8
JARIDA Januari 2016 Toleo na. 008 Mbinu bora za ECHO Afrika Mashariki!!!!! Katika toleo hili: 1. Kongamano la Arua 2. Matangazo 3. Rasilimali za ubunifu 4. Habari za ECHO A.M 5. Mbinu bora za ECHO A.M Matukio yajayo: Kongamano la mbinu bora katika maeneo ya wafugaji 1-3, Machi 2016 Nanyuki, Kenya; Kwa kujisajili tafadhali fungua hapa link

JARIDA - ECHOcommunity...Mafunzo yalilenga kubadilishana na kufanya marudio kati ya watendaji vifaa na mbinu wanazotumia na kwa pamoja kuboresha mbinu zilizopo. Kwa kawaida mafunzo

  • Upload
    others

  • View
    4

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: JARIDA - ECHOcommunity...Mafunzo yalilenga kubadilishana na kufanya marudio kati ya watendaji vifaa na mbinu wanazotumia na kwa pamoja kuboresha mbinu zilizopo. Kwa kawaida mafunzo

JARIDA

Januari 2016 Toleo na. 008 Mbinu bora za ECHO Afrika Mashariki!!!!!

Katika toleo hili: 1. Kongamano la Arua 2. Matangazo 3. Rasilimali za ubunifu 4. Habari za ECHO A.M 5. Mbinu bora za ECHO A.M

Matukio yajayo: Kongamano la mbinu bora katika maeneo ya wafugaji 1-3, Machi 2016 Nanyuki, Kenya;

Kwa kujisajili tafadhali fungua hapa link

Page 2: JARIDA - ECHOcommunity...Mafunzo yalilenga kubadilishana na kufanya marudio kati ya watendaji vifaa na mbinu wanazotumia na kwa pamoja kuboresha mbinu zilizopo. Kwa kawaida mafunzo

Organic Academy Leadership Course

Africa

January - November 2016 For more information, please visit www.ifoam.bio/academy Kongamano la nyanda za juu; 1-3, Novemba 2016, Addis, Ethiopia UNGEPENDA KUTANGAZA MAFUNZO? TUFAHAMISHE NA TUTATANGAZA www.ECHOcommunity.org Blogu ya Afrika Mashariki

SALAMU ZA MWAKA MPYA!!!

ECHO Afrika Mashariki inapenda kutoa salamu za mwaka mpya kwa wanachama washirika wake, wabia na wadau. ECHO inamshukuru Mungu kwa Baraka za mwaka uliopita ambazo zilipelekea kutimiza malengo ya kuwahudumia watu kwa kuwapatia “Mbinu bora” za kubadilisha Maisha yao ili kutimiza lengo la kupunguza njaa na kuboresha Maisha ya watu masikini!!! ECHO Afrika Mashariki inatangaza juu ya ushirikiano na nia ya kufanya kazi pamoja ili kuchangia zaidi katika matokeo haya katika mwaka 2016. Mungu na aendelee kuwabariki wote kwa kuchangia katika kufikia malengo haya ya pamoja!!!

Timu ya ECHO Afrika Mashariki katka picha ya pamoja (picha juu)

MATANGAZO

Hivi sasa ECHO inaendelea na maandalizi ya kongamano lake la pili lenye dhima “Mbinu bora katika sehemu za wafugaji” litakalofanyika kuanzia

tarehe 1-3 Machi, 2016 karika hoteli ya Sportsman’s huko Nanyuki, Kenya.

Kwa usajili na maelezo zaidi tafadhali bonyeza hapa link au tembelea www.echocommunity. Linalofuatia baada ya tukio hili, lingine litakuwa

kongamano la nyanda za juu huko Addis, Ethiopia kuanzia tare 1-3, Novemba,2016. Ungana na ECHO Afrika Mashariki kwa maelezo zaidi

