11
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] HABARI ZA NISHATI &MADINI Toleo No. 89 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Oktoba 16 - 22, 2015 Bulletin News http://www.mem.go.tz MKOMBOZI Soma habari Uk. 3 JK ameweka misingi sahihi kwa Rais Ajaye – Mwihava Bomba la gesi lenye ukubwa wa kipenyo cha inchi 36 na urefu wa kilomita 477 kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambalo linasafirisha gesi inayozalisha umeme katika kituo cha Kinyerezi I jijini Dar es Salaam Mtambo wa Kufua umeme Megawati 150 kutokana na Gesi Asilia wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam. Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba Rais Jakaya Kikwete

MEM 89 Online.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MEM 89 Online.pdf

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

Habari za nisHati &madini

Toleo No. 89 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Oktoba 16 - 22, 2015

BulletinNews

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI &MADINI

Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

Wabunge Soma habari Uk. 2

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2MKOMBOZI

Soma habari

Uk. 3JK ameweka misingi sahihi kwa Rais Ajaye – Mwihava

Bomba la gesi lenye ukubwa wa kipenyo cha inchi 36 na urefu wa kilomita 477 kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambalo linasafirisha gesi inayozalisha umeme katika kituo cha Kinyerezi I jijini Dar es Salaam

Mtambo wa Kufua umeme Megawati 150 kutokana na Gesi Asilia wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam.

Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba

Rais Jakaya Kikwete

Page 2: MEM 89 Online.pdf

2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Mohamed Saif

Hatimaye mradi mkubwa wa Kitaifa wa miundombinu ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara

na Songo Songo hadi Dar es Salaam umekamilika na kuzinduliwa.

Mradi huo ulizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete tarehe 10 Oktoba, 2015 katika hafla iliyofanyika Madimba mkoani Mtwara na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa, Mabalozi kutoka nchi mbalimbali na wananchi.

Rais Kikwete alisema hatua hiyo ni njia mojawapo kuelekea kwenye uchumi imara katika nyanja mbalimbali ikiwemo uanzishwaji wa viwanda kwani kutakuwa na nishati ya umeme yenye uhakika ambayo itazalishwa kwa kutumia gesi asilia.

Aliuelezea mradi huo kuwa ni mkubwa na wa aina yake kuwahi kufanyika nchini na utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la umeme na kuchochea maendeleo endelevu ya kiuchumi.

Rais Kikwete alizungumzia umuhimu wa suala la Uwajibikaji kwa Jamii yaani Corporate Social Responsibility (CSR) na kuliagiza Shirika La Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhakikisha linasaidia jamii inayozunguka mradi huo wa Madimba kwa kuchimba visima na kusaidia huduma nyingine.

“Suala la CSR halina mjadala, wananchi huku wana shida ya maji, lakini pia msiishie kwenye maji tu bali pia msaidie na mambo mengine. Hii sio hisani, ni wajibu wenu kufanya hivyo,” alisema.

Aidha, Rais Kikwete aliishukuru Serikali ya China kwa utayari wake wa kujenga miundombinu ya mradi husika na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya Tanzania na China.

Hayawi hayawi sasa yamekuwa…

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kituo cha Kuchakata Gesi cha Madimba mara baada ya kutembelea kituo hicho. Kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene na kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt James Mataragio.

>>> Rais Kikwete azindua mradi wa Kitaifa wa Miundombinu ya Kuchakata na Kusafirisha Gesi Asilia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akizindua jiwe la msingi la mradi wa Kuchakata na Kusafirisha Gesi Asilia kutoka Madimba (Mtwara) na Songo Songo (Lindi) hadi Dar es Salaam. Mtambo wa kuchakata Gesi Asilia uliopo Madimba Mkoani Mtwara

Page 3: MEM 89 Online.pdf

3BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

TahaririMEM

Na Badra Masoud

Five Pillars oF reForms

KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano

Bodi ya uhariri

MharIrI Mkuu: Badra MasoudMsaNIfu: Lucas Gordon

WaaNdIshI: Veronica simba, asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed saif, rhoda James ,

Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

increase eFFiciencyQUality delivery

oF Goods/service

satisFaction oF tHe client

satisFaction oF BUsiness Partners

satisFaction oF sHareHolders

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

Makubwa yamefanyika sekta ya Nishati

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

JK ameweka misingi sahihi kwa Rais Ajaye – Mwihava

Wengi tutakumbuka wakati Rais wa awamu ya nne Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alipoingia madarakani mwishoni mwa mwaka 2005 nchi yetu ilikuwa katika mgawo wa umeme na hadi ilipoingia mwaka 2006 mgawo huo wa umeme uliendelea kuwa mkali.

Mgawo huo ulitokana na kukauka kwa Mabwawa ambayo yanatumika kuzalisha umeme ambayo kwa kipindi hicho ndiyo yalikuwa chanzo kikubwa na pekee cha kuzalisha umeme.

Baadhi ya watafiti na wana mazingira walieleza kwamba kukauka kwa mabwawa hayo kunatokana na sababu kubwa mbili ambazo ni mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kilimo kinachofanywa na baadhi ya watu katika vyanzo vya maji (upstream) ambapo huchepusha maji na kushindwa kufuata mkondo wake.

Kutokana na mgawo huo wa umeme Serikali hiyo ya awamu ya nne kupitia Wizara ya Nishati na Madini iliamua kuchukua hatua za makusudi na madhubuti kuanza kukabiliana na hali hiyo ya mgawo na kipaumbele kikiwa ni kujenga mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati mbadala hususan gesi asilia.

Serikali iliruhusu Kampuni binafsi kuchimba gesi na kusafirisha pamoja na kuwauzia Makampuni binafsi, viwanda na TANESCO ili TANESCO nayo iweze kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia.

Ilipofika mwaka 2008 Serikali ilikamilisha ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa Ubungo I wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 102.

Mwaka 2009 mtambo mwingine ulikamilika wa Tegeta wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 45 na mwaka 2012 Serikali ilizundua mtambo wa Ubungo II (Megawati 105). Mitambo yote hiyo inazalisha umeme kwa kutumia gesi asilia na inamilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja.

Serikali pia ilijenga mitambo mingine ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ya Mtwara (Megawati 18) na Somangafungu mkoani Lindi (Megawati 7.5).

Ili kuwa na umeme wa uhakika katika gridi ya taifa kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa, Serikali ilijenga pia mtambo mwingine wa kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta mazito wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 60 uliopo Nyakato, Mwanza.

Kutokana na gesi asilia kugundulika kwa wingi katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania yaani Lindi na Mtwara, Serikali iliamua kujenga bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara na Lindi pamoja na mitambo ya kuchakata ambapo gesi hiyo inazalisha na kusafirishwa hadi kwenye mitambo ya kuzalisha umeme kwani gesi inayozalishwa na kuuzwa na watu binafsi haitoshelezi katika kuzalisha umeme.

Aidha, kutokana na bomba la gesi kujengwa na mitambo yake, Serikali iliona ni busara kujenga mtambo wa Kinyerezi I wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 150.

Mitambo yote ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia iliyojengwa na Serikali tangu mwaka 2008 hadi sasa 2015 imefikia jumla ya Megawati 484.5 ya umeme wote unaozalishwa na mitambo hiyo ya Serikali kupitia TANESCO. Hayo ni mafanikio makubwa katika sekta ya Nishati katika kipindi cha Serikali ya awamu ya nne.

Pamoja na kwamba Serikali ya awamu ya nne inaondoka madarakani mwishoni mwa mwaka huu lakini imeacha misingi mizuri na jitihada kubwa za kuendelea kuboresha sekta ya nishati hususan katika kuzalisha umeme.

Ni ukweli ulio wazi kwamba kukamilika kwa mtambo wa Kinyerezi I ndiyo mwanzo wa kuanza kwa ujenzi wa mitambo mingine ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ya Kinyerezi II, Kinyerezi III na Kinyerezi IV kwani zipo kila dalili za kuandaa na kuendelea kwa ujenzi huo kuwapo kwa eneo lenyewe ambapo mitambo hiyo itajengwa na wahusika wameshaanza kazi.

Hivyo tuna kila sababu ya kuipongeza Serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Mhe. Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwamba imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha kwamba upatikanaji wa umeme unaongezeka ili Taifa la Tanzania litakapofika mwaka 2025 liwe ni taifa la uchumi wa kati na mafaniko hayo yote yatatokana na kuwapo kwa umeme wa kutosha na wa uhakika.

Hii ni dhahiri kwamba maendeleo ya nchi yoyote duniani yanatokana na upatikanaji wa umeme wa uhakika hivyo lazima wote tutambue kwamba bila umeme hakuna maendeleo hivyo, umeme ni maendeleo.

Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava, amesema kuwa, Watanzania wanayo sababu ya kupongeza jitihada zilizofanywa

na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete katika sekta ndogo ya nishati hususan umeme kwani katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne hali ya uzalishaji umeme imeongezeka ikilinganishwa na ilivyokuwa awali.

Mhandisi Mwihava aliyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Mitambo ya kufua Umeme wa kiasi cha Megawati 150 Kinyerezi I jijini Dar es Salaam ,uzinduzi huo uliofanywa na Rais Kikwete mwanzoni mwa wiki na

kuhudhuriwa na wananchi wanaozunguka eneo ilipo mitambo hiyo, baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini, Mashirika ya Kimataifa, Uwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), baadhi ya watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini, watumishi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco),Wakandarasi waliojenga mitambo hiyo na wanaotarajia kujenga vituo vingine vya kuzalisha umeme vya Kinyerezi II na III.

