175
SURA YA SITA MJADALA JUU YA KUWEPO KWA MAJAZI Katika sehemu zilizotangulia tumenukuu itikadi za wanaoitwa Mawahabi au wanaojiita Al-Salafiyya au Ansaru Sunna na Maimamu wao watangulizi juu ya itikadi ya tajsim (kumfanya Allah kuwa ana kiwiliwili na viungo). Katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu 1 nilinukuu kiasi fulani baadhi ya itikadi hizo kisha nikasema: Sababu kubwa na chanzo cha Mawahabi kuwa na itikadi hizi za kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe, wakasema kuwa Mwenyezi Mungu ana mikono, miguu, uso, macho, anakwenda kwenye ardhi, anacheka, anakaa kitako kweli kweli, aliegemeza mgongo wake kwenye jabali huku akiandika Taurati n.k., ni kukanusha kwao kuwepo kwa majazi katika lugha ya Kiarabu na hasa hasa katika Qur-ani. Miongoni mwa walioandika kwa urefu na kukataa jambo hili ni Ibn Qayyim Al-Jawziyya. 2 1 - Uk. 32. 2 - Kama ilivyo katika kitabu chake Mukhtasar Al-Sawaaiq Al-Mursala j. 2 inaanzia uk. 231. Na kichwa cha habari “Heading” cha sehemu hio ni Sehemu Ya Kumvunja Taghuti (Shetani) Wa Tatu…Naye Ni Taghuti Wa Majazi. Lakini kitabu hiki sasa kimejibiwa kwa urefu na Sheikh Al-Khalili katika tafsiri yake Jawahiru Al-Tafsir: Juz-u Khaas. Katika tafsiri hio Sheikh Al-Khalili kaielezea Aya moja tu ya 7 ya Sura ya 3, ambayo imechukua karatasi 403, ambapo alichukua sehemu kubwa kwa kuzijadili hoja za Ibn Al-Qayyim juu ya suala la majazi. 1

MDAHALO WA KIMAPENZIxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1768672436/name/FIMBO+YA... · Web viewNa kwa tafsiri hio iliopokewa katika Hadithi, basi maana ya funguo za yaliojificha ambayo

  • Upload
    dinhtu

  • View
    506

  • Download
    10

Embed Size (px)

Citation preview

SURA YA SITAMJADALA JUU YA KUWEPO KWA MAJAZI

Katika sehemu zilizotangulia tumenukuu itikadi za wanaoitwa Mawahabi au wanaojiita Al-Salafiyya au Ansaru Sunna na Maimamu wao watangulizi juu ya itikadi ya tajsim (kumfanya Allah kuwa ana kiwiliwili na viungo). Katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu1 nilinukuu kiasi fulani baadhi ya itikadi hizo kisha nikasema:

Sababu kubwa na chanzo cha Mawahabi kuwa na itikadi hizi za kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe, wakasema kuwa Mwenyezi Mungu ana mikono, miguu, uso, macho, anakwenda kwenye ardhi, anacheka, anakaa kitako kweli kweli, aliegemeza mgongo wake kwenye jabali huku akiandika Taurati n.k., ni kukanusha kwao kuwepo kwa majazi katika lugha ya Kiarabu na hasa hasa katika Qur-ani. Miongoni mwa walioandika kwa urefu na kukataa jambo hili ni Ibn Qayyim Al-Jawziyya.2

Sasa tazama ajabu! Sheikh Kasim Mafuta kayapindua maneno yangu na badala yake akaninukuu sivyo!3 Anasema:

Ndugu msomaji kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa mambo ya dini yetu hii ya kiislamu na ukawa unashughulishwa na kufuatilia matatizo yanayo usibu umma huu mtukufu, bila shaka utaziona athari za wazi wazi za tofauti za wafuasi wa dini hii tukufu, tena baadhi ya tofauti ni zile tofauti nzito ambazo huwezi kutoa hukumu kwamba wote hao waliotofautiana wako katika haki. Na pengine unaweza kujiuliza ni nini sababu zilizowaingiza watu hawa katika tofauti hizi na itikadi potofu na batili? Ndugu Juma M. Al-Mazrui yeye anadai kwamba chanzo cha watu kutumbukia katika itikadi za batili: “Ni kukanusha kwao kuwepo kwa MAJAZI katika lugha ya kiarabu na hasa katika Qur’an”. Tazama kitabu chake “Hoja zenye Nguvu” ukurasa wa 32.4

Anaendelea Sh. Kasim kwa kusema:

1 - Uk. 32. 2 - Kama ilivyo katika kitabu chake Mukhtasar Al-Sawaaiq Al-Mursala j. 2 inaanzia uk. 231. Na kichwa cha habari “Heading” cha sehemu hio ni Sehemu Ya Kumvunja Taghuti (Shetani) Wa Tatu…Naye Ni Taghuti Wa Majazi. Lakini kitabu hiki sasa kimejibiwa kwa urefu na Sheikh Al-Khalili katika tafsiri yake Jawahiru Al-Tafsir: Juz-u Khaas. Katika tafsiri hio Sheikh Al-Khalili kaielezea Aya moja tu ya 7 ya Sura ya 3, ambayo imechukua karatasi 403, ambapo alichukua sehemu kubwa kwa kuzijadili hoja za Ibn Al-Qayyim juu ya suala la majazi. 3 - Kama utavyoona katika jawabu hii, kitabu chote cha Kasim Mafuta ni tadlis (ghushi) tupu! 4 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 35.

1

Juma hakusema kwamba vyanzo vya upotevu ni:Kutoshikamana na Qur’an na Sunna, Kumtii shetani na askari wake, Kufuata matamanio ya nafsi,Ujinga, Kiburi, Kufanya is’rafu katika matumizi ya majazi ndani ya Qur’an, na kuzipotosha tafsiri za baadhi ya aya kwa madai kuwa kuna majazi. Na nyinginezo miongoni mwa sababu zilizotajwa na Qur’an au Sunna. Bali yeye ameamua kutaja mambo hayo kuwa ndiyo vyanzo vya upotovu, na hali ya kuwa yeye mwenyewe ana yakini kwamba hawezi kututhibitishia kielimu kwamba itikadi hizo ni vyanzo vya upotevu kivipi?5

Anaendelea Sheikh Kasim Mafuta kwa kusema:

Tumebainisha katika kitabu hiki kwamba, chanzo na chimbuko kubwa la watu kutumbukia katika itikadi za batili ni kuiacha njia sahihi aliyotuwekea bwana Mtume Muhammad swalla llaahu alayhi wasallam, njia ya Qur’an na Sunna kwa ufahamu wa wema waliotangulia (maswahaba na wafuasi wao na maimamu waliokuja baada yao). Na si kama alivyodai mwandishi wa kiibadhi Juma Al-Mazrui, kwamba chanzo cha upotevu ni kupinga kuwepo kwa Majazi katika Qur’an. 6

Hayo ndio alioyasema Sheikh Kasim Mafuta katika kuyajibu yale nilioyasema mimi. Nami namwambia bwana Kasim Mafuta kwamba mimi sikusema “Chanzo cha upotovu ni kukataa majazi,” kama alivyodai yeye, bali nilichokisema ni hiki: “Chanzo cha Mawahabi kutumbukia katika itikadi HIZI ni kukanusha kwao kuwepo kwa majazi”. Sasa kama nilisema itikadi HIZI, suala ni kuwa je ni itikadi zipi hizo nilizozitaja na kuziashiria kwa neno HIZI? Utakumbuka kwamba mimi niliyasema hayo baada ya kunukuu zile itikadi za kudai kwamba Mungu ana mkono, mguu, macho n.k. Wewe, Sh. Kasim, umebadilisha na kusema Juma kasema kuwa asili ya upotovu ni kukataa majazi. Je huoni Sheikh kwamba unatumbukia katika kile kile ulichowatia aibu wenzako kwacho? Umedai kuwa Sheikh Al-Khalili kaubadilisha ubeti wa Ibn Al-Qayyim nao ubeti huo upo kama nitavyokuthibitishia nikifika mahala pake. Tena hata kama kweli ubeti huo mjengeko wake umebadilishwa, bado maana ya ubeti huo ni sawa sawa na maana iliomo katika ubeti uliomo katika Nuniyya ya Ibn Al-Qayyim. Wewe hapo ukaona umepata mwanya wa kuweza kutoa dukuduku lako ukimuiga Ali Al-Faqihi. Leo wewe umebadilisha maneno kwa mfumo ambao umeleta maana tafauti kabisa. Huoni kwamba unabeba jukumu na kujitwika mizigo?

5 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 37-38. Tulia tuli! Nitakuthibitishia kila kitu kwa hoja zitazoupozo moyo wako. 6 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 173.

2

Kwa hivyo ni wazi, kwa aliyeyatazama maneno yangu, kwamba mimi nauzungumzia upotovu maalumu, nao ni upotovu wa kumpachika Mungu viungo vya hakika; huo ndio ambao nimedai kwamba chimbuko lake ni kuyakanusha majazi, wala mimi sizungumzii upotovu kama vile ulevi na uzinifu. Ni akili ya mtu gani itayofikiria kwamba mtu anazini – kwa mfano – kwa sababu haamini majazi, au analewa kwa sababu haamini majazi?

Sasa narudia tena kuliweka wazi jambo hilo, labda kule hukulifahamu vizuri au umetaka kupotosha kwa kukusudia. Ninachokisema ni kuwa asili ya kuwepo itikadi za “Mungu ana mkono; mguu; macho n.k”, ni kuwa wenye itikadi hizi wanakanusha majazi, na kwa hivyo ulipotajwa mkono, basi wao wakaufasiri kuwa ni mkono kweli kweli; ulipotajwa mguu wakaufasiri kuwa ni mguu, n.k. Sasa je wewe hili unalipinga? Kama unalipinga tupe tafsiri ya maneno yako uliposema:

Kufanya is’rafu katika matumizi ya majazi ndani ya Qur’an, na kuzipotosha tafsiri za baadhi ya aya kwa madai kuwa kuna majazi…….7

……Na wengine wameona wauite “Usluubun min Asaalibil-Lugha” (utaratibu/mfumo katika taratibu za lugha) na njia hii ndiyo iliyokaribu na usahihi, ili kuwazuia watu wa batili wasiyapotoshe maandiko kwa kuupitia mlango huu. 8

Sasa kabla sijazungumza nilioyakusudia katika sura hii, ni vyema kwanza nikakunukulia nilioyasema katika kitabu changu kisha tuinukuu jawabu kamili ya Sh. Kasim Mafuta aliyonijibu ili tuweze kufikia natija sahihi. Katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu nilisema:

Sababu kubwa na chanzo cha Mawahabi kuwa na itikadi hizi za kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe, wakasema kuwa Mwenyezi Mungu ana mikono, miguu, uso, macho, anakwenda kwenye ardhi, anacheka, anakaa kitako kweli kweli, aliegemeza mgongo wake kwenye jabali huku akiandika Taurati, n.k., ni tatu:9

1) Kuzikubali Hadithi Ahadi katika mambo ya itikadi.2) Kuchukua Hadithi za kutunga.3) Kukanusha kwao kuwepo kwa majazi katika lugha ya Kiarabu

na hasa hasa katika Qur-ani. Miongoni mwa walioandika kwa urefu na kukataa jambo hili ni Ibn Qayyim Al-Jawziyya.

7 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 37-38. 8 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 51. 9 - Tazama ukweli kwamba haya mengine katika kitabu changu hayamo kwani kitabu hicho nilikuwa tayari ninakitayarisha kwa ajili ya chapa ya pili. Kwa hivyo, kipengele (1-2) ni ziada ambayo katika kitabu Hoja Zenye Nguvu chapa ya kwanza havimo.

3

Katika kitabu hiki tutazungumzia sula la tatu la kukataa majazi. Maana ya “Majazi” ni kutumika kwa neno tafauti na maana yake ya asili. Kwa mfano neno: “Simba”. Neno hili linamaanisha aina maalumu ya mnyama wa porini. Na hii ndio maana yake ya asili. Lakini nikisema kuwa Ali ndio simba wa kijiji hiki, makusudio huwa sio yule mnyama wa porini, bali ni kuwa Ali ni shujaa wa kijiji hiki. Na hii ndio maana ya “Majazi”: kutumika neno kinyume na maana yake ya asili. Sasa wao Mawahabi wanakataa kuwa katika Qur-ani kuna majazi. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu aliposema:

أيديهم فوق الله يد

Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao 10

wao wakasema kuwa Mwenyezi Mungu ana mkono. Masikini hawa hawakuifahamu Qur-ani wala lugha ya Kiarabu iliotumika kuteremshiwa Qur-ani. Sasa kwanini basi wakasema kuwa Mwenyezi Mungu ana mikono miwili tu na Aya ziko ziliozoonesha kuwa mikono yake ni mingi zaidi ya miwili? Anasema Mwenyezi Mungu:

ماء بأييد بنيناها والسNa mbingu tumezijenga kwa mikono

(yetu, mingi zaidi ya miwili).11

Sasa tafsiri na iwe hivi “Mwenyezi Mungu ana mikono mingi zaidi ya miwili” kama Aya hii inavyosema. Na alipotaja mkono mmoja basi iwe kataja mmoja katika hio mingi na halkadhalika alipotaja miwili awe kataja miwili katika hio mingi. Lakini kwa mujibu wa Aya hii mikono yake ni mingi zaidi ya miwili. Sasa kama ni hivi kwanini tena waseme ana mikono miwili tu? Ukiniambia: “Lugha ya Kiarabu inatumika katika wingi (tatu na kuendelea) kumaanisha mbili, na mbili kumaanisha wingi (tatu na kuendelea) na moja kumaanisha wingi vile vile.” Nitakujibu kwamba:

a) Katika lugha ya Kiarabu pia unatumika mkono kumaanisha nguvu, neema, uwezo n.k., kama utavyoona humu.

b) Kama unakubali kwamba wakati mwengine moja hutumika kumaanisha nyingi, basi umejijibu mwenyewe kwani haya ndio majazi yenyewe unayoyakataa: kutumika neno kinyume na maana yake ya asili. Kwani kwa asili moja ni moja; ikitumika kumaanisha tatu basi imetumika kinyume na maana yake ya asili.

10 - Sura ya 48 Aya ya 10. 11 - Sura ya 51 Aya ya 47.

4

Lakini haya yote yanatujuilisha kwamba hawa watu Mwenyezi Mungu hakuwapa nuru hata kidogo ya kukifahamu Kitabu chake. Sasa ukitaka kujua kwamba neno mkono katika lugha ya Qur-ani hutumika si kwa maana ya mkono wa kweli, soma Aya hizi zinazofuata kisha tia akilini, utafakari, uzingatie na kujiuliza je mkono uliotajwa katika Aya hizi ni mkono wa kweli. Anasema Mwenyezi Mungu:

البسط كل تبسطها وال عنقك إلى مغلولة يدك تجعل وال Wala usiufanye mkono wako kuwa wenye kufungwa

kwenye shingo yako wala usiukunjue wote.12

Je neno mkono hapa ni mkono wa kweli au maana yake ni kuwa usifanye ubakhili wala usifanye israfu? Kama ni mkono kweli kweli ndio uliokusudiwa hapa, basi mbona wenye kukataa majazi hawaendi na huku mikono yao ipo kati na kati tu baina ya shingo na kuikunjua yote?

Na anasema Mwenyezi Mungu:

األيد ذا داوود عبدنا واذكر Na mkumbuke mja wetu Dawud mwenye

mikono (mingi, yaani mwenye nguvu).13

Sasa je neno mikono hapa maana yake ni mikono hii ya viungo? Kama ndio basi Nabii Dawud alikuwa na mikono zaidi ya miwili kwa sababu Aya inasema األيد ذا (mwenye mikono mingi zaidi ya miwili). Bali hapa mikono maana yake ni nguvu.

Na akasema Mwenyezi Mungu katika Qur-ani:

واألبصار األيدي أولي ويعقوب وإسحق إبراهيم عبادنا واذكر

Na wakumbuke waja wetu Ibrahim, na Is-haq na Ya’aqub wenye mikono na macho.14

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu anamtaka Mtume wake (s.a.w.) awazingatie Mitume hao kwa sababu Mwenyezi Mungu kawapa mikono na macho. Sasa kwani sisi hatuna mikono na macho? Kwa hivyo, ni wazi kwamba mikono hapa maana yake ni nguvu; na macho maana yake ni busara na uwezo mkubwa wa kutazama mambo, kuyatafakari na kuyafahamu mambo hayo pamoja na hekima.

12 - Sura ya 17 Aya ya 29. 13 - Sura ya 38 Aya ya 18. 14 - Sura ya 38 Aya ya 45.

5

Kwa hivyo, mkono wa Mwenyezi Mungu maana yake ni nguvu za Mwenyezi Mungu: si kiungo kama wanavyosema baadhi ya watu. Na hivi ndivyo lugha ya Kiarabu inavyosema. Anasema babu yake Mtume (s.a.w.) wakati Mtume (s.a.w.) alipopotea katika mji wa Makka alipokuwa mdogo. Babu yake Mtume aliimba mashairi haya :

*** يدا لي اجعله و ربي اردده محمدا ولدي علي ردNirejeshee (é Mwenyezi Mungu) Muhammad

mwanangu**Mrejeshe é Mola wangu na umfanye kuwa mkono wangu.15

Sasa jiulize wewe vipi Mtume (s.a.w.) afanywe kuwa mkono wa babu yake? Ni wazi kwamba hapa babu yake Mtume anamuomba Mwenyezi Mungu amfanye Muhammad (s.a.w.) kuwa ni sababu ya yeye kupata nguvu au awe ni neema kwake.

Kwa kufahamu zaidi kuwepo kwa majazi katika Qurani soma Aya hii:

األسود الخيط من األبيض الخيط لكم يتبين حتى واشربوا وكلوا Aya hii inahusu mwezi wa Ramadhani, anasema Mwenyezi Mungu katika Aya hii:

Na kuleni na kunyweni mpaka ukubainikieni uzi mweupe kutokana na uzi mweusi. 16

Sasa tunawauliza wanaokataa majazi je nyuzi hizi mbili nyeupe na nyeusi zilizotajwa katika Aya hii ni nyuzi za kweli? Jawabu ni kuwa hizi si nyuzi za kweli kama za kushonea nguo, bali uzi mweupe ni kuchomoza kwa alfajiri sahihi ambayo huanza weupe katika upeo wa mashariki na uzi mweusi ni kiza cha usiku. Na kwa maana hio neno nyuzi katika Aya hii si hakika bali ni majazi (mithali). Hii ni Aya ambayo mmoja wa sahibu zangu alimtolea mtu mmoja anayekanusha majazi, na ikawa hana jawabu.

Al-Imamu Nur Al-Din Al-Salimi (r.a.) alipokuwa akizungumzia habari ya majazi, alisema kwamba Abu Tammam katika washairi wa zamani alitoa ushairi wake akasema: ةبآكال اءم ينقست ال (usininyweshe maji ya huzuni). Ikawa kuna mtu pale katika wanaopinga majazi. Akasema yule mtu kumwambia Abu Tammam: “Haya nipe hio gilasi yako nikutilie maji ya huzuni”. Yaani anakusudia kumwambia “Tangu lini wewe umesikia kwamba huzuni inanywewa?” Abu Tammam akamjibu yule mtu akamwambia: “Haya huu mkasi nikatie bawa lako la udhalili”. Abu Tammam naye anakusudia kumjengea hoja kwa kutumia Aya inayosema: “Na wainamishie (wazazi wako wawili) bawa la udhalili.”17 Yaani je

15 - Tumetaja marejeo huko mbele. 16 - Sura ya 2 Aya ya 187. 17 - Al-Imamu Al-Salimi: Tal’atu Al-Shams j.1 uk. 206.

6

bawa hapa ni bawa la kweli, na tangu lini na wapi umesikia kwamba mtu ana bawa? Kama si bawa basi elewa kwamba haya yote ni katika majazi ya lugha ya Kiarabu.

Na mimi siku moja nilijadiliana na hao wenye kukataa majazi. Nikamwambia yule bwana kama wewe unakataa majazi hebu soma Aya hii:

الله بحبل واعتصموا جميعاNa kamataneni na kamba ya Mwenyezi

Mungu kwa pamoja18

Nikamwambia haya niletee hio kamba ya kweli kweli ya Mwenyezi Mungu tukamatane nayo. Ikawa hana jawabu isipokuwa kuniambia: “Maudhui hii inahitaji utafiti”. Sasa tazama je kamba hapa katika Aya hii ni kamba ya kweli? Kila mtu anajua kuwa kamba hapa maana yake ni dini: si kamba ya kufungia ng’ombe. Sasa ikiwa umeyafahamu haya basi elewa kuwa makusudio ya mkono wa Mwenyezi Mungu ni nguvu zake. uso ni Dhati Yake, au katika sehemu nyengine limetumika neno uso kwa maana ya radhi zake. Macho kwa maana ya hifadhi yake. Na hivyo hivyo kila kitu kinafasiriwa tafsiri inayokubaliana na sifa za Mwenyezi Mungu.19

Hayo ndio nilioyasema katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu. Sasa natusome maelezo ya Sheikh Kasim Mafuta katika jawabu alionijibu.

JAWABU NILIOPATA KUTOKA KWA SH. KASIM MAFUTA

Anasema Sheikh Kasim bin Mafuta:

UCHAMBUZI YAKINIFU JUU YA SUALA LA MAJAZI

18 - Sura ya 3 Aya ya 103. 19 - Juma Al-Mazrui Hoja Zenye Nguvu uk. 32-36.

7

Ama madai ya kwamba umma umeingia katika upotevu kwa sababu ya kuitakidi kuonekana Allah kwa macho huko akhera ni madai batili kwa hoja tutakazo zitoa katika kitabu chetu hiki Inshaallaah. Na ama kuitakidi kwamba kuna waislamu ambao wataingia motoni kisha watatoka kwa sababu ya shafaa (uombezi):

Suala hili limethibiti kwa hoja zenye nguvu katika kitabu (Qur’an) na sunna sahihi za bwana Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam-.

Ama madai yake ya uwongo kuwa suala la kupinga kuwepo kwa majazi ndani ya Qur’an kuwa ndiyo chanzo cha kupotea watu, 20 ufafanuzi wake ni kama ufuatavyo:

Suala la kuwepo majazi na kutokuwepo kwake katika Qur’an na lugha ya kiarabu ni jambo ambalo maulamaa wametofautiana tangu zamani kama walivyotofautiana katika mambo mengine.

Ndugu Juma Al-Mazrui katika kitabu chake “Hoja zenye Nguvu” ukurasa wa 32 amefanya jaribio la kutaka kuuficha ukweli huo ambao uko wazi tena mbele ya macho yake na akafanya upotoshaji kwa makusudi dhidi ya watu anaowaita Mawahabi (akiwa ana wakusudia Ahlu sunna wal Jamaa) kwa kudai kwamba watu hao wamepotea, na chanzo cha upotevu wao huo ni kukanusha kuwepo kwa majazi katika lugha na Qur’an. Amesema ndugu Juma al Mazrui baada ya kichwa cha habari kisemacho:

CHANZO CHA KUTUMBUKIA KATIKA ITIKADI BATILI

Kisha akasema:

“Sababu kubwa na chanzo cha Mawahabi kuwa na itikadi hizi za kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe, wakasema kuwa Mwenyezi Mungu ana mikono, miguu, uso, macho…ni kukanusha kwao kuwepo kwa majazi katika lugha ya kiarabu na hasa hasa katika Qur’an. Miongoni mwa walioandika kwa urefu na kukataa jambo hili ni Ibn Qayyim Al-Jawziyya katika kitabu chake Mukhtasar Al-Sawaaiq Al Mursala….

Na maana ya “majazi” ni kutumika neno tafauti na maana yake ya asili…

Sasa wao Mawahabi wanakataa kuwa katika Qur’an kuna majazi”. Mwisho wa kunukuu.21

Kisha baada ya Sheikh Kasim kuyanukuu hayo, akajibu kwa kusema:

20 - Tazama mtu anavyopotoa maudhui huyo! Mimi ninasema kitu chengine na yeye anasema kitu chengine!21 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 38-39.

8

Majibu yetu yatakuwa katika nukta tatu:Nukta ya kwanza:Ni kuhusu maelezo yake kuhusu neno “Majazi”, kwa ufupi ni kwamba maelezo ya Juma kuhusu majazi yana upungufu alitakiwa aseme hivi: “Majazi ni kutumia neno katika isiyokuwa maana yake ya asili pamoja na kuwepo dalili inayozuia kukusudiwa maana yake ya asili kwa mafungamano ambayo yapo baina ya neno la asili na neno ambalo si la asili”. Kwa sababu ili maneno yawe ni majazi, ni lazima masharti matatu makuu yatimie, nayo ni:1-Kutumika neno katika isiyo kuwa maana yake ya asili.2-Lazima kuwepo na “QARINATUN MAANI’ATUN MIN IRADATI MA’ANAL ASLIY” dalili yenye kuzuia kukusudiwa maana ya asili.3-Lazima kuwepo na “ALAAQAH” mafungamano baina ya neno la asili na neno lisilo la asili.

Na likikosekana sharti moja kati ya haya matatu tuliyoyataja basi hakutakuwa na majazi na atakayedai kuwa ni majazi basi huyo ni mwongo mkubwa na hajui lugha ya kiarabu.22 Kwa mfano nikisema: “Nimemuona Simba anamla Swala”. Kwa mujibu wa misingi ya lugha ya kiarabu neno “Simba” hapa limetumika katika maana yake ya asili. Kwa sababu katika maneno haya hakuna: “QARINATUN MAANI’ATUN MIN IRADATI MA’ANAL ASLIY” dalili yenye kuzuia kuikusudia maana ya asili.

Na yanapotamkwa maneno hayo kila mwenye kusikia atakuwa ameelewa moja kwa moja kwamba simba aliyekusudiwa hapo ni simba mnyama mkali wa porini na wala si vinginevyo. Lakini mtu akisema; “nimemuona simba kwenye uwanja wa mapambano ameshika upanga”. Bila shaka hakuna atakayedhania kwamba simba aliyekusudiwa hapa ni yule mnyama pori, na sababu iliyozuia mtu asidhanie hivyo ni kauli ya msemaji; “ameshika upanga” maana simba asili hawezi kushika upanga, bali huyo ni mtu shujaa aliyefananishwa na simba kwa sababu ya ushajaa wake. Kwa hiyo kusema tu; kwamba majazi ni kutumia neno tafauti na maana yake ya asili, ni makosa kwa sababu tulizozitaja.23

JAWABU

Kwa kuanzia natutazame maneno yako uliposema:

22 - Kumbe wewe lugha unaijua na majazi umeyaelezea vizuri na ukatoa natija kwamba asiyesema hivyo huyo ni mwongo mkubwa: hajui lugha. Kisha wewe ukageuka ukayapinga majazi! Hii ni ajabu ilioje! 23 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 40-41. Tena Sheikh wewe majazi unayajua vyema, na umeyaelezea hapa kwa ulimi wa kalamu yako, halafu ukageuka na kuisapoti kauli ya wanaokanusha majazi!

9

Ama madai ya kwamba umma umeingia katika upotevu kwa sababu ya kuitakidi kuonekana Allah kwa macho huko akhera ni madai batili kwa hoja tutakazo zitoa katika kitabu chetu hiki Inshaallaah.

Na ama kuitakidi kwamba kuna waislamu ambao wataingia motoni kisha watatoka kwa sababu ya shafaa (uombezi):

Suala hili limethibiti kwa hoja zenye nguvu katika kitabu (Qur’an) na sunna sahihi za bwana Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam-.

Ninasema: kwamba maelezo juu ya vipengele hivi yatakuja in shaa Allah katika juzuu zenye kuzungumzia mas-ala ya kuonekana au kutoonekana kwa Allah; kama vile ambavyo maelezo juu ya suala la pili mahala pake ni juzuu inayohusu mas-ala ya kutoka au kutotoka motoni ambayo umedai kwamba Qur-ani imesema kwamba watu watatoka motoni. Lakini mukhtasari ninaotaka kukwambia hapa ni kuwa hii Qur-ani ipo kuanzia Suratu Al-Fatiha hadi Suratu Al-Nasi tuoneshe Aya moja tu iliosema kuwa watu watatoka motoni. Na ukituonesha basi mimi ni wa mwanzo kuwa Wahabi! Maelezo kwa urefu yatakuja katika sehemu yake in shaa Allah.

Ama maneno yako yasemayo:

Ama madai yake ya uwongo kuwa suala la kupinga kuwepo kwa majazi ndani ya Qur’an kuwa ndiyo chanzo cha kupotea watu, 24 ufafanuzi wake ni kama ufuatavyo:

Suala kuwepo majazi na kutokuwepo kwake katika Qur’an na lugha ya kiarabu ni jambo ambalo maulamaa wametofautiana tangu zamani kama walivyotofautiana katika mambo mengine.

Ninasema: maelezo juu ya kipengele cha kwanza nimeshayatoa kwamba hivyo sivyo nilivyosema. Ama kuhusu kipengele cha pili jawabu ni kuwa mazingatio hayapo katika kutafautiana kwa Maulamaa, bali mazingatio yapo katika usahihi wa dalili zilizotolewa. Ama lau kama Maulamaa wakitafautiana ndio jambo linazingatiwa basi kwanini tena tujibizane? Hayo yote, lau tafauti hio ilikuwa ni katika kauli zenye Maulamaa wengi, lakini leo kauli ya kukataa majazi ni kauli shaadh walioisema ni watu wachache hata wengine wakafika kusema:

24 - Tazama mtu anavyopotoa maudhui huyo! Mimi nasema kitu chengine na yeye anasema kitu chengine!

10

Majazi yapo katika lugha ya Waarabu kwa mujibu wa jumhur ya wanavyuoni, na akapinga Abu Is-haaq Al-Isfaraaini,25 na kupinga kwake huku kunatoa dalili tosha kwamba hakuichungulia lugha ya Waarabu, na kunatoa tangazo kwa sauti ya juu kabisa kwamba sababu ya tafauti (yake) hii ni kupitwa kwake na kuyasoma yale ambayo yanatakiwa ayasome katika lugha hii tukufu na yale yaliomo ndani yake miongoni mwa hakika na majazi ambayo hayajifichi hata kwa mwenye maarifa machache kabisa. Na (Abu Is-haaq huyo) ametoa ushahidi kwa (hoja) ambazo ni dhaifu kuliko nyumba ya buibui.26

Anasema Al-Qannubi:

Na miongoni mwa dalili za wazi juu ya udhaifu wa fahamu za watu hawa na uchache wa maarifa yao kwa Kitabu cha Allah Mtukufu na Sunna za Mtume wake (s.a.w.) na lugha ya Waarabu, ni kuyakanusha kwao majazi katika Kitabu (cha Allah) na Sunna za Mtume wake (s.a.w.) na lugha ya Kiarabu, pamoja na kuwa Umma umekaribia kukubaliana katika kuyathibitisha na wala hakuna aliyepinga isipokuwa wale walio shaadh (wachache waliopwekeka na kauli hio).27

Anasema Al-Suyuti: “Anayejingikiwa na majazi basi huyo yuko mbali na daraja ya (wenye) kufahamu; na upumbavu umemmaliza”.28 Kwa hivyo, kinachozingatiwa ni dalili: si ikhtilafu. Na dalili za kuwepo kwa majazi hazihitaji kusoma hata nusu kitabu; bali mtu yoyote, mwanachuoni na mtu wa kawaida, anazijua.

Ama tukirudi katika mas-ala ya taarifu (definition) nilioitoa. Ninamwambia Sheikh wetu Kasim bin Mafuta kwamba mwenye kutoa taarifu (definition) anapokusudia kuonesha mahiyya (kiini) ya kitu basi mara nyingi huwa anachukua kile kitu cha msingi tu. Na anapotoa Al-Ta’arifu bil-haddi (normative definition) ndio anakuwa anataja kiini na masharti yake.29 Na mimi katika kitabu changu sikukusudia kusomesha watu somo la balagha; 25 - Sahihi ni “Al-Asfarayiini”. 26 - Al-Shaukani Irshaadu Al-Fuhuul uk . 35. Lakini pamoja na hayo, Al-Imamu Al-Qannubi kanukuu maneno ya Imamu Al-Haramain katika kitabu chake Al-Talkhis akisema: “Kinachodhaniwa kwa Al-Ustaadh (Abu Is-haaq) ni kuwa hilo (la kukanusha majazi) halikuthibiti kutoka kwake”. Anasema Al-Qannubi: “Na vivyohivyo Al-Imamu Al-Ghazali kakanusha kunasibishwa kauli hio kwa Al-Ustaadh (Abu Is-haaq)”. Tazama Al-Qannubi Al-Saifu Al-Haad uk. 55. 27 - Tazama Al-Qannubi Al-Saifu Al-Haad uk. 55. 28 - Al-Suyuti Tarzu Al-’Imama nukulu kutoka katika kwa Al-Qannubi Al-Saifu Al-Haad uk. 56. 29 - Lakini ikiwa unataka lazima nitoe hio taarifu ulioitoa wewe, basi ungerudia kitabu changu Hali Sahihi Ya Kimaumbile uk. 14, ungeipata hio taarifu unayoitaka wewe. Huko nilisema kwamba majazi ni:

11

bali nilikusudia kuonesha kiini cha maudhui tu. Taarifu (definition) yangu niliposema “..na maana ya majazi ni kutumika neno tafauti na maana yake ya asili…” tayari imeshatoa kiini cha kile ninachotaka kukielezea. Ama mas-ala ya qarina na ‘Alaqa, hayo ni masharti ya majazi: si kiini cha majazi. Na kwa hivyo, usistaajabu wewe kuona kwamba hata wale wakuu wetu wanapotaka kuonesha kiini tu cha majazi nao hutoa taarifu (definition) kama hio nilioitoa mimi. Anasema Al-Imamu Al-Suyuti: “…Kwani majazi ni kulitumia neno kinyume na maahala pake”.30 Na anasema: “..Na majazi ni kuwa (mtu) akusudie kwayo kinyume cha maudhui yake (maana yake ya asili) kwa matumizi na kuleta maana”.31 Anasema: “Majazi katika neno pweke,32 na pia huitwa majazi ya kilugha, nayo ni kuitumia lafdhi pasina pale ilipowekwa mwanzo (kinyume na matumizi ya asili)”.33 Anasema Al-Imamu Al-Shaukani baada ya kutaja taarifu (definition) kama alioitaja Sheikh Kasim Mafuta: “Na ikasemwa kwamba (majazi) ni lafdhi iliotumika kinyume na mueko wake wa mwanzo kwa namna inayofaa”. 34 Na wengine wakasema kwamba majazi “Ni yalio kinyume cha hakika”.35 Anasema Al-Imamu Abu Is-haaq Al-Shirazi: “Ama Majazi, taarifu (definition) yake ni lile (neno) lililoondolewa kutoka katika ile (maana) ilioekewa”.36 Anasema Al-Amidi: “Na ukiwa unataka taarifu (definition) kwa njia yenye kuzikusanya zote (hizo) basi utasema: ‘Ni lafdhi yenye kujiweka katika matumizi yake au yenye kutumika kinyume na vile ilivyowekewa mwanzo katika fani ambayo kwayo kuna kusemezana kwa sababu ya ule uhusiano uliopo baina yake”. Utaona kwamba taarifu (definition) hii imelitoa neno qarina wakati taarifu (definitions) zilizotangulia zimelitoa neno qarina pamoja na neno ‘alaaqa. Anasema Al-Mamu Nuru Al-Din Al-Salim (r.a.):

** المتسع المجاز فهو مستعمال وضع له ما غير في يكن وإنNa ikiwa (lafdhi) kinyume na ilivyoekwa**Hayo ni

المعنى و الحقيقي المعنى بين رابطة لعالقة له وضع ما غير في استعمل لفظالحقيقي المعنى إرادة من مانعة قرينة مع المجازي

“(Majazi ni) neno ambalo limetumiwa kinyume na maana yake ya uhakika kwa kuwepo uhusiano wenye kufungamanisha baina ya maana ya uhakika na maana ya kimajazi, pamoja na kuwepo kifuatanishi cha maneno (context) chenye kuizuia maana ya uhakika”. Sheikh Kasim bin Mafuta ikiwa unataka lazima usome maelezo haya kutoka kwangu, basi rejea hicho kitabu changu nilichokutajia utayapata maelezo hayo. Lakini mimi sioni kwamba kuna ulazima wa kusema hivyo wakati wowote kama vile ambavyo wanavyuoni hawaoni ulazima huo wakati wowote. 30 - Al-Suyuti Al-Itqan j. 3, uk. 84. 31 - Al-Suyuti Al-Itqan j. 3, uk. 86. 32 - Al-Mufrad yaani neno lilopekeyake ambalo halikutegemezwa na jengine. 33 - Al-Suyuti Al-Itqan j. 3, uk.72. 34 - Al-Shaukani Irshaadu Al-Fuhuul uk . 33.35 - Al-Shaukani K.h.j.36 - Abu Is-haaq Al-Shirazi Al-Luma’a uk. 37.

12

majazi yenye kutoa nafasi, hivyo ikitumika.

*** وعل أصله عن تصرفه قرينة تكشفه قوشرطه ةNa sharti yake ni qarina yenye kuitoa**kutoka Asili yake; na mfungamano unaiweka wazi.37

Anasema katika Sherehe:

Majazi ni lafdhi iliotumika kinyume na ile maana ilioekewa kwa ajili ya kuwepo alaqa na qarina…..na alaqa na qarina ni masharti mawili ya majazi.38

Sasa baada ya haya, ninachotaka kumueleza Sheikh wangu Bwana Kasim bin Mafuta ni kuwa:

1) Unapotaka kuwasomesha watu somo la balagha basi ni lazima utoe hio taarifu ulioitoa wewe.

2) Ukitaka kutoa Al-Taarifu bil-haddi (normative definition) basi ni lazima utoe hio taarifu ulioitoa wewe.

3) Ikiwa lengo lako ni kuonesha msingi tu wa kitu na kiini chake, basi unatoa taarifu kama nilioitoa mimi.

4) Wakuu wetu kadha wa kadha wametoa taarifu kama hio nilioitoa mimi, kwa sababu hio niliokueleza.

5) Maneno qarina na ‘alaaqa si nguzo za taarifu ya majazi, bali ni masharti ya majazi. Na ndio maana ukaona kwamba wakati mwengine – kama nilivyokunukulia kauli tafauti – wanavyuoni huwa hawayataji maneno hayo kamwe.

6) Tafautisha baina ya kiini au nguzo za kitu na masharti yake.

Baada ya hayo, utaona makosa aliyoyatenda Sheikh Kasim mwana wa Mafuta aliposema: “Kwa hiyo kusema tu; kwamba majazi ni kutumia neno tafauti na maana yake ya asili, ni makosa kwa sababu tulizozitaja”.39 Tunasema: kusema hivyo si makosa, isipokuwa ukiongeza unakuwa umetaja masharti ya majazi: si kiini na msingi wa majazi. Kwa lugha nyengi ukiongeza unakuwa umeweka wazi zaidi. Ama ibara “Majazi ni kulitumia neno kinyume na maana yake ya asili” ni ibara ambayo tayari imeshajuilisha majazi ni nini, na kwahivyo mara nyingi wajuzi wanaitaja hio tu kama ulivyoona nukulu zao, isipokuwa ukiwa unataka kuwasomesha watu somo la balagha basi hapo utalazimika kusema kama hivyo ulivyosema wewe – kitabu changu Hoja Zenye Nguvu hakikuwa kitabu cha somo la balagh.

37 - Al-Salimi Shamsu Al-Usul uk. 23. 38 - Al-Salimi Tal’atu Al-Shamsi j. 1, uk. 199. 39 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 41.

13

Na kwa ujumla ni kuwa kweli taarifu (definition) ulioitaja wewe ni sahihi. Lakini nayo pia ina kosa dogo katika kipengele cha tatu kisemacho: Lazima kuwepo na “ALAAQAH” mafungamano baina ya neno la asili na neno lisilo la asili. Nawe ulitakiwa useme: “Lazima kuwepo na “ALAAQAH” mafungamano baina ya maana ya asili ya neno lililotumika na maana isio ya asili, au useme “Lazima kuwepo na “ALAAQAH” mafungamano baina ya maana ya asili na maana isio ya asili. Ama neno ni moja lile lile: hakuna katika majazi neno la asili lililopelekwa katika neno lisilo la asili: neno ni moja lile lile limepelekwa katika maana nyengine isio ya asili.40

Pia kuna makosa ya kinahau katika kipengele cha pili kisemacho: “QARINATUN MAANI’ATUN MIN IRADATI MA’ANAL ASLIY”, nawe ulitakiwa useme: “QARINATUN MAANI’ATUN MIN IRADATI Al-MA’ANA AL-ASLIY”, au kwa njia yako ya uandishi useme: “……AL-MA’ANAL ASLIY”.

