MEM 107 Online.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

  • Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    Habari za nisHati &madini

    Toleo No. 107 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Februari 18 - 24, 2016

    BulletinNews

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    http://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI &MADINI

    Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

    JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

    Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

    Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

    Wabunge Soma habari Uk. 2

    Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

    WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2Kampuni 300 zakutana na Profesa Muhongo

    MAGAMBA COAL LIMITEDSARA MASASI

    SINOTAN RENEWABLE ENERGYSUPER GROUP OF COMPANIES

    n Nia ni uwekezaji umeme

    Mkurugenzi Mkuu wa Super Group of Companies ambayo ni kampuni mama ya Kagera na Mtibwa Sugar Ltd, Seif Seif akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na kampuni hiyo.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza Mwenyekiti wa Kampuni ya Sinotan Renewable Energy, Alex Lema alipokuwa akielezea kuhusu mradi wa umeme wa upepo wa Makambako.

    Mwenyekiti wa kampuni ya Magamba Coal Limited, Jenerali Mstaafu Robert Mboma (katikati) akieleza jambo wakati wa mkutano na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto). Lengo lake ni kuwekeza katika kuzalisha umeme kwa makaa ya mawe.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa katika kikao na Bi.Sara Masasi aliyeambatana na Ujumbe wake kueleza nia yake ya kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 300 kutokana na Makaa ya Mawe ifikapo mwaka 2019.

  • BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Kampuni 300 zakutana na Prof. Muhongo

    Ili kutekeleza juhudi za Serikali za kutokomeza umaskini nchini, Serikali kwa kupitia Wizara ya Nishati na Madini imepanga kuongeza uzalishaji wa umeme

    kwenye gridi ya Taifa hadi kufikia Megawati 5,000 ifikapo mwaka 2020, na hatimaye Megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025, ili Tanzania iweze kufikia uchumi wa kati.

    Ili kuwezesha mipango hiyo, Wizara kuanzia mwanzoni mwa mwezi wa Februari mwaka huu, ikiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo imekuwa ikikutana na makampuni mbalimbali ya wawekezaji kutoka duniani kote, ili kusikiliza mapendekezo ya miradi yao ya uwekezaji katika sekta ya Nishati nchini kwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwemo upepo, jua, maji, mawimbi ya bahari, makaa ya mawe, gesi asilia na bayogesi.

    Ili kuwa na uelewa wa pamoja kati

    ya Wizara na Taasisi zake, Wawakilishi kutoka taasisi zilizo na zisizo chini ya Wizara ambazo ni, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) pamoja na Baraza la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira nchini (NEMC) walihudhuria.

    Profesa Muhongo amekuja na aina hii ya mazungumzo ya pamoja yanayohusisha Taasisi mbalimbali ili kupunguza urasimu kwa wawekezaji wa kuomba kukutana na taasisi hizo moja baada ya nyingine na badala yake wanakutanishwa kwa pamoja ili majadiliano hayo yaende kwa haraka na ufanisi zaidi.

    Katika kipindi cha takribani

    Wiki Mbili, Profesa Muhongo pamoja na watendaji wa Wizara na Taasisi wamekutana na kufanya mazungumzo na wawekezaji zaidi ya 300 kutoka kampuni za nje na ndani ambazo kati yake kuna wawekezaji wapya na wale waliokwisha anza utekelezaji wa miradi yao.

    Ili kuendana na kasi ya uongezaji wa nishati ya umeme nchini, Profesa Muhongo ameziagiza Taasisi zitakazoshiriki katika majadiliano na kampuni zilizoonyesha nia kuwekeza kuhakikisha kuwa majadiliano hayo yanafanyika ndani ya mwezi mmoja na si zaidi ya hapo.

    Wawekezaji wapya waliojitokeza waliweza kupata ushauri na muongozo kutoka taasisi hizo kuhusu jinsi ya kuanza miradi hiyo ili waweze kufikia maamuzi juu ya uwekezaji wao, huku wawekezaji walioanza kazi wakitathminiwa kuhusu maendeleo

    yao na changamoto wanazokumbana nazo na kujua jinsi gani Wizara inaweza kuwasaidia kusonga mbele kwa kutafutiwa ufumbuzi.

    Akizungumza katika mikutano mbalimbali na wawekezaji hao, Profesa Muhongo alisisitiza kuwa licha ya Serikali kuhitaji wawekezaji hao ili kuongeza kiasi cha umeme nchini lakini mwisho wa mikutano hii Serikali itaandaa kabrasha litakaloorodhesha kampuni zote zilizoonyesha nia ya kuwekeza na litawasilishwa katika taasisi mbalimbali za kifedha kwa ajili ya kuombewa fedha za utekelezaji hasa katika hatua ya upembuzi yakinifu.

    Profesa Muhongo amesisitiza kuwa nia ya serikali ni kufikia asilimia 75 ya wananchi wanaopata umeme ifikapo mwaka 2025 kutoka asilimia 40 ya sasa na kuongeza kiasi cha umeme katika gridi ya taifa kutoka Megawati 1,500 hadi 10,000 ifikapo 2025.

    Na Nuru Mwasampeta, Dar es Salaam.

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameitaka kampuni ya Sino-Tan Renewable

    Energy inayotaka kuzalisha umeme wa upepo katika eneo la Makambako Mkoani Njombe kuihakikishia Serikali kuwa ina uwezo wa kutekeleza mradi huo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia tarehe 15 Februari hadi 15 Machi 2016.

    Maagizo hayo yametolewa ofisini kwake wakati wa kikao baina ya Wizara na Kampuni hiyo iliyofika wizarani ili kueleza changamoto inazokumbana nazo katika kutekeleza mradi huo wa kuzalisha Megawati 100 za umeme.

    Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Alex Lema alisema upo mgogoro wa kuachia ardhi katika Kijiji cha Mtewele wilaya ya Wangingombe pamoja na kwamba halmashauri husika ilishatoa kibali kwa kampuni hiyo kutumia ardhi husika.

    Lema alieleza kuwa theluthi mbili

    za eneo la mradi zinapatikana katika wilaya ya Makambako wakati theluthi moja inayobaki ipo katika Wilaya ya Wangingombe ambako hasa ndiko kwenye mgogoro huo.

    Aidha Lema alitumia fursa hiyo kuiomba Wizara ya Nishati na Madini kuwa kiungo katika kuhakikisha mradi unafanikiwa kwa kuwashirikisha wadau wengine ambao ni Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbunge wa eneo husika pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wangingombe.

    Baada ya maelezo toka kwa Mwenyekiti huyo, Prof. Muhongo alimtaka Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Nishati Jadidifu, Edward Ishengoma kuteua

    maafisa wawili ili kufika katika eneo lenye mgogoro na kujionea sababu za wanakijiji hao kupinga eneo hilo kutumiwa na mradi huo na kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku mbili za ufuatiliaji.

    Aidha, Prof. Muhongo ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imebadili namna yake ya utendaji na kuwataka wawekezaji hao kuwasilisha mpango kazi wao ndani ya mwezi mmoja kutokana na uhitaji mkubwa wa nishati ya umeme wa kutosha na wa uhakika.

    Sino-Tan Renewable Energy yatakiwa kuonesha uwezo wa kuzalisha umeme

    Mwenyekiti wa Kampuni ya Sinotan Renewable Energy, Alex Lema akizungumza kuhusu utekelezaji wa mradi wa umeme wa upepo mjini Makambako.Wengine katika picha ni watendaji wa Wizara na Taasisi zinazohusiana na masuala ya nishati waliofika katika kikao hicho.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akifuatilia maelezo ya Mkurugenzi wa Kampuni inayowekeza katika umeme wa upepo mjini Makambako, Luka Buljani alipokuwa akitoa maelezo kuhusiana na mradi huo.

    2

  • 3BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    Five Pillars oF reForms

    KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano

    Bodi ya uhariri MharIrI Mkuu: Badra Masoud

    MsaNIFu: Lucas GordonWaaNdIshI: Veronica simba, asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed saif, rhoda James ,

    Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

    increase eFFiciencyQUality delivery

    oF Goods/servicesatisFaction oF

    tHe clientsatisFaction oF

    BUsiness Partners

    satisFaction oF sHareHolders

    tel-2110490FaX-2110389

    moB-0732999263

    Karibuni muwekeze katika Umeme

    tel-2110490FaX-2110389

    moB-0732999263

    Kampuni ya CHICO kutumbuliwa jipu isipokamilisha kusambaza umeme

    Ni takriban wiki mbili sasa kutoka tarehe 8 hadi 18 Februari Mwaka huu kuanzia bwawa la kuzalisha umeme Mtera na Dar es Salaam, ambapo Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiwa na watendaji wa Wizara pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini na taasisi nyingine wakiwamo TANESCO, TPDC, EWURA, STAMICO, NDC, TIC na NEMC walikutana na wawekezaji mbalimbali kuanzia wadogo hadi wakubwa, lengo likiwa ni kupata wawekezaji katika Sekta ya Nishati na hatimaye kuzalisha umeme.

    Prof. Muhongo alikutana na takriban Wawekezaji 300 walijitokeza kwa lengo la kufahamu taratibu mbalimbali za uwekezaji katika sekta hiyo ya umeme ambapo pamoja na mambo mengine, Wizara iliwaeleza taratibu za uwekezaji ikiwemo vyanzo vya umeme vilivyopo nchini.

    Vyanzo hivyo ni pamoja na Makaa ya mawe, maji, gesi, mawimbi ya bahari, joto ardhi, upepo, jua, mawimbi ya bahari, bayogesi na mabaki ya taka vyanzo vyote hivyo vipo katika maeneo mbalimbali hapa nchini na kwamba kinachohitajika ni mitaji, teknolojia kwa makampuni yenye nia ya kuwekeza.

    Yapo Makampuni yaliyoonyesha nia ya kutaka kuwekeza haraka iwezekanavyo na kwamba wapo tayari kwa mazungumzo ambapo Waziri aliwataka watendaji wa Makampuni yanayohusika ikiwamo TANESCO akiwa kama mnunuzi wa umeme, TPDC mwenye dhamana na nishati ya gesi, STAMICO mwenye dhamana ya kusimamia Makaa ya mawe na EWURA mwenye dhamana ya kupanga bei ya umeme na gesi kuhakikisha kwamba wanafanya mazungumzo ya kitaalamu na kuwasilisha taarifa kwa Waziri wa Nishati ifikapo Machi mwaka huu.

    Tunasema hiyo ni hatua nzuri aliyoionyesha Prof. Muhongo katika kuhakikisha maendeleo katika sekta ya Nishati yanafikiwa na hasa ikizingatiwa kwamba Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Pombe Magufuli amekuwa akisisitiza kuingia katika uchumi wa Viwanda.

    Ni jambo lililowazi kwamba unapozungumzia ukuaji wa viwanda katika taifa lolote duniani lazima uende sambamba na ukuaji wa sekta ya Nishati ambapo lazima kuwe na umeme wa uhakika na wa kutosha.

    Ili sekta ya umeme ikue hatuna budi kujikita zaidi katika kufanya kila linalowezekana kujenga mitambo ya kuzalisha umeme, kujenga miundombinu ya usafirishaji umeme na miundombinu ya usambazaji umeme ambapo uwekezaji wake kwa namna moja ama nyingine ni gharama kubwa ndiyo maana wizara iliona na vizuri kushirikisha pia sekta binafsi kufanya hivyo.

    Lengo hili la Wizara ni zuri katika kufikia pia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, kuifanya nchi yetu kufikia kipato cha Kati ambapo wawekezaji na Makampuni binafsi wakijitokeza katika kuwekeza katika umeme kwa vyovyote vile kiasi cha umeme katika gridi ya taifa kitaongezeka pamoja na miundombinu mingine ya umeme pia itaongezeka.

    Aidha, ni wazi kuwa upatikanaji wa umeme wa kutosha na wa uhakika utachochea uwekezaji wa viwanda na kupanua wigo wa ajira, kuongezeka kwa pato la taifa na hatimaye uchumi wa Tanzania kukua.

    Kwetu sisi tunasisitiza na kutoa wito wawekezaji wote walionyesha nia ya kuwekeza katika uzalishaji wa umeme kujenga mitambo hiyo nje ya Mkoa wa Dar es Salaam kwani kwa sasa Mkoa huo ndiyo wenye mitambo mingi ya uzalishaji umeme kuliko mikoa mingine nchini.

    Vilevile, Wizara inashauri uwekezaji wa mitambo ya kuzalisha umeme pia kuangalia mikoa ya Kusini hususan Lindi na Mtwara na hasa wale wanaolenga kutumia chanzo cha gesi asilia katika kuzalisha umeme.

    Kwa mara nyingine tena tunasema karibuni wawekezaji muwekeze katika umeme.

    Na Veronica Simba - Igunga

    Serikali imeiagiza Kampuni ya Chico iliyopewa tenda ya kusambaza umeme katika Mkoa wote wa Tabora kuhakikisha inakamilisha kazi hiyo kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili

    mwaka huu, la sivyo itachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwa kuipotezea muda Serikali.

    Vilevile, Kampuni hiyo italazimika kurejesha baadhi ya fedha ilizolipwa ili ibaki na malipo yanayolingana na kazi itakayokuwa imefanyika kufikia muda huo.

    Hayo yalisemwa Jumanne ya wiki hii, Februari 16, 2016, wilayani Igunga, mkoani Tabora na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akiwa katika ziara ya kikazi kukagua miradi mbalimbali ya Sekta za Nishati na Madini inayotekelezwa chini ya wizara yake.

    Kalemani alimpatia siku moja, Meneja wa Kanda husika wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika eneo hilo, kuhakikisha wanampatia taarifa ya lini Mkandarasi huyo atakamilisha kazi yake.

    Nimesikia malalamiko mengi kuhusu Mkandarasi huyu. Mbali ya kuwa nimeagiza akamilishe kazi yake kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili, nataka kufikia kesho mnipe taarifa rasmi ni lini atakamilisha kazi hiyo na taarifa hiyo ikijigongagonga, tutaondoka na mtu hapa, alisisitiza Naibu Waziri.

    Pia, Dkt. Kalemani alisema anataka kujua kiasi cha fedha alicholipwa Mkandarasi huyo ili iweze kulinganishwa na kazi aliyofanya. Kama itadhihirika tumemlipa kiasi kikubwa kisichoendana na kazi aliyofanya, tutamdai, alisema Dkt. Kalemani.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akisalimiana na baadhi ya Viongozi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Igunga alipowasili wilayani humo hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Wizara yake. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Zipollah Pangani.

    >>Inaendelea Uk. 4

  • 4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kalemani aliwataka Mameneja wa TANESCO na REA wa eneo hilo kumpatia taarifa ya kina kabla hajaondoka mkoani humo kwa nini zoezi la kuunganisha umeme wa REA Awamu ya Pili katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo linasuasua.

    Mathalani, kwa mujibu wa taarifa mliyowasilisha hapa, wilaya ya Nzega, hakuna hata mteja mmoja aliyeunganishiwa umeme. Lakini hata wilaya ya Igunga, waliounganishiwa ni wachache sana, hawafikii hata asilimia 50. Urambo vilevile, alisema.

    Dkt. Kalemani alisema kwa mujibu wa taarifa iliyopo, wananchi waliounganishiwa umeme wa REA Awamu ya Pili mkoani humo ni 5,000 ambao ni chini ya asilimia 20 ya malengo.

    Aliwataka wahusika watafakari kwa namna hiyo, itawezekanaje kufikia malengo ya Serikali ya kuwaunganishia umeme asilimia 75 ya wananchi ifikapo mwaka 2025.

    Naibu Waziri aliwataka watendaji wa REA kuhakikisha wanamsimamia ipasavyo Mkandarasi ili kuhakikisha kuwa ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili, kama alivyoagiza awali, shughuli zote za ujenzi

    na kuunganishia umeme wateja ziwe zimekamilika, ili miezi miwili inayobaki kufikia Juni, ambao ndiyo muda rasmi uliopangwa kukamilisha miradi ya REA Awamu ya Pili, zifanyike kazi za marekebisho madogo madogo.

    Aliagiza wananchi wote ambao wanastahili kuunganishiwa umeme wa REA kwa Awamu ya Pili, wawe wameunganishiwa kufikia mwishoni mwa mwezi huo wa Aprili. Hatuwezi kuingia REA Awamu ya Tatu pasipo kukamilisha ipasavyo Awamu ya Pili.

    Akizungumzia malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kuhusu baadhi ya vijiji kurukwa bila kuunganishiwa umeme na nguzo kupitishwa pembeni, Naibu Waziri aliwataka Watendaji husika wa TANESCO na REA kuhakikisha wanashughulikia suala hilo na kumpatia taarifa kabla ya kumaliza ziara yake ya siku tatu mkoani humo.

    Aliwaagiza wampatie orodha ya majina ya vijiji vilivyorukwa bila kupatiwa umeme na waeleze ni kwa nini vilirukwa. Pia, aliwataka waeleze vijiji hivyo viko kwenye mpango upi wa kupatiwa umeme, ili kama havikuwepo kwenye Mradi wa REA Awamu ya Pili, viingie katika Mradi huo Awamu ya Tatu.

    Alisisitiza kuwa Serikali haitakubali

    kuona wananchi wake wanakosa huduma ya umeme kwa sababu ya uzembe wa watu wachache.

    Naibu Waziri Kalemani pia alizungumzia suala la kukatika mara kwa mara kwa umeme kwamba ni suala lisilokubalika. Aliwataka watendaji wa TANESCO kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha umeme haukatiki mara kwa mara.

    Alisema Wizara imekwishawaelekeza TANESCO kuhakikisha Transfoma zote mbovu zinabadilishwa na zenye uwezo mdogo zinaondolewa na kuwekwa zenye uwezo mkubwa ili kuhimili mahitaji ya umeme ya wananchi. Wananchi wanapoongeza mahitaji, lazima pia nguvu ya umeme iongezeke.

    Dkt. Kalemani alisisitiza kuwa, endapo hatapatiwa taarifa yenye majibu ya kuridhisha kuhusu tatizo hilo la kukatika mara kwa mara kwa umeme wilayani Igunga, hatasita kuwawajibisha Mameneja wa TANESCO na watendaji husika.

    Naibu Waziri Kalemani anaendelea na ziara yake mkoani Tabora ambapo anatembelea miradi mbalimbali ya sekta za Nishati na Madini inayotekelezwa chini ya Wizara yake. Katika ziara hiyo ya siku 10, atatembelea pia Mkoa wa Kigoma na Geita.

    Kampuni ya CHICO kutumbuliwa jipu isipokamilisha kusambaza umeme>>INATOKA Uk. 3

    Sehemu ya umati wa wananchi wa Kijiji cha Matinje, Kata ya Mwashiku, wilayani Igunga wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini (hayupo pichani) alipowatembelea na kuzungumza nao hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Wizara yake.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani akizungumza na mmoja wa wananchi katika Kijiji cha Matinje, Kata ya Mwashiku, wilayani Igunga, alipowatembelea wananchi hao hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Wizara yake.

  • 5BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Makam wa Rais Mwandamizi kutoka kampuni ya PW Power Systems, Charles Levey, (kushoto) ambayo imeonesha nia ya ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 600 wa gesi asilia iliyogundulika nchini. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ameri Group ya Dubai, Ziad Barakat.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa kwenye mkutano na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na ujumbe wa kampuni ya Ameri Group kutoka Dubai walioonesha nia ya kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 600 kutokana na gesi asilia iliyogunduliwa nchini. Kikao kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.

    Na Zuena Msuya, Dar Es Salaam

    Kampuni ya Ameri Group yenye makazi yake nchini Dubai imeonyesha nia ya kuwekeza katika sekta ndogo ya gesi asilia

    kwa kuzalisha umeme wa megawati 600 unaotokana na nishati hiyo iliyogundulika nchini.

    Hayo yalibainishwa jijini Dar Es Salaam wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na ujumbe wa Kampuni hiyo ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ameri Group, Ziad Barakat aliyeambatana na Mkandarasi atakayetekeleza mradi

    huo pamoja na kampuni itakayofunga mashine za kufua umeme.

    Barakat alisema Kampuni hiyo inatarajia kuzalisha umeme wa megawati 600 unaotokana na gesi asilia ambapo katika awamu ya kwanza wataanza na megawati 300.

    Alisema kampuni hiyo tayari imewekeza katika baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Nigeria na Msumbiji na kuzalisha umeme unaotokana na gesi asilia.

    Tayari kuna kampuni ya PW Power systems ambayo itatekeleza ujenzi wa mradi huo na nyingine ya kufunga mitambo ya kufua umeme, nia yetu ni kuzalisha megawati 600 hapa Tanzania lakini tutaanza na megawati 300, alisema Barakat .

    Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliitaka kampuni hiyo kujadiliana pamoja na Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC) pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji( EWURA) ili kuona namna ambavyo kampuni hiyo itatekeleza mradi huo.

