12
IBFAN Africa COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005

COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Zijue-Haki-za-Uzazi-ka… · zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku 100 yenye

  • Upload
    others

  • View
    3

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Zijue-Haki-za-Uzazi-ka… · zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku 100 yenye

1

IBFAN Africa

COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005

Page 2: COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Zijue-Haki-za-Uzazi-ka… · zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku 100 yenye
Page 3: COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Zijue-Haki-za-Uzazi-ka… · zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku 100 yenye

1

KATIKA SHERIA MPYA YA KAZI TANZANIA

Kimetayarishwa na:Kituo cha Ushauri Nasaha,Lishe na Afya (COUNSENUTH)S. L. P. 8218Dar es SalaamSimu: +255 22 2152705 +255 755 165 112Barua pepe: [email protected]

Kwa kushirikiana na: Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na MichezoS. L. P. 1422 Dar es Salaam Simu: +255 22 2125609 Kimefadhiliwa na:IBFAN AfricaP. O. Box 781 Mbabane, Swaziland Tel: +268 404 5006

ISBN 9987-9017-2 -7 @ COUNSENUTH, 2005

Reprinting Sponsored by ILO, April, 2011

Sehemu yoyote ya kijarida hiki inaweza kunakiliwa kwa ajili ya matumizi yasiyo ya kibiashara ilimradi ionyeshwe kwamba taarifa hizo zimetoka kwenye kitabu hiki cha COUNSENUTH Information Series No. 9.

IBFAN Africa

IBFAN Africa

IBFAN Africa

Page 4: COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Zijue-Haki-za-Uzazi-ka… · zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku 100 yenye

2

Shukrani

Tunatoa shukrani za dhati kwa IBFAN Africa, ambao wamefadhili utayarishaji na uchapishaji wa kijitabu hiki.

Shukrani za pekee kwa Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo kwa kushirikiana na sisi katika hatua zote za utayarishaji wa kijitabu hiki. Shukrani pia kwa Taasisi zifuatazo zilizoshiriki kikamilifu katika kufanya kazi hii ifanikiwe: Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA), Wizara ya Afya - Huduma za Uzazi na Watoto na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Tunawashukuru watu mbalimbali waliohusika kwa namna moja au nyingine katika utayarishaji wa kijitabu hiki, hususan wafuatao: 1. Abubakar Rajabu Katibu Mkuu - Wizara ya Kazi,

Maendeleo ya Vijana na Michezo2. Hilda Missano TFNC3. Mary Chuwa TAMA4. Siham Ahmed TUCTA5. Hilda Makwinya Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana

na Michezo6. Teodesia Mbunda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia

na Watoto7. Regina Kutaga Wizara ya Afya, Huduma za Uzazi na

Watoto 8. Mary Materu COUNSENUTH9. Restituta Shirima COUNSENUTH10. Tuzie Edwin COUNSENUTH11. Belinda Liana COUNSENUTH12. Margaret Nyambo Hospitali ya Amana/ Manispaa ya lIala

Bila ushirikiano wao, kazi hii isingefanikiwa. Asanteni sana.

V. KainamulaMwenyekiti - COUNSENUTH

Page 5: COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Zijue-Haki-za-Uzazi-ka… · zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku 100 yenye

3

Utangulizi

Kijitabu hiki kimeandaliwa kwa nia ya kuwaelimisha waajiri, waajiriwa na jamii kwa jumla kuhusu haki za uzazi katika sheria mpya ya kazi Na. 6 ya mwaka 2004.

Taarifa zilizopo kwenye kijitabu hiki zitasaidia sheria hiyo kufahamika vizuri na hivyo kuwezesha wadau mbalimbali kuitumia ipasavyo ili kuboresha afya ya mama, mtoto na jamii na pia kuleta maendeleo. Vilevile wataweza kuchangia katika uboreshaji wa sheria hii.

