12
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] HABARI ZA NISHATI &MADINI Toleo No. 85 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Septemba 18 - 24, 2015 Bulletin News http://www.mem.go.tz Maonesho ya vito ARUSHA YAFANE Soma habari Uk. 5 UK 2 Sheria za mafuta, gesi zawakuna wawekezaji kutoka Norway >>> Yawe kama ya Thailand na Hongkong , yaongeze pato la Taifa

MEM 85 Online.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

Habari za nisHati &madini

Toleo No. 85 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Septemba 18 - 24, 2015

BulletinNews

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI &MADINI

Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

Wabunge Soma habari Uk. 2

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2Maonesho ya vito ARUSHA YAFANE

Soma habari

Uk. 5

UK2

Sheria za mafuta, gesi zawakuna wawekezaji kutoka Norway

>>> Yawe kama ya Thailand na Hongkong , yaongeze pato la Taifa

2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Mwandishi wetu, Bangkok- Thailand

Ubunifu na umakini katika sekta ya Madini umeelezwa kuwa ni muhimu kwani umepelekea baadhi

ya nchi ikiwamo Thailand na Hongkong kuingiza fedha nyingi zinazotokana na maonesho ya vito na usonara yanayofanyika kila mwaka katika nchi hizo.

Maonesho hayo ambayo hufuatana, huanzia katika mji wa Bangkok, Thailand na baadaye Hongkong ambayo hufanyika kila mwezi wa Septemba kila mwaka ambapo wauzaji wa madini ya vito na masonara mbalimbali wakubwa na wadogo hukutana katika maonesho hayo kutangaza na kuuza madini hayo.

Katika maonesho hayo pia, wanunuzi mbalimbali wakubwa na wadogo duniani huhudhuria ili kununua na kujenga mawasiliano ya kupata bidhaa hizo za madini ya vito kwa ajili kuuza kwenye nchi mbalimbali duniani.

Kwa hakika maonesho hayo huchangia fedha nyingi kwenye mapato ya nchi za Thailand na Hongkong na sababu hufanywa kila mwaka huku serikali za nchi hizo zikisimamia kwa dhati. Hii ni kutokana na kutambua kwamba nchi hizo zitapata mapato ya kutosha kutokana na kodi baada ya mauzo ya madini hayo ambayo yanaingizwa nchini humo kuuzwa.

Aidha, kwa upande mwingine pato linalotokana na utalii nalo huongezeka kutokana wageni kukodisha hoteli mbalimbali za nchi hiyo, halikadhalika kwa wageni ambao hutumia vyombo vya usafiri kama taxi, bajaji na pikipiki wakiwa nchini humo.

Vilevile, hata mama lishe katika nchi hizo nao hujikuta wakifanya biashara kuliko siku nyingine kutokana na wageni ambao hufika

kwa ajili ya maonesho kwani huvutiwa kula kwenye maeneo hayo pia ukiacha hotelini kwani vyakula vinatengenezwa katika hali ya usafi na ya kuvutia.

Mfano mzuri kwa mwaka huu pekee, Thailand imeweza kupokea makampuni zaidi ya 3000 yaliyofika katika maonesho ukiachilia mbali wanunuzi.

Uchumi wa nchi hizo unaendelea

kukua kila siku zinavyokwenda kutokana na ubunifu walionao ambapo wageni wengi wanaoshiriki maonesho hayo hushangazwa kwamba nchi hizo ambazo hazina madini mathalan Thailand wana kiasi kidogo sana cha dhahabu na Sapphire lakini wanatumia madini ya vito yaliyopo kwenye nchi nyingine ikiwamo Afrika kufanya maonesho na kuyatangaza ili kupata fedha.

Katika kipindi chote cha maonesho serikali za nchi hizo huhakikisha wafanyabishara wa vito na usonara wanaohudhuria maonesho hayo wanawekewa mazingira mazuri yasiyo na usumbufu wa ucheleweshaji wa aina yoyote huku wakiboresha usalama katika maonesho hayo hasa ikizingatiwa kwamba madini ya vito ni mali na yana thamani kubwa ikiwamo Almasi, Tanzanite, Sapphire na madini mengine mengi.

Kutokana na kwamba Serikali na wafanyabishara wa madini mbalimbali wa Tanzania kushiriki kwenye maonesho hayo mwaka huu, ni vizuri waandaaji wa maonesho ya Arusha Gem Fair, Tanzania yanayofanyika kila mwaka jijini Arusha wakajifunza kutoka kwenye nchi za Thailand na Hongkong kwani hakuna asiyeelewa kwamba Tanzania ina madini mengi ya vito.

Umefika wakati kwa Tanzania kuamka na kuandaa maonesho kama hayo ya Thailand na Bangkok ili kuwavutia wafanyabishara na wanunuzi wa madini ya vito na usonara kuja Arusha, Tanzania bila kukumbana na vikwazo visivyo na msingi ili baadaye tuweze kuufanya mji wa Arusha kuwa kituo na kitovu cha soko la vito na usonara barani Afrika kwani uwezo tunao, sababu tunayo na njia tunayo ya kufanya hivyo.

Maonesho ya vito Arusha yafane

PICHA ZOTE: Wafanyabiashara wa madini kutoka Tanzania wakionesha madini ya vito katika Banda la Tanzania jijini Bangkok, Thailand. Nchi ya Thailand hufanya maonesho hayo kila mwaka ambapo huwaingizia fedha nyingi za kigeni zinazotokana na mauzo ya vito pamoja na utalii unaotokana na wageni wanaoshiriki kwenye maonesho hayo kutoka nchi mbalimbali duniani.

3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

TahaririMEM

Na Badra Masoud

Five Pillars oF reForms

KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano

Bodi ya uhariri

Mhariri MkUU: Badra MasoudMSaNifU: Essy Ogunde

WaaNdiShi: Veronica Simba, asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, rhoda James ,

Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

increase eFFiciencyQUality delivery

oF Goods/service

satisFaction oF tHe client

satisFaction oF BUsiness Partners

satisFaction oF sHareHolders

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

Hatutaki aibu maonesho ya Vito Arusha

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

Awamu ya Pili Miradi ya Madini MbioniNa Asteria Muhozya, Dar es Salaam

Wizara ya Nishati na M a d i n i inatarajia kuzindua

Awamu ya Pili ya Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini kufuatia warsha ya uzinduzi itakayofanyika mjini Morogoro ikilenga kupata mrejesho wa utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi na kuangalia namna bora ya utekelezaji wa mradi Awamu ya Pili.

Akizungumza kuhusu miradi hiyo inayofadhiliwa na Serikali ya Tanzania

kwa kushirikiana na IDA, Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), Mhandisi Idrisa Yahya ameeleza kuwa, ongezeko la fedha za jumla ya kiasi cha dola za kimarekani milioni 50 unatarajia kuleta mafanikio katika sekta ya madini, kwa kuwa inatarajia kusaidia kuboresha faida zitokanazo na sekta ya madini nchini hususan kwa wachimbaji wadogo.

Aidha, aliongeza kuwa, mradi huo utalenga kufungamanisha sekta ya madini na sekta nyingine za kiuchumi, kuboresha rasilimali katika sekta husika, kuongeza uwazi na

uwajibikaji kwa kusaidia utekelezaji wa sera na sheria ya madini.

Vilevile alisema kuwa, mradi huo utaongeza uwazi na uwajibikaji katika kushughulikia masuala ya madini; kuwaongezea uwezo watumishi wa Wizara katika kusimamia sekta; na kuchochea uwekezaji katika sekta ya madini kupitia kuboresha taarifa za kijiolojia.

Pia, Mhandisi Idrisa alisema kuwa, warsha hiyo inatarajia kujadili mrejesho wa matokeo ya utekelezaji wa mradi kwa awamu ya kwanza , kutafuta taarifa na kujadili namna bora ya utekelezaji wa mradi awamu ya pili.

Miongoni mwa habari kubwa wiki hii ni habari ya kufanikiwa kwa maonesho ya vito na usonara katika nchi za Thailand na Hongkong na kuchangia kuongeza pato la taifa kwa kiasi kikubwa licha ya kwamba nchi hizo hazina madini mengi kama ilivyo Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika.

Miongoni mwa sababu zinazofanya maonesho hayo kufanikiwa ni uwepo wa mazingira mazuri ambayo huwavutia wafanyabishara na wanunuzi wa madini ikiwamo upatikanaji wa visa, wakifika kwenye viwanja vya ndege hawasumbuki kwa kusubiri muda mrefu kukamilisha taratibu na sheria za kuingiza madini hayo katika nchi hizo.

