101
1

Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

  • Upload
    others

  • View
    35

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

1

Page 2: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Order from:

E-mail: [email protected]: www.judeaharvest.info

2

Page 3: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

YaliyomoA UTANGULIZI 4

B MAMLAKA YA KIBIBLIA 5 -7

C THAMANI MUHIMU YA UJAZILIZAJI WA KUPANDIKIZA MAKANISA 8 - 13

D HATUA ZA UPANDIKIZAJI KANISA 14

1. Kuchagua Udongo (Utafiti) Mwitikio wa watu Utafiti Mashamba na Nguvu za kuvuna Ramani za Kiroho Ramani ya Soweto

141516192129

2. Kuuchimbua Udongo Kusudi la Maombi Maombi ya Kutembea

303133

3. Kupanda mbegu (Kupanda Kanisa) Kanisa la nyumbani Mikutano ya Injili (yenye lengo la kupanda makanisa) Uinjilisti wa nyumba kwa nyumba Filamu ya maisha ya Yesu Miundo ya upandaji kanisa

404145454546

4. Kutia mbolea kwenye udongo Kufundisha mafundisho ya msingi Toka uanafunzi hadi Uongozi Kupambana na vizuizi vya kiroho

47484850

5. Kuumwagilia maji udongo Utendajikazi wa Roho Kufundisha Chakula kigumu cha Neno Kuwapa Zana viongoz Mafunzo ya Uongozi Uwanja wa Mungu wa Mafunzo Kujifunza lugha ya Roho Mtakatifu

51525252535354

6. Kuyaondoa Magugu Kuvielewa vita vya Kiroho Kupambana na ngome katika kanisa Kupambana na ngome za Mahusiano

56575860

7. Kujiandaa kwa Mavuno Eneo la Kupewa zana Kuzidishwa Kuwa katika mwenendo wa Upandaji wa Makanisa

65666667

E Sifa za Mpanda Makanisa Awe na huruma kwa waliopotea Awe na ufahamu wa Kiufalme Awe na Maono Awapende watu, awe tayari kujidhabihu na kupata msaada wa kifamilia Awe na moyo wa kiutumishi, Bidii katika kazi, Mwaminifu na Mnyenyekevu

697070707172

F VIKWAZO VYA KUEPUKA 77

3

Page 4: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

UtanguliziBaada ya miaka ishirini ya uchunguzi na baada ya kuhusika kupandikiza makanisa 38 katika wakati wote huu, nimekutana mara nyingi sana na swali hili, “Mtu anawazaje kupandikiza kanisa?” Sijawahi vya kutosha kuwa na ufahamu wa kina kuandika kitu katika swala hili lakini hivi karibuni Bwana amenipa mzigo moyoni kuwashirikisha mambo kadhaa ya ujuzi wangu katika swala hili, kuhusu katika mandhari ya kiafrica.

Asubuhi ya leo wakati wa kufungua kinywa nikiwambia familia yangu juu ya jarida jipya la mafunzo ambalonaliandika juu ya upandikizaji kanisa. Kijana wangu wa miaka kumi na miwili, Dannie Jr. akasema, “Lakini Baba, hivi muhimu kweli? Nijambo la kawaida tu! unachofanya ni kupata watu wachache waliookolewa na kujenga jengo na hivyo tayari umesha maliza” Baada ya majibizano kidogo yasiyohaja kutamkwa nikamwambia “ Sawa kabisa kijana wangu, nilakawaida kimsingi.Nijambo la kimsingi kwa wanandoa kuwa na watoto na kama tu mwili wa Kristo basi liwe jambo la msingi kwa huu ‘’Mwili” kujizalia’’ kwa kujivuna sana akasema ‘’ Cha mno nini hapo’’ maelezo yangu yalimtosha niliposema, ‘’Mwanangu, tuseme engekuwa hujui ukweli kwamba siku moja, unapokuwa umeoa, unaweza kuzaa, ungefanya hivyo?’’

Makanisa mengi hayajui kwamba ni jambo la kimsingi kwamba wazaliane wenyewe kama makanisa na ndio maana nahisi ule uharaka wa kuandika jarida hili’’ Nataka kila Mchungaji na kila kanisa kujua kwamba huhitaji kipawa maalum kupandikiza kanisa jipya. Ni jambo la asili!Naamini nitawezakuweka msingi wa kushawishika kwangu toka kwenye maandiko kukusaidia kuelewa kwamba sio wazo jema tu bali ni msingi wa kibiblia wa kutimiza Agizo kuu katika Mathayo 28:19. Mimi si mwana Thiolojia lakini naamini kwa moyo wangu wote kuwa lazima iwe ni moyo na maono ya Baba yatakayotuhamasisha na kutusukuma kuimalizakazi ambayo ametupa.

Iwapo hatuushiriki moyo wake kwa waliopotea tutaendelea kujenga makanisa ambayo yana mtazamo wa ndani na kutumia hazina zetu kwa wale ambao wameishaokolewa wakipasha moto viti, hatutatumia nguvu zisizo na ukomo, “Kuwaburudisha ili kwamba warudi tena jumapili ijayo kujipatia mengi zaidi. Katika makanisa ya namna hiyo umisheni na uinjilisti ni mambo yanayo tokea nje ya kanisa na kuongozwa na wachache wanaojihisi kuitwa katika jukumu hilo, lakini walio wengi wapo tu kwaajili ya ‘’Maonyesho’’

Baada ya kuwepo katika nchi zaidi ya 23 na kuhubiri katika mamia ya makanisa, lazima nikubali kuwa kuna yaliyokuwa yanastahili kuchukuliwa kipekee mbali nasheria. Yapo makanisa na huduma duniani pote ambazo zinaongezeka kwa kiasi sana, wakipandikiza makanisa mahali yasipokuwapo, wengine jamii zao katika miji na mataifa.

Kanisa lako linaweza kuwa mojawapo kama Dannie Jr alivyosema, ‘’Nijambo la kawaida kimsingi!’’ Kaa nami kwa muda na nitakuhakikishia kuwa mwishowe utakubali.:‘’Ni la kawaida kimsingi’’

DANIE VERMEULEN

4

Page 5: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Msingi Wa Kibiblia Waupandikizaji Makanisa Kwa Kujaziliza

“Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha… Mwanzo 1:28

Kabla ya kuuweka msingi wa Kibiblia wa kupandikiza kanisa, lazima tulijibu swali hili wenyewe “Nini maono ya Baba kwa dunia?’’ Pindi tunapokuwa na upeo fulani wa uelewa wa moyo wa Baba kwa dunia iliyopotea, tutaanza kukubali mikakati yake.

AGIZO LA ADAMU NA HAWA.Adam na hawa viumbe wa mfano wake, wakijawa na utukufu wake, wakiasi haki yake, waliagizwa kwa amri ya sentensi moja: “Zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha”…

Waliumbwa na uzazi wa asili kulingana na maumbile yao.Walitarjiwa kutumia uzazi wao, ili kwamba kule kuijaza nchi kuwepo. Huu ulikuwa ndio mwanzo wa dunia iliyojaa watu wa aina ya Mungu- kizazi cha wanadamu kilicho na ushirika wa daima na Muumba wao- ufalme utakaoitawala dunia ya wanyama.

Mungu hakuwa na nia ya kuongeza kizazi hiki kwa kuendelea kuumba yeye zaidi, bali alichagua kwamba wajizidishe wao wenyewe. Hii inaonyesha kuzidisha kwa kurithiana kile ambacho amekiumba kwa mfano wake, akimpa mwanadamu ile raha ya kuumba pamoja na Mungu, kupitia uwezo wa asili uliowekwa ndani yake, mpaka hivi leo, kila mzazi anajawa na mshangao wakati kuzaliwa mtoto. Lile wazo la kuwa na sehemu katika uumbaji huu wa ajabu linastaajabisha mno.

Maono ya Baba yalikuwa kwamba kupanuka kwa kizazi cha wanadamu kulete kule kuijaza nchi. Maono yalikuwa dunia iliyojaa watu wenye kuudhihirisha utukufu wa Mungu, wakiishi katika hali ya haki kamilifu na wakifurahia uhusiano wa kina na Baba.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kuwa Adam wa kwanza alishindwa kupitia anguko la dhambi na hivyo kizazi chote cha wanadamu kikaanguka katika mzunguko wa kurithi dhambi na mauti. Je, hiyo ilibadili moyo wa Baba kwa dunia?La hasha. Tokea wakati Mungu alipotangaza “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke na kati ya uzao wako na uzao wake, huo utakuponda kichwa na wewe utauponda kisigino. (Mwanzo 3:15), Baba aliweka mpango wa ukombozi ambao ulimuhukumu shetani kushindwa. Mara tangazo hilo la mbinguni likatoa mwanga katika umilele wote, likitamka ahadi ya Adam wa Mwisho ambaye atakiponda kichwa cha shetani.

AGIZO LA ADAM WA MWISHOSasa hili linahusika vipi na upandikizaji wa kanisa? Hebu mruhusu Adam wa mwisho alipambanue. Alilichukua agizo la Adam wa kwanza kurejesha kila kitu ambacho Baba

5

Page 6: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

alikuwa nacho mwanzoni kwa ajili yetu (Matendo 3:21), Maono ya Baba ni kuona watu wote wanaokolewa na kupata kuijua kweli yote. Kristo Adam wa mwisho aliyekuja atukomboe toka katika vifungu vya dhambi na mauti. Alirejesha haki kwa kufanyika haki yetu. Alikuja kuusimika ufalme wa Mungu haka duniani kama ulivyo mbinguni.

