28
Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria (nola) Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 1

Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

  • Upload
    others

  • View
    22

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria (nola)

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 1

Page 2: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 2

Page 3: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

National Organisation for Legal Assistance (nola)P.O.Box 10096, Dar es Salaam -TanzaniaEmail: [email protected]: www.msaadawasheria.or.tz

c National Organisation for Legal Assistance (nola)

ISBN 9987 - 482 - 13 - 9

Kimehaririwa na : Mhe. Robert MakarambaKamishna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Michoro na Usanifu wa kurasa: Tibasima Arts Investments Ltd

Sheria za Urithi na Wosia

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 3

Page 4: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

ii Sheria za URITHI na WOSIA

DIBAJI

Sheria ni kanuni zinazoongoza shughuli na mahusiano ya watu waishio katika jamiifulani. Sheria inaelezea haki na wajibu wa wanajamii hao, inaweka masharti juu yamambo fulani, kuelezea makosa na adhabu iwapo makosa ama masharti yaliyotajwana sheria yatakiukwa. Sheria hazitungwi kwa ajili ya mtu mmoja mmoja, bali ni kwajamii nzima. Sheria lazima iwe na nguvu ya kutekelezeka, isibague watu wa tabakaama hali fulani na wengine, ijali maslahi ya wanajamii wote kwa ujumla wao, isiwena utata katika maana ama taathira yake, isitaje adhabu ama madhara kwa makosayaliyotendeka kabla haijatungwa, n.k.

Sheria lazima zieleweke kwa wahusika wote. Ni msingi kwa wanajamii kuzielewavema sheria za nchi yao, ili waepuke kuzivunja, lakini pia waweze kutambua palehaki zao zinapovunjwa, ili wawe na uwezo wa kudai haki hizo kwenye vyombovinavyosimamia haki, kama vile Mahakama.

Kwa hivi sasa sheria nyingi zinatungwa katika lugha ya Kiingereza, tena isiyo rahisikueleweka, hata kwa wale wanaoifahamu lugha hii. Hivyo ni dhahiri kuwawananchi walio wengi hawana uwezo wa kuzielewa sheria hizi na hivyo zinabakikuwa ni za matumizi kwa wanasheria na wasimamizi wa sheria tu. Pamoja naugumu wa lugha ya sheria, ni dhahiri kuwa watu wengi hasa waishio vijijini hawanauwezo wa kupata nakala za sheria hizi. Hii ni changamoto kubwa kwetu sote.

Vitini hivi vimeandaliwa kwa ajili ya kuwasaidia wanajamii, hasa waishio vijijini,kupata elimu juu ya sheria mbalimbali, ikiwemo miongozo, haki na wajibu, nataratibu mbalimbali za kisheria. Vitini hivi si mbadala wa sheria, bali ni vionjo tu vyasheria hizi katika lugha rafiki, inayoeleweka kwa wananchi walio wengi.

Tunatoa shukrani za pekee kwa wote walioshiriki kuandaa vitini hivi, wakiwemowaandishi, Kaleb Lameck Gamaya <Sheria ya Ardhi>, Charles Mutakyahwa Nkonya<Sheria za Urithi na Wosia>, Dotto Justo <Sheria ya Makosa ya Jinai na Mwenendo Wake>,Noel Kaganda <Sheria ya Ndoa na Mahusiano ya Familia>, Augustino Kusalika <Sheriaya Mikataba> na mimi Clement Mashamba <Taratibu za Kuendesha Mashauri ya MadaiMahakamani>. Zaidi ya hawa tunatoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Robert V.Makaramba, Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora, aliye hariri vitinihivi. Pia kwa wafanyakazi wote wa nola, kwa mchango wao katika uandaaji wavitini. Mwisho kabisa kwa wafadhili wetu, DANIDA, The Foundation for CivilSociety, Norwegian Peoples Aid, na UNHCR ambao mchango wao umefanikishakukamilika kwa awamu hii ya uchapishaji wa vitini. Kwa wote tunasema asantesana.

Clement Mashamba (Wakili)Mkurugenzi MtendajiShrikika la Kitaifa la Msaada wa Sheria

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 4

Page 5: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

1Sheria za URITHI na WOSIA

SEHEMU YA KWANZA

MIRATHI

Utangulizi

Kitini kinajadili sheria za urithi na wosia (mirathi) na kimegawanyika katikasehemu kuu tatu. Sehemu ya Kwanza inafafanua maana na aina za mirathi,maana, sifa na namna ya kuandika wosia; na Sehemu ya Pili inajadilitaratibu za kufungua mahakamani maombi ya kusimamia au kutekelezamirathi ya marehemu na Sehemu ya Tatu inajadili taratibu za namna yakuomba kusimamia mirathi.

Madhumuni makubwa ya hiki Kitini ni kuielewesha jamii kuhusu haki nawajibu katika kusimamia mirathi ili kuepukana na migogoro ya wanandugubaada ya kifo cha marehemu.

MIRATHI

Mirathi ni mali aliyoacha marehemu kwa ajili ya kurithishwa warithi wakehalali. Sheria imeweka taratibu maalum zinazoongoza ukusanyaji,uangalizi, usimamizi, ugawaji na umiliki wa mali za marehemu pamoja, nakulipa madeni aliyoacha marehemu wakati wa uhai wake au gharamazitokanazo na mazishi yake.

Sheria zinazohusu urithi nawosia (mirathi) hapa Tanzaniazimegawanyika katika sheria zamila, sheria za kidini na sheria zaserikali.

Sheria za Kimila

¨Tangazo la Sheria za Mila[The Local Customary (Declaration)(No.4) Order 1963, G.N.436/1963],Kiambatisho cha Pili – Sheriaza Urithi na Kiambatisho chatatu – Sheria za Wosia

Sheria za Kidini• Sheria ya Ndoa, Talaka na Urithi ya Waasia wasio Wakristu (The

Succession (Non Christian Asiatic) Ordinance, 1923,

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 5

Page 6: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

2 Sheria za URITHI na WOSIA

• Sheria ya Kiislamu ya Mirathi

Sheria za Kiserikali• Sheria ya Urithi ya India ya mwaka 1865 (The Indian Succession Act)• Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971

Utaratibu wa kukusanya, kutunza kugawa na kurithisha mali ya marehemuunasimamiwa na kuongozwa na sheria zifuatazo:

• Sheria ya Mirathi na Usimamizi wa Mali za Marehemu• Sheria ya Mahakama za Mahakimu ya mwaka 1985, Jedwali la Tano• Sheria ya Kabidhi Wasii Mkuu [Administrator General (Powers and

Functions) Act]• Sheria ya Usimamizi wa Mali za Thamani Ndogo, Sura ya 30 [The

Administration (Small Estates) Ordinance]

AINA ZA MIRATHI

Kuna aina kuu mbili za mirathi:

• Mirathi palipo na wosia

Mirathi ya aina hii inahusika ikiwa marehemu ameacha wosia, yaani tamkola maandishi au maneno yanayoweza kuthibitishwa na mashahidi, kwambaanataka mali, madeni yake yakusanywe, kutunzwa na hatimayekurithishwa na/au kumilikishwa kwa nani na/au kwa namna gani.Kwenye huo wosia marehemu pia hutaja ni nani angependa awe msimamiziwa mali na/au madeni yake ikiwa ni pamoja na kuyakusanya na kuyatunzahadi hapo mali au kulipa madeni hayo yatakapomilikishwa.

Endapo marehemu ameacha wosia na katika wosia huo amemtaja mtuatakayesimamia ukusanyaji wa mali na madeni na mgawanyo wa malina/au malipo ya madeni ya marehemu, mtu huyo hupeleka maombi yakemahakamani na mahakama ikiridhia humthibitisha kuwa mtekelezaji wawosia.

• Mirathi pasipo na wosia

Pale ambapo marehemu hakuacha wosia kwa maandishi au tamko juu yamgawanyo wa mali zake, warithi halali wa marehemu hulazimikakupendekeza kupitia kikao cha wana ukoo, mtu mmoja au zaidi kisha mtuau hao watu hupeleka maombi yao mahakamani na mahakama ikiridhiabasi itawateua kuwa wasimamizi wa mirathi.

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 6

Page 7: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

3Sheria za URITHI na WOSIA

SHERIA ZINAZOSIMAMIA MGAWANYO WA MALI YAMAREHEMU

Mgawanyo wa mali ya marehemu pale ambapo kuna wosia hufanywa kwakuzingatia huo wosia. Ugumu hujitokeza pale pasipo na wosia, ambapougawaji wa mali hutegemeana na sheria mbalimbali na wahusika. HapaTanzania sheria kadhaa zinazohusu ugawaji wa mali au urithishwaji wamali ya marehemu ambazo zinajadiliwa kwa kifupi katika sehemuinayofuata.

• Sheria ya Urithi ya India ya mwaka 1865

Sheria hii ilianza kutumika nchini India tangu mwaka 1865 lakini ililetwaTanzania (wakati huo Tanganyika), na Serikali ya Wakoloni waKiingereza. Sheria hii inaongoza na kusimamia mgawanyo wa mali zamarehemu pale ambapo itaonekana kwamba marehemu alikuwa hafuatiSheria za Kiislam wala Sheria za Kimila.

Kulingana na sheria hii, kamamarehemu ameacha mjane na watoto,

mjane atapata 1/3 na watoto 2/3 yamali yote ya marehemu. Lakini

kama marehemu hakuachawatoto, basi mjane atapata ½na ½ ya mali na nyingineinayobaki hugawanywa

sawasawa kati ya wazazi, kaka, nadada za marehemu.

Zingatio: Kwa mujibu wa sheria hii watoto wa nje ya ndoa hawana haki ya kurithiisipokuwa tu kama kuna wosia na katika wosia huo wawe wamerithishwa mali.

• Sheria ya Kimila

Ikibainika na kuiridhisha mahakama kwamba wakati wa uhai wakemarehemu aliishi kwa kufuata mila na desturi za kabila lake, basi mirathiitafuata sheria za mila za hilo kabila. Hapa Tanzaia yapo takribanimakabila yapatayo 120 hivi, ambayo kila moja linazo mila zake, hatahivyo kwa vile mengi ya makabila hayo ni ya Kibantu, nyingi ya hizomila hazipishani sana, ingawa zinaweza zikawepo tofauti ndogondogobaina ya kabila na kabila. Sehemu kubwa ya makabila hapa Tanzania

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 7

Page 8: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

4 Sheria za URITHI na WOSIA

yanafuata taratibu zamirathi za upande wakuumeni na baadhiupande wa ujombani.

Mwaka 1963 Serikali yaTanzania (wakati huoTanganyika), ilitoa tamko lakuzitambua Sheria za Milaza Ulinzi, Urithi na Wosia(Tangazo la Serikali Na.436/1963), zinazohusukanuni za urithi na wosia zawatu wa makabila yaTanzania Bara yanayofuatataratibu za urithi kwaupande wa kuumeni. Tamkohili licha ya kuweka bayanakanuni za urithi na wosia zamakabila hayo ziliweka piakanuni za kimila za ulinzi wa watoto waliofiwa na baba wakati wadogo,mrithi ambaye hayupo wakati wa kurithi na mke na watoto wa mtuanayekwenda safari ndefu.

Kulingana na Kanuni za Urithi za Kimila zilizotamkwa katika Tamko laSerikali Na. 436 la mwaka 1963, ambapo urithi hufuata upande wa ukoo wakiume, mgawanyo wa mali ya marehemu unakuwa kama ifuatavyo:

• Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya babayao

• Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake zitarithiwa na baba,mama, kaka, dada, wajomba na shangazi zake.

• Mtoto wa kiume wa nyumba kubwa hupata sehemu kubwa ya maliakifuatiwa na watoto wengine wa kiume, na mwisho watoto wakike wa nyumba yeyote ile hupata kiasi kidogo zaidi.

• Ijapokuwa kwa mujibu wa Sheria ya Kimila wajane hawajapewahaki ya kurithi, mjane mwenye watoto anayo haki ya kuishi nakutegemea watoto wake ambao watarithi mali ya marehemumumewe, yaani baba yao hao watoto.

• Mjane ambaye hana mtoto/watoto atabakia kwenye nyumba yamarehemu na kuitumia wakati wa uhai wake, na baada ya kifochake nyumba hiyo itagawiwa warithi halali wa marehemumumewe.