Aidha, watendaji katika kila eneo ikiwamo kwenye maonesho hayo hawachoki na wakati wote wapo tayari kutoa msaada unapohitajika kwa wafanyabishara na wanunuzi wa madini hayo ya vito na hata wageni mbalimbali wanaofika katika maonesho.

Kwa upande mwingine usalama ndani ya maonesho hayo pamoja na nchi hizo ni wa hali ya juu huku wakihakikisha kwamba wafanyabishara au wanunuzi wa madini hayo hawatapeliwi au kuibiwa wakati wakifanya biashara hizo watendaji na wafanyakazi katika maonesho hayo wakati wote wamekuwa wanyenyekevu na wasiochoka wala kukasirika.

Baada ya Serikali (Wizara), Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na wafanyabishara wa madini mbalimbali wa Tanzania kushiriki kwenye maonesho hayo mwaka huu tunaamini wanaondaa Maonesho ya Vito na Usonara Arusha mwakani watakuwa wamejifunza vya kutosha katika maonesho ya Thailand na Hongkong na wala hatuoni sababu ya wao kushindwa kufanya maonesho ya Arusha yakawa bora na ya kuvutia huku Serikali kwa upande mwingine ikipata mapato.

Ni lazima tuamke sasa kwa kuhakikisha maonesho tunayoandaa mwakani Arusha, Tanzania yawe kama ya maonesho ya Thailand na Hongkong ili kuwavutia wafanyabishara na wanunuzi wa madini ya vito na usonara kuja Arusha, Tanzania bila kukumbana na vikwazo visivyo na msingi kwa lengo la kuufanya mji wa Arusha kuwa kituo na kitovu cha soko la vito na usonara barani Afrika kwani uwezo tunao, sababu tunayo na njia tunayo ya kufanya hivyo.

Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Mhandisi Idrisa Yahya (kushoto) akieleza jambo katika moja ya shughuli za mradi wakati akikagua Jengo la Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC). Shughuli za uimarishaji na uendelezaji wa kituo hicho zilifanyika chini ya Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP). Wengine wanaosikiliza ni baadhi ya watumishi wa Wizara na watumishi wa Kampuni ya Kiure Engineering.

4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Veronica Simba – Bukoba

Serikali imesema mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao utatumia lugha za Kiswahili na Kiingereza

ili kuwawezesha watumiaji wake kuwa na uhuru wa kuchagua lugha ya kutumia.

Kufuatia hali hiyo, Serikali imewataka wachimbaji wadogo wanaomiliki leseni za madini nchini kuondoa hofu kuwa hawataweza kuutumia mfumo huo mpya kutokana na kile walicholalamikia kuwa mfumo unatumia lugha ya Kiingereza pekee.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni mjini Bukoba, Mkoani Kagera na Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Nuru Shaban wakati wa semina kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini kuhusu matumizi ya mfumo huo.

Mhandisi Shaban alisema kuwa Serikali ilizingatia umuhimu wa matumizi ya lugha zote mbili wakati wa kuandaa mfumo husika na kwamba tayari rasimu ya Kiingereza ilishakamilika wakati ile ya Kiswahili ikitarajiwa kukamilika hivi karibuni.

“Kilichochelewesha rasimu ya Kiswahili kukamilika ni kwa sababu ilipelekwa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa ajili ya kupitiwa na wataalam ili kuhakikisha lugha iliyotumika ni fasaha,” alifafanua.

Wakati huohuo, Mtaalam kutoka Kitengo cha Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Juma Masoud aliwataka wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini kuhakikisha wanawasilisha taarifa sahihi wakati wa zoezi la kusajiliwa kwenye mfumo huo mpya.

Alisema, Maafisa Madini watafanya kazi ya kuzungukia maeneo yote ya kazi wa wamiliki

wa leseni ili kujiridhisha na usahihi wa taarifa watakazokuwa wametoa wakati wa usajili.

Alisema, itakapobainika kuwa mmiliki wa leseni ametoa taarifa zisizo sahihi, atapewa taarifa kupitia akaunti yake kwenye mfumo mpya ikimtaka awasilishe taarifa sahihi na asipofanya hivyo, atafutwa kwenye mfumo.

Wizara ya Nishati na Madini inaendesha mafunzo kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini nchi nzima kuhusu mfumo mpya wa utoaji huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao.

