21
1 HOJA YA URAIA PACHA Pasian Letinan, MSc, P.Eng. CANTAN Policy Institute [email protected] http://www.cantanpi.org September 3, 2014 1.0 UTANGULIZI Duniani swala la uraia pacha siyo jipya, ukifuatilia historia ya uraia pacha, utagundua kwamba ni swala ambalo halikuwa rahisi sana kwa nchi nyingi duniani kulipatia ufumbuzi. Hata zile nchi zinazotambua uraia pacha kwa hivi sasa, zilipitia hatua ambayo ulipingwa vikali na kwa muda mrefu katika nchi hizo. Kabla sijatoa maoni yangu kuhusu mjadala unaoendelea Dodoma, ningependa kwanza kuangalia kwa kifupi historia ya upinzania dhidi ya uraia pacha na hatimaye kuruhusiwa kwake Marekani, Ulaya na Afrika hususan nchi za Afrika Mashariki. Baada ya kuchungua historua fupi ya upinzania na uungwaji mkono wa uraia pacha nitaangazia mchakato wa uraia pacha Tanzania hasa kwa kuzingatia makala iliyokuwa katika gazeti la Mwananchi la Agosti 17 kama hadidu ya rejea na hatimaye nitamalizia kwa kutoa maoni yangu ya jumla juu ya mchakato mzima unavyoendelea. 2.0 UPINZANI DHIDI YA URAIA PACHA 2.1 Marekani Upinzania dhidi ya uraia pacha una historia ndefu, si tu mataifa takriban yote duniani yaliupinga bali pia hata mashirika ya kimataifa yalifanya juhudi za makusudi kuzuia uraia pacha, kwa sababu ambazo zilikwa sahihi kwa mazingira ya dunia kwa wakati huo. Upinzani huu unaweza kuwa ulianza zamani zaidi, lakini kwa utafiti mfupi nilioufanya tuanzie 1849 mwanahistoria mmarekani George Bancroft, ambaye baadaye alikuwa balozi wa kwanza wa Marekani nchini Ujerumani alitoa hoja kwamba kukubali mtu kuwa uraia wa nchi mbili ni sawa na kukubali mtu kuwa na wake wawili (ikumbukwe kwamba kuwa na wake wawili ni jambo lisilokubalika kabisa kisheria nchini Marekani na nchi nyingi za magharibi) ... "one should as soon tolerate a man with two wives as a man with two countries; as sson bear with polygamy as the statue of double allegiance which common sense repudiates that it has not even coined a word to express it" (Tazama http://www18.georgetown.edu/data/people/mmh/publication-7319.pdf ).

HOJAYAURAIAPACHA

Embed Size (px)

Citation preview

1

HOJA YA URAIA PACHA

Pasian Letinan, MSc, P.Eng.

CANTAN Policy Institute

[email protected]

http://www.cantanpi.org

September 3, 2014

1.0 UTANGULIZI

Duniani swala la uraia pacha siyo jipya, ukifuatilia historia ya uraia pacha, utagundua kwamba ni swala

ambalo halikuwa rahisi sana kwa nchi nyingi duniani kulipatia ufumbuzi. Hata zile nchi zinazotambua

uraia pacha kwa hivi sasa, zilipitia hatua ambayo ulipingwa vikali na kwa muda mrefu katika nchi hizo.

Kabla sijatoa maoni yangu kuhusu mjadala unaoendelea Dodoma, ningependa kwanza kuangalia kwa

kifupi historia ya upinzania dhidi ya uraia pacha na hatimaye kuruhusiwa kwake Marekani, Ulaya na

Afrika hususan nchi za Afrika Mashariki. Baada ya kuchungua historua fupi ya upinzania na uungwaji

mkono wa uraia pacha nitaangazia mchakato wa uraia pacha Tanzania hasa kwa kuzingatia makala

iliyokuwa katika gazeti la Mwananchi la Agosti 17 kama hadidu ya rejea na hatimaye nitamalizia kwa

kutoa maoni yangu ya jumla juu ya mchakato mzima unavyoendelea.

2.0 UPINZANI DHIDI YA URAIA PACHA

2.1 Marekani

Upinzania dhidi ya uraia pacha una historia ndefu, si tu mataifa takriban yote duniani yaliupinga

bali pia hata mashirika ya kimataifa yalifanya juhudi za makusudi kuzuia uraia pacha, kwa sababu

ambazo zilikwa sahihi kwa mazingira ya dunia kwa wakati huo. Upinzani huu unaweza kuwa

ulianza zamani zaidi, lakini kwa utafiti mfupi nilioufanya tuanzie 1849 mwanahistoria mmarekani

George Bancroft, ambaye baadaye alikuwa balozi wa kwanza wa Marekani nchini Ujerumani

alitoa hoja kwamba kukubali mtu kuwa uraia wa nchi mbili ni sawa na kukubali mtu kuwa na

wake wawili (ikumbukwe kwamba kuwa na wake wawili ni jambo lisilokubalika kabisa kisheria

nchini Marekani na nchi nyingi za magharibi) ... "one should as soon tolerate a man with two

wives as a man with two countries; as sson bear with polygamy as the statue of double

allegiance which common sense repudiates that it has not even coined a word to express it"

(Tazama http://www18.georgetown.edu/data/people/mmh/publication-7319.pdf ).

2

Bancroft baadaye alirasimisha upinzani wake dhidi ya uraia pacha katika kile kilichoitwa

"Bancroft Treaties" ambayo ilizuia watu waliokuwa wakihamia Marekani (wakati huo wengi wao

kutoka Ulaya) au Wamarekani waliohamia nje kuwa na uraia pacha.

Mwaka 1874 aliyekuwa Rais wa Marekani wakati huo Ulysses Grant aliongea vikali kabisa dhidi

wa wamarekani kuwa na uraia pacha … "President U.G. spoke out against Americans claiming

the benefit of citizenship, while living on a foreign country, contributing in no manner to the

performance of the duties, to use the claims to citizenship of the United States simply as a shield

from the performance of the obligations of a citizen elsewhere (Tazama uk 701

http://www18.georgetown.edu/data/people/mmh/publication-7319.pdf )

Kwa upadne wake Rais Theodore Roosevelt akizungumzia swala la uraia pacha alisema ni

uwendawazimu ulio dhahiri, … "a self-evident absurdity" (Taz uk. 701

http://www18.georgetown.edu/data/people/mmh/publication-7319.pdf)

Wasiwasi wa Marekani ilikuwa ni kwamba endapo kungetokea vita Ulaya, basi wenye uraia pacha

wangeweza kuitwa na nchi zao asili kupigana upande wao badala ya nchi yao mpya yaani Marekani.

Hivyo kwa kuzuia uraia pacha, Marekani walikuwa na lengo la kuhakikisha raia wapya kutoka Ulaya

wanakata kabisa fungamano na nchi zao za asili hasa zile za kutumikia jeshini na pia maswala ya kulipa

kodi,na hoja hii itaeleweka vizuri ukiangalia historia ya Marekani.

Taifa la Marekani lilianza hapo 1776 baada ya majimbo 13 yaliyokuwa wakati huo makoloni ya

Uingereza, kutangaza kwamba yalikuwa yanajitambua kama madola huru na kwamba yalikuwa

yanaunda nchi mpya inayoitwa United States of America. Uhuru huu haukupatikana kwa ridaa ya

Waingereza, ni baada ya makoloni hayo kuingia vitani na Uingereza na chanzo hasa cha vita hiyo ni

bunge la Uingereza kupitisha sheria kuyataka makoloni hayo kulipa kodi kwa Uingereza. Kodi hiyo

ilikutana na upinzani mkali, fujo, ghasia na hadi vita kamili kati ya Uingereza na makoloni na katikati ya

vita hiyo makoloni yakaamua kujitangazia Uhuru. Hata baada ya uhuru huo, Uingereza haikuridhika

kuyaachia makoloni hayo kirahisi, kwanza ilikataa kutambua ukweli kwamba waliokuwa raia wake

kwenye hayo makoloni sasa eti si Waingereza tena ni Wamarekani. Lakini pia iliendelea na chokochoko

nyingine kama kutaka kuizuia Marekani kufanya biashara na Ufaransa. Uchokozi wa Uingereza

uliendelea hata ikafikia hatua ya Marekani kutangaza vita dhidi ya Uingereza mnamo 1812, vita

iliyodumu kwa takriban miana miwili na nusu, wenyewe Wamarekani wakiita ni vita ya pili ya uhuru

kulinda heshima ya utaifa wao.

Nimeeleza kwa kirefu kidogo swala hili la historia ya Uingereza na Marekani kwa vile upinzani wa

Marekani dhidi ya uraia pacha kwa kiasi kikubwa unatokana na historia hii, waliona uraia pacha ni hatari

kwamba kama watu wangeruhusiwa kuwa Wamarekani na papo hapo ni Waingereza kungekuwa na

3

uwezekano Uingereza kuwadai kodi kama ambavyo ilikuwa imetaka kufanya au pia wengine wangeweza

kupigana upande wa Uingereza iwapo vita ingetokea.

2.2 Ulaya

Nchi za Ulaya nazo zina historia ndefu ya uhasama wa kijeshi na kisiasa, ambao tunaweza kusema ulifikia

kilele chake katika vita kuu ya kwanza na ya pili ya dunia (kwa ajili ya kufanya makala isiwe ndefu sana

sina haja ya kuelezea kwa kirefu vita ya kwanza au ya pili ya dunia, nadhani historia hiyo inajulikana vya

kutosha; au ikiwa unataka kujua tumia google). Kwahiyo kulikuwa kutokuaminiana kati ya nchi na nchi

ndio maana nchi za Ulaya zilipinga swala la uraia pacha miaka iliyofuata baada ya vita kuu ya pili. Bila

kusahau pia kulikuwa na vita baridi kati ya makambi ya magharibi na mashariki iliyodumu tangu

kumalizika kwa vita vya pili vya dunia mpaka miaka ya mwanzo ya 1990. Katika mazingira kama hayo

hofu ya usalama ulichangia kwa kiaisi kikubwa kufanya uraia pacha usiruhusiwe kirahisi.

Mwaka 1963 nchi za Ulaya zilichukua hatua zaidi kupunguza uwezekano wa mtu kuwa na uraia zaidi ya

mmoja, … 1963 Council of Europe Convention on the Reduction of Cases of Multiple Nationality, the

summary states that: The convention aims to reduce as far as possible the number of cases of multiple

nationalities in the case of acquisition of a new nationality or the renunciation of one nationality, and the

legal consequence of persons concerned, including minor persons. (Council of Europe, 1963).

Pamoja na kwamba mkataba huu ulipitishwa na nchi 12 tu za Ulaya, kwa kiasi kukubwa uliakisi

mwelekeo wa mataifa mengi duniani wakati huo kwamba mtu hakutakiwa kuwa na uraia zaidi ya

mmoja.

2.3 Afrika, hususan Afrika Mashariki

Wakati wa kupata uhuru, miaka ya mwanzo ya 1960, nchi za Kiafrika hazikuruhusu uraia pacha. Hili ni

jambo lililotarajiwa kwa vile nchi nyingi zilirithi sheria nyingi kutoka mataifa ya Ulaya yaliyokuwa

yakizitawala, ambayo yenyewe kwa sababu za kihistoria kama nilivyoeleza hapo juu yalikuwa hayaupigii

upatu uraia pacha. Na kwa kweli wakati nchi hizi zinapata uhuru, miaka ya mwanzo ya sitini

kulikuwa hakuna Waafrika wengi waishio nje ya nchi zao, kiasi cha kuipa nguvu hoja ya uraia pacha. Kwa

hiyo siyo tu kwamba inaeleweka kwanini nchi nyingi za Kiafrika hazikuuruhusu bali pia hata kama

ungeruhusiwa wala ulikuwa hauhitajiki sana wakati huo.

Tukija karibu zaidi na nyumbani; Uganda na Kenya, washirika wenzentu wa Afrika Mashariki, nako

upinzani dhidi ya uraia pacha ulikuwa umeshamiri. Nchi zote hizo mbili zimeshakuwa na katiba tatu

4

mpaka sasa (Kenya: katiba ya Uhuru ya 1963, ya 1969 na mpya ya 2010 inayotumika sasa; Uganda:

Katiba ya Uhuru ya 1962, ya 1967 na ya 1995 inayotumika mpaka sasa). Kwa mujibu wa ripoti ya 2010

iitwayo Citizenship Law in Africa: A Comparative Study uliofanywa na Taasisi ya Open Society

Foundations, katika nchi za Afrika Mashariki Tanzania, Kenya na Uganda kumekuwa na upinzani wa

kihistoria dhidi ya uraia pacha kutokana na kuwa na shaka na idadi kubwa ya raia wenye asili ya kiasia

katika nchi hizo, hapa ninanukuu: … Kenya, Tanzania, and Uganda have historically been among those

countries most opposed to dual nationality because of suspicions about their large populations of Asian

descent. (Tazama uk 61: http://www.opensocietyfoundations.org/sites/default/files/citizenship-africa_20101118.pdf )

2.4 Jumuiya za Kimataifa; League of Nations & United Nations

Upinzani dhidi ya uraia pacha uliingia kwenye medani za kimataifa pia, League of Nations (mtangulizi wa

Umoja wa Mataifa) iliyoundwa mara tu baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia, lengo lake likiwa kuzuia

vita nyingine kama hiyo isitokee tena, ilisisitiza kwamba kila mtu anastahili uraia, lakini uraia mmoja tu;

pengine kwa kuzingatia uzoefu wa mahusiano yalikuwepo baina ya nchi na nchi mara tu baada ya vita ya

kwanza ya dunia, ninakuu. … League of Nations in its "Convention on Certain Questions Relating to

Conflict of Nationality Law, "Hague Convention" reflected the view that it is in the interest of the

international community to secure that all members should recognize that every person should have a

nationality and should have one nationality only" (League of Nations 1930)

Mwelekeo uliendelea kuwa huo baada ya vita kuu ya pili pale mwaka 1954 Umoja wa mataifa

(ulioundwa mara baada ya vita kuu ya pili, lengo kuu likiwa kuzuia vita baada ya Leauge of Nations

kushindwa kufanya kazi hiyo) kupitia tume yake ya sheria za kimataifa iliposema tena kuwa kila mtu

anastahili kuwa na utaifa, lakini utaifa wa nchi moja tu, … International Law Commission of the UN,

1954: All persons are entitled to possess one nationality but one nationality ony.

3.0 KUKUBALIKA KWA URAIA PACHA

3.1 Marekani

Marekani walilishughulikia swala hili kwa kukubali kimya kimya (recognize but not encourage, tazama

http://travel.state.gov/content/travel/english/legal-considerations/us-citizenship-laws-

policies/citizenship-and-dual-nationality/dual-nationality.html )

Pamoja na upinzani waliokuwa nao wanasiasa wa kimarekani juu ya uraia pacha, katiba yao haikupata

kuukataza. Ukiangalia sheria yao uhamiaji utaona wanaitolea maelezo kuwa inatambua uraia pacha,

lakini hawahimizi. Kwa hiyo Wamarekani wanaopata uraia wa nchi nyingine hawalazimiki kuukana uraia

5

wao wa Kimarekani, vivyo hivyo wale wahamiaji wanaopata uraia wa kimarekani kwa njia ya

kuandikishwa, hawalazimiki kwanza kuukana uraia wa nchi walizotoka.

Pamoja na kwamba uraia pacha haukutamkwa kinagaubaga kwenye katiba ya Marekani, lakini yapo

maamuzi ya mahakama kuu yaliyoutambua, kwa hivyo mtu unaweza kusema tayari kuna sheria ya kesi

(case law) inayotambua uraia pacha Marekani, hapa ninanukuu … Based on the U.S. Department of State

regulation on dual citizenship (7 FAM 1162), the Supreme Court of the United States has stated that dual

citizenship is a "status long recognized in the law" and that "a person may have and exercise rights of

nationality in two countries and be subject to the responsibilities of both. The mere fact he asserts the

rights of one citizenship does not without more mean that he renounces the other", (Kawakita v. U.S.,

343 U.S. 717) (1952). In Schneider v. Rusk 377 U.S. 163 (1964), the U.S. Supreme Court ruled that a

naturalized U.S. citizen has the right to return to his native country and to resume his former citizenship,

and also to remain a U.S. citizen even if he never returns to the United States.

(Tazama: http://en.wikipedia.org/wiki/United_States_nationality_law#Dual_citizenship )

3.2 Ulaya

Baada ya vita kuu ya pili, nchi nyingi za Ulaya zilianza kufungua mipaka yake, watu wake wakitembea

kwa urahisi zaidi kutoka nchi moja hadi nyigine na hata kufanya kazi nchi nyingine. Hii ilipelekea ndoa

baina ya watu wa mataifa mbali mabli. Nchi nyingi zikaanza kupata changamoto ya watoto waliozaliwa

katika ndoa za aina hiyo, ambao mara nyingi walirithi uraia wa wazazi wote wawili kwa kufuata taratibu

za kawaida zilizowekwa na nchi husika. Hali hii ilifanya uraia pacha kuwa ni jambo ambalo tayari

lilikwepo (de facto reality) pamoja na kwamba kisheria lilikuwa bado halijaruhusiwa (not allowed de

jure), ninanukuu … Dual citizenship could never be completely avoided, because people have always

moved across state borders and settled down. A case for dual citizenship thus usually arises, for example,

whenever a person is born within a country where the law of territoriality (jus soli) holds, but whose

parents are citizens of a country that observes the blood principle (jus sanguinis). Dual citizenship arises

when children are born in countries where the jus soli principle holds, while the countries of their parents'

origin apply the jus sanguinis principle.

Na kama nilivyoeleza hapo juu, sababu kubwa ya upinzani dhidi ya uraia pacha ulitokana na woga wa

usalama iwapo kungetokea mgogoro kati ya nchi na nchi. Kadri kitisho cha kutokea vita kati ya nchi hizo

kilivyopungua siku hadi siku ndivyo hofu ya usalama ilivyopungua. Kadhalika kumalizika kwa vita baridi

na kuingia kwa enzi ya utandawazi kulimaanisha kwenye geopolitical dynamics ni sera za kiuchumi

badala ya zile za kisiasa ndizo zilichukua kipaumbele.

