283
R A S I M U JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAARIFA YA MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA NNE KATIKA KIPINDI CHA 2005/2006 HADI 2014/2015 JULAI, 2015 1

Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne kuanzia 2005/2006 hadi 2014/2015

Embed Size (px)

Citation preview

1

R A S I M U

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

TAARIFA YA MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA NNE KATIKA KIPINDI CHA

2005/2006 HADI 2014/2015  

JULAI, 2015

2

YALIYOMOORODHA YA VIFUPISHOSURA YA KWANZA1. UTANGULIZISURA YA PILI2. KUJENGA MSINGI WA UCHUMI WA KISASA WA TAIFA LINALOJITEGEMEA2.1 UKUAJI WA UCHUMI2.1.1 Pato la Taifa2.1.2 Udhibiti wa Mfumuko wa Bei2.1.3 Kupungua kwa Umaskini2.1.4 Mapato ya Serikali2.1.5 Bajeti ya Serikali2.2 USIMAMIZI WA FEDHA ZA SERIKALI2.3 MAENDELEO YA SEKTA BINAFSI2.3.1 Maboresho ya Sera na Sheria2.3.2Ushiriki wa Sekta Binafsi katika kuendesha Uchumi2.3.3Kuimarisha Bandari na Vituo vya Mpakani

3

2.3.4 Usimamizi Sekta ya Fedha2.4 UWEKEZAJI NCHINISURA YA TATU3. SEKTA ZA UZALISHAJI MALI3.1 KILIMO3.1.1 Mikakati ya kuleta Mapinduzi ya Kilimo3.1.2 Ongezeko la Bajeti ya Kilimo3.1.3 Mpango wa Uwekezaji wa Ukanda wa Kusini (SAGCOT)3.1.4 Ruzuku ya Pembejeo3.1.5 Matumizi ya Zana Bora za Kilimo3.1.6 Ruzuku ya Viuatilifu3.1.7 Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo3.1.8 Huduma za Ugani3.1.9 Udhibiti wa Mbegu na Mbolea3.1.10 Uzalishaji wa Mazao nchini3.1.11 Akiba ya Chakula ya Taifa3.1.12 Uzalishaji wa Mazao ya Bustani3.1.13 Uzalishaji wa Mazao ya Mbegu za Mafuta3.1.14 Benki ya Kilimo

4

3.2 VYAMA VYA USHIRIKA3.3 UMWAGILIAJI3.3.1 Ongezeko la eneo la umwagiliaji3.3.2 Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Umwagiliaji3.4 UFUGAJI3.4.1 Utekelezaji wa Programu Kabambe ya Kuendeleza Sekta ya Mifugo3.4.2 Mradi wa Kopa Ng’ombe Lipa Ng’ombe3.4.3 Udhibiti wa Magonjwa ya Mifugo3.4.4 Ujenzi wa Mabwawa na Majosho3.4.5 Utafiti wa Mifugo na Huduma za Ugani3.4.6 Masoko ya Ndani ya Mifugo na Mazao yake3.4.7 Vituo vya Kuzalisha Mbegu Bora za Mifugo3.4.8 Kutenga Maeneo ya Malisho ya Mifugo3.4.9 Uzalishaji wa Vyakula vya Mifugo

5

3.5 UVUVI3.5.1 Vyuo Vya Uvuvi3.5.2 Udhibiti wa Uvuvi Haramu3.5.3 Kuimarisha Miundombinu ya Uvuvi3.5.4 Upatikanaji wa Mazao Bora na Usalama ya Uvuvi3.5.5 Kuimarisha Vikundi vya Ushirika vya Wavuvi3.5.6 Usimamizi wa Mazingira Katika Maeneo ya Uvuvi3.5.7 Uzalishaji wa Viumbe kwenye Maji3.6 WANYAMAPORI NA MISITU3.6.1 Kuboresha Miundombinu ya Hifadhi za Wanyamapori3.6.2 Misitu na Mazao yake3.6.3 Ufugaji Nyuki3.7 UTALII3.7.1 Vyuo na Hoteli za Kitalii3.7.2 Kutangaza Utalii wa Ndani3.7.3 Kutangaza Utalii wa Nje na Kutafuta Masoko Mapya

6

3.8 VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO3.8.1 Viwanda3.8.2 Biashara na Masoko3.9 MADINI3.9.1 Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa3.9.2 Kuimarisha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)3.9.3 Kuwajengea Uwezo Wachimbaji Wadogo wa Madini3.9.4 Ukaguzi wa MigodiSURA YA NNE4. HUDUMA ZA KIUCHUMI4.1 ARDHI4.1.1 Utawala wa Ardhi4.1.2 Mipango Miji4.1.3 Upimaji na Ramani4.1.4 Upimaji wa Mipaka ya Vijiji4.1.5 Mpango wa Taifa wa Matumizi Bora ya Ardhi4.1.6 Mfumo wa Teknolojia ya Kompyuta Katika Kutoa Huduma za Ardhi

7

4.1.7 Uanzishaji wa Miji Midogo (Satelite Towns)4.1.8 Mabaraza ya Ardhi4.2 NYUMBA4.2.1 Ujenzi wa Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)4.2.2 Ujenzi wa Majengo/Nyumba za Serikali4.2.3 Mikopo ya Ujenzi wa Nyumba4.3 NISHATI4.3.1 Utafutaji wa Gesi Asilia na Mafuta4.3.2 Ujenzi wa Bomba na Usambazaji wa Gesi Asilia4.3.3 Ujenzi wa Miundombinu ya Usafirishaji Umeme4.3.4 Usambazaji wa Umeme Vijijini4.3.5 Nishati Mbadala (Nishati Jadidifu)4.4 UJENZI4.4.1 Mfuko wa Barabara4.4.2 Ujenzi wa Barabara, Madaraja na Vivuko4.4.2.1 Barabara4.4.2.2 Madaraja4.4.2.3 Ujenzi wa Vivuko

8

4.5 UCHUKUZI4.5.1 Huduma za Usafiri wa Reli Jijini Dar es Salaam4.5.2 Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka4.5.3 Reli ya Kati4.5.4 Reli ya TAZARA4.5.5 Ununuzi na Ukarabati wa Injini (locomotives) na Mabehewa ya treni4.5.6 Bandari4.5.7 Usafiri wa Anga4.5.8 Ujenzi na Ukarabati wa Viwanja vya Ndege4.5.9 Kuimarisha Utabiri wa Hali ya Hewa4.6 MAENDELEO YA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO4.6.1 Utafiti4.6.2 Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano4.6.3 Huduma za Simu za Mkononi na Intaneti4.6.4 Huduma ya Mawasiliano Vijijini4.6.5 Mfumo wa Kuhakiki na Kusimamia Huduma za Mawasiliano

9

SURA YA TANO5. UWEZESHAJI WANANCHI5.1 UANZISHWAJI NA UIMARISHWAJI WA SACCOS NA VIKOBA5.2 MIRADI YA VIJANA5.3 MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKE5.4 BENKI YA WANAWAKE TANZANIA5.5 MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF)5.6 MKAKATI WA KURASIMISHA RASILIMALI NA BIASHARA TANZANIA (MKURABITA)5.7 AJIRA5.7.1 Kushughulikia Matatizo ya Wafanyakazi5.7.2 Usuluhishi na Uamuzi wa Migogoro ya Kikazi5.7.3 Usalama na Afya Mahali pa Kazi5.7.4 Usajili wa Vyama Huru vya Wafanyakazi na Waajiri5.7.5 Maslahi ya Watumishi wa Umma5.7.6 Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

10

SURA YA SITA6. HUDUMA ZA JAMII6.1 Elimu6.1.1 Elimu ya Awali na Msingi6.1.2 Elimu ya Sekondari6.1.3 Elimu ya Ualimu6.1.4 Mafunzo ya Ufundi6.1.5 Vyuo vya Maendeleo ya Jamii6.1.6 Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi6.1.7 Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi6.1.8 Elimu ya Juu6.1.9 Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Elimu6.1.10 Mikopo ya Elimu ya Juu6.1.11 Kuwianisha Mifumo ya Elimu

11

6.2 SEKTA YA AFYA6.2.1Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)6.2.2 Huduma za Maabara6.2.3 Huduma za Utafiti6.2.4 Mpango wa Taifa wa Damu Salama6.2.5 Huduma za Afya ya Kinywa6.2.6 Dawa na Vifaa Tiba6.2.7 Huduma za Mama na Mtoto6.2.8 Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI6.2.9 Udhibiti wa Ugonjwa wa Malaria6.2.10Upimaji na Tiba za Saratani ya Kizazi na Matiti6.2.11 Ajira za Watumishi wa Afya6.2.12 Mafunzo kwa Wataalam wa Afya6.2.13Kuboreshwa Huduma katika Hospitali Kuu

12

6.3 SEKTA YA MAJI6.3.1 Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini6.3.2 Uvunaji wa Maji ya Mvua6.3.3 Ujenzi wa Mabwawa ya Maji6.3.4 Uundaji wa Vyombo vya Watumiaji Maji6.3.5 Huduma ya Maji Mijini6.3.6Huduma ya Maji kwa Wasiokuwa na Uwezo6.3.7 Kupunguza Upotevu wa Maji Mijini6.3.8 Miradi Mikubwa ya Maji6.3.9 Visima Virefu vya Kimbiji na Mpera6.3.10 Ujenzi wa Bwawa la Kidunda6.3.11 Miundombinu ya Majitaka6.3.12Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za MajiSURA YA SABA7. MAENEO MENGINE MUHIMU7.1 SEKTA YA HABARI NA UTANGAZAJI7.1.1Usajili wa Magazeti, Redio na Televisheni7.1.2 Tovuti ya Wananchi

13

7.1.3 Shirika la Utangazaji Tanzania7.1.4 Mfumo wa Utangazaji wa Digiti7.2 SEKTA YA MICHEZO7.3 SEKTA YA SHERIA7.3.1 Katiba7.3.1 Utafiti na Urekebishaji wa Sheria7.3.2Uendeshaji wa Mashauri ya Madai na Jinai7.3.3 Mahakama7.3.4 Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo7.3.5 Huduma ya Usajili, Ufilisi na Udhamini7.3.2 Haki za Binadamu7.3.3 Utawala Bora7.3.4 Kuzuia na Kupambana na Rushwa7.3.5 Daftari la Kudumu la Wapiga Kura7.3.6 Muungano

14

7.3.7 SENSA YA WATU NA MAKAZI7.3.8 VITAMBULISHO VYA TAIFA7.4 ULINZI NA USALAMA7.4.1 Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)7.4.2 Uboreshaji wa Makazi ya Askari7.4.3Ujenzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC)7.4.4 Mradi wa Matrekta7.4.5 Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya7.5 HIFADHI YA MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI7.6 USAWA WA KIJINSIA7.6.1Ushiriki wa Wanawake Katika Uongozi na Maamuzi7.6.2Mapambano Dhidi ya Ukatili kwa Wanawake na Watoto7.7 MENEJIMENTI YA MAAFA7.8 KUHAMIA MAKAO MAKUU DODOMA7.9 KUZUIA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI7.10 MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

15

SURA YA NANE8. MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI8.1 SERA YA DIPLOMASIA YA UCHUMI8.2 USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA MASUALA MBALIMBALI YA KIMATAIFA8.3 KUONGEZA UWAKILISHI NJE YA NCHI KWA KUFUNGUA BALOZI MPYA8.4 MCHAKATO WA KUTAMBUA JUMUIYA YA WATANZANIA WANAOISHI UGHAIBUNI8.5 USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI8.5.1 Itifaki ya Umoja wa Forodha8.5.2Uundwaji wa Soko la Pamoja la Afrika Mashariki8.5.3Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki8.5.4Ushirikiano Katika Masuala ya Ulinzi na UsalamaSURA YA TISA9. HITIMISHO

16

ORODHA YA VIFUPISHO

AMCOS - Agricultural Marketing Cooperative SocietiesASA - Agricultural Seeds AgencyBASA - Bilateral Air Services AgreementBMUs - Beach Management UnitsBRELA - Business Registration and Licence AuthorityBRN - Big Results NowCAADP - Comprehensive African Agriculture Development ProgrammeCCM - Chama cha MapinduziCEIR - Centre for Emegency Information and ResearchCOSTECH - Commission for Science and TechnologyCRMP - Cooperative Reform and Modernization ProgrammeDAPPs - District Agricultural Development PlansDASIP - District Agricultural Sector Investment Projects

17

ENMRA - Elimu Nje ya Mfumo RasmiEPZ - Export Processing ZonesEPZA - Export Processing Zones AuthorityEWURA - Energy and Water Utilities Regulatory AgencyEWW - Elimu ya Watu WazimaIFMP - Implementation of Fisheries Management PlanIOS - International Organization for StandardizationKKK - Kusoma, Kuandika na KuhesabuKPL - Kilombero Plantation LimitedLAPF - Local Authorities Pension FundMACEMP - Marine and Coastal Environmental Management ProjectMIVARF - Marketing Infrastructure Value Addition and Rural Finance

18

SHD - Sichuan Hongda GroupSIDO - Small Industries Development OrganizationSMT - Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaSMZ - Serikali ya Mapinduzi ZanzibarSTAMICO - State Mining CorporationTANTRADE - Tanzania Trade Development AuthorityTCIMRL - Tanzania China International Mineral Resources LimitedTEHAMA - Teknolojia ya Habari na MawasilianoTFRA - Tanzania Fertilizer Regulatory AuthorityTGDC - Tanzania Geothermal Development Company LimitedTIB - Tanzania Investment BankTIC - Tanzania Investment Centre

19

TIRP - Tanzania Intermodal Rail Development ProjectMTUSATE - Mfuko wa Taifa wa Uendelezaji wa Sayansi na TeknolojiaMUKEJA - Mpango wa Uwiano Katika Elimu ya Watu Wazima na JamiiMUVI - Muunganisho wa Ujasiriamali VijijiniMVIWATA - Mtandao wa Vikundi vya Wakulima TanzaniaNARCO - National Research CompanyNDC - National Development CorporationNEMC - National Environment Management CouncilNFRA - National Food Reserve AgencyPSAs - Production Sharing AgreementsREA - Rural Energy AgencyREF - Rural Energy Fund

20

SACCOS - Savings and Credit Cooperative SocietiesSAGCOT - Southern Agriculture Growth Corridor of TanzaniaSEZ - Special Economic ZonesSHD - Sichuan Hongda GroupSIDO - Small Industries Development OrganizationSMT - Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaSMZ - Serikali ya Mapinduzi ZanzibarSTAMICO - State Mining CorporationTANTRADE - Tanzania Trade Development AuthorityTCIMRL - Tanzania China International Mineral Resources LimitedTEHAMA - Teknolojia ya Habari na MawasilianoTFRA - Tanzania Fertilizer Regulatory Authority

21

TGDC - Tanzania Geothermal Development Company LimitedTIB - Tanzania Investment BankTIC - Tanzania Investment CentreTIRP - Tanzania Intermodal Rail Development ProjectTMA - Tanzania Metrological AgencyTMAA - Tanzania Mining Audit AuthorityTNBC - Tanzania National Business CouncilTPA - Tanzania Ports AuthorityTPSF - Tanzania Private Sector FoundationTRCs - Teachers Resource CentresTRL - Tanzania Railways LimitedTSN - Tanzania Standard NewspaperUCSAF - Universal Communication Service Access FundVVU - Virusi Vya UKIMWIWMAs - Wildlife Management AreasWMO - World Metrological Agency

22

SURA YA KWANZA•UTANGULIZISerikali ya Awamu ya Nne kupitia Chama cha Mapinduzi iliingia madarakani tarehe 21 Desemba, 2005 chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kutokana na kazi nzuri iliyofanyika ya kuwaletea wananchi maendeleo, mwaka 2010, watanzania walikipa tena ridhaa Chama cha Mapinduzi kuongoza Serikali kwa kipindi kingine cha miaka mitano (2010-2015).

Katika kipindi chote cha miaka kumi, Serikali imefanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2005 na 2010 kwa kutekeleza miradi ya kipaumbele ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi. Aidha, huduma muhimu za jamii zikiwemo elimu, afya na maji zimeendelea kutolewa na Utawala Bora kuimarishwa.Taifa limeendelea kuwa na amani na utulivu na hivyo kutoa fursa kwa wananchi kufanya kazi za ujenzi wa Taifa na kujiletea maendeleo.

23

Katika kipindi cha miaka 10 ya Serikali ya Awamu ya Nne, uchumi wa nchi umekua kwa wastani wa asilimia 6.4 kwa mwaka. Ukuaji huu ni mzuri ikilinganishwa na nchi nyingi zinazoendelea kama Tanzania. Vilevile, mfumuko wa bei umeendelea kushuka, uwekezaji wa mitaji umeongezeka na pia nafasi za ajira. Sekta ya Kilimo ambayo ndiyo inayoajiri Watanzania wengi imeendelea kuimarika kupitia utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (Agricultural Sector Development Programme- ASDP).

Kupitia Programu hiyo, mwaka 2007 Serikali iliongeza msukumo kwa kutangaza azma ya KILIMO KWANZA yenye lengo la kuharakisha mapinduzi ya kilimo kwa kuwawezesha wakulima wadogo kufanya kilimo cha biashara. Sekta binafsi imeshirikishwa kikamilifu kuwekeza kwenye kilimo chenye tija kwa kushirikisha wakulima wadogo hususan kupitia Mpango wa Kuendeleza Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (Southern Agriculture Growth

24

Corridor of Tanzania - SAGCOT). Uboreshaji wa Sekta ya Kilimo umeongeza uzalishaji, upatikanaji na uhakika wa chakula ikiwa ni pamoja na ongezeko la bidhaa za kilimo zinazouzwa nje. Ujenzi wa barabara kuu na barabara za mikoa umefanyika na hivyo kuimarisha mtandao wa barabara nchini. Kutokana na juhudi hizo, mtandao wa barabara nchini umefikia jumla ya kilometa 35,000 ambapo kilometa 12,786 ni barabara kuu na kilometa 22,214 ni barabara za mikoa.

Huduma za Afya zimeendelea kuimarishwa na kuwezesha kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano. Vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua kutoka watoto 112 kwa vizazi hai 1,000 mwaka 2005 hadi vifo 54 kwa vizazi hai 1,000 mwaka 2015. Serikali pia imehakikisha wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na kufaulu wanakwenda sekondari kwa kuongeza idadi ya shule za Sekondari kutoka 1,745 mwaka 2005 hadi shule 4,576 mwaka 2015. Jitihada hizi zimeenda sambamba na ujenzi wa maabara kutoka 247 mwaka 2005 hadi 5,979 mwaka 2015. Aidha, idadi ya walimu na mabweni imeongezeka pia katika kipindi hicho.

25

Idadi ya wananchi wanaopata huduma ya umeme imeongezeka kutoka asilimia 13 mwaka 2005 hadi asilimia 36 ya Watanzania waishio Tanzania Bara mwaka 2014. Aidha, kiwango cha uunganishwaji umeme vijijini kimeongezeka na kufikia asilimia 17 mwaka 2014 kutoka asilimia 2 mwaka 2005.

Vilevile, jitihada kubwa imefanyika kuimarisha upatikanaji wa maji safi ambapo kiwango cha watu wanaopata huduma ya maji safi vijijini kimeongezeka kutoka asilimia 53.5 mwaka 2005 hadi asilimia 67.7 mwaka 2015. Serikali imeimarisha mawasiliano kwa kujenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano nchi nzima ambao umeunganishwa na Mikongo ya Mawasiliano ya Kimataifa. Kujengwa kwa mkongo huu kumepunguza gharama za mawasiliano nchini na kuchochea ukuaji wa uchumi.

26

Changamoto katika kipindi cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne zilitokana na Mdororo wa Uchumi wa Dunia ulioanza mwaka 2008 ambapo thamani ya Shilingi ya Tanzania ilishuka na hivyo kuathiri maeneo mengi ya uzalishaji. Mdororo wa uchumi umeathiri uzalishaji, ukusanyaji mapato ya ndani na pia hata upatikanaji wa fedha kutoka nje (mikopo na misaada). Hata hivyo, Serikali iliweka mkazo kuimarisha sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na viwanda ili kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa haraka.

Taarifa hii ina sura tisa (9) ambazo zimeelezea kwa kina mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne katika maeneo ya Ukuaji wa Uchumi, Sekta za Uzalishaji Mali, Huduma za Kiuchumi, Uwezeshaji Wananchi, Huduma za Jamii, Maeneo mengine Muhimu pamoja na Masuala yahusuyo Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.

27

Ni dhahiri kwamba mafanikio yaliyopatikana yametokana na juhudi kubwa zilizofanywa na viongozi katika ngazi zote kwa kushirikiana na wananchi. Kama ilivyo kwa Serikali yoyote inayomaliza kipindi chake, kuna kazi zilizoanza kutekelezwa ambazo zitakamilishwa na Serikali ya Awamu ya Tano kama ambavyo Serikali ya Awamu ya Nne ilikamilisha kazi zilizoanzishwa na Serikali ya Awamu ya Tatu.

Huu ndio msingi wa Dhana ya Utawala Bora ya kuendelea kutekeleza Mikakati na Mipango iliyoanzishwa kwa maslahi mapana ya wananchi wote na Taifa kwa ujumla. Watanzania wote wana wajibu wa kuyalinda mafanikio yaliyopatikana na kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea mafanikio zaidi.

28

SURA YA PILI•KUJENGA MSINGI WA UCHUMI WA KISASA WA TAIFA LINALOJITEGEMEASerikali ya Awamu ya Nne imechukua hatua madhubuti zinazolenga kujenga Taifa linalojitegemea kwa kukuza uchumi na kupunguza umaskini. Moja ya hatua hizo ni kuunda upya Tume ya Mipango, chini ya Ofisi ya Rais, na kuifanya kuwa chombo cha kubuni na kuishauri Serikali kuhusu sera na mikakati ya kiuchumi ya nchi yetu kwa upeo wa muda wa kati na muda mrefu. Kupitia Tume hiyo, Serikali imeitafsiri Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kwa kuandaa Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Miaka Kumi na Mitano (2011-2025) unaotekelezwa kwa vipindi vya miaka mitano mitano. Mpango wa kwanza wa Miaka Mitano ulianza kutekelezwa mwaka 2011/2012 na kumalizika mwaka 2015/2016. Ili kuharakisha utekelezaji wa Mpango wa Miaka Mitano na kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Serikali imeanzisha mfumo wa utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya mipango na Programu za maendeleo ya Taifa ujulikanao kama

29

“Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa” (Big Result Now – BRN!). Chini ya mfumo huo, miradi michache ya kipaumbele yenye uwezo wa kutoa matokeo makubwa kwa kipindi kifupi imeanishwa na kuanza kutekelezwa. Ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi hiyo unafanywa na chombo maalum kilichoundwa chini ya Ofisi ya Rais, Ikulu kijulikanacho kama President’s Delivery Bureau. Tayari miradi katika maeneo sita (6) imeshaanza kutekelezwa kupitia mfumo huo. Maeneo hayo ni Elimu, Maji, Uchukuzi, Kilimo, Nishati na Kuongeza Mapato ya Serikali.

Vilevile, Serikali imeainisha vikwazo vinavyokwamisha uwekezaji wa kasi wa Sekta Binafsi na kuanza kuvitafutia ufumbuzi chini ya BRN! Katika juhudi za kuboresha mazingira ya biashara maeneo sita ya kipaumbele yanatiliwa mkazo. Aidha, ili kufikisha huduma za afya karibu zaidi na wananchi, sekta ya afya imepewa msukumo mpya chini Mfumo wa Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa!

30

UKUAJI WA UCHUMI

• Pato la Taifa

Pato la Taifa kwa bei za soko limeendelea kuongezeka mwaka hadi

mwaka kutoka Shilingi milioni 19, 112,830 mwaka 2005 na kufikia

Shilingi milioni 79, 442,499 mwaka 2014 sawa na ongezeko la

Shilingi milioni 60,329,669. Tanzania ni moja ya nchi ambazo

uchumi wake umekua kwa kasi katika kipindi cha miaka 10

iliyopita. Ukuaji wa uchumi katika kipindi hicho ni wastani wa

asilimia 6.4 kwa mwaka, kiwango ambacho kinaridhisha

ikizingatiwa kuwa mwaka 2008 ulitokea mtikisiko wa kiuchumi

duniani na kuathiri Sekta mbalimbali za uchumi. Shughuli za

kiuchumi zilizochangia ukuaji huo ni pamoja na kilimo,

mawasiliano,viwanda,ujenzi na huduma.

31

Jedwali Na. 1: Mwenendo wa Pato la Taifa kwa Bei za Soko 2005- 2014

Mwaka Pato Ghafi la Taifa (000 SHS.)

Ongezeko Asilimia (%)

2005 19,112,830

2006 23,298,435 4,185,605 21.89

2007 26,770,432 3,471,997 14.90

2008 32,764,940 5,994,508 22.39

2009 37,726,824 4,961,884 15.14

2010 43,836,018 6,109,194 16.19

2011 52,762,581 8,926,563 20.36

2012 61,434,214 8,671,633 16.43

2013

2014

70,953,227

79,442,499

9,519,013

8,489,272

15.49

11.96

Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu

32

•Udhibiti wa Mfumuko wa BeiSerikali ya Awamu ya Nne imechukua hatua kadhaa za kudhibiti mfumuko wa bei ambao ulipanda kuanzia mwaka 2010 na kufikia asilimia 19.8 mwaka 2012 kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani. Hatua hizo ni pamoja na kupanua kilimo cha mazao ya chakula kwa kuongeza upatikanaji wa pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea, madawa na mbegu bora; kutekeleza mpango wa kulipa madeni ya kampuni za ufuaji umeme na kupandisha kiwango cha riba ya Benki Kuu inayotozwa kwa mikopo iendayo kwa taasisi za fedha nchini kutoka asilimia 7.58 hadi asilimia 12.58. Kutokana na juhudi hizo, mfumuko wa bei umedhibitiwa na kupungua hadi asilimia 5.6 mwaka 2013 na kuendelea kubakia kwenye tarakimu moja kama ilivyokuwa mwaka 2005 ulipokuwa wastani wa asilimia 4.35. Hadi kufika mwezi Machi, 2015 mfumuko wa bei ulifikia asilimia 4.3.

Mwaka 2005 2006 2007 2008 2009 2010 2011 2012 2013 2014

Mfumuko wa bei

4.35 6.7 6.4 13.5 12.2 5.6 19.8 12.1 5.6 4.8

Jedwali Na. 2: Wastani wa Mfumuko wa Bei 2005-2015 (%)

Chanzo: Ofisi ya Takwimu ya Taifa, miaka mbalimbali

33

•Kupungua kwa UmaskiniPato la wastani la Mtanzania limeongezeka kutoka Shilingi 360,865 mwaka 2005 hadi Shilingi 1, 725,290 mwaka 2014. Aidha, kwa mujibu wa Utafiti wa Mapato na Matumizi katika Kaya uliofanyika mwaka 2012, umaskini wa kipato (watu wanaoishi chini ya Shilingi 1,216 za Kitanzania kwa siku) umepungua kutoka wastani wa asilimia 34.4 mwaka 2007 hadi asilimia 28.2 mwaka 2012 sawa na wastani wa asilimia 6.2.

Vilevile, umaskini wa chakula (watu wanaotumia chini ya Shilingi 858 kwa matumizi ya chakula kwa siku) umepungua kwa wastani wa asilimia 2.1 kutoka asilimia 11.8 mwaka 2007 hadi asilimia 9.7 mwaka 2012. Hii inaonesha kuwa ukuaji wa uchumi unawafikia wananchi wengi na hivyo kupunguza umaskini wa kipato.

34

•Mapato ya Serikali

Mapato ya Ndani yameongezeka kutoka Shilingi bilioni 2,124.8 mwaka 2005 hadi Shilingi bilioni 10,510.56 Juni, 2014 sawa na ongezeko la asilimia 438.6. Ongezeko hilo limechangiwa na jitihada za Serikali kuendelea kuimarisha usimamizi wa ukusanyaji wa mapato ya kodi na yasiyo ya kodi pamoja na kuongezeka kwa shughuli za uchumi. Mafanikio hayo yametokana na hatua zilizochukuliwa na Serikali kudhibiti ukwepaji wa kodi kwa kuhakikisha kwamba kila anayestahili kulipa kodi analipa ipasavyo.

Hatua hizo ni pamoja na kupitia na kuimarisha matumizi ya mashine za utunzaji kumbukumbu za hesabu za biashara, kudhibiti biashara ya mafuta kwa kuweka vinasaba kwenye mafuta na kuongeza kodi kwenye mafuta ya taa ili kuondokana na tatizo la uchakachuaji wa mafuta ambao unasababisha upotevu mkubwa wa mapato ya Serikali. Kuongezeka kwa mapato hayo kumeiwezesha Serikali kuimarisha upatikanaji wa huduma za jamii pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

35

•Bajeti ya SerikaliKatika kipindi cha miaka kumi iliyopita (2005-2015) shughuli za Serikali zimepanuka kwa kiwango kikubwa na hivyo, kuongeza bajeti ya Serikali mwaka hadi mwaka. Bajeti ya Serikali imeongezeka kutoka Shilingi trilioni 4.18 mwaka 2005/2006 hadi Shilingi trilioni 19.67 katika mwaka 2014/2015 ikiwa ni ongezeko la Shilingi trilioni 14.49. Shughuli za Serikali na bajeti zimepanuka katika sekta za kipaumbele za kilimo, elimu, maji, umeme, afya na miundombinu.

Kufuatia ongezeko hilo, huduma mbalimbali zimeweza kuwafikia wananchi hususan walioko vijijini ambao hapo awali hawakuwa na huduma hizo muhimu za kiuchumi na kijamii.

36

USIMAMIZI WA FEDHA ZA SERIKALI

Serikali imeendelea kusimamia matumizi ya fedha za Umma kwa kuboresha mifumo ya kusimamia matumizi na kuiwezesha Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Hii ni pamoja na kupitisha Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya Mwaka 2008. Hatua nyingine zilizochukuliwa ni pamoja na kuongeza uwazi wa kujadili Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kupitia Bunge na kulipa Bunge uwezo mkubwa wa kushauri na kusimamia matumizi ya fedha za umma.

Juhudi hizo zimeendelea kuimarisha nidhamu ya matumizi ya fedha katika Ofisi, Wizara na Taasisi za Umma. Mathalan, Halmashauri zinazopata Hati Safi zimeongezeka kutoka asilimia 53 mwaka 2005 hadi asilimia 80 mwaka 2013. Aidha, watumishi wanaobainika kufanya ubadhirifu wa fedha za Umma wanachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

37

Hali ya akiba za fedha za kigeni hadi mwezi imekuwa ya kuridhisha kutokana na kuongezeka kwa mikopo ya kibiashara kutoka nje na kupungua kwa matumizi ya Serikali nje ya nchi. Akiba ya fedha za kigeni ilifikia Dola za Marekani milioni 4,388.6 mwishoni mwa mwezi Desemba, 2014 kiasi ambacho kinatosheleza uagizaji bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa zaidi ya miezi 4. Benki Kuu inaendelea kushiriki katika soko la fedha za kigeni kwa lengo la kuweka viwango sahihi vya ukwasi vinavyoendana na shughuli za kiuchumi.

MAENDELEO YA SEKTA BINAFSI• Maboresho ya Sera na Sheria

Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya biashara ili Sekta Binafsi iweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali na kufanya biashara nchini. Mazingira hayo yameboreshwa kwa kuandaa Sera, Sheria na Kanuni za Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Mwaka 2009, Serikali iliandaa Sera ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na kufuatiwa na maandalizi ya Sheria na Kanuni mwaka 2010. Sera, Sheria na Kanuni hizo zimeweka miongozo ya ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili kuongeza uwekezaji nchini.

38

Mwezi Aprili 2012, Serikali ilifanya marekebisho ya Sheria nne (4) zilizokuwa zinakinzana na Mazingira Wezeshi ya Biashara. Sheria hizo ni: Business Names (Registration) Act (Cap.213) kwa lengo la kupanua wigo wa uteuzi wa Wasajili wa Biashara ili kusogeza huduma ya usajili wa majina ya biashara karibu zaidi na wananchi; Companies Act (Cap. 212) ili kuruhusu uwepo wa kampuni zenye mwanahisa mmoja tofauti na awali ambapo ilitakiwa zaidi ya mtu mmoja kuanzisha na kusajili kampuni; Tanzania Trade Development Authority Act (Cap. 155) ili kuruhusu Taasisi ya TANTRADE kukusanya, kutangaza na kusambaza taarifa zinazohusu biashara na uwekezaji kwa wafanyabiashara na wawekezaji; na Merchandise Act (Cap. 355) ili kutoa tafsiri ya hakimiliki (Intellectual Property Rights) na bidhaa bandia na kuzuia utangazaji na uanzishaji wa tovuti za kuonesha bidhaa bandia.

Mabadiliko ya sheria hizo yatachangia kurahisisha ufanyaji biashara hapa nchini na hivyo kuongeza mchango wa sekta binafsi kwenye uchumi. Aidha, kutokana na umuhimu wa kuboresha mazingira ya biashara, Serikali imeandaa utaratibu wa kujumuisha suala la uboreshaji wa mazingira ya biashara katika mpango wa Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa (BRN!). Ili kuimarisha ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi imehusishwa na sasa itawezesha ubia huu kufanyika kwa ufanisi zaidi.

39

Ushiriki wa Sekta Binafsi katika kuendesha Uchumi

Serikali imeendelea kuratibu mashauriano na majadiliano kati ya Serikali na Sekta Binafsi kupitia Baraza la Taifa la Biashara (Tanzania National Business Council – TNBC). Baraza limeimarishwa na kuwa mhimili mkuu katika kuongoza majadiliano hayo kwa maendeleo ya nchi. Majadiliano yanafanywa baina ya pande hizi mbili kupitia Mabaraza ya Biashara yaliyoundwa katika ngazi ya Mikoa na Wilaya. Mafanikio yaliyopatikana kutokana na juhudi hizo ni pamoja na kubainisha kwa pamoja maeneo ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa kuzingatia mapendekezo na maazimio ya mikutano iliyofanyika kati ya Serikali na Wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi.

Serikali imewezesha mashauriano yenye tija kati yake na Sekta Binafsi kwa kuratibu na kusimamia zoezi la kuboresha mfumo wa uongozi wa Taasisi ya Kuendeleza Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation -TPSF). Zoezi hilo limeweka mfumo shirikishi utakaoiwezesha Taasisi hiyo kuwa na uwakilishi mpana zaidi wa makundi mbalimbali ya sekta binafsi yanayowakilishwa na Vyama vya Kibiashara. Chini ya mfumo huo mpya, Taasisi ya Sekta Binafsi imekuwa na sauti moja na uwezo mkubwa zaidi wa kutetea maslahi ya wanachama wake na pia kukabiliana na changamoto mbalimbali za Sekta Binafsi kwa pamoja.

40

Kuimarisha Bandari na Vituo vya Mpakani

Serikali imechukua hatua za kuboresha utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam ambapo, muda wa kutoa mizigo bandarini umepungua kutoka siku 12 mwaka 2011 hadi kufikia wastani wa siku 3 mwaka, 2015. Aidha, Serikali imeanzisha Kituo Kimoja cha Utoaji wa Huduma (One Stop Centre) kwenye Bandari ya Dar es Salaam ambapo wadau wote wanaotoa huduma bandarini hufanya kazi kwa kutumia mfumo mmoja wa Kompyuta ujulikanao kama Electronic Single Window System (ESWS). Hatua hiyo imeongeza ufanisi na kupunguza muda wa kutoa mzigo bandarini kufikia wastani wa siku 5 hadi 3, kiwango kinachopendekezwa kimataifa.

41

Aidha, ujenzi wa Vituo vya Utoaji wa Huduma kwa Pamoja Mipakani (One Stop Border Posts) katika mipaka ya Holili, Sirari na Mutukula ulikamilika na Kituo cha Holili kimekabidhiwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya uendeshaji. Ujenzi wa Vituo vingine vinne katika mipaka ya Horohoro/Lungalunga, Kabanga/Kobelo, Tunduma/Nakonde na Rusumo unaendelea na inatarajiwa utakamilika ifikapo mwishoni mwa mwaka 2014.

Vituo vya Utoaji wa Huduma kwa pamoja Mipakani vitawezesha huduma za kiforodha, uhamiaji, udhibiti wa ubora, viwango, usalama wa bidhaa na usalama kwa ujumla kukamilishwa katika upande mmoja wa mpaka. Hii ni tofauti na utaratibu wa sasa ambapo huduma hizo hufanyika katika pande zote za mipaka na hivyo kutumia muda mwingi katika kukamilisha taratibu hizo za forodha.

42

Jengo Jipya la kutolea Huduma mpakani, Horohoro Tanga

43

Usimamizi Sekta ya Fedha Serikali imeendelea kusimamia Sekta ya Fedha ambapo hadi kufikia Desemba 2014, jumla ya Benki zilizosajiliwa na kusimamiwa na Benki Kuu na kuanza kutoa huduma zimefikia 57 zenye matawi 660 nchi nzima. Upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi umeendelea kuongezeka kutokana na ubunifu wa mipango ya utoaji wa huduma za malipo ya rejareja kupitia simu za mikononi na huduma za uwakala wa mabenki (Agent banking services).

Kuongezeka kwa idadi ya benki na kupanuka mtandao wa matawi kumewezesha benki nyingi kufungua matawi yake Tanzania Bara na Zanzibar. Baadhi ya benki ambazo zina matawi pande zote mbili za Muungano ni NMB Bank Plc, CRDB Bank Plc, Exim Bank (T) Ltd na Tanzania Postal Bank.

44

Serikali pia imeendelea kusimamia Sekta ya Benki kwa kuendelea kuziongezea Benki zake mitaji ili ziweze kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi. Tathmini ya hali ya benki inaonesha kuwa, Sekta ya Benki nchini imeendelea kuwa imara na salama. Pamoja na mambo mengine, Benki hizo zina mitaji na ukwasi wa kutosha. Kiwango cha mitaji ikilinganishwa na mali iliyowekezwa kimeendelea kuongezeka na kufikia wastani wa asilimia 17.8 ikilinganishwa na kiwango cha asilimia 12 kinachotakiwa.

Kiwango cha mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu ikilinganishwa na kiwango cha amana kinachoweza kuhitajika katika muda mfupi kilifikia asilimia 37.1 ikilinganishwa na kiwango kinachohitajika kisheria cha asilimia 20 au zaidi. Aidha, hadi kufikia Desemba 2014, mabenki mengi yametimiza masharti mapya ya kuongeza mtaji kutoka Shilingi bilioni 5 hadi bilioni 15.

Riba katika masoko ya fedha zimeendelea kutegemea nguvu ya soko na hali ya ukwasi unaotokana na Sera za Fedha na Bajeti. Katika kipindi kilichoishia Novemba 2014, riba za dhamana za Serikali zilikuwa na wastani wa asilimia 13.8 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 14.8 katika kipindi cha Novemba

45

2013. Aidha, riba za mikopo kutoka kwenye benki zilibakia kwenye wastani wa asilimia 15.9 wakati zile za amana zikiwa kwenye wastani wa asilimia 8. Hata hivyo, riba za mikopo zinatarajiwa kushuka kutokana na kupungua kwa kasi ya mfumuko wa bei pamoja na matokeo ya uendeshwaji wa Mfumo wa Taarifa za Wakopaji.

Aidha, uamuzi wa Benki Kuu kupunguza sehemu ya amana za Sekta Binafsi ambazo benki zinatakiwa kuhifadhi katika Benki Kuu unatarajiwa kupunguza gharama za mitaji na hivyo kusababisha kushuka kwa riba za mikopo. Kutokana na jitihada hizo, hadi mwezi Desemba 2014, utoaji mikopo kwenye sekta binafsi umeongezeka na kufikia asilimia 20.

46

UWEKEZAJI NCHINISerikali imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja na kuangalia upya sera, miundo na sheria mbalimbali kuhusu ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi. Kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya biashara nchini, Taarifa ya Ulimwengu kuhusu Uwekezaji ya mwaka 2015 imeitaja Tanzania kuongoza nchi nyingine za Afrika Mashariki katika kuvutia wawekezaji kutoka nje. Takwimu zinaonesha kuwa thamani ya mitaji ya uwekezaji kutoka nje imeongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 1,229.4 mwaka 2011 hadi milioni 2,142 mwaka 2014 sawa na ongezeko la asilimia 74.2. Ongezeko hilo limechangiwa zaidi na sekta ya mafuta na gesi.

