6
Kukua na Kuenea Kiswahili nchini Tanzania. Wageni walipofika pwani ya Afrika Mashariki waliwakuta wenyeji tayari wana lugha yao ya mawasiliano, ambayo ni Kiswahili. Kiswahili pia kilitumika kama lugha ya kibiashara miongoni mwa wabantu. Hivyo wageni wa kwanza hawakuwa na sababu ya kutumia lugha nyengine zaidi yaKiswahili.Walilazimika kujifunza Kiswahili ili wakitumie katika shughuli zao mbalimbali za kibiashara zikiwemo shughuli za kibiashara, kidini na kiutawala. Wageni waliofika kwa nyakati tofauti katika pwani ya Afrika Mashariki ni waarabu, Wareno, Wajerumani na Waingereza. Kila kundi lililofika hapa likuwa na mchango wake katika kukuza na kueneza Kiswahili, pia wapo waodidimiza ustawi wa lugha hiyo. UKUAJI WA KISWAHILI NCHINI TANZANIA WAKATI WA WAARABU Kukua kwa lugha ni hali ya kuongezeka kwa msamiati wa lugha hiyo. Msamiati ni jumla ya maneno yanayotumiwa katika lugha fulani, ili lugha yoyote ikuwe lazima msamiati wake ukuwe. Wageni wa kwanza kuja Tanzania ni waarabu, kutokana na kuhusiana na Waarabu katika Nyanja mbalimbali. Ksiwahili kimechukua msamiati wa kiarabu ili kukuza msamiati wake, ni tabia ya lugha zinapotumika pamoja huathiriana na kuchukuliana maneno. Yasemakana kiingereza kimeathiriwa na kilatini kwa kiasi cha theluthi mbili. Kiswahili kimeathiriwa na lugha nyengine kama vile kihindi, kiajemi,kireno, Kijerumani, Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu n.k. Kiarabu ndicho chenye maneno mengi sana katika Kiswahili kuliko lugha ya taifa lolote jengine la kigeni, hii ni kwa sababu zifuatazo; (a) Bara Arabu ndiyo nchi ya kigeni iliyokuwa jirani zaidi na upwa wa Afrika Mashariki, hivyo watu wake waliingiliana zaidi na watu wa huku kuliko watu wengine wowote, maingiliano hayo hayakuwa ya kibiashara tu bali hata ya kindoa. (b) Lugha ya kiarabu ndiyo lugha iliyotumika kufundishia dini ya kiislamu, hivyo waswahili walijikuta wanaingiza maneno ya kiarabu katika Kiswahili. Sababu zilizochangia kukua kwa Kiswahili wakati wa utawala wa Waarabu 1. Dini.

Kukua Na Kuenea Kiswahili Nchini Tanzania

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Kukua Na Kuenea Kiswahili Nchini Tanzania

Kukua na Kuenea Kiswahili nchini Tanzania.

Wageni walipofika pwani ya Afrika Mashariki waliwakuta wenyeji tayari wana lugha yao ya mawasiliano, ambayo ni Kiswahili. Kiswahili pia kilitumika kama lugha ya kibiashara miongoni mwa wabantu. Hivyo wageni wa kwanza hawakuwa na sababu ya kutumia lugha nyengine zaidi yaKiswahili.Walilazimika kujifunza Kiswahili ili wakitumie katika shughuli zao mbalimbali za kibiashara zikiwemo shughuli za kibiashara, kidini na kiutawala.

Wageni waliofika kwa nyakati tofauti katika pwani ya Afrika Mashariki ni waarabu, Wareno, Wajerumani na Waingereza. Kila kundi lililofika hapa likuwa na mchango wake katika kukuza na kueneza Kiswahili, pia wapo waodidimiza ustawi wa lugha hiyo.

UKUAJI WA KISWAHILI NCHINI TANZANIA WAKATI WA WAARABUKukua kwa lugha ni hali ya kuongezeka kwa msamiati wa lugha hiyo. Msamiati ni jumla ya maneno yanayotumiwa katika lugha fulani, ili lugha yoyote ikuwe lazima msamiati wake ukuwe.

Wageni wa kwanza kuja Tanzania ni waarabu, kutokana na kuhusiana na Waarabu katika Nyanja mbalimbali. Ksiwahili kimechukua msamiati wa kiarabu ili kukuza msamiati wake, ni tabia ya lugha zinapotumika pamoja huathiriana na kuchukuliana maneno. Yasemakana kiingereza kimeathiriwa na kilatini kwa kiasi cha theluthi mbili. Kiswahili kimeathiriwa na lugha nyengine kama vile kihindi, kiajemi,kireno, Kijerumani, Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu n.k.

