BULLETIN 95 Online.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

  • Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    Habari za nisHati &madini

    Toleo No. 95 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Novemba 27 - Desemba 3, 2015

    BulletinNews

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    http://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI &MADINI

    Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

    JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

    Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

    Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

    Wabunge Soma habari Uk. 2

    Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

    WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

    Soma habari

    Uk. 3

    Baadhi ya wataalamu wa Kikosi-kazi cha uokoaji migodini wakiwa katika mafunzo.

    Serikali yajidhatiti kuepusha maafa migodini

    Marufuku kuchapisha kadi za Krismas na Mwaka Mpya

  • 2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Zuena Msuya na Remija Salvatory

    Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeunda Kikosi kazi Maalum cha Wataalam 17 na kuwapatia mafunzo maalum ya uokoaji

    kutokana na ajali zinazotokea katika Migodi ya Madini nchini.

    Mafunzo hayo yaliyofanyika hivi karibuni Mkoani Morogoro yaliwashirikisha pia Wakaguzi wa Madini kutoka sehemu mbalimbali nchini.

    Akifungua mafunzo hayo, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Mashariki, Mhandisi Juma Sementa alisisitiza umuhimu wa wataalam wanaounda kikosi kazi cha uokoaji kufanya mazoezi mara kwa mara ili kupata uzoefu na kujiweka tayari wakati dharura inapotokea.

    Aidha, Sementa aliongeza kuwa Serikali imezingatia kuwa na kikosi madhubuti cha uokoaji na hivyo imejipanga kuhakikisha kikosi hicho kinapatiwa mahitaji yote muhimu yanayohitajika ili kukiwezesha kukabiliana na ajali migodini muda wowote zinapotokea pasipo kupoteza muda.

    Unajua ajali hutokea wakati wowote, hivyo tutahakikisha kunakuwa na vifaa vyote stahiki vya uokozi muda wote. Nanyi tumieni mafunzo mliyopata kikamilifu katika kuhakikisha uokoaji unafanyika kama inavyotakiwa ili kuondoa hofu pindi ajali zinapotokea, alisema Mhandisi Sementa.

    Kwa upande wake, Mratibu wa mafunzo husika ambaye pia ni Mkaguzi wa Migodi kutoka Wizara

    ya Nishati na Madini, Mhandisi Assa Mwakilembe alisema mafunzo hayo ni muhimu hususan wakati huu ambapo sekta ndogo ya uchimbaji madini inazidi kukua hali inayosababisha kupanuka kwa shughuli za uchimbaji madini mdogo.

    Aliongeza kwamba mafunzo hayo yatatolewa pia katika maeneo ya wachimbaji wadogo pamoja na wa kati ili waweze kukabiliana na ajali za aina yoyote zinazotokea katika maeneo yao

    ya kazi.Akizungumza kwa niaba ya

    wenzake, mmoja wa wataalam wanaounda kikosi kazi cha uokozi, George Wandibha kutoka Ofisi ya Madini Songea, alisema mafunzo hayo ni muhimu kwao kwani yatawawezesha kutoa huduma ya uokoaji kwa ufanisi kama ilivyokusudiwa.

    Aidha, aliwataka wachimbaji wadogo kote nchini kutoa ushirikiano kwa timu ya uokoaji kwa kuhakikisha

    wanatoa taarifa za haraka kwa Ofisi yoyote ya Madini iliyo karibu na eneo husika pindi kunapotokea ajali ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za kitaalam kwa wakati na hivyo kuepusha madhara makubwa kutokea kwa maisha ya wahanga wa ajali.

    Mafunzo hayo ya uokoaji yalitolewa hivi karibuni na Wakufunzi wataalam kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya Acacia na yalihusisha nadharia na vitendo.

    Serikali yajidhatiti kuepusha maafa migodini

    Serikali yapiga marufuku uchapishaji kadi

    Serikali imepiga marufukku uchapishaji na utengenezaji wa Kadi za Krismasi na Mwaka mpya kwa gharama za Serikali au Tasisi ya Umma kwa mwaka

    huu.Katibu Mkuu kiongozi Balozi

    Ombeni Sefue amepiga marufuku wiki hii katika taarifa yake iliyotolewa na Ikulu.

    Balozi Sefue amesema kuwa kwa yeyote anayetaka kutengeneza kadi hizo afanye hivyo kwa gharama zake mwenyewe.

    Badala yake Balozi Sefue ameagiza kuwa fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji na uchapishaji wa Kadi ,zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, Idara na Taasisi za Umma zinadaiwa na wananchi au Wazabuni waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine ya kipaumbele. Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue

  • 3BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    Five Pillars oF reForms

    KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano

    Bodi ya uhariri MharIrI Mkuu: Badra Masoud

    MsaNIfu: Lucas GordonWaaNDIshI: Veronica simba, asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed saif, rhoda James ,

    Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

    increase eFFiciencyQUality delivery

    oF Goods/servicesatisFaction oF

    tHe clientsatisFaction oF

    BUsiness Partners

    satisFaction oF sHareHolders

    tel-2110490FaX-2110389

    moB-0732999263

    Hongera Sefue kupiga marufuku uchapishaji kadi za Sikukuu

    tel-2110490FaX-2110389

    moB-0732999263

    TPDC kufanya tafiti kwa ndege

    Wiki hii Serikali imepiga marufuku uchapishaji wa kadi za krismas na mwaka mpya kwa kutumia fedha za umma na badala yake fedha zilizotengwa kwa ajili hiyo zitumike kulipa wazabuni waliotoa huduma katika Wizara na taasisi mbalimbali za umma.

    Hatua hiyo imetangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi na kusisitiza kwamba kwa yeyote anayetaka kuchapisha kadi hizo basi afanye hivyo kwa kutumia gharama zake na si vinginevyo.

    Kwetu sisi tunaipongeza kwa dhati hatua hiyo kwani kimsingi haina maana yoyote kutengeza kadi hizo kwa gharama za Serikali huku tukiwa na madeni lukuki ya wazabuni ambao walituuzia vifaa na kutoa huduma mbalimbali.

    Hatua hii ni miongoni mwa baadhi ya hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na viongozi wetu wa juu za kubana matumizi na badala yake fedha hizo kutumika katika kutoa huduma muhimu na za msingi na ambazo zinaleta tija kwa wananchi.

    Tumeshuhudia hatua za hivi karibuni ambazo zimeleta tija kubwa na zilizowapa faraja kubwa Watanzania ikiwamo ya kutumia fedha zilizochangwa kwa ajili ya tafrija ya Wabunge kutumika kununulia vitanda, magodoro na mashuka ya wagonjwa katika Hospitali ya Maifa ya Muhimbili na wagonjwa wote waliokuwa wakilala chini kulala katika vitanda.

    Halikadhalika hatua ya kusitisha sherehe za Maadhimisho ya Uhuru za tarehe 9 Desemba, 2015 badala yake watu wafanye usafi kwani hatuwezi kusherehekea uhuru wakati baadhi ya ndugu zetu katika mikoa mbalimbali wakiugua kipindupindu na huku tukifahamu fika chanzo cha ugonjwa wa kipindupindu ni uchafu. Lazima tuondoe uchafu katika mazingira yanayotuzunguka.

    Vivyo hivyo, katika Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambapo Serikali pia imepiga marufuku sherehe badala yake fedha za sherehe ya maadhimisho hayo zitumike kuwanunulia dawa waathirika wa Ukimwi.

    Kwa hakika tunazipongeza na kuunga mkono hatua zote hizo za kubana matumizi na tutaendelea kutoa ushirikiano kwa hatua nyingine za kubana matumizi zitakazotolewa na viongozi wetu wa juu kwani Rais wetu John Pombe Magufuli alisisitiza Umoja na Mshikamano katika Ujenzi wa Taifa hivyo katika suala hili la kubana matumizi hatuna budi tushirikiane pamoja katika ujenzi wa Taifa letu.

    Tunasema hivyo kwa sababu Taifa lolote Duniani huendelea kwa kujengwa na wananchi wake kwa kila mmoja kuwajibika kwa nafasi yake, hivyo tunasisitiza kwamba Umoja wetu ndiyo utakaochochea ujenzi wa Taifa letu kusonga mbele.

