1
Kipindi chote cha kuanzia mwaka 2013 hadi sasa amekuwa akijihusisha na uelimishaji na uhamasishaji kupitia makongamano, warsha za vijana, pia uandishi kupitia Blog yake ya Jielimishe Kwanza! iliyobeba jina la kampuni iitwayo Jielimishe Kwanza! Social Enterprise yenye makao makuu jijini Dar es salaam, Tanzania. Kazula amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha mtazamo chanya katika nyanja za ajira, elimu, mazingira na biashara kupitia makala mbali mbali zilizosheheni ndani ya Blog yake maarufu iliyojinyakulia nafasi ya pili kitaifa kwa mwaka 2013 kama “The Best Inspirational Blog in Tanzania”. Hayuko nyuma sana katika kujiendeleza kielimu, mwanzoni mwa mwaka 2014 alianza kufanya shahada ya uzamili ya Sayansi ya Mazingira yenye vionjo vya Biashara na Ujasiriamali katika Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia- Nelson Mandela, Arusha-Tanzania. Nikinukuu moja ya sentensi katika mafunzo yake yahusuyo “mtazamo” anasema; “Mtazamo wako kukuhusu na kuwahusu wengine, unakuwa uhalisia wako kama ukiamini na kujichukulia…” Katika kitabu hiki anauliza “Mtazamo Wako Ni Upi? ” Ukizingatia kuwa Mtazamo Wako, Maisha Yako. Ungana naye hatua kwa hatua kupitia mkusanyiko wa makala zake kuhusu mtazamo ili kutambua mtazamo ulio nao na kuelekea kuwa na mtazamo chanya ulio na tija ya mafanikio na furaha maishani. Henry Kazula ni mwanzilishi na mmliki wa kampuni -“Jielimishe Kwanza! Social Enterprise” inayojihusisha na kutoa mafunzo ya kushawishi mabadiliko ya pamoja ndani ya jamii kwa vijana na wadau mbali mbali katika nyanja za mazingira, elimu, ajira, biashara, ujasiriamali na ujasiriamali jamii. Pia, Kazula ni mjasiriamali, mwandishi, mwelimishaji jamii, mhamasishaji wa hadhara na mtaalam wa masuala ya saikolojia ya malezi na mazingira, amekuwa bega kwa bega katika shughuli mbali mbali za maendeleo ya vijana na jamii kwa ujumla hasa alipokuwa akishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali kama; “Youth for Africa (YoA)” na “Global Platform-Actionaid Tanzania” yote ya jijini Dar es salaam katika ujasiriamali na ujasiriamali jamii, pia kuibua mbinu za pamoja kutatua changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana.

Kuhusu mwandishi henry kazula

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Kuhusu mwandishi henry kazula

 

Kipindi chote cha kuanzia mwaka 2013 hadi sasa amekuwa akijihusisha na uelimishaji na uhamasishaji kupitia

makongamano, warsha za vijana, pia uandishi kupitia Blog yake ya Jielimishe Kwanza! iliyobeba jina la kampuni

iitwayo Jielimishe Kwanza! Social Enterprise yenye makao makuu jijini Dar es salaam, Tanzania.

Kazula amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha mtazamo chanya katika nyanja za ajira, elimu, mazingira na biashara

kupitia makala mbali mbali zilizosheheni ndani ya Blog yake maarufu iliyojinyakulia nafasi ya pili kitaifa kwa mwaka

2013 kama “The Best Inspirational Blog in Tanzania”.

Hayuko nyuma sana katika kujiendeleza kielimu, mwanzoni mwa mwaka 2014 alianza kufanya shahada ya uzamili

ya Sayansi ya Mazingira yenye vionjo vya Biashara na Ujasiriamali katika Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia-

Nelson Mandela, Arusha-Tanzania.

Nikinukuu moja ya sentensi katika mafunzo yake yahusuyo “mtazamo” anasema;

“Mtazamo wako kukuhusu na kuwahusu wengine, unakuwa uhalisia wako kama ukiamini na kujichukulia…”

Katika kitabu hiki anauliza “Mtazamo Wako Ni Upi? ” Ukizingatia kuwa Mtazamo Wako, Maisha Yako. Ungana naye

hatua kwa hatua kupitia mkusanyiko wa makala zake kuhusu mtazamo ili kutambua mtazamo ulio nao na kuelekea

kuwa na mtazamo chanya ulio na tija ya mafanikio na furaha maishani.

Henry Kazula ni mwanzilishi na mmliki wa kampuni -“Jielimishe Kwanza!

Social Enterprise” inayojihusisha na kutoa mafunzo ya kushawishi mabadiliko

ya pamoja ndani ya jamii kwa vijana na wadau mbali mbali katika nyanja za

mazingira, elimu, ajira, biashara, ujasiriamali na ujasiriamali jamii.

Pia, Kazula ni mjasiriamali, mwandishi, mwelimishaji jamii, mhamasishaji wa

hadhara na mtaalam wa masuala ya saikolojia ya malezi na mazingira, amekuwa

bega kwa bega katika shughuli mbali mbali za maendeleo ya vijana na jamii

kwa ujumla hasa alipokuwa akishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali

kama; “Youth for Africa (YoA)” na “Global Platform-Actionaid Tanzania” yote

ya jijini Dar es salaam katika ujasiriamali na ujasiriamali jamii, pia kuibua

mbinu za pamoja kutatua changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana.