11
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] HABARI ZA NISHATI &MADINI Toleo No. 86 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Septemba 25 - Oktoba 1, 2015 Bulletin News http://www.mem.go.tz BENKI YA DUNIA yaridhishwa Mafanikio SMMRP Soma habari Uk. 3 Dira ya Madini Tanzania kuzinduliwa Januari, 2016 >>> ➢Wizara kuendelea kutoa ruzuku kwa Wachimbaji Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia), akibadilishana mawazo na Mwakilishi na Kiongozi wa Mradi wa SMMRP, Benki ya Dunia, Mamadou Barry (katikati) na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje wakati wa warsha ya ufunguzi wa Mradi wa SMMRP, Awamu ya Pili. UK 2

MEM 86 ONLINE.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MEM 86 ONLINE.pdf

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

Habari za nisHati &madini

Toleo No. 86 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Septemba 25 - Oktoba 1, 2015

BulletinNews

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI &MADINI

Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

Wabunge Soma habari Uk. 2

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2BENKI YA DUNIA yaridhishwa Mafanikio SMMRP

Soma habari

Uk. 3Dira ya Madini Tanzania kuzinduliwa Januari, 2016

>>> ➢Wizara kuendelea kutoa ruzuku kwa Wachimbaji

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia), akibadilishana mawazo na Mwakilishi na Kiongozi wa Mradi wa SMMRP, Benki ya Dunia, Mamadou Barry (katikati) na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje wakati wa warsha ya ufunguzi wa Mradi wa SMMRP, Awamu ya Pili.

UK2

Page 2: MEM 86 ONLINE.pdf

2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Asteria Muhozya, Morogoro

Wizara ya Nishati na Madini kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa

Rasilimali Madini (SMMRP) imezindua utekelezaji wa Awamu ya Pili ya mradi huo, huku ikifunga rasmi utekelezaji wa Mradi Awamu ya Kwanza ambao umewezesha Tanzania kupata mafanikio ya kujivunia kupitia sekta ya madini.

Akifungua warsha ya uzinduzi wa Mradi wa Awamu ya Pili iliyofanyika mjini Morogoro hivi karibuni, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava amesema kuwa, mradi wa awali ulifanikiwa kukamilisha malengo yaliyokusudiwa jambo ambalo limewezesha Benki ya Dunia kutoa nyongeza ya fedha ikiwemo kuongeza muda wa utekelezaji na kupanua mradi huo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.

Mhandisi Mwihava aliongeza kuwa, lengo kuu la kuongeza utekelezaji wa mradi kwa Awamu ya Pili ni kuboresha manufaa ya kijamii na kiuchumi yatokanayo na uchimbaji wa madini nchini kwa kuimarisha zaidi sehemu ya miradi ya kiuchumi na kijamii iliyokuwa inatekelezwa na mradi wa awali na hivyo kuhakikisha ukuaji mkubwa wa maendeleo pamoja na kupunguza umaskini.

Mwihava alitaja lengo Jingine la kuongeza utekelezaji wa mradi ni kushughulikia changamoto mbalimbali ikiwemo ya ugumu katika kutambua mazingira mazuri ya kijiolojia yanayofaa kwa uchimbaji mdogo wa madini, mafunzo duni na ukosefu wa vituo vya kujifunzia kwa wachimbaji.

Mwihava alisema kuwa, ili kutimiza azma hiyo, Wizara kupitia Mradi wa SMMRP II imekusudia kuanzisha vituo saba bora vya mfano katika maeneo ambayo yana wachimbaji wengi wa madini nchini ambapo vituo hivyo zitanufaika katika kuboresha teknolojia iliyopo ya uchenjuaji kama uchenjuaji usiotumia zebaki, matumizi salama ya zebaki na uchenjuaji kwa kutumia ‘cynide’.

Vilevile, Mwihava amesema kuwa, kupitia SMMRP, Wizara itaendelea kutoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia kwa kuongeza mipaka ya kijiolojia kwa Kanda zote kwa wale wanaostahili.

“Katika awamu hii jumla ya dola za Marekani milioni tatu (3) zimetengwa kufanikisha kazi hii na utoaji huu wa ruzuku utasaidia wachimbaji wadogo kuboresha teknolojia katika maeneo yao ya uchimbaji, kupata mafunzo na ujuzi maalum katika masuala ya

uchimbaji na kufanya mafunzo ya kibiashara,” amesisitiza Mwihava.

Aidha, Mwihava alisema kuwa, kupitia Wakala wake wa Jiolojia Tanzania (GST),kutafanyika utafiti katika maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za uchimbaji mdogo na yale yanayopendekezwa kwa ajili ya kuanzisha vituo vya uchenjuaji ili kufahamu mashapo yaliyopo na hivyo kuwezesha wachimbaji wadogo kufanya shughuli zao kwa uhakika zaidi.

Mwihava alisema kupitia mradi huo, Serikali inaendelea kuhamasisha Uongezaji Thamani Madini kwa kuendelea kukiwezesha kituo cha mafunzo cha TGC na kufanikisha Sheria ya Uongezaji Thamani Madini.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Benki ya Dunia ambaye pia ni Kiongozi wa Mradi wa SMMRP, Mamadou Barry, alipongeza hatua ambayo Tanzania imefikia katika kuendeleza Sekta ya Madini na kuongeza kuwa, kutokana na

mafanikio yaliyopatikana Awamu ya kwanza, Benki ya Dunia itaendelea kuisadia Tanzania ili kuhakikisha kwamba, sekta hiyo inachangia zaidi katika ukuaji wa uchumi ikiwemo kuhakikisha kwamba wananchi wa Tanzania wananufaika kupitia sekta hiyo.