kuhusiana na kongamano hili kupitia www.echocommunity.org

KONGAMANO LA ARUA ECHO Afrika Mashariki iliendesha kongamano huko Arua-Uganda- Mbinu bora za kufanya kazi katika maeneo yenye migogogoro- kuanzia tarehe 3-5, Novemba 2015, iliyofuatiwa na ziara ya matembezi kwenye mashamba mawili (Shamba la serikali la utafiti na Shamba la Eden la Anglican); tukio lilibarikiwa kupata wawasilishaji mada 34; ikijumuisha mada za asubuhi na mchana katika makundi madogomadogo. Nyingi kati ya dhima hizo zilihusiana zaidi na maelezo yanayohusiana na sababu/ vyanzo vya migogoro, mafunzo waliyopata na suluhisho baada ya migogoro ili kunusuru hali ili kuwezesha kusukuma maendeleo katika sehemu zilizoathiriwa na migogoro ambayo ni ya kisiasa, kidini au kikabila. Tukio lilikuwa ni la kuwafurahisha wafanyakazi wa maendeleo wanaofanya kazi katika maeneo yenye migogoro. Arua ilikuwa ni sehemu nzuri kufanya kongamano hilo kama ambavyo si kwamba imekuwa sehemu iliyoathiriwa na migogoro, lakini pia inapakana na sehemu nyingine za migogoro kama Sudan ya kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Congo (CONGO). Wafanyakazi wa ECHO waliratibu tukio hilo. Tathmini ya washiriki wote ilionesha matokeo chanya. Washiriki wote 62 waliojisajili walipatika pakiti za mbegu, nyingi kati ya hizo zikiwa mbolea ya kijani/mazao funika kwa ajili ya kurutubisha ardhi. Rasilimali za kongamano la Mbinu bora katika maeneo yenye migogoro, 2015 kwa sasa yanapatikana hapa

link.

Washiriki wa kongamano la Arua katika picha ya pamoja (picha juu)

Page 3: JARIDA - ECHOcommunity...Mafunzo yalilenga kubadilishana na kufanya marudio kati ya watendaji vifaa na mbinu wanazotumia na kwa pamoja kuboresha mbinu zilizopo. Kwa kawaida mafunzo

ECHO A.M NA AgriProFocus IMEWASAIDIA WAFUGAJI WA

NG’OMBE WA MAZIWA Darasa la maswala ya maziwa liliandaliwa kwa pamoja kati ya ECHO na AgriProfocus kwa wakulima 25 tarehe 30 Novemba na 1 Disemba kwenye kituo cha mafunzo ECHO , kuanzisha mkakati wa kuwasaidia wafugaji wa ng’ombe na mbuzi wa maziwa changamoto wanazokutana nazo kuzunguka kituo cha ECHO. Hii imeanzishwa kwa pamoja na AgriProfocus (SNV-Holand) na ECHO Afrika Mashariki.Mafunzo yaliandaliwa kwa ajili ya watendaji na wataalamu ambao wanawafundisha wakulima na watengenezaji katika sekta ya maziwa. Mafunzo yalilenga kubadilishana na kufanya marudio kati ya watendaji vifaa na mbinu wanazotumia na kwa pamoja kuboresha mbinu zilizopo. Kwa kawaida mafunzo ya AgriProfocus yanafanywa kwa ratiba ya siku mbili kwa mada moja husika. Mafunzo haya ya nne, kuhusu ulishaji, afya ya wanyama na uzalishaji, tarehe 30 Novemba hadi 1 Disemba yalifanyika katika kituo cha mafunzo cha ECHO Afrika Mashariki, yakiandaliwa kwa pamoja na Afisa mifugo wa wilaya Bwana. Julius Nangale. Huu ni mfano wa jinsi gani ECHO inaratibu shuguli tofauti tofauti za kupunguza umasikini. Nyingine ilikuwa kuonesha bustani ya mbogamboga na matunda yenye mimea mbalimbali na mbegu. ECHO pia ilionesha mbinu mbadala kama mtambo wake mpya wa biogesi na zana mbalimbali ambazo zinarahisisha shughuli za kilimo kama zana za kukokotwa na wanyama na mashine ya kukata chakula cha wanyama.