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 8

Page 9: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

5Sheria za URITHI na WOSIA

Zingatio: Watoto wa nje ya ndoa hawaruhusiwi kurithi chochote isipokuwa kamawalihalalisha kufuatana na mila za kabila husika. Mali ya marehemu inahusishamali yake binafsi na siyo vinginevyo.

• Sheria ya Kiislamu

Sheria ya Kiislamu ya Mirathi ni kama ilivyoanishwa katika vifungumabalimbali vya Kuruani Tukufu na kufafanuliwa katika makalambalimbali za wanazuoni wa Kiislamu. Hapa Tanzania Bara, Sheria yaKiislamu ya mirathi imeanishwa katika Tamko la Sheria za Kiislamu lamwaka 1967 (The Statements of Islamic Law, GN 222 of 1967). Tamko hilipamoja na kwamba halijawahi kutumika rasmi, ni mwongozo mzuri wahizo sheria.

Kama mirathi yeyote ile, mgawanyo wa mali ya marehemu kwa mujibuwa Sheria ya Kiislamu, huzingatia mambo muhimu matatu yafuatayo,kwamba:

(i) Mwenye mali awe alishakufa (maut al–muwarith)(ii) Pawepo na warithi halali wa marehemu (hayat al-warith), yaani

watoto wa marehemu ndugu wengine wa marehemu. Warithihawa ni lazima wawepo na wawe ni warithi hakikawanaotambulika kisheria wakati wa mauti ya marehemu

(iii) Marehemu ameacha mali (al- tarikah I al–mauruth)(iv) Urithi utokane na mali mali halisi na halali za marehemu na sio

nje ya hizo.Kabla ya mirathi lazima matatizo yafuatayo yawe yametatuliwakwanza: - Madeni yanayokabili mali za marehemu- Gharama za Mazishi- Utatuzi wa madeni mengine- Wosia uwe umefuatiwa- Warithi halali

Kulingana na mafundisho ya dini ya Kiislamu, wanazuoni wote kwa ujumlawanaafiki kuwepo kwa makundi yafuatayo kuwa ndio warithi halali kwamujibu wa dini ya Kiislamu:

(a) As’hab Al – Furud: Hili ni kundi la watu wanaopata urithi waokufuatana na muainisho wa bayana uliotolewa ndani ya KuruaniTukufu. Hawa kwa kawaida wapo kumi na mbili (12). Kati yao, wawili (2) hupatikana kwa njia ya mahusiano yakinyumba yaani mke na mume, wengine hutokana na undugu wadamu na uhusiano wa ukaribu kidugu, yaani jamaa.

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 9

Page 10: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

6 Sheria za URITHI na WOSIA

Kwa ujumla wao, ni kama ifuatavyo: (i) Mume, (ii) Mke, (iii) Mtotowa kiume, (iv) Mtoto wa kike, (v) Mama, (vi) Dada, (vii) Kaka, (viii)Mpwa, (ix) Dada wa kambo, (x) Kaka wa kambo, (xi) Babu mzaababa

(b) Asabah: Hawa ni wale wenye kupata urithi kutokana na albaki yamali yote baada ya wale warithi waliobainishwa kwenye Qur’ankupata sehemu yao.

(c) Hazina ya Umma: Kwa mujibu ya wanazuoni wa Kiislamu, kunamgawanyiko wa mawazo katika kuthibitisha uhalali wakuchukuliwa sehemu ya mali ya marehemu na kutolewa kamahazina ya umma. Mfano kundi linaloongozwa na Iman Hanafi naHanbal, wanapinga mali za marehemu kupelekwa katika hazinakusaidia jamii. Lakini wale wenye mtazamo wa mawazo kama yaMalik na Shafii wanaafiki suala la mali ya marehemu kuchukuliwana kurithishwa kwenye hazina ya jamii.

Mali za namna hii huwa ni mali ya jamii nzima na huwa chini yamsimamizi wake mkuu aliyechaguliwa na jamii yenyewe. Mfanokatika serikali ya mapinduzi Zanzibar, mali zitolewazo kama BaitulMal (haziina ya umma), zimewekwa chini ya uangalizi waKamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana.

(d) Dhawl – Arham: hili ni lile kundi la wale ndugu wasiotokana nadamu ya marehemu moja kwa moja.

ZINGATIO:

(i) Izingatiwe kwamba mgawanyo wa mali kwa mujibu wa dini ya Kiislamu,hufuata matabaka kama yalivyobainishwa hapo juu.

(ii) Kulingana na Sheria ya Kabidhi Wasii Mkuu, endapo mtu atakufa bila kuwa namrithi, au kwamba mali yake inaweza kupotea, basi hiyo mali itawekwa chini yaKabithi Wasii Mkuu, na endapo utapita muda wa miaka kumi na mbili (12) bilamtu yeyote kudai kitu chochote kuhusu mirathi hiyo, basi Kabidhi Wasii Mkuuataihamishia mali hiyo Serikalini.

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 10

Page 11: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

7Sheria za URITHI na WOSIA

SEHEMU YA PILI

WOSIA

Utangulizi

Kutokana na ukweli kwamba mwanadamu hapa duniani ni kiumbe wakupita tu na kwamba mara nyingi kifo hutokea kwa kushtukiza, ni vyemamwanadamu akajitayarisha kwa kuusia mali yake, ili pindi kifokikimchukua, mali hiyo igawiwe kadri muusia alivyotaka na hivyokuwaondolea warithi migogoro isiyokuwa ya lazima. Njia pekee na nzuri yakuusia mali ni kwa kuacha wosia.

Mara nyingi familia nyingi zimejikuta zikiingia kwenye mogogoro juu yamali aliyoiacha marehemu mara baada ya kifo chake, pengine hatakupelekea kuwepo na uhasama na hatimaye kuharibu hata uhusiano kati yawanandugu. Mara nyingi watoto na mjane au wajane ndio huathirika zaidinah ii migogoro ya mirathi.

Maana ya Wosia

Wosia ni kauli inayotolewa na mtu wakati wa uhai wake kwa hiari yakekuonyesha nia yake jinsi gani angependa mali yake igawanywe baada yakufa kwake.

Aina na sifa za wosia

Wosia unaweza kuwa wa namna mbili; wosia wa mdomo na wosia waulioandikwa (wa maandishi).

