7
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] HABARI ZA NISHATI &MADINI Toleo No. 87 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Oktoba 2 - 8, 2015 Bulletin News http://www.mem.go.tz Wachimbaji wadogo kupatiwa mafunzo Soma habari Uk. 2 Rais Kikwete kuzindua Miundombinu ya Gesi Asilia Mtwara >>> ➢Ni waliopewa ruzuku ya bilioni 7.2 Kamishna Msaidizi wa Madini, anayeshughulikia Uendelezaji wa Wachimbaji Wadogo, Julius Sarota akielezea jinsi madini ya shaba yanavyoweza kutambuliwa kupitia kipande cha mwamba alichokishika katika moja ya mafunzo kwa wachimbaji wadogo Tunduru mkoani Rukwa. UK 2 Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje

MEM 87 Online.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

Habari za nisHati &madini

Toleo No. 87 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Oktoba 2 - 8, 2015

BulletinNews

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI &MADINI

Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

Wabunge Soma habari Uk. 2

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2Wachimbaji wadogo kupatiwa mafunzo

Soma habari

Uk. 2Rais Kikwete kuzindua Miundombinu ya Gesi Asilia Mtwara

>>> ➢Ni waliopewa ruzuku ya bilioni 7.2

Kamishna Msaidizi wa Madini, anayeshughulikia Uendelezaji wa Wachimbaji Wadogo, Julius Sarota akielezea jinsi madini ya shaba yanavyoweza kutambuliwa kupitia kipande cha mwamba alichokishika katika moja ya mafunzo kwa wachimbaji wadogo Tunduru mkoani Rukwa.

UK2

Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje

2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Wa c h i m b a j i wadogo wa madini waliokidhi vigezo kwa ajili ya kupatiwa ruzuku ya

shilingi bilioni 7. 2 kutoka Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) kupitia Awamu ya Pili ya Utoaji Ruzuku kwa Wachimbaji Wadogo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Uchimbaji Mdogo Nchini, wanatarajiwa kupatiwa mafunzo ya namna ya kutumia fedha walizopewa kama ruzuku kuanzia tarehe 07 Oktoba, 2015 hadi tarehe 08 Oktoba, 2015.

Akizungumza na MEM Newsbulletin, Kamishna Msaidizi, anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje ofisni kwake hivi karibuni alisema lengo la mafunzo hayo yanayotarajiwa kufanyika mjini Dodoma ni kuwapa elimu wachimbaji wadogo wa madini 111 waliopewa ruzuku juu ya matumizi ya fedha walizokabidhiwa ili uchimbaji wa madini uwe na tija kwao.

Alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo katika sekta ya

madini na kuinua uchumi wa nchi, hivyo kubuni mbinu mbalimbali za kuboresha shughuli zao za madini kwa kuwapatia ruzuku pamoja na mafunzo mbalimbali juu ya sheria na kanuni za uchimbaji salama wa madini.

Aliongeza kuwa mara baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo, wachimbaji wadogo wanatarajiwa kutia saini na Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) kabla ya kuanza kutolewa kwa fedha na benki hiyo.

Alisisitiza kuwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya utiaji wa saini kati ya wachimbaji wadogo hao na Benki ya TIB.

Awali akizungumzia vigezo vilivyotumika katika kuwapata wachimbaji wadogo 111 walionufaika na ruzuku, Mhandisi Samaje alieleza kuwa ni pamoja na kuwa na leseni hai ya uchimbaji au biashara ya madini, cheti cha usajili kutoka katika mamlaka husika pamoja na kuwa na uzoefu usiopungua miaka miwili katika shughuli za uchimbaji wa madini, uchenjuaji au uongezaji thamani madini au uzoefu wa mwaka mmoja kwa shughuli zinazohusiana na uchimbaji wa madini ya ujenzi.

Alitaja vigezo vingine ni pamoja na kuwa na namba ya mlipa kodi, kuwepo kwa shughuli za uzalishaji katika mradi unaoombewa ruzuku, kuwa na kumbukumbu za ulipaji wa mrabaha, ada za mwaka, kodi na malipo mengine husika kwa kipindi kisichopungua miezi sita.

