64
Mimi ni Mwislamu Authorship Muhammed Ashraf Salah :

Iam muslim sawhilil

Embed Size (px)

Citation preview

Mimi ni

Mwislamu

Authorship

Muhammed Ashraf Salah

������� ���� � ������ : �� ��������� � ������ ����� �!� "#� $ �%�������&�����'

Mimi ni Mwislamu

Mimi ni Mwislamu

Kwa jina la Mungu wa RehemaKwa jina la Mungu wa RehemaKwa jina la Mungu wa RehemaKwa jina la Mungu wa Rehema

(�h�g�f�e�d�c� �b�a� �̀_�h�g�f�e�d�c� �b�a� �̀_�h�g�f�e�d�c� �b�a� �̀_�h�g�f�e�d�c� �b�a� �̀_

k�j�ik�j�ik�j�ik�j�i ) * +�,�- ./ :012

Na mtu anataka dini nyingine zaidi ya

Uislamu wala kukubali kuwa wakati ni

mmoja wa wenye kukhasiri Akhera

Al-Imran: 85

Mimi ni Mwislamu

Copyright, distribution and translation are

reserved for every Muslim

Legal Deposit No. 22274 / 2008

International Serial 977-6157-64-5

For charitable distribution call:

0020101459613

For suggestions e-mail:

[email protected]

WWW.Iam-Muslim.com

Mimi ni Mwislamu

(1) KUMWAMINI MWENYEZI MUNGU

Mimi ni Mwislamu…

• Ninamwamini Mwenyezi Mungu Pekee Asiye na mshirika na hakuna mola mwingine isipokuwa Yeye, Hakuzaa wala Hakuzaliwa, na hakuna kamwe kifano chake.

• Ameumba mbingu na ardhi, Naye Ndiye Anayezimiliki. Anayajua yaliyofichikana na yenye kuonekana. Yu Hai na Hafi, Anayasimamia mambo yote milele na Halali.

• Ana Majina Mazuri Kabisa na Sifa za Juu. Kati yake ni Majina tisini na tisa, mwenye kuyajua na kuyadhibiti vyema na akamwomba Mwenyezi Mungu Kwayo, ataingia peponi.

• Kati yake ni Sifa za Upweke, kwani Yeye Subhaanahu wa Taalaa ni Mmoja wa Dhati, Sifa na Vitendo, Aliyepwekeka, Aliye Pekee, Mkusudiwa, Mmiliki wa ufalme.

Mimi ni Mwislamu

• Na Sifa za Utukufu, kwani Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye habari ya kila jambo, Mwelekezaji wa manufaa, Haki, wa Mwanzo, wa Mwisho, wa Dhahiri, wa Siri, Mrithi, Mwenye Kubakia, Mkwasi, Mtakasifu, Mwenye Kushuhudia, Aliye Karibu, Mbora wa Kupangilia, Mwadilifu, Nuru ya mbingu na ardhi, Mwenye Utukufu na Ukarimu.

• Na Sifa za Uadhama, kwani Yeye ni Mshindi Asiyeshindika, Mwenye Sifa zote Tukufu, Mwenye Uadhama, Mwenye Sifa za Utukuzo, Mwenye Kulazimisha, Mwenye Nguvu, Aliye Imara, Mteza nguvu, Mweza, Mwenye uwezo wa juu, Mwingi wa Kunusuru, Aliye Juu, Aliye Juu ya vyote.

• Na Sifa za Uwezo, kwani Yeye ni Mwingi wa Ujuzi, Mwenye Kusikia, Mwenye kuona, Yu Hai,

Mwenye Kukamata, Mwenye Kukunjua, Mwenye Kushusha, Mwenye Kupandisha, Mwenye Kutukuza, Mwenye Kudhalilisha, Mwenye Kutoa, Mwenye Kuzuia, Mwenye Kunufaisha,

Mimi ni Mwislamu

Mwenye Kudhuru, Mwenye Kuhuisha, Mwenye Kufisha, Mwenye Kutanguliza na Mwenye Kuchelewesha.

• Na Sifa za Uumbaji, kwani Yeye ni Muumbaji, Msanifu wa Maumbile, Mtiaji Sura, Hakimpiti au Kumshinda kitu, Mbunifu, Mwenye Kuanzisha, Mwenye Kurejesha, Mwenye Kufufua, Mwenye Kukusanya, Mpaji Mkuu, Mfunguzi wa kila jambo, Mwingi wa Kuruzuku, Mwenye Kutajirisha, Mdhibiti wa idadi, Mwenye Kudhibiti mambo, Mwenye Kuhifadhi, Mlinzi na Muumbaji wa mbingu na ardhi bila ruwaza.

• Sifa za Rehma, kwani Yeye ni Mwingi wa Rehma, Mwingi wa Kurehemu, Mwingi wa Huruma, Mwenye Kuneemesha neema nzuri, Mwingi wa Penzi, Mtenda Wema, Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kusamehe, Mwingi wa Kukubali toba, Mwenye Amani, Mtoaji amani na imani, Mpole, Mwenye Kulipa vyema, Mkarimu, Mwenye Kuneemesha, Mwingi wa Kutoa, Mwenye Kusaidia, Mwenye Kujibu,

Mimi ni Mwislamu

Mkunjufu, Mwingi wa subira, Mvumilivu kwa Waja Wake, Latifu, Wakili, Mwenye Kutoa Misaada, Mwenye Kuombwa msaada na Mwenye Kukubali toba.

• Amemneemesha mwanadamu neema nyingi zisizo na hesabu. Na hakuna neema yoyote anayoneemeka nayo mja ila hutoka kwa Mwenyezi Mungu Pekee, kwani Yeye Ndiye Aliyemuumba na Akampa uhai, Akamfanya asikie na aone, Akamkirimu, kisha Akamruzuku na Akamfanyia wema.

• Kwa ajili hiyo, ni lazima mja amwabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake – nako ni kufuata amri Yake na kuacha makatazo Yake – kwa kuwa hastahiki yeyote kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke Yake.

• Vile vile, bila shaka Mwenyezi Mungu Anazijua hali zote za mja kati ya utiifu

Mimi ni Mwislamu

na uasi. Hivyo basi, ni wajibu moyo wa mja ujae haiba kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, utukuzo na mapenzi, na aone haya kumwasi na aachane na maasi, kwani Mwenyezi Mungu Humwona wakati akiyafanya.