Kiarabu ndicho chenye maneno mengi sana katika Kiswahili kuliko lugha ya taifa lolote jengine la kigeni, hii ni kwa sababu zifuatazo;(a) Bara Arabu ndiyo nchi ya kigeni iliyokuwa jirani zaidi na upwa wa Afrika Mashariki, hivyo watu wake waliingiliana zaidi na watu wa huku kuliko watu wengine wowote, maingiliano hayo hayakuwa ya kibiashara tu bali hata ya kindoa.

(b) Lugha ya kiarabu ndiyo lugha iliyotumika kufundishia dini ya kiislamu, hivyo waswahili walijikuta wanaingiza maneno ya kiarabu katika Kiswahili.

Sababu zilizochangia kukua kwa Kiswahili wakati wa utawala wa Waarabu1. Dini.Waarabu walipowasili walianza kueneza dini yao ya kiislam kwa wenyeji wa upwa wa Afrika. Waarabu walianzisha madarasa ambayo walitumia kufundishia waafrika dini ya kiislam, wafrika hao walifundishwa kusoma na kuandika kwa hati za kiarabu ili waweza kusoma na kuelewa Qur-an.

Lugha ya kufundishia katika madarasa hayo ilikuwa Kiswahili, hivyo waswahili walijikuta wanaingiza baadhi ya maneno katika Kiswahili. Kutokana na dini na elimu tumeweza kupata maneno ambayo tunatumia katika Kiswahili, maneno hayo ni kama vile; alajiri, alasiri, kurani, elimu, ratibu, inshallah.k

2. Utawala.Kutokana na kutawaliwa na waarabu,tumepata msamiati mwingi wa Kiswahili. Waarabu walitawala Pemba, Unguja na sehemu za pwani za bara. Kutokana na kutawaliwa kuna baadhi ya maneno ambayo yamechukuliwa kutoka lugha ya kiarabu na kuwa katika Kiswahili, maneno hayo ni kama vile sultani, mwinyi,utukufu, enzi n.k

3. Biashara.

Page 2: Kukua Na Kuenea Kiswahili Nchini Tanzania

Waarabu walipowasili katika mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki, walianza kufanya biashara na wenyeji,kutokana na maingiliano hayo ya kibiashara , waarabu walianza kuingiza maneno mengi ya kiarabu katika lugha ya Kiswahili. Kutokana na maingiliano hayo ya kibiashara, Kiswahili kilianza Kukua na Kuenea Kiswahili nchini Tanzania.kupanuka kwa kuongeza msamiati, na bila shaka hali hii ilisababihsa kukuwa kwa Kiswahili, mfano wa msamiati uliochukuliwa kutoka kwa waarabu na kingizwa katika Kiswahili ni jahazi, kodi, adesi n.k.

4. Waarabu na ndo za wabantu.Wageni hawa walikaa kwa miaka mingi sana katika pwani ya Afrika Mashariki, walijikuta walowezi ambao mila zao na Kiswahili zilianza kuchangamana kwa kiasi fulani. Hivyo, waarabu walijikuta wanatwa wake wa kibantu ili waishi kama mume na mke, lugha ambayo ilitumika sana katika maisha yao ya ndo ilikuwa ni Kiswahili.

Vile vile watoto waliozaliwa na wazazi wa kiarabu na kibantu walijifunza Kiswahili na kukitumia kama lugha yao ya awali. Malezi ya watoto hawa yaliegemea kwenye utamaduni wa Kiswahili, watoto hawa walikuzwa kwa lugha ya Kiswahili. Hata jamii ya watu wa pwani na Tanzania kwa ujumla waliwaita watoto hawa “Waswahili” baada ya maneno kama vile “Chotara”. Kwa ujumla utaona ndoa za waarabu na wabantu zilichangia pia katika kueneza lugha ya Kiswahili hapa nchini Tanzania.

KUENEA KWA KISWAHILI WAKATI WA UTAWALA WA WAJERUMANIWajerumani waliingia nchini Tanzania, baada ya ujio wa waarabu na wareno. Wajerumani walipoingia nchini Tanzania walikuta tayari Kiswahili kinatumika kwa kiasi fulani. Ujio wao kama wakoloni, ulichangia sana kuenea kwa lugha ya Kiswahili. Njia zizotumika kueneza Kiswahili nchini Tanzania wakati wa utawala wa Wajerumani zilikuwa kama ifuatavyo:

(a)Utawala.Kutokana na ukweli kuwa lugha ya Kiswahili ilikuwa imekwisha kuenea, Wajerumani waliamua kutumialugha hiyo katika shughuli zao za ki-utawala.Wajerumani walilazimika kujifunza lugha ya Kiswahili huko huko Berlin kabla ya kuja nchini, kujifunza huko kulisaidia kuenea kwa Kiswahili. Kwa shughuli za kiutawala hapa nchini, ukolni wa Kijerumani ulitoa mwongozo kwa viongozi wa nchini kujifunza na kutumialugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano katika utawala. Hii ilimaanisha kwamba wajumbe na maakida wote iliwabidi wajifunze lugha ya Kiswahili ili wawe viungo wazuri waserikali na wananchi.