Aliogeza vigezo vingine ni pamoja na kuwa na mpango kazi unaokidhi mahitaji ya uendelezaji wa jumuiya ya wachimbaji wadogo, kama ni uongezaji thamani awe na uthibitisho wa vyanzo vya upatikanaji wa madini ya vito vinavyotambulika kisheria, mradi unaoombewa ruzuku uwe endelevu na mwombaji awe na akaunti ya benki ya mradi husika.

Wakati huo huo akielezea lengo la awamu ya pili ya utoaji wa ruzuku, Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uendelezaji wa Wachimbaji Wadogo, Julius Sarota alisema kuwa ni kuwawezesha wanufaikaji wa ruzuku kuongeza uzalishaji kwa kupanua migodi au kuboresha uchenjuaji au uongezaji thamani madini na kuboresha huduma zitolewazo katika uchimbaji madini na ungezaji thamani madini .

Sarota alieleza kuwa malengo mengine ni pamoja na kuongeza

kipato, ajira na uwezo kwa wachimbaji ili kufanya uchimbaji mdogo kuwa tasnia ya ujasiriliamali, kuwakwamua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuongeza pato la taifa.

“Pia kupitia mpango huu tunataka kuwasaidia wakina mama au vikundi vyao vilivyo karibu na maeneo yaliyo karibu na maeneo ya uchimbaji madini kuongeza kipato kupitia kazi mbadala na kutoa mitaji ili kusaidia uendelezaji na ukuaji wa tasnia ya uchimbaji na uongezaji thamani madini wenye matokeo makubwa sasa, alisisitiza Sarota.

Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikiwawezesha wachimbaji wadogo wa madini kupitia ruzuku kupitia awamu tofauti, ambapo kupitia awamu ya kwanza iliyotekelezwa katika mwaka wa fedha 2013/14 wachimbaji au vikundi vya wachimbaji 11 vilifaidika kwa kila mmoja kupata wastani wa Dola za Marekani zisizozidi 50,000

Fedha hizi zilipatikana kupitia mradi wa Wizara hiyo wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ambao unapata fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia.

Wachimbaji wadogo kupatiwa mafunzo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa

kuzindua rasmi miundombinu ya gesi asilia kutoka Madimba Mkoani Mtwara tarehe 10 Oktoba, 2015.

Hayo yameelezwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt James Mataragio kwenye kikao chake na waandishi wa habari.

Imeelezwa kwamba mradi huo umegharimu kiasi cha Dola za Kimarekani bilioni 1.225 ambapo asilimia 95 ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Exim ya China na huku asilimia 5 zikiwa ni fedha za ndani.

Rais Kikwete kuzindua Miundombinu ya Gesi Asilia Mtwara

Nyumba za watumishi wanaofanya kazi katika kituo cha Kukachakata gesi. Madimba.

Mitambo ya kusafisha Gesi Asilia

3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

TahaririMEM

Na Badra Masoud

Five Pillars oF reForms

KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano

Bodi ya uhariri

Mhariri MkUU: Badra MasoudMSaNifU: Lucas Gordon

WaaNdiShi: Veronica Simba, asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, rhoda James ,

Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

increase eFFiciencyQUality delivery

oF Goods/service

satisFaction oF tHe client

satisFaction oF BUsiness Partners

satisFaction oF sHareHolders

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

Mafunzo kuhusu matumizi ya ruzuku yalete tija kwa wachimbaji

wadogo wa madini

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

GST waeleza faida miradi ya SMMRP

Wizara ya Nishati na Madini inatarajia kuendesha mafunzo kwa wachimbaji wadogo 111 waliopata ruzuku ya shilingi bilioni 7.2 kutoka katika Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) kupitia Awamu ya Pili ya Utoaji Ruzuku kwa Wachimbaji Wadogo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Uchimbaji Mdogo Nchini.

Lengo la mafunzo hayo yanayotarajiwa kufanyika Dodoma kuanzia tarehe 07 Oktoba, 2015 hadi tarehe 08 Oktoba, 2015 ni kuwapa elimu wachimbaji wadogo wa madini waliopewa ruzuku juu ya matumizi ya fedha watakazokabidhiwa ili uchimbaji wa madini uwe na tija kwao.

