwatuka na Mheshimiwa Martha JachiUmbulla ajiandae.

MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na kutoa shukrani napongezi kwa Serikali pamoja na Bunge letu Tukufu kwa kazinzuri inayoendelea kufanya kwa ajili ya nchi yetu nawananchi wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikubaliane na kuipongezaTRA kwa utaratibu walioufanya dhidi ya vijana wetu nahususan kwenye bodaboda. Hata hivyo, naomba vilevile kwautaratibu huo, TRA waweze kutambua na kutoa maelekezoambayo ni uniform kwa nchi nzima hususan kwawafanyabiashara wadogo wadogo wanaofanya biasharazao katika masoko madogo madogo ya kuuza vyakulapamoja na wale wajasiriamali wadogo wadogo wanaofanyakazi katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na stendi,kwa mfano, pale kwangu Maili Moja, Kibaha Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo kwa sababuulifika wakati TRA wakawa wanakwenda kutaka kudai kodiya mapato hata kwa wale wafanyabiashara wadogo

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

146

wanaouza mchele katika vizimba vya soko dogo lile la MailiMoja. Kwa hiyo, naomba kupitia spirit hiihii ya kuwaangaliahawa wafanyabiashara wa bodaboda, basi na hao wenginewaweze kuangaliwa ili na wenyewe waweze kufaidika nashughuli ndogondogo wanazozifanya za kiujasiriamali nawaweze kuji jenga il i hatimaye waweze kuwawafanyabiashara wakubwa na waweze kushiriki vyemakatika kulipa kodi na kuchangia katika pato la Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nizungumzienamna nzima ya kuchangamsha uchumi. Tunafahamu niana madhumuni ya bajeti ni pamoja na kuchangamsha auku-stimulate uchumi wa nchi. Tunaona wazi kwambatumekuwa tukipanga mipango mingi, hususan ya kilimo,tumenunua vifaa mbalimbali yakiwemo matrekta kwa wingikatika harakati za Kilimo Kwanza kwa maana ya kuboreshakilimo. Hata hivyo, ni ukweli usiofichika kwamba hata kamatungeendelea kununua matrekta mengi kiasi gani pamojana mitambo mingine mbalimbali kwa ajili ya kilimo ili tuwezekwenda kwenye kilimo cha biashara (commercial farming),kama Serikali haitaamua kwa makusudi kabisa kuwekautaratibu wa kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwa ajiliya kilimo, bado tutaendelea kutegemea mvua zisizofahamikana zisizokuwa na msimu maalum na matokeo yake hatatungelima na haya matrekta bado mkulima ataendeleakupata hasara kubwa na hataweza kuvuna mazao yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, rai yangu, naiomba Serikalikama tunavyokaa hapa tunapanga, fedha zinaendakwenye miundombinu ya barabara na mingeneyo, sasaumefika wakati wa kupanga fedha ziende katikamiundombinu ya umwagiliaji. Napenda kuona Serikaliinatengeneza miundombinu ya umwagiliaji katika maeneomwafaka ya kilimo ili wananchi na wale wote wanaotakakuendesha kilimo cha kisasa na kikubwa waweze kupata majiya umwagiliaji katika namna rahisi na kuweza kukuza kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo kwa sababu,tunazungumzia ukuaji wa uchumi mara kwa mara, lakiniukweli ni kwamba ukuaji huu tumeshindwa kuu-translate

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

147

kwenda kwa wananchi wengi wa Tanzania ambao niwakulima na wafugaji. Maana yake tunafahamu zaidi yaasilimia 70 ni wakulima na wafugaji na hawa katika suala hilibado hatujaweza kuwagusa katika kukuza uchumi wao. Kwahiyo, ni wazi kama tutafanya mapinduzi na hasa katikaumwagiliaji tutawagusa hawa wakulima. Kama tutafanyahivyo, tutaondokana na utaratibu wa vijana wengi wenyenguvu kuhama kutoka vijijini na kukimbilia mijini, maana hatahizi bodaboda karibu vijana wengi wanatoka vijijini. Sasamwisho kila kijana atakuwa na bodaboda na hata wakuipanda atakuwa hayupo. Nina imani tukiimarisha kilimo nahususan tukienda katika kilimo cha kisasa ikiwa ni pamoja nakuimarisha umwagiliaji, ni wazi vijana hawa watabaki vijijini,watazalisha na nchi yetu itakuwa na chakula cha kutoshana ziada, tutauza na hapo mkulima au mfugaji ataona ninamna gani uchumi unakua. Kama tutafanya hivyo,tutaondokana na migogoro kati ya wakulima pamoja nawafugaji, lakini na ule uhamiaji wa watu kwenda mijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kusisitiza hilo kwasababu ukiangalia trend ya mfumuko wa bei kwa mfanomwaka 2010/2011 na 2011/2012, average tulikuwatumekwenda mpaka kwenye inflation ya digits mbili, tulifikampaka 19, lakini uki-analyze utaona kabisa mchangomkubwa wa mfumuko huu wa bei ulikuwa unasababishwana chakula ambapo kilienda mpaka asilimia 40. Kwa hiyo,kama tutajikita sasa na kuhakikisha tunakwenda kwenyeukulima wa kisasa na Serikali ikawasaidia wananchi katikakutengeneza miundombinu hii ambayo ina gharama kubwa,ni wazi kuwa sasa hata ule ukuaji wa uchumi utamfikiamwananchi wa kawaida na wale walio wengi vijijini na kwamaana hiyo kila mtu atakuwa anafurahia ukuaji wa uchumikwa ujumla wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wazi kwamba badotunalo tatizo kubwa katika kusimamia hata hizi fedha kidogoambazo tunazikusanya. Naamini kama tutatangenezamfumo mpya na hususan kwa vijana wetu wengi

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

148

wanaomaliza shule na vyuo, tutafika mahali kutakuwa nanidhamu ya usimamizi wa fedha na hata hizi chache ambazotunazikusanya zitasimamiwa kwa ubora zaidi na zitawezakuleta tija. Tuchukulie mfano leo kijana anayemaliza chuokikuu au chuo chochote na anaenda kufanya kazi,anakabiliwa na mambo chungu nzima. Jambo la kwanzaanatakiwa atafute usafiri au gari, gari lile anatakiwa alinunuekwa fedha taslim (cash). Bado anakabiliwa na kujenga aukupanga nyumba ambapo anatakiwa alipe kodi ya mwakamzima na yenyewe ni cash, hata kama ni kujenga nyumbani kwa fedha taslimu. Kwa kweli katika hali hii tunasababishavijana hawa wanashindwa kuwa na nidhamu ya kusimamiakwa uadilifu fedha na kazi ambazo tunawapa. Nashauri kamakweli tunataka kuona vijana wetu wanakuwa waadilifu natunajenga kizazi kipya ambacho kitakuwa kinafanya kazi kwauadilifu na kuifanya nchi yetu iweze kusonga mbele nakuthamini fedha ambazo zinatokana na kodi zetu, ni wazikwamba sasa Serikali ianze kuangalia utaratibu mzima wakusaidia mfumo mzima ili vijana hawa wanapoingia katikamaeneo ya kazi waweze sasa kuingia katika utaratibu wamikopo na ili kuwaondolea adha na tamaa na ulazima wakukusanya fedha kwa haraka haraka ili waweze kupatamahitaji muhimu ambayo wanahitaji ili kuendesha maishayao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeyasema hayo kwasababu huo ndiyo ukweli ambao uko katika shughuli zetu zakila siku. Nina imani kama Serikali itajikita katika kuyaangaliahaya, tutafika mahali tutajikuta wote kwa ujumla wetuwakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara, tunakwendapamoja, tunaimba wimbo mmoja na hata ile gap kati yawalionacho na wasionacho itapungua. Tukifikia hapo, ninaimani tutaishi kwa amani na utulivu na tutaheshimiana nanchi yetu itaendelea kuwa kisiwa cha amani na maendeleotutayapata kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo machache,ninaomba kuunga mkono hoja, tuko pamoja. (Makofi)

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

149

MWONGOZO WA SPIKA

MWENYEKITI: Mheshimiwa Keissy.

MHE. ALLY K. MOHAMMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninataka Mwongozo wa Spika kwa mujibu wa Kanuni ya 68(7).

MWENYEKITI: Mheshimiwa Keissy unasemaje?