    Tunaunga mkono hatua zote za kubana matumizi na kiasi kikubwa cha fedha kutumika katika kuboresha huduma muhimu kwa wananchi ambao ndiyo waajiri wetu sisi watumishi wa Serikali.

    Na Augustine Kasale - TPDC

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Dkt. James Mataragio amesema Shirika limeanza tafiti za awali za

    mafuta na gesi asilia kwa kutumia ndege (Airbrone Gravity Gradiomery Survey).

    Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro katika zoezi la kupokea ndege ya utafiti kutoka kampuni ya CGG AVITION LTD ya nchini Kanada mwishoni mwa wiki hii.

    Utafiti huo utafanyika katika Kitalu cha Eyasi na Wembere na Mandawa hususan katika Mikoa ya Arusha, Shinyanga, Simiyu, Tabora na Lindi, alieleza Dkt. Mataragio.

    Alifafanua kuwa utafiti utafanyika kuanzia terehe 23 Novemba mwaka huu na utadumu kwa muda wa miezi mitatu hadi utakapokamilika mwezi Januari mwaka 2016.

    Hili ni zoezi la awamu ya kwanza na tumeamua kufanya utafiti huu maeneo haya kwa kuwa tumeona Kenya na Uganda hasa

    maeneo ya bonde la ufa yamegundulika kuwa na mafuta hivyo, hii inaashiria uwezekano mkubwa kwa nchi yetu kupata rasilimali hii, alisema Dkt. Mataragio.

    Aidha, alieleza kuwa utafiti huo unagharamiwa na TPDC kupitia fedha za mfuko wa maendeleo jumla ya shilingi bilioni 14 za Kitanzania na kwamba ni jambo la kujivunia nchi kugharamia utafiti kwa fedha za ndani kuliko kutegemea Wahisani.

    Aliongeza kuwa tarehe 14 Mwezi Novemba Shirika lilipokea ndege ya kwanza ambayo pia imekwisha anza utafiti kama huo katika Kitalu cha Ziwa Tanganyika Kaskazini.

    Pamoja na hayo, Dkt. Mataragio alisema kuwa uzalishaji wa gesi asilia ni mkubwa ukilinganisha na matumizi kwani kwa siku gesi huzalishwa kiasi cha futi za ujazo milioni 240 ilihali matumizi ni futi za ujazo milioni 140 za gesi kwa siku na kubaki ziada ya futi za ujazo milioni 100 za gesi kwa siku.

    Aliongeza kuwa sababu ya kutokuwa na uhitaji wa kutosha katika matumizi ya gesi hiyo ndiyo sababu ya kuwa na ziada ya futi hizo za ujazo.

    Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio akipewa maelezo ya jinsi ndege itakayofanya utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia inavyofanya kazi (ndani ya ndege) kutoka kwa Meneja wa Mradi Brett Robinson wa kampuni inayoendesha utafiti huo ya CGG AVITION LTD kutoka nchini Kanada katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Utafiti huo unagharamiwa na TPDC kutoka katika mfuko wa fedha za maendeleo.

    Ndege ya utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia inayotarajia kuanza utafiti katika kitalu cha Eyasi Wembere na Mandawa ikiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.

  • 4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Asteria Muhozya, Morogoro

    Wizara ya Nishati na Madini imepokea jengo la Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu za

    Kidigitali (Data Recovery Center) kutoka kwa Mkandarasi ambaye ni Kampuni ya G.E Engineering Limited katika makabidhiano ya awali yaliyofanywa Novemba 23 mwaka huu, mjini Morogoro baada ya kufanyika ukaguzi wa kina.

    Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), Mhandisi Idrisa Yahya alisema kuwa, kukamilika kwa kituo hicho kunatarajia kuondoa wasiwasi wa kupotea kwa kumbukumbu za takwimu mbalimbali (data) hususani zinazohusiana na leseni za madini ikiwemo pia kupunguza uhaba wa majengo ya kisasa ya ofisi za madini.

    Alisema kuwa, kituo hicho kimejengwa mahsusi kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu za kidigitali zinazohusu leseni, mpango ambao utasaidia Wizara ya Nishati na Madini kuhifadhi taarifa zake na za taasisi zilizo chini yake zinazohusu sekta ya madini.

