MEM 108 Online.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

  • Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    Habari za nisHati &madini

    Toleo No. 108 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Februari 25 - Machi 2, 2016

    BulletinNews

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    http://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI &MADINI

    Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

    JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

    Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

    Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

    Wabunge Soma habari Uk. 2

    Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

    WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2Gesi kuchochea mapinduzi ya uchumin Nyingine yagundulika Ruvu

    Dkt. Kalemani akataa utafiti wa GGM

  • BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Gesi kuchochea mapinduzi ya uchumiAsteria Muhozya na Zuena Msuya, Dar es Salaam

    Imeelezwa kuwa, Tanzania inatarajia kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi kupitia rasilimali ya Gesi Asilia ambayo inatajwa kuwa chachu

    ya ongezeko la nishati ya umeme jambo ambalo litachochea ukuaji wa viwanda nchini.

    Hayo yalielezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati akihitimisha vikao vyake na wawekezaji wa kampuni zinazofanya shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini, na kuwataka wawekezaji hao kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo kutokana mahitaji ya nishati hiyo nchini.

    Profesa Muhongo aliwaeleza wawekezaji hao msimamo wa Serikali kuhusu nishati hiyo kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vikubwa na vidogo huku rasilimali ya gesi asilia ikitajwa kuwa injini ya kufikia malengo hayo na kuwataka kuhakikisha kuwa gesi inapatikana nchini.

    Hatujagundua mafuta, lakini tuna hazina kubwa ya gesi ambayo inawezesha kufikia malengo hayo. Ni lazima kampuni hizi zibadili mwenendo wao wa namna ya kufanya kazi. Tunataka kasi zaidi katika suala hili na kuhakikisha gesi inapatikana. Tunataka umeme mwingi unaotokana na gesi, umeme nafuu na wa uhakika,alisisitiza Prof. Muhongo.

    Aliongeza kuwa, Serikali imelenga kujenga viwanda viwili vya Mbolea kutokana na gesi asilia na kuyataja maeneo ambayo viwanda hivyo vitajengwa kuwa ni Kilwa Mkoani Lindi na Mtwara, na kuongeza kuwa, ujenzi wa viwanda hivyo utachochea kilimo cha kisasa.

    Aidha, mbali na kutaja ujenzi wa viwanda vya mbolea, alisema kuwa, mipango mingine ya Serikali ni kujenga mitambo ya kusindika gesi ili pia Tanzania iweze kushindana na nchi nyingine kusafirisha gesi iliyosindikwa nje ya nchi, jambo ambalo litawezesha Serikali kupata fedha nyingi za kigeni.

    Tunataka kujenga mtambo wa kusindika gesi asilia Mkoani Lindi. Gharama za ujenzi huo zinatarajia kufikia kiasi cha Dola za Marekani Bilioni 30 na utakuwa mradi mkubwa zaidi kuwahi kutokea nchini. Tayari eneo la ujenzi wa mtambo huo limepatikana eneo la Likongo Manispaa ya Lindi, kiwanja Na.1, Kitalu A, alisema Prof. Muhongo.

    Pia alisema kuwa, mipango mingine ni kutumia gesi majumbani ili kuachana na matumizi ya mkaa ambayo yanatajwa kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira kwa kukata miti hovyo, na kuongeza kuwa, kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee matumizi ya mkaa kwa siku moja yanafikia kiasi cha magunia elfu hamsini (50,000).

    Vilevile, aliongeza kuwa, gesi asilia ni kichocheo kingine muhimu kitakachosaidia kuondokana na umaskini na kuongeza pato la Taifa ikizingatia kuwa, ongezeko la mahitaji ya kiuchumi yanapanda kutokana na kuongezeka la idadi ya watu wa

    kipato cha kati na kuongeza kuwa, tunataka Tanzania iondokane na umaskini kupitia rasilimali za gesi na mafuta.

    Aidha, mbali na nishati ya gesi asilia, Prof. Muhongo aliwaeleza wawekezaji hao kuwa, zipo rasilimali nyingine ambazo wawekezaji wanaweza kuwekeza nchini na kuzitaja kuwa ni nishati jadidifu, pamoja na vyanzo vingine vya upepo, mawimbi, umeme wa jua na makaa ya mawe.

    Wakati huo huo, Profesa Muhongo alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dodsal Hydrocarbons & Power (Tanzania) , Pilavullathil Surendran, kueleza kuhusu kampuni hiyo kugundua gesi asilia kiasi cha futi za ujazo trilioni 2.17, eneo la Bonde la Mto Ruvu na kueleza kuwa, taarifa zaidi juu ya ugunduzi huo itatolewa na Wizara.

    Ugunduzi huo mpya wa gesi katika mto Ruvu, mkoa wa Pwani kunaifanya Tanzania hadi sasa kuwa na hazina ya gesi yenye ukubwa wa futi za ujazo trilioni 57.27.

    Sheria mpya inatutaka kabla ya Waziri mwenye dhamana ya gesi kutangaza ugunduzi mpya wa gesi na mafuta, lazima ithibitishwe na Mamlaka ya Udhibiti wa bidhaa za petroli na gesi (PURA), alisisitiza Prof. Muhongo.

    Katika hatua nyingine, Prof. Muhongo aliahidi kukutana tena na wawekezaji wa umeme, mafuta na gesi ifikapo tarehe 1 Juni, tarehe 1 Septemba na tarehe 31 Novemba , mwaka huu ili kujadili maendeleo na hatua walizofikia katika utekelezaji wa miradi yao na kuongeza kuwa, Serikali itatoa ushirikiano mkubwa kwa kampuni hizo kuhakikisha zinatekeleza mipango yao kwa wakati.

    Profesa Muhongo alihitimisha vikao na wawekezaji katika kampuni za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi tarehe 24 Februari,2016 ambapo alianza kukutana na wazalishaji wadogo wa umeme wa chini ya megawati 20 unaotokana na maji mwezi Janurari, 2016, na wiki ya kuanzia tarehe 15 Februari,2016 alikutana na wawekezaji mbalimbali wenye nia ya kuwekeza katika sekta ndogo ya umeme.

    Baadhi ya Wawekezaji wa Kampuni za kutafiti na kuchimba mafuta na gesi nchini, wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) wakati wa kikao chake na wawekezaji hao.

    2

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza na wawekezaji wa kampuni za utafiti na uchimbaji wa Mafuta na Gesi (hawapo pichani). Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kelvin Komba, wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC, Dkt. James Mataragio na kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Albert Diliwa.

  • 3BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    Five Pillars oF reForms

    KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano

    Bodi ya uhariri MharIrI Mkuu: Badra Masoud

    MsaNIFu: Lucas GordonWaaNdIshI: Veronica simba, asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed saif, rhoda James ,

    Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

    increase eFFiciencyQUality delivery

    oF Goods/servicesatisFaction oF

    tHe clientsatisFaction oF

    BUsiness Partners

    satisFaction oF sHareHolders

    tel-2110490FaX-2110389

    moB-0732999263

    Miradi ya gesi, umeme haitaki longolongo!

    tel-2110490FaX-2110389

    moB-0732999263

    DKT. KALEMANI AKATAA UTAFITI WA GGM KUHUSU MIPASUKO

    Taifa la Tanzania limeingia katika historia ya nchi zilizo na rasilimali ya gesi asilia duniani baada ya ugunduzi wa gesi hiyo hapa nchini na kufanya sasa tuamini kwamba mapinduzi kiuchumi yanaweza kufanyika kupitia rasilimali hiyo ya Gesi asilia ambayo inatajwa kuwa chachu na kichocheo cha ukuaji wa uchumi pamoja na nishati ya umeme itakayowezesha kuongezeka kwa viwanda nchini.

    Waziri mwenye dhamana na Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo amethibitisha hayo wakati akihitimisha vikao vyake na wawekezaji wa kampuni zinazofanya shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini, na kuwataka wawekezaji hao kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo kutokana na mahitaji ya nishati hiyo nchini.

    Profesa Muhongo aliwaeleza wawekezaji hao msimamo wa Serikali kuhusu nishati hiyo kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vikubwa, vya kati pamoja na vidogo huku rasilimali ya nishati ikiwemo gesi asilia ikitajwa kuwa injini ya kufikia malengo hayo na kuhakikisha kuwa gesi inapatikana nchini.

    Alisisitiza kuwa, Serikali imedhamiria kujenga viwanda viwili vya Mbolea kutokana na gesi asilia, Kilwa Mkoani Lindi na Mtwara vitakavyochochea ukuaji wa kilimo cha kisasa nchini.

    Aidha, mbali ujenzi wa viwanda vya mbolea, alisema kuwa, mipango mingine ya Serikali ni kujenga mitambo ya kusindika gesi ili pia Tanzania iweze kushindana na nchi nyingine kusafirisha gesi iliyosindikwa nje ya nchi, jambo ambalo litawezesha Serikali kupata fedha nyingi za kigeni.

    Pia alisema kuwa, mipango mingine ni kutumia gesi hiyo majumbani ili kuachana na matumizi ya mkaa ambayo yanatajwa kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira kwa kukata miti hovyo, na kuongeza kuwa, kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee matumizi ya mkaa kwa siku moja yanafikia magunia elfu hamsini (50,000).

    Sambamba na hilo, Prof. Muhongo aliwaeleza wawekezaji hao kuwa, zipo rasilimali nyingine ambazo wawekezaji wanaweza kuwekeza nchini na kuzitaja kuwa ni upepo, mawimbi, makaa ya mawe na jua.

    Katika kutimiza azma ya Serikali ya kufikia katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 juhudi za kutafuta gesi bado zinaendela ambapo hivi karibuni katika eneo la Bonde la Mto Ruvu imegunduliwa gesi asilia kiasi cha futi za ujazo trilioni 2.17.

    Ugunduzi huo mpya wa gesi katika mto Ruvu, mkoa wa Pwani unaifanya Tanzania hadi sasa kuwa na hazina ya gesi ya kiasi cha futi za ujazo trilioni 57.27.

    Katika majumuisho ya mfululizo wa vikao vyake na wawekezaji, Prof. Muhongo aliahidi kukutana tena na wawekezaji wa umeme, mafuta na gesi ifikapo tarehe 1 Juni, tarehe 1 Septemba na tarehe 31 Novemba , mwaka huu ili kujadili maendeleo na hatua walizofikia katika utekelezaji wa miradi yao na kuongeza kuwa, Serikali itatoa ushirikiano mkubwa kwa kampuni hizo kuhakikisha zinatekeleza mipango yao kwa wakati.

    Sisi tunaungana na Waziri Muhongo kwamba umefika wakati sasa kwa wawekezaji wote waliokuwa wameanza miradi ya ujenzi wa mitambo ya umeme, utafutaji na uchimbaji wa gesi asilia kuongeza kasi ya utendaji wao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kwa wale ambao wameonesha nia ya kuwekeza katika sekta hizo za gesi na umeme kukamilisha taratibu kwa mujibu wa sheria ili waanze kutekeleza miradi hiyo mara moja.

    Na Veronica Simba Geita

    Serikali imesema haitambui utafiti uliofanywa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kuhusu malalamiko ya wananchi waishio jirani na Mgodi huo kuharibiwa

    nyumba zao na kupata ufa sehemu mbalimbali kutokana na milipuko inayofanywa na mgodi.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, alikataa kutambua utafiti huo, uliotoa majibu kwamba Mgodi hauhusiki na mipasuko inayolalamikiwa, akitoa sababu kwamba, si sahihi GGM kama watuhumiwa kujifanyia utafiti wao wenyewe.