    Aidha, Prof. Muhongo alizitaka Taasisi hizo kujadiliana kwa kina kuhusu masuala ya bei ya umeme ambayo kampuni hiyo itaiuzia TANESCO pamoja na masuala mengine ili wafikie muafaka kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi.

    Tanzania inahitaji umeme mwingi zaidi ili ifikapo mwaka 2025 iwe

    imefikia katika uchumi wa kati kama azma ya Serikali inavyoelekeza, pia Tanzania imesaini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Nishati Endelevu kwa wote( SE4ALL)ambao unaelekeza kuwa na nishati kwa kila mtu ifikapo mwaka 2030; Kwa mantiki hiyo tunahitaji wazalishaji umeme wasio wababaishaji,alisema Prof. Muhongo.

    Pamoja na mambo mengine, Prof. Muhongo alisema mara baada ya kampuni hiyo kujadiliana na TANESCO, EWURA pamoja na TPDC na kufikia makubalino; Serikali itaelekeza eneo ambalo kampuni hiyo itafua umeme wa gesi katika maeneo ambayo gesi asilia imegunduliwa kama ni Mtwara, Lindi, au Somangafungu.

    Kampuni ya Ameri Group yaonesha nia kuzalisha megawati 600

    Asteria Muhozya na Nuru Mwasampeta, Dar es Salaam

    Kutokana na mahitaji makubwa ya Nishati ya umeme barani Afrika, ambapo kiasi cha wananchi wake wapatao

    bilioni 1 wanatajwa kuwa bado wapo gizani Tanzania ikiwa miongoni mwao, imeelezwa kuwa, wawekezaji katika sekta hiyo wanavyo vyanzo vya uhakika vya kupata fedha za uwekezaji.

    Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa mwendelezo wa vikao vyake na wawekezaji katika sekta ya Nishati vilivyoanza tarehe 15-18 Februari, 2016, ambavyo vililenga

    kukutana na wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika vyanzo mbalimbali vya nishati vinavyopatikana nchini ili kuhoji na kubaini kampuni ambazo ziko tayari na zina uwezo wa kuwekeza.

    Prof. Muhongo amevitaja vyanzo hivyo kuwa ni pamoja na Mpango wa Serikali ya Marekani kusaidia maendeleo ya sekta ya umeme barani Afrika unaoitwa Power Africa Initiative ambao umetengewa Dola za Marekani zaidi ya Bilioni 6 ambapo Tanzania ni moja ya nchi zinazopewa kipaumbele katika mpango huo.

    Aidha, ameongeza kuwa, Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo ipo katika nafasi nzuri ya kufaidika na fedha za Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Nishati Endelevu kwa Wote (SE4ALL) ambapo mpango huo unaelekeza kuwa, ifikapo mwaka 2030 kuwe na

    upatikanaji umeme kwa wote na ongezeko maradufu la utumiaji umeme wa nishati jadidifu na matumizi bora.

    Pia, Profesa Muhongo ameeleza kuwa, kutokana na mahitaji ya umeme Duniani kupanda kwa asilimia 26 tayari kiasi cha Dola za Marekani

    trilioni 48 zimetengwa, ili kuongeza kiasi cha watumiaji wa nishati hiyo ifikapo 2020-2035, ambapo dola za Marekani trilioni 40 zikiwa zimetengwa kwa ajili ya kusambaza umeme na kiasi cha dola za Marekani trilioni 8 kwa ajili ya matumizi bora ya nishati.

    Vilevile, ameutaja mpango wa China Afrika Partnership ambapo kiasi cha Dola za Marekani bilioni 60 zimetengwa kwa ajili ya miundombinu , huku nishati ikipewa kipaumbele na kuongeza kuwa, kutokana na urafiki wa muda mrefu na mahusiano mazuri kati ya Serikali ya Tanzania na Watu wa China, Tanzania iko katika nafasi nzuri za kupata fedha hizo.

    Halikadhalika, Profesa Muhongo ameleeza kuwa, Umoja wa nchi za Ulaya (European Union) pia ni chanzo

    kingine kwa wawekezaji kupata fedha kwa kuwa, nishati imekuwa kipaumbele kwa taasisi hiyo.

    Wawekezaji makini macho yote sasa yapo Afrika. Tunataka fedha hizo zote zije Tanzania kuwekeza katika sekta ya nishati. Jipangeni vizuri mwende, Power Africa na sehemu nilizotaja, fedha za uhakika za umeme zipo. fedha,amesisitiza Prof. Muhongo.

    Aidha, kutokana na umuhimu na uharaka wa kutekeleza mipango hiyo, Profesa Muhongo amewataka wawekezaji ambao wako tayari kuwekeza nchini kuzingatia muda na ratiba ya kutekeleza majukumu yao na kuongeza kuwa, ikiwa kuna jambo litacheleweshwa na watendaji wa Serikali, tutachukua hatua, na ikiwa mwekezaji umeshindwa kwenda na muda wetu vizuri basi mradi wako utaachwa na wengine kupewa nafasi,ameongeza Muhongo.

    Profesa Muhongo amebainisha kuwa fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati zinapatikana katika maeneo ya gesi asilia, makaa ya mawe, nishati jadidifu umeme wa maji, upepo, umeme wa jua biogas na vyanzo vingine.

    Matumizi makubwa Sekta ya Umeme yaja

  • 6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Baadhi ya Watendaji kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara na Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia mada katika kikao kati ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo na Wawekezaji katika Sekta ya Nishati.

    Ni baadhi ya Watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wizara ya Nishati na Madini, na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakijadiliana jambo baada ya kikao cha wawekezaji sekta ya Nishati na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

    Picha 1 - 5 Baadhi ya Wawekezaji wakiwasilisha taarifa zao za uwekezaji kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). Baadhi ya maswali ambayo Profesa alihoji kutoka kwa wawekezaji hao ni uwezo wao kifedha, kiteknolojia,utaalam na uzoefu wa kazi katika vyanzo walivyochagua kuwekeza nchini.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akiongea jambo na baadhi ya wawekezaji mara baada ya kikao chake na wawekezaji ambao wameonesha nia kuwekeza katika vyanzo mbali mbali vinavyopatikana nchini na baadhi wamefika kupata taarifa kuhusu uwekezaji.

    KIKAO NA WAWEKEZAJI

    1 2 3

    4 5

  • 7BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amezitaka taasisi z inazos imamia

    miradi ya umeme nchini kuongeza kasi ya utendaji kazi ili Tanzania iweze kupata umeme wa uhakika.

    Profesa Muhongo aliyasema hayo katika kikao chake kilichokutanisha Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Kibo Mining na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wizara ya Nishati na Madini.

    Alisema kuwa ili nchi iweze kuwa na umeme wa uhakika unaozalishwa kwa wakati ni lazima taasisi zilizopo chini ya Wizara zikahakikisha zinaongeza kasi katika uwekezaji kwenye uzalishaji wa umeme kwa kushirikiana na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wenye vigezo ili uchumi wa nchi uweze kukua kwa kasi na kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025 ambayo ni kuhakikisha kuwa nchi inatoka katika kundi la nchi masikini duniani na kuingia katika kundi la nchi zenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

    Alisisitiza kuwa ili kufikia lengo hilo ni lazima taasisi zikaongeza kasi katika miradi yake ya umeme, kwa kushirikiana na wawekezaji mbalimbali na kuwataka kuondoa urasimu kwa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye miradi ya

    uzalishaji wa umeme nchini.Aliongeza kuwa nishati ni roho ya

    uchumi wa nchi na kusisitiza kuwa hakuna nchi yoyote duniani iliyopiga hatua bila kuwa na nishati ya umeme ya uhakika.

    Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuhakikisha kuwa sekta ya viwanda inakua kwa kasi na kutoa ajira hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi, hivyo nishati ya umeme inahitajika sana; bila nishati ya uhakika uchumi hauwezi kukua kwa kasi inayotakiwa, alisisitiza Profesa Muhongo.

    Waziri Muhongo aliendelea kusema kuwa nishati ya umeme ya uhakika itachangia ukuaji wa sekta za viwanda vidogo hasa maeneo ya vijijini, kilimo kukua kwa kasi na hivyo kunufaisha wananchi na pato la taifa kukua kwa kasi.

    Aidha Profesa Muhongo alilitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kushirikiana kwa pamoja katika hatua zote za uwekezaji nchini ili kuondoa mkanganyiko unaoweza kujitokeza kati ya Serikali na wawekezaji.

    TANESCO na EWURA naomba mshirikiane katika kila hatua, kwa kukaa meza moja na wawekezaji na kufikia mwafaka kabla hawajaanza kuwekeza, alisema Profesa Muhongo

    Awali Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Kibo Mining, Louis Coetzee akizungumza katika kikao hicho, alisema kuwa kampuni ya Kibo Mining ina mpango wa kuwekeza katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia makaa ya mawe ambapo

    itaanza na ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe wa Megawati 900 kwa awamu tofauti.

    Alisema awamu ya kwanza ambayo ni ujenzi wa mtambo wa kuzalisha Megawati 300 utakaogharimu Dola za Marekani milioni 800 utakamilika ifikapo mwaka 2019.

    Akielezea hatua iliyofikia ya maandalizi ya uwekezaji wa kampuni ya Kibo Mining Coetzee alisema kuwa kampuni hiyo iliyoanza maandalizi yake mwaka 2008 inakamilisha upembuzi yakinifu (feasibility study) katika mradi wake na kuongeza kuwa wana mpango wa kuanza ujenzi wa awamu ya kwanza mwaka 2017 baada ya taratibu zote kukamilika.

    Alisema mara baada ya ujenzi wa mtambo wa kwanza kukamilika mwaka 2019, umeme utakaozalishwa mbali na kutumika viwandani utaongezwa kwenye gridi ya taifa na hivyo kupunguza changamoto ya ukosefu wa umeme nchini.

    Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Kibo Mining, Louis Coetzee ( wa pili kutoka kulia) akielezea mikakati ya kampuni hiyo katika uwekezaji wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia makaa ya mawe mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake.

    Waziri Muhongo azitaka taasisi kuongeza kasi ya miradi ya umeme nchini

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( kulia) akimweleza Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Kibo Mining, Louis Coetzee (kushoto) fursa za uwekezaji nchini kwenye sekta ya umeme.

    Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Kibo Mining, Louis Coetzee akifafanua jambo katika kikao hicho.