Mfumo wa kutoa huduma za leseni kwa njia ya mtandao ulizinduliwa mapema mwezi Juni mwaka huu mjini Dodoma ili kutoa huduma za haraka, kuongeza uwazi na kumuwezesha mteja kusimamia leseni zake mwenyewe.

Mmoja wa wachimbaji wadogo wa madini – Bukoba akiuliza swali wakati wa semina kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini mjini humo, kuhusu mfumo mpya wa usajili wa leseni za madini kwa njia ya mtandao.

Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini – Kitengo cha Leseni, Juma Masoud akiwasilisha mada wakati wa semina kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini mjini Bukoba kuhusu mfumo mpya wa usajili wa leseni za madini kwa njia ya mtandao.

Afisa Madini Mkazi wa Bukoba, Ali Ali akifafanua jambo kwa washiriki wa semina (hawapo pichani) kuhusu Mfumo mpya wa utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao. Kulia ni Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini – Kitengo cha Leseni, Juma Masoud na Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Wadogo – Bukoba, Mtalemwa Baitani.

Maofisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini Makao Makuu – Dar es Salaam na wale wa Ofisi ya Madini – Bukoba, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina kuhusu mfumo mpya wa utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao mara baada ya semina hiyo iliyofanyika mjini Bukoba hivi karibuni.

KISWAHILI KUTUMIKA MFUMO MPYA WA LESENI ZA MADINI

5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

Na Greyson Mwase na Clinton Ndyetabula

Wadau pamoja na wawekezaji kutoka Norway wamefurahishwa na sheria ya gesi,

mafuta na ile ya uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uziduaji.

Wadau hao walifurahishwa mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene aliyefungua mkutano wa kibiashara kati ya Tanzania na Norway katika masuala ya gesi na mafuta.

Mkutano huo ulikutanisha Waziri wa Biashara na Viwanda kutoka Norway, Monica Maeland na ujumbe wa wadau, wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nchini humo na Waziri wa Nishati na Madini Nchini, George Simbachawene na wataalam na wawekezaji kutoka makampuni ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini. Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu biashara katika sekta za gesi na mafuta.

Waziri Simbachawene alisema katika kuhakikisha sekta za mafuta na gesi zinawanufaisha wananchi wote, Serikali iliamua kutunga sheria ya mafuta, gesi na ile ya uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uziduaji zenye lengo la kuweka mazingira bora ya uwekezaji katika sekta hizo.

Alisema sheria hizi ziko wazi kwa kuwa zinaelezea kwa kina kila eneo katika uwekezaji wa sekta ya mafuta na gesi ikiwa ni pamoja na usimamizi wake, uwazi na ushirikishwaji wa wananchi.

“Sheria hizi zinampa picha kamili mwekezaji kabla ya kuja kuwekeza nchini kwani zimeelezea kila eneo, sheria hizi zinasisitiza Serikali kuweka wazi faida ipatikanayo na uwekezaji katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi,” alisema Simbachawene.

Akielezea ushirikiano kati ya Tanzania na Norway katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta nchini, Simbachawene alisema kuwa nchi ya Norway ilianza kushirikiana na Tanzania tangu zamani hali iliyopelekea kugundulika kwa kiasi kikubwa cha gesi katika kisiwa cha Songosongo na kuokoa mabilioni ya fedha kutokana na gesi hiyo kutumika katika uzalishaji wa umeme nchini.

Alisema Norway kupitia kampuni yake ya utafutaji wa mafuta ya Statoil imekuwa ikishirikisha wazawa kwa kuwapatia mafunzo kazini, na kupelekea idadi ya wataalam wa mafuta na gesi kuongezeka nchini,

Aliongeza kuwa Norway

imekuwa ikitoa ufadhili kwa wanafunzi wa kitanzania, kusomea masuala ya mafuta na gesi na kusisitiza kuwa bado nchi ya Tanzania inahitaji wataalam zaidi katika masuala ya gesi na mafuta.

Wakati huohuo akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Biashara na Viwanda kutoka Norway, Monica Maeland alisema kutokana na sheria kuhusu mafuta na gesi kuwa wazi nchi ya Norway itaongeza nguvu zaidi katika uwekezaji kwenye sekta hizo ili nchi ya Tanzania iweze kupiga hatua kiuchumi.