    Badala yake, Dkt. Kalemani ameuagiza Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kufanya utafiti huo kwa siku tano kuanzia Jumatatu, Februari 29 mwaka huu na kuwasilisha taarifa yake ili Wizara ifanye maamuzi.

    Akizungumza mara baada ya kutembelea

    baadhi ya nyumba na majengo mengine ikiwemo Shule ya Msingi, zinazodaiwa kuathiriwa na milipuko ya Mgodi, katika maeneo ya Nyamalembo na Katoma wilayani Geita, Dk Kalemani alisema GST, ambao ni Wakala wa Serikali unaohusika na milipuko, watapitia kukagua nyumba na majengo yote yanayodaiwa kuathirika kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali akiwemo Diwani, Wenyeviti wa Vijiji husika pamoja na Wabunge wa maeneo hayo.

    Haiwezekani wewe unatuhumiwa kupasua, halafu unaweka mtaalamu kujichunguza mwenyewe, alisisitiza.

    Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kalemani alimwagiza Kaimu Afisa Madini wa Geita, Fabian Mshai kuuandikia barua uongozi wa Mgodi wa Geita, kuwataka ndani ya siku 14, watoe taarifa rasmi kimaandishi,

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (mwenye miwani), akiangalia mojawapo ya nyumba za wakazi wa maeneo jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), zinazodaiwa kuathiriwa na milipuko inayofanywa na Mgodi huo.

    >>Inaendelea Uk. 4

  • 4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    kama wanalitumia au hawalitumii eneo ambalo inasemekana Mgodi huo umeweka vigingi na umezuia wananchi wasilitumie kwa shughuli yoyote wakati Mgodi haulifanyii kazi.

    Dkt. Kalemani alisema kuwa, baada ya kukagua alibaini ni kweli Mgodi unamiliki eneo husika na wameweka vigingi kuzuia wananchi wasifanye shughuli yoyote ndani yake, lakini akasema utaratibu unautaka Mgodi kuwaruhusu wananchi kuendelea kutumia eneo hilo kuendeshea maisha yao ikiwa wao Mgodi hawalitumii.

    Huwezi ukaweka vigingi, ukasema hulitumii eneo, halafu humpi fidia mwananchi wa eneo husika na ukamwacha anaendelea kuzubaa asijue nini la kufanya.Alisema Dkt. Kalemani.

    Hata hivyo, Makamu Rais wa GGM anayeshughulikia Mahusiano na Maendeleo ya Jamii, Simon Shayo, alipoulizwa kuthibitisha endapo Mgodi uliandika barua ya kutoa zuio kwa wananchi wasitumie eneo hilo, alikana kuitambua barua hiyo hivyo Naibu Waziri akasema kwa kanusho lile, wananchi wanaweza kuendelea kulitumia kwa shughuli mbalimbali za kilimo, ufugaji na hata ujenzi.

    Wananchi muendelee na shughuli zenu katika eneo hilo kama kawaida mpaka pale Mgodi utakapokubali kuwafidia. Kama hawatawafidia,

    hakuna zuio la ninyi kutokufanya shughuli zenu. Mkae, muendelee na maisha yenu kama kawaida, alisema Dkt. Kalemani.

    Aliongeza kuwa, endapo Mgodi utaamua wananchi waondoke katika eneo husika, haitazuia kulipwa stahili za nyuma kutokana na muda waliopoteza.

    Tamko la Mgodi kuwa

    hawajawahi kuandika barua ya kuwazuia ninyi kuendelea na shughuli zenu, wote tumelisikia hapa. Sasa, tusubiri taarifa yao rasmi kimaandishi kama nilivyoagiza ili ikitofautiana na waliyosema hapa, tuchukue hatua za kisheria, alisisitiza.

    Aidha, Dkt. Kalemani aliwaagiza GGM kufikia Jumatatu, Februari 29 mwaka huu, wawe wamekarabati

    Shimo la Maji lililopo ndani ya eneo lao, ili kuzuia athari za maji hayo kufurika hadi nje ya eneo hilo na kufika katika makazi ya wananchi.

    Kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 2010, Kifungu cha 14, inawataka muweke mikingamo na kuzuia athari ya maji pamoja na mambo mengine.

    Akizungumzia agizo lililotolewa na Makam wa Rais, Samia Suluhu kutaka wananchi wanaozunguka Mgodi wa Geita wapewe miamba-taka kutoka mgodini, Naibu Waziri alisema, Tume iliyoundwa na Wizara kufuatilia na kutathmini jinsi kazi hiyo inavyoweza kutekelezwa, inakamilisha taarifa yake na utaratibu unatarajiwa kutolewa ifikapo Februari 28, mwaka huu.

    Pamoja na maagizo yote aliyoyatoa, Dk Kalemani alizitaka pande zote mbili, yaani wananchi na Mgodi, kuimarisha mahusiano mazuri baina yao kwani kuishi kwa kutumia sheria pasipo kuwa na mahusiano mazuri, haitawasaidia.

    Aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mgodi pale wanapofanya vizuri. Wakifanya vibaya, lazima sheria itachukua mkondo wake.

    Naibu Waziri Kalemani alikuwa katika ziara ya kikazi ya siku 10 ambayo aliihitimisha Mkoani Geita, Februari 24. Mikoa mingine aliyotembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Wizara yake pamoja na kukutana na wadau wa sekta za nishati na madini ili kujua changamoto zinazowakabili ni pamoja na Tabora na Kigoma.

    >>INATOKA Uk. 3

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akisaini Kitabu cha Wageni, ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Manguchie (katikati), kabla ya kuanza ziara yake wilayani humo kushughulikia kero mbalimbali za wananchi kuhusu masuala ya madini.

    Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Geita, Fabian Mshai, akisoma taarifa ya kazi ya Ofisi yake kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa ziara yake wilayani humo. Wengine pichani ni viongozi mbalimbali wa Serikali wa Wilaya, Kata na Vijiji pamoja na Maofisa wa Wizara.

    DKT. KALEMANI AKATAA UTAFITI WA GGM KUHUSU MIPASUKO

  • 5BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Mbunge wa Jimbo la Geita, Constantine Kanyasu, akizungumza na wananchi wa Geita wakati Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (mwenye miwani) alipofanya ziara ya kazi wilayani humo kutatua kero mbalimbali za wananchi kuhusu masuala ya madini.

    Mkazi wa Kijiji cha Katoma wilayani Geita, Malekela Emmanuel akitoa malalamiko yake kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kuhusu nyumba yake kuathiriwa na milipuko inayofanywa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wanaoishi jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, akisaini Kitabu cha Wageni katika Shule ya Msingi Nyamalambo. Shule hiyo ni miongoni mwa majengo yanayodaiwa kuathiriwa na milipuko inayofanywa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).

    Makamu Rais wa GGM anayeshughulikia Mahusiano na Maendeleo ya Jamii, Simon Shayo, akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kuhusu msimamo wa Mgodi kuhusiana na malalamiko ya wananchi kuathiriwa nyumba zao kutokana na milipuko inayofanywa na Mgodi huo.

    ZIARA NAIBU WAZIRI - GEITA

  • 6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Mohamed Saif

    Serikali imezitaka kampuni zilizo katika hatua ya utafiti wa gesi asilia na mafuta nchini kufanya tafiti kwa kutumia vifaa vya kisasa.

    Wito huo umetolewa hivi karibuni jijini Dar es salaam na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa mkutano wake na kampuni ya Ndovu Resources Limited ya Uingereza ambayo ina ubia na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)

    Profesa Muhongo alisema Serikali imedhamiria kuhakikisha kunakuwepo na umeme mwingi na wa uhakika na kwamba gesi asilia ni chanzo mojawapo cha nishati hiyo na hivyo ni muhimu utafiti ukafanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambayo haitumii muda mrefu.

    Alisema hadi hivi sasa wawekezaji waliojitokeza kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ni wengi na hivyo hakuna budi kuhakikisha utafiti unakamilika mapema ili kwenda na kasi ya Serikali.

    Profesa Muhongo alisema teknolojia imekua na hivyo kuna baadhi ya kampuni ambazo zimeonesha nia ya

    kufunga mitambo ya kufua umeme wa gesi ndani ya miezi 6. Ufungaji wa mitambo ya kisasa hauchukui muda mrefu; kwahiyo ni vyema mkaharakisha ili muanze uzalishaji mapema iwezekanavyo, alisema.

    Suala lingine ambalo Waziri Muhongo alisisitiza ni umuhimu wa uwajibikaji kwa jamii zinazozunguka maeneo ambayo miradi inatekelezwa.

    Profesa Muhongo alisema kuna vijana wengi kutoka masomoni ambao wanahitaji kufanya mafunzo ya kivitendo na hivyo alisisitiza kwamba ni vyema kampuni husika zikaandaa programu ya kuchukua vijana wanaohitaji mafunzo ya kivitendo (internship).

    Profesa Muhongo aliiagiza kampuni hiyo kukaa pamoja na mshirika wake ambaye ni TPDC ili waandae mpango kazi unaotekelezeka na kuuwasilisha wizarani kwa ajili ya kurahisisha ufuatiliaji wa mara kwa mara wa utekelezaji wake.

    Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo ya Ndovu Resources, Jay Bhattacherjee alisema tafiti zote zimeonyesha matokeo mazuri jambo ambalo alielezea kuwa litaongeza upatikanaji wa gesi asilia nchini kwa ajili ya matumizi mbalimbali mojawapo ikiwa ni kuzalisha umeme.

    Kikao hicho kilihusisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na taasisi zake likiwemo Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC),

    Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Ndovu Resources Limited, Balozi Isaya Chialo akifuatiwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Nchini, Thierry Murcia. Kulia kwa Profesa Muhongo ni Mkurugenzi Mkuu wa Ndovu Resources, Jay Bhattacherjee

    Fanyeni utafiti kisasa- Profesa Muhongo

    Na Veronica Simba - Buhigwe

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amekataa kupokea Taarifa ya utendaji kazi, kutoka kwa

    Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa wilaya mpya ya Buhigwe Mkoani Kigoma, Ntungwa Njegelo.

    Dkt. Kalemani alikataa kupokea taarifa hiyo Februari 19, alipokutana na Uongozi wa Wilaya hiyo mpya, kwenye Ofisi ya muda iliyopo wilayani humo, akiwa pamoja na watendaji mbalimbali kutoka wizarani, TANESCO na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

    Akizungumzia sababu za kukataa kupokea taarifa hiyo, Naibu Waziri alisema kuwa haijitoshelezi kutokana na kutoeleza kwa kina masuala mbalimbali muhimu ya kiutendaji katika wilaya hiyo.

    Kwa mfano, taarifa hii inaeleza vijiji 12 vimepata umeme lakini haielezi idadi hiyo ni kati ya vijiji vingapi. Pia, haielezi ni asilimia ngapi ya umeme imepatikana. Taarifa hii haiwezi kunisaidia maana nataka kutatua kero hivyo ni lazima nijue ukubwa wa tatizo.

    Kufuatia hatua hiyo, Naibu Waziri Kalemani alimwagiza Meneja huyo aandae taarifa mpya, yenye maelezo ya kina kuhusu utekelezaji wa miradi

    mbalimbali ya umeme hususani mradi wa REA (Umeme Vijijini) Awamu ya pili na kuiwasilisha kwake Jumatatu,

    Februari 22 mwaka huu.Aidha, Dkt. Kalemani alimwagiza

    Meneja huyo kufuatilia na kufanyia kazi malalamiko ya wananchi katika eneo lake, kuhusu kuwepo na mashimo yaliyochimbwa kwa ajili ya kusimika nguzo za umeme katika mashamba yao lakini yameachwa wazi kwa muda mrefu pasipo zoezi hilo kufanyika hivyo

    kuwazuia kuendelea na shughuli zao za kilimo.

    Awali, akiwasilisha taarifa kwa niaba ya wananchi wake kuhusu kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili kuhusiana na sekta ya nishati, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Mary Tesha alimwomba Naibu Waziri kusaidia ili mashimo yaliyochimbwa katika baadhi ya vijiji kwa ahadi ya kusimika nguzo za umeme, yafanyiwe kazi mapema ili wananchi waendelee na shughuli za kilimo katika mashamba yao.

    Vilevile, Dkt. Kalemani alisema pamoja na mapungufu kadhaa, Tanesco wamejitahidi kufanya kazi nzuri ya kuwaunganishia wananchi wa vijijini umeme kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

    Alimpongeza Mkandarasi mzalendo anayeunganisha umeme wa REA Awamu ya pili Mkoani Kigoma, Wilbroad Mutabuzi kupitia kampuni yake ya JV State Grid Electrical and Trchnical Works Ltd kwa kazi nzuri anayoifanya.

    Kuna baadhi ya maeneo tumekutana na matatizo ya wakandarasi kufanya kazi chini ya kiwango hivyo kuturudisha nyuma. Huyu Mkandarazi mzawa anayefanya kazi hiyo hapa Kigoma anajitahidi sana na namtaka aendelee hivyo.

    Alisema ameagiza zoezi la kuunganisha umeme wa REA Awamu ya pili likamilike ifikapo Mwezi Aprili mwishoni, hivyo wale wote waliopangwa kuunganishiwa umeme katika awamu hiyo, wanapaswa kuwa wamepatiwa huduma hiyo ndani wa kipindi hicho.

    Dkt. Kalemani aikataa Ripoti ya Meneja TANESCO

    Mkuu wa Wilaya mpya ya Buhigwe, Mary Tesha akiwasilisha taarifa kuhusu kero na changamoto mbalimbali kuhusu sekta ya nishati, zinazowakabili wananchi wake mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia), alipofanya ziara wilayani humo hivi karibuni.

  • 7BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Greyson Mwase na Latifah Boma, Dar es Salaam

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametaka kasi iongezwe katika

    mradi wa ujenzi wa kiwanda cha uchakataji na usindikaji wa gesi kimiminika (LNG) unaotarajiwa kuanza Mkoani Lindi mara baada ya taratibu za maandalizi kukamilika.

    Profesa Muhongo alisema hayo katika kikao cha kujadili hatua iliyofikiwa ya maandalizi ya ujenzi wa kiwanda hicho kilichoshirikisha watekelezaji wa mradi huo ambao ni Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Kampuni zinazojishughulisha na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini.

    Kampuni za utafiti wa mafuta na gesi zinayotekeleza mradi huo ni pamoja na Shell, Statoil, Ophir Energy, Pavilion na Exxon Mobil. Pia kikao hicho kilishirikisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST).

    Mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata na kusindika gesi kimiminika Profesa Muhongo aliiagiza TPDC kushirikiana kwa karibu na Kampuni hizo ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.

    Profesa Muhongo alisema

    Tanzania ina utajiri mkubwa wa gesi hivyo ni vyema wawekezaji wakachangamkia fursa hiyo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata na kusindika gesi kimiminika ambayo mahitaji yake ni makubwa duniani hususan katika bara la Asia.

    Ifikapo mwaka 2025 inatarajiwa kuwa mahitaji ya gesi duniani yatakuwa ni kiasi cha tani milioni 440 kwa mwaka hususan katika nchi za Asia ambazo ni karibu na Afrika, hii ni fursa ambayo tunatakiwa kuichangamkia ili kuendana na soko itakapofika kipindi hicho, alisema Profesa Muhongo.

    Profesa Muhongo aliendelea kusema kuwa gesi ya kimiminika imekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi zinazoendelea huku akitolea mfano wa Algeria ambayo ni nchi ya kwanza duniani kwa kuwa na kiwanda cha kuchakata na kusindika gesi kimimika ambayo kwa sasa imepiga hatua kubwa kimaendeleo.

    Katika maandalizi ya awali ya mradi huo, Profesa Muhongo alisisistiza uundwaji wa timu kwa ajili ya maandalizi ya mradi huo ikishirikisha wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Fedha na Mipango, Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Taasisi mbalimbali pamoja na wawakilishi kutoka katika Kampuni

    zinazofanya utafiti wa gesi na mafuta nchini ambazo ni mtekelezaji wa mradi huo.

    Alisisitiza kuwa ni vyema timu hiyo ikawa na wataalam wenye uzoefu mkubwa watakaofanya kazi kwa weledi na kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

    Aliagiza timu hiyo kukamilisha taratibu zote za maandalizi kabla ya mwezi Novemba, mwaka huu.

    Naye Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio alisema kuwa Shirika lake limekuwa likishirikiana na wabia wa ujenzi wa kiwanda hicho katika hatua zote za maandalizi ya awali na kuahidi kuongeza kasi ili kazi hiyo iweze kukamilika kwa wakati.

    Eneo la ardhi litakapojengwa kiwanda hicho cha kuchakata na kusindika gesi lipo katika kiwanja Na.1 -Kitalu A, Likongo katika Manispaa ya Lindi na lilipendekezwa na kuchaguliwa kwa pamoja kati ya TPDC na wawekezaji kutoka Kampuni za kimataifa za utafutaji mafuta na gesi asilia (IOCs) zinazofanya kazi zake hapa nchini.

    Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio akieleza jambo wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na wawekezaji wanaofanya utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini.

    Profesa Muhongo ataka kasi Kiwanda cha Uchakataji Gesi

    Meneja Biashara kutoka Kampuni ya Utafutaji wa Mafuta na Gesi nchini ya Statoil, Oivind Holm Karlsen (katikati) akielezea maendeleo ya miradi ya Kampuni hiyo nchini wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na wawekezaji wanaofanya utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akielezea fursa za uwekezaji nchini kwenye sekta ndogo ya gesi asilia wakati wa mkutano kati yake na Kampuni zinazofanya utafiti na uchimbaji wa gesi nchini.

  • 8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Veronica Simba - Kakonko

    Serikali imesema, wananchi wa kipato cha chini, hususan wa vijijini, wenye nyumba zenye kuanzia chumba kimoja hadi vinne, wataunganishiwa umeme

    pasipo kutandaza nyaya za umeme (wiring) kwenye nyumba zao.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, aliyasema hayo hivi karibuni wilayani Kakonko, Mkoani Kigoma, akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani humo kukagua miradi inayotekelezwa chini ya Wizara, hususan ya umeme vijijini, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

    Dkt. Kalemani alisema, badala ya kutandaza nyaya za umeme katika nyumba zao, wananchi hao watafungiwa kifaa maalum kijulikanacho kitaalam kama ReadyBoard (Umeme Tayari) kitakachowawezesha kutumia umeme kama kawaida.

    Alisema, utumiaji wa kifaa hicho ni teknolojia mpya itakayowasaidia wananchi wa kipato cha chini kuondokana na gharama kubwa za kutandaza nyaya ndani ya nyumba, ambazo mara nyingi husababisha wengi wao kushindwa kumudu gharama hizo na hivyo kukosa huduma muhimu ya umeme.

    Hata hivyo, Dkt. Kalemani aliweka bayana kuwa, watakaonufaika na huduma hiyo ni wale tu wenye kipato cha chini, wanaomiliki nyumba ndogo za kuanzia chumba kimoja hadi vinne. Wenye nyumba kubwa wataendelea na utaratibu wa kawaida wa kutandaza nyaya.

    Alisema, Serikali imefikia uamuzi huo, baada ya kuona wananchi wengi wa vijijini, ambao kipato chao ni duni, wanashindwa kunufaika na huduma ya umeme, licha ya Serikali kuwapelekea huduma hiyo kwa gharama nafuu kupitia Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na REA.

    Kama Serikali, tumedhamiria kuhakikisha asilimia 75 ya Watanzania wanatumia nishati ya umeme ifikapo mwaka 2025. Ili kufikia malengo hayo, ni lazima tuhakikishe tunawapatia huduma hiyo muhimu Watanzania wengi zaidi, na tuhakikishe wanawezeshwa kuitumia, hususani walioko vijijini, ambao wengi wao wana kipato cha chini, alisisitiza Naibu Waziri.

    Akifafanua zaidi kuhusu faida za kutumia kifaa hicho, Naibu Waziri alisema, wananchi watakaofungiwa ReadyBoard, watatumia shilingi 27,000 hadi 30,000 tu. Gharama hiyo inahusisha uwekaji wa nguzo, kuunganishiwa umeme nyumbani pamoja na kifaa husika.

    Alibainisha kuwa, kimsingi, umeme wa REA ni bure, isipokuwa mwananchi analazimika kulipia shilingi 27,000 tu kama tozo ya kodi ya Serikali (VAT). Tofauti na kulipia VAT, hakuna malipo hata thumni kwani Serikali imegharamia umeme huo.

    Aliongeza kuwa, Serikali inaangalia utaratibu wa kuondoa hata shilingi 6,000 inayotumika kulipia fomu kwa ajili ya maombi ya umeme kama njia ya kumwezesha mwananchi wa kipato cha chini kutumia huduma hiyo.

    Akizungumzia gharama za matumizi ya umeme, Dkt. Kalemani alisema, watumiaji wote wa umeme, ambao matumizi yao ni chini ya uniti 75, wanapaswa kulipia shilingi 100 tu za kitanzania kwa kila uniti moja. Alisema, gharama hiyo ni nafuu sana, hivyo hakuna sababu ya wananchi wa kipato cha chini kushindwa kutumia umeme kwani wako katika kundi hilo linalotumia umeme kidogo.

    Dkt. Kalemani alifafanua kuwa, wapo baadhi ya wananchi wanaotumia umeme chini ya uniti 75, lakini kwa bahati mbaya, wamewekwa katika kundi la watumiaji wakubwa wa umeme, hivyo wanapaswa kupeleka malalamiko katika Ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika maeneo yao ili wabadilishwe na kurudishwa katika kundi wanalostahili kuwa.

    Vilevile, aliwataka viongozi katika ngazi mbalimbali, kuanzia Kijiji hadi Mkoa, kuelimisha wananchi juu ya matumizi bora ya umeme, kwani wengi wanatumia umeme vibaya na hivyo kulazimika kulipia bili kubwa.

    Akizungumzia suala la kukatika mara kwa mara kwa umeme, Dkt. Kalemani alisema, Wizara yake imewaagiza Mameneja wa Tanesco wa Wilaya, Mkoa na Kanda nchi nzima, kuhakikisha wanarekebisha miundombinu mibovu ya umeme kama vile nguzo na transfoma ili kutatua tatizo hilo.

    Kwa hiyo, kukatika-katika kwa umeme kunakotokana na masuala ya kibinadamu, hakutarajiwi kuendelea baada ya Machi 31, mwaka huu.

    Aidha, aliwataka viongozi katika ngazi za Vijiji, Tarafa, Wilaya na hata Mkoa, kuhakikisha wanawasilisha majina ya vijiji ambavyo havikupangwa kupelekewa huduma ya umeme katika Mradi wa REA Awamu ya II, unaotarajia kukamilika ifikapo mwezi Juni mwaka huu, ili viingizwe katika Mradi wa REA Awamu ya III, unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.