MHE. ALLY K. MOHAMMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninaomba Mwongozo wako kwa mujibu wa Kanuni ya 68 (7)kinasema kwamba mtu anapozungumza asiwepo mwingineanayezungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu bajeti ya Wizara yaFedha, hapa kuna vitabu viwili; kitabu cha Makusanyo naMatumizi. Wabunge wengi wanazungumza tu namnaambavyo Serikali isikusanye mapato, hawaelezi Serikali ipatewapi mapato. Sasa sijui inakuwaje kwani sijasikia hataMbunge mmoja anasema hapa Waziri wa Fedha umesahausehemu fulani mapato yanavujishwa, wenyewe kazi yao nikusema punguza hiki, hiki na hiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Serikali ikipunguza kilakitu, huku tunaomba maji, umeme, barabara, fedha zitatokawapi? Sijasikia hata Mbunge mmoja anasema tumesahaukwenye kodi ya ng’ombe, hamna hata mtu mmoja ambayeamezungumza hilo hapa, wafugaji wa kuku hatujasungumza,lakini Wabunge wote ni mafuta shilingi mbili (2), sijui hiki nahiki. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sheria ya bajeti yaWizara ya Fedha lazima tuzungumze namna Serikaliitakavyopata mapato, ndiyo sheria. Mambo ya kuzungumzasijui hivi yalikwisha wakati wa Wizara, tulichangia wakati waWizara ya Kilimo, Wizara ya Maji, Wizara ya Mifugo, zotetumechangia. Sasa hapa tuisaidie Serikali yetu namnaitakavyokusanya pesa ili tujitegemee kwa asilimia mia kwamia au tupate asilimia 120, ndiyo tunavyotaka Wabunge

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

150

tuchangie namna hii. Kama hatuna uwezo, tukae kimya,tuwaache Wabunge ambao wana mawazo ya kuchangiaSerikali yetu ipate fedha. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo Mwongozo wangu.

WABUNGE FULANI: Sema naomba.

MHE. ALLY K. MOHAMMED: Ndiyo naomba namna hii,tuendelee kuchangia kusaidia Serikali, wapi Waziri wa Fedhakasahau au Kamati ya Bajeti imesahau wapi pa kupatafedha, tuchokonoe tupate fedha ili tuiwezeshe Serikali.(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mwongozo wako.(Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Keissy, majibu yaMwongozo huo nitautoa baadaye, ingawa na weweumenishangaza leo umeongeza hapa kodi ya kuku, tutozekodi kwenye kuku na kwenye ng’ombe, sasa sijui lengo lakolilikuwa kuomba na kuku nao watozwe kodi lakini nitatoamajibu ya Mwongozo huo baadaye. Tuendelee nauchangiaji halafu nitatoa majibu ya Mwongozo waMheshimiwa Keissy baadaye.

Waheshimiwa Wabunge, nil ikuwa nimemtajaMheshimiwa Clara Mwatuka atafuatia Martha Umbulla nabaadaye nitazungumza huo Mwongozo wa Keissy Mohamedtusipoteza kwanza muda wa kuchangia.

MHE. CLARA D. MWATUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ili nami niweze kusema machachejuu ya bajeti iliyopo mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza namshukuru Mungukwa jinsi anavyonipigania na kunishindania katika mengi. Pianikushukuru nawe kwa kunipa nafasi. Nachukua nafasi hiikuwapongeza Waziri na jopo lake zima kwa juhudiwaliyoifanya kuweza kuokoteza pesa hapa na pale kuweza

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

151

kuongezea kwenye Wizara zile ambazo zilikuwa zinamapungufu. Nawapongeza sana, muendelee na moyo huo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya yote, napendanitoe masikitiko yangu nikikujulisha wewe na Bunge nzima juuya mambo yanayofanyika Mtwara hivi sasa kwamba watuwanapigwa tangu wiki iliyopita hii wanapigwa mpaka juzisababu haijulikani. Sasa najiuliza ni yapi, ni ya gesi yaleyalena kama ni gesi kweli tupo katika nchi hii, kwa kweli sinaamani. Najiuliza hivi tupo nchi gani, Kusini kule au Mtwara hiini watu wa aina gani na hao wengine sehemu zinginewakoje? wa kweli ninasikitika, nasikitika hali hii ni mbaya sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha kushangaza ni kwambahata vyombo vya habari kimya, watu wamepigwa,wameumizwa, wamelazwa hospitalini, lakini hakuna taarifayoyote nchini juu ya matukio haya. Ina maana kwamba watuwa kule hawatakiwi katika nchi hii. Navyojieleza mimi, nafikirihata wenzangu nao wanasema eeh sisi siyo wa Tanzania hii.Kwa kweli Serikali naiomba ifanye juu chini jamani,tumeambiwa amri kuu ni upendo, tupendane, kwa ninitunachukiana? Yawepo hayo kwa sababu, lakini unakwendakumpiga mtu, Wanajeshi kwenda kuwapiga wananchi, raia,hawana silaha hawana nini. Mitutu, vifaru vimejaa hukoMtwara, wanapigwa mpaka Newala Mjini, sababu haijulikani.Kwa hiyo, naiomba Serikali ilitazama hili, ione na itende hakiyaani wale wanaotumwa kufanya kazi wanapitiliza. JuziUchaguzi Mdogo wa Kata ya Nima, magari matano yaWanajeshi na vifaru juu eti kwenye Uchaguzi wa Kata jamani,tunatoka wapi, tunakwenda wapi? Nasikitika sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kidogo tujuu ya bajeti iliyopo au hali iliyopo mbele yetu. Kwa kweli sipatila kusema kwa jinsi nilivyokatizika raha na nilivyo na huzunijuu ya hali inayoendeshwa kule Mtwara. Juzi hapa wakatiMheshimiwa Waziri wa Fedha alipotueleze hizo nyongeza,nyongeza zilizopatikana Wabunge hapa tulipiga makofi vizurisana, kushangilia kwamba kazi imefanyika nzuri. Ni kweli juhudi

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

152

wamefanya kubwa ya kupata fedha za kuongezea katikasehemu mbalimbali lakini tumeshangilia kitu chenyewewakati bado hatuna hakika kwamba itakuwa hivyo auimesemwa tu kama kawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba MheshimiwaWaziri na jopo lako iwe ni kweli hili ulilotufikishia kwamba fedhazitatolewa ndani ya wakati na kule zinakokwenda zikafanyiwekazi kama ilivyokusudiwa, isiwe zinatolewa kama zilizopitazingine, inaonekana huku zilitolewa lakini zinapotakiwakwenda hazijafika, haitakuwa na maana yoyote. Jamanikufanikisha kwa jambo siyo lazima pawe na kitu kwa wingisana, kidogo hichohicho kinaweza kufanyiwa kazi kwa makinikikaleta ufanisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa wengi wamelalamikakuhusu madeni ya Walimu, ni kweli siyo kwamba fedhahazikuwepo huko nyuma maana sasa nina imani kwa wingiwa fedha zilizopatikana sasa hivi madeni yote yatakwishalakini fedha zilikuwepo huko nyuma, mafisadi walikuwawakizitoa wapi si hizo hizo? Walimu wanafanya kazi katikamazingira magumu, tukawa tunasema hapa ooh, Waziriajiuzulu, ni kumwonea, kwa nini hatumwambii Rais basi ajiuzulusi mtu wake huyu, si kweli. Watoto wetu tumewapa Walimuwawafundishe, sasa Mwalimu hatujampa mazingira mazuriya kuipenda kazi yake, atafanyaje kazi? Mshahara mdogo,anapitwa hata na Bwana Shamba, Bwana Afya ambaowanafanya kazi usiku na mchana, hawapati mshahara wakutosha, ataipenda kazi hii, ataifanya kwa moyo,haiwezekani. Nyumba ya kulala tabu, anahangaika vijijiniajitafutie mwenyewe, apange huko kijijini na maisha yaende.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamedai kwa muda mrefuwakatishia wakati ule watafanya mgomo, mkawatishawakaacha, Walimu wavumilivu lakini mjue kwambaunapomchukua mtoto wako ukampa Ngaliba, wotetunamfahamu Ngaliba, jandoni kule, unawapeleka watoto,unakabidhi yule, kama hatakuwa na upendo na kamahutamwekea mambo yake vizuri, anajua mwenyewe cha

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

153

kuwafanya wale watoto. Sasa na Walimu nao hivyohivyo,kwa sababu hawatekelezewi yale wanayotaka basihawawezi kuipenda kazi wakaifanya kwa moyo. Hebutujaribu sasa tuwaongezee mishahara, madeni yaowanayodai tuwalipe, wapate nyumba, wale wanaoishikwenye mazingira magumu wapate hizo posho kwa ajili yamazingira magumu tuwape, hakika tutasema tulichelewawapi lakini tukibaki tu hivihivi mambo yatakwenda hivihivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwa wenzanguwakulima, hapa wamesema wameongeza hela kwenyekilimo lakini si jui itakuwa kama tunavyotegemea auwanavyotegemea wakulima baada ya kusikia bajeti hiikwamba imeongezewa sijui kama itakuwa hivyo. Kwa sababumkulima anaonekana kwamba ni nyuma toka zamani lakinini mchangiaji mzuri kwenye maendeleo ya nchi hii, hana chakusema hiki Serikali imenisaidia, hakuna. Tumesematunawatafutia masoko, makoso yapi, haya wanayokwendakukopesha. Sasa tuwasimamie vilivyo hizo fedha zifike hukozikafanyie kazi. Nil isema juzi hapa kwamba vijanawameacha uvivu hivi sasa wanafanya kazi za kujiendelezana kujipatia kipato. Sasa hapo walipoamua mwenyewevijana kufanya kazi basi tuwasimamie, wapewe mitaji iliwafanye kazi vizuri waweze kujitegemea. Tukiwaacha hivihivindiyo pale wanapokimbilia mijini kufikiria kwamba kule ndiyokuzuri lakini wengi walishaona kwamba hakuna faida yakwenda mijini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikia wenzanguwamezungumzia juu ya misahama ya kodi. Mimi kitu hiki namibado ninashangaa. Kwanza, niulize uwekezaji huu wananchihawawezi, wakipewa sehemu labda kwenye machimbo yamadini au sehemu yoyote ile, hawawezi wakawekeza,wakazalisha vizuri na Taifa likapata pato nzuri? Kwa sababuhivi sasa uwekezaji wote ni wa nje tu wakati wananchi wenyeuwezo wapo hata ndani humu wapo wengine ambaowanaweza wakashika sehemu fulani hata kwenye machimbohumu wakaendesha vizuri, kwenye hoteli wanawezawakawekeza, kwenye bahari humo, lakini kote hukotumewapa wageni. Sasa kinachosikitisha ni kwamba eti