Mwihava alisema kuwa, Rais Kikwete ameweka misingi sahihi kwa Rais ajaye wa Serikali ya Awamu ya Tano kutokana na kuwezesha ongezeko la vituo vya kufua umeme ukiwemo pia mradi mpya wa umeme wa Kinyerezi I na miradi mingine ya umeme inayoendelea kutekelezwa maeneo mbalimbali nchini.

“Umeweka rekodi ya kuwa Rais aliyeongeza megawati nyingi zaidi za umeme katika historia ya nchi yetu tangu uhuru ikiwa ni asilimia 60 ya mitambo yote iliyowekwa na Serikali tangu tupate uhuru mwaka 1961,” alisema Mwihava.

“Katika hili tuna kila sababu ya

>>> ➢Amtaja ndiye Kinara kuongeza uzalishaji umeme

>>> ➢➢Mramba - Kinyerezi I mitambo ya Kisasa

>>Inaendelea Uk. 5

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava akieleza jambo wakati wa uzinduzi wa Mitambo ya Kufua umeme wa gesi wa megawati 150 Kinyerezi I.

Page 4: MEM 89 Online.pdf

4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

JK ameweka misingi sahihi kwa Rais Ajaye – Mwihava

kupongeza jitihada zilizofanywa na Rais Kikwete, na hili limethibitisha jitihada zilizofanywa na, Chama Cha Mapinduzi (CCM). Pamoja na hayo unaondoka ukiwa umeacha miradi mikubwa ya umeme uliyo katika hatua mbalimbali ikiwemo ya Kinyerezi II hadi IV ambayo gharama za ukwekezji huo ni wa Serikali na sekta binafsi ambapo inafikia takriban Dola

za Marekani Bilioni 4 sawa na shilingi trilioni 8.

Mwihava pia aliitaja mitambo ya Kufua umeme iliyojengwa katika kipindi cha mwaka 2005-2010 kuwa ni pamoja na Vituo vya kufua Umeme vya Ubungo I kinachozalisha megawati 102, Ubungo II megawati 105, Tegeta megawati 42, Mtwara megawati 18, SomangaFungu megawati saba na nusu, Nyakato megawati 60 na Kinyerezi I megawati 150, ambavyo

vyote vinafanya jumla ya megawati 484.5, vyote vikiwa vimeunganishwa katika gridi ya taifa.

“JK amewezesha uwepo wa mitambo mipya ya kufua umeme kwa asilimia 47 ndani ya kipindi cha miaka 10. Haya ni mafanikio makubwa. Lakini vipo vituo vingine vinavyozalisha umeme nje ya gridi kama ilivyo kituo cha Kigoma”, alisema Mwihava.

Kwa upande wake Mkurugenzi

Mtendaji TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba aliielezea mitambo ya Kinyerezi I kuwa ni mitambo mipya na ya kisasa yenye teknolojia ya hali ya juu ambayo ni aina ya mitambo ambayo inatumika kuendesha ndege aina ya boeing.

“Huu ni uwekezaji mkubwa. Tanesco tutaendelea kutekeleza majukumu yetu kwa uadilifu hivyo wananchi tarajieni mabadiliko makubwa ya nishati ya umeme kutokana na mitambo yetu na miradi mingine kwani itakuwa mbadala wa vyanzo vya maji,”alisema Mramba.

Mramba aliongeza kuwa, mbali na Mradi wa Kinyerezi I, Tanesco inaendelea na utekelezaji wa miradi mingine ya umeme na kuutaja mradi wa Backbone wa Iringa hadi Shinyanga utakaozalisha Kv 400, Makambako- Songea – Ruvuma Kv 220 na mwingine kutoka Tanzania hadi nchini Kenya wa Kv 400.

“Matatizo yaliyopo sasa ni ya muda mfupi. Tutakuwa na umeme wa kutosha baada ya kukamilika kwa miradi hii, uunganishaji umeme kwa sasa umefikia asilimia 30 kutoka asilimia 10, wakati idadi ya watumiaji wa umeme imefikia asilimia 40,” aliongeza Mramba.

Kinyerezi I ni kituo kimojawapo kati ya vituo vinne vitakavyojengwa Kinyerezi Jijini Dar es Saalm ambapo kukamilika kwake kutawezesha uzalishaji wa umeme wa kiasi cha megawati 1290. Kituo cha kinyerezi I pekee kimegharimu takribani Dola za Marekani milioni 183 sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 400.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mhandisi Felschemi Mramba (wa pili kulia) akiweleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati), pamoja na wageni waliohudhuria halfa ya uzinduzi wa mitambo ya Kinyerezi I jijini Dar es Saalam kuhusu miundombinu ya kusafirisha umeme wakati wa Uzinduzi wa hiyo. Rais aliitembelea mitambo yote iliyopo Kinyerezi I kabla ya kuizindua rasmi.

>>Inatoka Uk. 3

Kasi ya uzalishaji wa umeme yahitajika - KikweteZuena Msuya na Nuru Mwasampeta.

Rais Jakaya Kikwete amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuongeza juhudi katika kujenga mitambo ya

kuzalisha umeme ili kupunguza mgawo unaoikumba nchi hivi sasa.

Rais Kikwete alisema hayo hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi 1 uliofanyika mwanzoni mwa wiki jijini Dar es Salaam ambacho kina uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi cha Megawati 150 kwa wakati mmoja pindi mashine zote nne zitakapowashwa.

Aidha ilielezwa kwamba megawati hizo 150 zitachangia kufikia kiasi cha megawati 350 zinazotarajiwa kuzalishwa katika mradi wa Kinyerezi 1 baada ya kukamilika kwa ujenzi na kuwashwa kwa

mitambo mingine mitatu iliyopo katika eneo hilo. Mitambo hiyo inatarajiwa kukamilika na kuwashwa ifikapo January 2016 hivyo kuchangia katika kupunguza tatizo la umeme linaloikabili nchi yetu hivi sasa, alibainisha.

Kikwete alisema kuwa kwa sasa Tanzania inakabiliwa na upungufu mkubwa wa umeme kutokana na ukame mkubwa ulioikumba nchi kwa mara ya kwanza na kusababisha baadhi ya uzalishwaji wa umeme kupungua na baadhi ya mitambo kama Kidatu kufungwa.

Kutokana na ukame huo, Kikwete ameitaka Tanesco kuongeza kasi ya kujenga mitambo mingine ya kuzalisha umeme kwa njia ya gesi, upepo, tungamo-taka na nyinginezo ili kuondokana na kutegemea umeme wa maji ambao sasa umekuwa si wa uhakika.

“Mabwawa tuliyokuwa tukiyategemea kuzalisha umeme yote yamekauka, ikiwemo Mtera ambayo

sasa imezima mitambo yake. Kidatu ambayo iko mbioni kuzimwa , Kihansi inazalisha robo ya uwezo wake,Hale, vile vile Nyumba ya Mungu hivyo ni lazima tuwe na mbadala wa kuzalisha umeme na tusirudi katika kutumia mafuta mazito yanayoiingiza nchi katika kutumia gharama kubwa za uzalishaji wa umeme”, alisema Rais Kikwete.

Aidha, alitaka kuharakishwa kwa ujenzi wa vituo vingine vya kuzalisha umeme ikiwemo Kinyerezi II,Kinyerezi III, na Kinyerezi IV ambapo ujenzi wa Kinyerezi II unatarajiwa kuanza mwanzoni kwa mwaka ujao mara tu baada ya kukamilika kwa mitambo yote Kinyerezi I na kukamilika ifikapo mwaka 2017.

Aidha Rais Jakaya Kikwete alibainisha kuwa Kenya ni nchi inayozalisha umeme kwa wingi ikifuatiwa na Tanzania lakini baada ya ugunduzi wa gesi asilia na kukamilika kwa ujenzi wa vituo vya kuzalisha umeme Tanzania itakuwa na

uwezo wa kuzalisha umeme wa ziada ambao utauzwa nchini humo.

Alisema nchi zilizoonesha nia ya kununua umeme toka Tanzania kuwa ni Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi pamoja na Zambia hivyo umeme utasaidia hata kukua kwa uchumi wan chi kutokana na kuuza nishati umeme.

Imebainika kuwa umeme unaotarajiwa kuzalishwa kutokana na gesi asilia kuwa ni megawati 1,220 kwa mchanganuo ufuatao; Kinyerezi I itazalisha megawatt 150, Kinyerezi II megawatt 240, Kinyerezi III megawatt 300 na mwisho ni Kinyerezi IV itakayozalisha megawatti 330

Kabla ya uzinduzi wa mradi huu mkubwa wa umeme mheshimiwa Rais alizindua bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara hadi Dar es Salaam pamoja na kituo cha kuchakata gesi asilia kilichopo Madimba mkoani Mtwara.

Page 5: MEM 89 Online.pdf

5BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Asteria Muhozya

Imeelezwa kuwa, kutokana na kukamilika kwa miundombinu ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara, Lindi hadi Dar es Saalaam

kunaifanya Tanzania kuingia katika orodha ya nchi zenye nishati ya gesi asilia.