Akielezea uzoefu wa Norway katika usimamizi wa sekta za gesi na mafuta Maeland alisema kuwa mara baada ya gesi kugunduliwa nchini humo, nchi hiyo ilikaribisha wawekezaji kutoka makampuni ya kimataifa katika utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi, kusomesha wataalam wake katika masuala ya gesi na mafuta na kuwekeza katika utafiti wa gesi na mafuta kwenye vyuo vikuu vya nchi hiyo.

Alisisitiza kuwa serikali ya Norway pia iliwekeza katika teknolojia kwa kununua vifaa vya kisasa katika utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta na kuhamasisha uwazi kwa wananchi.

“ Sekta za gesi na mafuta ni nyeti mno, hivyo uwazi unahitajika kwa wananchi, na kuwa sehemu ya uwekezaji huo na naipongeza Tanzania kwa kujumuisha uwazi katika sekta za gesi na mafuta,” alisisitiza Maeland.

Maeland alisisitiza kuwa serikali ya Norway iko tayari kushirikiana zaidi na nchi ya Tanzania katika uwekezaji katika sekta za gesi na mafuta, kubadilishana uzoefu ili kuinua uchumi wa nchi.

Sheria za mafuta, gesi zawakuna wawekezaji kutoka Norway>>> Simbachawene: Sheria zimezingatia uwazi na ushirikishwaji wazawa

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akifungua mkutano kuhusu biashara ya mafuta na gesi uliokutanisha wadau kutoka Tanzania na Norway uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Biashara na Viwanda kutoka Norway, Monica Maeland akielezea historia ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi katika nchi ya Norway.

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akisisitiza jambo katika kikao kati yake na Waziri wa Biashara na Viwanda kutoka Norway, Monica Maeland.

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akibadilishana mawazo na Waziri wa Biashara na Viwanda kutoka Norway, Monica Maeland (kushoto) kabla ya kuanza kwa mkutano kuhusu biashara ya mafuta na gesi uliokutanisha wadau kutoka Tanzania na Norway uliofanyika jijini Dar es Salaam. Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa sekta hizo.

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene katikati akimweleza Waziri wa Biashara na Viwanda kutoka Norway, Monica Maeland (wa tatu kutoka kushoto) mikakati ya serikali katika kuhakikisha wananchi wote wananufaika na ugunduzi wa gesi nchini.

6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Wanunuzi wa madini wakikagua madini ya vito kutoka kwa mfanyabiashara wa madini wa Tanzania katika banda la Tanzania kwenye maonesho kimataifa ya 56 ya Madini ya vito na usonara yanayofanyika mjini Bangkok, Thailand.

Ofisa kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), Stella akimpatia maelezo mmoja kati ya wanunuzi wa madini ya vito waliofika katika banda la Tanzania kutaka maelezo ya jinsi ya kuweza kununua madini hayo ya vito yanayopatikana Tanzania.

Picha ya pamoja kati ya ujumbe kutoka Wizara ya Nishati na Madini ya Tanzania na maofisa waandamizi wanaosimamia maonesho ya kimataifa ya Madini ya vito mara baada ya ufunguzi rasmi kufanyika jijini Bangkok, Thailand.

Wanunuzi wa Madini ya vito waliofika katika banda la Tanzania wakipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Wizara ya Nishati na Madini waliopo kwenye banda la Tanzania.

MAONESHO YA VITO NA USONARA BANGKOK

7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

MAONESHO YA VITO NA USONARA BANGKOK

Baadhi ya Madini ya Vito kutoka Tanzania yakiwa katika banda la Tanzania kwa ajili ya mauzo kwa Wafanyabiashara wa nchi mbalimbali waliofika katika banda hilo kununua kutoka kwa wafanyabiashara wa Tanzania.

Wafanyabiashara wa madini kutoka Tanzania wakionesha madini ya vito katika Banda la Tanzania jijini Bangkok, Thailand. Nchi ya Thailand hufanya maonesho hayo kila mwaka ambapo huwaingizia fedha nyingi za kigeni zinazotokana na mauzo ya vito pamoja na utalii unaotokana na wageni wanaokuja kushiriki kwenye maonesho hayo kutoka nchi mbalimbali duniani.

Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja (kulia) akisalimiana na mmoja wa wa washiriki wa maonesho hayo kutoka Tanzania

8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Veronica Simba - Geita

Wachimbaji wadogo wa madini nchini wameshauriwa k u t o o g o p a mabadiliko ya

teknolojia katika sekta husika na badala yake wayatumie vizuri ili yawasaidie kuboresha mazingira ya utendaji kazi wao na hivyo kukuza vipato vyao.