6

Kwa sababu hizo, mnamo 1997 Council of Europe lipitisha "European Convention on Nationality"

kimsingi kubadilisha sera yake ya mwaka 1963 juu ya uraia pacha, badala ya kusisitiza uraia mmoja tu

kwa kila mtu sasa nchi wanachama zikapewa jukumu la kutambua ama kutotambua uraia pacha na

baada yahapo nchi kadhaa za Ulaya zilianza kuruhusu uraia pacha.

3.3 Afrika/Afrika Mashariki

Kama nilivyogusia hapo juu siyo Waafrika wengi walikuwa wakiishi nje ya nchi zao wakati uhuru. Lakini

idadi ya Waafrika walio nje ya nchi zao imekuwa ikiongezeka kila kukicha. Kwa kutambua mchango wao

katika maendeleo ya nchi zao za asili, nchi za Afrika zimeanza kubadilisha sheria zake kuruhusu uraia

pacha ili kuwawezesha wale wananchi wake waishio ughaibuni kutopoteza uraia wao wa asili.

Kwa upande wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Burundi ilipitisha sheria kuruhusu uraia pacha

mwaka 2000 (kabla ya kujiunga na EAC), Rwanda iliruhusu mwaka 2004. Hata Uganda na Kenya ambao

walikuwa na wasiwasi kutokana na wingi wa raia wenye asili ya kiasia, walilazimika kubadilisha sheria

zao kutokana kuongezeka kwa kiasi cha fedha kinachotumwa nyumbani na raia walio nje. Hapa ninukuu

tena ile ripoti ya Open Society Foundation … The growing diaspora of people of African origin and the

economic significance of their remittances to and investments in their countries of origin, however, have

produced political pressure to change the law(tazama uk 61:

http://www.opensocietyfoundations.org/sites/default/files/citizenship-africa_20101118.pdf )

Katiba za Kenya za 1963 na 1969 hazikuruhusu Uraia pacha, ile ya 2010 ambayo ndiyo inatumika sasa

imeruhusu uraia pacha. Kwa Uganda katiba zote tatu, ya 1962, 1967 hata ile ya 1995 haikurusu uraia

pacha wakati ilipoanza kutumika. Kilichotokea Uganda kinafanana fanana na kinachotokea Tanzania

kwa hivi sasa. Wakati wa kuandika katiba yao mpya ya 1995, kulikuwa na Tume ya Odoki (sawa na Tume

ya Warioba kwa Tanzania) iliyoundwa kupita nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi. Tume hiyo, kwa

kuzingatia tawimu ilizokusanya, ilipendekeza uraia pacha usiruhusiwe na kwa hivyo katiba mpya ya 1995

ikaendelea kukataza uraia pacha.

Baada ya hapo kuliundwa tume ya mabadiliko ya katiba 2001-2003, ambayo ilichunguza tena swala la

uraia pacha. Nayo ikaja na msimamo ule ule, kwamba kutokana na maoni ya wengi, swala la uraia pacha

halikubaliki. Sababu kubwa za kukataa ni uaminifu, sababu za kiusalama na sababu za kiuchumi kwamba

wawekezaji wangekuja kutawala uchumi wa Uganda, ninanukuu, .. .The main arguments against dual

citizenship revolved around the issue of loyalty, and the security and sovereignty of Uganda. Fears were

also expressed that dual nationality investors would come to dominate the Ugandan economy.(tazama

uk 61 http://www.opensocietyfoundations.org/sites/default/files/citizenship-africa_20101118.pdf )

7

Pamoja na kwamba maoni ya tume ya mabadiliko ya katiba yalikataa uraia pacha lakini Serikali ya

Uganda ilileta mapendekezo kwa tume hiyo kwamba ilikuwa ni muhimu kuruhus uraia pacha ili

kuwawezesha wananchi wa Uganda waishio nje kutopoteza uraia wao. Mapendekezo hayo ya serikali

yalichukuliwa na tume na kupelekwa bungeni, hatimaye bunge likaridhia na hatimaye katika sheria ya

mabadiliko ya katiba ya mwaka 2005 ambapo uraia pacha uliruhusiwa. (Taz. Uk 61:

http://www.opensocietyfoundations.org/sites/default/files/citizenship-africa_20101118.pdf )

4.0 CHAKATO WA URAIA PACHA TANZANIA

4.1 Hoja za wasiounga mkono

Ukifuatilia kwa karibu utaona wale wapinzani wa uraia pacha hawana sababu mpya, ni zile zile ambazo

Wamarekani walikuwa nazo miaka ya 1800, ni hizo hizo nchi za Ulaya walikuwa nazo mara baada vita

kuu ya dunia miaka ya 1940 na katika kipindi cha chote cha vita baridi. Ni sababu hizo hizo wenzetu wa

Afrika Mashariki Kenya na Uganda walikuwa nazo. Sababu hizo zilikuwa na mantiki enzi hizo, lakini kwa

kweli ni hoja hafifu kuendelea kuzitumia sababu hizo hizo kwa mazingira ya dunia ya sasa.

Hapa nitachambua hoja za wapinzani wa uraia pacha Tanzania kwa kuzingatia makala yenye kichwa cha

habari “Uraia pacha, masilahi binafsi dhidi ya masilahi ya Taifa” iliyoandikwa kwenye gazeti la

Mwananchi toleo la Agosti 17, mwandishi akiwa aliyekuwa mmoja wa wajumbe wa Tume ya Warioba.

Nimechagua makala hii kwa sababu tu iliandikwa na aliyekuwa mjumbe wa tume, na wala siyo kwa

sababu hoja zake zina msingi. Pamoja na kwamba ni makala yake binafsi lakini kwa vile alikuwa mjumbe

wa tume, kwa akili ya kawaida mtu anaweza kufikiri kwamba uchambuzi wake huenda umeakisi

uchambuzi na vigezo walivyotumia tume kufikia uamuzi wa kutoingiza swala la uraia pacha katika rasimu

ya pili ya katiba; na kama ndivyo, basi uchambuzi wa tume katika hili kwa kweli ulipwaya. Sababu

zilizopo katika makala hiyo juu ya kwa nini uraia pacha haufai zimenukuliwa kwa wino mwekundu hapo

chini:

- Uraia pacha unaondoa ile dhana ya uaminifu usiogawika (indivisible loyalty) kwa nchi na Mamlaka Kuu

ya nchi. Kama ambavyo mtu hawezi kutumikia wakuu wawili kwa wakati mmoja, vivyo hivyo mtu hawezi

kutumikia (kwa maana ya uaminifu na utii) nchi zaidi ya moja.

Dunia imejaa historia ya majasusi wengi ambao hawakuwa na uraia wa pili, lakini waliuza siri za nchi zao,

kwa hivyo siamini kuwa kipande cha karatasi peke yake kinaweza kuwa ni kielelezo tosha kuonyesha

uaminifu wa mtu. Ukitaka kutafuta watu ambao hawana uaminifu wala huna haja ya kuvuka nje ya

mipaka, tazama hapo hapo nyumbani utakuta wakwepa kodi, utakuta wale wanaosaini mikataba mibovu

8

inayoliingizia taifa hasara kubwa. Sidhani kama hao ni waaminifu an wazalendo kuliko wale waishio

ughaibuni wakitegemea jasho lao huku wakidunduliza akiba kutuma hela nyumbani, wanaotumia muda

wao binafsi kujaribu kutangaza jina la Tanzania kwa kupitia matukio mbalimbali kama matamasha,

makongamano, mikutano n.k.

Ieleweke kwamba watu waliopo ughaibuni waliamua kubaki huko kutokana na fursa walizozipata. Lakini

kubaki kwao huko hakuna maana kwamba uzalendo wao basi ulikoma au kwa namna nyingine yoyote

hawaitakii mema Tanzania. La hasha, hivyo sivyo, isitoshe wengi wao bado wana familia zao Tanzania,

na wanaipenda Tanzania kuliko hata baadhi ya wale waliobaki nyumbani. Denmark ni moja ya nchi

ambazo zimepitisha sheria ya kuruhusu uraia pacha hivi majuzi, naomba nimnukuu waziri wa sheria wa

Denmark, Karen Hækkerup, katika hotuba yake bungeni mara baada ya bunge kupitisha sheria hiyo hapo

June 4, 2014: "… Katika dunia ya leo watu wengi wanachagua kuishi katika nchi za kigeni kwa sababu

mbalimbali, lakini bado wanakuwa na mapenzi makubwa kwa nchi zao za asili” (tazama:

http://cphpost.dk/news/dual-citizenship-approved-by-danish-parliament.9774.html). Naamini kwa

Watanzania ni hivyo hivyo, wapo wengi waliochagua kuishi nje, na kuishi kwao nje hakuwaondolei

uzalendo na mapenzi makubwa kwa Tanzania.

-Uraia pacha unadhoofisha usalama wa taifa. Nieleze kwa mifano tu, miezi kadhaa iliyopita kulitokea

uvumi kwamba ofisa wetu wa Jeshi la Wananchi, tena mwenye dhamana ya kutunza au kushughulika na

taarifa nyeti za kimawasiliano ametoweka. Sote tu mashahidi kihoro tulichokipata kipindi kile na zaidi

uvumi ulipozidi kuwa huenda amekimbilia nchi fulani ya jirani. Tukiwa na uraia pacha, hofu hii

itaongezeka maradufu, hasa pale wenye uraia pacha watakapopewa dhamana ya madaraka makubwa

na nyeti.