• Anafurahi kwa amali zake njema zinazomkurubisha kwenye radhi za Muumbaji wake Subhaanahuu wa Taala. Hivyo huzidi kufanya amali hizo hadi kufikia ngazi ya ihsani, kwani imani huzidi kwa matendo mema na hupungua kwa maasi.

• Asivutike kwenye matamanio, hawaa au bid'a, bali avutike kwa Mwenyezi Mungu Pekee huku akifuata maamrisho ya Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam. Asitafute kwa amali yake starehe ndogo ya dunia bali atafute kwayo malipo toka kwa Mwenyezi Mungu tu.

• Aidha, hakika Mwenyezi Mungu Ana huruma mno kwa mwanadamu kuliko huruma ya mama kwa mwanaye. Na rehma Yake imekienea kila kitu.

Mimi ni Mwislamu

Hivyo basi, ni wajibu kwa mja amwombe na anyenyekee Kwake katika haja zake za kidunia na za kiakhera, na wala asimwombe yeyote mwingine.

• Kwa vile hakuna faida yoyote ya kumwomba asiye Mwenyezi Mungu, kwa kuwa hamiliki uwezo ulio kamili isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hakuna asikiaye ya siri na minong'ono ila Mwenyezi Mungu, na hakuna anayemiliki makadirio isipokuwa Mwenyezi Mungu, basi kwa maana hiyo, hakuna wa kujibu dua isipokuwa Mwenyezi Mungu.

• Na kwa ajili hiyo, haijuzu kwa Mwislamu kuliomba kaburi, au kumwomba aliyezikwa humo vyovyote awavyo, kwa kuwa yeye hamsikii. Na kama hamsikii, basi ni vipi atamjibu au kumnufaisha? Hakika Mwenyezi Mungu Pekee Ndiye Mwenye Kunufaisha na Mwenye Kudhuru. Na kwa ajili hiyo, ni wajibu kwa Mwislamu asijenge msikiti juu ya makaburi, kwani Mtume Swalla

Mimi ni Mwislamu

Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam amelikataza hilo.

• Kadhalika, ni wajibu kwa mja alinganishe kati ya udhaifu wake na Nguvu za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kati ya umasikini wake na Utajiri wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kati ya ujinga wake na Elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kati ya unyonge wake na Utukufu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

• Na ajue kwamba utukufu ni wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waumini.

• Hivyo yampasa awe ni miongoni mwa Waumini hawa ambao hawatawakali isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu Pekee, wala hawaombi msaada isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, wala hawaombi kinga na kujilinda isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, wala hawaombi msaada wa dharura ila kwa Mwenyezi Mungu, wala hawamwogopi isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala hawataraji isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, wala

Mimi ni Mwislamu

hawamwombi isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala hawachinji isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wala hawaweki nadhiri isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wala hawaapi isipokuwa kwa Jina la Mwenyezi Mungu, wala hawaweki talasimu na hirizi (amali), wala hawasadiki wasemayo makuhani, watabiri (wanajimu) na wachawi, na wala hawawaendei.

• Na wao hawakosi rajua, na huwa na tahadhari ya mponyoko wa ndimi zao ili wasije kutelezea motoni. Hawasemi: "Amependa Mwenyezi Mungu na amependa fulani", "lau si Mwenyezi Mungu na wewe", "nimetawakali kwa Mwenyezi Mungu na kwako". Bali waseme: "Nimetawakali kwa Mwenyezi Mungu Pekee", "Amependa Mwenyezi Mungu kisha amependa fulani".

Maneno haya humsawazisha Mwenyezi Mungu na waja Wake, na ni katika shirki ndogo.

Mimi ni Mwislamu

• Na kama ilivyo wajibu kwetu kumwamini Mwenyezi Mungu, ni wajibu wetu vile vile tuwakatae mataghuti.

• Na kigogo wa mataghuti ni shetani na kila yule aliyeabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu naye akaridhia hilo.

• Na kati ya mataghuti hawa ni yule aliyetunga sheria zinazoharamisha Aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu, au kuhalalisha Aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu.

• Aidha, taghuti ni kila yule aliyelingania hilo, au akawaamuru watu hilo, au akahukumu kwa hilo, kwa vile ametaadi na akavuka mpaka wa kiumbe wa kusikia na kutii.

• Basi Allaah Pekee Ndiye Aliyewaumba wanadamu, na Ndiye Anayejua yanayowafaa, na kwa hivyo, hakuna yeyote awezaye kuwapangia sheria isipokuwa Yeye tu.

Mimi ni Mwislamu

(2) KUWAAMINI MALAIKA

• Ninaamini kuwepo malaika ambao Mwenyezi Mungu Amewaumba kutokana na nuru, na Akawafanya kuwa na mbawa mbili mbili, tatu tatu, na nne nne. Nao hawali, hawanywi, hawalali wala hawaoi. Amewaamuru kufanya kazi na kusimamia majukumu mbalimbali, nao hutekeleza hayo.

• Malaika siku zote humtii Mwenyezi Mungu bila kuchoka. Hawamwasi na humwogopa Mola wao toka juu yao. Kuna kati yao aliyesujudu toka siku Alipoziumba Mwenyezi Mungu mbingu na ardhi hadi siku ya Kiyama. Na atakaponyanyua kichwa chake atasema: "Subhaanak! Hatujakuabudu ukweli wa kukuabudu".

• Wao ni waja wa Mwenyezi Mungu na si wanawake, na wala si wasaidizi Wake, na wao watawaombea shifaa

Mimi ni Mwislamu

Waumini – kwa idhini ya Mwenyezi Mungu – siku ya Kiyama.

Kati ya malaika hawa, wapo:

• Walinzi ambao huwalinda viumbe na madhara.

• Watukufu waandishi ambao huandika matendo ya wanadamu, mema yao na mabaya yao.

• Wenye kumsabihi Mwenyezi Mungu. Hawa humsabihi Mwenyezi Mungu mchana na usiku na hawachoki mpaka siku ya Kiyama.

• Wenye kuvinjari ambao huhudhuria vikao vya dhikri, kisomo cha Qura-aan na vikao vya elimu.

• Wabebaji Arshi ambao idadi yao ni wanane. Ni viumbe wakubwa mno kati ya viumbe wa Mwenyezi Mungu. Ndege huruka toka ncha ya sikio la mmoja wao hadi shingoni kwa muda wa miaka mia tano.

Mimi ni Mwislamu

• Malaika wa mauti anayezitoa roho za viumbe kwa Amri ya Mwenyezi Mungu. Huyu ana wasaidizi wake.

• Israfil atakayelipuliza baragumu, kisha viumbe vyote vitakufa kabla ya kutokea Kiyama. Kisha litapulizwa jingine, na hapo watasimama viumbe wakiangalia.

• Mikaili anayesimamia jukumu la mvua.

• Ridhwaan ambaye ni mlinzi wa Pepo. Yeye ana wasaidizi wake walio mbioni kuwahudumia Waumini Peponi.

• Maalik ambaye ni mlinzi wa moto. Ana wasaidizi wake ambao viongozi wao ni kumi na tisa. Wana marungu ya chuma ya kuwaadhibu makafiri motoni - Mwenyezi Mungu Atuepushe na hayo.

• Mkuu wa Malaika ni Jibril aliyewakilishwa kupeleka wahyi kwa Manabii na Mitume.

Mimi ni Mwislamu

• Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam alimwona katika umbile lake. Kutokana na ukubwa wake, alizifunika peo za mbingu. Ana mbawa mia sita, naye ndiye aliyekikamata kijiji cha Lut kwa ncha ya ubawa wake, akakinyanyua hadi juu mbinguni, kisha akakipindua juu chini.

• Kuna malaika wengineo wengi zaidi ya hawa, na hakuna ajuaye askari wa Mola wako isipokuwa Yeye tu.

(¯̄̄̄�� ��°°°°� � � �� � � �� � � �� � � �±±±±�� ��²²²²�� ��³³³³� � � � � �� � � � � �� � � � � �� � � � � �µ´µµ́´µ´ ) *,34��:562

• Malaika huwapenda Waumini ambao Mwenyezi Mungu Huwapenda na huwaombea maghfira.

• Malaika mbali na nguvu zao hizi hupigana pamoja na Waumini.

Mimi ni Mwislamu

(3) KUVIAMINI VITABU

• Ninaviamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu Alivyoviteremsha kwa Mitume Wake, na kwamba katika asili ya kuteremshwa Kwake, ni Maneno ya Mwenyezi Mungu Aliyowafunulia ili waifikishe sheria na dini Yake. Vitabu vikubwa zaidi ni:

� Quraan Tukufu iliyoteremshwa kwa Mtume wetu Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam.

� Injili iliyoteremshwa kwa Iysa Alayhi Ssalaam.

� Taurat iliyoteremshwa kwa Musa Alayhi Ssalaam.

� Zaburi iliyoteremshwa kwa Daud Alayhi Ssalaam.

� Sahifa zilizoteremshwa kwa Ibrahim Alayhi Ssalaam.

Mimi ni Mwislamu

• Kati ya hivi, kuna vilivyopotolewa na kubadilishwa kabla ya kushuka Qur-aan.

• Na Qur-aan ndiyo iliyo juu ya Vitabu hivi, na ndiyo yenye kuongoza sheria zote na hukumu zake, na yenye kuondosha yale yote yenye kwenda kinyume na hukumu zake baada tu ya kuteremka kwake.

• Na kwamba Mwenyezi Mungu Hatokubali siku ya Kiyama ila amali kupitia uongofu wa Qur-aan. Hatokubali amali kwa kufuata Vitabu vilivyotangulia baada ya kuteremka Qur-aan kwa Mtume Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam.

• Na kwamba Qur-aan ni Maneno ya Mwenyezi Mungu ya miujiza. Maneno haya yana utukufu wake, na wala hayaingiliwi na batili kabla yake wala baada yake. Mwenye kuyasema, amesema kweli, na mwenye kuhukumia kwayo, amefanya uadilifu, na mwenye kuyafanyia kazi

Mimi ni Mwislamu

basi hakika ameongolewa katika njia iliyonyooka, mwenye kushikamana nayo amefuzu na kuokoka, na mwenye kuyakengeuka atakuwa ni katika wenye kuhiliki.

• Ni kwamba watu wa Qur-aan, hao ndio watu wa Mwenyezi Mungu waliokurubishwa Kwake, na kwamba mbora zaidi wa watu ni yule aliyejifundisha Qur-aan na akawafundisha watu, kwani Qur-aan hii itakuja siku ya Kiyama ikimwombea shifaa kila aliyeisoma, akaihifadhi na akaifanyia kazi, na itawaombea watu wake Pepo.

• Qur-aan huzitwaharisha nyoyo kutokana na shubha na matamanio yanayozichafua, huzikurubisha kwa Muumbaji Wake Subhaanahuu wa Ta'alaa, na huzihimiza kufanya kazi ili kufuzu na kupata neema za kudumu milele.

• Kati ya adabu za kusoma Qur-aan ni:

���� Kuwa twahara na wudhuu.

Mimi ni Mwislamu

���� Kuelekea Kibla.

���� Kukaa kwa adabu na heshima.

���� Kutoisoma kwa haraka.

���� Kuwa na unyenyekevu.

���� Kuonyesha huzuni kwa madhambi na kuvuka mipaka.

���� Kulia kutokana na kumwogopa Mwenyezi Mungu na Utukufu wa Maneno Yake.

���� Kusoma kwa sauti nzuri.

���� Kusoma kwa sauti ya chini ili kutowabughudhi wenye kuswali.

���� Kuzingatia maana ya maneno.

���� Kuhudhurisha moyo.

���� Kutaamuli kwa kina Aayah za Mwenyezi Mungu.

���� Tuwe na yakini kuwa kusimamisha hukumu za Kitabu hiki kwa watu ni moja kati ya sababu za kumakinishwa katika ardhi na kuwashinda maadui.

Mimi ni Mwislamu

Basi harakia ndugu yangu Mwislamu kwenda kwa Mola wako, na kikamate Kitabu hiki kwa hima. Kuwa na shime asikutangulie yeyote kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu Hufurahi zaidi kwa kurejea kwako Kwake kuliko wanavyofurahi watu kwa kurejea mtu wao aliyekuwa mbali.

Mimi ni Mwislamu

(4) KUWAAMINI MITUME

• Ninawaamini Mitume wa Mwenyezi

Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu

Aliwateua Mitume kati ya wanadamu,

Akawafunulia Sheria Yake kwa njia ya

wahyi, na Akawaamuru kuifikisha kwa

watu, na kwamba mwenye kuwatii

ataingia peponi, na mwenye kuwaasi

ataingia motoni.

• Kisha Akawatilia nguvu kwa miujiza

yenye kuonyesha ukweli wao ili

iwasaidie mbele ya wakadhibishaji, na

ili iwe ni hoja kwao.

• Na kwamba Mtume wa mwanzo ni

Nuhu, na wa mwisho wao ni

Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa

Aalihii wa Sallam.

Mimi ni Mwislamu

• Na kuwa Mitume hawa ni watu;

wanakula, wanakunywa,

wanaoa,wanaugua na wanakufa. Wao

ndio viumbe bora kabisa wa Mwenyezi

Mungu na wamehifadhiwa na maasi.

• Mitume wa Mwenyezi Mungu ni wengi.

Mwenyezi Mungu Amewataja baadhi

yao katika Qur-aan. Nao ni Muhammad

Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa

Sallam, Ibrahim Khalili wa Ar-

Rahmaan, Musa aliyesemeshwa na

Allaah, Iysa Neno la Mwenyezi Mungu

na Nuhu. Hawa ndio Mitume wenye

azma ya juu Rehma na Amani ziwe juu

yao. Pia Ismail, Is-haaq, Yakub,

Harun, Ayyub, Yunus, Sulayman,

Daawud, Yahya, Zakariya, Hud, Saleh,

Mimi ni Mwislamu

Yusuf, Shuayb, Ilyaas, Lut, Dhulkifl,

Idris, na wengi wengineo. Kati yao

kuna Aliowahadithia Mwenyezi Mungu

katika Qur-aan na wengineo

Hakuwahadithia.

• Jambo la kwanza walilolilingania

Mitume ni tawhid, na jambo kubwa

zaidi walilolikataza ni shirki, na wote

wamekuja na Uislamu na wito.

• wa tawhid. Lakini sheria zao na

mifumo ya kumwabudu Mwenyezi

Mungu Mtukufu ilitofautiana kutokana

na kutofautiana zama zao na nchi zao.

• Na kwamba Mitume walitoa bishara ya

kuja kwa Nabii Muhammad Swalla

Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam na

Mimi ni Mwislamu

wakawaamrisha kaumu zao

kumwamini Muhammad Swalla Allaahu

Alayhi wa Aalihii wa Sallam

atakapotumwa kwao.

• Tofauti kati ya Rasuli (Mtume) na

Nabii ni kuwa Rasuli ni yule

aliyefunuliwa sheria mpya na

akaamrishwa kuifikisha kwa watu.

Ama Nabii, ni yule aliyetumwa ili

kuithibitisha na kuipitisha sheria ya

Rasuli aliyemtangulia.

• Ninaamini kuwa mbora wa Mitume

mbele ya Allaah ni Muhammad Swalla

Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam

toka kwa mwana wa Ismaili bin

Ibrahim Alayhima Ssalaam. Allaah

Amemtuma kwa watu wote,

Mimi ni Mwislamu

Akahitimisha Unabii kwa Unabii wake,

na Utume kwa Utume wake.

• Akamtilia nguvu kwa miujiza,

Akamfanya bora kuliko Mitume wote.

Pia Ameufanya Utume wake kuwa

bora kuliko Utume wote uliotangulia,

na sheria yake kuwa bora kuliko

sheria zinginezo zilizopita, na Kitabu

chake Qur-aan kuwa bora kuliko

Vitabu vyote, na umati wake –

Waislamu – kuwa bora kuliko uma

nyinginezo.

• Na Mola wake Akampa mambo ambayo

Hakumpa yeyote katika Manabii

waliomtangulia. Kati ya mambo hayo

ni:

Mimi ni Mwislamu

(1) Al Wasiylah: Nayo ndiyo daraja ya

juu kabisa Peponi ambayo

Mwenyezi Mungu Amemwandalia

Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa

Aalihii wa Sallam.

(2) Al Kawthar: Nao ni mto Peponi

wenye kupita chini ya Arshi ya Ar

Rahman.

(3) Al Hawdh: Ni sehemu ambayo

Waislamu peke yao ndio

watakayokunywa siku ya Kiyama.

Siku ambayo watu watapatwa na

kiu kikali, na jasho litawafika hadi

magotini, viunoni na mabegani –

kila mmoja kwa mujibu wa amali

yake – na Waislamu watakunywa

hapo kwa vikombe atakavyowapa

Mimi ni Mwislamu

Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa

Aalihii wa Sallam kwa mikono yake

mitukufu. Baada ya hapo

hawatapatwa na kiu milele.

(4) Shafaa: Ni makamu ya kuhimidiwa

siku ya Kiyama. Hapo Mtume Swalla

Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam

ataomba shifaa kwa Mwenyezi

Mungu ili Waislamu waliofanya

maasi watolewe motoni, na

hatobakia ndani ya moto yeyote

anayeshuhudia kwamba hapana

Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu

na Muhammad ni Mtume wa Allaah.

Aliyefanya maasi hatosalia milele

motoni, bali atatoka baada ya

kutakaswa na maasi yake.

Mimi ni Mwislamu

Aliyewaamini Manabii wote na wala

hakumwamini Muhammad Swalla

Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam,

basi hatatoka motoni.

(5) Na kwamba Allaah Amemnusuru na

Akawanusuru askari wake na

wafuasi wake hadi siku ya Kiyama

kwa kuzagaza hofu ndani ya nyoyo

za maadui umbali wa mwendo wa

mwezi. Na hakuna Nabii yeyote

aliyepewa hili kabla yake

Muhammad Swalla Allaahu Alayhi

wa Aalihii wa Sallam.

(6) Na ardhi imefanywa kwake na

Waislamu kuwa msikiti (sehemu ya

kuswalia) na twahara, na

Mimi ni Mwislamu

haikufanywa hivyo kwa Manabii

waliomtangulia.

(7) Na Allaah Amemtuma kwa watu na

majini wote, lakini Mitume wengine

wametumwa maalumu kwa watu

wao tu.

(8) Na kuwa yeye ndiye wa mwanzo

kaburi lake kufunguka, na ndiye

mwombezi wa kwanza, na ndiye wa

kwanza kupewa shifaa, na ndiye wa

kwanza kugonga mlango wa Pepo.

Atakapougonga, mlinzi

wa Pepo Ridhwaan atamuuliza: "Nani

wewe?" Atajibu: "Muhammad". Ridhwaan

atamwambia: "Kwako nimeamrishwa

nisimfungulie yeyote kabla yako".

Mimi ni Mwislamu

Na kati ya miujiza ya Mtume Swalla

Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam ni:

� Kupasuka mwezi.

� Alilirejesha jicho la Qatada

lilipopofuliwa siku ya Uhud, macho yake

yakarudi yakawa mazima kabisa.

� Aliurejesha muundi wa Ibn Al

Hakam kama ulivyokuwa ulipovunjwa

siku ya Vita vya Badr.

� Aliutaka mti utamke shahada,

nao ukatamka shahada mbili mara tatu

mbele ya kafiri, naye akasilimu.

� Kigogo cha mti alichokuwa

akihutubia juu yake kililia wakati

alipokiacha na hakikunyamaza mpaka

alipoiweka mikono yake juu yake.

Mimi ni Mwislamu

� Alikifanya chakula kidogo kuwa

kingi baina ya mikono yake miwili, na

wakaweza kula na kushiba zaidi ya

watu 80 chakula cha kujaa viganja

viwili.

� Aliyafanya maji kidogo kuwa

mengi siku ya Hudaybiyah wakati jeshi

lilipobakiwa na bakuli moja tu ya maji.

Hapo Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa

Aalihii wa Sallam aliingiza mikono yake

ndani, maji yakaanza kububujika kati ya

vidole vyake kama chemchemu,

wakanywa maji Waislamu wote na

wakatawadhia maji hayo. Walikuwa

kiasi cha watu 1400.

� Alipelekwa usiku hadi Msikiti

wa Al Aqsa, na kisha alipandishwa hadi

Mimi ni Mwislamu

mbingu za juu na kukomea Sidrat Al

Muntahaa.

� Alielezea na kuhadithia habari

za umma zilizotangulia na Manabii wao

nailhali yeye hana kisomo; hajui

kusoma wala kuandika. Pia alielezea

matukio yatakayotokea siku za usoni

kwa kufunguliwa Fursi na Rome,

kusambaratishwa ufalme wa Kisra

aliyechanachana barua ya Mtume Swalla

Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam

aliyomtumia, pamoja na miujiza

mingineyo mingi.

� Muujiza mkubwa zaidi wa

Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii

wa Sallam ni Qur-aan Tukufu. Ni

Mimi ni Mwislamu

muujiza utakaosalia hadi siku ya

Kiyama.

� Kisha Allaah Ameunyanyua

utajo wake, Akaliandamisha jina la

Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii

wa Sallam na Jina Lake Subhaanahuu

wa Taalaa, na Akaifanya shahada ya

kuwa hapana mola isipokuwa Allaah na

kwamba Muhammad ni Mtume wa

Mwenyezi Mungu kuwa ndio jambo la

kwanza analoingia nalo mja katika

Uislamu,na jambo la mwisho analotoka

nalo duniani. Basi yeyote ambaye neno

lake la mwisho litakuwa ni "Laailaaha

illa Allaah", ataingia peponi.

• Ni wajibu wetu kwa upande wa

Mtume wetu Swalla Allaahu Alayhi

Mimi ni Mwislamu

wa Aalihii wa Sallam tusilitangulize

neno la kiumbe yeyote juu ya neno

lake, au rai ya yeyote hata kama ana

sauti kwa watu. Na ikiwa watu

watakutangulia kuhamia kwake, basi

hama wewe kwenda katika sunnah

yake katika kila jambo lako na wala

usimfuate mwingine zaidi yake. Ni

wajibu wetu tushikamane sote

pembezoni mwa amri yake na tumtii,

kwani mwenye kumtii Mtume, basi

huwa amemtii Mwenyezi Mungu.

(AAAA�� ��BBBB�� ��CCCC�� ��DDDD�� ��EEEE�� ��GFGFGFGF ) *7��8��:092:

• Na tusimwiite ila kwa kusema Mtume

wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu

Alayhi wa Aalihii wa Sallam.

Tusiseme (Muhammad) basi.

Mimi ni Mwislamu

• Tujipambe kwa adabu zake, na

tumwige katika hali zake zote; kulala

kwake, kula kwake, kutembea

kwake, kuswali kwake, kufunga

kwake, kutoa kwake sadaka, na

jihadi yake.

• Na tumpende zaidi kuliko nafsi zetu,

wana wetu, wazazi wetu na watu

wote.

• Na tumpende kila yule anayempenda

Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla

Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam

na kumfanya kiigizo chake, na

tumchukie kila yule anayemchukia

Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla

Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam

na wala hawajibiki na sheria yake.

Mimi ni Mwislamu

• Hivyo basi, ni lazima kwa Mwislamu

awapende Waumini, awanusuru,

ajifananishe nao, ashughulikie

mambo yao, asaidiane nao katika

mambo ya kheri, na awafanye kuwa

marafiki zake wa dhati.

• Ni wajibu kwake awabughudhi

makafiri na ukafiri wao, asiwatii,

asiungane nao dhidi ya Waislamu,

wala asisaidiane nao katika ubatilifu

wao, na wala asishiriki katika

sikukuu zao. Ni haramu kwake

kuwadhulumu, na linalotakiwa ni

kuwatendea haki.

• Ni wajibu wetu tuwapende Mama wa

Waumini; Wakeze Mtume Swalla

Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam,

Mimi ni Mwislamu

na tuwapende Maswahaba Wake

Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa

Sallam, kwani wao ndio bora wa

watu baada ya Manabii.

• Pia ni wajibu wetu tuihuishe Sunnah

yake Mtume Swalla Allaahu Alayhi

wa Aalihii wa Sallam, tuidhihirishe

sheria yake, na tubalighishe

ulinganio wake kwa watu wote.

Kisha tusubiri maudhi na kero

zinazotupata katika kuyapigania

hayo, kwani hayo hayaepukiki.

• Kwa vile Mwenendo wa Mwenyezi

Mungu uliopita kwa viumbe Vyake

unahukumia kuwa hakuna Nabii au

walii yeyote aliyelingania haki hii ila

alifanyiwa uadui na kuudhiwa.

Mimi ni Mwislamu

• Zindukana ndugu yangu Mwislamu!

Maudhi ya makafiri yasikufanye

ukaiacha dini yako. Kwani Mtume wa

Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu

Alayhi wa Aalihii wa Sallam

aliudhiwa wakati Maswahaba

walipokuwa wachache, nao pia

waliudhiwa wakafanya subira.

• Na wala usilegeze azma yako hata

kama watakwambia kuwa

unayoyazungumza ni upuuzi, una

misimamo migumu, au umepitwa na

wakati. Au wakisema: "ashachezewa

akili huyo". Kwani wewe una kiigizo

chema kwa Mtume wa Mwenyezi

Mungu, yeye ashaambiwa mshairi na

hata mwendawazimu.

Mimi ni Mwislamu

• Wala usisononeke ukiambiwa

mpotevu mwenye siasa kali. Hii ndio

tabia ya makafiri kwa Waumini.

(Ü�Û�Ú�Ù�Ø�×Ü�Û�Ú�Ù�Ø�×Ü�Û�Ú�Ù�Ø�×Ü�Û�Ú�Ù�Ø�× ) *���;��:5<2:

((Na wanapowaona, husema hakika

hawa bila shaka ni wapotevu)).

• Ikiwa watu wako makundi mawili, je

haikutoshi wewe kuwepo katika

kundi aliloko Mtume wako

Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa

Aalihii wa Sallam?!

• Achana nao hao mpaka ifike siku

ambayo dhalimu ataviuma vidole

vyake aseme: "Laiti mimi

ningeliifuata njia pamoja na Mtume".

Mimi ni Mwislamu

( \\\\�p�o�n�m����l�k�j��i�h�p�o�n�m����l�k�j��i�h�p�o�n�m����l�k�j��i�h�p�o�n�m����l�k�j��i�hqqqq ) *+�=,���:<>2:

• Wala usibabaike au kuchanganyikiwa

kama watakwambia kuwa wewe ni

gaidi au mwovu, kwani hayo ndio

madai ya madhalimu dhidi ya

Waumini duniani na akhera. Ni kuwa

pale Malaika watakapowaongoza

kwenda Jahannamu wakisunukia,

wataangalia humo kisha waseme:

(J�I�H���G�F�E�D�C�B�AJ�I�H���G�F�E�D�C�B�AJ�I�H���G�F�E�D�C�B�AJ�I�H���G�F�E�D�C�B�A ) *?:@<:2

((Na watasema: Mbona

hatuwaoni watu tuliokuwa

tukiwazingatia kuwa ni katika

waovu?))

Mimi ni Mwislamu

• Na hapa, Waumini (ambao makafiri

wamewaita kuwa ni waovu)

watawaita toka kwenye magorofa ya

juu kabisa ya Firdaws wakiwaambia:

(L�K�J�I�H�G�FL�K�J�I�H�G�FL�K�J�I�H�G�FL�K�J�I�H�G�F�� �� )*A�,-��:BB:2

� و�� ر��� ���(( �٤٤: ا���اف )) أن � و�

(( Hakika sisi tumeyakuta

Aliyotuahidi Mola wetu kuwa ni

kweli))

Mimi ni Mwislamu

(5) KUAMINI SIKU YA MWISHO

• Ninaiamini siku ya mwisho, nayo ni

iku ambayo dunia (nyumba ya amali)

itamalizika, na akhera (nyumba ya

malipo) itasimama, wema wakalipwa

Pepo, na waovu wakalipwa moto.

• Katika siku ya Kiyama, mizani

itawekwa, na kila mja atapewa

kitabu chake. Atakayepokea kitabu

chake kwa mkono wake wa kuume,

basi Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa

Aalihii wa Sallam atakuwa pamoja

naye Peponi. Ama yule atakayepokea

kitabu chake kwa mkono wake wa

kushoto, basi atakuwa pamoja na

Mimi ni Mwislamu

Firauni –laana ziwe juu yake–

motoni.

• Sirati itawekwa, atakayefanikiwa

kuivuka basi atafikia Peponi. Ama

ambaye kulabu zitamnyakua kutokana

na amali zake mbovu, basi

ataangukia motoni.

• Siku ya Kiyama ina dalili, ina alama

ndogo na ina alama kubwa.

• Miongoni mwa alama ndogo ni

kupotea uaminifu, kukithiri mauaji,

madaraka kukamatwa kwa mabavu

na mafasiki, na masuala muhimu

kuzungumziwa na wasiojua kitu.

• Na miongoni mwa alama kubwa ni

kuibuka Al Mahdi, kusimama ukhalifa

Mimi ni Mwislamu

wongofu utakaokwenda juu ya

misingi ya njia ya Utume kabla ya

kutokea Kiyama, na kudhihiri masihi

mwongo.

• Pia kuteremka Iysa Alayhi Ssalaam ili

awaongoze Waislamu, apigane na

makafiri, avunje vunje misalaba, aue

nguruwe, na azikatae dini zote

nyingine ila Uislamu tu.

• Basi haitobakia nyumba yoyote ya

mjini au ya mashambani ila

Mwenyezi Mungu Ataiingiza dini hii,

kwa heshima ya mwenye nguvu, au

kwa udhalili wa mnyonge.

• Vile vile kutoka Yaajuju na Maajuju.

Pia atatoka mnyama

Mimi ni Mwislamu

anayewasemesha watu, na jua

litachomoza toka magharibi, Qur-aan

itaondoshwa na mambo mengineyo.

• Basi yeyote atakayefanya amali ya

uzito wa atomu ikiwa ni ya kheri au

ni ya shari, ataiona siku ya Kiyama

ndani ya kitabu chake.

• Basi harakieni kwenye mambo ya

kheri kabla haujamalizka muda wa

kusajiliwa kwa kufa mja katika muda

ambao haujui yeyote ila Mwenyezi

Mungu Pekee.