“ Tanzania imekuwa ni nchi bora kwa kuwa na taarifa nzuri za Kijiolojia, Ofisi za Madini za Kanda zimeweshwa, Mfumo wa Utoaji Leseni Madini kwa njia ya mtandao unaendelea vizuri, lakini tunataka kuwawezesha zaidi wachimbaji wadogo wachangie pato la taifa, pia tunataka mabadiliko zaidi ili kuchochea uwekezaji kupitia madini”, alisema Mamadou.

Aidha, Mamadou aliiasa Serikali kutoridhika na mafanikio yaliyopatikana hivi sasa kupitia sekta husika na badala yake kuitaka sekta hiyo ichangie zaidi katika kuongeza ajira kwa vijana na pia iweze kuchochea fursa mbalimbali za kiuchumi kupitia sekta nyingine na kuziunganisha na sekta ya madini.

“Tumeshuhudia maendeleo makubwa katika sekta ya madini Tanzania, lakini hatupaswi kuridhika na mafanikio haya. Wananchi bado wanahitaji maendeleo zaidi kupitia madini. Siku zote Benki ya Dunia imekuwa pamoja katika kuleta mabadiliko haya, lakini tunataka kuona Tanzania inafaidika na yenye maendeleo kupitia madini ,” alisisitiza Mamadou.

Awali, akitoa taarifa kuhusu hatua mbalimbali zilizofanyika kuiendeleza sekta hiyo, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje alisema changamoto kadhaa zilizojitokeza awali zilichochea wazo la kuanzishwa kwa mradi wa SMMRP, na kutaja mafanikio

kadhaa, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009, jumla ya wachimbaji 123 wamepatiwa ruzuku, ambapo katika awamu ya kwanza mradi ulitoa jumla ya Dola za Marekani 500,000 na Dola za Marekani Milioni 3.5 sawa na shilingi bilioni 5.74, zilizotolewa katika awamu ya pili.

Akizungumzia kuhusu shughuli za Uongezaji Thamani Madini, Mhandisi Samaje alisema kuwa, SMMRP imefanikiwa kuimarisha kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) na kukifanya kuwa kituo bora cha mafunzo Afrika Mashariki kwa ukataji na unga’rishaji wa madini ya vito na usonara; utengenezaji wa bidhaa za mapambo na uchongaji wa vinyago vya mawe.

Vilevile, Samaje aliyataja mafanikio mengine kuwa ni kuboreshwa kwa mfumo wa utoaji na usimamizi wa leseni za madini (MCIMS) ili kuruhusu uombaji na ulipaji wa Ada za leseni kwa njia za mtandao. “Zoezi la kuondoa mrundikano wa maombi ya leseni umekamilika kwa asilimia 100 na hii imeimarisha uadilifu na uwazi wakati wa uombaji wa leseni mpya,” alisema Samaje.

Warsha hiyo ya ufunguzi wa Awamu ya Pili ya mradi wa SMMRP ilihudhuriwa na Ujumbe wa Benki ya Dunia, Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Makamishna Wasaidizi wa Madini, Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Maafisa wa Madini Wakazi, Asasi zisizo za Kiserikali, Wachimbaji wadogo na Makatibu Tawala kutoka wilaya za Mpanda, Geita, Butiama, Chunya, Lindi, Kyerwa, Bukombe ,Tunduru na Kahama.

Benki ya Dunia yaridhishwa Mafanikio Mradi wa SMMRP

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Washiriki wa warsha ya Ufunguzi wa Mradi wa SMMRP, katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo. Waliokaa kutoka kulia ni Meneja wa SMMRP, Mhandisi Idrisa Katala, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, Mwakilishi wa Benki ya Dunia na kiongozi wa mradi wa SMMRP, wa Benki hiyo, Mamadou Barry na mwakilishi kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST).

Page 3: MEM 86 ONLINE.pdf

3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

TahaririMEM

Na Badra Masoud

Five Pillars oF reForms

KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano

Bodi ya uhariri

Mhariri MkUU: Badra MasoudMSaNifU: Lucas Gordon

WaaNdiShi: Veronica Simba, asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, rhoda James ,

Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

increase eFFiciencyQUality delivery

oF Goods/service

satisFaction oF tHe client

satisFaction oF BUsiness Partners

satisFaction oF sHareHolders

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

Mafanikio SMMRP Awamu ya Kwanza yanastahili Pongezi!

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

Dira ya Madini Tanzania kuzinduliwa Januari, 2016

Wiki hii tumeshuhudia tukio la Uzinduzi wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini Awamu ya Pili (SMMRP) baada ya Awamu ya Kwanza ya Mradi kufungwa. Kupitia hotuba za viongozi wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo akiwemo Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, Wawakilishi wa Benki ya Dunia, Mamadou Barry; Rachel Perk na Meneja wa Miradi ya SMMRP, Idrisa Katela wote kwa nyakati tofauti walitaja mafanikio makubwa ambayo yamepatikana kupitia Awamu ya Kwanza ya utekelezaji Mradi huo jambo ambalo sote tunapaswa kujivunia.

Nasema tunapaswa kujivunia kwa kuwa mchango wa mradi huo unalenga kuboresha Sekta nzima ya Madini jambo ambalo litapelekea Serikali na wadau kunufaika. Tumeelezwa kuwa, Awamu ya Kwanza imewanufaisha si tu wachimbaji wadogo bali pia Taasisi za Serikali ambazo zinahusika moja kwa moja katika kuhakikisha kwamba sekta ya madini inazidi kuimarika na kuchangia zaidi katika pato la Taifa.

Kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika Awamu ya kwanza ikiwemo kukamilishwa kwa idadi ya mapitio ya sheria muhimu zikiwemo sheria ya Uongezaji Thamani Madini ambayo inasubiri kupitishwa na Bunge , vilevile Sheria ya Madini ya mwaka 2010 na Kanuni zake iliyorekebishwa. Jambo hili limeelezwa kuwa linalenga katika kuimarisha utawala bora na uwazi katika sekta ya madini. Ni wazi kwamba, kutokana na mapitio hayo ya Sheria na kanuni za Madini, Serikali imeonesha dhamira ya dhati katika kuhakikisha kwamba sekta ya madini inazidi kupiga hatua zaidi ikiwemo kuhakikisha kwamba inachangia zaidi katika pato la Taifa na wananchi wake wananufaika na rasilimali madini.

Vilevile, katika kuhakikisha kwamba Serikali inapata mapato stahiki kutokana na shughuli za uchimbaji madini, awamu ya pili ya mpango huo itahakakikisha kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawezeshwa ili kuongeza makusanyo yatokanayo na shughuli hizo. Lakini pia ili kuchochea uwekezaji katika sekta hiyo Wizara kupitia SMMRP tumeelezwa imekamilisha zoezi la high resolution airbone geophysical survey na kufikia asilimia 12.5 ya nchi yote. Hayo pia ni mafanikio kwasababu utafiti huo umesaidia kufahamu strakicha za kijiolojia ambazo zilikuwa hazijulikani hapo awali kwa kugundua miamba yenye madini ya almasi, dhahabu na tanzanite.

Aidha, katika mipango itakayotelekezwa awamu ya pili ya mradi huo, Serikali imekusudia kuanzisha vituo bora saba vya mfano katika maeneo ambayo yana wachimbaji wadogo wa madini wengi nchini na kuelezwa kuwa, vituo hivyo vitanufaika kwa kuboresha teknolojia iliyopo ya uchenjuaji. Haya pia ni mafanikio mengine kutokana na kwamba, vituo hivyo vitawezesha wachimbaji kufuata njia bora za uchenjuaji na hivyo kuepuka matumizi ya zebaki na kuzingatia matumizi salama.

Lakini pia tumeelezwa kuwa, awamu ya kwanza ya Mradi ilifanikiwa kuimarisha kituo cha Tanzania Gemological centre- TGC na kukifanya kuwa kituo bora cha mafunzo Afrika Mashariki kwa ajili ya ukataji na unga’rishaji wa madini ya vito (lapidary), usonara; Utengenezaji wa bidhaa za mapambo na uchongaji wa vinyago vya mawe.

Kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza, wadau na Watanzania hatuna budi kuunga mkono jitihada hizi ili kuwezesha mipango na malengo ya Serikali yaliyopangwa katika awamu hii yatakelezwe kwa mafanikio zaidi.

Na Greyson Mwase, Morogoro

Imeelezwa kuwa Tanzania inatarajia kuzindua Dira ya Madini Tanzania ambayo ni sehemu ya Dira ya Madini Afrika iliyoasisiwa mwaka 2009 na wakuu wa nchi zenye madini Afrika

mapema Januari, 2016 lengo likiwa ni kuboresha sekta ya madini nchini.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Mradi wa Biofueli, Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele, katika warsha kuhusu Dira mpya ya madini Afrika iliyofanyika mjini Morogoro.

Warsha hiyo ya siku tatu iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini ilikutanisha wataalam kutoka taasisi za serikali ambazo ni Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais- Tume ya Mipango, Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).

Pia ilikutanisha wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na taasisi zake kama vile Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Uendelezaji Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Nchini (TEITI), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Chuo cha Madini Dodoma (MRI).

Kiwele alisema kuwa mnamo mwaka 2009 wakuu wa nchi za Afrika zenye madini walikutana na kuanzisha Dira ya Madini Afrika lengo likiwa ni kuongeza uwazi na kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya madini.

Alisema dira hiyo pia ililenga katika kuboresha sera na sheria za madini katika nchi husika ili kuhakikisha kuwa shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini zinafuata kanuni na sheria pamoja na usalama wa wananchi.

Aliongeza kuwa kutokana na umuhimu wa sekta za madini, gesi na mafuta nchini, Tanzania imeanza utekelezaji wa Dira hiyo kwa kuwa na Dira ya Madini Tanzania ambapo imeanza kutoa mafunzo kwa wataalam kutoka katika taasisi za serikali kuhusu upitiaji wa mikataba ya madini, gesi na mafuta ili kuweza kuipitia na kuishauri Serikali kabla ya kusainiwa na kuepuka

makosa katika uingiaji wa mikatabaAlisema ili kuhakikisha kuwa sekta

za madini, gesi na mafuta zinasimamiwa ipasavyo, Serikali imeanza kutoa mafunzo kwa wataalam wake ndani na nje ya nchi ili waweze kushiriki katika sekta hizo na kuepuka gharama ya kutumia wataalam waelekezi kutoka nje ya nchi.

Aliendelea kusema kuwa Serikali imeanza kuhamasisha wananchi waishio katika maeneo yenye rasilimali za madini na gesi kushiriki katika uchumi wa sekta hizo kwa kuuza bidhaa na kutoa huduma kwa wekezaji.

Alisisitiza kwa kutambua hilo, Serikali imeandaa sera ya uwezeshaji wa wazawa katika kuhakikisha kuwa wananchi wazawa wanashirikishwa katika uchumi wa sekta ya gesi na kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa nchi.

Alisema mbali na madini, dira hiyo inalenga pia rasilimali nyingine kama vile gesi, mafuta pamoja na jotoardhi ambapo itawanufaisha Watanzania kwa kuhakikisha kuwa sekta husika zinasimamiwa kulingana na Dira ya Madini ya Afrika.

Mratibu wa Mradi wa Biofueli, Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na mikakati ya Serikali katika uendelezaji wa sekta za nishati, madini, gesi na mafuta katika warsha ya kuhusu Dira ya Madini Afrika iliyofanyika mjini Morogoro na kuwakutanisha wataalam kutoka Taasisi za Serikali.