Kama nilivyoeleza hapo juu usalama wa taifa ndiyo ilikuwa sababu kubwa iliyopeleka uraia pacha

kukataliwa katika nchi nying duniani. Sababu hii siyo ya kupuuza, lakini ningetarajia wanaitoa waeleze ni

kwa vipi usalama wa taifa wa Tanzania kwa mazingira yake na historia yake unahatarishwa na uraia

pacha? Hii sababu ilikuwa na matiki kwa wamarekani miaka ya 1800, kutokana na historia yao na

Uingereza kama nilivyoeleza hapo juu. Kadhalika ilikuwa na mantiki kwa nchi za Ulaya mwanzoni mwa

karne ya ishirini wakati wa vita kuu ya dunia na zama za vita baridi. Inawezekana kuwa ilikuwa na

mantiki kwa Uganda baada ya Idd Amin kuwafukuza wanachi wenye asili ya kiasia kutoka Uganda.

Inaweza kuwa ilikuwa na mantiki kwa nchi za Afrika miaka ya 60 mara baada ya Uhuru, maana walikuwa

na woga kwamba pengine wakoloni wangeweza kurudi. Siamini kama ina mantiki kwa Tanzania, miaka

50 baada ya Uhuru, zama za utandawazi. Haingii akilini kwamba tupo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki

na leo tunazungumzia kuunda shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki, na washirika wetu wote

wamesharuhusu uraia pacha na sisi bado tunasema usalama utakuwa hatarini.

9

Haitoshi tu kutoa kauli za jumla jumla kwamba uraia pacha unahatarisha usalama wa Taifa, bila

kubainisha ni kwa vipi. Huo mfano alioutoa Bwana Poleple wa uvumi kuhusu kuhusu ofisa wa Jeshi

aliyekimbia unafanya hoja yake izidi kuwa dhaifu kwa sababu mbili. Kwanza anatumia uvumi (hearsay)

kutaka kujenga hoja yake katika swala muhimu kama hili. Ingelikuwa ni mahakamani wangemwabia

ushahdi wa hearsay haukubailiki. Kwa hiyo ningemshauri uvumi auache mitaani ndipo mahala pake na

wala asiulete kwenye meza ya majadiliano ambapo tunazungumza maswala muhimu ya kitaifa, ajenge

hoja zake kwa kufanya uchambuzi yakinifu na siyo ule wa udhanifu. Pili, hata kama ingelithibitika kuwa

huo uvumi ulikuwa ni wa kweli, kwani tulikuwa na uraia pacha? Sasa sijui ni kwa vipi anataka kutumia

mfano huu kubainisha ubaya wa uraia pacha. Kimsingi ameonyesha kuwa usalama wa Taifa unaweza

kuingia mashakani hata bila ya kuwapo uraia pacha, kwa hiyo huo ni mfano ambao kwa kweli

ungepaswa kutolewa na watu wanotetea uraia pacha na wala siyo wale wanaoupinga.

- Kuna mifano ya jamaa zetu, ambao tuliwafahamu kama Watanzania, tukawasomesha kwa fedha za

walipa kodi wa Tanzania, wakahitimu na tukawapa dhamana na madaraka makubwa na nyeti. Leo hii

angalau wale ambao mimi nawajua hawako nasi tena. Wamekwenda kwenye ile nchi ambayo ni kama

ilizaliwa upya na inasemekana inapiga hatua kubwa kimaendeleo.

Kama alivyozungumzia swala la usalama, katika mfano huu pia kuna kujikanganya. Anadai kuna watu

wamewasomesha kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania, tukidhani ni Watanzania lakini mara baada ya

kuhitimu wakatokomea makwao. Nakubaliana na Bwana Polepole kuwa hilo kweli ni tatizo, lakini pia

niulize, ni kwa vipi tatizo hilo linahusiana na uraia pacha wakati limetokea tukiwa hatujaruhusu uraia

pacha. Ikiwa tatizo halikuletwa na uraia pacha, kutoruhusu uraia pacha kutaliondoaje?

Lakini pia tujiulize wageni wanaweza kuja nchini kinyemela na kunufaika kama raia wa Tanzania wakati

hatuna sheria ya uraia pacha, kweli itakuwa ni akili kuwakataa raia wetu kwa sababu tu wamechukua

uraia wa nchi nyingine kihalali?

Pengine alikuwa anataka kusema kwamba uraia pacha utaongeza tatizo hili. Inawezekana kuna chembe

za ukweli katika hilo, lakini bado atakubaliana na mimi kwamba bado uraia pacha siyo kiini cha tatizo hili.

Inatupasa tukae chini tutafute kiini cha tatizo hili, udhaifu uko wapi, nini chanzo chake na tuukate mzizi

wake badala ya kupendekeza majibu mepesi mepesi ambayo kwa kweli siyo jawabu ya tatizo hilo.

- Kama uraia pacha ukiwapo, itakuwa vigumu kusema hii ni siri na ni kwa masilahi ya taifa tena huenda

dhidi ya mataifa jirani kwa sababu hao wenzetu ambao pia watakuwa raia wa nchi jirani tutakuwa nao

tukitengeneza mambo hayo.

10

Sidhani kama hili ni tatizo, nchi zilizoruhusu uraia pacha huwa zinatunga sheria zinazoainisha ni namna

gani mtu anaweza kupata uraia pacha, haki zake, wajibu wake na mipaka yake. Kwa mfano Marekani

kama wewe siyo raia wa kuzaliwa huwezi kuwa Rais au Makamu wa Rais. Uganda, sheria yao imeanisha

maeneo kadhaa ambayo mtu mwenye uraia pacha hawezi kuhudumu.

Lakini pia ukiliangalia swala hili kwa mapana yake, watu hawahitaji kuwa raia pacha ili kutoa siri za nchi

zao. Zipo sababau mbalimbali ambazo zinawasukuma wafanye hivyo, mfano kusukumwa na dhamira

zao, au sababu za kifedha, wanalipwa kwa kuifanyia kazi nchi nyingine nk. Mfano unaovuma sana kwa

sasa hivi duniani ni ule wa Mmarekani mmoja Bwana Edward Snowden. Yeye alikuwa akifanya kazi

katika taasisi za usalama wa taifa lakini hakupendezwa na jinsi ambavyo vyombo hivyo vilikuwa vikitenda

kazi yao, akiona kama vinaingilia sana faragha za watu kama kufuatilia mawasiliano yao ya simu na barua

pepe. Akaamua kutoboa siri hiyo, ambayo ilisababisha sokomoko kubwa la kidiplomasia kwa Marekani.

Mtakumbuka kuwa simu walizokuwa wanasikiliza zilikuwepo mpaka za marais na viongozi wengine

duniani. Baada ya bwana Snowden kufanya hivyo Marekani ilihaha kweli kumkamata lakini Urusi

(hasimu wa Marekani) ikamkumbatia na kumpa hifadhi pamoja na kwamba yeye hakuwa na uraia wa

Urusi. Mfano huu unabainisha mambo mawili: Kwanza, Snowden hakuwa na uraia mwingine zaidi ya ule

wa Marekani, alisukumwa tu na dhamira yake, kwa hiyo ili mtu atoe siri hahitaji kwanza awe na uraia

pacha. Pili, Snowden alikaribishwa na Urusi pamoja na kwamba hakuwa na uraia wa Urusi, basi tu

wametaka kumpa hifadhi kwa vile amewaaibisha mahasimu wao. Vivyo hivyo raia yeyote wa Tanzania

hata bila ya uraia pacha anaweza kuihujumu nchi na kukimbilia nchi nyingine na akapewa uraia au

hifadhi ili mradi nchi hiyo ina maslahi katika hiyo hujuma iliyofanyika.

Mfano mwingine wa karibu zaidi na nyumbani ni ule wa Bwana John Githongo wa Kenya. Huyu

aliteuliwa na serikali mpya ya Kibaki 2003 kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maadili na Utawala Bora. Huyu

bwana kabla ya kuingia serikalini alikuwa anajulikana kwa rekodi yake ya kupigana na ufisadi katika

medani za kimataifa, akiwa katika shirika la Transparency International. Baada ya kuingia serikali juhudi

zake za kufagia ufisadi zilikumbana na vigingi vingi, hatimaye akakuta milungula mingine ilikuwa

ikiwahusisha mawaziri waandamizi na hata viongozi wa juu mpaka Makamu wa Rais. Akampelekea

taarifa hizi Rais Kibaki, ambaye hakuchukua hatua yoyote na wala hakuonyesha nia ya kumuunga mkono

katika jitihada zake. Huyu bwana aliamua kujiuzulu 2005, akiwa Uingereza, huku akiweka bayana sababu

za kujiuzulu kwake, barua yake ya kujiuzulu aliipeleka kwenye ubalozi wa Kenya Uingereza. Uingereza

walimpa hifadhi, wakihofia kuwa maisha yake yangekuwa hatarini iwapo angerudi Kenya. Serikali ya

Kenya ilisitishiwa misaada mingi kutokana na Bwana Githongo kufichua siri za uchafu uliokuwa

ukiendelea serikalini na hata mawaziri wengine kupigwa marufuku ya kusafiri katika baadhi ya nchi

zilizokuwa zikiipa Kenya misaada. Bwana Githongo wakati anafanya haya, Kenya ilikuwa bado

haijaruhusu uraia pacha, na Uingereza ilimpa hifadhi pamoja na kwamba alikuwa siyo raia wa Uingereza.

11

(Ukitaka kusoma zaidi: http://news.bbc.co.uk/2/shared/bsp/hi/pdfs/09_02_06_kenya_report.pdf). Kwa

hivyo kusema eti uraia pacha utasababisha mtu kutoa siri za nchi au atakimbilia nchi nyingine, si hoja,

mbona hayo yanafanyika bila ya uraia pacha.

Labda nimalizie kwa kuuliza swali la kizushi: Ni siri gani hasa hizo tunazotaka kuficha na ni nani tunataka

kumficha? Tunataka kuwaficha Marekani? Uingereza? Au Rwanda? Nchi kama Marekani na miguvu yao

yote, lakini mambo yao waliyokuwa wakidhani ni siri, wameyakuta yameanikwa hadharani katika

mtandao wa Wikileaks. Sisemi ni vibaya kuficha siri, lakini akili ya mwenzio changanya na yako.

- Tuchukue mfano mwingine, sasa tuna sera ya kuhudumu katika jeshi kisheria kwa vijana wetu kama

sehemu ya kujenga ushupavu na kuimarisha uzalendo wao, tukiwa na uraia pacha tujiandae kuwa na

Warundi, Wakongo, Wamarekani, Wakenya na Wasomali JKT tukiwafundisha uaminifu, utii na namna ya

kuipenda Tanzania kwa moyo wote hata na ikibidi mpaka tone la mwisho la damu yao.

Kama nilivyosema haitoshi tu kutoa kauli zenye vionjo vya hisia, lakini ukiziangalia kwa undani hazina

msingi wowote. Polepole hakutoa ushahidi wowote kuonyesha ni kwa vipi mtu akishakuwa na uraia

pacha basi moja kwa moja hiyo ni tiketi ya kukosa utii na uaminifu, kutoipenda ama kutoipigania

Tanzania.

Labda pia tuchunguze kidogo maana ya diaspora, … ukiangalia kamusi ya kiingereza ya Oxford (moja ya

Kamusi zinazoheshimika sana) utaona maana ya kwanza ya neno diaspora ni mtawanyiko wa Wayahudi

nje ya Israel, ama wayahudi wanaoishi nje ya Israel .. The dispersion of the Jews beyond Israel; Jews

living outside Israel, halafu baadaye ndiyo inasema ni mtawanyiko wa watu wowote nje ya maeneo yao

ya asili .. The dispersion or spread of any people from their original homeland. Kihistoria Wayahudi ndio

watu wa mwanzo duniani kutawanyika kutoka makazi yao ya asili, na ukisema diaspora ilikuwa na

maana ya wayahudi waishio nje ya Israel, lakini neno hili limekopwa kutoka kwa wayahudi na sasa

linamaanisha makundi yoyote ya watu waishio nje ya nchi zao za asili. Sasa Wayahudi kutokana na

historia yao ya kutawanyika, mara nyingi sana wanakuwa na uraia pacha, na katiba yao inaruhsu hata

zaidi ya uraia pacha (multiple citizenship, na kwa utafiti niliofanya, mtu hawezi kuukana uraia wa Israel,

… utaratibu wa kuukana upo lakini serikali ya Israel imeweka mchakato mgumu, kiasi kwamba ni kama

tu haiwezekani. Hata ukiishi nchi nyingine miaka mingi au ukiwa na uraia nyingi bado utaendelea kuwa

mwisrael). Lakini papo hapo Wayahudi ni kati ya watu wanaosifika kwa uzalendo kwa nchi yao. Wapo

wengi wana uraia wa nchi za magharibi lakini utakuta wanatumikia katika jeshi la Israeli. Kwa mfano

askari mmoja wa Israel aitwaye Gilad Shalit (ambaye pia ana uraia wa Ufaransa) mnamo mwaka 2006

alitekwa na wapiganaji wa Hamas, na akashikiliwa kwa kipindi cha miaka mitano kabla ya kuachiliwa

huru. Katika kukuru kakara za kutekwa wenzake wawili aliokuwa nao waliuawa. Angeweza kabisa kuishi

raha mustarehe ndani ya jiji la Paris lakini kwa uzalendo aliokuwa nao kwa Israel alikuwa radhi

12

kuipigania nchi yake hadi tone la mwisho (hapa nakopa maneno aliyotumia Polepole), na sidhani hapo

kuna atakayetilia shaka yoyote juu ya uzalendo wake kwa nchi yake. Wapo wengi ambao wana uraia wa

nchi za magharibi, lakini wanarudi nyumbani kupigana. Mfano huu unaonyesha wayahudi walio vinara

wa uraia pacha au zaidi (multiple citizenship) ni vinara pia kwa sifa ya uzalendo; na unakanusha hoja ya

Polepole kwamba uraia pacha unasababisha watu kukosa utii/uaminifu au watu kukosa uzalendo kwa

nchi yao.

- Zaidi ya yote, uraia pacha unavunja msingi wa haki ya usawa kwa sababu katika taifa moja, raia

wanawekwa katika mafungu, wale wenye uraia wa zaidi ya nchi moja, ambao wanakuwa na haki zote

nchini na haki zaidi kwingineko dhidi ya wale wenye uraia mmoja, ambao wana haki zote za hapa nchini

pekee, lakini wote wako sawa nchini.

Sielewi ni kwa vipi, uraia pacha unavunja haki ya usawa. Ieleweke kuwa mtu akiwa na uraia pacha

akiingia Tanzania atachukuliwa kama Mtanzania kwa mujibu wa sheria itakayowekwa, wala hataishi kwa

mujibu wa sheria za hiyo nchi nyingine ambayo ana uraia pacha. Uwezekano mkubwa ni kwamba

hatakuwa na haki zote sawa na watanzania ambao wana uraia mmoja, kutakuwa na baadhi ya haki

hatakuwa nazo kama sheria ya uraia pacha itakavyoainisha iwapo itapitshwa, mfano sheria hiyo inaweza

kusema mtu mwenye uraia pacha hawezi kuwa Rais, kufanya kazi kwenye taasis za usalama wa taifa n.k.

Na hili liko wazi, mbona hata katiba yetu ya sasa haiwaruhusu raia wa kuandikishwa kugomeba urais?

Vivyo hivyo itaainisha mipaka ya wazawa walio na uraia pacha.

Anaposema wenye uraia pacha watakuwa na haki zaidi kwingineko dhidi ya wale wenye uraia mmoja,

sioni kuna ubaya gani. Hii ni sawa na wale wanaosema kuwa wanaotaka uraia pacha wanataka kula huku

na huku. Mimi nikiwa na uraia wa Tanzania halafu nikaenda nchi nyingine nikapata uraia wa huko, hiyo

inaathiri vipi haki zako wewe uliyebaki Tanzania ukiwa na uraia mmoja? Na wewe kama unataka kuwa

na uraia pacha hujakatazwa kuutafuta kutoka nchi unayotaka kama sheria itakavyoanisha. Vinginevyo

kwa kweli hii itakuwa tu ile roho ya kwanini, na ni ubinfasi, mimi sipati kwanini mwigine apate, acha

tukose wote.

Ukweli mwigine ambao hatuwezi kuukataa ni kwamba popote pale huwa kunakuwa na fursa ambazo si

raia wote wanaweza kuzitumia, pamoja na kwamba kisheria zitatambulika ni kwa ajili ya wote.

Tuchukulie mfano pasi za kusafiria, raia yeyote anayo haki ya kuwa nayo lakini ni Watanzania wangapi

ambao wanazo na moja kwa moja wananufaika nazo kusafairia nchi za nje? Ni dhahiri kuwa ni wachache

sana. Je, hili suala halivunji usawa kwa misingi aliyoielezea Polepole? Na ziko sheria nyingi ambazo

zinatoa fursa kwa wote, lakini kiuhalisia wenye kutumia fursa hizo ni wachache lakini kwa manufaa

mapana ya taifa kwa ujumla. Wachache wanaopata fursa hizo wenyewe wananufaika lakini pia taifa

13

linanufaika. Vivyo hivyo kwa uraia pacha. Kwa hiyo si kweli kabisa kwamba usawa utavunjwa ikiwa uraia

pacha utaruhusiwa.

Suluhisho ndani ya Rasimu ya Katiba Toleo la Pili, kama ilivyoainishwa na Polepole

Ibara ya 59 ya Rasimu ya Katiba inawatambua na kuwapa hadhi maalumu watu wenye asili au nasaba ya

Tanzania na ambao wameacha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupata uraia wa

nchi nyingine wanapokuja Tanzania kwa masharti yatakayoainishwa na sheria za nchi.

Kama alivyoainisha Polepole, mapendekezo haya yalizingatia kuwa nchi itakapotambua uraia wa nchi

mbili, haitakuwa na msingi wa kikatiba na kisheria wa kuwazuia raia wa nchi nyingine kubaki na uraia

wao wanapokuwa raia wa kuandikishwa wa Tanzania kwa kuzingatia kuwa Jamhuri ya Muungano

inapakana na nchi nane na italeta changamoto ya usalama na ulinzi.

Nataka nimweleze tu kuwa si kweli, kwamba nchi itakapotambua uraia wa nchi mbili, haitakuwa na

msingi wa kisheria wa kuwazuia raia wa nchi nyingine kubaki na uraia wao wanapokuwa raia wa

kuandikishwa. Maana kinachopendekezwa hapa ni kulinda uraia wa watu wenye nasaba ya Tanzania.

