14
Ndani ... Waziri asisitiza umuhimu wa chakula Wanafunzi Bora 20 wapongezwa TEHAMA katika Shule za Msingi Uk.8 Uk.10 Toleo la 1/2013 ISSN NO: 1821-8717-1 Januari - Machi, 2013 P rofesa Eustella Bhalalusesa ameteuliwa kuwa Kamishna wa Elimu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Uteuzi wake ulianza Julai, 2012. Tunalenga katika Kuimarisha Ubora wa Elimu – Kawambwa Profesa Bhalalusesa, Kamishna wa Elimu S erikali inaweka msisitizo katika kuinua ubora wa elimu nchini ili kutoa wahitimu mahiri. Ili kufikia azma hiyo, Serikali itaimarisha na kuongeza miundombinu ya elimu, ikiwa ni pamoja na nyumba za mwalimu na maabara za sayansi; bila kusahau vifaa vya kufundishia na kujifunzia na kutoa motisha kwa walimu, wakufunzi na wahadhiri. Uk.11 Inaendelea uk. 5 Inaendelea uk. 6 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akishuhudia watoto wa shule ya msingi wanavyojifunza somo la TEHAMA mkoani Mtwara Jarida la Elimu WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

Tunalenga katika Kuimarisha Ubora wa Elimu – Kawambwa

Embed Size (px)

Citation preview

Nda

ni ..

. Waziri asisitizaumuhimu wa chakula

Wanafunzi Bora 20 wapongezwa

TEHAMA katika Shule za Msingi

Uk.8 Uk.10

Toleo la 1/2013 ISSN NO: 1821-8717-1 Januari - Machi, 2013

Profesa Eustella Bhalalusesa ameteuliwa kuwa Kamishna wa Elimu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Uteuzi wake ulianza Julai,

2012.

Tunalenga katika Kuimarisha Ubora wa Elimu – Kawambwa

Profesa Bhalalusesa, Kamishna wa El imu

Serikali inaweka msisitizo katika kuinua ubora wa elimu nchini ili kutoa wahitimu

mahiri. Ili kufikia azma hiyo, Serikali itaimarisha na kuongeza miundombinu ya elimu, ikiwa ni pamoja na nyumba za mwalimu na maabara za sayansi; bila kusahau vifaa vya kufundishia na kujifunzia na kutoa motisha kwa walimu, wakufunzi na wahadhiri.

Uk.11

Inaendelea uk. 5

Inaendelea uk. 6

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akishuhudia watoto wa shule ya msingi wanavyojifunza

somo la TEHAMA mkoani Mtwara

Jarida la ElimuWIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

Jarida la Elimu, 2013

YaliyomoWahaririMhariri Mkuu

Ntambi Bunyazu

---------------

MhaririTheresa Mbuligwe

---------------

Wahariri WasaidiziElizabeth Pancras

Oliva Kato

--------------

MsanifuRehema Maganga

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya

Ufundi

S.L.P. 9121, Dar es salaam

Simu:+255 2110146,

+255 2110150/2

Tovuti:www.moe.go.tz

Tahariri 3

Bodi ya Kitaalamu ya Walimu Kuanzishwa 4

Tunalenga Katika Kuimarisha Ubora wa Elimu – Kawambwa 5

Prof. Bhalalusesa, Kamishna wa Elimu 6

Mabadiliko ya Mihula ya Shule za Sekondari na Vyuo Vya Ualimu 7

TEHAMA Katika Shule za Msingi 8

Mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu Waonyesha Njia 9

Waziri wa Elimu Asisitiza Kuhusu Umuhimu wa Chakula Shuleni 10

Wanafunzi 20 Waliofanya Vizuri Zaidi Kidato cha Sita Mwaka 2012 Wapongezwa 11

Prof. Dihenga Astaafu Rasmi 12

Habari Katika Picha 13

1

Jarida la Elimu, 2013

Karibu katika toleo letu jipya la Jarida

la Elimu. Jarida hili ni moja ya njia

itakayotumiwa na Wizara katika kutoa

taarifa mbalimbali kuhusu masuala ya elimu.

Tuwahimiza wataalamu wa elimu kutumia jarida

hili kwa ajili ya kutoa maoni katika mambo yote

yanayohusu elimu.

Toleo letu la kwanza linatoa wito katika utoaji

wa elimu bora ili kusaidia jitihada zenye lengo la

kukuza ubora wa elimu nchini, kama kipaumbele

cha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Katika siku za karibuni, swali la jinsi ya kutoa

elimu yenye ubora limeamsha hisia za wadau

wa elimu. Ubora wa elimu unategemea ubora

wa kinachoingizwa, mchakato na matokeo yake.

Baadhi ya wadau wanaamini kwamba njia pekee

ya kufikia ubora wa elimu ni kuongeza kipato

cha mwalimu. Wazo la kuongeza mshahara wa

mwalimu ni muhimu sana kwa kuwa linaweza

kuwahamasisha walimu kufanya kazi kwa

juhudi zaidi, pamoja na kutatua matatizo yao

mengi. Kwa maoni yetu, kuongeza mshahara wa

mwalimu si njia pekee ya kuinua ubora wa elimu.