Page 4: MEM 86 ONLINE.pdf

4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Asteria Muhozya, Morogoro

Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), moja ya Taasisi iliyonufaika na utelekezaji wa

mradi wa awamu ya kwanza wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), umeeleza namna ilivyonufaika katika awamu hiyo, ikiwa ni pamoja na baadhi ya wachimbaji waliohudhuria warsha ya ufunguzi Awamu ya Pili ya mradi huo.

Akieleza zaidi kuhusu mafanikio hayo, Mtendaji Mkuu wa GST, Profesa Abdrulkarim Mruma alieleza kuwa, Serikali imekuwa ikiuwezesha Wakala huo kufanya kazi za utafiti na kuongeza kuwa, mradi wa SMMRP umesaidia kwa kiasi kikubwa na hivyo kuuwezesha wakala huo kufikia zaidi ya asilimia 18 ya maeneo yaliyofanyiwa tafiti za madini.

“Unajua shughuli za utafiti ni ghali sana na zinachukua muda mrefu, serikali imekuwa ikitusaidia kutekeleza tafiti zetu lakini SMMRP imetufanya tuongeze kasi zaidi ya kufanya tafiti za jiokemia na Jiofizikia”,alisema Prof. Mruma.

Naye mmoja wa wachimbaj wadogo wa kampuni ya Presicion ya Tanga, Debora Maimu alieleza kuwa, mradi wa SMMRP awamu ya kwanza umemuwezesha kuongeza idadi ya vifaa vya kukata na ku polish madini na hivyo kumwongezea uwezo wa kuzalisha zaidi.

“Mradi awamu ya kwanza umenisaidia sana kupanua soko na kujitangaza, awali nilikuwa sina uwezo wa kufanya hivyo. Nimefaidika na ninaweza kuyaelezea mafaniko yangu.”alisisitiza Maimu.

Kwa upande wake mchimbaji kutoka kampuni ya Kidee Mining Ltd ya Arusha, Allan, Mkitalu alieleza namna walivyonufaika na mradi wa awamu ya kwanza na kusema kuwa, walifaidika zaidi kwa kuwezeshwa kupata vifaa ambavyo wanavitumia katika shughuli za uchimbaji ambavyo vimewarahisishia utendaji kazi wao.

“Kwa kweli tumefaidika sana kwa kupata vifaa kupitia awamu ya kwanza ambavyo vimesaidia kuzifanya shughuli zetu za uchimbaji kuwa rahisi kuliko ilivyokuwa awali. Unajua uchimbaji unahitaji vifaa na uchimbaji ni vifaa, lakini bado kama wachimbaji tunahitaji kupata elimu zaidi za uchimbaji, naamini mradi wa pili utazingatia hilo.”alisema Mkitalu.

Awali akisoma taarifa kuhusu sekta ya madini, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje alieleza kuwa, zimekuwepo jitihada za kuwaelimisha wachimbaji wadogo ambapo mradi wa SMMRP ulifanikisha uandaaji wa miongozo kwa ajili ya mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika Nyanja za teknolojia ya uchimbaji na uchenjuaji madini, utunzaji wa mazingira, usalama na afya migodini na ujasiriamali katika masuala ya madini.

Pia, aliongeza kuwa, mradi umefanikiwa kununua vifaa vya kisasa ili kusaidia utendaji kazi kwa taasisi za serikali ikiwemo magari kwa ajili ya ofisi za kanda na zile za maafisa madini wakazi, Kituo cha

Jemolojia Tanzania (TGC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), GST, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Chuo cha Madini Dodoma (MRI).

Warsha hiyo ya ufunguzi wa Awamu ya Pili ya mradi wa SMMRP ilihudhuriwa na Ujumbe wa Benki ya Dunia, Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Makamishna Wasaidizi wa Madini, Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Maafisa wa Madini Wakazi, Asasi zisizo za Kiserikali, Wachimbaji wadogo na Makatibu Tawala kutoka wilaya za Mpanda, Geita, Butiama, Chunya, Lindi, Kyerwa, Bukombe ,Tunduru na Kahama.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, (GST), Profesa Abdrulkarim Mruma akiongea na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ambayo Wakala huo umepata katika utekelezaji wa SMMRP Awamu ya Kwanza. Uzinduzi wa Awamu ya mradi huo ilifanyika Morogoro hivi karibuni.

Mmoja wa wachimbaji wadogo wa Kampuni ya Presicion ya Tanga, Debora Maimu, alieleza kuwa, mradi wa SMMRP Awamu ya Kwanza. Maimu alieleza kuwa, mradi awamu ya kwanza umemuwezesha kuongeza idadi ya vifaa vya kukata na ku polish madini na hivyo kumwongezea uwezo wa kuzalisha zaidi.

Katibu Tawala wa Wilaya ya kahama, Mlele Ephrase akieleza jambo wakati wa kuchangia maoni na mapendekezo namna bora ambayo itasadidia mafanikio zaidi katika utekelezaji wa Mradi wa SMMRP Awamu ya pili. Wanaomsikiliza kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita, Gasto Kanyairita na kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Bukombe Paul Cheyo. Mbali na Makatibu Tawala hao, wengine waliohudhuria ufunguzi huo ni kutoka Wilaya za Mpanda, Geita, Butiama, Chunya, Lindi, Kyerwa, Tunduru na Kahama.

GST, Wachimbaji waeleza kunufaika na SMMRP

Page 5: MEM 86 ONLINE.pdf

5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

Serikali: Maslahi ya Kitaifa kwanzaNa Mohamed Saif

Serikali imeitaka Kamati ya Ufundi inayosimamia Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (Bulk Procurement Technical Committee)

kuepuka maslahi binafsi na badala yake kutanguliza maslahi ya Taifa mbele.

Wito huo umetolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Nishati Nchini, Mhandisi Hosea Mbise wakati wa kikao cha kwanza cha uzinduzi wa kamati hiyo.

