4
1 Kwa muda mrefu sasa rushwa inaonekana kuwa sugu katika sekta ya ardhi ambapo imeonekana sehemu ya ardhi ambayo imeonekana katika gazeti la serikali kama sehemu za wazi zilizotengwa kwa matumizi ya umma kuwa vimegawiwa kwa njia za kushukiwa kwa waendelezaji binafsi wala rushwa na watafutao utajiri, bado si jambo lililoisha. Licha ya ari, mwamko, na vitisho toka kwa waziri mpya wa ardhi na maendeleo ya makazi, Prof Anna Tibaijuka, juu ya zaidi ya viwanja thelathini (30) vya wazi katika manispaa ya Kinondoni pekee mjini Dar es Salaam viko katika hatari ya kuwa katika mikono ya waendelezaji wasio halali. Vitendo vya uporaji wa ardhi kupitia rushwa vimekuwa vikiongezeka kwa kasi na kuwa tatizo tete kwa Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla. Kiuhalisia kwa wananchi wa kawaida hakuna mabadiliko, waziri yupo kimya, mambo yanaenda kama kawaida hakika kuwa watu wananufaika sana kutokana na hali hii ya kuachiliwa mambo kwenda mrama. Katika hotuba aliyoitoa Mei 24, 2010 Rais Jakaya Kikwete wakati akifanya majumuisho ya ziara ya kukagua hali ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam alikiri kuwa yapo maeneo mengi ya wazi yaliyovamiwa na kuwa madiwani wanahusika na sakata hilo. Kufuatia kauli hiyo ya Rais Kikwete na malalamiko ya umma Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, bwana William Lukuvi alitembelea Manispaa ya Kinondoni tarehe 15 Juni 2010 na kubaini mapungufu kadhaa ya kiutendaji kuhusiana na masuala ya ugawaji wa ardhi yakiwemo maeneo ya umma yaliyozoeleka kuitwa viwanja vya wazi. Bwana Lukuvi aliunda kamati maalumu ya kuchunguza maeneo yote ya wazi yaliyovamiwa katika mkoa wa Dar es Salaam. Kamati hiyo iliundwa tarehe 18 Juni 2010 na pamoja na mambo mengine ilipewa hadibu za rejea ambazo ziliiongoza kamati tajwa kufanya kazi yake. Licha ya kwamba matokeo ya kamati hayajawahi kuwekwa wazi kwa umma, lakini imebainika kuwa manispaa ya Kinondoni ni miongoni mwa manispaa vinara katika uporwaji wa maeneo ya wazi jijini Dar es Salaam. Muda mfupi baada ya kushika nyadhifa mnamo Novemba 24, 2010 Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka aliahidi kuwachukulia hatua kali waporaji wa ardhi bila huruma. Matamshi yenye uthubutu na mamlaka yalirejesha matumaini kwa umma kuwa hatimaye wizara imempata kinara ambaye angeweza kuboresha mambo katika sekta hiyo. Katika kuonyesha uwezo mkubwa wa kushughulikia mambo, waziri aliamrisha uvunjwaji wa jingo binafsi katika sehemu nyeti ya ardhi pembezoni mwa fukwe ya barabara “ocean road beach area” na mkabala wa kiwanja cha gofu cha Gymkana. Aliwapa wamiliki binafsi wote notisi ya kuwataka kuhama na mkono wa sheria ungalifika na hakuna cha kuusimamisha. Lakini tangu kipindi hicho, inaonekana ule mchakamchaka na kuendelezwa kwa umakini sambamba na maneno ya Rais Rushwa yatafuna viwanja vya wazi Dar Mh. Prof. Anna Tibaijuka, Waziri wa Nyumba, Ardhi na Makazi Issue No. 006/11

Rushwa yatafuna viwanja vya wazi Dar

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Corruption Nemesis Eats Dar Open Spaces

Citation preview

Page 1: Rushwa yatafuna viwanja vya wazi Dar

1

Kwa muda mrefu sasa rushwa inaonekana kuwa sugu katika sekta ya ardhi ambapo imeonekana sehemu ya ardhi ambayo imeonekana katika gazeti la serikali kama sehemu za wazi zilizotengwa kwa matumizi ya umma kuwa vimegawiwa kwa njia za kushukiwa kwa waendelezaji binafsi wala rushwa na watafutao utajiri, bado si jambo lililoisha.

Licha ya ari, mwamko, na vitisho toka kwa waziri mpya wa ardhi na maendeleo ya makazi, Prof Anna Tibaijuka, juu ya zaidi ya viwanja thelathini (30) vya wazi katika manispaa ya Kinondoni pekee mjini Dar es Salaam viko katika hatari ya kuwa katika mikono ya waendelezaji wasio halali.

Vitendo vya uporaji wa ardhi kupitia rushwa vimekuwa vikiongezeka kwa kasi na kuwa tatizo tete kwa Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla. Kiuhalisia kwa wananchi wa kawaida hakuna mabadiliko, waziri yupo kimya, mambo yanaenda kama kawaida hakika kuwa watu wananufaika sana kutokana na hali hii ya kuachiliwa mambo kwenda mrama.

Katika hotuba aliyoitoa Mei 24, 2010 Rais Jakaya Kikwete wakati akifanya majumuisho ya ziara ya kukagua hali ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam alikiri kuwa yapo maeneo mengi ya wazi yaliyovamiwa na kuwa madiwani wanahusika na sakata hilo.

Kufuatia kauli hiyo ya Rais Kikwete na malalamiko ya umma Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, bwana William Lukuvi alitembelea Manispaa ya Kinondoni tarehe 15 Juni 2010 na kubaini mapungufu kadhaa ya kiutendaji kuhusiana na masuala ya ugawaji wa ardhi yakiwemo maeneo ya umma yaliyozoeleka kuitwa viwanja vya wazi.

Bwana Lukuvi aliunda kamati maalumu ya kuchunguza maeneo yote ya wazi yaliyovamiwa katika mkoa wa Dar es Salaam. Kamati hiyo iliundwa tarehe 18 Juni 2010 na pamoja na mambo mengine ilipewa hadibu za rejea ambazo ziliiongoza kamati tajwa kufanya kazi yake.

Licha ya kwamba matokeo ya kamati hayajawahi

kuwekwa wazi kwa umma, lakini imebainika kuwa manispaa ya Kinondoni ni miongoni mwa manispaa vinara katika uporwaji wa maeneo ya wazi jijini Dar es Salaam.

Muda mfupi baada ya kushika nyadhifa mnamo Novemba 24, 2010 Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka aliahidi kuwachukulia hatua kali waporaji wa ardhi bila huruma. Matamshi yenye uthubutu na mamlaka yalirejesha matumaini kwa umma kuwa hatimaye wizara imempata kinara ambaye angeweza kuboresha mambo katika sekta hiyo.

Katika kuonyesha uwezo mkubwa wa kushughulikia mambo, waziri aliamrisha uvunjwaji wa jingo binafsi katika sehemu nyeti ya ardhi pembezoni mwa fukwe ya barabara “ocean road beach area” na mkabala wa kiwanja cha gofu cha Gymkana. Aliwapa wamiliki binafsi wote notisi ya kuwataka kuhama na mkono wa sheria ungalifi ka na hakuna cha kuusimamisha. Lakini tangu kipindi hicho, inaonekana ule mchakamchaka na kuendelezwa kwa umakini sambamba na maneno ya Rais

Rushwa yatafuna viwanja vya wazi Dar

Mh. Prof. Anna Tibaijuka, Waziri wa Nyumba, Ardhi na Makazi

Issue No. 006/11

Page 2: Rushwa yatafuna viwanja vya wazi Dar

2

umerudisha nyuma juhudi za waziri kushughulikia uvamizi wa maeneo na upangiwaji pia uvamizi umeendelea kama tabia.

Bila kufata mtiririko, Mfumo wa ufatiliaji wa rushwa Tanzania (CTS) uliona maeneo ya wazi yaliyo katika hatua mbalimbali za uendelezwaji batili kwa matumizi ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo:

• Kiwanja Na. 1022 Kitalu E Sinza ambacho kuna ofisi ya afisa mtendaji na banda lenye vyumba vitano vya biashara na msingi wa jengo ambalo halijakamilika.

• Eneo karibu na kiwanja Na. 636 Kitalu E Sinza. Eneo lilibainika kuwa wazi ila limemegwa pande zote mbili na kuna matofali machache yamewekwa. Kamati ilielekeza kuwa Halmashauri irudishe mipaka ya kiwanja hiki na hatua ya kulitangaza kama eneo la wazi kwa mujibu wa sheria.

• Eneo karibu na viwanja Na. 281, 282, 283 na 287 Sinza B. Eneo hili limejengwa ofisi ya Mtendaji kata Sinza D. Kamati ilishauri kuwa eneo lililobaki litangazwe kama eneo la wazi kwa mujibu wa sheria na sehemu ilipojengwa ofisi ya kata eneo hilo lipimwe.

• Eneo karibu na viwanja Na. 411, 413,414 na upande mwingine kinapakana na 698 na 609 Sinza Block D, sehemu kubwa ya eneo hili ipo wazi na pia kimechimbwa kisima cha umma na kuna jiwe la msingi lenye shina la wakereketwa wa chama cha mapinduzi (CCM). Kamati ilishauri eneo lipimwe na kutumika kama eneo la wazi kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa sheria.

• Kiwanja Na. 814, 818 Sinza Block D. eneo

hili hutumika kama makazi ya watu na ndiyo waliondeleza eneo hilo. Kamati ilishauri Halmashauri kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini uhalali wa umiliki wa wananchi hao.

• Eneo jirani na viwanja Na. 480 na 481 Sinza Block D. Eneo hili lipo wazi na kamati imeshauri Halmashauri eneo hili lipimwe ili libaki kuwa wazi kwa matumizi yaliyokusudiwa. Bado haijafahamika kama halmashauri imepima eneo hili na kulitangaza kuwa wazi ili kuepuka wavamizi.

• Eneo jirani na kiwanja Na. 37 Sinza Block D ambalo kumejengwa msikiti na mmiliki wake hajulikani. Kamati ilishauri kuwa Halmashauri wafanye uchunguzi wa kina kubaini uhalali wa umiliki huu na hatua stahiki zichukuliwe. Bado haijafahamika endapo uchunguzi huo umeshafanyika au lah.

• Eneo jirani na viwanja Na. 75 na 77 Sinza Block D. Eneo hili limezungushiwa ukuta na mtu binafsi. Halmashauri ilishauriwa kufanya uchunguzi ili kubaini uhalali wa umiliki wa eneo hili na hatua stahiki zichukuliwe. Bado haijafahamika endapo uchunguzi umefanyika na ni hatua gani zilizochukuliwa.

• Eneo linalopakana na viwanja Na. 63, 99 Sinza Block D ambalo limejengwa Kanisa la Assemblies of God, Shule ya chekechea, ofisi ya CCM, gereji na pia kuna jengo la ghorofa limejengwa hapo. Halmashauri pia ilishauriwa kufanya uchunguzi wa kina na hatua stahiki zichukuliwe ili kubaini uhalali wa umiliki wa taasisi hizo (kanisa na CCM) na watu binafsi. Bado haikuweza kufahamika kuwa uchunguzi huo ulishafanyika na hatua gani zilizochukuliwa.

• Eneo lililopo mkabala na kiwanja Na. 475 Sinza B ambapo kumejengwa shina la wakereketwa wa CCM, mama lishe na pia kuna biashara ya pool inaendelea. Halmashauri ilishauriwa ifanye uchunguzi wa kina na hatua stahiki zichukuliwe. Bado haijafahamika endapo ushauri huo wa kamati ulizingatiwa na halmashauri.

• Eneo karibu na kiwanja Na. 23 Sinza C. Eneo hili hutumika limejengwa ofisi ya Afisa Mtendaji wa mtaa na pia kuna vibanda vya biashara. Kamati ilipendekeza kuwa sehemu ya ofisi imegwe na eneo lililobaki lipimwe na kutangazwa kama eneo la wazi. Haikuweza kufahamika kama ushauri huo ulikuwa umetekelezwa na halmashauri

• Eneo karibu na kiwanja Na. 24 Sinza

Page 3: Rushwa yatafuna viwanja vya wazi Dar

3

C, ambalo limengwa makazi ya watu. Halmashauri pia ilishauriwa ifanye uchunguzi wa uhalali wa umiliki na hatua stahiki zichukuliwe. Bado haikufahamika kama halmashauri imezingatia ushauri huu na ni hatua gani walizochukua.

• Eneo karibu Na. 765, 789, 790, na 797 Sinza C. Hapa kuna sehemu hutumika kama maegesho ya magari na pia kuna kibanda cha kukaangia chipsi. Kamati ilishauri kuwa Halmashauri itoe amri kuwa wamiliki wa magari kuondoa magari yao na pia upimaji ufanyike na kulitangaza eneo hilo kuwa wazi.

• Eneo la wazi lililozungukwa na viwanja Na. 21, 23, 25, 27, 29 Sinza B. Eneo hili kuna shina la wakereketwa wa CCM ,vibanda vya mama lishe, sehemu za kutengenezea mageti, magenge na kontena la kuuzia vinywaji vikali na baridi. Halmashauri ilishauriwa kuwaondoa wavamizi hawa ili eneo libaki kuwa wazi. Bado haijafahamika lini halmashauri itatekeleza ushauri huo.

• Eneo la wazi lililozungukwa na viwanja Na.72-74. Eneo limewekwa shina la wakereketwa wa CCM Kawawa kuna mama lishe na vioski. Kamati ilibaini kuwa eneo hili kwa mujibu wa mipango miji ni la wazi na kuishauri Halmashauri iwapeleke mama lishe kwenye maeneo yanayostahili na kupima eneo husika na kulitangaza kuwa wazi. Bado haijafahamika nini kimeshafanyika mpaka sasa juu ya maeneo hayo.

• Eneo la wazi linalozungukwa na viwanja Na. 1, 2, 89, 90, 141 na 142 Sinza E. Katika eneo hili kumejengwa nyumba za makazi, Baa na asilimia ndogo ya eneo lipo wazi (baadhi ya namba ya viwanja hivyo ni 655 na 690). Kamati ilishauri kuwa Halmashauri iendelee na uchunguzi na hatua stahiki zichukuliwe. Matokeo ya uchunguzi endapo kama ulifanywa hayajajulikana bado.

• Eneo la kiwanja cha michezo na Shule ya Msingi Sinza E. Kiwanja kimemilikishwa kwa CCM na kuna vibanda vimejengwa kuzunguka eneo lote na ndani linatumika kama maegesho ya magari. Kamati ilishauri kuwa eneo litumike kwa matumizi yaliyopangwa na shughuli ambazo hazihusiani ziondolewe. Bado haijafahamika kama halmashauri imeshawapa taarifa CCM kuhusu hili na kutangaza eneo husika kutumika kwa matumizi yaliyopangwa.

• Eneo la wazi jirani na viwanja Na. 77, 79,

81, 151-154, eneo hili limejengwa makazi ya watu na sehemu za biashara. Kamati imeshauri kuwa Halmashauri ifanye uchunguzi wa kina na kuchukua hatua zinazostahiki. Bado haijaweza kufahamika hatua ambazo halmashauri imechukua mpaka sasa.

• Viwanja Na. 9 na 10 Sinza A. Wamiliki wa viwanja hivi viwili wamefunga barabara ya kuingia eneo la wazi. Kamati ilishauri kuwa Halmashauri ichukue hatua ya kufungua barabara husika ili eneo la wazi litumike kwa matumizi yaliyopangwa. Bado haijafahamika nini kinachelewesha utekelezaji huo.

• Kiwanja Na. 846 Sinza A. Eneo hili limejengwa nyumba ya makazi na biashara. Katika eneo hili taratibu za kubadili matumizi inasemekana zilifuatwa, bado haijafahamika kuwa ni ukweli au uongo.

• Jirani na viwanja Na. 38, 40, 44, 46 na 48 Mtaa wa Kibesa Makurumla. Eneo hili limejengwa ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Makurumla. Kamati ilishauri kuwa eneo la ofisi limegwe na taratibu ya kubadilisha matumizi zifuatwe na eneo lililobaki litangazwe kuwa wazi na litumike kama sehemu ya starehe na michezo kwa mujibu wa sheria. Bado haijafahamika hatua ambazo Halmashauri imefikia kutekeleza ushauri huo.

• Jirani na viwanja Na. 18 na 19 Mtaa wa Malala Makurumla. Kuna wavamizi wasio rasmi wanalitumia eneo hili kama gereji. Kamati ilishauri kuwa wavamizi waondolewe na kutokana na uhaba wa maeneo ya wazi katika maeneo hayo, eneo hilo litumike kama kiwanja cha wazi. Bado haijafahamika utaratibu mbadala ambao halmashauri imeshaweka kwa ajili ya gereji husika.

• Jirani na viwanja Na. 73, 78, 80, 82, 84 na 86 Mtaa wa Mengo Makurumla, eneo hili limevamiwa na wavamizi wasio rasmi. Kamati ilishauri kuwa wavamizi waondolewe na kutokana na uhaba wa maeneo ya wazi katika maeneo hayo, eneo hilo litumike kama kiwanja cha wazi. Bado haijafahamika utaratibu mbadala ambao wajasiriamali wamewekewa na halmashauri.

• Eneo la wazi lililopo Mtaa wa Kagera Makurumla limevamiwa na na kuna ofisi ya CCM Tawi la Karume Kata ya Makurumla na pia kuna banda linalotumika kama sehemu ya biashara. Kamati ilibaini kuwa wahusika walishapewa notisi ya kuondoka na hivyo Halmashauri ichukue hatua ya kuwaondoa

Page 4: Rushwa yatafuna viwanja vya wazi Dar

4

wavamizi hao. Bado Halmashauri haijawaondoa wavamizi hao.

• Eneo la wazi nyuma ya Ubungo terminal (“buffer zone” ya reli) limejengwa vibanda vya biashara. Kamati ilibaini kuwa eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya reli hivyo basi vibanda hivyo viondolewe ili kuacha eneo litumike kama ilivyokuwa imepangwa. Bado haijafahamika utaratibu mbadala ambao Halmashauri imeuweka wa kuwapa wafanyabiashara hao maeneo ya biashara ikiwa bado kuna azma ya kuboresha matumizi ya reli kwa usafi ri wa ndani ya mkoa wa Dar es salaam.

• Eneo lipo jirani na kiwanja Na. 148 ambalo limejengwa nyumba ya makazi ya kudumu ya mtu binafsi. Kamati ilishauri kuwa Halmashauri iwasilishe taarifa kuhusu mwendelezaji huyo na kama ni mvamizi apelekewe notisi na kumtaka aondoe jengo hilo. Bado haijafahamika endapo taarifa ya halmashauri iliwashilishwa au lah!.

• Nyuma ya jengo la RUBADA na Kanisa la KKKT na Anglikana. Eneo hilo limejengwa shule ya msingi Ubungo Plaza kwa mpango wa MMEM. Kamati ilishauri kuwa eneo lililobakia litumike kwa matumizi michezo na burudani na si vinginevyo. Inasemekana kwa mujibu wa wakazi karibu ya eneo hilo, bado kuna baadhi ya watu wanalipangia mipango ya kulimega na kutumia kwa matumizi yao binafsi.

Ifahamike maeneo hayo yalitengwa kwa mujibu wa sheria (Public Recreation Grounds Cap. 320) na bado ni maeneo tegemewa na muhimu sana kwa umma mzima, ucheleweshwaji wa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa kamati una athiri sana maslahi ya umma

Swali linaloibuka linaendelea kuwa nini kimetokea katika mwamko uliowashwa na Rais na waziri husika? Je hakuna mtu yeyote ambaye anashuhudia uendelezwaji binafsi unaofanyika?

Baraza jipya la madiwani wa manispaa ya Kinondoni linatarajiwa kusimamia sheria, taratibu na kanuni kuhakikisha wahusika wote wa uvamizi na/au uuzwaji wa maeneo ya wazi wanachukuliwa hatua za kisheria jambo ambalo litasaidia kukomesha vitendo vya namna hiyo kujirudia.

Pia mamlaka husika za ardhi na manispaa, zinapaswa kufatilia kwa ukaribu na kutekeleza kila mapendekezo yaliyokuwa yametolewa na kamati hiyo jambo ambalo litasaidia mabadiliko katika manispaa ya Kinondoni na haswa kuonyesha kwa vitendo dhamira halisi ya kupambana na vitendo vya ukiukwaji wa sheria na rushwa vinavyokithiri katika sekta ya ardhi.

Uchunguzi wetu wa awali na ripoti zinaonyesha kwamba waendelezaji batili wanafanya kazi kwa ushirikiano na maafi sa wa ardhi wala rushwa sambamba na vyombo vya kusimamia sheria kuchukua maeneo ya wazi kwa ujira wa fedha na marupurupu mengine. Moja ya chama cha kisiasa imeonekana kikiwa pia kinaneemeka na biashara hiyo. Utembeleaji uliofanywa hivi karibuni unaonyesha bado mambo yanaendeshwa kikawaida, mchezo unaendeshwa kwa nguvu kubwa sana na kuna wanaonufaika na kuneemeka kutokana na matunda ya mchezo huo. Viwanja vya ukubwa huo vinasemekana kuwa kati ya TShs 50-300 milioni kutegemea ukubwa na eneo kiwanja kilipo.

Kipeperushi hiki kimetengenezwa na Agenda Participation 2000 (AP2000) kutokana na taarifa zinazopatikana katika CTS (Mfumo wa Ufuatiliaji wa Rushwa Tanzania) www.corruptiontracker.or.tz. AP2000 ni asasi isiyo ya kiserikali inaofanya kazi ya kuhamasisha utawala bora na inaendesha CTS. CTS inafadhiliwa na Ubalozi wa Finland na Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC)

Agenda Participation 2000 5th Floor, Ubungo Plaza, P.O Box 55756, Dar es Salaam, TanzaniaTel: + 255 22 2460036/ 2460039, Fax: + 255 22 2460040, Cell: 0754 844410Email: [email protected] Website: www.corruptiontracker.or.tz

ISBN No. 978-9987-944-3-2