David Sharland, akiwasilisha mada katika kongamano la Arua (Picha juu)

RASILIMALI ZA UBUNIFU Kituo cha mafunzo ECHO Afrika Mashariki kinawashauri watu kuja na kujifunza teknolojia mbalimbali za ubunifu ambazo ECHO inahamashisha chini ya mtandao wa kimataifa wa maendeleo ya mradi wa ubunifu (IDIN). ECHO Afrika Mashariki inatoa mafunzo ya kujenga uwezo wa ubunifu (CCB) yanayotolewa ili kufungua vipaji vya ubunifu kutoka kwa wanajamii ambayo yanaweza kutumika kutengeneza zana/ mashine rahisi. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Mratibu wa Ubunifu wa ECHO kwa barua pepe Harold Msanya at: [email protected]

Jesse (mbunifuu) akifanya majaribio ya mchine ya kahawa inayoendeshwa kwa baiskeli (picha juu)

Page 4: JARIDA - ECHOcommunity...Mafunzo yalilenga kubadilishana na kufanya marudio kati ya watendaji vifaa na mbinu wanazotumia na kwa pamoja kuboresha mbinu zilizopo. Kwa kawaida mafunzo

Wakulima wa maziwa kutoka vijiji vya jirani wametembelea wakulima wanne, na wakjadili muundo na vikwazo na wamahiri wa Kidachi kutoka chuo cha Wagenigen na timu ya ECHO (picha juu)

UANZISHWAJI WA MAKINGO UMEANZA KATIKA VIJIJI VYA

ILKUROT NA LENGIJAVE ECHO inakusanya samadi kwa baadhi ya wakulima ili kuanzisha kitalu chake cha miti ambacho kitakuwa kinazalisha maelfu ya miche ya miti kuanzia mwaka huu na kuendelea. Katika safari yake moja ya kuelekea kijiji cha Ilkurot, Mkulima, Lemali Mollel, aliomba msaada kutoka ECHO kwa Venance Mollel jinsi ya kupima makinga maji. Karne mbili zilizopita Mradi wa utunzaji mazingira wa kilimo mseto (SCAPA), uliwapimia wakulima katika kijiji hicho, lakini mbinu hiyo ilipotea. Venance alimfundisha Lemali kutumia mbinu ya ECHO ambayo imetambulika tena ambayo ni rahisi ya kupima maji ambayo wakulima wenyewe wanaweza kutengeneza na kutumia. Kwa kuongezea, Lemali aliwahusisha majirani zake kuweza kumsaidia kuchimba makingo, na walisaidiana kila mmoja kuanzisha.Wiki iliyofuata mvua kubwa ilianza kunyesha Ilkurot na jirani Lengijave, ikafurika mashamba na nyumba zilizoko kando kando ya njia za maji, kwenye baadhi ya mashamba iliweza kufunika na kuondoa udongo wa juu. Wakulima walichanganyikiwa kuona mashamba yao yamejaa maji na udongo wa juu kusombwa. Wakati katibu mkuu wa kijiji, Godson Emmanuel, alipotembelea shamba la Lemali na kuona wakulima wawili wametengeneza makingo ambayo yalikuwa yamejaa maji na hakukuwa na mmomonyoko wa udongo, alisema, “Ngoja

MAFUNZO YA KUJENGA UWEZO WA UBUNIFU

Wasimamizi wa wanafunzi na walimu wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) hivi karibuni walishiriki mafunzo ya kujenga uwezo wa ubunifu ili kuwezesha shughuli zao za kila siku za kuwasimamia wanafunzi katika kubuni miradi yao ya ubunifu. Mafunzo yamewafungulia njia ya kuwaongoza wanafunzi kufanya kazi nzuri ya kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii. Itawasaidia kuzingatia zaidi kubuni teknolojia zinazotatua changamoto zilizopo kwenye jamii, badala ya kufikiri zaidi kuhusu mitihani yao ya mwisho au teknolojia zinazoishiwa kuhifadhiwa. Matumaini ni kwa jamii na siyo kuendelea kuona changamoto zilezile mwaka hadi mwaka.ECHO Afrika Mashariki inafanya kazi pamoja na CAMARTEC na TWENDE ili kuwashawishi wanajamii na wafanyakazi wa maendeleo ambao wanashirikiana moja kwa moja na vyuo na wanafunzi wa vyuo kutoka ndani na nje ya nchi ili waweze kushirikiana ni kwa namna gani bora wanaweza kuisaidia jamii kutatua changamoto kwa kubuni teknolojia ambazo zinakidhi mazingira yao na kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka katika maeneo yao. Wasimamizi wa wanafunzi wa chuo cha ufundi Arusha wakiwa kwenye picha ya pamoja na wakufunzi wa mafunzo ya ubunifu Noela Byabachwezi, Bernard Kiwia na mfanyakazi wa ECHO Sophia Kasubi

