12
Novemba 2012 – Septemba 2013 Keep Your Promises ni kampeni ya kimataifa inayowaita watoa maamuzi kutimiza ahadi walizotoa kuhusu udhibiti afya na maji! ZANA YA KAMPENI www.keepyourpromises.org ON SANITATION AND WATER

Novemba 2012 – Septemba 2013 - End Water Poverty · ni pamoja na ahadi ya kuunda bajeti ya kando, na kuweka angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa udhibiti wa afya na usafi

  • Upload
    others

  • View
    2

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Novemba 2012 – Septemba 2013 - End Water Poverty · ni pamoja na ahadi ya kuunda bajeti ya kando, na kuweka angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa udhibiti wa afya na usafi

Novemba 2012 – Septemba 2013

Keep Your Promises ni kampeni ya kimataifa

inayowaita watoa maamuzi kutimiza ahadi walizotoa kuhusu udhibiti afya na maji!

ZANA YA KAMPENI

www.keepyourpromises.org

ON SANITATION AND WATER

Page 2: Novemba 2012 – Septemba 2013 - End Water Poverty · ni pamoja na ahadi ya kuunda bajeti ya kando, na kuweka angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa udhibiti wa afya na usafi

Keep Your Promises ni kampeni ya kimataifa inayowaita watoa maamuzi kutimiza ahadi walizozitoa kuhusu udhibiti afya na maji!

Watoa maamuzi wametoa ahidi nchini, kitaifa, kieneo na duniani kupata maji masafi ya kunywa na kudhibiti afya kwa nchi na jamii masikini sana duniani – lakini maneno hayatoshi! Ahadi hizi lazima zitimizwe ili kukomesha janga la kudhibiti afya na maji duniani.

Zana hii itakupa maelezo na msukumo unaohitaji ili kujiunga na kampeni. Kwa kuhusika, unaweza kuwaunganisha mamia ya maelfu ya watu duniani kote ambao wanachukua hatua ili kuhakikisha kwamba udhibiti msingi wa afya na maji masafi yanapatikana kwa KILA MTU!

Kampeni ya Keep Your Promises itaanza Novemba 2012 na itadumu kwa mwaka mmoja. Wafanya kampeni duniani watakuwa wakichukua hatua mwaka mzima na kuwakumbusha wanasiasa wao watimize ahadi walizotoa kuhusu udhibiti wa afya na maji.

Itakuwa mnamo na karibu na tarehe mbili muhimu, Siku ya Choo Duniani mnamo tarehe 19 Novemba 2012 na Siku ya Maji Duniani mnamo tarehe 22 Machi 2013, wafanya kampeni watakuja pamoja na kuungana ili kupanga hatua za kampeni ya halaiki duniani katika nchi za dunia. Mamia ya maelfu ya watu watachukua hatua katika tarehe hizi muhimu za kampeni ili kuhakikisha sauti zao zimesikiika!

Kampeni ya Keep Your Promises itafikia kilele chake katika Mkutano wa MDG kule New York mnamo September 2013, wakati maombi ya duniani ya Keep Your Promises yatawasilishwa kwa wafanya maamuzi ili kuwaomba wachukue hatua ili wahakikishe udhibiti afya na maji kwa wote.

Kampeni ya Keep Your Promises ni ya nchini, kitaifa, kieneo na ya duniani. Ahadi zimetolewa katika viwango vyote na tunadai kuona ahadi hizo zikitimizwa.

KEEP YOUR PROMISES KUHUSU UDHIBITI AFYA NA MAJI

UCHUNGUZI: KENYA

Katika Mkutano wa AfricaSan, Mbunge wa Kenya wa Maji na Umwagiliaji aliahidi mgao wa angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa maji na udhibiti afya. Baaadaye, katika Mkutano wa Ngazi za Juu wa Udhibiti afya na Maji katika mwaka wa 2012, serikali ya Kenya iliahidi pia kwamba watu milioni 20 zaidi wataweza kupata udhibiti wa afya na maji ya kunywa kufikia 2015.

Je, serikali inatimiza ahadi zake?