Mara baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo, Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye halfa ya utiaji wa saini kati ya wachimbaji wadogo hao na Benki ya TIB kabla ya fedha hizo kuanza kutolewa na benki hiyo.

Utoaji wa ruzuku kwa wachimbaji wadogo ni moja ya mikakati ya Serikali katika kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wa madini wanafanya kazi katika mazingira mazuri kwa kufuata sheria na kanuni za usalama katika uchimbaji wa madini.

Mbali na utoaji wa ruzuku, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikiendesha mafunzo kwa wachimbaji wadogo kuhusiana na sheria, kanuni za usalama katika uchimbaji wa madini pamoja na ujasiriliamali.

Awali, vigezo vilivyotumika katika utoaji wa ruzuku awamu ya pili ni pamoja na kuwa na leseni hai ya uchimbaji au biashara ya madini, cheti cha usajili kutoka katika mamlaka husika pamoja na kuwa na uzoefu usiopungua miaka miwili katika shughuli za uchimbaji wa madini, uchenjuaji au uongezaji thamani madini au uzoefu wa mwaka mmoja kwa shughuli zinazohusiana na uchimbaji wa madini ya ujenzi.

Vigezo vingine ni kuwa na namba ya mlipa kodi, kuwepo kwa shughuli za uzalishaji katika mradi unaoombewa ruzuku, kuwa na kumbukumbu za ulipaji wa mrabaha, ada za mwaka, kodi na malipo mengine husika kwa kipindi kisichopungua miezi sita.

Vigezo vingine ni pamoja na kuwa na mpango kazi unaokidhi mahitaji ya uendelezaji wa jumuiya ya wachimbaji wadogo, kama ni uongezaji thamani awe na uthibitisho wa vyanzo vya upatikanaji wa madini ya vito vinavyotambulika kisheria, mradi unaoombewa ruzuku uwe endelevu na mwombaji awe na akaunti ya benki ya mradi husika.

Malengo ya utoji wa ruzuku awamu ya pili ni pamoja na kuwawezesha wanufaikaji wa ruzuku kuongeza uzalishaji kwa kupanua migodi au kuboresha uchenjuaji au uongezaji thamani madini na kuboresha huduma zitolewazo katika uchimbaji madini na ungezaji thamani madini .

Malengo mengine ni pamoja na kuongeza kipato, ajira na uwezo kwa wachimbaji ili kufanya uchimbaji mdogo kuwa tasnia ya ujasiriliamali, kuwakwamua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuongeza pato la taifa.

Ikumbukwe kuwa mafunzo jinsi ya matumizi ya fedha za ruzuku ni muhimu ili wachimbaji wadogo wa madini waweze kufanya kazi katika mazingira bora na kupata faida na hivyo kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi

Rai yetu ni kuwaomba wachimbaji wadogo wa madini kuzingatia mafunzo watakayopewa ili waweze kusimamia vyema fedha watakazopewa, kupata faida, kujikwamua kiuchumi na hivyo kuwa na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia sekta ya madini.

Na Asteria Muhozya, Morogoro

Imeelezwa kuwa yapo manufaa makubwa na yanayotarajiwa kudumu kwa kipindi kirefu kutokana na utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST),

kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), ambapo pia manufaa hayo yanatajwa kuwa kichocheo kikubwa cha uwekezaji ndani na nje ya nchi na kuchangia ukuaji katika sekta ya madini nchini.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Mtendaji Mkuu wa GST, Profesa Abdulkarim Mruma, wakati akiwasilisha mada juu ya namna Wakala huo ulivyotekeleza awamu ya kwanza ya mradi na namna ulivyojipanga kutekeleza awamu ya pili ya mradi wa SMMRP katika warsha ya ufunguzi wa mradi wa SMMRP, Awamu ya pili uliofanyika mjini Morogoro hivi karibuni .