Aidha, ilielezwa kuwa, Tanzania inayo nishati ya kutosha kukidhi mahitaji muhimu kwa uwekezaji mkubwa, wa kati, wajasiriamali wadogo na uwepo wa nishati hiyo ni nguzo kubwa katika kuchochea maendeleo ya viwanda na ukuaji uchumi ikiwemo pia maendeleo ya jamii.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi James Mataragio wakati wa uzinduzi wa miundombinu ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia iliyofanyika mwishoni mwa wiki,

Madimba, mkoani Mtwara.Mataragio aliongeza kuwa,

kutekelezwa kwa mradi huo kutasaidia kwa kiwango kikubwa katika maendeleo ya nchi kutokana na ukweli kwamba, nishati ndiyo msingi mkuu wa maendeleo kwa nchi yoyote Duniani.

Vilevile, Mataragio alisema kuwa, kukamilika kwa mradi huo kuna faida nyingi ikiwemo wazalishaji wengine wa gesi asilia kuweza kulitumia bomba hilo bila masharti magumu na hivyo kuchochea uwekezaji.

Pia alieleza kuwa, matumizi ya gesi asilia kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo viwandani, taasisi, majumbani, matumizi ya magari na kuzalisha umeme yataongezeka na hivyo kusaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa kiwango kikubwa.

Alizitaja faida nyingine za mradi huo kuwa ni pamoja na kuongeza pato la Serikali kutokana na kodi, mrabaha na gawio kwa uuzaji

wa gesi asilia kwa wingi ikiwemo kuongeza pato kwa Halmashauri za Mtwara na Kilwa kupitia pato la kodi ya huduma.

Aliongeza kuwa, mradi huo utaokoa fedha za kigeni zinazotumika sasa kuagiza mafuta nje ya nchi kwa ajili ya kuzalisha umeme, kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti na kuleta unafuu kwa wananchi watakaotumia gesi asilia kwenye shughuli za kiuchumi ikiwemo kuchochea utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini.

Vilevile, alisema kuwa, mbali na faida hizo, mradi huo umesaidia upatikanaji maji safi kwa matumizi ya binadamu ambapo tayari kijiji cha Madimba kimeanza kupatiwa huduma ya maji ya kiasi cha lita 60,000 kwa siku na kutumiwa na zaidi ya wakazi 3000.

Tanzania yaingia katika orodha nchi zenye gesi asilia

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi James Mataragio, akiongea na waandishi wa habari katika mitambo ya kuchakata gesi Magimba, Mtwara

Moja ya visima vya maji safi vilivyojengwa kutokana na mradi wa gesi asilia. Visima hivi vina uwezo wa kuzalisha maji safi na salama lita 60,000 kwa siku ambayo yanatumiwa na zaidi ya wakazi 3000 wanaozunguka eneo la Madimba, mkoani Mtwara.

Mitambo ya kupokea gesi asilia iliyo katika eneo la SomangaFungu, wilayani Kilwa, mkoani Lindi. Gesi hiyo inapokelewa kutoka mitambo ya Kuchakata gesi iliyopo Madimba-Mtwara na SongoSongo, ambapo husafirishwa kuelekea katika kituo cha Kinyerezi I, Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufua umeme.

Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia uliopo katika eneo la Madimba, Mtwara.

Page 6: MEM 89 Online.pdf

6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Mohamed Saif

Imeelezwa kwamba kutokana na uzinduzi wa mradi mkubwa wa Kitaifa wa miundombinu ya kuchakata na kusafisha gesi asilia, upungufu wa umeme utakuwa

historia.Hayo yameelezwa kwenye hafla ya

uzinduzi wa mradi huo hivi karibuni Madimba Mkoani Mtwara na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene wakati akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kuzindua rasmi

mradi huo.Waziri Simbachawene alimpongeza

Rais Kikwete kwa jitihada zake za kuhakikisha mradi huo unafanikiwa. “Wapo baadhi ya Watanzania ambao wanahoji kuwa unapoondoka madarakani unatuacha achaje?, …nataka niwaambie Watanzania wenzangu Mheshimiwa Rais Kikwete aliikuta Tanzania ikiwa na kiasi cha gesi iliyogunduliwa cha futi za ujazo trilioni 8 lakini anatuacha na futi za ujazo trilioni 52,” alisema.

Alisema kuwa Serikali imewekeza kwa asilimia 100 katika mradi huo na kuongeza kwamba uamuzi wa Serikali kukubali kuwekeza katika mradi huo ni uamuzi unaoonesha namna Serikali ilivyodhamiria kutafuta suluhu ya changamoto za kusambaza gesi kwa watumiaji na pia kuondoa adha ya

ukosefu wa umeme wa uhakika nchini.“Uamuzi huu ni utekelezaji wa Ilani

ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2010 kuhusu upanuzi wa matumizi ya gesi asilia,” alisema Simbachawene.