Ama mfano ulioutoa wa kusema: “Nimemuona Simba anamla Swala” pia si mfano unaozungumziwa na wanavyuoni wa kubainisha maana ya uhakika wa neno. Bali kinachozungumzwa ni kuwa neno “Simba” peke yake bila ya kuwa katika sentensi, basi maana yake ya asili ni mnyama wa pori. Na kwa hivyo, nikilitamka neno “Simba” peke yake, basi mtu asidai kwamba “Nakusudia shujaa” kwani maana ya asili ya simba si shujaa, bali ushujaa ni sifa yake tu. Ama nikisema “Ali ni simba”, basi hapa inaeleweka kwamba nimelitumia neno hilo kimajazi kwa njia ya tashbihun baligh kwani simba anaeleweka ni nani na Ali anaeleweka ni nani; kumwita huyu kwa jina la yule ni kulitumia neno kinyume na maana yake ya asili nayo ndio majazi yenyewe. Ama mfano huu: “Nimemuona Simba anamla Swala”, si mfano pambanuzi kwani:

a) Hata Ali naye anakula swala na inawezekana ikawa mtu kamkusudia yeye kwa sababu ya ushujaa wake kama simba; na akamkusudia Said kuwa ni swala kwa sababu ya udhaifu wake. Lakini kilichozuia hapo isizingatiwe maana hio ya kimajazi ni kukosekana kwa qarina: si muundiko wa ibara hio, ama ibara hio kama inavyobeba uwezekano wa hakika vivyo hivyo ndivyo inavyebeba uwezakano wa majazi; kwani kama inavyojuzu kumwita ‘Ali kuwa ni simba kwa sababu ya ushujaa wake ndivyo inavyowezekana kumwita Said kuwa ni swala kwa sababu ya udhaifu wake, na kwa mantiki hio ibara ulioitoa ewe Sheikh wetu Kasim bin Mafuta si mfano sahihi

40 - Lakini haya hayana umuhimu mkubwa kwani hayana athari katika tafsiri. Umuhimu uko katika suala je majazi yapo au hayapo? Hili ndio muhimu.

14

katika maudhui hii, kwani kama hapo kumekosekana لفظية قرينة(qarina ya matamshi) jambo ambalo limepelekea kuyazingatia maneno hayo katika uhakika wake; basi elewa kwamba inawezekana ikapatikana حالية itayopelekea kuzingatiwa (qarina ya hali) قرينةibara hio hio kuwa ni majazi. Kwa hivyo, elewa kwamba kilichozuia hapo kuileta maana ya kimajazi si maneno “Anakula swala” kama ulivyodhania wewe, bali ni kwa sababu neno simba ni uhakika wa kitu fulani na hakuna kilichoutoa uhakika huo na kuupeleka katika maana nyengine.

b) Pili: ni kuwa tukijaalia kwamba huo mfano wako ni sahihi, na kwamba hivyo ulivyosema wewe ni sahihi, basi hii ina maana kwamba kilichosababisha kuyazingatia maneno “Nimemuona Simba anamla Swala”, kuwa yapo katika uhakika wake itakuwa ni hio qarina ulioitaja “anamla swala”; na sisi maudhui yetu ni qarina iliolitoa neno kutoka katika maana ya uhakika na kulipeleka katika maana ya kimajazi; si kulitoa neno katika maana ya kimajazi na kulipeleka katika maana ya uhakika au qarina iliolibakisha neno katika maana yake ya asili, kwani hakika ndio asili na kwa hivyo haihitaji qarina.

Ama kauli yako uliposema kuhusu qarina:

…..2-Lazima kuwepo na “QARINATUN MAANI’ATUN MIN IRADATI MA’ANAL ASLIY” dalili yenye kuzuia kukusudiwa maana ya asili.…………Lakini mtu akisema; “nimemuona simba kwenye uwanja wa mapambano ameshika upanga”. Bila shaka hakuna atakayedhania kwamba simba aliyekusudiwa hapa ni yule mnyama pori, na sababu iliyozuia mtu asidhanie hivyo ni kauli ya msemaji; “ameshika upanga” maana simba asili hawezi kushika upanga, bali huyo ni mtu shujaa aliyefananishwa na simba kwa sababu ya ushajaa wake.41 Kwa hiyo kusema tu; kwamba majazi ni kutumia neno tafauti na maana yake ya asili, ni makosa kwa sababu tulizozitaja.

Ninasema: dhahiri ya kutaja kwako mfano huo usemao:

..Na sababu iliyozuia mtu asidhanie hivyo ni kauli ya msemaji; “ameshika upanga” maana simba asili hawezi kushika upanga, bali huyo ni mtu shujaa aliyefananishwa na simba kwa sababu ya ushajaa wake.

41 - Jamani! Mtazameni huyu mtu anayekanusha majazi jinsi anavyoyachambua! Japo kuwa hukoseakosea katika vijipengele vidogo vidogo lakini msingi wa majazi kauelezea vizuri! Halafu akageuka kama siye, akayakanusha!

15

Maneno hayo ni sahihi kabisa, lakini ningependa kuongeza kitu kimoja, nacho ni kuwa maneno hayo yanamfanya asiyejua adhanie kuwa qarina siku zote inakuwa lafdhiyya tu au maqaaliyya (iliotajwa katika maneno ya msemaji); ilhali si mara zote hali inakuwa hivyo; bali wakati mwengine qarina inakuwa haliyya (inayofahamika tu katika maneno ya msemaji au hali yake pasina kutamkwa) na mara nyengine qarina inakuwa ‘aqliyya (ya kiakili).42 Na hizi zina njia nyingi mno ambazo kuzijua kwake kunategemea zaidi uwezo wa mtu wa kuifahamu lugha. Kwa mfano nikisema “Ali ni punda” hapa hutoona katika maneno haya qarina lafdhiyya iliolitoa neno punda kutoka katika maana yake ya asili au iliopelekea kutokumzingatia Ali kuwa ni punda wa kweli isipokuwa ukweli kwamba Ali na punda ni

ووضعا عرفا متغايراتان ni vitu viwili tafauti kikawaida na) حقيقتانkimuweko wao wa asili ya kilugha). Yaani nikisema “punda” anafahamika mnyama anayepandwa na kupakiwa mizigo, wakati nikisema Ali inajulikana kwamba namkusudia mtu. Na hapa hakuna qarina ya matamshi iliomtoa punda kutoka katika maana ya asili au kumfanya Ali kuwa si punda wa kweli isipokuwa kile kinachojulikana katika kawaida zetu kwamba huyu si yule na yule si huyu – ni hakika mbili tafauti. Sasa vipi tena nidai kuwa huyu ni yule. Hapa inaeleweka kwamba hayo ni madai ya kimajazi kwa njia ya tashbih (kukifananisha kitu kimoja na chengine). Ninasema: na kwa njia hii na ilio mfano wa hii ndio tunakanusha kuwa Allah ana mkono, uso n.k, kwani mkono – kwa mfano – uhakika wake wa kilugha unajulikana. Tulipojua kwa yakini kwamba uhakika wake wa kilugha hauwiyani na utukufu wa Allah, basi tumejua kwamba neno mkono wa Mungu limetumika kinyume na maana yake ya asili na kwa hivyo ni majazi ambayo ni wajibu kupewa maana inayowiyana na utukufu wa Allah.

Na mfano wa majazi ambayo qarina yake ni ‘aqliyya ni kama Aya isemayo: بالغيب ورسله ينصره من الله وليعلم (Na ili Allah amjue yule

atayemnusuru Yeye na Mtume wake katika hali ya ghaibu).43 Hapa kuna majazu hadhfi (majazi ya kuondoshwa kwa neno). Neno hilo lililoondoshwa ni neno dini, na maana ni “Na ili Allah amjue yule atayeinusuru DINI YAKE na Mtume wake katika hali ya ghaibu”, vyenginevyo hakuna mtu anayeweza kumnusuru Allah mwenyewe. Utaona kwamba hapa kuna majazi na wala hakuna qarina lafdhiyya iliotajwa ambayo imetujuilisha sisi kuwepo kwa majazi hayo isipokuwa kile kinachofahamika kiakili kwamba kiumbe hawezi kumnusuru Allah au kwa usahihi zaidi kwamba Allah mwenyewe yaani dhati yake hainusuriwi. Na kwa hivyo, qarina hapa ni ‘aqliyya. Maelezo haya yanakupa picha kwamba si kila mtu anaweza

42 - Tazama Dr. Wahbat Al-Zuhaili Usulu Al-Fiqhi j. 1, uk. 288. 43 - Sura 57, Aya 25.

16

kuyafasiri maandiko ya Kisharia, bali mwenye uwezo huo ni mtu alikusanya mambo mawili: elimu na kipaji – yote mawili kwa pamoja: si moja peke yake.

Kwa hivyo, qarina inaweza kutajwa kama wewe ulivyotoa mfano wa maneno: “simba kashika upanga” na inawezkana isitajwe lakini ikafahamika katika maneno kwa sababu kitu kimoja kimepewa jina la kitu chengine ilhali vitu viwili hivyo katika lugha vina uhakika tafauti kama vile: punda na Ali; Ali na jiwe; mkono na Mungu n.k., au kwa sababu udhahiri wa kilichotajwa ni kinyume na akili ya binaadamu.

Anaendelea Sheikh Kasim bin Mafuta kwa kusema:

Nukta ya pili; Sina shaka kuwa ndugu Juma na wengineo katika watu wa bid’a wanapokuwa wanataja neno; “Mawahabi” huwa wanawakusudia AHLU SUNNA WAL-JAMAA, nao ni wale ambao wanaziunga mkono hoja na dalili na kazi ya daawa alioifanya Sheikhul Islaam 44 Muhammad bin Abdul Wahaab ambaye amezaliwa mwaka 1115 H na kufariki mwaka 1206 H. Swali, Je ni kweli kwamba hao ambao ndugu Juma anawaita mawahabi ndio wanaopinga majazi? Maulamaa ambao wanapinga kuwepo kwa “Majazi” wako katika makundi mawili:a) wanaopinga kuwepo kwa majazi katika lugha na Qur’an.b) wanaopinga kuwepo kwa majazi katika Qur’an tu.a) Hawa wafuatao ni baadhi ya maulamaa waliopinga kuwepo kwa majazi katika lugha ya kiarabu na halikadhalika katika Qur’an:

44 - Huyu naye pia ni Sheikhul-Islam! Kaka yake anashuhudia kwamba hakuwa mwanachuoni kamwe. Kamrudi vikali sana na akamwambia: “Ufahamu wenu nyinyi bado hauzingatiwi (kwani hamuna elimu)”. Al-Sawaa’iqu Al-Ilaahiyya uk. 16. …. “Ninyi mumechukua fahamu zenu na mukafarikiana na kundi la waliowengi na mukaukafirisha umma wote wa Muhammad”. Uk. 17. ….. “Lau muliizingatia ibara hii vizuri basi mungelijua kwamba nyinyi mumeifasiri kinyume na maana yake…..kisha munadai kwamba maneno yenu na ufahamu wenu nyinyi ni makubaliano!” Uk. 21. … “…..mfano wa mtu kama nyinyi hawezi kufanya istimbat (hawezi kutoa hukumu kutoka katika Qur-ani na Hadithi) wala hawezi kufanya qiyas..” Uk. 34. …. “Hakika leo watu wamepata mtihani wa mtu anayejinasibisha na kufuata Qur-ani na Sunna (yaani ndugu yake Muhammad Abdil-Wahhab), na anatoa (hukumu) kutoka katika elimu zake wala hajali nani anakwenda kinyume naye. Na lau utamtaka awaoneshe maneno yake wanavyuoni basi hawaoneshi, bali anawalazimisha watu wachukue kauli yake na ufahamu wake na anayempinga yeye humwita kafiri…NAYE HANA HATA SIFA MOJA YA WATU WA IJTIHAD BALI (HANA HATA SIFA) MOJA KATIKA KUMI..LAKINI HUYAPIGIA DEBE MANENO YAKE KWA WAJINGA WENGI…”. Uk. 9. Hayo ni maneno ya Sheikh Sulaiman bin Abdil-Wahhab anamwambia ndugu yake Muhammed Abdul-Wahhab. Maelezo yake ni mengi, rejea kitabu hicho Al-Sawaaiqu Al-Ilahiyyya. Bali Al-Albani anashuhudia kwamba Muhammed Abdul-Wahab alikuwa hana elimu ya Hadithi kamwe. Bali vitabu vyake vinajishuhudisha hivyo, kwani ni vitabu visivyo na elimu kabisa hata mwanafunzi wa thanawi (sekondari) anaweza kuvitunga! Haya twendeni!

17

1- Imamu Abu Is’haaq Ibrahim bin Muhammad bin Mih’raan Al- Is’fraayiiniy Al-Shaafiy aliyefariki mwaka 418 H.2- Imamu Abu Aliy Al Hassan bin Ahmad bin Abdil-Ghaffaar Al-Fasawiy aliyefariki mwaka 377 H.3-Sheikhul Islaam Abul Abbaas Ahmad bin Abdul-Haliim Ibn Taymiyyah aliyefariki mwaka 728 H.4-Shamsud Din Abu Abdillahi Muhammad bin Abi Bakar mashuhuri kwa jina la Ibnul Qayyim al Jawziyyah aliyefariki mwaka 751 H.b) Na hawa wafuatao ni maulamaa ambao wamepinga kuwepo kwa majazi ndani ya Qur’an tu, lakini wakathibitisha kuwepo kwake katika lugha ya kiarabu:1-Muhammad bin Ahmad bin Abdillahi mashuhuri kwa Ibn Khuwayz Min’daad katika maulamaa wa madhehbu ya Ki-Maalik.2-Imamu Abul Abbaas Ahmad bin Ahmad Al-Twabariy Al-Shaafiy mashuhuri kwa Ibnul-Qaadhiy aliyefariki mwaka 335 H.

Ndugu msomaji kama ukiutazama kwa makini mwaka aliozaliwa Sheikh Muhammad bin Abdil-Wahab na mwaka waliokufa maulamaa hawa tuliowataja utagundua kwamba ndugu Juma al-Mazrui ni mwongo.

JAWABU

Mosi: sisi tunapotumia neno Wahabi hatukusudii Ahlu Sunna Wal-Jama’a, Ahlu Sunna ni madhehebu tatu na nusu zinazoeleweka – Shafi, Hanafi, Maliki na baadhi ya Hanbali. Hawa ndio watu wanaofuata Sunna. Na zinatosha kubainisha hilo zile adabu zao, uchaji wao na hata mijadala yao ilivyo, basi ni ya kiheshima na utulivu. Hawa wameishi Afrika Mashariki kwa karne nyingi hadi kufikia zama zetu hujasikiapo kumtukana mtu kwa sababu ya madhehebu yake, tafauti na nyinyi mulivyo duniani kote, ambapo hakuna sehemu yoyote ile ya dunia ambayo hamukuitia fitna! Ninatamani – ewe Sheikh Kasim bin Mafuta – lau Sheikh ‘Umar bin Sumait, Sheikh Sulaiman Al-‘Alawi, Sheikh Abdullah Salih Al-Farisi na walio mfano wa hao wangelikuwa hai ukakaa nao japo siku moja tu, kisha ukaona vipi Sunna inavyotekelezwa kimatendo. Lakini mwenzetu umekwenda kukaa na Mashekhe wa Suudia na Mawahabi wa Yemen, Sunna ya kweli utaipata wapi? Utayoipata huko ni Sunna ya kutukana watu na kuwakafirisha kama kitabu chako kinavyojishuhudisha chenyewe!

Kisha elewa kwamba miongoni mwa Ahlu Sunna wa kweli, ukiwachilia mbali jina, basi ni Ibadhi ndio wanaofuata Sunna za kweli wala hawakubadilisha kitu. Haya ninayokuambia ni kwa ushuhuda wa wasiokuwa Ibadhi kama nitavyokunukulia maneno yao katika juzuu nyengine za kitabu hiki, na ushahidi bora ni ule uliotolewa na mpinzani.

18

Nawe kama huniamini kama Ibadhi ndio Ahlu Sunna wa kweli, tokeni kikundi cha Mawahabi na kikundi cha Maibadhi mukaishi katika nchi hata ya kikafiri, kisha tazameni ni nani ambao tabia zao zitapendwa. Ahlu Sunna hujulikana – si kwa kujipachika jina hilo, bali – kwa tabia zao na mwenendo wao mzuri, na hili nyinyi ulimwengu mzima umeshuhudia kwamba hamunalo, munalolijua nyinyi ni kutukana watu na kumshambulia huyu na yule.45

Pili: ni kwamba ikiwa tutakubaliana na madai yenu kwamba Wahabi ni Ahlu Sunna je hio Jamaa yao iko wapi? Je wao ni wangapi duniani hata taarifu (definition) ya Ahlu Sunna Wa Al-Jamaa iwafae? Usiniambie kwamba Al-Jamaa (kundi kubwa) ni aliye katika haki hata akiwa mmoja kama ilivyopokewa kutoka kwa Ibn Mas-uud, kwani Ibadhi, Zaidia na Bohora watakuja kudai kwamba mmoja huyo aliye katika haki ni wao. Kwa hivyo, sisi tunapotaja Wahabi tunakusudia wafuasi wa Muhammad Abdul Wahhab, nao wako mbali mno na Sunna ya Mtume (s.a.w.) katika itikadi na katika akhlaqi, ijapokuwa wamedanganyika kwa kujipachika jina hilo na kuwarushia wenzao majina mabaya. Kwa hali yoyote ile, hili pia si muhimu, kwani sisi tunachokitaka ni nini unasema na una ushahidi gani: sio jina lako zuri la kujipamba au jina la mwenzio baya la kumpambua? Lakini kwa ufupi ni kuwa mimi katika kitabu changu na maandiko yagu yote, ninapotaja Mawahabi nawakusudia wafuasi wa Muhammad ‘Abdil-Wahhab pamoja na Maimamu wao wote watangulizi kama Ibn Taymiyya, Ibn Al-Qayyim, Ibn Batta, Al-Barbahari, na walio mfano wa hao.

Ama kuhusu wanavyuoni uliowataja kwamba wanakataa majazi, elewa kwamba hilo ni jambo lenye kuhitaji maelezo. Abu Is-haaq Ibrahim bin Muhammad bin Mih’raan Al-Is’fraayiiniy,46 kwa mfano, ambaye umemtaja kama ni Shafi. Yeye si Shafi katika itikadi; bali ni Shafi katika fiq-hi. Ama itikadi yake ni kama yenu ya kuwa Allah ana viungo. Na kwa sababu hii ndio maana Ibn Al-Qayyim akamtaja katika Ijtimaa’u Al-Juyuush na akasema: “Alikuwa ni katika Maimamu wakubwa wa Sunna wenye kuzithibitisha sifa (za Allah)”.47 Nawe Sheikh Mafuta unaelewa vyema nini Ibn Al-Qayyim anakusudia anaposema: “Alikuwa ni Imamu wa Sunna na 45 - Bali kanihadithia mwanafunzi mmoja wa Afrika Magharibi ambao kwao sasa Ibadhi imeingia kwamba mwanzo walipodhihiri Ibadhi huko watu walikuwa wakiwachukia wakidhania kuwa ndio wale wale Mawahabi wamekuja kwa sura nyengine. Na baada ya watu kujua kwamba kweli wao si Mawahabi na baada ya kuona mwenendo wao mzuri, sasa wamekuwa ni watu wenye kupendwa sana huko. Na haya yote ni kwa sababu Mawahabi huko wamefanya fitna isio na kifani hata ikapeekea kufa kwa watu wasiopungua thamanini katika fujo la siku moja. Hii ndio dini yenu enyi Kasim Mafuta!46 - Sahihi ni kumwita “Al-Asfaraayiini”, japo kuwa wanavyuoni wengi wamemwita hivyo. 47 - Tazam Ijtima’u Al-Juyuush uk. 111.

19

ni mwenye kuzithibitisha sifa za Allah” kwamba ni mwenye kuthibitisha kuwa Allah ana uso, mikono n.k. Kwa hivyo, Abu Is-haq huyu kukataa kwake majazi ni jambo la lazima wala hahisabiwi tena kuwa ni katika wanavyuoni wa Kishafi madamu katafautiana nao katika mambo ya misingi ya itikadi.

Hayo nilioyasema kuhusu Abu Is-haaq ni kwa kutegemea kile alichokisema Ibn Al-Qayyim katika kitabu chake hicho Ijtimaa’u Al-Juyuush kwamba Abu Is-haq huyo: “Alikuwa ni katika Maimamu wakubwa wa Sunna wenye kuzithibitisha sifa (za Allah)”. Vyenginevyo Imamu Al-Haramain na Al-Imamu Al-Ghazali – kama tulivyonukuu kabla – wanakanusha madai kwamba Abu Is-haaq alikuwa akikakanusha majazi.

Ama suala lako ulipouliza: “Je ni kweli kwamba hao ambao ndugu Juma anawaita mawahabi ndio wanaopinga majazi?” Suala hili – pamoja na majibu uliotoa – linaonesha kwamba hufahamu unachoambiwa! Ajabu mtu kukimbilia kujibu bila ya kufahamu anaambiwa nini! Nikisema kwamba Kasim Mafuta anaamini kwamba Mungu ana mikono haimaanishi kwamba ninakataa kwamba kuna wengine wenye kusema kwamba Mungu ana mikono. Bali maneno hayo yanathibitisha kwamba Kasim Mafuta anaamini kwamba Mungu ana mikono. Halkadhalika niliposema kwamba Mawahabi wanasema kuwa hakuna majazi, hio ina maana kwamba ninachokidai – kwa maneno yangu hayo – ni kwamba wao wanasema kuwa hakuna majazi: wala sidai kwamba hakuna mwengine yoyote yule aliyesema kuwa hakuna majazi. Sasa wewe unanijibu kwamba wako Maimamu waliokataa majazi kabla ya kuzaliwa Muhammad ‘Abdil-Wahhab. Jawabu hii ingelifaa lau mimi nilisema kwamba Muhammad ‘Abdil-Wahhab ni wa mwanzo kudai kutokuwepo kwa majazi. Kwa hivyo, ili uwe umenijibu jawabu sahihi niambie kwamba Mawahabi wanayakubali majazi. Na hapa itakubidi ufute usemi wako kwamba:

Na wengine wameona wauite “Usluubun min Asaalibil-Lugha” (utaratibu/mfumo katika taratibu za lugha) na njia hii ndiyo iliyokaribu na usahihi, ili kuwazuia watu wa batili wasiyapotoshe maandiko kwa kuupitia mlango huu.

Kwa ufupi, ni kuwa kauli ya kuwepo kwa majazi katika Qur-ani, Sunna na lugha ya Kiarabu, ndio kauli ya jumhur ya wanavyuoni katika madhehebu zote, na ndio yenye ushahidi wa wazi ambao haupingi ila ambaye hataki ukweli, au aliyepotea au mwenye akili finyu na udhaifu wa kufahamu. Tumetoa ushahidi kidogo katika sehemu tulionukuu yale nilioyasema katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu na nitaeleza tena baadae kwa urefu.

20

Na kwa hivyo, kauli yako uliposema:

Ndugu msomaji kama ukiutazama kwa makini mwaka aliozaliwa Sheikh Muhammad bin Abdil-Wahab na mwaka waliokufa maulamaa hawa tuliowataja utagundua kwamba ndugu Juma al-Mazrui ni mwongo”.

Kauli hii inaonesha jinsi ulivyokuwa jasiri katika kuwatukana watu bila hata ya kuwafahamu wanachokisema; inaonesha kiasi gani ulivyokuwa humuogopi Mola wako. Mimi nilichokisema ni kuwa Mawahabi wanakataa majazi. Wewe unaniambia kwamba wako maulamaa kabla ya kuwepo Mawahabi walikataa majazi kisha unaniita mwongo! Kwani mimi nilisema hakuna maulamaa hao hata nimekuwa mwongo? Na je tuseme kuwa wewe ni mwongo uliposema:

Ndugu Juma Al-Mazrui katika kitabu chake “Hoja zenye Nguvu” ukurasa wa 32 amefanya jaribio la kutaka kuuficha ukweli huo ambao uko wazi tena mbele ya macho yake na akafanya upotoshaji kwa makusudi dhidi ya watu anaowaita Mawahabi . 48

Na umesema:

Hakuna kitu kingine zaidi ya chuki kilichomfanya awaite Ah’lu Sunna kwa jina la Mawahabi, au Hashawiya, au Mujasima.49

Ninasema: je tuseme na wewe ni mwongo uliposema: “dhidi ya watu anaowaita Mawahabi” kwa sababu mimi siye niliyewaita watu hao Mawahabi na pia kwa sababu wako wengi mno duniani wanavyuoni na wasiokuwa wanavyuoni ambao wanawaita na wamewaita watu hao Mawahabi hata kabla ya kuzaliwa mimi kwa miaka mingi? Kama vile ambavyo jina “Hashwiyya” na jina “Mujassima” yametajwa na wanavyuoni wa karne nyingi. Anasema Al-Imamu Al-Subki Al-Ashafi: “Ama Al-Hashwiyya ni kikundi dhalili cha wajinga wanajinasibisha na (Al-Imamu) Ahmad na Ahmad yuko mbali nao”.50 Anasema Sheikh Al-Kawthari: “…..nao ni Al-Hashwiyya”.51 Bali Ibn Al-Qayyim anasema:

** ترايان ما الحشوي أم أنتم ذا بعد الخوارج دين على ذا من

48 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 39.49 - K.h.j. uk. 10.50 - Al-Subki Al-Kabir Al-Saifu Al-Saqil uk. 16. 51 - Al-Kawthari Takmilatu Al-Raddi ‘Alaa Al-Nuniyya kilicho pamoja Al-Saifu Al-Saqil cha Al-Subki Al-Kabir uk. 15.

21

Basi baada ya hayo ni nani aliye katika dini yaKhawaarij*****Munaonaje: ni nyinyi au ni Al-Hashwiy

... اإليمان ** راية حامل ــوي الحشــ لرأيتم أبصرتم لو والله

Wallahi lau mulitazama basi mungelimuona Al-Hashwiy**Kwamba ndiye aliyebeba bendra ya imani.52

Anasema Ibn ‘Assaakir:

العرش في حال سبحانه إنه والمجسمة الحشوية ن وإوقالتعليه جالس وهو له مكان العرش

Na wakasema Al-Hashwiyya na Al-Mujassima, kwamba Yeye Allah Mtukufu yupo katika ‘Arshi, na kwamba ‘Arshi ndio sehemu yake naye kakaa kitako juu yake.53

Anasema Al-Shahrastani:

…Na kundi la watu wa Hadithi Mahashwiyya….wamesema kwamba Mola wao wanayemuabudu ana sura ya mtu mwenye viungo na migawanyiko…na inajuzu kwake kuondoka (sehemu hadi sehemu) na kushuka na kupanda….54

Kwa hivyo, ni wazi kwamba jina hilo liko karne nyingi.55 Ama jina la Al-Mujassima na Al-Tajsim wamelizungumzia wanavyuoni wengi akiwemo Ibn Taymiyya kama tulivyomnukuu sana na wala hakuona kuwa hilo ni jina baya kama alivyosema:

Na hakuna yoyote katika Al-Salaf (watangulizi) aliyemlaumu mtu yoyote kwamba yeye (mtu huyo) ni mujassim (mwenye kusema kuwa Allah ni kiwiliwili). Wala (hakuna) aliyewalaumu mujasima (wenye kusema kuwa Allah ni kiwiliwili). Bali (Al-Salaf) waliwalaumu Al-Jahmiyya ambao waliyakanusha hayo (ya kuwa Allah ni kiwiliwili)!56……..

52 - Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 1, uk. 362. 53 - Ibn ‘Assaakir Tabyiin Kadhibi Al-Muftari uk. 150. 54 - Al-Shahrastani Al-Milal j. 1, uk. 117. 55 - Rejea pia Tafsiri Mafaatihu Al-Ghaib ya Al-Fakhru Al-Razi utaona akilitumia jina hilo katika sehemu tafauti za tafsiri yake. Tazama, kwa mfano, mas-ala ya kumi na mbili mlango wa pili katika tafsiri ya Suratu Al-Fatiha, mlango kuhusu “Sauti, herufi na hukumu zake”. 56 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 100.

22

…………………….Bali wanasema (Al-Imamu Ahmad na Maimamu wengine wa Sunna, kwamba) kuzithibitisha maana hizi ni haki zaidi kwa maana ya tajsim (kwa maana ya kumfanya Allah kuwa ni mwenye kiwiliwili) kuliko kuzithibitisha lafdhi zake bila ya (kuthibitisha maana yake).57

Halkadhalika ukisoma kitabu Al-Saifu Al-Saqil cha Al-Subki pamoja na Takmila yake cha Al-Kawthari,58 utaona wakilitumia jina hilo kwa wingi, na Al-Subki huyo kafa 756 A.H. Sasa:

1) Vipi unadai kwamba Juma Mazrui ndiye aliyekuiteni nyinyi Mawahabi, Hashwiyya, Mujassima?

2) Vipi utajitoa katika jina “mwongo” kwa mujibu wa misingi yako uliojijengea ya kuwaita watu waongo?

Sikiliza ewe Sheikh Kasim Mafuta! Elimu ni kufahamu: si kuhifadhi Hadithi nyingi. Mtu akisema kuwa “Mawahabi wanakataa kitu fulani” haileti maana kwamba hakuna mwengine anayekikataa kitu hicho. Isipokuwa ukiwa utajenga hoja kwa kutumia MafhubAl-Laqab nayo ni mafhumu dhaifu taqriban kwa makubaliano ya Umma mzima. Sheikh Kasim! Kwani tukisema kuwa Ibadhi hawaamini kuonekana kwa Allah inamaanisha kuwa huo ni uwongo kwa sababu wako wengine wasiokuwa Ibadhi ambao pia hawaamini kuonekana kwa Allah? Nyinyi ndugu zetu muna fahamu gani?

Anaendelea Sh. Kasim Mafuta kwa kusema:

Kwa mfano, baina ya Sheikh Muhammad bin Abdil Wahaab aliyezaliwa mwaka 1115 H na kufariki mwaka 1206 H na baina ya Imamu Abu Is’haaq al Isfraayiiniy aliyefariki mwaka 418 H, ambaye ni miongoni mwa wanaopinga kuwepo kwa “Majazi” utaona kuwa baina yao kuna miaka takriban 697, kabla ya kuzaliwa huyo wanaedai kuwa ndiyo muasisi wa huo uwahabi! Kwa miaka hiyo tayari upingaji wa majazi ulikuwepo duniani.

Sasa utasemaje kwamba Mawahabi wanapinga majazi na hali yakuwa huyo muasisi wa huo mnaouita uwahabi amezaliwa miaka 697 baada ya kauli hiyo ya kupinga majazi ? Au unataka kutuambia kwamba Imamu Abu Is’haaq Al-Isfraayiiniy alifufuka baada ya kuzaliwa Muhammad bin Abdul-wahab kisha akamfuata sheikh Muhammad bin Abdil-wahab? Au mnataka kutuambia kuwa hawa nao pia ni Mawahabi?59

57 - Ibn Taymiyya Bayanu Talbis Al-Jahmiyya j. 1, uk. 93. 58 - Tazama Takmila ya Al-Kawthari katika Al-Saifu Al-Saqil cha Al-Subki uk.17, 19. 59 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 42-43.

23

Ninasema: masuali haya yote, jiulize mwenyewe na ujijibu wewe, kwani msingi wake ni kunizulia kitu ambacho sikukisema. Kwa hivyo, hayo masuali jijibu wewe mwenyewe. Kisha baada hayo, Al-’Allama Sheikh Kasim Mafuta akasema:

JE WENYE KUPINGA MAJAZI WANA HOJA ZA KIELIMU?

Jambo muhimu la kulizingatia ni; je hao maulamaa waliopinga kuwepo kwa majazi, wamepinga kwa hoja na dalili za kielimu? Au ni kwa maneno matupu? Jawabu ni kama ifuatavyo:

Ukirejea kauli za maulamaa hao waliopinga kuwepo kwa majazi ima katika lugha ya kiarabu na Qur’an, au katika Qur’an tu, utagundua kwamba kuna hoja za msingi walizozitoa ambazo haitakiwi kuzipuuza, bali inatakiwa zitazamwe kielimu na kwa jicho la insafu. 60

Ninasema: Kuwepo kwa majazi ni kitu ambacho hata mtoto wa sekondari anakubaliana nako. Hakuna lugha yoyote duniani ambayo haina majazi. Na waliopinga kuwepo kwa majazi ni kwa sababu ya kuhofia kwao kuporomoka kwa itikadi zao: si kwa sababu majazi hayapo. Vyenginevyo mbona wao wenyewe wanalazimika kuyatumia? Hata lugha ya Kiswahili imejaa majazi. Nikisema: “Huyu ana mkono mkono” yaani ni mwizi; “Huyu ana ulimi” yaani ni msemaji; “Ana kichwa” yaani ana akili. Vyenginevyo watu wote wana mikono, ulimi na vichwa.

Anaendelea Sh. Kasim Mafuta kwa kusema:

Hizi zifuatazo ni baadhi ya hoja zao:

HOJA YAO YA KWANZA

Miongoni mwa hoja zao zinazowafanya kupinga kuwepo majazi katika lugha na halikadhalika katika Qur’an, ni kuwa maana ya maneno hufahamika kwa kuutazama mtiririko au muktadha (context) na dalili za uhalisia. Pia wakadai kuwa neno linapokuwa peke yake halileti maana kamili mpaka liwe katika sentensi, na linapo unganishwa katika sentensi

60 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 43.

24

huwa ule mtiririko wa maneno ndio unao ainisha maana husika ya neno hilo. 61

Ninasema: maneno hayo hayana ukweli hata chembe. Ulazima wa kufahamika kwa neno kwa kuutazama mtiririko au muktadha (context), ni katika hali mbili tu:

1) Neno linapotumika kinyume na maana yake ya asili, kama vile kulitumia neno mkono kwa maana ya nguvu. Hapa ndipo ambapo neno linaambiwa kuwa limetumika kimajazi na ndipo linapohitaji qarina lafdhiyya au haliyya au ‘aqliyya itayobainisha kwamba maana yake ya asili sio iliokusudiwa. Na hayo yote au mfano wa hayo umeyanena wewe mwenyewe kwa ulimi wa kalamu yako.

2) Neno linapokuwa ni mushtarak (asili ya neno hilo lina maana nyingi kwa pamoja). Kama – katika Kiswahili – nikitaja neno “mto” kisha nikanyamaza. Katika hali hii huwezi kujua ni mto gani nilioukusudia – je ni mto wa maji au wa kulalia. Na kwa hivyo hapa ni lazima kuwe na qarina itayobainisha makusudio yangu kama vile “nipe mto nilalie” au “ninakwenda mtoni kukoga”. Maneno “nipe…nilalie” na “ninakwenda…kukoga” ni qarina zilizobainishi ni mito gani hio nilioikusudia.

Katika hali mbili hizo, kama ulivyoona mifano nilioipiga, ndipo ambapo kuna ulazima wa kuwepo kwa qarina itayoainisha maana iliokusudiwa. Ama neno likiwa limetumika katika maana yake ya asili au si mushtarak basi hakuna haja ya kutazama mtiririko au muktadha (context). Na lau Sheikh Kasim bin Mafuta aliyarejea maneno yake alioyaandika mwenyewe, basi asingeliyasema maneno haya. Ebu jikumbushe maneno yako ulioyasema kabla kidogo:

Kwa sababu ili maneno yawe ni majazi, ni lazima masharti matatu makuu yatimie, nayo ni:1-Kutumika neno katika isiyo kuwa maana yake ya asili.2-Lazima kuwepo na “QARINATUN MAANI’ATUN MIN IRADATI MA’ANAL ASLIY” dalili yenye kuzuia kukusudiwa maana ya asili.3-Lazima kuwepo na “ALAAQAH” mafungamano baina ya neno la asili na neno lisilo la asili.

Na likikosekana sharti moja kati ya haya matatu tuliyoyataja basi hakutakuwa na majazi na atakayedai kuwa ni majazi basi huyo ni mwongo mkubwa na hajui lugha ya kiarabu62 …..

61 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 43.62 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 40. Tena Sheikh Kasim kumbe yeye majazi anayajua basi tu!

25

Hayo ni maneno yako mwenyewe! Ni wazi kwamba ikiwa masharti hayo hayakupatikana basi neno linabakia katika maana yake ya asili. Sasa vipi tena hapa unadai kwamba: “…Maana ya maneno hufahamika kwa kuutazama mtiririko au muktadha (context) na dalili za uhalisia”? Yaani – kwa lugha nyengine – neno halifahamiki mpaka utazame qarina (context).

Ama madai yako uliposema:

Pia wakadai kuwa neno linapokuwa peke yake halileti maana kamili mpaka liwe katika sentensi, na linapounganishwa katika sentensi huwa ule mtiririko wa maneno ndio unao ainisha maana husika ya neno hilo.

Tunasema: ikiwa neno likiwa peke yake halileti maana kamili na kwa hivyo hakuna majazi, basi pia na hakika isiwepo kwani neno peke yake halileti maana kamili; bali ni mtiririko (siyaq au sibaq) ndio inayobainisha maana husika! Na kwa hivyo, hizi lafdhi zote tukiichukua moja moja zinakuwa hazina maana yenye kufahamika!

Nasi tunasema kwamba neno linakuwa na maana yake ya uhakika nayo ni ile ambayo الذهن إلى yaani ni ile (inayokimbilia katika fahamu) يتبادرmaana ambayo mtu akilisikia tu neno hilo basi anaifahamu maana hio. Nikisema mkono, basi unaeleweka ni nini na hii ndio maana yake ya hakika. Ama kuwepo kwa neno katika sentensi, huko kunaweza kuonesha kwamba neno hilo halikutumika katika maana yake ya asili yaani ni majazi; wala haina maana kwamba neno halipewi maana yake ya uhakika linapokuwa peke yake.

Anaendelea Sh. Kasim Mafuta kwa kusema:

Mfano, neno “ رأس “ “Ra’asun” lina maana nyingi, lakini maana zote zinaainishwa na mtiririko wa maneno, kwa mfano mtu akisema: Ra’asul-Jabali, atakuwa hapa anakusudia kilele cha mlima.

Na kama atasema:

Ra’asul-Maali, atakuwa anakusudia msingi wa mali au rasilimali. Na kama atasema: Ra’asul-Insaani, atakuwa anakusudia kichwa cha binadamu. Na maana zote za neno hili zimeanishwa na mtiririko wa maneno, na wala hakuna binadamu yoyote anaeweza kututhibitishia kwa hoja na dalili kwamba maana ya asili ya neno “Ra’asi” ni kichwa cha binadamu, na katika sehemu nyingine zote ni Majazi. 63

63 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 44.

26

Ninasema: kwa maana hio mtu akisema “gari” wewe hujui kakusudia nini mpaka aseme “ninakwenda kutengeneza gari” au “ninakwenda kuitia petroli gari” au aseme: “nitasafiri kwa gari”? Na akisema “nyumba” wewe hufahamu anakusudia nini mpaka ataposema “ninakwenda kuezeka nyumba”. Akisema “mti” hufahamu kakusudia nini, mpaka ataposema “mti wenye matunda”. Akisema ndevu hujui kakusudia nini mpaka ataposema “ndevu za binaadamu au za mbuzi”. Akisema “tumbo” hufahamu kakusudia nini; mpaka ataposema “tumbo la mtu”. Hii ni akili gani? Hii ndio Al-Taqlid Al-A’amaa (kufuata kama kipofu). Basi ni hivyo: sisi tunapewa fikra nasi tunazichukua tu kwa sababu kazisema Ibn Al-Qayyim kana kwamba Ibn Al-Qayyim ni ma’asum.