    Alisisitiza kutokusahau maeneo muhimu kama Vituo vya Afya, Shule, Masoko, Magereza, Jeshi na mengine ya aina hiyo, ambavyo havikupangwa kwenye REA Awamu ya II, ili viingie katika REA Awamu ya III.

    Dkt. Kalemani atangaza neema kwa watumiaji umeme mdogo

    Fundi Umeme, akifunga umeme wa REA kama alivyokutwa na Msafara wa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, eneo la Buselesele Mkoani Geita hivi karibuni. Naibu Waziri alikuwa katika ziara ya kazi kukagua miradi ya umeme vijijini.

  • 9BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Teresia Mhagama, Dar es Salaam

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesaini leseni ya madini

    itakayoiwezesha kampuni ya Edenville International (T) Ltd ambayo ni kampuni tanzu ya kampuni ya Edenville Energy PLC ya nchini Uingereza kuchimba makaa ya mawe katika eneo la Mkomolo na Namwele Mkoani Rukwa kwa ajili ya kuzalisha umeme.

    Utiaji saini wa leseni hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini na kushuhudiwa na watendaji mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James Mdoe pamoja na watendaji wa kampuni ya Edenville.

    Naibu Katibu Mkuu, Profesa James Mdoe, alisema kuwa baada ya kupatikana kwa leseni husika kampuni hiyo itaanza kazi ya kuchimba madini hayo ya makaa ya mawe ifikapo mwezi Juni mwaka huu.

    Baada ya kuanza kuchimba makaa hayo mwezi Juni, kampuni hii imelenga kujenga mtambo wa kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 300 katika kipindi cha kati ya miezi 20 hadi 22 baada ya kupata cheti cha mazingira kutoka Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira, alisema Profesa Mdoe.

    Alisema kuwa umeme huo wa megawati 300 utazalishwa katika kipindi cha miaka 35 kwa kutumia hifadhi ya makaa ya mawe ambayo Kampuni hiyo imethibitisha kuwepo

    katika leseni yao kwenye eneo la Mkomolo, Mkoani Rukwa ambayo yanafikia tani milioni 173.

    Alieleza kuwa kiasi hicho cha umeme kinaweza kuongezeka endapo watagundua mashapo zaidi ya makaa ya mawe katika eneo lao lingine la Muze ambalo linaonesha dalili ya kuwa na makaa ya mawe mengi na lipo karibu na eneo la Mkomolo.

    Naibu Katibu Mkuu alisema kuwa katika kikao hicho wamekubaliana na kampuni ya Edenville kutekeleza masharti yote yaliyopo ndani ya leseni ikiwemo kutekeleza kazi zote zilizopangwa kufanyika kama Mpango Kazi wa kampuni hiyo unavyoelekeza.

    Tumewahimiza waishi maneno yao, mfano hapa wameeleza kuwa wanatarajia kuanza kuchimba makaa ya mawe mwezi Juni mwaka huu, inabidi watekeleze suala hilo ili mwisho wa siku tufikie lengo la kuzalisha umeme wa kutosha utakaowezesha nchi yetu kuwa na viwanda vingi ili Tanzania ifikie uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025, alisema Profesa Mdoe.

    Aliongeza kuwa Wizara itatoa ushirikiano kwa wawekezaji mbalimbali wanaojitokeza kuwekeza katika Sekta za Nishati na Madini na ndio maana Waziri Muhongo kuanzia mwanzoni mwa mwezi wa Pili mwaka huu amefanya mazungumzo na Kampuni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ili kusikiliza mapendekezo yao kuhusu uwekezaji wa umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwemo upepo, jua, maji, mawimbi ya bahari, makaa ya mawe, gesi asilia, bayogesi na joto ardhi ambapo Kampuni zaidi ya 300 zilijitokeza.

    Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Edenville, Cassiano Kaegele, alimshukuru Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Serikali ya Awamu ya Tano kwa juhudi mbalimbali wanazofanya katika kuhakikisha kwamba miradi mbalimbali inatekelezwa na kueleza kuwa kasi iliyopo sasa ikiendelea miradi mingi itatekelezeka na Tanzania haitalazimika kununua umeme kutoka nchi nyingine kwani ina vyanzo vya kutosha vya kuzalisha umeme huo.

    Naye Peet Meyer, Mjiolojia kutoka Kampuni hiyo ameeleza kuwa uchimbaji wa makaa ya mawe katika maeneo hayo utafanyika kwa njia ya mgodi wa wazi (opencast) katika miaka kumi ya kwanza na baadaye watachimba chini ya ardhi na kwamba makadirio ya gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 176. Leseni hiyo ya uchimbaji ni ya miaka kumi na Kampuni ya Edenville wanaweza kuihuisha tena baada ya miaka hiyo kupita.

    Kampuni ya Edenville International (T) Ltd yapata Leseni ya uchimbaji makaa ya mawe Mkoani Rukwa

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akisaini leseni ya madini itakayoiwezesha kampuni ya Edenville International (T) Ltd kuchimba makaa ya mawe katika eneo la Mkomolo na Namwele Mkoani Rukwa kwa ajili ya kuzalisha umeme. Wanaoshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (wa pili kulia), Kamishna Msadizi wa Madini anayeshughulikia Wachimbaji Wadogo, Julius Sarota (wa kwanza kulia), Mwanasheria wa Wizara, Abbas Kisuju (kushoto kwa Waziri) na Mhandisi Joseph Kumburu (kushoto kwa Mwanasheria).

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akisisitiza jambo mbele ya Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Taasisi na kampuni ya Edenville (T) Ltd kabla ya kusaini leseni inayoiruhusu Kampuni hiyo kuchimba makaa ya mawe katika eneo la Mkomolo na Namwele Mkoani Rukwa kwa ajili ya kuzalisha umeme wa megawati 300. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James Mdoe (hayupo pichani) na Kamishna Msadizi wa Madini anayeshughulikia Wachimbaji Wadogo, Julius Sarota (hayupo pichani).

    Watendaji kutoka kampuni ya Edenville (T) Ltd wakishuhudia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia), akisaini leseni hiyo. Kutoka kushoto mstari wa mbele ni Gwakisa Mwakyusa, Cassiano Kaegele, Mohj Pryor na Peet Meyer.

  • 10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ametaka kampuni zinazojishughulisha na

    shughuli za utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta nchini kuongeza kasi ya utafiti kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili sekta ya Gesi na Mafuta iweze kukua

    na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

    Profesa Muhongo alitoa kauli hiyo alipokutana na kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa vifaa na teknolojia katika utafutaji wa mafuta na gesi ya Schlumberger yenye makazi yake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili utendaji kazi wa kampuni hiyo.

    Kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam kilihusisha watendaji kutoka Wizara pamoja na taasisi zake ikiwemo Shirika la Maendeleo

    ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

    Alisema Tanzania kwa sasa ina utajiri mkubwa wa rasilimali ya gesi ambayo itachochea katika ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia umeme wa uhakika utakaotumika katika viwanda na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania.

    Aliendelea kusema kuwa ili

    sekta ya gesi na mafuta iweze kuwa na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi, Tanzania inahitaji wawekezaji watakaowekeza kwa kasi kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

    Alisisitiza kuwa serikali ipo tayari kushirikiana na mwekezaji yeyote mwenye nia ya kuwekeza kwenye sekta ya gesi na mafuta kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

    Kama Serikali tumedhamiria kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi zenye utajiri unaotokana na rasilimali za gesi na mafuta, hivyo tunapenda kushirikiana na wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa kutumia teknolojia ya kisasa, alisema Profesa Muhongo

    Profesa Muhongo aliihakikishia kampuni ya Schlumberger kuwa Serikali itafanya kazi kwa karibu nayo na kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika ili sekta ya gesi na mafuta iweze kukua kwa kasi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

    Awali akizungumza katika kikao hicho, Meneja Masoko kutoka kampuni ya Schlumberger, Abdul Adeshina alisema kampuni yake imekuwa ikitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kitanzania kwa asilimia 80 wanaofanya kazi katika kampuni hiyo.

    Aliongeza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika shughuli za utafiti wa mafuta na gesi nchini na kusisitiza kuwa kampuni hiyo ipo tayari kutumia teknolojia na vifaa vyake katika kuboresha shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi nchini.

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Meneja Masoko kutoka Kampuni ya Schlumberger, Abdul Adeshina (hayupo pichani) katika kikao hicho.

    Meneja Masoko kutoka Kampuni ya Schlumberger, Abdul Adeshina akielezea shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kusambaza vifaa na teknolojia kwa ajili ya utafiti wa mafuta na gesi nchini.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mbele) akiongoza kikao kati yake na kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa vifaa na teknolojia katika utafutaji wa mafuta na gesi ya Schlumberger. Pia kikao hicho kilihusisha watendaji kutoka Wizara pamoja na Taasisi zake likiwemo Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

    Waziri muhongo ataka teknolojia ya kisasa utafiti wa Mafuta, Gesi

  • 11BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Veronica Simba Kibondo

    Mto Malagarasi ulioko Mkoani Kigoma, unatarajiwa kuanza kuzalisha megawati 44.8 za umeme mara baada

    ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka ujao wa Fedha (2016/2017), kupitishwa na utekelezaji wake kuanza.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amesema uzalishaji huo wa umeme utatekelezwa kupitia mradi wa Igamba III.

    Aliyasema hayo hivi karibuni mjini Kibondo akiwa katika ziara ya kikazi, kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Wizara yake, hususan inayohusu umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

    Akifafanua zaidi kuhusu utekelezwaji wa Mradi huo, Naibu Waziri Kalemani alisema, Mtafiti aliyepewa kazi ya kutafiti kuhusu Mradi huo, aligundua kuwa, Igamba III inaweza kuzalisha umeme zaidi ya mara nne ya ule ulioainishwa awali katika utafiti wa Mradi wa Igamba II.

    Alisema, umeme utakaozalishwa kupitia Igamba III, utatosheleza mahitaji kwa watumiaji wa nishati hiyo katika Mkoa wa Kigoma na kubaki ziada kubwa, hivyo kuondoa kabisa tatizo la umeme katika mkoa huo.

    Kwa sasa, matumizi ya umeme kwa Mkoa wa Kigoma ni Megawati Sita kwa siku. Umeme utakaozalishwa kupitia Mto Malagarasi, utakuwa zaidi ya mara Saba ya mahitaji yenu, alisema.

    Akielezea mipango ya uzalishaji umeme kwa kutumia maji ya Mto Malagarasi, Naibu Waziri alisema, mwaka 2009, wakati wa utekelezaji wa Mradi wa Changamoto za Milenia

    (MCC), Mradi wa uzalishaji umeme wa Igamba II ulifanyiwa utafiti, ambapo ulipata ufadhili wa zaidi ya Dola Milioni 15 za Marekani.

    Alisema, kwa bahati mbaya, kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi huo, ilionekana hauwezi kutekelezeka kutokana na kugundulika kuwa kuna Vyura na Konokono katika Mto huo. Kutokana na Sheria za Mazingira za Kimataifa, Mradi ule ukasimamishwa.

    Dk Kalemani alieleza kuwa, kufuatia kusimamishwa kwa Mradi wa uzalishaji umeme wa Igamba II, Serikali iliamua kutumia pesa zilizokuwa zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wake, kununua

    Mashine za Umeme-Jua (Sola) katika Halmashauri za Mkoa wa Kigoma na maeneo mengine jirani. Maeneo hayo yalihusisha sehemu muhimu kama Hospitali, Shule mbalimbali na kwenye Masoko.

    Alisema kuwa, sehemu nyingine ya fedha hizo, ilitumika kukarabati miundombinu ya umeme ya mkoa wa Kigoma na maeneo jirani ya Halmashauri zote, zikiwemo Transfoma na Nguzo za umeme.

    Aidha, aliongeza kuwa, fedha nyingine iliyosalia, ilipelekwa kutekeleza miradi mingine ya kimaendeleo ya Watanzania.

    Naibu Waziri alisema, ili kuhakikisha wananchi wa Kigoma wanapata umeme wa uhakika na wa bei nafuu, Serikali iliamua kufanya utafiti mwingine wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji ya Mto Malagarasi, ambapo Mkandarasi aliyepewa kazi hiyo, amekamilisha utafiti wake na kilichobaki ni utekelezaji wa Igamba III.

    Naibu Waziri Kalemani, amehitimisha ziara ya kazi ya siku 10, kukagua miradi inayotekelezwa chini ya Wizara yake katika Mikoa ya Tabora, Kigoma na Geita.

    Mto Malagarasi kuzalisha Megawati 44 za umeme

    Sehemu ya Mtambo wa kuzalisha umeme wa mafuta unaomilikiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mjini Kigoma.

    Mwananchi wa Kijiji cha Malinzi, Kata ya Malinzi, Wilaya ya Kigoma, Hamza Poroto, akiuliza swali kuhusu huduma ya umeme wa REA, kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini (hayupo pichani), wakati wa ziara yake kijijini hapo hivi karibuni.

  • 12 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Kiwanda cha Chumvi chafutiwa LeseniNa Veronica Simba - Uvinza

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, amemwagiza Afisa Madini Mkazi wa Kigoma, Adam Juma

    kuandika hati ya makosa (default notice) ya siku 30, ili kufuta leseni ya mmiliki wa Kiwanda cha Chumvi Uvinza (Nyanza Mines (T) LTD).

    Dkt. Kalemani amechukua uamuzi huo kufuatia Mwekezaji huyo kutelekeza Mtambo wa kuchakata chumvi, ambao ni sehemu ya uwekezaji katika mgodi wake.

    Akizungumza na wananchi wanaoishi pembezoni mwa mtambo huo uliopo eneo la Uvinza, wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, Februari 19 mwaka huu, Naibu Waziri alisema Mwekezaji huyo amekiuka Sheria ya Madini na taratibu za uwekezaji, hivyo Serikali inalazimika kuchukua hatua stahiki.

    Serikali haiwezi kulifumbia macho suala hili, Mwekezaji huyu ametelekeza Mtambo huu kama chuma chakavu pasipo kuwekeza kama anavyopaswa, hivyo kuisababishia hasara Serikali kwa

    kutolipa kodi na mrabaha, alisema.Kufuatia hatua hiyo, Naibu Waziri

    Kalemani aliwaahidi wananchi hao kuwa Serikali itapata mwekezaji mwingine mapema ambaye atawapatia ajira ili waendelee kukidhi mahitaji yao.

    Tunataka aje mwekezaji anayeweza kufuata masharti ya uwekezaji na kuajiri watanzania, maana nafahamu wengi wenu mnategemea ajira kutoka Mtambo huu.

    Aidha, aliahidi kukutana na viongozi wa wananchi hao, ambao wengi walikuwa ni waajiriwa katika Mtambo huo ili kubainisha na kuainisha madai ya wale ambao hawajalipwa stahili zao, walipwe.

    Tutasimamia kuhakikisha, kabla hajafunga Mgodi, anawalipa wote wenye madai pamoja na kodi zote za Serikali anazopaswa kulipa. Pia, tutahakikisha anaacha mazingira katika hali nzuri ikiwemo kufukia mashimo aliyochimba kama sheria inavyomtaka.

    Akieleza zaidi kuhusu umuhimu wa Mgodi huo kwa ujumla, Naibu Waziri alisema kuwa, asilimia kubwa ya chumvi inayotumika nchini inatoka Uvinza.

    Alisema kuwa, kwa kuzingatia umuhimu wa Mgodi huo wa chumvi, Serikali inalazimika kuhakikisha

    anapatikana mwekezaji makini atakayewanufaisha watanzania kwani aliyepo ameshindwa kutimiza makubaliano ya mkataba baina yake na Serikali.

    Aliyataja baadhi ya makubaliano hayo kuwa ni kuajiri watanzania zaidi ya 2000, kulipa kodi za Serikali na kuendelea kurekebisha hali ya mazingira. Nimekagua, yote hayo hayafanyiki, alisema.

    Awali, wakati akikagua sehemu ya Mgodi huo ambayo inafanya kazi, Naibu Waziri aligundua kuwa wafanyakazi wake wanafanya kazi katika mazingira magumu pasipo kuwa na vifaa muhimu vya kujikinga kwa ajili ya usalama wao kama vile Kofia ngumu na Soksi za mikononi ambapo aliagiza wapatiwe vifaa hivyo ndani ya siku 30.

    Pia, alipozungumza na baadhi ya wafanyakazi katika Mgodi huo, walilalamikia kulipwa malipo duni.

    Suala jingine lililojitokeza wakati Naibu Waziri akizungumza na Uongozi wa Mgodi huo, kabla ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Mgodi, ni uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na kutumia kuni kuendeshea mitambo badala ya mafuta mazito kama Mpango wao wa kazi unavyoonesha.

    Ilibainika kuwa tayari, Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) lilishaupatia Mgodi huo maelekezo ya kutokata miti tena na kwamba yatumike mafuta mazito badala ya kuni ili kuhifadhi mazingira.

    Kutokana na matatizo mengi aliyoyabaini kabla hajatembelea eneo la Mtambo uliotelekezwa, Naibu Waziri awali, alifikia uamuzi wa kuunda Timu ya wataalamu wanne ambao aliwataka kufanya kazi kwa siku tatu kukagua na kumpatia taarifa kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo ulipaji wa mrabaha pamoja na maslahi ya wafanyakazi.

    Mgodi wa Chumvi Uvinza ulianza karne ya sita ukijulikana kama Nyanza Salt Mines, ambapo Serikali iliutaifisha mwaka 1967 kutoka kwa Wakoloni wa Kiingereza na kuuweka chini ya usimamizi wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC).

    Mwaka 1973, Mgodi uliwekwa chini ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kabla ya kubinafsishwa kwa mwekezaji Great Mining Corporation mwaka 1999, ambaye anaumiliki mpaka sasa.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini yuko katika ziara ya kikazi Mkoani Kigoma na baadaye ataelekea Geita.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia) akikagua Mgodi wa Chumvi Uvinza. Kushoto kwake ni Meneja wa Mgodi huo, Bonny Mwaipopo.

    Mmoja wa vibarua katika Mgodi wa Chumvi Uvinza (kulia), akitoa malalamiko kwa niaba ya wenzake kuhusu malipo duni wanayopatiwa mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk Medard Kalemani (kushoto). Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mrisho Gumbo.

    Sehemu ya Gofu lililokuwa Mtambo wa kuchakata Chumvi Uvinza.Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Uvinza.

  • 13BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Veronica Simba - Kasulu

    Imeelezwa kuwa mwenye mamlaka ya kutoa leseni za madini nchini ni Wizara ya Nishati na Madini pekee.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani alilazimika kutoa maelezo hayo hivi karibuni mjini Kasulu, baada ya kupokea taarifa ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Gerald Guninita iliyoeleza kuwa moja ya changamoto kubwa katika Wilaya yake ni mgogoro uliopo baina ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania na wachimbaji wadogo wanaojishughulisha na uchomaji chokaa.

    Wakala huo ulitoa idhini ya kuchoma chokaa kwa wachimbaji hao kwa masharti kadhaa, ikiwemo kulipia mrabaha kwa Wakala wa maeneo wanayomiliki. Hata hivyo, wachimbaji walikaidi na wanaendelea na shughuli hizo bila kulipa ushuru wowote kwa Wakala huo, alieleza Mkuu wa Wilaya.

    Mkuu huyo wa Wilaya, alimwomba Naibu Waziri Kalemani kutatua tatizo hilo kwa maelezo kwamba, Waziri mwenye dhamana na Maliasili, alishatoa agizo la kuwaondoa wavamizi wote ndani ya hifadhi za Serikali ikiwa ni pamoja na wachimbaji katika hifadhi za Makere.

    Kama unavyojua, shughuli za uchimbaji madini ni shughuli mtambuka zinazogusa sekta kadhaa kama nilivyoziainisha awali. Mvutano

    utaendelea endapo hapatafikiwa muafaka mzuri, alisisitiza Guninita.

    Akijibu taarifa ya Mkuu wa Wilaya pamoja na kutoa ufafanuzi, Naibu Waziri Kalemani alisisitiza kuwa, hakuna taasisi, wakala au mtu mwingine yeyote anayepaswa kutoa leseni ya madini isipokuwa Wizara ya Nishati na Madini pekee.

    Tutapanga utaratibu, tukutane na wenzetu wa Maliasili na Utalii kuzungumzia suala hili, alisema.

    Akifafanua zaidi, Dk Kalemani aliongeza kuwa, Kifungu namba 6 (1) cha Sheria ya Madini ya mwaka 2010, kimempa mamlaka Kamishna wa Madini pekee kutoa leseni ndogo za madini na Waziri wa Nishati na Madini kutoa leseni kubwa za madini.

    Aliendelea kufafanua kuwa, ikitokea kuna matatizo kwenye usimamizi wa leseni yoyote ya madini, mwenye dhamana ya kusimamisha leseni hiyo ni Kamishna wa Madini, kwa mujibu wa kifungu cha 6 (4) cha Sheria ya Madini.

    Vilevile, alieleza kuwa, Sheria hiyo ya Madini ya mwaka 2010, imempa mamlaka Kamishna wa Madini pekee, kukamata madini yaliyopatikana isivyo halali na kuyauza kwa kufuata utaratibu wa Tenda za Serikali.

    Alisema, leseni ya madini inaweza kutolewa katika eneo lolote bila kujali kuna misitu, shule wala kitu kingine chochote. Hata hivyo, baada ya kupata leseni, endapo iko kwenye eneo la Maliasili au eneo lolote lenye kugusa sekta nyingine, muhusika anapaswa

    kuomba kibali kutoka kwa sekta inayoguswa ili aweze kufanya shughuli zake.

    Aliongeza kuwa, Sheria ya Madini kupitia Kifungu namba 95 (1), kinampa uhuru mwenye mamlaka na sekta husika, aliyeombwa kibali, kukataa au kukubali shughuli za madini zifanyike katika eneo lake. Au anaweza kukubali

    kwa kutoa masharti, kwa mfano kuruhusu sehemu fulani ya eneo hilo itumike pasipo kuathiri shughuli nyingine za sekta yake.

    Ndiyo maana leseni nyingi ziko kwenye rasilimali ya Maliasili. Hata Mgodi wa Dhahabu wa Tulawaka ulioko Biharamulo, uko kwenye eneo la Maliasili, alifafanua.

    Wizara yatoa ufafanuzi utoaji Leseni za Madini

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa tatu kutoka kushoto) akikagua shughuli za uchimbaji dhahabu katika Machimbo ya Matinje yaliyopo Kata ya Mwashiku wilayani Igunga, wakati alipotembelea Machimbo hayo akiwa katika ziara ya kazi hivi karibuni. Kulia kwake ni Mbunge wa Manonga, wilaya ya Igunga, Seif Gulamali.

    TAOMAC wasisitiza ushirikiano na Serikali Sekta ya MafutaNa Zuena Msuya Dar Es Salaam,

    Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ameutoa hofu Umoja wa Kampuni za

    Mafuta Tanzania (TAOMAC) kwa kuwahakikishia kuwa ataendelea kushirikiana nao katika sekta hiyo kwa kuziangalia sheria na taratibu zilizopo.

    Prof. Muhongo aliyasema hayo jijini Dar Es Saalam wakati wa kikao chake na TAOMAC.

    Katika kikao hicho TAOMAC walitoa mapendekezo kadhaa ikiwemo kuimarisha ushirikiano katika masuala ya ulinzi na usalama kwenye miundombinu ya mafuta katika Bandari ya Dar Es Salaam.

    Prof. Muhongo alisema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na TAOMAC kwa kuwa inatambua umuhimu wa kampuni hizo katika uchumi wa nchi na kuziagiza kufanya biashara hiyo kwa njia halali, uaminifu na kufuata taratibu na sheria zilizowekwa.

    Aliongeza kuwa lengo la Serikali ni kuweka mazingira bora kwa kila Mtanzania wakiwemo wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa, ili kuisaidia Serikali katika kutimiza azma hiyo ni vyema kila mmoja akafuata taratibu na sheria za biashara anayoifanya

    kwa kujali maslahi mapana ya nchi na kuweka mbele uzalendo.

    Prof. Muhongo, aliwaahidi TAOMAC kushughulikia changamoto zinazowakabili katika sekta ya mafuta ikiwemo masuala ya ulinzi pamoja na malalamiko kuhusu huduma zisizoridhisha wakati wa kupokea mafuta.

    Sambamba na hilo Prof. Muhongo alisema wataangalia suala la kuongeza miundombinu ya kuhifadhi mafuta nchini ili kuondokana na changamoto za uwepo wa miundombinu isiyotosheleza mahitaji.

    Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu TAOMAC, Salum Bisarara aliyeambatana na wajumbe wa umoja huo alisema ameridhishwa na majibu ya Serikali yaliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na kwamba wanaimani kuwa kwa kasi hii ya Serikali ya awamu tano kero zao zitafikia tamati.

    Hata hivyo alimuahidi Waziri Muhongo kuwa watatekeleza kile alichowaagiza ili kutimiza azma ya Serikali katika kuleta maendeleo ya Taifa na mwananchi kwa ujumla.

    Bisarara ametoa wito kwa Kampuni na wafanyabiashara wa mafuta nchini kuzingatia sheria zilizowekwa kila mmoja aweze kufanya kazi halali na yenye kuleta tija kwa Taifa na wafanyabiashara wenyewe.

    Wajumbe wa umoja wa Kampuni za Mafuta wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, (hayupo pichani) aliyekuwa akitoa baadhi ya majibu ya hoja walizoziwasilisha kwakwe kuhusu sekta hiyo.

  • 14 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na. Issa Mtuwa(STAMICO) Mwanza

    Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limewawezesha wachimbaji wadogo na wanunuzi wa madini Kanda ya Ziwa kupata mafunzo

    maalum ya namna ya kutumia mfumo wa kielektroniki (Small Scale Mining Portal) ili kupata taarifa zinazohusu sekta ya uchimbaji mdogo wa madini ikiwemo masoko na bei za madini.

    Aidha, mafunzo yalihusisha pia matumizi ya mtandao wa Kompyuta na simu za mkononi katika kupata taarifa hizo.

    Akifungua mafunzo hayo wiki iliyopita jijini Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi, Mhandisi David Mulabwa alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa wachimbaji wadogo kwa kuwa yanawapa ufahamu mpana wa kujua masoko na bei za kila siku duniani kutoka kwa wanunuzi mbalimbali na pia kuwasaidia kuchagua mnunuzi mwenye bei nzuri zaidi yenye thamani halisi ya madini (Value for money)

    Aidha, Mhandisi Mulabwa alisema kuwa pamoja na kujua bei lakini mafunzo hayo yamelenga pia kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata taarifa mbalimbali zinazohusu madini na sekta ya uchimbaji mdogo kupitia mtandao huo.

    Akimkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi wa mafunzo hayo, Meneja

    Uchimbaji Mdogo kutoka STAMICO ambae ndiye Mratibu na muandaaji wa mafunzo hayo, Tuna Bandoma alimtaarifu mgeni rasmi kuwa miongoni mwa faida ya mafunzo hayo ni wachimbaji wadogo kusogezwa karibu na mlezi wao ambaye ni STAMICO.

    Aidha, aliwaarifu kuwa kupitia mfumo huo wachimbaji watapata taarifa mbalimbali zikiwemo orodha ya vifaa na bei zake pamoja na mahali vinapopatikana, taarifa za upatikanaji wa mitaji na teknolojia ya uchenjuaji wa

    madini kwa miradi yao ya uchimbaji na uchenjuaji madini.

    Pia Bandoma aliongeza kuwa, baada ya mafunzo hayo wachimbaji hao watakuwa na fursa ya kuuliza na kuwasiliana kuhusu masuala yanayowahusu hususan katika shughuli zao kwa kuingia na kufanya mawasiliano ya moja kwa moja na STAMICO kupitia ukurasa maalum ulioandaliwa mahususi kupitia tovuti ya mfumo huo (www.ssm-stamico.co.tz) na majibu yao watayapata moja kwa

    moja kupitia simu zao za mkononi. Bandoma alisema kuwa sekta ya

    uchimbaji mdogo imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za ukosefu wa vifaa na zana stahiki vya uchimbaji, ukosefu taarifa sahihi za masoko ya madini ya uhakika, ukosefu wa mitaji kwa miradi ya uchimbaji mdogo wa madini. Kutokana na changamoto hizo alidokeza kuwa STAMICO imeendelea na itaendelea kuzishughulikia kwa kutafuta majawabu stahiki kwa kusaidiana na wadau wengine kama Serikali kupitia Wizara, GST, SIDO na SMMRP.

    Alisema kuwa bado jukumu la msingi la STAMICO litaendelea kuwa kuwasaidia wachimbaji wadogo kitaalam kuboresha shughuli zao kwa kuongeza uzalishaji ulio bora zaidi.

    Naye Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo (MWEREMA), Mzakir Kasirate akizungumza wakati wa mafunzo hayo alisema anaishukuru STAMICO kwa kuandaa mafunzo hayo, kwani wamejifunza mengi na kupata uelewa mkubwa ikiwemo matumizi ya mfumo wa mtandao wa kompyuta kupata taarifa, kufuatilia bei ya soko la madini kutoka kwa wanunuzi mbalimbali lakini kubwa zaidi kupata nafasi ya kuuliza maswali kwa njia ya mtandao wa kompyuta na kupokea majibu kwa njia ya simu za mkononi.

    STAMICO iliratibu mafunzo hayo ambayo ni ya kwanza hapa nchini kutolewa na Shirika hilo kwa lengo la kuwaunganisha wachimbaji wadogo, wanunuzi wa madini na STAMICO kupitia mtandao huo na kuwezesha kupatikana kwa taarifa za uhakika na wakati zinazohusu bei za madini, vifaa na uchimbaji ulio salama.

    Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Kielektroniki katika kupata taarifa katika picha ya pamoja. Walio kaa kutoka kushoto ni; Ismail Sadik Mnunuzi wa Madini, Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogo mkoa wa Mwanza Richard Seni, Kamishina Msaidizi wa Madini kanda ya ziwa Victoria Magharibi Mhandisi David Mulabwa , Meneja Uchimbaji Mdogo kutoka STAMICO Tuna Bandoma, Mwakilishi wa SMMRP Veronica Nangale na Muniko Magoiga mchimbaji mdogo.

    Afisa Tehama Mwandamizi kutoka STAMICO Daudi Bupilipili akitoa mafunzo ya ufahamu wa matumizi ya mfumo wa Kielektroniki kwa wachimbaji wadogo na wanunuzi wa madini jijini mwanza Juzi. Walio kaa meza kuu kutoka kushoto ni; Mgeni rasmi Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya ziwa Victoria Magharibi Mhandisi David Mulabwa, Mwenyekiti wa Wachimbaji wa dogo mkoa wa Mwanza Richard Seni na Mwakilishi wa SMRRP Veronica Nangale

    Wachimbaji wadogo wapatiwa mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki

  • 15BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Latifah Boma, Dar es Salaam.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametoa wito kwa kampuni zinazofanya

    shughuli za utafiti na uchimbaji wa gesi asilia na mafuta nchini kutoa kipaumbele kwa Kampuni, wafanyabiashara na wafanyakazi wazawa pale nafasi za kazi au za utoaji huduma katika Kampuni hayo zinapopatikana.

    Profesa Muhongo alitoa wito huo wakati alipofanya mazungumzo na watendaji wa kampuni hizo Wiki hii jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya kampuni alizokutana nazo ni Maurel et Prom, Statoil, Pan African, Swala Oil, Dodsal Hydrocarbons, Beach Petroleum, Ndovu Resources pamoja na BG/Shell, ambayo imeundwa kwa ubia kati ya kampuni za kimataifa za BG na

    Shell. Mikutano hiyo pia ilihusisha

    Watendaji mbalimbali kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini ikiwemo Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA), Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

    Profesa Muhongo alieleza kuwa ushiriki wa Wazawa katika shughuli hizo za mafuta na gesi asilia, sio tu kwamba utapelekea Watanzania kufaidika na sekta hiyo bali pia utaongeza mahusiano mazuri kati ya wawekezaji na jamii zinazowazunguka.

    Aidha, Profesa Muhongo aliwapongeza wawekezaji hao kwa juhudi zao za kuendeleza jamii zinazozunguka maeneo wanapofanya shughuli za utafiti na uchimbaji wa

    gesi asilia na mafuta na alitoa wito kwa wawekezaji hao kusaidiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili kuwaunganishia umeme wananchi waliopo katika maeneo hayo kwani bado yana uhaba wa umeme.

    Profesa Muhongo vilevile aliitaka TPDC kuongeza juhudi kwenye kutangaza shughuli zake mbalimbali inazofanya nchini kwani wananchi wengi hawana taarifa ya kutosha juu ya maendeleo ya miradi katika sekta hiyo ya gesi.

    Ili kutimiza nia ya Serikali ya kuwa na nishati ya kutosha nchini, Profesa Muhongo aliwataka wawekezaji hao pamoja na taasisi zinazosimamia sekta hiyo kuongeza juhudi katika kuhakikisha gesi inapatikana kwani ina umuhimu mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

    Ili uchumi wa nchi uweze kufikia kiwango cha kati ifikapo mwaka 2025, Serikali imepanga kuendeleza na

    kujenga viwanda, ambavyo vitahitaji gesi kwa kiasi kikubwa, kwani gesi inatumika katika uzalishaji wa umeme na mbolea, viwanda vya saruji, viwanda vya kemikali pamoja na viwanda vinginevyo nchini, hivyo ni lazima kuongeza juhudi katika shughuli hizi mnazozifanya, alisema Profesa Muhongo.

    Profesa Muhongo ameweka ratiba ya kukutana na wawekezaji hao kila baada ya miezi mitatu ambapo atakutana nao tena mwezi Juni, Septemba na Novemba mwaka huu ili kutathmini mipango ya kazi baina yao na TPDC.

    Wawekezaji hao pia wamekutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa katikati ya wiki hii ambaye aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Kampuni hayo na kuyataka kuongeza juhudi katika shughuli za utafiti na uchimbaji wa gesi asilia nchini ili nchi iwe na gesi ya kutosha.

    Akiendelea na juhudi zake za kukutana na wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya Nishati nchini, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Wiki hii amekuwa na vikao na wawekezaji wanaofanya shughuli za utafiti wa mafuta na gesi nchini.

    Profesa Muhongo alieleza kuwa nia ya mikutano hiyo ni kukutanisha wadau wote wa miradi hiyo ili kujadili maendeleo ya miradi husika, changamoto wanazokutana nazo, maoni yao na taarifa zozote kutoka kwa wawekezaji hao ili kuzifanyia kazi kwa pamoja na hivyo kuziwezesha kampuni hizo kufanya kazi kwa ufanisi.

    Akijibu kuhusu hofu za baadhi ya wawekezaji juu ya changamoto wanazoziona zitajitokeza wakati wa utekelezaji wa Sheria ya Petroli ya mwaka 2015, Waziri Muhongo aliwasihi wawekezaji hao kuendelea na majukumu yao kwa kutumia sheria iliyopo na kama sheria hiyo itahitaji marekebisho basi yanaweza kufanywa baada ya kupima utekelezaji wake kwanza.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (aliyesimama) akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, kuzungmza na watendaji wa Kampuni zinazofanya shughuli za utafiti wa mafuta na gesi asilia nchini. Kushoto kwa Waziri wa Nishati na Madini ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akieleza jambo wakati wa mkutano baina yake na wawakilishi kutoka kampuni ya Maurel et Prom.

    Christopher Maitre (aliyesimama), Meneja kutoka Maurel et Prom, akielezea maendeleo ya miradi ya kampuni hiyo katika mkutano baina ya wawakilishi wa kampuni hiyo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

    MUHONGO ataka Wazawa kupewa Kipaumbele

  • 16 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    The party that is best able to understand a risk, control the likelihood of the risk occurring and/or minimize the impact of the risk should also be

    responsible for managing it. Some of the risks associated with infrastructures includes those borne from the supply side like Land availability and site acquisition so much legal and environment issues including permits and resettlements

    to be considered in which the public sector is best equipped to manage it, Constructions risks can results on the costs overruns, quality related issues of the facility, Operational Risks that involves operational related costs like salary, service interruptions that can result in revenue losses, these risks are allocated to private partner who are best equipped and incentivize to manage it. Some other risks comes that are borne from the

    demand side which is more related to the number of users of the facility or services. Financial, Currency, Political, legal and regulatory and Natural disaster risks are amongst the common risks elements associated with PPPs projects. Risks identifications and allocations between partners plays a major role in creating a win-win relationship between private and public sectors.

    To achieve risks identifications and

    allocations, in practice, Professionals usually deploy risk Matrix tool which is often used for contract drafting and negations of the project structures to facilitate discussion and outline all risks and their corresponding allocation. Risk Matrix is an important and key documents for PPPs projects, this document can be created early in the project development process, as it can greatly impact the attractiveness of the project for financiers and different interest private partners. Risk allocation will also influence profit margins sought by private investors.

    BUSINESS PERSPECTIVESalum Mnuna is MBA, Certified PPP specialist based in Dar es Salaam

    Can be reached via email [email protected] or WhatsApp 0767457817The views in the article are solely based on the knowledge of the author and should

    not be associated with his employer.

    Email: [email protected]

    Creating Attractive Financing environment of PPP Infrastructure projects through balanced risks allocations

    Public private partnership (PPPs) models are trending to become a common model of delivering public infrastructure around the globe. This is due to

    multiple reasons including the facts that governments are constrained in budgets, capacity, increasingly demands of infrastructure to stir economic growth by general public and the perceptions that PPPs offer greater value for money in comparison to tradition procurement. In Tanzania PPPs is still at its infant stages where PPPs Laws, environment and institutional arrangements has been put

    in place and capacity building programs are ongoing to equip personnel with much needed knowledge and skills to manage multimillion anticipated projects on economic development infrastructure.

    In Traditional Procurement the Public sector assumes all the risks associated with the projects unlike PPPs where optimal risks allocations drives the Value for money ( VfM) for the government by relieving some of the risk that cannot well be managed by public to private partner who is well equipped to manage and mitigate the impacts. Bear in mind PPPs projects are usually expensive for

    the Public sector and therefore engaging private sector should always be done with greater value for Money or over all greater positive net gain to the society in comparison to if it was to be procured traditionally.

    Risks allocations is important because it is critical factor to the success of the PPP project, if all the risks are shifted to one part say, the private partner, the project will be deemed to be too risky and there will be no interest from the private partner, and would scare banks and financial institutions to finance it, on the other hand if all the

    risks are allocated to the public partner, then will be no or limited motivations and incentives for private partner to innovate and perform efficiently. In this case using PPP Mechanism might not offer significant value, compared to traditional procurement, so finding the right balance of this allocation will be critical to the success of PPP Project. To find the balance, the risks should always be allocated to the part best equipped and have the capacity to manage them at low costs.

    Risks Identifications and Allocation

    By Salum Mnuna

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINI

    LESENI ZA MADINI ZENYE MALIMBIKIZO YA ADA

    Kamishna wa Madini anapenda kuwatangazia wamiliki wa leseni za madini zenye malimbikizo ya ada za leseni kuja kulipia leseni zao bila kukosa. Majina ya wamiliki na leseni husika zimeoneshwa kwenye orodha iliyochapishwa kwenye magazeti ya tarehe 18 Februari, 2016 ya Habari Leo, Uhuru na Daily News na vilevile katika gazeti la Al-Huda la tarehe 25 Februari, 2016. Majina hayo pia yanapatikana katika tovuti ya Wizara kwa anuani ya www.mem.go.tz. Watakaoshindwa kulipa madeni hayo ifikapo tarehe 16 Machi 2016, watachukuliwa hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni husika.

  • 17BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    GILAY SHAMIKA SENIOR ENGINEER & GEMOLOGISTTANZANIA MINERALS AUDIT AGENCY (TMAA)[email protected]

    Tanzanite T

    anzanite was formed over 600 million years ago when Mt. Kilimanjaro erupted caused a unique set of

    conditions to form deep within the earth - heat and pressure mixed with rare chemicals such as Vanadium to allow this exceptionally rare gem stone to form. These conditions remained constant for the entire 600 million years and Tanzanite grew. It was first discovered by man in 1967 when an enormous grassfire swept the land below Kilimanjaro Mountain.

    As Tanzanite is a brownish color in its rough state, the crystals lying on the surface were never noticed until when the grassfire had burnt the land and heated the stones. They turned bright, glittering violet-blue in the sunlight and attracted the attention of some Maasai tribesmen. Tanzanite was named by Tiffany & Company (New York) and for the first ten years after its discovery Tiffanys had the exclusive right to this lovely gem stone. Today, after the liberalization of the Tanzanian economy, it is a free market.

    To date the only known reserve of Tanzanite gemstone in the world is a strip of 8km by 1km at Merelani area in Manyara region, Northern of Tanzania on the slopes of the legendary Mt. Kilimanjaro at Merelani Tanzania.To remember this you can imitate Tanzanite Poem by Eng.Gilay Shamika;

    Tanzanite the uniqueness of Tanzania,

    Only Tanzanite in Tanzania,

    Only tanzanite with tantalizing tricolor,

    The stones on the foot of Mt.Kilimanjaro,

    The stones of 21st Century and

    The stones of December birthday.

    Geology Tanzanite is a thousand

    times rarer than diamonds and is trichroic, which means that in its rough form, it radiates three different colors from each of its crystallographic axes: blue, violet and burgundy. Tanzanites are found in Lelatema Antiform in Merelani, Manyara Region andits chemical formation is: 3Tsavorite + H2O + 5CO2 = 2Tanzanite + 3Quartz + 5Calcite

    Tanzanite is found within a relatively complex geological environment and is found in chocolate-tablet boudin structure, typically located in the hinges of isoclinal folds (folds dipping in the same direction) present in the ore body. The Geologists at Tanzanite one has identified two potential strips of these unique zones in the area and has named them as Upper Horizon and Lower Horizon.

    Unique features of Tanzanite to prove its natural

    Tanzanite is the only gemstones in the world that is trichroic. This means that when white light passes through, it breaks into 2 paths and creates 3 different colors - one axis will look violet, reddish brown and the third a blue-violet. The picture below shows the same Tanzanite crystal from 3 different angles showing its amazing trichroism. This is the confirmation that, the tanzanite you have is natural and not synthetic (manmade).

    Gemological properties of Tanzanite

    Gemological Properties of Tanzanite Unit of Measure Gem Species Zoisite Specific gravity 3.35 Hardness (Mohs Scale) 6.5 Toughness Fair Stability to light Stable Carat Weight Below 1-10 ,rarely 100 + Birthstone December

    Treatment and grading of tanzaniteTanzanite when heated at 600 centigrade it changes its color from pale blue/brown to deep blue/

    brown color. Though sometime in the market the grading includes AAA, AA and A, signifying A,B and C grade, but the grading within the country ( TanzaniteOne) the grading is as seen in the table below.

    Colour grading of Tanzanite ExplanationA Exceptional Colour, Eye Clean B Rare Deep Blue/other Colour, Eye Clean BSI B Colour-Slightly Included BI B Colour Included BL B Lighter Colour Grade, Eye Clean BLSI B Light-Slightly Included BLI B Light Included D Opaque Material(agreed to use D instead of O )

    Cut and polished Tanzanite

    Tanzanite in different lights; left side under white light and right side under incandescent light

    RoughTanzanite

  • 18 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Maonesho ya 5 ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yenye aina mbalimbali za vito zikiwemo

    Tanzanite , Ruby, Sapphire , Tsavori te , Rhodol i te , Spessart i te , Tourmaline,

    Chrysobery l na Almasi yanatarajiwa kuvutia

    Zaidi ya kampuni 100 za wafanyabiashara na wachimbaji madini ya Vito kutoka Tanzania na

    nchi zingine za Afrika Mashariki, Kati na Kusini; na zaidi ya wanunuzi 500 kutoka zaidi ya nchi 25

    ulimwenguni

    Jisajili na Ushiriki Sasa!!!

    Wasiliana na: Kamati ya Maandalizi AGF Simu: +255 784352299 or +255 767106773

    Barua pepe: [email protected]

    :ama Ofisi za Madini za Kanda

    Yameandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini

    kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA)

    Wafanyakazi STAMIGOLD washauriwa kuanzisha SACCOSNa Godfrey Francis- Stamigold

    Wafanyakazi wa mgodi wa Dhahabu wa Stamigold wamepewa mafunzo na kushauriwa kuanzisha

    Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) ili kujiletea maendeleo kiuchumi.

    Ushauri huo ulitolewa hivi karibuni mgodini hapo na wataalamu kutoka Wizara ya kilimo, Chakula na ushirika pamoja na Idara ya Maendeleo ya Ushirika Biharamulo, Thomas Mugwe na Emmanuel Maleo.

    Ilielezwa kwamba lengo la mafunzo hayo kwa wafanyakazi wa mgodi huo ni kuwawezesha kuhamasika na kutambulisha fursa na umuhimu wa kuunda SACCOS.

    Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Thomas Mugwe alisema SACCOS ni asasi ya fedha ambayo inajulikana kisheria kufuatia sheria Na. 20 ya mwaka 2003 ambayo inawataka watu wanaotarajia kujiunga pamoja kwa hiari yao kuweka fedha pamoja na kukopeshana.

    SACCOS inaundwa na watu waliojiunga pamoja kwa hiari yao ambao wamekubaliana kuweka fedha

    zao kwa pamoja na kukopeshana kwa malengo ya kujiendesha kiuchumi na kijamii, kama ilivyoainishwa katika sheria ya Vyama vya Ushirika, alisema.