Wosia wa maandishi lazima:• Uandikwe kwa kalamu ya wino na sio kalamu ya risasi (inayoweza

kufutwa futwa),• Muusia awe na akili timau• Utaje tarehe ulipoandikwa• Utaje kuwa muusia anayo akili timamu na anausia kwa hiari yake

mwenyewe,• Ushuhudiwe na mashahidi wanaojua kusoma na kuandika angalau

wawili (mmoja wa ukoo na mwingine mtu baki), kama muusia anajuakusoma na kuandika,

• Ushuhudiwe na mashahidi wasiopungua wane (wawili wa ukoo nawawili watu baki), kama muusia hajui kusoma na kuandika,

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 11

Page 12: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

8 Sheria za URITHI na WOSIA

• Wanaotarajia kuithi hawaruhusiwi kushuhudia wosia huo,• Usainiwe na muusia mbele ya mashahidi wake wakiona, kutia sahihi

yake au kama hajui kusoma, aweke alama ya dole gumba la kulia,• Utiwe sahihi za mashahidi,• Mashahidi wawe wamechaguliwa na muusia mwenyewe.

Katika shauri la Abdul Sadiki dhidi ya Wilfred Rutakunikwa, (1988)Mahakama Kuu ya Tanzania ilitamka kuwa kama muusia hajui kusomawala kuandika, wosia huo, kulingana na kanuni ya 19 na 21 ya LocalCustomary Law (Declaration) Order, Nambari 4 ya 1963, lazimaushuhudiwe na wanaukoo angalau wanne.

Kumbuka: Kadiri ya Jedwali la Tatu la Sheria ya Usimamizi wa Haki naMatumizi ya Sheria mbali mbali, Sura ya 358, wosia wa maandishiwaweza kubadilishwa kwa wosia mwingine wa maandishi unaotajakubadilisha wosia wa kwanza na unaofuata hatua zile zile kamailivyoainishwa hapo juu.Wosia wa mdomo lazima:• Ushuhudiwe na mashahidi wanne (wawili wa ukoo na wawili watu

baki),• Muusia awe na akili timamu• Kama mashahidi watakufa kabla ya muusia kufa, basi wosia

hautakubalika na urithi utagawanywa kadri ya mpango wa urithi usiowa wosia. Mwenyewe kama anataka kuusia mali zake, atoe wosiampya,

• Mashahidi wawe wamechaguliwa na muusia mwenyewe.

Katika shauri la John Ngomoi dhidi ya Mohamed Ally Bofu, (1988)Mahakama Kuu ya Tanzania ilitamka kuwa lengo la sharti kwambaangalau nusu ya mashahidi wa wosia wa marehemu lazima wawewanandugu, ni kulinda usalama wa mali za marehemu dhidi yaudanganyifu, kwani wosia uliozungukwa na mazingira ya udanganyifu nibatili.

Kumbuka: Kwamba Jedwali la Tatu la Sheria ya Usimamizi wa Haki naMatumizi ya Sheria mbali mbali Sura ya 358, inaweka bayana kwambakuandikisha wosia sio lazima, bali ni hiari ya muusia. Hata hivyo,kuandikisha wosia sio sababu ya kukubaliwa kama masharti yalioelezwahapo juu hayakutimizwa.

Ikumbukwe pia kwamba wosia wa mdomo hauwezi kufuta au kubadilishawosia wa maandishi, lakini wosia wa maandishi waweza kufuta aukubadilisha wosia wa mdomo ikiwa mashaidi walio hai bado wa wosiawa mdomo wataudhuria.

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 12

Page 13: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

9Sheria za URITHI na WOSIA

Kubatilishwa Wosia

Wosia waweza kubatilishwa ikiwa itathibitika kwamba muusiaamepungukiwa akili kwa sababu ya wazimu, ugonjwa, ulevi au hasira yagafla. Ni muhimu kukumbuka kwamba ni wahusika tu (warithi),wanaoruhusiwa kupinga wosia kwa sababu zilizotajwa hapo juu,

Jinsi ya Kurithisha Wosia

Kulingana na Sheria ya Usimamizi wa Haki na Matumizi ya Sheria mbalimbali, Sura ya 358, muusia anaweza kuusia mali yake yote bila kutaja kilakitu alichonacho wakati wa kufa kwake. Ikiwa muusia anapenda kuusiasehemu tu ya mali yake, basi sehemu iliyobaki itagawanywa kulingana namasharti ya urithi usio na wosia.

Mrithi Kunyimwa Urithi na Muusia

Kulingana na Sheria ya Usimamizi wa Haki na Matumizi ya Sheria mbalimbali, Sura ya 358, muusia anaweza kumnyima mrithi urithi wake ikiwamritihi:

• Amezini na mke wamtoa urithi,

• Amejaribu kumuua,amemshambulia, auamemdhuru vibayamtoa urithi au mamamzazi wa mrithi,

• Bila sababu ya haki,hakumtunza mtoawosia kutokana na njaana ugonjwa,

• Ameharibu mali yamuusia, uharibifu wakeutahesabika katikakukadiria kiwango chaurithi atakaostahilikupata.

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 13

Page 14: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

10 Sheria za URITHI na WOSIA

Kulingana na Sheria ya Kusimamia Mirathi ya Mali Ndogondogo, Sura ya30, dini sio sababu ya kumnyima mrithi urithi. Ikumbukwe kwamba muusiaakimnyima mrithi urithi wake, lazima ampe nafasi ya kujitetea mbele yakeau Baraza la Ukoo, na lazima atoe sababu za kumnyima urithi.

Lakini mrithi baada ya kujua amenyimwa urithi akikaa kimya bila yakujitetea mbele ya mtoa urithi au Baraza la Ukoo, hawezi tena baadayekupinga huo wosia. Kama mrithi hakuwa na habari za kunyimwa kwakeurithi, atatoa malalamiko yake kwenye Baraza la Ukoo ambao watamsikilizana wanao uwezo wa kukubali au kukataa. Ikibainika kwamba muusiaalimnyima mrithi urithi kimakosa, wosia utabadilishwa na urithiutagawanywa kulingana na urithi usio na wosia.