(b) Elimu.Utawala wa Wajerumani uliteua lugha ya Kiswahili itumike kama lugha ya kufundishia, na pia kutumika kama somo la kawaida katika shule za msingi. Baadhi ya shule hizo ni kama vile Tabora, Mpwapwa na Kilosa,kwa mtazamo huo, wanafunzi na walimu walijifunza Kiswahili ili wakitumia katika shughuli za elimu na hivyo kufanya lugha hiyo kuenea kwa urahisi.

(c) Shughuli za kilimo (Mashamba).Moja ya shughuli walizofanya Wajerumani, ilikuwa kuanzisha mashamba makubwa ya mazao ya biashara kama vile katani huko Tanga na kahawa huku Kilimanjaro na Bukoba. Katika mashamba haya kulikuwa na idadi kubwa ya vibarua kutoka sehemu mbalimbali za nchi,lugha iliyotumika ni Kiswahili, ambacho kilitumiwa na vibarua hao. Hivyo Kiswahili kilikuwa na ongezeko la watumiaji na kufanya lugha hiyo kuenea.

Page 3: Kukua Na Kuenea Kiswahili Nchini Tanzania

(d) Mahakama.Utawala wa Kijerumani ulitumia pia lugha ya Kiswahili katika shughuli za kimahakama. Wafanyakzai na wazee wa mahakama waliwahoji na kutoa hukumu kwa watuhumiwa kwa kutumialugha ya Kiswahili. Hivyo shughuli za kati ziliendeshwa kwa Kiswahili na kufanya kiswaili kienee chini ya utawala huu.

Kiswahili baada ya UhuruBaada ya uhuru kuna harakati mbalimbali zilizochukuliwa na serikali ya Tanzania katika kukiendelezana kukikuza kiswahili. Harakati hizo ni pamoja na kupendekezwa kuwa lugha rasmi 1962. Mnamomwaka 1964 kiswahili kilipendekezwa kuwa lugha ya taifa na kuwa kitatumika katika shughuli zote za kiserikali na kitaifa mfano katika elimu hususani elimu ya msingi.

Kundwa kwa Chombo cha usanifishaji ambacho kilikuwa na kazi ya kuhimiza maendeleo ya kiswahili,kutayaricha kamusi na vitabu mbalimbali vya sarufi na fasihi ya lugha ya kiswahili na kuandaawataalamu watakaoshughulikia usanifishaji wa kiswahiliPia baada ya uhuru kulianzishwa Taasisi mbalimbali zitakazoshughulikia lugha ya kiswahili. Mfano:-BAKITA, TUKI, TUMI, UKUTA, UWAVITA, Idara ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaamu.Baada ya uhuru nchini Tanzania kiswahili kilienea kwa kasi kubwa sana. Kuna sababu mbalimbali ambazo zilichangia kukua na kuenea kwa kiswahili hapa nchini. Baadhi ya sababu hizo ni pamoja na:-(a) kuteuliwa kwa kiswahili kuwa lugha ya Taifa.(b) Kiswahili kitumike katika Elimu, mfano kuwa lugha ya kufundishia katika shule za msingi.(c) kuundwa kwa vyombo mbalimbali vya kukuza na kuneza kiswahili.(d) Kiswahili kuwa Lugha rasmi na lugha ya Taifa.(e) Kiswahili kutumika katika shughuli mbalimbali za kidini, shughuli za kisiasa na kiutawala na shughuliza kiutamaduni.(f) Uchapishaji wa vitabu na majarida mbalimbali.

1. KISWAHILI KUWA LUGHA YA TAIFABaada ya uhuru mwaka 1962 kamati iliundwa ili kuangalia uwezekano wa kutumia kiswahili katika shughulizote rasmi, mfano bungeni na shughuli zote za kiofisi. Pia kiswahili kiliteuliwa kuwa lugha ya taifa 1964 ambapo katika shughuli zote za kitaifa zitaendeshwa kwa kutumia lugha ya kiswahili.

Hivyo kiswahili kilihimizwa kutumika katika mawasiliano yote hususani katika mawasiliano yote hasa katika shughuli za umma na Wizara zote, Serikali na Bunge, kiswahili kiliendelea kupanda hadhi zaidi wakati wa Azimio la Arusha la mwaka 1967 kwani azimio hilo lilitungwa na kuandikwa kwa lugha ya kiswahili.