“Zaeni ………”Agizo kwa Adam wa kwanza lilikuwa “Zaeni …..” Imeandikwa juu ya Adama wa mwisho kwamba “Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote” (Kolosai 1:15) “Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani cha kanisa naye ni mwanzo ni mzaliwa wa kwanza katika watu …(Kolosai 1: 18). Yesu anaonyesha kuzaa kwake kupitia mwili wake – kanisa. Kama vile Adam wa kwanza alivyofanywa kuzaa na kuongeza uzao wa mwanadam, kadhalika Adam wa mwisho amefanywa kuzaa na kuongeza mwili wake (Kanisa) ulimwenguni pote. Alisema “….Nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda” ( Mathayo 16:18).

Nabii Habakuki aliyatangaza maono ya Baba kwa ajili ya nchi aliposema “Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa Bwana, kama maji yaifunikavyo bahari”. (Habakuki 2:14) Baba atafanyaje haya isipokuwa imefanyika kupitia Bibi Arusi wake, Kanisa? Kanisa ndio lenye kuakisi na kuubeba utukufu wake. katika waraka wake kwa wakorintho anasema “Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano huo huo, toka utukufu hata utukufu, vile utukufu utakao kwa Bwana, aliye Roho” (2Korintho 3:18)

“……..mkaongezeke”Adam wa mwisho anatimiza maono ya Baba kupitia kulizidisha kanisa lake duniani pote. kupitia kuzaliana huku dunia inapokea ufahamu wa utukufu wa Bwana. Kanisa linapo ongezeka, linaleta uwepo wa mwili wake Kristo katika jamii.

Kama hii ni kweli basi upandikizaji wa makanisa wapaswa kuwa matokeo ya maisha kiasili ya kanisa, kama vile kuzaa kulivyo matokeo ya kiasili ya mahusiano ya ndoa.Stuart Murray anaandika, “Kazi ya upandikizaji makanisa yaweza kuhamasisha hitimisho kuwa, kuzaliana ni tabia ya msingi kama ilivyo kwa kiumbe yoyote kibaiolojia. Kanisa lenye afya haliendelei kwa ndani tu na kupanuka ukubwa wake na mguso wake kwa jamii, bali kiasili linaelezea uhai wake kwa upya wa muundo na maumbile.”1

Ellis na Mitchell wanasema, “Kama lipo kanisa ambalo halijafikiri juu ya kuzaliana …..wala halitarajii wala kutazamia kuwa hii ndiyo hali ya asili ya ukuaji, basi kanisa hilo ni tasa”2. Je, twende mbali zaidi na tuseme kwamba makanisa ambayo hayajihusishi na namna ya upandikizaji makanisa na yanabakia hivyo hivyo kwa miaka kadhaa, yaitwe pengine yasiyo ya kawaida? kama stuart Murray asemavyo, “ Pengine ingekuwa vema kuchukulia kuzalianakupitia upandikizaji wa kanisa kuwa kawaida, na kudumu kwa maadili ya miundo ya kidhehebu kwa zaidi yavizazi kadhaa, kutokuwa kawaida na tatizo.”3

KUONGEZEKA KWA KANISA KATIKA AGANO JIPYA.Iwapo kanisa ni mwili basi lina vichocheo “DNA” vyote muhimu ili kuzaliana. Tunaweza kusema kuwa Yerusalem na Antiokia yalikuwa makanisa ‘’Mama”.

1 Murray, Stuart: Church Planting, Laying foundations (Paternoster Press 1998) pp: 57, 582 Ellis, Roger & Mitchell Roger: Radical Church Planting (Cambridge: Crossway, 1992) p: 733 Murray, Stuart: p 59

6

Page 7: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Japokuwa mfano mzuri ni lile kanisa la Antiokia kupitia upandikizaji makanisa wa Barnaba na zaidi sana Paulo, makanisa yalizaliwa kutoka kanisa moja la mahali. Uzito wa huduma ya Paulo ulikuwa kanisa – huduma yake ilizaa kanisa lakini alitarajia bila ya shaka kuzidishwa kwa kanisa kuwepo.

7

Page 8: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Anamuandikia Timotheo, “Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo utawakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine” (2Timotheo 2:2) Hayakuwa matarajio tu ya Paulo bali katika sehemu kadhaa wa kadhaa ilitokea. Ilitokea huko Thesalonike (1Thesalonike 1:8)-Epafra alianzisha kanisa huko kolosai (Wakolosai 1: 7) na mtu mwingine alianzisha kanisa huko Loadikia (Wakolosai 2:1).

Jon Haley anasema, “Kwa Paulo, uaminifu kwa Agizo kuu ulimaanisha zaidi kuliko kuhubiri jumbe za kiuinjilisti hapa na pale.Ilimaanisha mfululizo wa majukumu ambayo yataleta ukomavu wa kanisa. Tunaweza kusema bila kuzidisha swala zima kuwa, kwa Paulo “Kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi “ (Mathayo 28:19) kulihusisha kupandikiza makanisa.“4

UFALME WA MUNGU UNAKUA KUPITIA KUONGEZEKA KWA KANISA

“….Mkaijaze nchi, na kuitiisha ….”Kristo, Adam wa mwisho alitangaza ufalme mpya (Mathayo 4:17).Maono ya baba kwa watu wake “kuijaza nchi na kuitiisha….”Yalidhihirika wazi katika maneno na huduma ya Yesu. Kuna “Kuijaza nchi” katika maandiko yafuatayo:

“Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu,jina lake Yohana. Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili ashuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.” (Yohana 1:6, 7) (NIV)

“Basi “Nami, nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu” (Yohana 12:32) (NIV)

“Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu mwokozi, mtu ambaye hutaka watu wote waokolewe na kupata kujua yaliyo kweli.” (1Timotheo 2:2) (NIV).

“Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote hapo ndiopo ule mwisho utakapokuja”. (Mathayo 24:14).(NIV)

“Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi …..”(Mathayo 28:19) (NIV)

“…..Ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii imani” (Warumi 16:25).

Hotuba ya kwanza ya Bwana Yesu ilikuwa kuutangaza ufalme mpya (Mathayo 3:2). Alisema atalijenga kanisa lake na kwamba milango ya kuzimu haitalishinda. Tunaweza kusema kwa hivyo, kuwa huu ufalme mpya umeundwa na makanisa, ya kwamba ataushinda ufalme wa giza, kuupenyeza na kuwakomboa walio kifungoni kupitia kanisa lake (Kolosai 1:18, Efeso 3:10-11, Warumi 5:17).

Pale nuru inapowaka giza hutoweka, wakati kanisa limepandwa kati ya jamii, ufalme wa Mungu umewadia katika jamii hiyo-nguvu iliyokinyume na ufalme wa giza lina maono ya kutimiliza utume wa Adam wa mwisho,…..kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi” (Yohana 3:8).(NIV)

Na-malizia kwa maneno ya Dk. C. Peter wagner. “Njia moja kubwa yenye ufanisi ya uinjilisti chini ya mbingu ni kupandikiza makanisa mapya.“5

4 Haley, Jon: Toward a Biblical Theology of Church Multiplication, p. 55 Wagner, C. Peter: Church Planting for a greater harvest, Regal Books p11

8

Page 9: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

THAMANI MUHIMU YA UJALIZAJI WA KUPANDIKIZA MAKANISA

KUJAZILIZA KUPANDIKIZA MAKANISA NI NINI?Kwa “kujaziliza “ tuna maana ni huduma ya kanisa kwa ajili ya kumfikia “kila mtu ‘’ “Yeyote “ na “wowote” kama ilivyoelezwa katika 1Timotheo 2 Petro. Vifungu hivi vina weka wazi kuwa Mungu anamtaka kila mtu, mwanaume na mwanamkena watoto kuisikia na kuilewa injilina kupata fursa ya kuamini na kutii kikamilifu kwa Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wao. sehemu muhimu pale ambapo Neno la Mungu linafundishwa na kuaminiwa.

Kupandikiza makanisa kwa kujaziliza (KMK) ni kibiblia hasa ni kulitimiza Agizo kuu, kwa namna ambayo kila mtu mwanaume, mwanamke au mtoto ana nafasi kukubali au kukataa injili kupitia ushuhudiaji wa kanisa la mahali. KMK ndiyo maono, mkakati na huduma ya kuyajaza mataifa, mikoa, miji, vijiji na ujirani kwa makanisa ambayo yataichukua injili kwa kila mtu katika lugha yake na kupitia utamaduni wao.

KUPANDIKIZA MAKANISA KUNAVUNJA NA KUVIPITA VIZUIZINionyeshe dhehebu linaloanguka, nitakuonyesha dhehebu lisilo na maono ya upandikizaji wa makanisa, nionyeshe nchi ambayo idadi yake ya wakristo haiongezeki au inapungua nami nitakuonyesha madhehebu ndani yake yasiyo na maono ya upandikizaji wa makanisa. Ni jambo la kutafakari, na bado kuna nchi kadhaa ambazo zinaonyesha ukuaji mkubwa wa uinjilisti tokea madhehebu na vikundi vya makanisa vilipokaa na kuazimia malengo maalum ya kitaifa ya kupandikiza makanisa. mifano ya nchi kama hizi ni Ufilipino, China,Brazil(hakika sehemu kubwa ya nchi za Amerika ya kilatini (Latin amerika) Ghana na Zimbabwe. katika kila bara la dunia hii kuna mashirika ya upandikizaji makanisa yanayovunja mipaka na vikwazo vya upinzani wa giza, na kuleta utukufu wa Bwana, uwepo halisi wa Kristo katika jamii zao mbali mbali.

Jim Montgomery. Mwanzilishi na Rais wa huduma ya Dawn, pengine ndiye mtu mwenye ufahamu mkubwa zaidi wa jambo hilo. Alifanya sehemu na muhimu katikia kuendeleza mkakati nyeti katika nchi ya Ufilipino katika miaka ya mwanzoni ya 1970 ambayo ingebadilisha Ufilipino milele. Mwaka 1974 ambapo karibu makanisa 75 na viongozi wa umisheni walijitoa kwa ajili ya lengo maalum kwa kila kijiji kuwa kanisa ifikapo AD 2000, Shirika hilo lilizaliwa likiitwa DAWN- kifupi cha Discpling a Whole Nation, yaani kufanya Taifa zima kuwa wanafunzi. Kwa nchi ya Ufilipino ilimaanisha kukua toka makanisa 5,000 hadi 50,000 katika miaka 26 tu 266!

February 2001 watakuwa wanaadhimisha – upandaji wa makanisa 50,000 katika miaka 26! Imetia mguso mkubwa nchini Ufilipino! Walijizalia tene na tena madhehebu mengi yalionyesha ukuaji na wakapita ukuaji wa makanisa mengi katika nchi zingine ulimwenguni, kwa nini? Walikuwa na maono ya kujaziliza makanisa katika kila (mahala jirani).

KUPANDA MAKANISA KWA KUJAZILIZA.

6 Montgomery, Jim: DAWN 2000, 7 million churches to go, Highland Books – p 34

9

Page 10: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Kupanda makanisa kwa kujaziliza ni maono yanayolenga katika kuhusisha Mwili mzima wa Kristo katika eneo husika,ama jiji au jimbo au nchi , kupanda kanisa mahali ambapo ni rahisi kufikia yeyote, ili kuweza kufanya Taifa kuwa wanafunzi (Mathayo 28:15) katika hatua hii lazima nieleze wazi kuwa agizo la Yesu kwetu halikuwa kufanya wanafunzi katika mataifa bali kufanya mataifa yote kuwa wanafunzi. Haya ni maono ya Taifa zima. Hivyo kuhusisha mwili mzima wa Kristo ni muhimu sana!

KWANINI KUPANDIKIZA MAKANISA KWA KUJAZILIZA?Zipo sababu kadhaa zaidi kuliko za msingi wa kibiblia, kwa nini kupandikiza kanisa kwa kujaziliza ndiyo njia bora ya uinjilisti, Hebu tuangalie baadhi.

1. Makanisa mapya hukua haraka kuliko ya ZamaniNikwanini makanisa mapya hukua kwa haraka zaidi kuliko yale ya zamani? Kwasababu uinjilisti ndio shughuli yao kubwa. Hupenya kuingia kaya mpya za ndugu na marafiki na kama kuna jengo , basi ule upya unaonekana zaidi, kitu kipya kinaonekana. Kadhalika ukumbuke kuwa ni rahisi kuzaa kuliko kufufua wafu.

2. Upandikizaji wa Makanisa huleta uhai mpya na afya kwenye KanisaMtoto mchanga analeta furaha kubwa nyumbani. Kanisa la kibaptisti la Kawil-huko Ufilipino lilipandwa mwaka 1986 na kufikia kilele cha mahudhurio 50, Mchungaji Armandela Merced alipo wasili hapo mnamo mwaka 1993 Kanisa lilikua limepungua kufikia washirika 8 tu! Pastor Arman akijua ni rahisi zaidi kuzaa kuliko kufufua wafu. Alilitumia lakelinalokufa kupanda kanisa jipya. Kwa kipindi cha miezi 6 walifanikiwa kupanda kanisa katika eneo la Imus lenye washirika 60! Palikuwa na mwitikio mkubwa huko Imus. lakini jambo la kushangaza ni kuwa kupitia kuzaa uamsho ukaja katika kanisa la Kawit. Washirika wakaongezeka hadi idadi ya kushangaza 96!

3. Makanisa ya aina mbalimbali yanahitajikaMakanisa yako kama watu, nayo yanamionekano tofauti. Mara nyingi muonekano wa kanisa hutegemea Mchungaji mwenyewe. Misukumo ya kitheolojia nayo huchangia na mara nyingi ndiyo hupanga Litrojia katika ibada, Mungu, kwa hekima yake isiyo na ukomo,aliumba namna mbalimbali za mionekano hiyo kiasi kwamba inakuwa vigumu kwa kusema” siwezi kupata Kanisa litakalo nifaa”. Tunahitaji kupanda makanisa mengi zaidi ambayo yatakuwa na watu wa namna mbalimbali.

Ni muhimu vile vile kutamka hapa kwamba tunahitaji makanisa ambayo yatashughulikia mahitaji ya vijana. Wanahitaji mahali ambapo watakuwa sawia na huru katika Inaeleweka vizuri kwamba kanisa la mtindo wa kizazi cha mwisho hautavutia kizazi hiki kipya.

4. Kupandikiza Kanisa hujenga viongozi wapyaPeter Wagner anasema “Makanisa mengi wamethibitisha ukweli kuwa kigezo muhimu sana kwa ukuaji na kupanuka kwa kanisa ni uongozi…kwa sehemu kubwa, makanisa yaliyopo bila ya kujua yameweka kizuizi kwa mashemasi na viongozi wa kawaida na matokeo yake ni kuwa kupanda juu kwa watu wapya katika nafasi za uongozi kwenye huduma ni vigumu. Lakini makanisa mapya yanafungua kwa upana mkubwa milango ya uongozi na changamoto za huduma na hatimaye mwili wote wa Kristo unanufaika”7

5. Kupandikiza Makanisa husaidia kudumu kwa madhehebuKatika kitabu chake “ Mavuno makuu kwa upandikizaji makanisa” Peter Wagner anasema hivi”Bila kubagua, makanisa yakuayo yamekuwa yale yanayosisitiza

7 Wagner, C. Peter: Planting churches for a greater harvest, Regal Books – p. 20

10

Page 11: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

upandikizaji wa makanisa” Madhehebu mengi yanazungumza juu ya ukuaji wa kanisa na wana nia ya kupandikiza makanisa, lakini hapo tu ndipo wanapofikia hawana mpango wala mkakati na kwa kawaida huwa na kiburi mno kuomba msaada popote. Katika Africa kusini, matukio ya kushangaza yametokea, ambayo mimi naamini yatakuwa na mguso kwa taifa hili. Dk. Isak Burger mwongozaji wa Apostolic faith Mission, anaunda mpango wa ukuaji kupitia upandikizaji makanisa nakwa namna yoyote ile ni dhehebu linalohusika!

Umoja wa kibaptisti nao pia wa maono halisi, Fungamano la Makanisa ya nyumbani katika Africa ya kusini, liliongezwa na Mchungaji Harold Weitsz, hivi sasa anaandika juu ya upandikizaji wa makanisa katika makabrasha yao na amewaomba Dawn Africa kuwasaidia katika eneo hili, lakini haya ni makundi yakuayo, Je, vipi kuhusu anguko hili? unaweza kufanya kile ambacho kanisa la Uingereza limefanya. Waliingia katika mradi wa Dawn na baada ya miaka 20 ya kushuka, sasa wanaonyesha ukuaji mkubwa.

6. Upandikizaji wa Makanisa ndiyo nyanja bora ya Uinjilisti kwa TaifaUchunguzi wa ukuaji wa kanisa katika nchi ya Peru umeonyesha ugunduzi wa kustusha, wameweka lengo la makanisa elfu hamsini (50,000) hadi kufikia mwaka 2003. Hiyo ilimaanisha makanisa mapya 6 kila siku! lakini hebu angalia,Mwaka 1989 walikuwa na makanisa 5,574 na idadi hiyo ikaongezeka hadi 12,915 mwaka 1995 – Wastani wa ukuaji kwa mwaka wa 15.03%. Mwaka 1989 walikuwa na washirika 750,000 katika makanisa yao idadi hii ikakua hadi kufikia 2,189,345 mwaka 1995 Wastani wa ukuaji kwa mwaka wa 19.55%! Hitimisho ni kuwa ukuaji wa washirika ni waharaka kunapokuwa na upandikizaji wa makanisa.

11

Page 12: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Sijui mbinu nyingine ambayo yaweza kuleta mguso mkubwa katika Taifa! Kama kanisa la Ufilipino singeliingia katika mpango wa Dawn wangelikuwa wamepanda makanisa 17,778 tu (yale yaliyokadiriwa) hadi mwaka 2000 badala ya 50,000!