ECHO, CAMARTEC na TWENDE kama mashirika washirika chini ya mradi wa IDIN inahamasisha teknolojia mbadala kwa pamoja kwa kuendesha mafunzo ya kujenga uwezo wa ubunifu kwa wanajamii wa Leguruki na vijiji vya jirani. Mafunzo yanalenga kufungua na kuendeleza mawazo ya ubunifu kwa wanajamii wote ili kuwawezesha waweze kutatua changamoto wanazokutana nazo katika shughuli zao za kila siku. Leguruki kuna maparachichi mengi; na moja kati ya changamoto nyingi wanazokutana nazo wanajamii wa huko ni ukosefu wa teknolojia ya kusaga mbegu za parachichi, kuwazuia mbwa wasile maparachichi yanayoanguka chini ya mti, na mbadala wa kufuga nyuki. Baada ya mafunzo ya ubunifu waliweza waliweza kubuni mashine rahisi ya kusaga mbegu ya parachichi na kuwa unga ambao unatumika kama kiungo cha chai kisichokuwa na kafeini.

Page 5: JARIDA - ECHOcommunity...Mafunzo yalilenga kubadilishana na kufanya marudio kati ya watendaji vifaa na mbinu wanazotumia na kwa pamoja kuboresha mbinu zilizopo. Kwa kawaida mafunzo

turudishe kijiji katika hali yake ya nyuma, kuanzisha tena makingo kijijini kote. Tunaweza kutunga sheria ndogondogo kwa watu wote kuzifuata. Maombi yametolewa na wanavijiji wote kuweza kujifunza mbinu rahisi; idadi ya wakulima waliokubaliana kwa hiari kuanzisha making imefikia 49.Ingawaje, ukizingatia nguvu ya viongozi wa kijiji kupambana na mafuriko ya hivi karibuni, maelekezo makubwa yametolewa ambapo kila kaya ambayo haijaanzisha makingo katika shamba lao watalipa faini ya Tsh. 200,000/=. Wiki moja kabla sheria mpya ndogo idadi ya wakulima waliopima na kuanzisha making ilikuwa 13. Kutokana na matokeo ya maelekezo ya viongozi wa kijiji idadi inaendelea kuongezeka. Katika picha hapo chini ikimuonesha mkulima wa kwanza wa kijiji cha Lengijave wakiangalia uharibibu uliofanywa na mvua za hivi karibuni, na kushirikisha mafunzo haya na mbinu mpya. Kama ambavyo ECHO ina kawaida ya kuyawezesha mashirika wazawa, imeendelea kuwezesha asasi ya kijamiii, RUCONET kufanya kazi pamoja kuwafundisha wakulima wengi zaidi kupata uelewa wa kupima makingo, na kupata mimea ya kupanda katika mifereji. Wakulima sasa wako tayari kujaribu njia mbalimbali za kupima na kuanzisha makingo.

Venance Mollel, Mkufunzi wa ECHO akimsaidia mwanajamii kuanzisha makingo katika kijiji cha Ilkurot.

KILIMO HIFADHI NA MBINU NYINGINE

Kikundi kilichokuwa kinatengeneza mashine ya kusaga mbegu ya parachichi wakiwasililisha mfano wa mashine yao ya kwanza wakati wa mafunzo ya ubunifu huko Leguruki.

HABARI ZA ECHO AFRIKA MASHARIKI

Kituo cha ECHO cha kanda kinashirikisha maelezo na rasilimali zinazohusu kilimo endelevu, mbinu mbadala kuzunguka kanda yote. Wajitolea wa ECHO, wanafunzi kwa vitendo na washauri wanafanya kazi kufikia malengo yake ya kushirikisha rasilimali na kutoa faida ya kujuana na fursa.