Profesa Mruma alisema kuwa, kuwezeshwa kwa mfumo mpya wa Mawasiliano ya Teknolojia katika Wakala huo chini ya SMMRP kunatarajia kutoa matokeo makubwa yatakayodumu kwa kipindi kirefu kwa kuwa mfumo huo wa teknolojia utasaidia kuboresha program kuhusu taarifa mbalimbali za kitafiti na kuzisambaza taarifa hizo jambo ambalo

litawezesha kutangaza taarifa muhimu kuhusu maeneo ya muhimu ya uwekezaji katika sekta ya madini ndani na nje ya nchi.

Vilevile, alisema kuwa, matumizi ya Teknolojia mpya katika utengenezaji wa ramani, upatikanaji wa data ni muhimu katika uendelezaji wa elimu ya Jiosayansi na madini hususani katika utafiti na uchimbaji wa madini katika nchi yoyote.

Warsha hiyo ilihudhuriwa na Ujumbe wa kutoka Benki ya Dunia, Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Makamishna Wasaidizi wa Madini, Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Maafisa wa Madini Wakazi, Asasi Wachimbaji wadogo na Makatibu Tawala kutoka wilaya za Mpanda, Geita, Butiama, Chunya, Lindi, Kyerwa, Bukombe ,Tunduru na Kahama.

Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), Mhandisi Idrisa Yahya (katikati) akijadiliana jambo na Watendaji kutoka Chuo Cha Madini Dodoma (MRI) (wa kwanza kushoto), Mhandisi Sudian Chiragwile, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jilojia Tanzania (GST), Profesa Abdrulkarim Mruma wakati wa warsha ya ufunguzi wa mradi wa SMMRP Awamu ya Pili.Wengine kutoka kulia ni Wawakilishi kutoka Benki ya Dunia, Rachel Perk na Mamadou Barry.

4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Mohamed Saif

Wizara ya Nishati na Madini kupitia Kitengo chake cha Leseni kinaendelea na mafunzo

maalumu kwa wachimbaji madini nchini kuhusu mfumo wa Huduma za Leseni kwa njia ya Mtandao ujulikanao kama Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP).

HISTORIA YA MFUMO WA UTOAJI LESENI

Inaelezwa kwamba hadi Mwaka 2000, Kitengo cha utoaji leseni kilikuwa Mkoani Dodoma. Mfumo wa utoaji leseni kwa hapo awali ulifanyika kwa njia ya mkono na hivyo kusababisha ucheleweshwaji mkubwa wa leseni.

Wakati huo leseni za uchimbaji mdogo zilipokelewa kwenye ofisi za Madini Wakazi na kupelekwa kwenye Ofisi za Madini Kanda, kisha kutumwa kwa telegram kwenda Dodoma. Kitengo cha Leseni Dodoma kilichambua maombi yote kwa mkono na kuandaa leseni ambazo zililetwa Dar es Salaam kwa ajili ya kusainiwa na Kamishna wa Madini au na Waziri wa Nishati na Madini.

Hali hiyo ilichangia changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ucheleweshaji wa kutolewa leseni kutokana na kutegemea hali ya mawasiliano kati ya ofisi za mikoani na Dodoma.

Akizungumzia mfumo huo wa zamani, Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Paul Masanja anasema kwamba mfumo huo ulikuwa na changamoto nyingi kwa kuwa ulitegemea umahiri na uadilifu wa Afisa aliyeshughulikia leseni na hivyo mara nyingine kufanya makosa na kusababisha migogoro na pia kusababisha baadhi ya waombaji kukosa leseni bila kuwepo na sababu ya msingi.

Changamoto nyingine ya mfumo huo wa awali, ilikuwa ni waombaji wa leseni kulazimika kusafiri kwenda kwenye ofisi za madini na mara nyingine kwenda hadi Dodoma kufuatilia maombi yao.

Mbali na hilo, Kamishna huyo anaeleza kwamba hapo awali ilimbidi mwombaji wa leseni kufyeka mipaka ya eneo analoomba na kuweka vibao na kisha kumleta Afisa madini ili kukagua eneo linaloombwa na hatimaye kwenda kufanya malipo ya maombi hayo kwenye ofisi ya Madini.

Pamoja na hayo yote, Mhandisi Masanja anaeleza kuwa bado ombi hilo lilikuwa na uwezekano wa kukataliwa au kukubaliwa.

“Hali hiyo ilichangia kuwakatisha tamaa baadhi ya waombaji wa leseni, hasa wananchi wanyonge. Vilevile maafisa wasio

waaminifu waliwapunja waombaji leseni wanyonge,” anaeleza Mhandisi Masanja.

Anabainisha kwamba mfumo uliokuwepo hapo awali vilevile ulichangia kuongezeka kwa vitendo vya rushwa na upendeleo usiokuwa na tija kwa Taifa.

Anaongeza kwamba licha ya mahangaiko waliyokuwa wanayapata waombaji leseni, Wizara pia ilikuwa na wakati mgumu wa kuhakikisha kwamba kumbukumbu zinatunzwa vyema ipasavyo kutokana na kwamba maombi yalikuwa yakifanywa kwa karatasi na vivyo hivyo kumbukumbu za leseni zilitunzwa kwenye madaftari.

Vilevile, anaeleza kwamba kulikuwa na ugumu wa kuchambua nyaraka za leseni na kuchora ramani kwa mkono (manually) ili kufuatilia uhai wa leseni, malipo ya ada na utendaji wa wamiliki wa leseni.

“Aghalabu leseni nyingi hazikuweza kuchambuliwa na hali hiyo iliathiri ubora wa utendaji wa Wizara na pia kasi ya kuwahudumia wananchi ilikuwa ndogo,” anasema Mhandisi Masanja.

MWANZO WA MABADILIKO

Anafafanua kwamba ilipofika mwaka 2007, Wizara ya Nishati na Madini ilianzisha Mfumo wa kisasa wa Utoaji na Usimamizi wa Leseni ujulikanao kama Mining Cadastral Information management System (MCIMS).

Anasema chini ya mfumo huo wa MCIM, ofisi zote za madini nchini ziliunganishwa kwa njia ya

mawasiliano ya kompyuta na hivyo kurahisisha mawasiliano kati ya ofisi hizo.

Chini ya mfumo huo wa MCIM, Mhandisi Masanja anaeleza kuwa “taarifa za leseni zimeweza kupatikana kila ofisi kwa wakati (Real-Time) tofauti na mfumo wa zamani uliotegemea mawasiliano ya barua na simu.”

Akifafanua zaidi, anasema mfumo huo unawezesha uchambuzi wa maombi ya leseni za madini kwa kutumia kompyuta na kwa kuzingatia Sheria na kanuni za Madini.

“Chini ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, waombaji wa leseni hawatakiwi tena kwenda kufyeka mipaka au kuweka alama za mipaka wakati wa kuwasilisha maombi ya leseni,” anafafanua.

Aidha, anasema waombaji wanaweza kuomba kuona ramani ya eneo husika kabla hawajatuma maombi ili kuhakiki kama eneo husika liko wazi ama vinginevyo.

Anasema huduma ya MCIMS imerahisisha huduma za wateja na kuongeza kasi ya utoaji leseni kwa kiwango kikubwa. Anaongeza kwamba mfumo huo umekuwa wa manufaa kwa wateja na kwa Wizara kwa kupunguza muda wa kutoa au kusubiri huduma za leseni.

Aidha, kwa maelezo yake Mhandisi Masanja, anabainisha kwamba mfumo huo umeongeza uwazi katika utoaji wa leseni unaovutia wawekezaji, na pia umewezesha Wizara kusimamia vizuri leseni zilizotolewa na pia uwekaji kumbukumbu na upataji taarifa kuwa bora zaidi

ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.

HALI ILIVYO HIVI SASAJitihada za Wizara ya Nishati na

Madini katika kuboresha huduma ya utoaji wa leseni za madini ziliendelea na inaelezwa kwamba katika kipindi cha Mwaka 2014/15, Wizara hiyo imeshughulikia uboreshaji wa mfumo wa MCIMS kwa lengo la kuwawezesha waombaji wa leseni za madini kujihudumia wenyewe (Self-Service) kwa kupitia mfumo wa Huduma za Leseni kwa njia ya mtandao yaani Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP).