Tunaamini kwamba kuna njia nyingine zaidi za

kufikia ubora wa elimu, ikiwa ni pamoja na kuinua

hadhi ya mwalimu katika jamii inayomzunguka, na

kuimarisha miundombinu ya shule.

Kuinua hadhi ya mwalimu katika jamii ni njia nzuri

na inayoweza kushawishi zaidi kuliko kuongeza

mshahara peke yake. Hii inatokana na ukweli

kuwa siku hizi tatizo la walimu si kipato peke

yake bali pia hadhi yao ambayo imeshuka

sana. Kama jamii itawaangalia walimu kama

watu muhimu wanaoelimisha na wanaohitaji

kuheshimiwa, kutakuwa na matokeo mazuri zaidi

kuliko tu kuongeza kipato chao. Uamuzi wa

jamii kuwaheshimu walimu utakuwa ni ishara ya

kuithamini elimu. Kwa hiyo kuinua hadhi ya mwalimu

kutamfanya mwalimu aridhike na hivyo kuongeza

ufanisi wake kuliko kumwongezea kipato peke

yake.

Aidha, kuimarisha miundombinu ya shule ni njia

nyingine muhimu ya kuinua ubora wa elimu.

Wanafunzi wanapata maarifa kutoka kwa walimu

wao na katika vitabu. Hii inawawezesha pia

kujifunza kwa udadisi na kufanya mazoezi kwa

vitendo peke yao wakati wowote. Hivyo, ni muhimu

kuwa na mbiundombinu mizuri ili kuwawezesha

wanafunzi kujifunza kwa ufanisi. Miundombinu ni

pamoja na maktaba, vyoo na maabara, ambavyo

vitawawezesaha wanafunzi kujifunza kwa vitendo.

Kwa hiyo, kuwepo kwa miundombinu muhimu katika

shule kutainua ubora wa elimu nchini.

Kwa sababu hiyo, tunaamini kuwa zipo njia

kadhaa za kuongeza ubora wa elimu kwa ufanisi

zaidi kuliko tu kuongeza kipato cha mwalimu.

Hii ni pamoja na kuinua hadhi yao katika jamii

na kuhakikisha kuwa kuna miundombinu bora

katika shule. Ni kwa msingi huo tunaihimiza jamii

kutambua umuhimu wa walimu wetu na kushirikiana

nao katika kuinua ubora wa Elimu nchini kwetu.

Tahariri

2

Jarida la Elimu, 2013

Serikali ipo katika maandalizi ya kuanzisha Bodi ya Kitaalamu ya Walimu

nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa maelekezo ya kitaalamu katika ufundishaji na kuchangia katika kuinua hadhi ya walimu na kiwango cha ufundishaji na ujifunzaji. Bodi

hii itawapa nafasi walimu wenyewe kuamua na kuimarisha misingi yao ya kitaaluma na kudumisha ubora wa kazi yao ya kitaalamu kupitia mamlaka moja, na hivyo kufanya elimu inayotolewa kuwa bora zaidi kutokana na ubora wa kitaaluma wa walimu.

Kazi ya Bodi itakuwa ni kusajili kusimamia na kuthibiti utaalamu na maadili ya taaluma ya ualimu kuweka viwango vya kitaalamu na kudhibiti na kusimamia ubora. Bodi hii pia itasimamia kanuni na vigezo vitakavyotumika katika kuidhinisha

programu za elimu ya ualimu. Bodi hii inatarajiwa kutekeleza majukumu yafuatayo: kusimamia uwepo wa chombo cha kisheria cha kudhibiti taaluma ya ualimu; kuweka viwango vya kitaalamu vya kufundishia na kuweka kanuni za maadili ya kitaalamu kwa ajili ya walimu wote; kushirikiana na

taasisi za elimu ya ualimu pamoja na mabaraza yanayotoa ithibati ya programu za elimu ya ualimu ya kitaifa na kimataifa, waajiri wa walimu, vyama vya walimu na asasi nyingine, pamoja na vyombo na watu wengine, kuhusu masharti ya usajili wa walimu na viwango

vingine vya kitaaluma kwa ajili ya walimu.

Kazi nyingine ya Bodi hii itakuwa ni kuchunguza malalamiko yanayotolewa dhidi ya walimu kwa misingi ya madai ya kudhalilisha taaluma pamoja na kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya

Bodi ya Kitaalamu ya Walimu Kuanzishwa

Inaendelea uk.6

Waziri wa Elimu na Mafunzo na Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa (katikati mwenye tai) akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa Wilaya ya Bagamoyo. wa kwanza kushoto ni Afisa kutoka British Council Tanzania.

3

Jarida la Elimu, 2013

Inatoka uk.1

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, amesema kwamba wizara yake kwa sasa imejiandaa kuinua ubora wa elimu katika ngazi zote za elimu na mafunzo, baada ya kazi nzuri iliyotokana na upanuzi wa Elimu ya Msingi, Sekondari na Elimu ya Juu. Aidha, Serikali

“Tumefanikiwa kuongeza uandiki shaji katika ngazi zote za elimu; kuanzia Elimu ya Awali, hadi Elimu ya Juu kwa kuongeza madarasa na miundombinu mingine, alisema Dkt. Kawambwa.

Ili kuinua ubora wa usimamizi wa shule na vyuo hivi, Wizara itaziimarisha taasisi zinazosimamia ubora wa elimu kama vile Idara ya Ukaguzi wa Shule, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (National Accreditation Council for Technical Education - NACTE) na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (Tanzania Council for Universities - TCU) ili ziweze kutekeleza vema majukumu yake muhimu ya kusimamia ubora wa elimu nchini.

Katika jitihada zake za kuipa mamlaka zaidi na uwezo, na hivyo kuongeza ufanisi katika ukaguzi wa shule na Vyuo vya Ualimu, Serikali inakusudia kuibadili Idara ya Ukaguzi wa Shule iliyopo ndani ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwa taasisi ya serikali inayojitegemea (wakala) ambayo itashughulika na ukaguzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu vilivyo vya serikali na visivyo vya serikali.

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ni chombo kilichoanzishwa kwa ajili ya kusimamia vyuo vyote visivyokuwa Vyuo Vikuu au Vyuo Vikuu Vishiriki vinavyotoa mafunzo ya ufundi katika ngazi za Cheti, Stashahada Shahada na tuzo nyingine zinazolingana na hizo. Baraza hili lina jukumu la kuratibu mafunzo ya Ufundi na Ufundi stadi

na kuanzisha mfumo wa kitaifa wa utoaji tuzo.

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ni chombo chenye mamlaka ya kutambua, kusajili na kutoa ithibati kwa vyuo vikuu vinavyoendeshwa nchini, pamoja na programu zinazotolewa na vyuo vikuu vya nje ambavyo havijasajiliwa na Tume. Aidha, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania huratibu utendaji wa vyuo vikuu vyote nchini ili kuleta ulinganifu katika mfumo wa elimu ya juu nchini.

Kufuatia kuongezeka kwa idadi ya shule na vyuo, idadi ya wanafunzi imeongezeka katika shule za Awali, Msingi, Sekondari, Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi, Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki.

Tanzania ipo kwenye hatua nzuri katika safari yake ya kuyafikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya kutoa Elimu ya Msingi kwa Wote. Sera ya utoaji wa Elimu ya Msingi bure imeleta mafanikio mazuri katika kuhakikisha uwepo wa fursa katika elimu na wanafunzi kubaki shuleni hadi wanapomaliza.

Idadi ya wanafunzi waliojiunga na Elimu ya Awali iliongezeka kutoka 638,591 (wasichana 319,974) mwaka 2005 hadi 1,034,729 (wasichana 504,304) mwaka 2012. Aidha, idadi ya wanafunzi (miaka 7-13) waliojiunga na shule za msingi iliongezeka kutoka 6,499,581 (asilimia 86.19) mwaka 2005 hadi 7,707,046 (asilimia 93.5) mwaka 2012. Uwiano wa mwalimu na wanafunzi katika shule za msingi uliimarika kutoka 1:56 mwaka 2005 hadi 1:46 mwaka 2012, na idadi ya wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza iliongezeka kutoka 243,359 (asilimia 49.3) mwaka 2005 hadi 522,379 (asilimia 53.6) mwaka 2012.

Katika Elimu ya Sekondari, idadi ya shule za sekondari iliongezeka kutoka 1,745 mwaka 2005 hadi

4,528 mwaka 2012. Aidha, idadi ya wanafunzi walioko katika shule za sekondari za kawaida (kidato I - IV) iliongezeka kutoka 489,942 (asilimia 10.3) mwaka 2005 hadi 1,802,810 (asilimia 71.2) mwaka 2012 na idadi ya wanafunzi wote katika shule za sekondari (kidato I - VI) iliongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,884,272 mwaka 2012.

Idadi ya vyuo vya ualimu nchini iliongezeka kutoka 52 mwaka 2005 hadi 105 mwaka 2012, na idadi ya wanachuo waliodahiliwa katika vyuo hivi iliongezeka kutoka 28,225 mwaka 2005 hadi 43,258 mwaka 2012, na hivyo kuwezesha utoaji wa walimu wengi zaidi.

Serikali imekusudia kuongeza idadi ya wahitimu wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi ili kutosheleza mahitaji ya soko la ajira. Idadi ya wanafunzi katika vyuo vya elimu ya ufundi iliongezeka kutoka 40,059 mwaka 2005/06 hadi 85,040 mwaka 2011/12.

Idadi ya vyuo vikuu vikuu na vyuo vikuu vishirikishi iliongezeka kutoka 23 mwaka 2005/06 hadi 49 mwaka 2012/13 na kufanya uandikishaji wa wanafunzi katika vyuo vikuu kuongezeka kutoka 40,719 mwaka 2005/06 hadi 166,484 mwaka 2012/13, na hivyo kuongeza idadi ya wahitimu wa Elimu ya Juu nchini. Aidha, Serikali iliongeza fedha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kutoka Shilingi bilioni 56.1 mwaka 2005/06 hadi Shilingi bilioni 326 mwaka 2012/13 na kufanya idadi ya wanafunzi wa Elimu ya Juu wanaopata mikopo kuongezeka kutoka 42,729 mwaka 2005/06 hadi 94,477 mwaka 2011/12.

Tunalenga katika Kuimarisha Ubora wa Elimu – Kawambwa

4

Jarida la Elimu, 2013

Inatoka uk.4

ulemavu wa mwili au akili; kushirikiana na mamlaka

nyingine za udhibiti wa walimu ili kuleta ufanisi katika

kubadilishana habari kitaifa na kukuza ulinganifu na

uthabiti katika kudhibiti taaluma ya ualimu nchini; kutoa

ushauri katika masuala ya kimaadili na ya kitaalamu

ambayo huathiri taaluma hii; kusimamia taaluma ya

ualimu, viwango vya kitaaluma vya walimu pamoja

na mbinu nyingine za kudhibiti taaluma na kuhifadhi

rejesta ya walimu nchini. Katika kutekeleza majukumu

yake, Bodi itazingatia matokeo ya ujifunzaji.

Uanzishwaji wa Bodi ya Kitaalamu ya Walimu unashabihiana na mkakati wa serikali wa kuhakikisha utoaji wa elimu bora ambapo uhuishaji wa kada ya ualimu ndio msingi wa utekelezaji. Vile vile Bodi hii inashabihiana na Bodi nyingine za kitaalamu zilizopo nchini kama vile Bodi ya Kitaalamu ya Madaktari, Bodi ya Usajili ya Wahandisi, Bodi ya Usajili ya Wahasibu, na nyinginezo.

Kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani, Bodi ya Kitaalamu ya Walimu itatoa utambulisho maalumu kwa walimu kama wataalamu nchini na pia itaweka utaratibu wa vigezo vya taaluma vilivyo sawa kwa jamii zote. Hivyo, Bodi italenga kuwapatia uwezo walimu kuwajengea uwezo mpana wanafunzi wao kitaaluma, kijamii kkwa kuzingatia misingi na utashi wa kujifunza ambazo zitawawezesha wanafunzi hao kujifunza kwa ufanisi. Vile vile, Bodi itaweka miundo itakayowahamasisha walimu kujituma katika kazi yao na walimu kwa pamoja kupenda kujitolea kuelimisha jamii ili elimu hii iweze kuleta maendeleo nchini.

Maandalizi ni kuwa Bodi ya a Kitaalamu ya Walimu itawalenga walimu wa kada na nyanja zote ndani na nje ya nchi. Bodi hii itafuata viwango vya kitaalamu vya kimataifa ili kuwapatia hadhi ya kimataifa yenye fursa ya kufanya kazi ya kufundisha popote duniani. Ni vema kila mwalimu achangamkie fursa ya kuwa mmojawapo katika Bodi ya Kitaalamu ya Walimu.

Bodi ya Kitaalamu ...

Prof. Bhalalusesa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Ricky Mpama, kufuatia kustaafu kwake mwaka 2008. Tangu wakati huo, Ofisi ya Kamishna wa Elimu imekuwa ikiongozwa na Makaimu Kamishna kama ifuatavyo: Leonard Musaroche, aliyekuwa Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari (2007 - 2009), Bw Aminiel Mrutu, Mkurugenzi Msaidizi wa Usajili wa Shule (2009 - 2010 ) na Bibi Marystella Wassena, Mkurugenzi wa Idara ya Ukaguzi wa Shule (2010-2012).

Kabla ya uteuzi wake, Profesa Bhalalusesa alikuwa Mkuu wa Shule Kuu ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Nipo tayari kwa changamoto mpya na ninatarajia kupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau wa elimu, serikali, sekta binafsi na umma kwa ujumla,” Profesa Bhalalusesa anasema.

Kwa mujibu wa Sheria ya Elimu, kifungu 353, Kamishna wa Elimu ndiye msimamizi mkuu wa taaluma katika shule na vyuo vya ualimu

vyote nchini. Kamishna wa Elimu ana jukumu la kusimamia sera na taratibu pamoja na kuweka viwango vya kudhibiti ubora wa elimu na mafunzo.

Viongozi wengine walioteuliwa hivi karibuni katika wizara ni Egbert N. Ndauka - Mkurugenzi wa Sera na Mipango; Issa Bakari - Mkurugenzi wa Elimu ya Ualimu; Zuberi M. Samataba - Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi; Paulina Mkonongo - Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari; na Jacob Kibona - Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi.

Prof. Bhalalusesa, Kamishna wa El imuInatoka uk. 1

5

Jarida la Elimu, 2013

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imefanya mabadiliko

katika mihula ya shule, ili wanafunzi wa ngazi zote katika shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu wawe na vipindi vya likizo vinavyofanana. Mabadiliko haya ya Mihula yanakwenda sambamba na marekebisho ya vipindi vya mitihani ya Taifa katika ngazi hizo. Mabadiliko haya yalianza kutumika Januari, 2013.

Kwa mujibu wa Waraka wa Elimu Namba 5 wa mwaka 2012, uliotolewa na Kamishna wa Elimu nchini, Profesa Eustella Bhalalusesa, kuanzia mwaka 2013, ratiba mitihani ya Taifa itakuwa kama ifuatavyo: Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (Septemba Wiki ya 2), Mtihani wa Kidato cha 4 (Novemba Wiki ya 1), Mtihani wa Kidato cha 6 (Mei Wiki ya 1, isipokuwa mwaka huu 2013 utafanyika mwezi Februari kama ilivyokuwa awali kabla ya

mabadiliko haya) na Mtihani wa Ualimu wa Stashahada ya Elimu, Mtihani wa Ualimu Daraja la IIIA na Mtihani wa Ualimu Daraja la III A Kozi maalum (Mei Wiki ya 1).

Kwa upande wa mihula ya masomo, kuanzia mwaka 2013, itakuwa kama ifuatavyo: Kidato cha 1-4 muhula wa kwanza ni Januari Wiki ya 1 - Juni Wiki ya 1, na muhula wa pili ni Julai Wiki ya 1 - Desemba Wiki ya 1; Kidato cha 5-6 muhula wa kwanza ni Julai Wiki ya 1 - Desemba Wiki ya 1 na muhula wa pili ni Januari Wiki ya 1 - Juni Wiki ya 1; Ualimu Stashahada na Cheti muhula wa kwanza ni Julai Wiki ya 1 – Desemba Wiki ya 1 na muhula wa pili ni Januari Wiki ya 1 - Juni Wiki ya 1.

Kutokana na mabadiliko yaliyofanyika, Profesa Bhalalusesa amefafanua kuwa Wanafunzi wote watapumzika Mwezi Juni na Desemba.

Tangu mwaka 2005, kumekuwepo na tatizo la kutofautiana kwa Mihula ya wanafunzi wa Elimu ya Sekondari ya Kawaida (Kidato cha Kwanza - cha Nne), Sekondari ya Juu (Kidato cha Tano na Sita) na Vyuo vya Ualimu. Aidha, muda wa kufanya mitihani ya Taifa kwa kidato cha Nne na Sita hutofautiana vilevile, na usahihishaji wa mitihani ya ngazi hizo za elimu umekuwa ukifanyika wakati wanafunzi baadhi ya ngazi za elimu wakiendelea na masomo Shuleni/Vyuoni.

Jambo hili limekuwa likiathiri maendeleo ya wanafunzi kitaaluma. Wasahihishaji wa mitihani hiyo pia, wamekuwa na muda mrefu wa kufanya kazi hiyo na kukosa muda wa kupumzika na kujikuta wanafanya kazi hiyo kwa mfululizo mwaka mzima. Hali hiyo, imesababisha baadhi ya walimu kutofanya kazi za kitaaluma kwa ufanisi kwenye vituo vyao vya kazi.

Mabadiliko ya Mihula ya Shule za Sekondari na Vyuo vya Ualimu

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Tambaza wakifanya majaribio ya Sayansi

6

Jarida la Elimu, 2013

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwa ushirikiano na

Ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa ilizindua mpango wa miaka mitano wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika shule za msingi. Mpango huo ambao unajulikana kama ‘Tanzania 21st Century Basic Education Programme’ (TZ - 21) umedhaminiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa ushirikiano na Marekani kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID), sekta binafsi kama vile ‘Cisco, Intel Corporation, Microsoft East, Southern Africa, Uhuru One’ na ‘Zanzibar Telecommunications’ (Zantel).

Mradi wa ‘Tanzania 21st Century Basic Education Programme’ ni jitihada za serikali za kuinua ubora wa elimu katika madarasa

ya chini ya shule za msingi, hususan katika kusoma, hisabati na sayansi, ili kuleta mafanikio katika ngazi za Elimu ya Juu. Mradi huu unatekelezwa katika mkoa wa Mtwara. Kutolewa kwa Elimu ya Msingi bure Tanzania kumeleta mafanikio makubwa sana nchini ambapo uandikishaji umeongezeka haraka sana ndani ya miaka 10 kutoka 59% hadi 96%.

Mradi huu una malengo makuu matatu. Lengo la kwanza ni kuimarisha muundo wa uendelezaji wa mwalimu kitaaluma pamoja na kutoa vifaa kwa ajili ya shule ili kuinua ubora wa ufundishaji katika kusoma, hisabati na sayansi kwa kutumia teknolojia katika madarasa.

Lengo la pili ni kuhimiza uanzishwaji wa TEHAMA katika madarasa kupitia mafunzo ya kina ya walimu juu ya namna ya kutumia teknolojia

mpya kwa ufanisi, pamoja na mwelekeo sahihi kuhusiana na mikakati ya kukabiliana na mabadiliko hayo.

Lengo la tatu la TZ - 21 ni kuanzisha Mfumo wa Usimamizi wa Habari za Elimu katika ngazi ya shule ambapo watumishi wa shule wataweza kukusanya na kusimamia taarifa ili kuleta ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji, kuimarisha utekelezaji wa maamuzi ya sera na kupima matokeo yake.

Timu ya mradi wa TZ - 21 inafanya kazi kwa kushirikiana na makampuni ya ndani na ya kimataifa yanayoongoza katika teknolojia ambayo yatautegemeza mradi kwa kutoa maunzi laini (hardware) na maudhui ya kieletroniki (e-content) kama sehemu ya mkakati wa kukuza TEHAMA kwa shule zote 846 katika Mkoa wa Mtwara.

TEHAMA katika Shule za Msingi

Waziri wa Elimu ya Mafunzo na Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa akizindua mafunzo ya TEHAMA kwa Walimu.

7

Jarida la Elimu, 2013

Serikali ya Tanzania imepata mkopo kutoka Benki ya Dunia kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa ajili ya kutekeleza

Mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, (STHEP) ambao unakusudia kujenga uchumi wa kisasa uliojaa maarifa na utakaohimili ushindani nchini Tanzania. Mradi huu ambao ni wa miaka saba, umedhamiriwa kutekelezwa katika awamu mbili nyumbufu ambazo ni Mpango wa Ukopeshaji Unaorekebika Kiurahisi - I (Adaptable Lending Programme - APL-1) na Mpango wa Ukopeshaji Unaorekebika Kiurahisi - II (APL-II). APL-1 ulitarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 5, kuanzia Julai 2008 na kumalizika Juni 2013.

Lengo la muda mrefu la mradi huu ni kuongeza uwezo wa Tanzania wa kutumia maarifa katika shughuli za kiuchumi kwa kujenga na kuimarisha mfumo wake wa Elimu ya Juu. Mradi huu unatarajiwa kuchangia katika Klasta Na. 1 ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA) ambapo moja ya malengo yake ni kuongeza uwezo wa sekta ya elimu ya juu katika kutoa wahitimu bora wanaokidhi mahitaji, hususan katika sayansi, teknolojia na uhandisi.

Fedha ya mkopo wa awamu ya kwanza (APL1) imeelekezwa zaidi katika: masomo ya sayansi na

teknolojia; taasisi za Elimu ya Juu; kuwajengea uwezo walimu wa shule za sekondari wenye shahada wanaofundisha masomo ya sayansi; kufanya upanuzi na kujenga uwezo wa taasisi za Elimu ya Juu; sekta ndogo za usimamizi na bodi za usimamizi wa Elimu ya Juu. Baadhi ya fedha ya APL -1 itawekezwa pia katika maandalizi kwa ajili ya uwekezaji mkubwa katika miundombinu na huduma ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Kupitia Mradi huu wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, jumla ya wahadhiri 187 wakiwemo 40 wanawake na 147 wanaume wamesomeshwa katika shahada za uzamili (Masters) na wahadhiri 191 wakiwemo 58 wanawake na wanaume 133 wamesomeshwa katika shahada za uzamivu (PhD).

Ili kuongeza nafasi za kusomea wanafunzi wa Elimu ya juu, Mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu umejenga majengo mapya 25 yenye uwezo wa kuchukua wanachuo 36,344 na ofisi za kutosheleza watumishi 1,640 katika vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki vya Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Sokoine, Chuo Kikuu cha Zanzibar, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Chuo Kikuu Ardhi, vyuo vikuu vishiriki vya Dar es Salaam na Mkwawa, Chuo cha Ufundi Arusha na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam.

Mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu Waonyesha Njia

Moja ya majengo yanayojengwa kupitia mradi wa STHEP

8

Jarida la Elimu, 2013

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa

amesisitiza kuhusu umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na Serikali na mashirika ya kimataifa katika kuchangia katika mpango wa chakula shuleni, kwani njaa imekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wanafunzi kuhudhuria masomo na hivyo kusababisha matokeo mabaya katika mitihani yao.

Dkt. Kawambwa aliyasema hayo katika uzinduzi wa mpango huo, katika Shule ya Msingi Kerege iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, unaotekelezwa na kampuni ya Kamal Group. Alisema kwamba sababu kubwa inayofanya wanafunzi washindwe kuhudhuria shule na kuwa na matokeo mabaya ni njaa, kusisitiza kuwa wanafunzi wanapopatiwa chakula shuleni

wanakuwa na mahudhurio mazuri.

Kitaifa, Mpango wa Lishe Shuleni unatekelezwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Duniani, kwa kusaidia kutoa chakula kwa wanafunzi ili kudhibiti utoro. Shirika la Mpango wa Chakula Duniani walikubali kutoa chakula katika maeneo ya majaribio ambapo katika shule za kutwa walitoa uji na chakula cha mchana.

Mpango huu ulianza kwa majaribio mwaka 2000 ukihusisha mikoa mitatu ikiwa na wilaya 11. Mikoa iliyohusika katika majaribio ilikuwa ni Dodoma, Arusha na Singida. Dodoma ilihusisha wilaya za Dodoma vijijini, Mpwapwa na Kondoa; Arusha ilihusisha wilaya za Ngorongoro, Monduli, Simanjiro

na Kiteto, wakati mkoa wa Singida ulihusisha wilaya za Singida Vijijini, Manyoni na Iramba. Katika mikoa hiyo ya majaribio shule 210 zilihusika zikiwa na wanafunzi 72,120.

Mpango huu wa majaribio katika mikoa hiyo ulilenga hasa maeneo yenye ukame ambapo mikoa ya Singida na Dodoma iliteuliwa. Mkoa wa Arusha ulichaguliwa kutokana na kuwa na shule za msingi za bweni zinazoendeshwa na Halmashauri. Shule hizi za bweni zilionekana kuzielemea Halmashauri na kufanya wanafunzi kuanza kutoroka shule kutokana na njaa iliyosababishwa na ukosefu wa chakula cha uhakika.

Katika shule za bweni zinazomilikiwa na Halmashauri kulitolewa uji na chakula cha mchana, wakati

Waziri wa Elimu Asisitiza kuhusu Umuhimu wa Chakula Shuleni

Inaendelea uk.12

Waziri wa Elimu na Mafunzo na Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa akisaidia kugawa uji kwa wanafunzi wa shule

9

Jarida la Elimu, 2013

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamewa-

pongeza wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani yao ya Kumaliza Kidato cha Sita mwaka 2012 pamoja na kuwakabidhi zawadi mbalimbali, ikiwemo kompyuta pakato (Laptop) na fedha taslimu shilingi 200,000 kila mmoja. Aidha, kila shule iliyotoa mwanafunzi au wanafunzi bora imezawadiwa shilingi milioni moja.

Hafla ya kuwapongeza wanafunzi hao kutoka shule nane za serikali na mbili za binafsi ilifanyika bungeni mkoani Dodoma baada ya Bunge kutengua kanuni na kuruhusu wanafunzi hao kuingia ukumbini na baadaye kuendelea

na shamrashamra za pongezi katika ukumbi wa Pius Msekwa.

Akizungumza wakati wa kuwa karibisha wanafunzi hao Bungeni, Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, pamoja na kuwapongeza aliwasihi wanafunzi hao kutumia vizuri uhuru watakaupata kwenye maisha yao ya vyuo vya Elimu ya Juu na kuhakikisha kuwa hawarudi nyuma katika maendeleo ya masomo yao, kwani huko kuna utawala binafsi zaidi tofauti na shule za sekondari.

Aidha, Waziri Mkuu alitaka utaratibu huo wa kuwatambua wanafunzi bora uwe endelevu na ikiwezekana wapatiwe fursa ya kuendelezwa katika vyuo vikuu

vya kipekee nje ya nchi hususan kwenye fani zitakazojenga uwezo wa Taifa.

Naye Spika wa Bunge, Mheshimiwa Anne Makinda, aliwasihi vijana hao kujiepusha na makundi mabaya ambayo yataweza kuzoretesha maendeleo yao katika masomo. Pia alizitaka shule nyingine kujitahidi kufanya vizuri.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dk. Shukuru Kawambwa, alisema kuwa hafla hiyo inafanyika ili kuwaenzi na kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri kwa mwaka 2012. Alisema kati ya wanafunzi 44,160 waliofanya mtihani huo mwaka 2012, wanafunzi

Wanafunzi 20 Waliofanya Vizuri Zaidi Kidato cha Sita Mwaka 2012 Wapongezwa

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo akitoa zawadi kwa mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri. Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Kassimu Majaliwa (kulia) na

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Selestine Gesimba (kushoto).

Inaendelea uk.12

10

Jarida la Elimu, 2013

40,775 walifaulu ambao ni sawa na asilimia 92.2. Dk. Kawambwa alisema kuwa kati ya waliofaulu, waliopata kiwango cha daraja la kwanza hadi la tatu ni 35,201.

Aliwataja wanafunzi hao na shule zao kuwa ni Faith Assenga, Immaculata Mosha, Rachel Sigwejo, Mary Kiangi, Nashivai Kivuyo, Evelyine Mapunga na Neema Munuo, wote kutoka shule ya Marian.

Wengine ni Neema Kiula (Kilakala), Ester Marcel (Ufundi Ifunda), Prisca Longo (Tabora wasichana), Zawadi Mdoe na Jamal Juma (Feza), Belinadino Mgimba (Minaki), Gwamaka Njobelo, Nickson Mwamsojo na Benson Maruchu (Mzumbe), Faridi Abdallah (Mpwapwa), Alex Isdor na Julius Luvanda (Kibaha) na Brighton Lema (Tabora Wavulana).

Halmashauri husika zilitoa chakula cha usiku. Vyakula vinavyotolewa katika mpango huu ni Mahindi, Njegere, Maharage, dengu, Mafuta ya kula na unga wa uji (Corn Soya Blend).

Mpango wa lishe shuleni ulipanuka zaidi mwaka 2010 na kufikia mikoa mitano ambapo Shinyanga na Manyara iliongezeka, na hivyo kufanya wilaya pia kuongezeka na kufikia 16. Wilaya zilizoongezeka katika mpango huu ni Shinyanga Vijijini, Meatu, Kishapu, Longido na Karatu. Aidha, idadi ya shule zilizohusika katika mpango huu ziliongezeka kutoka 210 zilizokuwemo hapo awali na kufikia 1,153.

‘Mpango wa Lishe Shuleni’ umeonekana kuongeza kiwango cha taaluma kwa kuwafanya wanafunzi wakae shuleni hadi

kuhitimu darasa la saba, kuongeza uandikishaji hasa katika maeneo ya wafugaji na maeneo ya ukame, kupunguza mdondoko na kuimarisha mahudhurio.

Kumekuwepo na mafanikio mengi katika mpango wa lishe ambapo uandikishaji kwa watoto wanaoanza darasa la kwanza, hasa wa kike, umeongezeka. Mahudhurio yameimarika, mdondoko umepu ngua kutoka asilimia 6 hadi asilimia 3, usikivu umeongezeka na afya za wanafunzi zimekuwa bora zaidi na pia jamii imejiongezea kipato kutokana na kuuza mazao yao yaliyonunuliwa na Shirika la Chakula Dunian (World Food Programme – WFP) na kutumika tena shuleni.

Changamoto zinazojitokeza katika mpango huu ni pamoja na kutokuwa endelevu kutokana na Halmashauri

kutoiweka programu hii katika bajeti zao kwa kuwa Wizara ya Elimu ni Shirika la Chakula Duniani tu ndio wanaochangia; ukosefu wa maeneo ya bustani shuleni; idadi ndogo ya wafadhili wenye kuchangia mpango huu wa chakula; ukosefu wa miundombinu kama vile majengo ya kuandalia chakula shuleni, bwalo la kulia chakula, pamoja na vifaa vya kuhifadhia na vya kuchukulia chakula na waandaaji wa chakula.

Aidha, kutokuwepo kwa maji safi na salama katika maeneo ya shule, uelewa mdogo wa jamii kuhusu umuhimu wa mpango wa chakula shuleni, ushiriki mdogo wa viongozi wa vijiji na serikali za mitaa, ukame, na uelewa na ujuzi mdogo wa wasimamizi wa mpango wa chakula shuleni unafanya utekelezaji wa mpango kuwa mgumu.

Prof. Dihenga Astaafu RasmiKatibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya

Ufundi, Profesa Hamisi O. Dihenga amestaafu rasmi utumishi wa umma mwezi Juni, 2012

baada ya kuitumikia Serikali katika nyadhifa mbalimbali hadi kufikia kuwa Katibu Mkuu kuanzia mwaka 2006 hadi alipostaafu kazi.

Katika uongozi wake akiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Dihenga amesimamia uanzishwaji/ uendeshaji wa mipango mbalimbali ya Elimu ikiwemo: ‘Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM), Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES), Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Juu (MMEJU), Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Ufundi (MMEU), Mradi wa

Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu’ na ‘Mkakati wa Maendeleo na Menejimenti ya Walimu’.

Watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Taasisi zake wataukumbuka ushirikiano wa hali ya juu aliokuwa nao Profesa Dihenga katika kuendesha shughuli za Wizara ya Elimu ambayo ni wizara muhimu na yenye changamoto nyingi.

Tunamuombea fanaka katika maisha yake baada ya kustaafu. Profesa Hamisi O. Dihenga

Inatoka uk.10

Inatoka uk.11Wanafunzi 20 Waliofanya Vizuri Zaidi...

Asisitiza Kuhusu Umuhimu wa Chakula Shuleni

11

Jarida la Elimu, 2013

Habari katika PichaWaziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Elimu na Utafiti wa Norway, Bibi Kristin Halvarsen (kushoto) na ujumbe wake, kuhusu masuala ya ushirikiano katika sekta ya Elimu.

Moja ya majengo yaliyojengwa kupitia Mradi wa STHEP

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillipo Mulugo akizindua Mradi wa kusomesha watoto wa kike 20,000 wa sekondari unaoendeshwa na Serikali kwa ushirikiano na shirika lisilo la kiserikali la Camfed.

Makamu wa Rais, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Chuo cha Ufundi Stadi Mkoani Lindi.

12

Jarida la Elimu, 2013

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi walioshinda shindano la uandishi wa Insha la nchi za Afrika Mashariki na Nchi wanachama wa SADC.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bibi Irina Bokova (wa kwanza kulia) na wa kwanza kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa akipokea mchango wa vitabu kwa ajili ya Shule za Msingi, kutoka Asasi isiyokuwa ya Serikali.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakitembelea Shule ya Sekondari Miono ambayo ni ya sayansi ya kidato cha tano na sita iliyoko Bagamoyo Mkoani Pwani

13