Na kwa ufupi, ni kwamba ikiwa neno “kichwa” kwa kulitaja tu halifahamiki nini makusudio yake, basi sababu si kwamba hakuna majazi na hakika, bali sababu itakuwa neno hilo litakuwa ni mushtarak. Neno mushtarak ni neno lenye maana nyingi wakati mmoja na zote ni maana za uhakika: si za kimajazi. Tumetoa mfano wa neno mto katika lugha ya Kiswahili, na tunatoa mfano wa neno عين ‘Ain katika lugha ya Kiarabu. Neno hili lina maana ya jicho, jasusi, chemchem, dhahabu n.k. Na kwa hivyo, nikisema Ain tu, kisha nikanyamaza huwezi kujua ninakusudia nini. Tafauti na‘ عينnikisema ‘Ain linaniuma. Hapa utafahamu kuwa ninakusudia jicho linaniuma. Ama maneno yenye maana moja ya kimsingi, hayo yanapotajwa huwa yanaeleweka wala hayahitaji qarina au kuwepo katika sentensi ili yaeleweke. Ama maana zake za kimajazi, hizo ndizo zinazohitaji kuwepo kwa Qaraain lafdhiyya au haliyya au ‘aqliyya. Na kwa mantiki hii nikisema kisu, mtu anafahamu ninakusudia nini; nikisema jiwe mtu anafahamu ninakusudia nini; nikisema chungwa mtu anafahamu ninakusudia nini n.k. Bali neno kichwa ukilitaja tu linafahamika ni kitu gani, na maana zake nyengine kama ra-sul mali (rasilimali) na ra-sul jabal (kichwa cha mlima yaani kileleni kwake), maana hizo ndizo ambazo hazifahamiki ili zitajwe namna hiyo – kwa kuwepo qarina. Hakuna Mwarabu yoyote utayemwambia “Ra-asun” (kichwa) akafikiria kwamba unakusudia juu ya mlima au rasilimali; bali ukilitaja tu neno hilo moja kwa moja Mwarabu anafahamu “kiungo cha mwili”. Kwa hivyo, madai yako hayo yametokana na kufuata kama bendera inavyofuata upepo: hayakutokana na tahqiq za kielimu!

Na kwa ufupi, ewe Sheikh Kasim Mafuta, ni kuwa hoja yako hio ni hoja ya Imamu wako Ibn Al-Qayyim. Naye kajibiwa jawabu ya uwazi na Al-Imamu Badru Al-Din Al-Sheikh Al-Rabbaani Ahmad bin Hamad Al-Khalili Al-Mufassir. Nakunukulia hoja ya Ibn Al-Qayyim halafu nakufatishia jawabu aliojibiwa. Anasema Ibn Al-Qayyim:

27

Kufarikisha kwenu baina ya hakika na majazi kwa kufuata kuifungamanisha katika moja ya lafdhi mbili kama vile الذل bawa) جناجla udhalili) na حرب na vilivyo mfano wake. Hakika (moto wa vita) نارya Waarabu hawakuzitumia lafdhi hizo ila katika hali ya kufungamanishwa. Na utafautishaji huu ni katika utafautishaji mbovu kabisa kwani lafdhi nyingi ambazo zimetumika katika maudhui yake (maana yake ya asili) basi wamejilazimisha kuzifungamanisha (hawazitumii peke yake) kama vile neno kichwa na bawa na mkono na mguu. Hakika yao (Waarabu) hawakuzitumia lafdhi hizi na zilizo mfano wa hizi isipokuwa kwa kuzifungamanisha na mwahala mwake na mule zinamotegemezwa, kama vile kichwa cha mnyama na kichwa cha maji na kichwa cha mtaji (ra-asul mali au rasilimali) na kichwa cha jambo. Halkadhalika neno جناح bawa. (Waarabu) hawakulitumia (neno hilo) ila katika hali ya kuliunganisha na kile ambacho hutegemezwa nacho kama vile الطائر الذل na ,(bawa la ndege) جناح .(bawa la udhalili) جناحAma mukilichukuwa neno bawa moja kwa moja (peke yake) bila ya kuliunganisha (na kitu) basi huwa halitoi maana yenye kuleta faida ya maana yake peke yake kamwe ukiachilia mbali kuwa ni hakika au majazi. Na ikiwa mutalizingatia katika hali ya kuunganishwa (na neno jengine) basi (neno hilo) linakuwa hakika katika kile kilichounganishwa nacho. Basi vipi kitu kilichotegemezwa na kitu kimoja kinakuwa hakika katika kitu hicho; halafu kinakuwa majazi katika kutegemezwa kwake na kitu chengine, ilhali kukinasibisha kwake na tegemezi hii ni sawa na kukinasibisha kwake na tegemezi nyengine. Bawa la Malaika (kwa mfano) ni hakika kwake. Allah anasema المالئكة جاعل أجنحة أولي رسال

ورباع وثالث مثنى (Ni mwenye kuumba Malaika kuwa ni wajumbe wenye mabawa mawili mawili, matatu matatu na manne manne). Atayesema kwamba Malaika hana bawa la kweli kweli, basi huyo ni mwongo, mzushi, mwenye kukikataa kile alichokithibisha Allah Mtukufu……….64

Hayo ndio maneno ya Ibn Al-Qayyim, nayo ni maneno ya kustaajabisha. Kwani mwenyewe kataja الذل na kuliingiza ,(bawa la udhalili) جناحbawa hili kuwa ni bawa la uhakika; nasi tunamuomba Ibn Al-Qayyim atuoneshe wapi duniani linapatikana bawa la uhakika la udhalili. Na kama Ibn Al-Qayyim ameshatangulia kwenda kwenye matendo yake alioyatanguliza, basi wafuasi wake wapo mmoja wao ni Sh. Kasim Mafuta. Tunaomba wafuasi watuoneshe wapi kuna bawa la uhakika la udhalili – je udhalili una bawa na linapatikana wapi? Kwa ufupi ni kuwa Ibn Al-Qayyim hapa anasema yale yale yaliosemwa na Al-’Allama Kasim Mafuta, kwamba neno moja tu peke yake huwa halitoi

64 - Ibn Al-Qayyim Al-Sawa’iq Al-Mursala uk. 247.

28

maana hadi pale litapowekwa katika sentensi au litapotegemezwa na neno jengine au kutegemezwa na mwahala mwake! Lakini akajibiwa na Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili kama ifuatavyo:

Na jawabu yake: ni kuwa hicho alichokisema ni madai yasio na ushahidi, kwani alioyataja kutoka kwa Waarabu kwamba wao hawavitaji (viungo) kama kichwa, na bawa na mkono na muundi na mguu ila kwa kuviunganisha kwa kuvitegemeza (na neno jengine) ni dai batili halina ushahidi wowote, na wapi ataupata ushahidi? Hakika ya kuvihusisha viungo hivi peke yake kwamba havitumiki ila katika hali ya kuviunganisha (na maneno mengine) hakuna yoyote aliyelisema katika walionukuu lugha (ya Kiarabu) kama vile Abu ‘Amri, Al-Khalil, Sibawayh, Al-Asma’iy, Al-Kisaai na wengineo. Na anayedai hivyo na alete ushahidi katika maneno yao. Na ikiwa (Ibn Al-Qayyim) anadai kwamba viungo vyote havitamkwi ila katika hali ya kuviunganisha (na mwahala mwake), basi hilo ni lenye kukataliwa kwa kuwepo ushahidi usiohisabika wenye kuonesha kinyume na hivyo. Na inatosha kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema: “.. ال ما فيها

سمعت أذن وال رأت Humo (Peponi) kuna mambo ambayo) ”عينjicho halijapata kuona wala sikio halijapata kusikia”. Basi kwa hakika ndani yake (Hadithi hii) jicho na sikio yametajwa bila ya kuyategemeza au kuyafungamanisha na (mwahala mwake)……………….......Na kuna pingamizi gani mtu akisema: قدم أو رجل أو يد أو رأس أو وجه لي بدا

األعضاء هذه من شيء أي أو شعر uso umenidhihirikia au) أوkichwa au mkono au mguu au nywele au chochote katika viungo hivi)?............Anasema ‘Umar bin Abi Rabi’a:

** ببنان زينت خضيب وكف جمرت حين معصم منها لي بدا

Ukanidhihirikia kutoka kwake mkono aliporembea Jamra Na kiganja chenye hina kimepambwa kwa ncha za vidole.

Ama mabawa ya Malaika ni hakika kwao, lakini hilo halitoi upinzani kwa waliosema kwamba bawa la udhalili ni majazi. Kwani inajulikana kwamba bawa ni kiungo cha kiumbe vyenye kuishi linafahamika kwa hisia na kulitumia (neno hilo bawa) kwa vitu visivyo vya hisia ni kiasi cha kutaka kuileta picha yake katika akili (kwa kuvifananisha na vitu) vya kihisia.65

Anachokisema Sheikh Al-Khalili, kwa ufupi, ni kuwa madai ya Al-Imam Ibn Al-Qayyim hayana ushahidi katika lugha ya Kiarabu, bali ni kinyume na ushahidi mwingi uliomo katika lugha ya Kiarabu. Na lau hakukuwa na ushahidi mwengine wowote ule isipokuwa Hadithi hio ya Mtume (s.a.w.) inayosema: “.. سمعت أذن وال رأت عين ال ما Humo (Peponi)) ”فيهاkuna mambo ambayo jicho halijapata kuona wala sikio halijapata

65 - Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Jawahiru Al-Tafasir: Juz’u Khaas uk. 191-193.

29

kusikia”, basi ungelitosha kubainisha ubatili uliomo katika madai ya Ibn Al-Qayyim. Kwani katika Hadithi hii mumetajwa neno jicho na neno sikio bila ya kutegemezwa na mwahala mwake yaani bila ya kusemwa “Jicho la binaadamu na sikio la binaadamu”. Na pamoja na hayo, imefahamika kwamba linalokusudiwa ni jicho la kweli na sikio la kweli. Hio – kwa mukhtasari66 – ndio jawabu aliojibiwa Ibn Al-Qayyim kwa madai yake hayo. Nayo inatosha kwa mwenye kutaka kutafuta ukweli.

Na kwa ziada ningependa kusema kwamba matumizi kama hayo ni mashuhuri kwa Waarabu ambapo wao huyatumia majina ya viungo bila ya kuyategemeza na mwahala mwake sawa ikiwa matumizi hayo ni ya kimajazi au ni ya hakika. Anasema Mtume (s.a.w.): “ يد ”المسلمون(Waislamu ni mkono).67 Utaona kwamba neno mkono hapa limetumika

اإلضافة عن hali ya kuwa halikutegemezwa na kitu nalo مجردةlimetumika kimajazi, na maana ni kuwa Waislamu ni kitu kimoja wanasaidiana. Na anasema Mtume (s.a.w.) katika Hadithi sahihi: العليا اليد

السفلى اليد من .(Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini) خيرYaani mwenye kutoa sadaka ni bora kuliko mwenye kupokea. Na Waarabu wa leo na wa kale husema: يد فالنلإن الفقه وقدما طولى افي Hakika fulani kwenye fiq-hi ana mkono mrefu na mguu) راسخةuliozama). Hapa mkono na mguu imetajwa bila ya kutegemezwa na sehemu zake: haikusemwa: “mkono au mguu wa binaadamu” na yote yametumika kimajazi kwa maana ya uwezo yaani mtu huyo ni mwenye uwezo mkubwa katika elimu ya fiq-hi. Wala usiniambie kwamba maana ya “mkono na mguu wa binaadamu” inafahamika kwa kutajwa kwa maneno “yeye ana mkono na mguu” kwani tunasema kwamba mkono na mguu wa binaadamu hapa sio iliokusudiwa, vyenginevyo isingelisemwa kuwa “ana mkono mrefu kwenye fiq-hi au mguu uliozama kwenye fiq-hi” kwani inaeleweka kwamba mkono haurefuki kwenye fiq-hi wala mguu hauzami kwenye fiq-hi.

Ama mfano mwengine wa kutumika kwa majina ya viungo pasina kutegemezwa na mwahala mwake na ikawa vimekusudiwa viungo vya kweli, ni Aya ya Qur-ani inayosema:

واألنف بالعين والعين بالنفس النفس أن فيها عليهم وكتبنان باألذن واألذن باألنف ن والس بالس

66 - Nimeikatakata jawabu hii kwa ajili ya kufupisha. 67 - Al-Rabi’u bin Habib Al-Jami’u Al-Sahih j. 4, uk. 354, Hadithi na. 903. Anasema mtiaji maelezo: “Kaitaja pia mwenye kitabu Kanzu Al-’Ummal uk. 441,442,443.

30

Tuliwaandikia juu yao humo (katika Taurati) kwamba nafsi kwa nafsi; na jicho kwa jicho; na pua kwa pua; na sikio kwa siko; na jino kwa jino.68

Yaani mtu huuliwa kwa kuua mtu; jicho la mtu hutofolewa atapotofoa jicho la mtu mwengine n.k. Pamoja na hayo, lakini utaona kwamba viungo vyote hivyo vimetajwa اإلضافة عن hali ya kuwa havikutegemezwa na مجردةkitu navyo vinafahamika ni kitu gani na nini makusudio yake. Baada ya haya, utaona kwa uwazi udhaifu uliomo katika hoja ya Ibn Al-Qayyim akiigwa na Kasim Mafuta.69

Na mfano wa Aya hio, ni Aya inayosema:

العين رأي مثليهم يرونهم كافرة وأخرىNa (kundi) jengine ni lenye kukufuru (wakawa) wanawaona (Waislamu) kuwa ni mara mbili ya wao kwa uoni wa jicho. 70

Hapa neno jicho halikutegemezwa na sehemu yake: haikusemwa “Uoni wa jicho la binaadamu”, ilhali sote tunajua kwamba hayo ndio makusudio.Na mifano myengine ni Aya kama:

دور تخفي وما األعين خائنة يعلم الص (Allah) anaijua khiyana ya macho na yale

ambayo vifua (mioyo) imeyaficha.71

Na Aya:

األعين وتلذ األنفس تشتهيه ما وفيها Na humo (Peponi) kuna kila yale ambayo nafsi

inayapenda na macho yanayafurahia.72

Na Aya:

وم شجرة إن ق البطون في يغلي كالمهل** األثيم طعام** الز

68 - Sura 5, Aya 45. 69 - Cha kusikitisha ni kuwa Kasim Mafuta yeye anawaambia watu kwamba wanawafuata Mashekhe wao tu bila ya kuhakiki: wakikosea nao wanakosea, wakati yeye kitabu chake kizima ni kufuata tu yasemwayo japo kuwa yana makosa ya wazi kama unavyojionea mwenyewe humu. 70 - Sura 3, Aya 13. 71 - Sura 40, Aya 19.

72 - Sura 43, Aya 71.

31

Hakika ya mti wa zaqqumi**Ni chakula cha waovu**Kama shaba ilioyayushwa inachemka katika matumbo.73

Na Aya:واعية أذن وتعيها تذكرة لكم لنجعلها

Ili tuifanye kuwa ni ukumbusho kwenu na ili sikio lenye kusikia lisikie.74

Na Aya:

األقدام به ويثبت قلوبكم على وليربط…Na ili (Allah) aifunge mioyo yenu (aipe nguvu)

na kwayo (maji ya mvua) aithibitishe miguu. 75

Sasa je bwana Kasim Mafuta bado wewe hujafahamu nini makusudio ya maneno: “Macho, vifua, matumbo, sikio, miguu, nyuso na mioyo” yaliotajwa katika Aya hizi kwa sababu haikusemwa: “Macho ya binaadamu au ya majini; vifua vya binaadamu au vya majini; matumbo ya binaadamu au ya majini; sikio la binaadamu au la jini; miguu ya binaadamu au ya majini n.k.?”

Na miongoni mwa dalili hizo ni kauli ya Al-Imamu ‘Ali bin Abi Talib (k.w.), aliposema:

** يا تنظري وال اللحظات إحبسي لعيني بالسرقات عينأقولNinaliambia jicho langu jizuie kidogo**Wala

usiangaliye ewe jicho kwa wizi.76

Hapa jicho limetumika katika maana yake ya uhakika. Na lafdhi ya pili ya jicho, haikutegemezwa na mahala pake. Naam! Mtu anaweza kudai kwamba jicho la pili limefahamika kwa qarina ya jicho la kwanza.77 Ninasema: huo

73 Sura 44, Aya 43-45. 74 - Sura 49, Aya 12.

75 - Sura 8, Aya 11. Aya nyengine ni Aya kama: نطمس أن قبل من......... ة يـوم وأنذرهم…أدبارها على فنردها وجوها إذ اآلزفـ........ الحناجر لدى القلوب

مع إن…..القلوب تطمئن الله بذكر أال...... ر الس ؤاد والبصـ ـان أولئك كـل والفـ ك عنه يخافون……………..مسئوال واألبصار القلوب فيه تتقلب يوما

Aya hizi zimetaja viungo (nyuso, migongo, myoyo, koo, masikio, macho, vifua) bila ya kuvitegemeza mwahala mwake, lakini bila ya shaka kimefahamika vyema nini kilichokusudiwa kwavyo. 76 - Al-Imamu ‘Ali Diwaanu ‘Ali uk. 52. 77 - Halkadhalika mtu anaweza akadai hivyo kuhusu baadhi ya Aya tulizozinukuu hapa. Na jawabu yetu ni moja kama hii tulioitoa hapa.

32

sio mjadala wetu: mjadala wetu ni kuwa je maana ya kiungo huwa haifahamiki hadi kitegemezwe na mwenyewe (yaani hadi isemwe jicho la mtu) au kinafahamika?

Na kwa hivyo, utaona kwamba Ibn Al-Qayyim mwenyewe pamoja na kukataa kwake kuwepo kwa majazi lakini vitabu vyake vimejaa majazi tena wakati mwengine huyataja kwa uwazi kama tutavyomnukuu baadae.

Ama kuhusu majazi ya mikono yasiotegemezwa na mwahala mwake, Ibn Al-Qayyim anafungua kitabu chake kwa kusema:

** يدان ذاك بفسخ للصدود ما األركان ثابت المحبة حكم

Hukumu ya mapenzi, nguzo zake ni imara**Upingaji78

hauna mikono miwili ya kubomoa hilo.79

Anasema mshereheshaji: Na mikono miwili ni uwili wa (neno) mkono, kwa maana ya uwezo.80 Sasa vipi tena Ibn Al-Qayyim anapinga majazi? Huku si kujigonga ambako kunaonesha kwamba hana hoja sahihi, bali anakimbia kuanguka kwa itikadi yake?

Anaendelea Sh. Kasim Mafuta kwa kusema:

HOJA YAO YA PILI

Itifaki iliyopo baina ya maulamaa wa lugha ya kiarabu kwamba mtu anaweza akayapinga maneno ambayo yanadaiwa kuwa ni majazi. Na kwa wakati huo huo akawa huyo mpingaji ni mkweli na yule mwenye kudai kuwa maneno hayo ni majazi pia akawa ni mkweli. Kwa mfano mtu akisema kwa kutumia majazi:

“Nimemuona simba ameshika upanga” akiwa anamkusudia mtu shujaa, kama akitokea mtu mwingine akisema huo ni uwongo! Huyo uliemuona wewe si simba, bali ni mtu shujaa, anakuwa huyu mwenye kutumia majazi ni mkweli na wakati huo huo huyu aliyepinga naye pia ni mkweli!

Kwa sababu hiyo wakasema wenye kupinga majazi: Kwa mujibu wa itifaki hiyo ni kwamba mtu akisema kwamba ndani ya Qur’an kuna majazi atakuwa moja kwa moja ameshasema kuwa ndani ya Qur’an kuna vitu

78 - Maana ya neno kwa neno ni “uzuiaji”, lakini ufasaha wa Kiswahili ni kusema “upingaji”. 79 - Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 1, uk. 16. 80 - Muhammad Khalil Harras Sha-hu Al-Nuniyya j. 1, uk. 16.

33

ambavyo kuna uwezekano wa mtu akasema kuwa ni uwongo na akawa huyo msemaji kwa wakati huo ni mkweli! Na bila shaka hilo si sahihi kwa itifaki ya waislamu wote, kwa sababu wamekubaliana waislamu wote duniani tangu hapo kale hadi sasa kwamba hakuna kitu chochote ambacho kiko ndani ya Qur’an kinachofaa kukipinga bali ukiipinga herufi moja tu utakuwa tayari umekufuru. 81

Ninasema: tazama watu walivyokuwa wachache wa kufahamu hawa! Hoja inasema:

Itifaki iliyopo baina ya maulamaa wa lugha ya kiarabu kwamba mtu anaweza akayapinga maneno ambayo yanadaiwa kuwa ni majazi. Na kwa wakati huo huo akawa huyo mpingaji ni mkweli na yule mwenye kudai kuwa maneno hayo ni majazi pia akawa ni mkweli.

Sasa ikiwa huyu ni mkweli na yule ni mkweli, kwanini tena unakanusha kuwa kuna majazi na huyu ni mkweli? Na kwanini pia usimpinge yule aliyekanusha kama huyu aliyethibitisha ni mkweli? Na ukiwa utampinga huyu aliyekanusha ni kwa nini umpinge naye ni mkweli? Ninasema: haiwezekani mtu mmoja akanushe kuwepo kwa kitu na mwengine adai kuwepo kwa kitu hicho hicho na wote wawe wakweli isipokuwa kutakuwa na hali mbili au moja ya mbili:

1) Mmoja wao atakuwa yuko sahihi na mwengine kakosea.2) Wawe hawajafahamiana: huyu anakusudia kitu kimoja; na yule

anakusudia kitu chengine kama nitavyozidi kukubainishia.

Kwa hivyo, kama umelifahamu hilo basi utakuwa umefahamu kwamba kuwaita watu hao wote kuwa ni wakweli ni kwa sababu aliyesema kwamba neno simba katika jumla ya maneno isemayo “Nimemuona simba ameshika upanga” si simba, basi makusudio yake ni kuwa huyo si simba wa kweli ambaye ni mnyama; na aliyemwita huyo kuwa ni simba basi makusudio yake pia ni kuwa huyo si simba mnyama bali ni mtu mwenye sifa ya simba ambayo ni sifa ya ushujaa, na kwa hivyo naye anakusudia kuwa huyo si simba wa kweli bali ni simba majazi. Kwa hivyo, hao tafauti zao ni lafdhiy za kimatamshi: si za uhakika. Kwani wote wanakubaliana kwamba huyo aliyeonekana kakamata upanga si simba wa kweli bali ni shujaa. Sasa upinzani uko wapi na nukta na logic (akili) iko wapi? Yaa Nas! Tusiwe wenye kufuata kama bendera: fulani kanena na miye nanena bila ya hata kufikiri vizuri. Madai hayo yote bado hayajabomoa kuwepo kwa majazi madamu uhakika wake upo tunauona.

81 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 44-45.

34

Anaendelea Sh. Kasim Mafuta kwa kusema:

Na hii itikadi ya kuwepo kwa Majazi ndani ya Qur’an inawafungulia watu mlango wa kuliingia jambo hilo la hatari. Kwa mfano, pale aliposema Allah:

والملك ربك وجاء صفا صفا“Na akaja Mola wako na Malaika safu safu “.82

Baadhi ya watu wakaigeuza maana ya aya hii wakasema hapana, hatakuja Mola Muumba wa kila kitu, bali itakuja amri yake! Kwa madai kwamba eti kuna “Majazul-Hadh’fi” majazi ya kuondosha kwa hiyo kuna kitu kimeondoshwa. Na kitu kilichowapa ujasiri wa kukana kwao kuja kwa Allah siku ya Qiyama ni pale walipofunguliwa mlango huo na hicho kitu kiitwacho “Majazi”. Kwa mfano, ukiwauliza kwa nini mmekimbilia kuitakidi kwamba hapo kuna majazi? Na hali yakuwa majazi si asili na hairuhusiwi kuiwacha asili na kukimbilia kwenye majazi mpaka itakapo shindikana maana ya asili? Wanadai kuwa asili imeshindikana, kwa sababu Allah hawezi kuja, na kitendo cha kuja kinaonyesha kuwa Allah ana mahali na hiyo ni sifa ya kiwiliwili, na kumpa Allah sifa hiyo ni kumfananisha na viumbe na kufanya hivyo ni kufru!!!

Madai haya si sahihi, kwa sababu kwanza, inatakiwa kukithibitisha kile ambacho Allah amejithibitishia nafsi yake kama anavyo stahiki, pamoja na kumtakasa na kufanana na viumbe, kama tutakavyo lifafanua suala hili mahali pake Inshaallah. Mwisho wa kunukuu.83

Ninasema: hilo la kubatilika kwa itikadi yenu ndilo munalolihofia kama ulivyosema mwenyewe: “Na hii itikadi ya kuwepo kwa Majazi ndani ya Qur’an inawafungulia watu mlango wa kuliingia jambo hilo la hatari”. Sasa ninachotaka kukwambia hapa ni kuwa batili haiondoshwi na batili; na maradhi hutibiwa kwa dawa sio kutibu maradhi kwa maradhi. Ikiwa kuna Aya watu wameipotoa – kama unavyodai – kwa kutumia majazi, basi hilo la kuyakanusha majazi halijawa dawa, kwani majazi yamethibiti kwa Qur-ani, Sunna na lugha ya Kiarabu. Dawa ni kubainisha tu kwamba katika Aya hio hakuna majazi. Ama kuyakanusha majazi kwa kuhofia kuanguka kwa itikadi yako, basi ni sawa sawa na mtu anayefanya jaribio la kutibu ugonjwa kwa kutumia ugonjwa mwengine; au anayerekebisha batili kwa kutumia batili nyengine?

Ama Aya isemayo:

82 - Suratul-Fajri (89) aya ya 22. 83 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 45-46.

35

والملك ربك وجاء صفا صفاNa akaja Mola wako na Malaika safu safu.84

Aya hii ni kweli jumhur ya wanavyuoni hawakusema kwamba Allah atakuja kweli kweli, bali hio ni kauli yenu na Maimamu wenu munaowafuata nyinyi. Hata hivyo, nao pia wamegongana katika kuifasiri Aya hio. Anasema Ibn Taymiyya akiwanukuu Mahanbali wenzake:

Na miongoni mwa (sababu) hizo, ni kwamba ikiwa (itikadi ya kuwa Allah ana) kiwiliwili itakataliwa kwa uwazi, basi italazimu kuikataa (itikadi ya kuwa Allah anafanya) harakati, kwa hivyo, ikiwa (harakati) zitakataliwa kwa uwazi, itakuwa vigumu (kuithibitisha) ile sifa ya mkusanyiko (wa siku ya kiama) iliokuja kwamba Allah atawachomozea (atawajia) watu wa siku ya kiama. Na kwamba Yeye (Allah) mwenyewe ndiye hasa atayewafanyia hisabu zao, kama alivyosema: “Na akaja Mola wako na Malaika safu safu”.85

Hayo ni maelezo ya Ibn Taymiyya akiwanukuu Mahanbali wenzake. Ama Ibn Al-Qayyim, yeye anasema:

Na kuja kwake (Allah siku ya kiama) si kufanya harakati wala si kuondoka (huko aliko) wala kubadilika kwani hayo ni pale ambapo mwenye kuja akiwa ni kiwiliwili au johari (kitu chenye kuchukua nafasi). Ilipothibiti kwamba yeye si kiwiliwili wala si johari wala si kitu chenye kufahamika (kwa akili tu) ambacho hakionekani wala kushikika (عرض); basi haikulazimika kwamba kuja kwake kuwe kwa harakati wala kuondoka.86

Kisha baada ya kunena hivyo, Ibn Al-Qayyim akapiga mifano inayofuata, akatongoa hivi:

Na lau ulizingatia hayo kwa kauli yao (Waarabu wanaposema) fulani kiama chake kimemjia ( قيامته فالنا جاءه ) na mauti yamemjia ,(جاءت) na maradhi yamemjia ;(الموت المرض na yaliofanana na hayo ,(جاءهkatika yale ambayo yapo, yanaingia kwake wala hayana mjo (wa kweli kweli) basi hilo lingelikubainikia.87

Na bila shaka hili alilolisema Ibn Al-Qayyim hapa ni jambo sahihi kabisa, kwani neno جاء kuja katika lugha ya Kiarabu na katika Qur-ani, kama vile

84 - Suratul-Fajri (89) aya ya 22. 85 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 27. 86 - Ibn Al-Qayyim Ijtima’u Al-Juyush uk. 88. 87 - Ibn Al-Qayyim Ijtima’u Al-Juyush uk. 89.

36

lilivyotumika kwa kitu chenye kuja kweli kweli, pia limetumika likitegemezwa katika mambo ambayo hayaji kweli kweli, yaani mambo ambayo hayana sifa ya kuhama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine. Na wala hakuna qarina isipokuwa ‘aqliyya, yaani yale yanayofahamika kiakili tu, na kwa hivyo, qarina ni haliyya hali halisi ilivyo au inayofahamika tu katika maneno. Mfano wa hayo ni kama Aya inayosema:

الموت أحدهم جاء إذا حتىMpaka mauti yakimjia mmoja wao.88

Na bila shaka mauti hayaji mjo wa uhakika yaani hayatoki sehemu moja kwenda nyengine, bali ni hali ambayo mtu inamfikia katika nafsi yake ambapo kiwiliwili chake kinatengana na roho yake. Ama kutoka sehemu moja kwenda nyengine, hii si sifa ya mauti bali ni sifa ya malaika wa mauti. Na kilichozuia tusiizingatie maana ya asili ya neno jaa (kuja) katika Aya hio Mpaka mauti yakimjia mmoja wao ni kile kinachofahamika kiakili kwamba mauti si kiwiliwili hata ikajuzu kuwa kifanye harakati ya kuhama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine.

Kama umelifahamu hilo, basi utakuwa umeelewa kwamba neno jaa (kuja) lililomo katika Aya: “Na akaja Mola wako na Malaika safu safu” ni lazima lifasiriwe kwa mujibu wa alivyo yule ambaye neno hilo limetegemezwa kwake naye ni Allah; kama vile ambavyo linafasiriwa neno hilo hilo katika Aya Mpaka mauti yakimjia mmoja wao kwa mujibu wa yalivyo yale ambayo neno hilo limetegemezwa kwake nayo ni mauti. Kwa maana nyengine ni kuwa, kama vile ambavyo Aya inasema kwamba mauti yanakuja ilhali hayaji mjo wa uhakika bali ni hali inayomfikia mtu tu kwa sababu mauti si kiwiliwili; basi vivyo hivyo neno kuja lililomo katika Aya inayosema: “Na akaja Mola wako na Malaika safu safu” linafasiriwa kuwa kuja huko kwa Allah si mjo wa kweli kweli ambao ni kuhama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine kwani Allah si kiwiliwili. Kwa ubainifu zaidi ni kuwa, maana ya asili, ya uhakika na ya kweli kweli ya neno kuja katika lugha ya Kiarabu – na nyenginezo – ni kufanya harakati za kuondoka kutoka sehemu hadi sehemu. Na hili ni muhali kwa Allah ambaye:

1) Hana mfano katika dhati yake wala katika sifa zake.2) Ambaye hahitaji chochote katika ulimwengu wala hamuhitajii

yoyote katika walimwengu bali amri yake anapotaka jambo husema kua nalo likawa; na ni mwenye uwezo wa moja kwa moja (

مطلقة .(absolute power قدرة

88 - Sura 23, Aya 99.

37

Na wala kuifasiri Qur-ani hivyo si kuyakataa maneno ya Allah alioyasema, bali ni kutafuta nini Allah kakikusudia katika usemi wake. Nasi tumelazimika kufasiri hivyo kwa sababu zile zile tulizozieleza kabla kwamba lugha ya Kiarabu ina migawanyiko miwili tu:

1) Hakika.2) Majazi.

Na kila neno la Kiarabu linakuwa na maana yake ya uhakika inayotumika katika lugha. Sasa mtu anapolifasiri andiko anatakiwa kwanza atazame je nini maana ya uhakika ya neno hilo katika lugha ya Kiarabu. Kisha baada ya kuipata hio maana ya uhakika ya neno hilo, ndio aitazame tena je maana hio ya uhakika inawezekana kusifiwa kwayo yule ambaye neno lenye maana hio limehusishwa naye? Ikiwa haiwezekani bila ya kuliletea neno hilo ta-awil, basi neno hilo huwa limetumika kimajazi na hapo inabidi zitazamwe maana zake za kimajazi. Kwa msingi huu basi, kama maana ya kuja katika lugha ni kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyengine, basi kuja ni sifa ya kiwiliwili kama alivyosema Ibn Al-Qayyim. Na kwa vile Allah si kiwiliwili basi huwezi kusema kwamba atakuja yeye mwenyewe kwa uhakika. Ukiniambia: “Atakuja kwa uhakika unaowiyana na utukufu wake”. Nitakujibu kwamba Allah kaiteremsha Qur-ani kwa lugha ya Kiarabu. Na lugha aliotuhubiria sisi kwayo ni lugha ile ile ya Waarabu wenyewe wanaoielewa. Na Waarabu hawana kwao maana ya kuja kwa hakika isipokuwa kuondoka sehemu moja kwenda nyengine. Vyenginevyo inakuwa kuja kwa maana ya kimajazi. Kwa mfano linapokuja jeshi la Zaid, basi Waarabu wanaweza wakasema kimajazi: زيد yaani jeshi ,(Zaid kaja) جاءlake limekuja: si yeye mwenyewe; au imekuja habari yake. Na lugha hii, kama vile ambavyo Waarabu walikuwa wakiitumia hapo kale, basi ndivyo wanavyoitumia leo hii. Hadi leo hii basi utawasikia Waarabu wakisema:

العراق بوش جوج yaani jeshi lake ,(Gorge Bush kaingia Iraki) دخلlimeingia Iraki: si yeye mwenyewe. Au العراق بوش جوج يوم جاء منذ (Tangu siku Gorge Bush aliokuja Iraki), yaani tangu siku jeshi lake lilipokuja. Na mfano wa hili ni kama Hadithi Qudsi inayosema:

هرولة أتيته يمشي أتاني فإن(Allah anasema: Mja wangu) akinijia naye anakwenda kwa miguu

(mwendo wa kawaida) basi mimi ninamjia mbio.

Ni wazi kwamba kuja kwa Mungu kulikotajwa hapa ni majazi, kwa sababu ya kuwepo qarina inayosema “mja wangu akinijia”, kwani hakuna mtu anayefunga safari ya uhakika akaenda kwa Allah kwa miguu; kama vile ambavyo hatujapata kusikia kwamba kuna mtu kajiwa na Allah kwa uhakika.

38

Baada ya hayo, sasa tazama kauli ya Al-Imamu Ahmad bin Hanbal. Sheikh Abdullah Al-Harari katika kitabu chake Al-Maqalatu Al-Sunniyya ananukuu yafuatayo:

Amesema Al-Bayhaqi katika manaqib89 ya Ahmad: “Katwambia Al-Hakim katuhadithia Abu ‘Amri bin Simak katuhadithi Hanbal bin Is-haaq kasema nimemsikia ami yangu Aba ‘Abdillah yaani (Al-Imamu) Ahmad anasema: ‘walinitolea hoja siku hio, yaani siku aliojadiliwa katika nyumba ya amiril-Mu-uminin, wakasema: ‘Suratul Baqara itakuja siku ya kiama na itakuja Suratu Tabarak. Basi (Mimi Ahmad bin Hanbal)90 nikawambia: ‘Hizo (zitazokuja) ni thawabu (za sura hizo: sio Sura zenyewe)”, Allah amesema:

ربك وجاء (Na akaja Mola wako), yaani utakuja uwezo wake, hakika ya Qur-ani ni mithali (mifano) na mawaidha.

Na akasema Al-Bayhaqi:

Katika haya kuna dalili kwamba yeye Ahmad alikuwa haitakidi kuwa kuja (kwa Allah) ambako kumetajwa katika Qur-ani; na kushuka (kwa Allah) kulikotajwa katika Sunna ni kuondoka kutoka katika sehemu moja kwenda nyengine kama dhati za viwiliwili zinavyokuja na kushuka. Bali huko (kuja kwa Allah) maana yake ni kudhihiri ishara zake na uwezo wake, kwani wao (hao waliojadiliana na Al-Imamu Ahmad) walipodai kwamba Qur-ani lau ilikuwa ni maneno ya Allah na ni sifa katika sifa zake basi isingelijuzu kwake kuwa ije. (Hapo ndipo) Abu Abdillah (Al-Imamu Hanbal) alipowajibu kwamba kinachokuja ni thawabu za kisomo ambacho anataka kukidhihirisha siku hio. Basi kule kukidhihirisha kwake akakuita kuwa ni kuja.91

Sasa baada ya hayo, Sheikh Kasim Mafuta anaweza kuchagua kauli anayoitaka na kuiita kuwa ndio kauli ya Al-Salafu Al-Salih au kauli ya Ahlu Sunna:

1) Kauli ya Ibn Taymiyya anayoinukuu kutoka kwa Mahanbali wengine bila ya kuipinga, bali kwa kuipa uzito zaidi. Nayo ni kauli inayosema kwamba Allah atakuja siku hio ya kiama yeye mwenyewe; na kwa hivyo yeye ni kiwiliwili kwani tukikataa kuwa ni kiwiliwili kuna hatari ya kutoweza kuithibitisha sifa hio ya kuja kwa Mwenyezi Mungu!

2) Kauli ya Ibn Al-Aqayyim katika Ijtimaau Jayshihi. Nayo ni kuwa Allah atakuja lakini si kwamba ataondoka huko aliko kwani kuondoka kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine ni sifa ya kiwiliwili na Allah si kiwiliwili.

89 - Habari zake njema. 90 - Al-Imamu Ahmad. 91 - Al-Harari, Abdullah Al-Maqalatu Al-Sunniyya Fii Kashfi Dhalati Ibn Taymiyya uk. 115.

39

3) Kauli ya Al-Imamu Ahmad, kwamba makusudio ya Aya hio (Na akaja Mola wako), ni kudhihiri kwa uwezo wake kama vile ilivyosemwa kuwa Suratul Baqara itakuja siku ya kiama yaani yatadhihiri malipo ya sura hio.

4) Na labda chaguo la nne linaweza kuwa katika kauli nilioiona na ambayo inastaajabisha kwa jinsi kichwa chake kinavyogongana na miguu yake. Nayo ni kauli nilioisoma katika maelezo ya Dr. Muhammad Khalil Harras katika Sharhu Al-‘Aqidati Al-Wasatiyya. Anasema Dr. Harras:

. فهذه خلقه من بائن عرشه فوق وهو ويدنو وينزل يجيء سبحانه وهوسبحانه كلها له أفعال

الحقيقة على

Naye Allah Mwenye kutakasika na kila upungufu anakuja na anateremka na anakurubia (kuwakurubia viumbe wake); Naye yuko juu ya arshi yake kapambanuka kutokana na viumbe wake. Haya yote ni matendo ya Allah mtukufu (ambayo anayatenda) kwa uhakika (si kwa majazi).92

Tazameni mantiki hii! Mungu anakuja kweli kweli na anashuka kweli kweli, lakini yuko kule kule aliko kakaa juu ya kiti chake hajaondoka! Na anavikurubia viumbe vyake kweli kweli lakini yuko juu mbinguni mbali na viumbe wake! Sasa huku ndiko kuja kweli kweli na ndiko kushuka kweli kweli; na huko ndiko kukurubia kweli kweli. Labda kesho watu wa skuli hii, kwa ufahamu wao huu, watatwambia kwamba Allah anakaa katika shingo za watu mkao wa kweli kweli, lakini unaomfalia Yeye au unaomstahikia Yeye, kwani Qur-ani inasema:

الوريد حبل من إليه أقرب ونحنNa sisi tupo karibu naye zaidi kuliko mshipa wa shingo (yake).93

Mshipa wa shingo wa mtu uko ndani ya shingo yake. Na Allah anasema yupo karibu zaidi na mtu kuliko mshipa wake mwenyewe uliomo ndani ya shingo yake. Sasa tuseme – kwa msingi wa kukataa majazi na ta-awil au kwa msingi wa kuzifasiri Aya kwa mujibu wa dhahiri yake (literally) – Allah anakaa katika shingo za watu?

Au labda kesho kutwa watu wa skuli hio watatwambia kwamba mtu anapokufa basi Allah anahudhuria na anakuwa yupo karibu zaidi kuliko watu waliohudhuria hapo, kwani Qur-ani inasema:

92 - Dr. Muhammad Khalil Haraas Sharhu Al-’Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 55. 93 - Sura 50, Aya 16.

