Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari -07!12!2015

Embed Size (px)

DESCRIPTION

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI -07-12-2015

Citation preview

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARITAARIFA YA MAKUSANYO KWA MAKASHA YALIYOONDOSHWA BANDARINI KINYUME CHA SHERIA KUFIKIA TAREHE 7 DISEMBA 2015 Ijumaa ya wiki iliyopita tuliwaita mahsusi kuwapeni taarifa ili muwajuze wananchi kuhusu hatua zilizochukuliwa kutekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli kwa wafanyabiashara walioondosha makasha Bandarini bila kulipa ushuru ili waweze kulipa ushuru huo ndani ya siku saba bila adhabu.

Wafanyabiashara wameendelea kuitikia wito kwa kulipa kodi iliyokwepwa na hadi kufikia leo hii TRA imeshakusanya kodi jumla ya shilingi 8,620, 768,976.70 Hii ni ongezeko la Sh 2,866,187,404.52 kuanzia tarehe 2 Disemba hadi leo. Baadhi ya waliolipa nyongeza hii ni wafuatao; S. S. Bakhresa & Co. Lt Sh.2,000,000,000.00 Tifo Global Trading Co. Ltd. Sh.310,000,000.00, IPS Roofing Co. Ltd. Sh.80,000,000.00, Red East Building Co. Ltd. 100,000,000.00, Zing Enterprises 325,644,200.00, Sapato N Kyando Sh.50,543,204.52Aidha, TRA na vyombo vya Dola vimeendelea kuchukua hatua dhidi ya watumishi ambao mwenendo wao unatia shaka ikiwa pamoja na kuwasimamisha kazi, kuwachunguza na kuwapandisha kizimbani. Katika zoezi hili mtumishi mwingine mmoja wa Idara ya Forodha amesimamishwa kazi kuanzia leo tarehe 7 Disemba 2015. Vilevile nachukua fursa hii pia kuwahakikishia wafanyabiashara wote kuwa TRA na Serikali kwa ujumla inathamini sana mchango wa wafanyabiashara waadilifu katika kukuza uchumi wa Taifa na itaendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini. TRA tunayoanza kuijenga upya ni rafiki kwa wafanyabiashara wanaolipa kodi. Tunawaahidi ushirikiano mzuri na TRA haina ugomvi na mfanyabiashara yeyote anayelipa kodi inayopaswa kulipwa. Tunawaomba wafanyabiashara waadilifu waendelee na biashara zao bila bugudha.

Hata hivyo TRA inazidi kusisitiza kuwa mfanyabishara yeyote ambaye alipitisha makasha au mizigo katika Bandari yoyote au kituo cha Forodha mipakani bila kulipa ushuru anatakiwa kulipa ndani ya muda wa msamaha uliotolewa na Mhe Rais ambao unaishia tarehe 11 Disemba. Baada ya tarehe 11 Disemba 2015 TRA itachukua hatua kali za kisheria kuhakikisha kodi iliyokwepwa pamoja na adhabu inalipwa. TRA hatutalala hadi kodi stahiki ikusanywe. Napenda pia kutumia fursa hii kuwaomba wananchi wasisite kutoa taarifa pindi wanapoona mwenendo wa watumishi wa TRA wasio waadilifu wanaowabugudhi na watoe taarifa mara moja kwa uongozi wa juu wa TRA. Simu ya Kiganjani ya Kaimu Kamishna Mkuu ni +255 787 570 714 na namba ya simu ya Naibu Kamishna Mkuu ni +255 784 228 095 Vile vile wananchi wanaweza kutujulisha kuhusu ukiukwaji wa maadili kwa watumishi wa TRA kwenye simu namba 0689 122 515 na kutuma ujumbe mfupi kwenye namba 0689 122 516.Nasisitiza tena kuwa TRA tunayoijenga sasa ni ya watumishi waadilifu na sio wanaotisha wafanyabiashara au wala rushwa. Tunawaomba wananchi watusaidie kwa kutupatia taarifa kwa siri kuhusu mienendo mibaya ya watumishi wa TRA na wale wanaojilimbikizia mali kwa njia zisizo halali maana sisi watumishi wa TRA tunaishi katika jamii na mnatufahamu. Tutawalinda watoa taarifa kwa mujibu wa sheria ya usiri kwa mtoa taarifa yaani The Whistleblower and Witness Protection Act, 2015 Mwisho, Uongozi wa TRA unapenda kuwahakikishia na kuwahimiza watumishi wake waadilifu wafanyakazi bila hofu, wazingatie sheria, kanuni na taratibu za kazi kwa mujibu wa Utumishi wa Umma. Katika zoezi linaloendelea la kubaini wale wanaochafua jina la Mamlaka ya Mapato hakuna mtumishi atakayeonewa.

Pamoja tunajenga Taifa letuKwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:

Kituo cha Huduma kwa wateja0800 780078

0800 750075

Au Mkurugenzi Huduma Na Elimu Kwa Mlipakodi

Simu: +25522-2119343

Barua pepe: [email protected]; [email protected]