    Mhandisi Idrisa aliongeza kuwa, kabla ya kujengwa kwa kituo hicho, taarifa zote zilikuwa zikihifadhiwa Makao Makuu ya Wizara na hivyo, kuona kuwa ipo haja ya kuwa na eneo zaidi ya moja la kuhifadhi kumbukumbu hizo.

    Tuliona kwamba sio sahihi kuwa na eneo moja la kuhifadhi kumbukumbu za kidigitali za madini hivyo kuona umuhimu wa kuwa na maeneo tofauti. Kituo hiki kinatarajia kukusanya kumbukumbu zote za madini nchini na zitahifadhiwa mahali hapa, alisema Mhandisi Idrisa.

    Aidha, aliongeza kuwa, mbali na kuwa na kituo cha kuhifadhi kumbukumbu, baadhi ya ofisi katika jengo hilo pia zinatarajiwa kutumiwa na Ofisi za Afisa Madini Mkazi wa Morogoro.

    Akizungumzia mikakati ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya mradi wa SMMRP (Additional Financing), Mhandisi Idrisa alisema kuwa awamu hiyo ya mradi inatarajiwa kuwezesha kukamilisha malengo ili kufika pale ambapo Serikali imepanga kufika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayosimamiwa na mradi huo.

    Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) cha

    Sehemu ya Jengo la Chuo cha Madini Dodoma litakalotumika kama Hosteli kwa ajili ya wanafunzi wa Chuo cha Madini Dodoma (MRI) Jengo hilo linakarabatiwa chini ya Mradi wa SMMRP kwa ufadhili wa Benki ya Dunia. Jengo hilo linatarajiwa kukabidhiwa rasmi kwa Chuo cha Madini tarehe 30 Novemba,2015.

    Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Uforo Ngowi (katikati), akimsikiliza Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), Mhandisi Idrisa Yahaya na Mkuu wa Kitengo cha IT, Wizara ya Nishati na Madini, Francis Fungameza.

    Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu za Kidijitali (Data Recovery Center) kuhusu taarifa za leseni za madini na taarifa za sekta ya madini. Kituo hicho kimejengwa chini ya Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB).

    Wizara ya Nishati na Madini, Francis Fungameza alieleza kuwa, uwepo wa kituo hicho utawezesha upatikanaji rahisi wa taarifa husika na kwamba uhakika na usalama wake utakuwa wa kiwango kikubwa.

    Kituo hiki kitawezesha kuwepo

    na uhakika wa uwepo wa taarifa hizi hususan taarifa za mfumo wa Huduma za Leseni za Madini kwa njia ya mtandao, aliongeza Fungameza.

    Uzinduzi rasmi wa Jengo hilo ambao kukamilika kwake kumechukua takriban wiki 38 chini

    ya usimamizi wa Mradi wa SMMRP ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia unatarajiwa kufanywa mara baada ya kuteuliwa kwa Waziri wa Nishati na Madini.

    Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotekeleza miradi mbalimbali ya sekta ya madini chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia. Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Benki ya Dunia ambaye pia ni Kiongozi wa Mradi wa SMMRP nchini, Mamadou Barry, wakati wa ufunguzi wa mradi wa SMMRP awamu ya pili, alinukuliwa akieleza kuwa, kutokana na mafanikio yaliyopatikana Awamu ya kwanza, Benki ya Dunia itaendelea kuisadia Tanzania ili kuhakikisha kwamba, sekta hiyo inachangia zaidi katika ukuaji wa uchumi ikiwemo kuhakikisha kwamba

    w a n a n c h i wa Tanzania wananufaika na sekta hiyo.

    Mwarobaini kuhifadhi kumbukumbu wapatikana

    Ni kupitia mradi wa SMMRP

  • 5BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Mtaalamu wa `Server` kutoka Kampuni ya IMEC, David Chikoya (aliyekaa) akiendelea na kazi ya kuhakiki mitambo katika chumba cha kuhifadhi kumbukumbu za kidigitali kuhusu sekta ya madini. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wataalamu kutoka Kampuni hiyo. Wa kwanza kutoka kulia ni Meneja Mradi wa SMMRP, Idrisa Yahaya akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA, Wizara ya Nishati na Madini , Francis Fungameza.

    Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu za Kidijitali (Data Recovery Center) kuhusu taarifa za leseni za madini na taarifa za sekta ya madini. Kituo hicho kimejengwa chini ya Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB).

    ZIARA KITUO CHA KUMBUKUMBU

    Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu (Data Recovery Center) kuhusu taarifa za leseni za madini na taarifa za sekta ya madini. Kituo hicho kimejengwa chini ya Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB).

    Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, pamoja na wakandarasi waliojenga Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu wakishauriana jambo mara baada ya kukagua jengo hilo, lililojengwa chini ya Mradi wa SMMRP kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

    Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika (katikati) akiwa sambamba na Maafisa kutoka Wizarani , Wakandarasi na washauri waliosimamia ujenzi wa Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu za Kidijitali za taarifa za leseni za madini na sekta nzima ya madini wakifanya ukaguzi wa kituo hicho kabla ya makabidhiano ya awali.

  • 6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    PICHANI wiki hii

    Jengo la Canteen kama linavyoonekana kwa ndani

    Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio akitoa maelezo ya jinsi ndege itakayofanya utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia inavyofanya kazi (ndani ya ndege) kutoka kwa Meneja wa Mradi Brett Robinson wa kampuni inayoendesha utafiti huo ya CGG AVITION LTD kutoka nchini Kanada katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Utafiti huo unagharamiwa na TPDC kutoka katika mfuko wa fedha za maendeleo.

    Sehemu ya Jengo la Chuo cha Madini Dodoma litakalotumika kama Hosteli kwa ajili ya wanafunzi wa Chuo cha Madini Dodoma (MRI) Jengo hilo linakarabatiwa chini ya Mradi wa SMMRP kwa ufadhili wa Benki ya Dunia. Jengo hilo linatarajiwa kukabidhiwa rasmi kwa Chuo cha Madini tarehe 30 Novemba,2015.

    Jengo linalotumiwa na wanafunzi wa Chuo Cha Madini Dodoma (MRI) kama linavyoonekana pichani. Jengo hilo limekarabatiwa na Mradi wa SMMRP

  • 7BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    The 5th International Arusha Gem Fair (AGF) will be held on 19th -21st April, 2016 at Mount

    Meru Hotel in Arusha

    Over 100 gemstone exhibitors from Tanzania and other countries from East, Central and Southern

    Africa will be hosted

    Over 500 gemstone buyers from 25 countries worldwide will participate.

    Register and Participate Now!!!

    Contact: AGF Organising Committee Tel: 0784-352-299; 0713-533-986

    & 0767-498-869.

    Email: [email protected]

    :or any nearby Zonal Mines Offices

    Organised by Ministry of Energy and Minerals in collaboration with

    Tanzania Minerals Dealers Association

    STAMICO yawanoa watumishi wake sheria ya mtandaoNa. Issa Mtuwa STAMICO

    Watumishi wa Shirika la Madini la Taifa- STAMICO, wamepatiwa mafunzo ya Sheria ya Makosa

    ya Mtandao (Cyber-crime Act) Na.14, 2015, ili kukuza uelewa wa Sheria hiyo mahali pa kazi.

    Mafunzo hayo yalifanyika hivi karibuni kwa nyakati tofauti kwa Watumishi wa STAMICO katika ofisi za Makao Makuu Dar es Salaam na Dodoma na hivyo kuwawezesha jumla ya Watumishi 88 kunufaika na mafunzo hayo.

    Akiongea mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo, Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA- STAMICO, Raymond Rwehumbiza alisema Shirika limeamua kutoa mafunzo hayo ili kuongeza uelewa na ufahamu wa matakwa ya Sheria husika kwa Watumishi na hivyo kuwawezesha kutambua wajibu na haki zao kwa mujibu wa Sheria.

    Sheria hii ni mpya na watumishi wamekuwa wakiisikia tu, lakini hawana ufahamu wa undani na namna inavyohusika katika utumiaji wa vifaa vya mawasiliano kama vile simu na mitandao, hivyo mafunzo haya yatatoa uelewa wa kutosha kwa watumishi, alifafanua.