40

وم بلغت إذا فلـــوال ( ونحن84) تنظـــرون حينئذ ( وأنتم83) الحلقـــتبصرون ال ولكن منكم إليه أقرب

Basi mbona (roho) inapofika katika koo**Nanyi wakati huo munatazama**Nasi tukaribu zaidi naye (huyo anayekufa) kuliko nyinyi lakini hamuoni.94

Sasa baada ya hayo, kwa upande wetu, tunaomuomba Sheikh Mafuta aturuhusu tumueleze kwanini tumeikubali tafsiri ya waliosema kuwa Aya hio: ربك وجاء (Na akaja Mola wako), kwamba haina maana ya kuwa Allah atakuja kweli kweli; bali itayokuja ni amri yake. Na katika kutoa kwetu maelezo hayo, itatubidi kutazama misingi miwili:

1) Kuifasiri Qur-ani kwa Qur-ani. Nayo ndio njia bora ya kumfahamu Allah anakusudia nini katika ujumbe wake.

2) Kuzitazama hoja za kiakili. Nazo zinakubalika ikiwa hazikugongana na andiko la wazi.

TAFSIRI YA QUR-ANI KWA QUR-ANI

Huu ndio msingi mkuu ambao wanavyuoni tangu zama za Masahaba walikuwa wakiutumia katika kuifahamu maana halisi ya Aya. Anasema Al-Imamu Ibn Taymiyya:

Ikiwa mtu atakuuliza, ni njia gani iliobora katika kuifasiri Qur-ani? Basi jawabu ya (suali) hilo ni kuwa njia sahihi zaidi katika hayo, ni kuwa Qur-ani ifasiriwe kwa Qur-ani, kwani kilichotajwa bila ya kufafanuliwa katika sehemu moja, hakika yake hufasiriwa katika sehemu nyengine. Kilichofupishwa katika sehemu moja basi huelezwa kwa urefu katika sehemu nyengine.95

Anasema Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Al-Mufassir:

…Ya kwanza ni Qur-ani yenyewe; hakika ya kitu bora kilichotumika katika kuifasiria Qur-ani ni Qur-ani yenyewe. Aya ngapi hazina ufafanuzi kisha ufafanuzi wake ukafunuliwa katika Aya nyengine. Na mara ngapi ujumla wa Aya moja unahusishwa na Aya nyengine….96

94 - Sura 56, Aya 83-85. 95 - Al-Harrani, Ibn Taymiyya Al-Nukatu Al-Mutammima uk. 89. 96 - Al-Khalili, Ahmad bin Hamad Jawahiru Al-Tafasir j. 1, uk. 20.

41

Ama mifano ya Aya ambazo huwezi kuufikia usahihi wa tafsiri yake ila kwa kuzifungamanisha na Aya nyengine kwa sababu ya kuondoshwa neno katika Aya moja au kwa kukosekana ubainifu, ziko nyingi. Mfano mmoja katika mifano iliosemwa na baadhi yao ni Aya isemayo:

يعلمها ال الغيب مفاتح وعنده هو إال

Na kwake Yeye Allah kuna funguo za yaliojificha; hakuna azijuaye ila Yeye tu.97

Amepokea Al-Bukhari kutoka kwa Mtume (s.a.w.) kwamba kaifungamanisha Aya hio na Aya isemayo:

وينز اعة الس علم عنده الله تدري إن وما األرحام في ما ويعلم الغيث لم وم نفس غدا تكسب ا ـــاذا

خبير عليم الله إن تموت أرض بأي نفس تدري

Hakika ya Allah anao ujuzi wa saa (ya Kiama kitakuwa wakati gani) na anateremsha mvua na anakijua kilichomo katika matumbo ya uzazi; na nafsi haijui (hata) nini itakichuma kesho; wala nafsi haijui itakufa katika ardhi gani; hakika Allah ni Mjuzi, Mwenye habari (ya kila kitu).98

Na kwa hivyo, Mtume (s.a.w.) akasema katika Hadithi hio: “Funguo za yaliojificha ni tano” kisha akasoma Aya hio tulioinukuu.99 Na kwa tafsiri hio iliopokewa katika Hadithi, basi maana ya funguo za yaliojificha ambayo yametajwa katika Aya 59 ya Sura ya 6, ni mambo hayo matano yaliotajwa katika Aya 34 ya Sura ya 31.

Na msingi huu wa kuifasiri Qur-ani kwa Qur-ani, utawakuta wanavyuoni wengi wamekwenda nao katika tafsiri zao. Mara ngapi utakuta katika tafsiri – kama ya Ibn Kathir – ikisemwa: “Aya hii ni kama Aya kadha”. Abu Hayaan, kwa mfano, kawapinga waliodai kuwa maana ya neno طائف taaifu lililotajwa katika Aya ya Qur-ani isemayo: طائف عليها فطاف

ربك من fataafa ‘alaihaa taaifum Rabbik, “Basi (shamba hio) ikatokewa na taaifu (tukio) juu yake litokalo kwa Mola wako,”100 kawapinga Abu Hayyaan waliodai kuwa maana ya neno hilo taaifu ni mahususi kwa tukio la usiku. Abu Hayyaan kawakatalia dai hilo kwa sababu Allah kasema katika 97 - Sura 6, Aya 59. 98 - Sura 31, Aya 34. 99 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 4778. Kwa maelezo zaidi tazama Fat-hu Al-Bari j. 9 uk.5531, katika sherehe ya Hadthi hio. 100 - Sura 68, Aya 19.

42

Aya nyengine ya Qur-ani: وا الذين إن هم إذا اتقــ ــ ــائف مس من ط يطان inna الشــ lladhina ttaqaw idhaa massahum taaifun mina shaytaan…. (Hakika wale wenye kumcha (Allah) basi taaifu (pepesi)101

ya shetani ikiwagusa…….).102 Anasema Abu Hayyaan kwamba hapa neno taaifu limetumika kumaanisha tukio la pepesi za shetani, nazo hazimpati mtu wakati wa usiku tu; bali hata mchana pia humsibu.

Halkadhalika Aya isemayo: حسنات سيئاتهم الله يبدل فأولئك “Basi hao Allah huyabadilisha mabaya yao (na kuyafanya) mema”103

wanavyuoni wengine wa tafsiri wameifungamanisha Aya hio na Aya nyengine yenye kusema: بدل ثم ظلم من إال وء بعــد حسنا إني ســ فــ

ور رحيم غفــ “Isipokuwa aliyedhulumu (aliyeidhulumu nafsi yake) kisha akabadilisha (na kufanya) mema baada ya maovu, basi Mimi ni Mwenye kusamehe sana; Mwenye kurehemu sana”.104 Wengine wamezifungamanisha Aya mbili hizi na wakasema kwamba makusudio ya kuyabadilisha maovu na kuyafanya kuwa ni mema si kwamba madhambi yake yanageuzwa kuwa thawabu; bali ni kuwafikishwa kwake kufanya mema akawa sasa anafanya mema badala ya mabaya aliokuwa akiyafanya.

Halkadhalika Aya inayosema: شيء بكل الله وكان محيطا (Na Allah kakizunguka kila kitu).105 Na Aya: محيط ورائهم من والله (Na Allah yuko nyuma yao kawazunguka).106 Aya hizi na zilizo mfano wa hizi, ikiwa utazichukua kwa udhahiri wake na ukatumia msingi wa balkafa (bila ya namna), basi utapata natija kwamba Allah kakizunguka kila kitu kweli kweli. Kisha unaweza ukatumia falsafa ya balkafa ukasema:: “lakini mzunguko unaomstahikia Yeye: si kama tunavyozunguka sisi”. Lakini ikiwa utakwenda na msingi wa kuifasiri Qur-ani kwa Qur-ani na ukazifungamanisha Aya hizo na Aya isemayo: بكل أحاط قد الله وأن

شيء علما (Na kwamba Allah kakizunguka kila kitu kwa ujuzi (kwa kukijua)),107 basi utaipata tafsiri au maana ya “Allah kukizunguka kitu” ambayo imetajwa katika Aya nyengine. Na kwa hivyo, maana ya Allah kukizunguka kila kitu – kwa mujibu wa mjumuiko huu wa Aya za Qur-ani – ni kuwa kakizunguka kila kitu kiujuzi yaani anakijua kila kitu kiukamilifu.

101 - Yaani tukio vile vile; hapa ni tukio lenye kutokana na shetani kwa hivyo wajuzi wa lugha wamelifasiri “pepesi”. 102 - Sura 7, Aya 201. 103 - Sura 25, Aya 70. 104 - Sura 27, Aya 11. 105 - Sura 4, Aya 126. 106 - Sura 85, Aya 20. 107 - Sura 65, Aya 12.

43

Halkadhalika Aya ya Qur-ani inayosema: الله في وجاهدوا (Na fanyeni jihadi katika Mwenyezi Mungu),108 ni Aya ambayo ndani yake kuna neno lililoondoshwa. Na neno hilo lililoondoshwa utalijua kwa kuitazama Aya nyengine inayosema: الله سبيل في وجاهدوا (..Na wakafanya jihadi katika njia ya Allah).109 Kwa hivyo, neno sabil (njia kwa maana ya dini) ndilo lililoondoshwa katika Aya ya mwanzo na limeweza kubainika kwa msada wa Aya hio ya pili. Halkadhalika katika Aya inayosema: “Na akaja Mola wako…”, tumeweza kujua kwamba neno amr (jambo) ndilo lililoondoshwa kwani ndilo lililotajwa katika Aya nyengine za Qur-ani, kama vile Aya inayosema ينظرون هل يأتي أو المالئكة تأتيهم أن إال

ربك أمر Hawana wanachokisubiri isipokuwa kujiwa na Malaika au iwajie amri (jambo) ya Mola wako.110

Na kwa msingi huo wa kulifungamanisha andiko moja na jengine ndio wanavyuoni wa jumhur wameweza kutoa natija kwamba katika Aya hio “Na akaja Mola wako…” kuna majazu hadhfi yaani majazi ya kuondoshwa neno, na kwamba neno lenyewe lililoondoshwa, kama tulivyosema, ni neno amri (jambo). Na hili la kuwepo kwa majazu hadhfi yaani majazi ya kuondoshwa neno katika Aya za Qur-ani si jambo geni: Aya kadha wa kadha zimekuja katika mfumo huo. Kwa mfano, Aya ya Qur-ani isemayo: هافي كنا التي القرية لئوس “Na kiulize kijiji ambacho tulikuwemo ndani yake”,111 ndani yake kuna majazu hadhfi, na asili yake Aya hio ni kusema: فيها أهل لئوس كنا التي القرية “Na waulize watu wa kijiji ambacho tulikuwemo ndani yake”, vyenginevyo kijiji hakiwezi kuulizwa kwani hakisemi. Halkadhalika, kama tulivyoeleza hapo nyuma kidogo, mfano wa hilo ni Aya isemayo: الله في وجاهدوا (Na fanyeni jihadi katika Mwenyezi Mungu), ambapo utaona kwamba neno njia kwa maana ya dini katika Aya hii limeondoshwa, na asili yake ni: وجاهدوا

الله سبيل في (Na fanyeni jihadi katika njia (yaani Dini) ya Mwenyezi Mungu), kama Aya nyengine ilivyolibainisha hilo kwa kusema:

الله سبيل في وتجاهدون (…Na mufanye jihadi katika njia ya Allah).112

Kilichobaki ni kujua kwanini wanavyuoni wa jumhur wamedai kwamba katika Aya “Na akaja Mola wako…” kuna majazu hadhfi yaani majazi ya kuondoshwa neno na kwa upande mwengine kwanini wao wamelikadiria neno lililoondoshwa kuwa ni amri (jambo). Tunasema: Ama kwanini 108 Sura 22, Aya 78.

109 - Sura 2, Aya 218. 110 - Sura 16, Aya 33. Maelezo kwa urefu juu ya Aya hizi yatakuja baadae in shaa Allah..111 - Sura 12, Aya 82.

112 - Sura 61, Aya 11.

44

wanavyuoni wamedai kwamba katika Aya “Na akaja Mola wako…” kuna majazu hadhfi, ni kwa sababu ambazo tumezitaja kabla kwamba maana ya kuja kweli kweli katika lugha ni kuhama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine. Na hili haliwezekani kwa Allah kwani:

a) Yeye si kiwiliwili, wakati kuja kwa namna hio ni sifa ya viwiliwili.

b) Yeye hahitaji kufanya harakati ili aweze kulifanya alitakalo, bali unatosha uwezo wake na elimu yake kufanya alitakalo kun fayakun, bila ya kukurupuka. Kama vile anavyowaruzuku viumbe wote wakati mmoja kwa elimu yake na uwezo wake bila ya kuwajia; ndivyo atavyowahukumu viumbe wake wote siku ya kiama wakati mmoja bila ya kuwajia.

c) Kuhitaji kwenda sehemu ili uweze kufanya kitu ni alama ya udhaifu na ukosefu wa uwezo kamili.

Ama kwanini wanavyuoni hao wamelikadiria neno hilo amri (jambo) na kwamba ndilo lililoondoshwa, ni kwa sababu tatu:

1) Aya nyengine zimetaja kuja kwa Allah wala huwezi kuzifasiri kuwa kuja huko ni kuja kwa uhakika.

2) Aya nyengine zimetaja kuja kwa amri (jambo) ya Mwenyezi Mungu.

3) Tukalazimika kuzifungamanisha hizi na zile ili kufikia maana sahihi.

AYA ZA KUJA KWA MUNGU KIMAJAZI

Ama Aya zilizotaja kuja kwa Allah, bila kutaja ndani yake neno amri (jambo) lakini ikawa kulikadiria neno hilo ni lazima, ni Aya kama:

أطرافها من ننقصها األرض نأتي أنا يروا أولمJe hawaoni kwamba tunaijia ardhi tunaipunguza pembeni mwake.113

Lafdhi ya Aya hii inasema kwamba Allah anaijia ardhi ili kuipunguza pembeni (mipaka) mwake. Lakini je ni kweli kwamba Allah anaijia ardhi kwa hakika? Bila shaka kila mwenye akili – licha ya mwenye alimu – anadiriki kwamba kuja huku kwa Allah kulikotajwa hapa ni kuja kwa amri yake – uwezo wake, nguvu zake n.k.

Na mfano mwengine ni Aya isemayo:

113 - Sura 13, Aya 41.

45

عليهم فخر القواعد نم بنيانهم الله فأتى قبلهم من الذين مكر قدقف وأتاهم وقهمـف من السيشعرون ال حيث من العذاب

Kwa hakika walifanya hila wale waliokuwa kabla yao, basi Allah AKAZIJIA nyumba zao katika misingi, basi mapaa yakawaangukia kutoka juu na adhabu ikawajia kutoka wasikokujua.114

Aya hii inazungumzia adhabu iliowafika baadhi ya makafiri. Miongoni mwa adhabu hizo ni kuwa Allah ALIKUJA AKAINGIA KWENYE MISINGI YA NYUMBA ZAO. Je hapa aliyekuja ni Allah akaingia chini ya misingi ya majumba au iliokuja ni amri yake pamoja na kuwa neno amri halikutajwa katika Aya hio? Ni wazi kwamba kule kuja kwa amri ya Mwenyezi Mungu ndiko kulikoitwa kuwa ni kuja kwa Mwenyezi Mungu. Na ibara za namna hii kwa Waarabu si ngeni. Waarabu husema: علي ilhali ,(Ali kaja) جاءhakuja yeye binafsi bali imekuja barua yake au jeshi lake au amri yake.

Mfano mwengine ni Aya isemayo:

لم حيث من الله فأتاهم الله من حصونهم مانعتهم أنهم وظنوا يحتسبوا

….Na wakadhania kuwa ngome zao zitawakinga kutokana na Allah, basi Allah AKAWAJIA kutokea wasikokufikiria.

Aya hii inazungumzia vita vya Waislamu na Mayahudi wa Banii Al-Nadhiir. Tunapata katika Aya hii kwamba Allah KAWAJIA Mayahudi hao kutokea katika sehemu ambayo wao hawakuitarajia. Je aliyekuja hapa ni Mwenyezi Mungu mwenyewe au ni adhabu ya Allah kupitia katika mikono ya waja wake?

Ukiniambia: “Lakini katika Aya hizi kuna qarina zenye kuonesha kwamba Allah hakuja mwenyewe”. Ukiniambia hivyo nitakujibu kwamba:

a) Qarina ni katika masharti ya majazi nawe huamini kuwepo kwa majazi. Au utayathibitisha majazi hapa na uyakatae kwengine?

b) Ikiwa unakubali kwamba hapa kuna qarina iliolitoa neno kuja katika maana yake ya asili na kulipeleka katika maana nyengine au kwamba kuna qarina yenye kuonesha kuwepo kwa neno amri (jambo) japo kuwa neno hilo halikutajwa, basi hii inamaanisha kwamba tumekubaliana kwamba majazi yapo. Ukiniambia kwamba “Aa huu ni uslubu tu si majazi”. Nitakujibu kwamba wanavyuoni wa fani za usuli wanasema kwamba ال

114 - Sura 16, Aya 26.

46

ا في إصطالحلمشاحة Hakuna kujadiliana katika maneno ya kitaalamu au ya kifani (technical terms). Yaani kinachozingatiwa ni uhakika wa kitu: si jina lake, na kwa hivyo je tuyaite hayo kuwa ni majazi au tuuite kuwa ni uslubu, hili si muhimu: kilichomuhimu ni je hapo kuna neno lililotumika kinyume na maana yake ya asili au halipo? Au kwa hapa je kuna neno lililoondoshwa au halipo? Ikiwa lipo neno hilo basi hayo ndio majazi yenyewe wanayoyakusudia wanavyuoni nawe unaweza kuyapa jina unalolitaka ikiwa jina majazi hulipendi. Kama halipo neno hilo lililotumika kinyume na maana yake ya asili au lililoondoshwa, basi itabidi utueleze je Aya hio inathibitisha kwamba Allah kazijia nyumba hizo kweli kweli akajitia chini ya misingi au – kama ilivyo katika dhahiri ya Aya nyengine – Allah kawajia Mayahudi na kuijia ardhi kweli kweli?

MJADALA NA AL-DARIMI

Lakini Sheikh ‘Uthman bin Said Al-Darimi, yeye anatafautisha baina ya Aya hizo au kama hizo na Aya isemayo: “Na akaja Mola wako na Malaika safu safu “.115 Anasema:

Tafauti iliopo baina ya Aya hizo zenye kusema kuwa Allah kawajia Banu Quraidha116 kutoka wasipopajua, na kwamba kazijia nyumba zao na kwamba kaijia ardhi, ni kuwa Aya hizi zinazungumzia adhabu iliowafika watu hao hapa duniani, wakati Waislamu wamekubaliana kwamba Mwenyezi Mungu hateremki isipokuwa siku ya kiama kwani siku hio Yeye anakuja kupitisha hukumu Yeye mwenyewe baina ya viumbe. Kwa hivyo, Siyaaq ya Aya hizo ni tafauti na Siyaaq ya Aya “Na akaja Mola wako na Malaika safu safu”.

Hayo ndio maneno yake.117 Nayo ni maneno ya ajabu kabisa, kwani:1) Kuja kwa Allah ama kuwe ni kwa hakika au ni kwa majazi.

Tukisema kuwa ni hakika basi ni vile maana ya neno kuja linavyomaanisha katika lugha ya Kiarabu. Na kuja kwa uhakika katika lugha ya Kiarabu – sawa na ilivyo katika lugha nyengine – ni

115 - Suratul-Fajri (89) aya ya 22. 116 - Hivi ndivyo alivyosema Al-Darimi. Lakini kilicho mashuhuri ni kuwa vita hivi vilikuwa baina ya Waislamu na Banii Al-Nadhir kama alivyosema Ibn Kathir, Al-Tabari, Al-Tabaatabaai, Al-Zamakhshari, Abdul-Razzaaq, Al-Sabuni na wengine. Kwa hivyo, alichokisema Al-Darimi ama itakuwa ni riwaya shaadha au kasahau au kosa la chapa. 117 - Maneno hayo sikuyanukuu neno kwa neno kwani ni marefu: nimenukuu nukta (points) zake tu kimaana. Tazama ‘Uthman Al-Darimi Al-Radu ‘Alaa Bishr Al-Marisi 50-51.

47

kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyengine. Na kuja huku kuna masharti yake:

a) Chenye kuja kiwe ni kiwiliwili.b) Kitoke sehemu kwenda nyengine. c) Sehemu kiliotoka ama kiwe bado kiko au kimeondoka. d) Kikiwa kimekuja huku na huko kilikotoka bado pia kipo,

basi chenye kuja hicho kitakuwa ni chenye kunyuuka au chenye kujizongoa.

e) Kikiwa kule hakiko: kimeondoka, basi hio ni alama ya kwamba chenye kuja kina udhaifu na kwamba hakiwezi kufanya kikitakacho ila kwa kuhama sehemu moja kwenda nyengine.

Hizo si kwamba ni hoja za kiakili tu, bali ndivyo ilivyo maana ya kilugha ya neno kuja. Wala usiniambie kwamba “Masharti haya ni sifa za viumbe, nasi hatuwezi kufanya Qiyas baina ya Muumba na kiumbe”. Kwani tunasema kwamba tunachokizungumzia sisi si mas-ala ya Qiyas, bali ni mas-ala ya madlulu lughawi (maana ya kilugha) ya neno kuja, kwamba neno kuja katika lugha ya Kiarabu haliwi ila na maana hio tulioieleza ikiwa neno hilo litatumika katika maana yake ya uhakika. Ama likitumika na kumaanisha maana nyengine zisizokuwa hizo basi linakuwa limetumika kimajazi: si uhakika wake wa kuja. Na hili ndilo kama lile alilolinena Al-Imamu Jua la Dini Ibn Al-Qayyim: “mauti yamekuja” ilhali mauti hayaji. Au kusema “habari imekuja” ilhali habari haiji bali inasimuliwa. Na kwa hivyo, ilipobainika kwamba Allah hawezi kuja kwa namna yoyote katika hizo tulizozieleza, basi elewa kwamba neno kuja lililotumika katika Aya hio ni kuja kimajazi na kwa hivyo ni lazima lifasiriwe kwa maana inayokubaliana na utukufu wa Allah.

Wala huwezi kusema:

Kuja kwake ni kuja ambako hatuwezi kukufahamu, bali ni kuja kunakokubaliana na utukufu wake, wala kuja huko hakuna mfano kwa sababu Yeye “ شيء كمثله .(Hana mfano wa kitu) ”ليس

Huwezi kutoa hoja hio na hoja yako ikanyooka mnyooko wa mtarimbo, kwani tunasema kwamba Aya isemayo: “Hana mfano wa kitu”, haikuja kubomoa maana za kilugha zilizomo katika lafdhi za Aya za Qur-ani, wakati ukisema “Kaja mjo wa uhakika lakini si kwa namna tunavyojua” basi unakuwa umei’attil (umeibomoa) maana ya neno kuja iliomo katika Aya kwani kuja mjo wa kweli kweli katika lugha ya Kiarabu unafahamika na kulitoa neno katika maana yake hio na kulipeleka katika maana nyengine

48

isiojulikana haikupokewa kamwe katika lugha.118 Katika lugha ya Kiarabu hakuna kusema “kaja mjo wa kweli lakini si kama tunavyojua sisi” bali kuna “Kaja kweli kweli” au “Kaja kimajazi”. Kwa maana hii, inakubainikia kwamba kanuni ya kutokumshabihisha Allah na viumbe iliojengeka katika Aya isemayo: “ شيء كمثله inabidi ,(Hana mfano wa kitu) ”ليسifungamanishwe na kanuni za kilugha ili kufikia maana sahihi, vyenginevyo itatubidi tuutendee kazi msingi mmoja na tuutupe msingi mwengine, nalo ni kinyume na kanuni “ إهماله من أولى النص Kulitendea kazi) ”إعمالandiko ni bora kuliko kulipuuza).

Wala haiwezekani kudai kwamba:

Kuja kwake ni kama kuwepo kwake; yaani kama vile ambavyo Yeye yupo na sisi tupo lakini kuwepo kwetu ni tafauti na kuwepo kwake; halkadhalika kuja kwake ni tafauti na kuja kwetu.

Pia hoja hio ni hoja dhaifu, kwani tunasema:a) Hiki ndio Qiyaas (ulinganisho) cha Kiumbe na Muumba

ambacho munakikataa, yaani Qiyaas kilichojengeka juu ya misingi ya uhakika wa kuja na uhakika wa kuwepo.

b) Kuja tunakokuzungumzia ni huku kunakoeleweka katika lugha ya Kiarabu na lugha nyengine: si kuja kwengine. Ama kuja kwengine – ikiwa kupo – basi kunahitaji ushahidi wake mwengine wa kilugha: ibainishwe kilugha kwamba neno kadha lina maana hio. Kwa hivyo, tuleteeni katika lugha ya Kiarabu kwamba kuna kuja kwa uhakika kusikokuwa huku tunakokujua.

c) Uhakika wa kuwepo (existence) unaofahamika katika lugha ya Kiarabu na nyengine hautafautishi baina ya kuwepo kwa kiumbe na kuwepo kwa Muumba. Yaani uhakika wa kuwepo hauna tafauti kwani kuwepo ni kinyume cha kutokuwepoعدم) non-existence) tu. Bali tafauti iko katika namna ya kuwepo huko: si uhakika wa kuwepo kwenyewe.

d) Kuwepo ni sifa ya ukamilifu bila ya sifa hio hakuna Mungu; ama kuja ni sifa ya udhaifu kwani ni sifa yenye kuonesha kuwa mjaji anahitajia na si mwenye uwezo mutlaq (usio mipaka). Bwana Kasim mwana wa Mafuta hawezi kupata chungwa ila atapolijia soko au kumuagiza mtu atayelijia soko; Allah jambo lake ni kun fayakun: hahitaji kuja ili ndio aweze kuwafanyia waja hesabu.

Jambo jengine: alilolidai Al-Darimi na kutafautisha kwalo baina ya Aya inayosema: “basi Allah AKAZIJIA nyumba zao katika misingi” na Aya: 118 - Bali kufanya hivyo ni majazi na ta-awil.

49

“Na akaja Mola wako na Malaika safu safu” ni kuwa katika Aya ya mwanzo inazungumzia kuja hapa duniani ili kuleta adhabu hapa duniani na:

Waislamu wamekubaliana kwamba Allah yuko juu ya ‘Arshi yake juu ya mbingu zake……; na wala hawakuwa na shaka kwamba Yeye atateremka siku ya kiama ili ahukumu baina ya waja wake….119

Nasi tunasema kwamba – kwanza – maneno haya hayana ukweli. Na bila shaka, pamoja na kuwa Ibn Taymiyya kakisifu sana na kukiusia sana kitabu hicho cha Al-Darimi, lakini tunamsubiri Sh. Kasim Mafuta labda kesho atamueka Imamu wake huyu, ‘Uthman Al-Darimi katika urodha ya waongo! Mimi simwiti mwongo, lakini ninazungumza kwa mujibu wa minhaj ya Sheikh Kasim Mafuta. Wapi kapata Al-Darimi kwamba:

Waislamu wamekubaliana kwamba Allah yuko juu ya ‘Arshi yake juu ya mbingu zake?” Na wapi kapata kwamba “Na wala hawakuwa na shaka (Waislamu) kwamba Yeye atateremka siku ya kiama ili ahukumu baina ya waja wake…?

Makubaliano haya yamo katika vitabu gani? Na ni Waislamu wangapi duniani tangu zamani hadi leo wenye itikadi hizo hata akadai kuwa Waislamu wamekubaliana?

Ama tukija katika tafauti hio alioisema Al-Darimi, tunakuta kuwa ni utafautishaji uliombali na tahqiq za kielimu, kwani::

1) Kinachozungumzwa hapa ni kuwa kutajwa kwa maneno “Kuja kwa Allah” haijaleta maana kwamba ni lazima kuja huko kuwe ni kuja kwa hakika. Hio ndio maudhui inayozungumzwa. Kisha kauli hii ikapatiwa ushahidi wa Aya hizo tulizozinukuu ikiwemo Aya isemayo: “basi Allah AKAZIJIA nyumba zao katika misingi.” Nasi tunakubaliana kwamba Allah hakuzijia nyumba hizo kweli kweli (physically). Kwa hivyo:

a) Hii ina maana kwamba neno kuja hapo ni majazi: si hakika.b) Kuja kwa Allah si lazima iwe kuja kweli kweli.c) Nadharia ya kwamba “tumsifu Allah vile alivyojisifu”

haikuweza kufanya kazi katika ulimwengu wa hakika, kwani hapa Allah anasema kaja na kuingia chini ya misingi ya nyumba, wakati hilo nyinyi hamulikubali.

Ukinambia:

119 - Tazama ‘Uthman Al-Darimi Al-Radu ‘Alaa Bishr Al-Marisi 50.

50

Aa! Unajua Allah kasema: ق ويوم ماء تشق ل بالغمام الس ونز المالئكة تنزيال Siku ambayo mbingu zitapasuka na Malaika

watateremka mteremko wa kweli kweli.120 Hapa imepokewa riwaya kwamba mbingu zitapasuka na Allah atakuja katika kipande cha mawingu. Na hili linathibitishwa na Aya inayosema: ينظرون هل إال

والمالئكة الغمام من ظلل في الله يأتيهم أن Hawana wanachokisubiri isipokuwa Allah awajie katika kivuli cha mawingu na Malaika.121 Basi ikaeleweka kwa mujibu wa maandiko haya kwamba Allah haji isipokuwa siku ya Qiyama.

Ukiniambia hivyo, nitakujibu kwamba:a) Aya mbili hizo – tukijaalia kwamba hiyo tafsiri uliozifasiri wewe ni

sahihi basi – hazijathibitisha kwamba Allah haji isipokuwa siku ya Qiama; bali zinathibitisha kwamba atakuja siku ya kiama. Na hii ni kwa mujibu wa tafsiri yako: si tafsiri ya jumhur. Ama kuzichukua Aya hizo na kuthibitisha kwazo kutokuja kwa Allah hapa duniani ni kuthibitisha kitu kwa njia ya Mafhumu Al-Laqab. Ubainifu wake ni kuwa iliposemwa kwamba Allah atakuja huko akhera; wewe ukadai kwamba basi duniani hatokuja. Na kwa msingi huu, ukaikataa sifa ya kuja iliomo katika Aya: “basi Allah AKAZIJIA nyumba zao katika misingi” na Aya: “Je hawaoni kwamba tunaijia ardhi tunaipunguza pembeni mwake” na Aya: “….Na wakadhania kuwa ngome zao zitawakinga kutokana na Allah, basi Allah AKAWAJIA kutokea wasikokufikiria”. Na Mafhumu Al-Laqab – kama unavyojua – haikubaliki katika kuthibitisha mas-ala ya dhana ya kifiq-hi, basi vipi itathibitisha mas-ala ya kiitikadi? Kwa hivyo, sisi bado tunasema kwamba kuja kwa Allah si lazima kuwe ni kuja kwa uhakika au kwa usahihi zaidi haiwezekani kuwe ni kuja kwa uhakika bali kuja kwake ni kuja kwa amri (jambo) yake.

b) Riwaya zilizotegemewa kutoa tafsiri hio ni riwaya za kutunga bila

shaka kama mutun zake zinavyojionesha.122 Riwaya moja imesimuliwa kutoka kwa Abu Huraira lakini katika sanad yake kuna Nu’aim bin Hammad. Naye wengine wamemkubali na wengine wamemkata na wakasema kuwa ni dhaifu na anasimulia Hadithi munkar.123 Na wengine wakasema kwamba alikuwa akitunga riwaya

120 - Sura 25, Aya 25. 121 - Sura 2, 210. 122 - Tazama riwaya hizo katika Uthman bin Said Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi j. 1, uk. 52-53. 123 - Anasema Al-Albani: “(Nu’aim) Bin Hammad mwenyewe ni dhaifu”. Al-Dhaifa j. 3, uk. 469, j. 13, uk. 393.

51

za kumtia aibu Abu Hanifa na kutunga riwaya za kuipa nguvu Sunna! Na wengine wakasema ni Imamu au ni mkweli lakini anakosea sana.124 Sanad hii huenda ikawa ina mpokezi asiyejulikana vile vile. Bali matn ya riwaya hii kama tutavyoijadili katika Hadithi za kuonekana kwa Allah ni matn mbovu ilioje. Riwaya ya pili imenasibishwa na Ibn Abbaas lakini katika sanad yake kuna Hammad bin Salama, naye ni dhaifu, tatamuelezea kwa urefu katika juzuu ya nne. Na katika sanad hii pia yumo ‘Ali bin Zaid bin Jud’aan naye ni dhaifu sana.125 Riwaya ya tatu imenasibishwa na Anas bin Malik, lakini katika sanad yake kuna Ibn Lahi’a naye ni dhaifu mwenye kuchanganyikiwa. Naam! ‘Abdul-Ghaniy anasema kwamba Hadithi zilizopokewa na wenye jina la “Abdullah”126 kutoka kwa Ibn Lahi’a ni sahihi. Ninasema: hata ikiwa hivyo basi ni kwa zile sanad zitazotimiza masharti mengine ya usahihi. Ama katika sanad hii, Ibn Lahi’a kaipokea Hadithi hio kutoka kwa Yazid bin Abi Habib kwa sigha ya ‘an’ana, na Ibn Lahi’a – mbali na udhaifu – pia ni mudallis (mwenye kughushi). Kwa hivyo, riwaya yake hapa haikubaliki kwa hali yoyote ile.127 Pili ni kuwa katika sanad hii kuna Sinan bin Sa’ad naye wemetafautiana kuhusu jina lake je ni Sinan bin Sa’ad au Sa’ad bin Sinan. Na kwa hivyo, Al-Imamu Ahmad, kaziwacha Hadithi zake kwani hajulikani jina lake hasa ni nani. Na Al-Juzjaani anasema “Hadithi zake ni wahi (dhaifu sana)”. Anasema Al-Nasai “Hadithi zake ni munkar”. Kisha mbali na hayo mpokezi huyu ni mwenye kuchanganyikiwa.128 Ama Hadithi ya nne na ya mwisho alioitolea ushahidi Al-Darimi imenasibishwa na Ibn Abbaas vile vile. Lakini katika sanad yake kuna Shahru bin Hawshab, naye ni dhaifu kama walivyosema kundi kubwa la wanavyuoni wa wapokezi na Hadithi. Bali mpokezi huyu katuhumiwa hata katika dini yake kwamba aliiba pesa katika beitil-mali na kwamba alifuatana na mtu wa Sham akamfanyia khiyana.129 Bila kusahau kwamba sanad hii ina wapokezi wengine ambao sikuwaona walipotajwa katika marejeo nilionayo, dhahir ni kwamba wapokezi hao hawajulikani. Wa Allahu A’alam!

124 - Tazama habari zake kwa urefu katika Tahdhibu Al-Tahdhib j.10, uk. 412, tarjama na. 833. 125 - Ibn Hajar Tahdhibu Al-Tahdhib j. 7, uk. 283-285, tarjama na. 545. 126 - Yaani majina yote yenye kumaanishwa “Waja wa Allah au waja wa Rahman n.k.”. 127 - Ibn Hajar Tahdhibu Al-Tahdhib j. 5, uk.327-332, tarjama na. 648. 128 - Ibn Hajar Tahdhibu Al-Tahdhib j. 3, uk. 409, tarjama na. 877. 129 - Ibn Hajar Tahdhibu Al-Tahdhib j. 4, uk. 324-326. tarjama na. 635.

52

2) Jambo la pili: ni kuwa ukweli kwamba Allah atahukumu baina ya waja siku ya kiama; hii bado haijawa qarina yenye kulazimisha kulifasiri neno kuja katika maana yake ya uhakika. Kwani:

a) Ulazima wa kuwepo katika sehemu fulani kikweli kweli (physically) wakati wa kufanya kitu haumuhusu Allah, bali huo unamuhusu kiumbe. Bwana Kasim Mafuta, kama tulivyosema kabla, akitaka chungwa pale sokoni Tanga, hawezi kulipata ila ende mwenyewe. Hii ikiwa tutasema kwamba Sh. Kasim Mafuta kaja kweli kweli au kaja hakika kununua chungwa. Vyenginevyo itambidi amuagize mtu mwengine. Na hapa itajuzu kusema kimajazi kwamba “Sh. Kasim Mafuta kaja kununua chungwa” yaani kaja mjumbe wake. Kama tunavyosema Rais wa Zambia kawambia Watanzania kitu kadha, na pengine msemaji kiuhakika ni balozi wake; ama Rais yeye kaamuru tu akiwa nchini kwake. Na hilo utalifahamu zaidi utapoifahamu maana ya:

b) العالمين الله عن غني (Allah katosheka (hahitaji chochote) kutokana na vilimwengu na walimwengu wote).130 Kudai kwamba Allah hapa atakuja kweli kweli kwani anakuja kuhukumu baina ya viumbe, ni kudai kwamba Yeye hawezi kuhukumu ila ahudhurie. Na hio si sifa ya Allah bali ni sifa ya hakimu kiumbe kwa sababu ya upungufu wake.

c) أراد إذا أمره إنما ( فيكون كن له يقول أن شيئا Hakika ya amri yake anapotaka kitu ni kusema kuwa nacho kinakuwa).131 Kwa hivyo, Allah anapotaka kitu chochote halazimiki kuwa ajikalifu au atoke sehemu kwenda sehemu ili kukifanya kitu hicho. Na kwa hivyo ndio maana Al-Imamu Al-Shafi akasema: “Allah alikuwepo kabla ya kuwepo sehemu. Akaumba sehemu naye (Allah) yuko katika sifa zake zile zile za tangu na tangu kama alivyokuwa kabla ya kuumba sehemu. Haimjuzikii Yeye kubadilika katika Dhati yake wala kubadilika katika sifa zake”.132

d) Riwaya inayomnukuu Sayyidna ‘Ali bin Abi Talib akisema kwamba “Allah atawahesabia watu (wote) wakati mmoja kama anavyowaruzuku wakati mmoja”. Nayo ndio moja ya maana za Aya isemayo الحساب سريع الله إن (Hakika ya Allah ni mwepesi wa kufanya hesabu),133 kwa mujibu walivyosema wajuzi. Yote haya yanathibitisha kwamba Allah kuwafanyia watu hesabu,

130 - Sura 3, Aya 97. 131 - Sura 36, Aya 82.

132 - Kikundi cha wapekuzi Ghayatu Al-Bayaan uk. 68. 133 - Sura 3, Aya 199. Aya hii iko katika Sura nyingi. Tazama tafsiri tafauti za wanavyuoni

utaona wakiinukuu riwaya hio ya Sayyidna ‘Ali (k.w.), hususan katika Aya 202 ya Sura ya pili.

53

hakujamaanisha kwamba ni lazima aje pale uwanjani mwenyewe. Au aje naye kabebwa na kiwingu au kabebwa na Malaika kama wanavyodai Mawahabi na Maimamu wao!

Baada ya hayo, utaona kwamba Aya tulizozinukuu zinathibitisha kwamba kuja kwa Allah si lazima iwe ni kuja kwa uhakika, kama tulivyoona kwamba Qur-ani inasema kwamba Allah:

1) Anaijia ardhi na kuipunguza pembeni.2) Kazijia nyumba na kujitia chini ya misingi.3) Kawajia Mayahudi wa Banii Al-Nadhir.

Na Aya zote hizo hazimaanishi kwamba Allah alikuja kweli kweli, bali ni ibara zenye kuonesha kuja kwa jambo lake. Kwa hivyo, Allah aliposema: “Na akaja Mola wako na Malaika safu safu”, maana yake ni kuja kwa jambo lake. Na kilichowapelekea wanavyuoni wa jumhur kuwa waifasiri Aya hio hivyo, ni:

1) Maana ya kilugha ya neno kuja haiwiyani na utukufu wa Allah pindipo tutasema kuwa kuja huko ni kuja kweli kweli. Kwani kuja kweli kweli hakuwi ila ni kuhama kutoka sehemu kwenda nyengine. Na hili lingekuwa sahihi lau Allah angelikuwa:

a) Anahitaji.b) Hawezi kufanya kitu ila akifate. c) Ni kiwiliwili.

2) Ulazima wa kuzifungamanisha Aya za Qur-ani ili zijifasiri zenyewe kwa zenyewe kwani Qur-ani ni wahyi na wahyi haugongani.