“Hatua hii muhimu inakusudia kuwapunguzia wananchi ugumu wa kupata huduma. Mfumo huu wa kujihudumia unafanana na mifumo inayotumiwa na TRA kwenye malipo ya leseni za magari au mifumo ya kununua LUKU iliyowekwa na TANESCO,” anafafanua Kamishna Masanja.

Anasema Mfumo wa OMCTP unakuwa kama kituo kimoja (one-stop-centre) ambacho kitatumiwa na wadau wa Sekta ya Madini walio nchini na walio nje ya nchi kuweza kujipatia huduma za leseni bila kulazimika kusafiri kwenda kwenye ofisi za Madini, pindi wanapokuwa wamesajiliwa ndani ya mfumo huo.

Kuna faida nyingi zinazopatikana ndani ya mfumo huo wa OMCTP kama anavyoeleza Mhandisi Masanja; “Kuongeza uwazi na kasi ya utoaji wa leseni za madini, wateja wataingiza maombi ya leseni wao wenyewe na hivyo kupunguza

Huduma ya utoaji leseni za madini sasa Mtandaoni

>>Inaendelea Uk. 5

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao. Wa pili kutoka kulia ni Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja na wa kwanza kushoto mbele ni Kamishna Msaidizi wa Madini- Sehemu ya Leseni, Mhandisi John Nayopa.

>>> ➢Maisha ya wachimbaji madini yamerahisishwa

5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

Sekta ya Nishati kuadhimisha miaka 10 ya MafanikioNa Zuena Msuya,

Wizara ya Nishati na Madini kupitia sekta ya Nishati inatarajia kuadhimisha miaka 10 ya mafanikio

katika sekta hiyo hivi karibuni.Akizungumza Jijini Dar Es

Salaam Mwenyekiti wa maandalizi ya mafanikio hayo Kamishna wa

Nishati nchini Mhandisi Hosea Mbise alisema kuwa maandalizi ya shughuli hiyo yanaendelea vizuri.

Mhandisi Mbise alisema mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, na hafla hiyo inatarajiwa kufanyika katikati ya mwezi Octoba kama Ratiba iliyopangwa haitabadilika.

Katika hafla hiyo Taasisi zote zilizo chini ya sekta ya Nishati ikiwemo Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini, (TPDC) watashiriki katika hafla hiyo.

Aidha wadau wote wa sekta ya Nishati zikiwemo Sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, Kampuni za mafuta na Gesi, pamoja

na balozi mbalimbali nchini pia zitahudhuria hafla hilo.

Mhandisi Mbise alisema hafla hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki wapatao 400 wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali hapa nchini, Taasisi za kiserikali, Mashirika ya umma, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wadau wote waliotoa mchango wao katika sekta ya Nishati.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Maandilizi ya hafla ya mafanikio ya miaka 10 ya Sekta ya Nishati inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni wakiwa katika moja ya vikao vya maalindilizi ya hafla hiyo katika ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini.

tatizo la mlundikano wa maombi kwenye ofisi za madini.”

Faida nyingine zinazotokana na mfumo huo kama anavyoeleza Kamishna huyo ni kwamba wateja (waombaji/wamiliki wa leseni za madini) na Serikali kuwa na uhakika na maombi yote yatakayowasilishwa. Vilevile watakuwa na uhakika na malipo yote yatakayofanywa kupitia mfumo huo na pia waombaji wa leseni wataweza kupata taarifa za leseni zao kila wakati na kujua wanapotakiwa kufanya malipo ya leseni au watakapotakiwa kutuma taarifa za utendaji kazi.

Aidha, anaongeza kwamba kupitia OMCTP, mawasiliano baina ya Wizara na wamiliki wa leseni yatakuwa rahisi zaidi na pia waombaji wa leseni wataweza kuhuisha taarifa za leseni zao kama vile anwani na namba za simu pindi taarifa hizo zitakapobadilishwa.

