46
FEBRUARY 15 – 22, 2014 MADA KUU: FAMILIA NA NDOA YA KIKRISTO Somo limeandaliwa na Mchungaji Rudatinya M. Mwangachuchu Katibu wa Wachungaji na Huduma za Familia wa Divisheni ya Mashariki ya Kati ya Afrika na kufasiriwa na: Mchungaji Stephen J. Letta Katibu wa Wachungaji, Huduma za Binafsi, Huduma za Familia, Shule ya sabato, na VOP. 1 MASOMO YA JUMA LA FAMILIA

memberfiles.freewebs.commemberfiles.freewebs.com/49/54/100695449/documents/Juma... · Web viewKuwa na ndoa bora utahitaji kuunda utamaduni (kanuni) baina yenu ninyi wawili. Ni aina

  • Upload
    ledung

  • View
    471

  • Download
    54

Embed Size (px)

Citation preview

FEBRUARY 15 – 22, 2014MADA KUU: FAMILIA NA NDOA YA KIKRISTO

Somo limeandaliwa na Mchungaji Rudatinya M. MwangachuchuKatibu wa Wachungaji na Huduma za Familia wa Divisheni ya Mashariki ya Kati ya Afrika

na kufasiriwa na:

Mchungaji Stephen J. LettaKatibu wa Wachungaji, Huduma za Binafsi, Huduma za Familia, Shule ya sabato, na VOP.

Union ya Kusini mwa Tanzania. (STU)

1. Juma la Maombi la Familia na Ndoa ya Kikristo

1

MASOMO YA JUMA LA FAMILIA

Utangulizi: Familia na mahusiano ni kiini cha Mpango wa Mungu wa Ukombozi. Familia ilianzishwa na Mungu wakati wa uumbaji kama taasisi ya mwanadamu iliyo kuu. Ni mandhari ya msingi ambako tabia inafunzwa na uwezo wa kuunda mahusiano ya karibu na Mungu pia na mwanadamu hukuzwa.

Mungu hujali kuhusu familia na hutaka kuwabariki wanafamilia kwa kiwango cha juu sana. Kama tunataka kuishuhudia mibaraka yake ikimwagwa kwa familia zetu, ni jambo la lazima kabisa tuwe tumeunganishwa naye kikamilifu. “Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu, na amani ya Mungu ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.” (Philippians 4:6, 7)

Kila mwanaume ama mwanamke huja kwenye ndoa akiwa na tabia zake za kipekee. Wote wawili wana mitazamo ya maisha inayoweza kutofautiana na ya mwenzake kabisa. Kama hawawezi kuyaona mambo kwa mtazamo wa pamoja, itakuwa vigumu sana kupata muafaka wa kuishi pamoja kwa amani. Hiyo haimaanishi kwamba hawawezi kufikia misimamo ya pamoja au kuelewana katika siku za usoni. Kufanya hivyo kunahitaji nidhamu ya hali ya juu ambayo watu wengi hawapo tayari kuipokea. Hiyo humaanisha kwamba wanahitaji nguvu kutoka nje ili kwanza iwaunganishe pamoja, na pili iwasaidie kuwa familia ya Kikristo iliyo kielelezo.

Zaidi ya hilo, ili familia ya Kikristo ili idhihirishe kwa ulimwengu nguvu na ubora wa mvuto wa Kikristo na athari zake katika jamii inayowazunguka, yapo mambo kadhaa wanayotakiwa kuyatimiza maishani mwao:

Jambo la kwanza na la muhimu kuliko yote, ni kile tukipatacho kwenye Neno la Mungu. “…Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.” Kumb. 6:4-9

Jambo la pili, la kuwa Mkristo anayeishi maisha yenye baraka, linaamuliwa na namna tunavyovitumia vyote, kanuni za Kikristo na kanuni njema za maisha zitokazo kwenye fungu hapo juu. Kumpenda Mungu kwa mioyo yetu yote, kwa roho zetu zote, na kwa nguvu zetu zote, ni ufunguo wa kupata ushindi

2

katika maisha ya Ukristo. Tunapotambua kanuni hii, tunatakiwa kuifundisha kwa watoto wetu, tukiwasimulia kuhusu Mungu wetu. Huu ndio utakaokuwa mzigo na wajibu wetu kwa Bwana wetu, na zoezi letu la kudumu la kiroho, litakalozifunga familia zetu pamoja.

Kule kufundisha na kuomba kwa ajili ya ulinzi wa familia zetu, kutatuletea Baraka za Mungu na kuwaonesha watu wengine kwamba ni vyema kuishi maisha ya Kikristo. Kwa njia hii, tutawaachia wao, kanisa lote la Kikristo, na ulimwengu wote kwa ujumla, urithi wa kiroho udunuo.

Jambo la tatu, kule kuendelea kurudia rudia kitu kile tukiaminicho kuwa muhimu maishani mwetu ndilo chimbuko la Baraka kwetu na kwa wengine. Akitoa maoni yake kuhusiana na fungu hilo hilo hapo juu, Parsons, anatangaza kwamba: “Aya hii ya Maandiko inaitwa Shema. Imeambatanishwa kwenye hotuba ya kuwaaga Wayahudi. Ni ombi la kwanza ambalo mtoto wa Kiyahudi hufundishwa. Wayahudi wengi bado hukariri Shema walau mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni; ni maneno ya mwisho Myahudi huyasema kabla ya kifo. Msisitizo maalumu unawekwa kwa maneno: ‘Bwana Mungu wetu, Bwana ni mmoja!’ Wanazuoni wa Kiyahudi hushauri kwamba Shema ni ushuhuda wa ukuu wa Mungu. Ni ahadi ya kuwa mtii kwa Mungu mmoja peke yake na tangazo la imani. (‘Hebrews for Christians’)

Biblia inatoa mapendekezo ya ziada yatakayotusaidia kuishi tukiwa tumeunganishwa kikamilifu na Mungu mwenyewe kupitia Neno Lake. Kamwe hapawezi kuwepo maisha ya Kikristo ambayo hayakujengwa juu ya Neno la Mungu. Mungu anapaswa kuwa msukumo na nguvu vinavyoileta familia pamoja; mafuta yanayosababisha familia kujongea na kutenda kulingana na viwango vya Ukristo vinavyowavuta wengine kuja kwenye upendo unaojali wa Yesu Kristo. Hii ndiyo njia pekee ambayo kama familia ya Mungu twaweza kung’aza maisha ya Kikristo, tunapoimarisha mahusiano na asili ya kila wema. Ellen G. White anakubali, na kuongezea hili kwa nguvu akisema:

“Utakatifu kwa Mungu unapoenea katika nyumba…Wazazi na watoto wanapaswa kujielimisha wenyewe kushirikiana na Mungu. Wanapaswa kuleta tabia na mienendo yao ipatane na mipango ya Mungu. (Adventist Home uk. 19)

“Mahusiano ya kifamilia yanapaswa kuwa yatakasayo katika mvuto. Nyumbani kwa Mkristo, kulikoanzishwa na kunakoendeshwa kulingana na mpango wa Mungu, ni msaada wa kushangaza katika kuunda tabia ya Kikristo…Wazazi na watoto wanapaswa kuungana katika kutoa huduma ya

3

upendo kwake Yeye ambaye pekee aweza kulidumisha pendo la kibinadamu kuwa safi na jema.” (Adventist Home uk. 19)

Mungu anatukuzwa na nyumba ya Kikristo. Kwa mujibu wa mama White anasema, “Baba na Mama wanaomfanya Mungu kuwa wa kwanza nyumbani mwao, wanaowafundisha watoto wao kuwa kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima, na kumtukuza Mungu mbele ya malaika na mbele za wanadamu kwa kuweka mbele ya ulimwengu, familia yenye utarabu bora, na yenye nidhamu – familia inayompenda na kumtii Mungu badala ya uasi dhidi Yake. Kristo siyo mgeni nyumbani kwao; Jina lake ni jina la nyumbani, linaloheshimika na kutukuzwa.” Analithibitisha hilo anapoandika: “Malaika wanafurahishwa na nyumba ambako Mungu ni mtawala mkuu na watoto wameelekezwa kuheshimu dini, Biblia, na Muumbaji wao. Familia hizo zinaweza kudai ahadi, ‘Wale wanaoniheshimu Nitawaheshimu.’ Kwa kuwa kutoka kwenye nyumba hiyo baba atatoka akienda kwenye shughuli zake, akiwa na roho iliyolainishwa na kunyenyekezwa na Mungu”. (Adventist Home uk. 27)

Mama White anatuhakikishia kwa mara nyingine tena kuwa, “Kuwepo kwa Kristo peke yake kunaweza kuwafanya wanaume na wanawake kuwa na furaha. Maji yote ya kawaida ya maisha, Yesu aweza kuyageuza kuwa divai ya mbinguni. Hivyo nyumba hugeuka na kuwa Edeni; na familia alama ya uzuri wa familia ya mbinguni. (Adventist Home uk. 28).

Kadri tutakavyokuwa tukiunganishwa pamoja katika juma hili la maombi ya familia ya Kikristo, tunatamani kujifunza mengi zaidi juu ya namna tunavyoweza kuwa tayari kuishi na kuwaonesha wengine wanaotuzunguka maisha ya Kikristo na kuwavuta kwa Kristo. Tuatakuwa tukiwatayarisha ili wawe tayari kwa ajili Yake anapokuja tena hivi karibuni. Ni tumaini letu kwamba maisha yetu yatabadilishwa yafanane naye, kama vile wanafunzi wa Agano Jipya, waliokuwa wazi sana katika kulifundisha kanisa la Kikristo kuhusu ni hatua zipi zinatakiwa kutunza ndoa na mahusiano hai, yenye afya na imara.

Maandiko ya Mitume yanapendekeza mfululizo wa mivuto na tabia iliyokusudiwa kuimarisha ulinzi na kupunguza mambo yaliyo kinyume. Mwandishi wa Waebrania anashauri kwamba “Upendano wa ndugu na udumu. Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.

Mtume Yakobo anatutia nguvu akisema “Ni nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa

4

hekima.” Yakobo 3:13. Yakobo anasema, kilicho muhimu siyo tu namna unavyoongea bali pia namna uishivyo. Anaendelea kusema kwamba namna tunavyotendeana isitokane na hisia bali itokane na ujuzi wetu juu ya njia za hekima za Mungu. Hekima ya kweli huanza na maisha matakatifu na hudhihirishwa kwa kuishi vema na wengine. Tena ni ya amani, na ya upole, ikibubujika neema na mibaraka, siyo ya joto siku moja na ya baridi siku inayofuata; haina pande mbili. Mnaweza mkaikuza jamii yenye afya na nguvu inayoishi sawasawa na mapenzi ya Mungu na inayofurahia matokeo yake ikiwa tu mtafanya bidii ya kuishi vizuri ninyi kwa ninyi, mkitendeana kwa kuheshimiana na kustahiana. (Yakobo 3:17, 18).

Mtume Paulo ana mengi ya kusema kuhusu kudumisha upendo katika mahusiano yetu. Tabia hizi, aliamini, huibuka kutoka katika mioyo yenye shukrani na maisha yaliyojazwa na neema ya Mungu. “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.” (Wakolosai 3:15).

“Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi. Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili. Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. (Warumi 12:9-17). Paulo anatuelekeza zaidi “Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote. (1Wathesalonike.5:15). Anatia moyo kuruhusu karama za Roho wa Mungu — “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria, (Wagalatia. 5:22, 23) tukiutia nguvu uhusiano wetu kwa kujimimina wenyewe “kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, tukichukuliana katika upendo”. (Waefeso 4:2)

Ushauri maalumu wa ndoa huja kutoka kwa Paulo pia. Yeye huona wazi kuwa heshima ni jambo la muhimu katika kujenga ndoa imara na mathubuti. Ushauri wake kwa wanandoa hufuata mara tu baada ya kuwaalika wote “hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo. (Waefeso. 5:21) “Enyi wake,” anasema, “watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.” (fungu la 22)

5

“Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake.” (fungu la 25)

Mme anapaswa kuwa chanzo cha upendo na atangulie katika kuonesha upendo na siyo kummiliki mkewe. Upendo wake kwa mkewe unapaswa kuwa “upendo unaojitambulisha kwa kutoa si kupokea peke yake” (fungu la 25), “upendo uliokusudiwa kuleta yaliyo bora kutoka kwa mkewe (fungu la 26). Upendo wa mume kwa mkewe unafananishwa na ule wa Kristo kwa kanisa lake, “maneno yake yanaamsha uzuri wa mke” (fungu la 26).

6

2. Mawasiliano mema msingi wa heshima na Upendo udumuo katika Ndoa ya Kikristo

Imejulikana kwamba tatizo kubwa linalovuruga na linaloendelea kuvuruga familia ni mawasiliano mabovu. Kama watu wangeweza kurekebisha njia zao za kuwasiliana nyumba nyingi zingeishi maisha yenye afya na furaha bila kujali udogo wa vipato vyao au mahali wanapoishi. Tungependa kuzishauri familia, njia zao za kuwasiliana katika kila jambo. Mtume Paulo anaongeza juu ya ushauri huu kwa kupendekeza kwamba “katika maisha mapya ya neema ya Mungu” wanandoa watendeane katika hali ya usawa, kila mmoja akimheshimu na kumfurahia mwenzake na kutafuta kuwa katika makubaliano, kuhurumiana, kupendana, na kunyenyekeana. (1Petro 3: 7, 8).

Biblia kwa mfululizo imekuwa ikiwaelekeza Wakristo namna ya kuishi kwa maelewano na maridhiano katika kila kona ya maisha. Yule anayetaka kuwa na nyumba aelewe kwamba kitu cha kwanza ni kutawala maneno. Tunajua hili lawezekana tu ikiwa watu wa hiyo familia watapenda kuishi kwa maelewano na kufanya kitu fulani ambacho kingesaidia kutimiza kusudi hili. Familia ni lazima zichukue uamuzi wa namna watakavyowasiliana kwa ufanisi kwa kuwa hili litawasaidia kukuza hali ya kiwango cha juu cha ukaribu katika ndoa, kujifunza kupatanisha migogoro na tofauti zao kwa namna iliyo nzuri na kuimarisha upande chanya wa ndoa yao.

Mawasiliano ya kifamilia huwa na nafasi muhimu katika kujenga na kulea familia. Mawasiliano mmazuri baina ya mume na mke na baina ya wazazi na watoto, hali kadhalika baina ya watoto wenyewe kwa wenyewe huimarisha mahusiano yenye upendo na uwiano katika familia. Kuboresha mawasiliano ya kifamilia huchochea upendo, kuaminiana na kuheshimiana, na zaidi sana, husaidia familia kukabiliana na hali za kupanda na kushuka za kifamilia na magumu yote inayoyapitia. (Iliwekwa January 5, 2011 na Stevedt 1954).”

Anaendelea kusema: “Vitabu vingi vya Biblia hufundisha kwamba mawasiliano mazuri ndicho chanzo cha uhakika cha furaha na faraja. Kwa kufanya hivyo familia ya Kikristo hujengwa. Katika kitabu cha Mithali 17:27, Neno la Mungu linatangaza, “Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa; Na mwenye roho ya utulivu ana busara.” Katika kitabu cha Yakobo 1:19, mwandishi anatuambia, “Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika.” Hii nadhani ndiyo kanuni ya kwanza ya mawasiliano. Watu wengi walijikuta kwenye mazingira ya matatizo, kwa sababu hawakuchukua muda wa kutosha kusikiliza na kutafakari ujumbe uliokuwa kwenye maneno. Tafadhali

7

chukua muda kucheua kabla hujasema lolote. Tusipokuwa waangalifu sisi kama wakristo mara nyingi tunaweza kujifanya tunamtii Mungu bila hata kusikiliza amri zake kwa kuwa tumezoelea mawasiliano mabovu kwenye familia zetu. Mazoea ya jambo hili huanzia nyumbani.

Siku moja kijana mdogo alikuwa anaendesha gari na alikuwa anakaribia kugongwa na binti mmoja aliyekuwa anaendesha kwa kasi na aliyekuwa amepoteza uthibiti wa gari lake. Huyu binti alimtukana Yule mvulana akisema “Nguruwe” huyu mvulana alijibu “Nyama ya Nguruwe” Alikuwa anashangaa inawezekanaje huyu binti amtukane wakati ni yeye aliyesababisha matatizo? Lakini mara tu huyu kijana alipokunja kona alikutana uso kwa uso na nguruwe (yule binti) akiwa amesimama katikati ya barabara. Binti alimwonya akome kumtukana. Wakati mwingi tumejikuta tukijibu watu, wakati katika uhalisia tulitakiwa tusikilize na na kuongeza umakini ili tuelewe kile watu wanachosema wanapopitisha ujumbe wao kwetu.

Amri inayotutaka tuwe wepesi kusikiliza, inatutaka kuwa tayari kusikiliza na kutii ujumbe wa Mungu. Wito wa kutaka tusiwe wepesi wa kuongea, unadai tuwe wakimya hadi tumeelewa ujumbe na namna ya kuutumia. Ni wito wa kujizuia tusije tukafanya vitendo vya haraka vitakavyoleta madhara. Changamoto ya ya kutokuwa wepesi wa kukasirika inatuonya dhidi ya hisia za kikatili na uchungu. Hatuwezi kumsikia Mungu iwapo tumejifunga kwenye hisia za chuki au visasi. Jamii yetu inatuhimiza kuelezea hisia zetu, ziwe njema au mbaya, zenye amani au zinazochoma, za Mungu au zisizo za Mungu. Yakobo 1:19, hata hivyo hutupatia picha ya mtu mwenye busara kama mtu aliye tayari kumsikiliza Mungu na wengine, atoaye majibu yake kwa uangalifu, na ajibuye kwa maneno yenye tahadhari (Lea 1999).”

Kuna baadhi ya dondoo zinazopendekezwa, ili kuboresha mawasiliano ya kifamilia. Kwa mara nyingine tena dondoo hizi zinaweza kuwa msaada pale tu familia zinapodhamiria kuboresha namna yao ya kuishi na wana dhamira ya kuwa na ndoa ya Kikristo yenye furaha. Tiba ya kwanza ya mawasiliano bora ni kusikiliza. “Hebu chukua muda kidogo usikilize na siyo tu kusikia. Funga TV au redio, weka kando kitabu unachosoma, sikiliza kile mtoto wako au mwenzi wako anachosema na ujaribu kuelewa hisia wanazojaribu kuziwasilisha kwako.”

Tiba ya pili ni maelewano mazuri “Unapaswa kuyachambua kwa uangalifu maneno unayotaka kuyasema. Ikiwa una hasira, umechukizwa au unahitaji kutoa hisia ambazo zinawea kuchochea migogoro au kuamsha hisia mbaya,

8

hakikisha unatumia neno “mimi”. Onesha hisia zako kwa kuelezea unavyohisi kuliko kutumia lugha inayoelekeza kidole kwa wengine. Hii itasaidia kunusuru hali ya hewa. Mara baada ya kuonesha hisia zako, mpe fursa mtu aliyekuwa anakusikiliza kukuuliza maswali. Mwombe mtu huyu kutumia sentensi za “mimi” pia, hiyo itakuza na kudumisha hali ya amani nyumbani kwako.”

Jambo la tatu, ni kufurahia. Ni vigumu kufurahia hasa wakati mwenzi ama mtoto wako anaporudia kile unachokijua tayari na ambacho kimekuwa kikirudiwa mara nyingi, lakini kumbuka kilicho muhimu mara nyingi siyo ujumbe, bali ni ule wakati mzuri wanaotaka wewe uwe pamoja nao. Tunapaswa kila mara kuvutiwa kwa dhati na kile wengine wanachotaka kusema. Kutoa usikivu wako usiogawanyika kwa wapendwa wako hata kwa kipindi kifupi cha wakati ni bora zaidi kuliko kutumia muda mrefu pamoja wakati mkiwa mmegawanyika na hampo pamoja.

“Jambo la nne, zoesha sauti yako kuwa tulivu na tamu hata pale hisia zako zinapokuwa juu. “Katika hali hiyo hiyo maneno mazuri; na sauti tamu na yenye kufikiria wengine daima huigusa mioyo na kuinua roho. Wakati huo huo uwe mwangalifu siyo tu kwa kile ukisemacho, bali pia namna unavyokisema na namna unavyojieleza mwenyewe mbele ya familia yako.”

Jambo la tano, Uwe mtu wa kuaminika na unayedumisha kujiamini; kuna watu ambao kwao ahadi ni kama haina maana yoyote; wanaendelea kutoa ahadi lakini kamwe hawatimizi yale wanayoahidi. Iamini familia yako na pokea kuaminiwa kutoka kwenye familia yako. Mwahidi mwenzi wako au mwanao unachoweza kukipata. Siku moja, nilimwahidi mwanagu kwamba ikiwa atakuwa wa kwanza darasani mwake nitamnunulia baiskeli; alinijulisha kuwa alikuwa wa tatu darasani mwake, lakini kwa kuwa ahadi yangu ilkuwa tu na lengo la kumhimiza, na sikutarajia kuwa alama zake zingebadilika ghafla hivyo, sikuwa tayari kumzawadia kama nilivyoahidi. Alifanya kazi kwa juhudi sana kiasi ilikuwa ni halali kumpatia nilichokuwa nimemwahidi.

Jambo la sita, daima tafuta na Tengeneza Muda Ulio Bora na Familia Yako. Wengi wana muda mzuri na watu wengine lakini kamwe hawana muda na familia zao. Mchungaji alikuwa anahubiri siku moja ya Sabato na alipotoa wito mwenzi wake na watoto wake walisimama na walipoulizwa kwa nini walifanya hivyo wakasema ilikuwa jambo jema wao kuwepo hapo kanisani kwa sababu ni hapo tu walipofurahia tabasamu tamu kutoka kwa mchungaji ambaye ni baba yao. Walikuwa hawajawahi kumwona mchungaji akiwa katika hali hiyo nzuri akiwa nyumbani kama alivyokuwa pale kanisani.

9

Ni kweli tunaweza kuwa na shughuli nyingi na tuliochoka tunaporudi nyumbani, lakini tukumbuke kwamba hizi kazi siku moja zitafikia ukomo wake lakini familia itabaki.

Jambo la saba, kuwa muwazi katika kujadili maswala na matatizo ni ufunguo mwingine wa kuboreshea mawasiliano ya familia. Haishauriwi kutumia majadiliano kulaumiana, badala yake kubadilishana mawazo yenye afya na utatuzi wa matatizo vitasaidia kuimarisha familia. Mawasiliano kwa kweli yana nafasi muhimu sana katika kuilea familia yako. Iruhusu familia yako kushirikisha wengine fikra zao, hisia zao, maoni yao na misisimko yao. Tianeni moyo kufanya mawasiliano kwa njia ya upendo, kutunzana, kuaminiana na kuheshimiana.

Kwa mujibu wa Stanley, na Susan L Blumberg, kuna mambo manne yanayojitokeza kwa familia zisizo na mawasiliano yasiyo na furaha kama: Kubembea, Kuwa na tafsiri hasi, Kutothaminiana, Kujitenga na Kutojihusisha.

Kujitukuza hutokea wakati mwenzi wa maisha asemapo kitu fulani ambacho si chema sana; na kisha mwenzi mwingine ajibupo kwa kusema kitu kilicho kibaya zaidi kwa mwenzake. Kabla hawajaendelea sana wawili hawa wanajikuta wakibwatizana, kile kilichoanza kama mazungumzo yasiyo na madhara yanaigeuza ndoa na kuitumbukiza kwenye maumivu makubwa. Tofauti kati ya wenzi wenye furaha na wasio na furaha ni ile namna wanavyoshughulikia migogoro kwenye ndoa zao. Wenzi wenye furaha hujua namna ya kutambua ujio wa Kubembea kabla hakujatokea na hubaki watulivu hadi dhoruba imepita.

Tafsiri hasi ni jambo jingine linaloharibu uimara wa ndoa. Mmoja wa wanandoa hutoa kauli au ishara, na hutafsiriwa katika hali iliyo hasi zaidi na mwenzi wa pili kuzidi vile ilivyokuwa ikimaanisha. Wanandoa wenye furaha huwa na mazoea ya kupeana faida ya kutilia shaka neno, na wakati wanapokuwa na shaka juu ya neno au kitendo huuliza ili kupata ufafanuzi kuliko kufikiria mabaya.

Kutothaminiana ni jambo jingine linalojitokeza kwa wenzi wasio na furaha. Hali hii hutokea wakati mume au mke wanapompuuzia mwenzi wake, kwa kutojali matakwa, mahitaji, na hisia vya wengine. Mtu aweza kutomthamini mwenzi wake kwa kumwongelea vibaya muda wote; kudharau kila kitu anachokisema; kuchukulia maumivu yao kama jambo la kawaida. Kwa mfano baada ya kurudi kazini amechelewa mke anasema: “Nimechoka sana!” na mume bila kuonesha huruma kidogo naye anasema “Na mimi pia nimechoka

10

sana.” Ingawa si jambo baya kuwa umechoka, ni tatizo kutojali hisia za mwenzi wako na kuanza kuzungumzia matatizo yako mwenyewe.

Kujitenga na kutojihusisha ni jambo la mwisho kati ya yale mambo manne yaliyoainishwa na utafiti wa ndoa wa Chuo Kikuu cha Denver uliotajwa hapo mwanzo.

Hii hutokea wakati mmoja wa wanandoa anapojiweka mbali na mwenzake akimkwepa kwa kadri inavyowezekana. Ni vigumu kushughulika na wanandoa walio katika hali hii (Markman, et al., 2001, pp. 13-31).

Sogeleaneni badala ya kukimbiana. Zungumzeni badala ya kushughulika na vitu vinavyowazuia kufurahiana. Mtegee sikio mkeo. Mtegee sikio mumeo. Zungumzeni vitu vya mzaha pamoja. Ukweli kwamba mnadumu kwenye mazungumzo utawaunganisha na kuifanya ndoa yenu kuwa yenye nguvu.

Ruhusu mwenzi wako akuvute. Jenga mazoea kwamba umefika hapo kutokana na mvuto wa mwenzi wako. Hiyo humfurahisha mwenzi wako; huwaunganisha. Ni sehemu ya gundi inayowaweka pamoja. Tatueni matatizo yenu yanayotatulika. Si kila tatizo lililo kati yenu linahitaji kutatuliwa. Kama mmeoana kwa miaka 10 au 15 hamuwezi kuwa vijana kama wakati mlipokuwa mmeoana. Lishughulikieni hilo. Ukweli ni kuwa hilo ni tatizo dogo ukilinganisha upendo Mungu alionao kwenu.

Mnaposhughulikia matatizo yanayotatulika, “lainisha ule mwanzo wa mazungumzo.” Kwa kuwa mwanamke kwa asili ndiye aliye mwepesi kutaka kutatua matatizo, epuka kumchokoza na kumtukana mume wako unaposhughulikia tatizo. Sekunde chache za mwanzo wa mazungumzo zitaamua sehemu iliyobaki itakuwaje. Anza na mambo matamu. Utafanikisha mengi ukija na mtazamo huu.

Karibu kwenye jamii ya wanadamu. Hukuolewa na mwanaume mkamilifu au hukuoa mwanamke mkamilifu. Hata mwenzako naye ni hivyo hivyo. Hakuna ndoa zilizokamilika kwa kuwa hakuna watu wakamilifu. Kama unaye mume anayekoroma au mke anayefanya hivyo, jaribu kuchukuliana naye, maana hakuna unachoweza kufanya zaidi ya hapo. Epuka kufikiria kwamba hutawezana na hali hiyo maana mbona kama unaishi jirani na mto unaweza kuchukuliana na kelele za maji yam to huo? Na wale waishio kando kando ya barabara kuu mbona huchukuliana na sauti za magari yanayopita hadi wanafikia kutoisikia kabisa kelele hiyo.

11

Kwa kawaida kunakuwa na malumbano kwenye familia zetu kwa kuwa mmoja hapendi chakula fulani au kuangalia mpira.

Kubali tofauti na amua kuishi na mtu uliyemchagua. Umesikia usemi: “Kama maisha yanakupa malimau tengeneza juisi ya malimao.” Tunawajua watu wengi waliokuwa wameoana na ambao waligeuka malimao. Wafanye kuwa juisi ya malimao na maisha yatakuwa bora zaidi kuliko yalivyokuwa miaka kadhaa iliyopita.

Chagua hali tofauti, mwitikio tofauti, mwitikio wa ushindi, na hali itakuwa inayochukulika. Hapa hatumaanishi kuwa mmoja amtumie mwenzake vibaya au ufanye mambo kwa kuigiza. Mambo hayo hayapaswi kuwepo kwenye ndoa. Ikiwa yapo basi mmoja wenu atafute msaada wa kitaalamu kuondoa hiyo tabia ya kuchukiza. Lakini usiitupe ndoa yako kwa kuwa tu mwenzi wako haonekani kama alivyokuwa anaonekana miaka 20 iliyopita.

Undeni tafsiri ya pamoja. Kwa kawaida watu huoana lakini huishi tofauti. Hawajihusishi na muda maalumu wa kuwa huru wa mwenzake; hawasali pamoja; hawasomi vitabu pamoja; hawapendi mapishi ya aina moja. Mume anapenda milima, mke anapenda ufukwe wa bahari; wanachukua likizo wakati tofauti. Kama mambo hayo sita mnayo mtakuwa na ndoa nzuri. Kuwa na ndoa bora utahitaji kuunda utamaduni (kanuni) baina yenu ninyi wawili. Ni aina ya utaratibu utakaowafunga pamoja, utakaokuwa na muziki utakaoeleweka na ninyi wawili tu.

Tumaini, Usalama, na kujitoa kikamilifu ni ni mambo ya msingi katika mahusiano yoyote, lakini kuwa nayo hakumaanishi unaweza kuuchukulia uhusiano wako kuwa ni kama jiwe. Mahusiano ni jambo linaloweza kuvunjika wakati wowote na ndiyo sababu 50% ya ndoa huishia kwenye talaka.

Willy anasema, “Wanandoa wenye furaha huendelea kuchumbiana, wakiambiana jinsi walivyo wazuri, na kufanya mambo pamoja.”

Mwenye hekima Suleiman, na mwandishi wa Yakobo, wote wawili wanazungumzia namna ya kuboresha na kudumisha mahusiano yenye afya – iwe kwenye ndoa; baina ya wazazi; baina ya watu wazima; baina ya wajumbe wa bodi; au baina ya mahusiano yoyote yenye maana maishani mwetu. (Gottman 1999).

12

3. Mtindo wa maisha na matumizi ya fedha katika Ndoa ya Kikristo

Moja ya mambo yaliyomshangaza sana Orbuch katika utafiti wake ni nafasi ya fedha katika migogoro ya ndoa. “Wengi wa walioachana wanasema kwamba fedha ilikuwa ni sababu namba moja ya migogoro katika miaka ya awali ya ndoa yao.” Aligundua pia kuwa, watu 6 kati ya 10 walisema, hawatashirikiana na wenzi wao gharama za maisha watakapokuwa na ndoa nyingine.” Orbuch anapendekeza kwamba kila mwanandoa atathmini mtazamo wake kuhusu matumizi na udundulizaji wa fedha na wayaongelee hayo katika siku za mwanzo za uhusiano. Anasema hakuna mpango unaowafaa wote, lakini wanandoa wanahitaji kuamua kanuni zao wenyewe na kuziheshimu.

Ndiyo maana haishangazi pale Biblia isemapo: “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.”1 Timotheo 6:10)

Ni kweli kuwa sote tunahitaji fedha maishani mwetu kwa sababu hakuna kitu unachoweza kukipata bila kutumia fedha. Lakini tatizo huanzia pale fedha inapokuwa kila kitu maishani mwako. Fedha ni lazima ionekane kama nyenzo ya thamani tunayoihitaji kuitumia. Tukiitumia vizuri itakuwa njema tu, lakini ikitumika isivyofaa itatudhuru. Hii humaanisha kwamba tatizo siyo fedha bali namna tunavyoitumia.

Kanuni kadhaa za kutuongoza kutumia fedha:

Mithali 6:6-11 inatupa hekima kuhusiana na uvivu na matokeo yake mabaya. Tunashauriwa kuiga kutoka kwa chungu (mchwa) afanyaye kazi ya kujihifadhia chakula. Katika kufanya hivyo chungu huhakikisha kwamba kuna chakula cha kutosha kwenye ghala cha kuwafaa wakati wa mvua. Kanuni ya kwanza ni kufanya kazi kwa juhudi ili kuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya chakula na mahitaji mengine. “Mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.” (Mithali 6:6)

Kanuni ya Pili: Usipagawe na kupata fedha. Mtu wa namna hiyo, kwa mujibu wa Maombolezo 5:10, kamwe hawezi kuwa na utajiri wa kutosha kumridhisha na hivyo atapaswa daima kuendelea kutaka zaidi na zaidi. Wakiwa wametawaliwa na roho hii ya kutaka zaidi na zaidi, familia nyingi zimeharibika. Baba anayeondoka nyumbani na kukaa mbali sana na familia yake kwa muda mrefu ili kupata fedha zaidi anaiweka familia yake katika

13

mazingira ya hatari. Hali ni hiyo hiyo pia kwa mke. Familia zilizovunjika ni kilio cha kila siku lakini wengi wasingependa kuibadili hali hii. Ukweli ni kuwa familia nyingi zinateseka zaidi kutokanan na tatizo la kupata fedha zaidi kuliko ukosefu wa fedha.

Kanuni ya Tatu: Matumizi ya fedha. Tunatiwa moyo pia kuwa mawakili wema kwa kile Mungu alichotupa.

MASWALA YA FEDHA NYUMBANI

Mungu anawataraji watu wake wawe wenye kutafakari na watunzaji. Angependa wajifunze kutumia mali kwa uangalifu, na wasipoteze chochote. Counsel for the Church uk. 154

Familia za siku hizi zinatambulika kwa matumizi yasiyo na busara ya mali zao. Ni jambo la kushangaza kuona kiasi kikubwa cha fedha kikitumika katika kununulia nguo, chakula na samani. Baadhi hutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya harusi zao hata pale ambapo mishahara yao haiwaruhusu. Wanaishi kuilemea jamii. Mipango ya siku za usoni haiwekwi vizuri. Wengi huchagua kuanza maisha yao ya kifamilia wakiwa na madeni makubwa kutoka kwenye mabenki bila kuzingatia nini kitatokea mbeleni. Biblia ina hekima ambayo ingetusaidia katika kufanya maamuzi kuhusu namna ya kupanga. Katika Luka 14:28 Yesu akizungumzia kuhusu kujenga mnara anasema hivi: “Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?”