Sasa baada ya hayo tumebakiwa na suali moja nalo ni kuwa: ikiwa tumeweza kuthibitisha kwamba kuja kwa Mungu si lazima iwe ni kuja kwa kweli kweli na kwamba kutajwa kwa maneno kuja kwa Mungu kunaashiria kuwepo kwa majazu hadhfi (majazi ya kuondoshwa neno) katika maneno hayo, je ni Aya gani hizo zilizotoa tafsiri yenye kuonesha kwamba neno amri (jambo) ndilo lililoondoshwa katika Aya والملك ربك وجاء صفا .(Na akaja Mola wako na Malaika safu baada ya safu) صفا

AYA ZENYE KUONESHA KUONDOSHWA KWA NENO AMRU (JAMBO)

Tunasema kwamba chenye kubainisha kuondoshwa kwa neno hilo ni Aya zenye kuzungumzia adhabu zilizowafika baadhi ya watu na Aya zenye kuzungumzia yatayowafika watu kwa kutumia ibara kuja kwa jambo au kwa amri ya Allah. Kwa mfano Aya kama:

54

ا ربك أمر جاء لم Ilipokuja amri ya Mola wako.134

Anasema Allah:أمرنا جاء فإذا

Basi itapokuja amri yetu.135

Anasema Allah:

ا أمرنا جاء ولمIlipokuja amri yetu.136

Anasema Allah:

ا أمرنا جاء فلمBasi ilipokuja amri yetu.137

Anasema Allah:

ينظرون هل ربك أمر يأتي أو المالئكة تأتيهم أن إال

Hawana wanachokisubiri isipokuwa kujiwa na Malaika au iwajie amri ya Mola wako.138

Anasema Allah:

الغرور …… بالله كم وغر الله أمر جاء حتى األماني تكم وغر

….Na yakakudanganyeni matamanio (ya nafsi zenu) mpaka jambo la Allah likaja139 na mdanganyi (Ibilisi) akakudanganyeni na (habari) za Allah.140

Na Aya hizi ziko nyingi: hatuna haja ya kurefusha. Kisha elewa kwamba Aya hizi na zilizo mfano wa hizi, Wanavyuoni huwa wanatafautiana katika

134 - Ilipokuja amri ya mola wako ya kuwaangamiza Fir’awna na wafuasi wake. Sura 11, Aya 101. 135 - Sura 23, Aya 27. Sura 11, Aya 40 أمرنا جاء إذا . حتى136 - Sura 11, Aya 58. 137 - Sura 11, Aya 66. 138 - Sura 16, Aya 33. 139 - Yaani mauti. 140 - Sura 57, Aya 14.

55

kulifasiri neno amr lililomo ndani yake. Al-Imamu Ibn Jarir, kwa mfano, ananukuu kauli ya mmoja wa Wanavyuoni akisema kuhusu Aya inayosema:

أمرن جاء إذا احتى . Anasema: “itapokuja amri yetu ambayo tulimuahidi kuwa itawajia kaumu yake miongoni mwa mafuriko ambayo yatawagharikisha”.141 Ni wazi kwa mujibu wa tafsiri hii kwamba limetumika neno amr kwa maana ya jambo. Ndio maana akasema “itawajia kaumu yake miongoni mwa mafuriko ambayo yatawagharikisha”.

Wengine hulifasiri kwa maana ya amri ambao wingi wake kwa Kiarabu huwa ni awaamir. Na wengine hulifasiri kwa maana hio ya mwanzo yaani jambo, na wingi wake kwa Kiarabu linakuwa umuur. Sh. Al-Sabuni katika tafsiri ya Aya: ا أمرنا جاء فلم , anasema: “Yaani ilipokuja amri yetu ya kuwaangamiza wao, basi tulimuokoa (Nabii) Salih (a.s.)”. Ni wazi kwa tafsiri hii kwamba, neno amri hapa limetumika kwa maana ya kuamuru.

Baada ya hayo, sasa naturudi katika Aya zetu. Tunasema: ukiniambia:

Aaa! Unajua kwamba Aya hizo zinasema kwa uwazi kwamba itakuja au imekuja amri yake, na wala hazijakataa kwamba Yeye Allah atakuja. Na kwa hivyo, kuthibitisha kutokuja kwake kwa kutumia Aya hizo ni kuthibitisha kitu kwa kutumia Mafhumu Al-Laqab. Ubainifu wake ni kuwa iliposemwa kuwa amri yake itakuja, wewe ewe Juma Mazrui ukasema kuwa basi Yeye hatokuja. Na hii ni hoja dhaifu.

Ukiniambia hivyo, nitakujibu kwamba msingi wa hapa si Mafhumu Al-Laqab ambao ndio ulizaa natija hio, bali msingi wa hapa ni kuwa maana ya uhakika wa kilugha ya neno جاء kuja haiwezekani kuitumia kwa Allah kwa sababu ambazo tumezieleza sana na kuzikariri. Na kwa hivyo, haikubakia ila maana ya kimajazi ya neno hilo. Na hakuna maana ya kimajazi inayotoa maana sahihi ila tuseme kwamba maana ya “Atakuja Mola wako” ni “Itakuja amri ya Mola wako” kwani mfumo huu ndio uliomo katika Aya nyengine, na tafsiri bora ni ya kuifungamanisha Aya moja na nyengine. Ukiniambia:

Lakini – kama alivyosema Al-Imamu Al-Darimi – kwamba kuna tafauti ya Aya kama hizo ulizozitoa na Aya hio ya Surat Al-Fajr, kwani Aya hizo zinazungumzia adhabu ya dunia, wakati Aya hio ya Surat Al-Fajr inazungumzia kuja kwake huko akhera, naye anakuja ili kufanya hukumu.

Ukiniambia hivyo, nitakujibu kwamba:

141 - Al-Tabari, Muhammad bin Jarir Jaami’u Al-Bayaan j. 12, uk. 46.

56

1) Hii ina maana kwamba wewe umekufahamu kwamba kule kufanya kwake hukumu baina ya viumbe wake kuwa ndio qarina ambayo inaonesha kwamba Allah atahudhuria pale uwanjani mwenyewe. Nasi tunasema kwamba Allah hahitaji kutoka sehemu moja kwenda nyengine ili ndio aweze kufanya chochote akitakacho kwani yeye ni العالمين عن غني (Kajitosheleza: hahitaji chochote katika vilimwengu na walimwengu).

2) Hakuna tafauti yoyote ile kwa Allah baina ya dunia na akhera, kwani Yeye habadiliki wala haathiriwi na nyakati wala mwahala wala hapitikiwi na hali tafauti. Yeye kakamilika katika Dhati yake: kama alivyokua ndivyo alivyo na ndivyo atavyokua milele na milele; na ni mkamilifu katika sifa zake wala hahitaji sifa za ziada. Na kwa hivyo, ikiwa duniani kawaadhibu watu na akawahukumu watu kwa baadhi ya makosa yao bila ya kuwajia – kama Aya tulizozinukuu na nyenginezo nyingi zinavyothibitisha – bila ya kuja Yeye mwenyewe, basi hakuna ulazima kwamba akhera asiweze kuwahukumu watu ila kwa kuhudhuria Yeye mwenyewe. Na kwa hivyo, kimepokelewa kutoka kwa Al-Imamu Ali (k.w.) kile tulichokinukuu kabla kwamba “Allah atawahukumu watu wakati mmoja kama anavyowaruzuku wakati mmoja”. Na bila shaka mwenye uwezo huu basi hahitaji kuwepo ili ndio apitishe hukumu.

TUNARUDI KATIKA MJADALA WA MAJAZI

Hayo ndio maelezo yetu kwa ufupi kuhusu Aya hio inayosema: “Na atakuja Mola wako na Malaika safu safu”. Baada ya hayo, sasa naturudi katika mjadala wa majazi pamoja na Sheikh wetu Al-’Allama Kasim bin Mafuta. Anasema Sheikh Mafuta:

HOJA ZA WENYE KUTHIBITISHA MAJAZI

Wakajitetea wenye kuthibitisha kuwepo majazi ndani ya Qur’an kwa kusema: Majazi ni sehemu katika fasihi za lugha ya kiarabu, na hii Qur’an imeshuka kwa lugha ya kiarabu. Na kila ambacho kinafaa kuwepo katika lugha ya kiarabu kinafaa kuwemo ndani ya Qur’an. Na miongoni mwa mambo yaliyomo ndani ya lugha ya kiarabu ni haya majazi. Kwahiyo, tunapata natija kwamba “Majazi” yamo katika Qur’an.

MAJIBU YA WENYE KUPINGA

57

Wakawajibu wenye kupinga kuwepo majazi ndani ya Qur’an kama ifuatavyo:

Tumewakubalia (AL-MUQADDIMATU AL-SUGH’RAA) kwamba majazi yamo katika lugha ya kiarabu, lakini hatuwakubalii (ALMUQADDIMATUL-KUBRAA) kwamba kila kilichomo katika lugha ya kiarabu kinafaa kuwemo ndani ya Qur’an, bali sisi tunasema kinyume chake, kwamba; kuna baadhi ya vitu vimo katika lugha ya kiarabu, lakini havifai bali ni haramu kuitakidi kuwemo ndani ya Qur’an.

Kwa mfano;Katika elimu ya balagha sehemu ya Badi’i katika sehemu ya “Muhassinaatul-Ma’anawiyyah” (vitu vyenye kupendezesha maana), kuna kitu kinachoitwa “AL-HAZ’LU” (mzaha/utani). Kitu hiki kimo ndani ya lugha ya kiarabu, lakini huwezi kusema kwamba maadamu kimo kwenye lugha, basi kinafaa kuwemo ndani ya Qur’an, kwa sababu Allah anasema kuhusu Qur’an:

بالهزل هو وما *فصل لقول إنه“Kwa hakika hii (Qur’an) ni kauli kupambanua142 (13) Na wala si mzaha (14)”. 143

Miongoni mwa fani za lugha ya kiarabu ni suala la utani, lakini ndani ya Qur’ani hakuna utani na mwenye kuitakidi kuwa katika Qur’an kuna utani atakuwa tayari amekufuru. Halikadhalika ndani ya lugha ya kiarabu kuna kitu katika milango ya elimu ya balagha kiitwacho “al Ruju’u” kujirudi, msemaji anaweza kusema neno halafu hapo hapo anajikadhibisha mwenyewe kwa kuwa alisema maneno hayo bila ya uhakika, kutokana na kuweweseka, au hofu, au kuzidiwa na mapenzi n.k.

Halikadhalika kuna kitu kitachoitwa “Hus’nu Ta’alili” kutoa sababu ya kitu ambayo si halisia. Mfano mtu akisema: Mvua imenyesha mjini kwetu kwa sababu ya kutuona144 haya. Mambo haya na mengineyo ambayo sikuyataja, yamo katika lugha ya kiarabu lakini hayamo na wala hayafai

142 - Sahihi ni kuifasiri Aya hio: “Kauli pambanuzi” au “kauli yenye kupambanua” kwani masdar hapa imetumika kwa maana ya sifa, kama inavyosemwa: العدل Imamu) اإلمامuadilifu) yaani “Imamu muadilifu” au “Imamu mwenye uadilifu”. Na katika Qur-ani Allah anasema: صالح غير عمل إنه “Yeye (mtoto wa Nabii Nuha) ni matendo yasio mema” Sura 11, Aya 46, yaani “Yeye ni mtendaji wa yasio mema”. Na bila shaka itakuwa ajabu ilioje ikiwa mtu ataifasiri Aya hio kuwa maana yake ni “Yeye (mtoto wa Nabii Nuha) ni matendo yasio mema” badala ya kusema: “Ni mtendaji wa yasio mema”. Kwa hivyo, kutumika kwa masaadir katika sehemu hizi ni kwa ajili ya mubaalagha kana kwamba Qur-ani ndio upambanuzi wenyewe kwa jinsi inavyopambanua mambo; na kana kwamba Imamu ndio uadilifu wenyewe kwa jinsi alivyo muadilifu; na kana kwamba mtoto wa Nabii Nuhu ndio uovu wenyewe kwa jinsi alivyokuwa muovu. Wa Allahu A’alam!143 - Suratul-Twaariq (86) aya ya 13-14.

144 - Dhahir ni kuwa hili ni kosa la chapa na sahihi ni “kutuonea haya.”

58

kuwemo katika Qur’an, bali kuitakidi kuwemo ndani ya Qur’an ni ukafiri. Kwa hiyo madai ya kwamba kila kilichomo kwenye lugha ya kiarabu kinafaa kuwemo ndani ya Qur’an, madai hayo hapa yanaporomoka.145

JAWABU

Kwa kuanzia ni kuwa mimi nastaajabishwa sana na wewe Sheikh Kasim Mafuta! Wewe unatafuta ile hoja unayodhania kuwa ni dhaifu na ambayo haina msingi wowote wewe ndio unaijadili na unawacha kujadili mambo ya msingi! Hujui ewe Sheikh Kasim kwamba tafauti katika juz-iyyaat (vijisehemu vya jambo) haimaanishi kutokuthibiti kwa asasiyyaat (misingi) yake? Kwa mfano, kutafautiana kwa wanavyuoni juu ya Hadith Mursal: kwamba je aina hio ya Hadithi inafaa kutumika kama ni hoja ya Kisharia au haifai, hakubomoi ukweli wa kuwepo kwa Hadithi dhaifu.

Halkadhalika – kama tulivyonena na kukariri – cha muhimu kukielewa ni hii tafauti baina ya kuwepo kwa uhakika wa kitu na kuzuka kwa jina lake la kitaalamu. Jina sala ya tarawehe – kwa mfano – limezuka, lakini uhakika wa sala yenyewe ulikuwepo tangu enzi ya Mtume (s.a.w.). Kwa hivyo, kinachotazamwa ni je hao walioita fani hio kuwa ni Hazlu (mzaha/utani) wanakusudia nini? Baada ya kukipata hicho wanachokikusudia wao ndio kinatazamwa je katika Qur-ani kimo au hakimo. Hazlu wanayoikusudia watu wa balagha si ile yenye kufasiriwa “utani au mzaha” kama ulivyodhania wewe. Nimesema na ninakariri kwamba technical terms (maneno ya kifani) huwa hayatazamwi katika maana yake ya kilugha, bali yanatazamwa nini kinakusudiwa kwayo. Nimekupa mfano wa neno sala ya tarawehe, na nakuongezea mfano wa neno tajaahul ambalo ukilifasiri kilugha maana yake ni kujifanya kuwa hujui nawe unajua. Lakini katika fani ya balagha haikusudiwi hivyo, zinazokusudiwa ni zile nukat za kibalagha kama vile kuonesha kulaumu, kugomba, kustaajabu, kudharau n.k.

Mfano mwengine wa nyongeza ni neno makruh. Unaelewa vyema kwamba katika dhana (concept) ya Qur-ani, neno makruh limetumika kwa mambo yalioharamishwa. Kwa mfano, Allah baada ya kutaja mambo kadha wa kadha alioyaharamisha kama vile kuua; kula mali ya yatima; kupunja katika vipimo n.k., aliishia kwa kusema:

ربك عند سيئه كان ذلك كل مكروهاYote hayo ubaya wake ni makruhu (wenye

kuchukiza) kwa Mola wako.146

145 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 46-47.146 - Sura 17, Aya 38.

59

Wakati Allah anasema hivyo, utakuna neno makruh kwa wanavyuoni wa fiq-hi linatumika kwa kitu ambacho ukikifanya hupati dhambi na ukikiwacha unapata thawabu zaidi. Sasa huwezi kudai kwamba “si kweli hakuna kitu makruh” kwa sababu katika dhana ya Qur-ani neno hilo limetumika kumaanisha kitu haramu. Huwezi kudai hivyo na hoja yako ikanyooka, bali unachotakiwa ni kutazama je wale waliozigawa hukumu za kifi-qhi migawanyiko hio ya makruh, haramu n.k., wanakusudia nini? Tena: je kile wanachokikusudia wao kipo au hakipo? Hivi ndivyo unavyofanywa utafiti wa kitaalamu.

Halkadhalika neno مفعول “mtendwa”, ukiwa utalichukulia kilugha basi – katika sentensi fulani fulani – huwezi kusema kuwa Allah ni mtendwa kwani – kilugha – mtendwa ni mwenye kufikiwa na kitendo cha mtenda. Lakini watu wa nahau wanaposema فاعل “mtenda” na مفعول “mtendwa”, huwa hawakusudii maana zake za kilugha. Na kwa hivyo, katika maneno kama علي qawiya ‘Ali (Ali kapata nguvu), Ali قويanaitwa kuwa ni mtenda ilhali hapa hajatenda kitu; na katika maneno kama:

الله Allah anaitwa mtendwa ilhali ,(nimemuomba Allah) دعوتhajatendwa kitu kwani Yeye kamwe hafikiwi na kitendo cha yoyote. Kwa hivyo, tunapozungumzia technical terms (maneno ya kifani) huwa hatutazami maana zake za kilugha tu, bali kinachotazamwa ni nini kinakusudiwa kwayo. Na ndio maana wanavyuoni wakasema yale tulioyanukuu kabla: ا في مشاحة إصطالحلال (Hakuna kujadiliana katika maneno ya kitaalamu au ya kifani).

Ama maneno yako uliposema:

Katika elimu ya balagha sehemu ya Badi’i katika sehemu ya “Muhassinaatul-Ma’anawiyyah” (vitu vyenye kupendezesha maana), kuna kitu kinachoitwa “AL-HAZ’LU” (mzaha/utani). Kitu hiki kimo ndani ya lugha ya kiarabu, lakini huwezi kusema kwamba maadamu kimo kwenye lugha, basi kinafaa kuwemo ndani ya Qur’an, kwa sababu Allah anasema kuhusu Qur’an:

بالهزل هو وما *فصل لقول إنه“Kwa hakika hii (Qur’an) ni kauli kupambanua (13) Na wala si mzaha (14)”.

Ninasema: maneno hayo hayakufai wewe ewe Sheikh Kasim mwana wa Mafuta, kwani kama Qur-ani ilivyosema:

بالهزل هو وما *فصل لقول إنه“Kwa hakika hii (Qur’an) ni kauli kupambanua (13) Na wala si mzaha (14)”

60

ndivyo ilivyosema: بهم يستهزئ الله

Allah atawacheza shere (atawafanyia mzaha).147

Sasa je neno yastahziu (atawafanyia mzaha), utalitoa katika maana yake ya asili na kuliletea ta-awil? Ukifanya hivyo utakuwa umethibitisha majazi na ta-awil katika sifa za Allah. Jambo hilo kwenu nyinyi ni kuyapotoa maandiko! Ukisema “ndio atafanya mzaha”, basi kwa mujibu wa maelezo yako utakuwa umethibitisha itikadi haramu katika Qur-ani na umekufuru. Sasa hapa nakuachia kazi wewe mwenyewe urekebishe fikra zako na kujichagulia minhaj (methodology) itayokufikisha nchi kavu kwa salama na amani – je ni kuyakubali majazi na ta-awil au ni kuyakanusha?

Naturudi katika kulitazama neno Hazl linalotumika katika fani ya balagha. Tunasema: ukirudi katika neno hilo, utakuta kwamba wao hawakusudii kufanya utani kwa maana ya maskhara yasio na ukweli ndani yake, bali wanakusudia kwamba mjengeko wa ile ibara kana kwamba inakusudiwa utani kumbe ni kitu cha kweli. Anasema Jalalu-Din Abu ‘Abdi-Llah:

ومثاله تفسيره عن تغني فترجمته الجد به يراد الذي الهزل ومنهالشاعر قول

للضب ** أكلك كيف ذا عن عد فقل مفاخرا أتاك تميمي ما إذا

Na katika hayo ni Hazlu (utani) inayokusudiwa Jiddu (seriousness au ukweli), basi tarjama (heading) yake inatosha: hakuna haja ya maelezo. Na mfano wake ni kauli ya mshairi aliposema:

Ikiwa mtu wa kabila la tamimi atakujia akijifakharisha**Mwambiye wachana na hayo; vipi na kula kwako dhabb.148

Maneno “Vipi na kula kwako dhabb”149 yaani wajifakharisha nini nawe wala dhabb? Maneno hayo yanaonekana kama ni utani ndio maana yakaitwa Hazl, lakini makusudio yake si utani bali makusudio yake ni kuonesha kumdharau yule aliyejifakharisha. Hii ndio Hazl wanayoikusudia kwenye elimu ya balagha: si utani kwa maana ya kudanganya au utani usio na maana.

147 - Sura 2, Aya 15. 148 - Jalalu-Din Abu ‘Abdi-Llah Al-Idhaahu Fii ‘Ilmil Balagha j. 1, uk. 351.

149 - Dhabbu ni mdudu kama kenge lakini yeye ni mdogo. Urefu wake ni kama guruguru lakini yeye mpana kidogo. Watu wengine huko kwetu wanamfasiri “kenge” lakini kwa

kweli huyu si kenge kafanana naye tu.

61

Ama utani au Hazlu kwa maana ya kufanya maskhara, huu hata kama upo katika jamii za Waarabu na katika kila jamii pamoja na kuandikwa katika literature (Adab) zao, lakini huu si katika muundiko wa lugha; tafauti na alivyo faa’il (mtenda) na maf’ul (mtendwa) na majazi ambazo ni sehemu za miundiko ya lugha. Ama utani au Hazlu kwa maana ya kufanya maskhara hayo ni katika utamaduni (tradition) wa Kiarabu bali ni katika utamaduni wa binaadamu wote. Na sisi suala letu ni muundiko wa lugha ya Waarabu: si utamaduni wa Waarabu.

Ama “al Ruju’u”, si maana yake kujirudi kwa maana ya kuwa “msemaji anaweza kusema neno halafu hapo hapo anajikadhibisha mwenyewe” kama ulivyodhani wewe! Bali maana ya fani hii ni kukanusha ukamilifu wa kitu au kuikanusha dhana (mafhum au concept) fulani ya kitu na kuithibitisha dhana hio kwa njia nyengine. Al-‘Allama Al-Tiybi anatoa mfano wa Al-Ruju’u ya kibalagha kwa beti hizi:

* دروعا حسبتهم لألعادي* *****وإخوان ولكن فكانوها** صائبات سهاما فؤادي *****وخلتهم في ولكن فكانوها

** ودادي من ولكن صدقوا لقد القلوب منا صفت قد وقالوا1) Na ndugu niliwafikiria kuwa ni ngao**Basi nao wakawa hivyo

lakini (ngao zenyewe) ni za (kuwakinga) maadui (si za kunikinga mimi).

2) Na niliwadhania kuwa ni mishare yenye kuisibu (shabaha)**Basi wakawa hivyo lakini (shabaha yenyewe) ni katika kifua changu (wakanipiga mimi).

3) Na wakasema mioyo yetu sasa imesafika**Wamenena kweli lakini (imesafika) kutokana na mapenzi yangu (hainipendi).

Hii ndio Al-Ruju’u inayozungumzwa katika fani ya balagha. Utaona kwamba mshairi kathibitisha kwamba watu hao ni ngao; kisha akakanusha kuwa ngao hizo ni za kumkinga yeye; kisha akathibitisha kwamba ni ngao za kuwakinga maadui. Kwa hivyo, kwa ufupi, ni kuwa yeye hajakataa kwamba hizo ni ngao lakini si ngao za kumkinga yeye bali ni za kuwakinga watu wengine. Hii ndio Al-Ruju’u inayokusudiwa katika balagha.

Halafu Al-‘Allama Al-Tiybi akatoa mfano wa Al-Ruju’u kwa Aya isemayo:

للمؤمنين ويؤمن بالله يؤمن لكم خير أذن قل أذن هو ويقولون

62

(Makafiri) wakasema kuwa yeye (Mtume) ni sikio (kila aambiwalo alisikiliza tu); sema (kweli) ni sikio lakini ni sikio la kheri kwenu: anamuamini Allah na kuwaamini waumini….150

Utaona katika Aya hii kwamba Allah mwanzo anawapinga makafiri kwa kumwita Mtume sikio kwani maana walioikusudia wao si ya kweli: wao wanakusudia kwamba Mtume (s.a.w.) chochote anachoambiwa, basi yeye anakisikiliza na kukikubali; kisha Allah akathibitisha kuwa kweli yeye ni sikio yaani ni mwenye kusikia kila kitu lakini ni katika mambo ya kheri tu. Kwa hivyo, hapa kuna kukadhibisha na kuthibitisha na hii ndio maana ya Al-Ruju’u inayozungumziwa na watu wa balagha.

Ama “Hus’nu Ta’alili” kutoa sababu ya kitu ambayo si sahihi, pia si mfumo wa lugha bali ni madai tu ya adiib (mtu wa literature) katika kuipamba lugha yake. Kwa lugha nyengine husnu ta’alil ni fikra: si muundiko wa lugha: muundiko wa lugha ni ule ambao Waarabu wote wanautumia kama: taqdim na ta’akhir; al-muqaabala; al-mushaakala; majaz n.k.

Kwa hali yoyote ile ikiwa tutasalimu amri kwamba si kila kilichomo katika lugha ya Kiarabu kimo ndani ya Qur-ani; suali ni kuwa je baadhi ya yaliomo ndani ya lugha ya Kiarabu yamo katika Qur-ani au yote hayamo? Bila shaka jawabu yako hapa haitotafautiana na binaadamu yoyote kwamba baadhi ya yaliomo ndani ya lugha ya Kiarabu yamo katika Qur-ani. Sasa je katika hayo baadhi ya yaliomo ndani ya Qur-ani, majazi nayo yamo au hayamo? Nadhani hili ndilo suali la kujiuliza na kulitafutia jawabu ili tuweze kuufikia ukweli.

Sasa ili tukuthibitishie hilo, natuanze kwa kutoa ta’arifu (definition) ya majazi. Natuache majina (majazi au uslub); na twende kwenye uhakika. Wanaoamini majazi wanasema: “Majazi ni neno lililotumika kinyume na maana yake ya asili”.151 Kilichobaki ni kujiuliza: je katika Qur-ani hakuna maneno yaliotumika kinyume na maana yake ya asili. Soma Aya zifuatazo halafu niambie je maneno yaliomo humo yametumika kwa maana gani. Anasema Allah:

النور إلى الظلمات من يخرجهم آمنوا الذين ولي الله

Allah ni Msimamizi wa Waumini: anawatoa katika kiza (na) kuwapeleka kwenye nuru. 152

150 - Sura 9, Aya 61. 151 - Hapa natoa ta’arifu yenye kubainisha uhakika wa kitu: sitoi masharti ya majazi. 152 - Sura 2, Aya 257.

63

Tazama neno “kiza” na neno “nuru”. Uhakika wa maneno hayo sio uliokusudiwa hapa, bali maana ni: “Allah anawatoa walioamini kutoka katika upotovu na kuwaingiza katika uongofu”. Upotovu umefananishwa na kiza kwa sababu ya kuwa mpotovu anayumbayumba katika upotovu wake kama vile anavyoyumbayumba mtu aliye katika kiza; na uongofu umefananishwa na nuru kwa sababu mtu katika nuru anaona vizuri na anakwenda sawa sawa. Vyenginevyo hakuna nuru ya kweli ambayo Waumini huingizwa humo au kiza cha kweli ambacho Waumini hutolewa kutoka humo.

Anasema Allah: الله بحبل واعتصموا جميعا

Na kamataneni na kamba ya Allah kwa pamoja.153

Sheikh Mafuta! Hii kamba ya kweli kweli ya Mwenyezi Mungu inapatikana wapi ili nasiye tupatekushikana nayo? Au utaniambia kwamba kamba hapa ina maana ya dini ili tukubaliane kwamba neno kamba hapa limetumika kinyume na maana yake ya asili?

Allah anasema: ثقفوا ما أين الذلة عليهم ضربت الناس من وحبل الله من بحبل إال

Wamepigwa udhalili popote walipo, isipokuwa (wakishikana) na kamba ya Allah na kamba ya watu. 154

Sijui tunakubaliana kwamba kamba ya Allah ni dini yake; na kamba ya watu ni msaada wao? Kama hatukubaliani hivyo, basi Sh. Kasim tueleze nini maana ya kamba hizi na zinapatikana wapi.

Anasema Allah:والنهار الليل مكر بل

Bali (ni) vitimbi vya usiku na mchana.155

Jamani! Usiku na mchana una vitimbi? Au hapa kuna majaz hadhf (majazi ya kuondosha neno) na maana ni: “Bali vituko vyenu mulivyokuwa mukivifanya usiku na mchana?” 153 - Sura 3, Aya 103. 154 - Sura 3, Aya 112.. 155 - Sura 34, Aya 33.

64

Anasema Allah:راط اهدنا المستقيم الص

Tuongoze njia ilionyooka.156

Hii njia ya kweli kweli ilionyooka tunayomuomba Allah atuongoze iko wapi? Je si maana yake kwamba tuongoze katika dini sahihi? Na kwa hivyo, neno njia hapa limetumika kinyume na maana yake ya asili.

Anasema Allah:األيد ذا داوود عبدنا واذكر

Mkumbuke mja wetu Dawud mwenye mikono mingi (zaidi ya miwili).157

Jamani! Huyu Nabii Dawud alikuwa na umbo la namna yake peke yake? Aya inasema alikuwa na mikono mingi zaidi ya miwili. Ukinambia: “Aa! Unajua katika lugha ya Kiarabu inatumika nyingi kumaanisha mbili na moja kumaanisha nyingi na mbili kumaanisha nyingi”. Dai hili nimeshakujibu sana kwamba hayo ndio majazi yenyewe yaani kutumika neno kinyume na maana yake ya asili. Vyenginevyo wapi umepata kusikia kwamba moja ni mbili au ni tatu na kuendelea?

Anasema Allah:الغيب مفاتح وعنده

Naye ana funguo za (mambo) ya ghaib.158

Je funguo hizi ni funguo za kweli au ni elimu ya ghaib? Au tuseme ghaib ina kufuli za kweli kweli na funguo zake za kweli kweli anazo Allah?

Anasema Allah: األرض لكم جعل الذي هو مناكبها في فامشوا ذلوال

Yeye (Allah) ndiye aliyekufanyieni ardhi kuwa dhalili, basi nendeni (mutembee) katika mabega yake. 159

156 - Sura 1, Aya 6. 157 - Sura 38, Aya 17. 158 - Sura 6, Aya 59. 159 - Sura 67, Aya 15.

65

Tunasubiri labda Sheikh Mafuta atatujuilisha mabega haya ya ardhi yako sehemu gani. Au atatwambia kwamba mabega hapa ni kwa maana ya pande (sehemu) ili iwe neno hilo hapa limetumika kinyume na maana yake ya asili.160

Anasema Allah:

ــزل بالذي آمنــوا الكتـاب أهل من ائفةط وقالت آمنــوا الذين على أن آخره واكفروا النهار وجه

Na wakasema baadhi ya watu wa Kitabu: kiaminini kile walichoteremshiwa walioamini (katika) USO wa mchana na mukufuru mwishoni mwake (mwishoni mwa uso huo). 161

Bwana Kasim upo? Ivo huu mchana nao una uso bwana Kasim? Allah anasema النهار وجه (Uso wa mchana). Au utaniambia kwamba uso hapa una maana ya mwanzo; na kwa hivyo maana ni mwanzo wa mchana? Basi kama ni hivyo, ni kipi kinachozuia neno “Uso wa Allah” isiwe dhati yake au radhi zake?

Anasema Allah:

ياح يرسل الذي وهو الر رحمته يدي بين بشرا

Naye ndiye anayetuma upepo hali ya kuwa ni bishara baina ya mikono miwili ya rehema yake.162

Jamani! Ivo hii rehema ya Allah ina mikono miwili? Au maana ni: “Naye ndiye anayetuma upepo hali ya kuwa ni bishara itokayo katika rehema yake”. Na kwa hivyo, neno “mikono miwili” ni majazi: limetumika kinyume na maana yake ya asili.

Anasema Allah:حمة من الذل جناح لهما واخفض الر

Na wainamishie (wazee wako wawili) bawa la udhalili wa huruma. 163

160 - Naam! Neno mankib lina maana nyengine, lakini zote hizo ni maana za kimajazi: si za hakika. 161 - Sura 3, Aya 72. 162 - Sura 7, Aya 57. 163 - Sura 17, Aya 24.

66

Labda kesho tutaambiwa kwamba udhalili una bawa lakini bawa lake si kama bawa la ndege!

Anasema Allah:{ للمؤمنين جناحك {واخفض

Na inamisha bawa lako kwa waumini.164

Hapa Mtume (s.a.w.) anaambiwa ainamishe bawa lake. Tunahofia kwamba lugha hii wenzetu itawashinda na kutwambia kuwa bawa hili ni bawa la kweli! Wallahu Al-Musta’aan!

Anasema Allah:العجل قلوبهم في وأشربوا

Na wakanyweshwa ndama katika mioyo yao. 165

Jamani! Ni nani anaweza kumnywa ndama? Na ndama ananywewa? Ni wazi kwamba hapa kuna majazu hadhfi (majazi ya kuondoshwa kwa neno) nalo ni mapenzi na kwa hivyo maana ya Aya hio ni “Walinyweshwa mapenzi ya kupenda ibada ya ndama”. Yaani waliipenda mno ibada yao hio ya kuabudu ndama.

Anasema Allah:ر ربهم عند صدق قدم لهم أن آمنوا الذين وبش

Wabashirie wale walioamini kwamba wana mguu wa ukweli kwa Mola wao. 166

Jamani! Ukweli nao una mguu? Basi hatuachi sisi kufuata kama bendera kwa sababu tu msemaji ni Ibn Al-Qayyim na Ibn Taymiyya!

Anasema Allah:

( أو13) رقبة ( فك12) العقبة ما أدراك ( وما11) العقبة اقتحم فال ( أو15) مقربة ذا ( يتيما14) مسغبة ذي يوم في إطعام ذا مسكينا(16) متربة

164 - Sura 15, Aya 88. 165 - Sura 2, Aya 93. 166 - Sura 10, Aya 2.

67

Basi je ameshaukata mlima?* Na nini kinachokujuilisha, ni nini mlima huo?* (Ni) kuifungua shingo* Au kumlisha katika siku yenye njaa* Yatima aliye na ukaribu (ujamaa)*Au masikini mwenye dongo. 167

Sasa ebu Bwana Kasim bin Mafuta yahesabu majazi yaliomo katika Aya hizi:

4) Neno ‘Aqaba. Maana yake ni njia yenye mawe mawe kwenye mlima.

5) Allah akauliza: je hio ‘Aqaba (njia yenye mawe mawe kwenye mlima) unaijua ni nini?

6) Kisha akabainisha kwamba ‘Aqaba (njia yenye mawe mawe kwenye mlima) ni:

a) Kumlisha masikini.b) Kuifungua shingo. Hapa jiulize tena: nini maana ya

kuifungua shingo katika Aya hio: ni shingo tu au ni mtu kamili? Shingo hapo ni kwa maana ya mtumwa.

Kwa hivyo kuyafanya hayo, basi Allah kakuita kuwa ni kuupanda mlima. Je bado tu mtu aliyejifungua pingu za kubururwa atakubaliana na madai kwamba katika Qur-ani hakuna majazi (maneno yaliotumika kinyume na maana yake ya asili)?

Allah anasema:رمى الله ولكن رميت إذ رميت وما

Hukurembea uliporembea, lakini Allah ndiye aliyerembea.168

Anasema Al-Imamu Badru Al-Din, Sheikh Al-Mufassirin Al-Khalili:Nanyi munaona vipi Aya ilivyokusanya baina ya kukataa kwamba Mtume (s.a.w.) karembea katika kauli yake Allah رميت وما (Na hukurembea); na baina ya kuthibitisha kuwa karembea katika kauli yake Allah رميت إذ (Uliporembea). Kisha hatima yake, Aya ikakutegemeza kurembea huko kwa Allah (subhanahu wa ta’aala) ikasema: رمى الله ولكن (Lakini Allah ndiye aliyerembea). Basi ivo inasemwa kuwa kile alichokataliwa Mtume (kuwa hakukifanya katika Aya hii) ndicho alichothibitishiwa (kuwa kakifanya), nacho ndicho hicho hicho ambacho mwishowe kimenasibishwa na Allah (kuwa ndiye aliyekifanya). Hapana! Bali alichokataliwa (Mtume s.a.w. kukifanya) ni kukupa tawfiki kule kurembea kwa kulisibu lengo la kile kinachorembewa, na hili ndilo ambalo kiumbe hana uwezo nalo, kwani hilo ni jambo la Allah……169

167 - Sura 90, Aya 11-16. 168 - Sura 8, Aya 17. 169 - Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Jawahiru Al-Tafasir, Juz-u Khaas uk. 77-78.

68

Hio ni mifano michache sana katika mingi iliomo katika Qur-ani. Je katika Aya hizo hakuna majazi? Je maneno yaliotumika katika Aya hizo yametumika kumaanisha maana zake za asili? Kwa kweli ndugu zetu haki hawaitaki: wao wana msimamo wao huo, basi ni huo huo tu hata kama unapingana na ushahidi wa wazi. Bwana Kasim Mafuta! Kuna msemo wa kizungu wenye kusema “Unaweza kumchukua farasi hadi kwenye mto; lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji”. Mimi nimeshakuonesha majazi katika Qur-ani – na nitazidi kukuonesha baadae – lakini siwezi kukulazimisha kurudi katika haki. Natuendelee na kuzitazama hoja za Sheikh Kasim Mafuta.

KICHANGUZI CHA KULLIYYATUN MUUJIBAH NI “JUZ’IYYATUN SAALIBAH”.

Anasema Sheikh wetu Kasim bin Mafuta:

Na kwa kuzitumia njia za kimantiki (logic) wanasema kwamba;سالبة” جزئية الموجبة الكلية نقض“

“Kichanguzi cha Kulliyyatun Muujibah” ni “Juz’iyyatun Saalibah” Kwamfano: “Kulliyatun Muujibah” kama vile ukisema: kila ambacho kimo kwenye lugha ya kiarabu kinafaa kuwemo katika Qur’an. Maneno hayo yanavunjwa na “Juz’iyyatun Saalibah” ambayo ni kusema: Kuna vitu vingi vimo katika lugha ya kiarabu lakini havifai kuwemo kwenye Qur’an. Na msingi huu (Juz’iyyatun Saalibah” ukithibiti kwa hoja basi msingi huo wa kwanza (Kulliyyatun Muujibah) unaporomoka. Na hapo nyuma tumekuthibitishia kuwepo katika lugha ya kiarabu vitu vingi ambavyo kudai kwamba vimo ndani ya Qur’an ni haramu. Tazama maelezo hayo kwa urefu zaidi katika kitabu “Man’u Jawazil-Majaazi” cha Imamu wa tafsiri katika zama hizi Sheikh Muhammad al-Amin bin Muhammad al-Shin’qitwiy.

JAWABU

Hapa napenda kutoa pongezi zangu kwamba leo Ahlu Sunna wewe unatumia au unasapoti mantiki (logic) kuunga mkono hoja yako. Siisahau jawabu ya Dr. Bakr Abu Zaid aliomjibu mwanachuoni wa Kishia katika mkutano wa fiq-hi uliofanyika hapa Oman ambapo mwanachuoni huyo alitoa hoja kwa kanuni ya mantiki (logic), Dr. Bakr Abu Zaid akamwambia: “Hio ni kanuni ya mantiki (logic) na wanavyuoni hawakutegemea mantiki (logic) katika kuthibitisha hukumu za kisharia”.170 Sheikh Kasim! Mantiq si elimu inayotegemewa katika uwanja wa Sharia. Bali wengine wanasema –

170 - Au maneno yalio na maana hio.

69

nami nawaunga mkono – kwamba mantiki si elimu kamwe. Qur-ani na Sunna zina fani zake za kuzifasiria muhimu yao ni fani za lugha (Nahau, Sarfu na Balagha).

Kwa ufupi ni kuwa hio ni hoja ya kuunda isio na msingi, kwani kama tulivyoeleza kwamba ikiwa kila kilichomo katika Kiarabu hakimo katika Qur-ani, suali ni kuwa je baadhi ya yaliomo katika Kiarabu yamo katika Qur-ani au hayamo? Kama yamo, je majazi katika hayo baadhi ya yaliomo katika Qur-ani, nayo yamo? Kama hayamo, basi tuletee kamba tulioamrishwa kushikamana nayo katika Aya:

الله بحبل واعتصموا جميعاNa kamataneni na kamba ya Mwenyezi Mungu kwa pamoja.171

Sheikh Mafuta una deni la kamba hii, utuletee au utwambie inapopatikana. Hapa sitaki kurefusha kwani maelezo yakutosha yametangulia na nyongeza nyingi itakuja in shaa Allah.

Anasema Sheikh Kasim Mafuta:

HOJA YAO YA TATU

Pia ukitazama kwa makini utakuta kuwa hakuna vigezo na vidhibiti vya uhakika katika kuitolea Ta’arif (definition) sahihi “Majaazi al-Mur’sal” (Absolute Metaphor), na matumizi yake, na hilo linasababisha mgongano katika matumizi yake kilugha jambo ambalo ni muhali kuwemo katika Qur’an. Kwa mfano mtu akisema: “Nimeingiza kidole sikioni”. Kwa mujibu wa maelezo ya wenye kudai kuwepo majazi wanasema kuwa hapo kuna “Majaazul-Mursal” (Absolute Metaphor) na maana yake ni kwamba umeingiza baadhi ya kidole, kwa sababu kidole chote hakiingii sikioni, kwa hiyo utakuwa umekitaja kidole lakini makusudio ni baadhi yake.