Waombaji na wamiliki wa leseni nchini hawana budi kupokea uzinduzi huo wa OMCTP kwa moyo mkunjufu kwani hatimaye

kilio chao juu ya changamoto mbalimbali zilizokuwa zikihusishwa na huduma isiyoridhisha ya utoaji leseni nchini zimepatiwa tiba mujarabu.

Akifafanua zaidi kuhusu huduma hiyo ya OMCTP, Kamishna Msaidizi wa Madini Sehemu ya Leseni, Mhandisi John

Nayopa anasema changamoto zilizokuwepo kwenye mifumo ya awali hivi sasa itakuwa ni historia.

Mhandisi Nayopa anaeleza kwamba tayari mafunzo kuhusu mfumo huo wa OMCTP yanaendela kutolewa kwa wachimbaji madini kote nchini.

Anaeleza umuhimu wa

mafunzo hayo na kuwataka wachimbaji wa madini, waombaji na wamiliki wa leseni kuhakikisha wanafuatilia kwa umakini mafunzo hayo yanayotolewa na Wizara.

“Ni vyema mafunzo juu ya mfumo huo wa OMCTP yanayoendelea kwa wachimbaji madini kote nchini yakapewa umuhimu wa kipekee na wachimbaji wenyewe. Ieleweke kwamba lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wao wenyewe katika kutumia na kufaidika na mfumo huu”, anasema.

Mhandisi Nayopa anawatoa hofu wamiliki wa leseni za uchimbaji mdogo ambao wameonesha shaka kuhusu uwezo wao katika kutumia mfumo wa OMCTP kuwa Wizara imeweka vifaa katika ofisi zote za Madini kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wenye matatizo ya matumizi ya mfumo huo.

Ni wakati muafaka sasa kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini kujisajili kwenye Ofisi za Madini ili kuanza kutumia mfumo huo mpya. Inaelezwa kwamba tayari usajili umekwishaanza.

Huduma ya utoaji wa leseni za madini sasa ni kwa Mtandao>>Inatoka Uk. 4

Kupitia mfumo mpya wa Huduma za Leseni kwa njia ya Mtandao (OMCTP), wachimbaji wadogo wa madini wataweza kuingiza ama kubadili taarifa za leseni zao wakiwa huko huko migodini bila kufika kwenye ofisi za madini

6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

APPOINTMENT OF DIRECTORS TO CONSTITUTE THE BOARD OF DIRECTORS OF TPDC

2nd October, 2015:

The desire to appoint a Competent Board of Directors

The Ministry of Energy and Minerals (MEM) of the Government of the United Republic of Tanzania as mandated under the Public Corporations Act and, in that on behalf of the Shareholder of Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC), would like to recruit able and competent Tanzanians to constitute and serve in the Board of Directors of TPDC.

It is desired that upon their appointment as such as required under the Law, members of the Board of Directors of TPDC will lead and govern this strategic Corporation to highest levels of performance in terms of: investing strategically in the entire petroleum value chain, provision of reliable and quality oil and natural gas to the Nation, and managing prudently the petroleum resource and other resources of the Corporation for the benefit of the present generation and future generations.

In short, it is expected that under the governance of this Board of Directors, TPDC shall go forward in recording desirable positive contributions to the wellbeing of the Nation in all respects; thus, satisfying the needs and desires of its shareholder, the Government; investors; customers; development partners; and other stakeholders.

In these regards, MEM shall closely monitor the performance of the Board of Directors as required under the Law, and in line with pre- agreed Key Performance Indicators (KPIs). The KPIs shall reflect the expectations outlined in major policy documents of the Government, the laws governing the sector, TPDC’s contractual obligations and those of its customers and other stakeholders.

Qualifications/Qualities of individuals to be appointed as members of the Board of Directors

MEM therefore desires that the Board of Directors of TPDC shall be composed of individuals who have demonstrated significant achievements in their respective professional careers, in business management and their service in either public or private sector, or both.

The aspirants must possess requisite knowledge; intelligence and experience to enable them make significant positive contribution in the Board of Directors’ decision making process.