Mhandisi Mbise aliitaka Kamati hiyo kuhakikisha kwamba masuala yenye maslahi ya kitaifa kwenye Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (BPS) yanazingatiwa ikiwa ni pamoja na usalama wa ugavi na hali ya dharura ambayo inaweza kuwa na athari kubwa kwenye upatikanaji wa bidhaa za mafuta.

Alisema jukumu kuu la kuundwa kwa Kamati hiyo ni kusimamia mchakato wa kuibadili Kampuni ya Uratibu wa Uagizaji wa Mafuta (PIC) kuwa Wakala wa Serikali (Bulk Procurement Agency) ambao utafanya

shughuli zake chini ya Wizara ya Nishati na Madini.

Kamati hiyo imeundwa kwa mujibu wa Kanuni ya Uagizaji wa Mafuta ya Mwaka 2013 ijulikanayo kama The Petroleum Bulk Procurement Regulations, 2013 ambayo inaelezea lengo la kuundwa kwake na kubainisha majukumu yake.

Aidha, kwa mujibu wa Kanuni hiyo, mwenye mamlaka ya kuteua wajumbe wa kamati hiyo ni Waziri wa Nishati na Madini.

Mhandisi Mbise alisema Kamati hiyo inaundwa na wataalamu kumi

(10) na huku Mwenyekiti wake akiwa ni Stanley Marisa ambaye ni Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia masuala ya Petroli.

Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria kikao hicho cha kwanza cha Kamati hiyo ni Anna Ngowi (Wizara ya Nishati na Madini), Magreth Chuwa (Wakala wa Vipimo na Mizani), Salum Bisarara (TAOMAC), Michael Mjinja (PIC), Vija Nair (Gapco), Orlando D’Costa (Augusta Energy) na Adam Elinewinga (Puma Energy).

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ufundi inayosimamia Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (Bulk Procurement Technical Committee) wakiendelea na kikao chao cha kwanza

Kamishna wa Nishati, Mhandisi Hosea Mbise (kushoto) akizungumza jambo. Kushoto kwake ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uratibu wa Uagizaji wa Mafuta (PIC), Michael Mjinja.

Mtwara, Lindi kupata mtambo wa MW 20Na Zuwena Msuya na Clinton Ndyetabula, Dar es Salaam

Serikali imesema itapeleka Mtwara mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi wa kiasi cha Megawati 20 kutoka Dar es salaam ili

kuimarisha upatikanaji wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara katika kipindi cha mwezi mmoja baada ya umeme wa gesi kuanza kutumika.

Hayo yalielezwa hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene wakati alipotembelea mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Simbachawene alisema kuwa mtambo huo wa kuzalisha umeme wenye uwezo wa kutembea kutoka eneo moja kwenda jingine utasaidia kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme wa uhakikika kwa wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara wakati huu ambapo mkoa wa Mtwara uko katika hatua nzuri ya

kuzalisha umeme wa Megawati Mia Sita (600).

“Baada ya umeme huu wa gesi kuanza kutumika, sasa Tanzania kuwa katika uchumi wa kati na ni busara kwa mikoa ya Mtwara na Lindi kuwa na umeme wa uhakika wajivunie uwepo wa rasilimali hiyo ndani ya ardhi yao ambayo inatumika nchi nzima, alisema Simbachawene.

Aidha, alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania kuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali pale Serikali inapoandaa miradi ya maendeleo kwa kuwa, yanatarajiwa kulinufaisha Taifa kwa ujumla.

“Watu wa Mtwara na Lindi bwana! Walikuwa wabishi lakini sasa hivi mambo ni mazuri kabisa! jamani watanzania tusipingane na maendeleo”, alisema Simbachawene.

Katika ziara hiyo, Waziri Simbachawene alitumia nafasi hiyo kuwataka wawekezaji kuwekeza kwa wingi katika miradi ya umeme.

Mtambo wa kuchata gesi asilia uliopo makao makuu ya TANESCO (Ubungo II Gas Plant) unaojulikana kwa jina la Symbion kama unavyoonekana pichani.

Page 6: MEM 86 ONLINE.pdf

6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), Awamu ya pili unatarajiwa kuwa

na manufaa zaidi katika sekta ya madini kutokana na malengo na mipango ya mradi huo ikiwemo kuhakikisha kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawezeshwa ili kuhakikisha inaingiza masuala ya uchimbaji mdogo katika mfumo wa kodi.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha mada ya namna mradi wa awamu ya pili utakavyotekelezwa, Meneja Mradi wa SMMRP, Mhandisi Idrisa Katela, alisema kuwa, utekelezaji wa Awamu hiyo unalenga masuala kidhaa ambayo yatawezesha kuimarisha na kuendeleza sekta, ikiwemo kuanzisha vituo bora vya mfano katika maeneo ambayo yana wachimbaji wadogo wengi wa madini ili vituo hivyo vinufaike katika kuboresha teknolojia iliyopo ya uchenjuaji.

Aliitaja mikoa ambayo vituo hivyo vinakusudiwa kujengwa kuwa ni pamoja na Mara, Mbeya, Geita, Kagera, Simiyu, Ruvuma, Lindi na Katavi na kuongeza kuwa, ili kuhakikisha kwamba senta hizo zinakuwa na tija, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) litasimamia uendeshaji wa vituo hivyo ikiwemo kutoa huduma za kitaalamu kwa wachimbaji pale zitakapohitajika.

Aidha, aliongeza kuwa, Kituo cha Jemolojia Tanzania, (TGC) kitaendelea kuwezeshwa ili kukifanya kuwa kituo kikubwa na bora katika Ukanda wa Afrika Mashariki kwa kutoa mafunzo , ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito.