7 Makanisa mapya yanaweza kayaamasisha yaliyopo.

Ni jambo la kusikitisha kwamba mara nyingi kunapokuwa na kanisa kubwa jipya lenye nguvu linaanza kati ya jamii ambapo yapo makanisa mengine, mara nyingi kunakuwa na uadui dhidi ya lile kanisa jipya, Wachungaji wanaogopa kupoteza washarika kwa kanisa jipya. Ushauri wangu kwa Wachungaji ni huu: Endelea kuotesha majani mabichi kanisani na kondoo hawatapotea.

Makanisa ya zamani ambayo yamedumaa mara nyingi hupata “Changamoto toka kwa yale mapya katika kuwajali washarika wao zaidi na kuwaangalia vizuri zaidi, Makanisa mapya huongeza kiwango cha hali ya Kiroho.

Kanuni ya muhimu kwa jamii yoyote yenye kanisa zaidi ya moja ni kujiona wote kuwa sehemu kundi ambalo Kristo ameliita ili “Kuziharibu kazi za yule mwovu” (1Yoh, 3:8) Pindi ambapo Mchungaji anaweza kuomba watendakazi wengi zaidi waje kwenye uwanja wa mavuno anapofanyia yeye kazi, hakika amekuwa mhudumu wa kweli wa Ufalme wa Mungu.

8. Upandikizaji wa Makanisa utaleta Ufalme mpya na huruma kwa waliopotea.Ni vigumu kuamini kwamba makanisa mengi hutumia hazina zao 90% kwa wale ambao tayari wameokolewa, Kanisa la kawaida tu hutumia angalau 90% ya fedha zake kwa washarika wake ambaowameshasikia Injili tana na tena. Mchungaji wa kawaida anatumia asilimia 90% ya muda wake kwa washarika ambao wameshaokolewa.

Tunaweza tukaendelea zaidi na zaidi. Nakanisa yanadumaa yanapokuwa yanajijali zaidi kwa ndani maisha yao ya kikanisa, wakati yanapoelemewa na mahitaji na shida zao tu. Makanisa ya namna hiyo yanapoteza maono na yanaangukia kwenye “Udini” badala ya kuwa wafisaji na watendaji katika Ufalme wa Mungu.

Nalipokuwa mtoto nilangalia wafanyakazi wa mashamba siku ya jumapili mchana wakikusanya mbwa wao kwenda kuwinda sungura. Wakati palikuwa hapana sungura wa kukamata hawa mbwa walibwekeana na kuumana, lakini punde tu sungura alipoonekana walisahauliana na wakaenda kumkamata na kumua sungura. Kadhalika ndani ya kanisa kunapokuwa hakuna maono kwa waliopotea, washarika wataanza kuumana na kubwekeana. Baada ya miaka ishirini na mbili ya huduma ya Uchungaji nimetambua huu ukweli kuwa halisi.

12

Page 13: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Wakati kanisa linapo husika na upandikizaji wa makanisa, huruma na shauku mpya kwa waliopotea itakuwa dhahiri, Ni kama mama akizaa mtoto mwingine.

9. Upandikizaji utaleta Maono ya dunia katika Kanisa.Mara nyingi, Wakristo wanajificha kwenye kuta za kanisa, wanaambiwa wasi “Changamane na dunia” na hata wanaogopa kusoma magazeti ya kidunia na vitabu vingine. Inasikitisha, tunahitaji kujua kinachoendelea katika dunia tunamoishi.

Wapo maelfu ya wakristo ambao hawajui chochote juu ya wasio fikiwa hapa duniani, juu ya Dirisha 10/40 au upotevu wa kizazi x! Makanisa yanayojihusisha na upandikizaji wa makanisa daima huwatafuta wale wasio na kanisa, wasio fikiwa na walio sahauliwa. Ni hapo ndipo macho yao sasa yanapo funguliwa na wanayatambua mavuno.

Ninahamasika mno ninaposikia makanisa ambayo hupandikiza makanisa katika jamii za mila tofauti, wakifanya juhudi kuifikia “Miisho ya nchi”. Moja ya nyakati za kusisimua sana za maisha yangu kama Mchungaji ilikuwa ni pale nilipohusika na upandikizaji wa makanisa katika nchi ya Malawi kwenye kabila la Wayao, jamii isiyofikiwa umbali wa Km. 2300 tokea Kanisani kwangu Afrika ya Kusini. Washarika wangu wallijijengea maono ya kiulimwengu!

10. Upandikizaji Makanisa husisitiza kanuni ya kupanda na kuvuna.Ni kanuni ya kibiblia kuwa “chochote apandacho mtu ndicho atakacho vuna” (Wagalatia 6:7) Iwapo tunazungumzia “Kupanda” basi bilashaka pia tunazungumzia “Kuvuna”. Tunapowekeza fedha katika upandaji kanisa tunahitaji kutarajia mavuno ya kifedha kwa kupandikiza kanisa, kama tukipanda kwa kuwekeza watu tabiri kwamba tutavuna nini?

HATUA ZA VITENDOIwapo Taifa litaingia katika upandikizaji kanisa kwa kujaziliza, basi mkakati wa aina ya Dawn ni muhimu. Jim Montgomery8 anatoa vidokezo 12 kwa ajili ya mkakati wa Dawn. Anasema “Ni mkakati ambao :

1. Una msingi katika Kristo katika msisitizo wake wa kuona kuwa amefanyika kuwa sehemu ya kila jamii ya watu 500 hadi 1000 duniani.

2. Umejengwa katika mpango madhubuti wa Mungu ambaye hapendi awaye yote apotee.

3. Umelenga katika kuitamalaki nchi kimpangilio.

4. Huchukua manufaa ya viwango vya kihisia na kiutendaji vya nchi nzima.

5. Huitambua ile nguvu kuu ya ajabu iliyo katika taarifa.

6. Hutoa ujumbe wa kinabii kwa kanisa..

7. Hukusanya nguvu kuu zilizopo ilikufanyia kazi lengo linalo pimika na lenye mpaka wa muda.

8. Husisitiza mbinu iliyobora chini ya mbingu.

8 Montgomery, Jim: DAWN 2000, 7 million churches to go, Highland Books – p. 170

13

Page 14: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

9. Husaidia mwili wa Kristo kutendakazi kama mwili:

10. Hutia moyo masharika ya kikanisa kufanyakazi “bega kwa bega”

11. Hutoa muundo wa rejea kwa ajili ya mikakati ya kitaifa na kimataifa kwa ajili ya kufanya mataifa kuwa wanafunzi.Kila moja ya vidokezo hivi 11 kina nguvu, vinapowekwa pamoja katika namna ya mfanano, hazina yake ni kubwa mno kuliko inavyoweza kueleweka.

JINSI YA UPANDIKIZAJI KANISA KWA KUJAZILIZA UTENDAVYO KAZIDk. Murry Moerman, akitwaa toka kwa Montgomery, anafanya taswira ya jinsi ambavyo upandikizaji makanisa kwa kujaziliza unavyofanyakazi, unavyotofautiana kutoka Taifa hadi Taifa na pia hali na hali ya kimazingira na pamoja na hayo vidokezo kadhaa ni vya muhimu:

Mtu au kundi la watu wenye shauku ya kuifikia nchi yao kama alivyo kuwa John Knox wa Scotland, ambaye alimlilia Mungu akisema “Nipe Scotland au nife!”

Kamati ya uwakilishi ya kitaifa ambayo inatendakazi kwa kuyashiriki maono na kuwa tayari kutoa hazina za kibinafsi na hata kishirika kuongoza hatua hizi rahisi kabisa.

Kukusanya na kurejea upya taarifa muhimu zinahusiana na jeshi la wavunaji na uwanja wa mavuno katika nchi, katika hili kwa weza kupatikana “ujumbe wa kinabii, “Jinsi Mungu anavyoliona kanisa lake katika Taifa na nini anachosema kwa watu wake.

Mikutano ya mara kwa mara ya kitaifa na kimkoa kwa viongozi kutafakari kile ambacho Mungu anaweza kuwa amesema na jinsi ambavyo kila dhehebu linaweza kuitikia kile ambacho Mungu amekusudia kukikamilisha, Mikutano hii mara nyingi imeitwa “Makongamano” kusisitiza eneo muhimu la kufanya maamuzi yatokanayo na mwitikio. Malengo yatawekwa na kufikiwa upya, maaendeleo kuadhimishwa, maombi kwa ajili ya uamsho kuhuishwa na kujitoa upya kufanyika.

Kujitoa kuendelea na kazi mpaka Yesu arudi: Kuhamasika na kuanzisha maombi, kuratibu jeshi la uvunaji na maendeleo ya uvunaji katika eneo husika, kusambaza taarifa, matangazo na makongamano na kushirikishana miundo na rasilimali za upandikizaji makanisa.

14

Page 15: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

15

HATUA ZA

UPANDIKIZAJI

WA MAKANISA

1. Kuchagua Udongo

- Utafiti -

Page 16: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

1. KUCHAGUA UDONGO

1 Wakorintho 3:6-10“Mimi nilipanda, Apollo akatia maji: bali mwenye kukuza ni Mungu, 7. Hivyo apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. 8. Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake sawasawa na taabu yake mwenyewe. Maana sisi tu wafanyakazi pamoja na Mungu ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la mungu.10. Kwa kadiri ya neema ya Mungu uliyopewa, mimi kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi na mtu mwingine anajenga juu yake, lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.