HIFADHI YA MBEGU ECHO AFRIKA MASHARIKI Hifadhi ya mbegu/ Shughuli za mbegu: Hifadhi ya mbegu ECHO Afrika Mashariki imeanza kukusanya na kutambulisha mbegu za miti ya asili / miti ya kigeni na kuzalisha miche katika kitalu cha miche ya miti. Miche sasa inapatikana katika kitalu cha miti ECHO kwa ajili ya kupanda.Wakulima/Wafanyakazi wa maendeleo/ Mashirika ya kijamii yanayopendelea kupanda miti tafadhali wafike kuchukua miche au mbegu kama pakiti ndogondogo tayari zimetengenezwa na hifadhi ya mbegu ECHO na miche inapatikana katika bustani ya miti. Pakiti ndogondogo za mbegu zinatengenezwa kwa ajili ya washirika wa ECHO kwa ajili ya kugawa bure.Kuna aina mbalimbali za miche ya miti ambayo ECHO inauza kwa bei rahisi. ECHO kila wakati inawakaribisha watu waje wajipatie mbegu za miti ya asili/kigeni ili waweze wakapande kwenye maeneo yao.Tafadhali kumbuka kuwa unapopanda mti; unatunza mazingira na unaacha urithi mzuri kwa wajukuu zako!!!!!!! Hhhh hhhh hhh

Page 6: JARIDA - ECHOcommunity...Mafunzo yalilenga kubadilishana na kufanya marudio kati ya watendaji vifaa na mbinu wanazotumia na kwa pamoja kuboresha mbinu zilizopo. Kwa kawaida mafunzo

ECHO Afrika Mashariki inaheshimu sehemu ya kilimo hifadhi kadiri inavyoendelea kutekeleza katika eneo la bustani ya maonesho kwa kulima aina mbalimbali za mazao funika kwa kulima lenyewe au kuchanganya na mazao mengine chini ya mfumo wa matandazo ili kuwezesha udongo kuwa na unyevu na kuboresha rutuba ya udongo. ECHO A.M inawashauri watu kuja na kujifunza mbinu bora za kilimo hifadhi katika maeneo yao ukizingatia kuwa kuna kesi mbalimbali za uharibifu wa ardhi kuzunguka kanda hii. Wakulima wengi kuzunguka kituo cha mafunzo cha ECHO wanakuja na kutafuta ushauri ni kwa jinsi gani wanaweza kuboresha ardhi yao iliyoharibika. Zaidi ya hayo ECHO A. M inaonesha shughuli zake kwa kuwa na bustani za maonesho kwa kuonesha mbinu mbalimbali ikiwemo upandaji wa miti ya malisho, uzalishaji wa mbogamboga, mbinu za upandaji migomba, upandaji wa mbogamboga za kudumu zenye kiwango kikubwa cha protini ikiwemo majani ya mihogo (kisamvu) mlonge, Chaya na viazi vitamu, utengaji wa mfumo wa mimea mbalimbali ambayo inaweza kuchanganyikana na mengineyo. Unakaribishwa kutembelea na kujifunza mbinu bora za kilimo hifadhi!!!!!!

Makingo yaliyooteshwa majani ya malisho, miti pampja mimea jamii ya mikunde .Contours with intercropped fodder.

Picha juu ikionesha kitalu cha miti ya asili katika bustani ya miti.

UMOJA WA IDDS Umoja wa IDDS ni wa wabunifu wazawa lililoanzishwa kwa lengo la kukutana na kushirikishana mafanikio na changamoto wanazokutana nazo wanapooendeleza ubunifu wao. Pamoja na mambo mengine wanapata nafasi ya kujifunza teknolojia nyingine pia. Miezi miwili iliyopita wanachama wa umoja wa IDDS walishiriki katika tukio la kujifunza kwa siku mbili kuhusiana na teknolojia ya biogesi. Teknolojia ya biogesi inatambulika kama njia bora ya kuhakikisha usafi wa kudhibiti uchafu wa wanyama kwa sababu ya faida nyingi zinazotokana nayo ikiwemo nguvu ya kupikia na uzalishaji wa mboji. Washirika walipata nafasi ya kujionea aina tofautitofauti za mitambo ya biogesi ikiwemo mtambo unaotumia kinyesi cha wanyama na binadamu iliyobuniwa kwa ajili ya maeneo makavu kiasi, na chaguzi rahisi kwa ajili ya biogesi ya karatasi ya plastiki iliyobuniwa na ECHO mwezi Octoba, 2015.