Lazima izingatiwe kwamba, kama si kwa sababu tulizozitaja hapo juu,mirathi ya marehemu, kwa marehemu aliyeacha wosia, lazima isimamiwekadiri ya matakwa ya marehemu yanavyobainisha. Katika shauri la JuliusPero dhidi ya Cosmas Raphael, (1983) Mahakama Kuu ya Tanzaniailitamka kuwa shauku ya muusia kama inavyobainika katika wosia,lazima ifuatwe.

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 14

Page 15: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

11Sheria za URITHI na WOSIA

SEHEMU YA TATU

TARATIBU ZA KUOMBA MIRATHIMAHAKAMANI

MIRATHI YENYE WOSIA

Ndani ya siku thelathini (30) tangu kufariki marehemu, wahusikawanapaswa kusajili kifo cha marehemu kwenye Ofisi ya Vizazi na Vifoambayo iko kwa Mkuu wa Wilaya katika kila Wilaya Tanzania Bara. Kamawahusika watachelewa kusajili kifo ndani ya hizo siku (30), basi wanapaswakufika Ofisi hiyo ya vizazi na vifo kwa maelezo.

Kifo kinasajiliwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambako kifo hichokilitokea na sio katika wilaya yeyote ile. Kama kuna matatizo kuhusu wapikifo kisajiliwe, wahusika wanaweza kuwasiliana na Msajili Mkuu wa Vizazina Vifo, Makao Makuu, Dar es Salaam.

Mara baada ya usajili wa kifo cha marehemu waombaji wanawezakufungua maombi ya mirathi mahakamani. Maombi hayo huambatanishwana nakala ya:• Wosia alioacha marehemu• Cheti cha kifo cha marehemu

Mhusika anaweza kufungua maombi ya mirathi katika Mahakama yaMwanzo, Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Hakimu Mkazi naMahakama Kuu, kufuatana na thamani ya mali, mahali mali ya marehemuilipo, au mahali ambapo marehemu kabla ya kifo chake alifanya makaziyake ya kudumu.

Baada ya kuwasilisha maombi ya mirathi, mahakama kwa kawaida hujazafomu za “Taarifa ya Kawaida” kulingana na mahakama ambako mirathihiyo ilifunguliwa.

• Kama mirathi imefunguliwa katika mahakama za chini yaMahakama Kuu, tangazo hilo hutolewa katika gazeti la kawaidalinalosomwa na watu wengi, au katika mbao za mahakama namirathi hutolewa baada ya siku thelathini tangu tangazo kutolewa.

• Kama mirathi imefunguliwa katika Mahakama Kuu, tangazo hilohutolewa katika magazeti la serikali, na mirathi hutolewa baada yasiku tisini (90) tangu tangazo kutolewa.

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 15

Page 16: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

12 Sheria za URITHI na WOSIA

Lengo la tangazo hilo nikuwawezesha walewasioridhika na usimamizi huokupeleka pingamizimahakamani na kumzuia mtuhuyo asipewe usimamizi wamirathi au asiteuliwe kuwamtekelezaji wa mirathi hiyo.Mahakama hata hivyo inauwezo wa kufupisha kipindihiki cha tangazo la siku 30 au90, kwa kutoa tangazo la mudamfupi zaidi.

Baada la siku 90 kumalizika aumuda mfupi zaidi uliowekwana mahakama bila pingamizikutolewa, mahakamaitamthibitisha muombaji kuwa mtekelezaji wa wosia wa marehemu.Endapo mwombaji ni mtekelezaji tu wa wosia wa marehemu atalazimikakutekeleza, na/au kuendeleza taratibu za kugawa mali za marehemu kamaifuatavyo:-

• Kukusanya mali na madeni ya marehemu na pia kutambua anaowadaina/ au wanaomdai

• Kutayarisha taarifa ya awali ya maelezo / ufafanuzi wa mali zote namadeni ya marehemu (inventory), na kuiwakilisha mahakamani katikakipindi cha miezi sita tangu kuthibitishwa kwake na mahakama. Hatahivyo mahakama inaweza kurefusha muda huo kadri itakavyoona infaa.

• Msimamizi/mtekelezaji wa wosia atagawa mali kwa mujibu wa wosia.

• Kutoa taarifa ndani ya miezi 6 ya ukamilishwaji wa zoezi la ugawaji wamali za marehemu mahakamani na mahakama kujiridhisha kama zoezihilo limeendeshwa sawa. Hata hivyo mahakama inaweza kurefushamuda huo kadri itakavyoona infaa.

• Mahakama kufunga jalada la mirathi kama zoezi la ugawajilimeendeshwa sawa na kukamilika.

Kwa maelezo zaidi angalia Sheria ya Mirathi na Usimamizi wa Mali yaMarehemu

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 16

Page 17: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

13Sheria za URITHI na WOSIA

MIRATHI PASIPO NA WOSIA

Ndani ya siku 30 thelathini tangu alipofariki marehemu wahusikawanapaswa kusajili kifo cha marehemu kwenye Ofisi ya Vizazi na Vifoambayo iko kwa Mkuu wa Wilaya wa kila wilaya Tanzania Bara. Kamawahusika watachelewa kusajili kifo ndani ya siku (30), basi wafike kwenyeOfisi hiyo ya vizazi na vifo kwa maelezo.

Kifo kinasajiliwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya iliyopo mahali kifokilipotokea, na sio katika wilaya yeyote ile. Kama kuna matatizo kuhusuwapi kifo kisajiliwe, wahusika wanaweza kuwasiliana na msajili Mkuu waVizazi na Vifo, Makao Makuu, Dar es Salaam.

• Msimamizi au wasimamizi wa mirathi huteuliwa au kuchaguliwa nakikao cha wanandugu au ukoo

• Mwombaji hupeleka maombi yake mahakamani akiomba kuteuliwakuwa msimamizi wa mirathi. Maombi hayo huambatanishwa na vituvifuatavyo:-- nakala cheti cha kifo cha marehemu,- nakala ya kikao cha wanandugu cha kumchagua msimamizi wa

mirathi,- tamko la mwombaji kwanba atasimamia mirathi kwa uaminifu,- kiapo cha wanandugu kwamba wanamteua mwombaji kuwa

msimamizi wa mirahti,- kiapo cha mashahidi wakimdhamini mwombaji na kwamba wako

tayari kutoa fidia- endapo mwombaji atashindwa kusimamia vizuri.