2. KUUNDWA KWA VYOMBO VYA UKUZAJI NA UENEZAJI WA KISWAHILITanzania baada ya uhuru ilifanya jitihada za kuunda vyombo mbalimbali vya kukuza na kueneza kiswahili katika nyanja mbalimbali mfano wa vyombo hivyo ni UWAVITA,BAKITA, TUMI,TUKI, Taasisi ya Elimu,TAKILUKI na Chama cha Kiswahili Chuo Kikuu Dar es salaam.

3. KUTUMIKA KATIKA ELIMUKiswahili licha ya kutumika katika shughuli mbalimbali za kiserikali, kilipendekezwa kutumika Katika shule za Msingi na kufundishwa katika elimu ya sekondari kama somo na katika vyuo vikuu wanatoa shahada mbalimbali za lugha ya kiswahili. Pia katika Elimu ya watu wazima ambao hawakujua kusoma na kuandika.

Page 4: Kukua Na Kuenea Kiswahili Nchini Tanzania

Watu hawa walijifunza masomo mbalimbali kwa lugha ya kiswahili na kuwafanya watu wengi kujua kusoma, kuandika na kuzungumza lugha ya kiswahili fasaha. Kampeni hii ilikuwa kwa nchi nzima ambapo walijifunza elimu ya Afya, Siasa,Kiswahili, Kilimo na ufundi kwa lugha ya kiswahili na kuwafanya watu wengi kuzungumzakiswahili sanifu.

4. VYOMBO VYA HABARITangu uhuru ulipopatikana kuna vyombo mbalimbali vya habari vilivyoanzishwa. Vyombo hivi hutumika kueneza kiswahili kwa kiasi kikubwa na hufikiwa na watu wengi licha ya kuwepo kwa changamoto za kiuchumi. Vyombo hivyo ni magazeti na majarida mbalimbali ambayo huandikwa kwa lugha ya Kiswahili lakini kuna redio na runinga ambazo matangazo yake hutangazwa kwa lugha ya kiswahili. Hivyo kukifanya kiswahili kuenea kote ndani na nje ya nchi.

5. BIASHARAShughuli za kibiashara nchini husaidia kuenea na kukua kwa kiswahili kutokana na kuwepo kwa makabila tofauti tofauti ambapo wafanyabiashara huweza kuunganishwa kwa lugha ya kiswahili. Hivyo kiswahili hudumishwa na kutumika katika biashara hizo.

6. SHUGHULI ZA SIASA NA UTAWALATangu wakati wa harakati za kupigania uhuru kiswahili kimetumika kama nyenzo muhimu kuwaunganisha wananchi. Shughuli nzima za kisiasa zimetumia lugha hii katika kujiimarisha; mfano wakati wa chama kimoja, Azimio la Arusha na Mfumo wa vyama vingi Kiswahili kimetumika kama njia kuu ya mawasiliano.

Pia katika utawala chama kinachotawala kimekuwa na harakati za kukiendeleza kiswahilli katika nyanja zote. Ambapo kiswahili kimekuwa kikitumika katika shughuli zote za kiutawala. Hivyo shughuli za kisiasa na kiutawala zimechangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza, kukieneza na kukiendeleza kiswahili.

7. UANDISHI NA UCHAPISHAJI WA VITABUKuibuka kwa waandishi wa vitabu mbalimbali vya kiswahili vya sarufi na fasihi ambavyo vilichambua kwa kina mambo mabalimbali yahusuyo lugha ya kiswahili na utamaduni wake, mfano : Nkwera,Shabani Robart, Mathias Mnyapala na Shaffi Adam Shaffi. Waandishi wengine chipukizi walijitokeza na wanaendelea kujitokeza katika tasnia hii ya uandishi wa vitabu.

8. SHUGHULI ZA KIUTAMADUNIShughuli za kiutamaduni zimechangia kueneza kukuza na kuendeleza lugha ya kiswahili. Shughuli hizo ni pamoja na harusi, misiba, matanga na sherehe mbalimbali za kijamii ambazo zimesaidia kukiendeleza kiswahili kwa kuwa huwakutanisha watu tofauti tofauti katika shughuli hizo, ambapo huwalazimu kutumia lugha ya kiswahili katika mawasiliano na kufanya kiswahili kuendelea.Pia katika Sherehe mbalimbali vikundi vya sanaa na muziki vinavyotumia lugha ya Kiswahili kutumbuiza. Vikundi vingine huandaa nyimbo zao kwa ajili ya kukieneza kiswahili.

www.news4timeblog.com Tanzania