  • 8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Prof. Muhongo ataka wawekezaji makini sekta ya NishatiNa Asteria Muhozya, Dar es Saalam

    Imeelezwa kuwa, mbali ya kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya kuifanya Tanzania kuwa na umeme wa kutosha ifikapo mwaka 2025, Serikali pia imeazimia kufikia

    malengo ya Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Nishati Endelevu kwa Wote (SE4ALL) ifikapo mwaka 2030.

    Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati na Madini katika vikao baina yake na wawekezaji wa Kampuni mbalimbali katika sekta ya Nishati vilivyoanza tarehe 15- 18 Februari, 2016, kwa lengo la kujadili namna kampuni hizo zinavyoweza kufanya kazi na Tanzania hususan katika kuzalisha umeme ili kuweza kufikia malengo tarajiwa ya Taifa kuwa na umeme mwingi, nafuu na wa uhakika.

    Mpango wa SE4ALL unalenga katika upatikanaji umeme kwa wote ifikapo mwaka 2030, ongezeko maradufu la utumiaji wa nishati jadidifu na matumizi bora. Rasilimali za kufikia huko tunazo na hivyo tunahitaji

    wawekezaji makini,alisisitiza Profesa Muhongo.

    Prof. Muhongo amesema Tanzania inahitaji kufikia malengo hayo yote, hali ambayo imefanya Wizara kuongeza jitihada za kuhakikisha inakutana na wawekezaji mbalimbali ambao wameonesha nia ya kuwekeza katika sekta hiyo ili kuweza kuhoji na kubaini kampuni ambazo zina uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha ili kuchochea shughuli mbalimbali za kiuchumi.

    Aliongeza kuwa, japokuwa Taifa lina uhitaji mkubwa wa nishati hiyo, lakini suala la kumpata mwekezaji makini, mwenye uwezo kiteknolojia, kifedha na uzoefu wa kutosha ni jambo ambalo Serikali inalichukulia kwa uzito mkubwa ili kufikia malengo tarajiwa.

    Ameongeza kuwa, Serikali imelenga katika kuhakikisha kwamba, nishati inasaidia kuwezesha ukuaji wa uchumi, kuondoa umaskini na kuongeza pato la taifa kwa miongo kadhaa na hivyo kutumia fursa hiyo kuwakaribisha wawezekaji kupitia vyanzo mbalimbali vya nishati vinavyopatikana nchini,

    ikiwemo makaa ya mawe, gesi asilia, jotoardhi, upepo, jua na nishati nyingine.

    Akizungumzia kuhusu nishati ya makaa ya mawe amesema ni wakati sasa wa Serikali kuongeza nguvu zaidi ili makaa hayo yaweze kuzalisha umeme nchini, ikizingatiwa kwamba, Taifa linayo akiba ya kutosha ya makaa hayo nchini.

    Kama Taifa tunataka kuweka nguvu kubwa katika rasilimali ya makaa ya mawe, si jambo zuri hata kidogo kutokuzalisha hata megawati moja ya makaa ya mawe wakati rasilimali za kutosha zipo. Ikiwa tunahitaji umeme nafuu na wa uhakika, makaa ya mawe yatakuwa na mchango mkubwa katika hili. Aidha, alitumia fursa hiyo kuzitaka kampuni ambazo ziko katika hatua za kukamilisha taratibu zinazotakiwa hususani zile zinazolenga kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe, kuongeza kasi ya utendaji ili kuhakikisha kwamba, suala hilo halichukui muda mrefu.

    Miongoni mwa Kampuni ambazo zimeonesha nia ya kuwekeza katika kuzalisha umeme kwa kutumia makaa

    ya mawe ni Kampuni ya Edenville Energy plc, ambayo tayari imefanya utafiti katika maeneo ya Mkomolo na Namwele, mkoani Rukwa , ambapo kampuni hiyo imelenga kuzalisha megawati 300 kwa kutumia makaa ya mawe, na uwezo wa kuendelea kuzalisha kwa kutumia makaa hayo kwa kipindi cha miaka 35 kutokana na rasilimali iliyopo maeneo hayo.

    Tanzania inatajwa kuwa tayari imetia saini Mpango wa Umoja wa Mataifa ya Nishati Endelevu kwa Wote (SE4ALL) ifikapo mwaka 2030, ambao utaiwezesha kufaidika na fedha zitakazotolewa ili kuendeleza miradi ya nishati. Aidha, bado iko katika nafasi nzuri ya kufaidika na mpango huo wa SE4 ALL, pia ndio nchi iliyoiwakilisha Afrika katika maandalizi ya mpango huo.

    Profesa Muhongo ameanza kukutana na wawekezaji mbalimbali katika Sekta ya Nishati ikiwa ni jitihada za Serikali kufanya kazi na wawekezaji wa ndani na nje katika sekta hiyo ili kuwezesha ongezeko la nishati hiyo nchini.

    Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Edenville Energy, Mark Pryor (aliyesimama) akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya Kampuni hiyo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati). Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe, Watendaji Wakuu kutoka Wizarani, Taasisi zilizo chini ya Wizara ikiwemo EWURA, Wakala la Nishati Vijijini (REA), Wakala wa Jilolojia Tanzania (GST), Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akiongoza kikao chake na Kampuni ya ya Edenville Energy. Kampuni hiyo imeonesha nia ya kuwekeza katika uzalishaji umeme kwa kutumia makaa ya mawe. Kampuni ya Edenville Energy plc, inalenga kuzalisha Megawati 300 za umeme. Vilevile, kutokana na rasilimali inayopo ya makaa hayo katika maeneo ya utafiti ya kampuni hiyo kutawezesha uzalishaji kuchua hadi miaka 35.

    Baadhi ya Watendaji kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara na baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakifuatilia kikao baina ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo na wawekezaji katika sekta ya Nishati.

    Mtendaji Mkuu wa Kampuni Tanzu ya Kuendeleza Jotoardhi Tanzania (TGDC) Mhandisi Boniface Njombe (Kushoto) akibadilishana kadi za mawasiliano na mmoja wa wawakilishi wa Kampuni ya Power Machine waliokutana pia na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.

  • 9BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Mohamed Saif

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo a m e w a t a k a watendaji wa taasisi

    zilizo chini ya wizara kufanya kazi kwa kutanguliza maslahi ya Taifa.

    Aliagiza hayo hivi karibuni katika kikao chake na mwekezaji wa kampuni ya Mkonge Energy Systems (MeS) Limited ya jijini Tanga kupitia kampuni tanzu ya Tanzania Masigira Power Limited (TMPL) ambao wameonesha nia ya kuzalisha umeme kiasi cha Megawati 71 wilayani Songea mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na kampuni ya China ya Sino Hydro Hong Kong Holding Limited (SHKHL) inayomilikiwa na Power China.

    Katika kikao hicho Waziri Muhongo Alizitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha wanashirikiana katika majadiliano mbalimbali ya miradi ya umeme nchini ili kuharakisha utekelezaji wake.

    EWURA na TANESCO fanyeni kazi kwa pamoja ili miradi iende kwa kasi; tulipende Taifa letu na tufanye maamuzi kwa maslahi ya Taifa. Kaeni pamoja mjadiliane na sio kila mmoja kivyake, alisisitiza.

    Alisema kuwa Serikali haitokubali miradi ikwame kwa uzembe na hivyo aliagiza hadi kufikia tarehe 15 mwezi Machi mwaka huu majadiliano kuhusu miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme yawe yamekamilika. Na

    ndani ya miezi mitatu ijayo lazima miradi mipya ya kuzalisha umeme iwe imejulikana na kuanza kutekelezwa, alisema.

    Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mwenyekiti wa Kampuni ya Mkonge Energy Systems (MeS), Salum Shamte alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 2008 baada ya Serikali kutangaza kuwa kampuni binafsi nazo zinaruhusiwa kuzalisha umeme na kuiuzia TANESCO.

    Alisema awali kampuni hiyo ilikuwa inazalisha umeme wa maji kiasi cha kilowati 300 kwa matumizi yake ya Kiwanda cha Mkonge na kufuatia tangazo hilo la Serikali, ndipo kampuni tanzu ya MeS ikaanzishwa.

    Alisema kuwa tayari upembuzi yakinifu umekamilika na kwamba kupitia mradi huo wa Masigira, kampuni tanzu ya TMPL itajenga njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 33 ya kilomita 14 kutoka Mahanje hadi Madaba ambapo kutakuwa na kituo cha kupoozea umeme.

    Aidha, mbali na mradi wa Masigira, Shamte alieleza kuwa wanayo miradi mingine midogo ya kuzalisha umeme ambayo ni mradi wa Kiwira wa Megawati 43.2 uliopo wilayani Tukuyu, Mkoani Mbeya ulio chini ya kampuni tanzu ya Kiwira Energy Limited (KEL) ya ubia wa MeS na kampuni ya Frontier Investment Management ya Denmark.

    Mradi mwingine ambao Shamte aliuzungumzia katika kikao hicho ni mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia mabaki ya mkonge kiasi cha megawati 11.2 ambao alisema upo chini ya kampuni mama ya MeS.

    Mkutano huo ni moja kati ya mikutano inayoendelea kwa wiki hii baina ya Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake pamoja na wawekezaji lengo likiwa ni kuwawezesha kupata maelezo ya kina kuhusu fursa zilizopo nchini na pia kuiwezesha Wizara kupata maelezo kutoka kwa Wawekezaji hao kuhusu uwezo wao wa kutekeleza miradi wanayokusudia.

    Muhongo ataka watendaji watangulize maslahi ya Taifa

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao chake na mwekezaji kutoka kampuni ya Mkonge Energy Systems (MeS) Limited ya jijini Tanga. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Salum Shamte.

    Wawakilishi kutoka kampuni ya Mkonge Energy Systems wakifurahia jambo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia). Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya MeS, Juma Shamte akifuatiwa na Mwenyekiti wa MeS, Salum Shamte.

    Wajumbe wa mkutano baina ya Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zilizo chini yake pamoja na mwekezaji, kampuni ya Mkonge Energy Systems (MeS) Ltd ya jijini Tanga. Mikutano baina ya wizara hiyo na wawekezaji wa uzalishaji umeme inaendelea chini ya uenyekiti wa Profesa Sospeter Muhongo.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiagana na Mwenyekiti wa Kampuni ya MeS, Salum Shamte mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina ya wizara na kampuni hiyo.

  • 10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Teresia Mhagama, Tarime

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameipa siku 30, Kamati aliyoiunda

    ya kutathmini kero za wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara ambapo Kamati hiyo inatakiwa kutoa ripoti tarehe 23 Machi 2016.