Akizungumzia suala la ruzuku, Katela alisema, mradi utatoa ruzuku wa wachimbaji wadogo na Taasisi za Kijamii zinazojishughulisha na shughuli zinazokwenda sambamba na masuala ya uchimbaji ili kuwawezesha kukuza shughuli za uchimbaji, kuwezesha uongezaji thamani, kupata ujuzi zaidi.

Vilevile, aliongeza kuwa, awamu ya pili ya mradi imekusudia kuhamasisha jamii zinazozunguka maeneo ya migodi na ambazo zimeathirika na shughuli za uchimbaji kuanzisha kazi mbadala tofauti na zile za uchimbaji mdogo.

“Tumefanikiwa katika awamu ya kwanza, lakini sisi kama wadau, tunatakiwa kusimamia kikamilifu utelekezaji wa mradi huu kuhakikisha kwamba wachimbaji wananufaika na kuchangia zaidi katika pato la taifa lakini wakati huo, watanzania na halmashauri pia zinanufaika na pia kuiwezesha sekta kupiga hatua zaidi,” alisisitiza Katela.

“Nina imani kuwa, nyongeza

ya jumla ya kiasi cha dola za kimarekani milioni 50 inatarajia kuleta mafanikio katika sekta ya madini, kwa kuwa inatarajia kusaidia kuboresha faida zitokanazo na sekta ya madini nchini hususan kwa wachimbaji wadogo.

Aidha, aliongeza kuwa, mradi huo utalenga kufungamanisha sekta ya madini na sekta nyingine za kiuchumi, kuboresha rasilimali katika sekta husika, kuongeza uwazi na uwajibikaji kwa kusaidia utekelezaji wa sera na sheria ya madini.

Akichangia katika warsha hiyo, mwakilishi wa Benki ya dunia na mjumbe wa masuala ya SMMRP, Rachel Perk alieleza changamoto ya kuhakikisha kuwa, wanawake wanashirikishwa kikamilifu katika sekta na kuongeza, “mafanikio makubwa yamepatikana katika awamu ya kwanza lakini tunatarajia mafanikio zaidi ikiwemo ushiriki mkubwa zaidi wa wanawake katika sekta, tunatarajia kutakuwa na maboresho zaidi katika awamu hii ikiwemo kuhakikisha kwamba taifa linanufaika zaidi kupitia sekta hii,” alisema Perk.

Warsha hiyo ya ufunguzi wa Awamu ya Pili ya mradi wa SMMRP ilihudhuriwa na Ujumbe wa Benki ya Dunia, Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Makamishna Wasaidizi wa Madini, Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Maafisa wa Madini Wakazi, Asasi zisizo za Kiserikali, Wachimbaji wadogo na Makatibu Tawala kutoka wilaya za Mpanda, Geita, Butiama, Chunya, Lindi, Kyerwa, Bukombe ,Tunduru na KahamaB

SMMRP Awamu ya pili, mikakati kabambe>>> Kuanzisha vituo saba vya mfano , TRA kuhusishwa

Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), Mhandisi Idrisa Katela akieleza jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu mpango wa Utekelezaji wa SMMRP awamu ya pili katika warsha ya ufunguzi wa mradi huo iliyofanyika hivi karibuni mjini Morogoro.

Mwakilishi wa Benki ya Dunia (WB) na mjumbe wa Mradi wa SMMRP, Rachel Perk alieleza jambo wakati wa ufunguzi wa Mradi wa SMMRP Awamu ya pili. Wanaomsikiliza kutoka kulia ni Meneja wa Mradi wa SMMRP, Idrisa Katela, Mwakilishi na Kiongozi wa Mradi wa SMMRP, Benki ya Dunia Mamadou Barry, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava na Kaimu Kamishna wa Madini, Ally Samaje.

Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Wachimbaji Wadogo Julius Sarota akieleza jambo wakati wa ufunguzi wa mradi wa SMMRP awamu ya pili. Anayemfuatilia (kushoto ni Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Assah Mwakilembe. Wengine ni washiriki wa warsha hiyo

Sehemu ya Washiriki wa warsha ya ufunguzi wa Mradi wa SMMRP Awamu ya pili, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyoendelea wakati wa ufunguzi a warsha hiyo.

Page 7: MEM 86 ONLINE.pdf

7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

WARSHA KUHUSU DIRA YA MADINI AFRIKA

Washiriki kutoka Taasisi za Serikali wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa kwa nyakati tofauti na watoa mada (hawapo pichani)

Mtaalam kutoka Kitengo cha Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Philipo James akielezea utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal) kwenye warsha kuhusu Dira ya Madini Afrika iliyofanyika leo mjini Morogoro. Warsha hiyo iliyokutanisha watalaam kutoka Taasisi za Serikali, ililenga kuwajengea uwezo kuhusu sekta ya madini nchini.

Wajumbe kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia na kunukuu kumbukumbu za mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa

Mtaalam kutoka Kitengo cha Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Philipo James akisisitiza jambo katika warsha hiyo

Mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Sehemu ya Nishati Jadidifu Mhandisi Styden Rwebangila akipitia mada mbalimbali kabla ya kuwasilishwa katika warsha hiyo.

Page 8: MEM 86 ONLINE.pdf

8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Baadhi ya Washiriki wa warsha ya ufunguzi wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Awamu ya Pili wakibadilishana mawazo baada ya ufunguzi wa warsha hiyo iliyofanyika Mjini Morogoro na kuhuduhuriwa na Ujumbe wa Benki ya Dunia, Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Makamishna Wasaidizi wa Madini, Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Maafisa wa Madini Wakazi, Asasi zisizo za Kiserikali, Wachimbaji wadogo na Makatibu Tawala kutoka wilaya za Mpanda, Geita, Butiama, Chunya, Lindi, Kyerwa, Bukombe ,Tunduru na Kahama.