Kwakua Paulo alitumia lugha ya kikulima kuelezea kuzaliwa kwa kanisa lilikuwa Korintho,mimi nitatumia lugha hiyo ya kilimo pia.Kadhalika ni lugha mwafaka katika Afrika.Tunazielewa vema hatua za kilimo.

1. 1. Tafuta udongo wenye rutuba – Mwitikio wa watu.Mkulima yeyote ambaye anataka kupanda mbegu itakayotoa mavuno mazuri kwanza anachagua udongo vizuri kwa uangalifu mkubwa. Aina fulani za udongo hazifai kabisa kwa ajili ya kilimo. Katika hatua za upandikizaji wa kanisa ni muhimu kwanza kuangalia mwitikio wa watu. Sisemi kwamba iwapo watu watakosa mwitikio mzuri basi waachwe tu. Vinginevyo, upo wakati ulio mwafaka ambapo kijiji fulani, eneo jirani au hata watu binafsi wanamwitikio kwa sababu mbalimbali.

1. 2. UtafitiNi muhimu kuwa utafiti ufanyike kwenye udongo husika ila kwamba ujue ni aina gani ya zao latakalo faa, kwa udongo huo husika. Hii ndiyo habari ya utafiti, utafiti ni hatua ya kukusanya taarifa zinazo turuhusu kutathmini na kupima jukumu husika na kuweka malengo, mipango na kipaumbele cha upandikizaji wa makanisa ni muhimu kwamba, kwanza mpandaji afanye utafiti wenye nyanja tatu:

Eneo la Mavuno.Utambulisho, mahali, maelezo na hali ya watu, ikijumuisha makundi yote ya kimbari, kilugha na kijamii katika kila jamii ya mji husika.

Nguvu ya UvunajiUtambulisho, mahali, maelezo na hali ya madhehebu yote, makutaniko ya mahali, mawakala wa umisheni na mashirika ya kikanisa.

Ramani ya Kiroho (Kazi za mapepo)Uchoraji wa ramani ya Kiroho ni kuutafiti mji ili kugundua kila vipenyo ambavyo shetani amevifanya, ambavyo vinazuia uenezaji wa injili na uinjilisti wa mji kwa ajili ya Kristo. Lazima tujifunze kuiona dunia kama jinsi ilivyo, na wala si kama inavyoonekana tu, kuchora ramani ya Kiroho kunahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulingo wa Kiroho kwenye sehemu na mazingira katika dunia yenyewe halisi. Ni njia ambayo kwayo twaweza kuona kilichopo uvunguni mwa dunia inayoonekana kimwili.

16

Page 17: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

UTAFITI

MaanaNi hatua ya kukusanya taarifa ambazo zinaturuhusu kutathmini na kupima jukumu na kuweka malengo, mipango na kipaumbele kwa ajili ya kulitimiza Agizo kuu.

KUNA HEKIMA KATIKA KUWA NA TAARIFA.Sulemani pia ali hakiki thamani isiyo pimika ya taarifa na ufahamu. Kitabu cha Mithali kimejaa kauli zenye kushawishi juu ya umuhimu wa kuwa na taarifa, hebu tuangalie mistari kadhaa ya maandiko yenye kusisimua:a) Mithali 13:16

“Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa” (NIV)

b) Mithali 14:1“Mjinga huamini kila Neno, bali mwenye busara huangalia sana aendavyo”(NIV)

c) Mithali 15:14“Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa”.(NIV)

d) Mithali 18:13“Yeye ajibuye kabla hajasikia ni upumbavu na aibu kwake”(NIV)

e) Mithali 24:3-4“Nyumba hujengwa kwa hekima, na kwa ufahamu huthibitika, na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa, vitu vyote vya thamani na vya kupendeza”.(NIV)

17

Page 18: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Utafiti – Nguvu Ya Taarifa Na Roy Wingerd

Taarifa juu ya Uwanja wa Mavuno na nguvu ya mavuno ni msaada kwetu Iwapo tuna imani ya kuziamini ahadi za Mungu na kama tupo radhi kuzitii amri zake.

Wakati kazi yote ya utafiti itakapo kamilika – yaani, ukaguzi wote, Mawasiliano, Kunakili, Kupiga hesabu, Kutathmini na kuandika – watu wachache, kama wapo, watakuwa wameletwa katika “Ujuzi wa ile KWELI” na hivyo wameokolewa. Utafiti sio shughuli ya kiunjilisti ambayo inawaongoza watu kwa Yesu kwa imani na kuwa wanachama wenye kuwajibika katika kanisa lake.

Na bado utafiti na taarifa ni vya thamani kubwa katika utekelezaji wa Agizo kuu. Picha halisi ya upana wa mashamba ya mavuno ya dunia daima ni zana kubwa Mungu anayoitumia kuwapa watu wake mzigo kwa waliopotea. Taarifa toshelevu, sahihi na zinazo kwenda na wakati. Zinapotafsiriwa inavyo stahili kwa usahihi, yaweza kulisukuma kanisa kwenye Uinjilisti na upandikizaji kanisa wenye ufanisi mkubwa.

Tumepewa muundo wa kutuonyesha umuhimu wa utafiti, kwa jinsi wana wa Israel walipokuwa wakijiweka tayari kuingia nchi ya Ahadi, Musa aliamriwa na Mungu kutuma watu kumi na wawili waende wakaipeleleze nchi ya Kanaani. Ni dhahiri kuwa watu hawa kumi na wawili walikuwa mahiri katika mbinu za upelelezi wa nchi, wakifanya upembuzi makini, wakinukuu taarifa na kufanya mahitimisho. Waliporudi walitoa taarifa ya kile walichokiona kwa Musa.

Kumi kati ya wale wapelelezi “Walifanya mioyo ya watu iyeyuke kwa hofu” Maelezo yao ya vikwazo vilivyokuwa mbele yao, Yaliwafanya waanze manung’uniko, “….Ingalikuwa heri kama tungalikuta katika nchi ya Misri …..mbona Bwana anatuleta katika nchi hii ili tuanguke kwa upanga?” (Hesabu 14:2,3) Lakini Kalebu na Yoshua “walimtafuta Bwana Mungu wao kwa utimilifu” (Yoshua 14:8). “Wakawatuliza watu mbele ya Musa, wakasema, Natupande mara tukaitamalaki, maana twaweza kushinda bila shaka”. (Hesabu 13:30). Wakiwatia imani walisema, “Msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu: uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye Bwana yu pamoja nasi” (Hesabu 14:9).

Ni nini kilichofanya tofauti kati ya hao wawili na wale wengine? Je, haikuwa ukweli kuwa wale wapelelezi kumi watumainia nafsi zao wenyewe wakati Joshua na Kalebu walimtumainia Mungu kwa ukamilifu, wote waliwaona wale majitu katika nchi. Walio wengi walijiona dhaifu na wanyonge kwa kujilinganisha. Kalebu na Yoshua, hawakuupoteza ujasiri wao kwa sababu hawakupoteza machoni yao kwa Yeye aliye mkuu kuliko mijitu yote.

Kalebu na Yoshua wanatufundisha kuwa nguvu ya taarifa haimo katika taarifa zenyewe tu, bali katika imani, kushawishika na tabia ya yule ambaye amekabidhiwa hiyo taarifa, Maono, Kujitoa,na Ujasiri, Kujiweka wakfu, Kung’ang’ania – mambo tuyaonayo kwa watu hawa – ndiyo uvuvio kwa awaye yote ambaye atatoa maisha yake kulikamilisha Agizo kuu.Imani ya watu wa jinsi hii ndiyo inayoazimu iwapo nguvu iliyoachiliwa katika taarifa husika itakuwa endelevu na yenye kutia motisha au yenye kuharibu na kudhoofisha.

18

Page 19: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Mungu angalimuambia Musa na Waisrael kila kitu kilichokuwapo kujulikana juu ya magumu ambayo wangekabiliana nayo katika kuiteka nchi ya Ahadi.

Jukumu la kuiteka nchi ya kanaani lawezakuwa sambamba na jukumu la kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi katika agano Jipya. Kwa jinsi ile ile Bwana hajatuambia kila kitu tunachohitaji kujua ili kuwafanya watu kuwa wanafunzi. Leo, zaidi hata ya awali,”Wapelelezi “ Lazima watumweili kugundua watu wote wako jinsi gani, wako wapi, na ni kina nani.Hii sio jukumu dogo. Na katika hatua za kujifunza kanisa na mataifa tutakumbana na “Majitu” mengi, tutakuwa na mwitikio gani? Wakati watu wa imani watakapowasilisha taarifa za Mashamba ya mavuno na kanisa la Taifa, yaweza kuusaidia mwili wa Kristo, Viongozi wa kanisa, wainjilisti, wapanda Makanisa, Washsrika – kupata picha ya kile ambacho Mungu Roho amekuwa akifanya. Yaweza kuwahamasisha kuweka malengo na kufanya mipango ya kulikamilisha Agizo kuu katika nchi yao asilia.