End Water Poverty inafadhiliwa na WaterAid, Tearfund na Dutch WASH Alliance

Page 3: Novemba 2012 – Septemba 2013 - End Water Poverty · ni pamoja na ahadi ya kuunda bajeti ya kando, na kuweka angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa udhibiti wa afya na usafi

Licha ya maendeleo ya miaka michache iliyopita, watu bilioni 2.5 bado wanaishi bila choo kisafi na watu milioni 783 bado wanakosa kupata maji masafi1. Ukosefu wa huduma kama hizo muhimu huunda shida kuu kwa nchi zinazokua – kwa hivyo kudhoofisha mifumo ya afya, elimu, maendeleo ya kiuchumi, na maendeleo ya usawa wa kijinsia.

Karibu watoto 2,000 wanakufa kila siku kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuiliwa yanayohusiana na maji, kwa hivyo kuifanya ya pili inayoua sana watoto duniani2. Janga hili linaathiri pia uchumi ya nchi zinazokua – katika mataifa ya Sahara kusini, inakadiriwa asilimia 5 ya mapato ya serikali hupotea kwa sababu ya magonjwa na vifo vinavyosababishwa na maji machafu na udhibiti duni wa afya3. Lakini janga hili linaweza kutatuliwa! Janga la maji na udhibiti afya linasababishwa kimsingi na ukosefu wa hiari ya kisiasa. Kushinda janga hili kunahitaji serikali kuu na ya mitaa kutimiza neno lao na kutekeleza ahadi walizotoa kuhusu udhibiti afya na maji. Keep Your Promises!

1 UNICEF, Water, Sanitation and Hygiene Annual Report, 2008 2 WaterAid 2012/WHO 2008/The Lancet 20123 UNDP, Ripoti ya Maendeleo ya Wanadamu, 2006

NINAWEZAJE KUHUSIKA?

ORODHA YA UKAGUZI YA HATUA!

2

1

3

4

5

6

Pakua maombi ya jumla kutoka kwa www.keepyourpromises.org na uanze kukusanya saini

Fanya Usikilizaji wa Keep Your Promises mnamo na karibu na Siku ya Choo Duniani, 19 Novemba 2012

Panga Matembezi nchini na uhusike katika Matembizi ya Duniani ya Maji na Udhibiti afya mnamo na karibu na Siku ya Maji Duniani, 22 Machi 2013

Kagua maelezo ya nchi yako kwenye www.WASHwatch.org na uongeze visasisho vipya kuhusu udhibiti afya na maji

Je, kuna uchaguzi wa nchini au wa kitaifa unaokuja katika eneo lako? Panga kampeni ya uchaguzi kuhusu udhibiti afya na maji na uhakikishe wagombeaji wamegundua!

Jiunge na majadiliano ulimwenguni kuhusu ni nini kinachopaswa kubadilisha Malengo ya Maendeleo ya Mileniamu katika mwaka wa 2015.

WATU BILIONI 2.5 BADO WANAISHI BILA CHOO SALAMA

WATU MILIONI 783 BADO WANAKOSA KUPATA MAJI MASAFI

JANGA LA UDHIBITI AFYA NA MAJI

Page 4: Novemba 2012 – Septemba 2013 - End Water Poverty · ni pamoja na ahadi ya kuunda bajeti ya kando, na kuweka angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa udhibiti wa afya na usafi

TIMIZA AHADI HIZIWatoa maamuzi tayari wametoa ahadi nyingi za kupata maji na udhibiti afya duniani katika makubaliano ya kitaifa, kieneo na ya kimaitafa. Sasa ni wakati wa kubadilisha maneno haya kuwa hatua na kufanya maendeleo ya kweli kuwadia kutoa udhibiti afya na maji kwa wote, ikiwa ni pamoja na jamii masikini na zilizotengwa.

AHADI ZILIZOTOLEWA KUHUSU UDHIBITI AFYA NA MAJI ZINAJUMUISHA:

Nchi 32 zilitia saini Azimio la eThekwini mnamo mwaka wa 2008. Walitoa ahadi kadhaa ikiwa ni pamoja na ahadi ya kuunda bajeti ya kando, na kuweka angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa udhibiti wa afya na usafi.

3 Azimio la eThekwini na mpango wa hatua

wa AFRICASAN

Keep Your Promises!