Wakiwa wanaifanyia kazi “Qaaidah” (kanuni) iliyopo katika “Majaazil Mursali” (Absolute Metaphor) isemayo: “Min It’laaqil-Kulli wa Iraadatil-Ba’adhi” (ni kukitaja kitu kizima lakini makusudio ni baadhi yake)”. Lakini ukifanya utafiti wa kina utagundua kwamba wenye kuitumia “Qaaidah” (kanuni) hii wameshindwa kuidhibiti kitaalamu, kiasi ambacho inafikia kuifanya sehemu kubwa ya lugha ya kiarabu kama si yote kuwa ni Majazi! Jambo ambalo si sahihi.

Kwa sababu wanakubaliana wataalamu wote wa lugha ya kiarabu kwamba matumizi ya maneno katika maana zake za asili ni mengi zaidi kuliko

171 - Sura ya 3 Aya ya 103.

70

maana za ki-Majazi. Na hilo linapingana na kanuni hiyo na nyinginezo za kimajazi. Kwa kuitumia “Qaaidah” hiyo ya kukitaja kitu kizima lakini makusudio ni baadhi yake, kunavunja itifaki hiyo. Kwamfano, mtu akisema: Nimekula wali, au Nimekunywa maji, au Nimekwenda Makka. Kwa mujibu wa kanuni hiyo yanakuwa maneno yote hayo ni “Majazi” hata kama wenye kuyathibitisha hawasemi hivyo, lakini kanuni hiyo waliyoiweka ndiyo inavyoelekeza, kwa sababu utaambiwa wewe umekula baadhi ya wali na hukula wali wote. Na utaambiwa kuwa umekunywa baadhi ya maji na hukunywa maji yote. Na umefika baadhi ya sehemu za jiji la Makka na hukufika Makka yote, pengine umefika Mina, Aziiziyyah, Ajyaad, Ghaza na katika msikiti mtukufu, lakini hukufika Misfala, wala Hafaair, wala Ka’akiyyah na sehemu nyinginezo katika mitaa ya Makka, kwa hiyo ukisema nimefika Makka ni majazi kwa kuwa umetaja Makka lakini makusudio yako ni baadhi yake.

Halikadhalika ukisema nimekaa msikitini, au nyumbani, au darasani, au ofisini, maneno yote hayo ni majazi kwa sababu kiuhakika kabisa utakuwa hukukaa katika msikiti wote bali umekaa katika baadhi ya eneo la msikiti, au nyumba, au darasa, au ofisi. Hivyo basi, kwa sababu ya kukosekana udhibiti ulio makini wa suala hili ndiyo baadhi ya maulamaa wakasema kuwa maneno yote hayo ni hakika na wala si majazi na mtiririko wa maneno (context) ndiyo ulio ainisha maana ya maneno hayo.

JAWABU

Uchambuzi wako huu unaashiria mambo mawili:1) Huwezi kufanya tahqiq ya yanayosemwa.2) Hukuifahamu vyema “Majaazul-Mursal”.

Na kabla ya yote natuanzie na madai yako uliposema:

Kwa sababu wanakubaliana wataalamu wote wa lugha ya kiarabu kwamba matumizi ya maneno katika maana zake za asili ni mengi zaidi kuliko maana za ki-Majazi. Na hilo linapingana na kanuni hiyo na nyinginezo za kimajazi. Kwa kuitumia “Qaaidah” hiyo ya kukitaja kitu kizima lakini makusudio ni baadhi yake, kunavunja itifaki hiyo.

Tunauliza: makubaliano haya yako wapi? Hili ndilo tatizo lenu: kitu musichokijua au mukitakacho basi munakipamba kwa usemi: “Umma umekubaliana” au “Al-Salafu Al-Salih wamekubaliana” au ‘Hakuna khilafu

71

juu ya hili”. Ilikuwa useme kwamba jumhur ya “wataalamu wa lugha wanasema kwamba matumizi ya maneno katika maana zake za asili ni mengi zaidi kuliko maana za ki-Majazi”. Ama makubaliano ya wote hayapo. Ibn Al-Jinni – kwa mfano – anasema: “Asilimia kubwa ya lugha ni majazi”.172 Anasema Ibn Al-Qayyim: “Na kwa hakika baadhi ya Maimamu wa nahau wamesema kwamba asilimia kubwa zaidi ya lugha ni majazi”.173

…. “Na Jahmu (bin Safwaan) kajipa (kanuni kwamba) asilimia kubwa ya lugha ni majazi”. 174 Anasema Abu Al-Balqaa: “Asilimia kubwa zaidi ya lugha ni majazi”.175

Hivi ndivyo walivyosema Maimamu hao. Lakini ninavyoona mimi ni kuwa hakuna khilafu ya hakika baina ya waliosema kuwa majazi ni mengi zaidi kuliko hakika na waliosema kuwa hakika ndio nyingi zaidi kuliko majazi. Na tahrir ya hayo ni kuwa maneno mengi yanakuwa kiasili yana maana kadha; kisha yanatumiwa kwa maana nyengine ilio karibu na ile ya asili kwa sababu ya kuwepo munasaba au alaaqa (uhusiano) baina ya maana ya asili na ile iliotumiwa baadae. Kisha ile maana ya pili inatumika sana na kuenea hadi inafika kwamba neno hilo likitajwa tu basi huwa haifahamiki ila ile maana ya pili: isio ya asili. Na hapa inakuwa maana ya pili ndio ya uhakika kama walivyosema: حقيقةال لحقالمجاز كثرإذا (Matumizi ya majazi yakikithiri basi huuganishwa na hakika).176 Mfano mmoja mzuri ni neno kitabu. Maana ya asili kabisa ya neno kitabu katika lugha ya Kiarabu ni kitu “chenye kukusanya” au “chenye kuunganisha”. Anasema Al-Imamu Al-Baghawi:

Na asili ya kitabu ni kuunganisha na kukusanya. Na (kikosi cha) jeshi huitwa katiiba kwani (majeshi) wanakusanyika pamoja. Na kitabu kimeitwa kitabu kwa sababu ya kukusanya herufi (na kuziunganisha na) herufi nyengine.177

Hio ndio maana ya asili ya neno hilo. Lakini maana hio imehajiriwa kabisa, na leo ukitaja kitabu, basi kinajulikana papo hapo kuwa unakusudia haya

172 - Ibn Jinni, Al-Khsaais j. 2, uk. 308. Na akainuku pia kauli hii Al-Imamu Al-Shaukani katika Irshaadu Al-Fuhuul uk . 36. 173 - Ibn Al-Qayyim Al-Sawaa’iqu Al-Mursala j. 451. 174 - Ibn Al-Qayyim Al-Sawaa’iqu Al-Mursala j. 456. 175 - Abu Al-Balqaa Al-Kulliyyaat j. 1, uk. 1600. 176 - Yaani neno la kimajazi likiwa linatumika sana katika hali hio, basi baadae matumizi yake hayo yanakuwa si majazi tena bali ni hakika. Tazama Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 12, uk. 156, babu ghalat man qaala innahu majaz.Tazama pia kichwa cha habari kilichomo katika kitabu Al-Khasaais cha Ibn Jinni j. 2, uk. 308. Dr. Al-Buti Al-Salafiyya uk. 81-82. 177 - Al-Baghawi Ma’aalimu Al-Tanzil j. 1, uk. 81.

72

maandishi yaliomo katika karatasi au karatasi zenye maandishi. Maana hii ya pili baadae ilizagaa na ikageuka kuwa sasa ndio maana ya uhakika ya neno hilo; wakati ukitazama asili ya neno basi maana hii ya pili ni majazi. Mfano wa pili ni neno kafiri. Asili ya kilugha ya neno kafiri ni mwenye kufukia au mwenye kufunika. Na kwa sababu hii, mkulima kaitwa kafiri kwa sababu anazifunika mbegu kwa udongo wakati anapopanda mimea, kama ilivyo katika Aya ya Qur-ani inayosema:

{ يكون ثم مصفرا فتراه يهيج ثم نباته ار الكف أعجب غيث كمثل {حطاما

Ni kama mvua ambayo mimea yake huwafurahisha wakulima, kisha yakakauka ukayaona yamepiga umanjano, kisha yakawa mabuwa..”.178

Na kwa tahrir hii, ynabainika makusudio ya wale waliosema kwamba asilimia kubwa zaidi ya lugha ni majazi kwani ni kweli kwamba asilimia kubwa ya maneno ya Kiarabu yako hivyo. Na yanabainika makusudio ya wale waliosema kwamba asilimia kubwa ya maneno ya Kiarabu ni hakika: si majazi, kwani baada ya yale maneno kuhamishwa kutoka katika maana yake ya asili na kuja katika maana ya pili na maana hio ya pili ikaenea na kuzagaa hadi kufikia kwamba neno hilo linapotajwa haifahamiki ila kwa maana yake hio ya pili basi maana hio ya pili inakuwa sasa ni hakika. Na pia kwa tahriri hii unaondoka mgongano baina ya rai mbili za wataalamu wakuu. Wallahu A’alam.

Tukirudi katika maelezo yako, tunasema: lau tutakubaliana na wewe juu ya hayo ulioyasema, basi hii ina maana kwamba Majaazul-Mursal ni batili: hayakuthibiti. Na kubatilika kwa kuwepo kwa aina moja ya Majazi, hakujabatilisha kuwepo kwa asili ya majazi au kuwepo kwa aina nyengine za majazi. Cha kufahamu ni kuwa sisi hatuzungumzii hizi juz-iyyat (vijisehemu vya kitu), bali tunazungumzia kulliyyat (misingi ya kitu); ama juz-iyyat, watu wanaweza wakatafautiana juu yake ilhali wamekubaliana juu ya kuwepo kwa kulliyyat (misingi). Nimekupa mfano wa tafauti za wanavyuoni juu ya kuitumia Hadithu Mursal kwamba hilo halibomoi uhakika wa kuwepo kwa aina nyengine za Hadithi dhaifu. Kwa hivyo, lau tatasalimu amri mbele ya mantiki yako hii ya kutokuwepo kwa Al-Majazu Al-Mursal je huko kunabomoa kuwepo kwa majazi mengine hususan ukizingatia ukweli kwamba ushahidi wa wazi umesimama juu ya kuwepo kwa majazi hayo?

178 - Sura 57, Aya 20.

73

Ama nukta nyengine ni kuwa kuna tafauti kubwa baina ya majazu mursal na mifano uliotoa. Mfano wa kwanza uliotoa ni: “Nimeingiza kidole sikioni”. Haya kweli ni majazu mursal, lakini itakuwa hivyo pindipo utayazungumzia kwa lugha ya Kiarabu: si kwa lugha ya Kiswahili. Na hii ni kwa sababu katika lugha ya Kiarabu kidole ni kile kiungo kizima. Ama sehemu ya mwisho tu ina jina lake mbali nalo ni banaan (fingertips). Sasa wewe ulipotumia jina la kiungo kizima kwa kumaanisha jina la sehemu ya kiungo hicho, ndipo ilipodhihiri kwamba umetumia neno kinyume na maana yake ya asili, kwani kiungo hicho kamili kina jina tafauti na jina la sehemu yake ya mwanzo ambayo ndio ulioitia wewe masikioni mwako.

Ama mfano wako uliposema: Nimekula wali, huu si mfano sahihi, kwani utaposema hivyo kwa lugha ya Kiarabu ama utatumia alifu na lamu useme:

األرز Ukisema hivi, basi alifu na lamu .(Nimekula wali) أكلتimeshabainisha makusudio kwani alifu na lamu hapa ama zinamaanisha:يدهعال فيرعلتا (1 (Al-taarif Al-‘ahdi) nayo ima ni ذكري au عهد Na hii ina maana kuwa wali ulioula ni wali maalumu, kwa maana .ذهنيya kwamba si wali wote. Na kwa hivyo, maneno haya si majazi bali ni hakika kwani vyombo vya lugha vimeshabainisha makusudio.2) Au iwe الجنس الماهية pia huitwa لتعريف الحقيقة au لبيان .لبيانKwa maana hii itakuwa lengo lako uliposema األرز Nimekula wali, ni أكلتkubainisha uhakika wa ulichokila tu. Katika hali hizi mbili, inakuwa hakuna األرز :katika maneno (ujumla) عموم Nimekula wali , hata ikafaa أكلتkuuliza “je ulioula ni wali wote au ni baadhi tu” kwani vyombo vya lugha vimeshabainisha makusudio.

Vyenginevyo, ikiwa utasema: أرز اأكلت akaltu urzan (Nimekula wali), bila ya kuweka alifu na lamu katika neno urz, basi sigha (form) hii ni في نكرة

اإلثبات (ujumla) عموم nakira fii siyaaqi al-ithbaat, nayo pia haina سياقndani yake, hata ikafaa kuuliza “je ulioula ni wali wote au ni baadhi tu”. Kwa hivyo, mfano huu si mfano sahihi.

Ama mifano ya: Nimekwenda Makka…nimekaa msikitini, au nyumbani, au darasani, au ofisini, haya yote si majazi, wala si sawa na kusema: أدخلت

األذن في Ubainifu wa .(nimeingizi kidole changu kwenye sikio) إصبعيhaya ni kuwa sehemu ya Makka inaitwa Makka kama vile ambavyo sehemu ya Pemba ni Pemba; sehemu ya msikiti inaitwa msikiti – yote hayo huitwa hivyo kwa uhakika. Ama ncha za vidole (banaan) ambazo ndizo unazozitia katika sikio, katika lugha ya Kiarabu zinaitwa vidole kimajazi.

Hayo ndio maelezo yalionibainikia kuhusu suala hili. Kwa hali yoyote ile itayokuwa, ubainfu wa mwanzo unakutosha kukuongoza kwamba lau

74

tutasalimu amri juu ya maelezo yako ulioyatoa hapa, basi upeo uliomo katika maelezo hayo ni kuwa majazu mursal si sahihi, na kutokuwa sahihi kwa majazu mursal hakumaanishi ubatili wa majazi mengine.

Baada ya hayo tumebakiwa na mambo mawili:1) Tuelewe kwamba waliozungumzia majazu mursal wanakusudia

nini. 2) Je hicho walichokizungumzia kipo au hakipo.

MAKUSUDIO YA MAJAZU MURSAL

Ama suala la mwanzo ni kuwa waliozungumzia kuwepo kwa majazu mursal wanakusudia “Kutumika neno kinyume na maana yake ya asili kwa uhusiano usiokuwa wa kutaka kukifananisha kitu kimoja na chengine; na kwa kuwepo qarina inayoizuia maana ya asili”. Sasa mchambuzi huwa hatazami hii istilahi (techinical term): je tuite majazu mursal au tuite uslub; hili si muhimu katika ulimwengu wa uchambuzi, bali anatazama uhakika wa kile kilichosemwa – kama tutavyoeleza zaidi baadae – je kipo au hakipo? Kwa hivyo, cha kujiuliza hapa ni kuwa je maneno yaliotumika namna hio yaani yaliotumika kinyume na maana yake ya asili bila ya kukusudia kufanya tashbih (kufananisha) yapo au hayapo? Kama hayapo, basi itakuwa kweli hakuna kitu majazu mursal; kama yapo basi hii ina maana kwamba uhakika wa kitu hicho upo ama jina ukipenda kuita majazu mursal ita hivyo; kama hupendi tafuta jina jengine ukiite, sisi hatugombanii majina bali tunazungumzia uhakika wa kitu, kwani kama tulivyonukuu zaidi ya mara moja kwamba wataalamu wanasema: ا في مشاحة إصطالحلال Hakuna kujadiliana katika maneno ya kitaalamu au ya kifani (technical terms). Pia kasoro zilizomo katika vijipengele vya kitu, havibomoi uhakika wa misingi ya kitu hicho.

Sasa ili ujue kwamba kitu hicho (majazu mursal) kipo, soma mfano mmoja ufuatao – na mifano iko mingi imetajwa katika vitabu vya balagha. Anasema Allah:

( تصلى3) ناصبة ( عاملة2) خاشعة يومئذ وجوه (4) حامية ناراNyuso siku hio zitahizika*Zitakuwa ni zenye kufanya kazi ngumu*Zitauingia moto mkali.179

Hapa utaona kwamba kumetajwa nyuso kuwa ndizo zitazoingia motoni, bila ya kutajwa mtu kamili ilhali atayeuingia moto ni mtu kamili: si uso tu. Kwa

179 - Sura 88, Aya 2-4.

75

hivyo, imetajwa sehemu ya kitu na kilichokusudiwa ni kitu kamili. Wala haikukusudiwa kufananishwa kitu kimoja na chengine. Hiki ndicho wataalamu wanachoita Al-Mjazu Al-Mursal. Je kipo au hakipo? Narudia tena: sizungumzii majina: ninazungumzia uhakika wa kitu (facts au .(حقائق

KUICHEZEA LUGHA NA QUR-ANI

Anasema Sheikh Al-‘Allama Kasim bin Mafuta:

Pia maulamaa wanaopinga kuwepo kwa majazi wanapowahoji na kuwapa changamoto (challenge) wenye kuthibitisha kuwepo kwa majazi hawapati majibu yoyote ya kuridhisha ndipo pale wakalipinga suala hili ili:-Lugha ya kiarabu isichezewe.-Ili watu wa batili wasipate nafasi ya kuichezea Qur’an kwa kupotosha maana yake kwa madai ya kwamba kuna majazi, na hili walilolifikiria ndilo lililotokea.

Kwa sababu wamejitokeza baadhi ya watu wakazipotosha aya nyingi zinazotaja sifa za Allah kwa madai kwamba kuna majazi kwa madai ya kumtakasa Allah na sifa za viumbe na hatima yake wakaingia katika upotofu.

Mpaka hapo itabainika kwamba;

Kupinga kuwepo kwa Majazi ndani ya Qur’an ili kufunga milango ya kuwaingiza watu kwenye upotofu ndiyo msimamo sahihi na wa haki na unaokubaliana na akili180 zaidi kuliko kudai kinyume chake. Mwisho wa kunukuu.

JAWABU

Hayo ndio maneno ya Sheikh huyo wa Pongwe Tanga, nayo si maneno madhubuti. Kwani wanaopinga kuwepo kwa majazi wanapewa jawabu za wazi kabisa, lakini huwezi kumlazimisha farasi kunywa maji; unachoweza ni kumchukua hadi mtoni. Vyengine, tupeni maana ya kamba iliotajwa katika Aya:

الله بحبل واعتصموا جميعاNa kamataneni na kamba ya Allah kwa pamoja.

Na katika Aya:

180 - Akili ya nani?!

76

ثقفوا ما أين الذلة عليهم ضربت الناس من وحبل الله من بحبل إالWamepigwa udhalili popote walipo, isipokuwa (wakishikana)

na kamba ya Allah na kamba ya watu.

Na mutupe maana mkono uliotajwa katika Hadithi:“ يد ”المسلمون

Waislamu ni mkono.181

Na Hadithi:السفلى اليد من خير العليا اليد

Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini.

Na ubeti wa babu yake Mtume (s.a.w.) aliposema:

*** يدا لي واجعله ربي اردده محمدا ولدي علي ردNirejeshee (é Mwenyezi Mungu) Muhammad

mwanangu Mrejeshe é Mola wangu na umfanye kuwa mkono wangu.182

Na mutupe maana ya neno jua lililotajwa katika ubeti wa mashairi yasemayo:

** الشمس من تظلني شمس عجب ومن تظلني قامتAlisimama akanifunika kivuli, na ni ajabu** Jua linanikinga (linanipa kivuli) dhidi ya jua.

Jamani! Wapi mumepata kuona kwamba jua linamziba (linamzinga) mtu asipigwe na jua? Haya! Twambie Sheikh Kasim bin Mafuta! Haya si majazi ni nini?

Kwa hivyo:1) Ni wazi kwamba nyinyi ndio munaoichezea lugha ya Kiarabu kwani

lugha inathibitisha kuwepo kwa majazi; nyinyi munakanusha. 2) Nyinyi ndio munaochezea Qur-ani, kwani Qur-ani inathibitisha

kuwepo kwa majazi tena kwa wingi sana; nyinyi munakanusha.

Ama kauli yako uliposema:

181 - Al-Rabi’u bin Habib Al-Jami’u Al-Sahih j. 4, uk. 354, Hadithi na. 903. Anasema mtiaji maelezo: “Kaitaja pia mwenye kitabu Kanzu Al-’Ummal uk. 441,442,443. 182 - Ubeti huu niliuhifadhi miaka mingi kutoka katika kitabu kiitwacho ‘Uyuunu Al-Taarikh kiasi cha kwamba sikumbuki tena juzuu na ukurasa. Lakini nimeukuta tena katika kitabu Al-Ma’arifa Wa Al-Ta’arikh cha Al-Fasawi j. 3, uk. 281 kwa lafdhi isemayo:

يدا ... عندي واصطنع ربي أردده محمدا راكبي إلي رد

77

Ili watu wa batili wasipate nafasi ya kuichezea Qur’an kwa kupotosha maana yake kwa madai ya kwamba kuna majazi, na hili walilolifikiria ndilo lililotokea.

Ninasema: hiki ndicho munachokiogopa. Munachokiogopa katika kuyakanusha majazi ni kuanguka kwa itikadi zenu batili za tashbihi na tajsim. Nami ninakwambia ewe Sheikh Kasim Mafuta, tukijaalia kuwa hizo itikadi zenu za Mungu mwenye viungo na sura ya binaadamu kuwa ndio itikadi sahihi, na itikadi zetu za kumtakasa Allah kutokana na sifa za viumbe ndio batili, basi ilivyo ni kuwa huwezi kutibu batili kwa batili. Huwezi kukataa majazi kwa kukimbia Mungu wako mwenye mikono asije akakatwa mikono yake; majazi yapo yapo tu, na hamuna uwezo wa kuyakanusha kwa hoja hata mukikusanyika Mawahabi wa dunia nzima – binaadamu na majini pamoja.

Ama kauli yako uliposema:

Mpaka hapo itabainika kwamba: kupinga kuwepo kwa Majazi ndani ya Qur’an ili kufunga milango ya kuwaingiza watu kwenye upotofu ndiyo msimamo sahihi na wa haki na unaokubaliana na akili zaidi kuliko kudai kinyume chake.

Ninasema: upotofu ni kukikanusha kitu kilichothibiti katika Qur-ani au Sunna. Sisi tumekuthibitishia kwa Aya nyingi za Qur-ani, kwamba kuna majazi, na wewe umetoa hoja za kifalsafa ya Kigiriki. Kilichobaki utwambie je maneno hayo yaliotumika katika Aya hizo na Hadithi hizo na maneno hayo ya Waarabu yametumika katika maana yake ya asili, au yametumika kinyume na maana yake ya asili ili tuweze kutoa hukumu adili juu ya kuwepo kwa majazi na kutokuwepo.

Anaendelea Sheikh Kasim kwa kusema:

Na ama baadhi ya mifano ambayo hutolewa kama ni hoja ya kuwakandamiza wenye kupinga majazi Imamu Ibnul-Qayyim katika kitabu chake “AL-SWAWAAI’QUL-MUR’SALA” ameyajibu kwa ufundi mkubwa mno. Kadhalika Imamu wa Tafsiri na Usuul katika zama hizi sheikh Muhammad al-Amin al-Shanqitwiy pia amezijibu hoja nyingi tena kwa ufanisi wa hali ya juu kwa mwenye kutaka faida na arejee kwenye kitabu chake: “MAN’U JAWAAZIL-MAJAZI” Na ukizitazama kwa makini hoja zao utagundua kwamba tofauti ni ya kimatamshi, hawa wameona utaratibu huo wauite “Majazi”, na kwa hakika hilo lina mapungufu mengi kama tulivyo thibitisha hapo nyuma.

78

Na wengine wameona wauite “Usluubun min Asaalibil-Lugha” (utaratibu/mfumo katika taratibu za lugha) na njia hii ndiyo iliyokaribu na usahihi, ili kuwazuia watu wa batili wasiyapotoshe maandiko kwa kuupitia mlango huu.

JAWABU

Ama kuhusu kitabu Al-Sawaai’qul-Mur’sala cha Al-Imamu Shamsu Al-Din, Ibn Al-Qayyim Al-Zar’i, nakujuilisha kwamba kitabu hicho kimejibiwa hoja moja moja na Al-Imamu Badru Al-Din, Sheikh Al-Mufassirin, Mujthid Al-’Asr, Al-Allama Al-Jami’u Ahmad bin Hamad Al-Khalili Al-Mufassir. Jawabu hio inaitwa Jawaahiru Al-Tafsir Juz-u Khaas, tafadhali itafute uisome. Utakuta humo yenye kuupoza moyo wako. Ninachotaka kukwambia ni kuwa wakuu wako kule Suudia kimewashinda kukijibu kama walivyoshindwa kutoa jawabu sahihi kwa kitabu Al-Haqqu Al-Damigh. Lakini tatizo lenu wenzetu ni kuwa hamuna munachokijua isipokuwa Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim!

Bali kitabu hicho cha Ibn Al-Qayyim, hakina hoja isipokuwa shubuhati tupu. Watu wanakwambieni “Haya majazi” nyinyi hamuna jawabu ya kuyakataa; halafu munasema hakuna majazi, sasa kama hakuna majazi hiki ni nini? “Huu nchele” wewe huwezi kuukataa kwani unauona kuwa kweli “ni nchele” lakini unashikilia kauli yako “hakuna nchele”. Basi haya bakieni hivyo hivyo kufuata kama bendera au al-taqlidu al-a’ama.

Ama kauli yako uliposema:

Na wengine wameona wauite “Usluubun min Asaalibil-Lugha” (utaratibu/mfumo katika taratibu za lugha) na njia hii ndiyo iliyokaribu na usahihi, ili kuwazuia watu wa batili wasiyapotoshe maandiko kwa kuupitia mlango huu.

Ninasema: yote haya yanaonesha yale yale tulioyasema na kuyakariri kwamba ima ukweli huutaki au hujui kuhakiki mambo! Sisi bwana hatutafautiani katika majina: bali tunatafautina katika uhakika wa kitu – je kipo au hakipo. Majazi ni “kutumika neno kinyume na maana yake ya asili”. Je uhakika wa matumizi haya upo au haupo? Kama upo basi hayo ndio majazi yenyewe ukiwa utayaita majazi au “Usluubun min Asaalibil-Lugha” (utaratibu/mfumo katika taratibu za lugha). Sheikh Kasim upo? Haya majina ni istilahiyya (technical terms) zilizoekwa na wanavyuoni ili kurahisisha kufahamiana katika uwanja wa elimu; ama uhakika wa kile kitu ndio wa kuzungumziwa.

79

Hadi hapa tutakuwa tumefika mwisho wa kuzijadili shubuhati za Sheikh Mafuta kuhusu Majazi. Sasa natuchukue fursa hii kwa kulielezea tena suala la majazi kwa ufupi ili tuweze kuwa katika ubainifu juu ya jambo hili.

MAELEZO ZAIDI JUU YA KUWEPO KWA MAJAZI Baada ya mjadala huo sasa natuizungumzie maudhui hii kwa ufupi. Elewa ndugu msomaji kwamba jumhur (majority) ya Wanavyuoni wa Kiislamu katika madhehebu zake tafauti wanasema kuwa majazi ni kitu kilichopo katika Qur-ani, Hadithi za Mtume (s.a.w.) na lugha ya Kiarabu. Kama vile ambavyo Al-Salaf Al-Saalih (watangulizi wema, Masahaba na wanafunzi wao) wote wametumia majazi katika maneno yao ya kawaida (prose) na mashairi yao hata kama jina hilo halikuwepo. Wakati – kwa upande wa pili – wengine wachache sana – aghlabu ya wachache hao ni baadhi ya watu wa madhehebu ya Hanbali – wamekanusha kuwepo kwa majazi! Sababu iliowafanya watu hao wayakanushe majazi, si kwamba majazi hayapo, bali ni kuwa kukubali kuwepo kwa majazi kutapelekea kuibomoa itikadi yao ya kuwa Allah ana viungo, ambavyo ukweli wake ni kuwa vimetajwa katika Qur-ani na Hadithi kimajazi (figuratively)! Na kwa sababu hio ya kukanusha kwao majazi, basi Allah aliposema: “Mkono wa Allah uko juu ya mikono yao”183 na akasema “Nini kilichokuzuia usimsujudie yule niliyemuumba kwa mikono yangu miwili”,184 wenye kukanusha kuwepo kwa majazi wakasema kuwa Allah ana mikono kweli kweli!

Miongoni mwa waliokuwa mstari wa mbele katika kukanusha kuwepo kwa majazi ni Al-Imamu Ibn Taymiyya na mwanafunzi wake Al-Imamu Ibn Al-Qayyim.185 Lakini hoja walizozitegemea juu ya ukanushaji wao huo ni dhaifu kuliko nyumba ya buibui! Hoja yao kubwa ni kuwa wanavyuoni wa lugha wa mwanzo hawakuigawa lugha ya Kiarabu katika migawanyiko miwili hio ya majazi na hakika, bali hayo yalifanywa na waliokuja baadae!186 Anasema Ibn Taymiyya:

183 - Sura ya 48 Aya ya 10.184 - Sura 38, Aya 75.185 - Ibn Qayyim kaandika kitabu maalumu juu ya kukanusha majazi, na akarefusha sana kwa hoja ambazo hazina kichwa wala miguu. Hoja hizo zimejibiwa moja moja na Sheikh Al-Khalili katika tafsiri yake Jawahiru Al-Tafasir Juzuu Khas. Anayetaka kuona jawabu juu ya dai moja moja la Ibn Al-Qayyim na-arejee tafsiri hio. 186 - Hoja zao nyengine ni kama alivyozileta Sheikh Mafuta. Na umejionea mwenyewe udhaifu wa hoja hizo.

80

Hakika ya wengi katika hawa (wenye kukubali majazi) wameigawa lugha (sehemu mbili): majazi na hakika….bali Maimamu wa lugha kama Al-Khalil, Sibawayh, Al-Kisaai, Al-Farraau na walio mfano wa hao, na Abu ‘Amri bin Al-’Alaa na Abu Zaid Al-Ansari na Al-Asma’i na Abu Amri Al-Shaibani na wengineo hawakuigawa (lugha) kama walivyoigawa hawa.187

Na hoja hio akaikariri Ibn Al-Qayyim kwa kusema:

Wala hakuna yoyote katika Waarabu kamwe aliyesema kwamba neno hili ni hakika na hili ni majazi; wala hakuna hayo katika maneno ya walionukuu lugha ya Waarabu kwa kuzungumza nao mdomo kwa mdomo au kwa kupitia kwa mtu mwengine; kama vile ambavyo hakuna (suala la kuwepo kwa majazi) katika maneno ya Masahaba, wala Tabiina (wafuasi wao) wala Tabii Tabiina (wafuasi wa wafuasi) wala yoyote katika Maimamu Wanne.188

Na akasema Ibn Al-Qayyim:

Na itapoeleweka kwamba migawanyiko ya maneno katika hakika na majazi si migawanyiko ya Kisharia, wala ya kiakili wala ya kilugha, basi (utakuwa umeelewa kwamba migawanyiko hio) ni ya kifani tu (kiistilahi). Na fani hii imejitokeza baada ya karne tatu zenye ubora kwa mujibu wa andiko. 189

Hayo ndio maelezo ya Maimamu wawili hao: Ibn Al-Qayyim na Sheikh wake Ibn Taymiyya, nayo si maneno yenye uzito katika mezani ya elimu kwani:

1) Kama vile ambavyo Masahaba na Wafuasi wao hawakusema kuwa haya ni majazi, pia hawakukanusha kuwepo kwa majazi.

2) Ikiwa kutokuigawa kwao lugha katika migawanyiko ya majazi na hakika ni dalili kwamba hakuna majazi, basi inabidi kwamba na hio pia iwe dalili ya kutokuwepo kwa hakika, kwani hawakutaja mgawanyiko huu wala ule!

3) Kinachozingatiwa ni ushahidi wa kitu: si nani kakisema au hakukisema; lini kimesemwa au hakikusenwa.

4) Nne – na ndio muhimu – ni kuwa Maimamu wawili hawa wameshindwa kutafautisha baina ya kuwepo kwa uhakika wa kitu (the existence of a fact) na kuvumbuliwa kwa neno la kifani au la

187 - Ibn Taymiyya Majmu’u Al Fatawa j. 20 – juzuu inayohusu Usulu Al fiqh – uk. 230, na mfano wake katika j. 8, uk. 65.188 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasar Al Sawaiq Al Mursala uk. 231-232.189 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasar Al Sawaiq Al Mursala uk. 233. Kasahau Ibn Al-Qayyim kwamba kinachozingatiwa si wakati bali ni dalili.

81

kitaalamu la kitu hicho (the rise of a technical word). Uhakika wa majazi ulikuwepo tangu enzi ya Mtume (s.a.w.) na kabla yake, lakini neno lake la kifani ndilo ambalo limeundwa baada ya kuundwa kwa fani za elimu. Kwa mfano, enzi ya Mtume (s.a.w.) hakukuwa na elimu ya Nahau, wala Sarfu, wala Usulu Al-fiqhi wala Tajwid, wala ‘Ulumu Al-Hadith – yaani majina ya fani hizo zote yalikuwa hayapo. Hizi zote ni fani ambazo zimeundwa baadae lakini uhakika wa fani hizo ulikuwepo tangu zamani. Waarabu husema kwa mfano: “Ali yadh-habu” watu wa Nahau husema kuwa Ali ni “Mubtada (kianzilishi)”. Sasa maneno “Ali yadh-habu” yalikuwepo tangu enzi ya Mtume (s.a.w.), lakini jina la kifani au la kinahau la kuuita muundo huu kuwa ni “Mubtada (kianzilishi)” ndilo lililogunduliwa baadae – uhakika ulikuwepo na jina la kifani limefuata baadae. Halkadhalika nikisema Hadithi hii ni dhaifu au hasan au maudhui au mursal au mu’allaq au mawquf, majina yote haya yamepangwa na wataalamu wa Hadithi: hayakuwepo katika enzi ya Mtume (s.a.w.) wala katika enzi ya Masahaba, lakini uhakika wake ulikuwepo. Kwa kufahamu zaidi tazama ukweli kwamba wanasayansi leo wanagundua vitu vilivyokuwepo miaka nenda miaka rudi ndani ya miili yetu na katika ulimwengu, kisha baada ya ugunduzi huo wanavipa majina vitu hivyo – uhakika wa vitu hivyo ulikuwepo lakini majina ni ugunduzi wao. Sasa leo itakuwa ni jambo la ajabu ikiwa atatokea mtu atasema kwamba si kweli: hakuna sayari inayoitwa pluto kwani waliotangulia hawakuitaja! Kwa hivyo, uhakika wa sayari hio upo na ulikuwepo tangu ulipoumbwa ulimwengu; na jina ndilo waliloliunda watu ili kurahisisha kufahamiana katika masomo na mazungumzo yao. Kwa hivyo, halkadhalika majazi: uhakika wake ulikuwepo lakini jina ndilo ambalo limeundwa na watu, na kuchelewa kwa Technical term (jina la kifani) hakumaanishi kutokuwepo kwa uhakika wa kitu.

Ama madai ya Ibn Taymiyya aliposema:

..Hakuna shaka kwamba wengi wa hawa wameyagawa (maneno ya Kiarabu) mgawanyiko huo (wa hakika na majazi), lakini hakuna katika wao Imamu wa fani yoyote katika fani za kiislamu wala tafsiri, wala Hadithi wala fiq-hi wala lugha wala nahau, bali Maimamu wa nahau kama Khalil, Sibawayh, Al-Kisaai…………hawakuigawa (lugha) kama walivyoigawa hawa.190

190 - Ibn Taymiyya Majmu’u Al Fatawa j. 20 – juzuu inayohusu Usulu Al fiqh – uk. 230, na mfano wake katika j. 8, uk. 65.

82

Na madai ya Ibn Al-Qayyim aliposema:

…..Kama vile ambavyo hakuna (suala la kuwepo kwa majazi) katika maneno ya Masahaba, wala Tabiina (wafuasi wao) wala Tabii Tabiina (wafuasi wa wafuasi) wala yoyote katika Maimamu Wanne.191

Utaona kwamba maneno hayo yako mbali mno na tahqiqi za kielimu. Bali maneno hayo yanatokana na ile ile kawaida yao ya kila kitu chao wanachokitaka wao basi inakuwa: “Umma umekubaliana” na inakuwa: “Hii ndio kauli ya Al-Salaf Al-Saalih (watangulizi wema)” japo kuwa ukweli uko kinyume na hivyo!

Naturudi katika madai kwamba hakuna yoyote katika hao ambao Ibn Al-Qayyim na Sheikh wake wamewataja aliyezigawa lafdhi za lugha ya Kiarabu migawinyiko hio ya majazi na hakika. Tunasema: ama iwe Ibn Al-Qayyim na Ibn Taymiyya wanakusudia, kwa maneno hayo, kwamba:

1) Hakuna yoyote aliyelitaja neno majazi.2) Au iwe wanakusudia kwamba hakuna aliyetumia majazi (yaani

aliyelitumia neno kinyume na maana yake ya asili) hata kama hakuliita majazi.

Ama nukta ya mwanzo utaona ni kinyume na mengi yaliotajwa na wanavyuoni watangulizi. Miongoni mwa hao ni yule ambaye Ibn Taymiyya mwenyewe katoa wasia wa kuwa kitabu chake kisomwe. Huyu si mwengine bali ni ‘Uthman bin Said Al-Darimi. Anasema ‘Uthman Al-Darimi akimjibu Bishr Al-Marsi:

مجاز على بقلوبهم، الناس يعقله الذي المجاز على يجوز هذا فمثلالعرب كالم

Mfano wa (maneno haya) unajuzu kwa misingi ya majazi wanayoyaelewa watu kwa nyoyo zao; kwa misingi ya majazi ya lugha ya Waarabu.192

Na anasema:

المجاز على جائز المعروف في ههنا هذا

Hili hapa kama inavyojulikakana linafaa kwa misingi ya majazi.193

191 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasar Al Sawaiq Al Mursala uk. 231-232.192 - ‘Uthmaan bin Said Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi j. 1, uk. 29. 193 - ‘Uthmaan bin Said Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi j. 3, uk. 156.

83

Na anasema:المجاز على مثل الزرع ضحك

Konde imecheka ni mfano wa kimajazi. 194

Na anasema:

معنى على وتسمع تتراءى والقصور الجبال الكالم مجاز في يقال وقدبعض يقابل بعض ــــأنها اـــها

األصوات وتبلغها

Na huenda ikasemwa katika maneno ya kimajazi kwamba milima na majumba yanaonana na yanasikia kwa maana kwamba yanaelekeana na kufikiwa na sauti. 195

Hayo ni maneno ya ‘Uthman Al-Darimi (280 A.H.), yamo ndani ya kitabu ambacho Ibn Taymiyya alikuwa anausia sana kuwa tukisome ili tupate kumjua Mungu mwenye viungo! Sasa vipi tena wanadai kwamba hakuna aliyetaja majazi katika karne tatu za mwanzo wala hakuna Imamu yoyote wa fani za elimu aliyeyataja? Hapa inakubainikia ndugu msomaji ukweli kwamba watu hawa wanapenda kuwasingizia Al-Salaf katika itikadi zao wanazozitaka wao. Halafu wanakuwa mabingwa wakubwa wa kuwaita watu waongo! Sasa sijui Sheikh Kasim Mafuta atawaingiza Maimamu wawili hawa katika orodha ya waongo au vipi?

Ama Al-Jahidh (250 A.H.), yeye anasema kuhusu Aya isemayo:

اليتامى أموال يأكلون الذين إن بطونهم في يأكلون إنما ظلما نارا وسيصلون سعيرا

“Hakika wale wanaokula mali za mayatima kwa dhulma, kwa hakika wanakula moto katika matumbo yao na watauingia moto mkali…….”.196Anasema Al-Jahidh katika kitabu chake Al-Hayawaan197 kuhusu Aya hio: “ آخر مجاز 198.(Na haya ni majazi mengine) ”وهذا

Ama Al-Imamu Al-Shafi (150-204 A.H.), yeye kanukuliwa na Al-Bazdawi (483) akisema:194 - ‘Uthmaan bin Said Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi j. 3, uk. 176. 195 - ‘Uthmaan bin Said Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi j. 1, uk. 50. 196 - Sura 4, Aya 10. 197 - J. 5, uk. 25. 198 - Nukulu kutoka kwa Dr. Zakariya Qira-atu Jadaliyya uk. 138. Na Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Jawaahiru Al-Tafsir Juz-u Khaas uk. 122.