Katika 1 Wafalme 4, tunasimuliwa kisa cha kuvutia cha mjane aliyesumbuliwa na madeni ya mume wake baada ya kufa. Mdai huyu alitaka alipwe fedha yake bila kujali madhara yatakayotokea. Hali ilikuwa nzito kiasi kwamba hakuwa tayari kuwaachilia watoto wake hivyo aliwachukua kuwa utatuzi wa tatizo. Mwanamke huyu aliamini kwamba mume wake alikuwa mtu wa Mungu.a Angalia alivyosema kwenye fungu la 1, “Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha Bwana.” Kwa nini alikuwa na deni hili? Hatujui na si jambo muhimu katika kisa hiki. Hata hivyo alikuwa ameelemewa na madeni. Ni wangapi kati yetu tuna madeni? Nadhani ni wengi. Kwa nini? Sijui.

Tunaishi katika ulimwengu wenye madeni. Kote kutuzunguka kuna mabenki yanayotoa mikopo na watu wengi sasa ni watumwa wa mabenki haya. Tatizo siyo kupata mikopo, lakini swali ni kwa sababu gani unachukua huo mkopo na umejiandaaje kuulipa. Familia nyingi zinaumia kwa sababu chochote wanachopata kinatumika vibaya katika mambo yasiyo ya lazima na mwisho

14

wa siku mambo hayo huiletea familia msongo. Kila sikukuu ni chanzo cha madeni: harusi, mazishi, mahafali, simu n.k.

“Wengi, wengi sana hawajajielimisha wenyewe kwamba wanaweza kuthibiti matumizi yao kulingana na mapato yao. Hawajifunzi kuchukuliana na mazingira, na wanakopa, na kukopa tena na tena na kuelemewa na madeni, na matokeo yake wanakatishwa tama na kushushwa moyo.” (Adventist Home uk. 374)

“Inakupasa kuona kuwa husimamii maswala yako ya fedha katika namna itakayokuingiza kwenye deni. Wakati mtu anapokuwa kwenye deni, yupo ndani ya mojawapo ya mitego ya shetani, anayoitega ili kuzinasa roho. Dhamiria kutojitumbukiza kamwe kwenye deni lingine. Jinyime vitu maelfu kuliko kujiingiza kwenye deni. Epuka deni kama ambavyo ungeepuka ndui.” Counsels for the Church uk.155.

Kama unazo tabia za ufujaji wa mali, zikate mara moja tabia hizo kutoka kwenye maisha yako. Ni mpaka utakapofanya hili, utaendelea kuwa mhitaji milele zote. Tabia za kutumia vizuri mali, ujasiriamali, na kujinyima ni sehemu bora zaidi kwa wanao kuliko hazina ya utajiri. (Adventist Home uk. 375)

Sisi ni wasafiri na wapitaji hapa duniani. Hebu tusitumie mali zetu kwa kuridhisha matamanio yetu ambayo Mungu angetutaka tuyashinde. Hebu tuiwakilishe vizuri imani yetu kwa kujizuia na matamanio yetu. (Adventist Home uk. 375)

Jambo jingine muhimu tunalopaswa kujifunza katika upande wa matumizi ya fedha katika familia zetu ni tabia ya kudunduliza. Hatuwezi kutawala fedha vizuri kama tutazungumzia kutumia au kuweka bajeti bila kamwe kuzungumzia umuhimu wa kudunduliza kwa ajili ya nyakati za changamoto. Njia bora zaidi ya kujizuia na kuwa na matumizi mazuri ya fedha ni kwamba kabla ya kutumia fedha kwanza tafuta ushauri kutoka kwa mwenzi wako. Kumbuka mume au mke hampaswi kamwe kujadili maswala yenu ya fedha na wazazi wenu. Ikiwa kama wazazi mtaamua kuhitaji ushauri wa ziada kutoka kwa wazazi au familia, nendeni kwao mkiwa pamoja kama familia.

Kumiliki akaunti za pamoja ingekuwa ufumbuzi mwingine mzuri. Mtu fulani alishawahi kusema kwamba wakati wanandoa wanapomiliki hundi ya pamoja, wanalazimika kuwasiliana kuhusu fedha na namna itakavyotumika. Mara nyingi inachochea haja ya kuwa na bajeti ya nyumbani ili mmoja wa wanandoa asije akatumia zaidi katika eneo husika.

15

Kwa sababu ya umuhimu wa fedha katika familia, ni jukumu letu kama wazazi kuwafundisha watoto wetu kuhusu fedha. Kwa sababu tunajua kwamba wakati wowote kutakapotokea misuguano katika nyumba kuhusu fedha, misuguano hii itawaathiri watoto. Wajulishe watoto kanuni za Mungu kuhusu fedha wanapokuwa na uwezo wa kuelewa, ukiwaandaa kwa familia zao za siku za usoni. Biblia iko wazi kuhusu jambo hili. “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.” (Mithali 22:6). Ellen G. White anaongezea hivi: “Hebu wazazi watafute kufinyanga na kuelekeza akili za watoto wao vilingane na neno la Mungu. Hebu wawafundishe katika namna ambayo watoto wao watafanana na Yesu Kristo.

Nyumba ya Kikristo inapaswa kuwa nyumba inayoongoza katika namna wanavyotumia utajiri wao kwa kuonesha mfano bora kwa wale wanaokutana nao.

16

4. Jukumu la Baba katika Familia ya Kikristo

Kwa mujibu wa Dr. Tony Evans, kuna majukumu matano ya mume kwa mkewe. Nitachukua mawili tu. Wajibu wa kwanza wa mwananume kwa mkewe, ni kumpenda (Neno la Kiyunani Agape). Neno upendo linawaongoza watu katika mchanganyo kwa sababu upendo limekuwa neno lisiloeleweka. Tunawasikia watu wakisema kwamba “Naipenda kazi yangu. Naipenda nchi yangu na Napenda kula viazi vitamu.” Hizi zote ni aina za upendo ambazo ni tofauti na kile Mungu alichowaamuru wanaume wawe nacho kwa wake zao.

Evans anaongeza hivi: Unaona, wakati Maandiko yanapozungumzia upendo, yanazungumzia kuhusu kafara ambayo unaifanya kwa ustawi wa mtu mwingine. Unaweza tu kuupima upendo kwa kafara yako, siyo kwa kile unachokifaidi. Kama unazungumzia kuhusu kumpenda mke wako, na kwa kusema hivyo unamaanisha kwamba hukufanyia mambo mengi mazuri, huo sio upendo. Huo ni upendo wake kwako. Kusema kwamba mume anampenda mke wake ni kuzungumzia kafara unayoifanya kwake. (Waefeso 5:25). Biblia husema: “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake!” Hii humaanisha kwamba upendo ni kutoa zaidi kuliko kupokea. Wanaume wanatakiwa kutoa bila kudai cha kulipwa. Kwa mujibu wa mtume Paulo kwa Wakolosai, Paulo alisema upendo ni kitu fulani kitamu na si kichungu. “Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.” Wakati wowote mwanaume awapo mchungu kwa mkewe hawi kinyume na huyo mwanamke peke yake bali anamkosea Mungu aliyetoa agizo hili pia.

Nakubaliana na Evans kwamba wakati “mwanaume anapozungumzia upendo anazungumzia kuhusu upendo. Kuzungumzia kuhusu upendo ni kuzungumzia kuhusu Kalvari. Kuzungumzia kuhusu upendo ni kuzungumzia kuhusu Mwokozi. Tunaye Mwokozi katika Kristo, na wake zetu wanapaswa kuwa na Mwokozi ndani yetu. Tunaye mkombozi katika Kristo. Na wenzi wetu wanapaswa kuwa na Mkombozi ndani yetu. Unapozungumzia kumpenda mke wako unazungumzia kuhusu kubeba msalaba. Uhusiano wa kindoa unafananishwa na uhusiano uliopo baina ya Kristo na kanisa lake. Mwanaume ana nafasi nyumbani kama ile Yesu aliyonayo kanisani. Kama mwanaume anavyomchukua Yesu kuwa mtu wake anayemkubali sana, ndivyo ilivyo pia katika ndoa.

Wajibu wa pili na ambao ningependa kuusisitiza ni ule wa kukaa na mke, 1 Petro 3:7, “Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa

17

mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.”

“Waume wengi wamezitelekeza familia zao kwa ajili ya kutafuta mali za kuboresha familia zao. Lakini kile ambacho Mungu alimwamuru mwanaume ni kukaa na mke wake. Kwa mujibu wa Evans, “Hii haimaanishi kuishi tu kwenye nyumba moja naye. Neno la Kiyunani lililotumika kumaanisha “kukaa” ni kukaa karibu kwa maelewano, kujipanga kwa ukaribu, kuwa na ujirani naye” inamaanisha ni kukaa kwa ukaribu zaidi.

Wanaume wengi wana mawazo haya, Ninaenda nje, mimi ndiye mtoaji, na wewe ni mke, utakaa nyumbani. Unafanya kazi yako, nafanya yangu” Hapo ndipo tatizo lilipo. Nyumbani ni kazini pako! Kazi ya mwanamke ni kumsaidia mume, lakini hapaswi kubadili nafasi yako kama mume. Unatakiwa kufanya kazi na mkeo kwa ukaribu ili kujenga roho ya maridhiano ndani yenu. Ili kufanya hilo mnatakiwa kuwa pale.” Wakati wowote mali unazomnunulia zinapokuwa badala ya kuwepo kwako, ndipo huendelei kuishi naye zaidi.

Huwezi tu ukaja nyumbani na kuanza kuwasha TV, unatakiwa uje nyumbani na kuanza kufanya naye kazi, na kuzungumza naye! Wakati fulani hiyo huashiria kuwa unatambua uzuri wake. Ama waweza mweleza maneno mazuri kama, hukuweza kuifanya akili yako isimfikirie siku nzima. Ama waweza kuanika nguo yeye akiwa anaendelea kufua. Wakati mwingine waweza tandika upande mmoja wa kitanda yeye akiwa anatandika upande ule mwingine. Kwa nini? Kwa sababu siyo mtumwa wako. Hapana! Hilo halikuwa kusudi la Mungu; alitolewa kwako awe masaidizi.

Kama Wakristo tunashangazwa kwa nini wanaume hawawajibiki leo. Kwa familia nyingi, wajibu wa baba unashuka na mama anachukua nafasi kwa kuwa hayupo. Biblia inapendekeza kwa msisitizo nafasi ya baba kama mkuu wa familia. Hakuna mwingine anayeweza kuziba nafasi hiyo; unapaswa kuwa pale. Watoto wako wanatakiwa kujifunza namna ya kumwona Mungu kama baba kupitia kwako. Ingawa majaribu yanaweza kuibuka katika maisha ya wanandoa, mume na mke wanatakiwa kuhifadhi roho zao katika pendo la Mungu. Baba anapaswa kumwangalia mama wa watoto wake kama mmoja anayestahili upendo, uangalizi, na kuhurumiwa. (Adventist Home uk. 178)

Siri ya Umoja wa Familia. Ellen G. White ana kauli kali ambazo tungependa tuzitoe kwenu ili mzielewe vizuri na ziwe na mvuto wa pekee maishani mwenu. Yeye anasisitiza na kutuhakikishia kwamba chanzo cha

18

migawanyiko na malumbano katika familia na kanisani ni kujitenga na Kristo. Ndiyo, kumsogelea Kristo ni kusogeleana sisi kwa sisi. “Siri ya umoja wa kweli kanisani na katika familia siyo diplomasia, siyo utawala, siyo juhudi isiyo ya kibinadamu ya kushinda matatizo – ingwa hii nayo inahitajika – lakini ni umoja na Kristo. (Adventist Home uk. 179)

Kila aliye mume na baba angesoma ili “kuelewa maneno ya Kristo, siyo kwa kuegemea upande mmoja, ule wa utii wa mwanamke kwa mumewe, bali katika nuru ya msalaba wa Kalvari, kusoma ili kujua nafasi yake katika mzunguko wa familia.” “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno.” Yesu alijitoa mwenyewe afe msalabani ili kusudi kutusafisha na kutulinda na dhambi na uchafu kwa mvuto wa Roho Mtakatifu. (Adventist Home uk. 117)

Wakati fulani tunapokuwa hatuzungukwi na hali safi na takatifu, tunaonesha roho ya ukatili nyumbani. “Mtu afanyaye hivi anafanya kazi kwa ubia na mawakala wa shetani. Ilete nia yako katika kutii mapenzi ya Mungu. Fanya yote yaliyo katika uwezo wako kufanya maisha ya mkeo kuwa ya kuvutia na yenye furaha. Lichukue neno la Mungu kama mtu wako wa kukushauri. Ukiwa nyumbani ishi mafundisho ya neno. Ndipo utayaishi kanisani na utayachukua mahali pako pa kazi. Kanuni za mbinguni zitaboresha shughuli zako zote. Malaika wa Mungu watashirikiana nawe, wakikusaidia kumfunua Kristo katika ulimwengu. (Adventist Home uk. 213)

19

5. Jukumu la mke katika familia ya Kikristo

Tony Evans alikuwa sahihi aliposema kwamba Mungu aliwaita mume na mke kuhudumiana. “Ndoa ni taasisi iliyosimikwa na Mungu, muunganiko mtakatifu, amabapo mume anamhudumia mke, na mke anamhudumia mume. Kitu kibaya ambacho mwanaume aweza kukifanya ni kuoa mke asiye sahihi. Suleimani analithibitisha hili katika Mithali 27:15, “Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi, Na mwanamke mgomvi ni sawasawa.” Kwa kweli hakuna kitu kinachoweza kuwa kibaya kama kutumia siku zote za maisha yako na mwanamke mwovu, hali ni hiyo hiyo pia kwa mwanaume.

Mungu aliwaumba kwa makusudi mwanaume na mwanamke ili waishi pamoja kwa maelewano na kila mmoja akifidia mapungufu ya mwenzake. Wale waliooana waliokuwa hawalijui hili, ni wakati wa kufahamu kanuni hii, na wale ambao hawajaoa na kuolewa wajitahidi kulifikia hili. Wajibu wa kwanza ambao mwanamke mwema anatakiwa kuutimiza ni kumsaidia mwanaume wake. Mwanzo 2:18, “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”

Tunaishi katika zama za usawa na ukombozi wa wanawake unaosukumwa na kiu ya madaraka. Ingawa Biblia inafafanua mahusiano mema yaliyoanzishwa na Mungu mwenyewe, ambapo mwanamke ni msaidizi na mume ni kichwa cha familia; mambo haya mawili yanaonekana ya kigeni kwenye jamii ya kisasa. Hata hivyo ndivyo Mungu alivyotaka iwe. Kama kila mmoja katika familia atatimiza wajibu wake kulingana na mpango wa Mungu, hapatakuwa na sababu ya kupigania haki za kila mmoja. Baba atachukua nafasi kama ya Yesu kwa kanisa lake; na mke na watoto watakuwa watii kwa baba kama wakristo walivyo watiifu kwa kiongozi wao Yesu Kristo.

“Evans anathibitisha kwamba: “Moja ya sababu zinazofanya wanaume wafanye vibaya ni kwa sababu mwanamke hamsaidii, anaitumia ndoa kujisaidia mwenyewe. Ana mtazamo tofauti wa mahusiano. Badala ya kuwa mshirika wake na kuja karibu naye na kuongeza mahusiano yao na Mungu, anakuwa sehemu ya upinzani, hashirikiani na ajenda ya Mungu kwa familia, bali anaitumia kama mahali pa kujitimizia haja zake mwenyewe. Na wakati mwanamke anapokosa shabaha kwamba tarajio la kwanza la Mungu kwake katika mahusiano yake na mumewe ni kuwa msaidizi, ndipo hali ya hewa iliyo kinyume inapozaliwa nyumbani ambayo ni vigumu kuishinda.”

20

Jambo la pili, hata ingwa mume hatendi yale anayopaswa kutenda, kumbuka kuwa ufumbuzi ni kumsaidia pale alipo dhaifu ili kusudi familia iendelee kuwa imara. Hawa wawili wameumbwa ili wasaidiane. Hii humaanisha kufidia pale udhaifu unapopatikana. Mke si mkamilifu, na mume naye pia. Wajibu wa kila mmoja ni kujenga daraja. Ni vizuri kila siku kukumbuka kwamba kuna wageni wasioonekana. Yesu ameahidi kuwa pamoja nasi daima; lakini ni lazima tumpokee kama Bwana wa familia yetu kama tunahitaji kweli ushindi katika ndoa yetu.

Kile ambacho mwanamke anatakiwa kufahamu ni kwamba mwananume hawezi kuwa mwanamke. Mungu amewaumba kwa namna hiyo. Kila mmoja atimize wajibu wake wa kuwa vile Mungu alivyokusudia awe. Kubadilishana majukumu hakuwezi kumshusha yeyote. “Sasa, wanawake, ikiwa Mungu anawatarajia muwasaidie wanaume zenu, hiyo yenyewe humaanisha mwanaume wako anahitaji msaada!” Evans.

Ni kilio cha wanawake wengi kwamba wanaume wanatumia vibaya madaraka na uongozi ambao Mungu aliwapatia. Wanakosea na wanatawala kwa fimbo ya chuma na kuwasaga walio chini yao. Ni nini ingepaswa iwe mwitikio wa mwenza katika mazingira haya? Kwa mara nyingine tena ni kuomba na kumsaidia ndiyo ufumbuzi unaoweza kuleta matunda. Wanaume wanahitaji msaada na ni wewe ndiye wa kusaidia. Pale usipoweza mumeo pia atakusaidia. Tunapaswa kutegemeana. “Huwezi kulalamika kwamba hayupo vile alivyopaswa kuwa ikiwa wewe mwenyewe hutimizi majukumu yako kama msaidizi! Mungu alikufanaya msaidizi kwa sababu kwa ukweli mwanaume anahitaji msaada. Anahitaji sana mtu fulani wa kuja karibu naye aliye tofauti na yeye, ili kumkamilisha, na hivyo kutimiza mpango wa Mungu.

Mithali 31:10, “Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.” Wanawake wanapaswa kujiona kwa namna ile ambayo Mungu alitaka wawe. Mwanamke akijiona katika ile thamani yake halisi, atatekeleza majukumu yake bila ulalamishi. Evans anaiweka kwa namna hii:

Wanawake wengi wanajitazama kwa mtazamo wa chini unaowafanya kuwa wake dhaifu. Unapojitazama mwenyewe na kujilinganisha na dhahabu isiyo na thamani, kama ulivyo machoni pa Mungu, basi utatenda kwa nama hiyo hiyo. Ikiwa unajitazama kama kito cha mbadala, utaishi namna hiyo hiyo. Mithali 31 inaongelea mwanamke halisi. Siyo mwanamke aliyeundwa na vipodozi, vito n.k. hadi unakaribia kutotambua umfananishe na nini, lakini ni mwanamke mwadilifu. Na maandiko yanasema mtu anapompata aina hii ya mwanamke, mke wa kweli na mwadilifu; amepata kipande cha kito chenye

21

thamani. Na muhuri wa mwanamke huyu ni nini? Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake. Mithali 31:12. Atamtendea mema na siyo mabaya siku zote za uhai wake. Sasa ikiwa mume wako angeulizwa unamtendea jambo gani jema, angekuwa na jibu? Msaidie aingiapo msaidie atokapo. Biblia inasema: “Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo. Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali. Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao. Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.” Mithali 31:13-16.

“Huyu si kama wanawake wa kisasa wanaofanya kazi zao wenyewe, wenye fedha zao wenyewe na akaunti za wenyewe na wanaoandika hundi zao wenyewe. Wanaotumia fedha zao kununulia nguo za gharama kubwa, vito na vitu vingi vingine vinavyoonesha kwamba wana nguvu na hawahitaji mtu mwingine yeyote kuwatawala au kuwasaidia kwa namna yoyote. Huyo siyo mwanamke mcha Mungu. Kwa sababu mwanamke mcha Mungu, wakati akitumia stadi hizo huko nje, daima hurudisha fedha nyumbani kwa ajili ya kupamba nyumba na kumpendezesha mumewe. Hakuna mashindano ya fedha.” Evans

Changamoto ya tofauti. Tunapaswa kuishinda changamoto ya tofauti kwa upendo na kwa kumwelewa Mungu mwanzilishi wa ndoa. Mshauri anayeheshimika wa mambo ya ndoa Dr. Carl Whitaker (1988) amesema: ndoa yenye afya kwa kweli ni muunganiko wa tamaduni mbili za kigeni. (uk.202). Hatimaye, namna tunavyoshughulikia tofauti zetu huamua ubora wa ndoa na familia zetu. Ubora wa mahusiano ya familia zetu za kikanisa pia unategemea namna tunavyoshughulikia tofauti zetu kama waumini.

Na kama unaipenda kazi yako sana kiasi kwamba mumeo hafaidiki na ile kazi yako unayoipenda, basi wewe si mwanamke mcha Mungu. Umejinunulia uongo kwamba wewe ni mwanamke uliye hivyo, unafanya mambo yako mwenyewe, na kwamba mwanaume kwako ni usumbufu tu. Lakini kwa sababu wanawake wengi wamefungua akaunti za benki, na wanatumia fedha zao wenyewe kwa ajenda zao wenyewe na mwanaume hana uzuri wowote, basi mibaraka ya Mungu haitakuwepo maishani mwao au nyumbani mwao. Nyumba zao zilizizokuwa na uchaji wa Mungu zitakuwa nyumbaz isiyo na Mungu.

Unapoanza kuishi maisha yako ya ndoa bila kufikiria ustawi wa mume wako, umejiunga na yule adui katika kuimomonyoa ndoa yako. Mungu hakukupa

22

mume ili uendelee kuwa mwanamke anayejitegemea akiishi peke yake. Alikupa mume ili kusudi muwe washirika na yeye, ukimsaidia kwa kutumia karama zako, stadi zako, na uwezo wako aliokubariki nao, kwa ajili ya ustawi wa nyumba nzima. Wakati kazi yako inapokutaka wewe uache wajibu wako kama mke na mama, unakuwa upo kwenye mstari uliopotoka, na huo siyo wito kutoka kwa Mungu.

23

6. Kulea

Malezi ni nini?

Malezi, kwa mujibu wa Wikipedia encyclopedia “ni mchakato wa kuinua na kutegemeza makuzi ya kimwili, kihisia, kijamii, na kiakili ya mtoto tangu utoto hadi utu uzima. Malezi humaanisha shughuli za kumkuza mtoto zaidi kuliko mahusiano ya kibaolojia.” Inahusisha kulea uzoefu, stadi, sifa, na majukumu.