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

154

asilimia tatu, wewe mwenye chako upewe Sh.3 katika kilaSh.100, hivi inaingia akilini jamani, yaani hatujihurumii? Sasatunapata shida, nchi maskini wakati utajiri umejaa, tunaukaliatu, tunawapa wenzetu wananufaika, wanakuja kuchukuawanakwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naamini mikataba hiiinakuwa miwili, kwamba ule wa asilimia tatu ndiyo wakujulikana Kitaifa, lakini upo mkataba wa siri, haiwezikani,tutafika wapi? Basi tuwape wananchi wao wawekeze iliwakila hao ni afadhali kwamba watalia nchini humuhumukuliko wale wanaochukua na kwenda nje huko. Jamani, kwakweli Tanzania tunasikitisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo mengine yale yakusema kwamba tuchukue hiki hapa tufanyie hiki kwa ajiliya nje tunaweza sana, lakini kwa ajili ya Taifa tupo mbali sana.Mimi naomba safari hii bajeti hii iliyoongezwa vizuri wotetukafurahia hapa ndani basi na iwe hivyo, wale waliopewanafasi hizo waone kwamba hapa mimi ni kama nyabara,nasimamia kitengo hiki kifanye kazi vizuri iwe manufaa kwanchi na siyo kwamba unafanya hivyo kwa faida yako,hapana. Tumekula viapo kuanzia kwenye vyama na hapakila siku tunakula viapo, tuwe waaminifu na utii pia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu zangu hivi sasainaonekana kwamba aliyepata amepata, wengine kamawewe hukupata usipige kelele, ukipiga kelele, wanasema ulietu, watu wanakwenda, siyo kweli. Mheshimiwa Yahayaamesema hapa kwamba hakuna anayekwenda nazokwenye sanduku au watamfungashia mzigo huo kwenyesanduka akaenda nao, hakuna, haya yote tunayaachahapahapa. Tufanye kwa manufaa ya nchi, wote wajisikiekwamba hapa leo sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe kila mmoja ambayeamepewa nafasi ya kuongoza na kwa mfano nyie wenzanguMawaziri maana ndiyo mlioshika usukani, naomba Munguawabariki, awapeni afya njema na muwe na moyo hasa wa

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

155

uzalendo maana Wizara yako ikifanya vizuri ni sifa yako weweWaziri. Kwa hiyo, mfanye kazi kwa uchungu, watu waletunaowasimamia wa chini yetu basi tuwasimamie vizuri iliwewe unufaike pamoja na watu wako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema ahsante na Munguawabariki. Ahsante sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mama Clara Mwatuka.Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na MheshimiwaMartha Umbulla na Mheshimiwa Charles Mwijage ajiandae,halafu tutamsikia Rukia Kassim Ahmed.

MHE. MARTHA J. UMBULLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza kabisa nikushukuru wewe kwa kunipa fursa hii nanimshukuru sana Mwenyezi Mungu ambaye ameniwezeshamimi kumudu majukumu yangu yote nikiwa na afya njema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie fursa hii piakuwapongeza wananchi wa Dongobeshi, Wilaya ya Mbulu,kwa kukipa kura nyingi Chama cha Mapinduzi japokuwahazikutosha, lakini iwe fundisho kwetu na kujipanga upya,wasife moyo, ipo siku Mungu atatusaidia tutaikomboa Katayetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya utangulizi huo,naomba nijielekeze katika kuchangia bajeti yetu. Nichukuefursa hii pia kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri naManaibu Waziri wake, ni watu makini na Watanzania wanaimani kubwa nao kwa kuwa bajeti hii inaweza ikawakomboakatika lindi la umaskini walionao na kwa ubunifu wao naaminikwamba bajeti ndiyo njia pekee ya kuweza kuwasaidiawananchi ili watokane na umaskini. Kubuni namna bora yakutengeneza na kutekeleza na kusimamia bajeti, ndiyo njiapekee ya kuweza kuinua uchumi wa nchi yetu na pato laTaifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata tukipanga bajeti nzurinamna gani kama ambavyo Waheshimiwa Wabungewengine wamesema kama bajeti haigusi mtu wa chini ama

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

156

wananchi walio wengi maskini vijijini bado bajeti hiyo haiwezikuwa na manufaa kwa Watanzania. Nasema hivyo kwasababu umaskini wa nchi unapimwa kwa vigezo vya umaskiniwa wananchi wake, namna wanavyoishi katika nyumba zilizoduni vijijini, namna ambavyo hawana uhakika wa chakulana namna ambavyo wana matatizo mengi ya hapa na pale,hiyo bado inaweka nchi katika rank ya kuwa nchi maskinikutokana na hali duni ya wananchi wake. Kwa hiyo,naiomba Serikali iweze kuangalia ni namna gani bajeti zetutunazopanga mwaka hadi mwaka ziweze kugusa moja kwamoja wananchi walio wengi vijijini. Naipongeza Serikali kwanamna ya pekee kwa kuwa, imeweza kusikia kilio chaWabunge, wameongeza fedha katika maeneo mbalimbaliambavyo Wabunge walisisitiza ili kupunguza ukali wa umaskinivijijini, lakini bado ninaishauri Serikali kwamba iendeleekupanga mwaka hadi mwaka ili hatimaye tujikomboe na lindila umaskini unaowakabili wananchi watu wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru bajeti hii piaimeweka vipaumbele, najua kwamba vipaumbele huwavinatokana na mahitaji ya jamii husika. Kwa mfano,vipaumbele vya Mkoa wa Kigoma haviwezi kuwa sawa navipaumbele vya Mkoa wa Manyara. Ukimuuliza mwananchiwa Wilaya ya Kiteto, atakwambia umeme kweli ninauhitaji,maji ninayahitaji, barabara ninahitaji, lakini kusema kweli mimiardhi yangu ambayo inanililisha, inanipa maisha, inasomeshawatoto wangu bado imeporwa na kwa miaka mitano ninamigogoro hii ambayo haitatuliwi. Sasa naishauri Serikali vilevilekwamba isiendelee kufumbia macho migogoro ya ardhi.Migogoro ya ardhi imefika mahali pabaya, inapoteza maishakwa baadhi ya maeneo ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri pia Serikali kwambaiweke namna ambavyo bajeti sasa itaelekeza wataalamwaweke mipangilio ya matumizi bora ya ardhi ili tuondokanena migogoro ya ardhi. Leo hii ardhi inapoteza maisha yaWatanzania. Katika miaka mitano, kumi ijayo itaendeleakupoteza maisha ya Watanzania kwenye maeneo yenyemigogoro kwa sababu ardhi haiongezeki na Watanzaniatunaongezeka kwa asilimia saba hadi kumi. Sasa bila