Kwamba ukishakuwa wewe Mtanzania kwa kuzaliwa ubaki kuwa Mtanzania hata kama umepata uraia

wa nchi nyingine na wala si kwa Watanzania wa kuandikishwa. Kama nilivyosema hapo juu katiba tayari

inakataza mtu ambaye ana uraia wa kuandikishwa asigombee uraisi wa nchi. Kwa nini msingi huo

usiendelee kutumika kuwakataza raia wa kujiandikisha wasiwe raia wa nchi nyingine zaidi ya Tanzania.

Maana mtu ameomba uraia, kila nchi ina masharti yake, sisi ndio masharti yetu, kama mtu hakubaliani

nazo hapati uraia.

Ninadhani ni swala la msingi pia kabisa kuainisha hapa kwamba kuna uraia pacha wa aina mbili:

Emigrant dual citizenship: Hii ina maana nchi inaruhusu raia wake wenye uraia wa kuzaliwa kupata uraia

wa nchi nyingine bila kupoteza uraia wa wao wa kuzaliwa.

Immigrant dual citizenship: Hii ni pale nchi inaporuhusu wahamiaji walioingia kupata uraia kwa njia ya

kuandikishwa ama kunasibishwa lakini bila kulazimika kupoteza uraia wa nchi zao za asili.

Hivi ni vitu viwili tofauti, tofauti hii inakuwa siyo muhimu sana iwapo sheria inaruhusu aina zote mbili,

kama ilivyo katika nchi nyingi zilizoruhusu uraia pacha. Lakini tofauti hii ni muhimu kuizingatia pale

inapotokea nchi inaruhusu aina moja na kukataza aina nyingine. Kwa mfano raia wa Ujerumani

wanaopata uraia wa nchi nyingine wanaruhusiwa kuendelea kuwa na uraia wa kijerumani kama bado

wana familia zao zilizobaki Ujerumani. Lakini wakati huo huo wahamiaji wanaopata uraia wa Kijerumani

kwa njia ya kuandikishwa ni lazima waukane uraia wa nchi zao za asili. (Taz uk. 24

14

https://www.mah.se/upload/Forskningscentrum/MIM/Publications/WB%203.01.pdf). Kwa hiyo

Ujerumani inaruhusu emigrant dual citizenship, lakini hairuhusu immigrant dual citizenship. Ujerumani

siyo tu kwamba inaruhusu emigrant dual citizenship bali inawahimiza watu wenye asili ya kijerumani

ambao wamepata uraia wa nchi nyingine kutoukana uaria wao wa kijerumani. (Taz uk. 708

http://www18.georgetown.edu/data/people/mmh/publication-7319.pdf )

Kwa hiyo kama woga kwa swala la uraia pacha ni juu ya wale raia wa kutoka nchi nyingine

watakaochukua uraia Tanzania, basi hao hatuna lazima ya kuwapa uraia pacha. Tunaweza kuruhusu

Watanzania wenye uraia wa kuzaliwa kuendelea kuwa na uraia wa Tanzania pindi wanapopata uraia wa

kuandikishwa wa nchi nyingine (emigrant dual citizenship) na wakati huo huo kuwataka wale

watakaoomba uraia wa kuandikishwa Tanzania waukane kwanza uraia wao, kwa maana nyingine

kutoruhusu immigrant dual citizenship. Hii inaweza kuonekana kama ubaguzi, lakini kama kweli

tunaweza kuonyesha tuna sababu za kimsingi basi watu watazielewa, sioni kama itakuwa ni tatizo, kama

ukiona sababu hizo hazieleweki basi zitakuwa ni sababu zisizokuwa na msingi.

Hata ukiangalia mfano mwingine wa katiba za majirani zetu wa Kenya na Uganda, wote wameruhusu

uraia pacha lakini ukisoma katiba zao utaona tafsiri tofauti.

Ile ya Uganda imeruhusu uraia pacha kwa raia wake wa kuzaliwa pamoja na wale watakaopata uraia wa

Uganda kwa njia ya kuandikishwa. Ninakuu hapa katiba ya Uganda ya 1995 kama ilivyobadilishwa 2005,

ibara ya 15 ibara ndogo ya kwanza na ya pili:

15. Dual citizenship.

(1) A citizen of Uganda of eighteen years and above, who voluntarily acquires the citizenship of a country

other than Uganda may retain the citizenship of Uganda subject to this Constitution and any law enacted

by Parliament.

(2) A person who is not a citizen of Uganda may, on acquiring the citizenship of Uganda, subject to this

Constitution and any law enacted by Parliament, retain the citizenship of another country.

Lakini ya Kenya imeruhusu uraia pacha kwa wale raia wa kuzaliwa tu, haitamki chochote juu ya

watakaopata uraia kwa njia ya kuandikishwa, ninanukuu hapa katiba ya Kenya ya 2010, ibara ya 16.

Dual Citizenship

16. A citizen by birth does not lose citizenship by acquiring the citizenship of another country.

Uzoefu wa nchi nyingine

Uzoefu wa nchi ya India na Ethiopia ambazo hazina na zimesita kutoa uraia wa nchi mbili kwa sababu za

kiulinzi na usalama, lakini zimetoa hadhi maalumu kwa watu wenye asili na nasaba ya nchi hizo, ambao

wameacha kuwa raia wa nchi hizo.

15

Katika Katiba ya India, watu hao wanaitwa ‘Persons of Indian Origin’ na wana hadhi maalumu. Kwa

mujibu wa sheria za India, mtu mwenye asili au nasaba ya India hadi kizazi cha nne, atapata hadhi ya

‘Person of Indian Origin (PIO)’, isipokuwa kwa raia wa nchi za Afghanistan, Bangladesh, Bhutan, China,

Iran, Nepal, Pakistan na Sri-Lanka.

Kama anataka kutafuta uzoefu wan chi nyingine, mimi nadhani ingekuwa na mantiki zaidi kama

angeangalia nchi majirani zetu wa Afrika Mashariki ambao tunafanana nao zaidi kijiografia, kihistoria na

kiutamaduni. Na tuna fungamano nao kubwa za kiuchumi, kijamii na kisiasa katika jumuiya ya Afrika

Mashariki. Sielewi kwa nini Polepole anavuka mabara na bahari kwenda kujilinganisha na India ambao

hatufanani nao, halafu anaacha washirika wenzetu katika Afrika Mashariki, Kenya, Uganda, Rwanda na

Burundi, ambao tunafanana nao zaidi, na ambao wote wameruhusu uraia pacha.

5.0 MAONI MENGINE YA JUMLA

5.1 Hofu ya kuwa na Rais mgeni

Nimesoma mahala pengine mtandaoni, moja ya hofu ya uraia pacha ni pamoja na kwamba eti ipo siku

Tanzania inaweza kujikuta ina rais mgeni. Ni vizuri ikawekwa wazi kuwa nchi zenye uraia pacha zina

sheria zinazoainisha masharti yake. Mathalani, nchini Canada aliwahi kuteuliwa Gavana Michaelle Jean

(ambaye kwa Canada kiitifaki yupo juu ya Waziri Mkuu) ambaye alikuwa pia na uraia wa Ufaransa. Kwa

utaratibu wao alilazimika kwanza kuukana uraia wa Ufaransa kabla ya kuchukua nafasi hiyo. Vivyo hivyo

kwa Tanzania masharti yanaweza kuwekwa kuwa wenye uraia pacha kuna mambo hawawezi kushiriki

iwapo wana uraia wa nchi nyignine au mpaka watakapokana uraia huo. Hili ni jambo la kawaida ili

kuondoa mgongano wa kimaslahi.

5.2 Uzalendo

Sababu nyingine inayovuma sana ni ile ya kusema uraia pacha utaathiri uzalendo. Mimi nadhani kama

mtu leo ni mzalendo, kesho hawezi kukosa uzalendo kwa vile tu kachukua pasi ya kusafiria ya nchi

nyingine. Uzalendo uko kwenye moyo wa mtu sio swala la kupima kwa idadi ya pasi za kusafiria mtu

alizobeba. Kama mtu siyo mzalendo, basi siyo mzalendo tu potelea mbali ana passport moja au mbili.

Mfano nimesoma juu ya Mtanzania mmoja, mwalimu wa chuo kikuu fulani huko Marekani na ambaye

amechukua uraia wa Marekani. Miaka michache iliyopita kwa juhudi zake aliweza kufanikisha kuwaleta

madiwani kutoka kanda ya ziwa kuja kujifunza kazi za halmashauri za miji kwenye chuo chake, pasipo

16

gharama yoyote kwa upande wa madiwani. Je huyu si mzalendo kwasababu ya kuchua pasi ya kusafiria

ya Marekani? Ninamini inawezekana kabsia kwa Mtanzania anayeishi New York kuwa mzalendo sawa na

yule anayeishi Mbagala au hata zaidi.

5.3 Usalama wa Taifa

Kama nilivyoeleza hapo juu sababu ya usalama imepitwa na wakati kwas asa. Inatakiwa tu katiba

itambue uraia pacha wa namna mbili, kwanza kwa wantanzania ambao ni raia wa kuzaliwa wanaopata

uraia wa nchi nyingine, na wale raia wa kuandikishwa ambao tayaro wana uraia wa nchi walikotoka.