    Kamati hiyo itakuwa na makundi

    mawili yatakayofanya kazi sambamba kwa kuzunguka katika vitongoji tofauti vinavyozunguka mgodi kuanzia tarehe 22 Februari, 2016.

    Timu hiyo itaundwa na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Sehemu ya Leseni, Mazingira, Ukaguzi wa Migodi na Idara ya Sheria.

    Wataalam wengine watakaounda Kamati hii ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Watathmini kutoka Wizara ya Ardhi, Baraza la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira ( NEMC) na Wizara ya Maji na Umwagiliaji, alisema Profesa Muhongo.

    Aliongeza kuwa Wajumbe wengine ni Wenyeviti wa Vitongoji vitakavyozungukiwa na Kamati, Wawakilishi wa Mbunge wa Tarime Vijijini, Mgodi wa Acacia North Mara na Wizara ya Mambo ya Ndani.

    Alisema kuwa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Tarime, Halmashauri ya Tarime na Vyombo vya Usalama wilayani humo havitashiriki katika Kamati husika kwani baadhi ya tuhuma za wananchi zimeelekezwa katika Ofisi hizo.

    Kila upande unaohusika na zoezi hilo ulitakiwa kuwasilisha majina ya wajumbe wa Kamati kwa Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, siku ya Jumanne tarehe 16 Februari, 2016.

    Alieleza kuwa Mwenyekiti na Makamu wa Kamati hiyo watatoka Wizara ya Nishati na Madini na kwamba kamati itafanya kazi katika siku zilizopangwa na si vinginevyo na mwenendo wa Kazi wa Kamati husika utakuwa ukifuatiliwa katika kila wiki.

    Baada ya zoezi la upangaji wa Kamati hiyo kukamilika, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, alimshukuru Waziri wa Nishati na Madini na serikali kwa ujumla kwa kulipa uzito jambo hilo ambalo halikutafutiwa ufumbuzi kwa miaka kadhaa na kuitakia kamati kila la heri katika utendaji kazi ili kila mtu apate haki yake anayostahili.

    Naye Meneja Uendelezaji, Mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara, Abel Yiga kwa niaba ya Mgodi huo amemshukuru Profesa Sospeter Muhongo kwa kufika wilayani Tarime ili kutatua changamoto kati ya Mgodi na wananchi kwani wamekuwa wakiwasilisha changamoto zao katika ngazi mbalimbali za uamuzi lakini utatuzi bado haujapatikana.

    Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga pia ametoa pongezi kwa Profesa Muhongo kwa kutoa muongozo utakaopelekea kupata suluhisho la kero zinazowapata wananchi wanaozunguka mgodi pamoja na kero ambazo mgodi unazipata katika utekelezaji wa majukumu yake.

    Alitoa wito kwa wananchi wilayani Tarime kuwa na imani na Kamati hiyo na kila upande ukubaliane na taarifa itakayotolewa na Kamati husika.

    Baadhi ya kero zitakazofanyiwa kazi na Kamati hiyo ni pamoja na suala la fidia kwa wananchi waliopisha Mgodi, utegeshaji wa nyumba ndani ya eneo la Mgodi, athari za mitetemo inayotokana na upasuaji wa miamba, ajira kwa watanzania ndani ya mgodi, utoaji wa huduma katika mgodi na masuala mengine yatakayojitokeza wakati zoezi la tathmini litakapoanza.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Nyakungulu wilayani Tarime ambaye alikuwa akiwasilisha kero za wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara wakati Profesa Muhongo alipofanya ziara ya kikazi wilayani Tarime.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia) akioneshwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga baadhi ya nyumba zinazodaiwa kutegeshwa kwa ajili ya kulipwa fidia katika moja ya maeneo yanayozunguka mgodi wa Dhahabu wa Acacia North Mara. Profesa Muhongo alifika katika eneo la Nyamongo linalozunguka mgodi huo ili kuzungumza na wananchi na kukagua athari ambazo zinadaiwa kusababishwa na mgodi katika eneo hilo.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kulia) akitembelea maeneo yanayolalamikiwa na wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia NorthMara wakati alipofanya ziara ya kikazi wilayani Tarime. Kulia kwa Waziri ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, na kulia kwa Mbunge ni Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga.

    Kero za wanaozunguka mgodi wa acacia north mara kutathminiwa kwa siku 30

  • 11BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Mohamed Saif- Morogoro

    Wizara ya Nishati na Madini kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini imepokea jengo

    la Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu za Kidigitali (Data Recovery Center) cha mjini Morogoro kutoka kwa Mkandarasi ambaye ni Kampuni ya G.E Engineering

    and Construction Limited. Akizungumza hivi karibuni, kwa

    niaba ya Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), Mhandisi Idrisa Yahya, wakati wa makabidhiano hayo Msanifu Majengo (Architect) wa SMMRP, Joseph Ringo alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa Kituo hicho ni kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali za kidigitali hususan zinazohusiana na leseni za madini.

    Alisema kituo hicho kitasaidia Wizara

    ya Nishati na Madini kuhifadhi taarifa zake pamoja na za taasisi zilizo chini yake jambo ambalo alisema litasaidia kuhifadhi kumbukumbu sahihi na za wakati hata kama endapo ikitokea ajali yeyote kwenye mfumo mama uliopo wizarani na kwenye taasisi zake.

    Aliongeza kwamba awali kabla ya kujengwa kituo hicho, taarifa zote zilikuwa zikihifadhiwa Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini na alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo kutasaidia kuwa na eneo lingine la

    kuhifadhia kumbukumbu husika mbali na hilo la awali.

    Aliendelea kueleza kuwa mbali na kutumika kama Kituo cha kutunzia kumbukumbu, jengo hilo pia litatumika kama Ofisi ya Afisa Madini Mkazi na hivyo kupunguza uhaba wa majengo ya ofisi za madini.

    Ilielezwa kwamba ujenzi wa jengo hilo chini ya usimamizi wa mradi SMMRP umechukua takriban wiki 38 hadi kukamilika kwake na kukabidhiwa rasmi.

    Wizara yakabidhiwa rasmi jengo la Morogoro

    Jengo la Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu za Kidigitali (Data Recovery Center) la mjini Morogoro ambalo ujenzi wake umekamilika na kukabidhiwa rasmi.

    Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika akikabidhiwa funguo za jengo la Kituo cha kuhifadhia kumbukumbu cha Morogoro na Mkandarasi aliyejenga jengo hilo kutoka kampuni ya GE Engineering and Construction Ltd, Mhandisi Samson Shoo (kulia). Wanaoshuhudia ni Msanifu Majengo wa SMMRP, Arch. Joseph Ringo (kulia), Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini na washauri waliosimamia ujenzi wa jengo hilo.

    Msanifu Majengo wa SMMRP, Arch. Joseph Ringo (kulia) akitia saini Hati ya Makabidhiano mara baada ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika.

  • 12 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    cseec yawasilisha mapendekezo miradi ya umemeNa Mohamed Saif

    Kampuni ya China Sinogy Electric Engineering Co. Ltd (CSEEC) ya nchini China kwa

    kushirikiana na kampuni za Coal Energy Co Ltd, Star Energy Co Ltd na Sun Power Co Ltd za Tanzania zimewasilisha mapendekezo ya uwekezaji wa miradi mitatu ya uzalishaji umeme.

    Kampuni hizo ziliwasilisha mapendekezo ya miradi hiyo ya kuzalisha umeme hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika mikutano iliyomalizika baina ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na wawekezaji wa uzalishaji umeme.

    Akizungumza katika mkutano huo, Meneja Msaidizi wa CSEEC, Huang He aliitaja miradi ya uzalishaji umeme ambayo kampuni hizo zinahitaji kuwekeza kuwa ni mradi wa umeme wa makaa ya mawe wa megawati 1,200; umeme wa gesi asilia wa megawati 1,440 na mradi wa umeme wa jua wa megawati 100.

    Akielezea mradi wa makaa ya

    mawe, He alisema mradi huo ni kwa makaa ya mawe ya Kiwira ambapo kutajengwa mitambo ya kuzalisha megawati 600 na Ngaka ambapo kutajengwa mitambo ya megawati 600 na hivyo kufanya jumla ya umeme utakaozalishwa kwa makaa ya mawe kufikia megawati 1,200.

    Kuhusu mradi wa uzalishaji umeme wa gesi asilia, He alisema mitambo itajengwa katika maeneo matatu tofauti ambayo ni Kilwa- mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 480; Mkuranga kutajengwa mitambo ya kuzalisha megawati 480 na Bagamoyo mitambo ya kuzalisha megawati 480 ambapo jumla yake itakuwa megawati 1,440.

    Aidha, mradi wa tatu ambao ulipendekezwa na kampuni hiyo ni wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya jua ambao He alisema kwamba utajengwa Mkoani Shinyanga na utazalisha jumla ya megawati 100.

    Kampuni ya CSEEC ni kampuni tanzu ya China National Machinery Industry Corporation (Sinomach) wakati kampuni za Star Energy Co Ltd, Coal Energy na Sun Power Co Ltd ni kampuni tanzu za Super Group of Companies Tanzania.

    Kampuni za sukari nchini kuiuzia umeme TANESCONa Mohamed SaifKampuni ya Super Group

    of Companies kupitia kampuni zake tanzu za Kagera Sugar Limited na Mtibwa Sugar Limited imesema ina malengo ya kuzalisha umeme na kuliuzia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

    Hayo yalielezwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika mkutano kati ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na ujumbe wa kampuni hizo ukingozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Super Group of Companies, Seif Seif aliyeambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kagera Sugar Ltd, Ashwin Rana.

    Akizungumza katika mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Rana alisema kwa sasa kampuni hizo zinazalisha umeme kwa matumizi ya viwanda vyake ambapo kwa kiwanda cha Kagera umeme unaozalishwa ni kiasi cha megawati 5 na kwa upande wa Mtibwa umeme unaozalishwa ni megawati 9.

    Hata hivyo alisema lengo lililopo ni kuongeza uzalishaji wa umeme kwa kila kiwanda na alibainisha kuwa umeme utakaozalishwa ni mwingi kuliko mahitaji na hivyo ziada itakayopatikana itauzwa kwa TANESCO.

    Alifafanua kwamba kwa upande wa Kagera Sugar kiasi cha megawati 23 kitazalishwa ambapo kati ya hizo megawati 13 zitatumika kwa matumizi ya kiwanda na megawati 10 za ziada zitauzwa kwa TANESCO na kwa upande wa Mtibwa Sugar ni kwamba kiasi cha Megawati 30 kitazalishwa ambapo megawati 20 zitatumiwa kiwandani na megawati 10 zilizobaki zitauzwa kwa TANESCO.

