48
Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Taasisi ya Elimu Tanzania Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 1 25/04/2019 12:13

Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

  • Upload
    others

  • View
    77

  • Download
    4

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

i

Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II

Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini

Taasisi ya Elimu Tanzania

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 1 25/04/2019 12:13

Page 2: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

ii

© Taasisi ya Elimu Tanzania, 2018

Toleo la Kwanza, 2018

ISBN: 978 - 9976 - 61 - 803 - 7

Taasisi ya Elimu TanzaniaS.L.P. 35094Dar es Salaam

Simu: +255 22 2773005 / +255 22 277 1358Faksi: +255 22 2774420Baruapepe: [email protected]: www.tie.go.tz

Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kutafsiri, kupiga chapa, kurudufu au kutoa andiko hili kwa namna yoyote ile bila idhini ya maandishi ya Taasisi ya Elimu Tanzania.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 2 25/04/2019 12:13

Page 3: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

iii

Yaliyomo

Ukurasa

Utangulizi ............................................................................................. iv

Shukurani............................................................................................. ix

Vifupisho............................................................................................... x

Sura ya KwanzaLugha ya mazungumzo ........................................................................... 1

Sura ya PiliUtambuzi wa sauti .................................................................................. 8

Sura ya TatuUtambuzi wa sauti za herufi ................................................................... 13

Sura ya NneKusoma kwa ufasaha .............................................................................. 23

Sura ya TanoKusoma kwa ufahamu ............................................................................. 29

Faharasa ................................................................................................. 36

Marejeleo ............................................................................................... 37

Kiambatisho .......................................................................................... 38

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 3 25/04/2019 12:13

Page 4: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

iv

Utangulizi

UsuliMafunzo kazini kwa walimu ni muhimu katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji. Mafunzo haya humwezesha mwalimu kujenga umahiri wa kutekeleza mtaala wa darasa la I na II kwa ufanisi.

Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha stadi ya kusoma. Aidha, utajifunza namna ya kumwezesha mwanafunzi kukuza lugha ya mazungumzo katika mawasiliano, kubainisha sauti mbalimbali katika mazingira, kutambua sauti za herufi, kusoma kwa ufasaha, kusoma kwa ufahamu na kusikiliza. Hivyo, itakuongezea maarifa katika kufundisha stadi ya kusoma.

Lengo la moduliLengo la moduli hii ni kukuwezesha kujenga umahiri wa kufundisha stadi ya kusoma kwa ufanisi kwa wanafunzi wa darasa la I na II.

Walengwa Walengwa wa moduli hii ni walimu wanaofundisha darasa la I na II. Moduli hii inaweza kutumiwa pia na walimu wakuu, maafisa elimu kata, wathibiti ubora wa shule na wadau wengine wa elimu.

Jinsi ya kutumia moduliUnatakiwa kusoma moduli hii na kufanya shughuli mbalimbali zilizoainishwa. Utashirikiana na wenzako kama itakavyokuwa imeelekezwa. Aidha, unatakiwa kuwashirikisha wenzako juu ya changamoto mbalimbali ulizokumbana nazo katika ufundishaji na ujifunzaji ili kujadiliana kwa pamoja namna ya kuzitatua. Pia mwalimu katika ufundishaji wako zingatia watoto wenye mahitaji maalum.

Muundo wa moduliModuli hii imegawanyika katika sura tano ambazo ni: lugha ya mazungumzo, utambuzi wa sauti, utambuzi wa sauti za herufi, kusoma kwa ufasaha na kusoma kwa ufahamu. Kila sura ina utangulizi, umahiri wa kujifunza na jaribio la awali ambapo utajipima uelewa wako kabla ya kuanza kusoma sura husika. Vilevile, yapo maudhui utakayojifunza katika sura inayohusika, kazi za kufanya, tafakuri na jaribio baada ya kujifunza ambalo utalifanya ili kupima ulichojifunza. Mwishoni

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 4 25/04/2019 12:13

Page 5: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

v

mwa moduli kuna shughuli mbalimbali utakazozifanya zilizopo katika Jumuiya za Ujifunzaji.

Utaratibu wa utoaji mafunzoMuda wa mafunzo haya ni mwaka mmoja. Mwalimu unatakiwa kukamilisha moduli zote tano ambazo ni: moduli ya kufundisha kuhesabu, kuandika, kusoma, masuala mtambuko na utekelezaji wa mtaala wa darasa la I na II.

Utakabidhiwa moduli zote na utajifunza mwenyewe katika kituo chako cha kazi. Unapaswa kusoma na kufanya shughuli zote zilizoainishwa katika kila moduli. Mwalimu unatakiwa kujipangia utaratibu kwa kuzisoma moduli hizo kwa ukamilifu na kwa muda uliopangwa. Sambamba na hilo, kutakuwa na jumuiya za ujifunzaji katika ngazi ya shule na vituo vya walimu vya ujifunzaji ndani ya kata ambapo utakutana na walimu wengine kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, mafanikio na changamoto mlizokutana nazo katika ujifunzaji. Ujifunzaji katika jumuiya utaongozwa na shughuli zilizoainishwa mwishoni mwa kila moduli.

Katika kuhakikisha kwamba mafunzo haya yanafanyika kwa ufanisi, mnapaswa kukutana angalau mara moja kwa wiki katika ngazi ya shule; mara moja kwa mwezi katika vikundi vya walimu vya ujifunzaji ndani ya kata na mara mbili kwa mwaka katika vituo vya walimu vya ujifunzaji ngazi ya kata. Kabla hujajifunza maudhui katika kila sura, unapaswa kufanya jaribio ambalo linaakisi maudhui ya sura husika. Baada ya kujifunza maudhui ya sura hiyo utafanya jaribio ili kupima uelewa wako baada ya kusoma sura husika ya moduli. Vilevile, utapewa kazimradi za kufanya ambazo zitajumuishwa katika upimaji utakaofanyiwa.

Upimaji wa mafunzoUpimaji wa mafunzo utafanyika ili kubaini kama umejenga umahiri uliokusudiwa. Upimaji utahusisha mambo yafuatayo:

i. Mkoba wa kazi ambao utajumuisha kazi za vikundi, zana za kufundishia na kujifunzia, machapisho mbalimbali uliyotumia katika kujifunza na majibu ya shughuli mbalimbali ambazo umezifanya katika moduli husika

ii. Kazimradi itakayohusisha zana zinazogusa umahiri husika uliopo katika Mtaala na Muhtasari wa darasa la I na II ambazo zitahakikiwa mwisho wa mafunzo

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 5 25/04/2019 12:13

Page 6: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

vi

iii. Uangalizi wa ufundishaji ndani na nje ya darasa utafanyika mara tatu kwa muda wote wa mafunzo. Uangalizi huu utafanywa na Mwalimu Mkuu, Afisa Elimu Kata na Mthibiti Ubora wa Shule. Zana itayotumika katika uangalizi itatoka kwenye kiongozi cha mthibiti ubora wa shule

Upimaji wa mafunzo utafanywa na walimu wakuu katika ngazi ya shule na maafisa elimu kata katika ngazi ya kata. Aidha, wathibiti ubora wa shule na maafisa elimu ngazi ya wilaya watasimamia zoezi zima la ujifunzaji na upimaji ili kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa yana ubora uliokusudiwa.

Unapaswa kufaulu kwa kiwango kisichopungua alama C ili kuweza kutunukiwa cheti cha kukutambua kama mwalimu wa darasa la I na II uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali la 1 na 2:

Jedwali la 1: Mwongozo wa upimajiMkoba wa kazi Kazi mradi Uangalizi wa ufundishaji Jumla

20 20 60 100

Jedwali la 2: Viwango vya ufauluAlama Daraja Kiashirio

75 – 100 A Bora64 – 74 B Vizuri sana44 – 63 C Vizuri35 – 43 D Inaridhisha0 – 34 F Dhaifu

Ufuatiliaji na tathmini ya mafunzo Kwa kuwa mafunzo yatafanyika katika ngazi ya shule, na vituo vya ujifunzaji ndani ya kata. Walimu wakuu, maafisa elimu kata, wathibiti ubora wa shule na maafisa elimu wa wilaya ndiyo watakaokuwa wafuatiliaji wakuu wa mafunzo haya. Kutakuwa pia na ufuatiliaji katika ngazi ya taifa ikijumuisha Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia (WyEST) kitengo cha elimu ya ualimu na idara ya usimamizi wa elimu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 6 25/04/2019 12:13

Page 7: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

vii

(OR-TAMISEMI). Tathmini ya utekelezaji wa Programu ya Mafunzo kazini kwa walimu wa darasa la I na II itafanyika baada ya kumaliza mafunzo. Lengo la tathmini hii ni kuona kama mafunzo yametekelezwa kama yalivyopangwa na kubaini changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji kwa ajili ya kuboresha. Tathmini hii itahusisha wadau mbalimbali kuanzia ngazi ya shule hadi taifa. Zana za kufanyia tathmini zitaandaliwa na TET kwa kushirikisha wadau wanaohusika. Baada ya tathmini kukamilika, maboresho yatafanyika katika maeneo yanayohusika na mafunzo yataendelea. Tathmini zitafanyika pale inapobidi kulingana na mahitaji.

Tafsiri ya alama Katika moduli hii kuna alama mbalimbali zinazokuwezesha kutambua shughuli zinazotakiwa kufanyika wakati wa usomaji.

Alama Maelezo

Lengo au malengo yanayopaswa kufikiwa na msomaji wa programu hii katika sura

Zingatia vidokezo au wazo muhimu na kulikumbuka

Maswali ya kujiuliza kabla au hata wakati wa kuendelea kusoma

Muhtasari uliotolewa kuhusu sura inayohusika

Marejeleo yaliyotumika ambayo yanapendekezwa uyasome ili kuelewa zaidi

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 7 25/04/2019 12:13

Page 8: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

viii

Alama Maelezo

Tafakuri ambayo utaifanya katika sura inayohusika. Aidha, maswali hayo unaweza kuwashirikisha wenzako kwa majadiliano zaidi

Kazi ya kufanya

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 8 25/04/2019 12:13

Page 9: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

ix

Shukurani

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inatambua na kuthamini mchango muhimu wa washiriki waliofanikisha uandishi wa moduli hii ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II.