Kwa mujibu wa chanzo hicho hicho, kwa upande wa wanadamu, hili kwa kawaida hufanywa na wazazi wa kibaolojia wa mtoto anayehusika, ingawaje serikali na jamii zina wajibu wake pia. Katika hali nyingi, watoto yatima au waliotelekezwa hupokea matunzo ya malezi kutoka kwa watu wasio na uhusiano nao wa damu. Wengine huweza kuchukuliwa na wasamaria wema na kuwafanya watoto wao, au kuchuliwa na jamaa ya karibu, au kuwekwa kwenye vituo vya kulelea watoto yatima.

“Kutokana na yaliyoelezwa hapo juu, moja ya maeneo magumu kuliko yote katika jukumu la malaezi ni swala linalozunguka jukumu la kuwa mlezi katika kusomesha, kutoa adhabu, na kurithisha tabia njema. Ya pili ni kuweza kutengeneza mazingira ya kufaa kwa ajili ya ustawi wa watoto. Ulimwengu huu ambako sanamu huonekana kuwa kila kitu hutoa shinikizo kubwa kwa watoto wetu – shinikizo la kufanikiwa, shinikizo la kuipata elimu, shinikizo la tabia njema, shinikizo la kutaka uonekane mwanariadha au mwembamba, shinikizo la kuvaa kwa mtindo unaokubalika kwa wakati huo. Uwezekano wa kushindwa ni mkubwa siku hizi zenye vipaumbele vya taswira. Uwezekano wa kutoendana nao ni mkubwa kuliko hapo zamani.” (Victor Marley, katika kitabu chake: Parenting for Growth.)

Kwetu sisi, kama kanisa la Kikristo, tunaundaje mipaka yenye uhalisia na ufanisi kwa watoto wetu? Tunawezaje kuhakikisha kwamba wanakua katika tabia za uaminifu, uwajibikaji, uadilifu, na ukomavu? Jukumu la mzazi ni gumu sana lakini la muhimu. Hakuna anayeweza kulikwepa. Taswira ya jamii tuliyonayo leo inashikika. Tunapaswa kuhakikisha kwamba hatuendelei na makosa yale yale ya nyuma tukijifanya tunayasahihisha. Kwa mfano jamii yetu leo inalazimishwa kumfikiria mwanamke katika kila jambo wanalofanya. Wanawake wanapendelewa mara nyingi. Hupanda kwenye nafasi za juu kwa sababu ya jinsia yao. Kama jamii ingekuwa inawajibika na aminifu kwao, ingekuza uelewa kuwa wapo hapo walipofikia kwa kuwa wanastahili na siyo kwa sababu ya upendeleo wa wanawake. Hii itawajulisha kwa mara nyingine

24

tena ya kuwa ni lazima ufanye kazi kwa bidii, kwa sababu ndiyo ukweli hapa duniani kama unataka kuwa na mafanikio.

Malezi ya Kiroho

“Ni jambo la ajabu unapowaza kuwa Mungu aliweka nguvu hiyo isiyomithilika ndani ya mume na mke, kwamba kutokana na upendo wao, maisha mapya yaletwe duniani. Na ni upendeleo na jukumu la kiushangaza kulea watoto wako kwa upendo huo unaofanana na wa Kristo, kwamba wakue wakimstaajabia na kumwabudu Baba yao wa Mbinguni! Malezi ya Kiroho ni malezi yaliyojengwa katika Biblia.”

Je, haishangazi kujua kwamba Mungu ndiye wa kwanza kuifanya kazi hii ya malezi? (Ufunuo 3: 19). Kwa wale awapendao huwaadhibu lakini pia yupo tayari kuzungumza na watoto wake ili awalete kwenye uelewa mzuri. “Je, tokea wakati huu hutanililia, Ee Baba yangu, wewe u kiongozi wa ujana wangu? Je! Ataishika hasira yake hata milele? Ataishika hata mwisho? Tazama, umesema hivyo, bali umetenda mambo mabaya, umefuata njia yako mwenyewe. Mungu anatoa ushauri mwema kwa Israeli kwenye fungu la 22 “Rudini, enyi watoto waasi, mimi nitaponya maasi yenu. Tazama, tumekuja kwako; maana wewe u Bwana, Mungu wetu. Na Mungu anatoa mashauri mema kwa wazazi kupitia nyaraka za mtume Paulo namna hii: “Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.” (Waefeso 6:4)

Malezi ni mojawapo ya kazi muhimu mno na yenye changamoto, Mungu aliyowapatia wanadamu. Katika kitabu ‘Child Guidance,’ Ellen White anatuambia, “Hakuna kazi ya juu iliyowahi kupewa wanadamu wafao zaidi ya kuchonga tabia.” Uk. 163).

Ni tabia ya Kikristo inayowapatia watoto wetu mambo muhimu ya kiroho na kihisia ambavyo ni vya lazima ili kufanikiwa katika mahusiano yao. Wazazi wanatekeleza jukumu muhimu na la maana katika kusimamia makuzi ya tabia ya watoto wao na kujumuika nao nyumbani na kwa marafiki zao.

Kuunda Mazingira yaliyo Safi

Kwa hiyo malezi ni ya kwanza, kuunda mazingira yaliyo safi ambamo watoto watakuwa wakiongozwa kwenye mazingira mazuri ya Kikristo. Ellen G. White alisema katika kitabu chake cha Adventist Home yafuatayo: “Kila familia ya Kikristo ni lazima iwe na sheria; na wazazi ni lazima kwa maneno yao, na

25

kwa vitendo vyao wenyewe kwa wenyewe, watoe kwa watoto, mfano bora na ulio hai ambao wangetamani watoto wao wawe nao. Usafi katika matamshi na tabia njema ya kweli ya Kikristo ni lazima vioneshwe daima.

Wafundishe watoto na vijana kujiheshimu wenyewe, kuwa wakweli kwa Mungu, wakweli kwa kanuni; wafundishe kuheshimu na kutii sheria ya Mungu. Kanuni hizi zitatawala maisha yao na zitapelekwa nje kwa wenzao wanaoshirikiana nao. Watatengeneza mazingira safi – ambayo yatakuwa na mvuto wa kuzitia moyo roho dhaifu katika njia iendayo juu kwenye utakatifu na mbinguni.

“Hebu kila somo liwe na tabia inayoinua na iboreshayo, na kumbukumbu zilizoandikwa kwenye vitabu vya mbinguni zitakuwa katika namna ambayo hutaaibika kuviangalia siku ya hukumu.” (Adventist Home uk. 16.3).

Mtume Paulo katika barua yake kwa Wathesalonike anasema hivi: “Vile vile, kama mjuavyo, jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo na kushuhudia, ili mwenende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.” (1 Thessalonians 2: 11-12).

Malezi ni msuguano baina ya uhuru na adhabu:

Malezi ni jukumu zito la kuwakuza watoto wafanyao maamuzi mazuri katika mazingira magumu, wakiyapinga mashauri yasiyofaa ya watoto wa umri wao, na wakitoa mvuto mzuri kwa watu wanaowazunguka. Katika kanuni zote tulizozungumzia zinazohusu kulea, yenye changamoto kubwa zaidi ni namna ya kumwadabisha mtoto. Unaweza kuichagua kanuni nyingine yeyote kama malezi ya msingi, lakini mimi nimechagua hii ili kuanza nayo. Kwa sababu naamini kuwa nidhamu ni ya muhimu kila mahali, kuanzia nyumbani, shuleni na baadaye kazini ambako kazi njema itategemea nidhamu. Kwangu mimi ni muhimu kushughulikia nidhamu kuanzia nyumbani, ili watu wawe na zana za kuyakabili maisha.

Kwa hiyo ni sawa kumfundisha mtoto wako majukumu kupitia nidhamu (adhabu). Kila mzazi angetamani watoto wake wangekuwa na mipangilio katika kazi, lakini wanaonekana daima kuwa na udhuru. Ikiwa watoto wako wanakuchanganya haupo peke yako. Hapa tunapendekeza kazi za kawaida ambazo unaweza kuzifanya nyumbani ili kujenga nidhamu

Unawezaje kuwafanya watoto wako wasafishe vyumba vyao bila kinyongo? Maswala mengine ya watoto ambayo wazazi wamelalamikia ni kulundika nguo chafu, kuweka vyombo vichafu kwenye karo, kutofagia sakafu chafu au

26

kazi nyingine yoyote utakayowatuma. Vijana wakubwa hujifunza masomo ya maana kama uwajibikaji, Kujitegemea, na stadi za kufanya maamuzi. Hata ingawa jambo hili laweza kusababisha migongano, kuwafanya watoto wako wasaidie kazi za nyumbani ni jambo lenye faida kwa namna nyingi. Licha ya kuwa ni nyongeza ya stadi muhimu za maisha, itakupatia muda wa ziada wa kukaa nao.

Kushugulika na Udhuru

Kila mzazi anajua inafananaje kushughulikia udhuru wa watoto. Wengi wao, watapata udhuru ili wasifanye kile wanachotakiwa kufanya kwa ratiba ya kila siku. Yafuatayo yalipendekezwa na uchunguzi unaohusu kuwarudi watoto.

“Kila mzazi ameshawahi kushughulika na udhuru wa watoto wake. Na unaendelea kufikiri kwamba kama angefanya kazi alizopangiwa badala ya kutoa udhuru na kubisha, angekuwa ameshamaliza! Tumia vidokezo vifuatavyo kuwasaidia watoto kukubali kazi wanazopangiwa.

Chambua matokeo pale mtoto wako anapokataa kufanya majukumu yake.

Kwa mfano, ikiwa mtoto wako hataki kuosha vyombo, mkataze asitazame video, TV, na michezo mingine iliyopo hapo nyumbani anayoipenda, hadi amalize kazi aliyopewa.

Unda ratiba ambayo majukumu hutangulia na kisha kufuatiwa na maburudisho. Kwa njia hiyo, ikiwa mtoto wako huwa anamangamanga anapopewa kzi za kufanya, muda wake wa maburudisho utaendelea kupungua. Vijana wakubwa wao huja na udhuru wa ajabu wakati wasipotaka kuacha michezo yao. Nenda nao katika shughuli waifanyayo na jaribu kufanya nao hiyo kazi wanayoilalamikia. Wafundishe watoto tofauti kati ya udhuru wa kweli na uvivu. Udhuru wa kweli unamaanisha kwamba kuna kitu kimejitokeza kinachofanya iwe vigumu kutekeleza jukumu kama lilivyokuwa limepangwa, kama vile kuumwa. Udhuru wa kweli humaanisha kwamba bado utahitaji kulifanya lile jukumu, ila utachukua muda mrefu zaidi kulikamilisha. Udhuru wa uvivu ni ule ambao mtoto wako huutumia kwa sababu tu hataki kuifanya ile kazi.

