29
[Type text] Page 1 UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARA KWA KUONGEZA PATO LA FAMILIA MUZEZA DISTRICT COUNCIL KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI KIBIASHARA

UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

  • Upload
    others

  • View
    68

  • Download
    7

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

[Type text] Page 1

UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARA

KWA KUONGEZA PATO LA FAMILIA

MUZEZA DISTRICT COUNCIL

KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI KIBIASHARA

Page 2: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 2

UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI

1. Utangulizi

2. Banda bora la kuku

3. Njia za ufugaji wa kuku chotara

4. Utunzaji wa kuku chotara

5. Utunzaji wa vifaranga

6. Utengenezaji wa chakula cha kuku

7. Magonjwa ya kuku

8. Masoko

UTANGULIZI

Asilimia 75% ya Watanzania ni wafugaji wa kuku wa asili. Kila mtanzania

anaweza kufuga kuku bila kujali hali ya kipato kwa kuwa kuku wa asili

wanavumilia magonjwa na wanakubali mazingira yote ya ufugaji. Kuku wa asili

wamekuwa wakifugwa holela bila kuzingatia kanuni bora za ufugaji wa kuku

hivyo kupelekea mazao duni na hata kupungua kwa idadi ya kuku wa asili.

Hivyo ipo haja ya kuboresha mazingira na kufuata kanuni za ufugaji bora.

Lengo ni kuongeza uzalishaji wa mayai kutoka mayai 60 hadi mayai 100 kwa

kuku kwa mwaka na kuongeza uzalishaji wa nyama ya kuku kutoka kilo 1 hadi

kilo 2.5 kwa kuku kwa kipindi cha miezi sita.

Page 3: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 3

SURA YA KWANZA.

BANDA LA KUKU

Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali. Banda bora la

kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

Lijengwe kwenye sehemu ambayo inaweza kufikika kwa urahisi.

Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa

hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na

wanyama hatari, Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama

wa chakula na

kujiongezea kipato.

Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika

kwa urahisi.

Lijengwe sehemu yenye mwinuko isiyotuama maji, isiyo na upepo mkali

na iwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu.

Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala

Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji, kutagia, kuatamia na sehemu

ya kulelea vifaranga

Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku na kuweka vyombo

vya chakula na maji

Kwenye mazingira ya joto banda liwe la ukuta mfupi na sehemu kubwa

wazi yenye wavu hadi kufikia kwenye paa

Page 4: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 4

Kwenye mazingira ya baridi banda liwe na ukuta mrefu unaokaribia paa

na sehemu ndogo tu iwe wazi yenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga.

Sehemu nzuri ya kujenga banda ni:

Ile inayofikika kwa urahisi

Ile yenye mwanga wa kutosha

Isiyo na upepo mkali

Isiyoruhusu maji kusimama au kuingia ndani.

Sifa za banda

1. Sakafu – inaweza kuwa ya saruji, mbao au iliyosiribwa kwa udogo

2. Isipitishe unyevu, isiwe na nyufa na iwe rahisi kusafishwa

Ukuta

Ukuta lazima uwe imara ili kuweza kushikilia paa,

Ukuta unaofaa uwe wa matofali ya saruji au matofali ya kuchoma , pia

kuna uweaekano wa kutumia miti, fito, mabanzi na mabati. Kama

ukitumia mabanzi au fito ni vyema kuondoa magamba na kupaka dawa

kwa ajili ya kuzuia mchwa.

Katika sehemu za joto, ukuta ujengwe mita moja kutoka chini kwenda juu

na sehemu iliyobaki izibwe kwa kutumia wavu ili kuingiza hewa na kuzuia

wanyama wakali, sehemu za baridi ukuta ujengwe kutoka chini hadi juu

ilimradi kuwe na madirisha ya kutosha kupitisha hewa

Ni muhimu kusiriba ukuta ili kuzuia nyufa vile vile inarahisisha kusafisha

nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu

Paa:

Liwe imara na lisilovuja

Liezekwe kwa kutumia mabati , nyasi, madebe, makuti au vigae

Page 5: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 5

Vipimo vya banda

Kuku wanahitaji nafasi tofauti kutegemea na umri aina na njia za ufugaji

Kwa muda wa majuma manne ya mwanzo eneo la mita mraba1 au eneo la

hatua moja linatosheleza vifaranga 16. Banda lenye eneo la mita mraba 16

linaweza kulea vifaranga 320 hadi majuma 4. Baada majuma manne ya umri

nafasi iongezwe.