• Wakamwosha jamaa zake,

wakamvisha sanda, wakamswalia,

wakamzika. Kisha akajiwa na Malaika

wawili; Munkari na Nakiyr,

Mimi ni Mwislamu

wakamkalisha kitako na kumwuuliza:

"Nani Mola wako? Nini dini yako?

Nani Nabii wako?"

• Ikiwa atajibu kuwa: "Allaah ni Mola

wangu, na Uislamu ndiyo dini yangu,

na Muhammad Swalla Allaahu Alayhi

wa Aalihii wa Sallam ndiye Nabii

wangu na Mtume wangu" – na Allaah

Akamwezesha hilo – basi

itafunguliwa katika kaburi lake

harufu ya rayhaan hadi peponi,

akaona mashukio yake huko, na

makasri yake na ufalme wake. Hapo

atashangilia kwa furaha kubwa, na

kaburi lake litapanuliwa upeo wa

macho.

Mimi ni Mwislamu

• Na ikiwa ni katika makafiri, basi

hatoweza kujibu chochote, kwani

majibu wakati huo si kwa akili au

werevu wa mtu.

• Bali Mwenyezi Mungu Huwathibitisha

na kuwaimarisha watu wa imani

wakati huo kwa yale

waliyoyatanguliza kati ya amali

njema zilizosimamia juu ya tawhid,

utekelezaji wa faradhi, kushiriki

jihadi, kutenda mema, kuamrisha

mema, kukataza mabaya, kutoa

sadaka, kusoma Qur-aan, kufunga

siku za joto kali, na kusimama

kuswali muda mrefu usiku wa baridi

kali.

Mimi ni Mwislamu

• Ama akiwa ni katika makafiri, basi

kaburi lake humbana hadi mbavu

zake zikaingiana katika mwili wake,

na kaburi lake huwa ni shimo katika

mashimo ya motoni kwa sababu ya

amali zake mbaya.

• Basi jitahidi ndugu yangu Mwislamu,

kwani leo ni amali na hakuna hisabu,

lakini kesho ni hisabu na hakuna

amali.

• Na siku hiyo, Waislamu watiifu

wataingia Peponi peke yao, kwa vile

Mwenyezi Mungu Hatoikubali dini

yoyote siku ya Kiyama isipokuwa

Uislamu.

Mimi ni Mwislamu

• Ndani ya Pepo kuna neema ambazo

hakuna sikio lililowahi kuzisikia, wala

jicho lililowahi kuziona, wala hata

kuwaziwa katika akili ya

mwanadamu. Neema zake zitasalia

milele wala hazitomalizika, na

waliomo humo hawatakufa milele.

Neema kubwa zaidi ya zote humo, ni

kuuangalia Uso wa Mwenyezi Mungu

Mola wa walimwengu wote.

• Na waasi, waovu na makafiri

wataingia motoni. Ndani ya moto,

kuna adhabu zisizoweza kuvumilika

Alizoziandaa Mwenyezi Mungu kwa

ajili ya makafiri. Milima mirefu thabiti

haiwezi kuzivumilia adhabu hizi, na

Mimi ni Mwislamu

hao wataadhibiwa humo bila

kupumzishwa.

• Na humo, wafuasi wa mataghuti

wataomba adhabu iongezwe

maradufu kwa wakubwa wao

waliowapoteza. Na hapo Mwenyezi

Mungu Ataamuru adhabu iongezwe

maradufu kwa wote.

• Basi thibiti ndugu yangu Mwislamu

juu ya haki hii, wala usidanganyike

kabisa kuona kuwa wavunjaji sheria

ni wengi zaidi, kwani ikiwa wewe

utawatii na ukawafuata wengi

waliomo ardhini, basi watakupoteza

njia ya Mwenyezi Mungu. Nawe pita

pamoja na wenye kupita kuelekea

kwa Mwenyezi Mungu.

Mimi ni Mwislamu

• Kwani kundi katika umma wa

Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa

Aalihii wa Sallam litaendelea kuwa

juu ya haki likiwa na nguvu, hawezi

kuwadhuru yeyote aliyekwenda nao

kinyume au aliyewasaliti mpaka siku

ya Kiyama.

• Basi ni mbinu zipi za kuzijua ngazi

hizo za kupanda juu, na kuokoka na

ngazi hizo za kuporomokea chini? Na

ni mbinu zipi za kuwafikia

waliotangulia wenye kukurubishwa,

na kujiweka mbali na wapingaji

wenye kuangamia? Bila shaka ni toba

ya kweli ya kusahihisha na

kurekebisha yaliyopita, na amali

njema za kuweka sawa umri

Mimi ni Mwislamu

uliosalia, na kuweka nia ya kweli ya

kunyooka na kutokengeuka.

• Basi kuwa pamoja na watu kwa

kiwiliwili chako, ukiuza, ukinunua,

ukioa na ukiiamirisha ardhi kwa yale

Aliyokuhalalishia Mwenyezi Mungu.

• Wala moyo wako usifungamane na

kitu chochote cha kidunia, bali nenda

na moyo wako pale ambapo

unatakikana uwe, huko chini ya Arshi

ya Ar Rahmaan, na sujudu kwa moyo

wako sijdah ambayo utaendelea

kuisujudu hadi siku ya Kiyama.

Mimi ni Mwislamu

(6) KUAMINI QADHAA NA QADARI

• Nako ni kuamini kwamba Mwenyezi

Mungu Anayajua yote yaliyomo

ulimwenguni, yote yanayofanyika na

yatakayotokea hadi siku ya Kiyama.

Hata chembe ndogo mno, Yeye

Hakosi kuijua. Na kwamba Yeye

Anavijua vitendo vya waja, riziki zao,

muda wao wa kuishi, na nani kati yao

atakuwa wa peponi, na nani kati yao

atakuwa wa motoni kabla

Hajawaumba.

• Na kwamba Mwenyezi Mungu

Ameyaandika makadirio haya katika

Lawh Al Mahfuudh kabla hata

Hajaziumba mbingu na ardhi kwa

miaka elfu hamsini, na kwamba Lawh

Mimi ni Mwislamu

Al Mahfuudh hii hakuna malaika wa

karibu au hata Nabii aliyetumwa

awezaye kuichungulia.