Haki za uzazi katika sheria mpya ya kazi Tanzania

Haki za uzazi ni nini? Ni haki zinazomwezesha mwanamke mwajiriwa kutimiza majukumu yake ya uzazi na kufanya kazi au kuzalisha bila kubaguliwa, kubugudhiwa au kupoteza ajira.

Likizo ya uzazi ikiwa ni moja ya haki za uzazi, humpa mama muda wa kumuwezesha kutoa matunzo muhimu kwa mtoto katika miezi ya mwanzo ya maisha yake, ikiwa ni pamoja na kumnyonyesha. Vilevile likizo ya uzazi humpa mwanamke mwajiriwa muda wa kupumzika na hivyo kusaidia mwili wake kurudi katika afya na hali ya kawaida baada ya kujifungua. Kwa mantiki hiyo, ni muhimu mwajiri na mwajiriwa kufahamu vizuri haki hizo na wajibu wao katika utekelezaji wa sheria hiyo. Sheria mpya ya kazi Tanzania inasema nini kuhusu likizo ya uzazi? ✵ Mwanamke mwajiriwa anapaswa kumfahamisha mwajiri

wake nia ya kuchukua likizo ya uzazi angalau miezi mitatu kabla ya tarehe ya makisio ya kujifungua. Pia anatakiwa kuambatanisha kielelezo cha daktari.

✵ Mama ana haki ya kupewa likizo ya uzazi sio chini ya siku 84 yenye malipo.

Page 6: COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Zijue-Haki-za-Uzazi-ka… · zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku 100 yenye

4

✵ Mama aliyejifungua mtoto zaidi ya mmoja (mapacha au zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku 100 yenye malipo.

✵ Mama ana haki ya kuchukua likizo yake ya mwaka (siku 28) katika mwaka huohuo aliopata likizo ya uzazi. Aidha, sheria inaruhusu mama kujadili na mwajiri wake kama kuna uwezekano wa kuunganisha likizo hiyo ya mwaka na likizo yake ya uzazi.

✵ Likizo ya uzazi inaweza kuchukuliwa wiki nne kabla ya kujifungua au mapema zaidi iwapo kuna uthibitisho wa daktari kwamba ni muhimu kufanya hivyo kwa ajili ya afya ya mama au mtoto.

✵ Mwanamke ana haki ya kupewa tena likizo ya uzazi ya siku

84 yenye malipo endapo mtoto wake atafariki katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuzaliwa.

Chanzo: IBFAN Africa

Page 7: COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Zijue-Haki-za-Uzazi-ka… · zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku 100 yenye

5

✵ Mwajiri haruhusiwi kumpa mwanamke mwenye mimba au anayenyonyesha kazi ambazo zinahatarisha afya yake au ya mtoto. Endapo mama alikuwa anafanya kazi ambayo inaweza kusababisha hatari kwake au kwa mtoto; mwajiri anapaswa kumpatia kazi mbadala bila ya kwenda tofauti na mkataba au makubaliano ya ajira yake.

✵ Inapobidi mwanamke kubadilishiwa kazi kutokana na hali ya uzazi; hairuhusiwi kupewa kazi inayompunguzia kipato au marupurupu aliyokuwanayo awali.

✵ Mama mwajiriwa haruhusiwi kurudi kazini katika kipindi cha wiki sita za mwanzo tangu kujifungua isipokuwa pale tu atakapokuwa ameruhusiwa kufanya hivyo na daktari.

✵ Mwajiri haruhusiwi kumuachisha kazi mwanamke kutokana na sababu zinazohusiana na ujauzito au kujifungua.

✵ Kisheria, mwajiri anawajibika kumpa mwanamke mwajiriwa likizo nne tu za uzazi katika kipindi chote cha ajira.

Chanzo: IBFAN Africa

Page 8: COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Zijue-Haki-za-Uzazi-ka… · zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku 100 yenye

6

Muda wa kumnyonyesha mtoto wakati wa Kazi✵ Mama anayenyonyesha ana haki ya kupewa muda wa

saa mbili kwa siku wakati wa kazi kwenda kumlisha/ kumnyonyesha mtoto wake.