    Alisema kuongezeka huko kwa uzalishaji umeme kutasaidia TANESCO kuwa na umeme mwingi na vilevile kwa upande wa Kagera kutasaidia kupunguza haja ya kununua umeme kutoka nje ya nchi. Tunao uwezo wa kuanza kuzalisha na kuiuzia umeme TANESCO ndani ya miaka miwili, alisema.

    Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipongeza wazo hilo la kuongeza uzalishaji wa umeme na kuagiza wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake kuka pamoja na kampuni hiyo kujadili kwa kina kuhusiana na miradi husika.

    Profesa Muhongo alitoa mwezi mmoja wa kukamilika kwa majadiliano hayo na aliagiza ifikapo tarehe 16 mwezi Machi awe amepatiwa mrejesho wa kuanza kwa utekelezaji wa miradi hiyo.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya Super Group of Companies Tanzania, Nassor Seif (katikati) na Meneja wa kampuni ya CSEEC, Liang Tiansheng (kushoto).

    Mkurugenzi Mtendaji wa Kagera Sugar Ltd, Ashwin Rana akiwasilisha mada wakati wa mkutano. Wengine katika picha ni Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zilizo chini yake.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kagera Sugar Ltd, Ashwin Rana (hayupo pichani). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Madini, Profesa James Mdoe

  • 13BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Mohamed Saif

    Kampuni ya Rukun Al Yaqeen I n t e r n a t i o n a l maarufu kama Ray International

    Group ya nchini Oman imesema ipo tayari kuwekeza kwenye sekta nishati nchini.

    Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na wawekezaji, Mwenyekiti wa kampuni hiyo Dkt. Tahir Al-Kindi alisema kampuni yake inao uzoefu wa muda mrefu na inatumia teknolojia ya kisasa.

    Alisema kuwa kampuni hiyo ni kampuni mama ambapo ndani yake zipo kampuni tanzu kadhaa ambazo takriban zote zinajihusisha na masuala yanayohusu sekta ya nishati.

    Dkt. Tahir alitaja baadhi ya shughuli na huduma zinazotolewa na kampuni zake kuwa ni utengenezaji wa nguzo imara za zege, utaalamu na teknolojia ya kisasa ya

    matengenezo ya miundombinu ya umeme bila kukata umeme, utaalamu na teknolojia ya kisasa ya usafishaji wa visima vya mafuta na gesi na utoaji wa mafunzo katika nyanja mbalimbali hususan kuhusiana na masuala ya nishati.

    Akizungumzia suala la mafunzo, alisema mipango iliyopo kwa kampuni hiyo kupitia kampuni yake tanzu ya Ray International Skills Development, ni kuanzisha chuo cha mafunzo nchini Tanzania ambacho kitakuwa kitovu cha mafunzo ya aina hiyo kwa Afrika Mashariki na nchi nyingine za jirani.

    Tunataka kuifanya Tanzania kitovu cha mafunzo haya; yani watu kutoka nchi nyingine za jirani ambao watahitaji mafunzo tunayotoa waje hapa Tanzania, alisema.

    Alitaja baadhi ya programu zinazotolewa na kampuni hiyo kuwa ni mafunzo ya shughuli za migodini; mafunzo ya shughuli za utafiti kwenye rasilimali madini, mafuta na gesi; mafunzo ya matengenezo ya

    vifaa vya migodini na mafunzo ya usalama mahala pa kazi.

    Kwa upande wake Profesa Muhongo aliagiza watendaji wa wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania

    (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kukaa pamoja na kampuni hiyo ili kujadili kwa kina mapendekezo ya kampuni hiyo.

    Katika kikao hicho, Mwenyekiti huyo wa Ray International Group aliambatana na mwenyeji wake ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Super Group of Companies Tanzania, Seif Seif.

    Na Malik Munisi, TPDC

    Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limekutana na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ikiwa ni mwendelezo wa shirika hilo

    kutoa elimu kwa wadau mbalimbali.Katika kikao kiliofanyika hivi

    karibuni kwenye kituo cha Kuchakata na kusafirisha gesi asilia Madimba Mtwara ambapo Madiwani hao walipata fursa ya kusikia mada mbalimbali zilizolenga kutoa elimu zaidi kuhusu masuala ya mafuta na gesi zilitolewa na wataalam

    kutoka TPDC. Akizungumza katika kikao hicho,

    Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Ally alisema ugunduzi wa gesi mkoani Mtwara umekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo na kuitangaza Mtwara na Tanzania Duniani.

    Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wakazi wa Wilaya ya Mtwara kuchangamkia fursa zinazotokana na miradi ya mafuta na gesi na kuongeza kuwa, Mtwara ina ardhi yenye rutuba nzuri na kilimo na kumekuwa na ongezeko la wageni siku hadi siku jambo ambalo linachangia kutanuka kwa soko la chakula.

    Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchakataji, Usafirishaji na Usambazaji wa gesi asilia kutoka TPDC, Dkt. Wellington Hudson akisoma hotuba ya TPDC kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa, Serikali imefanya uwekezaji wa kimkakati kwa kujenga miundombinu ya gesi nchini na kusisitiza kuwa, ili azma ya Serikali ifikiwe ni lazima miundombinu hiyo ilindwe na kutunzwa kwa kushirikiana kwa pamoja kati ya Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi wenyewe ambao ndio walinzi wa kwanza.

    Vilevile, Dkt. Hudson alitoa rai kwa madiwani kuwahamasisha wananchi wanaoishi maeneo ambayo miundombinu ya gesi imepita au mahali ilipo kuilinda kwa kuwa ni ni mali yao.

    Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Musa Ndazigula alitoa shukrani kwa elimu iliyotolewa na TPDC na kushauri kuwa utoaji wa elimu uwe endelevu na kusisitiza kuwa, utoaji wa taarifa na elimu ni muhimu kwa kuwa itasaidia kuziba ombwe ambalo linaweza kuharibu mipango mizuri ya Serikali.

    TPDC yatoa elimu ya mafuta, gesi kwa Madiwani Mtwara

    Mkurugenzi wa utafiti na uendelezaji wa mafuta na gesi kutoka TPDC, Kelvin Komba akitoa mada kwa Madiwani wa Halmashauri ya Mtwara, Madimba.

    Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Ally (mwenye mtandio mwekundu) akipata maelezo kuhusu kiwanda cha kuchakata gesi asilia wakati wa ziara ya mafunzo kwa madiwani iliyofanyika katika kiwanda cha Madimba, Mtwara.

    Kampuni ya Oman yavutiwa kuwekeza nchini

    Mwenyekiti wa kampuni ya Ray International Group, Dkt. Tahir Al-Kindi akielezea shughuli zinazofanywa na kampuni yake katika mkutano na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).

  • 14 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akimpa zawadi ya picha, Balozi wa China nchini, Lu Youqing, mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Tatu wa Wanasayansi Vijana Duniani.

    ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, DKT. MEDARD KALEMANI MKOANI TABORA

    Mmoja wa wachimbaji wadogo wadogo wa madini katika Machimbo ya Matinje yaliyopo Kata ya Mwashiku wilayani Igunga, akimwonesha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati) kipande cha dhahabu baada ya kuchekecha udongo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Manonga wilayani Igunga, Seif Gulamali.

    Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Jackline Liana akimshukuru Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani na Ujumbe wake kwa kutembelea Wilaya hiyo wakati Naibu waziri akiwa katika ziara ya kikazi.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini (wa pili-kushoto) akiangalia Shimo linalochimbwa madini ya dhahabu katika machimbo ya Matinje wilayani Igunga, wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora hivi karibuni. Shimo hilo lina urefu wa mita 60.

    Wananchi mkoani Tabora, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini (hayupo pichani), alipotembelea vijiji mbalimbali na kuzungumza na wananchi akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo hivi karibuni kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Wizara.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (mwenye Suti), akishuhudia zoezi la uchujaji wa tope linalosadikiwa kuwa na dhahabu, alipotembelea Machimbo ya Matinje yaliyoko wilayani Igunga hivi karibuni.

  • 15BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, DKT. MEDARD KALEMANI MKOANI TABORA

    Mwekezaji wa Madini wilayani Igunga, Bilal Soud, akimkabidhi Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani, taarifa kuhusu eneo, majengo na visima vya maji alivyokuwa anamiliki ambavyo amevikabidhi kwa wananchi wa Kijiji cha Matinje wilayani Igunga.

    Mmoja wa wananchi katika Kijiji cha Chamipulu Kata ya Mwangoye, akiwasilisha maoni kuhusu changamoto zinazowakabili kuhusu huduma ya umeme kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora hivi karibuni.

    Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati-Magharibi, Humphrey Mmbando na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Jackline Liana, wakijadili jambo nje ya Ofisi ya Wilaya hiyo, wakati Naibu Waziri alipokuwa ziarani kikazi katika Mkoa wa Tabora hivi karibuni.

    Wawekezaji katika sekta ya madini wa Kampuni ya NMDC Limited kutoka India, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa kikao kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nzega hivi karibuni.

    Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Jackline Liana (Kulia), Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (wa pili-kulia) pamoja na baadhi ya maofisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakiwa katika kikao na wawekezaji wa Madini wa kampuni ya NMDC Limited kutoka India.

  • 16 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Latifah Boma, Dar es Salaam

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo a m e w a t a k a wawekezaji katika

    sekta za Nishati na Madini kufanya utafiti wa kutosha katika maeneo husika kabla ya kuendelea na utekelezaji wa miradi yao.

    Prof. Muhongo aliyasema hayo katika mkutano baina yake na wawakilishi kutoka Kampuni ya Lake Holdings ukiwa ni moja kati ya mikutano kadhaa inayoendelea katika wiki nzima baina ya Wizara na wawekezaji wa sekta hizo.

    Kampuni hiyo iliyosajiliwa mwaka 2012, ina mpango ya kujenga kituo cha kuzalisha umeme chenye uwezo wa Megawati 300 hadi Megawati 450 wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma, ambao ni mkubwa zaidi ukilinganishwa na mradi wa awali wa Kampuni hiyo katika Kata ya Kiwira, Wilayani Rungwe, Mkoani Mbeya, ambao ulilenga Megawati 200 za umeme.

    Akizungumza katika mkutano huo, Mratibu wa mradi huo, Profesa Runyoro, alieleza kuwa changamoto kuu waliyoipata katika kutekeleza mradi huo ni upatikanaji wa makaa ya mawe,

    ambayo yanahitajika kwa kiasi kikubwa (tani milioni moja), ili kuwezesha mradi huo, na kuongeza kuwa, maeneo mengi yameshachimbwa na watu wengine.