Alisema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kwamba gesi asilia inapatikana kwa ajili ya kuzalisha umeme na wananchi wengi zaidi kupata gesi kwa matumizi ya majumbani na viwandani.

Aliongeza kuwa “ni wazi kwamba matumizi hayo ya gesi asilia yataongeza kasi ya ukuaji uchumi kwa mtu mmoja mmoja na kwa Taifa kwa ujumla,” alisema Simbachawene.

Waziri Simbachawene alisema kutokana na mradi huo, viwanda nchini vitaongezeka na kubainisha kwamba tayari Kampuni ya Dangote imefungua kiwanda cha kuzalisha saruji.

Alisema kiwanda hicho kitatoa ajira kwa Watanzania wengi na hivyo kupunguza tatizo la ajira nchini. Aidha, mbali na kiwanda hicho, Simbachawene alisema viwanda vingine vitakavyojengwa ni vya mbolea na vya plastic.

“Kampuni ya Dangote imefungua kiwanda cha kuzalisha saruji kitakachokuwa kikubwa katika Afrika na kitatoa ajira kwa Watanzania 1,366 ambapo 697 watakuwa vibarua na 699 watakuwa ni wa kudumu katika fani mbalimbali,” alisema.

Waziri Simbachawene aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kuunga mkono dhamira ya Serikali kwa kutoa vibali kwa mashirika yake hususan China Petroleum Technology and Development Corporation (CPTDC) pamoja na Benki ya Exim ya China kuweza kufanya tathmini ya mradi na kukubali kutoa mkopo wa masharti nafuu na hivyo kufanikisha kukamilika kwa mradi huo.

Vilevile Simbachawene aliwashukuru Mawaziri waliomtangulia katika Wizara ya Nishati na Madini ambao ni William Ngeleja na Profesa Sospeter Muhongo kwa mchango wao katika mafanikio ya ujenzi na hatimaye kukamilika kwa miundombinu husika.

Kufuatia kukamilika kwa Mradi wa Kitaifa wa Gesi Asilia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akikagua Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt James Mataragio akifuatiwa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.

>>> Upungufu wa Umeme kuwa historia>>> Viwanda kuongezeka, ajira nyingi kuzalishwa

Baadhi ya Wananchi waliohudhuria hafla ya kihistoria ya uzinduzi wa mradi wa miundombinu ya kusafisha na kusafirisha gesi kwenye eneo la Madimba, Mkoani Mtwara hivi karibuni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali pamoja na Wakandarasi wa Mradi kutoka Kampuni za CPTDC, CPE na CC za China mara baada ya kukagua Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba.

Page 7: MEM 89 Online.pdf

7BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Ufahamu undani wa Mradi wa Kitaifa wa miundombinu ya Gesi Asilia…Mohamed Saif na Teresia

Mhagama

Ni tukio la kihistoria kuwahi kufanyika nchini ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete

alizindua rasmi mradi mkubwa wa kitaifa wa Miundombinu ya Kuchakata na Kusafirisha gesi asilia.

Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika hivi karibuni kijijini Madimba ambapo kumejengwa miundombinu ya kuchakata gesi asilia na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa, mabalozi wa nchi mbalimbali na mamia ya wananchi wa Mkoani Mtwara na maeneo mengine ya Tanzania.

Awali, akitoa maelezo ya utangulizi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt James Mataragio alisema miundombinu ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia imekamilika na inamilikiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kwa asilimia 100.

Akiuelezea mradi huo, alisema bomba la gesi lina uwezo wa kusafirisha gesi asilia kiasi cha futi za ujazo milioni 784 kwa siku kwa kiwango cha juu bila mkandamizo (compression) na matumizi yakiongezeka zaidi linaweza kusafirisha kiasi cha futi za ujazo hadi milioni 1,002 kwa siku kwa kuongezea mgandamizo pale Somanga-Fungu.

Alisema usafirishaji wa gesi asilia katika bomba hilo kubwa kutoka mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam lenye ukubwa wa kipenyo cha inchi 36 na urefu wa kilomita 477 umeenda sambamba na kukamilika kwa mitambo ya kuchakata gesi hiyo iliyojengwa katika eneo la Madimba mkoani Mtwara na Songosongo mkoani Lindi.

Hii ni kusema kwamba gesi hiyo itasafishwa katika vituo vya Madimba na Songo Songo kabla ya kusafirishwa

katika bomba hilo ambapo mitambo ya Madimba inao uwezo wa kuchakata gesi futi za ujazo zipatazo milioni 210 kwa siku na mitambo ya Songo Songo ina uwezo wa kuchakata gesi futi za ujazo zipatazo milioni 140 kwa siku.