Baadhi ya Washiriki wa warsha ya ufunguzi wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), Awamu ya Pili wakifuatilia jambo wakati wa ufunguzi huo.

Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia na Kiongozi wa Mradi wa SMMRP, Mamadou Barry akiwasilisha mada wakati wa warsha ya ufunguzi wa Mradi wa SMMRP, Awamu ya Pili.

Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Mhandisi Subian Chilangwire akieleza jambo wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo. Chuo cha Madini Dodoma ni miongoni mwa Taasisi ambazo zilinufaika kwa kununuliwa vifaa na Mradi wa SMMRP, Awamu ya Kwanza.

WARSHA YA UFUNGUZI WA MRADI WA SMMRP AWAMU YA PILI

Page 9: MEM 86 ONLINE.pdf

9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

Baadhi ya Washiriki wakifuatilia warsha ua ufunguzi wa Mradi wa SMMRP Awamu ya Pili, kutoka Kushoto ni Mkuuu wa Kitengo cha Mazingira, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Gidion Kasege, Kamishna Msaidizi wa Madini, Songea, Mhandisi Victor Mahobe na Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

WARSHA YA UFUNGUZI WA MRADI WA SMMRP AWAMU YA PILI

Meza Kuu pamoja na washiriki wengine wa warsha ya ufunguzi wa Mradi wa SMMRP Awamu ya pili wakifutilia uwasilishaji wa mada wakati wa warsha hiyo.

Baadhi wa Wajumbe ya Sekretarieti ya warsha ya ufunguzi wa Mradi wa SMMRP Awamu ya pili wakiendelea na majukumu yao wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo.

Mshehereshaji wa warsha ya ufunguzi wa Mradi wa SSMRP awamu ya Pili, Mhandisi, Assah Mwakilembe (aliyesimama) akiongea jambo wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo. Wengine wanaomsikiliza Meza Kuu , kutoka kushoto ni Meneja Mradi wa SMMRP, Mhandisi Idrisa Katela, Mwakilishi na Kiongozi wa Mradi wa SMMRP Benki ya Dunia, Mamadou Barry, Kaimu Katibu Mkuu , Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje na Mjumbe wa Mradi wa SMMRP Benki ya Dunia Rachel Perk.

Page 10: MEM 86 ONLINE.pdf

10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Watanzania tujivunie Mradi wa Gesi-SimbachaweneNa Zuwena Msuya na Clinton Ndyetabula, Dar es Salaam

Waziri wa Nishati na Madini George S i m b a c h awe n e a m e s e m a W a t a n z a n i a

wanahaki ya kujivunia kuwa na mradi mkubwa na wa kwanza wa umeme wa gesi tangu nchi ipate uhuru kutokana na hazina ya gesi asilia iliyogunduliwa nchini.

Simbachawene alisema hayo hivi karibuni jijini Dare Es Salaam alipotembelea mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi ya Ubungo ambayo inapokea gesi inayozalisha umeme kutoka Kinyerezi I na kuuingiza katika gridi ya Taifa.

Alisema wakati wa michakato na mipango ya kutekeleza mradi huo likiwemo bomba la kusafirisha gesi kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara inaanza, changamoto nyingi zilijitokeza, lakini Serikali kwa kutambua umuhimu wa rasilimali hiyo kwa wananchi wake na Taifa kwa ujumla ilisimama imara hadi kufanikisha mradi huo ambayo sasa matunda yake yanaonekana.

“Mradi huu wakati unanza kulikuwa na sarakasi za kila aina, fujo pamoja na vurugu, vitimbwi na vitisho vya kila aina ili kukatisha tamaa, lakini Serikali ilikuwa na misimamo thabiti na kusimama kitede na hatimaye leo hii umeme wa Mtwara unaangaza nchini nzima,” alisema Simbachawene.

Alifafanua kuwa, kwa sasa zoezi la uingizaji wa umeme huo katika gridi ya Taifa unafanyika kwa awamu na utakamilika baada ya mwezi mmoja kutegemea na msukumo wa gesi unavyoendelea kuimarika kwenye bomba jipya; zoezi hilo litaendelea hadi litakapo kamilika kabisa baada ya msukumo wa gesi kwenye bomba

kufika kiwango cha 55 kwa kipimo cha Bars.

Halikadhalika, Simbachawene aliweka wazi kwamba baada ya kuwasha Megawati 90 kwa mitambo ya ubungo II na Symbion, kinachufuata ni kuwasha mtambo wa Symbion wa megawati 20, kisha megawati 40 wa Symbion, ukifuatiwa na mtambo wa megawati 75 wa Kinyerezi, baadaye mtambo wa Ubungo II wa megawati 35 na hatimaye kuwasha mitambo ya Kinyerezi ya Megawati 75 na kutoa jumla ya Megawati 335.

Aidha amewapongeza watanzania kwa kuwa na moyo wa uvumilivu na kuwaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza wakati wote wa zoezi la majaribio ya kusukuma gesi kutoka Mtwara hadi Kinyerezi Dar es Salaam na baadaye umeme kuingizwa katika gridi ya Taifa na kwamba waendelee kuiamini Serikali yao kwani ni sikivu na inalengo la kuboresha maendeleo ya wananchi wake na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba alisema kuwa, mara baada ya kuwasha umeme huo wa gesi mitambo iko katika hali nzuri na hakuna hitilafu yoyote ya kiufundi iliyojitokeza kutokana na zoezi hilo.

“Kwakweli hali ya mitambo ni nzuri tumejiridhisha, zoezi hili litaendelea kama ilivyokusudiwa na ndani ya mwezi mmoja tunaimani tutafanikisha zoezi hili ili watanzania waondokane kabisa na tatizo la kukatika kwa umeme,” alisema Mhandisi Mramba.

Mradi wa mradi mkubwa wa umeme wa gesi iliwemo bomba la kusafirisha gesi kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara umegharimu Dola za Marekani bilioni 1.22 tangu kuanzishwa hadi kukamilika kwake.

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mpango wa Mabadiliko Makubwa Sasa (BRN) wa Wizara ya Nishati na Madini, Juma Mkobya, (kulia) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (wakwanza kushoto) wakati wa ziara yake ya siku mmoja Makao Makuu ya (TANESCO)

Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene akiwaeleza waandishi wa habari pamoja na wajumbe wengine juu ya mtambo

Wajumbe kutoka Taasisi mbalimbali pamoja na waandishi wa habari wakiambatana na Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene wakati wa ukaguzi wa mitambo ya kuchakata gesi asilia ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Page 11: MEM 86 ONLINE.pdf

11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

Na Jacqueline Mattowo-STA-MIGOLD

Kampuni ya STAMIGOLD kupitia mgodi wake wa dhahabu wa Biharamulo uliopo wilayani Biharamulo

Mkoani Kagera hivi karibuni umefanikisha zoezi la upimaji wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi kwa wanawake zaidi ya 200 waishio vijiji vya Mavota na Mkunkwa vilivyopo takribani kilomita 7 kutoka eneo la mgodi.

Zoezi la upimaji lilifanyika katika zahanati ya kijiji cha Mavota kwa muda wa siku tatu chini ya wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI) Kanda ya Mwanza kwa kushirikiana na Madaktari wa kliniki ya mgodi.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya zoezi la upimaji kuhitimishwa, Meneja Mkuu wa mgodi huo, Mhandisi Dennis Sebugwao alisema kuwa uwezeshaji wa upimaji huo ni sanjari na utaratibu uliowekwa na kampuni wa kujali afya za wafanyakazi wake.

“Kampuni inajali sana afya za wafanyakazi wake na katika kutekeleza hilo tuliamua kufanya

utaratibu wa upimaji wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi mara baada ya wazo hilo kutolewa na wafanyakazi wanawake hapa mgodini mnamo mwezi Mei mwaka jana,” alisema.

Alisema kuwa Mwaka jana baadhi ya wafanyakazi waliopimwa walikutwa na matatizo na hivyo kuona kwamba kuna umuhimu wa kufanya vipimo mara kwa mara.

“Hilo lilitufanya tufikirie kuwa yawezekana kuna wanawake katika jamii zinazozunguka mgodi wenye matatizo kama hayo hivyo kupata wazo la kuwaleta UMATI kwa awamu nyingine ambapo kama kampuni tulidhamiria kufanya vipimo hivyo kwa wanawake 500 waishio jirani na mgodi,” alisema.

Kwa upande wake Mtaalam wa magonjwa ya saratani ya matiti na mlango wa kizazi Milka Eyembe kutoka UMATI alisema kuwa kuna aina nyingi za saratani lakini takwimu zinaonyesha saratani ya mlango wa kizazi ndio saratani ya kwanza inayoongoza kusababisha vifo kwa wanawake wengi hapa nchini.

“Ningependa kutoa ushauri kwa akina mama kujiwekea utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili kugundua mapema pale kunapokuwa na tatizo hili kwani

kina mama wengi hugundua wana matatizo tayari saratani ikiwa imesambaa na kuwa katika hatua ambayo matibabu yake ni magumu na ya gharama kubwa hivyo kusababisha vifo,” alisema Eyembe.

Eyembe aliongeza kuwa jumla ya wanawake 221 kutoka vijiji vya Mavota na Mkunkwa walifanyiwa vipimo vya saratani ya matiti na mlango wa kizazi pamoja na vipimo vya virusi vya UKIMWI (VVU) ambapo kati ya wanawake hao waliopimwa, wanawake 10 waligundulika wana dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi na kupatiwa matibabu na mmoja aliyegundulika kuwa na saratani aliandikiwa barua kwenda Hospitali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza.

Mmoja wa akina mama walionufaika na zoezi la upimaji, Elda Cleophace mkazi wa kijiji cha Mavota , aliishukuru kampuni ya STAMIGOLD kwa kufanikisha zoezi hilo na kukiri kuwa tangu azaliwe hajawahi kufanya vipimo hivyo wala kusikia huduma hiyo

kufanyika katika kijiji cha Mavota. “Hapa kijijini ulienea uvumi

ambao uliwafanya wanawake wasipime lakini nawashauri kina mama wenzangu ambao walisita kujitokeza na wanawake wote kupuuza uvumi wa aina hii na kujitokeza kupimwa afya zao. Naomba mgodi uwe unatuletea huduma kama hizi mara kwa mara kwani zinasaidia kutambua afya zetu” Alieleza Bi. Cleophace.

Zoezi la upimaji lilihitimishwa katika kliniki ya mgodi ambapo jumla ya wanawake 8 walijitokeza kupima miongoni mwao wakiwa wafanyakazi wapya na wengine waliokuwa wanarudia zoezi la upimaji kutokana na kukutwa na dalili za awali za ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi mnamo mwaka jana ambapo kitaalam mgonjwa hushauriwa kurudia vipimo kuangalia matokeo ya matibabu baada ya mwaka mmoja na wote waliorudia walithibitika kupona.

STAMIGOLD yafanikisha upimaji wa saratani kwa wanawake zaidi ya 200

Rebeca Peter (kushoto) akizungumza na Mtaalam wa magonjwa ya saratani ya matiti na mlango wa kizazi. Kulia ni Mtaalamu kutoka UMATI, Milka Eyembe wakati wa zoezi la upimaji katika Kliniki ya mgodi.

Mkazi wa kijiji cha Mavota, Restuta Paskali akielezea waandishi wa habari namna alivyonufaika na zoezi la upimaji wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi lililofanyika katika Zahanati ya kijiji cha Mavota kwa msaada wa STAMIGOLD.