Kufanya kazi usiku

✵ Mwanamke mjamzito asipangiwe kazi za usiku kuanzia miezi miwili kabla ya kujifungua, au pale atakapoonyesha kwa mwajiri cheti cha daktari kinachoeleza kwamba hali yake haimruhusu kufanya kazi usiku.

✵ Mama anayenyonyesha asipangiwe kazi usiku katika miezi miwili baada ya kujifungua; isipokuwa mama akiomba na akiwa na cheti cha daktari kinachothibitisha kwamba afya yake au ya mtoto haitahatarishwa kwa kufanya kazi hizo.

✵ Mama anayenyonyesha asipangiwe kazi usiku hata baada ya miezi miwili iwapo ana cheti cha daktari kinachoonyesha hali yake au ya mtoto wake hairuhusu kufanya kazi usiku.

Chanzo: URC/QAP

Ubaguzi katika ajiraMwajiri haruhusiwi kwa wazi au kificho kumbagua mwajiriwa kutokana na jinsia yake, ujauzito, hali ya kuolewa, kulea au majukumu ya kifamilia.

Page 9: COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Zijue-Haki-za-Uzazi-ka… · zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku 100 yenye

7

Likizo ya uzazi kwa baba mwajiriwa

✵ Sheria mpya inaruhusu likizo ya siku zisizopungua tatu zenye malipo, kwa baba wa mtoto aliyezaliwa. Siku hizo zichukuliwe katika muda wa wiki moja ya kwanza tangu kuzaliwa kwa mtoto. Kwa kawaida likizo hiyo ya siku 3 hutolewa mara moja tu katika mzunguko wa likizo ya mwaka bila ya kujali idadi ya watoto watakaozaliwa katika kipindi hicho.

✵ Likizo hiyo inampa baba fursa ya kumhudumia mama na mtoto, kumsaidia mama kujenga msingi mzuri wa kumlisha mtoto na pia kutafuta mahitaji ya familia.

✵ Baba wa mtoto aliyezaliwa anaweza pia kupewa likizo isiyopungua siku 4 yenye malipo, wakati wa kuuguliwa na mtoto, kifo cha mtoto au kifo cha mwenzi wake.

✵ Likizo hiyo ya siku 4 hutolewa mara moja katika kipindi cha mzunguko wa likizo ya mwaka bila kujali idadi ya matukio yaliyojitokeza katika kipindi hicho. Hata hivyo, mwajiri anaweza kuidhinisha mwajiriwa kuchukua siku zaidi zisizo na malipo kulingana na tatizo alilopata.

Faida za likizo ya uzazi

Faida kwa mwajiri ✵ Inaongeza ari na uwajibikaji wa mwajiriwa kwa kutambua

kwamba mwajiri anamjali. ✵ Inapunguza mahudhurio hafifu yanayoweza kusababishwa

na mama kutokuwepo kazini kwa ajili ya kuuguza mtoto.✵ Inaweza kupunguza idadi ya waajiriwa wanaoacha kazi.✵ Inapunguza gharama za matibabu kwa ajili ya wafanyakazi

kwani mtoto aliyenyonya ipasavyo huwa na kinga thabiti dhidi ya maradhi.

✵ Inaongeza kiwango cha uzalishaji kwani waajiriwa hawatatumia muda wa kazi kwa ajili ya matatizo ya kifamilia kama vile kuuguza mtoto.

Page 10: COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Zijue-Haki-za-Uzazi-ka… · zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku 100 yenye

8

Faida kwa mtoto ✵ Mtoto anapata muda wa kutosha kunyonya au kulishwa

ipasavy o. ✵ Inasaidia kujenga uhusiano wa karibu kati ya mama na

mtoto. ✵ Inapunguza hatari ya mtoto kufa kwa utapiamlo au maradhi

mbalimbali, kwani maziwa ya mama humwongezea mtoto kinga

Faida kwa mama ✵ Inamuwezesha mama kunyonyesha na hivyo kupunguza

uwezekano wa kupata saratani ya matiti au mfuko wa uzazi.