Idadi ya kuku katika eneo la mita za mraba.

Aina ya kuku

Njia za ufugaji Kuku wa mayai Kuku wa nyama

Sakafu ya matandazo 3 - 4 6 - 8

Ufugaji wa kwenye

vichanja maalumu vya

chuma

8 - 12 15 - 25

Vifaa vinavyohitajika katika banda la kuku:

Vyombo vya maji – maalumu vya plastiki au bati vya kuweka maji kwa ajili

ya kuku, unaweza kutumia sahani na kopo jaza maji kwenye kopo kisha

lifunike na sahani na ligeuze hii ni kwa ajili ya vifaranga, kwa ajili ya kuku

wakubwa unaweza kutumia sufuria, vungu, madebe au karai.

Vyombo vya chakula- kwa ajili ya vifaranga ni chano za mayai, makasha

yaliyobebea vifaranga na vyombo maalumu vya bati au plasitiki. Kwa

kuku wakubwa ni vile vyombo maalumu vilivyotengenzwa kwa mbao au

bati.

Viota – kuna aina mbili za viota ambavyo vinatumika kwa ajili ya kutagia

mayai

Page 6: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 6

1. aina ya kwanza ni kiota cha kuku mmoja mmoja , kila kiota

kinaweza kutumiwa na kuku watano kwa zamu. Vipimo vya

kila kiota viwe SM 30 upana, SM 30 urefu na SM 35 kina,

upande wa mbele uwe wazi lakini SM 10 za kwanza kutoka

chini zizibwe kwa mbao

2. Aina ya pili ya kiota cha jumla, kinaweza kutumiwa na kuku

watano hadi sita kwa wakati mmoja vipiomo view SM 30

upana , SM150 urefu na SM55 kina.

Sifa za kiota

Kiwe na giza kiasi, giza hupunguza tabia ya kuku kula

mayai na kudonoana

Kiwe kimewekwa mahali ambapo ni rahisi kwa kuku

kuingia na kutoka.

Page 7: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 7

SURA YA PILI

NJIA MBALIMBALI ZA UFUGAJI WA KUKU

Kuku huweza kufugwa kwa kutumia njia mbalimbali kutegemea ukubwa wa

eneo na uwezo wa mfugaji, kuna njia tatu za ufugaji wa kuku nazo ni :

Ufugaji huria- kuku huachwa wenyewe wajitafutie chakula na maji ,

ufugaji huu hutumika sana kwa kuku wa asili na hakuna utaratibu wowote

wa kuwapatia chakula cha ziada

Faida-

haina gharama kubwa

Kuku wanapata mzoezi yakutosha

Hasara-

Huharibu mazingira, hula mazao hasa nafaka

Ni rahisi kuku kuathriwa na wezi, wanyama wakali au hali

mbaya ya hewa.

Ni rahisi kuambukizwa na kusambaza magonjwa

Wanaweza kutaga mayai vichakani

Ukuaji wake ni hafifu

Kuna uwezo wa kuhamia nyumba nyingine.

Page 8: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 8

Ufugaji ndani ya uzio- huu ni ufugaji unaofanyika katika sehemu

iliyozungushiwa uzio . Kuku hujitafutia chakula chao wenyewe na kuna

utaratibu wa kuwapaokatia maji na chakula cha ziada. Ndani ya uzio

kuna banda ambalo kuku wanaweza kulala, kuingia na kutoka wakati wa

mchana. Ufugaji huu unatumika kwa kuku chotara na kuku wa kisasa.

Faida-

Gharama yake ni nafuu

Ni rahisi kuelewa kiwango cha utagaji na utotoaji

wao

Si rahisi kuku kuathiriwa na wezi, wanyama wakali au

hali mbaya ya hewa

Si rahisi kuambukizwa magonjwa mbali mbali

Hasara-

Gharama za ujenzi wa uzio na vifaa kwa ajili ya

chakula na maji

Njia hii inahitaji eneo kubwa

Ufugaji ndani ya Banda – kuku hufugwa ndani ya banda wakati wote na

hupatiwa maji na chakula. Njia hii hutumika zaidi kwa ufugaji wa

kibiashara

Faida

Kuku wengi huweza kufugwa katika eneo dogo

Nirahisi kuwahudumia

Sio rahisi kuambukizwa magonjwa kutoka nje

Page 9: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 9

Wanakuwa na usalama wa uhakika

Hasara Gharama za mwanzo zinahitaji mtaji mkubwa

Ugonjwa unapotokea ni rahisi kuambukizana

Ufugaji huu unahitaji utaalamu wa kutosha

SURA YA TATU

UTUNZAJI WA KUKU WA ASILI/CHOTARA

KUCHAGUA KUKU BORA JIKE WA ASILI WA KUFUGA.

Aina za kuku wa asili wanaopatikana hapa nchini ni pamoja na Kuchi (Kuza),

Poni (Kishingo), Njachama, Kinyavu, Mbuni na Tongwe (Msumbiji). Mfugaji

anaweza kuongeza uzalishaji kwa kuchagua kuku mwenye sifa zifuatazo:-

Uwezo wa kutaga mayai mengi (kati ya 15-20) katika mzunguko mmoja

wa utagaji (Jedwali Na 10),

Uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga wengi,

Uwezo wa kustahimili magonjwa,

Anayetoka maeneo yasiyo na magonjwa; na

Umbo kubwa na kukua haraka.

MASUALA YA KUZINGATIA WAKATI WA KUMCHAGUA KUKU MTAGAJI WA

KIENYEJI.

Viungo vya mwili (Sifa)

Macho

- Maangavu, yenye wekundu kwa mbali na makubwa yamejaa kwenye soketi

za macho.

Page 10: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 10

Mdomo

- Wenye rangi ya njano kwa mbali Kisunzu/upanga

- Chekundu, laini, kimelala kidogo upande na kinang’aa Shingo

- Iliyosimama Umbali kati ya kidari na nyonga

- Upana wa vidole 3-4 vya mpimaji Upana wa nyonga

- Upana wa vidole 3 vya mpimaji

KUCHAGUA KUKU BORA WA KISASA.

Kuku bora wa kisasa kwa ajili ya mayai au nyama ni mwenye sifa zifuatazo:-

Uwezo wa kuanza kutaga wakiwa na umri mdogo (miezi 5 - 6)

kutegemeana na koo,

Umbo kubwa na anayekua haraka (kilo 1.5-2.0 kwa kipindi cha wiki 8-12)

kutegemea na koo kwa kuku wa nyama,

Anayetaga mayai mengi (250 au zaidi) kwa kuku wa mayai kwa mwaka;

na

Awe na uwezo wa kutaga katika umri wa miezi 6 - 8.

KUCHAGUA JOGOO BORA WA MBEGU.

Jogoo wa mbegu anatakiwa awe na sifa zifuatazo:

Achaguliwe kutoka kwenye koo zenye sifa ya kutaga mayai mengi,

Mrefu, umbo kubwa, miguu imara na yenye nguvu,

Awe machachari, ushawishi kwa mitetea na ari ya kupanda; na

Uwezo wa kupanda akiwa na umri wa miezi 7 – 10.

Page 11: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 11

MAYAI KWA AJILI YA KUTOTOA VIFARANGA.

Uchaguzi wa Mayai

Mayai kwa ajili ya kutotoa vifaranga yawe na sifa zifuatazo:-

Yaliyorutubishwa na jogoo,

Yasiwe na nyufa,

Yasiwe na maganda tepetepe,

Yasiwe na kiini kilichovunjika,

Yawe na ukubwa wa wastani; na

Yasiwe yamekaa zaidi ya wiki 2 baada ya kutagwa.

Wastani wa jogoo mmoja kwa majike kumi (10).

KUCHAGUA MAYAI YA KUANGULIWA.

Mayai yanayofaa kuanguliwa yawe na ukubwa wa wastani, yasiwe na nyufa,

yasiwe ya mviringo kama mpira, yasiwe na uchafu, mayai mazuri ni yale

yaliyotagwa na kuku aliyepandwa na jogoo.

UANGUAJI WA VIFARANGA WA ASILI.

Kwa kawaida kuku mmoja anaweza kuatamia mayai 12 hadi 15 kwa mara

moja, kuku awekewe mayai ya kuatamia wakati wa kuatamia unapofika,

inashauriw a kumwekea kuku mayai ya kuatamia wakati wa usiku kwani

akiwekewa mchana anaweza kuyaacha.

Kutayarisha kuku wa kuatamia:- kuku wanaotazamiwa kuatamia lazima

wachaguliwe kwa makini siku mbili kabla ya kuatamia ili kuhakikisha kwamba

hawana chawa, utititri au viroboto. Kuwepo kwa wadudu hao husababisha

kuku wasitulie kwani huwakosesha raha hali hii husababisha kuanguliwa kwa

vifaranga vichache.

Page 12: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 12

SURA YA NNE

UTUNZAJI WA VIFARANGA.

Kuku chotara wanahitaji matunzo bor a. endapo unahitaji kupata kuku wengi

nakuongeza kipato au kuboresha lishe ya familia, basi inakubidi uwatunze

vifaranga vizuri kwa kuhakikisha hawafi ovyo.

Vifaa kwa ajili ya kuwapatia joto vifaranga – joto ni la muhimu katika uhai wa

vifaranga , katika juma la kwanza joto linalostahili katika sehemu ya kulea ni

350C joto hili lipunguzwe kwa 20C kila baada ya juma moja hadi kufikia 270C

katika juma la tano. vifaranga wanaweza kupatiwa joto kwa kutumia vyombo

mbalimbali vya umeme, taa za chemli au jiko la mkaa

UFUATILIAJI WA VIFARANGA KUANZIA WIKI 1 – 4.

WIKI YA KWANZA

Siku ya kwanza hadi ya tano (1 – 7) vifaranga wapewe

Chick formula (dawa ya vitamini ya vifaranga) kwenye maji kwa muda

wa siku 5

Chakula cha vifaranga cha kuanzia

Chanjo ya mdondo angalau kati ya siku ya 5 hadi 7.

Vifaranga wawekwe kwenye banda safi lililowekwa maranda (yasiwe

mepesi yenye vumbi kwani yatawaletea vifaranga mafua

Vifaranga wakae na mama yao ili awapatie joto (kuwatamia) au

wawekwe kwenye chumba maalumu chenye joto.

WIKI YA PILI

Page 13: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 13

Siku ya 8 – 14

Vifaranga waendelee na chakula cha vifaranga

Siku ya 12 hadi 14 wapewe dawa ya kinga ya kuvaa makoti (kuhara

damu)

WIKI YA TATU

Siku ya 15 – 21

Chakula cha vifaranga kiendelee

Vifaranga warudie kupewa dawa/vitamin ya vifaranga (chick formula )

kwa muda wa siku tano

Siku ya 20 – 21 wapewe dawa ya minyoo ya kuku. Dawa ya minyoo

inatakiwa uwape kuku wote ulio nao bila ya kujali kundi. Baada ya miezi

mitatu kuku wote wanatakiwa kupewa dawa ya minyoo tena.

Banda la kuku (vifaranga) lifagiliwe na kuwekwa tena maranda safi

Kama uliwapa chanjo ya kuchanganya na maji inabidi urudie siku ya 25.

WIKI YA NNE : Rudia dawa ya kuvaa makoti (Esb3)

Vifaranga waendelee na chakula

Vifaranga wapewe dawa za kinga ya magonjwa mbalimbali kulingana

na ushauri wa mtaalamu

Madawa hayo ni kama

Antibiotic zilizochanganywa na vitamini (OTC Plus)

Madawa aina ya salfa- Trisulmycine, S-Dime, Fluquine

Page 14: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 14

SURA YA TANO

UTENGENEZAJI CHAKULA CHA KUKU

Chakula cha kuku lazima kiwe na viini lishe muhimu kama vile:-

Protein.

Wanga.

Madini.

Vitamini.

Hakikisha chakula unachotengeneza kinakuwa na mchanganyiko wa

vyakula vifuatavyo

Vyakula vya kujenga mwili kama vile ya kunde, samaki, mashudu ya

ufuta, pamba na alizeti.

Vyakula vya kulinda mwili na kukinga mwili usipate maradhi kam

kabichi, michicha, majani ya mapapai na nyasi mbichi.

Vyakula vinavyojenga mifupa kama vile aina ya madini, chokaa,

mifupa iliyosagwa, chumvi. Ukosefu wa vitamini na madini kama

kalisiamu na Fosforasi husababisha matege, kukunjamana kwa vidole,

kufyatuka kwa misuli ya goti na kupofuka macho.

Mambo ya kuzingatia kabla ya kutengeneza chakula cha kuku

Jinsi ya kupata vyakula vya aina mbalimbali

Kiasi cha viini lishe vinavyohitajika kulingana na umri wa kuku kwa mfano

vifanga wanahitaji protein asilimia 18 hadi 22, kuku wanaokuwa

Page 15: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 15

wanahitaji asilimia 17 hadi 19, kuku wa mayai wanahitaji asilimia 15 hadi

17

Viwango vya uchanganyaji wa aina za vyakula mbalimbali

Mchanganyiko wa chakula cha kuku chotara Kg 30

1. Pumba za mahindi debe - 2

2. Mashudu ya pamba/alizeti kg - 4

3. Dagaa zilizosagwa kg 1

4. Mifupa iliyosagwa kg 1

5. Chokaa ya mifugo kg 1

6. Damu iliyosagwa kg 1

7. Lukina iliyokaushwa debe ½

8. Chumvi ya kawaida vijiko vikubwa 2

9. Madini premix kg 1/8

10. DCP vijiko 3

Mfano wa chakula cha vifaranga kuanzia siku ya kwanza hadi majuma manne:

VYAKULA KIASI (KG)

Mahindi 30

Pumba za mahindi 20

Soya 18

Page 16: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 16

Mashudu ya alizeti 20.5

Dagaa zikaangwe kuua wadudu 5

Mifupa iliyosagwa 3

Damu iliyosagwa 1

Chumvi 0.5

Vitamini 2

Mfano wa chakula cha kukuzia kuanzia juma la nne.

VYAKULA KIASI (KG)

Mahindi 45

Pumba za mahindi 20

Soya 20

Mashudu ya pamba 5

Dagaa zikaangwe kuua wadudu 2.5

Mifupa iliyosagwa 4

Damu iliyosagwa 1

Chumvi 0.5

Vitamini 2

Page 17: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 17

Mfano wa chakula cha kuku mayai kuanzia juma la nne hadi ishirini

VYAKULA KIASI (KG)

Mahindi 45

Pumba za mahindi 25

Soya 5

Mashudu ya alizeti 12.5

Dagaa zikaangwe kuua wadudu 4

Chokaa 3

Damu iliyosagwa 3

Chumvi 0.5

Vitamini 2

Mfano wa chakula cha kuku wa mayai kuanzia juma la ishirini na kuendelea

VYAKULA KIASI (KG)

Mahindi 50

Pumba za mahindi 15.5

Soya 18

Page 18: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 18

Mashudu ya pamba 5

Dagaa zikaangwe kuua wadudu 4

Mifupa iliyosagwa 3

chokaa 2

Chumvi 0.5

Vitamini 2

Page 19: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 19

SURA YA SITA

MAGONJWA YA KUKU

Magonjwa husababishwa na virusi, bacteria, vimelea, minyoo, viroboto,

chawa, utitiri, lishe duni na uchafu

KUWATENGA WAGONJWA- kuku wagonjwa watengwe mbali na kuku

wagonjwa ili ugonjwa usisambae kwa kuku wote

Kuku huweza kushambuliwa na magonjwa mbalimbali ambayo

husababisha hasara kubwa kubwa kwa mfugaji . hasara hiyo ni kama vile

Gharama ya matibabu

Kudumaa kwa kuku

Vifo vya kuku

Upungufu wa mayai

JINSI YA KUZUIA MAGONJWA (KANUNI)

USAFI – ni muhimu sana kwa ajili ya kuzuia magonjwa

CHANJO- kuku wapatiwe chanjo dhidi ya ugonjwa wa kideri (Mdondo)

KUNYWESHA DAWA ZA MINYOO – kuku wapatiwe dawa za minyoo kila

baada ya miezi mitatu

Magonjwa yanayosababishwa na virusi

Mdondo – new castle

Dalili za ugonjwa

Kuku kukohoa

Page 20: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 20

Kuhema kwa shida

Hutokwa na ute mdomoni na pua

Hupatwa kizunguzungu

Kuharisha mharo wa kijani na njano

Hatimaye kuku hufa gafla

Vifo huweza kufikia asilimia 90

Kinga na tiba

Usafi wa banda na vyombo

Usafi wa mazingira na kuchoma mizoga inayoweza kuletwa na

ndege

Usiruhusu watu kuingia kwenye banda ovyo

Kuku wapewe kinga wakiwa na umri wa siku 5-7

hakuna tiba dhidi ya ugonjwa huu Ndui ya kuku

kuku hupatwa na vipele vya mviringo kwenye upanga, masikio,

miguu na sehemu zisizo na manyoya.

Vifo vichache kwa kuku wa kubwa, wadogo hufa nusu ya kundi

Kinga na tiba

Kuku wapewe chanjo wakiwa na umri wa miezi 2

Wapewe vitamin na antibiotic

Usafi wa banda na mazingira

Page 21: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 21

Hakuna tiba

Mafua makali ya ndege

Dalili

Kupumua kwa shida

Kukohoa na kupiga chafya

Kutokwa na machozi

Kuku kupinda shingo na kuanza kuzunguka

Kuvimba kichwa

Kuharisha kinyesi chenye majimaji , rangi ya kijani na baadaye

kinyesi cheupe

Kinga na tiba

Ukiona dalili hizo toa taarifa kwa Daktari/mtaalamu aliye karibu

nawe

Ugonjwa huu hauna tiba Homa ya matumbo

Dalili

Kuku huharisha mharo wa kijani

Vilemba na upanga hupauka kutokana na upungufu wa damu

Manyoya husimama

Vifo huweza kufikia asilimia 50

Kinga na tiba

Page 22: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 22

Usafi wa banda

Tibu kwa kutumia dawa zinazoshauriwa na wataalamu kama

vile Esb3

Kipindupindu

Dalili

Kuku huhara mharo wa njano

Husinzia na kulegea

Hulala kichwa kikining’inia kwenye mabawa

Magoya husimama

Hushindwa kusimama hatimaye hufa

Vifo huweza kufikia asilimia 50

Kinga na tiba

Usafi wa banda, vyombo na mazingira yake

Tumia dawa ya chanjo kwa kufuata ushauri wa mtengenezaji

wa chanjo

Ugonjwa huweza kutibika kwa dawa aina ya sulfa

Mafua ya kuku Coryza

Dalili

Kuvimba uso na macho

Kamasi hutiririka toka puani na mdomoni

Page 23: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 23

Hukohoa

Huhema kwa shida na kukoroma

Mayai hupungua asilimia 10 - 40

Kinga na tiba

Usafi wa b anda na mazingira yake

Kuku wagonjwa watengwe na ikibidi wachinjwe

Wapewe dawa ya chanjo siku 2 kabla ya kuanzwa

CTC 30%

MINYOO.

Ni wa wadudu wanaoleta madhara kwa kuku na hata kwa wanyama

wengine. Kuku hupata minyoo kwa kula vyakula vyenye kinyesi chenye wadudu

waha

Dalili

Kuku hudumaa

Manyoya huwa hafifu

Damu hupungua

Kupungua uzito na kukonda

Utagaji wa mayai hupungua

Minyoo huweza kuonekana kwenye kinyesi

Kinga

Page 24: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 24

Safisha banda kwa dawa ya kuuwa wadudu

Badilisha matandazo

Safisha vyombo vya chakula na maji

Tenganisha kuku wakubwa na wadogo

Kuku wapewe dawa za kuzuia minyoo kila baada ya miezi

mitatu

Kwa ushauri zaidi Muone mtaalamu wa mifugo.

MASOKO:

Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa

ya msingi yatakayomsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya

juu katika biashara anayoifanya:

Kwanza kabisa ajiulize kama bidhaa anayozalisha ina soko? Na kama soko lipo:

• Lipo wapi na hali ya miundombinu za kulifikia iko vipi ( ili afahamu gharama ya

kufika sokoni kama utaamua kuuzia sokoni).

• Bidhaa inahitajika kwa wingi kiasi gani na wakati gani sokoni

• Soko linahitaji bidhaa yenye sifa zipi ( ubora n.k. ili uzalishe sawa na matakwa

ya soko n.k)

• Kama wanunuzi watakuwa na utayari kununulia unakozalishia, je unao uwezo

wa kutosheleza mahitaji yao (ili uweze kujipanga kukidhi mahitaji kwa kuongeza

uzalishaji au kwa kuungana na wazalishaji wengine).

• Linganisha bei ya bidhaa sokoni na bei ya kuuzia unakozalishia (ili ujue palipo

na faida zaidi kwako baada ya kuondoa gharama za kufuata soko) Ila ukiamua

Page 25: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 25

kuuzia sokoni hakikisha unao uwezo wa kushindana na wauzaji wengine huko

sokoni.

Majibu ya maswali haya ndiyo yatakayokupa msingi wa kujipanga kiuzalishaji ili

hatimaye upate faida. Hivyo hata kabla hujaanza kuzalisha fahamu haya

yaliyotajwa hapa juu.

(a) Kutafuta na kutumia taarifa za masoko ya sehemu tofauti:

Kwa kadri utakavyokuwa unaendelea kuzalisha, mabadiliko mbali mbali

yatatokea kuhusiana na uzalishaji wako na hata kuhusiana na soko la bidhaa

unayozalisha kwa maana ya kuku.

Ili uendane na mabadiliko yanayotokea ni muhimu mzalishaji upate taarifa za

hali ya soko mara kwa mara. Taarifa hizi zitakusaidia kufanya maamuzi

yatakayokuwezesha kuendelea kupata faida.

Taarifa za masoko zinaweza kupatikana kwa wazalishaji kadhaa kuungana na

kuunda umoja wao. Katika umoja huo wawakilishi wachache wanakuwa na

jukumu la kutafuta taarifa za masoko ya kuku sehemu mbali mbali ambako

kunaweza kuwapa wazalishaji tija zaidi.

Walio katika umoja huo watatumia taarifa hizo kufanya maamuzi ya kuuza kwa

faida zaidi kwa pamoja au kwa mmojammoja kutegemeana na hali halisi.

Watoa taarifa pia watafanya mawasiliano ya kuwajulisha wanunuzi juu ya

upatikanaji wa kuku kwenye maeneo wanakozalishiwa.

(b) Mbinu zaidi ya kupata masoko mazuri:

(i) Umoja wa kuzalisha na kuuza;

Kwa kawaida kama bidhaa ina soko, wateja hupatikana kwa urahisi pale

wanapohakikishiwa upatikanaji wa bidhaa kwa wingi katika sehemu moja.

Page 26: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 26

Katika hali hii, wanunuzi huwa tayari hata kununua kwa bei ya juu zaidi kwa

sababu ya kupunguza muda na gharama ya kutafuta bidhaa ya kutosha

kupeleka sokoni.

Kwa upande wa kuku jambo hili linawezekana kama mfugaji atafuga kuku

wengi wa umri usiopishana sana kwa wakati mmoja. Watakapofikia kimo

kinachofaa kuuza utawauza wengi kwa wakati mmoja na kwa faida zaidi.

Mahali ambapo mfugaji mmoja mmoja hawezi kukidhi wingi wa hitaji la

wanunuzi, wafugaji kadhaa wanaweza kuunda umoja wao wa kuzalisha (kila

mmoja kwake ) na kuuza kwa kipindi kimoja na kupata faida zilizotajwa hapa

juu.

Faida nyingine ya kuuza katika umoja ni kuongezeka kwa uwezo wenu wa

kupanga na kusimamia bei mnayotaka kuuzia. Sauti na uamuzi wenu wa

pamoja utawapa nguvu ya kusimamia bei yenu mnayoipanga dhidi ya bei za

chini wanazotaka wanunuzi. Uwezo wako wa kusimamia bei unayoitaka ni

mdogo ukiuza peke yako.

Chama cha akiba na mikopo ni kikundi cha watu waliojiunga kwa hari yao

kufanya ushirika wa kuweka akiba zao kwa pamoja na kutoa mikopo kwa

urahisi kutokana na akiba zao.

Kwa wafugaji wa kuku kibiashara wanashauriwa kuwa na chombo cha namna

hii kitakachokuwa na utaratibu wa wanachama kuweka na pia wanachama

hawa kuwa na fursa ya kukopa kwa lengo kubwa la kuendeleza ufugaji wao

wa kuku kibiashara.Ufugaji wa kibiashara ungehitaji kuongeza mtaji mara kwa

mara kulingana na mahitaji ya soko husika. Mfumo wa kuweka na kukopa

utakuwa chanzo kizuri na cha kuaminika kukidhi haja ya mtaji endelevu kwa

wafugaji wa kuku.

Page 27: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 27

Michango kwa ajili ya akiba inaweza kutokana na makato ya mapato

yanayotokana na mauzo ya bidhaa za kuku ( vifaranga,mayai, kuku n.k. ). Au

kiwango maalum kwa wakati maalum kinaweza kuwekwa na wanachama ili

kitolewe kwa utaratibi wanaokubaliana.

Wanachama wanaweza kukopa kutoka kwenye chama chao kwa ajili ya

ununuzi wa mahitaji, mbalimbali ya kuku kama:

• Madawa

• Vyakula

• Ukarabati au ujenzi wa mabanda ya kuku n.k

(ii) Faida za chama kama hiki ni:

• Wanachama watapata sehemu ya kuhifadhi pesa yao kwa usalama kwa ajili

ya matumizi ya baadaye.

• Masharti ya kukopa ni nafuu kuliko vyombo vingine vya kifedha.

• Wanachama hujifunza misingi ya kushirikiana, mahusiano na kusaidiana.

• Wanachama hupata maarifa ya ziada kuhusu maswala ya kifedha.

Chama cha namna hii, lazima kiwe na kanuni za kukiongoza ambazo hutungwa

na wanachama wenyewe.

Kanuni hizi zilenge kulinda malengo ya chama na kila mwanachama

anawajibika kuzizingatia.

(iii) Mambo makuu ya kuzingatia katika katiba ni:

• Malengo ya chama

Page 28: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 28

• Haki, wajibu na malengo ya wanachama

• Viwango vya viingilio

• Hisa na michango

• Uongozi na majukumu

• Vikao na mikutano

• Utunzaji wa kumbukumbu

• Mikopo na riba

• Taratibu za kutoa mikopo

• Migawanyo ya faida

(iv) Mambo ya msingi ya kusimamia na kuendesha chama cha Akiba na

Kukopa ni pamoja na:

Uhiari wa wanachama

Uongozi uwe wa kidemokrasia

Kusiwe na urasimu

Chama lazima kiwe na vitabu vitakavyotumika kuweka kumbukumbu ya

hifadhi za fedha za wanachama

Uwekaji wa akiba uwe wa mara kwa mara

Mkopo ulipwe kwa muda uliopangwa

Fedha za chama ziwekwe benki au kwenye masanduku maalum ya

kutunzia kwa utaratibu uliopendekezwa Mahesabu ya chama yafanyiwe

ukaguzi mara kwa mara.

Page 29: UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARAmuhezadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/UFUGAJI...nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu Paa: Liwe imara na lisilovuja Liezekwe kwa kutumia

Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.

[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 29

Kikundi kama hiki kinaunganisha nguvu pamoja na kupunguza tatizo la kupata

huduma ya kifedha hasa katika maeneo ya vijijini.Hata hivyo jambo la msingi la

kufanikisha malengo ya vyombo hivi ni kuzingatia kanuni zilizowekwa na

wahusika. Vilevile utaalam wa kutosha wa kuendesha na kusimamia chombo

vya namna hii ni muhimu uwepo.

(Kwa ushauri zaidi wanachama wamuone Afisa Ushirika aliyepo karibu yao).