TET inatoa shukurani za dhati kwa mchango uliotolewa na wataalamu wafuatao walioshiriki kutayarisha moduli hii:

Waandishi: Anna Godwin, Zaina Kobelwa, Josephat Luoga, Wilhelmi Galishi, na Virigirio Bangi

Wahariri: Dkt. Richard Shukia na Mussa R. Kaoneka

Msanifu: Rehema H. Maganga

Wachoraji: Alama Art and Media Production

Mratibu: Monica W. Manyanga

Aidha, TET inatoa shukurani za pekee kwa Shirikia la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ‘UNICEF’ kwa kufadhili uandishi na ujaribishaji wa moduli hii.

Mwisho, TET inatoa shukurani kwa Global Partnership for Education (GPE) chini ya mpango wa kuboresha ufundishaji wa stadi ya kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) unaojulikana kama Literacy and Numeracy Education Support (LANES) kwa kufadhili uhakiki na uchapaji wa moduli hii.

....................................Dkt. Aneth A. Komba Mkurugenzi MkuuTaasisi ya Elimu Tanzania

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 9 25/04/2019 12:13

Page 10: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

x

Vifupisho

GPE Global Partnership for Education

KKK Kusoma, Kuandika na Kuhesabu

LANES Literacy and Numeracy Education Support

OR-TAMISEMI Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

TET Taasisi ya Elimu Tanzania

UNICEF United Nations Chidren's Fund

WyEST Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 10 25/04/2019 12:13

Page 11: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

1

Sura ya Kwanza

Lugha ya mazungumzo

Lugha ya mazungumzo ni lugha inayotumika katika mawasiliano kwa kutumia mdomo. Lugha rasmi ya mawasiliano nchini Tanzania ni Kiswahili. Mawasiliano hayo hutegemea aina ya wahusika, mazingira, umri na maudhui ya mazungumzo baina ya wazungumzaji. Hivyo, lugha ya mazungumzo inahitaji umahiri katika kusikiliza ili mtu aweze kuelewa. Lugha ya mazungumzo ni moja kati ya stadi za awali itakayomsaidia mwanafunzi kuanza kujifunza kusoma. Mwanafunzi akifundishwa namna nzuri ya kufanya mazungumzo kwa kutumia mbinu mbalimbali atakuwa na uwezo wa kusikiliza na kuzungumza kwa ufasaha.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii utajenga umahiri katika: i. kusalimiana na kuagana vizuri

ii. kujitambulisha na kutambulisha wengine

iii. kutumia lugha ya heshima katika mazungumzo

iv. kutumia lugha katika kuomba ruhusa na kuomba vitu

v. kusimulia habari yoyote ikiwemo hadithi na matukio mbalimbali

Jaribio kabla ya kujifunza

Jaribio hili linalenga kupima uelewa ulionao kabla ya kujifunza maudhui ya sura hii. Fanya jaribio hili kabla ya kuanza kujifunza.

1. Nini maana ya lugha ya mazungumzo?

2. Ni kwa namna gani utakuza lugha ya mazungumzo kwa mwanafunzi aliyeathiriwa na lugha mama?

3. Andaa wimbo utakaowafundisha wanafunzi namna ya kuagana wanapotoka shuleni.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 1 25/04/2019 12:13

Page 12: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

2

1.1 Kusalimiana na kuagana

Kusalimia ni mazungumzo yenye maudhui ya kujuliana hali. Pia, ni utamaduni unaoonesha heshima katika rika zote na nyakati mbalimbali. Baadhi ya maneno yanayotumika katika salamu ni kama vile shikamoo, marahaba, habari, hujambo, habari ya asubuhi, na habari ya jioni. Vilevile, wanafunzi wafundishwe kuwa katika kusalimiana kuna matendo yanatumika kama vile kushikana mikono. Kusalimiana kwa kushikana mikono hutegemea mila, desturi na jinsi ya watu kulingana na mazingira.

Kuagana ni kipengele kimojawapo cha stadi ya kuzungumza ambacho mwanafunzi anatakiwa ajifunze na kujua namna ya kukitumia katika kuagana kwa nyakati tofauti. Baadhi ya maneno yanayotumika katika kuagana ni kama vile kwaheri, usiku mwema, tutaonana kesho au baadaye. Vilevile, wanafunzi wafundishwe kuwa katika kuagana kuna matendo yanayotumika kama vile kupungiana mikono.

Unafikiri kuna tofauti kati ya kusalimiana na kuagana?

Katika maisha yetu ya kila siku, matendo ya kusalimiana na kuagana yanajitokeza katika lugha tunayoitumia kwa kuzingatia nyakati, rika, mazingira na tamaduni mbalimbali. Hivyo, kusalimiana na kuagana ni sehemu muhimu ya mawasiliano.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 2 25/04/2019 12:13

Page 13: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

3

Kielelezo namba 1: Bibi akisalimiana na mjukuu

Katika kukuza stadi ya kuzungumza kwa mwanafunzi wa darasa la I na II unaweza kutumia mbinu mbalimbali ili kumwezesha mwanafunzi kuelezea shughuli za kila siku, kujadili picha, kujibizana, kusimulia hadithi na kuigiza. Katika kufanya hayo yote kumbuka kumsaidia mwanafunzi kutamka matamshi kwa usahihi huku akizingatia lafudhi, kiimbo, kasi stahiki, upatanisho wa kisarufi, msamiati sahihi kwa kila umahiri na kuwa na mtiririko mzuri wa matukio.

Waongoze wanafunzi kuandaa igizodhima kuonesha jinsi ya kuwasalimia watu wazima na wanafunzi wenzake kwa nyakati tofautitofauti. Chunguza na kisha uandike taarifa fupi kuhusu lugha iliyotumika katika salamu hizo.

Ni vizuri kumpatia mwanafunzi shughuli zinazohusu kusalimiana na kuagana kwa kuzirudiarudia. Hii itamwezesha mwanafunzi kuendelea kujenga umahiri katika stadi ya mazungumzo ambapo kwa ujumla itamsaida kuitumia lugha kwa ufasaha.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 3 25/04/2019 12:13

Page 14: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

4

1.2 Kujitambulisha na kutambulisha wengine

Unafikiri ni njia gani nzuri inayoweza kutumiwa na wanafunzi kujitambulisha na kutambulisha wengine?

Hebu fikiria wimbo mzuri utakaowawezesha wanafunzi wako kujitambulisha na kutambulisha wengine. Pia, unaweza kutumia mbinu ya kuwaambia wanafunzi waulizane majina yao na mahali wanapoishi.

Kuna namna mbalimbali za kujitambulisha na kutambulisha wengine zinazotumika katika shughuli kama vile mikutano, warsha na semina darasani au nje ya darasa. Katika kuwafundisha wanafunzi kujitambulisha na kutambulisha wengine unaweza kutumia nyimbo, maigizo na michezo au kwa kuzungumza wao kwa wao.

Utambulisho ni dhana pana iliyobeba mambo mengi ndani yake. Mambo hayo ni kama vile utamaduni, mila, desturi, lugha, historia ya jamii, mavazi, chakula, siasa, imani na uchumi. Kwa hiyo, utambulisho unaweza kutumika kuwabainisha wazungumzaji fulani kuwa wanatoka jamii moja au jamii tofauti.

Pamoja na upana wa dhana hii unapaswa kujua kuwa mwanafunzi wa darasa la I na II anapaswa kujua kujitambulisha na kuwatambulisha watu wengine. Baadhi ya vipengele ambavyo ni muhimu sana kutolewa maelekezo kwa umri na mazingira yao ni jina lake, jina la mzazi au mlezi wake, majina ya marafiki zake, umri wake na mahali anapoishi. Kujitambulisha na kuwatambulisha watu wengine husaidia kufahamiana. Kwa ujumla, uwezo wa mwanafunzi kujitambulisha na kutambulisha watu wengine ni kiashirio muhimu cha kuonesha jinsi mwanafunzi alivyokuza stadi ya kuzungumza katika kuwasiliana.

Ni changamoto gani unazoweza kukutana nazo katika ufundishaji wa kujitambulisha na kuwatambulisha wengine? Unawezaje kuzitatua?

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 4 25/04/2019 12:13

Page 15: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

5

1.3 Kutumia lugha ya heshima katika mazungumzo

Lugha ya heshima na yenye staha inasisitizwa kutumiwa na rika zote katika mazungumzo ili kujenga nidhamu ya matumizi ya lugha yetu. Lugha ya heshima ni moja ya maadili tunayopaswa kumjengea mwanafunzi wa kitanzania. Hivyo, kutumia lugha ya heshima ni moja kati ya vipengele muhimu katika kujifunza stadi ya mazungumzo.

Bila shaka umewahi kuwa katika mazingira ambapo watu wawili walianza kuzungumza na baadaye wakaishia katika ugomvi. Je, unadhani ni lugha gani iliyotumika na kusababisha hali hiyo?

Kila mtindo wa lugha una matumizi yake kulingana na muktadha na maudhui yanayohusika. Kumbuka kwamba lugha ya heshima katika mazungumzo huleta amani na maelewano baina ya wazungumzaji. Hivyo basi, lugha ya heshima inapaswa kutumika katika mazungumzo kati ya mtu na mtu ili kuonesha staha na thamani ya mtu.

1. Elezea umuhimu wa kutumia lugha ya heshima katika mazungumzo mahali popote.

2. Taja na kuelezea mbinu tatu utakazotumia kufundisha lugha ya heshima katika mazungumzo.

1.4 Kutumia lugha katika kuomba ruhusa na kuomba vitu

Katika kutumia lugha ya mazungumzo huwezi kukwepa kuzungumzia lugha inayotakiwa kutumika katika kuomba ruhusa au kuomba kitu chochote kwa mtu. Kuomba ruhusa au kitu ni moja ya utaratibu katika matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa kutumia maneno. Kwa mfano, katika mazingira ya shuleni, ndani ya darasa mwanafunzi anaweza kuomba ruhusa ya kutoka nje. Katika mazingira ya nyumbani mwanafunzi anapotaka kuchukua kitu ni vizuri akaomba kwa mfano: "mama, naomba chungwa" au "dada naomba kwenda kucheza na rafiki yangu wa nyumba ya jirani".

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 5 25/04/2019 12:13

Page 16: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

6

1.5 Kusimulia habari, hadithi na matukio mbalimbali

Bila shaka uliwahi kusimulia hadithi au habari yoyote inayohusu jambo ambalo ulilipata kutoka katika vyanzo mbalimbali kama vile; redio, magazeti na runinga. Hadithi ni masimulizi yenye mfuatano wa matukio ambayo yanaweza kuwa ya kubuni au ya kweli yanayoweza kufurahisha au kuhuzunisha. Malengo ya hadithi hutegemea hadhira, dhima na mafunzo yanayotarajiwa. Mbali na kusimulia matukio kwa njia ya hadithi unaweza kutumia nyimbo, majigambo, ngonjera na mbinu nyingine nyingi.

Unapomwambia mwanafunzi asimulie tukio lolote unamjengea stadi gani ya lugha?

Mwanafunzi akiwa na uwezo wa kusimulia tukio lolote au hadithi na kuelezea kwa maneno yake mwenyewe inaashiria kwamba ana stadi ya kuzungumza.

Chagua hadithi fupi kwenye kitabu cha kusoma, kisha wasomee wanafunzi, baada ya hapo waambie wasimulie hadithi hiyo wao wenyewe.

Nafikiri umewasikiliza wanafunzi wako wakiwa wanasimulia hadithi hiyo na jinsi walivyoielewa kwa maneno yao wenyewe. Je, umekutana na changamoto zipi zitakazokufanya urudie kuisimulia hadithi hiyo ili warudie tena kusimulia na kukuza lugha ya mazungumzo?

Kumfundisha mwanafunzi lugha ya mazungumzo humsaidia kuwasiliana na wenzake na jamii yake. Lugha ya mazungumzo inatakiwa kukuzwa si kwa wanafunzi tu bali kwa mtu mwingine yeyote. Watu wengi wanashindwa kutoa mawazo na michango yao katika jamii kutokana na tatizo la kukosa umahiri wa lugha ya mazungumzo.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 6 25/04/2019 12:13

Page 17: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

7

1. Unafundisha darasa lenye wanafunzi 45 (arobaini na tano), wanafunzi watatu kati yao wanazungumza lugha mama (lugha ya kwanza au ya kabila lao) na wanafunzi wawili kati yao wanashindwa kutamka baadhi ya maneno ya Kiswahili. Utatumia mbinu gani za kufundishia na kujifunzia ili kuwawezesha kukuza lugha ya mazungumzo?

2. Unafikiri kusalimiana, kuagana, kujitambulisha na kutambulisha watu wengine, kutumia lugha ya heshima na kusimulia hadithi kutafanikisha kukuza lugha ya mazungumzo? Kwa vipi?

3. Pendekeza njia nyingine zinazoweza kutumika katika kukuza lugha ya mazungumzo.

Hongera kwa kumaliza kujifunza sura ya lugha ya mazungumzo ambapo umeweza kujenga umahiri katika stadi ya lugha ya mazungumzo, kusalimiana na kuagana, kujitambulisha na kutambulisha wengine. Pia tumejadili kutumia lugha ya heshima katika mazungumzo, Kutumia lugha katika kuomba ruhusa na kuomba vitu. Vilevile, tumejifunza kusimulia habari, hadithi na matukio mbalimbali. Hivyo katika kuendelea kujenga umahiri wa lugha ya mazungumzo unapaswa kumshirikisha mwanafunzi katika shughuli mbalimbali wakati wa kufundisha. Hii ni kwa sababu mwanafunzi anapopata nafasi ya kufanya mazoezi mengi ya kuzungumza huelewa haraka na kwa urahisi.

Jaribio baada ya kujifunzaJaribio hili linalenga kupima umahiri ulioupata baada ya kujifunza maudhui ya sura hii. Ni muhimu kufanya jaribio hili.

1. Nini maana ya lugha ya mazungumzo?2. Ni kwa namna gani utakuza lugha ya mazungumzo kwa mwanafunzi

aliyeathiriwa na lugha mama?

3. Andaa wimbo utakaowafundisha wanafunzi namna ya kuagana wanapotoka shuleni.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 7 25/04/2019 12:13

Page 18: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

8

Sura ya Pili

Utambuzi wa sauti

Karibu tena katika sura ya pili ambayo itakuwezesha kutambua na kubainisha sauti mbalimbali zinazotolewa na viungo mbalimbali vya binadamu zikiwamo sauti za lugha. Pia, utaweza kujifunza kusikiliza na kuzibainisha sauti za ndege, wanyama na vitu mbalimbali kutoka katika mazingira yanayokuzunguka.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii utajenga umahiri katika:i. kubaini sauti mbalimbali zinazotolewa na wanyama na ndege

ii. kubaini sauti zinazotolewa na viungo vya mwili wa binadamu

iii. kuigiza sauti mbalimbali kulingana na picha na vitu vinavyotoa sauti

Jaribio kabla ya kujifunza

Jaribio hili linalenga kupima uelewa ulionao kabla ya kujifunza maudhui ya sura hii. Fanya jaribio hili kabla ya kuanza kujifunza.

1. Eleza njia tatu ambazo utazitumia ili kuwasaidia wanafunzi kutamka sauti

za herufi.

2. Fafanua zana tatu za ufundishaji na ujifunzaji utakazozitumia wakati wa

kufundisha sauti za herufi.

3. Taja mbinu tatu unazoweza kuzitumia katika kuwaongoza wanafunzi kutenganisha sauti za wanyama na ndege.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 8 25/04/2019 12:13

Page 19: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

9

2.1 Kubaini sauti mbalimbali zinazotolewa na wanyama na ndege

Wanyama na ndege ni viumbe hai. Wote wana sifa zinazowafanya waitwe viumbe hai. Baadhi ya viumbe hai hutoa sauti ambazo hutumika katika mawasiliano yao sambamba na mifumo mingine ya mawasiliano.

Je, unaweza kuigiza sauti tofautitofauti za wanyama na ndege unaowafahamu? Igiza sauti hizo.

Bila shaka unaweza kuigiza na kutofautisha sauti hizo. Kwa mfano, unaweza kutofautisha sauti ya ng’ombe, mbuzi na ndege kama vile kuku, bata, njiwa na wengine wengi. Mwalimu, unapokuwa darasani unaweza kuwaambia wanafunzi waigize sauti za wanyama na ndege walizowahi kuzisikia. Aidha, kwa kutumia majina ya wanyama, ndege na vitu mbalimbali utaweza kumsaida mwanafunzi kubaini na kutamka sauti za mwanzo na za mwisho katika majina hayo. Kwa kusikiliza na kuzibainisha sauti zinazosikika katika mazingira yanayomzunguka mwanafunzi kutamwezesha kufanya mazoezi ya kutamka sauti za herufi bila shida.

1. Andika majina ya wanyama walioko katika mazingira yako katika kadi na kisha waongoze wanafunzi kutamka majina ya wanyama hao na kuigiza sauti zao.

2. Bainisha sauti ambazo zimewashinda wanafunzi kutamka kwa usahihi na kwa sauti kisha chunguza kwa nini wameshindwa kuzitamka. Buni mbinu ya kuwasaidia.

3. Andika changamoto ulizokutana nazo wakati wa kutamka na kuigiza sauti za wanyama hao.

Kabla ya kuanza kufundisha kutamka sauti za herufi ni muhimu kurejea katika mazingira yanayokuzunguka ili kusikiliza na kubainisha sauti za wanyama, ndege na wanadamu ili kuandaa na kuzifanyia mazoezi ala za sauti hizo.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 9 25/04/2019 12:13

Page 20: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

10

2.2 Kubaini sauti zinazotolewa na viungo vya mwili wa binadamu

Bila shaka unatambua kuwa kuna viungo vya mwili wa binadamu ambavyo vinatumika kutolea sauti. Je, unaweza kuvitaja viungo hivyo? Kwa kutumia vitendo utabaini kuwa viungo hivyo vinatoa sauti tofauti tofauti. Kwa mfano, kupiga makofi kunatoa sauti zinazosikika tofauti na sauti zinazotokana na kupiga mbinja au kuchapa miguu chini. Pia, kutumia ulimi na midomo kunatoa sauti tofauti na sauti zinazotolewa na viungo vingine.

Taja viungo vya mwili wa binadamu vinavyoweza kutoa sauti kisha waongoze wanafunzi kutumia viungo hivyo kutoa sauti.

Katika kufundisha utambuzi wa sauti ni vema kutumia zana na mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kumjengea mwanafunzi umahiri katika kutambua na kutamka sauti za herufi. Zana hizo zinaweza kuwa filimbi, ngoma, vuvuzela na zeze zinazowezesha kufikia umahiri wa kusikiliza na kubainisha sauti kwa urahisi.

2.3 Kuigiza sauti mbalimbali kulingana na picha za vitu vinavyotoa sauti

Katika mazingira yetu tumezungukwa na vitu mbalimbali vilivyo na uhai na visivyo na uhai. Vilevile, tunaweza kuona picha za vitu hivyo.

Je, unafahamu kuwa baadhi ya vitu hivyo hutoa sauti?

Vitu mbalimbali hutoa sauti ikiwa vitagongwa, kuguswa, kuangushwa, kusuguliwa, kupulizwa, kusukumwa, kuvutwa au kuinuliwa. Kwa kutumia picha unaweza kuigiza sauti au kufanya vitendo vitakavyoonesha kuwa wanyama na vitu hutoa sauti. Kwa mfano, unaweza kutumia picha ya pembe ya mnyama kuigiza sauti kwa kupuliza au kuwa na picha ya mbuzi na kuigiza sauti ya mbuzi na kadhalika.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 10 25/04/2019 12:13

Page 21: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

11

Hata hivyo, unaweza kutumia vitu halisi kama vile kijiko na chupa ya kioo na kuvigonganisha taratibu kiasi cha kutoa sauti. Hii itakusaidia katika kuwawezesha wanafunzi kutambua kuwa tunaweza kutengeneza na kubaini sauti za vitu mabalimbali pale tunapoviona vikiwa halisi au kuona picha zake. Pia, utaweza kuwasaidia wanafunzi waigize sauti mbalimbali kutokana na vitu vinavyowazunguka.

1. Tengeneza vikaragosi vya wanyama kwa kutumia makunzi mbalimbali yanayopatikana katika mazingira na kuwaonesha wanafunzi ili waigize sauti zao.

2. Tengeneza vifani vya ndege kama kuku, bata, njiwa, mbuni na kunguru kwa kukata maboksi magumu ili kupata maumbo ya ndege hao kisha wanafunzi waigize sauti zao.

Kumbuka kwamba kwa kutumia zana utamjengea mwanafunzi dhana ya mnyama au kitu husika, kumbukumbu ya kudumu na kumfanya ashiriki kikamilifu katika ujifunzaji. Hivyo, zitamrahisishia kupata umahiri katika stadi za awali za utambuzi wa sauti za herufi.Mwalimu, yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia wakati unafundisha sura hii ya utambuzi wa sauti:

i. Anza kufundisha sauti za wanyama, ndege na vitu mbalimbali wanavyovifahamu wanafunzi. Kwa mfano sauti za mbuzi, ng’ombe, paka, kuku na bata

ii. Kuwasisitiza wanafunzi kuwa makini kusikiliza sauti za vitu na viumbe vinavyowazunguka kwani ufundishaji wa sauti unaendana na kusikiliza. Mwanafunzi mwenye mahitaji maalumu ya kielimu ahudumiwe sawasawa na mahitaji yake

iii. Mazoezi mengi ya kusikiliza na kutamka sauti za maneno ndiyo njia bora ya kufundisha utambuzi wa sauti

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 11 25/04/2019 12:13

Page 22: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

12

Jadili na mwenzako ni kwa namna gani unaweza kufundisha ubainishaji wa sauti mbalimbali katika mazingira.

Hongera kwa kumaliza sura ya utambuzi wa sauti. Katika sura hii umejifunza namna ya kubaini sauti za wanyama, ndege, sauti zinazotolewa na viungo vya mwili wa binadamu na vifaa vingine vinavyotoa sauti. Vilevile, umejifunza kuigiza sauti mbalimbali kulingana na picha za vitu vinavyotoa sauti kwa kutamka sauti za mwanzo na za mwisho .

Jaribio baada ya kujifunza

Jaribio hili linalenga kupima umahiri ulioupata baada ya kujifunza maudhui ya sura hii. Ni muhimu kufanya jaribio hili.

1. Eleza njia tatu ambazo utazitumia kuwasaidia wanafunzi kutamka sauti

za herufi.

2. Fafanua zana tatu za ufundishaji na ujifunzaji utakazozitumia wakati wa

kufundisha sauti za herufi.

3. Taja mbinu tatu unazoweza kuzitumia katika kuwaongoza wanafunzi kutenganisha sauti za wanyama na ndege.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 12 25/04/2019 12:13

Page 23: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

13

Sura ya Tatu

Utambuzi wa sauti za herufi

Karibu katika sura hii inayohusu utambuzi wa sauti za herufi ambayo inalenga kukujengea uwezo wa kumwezesha mwanafunzi kutambua na kubaini sauti za herufi katika lugha.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii utajenga umahiri katika: i. kufafanua dhana ya sauti za herufiii. kumwezesha mwanafunzi kubainisha sauti za herufi za irabu na

konsonantiiii. kumwezesha mwanafunzi kuhusianisha sauti na herufi za irabu na

konsonantiiv. kumwezesha mwanafunzi kuunganisha na kutamka sauti za irabu

na konsonanti ili kuunda silabiv. kumwezesha mwanafunzi kuunganisha silabi kuunda nenovi. kumwezesha mwanafunzi kuunganisha na kutenganisha maneno

katika sentensi

Jaribio kabla ya kujifunza

Jaribio hili linalenga kupima uelewa ulionao kabla ya kujifunza maudhui ya sura hii. Fanya jaribio hili kabla ya kuanza kujifunza.

1. Taja ala tatu za sauti.2. Andaa maneno kumi yenye silabi mwambatano ili kuunda sentensi tano

kwa ufasaha.3. Bainisha mbinu utakazozitumia kumsaidia mwanafunzi kutamka sauti za

herufi kwa urahisi.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 13 25/04/2019 12:13

Page 24: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

14

3.1 Dhana ya sauti za herufi

Sauti za herufi ni vitamkwa vinavyotokana na ala za sauti katika mfumo wa hewa kutoka mapafuni kuelekea nje kupitia chemba ya kinywa na pua.

Ala za sauti na mahali pa kutamkia

1. Midomo 2. Meno3. Ufizi 4. Kaakaa gumu5. Kaakaa laini6. Uvula (kidaka tonge)7. Ncha ya ulimi8. Pembe ya ulimi9. Sehemu ya mbele ya ulimi10. Sehemu ya nyuma ya ulimi11. Shina la ulimi12. Koromeo13. Glota.

Mahali pa kutamkia:1. Midomo: hutoa sauti (p, b, m, w). Mfano wa maneno ni pipa, beba, mimi na

wewe.2. Midomo meno: hutoa sauti (f, v). Mfano wa maneno ni fua, vua, na vaa.3. Meno: hutoa sauti (th, dh). Mfano wa maneno ni thamani, na dhahabu.4. Ufizi: hutoa sauti (t, d, n, l, r, s, z). Mfano wa maneno ni tua, dua, nuna, sasa,

na zana.5. Kaakaa gumu: hutoa sauti (j, y, sh, ch, ny). Mfano wa maneno ni jani, yai,

shule, chui, na nyanya.6. Kaakaa laini: hutoa sauti (k, g, gh, ng’). Mfano wa maneno ni kisu, gumu,

ghali, na ng’ombe.7. Glota: hutoa sauti (h). Mfano wa maneno ni huyu, na hewa.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 14 25/04/2019 12:13

Page 25: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

15

Eleza tofauti iliyopo kati ya sauti na jina la herufi kwa kutumia uzoefu wako wa kufundisha.

Herufi ni alama ya maandishi inayowakilisha kitamkwa katika lugha.

Alama ya sauti ni umbo la sauti ya herufi husika katika maandishi.

Silabi ni kifungu cha sauti kinachotamkwa kwa pamoja kama kifungu kimoja cha sauti. Silabi zinaweza kuundwa na irabu peke yake katika maneno kama vile ua ambapo kuna silabi mbili, u na a au kwa kuweka pamoja konsonanti na irabu katika maneno kama vile kaka ambapo kuna silabi ka na ka. 3.2 Kubainisha sauti za herufi

Kubaini sauti za herufi ni jambo la kwanza lakini hufuatiwa na kuhusianisha sauti hiyo na herufi. Kwa hiyo, tunaweza kusema kwamba kila herufi ya Kiswahili ina sauti yake na kufanya itambulike kuwa herufi moja kwa sauti moja. Kila herufi inawakilisha sauti moja na kila sauti huwakilishwa na herufi moja.

Kwa kutamka bainisha sauti za herufi unazozifahamu.

Kuna aina mbili za herufi za Kiswahili. Aina hizo ni konsonanti na irabu. Irabu ni herufi ambazo wakati wa utamkaji wake hakuna kizuizi katika mkondo hewa unaotoka mapafuni kwenda nje. Herufi hizo ni: a, e , i , o na u.Konsonanti ni herufi ambazo wakati wa utamkaji wake kunakuwa na kizuizi katika mkondohewa unaotoka mapafuni kwenda nje kupitia chemba ya kinywa au pua. Mfano wa herufi hizo ni: b, ch, d, f, g, h, j, k, l, m, n, p, r, s, t, v, w, y, na z. Vilevile kuna herufi mwambatano ambazo utamkaji wake ni sawa na sauti za herufi za konsonanti nazo ni ny, mb, sh, th, nch, mbw, ndw.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 15 25/04/2019 12:13

Page 26: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

16

1. Andaa kadi za herufi za konsonanti na irabu. Gawa kadi katika makundi hayo na kisha tamka sauti ya herufi hiyo ili mwanafunzi aoneshe kadi yenye herufi hiyo.

2. Kwa kutumia kadi hizo za herufi onesha kadi ya herufi kwa wanafunzi ili watamke sauti ya herufi hiyo.

3. Andaa kadi, mti wa herufi mwambatano na chati ya herufi mwambatano. Tumia zana hizo ili wanafunzi waweze kubainisha sauti zake.

Weka kazi yako katika mkoba wa kazi

Sisitiza wanafunzi, waangalie mdomo wako wakati unapotamka sauti inayohusika.

3.3 Kuhusianisha sauti na herufi

Baada ya kubaini sauti za herufi sasa tuone namna ya kuhusianisha sauti hizo na herufi husika. Kama ilivyoelezwa hapo awali kila herufi ina sauti yake na katika lugha ya Kiswahili herufi moja huwa na sauti moja.

Sauti b,ch,d, k, l,m, n, p. Hizi ni herufi za aina gani? Sauti ny, mb, sh, nj, nch, fy, nz, mbw, chw, ngw. Hizi ni herufi za aina gani? Sauti a, e, i, o, u. Hizi ni herufi za aina gani?

Bila shaka, umeweza kufikiri na kubaini kwamba ni herufi mwambatano, herufi za konsonanti na herufi za irabu. Herufi mwambatano zinaundwa na herufi mbili au zaidi za konsonanti. Iwapo zitaongezewa irabu mwishoni mwa herufi hizo tunapata silabi mwambatano.

Uhusianishaji wa herufi na sauti mojamoja unamwezesha mwanafunzi kubaini, kuhusianisha na kutamka herufi na kusoma silabi na maneno bila shida. Hivyo basi, zoezi la kuhusianisha herufi mojamoja ni lazima liwekewe msisitizo zaidi wakati wa ujifunzaji wa mwanafunzi.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 16 25/04/2019 12:13

Page 27: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

17

1. Andaa kadi za herufi na gawa kadi hizo kwa wanafunzi ili wahusianishe na herufi zilizomo katika chati.

2. Taja na fafanua mbinu au michezo utakayotumia kumwezesha mwanafunzi kuhusianisha sauti na herufi.

Kumbuka njia na mbinu ulizotumia kuhusianisha sauti na herufi mojamoja ndizo njia utakazotumia kuhusianisha sauti na herufi mwambatano.

Unafikiri kuna umuhimu wa kufundisha uhusiano uliopo kati ya herufi kubwa na ndogo kwa mwanafunzi wa darasa la I na II?. Kwa nini?

Kumbuka kurejea herufi zote za konsonanti na irabu ili kutambulisha herufi kubwa sambamba na kujua matumizi yake. Herufi kubwa huonekana na kutumiwa katika stadi ya kuandika. Katika kufundisha ni muhimu kutumia kadi za herufi ndogo na kubwa na chati ya herufi ndogo na kubwa ili kujenga kumbukumbu ya kudumu kwa mwanafunzi. Herufi kubwa hujitokeza katika maeneo mbalimbali kama vile; mwanzo wa jina la mtu, mahali, vitu, mwanzo wa sentensi na baada ya kituo katika habari au alama ya kushangaa na kuuliza.

Onesha mfano wa kufundisha matumizi ya herufi kubwa kwa kutumia jina la mwanafunzi mmojawapo.

3.4 Kuunganisha na kutenganisha sauti za herufi zinazounda maneno

Kuunganisha na kutenganisha sauti ni mbinu inayomwezesha mwanafunzi kuwa na uwezo wa kutamka na kusoma maneno kwa urahisi zaidi. Unaelewa nini kuhusiana na dhana ya kuunganisha na kutenganisha sauti katika kufundisha uundaji wa maneno?

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 17 25/04/2019 12:13

Page 28: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

18

Kuunganisha sauti: unaweza kuunganisha sauti kupata silabi, neno, sentensi na hata kifungu cha habari. Hivyo basi kuunganisha sauti kunategemea umakini katika kusikiliza mfuatano wa sauti mojamoja na jinsi zinavyotamkwa kisha kuunganishwa ili kuunda neno. Kwa mfano, sauti: /k/+/a/ tunapata silabi ka silabi:/ka/ +/ka/ tunapata neno kaka

Kutenganisha sauti: unaweza kutenganisha sauti kwa kuondoa sauti mojamoja katika neno. Kwa mfano, kutenganisha neno sokoni /s/-/o/-/k/-/o/-/n/-/i/

Kumbuka: njia hizi mbili ndizo zitakazokusaidia kumwezesha mwanafunzi kuwa na uwezo wa kusoma na kutamka maneno. Kwa kutumia mbinu hizi, mwanafunzi atakuwa na uwezo wa kutenga neno katika sauti mojamoja na kuliunganisha na kisha kulitamka kwa urahisi.

1. Andaa maneno matano na kuwaelekeza wanafunzi kutenga na kusoma silabi zinazounda meneno hayo.

2. Andaa chati ya herufi, uwaelekeze wanafunzi kutumia chati hiyo kujenga silabi na kutumia silabi hizo kuunda maneno na kuyasoma kwa sauti.

Pamoja na shughuli uliyoifanya hapo awali, endelea na zoezi hili darasani ili kuimarisha maarifa na kukuza umahiri katika ufundishaji wa kutenganisha na kuunganisha herufi, kuunda maneno na baadaye sentensi.

Hatua ya 1Kwa kutumia kadi andaa maneno kadhaa yanayofahamika kwa wanafunzi, kisha andaa kadi za herufi mojamoja za maneno hayo.

Hatua ya 2Onesha kadi za herufi zinazounda neno ili wanafunzi watamke na kuunganisha sauti hizo.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 18 25/04/2019 12:13

Page 29: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

19

Hatua ya 3Onesha kadi yenye neno zima ili wanafunzi watenge sauti katika neno hilo. Ikiwa kutakuwa na wanafunzi ambao watashindwa kutamka baadhi ya sauti na maneno, orodhesha sauti hizo na kisha fikiria jinsi utakavyowawezesha kuzitamka katika kipindi kijacho.

Njia hii uliyoitumia kutenganisha sauti katika neno na kuunganisha sauti kupata neno ndiyo njia utakayoitumia kutenganisha na kuunganisha silabi katika neno. Kadhalika katika kuunda maneno mengine.

Silabi katika lugha ya Kiswahili zinaundwa katika miundo minne tofauti kama ifuatavyo:

i. Irabu peke yake: Kwa mfano, neno ‘ua’ litakuwa /u/a/ u ni silabi na a ni silabi

ii. Konsonanti na irabu: kwa mfano silabi /ba/ta/ hivyo /ba/ na /ta/ni silabi

iii. Konsonanti mbili na irabu: Kwa mfano, neno ‘mt/u’ /m/tu/ hivyo m ni silabi, m/to/to

iv. Konsonanti tatu na irabu katika kila silabi: kwa mfano nywa,n/g/w/a,nzwi

Ili kufundisha kutenganisha na kuunganisha sauti na silabi katika neno kuna hatua za kufuata ili kujenga umahiri kwa wanafunzi. Njia hizo ni:

i. Andaa kadi za silabi unazotaka kufundisha sauti zake

ii. Gawa kadi hizo kwa wanafunzi kulingana na idadi ya silabi

iii. Waelekeze wanafunzi kuzinyanyua juu ili kila mwanafunzi aweze kuona kwa urahisi

iv. Tamka sauti ya herufi au silabi husika na wanafunzi wakikufuatisha huku zikiinuliwa juu zile zilizotamkwa ili kuunda silabi au neno

v. Baada ya kuziinua kadi zote juu wanafunzi watamke sauti mojamoja kwa mfuatano

vi. Kisha watamke neno zima au silabi nzima kwa sauti

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 19 25/04/2019 12:13

Page 30: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

20

1. Onesha namna utakavyounganisha silabi za herufi mwambatano na silabi za kawaida ili kuunda maneno yenye silabi tatu.

2. Kwa kutumia njia ya kutenga sauti katika neno onesha jinsi utakavyotenganisha silabi mwambatano katika neno.

Kumbuka kuwauliza wanafunzi maswali ya papo kwa papo; mfano silabi ba imeundwa na sauti zipi? Vilevile, hakikisha kwamba katika kila hatua wanafunzi wanaweza kutamka sauti husika ya herufi. Wale ambao wanahitaji msaada wa kiutalaamu wasaidiwe mapema. Wanafunzi wasitumike kama bango la kutundikia kadi bali mwalimu utafute njia nyingine kama vile mti wa maneno au egemeo lenye matawi sawia ili kila mwanafunzi ajifunze kikamilifu.

3.5 Kuunganisha na kutenganisha maneno katika sentensi

Bila shaka unakumbuka dhana hizi mbili za kuunganisha na kutenganisha sauti na silabi katika maudhui yaliyopita.

Unafikiri utenganishaji au uunganishaji uliouona awali unaweza kutumika kutenganisha maneno katika sentensi na kuunganisha maneno ili kupata sentensi? kwa vipi?

Njia hizo utakazozitumia katika kuunganisha maneno na kuunda sentensi ni za msingi katika kukuza stadi ya kusoma kwa ufasaha.

Ni vizuri kuzingatia idadi ya maneno katika sentensi kulingana na ngazi ya darasa na wanafunzi husika kwani kwa darasa la I mwanafunzi hufundishwa sentensi sahili tu ikiwa na maneno yasiyozidi nane. Kwa darasa la juu zaidi, maneno yanazidi kuongezeka katika sentensi kulingana na uwezo wa wanafunzi.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 20 25/04/2019 12:13

Page 31: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

21

Kama ilivyo katika kutenganisha silabi katika neno pia tunaweza kutenganisha maneno katika sentensi. Kumbuka kwamba mbinu na namna ya kutenganisha sauti, silabi, hazitofautiani na kutenganisha maneno katika sentensi.

1. Andaa maneno katika kadi au chati ya sakaneno. Kisha waongoze wanafunzi kusoma na kutumia maneno hayo kuunda sentensi.

2. Andaa kadi za sentensi au chati ya sentensi, kisha ongoza wanafunzi kutenganisha na kuyasoma maneno yaliyounda sentensi hizo.

Wawezeshe wanafunzi kusoma kila neno utakalotumia katika kuunda sentensi na silabi zinazounda maneno hayo. Kadi za herufi, silabi, maneno na sentensi zitumike kumjengea mwanafunzi kumbukumbu ya kudumu na uwezo wa kutambua sauti za herufi katika sentensi nzima.

Onesha kwa mfano namna utakavyotumia zana kama vile kadi za

herufi, chati za herufi, chati ya sakaneno, mti wa herufi, chati ya sentensi na kadi mkunjo kumfundisha mwanafunzi kuunda silabi, neno na sentensi.

Hongera kwa kumaliza sura ya utambuzi wa sauti za herufi. Katika sura hii tumejadili dhana ya sauti za herufi, kubainisha sauti za herufi, kuhusianisha sauti za herufi. Vilevile, tumejifunza kuunganisha na kutenganisha sauti za herufi zinazounda maneno. Mwisho tumejifunza kuunganisha na kutenganisha maneno katika sentensi.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 21 25/04/2019 12:13

Page 32: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

22

Jaribio baada ya kujifunza

Jaribio hili linalenga kupima umahiri ulioupata baada ya kujifunza maudhui ya sura hii. Ni muhimu kufanya jaribio hili.

1. Taja ala tatu za sauti.

2. Andaa maneno kumi yenye silabi mwambatano ili kuunda sentensi tano kwa ufasaha.

3. Bainisha mbinu utakazozitumia kumsaidia mwanafunzi kutamka sauti za herufi kwa urahisi.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 22 25/04/2019 12:13

Page 33: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

23

Sura ya Nne

Kusoma kwa ufasaha

Karibu katika sura ya nne inayohusu kusoma kwa ufasaha. Kusoma kwa ufasaha ni uwezo wa kusoma matini kwa kasi stahiki, hisia, kutumia matamshi na kiimbo sahihi. Umahiri wa kusoma unahusisha mambo kadhaa ya msingi yakiwamo kasi, usahihi na hisia.

Kusoma kwa kasi ni kusoma kwa kiwango kinachotakiwa cha usomaji ambacho si cha kasi sana wala polepole sana. Mwanafunzi anatakiwa kusoma kwa kasi stahiki kwa kuzingatia idadi ya maneno arobaini aliyoyasoma kwa dakika moja.

Kusoma kwa usahihi ni kusoma maneno na kutamka kwa usahihi, kasi stahiki na kwa hisia maneno yote kwa kuzingatia sauti yake (kiimbo) sahihi na maana inayohusika. Hivyo, kuna maneno yanayofanana katika kuandika, isipokuwa yanatofautiana katika matamshi. Mfano neno “barabara”

Kusoma kwa hisia ni hali ya kusoma kwa kuzingatia alama za uandishi zinazo onesha hisia ya msomaji mfano alama ya mshangao (!). Kupanda na kushuka kwa sauti na lafudhi ya lugha katika kutamka maneno.

Kufundisha kusoma kwa ufasaha katika kusoma matini yoyote husaidia kukumbuka ulichokisoma na kupata maana ya kile unachokisoma na kusoma kwa kasi inayotakiwa.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii utajenga umahiri katika:

i. kufafanua dhana ya kusoma

ii. kumwezesha mwanafunzi kusoma kwa ufasaha herufi, silabi, maneno na sentensi kwa kutumia chati na vifungu vya habari

iii. kumwezesha mwanafunzi kusoma hadithi fupi kwa kuzingatia alama za uandishi

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 23 25/04/2019 12:13

Page 34: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

24

Jaribio kabla ya kujifunza

Jaribio hili linalenga kupima uelewa ulionao kabla ya kujifunza maudhui ya sura hii. Fanya jaribio hili kabla ya kuanza kujifunza.1. Eleza maana ya kusoma kwa ufasaha.2. Fafanua mambo matatu ya kuzingatia unaposoma kwa ufasaha.

3. Andika kweli kwa sentensi sahihi na si kweli kwa sentensi isiyo sahihi. i. Mwalimu anatakiwa kufundisha sauti za herufi kabla ya kufundisha

silabi.ii. Silabi ni lazima itokane na konsonanti na irabu tu.

Kusoma kwa ufasaha husaidia kupata ufafanuzi zaidi wa kile kinachosomwa na kujenga kumbukumbu ya kilichosomwa.

4.1 Dhana ya kusoma

Kusoma ni uwezo wa kubaini maumbo ya herufi (maandishi) kwa kutazama au kupapasa na kupata maana iliyokusudiwa na mwandishi.

Kusoma huhusisha vitendo kama vile namna ya kukaa, kupepesa macho, namna ya kushika kitabu au chapisho lolote, kasi stahiki na hisia. Chunguza mwanafunzi wakati anasoma habari kimya au kwa sauti kama anatenda ipasavyo.

Kielelezo namba 1: Mwanafunzi anasoma kitabu

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 24 25/04/2019 12:13

Page 35: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

25

Jambo jingine la muhimu ni kuhakikisha kuwa mwanafunzi anasoma kwa mwendo na kasi stahiki ili aweze kuelewa anachokisoma katika matini.

1. Tengeneza kitabu rahisi cha hadithi ihusuyo chanzo cha asali ya nyuki. Kwa kutumia kitabu hicho wanafunzi wasome ili uone namna wanavyotembeza macho.

2. Andaa habari yenye kuibua hisia kwa msomaji. Kisha wanafunzi wasome ili kupima kasi ya usomaji na wanavyowasilisha hisia zao wakati wanasoma habari hiyo.

Ili mwanafunzi wa darasa la I na II aweze kujifunza vizuri kusoma kwa ufasaha inabidi apewe mazoezi mengi ya kusoma kwa sauti na siyo kimya kwani kwa kufanya hivyo utakuwa unamsaidia kusahihisha matamshi pale anapokosea.

4.2 Kusoma kwa ufasaha herufi, silabi, maneno na sentensi kwa kutumia vifungu vya habari

Kusoma kwa ufasaha ni zao chanya la kusoma sauti za herufi, silabi na maneno kwa ufasaha. Hivyo, ni muhimu kufundisha na kujifunza ili kuwa mahiri zaidi katika kusoma kwa ufasaha. Katika kusoma kwa ufasaha ni muhimu kuzingatia kasi stahiki, usahihi wa matamshi katika kusoma maneno kwa kuzingatia kiimbo na hisia yaani kupanda na kushuka kwa sauti katika usomaji wa habari.

Kwa kutumia kifungu cha habari au hadithi, onesha mfano wa namna ya kusoma kwa ufasaha na kasi stahiki. Kisha waambie wanafunzi wasome kwa ufasaha na kasi stahiki. Unafikiri kwa nini ufasaha unasisitizwa katika kusoma habari?

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 25 25/04/2019 12:13

Page 36: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

26

Ufasaha unasisitizwa katika kusoma habari ili kumjengea mwanafunzi umahiri katika stadi ya kusoma kwa ujumla. Pia, unasisitizwa kumfanya msomaji apate maana ya yale yaliyoandikwa kwani kwa kutosoma kwa ufasaha neno moja kunaweza kupoteza maana ya kile kilichokusudiwa. Mwanafunzi anaposoma kwa kusitasita hushindwa kukumbuka alichosoma baada ya kumaliza kusoma habari husika.

1. Andaa habari/hadithi yenye maudhui ya bustani ya mbogamboga kisha isome kwa wanafunzi kama mfano ili wajifunze namna ya kusoma kwa ufasaha kutoka kwako.

2. Kwa kutumia hadithi au habari hiyo waelekeze wanafunzi waisome kwa ufasaha.

Katika kumsaidia mwanafunzi kujenga umahiri wa kusoma kwa ufasaha ni muhimu kutumia saa ili kuweza kubaini ni maneno mangapi mwanafunzi ameweza kuyasoma kwa ufasaha kwa dakika moja. Mwanafunzi wa darasa la I na II anatakiwa kuwa na uwezo wa kusoma maneno yasiyopungua arobaini kwa dakika moja.

4.3 Kusoma hadithi fupi kwa kuzingatia alama za uandishi

Alama za uandishi ni moja ya vigezo vikubwa katika kusoma na kuandika kwa ufasaha. Hivyo, tunaweza kusema kwamba ikiwa mwandishi hakufuata utaratibu wa uandishi ikiwamo alama za uandishi, na msomaji atasoma bila kuzingatia alama hizo jambo ambalo litaondoa ladha katika usomaji wake.

Unafikiri ni alama zipi za uandishi ambazo mwanafunzi wa darasa la I na II anatakiwa kuzitambua na kuzitumia?

Alama za uandishi ni muhimu sana kwa msomaji ili kujenga hisia na mtiririko unaoeleweka. Kwa wanafunzi wa darasa la I na II ni vema wakatambulishwa na kuelekezwa kutumia alama nne za uandishi ambazo ni nukta (.), mkato (,), alama ya mshangao (!) na alama ya kuuliza (?).

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 26 25/04/2019 12:13

Page 37: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

27

Ili kujenga umahiri katika kusoma kwa ufasaha ni lazima uzingatie alama za uandishi zilizopo katika habari au hadithi husika ikiwa ni pamoja na kupanda na kushuka kwa sauti pale inapotakiwa ili kujenga dhana halisi ya kile unachosoma.

Andaa kifungu linganifu cha habari chenye aya mbili na alama hizi . , ! ? na kisha wasomee wanafunzi aya hizo kwa kufuata alama za uandishi na kasi stahiki. Watake wanafunzi warudie kusoma kwa sauti kifungu hicho cha habari kwa kufuata alama za uandishi.

Kusoma kwa hisia ni namna nyingine itakayokupa ishara kwamba msomaji anasoma kwa ufasaha akionesha kupanda na kushuka kwa sauti. Wakati mwingine msomaji anaweza kuelezea yanayofanyika katika hadithi kwa kukunja uso ikiwa amechukizwa, kutikisa kichwa kama amesikitishwa na kuonesha furaha au huzuni.

Andika habari au hadithi yenye kuibua hisia na kusisimua. Habari au hadithi hiyo iwe na maudhui yoyote yatakayoendana na wanafunzi wa darasa la I na II .

(Unaweza kutumia kitabu rahisi katika ufundishaji wako)

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ya kuzingatia wakati wa kufundisha na kujifunza kusoma kwa ufasaha:

i. Kuanza kusoma herufi, silabi, maneno na sentensi kwa kasi stahiki

ii. Kutumia machapisho mbalimbali yaliyopo darasani na nje ya kuta za darasa

iii. Kuandaa hadithi kulingana na ngazi ya wanafunzi. Kama ni darasa la kwanza hakikisha kwamba hadithi yake inakuwa na maneno ambayo amejifunza awali

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 27 25/04/2019 12:13

Page 38: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

28

Fafanua kwa mifano namna utakavyomfundisha mwanafunzi matumizi ya alama za uandishi katika kusoma kwa ufasaha.

Hongera kwa kuimaliza sura hii ya kusoma kwa ufasaha ambayo itamjengea mwanafunzi umahiri katika kusoma kwa ufasaha na kusikiliza kwa ufahamu, hivyo kuwa na uwezo wa kujieleza kulingana na mahitaji yake. Ufasaha unajengwa hata kabla ya kuanza shule kwa sababu unaonekana hata katika mazungumzo ya kawaida. Ikumbukwe kwamba mwanafunzi hujifunza kusoma kwa ufasaha kulingana na mazingira yake. Ikiwa jamii inayomzunguka inakosea katika matamshi fulani, mwanafunzi naye ataathirika kwa kuwa na matamshi yasiyo sahihi. Hivyo basi, ni muhimu kusisitiza kusoma kwa ufasaha kuanzia ngazi ya darasa la I na II ili kujenga msingi ulio bora kwa mwanafunzi husika.

Jaribio baada ya kujifunza

Jaribio hili linalenga kupima umahiri ulioupata baada ya kujifunza maudhui ya sura hii. Ni muhimu kufanya jaribio hili.

1. Eleza maana ya kusoma kwa ufasaha.2. Fafanua mambo matatu ya kuzingatia unaposoma kwa ufasaha.

3. Andika kweli kwa sentensi sahihi na si kweli kwa sentensi isiyo sahihi. i. Mwalimu anatakiwa kufundisha sauti za herufi kabla ya kufundisha

silabi.ii. Silabi ni lazima itokane na konsonanti na irabu tu.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 28 25/04/2019 12:13

Page 39: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

29

Sura ya Tano

Kusoma kwa ufahamu

Karibu katika sura ya tano inayohusu kusoma kwa ufahamu kunakohusisha kutafsiri, kuchambua na kutathmini matini. Kusoma kwa Ufahamu ni uwezo wa kuelewa na kutafsiri matini iliyosomwa. Ili kujiridhisha kama mwanafunzi amesoma kwa ufahamu ni lazima atoe mrejesho wa kile alichokisoma kwa kujibu maswali ya ufahamu na kubaini msamiati, kufupisha habari na kuisimulia kwa maneno yake mwenyewe. Vilevile aweze kuhusianisha alichokisoma na maisha ya kila siku. Aidha, kusoma kwa ufahamu humjengea mwanafunzi stadi za kutafsiri na kuelezea picha, kutabiri matukio na kueleza sifa na matendo ya wahusika katika hadithi.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii utajenga umahiri katika: i. kutabiri matukio na kuelezea sifa za wahusika katika hadithiii. kusoma kifungu cha habari na kubaini msamiatiiii. kujibu maswali ya ufahamu kutokana na kifungu cha habariiv. kuhusianisha hadithi na maisha ya kila sikuv. kutafsiri na kuelezea picha.

Jaribio kabla ya kujifunza

Jaribio hili linalenga kupima uelewa ulionao kabla ya kujifunza maudhui ya sura hii. Fanya jaribio hili kabla ya kuanza kujifunza.

1. Fafanua maana ya kusoma kwa ufahamu.2. Eleza kwa ufupi maana ya msamiati.3. Kuangalia picha ni mbinu mojawapo ya kutabiri matukio katika

kusimulia hadithi. Taja mbinu nyingine unazozijua.

4. Jadili umuhimu wa kusoma kwa ufahamu.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 29 25/04/2019 12:13

Page 40: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

30

5.1 Kutabiri matukio na kuelezea sifa za wahusika katika hadithi

Kutabiri ni uwezo wa kubashiri kuhusu matokeo yajayo kulingana na mtiririko wa matukio yalivyo katika habari.

Unawezaje kutabiri matukio katika hadithi?

Katika hadithi au habari nyingi unaweza kutabiri matukio lakini si kila habari unaweza kuitabiri kwani utabiri hutegemea habari yenyewe kwa kuwa mwandishi mwingine huandika habari yake kwa namna ambayo kutabiri tukio litakalofuata inakuwa vigumu. Utabiri wa matukio katika habari ni ishara nzuri inayothibitisha kuwa msomaji amesoma na kuelewa habari au hadithi inayohusika kwa ufahamu.

Mwalimu, kwa kutumia kifungu cha habari/hadithi au jalada la kitabu unaweza kuwaongoza wanafunzi kutabiri kwa kuwapa nafasi ya kusoma habari/picha na kuwapa muda mfupi wa kujadili kile kinachoweza kufuata katika habari/picha hiyo. Kuwapa wanafunzi nafasi ya kufikiri kutawajengea udadisi, kukuza fikira zao na kuwa wachunguzi. Kwa mfano unaweza kutumia kifungu hiki; "baada ya kupata taarifa kuwa vitu vimeibwa nyumbani kwao walihuzunika sana na wakaacha kucheza mpira". Kisha kuuliza swali hili: Unafikiri walifanya nini? Swali kama hilo halilengi tu kujua kama anakumbuka bali kunamfanya afikiri katika kiwango cha juu zaidi.

1. Andaa kifungu cha habari kisha wasomee wanafunzi na kusitisha kusoma kila baada ya mistari michache au aya moja kisha waulize wanafunzi wafikirie kile kitakachotokea baadaye.

2. Fanya ufuatiliaji katika kila habari ili ugundue kiwango cha uelewa wa wanafunzi wako na kuwasaidia pale wanapohitaji msaada.

3. Toa matokeo ya ubashiri ili wafahamu kama wameweza kubashiri kwa usahihi na kama wamekosea wasahihishe.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 30 25/04/2019 12:13

Page 41: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

31

5.2 Kuhusianisha hadithi na maisha ya kila siku

Husianisha hadithi uliyowasimulia au waliyoisoma kisha wanafunzi wenyewe waihusianishe na maisha yao ya kila siku kwa kuchambua wahusika walioko katika habari na uhusika waliouvaa. Kwa mfano, mhusika kuonekana mwenye upendo, ushirikiano, uchoyo, uchafu, uvivu au ujasiri.

Hebu fikiri, unaweza kuhusianisha hadithi yenye wahusika viumbe kama wanyama na wadudu na maisha yetu ya kawaida?

Ikiwa wahusika hao wamevaa uhusika wa binadamu lakini ni vikaragosi vya udongo au wanyama kama vile; twiga, tembo au ndege waeleze wanafunzi kuwa wanawakilisha binadamu.

Tumia ‘kitabu rahisi’kuandika hadithi fupi yenye wahusika ambao ni binadamu na maudhui ya matumizi ya simu ya mkononi katika kupeana taarifa, kisha wasomee wanafunzi au wape wasome wenyewe. Waulize kuhusu wahusika katika hadithi hiyo.

Kumbuka kwamba unaweza kutumia wahusika kama vile; wanyama na wadudu katika kuelezea tukio fulani. Jambo la msingi ni kumfafanua mhusika huyo kutoka katika hali yake ya kuwa mdudu hadi katika maisha na mazingira ya binadamu ili mwanafunzi aweze kupata ujumbe ulioukusudia.

Unatakiwa kuwaambia wanafunzi waeleze walichojifunza kutokana na wahusika katika habari au hadithi waliyoisoma. Ikiwa kitabu kinachotumika kina picha, hakikisha wanafunzi wanaziona picha hizo. Maswali kuhusu wahusika yanaanzia katika wasifu wa nje. Katika kujenga ufahamu zingatia maswali unayoyatoa kuanzia katika picha kama idadi ya wahusika, jinsi zao, matendo wanayoyafanya na mambo mengine yanayofanyika katika habari hiyo ili kujenga ufahamu.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 31 25/04/2019 12:13

Page 42: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

32

5.3 Kusoma kifungu cha habari, kubaini msamiati na kujibu maswali ya ufahamu

Kifungu cha habari lazima kizingatie ngazi ya darasa, uelewa, umri na mazingira yanayomzunguka mwanafunzi. Kwa kuzingatia hayo huna budi kuwa na hadithi au habari zinazosadifu mambo hayo ili kufikia malengo ya ujumbe uliotarajia wanafunzi wako waupate.

Je, utajuaje kama hadithi uliyowasomea wanafunzi au waliyoisoma wenyewe ina misamiati?

Msamiati ni jumla ya maneno yote yanayounda na kutumika katika lugha. Katika ufundishaji wa msamiati maneno haya hufahamika kama maneno anayokutana nayo mwanafunzi kwa mara ya kwanza au maneno mapya. Ili habari au hadithi uliyoitoa ieleweke kwa wanafunzi wako na wapate mafunzo uliyotarajia ni vema ukafafanua maneno mapya yote yaliyotumika katika hadithi hiyo. Unaweza kutumia picha au kitu halisi kuelezea maneno hayo. Ni vyema pia uyaandike ubaoni maneno yote yaliyoonekana kuwa mapya kwa wanafunzi. Hii itawasaidia wanafunzi wakati wa kusoma habari au hadithi kupata maana fasaha ya maneno hayo na kuwa na ufahamu zaidi kwa kile watakachokisoma.

1. Andaa kifungu cha habari kisichozidi aya mbili kinachohusu ‘Shule yetu’ au ‘Nyumbani kwetu’ ili wanafunzi wasome kwa ufahamu na ubainishe msamiati uliojitokeza katika habari hiyo.

2. Bainisha mbinu utakazozitumia katika kufundisha msamiati huo kwa mwanafunzi wa darasa la I na II .

Baada ya mwanafunzi kusoma kifungu cha habari au hadithi na kuelewa maneno yote yaliyotumika katika habari hiyo ni dhahiri kuwa atakuwa na uwezo wa kujibu maswali yanayotokana na habari hiyo. Ikiwa mwanafunzi wako atakuwa na ufahamu mzuri wa habari katika hatua hii, ataweza kufanya mambo yafuatayo kuhusu habari hiyo.

i. Kutabiri matukioii. Kujenga taswira kutokana na habari au hadithi husikaiii. Kuhusianisha hadithi aliyoisoma na hadithi nyingine alizowahi kuzisikia

kimaudhui

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 32 25/04/2019 12:13

Page 43: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

33

iv. Kufupisha habari au hadithi hiyo kwa maneno yake mwenyewe

v. Kuhusianisha habari au hadithi hiyo na maisha ya kila siku

Mambo yafuatayo ni muhimu kuzingatiwa wakati unafundisha ufahamu katika ngazi yoyote ya darasa.

i. Kuzingatia utambuzi wa sauti za herufi kwa usahihi

ii. Kuuliza maswali yenye kufikirisha kulingana na ngazi husika;

iii. Kuzingatia alama za usomaji

iv. Kumsikiliza mwanafunzi kwa makini ili kumsaidia pale anaposhindwa wakati wa ujifunzaji.

Vilevile, kumbuka kuwauliza wanafunzi maswali yenye kujenga kumbukumbu, kufikirisha na kuhusianisha na mazingira yao. Uelewa wa wanafunzi unatofautiana baina yao. Hivyo, hakikisha unatoa maswali yanayopima ngazi nyingi za ufahamu ili kuwasaidia katika vipindi vitakavyofuata.

1. Tumia kitabu rahisi kuandika hadithi (hadithi ziwe tatu zenye maudhui tofauti).

2. Taja na fafanua mbinu nne utakazotumia katika kufundisha msamiati.

5.4 Kutafsiri na kuelezea picha

Ufahamu haujengwi kwa kusoma maandishi tu bali hata kwa kutumia picha, yaani kutafsiri na kuelezea picha husika. Kwa kutumia kitabu rahisi cha picha unaweza kuwapa wanafunzi nafasi ya kutafsiri na kuelezea picha hizo na kupata ujumbe uliotarajiwa.

Je, unawezaje kusoma picha kwa sauti?.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 33 25/04/2019 12:13

Page 44: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

34

Hakika inawezekana kwa njia ya kujiuliza maswali au kuwauliza wanafunzi maswali ya udadisi kuhusu picha hiyo. Katika kusoma picha unahitaji uwezo mkubwa wa kutafsiri na kueleza alichokiona kwa kutumia lugha fasaha. Mwalimu ukitumia picha katika kufundisha ufahamu utamwezesha mwanafunzi kujenga udadisi, kuwa mchunguzi na kukuza kipaji. Inawezekana akapenda kuwa msanii kupitia picha hizo na inaweza pia kumvutia na kuvuta usikivu wake maradufu. Hata hivyo haya yanaweza kutokea ikiwa tu picha ina mvuto na uwezo wa kumjengea mwanafunzi uelewa wa mazingira yake halisi.

1. Andaa chati ya picha yenye mfululizo wa picha za matukio kuhusu huduma ya kwanza.

2. Andaa kitabu rahisi cha picha za wanyama.

Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia wakati unaandaa pichaili kujenga ufahamu wa mwanafunzi:i. Picha iwe ya kuvutia na yenye rangi na maudhui maalumuii. Iwe kubwa na ya kuonekana vizuri kwa wanafunziiii. Isiwe ya kutisha bali ya kusisimua iv. Iwe yenye kujenga maadili kwa wanafunziv. Izingatie maudhui unayotarajia kufundishavi. Iwe inajieleza yenyewe hata bila kuwekewa maandishi yoyote

Andaa maswali kuhusiana na hadithi/habari zenye kuwawezesha wanafunzi kuhusianisha na maisha yao ya kila siku.

Maswali yawe ya kumfanya mwanafunzi kutathimini, kutafakari na kutumia maarifa aliyoyapata kutoka katika habari au hadithi aliyoisoma/aliyoisikia.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 34 25/04/2019 12:13

Page 45: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

35

Ufundishaji wa kusoma kwa ufahamu katika darasa la I na II huwa unakuwa rahisi ikiwa mwalimu atakuwa mbunifu wa kutumia vitabu vya hadithi na mazoezi mengi ya kusoma na kusikiliza. Ikiwa utazingatia mambo ya msingi katika sehemu hii utakuwa mahiri katika uandishi wa hadithi fupi za watoto zenye maudhui mbalimbali kulingana na ngazi yao ya darasa.

Stadi ya kusoma na kusikiliza kwa ufahamu ndiyo msingi muhimu katika kujifunza. Hivyo, zinatakiwa kuendelezwa na kukuzwa kadiri mwanafunzi anavyopanda ngazi kielimu. Ufundishaji huu katika ngazi za juu utategemea masomo na maudhui.

Ni muhimu usomaji kwa ufasaha na usikilizaji usisitizwe katika kila nyanja ili kumfanya mwanafunzi kuwa na uwezo wa kufahamu kila anachojifunza.

Jaribio baada ya kujifunza

Jaribio hili linalenga kupima umahiri ulioupata baada ya kujifunza maudhui ya sura hii. Ni muhimu kufanya jaribio hili.

1. Fafanua maana ya kusoma kwa ufahamu.2. Eleza kwa ufupi maana ya msamiati.3. Kuangalia picha ni mbinu mojawapo ya kutabiri matukio katika kusimulia

hadithi. Taja mbinu nyingine unazozijua. 4. Jadili umuhimu wa kusoma kwa ufahamu.

Jumuiya ya ujifunzajiMaswali yafuatayo yataongoza majadiliano katika jumuiya za ujifunzaji

1. Ni kitu gani ulichojifunza katika moduli hii ambacho kimekusaidia katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji kwa mwanafunzi wa darasa la I na II ?

2. Changamoto gani ulizokutana nazo wakati wa ujifunzaji wa moduli hii?

3. Je, ni mbinu gani ulizozitumia katika kutatua changamoto hizo?

4. Unadhani nini kifanyike ili kuimarisha stadi ya kusoma kwa wanafunzi wa darasa la I na II.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 35 25/04/2019 12:13

Page 46: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

36

Faharasa

Mahitaji Maalumu Uhitaji wa uangalizi na huduma za kipekee kwa mwanafunzi kulingana na hali au utendaji wake.

Makunzi Ni malighafi ambayo hutumika katika kutengenezea zana za kufundishia na kujifunzia.

Mkoba wa Kazi Ni jalada au kifaa kinachotumika kuhifadhia kazi za mwalimu alizozifanya hatua kwa hatua katika nyakati tofauti za ujifunzaji ambazo zitatumika katika upimaji ili kutathimini maendeleo ya ufundishaji na ujifunzaji.

Umahiri Ni uwezo wa kufanya jambo kwa ufanisi mkubwa.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 36 25/04/2019 12:13

Page 47: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

37

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2014). Moduli ya Mwalimu kwa Darasa la I-II: Kusoma kwa ufahamu. Dar es Salaam.

Taasisi ya Elimu Tanzania (2015). Mwongozo wa Mwalimu wa Kufundishia Stadi ya kusoma na Kuandika kwa Elimumsingi Darasa la I na II . Dar es Salaam.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (2014). Moduli ya Mwalimu kwa Darasa la I-II: Sauti ya Herufi, Jina la Herufi na Silabi. Dar es Salaam.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (2015). Muhtasari wa Elimumsingi Darasa la I. Dar es Salaam: Taasisi ya Elimu Tanzania.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (2015). Muhtasari wa Elimumsingi Darasa la II. Dar es Salaam: Taasisi ya Elimu Tanzania.

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 37 25/04/2019 12:13

Page 48: Moduli ya Kufundisha Kusoma Darasa la I na II ya Kusoma I-II... · 2020. 4. 2. · darasa la I na II kwa ufanisi. Moduli hii imeandaliwa kwa lengo la kukujengea umahiri wa kufundisha

38

Kiambatisho

1. Sauti za midomo: Hizi ni sauti zinazotamkwa kwa kukutanisha mdomo wa chini na mdomo wa juu katika kutamka sauti fulani.

Sauti za midomo ni (p, b, m, w)

Mfano wa maneno: pipa, beba, mimi, wewe.

2. Sauti za midomo meno: Hizi ni sauti zinazotolewa kwa kukutanisha midomo ya chini na meno ya juu. Sauti hizo ni (f, v).

Mfano wa maneno: fua, vua, vaa

3. Sauti za meno: Hizi ni sauti ambazo wakati wa kuzitamka ncha ya ulimi hugusana na meno ya juu. Sauti hizi ni (th, dh).

Mfano wa maneno: thamani, dhahabu

4. Sauti za ufizi: Hizi ni sauti ambazo zinapotamkwa ncha ya ulimu hugusana na ufizi. Sauti za ufizi ni (t, d, n, l, r, s, z).

Mfano wa maneno: tua, dua, nuna, sasa, zana.

5. Sauti za kaakaa gumu: Hizi ni sauti ambazo zinapotamkwa bapa la ulimi hugusana na kaakaa gumu.

Sauti hizi ni (j, y, sh, ch, ny)

6. Sauti za kaakaa laini: Sauti hizi hutolewa wakati sehemu ya nyuma ya ulimi inapogusana na kaakaa laini. Sauti hizi ni (k, g, gh, ng’).

Mfano wa maneno: kisu, gumu, ghali, ng’omba.

7. Sauti za glota: Sauti hizi hutamkwa pale ambapo nyuzi sauti zinapofunga na kuruhusu hewa ya kuanzia kwenye glota kutumika kutoa sauti hiyo. Sauti hii ni (h).

Mfano wa maneno: huyu, hewa

Moduli ya Kusoma I-II 9.indd 38 25/04/2019 12:13