84

الطالق بلفظ يقع والعتاق مجازا التحرير بلفظ يقع الطالق إن

مجازا

Hakika ya talaka inasibu kwa kutumia lafdhi ya ukombozi199 kimajazi, na kuachia huru mtumwa kunasibu kwa kutumia lafdhi ya talaka kimajazi.200

Na – kama alivyoyataja kwa uwazi – Al-Imamu Al-Shafi pia kaashiria juu ya kuwepo kwa majazi katika kitabu chake Al-Risala hata kama hakuyataja kwa jina, lakini alisema:

... سياقه في يعرف وظاهرا بلسانها العرب بكتابه الله خاطب فإنماظاهره غير يراد أنه

Kwa hakika Allah kazungumza na Waarabu katika Kitabu chake kwa lugha yao….na (andiko) dhahir (wakati mwengine) linafahamika katika mtiririko wake (siyaaq yake) kwamba halikukusudiwi udhahiri wake.201

Halkadhalika kasema Al-Imamu Al-Shafi katika Diwani yake:

كليلة عيب كل عن الرضا تبدي ***عين السخط عين ولكنالمساوي

Jicho la kuridhia limechoshwa na kila aibu (halijishughulishi na aibu za watu); na jicho la chuki (kazi yake ni) kudhihirisha maovu (ya watu).202

Sasa tuseme Al-Imamu Al-Shafi anakusudia kusema kwamba neno kuridhia na neno kuchukia yana macho kweli kweli?

Hayo ni maneno ya Al-Imamu Al-Shafi, nayo yako wazi juu ya suala la kuwepo kwa majazi. Kwa hivyo, ni wazi kwamba Al-Imamu Al-Shafi kazungumzia majazi hata kama katika nukulu mbili hizi za mwisho hakuyapa jina hilo, na jina – kama tulivyosema na kukariri – si muhimu: kilicho muhimu ni uhakika wa kitu.

199 - Yaani lau mtu atamwambia mkewe “nimekuweka huru au nimekupa uhuru au wewe uko huru”.. 200 - Yaani lau mtu atamwambia mtumwa wake “Anta Taaliq” (nimekuacha), basi mtumwa huyo anakuwa huru. Lakini nijuavyo mimi ni kuwa lafdhi kama hizi ni kinaya kwa hivyo, mke haachiki wala mtumwa hakomboki ila iwe niya ya muachaji na mkomboaji ni kuwacha na kukomboa. 201 - Al-Imamu Al-Shafi Al-Risala uk. 52. 202 - Al-Shafi Diwaan uk. 131.

85

Ama Al-Imamu Al-Ash’ari,203 yeye kanukuliwa na Ibn Al-Qayyim akithibitisha majazi. Anasema Ibn Al-Qayyim:

على العبد وفعل الحقيقة على لله فعل العباد أفعال بل فرقة وقالتاألشعري قولي أحد وهذا المجاز

Na wengine wakasema: ‘Bali vitendo vya waja kiuhakika ni vitendo vya Allah,204 na ni vitendo vya mja kimajazi (tu), na hii ni moja ya kauli mbili za Al-Ash’ari.205

Anasema Ibn Taymiyya:

أحمد . اإلمام كالم في إال األئمة من أحد كالم في المجاز لفظ يعرف ولمكتبه فيما الرد من فإن

والجهمية الزنادقة القرآن )على مجاز من : ((.)هذا ولم.. فتاواه في وقالأحد بــهذا من ينطق

في إال األئمة من أحد كالم في المجاز لفظ يعرف ولم واألئمة السلفأح اإلمام فإن ــكالم ه ــــمد

والجهمية الزنادقة على الرد من كتبه فيما القرآن ((قال مجاز من )).هذا

Na neno majazi halikujulikana kwa yoyote katika Maimamu isipokuwa katika maneno ya Al-Imamu Ahmad. Hakika katika maandiko yake ya kuwajibu mazindiki na Jahmiyya (basi kuna maelezo yasemayo): ‘Haya ni majazi ya Qur-ani’.206 …..na akasema Ibn Taymiyya katika Fatawa zake: ‘Na hakuna yoyote katika Al-Salaf na Maimamu aliyelitamka (neno) hili, wala majazi hayakujulikana katika maneno ya yoyote miongoni mwa Maimamu isipokuwa katika maneno ya Al-Imamu Ahmad hakika yake kasema katika maandiko yake ya kuwarudi Al-Zanaadiqa na Al-Jahmiyya: “Haya ni majazi ya Qur-ani”.207

Na maneno alioyaashiria Ibn Taymiyya katika nukulu hio, ni maneno yalio katika kitabu kilichotungwa na kubandikwa nacho Al-Imamu Ahmad kiitwacho Al-Radu ‘Alaa Al-Zanaadiqa Wa Al-Jahmiya ambacho ndani yake kuna maneno haya:

لموسى ا قوله وأما عشر السابعة أسمع )لمسألة معكما إننيآخ (وأرى موضع في إنا ) رـــــوقوله

مستمعون قال )معكم كيف معكما )وقالوا أخرى (إنني آية في إنا)وقالمستمعون كوا ــــفش (معكم

203 - Kazaliwa mwaka 260 A.H. 204 - Kwa maana kwamba Allah ndiye aliyeviumba. 205 - Ibn Al-Qayyim Shifaau Al-‘Alil uk. 93. 206 - Ibn Taymiyya Iqaamatu Al-Dalil ‘Alaa Ibtali Al-Tahlil j. 3, uk. 392. 207 - Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 12, uk. 156, babu ghalat man qaala innahu majaz.

86

قوله أما ذلك أجل من القرآن معكم )في اللغة (إنا مجاز في فهذا

Mas-ala ya kumi na saba: ama kauli yake Allah aliposema: “Hakika Mimi niko pamoja nanyi ninasikia na ninaona”208 na kauli yake katika sehemu nyengine “Hakika ya sisi tuko pamoja nanyi tunasikiliza”.209 Basi (Al-Jahmiyya) wakasema: ‘Vipi (Allah) aseme: ‘Hakika Mimi niko pamoja nanyi’ na aseme katika Aya nyengine “Hakika Sisi tuko pamoja nanyi tunasikiliza”. Basi wao (Al-Jahmiyya) wakawafanya watu waishuku Qur-ani. (Lakini jawabu ni kuwa) ama kauli yake “Hakika Sisi tuko pamoja nanyi” haya ni katika majazi ya lugha. 210

Sasa kilichobakia ni kuwa Sh. Kasim Mafuta amuweke Imamu wake Ibn Taymiyya katika orodha ya waongo kwani kilichonukuliwa kutoka kwa Al-Imamu Ahmad ni: " معكم " إنا قوله اللغة أما مجاز في فهذا “Ama kauli yake ‘Hakika Sisi tuko pamoja nanyi’ haya ni katika majazi ya lugha. Ibn Taymiyya kamnukuu Al-Imamu Ahmad akisema: (( من هذا

القرآن Haya ni majazi ya Qur-ani. Kwa mujibu wa vipimo vya((مجازbwana Kasim, huu ni uwongo! Kama vile alivyomwita Sh. Al-Khalili kuwa ni mwongo kwa sababu kama hii au inayofanana na hii. Sikusudii chochote hapa isipokuwa kutaka kuwaonesha walimwengu jinsi Kasim Mafuta alivyokuwa na fahamu finyu, vyenginevyo huu hauitwi kuwa ni uwongo bali ni ama kughafilika au kuyanukuu maneno kimaana.

Anasema Ibn Taymiyya:

الناشي العباس كأبي طائفة وقالت فيهما حقيقة أنه على فالجمهورجل و عز الرب في حقيقة إنها

المخلوق في مجاز

Basi jumhur wanasema kwamba hilo (jina ambalo huitwa Muumba na kiumbe)211 ni hakika kwa wote wawili (Muumba na kiumbe), na wengine kama vile Abu ‘Abbaas Al-Nnashi wanasema kwamba hayo (majina ya namna hio) ni hakika kwa Allah212 na ni majazi kwa viumbe.213

208 - Sura 20, Aya 46. 209 - Sura 26, Aya 15. 210 - Al-Raddu ‘Alaa Al-Zanaadiqa Wa Al-Jahmiyya kilichonasibishwa na Al-Imamu Ahmad na kuhakikiwa na Daghish Al-‘Ajmi uk. 193. 211 - Kama vile majina عالم أو قادر أو aliye hai, au mwenye uwezo au mwenye حيelimu.212 - Yaani muweza wa hakika – kwa mfano – ni Allah. 213 - Ibn Taymiyya Al-Jawaabu Al-Sahih j. 3, uk. 294.

87

Hayo ni maneno anayoyanukuu Ibn Taymiyya mwenyewe kutoka kwa Abu Abbaas Al-Nnashi. Na Abu Abbaas huyu kafa mwaka 293.214 Baada ya yote hayo yaliosemwa na ‘Uthman Al-Darimi, Al-Jaahidh, Al-Shafi, Ahmad na Abu ‘Abbaas Al-Nnaashi, na mengine katika haya kayanukuu Ibn Taymiyya mwenyewe na Ibn Al-Qayyim mwenyewe, bado kutabakia ukweli katika kudai kwamba:

1) Hakukuwa na Imamu wa fani yoyote ile ambaye kayataja majazi.2) Majazi hayakutajwa na yoyote yule katika karne tatu za mwanzo.

JAWABU YA BADRU AL-DIN AL-KHALILI

Sasa baada ya hayo, natutazame jawabu ya Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Al-Mufassir juu ya maneno hayo ya Ibn Al-Qayyim na Sheikh wake, Ibn Taymiyya. Anasema Sheikh Al-Khalili:

Ama Maimamu wanne (wa Kisuni) wameyataja majazi kwa uwazi au kwa kuashiria. Na miongoni mwa walioyataja kwa uwazi ni Abu Hanifa aliposema:

في بل الحكم، في ال التكلم في الحقيقة عن خلف المجاز إنأصل الحكم

Hakika ya majazi ni badala ya hakika215 katika kusema: si katika hukumu, ama katika hukumu (majazi) ni asili.216

Na akanukuu ‘Alaau Al-Din Al-Bukhari kutoka kwake (Abu Hanifa akisema) kwamba hakika na majazi ni katika sifa za lafdhi kwa makubaliano ya watu wa lugha.

214 - Al-Dhahabi Al-Siyar j. 11, uk. 134-135. 215 - فرع الحقيقة أي عن (Yaani ni tawi au yanatokana na uhakika) katika kusema si katika hukumu. Kuyafahamu maneno haya inabidi ufahamu hukumu ni nini na kusema ni nini. Kusema ni ile lafdhi ya hakika ulioitumia kwa kukusudia majazi, kama neno simba katika jumla ya maneno inayosema: “Ali ni simba”. Na hukumu ni ile sifa iliomo katika lafdhi hio nayo ni “Ushujaa”. Sasa je hii hukumu, ambayo kwa hapa ni ushujaa, ni asili: si majazi; na majazi ni hili tamko “Simba” tu, au ni kinyume chake? Abu Hanifa anaona kwamba hukumu, ambayo kwa hapa ni ushujaa, ni jambo la asili; na tawi yaani majazi yapo katika lile tamko ambalo kwa hapa ni neno simba. Kwa ufafanuzi zaidi, tazama Dr. Al-Zuhaili Usulu Al-Fiqhi j. 1, uk. 293 216 - Tazama Kashfu Al-Asraari ‘An Usuli Fakhri Al-Islaam Al-Bazdawi cha ‘Alaau Al-Din Al-Bukhari, j. 2, uk. 145-146, chapa ya Daru Al-Kitaab Al-’Arabi. Ninasema: maelezo haya pia kayanukuu Dr. Al-Zuhaili katika Usulu Al-Fiqhi j. 1, uk. 293.

88

Na mfano wake ni kauli ya Al-Imamu Ahmad (bin Hanbal aliposema): اللغة: مجاز فهذا معكم إني ,Kauli yake: mimi niko na nyinyi) قوله

haya ni majazi ya lugha);217 hakika yake (maneno hayo ya Al-Imamu Ahmad) yako wazi kabisa katika kuthibitisha majazi pamoja na kuwa Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim wamefanya jaribio la kutaka kuleta ta-awil kwamba makusudio yake ni kuwa hilo linajuzu katika lugha.218 Bali miongoni mwa masahibu wa Ahmad wako wale ambao walikuwa karibu naye zaidi kwa zama ambao waliyafasiri maneno hayo ya Ahmad katika udhahiri wake katika kuthibitisha majazi. Na hili wamelikiri Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim wenyewe waliposema: ‘Na wameshikana na maneno haya ya Ahmad wale wenye kunasibika na madhehebu yake (wakasema) kwamba katika Qur-ani kuna majazi, kama vile Al-Qadhi Abu Ya’alaa, Ibn ‘Aqil, Abu Al-Khattab.219……

Ama (Al-Imamu) Malik na (Al-Imamu) Al-Shaafi hata kama hawakuyataja majazi kwa jina lake220 lakini wameyathibitisha kwa (ibara) zenye kuyaonesha (hayo majazi)…Katika tafsiri ya Qur-ani ya (Al-Imamu) Malik kuna tafsiri ya maneno kimajazi. Mfano wa hayo ni kile kilichosimuliwa na Ibn Al-Qaasim kutoka kwake (Al-Imamu Malik) kuhusu Aya isemayo:

تأويله يأتي يوم (Siku itayokuja hatima yake). Kasema: ‘Nimemsikia Malik akisema تأويله (Hatima yake) ni malipo yake.221 Na Ibn Wahb kapokea kutoka kwake (Al-Imamu Maalik) kwamba kasema kuhusu Aya isemayo: رهم الله بأيام وذك (Wakumbushe siku za Allah), (anasema Malik kwamba, Allah) anakusudia (wakumbushe kuhusu) neema zake na ataya zake kwao.

Ama Al-Shafi amethibitisha majazi, aliposema…222 Bali Al-Bayhaqi kamnukuu (Al-Imamu Al-Shaafi) akiyataja majazi kwa uwazi kwa maana yake ya kifani, na hayo ni katika kauli yake Mtume (s.a.w.) aliposema:

عاتقه عن العصا يضع ال فرجل جهم أبو Ama Abu Jahm, yeye ni) أما

217 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasar Al-Sawaa’iqi Al-Mursala uk. 232. 218 - Nimeinukuu kauli hii ya Al-Imamu Ahmad kabla, lakini sikunukuu madai haya ya Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim, kwani madai hayo nimeyanukuu hapa kutoka kwa Sheikh Al-Khalili. 219 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasar Al-Sawaa’iqi Al-Mursala uk. 232. 220 - Anakusudia katika yale yaliomo katika vitabu vyao wenyewe. Vyenginevyo Al-Imamu Al-Shafi kanukuliwa na Al-Bazdawi akiyataja majazi kwa jina lake la kifani kama tulivyonukuu kabla na kama Sheikh mwenyewe alivyomnukuu kupitia kwa Al-Bazdawi na Al-Bayhaqi. 221 - Al-Qabsu fii Sharhi Al-Muwattai cha Al-’Allama Ibn Al-’Arabi j. 4, uk. 203. 222 - Maneno ya Al-Imamu Al-Shafi tumeshayanukuu kabla, nayo ni:

... غير يراد أنه سياقه في يعرف وظاهرا بلسانها العرب بكتابه الله خاطب فإنماظاهرهKwa hakika Allah kazungumza na Waarabu katika Kitabu chake kwa lugha yao….na (andiko) dhahir (wakati mwengine) linafahamika katika mtiririko wake (siyaaq yake) kwamba halikukusudiwi udhahiri wake.

89

mtu ambaye mkwaju hauondoi mabegani mwake),223 naye (Al-Bayhaqi) akakubaliana naye.224………..

Ama madai ya Ibn Al-Qayyim akimfuata Sheikh wake Ibn Taymiyya kwamba majazi hayapo katika maneno ya Al-Khalil na Sibawayh na Al-Farraa na Al-Asma’i na mfano wa hao, ni madai yaliosimama juu ya msingi wa kusukuma, kwani wote hawa walikuwa wakifahamu vyema nini tafauti ya hakika na majazi, na hayo yako wazi katika maneno yao: ni sawa tu wakiwa wameyataja majazi kwa uwazi au hawakuyataja kwa uwazi. Na hakuna shaka kwamba Abu ‘Amri bin Al-’Alaa ndiye aliyewatangulia kwa zama wote hao waliowataja, naye kataja Al-Isti’ara kwa uwazi nayo (hio Al-Isti’ara) ni majazi bora yao na ndio majazi yalio bayana zaidi. Na hayo ni katika yale alioyasimulia Ibn Rashiq Al-Qayrawaani kutoka kwake katika kitabu Al-’Umda, kwamba alisema kuhusu ubeti wa Dhu Al-Rumma:

ذو حتى به ** ىأقامت الفجر مالءته الثريا وساق والتوى العودAlikaa huko mpaka kijiti kikakauka na akapinda***Na kizibau225 cha (nyota za) thuraiya kikaendeshwa na alfajiri.

Akasema baada ya ubeti huo:

اللفظة؟ هذه له استعار وإنما له، مالءة وال مالءة له صير كيف ترى أالHuoni namna alivyoifanya (thureyya kuwa ina) kizibau wala haina kizibau, bali neno hili kaliazima tu (ni isti’aara yaani kalitumia kimajazi).226 …..

Kama vile ambavyo kwamba Abu Zaid Al-Qurashi kayataja majazi kwa uwazi katika kitabu chake Jamharatu Ash’aari Al-’Arab, na akataja ushahidi wake kwa urefu katika Qur-ani na maneno ya Waarabu ya kawaida (prose) na ya utenzi.

Na katika maelezo ya Sibawayh kaashiria majazi ya kuondoshwa (kwa neno) na mengineo, isipokuwa yeye kayaita ittisaa’an (kutoa nafasi kwa lugha ya Kiarabu). Mfano wa hayo ni kauli yake aliposema: ‘Huu ni mlango wa matumizi ya kitendo katika tamko si katika maana kwa sababu ya ittisaa’i yao katika lugha………(Na akasema kuhusu Aya isemayo)فيها كنا التي القرية لئوس ……… (Na kiulize kijiji ambacho tulikuwemo ndani yake)…(kasema Sibawayh): ‘Hakika anakusudia (waulizeni) watu wa kijiji…227

223 - Yaani anapiga sana. 224 - Al-Bayhaqi Manaqibu Al-Shafi’i j. 2, uk. 239. 225 - Kizibau cha nguo. 226 - Abu Al-Husain bin Rashiq Al-Qayrawaani Al-’Umda Fii Mahaasini Al-Shi’ir Wa Aadaabih j. 1, uk. 428, chapa Daru wa Maktaba Hilal.

90

Baada ya hayo utaona kwamba:1) Ibn Al-Qayyim na Ibn Taymiyya wamesukuma tu kuhusu suala la

kuyakataa kwao majazi kutoka kwa watu wa karne tatu za mwanzo. Na hii ni kawaida yao na wafuasi wao wote katika kila kitu wasichokijua au wasichokitaka, basi wao husema “Hakuna yoyote aliyesema” au “Al-Salafu Al-Salih wamekubaliana”.228

2) Wameshindwa kujua baina ya kuwepo kwa kitu na baina ya kuanza kwa jina lake la kitaalamu.229 Majazi yalikuwepo tangu enzi ya Mtume (s.a.w.) na kabla; na jina lake la kifani ndilo lililokuja baadae.

Sasa baada ya hayo, natutazame ushahidi wa kuwepo kwa majazi katika Qur-ani, Hadithi na lugha ya Kiarabu.

MAJAZI KATIKA QUR-ANI

Majazi kama tulivyosema ni kulitumia neno kinyume na maana yake ya asili. Tumenukuu sana huko nyuma ushahidi wa Qur-ani juu ya kuwepo kwa matumizi ya namna hio. Lakini kwa kuwa mlango huu ndio hasa nilioufanya ili kuthibitisha hilo basi hatuna budi kunukuu ushahidi japo kidogo juu ya kuwepo kwa majazi. Nitatumia neno majazi kumaanisha majazi yenyewe, kinaya, tashbihi, tawria au isti’ara: zote hapa nitazipa jina la majazi kwa kuzingatia kwamba zote zimetumika kinyume na maana yake ya asili.230

Baada ya hayo elewa ndugu msomaji mwenye kutafuta ukweli kwamba Aya nyingi za Qur-ani zina majazi lakini nachukua mifano miwili mitatu:

227 - Rejea Al-Imamu Badru Al-Khalili Jawaahiru Al-Tafsir Juz-u Khaas uk. 120-126. Bila kusahau kwamba nimeyabutua maneno yake ili kufupisha. Pia elewa kwamba Ibn Al-Qayyim na Ibn Taymiyya wana shubuhat nyengine nyingi walizozileta juu ya maudhui hii, lau tutazijadili itatubidi tufanye juzuu kamili juu ya maudhui hii. Shubuhati hizo zimejibiwa kiufundi na kwa uwazi na Sheikh Al-Khalili katika Jawaahiru Al-Tafsir Juz-u Khaas anayetaka naa arejee huko, labda tukiona kwamba kuna haja ya kukifasiri kitabu hicho tutafanya hivyo inshaa Allah ili uone kwamba hawa watu hawana hoja bali ni kubabaisha watu tu. 228 - Na hapa watu – hususan wa madhehebu za Kisuni – inawabidi wayahadhari sana maneno ya watu hawa na nukulu zao: wasije wakadanganyika na propaganda zao wanaposema “Ahlu Sunna” au “Al-Salaf” au “Umma”. Ahlu Sunna, na Al-Salaf na Umma kwao ni Ibn Batta, Al-Sijzi, Ibn Zaaghun na walio mfano wa hao. Na watu wa bidaa ni wafuasi wa madhehebu tatu za Kisuni, Ibadhi, Shia na Zaidia! 229 - Wala hawakushindwa kujua, lakini hawakutaka tu! 230 - Na hii ndio kauli ya aghlabu ya wajuzi.

91

1) Allah anasema: “ الله وجه فثم تولوا فأينما ” “Popote mutapoelekea basi kuna uso wa Mwenyezi Mungu”.231 Neno lililotumika hapa kumaanisha uso ni neno wajhu. Maana ya msingi ya wajhu – kama nilivyoliweka katika Aya – ni uso. Sasa je hii ndio maana iliokusudiwa hapa? Kama ndio basi maana itakuwa Allah ana uso, na uso huo unapatikana kila sehemu popote utapoelekea. Na hili – kama unavyoona – si kwamba litagongana na akili ya kila Muislamu tu, bali pia – litagongana na itikadi ya skuli hio ya Mawahabi na Maimamu wao kwamba Allah yuko mbinguni hali ya kuwa yuko mbali na viumbe madamu uso wake uko kila sehemu! Kwa hivyo, neno uso hapa limetumika kimajazi na maana ni kuwa popote utapoelekea basi Allah yupo232 kama alivyosema katika Aya nyengine كنتم ما أين معكم وهو (Naye yuko pamoja nanyi popote mulipo). Yaani elimu yake ipo pamoja nanyi: si kuwepo kidhati (physically). Au radhi zake utazipata kwa mujibu wa tafsiri nyengine.

2) Allah anasema: “ وجهه إال هالك شيء Kila kitu kitaangamia) ”كلisipokuwa uso wake (Allah).233 Sasa ikiwa tutalifasiri neno uso kwa maana yake ya asili au ya uhakika na tukaitakidi kuwa Allah ana viungo vyengine (miguu, mikono n.k), ikiwa tutakwenda na tafsiri za namna hii, basi Aya hii inaonesha kuwa vitu vyote hivyo vitaangamia na utaobaki ni uso wa Allah tu: miguu yake, mikono yake na sisi na vitu vyote hivyo vitaangamia! Hii ndio dhahiri ya Aya inavyosema. Lakini ikiwa tutaifasiri Aya hio kimajazi tukasema kuwa neno uso hapa maana yake ni dhati (the essence or the person of Allah), basi tafsiri haitokupa tabu kwani maana ni kuwa kila kitu kitaangamia isipokuwa Dhati ya Allah yaani isipokuwa Allah mwenyewe. Utakumbuka kwamba njia bora ya kuzifasiri Aya za Qur-ani ni kuitazama Qur-ani yenyewe, kwani Qur-ani inajifasiri yenyewe katika maneno yake, sentensi zake na siyaaq zake. Na matumizi ya neno uso kwa maana ya dhati yamekuja katika Aya nyengine za Qur-ani kama vile Aya isemayo:

حامية * * نارا تصلى ناصبة عاملة خاشعة يومئذ وجوهNyuso siku hio zitadhalilika**zikiwa zimetenda kazi nzito** zitaingia moto mkali.234

Sasa jiulize wewe je zitakazoingia motoni ni nyuso tu? Bila shaka ni watu wenyewe. Kwa hivyo, neno uso hapa ni kwa maana ya dhati yaani mtu mwenyewe mzima, na kwa hivyo haya – kama tulivyoeleza kabla – ni majazi. Halkadhalika katika Aya hio isemayo: وجهه إال هالك شيء كل231 - Sura 2, Aya 115.232 - Yaani elimu yake ipo na radhi zake zipo utazipata. 233 - Sura 28 Aya 88.234 - Sura 88 Aya 2-3-4.

92

(Kila kitu kitaangamia isipokuwa uso wake (Allah), maana yake ni kuwa kila kitu kitaangamia isipokuwa Dhati ya Mwenyezi Mungu, yaani Allah mwenyewe ndiye atayebakia, na kwa hivyo neno hilo uso limetumika katika Aya hiyo kimajazi (figuratively). Na utakumbuka – ewe msomaji mwenye kutaka haki – kwamba Waarabu hutumia neno uso kumaanisha dhati. Kama vile wanaposema وجهك (Nimeujia au nimeukusudia uso wako) قصدتyaani nimekujia au nimekukusudia wewe. Na miongoni mwa hayo ni kauli ya mshairi aliposema:

** بالفالح يأتي حمن الر إلى ناظرات بدر يوم 235وجوه

Nyuso siku ya (vita vya) Badri zilimtazamia Mwenyezi Mungu alete ushindi.236

Maana ya neno zilimtazamia lililomo katika ubeti huu ni kuwa nyuso siku hio zilimngojea na kumtarajia Allah alete ushindi. Na inaeleweka kwamba zenye kungojea si nyuso tu: bali ni nyuso na kiwiliwili chote na nyoyo na akili na fikra.

3) Allah anasema:

سبيال وأضل أعمى اآلخرة في فهو أعمى هذه في كان من

Atayekuwa kipofu katika dunia hii, basi akhera atakuwa kipofu na mwenye kupotea njia zaidi.237

Maana ya asili au ya uhakika au ya msingi ya neno kipofu ni “Asiyeona”. Lakini je hii ndio maana ya Aya hii na kwa hivyo vipofu akhera wataingia motoni!? Bila shaka neno hilo halikutumika hapo kwa maana yake hio ya asili, bali maana ni “Atayekuwa mpotovu katika dunia basi akhera atapotea zaidi”, na kwa hivyo neno hilo limetumika kimajazi (figuratively).

4) Anasema Allah: حمة من الذل جناح لهما واخفض الر

Na wainamishie (wazee wako wawili) bawa la udhalili wa huruma. 238

Jamaa! Hata huu udhalili nao una bawa? Na bawa hili lapatikana wapi?

235 - (( بالخالص (( أخرى رواية وفي236 - Sheikh Al-Khalili Alhaqu Al-Damigh uk. 46. 237 - Sura 17, Aya 72. 238 - Sura 17, Aya 24.

93

Anasema Allah:ر ربهم عند صدق قدم لهم أن آمنوا الذين وبش

Wabashirie wale walioamini kwamba wana mguu wa ukweli kwa Mola wao. 239

Jamaa! Ivo ukweli nao una mguu? Na uko wapi mguu huo?

5) Anasema Mwenyezi Mungu:

البسط كل تبسطها وال عنقك إلى مغلولة يدك تجعل وال Wala usiufanye mkono wako kuwa wenye kufungwa

kwenye shingo yako wala usiukunjue wote.240

Je neno mkono hapa ni mkono wa kweli au maana yake ni kuwa usifanye ubakhili wala usifanye israfu? Kama ni mkono kweli kweli ndio uliokusudiwa hapa, basi Waislamu tunatakiwa mikono yetu daima iwepo kati na kati tu baina ya shingo na kuikunjua yote: tusije tukaikunjua yote wala tusiikunje!

6) Anasema Allah:

م تسمع أفأنت إليك يستمعون من ومنهم ) يعقلون ال كانوا ولو الص يبصرون ال كانوا ولو العمي تهدي أفأنت إليك ينظر من ( ومنهم42

(34(

Na miongoni mwao wako wanaokusikiliza, basi wewe utawasikilizisha viziwi hata kama hawafahamu?**Na miongoni mwao wako wanaokutazama, basi wewe utawaongoza vipofu hata kama hawaoni?241

Basi tuseme kwamba vipofu na viziwi waliotajwa katika Aya hizi ni vipofu na viziwi wa kweli au ni watu waliofananishwa tu na vipofu na viziwi kwa sababu ya kutokusikiliza kwao maamrisho ya Allah na kutokuyafuata?

7) Anasema Allah:يرجعون ال فهم عمي بكم صم

Viziwi, mabubu, vipofu, kwa hivyo wao hawatorejea.242

Na anasema:239 - Sura 10, Aya 2. 240 - Sura ya 17 Aya ya 29.241 - Sura 10, Aya 42-43. 242 - Sura 2, Aya 18.

94

م الله عند الدواب شر إن يعقلون ال الذين البكم الصHakika ya viumbe waovu kabisa kwa Mwenyezi Mungu ni viziwi,

vipofu ambao hawafahamu (kwa akili zao).243

Je na haya pia si majazi? Hatuna haja ya maelezo, kwani ikiwa mtu anahitaji kusoma Sharhu Ibn ‘Aqiil ili ajue jaar na majrur basi hahitaji kusoma hata alifu inani ili ajue kwamba maneno haya hayakutumika kwa uhakika wake?

MAJAZI KATIKA HADITHI

Natoa mifano kidogo tu: mifano iko mingi mno. Allah anasema katika Hadithi Qudsi:

إزاري والعظمة ردائي الكبرياءUkuu ndio vazi langu la juu na utukufu

ndio vazi langu la chini.244

Allah anasema katika Hadithi hii Qudsi: “Ukuu ndio vazi langu la juu na utukufu ndio vazi langu la chini”. Kwa hivyo, ikiwa tutakataa kuwepo kwa majazi basi natuseme kuwa Allah anavaa nguo mbili kanzu na seruni, kanzu yake inaitwa kibriyaa (ukuu); na seruni yake inaitwa Al-‘Adhama (utukufuu au ukuu)!!!

Katika Hadithi nyengine Qudsi, Allah anasema:

يزال.... وما عليه، افترضت مما إلي أحب بشيء عبدي إلي تقرب ومابالنـــوافل إلي يتقرب عبدي

أحبه، به حتى يبصر الذي وبصره به، يسمع الذي سمعه كنت أحببته فإذاب يبطش التي ها ـــــويده

بها يمشي التي ورجله

….Na mja wangu hajikurubishi kwangu kwa kitu nikipendacho zaidi kuliko yale niliomfaradhishia. Na mja wangu anaendelea kujikurubisha kwangu kwa (kufanya) nawafil (ibada zisizo za lazima) mpaka ninampenda. Basi nikimpenda ninakuwa (Mimi Mungu ndio) sikio lake analosikia kwalo, na jicho lake analoonea na mkono wake anaoshikia na mguu wake anaoendea.245

243 - Sura 8, Aya 22. 244 - Ibn Maja Al-Sunan Hadithi na. 4174-4175.245 - Kaipokea Al-Bukhari na akainukuu Al-Imamu Al-Nawawi Riyaadhu Al-Saalihin uk. 58, Hadithi na. 95.

95

Jamani hebu nikuulizeni na nikuombeni tuweke ushabiki na umadhehebu kando japo kwa dakika tano. Ivo kweli inawezekana kukataa majazi (metaphor) na kwa hivyo kuifasiri Hadithi hii literally (neno kwa neno kama ilivyo)? Kama ni hivyo, basi Allah anasema hapa kuwa Yeye ni masikio, macho, mikono na miguu ya mawalii wake, kwa hivyo viungo vya mawalii ndio Mungu mwenyewe au ndio sehemu za Mungu! Bila shaka maana hio haiingi akilini – huhitaji kuwa mwanachuoni; na maana inayofahamika kiakili ni kuwa mawalii wanasikiliza yanayomridhisha Allah, na kwa hivyo Allah kajiita Yeye mwenyewe kuwa ndio masikio yao; wanatazama, wanashika na wanayaendea yanayomridhisha Allah. Kwa hivyo, sikio la Allah, jicho lake, mkono wake na miguu yake iliotajwa katika Hadithi hii ni majazi (metaphor) na maana yake ni kama tulivyoeleza.

Lakini nilipojadiliana na baadhi ya ndugu zetu, mmoja wao aliniambia kwamba hili liko wazi katika Hadithi hio. Baadae – baada ya kupekuwa – nikamkuta Sheikh Al-Khalili akiwanukuu baadhi ya wanavyuoni wao wakisema hivyo hivyo. Kisha Sheikh Al-Khalili akajibu kwamba hilo si sahihi kwani maneno: mkono, miguu, macho na masikio, yote haya yana maana zake za uhakika wa kilugha ambao yanapotajwa tu maneno hayo mtu haufahamu isipokuwa uhakika huo. Unapotaja mguu, kwa mfano, mtu hakufahamu isipokuwa kwamba umekusudia kiungo maalumu ambacho tunakijua sote. Na kwa hivyo, ikiwa uhakika wa viungo hivyo wa kilugha sio uliokusudiwa katika Hadithi hio basi ni wazi kwamba maneno hayo yametumika kimajazi – yametumika kinyume na maana yake ya asili.

Hadithi nyengine inasema:

: رب وأنت أعودك كيف رب يا قال تعدني فلم مرضت آدم ابن يا : عل أما قال أن ــالعالمين؟ مت

....... عنده لوجدتني عدته لو أنك علمت أما تعده؟ فلم مرض فالنا عبدي

Ewe Binaadamu we! Mimi niliumwa basi wewe hukuja kunijuia!246 Atasema (binaadamu): ‘ewe Mola wangu! Vipi nije kukujuia nawe ni Bwana wa ulimwengu? Atasema (Allah) kwani hujui kwamba mja wangu fulani kaumwa wewe hukwenda kumjuia? Hujui kwamba lau ulikwenda kumjuia basi ungelinikuta mbele yake..247

Hadithi hii bila shaka lau haitofasiriwa kwa misingi ya kimajazi basi itakuwa ni mushkeli mkubwa na yatakuwa maneno ya Kisharia

246 - Kunijuia ni Kipemba, Kiunguja kunijulia, sijui Kitanga wanasemaje, lakini maana yake ni kwenda kumtazama mgojwa. 247 - Muslim Al-Sahih Hadithi na. 2569.

96

yanagongana ambapo sehemu moja inathibitisha kitu na ya pili inakikanusha kitu hicho hicho. Tazama maneno: “Mimi niliumwa basi wewe hukuja kunijuia” je maneno haya inawezekana kuyanasibisha na Mwenyezi Mungu kwa udhahiri wake? Je inawezekana kusema kuwa Allah anaumwa lakini kuumwa kwake si kama kuumwa kwetu? Sasa tazama ukweli kwamba Allah mwenyewe kayafasiri maneno hayo akasema:

Kwani hujui kwamba mja wangu fulani kaumwa wewe hukwenda kumjuia? Hujui kwamba lau ulikwenda kumjuia yeye basi ungelinikuta mbele yake.

Jambo hili linabainisha kwamba kuumwa kulikotajwa mwanzo si hakika bali ni majazi, na kuumwa kwa pili – kuumwa kwa mja – ndio hakika. Vyenginevyo, ukiwa utakataa majazi basi itakubidi useme:

1) Hadithi hii inajigonga. 2) Au Allah anaumwa kweli.3) Tukienda kumtazama mgonjwa tutamkuta Allah yupo mbele yake,

na hili halijawahi kutokea. Sijui labda wale wenye kukataa majazi – akina Kasim Mafuta na wenzake – wao wakenda kuwatazama wagonjwa humkuta Mungu huko, na kwa hivyo kauli yao ya kuwa Mungu haonekani hapa duniani huko inakuwa haitendi kazi!

4) Kwa hivyo, kukataa majazi kunaifanya riwaya hii iwe na mgongano au tuwe na itikadi ya tashbihi ilio wazi bali tuwe na itikadi ambayo haikubaliani na matokeo yalivyo.

Hadithi nyengine inasema:تقربت ذراعا إلي تقرب وإذا ذراعا، إليه تقربت شبرا إلي العبد تقرب إذا

أتاني وإذا باعا، إليههرولة أتيته يمشي

Mja wangu akijikurubisha kwangu shubiri moja basi Mimi najikurubisha kwake dhiraa nzima; na akijikurubisha kwangu dhiraa moja, basi Mimi najikurubisha kwake pima nzima; na anayenijia naye anakwenda (mwendo wa kawaida), basi Mimi namjia hali ya kuwa nakwenda mbio (natroti).248

Katika jambo lenye kuonesha kuwa Mawahabi wanasoma lakini hawafahamu ni kusema kwao kwamba har-wala (mwendo wa mbio au kutroti) ni katika sifa za Mwenyezi Mungu wakitegemea Hadithi hii! Hii inaonesha kuwa hawa watu Allah hakuwapa fahamu hata kidogo hata wakihifadhi maelfu ya Hadithi. Tazama qarina za Hadithi hii halafu jiulize

248 - Kaipokea Al-Bukhari na akainukuu Al-Imamu Al-Nawawi Riyaadhu Al-Saalihin uk. 58, Hadithi na. 96.

97

je kweli uliokusudiwa hapo ni mwendo wa kweli? Tazama nukta mbili zifuatazo:

1) Mja – kwa mujibu wa dhahiri ya Hadithi hii – anakwenda kwa

miguu huko aliko Allah. Jamani! Wapi tumepata kusikia kuwa kuna mtu anakwenda kwa miguu kumfuata Allah huko aliko? Bila shaka maana ni kuwa anayefanya wema kidogo kwa ajili ya Allah, Allah anamlipa mengi kuliko ule wema wake.

2) Allah anakuja mbio mbio kwa mja! Wapi tumepata kusikia kwamba kuna mja kajiwa na Allah miongoni mwa Manabii, Masahaba au Mawalii wakubwa, na wote hawa ndio walio mstari wa mbele katika uchaji?

Kwa hivyo, ni wazi kwamba lafdhi zote hizi ni majazi; wala huwezi kuifasiri Hadithi hio katika uhakika wake kwani uhakika wake haukubaliani na akili wala haukubaliani na matokeo yalivyo.

Hadithi nyengine inasema:

: : الدهر وأنا الدهر وأنا وادهراه يقول آدم ابن يشتمني وجل عز الله قال

Kasema Allah Mtukufu (katika Hadithi Qudsi): ‘Binaadamu ananitukana, anasema: ‘E dahari weee! Na Mimi (Mungu) ndio dahari; na Mimi (Mungu) ndio dahari.249

Na lafdhi nyengine ya Hadithi hii ni:

والنهار الليل بيدي الدهر وأنا الدهر آدم ابن يسب

Binaadamu anatukana dahari, na Mimi (Allah) ndio dahari yenyewe; mikononi kwangu kuna usiku na mchana.250

Kwa hivyo, kwa wale wanaokataa majazi basi wasipate tabu ya kumjua Mola wao: Mola wao ni hizi zama (dahari) kama Hadithi inavyosema. Na kwa sababu msingi ni kuwa:

Tunakithibitisha kile ambacho Allah na Mtume wake wamekithibitisha na kukikanusha kile walichokikanusha, bila ya kukiletea ta-awil (kukiletea tafsiri ya ndani) wala tahrif (kukipotoa) wala tashbih (kukifananisha),

249 - Ibn Abi ‘Aasim Sunna j. 1, uk. 410, Hadithi na. 611. 250 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 7491. Muslim Al-Sahih Hadithi na. 2246. Lafdhi ni ya Muslim.

98

basi maana na iwe:1) Allah ni dahari.2) Lakini yeye ni dahari si kama dahari.