Ushauri huo umetolewa hivi karibuni mjini Geita na Mwenyekiti wa Chama cha Watafutaji na Wachimbaji Madini Wadogo, mkoani humo (GEREMA), Christopher Kadeo, wakati wa Semina kwa wachimbaji hao kuhusu mfumo mpya wa utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao.

Kadeo aliwashauri wachimbaji wenzake kujisajili kwa wingi na kwa wakati katika mfumo huo mpya ulioanzishwa na Wizara ya Nishati na Madini unaolenga pia kuboresha huduma za utoaji na usimamizi wa leseni za madini nchini.

“Baada ya mafunzo haya tuliyopatiwa na Wizara, ninatarajia sisi wachimbaji na wamiliki wa leseni za madini Geita tuchangamkie zoezi la kujisajili kwenye mfumo huu, ikiwezekana ndani ya wiki moja wote tuwe tumeshakamilisha usajili,” alisisitiza Kadeo.

Alisema, uwezekano wa kuutumia mfumo huo mpya kwa ufanisi ni mkubwa akitoa mfano wa mfumo wa utangazaji kupitia Runinga ulivyobadilishwa kutoka analogia kwenda digitali, “nasi katika Sekta ya Madini tusing’ang’anie kutumia analogia, tukubali kuhamia katika mfumo wa

digitali ili tuweze kunufaika zaidi.”Mwenyekiti huyo wa

wachimbaji madini alisema kuwa kuogopa mabadiliko ni suala ambalo limekuwa likirudisha nyuma maendeleo ya nchi katika nyanja mbalimbali na kuwataka watanzania kuondokana na uoga huo.

Vilevile, Kadeo aliwataka wachimbaji na wamiliki wa leseni za madini kuzitumia ofisi za madini zilizoko katika maeneo yao pale wanapohitaji ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayohusu sekta hiyo badala ya kusikiliza maneno ya mitaani.

Kwa upande wake, Mtaalam kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Geita, Musimu Kabasa aliwataka wachimbaji na wamiliki wa leseni za madini kutokimbilia Mahakamani pindi wanapokuwa na migogoro baina yao ama watu au vikundi mbalimbali katika jamii bali wawaone Maofisa wa Madini ili waweze kuwasaidia kusuluhisha na kutatua migogoro hiyo.

Alisema Maafisa Madini, wanafanya kazi chini ya Kamishna wa Madini ambaye amepewa Mamlaka kisheria kutatua migogoro inayohusu sekta hiyo.

“Si busara kukimbilia Mahakamani kila mnapokutana na migogoro ambayo inaweza kutatuliwa au kusuluhishwa na Kamishna wa Madini nchini. Mkumbuke kuwa Kamishna ni mtaalam wa sekta husika, yeye na wataalam walio chini yake wanaielewa vema sekta ya madini hivyo ni rahisi kwao kutatua migogoro hiyo,” alisisitiza Kabasa.

Semina kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini kuhusu mfumo mpya wa usajili wa leseni za madini kwa njia ya mtandao iliyofanyika Geita, ni mwendelezo wa semina zinazoendelea kufanyika nchi nzima chini ya Wizara ya Nishati na Madini kupitia Kitengo chake cha Leseni.

Wachimbaji Madini Waaswa kutoogopa TEKNOLOJIA

Baadhi ya wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini mjini Geita wakiwa katika semina kuhusu mfumo mpya wa utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao, iliyofanyika hivi karibuni mjini humo.

Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini – Kitengo cha Leseni, Mhandisi Nuru Shaban

Kaimu Ofisa Madini Mkazi wa Geita, Godfrey Kelaka

Mwenyekiti wa Chama cha Watafutaji na Wachimbaji Madini Wadogo (GEREMA), Christopher Kadeo

Ofisa kutoka Ofisi ya Madini – Geita, Fabian Mshai

9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

Na Veronica Simba - Kahama

Serikali imesema wachimbaji wadogo wa madini wanaruhusiwa kumiliki idadi yoyote ya leseni za madini ilimradi waweze

kuzifanyia kazi.Hayo yalisemwa hivi karibuni

mjini Kahama na Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Kitengo cha Leseni, Mhandisi Nuru Shabani wakati akiwasilisha mada kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao, wakati wa semina iliyofanyika mjini humo.

“Mchimbaji mdogo anaruhusiwa kumiliki idadi yoyote ya leseni anazoweza kumudu kuzifanyia kazi. Kwa upande wa wachimbaji wakubwa, wao wanaruhusiwa kumiliki leseni zisizozidi 20 lakini pia sheria inawataka wawe na uwezo wa kuzifanyia kazi,” alisema Mhandisi Shabani.

Mhandisi Shabani alitoa ufafanuzi huo kufuatia swali lililoulizwa na mmoja wa washiriki wa semina hiyo, ambaye alitaka kufahamu idadi ya leseni anazopaswa kumiliki mchimbaji mdogo wa madini.

Akifafanua zaidi kuhusu umuhimu wa wamiliki wa leseni kuzifanyia kazi, Mhandisi Shabani alisema, kwa yeyote anayemiliki leseni na kuliacha eneo husika pasipo kulifanyia kazi, sheria inaelekeza kuwa mtu huyo anyang’anywe leseni yake.

Alisema, mfumo mpya wa utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao umeweka mazingira wezeshi kwa mmiliki wa leseni ambaye hafanyii kazi eneo lake, kutambulika kwa urahisi na hivyo hakuna namna ambayo mhusika anaweza kufanya udanganyifu kwa Serikali kwa kuhodhi eneo pasipo kulifanyia kazi.

Wizara ya Nishati na Madini ilizindua mfumo wa kutoa huduma za leseni kwa njia ya mtandao mapema mwezi Juni mwaka huu mjini Dodoma ili kutoa huduma za haraka, kuongeza uwazi na kumuwezesha mteja kusimamia leseni zake mwenyewe.

Ni kwa kuzingatia umuhimu wa matumizi ya mfumo huo mpya kwa wadau wa sekta ya madini nchini, Wizara kupitia Kitengo cha Usimamizi wa Leseni inaendesha zoezi nchi nzima kuwaelimisha wadau hao namna mfumo huo unavyofanya kazi.

Ruksa wachimbaji wadogo kumiliki leseni kadri wawezavyo

Ofisa Madini Mkazi wa Kahama, Sophia Omar, akifungua mafunzo kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini kuhusu matumizi ya huduma mpya ya utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao. Mafunzo hayo yamefanyika hivi karibuni mjini Kahama ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo yanayotolewa na Wizara ya Nishati na Madini kwa wachimbaji wadogo nchi nzima.

Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini Mkoani Shinyanga (SHIREMA), Bahati Kalekwa akitoa neno la shukrani kwa Wizara ya Nishati na Madini kuandaa na kuendesha mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini kote kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao.

Juma Masoud akiwasilisha mada kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni wilayani Kahama, kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao. Semina hiyo imefanyika hivi karibuni mjini Kahama ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo yanayotolewa na Wizara ya Nishati na Madini kwa wachimbaji wadogo nchi nzima.

10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Wizara ya Nishati na Madini inasikitika kutangaza Kifo cha Mfanyakazi wake Edward D. Mwaisopo, kilichotokea tarehe 05/09/2015, Mkoani Dodoma.

Marehemu aliajiriwa na Wizara ya Nishati na Madini katika Chuo cha Madini Dodoma kama Fundi Sanifu Migodi mwaka 2002. Pia alijiendeleza katika Chuo cha Madini Dodoma katika Fani ya Jiolojia mwaka 2005 hadi mwaka 2008 alipohitimu na kupata Stashahada ya Jiolojia.

Mwaka 2010 alihamishiwa Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini Dar Es Salaam hadi mwaka 2011 alipohamia Dodoma katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi.

Marehemu ameacha Mjane na Watoto watatu (3) wawili wa Kike na mmoja wa kiume.

Mpango Mkakati wa Mawasiliano Sekta ndogo ya Gesi na Mafuta

TANZIA

02/10/1968 - 05/09/2015Bwana Ametoa na Bwana

Ametwaa jina lake Lihimidiwe.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava na baadhi ya watendaji wa Wizara, akiwa na ujumbe kutoka Shirika la Maendelo la Ujerumani( GIZ ) waliofadhili Mpango Mkakati wa Mawasiliano Sekta ndogo ya Gesi na Mafuta, ujumbe huo umefika wizarani ili kuona hatua iliyofikiwa juu ya mkakati huo.

Mhandisi Ngosi Mwihava

11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

STATE MINING CORPORATION (STAMICO)

INVITATION FOR EXPRESSION OF INTEREST (EOI) FOR FORMING A JOINT VENTURE COMPANY (JVC) FOR BUHEMBA GOLD MINE RE-DEVELOPMENT PROJECT AND PROCESSING OF OLD GOLD TAILINGS.

TENDER NO. PA/133/2015/2016/HQ/C/01

1. State Mining Corporation (STAMICO), a state owned corporation (100%) of the United Republic of Tanzania, is seeking a joint venture partner on Buhemba mine re-development project and Processing of Tailings. The joint venture partner will provide equity capital financing of the project and shall participate in the operations of the project.

2. STAMICO is the owner of Buhemba property through prospecting license PL 7132/2011. The licensed area lies approximately 50 kilometers south-east of Musoma Town in the new Butiama district, Mara Region and covers 8.18 square Kilometers in area. The property is potential for an insitu hard rock and tailings inferred resources estimated at 610,590 ounces and 50,000 ounces of Gold, respectively.

The Main objective of STAMICO is to seek for a joint venture partner with sound technical capability and financial Capacity to undertake the following activities:

I. Exploration, mining, processing and marketing of gold

II. Processing of old gold tailings existing in the project area

3. STAMICO is inviting sealed Expression of Interest from technically and f i n a n c i a l l y competent companies/consortium to partner in developing and operating the Buhemba Gold Mine hard rock resources and processing old gold tailings and mineralized waste rocks.

4. Interested companies are requested to provide information indicating that they are capable and qualified to re-develop the Buhemba Gold Mine project and

processing of tailings by submitting the following:

a) C o m p a n y particularsi. Name and country of the company/consortium ii. C o m p a n y ’ s registration certificateiii. C o m p a n y ’ s physical and postal address, fax and website address of its headquarters and branches if anyiv. Organization setup including names and nationality of

directors of the company/consortium. In case of consortium, submission should include original documents of powers of Attorney authorizing leading partner to represent and act on behalf of the consortium.

b) Technical capabilityi. Details of company’s experience in the

mining field, at least five (5) years of experience in exploration, development and or management of medium to large scale gold mines

ii. Processing of tailings and mineralized waste rocks

iii. Number and Credentials (CVs) of professional experts in the field of exploration, mining, processing, metallurgy, mechanical, electrical, civil, environment, safety and occupational health owned by the company.

c) Financial capabilityi. Submission of latest three years audited

financial statements of the company/individual companies within the consortium in an International Financial Reporting Standards (IFRS).

ii. Proof/Availability of Equity Contributioniii. Percentage of loan capital and sources of

such capital. Note that STAMICO will participate in raising capital from local financial institutions if required; and

iv. Readiness to pay signature bonus to STAMICO immediately after winning the tender.

d) Other informationi. Proposal to use local expertise and promote

local content on services in line with the

Mining Act, 2010ii. Proposed Joint Venture structure iii. Interested foreign joint venture partners

should also state on the availability of funds to finance the project and/or availability of a Government guarantee for internal and external bank loans will be an added advantage

iv. Any other information which the company may consider relevant to support its proposal.

v. For non-African based applicants, provide experience in running mining related projects in African countries

5. Companies will be shortlisted in accordance with the procedures set out in the Public Procurement Act No. 7 of 2011 and the Public Procurement Regulations – Government Notice No. 446 of 2013.

6. Selection will base on the criteria set out in item four (4) above and shortlisted companies will be invited to obtain tender documents and submit their technical and financial proposals for final consideration.

7. Interested eligible companies may obtain further information on the project profile from the office of the Tender Board Secretary of the State Mining Corporation from 9:00 to 15:00 hours from Monday to Friday inclusive except on public holidays.

8. EOI should be delivered to STAMICO’s Tender Board Secretary at the physical address and clearly marked “Expression of Interest for forming a joint venture Company for Buhemba gold mine re-development project and processing of existing old gold tailings”.

MANAGING DIRECTORState Mining Corporation (STAMICO)Plot No. 417/418, UN RoadP.O. Box 4958Dar es Salaam

9. The deadline for submission of the Expression of Interest is by Thursday 15th October 2015 at 14:00 Hours (EAT). Late submission of Expressions of Interest shall not be accepted for evaluation irrespective of the circumstances.

MANAGING DIRECTORSTATE MINING CORPORATION

12 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini