20
Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikisha viwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji Jarida la Baraza la Habari Tanzania Toleo la 148, Desemba, 2019 ISSN 0856-874X MCT yajipanga kwa changamoto Sheria ya Haki ya Kupata Habari kurahisishwa Vyanzo vya habari vyabanwa zaidi Uk5 Uk 13 Uk 10 Mwaka wa mafanikio

Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

  • Upload
    others

  • View
    11

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikishaviwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji

Jarida la Baraza la Habari TanzaniaToleo la 148, Desemba, 2019ISSN 0856-874X

MCT yajipanga kwa changamoto

Sheria ya Haki ya Kupata Habari kurahisishwa

Vyanzo vya habari vyabanwa zaidi

Uk5 Uk 13Uk 10

Mwaka wa mafanikio

Page 2: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

BODI YA UHARIRI:Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji – MCTDavid Mbulumi Meneja ProgramuHamis Mzee Mhariri

MAWASILIANOKwa Maoni na Malalamiko:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzani (MCT)S.L.P. 10160, Dar es SalaamSimu: +255 22 27775728, 22 2771947Simu ya Kiganjani: +255 784 314880Fax: + +255 22 2700370Baruapepe: [email protected]: www.mct.or.tzFacebook:- www.facebook.com/mediacounciltanzania Twiter:- www.twitter.com/mctanzania

2

TAHARIRIJarida la Baraza la Habari Tanzania

Hatua hii ni muhimuHabari ni nguvu na kuwa na

wananchi waliohabarika ni jambo muhimu kwa maendeleo kwa jumla.

Kupitishwa kwa sheria ya Haki ya Kupata Habari lilikuwa ni jambo muhimu na hatua nzuri.

Hata hivyo utekelezaji wa sheria hiyo una changamoto kwa kuwa imebainika kwamba umma kwa jumla hauielewi na hata maofisa wa serikali nao hawaielewi.

Hali hii ndiyo imefanya Baraza la Habari Tanzania (MCT) kuanzisha mazungumzo na Wizara ya Katiba na Masuala ya Sheria kwa lengo la kutoa mafunzo kwa maofisa wa serikali.

Jitihada za awali za Baraza kuangalia ufanisi wa sheria hiyo mwaka jana (2018) ulibaini changamoto kadhaa kama vile wananchi wengi hawakuwa na taarifa kuhusu sheria hiyo.

Hata hivyo utafiti uliofanyika mwaka huu umebaini kuna maboresho kiasi. Baadhi ya watafuta taarifa waliweza kupewa taarifa hizo na wengine walielekezwa watu wa kuwatafuta kwa taarifa na wengine waliambiwa kuwa watapata ama kutopata taarifa ndani ya siku 30 kama sheria inavyotaka.

Ingawa haya ni maendeleo mazuri lakini isiwe chanzo cha kubweteka. Na hii ndiyo sababu ya kupokea jitihada ya MCT ya kurahisisha sheria hiyo kwa kutumia chapisho ambalo litaeleweka kwa urahisi na wananchi.

Chapisho hili litakuwa la vibonzo na litaanza rasmi mwakani(2020).

Ni wazi kwamba hatua hiyo ya kurahisisha sheria hiyo itasaidia katika kuelimisha sehemu kubwa ya wananchi na kuwahamasisha kuitumia na kupata matokeo mazuri na kuwawezsha kufanya maamuzi stahiki pamoja na kuwawajibisha viongozi wao.

MCT, MSHINDI WA TUZO YA IPI 2003

FREE MEDIA PIONEER

Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar, Aime Duwe, akichangia katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) uliofanyika katika hoteli ya Sea shells Jijini Dar es Salaam Novemba 29, 2019.

Page 3: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

3

Habari

Toleo la 148, Desemba, 2019

Na Mwandishi wa Barazani

Wakati mwaka 2019 una-ishia, Baraza la Habari Tanzania (MCT) linau-angalia mwaka huo

kwa fahari baada ya kupata ush-indi wa kihistoria dhidi ya sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016 katika Mahakama ya Af-rika Mashariki (EACJ).

Kati ya vifungu 18 vya sheria hiyo ambavyo vilipingwa katika kesi iliyowasilishwa na Baraza na washirika wake vifungu 16 vilionekana na Mahakama hiyo kuwa vinakiuka mkataba wa ushirikiano wa Afrika Mashariki ilipotoa hukumu yake Machi 28, 2019.

Washirika wa MCT katika kesi hiyo kupinga Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Umoja wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

Sheria hiyo ilipitishwa na Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016.

Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika mahakama ni mwelekeo mpya wa Baraza , washirika wake na wadau wa habari wa kwenda mahakamani kupinga sheria kandamizi dhidi ya vyombo vya habari, ikiwa ni mabadiliko kutokana na msimamo wa muda mrefu kutopenda

kwenda mahakamani kwa mtazamo kuwa ni upotezaji wa muda na kesi huchukua muda mrefu.

Katika kesi hiyo ya kupinga Sheria hiyo ya Huduma ya Vyombo vya Habari, Mahakama ya Afrika Mashariki iliamuru serikali ya Tanzania kufanya marekebisho ili sheria hiyo iende sawa na Mkataba wa Afrika Mashariki, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa MCT uliofanyika Dar es Salaam Novemba 29, 2019 walielezwa katika Ripoti ya Utekelezaji ya Katibu Mkuu wa Baraza.

Licha ya hukumu hiyo ya Mahakama ya Afrika Mashariki, serikali inasuasua kuitekeleza.

Kuna kesi kadhaa zilizo katika hatua mbalimbali zinazopinga sheria zinazohusu vyombo vya habari ama kanuni zake.

Kutokana na jitihada za Baraza, Mkutano Mkuu uliambiwa kwamba waandishi watatu waliotiwa hatiani kwa makosa ya kubambikiwa kesi ya unyang’anyi kwa kutumia nguvu na kufungwa na Mahakama Kuu ya Wilaya ya Magu miaka 30, Mahakama imeamuru kesi yao isikilizwe upya.

Mahakama Kuu ilitupilia mbali

2019 mwaka wa mafanikio kwa MCT

Wajumbe Mkutano Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania uliofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 29, 2019 wakiwa katika picha ya pamoja.

Endelea Ukurasa wa 4

l Baraza lapata mafanikio ya kihistoria

Page 4: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

4

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Magu na kuamuru kesi inayowakabili waandishi Christopher Gamaina wa Raia Mwema, Zephania Mandia wa Channel Ten na Manga Msabaha wa gazeti la Mzawa kusikilizwa upya.

Jaji wa Mahakama Kuu alitupilia mbali ushahidi wote wa upande wa mashitaka na kuamuru kesi hiyo isikilizwe na hakimu mwingine. Kesi hiyo inaendelea katika Mahakama ya Magu.

Katika mwaka huo, ripoti ya Katibu Mtendaji matukio 73 ya ukiukaji wa uhuru wa habari yameripotiwa ambapo 33 yalithibitishwa na kurekodiwa katika Rejista ya Ukiukaji wa Uhuru wa Habari inayosimamiwa na MCT.

Kuhusu usalama wa waandishi, hatua zimechukuliwa kuzungumza na serikali kuhusu sheria za habari pamoja na usalama wa waandishi.

Ripoti hiyo imeeleza wazi kwamba usalama wa waandishi wa habari ni muhimu kwa sababu unawezesha vyombo vya habari kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Mikutano na Wizara ya Habari iliandaliwa na kwamba Baraza liliandika barua mbili za kumkumbusha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ahadi yake aliyoitoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru Duniani Mei 3, 2019 kukutana na wadau wa habari na kujadili masuala mbalimbali ikiwa pamoja na yanayohusu sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu pia walielezwa kuhusu jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Baraza kushirikisha vyombo vya kikanda na mtandao wa kimataifa na wadau.

Miongoni mwa taasisi za kimataifa ambazo Baraza lilifanyakazi nazo, ripoti hiyo imeonyesha ni pamoja na Kamati ya Kutetea Waandishi wa Habari (CPJ) katika kampeni kuhusu alipo mwanahabari Azory Gwanda aliyetoweka baada ya kuchukuliwa na watu wasiojulikana Novemba 21, 2017.

Baraza pia limechukua hatua

ya kutaka kupata hadhi ya kuwa mwangalizi katika Umoja wa Afrika. Limewasilisha maombi yake na mchakato unaendelea.

Mkutano ulifahamishwa kuwa Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kipindi cha mpito wa Chama cha Mabaraza ya Habari ya Afrika Mashariki katika mkutano uliofanyika Kisumu , Kenya Novemba 2, 2019 katika siku ya kimatifa ya kupinga msimamo wa kutochukua hatua dhidi ya uhalifu dhidi ya wanahabari.

Baraza liko katika mchakato wa

kuandaa andiko kuhusu hali ya Uhuru wa habari na Uhuru wa Kujieleza nchini litakaloonyesha mwelekeo na matukio ya ukiukaji.

Andiko hilo linapitiwa na litakapomalizika litawasilishwa katika Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika (ACHPR) na Umoja wa Mataifa.

Shughuli za uragbishi na uzengezi zilifanyika wakati wote na Baraza kwa kushiriki katika vipindi vya redio na runinga, kuandika mada na makala kuhusu ukiukaji na kuchapisha makala kuhusu kueneza sheria ya Haki ya Kupata Taarifa (ATI).

Makamu wa Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Hassan Mitawi akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Baraza uliofanyika Novemba 29, 2019 Jijini Dar es Salaam.

2019 mwaka wa mafanikio kwa MCT Inatoka Ukurasa wa 3

Page 5: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limejipanga kutekeleza na kutimiza ma-jukumu yenye changamoto

mwaka 2020.Kamati ya Fedha na Utawala ya

Bodi ya Baraza hilo imepitisha Mpango wa mwaka na Bajeti ya Baraza kwa mwaka 2020.

Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati hiyo, Kajubi Mukajanga ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza, Kamati hiyo iliyoketi Desemba 4 chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais wa Baraza, Hassan Mitawi, tangu 2007/8 shughuli za Baraza zinazingatia mipango mkakati ya miaka minne mine inayopitishwa.

Mwishoni mwa kila mwaka , Sekretarieti hupanga mpango na bajeti kuzingatia mahitaji ya

kimkakati na vipaumbele. Mukajanga alisema kuwa

Novemba 2019 Sekretariet ilienda katika kikao cha kujitathmini kwa kupitia utendaji wa Baraza kwa mwaka unaomalizika na kupanga mpango na bajeti ya 2020 ambapo masuala kadhaa ikiwemo kuhimiza kufutwa kwa sheria kandamizi dhidi ya vyombo vya habari Tanzania Bara, kuendeleza shughuli za Umoja wa Haki ya Kupata Habari (CoRI) katika pendekezo la kamati ya pamoja ya serikali na wadau ya marekebisho ya sheria ya habari vimepewa kipaumbele katika mpango wa mwaka 2020.

Masuala mengine ni pamoja na kuendelea kuunga mkono ufunguaji mashitaka, kushirikiana na wadau wa kikanda na kimataifa, kuieneza sheria ya Haki ya Kupata habari, kushiriki katika mchakato wa kisheria wa sheria

mpya ya habari ya Zanzibar ikiwa pamoja na kushauriana na serikali kwa ngazi za juu na kuendeleza juhudi za kuhamasisha kutumia kesi mahakamani, mchakato wake na matokeo.

Kiubunifu kuendeleza kampeni za vyombo vya habari kufanya kampeni kuhamasisha na kuelewesha kuhusu ukiukaji wa uhuru wa habari ikiwamo pamoja na kutumia mitandao yenye ushawishi, kufanya kampeni Zanzibar na Bara kuhusu shughuli za usuluhishi na upatanishi za MCT, kufanya vikao vya upatanishi, kuandaa Tuzo za 11 za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT), na kupitia na kuchapisha Kanuni za Maadili za Wanataaluma ya Habari.

Kuendesha mafunzo ya menejimenti ya habari kwa wanawake na kusambaza sera ya jinsia na habari na kuendeleza shughuli kuhusu Mtaala wa uandishi wa habari wa kitaifa utakaopitiwa pia ni miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaumbele na Baaraza.

Kamati pia ilielezwa kuwa menejimenti imeamua kutumia watumishi wa kujitolea kuendeleza malengo ya Baraza na kwamba Baraza limepanga kufanya mkutano wa mapitio katika nusu ya pili ya mwaka 2020, kutathmini mafanikio ya kupata fedha na utekelezaji wa mipango.

5

Habari

Toleo la 148, Desemba, 2019

MCT yajipanga kutekeleza majukumu yenye changamoto 2020

Kamati ya Fedha na Utawala ya Bodi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) ikiwa katika kikao Desemba 4, 2019. Kutoka Kushoto ni wajumbe wa Kamati Anna Henga, Bakari Machumu, Mwenyekiti wa Kamati na Makamu wa Rais wa MCT , Hassan Mitawi, Katibu wa Kamati na Katibu Mtendaji wa Baraza, Kajubi Mukajanga. Wa pili kulia ni mjumbe wa Kamati , Wallace Mauggo na kulia ni Meneja Raslimali Watu na Utawala , Ziada Kilobo. Picha: Said Hassan

Page 6: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

6

Utaratibu

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

16

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Baraza la Habari Tanzania ni chombo huru kilichoundwa na wadau wa vyombo vya habari kusimamia weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

Je! Una malalamiko juu ya habari au makala iliyotoka gazetini au kipindi chochote kilichorushwa hewani na radio au luninga?

Kama una malalamiko, basi wasiliana na mhariri wa gazeti au chombo husika cha habari. Ikiwa hutaridhika na hatua za chombo hicho cha habari, basi peleka malalamiko yako Baraza la Habari Tanzania. Baraza litashughulikia shauri lako haraka kwa misingi ya maridhiano na uungwana.

Jinsi ya kupeleka shauri katika Baraza• Kabla ya kuleta shauri katika Baraza dhidi ya chombo cha habari chochote au

mwandishi wa habari yeyote, mlalamikaji ajiridhishe kuwa juhudi za kuleta maelewano na kupata upatanishi kati yake na walalamikiwa zimeshindikana.

• Mlalamikaji anapaswa kuhakikisha kwamba wakati malalamiko yanaletwa kwenye Baraza habari zinazolalamikiwa hazikuchapishwa au kutangazwa zaidi ya wiki 12 zilizopita.

• Malalamiko yoyote yaletwayo kwenye Baraza sharti yawe katika maandishi na yaonyeshe tarehe, jina la chombo cha habari kilichochapisha au kutangaza habari zinazolalamikiwa. Baraza linaweza kukiamuru chombo cha habari au gazeti kumuomba radhi mlalamikaji na, au kumpa nafasi ya kujibu, au kutoa amri yoyote itakayoona inafaa na ambayo ipo ndani ya mamlaka yake.

• Iwapo mlalamikaji hataridhika na uamuzi wa Baraza anaweza kutafuta njia nyingine za kutatua shauri lake ikiwemo kulipeleka mahakamani. Hata hivyo, hatatumia uamuzi wa Baraza kama ushahidi Mahakamani. Hata hivyo, Mahakama inaweza kulialika Baraza wakati wowote kama “rafiki wa mahakama” (Amicus Curiae’) pale itakapohitaji ushauri wa kitaalamu kuhusu mambo ya habari.

Kwa mawasiliano na Baraza:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzania,Josam House, Kitalu B, Ghorofa ya Kwanza, Upande B, S.L.P 10160, Simu+255 22 2775728/ +255 22 2771947,Nukushi +255 22 2700370, Simu ya Kiganjani +255 732 998310Barua Pepe: [email protected]: mct.or.tz

BARAZA LA HABARI TANZANIA

Page 7: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Mwelekeo wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Baraza la Habari Tanzania ulio-fanyika Novemba 29,

ulikuwa wa matumaini. Hali iliyojitokeza kwa wajumbe

kutoka mikoa mbalimbali ilikuwa ya bashasha wakibadilishana salamu na kujitambulisha.

Mkutano ulianza kwa kukaribisha wanachama wapya wa Baraza kwa kuwakabidhi vyeti vya

uanachama.Kadri mkutano ulivyoendelea ,

wajumbe walifahamishwa na kujadili masuala muhimu ikiwamo suala la Baraza kujitegemea katika uendeshaji wake na kuliimarisha. Waliambiwa katika taarifa ya Katibu Mtendaji kuwa mkakati wa kupata mapato umetayarishwa na unafanyakazi.

Kutokana na uamuzi uliochukuliwa katika Mkutano wa 20 uliofanyika Zanzibar Oktoba 5, 2018 kwa waendesha mitandao ya kijamii – bloggers - kuwa

uanachama wa Baraza, wajumbe wa Mkutano wa 21 waliidhinisha ada ya wanachama yao ya kila mwaka kuwa sh. 100,000.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, Kajubi Mukajanga alifafanua wakati wa mkutano huo kuwa vituo vya redio ambavyo ni wanachama na vinavyorusha matangazo yao mtandaoni havihusiki na ada hiyo mpya.

Wajumbe pia walipokea ripoti ya Katibu Mtendaji kuhusu fedha za Baraza.

Mukajanga alisema Baraza kwa mara nyingine limepata hati safi ya ukaguzi kwa mwaka 2018, hali ambayo imekuwapo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1995.

Mkutano Mkuu uliiteua tena kampuni ya ukaguzi ya Auditax International kukagua hesabu za Baraza kwa kipindi kinachoishia Desemba 31, 2019.

Mkutano Mkuu huo ukiwa chini ya uenyekiti wa Makamu Rais wa MCT, Hassan Mitawi, pia ulisikia hali ya wasiwasi kuhusu hofu inayotamalaki nchini na hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.

Mitawi na Katibu Mtendaji wa Baraza Mukajanga licha ya kuzingatia suala hilo la hofu, wametaka vyombo vya habari kuwa makini na kuzingatia uzalendo katika utendaji wao.

7

Habari

Toleo la 148, Desemba, 2019

MCT yafanya Mkutano Mkuu kwa mafanikio Dar

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Baraza la Habari Tanzania wakichukua nafasi zao kabla ya kuanza mkutano huo Novemba 29, Jijini Dar es Salaam .

Page 8: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

98

Toleo la 148, Desemba, 2019

Picha

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Picha

Wawakilishi wa vyombo vya habari vilivyojiunga na Baraza la Habari Tanzania (MCT) wengi wao wakitoka radio, wakipokea vyeti vya kuwa wanachama wapya kutoka kwa Makamu Rais wa Baraza, Hassan Mitawi. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza, Kajubi Mukajanga.

Page 9: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Na Mwandishi wa Barazani

Baraza la Habari Tanzania (MCT) liko katika mchakato wa kutoa chapisho la Sheria ya Haki ya Kupata H

abari iliyorahisishwa ili watu wengi zaidi waielewe.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza waliambiwa katika ripoti ya Katibu Mtendaji kuwa chapisho hilo litakuwa la vibonzo na litazinduliwa mapema mwakani.

Licha ya kuwepo kwa sheria hiyo, ripoti hiyo imeeleza kuwa Baraza limebaini kwamba kuna baadhi ya

changamoto katika kupata habari kutoka kwa maofisa wa serikali na limeamua kufanya utafiti ili kupata matokeo halisi kuhusu habari zinavyotolewa katika ofisi za serikali.

Katika miezi mitatu – Julai hadi Septemba, 2018 Baraza lilitumia waratibu wa klabu za uandishi wa habari kuomba taarifa katika ofisi mbalimbali za serikali na matokeo yake hayakuwa mazuri ambapo ilibainika kuna changamoto mbalimbali kwa umma ikiwemo kutokujua uwepo wa sheria hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Katibu Mtendaji, utafiti huo ndiyo

umekuwa msingi wa majadiliano kati ya Baraza na Wizara ya Katiba na Masuala ya sheria kuhusu kutoa mafunzo kwa maofisa wa serikali.

Ripoti hiyo kuhusu ufanisi wa sheria hiyo ilisambazwa kwa wahariri, wanachama wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRi), wadau wa habari na watetezi wa haki za binadamu wakati wa mkutano wa kilele wa MCT na Wahariri uliofanyika mjini Tanga Novemba 29 hadi 30, 2018.

Mwaka 2019, waratibu wa klabu za uandishi walipewa kazi na Baraza kufanya utafiti wa kufuatilia kuanzia Septemba hadi Oktoba , 2019 ambayo imekamilika.

Hata hivyo kuna maboresho katika utoaji wa habari ambapo taarifa za awali zimeonyesha kuwa asilimia 22 za watafuta habari walipatiwa taarifa zote walizohitaji na huduma ya majibu kwa wanaotaka taarifa imekuwa nzuri ambapo wahitaji hupewa mawasiliano ya wapi wafuatilie.

Asilimia 78 ya wahitaji taarifa wameambiwa kama watapata taarifa au hapana katika kipindi cha siku 30 kama inavyotakiwa kisheria. Ripoti kuhusu zoezi la utafiti huo itachapishwa na kusambazwa.

10

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

MCT kurahisisha Sheria ya Haki ya Kupata Habari

Meneja wa Fedha wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Mustapha Tarimo na Meneja Raslimali Watu na Utawala wa Baraza, Ziada Kilobo wakiwasilisha ripoti katika Mkutano Mkuu wa Baraza.

Page 10: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Bodi ya wadhamini ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) imekutana Desemba 3, 2019 na kujadili masuala

muhimu yahusuyo Baraza. Kulingana na Katibu wa Bodi

hiyo, Kajubi Mukajanga ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza, wajumbe wa Bodi hiyo chini ya Mwenyekiti wao Profesa Geoffrey Mmari , walipokea ripoti na maendeleo kuhusu Baraza kujitegemea iliyoandaliwa na Sekretarieti.

Wajumbe wengine wa Bodi ya wadhamini ni Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba na Jaji mstaafu Agusta Bubeshi.

Bodi ya wadhamini pia ilijadili kuhusu hali ya sasa ya vyombo vya habari nchini.

Bodi hiyo hukutana mara moja kwa mwaka ila yaweza kukutana mara nyingi zaidi ikitakiwa kufanya hivyo na Bodi ya Baraza. Mwaka jana pia ilikutana Desemba.

11

Habari

Toleo la 148, Desemba, 2019

Bodi ya wadhamini MCT yakutana

Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya Baraza la Habari Tanzania, Kajubi Mukajanga akizungumza katika kikao cha Bodi hiyo ilipokutana Desemba 3, 2019. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Geoffrey Mmari na kushoto ni mjumbe wa Bodi jaji mstaafu Agusta Bubeshi. Wapili kulia ni mjumbe wa Bodi, Joseph Warioba – Waziri Mkuu mstaafu na Makamu wa rais na kulia ni Meneja Raslimaliwatu na Utawala wa MCT, Ziada Kilobo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Baraza la Habari Tanzania, Profesa Geoffrey Mmari akiongoza kikao cha Bodi hiyo Desemba 3, 2019. Kulia ni Kajubi Mukajanga Katibu wa Bodi hiyo na ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza .

Page 11: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Na Mwandishi wa Barazani

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi

Mukajanga amesema Mfanyabiashara maarufu, Ali Mufuruki aliyefariki hivi karibuni amelisaidia sana Baraza hilo.

“Alituletea uzoefu wa sekta binafsi katika shughuli zetu… ilikuwa ya manufaa sana”, Mukajanga alisema kuhusu Mufuruki aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Baraza kati ya Juni 2014 hadi Juni 2017.

“Aliingiza uongozi wa kishirika na ujuzi wa ujasiriamali wa binafsi mambo ambayo yalitusaidia sana”,

alisema Mukajanga akionyesha wazi kuwa na huzuni.

Baraza alisema linamkumbuka Mufuruki kwa mchango wake mkubwa alipokuwa mjumbe wa Bodi.

Katika Bodi alikuwa mjumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala.

“Tunamshukuru Mungu kwa muda ambao Mufuruki alilitumikia Baraza, alisema na kusisitiza kuwa kifo chake ni pigo kubwa na kimeleta mshtuko mkuwa pia kwetu”.

Mufuruki alifariki katika hospitali moja nchini Afrika Kusini alikokuwa ameenda kwa matibabu.

Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam wakiwemo wafanyabiashara na viongozi wa

kisiasa walitoa heshima zao za mwisho kwa Mufuruki Desemba 10, 2019 katika Kituo cha Kimataifa cha

Mikutano cha Mwalimu

Nyerere.

12

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

MCT yamlilia Mufuruki Habari

Mfanyabiashara maarufu , Ali Mufuruki aliyefariki akipata matibabu Afrika Kusini.

Page 12: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Gervas Moshiro

Mara baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwishoni mwa Novemba 2019, Balozi

za Marekani na Uingereza zilitoa matamko ya kuwa uchaguzi huo haukuwa halali. Vyombo vya habari vya nje viliutangazia ulimwengu msimamo huo wa nchi hizo. Vyombo vya habari vya nchini ambavyo hadi wakati huo vilikuwa vimejikita zaidi kutangaza kususiwa kwa uchaguzi huo, havikuweza vyenyewe kutathmini hali hiyo na kudiriki kuonesha kasoro za uchaguzi huo na madhara yake.

Vyombo vya mtandaoni vilinukuu maoni machache kutoka kwa wanasiasa machachari na wanaharakati wengine waliothubutu kuikosoa bayana serikali, lakini pia kuna vyombo vingine vilikuwa na ujasiri wa kukariri kile walichosema wanadiplomasia, pengine kwa kudhani kuwa wasingewajibishwa kwa kutoa matamko hayo kwani tayari wakubwa walikwisha kuutangazia ulimwengu kasoro hizo.

Lahaula! Kumbe ‘Kaka mkubwa’ alikuwa macho na kuwashukia kwa kishindo kwa kukataza wanahabari nchini kunukuu taarifa zozote zinazotolewa na mataifa au mashirika ya nje kwenye uandishi wao. Naelewa inakatisha tamaa kama anavyodai Mkurugenzi wa Habari kuwa mara nyingi amekuwa akiviasa vyombo vya habari bila mafanikio. Dawa anayoona imebaki sasa ni kutumia mkono mzito wa serikali, ikiwemo mkondo wa sheria.

Sikutarajia msemaji wa serikali kupenda matamshi yale ya wanadiplomasia au vyombo vya habari vilivyokariri matamshi yao kuhusiana na uchaguzi ule, lakini angalau tungebainishiwa ni tunu gani ya kitaaluma iliyokuwa inakashifiwa. Vitisho hutolewa na adui, lakini kwenye jamii ambapo katazo halifahamiki wala kuridhiwa, ni kuzidisha vitisho ambavyo tayari vimefurika. Elimu ingetumika kabla ya kurejelea sheria na hasa kwa kufahamu au kuamini kuwa bado demokrasia yetu ni changa.

Natarajia wasimamizi wa sekta ya

habari kufahamu vyema uwili wa tasnia: wanahabari na waandishi wa habari. Kuna tofauti kubwa katika utayarishaji wa maudhui ya pande hizo mbili kwa malengo, mkabala na aina ya maudhui. Inaelezea hata ni kwa nini kuna kazi mbili tofauti zinazotambulika: maafisa mawasiliano dhidi ya waandishi wa habari.

Mambo mawili yahitaji kufafanuliwa: kupotosha habari na uvumi ambayo Mkurugenzi wa Habari anadai yanahujumu serikali. Ingekuwa ndio mimi kwenye viatu vyake ningeanza kwa kutathmini ukweli wa mambo hayo, licha ya kwamba naelewa wakati mwingine wakubwa zaidi wanashinikiza hatua fulani zichukuliwe, halafu ningeyaweka bayana kwa vyombo vya habari ili na wananchi waelewe masuala hayo, ikiwezekana hata kuanzisha mjadala wa jamii.

Ikiwa vyombo vya habari havitaripoti nipendavyo, kuna mwanya wa kutumia chombo chochote cha habari kwa kulipia utoaji wa taarifa hizo. Bila serikali kujitokeza na yenyewe kutangaza mambo yake kivyake, itashindwa na nguvu za wenye uchumi mkubwa.

Hata hivyo nampongeza Mkurugenzi huyo kupiga vita utoaji wa habari za uongo na uchochezi. Juhudi zaidi zahitajika kuondoa kabisa kwenye vyombo vya habari hapa nchini udhaifu huo.Hatua ichukuliwe kwa vyombo vyote kusiwe na ubaguzi wa kupendelea vyombo vinavyoitwa vya “kimkakati”.

Wakati mwingine tunachukulia, pengine kwa makosa, kuwa yeyote aliye kwenye chombo cha habari ni mwelewa na ana mtizamo unaotakiwa. Mtizamo au mwelekeo ni zao la utamaduni na hasa pale inapohusiana na uzalendo. Je, mfumo wetu wa elimu na utamaduni wa kazi unawapa watu maarifa na moyo wa uzalendo? Inahitajika makuzi ya namna fulani kumfanya mtu ajitambue na kufanya uamuzi wa kuchapisha kizalendo anapokabiliwa na mtanziko.

Wakati wa utawala wa awamu ya Mwalimu Julius Nyerere vyuo vya siasa na maendeleo vilianzishwa katika kanda kadhaa nchini na viongozi wote waandamizi, wakiwemo wanahabari walitakiwa kuhudhuria bila malipo.

Jeshi la Kujenga Taifa lilikuwa na jukumu kama hilo kwa vijana waliofuzu elimu ya juu. Baadhi ya waliohudhuria mafunzo hayo wapo kwenye vyombo vya habari hivi sasa, na nitashangaa ikiwa kazi zao hazidhihirishi uzalendo waliofunzwa.

Nakumbuka semina moja iliyoendeshwa na mtaalam wa Thomson Foundation (Uingereza) miaka ya tisini mwanzoni kwa maafisa habari na akawauliza: “Mnamtumikia nani?” Kwa mshangao, neno ‘wananchi” au “umma” halikuwatoka mdomoni. Walijibu: serikali. Sijui jibu lingekuwa nini kama wangeulizwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya binafsi.

Sipo kwenye mawazo ya Rais, lakini huenda akakubaliana nami kuwa moja ya vitu vinavyomfanya kuteua viongozi wa taasisi wenye elimu ya juu kabisa ni kuhakikisha uamuzi wao wakati wote unatosheleza uwanda wote wa changamoto zinazoweza kukabili taaluma, taasisi, sekta na nyinginezo bila kuruhusu upungufu usio wa lazima.

Nia ya makala haya ni kujadili kuendelea kupungua nafazi za utendaji wa vyombo vya habari, maadam sasa vyanzo vya habari navyo vimeanza kupigwa vita, ikinishawishi kuamini kuwa huu ni mkakati uliopangwa wa kusambaratisha uandishi wa habari.

Kwa miaka kadhaa, hasa wakati wa awamu ya kwanza na ya tano ya serikali, nimesikia baadhi ya wanasiasa wakilaani vyombo vya habari kuwa vinatumiwa na maadui kuhujumu nchi. Ni kweli wakati wa awamu ya kwanza, vyombo vya habari vya nchi za magharibi vilikuwa vinachafua sana taswira ya nchi kwa kuwa Mwalimu Nyerere aliifanya nchi kuwa na itikadi ya kijamaa iliyokinzana na ubepari uliokumbatiwa na mataifa hayo yaliyokuwa marafiki wetu awali. Vyombo vyetu vya habari nchini vilifahamu hali hiyo na vikawa macho, wakati mwingine kujibu mapigo kila nchi inapoandikwa vibaya kwenye vyombo vya nje.

Hata hivyo, japo sasa tuko kwenye mrengo wa ubepari, tunachukuliwa kuwa wakorofi kwa sababu

13

Toleo la 148, Desemba, 2019

Maoni

Kubana vyanzo vya habari ni unyanyasaji wa taaluma

Endelea Ukurasa wa 14

Page 13: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

14

Maoni

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

tunapungukiwa tunu muhimu kama haki za binadamu,usawa kitaifa na haki ya maisha kama inavyotajwa kwenye katiba ya nchi.

Kama nikisoma Kifungu cha 3 cha katiba ya nchi kinachosema: ‘Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa’, na kutathmini uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kigezo hicho na kukuta kuna tatizo, kuna ubaya gani nikisema hivyo?. Inabidi sasa tujue kuwa maadam bado tunajitangaza kuwa ni nchi ya kidemokrasia, wengine watatupima kwa vigezo vya demokrasia vinavyotumika kwingineko, na hii inaweza kusemwa na mwanadiplomasia au mwingine yeyote. Ni juu yetu kuwaelimisha kuhusu tofauti ya demokrasia yetu kama itakuwa na vigezo totauti visivyo kwenye demokrasia kongwe. Kama vigezo hivi vingekuwa bayana, vyombo vya habari vyenyewe vingewajibu wale wanadiplomasia au hata kukataa kuchapisha malalamiko yao.

Siamini kuwa kuna mashirika ya nje yanayoshawishi vyombo vya habari nchini kuandika maoni yasiyokubalika kitaaluma au kinyume na maadili, labda iwe kwenye vile vyombo vinavyojipambanua kuwa ni vya “kimkakati” ambavyo yaonekana vimeandikishwa kwa lengo la kupotosha. Maudhui yake mengi yanapingwa na wanataaluma lakini mamlaka za usimamizi zinakaa kimya. Kama jina linavyoashiria –‘vyombo vya kimkakakti’ viko kwa kazi inayovihitaji ili iweze kufanikishwa. Taifa bado halijaifahamu vyema dhana hii mpya ya vyombo vya habari vya kimkakati na namna vitakavyojiweka kwenye mfumo wa mawasiliano nchini.

Natoa changamoto kwa wanahistoria watupe mifano ya nchi zilizotumia vyombo vya kimkakati visivyozingatia maadili ya taaluma na ni nini kilikuwa matokeo yake.

Nakumbukuka historia ya Ujerumani chini ya chama cha Manazi na Italia chini ya Benito Mussolini. Mkakati wao mkuu ulikua kupotosha habari ambapo ulizaa mashujaa waliogeuka kuwa wahalifu wakubwa waliosababisha vita vya dunia na madhara yake yakiwa nasi hadi hii leo. Habari chini ya Waziri Goebbels wa Ujerumani ikawa ndiyo wizara kubwa ya serikali, watu wakiwa wanatega kusikia nini kipya atakachoamuru mkubwa siku hiyo.

Jambo hilo huwa hivi. Inaanza kwa kuondosha taasisi zinazowawezesha wananchi kuwa na nguvu, kama vile vyombo vya habari. Uanzishaji wa vyombo vya habari vya kimkakati ni ishara kuwa mchakato huo umekwisha kuanza – utoaji wa propaganda.

Hatua inayofuata ni kufifisha vyombo vya habari vilivyozoeleka ama kwa kuviingiza kwenye utaratibu wa utoaji wa propaganda au kuviua kiuchumi. Kuna ripoti nyingi hadi sasa zinazoonesha jinsi baadhi ya viongozi katika ngazi mbalimbali na vyombo vya dola wanavyodhalilisha vyombo vya habari, kuvifanya visiweze kutenda kazi itakiwavyo kitaaluma.

Ripoti za kisomi zilizofadhiliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) zinaonesha kuwa baadhi ya vyombo vya habari vimeanza kuacha majukumu yake ya kuwa jicho la jamii, na hivyo kuachilia uonevu na ukandamizaji kushamiri. Wanahabari wanaogopa kuchunguza maovu kwa kutojua mamlaka zitawafanya nini. Tumekuwa tunasikia makaripio yakitolewa na wakubwa kila inapotolewa habari wasioipenda kwenye vyombo vya habari. Wanataka vyombo vya habari viendane na wanavyotaka, la sivyo vifyate mkia.

Kuhusu kuua kiuchumi kama tayari ilivyokwisha ripotiwa katika makala kadhaa zilizotangulia, hali ni mbaya na wahariri wanakiri kuwa huenda baadhi ya vyombo vikajifunga. Mbaya wao ni kanuni ya sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari inayompa Mkurugenzi wa Habari ukiritimba wa kutoa matangazo yote ya serikali. Na kama inavyotarajiwa, hisani huanzia nyumbani, anatoa matangazo hayo kwa vyombo vinavyokubali na kuendeleza maslahi ya serikali au vyombo rafiki. Sitarajii utaratibu huu kubadilika kama sheria haijabadilishwa kurejesha utaratibu huria wa zamani. Kuna haja ya kutumia mahakama au bunge au kuacha kulalama.

Kuendelea kuweko kama chombo

cha habari maana yake ni kukubali kubadilika kwa kupenda na kuunga mkono yafanywayo na serikali bila kujali matokeo yake. Waasisi wa mkakati watafurahi kuona vyombo vyote vya habari vina mwelekeo mmoja na hivyo kuweza kuvitumia kuendesha utawala wa nchi. Hii ndiyo hali inavyokuwa katika utawala wa chama kimoja usiokuwa na uanuwai wa vyombo vya habari. Utaratibu huu tulikuwa nao miaka ya sitini, sabini, themanini na kuuacha miaka ya tisini baada ya kutoona manufaa yake.

Kabla ya uliberali wa 1992, vyombo vya habari nchini vilikuwa radio moja ya taifa, gazeti moja la kiingereza na moja la Kiswahili. Hakukuwa na runinga wala vyombo vya mtandaoni. Machapisho mengine yalikuwa ya taasisi za serikali na yakiwa hayana mchango sana katika kuhabarisha jamii masuala yawahusuyo kila siku. Kulikuwa hakuna mawazo mbadala.

Kufufua mfumo huo kunahitaji mtu mwenye maono na kipaji cha ziada ili ukubalike zama za sasa. Kuanzishwa kwake pekee kutazua upinzani mkubwa kwa vile madhara yake yanafahamika. Iweje, mfumo huo hauna nafasi katika zama za sasa kutokana na maendeleo ya teknolojia ya habari. Kuna nchi kama China zinajaribu kudhibiti uanuwai wa vyombo na mawazo lakini zinashindwa. Habari anuwai kutoka vyanzo anuwai ni sehemu ya maisha ya binadamu kwa sasa.

Siasa za vyama vingi na vyombo vya habari anuwai ni pete na kidole. Vyombo vya habari wakati mwingi vinatafuta habari kutoka vyama vya siasa kwa sababu katika mabishano na msuguano wa kuwania madaraka, kunatokea msisimko unaofurahisha watu. Kuweko kwake kumejikita katika uhalisia wa binadamu, na ndivyo tulivyo. Tumepitia wakati wa siasa za chama kimoja na kuona hazina tija kwa huko tuendako, na ndio maana hata Baba wa Taifa Mwl. Nyerere aliunga

Inatoka Ukurasa wa 13

Kubana vyanzo vya habari ni unyanyasaji wa taaluma

Endelea Ukurasa wa 18

Page 14: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

New York

Idadi ya wanahabari waliofungwa kutokana na kutekeleza kazi zao duniani imefikia 250 kwa mwaka wa nne mfululizo, huku China na

Uturuki zikiongoza katika ufungaji wa wanahabari, Kamati ya Kutetea waandishi imeripoti.

Hadi Desemba 1, 2019, CPJ imebaini kuwepo waandishi 250 kwenye magereza na asilimia 98 wakiwa waandishi wa nchi husika. Baada ya China, Uturuki, Saudi Arabia na Misri, nchi zinazoongoza kwa kufunga wanahabari ni Eritrea, Vietnam na Iran.

Katika ripoti yake iliyotolewa Desemba 11, 2019 CPJ imeeleza kuwa Rais Xi Jinping wa China amezidi kubana hatua za nchi yake dhidi ya vyombo vya habari ambapo waandishi 48 wako gerezani.

Uturuki ikiwa imeondoa kabisa uandishi wa habari huru kwa kufungia zaidi ya vyombo vya habari 100 na kuwafunguliwa mashitaka ya ugaidi wafanyakazi wake, ilikuwa na waandishi 47 gerezani mwaka 2019.Wengine kadhaa wakikabiliwa na mashtaka ama wamefungwa ama wako nje kwa dhamana.

“Kufungwa kwa mwandishi mmoja ni ukiukaji mbaya wa haki wenye madhara makubwa kwa familia, marafiki na jamaa”, amesema Joel Simon, Mkurugenzi Mtendaji wa CPJ.

“Lakini kufungwa kwa mamia ya wanahabari – kila mwaka ni tishio kwa mfumo wa taarifa ambao sote tunautegemea. Serikali kandamizi zinatumia mbinu katili kuzinyima jamii zao na dunia kwa jumla habari muhimu” , aliongeza.

Ukandamizaji, kuyumba kwa jamii na maandamano katika Mashariki ya Kati kumesababisha waandishi wengi wa habari kufungwa hasa Saudi Arabia ambao idadi yao ilifikia 26 mwaka 2019 ikiiweka sawa na Misri ikiwa ni nchi ya tatu kwa kufunga wanahabari duniani.

Siasa ni sababu kubwa ya

kufungwa kwa wanahabari ikifuatiwa na haki za binadamu na rushwa. Wakati wanahabari wengi waliofungwa duniani wanakabiliwa na mashtaka dhidi ya serikali, idadi ya waliofungwa kwa habari feki imepata kufikia 30; mwaka 2012 ilibaini kuwa ni mwanahabari mmoja tu duniani alikabiliwa na tuhuma

hizo. Nchi kandamizi kama Russia na Singapore mwaka uliopita zimefanya kuwa kosa la jinai uchapishaji wa habari feki.

Orodha ya CPJ ni sehemu tu ya waliomo magerezani kwa kuwa haijumuishi wanahabari waliofungwa ama kuachiwa katika kipindi cha mwaka mzima.

15

Habari

Toleo la 148, Desemba, 2019

Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Kutetea Waandishi wa Habari (CPJ) Simon Joel.

Waandishi 250 wafungwa duniani mwaka wa nne mfululizol Serikali kandamizi zatumia mbinu za kikatili kunyima jamii na

dunia habari muhimu, asema Mkurugenzi Mtendaji wa CPJ

Page 15: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

16

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Habari

Kitabu hiki ni muhimu na cha lazima kwa waandishi wa habari na wahariri kukisoma ili kuelewa takwimu na jinsi ya kuzitumia kwa usahihi katika habari

Page 16: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Na Mwandishi wa Barazani

Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri (TEF) umepitisha mabadiliko

ya katiba kuiwezesha kutimiza masharti ya usajili mpya.

TEF huko nyuma ilisajiliwa kama kampuni lakini mahitaji ya sheria mpya yanataka taasisi kama hizo zisajiliwe kwa masharti mapya vinginevyo zinajifuta.

Katika mkutano mkuu uliofanyika Desemba 9, 2019 katika jengo la mkoa la NSSF Jijini Dar es Salaam wanachama wa TEF kwa kauli moja waliidhinisha marekebisho ya katiba kuisajili kuwa Amana.

Waliokuwa wajumbe wa Bodi ya TEF sasa wanakuwa wadhamini na itakuwa na Sekretarieti na Mtendaji Mkuu.

Aidha TEF itakuwa na Bodi ya Wakurugenzi.

Jambo lingine jipya katika katiba mpya ni kuwa taasisi zinaweza kuwa wanachama wa

TEF. Chombo chochote cha habari

kinachotaka kuwa mwanachama kinawasilisha maombi yake katika TEF kwa maandishi kwa mtendaji wake mkuu.

Kwa upande wa wanachama binafsi, uanachama huo uko wazi kwa mtu yeyote anayetambulika ama ameajiriwa kama mhariri ama mhariri mkuu, mhariri mtendaji, mhariri wa habari, mhariri wa kitengo ama aliyefanyakazi katika tasnia kwa kipindi kisichopungua miaka 10 na mwenye sifa kuwa mhariri.

TEF itakuwa na wanachama washiriki. Shirika la kigeni ama mtu binafsi wa ngazi za juu katika chombo cha habari anaweza kuomba uanachama wa aina hiyo.

TEF mpya pia itakuwa na wanachama wa heshima. Hawa watakuwa wanateuliwa na Mkutano Mkuu.

Mchakato wa kupitisha katiba mpya ulisimamiwa na Kaimu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile ambaye aliwapongeza wajumbe waliohudhuria mkutano

huo kwa kupitisha mabadiliko hayo, hatua itakayoharakisha usajili wa Jukwaa.

Akiwasilisha ripoti kuhusu shughuli za TEF kwa mwaka , Katibu wa TEF, Neville Meena alisema hali katika vyombo vya habari si nzuri kwa kuwa wahariri wengi wamepoteza kazi.

Alisema wahariri wameachishwa katika kampuni za Mwananchi Communications, The Guardian Limited na New Habari.

Pia alisema licha ya matatizo ya kiuchumi, TEF inachechemea kupata mapato kutoka katika miradi inayotekeleza na baadhi ya mashirika kama vile mradi wa watoto na UNICEF.

Hata hivyo baadhi ya wajumbe kwenye mkutano huo hawakupendezwa na ripoti hiyo ya juu juu kuhusu shughuli za Jukwaa na kuhimiza kuwepo taarifa ya kina.

Ripoti ya kina, walisema, itawapa wanachama fursa ya kupitia na kuijadili kwa ukamilifu.

17

Habari

Toleo la 148, Desemba, 2019

TEF yabadili katiba Wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) waliohudhuria mkutano mkuu wa jukwaa hilo wakiwa katika picha ya pamoja.

Page 17: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

mkono mageuzi kuingia vyama vingi, na kukubali kuua taasisi alizoanzisha mwenyewe kwa imani kuwa bila fikra na mawazo mbadala, hakuna demokrasia inayotajwa na katiba ya nchi.

Pamoja na kukubali busara za Baba wa Taifa , tusisahau urithi wa kudumu aliyotuachia – kujikosoa kama nguzo kuu ya demokrasia. Aliandika hata kitabu, Tujisahihishe, kuhakikisha rika zote na zijazo zinapata hekima hiyo kama tunu ya milele. Anayeamini kuwa demokrasia inajengwa bila kujikosoa anakosea, na kwa hakika ni moja ya kazi kuu ya vyombo vya habari, kutoa fursa na jukwaa kwa wananchi kujisahihisha.

Ukosoaji kwenye vyombo vya habari ni wa kudumu, na namna pekee ya kuukwepa ni kutenda majukumu katika kiwango kinachokubalika. Wakati mwingine katika kutafuta kilicho bora zaidi huzua nako malalamiko. Njia pekee ni kuelezea kukwama huko au mabadiliko yoyote kwa uwazi kabisa kupitia vyombo vya habari. Ukosoaji hauna madhara kabisa ikiwa unafanywa kupitia vyombo vya habari. Utafiti ni chanzo muhimu cha habari mpya kwa wanahabari. Katika vyombo vya habari vyenye uwezo, kuna vitengo kamili kwa ajili ya utafiti na taarifa muhimu zenye maslahi kwa umma huibuliwa na kufanya chombo kupendwa na watu.

Uchungu ulikuja wakati sheria ya Takwimu ilipokataza uchapishaji wa data isiyokuwa na ithibati ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Tunakumbuka msukosuko aliopata mkuu wa TWAWEZA Aidan Eyakuze 2018 alipochapisha data kuonesha kuwa upendo kwa Rais umekuwa ukishuka. Hakuna ajuaye ingekuwaje kama data hiyo ingeonesha kuwa mapenzi hayo yameongezeka. Japo baadaye Aidan alisamehewa na washtaki wake COSTECH, Idara ya Uhamiaji ilijiunga hapo na kuendeleza mateso hayo kwa kuanza kufuatilia uraia wake na mengine mengine.

Hii ni mara ya pili taasisi hiyo yenye kutafiti mambo ya elimu inajikuta kwenye mikono ya serikali. Mgongano mkubwa ulikuwa wakati wa utawala wa awamu ya tatu wa Rais Benjamin Mkapa TWAWEZA ,ikiongozwa na Rakesh Rajani, iliposhutumiwa kudhalilisha taifa kwa kuchapisha picha na taarifa zenye kuonesha utoaji elimu ya msingi katika mazingira duni kabisa. Alisamehewa baada ya kuomba

radhi. Neno muhimu hapa ni uzalendo. Tamko hasi, liwe lastahili au sivyo linachukuliwa kuwa ni kosa. Tunahitaji kufahamu vigezo vinavyofanya taarifa au habari kuwa ya kizalendo katika uandishi wa habari.

Tunapenda kurejelea kazi ya vyombo vya habari kama kioo cha jamii. Katika taasisi, dhima huainishwa na kutekelezwa na watu wenye maarifa stahiki, ujuzi na mwelekeo kutosheleza mahitaji ya jamii. Kufanya kazi vizuri inavyotakiwa ni matarajio na ni jambo la kawaida. Jamii inategemea uchunguzi wa vyombo vya habari kuweza kufahamu watu au taasisi ambazo hazitekezi majukumu yao inavyotakiwa.

Kulaumu au kukosoa mtu kwa kutotekeleza majukumu yake ipasavyo, sio kukosa uzalendo kwa vile vyombo vya habari vimeundwa kwa madhumuni hayo. Hatutakiwi kuparaganya dhima ya vyombo vya habari kwa kuvitwisha majukumu kupendezesha nafsi ya mtu. Yanatakiwa kuwa majukumu yanayopendelewa na jamii nzima. Muhimu zaidi ni kwamba lawama haitakiwi kufanywa jinai.

Mwanzoni mwa Disemba 2019, TWAWEZA walitoa ripoti yenye kuonesha umuduji wa elimu katika shule za msingi nchini. Data nyingine ilikuwa hasi na nyingine chanya. Wakati huu uongozi wa TWAWEZA haukupata msukosuko kwa kuwaeleza wananchi ukweli baada ya kulegeza masharti kwenye kanuni zinazohusika. Ni juu ya mamlaka za elimu kurekebisha kasoro zilizoibuliwa baada ya ukweli kufahamika.

Kukumbushwa uozo katika jamii ndiko kunakofanya wabia wa maendeleo – wa ndani na nje ya nchi kuwa macho na hili ni jukumu halali la vyombo vya habari.

Hii inanikumbusha umuhimu wa kupata habari na ni kwa nini watu walipigania kupata sheria ya kuhakikisha wananchi wanapata habari ilivyoainishwa kwenye katiba Kifungu 18(d), “Kila mtu ..(d) anayo

haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii”.

Kupewa taarifa ni haki ya msingi na inatambuliwa vyema na sera ya habari ya 2003 , inayotaja taasisi ambazo kwazo haki hii itatekelezwa: vyombo vya habari, taasisi za mafunzo ya habari na mamlaka za usimamizi. Serikali inatajwa kuwa ndiye mbia mkubwa na inatakiwa iwezeshe wabia wengine kwa nyenzo na mazingira mwafaka ya kisheria ili viweze kutekeleza majukumu yao. Ni vibaya kudharau mahitaji yao hasa yanayohusiana na kujimudu na uendelevu kitaaluma.

Kuwa serikali ya kidemokrasia kunahitaji utekelezaji wa upataji wa habari kwa kuimarisha vyombo vinavyotoa habari kwa umma. Vyombo binafsi bado vinalalamikia mazingira binyifu ya kisheria na sasa hili la kiuchumi kwa kunyimwa matangazo litafanya utendaji wao kuwa mgumu zaidi. Hii inadhoofisha vyombo hivyo kwa faida ya vile vinavyojiita vya ‘kimkakati’. Inaua madhumuni ya upataji wa habari uliokusudiwa kisheria na kikatiba.

Kuhusu vitisho vya Mkurugenzi wa Habari kuwa ameonya mara nyingi vyombo korofi na sasa lazima wakumbane na mkono wa sheria kama hawataacha kunukuu taarifa ambazo zinafahamika na ziko wazi kama hewa tuivutayo, ni aina nyingine ya ukandamizaji. Ni vitisho. Kuonya na kutisha, kunaelimisha?

Hii si hali nzuri kwa jamii iliyo huru na hii sio aina ya uhuru uliotafutwa wakati wa kupata uhuru kutoka kwa wakoloni. Jambo moja ni dhahiri, baadhi ya watendaji hawaelewi maana ya katiba ya nchi. Kama mahakama ziko huru kama katiba inavyotamka, basi vitisho vitaogopwa tu ikiwa mahakama hazitatumiwa ipasavyo. Bado tuna imani na mahakama zetu kama kimbilio la mwisho la kutoa haki.

Maoni

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

18

Inatoka Ukurasa wa 14

Kubana vyanzo vya habari ni unyanyasaji wa taaluma

Page 18: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Na Mwandishi wa Barazani

Hatimaye waandishi wa habari Tanzania wamepata chama cha wa-fanyakazi kilicho hai ku-

fuatia uchaguzi wa viongozi wa chama kipya cha Waandishi wa habari na watumishi wa vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA).

Mwenyekiti mpya wa JOWUTA, Claud Gwandu, alisema katika hotuba yake ya awali kuwa mafanikio ya chama hicho yatategemea waandishi wenyewe.

Alitoa mwito kwa waandishi nchini kote kutumia chama hicho kupigania haki na maslahi yao kwa maendeleo yao kwa jumla.

"Naomba kila mmoja …tushirikiane kujenga JOWUTA na ili kufanikiwa katika suala hili, ni jukumu la kila mmoja wetu kupata wanachama 10 ili kwa pamoja tuweze kupigania haki zetu kisheria”, alisema.

Pia alitoa mwito kwa wanachama kulipa ada zao kila mwezi kuwezesha chama hicho kufanyakazi kwa ufanisi katika kutetea maslahi ya wanachama.

Katika uchaguzi uliofanyika Dodoma Novemba 30, 2019, Gwandu alimpiku Tuma Sitta baada ya kupata kura 30 dhidi ya 17.

Kenneth Ngelesi aliyesimamia uchaguzi huo alimtangaza Gwandu kuwa amechaguliwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa JOWUTA.

Pia alitangaza kuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikuwa na mgombea mmoja - Ramadhan Libenanga ambaye alipata kura 43 wakati nne zilimkataa.

Suleiman Msuya alichaguliwa Katibu Mkuu kwa kupata kura 44 , moja

iliharibika na tatu zilimkataa wakati Said Mmanga ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mpito wa JOWUTA, alichaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu baada ya kupata kura 46 za ndiyo na mbili za hapana.

Maurine Odunga alipata kura 46 za ndiyo na kuwa Mweka hazina wa Chama hicho.

Veronica Ignatus, Mussa Juma na

Saphia Ngalapi walichaguliwa Wadhamini wa chama hicho.

Wanachama 48 wa JOWUTA kati ya 61 waliothibitisha kushiriki walihudhuria mkutano huo wa uchaguzi, walihudhuria.

Usajili wa JOWUTA na uchaguzi wa viongozi wake unafuatia kufutwa kwa chama cha TUJ ambacho hakikuwa kikifanyakazi kutokana na udhaifu wa uongozi..

JOWUTA yachagua viongoziHabari

Toleo la 148, Desemba, 2019

19

Mwenyekiti mpya wa Chama cha Waandishi na Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) Claud Gwandu akizungumza katika mkutano wa uchaguzi wa chama hicho. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Ramadhan Libenanga na kulia ni Katibu Mkuu, Suleiman Msuya.

Na Mwandishi wa Barazani

Uongozi mpya wa Chama cha Waandishi wa Habari na Watumishi wa Vyombo vya Habari (JOWUTA) wametoa

mwito kuntu kwa Jukwaa la Waha-riri Tanzania (TEF) wakihimiza wa-

nahabari kujiunga na kulipa michango yao ya wanachama katika chama hicho kichanga cha wafan-yakazi.

Katibu Mkuu , Selemani Msuya, amewaambia wahariri katika mkutano mkuu wa TEF uliofanyika Desemba 9, 2019 kwamba ni muhimu kila mmoja atimize wajibu wake.

Msuya, mwandishi anayefanyakazi Tanzania Daima alimwomba kila mmoja kuchukulia suala la JOWUTA kama suala linalomhusu.

Kwa JOWUTA kufanyakazi kama chama halisi cha wafanyakazi kinahitajika kuwa na wanachama 500. Hadi sasa kina wanachama 120.

Wanachama wengi zaidi wanahitajika kujiunga chama hicho, Msuya aliwaambia wahariri alipozungumza nao kwa niaba ya Mwenyekiti wa JOWUTA, Claud Gwandu.

Alisema kuwa ada ya kujiunga ni sh. 10,000 na mchango wa kila mwezi wa mwanachama ni sh. 5,000.

Katibu Mkuu JOWUTA atoa mwito kwa wahariri

Page 19: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Na Mwandishi wa Barazani

Waandishi wa habari watatu Christopher Gamaina wa Raia Mwema, Zephania Mandia wa Channel Ten

na Manga Msabaha wa gazeti la Mzawa waliokuwa wakikabiliwa na shitaka la unyang’anyi kwa kutumia nguvu, wako huru baada ya upande wa mashitaka kuomba wafutiwe shi-taka hilo.

Kwa mujibu wa mwandishi Gamaina, baada ya kesi hiyo kutajwa mara kadhaa, upande wa Jamhuri kupitia kwa Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Chacha, uliomba kuondoa/kufuta shitaka hilo mahakamani, ambapo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Magu, Eric Kimaro alikubaliana na ombi hilo, hivyo kutoa uamuzi wa kuwaachia huru Desemba 20, 2019.

Gamaina amemwandikia rasmi Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Kajubi Mukajanga Desemba 30, 2019 kushukuru kwa msaada wa kisheria uliotolewa na Baraza.

“Ninaomba kuwasilisha kwako kama si Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa jumla shukrani nyingi kutokana na msaada wa kisheria mliotupatia kwa kutuwekea mawakili wa utetezi, Linus Amri na Mutalemwa waliotukatia rufaa baada ya kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela pamoja na wenzangu, Zephania Mandia na Manga Msalaba, Aprili 18, 2019.

“ Hukumu hiyo ilitokana na Kesi Namba 11/2018 ya unyang’anyi wa kutumia nguvu tuliyobambikwa na Polisi kutokana na utekelezaji wa majukumu yetu ya uandishi wa habari” ameeleza Gamaina.

Kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Edmund Kente.

Gamaina ameeleza kuwa baada ya mawakili, Amri na Mutalemwa kuwakatia rufaa kupinga hukumu

hiyo, kesi hiyo ilisikilizwa na Jaji Mohamed Siyani katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, ambapo Julai 27, 2019 Jaji huyo alitoa uamuzi wa kufuta kifungo hicho na kuelekeza kesi irudi kusikilizwa upya kwa hakimu mwingine katika Mahakama ya Wilaya ya Magu.

Kutokana na uamuzi huo, Gamaina amesema walitolewa katika Gereza Kuu Butimba mkoani Mwanza na kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Magu Agosti 5, 2019 ambapo waliachiwa kwa dhamana kusubiri kesi hiyo ianze kusikilizwa upya.

“Ni ukweli usiopingika kwamba hatua hiyo ya mimi na wenzangu kuachiwa huru imetokana na utetezi mahiri wa mawakili Amri na Mutalemwa sambamba na Mwenyezi

Mungu kwa upande mwingine”, ameeleza Gamaina katika barua ya kushukuru Baraza la Habari.

“ Nikiwa nimejawa furaha ya kuachiwa huru, ninarudia kuishukuru ofisi yako [MCT] kwa dhati ya moyo kwa kukubali kugharimia mawakili hao kwa ajili ya kututetea hadi kutuwezesha kuachiwa huru” ameeleza.

Ametoa mwito kwa MCT iendelee na moyo huo wa kutoa msaada wa kisheria kwa waandishi wa habari wanaopata matatizo ya kuonewa na kushitakiwa kutokana na utekelezaji wa majukumu ya uandishi wa habari nchini.

Gamaina amemaliza barua hiyo kwa kusema“Mungu wabariki wanahabari, bariki MCT, bariki Tanzania, Amina”.

Waandishi wafutiwa kesi ya unyang’anyi na kuachiwa huru

Wanahabari Christopher Gamaina(kushoto) na Zephania Mundia (kulia) wakiwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi ya Mwanza (MPC), Edwin Soko baada ya kuachiwa kwa dhamana.

20

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

l Waishukuru MCT kwa msaada wa kisheria

Page 20: Mwaka wa mafanikio - MCT...Bunge Novemba 5, na kuidhinishwa haraka haraka na Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2016. Kukabiliana na sheria hiyo mpya ya habari katika

Na Mwandishi wa Barazani

Juhudi zaidi zitawekwa ili ku-fanikisha kupatikana sheria mpya ya habari ya Zanzibar, wajumbe wa Mkutano Mkuu

wa 21 wa Baraza la Habari Tanza-nia (MCT) wameelezwa.

Baraza ambalo limehusika katika uragbishi na uzengezi wa sheria hiyo mpya ya habari Zanzibar tangu 2010, mwaka 2019 lilitekeleza shughuli kadhaa kufanikisha lengo hilo.

Ripoti ya Katibu Mtendaji wa Baraza katika mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam Novemba 21, imeeleza kuwa miongoni mwa shughuli zilizofanywa na Baraza ni pamoja na kuwasilisha mada kuhusu sheria ya habari ya Zanzibar na umuhimu wa kuharakisha mchakato wa sheria mpya ya habari

Visiwani wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Mei 3, 2019.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa moja ya maazimio yaliyofikiwa wakati wa maadhimisho hayo ni kufuatilia kila hatua za mchakato huo ili kufanikisha kupatikana sheria hiyo.

Ofisi ya MCT ya Zanzibar ilimpakazi mwanasheria kupitia mapendekezo ya muswada wa sheria hiyo mpya ili kuwezesha Baraza kuweka mchango wake kwa Wizara baada ya kuhudhuria mkutano uliofanyika Juni 3 na 4 ulioitishwa na Idara ya Habari ambao ajenda yake kuu ilikuwa kujadili muswada wa sheria hiyo mpya.

Mwezi mmoja baadaye Julai 9, 2019 na Julai 28, 2019 Baraza liliandaa mkutano na Kamati ya Zanzibar ya Sheria mpya ya habari ikijumuisha WAHAMAZA, TAMWA Zanzibar, Kituo cha Sheria cha

Zanzibar, Klabu za waandishi za Pemba na Zanzibar.

Matokeo ya Mkutano huo ni kuhitajika kuwepo na uwakilishi mpana kujumuisha wadau wengi zaidi wakiwemo wawakilishi wa serikali ili kupata maoni zaidi ya jinsi ya kufanikisha suala hilo.

Waziri wa Habari, Utalii na mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo aliiambia MCT wakati wa mkutano wa Oktoba 21, 2019 kwamba Wizara yake imekamilisha ngwe yake na inatarajia kuwasilisha muswada kwenye kamati ya makatibu wakuu wa wizara zote kwa michango zaidi.

Zanzibar imepanga kufuta sheria mbili – Sheria ya Tume ya Utangazaji ya 7 ya mwaka 1997 na Sheria ya Usajili wa Magazeti na Vitabu namba 5 ya mwaka 1988 kuwezesha kuwa na Sheria mpya ya Huduma ya Vyombo vya Habari.

21

Habari

Toleo la 148, Desemba, 2019

Meneja Programu wa Baraza la Habari Tanzania, David Mbulumi akitoa taarifa katika mkutano mkuu wa Baraza la Habari Tanzania(MCT) uliofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 29,2019.

Juhudi zaidi za kupata sheria mpya ya habari Z’bar