27

7. Uchaguzi wa Mwenzi wa Maisha

Ndoa ni kitu cha muhimu sana na amabcho hakitakiwi kuchukuliwa kwa wepesi. Ni kitu kitakachoelekeza na kuathiri maisha yako katika ulimwengu huu na katika ulimwengu ujao. Mkristo wa kweli kamwe hawezi kuendelea na mipango yake kwenye welekeo huu bila kuwa na hakika kama Mungu ameafiki mpango wake. Ellen G. White anashauri kwamba “tusitafute kutaka kujiridhisha wenyewe, lakini tujisikie kuwa ni lazima Mungu atuchagulie. Hatupaswi kujiridhisha wenyewe, kwa kuwa Kristo hakujiridhisha mwenyewe. Nisieleweke kumaanisha ya kwamba mtu yeyote atapaswa kumwoa yule asiyempenda. Hiyo ingekuwa dhambi. Lakini viini macho na misisimko ya mwili isiruhusiwe kutuongoza kwenye maangamizo. Mungu anahitaji moyo wote, upendo ule mkuu.” {CCh 112.1}”

Upendo ni wa lazima katika ndoa, lakini ni lazima uwiane na uelewa dhahiri wa kile kinachotokea katika maisha halisi. Vijana wengi hujitumbukiza kwenye ndoa bila kuangalia matokeo ya maamuzi yao. Kwa mara nyingine tena Ellen G. White anatoa maelekezo mazuri katika kutafuta mwenzi wa maisha. “Wale wanaotafakari ndoa wanatakiwa kufikiria ni nini itakuwa tabia na mvuto wa nyumba wanayokusudia kuianzisha, watakapokuwa wazazi. Wajibu mtakatifu umewekwa juu yao. Ustawi mzuri wa watoto wao katika ulimwengu huu na katika ulimwengu ule ujao, unawategemea wao. Kwa kiasi kikubwa wao ndio wanaoamua muhuri wa kimwili na kiroho ambao watoto hao wataupokea. Na tabia ya nyumbani inategemea hali iliyoko kwenye jamii; mvuto wa uzito wa kila familia, utaamua kama mzani utapanda juu au utashuka chini.

Ushauri wake ni kwamba “uangalifu mkubwa ni lazima ufanyike na vijana wa Kikristo katika kuunda urafiki na katika kuchgua mwenzi wa maisha. Uwe macho, isije ikawa kile ukidhaniacho kuwa ni dhahabu kikageuka kuwa chuma cha kawaida. Ubia katika mambo ya ulimwengu huwa na kawaida ya kuweka vipingamizi katika njia ya huduma yako kwa Mungu, na roho nyingi zinaangamizwa na umoja usio na furaha, (uwe wa biashara ama wa ndoa,) na wale ambao hawawezi kamwe kuinuka au kuwa bora.” (CCh 112)

Imegundulika kwamba baadhi ya vijana wakati fulani wana vipaumbele visivyoweza kudumu. Baadhi huangalia afya, wengine umaarufu na wanasahau kwamba yote haya yaweza kudumu kwa muda kitambo ikiwa hayakujengwa juu ya tabia maalumu. Pima kila hatua, na angalia kila maendeleo ya tabia ya yule unayemfikiria kuungana naye kwa maisha yote.

28

Hatua unayokwenda kuichukua ni moja iliyo muhimu kuliko zote katika maisha, na hivyo isiingiliwe kwa haraka.

Unaweza kupenda, lakini usipende kiupofu. Kagua kwa uangalifu ili uone ya kama maisha yako ya ndoa yatakuwa yenye furaha ama yasiyo na maelewano na mabaya. Hebu maswali yangeulizwa, je, muunganiko huu utapanua eneo langu la kutumika? Ikiwa maswali haya hayaleti majibu yenye utata, basi kwa hofu ya Mungu songa mbele. (CCh 112)

Uchaguzi wa mwenzi wa maisha ni lazima uwe ule utakaozingatia hali za kimwili, kiakili, na kiroho za wazazi na watoto katika kubariki wanadamu wenzao na kumtukuza Muumbaji

Sifa zinazoangaliwa kwa mke mtarajiwa.

a. Hebu mvulana amtafute yule ambaye atasimama upande wake, aliye na uwezo wa kuchukua sehemu ya mzigo wake, yule ambaye mvuto wake utamwinua na kumtakasa, na atakayemfanya mwenye furaha maisha yake yote.

b. Kwa mujibu wa Biblia: “Mke mwema atoka kwa Bwana. Moyo wa mumewe humwamini. Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu. Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema, Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote. Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana.”

Haya ni mambo yatakayozingatiwa:

1. Yule utakayeoana naye ataleta furaha nyumbani kwako? 2. Je huyu mwanamke ni mjasiriamali, au atakapoolewa siyo tu atafuja

mapato yake yote, bali atafuja pia mapato yako ili kujilisha upepo au kupenda mwonekano? Kanuni zake ni sahihi katika welekeo huu?

3. Huyu mwanamke anacho chochote cha kumsaidia kumudu maisha?... Ninajua kwamba kwa akili za mwanaume aliyebanwa na upendo na fikra za ndoa, maswali haya yatatupiliwa mbali kana kwamba hayatakuwa na matokeo katika maisha ya baadaye. Lakini mambo haya ni lazima yazingatiwe kwa sababu yana mchango katika maisha yako ya baadaye.

4. Katika uchaguzi wako wa mke chunguza tabia yake. Atakuwa mtu mwenye uvumilivu? Au ataghairi kumtunza mama yako na baba yako katika wakati ambao wanahitaji mtoto mwenye nguvu naye ataenda

29

kwenye mipango yake ya kuifurahisha nafsi yake mwenyewe, na kumwacha baba na mama ambao badala ya kumpata binti anayejali watampoteza pia kijana wao?

Sifa zinazoangaliwa kwa Mume mtarajiwa:

Kabala hajatoa mkono wake kwake kwenye harusi, kila mwanamke anatakiwa kujiuliza kama yule anayekwenda kuunganisha naye mustakabali wa maisha anastahili.

1. Taarifa zake za mambo ya huko nyuma zikoje?2. Je, maisha yake ni safi?3. Je upendo anaoonesha ni wa kweli, unaoinua tabia, au ni msisimko tu?4. Anazo tabia zitakazomfanya kuwa mwenye furaha?5. Naweza kuipata furaha na amani ya kweli nikiwa karibu naye?6. Ataruhusiwa kuhifadhi haki zake za msingi, au atalazimishwa kusalimisha

maamuzi na dhamira yake kwa mumewe?7. Anaweza kuheshimu madai ya Mwokozi kuwa Ndiye mkuu kuliko wote?8. Je, mwili na roho, mawazo na makusudi, yatahifadhiwa safi na matakatifu?

Maswali haya yanabeba umuhimu mkubwa kwa ustawi wa kila mwanamke anayeingia kwenye mahusiano ya ndoa.

Hebu mwanamke anayetamani muunganiko wenye amani, na wenye furaha, anayetaka kujiepusha na misiba na huzuni za baadaye ajiulize kabla hajatoa upendo wake.

1. Mpenzi wangu anaye mama? 2. Alama kubwa ya tabia yake ni nini?3. Je, anatambua jukumu lake kwa huyu mama?4. Anajali furaha na matakwa yake? 5. Kama hamweshimu na kumtii mama yake, ataonesha heshima na

upendo, wema na usikivu, kwa mkewe? 6. Wakati upya wa ndoa utakapokwisha, bado ataendelea kunipenda? 7. Atayavumilia makosa yangu, au atakuwa mkosoaji, mkali, na dikteta? 8. Upendo wa kweli utayafunika makosa mengi. Upendo hautayagundua. 9. Hebu binti ampokee kama mwenzi wa maisha yule tu mwenye tabia

zilizo safi za kiume, yule ambaye anatia moyo, mwaminifu na yule ampendaye na kumcha Mungu.

10. Waepuke wale wasioheshimu watu. 11. Waepuke wale wapendao uvivu. 12. Waepuke wale wanaodhihaki mambo matakatifu.

30

13. Epuka kuunganika na atumiaye lugha chafu.14. Epuka na yule anayetumia hata glasi moja ya pombe. 15. Usisikilize mashauri ya mtu ambaye hatambui wajibu wake kwa

Mungu.

Ukweli safi utakasao roho utakupatia nguvu kujiondoa kutoka kwa mtarajiwa anayevutia na ambaye umejua hampendi na kumcha Mungu, na asiyejua lolote kuhusu kanuni za haki ya kweli. Tunaweza daima kuchukuliana na madhaifu ya marafiki zetu na kutojua kwao, lakini kamwe hatuwezi kushirikiana nao.

Upendo ni Zawadi ya Thamani kutoka kwa Yesu

Upendo ni zawadi ya thamani tunayoipokea kutoka kwa Yesu. Upendo wa kweli na mtakatifu siyo hisia, bali ni kanuni. Wale wanaoongozwa na upendo wa kweli si vipofu au wasio na akili. Kuna upendo mchache na adimu wa kweli na wa kujitoa kikweli kweli. Tamaa ndiyo inayoitwa upendo

Kanuni za upendo wa kweli zipo juu na takatifu, na zipo tofauti na upendo uamshwao na tamaa, ambao hufa ghafla unapoumizwa na kutingishwa.

Upendo ni mmea unaokuzwa kimbingu, na ni lazima ulishwe na kukuzwa. Mioyo yenye upendo, maneno ya kweli, yenye upendo, vitafanya familia yenye furaha na kutoa mvuto unaoinua kwa wote walio kwenye mzunguko wa mvuto wao.

Wakati upendo safi hukubaliana na Mungu katika mipango yake yote, na huwa katika mapatano makamilifu na Roho wa Mungu, msisimko utakuwa kichwa ngumu, wenye harara, usiotumia akili, usiokubaliana na vizuizi vyote, na hukifanya kile ilichokichagua kuwa sanamu yake. Katika njia zake zote yule aliye na upendo wa kweli, neema ya Mungu itaonekana. Ukatikati, maisha rahisi, udhati, uadilifu, na dini vitaonekana katika kila hatua atakayopiga kuelekea muunganiko wa ndoa.

Wale waliotawaliwa hivyo hawatatekwa kujumuika na mwingine itakayomletea hasara ya kupoteza mvuto wa mkutano wa maombi na huduma za kidini. Upendo wao kwa ukweli hautakufa kwa kupuuza fursa na upendeleo ambao Mungu aliutoa kwao kwa neema.

Upendo ule ambao hauna msingi wa maana zaidi ya kuridhisha tamaa za mwili utakuwa kichwa ngumu, mpofu na usiotawaliwa. Heshima, kweli, na kila nguvu njema ya akili iliyoinuliwa zitaletwa chini ya utumwa wa tamaa. Mtu aliyefungwa katika minyororo hii ya kiwendawazimu mara nyingi ni

31

kiziwi kwa sauti ya akili na dhamiri; hakuna hoja wala wito utakaomwongoza kuona ubaya wa msimamo wake.

Upendo wa kweli si tamaa yenye nguvu na inayochoma. Kinyume chake ni tulivu na ya ndani sana kwa asili yake. Inaangalia ng’ambo ya yale yanayoonekana, na inavutiwa na ubora tu. Umejaa hekima na unachuja mambo, na kujitoa kwake ni halisi na kunakodumu.

Upendo ulio nje ya himaya ya misisimko na tamaa, huwa wa kiroho, na hudhihirika katika maneno na vitendo. Mkristo ni lazima awe na huruma na upendo viliyotakaswa, ambamo ndani yake hakuna kukosa subira. Hofu, kukosa adabu, na tabia za kijeuri, lazima zilainishwe na neema ya Kristo.

32

8. Maombi na Masomo ya Biblia ni vya lazima ili kufanya maamuzi yaliyo sahihi

Ikiwa imeanzishwa na Mungu, ndoa ni taasisi takatifu na isiingiwe katika roho ya ubinafsi. Wale wanaotafakari hatua hii ni lazima kwa unyenyekevu na kwa maombi watafakari umuhimu wake na kutafuta ushauri wa Mungu ili wajue kama wanakwenda kwa njia inayopatana na mapenzi ya Mungu. Maelekezo yaliyotolewa kwenye Neno la Mungu kuhusiana na jambo hili ni lazima yazingatiwe kwa uangalifu. Mbingu huziangalia kwa furaha ndoa zilizoundwa zikinia kufuata maagizo yaliyotolewa na Maandiko.

Ikiwa kuna somo lolote ambalo linapaswa kuangaliwa kwa akili iliyotulia na maamuzi yasiyoongozwa na misisimko, ni somo la ndoa. Ikiwa kuna wakati Biblia itahitajika kama mshauri, basi ni huo wakati ambao haijachukuliwa hatua ya kuwafunga pamoja watu wawili kwa maisha yao yote. Lakini mawazo yaliyopo ni kwamba kwa jambo hili hisia ni lazima ziongoze, na kwa mara nyingi ugonjwa wa mapenzi unateka swala zima na kuelekeza kwenye maangamivu. Ni katika eneo hili ambapo vijana huonesha uwezo mdogo wa akili kuliko katika maeneo mengine; ni hapa ambapo hukataa kushaurika. Swala la ndoa linaelekea kuwa na nguvu inayowaroga. Hawajitoi kwa Mungu. Akili zao zimefungwa minyororo na wanasonga mbele kisirisiri, kana kwamba wanahofia mipango yao isitibuliwe na mtu mwingine.

Wengi wanaabiri katika chombo cha hatari. Wanahitaji rubani; lakini wanasita kupokea msaada unaohitajika sana, wakijihisi kuwa wana uwezo wa kukigeuza chombo kuelekea kilikotoka bila kujua ya kuwa ki karibu kugonga mwamba utakaosababisha kutokea kwa dhoruba ya imani na furaha…hadi watakapokuwa wasomaji makini wa Neno (Biblia), watafanya kosa kubwa litakalowaondolea furaha yao na furaha ya wenzao, kwa sasa na kwa wakati ujao.

Kama wanaume na wanawake wana tabia ya kuomba mara mbili kabla hawajaingia katika uchumba, watapaswa kuomba mara nne kwa siku hasa wakati swala hilo linapotarajiwa. Ndoa ni kitu kitakacholeta mvuto na kuathiri maisha yako sasa katika ulimwebgu huu na ulimwengu ule ujao…

Ndoa Yenye Furaha na Isiyo na Furaha? “Ikiwa wale wanaofikiria kuwa na ndoa wasingependa kuwa na dalili za huzuni baada ya kuoana, ni lazima walifanye kuwa somo makini na la dhati sasa. Hatua hii ikichukuliwa bila busara ni mojawapo ya njia zenye ufanisi mkubwa katika za kuwaharibu vijana wa kike na wa kiume wenye kutegemewa. Maisha huwa mzigo, na laana, hakuna mtu anayeweza kuharibu furaha ya mwananmke na kufaa

33

kwake, na kufanya maisha kuwa mzigo unaoulemea moyo kama mume wake mwenyewe; na hakuna mtu anayeweza kufanya moja ya mia katika kuhafifisha matumaini na njozi za mwanaume, kutengua nguvu zake na kuharibu mvuto na matarajio yake, kama mke wake mwenyewe. Ni kutoka kwenye wasaa wa ndoa ambako wanaume wengi na wanawake wengi hupanga ushindi wao au kushindwa kwao katika maisha haya, na matumaini ya maisha ya baadaye.” (Adventist Home uk. 43)

Nyingi za ndoa za wakati wetu na namna ambavyo zinafanywa ni moja ya dalili za siku za mwisho. Wanaume na wanawake ni ving’ang’anizi na vichwa ngumu kiasi ambacho Mungu anaachwa kando ya mipango yao. Dini inawekwa kando, kana kwamba haina nafasi katika jambo hili nyeti na muhimu.

Epuka Ndoa baina ya Mkristo na Asiyeamini. – Ellen G. White anawaonya vijana wasioane na wasioamini. Na wale wasioamini ni wale wasioshiriki imani na kanuni za kanisa pamoja nasi. Tofauti moja katika imani yaweza kuharibu uzuri wa ndoa yako milele. Alisema: kuna kutothamini kukubwa kwa kutisha katika ulimwengu wa Kikristo, kwa kutothamini mafundisho ya neno la Mungu kuhusiana na ndoa baina ya wakristo na wasioamini. Wengi wajidaio kumpenda na kumcha Mungu huchagua kufuata akili zao zilizopinda kuliko kuchukua mashauri ya Hekima Isiyo na Ukomo. Katika jambo nyeti lihusulo furaha na ustawi wa wote wawili katika ulimwengu huu na ule ujao, maamuzi king’ang’anizi yameruhusiwa kutawala. (Adventist Home uk. 61)

Si jambo la kushangaza ndoa nyingi changa zimeharibiwa na ziko kinyume na kanisa. Vijana wengi amabo hawajaongoka wanafanya mchezo wa kubatizwa ili tu kuwapata mabinti wa Kikristo kutoka makanisani mwetu na ambao baadaye hubadilika na kurudia vile vile kama walivyokuwa huko nyuma. “Ni jambo la hatari kuunda ushirika wa kidunia. Shetani anatambua wazi kuwa wasaa unaoshuhudia ndoa za vijana wengi wa kiume na wa kike hufunga historia ya uzoefu wao wa kidini na kufaa kwao. Wamempoteza Kristo. Wanaweza kwa nyakati kujaribu kuishi maisha ya Kikristo, lakini jitihada zao zote zinatendwa zikikinzana na mvuto wa upinzani kutoka upande mwingine. Hapo mwanzo ilikuwa furaha na jambo la kujivunia kuzungumza kuhusu imani na tumaini lao; lakini sasa hawapo tayari kutaja jambo hilo, wakijua kuwa mtu waliyeungana naye kuelekea hatima moja, hafurahii hayo. Matokeo yake, imani katika ukweli wa thamani hufa moyoni, na shetani kwa werevu mkubwa huwatandazia wavu wa kutoamini. (Adventist Home uk. 66)

34

Ushauri wa wazazi wamchao Mungu

Huku tukiwa na huzuni nyingi zitokazo kwenye ndoa, ni kwa nini vijana wasingekuwa na hekima zaidi? Kwa nini waendelee kujisikia kwamba hawahitaji ushauri wa watu wenye umri mkubwa na wenye uzoefu? Kwenye biashara, wanaume kwa wanawake huonesha tahadhari kubwa. Kabala ya kujiunga na biashara yoyote muhimu, hujiandaa kwa kazi yao. Muda, fedha, na uchunguzi wa uangalifu hufanyika kwa jambo hilo, wasije wakafanya makosa katika shughuli zao. Ni tahadhari kubwa kiasi gani ingehitajika katika kuingia kwenye mahusiano ya ndoa; mahusiano ambayo yataathiri vizazi vijavyo na maisha ya baadaye! Kinyume chake huingiliwa kwa matani na wepesi, kwa tamaa na misisimko, upofu na ukosefu wa akili iliyotulia. Maelezo sahihi kuhusu jambo hili ni kuwa Shetani anatamani kuona machungu na machafuko duniani, na anatandaza wavu wake kunasa roho. Anafurahia kuwaona watu hawa wasiozingatia wakipoteza furaha yao katika ulimwengu huu, nwa wakipoteza kaya zao katika ulimwengu ule ujao.

Je watoto wachukue ushauri kutoka kwenye tamaa zao na mivuto yao bila kuzingatia ushauri na hukumu za wazazi wao? Baadhi huonesha kutotaka mawazo yaliyo katika maoni ya wazazi wao, wala kuheshimu maamuzi yao ya kiutu uzima. Ubinafsi umefunga mlango wa mioyo yao na kujielekeza kwenye hisia. Akili za vijana zinahitaji kuamshwa kuhusiana na jambo hili. Amri ya tano ndiyo amri pekee yenye ahadi, lakini inachukuliwa kwa wepesi na inapuuzwa kwa madai ya wapendanao. Kutojali upendo wa mama, kutoheshimu matunzo ya baba ni dhambi zitakazosimama zikiwa zimeandikwa dhidi ya vijana wengi.

Moja ya makosa makubwa yanayopendekezwa katika jambo hili ni kwamba vijana na wasio na uzoefu wasibugudhiwe, waachwe kuingiliwa kwenye uzoefu wao wa mapenzi. Kama kuna jambo ambalo lingehitajika kutazamwa kutoka kona zote ni hili. Msaada wa uzoefu wa wengine na upimaji wa uangalifu na uliotulia wa jambo hili kwa pande zote ni wa muhimu. Ni jambo ambalo limeshughulikiwa kwa wepesi na sehemu kubwa ya watu. Mchukueni Mungu na wazazi wenu wamchao Mungu katika mashauri yenu, marafiki zangu vijana. Ombea juu ya jambo hilo.

Mnauliza, hivi mzazi anatakiwa kuchagua mwenzi bila kushirikisha hisia za mvulana au binti yake? Naliweka swali hilo kwenu kama ambavyo

35

lingetakiwa kuwa: Hivi inafaa mvulana au binti achague mwenzi bila kwanza kushauriana na wazazi, wakati hatua hiyo itaathiri furaha ya wazazi? Na baada ya kushauriwa na wazazi, inampasa kijana kuendelea kufuata mipango yake mwenyewe kinyume na ushauri na maoni ya wazazi?

Ninajibu kwa ujasiri: Hapana. Amri ya tano inakataza jambo hilo. “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.” Hii ni amri yenye ahadi ambayo Mungu ataitimiza kwa wale wanaoitii. Wazazi wenye busara kamwe hawatachagua mwenzi kwa ajili ya watoto wao bila kuheshimu mapenzi yao. Lakini inawapasa kusisitiza kile kilicho chema hata kama watoto wao hawatahiari kuzingatia ushauri wao mwema. Wanatakiwa kutimiza wajibu wao kama wazazi.

Baba na mama wanapaswa kukubali jukumu lililowekwa kwao la kuongoza hisia za vijana ili waweze kuwapata wenzi wafaao. Wanatakiwa walione kuwa ni jukumu lao, kupitia mafunzo na vielelezo vyao wenyewe, kwa msaada wa neema ya Mungu, kuifinyanga tabia ya watoto wao kuanzia katika miaka ya awali ili wawe safi na bora watakaovutwa kwa yaliyo mema na ya kweli. Vinavyofanana huvutana. Vinavyofanana hupendana. Hebu upendo dhidi ya ukweli na usafi na wema vipandikizwe mapema katika roho, na kijana atatafuta ushirika na wale wenye kuwa na tabia hizi tu.

Ukristo kuwa Mvuto Unaotawala. – Ukristo unatakiwa kuwa mvuto unaotawala katika mahusiano ya ndoa, lakini mara nyingi nia iliyowaongoza watu kwenye muunganiko huu havioani na kanuni za Kikristo. Shetani anatafuta daima kuimarisha nguvu zake dhidi ya watu wa Mungu kwa kuwashawishi kuingia katika ushirika na watu wake, na ili alikamilishe hili huamsha tamaa zisizo takatifu mioyoni. Lakini Bwana katika neno lake ameelekeza vizuri watu wake wasiungane na watu hao wasio na upendo wake ndani yao. (Adventist Home uk. 94)

Hitimisho:

Juma hili ni ukumbusho kwa kanisa kuwa ndoa ya Kikristo siyo furaha ipatikanayo kiajali, bali ni jambo linalopangwa vizuri ambapo kila mmoja hushiriki. Ili kuwa na ndoa ya Kikristo, wazazi na viongozi wa kanisa, wanapswa kushirikiana kuwaandaa vijana kabla hawajachgua wenzi wao, wakiwa hawajajiandaa jambo linaloweza kuwasababishia kuanguka kwenye mitego ya mwovu. Hata baada ya uchaguzi mzuri, vijana bado wanahitaji hekima ya kanisa. Utunzaji maalumu unatakiwa kuwekwa ili wakue chini ya nguvu na uongozi wa Roho Mtakatifu kwa kuwafundisha Biblia na Maandiko

36

ya Ellen G. White kuhusu ndoa na maisha bora. Mungu Mwenyezi alibariki kanisa lake.

37