Lakini kifungu nambari mbili kitabomolewa na ukweli kwamba Allah kawalaumu watu hao kwa kuitukana dahari na kwamba Yeye ndio dahari, na bila shaka dahari wanayoitukana watu hao ni hii tunayoijua ya mabadiliko ya usiku na mchana: si: “dahari lakini si kwa namna tunayoijua”. Kwa hivyo, natija ya kukataa majazi ni kuwa mabadiliko ya usiku na mchana (dahari) ndio Mungu mwenyewe! Huu ni ujuha wa mwisho duniani?

Anasema Mtume (s.a.w.):

السيوف ظالل تحت الجنةPepo iko chini ya vivuli vya panga.251

Tazama ewe mwenye akili timamu! Je utaichukua Hadithi hii literally (neno kwa neno) au utaifasiri kwamba anayetaka pepo basi akapigane jihadi? Vyenginevyo basi natusema kuwa pepo ziko kwenye vivuli vya panga: tuziweke panga zetu kwenye jua na zikitoa kivuli basi hapo ndipo kwenye pepo!

Anasema Mtume (s.a.w.):

عاتقه عن عصاه يضع فال جهم أبو ا .......أمAma Abu Jahm ni mtu ambaye mkwaju hauondoi begani kwake.252

Yaani anapiga sana. Au utakataa majazi uniambie kuwa maana yake ni kuwa Abu Jahm alikuwa akitembea na bakora begani kila wakati: haiweki chini.

Bali Hadithi inasema kwamba Allah ana wembe mkali zaidi kuliko wa baba yake Abu Al-Ahwas kama alivyosimulia Al-Bayhaqi katika kitabu Al-Asmaau Wa Al-Sifaat.253

MAJAZI KATIKA LUGHA YA KIARABU

251 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 2818. Muslim Al-Sahih Hadithi na. 1902. 252 - Muslim Al-Sahih Hadithi na. 1480. 253 - J. 2, uk. 176, Hadithi na. 742.

99

Mashairi ya Waarabu na maneno yao ya kawaida (prose) yamejaa majazi kama vile ambavyo sisi Waswahili lugha yetu imejaa majazi pia. Waswahili huwa tunasema:

1) “Yakhe kijana yule ana mkono mkono”! Yaani ni mwizi.2) “Yakhe yule ana ulimi mrefu au ana mdomo sana”! Yaani ana

maneno mengi au mtukanaji.3) “Yakhe mguu huu ni wako”! Yaani nimekujia wewe. Lakini

inaonekana lau Sharia yetu ilikuwa kwa lugha ya Kiswahili na Sheikh Kasim Mafuta akawa ndiye Kadhi, basi angelitukata miguu na mikono sote kwa ufahamu wake wa lugha. Kwa sababu ungelimwambia “Sheikh huu ni mguu wako” yeye angechukua panga akaukata akauchukua mwenyewe!

4) “Yakhe nakupa mkono”! Yaani nakusapoti: nakubaliana na wewe au nakupongeza

5) “Aaa! Mimi sitii mkono wangu”! Yaani mimi sijitii katika jambo hilo: sijihusishi.

6) “Ama yakhe saa zenda”! Au “Siku zenda”! Na bila shaka saa na siku haziendi, bali zinapita.

7) “Biashara inakwenda vizuri”! Yaani bidhaa zinauzwa kwa wingi, vyenginevyo biashara haiendi.

8) “Yakhe Omari kazi kaiwekea mguu”! Yaani kaizuia. 9) “Aaa Bwana usiniangushe wee”! Yaani usinikoseshe yale

niyatakayo.10) “Omari kamvunjia fulani nyumba”. Hii haina maana kwamba Omari

alichukua mtaimbo akaenda kubomowa matufali ya nyumba ya fulani, bali haya ni majazi ya kinaya cha Kiswahili na maana yake ni kuwa “Omari anafanya machafu na mke wa fulani”. Mke katika Kiswahili kaitwa nyumba kwani nyumba inaimarika kwa kuwepo yeye, na akihama mke mara nyumba huanguka254 kwa kukosa kushughulikiwa.

11) “Mazoea kilema”. Ilhali mazoea si kilema cha kweli.12) “Mtu kidole”. Ilhali mtu si kidole.13) Siisahau kauli ya mwalimu wangu wa chuo nilipomsikia akisema

maneno yenye maana kwamba: “Naona juu kushagogwa”.! Hiki ni Kipemba. Kiunguja na kistandard ni: “Naona juu kumenuna”. Lakini mtu huyo aliposema juu kushagogwa anakusudia: “Mawingu yametanda”.

Hio ni baadhi ya mifano ya balagha ya Kiswahili. Sasa kama umeyaelewa hayo, basi elewa kwamba lugha ya Kiarabu ni tajiri zaidi katika balagha ya

254 - Hasa ikiwa ni ya makuti au nyasi.

100

namna hio. Lakini wale ambao wanadhania kuwa kujua balagha ni kujua yale maneno ya kifani technical terms tu yaliyowekwa na wanavyuoni ili kurahisisha darsa zao, basi siku zote huwa wanataabika katika kuyafasiri maneno ya Allah na Mtume wake. Ndugu wasomaji! Kujua balagha sio kujua Hazl (mzaha) au tauria (kugubuka) au maneno mengine ya kifani, bali kujua balagha ni kuweza kujua maana halisi ya maandiko kwa misingi ya lugha ilivyo, yaani kuweza kujua Allah – katika Aya kadha – na Mtume (s.a.w.) katika Hadithi kadha – wanakusudia nini: sio wametamka nini tu. Vyenginevyo hizi istilaahat zote za balagha, Masahaba hawakuwahi kuzijua, ilhali wao ndio wajuzi wao wa lugha ya Kiarabu.

Baada ya hayo, sasa tazama mifano miwili mitatu ya balagha ya Kiarabu. Anasema Mshairi wa kiarabu:

** أعددها وال منها أعد سابغة علي أياد لهAna mikono (mingi) imenienea juu yangu**Naihisabu

lakini siwezi kuihisabu (kwa wingi).255

Jiulize wewe je huyu mtu alikuwa na mikono mingapi mpaka ikafika hadi kuwa mtu hawezi kuihisabu. Bila shaka mshairi anakusudia kusema kwamba takrima na ataya alizopewa ni nyingi na kwa kuwa mkono ndio unaotoa ataya hizo basi ataya zimepewa jina la mkono.

Anasema mshairi:

*** إليه العباد رب محصيه لست ذنبا الله والعمل الوجهأستغفر

Ninamuomba Allah msamaha kwa dhambi nisizozihesabu***Bwana wa waja kwake yeye unakwenda USO na matendo.

Bila shaka neno uso hapa halikukusudiwa uso-kiungo, bali maana ni القصد (makusudio), yaani ikhlas.

Anasema mshairi:

** غائظة ألعدائها وأخرى يرتجى خيرها يد يداك

Mikono yako miwili; mkono mmoja kheri yake inatarajiwa; na mkono wa pili una hasira kwa maadui wake.

255 - Katika kitabu Dawaawiinu Al-Shi’iri Al-‘Arabi j. 47, uk. 227, ubeti huo umeandikwa:سابقة إلي أياد أعددها ** له وال منها أعد

Ana mikono imenitangulia** Naihisabu lakini siwezi kuihisabu (kwa wingi).

101

Tazama jinsi Waarabu wanavyoitumia lugha yao! Maneno haya lau yalikuja katika Qur-ani au Hadithi basi Mawahabi wangelishindwa kuyafahamu, na wangelisema: “Allah ana mikono miwili; mkono wake mmoja unatoa kheri; wa pili una hasira kwa maadui wa Allah”. Ilhali inaeleweka hapa kwamba mkono-kiungo si makusudio ya maneno hayo kamwe, vyenginevyo asingelisema kwamba una hasira, kwani mkono-kiungo hauna hasira.

Anasema Al-Imamu ‘Ali bin Abi Talib (k.w.):

** والرسوم المعالم ستخبرك تقضت أمم عن األيام سلZiulize siku kuhusu umma zilizoangamia**Alama na

mabaki yatakupa habari256

Sayyidna ‘Ali (r.a.) anatwambia tuziulize siku, sasa je siku kweli zinaulizwa? Kisha anatwambia kwamba alama na mabaki ya umma zilizopita zitatoa habari. Je haya ni kweli ikiwa tutayafasiri maneno hayo kama yalivyo: ni kweli alama zinasema?

Anasema Al-Imamu Al-Shafi:

** القضاء حكم إذا نفسا وطب تشاء ما تفعل األيام دعZiache siku zifanye zitakayo**Na poa moyo

wakati qadhaa257 itapohukumu.258

Sasa je ni kweli siku zinafanya kitu? Siku ni mapinduko ya nyakati: usiku na mchana na anayekadiria matokeo mema na mabaya ni Allah: si siku. Lakini pamoja na hayo, Al-Imamu Al-Shafi anatwambia kwamba tuziwache siku zifanye zitakayo. Haya ndio yale wataalamu wanayoita al-majazu al-’aqliy (majazi ya akili). Kama kusema “dawa hii imeniponesha” ilhali Allah ndiye aliyekuponyesha na dawa ni sababu tu.

Sina haja ya kurefusha kwa vile ushahidi mwengine mwingi nimeunukuu hapa na pale. Kwa haya machache inakubainikia ukweli kwamba majazi yapo katika Qur-ani, Sunna na lugha ya Kiarabu bali katika lugha za binaadamu wote, na wala hayakanushi majazi isipokuwa mtu asiyekuwa na fahamu hata kidogo au mwenye fahamu yake lakini anafanya kibri dhidi ya ukweli. Na kilicho wazi kabisa – kama yanavyofahamika maneno ya Sh. Kasim mwenyewe – ni kuwa wanaokataa kuwepo kwa majazi wanayakataa 256 - Diwan Al-Imami ‘Ali uk. 99, mashairi nambari 154. 257 - Maamuzi ya Allah. 258 - Al-Imamu Al-Shafi Diwaan Al-Shafi uk. 18.

102

kwa kuhofia kuanguka kwa itikadi yao batili ya mungu-mtu (man-god or god-incarnate).

MAWAHABI HAWAJUI WAKISEMACHO!

Anasema Sheikh Al-Khalili:

Na miongoni mwa ajabu nilioisikia ni kwamba mimi nilikuwa katika hiwaar (discussion au mjadala) pamoja na mmoja wa Hashwiyya wenye kukanusha majazi, basi ikawa miongoni mwa alioyasema ni kuwa: ‘Ni dalili gani iliosema kwa uwazi kwamba (neno) hili ni hakika na hili ni majazi katika Qur-ani au Sunna au yale yaliopokewa kutoka kwa Salaf wa Umma miongoni mwa Masahaba na wafuasi wao? Nami nikamwambia: ‘Ni dalili gani iliosema kwa uwazi ikaielezea dalili ya kisharia kwamba ni Aam‘ عام (ya ujumla) na nyengine kuwa ni ?Khaas (mahususi) خاص Akasema: ‘Kwa kuwa imepokewa kauli ya Mtume (s.a.w.) akisema kwamba: ‘Sisi Manabii haturithiwi’259 pamoja na kwamba Allah kasema (katika Qur-ani): األنثيين حظ مثل للذكر أوالدكم في الله يوصيكم (Allah anakuusieni kuhusu watoto wenu mwanamme (katika kurithi) apate sawa na fungu la wanawake wawili),260 tukajua kwamba Hadithi hio imeuhusisha ujumla uliomo katika Aya hii; basi tukajua kwamba andiko khaas (specific au exceptional) linabomoa andiko Aam‘ عام (la ujumla)’.

Na nimestaajabishwa na ufinyu wa upeo wa watu hawa na kufinyika kwa akili zao na kupooza kwa fahamu zao,261 kwa sababu suali lilikuwa ni kuhusu kuwepo kwa nassu (andiko linalotamka kwa uwazi) kwamba hii ni Khaas (mahususi au specific au خاص Aam (ya ujumla) na hii ni‘ عامexceptional): wala halikuwa suali kuhusiana na kuwepo kwa عموم (ujumla) na kuwepo خصوص (uhusishaji) kama vile alivyonilazimisha mimi nimletee nassu (andiko la wazi lenye kusema) kwamba haya ni majazi na hii ni hakika…….262

Basi hivyo unavyoona akili ya mtu huyo aliyejadiliana na Sheikh Al-Khalili, ndivyo zilivyo akili za watu hao hata Maimamu wao wakubwa.263 Wallahi

259 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 4036. Muslim Al-Sahih Hadithi na. (49) 1757-(51) 1758. 260 - Sura 4, Aya 11. 261 - Msemaji ni Sheikh Al-Khalili. 262 - Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Jawaahiru Al-Tafsir Juz-u Khaas uk. 111-112. Kisha baada ya hapa Sheikh akanukuu Aya zenye kuonesha kuwepo kwa majazi katika Qur-ani. 263 - Siisahau kauli ya kijana mmoja alieniambia: “Wale ni watu wa kuombewa dua, kwani si watu wa akili na fahamu”.

103

ukisoma kitabu Al-Raddu ‘Alaa Bishr Al-Marisi cha ‘Uthman Al-Darimi ambacho Ibn Taymiyya kakiusia sana, basi utastaajabishwa sana na ‘aqliyya (mentality au fikra) ya kiumbe huyu pamoja na kuwa kahifadhi maelfu ya Hadithi? Bishr Al-Marisi anasema vyengine; yeye anamjibu vyengine!

Sasa baada ya hayo, tazama vichekesho vyengine vyenye kuliza, navyo ni vichekesho vya kujigonga kwa Ibn Al-Qayyim mwenye kukanusha/kuthibitisha majazi للمجاز المثبت .النافي

KUJIGONGA KWA IBN AL-QAYYIMKUYATUMIA KWAKE MAJAZI

Sasa baada ya hayo – ukipenda kucheka au kulia – tazama maajabu ya Ibn Al-Qayyim! Ibn Al-Qayyim pamoja na kuwa kakanusha majazi kwa kututungia kitabu kilichochukua sehemu kubwa juu ya kulielezea suala hilo, lakini yeye na wengine wengi hawakuacha kuyatumia majazi, bali na wakati mwengine kuyataja kwa jina. Tazama ukweli kwamba Ibn Al-Qayyim, kitabu chake ambacho ndani yake anakataa majazi, kakiita Al-Sawaai’qu Al-Mursala (Mapigo ya radi yalioachiwa)! Sasa jamani! Kitabu ni radi, au yaliomo ndani ya kitabu ni radi za kweli? Na akakiita kitabu chake chengine Madaariju Al-Saalikin (Njia za wenye kushika njia au wenye kupita). Na namna hivyo unawakuta katika vitabu vyao mbali mbali wanatumia ibara za kimajazi. Tazama maneno ya Ibn Al-Qayyim kuhusu dunia; anasema:

... عذبتهم بعد سمها كؤوس سقتهم شراب أمر وأذاقتهم العذاب بأنواع بحبها..... فسكروا خمرها وسكؤ

….(Dunia)..imewaadhibu kila namna; na ikawaonjesha kinywaji kichungu chao; imewanywesha gilasi za sumu yake baada ya gilasi za pombe yake, basi wakalewa kwa kuipenda (hio dunia)!264

Sasa hebu tujiulize je Ibn Al-Qayyim kayakusudia maneno haya katika maana yake ya uhakika kwamba dunia inawanywesha watu sumu na pombe na kinywaji kibaya chao na watu wakalewa kweli kweli kwa sababu ya kuipenda! Na vipi mtu analewa kweli kweli kwa kupenda!

Na kabla ya hapo, Ibn Al-Qayyim kasema:

والروح القلب بعين أدرك الذي فذلك

264 - Ibn Al-Qayyim Madariju Al-Saalikin 3, uk. 190-191.

104

Hayo ndio aliyoyadiriki kwa jicho la moyo na roho.265

Sasa moyo una jicho la kweli; roho ina jicho la kweli? Au ni uoni kwa maana ya basira (uoni wa moyo) si kwa maana ya basar (uoni wa jicho)? Namna hivi utaona mtu huyu anavyojigonga mwenyewe.

Na katika Nuniyya yake, Ibn Al-Qayyim anafungua kitabu chake kwa kusema:

** يدان ذاك بفسخ للصدود ما األركان ثابت المحبة حكم

Hukumu ya mapenzi, nguzo zake ni imara**Upingaji266

hauna mikono miwili ya kubomoa hilo.267

Anasema mshereheshaji: Na mikono miwili ni uwili wa (neno) mkono, kwa maana ya uwezo.268 Sasa vipi tena Ibn Al-Qayyim anapinga majazi? Huku si kujigonga ambako kunaonesha kwamba hana hoja sahihi, bali anakimbia kuanguka kwa itikadi yake ya mungu mtu?

KUKARIBIA KWAKE KUYATAJA MAJAZI

Ama kuyataja kwake majazi kwa kuyaashiria kulikokaribia kuyataja kwa uwazi ni kama alivyosema Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Al-Mufassir. Anasema:

Na Ibn Al-Qayyim kayabomoa mwenyewe yale alioyajenga hapa ya kukanusha majazi, kwa kuyakiri kwake majazi bila ya kujua wakati alipoifasiri Hadithi isemayo: “ لسانه عني Ukateni ulimi) ”اقطعواwake kutokana na mimi), kwamba makusudio yake ni kumnyamazisha yule mwenye kusifu kwa kumpa tunza ili iikate ulimi wa maneno yake. Na akaifasiri Hadithi (ya Mtume s.a.w.) isemayo: من سيف خالدا إن

الله ,(Hakika ya Khalid ni upanga katika panga za Allah) سيوفkwamba maana yake ni kuwa anawaua washirikina kama upanga

265 - Ibn Al-Qayyim Madariju Al-Saalikin 3, uk. 190. 266 - Maana ya neno kwa neno ni “uzuiaji”, lakini ufasaha wa Kiswahili ni kusema “upingaji”. 267 - Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 1, uk. 16. 268 - Muhammad Khalil Harras Sha-hu Al-Nuniyya j. 1, uk. 16.

105

usio na ala (ghala) ambao hauhitaji kuchoolewa; na Hadithi inayosema kwamba Hamza ni ورسوله الله أسد من simba) أسدkatika simba wa Allah na Mtume wake), kwamba maana ni kuwa Hamza anawawinda maadui wa Allah.269

KUYATAJA KWAKE MAJAZI KWA JINA LAKE LA KIFANI

Baada ya kuona jinsi Ibn Al-Qayyim alivyoyatumia majazi, sasa tazama jinsi Ibn Al-Qayyim huyo huyo anavyoyataja majazi kwa uwazi. Anasema:

الظاهر في يدخل وإنما المنصوص في يدخل ال والتأويل المجازالمحتمل

Majazi na ta-awil hayaingii katika maandiko ya wazi, bali yanaingia katika maandiko dhahir yenye uwezekano (huu na ule).270

Anaendelea Ibn Al-Qayyim:

: .... ألفاظ أكثر قيل الفعل في الضمير استتار معنى ما قيل فإنوا والتشبيه االستعارة على محمول تسامح....لالنحاة

Ikiwa itasemwa nini faida ya kujificha kwa dhamiri (pronoun) katika kitendo?….Basi jawabu ni kuwa asilimia kubwa ya lafdhi za watu wa nahau zinafasiriwa kwa njia ya isti’ara (majazi) na tashbihi na tasamuh.271

Anaendelea Ibn Al-Qayyim:

على واستدالله معا، والمجاز الحقيقة إرادة يمتنع ال أنه على قوله أما : بقولهم أحد “ذلك القلم

مثنى اسم اللسانين ألن فيه حجة فال مقـــام اللسانين، قائم فهوبأحدهما أريد باسمين النــــطق

مجاز وباآلخر الحقيقة

Ama kauli yake (aliposema) kwamba hakuna pingamizi katika kukusudia (matumizi ya) hakika na majazi kwa pamoja (katika neno moja) na kutoa kwake ushahidi kwa msemo wao unaosema: ‘Kalamu ni moja ya ndimi

269 - Na Hadithi nyengine nyingi zenye majazi ambazo Ibn Al-Qayyim kayatoa maneno yake katika maana ya asili na kuyapeleka katika maana hizo za kimajazi. Tazama maelezo hayo katika Jawaahiru Al-Tafsir Juz-u Khaas uk. 288-289. Na maneno ya Ibn Al-Qayyim mwenye kujigonga utayapata katika Mukhtasar Al-Sawaa’iqi Al-Mursala uk. 272-273. 270 - Ibn Al-Qayyim Badaai’u Al-Fawaaid j. 1, uk. 19. 271 - Ibn Al-Qayyim Badaai’u Al-Fawaaid j. 1, uk. 111.

106

mbili’, hakuna hoja ndani yake kwani neno lissanain (ndimi mbili) ni uwili, kwa hivyo limechukua nafasi ya kuyatamka majina mawili, moja lao limekusudiwa uhakika (wake) na jengine ni majazi. 272

Anasema Ibn Al-Qayyim:

فاألوقات الحقيقة في وأما مجازا المعاني بهذه توصف قد األوقات ألنالفلك فإذا........ هي

جعتها وإذا الزمان، مرور من ألنها حقيقة فاللفظ ظرفا، المرة جعلتمجاز فاللفظ مصدرا

Kwani nyakati huenda zikasifiwa kwa maana hizi kimajazi ama katika uhakika nyakati ni falaki……………………Ikiwa (neno) marra utalijaalia kuwa ni dharfu basi tamko hilo litakuwa ni hakika, kwani linatokana na neno mururi azzamaan (kupita kwa zama); na ukilijaalia kuwa ni masdar (chimbuko) basi tamko hilo litakuwa ni majazi. 273

Anasema Ibn Al-Qayyim:

في له ومثبتا علـيه داال اللــفظ جـــعل ما باللفظ يقصد إنما فالمـــعرضيخرج لم فهو الجملة،

الكالم، حدود عن والمجاز بتعريضه حقيقة فيه الكالم فإن

Mwenye kuashiria,274 kwa hakika anakusudia kwa tamko lake kitu ambacho andiko hilo linakimaanisha (kimo ndani ya lafdhi hio) na ambacho kwa ujumla linakithibitisha, kwa hivyo yeye – kwa kuashiria kwake huko huwa hajatoka katika mipaka ya maneno, kwani maneno ndani yake kuna uhakika na majazi. 275

Anaendelea Ibn Al-Qayyim:

272 - Ibn Al-Qayyim Badaai’u Al-Fawaaid j. 3, uk. 59. 273 - Ibn Al-Qayyim Badaai’u Al-Fawaaid j. 2, uk. 286. 274 - Maana ya kuashiria huku ni kama mtu kusema maneno kadha na maneno hayo yakawa yana maana mbili: maana ya mbali na maana ya karibu. Mwenye kusikiliza akaifahamu ile maana ya karibu. Na lengo ni kujiepusha na shari ya mtu. Na kwa hivyo, ikapokewa riwaya ikisema kwamba: الكذب عن لمندوحة المعاريض في Hakika kuashiria kunampa) إنmtu nafasi asiingie katika uwongo). Mfano wake ni kama watu wanayemtafuta mke wa fulani ili wamdhuru wakakutana naye wakamuuliza: ‘huyu ni nani?’ Akawajibu: “huyu ni ndugu yangu”. Wao wakafahamu ni ndugu yake katika nasaba, na hio ndio maana ya karibu, kumbe yeye anakusudia kuwa ni ndugu yake katika dini – Muislamu mwenzako, na hii ndio maana ya mbali nayo ndio ulioikusudia. Kwa hali hii, anakuwa hakusema uwongo na kajiepusha na shari zao. 275 - Ibn Al-Qayyim Ighaathatul Lahafaan uk. 413, chapa Al-Maktaba Al-Tawfiqiyya, tahqiq: ‘Abdul-Hakim Muhammad ‘Abdil-Hakim.

107

لك مسلمين سمنا أي التسمية بمعنى مجاز الله إلى الجعل هذا ونسبةج أي ــــــــوكلذلك أئمة علناهم

الحقيقة فمنهم وضالل رشد أئمة أنفسهم جعلوا وهم كذلك سميناهمالمجاز ومنه

Na kulinasibisha (neno) jaala kwa Mwenyezi Mungu ni majazi kwa maana ya kuita jina (na maana yake ni) ‘tuite sisi kuwa ni wenye kujisalimisha kwako’; halkadhalika (Aya isemayo) “Na tukawajaalia (tukawafanya) kuwa Maimamu”276 yaani tuliwaita hivyo, nao wakajifanya wenyewe kuwa ni Maimamu wa uongofu na upotufu, basi kutoka kwao ni hakika na kutoka kwake (Allah) ni majazi.277

Anaendelea Ibn Al-Qayyim, akinukuu maneno ya Sheikh wake Ibn Taymiyya:

معنى..... به فيعني معناه في ظاهرا اللفظ كون التوهم سبب يكون أوينـــوي بأن باطنا يحتملهحقيقته دون اللفظ .....مجاز

Au iwe sababu ya kukosea ni kuwa tamko ni dhahiri katika maana yake, yeye akusudie maana (yake nyengine) ambayo inawezekana kuwemo katika undani wake kwa maana kwamba akusudie majazi pasina hakika.278

Anasema Ibn Al-Qayyim:

األكثرين: عند مجازا فقط اثنين في استعماله يصح الجمع اسم أن الثاني..... بعضهم عند وحقيقة

Pili: ni kwamba jina la wingi (plural) linafaa kulitumia kwa wawili (lakini) kimajazi tu kwa mujibu wa (wanavyuoni) walio wengi, (na inafaa kulitumia hivyo) kwa hakika kwa mujibu wa baadhi yao.279

Anasema Ibn Al-Qayyim:

: إال الثالث، وبعض اثنين في الجمع استعمال صح وإن أنه الثاني الجوابوالحقيقة مجاز، أنه

ومجازه، حقيقته بين اللفظ دار وإذا اللفظ، وفق على المعنى يكون أنبه أولى فالحقيقة

276 - Sura 21, Aya 73. 277 - Ibn Al-Qayyim Shifaau Al-’Alil uk. 100. Nayo ni maneno ya Ibn Taymiyya katika Kitabu Iqaamati Al-Dalil j. 1, uk. 145.278 - Ibn Al-Qayyim I’ilaamu Al-Muwaqqi’iin j. 3, uk. 246. Ibn Al-Qayyim kaanza maneno haya kwa kusema: عنه الله رضي شيخنا Kasema Sheikh) قال wetu Allah amuwie radhi), kwa dhahir haya katika nukulu hii ni maneno ya Ibn Taymiyya; yeye anayanukuu tu. 279 - Ibn Al-Qayyim Zaadu Al-Ma’aadi j. 5, uk. 475.

108

Jawabu ya pili: ni kuwa hata kama ni sahihi kutumia wingi katika vitu viwili na sehemu ya kitu cha tatu, lakini hayo ni majazi; ama hakika ni kuwa maana iende kwa mujibu wa tamko; na tamko ikiwa lipo baina ya uhakika wake na majazi yake basi uhakika ndio uliobora zaidi (kuzingatiwa).280

IBN TAYMIYYA NA MAJAZI

Kama ulivyoona kwamba Ibn Al-Qayyim kakanusha majazi kisha akageuka na kuyatumia bali na akayataja kwa jina. Pia tumeona katika nukulu moja ya Ibn Al-Qayyim aliomnukuu Sheikh wake, Ibn Taymiyya, kwamba naye – katika nukulu hio – kayathibitisha majazi. Sasa tazama maneno mengine ya mwalimu mkuu, Ibn Taymiyya, ambaye pia alikuwa mstari wa mbele katika kuyakanusha majazi. Anasema:

بالخلق يليق الذي المعنى على الظاهر أطلق من خطأ لك يبين أن ،والذي : أحدهما نوعان األلفاظ

أسد قيل إذا فهذا والكلب والبحر والحمار األسد كلفظ مفرد معناه مارسوله وأسد ق ،الله يلــــــأو

قيل أو بحر الخيل من الجواد أو السخي أو للعالم قيل أو حمار للبليدث مجاز فهذا كلب إن ـلألسد م

المراد تبين قرينة به لفرس كقرنت وسلم عليه الله صلى النبي ،قول : طلحة وج ))أبي دناه ـــــإن

على ))وقوله: ، ((لبحرا الله سله الله سيوف من سيف خالدا إنلعثم . ((المشركين ان: ــوقوله

قميصا )) قمصك الله : ((إن في الله يمين األسود الحجر عباس ابن وقولاستل , فمن مه ـاألرض

ربه بايع فكأنما ..…وصافحه

Na chenye kukubainishia kosa la wale wenye kuitumia maana ya dhahiri pasina kuifungamanisha na kitu kwa mujibu wa maana yenye kuwiyana na viumbe, ni kwamba matamshi yako ya aina mbili: Moja yao ni tamko ambalo lina maana pweke (halikuunganishwa na tamko jengine) kama vile tamko: simba, punda, bahari, mbwa. (Tamko la namna) hii pindipo itasemwa: ‘Huyu ni simba wa Allah na Mtume wake’, au ‘akaitwa mtu mwenye fahamu nzito kuwa ni punda’, au ‘mwanachuoni au mkarimu au farasi mwenye mwendo akaitwa kuwa ni bahari’ au ‘simba akaitwa mbwa’ basi haya ni majazi. Kisha ikiwa hayo yataambatana na qarina yenye kubainisha nini makusudio yake kama vile kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema kuhusu farasi wa Abi Talha: ‘Kwa hakika sisi tumemuona kuwa ni bahari’ na kauli yake ‘Hakika Khalid ni upanga katika panga za Allah;

280 - Ibn Al-Qayyim Zaadu Al-Ma’aadi j. 5, uk. 476.

109

kauchooa dhidi ya makafiri” na kauli yake kwa ‘Uthman: ‘Hakika ya Allah kakuvisha kanzu’ na kauli ya Ibn ‘Abbaas: ‘Jiwe jeusi ni mkono wa kuume wa Allah katika ardhi’ atayelishika au kulipa mkono basi ni kana kwamba kambai’i281 Mola wake……….. 282

Anaendelea Ibn Taymiyya:

بل قالوا بما ولعنوا أيديهم غلت مغلولة الله يد اليهود وقالت قوله فيك ينفق مبسوطتان يفـــيداه

اللفظ من ظاهرة عرفية حقيقة وهي مشهور يشاء مجاز هي أو

Katika kauli yake Allah: “Na Mayahudi wakasema kuwa mkono wa Allah umefungwa; mikono yao ndio iliofungwa na wakalaaniwa kwa walioyasema; bali mikono yake miwili imekunjuliwa anatoa (riziki) namna apendavyo” nayo (Aya hii) ni uhakika wa kikawaida uliowazi katika tamko au ni majazi yalio mashuhuri.283

KASIM MAFUTA NAYE AJIGONGA

Kasim Mafuta naye anena:

Pamoja na kwamba inawezekana likatumika neno katika maana nyingine isiyokuwa ya asili, lakini mpaka ishindikane kutumika maana ya asili, kisha kuweko na dalili itakayotufahamisha kushindikana matumizi hayo ya asili ya neno hilo na kwenda nje ya asili yake.

Suali! Pale inaposhindikana kulitumia neno katika maana ya asili na ikabidi kulitumia katika maana isio ya asili, je ile maana isio ya asili inakuwa ni hakika au majazi? Usiniambie ni uslubu kwani – kama nilivyokueleza sana – hatuzungumzii majina ya kifani: tunazungumzia uhakika wa kitu. Suali ni kuwa je neno hilo linakuwa liko katika matumizi ya asili au limetoka katika maana ya asili?

Bila shaka maneno hayo ya Sheikh Kasim bin Mafuta, yanaashiria bali yanatongoa kwamba majazi ni kitu kilichopo. Na hili linapata nguvu kwa maelezo yake mengine aliposema:

Kwa sababu ili maneno yawe ni majazi, ni lazima masharti matatu makuu yatimie, nayo ni:

281 - Kaekeana ahadi na Allah. 282 - Ibn Taymiyya Iqaamatu Al-Dalili j. 4, uk. 82. 283 - Ibn Taymiyya Iqtidhaau Al-Siraat j. 1, uk. 20.

110

1-Kutumika neno katika isiyo kuwa maana yake ya asili.2-Lazima kuwepo na “QARINATUN MAANI’ATUN MIN IRADATI MA’ANAL ASLIY” dalili yenye kuzuia kukusudiwa maana ya asili.3-Lazima kuwepo na “ALAAQAH” mafungamano baina ya neno la asili na neno lisilo la asili.

Na likikosekana sharti moja kati ya haya matatu tuliyoyataja basi hakutakuwa na majazi na atakayedai kuwa ni majazi basi huyo ni mwongo mkubwa na hajui lugha ya kiarabu284 …..

Lakini baada ya yote hayo, Sheikh Kasim kajikanganya mwenyewe na kujigonga kwa kuyakanusha kwake majazi katika sehemu nyengine za kitabu chake na kukubaliana na wale wenye kuyakanusha. Na hili linatoa jawabu ya wazi kwamba ndugu yetu hayuko katika haki wala haki haitaki wala hakuyakanusha majazi kwa sababu ya kuwa kakinai kwa hoja na dalili. Tazama maneno yake mengine kisha linganisha na hayo yaliotangulia:

JE WENYE KUPINGA MAJAZI WANA HOJA ZA KIELIMU?

Jambo muhimu la kulizingatia ni; je hao maulamaa waliopinga kuwepo kwa majazi, wamepinga kwa hoja na dalili za kielimu? Au ni kwa maneno matupu? Jawabu ni kama ifuatavyo:

Ukirejea kauli za maulamaa hao waliopinga kuwepo kwa majazi ima katika lugha ya kiarabu na Qur’an, au katika Qur’an tu, utagundua kwamba kuna hoja za msingi walizozitoa ambazo haitakiwi kuzipuuza, bali inatakiwa zitazamwe kielimu na kwa jicho la insafu. 285

Anaendelea Sheikh Ibn Mafuta kwa kusema:

Pia maulamaa wanaopinga kuwepo kwa majazi wanapowahoji na kuwapa changamoto (challenge) wenye kuthibitisha kuwepo kwa majazi hawapati majibu yoyote ya kuridhisha ndipo pale wakalipinga suala hili ili:-Lugha ya kiarabu isichezewe.-Ili watu wa batili wasipate nafasi ya kuichezea Qur’an kwa kupotosha maana yake kwa madai ya kwamba kuna majazi, na hili walilolifikiria ndilo lililotokea.

Kwa sababu wamejitokeza baadhi ya watu wakazipotosha aya nyingi zinazotaja sifa za Allah kwa madai kwamba kuna majazi kwa madai ya

284 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 40. Tena Sheikh Kasim kumbe yeye majazi anayajua basi tu!285 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 43.

111

kumtakasa Allah na sifa za viumbe na hatima yake wakaingia katika upotofu.

Mpaka hapo itabainika kwamba;

Kupinga kuwepo kwa Majazi ndani ya Qur’an ili kufunga milango ya kuwaingiza watu kwenye upotofu ndiyo msimamo sahihi na wa haki na unaokubaliana na akili286 zaidi kuliko kudai kinyume chake. 287

Ni wazi kwamba Sheikh Kasim, sawa na Maimamu wake Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim, anakikanusha hapa kile ambacho kakithibitisha kule. Na hii ndio natija ya kukamatana na batili. Na lau ungelikuwa ewe Sheikh Kasim mwanangwa wa Mafuta hukuyathibitisha majazi kwa maneno yako yoyote yale isipokuwa kitendo chako cha kumwita Ibn Al-Qayyim kwa jina la “Shamsu Al-Din (Jua la dini)”,288 basi kingelitosha kitendo chako hicho kuonesha kuwa umejigonga, vyenginevyo wapi umesikia kwamba Ibn Al-Qayyim au mwanachuoni mwengine yoyote yule ni jua la kweli kweli la dini? Bali wapi umesikia kwamba dini ina jua (sayari). Wa Allahu Al-Musta’aan!

MUKHTASARI NA NUKTA MUHIMU

Baada ya mzunguko huu mrefu,289 ndugu Muislamu sina budi kusema kwamba imekubainikia kwa uwazi – nawe umo katika kuzipekuwa karatasi za kitabu hiki – kwamba:

1) Majazi ni neno lililotumika kinyume na maana yake ya asili.2) Maneno ya namna hio yamo kwa wingi katika Qur-ani, Sunna

(Hadithi za Mtume s.a.w.) na lugha ya Waarabu, kama vile ambavyo yamo katika lugha nyengine za binaadamu.

3) Waliokataa kuwepo kwa majazi hawakuja na hoja yoyote ilioweza kuthibitisha kwamba yale maneno yaliomo katika Qur-ani kama vile dini ya Kiislamu kuitwa kuwa ni kamba au msaada wa watu pia nao kuitwa kuwa ni kamba na mengineo, yametumika katika maana yake ya uhakika, ili iwezekane kuyakanusha majazi kwa hoja sahihi.

4) Sheikh Kasim Mafuta naye – akiwafuata Maimamu wake, Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim – kajitumbukiza katika kitu

286 - Akili ya nani?! 287 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 50.288 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 42. 289 - Lakini usije ukadhania kwamba nimerefusha kama inavyotakiwa; laa, sio hivyo, mas-ala haya ni marefu yanahitaji juzuu yake peke yake. Tukijaaliwa nitavizungumia vipengele vyengine katika kazi nyengine. Kwa hapa natarajia kwamba maudhui hii imefahamika vya kutosha.

112

kitachomfanya dahari nzima achekwe kwa kuandika kitabu akakanusha kuwepo kwa majazi! Lakini kama ulivyoona, Sh. Kasim kashindwa kutoa hoja yoyote ya kimaandiko ilioweza kubomoa hoja za kimaandiko tulizozitoa. Bali hata kuzinukuu zile hoja zetu kikamilifu hakuzinukuu kwani kajua kwamba lau atazinukuu kikamilifu basi kila atayezisoma hawezi kukubaliana naye. Alichotegemea yeye ni falsafa na logic, lakini yote hayo yamefeli kuthibitisha madai yake au kubomoa madai yetu.

5) Ibn Al-Qayyim na Ibn Taymiyya – kama kawaida yao – wakadai kwamba hakuna katika Al-Salaf na wanavyuoni wakuu wa lugha na fani nyengine za elimu walioyataja majazi.

6) Tumethibitisha kimaandiko kwamba:a) Wako ambao hawakuyataja majazi kwa jina lakini

wameyatumia, kama vile maneno ya Al-Imamu ‘Ali katika mashairi yake tulioyanukuu.

b) Wako walioyataja majazi kwa jina jengine, kama vile Sibawayh na Al-Imamu Al-Shafi katika kitabu chake Al-Risala na wengine wengi. Lakini hili la kutaja jina – kama tulivyokariri – si muhimu, kwani kinachotazamwa ni uhakika wa kitu: si jina lake.

c) Wako walioyataja kwa jina lake la kifani, kama ‘Uthman Al-Darimi, Al-Imamu Ahmad, Al-Imamu Abu Hanifa, Abu ‘Abbaas Al-Nnaashi, Al-Imamu Al-Shafi – kama ilivyo katika nukulu ya Al-Bazdawi – na wengine.

d) Kwa hivyo, madai ya Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim kwamba Al-Salaf hawakuyataja majazi hayana ukweli. Watu hawa wamekuwa na kawaida hio ya kila wakitakacho wao, basi wao huwatupia mzigo Al-Salaf ili wapate kuitangaza biashara yao. Na hapa inawapasa watu – hasa hasa huko kwetu Afrika Mashariki – wazinduke na propaganda za Kiwahabi za kwamba wao wanafuata Al-Salaf. Wallahi! Al-Salaf na wao ni umbali wa mashariki na magharibi, labda ikiwa wanakusudia Ibn Batta, Al-Hakkaari na walio mfano wa hao: si Al-Salaf Masahaba.

7) Hata kama kweli Al-Salaf hawakuyataja majazi, basi huo si ushahidi kwamba majazi hayapo kwani:

a. Kinachozingatiwa ni dalili: si chengine. Na dalili Wa-Lillahi Al-Hamdu zipo kwa wingi kama tulivyonukuu baadhi yake.

b. Tunachozungumzia ni uhakika wa kuwepo kwa majazi nalo ni neno lililotumika kinyume na maana yake ya asili: si kuwepo kwa technical term (jina la kifani), vyenginevyo fani zote – nahau, balagha, sarfu, pamoja na majina yanayotajwa ndani yake – zilikuwa hazipo. Lakini uhakika wake ulikuwepo.

113

8) Kwa haya machache, natarajia ndugu msomaji, imeweza kukubainikia haki ni ipi na batili ni ipi juu ya maudhui hii.

114