    Alisema kabla ya kukisajili chama hicho, kwa mujibu wa sheria wanapaswa kuchukua hatua za awali kadri watakavyoona inafaa ili kusaidia uundaji wa chama hicho.

    Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kufanya mikutano na mijadala yenye tija itakayosaidia kuibua changamoto na matatizo yanayoikabili jamii husika ili kupatikane kwa makubaliano ya pamoja ya namna ya kukabiliana na changamoto hizo.

    kisheria, kuboresha maisha yao kwa kuanzisha ushirika wa Akiba na Mikopo kwa malengo ya kusaidiana kwa kuweka akiba na kupata mikopo yenye masharti na riba nafuu.

    Aliongeza kwamba SACCOS inaanzishwa na watu wasiopungua 20 kwa mujibu wa sheria ya vyama vya Ushirika ya mwaka 2003 na watu 20 wanaruhusiwa kuanzisha chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo.

    Hata hivyo uzoefu umeonesha kadri idadi inavyoongezeka ndivyo chama kinavyokuwa na fursa kubwa zaidi ya kujenga mtaji, mfuko wa kukopeshana na kupanua soko au wateja wanaohudumiwa.

    Alisema endapo wahusika

    wataamua kwa hiari yao kuanzisha SACCOS watatoa taarifa kwa Afisa Ushirika wa eneo husika ili aje kutoa

    muongozo au maelekezo ya namna ya uanzishwaji wake.

    Baadhi ya wafanyakazi wa Stamigold wakifuatilia mafunzo ya uundaji na uendeshaji wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) kutoka kwa Afisa ushirika (hayupo pichani).

  • 19BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Energy investment opportunities Invest in Tanzania Priority areas; Lindi & Mtwara

    The Ministry of Energy and Minerals is responsible for overseeing the overall development of the energy sector in Tanzania. It works hand in hand with various stakeholders, both public and private sectors to deliver its mission. To attract private capital into the sector, the Government has taken several initiatives to improve institutional set up, legal and regulatory frameworks including restructuring of the State Owned Companies. The restructuring aims at enhancing efficiency in the provision of services.

    1. POLICY AND LEGAL FRAMEWORK

    The energy sector has the following guiding instruments in place which assist in discharging its duties.

    1. National Gas Utilization Master

    Plan (under prep);2. National Energy Policy 2015; 3. Petroleum Act, 20154. Model Production Sharing

    Agreement, 2013; (MPSA);5. Public-Private-Partnership Act,

    20106. Electricity Act, 2008;7. Rural Energy Act, 2005;8. Environmental Management Act,

    2004;9. Income Tax Act, 2004;10 Occupational Safety and Health

    Act, 2003;11. Energy and Water Utilities

    Regulatory Authority Act, 2001;

    2. RESOURCES POTENTIAL

    Tanzania has abundant indigenous energy resources which include natural gas, hydropower, coal, geothermal, solar, uranium, biomass, and wind. As summarized hereunder, much of the resources is undeveloped.

    RESOURCE POTENTIAL APPLICATION EXPLANATIONS & COMMENTS

    1. Large hydro 4,700 MW 12% harnessed for power generation

    Installed capacity is only 561 MW

    Natural Gas Enormous deposit

    More than 55 tcf discovery, currently used for 711 MW power generation and some domestic applications

    More explorations are ongoing

    2.Small microhydro

    500 MW 5% harnessed for power generation

    Less than 100 MW has been exploited

    3.Biomass Woodland and agricultural residues

    Electricity generation from biomass in the country is more than 35MW, some of which is grid-fed

    Electricity is generated mainly from woodlogs and agricultural residues from agro-based industries

    4.Solar 200Wm-2 >6MW electricity installed capacity

    The average sunshine is more than 9 hours per day

    5.Wind Speed: 0.8 - 4.8 m/s

    Some area over 8m/s

    Already > 100 MW capacity is lined in the Power System Master Plan 2009-2033

    Potential sites for investment in wind energy include the area around Makambako in Iringa, Kititimo in Singida, and Mgagao in Kilimanjaro region

    6.Geothermal More than 5000 MW

    Not exploited Among 50 sites, only one (Ngozi in Mbeya Region) has undergone detailed study. Tanzania Geothermal Development Company Ltd. has been established.

    7.Coal 1.2 5 billion tonnes

    < 150,000t/year The Government is discussing with potential investors (public and private) on identified projects development.

    9. Nuclear Uranium deposits exists in Dodoma, Ruvuma and Singida Regions

    Not exploited Private sector has shown interest to develop the resource

    11.Tidesl/waves Significant Not exploited No assessment yet

    3. POWER SECTORThe interconnected grid system installed

    capacity has reached 1,516.24 MW in the grid system, whereas 561.84MW is hydro based, 711 MW from natural gas and 243 MW from heavy oil plants. Maximum Demand in the national grid system is 988.34 MW. Currently electricity Customer base is about 1.5 connections. Access to Electricity is about 40% while connection level is 30%;

    Supply of reliable and quality electricity is a pivot for economic development of every nation. The countys priority initiative is to effectively utilize available indigenous fuels for Sustainable Power Generation. The fast growing power demand in the country of about 10 -15% offers a good opportunity for both local and foreign investors to participate in the development of the Tanzanian power industry;

    The Government has completed construction of a 547km, 36 inch diameter Natural Gas pipeline from Mtwara to Dar es Salaam that will supply enough gas for power generation plants as well as for industrial and domestic consumption has been completed;

    The addition gas fired power plants is as shown below under construction or commissioning stage include: Kinyerezi I (150MW) in commissioning stage while its extension for 185 MW is being negotiated; Kinyerezi II (240MW) construction has started; Kinyerezi III (300MW), and Kinyerezi IV (330MW) still being negotiated; 600 MW to be located at Mtwara (negotiation stage); and 320MW to be located at Somanga fungu;

    Two Wind power plants of 50MW each at Singida; and Development of coal fired power plants: Mchuchuma (600MW), Ngaka (400MW) and Kiwira (200MW) which are still in discussions;

    Several transmission line under construction including Iringa Shinyanga 400 kV, and Makambako Songea 220kV. Rehabilitation of existing power transmission infrastructures as well as new infrastructures for power evacuation to load centers in the north western part of the country where mining activities are concentrated are going on.

    In the long term planning horizon the Government will continue to invest in power generation using Natural gas, coal, hydro, Renewable Energies ( Geothermal, Solar , Wind and Biomas); Extension of grid network to reach the isolated areas, and construction of power interconnector projects to enable power trading with neighboring countries that will improve power security in the region.

    4. INVESTMENT OPPORTUNITIES5.1 PETROLEUM SUB-SECTOR

    Exploration of oil and gas (open acreages in deep-sea in the Indian Ocean, inland basins and Lake Tanganyika North Block;

    Construction of petrochemical industries;

    Construction of infrastructure for transportation and distribution of natural gas in Mtwara, Lindi, Dar-es-Salaam and neighboring regions;

    Construction of oil pipelines from Dar-es-Salaam to other neighboring countries;

    Establishment of the storage facilities for petroleum products - transit fuel.

    Several transmission line under construction including Iringa Shinyanga 400 kV, and Makambako Songea 220kV. Rehabilitation of existing power transmission infrastructures as well as new infrastructures for power evacuation to load centers in the north western part of the country where mining activities are concentrated are going on.

    In the long term planning horizon the Government will

    continue to invest in power generation using Natural gas, coal, hydro, Renewable Energies ( Geothermal, Solar , Wind and Biomas); Extension of grid network to reach the isolated areas, and construction of power interconnector projects to enable power trading with neighboring countries that will improve power security in the region.

    4. INVESTMENT OPPORTUNITIES

    5.1 PETROLEUM SUB-SECTOR Exploration of oil and gas (open acreages in deep-sea in the

    Indian Ocean, inland basins and Lake Tanganyika North Block;

    Construction of petrochemical industries; Construction of infrastructure for transportation and

    distribution of natural gas in Mtwara, Lindi, Dar-es-Salaam and neighboring regions;

    Construction of oil pipelines from Dar-es-Salaam to other neighboring countries;

    Establishment of the storage facilities for petroleum products - transit fuel.

    5.2 HYDRO POWER PROJECTS SN PROJECT NAME FEASIBILITY STATUS REMARKS 1. Malagarasi Stage III, 44.7

    MW Feasibility Study completed in September,

    2011 ESIA Certificate was issued by NEMC in

    May, 2013

    No potential financier is committed

    2. Rumakali 222 MW Feasibility Study and ESIA study were completed in May, 1998

    No potential financier is committed

    3. Steiglers Gorge Phase I 1 1,048 MW

    Pre - Feasibility Study was completed in 2012

    ESIA study ongoing

    No potential financier is committed

    4. Songwe Manolo (Lower) 177.9 MW

    Feasibility Study was completed in April,

    No potential financier is committed

    SN PROJECT NAME FEASIBILITY STATUS REMARKS Manolo (Lower) 158.9 MW

    2014

    ESIA study of Lower Manolo was completed in 2015 Manolo (Lower)

    29.4 MW

    5. Mpanga 160 MW Pre - Feasibility Study was completed in June2010

    ESIA Certificate was issued by NEMC in 2012

    No potential financier is committed

    6. Masigira 118MW Preliminary study was completed in March,1997

    Feasibility Study and ESIA study is on going

    No potential financier committed

    7. Lower Kihansi Expansion 120 MW

    Preliminary study was completed in Mar-1997

    No potential financier committed

    8. Upper Kihansi 47 MW Pre- Feasibility Study was completed in October, 1990

    No potential financier committed

    9. Kakono 87 MW Feasibility Study and ESIA study were completed in September, 2014

    NEMC is reviewing the ESIA report

    No potential financier committed

    10. Iringa

    Ibosa 36 MW Pre- Feasibility Study was completed in May-2013

    Under preparation for ESIA study by RUBADA

    No potential financier committed

    Nginayo 52MW

    11. Mnyera

    Ruaha 60.3 MW Pre- Feasibility Study was completed in June, 2012

    ESIA study was completed in 2014 Under examination of ESIA report by NEMC

    No finacial commmited Mnyera 137.4 MW

    Kwanini 143.9 MW Pumbwe 122.9 MW Taveta 83.9 MW Kisingo 119.8 MW

    5.3 TRANSMISSION LINES PROJECTS:

    Northwest Grid Power Project Nyakanazi to Mbeya 220 kV transmission line It mainly consists of five 220 kV Substations: Nyakanazi, Kigoma, Mpanda Sumbawanga and Mbeya; about 1148km of 220kV high tension Transmission line.

    Iringa Mbeya 400 kV Transmission Line in Tanzania The project will involve construction of a 292 km 400 kV Transmission line from Iringa to Mbeya together with associated substation.

    Dar es Salaam Morogoro-Dodoma 400 kV Transmission Line

    The project will involve construction of a 451km 400kV Transmission line from Dar es Salaam to Dodoma via Morogoro together with upgrading the 400/220kv Substation at Morogoro.

  • 20 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIAMINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIAMINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

    TANZANIA: SUSTAINABLE MANAGEMENT OF MINERAL RESOURCES PROJECT [SMMRP] [IDA

    CREDIT No.: 45840]INVITATION FOR BIDS FOR THE PROCUREMENT

    OF PORTABLE XRF FOR ELEMENT DETECTION FOR ZONAL MINES OFFICES

    [IFB No.: ME/008/SMMRP/G/83]

    Date: 25th February, 2016

    1. The United Republ