    Mafunzo hayo pia yalilenga kuwafahamisha watumishi makatazo

    mbalimbali kufuatia Sheria hiyo ya Makosa ya Mtandao, kuwakinga na makosa ya mitandao na kulinda taswira ya Shirika, kwani inapotokea Mtumishi wa Umma ametenda makosa ya mtandao, doa lake huathiri kwa kiwango kikubwa taswira ya ofisi anayofanyia kazi.

    Naye Afisa TEHAMA Mwandamizi wa STAMICO, Daudi Bupilipili ambaye alikuwa Mwezeshaji wa mafunzo husika, alisema ni kosa kisheria kwa mtu yeyote kusambaza ujumbe wowote usiofaa uliotumwa kwa njia ya mtandao hata kama msambazaji hakuhusika katika kuuandaa ujumbe huo, kwani atakuwa amesaidia kutenda kosa kwa kuusambaza.

    Kupitia mafunzo haya napenda kuwaelimisha kuwa ukipata ujumbe usiofaa kupitia barua pepe yako ufute mara moja na usiusambaze kwa wengine, alisisitiza Bwana Bupilipili.

    Aliyataja baadhi ya makosa yaliyoainishwa katika Sheria hiyo kuwa ni kuandika na kusambaza ujumbe wenye uchochezi wa namna yoyote ile, kusambaza picha zisizo na maadili, picha za utupu na ujumbe wa kumkashifu au kumshambulia mtu mtandaoni kwa namna yeyote ile.

    Makosa mengine ni kusambaza taarifa isiyokuwa na uthibitisho, kufanya udanganyifu wa aina yoyote kwa kutumia mitandao na kuruhusu mtu mwingine kutumia simu yako ya

    mkononi kwa nia ya kutenda uhalifu. Wakizungumza mara baada ya

    mafunzo, baadhi ya Wafanyakazi walisema mafunzo husika yatasaidia kuongeza uelewa katika masuala ya kisheria hususan inayohusu mtandao na hivyo kuepukana na uvunjifu wa sheria husika.

    Kwa upande wake, Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma wa STAMICO, Koleta Njelekela aliwashukuru waandaji wa mafunzo hayo na kuwaasa watumishi kuzingatia mafunzo husika ili kuboresha matumizi sahihi ya mtandao sehemu ya kazi na hivyo kuepuka kuathiri taswira ya Shirika.

    Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA-STAMICO Bw. Raymond Rwehumbiza akitoa mafunzo kuhusu Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cyber-crime Act) Na.14, 2015 kwa Watumishi wa Shirika hilo katika ofisi za STAMICO Makao Makuu, zilizopo jijini Dar es Salaam

  • 8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Tembelea tovuti yetu www.mem.go.tz usome Toleo Maalum la ENERGY SECTOR- QUARTELY DIGEST

    Picha N0. 1, 2 na 3 ikionesha sehemu ya Jengo la GST Dodoma ambalo limejengwa kupitia Mradi wa SMMRP chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia. Aidha, jengo hilo pia litatumika kama ofisi kwa ajili ya viongozi waandamizi wa Wizara.

    Meneja Mradi wa SMMRP, Mhandisi Idrisa Yahya, (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Caroline Msika na Maafisa kutoka Wizara ya Nishati wakijadiliana jambo mara baada ya ukaguzi wa jengo la GST ambalo limejengwa chini ya mradi wa SMMRP.

    2

    43

    1GST yanufaika na SMMRP

  • 9BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Picha 3 na 4, kikao baina ya Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, GST na Wakandarasi wa kampuni ya W&B wakijadiliana jambo kabla ya kuanza ukaguzi wa Jengo la GSTambalo limejengwa chini ya Mradi wa SMMRP kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

    Picha N0. 1 na 2 Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, GST, kampuni ya W& B na washauri wakikagua jengo la GST ambalo limejengwa kupitia Mradi wa SMMRP.

    Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Jilojia Tanzania (GST), Prof. Abdulkarim Mruma, wakati walipofika kwa Wakala huo kukagua Jengo la GST kabla ya makabidhiano ya awali.

    3

    54

    GST yanufaika na SMMRP

    1

    2