    Akizungumzia suala hilo, Profesa Muhongo aliwataka wawekezaji kwenda wenyewe katika maeneo hayo ili kujua kiasi cha makaa ya mawe

    yanayopatikana kwani mradi huo ni mkubwa na utahitaji uwekezaji wa kiasi kikubwa na hivyo kuwataka kufanya Geographical Mapping na kisha kutoa majibu baada ya mwezi mmoja.

    Aidha, alilitaka Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kufanya kazi

    kwa karibu na Kampuni hiyo ya Lake Holdings ili waweze kuafikiana juu ya swala hilo, ili wawekezaji hao waweze kupata maeneo ya kuchimbia makaa ya mawe.

    Vilevile aliwataka wawekezaji hao kutochukua maeneo na kuyaacha na hivyo kupoteza muda wa Watanzania, badala yake aliwataka wayafanyie kazi ili Watanzania waweze kunufaika na rasilimali hiyo.

    Na Veronica Simba Nzega

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.. Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),

    kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwafikisha Mahakamani wadaiwa wake sugu hususan Kampuni na watu binafsi.

    Dkt. Kalemani alitoa agizo hilo jana wilayani Nzega, akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Tabora kukagua miradi mbalimbali ya sekta za nishati na madini inayotekelezwa chini ya Wizara yake.

    Alisema, Serikali ilikwishaanza kulipa madeni yake kwa TANESCO, hivyo hakuna budi Kampuni na watu binafsi wanaodaiwa na Shirika hilo kulipa madeni yao pia.

    Meneja wa TANESCO, Sheria ya Umeme inakuruhusu kuwachukulia hatua wadaiwa waliogoma kulipa madeni yao. Wapeleke Mahakamani.

    Katika kuhakikisha agizo lake linapewa uzito unaostahili, Naibu Waziri aliwaagiza Mameneja wa TANESCO wa Mkoa wa Tabora kumpatia orodha ya majina ya wale wote wanaodaiwa na Shirika hilo mkoani humo ifikapo Ijumaa, Februari

    19 mwaka huu.Mnipatie orodha hiyo ifikapo

    Ijumaa, iwe ni kampuni ya mtu mzito au mtu mwingine yeyote, alisisitiza. Aliongeza kuwa, ni lazima hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya waliokaidi kulipa kwani kitendo hicho ni kuihujumu TANESCO.

    Naibu Waziri alisema Serikali imedhamiria kukusanya mapato yote stahiki kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wake, hivyo alimwambia Meneja wa TANESCO Mkoa wa Tabora kuwa asipochukua hatua kama alivyomwagiza, hatasita kumuwajibisha yeye mwenyewe.

    Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kalemani ameagiza kuwa Makandarasi wote wanaojihusisha na shughuli za kutandaza waya na vifaa vingine kwa ajili ya kuunganisha umeme majumbani na katika majengo mbalimbali (wiring), kujisajili katika Ofisi za Wilaya za TANESCO.

    Alisema, agizo hilo linafuatia kuwepo na wimbi la matapeli maarufu kama vishoka ambao hufanya kazi hiyo ya kuunganisha umeme pasipo kuwa na utaalam husika.

    Aidha, aliwataka wananchi kutofautisha kazi zinazofanywa na TANESCO na zile zinazofanywa na Makandarasi binafsi katika zoezi zima la kuunganisha umeme.

    Alisema, kazi ya TANESCO ni kusimika nguzo za umeme na kuunganisha Waya unaoingiza umeme katika nyumba au jengo husika lakini si kazi ya Shirika hilo kufunga Waya na Vifaa vya umeme ndani ya nyumba au jengo.

    Wananchi wengi wamekuwa

    wakilalamika sana kwamba wanatapeliwa kwa kutozwa fedha nyingi na/au kufungiwa vifaa vya umeme visivyo na ubora kwenye nyumba zao. Mara nyingi lawama hizo huelekezwa TANESCO.

    Dkt. Kalemani alisema, ndiyo maana Serikali kupitia Wizara yake, imeamua kuwa Makandarasi wote wanaojihusisha na shughuli hizo wasajiliwe katika Ofisi za TANESCO za Wilaya ili wafahamike na hivyo kuwaepushia wananchi adha ya kutapeliwa.

    Dkt. Kalemani aagiza wadaiwa sugu wa umeme washughulikiwe

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ishihimulwa, Kata ya Bukumbi, wilaya ya Nzega hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora.

    Wawekezaji watakiwa kufanya tafiti

    Mratibu wa Mradi, Profesa Runyoro (wa Tano kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Lake Holdings Bw. Khalid Hassan Mohamed (wa nne kulia), wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profes Sospeter Muhongo (katikati) akizungumzia kuhusu mradi wa kampuni hiyo wa kujenga kituo cha kuzalisha umeme chenye uwezo wa Megawati 300 hadi Megawati 450 wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma.

  • 17BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Veronica Simba - Nzega

    Serikali imetoa siku tano kwa mwekezaji wa madini ambaye ni Kampuni ya NMDC Limited kutoka India, kushughulikia

    utaratibu wa kuwalipa fidia wananchi wa Kata ya Ntobo iliyopo wilayani Igunga, mkoa wa Tabora, walioachia ardhi yao kumpisha mwekezaji huyo.

    Agizo hilo lilitolewa Februari 17 na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani, wilayani Nzega alipokutana na viongozi wa Kampuni hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya wizara yake.

    Akiwa wilayani Igunga, Naibu Waziri alipokea taarifa kuwa mwekezaji huyo alipewa leseni Nne za uchimbaji madini wa kati mwaka 2012 lakini mpaka sasa hajaanza shughuli za uzalishaji kutokana na kutolipa fidia za maeneo ya wakazi wa eneo hilo.

    Kutokana na taarifa hiyo, Naibu Waziri aliagiza kukutana na Mwekezaji huyo ambapo walikutana naye juzi akiwa wilayani Nzega akiendelea na ziara yake.

    Katika kikao hicho, ilibainika kuwa, kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni 20.7 zinadaiwa kama fidia kwa wananchi waliopisha eneo husika.

    Ilielezwa kuwa, ulipaji huo wa fidia umekwama kutokana na mwekezaji huyo kutotaka kulipa fidia yote kwa wakati mmoja bali anataka alipe fidia kidogo kwa kuanzia na eneo dogo kati ya lile analomiliki ambalo anadai ndilo

    atakaloanza kufanyia kazi.Aidha, alidai kwamba atakuwa

    analipa fidia kwa eneo lililobaki kulingana na atakavyokuwa akilitumia.

    Akizungumza katika kikao hicho, Kamishna Msaidizi wa Madini wa Kanda ya Kati-Magharibi, Humphrey Mmbando alimweleza Naibu Waziri kuwa, wananchi wa eneo husika wanalalamika kuwa tangu eneo lao lichukuliwe na mwekezaji huyo, shughuli zao zilizokuwa zikifanyika katika eneo hilo zimesimama na hivyo wanahitaji kulipwa fidia stahiki.

    Kamishna Mmbando aliongeza kuwa, kufuatia malalamiko ya wananchi, Ofisi yake ilimtaka mwekezaji huyo awe ametoa majibu ya namna atakavyoshughulikia madai ya wananchi ndani ya siku 10 ambayo ilikuwa ni juzi, Februari 17, wakati kikao hicho kikikaa.

    Kutokana na maelezo hayo, Naibu Waziri alitoa siku tano zaidi kwa mwekezaji huyo ili ashughulikie mambo kadhaa katika kutatua mgogoro huo.

    Ndani ya siku hizo tano, Naibu Waziri alimuagiza mwekezaji huyo, atoe taarifa rasmi ya kimaandishi kwa Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Magharibi kuwa anakusudia kufanya uzalishaji kwa kuanzia na eneo dogo ndani ya leseni yake.

    Pia, alimuagiza mwekezaji huyo kumwomba Mthaminishaji wa Serikali kufanya uthamini kwa kujikita katika eneo lile tu ambalo anakusudia kuanza kulifanyia kazi.

    Vilevile, Naibu Waziri alimuagiza mwekezaji huyo kuzungumza na

    wananchi husika ili wakubaliane kiasi cha fidia atakachotoa kwao kwa kuzuia shughuli zao za kujipatia kipato katika eneo hilo kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

    Mbali na maagizo hayo, Naibu Waziri alimuagiza mwekezaji huyo awaruhusu wananchi kuendelea na shughuli za uzalishaji katika eneo ambalo atakuwa hajaanza kulifanyia kazi.

    Nimewapa siku tano zaidi, mfanyie kazi maagizo niliyoyatoa vinginevyo, tutachukua hatua nyingine stahiki za kisheria dhidi yenu.

    Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kalemani ameagiza kufutwa kwa leseni zote za madini ambazo

    hazifanyiwi kazi na maeneo hayo kugawiwa kwa wachimbaji wadogowadogo ili wayafanyie kazi na kulipa mrabaha kwa Serikali.

    Kwa kuanzia, katika eneo hili, nimeagiza leseni za utafutaji wa madini za kampuni za Kilimanjaro Mine na Mabangu Resources ziandikiwe taarifa ya kufutwa na tutaendelea na maeneo mengine, alisema.

    Alisema kuwa kuna wawekezaji wengi ambao wamekuwa wakishikilia maeneo kwa muda mrefu pasipo kuyafanyia kazi na hivyo kuikosesha Serikali mapato yatokanayo na kodi, pia kuwakosesha wananchi maeneo ya kufanyia kazi.

    Awali, Naibu Waziri alitembelea Machimbo ya Madini katika Kijiji cha Matinje B, Kata ya Mwashiku wilayani Nzega ambapo mbali na kumpongeza mmiliki wa machimbo hayo, Jason Shinyanga, kwa kulipa mrabaha wa Serikali, alimuagiza kuboresha mazingira ya uchimbaji katika eneo hilo.

    Meneo aliyoagizwa kuboresha ni pamoja na kujenga nyumba za kulala watumishi wake pamoja na vyoo bora. Tunakupa taarifa ya siku 60 urekebishe dosari hiyo, usiporekebisha, tutasahau kama umelipa mrabaha au la, alisisitiza Naibu Waziri.

    Aidha, Naibu Waziri aliwashauri wananchi wanaojishughulisha na uchimbaji kuhakikisha wanapata ushauri wa kitaalamu kutoka ofisi za madini katika maeneo yao kabla hawajaanza shughuli hizo.