Kisha bunge litunge sheria ya uraia itakayosimamia mambo wanayoruhusiwa na wasiyoruihusiwa

Watanzania wa kuzaliwa wenye uraia pacha. Inawezekana kabisa kutowaruhusu kushika uongozi ngazi

fulani ama kutowaruhusu kufanya kazi katika nafasi nyeti mfano idara ya usalama wa taifa, jeshi nk.

Halafu vile vile kuwe na ibara ndogo itakayosimamia utaratibu wa raia wa nje kupata uraia wa Tanzania,

vile vile kunakuwa na haki, wajibu na mipaka vinavyoendena na uraia wa aina hiyo. Ile aliyosema bwana

Polepole kwamba huwezi kuruhusu uraia pacha kwa watanzania wa kuzaliwa halafu ukawanyima wa

kuandikishwa siyo jambo ambalo haliwezekaniki kama yeye anavyotaka tuamini. Nchi nyingine zinafanya

hivyo. Na mbona katiba yetu ya sasa tayari inawabagua? Ibara ya 39(1) inasema moja ya sifa ya

mgombea urais lazima awe ni raia wa kuzaliwa, kwa hiyo hawana haki zote sawa na raia wa kuzaliwa.

5.4 Swala la Jumuiya ya Afrika Mashariki

Wale wanotumia usalama wa Taifa kama sababu ya kutoruhusu uraia pacha, bado kuna kitu kimoja

ambacho hawajaeleza vizuri. Kama tujuavyo tupo kwenye mchakato wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

ambako tayari kuna muungano wa forodha (customs union), soko la pamoja (common market).

Muungano wa sarafu (moneytary union) ulipitishwa mwishoni mwa mwaka jana na wakuu wa nchi za

jumuiya hiyo. Hatimaye lengo la nchi hizi ni kuwa na shirikisho la Afrika Mashariki. (tazama ripoti ya

Wako:

http://www.eac.int/federation/index.php?option=com_docman&task=doc_download&gid=140&Itemid

=136 )

Kwa hiyo utaona tayari Tanzania tuna fungamano za karibu kabisa na wenzetu wa Afrika Mashariki, na

huenda baadaye tukawa ni nchi moja chini ya shirikisho. Wenzetu wote wa Afrika Mashariki tayari

wameruhusu uraia pacha.

Swali ambalo ningewauliza wanaopinga uraia pacha Tanzania, mtawazuia vipi raia wa Afrika Mashariki

ambao wana uraia pacha kuingia Tanzania kwa kutumia mwavuli wa nchi zao za Kenya, Uganda, Rwanda

na Burundi? Hamwoni kwamba Wakenya, Waganda, Wanyarwana na Warundi waliochukua uraia wa

nchi nyingine watakuwa na fursa zaidi Tanzania kuliko Watanzania wenye uraia pacha? Tuchukue mfano

17

mdogo: Ikiwa Mtanzania na Mkenya wanaoshi Marekani na wote wamechukua uraia wa Marekani

watakuja Tanzania, Mkenya ataingia kirahisi kama raia wa Afrika Mashariki lakini Mtanzania ataingia kwa

viza kama Mmarekani. Sasa kama ni “dhambi” ya kuchukua uraia wa nchi nyingine Mkenya na

Mtanzania wameitenda dhambi ile ile, lakini Tanzania “inamwadhibu” zaidi Mtazania kuliko Mkenya. Hii

si sawa wala si haki.

Swali la pili, kuwa na shirikisho kimsingi maana yake ni kuwa nan chi moja, ambayo kwa vitu muhimu

kama uraia ni lazima iwe na sheria moja. Sasa ikiwa upande mmoja Tanzania iko katika mchakato

kuelekea shirkisho na upade mwingine wanakataa kuruhusu uraia pacha wakati washirika wake wa

Afrika Mashariki wameruhusu ni kuwa na sera zinazopingana, huu ni wakati mwafaka wa kuliangalia

hilo.

5.5 Faida za Uraia Pacha

Makala ya bwana Poleple imeegemeea upande mmoja, ubaya wa uraia pacha, haikuzumgumzia hata

kidogo faida zake. Katika hotuba ya Rais kwenye Mkutano na Watanzania waishio nje ya nchi Agost 14,

2014 alibainisha faida za mbalimbali za diaspora, ambazo kwa kiwango kikubwa zina uhusiano wa moja

kwa moja na na uraia pacha. Nitamalizia makala hii kwa kuzungumzia kidogo mbili kati ya sababu hizo.

5.5.1 Remittance, yaani fedha zinazotumwa nyumbani na watu walioko nchi za nje.

Nadhani hili limeshazungumzwa sana kwa hivyo linaeleweka, ila ningependa nigusie kitu kimoja. Katika

utafiti uliofanywa na mwanataaluma mmoja, raia wa Ghana, Adams Bodomo, alibaini kwamba kwa

mwaka 2010 fedha zilizotumwa nyumbani na Waafrika waishio nje zilikuwa nyingi kuzidi zile zilitolewa

na wahisani wa magharibi kama msaada wa rasmi wa maendeleo (Official Developmet Aid). Kwa mwaka

2010 pekee, Waafrika waishio nje walituma nyumabni jumla ya dola za kimarekani bilioni 50.8 wakati

misaada ya maendeleo kwa Afrika (ODA) ilikuwa bilioni 43.

Takwimu hizi zinaonyesha kiasi cha fedha kilichotumwa kwa njia rasmi tu (kama Western Union,

Moneygram nk), lakini Bw Bodomo anakisia kwamba karibu robo tatu ya fedha zinazotumwa Afrika

zinapitia njia zisizo rasmi, kwa mfano mtu anaweza kutuma hela nyumbani kupitia rafiki yake

anayekwenda likizo. Kwa hiyo anakisia kama ukihesabu zote hizo, basi fedha zinazotumwa nyumbani na

Waafrika waishio nje huenda zikapindukia zile zinazotelewa kama msaada rasmi wa maendeleo karibu

mara tatu au nne. (Ukitaka kusoma zaidi tazama http://www.bbc.com/news/world-africa-22169474 )

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba nchi yetu itaendelea kuhitaji misaada ya wahisani kwa muda

mrefu ujao. Lakini tafiti zinazofanywa zinaonyesha kuwa nchi zinazoendelea zinaweza zikapata fedha

18

nyingi zaidi kutoka kwa raia wake waishi ughaibuni. Nchi nyigni za Afrika zimetambua hilo, kwa takwimu

za Benki ya Dunia, karibu nusu ya nchi za bara la Afrika, sasa zinaruhusu namna fulani ya uraia pacha

(tazama jedwali uk. 25, http://siteresources.worldbank.org/EXTDECPROSPECTS/Resources/476882-

1157133580628/DfD_overview.pdf ; kuna ripoti ya taasisi nyingine pia ya 2010, taz. ukursa 62:

http://www.opensocietyfoundations.org/sites/default/files/citizenship-africa_20101118.pdf )

Tanzania imelitambua hilo, rejea hotuba wa Rais Kikwete katika mkutano wake na raia waishio nje

tarehe August 14 Dar es Salaam, akinukuu takwimu za Benki ya dunia alibainisha kuwa kwa mwaka 2013

kulikuwa na watu milioni 220 waliokuwa wakiishi nje ya nchi zao, ambao walituma nyumbani kiasi cha

dola za kimarekani bilioni 581, na inakadiriwa kiasi hicho kitaongezeka kufikia bilioni 681 ifikapo mwaka

2016 (ongezeko la asilimia 17). Akiendelea kunukuu takwimu hizo Rais alisema kwa mwaka 2011

Tanzania ilipokea dola za kimarekani milioni 10.2 wakati Kenya ilipokea bilioni 1.2. Rais alisema kuwa

kiasi Tanzania ilichopokea ni kidogo (kama ambavyo wapinzani wengi wa uraia pacha wanavyodai), lakini

alikuwa pia mwepesi kukiri kwamba kiwango hiki kinachotumwa kinategemea idadi ya watu wanaoishi

nje na watu hao wana shughuli gani huko; na alienda mbali zaidi kusema kwamba Tanzania kwa historia

yake haijawa na watu wengi wanaoishi nje, wengi wakienda kusoma nje walikuwa wanarudi.

Katika hotuba ya Rais tunaweza kubaini vitu vichache: Kwanza kiwango kinachotumwa na watu walio nje

kitaendelea kuongezeka. Rais hakutoa sababu za ongezeko hilo lakini mimi nadhani ni kutokana na

utandawazi kuendelea kushamiri basi watu wengi zaidi watavuka mipaka kwenda kuishi nchi za nje. Ili

Tanzania iweze kuongeza mgao wake katika hela zinazotumwa kutoka diaspora kwanza ni lazima idadi

ya Watanzania wanaoishi nje iongezeke, hilo halina ubishi, hata Rais amekiri kiwango kinachotumwa

kinategemea idadi ya watu.

Pia Rais amegusia pia kuwa swala siyo idadi ya watu peke yake, bali pia wanafanya shughuli gani? Ikiwa

watu wana kazi nzuri zenye kipato kikubwa vivyo hivyo wataweza kutuma nyumbani hela nyingi zaidi.

Ikiwa wanafanya shughuli ambazo kipato chake ni kujikimu tu basi hawatakuwa na hela nyingi za

kutuma nyumbani.