✵ Inamuwezesha mama kunyonyesha maziwa yake pekee na mara nyingi, hivyo kuzuia ujauzito iwapo mama hajapata hedhi katika miezi 6 ya mwanzo.

✵ Inachangia kupunguza gharama za matibabu kwani mtoto anayenyonya maziwa ya mama huwa na kinga thabiti dhidi ya maradhi mbalimbali.

✵ Husaidia mama kupata matunzo ya kuboresha lishe na afya yake.

Faida kwa Taifa ✵ Inachangia kupunguza vifo vya watoto. ✵ Inaboresha afya ya mama na hivyo kumuwezesha kufanya

kazi na kuzalisha. ✵ Inachangia katika kutunza mazingira, kwani kunyonyesha

hakuachi mabaki kama vile makopo. ✵ Inapunguza matumizi ya fedha za kigeni kwa ajili ya

kuagiza maziwa mbadala na dawa kutoka nje ya nchi.

Page 11: COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Zijue-Haki-za-Uzazi-ka… · zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku 100 yenye

9

Mambo muhimu ya kukumbuka

✵ Mama aanze kunyonyesha mtoto wake mara anapozaliwa. ✵ Mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama pekee mpaka

anapotimiza umri wa miezi sita.✵ Atimizapo umri wa miezi sita, mtoto aanze kupewa vyakula

vya nyongeza huku akiendelea kunyonyeshwa hadi kutimiza umri wa miezi 24 na zaidi.

✵ Mama anayefanya kazi awasiliane na wahudumu wa afya ili kuelekezwa njia zinazomuwezesha kuendelea kumnyonyesha mtoto baada ya kumaliza likizo ya uzazi.

✵ Ikumbukwe kuwa chakula cha mtoto mwenye umri chini ya miezi sita ni maziwa pekee.

✵ Mama ale mlo kamili wenye mchanganyiko wa vyakula mbalimbali wakati wa ujauzito na wakati anaponyonyesha.

✵ Mwanamke mjamzito au anayenyonyesha atumie virutubishi vya nyongeza kama inavyoelekezwa na mtaalamu wa afya.

✵ Mama aliyejifungua apate muda wa kutosha wa kupumzika wakati wa mchana.

Hitimisho

Likizo ya uzazi ina faida kwa mwajiri, mwajiriwa, familia na taifa. Inamuwezesha mwanamke aliyeajiriwa kumpa mtoto matunzo muhimu katika miezi ya mwanzo ya maisha yake na kutayarisha mpangilio wa matunzo ya mtoto atakaporudi kazini. Hivyo huchangia kwa kiasi kikubwa katika uwajibikaji na ufanisi wa kazi.

Wadau mbalimbali wanashauriwa kutoa mapendekezo ya kuboresha sheria hii.

Page 12: COUNSENUTH Information Series No.9 September 2005counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Zijue-Haki-za-Uzazi-ka… · zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku 100 yenye

10

IBFAN Africa

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

MKURUGENZI MTENDAJI Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na AfyaS. L. P. 8218 Dar es Salaam Simu/Faksi: +255 22 2152705Email: [email protected]

KATIBU MKUUWizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, na Michezo S. L. P. 1422 , Dar es Salaam Simu: +255 22 2110877

Kuhusu COUNSENUTH

Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH) ni asasi isiyo ya kiserikaii yenye makao yake Dar Es Salaam. Dhumuni la COUNSENUTH ni kuboresha Lishe na Afya ya Watanzania kwa kutoa elimu ya lishe na unasihi kwa kushirikiana na taasisi, asasi na vikundi mbalimbali katika jamii.