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

157

kupangilia vizuri ardhi tuliyonayo, kwa kuweka wataalam nabajeti ambayo inaweza ikasaidia katika eneo hilo, italetamatatizo na wananchi wataendelea kupata migogoro mingi,watapoteza muda wa kuzalisha na hilo litakuwa siyo jamboambalo litaleta maendeleo kwa wananchi kulingana navipaumbele vyao. Serikali yetu ipangilie bajeti kwa kujalivipaumbele vya jamii katika maeneo yao ili ilete utulivu nakuongeza uzalishaji kwa sababu kwa namna hiyo piawananchi wataweza kuongeza kipato na mapato ya Taifaletu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la lingine ambalonataka kuchangia ni la kunusuru maisha ya vijana. Ubunifuwa kutekeleza mipango ya bajeti ufanyike ukilenga vijanawa leo. Kwa muda mrefu, Serikali yetu imelenga wanawake,tunashukuru na matatizo ya wanawake siyo dhahiri kulinganana matatizo ya vijana. Kwa sababu wanawake hawawezikuzurura mitaani pamoja na shida walizonazo, kwa sababuwana majukumu mengi ya kulea lakini vijana wanazururamitaani kama hawana shughuli ya kufanya na wanapangamipango mibovu kwenye magenge ambayo yanahatarishasiyo maisha yao tu bali hata ya Taifa. Kwa hiyo, naomba nanaishukuru pia Serikali kwa kuwa imeshaangalia kipaumbelecha vijana lakini basi iendelee kubuni ni kwa namna ganivijana hawa kwa wingi wao wanaweza wakawezeshwa iliwaweze kuendeleza Taifa letu kwa sababu ni kundi kubwana kundi muhimu katika jamii ya Watanzania. Naomba kundihili lilengwe zaidi si tu ili kunusuru maisha yao bali maisha yaTaifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia kwa mfano Mkoawetu wa Manyara, tunashukuru Mungu vijana wetuwanapenda sana kulima na kufuga lakini hawana mitaji.Ndiyo maana hata ukiangalia maambukizi ya VVU katikaMkoa wa Manyara yako chini, tunamshukuru Mungu ni kwasababu vijana wanajishughulisha sana ukilinganisha na vijanakatika maeneo mengine. Tunaomba mitaji iweze kupatikanakwa ajili ya vijana, ile benki iliyotajwa ya vijana basi iwezekuwekewa fungu la kutosha ili vijana wetu waweze kujisaidia

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

158

katika kuendeleza maisha yao na kuzalisha kwa wingi ilituweze kuinua pato letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo natakakuchangia ni la barabara. Sambamba na pongezi kwaSerikali kujenga barabara katika nchi yetu lakini naombaujenzi wa barabara sasa uelekezwe zaidi katika maeneo yauzalishaji. Kuna maeneo kwa sababu kuna fursa tu ya kujengabarabara na barabara zimejengwa mpaka vichochoroni,lakini kuna maeneo hawajawahi kuona lami mfano katikaWilaya zetu za Mkoa wa Manyara. Tunashukuru Wilaya mbiliau tatu hivi zina barabara zinazopita kutoka kwa mfanoWilaya ya Hanang ina barabara ile inayotoka Arusha kwendaSingida ni barabara ya lami, hali kadhalika na Babati lakiniWilaya ya Kiteto hawajawahi kuona lami na kama,tunavyojua kati ya Wilaya zinazozalisha sana katika nchi yetuni Wilaya ya Kiteto. Barabara ya kutoka Kibaya kujaNjiapanda ya Dar es Salaam na Dodoma ni barabaramuhimu sana na tunaomba chondechonde MheshimiwaWaziri wa Ujenzi atanisikia huko alipo, barabara hii iwekewelami kwa sababu inasomba mazao ambayo yanakwendasoko kubwa la Kimataifa la Kibaigwa na barabara hiiinaharibika kila mara kwa sababu ya magari mengiyanasomba mazao. Kwa hivyo, tunaomba MheshimiwaWaziri aiwekee bajeti ili barabara hii itengenezwe ni muhimusana kwa uzalishaji wa mazao kutoka Wilaya yetu ya Kitetolakini vilevile iweze kurahisisha usafiri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara inayotoka ndaniya Wilaya ya Mbulu kupita kwenye mlima wa Magala kwendampaka Njiapanda ya kwenda Arusha. Hata Marais wetuwameshapita barabara hii, najua ni ya TANROAD lakininikiangalia baadhi ya Wilaya zina barabara za lami mpakavichochoroni, najiuliza kulikoni. Kwa nini barabara za maeneoyanayozalisha mazao kwa wingi ambayo inainua pato laTaifa letu zisiweze kupewa kipaumbele na bajeti zetu naSerikali lakini zinaweza kujenga barabara ambazo zinamanufaa lakini basi si kipaumbele cha Taifa letu? Naombakwa nafasi hii Serikali iweze kuangalia kipaumbele kwabarabara za maeneo yanayozalisha kwa wingi.

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

159

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Wilaya ambazo miaka50 ya Uhuru hazijaweza kuona lami. Mfano Wilaya ya Mbuluilikuwa na lami ya Mjerumani, ya zamani sana na ikatobokampaka tukaomba kwamba waikwangue bora tubaki nabarabara ya vumbi lakini basi kwa bahati nzuri wamejengabarabara lakini ndio laini hiyo moja hatuna barabarazinazokwenda kwenye maeneo ya uzalishaji. Wilaya yaMbulu inazalisha mazao kwa maeneo mengine hata marambili kwa mwaka na mazao mengine yanaozea vijijini. KuleMbulu Kwerumus na Maisara wanalima mazao mengi viazimviringo na viazi vitamu, lakini vinaozea kule kwa sababubarabara ni za shida na milima na mabonde. Kwa hiyo,naomba kwa nafasi hii nimwombe Mheshimiwa Waziri awezekuangalia barabara zile zinazokwenda kwenye maeneo yauzalishaji zipewe kipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niliona nichangie maeneohaya machache, napenda kuunga mkono hoja, nakushukurukwa kunipa nafasi ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa MarthaJachi Umbulla. Mheshimiwa Charles Mwijage alikuwaazungumze Mheshimiwa Gaudence Kayombo lakini simwonindani ya ukumbi nitampa nafasi Mheshimiwa Rukia Kassim.

MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia bajetikuu ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yametokea maambuzimakubwa, mlipuko wa ugonjwa wa malaria katika Wilayaya Muleba. Nachukua fursa hii kuishukuru Serikali hasahasaWizara ya Afya namna mlivyoitikia na kuwajali watu waWilaya ya Muleba, Mwenyezi Mungu awaongezee moyo huo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapa pole wananchi waMuleba ambao mmepata matatizo hayo, tulipojikwaatunajua na mkirejea swali langu la Mkutano huu wa Kumi naMoja nililouliza Wizara ya Afya ikashindwa kunijibu ilichopaswa

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

160

kunijibu ndiyo hayo majanga yametupata tutakaa chinitutazungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia bajeti yaSerikali, niwapongeze Mheshimiwa Dkt. Kapteni Chiligati, AlhajKeissy na Professa Msolwa, ndio mimi nitaazima busara zaokatika kuboresha au kusherehesha mchango wangu.

MWENYEKITI: Alhaj Keissy yupi Mheshimiwa Mwijage?

MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Ally Keissy Mabodi sijuinyie mnamwitaje.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge Keissy!

MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mbunge wa Nkansi.(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, busara nyingine nitaazimabusara ya rafiki yangu Mama Chichi, Mama Chichi ni mamawa Kichina, nilikutana naye siku moja nikamwuliza nipe siri yamaendeleo ya China. Akasema China imeendelea kwasababu ya mambo matatu. China iliwekeza kupita kiasikatika elimu, elimu hii mnayoijua lakini zaidi elimu ya MafundiMchundo. Ndio maana nampongeza sana Profesa Msolwakwa mchango wake. Tunahitaji kuwa na wanafunzi wengi,watu wengi waliofundishwa ufundi stadi ambao wanapokujakufanya kazi wanaweza kufanya kazi zilizo nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, akasema zaidi Wachinawalitoa elimu ya uzalendo yaani mtu anakwenda shuleniunafundishwa uzalendo na una-disco mpaka unauelewauzalendo. Akaenda zaidi, Wachina walifanikiwa hapowalipofika kwa sababu walitunga sera, falsafa kubwa yaWachina kutunga sera lazima utunge sera ambayoinawalenga watu, ukitunga sera na haiwalengi watuumekosea. Kitu cha tatu, Wachina waliwekeza katika soundau propaganda. Wamepiga propaganda sanaukichanganya mambo hayo matatu mambo yanakwenda.(Makofi)

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

161

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwa MheshimiwaKeissy. Serikali kupitia TRA imeanzisha utaratibu wa kufunguamizigo ya watu na kuikagua, mfumo huo ni subjective. Serikaliimewahi kufanya hivyo miaka ya 1980, mimi niko kwenyemaeneo ya bandari tangu mwaka 1984 iliwahi kufanya hivyo.Suluhisho ni lipi Waziri wa Fedha? Nenda kanunue scanners,funga scanners, sasa hivi kuna scanner nyingine ni mobile,kwa nini pembe za ndovu zinapita Tanzania? Mozambiquewamefunga scanners, Namibia wafunga scanners, Kenyawamefunga scanner, scanner kwa mizigo yote inayoingia namizigo yote inayoondoka. Wananchi wataishiwa mashakakama container linapita watu wanadhani kuna matofali yadhahabu, linasimamishwa inaletwa mobile scanner wana-scan kila mtu anakuwa na amani ya moyo fullstop, kufunguamizigo, utafungua mizigo mingapi? Sheria ya Forodha,inasema utoe jora la nguo upime yadi kwa yadi weweutapima makontena 100 utayaweza, that is subjective. Letascanner, ni rahisi ukakopa scanner hata kama ni za shilingibilioni 100 ukaweza kuokoa hayo mabilioni ambayounapoteza kwa mwaka. Ushauri wangu ndio huo, nadhanikwa kufanya hivyo tutapata fedha nyingi na mnaweza kukutafedha mtakazookoa mtaweza kupunguza tozo na ushurumwingine kwa wananchi, pale tunapoteza fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie kwenye Wizaraya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo. Mimi ni mvuvi na nikokwenye Mambo ya Maendeleo ya Mifugo. Tuliomba fedhaziongezwe, tumeongezewa shilingi bilioni ishirini, nashaurikatika fedha zile zichukuliwe angalau shilingi bilioni tanoziwekezwe makusudi katika kilimo cha samaki. Wachinawamejifunza kilimo cha samaki Tanzania. Tuwekeze katikakilimo cha samaki ambao wananchi wakifuga samaki basiwatapata kile kipato. Kilimo cha samaki kikikua wananchiwatakuwa na uchumi utakua na wananchi wenyewe.Bwawa la samaki la mita 20 kwa 30 lililowekewa vinyoleo vyakuongeza oxygen ukiwekeza shilingi milioni kumi unapatamilioni sitini katika miezi minne, hakuna biashara inalipa kamahiyo. (Makofi)

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

162

Mheshimiwa Mwenyekiti, twende kwenye shughuli yaMheshimiwa Waziri ya kuongeza bei ya mafuta ili yawezekupata kipato. Mwaka 2007, Serikali iliweka gharama yamafuta fuel levy ili kujenga na ku-maintain barabara. Sh.200ya mwaka 2007 sio Sh.200 ya leo. Naunga mkono Serikalikwa kuongeza Sh.63 kwenye fuel levy ili tujenge barabara.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Ujenzi alisimamaBungeni akasema Mwijage barabara yako ya Muhutwe,Kamachumu itajengwa, jungu kuu halikosi ukoko, nakuungamkono kusudi ujenge barabara yangu, nakuunga mkonokusudi mpate fedha ya kutosha kujenga daraja la Kishara,nakuunga mkono kusudi Wabunge wote hawa wanaotakabarabara zao zipandishwe daraja waweze kupandishiwadaraja. Ni kwa misingi hiyo tunakuunga mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, shilingi hamsini za REA,kimsingi mimi ningekuwa na uhuru wa kusema ningesemahizi fedha ziongezwe. REA kwa miaka mitatu kilawanachoahidiwa hawapewi. Busara ya Kamati ya Nishati nikwamba REA sasa ipewe fixed amount kama tozo kusudituwe na uhakika kiasi gani tumemtengea REA na ile fedhaizuiliwe iwe ringfenced. Naunga mkono ongezeko la shilingihamsini kama fedha ya umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Keissyamesema sisi hatuna mjomba Ulaya, hatuna shangazi,wajomba wengine anasema watatuumiza, kwa hiyo tujifungemkanda sisi kusudi tuweze kuwekeza katika sekta hizo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri waFedha atakapokuwa ameweka michanganuo yake hiyokatika bei za mafuta atakuja kuona kitu ambacho si chakawaida katika soko. Atakuwa ame-load ushuru Sh.713kwenye petroli na Sh.515 kwenye pampu haitapendeza.Lazima achezee hesabu zake, apunguze kwenye petrolikusudi awasaidie zaidi hawa watu wanaolalamikiwa wabodaboda lakini upunguze kuna wafanyakazi wa Serikali,

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

163

Walimu wamenunua vile vigari vidogo vinavyotumia petroliuweze kuwasaidia hawa watu kusudi na wenyewe wawezekupata nafuu. Waziri asiwe na wasiwasi, achezee matrix,achezee tarakimu zake ataweza kuona kabisa atabaki nakiasi cha fedha anachokitaka cha shilingi trilioni 1.714, hamnatatizo ataweza kuzipata. Afanye homework, awatume vijanawake wafanye homework atafika pale lakini mimi naungamkono zoezi la kujinyima, kujifunga mkanda kusudi tuwezekupata fedha za kuendeleza nchi zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la mazaoya wakulima. Naishukuru Serikali imetoa tamko kwambaSheria ya Ushirika italetwa Bungeni na iletwe, wakulima wanahali mbaya, ushirika unapashwa kuangalia upya. Nimekuwanikipata message leo kwamba mkulima wa kahawaanachopata ni asilimia 30 ya bei ya soko la dunia, kilichobakihapa ni ukiritimba wa Tanzania Coffee Board na Vyama vyaUshirika. Naomba hiyo sheria ije na inapokuja ilenge mambohayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa na tatizo la watuwa korosho, nimewahi kulisema hapa katika swali lanyongeza. Tunapashwa Serikali tuwekeze fedha nyingi,tuokoe zao la korosho kwa kui-brand korosho ya Tanzania,tuache watu wa kati, twende sokoni, tumia fedha nyingi, itwill be costly, peleka watu waende kwenye soko Marekanina Ulaya wakiitengeneza na kuiuza na kui-brand korosho yaTanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru leo asubuhi Waziriwa na Biashara na Viwanda ametangaza ujio wa kiwandakikubwa cha Kijapan kitakachokula pamba yetu. Nimatumaini yetu kwamba kitaleta na ma-designer wa nguonzuri, tusingependa kuona mwekezaji anakuja kuwekezaTanzania anatengeneza nguo ambazo sisi hatuzipendi,tumeshazoea suti nzuri nzuri. Kwa hiyo, waje watengenezenguo hapa lakini watutengenezee nguo nzuri,wakitutengenezea nguo ambazo hazivutii na yenyewe hiyoitakuwa counter productive.

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

164

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwa watu wa TRAtena. TRA baada ya mabadiliko haya ya bei, mtakuwa naexposure ya Sh.530 kwa dizeli ukilinganisha na mafuta yandege. TMMA mnapaswa muisaidie TRA na EWURA muisaidieTRA ili tuweze kudhibiti kimsingi mafuta ya dizeli yanayoingiakwenye migodi. Haiwezekani jenereta iliyopangiwa kutumiadizeli lita 10,000 kwa mwaka ikatumia lita 100,000. Tungetakahizo Mamlaka za Serikali ziweze kusimamiwa, ziwezekuhakikishiwa kwamba zinatumia mafuta yale ambayo walemanufacturers, OEM (Original Equipment ManufacturersRecommendation) waliyoyasema na lazima hizi Mamlakaziwe taxed. Nashauri Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajetimuwaite hawa watu wa TMMA, muwaite hawa watu wa TRAmuwaulize watafanya nini? Kwa sababu Sh.530 ni motishatosha kwa mtu kuweza kufanya kitu anachotaka kufanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napokuja kwa MheshimiwaComrade Chiligati tuzungumze tax culture. Inaweza kuletamashaka uongezaji wa kodi. Serikali inafanya vibaya auinakwenda kinyume na kanuni za uchumi kwa ku-tax rawmaterials, kwa ku-tax petroli, lakini iko haja sasa tutumie mbinuzote…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa hiyo ni kengele ya pili.

MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana. Nilikuwa namsikiaMheshimiwa mmoja kule anasema kwa sababu ya busaraza Mheshimiwa Keissy Mabodi, nikuongezee dakika 10 lakiniKanuni hairuhusu. Kwa hiyo, naomba tu tuendelee namchangiaji anayefuata. Atafuata Mheshimiwa Rukia KassimAhmed, Mheshimiwa Richard Ndassa ajiandae na kamamuda utaturuhusu Mheshimiwa Kilufi naye atapata nafasi yakuchangia.

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

165

MHE. RUKIA KASSIM AHMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana nami kunipa fursa hii nikaweza kuchangiakatika bajeti hii ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kuchangia,napenda nikipongeze chama changu cha CUF kwa ushindimkubwa tulioupata kule Pemba na kesho tutaingiza medaliya dhahabu Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hivyo,naanza na kuchangia bajeti ya Serikali. Mimi naanza nakusema kuwa fedha za bajeti ya maendeleo ni ndogo sana,ni asilimia 31. Katika hizi asilimia 31, asilimia 21 inategemewakutoka kwa wafadhili. Hali za wafadhili wetu tunazijua zinamasharti magumu. Je, pale ambapo fedha hizihazitopatikana ina maana hakutokuwa na shughuli zozoteza maendeleo katika nchi hii? Mwaka jana tuliahidiwakupewa shilingi trilioni 1.89, lakini matokeo yake tulipata shilingitrilioni 1.23 sawa na asilimia 65. Je, Mheshimiwa Waziri waFedha ikiwa tutakosa fedha hizi tutafanyaje? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kutoka hapo,nataka sasa nizungumzie vyanzo vya mapato. Siku zoteSerikali inang’ang’ania na vyanzo vya mapato hivyohivyo,hatubadilishi. Kila siku tukitaka kuongeza mapato tunaanzakusema kama tutaongeza ushuru katika vinywaji baridi, bia,soda, sigara na kadhalika. Mimi nasema hivi kila sikututaendelea kutwanga maji kwenye kinu? Kuna sentensi mojamimi inaniudhi sana katika bajeti kila mwaka naionawanasema kama ushuru wa cigar utaendelea kubakiapalepale asilimia 30. Mimi nataka nikuulize Mheshimiwa Waziriwa Fedha hivi ni Watanzania wangapi wanaovuta cigarhapa nchini? Nataka uniambie ni kiasi gani cha mapatotunachoingiza kutoka katika hizo cigar hata ikawa kila sikutunang’ang’ania na mambo haya? Tunaacha kuzungumziani kiasi gani cha mapato tunayoongeza kutoka katika sektaya madini, tunakwenda ku-deal na cigar. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ina madini mengisana. Mimi nataka niseme katika Mkoa unaoongoza kwa

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

166

umaskini uliokithiri ni Geita. Ukiacha Geita ni Bunda na Igungalakini Geita kuna migodi miwili mikubwa, hivi jamanihatuwaonei huruma Watanzania wale walioko Geita?Hakuna maji, hakuna umeme, nyumba zenyewe ziko‘dhoofulihali’, hivi kweli Serikali haioni tunawaachiawawekezaji wakubwa wanakuja wakichukua dhahabu zetuwakipeleka nje, lakini Watanzania wale wabakia katika haliya umaskini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi jamani tutakwendakusema nini kesho mbele ya Mungu? Serikali iwapatie majisafi na salama kutokana na kile kinachopatikana kule kwao.Wapatiwe barabara ingawa mambo haya mimi nasemakuwa si maendeleo wakipewa mambo haya kwa sababu niwajibu wa Serikali kuwapatia maji safi na salama pamoja nabarabara. Sijapata kusikia mkono ukipewa shukrani na mguukwa kuutoa mwiba, huu ni wajibu wake. Pia tukiwapatia walewatu wa Geita maji safi na salama, hatuwezi kusema nimaendeleo ni sawasawa na nyumba kwenye nyumba lazimakuwe na mwiko na sufuria, ni kitu cha kawaida katika nyumbakuwemo. Sasa leo tunawaachia wawekezaji wakubwa, walehawakuja hapa kutembea wamekuja kwa biashara, kwa niniSerikali haiwatozi ushuru? Kila siku kilio cha Watanzania ni hiki,tutaiacha nchi inateketea, twaachiwa mashimo na mpango,watu wanabakia tukiangalia, wanakwenda kutumia watuhuko ulaya. Jamani tumuogopeni na ‘mchana kusudi atavaakusudi’ tutakuja kusutwa huko tunakokwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,mimi nataka niende kwenye kodi ya mishahara. Serikaliimesema kuwa imewapunguzia mishahara kwa 1% yaanikutoka 14% mpaka 13% huku ni kuwadhihaki watumishi waSerikali. Tunasema kama uchumi unakua, ni kweli unakualakini bado chakula kiko vilevile, bei iko juu, kuna gharamaza usafiri, kuna gharama za kodi ya majumba wanazo kodi,kuna gharama za maji, kuna gharama za umeme, hivi 1% hiitunayoitoa ni kweli tumewapa unafuu hawa wafanyakazi waSerikali? Huku ni kuwadhihaki na naiomba Serikali itafute ninmana gani ya kuwasaidia watumishi hawa wa Serikali.(Makofi)

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

167

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ninatoa ushauri,naomba tuwapunguzie kwa 3%, nakisi hii tuitoe kwenyevocha za simu. Matumizi ya simu Tanzania yamekuwamakubwa na ni kwa sababu hizi vocha ni rahisi. Humu tunawatu wana miaka 65 kazi yao ni kusikil iza simu nakudanganywa na watoto wadogo wakiitwa baby. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wengine ndoa zinavunjikakwa sababu ya simu hizi za mkononi. Watoto wetu wanafelikutokana na kuchati kwenye simu, kila wakati wanachati nakutuma message. Mimi naiomba Serikali tuongeze kodikwenye vocha za simu, 3% tupeleke kwenye mishahara ilitusaidie watu, anayetaka kuitwa baby basi atagharamika.(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kutoka hapo,nataka niende kwenye sekta ya elimu. Karibu 80% ya watotowetu wameacha kusoma masomo ya sayansi na wanasomamasomo ya arts, hivi kweli sisi wenyewe hatujaliona hili?Wataalam wengi tulionao ni kuanzia miaka 60 na kwendajuu, umri wetu ni mfupi, hatusomeshi watoto na hii yoteinatokana na mwanzo mbovu wa watoto kwenye masomoya hisabati na sayansi. Mimi naishauri Serikali ili kuondokanana hili na ili tuweke akiba vizuri, tusomeshe watoto wetumasomo ya sayansi. Naishauri Serikali kila Wilaya ittengweshule moja ipewe vifaa vya maabara vya kutosha na Walimuwazuri tuwasomeshe watoto wetu sayansi ili tuwe na akibaya baadaye. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MHE. RUKIA KASSIM AHMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,kama kengele siyo yangu niambie niendelee.

MWENYEKITI: Hiyo siyo ya kwako ni ma-baby tuwalikuwa wanakusikiliza kwa makini. (Kicheko)

MHE. RUKIA KASSIM AHMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,ikiwa tutawasomesha watoto wetu masomo ya sayansi,

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

168

tutakuwa tumejiwekea akiba ya baadaye lakiniinavyoonekana Serikali hili hawajaliona. Hebu tufanyenitathmini, tuangalie watoto wetu namna wanavyokuwawanaacha masomo ya sayansi na kusoma masomo ya arts.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kutoka hapo,naomba niseme hivi jamani Serikali haioni jinsi Wazanzibartunavyonyanyasika katika Jamhuri hii ya Muungano?Wazanzibar sisi Wabunge tuliomo humu ndani tunashindwakuleta magari yetu hapa kwa sababu ya kutozwa ushurumkubwa. Mkenya anaweza kutoka na gari lake Kenyaakalipa dola ishirini na akaweza kutembea na akafanyashughuli zake. Sisi tunaoambiwa kama ni Watanzaniatuliokamilika, tunashindwa kuleta magari yetu hapa kutokanana ushuru ulivyo mkubwa. Sasa kila tukisema kuwa hii ni kerowenzetu hamuioni? Jamani ‘mwajua kuwa ukerezwaomwisho wake huanguka’ au ndiyo nia mliyoikusudia hiyo?Mimi naishauri Serikali sana kwa nia safi kabisa kuwa kero hiituondosheeni, tumechoka, tena tumechoka sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naomba kukaa kitako. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Rukia.Kwa kweli leo misamiati yako imetuacha hoi kabisa,‘ukerezwao mwishowe huanguka’. Waheshimiwa Wabunge,nimwite Mheshimiwa Ndassa na nadhani Mheshimiwa Kilufianaweza kupata nafasi, Mheshimiwa Ndassa tafadhali.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa nafasi hii ya jioni na mimi nitoe mchangowangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nitamke kuwanaiunga mkono hotuba ya Waziri wa Fedha, hotuba ya Waziriwa Mahusiano Mheshimiwa Wasira lakini niipongeze sanaKamati ya Mtemi Chenge kwa mapendekezo mazuri sanaambayo nina uhakika Serikali itayafanyia kazi vizuri. Naombasana Serikali, kuna mapendekezo ya muda mfupi, ya muda

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

169

mrefu na ya kati. Kwa hiyo, yale ya muda mfupi MheshimiwaWaziri wa Fedha na Mheshimiwa Wasira basi mngeyachukuana kuyafanyia kazi, hivyohivyo na mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumze kuhusuumeme. Nenda popote pale duniani, nenda uendako,umeme ni kila kitu. Maendeleo yoyote duniani pasipoumeme, usitegemee utapata maendeleo. Kwa hiyo, miminaomba sana Wizara ya Fedha, pesa ambazo zimetengwakwa ajili ya umeme, zitumike kwa kazi nyingine yoyote ile ilaziende kwenye umeme. Narudia, pesa ambazo zimepitishwakwa ajili ya umeme, kwa maana ya ujenzi wa miundombinuna kujenga umeme vijijini kupitia mpango wa REA, zisitumikekwa nyingine yoyote ile i la zifanye kazi ya kujengamiundombinu ya umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niiombe Serikali kwasababu kutakuwa na bomba la gesi, tufanye juu chini ili ndaniya miezi 18 bomba hilo liwe limekamilika. Likishakamilika, ninauhakika gharama za umeme kwa Watanzania zitapunguasana. Tusifanye ajizi, kama tunavyopanga vitu kwavipaumbele hivyohivyo, naomba Serikali isisite kutekeleza.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye suala lingineambalo nafikiri wenzetu Wizara ya Fedha na Wizara yaMawasiliano sijui huwa kunakuwa na kigugumizi gani. Bandariya Dar es Salaam, ule ni mgodi, ni sehemu ambayo Tanzaniatunaweza kuvuna pesa nyingi kwelikweli lakini nashangaatumeachia tu. Ukichukua nchi sita zinazopitisha mizigo yakepale Dar es Salaam kama kungekuwa na usimamizi mzuri naWaheshimiwa Wabunge kila mara tumekuwa tukisema lakinihakuna kinachofanyika. Bandari ya Dar es Salaam baadaya kwenda pale Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe ambayeninampongeza sana kwa kazi yake nzuri anayofanya mapatoyaliongezeka sana lakini unajiuliza hivi huko nyumakulikuwaje? Kama mapato yaliongezeka, tatizo lilikuwa ninini? (Makofi)

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

170

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa liko sehemumbili TRA na TPA rushwa imezidi. Niiombe Serikali nanimwombe Mheshimiwa Waziri wa Fedha atakapokujawakati anafanya majumuisho, atuambie ana mikakati ganiya kuboresha bandari ya Dar es Salaam, ana mikakati ganikuzuia wizi uliopo, ana mikakati gani kuzuia upotevu wa mizigobandari ya Dar es Salaam mizigo, pale mizigo inapotea sanana kila mtu anafahamu. Nimesema Bandari ya Dar es Salaamni mgodi ambao unaweza kutuingizia pesa nyingi sana hasatukisimamia vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni misamaha ya kodi.Mheshimiwa Waziri wa Fedha bado hujaamua kuhusu sualala misamaha ya kodi.