Alisema jumla ya gharama za ujenzi wa mradi huo wa kusafisha na kusafirisha gesi mpaka kukamilika kwake ni Dola za Marekani zipatazo bilioni 1.225, ambapo asilimia 95 ni mkopo kutoka Benki ya Exim ya China na huku asilimia 5 ikitoka Serikalini.

Alieleza kwamba gharama hizo zimegawanyika ambapo mtambo wa kusafisha gesi asilia wa Songo Songo umegharimu Dola za Marekani 151,735,000; Mtambo wa Kusafisha gesi asilia wa Madimba umegharimu Dola za Marekani 197, 877,000 na Bomba la kusafirisha gesi asilia limegharimu kiasi cha Dola za Marekani 875, 715,000. Miundombinu hii inamilikiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kwa asilimia 100.

Katika kuhakikisha kuwa gesi hii inawafikia wananchi wengi nchini, alisema Serikali imeweka matoleo/viunganishi katika sehemu mbali mbali ili kuwezesha kusambaza gesi katika maeneo mbalimbali ambapo bomba kuu linapita na huku akitaja maeneo hayo kuwa ni Mtwara mjini, Lindi, Somanga Fungu, Kilwa na Mkuranga.

Ni dhahiri kuwa uwepo wa gesi asilia utainufaisha Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo kuzalisha umeme, kutumika kama nishati viwandani, taasisi, majumbani, kwenye magari kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti na kuleta unafuu kwa wananchi watakaotumia gesi asilia kwenye shughuli zao za kiuchumi.

Vilevile alisema gesi italinufaisha Taifa kuongeza Pato la Serikali kutokana na kodi, mrabaha na gawio kwa uuzaji wa gesi asilia, kuongeza pato kwa Halmashauri za Mtwara na Kilwa kupitia pato la kodi ya huduma (Service Levy) ambayo ni asilimia 0.3 ya mauzo ya gesi asilia na hivyo kuokoa fedha za kigeni zinazotumika kuagiza mafuta nje ya nchi kwa ajili ya kuzalisha umeme.

Ufunguzi rasmi wa kazi ya kutandaza bomba kutoka Madimba hadi Dar es Salaam, ulifanywa na Rais Jakaya Kikwete kwa kuweka jiwe la msingi katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 8 Novemba 2012.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt James Mataragio akitoa maelezo ya utangulizi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa miundombinu ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia iliyofanyikia Madimba Mkoani Mtwara

>>> Rais Kikwete auzindua rasmi tarehe 10 Oktoba, 2015>>> Unamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100>>> Ni mkubwa na wa aina yake kuwahi kufanyika nchini>>> Umegharimu Dola za Marekani zipatazo bilioni 1.225

Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba

Hatua mbalimbali za ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kabla ya kukamilika kwa mradi huo

Page 8: MEM 89 Online.pdf

8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akikagua Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba. Kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt James Mataragio. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akifuatiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava.

2. Mtambo wa Kuchakata Gesi Asilia wa Madimba, Mkoani Mtwara

3. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete (kulia) akisikiliza maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (hayupo pichani). Kulia kwake ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing na anayemfuatia ni Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.

4. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba. Kulia kwake ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu. Kushoto kwake ni Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete. Wengine ni Viongozi mbalimbali wa Kitaifa.

5. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete akipatiwa maelezo na Meneja Mitambo ya Kuchakata Gesi Asilia, Mhandisi Sultan Pwaga (aliyenyoosha mikono) kuhusu Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia wa Madimba. Wengine katika picha ni viongozi mbalimbali wa Kitaifa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mradi.

HAFLA YA UZINDUZI WA MIUNDOMBINU YA KUCHAKATA NA KUSAFIRISHA GESI ASILIA

1

4

5

2

3

Page 9: MEM 89 Online.pdf

9BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini.

UZINDUZI MTAMBO WA KUZALISHA UMEME KWA KUTUMIA GESI ASILIA KINYEREZI I

Picha N0. 1, 2, ikionesha baadhi ya mitambo ya kufua umeme iliyopo katika eneo la Kinyerezi I, jijini Dar es Salaam. Picha N0. 3 ni kituo cha kupooza na kusambaza umeme kichopo Kinyerezi I jijini Dar es Salaam

1

2 3

Page 10: MEM 89 Online.pdf

10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Baadhi ya Wananchi wanaoishi eneo la Kinyerezi waliohudhuria uzinduzi wa Mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi I wakifuatilia hafla ya uzinduzi

Baadhi ya wageni mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini, TANESCO, mashirika ya Maendeleo, viongozi wa Kitaifa na wawakilishi kutoka Balozi mbalimbali nchini wakifuatilia hafla ya uzinduzi.