Uwekezaji katika shughuli za umeme na gesi uliongezeka kwa kasi kubwa kutoka uwekezaji wa chini ya Dola za Marekani milioni 3.0 mwaka 2008 hadi Dola za Marekani milioni 290.4 mwaka 2013. Kutokana na uwekezaji huo, jumla ya futi za ujazo trilioni 53.2 za gesi zimekwishagunduliwa nchini. Aidha, katika kipindi hicho kumekuwa na ongezeko la uwekezaji katika ujenzi wa miundombinu, kilimo na viwanda, ujenzi na uchukuzi ambavyo vimeendana na ongezeko la ajira katika sekta hizo.

47

Sekta Idadi ya Miradi

Miradi mipya Miradi ya upanuzi

Miradi ya wazawa

Miradi ya wageni

Miradi ya ubia

Ajira Dhamani ya wekezaji US$ M

Kilimo 382 285 97 150 114 118 171,795 12,287.72

Maliasili 49 37 12 14 11 25 9,320 181.83

Utalii 1,809 1342 467 1128 305 376 94,884 6,726.82

Uzalishaji Viwandani 2062 1605 457 762 717 583 201,214 12,559.80

Mafuta na Madini 11 7 4 3 3 5 1,014 123.59

Majengo ya Biashara 1,087 916 170 606 242 236 145,372 8,991.97

Usafirishaji 1,100 864 236 675 193 232 107,159 5,989.63

Huduma 145 128 17 28 62 55 17,711 1,459.65

Kompyuta 12 10 2 2 5 5 345 50.96

Huduma za Fedha 62 32 30 13 15 34 12,762 368.27

Mawasiliano 70 53 17 19 13 37 29,958 13,417.60

Nishati 40 36 4 16 8 17 10,411 5,431.38

Rasilimali Watu 248 198 50 169 34 45 21,656 992.17

Miundombinu 41 32 9 22 6 13 141,497 84,836.46

Utangazaji 47 40 7 40 2 5 3,687 436.55

JUMLA 7,165 5,585 1,579 3,647 1,730 1,786 968,785 153,854.41

Jedwali Na.3: Miradi iliyosajiliwa nchini Januari, 2005 hadi Juni, 2014

Chanzo: Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), 2014.

48

SURA YA TATUSEKTA ZA UZALISHAJI MALI

i. KILIMO Serikali imechukua hatua za kuimarisha Sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya kijani kwa kuanzisha na kutekeleza Mipango na Programu mbalimbali zinazolenga kuendeleza Sekta ya Kilimo nchini.

Mikakati ya kuleta Mapinduzi ya KilimoKatika kipindi cha miaka 10 ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne, Sekta ya Kilimo imeimarishwa kwa kiwango kikubwa. Serikali imetekeleza kwa mafanikio Programu mbili kuu ambazo ni Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (Agricultural Sector Development Programme –ASDP) na Programu ya Mageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika (Cooperative Reform and Modernization Programme – CRMP). Aidha, Serikali ilitangaza azma ya KILIMO KWANZA kwa lengo la kuongeza msukumo zaidi katika sekta ya kilimo na kuleta mapinduzi ya kilimo kwa kuwezesha wakulima wadogo kufanya kilimo cha kibiashara.

49

Kupitia azma hiyo, Serikali imeendeleza jitihada za kushirikisha sekta binafsi katika kuwekeza kwenye kilimo kupitia mipango mingine kama vile Mpango wa Kuendeleza Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (Southern Agriculture Growth Corridor of Tanzania –SAGCOT) na Programu ya Kuendeleza Kilimo Afrika (Comprehensive African Agriculture Development Programme – CAADP) ambapo Mpango wa Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo (Tanzania Agriculture and Food Security Investment Plan –TAFSIP) umeandaliwa.

Kupitia Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo I (ASDP I), iliyoanza kutekelezwa mwaka 2006, Serikali imezijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kupanga na kutekeleza Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (District Agricultural Development Plans-DADPs). Serikali imehakikisha kuwa asilimia 75 ya rasilimali zinazowekezwa chini ya ASDP zinaelekezwa katika wilaya na vijiji kupitia DADPs kwa lengo la kuongeza tija ya rasililimali hizo katika kilimo.

50

Kutokana na juhudi hizo za Serikali, uzalishaji wa chakula nchini umeongezeka kutoka tani milioni 9.66 mwaka 2005 hadi tani milioni 16.0 mwaka 2014. Kati ya kiasi hicho, tani milioni 9.8 ni nafaka na tani milioni 6.2 ni mazao yasiyo nafaka. Kutokana na ongezeko hilo, taifa limeweza kujitosheleza kwa chakula kwa wastani wa asilimia 125 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 95 mwaka 2005. Utoshelevu huo ni asilimia 121 nafaka na mazao yasiyo ya nafaka ni asilimia 134. Ongezeko la uzalishaji wa chakula limesababisha bei za vyakula kushuka na hivyo kuchangia kupunguza mfumuko wa bei.

Ongezeko la Bajeti ya KilimoSerikali imeendelea kuongeza bajeti ya Sekta ya Kilimo mwaka hadi mwaka. Mwaka 2005/2006 bajeti ya Sekta ya Kilimo ilikuwa Shilingi Bilioni 233.3 na mwaka 2014/2015 bajeti ilifikia Shilingi Bilioni 1,084.7 ikiwa ni ongezeko la Shilingi Bilioni 851.4 sawa na asilimia 365. Ongezeko hili limewezesha kuongezeka kwa uwekezaji katika sekta ya kilimo.

51

• Mpango wa Uwekezaji wa Ukanda wa Kusini (SAGCOT)Serikali imeanzisha mpango wa kukibadilisha kilimo kutoka kilimo cha kujikimu na kuwa cha kisasa na cha kibiashara kwa kutumia mitaji, teknolojia na ubunifu. Dhana hii inatekelezwa kwa kuanzisha Kanda za kilimo kulingana na hali ya hewa, aina za udongo na masuala mengine muhimu. Kwa kuanzia, Serikali imeanza kutekeleza dhana hiyo katika ukanda wa kusini unaojulikana kama Southern Agriculture Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT).

Kituo cha Kuratibu Utekelezaji wa Mpango huo (SAGCOT Centre) kimeanzishwa. Mafanikio ya Mpango huo ni pamoja na uwekezaji uliofanywa na Kampuni ya ‘Kilombero Plantation Limited’ (KPL) katika uzalishaji wa mpunga katika shamba la Mngeta, Wilayani Kilombero ambapo wakulima wadogo zaidi ya 3,000 kutoka katika vijiji vinavyozunguka shamba hilo wamenufaika na uwekezaji huo kwa kupata teknolojia mpya na soko la mazao yao. Wakulima hao wameweza kuongeza uzalishaji wa mpunga kutoka tani mbili (2) hadi nane (8) kwa hekta.

52

Kupitia SACGOT, maeneo zaidi ya uwekezaji yanaendelea kuainishwa na kupimwa. Tayari shamba la Ngalimila wilayani Kilombero lenye ukubwa wa hekta 5,128 limepimwa. Vilevile, upimaji wa eneo lenye ukubwa wa hekta 105,000 unaendelea kukamilishwa ikiwa ni pamoja na kuwekewa mipango ya matumizi bora ya ardhi tayari kwa uwekezaji. Utaratibu huu umewezesha wakulima wadogo kuunganishwa na masoko na kupata pembejeo kwa uhakika zaidi.

• Ruzuku ya Pembejeo Serikali imeendelea kutekeleza Mpango wa Ruzuku ya Pembejeo kwa kuongeza bajeti kutoka Shilingi bilioni 7.5 mwaka 2005/2006 hadi Shilingi bilioni 299.3 mwaka 2013/2014, ongezeko la Shilingi bilioni 291.8 sawa na asilimia 3,891. Kutokana na juhudi hizo, upatikanaji wa pembejeo za kilimo hususan mbolea, mbegu bora na dawa za mimea umeongezeka. Upatikanaji wa mbolea uliongezeka kutoka tani 241,753 mwaka 2005/2006 hadi kufikia tani 342,798 mwaka 2014/2015. Upatikanaji huo wa mbolea kwa wakulima ni sawa na asilimia 70.7 ya makisio ya mahitaji ya mbolea ya tani 485,000 kwa mwaka.

 

53

Kwa ujumla, Kaya milioni 2.5 za wakulima zimenufaika na ruzuku ya mbolea, mbegu bora za mahindi na mbegu bora ya mpunga hadi kufikiamwaka 2013/2014.

Kutokana na ruzuku ya pembejeo, wakulima walionufaika waliongeza tija na uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga. Uzalishaji wa mahindi umeongezeka kutoka wastani wa gunia 5 hadi gunia 15 kwa ekari moja. Uzalishaji wa mpunga umeongezeka kutoka wastani wa gunia 4 hadi gunia 20 kwa ekari moja.

Kutokana na ongezeko hilo, idadi ya wakulima wanaonufaika na pembejeo za kilimo kwa utaratibu wa vocha imeongezeka ambapo mwaka 2008/2009 kaya 737,000 zilinufaika na ilipofika mwaka 2013/2014, Serikali ilitoa ruzuku zilizonufaisha kaya 932,100 ambazo zilitumia tani 124,685 za mbolea na tani 9,621 za mbegu.

54

Matumizi ya Zana Bora za KilimoSerikali imeendelea kuhimiza matumizi ya zana bora za kilimo ambapo matrekta yanayotumika kwa kilimo (operational) yameongezeka kutoka 7,210 mwaka 2005 hadi 10,064 mwaka 2014. Matrekta ya mkono (power tillers) yameongezeka kutoka 281 mwaka 2005 hadi 6,348 mwaka 2014. Mwaka 2012, Serikali iliingiza matrekta na zana nyingine za kilimo 1,860 na kuuzwa kwa bei nafuu kwa wakulima kupitia mikopo kwa vikundi vya wakulima. Aidha, majembe yanayokokotwa na wanyama yameongezeka kutoka 1,307,655 hadi 1,589,258. Upatikanaji wa zana hizo umewezesha kuongezeka kwa eneo linalolimwa kwa kutumia trekta kufikia asilimia 14 kutoka asilimia 10 mwaka 2005 na eneo linalolimwa kwa wanyama kazi kutoka asilimia 20 hadi asilimia 24 katika kipindi hicho. Aidha, matumizi ya jembe la mkono yamepungua kutoka asilimia 70 hadi asilimia 62.

55

Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akikagua Powertillers na zana nyingine za mafunzo baada ya kufungua Kituo cha Utafiti na Mafunzo ya Wakulima kilichopo Dakawa

Mkoani Morogoro

56

Ruzuku ya ViuatilifuSerikali imeendelea kutoa ruzuku ya viuatilifu kwa wakulima wanaozalisha zao la korosho katika Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Tanga, na Pwani. Zaidi ya tani 8,600 za dawa na lita 980,000 za dawa ya maji za ruzuku ya viuatilifu vya zao la korosho zimetolewa na kusambazwa kwa wakulima kuanzia mwaka 2005 hadi 2014. Aidha, ruzuku ya viuatilifu vya zao la pamba ilitolewa kwa wakulima wa Mikoa ya Shinyanga, Mara, Kigoma, Manyara, Mwanza, Singida, Tabora, Iringa, Morogoro na Pwani. Viuatilifu vilivyotolewa vilitosheleza eneo la ekari 1,537,500 na wakulima 576,710 wamenufaika na ruzuku hiyo. Pamoja na viuatilifu vya zao la pamba, Serikali pia ilitoa ruzuku za mbegu ya pamba kwa wakulima 576,710 katika mikoa inayozalisha zao la pamba. Ruzuku pia ilitolewa kwa ajili ya uzalishaji wa miche bora ya chai na kahawa na kusambazwa kwa wakulima. Hadi kufikia mwaka 2013/2014, ruzuku iliyotolewa imefanikisha uzalishaji wa zaidi ya miche bora ya chai milioni 30 na miche bora ya kahawa milioni 40 ambayo ilisambazwa kwa wakulima katika maeneo yanayolima mazao hayo.

57

•Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo

Serikali imeendeleza jitihada katika kuongeza uzalishaji wa mbegu bora ambapo upatikanaji umeongezeka kutoka tani 10,477 mwaka 2005 hadi kufikia tani 36,410.46 Aprili, 2015 sawa na ongezeko la asilimia 248. Kiasi hiki ni sawa na asilimia 60 ya mahitaji. Makisio ya mahitaji ya mbegu bora za kilimo zikiwemo mbegu za nafaka, mikunde, mbegu za mafuta na mboga ni tani 60,000 kwa mwaka ambapo uzalishaji wa ndani umefikia tani 21,407.29 kwa mwaka na uingizaji wa mbegu kutoka nje ya nchi ni tani 15,003.17 kwa mwaka. Hivyo, upungufu ni tani 23,589.54.

• Huduma za UganiSerikali imeongeza udahili wa wanafunzi wanaojiunga na vyuo katika fani ya kilimo kwa lengo la kufikisha huduma za ugani kwa wakulima wengi zaidi. Idadi ya vyuo vinavyotoa mafunzo ya kilimo imeongezeka kutoka vyuo 9 mwaka 2005 hadi kufikia vyuo 15 mwaka 2014. Wahitimu wote wanaofaulu wamekuwa wakiajiriwa moja kwa moja na Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali za Mitaa kila mwaka. Idadi ya Maafisa ugani walioajiriwa na Serikali imeongezeka kutoka 3,379 mwaka 2005 hadi 7,974 mwaka 2014 ambapo maafisa ugani 5,119 walikuwa na Astashahada na 2,855 Stashahada. Lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila Kijiji kinakuwa na afisa ugani.

58

Serikali imeendelea kutoa vitendea kazi kwa maafisa ugani ili kuboresha huduma za ugani kwa wakulima. Pikipiki 2,343 na baiskeli 3,389 zimenunuliwa na kugawiwa kwa maafisa ugani kote nchini. Aidha, magari 106 yamenunuliwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya shughuli za huduma za ugani. Serikali imeandaa na kusambaza Mwongozo wa Kuanzisha na Kuendesha Mashamba Darasa kwenye Halmashauri zote nchini kwa lengo la kuongeza mbinu shirikishi katika huduma za ugani. Mbinu shirikishi imewawezesha wataalam wa kilimo kuwafikia wakulima wengi kwa wakati mmoja na hivyo, kuwezesha kuongezeka kwa Mashamba Darasa kutoka 1,965 yenye wakulima 51,623 mwaka 2006 hadi mashamba darasa 16,512 yenye jumla ya wakulima 345,106 mwaka 2014. Kutokana na jitihada hizo, kiwango cha wakulima wanaopata huduma za ugani kimeongezeka kutoka asilimia 35 mwaka 2005 hadi asilimia 45 mwaka 2014.

•Udhibiti wa Mbegu na Mbolea Serikali imeanzisha Wakala wa Mbegu wa Taifa (Agricultural Seed Agency-ASA) kwa lengo la kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora kwa bei nafuu. ASA imeunda ushirikiano na Jeshi la Kujenga Taifa na Jeshi la Magereza ambapo kupitia mkakati huo imezalisha miche bora ya matunda 487,000 na vipando vya muhogo 15,641,866 na miche bora ya matunda 55,165,251. Vilevile, ASA imezijengea uwezo kampuni binafsi za mbegu za Watanzania 14 kwa kuzipatia mafunzo ya teknolojia ya uzalishaji wa mbegu bora.

59

Udhibiti wa Mbegu na Mbolea Serikali imeanzisha Wakala wa Mbegu wa Taifa (Agricultural Seed Agency-ASA) kwa lengo la kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora kwa bei nafuu. ASA imeunda ushirikiano na Jeshi la Kujenga Taifa na Jeshi la Magereza ambapo kupitia mkakati huo imezalisha miche bora ya matunda 487,000 na vipando vya muhogo 15,641,866 na miche bora ya matunda 55,165,251. Vilevile, ASA imezijengea uwezo kampuni binafsi za mbegu za Watanzania 14 kwa kuzipatia mafunzo ya teknolojia ya uzalishaji wa mbegu bora.

Serikali imeanzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Regulatory Authority-TFRA) ili kuhakikisha kuwa mbolea inayouzwa kwa wakulima ina ubora unaotakiwa kisheria. Hadi mwaka 2013/2014, Mamlaka hiyo imesajili wafanyabiashara wa mbolea 720 na kuwapa leseni za kufanya biashara ya mbolea na bidhaa nyingine zinazohusika na mbolea. Aidha, tafiti mbalimbali za mbolea ikiwemo mbolea ya Minjingu Rock Phosphate ziliendelea kufanyika katika Vituo vya Utafiti vilivyopo katika Kanda za Mashariki, Nyanda za Juu Kusini na Nyanda za Juu Kaskazini na Kanda ya Ziwa. Utafiti huo umeonesha

60

Zao 2005/06 2006/07 2007/08 2008/09 2009/10 2010/11 2011/12 2012/13 2013/14

Pareto 2,800 1,500 2,300 1,500 3,320 5,000 5,600 6,100 7,000

Tumbaku 56,463 65,299 57,454 58,702 60,900 130,000 93,000 74,240 100,000

Korosho 77,158 92,232 99,107 79,068 74,169 121,070 127,000 121,704 127,939

Mkonge 27,000 27,794 33,000 33,208 26,363 35,000 35,000 23,344 41,104

Sukari 263,317 192,535 265,434 279,605 279,850 263,461 317,000 286,380 293,011

kwamba mbolea ya Minjingu inafaa kutumiwa kwenye maeneo mengi nchini na hivyo kuongeza tija na uzalishaji. •Uzalishaji wa Mazao nchiniSerikali imeimarisha uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini kote ambapo tija na uzalishaji wa mazao mengi umeongezeka. Jedwali Na.4 linaonesha ongezeko la baadhi ya mazao muhimu ya biashara.

Jedwali Na.4: Mwenendo wa Uzalishaji wa Mazao ya Asili ya Biashara (tani) 2005/2006 – 2013/14

61

•Akiba ya Chakula ya Taifa

Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (National Food Reserve Agency – NFRA) imekuwa ikitenga fedha kila mwaka kwa ajili ya ununuzi wa akiba ya chakula na kukihifadhi kwa ajili ya tahadhari ya kukabiliana na upungufu wa chakula unaoweza kutokea kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukame, mafuriko na maafa mengine. Uwezo wa NFRA kununua chakula umeongezeka kutoka tani 100,000 mwaka 2004/2005 hadi kufikia zaidi ya tani 280,000 mwaka 2014/2015. Aidha, NFRA imekuwa mkombozi kwa wakulima kutokana na kununua chakula kwa bei nzuri katika maeneo ambayo wanunuzi binafsi hawawezi kufika na hivyo kuwa kichocheo cha kuongeza uzalishaji katika maeneo hayo kutokana na kuwa na uhakika wa soko. Hata hivyo, Serikali inaendelea kufanya utafiti na tathmini kuhusu namna bora zaidi ya kushughulikia suala la akiba ya chakula ya taifa ambayo pamoja na mambo mengine itahusisha wakulima, wafanyabiashara na pia mazao mengine.

62

Mhe. Mizengo P. Pinda (Mb.) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikagua akiba ya mahindi wakati alipotembelea Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (National Food Reserve Agency – NFRA) mjini Arusha. Serikali imeongeza uwezo wa kuhifadhi chakula kutoka tani 100,000 mwaka 2005 hadi kufikia tani 280,000 mwaka 2014.

63

•Uzalishaji wa Mazao ya Bustani

Serikali imeendelea kuhamasisha uwekezaji katika uzalishaji wa mazao ya bustani kama vile matunda, mboga, maua na viungo. Serikali inatekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kuendeleza Mazao ya Bustani (National Horticulture Development Strategy 2012-2021) na Mwongozo wa Mbinu Bora za Kilimo cha Mazao ya Bustani (Horticultural Crops Good Agricultural Practices - GAP), pamoja na kuwekeza kwenye ujenzi wa miundombinu ya ukusanyaji, uhifadhi na uzalishaji wa miche bora ya mazao ya bustani.

Kutokana na jitihada hizo, uzalishaji wa matunda umeongezeka kutoka tani 1,211,058 mwaka 2005 hadi kufikia tani 4,574,240 mwaka , 2015. Vilevile, uzalishaji wa mboga umeongezeka kutoka tani 582,310 mwaka 2005 hadi tani 1,041,375 Aprili, 2015. Aidha, uzalishaji wa maua umeongezeka kutoka tani 5,862 mwaka 2005 hadi tani 11,140 Aprili, 2015. Ongezeko la mazao ya bustani limechangia kupunguza umasikini wa kipato na kuimarisha lishe nchini.

64

Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisikiliza maelezo kutoka kwa mkulima wa Nyanya, Judith Munisi wa kikundi cha Upendo Jegestal alipotembelea Kituo cha Habari na Mafunzo (Shamba Darasa) cha Jegestal – Lushoto Mwaka, 2014.

65

Uzalishaji wa Mazao ya Mbegu za Mafuta

Serikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi imeendelea kuimarisha uzalishaji wa mazao ya mafuta ikijumuisha alizeti, karanga, ufuta na michikichi. Kutokana na uwekezaji katika viwanda vidogo na vya kati vya kusindika mafuta katika mikoa ya Manyara, Dodoma, Njombe, Mbeya, Rukwa, Singida na Kigoma, uzalishaji umeongezeka kutoka tani 1,389,947 mwaka 2005/2006 hadi kufikia tani 5,930,000 mwaka 2015 (Jedwali Na. 5). Uzalishaji wa alizeti umeongezeka zaidi ikilinganishwa na mazao mengine ambapo uzalishaji umefikia tani milioni 2.87 mwaka 2014/2015 kutoka tani 373,391 za mwaka 2005/2006.

66

Zao 2006 2007 2008 2009 2010 2011 2012 2013 2014 2015

Alizeti 373.4 369.8 418. 304.7 313.1 786.9 1,125.0 2,625.0 2,755.0 2,878.5

Karanga 783.7 408.1 396.8 347.9 465.3 651.4 810.0 1,425.0 1,635.7 1,835.9

Ufuta 221.4 155.8 46.8 90.0 144.4 357.2 456.0 1,050.0 1,113.8 1,174.5

Mawese 11.4 12.5 - 14.2 16.1 17.0 24.8 40.5 41.0 41.4

Jumla 1,389.9 946.2 861.8 756.8 938.9 1,812.5 2,415.8 5,140.5 5,545.6 5,930.4

Jedwali Na. 5: Mwenendo wa Uzalishaji wa Mbegu za Mafuta mwaka 2006 – 2014 (Tani ‘000)

Chanzo: Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

67

•Benki ya KilimoSerikali imekamilisha maandalizi ya kuanzisha Benki ya Kilimo kwa kutenga Shilingi bilioni 100 kama mtaji wa kuanzisha Benki hiyo. Mtaji huo utaendelea kuongezwa kwa kutenga fedha kwenye Bajeti ya Serikali kila mwaka na kutafuta misaada na mikopo yenye riba nafuu hadi utakapofikia mtaji wa Dola za Marekani milioni 500 zinazolengwa. Benki hiyo inalenga kuwanufaisha wakulima kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu ili kukabiliana na changamoto ya riba kubwa ya mikopo kutoka benki nyingine zisizo za kilimo.

Serikali imekamilisha muundo wa Benki hiyo na kuteua Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Mtendaji Mkuu wa muda. Vilevile, baadhi ya wataalamu wameanza kuajiriwa katika Benki hiyo. Aidha, Serikali imeongeza jumla ya Shilingi bilioni 55 kupitia Dirisha la Kilimo kwenye Benki ya TIB kati ya kipindi cha Januari 2011 hadi Desemba 2013.

68

•VYAMA VYA USHIRIKAIdadi ya Vyama vya Ushirika imeongezeka kutoka 5,832 mwaka 2005 hadi 9,604 mwaka 2014. Vyama hivyo vinajumuisha Vyama vya Msingi vya Ushirika wa Mazao (Agricultural Marketing Cooperative Societies – AMCOS), Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (Savings and Credit Cooperative Societies – SACCOS), Umwagiliaji, Mifugo, Uvuvi, Nyumba, Madini, Viwanda, Walaji, Huduma, na aina nyingine za Vyama vya Ushirika. Idadi ya Vyama vya Ushirika vya mazao ilifikia 2,619, na SACCOS zimeongezeka kutoka 1,875 mwaka 2005/2006 na kufikia SACCOS 5,559 mwaka 2013. Idadi ya wananchi waliojiunga na kunufaika na huduma za SACCOS imeongezeka kutoka 291,368 mwaka 2005/2006 hadi 1,153,248 mwaka 2013. Uwekezaji wa wananchi katika SACCOS kupitia akiba, amana na hisa umeongezeka kutoka Shilingi bilioni 85.6 mwaka 2005 hadi kufikia Shilingi bilioni 463 mwaka 2013 ikiwa ni ongezeko la takribani asilimia 541. Serikali pia imeongeza huduma za kifedha kupitia Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (SACCOS). Vilevile, kumekuwa na ongezeko la mikopo iliyotolewa na SACCOS kwa wanachama wake kutoka Shilingi bilioni 65.7 mwaka 2005/2006 hadi kufikia Shilingi bilioni 893 kwa mwaka 2013 ikiwa ni takriban asilimia 13. Mikopo iliyochukuliwa na wanachama imetumika katika uwekezaji kwenye shughuli za biashara, kilimo, viwanda vidogo vidogo, ufugaji, ujenzi wa nyumba, kulipa karo za shule, matibabu na ununuzi wa zana za kilimo.

69

•UMWAGILIAJI

Ongezeko la eneo la umwagiliajiSerikali imeandaa Sera ya Umwagiliaji ya Taifa ya mwaka 2010 na kuunda Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ambayo imewezesha kuendeleza eneo la umwagiliaji kiasi cha kufikia hekta 461,326 mwaka 2014/2015 ikilinganishwa na hekta 264,388 za mwaka 2005/2006 sawa na ongezeko la asilimia 74.5. Idadi ya wakulima walionufaika na huduma za kilimo cha umwagiliaji kupitia Programu ya maboresho ya ASDP imeongezeka kutoka wakulima 313,786 mwaka 2005 hadi kufikia wakulima 468,892 mwaka 2013.

70

Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wakulima wa Mpunga kuhusu kilimo cha umwagiliaji alipotembelea mashamba ya Skimu ya umwagiliaji Mombo mkoani Tanga.

• Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya UmwagiliajiSerikali imeendelea kujenga na kukarabati Skimu mbalimbali za umwagiliaji kama inavyoonekana katika kiambatisho Na. 1. Ujenzi na ukarabati wa skimu za umwagiliaji umeongeza tija katika uzalishaji wa mazao mbalimbali kwa kuongeza uhakika wa upatikanaji wa maji katika uzalishaji mazao.

71

UFUGAJI

Utekelezaji wa Programu Kabambe ya Kuendeleza Sekta ya Mifugo Serikali imeanzisha na kutekeleza Programu Kabambe ya Kuendeleza Sekta ya Mifugo na Ufugaji. Kupitia utekelezaji wa Programu hiyo, uzalishaji wa mazao ya mifugo (maziwa, nyama na Mayai) umeongezeka. Uzalishaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita bilioni 1.4 mwaka 2005 hadi lita bilioni 2.06 mwaka 2015 sawa na ongezeko la asilimia 47. Idadi ya ng’ombe bora wa maziwa imeongezeka kutoka 510,000 mwaka 2005 hadi kufikia 780,000 mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko la asilimia 52. Uzalishaji wa nyama umeongezeka kutoka tani 378,509 mwaka 2005 hadi tani 597,757 mwaka 2015, sawa na ongezeko la asilimia 58. Vilevile, unenepeshaji wa ng’ombe umeongezeka kutoka ng’ombe 62,000 mwaka 2008 hadi ng’ombe 213,000 mwezi Februari 2015. Unenepeshaji huo unafanyika katika Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Arusha, Rukwa, Tabora, Tanga, Pwani na Kilimanjaro. Aidha, uzalishaji wa mayai umeongezeka kwa asilimia 133 kutoka mayai Bilioni 1.8 hadi mayai Bilioni 4.2 katika mwaka 2015. Pia, uzalishaji wa vifaranga vya kuku wa nyama na wa mayai umeongezeka kutoka vifaranga milioni 26.8 hadi milioni 64 mwaka 2015. Mashamba makubwa ya kuzalisha vifaranga yameongezeka kutoka mashamba 10 mwaka 2005 hadi mashamba 21 Februari, 2015.

72

Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikagua mradi wa ufugaji kuku katika kambi ya Ruvu JKT mkoani Pwani. Uzalishaji wa kuku nchini umeongezeka kutoka kuku milioni 30 mwaka 2005 hadi milioni 61 mwaka 2014.

73

Mradi wa Kopa Ng’ombe Lipa Ng’ombe

Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2005 hadi Februari 2015, Serikali imesambaza jumla ya mitamba 70,862 na mbuzi wa maziwa 13,517 kupitia Mpango wa Kopa Ng’ombe/Mbuzi, Lipa Ng’ombe/Mbuzi katika mikoa yote nchini. Aidha, Mashamba ya Kuzalisha Mifugo ya Sao Hill, Nangaramo, Kitulo, Ngerengere na Mabuki yameimarishwa kwa kukarabati nyumba 40 za watumishi na kupatiwa vitendea kazi kama vile magari, matrekta na zana zake pamoja na mashine za kukamulia. Vilevile, mashamba hayo yalipatiwa jumla ya ng’ombe wazazi 3,495 na madume 230.

74

Udhibiti wa Magonjwa ya MifugoSerikali imeendelea na jitihada za kudhibiti magonjwa ya mifugo ikiwemo ugonjwa wa Homa ya Mapafu ya Ng’ombe. Jumla ya dozi milioni 25.7 za chanjo zenye thamani ya Shilingi bilioni 2.93 zimetumika kuchanja ng’ombe milioni 24.4 katika Mikoa ya Pwani, Tabora, Kagera, Kigoma, Shinyanga, Singida, Iringa, Mbeya na Rukwa. Pia, Serikali imeendelea kutoa ruzuku ya dawa za kuogeshea mifugo ambapo hadi mwezi Februari, 2015 jumla ya Shilingi bilioni 20.3 zimetolewa kama ruzuku na kununua jumla ya lita milioni 1.32 za dawa za kuogesha mifugo kwa mikoa yote Tanzania Bara. Kutokana na juhudi hizo, vifo vya ndama vimepungua kutoka wastani wa asilimia 40 hadi chini ya asilimia 10 katika maeneo yaliyozingatia taratibu za uogeshaji. Aidha, udhibiti wa ugonjwa wa Ndigana Kali ya Ng’ombe kwa njia ya chanjo umeendelea kufanywa ambapo ng’ombe 810,000 walipatiwa chanjo ya kinga na kupunguza vifo vya ndama kutoka asilimia 85 hadi asilimia 5.

75

Ujenzi wa Mabwawa na Majosho

Serikali kupitia Mipango ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Wilayani na Sekta Binafsi, imejenga malambo 1,008, majosho 2,364, maabara 104 za mifugo na visima virefu 101. Aidha, Serikali imekarabati jumla ya malambo 370, majosho 499 na hivyo kuongeza idadi ya majosho kutoka 2,177 hadi 3,637. Kuwepo kwa malambo kumewezesha mifugo kupata maji hususan wakati wa kiangazi pamoja na kupunguza uhamaji wa wafugaji na migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

Utafiti wa Mifugo na Huduma za UganiSerikali imeanzisha Wakala wa Mafunzo ya Mifugo kwa lengo la kuboresha na kuimarisha mafunzo ya wataalam wa mifugo. Wakala hiyo ina kampasi 8 ambazo ni Morogoro, Tengeru, Mpwapwa, Buhuri, Madaba, Temeke, Kikulula na Mabuki. Aidha, idadi ya wanachuo wanaodahiliwa katika Vyuo

76

vya Mafunzo ya Mifugo katika ngazi za Astashahada na Stashahada imeongezeka kutoka 738 kwa mwaka katika mwaka 2005/2006 hadi 2,451 kwa mwaka katika mwaka 2014/2015.

Vilevile, katika kipindi cha miaka 10, Serikali imeongeza ajira za wagani wa mifugo katika Halmashauri mbalimbali nchini kutoka 2,270 mwaka 2005 hadi kufikia 8,541 mwaka 2015 sawa na ongezeko la asilimia 276. Aidha, jumla ya vikundi 1,820 vya wafugaji vimeundwa na vinajihusisha na ufugaji bora wa ng’ombe wa maziwa (Mbeya, Arusha na Tanga), uboreshaji ng’ombe wa asili (Morogoro, Dodoma, Mwanza na Shinyanga), mbuzi wa maziwa (Arusha na Manyara), kuku wa asili (Dodoma na Singida), kuku wa kisasa (Morogoro na Mwanza), kondoo (Arusha na Manyara), udhibiti wa ndorobo (Tanga), nguruwe (Rukwa na Mbeya) na sungura (Morogoro na Mtwara).

77

Masoko ya Ndani ya Mifugo na Mazao yake

Serikali imeanzisha Mkakati wa Kufufua na Kuendeleza Sekta na Viwanda vya Ngozi unaotekelezwa katika Halmashauri 75 za mikoa 18 kwa kutumia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Mifugo. Utekelezaji wa Mkakati huo umesaidia kuongeza usindikaji wa ngozi unaofanyika nchini kutoka vipande 790,000 venye thamani ya Shilingi bilioni 1.9 mwaka 2005 hadi vipande milioni 3.78 vyenye thamani ya Shilingi bilioni 71.5 mwaka 2014. Jumla ya wafugaji 6,047, wachinjaji na wachunaji 4,285 wamepatiwa mafunzo kuhusu Mkakati wa Kufufua na Kuendeleza Sekta ya Viwanda vya Ngozi nchini. Aidha, jumla ya machinjio 67 yamefanyiwa ukarabati. Hatua hizo zimeongeza ubora na thamani ya ngozi pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania.

Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi na kuhamasisha Sekta Binafsi kujenga viwanda na machinjio ya kisasa katika maeneo mbalimbali nchini. Viwanda na machinjio hayo ni pamoja na ‘Sumbawanga Agricultural and Animal Feeds Industries’, Iringa, Chobo (Mwanza), Triple S (Tandani

78

(Mkuranga), Kiliagro (Arusha), Mtanga Foods Limited (Kilolo), Alpha Choice (Magu), ORPUL (Simanjiro), Xinghua International (Shinyanga), Engahay (Babati).

Idadi ya viwanda vya kusindika maziwa imeongezeka kutoka 22 hadi 74 kati ya mwaka 2005 na 2014. Uwezo wa usindikaji wa maziwa kwa siku pia umeongezeka kutoka lita 56,580 mwaka 2005 hadi lita 139,800 mwezi Februari, 2015 sawa na ongezeko la asilimia 147. Vituo 22 vya kukusanyia maziwa vimejengwa katika mikoa ya Arusha, Mara, Tanga, Iringa, Manyara, Kilimanjaro, Morogoro, Rukwa, Kagera na Mwanza. Pia, matenki matatu (3) ya kupoza maziwa yamepelekwa katika Vyama vya Wafugaji Siha, Njombe na Pongwe (Tanga) ili kuongeza ukusanyaji na usindikaji wa maziwa.

79

Vituo vya Kuzalisha Mbegu Bora za MifugoSerikali imeongeza vituo vya uhamilishaji kutoka kituo kimoja cha Arusha mwaka 2005 hadi kufikia vituo nane (8) mwezi Februari, 2015 ambavyo vipo katika Mikoa ya Mbeya, Katavi, Mwanza, Pwani, Dodoma, Lindi na Sao Hill (Iringa) kinachoendelea kujengwa. Aidha, dozi 755,584 za mbegu bora zimezalishwa na kusambazwa kwa wafugaji na ng’ombe 955,360 wamehamilishwa. Vilevile, wataalam 1,378 kutoka maeneo mbalimbali wamepata mafunzo ya uhamilishaji.

Serikali kupitia NARCO imetenga vitalu 124 vya ufugaji ambapo vitalu 96 vimemilikishwa kwa wawekezaji binafsi ambao wameviimarisha kwa kujenga miundombinu ya maji, malisho, majosho, nyumba za watumishi na ofisi. Hadi kufikia mwaka 2014, jumla ya ng’ombe 36,820, mbuzi na kondoo 8,612 waliwekezwa katika vitalu hivyo. Wawekezaji Watanzania 400 walipata ushauri na mafunzo ya kusimamia ufugaji wa kisasa kutoka NARCO. Katika kipindi hicho, jumla ya ng’ombe 72,182 wameuzwa na NARCO ambapo kati ya hao ng’ombe 21,635 walinenepeshwa.

80

Kutenga Maeneo ya Malisho ya Mifugo

Serikali imeendelea kuhimiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kutenga ardhi kwa ajili ya shughuli za ufugaji kwa kuzingatia Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye vijiji kote nchini. Kutokana na jitihada hizo, maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za ufugaji yameongezeka kutoka hekta 930,279 mwaka 2005 hadi hekta milioni 1.95 mwaka 2015. Maeneo hayo yapo katika mikoa 22, wilaya 81 na vijiji 620. Aidha, Serikali imechukua hatua za kuhamasisha ufugaji wa kisasa ikiwa ni pamoja na kuanzisha na kuvijengea uwezo vituo vya uzalishaji wa mbegu bora za malisho katika mashamba ya Vikuge (Kibaha), Langwira (Mbarali), Mabuki (Misungwi), Buhuri (Tanga), Kizota (Dodoma Manispaa), Kongwa (Kongwa), Mivumoni (Muheza) na Sao Hill (Mufindi). Uzalishaji wa mbegu bora za malisho kwenye mashamba hayo umeongezeka kutoka tani 15.7 mwaka 2005 hadi tani 48.5 mwezi Februari, 2015.

81

Vilevile, uzalishaji wa hei katika mashamba ya Serikali umeongezeka kutoka marobota 109,000 mwaka 2005 hadi 500,000 mwezi Februari, 2015. Wazalishaji binafsi wa malisho bora wameongezeka kutoka wawekezaji 6 mwaka 2005 hadi 40 mwezi Februari, 2015 ambapo uzalishaji wa hei kwenye mashamba ya wawekezaji umeongezeka kutoka marobota 69,100 mwaka 2005 hadi 457,860 mwezi Februari, 2015. Uzalishaji wa Vyakula vya Mifugo

1.Serikali imeendelea kuhamasisha Sekta Binafsi kushiriki katika uzalishaji wa vyakula vya mifugo ambapo uzalishaji umeongezeka kutoka tani 559,000 mwaka 2005 hadi tani 1,200,000 mwezi Mei, 2015. Idadi ya viwanda vya kuzalisha vyakula vya mifugo imeongezeka kutoka viwanda 6

82

mwaka 2005 hadi 80 mwezi Februari, 2015 vikiwa na uwezo wa kusindika tani milioni 1.4 za vyakula hivyo kwa mwaka. Viwanda hivyo vipo katika mikoa ya Dar es Salaam (34), Kilimanjaro (6), Mbeya (5), Mwanza (10), Shinyanga (3), Singida (1), Dodoma (1), Lindi (1), Morogoro (3), Arusha (7) na Pwani (9).

UVUVI Serikali imeendelea kutekeleza Mradi wa Usimamizi wa Mazingira ya Ukanda wa Pwani na Bahari (Marine and Coastal Environmental Management Project – MACEMP) katika Halmashauri 16 za pwani ya Bahari ya Hindi kwa upande wa Tanzania Bara, na wilaya 10 kwa upande wa Zanzibar. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuimarishwa kwa usimamizi wa rasilimali za uvuvi, kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi Bahari Kuu, kuimarishwa kwa uhifadhi wa rasilimali za uvuvi katika Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu na kuwezesha udhibiti wa ubora na usalama wa mazao ya uvuvi.

83

Vyuo Vya UvuviSerikali imeendelea kuviimarisha Vyuo vya Uvuvi kwa kuvijengea uwezo wa kuandaa wataalam wa Sekta ya Uvuvi kupitia Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi. Kwa sasa wakala una vyuo vitano ambavyo ni Nyegezi (Mwanza), Mbegani (Pwani), Gabimori (Mara), Kibirizi (Kigoma) na Mikindani (Mtwara) ikilinganishwa na vyuo viwili mwaka 2011/2012. Kutokana na hatua hizo udahili wa wanafunzi umeongezeka kutoka 127 mwaka 2005 hadi 1,215 mwezi Februari, 2015. Aidha, idadi ya wagani wa uvuvi imeongezeka kutoka 103 mwaka 2005 hadi 664 mwezi Mei, 2015. Pia, wavuvi 3,719 na wafugaji wa samaki 447 walipatiwa mafunzo ya muda mfupi. Vilevile, idadi ya wakufunzi wenye shahada wameongezeka kutoka 7 mwaka 2005 hadi kufikia wakufunzi 54 mwezi Februari, 2015.