In light of Government policies and priorities on one hand, and the Company’s Mission and Vision on the other hand, the individuals are expected to possess qualifications and qualities and experience that will add value in the energy sector and the petroleum sub-sector in particular. Specifically, the following qualities are considered desirable to any candidate aspiring to become member of the Board of Directors of TPDC:

1. Education: it is desirable that a candidate should hold a degree from a respected college or university majoring in the fields of, natural sciences, economics, finance, engineering, law, or management/administration. Possession of a Masters or doctoral degree will be an added advantage;

2. Experience: a candidate must have extensive experience (not less than 10 years) in his/her professional career and must demonstrate positive track record of performance in management in either public or private service, or both. An ideal candidate should have sufficient experience to fully appreciate and understand the responsibilities of a director in a challenging company like TPDC;

3. International Experience: experience working in either senior management or as director in international organizations/corporations relevant to the petroleum industry will be considered as an advantage to a candidate’s profile;

4. Individual Character and Integrity: a candidate must be a person of highest moral and ethical character, impeccable record and integrity. In this regard, a candidate must exhibit independence and demonstrate personal commitment to serve in the Company’s and public interests;

5. Personal Qualities: a candidate must have personal qualities that will enable him to make substantial active contribution in the Board’s decision-making process. These qualities include intelligence, self-assuredness, independence, highest ethical standing, practical knowledge to corporate governance standards,

willingness to ask difficult questions, inter-personal skills, proficiency in communication skills and commitment to serve,

6. Knowledge of the Sector: a candidate must have sufficient knowledge of TPDC’s work and situation and issues affecting the energy sector and the petroleum sub-sector in Tanzania. In this regard, a candidate must have particular knowledge of TPDC’s or rather, the energy sector’s stakeholders’ desires, needs and challenges, like those of the Government, development partners, investors, regulators, customers, etc.

7. Courage: a candidate must be able and willing to make right decisions at all times, even if the same would make the person look difficult or unpopular;

8. Availability: a candidate must be willing to commit, as well as have, sufficient time available to discharge his or her duties as member of the Board of Directors. Therefore, a desirable candidate should not have other corporate board memberships;

9. Compatibility: a candidate should be able to develop good working relationship with other members of the Board of Directors and members of senior management of the Company; and

10. Conflict of Interest: a candidate must not be in a position of conflict of interest with Company’s activities.

Invitation to apply: MEM invites candidates who possess the mentioned qualifications and qualities to apply to be considered for appointment as directors and serve in the Board of Directors of TPDC. Interested candidates must write and submit their applications by Friday, 16th October, 2015 demonstrating their respective qualifications and qualities, attaching photostat copies of their testimonials and detailed CVs to;

The Permanent Secretary,Ministry of Energy and Minerals,

5 Samora Machel Avenue,P.O.BOX 2000,

11474, DAR ES SALAAM.Email: [email protected]

7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya ‘Nishati na Madini’ Karibu tuhabarishane na

tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA (TPDC)

TAARIFA KWA UMMAShirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini, wanayo furaha kuwafahamisha kwamba,ujenzi wa miundombinu ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia, kutoka Madimba-Mtwara na Songosongo-Lindi hadi Dar es salaam umekamilika.

Kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu hii, kutafungua historia mpya ya uchumi wa nchi yetu, kwani kutawezesha upatikanaji wa nishati ya uhakika, na hivyo kukuza uchumi na kuongeza pato la Taifa.

Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atazindua miundo mbinu hii – Tarehe 10/10/2015 huko Madimba, Mtwara.

Wote mnakaribishwa kushuhudia tukio hili la kihistoria nchini kwetu.

‘Gesi asilia, kwa maendeleo ya Taifa’

Imetolewa na:Mkurugenzi MtendajiShirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

 

Extractive Inter-stakeholders Forum (EISF) in Collaboration with the Ministry of Energy and Minerals

(MEM) Invites You to participate and exhibit    

The TANZANIA OIL, GAS AND MINERALS BUSINESS AND SUPPLY CHAIN

Creating awareness on the Extractive Industry Value Chains, Financing, Marketing and Business Opportunities

The event will be held on 24-25 March 2016 at Hyatt Regency Dar es Salaam - The Kilimanjaro