• Hata kijusi kinapokuwa ndani ya

tumbo la uzazi la mama yake,

Mwenyezi Mungu Huwaamrisha

Malaika waandike kama ni cha kike

au kiume, waandike na riziki yake,

amali yake, muda wake wa kuishi na

hatima yake (ima peponi au motoni).

Pia waandike mazuri na mabaya

atakayokabiliana nayo.

• Kisha unapoingia usiku wa cheo

(Laylatul Qadr), huteremka

makadirio ya mwaka mzima toka

Lawh al Mahfuudh kati ya ajali za

watu, riziki zao, nani kati yao atahiji

mwaka huo na mengineyo. Katika

Mimi ni Mwislamu

usiku huo, hukadiriwa mambo ya

mwaka mzima.

• Kisha huteremka makadirio ya kila

siku kwa nyakati zake na watu wake,

hapo Mwenyezi Mungu Huwanyanyua

watu na wengine Huwashusha.

• Na tuamini kuwa Mapendeleo ya

Mwenyezi Mungu ndiyo yawayo,

Alilolitaka huwa na Asilolitaka haliwi.

Mwenyezi Mungu Hana wa

kumshinda, na Yeye Ndiye Mwenye

kuzipindua nyoyo. Humwongoa

Amtakaye kwa fadhila Zake na rehma

Zake, na Humpoteza Amtakaye kwa

Uadilifu Wake na Hekima Yake,

kwani Yeye Ndiye Ajuaye zaidi nani

anastahiki uongofu na nani

anastahiki upotevu.

Mimi ni Mwislamu

• Na Mwenyezi Mungu Haulizwi yale

Ayafanyayo lakini watu huulizwa.

• Na tuamini kuwa Mwenyezi Mungu

Amekiumba kila kitu, na hakuna

chembe yoyote ndogo ulimwenguni

isipokuwa Mwenyezi Mungu

Ameiumba na Akaumba kutikisika

kwake na kutulia kwake.

• `Na kwamba Yeye Amewaumba waja

na vitendo vyao, na kwamba Yeye

Amewaumbia waja uwezo na

mapendeleo yao ili wajichagulie

wenyewe vitendo vyao.

• Na kwamba Mwenyezi Mungu

Mtukufu Amewaamuru viumbe Wake

wamtii, na Akawaahidi kuwapa Pepo

Yake wakifanya hivyo, na

Amewakataza kumwasi Yeye, na

Mimi ni Mwislamu

Akawapa onyo la kuwaingiza ndani

ya moto Wake wakifanya hivyo, na

wala Hakuwakalifisha kazi isipokuwa

ile ambayo wanaweza kuifanya. Na

hapo wakagawanyika makundi

mawili: Waumini na makafiri; kwa

hiari yao wenyewe, kwa mapendeleo

yao wenyewe na kwa uwezo wao

wenyewe, na yote hayo Mwenyezi

Mungu Amewaumbia.

• Na kwamba thawabu na adhabu

hutokana na kuifuata sheria, si kwa

kutangulia Elimu ya Mwenyezi Mungu

kwao. Basi yeyote atakayefanya amali

yoyote ya kheri ya uzito wa atomu,

atalipwa kwayo. Na yeyote atakayefanya

amali yoyote ya shari ya uzito wa

atomu, basi ataadhibiwa kwayo.

Mimi ni Mwislamu

• Na kwamba kinachozingatiwa ni

mwisho wa matendo, na kwamba kila

mja ni mwenye kuendeshwa katika

lile aliloumbiwa kati ya kufurahika

Peponi au kupata shakawa motoni.

• Na kwa ajili hiyo, ni wajibu kwa mja

aogope mwisho mbaya, na aendelee

daima kumwomba Mwenyezi Mungu

na amhitajie, Amhidi katika njia

iliyonyooka, na adumu kumwomba

Amsaidie katika kumtii, na ajilinde

Kwake na maasia, kwa vile mja hana

hila wala nguvu zozote za kuyafanya

hayo ila kwa Uwezo wa Mwenyezi

Mungu.

• Na kwamba Waumini Huridhia

Qadhaa ya Mwenyezi Mungu na

Qadari Yake; ya kheri yake na ya

Mimi ni Mwislamu

shari yake, katika misukosuko na

katika furaha, na wana yakini kuwa

hawezi yeyote kuwanufaisha

isipokuwa kwa Qadari ya Mwenyezi

Mungu, na wala hawadhuru

isipokuwa liwe lisha andikwa na

Mwenyezi Mungu.

• Na mja hatopata utamu wa imani

mpaka pale atakapojua kwamba

lililompata lisingekuwa la kumkosa,

na lililomkosa lisingekuwa la

kumpata.

Na mwisho naomba nikisema:

"Ninamhimidi Mwenyezi Mungu, na

ninamwomba Aniingize Peponi mimi na

Waislamu wengine, na Anilinde na moto

mimi na Waislamu wengine". Aamiyn.

Mimi ni Mwislamu

Mimi ni Mwislamu

� �_�`�a�b��c�d�e�

f�g�h�i�j�k �� �

]٨٥:ل ���ان[

������������٠٠٢٠١٠١٤٥٩٦١٣٠٠٢٠١٠١٤٥٩٦١٣٠٠٢٠١٠١٤٥٩٦١٣٠٠٢٠١٠١٤٥٩٦١٣א���� ��א��א���������� ���[email protected]*(#א)�'�א��������א�& ��א%�$#"! � �

WWW.Iam-Muslim.com

� �

١٤٣١������ J�٢٠١٠�,� �

���W٢٢٢٧٤L٢٠٠٩���א���א� �

� ٠١٢٠١٥٢٩٠٨: א�0123'������������W٠١٠٥٠١٣١٥١٠١٠٥٠١٣١٥١٠١٠٥٠١٣١٥١٠١٠٥٠١٣١٥١א%.א-���

� !" "!# و $%& �&'(% � ,+ ا&*�'ق

Mimi ni Mwislamu

��4��$��56���67�8�9��:;���4"�<

�� �����������

� �� �� �

��� � � ���� � � � ��������� �������� ������ ���� ���

٠١٠٦٧١٤٧٦٨

�!"� �� ���������# $��% &�'��� ()��� ���� ����

٠١٢٥٨٣٤٥٧٤

����ــ�����ــ�����ــ�����ــ