MDG ina ahadi ya kupunguza nusu, kabla ya 2015, mgao wa watu bila maji masafi ya kunywa na udhabiti msingi wa afya. Ijapokuwa lengo la maji limefikiwa, watu milioni 783 bado wanakosa maji salama. Kwa sasa, lengo la udhibiti afya bado halijafikiwa, na kwa kiwango cha sasa cha maendeleo itakuwa zaidi ya miaka mia mbili hadi lengo la MDG lifikiwe katika mataifa ya Sahara Kusini.

Malengo ya Maendeleo ya

Mileniamu (MDGs)

Keep Your Promises!

Nchi zinazokua, nchi zinazofadhili na benki za maendeleo zilihusika katika Mkutano wa kihistoria wa Ngazi za Juu mnamo Aprili 2012. Kila mmoja alichapisha taarifa inayoorodhesha hatua watakazochukua kuhusu maji na udhibiti afya kati ya miaka miwili ijayo. Ng'amua zaidi katika www.keepyourpromises.org na www.sanitationandwaterforall.org.

Mkutano wa Ngazi za Juu wa Udhibiti afya na Maji

kwa Wote (SW) 2012

Keep Your Promises!

2

1

Jinsi unavyohusika katika kampeni ya Keep Your Promises kutategemea na ahadi ulizotoa katika eneo au nchi yako. Ahadi kuhusu udhibiti afya na maji iliyotolewa na nchi fadhili kama vile Uholanzi itakuwa tofauti sana na ahadi zilizotolewa na serikali kuu ya Ethiopia. Huenda pia serikali yako imetoa ahadi kadhaa katika viwango vya kieneo au kitaifa. Kwa mfano, nchi nyingi za Afrika zilitia saini Azimio la eThekwini na nchi kadhaa za Asia Kusini zilitia saini Azimio la Kolombo. Katika kiwango cha nchini, manispaa au kijiji, huenda ahadi zilitolewa kuhusu udhibiti afya na maji – pengine wakati wa Matembezi ya Duniani ya mwaka uliopita ya Maji na Udhibiti afya, au katika mkutano wa baraza la mtaa.

Page 5: Novemba 2012 – Septemba 2013 - End Water Poverty · ni pamoja na ahadi ya kuunda bajeti ya kando, na kuweka angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa udhibiti wa afya na usafi

Utambuaji wa maji na udhibiti afya kama haki ya binadamu: Mnamo mwaka wa 2012 Baraza Kuu la UN na Baraza la Haki za Binadamu la UN lilichukua maamuzi ya kutambua maji masafi ya kunywa na udhibiti afya kama haki msingi za binadamu. Uchunguzi wa hivi karibuni ulionyesha karibu asilimia 80 ya nchi zilizohusika zilitambua kabisa haki ya maji na zaidi ya asilimia 50 walitambua kabisa haki ya udhibiti afya4. Hata hivyo mengi yanahitajika kufanyika ili kuhakikisha kwamba serikali zote zinatambua haki ya maji na udhibiti afya, na kwamba wabadilishe haya kuwa hatua. Ng'amua zaidi katika www.righttowater.info.

4 Ripoti ya GLAAS, 2012

Katika mkutano wa SACOSAN IV, Nchi 8 za Asia ya Kusini zilijitolea kutoa udhibiti afya kwa watu milioni 700 wa Asia Kusini ambao bado wanaenda choo mahali wazi. Waliahidi kuongeza ufadhili wa udhibiti afya na usafi na kuweka bajeti mahususi ya mipango ya udhibiti afya na usafi.

SACOSAN IV na Azimio la

Kolombo

Keep Your Promises!

4Katika mwaka wa 2007, nchi 17 kutoka Marekani Latino zilitia saini azimio la LatinoSan na zikajitolea kupatia kipaumbele udhibiti afya katika sera za maendeleo ya taifa na kuimarisha ushirikiano wa serikali za ndani.

LatinoSan

Keep Your Promises!

5

Nchi nyingi zinazokua na zinazofadhili pia zimetoa ahadi zao na mipango ya kuboresha matoleo ya maji, udhibiti afya na usafi. Serikali za mitaa na mamlaka ya mji au kijiji huenda pia zimetoa ahadi za kujenga vyoo, kuboresha utoaji maji au kutoa vyoo vya kando vya wavulana na wasichana katika shule ya hapo.

Ahadi za kitaifa na mtaa

Keep Your Promises!