UZINDUZI MTAMBO WA KUZALISHA UMEME KWA KUTUMIA GESI ASILIA KINYEREZI I

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Tonia Kandiero (wa pili kulia) pamoja na wageni wengine alipowasili eneo la Kinyerezi I, jijini Dar es Saalam

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi (TANESCO), Dkt. Mighanda Manyahi (wa pili kulia) kwa niaba ya TANESCO akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete zawadi ya picha inayoonesha baadhi ya miradi mikubwa ya umeme iliyotekelezwa kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne. Wengine wanaoshuhudia kutoka kushoto ni kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava, na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadik

Baadhi ya Watumishi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa mitambo ya Kufua umeme ya megawati 150 ya Kinyerezi I.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).

Page 11: MEM 89 Online.pdf

11BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMAUMILIKI WA MITAMBO YA UZALISHAJI UMEME

Hivi karibuni zimeibuka taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zikimnukuu Waziri wa Nishati na Madini, George B. Simbachawene akisema kuwa mitambo yote ya uzalishaji umeme nchini inamilikiwa na Kampuni binafsi.

Tunapenda kuutaarifu Umma kuwa taarifa hizi ni za uongo kwani Waziri Simbachawene hajawahi kutoa tamko la kuwa mitambo ya kuzalisha Umeme yote nchini ni ya kampuni binafsi bali alichosema ni kuwa, baadhi ya mitambo ni ya kampuni binafsi na mingine inamilikiwa na Serikali.

Mitambo inayomilikiwa na Serikali ni:-

1 Kinyerezi I (Gesi) yenye uwezo wa MW 150 ambapo MW 35 zimewashwa leo 12 Oktoba 2015;

2 Ubungo I (Gesi) yenye uwezo wa MW 102 ambayo kwa sasa inazalisha MW 85;

3 Ubungo II (Gesi) yenye uwezo wa MW 105 ambayo kwa sasa inazalisha MW 70;

4 Tegeta (Gesi) yenye uwezo wa MW 42 ambayo kwa sasa inazalisha MW 42;

5 Nyakato (Mafuta) yenye uwezo wa MW 60 ambayo kwa sasa inazalisha MW 42;

6 Kidatu (Maji) yenye uwezo wa MW 204 ambayo kwa sasa inazalisha MW 27;

7 Kihansi (Maji) yenye uwezo wa MW 180 ambayo kwa sasa inazalisha MW 45;

8 Pangani (Maji) yenye uwezo wa MW 68 ambayo kwa sasa inazalisha MW 17;

9 Nyumba ya Mungu (Maji) yenye uwezo wa MW 8 ambayo kwa sasa inazalisha MW 5;

10 Hale (Maji) yenye uwezi wa MW 21 ambayo kwa sasa inazalisha MW 4; na

11 Mtera (Maji) yenye uwezo wa MW 80 ambapo mitambo yake imezimwa (MW-0);

Kwa hiyo, Jumla ya kiasi cha umeme kinachopatikana katika mitambo hiyo kwa sasa ni Megawati 337 kati ya Megawati 870 zinazotakiwa kuzalishwa.

Mitambo inayomilikiwa na watu binafsi ni:- 1 IPTL (Mafuta) yenye uwezo wa MW100

ambayo kwa sasa inazalisha MW 80;2 Aggreko (Mafuta) yenye uwezo wa MW

70 ambayo kwa sasa inazalisha MW 70;3 SONGAS(Gesi) yenye uwezo wa

MW180 ambayo kwa sasa inazalisha

MW 158; na4 Symbion (Gesi) yenye uwezo wa MW

112 ambayo kwa sasa inazalisha MW 74.

Hivyo mitambo hii ya watu binafsi inazalisha umeme wa kiasi cha Megawati 382 kati ya Megawati 462 zinazohitajika.

Ieleweke kuwa Serikali inajitahidi kuiwasha mitambo hiyo yote inayomilikiwa na Serikali na Binafsi ili izibe pengo la umeme wa maji ambao umepungua kutoka MW 561 hadi MW 88. Ili nchi isiwe na mgawo wa umeme zinahitajika MW 1332 ambapo kwa sasa kiasi cha umeme kinachopatikana ni Megawati 719.

Awali tulikuwa na upungufu wa megawati takribani 450 lakini tumefanya juhudi za kuwasha mitambo mbali mbali tangu wiki iliyopita na sasa upungufu uliobaki ni kati ya MW 200 na 250.

Serikali kupitia TANESCO inatoa rai kwa Watanzania kuendelea kuvumilia kipindi hiki cha mpito kwani inajitahidi kwa hali na mali kuwasha mitambo iliyobaki ya gesi ya Kinyerezi yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 150 hivyo hadi ifikapo tarehe 20 Oktoba, 2015 hali ya upatikanaji wa umeme itaanza kutengemaa.

Asanteni na poleni kwa usumbufu unaojitokeza.

Imetolewa na;a WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene