24
TOLEO LA 1 | VOLUMU 46 JANUARI- MACHI, 2018 ISSN- 0856- 5905 YALIYOMO TGNP Mtandao

YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

  • Upload
    others

  • View
    5

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

TOLEO LA 1 | VOLUMU 46 JANUARI- MACHI, 2018

ISSN- 0856- 5905YA

LIY

OM

O

TGNP Mtandao

Page 2: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

Kuhusu Jarida: Toleo la 1, 2018

Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na masuala yanayohusu ukombozi wa mwanamke kimapinduzi na usawa wa kijinsia.

Bodi ya UhaririLilian Liundi-MwenyekitiHappy Maruchu- MjumbeDeogratius Temba-MjumbeMonica John- Mjumbe Grace Kisetu- Mjumbe Davice Collins-MjumbeMelkizedeck Karol-Mjumbe

MhaririMonica John

Mmiliki na mchapishajiTGNP MtandaoS. L. P 8921 Dar es salaam, TanzaniaSimu: +255 022 2443025/ 2443450/ 2443286; 0754 784050Barua pepe: [email protected]@tgnp.orgTovuti: www.tgnp.orgJarida hili linatoka kila baada ya miezi mitatu (kila robo mwaka). Hugawanywa kwa wadau husika wakiwemo wanaharakati wote nchini Tanzania.

Angalizo: Maoni yaliyotolewa ndani ya jarida hili na wachangiaji binafsi siyo lazima yawakilishe maoni ya mchapishaji. Mchapishaji huangalia usahihi wa habari zenyewe hawajibiki kwa makosa yamefanywa kwa nia njema.

Tahariri:Karibu tena kwenye Jarida lako la ULINGO wa Jinsia toleo la kwanza kwa mwaka huu 2018.

Katika jarida hili tumewaandalia makala mbalimbali ambazo tunaamini zitakuhabarisha, kukuelimisha na kukuburudisha katika muktadha mzima wa harakati za ukombozi wa wanawake kimapinduzi. Lengo hasa ni kuhakikisha tunaijenga Tanzania yenye kuzingatia na kuheshimu usawa wa kijinsia katika nyanja zote ikiwemo kushika nafasi za uongozi na mgawanyo sawa wa rasilimali za umma.

Toleo hili ni maalum kwa kukupatia matukio mbali mbali yaliyojiri kutokana na shughuli mbalimbali za kiharakati zinazofanywa na TGNP Mtandao na wadau wake katika kuhakikisha taifa letu linapata maendeleo endelevu.

Habari kuu katika toleo hili lenye mchangayiko wa makala ni kongamano la kubwa na la kipekee, la wanawake na uongozi lililoratibiwa na TGNP Mtandao kwa mara ya kwanza. Kongamano hilo lililokuwa na mada kuu isemayo, “Kutambua na kusherekea uongozi wa mwanamke jukwaani na nyuma ya pazia juu” lililenga kutambua michango na ushawishi wa wanawake katika kuendeleza agenda ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi na uwezeshaji wanawake nchini, pamoja na kutoa fursa/jukwaa kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na kujifunza miongoni mwa mwao.

Makala nyingine zilizopo ni pamoja na kampeni ya Hakeketwi Mtu 2018, Kampeni ya “Mpe Mabawa”, mafunzo ya tafakuri ya ushirikiano, warsha ya Madiwani, klabu za Jinsia mashuleni zinavyotumika kupunguza ukatili wa kijinsia nchini, wito wa kutenga bajeti kwa ajili ya taulo za kike wakati wa hedhi na maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji pamoja na historia ya Mhe. Anna Makinda, Spika wa kwanza mwanamke katika Bunge la Tanzania. Kupitia Makala hizi zitakupa nafasi ya kutafakari kwa kina masuala muhimu na kuendelea kujenga mijadala ya kina pale ulipo kwa kuhusianisha makala hizi na hali halisi ya mahali unapoishi.

Zaidi, kumbuka kumpatia na mwenzako jarida hili mara utakapo maliza kusoma ili kusambaza maarifa haya kwa watu wengi zaidi.

Mwisho, tunakutakia usomaji mwema na ulifurahie jarida hili. Kutoka kwa jarida hili ni mwanzo wa maandalizi ya toleo lingine.

Mhariri.

2 | ULINGO WA JINSIA2 | ULINGO WA JINSIA

Page 3: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

Kongamano la kwanza la wanawake na uongozi: Kutambua na kusherekea uongozi wa mwanamke jukwaani na nyuma ya paziaNa Mwandishi Wetu

Kuanzia kushoto ni Prof. Ruth Meena- mwanachama wa TGNP, Mhe. Mama Anna Makinda, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Scholarstica Kimaryo -Mkurugenzi wa shirika la Maadili leadership Solutions, Rachel Madundo,

Mwenyekiti wa Vituo vya taarifa na maarifa Wilaya ya Kishapu na Mhe. Esther Bulaya – Mbunge wa Bunga Mjini.

Kwa mara ya kwanza TGNP Mtandao imeratibu kongamano la wanawake na uongozi lililofanyika tarehe 27 Februari katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo liliwaleta pamoja zaidi ya washiriki 250, wakiwemo baadhi ya viongozi wanawake wastaafu na waliopo madarakani kuanzia ngazi ya jamii hadi ya taifa (mawaziri, madiwani, watendaji wa kata na vijiji, wabunge n.k), watia nia waliowania nafasi mbalimbali za uongozi 2015, wanaharakati vijana, wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa, washiriki wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) na vyombo vya habari. Kongamano hilo, la kipekee ambalo kwa mara ya kwanza liliwaleta wanawake viongozi bila kujali itikadi, dini, hali ya uchumi au umri, lilikuwa na lengo la kutambua michango na ushawishi wa wanawake katika kuendeleza agenda ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake nchini, pamoja na kutoa fursa/jukwaa kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na

kujifunza miongoni mwa mwao na kupanga mikakati ya jinsia ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi.

Akizungumza wakati wa kuwakaribisha washiriki, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Bi Lilian Liundi alielezea hali ya ushiriki wa wanawake katika uongozi nchini na kutoa wito kuwa pamoja na juhudi za wadau mbalimbali ikiwemo serikali bado juhudi zaidi zinahitajika ili kuongeza idadi ya wanawake katika nafasi mbalimbali za maamuzi nchini kufikia lengo la 50/50 katika uongozi. .

“Takwimu za Inter-Parliamentary Union (IPU) zinaonyesha kuwa hadi Januari mwaka 2017, Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa Afrika Mashariki na nafasi ya 25 duniani kwa kuwa na 36.4% ya wanawake wabunge ambapo Rwanda ndio nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na 61.3%.” Bi Liundi Alifafanua.

JANUARI- MACHI, 2018 | 3

Page 4: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

Wito umetolewa kwa vijana wote wa Afrika kujenga mustakabali wao sasa badala ya kusubiria baadae.

Akiongea katika warsha ya vijana iliyofanyika kuelekea mkutano mkuu wa nane wa Afrika juu ya haki za afya ya uzazi, mkuu wa kitengo cha vijana kutoka Umoja wa nchi za Africa (AU) Bi. Prudence Ngweya alieleza umuhimu na uhitaji wa kuwashirikisha vijana katika kufikia agenda ya 2063 ya Afrika tunayoitaka na malengo ya maendeleo endelevu.

“Afrika inaweza kushinda changamoto zote zilizopo mbele yake kupitia vijana. Tunaamini mustakabali wa vijana ni leo na si kesho.” Alisisitiza Bi. Ngweya.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la umoja wa mataifa linalojihusisha na idadi ya watu (UNFPA) kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dr. Juliita Onabanjo alisema kuwa Afrika ijayo itabadilishwa na vijana. Akisisitiza “Kama mtu mzima, naamini kwa dhati kuwa kwa ajili ya maendeleo ya Afrika, vijana ndio kitu bora na pekee tulicho nacho.”

Aidha, mwakilishi wa vijana kutoka umoja wa mataifa (UN), Bi. Jayathma Wickramanayake ambaye aliwashilisha hotuba na pia kushiriki katika moja ya mdahalo wa vijana juu ya kuunganisha mgawanyiko wa

idadi ya watu uliopo Afrika “Harnessing Demographic Dividends in Africa” aliweka mkazo juu ya umuhimu wa elimu ya Afya ya Uzazi na haki kwa vijana na uhitaji wa kutokomeza mila potofu.

“Katika karne hii hatuwezi ruhusu watoto kuozwa wala watoto kuzaa watoto.” Alisisitiza akiongezea, “Tunatakiwa kuhakikisha kuwa vijana ndio msingi wa mabadiliko. Vijana wanatakiwa kuwa mhimili katika utekelezaji wa programu zinazoendelea katika jamii zetu.”

Nae, Waziri katika ofisi ya Rais nchini Afrika Kusini Mhe. Jeff Radebe katika hotuba yake ya ufunguzi alisema kuwa wanawake na vijana wameendelea kuwa kundi linaloachwa nyuma katika jamii.

“Japokuwa vijana chini ya miaka 15 ni takribani asilimia 41 ya idadi ya watu wote Afrika kulingana na takwimu za Benki ya Dunia, takribani asilimia 60 ya kundi la vijana wote Afrika hawana ajira.” Mhe. Radebe alielezea akiongoza, “kwa kutambua ukubwa wa tatizo na kufanya jitihada za kutatua hali iliyopo sana na inayotabirika Umoja wa Africa (AU) walitangaza mwaka 2017 kuwa mwaka wa kuunganisha mgawanyiko wa idadi ya watu uliopo Afrika “Harnessing the Demographic Dividend” kwa kuwekeza kwa vijana”

Wito kwa Vijana wa Afrika: “Jenga mustakabali wako leo”Na Monica John.

Aliongeza, “kwa kuzingatia kanuni ya Malengo ya ya Kidunia ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ya kutomwacha mtu nyuma, kongamano hilo linahakikisha ushiriki wa watu umri mbalimbali ili kuleta majadiliano yenye tija ambayo yataleta chachu ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi.” Kwa upande wake Mgeni rasmi katika kongamano hilo, Mbunge wa Hanang Dkt. Mary Nagu alisisitiza juu ya nguvu ya idadi ya wanawake hasa katika uchaguzi. Akisema, “Wanawake ni zaidi ya 50% ya idadi ya wananchi wote Tanzania. Hatuna budi kuitumia vizuri idadi yetu ili tuweze kuongeza idadi ya wanawake katika nafasi mbalimbali za maamuzi. Tuna nguvu na uwezo wa kuwawezesha wanawake wenzetu kushika nafasi za uongozi kwa kupitia kura zetu.”

Dkt Nagu, pia aliwakumbusha wanawake walioshika nafasi mbalimbali za uongozi kutumia nafasi hizo kuhakikisha kuwa mahitaji ya wanawake na makundi yaliyo pembezoni yanashughulikiwa. TGNP Mtandao inaamini kwenye uongozi wenye kuleta mabadiliko na ulioshirikishi: kiongozi anapaswa kuwa mwaminifu, muwajibikaji na kuwa na uwezo wa kuhamasisha na kuunganisha jamii ili kuhakikisha haki za kijamii, usawa na haki za binadamu zinazingatiwa. Ni kwa kupitia majukwaa kama Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS), Tamasha la Jinsia, majukwaa ya wanawake wanaharakati na viongozi vijana, vitovu vya jinsia mashuleni na vituo vya taarifa na maarifa, TGNP Mtandao imekuwa ikilea na kukuza viongozi wanawake watakaoleta tija katika maendeleo katika jamii yetu na nchi kwa ujumla. Lengo kuu limekuwa ni kuhamasisha ushiriki wa wananchi hasa wanawake katika nafasi mbalimbali za maamuzi kunanzia ngazi ya jamii hadi taifa.

4 | ULINGO WA JINSIA

Page 5: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

Wito kwa Vijana wa Afrika: “Jenga mustakabali wako leo”

Mhe. Radebe aliwataka vijana wa kiafrika kuwa wasimamizi na walinzi wa maendeleo yao kama ilivyotamkwa katika kifungu cha 26 cha Mkataba/maazimio ya Afrika kwa vijana ‘African Youth Charter’ na kwa upande mwingine, kuzitaka serikali za Afrika kutekeleza na kwa umoja kuwekeza katika kuwawezesha na kuwainua vijana na wanawake.

Warsha hiyo ya vijana iliyofanyika mwezi wa pili jijini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini, iliratibiwa na shirika la AIDS Foundation South Africa (AFSA) kwa kushirikiana na Youth Lab nchini Afrika Kusini na mashirika mengine. Mkutano huo ulikuwa na mada kuu isemayo “Kuendeleza upatikanaji wa afya ya uzazi na haki kwa wasichana na wanawake katika bara la Afrika (advancing SRHR of Girls and Women in Africa)” na uliwakutanisha zaidi ya vijana 150 kutoka mataifa 16 barani Afika ikiwemo Tanzania, kujifunza, na kubadilishana uzoefu wa mikakati inayofanya kazi na kuleta tija katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi kwa vijana.

Mwandishi wa makala

haya ni Mtaalamu

wa Mawasiliano toka

TGNP Mtandao na

Mmoja wa washiriki

wa mkutano huo

JANUARI- MACHI, 2018 | 5

Baadhi ya Washiriki wa warsha ya Vijana iliyofanyika kuelekea mkutano mkuu wa nane wa Afrika juu ya haki za afya ya uzazi (African Conference on Sexual Health and Rights) katika moja ya vikundi vya majadiliano kuhusu kukabiliana mila na tamaduni

potofu zinazokwamisha watoto wa kike kufikia ndoto zao.

Page 6: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

Shelagh Savage mwakilishi kutoka Taasis ya elimu ya kimataifa ya Coady akifanya uwezeshaji wakati wa warsha.

Tafakuri kuhusu ushirikiano: TGNP Mtandao na Chuo cha Mafunzo ya Kijinsia waratibu warsha ya siku mbili. Na Davice Collins, TGNP Mtandao

TGNP Mtandao na Taasisi ya Mafunzo ya Kjinsia (GTI) kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Crossroad International (CI) la nchini Canada pamoja na Taasisi ya Elimu ya Kimataifa ya Coady huko Canada waliendesha warsha ya siku mbili kuanzia tarehe 16-17 Januari katika ofisi za TGNP Mtandao jijini Dar es salaam. Warsha hiyo iliwaleta pamoja takribani washiriki 26, wakiwakilisha asasi za kiraia, vyuo vya elimu ya juu, makundi ya vijana, watu wenye ulemavu na maafisa wa serikali kutoka Dar es Salaam.

Malengo makuu ya warsha hiyo yalikuwa ni kutafakari upya na kuweka mikakati juu ya masuala ya

ushirikiano (rethinking partnership) katika ngazi zote na kuongeza uwezo wa kushirikiana bila kujali tofauti ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Warsha hiyo pia ililenga kujenga ujuzi wa pamoja ili kuleta tija na usawa katika ushirikiano.

Akitoa neno la ukaribisho, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Bi Lilian Liundi alieleza faida na manufaa ya ushirikiano katika kujenga harakati la vuguvugu la wanawake lenye nguvu. “Ni kupitia ushirikiano na Crossroads International (CI) ndipo TGNP Mtandao iliweza kuanzisha ushirikiano wa utatu pamoja na Taasisi ya Kimataifa ya Coady

iliyoko nchini Canada ili kuendesha na kupanga mafunzo ya kikanda na TGNP Mtandao na Chuo cha Mafuzo ya Jinsia (GTI). Warsha hii ni mwanzo wa tu ushirikiano huo” Alisisitiza.

Kwa upande wake Profesa Saida Yahya Othman mwanachama wa TGNP Mtandao ambaye pia alikuwa mgeni rasmi alifafanua misingi na umuhimu wa ushirikiano katika kuleta maendeleo yenye tija hasa katika kushirikishana uzoefu na ujuzi ili kufikia malengo ambayo isingekua rahisi kuyafikia kwa kujitegemea binafsi au kama shirika moja moja.

6 | ULINGO WA JINSIA

Page 7: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga imepongezwa kwa kuweza kutenga bajeti yenye mrengo wa kijinsia katika bajeti ya mwaka 2016/2017 na hivyo, kuifanya halmashauri hiyo kupata tuzo iliyotolewa na Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Mama samia suluhu wakati wa Tamasha la Jinsia la 13 lililoandaliwa na TGNP Mtandao Septemba 2017.

Hayo yalielezwa hivi karibuni na Katibu wa Mtandao wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu vinavyoratibiwa na TGNP Mtandao Peter Nestory, wakati akiwasilisha mapendekezo ya wanajamii katika kikao cha baraza la madiwani, kupitia hoja binafsi waliyoiandaa.

Hoja hiyo binafsi ililenga kuitaka Halmashauri hiyo kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuboresha mazingira ya shule kwa mtoto wa kike kwa kukabiliana na changamoto zinanazo mkabili mtoto wa kike kama ukosefu wa taulo za kike mashuleni, ukosefu wa vyumba maalumu vya kujihifadhi watoto wa kike wanapokuwa katika hedhi.

Prof. Saida aliongezea “Malengo haya ya warsha yaliyosheheni yatasadia kujenga mfumo wa ushirikiano, kuchambua washirika wenye uwezo, na kuendeleza mikakati ya kuimarisha ushirikiano. Kama mwanachama wa TGNP Mtandao na mkufunzi, binafsi napenda kuwashukuru shirika la kimataifa la CI kwa kuunga mkono mpango huu muhimu.”

Shelagh Savage mwakilishi kutoka Taasisi ya elimu ya Kimatifa Coady ambaye pia alikuwa ni mwezeshaji wa warsha hiyo alifafanua kuwa ushirikiano ni zaidi ya msaada wa kifedha, ila pia una jumuisha ujuzi ambao ni wa msingi. “Kabla ya kufanya ushirikiano, taasisi inatakiwa kuzingatia malengo ya pamoja, manufaa ya pamoja na uainishaji wa majukumu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.”

Warsha hii ni matokeo ya ushirikiano wa pamoja kati ya TGNP Mtandao na shirika la kimataifa la Crossroad (CI), Shirika la kimataifa la maendeleo la Canada linalojihusisha na kupunguza umaskini na kuongeza haki za wanawake duniani. CI imekuwa ikishirikiana na TGNP Mtandao katika shughuli mbalimbali zikiwemo mafunzo, utafutaji wa rasilimali na kubadilishana uzoefu. Kama sehemu ya kuimarisha mahusiano hayo kati ya GTI na Coady, CI imewezesha ushirikiano wa mashirika matatu yaani TGNP Mtandao, GTI na Coady. Ushirikiano huu unalenga kutoa fursa ya kuratibu mafunzo na warsha mbalimbali kwa pamoja. Baadhi ya mafunzo yanayotarajiwa kutolewa TGNP Mtandao na GTI jijini Dar es salaam hapo baadae mwaka huu ni pamoja na zana na mikakati ya wajibu na uwajibikaji wa wananchi, na mafunzo ya uongozi kwa vijana.