6 Ng'amua zaidi kuhusu ahadi serikali yako kuu imetoa kuhusu udhibiti afya na maji, katika www.keepyourpromises.org.

Tunakaribisha ahadi zote zilizotolewa na watoa maamuzi lakini nyingi kati ya hizo bado hazijatekelezwa au kutimizwa. Kusuluhisha janga la udhibiti afya na maji kunahitaji watoa maamuzi kutimiza neno lao na kutekeleza ahadi walizotoa.

Ni wakati wa kuelezea serikali kuu na za mtaa:

“Timiza Ahadi Zako kuhusu Udhibiti afya na Maji!”

Page 6: Novemba 2012 – Septemba 2013 - End Water Poverty · ni pamoja na ahadi ya kuunda bajeti ya kando, na kuweka angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa udhibiti wa afya na usafi

KALENDA YA KAMPENI 22 MACHI

2013:

SIKU YA MAJI DUNIANI Jiunge na Matembezi ya Duniani ya Maji na Udhibiti afya yanayofanyika tarehe 16 hadi 24 Mach 2013 kwa kupanga Matembezi katika eneo lako. Mwalike mtoa uamuzi wako na umuulize atimize ahadi alizotoa kuhusu udhibiti afya na maji!

Mwaka uliopita zaidi ya watu 370,000 kutoka nchi 70 walihusika katika Matembezi ya Duniani ya Maji na Udhibiti afya – tufanye mwaka huu uwe mkubwa na bora zaidi! Tuelezee ni wapi na lini utatembea au utapata Matembezi karibu na wewe kwenye tovuti: www.worldwalksforwater.org.

19 NOVEMBA 2012:

SIKU YA CHOO DUNIANI NA

UZINDUZI WA MAOMBI YA KIMATAIFA YA TIMIZA AHADI ZAKO Mnamo na karibu na Siku ya Choo Duniani, 19 Novemba 2012, Usikilizaji wa Timiza Ahadi zako utafanyika katika nchi na jamii kote duniani. Usikilizaji huu ni midahalo ya umma, mazungumzo au mikutano ambayo wafanya kampeni watawaomba watoa maamuzi kutimiza ahadi nyingi za nchini, kitaifa na kieneo walizotoa ili kupata udhibiti afya, maji na usafi kwa raia wao.

Maafisa wa mtaani, wafanyikazi wa umma, mawaziri wa serikali na watoa maamuzi wengine wataulizwa kuripoti maendeleo waliyoyafanya kuhusu ahadi zao za udhibiti afya, maji na usafi na kushiriki mipango yao ya kuhakikisha ahadi zao zimezingatiwa na malengo yamefikiwa.Usisitizaji sio kuwaomba watoa maamuzi kutoa ahadi mpya, lakini kuwaomba waonyeshe maendeleo wazi kuwadia malengo ambayo wameyaweka tayari.

Je, mtoa uamuzi wako wa nchini au wa kitaifa ametoa ahadi ya kuboresha hali ya udhibiti afya, maji na usafi katika eneo au nchi yako?

Panga Usikilizaji ili uwaulize kuhusu maendeleo yako kuwadia ahadi hii na uwakumbushe wahakikishe ahadi hii imetimizwa. Pakua zana yenye mawazo na vidokezi vingi vya kupanga Usikilizaji wako mwenyewe katika www.keepyourpromises.org.

Siku ya Choo Duniani itashuhudia pia uzinduzi rasmi wa maombi ya duniani ya Timiza Ahadi Zako! Pakua ombi kutoka kwa www.keepyourpromises.org na uanze kukusanya saini leo!

Kagua tovuti rasmi ya

Siku ya Choo Duniani katika www.worldtoiletday.org ili ujifunze, ushiriki na

uchukue hatua ya udhibiti afya. Tovuti hiyo inaalika kila mtu

kuhusika katika mada ya mwaka huu “Ninajali, je

wewe?”

Page 7: Novemba 2012 – Septemba 2013 - End Water Poverty · ni pamoja na ahadi ya kuunda bajeti ya kando, na kuweka angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa udhibiti wa afya na usafi

Tumia muda huu kukusaidia kupanga kampeni yako. Tumejumuisha tarehe muhimu kwa ajili ya shajara yako!

Kampeni ya Keep Your Promises itafikia kilele katika Mkutano wa UN MDG mnamo Septemba 2013, wakati viongozi wa duniani watakutana kuhakiki Malengo ya Maendeleo ya Mileniamu na kuweka mpangilio mkuu wa maendeleo ambao utatumika. Tutawasilisha ombi letu katika Mkutano huu na kuwaomba watuoa maamuzi wote kutimiza ahadi

zao kuhusu udhibiti afya na maji na kuongezea juhudi za kuhakikisha udhibiti afya na maji salama ya kunywa kwa kila mtu.

Kuwadia Septemba 2013, kila mtu atajiunga pamoja katika tarehe mbili muhimu: Siku ya Choo Duniani mnamo tarehe 19 Novemba 2012 na Siku ya Maji Duniani mnamo tarehe 22 Machi 2013. Kwa mwaka uliosalia, tumia nyenzo hizi ili kuwafanya watoa maamuzi wako kuwajibika kuhusu tarehe muhimu katika nchi yako. Je, ni ahadi zipi walizotoa kuhusu udhibiti afya na maji? Je, wamezitimiza?

23 SEPTEMBA 2013: MKUTANO WA UN MDG KUHUSU MPANGILIO WA MAENDELEO WA BAADA YA 2015 Kampeni hii itafikia kilele katika mkutano huu na kuwasilishwa kirasmi kwa ombi kwa viongozi wa ulimwengu kule New York. Hakikisha umeongeza saini za ombi lako kwa jumla kuu ili tuweze kuwaeleza watoa maamuzi kwamba mamia ya maelfu ya watu

duniani kote wanataka kuwaona wakitimiza ahadi zao kuhusu udhibiti afya na maji.

Katika mkutano huu, viongozi wa duniani watakuwa wakijadili mipango mipya ya

maendeleo ya kijumla baaada ya muda wa MDG kuisha katika mwaka wa 2015. Tunataka kuhakikisha udhibiti afya na maji yamepewa uzito unaofaa. Tutawaomba watoa maamuzi kufanya kazi ili kuhakikisha kwamba kila

mmoja, kila mahali anaweza kupata udhibiti afya na maji salama ya kunywa.

Unaweza kukusanya saini

za ombi la Timiza Ahadi Zako mwaka mzima.

Tumia maombi hayo katika nchi yako ili kuwaomba wanasiasa wako kutimiza

ahadi zao!

Kisha tutahesabu ni watu wangapi duniani wametia saini maombi na tuhakikishe viongozi wa duniani wamejua katika

Mkutano wa MDG kule New York. Tutawaita watoa maamuzi wote, kila mahali kutimiza ahadi zao

kuhusu udhibiti afya na maji.

Page 8: Novemba 2012 – Septemba 2013 - End Water Poverty · ni pamoja na ahadi ya kuunda bajeti ya kando, na kuweka angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa udhibiti wa afya na usafi

HATUAZA KAMPENI UNAZOWEZA KUFANYA MWAKA MZIMAJanga la maji na udhibiti afya limeendelea kwa muda mrefu sana – ni wakati wa kuuliza serikali kuu na za mitaa kutimizia ahadi zaoKampeni ya The Keep Your Promises itaendeshwa kwa mwaka mzima na kilele chake kitakuwa Septemba 2013, wakati tutawasilisha maombi ya jumla kwa viongozi wa duniani. Wafanya kampeni duniani kote watakuja pamoja na kuchukua hatua Siku ya Choo Duniani na Siku ya Maji Duniani, lakini zile siku zingine za mwaka huenda ukataka kuzingatia ahadi na tarehe muhimu ambazo ni maalum kwa nchi yako au eneo lako.

KUKAMPENI WAKATI WA CHAGUZI Je, kuna uchaguzi wa manispaa, eneo au kitaifa unaofanyika katika nchi yako wakati wa kipindi hiki? Wanasiasa wanahitaji kupiga kura ili kuchaguliwa, kwa hivyo chaguzi ni wakati mzuri wa kupata ahadi na kusisitiza mahitaji ya maji na udhibiti afya katika ajenda ya kisiasa. Tumetengeza Zana ya Uchaguzi ya kukusaidia kufanya hivyo. Zana hiyo hutoa mwongozo tondoti wa upangaji, utengenezaji, na utekelezaji wa kampeni nzuri ya kufanya wanasiasa kukaa na kuzingatia! Ipakue kutoka www.keepyourpromises.org na uanze leo kampeni yako ya uchaguzi ya Timiza Ahadi Zako!

WASHwatch Tovuti ya www.WASHwatch.org ni zana ya mtandaoni ya kufuatilia sera ya serikali na ahadi za bajeti kuhusu maji na udhibiti afya. Tovuti hii rahisi kutumia ni njia nzuri ya kukagua kama serikali inatimiza ahadi zake! Ina maelezo mapya kuhusu viwango vya kufikia maji na udhibiti afya na visasisho kuhusu mgao wa bajeti. Mtu yeyote anaweza kuongeza maelezo na kuwacha maoni kwenye tovuti hii. Kagua visasisho vipya kuhusu ahadi ya nchi yako na ung'amue ni maendeleo gani yaliyofanywa! Unaweza kupata mwongozo wa kutumia WASHwatch katika www.keepyourpromises.org.

BAADA YA 2015 Malengo ya Maendeleo ya Mileniamu (MDG) yanaisha muda wake katika mwaka wa 2015 na hakuna uamuzi uliofanywa kuhusu itakayoibadilisha: Huenda kukawa na malengo tofauti yaliyowekwa, au hata mpangilio mpya wa maendeleo. Mchakato wa UN wa kuunda mpangilio wa baada ya 2015 unaendelea kwa sasa, na tunahitaji kuhakikisha kwamba sauti ya raia inasikiika ili maji na udhibiti afya upate uzito unaofaa. Ng'amua zaidi kuhusu jinsi ya kuhusika katika mashauriano ya UN kuhusu mpangilio wa baada ya 2015 katika www.keepyourpromises.org.

Page 9: Novemba 2012 – Septemba 2013 - End Water Poverty · ni pamoja na ahadi ya kuunda bajeti ya kando, na kuweka angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa udhibiti wa afya na usafi

VIDOKEZO VYA KAMPENISOMANi muhimu kujua ni ahadi zipi serikali yako ya mtaa au ya kitaifa ilitoa ili uweze kuifanya iwajibike. Huenda waliahidi kutumia asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa maji na udhibiti afya, kwa mfano, au pengine walijitolea kuongeza upatikanaji wa udhibiti afya katika maeneo ya mashambani kwa asilimia 30. Angalia vijipicha vya nchi vinavyopatikana kutoka kwa www.keepyourpromises.org. Punde tu unapojua ahadi zilizotolewa, unaweza kuangalia kwamba serikali yako inafanya kazi kuwadia kuzitimiza.

KUWA KATIKA VYOMBO VYA HABARIVyombo vya habari ni muhimu katika kuhakikisha kwamba kampeni imefanikiwa, kwa hivyo hakikisha hatua zako ziko kwenye habari kwa kutuma ripoti kwa gazeti la eneo lako au idhaa ya redio. Watoa maamuzi wa eneo lako watafurahia kuonekana kwenye vyombo vya habari ikiwa itamaanisha umaarufu bora kwao – na unaweza kuitumia kama nafasi ya kuwaomba hadharani wadhibitishe upya ahadi zao za udhibiti afya na maji!

NENDA MTANDAONIKampeni ya dijitali ni njia nzuri ya kueneza ujumbe wa Timiza Ahadi Zako na kuunganika na wafanya kampeni wengine duniani kote. Tumia vyombo vya habari vya jamii kama vile Facebook na Twitter kutangaza matukio yako na kuwafikia wasaidizi. Unganika na kampeni ya Timiza Ahadi Zako katika: www.twitter.com/WASHpromises na www.facebook.com/keepyourWASHpromises ili ufuate visasisho vipya vya kampeni na ushiriki hatua zako za kampeni.

UCHUNGUZI: UHOLANZI

Waziri wa Uholanzi wa Mambo ya Ulaya na Ushirikiano wa Kimataifa Ben Knapen alitangaza uvumbuzi mpya kati ya Uholanzi na Uingereza katika Mkutano wa Nganzi za Juu wa SW mnamo Aprili 2012, ambao utaleta maji na udhibiti afya kwa watu wengine zaidi milioni 10 katika nchi tisa katika Afrika Magharibi na ya Kati. Omba serikali ya Uholanzi itimize ahadi zao kuhusu udhibiti afya na maji!

UCHUNGUZI: PAKISTANI• Serikali ya Pakistani imeahidi kuboresha ufikiaji wa

udhibiti afya kwa watu milioni 20 kabla ya 2015 katika Mkutano wa Ngazi za Juu wa SWA mnamo Aprili 2012.

• Kwa kuongezea, serikali iliahidi kuanzisha Jopo maalum kuhusu udhibiti afya mashambani na mjini kabla ya Desemba 2012 na kuanzisha mpangilio wa kitaifa wa ufuatiliaji kabla ya 2013.

• Kama mtia saini Azimio la Kolombo, Pakistani imeahidi pia kuhakikisha kwamba kila shule mpya na iliyopo ina vyoo vinavyofanya kazi, na vinavyofaa watoto, zingine za kando za wasichana na wavulana. Omba serikali kutimiza ahadi zake!

Page 10: Novemba 2012 – Septemba 2013 - End Water Poverty · ni pamoja na ahadi ya kuunda bajeti ya kando, na kuweka angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa udhibiti wa afya na usafi

Ombi hili litawaomba watoa maamuzi wote kutimiza ahadi zao za kuchukua hatua ya kutamatisha janga la maji na udhibiti afya, na kufikia udhibiti afya na maji kwa wote.

Ombi hili litawasilishwa kwa viongozi wa duniani katika Mkutano wa MDG mnamo Septemba 2013. Lakini hiyo sio yote! Unaweza pia kutumia ombi hili katika nchi yako mwenyewe ili kulenga watoa maamuzi wako.

Unaweza kuendelea kukusanya saini hadi wakati wa Mkutano wa MDG mnamo Septemba 2013!

Tukusanye nyingi kama tuwezavyo na tuwaonyeshe watoa maamuzi kwamba dunia inatazama!

Waulize watu katika familia yako, shirika na jamii ya eneo lako kutia saini. Unaweza pia kumuuliza mwanasiasa wako. Pakua ombi kutoka www.keepyourpromises.org.

Je, nifanye nini ninapokusanya saini?Wasilisha ombi kwa mtoa maamuzi wa eneo au taifa lako na uwaombe watimize ahadi zao kuhusu udhibiti afya na maji!

Tufahamishe:• Je, ni watu wangapi hadi sasa wametia saini ombi katika nchi yako.• Iwe ulibinafsisha ombi na kuliwasilisha kwa mtoa uamuzi katika nchi yako.

Tuelezee ni ahadi gani ya udhibiti afya na maji uliwaomba watekeleze.

Tufahamishe katika: www.keepyourpromises.org. Kisha tutakuongeza kwenye kihesabio chetu ambacho kinaonyesha idadi ya watu duniani ambao wamechukua hatua katika kuunga mkono Timiza Ahadi Zako. Tunavyokusanya zaidi, ndivyo wanasiasa duniani kote wana uwezekano wa kutusikiliza!

Unaweza kupakua ombi na kisha ulihariri ili ulifanye linalofaa maudhui ya eneo au taifa lako!

Jumuisha mahitaji yako mwenyewe ya kampen katika ombi, kwa mfano ukiomba kutengenezwa kwa vyoo katika mji au kijiji chako, au kuongeza mgao wa mapato ya serikali yanayotumiwa kuhusu udhibiti afya na maji. Kisha unaweza kukusanya saini katika jamii ya eneo lako na uwasilishe ombi kwa mtoa maamuzi wa eneo au taifa lako.

JE, NI NINI?

OMBI

ITATUMIKA AJE?

NA USIKOME HAPO!

KU

SAN

YA

SAIN

I

BINAFSISHA OMBI NA ULITUMIE

KATIKA NCHI YAKO

TIMIZA AHADI ZAKO

Page 11: Novemba 2012 – Septemba 2013 - End Water Poverty · ni pamoja na ahadi ya kuunda bajeti ya kando, na kuweka angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa udhibiti wa afya na usafi

MATUMIZI BORA YA FEDHA

Ufadhili wa udhibiti afya na maji unahitaji kuwa umelengwa vyema zaidi ili kuhakikisha kwamba nchi masikini na jamii zinazoathirika sana zimefikiwa. Hii inamaanisha kuhakikisha kwamba serikali zinatumia pesa vizuri zaidi, na kupatia kipaumbele maeneo magumu kuyafikia (kama vile maeneo ya mashambani) katika nchi ambazo hazijaendelea kabisa.

FANYA UDHIBITI AFYA NA MAJI KIPAUMBELE ZAIDI YA 2015

Malengo ya Maendeleo ya Mileniamu yanaisha muda wake mwaka wa 2015, na kwa sasa mipango ya maendeleo ambayo yataifuata hayajaamuliwa. Timiza Ahadi Zako inaomba udhibiti afya na maji kuwa kipaumbele kitaifa, kieneo, na duniani baada ya 2015.

PESA ZAIDI Ufadhili zaidi unahitaji ili kuwafikia watu zaidi na huduma za udhibiti afya na maji salama. Watoa maamuzi wameahidi kuongeza ufadhili ili kufikia watu zaidi na huduma hizi lakini kwa sasa tunahitaji kuwafanya wawajibike na tuhakikishe kwamba wanatimiza ahadi zao! Thawabu ni kubwa – kwa kila $1 iliyowekezwa katika maji na udhibiti afya, wastani wa $4 hurejeshwa katika uzalishaji ulioongezeka5.

BORESHA UWAZI

Serikali kuu zinahitaji kuwa wazi zaidi kuhusu kiwango cha pesa wanachokitumia kwa udhibiti afya na maji. Zinahitaji pia kuifanya kuwa rahisi kufuatilia maendeleo yanayofanywa, ili wafanya kampeni waweze kusema kirahisi ikiwa serikali inatimiza ahadi zake.

TIMIZA AHADI ZAKO KUHUSU UDHIBITI AFYA NA MAJI:JE, NI NINI TUNACHOKITAKA?Komesha Umasikini wa Maji inaomba kubadilishwa kwa hatua kutoka kwa serikali zote ili kutimiza ahadi zao za kuboresha ufikiaji udhibiti wa afya na maji. Kwa kuongezea, tunaomba serikali kwenda zaidi ya ahadi hizi na kufanya kazi kuwadia kufikia ufikiaji wa kijumla wa udhibiti msingi wa afya na maji masafi ya kunywa.

Kampeni ya The Keep Your Promises ina mahitaji 4 kuu:

Unaweza kutumia mahitaji haya manne ya kampeni wakati unakutana na mwanasiasa wa eneo lako au afisa wa serikali. Kumbuka kuomba pia ahadi mahususi ya eneo au ya kitaifa itimizwe, kwa mfano ahadi ya kufungua vyoo katika eneo lako, au utoaji maji ilioboreshwa ipatikane kwa kila mtu katika kijiji chako.

Kampeni hii ya duniani ni nafasi ya watu duniani kote kuja pamoja na ujumbe wazi, wa pamoja: Timiza Ahadi Zako kuhusu Udhibiti Afya na Maji!

1

3 4

2

Viongozi wa dunia,

Tunawaomba watoa maamuzi wote kutimiza ahadi zao za kuchukua hatua ya kutamatisha janga la maji na udhibiti afya, na kufanya kazi kuwadia kutoa udhibiti afya na maji kwa wote.

Jina:

Nchi:

Viongozi wa dunia,

Tunawaomba watoa maamuzi wote kutimiza ahadi zao za kuchukua hatua ya kutamatisha janga la maji na udhibiti afya, na kufanya kazi kuwadia kutoa udhibiti afya na maji kwa wote.

Katika [nchi], tunaomba [mtoa maamuzi] kutimiza ahadi yake ya [ahadi iliyotolewa].

Jina:

Nchi:

Pakua ombi halisi kutoka www.keepyourpromises.org.

5 Hutton, gharama kwa jumla na faida za kunywa maji na uvumbuzi wa udhibiti afya ili kufikia lengo la MDG na kuenea duniani, WHO, Geneva, 2012

ON SANITATION AND WATER ON SANITATION AND WATER

Page 12: Novemba 2012 – Septemba 2013 - End Water Poverty · ni pamoja na ahadi ya kuunda bajeti ya kando, na kuweka angalau asilimia 0.5 ya mapato ya serikali kwa udhibiti wa afya na usafi

ENDWATERPOVERTY