    Pia, aliwataka kuhakikisha wanakuwa na leseni halali za kuendeshea shughuli hizo za uchimbaji ili pamoja na mambo mengine kuongeza thamani ya maeneo yao pindi wanapotaka kuyauza au kuingia ubia na wawekezaji wa kati na wakubwa.

    Naibu Waziri Kalemani ampa siku tano mwekezaji kushughulikia ulipaji fidia

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati), akiongozwa na baadhi ya viongozi wa Machimbo ya Dhahabu ya Matinje yaliyopo katika Kijiji cha Matinje Kata ya Mwashiku wilayani Igunga. Naibu Waziri alitembelea Machimbo hayo hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani (Mwenye Suti-katikati) akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Machimbo ya Matinje yaliyopo Kata ya Mwashiku wilayani Igunga, Charles Nogu, wakati alipotembelea Machimbo hayo akiwa katika ziara ya kazi hivi karibuni.

  • 18 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Pivotech, Joshua Ibrahim (mwenye suti ya kijivu), akieleza kuhusu uwezekano wa kuanzisha mradi ya bayogesi nchini, wakati wa kikao baina ya kampuni hiyo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), kilichofanyika wiki hii jijini Dar es Salaam.

    Profesa Emmanuel Batamuzi (mwenye suti ya bluu), kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine akizungumzia uwezekano wa kuanzisha mradi wa bayogesi nchini, wakati wa kikao baina ya Kampuni ya Pivotech na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati ), kilichofanyika wiki hii jijini Dar es Salaam.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwaelekeza jambo wawakilishi wa Kampuni ya Pivotech kuhusu kuanzisha mradi wa bayogesi nchini, mwanzoni mwa wiki.

    KIKAO BAINA YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, PROFESA SOSPETER MUHONGO NA KAMPUNI YA PIVOTECH

  • 19BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Kampuni ya Ram Nuclear kutoka Senningerberg yaonesha nia ya Kuwekeza Kwenye Umeme Wa Uranium

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa akifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja Mkuu kutoka Kampuni ya Ram Nuclear yenye makazi yake Senningerberg, Bastian Ringsdorf (hayupo pichani) katika kikao chake na kampuni hiyo pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake.

    Meneja Mkuu kutoka Kampuni ya Ram Nuclear yenye makazi yake Senningerberg, Bastian Ringsdorf akifafanua jambo katika kikao kati ya kampuni hiyo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini.

    Baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Nishati na Madini wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja Mkuu kutoka Kampuni ya Ram Nuclear yenye makazi yake Senningerberg, Bastian Ringsdorf (hayupo pichani)

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa, akifafanua jambo katika kikao kati ya kampuni hiyo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini.

    Meneja Mkuu kutoka Kampuni ya Ram Nuclear yenye makazi yake nchini Senningerberg, Bastian Ringsdorf (mbele wa kwanza kulia) akielezea uzoefu wa kampuni hiyo katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia madini ya urani katika kikao chake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake.

  • 20 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIAMINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIAMINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

    CALL FOR INTERVIEW PRESS RELEASE FEBRUARY 15, 2016

    On behalf of the State Mining Corporation (STAMICO), the Permanent Secretary of the Ministry of Energy and Minerals invites the following shortlisted applicants for the post of Board Directors of the STAMICO to attend oral interview to be held on 22nd February, 2016 from 9:00am at TEITI Conference Hall, International House 4th Floor, Dar es Salaam.

    APPLICANTS FOR THE POST OF DIRECTORS TO CONSTITUTE THE BOARD OF DIRECTORS OF STAMICO

    General Conditions

    1) Applicants must come with their original certificates of Bachelor/Masters Degree and any other supporting documents.

    2) The Ministry will not cover any costs involved in the interview including food, transport and accommodation.

    Note: Applicants whose names are not found on the above list should consider themselves unsuccessful.

    Permanent Secretary,Ministry of Energy and Minerals,

    P. O. Box 2000,DAR ES SALAAM.

    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

    CALL FOR INTERVIEW

    On behalf of the State Mining Corporation (STAMICO), the Permanent Secretary of the Ministry of Energy and Minerals invites the following shortlisted applicants for the post of Board Directors of the STAMICO to attend oral interview to be held on 22nd February, 2016 from 9:00am at TEITI Conference Hall, International House 4th Floor, Dar es Salaam. APPLICANTS FOR THE POST OF DIRECTORS TO CONSTITUTE THE BOARD OF DIRECTORS OF STAMICO S/N NAME AND ADDRESS S/N NAME AND ADDRESS 1. Mgelwa Mgendwa Ilangali,

    P.O Box 63021, DAR ES SALAAM.

    2. Mrisho Said Masebu, P.O. Box 11578, MWANZA.

    3. Mr. Gosbert Josue Kagaruki, P. O. Box 21775. DAR ES SALAAM

    4. Mr. Chacha Werema Chambiri, P. O. Box 11727, DAR ES SALAAM

    5. Emanuel William Massano, P. O. Box 45511, DAR ES SALAAM.

    6. Abdallah H. Musa, P.O Box 5556, DAR ESSALAAM.

    7. Sebastian Sylvester Ndile, P. O. Box 396, MWANZA.

    8. Didace M. Tangatya, P.O Box 798, DODOMA. S/N NAME AND ADDRESS S/N NAME AND ADDRESS

    9. Isaka Bisansaba P.O. Box 10217, MWANZA.

    10. Manyama M. Makweba, P.O Box 833, DODOMA.

    11. Witness Shilekirwa, Wiscon Associates, P. O. Box 78999, DAR ES SALAAM.

    12. Dr. Lightness J. Mnzava, P.O Box 77213, DAR ES SALAAM

    13. Lucy P. Nambuo, P.O. Box 20766, DAR ES SALAAM.

    14. Prof. Romuald Haule, St. Augustine University of Tanzania, P. O. Box 2622, MBEYA.

    15. Eng. Wanzagi Mkongwe Wansakya P.O Box 11824, MWANZA.

    16. Dr. Hilbrand Shayo, TIB Development Bank, P. O. Box 9373, DAR ES SALAAM

    General Conditions

    1) Applicants must come with their original certificates of Bachelor/Masters Degree and any other supporting documents.

    2) The Ministry will not cover any costs involved in the interview including food, transport and accommodation.

    Note: Applicants whose names are not found on the above list should consider themselves unsuccessful.

    Permanent Secretary, Ministry of Energy and Minerals, P. O. Box 2000, DAR ES SALAAM.

    1. On 04th February, 2016, the Chief Executive of Tanzania Royalty Exploration Corporation issued a News Release, entitled Tanzania Royaltys subsidiary Tanzam provides notice of Force Majeure under agreement with STAMICO (State Mining Company) owned by the Tanzania Treasury. The Press release was wired to the stock markets and became public on 5th February 2016. The press Release indicated that the Force Majeure was being declared due to an invasion and forced occupation of the Buckreef mine by illegal miners. The Press release goes further to suggest that the invasion was instigated by the Deputy Minister for Energy and Minerals during his recent visit to Buckreef mine.

    2. Unfortunately, The News Release by Tanzania Royalty Exploration Corporation regarding the Buckreef mine JV contains misleading information regarding the state of affairs at Buckreef Mine, and appears to have been designed to portray the Deputy Minister, the Government of Tanzania and Tanzanians as being unruly and not law abiding.

    3. It is not the intention of this Press Release to dwell on the Contractual matters between Tanzam and STAMICO, neither do we wish to discuss the effect of the declared Force Majeure. We, however would like to reiterate the Governments dissatisfaction with the poor progress of re-establishing mining at Buckreef mine, which was the main message of the Deputy Minister when he visited the mine on 6th January, 2016. In view of many milestones that were not met by the JV group in 2015, the Deputy Minister required the mining operator to start active mining within fourteen days. This was not unlawful directive as portrayed in TANZAMs News release, as the company had made several promises to commission the mine in 2015. Tanzam came in as a Joint Venture Partern with STAMICO, with a promise to commission a medium-scale mine by May, 2014.

    4. On 8th February, 2016, the Commissioner for Minerals visited the Buckreef mine. The Commissioners visit coincided with TANZAMs unilateral declaration of Force Majeure and the unannounced suspension of all activities on the Buckreef mine. On inspecting the mine premises, in particular the South Pit, the Commissioner and his hosts noted nothing unusual as there were no single artisanal miner found in the vicinity of South Pit and there was as such no security threat as indicated in TANZAMs Press Release. Sporadic artisanal mining activities were reported to occur at the margins of the Buckreef portfolio and away from the operations area. Moreover, there was no security issue that was reported by the Company to Government in recent days.

    5. We believe, any grievances that the investor had or continues to have, would have been attended to by Government according to existing laws. However, the use of press for malicious purposes like the News Release in question, is not helpful neither it is ethical. This is more disturbing when the information disseminated is utterly incorrect as in the case of the status of the Buckreef Mine.

    6. We wish to inform the public that the Buckreef mine is secure and there is no invasion or forced occupation of the mine at present. The onus is for JV partners to develop the mine according to the authorised timeline, and in accordance with the Licence conditions.

    7. The Government will continue to work with responsible investors to ensure smooth development of the mineral sector in Tanzania, within the existing legal and regulatory regimes. We also call upon the investors to avoid unnecessary disputes with Government or local communities and to try as much as possible to seek redress through the provided legal and administrative channels, which for the case of Tanzania, they are always welcoming and very transparent.

  • 21BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Maonesho ya 5 ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yenye aina mbalimbali za vito zikiwemo

    Tanzanite , Ruby, Sapphire , Tsavori te , Rhodol i te , Spessart i te , Tourmaline,

    Chrysobery l na Almasi yanatarajiwa kuvutia

    Zaidi ya kampuni 100 za wafanyabiashara na wachimbaji madini ya Vito kutoka Tanzania na

    nchi zingine za Afrika Mashariki, Kati na Kusini; na zaidi ya wanunuzi 500 kutoka zaidi ya nchi 25

    ulimwenguni

    Jisajili na Ushiriki Sasa!!!

    Wasiliana na: Kamati ya Maandalizi AGF Simu: +255 784352299 or +255 767106773

    Barua pepe: [email protected]

    :ama Ofisi za Madini za Kanda

    Yameandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini

    kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA)

    Ijumaa, Februari 19, 2016kuanzia saa 3: 00 kamili usiku.

    USIKOSE KUMTAZAMA

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa SOSPETER MUHONGO, akizungumzia siku 100 za utawala wa Serikali ya awamu ya tano ,katika Televisheni ya taifa TBC