Ili tupate mwangaza zaidi juu ya maswala hayo ambayo Rais ameyaibua, hebu na tuangalie taarifa ya

Benki ya Dunia, Harnessing Diaspora Resources for Africa ya mwaka 2011. Ripoti hiyo ilionyesha kuwa

Nigeria ndiyo nchi ya Afrika inayoongoza kwa kuwa na wahamiaji wengi zaidi Marekani, 211,000, Kenya

ikiwa na 85,000. Katika takwimu hizo Tanzania hata haikutajwa, ikimaanisha idadi ya wantanzania

walioko huko ni ndogo mno kuweza hata kuingia kwenye takwimu. (Taz jedwali uk.5

http://siteresources.worldbank.org/EXTDECPROSPECTS/Resources/476882-

1157133580628/DfD_overview.pdf ). Naamini ikiwa utaangalia takwimu za Waafrika wanaoishi nchi

19

nyingine, mfano za Ulaya, hazitatofautiana sana na hizi za Marekani, Tanzania itakuwa na watu

wachache. Sasa kwa takwimu hizo huwezi kushangaa ikiwa Tanzania inapokea fedha kidogo kulinganisha

na nchi nyingine.

Ripoti hiyo hiyo ya benki ya dunia, inaonyesha ni rahisi zaidi kwa wahamiaji kupata kazi nzuri zenye

kipato kikubwa ikiwa watachukua uraia wa nchi hizo. Na utafiti umeonyesha kuwa nchi zinazoruhusu

uraia pacha zimepokea fedha nyingi zaidi zinazotumwa kutoka diaspora kwa vile raia wao wako radhi

zaidi kuchukua uraia wa nchi walizohamia. Hapa ninanukuu …

Holding dual citizenship provides an important link between diasporas and their home countries.

It can also improve both a diaspora's connection with its origin country and its integration into the

destination country. Citizenship and residency rights are important determinants of a diaspora's

participation in trade, investment and technology transfer with its origin country and make it easier to

travel and own land. Origin countries that allow dual citizenship also benefit because their migrants are

then more willing to adopt the host country's citizenship, whci can improve their earnings and thus their

ability to send remittances and invest in the origin country.

Immigrants from some countries that allowed dual citizneship during the 1990s and 2000s (Brazil,

Colombia,Costa Rica, teh Dominican Republic and Ecuador) have experienced a rise in earnings in the

United States, because they acquired legal status and can have access to better jobs.

Kwa utafiti huo wa Benki ya Dunia ni dhahiri kwamba kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya uraia

pacha na kiasi cha fedha kinachotumwa nyumbani, kwa hiyo ni wakati mwafaka kwa Tanzania kuruhusu

uraia pacha. Uraia pacha utawapa motisha Watanzania wengi zaidi kuishi nje na kupata kazi nzuri zaidi,

na moja kwa moja kiasi cha fedha watakachotuma nyumbani kitaongezeka.

Tuchukue mfano mwingine: Tuseme kuna Mtanzania yuko kwenye nchi iliyoendelea, kama Marekani,

Canada, Ufaransa au nchi nyingine yoyote, akajisomesha mwenyewe hadi kuhitimu uhandisi kwenye

mambo ya Nuclear Physics halafu baada ya kuhitimu akapata kazi nzuri kwenye kinu kimojawapo cha

nyuklia katika nchi hiyo lakini sharti lazima awe raia. Mtu huyo inabidi aidha achukue uraia apate hiyo

kazi nzuri yenye kipato kikubwa au akatae kuchukua uraia afanye kazi za chini ya viwango ambazo

hatalazimika kuchukua uraia wa nchi hiyo lakini ambazo mshahara wake siyo mzuri sana, ni kipato cha

kujikimu tu.

Unaweza kusema asichukue hiyo kazi arudi nyumbani Tanzania. Ndiyo, anaweza kurudi, lakini hatatumia

utaalamu wake aliosomea wa uhandisi katika mambo ya nuclear physics. Anaweza kubahatisha kazi

nyumbani lakini anaweza asipate kazi, na hata akipata hiyo kazi nyumbani itakuwa ni kazi ambayo hana

20

utaalamu nayo kwa vile Tanzania hatuna kinu cha nyuklia. Kwa maana nyingine elimu yako aliyoipata

kwa kujinyima na utaalamu wake vitakuwa havitumiki na hii itakuwa hasara kwake binafsi na kwa taifa

pia. Sasa hapa busara ingekuwa ni kwamba aache kuchukua kwasababu ya uzalendo? Au akae Marekani

akifanya kazi za chini ya viwango? Au arudi Tanzania na elimu yake iwe ni bure, .. maana utaalamu wake

hataweza kuutumia Tanzania?

5.5 .2 Ushawishi

Mnapokuwa na idadi kubwa ya raia wenu katika nchi fulani na ikiwa wana uraia wa nchi hiyo, basi

inawezekana kabisa watu hao kushawishi sera za nchi hiyo juu ya nchi yenu.

Mfano mzuri ni Israel na Marekani. Mara nyingi sera za Marekani ni lazima ziipendelee Israel sababu

mojawapo ni kwamba Marekani ina raia wenye asili ya kiyahudi na wenye ushawishi mkubwa katika

siasa za Marekani. Mgombea urais yeyote wa Marekani ni lazima ajikombe kwa Israel kusudi apata

uungwaji mkono na Wayahudi waishio Marekani.

Mfano mwingine, Canada kuna watu wengi wenye asili ya Ukraine. Wanasiasa wengi watataka kuwa na

sera nzuri kwa Ukraine vinginevyo watakosa kura za hao raia wenye asili ya Ukraine kwenye uchaguzi

utakaofuata. Kwa mfano wakati wa mgogoro wa Urusi na Ukraine, Waziri Mkuu wa Canada ndiye

aliyekuwa kiongozi wa kwanza wa magharibi kwenda Ukraine kubainisha kwama anaiunga mkono

Ukraine dhidi ya Urusi, na wameipatia Ukarine mabilioni ya dola. Watu wanaweza wasione moja kwa

moja lakini ile ilikuwa ni kampeni ya uchaguzi, anajua Canada kuna uchaguzi mwaka ujao hivyo anataka

kujihakikishia kura za raia wa Canada wenye asili ya Ukraine.

Vivyo hivyo ndivyo ilivyokuwa wakati wa maafa asilia, tufani Haiyan ilipoikumba Philippines mwishoni

mwaka 2013. Serikali ya Canada ilikuwa mstari wa mbele kusaidia, kupeleka misaada ya kibindamu na

kuahidi kwamba katika michango yoyote itakayokusanywa na jamii zozote kwa ajili ya maafa hayo, basi

serikali nao wangetoa kiwango kama hicho hicho. Kwa namna moja ile ilikuwa ni kampeni ya kusaka kura

za Wafilipino ambao ni jamii kubwa Canada.

Tanzania haijafikia kiwango hicho cha kushawishi maswala ya sera, lakini ile kuwa na jumuiya za

Watanzania sehemu mbali mbali duniani nako si haba sana. Ile peke yaje inawafanya watu wa nchi hizo

wasikie Tanzania, na huenda wakapatwa na tashwishi ya kujua zaidi na hatimaye huenda hata

wakaamua kuja kama watalii Tanzania. Jumuiya hizi pia hujishughulisha na shughuli mbali mbali za

kuonyesha utamaduni wa mtanzania katika nchi wanazoishi. Sasa ingekuwa ni wakati wa jumuiya hizi

kuungwa mkono, kuziwezesha zaidi katika hayo wanayofanya sasa na hata hatimaye kukua kiasi cha

21

kuwa na usawishi katika maamuzi ya kisera katika nchi wanazoishi. Kuruhusu uraia pacha ingekuwa ni

namna moja ya kuziunga mkno na kuziwezesha.

6.0 HITIMISHO

Rais aligusia kwenye hotuba yake kwamba haitawezekana kwa nchi kuendelea kwa fedha zake yenyewe,

ni lazima ipate mitaji kutoka nje. Tumeshaona inawezekana Watanzania wakatuma hela kuzidi zile

zinazokuja kama misaada. Tuchukue hatua za makusudi kuelekea hali hiyo, kuruhusu uraia pacha ni

hatua moja kuelekea huko.

Isitoshe, zile zama za vita baridi zimekwisha, hizi ni zama za utandawazi. Na mojawapo ya sifa zake ni

watu kuweza kufanya kazi katika nchi nyingine, “movement of labour”. Katika zama hizi za utandawazi,

tusiifanye Tanzania kuwa ni nchi ya kupokea wafanyakazi wa kigeni tu, na sisi tutoe watu wetu kwenda

nchi za nje, huko wataongeza utaalamu zaidi wakiamua kubaki huko nchi itafaidika kwa fedha

watakazotuma nyumabni, wakiamua kurudi nyumbani nchi itafaidika zaidi kwa utaalamu na “exposure”

watakayopata. Lakini yote mawili yatahitaji waweze kuwa raia wan chi hizo ndipo wataweza kupata kazi

nzuri zaidi na kuongeza maarifa yao. Siyo wengi watakaokuwa radhi kupoteza uraia wa Tanzania pindi

watakapochukua uraia wa nchi nyingine, kwa hiyo ni wakati mwafaka wa kuruhusu uraia pacha.