84

Udhibiti wa Uvuvi Haramu

Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa samaki na mazao ya uvuvi. Doria za nchi kavu na kwenye maji zimefanyika katika maeneo mbalimbali ya nchi kavu na kwenye maji katika ukanda wa Maziwa makuu na madogo, Pwani ya Bahari ya Hindi, Mito na Mabwawa. Katika maeneo ya Pwani ya Bahari ya Hindi zimefanyika doria kwa siku kazi 25,836. Matokeo ya doria hizo ni kukamatwa kwa kokoro 2,270, kamba za kokoro mita 301,904, monofilament 12,595, mabomu 308, mitungi ya gesi 271, samaki wa mabomu kilo 5,665, na watuhumiwa 2,419 kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Aidha, vituo vipya vya doria ukanda wa Pwani vya Horohoro, Kilwa, Mafia na Mtwara vimeanzishwa na boti 16 kununuliwa kwa ajili ya kudhibiti uvuvi haramu. Katika maeneo ya maziwa, doria za majini na nchi kavu zimefanyika na kuwezesha kukamatwa kwa samaki wachanga kilo 101,461, makokoro 3,194, nyavu za makila chini ya nchi tano 25,725, nyavu za timba 17,739,, magari 22, mitumbwi 186, injini 18 na watuhumiwa 1,752 kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

85

Mafunzo ya ufahamu wa hali ya rasilimali ya uvuvi yameendelea kutolewa na wadau kuhamasishwa kushiriki katika kusimamia rasilimali za uvuvi ikiwemo kuendesha doria mbalimbali. Jumla ya wadau 28,145 katika mialo wakiwemo wanajeshi, wamiliki wa mitumbwi, wachakata samaki, wafanyabiashara ya samaki na wadau kutoka makundi mengine wamepatiwa mafunzo. Vilevile, mafunzo kuhusu uvuvi endelevu na athari za uvuvi haramu kwa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa 883 wakiwemo Madiwani 146, Wenyeviti/Meya wa Halmashauri 13, Wakurugenzi wa Halmashauri 11, Maafisa Uvuvi wa Wilaya13, Wenyeviti wa Vijiji 350 na Watendaji wa vijiji 350 yamefanyika.

Kuimarisha Miundombinu ya UvuviSerikali imeimarisha miundombinu muhimu ya uvuvi kwa kujenga na kuboresha mialo mitatu (3) ya kisasa ya kupokelea samaki katika Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi chini ya mradi wa MACEMP. Mialo hiyo ni Kilindoni

86

(Mafia), Nyamisati (Rufiji) na Masoko Pwani (Kilwa). Katika Ukanda wa Ziwa Victoria mialo 19 ilikarabatiwa na mialo 6 ya kisasa ilijengwa chini ya Mradi wa Implementation of Fisheries Management Plan (IFMP) katika maeneo ya Marehe (Missenyi), Kukimbaitare (Chato), Bwai (Musoma), Sota (Rorya), Kigangama (Magu), na Kahunda (Sengerema). Vilevile, katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika mialo minne (4) ya kisasa ya kupokelea samaki ya Kibirizi (Ujiji – Kigoma), Muyobozi (Kigoma), Ikola (Mpanda Vijijini) na Kirando (Nkasi) imejengwa. Aidha, Serikali kupitia Halmashauri ya Sumbawanga kwa kushirikiana na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) imejenga Soko la Samaki Kasanga ambalo litawezesha wavuvi kupata soko la uhakika la kuuzia mazao ya uvuvi na kuongeza kipato.

87

Upatikanaji wa Mazao Bora na Usalama ya Uvuvi

Serikali imeimarisha Maabara ya Taifa ya Uvuvi iliyopo Nyegezi, Mwanza kwa kuipatia vifaa vya maabara na kujenga uwezo kwa watumishi. Pia, Serikali imeendelea kutoa mafunzo kuhusu teknolojia mbalimbali za uhifadhi na uchakataji wa mazao ya uvuvi. Wadau 1,493 kutoka Halmashauri za Majiji ya Mwanza (185), Bukoba - Kagera (180), Musoma – Mara (150) na Tanga (180); Manispaa ya Ilala (44), Kigoma – Ujiji (24), na Wilaya za Pangani (40), Muheza (120), Mafia (80), Mtwara Vijijini (52), Lindi Vijijini (78), Mkuranga (50), Bagamoyo (40), Nkasi (130), Sumbawanga (50) na Mpanda (80) walipata mafunzo. Vilevile, Serikali imeendelea kuhamasisha Sekta Binafsi kuwekeza katika uvuvi ikiwemo kuanzisha viwanda vya kuchakata samaki ambapo hadi sasa vimeanzishwa viwanda 48 vya kuchakata samaki na maghala 84 ya kuhifadhi mazao ya uvuvi.

88

Kuimarisha Vikundi vya Ushirika vya Wavuvi

Serikali imewezesha uanzishwaji wa vikundi 659 vya usimamizi shirikishi wa rasilimali za uvuvi (BMUs) na kufanya idadi ya BMUs nchini kote kufikia 749. Kati ya hizo, BMUs 511 zimesajiliwa na zinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria ndogo na mipango kazi yao. Kutokana na kuanzishwa kwa vikundi hivyo, jumla ya wanachama 124,434 wameandikishwa kwenye BMUs, kati yao wanaume ni 92,386 na wanawake 32,048. Pia, mafunzo ya uongozi, utawala bora na usimamizi wa fedha za Vikundi yalitolewa kwa viongozi wa BMUs hizo 433 yakijumuisha Wenyeviti, Makatibu, Wahasibu na Mabaharia. Aidha, watendaji 388 wa v ijiji wamenufaika na mafunzo hayo.

89

Usimamizi wa Mazingira Katika Maeneo ya Uvuvi

Serikali imeendelea kutoa elimu kuhusu uanzishwaji na utekelezaji wa miradi midogo ya utunzaji wa mazingira ikiwemo ya upandaji miti na uchimbaji wa malambo kwa ajili ya kupata maji safi ya kunywa mifugo, kilimo na ufugaji. Taarifa mbalimbali kuhusu utafiti na usimamizi endelevu wa rasilimali za uvuvi ziliandaliwa na kusambazwa kupitia magazeti, vipindi vya radio na luninga. Serikali imeendelea kuhimiza wananchi kuendesha shughuli mbadala za kiuchumi ili kupunguza shinikizo la uvuvi kwenye maji ya asili na maeneo tengefu. Katika ukanda wa Pwani jumla ya vikundi 230 viliwezeshwa kupitia mradi wa MACEMP kutekeleza miradi mbadala ya kiuchumi ikiwemo ufugaji nyuki, ufugaji samaki, kilimo cha bustani, ufugaji ng’ombe, mbuzi na kuku, ukulima wa mwani, ususi, ushonaji pamoja na usindikaji wa chumvi.

90

Uzalishaji wa Viumbe kwenye Maji

Vituo kumi (10) vya ukuzaji viumbe kwenye maji vya Ruhila (Songea), Mwamapuli (Igunga), Nyigedi (Lindi), Nyamirembe (Chato), Mwanza, Bukoba, Kigoma, Musoma, Kilimanjaro, Machui (Tanga) na Mbegani (Bagamoyo) vimeanzishwa na kituo cha Kingolwira (Morogoro) kimekarabatiwa. Vituo hivyo pamoja na vituo 6 vya binafsi vimewezesha uzalishaji wa vifaranga vya samaki kuongezeka kutoka 200,000 mwaka 2005 hadi 4,199,140 mwezi Februari, 2015. Vifaranga hao wamesambazwa kwa wafugaji wa samaki kote nchini. Idadi ya mabwawa ya kuzalisha viumbe kwenye maji imeongezeka kutoka 13,011 mwaka 2005 hadi 21,300 Mei, 2015. Aidha, idadi ya wafugaji imeongezeka kutoka 11,245 mwaka 2005 hadi 20,493 mwezi Februari, 2015.

91

WANYAMAPORI NA MISITUKuboresha Miundombinu ya Hifadhi za Wanyamapori

Serikali imeelekeza nguvu katika kuhifadhi, kulinda, kuendeleza, kudumisha, kuboresha na kuvuna maliasili ya wanyamapori kwa manufaa ya Taifa na kuwezesha jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi kunufaika na rasilimali zilizopo. Katika kipindi cha kuanzia 2005 hadi 2014, Serikali iliidhinisha jumla ya maeneo 19 kuwa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (Wildlife Management Areas -WMAs). Jumuiya hizo zimewezeshwa kwa kupatiwa na Serikali jumla ya Shilingi milioni 917.1 ambazo zilitokana na mgao wa uwindaji wa kitalii. Aidha, kupitia Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania, Serikali imechangia jumla ya Shilingi bilioni 2.4 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wananchi wanaoishi jirani na hifadhi ikiwemo ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na sekondari, zahanati, ofisi za vijiji na visima vya maji. Katika mapambano dhidi ya ujangili wa wanyamapori ndani na nje ya maeneo ya hifadhi, kati ya mwaka 2006 na 2014, Serikali iliendesha doria zilizowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 17,084 na silaha 4,111 za aina mbalimbali na kesi 6,803 kufunguliwa katika vituo mbalimbali.

92

Kati ya kesi hizo, kesi 2,734 zenye watuhumiwa 2,246 zilimalizika kwa watuhumiwa kutozwa faini ya jumla Shilingi milioni 652.3 na watuhumiwa 210 walihukumiwa vifungo jela.

Misitu na Mazao yakeSerikali imeendelea kuhifadhi, kulinda na kuhamasisha matumizi endelevu ya misitu ikiwemo kurejesha mipaka yenye jumla ya urefu wa kilometa 13,237 katika misitu 116 iliyohifadhiwa nchini. Vilevile, mawe ya mipaka 2,416 na mabango ya taarifa/tahadhari 3,725 yalisimikwa pamoja na kufyeka mipaka ili kuweka bayana mipaka kwa kutumia alama za kudumu na kuondoa dhana kwamba mipaka ya misitu ya hifadhi haifahamiki.

93

Ufugaji NyukiSerikali imeendelea kuimarisha sekta ya ufugaji nyuki kwa lengo la kuchangia kuongeza ajira na kupunguza umaskini. Aidha, wananchi wamehamasishwa kushiriki katika ufugaji nyuki nchini pamoja na kupatiwa Mafunzo kuhusu mbinu bora za ufugaji nyuki ambapo wafugaji nyuki 7,320 kutoka vikundi 330 katika vijiji 921 vya wilaya 30 walipatiwa mafunzo ili kuboresha uzalishaji wa mazao ya nyuki.

Wafanyabiashara 50 na wafugaji 241 wamepatiwa mafunzo ya kuhakiki ubora wa mazao ya nyuki na taratibu za kufanya biashara ya mazao ya nyuki. Vile vile, watanzania 839 walishiriki katika Kongamano la Apimondia, 2014 lililokuwa na washiriki 941. Kongamano hilo limetoa elimu kuhusu mbinu za kulinda ubora wa mazao ya nyuki: umuhimu wa nyuki katika uchavushaji wa mimea; magonjwa ya nyuki; na jinsi wafugaji wa nyuki watakavyokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

94

Jumla ya mizinga 14,076 imetengenezwa na kusambazwa kwa wananchi waishio karibu na hifadhi za misitu katika Mikoa ya Pwani, Morogoro, Mbeya, Rukwa, Iringa, Tabora, Shinyanga, Katavi, Ruvuma, Mtwara, Lindi, Kilimanjaro, Tanga Arusha, Singida, Manyara na Dodoma. Kutokana na juhudi hizo, jumla ya tani 3,253 za nta zenye thamani ya Shilingi bilioni 21.3 na tani 2,633 za asali zenye thamani ya Shilingi bilioni 5.9 zimepatikana katika kipindi cha kuanzia mwaka 2005 hadi 2013.

95

Mhe. Mizengo P. Pinda (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipata maelezo ya bidhaa za asali kutoka kwa mmoja wa Wajasiriamali katika Maonesho Maalum ya bidhaa za mazao ya nyuki yaliyofanyika mwezi Novemba, 2014 Jijini Dar es Salaam.

UTALII Serikali imeimarisha Sekta ya Utalii kwa kuweka mazingira wezeshi pamoja na kuhamasisha Sekta Binafsi kuwekeza katika Sekta hiyo kwa lengo la kuongeza utalii wa ndani na wa nje. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na ujenzi wa vyuo vya utalii, hoteli zenye hadhi, uimarishwaji na ujenzi wa miundombinu inayowawezesha watalii kufika kwa urahisi kwenye maeneo yenye vivutio vya utalii.

Vyuo na Hoteli za KitaliiSerikali imekijengea uwezo Chuo cha Taifa cha Utalii kwa kujenga Kampasi ya Bustani na hivyo kuwa na kampasi tatu ambazo zimeongeza udahili wa

96

wanafunzi katika tasnia ya hoteli na utalii nchini. Kampasi ya Bustani ilikamilika Desemba, 2011. Kutokana na kufunguliwa kwa Kampasi hiyo, udahili umeongezeka kutoka wanafunzi 186 mwaka 2010/2011 hadi 218 mwaka 2014/2015. Hadi kufikia mwaka 2014 idadi ya hoteli za kitalii nchini zimefika 300.

Kutangaza Utalii wa Ndani

Serikali imeendelea kutumia fursa za maonesho mbalimbali ya ndani yakiwemo maonesho ya Sabasaba, Nanenane, Karibu Travel Fair, Siku ya Utalii Duniani kuhamasisha na kukuza utalii wa ndani. Aidha, Serikali imekuwa ikihamasisha utalii wa ndani kwa kuandaa matembezi katika vivutio vya utalii nyakati za sikukuu yenye kampeni ijulikanayo kama “Utalii uanze kwa Mtanzania Mwenyewe”. Matokeo ya jitihada hizo ni kuongezeka kwa idadi ya watalii wa ndani kutoka 567,062 mwaka 2010 hadi 1, 003,496 mwaka 2015.

97

Kutangaza Utalii wa Nje na Kutafuta Masoko Mapya

Serikali imeendelea kutekeleza Mkakati wa Kutangaza Utalii (2012 - 2016) ambao unalenga kuongeza idadi ya watalii. Moja ya jitihada zilizowekwa ni kutangaza vivutio vya utalii katika masoko mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na masoko mapya ya nchi za Urusi, Brazili, Afrika ya Kusini, Japan, China, India na Singapore.

Jitihada nyingi zimefanyika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kimataifa kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ziara za viongozi, vyombo vya habari vya kimataifa, na michezo ya kimataifa. Vilevile, Serikali imewezesha wachezaji nyota wa kimataifa wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid ya Hispania kuja Tanzania na kutembelea vivutio vya utalii na kuvitangaza kimataifa. Pia, Serikali imefanikisha kuweka matangazo kwenye viwanja sita vya Ligi kuu ya mpira wa miguu ya Uingereza (English Premier League) na katika kiwanja cha Seattle Sounders nchini Marekani.

98

Matangazo ya vivutio vya Utalii katika viwanja vya Seattle Sounder 2012 nchini MarekaniVivutio vitatu vya utalii vya Tanzania ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Mbuga ya Wanyama ya Serengeti na Bonde la Hifadhi la Ngorogoro vimefanikiwa kuwa kati ya Maajabu Saba ya Asili ya Afrika (New Seven Wonders of Africa). Katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne, idadi ya watalii kutoka nje waliotembelea nchini imeongezeka kutoka watalii 612,754 mwaka 2005 hadi kufikia watalii 1,140,156 mwaka 2014. Mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kutoka Dola za Marekani million 823.05 mwaka 2005 hadi Dola millioni 1,853 mwaka 2014.

99

VIWANDA, BIASHARA NA MASOKOViwandaKatika kuendeleza uwekezaji wa viwanda, Serikali imechukua hatua mbalimbali za kutenga maeneo maalum ya uwekezaji katika mikoa 20 ya Tanzania Bara. Maeneo yaliyotengwa yameendelea kuwekewa miundombinu ya msingi itakayovutia Sekta Binafsi kujenga viwanda na kuzalisha. Hatua hiyo imelenga kupunguza baadhi ya changamoto zinazowakabili wawekezaji wanaotaka kuanzisha viwanda nchini. Mchango wa Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 8.87 mwaka 2005 hadi asilimia 9.92 mwaka 2013. Takriban miradi mipya ya viwanda 1,547 ilisajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kati ya mwaka 2005 na 2014 na miradi 751 ilipewa leseni za kudumu na BRELA za kuanzisha viwanda.

100

Viwanda vya nguo na mavazi vimeongezeka kutoka viwanda vinavyofanya kazi 17 mwaka 2005 hadi viwanda 22 mwaka 2014. Aidha, uzalishaji wa nguo umeongezeka kutoka mita za mraba milioni 91.5 hadi mita za mraba milioni 97.4 katika kipindi hicho. Aidha, Viwanda vya chuma vimeongezeka kutoka vinane (8) mwaka 2005 hadi kufikia ishirini na mbili (22) mwaka 2014.Kutokana na ukuaji wa Sekta ya Viwanda, ajira katika sekta hiyo imeongezeka kutoka 89,316 mwaka 2005 hadi kufikia 126,882 mwaka 2014. Katika ajira hizo, viwanda vinavyoongoza ni viwanda vya kusindika vyakula (ajira 51,759), ufumaji na ushonaji (ajira 14,165); tumbaku na sigara (ajira 7,968).

101

Viwanda vya SarujiSerikali imewezesha kuanzishwa kwa viwanda vipya vya Saruji Nane (8) katika maeneo mbalimbali nchini. Viwanda hivyo ni Kiwanda cha Dangote mjini Mtwara, Kiwanda cha Rhino Mkuranga, Maweni Tanga, Kiwanda cha Kisarawe; Kiwanda cha Lake Cement; Kiwanda cha Kilwa Cement; kiwanda cha “Arusha Cement”; na kiwanda cha MEIS cha mjini Lindi. Kutokana na juhudi hizo, uzalishaji wa saruji umeongezeka kutoka tani milioni 2.58 mwaka 2012 hadi tani milioni 4.4 mwaka 2014, sawa na ongezeko la asilimia 70.5. Ongezeko hili limewezesha kupunguza uhaba wa saruji na ongezeko la bei ya saruji. Aidha, ujenzi wa viwanda hivi vipya umechochea kasi ya ukuaji wa uchumi, hususan katika sekta ya ujenzi wa miundombinu na makazi na kuzalisha ajira nyingi.

Viwanda vya NgoziSerikali inatekeleza Mkakati Unganishi wa Kufufua na Kuendeleza Viwanda vya Ngozi ambao umewezesha kuanzishwa kwa viwanda vipya vya ngozi vya Open Enterprises Morogoro, Super Leather Ltd (Leather Product Manufacturing) na Morogoro Leather Community mjini Morogoro na kiwanda cha Petrocity Tannery (Leather Processing) jijini Mwanza. Miradi mingine ya kusindika ngozi imeanzishwa ikiwemo ya Tanmbuzi Co. Himo - Mkoani Kilimanjaro; Bhat Bangla Agritech (T) Ltd. Ya mjini Dodoma;

102

Zhung FU International Co. Ltd. (Leather Production and Plastic Footwear) cha Mkuranga; “Xinghua International Ltd” kilichoko Shinyanga; “Meru Tannery” cha Arusha; na Boggosh kilichopo Mwanza. Usindikaji wa ngozi umeongezeka kutoka futi za mraba 6,038,000 mwaka 2005 hadi futi za mraba 45,000,000 mwaka 2013/14 kwa kiwango cha wet-blue. Aidha, mauzo ya bidhaa za ngozi yameongezeka kutoka Shilingi bilioni 1.6 mwaka 2005 hadi kufikia Shilingi bilioni 63 mwaka 2013/14. Ajira katika sekta ndogo ya ngozi imeongezeka kutoka ajira 280 mwaka 2005 hadi 755 mwaka 2014.

103

Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiangalia kiatu aina ya buti katika Banda la Jeshi la Magereza wakati wa Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam, mwaka 2014.

Maendeleo ya Viwanda Vidogo Serikali kupitia Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) imeendelea kuzalisha na kusambaza teknolojia za uzalishaji kwa wananchi. Kupitia vituo vya uendelezaji wa teknolojia vilivyopo Mbeya, Arusha, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Shinyanga na Kigoma, SIDO imezalisha jumla ya teknolojia mpya 1,715 na zana mpya aina 604 na kuzisambaza kwa wananchi. Zana zilizozalishwa ni pamoja na jembe la kukokotwa na wanyamakazi, mashine za kupandia, pampu za maji, mashine ya kuvunia, mashine ya kupura mtama na mashine za kupukuchua nafaka. Zana zingine zilizozalishwa ni pamoja na zana za ubanguaji wa korosho, usindikaji wa mihogo, usindikaji wa vyakula, upunguzaji wa matumizi ya miti na mazao yake kama nishati. Zana nyingine ni zile za ufungashaji wa vyakula vilivyosindikwa, vifaa vya

104

ujenzi hasa matofali, utengenezaji wa chokaa na chaki, ukamuaji mafuta ya kupikia, utengenezaji wa sabuni na usindikaji ngozi kwa kutumia njia za asili. Teknolojia hizo zimesaidia kuimarisha na kuongeza ubora wa bidhaa za wajasiriamali, kurahisisha kazi ya kilimo na hatua za awali za usindikaji wa mazao ya shamba. Mwaka 2010, Serikali ilifanya utafiti wa Biashara ndogo, Viwanda Vidogo na Vya Kati (Micro, Small and Medium Enterprises - Baseline Survey) na kukamilika mwaka 2012. Matokeo ya utafiti huo yamebainisha kuwa kuna jumla ya wajasiriamali wadogo milioni tatu nchini ambapo wengi wao wamejikita katika sekta ya biashara na huduma, na kwamba asilimia 54.3 ya wajasiriamali hao ni wanawake. Utafiti huo pia umeonesha kwamba sekta ya viwanda vidogo na biashara ndogo inachangia kiasi cha asilimia 27 katika pato la taifa na kutoa ajira za moja kwa moja kwa Watanzania zaidi ya milioni 5.

105

Programu ya Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI)Serikali imeendelea kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Programu ya Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) inayotekelezwa kwa kuzingatia mlolongo wa thamani kwa mazao ya alizeti, mihogo, matunda na nyanya ili kuongeza kipato kwa wakulima na kupunguza umaskini. Programu hiyo inatekelezwa katika wilaya 19 za mikoa sita. Wilaya hizo ni: Iringa Vijijini, Kilolo, Simanjiro, Hanang, Babati, Bagamoyo, Rufiji na Mkuranga. Wilaya nyingine zilizopo kwenye Programu hiyo ni Songea Vijijini, Namtumbo, Mbinga, Sengerema, Kwimba, Ukerewe, Muheza, Korogwe, Kilindi na Handeni. Programu hiyo imetoa huduma za kuunganisha wajasiriamali na masoko kwa kaya 92,910 kwa kuziwezesha kuanzisha miradi 15,580 midogo vijijini, urasimishaji wa vikundi vya uzalishaji 65,308 na upatikanaji wa ajira 39,574.

Aidha, Programu hii imesaidia kuimarisha mifumo ya kusambaza mbegu bora na pembejeo. Baadhi ya wakulima wamepewa mafunzo ya kuzalisha mbegu bora za mazao na kuanzisha mashamba ya mbegu hizo na kuwafanya wajasiriamali wa kudumu wa mbegu hizo. Juhudi hizi zimewezesha ongezeko la uzalishaji katika eneo la mradi. Kwa mfano,

106

uzalishaji wa zao la alizeti umeongezeka kutoka wastani wa kilo 245 hadi kilo 560 kwa ekari; uzalishaji wa nyanya umeongezeka kutoka wastani wa tani 20 hadi tani 30 kwa ekari; na uzalishaji wa muhogo kutoka tani 6 hadi tani 9 kwa ekari.

Maeneo ya Uzalishaji Kwa ajili ya Uuzaji NjeSerikali imeendelea kuhamasisha uwekezaji kupitia Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa ajili ya Mauzo ya Nje (Export Processing Zones-EPZ) na Maeneo Maalum ya Uchumi (Special Economic Zone- SEZ). Eneo Maalum la Kiuchumi la Benjamin William Mkapa lilikamilika mwaka 2010. Maeneo maalum matano ya viwanda ya Millennium Business Park, Hifadhi EPZ, Global EPZ, Kamal Industrial Estate, na Kisongo EPZ yameanzishwa. Kuanzishwa kwa maeneo hayo kumewesha kampuni 118 kuendesha shughuli za uzalishaji na kuchangia fursa za ajira ya moja kwa moja zinazofikia 32,000 na mauzo ya nje kufikia dola milioni 650.

107

Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikagua Eneo Maalum la Kiuchumi la Benjamin William Mkapa lililopo Mabibo jijini Dar es Salaam.

108

Maeneo Maalum ya Kiuchumi

Serikali imeainisha na kutenga Maeneo Maalum ya Kiuchumi (SEZ) kwa lengo la kukuza mchango wa maeneo hayo kwenye uchumi wa nchi. Maeneo hayo ni pamoja na Bagamoyo SEZ; China-Tanzania Logistics Centre; Mtwara Free Port Zone; na Kigoma SEZ. Kupitia EPZA, kampuni saba zimeonesha nia ya kuwekeza katika “Eneo Maalum la Bandari Huru” la Mtwara (Mtwara FreePort Zone) lenye jumla ya hekta 110. Uwekezaji huo utahusisha kampuni zinazotoa huduma kwenye sekta ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi.

Serikali imeimarisha ushiriki wa Sekta Binafsi katika uwekezaji na biashara ili kushiriki vema katika soko la ushindani kwa kuipa nguvu ya kisheria Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje (EPZA) na Maeneo Maalum ya Uwekezaji (Special Economic Zones – SEZ). Jumla ya maeneo maalum ya uwekezaji yametengwa katika Mikoa Ishirini (20) yakiwemo ya TAMCO - Kibaha, Kange - Tanga na KMTC - Kilimanjaro.

109

Maeneo hayo yanaendelea kuwekewa miundombinu ya msingi itakayovutia Sekta Binafsi kujenga viwanda na kufanya biashara. Hatua hiyo inalenga kupunguza changamoto ya upatikanaji wa ardhi kwa wawekezaji wanaotaka kuanzisha viwanda nchini. Jitihada za kutenga maeneo maalum katika maeneo yaliyobaki hususan mikoa mipya ya Simiyu, Katavi, Geita na Njombe zinaendelea. Aidha, Serikali inaendelea na jitihada za kutafuta fedha kwa ajili ya maeneo ya Bandari - Mtwara, Bunda-Mara, na Mererani – Manyara.

Mradi wa Makaa ya Mawe na ChumaSerikali kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (National Development Corporation –NDC) imeingia ubia na Kampuni ya Sichuan Hongda Group (SHG) ya China ambapo kampuni ya Tanzania China International Mineral Resources Limited (TCIMRL) imeanzishwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na chuma cha Liganga. Serikali inamiliki hisa asilimia 20 na asilimia 80 zinamilikiwa na Kampuni ya SHG. Kazi ya utafiti ili kubaini wingi na ubora wa madini ya chuma na makaa ya mawe imekamilika na kuthibitika uwepo wa mashapo (reserves) ya makaa ya mawe tani milioni 370 katika eneo la kilometa za mraba 30 kati ya 140 zilizotengwa kwa ajili ya mradi huo.

110

Inakadiriwa kuwa kiasi cha tani milioni 3.0 za makaa ya mawe kitazalishwa kwa mwaka na kinatarajiwa kuzalisha umeme wa zaidi ya Megawati 600 zitakazotumika katika uchenjuaji na uyeyushaji wa madini ya chuma na ziada kuingizwa kwenye gridi ya Taifa. Aidha, mashapo ya madini ya chuma yamebainika kuwa ni tani milioni 219 katika eneo la Kilometa 10 za mraba kati ya Kilometa 166 za mradi. Kampuni hiyo inatarajia kuzalisha tani milioni 2.9 kwa mwaka ambapo tani milioni 1 za bidhaa mbalimbali za chuma zitakuwa zinazalishwa kila mwaka. Hadi sasa, kiasi cha Shilingi trilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya chuma zimepatikana na ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwaka huu wa 2015.

Biashara na Masoko

Serikali ya Awamu ya Nne imechukua hatua madhubuti za kuimarisha biashara nchini kwa kuhakikisha kwamba bidhaa zinazozalishwa zinakuwa na ubora wa hali ya juu ili ziweze kupata masoko ndani na nje ya nchi.

111

Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiangalia bidhaa baada ya kutembelea banda la Maonesho ya Wajasiriamali wenye Ulemavu.

Programuu ya Utambulisho wa Kitaifa wa BidhaaSerikali imewezesha Sekta Binafsi kupata usajili wa kutumia nembo za mistari (bar codes) na huduma nyingine zinazotolewa na Kampuni ya Kimataifa ya GS1 yenye Makao Makuu huko Brussels, Ubelgiji. Kupatikana kwa bar codes, kutawezesha bidhaa za Tanzania kutambulika kimataifa na kupunguza gharama kwa wafanyabiashara wa Tanzania ambao walikuwa wakipata huduma hiyo kutoka nchi nyingine kwa gharama kubwa. Bidhaa za Tanzania zimepewa namba 620 ya utambulisho. Hadi kufikia mwezi

112

Aprili, 2012, jumla ya wazalishaji 151 wamesajiliwa kutumia huduma hiyo na bidhaa 3,000 ambazo ziko sokoni zina mfumo huo wa utambuzi.

Ongezeko la Mauzo ya Bidhaa Nje ya NchiSerikali imehamasisha Jumuiya ya Wafanyabiashara kuhusu fursa za masoko zilizopo ndani ya nchi, kikanda na kimataifa kwa kutoa taarifa kupitia Taasisi zinazowawakilisha. Kutokana na juhudi hizo pamoja na kuongezeka kwa kazi ya kutatua vikwazo vya ufanyaji biashara, thamani ya mauzo ya bidhaa nje iliongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 1,917.6 mwaka 2006 hadi dola za Marekani milioni 5,348.9 mwaka 2014.

Kielelezo Na. 3.1 Thamani ya Mauzo ya Bidhaa Nje ya Nchi

Chanzo: Wizara ya Viwanda na Biashara.

113

Uendelezaji wa Miundombinu ya MasokoSerikali imeendelea kuboresha miundombinu ya masoko katika mikoa na mipakani ili kukuza biashara ya ndani na Kikanda. Uboreshaji wa miundombinu hiyo umempatia mwananchi uhakika wa soko la mazao yake. Katika kipindi cha Awamu ya Nne, Serikali imejenga jumla ya masoko 10 ya mikoani, mengi yakiwa katika maeneo ya kimkakati ya mipakani.

Masoko yaliyojengwa ni Nyamugali lililopo katika mpaka wa Tanzania na Burundi; na Masoko ya Mkenda na Mtambaswala yaliyopo katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji. Aidha, ujenzi wa masoko matano ya mipakani katika maeneo ya Kabanga- Ngara, Nkwenda - Karagwe, Murongo – Karagwe, Remagwe –Tarime, na Busoka - Kahama upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake. Uboreshaji miundombinu ya masoko unajumuisha pia uboreshaji miundombinu mingine kama barabara na uongezaji thamani ili kuyafikia masoko hayo kirahisi.

Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya biashara na masoko kwa kuchukua hatua mbalimbali. Moja ya hatua hizo ni pamoja na kujenga miundombinu ya masoko ya mazao katika Hamashauri zote nchini. Masoko 7 yalijengwa mipakani katika mikoa ya Kagera, Mara, Shinyanga na Kigoma kupitia Mradi wa District Agricultural Sector Investment Project (DASIP). Masoko mengine yanaendelea kujengwa katika mipaka ya Mtukula, Murongo, Nkwenda, Kabanga Manyovu, Sirari na Isaka.

114

Kupitia Programuu ya Uendelezaji Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (Marketing Infrastructure Value Addition and Rural Finance - MIVARF), Serikali imekarabati jumla ya kilomita 555.3 za barabara katika wilaya 8 kwa kiwango cha changarawe. Wilaya hizo ni Mbulu, Mbarali, Kwimba, Rufiji, Songea Vijijini, Kahama, Singida Vijijini na Lushoto. Kupitia Programu hiyo, jumla ya maghala 15 yenye uwezo wa kuhifadhi tani 1,000 za mazao kila moja yamejengwa katika Wilaya za Iringa Vijijini, Njombe Vijijini, Same, Songea na Mbarali. Maghala matatu katika Halmashauri za Sumbawanga, Mbulu na Kibaha yalifanyiwa ukarabati. Ujenzi na ukarabati wa maghala hayo umesaidia kupunguza upotevu wa thamani ya mazao baada ya kuvunwa kwake.

115

Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akikagua ujenzi wa Soko la Kisasa (Shopping Mall) Wilayani Ilemela, Mkoa wa Mwanza.

Mfumo wa Stakabadhi za GhalaSerikali ilianzisha Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, ili kuwapatia wananchi bei nzuri ya mazao yao pamoja na uhakika wa sehemu ya kuyahifadhi. Hatua hiyo imewezesha wananchi kuondokana na unyonyaji uliokuwa ukifanywa na wafanyabiashara wa kati hapo awali. Manufaa ya mfumo huo yamejionesha wazi kwenye mazao ya Kahawa na Korosho ambapo wakulima wa korosho kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara wamefaidika kwa kupata bei nzuri ya korosho ikilinganishwa na wakulima wa maeneo mengine.

Mfumo huu umeonesha mafanikio dhahiri kwenye zao la korosho kwa kuongeza uzalishaji kutoka tani 92,573 mwaka 2006/07 hadi kufikia tani 196,000 katika msimu wa 2014/2015. Bei ya wastani ya mkulima imeongezeka kutoka Shilingi 450.00 hadi kufikia 1,350.00 kwa kilo, Ushuru

116

wa mauzo nje kutoka Shilingi milioni 44 hadi bilioni 43.2 mwezi Januari, 2015. Ushuru wa halmashauri zote katika eneo linalolima korosho na waliotumia mfumo huu umeongezeka zaidi ya mara dufu.Mafanikio yaliyopatikana katika zao la korosho yameifanya Serikali kufanya marekebisho ya Sheria ili kuwezesha mfumo huo sasa kutumika kikamilifu kwenye mazao mengine baada ya kufanyiwa majaribio katika mazao ya Ufuta, Alizeti, Mahindi, Mbaazi na Mpunga na sasa kuanzishwa Soko la Bidhaa Tanzania.

Matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala yamewezesha wakulima kupata mikopo kutoka Benki za CRDB, NMB, Kilimanjaro Co-operative Bank na Benki ya Maendeleo ya Wanawake. Mikopo iliyotolewa na Benki hizo imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 36.2 katika msimu wa mwaka 2007/08 hadi Shilingi bilioni 53.03 katika msimu wa mwaka 2014/15. Kwa ujumla tangu mfumo huu uanze kutumika kwa mujibu wa sheria, jumla ya Shilingi billioni 335.4 zimetolewa kama mkopo kwa wakulima.

Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikagua mahindi yanayouzwa katika soko la kimataifa la mazao la Kibaigwa wilayani Kongwa mkoani Dodoma. Soko hili limefanikiwa kupokea tani za mazao 532,854 na kusafirisha tani 529,143 za mazao tofauti kwa mwaka 2004 hadi 2010.

117

MADINIMchango wa Sekta ya Madini katika Pato la TaifaUsimamizi na utekelezaji mzuri wa Sera ya Madini ya mwaka 2009 umewezesha mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa kuongezeka kutoka asilimia 2.9 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 3.5 mwaka 2014. Mauzo ya madini nje ya nchi yameongezeka kutoka Dola za Marekani Milioni 727.45 mwaka 2005 hadi Dola za Marekani Milioni 1,744.5 mwaka 2014. Aidha, Sheria ya Madini ya mwaka 2010 imewezesha kuongezeka kwa mapato ya Serikali kutokana na kuanza kutumika kwa viwango vipya vya mrabaha. Mapato ya Serikali kutokana na uchimbaji mkubwa wa madini yameongezeka kutoka takriban Shilingi bilioni 60.4

118

mwaka 2005 hadi kufikia Shilingi trilioni 2.51 mwaka 2014 sawa na ongezeko la asilimia 4,055.

Kutokana na jitihada za Serikali kwenye Sekta ya Madini, uwekezaji wa migodi mipya mitatu (3) ya Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi (Shinyanga), Mgodi wa Dhahabu wa New Luika (Mbeya) na Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka (Ruvuma) umefanyika. Aidha, katika kipindi hicho, miradi mbalimbali ya madini iliendelezwa na kufikia hatua ya kuanzisha mgodi. Miradi hiyo ni pamoja na Kabanga Nickel (Kagera), Mradi wa Urani wa Mkuju (Ruvuma), Dhahabu Nyanzaga (Mwanza), Mradi wa Nickel wa Dutwa (Simiyu), Mradi wa Panda Hill Niobium (Mbeya) na Miradi ya Chuma Liganga na Makaa ya Mawe Mchuchuma (Njombe). Kutokana na uwekezaji huo, ajira rasmi kwenye migodi mikubwa nchini imeongezeka kutoka waajiriwa 3,517 mwaka 2005 hadi takriban waajiriwa 15,000 mwaka 2014. Aidha, ununuzi wa bidhaa za ndani (local procurement) kwenye migodi mikubwa umeongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 230.41(sawa na asilimia 41 ya manunuzi yote) hadi Dola za Marekani milioni 536.56 (sawa na asilimia 54 ya manunuzi yote) katika kipindi hicho.

Kuimarisha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)Mwaka 2008, Serikali ilitengua uamuzi wa Mwaka 1996 wa kulibinafsisha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na kuanza rasmi kuliboresha mwaka 2013 ili kuliwezesha kushiriki ipasavyo katika shughuli za uchimbaji wa

119

Jedwali Na. 6 Ongezeko la mapato yatokanayo na sekta ya madiniMwaka 2005 2006 2007 2008 2009 2010 2011 2012 2013 2014

%ya Pato la Taifa 2.9 3.2 3.5 3.4 3.3 3.3 3.3 3.5 3.3 3.5

Thamani ($

milioni)

727.5 835.9 982.7 1,075.9 1,103.4 1,508.7 1,980.2 2,302.5 1,918.9 1,744.5

120

madini na hatimaye kukuza uchumi wa Taifa. Kufuatia uamuzi huo, Serikali imenunua Mgodi 0 wa Tulawaka uliokuwa unamilikiwa na Kampuni ya Barrick Gold Limited na Pangea Minerals Limited kwa gharama ya Dola za Marekani milioni tano (5) na imesajili Kampuni Tanzu ya Stamigold Company Limited itakayoendesha mgodi huo. Mkataba wa uhamishaji wa umiliki wa mgodi huo ulisainiwa baina ya STAMICO na Pangea Minerals Limited (PML) kampuni tanzu ya ABG mwezi Novemba, 2013 kwa lengo la kuhamisha mitambo ya uchenjuaji, maeneo ya uchimbaji pamoja na Kambi ya Uchimbaji (Mining Camp). Kufuatia uhamisho huo, STAMICO imeanza uzalishaji mwezi Julai, 2014 na kufanikiwa kutoa mkuo (gold bar) wa kwanza wa dhahabu wa kilo 25 wenye thamani ya Shilingi bilioni 1.5. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Septemba, 2014 kiasi cha dhahabu kilichozalishwa kilifikia kilo 103.1 zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 3.29 sawa na Shilingi bilioni 5.4. Aidha, Watanzania 340 wameajiriwa kwenye mgodi huo.STAMICO pia iliingia ubia na Kampuni ya TANZAM 2000 (STAMICO hisa 45 na TANZAM hisa 55) kwa mradi wa uendelezaji upya wa mgodi wa Buckreef. Aidha, STAMICO imepata mbia Kampuni ya Manjaro Resources ya Australia kwa ajili ya kuendeleza mgodi wa dhahabu wa Buhemba ambapo Serikali itamiliki hisa asilimia 40 na kupata gawio la asilimia 30 ya thamani ya dhahabu itakayozalishwa.

121

Katika hatua nyingine, mwezi Desemba, 2013, Serikali iliingia mkataba na Tanzanite One Mining Limited (TML) wa uendeshaji Mgodi wa Tanzanite uliopo Mererani kwa ubia wa hisa kwa uwiano wa 50:50. Kupitia mkataba huo, TML ina jukumu la kuendesha mgodi (operator) na STAMICO ni Mbia ambapo hushiriki katika kusimamia maendeleo ya mgodi.