MBUNGE FULANI: Wako holiday.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Naambiwa huku sijui mkoholiday. Katika kitabu chako, ukurasa wa 44 unasemakuangalia upya misamaha ya kodi kwa lengo ya kuipunguza.Ukienda ukurasa wa 62, unasema aidha, Serikali inakamilishakazi ya utafiti wa kuchambua misamaha. Hivi mnachambuampaka lini, ni utafiti ni upi ambao hamuujui mpaka leo?Mnatafiti, mnachambua, mnatafiti, mnachambua, hivimisamaha hii hamuijui? Hivi mnataka Wabunge waseme ninindiyo muelewe? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnalalamika kuhusumapato, mapato yako pale, yanavuja pale kwa sababu yamisamaha mingi na kila Mbunge amekuwa akisema humu,tumekuwa viziwi. Naomba sana Mheshimiwa Dkt. Mgimwa,Waziri wa Fedham, ili tupunguze utegemezi ni pamoja nakupunguza mianya ya misamaha ya kodi. Tukifanya hivyo,nina uhakika tutafika mbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa kuiombaSerikali kwa sababu kutakuwa na bomba la maji kutoka ZiwaVictoria, Waziri wa Maji tafadhali sana, maji yanatoka Magu.Katika Kata ya Mwabomba, Kalalo, Nyambiti, Wala,Bhujingwa, bomba hilo lipite sehemu hizo. (Makofi)

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

171

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.(Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Ndassa.Mchangiaji wetu wa mwisho nilisema atakuwa MheshimiwaKilufi.

MHE. MODESTUS D. KILUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ili na mimi niwezekuchangia bajeti hii ya mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sanaMheshimiwa Spika kwa utaratibu huu mpya wa bajeti ambaoumetushirikisha vya kutosha Waheshimiwa Wabunge namichango yetu mingi imefikiriwa na ninashukuru sanakwamba kwa sasa tunaweza tukaenda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna kinachowezakufanyika katika Taifa lolote lile kama uchumi wake siyo mzuri.Ni uchumi tu unaoweza kutufanya Walimu wetu wapatemishahara ya kutosha, Idara zote za Serikali ziweze kufanyakazi vizuri, barabara zetu ziweze kutengenezwa vizuri, kilimokiweze kuendeshwa vizuri. Hakuna nchi iliyoendelea kiuchumibila kuwa na miiko. Tanzania tutacheza, tutasema sana hapalakini kama hatujiwekei miiko ya kudhibiti hali ya uchumikatika nchi hii, hatuwezi kupata maendeleo hata kidogo. Ninauhakika hata nchi zilizoendelea zina miiko. Tanzania hatunamiiko na sijui tunaogopa kitu gani. Tuna uchumi mzuri, sisi siyomaskini nchi hii siyo masikini kama ni umasikini basi tunao waaina nyingine siyo umasikini wa rasilimali. Rasilimali tunazo zakutosha, sasa ni jukumu letu kujiuliza wapi tunakwama nawapi tunajikwaa. Tatizo hatuna miiko, watu wanafanyawanavyotaka hakuna uwoga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale bandarini, namshukurusana Mheshimiwa Mwaijage alikuwa anasema kuna chombokinaitwa scanner kinatazama kila kitu kilichopo kwenyekontena, ni kitu ambacho kingetuokolea uchumi mkubwasana pale bandarini lakini Mheshimiwa Mwijageamezungumza mara nyingi, ukienda kwenye Hansard

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

172

utakuta, nimelikuta mimi lakini ushauri huo hauchukuliwi. Kunanini pale bandarini tunapoteza fedha nyingi? Watuwanaofanya kazi Bandari, wameishi peponi kwa muda mrefusana na hawakutegemea kama kuna siku kutakujamabadiliko. Tupeleke scanner ikachunguze makontena yaleyanapoingia waone kila kitu kilichomo mle ndani ili watuwasikwepe, tunapoteza fedha nyingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye migodi yetu kunafedha nyingi zinapotea kule. Nchi hii kama tungedhibitiuchumi, siyo maskini sisi. Kwa nini Watanzania tunawavishaumaskini sisi tuliopewa majukumu ya kusimamia uchumi waTaifa hili? Tofauti ya mapato inajenga chuki katika jamii.Watanzania hawatatuvumilia kuona rasil imali zaohazisimamiwi vizuri, watu wanaishi kwa shida, watumishimishahara haitoshi, Walimu wanahangaika, wafanyakaziwastaafu wanapata shida, tumethubutu hata Wanajeshiwastaafu kutowalipa vizuri, wanalalamika, tunakwenda wapina uchumi tunao? Tatizo ni kudhibiti tu. Mimi naunga mkonoyeyote atakayehusika na ubadhirifu wa mali ya ummaanyongwe kama Mheshimiwa Keissy alivyosema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawahakikishieni nduguzangu, hakuna Mtanzania atakayepinga kuwa anayehujumuTaifa hili anyongwe na kufilisiwa mali zake hata tungepigakura za maoni, wote wangetuunga mkono. Tunaogopa ninikufanya maamuzi haya makubwa ili tulinde uchumi wa nchihii, tunachoogopa kitu gani? Kwa nini tusiweke sheria tupitishehapa Bungeni, Wabunge wote tupo tupitishe kwamba yeyoteatakayejihusisha na uhujumu uchumi wa Taifa hili anyongwena afilisiwe mali zake, tukifanya hivyo, nina uhakikatutakwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasimama hapo kamaMbunge kutoka Jimbo la Mbarari, nimetumwa naWanambarari kuangalia keki hii, wanasikiliza shilingi trilioni 18Mbarari ni nini kitafanyika. Wanaangalia na wenyewe kuwatumempeleka mwenzetu kule je, Mbarari tunapata kitu gani?Nawaomba ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge, rasilimalihizi zigawanywe sawasawa. Kama tatizo la maji liko Mkoa

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

173

fulani na Mbeya na Mbarari vilevile tuna tatizo la maji. Kamakipaumbele ni maji basi na Mbarari kipaumbele hichokiangaliwe. Kama tatizo ni barabara basi na Mbarariziangaliwe. Katika shilingi trilioni 18 haiwezekani mimi Mbararinikarudi sina kitu, barabara hakuna, bahati mabayaMheshimiwa Magufuli hayupo nilimwomba barabara yaRujewa – Madibila ni ahadi ya muda mrefu lakini utekelezajiwake ni hadithi, Wanambarari tumechoka kusikiliza hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeomba kabarabarakadogo tu, kana sifa zote za kiuchumi ka kutoka Igawakwenda Ubaruku kuchukua mchele unaokobolewa kwenyeviwanda pale ambao unaingia Dar es Salaam kila siku nayenyewe naahidiwa, inajengwa nusu kilomita kwa mwaka,kilomita kumi na nane itajengwa kwa miaka mingapi? Kamani sifa uchumi upo, barabara ile kila siku mchele unapitishwakwenda Dar es Salaam kwa nini barabara ile isijengwe?Sikubaliani na Wanambarari hawakubali kabisa. Kama niuzalishaji tunafanya, Mbarari tunaongoza kwa scheme nyingiza umwagiliaji lakini barabara zake ndiyo hizo haziimarishwi,kwa nini? Kuna nini? Kuna upendeleo kwenye kugawarasilimali za Taifa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekuwa nikiangaliaWizara ya Elimu, shule za msingi, shule za sekondari namnazitakavyoboreshwa. Mbarari mimi sina shule nyingi sana lakininimepewa shule tano, saba. Kuna mahali wana shule 150wamepewa shule 100, hivi kwa nini uwiano huu wenye shulechache zisichukuliwe zote? Hata na mimi mnanipa hesabuza shule saba, shule zangu hata 30 hazifiki, kwa nini shule zotezisipewe hiyo huduma? Ili wenye shule 100 watusubirie sisiwenye chache zinazozidi ndiyo wachukue wenyewe. Niupendeleo ambao haukubaliki, keki ya Taifa ni lazimatugawane sawasawa, haiwezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema Mheshimiwa Waziriwa Elimu kama ananisikiliza, shule za Mbarari kama ataiachahata moja mimi sitakubaliana hata kidogo. Nina shulechache, watu wamepewa shule 100, watu wamepewa shule50, Mbarari chache zile eti nimepewa tano, sita, kwa nini?