Ili mwombaji aweze kupewa usimamizi wa mirathi lazima maombi yakeyazingatie na kutaja kwa kiwango cha kuithibitishia mahakama hayayafuatayo:-• Tarehe na mahali kilipotokea kifo cha marehemu,• Familia na ndugu wengine wa marehemu,• haki au mamlaka ambayo kwayo mwombaji anapata uwezo wa kuleta

maombi mahakamani,• orodha ya mali/madeni ya marehemu anayoweza kukusanya,• kwamba amefanya utafiti wa makini na kujilidhisha kwamba hakuna

wosia alali uliogunduliwa,• kwamba maombi kama hayo yamewahi kufanyika katika mahakama

yoyote ndani au nje ya nchi au la.

Baada ya kuwasilisha maombi ya mirathi, mahakama kwa kawaida hutoatangazo la mirathi kwa muda wa siku 90 kwenye Gazeti la Serikali

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 17

Page 18: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

14 Sheria za URITHI na WOSIA

linalosomwa na watu wengi au katika mbao za mahakama. Lengo nikuwawezesha wale wasioridhika na usimamizi huo kupeleka pingamizimahakamani. Vile vile mahakama ina uwezo wa kufupisha kipindi hiki chaTangazo la siku 90, kwa kutoa tangazo la muda mfupi zaidi,

Baada ya kuwasilisha maombi ya mirathi mahakamani, mahakama kwakawaida hujaza fomu za

“Taarifa ya Kawaida” kulingana na mahakama ambako mirathi hiyoimefunguliwa.

• Kama mirathi imefunguliwa katika mahakama za chini ya mahakamakuu, tangazo hutolewa katika gazeti la kawaida linalosomwa na watuwengi au katika mbao za mahakama na (30) mirathi hutolewa baada yasiku therathini tangu tangazo kutolewa.

• Kama mirathi imefunguliwa katika Mahakama Kuu, tangazo hutolewakatika magazeti la serikali na mirathi hutolewa baada ya siku tisini (90)tangu tangazo kutolewa.

ZINGATIO: Kama tulivyoona kuhusiana na mirathi yenye wosia, lengo lamuda huo wa tangazo ni kuwawezesha wale wasioridhika na usimamizihuo kupeleka pingamizi mahakamani na kuzuia mtu huyo asipeweusimamizi wa mirathi au asiteuliwe kuwa mtekelezaji wa wosia (mirathi)ya marehemu. Hata hivyo Mahakama ina uwezo wa kufupisha kipindihiki cha tangazo la siku 30 au 90, kwa kutoa tangazo la muda mfupi zaidi.

Mwombaji ambaye sasa ni msimamizi wa mirathi ya marehemu atalazimikakutekeleza, na/au kuendeleza taratibu za kugawa mali za marehemu kamaifuatavyo:-

• Kukusanya mali na madeni ya marehemu na pia kutambua anaowadai.

• Kutayarisha taarifa ya awali ya maelezo / ufafanuzi wa mali zote namadeni ya marehemu, na kuiwakilisha mahakamani katika kipindi chamiezi sita tangu kuthibitishwa kwake na mahakama. Hata hivyomahakama inaweza kurefusha muda huo kadri itakavyoona infaa.

• Msimamizi wa mirathi atagawa mali kwa warithi halali wa marehemukama walivyobainishwa na kutajwa katika maombi ya usimamizi wamirathi, kwa mujibu wa sheria husika yaani kama ni sheria ya mila, diniau serikali.

• Kutoa taarifa ndani ya miezi 6 ya ukamilishwaji wa zoezi la ugawaji wamali za marehemu mahakamani na mahakama kujiridhisha kama zoezihilo limeendeshwa sawa. Hata hivyo mahakama inaweza kurefusha

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 18

Page 19: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

15Sheria za URITHI na WOSIA

muda huo kadri itakavyoona infaa.

• Mahakama kufunga jalada la mirathi kama zoezi la ugawajilimeendeshwa sawa na kukamilika.

PINGAMIZI KWA MAOMBI YA MIRATHI

Pingamizi

Lengo la kutoa tangazo la mirathi katika gazeti la serikali (Ndani ya kipindicha siku 90 au pungufu (chini ya hapo), au taarifa ya kawaida (ndani ya kipindicha siku 30 au pungufu (chini ya hapo), ni kutoa fursa kwa yeyoteasiyeridhika na kuthibitishwa kwa mtekelezaji wosia ama kuteuliwa kwamsimamizi wa mirathi, kupeleka pingamizi lake mahakamani.

Kwa njia ya pingamizi, mtoa pingamizi hutoa sababu za kupingauthibitishwaji au uuteuliwaji wa mtekelezaji au msimamizi wa mirathi yamarehemu. Baada ya kuwasilisha pingamizi mahakamani, maombi yamirathi huchukua mfumo wa shauri la kawaida la daau na mwombaji wamirathi hupewa muda wa kujibu malalamiko ya mweka pingamizi.

Hivyo mahakama husikiliza pingamizi hilo na inaporidhika na sababuzitolewazo katika pingamizi, inaweza kubatilisha uthibitishwaji wamtekeleza mirathi au kukataa uteuzi wa mwombaji usimamizi wa mirathi.

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 19

Page 20: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

16 Sheria za URITHI na WOSIA

Hata kama muda wa kuwasilisha pingamizi utapita na mahakamaikamthibitisha au kumteua mtekelezaji au msimamizi wa mirathi, endapoitathibitika kwamba kulikuwapo na kughushi ,au udanganyifu kuhusianana usimamizi,au utekelezaji wa mirathi, basi maombi yanaweza kupelekwamahakamani kutaka mtekelezaji au msimamizi aondolewe na/ auusimamizi wake kutenguliwa.