Kuwajengea Uwezo Wachimbaji Wadogo wa MadiniKatika kipindi cha Mwaka 2005 - 2014, jumla ya kilometa za mraba 1,638.9 ambazo ni sawa na hekta 163,890 katika maeneo 22 zimetengwa kwa ajili ya uchimbaji mdogo. Maeneo hayo yanaweza kutoa takriban leseni 16,389 za wastani wa ukubwa wa hekta 10 kila moja. Aidha, katika kipindi hicho, jumla ya leseni 8,800 za uchimbaji mdogo zilitolewa ikilinganishwa na leseni 4,056 zilizotolewa katika maeneo matatu (3) yaliyotengwa katika kipindi cha kabla ya mwaka 2005. Kutokana na juhudi hizo, idadi ya wachimbaji wadogo imeongezeka kutoka watu 500,000 mwaka 2005 hadi watu 2,000,000. Mwaka 2009, Serikali ilianza kutoa mikopo kwa kampuni za kutoa huduma za ukodishaji wa vifaa kwa wachimbaji wadogo. Kampuni 3 zilikopeshwa kiasi cha Shilingi milioni 488 ili kutekeleza lengo hilo. Aidha, katika mwaka huo vikundi viwili (2) vya akina mama vilikopeshwa jumla ya Shilingi milioni 85 ili kuanzisha vituo vya uongezaji thamani kwa madini ya vito.

122

Mwaka 2009, Serikali ilianza kutoa mikopo kwa kampuni za kutoa huduma za ukodishaji wa vifaa kwa wachimbaji wadogo. Kampuni 3 zilikopeshwa kiasi cha Shilingi milioni 488 ili kutekeleza lengo hilo. Aidha, katika mwaka huo vikundi viwili (2) vya akina mama vilikopeshwa jumla ya Shilingi milioni 85 ili kuanzisha vituo vya uongezaji thamani kwa madini ya vito. Vilevile, kuanzia mwaka 2011 Serikali ilianza kutenga fedha kwenye Bajeti yake kwa ajili ya kuwezesha wachimbaji madini wadogo. Jumla ya Shilingi bilioni 1.39 zimekwishatolewa kufikia mwezi Machi, 2015 kwa ajili ya uwezeshaji wa miradi 16 ya uchimbaji mdogo.  Kuanzia mwaka 2013, Serikali ilianza utaratibu wa kutoa mikopo ya masharti nafuu na ruzuku kwa wachimbaji wadogo kupitia Benki ya Maendeleo ya TIB. Hundi za awamu ya kwanza za ruzuku hiyo zenye jumla ya Dola za Marekani 537,000 sawa na Shilingi milioni 880.68 zilikabidhiwa kwa walengwa mwezi Aprili, 2014. Hata hivyo, kutokana na wengi wa wachimbaji wadogo kukosa sifa za kupewa mikopo kupitia TIB, Serikali imeamua kuboresha masharti ya mikopo hiyo ambapo sasa itatolewa kwa utaratibu wa ruzuku.

123

Vilevile, kuanzia mwaka 2011 Serikali ilianza kutenga fedha kwenye Bajeti yake kwa ajili ya kuwezesha wachimbaji madini wadogo. Jumla ya Shilingi bilioni 1.39 zimekwishatolewa kufikia mwezi Machi, 2015 kwa ajili ya uwezeshaji wa miradi 16 ya uchimbaji mdogo.  Kuanzia mwaka 2013, Serikali ilianza utaratibu wa kutoa mikopo ya masharti nafuu na ruzuku kwa wachimbaji wadogo kupitia Benki ya Maendeleo ya TIB. Hundi za awamu ya kwanza za ruzuku hiyo zenye jumla ya Dola za Marekani 537,000 sawa na Shilingi milioni 880.68 zilikabidhiwa kwa walengwa mwezi Aprili, 2014. Hata hivyo, kutokana na wengi wa wachimbaji wadogo kukosa sifa za kupewa mikopo kupitia TIB, Serikali imeamua kuboresha masharti ya mikopo hiyo ambapo sasa itatolewa kwa utaratibu wa ruzuku.

124

Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimkabidhi mchimbaji mdogo wa madini kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Mwalazi Bw. Juma Digalu, hundi ya Dola za Marekani 50,000 ikiwa ni Ruzuku ya Serikali kwa wachimbaji wadogo kupitia Benki ya Maendeleo TIB, mjini Dodoma, 2014.Vilevile mwaka 2009 Serikali imeanzisha Kituo cha Uongezaji wa Thamani Madini Arusha (Tanzania Gemological Centre - TGC) kwa lengo la kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo juu ya namna ya kuongeza thamani madini wanayozalisha.

Ukaguzi wa Migodi

Mwaka 2009, Serikali ilianzisha Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) kwa lengo la kuhakikisha kuwa inapata mapato stahiki kutokana na shughuli za uzalishaji na biashara ya madini nchini. Pia, Wakala ilipewa jukumu la kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinafanyika kwa kuzingatia uhifadhi na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya migodi. Kutokana na ukaguzi wa TMAA, Serikali imeweza kukusanya kodi ya mapato jumla ya Shilingi bilioni 537.9 kutoka katika migodi ya Geita, Golden Pride, Tulawaka na Mwadui.

125

Aidha, Serikali ilikusanya malipo mbalimbali baada ya kubainika kutolipwa na migodi, ambapo jumla ya Shilingi bilioni 17.06 zililipwa Serikalini na migodi mikubwa na ya kati iliyokaguliwa katika kipindi cha mwaka 2005 hadi Agosti, 2014. Malipo hayo yanajumuisha mrabaha, kodi ya zuio na ushuru wa huduma.

Aidha, utunzaji wa mazingira umeimarika kwenye maeneo ya migodi mikubwa nchini kutokana kaguzi za mara kwa mara zinazoendeshwa na Wakala kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

126

SURA YA NNEHUDUMA ZA KIUCHUMI

i. ARDHISerikali imeendelea kutekeleza maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM kuhusu maendeleo ya ardhi kwa kudumisha na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana. Mafanikio makubwa yamepatikana katika kipindi cha miaka 10 ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Utawala wa ArdhiSerikali imeendelea kusimamia Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 na Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999 ili kuwawezesha wananchi hususan maskini kumiliki ardhi kama mtaji muhimu kwa ajili ya makazi, kilimo, kuanzisha biashara mbalimbali na hivyo kukuza ajira na kupunguza umaskini. Chini ya sera na sheria hizo, kila Mtanzania ana fursa sawa ya kumiliki ardhi tofauti na nchi takriban zote duniani. Kwa mfano, katika nchi za kiafrika ardhi inamilikiwa na watu matajiri, kifalme au kiukoo. Katika mfumo huo wa umilikaji ardhi, watu maskini hawana fursa yoyote ya kumiliki ardhi kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

127

Ili kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi, Serikali imeanzisha Kanda nane (8) za Utawala wa Ardhi kwa ajili ya kusimamia upangaji, upimaji na kutoa hatimiliki. Kanda hizo ni Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), Ziwa (Mwanza), Kaskazini (Moshi), Magharibi (Tabora), Kati (Dodoma), Kusini (Mtwara), Kanda ya Mashariki (Morogoro) na Kanda ya Dar es Salaam inayohudumia Mkoa wa Dar es Salaam. Aidha, jumla ya Hati miliki 164,275 zimetolewa kwa wananchi na taasisi kuanzia mwaka 2006 hadi Machi, 2015.

Mipango MijiSerikali ya Awamu ya Nne imezijengea uwezo Halmashauri za Miji na Wilaya ili ziweze kupanga miji, kupima viwanja na kuuza kwa wanaohitaji kwa kutumia fedha za Mfuko wa Mzunguko (Development Revolving Fund). Halmashauri mbalimbali nchini zimekopeshwa jumla ya Shilingi bilioni 4.7 kwa ajili ya kupima viwanja. Halmashauri hizo ni kama inavyoonekana katika jedwali namba 7.

128

Na Halmashauri Fedha zilizotumika (000,000)

Idadi ya Viwanja vilivyopimwa

1 Jiji la Mwanza 1,230 3,500

2 Jiji la Mbeya 600 5,000

3 Manispaa ya Morogoro 400 4,000

4 Mji wa Kibaha 470.4 500

5 Wilaya ya Bagamoyo 600 3,000

6 Manispaa ya Kinondoni 600 5,000

7 Manispaa ya Ilala 400 1,000

8 Manispaa ya Temeke 400 3,000

Jedwali Na.7 Upimaji wa Viwanja Katika Halmashauri

Hadi kufikia Novemba 2014, jumla ya Shilingi bilioni 3.9 zimerejeshwa. Aidha, Halmashauri za Wilaya 48 zimekopeshwa jumla ya Shilingi bilioni 6.9 kwa ajili ya kupima viwanja. Vilevile, Serikali imefanya uthamini na kulipa fidia stahiki kwa wamiliki wa asili wa ardhi ili kupata ardhi huru ya kupima viwanja katika Miji Mikuu ya Mikoa.

129

Upimaji na RamaniSerikali imekamilisha kujenga Mtandao Mpya wa Alama 688 za Msingi za Upimaji Ardhi Nchini (National Geodetic Control Network - NGCN). Mtandao wa Alama hizo, utarahisisha upimaji wa ardhi kwa matumizi mbalimbali na kupunguza gharama za upimaji nchini. Kutokana na hatua hiyo, Serikali imekamilisha upimaji picha na uhakiki wa ardhini kwa ajili ya utayarishaji wa ramani za msingi za Kitalu cha Kiomboi za uwiano wa 1:50,000 na upimaji picha na uhakiki wa ramani katika miji 10 ya Kanda ya Kusini katika uwiano wa 1:2,500. Aidha, Serikali inaendelea kuandaa na kusanifu ramani za msingi za maeneo ya Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera, Mara, Kigoma, Mtwara, Lindi, Ruvuma, Mbeya na Iringa; kutayarisha ramani za Jiji la Dar es Salaam na miji 15 katika Kanda ya Kaskazini Mashariki; na upigaji picha za anga, uhakiki ardhini na uandaaji wa picha za satellite (geo-referencing) katika miji 45 na Vitalu vya Mikoa ya Kagera, Kigoma, Mbeya na Jiji la Dar es Salaam.

Upimaji wa Mipaka ya VijijiJumla ya mipaka ya vijiji 10,500 imepimwa na kutoa vyeti vya ardhi kwa kijiji 10,341 nchini. Aidha, wananchi wameendelea kumilikishwa ardhi vijijini kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na kijamii ambapo jumla ya hakimiliki za kimila 175,289 ziliandaliwa na hati 169,362 zilitolewa kwa wananchi katika vijiji vilivyopimwa na kupewa vyeti vya ardhi vya vijiji.

130

Mpango wa Taifa wa Matumizi Bora ya ArdhiSerikali imeandaa Mipango ya Matumizi ya Ardhi kwa njia shirikishi katika vijiji 1,215 vilivyopo katika wilaya 32 nchini. Wilaya hizo ni Ngorongoro, Longido, Monduli, Kilolo, Muleba, Mpanda, Kilwa, Lindi, Nachingwea, Babati, Rorya, Tarime, Mbarali, Chunya, Kilosa, Kilombero, Ulanga, Mvomero, Mtwara, Newala, Geita, Makete, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe, Mafia, Rufiji, Namtumbo, Bariadi, Muheza, Mkinga na Pangani.

Vilevile, kwa kushirikiana na Halmashauri mbalimbali, Serikali imepima mashamba 178 katika mikoa ya Arusha na Morogoro ili kuingizwa kwenye Hazina ya Ardhi kwa ajili ya wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Mfumo wa Teknolojia ya Kompyuta Katika Kutoa Huduma za ArdhiSerikali inaendelea kuimarisha Mfumo wa Utunzaji wa Kumbukumbu za Ardhi kwa kuziunganisha Halmashauri za Miji na Wilaya 136 katika Mfumo wa Teknolojia ya Kompyuta (LRMS) wa kutunza kumbukumbu za ardhi na kukadiria kodi ya pango la ardhi. Mfumo huo unalenga kuboresha utaratibu wa upatikanaji wa hatimiki za ardhi na kusogeza huduma za upimaji, upangaji na usimamizi wa ardhi karibu na wananchi.  

131

Uanzishaji wa Miji Midogo (Satelite Towns)Serikali imeanzisha Miji midogo (Satelite Towns) ili kudhibiti msongamano wa watu na magari katika Jiji la Dar es Salaam kupunguza gharama za uzalishaji na uendeshaji na kupunguza ongezeko la makazi holela katika maeneo ambayo hayajapangwa. Aidha, Serikali imeunda Wakala wa kusimamia uendelezaji Mji Mpya wa Kigamboni ambao ni Mamlaka ya Upangaji wa eneo la Mji Mpya Kigamboni lenye Kata tisa za Kigamboni, Tungi, Vijibweni, Mjimwema, Kibada, Somangila, Kisarawe II, Kimbiji na Pemba Mnazi. Aidha, Rasimu ya Mpango Kabambe wa Mji Mpya wa Kigamboni imeandaliwa, ujenzi wa daraja la Kigamboni na barabara kiunganishi unaendelea chini ya Wizara ya Ujenzi; eneo la upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam katika Kata ya Vijibweni limebainishwa na utaratibu mpya wa uendelezaji wa Mji huo ulipitiwa na kuridhiwa na wadau wa Kigamboni.

Serikali imefanya uthamini katika eneo la Uvumba, Kata ya Kibada litakalotumika kwa ujenzi wa makazi mbadala ya wananchi watakaopisha ujenzi wa miundombinu. Serikali pia inaendelea na kutayarisha Mipango Kabambe ya Kawe (ekari 240.0), Luguruni (ekari 156.53) na Uvumba, Kigamboni (ekari 202.0) katika Mkoa wa Dar es Salaam. Vilevile, Serikali imetayarisha Mipango Kabambe ya kuendeleza maeneo ya Burka/Matevesi (ekari 579.2) na Usa River (ekari 296.0) katika Mkoa wa Arusha. Mchakato wa kuanza ujenzi na kuwapata wawekezaji wenza kwenye maeneo haya unaendelea.  

132

Mabaraza ya ArdhiSerikali imeendelea kuboresha utendaji kazi wa Mabaraza ya Wilaya na Nyumba ambayo yamefikia 49 kutoka 39 mwaka 2005. Mabaraza 26 yameundwa katika Wilaya za Kilombero, Simanjiro, Karatu, Njombe, Rungwe, Tarime, Geita, Mbinga, Same, Chato, Maswa na Kondoa. Wilaya nyingine ni Korogwe, Ukerewe, Geita Iramba, Nzega, Manyoni, Kilosa, Tunduru, Mpanda, Kyela, Muleba, Ngara, Karagwe na Ngorongoro. Sambamba na Mabaraza hayo, jumla ya Wenyeviti 49 wa Mabaraza wameajiriwa katika Wilaya zenye migogoro mingi. Wilaya za Ilala, Temeke, Kinondoni, Kibaha, Arusha, Morogoro, Mwanza, Dodoma, Musoma na Bukoba yalipewa Wenyeviti wawili wawili. Aidha, idadi ya siku za vikao iliongezwa kutoka viwili hadi vinne kwa wiki. Mabaraza haya yameweza kupokea mashauri 72,518 kwa mwaka ambapo asilimia 90 ya mashauri hayo yamesikilizwa na kutolewa uamuzi.

NYUMBASerikali imehamasisha wananchi kujenga nyumba bora kwa kutumia vifaa na teknolojia rahisi za ujenzi. Aidha, kwa kuzingatia mazingira halisi ya Mijini na kasi ya ukuaji wa Miji, Sheria ya Miliki ya Sehemu za Jengo Na.16 ya mwaka 2008 (The Unit Titles Act No. 16 of 2008) imetungwa. Sheria hiyo

133

inawezesha mwananchi kupata hatimiliki ya sehemu ya jengo. Hii itawezesha kipande kimoja cha Ardhi hasa Mijini kuwanufaisha Wananchi wengi, na kuongeza Soko la Nyumba na Mapato ya Serikali. Vilevile, Sheria ya Mikopo ya Nyumba Na. 17 ya Mwaka 2008 (The Mortagage Financing Act No. 17 of 2008) imetungwa ili kupunguza tatizo la kupata mikopo ya ujenzi na ununuzi wa nyumba.

Ujenzi wa Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linatekeleza mkakati wa ujenzi wa nyumba za makazi kwa ajili ya kuuza na kupangisha; ujenzi wa majengo ya vitega uchumi; na kuzifanyia matengenezo nyumba na majengo mbalimbali. Shirika la Nyumba la Taifa limekamilisha ujenzi wa nyumba za makazi 395 kwa ajili ya kuuza na kupangisha kwa gharama ya Shilingi bilioni 17.7. Nyumba hizo zimejengwa katika maeneo ya Boko, Mbezi Beach na Mbweni JKT (Dar es Salaam); Ruangwa (Lindi); Chato (Geita); Chalinze (Pwani); Medeli (Dodoma); Kibla na Mtaa wa Haile Selasie (Arusha). Majengo matatu ya vitega uchumi yamekamilishwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 44.9 katika miji ya Iringa, Kigoma, Arusha, Jiji la Dar es Salaam na Manispaa ya Shinyanga na majengo 73 yanaendelea kujengwa kwa ushirikiano na Sekta Binafsi kwa gharama ya Shilingi bilioni 131.

134

Majengo 25 yamekamilika na ujenzi wa majengo mengine 48 unaendelea katika Majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Manispaa ya Morogoro. Aidha, kwa upande wa ujenzi wa nyumba za makazi na biashara, nyumba zimeongezeka kutoka 4,814 mwaka 2005 hadi kufikia 6,494 mwaka 2014 kwa gharama ya Shilingi bilioni 387. Kati ya nyumba hizo, nyumba 2,475 ni za gharama nafuu na nyumba 3,425 ni za gharama ya kati na juu.

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizindua mradi wa ujenzi wa Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa.

135

Ujenzi wa Majengo/Nyumba za Serikali

Katika kipindi cha Mwaka 2005 hadi 2014, Serikali imetekeleza miradi 95 ya ujenzi wa nyumba na majengo ya Serikali yenye thamani ya Shilingi bilioni 71.2. Kati ya miradi hiyo, miradi 60 yenye thamani ya Shilingi bilioni 26.4 ni ya ujenzi wa nyumba za viongozi na ofisi za Serikali na miradi 35 yenye thamani ya Shilingi bilioni 44.5 ni ya ujenzi wa nyumba za Watumishi wa Umma na majengo ya biashara. Aidha, katika miradi iliyotekelezwa, jumla ya nyumba 173 za makazi ya viongozi wa Umma zilikamilika na nyumba 31 zinaendelea kukamilishwa. Kwa upande wa nyumba za makazi ya watumishi wa Umma, jumla ya nyumba 643 zilikamilika na nyumba 270 zinaendelea kukamilishwa.

Serikali pia imenunua jumla ya viwanja 2,990 na maeneo makubwa 9 (housing estates) katika mikoa yote ya Tanzania Bara kwa ajili ya kujenga nyumba za watumishi wa umma. Serikali inamiliki viwanja katika maeneo ya Nzuguni (Dodoma), Bunju na Gezaulole (Dar es Salaam) vinavyotarajiwa kuendelezwa katika mradi maalum wa ujenzi wa nyumba 10,000.

136

Mikopo ya Ujenzi wa Nyumba1.Serikali imeendelea kutoa mikopo kwa Watumishi wa umma kwa ajili ya kujenga nyumba. Jumla ya Shilingi bilioni 5.4 zimekwishatolewa ambapo watumishi 1,169 wamenufaika tangu kuanzishwa kwa mfuko huo mwaka 2008.

NISHATI2.Serikali imechukua hatua za kuboresha Sera na Sheria mbalimbali kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa Sekta ya Nishati. Hatua hizo ni pamoja na kuandaa Sera ya Gesi Asilia ya mwaka 2013 ambapo itaweka usimamizi thabiti katika Sekta ya Gesi Asilia; kurekebisha Sera ya Nishati ya mwaka 2003 ili kuwa na Sera ya Nishati ambayo ipo katika hatua ya ukamilishwaji; kufanya maandalizi ya kutunga Sera ya Petroli na Sera ya Ushiriki wa Wazawa kwenye Rasilimali za Mafuta na Gesi Asilia. Aidha, Serikali imetunga Sheria mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sheria iliyoanzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA); Sheria iliyoanzisha Wakala wa Nishati Vijijini (REA); Sheria Mpya ya Umeme ambayo imeruhusu sekta binafsi kushiriki katika kuzalisha na kuuza umeme; Sheria ya Petroli ambayo imeboresha usimamizi wa Sekta ya Petroli kwa kujenga mazingira ya ushindani wenye tija na kudhibiti upandaji holela wa bei za mafuta.

137

Utafutaji wa Gesi Asilia na MafutaSerikali ilielekeza juhudi za utafutaji mafuta na gesi asilia kwa kuvutia wawekezaji katika kina kirefu baharini na mabonde ya ufa. Kwa mara ya kwanza Serikali ilitoa leseni za utafutaji mafuta na gesi katika mabonde ya Ziwa Tanganyika, Malagarasi, Kilosa, Kilombero, Pangani, Ruhuhu, Kyela na Tanga. Serikali imesaini mikataba 24 ya uzalishaji na ugawanaji wa mapato (Production Sharing Agreements - PSAs). Idadi hiyo ni kubwa ikilinganishwa na mikataba 13 iliyosainiwa kati ya Mwaka 1952 hadi 2004.

Katika kipindi cha Mwaka 2005 hadi Septemba, 2014 idadi ya visima vya utafutaji mafuta vilivyochorongwa vilikuwa 45. Kati ya visima hivyo, visima 20 viligundulika kuwa na gesi. Idadi hii ni kubwa kwa kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya utafutaji wa mafuta na gesi hapa nchini. Wastani wa uchimbaji visima kati ya Mwaka 1952 na Mwaka 2004 ulikuwa chini ya kisima kimoja (1) kwa mwaka. Wastani huo kwa kipindi cha Mwaka 2005 na Mwaka 2014 ulifikia visima 5 kwa mwaka.Mafanikio makubwa yamepatikana katika kipindi cha Mwaka 2005 hadi 2014, ambapo gesi asilia iligunduliwa nchi kavu katika maeneo ya Mkuranga Mwaka 2007, Nyuni wilayani Kilwa Mwaka 2008 na Ntorya wilayani Mtwara Mwaka 2012. Aidha, mwaka 2010 ugunduzi wa kwanza wa gesi asilia katika kina kirefu baharini ulifanyika katika kitalu namba 4 (Kisima cha Pweza -1).

138

Kisima hicho kilichochea juhudi za Serikali katika utafutaji wa mafuta na gesi baharini ambapo hadi Septemba, 2014 visima 27 vilichorongwa. Hadi mwezi Machi 2015, hazina ya gesi asilia iliyogunduliwa ilifikia futi za ujazo trilioni 55.08 ikilinganishwa na futi za ujazo trilioni 8 mwaka 2005. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 587.5 ya hazina iliyokuwepo mwaka 2005.

Ujenzi wa Bomba na Usambazaji wa Gesi Asilia

Visima vinne vya uzalishaji gesi asilia vilivyopo Mnazi Bay Mtwara vilikamilishwa kati ya Mwaka 2006 na 2007. Pia, ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi asilia yenye uwezo wa kusafisha hadi futi za ujazo milioni 10 kwa siku (10 mmscfd) ulikamilishwa. Bomba lenye urefu wa kilometa 27 na uwezo wa kusafirisha gesi hadi futi za ujazo milioni 70 kwa siku (70 mmscfd) kutoka Mnazi Bay hadi Mtwara Mjini limekamilika. Mtambo wa kufua umeme ulisimikwa Mtwara Mjini na ufuaji umeme kwa kutumia gesi ya Mnazi Bay ulianza Mwaka 2006. Vilevile, miundombinu ya kusafirishia umeme kutoka Mtwara kwenda miji ya Lindi na Masasi ilikamilika. Kupitia Mradi huo, Miji ya Mtwara, Lindi na Masasi inapata umeme wa uhakika tangu Mwaka 2006 mradi huo ulipoanza, ambapo matumizi ya gesi kwa siku ni futi za ujazo milioni mbili (2 mmscfd). 

139

Mwezi Juni, 2012 Serikali ilisaini makubaliano ya mkopo nafuu na Benki ya Exim ya China kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi

asilia na bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mnazi Bay - Mtwara na Songosongo Kisiwani (Lindi) hadi Dar es Salaam lenye urefu wa kilomita 542. Gharama za mradi huo ni Dola za Marekani milioni 1,225.3, sawa na Shilingi

trilioni 1.96. Ujenzi wa Bomba hilo umekamilika. Vile vile, Ujenzi wa nyumba za wafanyakazi 16 katika eneo la Songosongo na madimba umekamilika. Aidha, ujenzi wa mitambo ya kasafisha gesi asilia katika eneo la Madimba, Mtwara

umefikia asilimia 99 na mitambo ya Songo Songo Lindi umefikia asilimia 97. Mitambo na bomba hilo inatarajiwa kuanza kufanya kazi ifikapo Septemba, 2015.

Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikagua ujenzi wa Bomba la Gesi Asilia mkoani

Mtwara.

140

Ujenzi wa Miundombinu ya Usafirishaji UmemeSerikali ya Awamu ya Nne iliweka mikakati mahsusi ya kuongeza uzalishaji wa umeme ili kufikia lengo la kuzalisha MW. 2,780 ifikapo Mwaka 2015/2016. Katika kipindi cha Mwaka 2005 hadi Oktoba, 2014, Serikali imefanikiwa kuongeza kiasi cha umeme kinachozalishwa na kuingizwa katika Gridi ya Taifa kutoka MW. 891 Mwaka 2005 hadi kufikia MW. 1,396 mwezi Oktoba, 2014 sawa na ongezeko la asilimia 57.

Hatua hii imefikiwa kutokana na utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme ikiwemo ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa MW. 100 wa Ubungo I; ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa MW. 45 waTegeta; ujenzi wa mtambo wa kufua umeme, wa MW. 105 wa Ubungo II; ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa MW 60 wa Mwanza; na kukamilika kwa mradi wa umeme wa Somanga Fungu, MW. 7.5. Miradi mingine inaendelea kukamilishwa ikiwa ni pamoja na mradi wa Kinyerezi I wa MW. 150 utakaotumia gesi asilia ambao hadi Juni, 2015, ulikuwa umefikia asilimia 90 ya utekelezaji.

141

Serikali ya Awamu ya Nne ilipoingia madarakani mwaka 2005, idadi ya Watanzania waliounganishiwa umeme (connection level) ilikuwa asilimia 10 na wananchi waliokuwa wakipata huduma ya umeme (access level) walikuwa asilimia 13. Kufuatia jitihada mahsusi za Serikali ikiwemo punguzo la gharama za kuunganisha umeme pamoja na uwezeshaji chini ya Mfuko wa Nishati Vijijini (Rural Energy Fund - REF), kiwango cha uunganishwaji umeme vijijini kimeongezeka kutoka asilimia 2 Mwaka 2005 hadi asilimia 17 Mwaka 2014. Lengo la Serikali lilikuwa kuwawezesha Watanzania asilimia 30 kuunganishiwa umeme ifikapo Mwaka 2015/16. Hadi kufikia Machi 2014, wananchi wanaopata huduma ya umeme walifikia asilimia 36 ya Watanzania waishio Tanzania Bara.

Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akibofya kitufe huku akishuhudiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) Bw. Daniel Wolde Johannes na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Alfonso Lendhardt kuashiria uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani kupitia MCC April 2013.

142

Usambazaji wa Umeme VijijiniSerikali ilitekeleza awamu ya kwanza ya mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini kwenye baadhi ya maeneo katika mikoa 25 ya Tanzania Bara. Chini ya mradi huo, wilaya 17 zimeunganishiwa huduma za umeme na kufanya Makao Makuu ya Wilaya zilizopata umeme kufikia 125 kati ya Wilaya 135 zilizopo. Aidha, kupitia REA, Serikali imepeleka umeme kwenye maeneo mbalimbali ya uzalishaji mali na huduma za jamii. Jumla ya Shule za Sekondari 1,845; zahanati na vituo vya afya 898 na hospitali 96 zilipatiwa umeme katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara pamoja na vijiji 4,718 kupitia REA. Awamu ya pili inaendelea kutekelezwa ambapo lengo ni kufikisha umeme vijijini katika mikoa yote ya Tanzania Bara pamoja na kufikisha umeme kwenye Makao Makuu ya Wilaya zilizopo kwenye mpango. Jedwali Namba 8 linaonesha idadi ya vijiji vilivyopata umeme kupitia REA.

143

Mkoa Wilaya Idadi ya vijiji

Arusha Arusha, Arumeru, Monduli, Ngorongoro na Longido 198

Dodoma Dodoma, Mpwapwa, 205

Iringa na Njombe Makambako, Ludewa, Makete na Iringa Vijijini 252

Kagera Ngara na Karagwe 85

Kigoma Kibondo, Kasulu na Kigoma Vijijini 102

Kilimanjaro Moshi, Rombo, Hai, Mwanga na Same 466

Lindi Kilwa, Nachingwea, Ruangwa na Lindi Vijijini 92

Mara Bunda, Butiama, Musoma, Rorya, Serengeti na Tarime 155

Manyara Babati, Hanang, Mbulu na Simanjiro 194

Mbeya Chunya, Mbozi, Rungwe, Ileje na Mbeya Vijijini 338

Morogoro Mvomero, Kilosa, Kilombero, Ulanga na Morogoro Vijijini 280

Mtwara Newala, Masasi, Tandahimba, Nanyumbu na Mtwara vijijini 119

Jedwali Na.8 Miradi ya Umeme Vijijini

144

Mwanza Nyamagana, Misungwi, Sengerema, Magu na Ilemela 286

Pwani Kisarawe, Bagamoyo, Mkuranga, Kibaha na Mafia 223

Ruvuma Songea, Namtumbo, Mbinga na Tunduru 110

Rukwa Nkasi na Sumbawanga 50

Singida Manyoni, Iramba, Ikungi na Singida 139

Tabora Urambo, Kaliua na Nzega 172

Tanga Korogwe, Handeni, Muheza, Kilindi na Lushoto 373

Katavi 9

Geita 62

Simiyu 126

JUMLA 4,718

Chanzo: Wizara ya Nishati na Madini, 2015.

145

Nishati Mbadala (Nishati Jadidifu)Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kupunguza utegemezi wa umeme unaozalishwa kwa kutumia vyanzo vya maji. Hatua mojawapo ni uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati jadidifu (renewable energy). Serikali imekamilisha utafiti wa kijiolojia, kijiofizikia katika eneo la Ziwa Ngozi mkoani Mbeya kwa ajili ya kuzalisha umeme kutokana na Jotoardhi (Geothermal). Utafiti unafanyika katika maeneo ya Mbaka na Ziwa Ngozi kwa ajili ya uhakiki wa uwezo wa kufua umeme kutokana na jotoardhi.

Aidha, Serikali imeanzisha Kampuni inayoitwa Tanzania Geothermal Development Company Limited (TGDC) itakayoratibu utafiti, uchorongaji visima, uendelezaji wa jotoardhi na kutoa ushauri wa kitalaamu.

UJENZI Mfuko wa Barabara

Serikali imeendelea kuongeza fedha katika Mfuko wa Barabara kutoka Shilingi bilioni 73.08 mwaka 2005 hadi Shilingi bilioni 751.7 mwaka 2014. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 928.6 kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 4.

146

Kielelezo Na.4 Mapato ya Fedha za Mfuko wa Barabara (2005/06 - 2014/15)

Chanzo: Mfuko wa BarabaraUjenzi wa Barabara, Madaraja na Vivukoi. Barabara Katika kipindi cha mwaka 2005 - 2015, jumla ya kilometa za Barabara Kuu na za Mikoa zenye urefu wa kilomita 17,762 zimekuwa katika hatua mbalimbali za ujenzi. Barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 5,568

147

zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami. Kati ya hizo, barabara zenye urefu wa kilometa 1,226 zilianzishwa na Serikali ya Awamu ya Tatu na kukamilishwa na Serikali ya Awamu ya Nne na kilometa 4,342 zilianzishwa na kukamilishwa na Serikali ya Awamu ya Nne. Aidha, barabara zenye jumla ya kilometa 3,873 zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami. Vilevile, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umekamilika kwa barabara zenye urefu wa kilometa 4,965 na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina unaendelea kwenye barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 3,356. Jedwali namba 9 linaonesha taarifa hizo kwa ufupi.

Jedwali Na 9: Muhtasari wa Miradi ya Barabara na Madaraja iliyotekelezwa katika kipindi cha Awamu ya Nne (2005-2015)

148

A: Miradi iliyosainiwa kabla ya 2005 na kukamilika kipindi

cha Awamu ya Nne

Aina ya Mradi Urefu (Km.) Idadi (Na.)

Barabara 1,226

Madaraja 2

B: Miradi iliyosainiwa baada ya 2005 na kukamilika kipindi

cha Awamu ya Nne

Barabara 4,342

Madaraja 10

C: Miradi iliyosainiwa baada ya 2005 na utekelezaji wake

unaendelea

Barabara 3,873

Madaraja 5

D: Miradi iliyofanyiwa Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina

na ujenzi haujaanza.

Barabara 4,965

Madaraja 8

E: Miradi ambayo Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina

unaendelea.

Barabara 3,356

Madaraja 5

Jumla 17,762 30

Jedwali Na 9: Muhtasari wa Miradi ya Barabara na Madaraja iliyotekelezwa katika kipindi cha Awamu ya Nne (2005-2015)

149

Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga wilayani Biharamulo mkoani Kagera.

150

Madaraja

Serikali imekamilisha Daraja la Umoja (Unity Bridge) na kujenga madaraja mengine kumi na moja (11) ambayo ni Rusumo (Kagera), Mwanhuzi (Simiyu), Kikwete (Kigoma), Nangoo (Mtwara), Ruhekei (Ruvuma), Mbutu (Tabora), Mwatizi (Morogoro), Ruvu (Pwani), Nanganga (Mtwara), Maligisu (Tabora) na daraja la waenda kwa miguu Mabatini (Mwanza). Pia, Serikali inaendelea kukamilisha madaraja makubwa 5 ya Kigamboni (Dar es Salaam), Kilombero (Morogoro), Kavuu (Katavi), Sibiti (Singida) na Lukuledi II (Mtwara). Vilevile, madaraja makubwa 13 yako kwenye maandalizi ya kujengwa. Madaraja hayo ni madaraja ya Momba (Mbeya), Mwiti (Mtwara), Simiyu (Mwanza/Mara), Wami (Pwani), Ruhuhu (Ruvuma), Ubungo Interchange (Dar es Salaam), TAZARA (Dar es Salaam), Selander (Dar es Salaam), Ruvu Chini (Pwani), Daraja jipya la Wami Chini (Pwani), Kirumi (Mara), Pangani (Tanga) na daraja la waenda kwa miguu la Furahisha (Mwanza). 

151

Daraja Urefu wa Daraja (m) Urefu wa Barabara za maingiliano (Km.)

Umoja (Mtwara) 720 5.0

Mwanhuzi (Simiyu) 38.6 -

Malagarasi (Kigoma) 200 48.0

Nangoo (Mtwara) 102.7 -

Ruhekei (Ruvuma) 60 0.12

Nanganga (Mtwara) 77.2 0.57

Maligisu (Mwanza) 40 3.0

Mbutu (Tabora) 40 3.0

Mwatisi (Morogoro) 60 0.12

Kilombero (Morogoro) 384 9.142

Sibiti (Singida) 82 25.0

Lukuledi (II) (Mtwara) 27 1.0

Kigamboni (Dar es Salaam) 680 2.5

Jedwali Na 10: Madaraja yaliyojengwa na Kukarabatiwa (2005 – 2014)

152

Ujenzi wa Vivuko Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya vivuko. Miradi inajumuisha ununuzi, ukarabati na ujenzi wa maegesho ya vivuko kwa upande wa Tanzania Bara. Vivuko 24 vinaendelea kutoa huduma katika sehemu mbalimbali za nchi. Vivuko vinavyotoa huduma vimeongezeka kutoka vivuko tisa (9) mwaka 2005 hadi kufikia vivuko 28 mwaka 2015. Hili ni ongezeko la vivuko 19 sawa na asilimia 211 ambapo jumla ya Shilingi bilioni 47.3 zimetumika katika ununuzi. Pia, Serikali imefanya ukarabati mkubwa wa vivuko sita (6) ili viendelee kutoa huduma bora kwa wananchi. Vivuko hivyo ni MV Kigamboni, MV Sengerema, MV Chato, MV Sabasaba, MV Kome I (sasa MV Mara) na MV Geita (sasa MV TEMESA).

153

UCHUKUZISerikali imechukua hatua mbalimbali zenye lengo la kuongeza ufanisi na kukuza sekta ya uchukuzi. Hatua hizo ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu na huduma za barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege. Juhudi hizo za Serikali zimewezesha Sekta ya Uchukuzi kukua kutoka asilimia 6.4 mwaka 2005, hadi asilimia 7.1 mwaka 2014. Aidha, uchangiaji wa Sekta ya Uchukuzi katika pato la taifa umeongezeka kutoka asilimia 5.4 mwaka 2005 hadi asilimia 5.8 mwaka 2014.

Huduma za Usafiri wa Reli Jijini Dar es SalaamKutokana na msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam unaosababishwa na ongezeko la magari, idadi ya watu pamoja na hali halisi ya miundombinu ya barabara na reli, mwaka 2012, Serikali ilichukua hatua ya kuanzisha huduma ya usafiri wa treni Jijini kwa kutumia njia za reli za TAZARA na Reli ya Kati. Huduma hizo zinatolewa na Kampuni ya Reli (TRL) kati ya stesheni za Dar es Salaam na Ubungo Maziwa na TAZARA kuanzia stesheni za Mwakanga hadi Kurasini, Dar es Salaam. Kampuni ya Reli (TRL) imekuwa ikisafirisha abiria 1,343,763 kwa siku sawa na wastani wa safari 123 za daladala kwa siku na kwa upande wa TAZARA wastani wa abiria 1,460,506 kwa siku walisafirishwa sawa na wastani wa safari 133 za daladala kwa siku.

154

Serikali imeweka mipango na mikakati ya kuboresha na kupanua huduma ya usafiri wa treni ya abiria Jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kuongeza eneo la ujenzi wa miundombinu na uboreshaji wa usafiri jijini kutoka umbali wa kilometa 20 za sasa hadi kilometa 50 ili kujumuisha Wilaya za Kibaha, Kisarawe, Mkuranga na Bagamoyo. Aidha mwezi Oktoba, 2014, Serikali kupitia Kampuni ya Reli (TRL) ilitiliana saini mkataba na mwekezaji kwa ajili ya kuanza mradi wa treni za kisasa zijulikanazo kama Diesel Multiple Unit

(DMU). Treni hizi zitatoa huduma ya usafiri wa abiria kutoka Stesheni ya Dar es Salaam hadi Pugu kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA).

Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka yenye urefu wa kilometa 20.9 inayoanzia eneo la Kimara hadi Kivukoni ikijumuisha matawi ya Magomeni hadi Morocco na sehemu ya barabara Msimbazi hadi Kariakoo. Barabara hiyo itakuwa na jumla ya Vituo Vikuu (Terminals) vitano (5) katika maeneo ya Kimara, Ubungo, Morocco, Kariakoo na Kivukoni, na vituo vidogo 27 vitakavyokuwa na uwezo wa kuhudumia mabasi 65 kwa saa kwa kila mwelekeo. Mabasi yatakayotumika yatakuwa na uwezo wa kubeba kati ya abiria 140 mpaka 160. Pia , kutakuwa na mabasi ya ukubwa wa kati ya abiria 50 mpaka 80 yatakayotumia barabara ndogo za Jiji kuleta abiria kwenye barabara kuu. Lengo likiwa kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.

155

Sehemu ya barabara ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka unaotekelezwa Jijini Dar es Salaam.

Reli ya KatiSerikali imeendelea kushirikiana na Serikali za Rwanda na Burundi katika uendelezaji wa mradi wa ujenzi wa reli ya Dar es Salaam – Isaka – Keza - Kigali (Km 1,464) na Keza – Musongati (Km 197) kwa kiwango cha kimataifa. Upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa reli hiyo umekamilika na usanifu wa kina unaendelea.Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa kuwezesha huduma ya Reli kufanya kazi kwa ufanisi kwa kushirikiana na mifumo mingine ya usafiri (Tanzania Intermodal Rail Development Project - TIRP). Mradi wa ukarabati wa reli unatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2019. Aidha, ili kutekeleza mradi huo, mwezi Julai, 2014 Serikali kupitia RAHCO ilisaini mkataba wa Dola za Marekani milioni 300 (takriban Shilingi bilioni 500) kutoka Benki ya Dunia. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kutandika reli nzito za ratili 80 kwa yadi

156

kwa urefu wa Kilomita 308. Reli hizo ni DSM – Pugu (Km. 20), Mpiji - Kilosa (Km. 249) na Igalula - Tabora (Km. 39).Mradi wa kutandika reli za ratili 80 kwa yadi kati ya stesheni za Kitaraka na Malongwe yenye urefu wa Km. 89 ulioanza mwezi Septemba, 2012 ulikamilika mwezi Februari, 2014. Kukamilika kwa ujenzi wa njia ya reli kati ya stesheni za Malongwe na Kitaraka kunafanya reli zilizotandikwa zenye uzito wa ratili 80 kwa yadi kati ya Dar es Salaam na Tabora kufikia jumla ya km 527. Aidha, madaraja ya Km. 293 na Km. 303 kati ya Kilosa na Munisagara na kati ya Bahi na Kintiku yalikarabatiwa.

Reli ya TAZARAReli ya TAZARA huanzia katika Jiji la Dar es Salaam na kuishia katika mji wa New Kapiri Mposhi, Zambia ikiwa na urefu wa Km. 1,860. Kwa upande wa Tanzania, reli hii ina urefu wa Km. 975 na kwa upande wa Zambia ina urefu wa Km. 885.Kwa kutambua umuhimu wa usafiri wa reli, katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2014, Serikali imetoa jumla ya Shilingi bilioni 36.4 kwa ajili ya kuboresha huduma za TAZARA; Shilingi bilioni 4.78 kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi na Shilingi bilioni 4.75 kwa ajili ya kulipa malimbikizo stahili ya watumishi wastaafu wa TAZARA wa upande wa Tanzania. Katika mwaka 2014/2015, Serikali ilitenga Shilingi bilioni 66.0 ili kuongeza mtaji wa uwekezaji na uendeshaji.

157

Miradi inayotarajiwa kutekelezwa ili kuboresha miundombinu na utoaji wa huduma za reli ya TAZARA ni pamoja na kufanya matengenezo kwenye madaraja 265 kwa kuweka mataruma mapya ya mbao na kuweka mawasiliano yanayotumia Mkongo wa Taifa; kuimarishwa uwezo wa karakana ya Dar es Salaam, mgodi wa machimbo ya kokoto na matengenezo ya kiwanda cha mataruma ya zege cha Kongolo; kufanya upembuzi wa kina wa ujenzi wa tawi la reli ya Mlimba – Liganga – Mchuchuma (Km. 260), Uyole – Kiwira – Itungi (Km. 75) na Tunduma - Kasanga Port - Sumbawanga (Km. 400). 

Ununuzi na Ukarabati wa Injini (locomotives) na Mabehewa ya treniSerikali imeingia mkataba wa kununua injini mpya 13 za treni zenye nguvu ya HP 2,200. Mkataba huo ulisainiwa mwezi Aprili, 2013 na malipo yote yameshafanyika. Injini mpya 7 za treni kati ya injini 13 zilizoagizwa zimewasili mwezi Mei, 2015 na injini 6 zilizobaki zinategemewa kuwasili wakati wowote. Upatikanaji wa injini hizo utaongeza uwezo wa kusafirisha mizigo kwa tani 364,000 zaidi. Aidha, mwezi Machi, 2014 Serikali iliingia mkataba wa kununua mabehewa 274 mapya ya mizigo na malipo yamekamilika. Mkandarasi anaendelea na kazi ya ujenzi wa mabehewa hayo na tayari mabehewa 197 yameshawasili nchini mwezi Mei, 2015 na mengine yaliyobaki yanatarajiwa kuwasili nchini hivi karibuni.

158

Pia, Serikali imeingia mkataba wa kununua mabehewa mapya 22 ya abiria ambayo malipo yake yamekwishafanyika. Mabehewa hayo yaliyowasili nchini mwezi Desemba, 2014 na kuzinduliwa tarehe 1 Aprili, 2015 yanatarajiwa kupunguza tatizo la usafiri na msongamano wa abiria katika Reli ya Kati. Mabehewa hayo yameongeza idadi ya treni za abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma na Mwanza kufikia tatu (3) kwa juma kutoka mbili (2) za sasa. Vilevile, Serikali imeshalipia mabehewa 34 mapya ya breki. Mabehewa 17 kati ya 34 yamewasili nchini mwezi Februari, 2015 na mabehewa 17 yaliyobaki yatawasili nchini hivi karibuni. Serikali kupitia TRL iliunda upya injini nane (8) za treni katika karakana ya TRL iliyopo mjini Morogoro. Kazi hiyo ilikamilika mwezi Oktoba, 2014. Uundaji upya wa injini hizo utasaidia kuongeza uwezo wa kusafirisha mizigo kwa tani 224,000 zaidi. Vilevile, ukarabati wa mabehewa 89 ya mizigo na mabehewa 31 ya abiria umekamilika.

159

Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikagua moja kati ya mabehewa mapya 22 ya abiria yaliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kuboresha huduma za Kampuni ya Reli Tanzania (TRL). Kununuliwa kwa mabehewa hayo kutaimarisha huduma za usafiri wa treni ya abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma na Mwanza.

Bandari

Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania ilitayarisha Mpango Kamambe wa Miaka Ishirini wa Kuendeleza Bandari (Ports Master Plan, 2008-2028. Lengo la Mpango huo ni kuzifanya bandari zote nchini kuongeza mchango katika maendeleo ya nchi na kuongeza usafirishaji wa mizigo kwa nchi jirani zinazotumia bandari zetu. Mpango huo unatoa dira na mwongozo wa kuendeleza bandari zote na ulianza kutekelezwa tangu mwaka 2008.Kutokana na juhudi zilizofanyika za kuimarisha Bandari ya Dar es Salaam, shehena katika bandari zimeongezeka kutoka tani milioni 6.7 zilizosafirishwa mwaka 2005 hadi kufikia tani milioni 14.4 zilizosafirishwa katika mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko la asilimia 114.6. Huduma za Bandari ya Dar es Salaam zimeendelea kuwa bora ambapo muda wa meli kukaa

160

bandarini kwa ajili ya kupakia au kupakua mizigo umepungua kutoka siku 12 mwaka 2006 hadi siku 3.1, mwaka 2015. Aidha, uwezo wa bandari kupakua magari kwa kila zamu moja ya saa nane umeongezeka hadi kufikia magari 852.Serikali imesogeza huduma za bandari karibu na wateja, hususan katika nchi jirani ambapo tarehe 1 Mei, 2014, Mamlaka ya Bandari ilifungua ofisi zake mjini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC). Kupitia ofisi hiyo, wateja walioko DRC hawalazimiki kwenda Dar es Salaam wakiwa wamebeba fedha kwa ajili ya kulipia mizigo yao.

Hivi sasa, wateja watalipia huduma za bandari wakiwa DRC na watapokea mizigo yao bila kuhitajika kufika Dar es Salaam. Huduma kama hizo zitaanzishwa katika nchi za Zambia, Burundi na Rwanda.Kuanzia Februari, 2014 Bandari ya Dar es Salaam ilianza kutoa huduma zote kwa saa 24 kwa siku baada ya wadau wote wa Bandari kusaini mkataba wa kutoa huduma katika Bandari ya Dar es Salaam kwa saa 24 kwa siku. Aidha, Benki za NMB na CRDB, tayari zimeanzisha huduma za kibenki ndani ya bandari.

161

Serikali ipo kwenye mchakato wa ujenzi wa Gati mpya Na. 13 na 14. Kazi za ujenzi zinatarajiwa kuanza mwezi Julai, 2015. Kukamilika kwa mradi huo kutaongeza uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam kuhudumia shehena ya makasha (containers) kutoka makasha 600,000 hadi 1,200,000 kwa mwaka.

Aidha, maandalizi ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo yanaendelea ambapo katika hatua za awali, Serikali ilisaini makubaliano (Framework Agreement) na Serikali ya watu wa China mwezi Machi, 2013, ili kampuni ya China Merchant Holdings International Limited (CMHI) iendeleze eneo la Special Economic Zone (SEZ) lililopo mjini Bagamoyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Bandari ya Mbegani.

Bandari ya Tanga imeongezewa uwezo wa kuhudumia shehena kwa kununua tishari kubwa mbili kwa ajili ya kuongeza uwezo wa bandari kuhudumia shehena. Aidha, Gati jipya la kisasa limejengwa katika Bandari ya Kilindoni Mafia. Ujenzi ulikamilika mwezi Septemba, 2013 na kufunguliwa rasmi mwezi Oktoba, 2013. 

Usafiri wa AngaSerikali imeendelea kuimarisha usafiri wa anga kwa kuchukua hatua kadhaa. Hadi kufikia mwaka 2015, Serikali imeingia Mikataba ya Usafiri wa Anga Bilateral Air Services Agreements - BASA na nchi 54 ikilinganishwa na mikataba 41 iliyokuwepo mwaka 2005.

162

Kati ya mikataba ya BASA iliyopo sasa, mikataba ya nchi 22 ndio ambayo kampuni au mashirika yake ya ndege yanatoa huduma kati ya Tanzania na nchi husika. Mashirika ya ndege ya ndani na nje ya nchi yanayotoa huduma nchini kwa sasa ni 27. Safari za ndege kati ya nchi hizo na Tanzania zimeongezeka kutoka safari 78 mwaka 2005 hadi safari 175 kwa juma mwaka 2014.

Aidha, hadi kufikia mwaka 2014, jumla ya kampuni 55 za usafiri wa ndege zilikuwa zinatoa huduma ndani na nje ya nchi ikilinganishwa na kampuni 29 zilizokuwa zikitoa huduma katika mwaka 2005. Hili ni ongezeko la asilimia 89.7. Idadi ya abiria wanaowasili na kuondoka katika viwanja vya ndege nchini imeongezeka kutoka abiria 2,172,519 mwaka 2005 hadi abiria 4,670,380 mwaka 2013 ikiwa ni ongezeko la asilimia 115. Ongezeko hilo la abiria limetokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukua kwa uchumi ambapo kumewezesha wananchi kumudu gharama za usafiri wa anga; kuongezeka kwa utalii nchini kutokana na Serikali kutangaza vivutio vya utalii kimataifa; Kiwanja cha Ndege cha Songwe kuanza kutoa huduma tarehe 16 Januari, 2013 na kukarabatiwa kwa viwanja vya ndege vya Kigoma, Arusha, Mpanda, Musoma na Tabora.

163

Ujenzi na Ukarabati wa Viwanja vya NdegeSerikali imekarabati na inaendelea kupanua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kazi zilizofanyika ni pamoja na kukarabati barabara ya kuruka na kutua ndege; ukarabati na upanuzi wa barabara za kiungio; ukarabati wa maegesho ya ndege; ukarabati wa mfumo wa taa za kuongoza ndege (Precision Approach) pamoja na ukarabati wa mfumo wa maji taka ulioanza mwezi Oktoba, 2008 na kukamilika mwezi Januari, 2011. Baada ya kukamilika kwa mradi huo, Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kimeongeza uwezo wake wa kuhudumia ndege kutoka ndege 7 hadi ndege 30 kwa saa na kukidhi mahitaji ya ndege kubwa na za kisasa za abiria duniani.  Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (Terminal III) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere ulianza rasmi mwezi Januari, 2014 baada ya kukamilika kwa kazi ya usanifu wa kina. Mradi huo ni mkubwa katika historia ya usafiri wa anga nchini na unatekelezwa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza itahusu ujenzi wa jengo lenye uwezo wa kuhudumia abiria milioni 3.5 kwa mwaka kwa gharama ya Shilingi bilioni 293. Awamu hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2015. Awamu ya pili ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria inatarajiwa kuanza mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa awamu ya kwanza. Ujenzi wa awamu ya pili utakaogharimu Shilingi bilioni 225 utaongeza uwezo wa jengo kuhudumia abiria milioni 6 kwa mwaka na hivyo JNIA kuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 7.2 kwa mwaka.

164

Mradi huo utakuwa na maegesho ya ndege za aina zote ikiwemo ndege kubwa kama vile Airbus 380. Pamoja na ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (Terminal III), Serikali inaendelea kufanya ukarabati na upanuzi wa jengo la abiria linalotumika sasa (Terminal II) kwa lengo la kuongeza uwezo wake wa kuhudumia abiria. Serikali imejenga Kiwanja cha Ndege cha Songwe ambacho kilianza kutoa huduma za uendeshaji wa ndege mwezi Januari, 2013. Kuanzia mwezi Januari, 2013 ndege zinafanya safari za kibiashara kati ya Uwanja huo na viwanja vingine nchini. Hivi sasa ndege mbalimbali zinatoa huduma za abiria na mizigo kwa wananchi wa Mbeya na mikoa ya jirani kupitia kiwanja hicho. Pamoja na kuanza kutumika kwa kiwanja hicho, kazi ya ujenzi wa jengo kubwa la abiria inaendelea na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2015. Serikali imekarabati pia viwanja vya ndege vya Arusha, Mafia, Mpanda, Kigoma, Tabora, Mwanza, Bukoba na Mtwara pamoja na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA).

Muonekano wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa

Mwalimu Nyerere baada ya kukarabatiwa.

165

Kuimarisha Utabiri wa Hali ya HewaSerikali imeendelea kuimarisha shughuli za utabiri wa hali ya hewa. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (Tanzania Meteorological Agency - TMA) imeendelea kutoa huduma za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kutoa tahadhari ya majanga yanayosababishwa na hali mbaya ya hewa pamoja na kubadilishana taarifa na data za hali ya hewa katika mtandao wa dunia kulingana na makubaliano ya kimataifa. Huduma za utabiri wa hali ya hewa zimeendelea kutolewa kila siku, kila bada ya siku 10, mwezi, mwelekeo wa msimu na tahadhari dhidi ya majanga yanayosababishwa na mafuriko, ukame na upepo mkali ili kusaidia wananchi kupanga shughuli zao za kila siku za kimaendeleo. Aidha, takwimu na data zilizosaidia utekelezaji wa majukumu ya sekta za ujenzi; kilimo; usafiri na usafirishaji; maji; nishati; utalii na masuala ya tafiti mbalimbali zimeendelea kutolewa. Huduma ya utabiri wa hali ya hewa imeboreshwa kutoka asilimia 60 katika mwaka 2005 hadi kufikia wastani wa asilimia 80 katika mwaka 2014. Hatua hiyo imeongeza imani ya wananchi juu ya utabiri unaotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa katika kuokoa maisha ya wananchi na mali zao. Aidha, TMA kwa kushirikiana na WMO imeingia mkataba wa utaratibu wa mfumo wa usimamizi wa utoaji huduma zenye viwango bora kimataifa kwa ajili ya huduma za hali ya hewa kwenye sekta ya usafiri wa anga ambapo TMA ilipata cheti cha kutoa huduma bora zinazotambuliwa Kimataifa mwezi Februari, 2011.  

166

Vilevile, Serikali kupitia TMA imeanza kutumia magazeti matano, radio 23, vituo vya televisheni sita, kampuni za simu za Tigo na Vodacom na mitandao mbalimbali ya kijamii kusambaza taarifa za hali ya hewa. Lengo ni kuhakikisha kuwa taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinawafikia walengwa kwa urahisi.

MAENDELEO YA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO Utafiti

Serikali imedhamiria kukuza shughuli za utafiti kwa kuamua kutenga asilimia moja ya Pato Ghafi la Taifa (GDP) kila mwaka kwa ajili ya Utafiti na Maendeleo. Dhamira hiyo ya Serikali imewezesha fedha kwa ajili ya shughuli za utafiti kuongezeka kutoka Shilingi bilioni 1 mwaka 2005 hadi Shilingi bilioni 21.5 kwa mwaka mwaka 2014. Aidha, Serikali imeanzisha Mfuko wa Taifa wa Uendelezaji Sayansi na Teknolojia (MTUSATE) na kuimarisha Tume ya Sayansi na Teknolojia (Commission for Science and Technology - COSTECH) ili kiwe chombo kinachounganisha watafiti na wagunduzi wote nchini. Kutokana na juhudi hizo, tafiti zifuatazo zimefanyika: Utafiti wa uzalishaji wa mbegu bora ya maharage ya soya inayotoa mazao mengi kwa ekari;Lishe ya mazao na mimea ya misitu iliwayo;Mchango wa misitu midogo katika kuongeza pato la taifa;Mimea yenye viuatilifu vyenye uwezo wa kuua mbu na kuzuia ugonjwa wa malaria nchini;Mashine ndogo inayoweza kuhamishika ya bayogesi (compact portable biogas) imehawilishwa ili kupunguza utegemezi wa nishati ya mkaa na kuni ambazo huchochea uharibifu wa mazingira.

167

Katika kutekeleza hayo, Sheria ya Uendelezaji wa Sayansi na Teknolojia imeandaliwa na maboresho ya mifumo ya sayansi, teknolojia na ubunifu inaendelea kukamilishwa. 

Mkongo wa Taifa wa MawasilianoSerikali imejenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa lengo la kufikisha huduma za mawasiliano kwa Wananchi kwa uharaka zaidi, uhakika na kwa gharama nafuu. Jumla ya kilomita 7,560 zimejengwa kwa awamu mbili. Gharama za mawasiliano zimepungua kwa kiasi kikubwa kufuatia kujengwa kwa mkongo. Aidha, Mkongo wa Taifa umeunganishwa na mikongo mingine ya Kimataifa ya SEACOM, EASSY na SEAS. Awamu ya Tatu ya ujenzi ambayo itaziunganisha Unguja na Pemba kwenye Mkongo wa Taifa imeanza Mwezi Desemba, 2013 na inatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti, 2015. Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umeunganisha mawasiliano na nchi za jirani za Malawi, Zambia, Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya. Hadi sasa, ujenzi wa Mkongo huo umewasaidia watoa huduma na kuendelea kuharakisha maendeleo ya Taifa kwa wananchi kupata fursa ya kutumia TEHAMA katika kupambana na umaskini na kujiletea maendeleo kwa kasi zaidi.

Huduma za Simu za Mkononi na IntanetiSerikali imeendelea kuboresha mazingira ya ukuaji wa Sekta ya Mawasiliano nchini na hivyo kufanya Sekta hiyo kukua kwa kasi.

168

Idadi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini imeongezeka maradufu na kufikia laini za simu milioni 32.01 mwezi Desemba, 2014 kutoka milioni 2.96 mwaka 2005. Aidha, gharama za kupiga simu zimepungua hadi kufikia Shilingi 34.92 kwa dakika mwaka 2014 kutoka Shilingi 115 mwaka 2005.  Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine imeendelea kuboresha mfumo wa intaneti na hivyo, wananchi wanaoutumia mfumo huo kuongezeka kutoka milioni 3.6 mwaka 2005 hadi watumiaji milioni 11.4 mwaka 2014. Gharama za huduma za intaneti zimepungua kutoka wastani wa Shilingi 36,000 kwa Gigabyte mwaka 2005 hadi wastani wa Shilingi 9,000 kwa Gigabyte mwaka 2014. Gharama za usafirishaji wa mawasiliano kwa masafa marefu (Kilomita 1,000 kwa kasi ya megabyte 2 kwa sekunde) nazo zimeendelea kushuka kutoka wastani wa Dola za Marekani 20,000 mwaka 2006 hadi wastani wa Dola za Marekani 160 mwaka 2014. Aidha, kumekuwa na ongezeko la huduma nyingine kupitia mawasiliano ya simu za mkononi kama vile, miamala ya kifedha, ununuzi wa huduma na bidhaa kwa kutumia miamala ya kibenki, taarifa za masoko, hali ya hewa na mijadala ya masuala mbalimbali ya kijamii. Inakadiriwa kuwa watumiaji wapatao milioni 12.3 wanatumia huduma za miamala ya kibenki kwa kutumia simu za mikononi.

169

Huduma ya Mawasiliano VijijiniSerikali imeendelea kuweka mazingira na kushawishi Sekta Binafsi kufikisha mawasiliano kwenye maeneo ya vijijini yasiyokuwa na mvuto kibiashara kwa kuanzisha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF). Kupitia Mfuko huo, kampuni za simu zimeridhia kwa hiari kupeleka mawasiliano kwenye Kata 163 kwa awamu ya kwanza A. Katika awamu ya kwanza A kampuni za simu zitapeleka mawasiliano kwenye Kata 44 kwa gharama zao na Kata 33 kwa ruzuku ya UCSAF. Hadi mwaka 2014, jumla ya Kata 52 zenye Vijiji 316 vimefikishiwa huduma za mawasiliano kupitia Mpango huo. Aidha, Serikali imetia saini makubaliano na watoa huduma za mawasiliano kufikisha huduma hizo katika Kata nyingine 163 zenye Vijiji 922. Wananchi 1,211,841 watanufaika na juhudi hizo.

Mfumo wa Kuhakiki na Kusimamia Huduma za Mawasiliano1.Serikali imesimika Mfumo wa Kusimamia Mawasiliano ya Simu Nchini. Lengo la kujenga Mfumo huo ni kubaini takwimu zinazopita katika mitandao ya mawasiliano. Mfumo huo unaweza kutoa takwimu za mawasiliano yanayofanyika ndani na nje ya nchi; kutambua mapato na miamala ya fedha; kufuatilia na kugundua mawasiliano ya ulaghai; na kutambua taarifa za laini ya simu na za kifaa cha mawasiliano.

170

Mfumo huo umeanza rasmi kutumika mwezi Oktoba, 2013 na kwa kipindi cha Oktoba hadi Novemba, 2014 umeweza kuiingizia Serikali jumla ya Shilingi bilioni 24.6 ambazo zisingeweza kupatikana bila kuwekwa kwa mfumo huu.

Serikali imeendesha na kuratibu mpango wa kusajili simu za kiganjani ambao unatambuliwa na Sheria ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 kwa lengo la kuimarisha matumizi ya masuala ya mawasiliano na haki za watumiaji. Sheria hiyo imeelekeza kuanzishwa kwa masjala ya namba za utambulisho wa simu zote za mikononi (CEIR Register) ili kuhifadhi taarifa za vifaa vya simu na kuwezesha utambuzi wa vifaa hivyo pale itakapohitajika hususan kwa matumizi ya simu yanayokiuka sheria. Idadi ya laini za simu zilizosajiliwa hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2014 ni 31,124,052 sawa na asilimia 98 ya laini zilizopo.

171

SURA YA TANO

UWEZESHAJI WANANCHISerikali imeendelea kuratibu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 ambapo mapitio ya Sheria Na.16 ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yamefanyika. Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekamilisha Mwongozo wa Kitaifa wa Ufundishaji Ujasiriamali utakaosaidia kutoa mafunzo ya ujasiriamali kuanzia ngazi ya shule za awali hadi vyuo vikuu. Mwongozo huo umeandaliwa ili masomo ya ujasiriamali, uwezeshaji, urasimishaji wa biashara, kilimo, ufugaji na uvuvi yaweze kutolewa kwa wananchi wengi.

Serikali kwa ushirikiano na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kupitia Programu ya Ruzuku ya Kuchangia (Matching Grants Programme) imetekeleza Mpango wa Maendeleo ya Biashara (Tanzania Business Development Scheme-TBDS) na Mpango wa Kusaidia Vyuo vya Elimu ya Juu Kubuni Kozi Mpya za Kuongeza Ujuzi na Ufanisi Kazini (Tanzania Innovation Applied Research Scheme). Programu hiyo imewezesha kampuni 1,728 kusajiliwa. Kati ya hizo, kampuni 786 zilipata kiasi cha Shilingi bilioni 7.8 kama ruzuku kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza miradi ya kiuchumi. Aidha, Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) imeanzisha Mfuko wa Ufundi na Utafiti, ambapo kiasi cha Shilingi bilioni 16.5 zimetolewa kwa Vyuo vya Elimu ya Juu tisa (9) kwa ajili ya kununulia vifaa vya kufundishia.

172

UANZISHWAJI NA UIMARISHWAJI WA SACCOS NA VIKOBA Serikali imeendelea na jitihada za kuhamasisha uanzishwaji wa Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOs) nchini hatua iliyowezesha ongezeko la Vyama hivyo kutoka 1,875 mwaka 2005 hadi 9,468 mwaka 2014. Aidha, elimu imeendelea kutolewa na kuwezesha SACCOS kuwa na uongozi bora. Vilevile, Mafunzo ya ujasiriamali yametolewa ambapo wanachama 1,361 wa SACCOS na AMCOS wamepata mafunzo yaliyowawezesha kunufaika na mikopo ya Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi kwa kushirikiana na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), Maafisa Ushirika wa Wilaya, na Benki ya CRDB.

Vilevile, Serikali inashirikiana na Serikali ya Ubelgiji kutekeleza Mradi wa Kuendeleza Shughuli za Kiuchumi za Kuongeza Kipato katika Mikoa ya Kigoma na Pwani. Chini ya mradi huo, vikundi vya kiuchumi 120 vyenye wanachama 3,600 vilipata elimu na mafunzo ya ujasiriamali na uendeshaji wa VICOBA. MIRADI YA VIJANASerikali imechukua hatua za kuwawezesha vijana kujiajiri kupitia miradi mbalimbali. Serikali kupitia Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA) imeandaa mafunzo ya elimu ya ufundi Stadi kwa vijana ambao hawakupata fursa ya kujiunga na elimu ya sekondari na elimu ya juu. Jumla ya vijana 4,000 wamepatiwa mafunzo katika fani za uongozi wa hoteli, ufundi magari, ujenzi na umeme. cha

173

Aidha, Serikali imeendelea kutoa mafunzo maalum yanayolenga kuwapatia vijana uwezo wa kupenda kazi na kujiajiri. Elimu ya ujasiriamali imetolewa kwa vijana 3,700 wenye viwango tofauti vya elimu kuanzia elimu ya msingi, sekondari na vyuo. Serikali imeandaa na kuanza kutekeleza Programu ya Kukuza Ajira kwa Vijana.

Programu hiyo imepangwa kutekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza ya miaka mitatu inatarajiwa kutoa fursa za ajira zipatazo 840,000 kwa vijana wa kada mbalimbali. Mkakati wa Programu hii utahusisha kuwajengea vijana uwezo na ujuzi katika stadi mbalimbali za kazi na ujasiriamali, kuwapatia mitaji, nyenzo na vifaa vya uzalishaji mali, kuhamasisha mazingira wezeshi kisera na kwapatia maeneo ya uzalishaji na biashara.

Serikali imeimarisha vituo vinavyotoa mafunzo kwa vijana kwa kuvifanyia ukarabati. Katika Kituo cha Mafunzo ya Vijana Sasanda, kumejengwa zizi la ng’ombe, jengo la kufugia nyuki na bwawa la kufugia samaki. Katika Kituo Ujasiri Marangu, kumejengwa uzio eneo la kituo na kufunga umeme. Katika Kituo cha Mafunzo ya Vijana cha Ilonga, ukarabati wa mfumo wa maji safi na taka, na jengo la utawala umefanyika.  Serikali imeendelea kuimarisha Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa kuzitaka Halmashauri zote kutenga asilimia tano ya mapato yake kwa ajili ya Mfuko huo.

174

Halmashauri 40 kati ya 155 zimetenga asilimia tano kutoka kwenye mapato yao kwa ajili ya mikopo ya vijana ambapo jumla ya vijana 856 walinufaika na kupewa mikopo ya SACCOS katika Halmashauri za Wilaya za Magu, Ukerewe, Nyamagana na Ilemela (Mwanza), Karagwe (Kagera), Chemba (Dodoma), Busega (Simiyu), Babati (Manyara), Kigoma Ujiji (Kigoma), Lindi, Kilwa (Lindi) na Halmashauri zote za Mkoa wa Tanga.

MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKEKatika kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuinua hali zao kimaisha, Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake umenufaisha vikundi 3,119 vyenye jumla ya wanawake 23,769. Aidha, idadi ya wanawake waliopata mikopo kutoka katika Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake imeongezeka kutoka wanawake 3,008 mwaka 2005 hadi kufikia wanawake 23,769 mwaka 2014. Kiasi cha fedha kilichokopeshwa kimeongezeka kutoka Shilingi milioni 260 mwaka 2005 hadi kufikia Shilingi Bilioni 1.9 mwaka 2014. Jumla ya Mikoa 25 ya Tanzania Bara ilipelekewa fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake kwa ajili ya kuwakopesha wanawake.  

BENKI YA WANAWAKE TANZANIASerikali ya Awamu ya Nne imeanzisha Benki ya Wanawake kwa lengo la kuwawezesha wanawake na wajasiriamali wengine kupata huduma za kifedha zenye masharti nafuu. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009, Benki hiyo imefungua matawi mawili katika Mtaa wa Posta ya Zamani na (Tawi la

175

Mkwepu) na Mtaa wa Aggrey/Likoma (Tawi la Mjasiriamali) katika eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Aidha, idadi ya vituo vya kutolea mikopo imeongezeka kutoka vituo 18 mwaka 2012/13 hadi kufikia vituo 81 mwaka 2013/14. Matawi na vituo hivyo vimewezesha kuongeza idadi ya wajasiriamali waliopata mikopo kupitia Benki ya Wanawake Tanzania, hususan wanawake kutoka wajasiriamali 689 mwaka 2010 hadi wajasiriamali 42,648 mwaka 2014.

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Akizindua Benki ya Wanawake Tanzania, Jijini Dar es Salaam, tarehe 4 Septemba,

2009.

176

Serikali kupitia Benki ya Wanawake imeendelea kutoa huduma za mikopo kwa wananchi katika Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Ruvuma, Mbeya, Iringa na Njombe.

Katika kipindi cha 2009 hadi 2014, jumla ya mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 24.9 imetolewa kwa wananchi 12,992 wakiwemo wanawake 11,350 sawa na asilimia 87 na wanaume 1,642 sawa na asilimia 13. Mikopo hiyo imewawezesha wajasiriamali kujiajiri katika shughuli mbalimbali za uzalishaji na hivyo kuinua kipato chao.

177

Chanzo: Benki ya Wanawake Tanzania, 2014Pamoja na Mifuko ya Vijana na Wanawake, Serikali pia imetoa mikopo kwa wananchi kwa kupitia mifuko mbalimbali kama inavyoonekana katika Jedwali Na.12.

Mkoa Idadi ya Wateja Mikopo Iliyotolewa Jumla

Wanawake Wanaume Wanawake Wanaume

Dar es Salaam 5,152 770 17,916,780,000 2,677,220,000 20,594,000,000

Dodoma 2,300 284 1,278,530,000 340,470,000 1,619,000,000

Mwanza 1,554 253 932,384,000 225,616,000 1,158,000,000

Ruvuma 1,142 186 633,582,000 238,600,000 872,182,000

Mbeya 558 69 252,700,000 78,300,000 331,000,000

Iringa 412 51 164,828,000 20,372,000 185,200,000

Njombe 232 29 92,916,000 11,484,000 104,400,000

Jumla 11,350 1,642 21,271,720,000 3,592,062,000 24,863,782,000

Jedwali Na.11: Kiasi cha Mikopo Kilichotolewa kwa Wajasiriamali kupitia Benki ya Wanawake Tanzania

178

Mfuko/Mpango Thamani ya Mikopo iliyotolewa (Bilioni) Wanufaika

Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi (Mwananchi Empowerment Fund) 9.5 10,073

Mpango wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Kuongeza Ajira 50.6 76,546

Mfuko wa Kuendeleza Wajasiriamali 36.4 67,720

Mfuko wa Maendeleo ya Vijana* 1.22 244

Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake 5.44 500,000

Mradi wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo (SELF) 57.1 95,034

Mfuko wa Pembejeo za Kilimo 6.17

Mfuko wa Rais wa Kujitegemea 53.2 27,600

Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Mauzo ya Nje 853.98

Mfuko wa Kudhamini Mabenki na Taasisi za Fedha kwa ajili ya kutoa mikopo kwa miradi midogo na ya

kati

7.01

Jumla 1,080.62 777,217

Jedwali Na. 12: Mikopo Iliyotolewa na Mifuko Mbalimbali ya Uwezeshaji Hadi Desemba, 2013

Chanzo: Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, 2014.*SACCOS 244 zilihusika katika utoaji wa mikopo hiyo.

179

MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF)Serikali imeendelea na jitihada za kupunguza umaskini kwa kusimamia utekelezaji wa Awamu ya II na III ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF). Awamu ya II pamoja na mambo mengine, ililenga kuhamasisha jamii yenye kipato cha chini kujiwekea akiba na kuwekeza. Kupitia Mpango huo, jumla ya vikundi 1,620 vyenye wanachama 20,869 kwa upande wa Tanzania Bara na vikundi 158 vyenye wanachama 1,843 Zanzibar viliundwa na kupewa mafunzo na hivyo kuwekeza. Hadi kufikia Juni 2013, vikundi hivyo viliweza kuweka akiba ya Shilingi milioni 710. Kati ya fedha hizo, Shilingi milioni 499 zilikuwa zimetolewa kama mikopo nafuu kwa wanachama. Kiwango cha marejesho ya mikopo hiyo kilikuwa ni asilimia 76.

Katika Awamu ya III ya TASAF, Serikali pamoja na mambo mengine imelenga kuhawilisha fedha kwa kaya maskini kwa masharti ya kaya hizo kupeleka watoto shule na watoto wadogo wa chini ya miaka 5 kupelekwa kliniki. Kupitia Mpango huo, kaya maskini 580,844 zimetambuliwa nchini na 436,275 zimeandikishwa kwenye Mpango. Kati ya kaya zilizoandikishwa, kaya 260,173 zimewezeshwa jumla ya Shilingi bilioni 33.3. Uhawilishaji unaendelea katika maeneo mengine kwa mujibu wa Kalenda ya Malipo ya kila baada ya miezi miwili.

180

MKAKATI WA KURASIMISHA RASILIMALI NA BIASHARA TANZANIA (MKURABITA)

Serikali ya Awamu ya Nne inaendelea kutekeleza Mkakati wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) pamoja na kuifanyia marekebisho Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999, ambayo imeongeza uhai wa leseni za makazi kutoka miaka miwili hadi mitano. Katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2014, Serikali kupitia MKURABITA imetambua nyumba 311,261 nchini kwa ajili ya kupatiwa leseni za makazi katika Mikoa ya Dar es Salaam (nyumba 274,617), Kilimanjaro (nyumba 1,119), Mwanza (nyumba 25,929), Dodoma (nyumba 5,651) na Tanga (nyumba 3,945). Aidha, Leseni za Makazi 160,500 zimeandaliwa na kati ya hizo leseni 98,787 zimetolewa kwa wananchi. Leseni hizo zinatumiwa na wananchi kama dhamana ili kupata mikopo katika vyombo vya fedha. Pia, Serikali imekamilisha zoezi la urasimishaji wa makazi holela 1,970 katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kutoa elimu ya urasimishaji na kuzuia makazi holela kwa wataalam wa Halmashauri zilizoko katika Mikoa ya Singida, Shinyanga, Dodoma na Tabora. Katika kipindi cha kuanzia 2008/2009- 2013/2014, upimaji wa ardhi umefanyika ambapo mashamba 84,886 yamepimwa na Hatimiliki 70,033 kuandaliwa katika wilaya 39. Vilevile, Serikali imeshiriki katika ujenzi wa masjala 42 katika Wilaya 15. Aidha, masjala za vijiji 17 zimejengwa na kukarabitiwa katika wilaya 6, na ujenzi wa masjala katika vijiji 25 unaendelea.

181

AJIRASerikali imeendelea kuandaa na kusimamia mazingira ya kazi; kuhakikisha kuwa yapo mazingira mazuri ya utekelezaji wa viwango vya kazi, usawa, kazi za staha, kukuza fursa za ajira pamoja na kusimamia masuala ya Hifadhi ya Jamii kwa kusimamia Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo kuhusu Kazi na Ajira. Kutokana na Sera nzuri za kuishirikisha Sekta Binafsi kwenye uchumi nchini, fursa za ajira zimeendelea kupatikana kama inavyooneshwa katika jedwali Na.13.

WaajiriwaMwaka

2010 2011 2012 2013

Wanaume 810,427 845,569 947,545 1,126,534

Wanawake 465,883 513,527 564,501 669,740

Jumla 1,276,310 1,359,096 1,512,046 1,796,274

Jedwali Na 13: Mchanganuo wa Jumla ya Ajira kwa Jinsia kuanzia 2010 -2013

Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu

182

Kushughulikia Matatizo ya WafanyakaziSerikali imeendelea kuwa karibu na wafanyakazi na kuhakikisha kuwa inashughulikia matatizo yao kwa wakati. Kutokana na usimamizi huo mafanikio yafuatayo yamepatikana:

i. Uundwaji wa vyombo vya ushirikishwaji wa wafanyakazi ili kuwawezesha kushiriki katika maamuzi mbalimbali yanayowagusa. Vyombo hivyo ni pamoja na Baraza la Ushauri wa Masuala ya Kazi, Jamii na Uchumi (LESCO) na Bodi 8 za Mishahara za Kisekta.

ii. Katika kipindi cha 2005 – 2014, jumla ya kaguzi za kazi 420,350 zimefanywa ambazo ni sawa na wastani wa kaguzi 40,000 kwa mwaka kwa lengo la kuhakikisha waajiri wanafuata Sheria za kazi ipasavyo.

Usuluhishi na Uamuzi wa Migogoro ya KikaziSerikali imeendelea kuhimiza maelewano baina ya waajiri na wafanyakazi, na kuhamasisha uzuiaji na utatuzi wa migogoro ya kikazi kwa njia ya usuluhishi na uamuzi. Katika kutekeleza azma hiyo, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi

183

ilianzishwa mwezi Mei, 2007. Hadi sasa, Tume hiyo imepokea na kusajili jumla ya migogoro ya kikazi 76,230 ambapo kati ya hiyo, migogoro 73,180 sawa na asilimia 96 ilitatuliwa.

Usalama na Afya Mahali pa KaziSerikali imeendelea kusimamia na kufuatilia uzingatiaji wa usalama na afya mahala pa kazi. Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali imepitisha Sera ya Taifa ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2010 pamoja na kuanzisha na kuimarisha Wakala wa Afya na Usalama mahali pa kazi yenye jukumu la kufanya kaguzi mahala pa kazi ili kuhakikisha kuwa Sheria na taratibu zinafuatwa.

Jumla ya kaguzi za kawaida 816,054 na kaguzi maalum 138,435 zilifanyika na wafanyakazi 435,063 walipimwa afya zao iii kubaini matatizo na athari wanazozipata kutokana na maeneo wanayofanyia kazi kuwa na upungufu na kutozingatia masuala ya afya na usalama kazini. Jumla ya kampuni 46 zilizotozwa faini na kampuni nne (4) zilifungiwa kutoa huduma kutokana na ukiukaji wa Sheria.

184

Usajili wa Vyama Huru vya Wafanyakazi na WaajiriSerikali imeendelea kuhimiza na kufuatilia haki mbalimbali za wafanyakazi na waajiri, ikiwemo haki ya kuanzisha, kujiunga na kushiriki katika shughuli mbalimbali halali za vyama vya wafanyakazi na waajiri. Jumla ya Vyama vya Wafanyakazi sita (6), Chama cha Waajiri kimoja (1) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi moja (1) limesajiliwa kati ya mwaka 2006 hadi 2014. Lengo ni kuongeza na kuboresha wigo wa ushiriki, majadiliano na utetezi wa haki za wafanyakazi na waajiri katika sehemu za kazi. Kutokana na usajili huo, Vyama vya Wafanyakazi vilivyopo sasa ni 24, Vyama vya Waajiri viwili (2), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi moja (1) na Shirikisho la Mashirikisho ya Afrika Mashariki (EATUC) moja.

Maslahi ya Watumishi wa UmmaSerikali imeendelea kuboresha maslahi ya Watumishi wa Umma kwa kutunga Sera ya Malipo ya Mishahara na Motisha Katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2010 na kuanzisha Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma. Bodi hiyo ina wajibu wa kumshauri Rais kuhusu viwango vya mishahara na maslahi mbalimbali katika Utumishi wa Umma. Jitihada hizo za Serikali zimewezesha kuongezeka kwa mishahara ya watumishi mwaka hadi mwaka. Kwa wastani, mishahara ya Watumishi wa Umma kwa mwezi imeongezeka kutoka Shilingi 152,849 mwaka 2005/2006 hadi Shilingi 596,525 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 290.

185

Aidha, kima cha chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma kwa mwezi kimeongezeka kutoka Shilingi 65,000 mwaka 2005/2006 hadi Shilingi 265,000 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 308 kama invyoonekana kwenye kielelezo Na.5

Kima cha Chini na Wastani wa Mishahara, 2005/6 – 2014/15

Chanzo: Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma

186

Katika hatua nyingine, Serikali ya Awamu ya Nne imefanikiwa kupunguza kiwango cha Kodi ya Mapato kwa Watumishi (PAYE) kutoka asilimia 18 mwaka 2005/2006 hadi asilimia 12 mwaka 2014/2015. Hatua hiyo ilichukuliwa na Serikali kama njia ya kuongeza kipato kwa watumishi.

Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

Kuanzia mwaka wa 2008/2009 hadi 2012/2013, Mashirika ya Hifadhi ya Jamii yameongeza wanachama wao kwa kiasi kikubwa. Idadi ya Wanachama wa Mashirika hayo imeongezeka kutoka 839,261 mwaka 2008/2009 hadi 1,301,967 mwaka 2012/2013 sawa na ongezeko la asilimia 55. Kwa ujumla kila Shirika la Hifadhi ya Jamii limeongeza idadi ya wanachama. Idadi ya wanachama wa NSSF, imeongezeka kutoka 371,911 mwaka 2008/2009 hadi 593,032 mwaka 2012/2013 sawa na ongezeko la asilimia 59; PPF imeongeza wanachama kutoka 104,684 mwaka 2008/2009 hadi 224,193 sawa na ongezeko la asilimia 114. Aidha, PSPF imeongeza wanachama kutoka 266,045 mwaka 2008/2009 hadi 320,860 mwaka 2012/2013 sawa na ongezeko la asilimia 21; LAPF imeongeza wanachama kutoka 66,394 mwaka 2008/2009 hadi 104,840 sawa na ongezeko la asilimia 58 na GEPF imeongeza wanachama kutoka 30,227 mwaka 2008/2009 hadi 59,042 mwaka 2012/2013 sawa na ongezeko la asilimia 95. Ongezeko la wanachama katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeoneshwa katika Jedwali Na. 14 .

187

Mfuko/Mwaka 2008/09 2009/10 2010/11

2011/12 2012/13

Ongezeko

NSSF 371,911 383,808 521,629 543,685 593,032

59%

PPF 104,684 160,068 180,046 203,981 224,193

114%

PSPF 266,045 288,055 306,514309,767 320,860

21%

LAPF 66,394 73,833 80,529 91,852 104,840

58%

GEPF 30,227 35,279 41,879 52,670 59,042

95%

NHIF

Jumla 839,261 941,043 1,130,597 1,201,955 1,301,967

55%

Jedwali Na. 14. Uanachama Katika Mashirika ya Hifadhi za Jamii, 2008-2013

Aidha, uwekezaji wa Mashirika hayo umeongezeka kutoka Shilingi bilioni 3,147.03 hadi bilioni 5,343.13 kati ya mwaka 2009/2010 hadi mwaka 2012/2013 sawa na ongezeko la asilimia 12. Mifuko yote imeonesha mafanikio ya kuridhisha katika uwekezaji kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 15.

Chanzo: Mamlaka ya Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), 2013.

188

Mwaka/Mfuko

2009/10 2010/11 2011/12 2012/13

LAPF 277.52 365.99 490.36 570

PPF 667.98 835.83 1,022.42 1,022.42

PSPF 794.75 866.53 970.85 978.226

NSSF 1,029.21 1,216.62 1,800.12 2,073.615

GEPF 85.94 99.21 134.97 173.769

NHIF 291.64 373.15 408.57 524.755Jumla 3,147.04 3,757.33 4,827.29 5,342.785

Jedwali Na. 15 Thamani ya Uwekezaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (Bilioni za Kitanzania)

Vilevile, michango ya Wanachama katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeongezeka katika kipindi cha miaka mitano (2008/2009 hadi 2012/2013). Michango imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 749.9 mwaka 2008/2009 hadi Shilingi bilioni 1,607.9 mwaka 2012/13 sawa na ongezeko la asilimia 17. Kila mfuko ulikuwa na ongezeko la uchangiaji kama invyoonekana katika Jedwali Na. 16.

Chanzo: Mamlaka ya Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), 2013.

189

Mfuko/ Mwaka 2008/09 2009/10 2010/11

2011/12 2012/13

Ongezeko

NSSF 255.27 300.09 356.51

420.24 475.806

86%

PPF 126.96 147.65 187.50

229.022 251.72

98%

PSPF 227.4 239.25 392.9444.099 516.543

127%

LAPF 47.05 54.24 80.589.06 119.175

153%

GEPF 13.79 16.32 25.6930.15 37.299

170%

NHIF 79.39 90.08 134.89163.46 207.43

161%

Jumla 749.86 847.63 1177.991,376.04 1607.968

114%

Jedwali Na.16: Michango ya Wanachama wa Mifuko ya Jamii (Bilioni za Kitanzania).

Chanzo: Mamlaka ya Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), 2013.

190

SURA YA SITAHUDUMA ZA JAMII

ElimuSerikali imeendelea kutekeleza azma ya kuboresha na kupanua elimu katika ngazi zote kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya juu ili kutoa elimu shindani na yenye kumwezesha mwananchi kuhimili ushindani katika soko la ajira na pia kujiajiri. Serikali inatumia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 kutoa miongozo ya jumla ya masuala yote ya elimu na mafunzo kwa ngazi zote. Sera hiyo imelenga kuongeza fursa, ufanisi na ubora wa elimu na mafunzo ili kuliwezesha taifa kufikia Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ya kuwa na viwango vya rasilimali watu kwa nchi yenye uchumi wa kati. Sera imezingatia mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisayansi na kiteknolojia na changamoto za elimu na mafunzo kitaifa, kikanda na kimataifa.

Elimu ya Awali na MsingiSerikali imeendelea kuhimiza uandikishaji wa wanafunzi katika madarasa ya elimu ya awali na hivyo kufanya uandikishaji kuongezeka kutoka wanafunzi 638,591 mwaka 2005 hadi wanafunzi 1,026,466 mwaka 2013. Aidha, idadi ya shule za msingi zenye madarasa ya elimu ya awali imeongezeka na kufikia shule 12,046 kati ya 15,576 za msingi za Serikali zilizopo.

191

Idadi ya wanafunzi walioandikishwa darasa la kwanza imeongezeka kutoka 1,348,437 mwaka 2005 hadi wanafunzi 1,430,231 mwaka 2013. Idadi ya shule za Msingi imeongezeka kutoka shule 14, 257 mwaka 2005 hadi shule 16,343 mwaka 2013. Serikali inasisitiza matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji ambapo wadau mbalimbali wa maendeleo wanashirikishwa kikamilifu kwa lengo la kuinua ubora wa elimu nchini. Mwaka 2012, Serikali ya Marekani kupitia Shirika la USAID ilifadhili utoaji wa kompyuta katika shule zote za msingi katika mkoa wa Mtwara kupitia mradi wa elimu wa Tanzania ya Karne. ya 21 (TZ21). Tangu mradi huo uanze, shule 90 za msingi, vituo vinne (4) vya ualimu (Teachers Resource Centres - TRCs) na Ofisi ya Afisa Elimu wa Mkoa wa Mtwara pamoja na ofisi za Maafisa Elimu wa Wilaya za Mkoa wa Mtwara wamewekewa vifaa vya mtandao wa Intaneti.

Elimu ya SekondariSerikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa wanafunzi wengi wanaomaliza elimu ya msingi wanapata nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari. Hatua zilizochukuliwa zinawezesha, idadi ya Shule za Sekondari kuongezeka kutoka 1,745 mwaka 2005 hadi shule 4,576 mwaka 2014 sawa na ongezeko la asilimia 162.2. Aidha, idadi ya wanafunzi wanaoendelea na elimu ya sekondari baada ya kumaliza elimu ya msingi imeongezeka kutoka wanafunzi 196,391 mwaka 2005 hadi wanafunzi 411,127.

192

Vilevile, jumla ya nyumba za walimu 492 zimejengwa katika kipindi hicho na Maktaba za Shule zimeongezeka kutoka 401 hadi 1,024. Pia, idadi ya maabara imeongezeka kutoka 1,478 mwaka 2005 hadi 4,237 zilizokamilika, na 5,974 zipo katika hatua mbalimbali ya ujenzi hadi kufikia mwezi Machi, 2015.

Serikali imeendelea kujenga, kukarabati na kuboresha mazingira na miundombinu ya utoaji elimu ya sekondari nchini. Utekelezaji wa Mradi wa MMES II umeendelea kwa kufanya ukarabati wa shule 1,200 (shule 264 za awamu ya kwanza, shule 528 za awamu ya pili na shule 408 za awamu ya tatu). Idadi ya walimu wa shule za sekondari imeongezeka kutoka walimu 23,905 mwaka 2005 hadi walimu 73,407 mwaka 2014 Vilevile, Miongozo ya Walimu katika kufundisha masomo ya Sayansi kwa vitendo imeandaliwa na kusambazwa katika shule zote za sekondari nchini. Aidha, nakala 1,985,530 za vitabu vya Kemia, Biolojia, Fizikia na Hisabati zimesambazwa katika shule zote za Sekondari nchini .

193

Mhe. Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoa zawadi kwa mwanafunzi bora zaidi katika masomo ya Sayansi wakati

wa Wiki ya Elimu, Juni 2015.

194

Elimu ya UalimuSerikali imeendelea kupanua mafunzo ya ualimu ili kuhakikisha kuwa walimu wa kutosha wanapatikana kukidhi idadi ya wanafunzi wanaoendelea kuongezeka. Idadi ya Vyuo vya Ualimu imeongezeka kutoka 52 mwaka 2005 hadi 106 mwaka 2014. Aidha, udahili wa wanachuo katika Vyuo vya Ualimu umeongezeka kutoka wanachuo 26,224 mwaka 2005 hadi wanachuo 35,645 mwaka 2014.

Serikali imeanzisha Stashahada ya Elimu ya Awali katika vyuo 19, Stashahada ya Elimu ya Msingi katika vyuo 3, Stashahada ya Juu ya Elimu ya masomo ya Sayansi katika vyuo 3, Stashahada ya Juu ya Elimu ya masomo. ya Lugha katika chuo 1 na Stashahada ya Elimu Michezo katika chuo 1.

Lengo ni kuandaa walimu mahiri watakaofundisha elimu ya awali, msingi na sekondari kwa kuwajengea uwezo wa kumudu maarifa na stadi muhimu katika kutekeleza mitaala kwa ufanisi shuleni. Kutokana na juhudi hizo, idadi ya walimu imeongezeka kutoka 135,013 mwaka 2005 hadi 189,489 mwaka 2013 kwa shule za msingi na kutoka 21,450 hadi 73,407 kwa shule za sekondari katika kipindi hicho kama inavyoonekana katika jedwali lifuatalo.

195

  MSINGI SEKONDARI

MWAKA SERIKALI BINAFSI JUMLA SERIKALI BINAFSI JUMLA

2005 132,409 2,604 135,013 12,592 8,858 21,450

2006 148,607 3,275 151,882 14,051 6,185 20,236

2007 153,027 3,637 156,664 17,755 6,665 24,420

2008 149,433 5,462 154,895 25,240 12,576 37,816

2009 151,476 5,709 157,185 26,432 7,522 33,954

2010 159,081 6,775 165,856 30,252 10,255 40,517

2011 167,111 8,338 175,449 39,934 12,212 52,146

2012 171,986 9,001 180,987 51,469 13,617 65,086

2013 179,322 10,165 189,489 58,028 15,379 73,407

Jedwali Na.14 Ongezeko la Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari nchini

Serikali imeanzisha mfumo wa TEHAMA katika vyuo 34 vya Serikali na kuwajengea uwezo wakufunzi juu ya matumizi ya TEHAMA katika kufundisha na kujifunza. Aidha, miundombinu ya Vyuo vya Ualimu Patandi, Bustani na Vikindu imeimarishwa ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Chanzo: Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

196

Mafunzo ya Ufundi

Serikali imeongeza kasi ya upanuzi wa elimu ya ufundi na mafunzo ya Ufundi stadi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wadau wa Sekta Binafsi kuwekeza kwenye mafunzo hayo. Kutokana na jitihada hizo, Vyuo vya Elimu ya Ufundi vimeongezeka kutoka 240 mwaka 2005 hadi 287 mwaka 2014 na Vyuo vya Ufundi Stadi vimeongezeka kutoka vyuo 672 mwaka 2005 hadi vyuo 750 mwaka 2014. Udahili wa wanafunzi katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi kwa mwaka umeongezeka kutoka 40,059 mwaka 2005 hadi 113,080 mwaka 2014. Kwa upande wa vyuo vya ufundi stadi, udahili kwa mwaka umeongezeka kutoka wanafunzi 78,586 mwaka 2005 hadi kufikia wanafunzi 145,511 mwaka 2014. Vilevile, ujenzi wa vyuo vipya vya ufundi stadi vya Manyara, Lindi, Pwani na Kipawa TEHAMA umekamilika.

Vyuo vya Maendeleo ya JamiiWataalam wa Maendeleo ya Jamii ni kada muhimu katika kuraghibisha ushiriki wa jamii katika shughuli za maendeleo. Udahili wa wanafunzi katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kwa mwaka umeongezeka kutoka wanafunzi 940 (wanawake 513 na Wanaume 427) mwaka 2005 hadi wanafunzi 3,634 (wanawake 2,407 na wanaume 1,227) mwaka 2014.

197

Ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kutoka vyuo vinne (4) mwaka 2005 (Tengeru, Buhare, Rungemba na Misungwi) hadi kufikia vyuo nane (8) mwaka 2014 (Tengeru, Buhare, Rungemba, Misungwi, Uyole, Mlale, Ruaha na Mabughai). Idadi ya wahitimu katika Vyuo hivyo imeongezeka kutoka wahitimu 477 mwaka 2005 hadi wahitimu 2,940 mwaka 2014.

Vyuo vya Maendeleo ya WananchiKutokana na maboresho yaliyofanyika katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi, udahili wa washiriki katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi umeongezeka kutoka washiriki 24,658 mwaka 2005 hadi kufikia washiriki 40,692 mwaka 2014. Katika kipindi hicho, jumla ya washiriki 36,838 walihitimu

katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi, kati yao 22,939 ni wanaume na 13,899 wanawake. Aidha, wahitimu 33,319 sawa na asilimia 90.44 ya wahitimu wote wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi wamejiajiri na kuajiri wengine katika shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile ufundi umeme wa majumbani, umeme wa magari, uungaji vyuma, umakanika, ushonaji, kufungua maduka ya pembejeo za kilimo, maduka ya dawa za mifugo, maduka ya vifaa vya umeme na ujenzi. Vilevile, wahitimu 3,047 sawa na asilimia 8.27 ya wahitimu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi wameajiriwa katika kampuni za watu binafsi na Taasisi mbalimbali za Serikali.

198

Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo RasmiSerikali imeendelea kuhimiza na kuboresha Elimu ya Watu Wazima (EWW) na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi (ENMRA). Mfumo wa ukusanyaji, utunzaji na matumizi ya taarifa za Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi umeboreshwa kwa kutoa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata 120 na maafisa Elimu ya Watu Wazima wa Wilaya 30. Serikali imeendelea kuhimiza utekelezaji wa Programu ya Mpango wa Uwiano katika Elimu ya Watu Wazima na Jamii (MUKEJA) ambapo uandikishaji wa vijana na watu wazima katika madarasa ya kisomo kuanzia mwaka 2005 unaonesha idadi ya wanawake wanaojiandikisha ni kubwa kuliko wanaume. Kwa mfano, mwaka 2005 idadi ya wanakisomo wote ilikuwa 1,900,255 ambapo wanawake walikuwa 1,051,478 (55%); mwaka 2010 idadi ya wanakisomo ilikuwa 924,693 ambapo wanawake walikuwa 473, 785 (51.2%); mwaka 2014, jumla ya Wanakisomo ilikuwa 828, 469 ambapo wanawake walikuwa 431,085 (52%). Takwimu hizo zinaonesha kuwa wanawake wamepata mwamko wa kujiunga na madarasa ya kisomo kutokana na majukumu waliyo nayo ya kutunza familia na uzalishaji mali.

Serikali inaendelea kuandaa na kutekeleza Mpango wa Elimu ya Watu Wazima wenye Manufaa nchini hatua kwa hatua. Uzinduzi na utekelezaji wa Mpango wa Ndiyo Ninaweza umefanyika katika wilaya 9 za majaribio ambazo ni Dodoma Manispaa, Ilemela, Songea Manispaa, Temeke, Ilala, Kinondoni, Mwanga, Bagamoyo na Mkuranga. Lengo ni kuwawezesha wananchi

199

Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) na kuwapatia walengwa (vijana na watu wazima) maarifa muhimu kwa maisha yao ya kila siku.

Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizindua Mpango wa Utambuzi wa Ujuzi Nje ya Mfumo Rasmi

Elimu ya Juu.Serikali imefanya upanuzi wa elimu ya juu na kuwezesha watanzania wengi kupata elimu ya ngazi hiyo. Vyuo Vikuu nchini vimeongezeka kutoka 23 mwaka 2005 had 46 mwaka 2014.

200

Aidha, udahili katika vyuo vikuu kwa mwaka umeongezeka kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 204,175 mwaka 2013 ambapo wanafunzi wa kike waliodahiliwa mwaka 2013 ni 74,498 sawa na asilimia 36.5. Ongezeko katika udahili umewezesha ushiriki rika kwa elimu ya juu kuongezeka kutoka asilimia 1.27 mwaka 2005 kufikia asilimia 5.5 mwaka 2014.

Mhe. Mizengo P. Pinda (Mb.) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikagua vifaa vya maabara katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine.

201

Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Elimu

Mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu umeboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kumbi za mihadhara (lecture theaters) kwa baadhi ya Vyuo Vikuu, madarasa na vyumba vya kufanyia semina, maabara, karakana (workshops), maktaba na ofisi za wanataaluma. Mradi umegharamia ujenzi wa majengo mapya 25, ikiwa ni pamoja na kuyafanyia ukarabati majengo yaliyokuwepo katika Vyuo Vikuu saba (7) ambavyo ni Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar-es-Salaam, Taasisi ya Teknolojia Dar-es-Salaam, Chuo Kikuu cha Ardhi na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Mbali na miundombinu hiyo, mradi uliwezesha ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kufundishia na kujifunzia katika Taasisi 16 za Elimu ya Juu. Ununuzi huo ulilenga katika maeneo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), vifaa vya maabara, vitabu vya kiada na magari.

202

Jengo lenye Vyumba vya Mihadhara na Ofisi za Walimu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa.

203

Mikopo ya Elimu ya Juu

Serikali imeendelea kugharamia wanafunzi wa elimu ya juu nchini kwa kutoa mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wenye sifa. Idadi ya wanafunzi wanaopata mikopo kwa mwaka imeongezeka kutoka 42,729 mwaka 2005 hadi wanafunzi 214,722 mwaka 2014. Kiwango cha urejeshaji wa mikopo kwa wahitimu walionufaika na mikopo hiyo kimeongezeka kutoka asilimia 30 mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 39 mwaka 2014. Utoaji mikopo umeimarishwa kwa kuzingatia uhitaji wa mwombaji badala ya ule wa awali wa kutumia ufaulu wa Daraja la I na la II ambao ulionekana kunufaisha zaidi wanafunzi kutoka familia zenye uwezo.

Katika mwaka wa masomo 2013/2014, Serikali ilianza kutumia Mfumo wa Kielektroniki unaowezesha wanafunzi kutuma maombi ya mkopo bila kulazimika kufika kwenye Ofisi ya Bodi ya Mkopo. Jumla ya wanafunzi 115,322 waliomba mkopo kupitia mfumo huo na kutuma viambatisho vya maombi yao kwa njia ya EMS.Jedwali lifuatalo linaonyesha ongezeko la wanafunzi walionufaika na mikopo pamoja na kiasi cha mikopo iliyotolewa.

204

Mwaka Idadi ya wanafunzi Kiasi cha mkopo kilichotolewa

2005/2006 42,229 56,000,371,483

2006/2007 47,554 76,071,839,629

2007/2008 55,687 110,873,883,141

2008/2009 58,798 139,093,681,094

2009/2010 72,035 197,348,958,875

2010/2011 92,791 231,8555,927,151

2011/2012 94,773 322,031,207,695

2012/2013 96,615 318,127,765,781

2013/2014 94,477 326,000,000,0000

Kuwianisha Mifumo ya ElimuSerikali imejipanga vyema kuhakikisha kuwa Watanzania wanakuwa na kiwango

cha elimu kinachoshabihiana na viwango vya elimu kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuwawezesha kuwa na fursa sawa za kupata ajira kama inavyoainishwa katika Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nchi wanachama zimeidhinisha Mikakati ya Uwianishaji wa Mitaala katika Maeneo ya Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Sekondari, Mafunzo ya Ualimu, Mafunzo ya Makundi Maalum, Mafunzo ya Ufundi na Ufundi Stadi, Mafunzo Nje ya Mfumo Rasmi na Elimu ya Watu Wazima.

Jedwali Na.15: Mikopo ya Elimu ya Juu

205

Ngazi ya Kituo

Mwaka 2005 Mwaka 2014

Serikali Binafsi Jumla Serikali Binafsi Jumla

Zahanati 3,183 1,289 4,472 4,469 1,886 6,355

Vituo vya

Afya

341 140 481 489 160 649

Hospitali 95 124 219 114 129 243

Jumla 3,619 1,553 5,172 5,072 2,175 7,247

SEKTA YA AFYAMpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)Serikali imeendelea kuimarisha, kuboresha na kujenga vituo vya kutolea huduma za afya katika ngazi mbalimbali ili kusogeza huduma hizo karibu zaidi na wananchi. Utekelezaji wa Sera ya Afya ya mwaka 2007 na Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007 – 2017 umeleta mafanikio makubwa katika Sekta ya Afya. MMAM ni mpango wa miaka 10 unaotekelezwa na Serikali kuanzia mwaka 2007 hadi 2017 kwa lengo la kupambana na adui maradhi kwa kuhakikisha kwamba huduma bora za afya ya msingi zinawafikia wananchi wote. Kupitia MMAM, vituo vya kutolea huduma za afya na ustawi wa jamii vimeongezeka kutoka vituo 5,172 mwaka 2005 hadi 7,247 mwaka 2014, sawa na ongezeko la vituo 2,075. Kati ya vituo vyote vilivyopo nchini, vituo 5,072 ni vya Serikali na 2,175 ni vya taasisi binafsi. Jedwali Na. 16 linaonesha umiliki wa vituo vya kutolea huduma za Afya.

Chanzo: Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, 2014

206

Vilevile, Taasisi za Mafunzo ya Afya zimeongezeka na kuimarishwa ili kujenga uwezo wa watumishi na kukidhi mahitaji ya utoaji wa huduma bora kwenye ngazi zote za vituo vya kutolea huduma za afya. Pia, Serikali imeimarisha upatikanaji wa vifaa, vifaa tiba na dawa katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya. Aidha, Serikali imeweka mfumo wa rufaa katika utoaji wa huduma za afya na kuanzisha Timu za Ushauri zinazotumia mobile clinics kutoa huduma za madaktari bingwa kwenye vituo vilivyo maeneo ya mbali ili kupunguza rufaa zisizo za lazima.

JEDWALI NA.16 MWENENDO WA UPATIKANAJI WA WATAALAM KADA MBALIMBALI ZA AFYA

Mwaka Madaktari Daktari Wasaidizi

Madaktarina

Daktari Wasaidizi

Wauguzi Wateknolojia wa Maabara Wafamasia

2006 1,048 1,223 2,271 15,961 1,277 1,309

2008 1,176 1,567 2,743 16,786 1,316 1,387

2009 1,328 1,690 3,018 17,606 1,522 1,449

2010 1,447 1,860 3,307 18,447 1,643 1,490

2011 1,655 1,953 3,608 19,361 1,780 1,560

2012 2,225 1,789 4,014 20,034 2,054 1,601

2013 2,283 1,913 4,196 20,800 2,180 1,636

2014 2,325 1,914 4,239 22,942 2,378 1,674

Chanzo: Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

207

Huduma za MaabaraSerikali imeimarisha na kuboresha huduma ya uchunguzi wa magonjwa katika ngazi mbalimbali. Maabara za Hospitali za Rufaa, Mikoa na Wilaya zimepatiwa mashine za kuchunguza damu, uwezo wa figo na ini, pamoja na chembe chembe za kinga (CD4) kwa ajili ya uanzishwaji na ufuatiliaji wa matibabu kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI.

Aidha, Serikali imeiwezesha Maabara ya Taifa ya Afya za Jamii iliyopo katika Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa kuipatia vifaa na mashine za kuchunguza magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ya milipuko. Uwepo wa vifaa na mashine hizo za kuchunguza magonjwa umeongeza ufanisi katika kutoa huduma za afya nchini. Katika hatua nyingine, Serikali imeiwezesha Maabara ya NIMR ambayo ni Maabara ya Kimataifa ya Rufaa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kusimamia na kutoa mafunzo ya Uhakiki wa Ubora wa Huduma za Maabara.

208

Huduma za UtafitiSerikali kupitia Taasisi zake za utafiti imeendelea kufanya utafiti wa masuala ya afya kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi. Tafiti za UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na Magonjwa mengine ya Tropiki zimeendelea kufanyika kwa kutathmini huduma mpya za magonjwa hayo kwa kutumia chanjo, dawa na vipimo vya maabara; tafiti za awali; majaribio; tafiti za kiepidemiolojia; tafiti za kuboresha huduma na sayansi jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kitaifa na kimataifa.

Tafiti za malaria zimeonesha kupungua kwa ukubwa wa Malaria katika eneo la Kaskazini Mashariki ya Tanzania. Aidha, utafiti wa chanjo ya malaria uliofanywa wilayani Korogwe umeonesha uwezo mkubwa wa kinga kwa watoto na tathmini za usugu wa Mbu dhidi ya Viuatilifu vinavyotumika kusindika vyandarua umeonesha kuwa kuna usugu wa asilimia 8-11. Vilevile, baadhi ya tafiti za UKIMWI zilizofanyika zimeonesha kuimarika kwa mfumo wa ufuatiliaji wa utumiaji wa dawa za kurefusha maisha kwa wagonjwa.

209

Mpango wa Taifa wa Damu SalamaSerikali imeimarisha huduma za upatikanaji wa damu salama inayokidhi mahitaji kwa kuongeza vituo vya damu salama vya kanda kutoka vinne (4) mwaka 2005 hadi vinane (8) mwaka 2014. Vituo hivyo ni Kanda ya Kaskazini (Moshi), Kanda ya Kusini (Mtwara), Kanda ya Magharibi (Tabora), Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam), Kanda ya Ziwa (Mwanza), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), Kanda ya JWTZ (Lugalo) na Kanda ya Zanzibar (Unguja).

Vilevile, Serikali imeanzisha vituo vidogo vitano (5) vya kukusanya na kusambaza damu (Satelite Blood Collection Sites) ambavyo vipo Mnazi Mmoja, Morogoro, Hospitali ya Mkoa Dodoma, Viwanja vya Ilulu Mkoani Lindi na Kigoma. Ufunguzi wa vituo hivyo umesaidia kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi na hivyo kuongeza idadi ya wachangiaji damu kwa hiari kutoka asilimia 20 mwaka 2005 hadi asilimia 81 mwaka 2014. Ukusanyaji damu umeongezeka kutoka chupa 52,000 hadi 162,367 kwa mwaka katika kipindi hicho. 

210

Huduma za Afya ya KinywaSerikali imeendelea kuvijengea uwezo vituo vya tiba na huduma ya kinywa na meno nchini kwa kuweka vifaa vya tiba ya meno kwenye Halmashauri za wilaya 91 nchini. Aidha, vituo vinavyotoa huduma za afya ya kinywa vimeongezeka na kufikia hospitali 136, vituo vya afya 63 na zahanati tatu (3) nchini. Vilevile, vipo vyuo sita (6) vinavyotoa mafunzo kwa wataalam wa afya ya kinywa ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba Muhimbili kinachotoa Shahada ya Uzamili. Hospitali ya Taifa Muhimbili imefunga mashine 26 mpya za kisasa za tiba ya meno na kuanzisha maabara mpya ya kisasa ya kutengeneza meno bandia. Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Dodoma na Ruvuma zimewekewa mashine za kisasa za tiba ya meno.

Dawa na Vifaa TibaBohari ya Dawa imejengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa na vifaa tiba nchini. Kwa kutumia mikakati mbalimbali, Bohari ya Dawa imeimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba. Serikali imejenga au kukodi maghala sehemu mbalimbali nchini kwa lengo la kuongeza uwezo wa kuhifadhi dawa na vifaa tiba ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma. Uwezo wa Bohari ya Dawa kuhifadhi dawa na vifaa tiba umeongezeka kutoka mita za mraba 26,854 mwaka 2005 hadi mita za mraba 58,939 mwaka 2014.

211

Hatua hizo zimesaidia kuongeza kiwango cha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma nchini kutoka asilimia 55 mwaka 2005 hadi asilimia 89 mwaka 2014. Aidha, Serikali imeiwezesha Bohari ya Dawa kufikisha dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ikilinganishwa na utaratibu wa awali ambapo dawa na vifaa tiba vilikuwa vinafikishwa kwa Mganga Mkuu wa Wilaya. Aidha, bajeti ya ununuzi na usambazaji wa dawa na vifaa tiba imeongezeka mara tano zaidi kutoka Shilingi bilioni 40.6 mwaka 2005 hadi Shilingi bilioni 228 mwaka 2015. Ongezeko hilo limetokana na jitihada za dhati za Serikali katika kukabiliana na maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria.

Moja ya ghala la Bohari Kuu ya Dawa kwa ajili ya kuhifadhi Dawa katika Kanda

212

Huduma za Mama na MtotoSerikali imetekeleza afua mbalimbali zilizopunguza vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano (5) ikiwa ni pamoja na kuwajengea watoa huduma za afya uwezo wa kuwahudumia watoto wachanga wanapozaliwa kwa kuwapatia tiba stahiki. Aidha, Serikali imeongeza bajeti ya ununuzi na usambazaji wa vifaa muhimu kwa ajili ya huduma za mama na mtoto. Hatua hizo zimesaidia kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) kutoka 112 kwa vizazi hai 1,000 mwaka 2005 hadi 54 kwa vizazi hai 1,000 mwaka 2014. Aidha, Taarifa ya Kimataifa ya “Interagency Child Mortality Estimate’’ ya Septemba 2013, imeonesha kuwa Tanzania imeweza kufikia Lengo Namba 4 la Maendeleo ya Milenia kabla ya Mwaka 2015 la kuwa na vifo visivyozidi 54 kwa kila vizazi hai 1000.

Serikali inatekeleza Mpango wa Kuzuia Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ambapo hadi kufikia mwaka 2014 vituo 5,200 vinatoa huduma hiyo ikilinganishwa na vituo 544 vilivyokuwa vikitoa huduma hiyo mwaka 2005. Asilimia 97 ya vituo hivyo inavotoa huduma ya afya ya uzazi hutoa huduma ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Kutokana na ongezeko hilo, idadi ya wajawazito wanaoishi na VVU waliopata huduma ya kuzuia maambukizi ya VVU kwenda kwa mtoto imeongezeka kutoka wajawazito 255,913 mwaka 2005 hadi wajawazito 1,720,991 mwaka 2014.

213

Upimaji wa VVU kwa wajawazito umeongezeka kutoka wajawazito 206,721 mwaka 2005 hadi 1,353,106, sawa na asilimia 73 ya waliopimwa maambukizi ya VVU mwaka 2014. Vilevile, wajawazito na watoto wachanga waliokutwa na maambukizi ya VVU walipatiwa dawa za kupunguza makali ya VVU na kupunguza maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Jumla ya wanawake 73,960 na watoto 63,868 walipatiwa dawa za ARV mwaka 2014 ikilinganishwa na wanawake 13,873 na watoto wachanga 7,424 waliopatiwa ARVs mwaka 2005.

Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWISerikali imeendelea kutoa huduma mbalimbali kwa lengo la kupambana na ugojwa wa UKIMWI. Huduma zilizotolewa zimesaidia kushuka kwa kiwango cha maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kutoka asilimia 7 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2012. Aidha, kiwango cha maambukizi ya VVU kutoka kwa mama wajawazito kwenda kwa watoto kimepungua kutoka asilimia 26 mwaka 2010 hadi asilimia 15 mwaka 2012. Vilevile, idadi ya Vituo vya Upimaji na Ushauri vimeongezeka kutoka vituo 521 mwaka 2005 hadi 4,391 mwaka 2014. Idadi ya wananchi wanaopatiwa huduma hiyo imeongezeka kutoka watu 365,189 mwaka 2005 hadi kufikia watu 25,468,564 mwezi Desemba, 2014.

214

Huduma ya matunzo na tiba kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI zimeongezeka kutoka vituo 96 mwaka 2005 hadi vituo 1,300 mwaka 2015 na idadi ya watu walioanzishiwa dawa za kupunguza makali ya VVU, imeongezeka kutoka 16,199 mwaka 2005 hadi watu 640,048 Desemba, 2014. Tafiti zilizofanyika, zimebainisha kwamba, tohara kwa wanaume ni afua inayoweza kupunguza maambukizi ya UKIMWI kwa asilimia 60. Hivyo, Serikali ilianza kutekeleza afua hiyo mwaka 2010 na hadi mwaka 2014 wanaume 1,138,000 wamekwishafanyiwa tohara.

Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipima Virusi vya UKIMWI wakati wa Uzinduzi wa kampeni maalum ya upimaji wa hiari wa VVU mwaka 2007. 

215

Udhibiti wa Ugonjwa wa MalariaSerikali kwa kushirikiana na wadau wengine imeendelea kutekeleza afua mbalimbali za kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa malaria nchini. Utekelezaji huo ni pamoja na Serikali kusambaza (bila malipo) vyandarua 8,753,438 vyenye viuatilifu kwenye kaya zenye watoto wenye umri chini ya miaka mitano (5). Aidha, vyandarua 7,785,787 viligawiwa kwa wajawazito na vyandarua 4,960,111 kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja (1), kupitia Mpango wa Hati Punguzo. Vilevile, jumla ya vyandarua 26,371,329 viligawiwa kwa wananchi bila malipo kupitia Kampeni zilizolenga Watoto chini ya miaka 5 (U5CC) na ngazi ya Kaya (UCC).

Serikali pia inatekeleza, Mpango wa Upuliziaji wa Viuatilifu Ukoko ndani ya Nyumba vya kuua mbu wanaoeneza malaria ambapo katika Mikoa ya Kagera, Mwanza, Mara na Geita zaidi ya kaya 1,440,000 zenye watu 6,500,000 zimenufaika. Kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika Kanda ya Ziwa, Mpango huo unatarajiwa kutekelezwa katika mikoa ya Kigoma na Lindi.Serikali inatekeleza Mkakati wa Udhibiti wa Viluwiluwi vya Mbu katika Mazalia (aquatic stage) kwa kutumia viuadudu vya kibayolojia (biolarvicides). Mkakati huo ulioanzishwa katika Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam unatarajiwa kutekelezwa kwa awamu katika miji yote ya Wilaya nchini.

216

Aidha, Serikali imekamilisha ujenzi wa Kiwanda cha Viuadudu (Bio – Larvicides) kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha kitakachozalisha viuadudu vya kukidhi mahitaji nchini na hata nchi jirani. Utekelezaji wa afua hizo, umechangia kuokoa maisha ya watoto 60,000 ambao wangefariki kwa ugonjwa wa malaria kila mwaka. Vile vile, idadi ya wagonjwa wa malaria imepungua kutoka 326 kwa kila watu 1,000 mwaka 2009 hadi kufikia wagonjwa 161 kwa kila watu 1,000 mwaka 2014.

Upimaji na Tiba za Saratani ya Kizazi na Matiti

Serikali imechukua hatua mbalimbali za kupunguza ongezeko la saratani kwa kufanya utambuzi na kutoa huduma za tiba mapema kwa saratani ya kizazi kwa wanawake. Vituo zaidi ya 200 vinavyotoa huduma za upimaji, matibabu na utambuzi wa dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi vimeanzishwa katika Mikoa 19. Vilevile, chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi (HPV vaccine), imeanzishwa na inaendelea kutolewa ambapo jumla ya wasichana 17,000 wamepatiwa chanjo hiyo.

217

Ajira za Watumishi wa AfyaSerikali imeendelea kuajiri watumishi wa afya wa kada mbalimbali ili kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini pamoja na kuzisogeza huduma hizo karibu na wananchi. Serikali imeajiri jumla ya wataalam 55,608 kuanzia mwaka 2005 hadi 2014. Watumishi hao wamepangiwa vituo vya kazi katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya nchini.

Mafunzo kwa Wataalam wa AfyaSerikali imeendelea kuvijengea uwezo Vyuo vinavyotoa mafunzo kwa wataalam wa afya ili kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa ambapo idadi hiyo kwa mwaka imeongezeka kutoka wanafunzi 2,811 mwaka 2005/06 hadi kufikia wanafunzi 11,807 mwaka 2014/15. Ongezeko hilo linaendana na utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi unaohitaji ongezeko la wataalam wa afya ili kukidhi mahitaji ya ongezeko la zahanati na vituo vya afya nchini. Hivyo, Serikali imevuka lengo la kudahili wanafunzi 10,000 waliotarajiwa kudahiliwa ifikapo mwaka 2017.

218

Kuboreshwa Huduma katika Hospitali KuuHospitali ya Taifa Muhimbili

Serikali imeboresha upatikanaji wa huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa majengo ya kutolea huduma mbalimbali. Serikali pia imekamilisha ujenzi wa Kituo cha Matibabu na Mafunzo ya Magonjwa ya Moyo na kuanzisha huduma mpya za upasuaji mkubwa wa moyo ambazo zimeanza kutolewa mwezi Mei, 2008. Hadi Desemba 2012, jumla ya wagonjwa 480 wamepatiwa huduma hiyo. Utoaji wa huduma hiyo umeweza kuokoa takriban Shilingi bilioni 4.8 ambazo zingetumika kuwapeleka wagonjwa hao nje ya nchi kutibiwa.

219

Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akioneshwa moja ya vifaa vya kisasa vinavyotumika kuchunguza maradhi ya moyo kwenye ufunguzi rasmi wa Kituo Kipya cha Moyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, 2014. Serikali imeiwezesha Hospitali ya Taifa Muhimbili kutoa huduma ya kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo, ambapo kufikia mwaka 2014, huduma hiyo imetolewa kwa watu 1,198 (wanaume 849 na wanawake 349). Pia, hospitali hiyo imepanua huduma za uchunguzi na tiba kwa kutumia upasuaji kupitia tundu dogo (endoscopy). Huduma hiyo inawafanya wagonjwa walazwe kwa muda mfupi na hata kuruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kufanyiwa upasuaji. Huduma ya matibabu ya saratani kwa watoto pia imeanza kutolewa sanjari na kufunga mitambo na vifaa vya kisasa vya kuchunguza magonjwa mbalimbali kama vile MRI, CT – Scanner na ELISA.

220

Hospitali ya Rufaa ya BugandoSerikali imekarabati Hospitali ya Rufaa ya Bugando inayohudumia wakazi wa mikoa nane (8) ya Kanda ya Ziwa yenye wakazi wapatao milioni 16 na kufunga mitambo. vifaa na mashine za kisasa ambazo zimeiwezesha hospitali hiyo kuanzisha matibabu ya saratani kwa njia ya mionzi (Oncology & Nuclear Medicine) na huduma za upasuaji mkubwa wa moyo. Hadi kufikia mwezi Septemba 2014, jumla ya wagonjwa 81 wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo. Huduma za afya kwa njia ya mtandao zimeboreshwa ambapo daktari bingwa nje ya nchi hushirikiana na madaktari bingwa wa Bugando kutoa huduma kwa wagonjwa nchini. Aidha, katika kipindi cha mwaka 2008 hadi 2012, Hospitali hiyo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Katoliki cha Sayansi ya Tiba, Bugando (CUHAS) imefundisha madaktari 397 pamoja na Wataalam wengine 949 waliobobea katika fani mbalimbali.

Hospitali ya Rufaa ya KCMCHospitali ya Rufaa ya KCMC imewezeshwa na Serikali kutoa huduma za matibabu ya mifupa, magonjwa ya njia ya mkojo na figo (Urology), magonjwa ya ngozi, magonjwa ya pua, masikio na koo. Aidha, Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Tumaini imeendelea kutoa mafunzo ya taaluma za afya ikiwa ni pamoja na shahada za uzamili na uzamivu katika fani mbalimbali za afya.

221

Hospitali ya Rufaa MbeyaSerikali imeboresha Hospitali ya Rufaa Mbeya ambapo mafanikio

makubwa yamepatikana ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa miondombinu ya kutolea huduma kama majengo, mitambo, vifaa tiba na wataalam. Maabara ya hospitali hiyo ilipata ithibati ya kimataifa na ni maabara pekee nchini yenye ‘bio safety level 3’. Vilevile, mitambo na vifaa vya kisasa vimesimikwa katika hospitali hiyo ili kuinua kiwango cha huduma inazotoa. Mitambo na vifaa hivyo ni pamoja na Autoclave kubwa (400lts) kwa ajili ya utakasaji wa vyombo vya upasuaji; mashine mpya ya kutolea dawa ya nusu kaputi na mashine za kusaidia mgonjwa kupumua anapozidiwa.

Hospitali ya Rufaa Mbeya ilianza kutumia Programu za Kielektroniki mwaka 2009 kama njia ya kuboresha huduma zake na udhibiti wa rasilimali. Programu hizo zinaunganisha taarifa zote za mgonjwa ikiwa ni pamoja na maelezo ya daktari, vipimo, utoaji dawa kwa wagonjwa wa bima na huduma nyingine zote. Kila chumba cha daktari na wodi zote zimeunganishwa katika mtandao wa kompyuta. Utaratibu huu umeimarisha utunzaji wa kumbukumbu za wagonjwa na taarifa mbalimbali za hospitali.

222

Taasisi ya Saratani ya Ocean RoadTaasisi ya Saratani ya Ocean Road imeimarishwa ili iweze kutoa matibabu

ya aina mbalimbali za saratani ambapo kwa sasa inatoa huduma kwa wastani wa wagonjwa 2,500 kwa mwaka. Vifaa vya Tiba kwa Mtandao (Telemedicine), mashine za kutibu saratani kwa mionzi aina ya Centron Equinox pamoja na mashine ya High Dose Rate Intracavitary zimesimikwa katika Taasisi hiyo. Mashine hizo zina ufanisi wa hali ya juu katika kutibu saratani ya shingo ya kizazi. Huduma nyingine zilizoboreshwa ni pamoja na;

i. Kununua mashine mbili za “Cobalt 60” zenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.5;

ii. Kununua mashine mbili (intracavitary unit) zenye thamani ya Shilingi milioni 200 na simulator na Treatment Plan Unit vyenye thamani ya Shilingi milioni 280;

iii. Kununua Gamma Camera mbili kwa Shilingi milioni 800;iv. Kujenga Wodi mpya yenye uwezo wa vitanda 257.Katika kuhakikisha ubora wa watumishi, Taasisi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Muhimbili, imeweza kufundisha wataalamu wa saratani katika kiwango cha shahada ya kwanza na ya uzamili wapatao 40 katika kipindi cha miaka mitatu.

223

Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)Serikali imeimarisha Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na kuiwezesha kutoa huduma za upasuaji ambazo awali hazikuwepo nchini. Huduma hizo ni pamoja na kubadilisha mifupa ya nyonga; kubadilisha mifupa ya goti; kufanya upasuaji mkubwa wa saratani ya ubongo; upasuaji mkubwa wa Uti wa Mgongo; na tiba ya majeruhi hasa walioumia ubongo na waliovunjika ambao wengi wao wanafanyiwa upasuaji ndani ya masaa 24. MOI pia imeanzisha masomo ya uzamili katika fani ya upasuaji wa mifupa na majeruhi.

Jengo jipya la Hospitali ya Muhimbili kitengo cha MoI

224

Ujenzi wa Hospitali ya Kisasa na Kampasi ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Eneo la Mloganzila

Serikali imeanza ujenzi wa Hospitali ya Kisasa na Kampasi mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi katika eneo la Mloganzila. Hospitali hiyo itakayokuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 603 kwa wakati mmoja itajengwa kwa gharama ya Dola za Marekani 94,540,000. Kati ya fedha hizo, kiasi cha Dola 76,500,000 ni mkopo nafuu kutoka Serikali ya Korea ya Kusini na Dola 18,040,000 ni mchango wa Serikali ya Tanzania. Mradi huo utakapokamilika utawezesha Chuo Kikuu cha Muhimbili kuongeza uwezo wa kuchukua wanafunzi kutoka idadi ya sasa 3,100 hadi kufikia 15,000 na hivyo kupunguza uhaba wa wataalam wa afya nchini.

Vilevile, Serikali imeanza mchakato wa kununua na kuweka vifaa tiba kufuatia kusainiwa Mkataba na Mtaalamu wa kuweka vifaa hivyo Desemba, 2014. Lengo ni kuhakikisha kwamba hospitali hiyo itakapokamilika vifaa hivyo viweze kutumika mara moja. Aidha, ujenzi wa kilomita 4 za barabara ya lami kutoka eneo la mradi hadi Kibamba katika Barabara Kuu ya Morogoro unaendelea na upo katika hatua za ukamilishwaji. Vilevile, umeme wa muda umefikishwa katika eneo la mradi pamoja na miundombinu ya maji.

225

SEKTA YA MAJI

Serikali imeendelea kutekeleza Sera ya Maji ya Mwaka 2002 ambayo imeweka mwongozo mzuri wa maendeleo ya Sekta ya maji katika kuendeleza, kutunza na kusimamia matumizi endelevu ya vyanzo vya maji. Katika kutekeleza Sera hiyo, Serikali iliandaa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji ya (2006 – 2025) ambayo inatekelezwa kwa awamu za vipindi vya miaka mitano. Awamu ya kwanza ilianza kutekelezwa mwaka 2007/2008 na kukamilika mwezi Juni, 2014 ambapo miradi mbalimbali ya maji imekamilika.

Awamu ya kwanza ya Programu iligawanywa katika Programu ndogo nne (4) ambazo ni; Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji; Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini; Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mijini, na Kuimarisha na Kuzijengea Uwezo Taasisi zinazotekeleza Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji. Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Programu hiyo ulianza Julai, 2014.

226

Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini

Serikali imeimarisha huduma za maji vijijini kwa kukarabati, kujenga na kupanua miundombinu ya maji katika maeneo ya vijijini. Serikali ilianza kutekeleza Mradi wa Maji kwa Vijiji 10 kwa Kila Halmashauri. Mpango huo ulioanza kutekelezwa mwezi Julai, 2006 umewezesha kutekelezwa kwa miradi 1,555 nchini kote. Aidha, ujenzi wa miradi 763 ya maji iliyopo katika vijiji 830 unaendelea. Kati ya miradi hiyo, miradi 290 imekamilika na miradi 473 ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Vilevile, mwaka 2007 Serikali ilianza

kutekeleza miradi ya maji yenye kuleta matokeo ya haraka (Quickwins) ambapo hadi kufikia Septemba 2014, jumla ya miradi 4,560, yenye vituo vya kuchotea maji 9,546 imejengwa au kukarabatiwa. Hatua hiyo imeongeza upatikanaji wa huduma ya maji kwa watu 2,386,500 waishio vijijini.

Kupitia Mpango wa “Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa (BRN!), Serikali imeongeza vituo vya kuchotea maji kutoka vituo 16,062 vilivyokuwepo kabla ya Mpango huo kuanza hadi vituo 32,977 ilipofika mwezi Juni, 2014. Kukamilika kwa miradi hiyo kumeongeza upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa wakazi 8,244,250 waishio vijijini. Kiwango cha watu wanaopata huduma ya maji safi vijijini imeongezeka kutoka asilimia 53.5 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 67.7 mwaka 2015.

227

Uvunaji wa Maji ya MvuaKatika kukabiliana na uhaba wa maji kwenye maeneo kame nchini, Serikali ilielekeza kila Halmashauri kuandaa Mpango wa miaka mitano (5) na kutunga Sheria ndogo zinazohakikisha kuwa michoro ya nyumba zote zinazojengwa inajumuisha mifumo ya miundombinu ya kuvuna maji ya mvua kabla ya ujenzi wake kuidhinishwa. Hadi kufika mwezi Aprili 2015, Halmashauri mbalimbali nchini zimejenga matanki 800 ya lita kati ya 1,000 na 5,000 ya kuvuna maji ya mvua kwenye shule, zahanati na taasisi nyingine. 

Ujenzi wa Mabwawa ya MajiSerikali imeendelea kujenga na kukarabati mabwawa ya maji katika maeneo kame nchini ili kuwapatia wananchi huduma endelevu ya maji. Mabwawa ya Iguluba (Iringa) na Wegero (Meatu) yamekamilika. Mabwawa ya Sasajila (Dodoma), Habiya (Itilima), Seke Ididi (Kishapu), Matwiga (Chunya), Kawa (Nkasi), Mwanjoro (Butiama) na Kidete (Kilosa) yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi. Ujenzi wa mabwawa ya Habiya, Seke Ididi na Matwiga umeanza mwezi Juni, 2014.

228

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Nachingwea mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Shilingi Bilioni 34.6 unaojumuisha Wilaya za Nachingwea na Masasi

mkoani Mtwara.

229

Uundaji wa Vyombo vya Watumiaji Maji

Serikali imeelekeza Halmashauri zote nchini kusajili vyombo vya watumiaji maji ili kuhakikisha kuwa uendeshaji na usimamizi wa miradi ya maji unafanyika kwa mujibu wa sheria. Hatua hiyo imesaidia kuongeza idadi ya vyombo vya watumiaji maji vilivyosajiliwa kisheria kutoka vyombo 75 mwaka 2005 hadi vyombo 909 mwezi Aprili, 2015.

Vilevile, mafunzo mbalimbali yametolewa kwa vyombo hivyo ili kuvijengea uwezo wa kuendesha shughuli zake ikiwa ni pamoja na mafunzo ya uendeshaji, utunzaji wa fedha, matengenezo madogo ya mradi na njia mbalimbali za utoaji wa taarifa za maendeleo ya mradi.

230

Huduma ya Maji MijiniSerikali imetekeleza miradi mbalimbali yenye lengo la kuboresha huduma za Maji Mijini. Miradi hiyo hutekelezwa na Mamlaka 23 za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwenye Miji Mikuu ya Mikoa, Mamlaka zaidi ya 100 za Miji Mikuu ya Wilaya na Miji Midogo pamoja na Miradi nane (8) ya Kitaifa. Mamlaka hizo zinasimamiwa na Bodi za Wakurugenzi ambapo wakazi wapatao 6,584,810 wanapata huduma ya maji kutoka katika Mamlaka hizo. Kiwango cha upatikanaji maji kwa wakazi wa Miji Mikuu ya Mikoa kimeongezeka kutoka asilimia 74 mwaka 2005 hadi asilimia 86 mwaka 2014. Katika Jiji la Dar es Salaam kiwango kimeongezeka kutoka asilimia 55 hadi asilimia 68 katika kipindi hicho. Aidha, hali ya upatikanaji wa maji katika Miji Mkuu ya Wilaya, Miji Midogo na Miradi ya Kitaifa ni asilimia 53. Vilevile, Uzalishaji maji umeongezeka kutoka mita za ujazo 273,959 kwa siku mwaka 2005 hadi kufikia mita za ujazo 384,353 mwaka 2014, sawa na ongezeko la asilimia 40.

Mhe. Mizengo P. Pinda (Mb.) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizindua Mradi wa Maji katika Mji Mdogo  wa Kibaigwa wilayani Kongwa. Chanzo: Wizara ya Maji

231

Huduma ya Maji kwa Wasiokuwa na UwezoMamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Miji Mikuu ya Mikoa hutoa huduma ya maji bila gharama kwa kaya zisizokuwa na uwezo. Jumla ya kaya 2,000 katika mamlaka hizo hupatiwa lita 160 kwa siku kwa kila Kaya sawa na takriban lita 5,000 kwa mwezi.

Kupunguza Upotevu wa Maji MijiniSerikali imeendelea kukarabati miundombinu ya maji kwa lengo la kupunguza upotevu wa maji. Hali hiyo imepunguza upotevu wa maji kwenye miji hiyo kutoka zaidi ya asilimia 50 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 35 mwezi Machi, 2015. Lengo ni kupunguza upotevu huo hadi kufikia asilimia 20 ya maji yanayozalishwa, kiwango kinachokubalika Kimataifa.

Kupungua kwa upotevu huo wa maji kumechangiwa pia na ukarabati mkubwa wa miundombinu ya maji uliofanyika katika miji ya Arusha, Moshi, Tanga, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Songea, Iringa, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Musoma na Bukoba, pamoja na jitihada za kupambana na uvujaji maji katika Mamlaka zote. Kutokana na hali hiyo, makusanyo ya maduhuli katika Mamlaka hizo yameongezeka kutoka Shilingi bilioni 22 mwaka 2005 hadi kufikia Shilingi bilioni 78 mwaka 2014. Ongezeko hilo limeziwezesha Mamlaka hizo kujiendesha zenyewe kwa kulipa gharama za uendeshaji, kuchangia katika uwekezaji na mishahara ya watumishi wake na hivyo kuipunguzia mzigo Serikali.

:

232

Miradi Mikubwa ya MajiSerikali imetekeleza miradi mikubwa ya maji kwa lengo la kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata maji safi na salama. Miradi mikubwa ifuatayo imetekelezwa kwa mafanikio makubwa.

Mradi wa Maji wa Kahama – ShinyangaSerikali imekamilisha kazi ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kutoa maji Ziwa Victoria hadi miji ya Kahama na Shinyanga. Mradi huo ulikamilika mwaka 2009 na uligharimu jumla ya Shilingi bilioni 252. Mradi huo ni mkubwa kuliko miradi yote ya maji iliyotekezwa nchini kwa kutumia fedha za ndani za Serikali. Mradi huo umesanifiwa kuhudumia wananchi wapatao 1,000,000. Kukamilika kwa mradi huo kumeboresha huduma ya maji katika miji ya Shinyanga, Kahama na Vijiji vipatavyo 76 vilivyo kandokando ya bomba kuu. Mradi wa Maji ChalinzeSerikali inatekeleza Mradi wa Maji Chalinze kwa ajili ya kusambaza maji katika vijiji vya Wilaya za Bagamoyo na sehemu ya Morogoro Vijijini. Awamu ya Kwanza ya mradi huo iliyogharimu Shilingi bilioni 23.4 imekamilika na kuwanufaisha wananchi 180,000. Ujenzi wa Awamu ya Pili ya mradi huo unaendelea na unalenga kuvipatia maji vijiji 47 vikihusisha vijiji 42 vya mkoa wa Pwani na vijiji 5 vya Mkoa wa Morogoro. Mradi huo ukikamilika, unatarajiwa kuwanufaisha wakazi 197,648 wa Wilaya za Bagamoyo, Kibaha na Morogoro Vijijini. Utekelezaji wa Awamu ya Tatu unatarajiwa kukamilika mwaka 2016 na kugharimu Dola za Marekani milioni 49.

233

Huduma ya Maji Safi na Majitaka Jijini Dar es Salaam

Serikali inatekeleza mpango wa kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama na uondoshaji majitaka katika Jiji la Dar es Salaam na Miji ya Kibaha na Bagamoyo. Madhumuni ya mpango huo ni kuongeza wingi wa maji kutoka lita milioni 300 kwa siku za sasa hadi lita milioni 756 kwa siku ifikapo mwaka 2017. Utekelezaji wa Mpango huo ulioanza mwaka 2011, umewezesha kupanuliwa kwa Mtambo wa Kusafisha Maji wa Ruvu Chini na kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 180 hadi lita milioni 270 kwa siku ilipofika mwaka 2014.

Aidha, ujenzi wa bomba la maji lenye urefu wa kilomita 55.9 la kusafirisha maji na ujenzi wa kingo za Mto Ruvu katika eneo la Kidogozero unaendelea. Vilevile, kazi ya kulaza bomba kuu la kutoka mtamboni hadi Kibamba, pamoja na ujenzi wa tanki jipya la Kibamba umekamilika. Upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu unatarajiwa kuongeza uwezo wa mtambo kuzalisha maji kutoka lita milioni 82 kwa siku hadi lita milioni 196 kwa siku. Hatua hiyo inatarajiwa kupunguza tatizo la uhaba wa maji unaotokana na kasi ya ukuaji wa Miji ya Mlandizi, Kibaha na Jiji la Dar es Salaam.

234

Visima Virefu vya Kimbiji na Mpera

Serikali imeanza kazi ya kuchimba visima 20 virefu kwa awamu katika maeneo ya Kimbiji na Mpera. Visima hivyo vikikamilika vitakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 260 kwa siku. Awamu ya Kwanza ya mradi huo imekamilika na ulipaji wa fidia kwenye eneo la mita 60 kuzunguka kila kisima katika maeneo ya Kimbiji na Mpera umekamilika. Aidha, uthamini katika maeneo ya ujenzi wa njia za mabomba na barabara kuelekea kwenye visima umeanza.

Ujenzi wa Bwawa la KidundaSerikali imeanza mchakato wa kujenga Bwawa la Kidunda ili kuhakikisha

kwamba maji katika mto Ruvu yanakuwepo kipindi chote cha mwaka na kuzalisha umeme wa megawati 20. Kazi ya usanifu wa bwawa imekamilika na tathmini ya athari za kimazingira na kijamii kwa ajili ya ujenzi wa barabara kuelekea eneo la ujenzi wa Bwawa la Kidunda imekamilika.

Kazi ya uthamini kwa ajili ya malipo ya fidia kwenye njia ya umeme imekamilika na Awamu ya Kwanza ya ulipaji fidia imekamilika. Aidha, Serikali kupitia DAWASA na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro inaandaa viwanja 1,000 kwa ajili ya kuwahamishia waathirika wa mradi pamoja na barabara kwenda makazi mapya kwa gharama ya Shilingi bilioni 1.3.

235

Miundombinu ya Majitaka1.Miundombinu ya majitaka imejengwa na baadhi yake kupanuliwa katika Miji ya Arusha, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Tabora, Moshi, Tanga, Songea na Iringa. Hii imeongeza huduma ya uondoaji majitaka kwa wakazi wanaoishi kwenye miji hiyo kutoka asilimia 17 mwaka 2006 hadi asilimia 20 mwaka 2014.

Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za MajiSerikali imefanya jitihada za kuweka mfumo endelevu wa kusimamia, kuhifadhi, kudhibiti matumizi ya maji na kugawa maji yaliyopo kwa uwiano kulingana na mahitaji ya sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuanzishwa kwa Bodi ya Taifa ya Maji na Bodi za Maji za Mabonde tisa (9) nchini zenye wajumbe kutoka Sekta mbalimbali. Bodi hizo zimepewa uwezo wa kisheria wa kutoa vibali vya kutumia maji ambapo hadi mwezi Aprili 2014, jumla ya vibali 3,731 vya kutumia maji na vibali 33 vya utupaji wa Majitaka vimetolewa chini ya Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya mwaka 2009 ikilinganishwa na vibali 235 vilivyokuwa vimetolewa mwaka 2005.

236

Serikali inaandaa Mipango Shirikishi ya Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji kwa lengo la kuwawezesha wadau mbalimbali kutekeleza majukumu yao katika kutunza vyanzo vya maji, kudhibiti matumizi ya maji na kupunguza migogoro ya watumia maji. Mipango sita (6) kati ya tisa (9) imekamilika na Jumuia za Watumia Maji zimeongezeka kutoka 56 mwaka 2005 hadi 99 mwaka 2014.

Serikali inashirikiana na Jumuia hizo katika utoaji wa elimu na uhamasishaji kuhusu Sera ya Maji ya mwaka 2002 kwa jamii na makundi mbalimbali.

237

SURA YA SABA

MAENEO MENGINE MUHIMU1. SEKTA YA HABARI NA UTANGAZAJI Usajili wa Magazeti, Redio na TelevisheniKatika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne, idadi ya magazeti na majarida

yaliyosajiliwa imeongezeka kutoka magazeti na majarida 504 mwaka 2005 hadi 833 Desemba, 2014 sawa na ongezeko la asilimia 65. Aidha, vituo vya redio vimeongezeka kutoka vituo 59 mwaka 2005 hadi vituo 93 Desemba, 2014. Vilevile, vituo vya televisheni 28 vimesajiliwa na kuongeza wigo wa kupata matangazo, kuhabarisha, kuburudisha na kuelimisha umma wa Tanzania.

Serikali imeendelea kuifanyia maboresho Kampuni ya Magazeti (TSN) na hivyo kuiwezesha kuanzia gazeti jipya la HABARILEO pamoja na kuongeza kurasa katika magazeti yaliyokuwepo ya Daily News na Sunday News. Tovuti ya Wananchi Serikali ilianzisha tovuti ya wananchi mwaka 2007 kwa ajili ya wananchi kutoa maoni na hoja mbalimbali kuhusu utekelezaji wa shughuli za Serikali na Utumishi wa Umma kwa ujumla. Hadi kufikia mwaka 2013, tovuti ya wananchi ilikuwa imepokea hoja 117,243 na kati ya hizo, hoja 78,258 zilizoihusu Serikali zilishughulikiwa.

238

Shirika la Utangazaji Tanzania

Serikali imeendelea kuboresha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuimarisha mtizamo wa idhaa za matangazo yake na kuanzisha TBC1, TBC Taifa, TBC FM na TBC Internatinal. Mitambo ya Frequency Modulation (FM) imewekwa katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mbeya, Tabora, Kigoma, Mwanza, Mara, Kagera, Tanga, Lindi, Singida, Rukwa, Shinyanga, Iringa, Manyara, Katavi, Kilimanjaro, Ruvuma (Songea na Tunduru), Mtwara, Morogoro, Pwani, Zanzibar na Pemba.

Aidha, TBC imejenga mitambo ya kurushia matangazo ya FM ya idhaa ya Kimataifa katika mikoa ya Arusha, Dodoma na Mwanza. Vilevile, imejenga mitambo ya kurushia matangazo ya televisheni katika mfumo wa dijiti katika Mikoa 14 ambayo ni Shinyanga, Geita, Dar Es Salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Kilimanjaro, Ruvuma (Songea na Tunduru), Tanga, Morogoro, Pwani, Zanzibar, Pemba na Mbeya. 

239

Mfumo wa Utangazaji wa DigitiSerikali imekamilisha dhamira yake ya kuhama kutoka mfumo wa analojia kwenda dijiti. Utelelezaji huo ulioanza tarehe 31 Desemba, 2012 kwa kuzima mitambo ya analojia katika Mkoa wa Dar es Salaam, Mbeya, Tanga, Mwanza, Arusha, Dodoma, na Moshi umekamilishwa mwezi Aprili, 2015 kwa kuzima mitambo ya analogia katika Miji ya Lindi na Mtwara. Hatua hiyo imeifanya Tanzania kufikia makubaliano ya kubadili teknologia ya utangazaji kutoka analojia kwenda digiti kabla ya tarehe 17 Juni, 2015 iliyowekwa kimataifa. Tanzania ni moja ya nchi chache barani Afrika ambazo zimetekeleza uhamiaji huo kwa mafanikio makubwa. Mafanikio hayo yamewafanya wataalam kutoka nchi mbalimbali kuja kujifunza utekelezaji wa mpango huu.  

SEKTA YA MICHEZO  Serikali imeendelea kudumisha na kukuza michezo kwa kuboresha miundombinu ya michezo. Eneo la Changamani la Michezo (Sports Complex) limeendelea kujengwa, Jijini Dar es Salaam kwa awamu ya kwanza ambayo ni uwanja wa kisasa wenye viwango vya Olimpiki, ukiwa na viwanja vya mpira wa miguu na riadha. Uwanja huo wenye uwezo wa kuingiza watu 60,000 wakiwa wamekaa ulikabidhiwa baada ya uwekaji wa TARTAN Januari, 2009. Aidha, ukarabati wa Uwanja wa Uhuru kwa kujengwa umbo jipya (U) pamoja na kuezekwa paa lake umekamilika. Uwanja huo sasa una uwezo wa kuchukua watu 20,000 wakiwa wameketi.

240

Uwanja wa Mpira wa Kisasa – Dar es SalaamSEKTA YA SHERIAKatiba

Serikali imeendelea kusimamia utekelezaji wa Katiba na Sheria za nchi katika uendeshaji wa shughuli za umma na binafsi, na hivyo kuweka misingi imara ya kuendelea kuwepo kwa amani na utulivu nchini. Aidha, Serikali imesimamia na kuratibu mchakato wa kihistoria wa kuandika Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotokana na maoni ya wananchi. Hatua muhimu za kuandika Katiba Mpya zilizokamilika ni pamoja na Kutunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyojumuisha wajumbe wa makundi mbalimbali ya jamii kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. Tume hiyo ilikusanya maoni ya wananchi na kuandaa Rasimu ya Kwanza na ya Pili ya Katiba. Hatua nyingine iliyokamilika ni Kuundwa kwa Bunge Maalum la Katiba ambapo Rasimu ya Katiba ilijadiliwa na Bunge Maalum la Katiba na hatimaye kupatikana kwa Katiba Inayopendekezwa. Hatua iliyobakia ni wananchi kuipigia Kura ya Maoni Katiba hiyo.

241

Mhe. Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Dkt.Mohamed Ali Shein Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa wameinua juu Katiba Inavyopendekezwa mara baada ya kukabidhiwa na Spika wa Bunge la Katiba, Mjini Dodoma........2014.

Utafiti na Urekebishaji wa SheriaSerikali imeendesha tafiti mbalimbali za kisheria kwa lengo la kuimarisha mfumo wa sheria nchini. Matokeo ya tafiti hizo yamewezesha kutungwa kwa Sheria ya Mtoto, Sura ya 13; Sheria ya Kutambua Ushahidi wa Kielektroniki ya mwaka 2007; Sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009, Sheria ya Walemavu, Sura ya 183; na Sheria 188 zimefanyiwa marekebisho ili ziweze

242

Uendeshaji wa Mashauri ya Madai na JinaiSerikali imesogeza huduma za kisheria karibu zaidi na wananchi kama moja ya njia muhimu ya kuharakisha maendeleo ya nchi. Jitihada hizo zimesaidia kuanzisha vituo vya huduma za kuendesha mashauri katika Mikoa na Wilaya. Jumla ya Mashauri 5,085 ya madai yaliendeshwa kati ya mwaka 2005 na 2015 ambapo Mashauri 1,379 yalihitimishwa. Aidha, Mashauri ya Jinai 233,512 yaliendeshwa na Mashauri 124,769 kuhitimishwa. Vilevile, Mashauri 132 ya Katiba, 80 ya Uchaguzi yaliendeshwa ambapo Mashauri 17 ya Katiba yalihitimishwa na Mashauri yote 80 ya Uchaguzi yalihitimishwa.

Serikali imefungua Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika mikoa 14. Kufunguliwa kwa ofisi hizo kumefanya Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali mikoani kuongezeka kutoka 11 mwaka 2005 hadi 25 mwaka 2014. Aidha, Serikali imeajiri Mawakili wa Serikali wapya 422 na kuwapeleka katika mikoa mbalimbali nchini. Vilevile, jumla ya mikataba 3,427 ilifanyiwa upekuzi wa kuhakikiwa na kutolewa ushauri wa kisheria katika kipindi hicho.

243

Mahakama

Katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2014, Serikali imefanikisha kutungwa kwa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama (The Judicial Administration Act, No.4/2011). Sheria hiyo imebadili muundo wa Mahakama kwa kuanzisha nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Msajili Mkuu wa Mahakama. Mtendaji Mkuu wa Mahakama ndiye msimamizi mkuu wa masuala ya utawala katika mahakama akisaidiwa na Watendaji wengine wa Mahakama. Msajili Mkuu wa Mahakama anasimamia shughuli za kuendesha mashauri na majukumu mengine ya msingi (Judicial functions). Hatua hiyo imeongeza ufanisi katika shughuli za utoaji haki nchini.

Idadi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani imeongezeka kutoka Majaji tisa (9) mwaka 2005 hadi 16 mwaka 2014. Idadi ya Majaji wa Mahakama Kuu imeongezeka kutoka Majaji 35 mwaka 2005 hadi Majaji 78 mwaka 2014 na Mahakimu Wakazi wameongezeka na kufikia zaidi ya 900 nchini. Ongezeko la watumishi wa mahakama pamoja na utaratibu wa kutenganisha majukumu ya kiutawala na kazi za kimahakama umepunguza mlundikano wa mashauri mahakamani. Aidha, Mahakama imeanzisha utaratibu wa kupima utendaji kazi wa Mahakimu na Majaji kwa kigezo cha idadi ya mashauri wanayoamua. Chini ya utaratibu huo, kila Jaji wa Mahakama ya Rufani anatakiwa kumaliza wastani wa mashauri 1,200 hadi 1,400 kwa mwaka na Mahakama Kuu wastani wa mashauri 220 kwa mwaka.

244

Mahakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na Wilaya wamewekewa lengo la kila mwaka kuamua mashauri 250 hadi 300. Aidha, Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara inatumia TEHAMA na mifumo ya kielektroniki katika kusikiliza mashauri na kutunza kumbukumbu. Viwango vya posho ya Wazee wa Baraza vimeongezewa kutoka Shilingi 1,500 mwaka 2005 hadi Shilingi 5,000 kwa kila shauri linalohitimishwa. Ongezeko la viwango hivyo, limeongeza ufanisi katika utendaji wa kusikiliza Mashauri na kupungua malalamiko na manung’uniko ya siku nyingi ya watendaji hao. Vilevile, mazingira ya kufanyia kazi kwa Majaji, Mahakimu na watumishi wa ngazi zote za mahakama yameboreshwa kwa kununua vifaa vya kisasa kama magari, pikipiki na samani kwa lengo la kurahisisha kazi na kuongeza ufanisi. 

Mafunzo ya Uanasheria kwa VitendoSerikali imeanzisha Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo kwa lengo la kuandaa, kuendesha na kutoa mafunzo ya uanasheria kwa vitendo kwa wahitimu wa Shahada ya Kwanza katika fani ya Sheria. Mafunzo yanayoendeshwa ni mahsusi kwa ajili ya wahitimu ambao wanatarajia kujiunga na utumishi wa umma au wanaotarajia kufanya kazi za uwakili wa kujitegemea. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kukamilika kwa majengo ya kudumu ya Taasisi yaliyopo maeneo ya Sinza, Dar es Salaam, yaliyojengwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 16.

245

Hadi kufikia mwezi Juni 2014, Taasisi hiyo imedahili jumla ya wanafunzi wa sheria 4,189. Kati yao, wanafunzi 3,348 wamehitimu na wengine 841 wanaendelea na mafunzo. Kati ya waliohitimu mafunzo, wanafunzi 1,708 walifaulu na kutunukiwa Stashahada ya Uzamili.

Huduma ya Usajili, Ufilisi na UdhaminiMwaka 2006, Serikali ilifanya mabadiliko ya kisheria ili kuanzisha Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) iliyochukua nafasi ya iliyokuwa Idara ya Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali. Lengo la hatua hiyo ni kuimarisha uwezo wa Serikali wa kusajili matukio muhimu ya binadamu; kupunguza utegemezi wa Idara ya Kabidhi Wasii Mkuu kifedha kwenye Hazina Kuu ya Serikali na kuwa moja ya vyanzo vya mapato ya Serikali. Hatua hiyo imesaidia kuongeza usajili wa matukio muhimu ya binadamu kutoka vizazi 284,907 mwaka 2005 hadi 600,622 mwaka 2014; vifo 36,758 hadi 53,241; na ndoa 10,064 hadi 17,479.

Aidha, huduma za usajili wa matukio muhimu ya binadamu zimesogezwa hadi katika ngazi ya Mikoa na Wilaya. Hivi sasa Wakala unatekeleza mkakati wa uandikishaji wa vizazi utakaowezesha kufikiwa kwa lengo la asilimia 85 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 100 ifikapo mwaka 2025.

246

Haki za BinadamuSerikali imeendeleza jitihada za kukuza, kulinda na kuhifadhi haki za binadamu na Utawala wa Sheria nchini. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuanza kutoa huduma zake katika Mikoa ya Lindi, Mwanza, Mjini Magharibi na Pemba. Vilevile, Serikali imeanzisha mfumo wa kielektroniki wa kupokea malalamiko toka kwa wananchi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu. Hatua hiyo imechangia kuongeza upatikanaji wa huduma zitolewazo na Tume ya Haki za Binadamu kwa Wananchi wengi zaidi. Idadi ya malalamiko yanayowasilishwa Tume kwa mwaka imeongezeka kutoka 9,455 mwaka 2006 hadi 25,921 mwaka 2014. Aidha, uwezo wa Tume wa kushughulikia malalamiko kwa mwaka umeongezeka kutoka malalamiko 3,021 mwaka 2005 hadi malalamiko 18,501 mwaka 2014.

Serikali imeendelea pia kutekeleza majukumu yake yanayotokana na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa ambayo Tanzania imeridhia. Aidha, Taarifa za utekelezaji wa Haki za Binadamu imekuwa ikiandaliwa na kuwasilishwa kwenye vyombo husika vya Kikanda na Kimataifa. Utekelezaji wa mikataba hiyo umechangia katika kuboresha haki za binadamu nchini ambapo Sheria mbalimbali zimetungwa zenye lengo la kuendeleza haki hizo ikiwemo Sheria ya Haki za Mtoto Na. 21/2009 na Sheria ya Watu wenye Ulemavu Na,9/2010.

1.

247

Utawala BoraSerikali imeendelea kutekeleza dhana ya Utawala Bora ili kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kuwa na imani na Serikali yao. Programu za maboresho zimeendelea kutekelezwa ili kuimarisha utawala bora na uwajibikaji. Kupitia Programu hizo, malalamiko 1,575 yamepokelewa ambapo malalamiko 764 yaliyohusu ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma yalichambuliwa, kuchunguzwa na hatua stahiki kuchukuliwa. Aidha, Fomu 60,948 za Tamko la Rasilimali, Maslahi na Madeni zilirejeshwa sawa na asilimia 77 ya Fomu 78,786 zilizosambazwa.

Mashauri 46 ya ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma yameshughulikiwa. Katika mashauri 27 kati ya mashauri yaliyoshughulikiwa, ilithibitika kuwepo kwa ukiukaji wa Sheria hiyo ambapo adhabu mbalimbali zilitolewa ikijumuisha Onyo, Onyo Kali na Faini. Hatua hizo zimeboresha upatikanaji wa huduma kwa umma, kupanua demokrasia na kuongeza kasi ya utoaji maamuzi ya mashauri katika Mahakama za Mwanzo na za Wilaya.

248

Kuzuia na Kupambana na Rushwa Serikali imeendelea kushirikiana na wananchi katika jitihada za kuzuia na kupambana na rushwa. Kutokana na jitihada hizo, kesi mpya zilizofunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini ziliongezeka kutoka 50 mwaka 2005 hadi kesi 1,900 mwaka 2014. Katika uwiano, kesi ambazo Serikali ilishinda mwaka 2013 hadi 2014 ni nyingi kuliko ilizoshindwa na washtakiwa kuachiwa/kuchukuliwa hatua za kiutawala. Aidha, katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha mwaka 2005 hadi Juni, 2014, Serikali imefanikiwa kuokoa kiasi cha mali yenye thamani ya Shilingi bilioni 86.7. Kiasi hiki ni ongezeko la Shilingi bilioni 84.2 ikilinganishwa na mwaka 2005 ambapo ziliokolewa Shilingi bilioni 2.5. Daftari la Kudumu la Wapiga KuraKatika mkakati endelevu wa kuimarisha na kukuza demokrasia nchini, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya uchaguzi imekuwa ikiboresha Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kila inapoonekana kuna ulazima. Mwaka 2008, daftari hilo liliboreshwa na kuonesha kuwa wapiga kura wamefika 18,014,667 kutoka 15,935,493 waliokuwepo mwaka 2005. Aidha, uboreshaji kwa awamu ya pili ulifanyika mwaka 2010 ambapo wapiga kura walioandikishwa walifikia milioni 21.8 sawa na asilimia 86 ya watu wote wenye umri wa kupiga kura. Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea na mchakato wa kuboresha Daftari hilo kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambapo inatumia mfumo wa kielektroniki ujulikanao kama Biometric Voters Registration (BVR).

249

MuunganoSerikali ya Awamu ya Nne imefanya jitihada kubwa kuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa mwaka 1964. Katika kipindi hicho, wananchi wa pande zote mbili za Muungano wameongeza ukaribu wao kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kutokana na juhudi za Serikali zote mbili za kuweka mazingira wezeshi kupitia mazungumzo yenye lengo la kutatua changamoto zinazoukabili Muungano. Kamati ya pamoja ya kujadili changamoto za Muungano chini ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekutana mara kwa mara na kujadili changamoto za Muungano. Pamoja na vikao hivyo, Wizara na Sekta nyingine zisizo za Muungano zimekuwa zikikutana na kujadili namna ya kushirikiana katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii. Vikao hivyo vimeimarisha ushirikiano wa pande zote mbili na kuwaweka watendaji karibu zaidi. Baadhi ya changamoto zilizopatiwa ufumbuzi ni:

Utekelezaji wa Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu wa Utawala BoraSheria Na.7 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ya mwaka 2001 inayosimamiwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ilikuwa haitekelezwi Zanzibar. Hivyo, Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Oktoba, 2006 ili kukidhi matakwa ya Tume kufanya kazi pande mbili za Muungano. Kwa sasa Tume imefanya kazi pande zote mbili za Muungano.

250

Uvuvi kwenye Ukanda wa Uchumi wa Bahari Kuu Ukanda wa Uchumi katika Bahari Kuu unasimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo, Sheria Na.1 ya Mamlaka ya Uvuvi katika Ukanda wa Bahari Kuu ya mwaka 1998 haikuhusisha taasisi za SMZ katika utekelezaji wake. Hivyo Sheria ilifanyiwa marekebisho mwezi Februari, 2007 na kutambua taasisi zinazohusika na matumizi ya Bahari Kuu kwa upande wa Zanzibar na kuzijumuisha katika Kamati ya Utendaji ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu. Hivi sasa, Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu ni moja, yenye Makao Makuu Zanzibar. Utekelezaji wa Sheria ya Usafiri wa MajiniMasuala yote yanayohusu uchukuzi na usalama wa njia ya majini katika mikataba yote ya kimataifa inayoihusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanatekelezwa kupitia Sheria ya Merchant Shipping ya mwaka 2003. Baada ya mashauriano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Kimataifa la Usafiri Baharini (International Maritime Organization – IMO), imekubalika kuwa Zanzibar iwe na Mamlaka yake ya Usafiri Majini (Zanzibar Maritime Authority) chini ya Sheria yake ya Maritime Transport iliyoanza kutumika mwaka 2006. Kupitia Sheria hiyo, Zanzibar inatekeleza baadhi ya majukumu kulingana na mikataba ya kimataifa chini ya usimamizi wa Serikali ya Muungano wa Tanzania. Mgawanyo wa Mapato ya Misaada na Uwezo wa Zanzibar Kukopa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikipata misaada mbalimbali kutoka kwa Washirika wa Maendeleo na nchi wahisani kwa ajili ya kutekeleza Programu za maendeleo. Hata hivyo, mgawanyo wa mapato hayo umekuwa na changamoto katika pande mbili za Muungano. Pande mbili za Muungano zimeridhia Zanzibar iendelee

251

kupata mgao wa asilimia 4.5. Aidha, Zanzibar imepewa mamlaka kukopa ndani na nje ya nchi. Kwa mikopo ya nje, SMZ inakopa kupitia udhamini wa Serikali ya Muungano ambapo SMT huhamisha mkopo unaoombwa kutoka nje kwenda SMZ. Serikali zote mbili zinashirikiana katika maandalizi ya bajeti, ikiwemo mapendekezo ya upatikanaji wa misaada na mikopo ya kibajeti kutoka nje.

Kodi nyinginezoPande mbili za Muungano zinajadiliana na SMZ ipate sehemu ya mapato yanayokusanywa kutoka kwenye Kodi ya Mishahara ya Wafanyakazi (PAYE) na kuingizwa kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina wa SMZ wakati utaratibu wa kurekebisha Sheria unaendelea.

Wafanyabiashara wa Zanzibar kutozwa kodi mara mbiliKuwepo kwa tofauti ya ukadiriaji wa viwango vya thamani za bidhaa, na kodi ya forodha baina ya Ofisi za TRA zilizopo Tanzania Bara na zile zilizopo Zanzibar, kumeleta changamoto kwa wafanyabiashara wa Zanzibar. Katika kuhakikisha kuwa changamoto hizo hazijitokezi tena, pande mbili za Muungano zimekubaliana kuwa mfumo unaotumika sasa wa tathmini uendelee katika kipindi cha mpito, wakati TRA ikifanya tathmini ya mfumo wa kodi ya forodha ili kubaini faida na upungufu uliopo.Mwaka 2014, Muungano wa Tanzania ulitimiza miaka 50 ukiwa umefanya mambo mengi makubwa kwa manufaa yapande mbili za Muungano.

252

Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yalifanyika kwa mafanikio makubwa kwa kuandaliwa maonesho na sherehe mbalimbali za kumbukumbu ya Tukio hilo muhimu. Matarajio ya Watanzania wengi ni kwamba muungano huo ambao ni wa wananchi utaendelea kuimarika zaidi na wananchi wa pande zote mbili kutumia fursa nyingi za uchumi zinazopatikana pande zote mbili za Muungano kujiletea maendeleo.

SENSA YA WATU NA MAKAZISerikali imekamilisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012. Zoezi hilo lilikamilika kwa ufanisi mkubwa na kuwezesha kupatikana kwa takwimu sahihi zitakazotumika katika kupanga mipango ya maendeleo na kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma nchini. Matokeo ya Sensa yameonesha kwa idadi ya watu nchini Tanzania ni 44,928,923 ambapo watu 43,625,354 wapo Tanzania Bara na watu 1,303,569 wapo Zanzibar. Aidha, Serikali imetoa machapisho mbalimbali yanayotafsiri matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi katika makundi mabalimbali ya kijamii na kiuchumi ili ziweze kutumika katika kupanga mipango ya maendeleo. Vilevile, mfumo wa kompyuta wa kutunza takwimu umeandaliwa ambapo takwimu za Sensa zinapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (www.nbs.go.tz).

253

VITAMBULISHO VYA TAIFA Serikali ilianzisha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) mwaka 2008 kwa lengo la kujenga Mfumo wa Utambuzi na Usajili wa Watu wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wakiwemo raia wa Tanzania, wageni wakaazi na wakimbizi wanaoishi kihalali hapa nchini. Mfumo huo unashirikisha taarifa za NIDA na taasisi nyingine kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za Serikali na sekta binafsi kwa wananchi. Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imeanza zoezi la utambuzi na usajili wa watu ambapo hadi kufikia mwezi Septemba, 2014 imesajili watu 4,816,979 katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na Morogoro.  

ULINZI NA USALAMASerikali imefanya jitihada kubwa za kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka yote pamoja na kulinda maisha na mali za raia. Jitihada zilizofanyika ni pamoja na utoaji wa mafunzo kwa askari, ujenzi wa makazi bora na ununuzi wa vifaa vya kisasa.

254

Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mujibu wa Sheria yalirejeshwa mwaka 2013 kwa vijana waliohitimu kidato cha sita. Mafunzo hayo yalianza kutolewa mwezi Machi, 2013 ambapo takriban vijana 38,200 wamehitimu mafunzo hayo hadi kufikia mwezi Januari, 2015. Malengo ya mafunzo hayo ni pamoja kuwajengea uzalendo, ukakamavu, maadili mema, utaifa na kuwafunza stadi za kazi vijana wa Tanzania.

Uboreshaji wa Makazi ya AskariSerikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya wanajeshi unaogharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 300. Lengo la mradi huu ni kupunguza uhaba wa nyumba kwa ajili ya makazi ya Maafisa na Askari. Mikoa inayohusika kwenye mpango huu wa ujenzi ni Arusha (nyumba 792), Dar es Salaam (2,288), Dodoma (592), Kagera (144), Kigoma (160), Morogoro (616), Pwani (840), Pemba (320) na Tanga (312). Mradi huu ulizinduliwa rasmi tarehe 15 Mei, 2013 na utakamilika ifikapo Septemba, 2017. Katika awamu ya kwanza ya mradi huu zinajengwa nyumba 6,064 kwa kuzingatia vipaumbele na mahitaji. Jumla ya nyumba 3,096 zilizokuwa zikijengwa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zimekamilika. Ujenzi na ukarabati mkubwa umefanyika katika majengo ya hospitali kuu za jeshi kanda za Zanzibar (Bububu), Mbeya na Tabora (Mirambo). Aidha, Hospitali Kuu ya Jeshi (Lugalo) imepandishwa hadhi na kuwa Hospitali Kuu ya Rufaa.

255

Baadhi ya nyumba za Wanajeshi zilizojengwa eneo la Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya

Wanajeshi.

Kwa upande wa nyumba za Jeshi la Polisi, maghorofa 90 katika maeneo ya Dar es Salaam, Pemba na Unguja yenye makazi 394 ya askari yamejengwa. Katika kipindi hicho pia, maghorofa 15 ya askari wa vyeo vya chini ya kuwezesha kuishi askari 60 yamejengwa katika mikoa ya Mara, Mwanza na Kagera. Aidha, jumla ya mabweni 14 kwa ajili ya askari wapya yamejengwa nchi nzima na nyumba 242 za askari polisi zimejengwa. Nyumba hizo zimejengwa na kukamilika katika mikoa ya Arusha na Dar es Salaam.

256

Ujenzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC)

Serikali imejenga Chuo cha Ulinzi cha Taifa ambacho kimekamilika tangu mwaka 2011 na uzinduzi wake ulifanyika tarehe 10 Septemba, 2012. Chuo hicho kimeanzishwa kwa ajili ya kutoa mafunzo ya uongozi wa masuala ya ulinzi na usalama wa Taifa kwa maafisa waandamizi Jeshini na Serikalini.

Kuanzishwa kwa Chuo hicho, kimesadia kupunguza gharama za kuwasomesha Maafisa na Viongozi wa Jeshi na Serikali nje ya nchi.

Mradi wa MatrektaSerikali kupitia Shirika la SUMA JKT, imeendelea na mradi wa kuleta nchini matrekta na zana zake ikiwa ni mpango maalum wa Serikali katika kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya ‘Kilimo Kwanza’ inayolenga kupunguza matumizi ya jembe la mkono na kuongeza zana za kisasa. Matrekta 1,840 na zana za kilimo zenye thamani ya Shilingi bilioni 53.67 ziliingizwa nchini na SUMA JKT. Matrekta na zana hizo zimeuzwa kwa mkopo kwa wadau mbalimbali zikiwemo Halmashauri za Wilaya, Vikundi vya Uzalishaji mali, SACCOS na watu binafsi ikiwa ni hatua ya kuunga mkono kauli mbiu ya Kilimo Kwanza.

257

Baadhi ya Matrekta ya Mradi wa SUMA JKT yakiwa katika eneo la Kambi ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam. Matrekta 1,840 na zana za kilimo yaliuzwa kwa mkopo kwa wadau mbali mbali zikiwemo Halmashauri za wilaya, vikundi vya uzalishaji mali, SACCOS na watu binafsi WAN

258

Mapambano dhidi ya Dawa za KulevyaSerikali imeendelea kutekeleza Sheria ya Kuzuia Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya Namba 9 ya mwaka 1995. Mafanikio yafuatayo yamepatikana:

•Ushirikiano miongoni mwa vyombo vya udhibiti umejengwa na hivyo kuongeza ukamataji wa dawa za kulevya na watuhumiwa. Jumla ya kilo 3,144.43 za heroin, kilo 356.3 za cocaine, kilo 210,335.80 za bangi na kilo 44,570.80 za mirungi zilikamatwa hadi kufika mwaka 2014;

•Kuimarika kwa huduma muhimu kwa waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya;•Kuundwa kwa Kikosi Kazi katika ngazi ya taifa kinachojumuisha vyombo vya Ulinzi na Usalama ili kuhusika na mapambano dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya;•Kuongezeka uelewa wa tatizo la dawa za kulevya miongoni mwa jamii.Jumla ya watumiaji dawa za kulevya 20,626 walifika katika vituo vya tiba kupata huduma za tiba. Aidha, watumia dawa aina ya heroin 1,805 wanaendelea kupata tiba katika vituo vya Mwananyamala, Temeke na Muhimbili.

Katika juhudi za kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya, Sheria ya Kupambana na Dawa za Kulevya imehuishwa ili iweze kukabiliana na changamoto mpya katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya. Kupitia sheria hiyo, Mamlaka ya Udhibiti itakayokuwa na nguvu zaidi kuliko ilivyoTume.

259

HIFADHI YA MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJISerikali imeimarisha usimamizi katika utekelezaji wa Sera ya Mazingira ya mwaka 1997 pamoja na Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004. Katika kufanikisha utekelezaji huo, Serikali ilianzisha Programuu ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira (Enviromental Management Act Implemetation Support Programume –EMA ISP) mwaka 2005 kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa sheria hiyo.  Mafanikio yaliyopatikana kupitia Programu hii ni pamoja na kuandaa Kanuni za Sheria ya Mazingira, kuhuisha masuala ya Mazingira katika Mipango ya Maendeleo, kuandaa na kusambaza miongozo kuhusu hifadhi ya mazingira, kufanya tathmini ya athari za mazingira za miradi mbalimbali, kufanya tathmini za kimkakati za mazingira, kuimarisha usimamizi wa viwanda na biashara ili kuzingatia hifadhi ya mazingira, kutunga Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira na kutoa elimu ya mazingira kwa Umma. Serikali pia imetekeleza Mikakati na Miradi mbalimbali ya hifadhi ya mazingira kama vile Mkakati wa Kuhifadhi Mazingira ya Ardhi na Vyanzo vya Maji; Mkakati wa Kutunza Vyanzo vya Maji na Misitu; Tuzo ya Rais ya Kutunza Vyanzo vya Maji, Kupanda na Kutunza Miti; Mkakati wa Kuratibu Kampeni ya Upandaji Miti; na Mkakati wa Hatua za Haraka za Kuhifadhi Mazingira ya Bahari, Ukanda wa Pwani, Maziwa, Mito na Mabwawa. Kati ya mwaka 2007 na 2013, jumla ya miti 1,258,002,967 ilipandwa kama inavyoonekana kwenye dekwali Na.17.

260

MWAKA ILIYOPANDWA ILIYOSTAWI ASILIMIA (%)

2007/2008 245,970,955 213,872,564 87

2008/2009 267,956,464 190,988,377 71

2009/2010 208,868,230 162,277,018 78

2010/2011 180,798,223 141,470,900 78

2011/2012 145,156,884 108,171,349 75

2012/2013 209,252,211 142,868,916 68

JUMLA 1,258,002,967 959,649,124 76

Jedwali Na.17: Idadi ya Miti iliyopandwa Nchini na Kustawi katika Kipindi cha mwaka 2007 – 2013

Chanzo: Ofisi ya Makamu wa Rais

261

USAWA WA KIJINSIA Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha kwamba usawa wa kijinsia unazingatiwa katika jamii ili kuwezesha wanawake kushiriki, kumiliki na kunufaika kwa usawa katika fursa za maendeleo. Katika kipindi cha 2005 hadi 2014, mafanikio makubwa yamepatikana katika kufikia azma ya Serikali ya usawa wa kijinsia kiuchumi, kijamii na kisiasa

• Ushiriki wa Wanawake Katika Uongozi na MaamuziUshiriki wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi na maamuzi umeongezeka ambapo idadi ya Mawaziri wanawake imeongezeka kutoka 6 kati ya Mawaziri 25 mwaka 2005 hadi kufikia 10 kati ya Mawaziri 32 mwaka 2013; Wakuu wa Wilaya wameongezeka kutoka 20 kati ya Wakuu wa Wilaya 104 mwaka 2005 hadi kufikia 53 kati ya Wakuu wa Wilaya 144 mwaka 2013; Majaji wanawake wameongezeka kutoka 8 kati ya Majaji 50 mwaka 2005 hadi kufikia 24 kati ya Majaji 67 mwaka 2013; na Wabunge Wanawake wameongezeka kutoka 62 kati ya Wabunge 288 mwaka 2005 hadi kufikia 127 kati ya Wabunge 352 mwaka 2015.

Mapambano Dhidi ya Ukatili kwa Wanawake na WatotoSerikali imeendeleza jitihada za kuzuia na kupambana na ukatili dhidi ya wanawake kupitia kampeni mbalimbali na maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Kutokana na jitihada hizo, mwamko wa jamii katika kutoa taarifa za matukio ya vitendo vya ukatili kwenye Mamlaka husika umeongezeka.

262

Matukio 42,019 ya ukatili dhidi ya binadamu yakijumuisha mauaji, kubaka, kulawiti, kutupa watoto, wizi wa watoto, usafirishaji wa binadamu na kunajisi yalitolewa taarifa kwenye Mamlaka husika. Jeshi la Polisi limeanzisha Dawati la Jinsia na Watoto kwenye vituo vya polisi karibu nchi nzima. Hili ni Dawati maalum linalohudumiwa na watendaji waliopewa mafunzo maalum kwa ajili ya kushughulikia makosa ya unyanyasaji wa kijinsia tofauti na hapo awali ambapo hapakuwa na utaratibu maalum wa kushughulikia makosa hayo. 

MENEJIMENTI YA MAAFASerikali imeendelea kuhakikisha kwamba Taifa linajikinga, linajiandaa, linakabili na kurejesha hali endapo maafa/majanga yanayotokea. Maafa au majanga yanayotokea yanaweza kuwa ni yale ya asili au kusababishwa na shughuli za binadamu. Maafa hayo yamekuwa yanasababisha vifo, uhaba mkubwa wa chakula na hata kukosa amani na utulivu. Kati ya mwaka 2005 na 2014 Serikali ilitoa chakula cha msaada kiasi cha tani 578,459.06 zenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 200 kwa zaidi ya wananchi milioni 3 waliokumbwa na njaa katika maeneo mbalimbali nchini. Serikali pia, iliwawezesha wakulima wasio na uwezo kupata mbegu katika mikoa iliyoathirika na ukame. Jumla ya Shilingi bilioni 15.72 zilitumika kukabiliana na maafa mbalimbali yakiwemo mafuriko yaliyotokea katika maeneo nchini kati ya mwaka 2006 na 2014.

263

Aidha, Serikali ilitoa Shilingi bilioni 2.31 ununuzi wa mifugo kwa ajili ya familia za wafugaji zilizopoteza mifugo kutokana na ukame mkubwa uliokumba Mikoa ya Arusha na Manyara. Vilevile, Serikali ilitoa jumla ya Shilingi bilioni 11.59 kwa ajili ya wananchi walioathirika na milipuko ya mabomu katika eneo la Mbagala na eneo Gongolamboto.

Serikali imeendelea kuzijengea uwezo Halmashauri na vyombo vya dola katika kudhibiti na kukabiliana na majanga ya aina mbalimbali. Mipango ya Wilaya ya kujiandaa na kukabiliana na maafa pamoja na Mikakati ya Mawasiliano imeandaliwa na kusambazwa kwenye Halmashauri za Wilaya kumi (10) ambazo ni; Dodoma (Mpwapwa, Chamwino na Kondoa); Shinyanga (Shinyanga (V), na Kishapu); Simiyu (Maswa, Bariadi, na Meatu); Kilimanjaro (Same na Mwanga).

KUHAMIA MAKAO MAKUU DODOMASerikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha inahamia Dodoma. Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kutenga eneo kwa ajili ya Ujenzi wa Mji wa Serikali karibu na Ikulu ya Chamwino. Aidha, Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) imeendelea na uboreshaji miundombinu ya Dodoma ili kuharakisha azma hiyo. Miundombinu hiyo ni barabara, umeme; huduma za maji safi, maegesho; maeneo ya wazi, ujenzi wa maeneo ya mandhari; mitaro ya maji ya mvua; na upandaji wa maua na nyasi. Mipango ya matumizi bora ya ardhi imeandaliwa kulingana na kasi ya upanukaji wa mji.

264

Mipango ya maendeleo na ramani za makazi pia zimeandaliwa na uboreshaji na uhalalishaji wa maeneo yaliyojengwa kiholela umefanyika.Serikali imeweka mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma (Hekta 5,000), Chuo cha Upelelezi cha Polisi (Hekta 127), Chuo cha Jesuit Fathers (Hekta 180), Eneo la Uwekezaji kwa ajili ya Ujenzi wa Majengo mbalimbali (Real Estate Development) la Ndejengwa karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma (Hekta 500) na Uwanja wa Nane Nane (Hekta 160).

Vilevile, Serikali inaendelea kuhamasisha Sekta Binafsi kushiriki katika ujenzi wa hoteli za kisasa, viwanda pamoja na Taasisi kama vile shule, hospitali na nyumba za ibada katika maeneo ya Manispaa ya Dodoma yaliyotengwa na yatakayoendelea kutengwa. Utoaji wa maeneo hayo kwa wawekezaji unaendelea ambapo hadi mwaka 2014 Manispaa imetoa viwanja vyenye ukubwa wa mita za mraba 783,054 kwa ajili ya makazi, mita za mraba 1,539,400 kwa Taasisi na mita za mraba 285,000 kwa ajili ya majengo ya biashara ili kukidhi mahitaji ya Makao Makuu ya Nchi. Aidha, viwanja vya makazi vyenye mita za mraba 2,433,900 vimepimwa na miundombinu ya umeme, barabara na maji imewekwa katika maeneo ya Ndejengwa. CDA pia imetenga mita za mraba 410,000 kwa ajili ya hoteli za kisasa na majengo makubwa ya biashara (Shopping Malls) mita za mraba 204,400 kwa ajili ya viwanda, mita za mraba 1,569,900 kwa ajili ya Taasisi na mita za mraba 160,400 kwa ajili ya maeneo ya kuchezea watoto katika eneo la Njedengwa.

265

Serikali pia imekamilisha ujenzi wa majengo yenye hadhi ya Makao Makuu kwa ajili ya Ofisi za Wizara ya Fedha, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kumbukumbu za Nyaraka za Taifa, LAPF na Benki Kuu. Aidha, Shirika la Nyumba la Taifa limejenga nyumba za makazi eneo la Medeli Mkoani Dodoma kwa ajili ya watumishi watakaohamia Makao Makuu.

KUZUIA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWISerikali ya Awamu ya Nne imendeleza jitihada za kupambana na ugonjwa wa UKIMWI ambao umekuwa tishio kubwa katika Maendeleo ya Taifa. Mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 10 ni pamoja na:

Kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI na kupitia Mkakati wa Pili wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI kuandaa Mkakati wa Tatu wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2013/14 -2017/18; Kutekeleza mpango wa matunzo na matibabu kwa Watu Wanoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) ambapo idadi ya WAVIU waliojiunga na huduma ya matunzo na matibabu imeongezeka kutoka 403,378 mwaka 2008 hadi 1,366,402 ongezeko la asilimia 238.8. Idadi hii ni sawa na asilimia 68 ya watu wanaoishi na VVU. Aidha, Vituo vinavyotoa huduma ya matunzo na matibabu imeongezeka kutoka vituo 700 mwaka 2008 hadi vituo 1,209 sawa na asilimia 73. Kutekeleza huduma za kuzuia maambukizo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ambapo wanawake wajawazito WAVIU 75,866 sawa na asilimia 77.5 ya wanawake wajawazito wanaoishi na VVU walipata huduma ya ARVs ili kupunguza hatari ya maaabukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

266

•Kuunda Mabaraza ya Watu Waishio na Virusi vya UKIMWI kwa lengo la kulinda na kutetea masuala yote yanayowahusu WAVIU nchini na kufanya uraghabishi wa VVU na UKIMWI ili kuongeza mwitikio wa jamii. Hadi kufika Desemba, 2014, jumla ya Mabaraza 92 ya Wilaya (district clusters) yameanzishwa.•Kufanya utafiti wa kubainisha viwango vya maambukizi ya VVU kwa lengo la kufahamu ukubwa na mwenendo wa maambukizi ya UKIMWI, ufahamu wa jamii kuhusu kinga, tiba na vichocheo vya maambukizi ya Ugonjwa wa UKIMWI. Utafiti uliofanyika umeonesha dalili za kushuka kwa kiwango cha ushamiri wa Virusi vya UKIMWI kwenye jamii kutoka asilimia 7% mwaka 2003/04 hadi asilimia 5.7 mwaka 2007/08 na asilimia 5.3 mwaka 2013. •Kutoa elimu ya VVU na UKIMWI kwa jamii kwa kupitia vyanzo mbalimbali vya habari ikiwemo radio, luninga, magari 21 ya sinema mikoani, machapisho na majarida mbalimbali juu ya VVU na UKIMWI ikiwa pamoja na mawasiliano juu ya ubadilishaji wa tabia zinazosababisha kupata maambukizi ya VVU.Kutokana na juhudi hizo za Serikali, taarifa na takwimu za hivi karibuni zimeonesha kupungua kwa kasi ya ushamiri wa VVU na huduma ya matibabu kuendelea kuimarika. Lengo la Serikali ni kuwa na Sifuri Tatu (hakuna maambukizi mapya, hakuna vifo vinavyotokana na VVU na hakuna unyanyapaa wa waathirika. Aidha, Serikali imeanzisha Mfuko wa UKIMWI (AIDS Trust Fund) utakaowezesha nchi kuwa na fedha za ndani za kutosha kwa ajili ya kudhibiti UKIMWI na kupunguza utegemezi kutoka kwa wahisani. Mfuko huo unategemea kuchangia karibu asilimia 40% ya mahitaji ya fedha kwa ajili ya kukabiliana na UKIMWI nchini.

267

Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwet,e Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikabidhi hundi kwa uongozi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kwa ajili ya kuwezesha Asasi za Kiraia zinazojihusisha na mapambano ya VVU na UKIMWI.

268

MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAASerikali imeendelea kuboresha huduma na kupeleka madaraka kwa wananchi kupitia Sera ya Ugatuaji wa Madaraka. Serikali imeanzisha maeneo mapya ya utawala ikiwa eneo na Mikoa mipya minne ya Katavi, Geita, Simiyu na Njombe. Aidha, Serikali imeanzisha Wilaya mpya 19 za Chemba, Ikungi, Mkalama, Busega, Itilima, Mbogwe, Kyerwa, Nyang`hwale, Kakonko, Buhigwe, Uvinza, Butiama, Kaliua, Kalambo, Mlele, Momba, Wanging`ombe, Nyasa na Gairo. Lengo ni kupeleka huduma karibu na wananchi na pia kutoa huduma kwa haraka, ufanisi, weledi na kiwango kinachotakiwa.

Serikali ilizipa hadhi ya kuwa Halmashauri za Miji Mamlaka za Miji midogo ya Njombe, Mpanda, Kahama, Masasi, Handeni, Nzega, Kasulu, Makambako na Tunduma na kufanya idadi ya Halmashauri za Miji kuongezeka na kufikia 13 mwaka 2014. Aidha, Halmashauri za Wilaya za Bahi, Chamwino, Rorya, Misenyi, Chato, Nanyumbu, Mkinga, Siha, Meru, Arusha, Longido zilianzishwa. Halmashauri za Manispaa za Arusha, Tanga na Mbeya zilipewa hadhi ya Jiji. Halmashauri ya Mji wa Lindi pamoja na Halmashauri za Wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke kutoka Jiji la Dar es Salaam zilipewa hadhi ya Manispaa. Vilevile, Manispaa ya Ilemela ilianzishwa kutoka Jiji la Mwanza.

Serikali imesimamia uanzishwaji wa maeneo mapya ya utawala na kufanya maeneo hayo kuongezeka na kufikia Kata 3,804, Vijiji 12,275, kutoka vijiji 10,376 mwaka 2005 Mitaa 3,922 toka 2,626 na Vitongoji 64,669 kutoka 57,137 katika kipindi hicho

269

SURA YA NANE MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKISERA YA DIPLOMASIA YA UCHUMISerikali imeendelea kutekeleza Sera ya Mambo ya Nje inayosisitiza diplomasia ya uchumi. Ziara za Viongozi wa Kitaifa nje ya nchi zimekuwa na mafanikio makubwa. Kutokana na Tanzania kuendelea kuheshimika kimataifa, viongozi wa mataifa mbalimbali walifanya ziara nchini na kuiwezesha Tanzania kunufaika katika uwekezaji kutoka nje katika sekta mbalimbali. Viongozi mashuhuri wa Kimataifa waliotembelea Tanzania ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Xi Jinping aliyetembelea nchi yetu mwaka 2013 na kuwezesha kusainiwa kwa mikataba 16 ya miradi mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na Tanzania.

Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Mkongo wa Taifa na Ujenzi wa Bandari kwenye Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo. Vilevile, ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani mwaka 2013 imeifanya nchi yetu kuwa moja ya nchi saba za Afrika zitakazonufaika na mradi wa uzalishaji wa umeme utakaogharimiwa na Serikali ya Marekani kwa kiasi cha Dola za Marekani bilioni 7 huku Washirika wengine wa Maendeleo wakitoa Dola za Marekani bilioni 9.

270

Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa bidhaa mbalimbali za Kitanzania zinaendelea kutambulika na kupata soko katika masoko mbalimbali ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania ni mwanachama. Mwaka 2008 nchi yetu ilisaini Makubaliano ya Kuanzisha Soko la Pamoja la Jumuiya za SADC, EAC na COMESA na hivyo kuongeza wigo wa soko la bidhaa zinazozalishwa nchini. Aidha, Serikali imeingia makubaliano ya kupanua wigo wa soko la bidhaa za ndani na nchi nyingine duniani. Kwa mfano, kupitia Kongamano la ”Forum on China-Africa Cooperation” (FOCAC) idadi ya bidhaa za Afrika zinazoweza kuingizwa kwenye soko la China bila kulipia ushuru imeongezeka kutoka 187 hadi 440. Mazao ya tumbaku na bidhaa za baharini ni miongoni mwa bidhaa ambazo Tanzania imeingia makubaliano ya kuziingiza moja kwa moja katika soko la China.Serikali imefanikisha ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere kilichopo Jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kimejengwa kwa msaada wa Serikali ya Watu wa China na kuwa kivutio kikubwa cha mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa na hivyo kutoa fursa za biashara kwa mahoteli, vyombo vya usafiri na maduka ya bidhaa, na kuongeza shughuli za utalii wa mikutano nchini. Kituo hicho kilitumika katika Mkutano mkubwa wa Kimataifa wa Smart Partinership Dialogue uliofanyika mwezi Juni, 2013 ambao uliwaleta Tanzania Viongozi ishirini na washiriki takriban mia nane. Utalii wa mikutano (Conference Tourism) ni moja ya nyenzo muhimu ya kutangaza na kukuza utalii, kwa kuwa washiriki huamua kutembelea vivutio baada ya mikutano, au kurejea baadae kwa ajili ya kutalii baada ya kuwa na ufahamu na nchi hiyo.

271

Jengo la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (Julius Nyerere International Convention Centre-JNICC)

272

USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA MASUALA MBALIMBALI YA KIMATAIFA

Tanzania imeendelea kutoa mchango mkubwa katika kuleta maendeleo na ustawi kwa Jumuiya ya Kimataifa. Kwa kutambua mchango wa nchi yetu, mara kadhaa Tanzania imeongoza mataifa mengine katika shughuli za kurejesha amani, utulivu na maelewano hususan katika eneo la Maziwa Makuu. Jitihada za Tanzania katika kuleta amani, utulivu na maelewano ni pamoja na jukumu la kuongoza Vikosi vya Kulinda Amani vilivyopo Darfur nchini Sudan tangu mwezi Juni, 2013, na jukumu la kuongoza vikosi vya kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu mwezi Aprili, 2014. Utekelezaji wa majukumu hayo umeiletea heshima kubwa nchi yetu na kuonesha mchango mkubwa wa Tanzania katika ujenzi na ulinzi wa amani. KUONGEZA UWAKILISHI NJE YA NCHI KWA KUFUNGUA BALOZI

MPYASerikali imeendelea kutekeleza Mpango wake wa miaka 15 wa kufungua balozi mpya, kununua, kujenga na kukarabati majengo ya ofisi na makazi katika balozi. Katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2014, Serikali imefanikiwa kufungua balozi tano (5) katika miji ya Muscat (Oman); Kuala Lumpar (Malaysia); Brasilia (Brazil); The Hague (Uholanzi) pamoja na Moroni, (Comoro). Aidha, Serikali imejenga jengo la Ofisi ya ubalozi New Delhi nchini India, kununua majengo ya Ofisi ya Ubalozi Washington D.C. na New York nchini Marekani na Paris nchini Ufaransa. Vilevile, Serikali imefanya ukarabati wa majengo ya ofisi na makazi yaliyopo Maputo, Brussels, Ottawa, Nairobi na Tokyo.

273

Jengo la Ubalozi wa Tanzania mjini New Delhi nchini India

MCHAKATO WA KUTAMBUA JUMUIYA YA WATANZANIA WANAOISHI UGHAIBUNI

Serikali ilianzisha mchakato wa kuzitambua Jumuiya za Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) ili waweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa lao. Kongamano la Kwanza la Jumuiya za Watanzania waishio nje ya nchi lilifanyika nchini mwezi Agosti, 2014 na kushirikisha Watanzania kutoka nchi mbalimbali. Matokeo ya jitihada hizo yameanza kuonekana kwa Jumuiya kadhaa za Watanzania waishio nje ya nchi kuonesha nia ya kurudi nchini na kuwekeza katika maeneo mbalimbali. Kwa mfano, Kampuni ya Kilimo Bora inayomilikiwa na Watanzania waishio Canada na Marekani imeonesha nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha zao la ufuta kwa ubia na mwekezaji kutoka Canada. Vilevile, Kampuni inayomilikiwa na Watanzania waishio Edinburg, Scotland imeonesha nia ya kushirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kutafuta vyanzo vya mitaji huko Scotland.

274

USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKISerikali imedhamiria kuhakikisha kwamba Watanzania wananufaika ipasavyo na fursa za kiuchumi na kijamii zinazotokana na mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha, Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara ili kuvutia uwekezaji na ukuaji wa biashara nchini. Matokeo ya jitihada hizo ni kupanuka kwa soko la bidhaa za ndani na kuongezeka kwa shughuli za uwekezaji kutoka nchi wanachama. Kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania imesaini makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi baina yake na Nchi za Jumuiya ya Ulaya ambao utainufaisha nchi yetu katika kupata fursa za masoko ya Nchi za Ulaya.• Itifaki ya Umoja wa ForodhaItifaki ya Umoja wa Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilianza kutekelezwa tarehe 1 Januari, 2005 ikilenga kukuza biashara, kuongeza ufanisi katika uzalishaji, kuongeza uwekezaji wa ndani baina ya nchi Wanachama na kuendeleza viwanda. Katika kipindi chote cha utekelezaji wa Itifaki hiyo, Tanzania imepata mafanikio makubwa hususan katika eneo la biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Thamani ya bidhaa za Tanzania zilizouzwa katika Nchi Wanachama imeongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 142.0 mwaka 2005 hadi Dola za Marekani milioni 1,120.1 mwaka 2013 ikiwa ni ongezeko la Dola za Marekani milioni 978.10. Bidhaa zilizochangia katika ongezeko hili ni pamoja na nafaka, karatasi, mbolea, vifaa vya umeme, mashine, bidhaa za mafuta na vimiminika, vyandarua, bidhaa za plastiki, na chai.

275

Bidhaa nyingine ni saruji, matunda, chuma, samaki, ngano, sukari na nguo. Aidha, thamani ya biashara ya jumla (total trade) ya Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki imeongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 317.9 mwaka 2005 hadi Dola za Marekani Milioni 1,515.0 mwaka 2013. Ongezeko hilo limeongeza mgao wa biashara (market share) ya Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka asilimia 15.2 mwaka 2005 na kufikia asilimia 26.1 mwaka 2013 ikiwa ni nafasi ya pili baada ya Kenya. Utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki umechangia katika jitihada za Serikali za kuvutia na kukuza uwekezaji hapa Nchini. Utekelezaji wa Itifaki hiyo umewezesha idadi na thamani ya miradi ya uwekezaji kutoka Nchi Wanachama kuongezeka kutoka miradi 35 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 39.6 mwaka 2005 hadi kufikia miradi 244 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 676.5 mwaka 2013. Aidha, katika kipindi hicho miradi hiyo imezalisha jumla ya ajira 15,721 kwa Watanzania. 

276

• Uundwaji wa Soko la Pamoja la Afrika Mashariki Soko la Pamoja la Afrika Mashariki ni hatua ya pili ya mtangamano wa Afrika Mashariki na ilianza kutekelezwa mwaka 2010. Lengo lake ni kufungua fursa za uhuru wa kuuza bidhaa, uhuru wa kufanya biashara ya huduma, uwekezaji, uhuru katika soko la mitaji, fursa za kuanzisha shughuli za kiuchumi na uhuru wa kupata ajira katika maeneo yaliyofunguliwa katika Nchi Wanachama. Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja, Tanzania imefungua milango ya ajira katika Sekta zinazokabiliwa na uhaba kama vile Walimu wa vyuo vya elimu ya juu na vyuo vikuu wenye shahada ya uzamivu; Walimu wa shule za sekondari katika fani za Hisabati, Fizikia na Baiolojia; Walimu wa shule za msingi zinazofundisha kwa lugha ya kiingereza wenye angalau shahada ya kwanza; Walimu wa vyuo vya Kilimo, Ufundi Stadi wenye kiwango cha elimu cha angalau shahada ya pili katika fani husika, Wauguzi na wakunga. Kufunguliwa kwa maeneo haya kumevutia uwekezaji na teknolojia na kuimarisha ushindani wa ndani.

277

• Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika MasharikiNchi Wanachama wa Afrika Mashariki zimesaini Itifaki ya Umoja wa Fedha Mwezi Novemba 2013 ikiwa ni msingi katika kuwa na Sarafu moja ya Nchi Wanachama. Hatua hiyo itaweza kukuza biashara na uchumi wa nchi yetu na kupunguza gharama za kufanya biashara baina ya nchi za Jumuiya na kuongeza mauzo ya bidhaa za Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.• Ushirikiano Katika Masuala ya Ulinzi na Usalama

Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeendelea kuandaa na kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi ambapo mazoezi mawili yalifanyika nchini kati ya mwaka 2009 na 2013. Nchi Wanachama zinashirikiana pia katika masuala ya kiufundi hususan katika ununuzi wa vipuri na matengenezo ya vifaa vya kijeshi, kupeana taarifa mbalimbali za kiutafiti, kuwa na mafunzo ya pamoja na masuala ya utamaduni ambapo kila mwaka Majeshi ya Nchi wanachama hufanya mashindano ya michezo mbalimbali.

Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeendelea kutekeleza Mpango Mkakati wa Amani na Usalama wa Jumuiya (The EAC Strategy for Regional Peace and Security) ambapo Nchi Wanachamna hubadilishana taarifa za kiusalama na mbinu zinazotumiwa na wahalifu; kubadilishana Programu za mafunzo ya usalama; kuanzisha mfumo wa kuimarisha operesheni za pamoja; kupambana na dawa haramu za kulevya.

278

Aidha zinashirikiana kwa Viongozi wa vyombo vya usalama kutembeleana; kuanzisha mfumo wa kudhibiti wakimbizi; kupambana na ugaidi; kupambana na wizi wa mifugo; kutekeleza mradi wa kudhibiti kusambaa kwa silaha haramu ndogo ndogo na nyepesi; kusimamia mpango wa kuimarisha usalama katika Ziwa Victoria; kuandaa mfumo wa kushughulikia migogoro katika kanda; na kuanzisha mfumo wa kudhibiti majanga. Aidha, nchi wanachama zimesaini Itifaki ya Amani na Usalama ya Afrika Mashariki mwezi Februari, 2013 ikiwa na lengo la kushughulikia changamoto mtambuka za kiusalama zilizopo na zinazojitokeza katika nchi wanachama.

279

SURA YA TISA

•HITIMISHOMafanikio yaliyopatikana tangu Serikali ya Awamu ya Nne ilipoingia madarakani ni makubwa kwani malengo yaliyowekwa yamefikiwa kwa kiasi kikubwa. Licha ya changamoto ya hali ya mdororo wa uchumi duniani ulioanza mwaka 2008 pamoja na ukame uliotokea mwaka 2007 na madhara yake kuendelea kwa miaka kadhaa, uchumi umekua kwa kasi nzuri ikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara. Ukuaji huo wa uchumi umewezesha ongezeko la mapato ambayo yametumika kutekeleza miradi ya kipaumbele.

Ujenzi na ukarabati wa miundombinu muhimu umewezesha usafiri na usafirishaji kuimarika na hivyo kuwezesha bidhaa na pembejeo kuwafikia wananchi kwa urahisi na kwa wakati. Vilevile, kufika kwa nishati ya umeme maeneo mengi vijijini kumebadili sura ya vijiji hivyo na hivyo kubadili maisha ya wanachi hao kwa kiasi kikubwa. Hii ni pamoja na kuimarika kwa mawasiliano ya simu ambayo yamefika katika vijiji vingi nchini.

280

Katika sekta ya elimu, hatua kubwa imepigwa kwani wanafunzi wanaojiunga na shule za sekondari wameongezeka kwa kiasi kikubwa na pia wengi sasa wanajiunga na elimu ya juu ikilinganishwa na hapo awali. Hii imetokana na jitihada zilizofanyika za kujenga shule mpya za kata na kuongezeka kwa vyuo vya elimu ya juu pamoja na kuongeza fedha za kuwakopesha wanafunzi wa elimu ya juu. Afya za wananchi pia zimeimarika, hususan kupungua kwa kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa malaria ambapo kiwango kimepungua kutoka asilimia 18 hadi 9 mwaka 2014. Hii imetokana na jitihada za Serikali za kugawa vyandarua vyenye viuatilifu na pia kunyunyuzia dawa ya ukoko katika baadhi ya mikoa.

Kwa kutazama mwelekeo mzuri wa ukuaji wa uchumi pamoja na hali ya utulivu na amani vilivyopo nchini, kuna matumaini makubwa kwamba Tanzania itazidi kusonga mbele kimaendeleo kwa kuongeza uwekezaji kwenye sekta za kipaumbele hali itakayowezesha kufikia lengo la kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025. Uwekezaji unaoendelea kufanywa na Serikali kwenye miundombinu ya msingi pamoja na sera nzuri za kuvutia Sekta Binafsi kuwekeza mitaji nchini vitaendelea kuwa muhimu katika miaka ijayo.  

281

Kwa ujumla, Serikali imetekeleza vizuri Ilani ya CCM ya mwaka 2005 na 2010 kwa kuzingatia Mwelekeo wa Sera za CCM zilizoweka misingi ya usawa, uwazi na maendeleo ya watu. Miradi mingi iliyoanzishwa ikiwemo ile iliyoanzishwa na Serikali zilizotanguliwa imekamishwa na utekelezaji wa miradi mingine ipo kwenya hatua mbalimbali. Miradi ambayo haijakamilika itaendelea kukamilishwa na Serikali ya Awamu ya Tano na ni wajibu wa kila mtanzania kuhakikisha kwamba anafanya kazi kwa bidii na maarifa ili kujiletea maendeleo kwani maendeleo ya kweli yanaletwa na watu kwa kushirikiana na viongozi wanaowachagua.

282

 Mungu Ibariki Afrika,

Mungu Ibariki Tanzania.

283

Na Jina la Mradi/Sehemu ilipo Eneo (Ha)

1 Mahiga (Kwimba) Mkoa wa Mwanza. 242 Ujenzi wa Bwawa na Mifereji na miundombinu ya mashambani kwa gharama ya Shilingi.

1,970,000,000.

2. Ilujamate (Misungwi), Mkoa wa Mwanza. 185 Ujenzi wa banio na Mifereji mkuu kwa gharama ya TShs. 220,000,000 kupitia mfuko wa PIDP/IFAD

3. Nyashidala (Misungwi), Mkoa wa Mwanza. 132 Ujenzi wa banio na Mifereji mkuu kwa gharama ya TShs. 220,000,000 kupitia mfuko wa PIDP/IFAD

4. Iwelyangula (Shinyanga mjini), Mkoa wa Shinyanga. 150 Ujenzi wa banio na Mifereji mkuu kwa gharama ya Shs. 480,000,000.

5. Mwamalili (Shinyanga mjini), Mkoa wa Shinyanga. 400 Ujenzi wa banio na Mifereji mkuu kwa gharama ya Shs. 487,000,000.

6. Irienyi (Lorya), Mkoa wa Mara. 80 Ukarabati na ujenzi wa mifereji ulianza kwa gharama ya Shs. 751,000,000.

7. Maliwanda (Bunda), Mkoa wa Mara. 90 Ujenzi wa bwawa na Mifereji na miundombinu ya shambani kwa gharama ya shs. 1,400,000,000.

Kiambatisho Na. 1: Skimu za Umwagiliaji zilizojengwa/Kukarabatiwa