Wakati taarifa zile zile zinapowasilishwa na watu wasio na imani, zaweza kulifanya kanisa lirudi nyuma kwa hofu kwa kuona jukumu linaloonekana kutowezekana, Wake na Waume wanawasilisha taarifa sahihi kwa imani jasiri na uhodari usiozuilika wanaifungulia nguvu halisi ya taarifa.

Kalebu na Yoshua, watafiti, hawakupoteza maono ya yule ambaye mamlaka na uweza wote Mbinguni na Duniani amepewa (Mathayo 28:18). Hivyo nasi pia yatupassa kuelewa na kuenenda katika “Nguvu yake kuu isiyolinganishwa kwetu sisi tuaminio” (Efeso 1:18-23). Utafiti ni sehemu muhimu sana ya mkakati wa DAWN. Lakini kitendo cha kukusanya taarifa zilizo nyeti, sahihi zinazoenda na wakati na zenye kuhamasisha sio hakikisho kuwa kanisa litasimama juu na kusema “Natuende tukawafanye watu wote kuwa wanafunzi, kwa kuwa hakika twaweza kufanya hivyo”. Lazima tuunganishe taarifa za namna hiyo na imani, ”Kwa kuwa pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu!”(Ebrania 11: 6)

Macho ya Bwana yanatafiti ulimwengu wote, kutia nguvu wale ambao mioyo imejitoa kikamilifu kwake. 2 Nyakati 16: 9 Je, atawaona watu wa imani ambao watasimama dhidi ya upinzani wowote na kuliita Kanisa kusonga mbele na “Kuitamalaki nchi? Bwana Yesu Kristo anatafuta watu kutoka katika kila Taifa ambao hawaogopi wala hawaoni aibu kusema “Natuihubiri kwa kila mtu na kupanda makanisa kila mahali: Kwa kuwa kwa msaada wa Bwana Yesu tunaweza hakika!”

19

Page 20: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

KUUELEWA UWANJA WA MAVUNO NA JESHI LA WAVUNAJI

UWANJA WA MAVUNO

Utambulisho, Mahali, Maelezo na hali ya watu, pamija na vikundi vyote vya kijadi, kikabila na kijamii katika jamii zote za njia husika.

MASWALI JUU YA UWANJA WA MAVUNO

Utambulisho.

Niwatu gani wanaounda mji au eneo husika? Ni vikundi gani vya watu walio hapo na ni lugha gani wanayozungumza? kuna mgawanyo gani wa madaraja ya kijamii? Ni nani walio maskini na wakiwa?

Eneo Eneo limegawanywa vipi kijiografia?

Mahali Ni nini hali ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kidini ya mji?Ni nini hali ya kimaadili ? Ni nini dhambi ya Mababa?Ni nini sababu ya hali hizi? Ni nini mahitaji ya msingi ya Jamii? Ni nini kiwango na aina ya umaskini na mikandamizo.

Hali Ni nini idadi ya watu, Mjini na Vijijini, idadi ya Wanawake, Wanaume, Watoto,Vijana na watu wazima katika mjihusika, kuna nyumba ngapi au kaya ngapi? Ni nini idadi ya watu wa kila Kabila na vikundi vya watu?

JESHI LA WAVUNAJIUtambulisho, Mahali, Maelezo na hali ya madhehebu, makutaniko, wakala wa Umishenari, na taasisi za kikanisa.

MASWALI JUU YA JESHI LA WAVUNAJI:

Utambulisho Madhehebu gani yaliyopo, makanisa ya mahali, vikundi vya kimishenari na muungano

wa kimakanisa ambayo yanaweka nguvu katika mji?

Eneo Yako wapi? Wafanya kazi gani katika mjihuu? Wanafanya kazi kati ya watu wa kundi gani?

Maelezo Ni madhehebu gani yaliyo na malengo na mipamgo ya ukuaji? Ni huduma zipi ambazo

kumekuwa na matokeo ya makanisa kuanzishwa? Ni mbinu gani zilizo na ufanisi mkubwa kwa upandikizaji wa kanisa na Uinjilisti? Huduma gani zingine zenye kutegemeza na kuhusika moja kwa moja na upandikizaji kanisa?

20

Page 21: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Hali Ni makanisa mangapi, washarika, wachungaji na watendakazi wengine waliopo katika

kila kanisa? Wanaongezeka kwa kiasi gani? Ni watu wangapi wanahudumiwa na kila taasisi ta kikanisa? Kuna Wamishenari wangapi wa kigeni katika eneo hilo?

RAMANI ZA KIROHOMAANA.Kuchora ramani za Kiroho ni kuutafiti mji kugundua kila aina ya vipenyo vya shetani alivyovifanya, ambavyo vinazuia kuenea kwa Injili na kufanyika kwa Uinjilisti katika mji husika. (Andy Jacobs)

Nakubaliana na George Otis Jnr, pale aliposema kuwa, “Lazima tujifunze kuiona dunia kama kihalisi na wala sio kama tu inavyoonekana” Kadhalika akaupa jina mtazamo huu mpya wa vitu – “Ramani za Kiroho”. Hii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya vionekanavyo. Kupiga ramani za kiroho ni mbinu ambayo kwayo twaweza kuona yale yaliyo chini ya dunia halisi ionekanavyo.

NGOME ZA ENEOKUNA MSINGI WA KIBIBLIA?Wengi wanatishika sana kwa neno au dhana nzima ya “ngome za eneo” kwa kuwa tu kwamba neno la ziada la kibiblia. Japokuwa ni neno la ziada kibiblia, si neno lisilo la ki- biblia wala dhana iliyo nje ya biblia. Je, kuna kuungwa mkono kwa dhana hii ya ngome za eneo? Naamini kupo. Hebu na tuangalie kwa ufupi mifano miatu.

MIFANO YA NGOME ZA ENEO KATIKA AGANO LA KALE.1. Mahali pa juu.Hesabu 33:51-52“Nena na wana wa Israel uwaambie, Mtakapovuka mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani: [52] Ndipo mtakapo wafukuza wenyeji wote wan chi hiyo mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu, na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunja vunja mahali pao pote palipoinuka…”

Moja ya vikwazo vya anguko kwa Israel ni “Mahali pa juu” Kwa nini?Hizi zilikuwa ni milki halisi za maeneo za mapepo mabaya ambapo shughuli zao zilianzia. Mapepo walilinajisi Taifa zima tokea mahali hapo, kuvunja ngome hii dhidi ya Israel iliwapasa kupaharibu hapa “Mahali pa juu”.

Mungu aliona mahali hapa kuwa ni uzinzi wa Kiroho. Ilikuwa moja ya sababu ya utumwa wa Babeli

2. Bel MardukYeremia 50:2-3“Tangazeni katika mataifa, mkahubiri na kutweka bendera, hubirini msifiche semeni, Babeli amefedheheka Merodaki amefadhaika, sanamu zake zimeaibishwa, vinyago vyake vime vimefadhaika. [3] Maana toka kaskazini Taifa limekuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa, wala hapana mtu atakaye kaa humo, wamekimbia, wamekwenda zao, Wanaadamu na wa Wanyama pia”.

Neno “Bel au Baali ni neno shina la “Bwana” na katika aya hii limetumika kwa Merodaki kama Bwana Merodaki.Alikuwa ndiye “mungu wa Taifa la Babeli” au ndiye aliyekuwa ngome kuu juu ya Taifa hilo.

21

Page 22: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

3. Mkuu wa Uajemi (Daniel 10)Hapakuwa na mkuu hasa juu ya Uajemi. Hapakuwa shaka ilikuwa ni ngome tu ya eneo.

MIFANO YA NGOME KATIKA AGANO JIPYA1. Artemi wa EfesoArtemi ni jina la Kiyunani la Diana (Kirumi) ambaye ndiye aliyekuwa roho yenye kutawala katika Efeso. Viongozi wa mji wa Efeso walighadhibika mno na huduma ya Paulo mtume kiasi kwamba waliogopa kuwa hekalu la mungu wa Diana litadharauliwa na hadhi yake kuharibiwa. (Matendo 19:27). Watu walimwita “mwokozi” “bwana” na “malkia wa Anga”. alivaa alama zile za kinajimu kuzunguka nguvu shingo yake na “alikuwa na mamlaka na uwezo wenye nguvu katika hatima ya kinajimu” – Clinton E. Anold. Waefeso, nguvu na miujiza uk. 27

2. Kahaba Mkuu (Ufunuo 17)Sura yote hii inaonyesha jinsi roho hii ya kipepo ilivyo ngome ya eneo husika.

KANUNI TISA ZA RAMANI ZA KIROHO.1) Lazima iwe na msingi katika Neno la Mungu na mafunuo yake.

2) Wale wahusikao na kupiga ramani na vita vya kiroho wanahakikisha kuwa wanaishi katika utakatifu.

3) Wawe chini ya mamlaka ya kiroho, katika kanisa la mahali.

4) Utafiti uwe kwa maongozi ya Roho Mtakatifu na sio hatua za kisayansi.

5) Wahusikao wawe na mtazamo wa matumaini.

6) Wawe na umoja kamili.

7) Wahusikao wasiwe waongofu wachanga ambao hawaja komaa kiroho.

8) Hatimaye wazee wa mji lazima waongoze.