Ni wakati gani Mahakama inaweza kubatilisha uthibitishwaji waMtekeleza mirathi au kukataa uteuzi wa Msimamizi wa mirathi:

Kwa mujibu kifungu namba 49(1) cha Sheria ya Mirathi na Usimamizi waMali ya Marehemu, (Probate and Administration of Estate Act,) Sura ya 352,mahakama yaweza kubatilisha uthibitishwaji wa mtekelezaji mirathi aukufuta uteuzi wa msimamizi wa mirathi, endapo yatabainika yafuatayo:

(i) Kwamba mwenendo wa kupata utekelezaji au usimamizi wamirathi ulikuwa na dosari za msingi,

(ii) Kwamba utekelezaji au usimamizi wa mirathi ulipatikana kwaudanganyifu baada ya kutoa mapendekezo ya uwongo au baada yakuificha mahakama habari muhimu na za msingi katika mirathihiyo,

(iii) Kwamba utekelezaji au usimamizi wa mirathi ulipatikana kwa njiaya malalamiko ya uwongo juu y jambo la muhimu la kisheria ilikuthibitisha kupatikana kwa utekelezaji au usimamizi wa mirathi,ingawa mlalamiko hayo yalifanywa kwa kutojua au bila nia mbaya,

(iv) Kwamba utekelezaji au usimamizi wa mirathi umekuwa hainamaana na haitekelezeki,

(v) Kwamba mtu aliyepewa utekelezaji au usimamizi wa mirathi, kwamakusudi ameamua kutopeleka orodha ya mali za marehemukulingana na sehemu ya kumi na mmoja ( XI) ya Sheria ya Mirathina Usimamizi wa Mali za Marehemu, Sura ya 352 au chini ya sheriahiyo hiyo, amepeleka mahakamani orodha au taarifa ya uwongo yamgawanyo wa maliza marehemu,

Basi ikilidhika kwamba mirathi imeendeshwa kinyume na taratibu sahihizinazoongaza mirathi kisheria na /au kinyume cha masilahi ya warithi,mahakama huwafutia uthibitishwaji au uteuzi, mtekelezaji au msimamiziwa mirathi na badala yake huagiza mtu mwingine ateuliwe na kupewamadaraka ya usimamizi wa mirathi hiyo.

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 20

Page 21: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

17Sheria za URITHI na WOSIA

ANGALIZO:

(a) Kwamba baada ya kuthibtishwa kuwa mtekelezaji au kuteuliwakuwa msimamizi wa mirathi, mtekelezaji au msimamizi wamirathi anapaswa, kutayarisha taarifa ya awali ya maelezo /ufafanuzi wa mali zote na madeni ya marehemu (inventory), nakuiwakilisha mahakamani katika kipindi cha miezi sita (6) tangukuthibitishwa au kuteuliwa kwake na mahakama; anapaswakugawa mali kwa warithi halali wa marehemu kamawalivyobainishwa na kutajwa katika wosia au katika maombi yausimamizi wa mirathi, kwa mujibu wa sheria husika yaani kamani sheria ya mila, dini au serikali; na mwisho kutoa taarifa ndaniya miezi 6 ya ukamilishwaji wa zoezi la ugawaji wa mali zamarehemu mahakamani na mahakama kujiridhisha kama zoezihilo limeendeshwa sawa, hivyo kufinga jarada.

(b) Kutopeleka taarifa ya kukamilika kwa usimamizi wa mirathikama inavyotajwa na sheria, sio tu ni sababu tosha ya mahakamakubatilisha au kutengua uthibitishwaji au uteuliwaji wamtekelezaji au msimamizi wa mirathi bali pia ni kosa la jinai.Hivyo mtekelezaji au msimamizi wa mirathi ni lazima atimizemajukumu yake.

MAOMBI YA KUPEWA USIMAMIZI WA MUDA WAMIRATHI

Wakati maombi ya kuomba usimamizi au utekelezaji wa mirathiyanaendelea mahakamani, mwombaji anaweza kuioomba mahakamakuiomba mahakama impe usimamizi wa mirathi wa muda.

Msimamizi aliyepewa usimamizi wa muda anakuwa na majukumu sawa namsimamizi aliyethibitishwa au kuteuliwa namahakama ya kukusanya nakutunza mali ya marehemu, isipokuwa hawezi kugawa mali ya marehemukwa warithi.

Lengo la kutoa usimamizi huu wa muda, ni kuwawezesha wawezekutimiza majukumu ya haraka kama vile matunzo kwa watoto na mjane.

WAJIBU WA MAHAKAMA KATIKA KUTHIBITISHAMTEKELEZAJI AU KUCHAGUA] MSIMAMIZI WAMIRATHI

Endapo mtu ameomba kuthibitishwa au kuteuliwa kuwa mtekelezaji aumsimammizi wa mirathi, mahakama inao wajibu wa kuchunguza kwa

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 21

Page 22: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

18 Sheria za URITHI na WOSIA

makini na kujiridhisha kwamba mtu huyo anayeomba kuthibitishwa aukuteuliwa kuwa mtekelezaji au msimamizi wa mirathi, anayo maslahikatika mirathi hiyo na ataweza kufanya kazi hiyo kwa makini na uaminifumkubwa kulingana na matakwa ya marehemu (kama yanaweza kubainika)katika kusimamia mali hizo.

Katika shauri la Seifu Marare dhidi ya Mwadawa Salum, (1985) MahakamaKuu, kupitia Jaji Katiti, ilisema kwamba wajibu wa mahakama katikakuchagua msimamizi wa mirathi, ni kuchagua mtu ambaye ana maslahikatika mirathi hiyo na amabaye angeweza kusimamia mirathi ya hiyokulingana na matakwa ya marehemu kama yanaweza kubainika.

WAJIBU WA MTEKELEZAJI AU MSIMAMIZI WAMIRATHI

Kadiri ya Jedwali la tano la Sheria ya Mahakama za Mahakimu na fungu la99 la Sheria ya Mirathi na Usimamizi wa mali za marehemu, inabainishwakwamba mtekelezaji au msimamizi wa mirathi ya marehemu ndiyemwakilishi wa marehemu kisheria na mali zote za marehemu zikomikononi mwake. Hivyo mtekelezaji au msimamizi wa mirathi yamarehemu anao wajibu na au majukumu kama inavyoainishwa hapa chini:

(i) Kukusanya mali zote za marehemu kwa uaminifu na uangalifumkubwa,

(ii) Kupeleka orodha ya mali ya marehemu au madeni alivyo wezakukusanya,

(iii) Kupokea na kulipa madeni halali ya marehemu, ikiwani pamoja nakulipa gharama zitokanazo na usimamizi,

(iv) Kugawanya mali iliyobaki kwa warithi halali wa marehemu,

(v) Kuifahamisha mahakama juu ya ugawaji wa mali za marehemuulivyofanyika na kama umekamilika au muda zaidi uongezwe iliaweze kukamilisha ugawaji wa mali ya marehemu na kuiwezeshamahakama kufunga jalada la mirathi,

(vi) Kulingana na fungu la 100 la Sheria ya Mirathi na Usimamizi waMali za Marehemu, mtekelezaji au msimamizi wa mirathi anawezakushitaki au kushitakiwa katika shauri lolote jipya au ambalomarehemu ama alianzisha au lilifunguliwa dhidi yake,

(vii) Kadri atakavyoona inafaa, na kadiri ilivyo kwa masilahi ya warithi,mtekelezaji au msimamizi wa mirathi, anaweza kuuza maliinayohamishika kutoka katika mirathi ya marehemu,

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 22

Page 23: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

19Sheria za URITHI na WOSIA

(viii) Mtekelezaji au msimamizi wa mirathi hawezi kutengeneza au kupatafaida kutokana na usimamizi wake,ispokuwa kama wosia umesema hivyo

ZINGATIO: kumekuwepo na dhana potofu kwa watekelezaji au wasimamiziwa mirathi walio wengi, kwamba baada ya mtu kuthibitishwa au kuteuliwakuwa mtekelezaji au msimamizi wa mirathi, basi amerithishwa mali hizomoja kwa moja na anaweza akafanya anavyotaka juu ya mali hizo. Kwamakala hii tunapenda kusisitiza kuwa hiyo ni dhana potofu. Baada yakuteuliwa au kuchaguliwa kuwa msimmizi wa mirathi, anao wajibu wakukusanya mali na kuzigawa kwa walithi halali wa marehemu, katika mudauliopangwa na kutoa taarifa mahakamani kwamba zoezi hilo limefanyikasalama na limekamilika. Kinyume na hapo, anatenda kosa la jinai.

HAKI ZA WARITHI DHIDI YA MTEKELEZAJI/MSIMAMIZI WA MIRATHI

Endapo mtekelezaji au msimamizi wa mirathi amesimamia au ametumiamirathi ya marehemu vibaya, warithi halali wa marehemu, pamoja na mambomengine, waweza kufanya yafuatayo:

(i) Kulingana na fungu namba 49(1)(e) na (2) cha Sheria ya Mirathi naUsimamizi wa Mali za Marehemu, Sura ya 352, warithi hao,wanaweza kuiomba mahakama kumfutia utekelezaji au usimamizi wamirathi na hivyo kulazimika kurudisha mahakamani hati zotezilizotolewa na mahakama kuthibitishautekelezaji au usimamizi wake wamirathi, ili mahakama iwezekumchagua mtu mwingine.

(ii) Kama amekataa kurudishamahakamani hati zotezilizotolewa nam a h a k a m ak u t h i b i t i s h autekelezaji auu s i m a m i z iwake wam i r a t h i ,w a r i t h iw a w e z a

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 23

Page 24: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

Vitini vingine vilivyochapishwa na Shirika la Nola

1. Sheria ya Mikataba

2. Taratibu za kuendesha Mashauri ya Madai Mahakamani

3. Taratibu za Mashauri ya Ardhi

4. Sheria ya Ndoa na Mahusiano ya Familia

5. Sheria ya Makosa ya Jinai na Mwenendo wake

20 Sheria za URITHI na WOSIA

kumshitaki chini ya fungu namba 51 kifungu cha pili, na akikutwana hatia anweza kutozwa faini au kifungo kisichozidi miezi mitatuau vyote faini na kifungo,

(iii) Kama mtekelezaji huyo na/au msimamizi wa mirathi amesimamiavibaya au ameharibu mali ya marehemu, warithi au mtu yeyotemwenye maslai na usimamizi huo, anaweza kumfikishamahakamani akimtaka alipe fidia kwa uharibifu au hasaraaliyosababisha. Katika shauri la Safiniel Cleopa dhidi ya JohnKadeghe (1984) Mahakama Kuu, kupitia Mheshimiwa Jaji Chua,ilisema kwamba msimamizi ambaye ameharibu, kutumia vibaya aukusababisha hasara kwenye mali ya marehemu, lazima arekebishehasara au uharibifu huo.

HITIMISHO

Ni jambo la busara kwamba kila mtu atayarishe wosia wakati wa uhai wakeili kuacha msingi mzuri wa mgawanyo wa mali zake atakapoaga dunia.Ingawa bado mahakama katika mazingira fulani, yaweza kubatilisha wosiawa marehemu kama tulivyoona hapo juu, mgawanyo wa mali zamarehemu, utegemea maelezo na maelekezo katika wosia.

Ikumbukwe kwamba, usimamizi wa mirathi sio kurithishwa mali zamarehemu. Msimamizi wa mirathi ni mdhamini tu. Kazi yake ni kukusanyamali na kuirithisha kwa wanufaika wa mirathi ya marehemu. Kama yeye nimmoja wapo wa wanufaika, anapaswa kupata sehemu yake halali kamawengine.

Usimamizi wa mirathi, umepewa muda maalum wa ukomo hivyo lazimamsimamizi ajitahidi kutimiza majukumu yake ya kukusanya mali nakuzigawa kwa wanufaika katika muda uliopangwa na sheria. Kushindwakutimiza kazi za usimamizi wa mirathi kwa muda uliopangwa, mahakamainaweza kumfutia msimamizi au mtekelezaji usimamizi au utekelezaji wakekulingana na hali itakavyokuwa.

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 24

Page 25: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

21Sheria za URITHI na WOSIA

MAELEZO YA KUJIKUMBUSHA

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 25

Page 26: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

22

MAELEZO YA KUJIKUMBUSHA

Sheria za URITHI na WOSIA

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 26

Page 27: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:17 PM Page 27

Page 28: Kimetayarishwa na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria ... · • Watoto wa kiume na wa kike ndio warithi pakee wa mali ya baba yao • Kama marehemu hakuacha watoto, mali zake

ISBN 9987 - 482 - 13 - 9

National Organisation for Legal Assistance (nola)P.O.Box 10096, Dar es Salaam-Tanzania

Tel: +255 22 22772547 • Fax: +255 22 2771269Email: [email protected] Website: www.msaadawasheria.or.tz

Urith na wosia.qxd.qxp 11/16/2006 8:18 PM Page 28