Jamii Kishapu yataka Kutengwa bajeti kwa ajili ya taulo za kike wakati wa hedhiNa Kadama Malunde- http://www.malunde.com

Wanaharakati ngazi ya jamii kupitia mtandao wa vituo cha taarifa na maarifa wilayani Kishapu wakiwasilisha taarifa ya mtandao wao katika kikao cha baraza la madiwani. Wapili kutoka kulia ni katibu wa mtandao huo, Peter Nestory.

JANUARI- MACHI, 2018 | 7

Page 8: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

Pia, wameishauri halmashauri kupitia bajeti ya mwaka 2018/19 kuongeza bajeti iliyotengwa kwa ajili ya maendeleo ya wanawake, vijana na watu wanaoishi na ulemavu ili kufikia malengo ya kuwezesha na kuinua kiuchumi makundi hayo.

“Kupitia mapendekezo yetu tunashauri shilingi milioni 40 zilizotengwa kwenye bajeti ya mwaka 2018/2019 kwa ajili ya kuwezesha makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ziongezwe hadi kufikia shilingi milioni 100 au zipelekwe eneo moja tu kwani haziwezi kukidhi malengo. Katika bajeti ya mwaka uliopita walitenga shilingi milioni 82 kwa ajili ya makundi hayo na hazikutosha.” alisema Katibu huyo.

Pia waliitaka halmashauri na serikali kupitia wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto kuchukuwa hatua za makusudi ili kuweza kukamilisha ujenzi zahanati na vituo vya afya pamoja na kuboresha upatikanaji wa vifaa tiba na madawa hatua itakayosaidia kuepusha vifo vya mama na mtoto chini ya miaka mitano.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. Boniface Butondo alisema halmashauri hiyo inatambua jitihada kubwa

zinazofanywa na TGNP Mtandao kupitia Vituo vya Taarifa na Maarifa katika kuibua changamoto mbalimbali za kijamii.

“Naahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyowasilishwa kwenye kikao hicho na wanavituo vya taarifa na maarifa kwa niaba ya wanajamii juu ya bajeti ya halmashauri ya mwaka 2018/2019.” Aliahidi Mhe. Butondo.

Mhe. Butondo aliendelea kusema kuwa mtandao huo uliiwezesha halmashauri hiyo kupata tuzo heshima ambayo ilikabidhiwa kwao na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 iliyozingatia mrengo wa kijinsia ambayo iliwawezesha watoto wa kike kupata pedi/taulo na kuahidi kuzingatia ushauri huo.

Naye, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mhe. Stephen Magoiga alisema hoja na mapendekezo ya wanajamii yaliyowasilishwa na katibu wa mtandao wa vituo vya taarifa na maarifa wa wilaya ya Kishapu yatajibiwa kwa maandishi yakiambatana na ufafanuzi wa mikakati iliyopo na hatua ziliyochukuliwa.

8 | ULINGO WA JINSIA

Page 9: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

Washiriki wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji yaliyofanyika katika kata ya kipunguni ambako hivi karibuni kipindi cha ukeketaji kitaanza

Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji: Hakeketwi Mtu 2018Na Monica John,

TGNP Mtandao kwa kushirikiana na kituo cha taarifa na maarifa Kipunguni wameadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji. Maadhimisho yalifanyika tarehe 7 Februari katika kata ya Kipunguni. Maadhimisho hayo yaliwaleta pamoja washiriki 130 (78 ke, 52 me) wakiwemo watumishi wa TGNP Mtandao, wanachama wa sauti ya jamii Kipunguni, wawakilishi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi, maafisa wa serikali za mtaa, wanafunzi, viongozi mashuhuri, wananchi kutoka mitaa ya Kivule, Chanika, Kitunda, Mzinga na Mabibo pamoja na wanahabari.

Maadhimisho hayo yalilenga kuandika na kuweka kumbukumbu za safari ya harakati za kupambana na ukeketaji ikiwemo kuweka kumbukumbu za hadithi za mafanikio na ushuhuda kutoka kwa washiriki namna ambavyo wanakabiliana na vitendo vya ukeketaji pamoja na kuweka mikakati ya pamoja na kwa umoja kupambana na vitendo hivyo.

Akifungua maadhimisho hayo, Afisa Programu Mwanamizi wa TGNP Mtandao Idara ya Ujenzi wa Harakati na Nguvu za Pamoja Bi Anna Sangai alielezea kuwa, “Kuna njia au mbinu mbalimbali

ambazo hutumia kukeketa. Kuna watu wanatumia kemikali kwa watoto wachanga kuwakeketa, wengine wanawavalisha watoto wa kike mavazi ya kiume na kusema wanaenda kuwatairi, wengine wanatumia kucha kuondoa hicho kiungo hasa kwa watoto wachanga lakini kiuhalisia, ni namna ambavyo wanafanya ukeketaji kimya kimya”.

Bi Sangai alimtaka kila mtu kuwajibika kuwalinda watoto dhidi ya mila potofu kama vile ukeketaji.

Miongoni mwa masuala yaliyouibuliwa katika maadhimisho hayo ni pamoja na kutolewa elimu zaidi juu ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji hasa kwa polisi waliopo katika madawati ya jinsia ili kuweza kuongeza umakini wao katika kupambana na vitendo hivyo.

Pia, washiriki walitaja changamoto ya ufinyu wa rasilimali fedha kwa ajili ya madawati ya jinsia unaokwamisha msaada wao katika kufanyia kazi matukio ya ukatili yanayoripotiwa katika madawati hayo. “Ni muhimu Serikali ikatenga fedha za kutosha kwa

JANUARI- MACHI, 2018 | 9

Page 10: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kutoka wilaya za Kinondoni, Temeke na Ubungo wakiwasilisha maswala yalioibuliwa katika utafiti shirikishi zlizofanywa katika shule zao.

Vitovu vya Jinsia Kupunguza Ukatili wa Kijinsia Nchini Na Hellen Nachilongo- Gazeti la The Citizen

“Tangu kuanzishwa kwa klabu

ya jinsia shuleni kwetu, wanafunzi wamekuwa na uelewa juu ya masuala na aina mbalimbali za ukatili wa kijinsia na wanauwezo wa kupambana na vitendo hiyo vya kikatili.”

ajili ya madawati ya jinsia ili kuweza kurahisisha kazi zao za kupambana na ukatili wa kijinsia katika jamii.” Mzee Khamis mmoja wa washiriki alipendekeza na kusisitiza.

Aidha, washiriki waliguswa na suala la kutoa msaada kwa wasichana wanaotoroka nyumbani kwa hofu ya kukeketwa. Washiriki walisema kuna umuhimu wa wasichana hawa kusaidiwa kwa kupatiwa mahitaji muhimu kama vile malazi, chakula na makazi, na hivyo, kuyataka mashirika kutengeneza vituo salama vitakavyowawezesha wasichana hawa jasiri kupata mahitaji yao muhimu wanapotoroka kukekektwa. Zaidi, washiriki wameitaka TGNP Mtandao kuanzisha

Vitovu vya jinsia katika shule ya sekondari Misitu ili kuwawezesha na kuwajengea uwezo baadhi ya wasichana katika shule hiyo walionaza kushiriki katika harakati za kupambana na ukeketaji ili pia waweze kuwahamasisha wanafunzi wengine kushiriki katika kutoa elimu na mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto hususani ukeketaji.

Siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji ni siku inayofadhiliwa na umoja wa mataifa (UN) kutoa elimu juu ya madhara ya ukeketaji. Siku hii huadhimishwa kila mwaka tarehe 6 Februari kama sehemu ya jitihada za umoja wa mataifa kutokomeza ukeketaji. Maadhimisho haya yalianza rasmi mnamo mwaka 2003.

Ukatili wa jinsia ni suala la kiafya na haki za binadamu duniani. Suala hili limekithiri zaidi katika nchi zinazoendelea kama Tanzania. Wanawake na watoto katika nchi nyingi zinazoendelea wameathiriwa zaidi na ukatili wa kimwili na kihisia kwa sababu ya jinsia yao. Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoo kunahitaji nguvu ya pamoja na kushirikisha mikakati mbalimbali.

Ili kutokomeza ukatili wa kijinsia nchini, TGNP Mtandao inatoa elimu katika shule za msingi na sekondari ili kuwahamasisha kuanzisha vitovu vya jinsia katika shule hizo. Jitihada hizi zinalengo la kuzuia kusambaa na athari za vitendo vya ukatili.

Kupitia jitihada hizi, TGNP Mtandao imeweza kuelimisha walimu tisa (10) wa shule za sekondari (5)

10 | ULINGO WA JINSIA

Page 11: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

na msingi (5) na kuhakikisha kuwa vitovu vya jinsia zimeanzishwa katika shule hizo. Shule hizo ni pamoja na shule za sekondari Mabibo wilayani Ubungo, Makumbusho wilayani Konondoni, Kivule wilayani Ilala, Maganzo na Ukenyenge wilayani Kishapu ambapo shule za msingi ni Mchangani wilayani Kinondoni, Umoja wilayani Ubungo, Kilimani wilayani Ilala, Magoto na N’ereng’ere wilayani Tarime.

Mwalimu wa shule ya msingi Kilimani Bw. Jagita Maryango anasema kuwa wanafunzi mara nyingi wanakumbana na vitendo vya ukatili lakini hukosa majukwaa ya kuongelea na kutoa taarifa juu ya vitendo hivyo ili viweze kuchukuliwa hatua.

Bw. Maryango alieleza kuwa waalimu wananafasi kubwa ya kuzuia vitendo vya kikatili kwa watoto wa kike na wa kiume wawapo shuleni na zaidi, msaada mkubwa unahitaji kuhakikisha watoto wanakuwa salama.

Mbali na hilo, alielezea kuwa shule ni sehemu nzuri ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa sababu wanafunzi wanatumia masaa mengi wakiwa shuleni kuliko sehemu nyingine. Hii ina maanisha kuwa jitihada zote zinazolenga kutokomeza ukatili zitafanikiwa zaidi zikianzishwa katika shule tofauti tofauti kuliko sehemu nyingine yoyote.

“Tangu kuanzishwa kwa vitovu vya jinsia shuleni kwetu, wanafunzi wamekuwa na uelewa juu ya masuala na aina mbalimbali za ukatili wa kijinsia na wanauwezo wa kupambana na vitendo hiyo vya kikatili.” anasema Mwalimu huyo.

Aliendelea kuelezea kuwa wakati vitovu vya jinsia inaanzishwa shuleni hapo, wanafunzi wachache sana waliweza kujitokeza kujiunga na vitovu hivyo lakini kwa sasa klabu hiyo ina zaidi ya wanafunzi 80 na ni matajario yake wanafunzi wataongezeka zaidi kutokana na kuona umuhimu wa kujiunga katika vitovu hivyo.

Aidha mwalimu huyo anaendelea kusema kuwa shule zenye klabu za jinsia zinafanya vizuri sana kwani wanafunzi wake wanauwezo wa kuzungumza kwa uwazi juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia kwa wazazi, waalimu na jamii kwa ujumla. Wanafunzi wamekuwa wajasiri katika kujielezea bila woga au kusita jambo ambalo linasaidia katika kutokomeza vitendo vya

ukatili shuleni kwa sababu wanafunzi wengine wanajua hatua za kuchukua wanapokumbana na vitendo vya ukatili.

Kwa upande wake mwalimu wa shule ya msingi Kivule Bi Stella Lugendo anasema kuwa elimu ina mchango mkubwa katika kupinga mila na tamaduni potofu zilizopo katika jamii zinazopelekea ukatili wa kijinsia. Akiongezea, “Juhudi za pamoja zinahitajika ili kuhakikisha mizizi ya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana inang’olewa. Na njia nzuri ya kutokomeza ukatili ni kuhakikisha hautokei kabisa kwa kupambana na visababishi vya vitendo hivi.

Nae, Mkuu wa wilaya ya Ubungo Bw. Kisare Makori amewataka wanaharakati wanaopambana na ukatili wa kijinsia kuja na mapendekezo yatakayoisaidia serikali kutengeneza mitaala kuhusu masuala ya jinsia.

Aliongezea kuwa kama ilivyo kwa somo kama hesabu, sayansi na masomo mengine, Elimu ya jinsia inapaswa kuwa moja ya masomo yanayofundishwa shuleni ili kusaidia kutokomeza vitendo vya ukatili kwa kusaidia wanafunzi kujua madhara ya vitendo hivyo. Kwa kulisoma kama mojawapo ya masomo, wanafunzi watajua haki zao na namna ya kijilinda dhidi ya ukatili wa kijinsia.

“Ukatili wa kijinsia bado ni changamoto nchini. Takwimu zinaonyesha kuwa 42% ya wanawake walioolewa wamekumbana na vitendo vya ukatili wa kingono kutoka kwa waume zao. Hata hivyo, kama masuala ya jinsia yatafundishwa kwa wanafunzi itawasaidia watoto wa kiume kujua madhara yatokanayo na kuwakatili wenzi wao na hivyo, kuwahamasisha wasiweze kutenda vitendo hivyo kwa wenzi wao wanapokuwa. Na kwa upande wa watoto wa kike, itawasaidia kujua namna ya kujilinda dhidi ya vitendo hivyo.” Anasema mkuu huyo wa Wilaya.

Wanafunzi ni wahusika wa msingi tukifikiria kusambaza njia mbalimbali za kuzuia ukatili wa kijinsia nchini. Watakuwa wakubwa wakiwa na akili na fikra kuwa ukatili kijisnia hauvumiliki na hivyo watachukua hatua kuukomesha na kuutokomeza.

Vitovu hizi za jinsia zinatengeneza mwanzo mzuri katika kuendeleza mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

JANUARI- MACHI, 2018 | 11

Page 12: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

12 | ULINGO WA JINSIA

12

8 9

65

Page 13: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

JANUARI- MACHI, 2018 | 13

3

4

7 1. caption missing

2. Diwani wa Ijombe wilayani Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa

shule ya sekondari Igawii, Stimar Hepa John akichangia kwenye mjadala wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.

3. Diwani wa Kata ya Mshewe ya Wilaya ya Mbeya vijijini, mkoani Mbeya, Esther Mbega akishiriki kwenye mjadala wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam

4. Wanaharakati wa Sauti Jamii Kipunguni wakiwa na watoto mbalimbali wa kata ya hiyo wakiwa wameshika mabango yenye jumbe tofauti tofauti kuashiria kuchoshwa na vitendo vya ukeketaji vilivyoshamili katika kata hiyo, mapema jana katika uzinduzi wa kampeni ya Akeketwi mtu mwaka 2018.

5. Watoto kutoka mitaa mbalimbali ya kata ya Kipunguni wakilifuata gari la matangazo la Sauti Jamii Kipunguni na kuzipokea kwa furaha huduma mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ikiwa ni kugawa vipeperushi na kutoa elimu bure, mapema jana katika uzinduzi wa kampeni ya Akeketwi mtu mwaka 2018.

6. Mwanaharakati wa Sauti Jamii Kipunguni Bi. Tausi Msangi akibandika karatasi yenye ujumbe(posters) katika moja ya duka la dawa linalopatikana katika kata ya kipunguni, mapema jana katika uzinduzi wa kampeni ya Akeketwi mtu mwaka 2018.

7. caption missing

8. Wanaharakati wa kata ya kipunguni wakicheza kwa pamoja na watoto wa kata hiyo mara baada ya kuwapa elimu juu ya kupinga ukeketaji na rushwa ya ngono mapema jana jijini Dar es salaam.

9. Mchungaji wa kanisa la Sinai Pentecostal Ndugu. Imani Juma Feruzi akibandika karatasi yenye ujumbe(posters) katika pikipiki mapema jana, katika uzinduzi wa kampeni ya akeketwi mtu mwaka 2018 iliyoandaliwa na Sauti Jamii Kipunguni ili kupinga vitendo vya Ukeketaji na Rushwa ya ngono.

Page 14: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

Hakeketwi Mtu 2018: Kipunguni Waanzisha Kampeni ya Kupinga Ukeketaji Na. Vicent Macha- www.habari24.blogspot.com

Kituo cha taarifa na Maarifa -Sauti Jamii Kipunguni kimezindua kampeni mahsusi ya kupinga ukeketaji kwa kutoa elimu mtaa kwa mtaa, kugawa vipeperushi pamoja na kubandika mabango yenye jumbe mbalimbali katika kata hiyo.

Akiongoza kampeni hiyo Mwenyekiti wa kituo hicho Bw. Selemani Bishagazi alisema kuwa lengo kuu la kampeni hiyo ni kupinga vitendo vya ukeketaji vinavyotarajiwa kutekelezwa mwaka huu. Akidai, “Mwaka 2018 ni mwaka wa ukeketaji hususani kwa makabila yanayotoka mikoa ya mara ambayo wakazi wengi wa kata hiyo hutoka katika mkoa huo.” Bw. Bishagazi alieleza kuwa watekelezaji wakuu wa ukeketaji ni watu wanaoishi katika jamii na kesi zake zinakuwa ngumu

kusikilizwa kutokana na kwamba watekelezaji wa hayo ni ndugu kama vile baba, mama au shangazi hivyo kuleta ugumu kwa mtoto kutoa ushahidi kwa kuogopa kuwa mzazi wake au ndugu yake atafungwa kwa sababu yake.

“Wanaharakati wengi wamekuwa wakisubiri zoezi la kukeketa lianze ndipo waanze kuwakamata wahusika wakiwa tayari wameshakeketa, lakini kwetu sisi tumeona tuzuie kabla watoto hawa hawajafanyiwa ukeketaji ili kuweza kuwakomboa juu ya mila na tamaduni mbaya kama hizi” alifafanua Bishagazi akiongezea, “Kampeni hii itakuwa ni endelevu lakini pia tutajaribu kuwa karibu na wananchi ili waweze kutupa taarifa mbalimbali kuhusu wakeketaji na tutakaa nao chini kuwapa elimu juu ya madhara ya ukeketaji ili waachane na mila

potofu ya kukeketa na waweze kuwa watu wema katika jamii”.

Kwa upande wake Tausi Msangi mmoja wa washiriki katika uzinduzi wa kampeni hiyo ameelezea kufurahishwa na kuanzishwa kwa kampeni hiyo akiamini kuwa jamii kubwa ya Kipunguni na nje ya Kipunguni wataweza kufikiwa ili kushiriki katika kutoa taarifa za vitendo vya ukeketaji katika maeneo yao.

“Mwitikio wa wananchi kuhusu kampeni hii unaonekana kuwa chanya kwani wamekubali kushiriki katika kutoa taarifa za ukeketaji katika maeneo yao wakati msimu utakapokaribia. Na kwa upande mwingine, nimeshuhudia baadhi ya kina mama wakianza kukosoana kutokana na kuendekeza vitendo vya ukeketaji.” Alifafanua Tausi.

Wanaharakati kutoka wa kata ya Kipunguni jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Hakeketwi mtu 2018,

14 | ULINGO WA JINSIA

Page 15: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

Madiwani watakiwa kushirikiana na wananchi katika maendeleoNa Rabi Hume- www.Dewjiblog.co.tz

Afisa Programu ya Ujenzi wa Harakati na Nguvu za Pamoja wa TGNP Mtandao Bw. Deogratius Temba akiendesha mjadala wa kubadilishana uzoefu baina ya Madiwani juu ushirikiano kati ya wananchi na viongozi wao katika kuleta maendeleo katika kata zao.

Madiwani wametakiwa kushirikiana na wananchi katika uandaaji na utekelezaji wa shughuli za maendeleo badala ya kujiamulia wenyewe. Hayo yalieleza katika warsha iliyoandaliwa na TGNP Mtandao, ikwakutanisha madiwani 30 kutoka halmashauri za Kishapu (Shinyanga), Tarime (Mara), Mbeya (Mbeya), Morogoro Vijijini (Morogoro) na manispaa za Ilala, Kinondoni na Ubungo (Dar es salaam).

Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar e salaam, ilitoa nafasi kwa madiwani hao kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao.

Akiongea katika Warsha hiyo, Afisa Programu ya Ujenzi wa Harakati na Nguvu za Pamoja wa TGNP Mtandao Bw. Deogratius Temba

alisema “shughuli za maendeleo zinawahusu wananchi moja kwa moja hivyo viongozi hasa madiwani wanaochaguliwa na wananchi hawana budi kuwashirikisha wapiga kura wao.”

Madiwani hao pia walipata fursa ya kushirikishana masuala ya kijinsia hasa kwa kuchambua bajeti zao za Halmashauri kwa kuzingatia mrengo wa kijinsia na namna wamezingatia na kufanikiwa kutenga rasilimali kuhakikisha zinakidhi mahitaji ya kijinsia. Katika kujifunza, madiwani hao piawalitembelea kituo cha taarifa na maarifa Kipunguni na kujionea mradi wa kilimo cha kisasa unaotekelezwa katika eneo hilo kama sehemu ya kupambana na ukeketaji na uwezeshaji wanawake na vijana kiuchumi na kujinfunza jinsi wananchi walivyofanikiwa kuleta maendeleo kwa kushirikiana

na viongozi ikiwepo kupambana na ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji.

Diwani wa Kata ya Ijombe wilayani Mbeya Mhe. Stimar Hepa John alisema kwamba wakati umefika kwa wananchi wengi kutambua shughuli za TGNP Mtandao, akiongezea, “Naona kwamba TGNP Mtandao ina jukumu kubwa nchini Tanzania na hivyo inastahili kuwa kila mahali kuwasaidia watanzania kujiimarisha katika nyanja zote.”

Miongoni mwa maazimio yaliyotolewa na Madiwani hao kwa Halmashauri zao kufanyia kazi ni pamoja na namna ya kusimamia Mfuko wa Maendeleo wa wanawake na kutekeleza dhana ya viwanda.

Kwa mujibu wa Ofisa Programu uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deo Temba mambo mengine waliyokubaliana ni kushawishi na kufuatilia ongezeko kila zahanati na vifaa vya kujifungulia na kuhimiza uwekaji wa mikakati ya kupambana na ukatili wa jinsia na kuunda kamati za ulinzi za mtoto.

TGNP Mtandao ni asasi ya kiraia inayo fanya kazi na wanajamii kwa kipindi cha Zaidi ya miaka 25 kwa kushirikiana na mashirika mengine yasiyokua ya kiserikali, jamii, taasisi za serikali, Wizara, Halmashauri na Kamati za Bunge za kisekta kwa ajili ya majadiliano, mashauriano na mafunzo ya namna ya kuboresha huduma za jamii kama afya, maji na elimu kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

JANUARI- MACHI, 2018 | 15

Page 16: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

Jasmin Ramadhan (15), Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mungaa na mwanachama wa klabu ya “Sauti za Wanafunzi” akitoa hoja yake wakati wa mdahalo juu ya ukeketaji

Hivi ndivyo wanafunzi wanavyoshiriki katika kutatua changamoto za ndoa za utotoni na ukeketaji.

Na Mwandishi Wetu

“Nakumbuka binamu yangu alifariki kutokana na kutokwa na damu nyingi sana baada ya kukeketwa wiki tatu tu baada ya kuzaliwa. Nilighazibika sana kutoka na hilo, Ni lazima sasa nihakikishe jamii inaachana na vitendo hivi vya kinyama”

Vijana ni tunu ya thamani kwa nchi na kuwekeza kwa vijana kutaleta mabadiliko makubwa ya kijamii na kiuchumi katika nchi. Hata hivyo, kundi hili linakabiliwa na changamoto zikiwemo ukatili na uhalifu, kukosa ajira, na magonjwa yakuambikiza kama UKIMWI, ambazo zinasababisha vijana kukosa haki zao na mwishowe kuigharimu jamii kiuchumi. Kuiwezesha jamii kwa kutoa elimu

ni njia mojawapo muhimu katika kutokomeza ndoa za utotoni na vitendo vya ukeketaji. Vijana wakike na wakiume wakielewa juu ya haki za binadamu na pia kujua stadi za maisha wanaweza kukabiliana na athari za mila potofu na vitendo vya kikatili wanavyoweza kufanyiwa.

Kwa sababu hiyo shirika la Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF)-linalofanya kazi mkoani

Singida lilitambua kuwa kupitia mijadala ya kijamii juu ya madhara na ndoa za utotoni na ukeketaji kiafya, kiuchumi na ukiukwaji wa haki za binadamu inasaidia watu wengi kuanchana na mila hizo potofu.

Mkoa wa Singida ni moja ya mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotoni na ukeketaji nchini. Kupitia mradi unaosimamiwa na SPRF’s Aware Project, klabu zinazojulikana kama

16 | ULINGO WA JINSIA16 | ULINGO WA JINSIA

Page 17: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

“Tuliona umuhimu wa kuwashirikisha shule ya sekondari

Makiungu maarifa na elimu tuliyo nayo ili kuweza kuungana nao katika kuielemisha jamii. Ijapokuwa tulilazimika kutembea umbali wa kilometa 2.5 kufika shuleni hapo, ilikuwa ni jambo la busara kufanya.

Sauti za Wanafunzi zilianzishwa katika shule nne katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida. Moja ya shule inayofanya vizuri katika kutekeleza mradi huo ni Shule ya Sekondari Mungaa.

“Tumehamasika sana baada ya kuanzishwa kwa klabu hii shuleni kwetu, tumejifunza juu ya masuala ya ndoa za utotoni na ukeketaji na athari zake na tupo tayari kuelimisha wanafunzi na jamii yetu juu ya masuala haya”. Anasema Joseph Damian (18), mwenyekiti wa klabu hiyo

“Tumeweza kufanya midahalo na majadiliano kuhusu ndoa za utotoni na ukeketaji. Kwa pamoja tumeweza kuainisha visababishi na kutoa suluhisho la kuweza kuondokana na mila hizo potofu.” Anaongezea Joseph kwa ujasiri Licha ya kuwa klabu haikuwa na muda mrefu toka ianzishwe, imefanikiwa kufanya baadhi ya shughuli ikiwemo midahalo shuleni hapo ambapo zaidi ya wanafunzi 300 walishiriki na pia kufanya mdahalo na shule za jirani ikiwemo shule ya sekondari Makiungu.

“Tuliona umuhimu wa kuwashirikisha shule ya sekondari Makiungu maarifa na elimu tuliyo nayo ili kuweza kuungana nao katika kuielemisha jamii. Ijapokuwa tulilazimika kutembea umbali wa kilometa 2.5 kufika shuleni hapo, ilikuwa ni jambo la busara kufanya.” Anaelezea Jasmin Ramadhan (15), mwanachama wa klabu hiyo Wanafunzi hawa hawatoi elimu hiyo kwa wanafunzi wenzao tu bali hata kwa familia zao na jamii inayowazunguka. Natalia Michael (18) mwanachama

mwingine wa klabu hiyo anasema “Nakumbuka binamu yangu alifariki kutokana na kutokwa na damu nyingi sana baada ya kukeketwa wiki tatu tu baada ya kuzaliwa. Nilighadhibika sana kutoka na hilo, Ni lazima sasa ni sasa nihakikishe jamii inaachana na vitendo hivi vya kinyama”.

“Nilizingumza na bibi yangu na baadhi ya bibi wengine kuhusu ukeketaji na madhara yake, lakini ilikuwa ngumu sana kuwashawishi kwani hawakuweza kukubaliana na mimi kirahisi kuwa ukeketaji unaweza kusababisha kifo. Na hii ni kwa sababu wana uzoefu na hawakufariki kutokana na ukeketaji.” anaelezea mwanafunzi mwingine, Timothy Francis

Kulingana na maelezo ya Mwenyekiti wa klabu, Joseph Damian, Klabu hiyo ina mipango ya kufikia shule nyingi zaidi na pia kuwafikia wanawake na watoto wa kike wenye mimba ili kuwaelimisha madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike, lengo likiwa ni kuona ukeketaji unatokomea mkoani Singida.

“Tunajua kuwa siku hizi ukeketaji unafanywa kwa vichanga na hivyo, tunatambua kuwa kama hii elimu itawafikia wanawake wenye mimba itahamasisha wanawake hao kuwalinda watoto wao pindi wanapozaliwa. Na hivyo, bado tunaweka mikakati ya namna gani tunaweza kuwafikia na kutoa elimu kwao kwani tunakabiliwa na changamoto ya usafiri kutokana na jamii yetu ina eneo kubwa sana kufikika bila usafiri.” Anafafanua Joseph

JANUARI- MACHI, 2018 | 17

Page 18: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

TGNP Mtandao imezindua kampeni yake ya ‘MPE MABAWA’ yenye lengo la kuhakikisha mtoto wa kike anafurahia maisha yake shuleni kwa kupata taulo za kike bure.

Akizungumza katika Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS), Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa Nguvu za Pamoja wa TGNP, Grace Kisetu alisema kampeni hiyo ina dhumuni la kumuwekea mtoto wa kike mazingira salama yatakayomuwezesha kufanya vizuri kwenye masomo pindi awapo shuleni.

“Kupitia kampeni hii ya Mpe Mabawa, tunalenga kuvunja ukimya kwa kuhakikisha kuwa suala la hedhi linoangelewa kwa uwazi, pia, kuboresha mazingira ya shule kwa kuhakikisha upatikanaji wa matundu ya vyoo ya kutosha, maji yakutosha, taulo za kujihifadhi watoto wa kike, vyumba vya

kujisitiria pamoja na waalimu walezi.” Alifafanua Bi. Grace akisisitiza, “suluhu ya kudumu ni utengwaji wa bajeti za kutosha kuhakikisha upatikanaji wa taulo, ambapo tunafanya uchechemuzi kuhakikisha bajeti yenye mrengo wa kijinsia. Tayari tumeshaanza katika ngazi ya halmashauri pamoja na wadau wengine kama wabunge.”

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalumu CHADEMA Mhe. Upendo Peneza alisema ili kufanikisha lengo hilo, kuna hitajika nguvu ya pamoja baina ya wadau kwani bila kufanya hivyo, itakuwa ni kupoteza nguvu.

Mhe. Peneza aliendelea kusema kuwa serikali ikikubali kuongeza kiasi cha shilingi 5000 katika fedha inazopeleka shuleni kwa ajili ya elimu bure, pedi bure kwa wanafunzi wa kike kuanzia darasa la tano mpaka kidato cha nne

zinaweza kupatikana.

“Jumla ya wanafunzi wasichana ambao wanahitaji taulo za kike ni kuanzia darasa la tano mpaka kidato cha nne, kama serikali itaongeza shilingi 5000 kwenye fedha za ruzuku (capitation grants) inaweza kumaliza tatizo hilo”. Mhe. Peneza alisisitiza akiongeza “Mpaka sasa tumeshapata mafanikio kupitia hoja hii, suala hili limeingizwa kwenye mapendekezo ya kamati ya bunge la mwaka na ikipitishwa itakuwa ni azimio la bunge”.

Kwa upande wake mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya secondary mabibo, alisema kuwa amefurahishwa sana na kuanzishwa kwa hizo kampeni kwani zitasaidia sana kuhakikisha watoto wa kike wanahudhuria vema masomo yao hata wakiwa katika siku zao.

“Shuleni wanafunzi wengi wa kike wanaomba ruhusa wakipata hedhi wakiwa shuleni aidha kwa sababu ya kukosekana kwa taulo za kijihifadhi, au kukosekana kwa dawa za kutuliza maumivu ya tumbo. Ushiriki wa wanawake katika uongozi hautoweza patikana kama watoto wa kike hawataweza kuhudhuria masomo kikamilifu.” Alifafanua mwanafunzi huyo.

Mwisho washiriki walitoa mapendekezo mbalimbali ikiwemo kuhakikisha kuwa fedha zinazopelekwa shuleni zinaandikwa kabisa kuwa ni kwa ajili ya taulo za hedhi, na pia, kutumia fursa ya uchaguzi unaokuja kuhakikisha wagombea wanalibeba suala hilo kama moja ya agenda zao za kampeni.

Mbunge wa viti Maalumu, Mhe. Upendo Peneza akiwasilisha mikakati yake upatikanaji wa taulo za kike mashuleni kwa washiriki wa Semina za Jinsia na Maendeleo zifanyikazo katika ofisini za TGNP Mtandao.

Kampeni ya “Mpe Mabawa”: Hii ndio namna ya kumsaidia mtoto wa kike akiwa hedhini Na. Hellen Urio, TGNP

18 | ULINGO WA JINSIA

Page 19: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

KUTANA NA SPIKA WA KWANZA MWANAMKE TANZANIA

MHE. ANNA MAKINDA

Je unajua Tanzania ilichukua miongo

mingapi tangu uhuru kuwa na Spika

mwanamke wa kwanza? Na spika huyo ni

nani?

Je unajua ilimchukua miaka kumi

bungeni kuweza kuwania nafasi ya

uspika?

Je unajua pamoja na kuwa mzoefu,

katika shughuli za bunge, bado kuna

walodai kwamba amepewa? Amebebwa?

Hata hivyo mama huyu hakuterereka

aliliongoza Bunge kwa makini

akizingatia kanuni na kutumia busara

kubwa kusimamia mhe. e. imili huu

muhimu wa serikali

Huyu siyo mwingine ni Mhe. e.

e. Anna Makinda, Spika wa kwanza

mwanake kuliongoza Bunge la Jamhe.

e. uri ya Muungano wa Tanzania

Ebu tudodose kwa ufupi safari ya huyu shujaa mwanamke aliyekuwa na uthubutu wa kuwania kiti hiki kilichokuwa kimehodhiwa na wanaume tangu tupate uhuru mwaka 1961 hadi mwaka 2010. Mhe. Anna Makinda.

Maisha ya utotoAnna Makinda alizaliwa Julai 26 mwaka 1949 mkoani Njombe zamani ikiwa sehemu ya mkoa wa Iringa akiwa mtoto wa nne kati ya watoto watano wa familia ya mzee Japhet Wilson Makinda na mama Emelia Tulaleka Samunyuha. Baba na babu mzaa baba walikuwa wasomi na watu wenye kujiweza kiuchumi.

Je kisomo cha wazazi na uwezo wa kiuchumi kiliinufaishaje familia ya Anna? Kuna usemi usemao: Ukimsomesha mwanamke utasomesha familia nzima, lakini ukimsomesha mwanaume, umemsomesha mtu mmoja. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa familia hii ya Anna Makinda. Baba yake Anna Makinda alikuwa msomi aliyebobea katika masomo ya sheria na alisoma chuo cha Edinburgh kilichopo nchini Uingereza. Baadaye akashika nyadhifa mbalimbali wakati wa ukoloni na baada ya uhuru, ikiwa ni pamoja na kufundisha sheria, ukuu wa wilaya, afisa tawala, na hatimaye mkuu wa mkoa. Babu yake Anna naye alikuwa msomi mwanasheria na mfanya biashara. Elimu ya baba na vyeo vyake vyote havikuwa wezeshi kwa Anna wala ndugu zake walozaliwa nao.

Kulikoni?Baba mzazi aliamua kuoa wake wengine wawili, hivyo akawa na wake watatu. Mama mzazi wa Anna aliyekuwa mke wa kwanza akatekelezwa akalazimika kuishi maisha duni. Wakati alipoteuliwa kuwa mkuu wa mkoa, baba yake Anna alimrudisha mama yake kijijini Lupembe

JANUARI- MACHI, 2018 | 19

Page 20: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

alikolazimika kufanya kazi nyingi ili kuikimu maisha ya familia yake. Mhe. Anna anakiri” Mama alilima, alipika pombe na kufanya biashara ndogo ndogo ili aweze kutupatia mahitaji ya lazima”. Manyanyaso aliyoyapata mama, anakiri Mhe. Anna yalikuwa kichocheo kikubwa kilchomfanya yeye asome kwa bidii ili amkomboe mama yake katika mateso makubwa aliyokuwa akiyapata alipokuwa akiwalea.

Maisha ya shule: masomo, michezo na uongoziAnna Makinda aliweza kuunganisha masomo, michezo na uongozi katika maisha yake yote ya shule ya msingi, sekondari, na hata chuo kikuu. Akiwa shule ya kati (Middle School) ya Peramiho alipenda hisabati, alishiriki kwenye michezo hasa mpira wa kikapu, na mbio. Nyota yake ya uongozi ilianza hapa kwani alichaguliwa kuwa kiranja mkuu wa shule hiyo. Alipochaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya wasichana ya Masasi enzi hizo ikijulikana kama Salvatory College, aliamua kushiriki kwenye masuala ya siasa kwa kujiunga naChama cha TANU na kuchaguliwa mwenyekiti wa Tawi la Vijana wa TANU shuleni hapo. Hatimaye, alipochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita shule ya Marian College inayojulikana sasa hivi kama Kilakala, alichaguliwa kuwa Raisi wa serikali ya wanafunzi na mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa TANU. Akiwa rais wa serikali ya wanafunzi, alibuni mfumo wa uongozi unaofanana na uongozi wa kitaifa, akiwa na rais, waziri mkuu, na mawaziri.

Anna aliwezaje kumudu masomo, michezo, siasa na uongozi?Siri ya kuweza kuwa na uwiano sawia katika majukumu mengi ni moja tu! “Kupanga matumizi ya Muda” Anakiri Mhe. Anna makinda. Mpango wa matumizi ya muda ni changamoto kubwa kwa watanzania wengi. Ni wachache

sana tunatamuba kwamba muda ni rasilimali ambayo ikishatumiwa haiwezi kurejeshwa. Mpangilio mzuri wa muda ulimwezesha Mhe. Anna Makinda aweze kumudu majukumu mengi tangu akiwa mtoto, akimsaidia mama yake kwenye majukumu ya nyumbani, akisoma huku akipewa majukumu ya uongozi, pamoja na kushiriki katika michezo.

Shughuli hizi zilimjengea, kujiamini, kupenda kazi na ukakamavu. Vyote hivi vilizidi kuimarishwa pale ambapo alijiunga na jeshi la kujenga taifa baada ya kuhitimu kidato cha sita. Jeshi lilimjengea nidhamu ya dhati siyo ya woga, ukakamavu, uthubutu, na nidhamu ya kazi. Vilevile, vilimwezesha kutambua kwamba tofauti za jinsia zimeumbwa kwani mambo mengi aliyozania ni magumu aliyamudu.

Maisha ya chuo cha uhasibu

Baada ya kuhitimu masomo ya sekondari na mafunzo ya jeshi, Anna alichaguliwa kujiunga na masomo ya uhasibu kwenye Taasisi ya Maendeleo ya Mzumbe (IDM) kwa sasa inajulikana kama Chuo Kikuu Cha Mzumbe akisoma uhasibu lakini akajikita kwenye masomo ya ukaguzi. Kozi hii ilikuwa mpya ikijulikana kama Certified Public Accountancy na waliisoma kwa miaka minne. Masomo ya uhasibu yalihitaji msingi mzuri wa masomo

ya hisabati. Mfumo wa elimu wakati ule haukuwezesha watoto wengi wa kike wapende hisabati, hivyo ni wasichana wachache sana waliweza kumudu masomo ya hisabati. Katika darasa la wanafunzi 58, walikuwa wanafunzi wa kike wawili tu kwenye kozi hii.

Licha ya kuwa wanawake wachache, bado Anna alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana, na mjumbe kwenye Bodo ya IDM. Hakika, kipaji chake cha uongozi kilionekana popote alipokuwa katika maisha yake yote ya masomo. Mwaka 1975 alijiunga na chuo cha fedha (IFM) kwa mwaka mmoja akichukua kozi ya awali ya CPA. Akiwa kati ya waanzilishi wa kozi hii, na hatimaye wakaunda bodi ya taifa ya uhasibu (National Board of Accountancy) Kozi hii ilimwezesha kuwa kati ya wahasibu wachache walioidhinishwa.

Maisha ya kazi na maaumzi ya kuingia siasa Baada ya kuhitimu stashahada ya uhasibu mwaka 1975, Anna Makinda aliajiriwa na shirika la ukaguzi Tanzania (TAC) akiwa kwenye uangalizi lakini baadaye alipata mkataba wa kudumu. Baada ya kuthibitishwa aliamua kuacha ajira rasmi na kujitosa kwenye kinyanganyiro cha siasa. Uamuzi huu uliwashangaza wahasibu wenzake. Kwanza hawakuona kabisa uhusiano ulokuweko kati ya fani ya uhasibu na siasa. Vile vile, walimshangaa Anna kuchagua ubunge wenye mshahara kidogo sana na kuacha uhasibu uliokuwa na mshahara mnono. Hata hivyo, huu ulikuwa uelewa finyu wa kazi za ubunge. Masomo ya uhasibu na ukaguzi pamoja na safari yake yote ya shule na chuo, yalimjengea Mhe. Anna Makinda msingi mzuri wa maisha yake ya siasa na wadhifa mbalimbali aliyozifanya hadi kufikia ngazi ya uspika. Vile vile, Anna hakuingia siasa kwa tama ya fedha, yeye alikuwa na maono, ya utetezi,

20 | ULINGO WA JINSIA

Page 21: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

uwakilishi na huduma.

Kazi za mbunge na ujuzi wa mahesabuBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni muhimili mmojawapo wa utawala ambao kazi kubwa ni pamoja na kutunga sheria, kusimamia matumizi ya mapato ya taifa pamoja na kuidhinisha bajeti ya serikali. Kimantiki, mbunge mwenye ujuzi wa mahesabu na utaalam wa ukaguzi wa matumizi ya fedha, ni hazina kubwa katika shughuli ya kuisimamia serikali kwenye kutumia fedha za walipa kodi wake. Kisomo chake na fani ya uhasibu vimechangia sana katika kumkuza kisiasa na kmwezesha kufanya kazi za siasa na uongozi kwa uledi mkubwa. Mhe. Anna aliingia Bungeni kwa mara ya kwanza, akiwa na umri wa miaka 23 tu, ilimchukua miezi sita kabla hajachangia chochote bungeni. Alikuwa akisoma Hansard, akasoma kanauni za bunge, ili aweze kuelewa majukumu yake, mipaka yake na kanuni za bunge. Msomi yoyote mahiri, hatoi hoja bila utafiti.

Mjumbe wa kamati za bunge Mhe. Anna makinda anaamini kwamba fani ya uhasibu na ukaguzi wa fedha ulimwezesha kushiriki kwa makini katika kamati zote alizowahi kuchaguliwa na hasa hasa kamati ya mahesabu (accounts committee) Kamati yake ilihusika kwenye kufanya uchunguzi wa kina kwenye ubadhilifu na hujuma ya sukari. Mhe. Anna anakiri kwamba alichangia vizuri katika uchunguzi wa awali na hatimaye kuandika ripoti iliyoonesha mapungufu ya kiuutendaji na kiusimamizi kwa watendaji. Kutokana na uchunguzi huu baadhi ya viongozi ikiwa ni pamoja na waziri husika waliwajibishwa kwa kulazimishwa kujiuzulu. Vilevile, kutokana na ripoti hii, kulionekana umuhimu wa mwanasheria mkuu wa serikali kushiriki bungeni.

Hata hivyo, kutokana na msimamo wake mkali kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma alijijengea maadui wengi ikiwa ni pamoja na wanachama wenzake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Jambo ambalo halikumkatisha tamaa, wala kumpa woga. Badala yake kumjengea imani kwa viongozi wake hususani maraisi wa awamu zote nne walimpa nyadhifa mbalimbali za uwaziri katika wizara mbalimbali, na ukuu wa mkoa, kuteuliwa kwenye bodi mbalimbali na hatimaye kujenga imani na wabunge waliomchagua kuwa spika mwanamke wa kwanza.

UwaziriMhe. Anna Makinda alikuwa waziri katika awamu zote tatu chini ya Mwl. Julius Nyerere, Mhe. Al Hasan Mwinyi, Mhe. Benjamin Mkapa na Mhe. Jakaya Kikwete. Mhe. Anna aliingia Bungeni akiwa na miaka 23 na akanza kupewa wadhifa wa uwaziri akiwa na miaka 33. Wakati wa uongozi wa rais Mwl. Julius Nyerere, Mhe. Makinda alichaguliwa kuwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu akiwa anasimamaia masuala ya sera na udhibiti wa majanga chini ya waziri mkuu marehemu Sokoine. Katika serikali ya awamu ya Pili ya rais Ally Hassan Mwinyi, aliteuliwa kuwa waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na watoto, wizara aliyoiongoza hadi mwaka 1995. Akiwa waziri katika wizara hiyo, ni waziri pekee aliyefanikiwa kuunda bunge la watoto Tanzania akiwashirikisha watoto wawili wawili kutoka kila mkoa na kuwafundisha habari za bunge hasa kutetea haki za watoto. Ukuu wa mkoaBaada ya uchaguzi wa mwaka 1995-2000, Mhe.Makinda kwa mara nyingine alishinda ubunge kupitia jimbo la Njombe kusini. Hata hivyo, aliyekuwa rais waserikali ya awamu ya tatu Mhe. Benjamini Mkapa alimteua Mhe. Anna kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma. Mhe. Makinda

akiwa na kofia mbili yaani ya ubunge na ukuu wa mkoa aliweza kuzifanya kazi zote kwa ufasihi mkubwa licha ya changamoto mbalimbali alizokutana nazo katika kazi.

Nafasi za uongozi nje ya nchiMhe. Makinda ni moja ya wanawake walioaminika na nchi mbalimbali duniani kutokana na utendaji na ufanisi wao katika kazi. kwa mfano, alipokuwa waziri wa Maendeleo, wanawake na watoto alichaguliwa kuwa rais wa bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Watoto Duniani (UNICEF) nafasi iliyomwezesha kutembelea nchi nyingi duniani katika utetezi wa watoto. Vilevile, aliwahi kuchaguliwa kuongoza ukwaa la wabunge wa SADC (SADC Parliamentary Forum). Pia, alifanya kazi na Pan African News Agency kama katibu na baadaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa PANA. Shughuli za kikanda na za Kimataifa ziliongezea upeo wake wa kutambua muktadha unaokabili wanyonge na hususani watoto na wanawake.

Nafasi ya unaibu spika wa bunge la TanzaniaBaada ya uchaguzi wa mwaka 2005, Mhe. Makinda alishinda kwa mara nyingine tena ubunge kupitia jimbo la Njombe Kusini na pia, aligombea nafasi ya unaibu spika. Kutokana na uzoefu wake na utendaji wake mzuri katika masuala ya bunge, akiwashinda wagombea wengine aliweza kuchaguliwa kuwa naibu wa spika wa bunge la Tanzania, wakati marehemu mzee Samuel Sitta alichaguliwa kuwa Spika. Akiwa naibu spika aliweza kuisimamia serikali katika masula mbalimbali yakiwemo ya Escrow, Richmond yaliyosababisha mawaziri wengi kuachia ngazi ikiwemo kuvunjwa kwa baraza la mawaziri. Pia Mhe. Makinda alimshauri Spika kuhusu kutenganisha muhimili wa bunge na serikali na kusimamia kanuni na taratibu za bunge kwa umakini.

JANUARI- MACHI, 2018 | 21

Page 22: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

Uzoefu alioupata kama naibu Spika ulimpa uthubuti wa kuwania kiti cha uspika.

SPIKA WA KWANZA MWANAMKE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Makinda aliamua kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya spika wa bunge la Tanzania mwaka 2010. Katika kinyang’anyiro hicho alikuwa na wagombea wengine wanaume akiwemo aliyekuwa spika wa wakati ule Mhe. Samwel Sita na mwingine kutoka upinzani Mwanasheria Mabere Marando. Baaada ya uchaguzi na matokeo kutoka, Mhe. Makinda aliweza kuvunja rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza spika wa bunge la Tanzania katika bunge la kumi kwa kupata kura 265 dhidi ya Marando aliyepata kura 53 na kura 9 ziliharibika. Kwa hiyo, mwaka 2010 Mhe. Anna Makinda akawa spika wa kwanza mwanamke katika historia ya Bunge na Tanzania. Japo safari yake ilikuwa na changamoto nyingi bado aliweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kujiamini na aweza kukubalika kitaifa na kimataifa.

Ni nini kilichomwezesha Anna Makinda kushinda?

Sikiliza Sauti Za Wabunge Wenzake.

Ushindi wa Mhe. Makinda

Mhe. Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa mjini, alisema yeye anaona alibebwa kutokana na mkataba wa SADC ambao ulikuwa unataka usawa wa jinsia wa 50 kwa 50.

Mhe. Cecilia Pareso, Mbunge wa viti maalumu kutoka Chama cha Demockasia na Maendeleo (CHADEMA) alisema kuwa ushindi wa Mhe. Anna ulitokana na uzoefu wake wa muda mrefu bungeni.

Mhe.Maulid Mtulia, Mbunge wa Kinondoni- Dar es salaam kupitia CUF aliorodhesha sababu kuu tatu: “Kwanza, Mhe. Anna Makinda ni mbunge aliyelitumikia bunge kwa muda mrefu tangu Tanzania ikiwa chini ya chama kimoja mpaka tunaingia kwenye mfumo wa vyama vingi. Pili, Mhe. Anna aligombea wakati ambapo kulikuwa na vuguvugu la usawa wa kijinsia duniani na tatu, Mhe. Anna alikuwa na vigezo vilivotosheleza sifa za uspika.

Mhe. January Makamba, mbunge wa Bumbuli- Tanga alisema kwamba huwezi kumlinganisha Mhe. Anna Makinda na mbunge yeyote maana yeye alipikwa kisiasa kwa sababu Mhe. Anna yeye aliingia bungeni toka akiwa na umri mdogo sana kuliko wabunge wengine. “Ni mama ninayemwona kuwa na ueledi kubwa kisiasa na kipaumbele chake ni kufanya kazi kwa bidii katika kila eneo alilopewa kulisimamia”.

Kazi za usipika

Wabunge wanasema nini kuhusu utendaji wake wa kazi?Mhe. Faustine Ndungulile, mbunge wa Kigamboni Dar es salam kupitia CCM alisema, “Mimi ninamwona Mhe. Makinda kama mama na mlezi wa wabunge wengi, mimi nikiwa mmojawapo. Tulipoingia bungeni alitufundisha mambo mengi ikiwa

ni pamoja na kanuni za bunge, jinsi ya kujenga hoja, kuvaa na kuishi kama wabunge. Aliongeza kuwa pamoja na changamoto alizokutana nazo bado mama Makinda alikuwa mvumilivu na mwenye upendo kwa wabunge wote; hakuwa na visasi. Haya yanathibitishwa na yeye mwenyewe aliposema, mimi sina uadui na mtu yeyote na kwamba nitafanya kazi na watu wote bila kujali itikadi za kisiasa.

Naye, Mhe. Pareso anasema kwamba tofauti ya Spika Makinda na wengine ni kwamba wakati wa mama Makinda adhabu kwa waheshimiwa wabunge waliokosea hazikuwa kubwa kama ilivyo sasa ambapo mbunge anaweza kupewa adhabu kubwa ya kufungiwa muda mrefu jambo ambalo ni kinyume cha kanuni za bunge. Anaongeza kuwa Mhe. Anna Makinda alikuwa mvumilivu na aliliongoza bunge kwa busara na si kama ilivyo sasa ambapo bungeni hakuna nidhamu.

Mhe. Halima Mdee Mbunge wa jimbo la Kawe- Dar es salaam kutoka CHADEMA alisema, mama Makinda alikuwa na uwezo mkubwa wakukidhi masuala yote ya kuwa spika, alikuwa akipenda watu, msikivu, muelewa na jasiri wa kuthubutu bila kusita. Aliendelea kusema kwamba akimfanansha na mtangulizi wake marehemu Samwel Sita, mama Makinda alijitahidi sana kufuata kanuni za bunge na alikuwa mvumilivu maana alipata changamoto ambapo wanaume wengi hawamkupokea vizuri na walisema asingeweza kuongoza bunge. “Kutoka kwake mimi binafsi nilijifunza kuwa kabla ya kusema jambo hakikisha umesoma kila kitu vizuri na kuelewa”. Pamoja na hayo Mhe. Mdee anaongeza kuwa mama Makinda alitetea sana chama cha wanawake wabunge na kutufundisha mengi.

Kwa upande wake Mhe. Suzan Lyimo, mbunge kutoka CHADEMA

22 | ULINGO WA JINSIA

Page 23: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

Mhe. Anna Makinda lipokabidhiwa tuzo na TGNP Mtandao kutambua mchango wake katika kuimarisha usawa wa kijinsia nchini kwa kuwa spika wa kwanza mwanamke Tanzania. Tuzo hii ilitolewa wakati wa tamasha la 14 Jinsia la mwaka 2017

Mafunzo yatokanayo na simulizi ya Mhe.Anna Makinda

Safari ya Mhe. Anna Makinda ni safari yenye mafunzo mengi kwa

wanaharakati watetezi wa haki za wanawake.

qFunzo la kwanza ni kuwa na ndoto na maono na kuyafanyia kazi.

Alitambua kipaji chake na akifanyia kazi ya kukikuza pindi fursa

ilipojitokeza tangu akiwa mtoto.

qKujiamini na uthubutu kulimwimarisha katika utendaji wake wa kazi.

qAliwatendea haki watu wote bila kujali itikadi, kama shuhuda

zilivyojieleza

qMhe. Anna hakukimbia changamoto, alitafuta njia ya kukabiliana nazo

qAliacha alama za kudumu kwa wale wote aliogusa maisha yao kwa kufanya

na kutetea, pamoja na kuwafundisha wenzanke kile alichokijua, na

kukiamini.

alisema mama Makinda alikuwa mama jasiri, mzoefu aliyejiamini na kuzijua vizuri kanuni za bunge ambapo uzoefu wake wa uongozi katika nyadhifa mbalimbali ulimsaidia kulifanya bunge kuwa moja kwa kutenda haki. Anaongezea kuwa unyenyekevu na upendo wa mama Makinda, uvumilivu na kuishi kwake kama mama /mlezi kulimsaidia sana. “Nawashauri wabunge wengine wanawake tumuige mama Anna Makinda kwa kuwa na nidhamu, upendo, unyenyekevu, kupenda kusoma kwa bidii ili kuacha alama kama yake”.

Kwa upande wa Mhe. Zitto Kabwe (ACT) alisema “Mimi nimejifunza mengi wakati nilipoingia bungeni chini ya uongozi wa Mama Makinda kama kuwa na taarifa kamili na yenye uthibtisho kabla ya kuongea bungeni. Hili nilijifunza kwa Mama Makinda kwa vile ujuzi wake ulimpelekea kujua miongozo yote ya Bunge na hakuteteleka kwenye maamuzi yake. Aliona pia kuwa mwanamke kulimpelekea kufanya kazi za jitihada na umakini maana kila wakati alikuwa anaonekana kwa jicho la mwanamke na sio Spika. Kwa ujumla alifanya kazi

nzuri na watu wote hasa wabunge wanajua hilo.”

Mhe. Tundi Lissu, mbunge wa Singida kupitia CHADEMA anasema “Mimi nilimfurahia sana Mhe. Anna Makinda maana alikuwa kila mara akinikumbusha enzi zangu za harakati na TGNP. Nilipenda majadiliano na mazungumzo na Mhe.Spika wakati mwingi tukiwa tunajibishana bungeni na baadaye kukutana baada ya bunge na kuongea pembeni. Nilipata funzo zuri sana la kujua kuvumilia na kuongea pale inapotakiwa. Nilijifunza pia kuwa chochote unachotaka lazima ukifanyie kazi maana niliona mama Makinda alipenda kuwa mbunge, akafanya bidii na kukaa bungeni kwa zaidi ya miaka 25 hadi akafikia kuwa Spika. Hili ni jambo la kuigwa na linatoa changamoto kwangu mimi binafsi ili niweze kufikia malengo yangu.”

Mhe. Maryam Msabaha mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA alisema “Mama Makinda amesaidia sana wabunge wanawake kwa kuwafunda kila wakati jinsi ya kuishi na kufanya kile kilicho waleta bungeni na wajiepushe kulaghaiwa na wanaume wenzao wenye nia ya kuwatumia na hatimaye kuwadharau na kuwadhailisha”.

JANUARI- MACHI, 2018 | 23

Page 24: YALIYOMO - TGNP · Ulingo wa Jinsia ni Jarida linalomilikiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Jarida hili linawakilisha sauti za wanaharakati kuhusu Maendeleo, uchumi, haki na

S.L.P 8921, Dar es Salaam,Simu: 022 2443025Tovuti: www.tgnp.org

Tgnpmtandao

24 | ULINGO WA JINSIA24 | ULINGO WA JINSIA