HITIMISHORamani za Kiroho ni kama kikosi cha upelelezi cha kijeshi, kupitia hicho, tunakwenda nyuma nyuma ya mipaka ya adui kumwelewa adui na mipango yake na jinsi alivyo jiimarisha. Kama vile Kyell Sjoberg asemavyo tunafanya “Upelelezi wa Kiroho”.

Mfano mzuri wa kibiblia ni wale wapelelezi waliotumwa katika nchi ya Ahadi na Musa baadae Yoshua. Kuna mambo yanayoshabikiana kiroho yanayoweza kuonekana katika mikakati hiyo.

22

Page 23: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

JINSI YA KUCHORA RAMANI ZA KIROHOEzekiel 4:1-3

“Wewe nawe, Mwanadamu, jipatie tofali uliweke mbele yako, kisha chora juu yake mfano wa mji, yaani, Yerusalemu [2] ukauhusuru, Ukajenge ngome juu yake, na kufanya boma

juu yake: ukaweke makambi juu yake, na kuweka magogo ya kuubomoa yauzunguke pande zote [3] Kisha ukajipatie bamba la chuma, ukalisimamishe liwe ukuta wa chuma

kati yaw ewe na mji huo, ukaulekeze uso wako juu yake, nao utahusuriwa, nawe utauhusuru. Hili liakuwa ishara kwa nyumba ya Israel”.

Hakuna mfumo au kanuni maalum iliyowekwa kwa ajili ya ramani za kiroho, lakini hebu tuone mapendekezo ya Peter Wagner juu ya kupiga ramani za kiroho mjini pako.

HATUA YA KWANZA: KUSANYA TAARIFAKufuatia maongozi ya Wachungaji kama Harold Caballeros, nitaigawanya hatua hii ya kukusanya taarifa katika sehemu tatu;

1) Utafiti wa Kihistoria2) Utafiti Halisi3) Utafiti wa Kiroho

Kama ungependa kugaawa majukumu kwa vikosi vitatu kama vile Caballeros afanyavyo ni mapendekezo yako. Lakini ina ina manufaa yake iwapo ipo nguvu kazi ya kutosha.

1. UTAFITI WA KIHISTORIA

I. HISTORIA YA MJIA. Kuanza kwa Mji

1) Ni watu gani walioanzisha Mji?2) Nini zilizokuwa sababu za mmoja mmoja au za pamoja za kuuanzisha Mji? Imani

na falsa zao zilikuwa nini? Maono yao yalikuwa nini kwa siku za usoni za Mji ule?3) Nini maana na muhimu wa jina la asili la Mji huo?

Je, jina limebadilishwa? Je, kuna majina au alama nyingine mashuhuri za mji? Je, majina haya yana maana? Je, yana husiana na dini ya aina yoyote? Je, ni

majina ya kipepo au nguvu za giza? Je, yanaashiria baraka? Je, yanaonyesha karama ya ukombozi kwa mji ule? Je, yanaonyesha tabia za watu wa mji huo?

B. Historia ya Baadae ya Mji1. Mji huo umechukua nafasi gani katika maisha na tabia ya Taifa kwa ujumla?2. Viongozi mashuhuri walipochipukia katika mji, walikuwa na maonu gani kwa ajili ya

mji ule.3. Je, wamekuwa na mabadiliko makubwa kwenye serikali au katika uongozi wa

kisiasa wa mji?4. Je, kumekuwa na mabadiliko yoyote muhimu ya kiuchumi wa mji? kushuka

kiuchumi? Teknolojia? Viwanda? Ugunduzi wa maliasili?5. Je, kumekuwa na wahamiaji gani muhimu? Je, kumekuwa na kuingia kwa lugha ya

kigeni au utamaduni wa kigeni katika mji huo kwa ujumla?6. Je, wahamiaji au watu walio wachache wametwendwa vipi? Makundi ya kikabila na

kijamii tofauti yamehusiana vipi kati yao? Je, kanuni au sheria za mji zimeruhusu ubaguzi wa aina yoyote ile?

7. Je, viongozi wa mji wamevunja makubaliano, au maagano yoyote?8. Je, kuna vita vyovyote ambavyo vimeuathiri mji huo? Je, kumewahi kupiganwa vita

yoyote katika mji huo? Je, kulikuwa na umwagaji damu?

23

Page 24: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

9. Mji umewatendeaje maskini na wanaonewa? Je, viongozi wa mji wamekuwa na tabia ya tama? Je, kuna udhihirisho wowote wa rushwa kati ya viongozi wa kisiasa, kiuchumi au viongozi wa kidini au taasisi mbalimbali?

10. Kuna majanga gani ambayo yameuathiri mji?11. Ni miziki ya aina gani ya miziki ambayo watu husikiliza kuna ujumbe gani

wanaopokea katika miziki hiyo.12. Je, mji unayo kauli mbiu au msemo wake? Kunamaana yoyote ya kauli au msemo

huo?13. Ni maneno gani matano watu walio wengi wanayatumia kuonyesha muonekano

chanya wa mji wao hivi leo? Ni maneno gani matano watakayo tumia kuonyesha mwonekano usiofaa wa mji huo?

II. HISTORIA YA KIDINI KATIKA MJI A. Historia ya Dini zisizo za Kikristo1. Nini uliokuwa mtazamo wa kidini na tabia za watu walioishi mahali pale kabla mji

haujaanzishwa? 2. Je, fikra za kidini zilipewa kipaumbele wakati wa kuuanzisha?3. Je, watu wasio wakristo wameingia katika mji kwa wingi wa kutisha?4. Vikundi gani vya siri (kama Freemason) vimekuwepomjini? 5. Vikundi gani vya wachawi, vya kishetani au vyama kama hivyo vya siri (cults)

vimekuwa vikifanya kazi hapo mjini?

B. Ukristo1. Ni lini, kama ndivyo, Ukristo ulipoingia mjini hapo? kwa namna gani?2. Je, mmoja wa viongozi wa kikristo amewahikuwa katika Freemason?3. Jamii ya Kikristo imekuwa na nafasi gani katika hili.4. Je, Ukristo hapo unakuwa unadumaa au unashuka?

C. Mahusiano1. Je, kumewahi kuwa na mapambano kati ya dini katika mji huo?2. Je, kumewahi kuwa na magombano kati ya Wakristo?3. Ni nini historia ya migawanyiko katika kanisa.

2. UTAFITI HALISI.1. Pata ramani mbalimbali za mji, hasa za zamani. Kuna mabadiliko gani yaliyotokea

katika hali ya nchi kwenye mji?2. Ni kina nani walioubuni mji? Je, walikuwa waabudu shetani?3. Je, kuna alama au ishara zozote zionekanazo zilizotiwa katika mchoro wa mwanzo

wa kuubuni mji?4. Je, kuna umuhimu wowote kwenye kubuni mahali au uhusiano wa sehemu za

majengo makuu hasa yale yanayowakilisha nguvu za Kisiasa, Kiuchumi,Kielimu au Kidini katika mji? Je, waabudu shetani waliweka jiwelolote lamsingi?

5. Je, kumekuwepo na umuhimu wowote wa kihistoria katika sehemu ya kiwanja ambapo moja ya majengo haya yapo? Ni nani aliyekuwa Mmiliki wa ardhi hiyo.

6. Nini historia ya maeneo ya kupumzikia ya mji? Nani aliyeyaanzisha na kuyajenga? Majina ya maeneo hayo yaweza kuwa na umuhimu wowote.

7. Nini historia ya awali na umuhimu wa sanamu na kumbukumbu za mji? Je, zinaakisi tabia au sifa za kipepo au kumtukuza muumbwa badala ya Muumba?

8. Kuna kazi gani ya kisanii iliyoonyeshwa katika mji, hususani katika majengo ya kijamii, makumbusho au majumba ya maonyesho? Tafuta sanaa za kipepo na zenye kuamsha tamaa.

9. Je, kuna maeneo ya ugunduzi wa mambo ya kale katika mji? yanaweza kuwa na maana gani?

24

Page 25: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

10. Vituo vya dhambi zinazoonekana kama kliniki za kutoa mamba, maduka ya vitabu au picha za ngono, au majumba ya sinema hizo chafu, maeneo ya ukahaba, kamari , maaba ya usiku kucha, vitendo vya mashoga n.k. Viko maeneo gani?

11. Ni yapi maeneo yanayozingatia tama, unyonyaji, umaskini, ubaguzi, vitendo vya mapigano, magonjwa au ajali za mara kwa mara?

12. Ni yapi maeneo ya wakati uliopita au uliopo ya umwagaji damu kwa mauaji, vita au uchinjaji?

13. Je, ilipo miti, vilima, mawe au mito inaunda sura au mfumo wowote muhimu?14. Je, kuna alama zozote za ardhini zenye majina ambayo yaweza kumtukuza Mungu?15. Ni eneo gani lililo juu zaidi kijografia katika mji na ni kitugani kilichojengwahapo? Hii

yaweza kuwa kauli ya mamlaka.16. Kanda au maeneo yapi au jirani na mji wako yanayoonekana kuwa na tabia za

kipekee? Jaribu kutambua maeneo ya mji yanayoonekana kuwa na maeneo tofauti ya kiroho.