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

174

Kama kweli tunataka kugawa uchumi wa wananchi waTanzania kwa usawa, kwa nini? Haiwezekani kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna miradi mingi ya kilimocha umwagiliaji, Mwenda mtitu inakwenda vizuri, ni ahadiya Serikali, naishukuru sana Serikali kwamba ule mradiunakwenda vizuri na nina uhakika utakamilika. Tuna ujenziwa Hospitali ya Wilaya, naishukuru Serikali unakwenda vizuri,naomba jitihada hizo ziendelee. Tuna mradi wa kujengabwawa kubwa Madibila pale ambalo litamwagilia hekta3,600 Mheshimiwa Rais aliahidi, nashukuru sana na jitihadanimeona zinaendelea na mahali pengine pengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina tatizo la umeme katikaWilaya ya Mbarari. Katika Kata 20 ni Kata nne tu zimepitiwana umeme hivi mnataka kusema Mbarari ni wapi?

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa kengele ya pili.

MHE.MODESTUS D.KILUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. (Makofi)

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. MASOUD ABDALLA SALIM: Mwongozo wa Spika.

MWENYEKITI: Miongozo tena.

MHE. MASOUD ABDALLA SALIM: MheshimiwaMwenyekiti, kidogo tu naomba Mwongozo wako kwakutumia Kanuni ya 68 (7) na ninaomba niseme yaleyaliyonisukuma kuomba Mwongozo huu. Katika hotuba yaMheshimiwa Clara Diana Mwatuka, akitoa maelezo yakehapa wakati akichangia, alieleza masikitiko yake na akasemaanakosa imani na nguvu ya kuweza kuchangia ambapo kunabaadhi ya Watanzania wenzetu ambao wanaendeleakunyanyasika, kupigwa na kuumizwa. Hili ni jambo kubwa,

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

175

halistahamiliki, linahitaji kupatiwa ufumbuzi wa kudumu naSerikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Clara Mwatukawakati akiendelea na mazungumzo yake alieleza waziwazikuwa tatizo hili linasukuma hata Wanajeshi kuingia katikanyumba za watu. Je, Serikali katika hili, kwa nini linaachiwalinaendelea hivi na Watanzania wanaendelea kuumizwa nahawa ni wananchi wetu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mwongozo wakojuu ya tatizo hili ambalo linaendelea kutokea huko Mtwara,nashukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kombo.

MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO: MheshimiwaMwenyekiti, naomba Mwongozo wako. Kesho ni Alhamis …

MWENYEKITI: Kanuni ya ngapi?

MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO: MheshimiwaMwenyekiti, Kanuni ya 64(7). Kesho ni Alhamis, sisi Wabungetuna fursa ya kumuuliza Waziri Mkuu maswali moja kwa mojalakini hii ni wiki ya tatu hatujapata nafasi hiyo, tunaombaufafanuzi kama kesho tutapata nafasi hiyo?

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naona mudaumebaki kidogo lakini nitajibu hiyo miongozo ya Wabunge.

Mheshimiwa Kombo, kesho ni Alhamis na ni kipindi chamaswali kwa Waziri Mkuu, kwa taarifa ambazo zilikuwa rasmikabisa ndani ya Bunge Mheshimiwa Waziri Mkuu alikuwasafarini na si taarifa tu ndani ya Bunge na sisi wote tumekuwatukimshuhudia akifanya kazi mbalimbali kupitia kwenyevyombo vya habari. Kwa hiyo, kwa taarifa hii naomba niiarifuOfisi ya Katibu wa Bunge, wataendelea kuwasiliana naMheshimiwa Waziri Mkuu kama atakuwa yupo kwa ajili yamaswali kesho asubuhi, utaratibu wa shughuli za BungeWabunge wote tunaupata kupitia muundo mpya wa

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

176

utendaji kazi wa Bunge kwenye simu zetu huwa tunapewaajenda za shughuli za Bunge za siku inayofuata. Kwa hiyo,kama Mheshimiwa Waziri Mkuu atakuwa amerudi, ratiba hiyotutaipata na tutapewa taarifa rasmi na niwaombe Makatibuwangu mnaonisaidia kuniongoza hapa mbele leo, hilo sualapia mlipatie ufafanuzi ili Waheshimiwa Wabunge wajue kamawanatakiwa kuja mapema kwa ajili ya shughuli hiyo ama vipi.

Mheshimiwa Masoud umezungumzia suala la hotubaya Mhesmiwa Clara, naomba nimwombe Mheshimiwa Claraawasilliane na Waziri husika, amweleze kile ambacho alikuwaanakizungumza kwa sababu hata hivyo katika kuchangiahotuba hii, nimechukua tu nafasi yangu kama Kiti kumvumiliakwa sababu ajenda aliyokuwa anazungumza kwa mujibu waKanuni ilikuwa siyo ajenda ambayo iko Mezani. Kwa hiyo, kwanafasi yake angeweza kutumia Kanuni nyingine naakalizungumza suala hilo lakini kwa uzito wa jinsi alivyosema,namwomba sana Mheshimiwa Clara awasiliane na Wazirihusika, nadhani anaweza kupata maelezo mazuri na ya kinana ninaamini kwa jinsi ninavyomjua Waziri husika atapatanafasi ya kumsikiliza vizuri na ataweza kupata suluhu ya ninikinachofanyika na anaweza akasaidia kujua nini chakufanya.

Mwongozo mwingine ambao nilikuwa nimeombwahapa ndani niliombwa na Mheshimiwa Keissy na MheshimiwaKeissy alitaka kujua kwa nini hawa Waheshimiwa Wabungewanapochangia hawazungumzia kutoa na wao ushauri kwaSerikali ni namna gani Serikali ifanye ili kuweza kuongezamapato badala yake wanachangia tu na ndipo hapoalipokuwa anashauri hata yeye kuwa mpaka kukuwanaweza kutozwa kodi ili kuongeza uchumi na pato la Taifa.

Waheshimiwa Wabunge, Kanuni ya 106 inasimamiamjadala kuhusu hotuba ya bajeti na nitasoma Kanuni ya 106(1) ambayo inasema:-

“Mjadala kuhusu hotuba ya bajeti ya Serikaliutaendelea kwa siku zisizozidi saba ambapo dakika zisizozidi

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462350218-HS-11-52-20… · jambo hilo. Ukisema sasa tunakwenda kuzivunja zile Kata

19 JUNI, 2013

177

kumi zitatolewa kwa kila Mbunge anayetaka kuchangiahotuba hiyo”. Hiyo tunakwenda nayo hivyo.

Kanuni ya 106(2) inasema:-

“Katika hatua hii, majadiliano yatahusu mambo yajumla kuhusiana na hali ya uchumi…”

Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge wanachokifanyahapa ni kuzingatia ile Kanuni, kuzungumza mambo ya jumlakuhusiana na hali ya uchumi lakini hata hivyo ushauri pia nabusara alizozitoa Mheshimiwa Keissy nazo zina manufaa.Tunapozungumza hali ya jumla ya uchumi wetu, ni vizuri sanaWaheshiumiwa Wabunge kama pia tutajikita kuishauri Serikali,nini kifanyike ili kuongeza mapato, kubana matumizi nakujenga uchumi imara wa nchi yetu ya Tanzania. Kwa hiyo,hayo pia ni mawazo yenye busara tu ambayo nadhanitukiyafuata pia yana nafasi nzuri ya kuweza kujenga nakuisaidia Serikali yetu.

Niendelee kuwaarifu Waheshimiwa Wabunge naWatanzania wote, Wabunge wanapochangia wanazingatiaKanuni niliyoisoma na Kanuni hiyo inasema ni lazimakuzungumzia mambo ya jumla yanayohusiana na hali yauchumi wa nchi yetu. Baadaye tutakapokuja kwenyekuhitimisha, Mheshimiwa Waziri, mtoa hoja au watoa hoja,watayatizama mambo haya yote na kuona namna ganitunaweza kufanya ili kuboresha uchumi wa nchi hii.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya hayo, naombaniwashukuru kwa siku hii ya leo, naahirisha shughili hizi zaBunge mpaka kesho saa tatu asubuhi ndani ya ukumb huuwa Bunge.

(Saa 1.45 Usiku Bunge liliahirishwa Mpaka Siku ya Alhamisi,Tarehe 20 Juni, 2013, Saa Tatu Asubuhi)