Wanachama wa umoja wa IDDS katika picha ya pamoja wakati wa mafunzo ya biogesi yaliyofanyika CAMARTEC

Page 7: JARIDA - ECHOcommunity...Mafunzo yalilenga kubadilishana na kufanya marudio kati ya watendaji vifaa na mbinu wanazotumia na kwa pamoja kuboresha mbinu zilizopo. Kwa kawaida mafunzo

Wanachama wa umoja wa IDDS walipotembelea CAMARTEC na ECHO kujionea aina mbalimbali za mitambo ya biogesi ikiwemo mtambo wa kujengea wa CAMARTEC na mtambo wa karatasi ngumu ya plastiki ya ECHO.

MRADI WA PAMOJA-KOTIDO, KARAMOJA, UGANDA Mshauri wa mambo ya kiufundi wa ECHO wa mradi wa pamoja huko Kotido, Karamoja Uganda ameripoti kuhusiana na chanjo ya tatu ya ndigana baridi iliyofanyika katika vijiji 8 vya Kaunti ya Kacheri, Kotido Karamoja kuanzia 10-15 Novemba, 2015. Wakati wa kampeni ndama 760 walichanjwa, wakapata dawa ya minyoo na kuvikwa pete. Wanawake kadhaa walihusika wakati wa chanjo, watu walioshiriki kutoka wilayani kusherehekea tukio hilo, ambalo lilikuwa na umuhimu kwa wote waliohudhuria, wakiwemo wanawake na wachungaji. Kushindwa kwa mazao mengi kote mkoani. Siku moja wakati wa kutoa chanjo ya ndigana baridi, watu waliondoka ili kwenda kujipatia chakula cha msaada kutoka WFP kilichotolewa na kijiji. Ushuhuda kwa wanaofuga ng’ombe kuhusu ubora wa chanjo ulitolewa jioni wakati wa kuangalia video na uhamasishaji; ndama waliochanjwa katika kampeni iliyopita ni wakubwa kuliko wengine wa umri wao, na wanaendelea vizuri kwa ujumla.

Picha juu watu wakikusanyika katika chanjo ya tatu huko, Kotido, Karamoja

Page 8: JARIDA - ECHOcommunity...Mafunzo yalilenga kubadilishana na kufanya marudio kati ya watendaji vifaa na mbinu wanazotumia na kwa pamoja kuboresha mbinu zilizopo. Kwa kawaida mafunzo

Imehaririwa na : Erwin Kinsey Charles (Bonny) Bonaventure, Sophia Kasubi na Rose Dusabeyezu

Wanaume na wanawake wakikusanyika kwa ajili ya chanjo ya 3 huko Kotido, Karamoja, (picha juu)

Unahitaji kushauriwa? (Kwa malipo au bure): Kituo cha kanda cha ECHO kinatoa fursa kwa washirika wengine kupata ushauri bure au kwa malipo kulingana na asili ya hitaji lako. Njoo utembelee!! -Wanafunzi wa club ya Roots & Shoots wameendelea na ratiba yao ya kawaida ya kutembelea ECHO Afrika Mashariki kwa madhumuni ya kujifunza . Hivi sasa ECHO inafanya maandalizi ya matembezi ya mwanzilishi wa Roots & Shoots, Dr. Jane Goodall katikati ya mwezi wa Pili, 2016! -Kituo cha ECHO kinapokea makundi ya watu, washirika wa mashirika ya kijamii na mtu mmoja wanaotaraji kupata ushauri kulingana na mahitaji yao. Robert Shimaingo kutoka Zambia amewasiliana na ECHO kuja kujifunza shughuli zake na kuweza kupeleka mbinu mbadala na mbinu bora kwa matumizi katika nchi yake.

Robert kwenye picha juu wakati alipotembelea mmoja kati wa majirani wa ECHO huko kijiji cha Ilkurot.