3. UTAFITI WA KIROHOA. Wasio – Wakristo

1. Miungu na roho zitawalazo zinahusika na mji kwa wakati uliopo au uliopita majina yao ni nani?

2. Ni yapi maeneo yao ya mahali pa juu, madhabahu, mahekalu, sanamu za ukumbusho au majengo yanayohusiana na uchawi, mambo ya giza, ubashiri, ushetani, Freemason, Mormon, dini za kimashariki, mashahidi wa Yehova na wengineo, Je, kuna mfumo unaonyeshwa nao wenye ramani wanapowekwa kwenye nafasi zao?

3. Je, maeneo ya ibada za kipagani tokea zamani, hata kabla ya mji kuanza ni yapi?4. Kuna vituo gani vya kitamaduni ambavyo vyaweza kuwa na sanaa au michoro

nayohusishwa na ibada za kipagani?5. Je, kuna kiongozi yeyote wa mji ambaye kwa kujua amejitoa kwa miungu ya

kipagani au mamlaka yoyote.6. Je, kuna laana zozote ambazo zilitolewa na wakaazi wa mwanzo wa mji au

waanzilishi wa mji?

B. Wakristo1. 1Wajumbe wa Mungu wamepokelewaje na mji huo?2. Je, Uinjilisti umekuwa mgumu au rahisi?3. Makanisa yako upande gani? Ni yapi uyaonayo kama makanisa yenye kutoa?

4. Ni nini afya ya kanisa katika mji huo?5. Ni viongozi gani wa Kikristo wanaotambulika kama “wazee wa mji”?6. Je, ni rahisi kuomba katika maeneo yote ya mji?7. Ni nini hali ya umoja kati ya viongozi wakristo katika madhehebu na vikundi vya

kikabila.8. Ni ni mtazamo wa viongozi wa mji kuhusiana na maadili ya Kikristo?

C. Kimafunuo1. Ni kitu gani ambacho waombeaji waliokomaa wanasikia toka kwa Mungu juu ya

mji husika.2. Ni nini utambulisho wa mamlaka za kiroho zionekanazo kuutawala mji wote au

eneo fulani la maisha ya mji au mahali?

25

Page 26: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

HATUA YA PILI: KUFANYIA KAZI TAARIFA.Faidaza kuwa na wachangiaji kadhaa kwenye kitabu kama hiki ni kuwa wanatoa nuru ya tokea mitazamo tofauti ili kufikia kiwango na mikakati nyeti kukabili vita vya kiroho kwa kiwango cha juu. Tumeona jinsi Cindy Jacobs alivyoongoza wachungaji wa Resistensia katika toba. Tumemwona rafikiye Kell Sjoberg alipenyeza kikundi cha kishetani katika nchi ya Sweden na kuona jinsi Harold Caballeros alivyolipata jina la mtu wa mamlaka ya kiroho kwenye kurasa za gazeti la Guatemala. Tumemwona Bob Bakett akiendesha gogo la mashua hadi kwenye gati ya Hemet. Kadhalika tumemwona Victor Lorenzo akiunganisha msalaba wa kusulubia katikati ya duka kubwa katika mji wa Laplata, na Bev Klopp akitubu katika majengo ya siri chini ya ardhi mjini Seatle. Wote hao wameona faida fulani katika mbinu waliyoitumia, lakini hakuna kati yao aliyetaka kuwa wengine watumie njia yake.

Kupitia maombi, Mungu atawaonyesha viongozi mji kwa mji, ni mkakati upi ufaao zaidi kwa hali yao. Vinginevyo kuna kanuni ya kuhudumia mji kulingana na hali na mazingira yao maalum. katika kitabu cha kwanza cha mfululizo huu, Maombi ya mapambano, ambapo zitafanana na kanuni za kuuteka mji, ambazo nilizielezea humo. Kwa faida ya wale ambao hawajakisoma kitabu hicho au wale waliosahau, nitaorodhesha kanuni sita hizo bila ya maelezo ya ziada.

Kanuni ya 1. Eneo Chagua eneo la kijiografia linalofikika kwa urahisi kwa mipaka itambulikanayo ya Kiroho.

Kanuni ya 2. WachungajiPata umoja wa wachungaji na viongozi wengine wa Kikristo katika eneo hilo na muanze kuomba pamoja mara kwa mara.

Kanuni ya 3. Mwili wa KikristoOnyesha wazi kuwa juhudi hizo sio kazi ya Wapentecoste na wanauamsho tu, bali mwili wote wa Kristo.

Kanuni ya 4. Maandalizi ya Kiroho.Hakikisha ushiriki wa viongozi na wakristo wengine Kiroho, kupitia toba, Unyenyekevu na utakatifu.

Kanuni ya 5. Utafiti Tafiti historia ya nyuma ya mji ili kuzigundua nguvu za Kiroho ziuundazo mji.(Hii ilishakiwa katika sehemu ya kwanza ya sura hii “Kukusanya Taarifa”).

Kanuni ya 6. WaombeajiTendakazi na waombeaji wenye wito na vipawa katika vita vya kiroho vya ngazi ya juu ili kutafuta mafunuo ya Mungu juu ya (a) Kipawa au Kipawa cha ukombozi cha mji husika (b) Ngome za shetani za mji (c) Roho zitawalazo zenye jukumu juu ya mji huo (d) Dhambi ya pamoja ya wakati uliopo na uliopita ambayo hainabudi kutubiwa (e) Mpango wa Mungu wa kushambulia na wakati hasa wa kufanya hivyo.

JINSI YA KUZISHUHULIKIA TAARIFA.Ni vigumu mno kuchanganua taarifa za utafiti na takwimu katika hali ya maandiko. Ni muhimu kuweka taarifahizi katika ramani. Ramani ni kama picha ielezeayo hadithi. Kuelezea hili nitakupa kisa cha kujifunza na mfano wa ramani.

26

Page 27: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Soweto – Afrika ya kusini.Soweto inawakazi milioni mbili. Ilikuweza kufanya upandikizaji wa kanisa ni muhimu kufanyia utafiti mji huu. Aina ya taarifa inayohitajika zaidi ilikuwa;

Makanisa ya Kikristo- yako mangapi, yako wapi na ni watu wangapi wanao hudhuria kanisani hapo? Kadhalika tunaweka ainisho kati ya makanisa ya kiinjilisti na makanisa makongwe. Hii itatueleza jambo juu ya Jeshi la wavunaji.

Makanisa ya imani potofu – yako mangapi, yako wapi na ni watu wangapi wahuhudhuriaoa makanisa hayo?Hii ni sehemu ya utafiti katika uwanja wa mavuno.

Maeneo ya Unywaji (Bar, Madanguro n.k ). Yako mangapi, na yako wapi? Ulevi wa pombe ni ngome kubwa katika Afrika.

Maeneo ya Kamari – Tuanfanya utafiti juu ya maeneo ya kamari kwa sababu hizohizo hapo juu.

Waganga wa Kienyeji – Afrika bado imeelemea mno katika shughuli za uganga wa kienyeji. Wanamguso mkubwa sana katika jamii. Hii pia ni sehemu kubwa ya Ramani za Kiroho.

Katika ukurasa wa 26 kuna ramani ya eneo mojawapo la kitongoji cha Soweto. Matokeo ya kushangaza ya utafiti huu yalikuwa;

Idadi ya wakazi - 86,000 Makanisa - 7 (wastani 100) Makanisa ya imani potofu - 15 Waganga wa kienyeji - 18 Maeneo ya unywaji - 75

Takwimu pamoja na ramani hutupa picha ifuatayo

Jeshi la wavunaji;Unaweza kuana matandao wa kuenea kwa makanisa (yalipo). Unaweza sasa ukaazimu ukubwa wa Jeshi la Wavunaji. Kamawastani wa kanisa ni washirika 100 na yako makanisa7 inamaana ukubwawa Jeshi la Wavunaji ni kati ya watu 700 na 1000.

Uwanja wa Mavuno;Iwapo idadi ya watu ni 86,000 na Jeshi la Wavunaji ni 1000 basi uwanja wa mavuno ni 85,000. Hii inakuambia kwamba unahitaji kuweka lengo la angalau makanisa 85 katika eneo hili.

Ramani ya Kiroho;Ramani hukuambia ngome hizi zilipo. Kwakuwahii ni jamii inayo badilishwa kupitia upandikizaji wa makanisa utaweza kuona kupungua kwa maeneo ya kunywea pombe na waganga wakienyeji.Taarifa hizi pia hutusaidia katika maombezi na uinjilisti. Hata hivyo taarifa hizi ZiSIANGUKIE mikononi mwa watu wasio husika! Yaweza kusababisha muitikio usio stahili kwa watu utakao kuwafikia.

27

Page 28: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

28

Page 29: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

29

HATUA YA

UPANDIKIZAJI

KANISA

2. Kuchimbua Udongo

- Maombi -

Page 30: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

2. KUUCHIMBUA UDONGOJambo linalofuata alifanyalo mkulima, ni kulima ardhi ule udongo mgumu unahitaji kuchimbuliwa na kulainishwa kwa ajili ya hatua zifuatazo za upandaji.

Kadhallika, jamii ila ambamo utakwenda kupanda kanisa inahitaji kufunguliwa na kulainishwa kwa ajili ya Injili. Hii yaweza kufanyika kwa maombi tu.

2.1 MAOMBIPasipo na Maombezi ya kina na subira katika kusikia mkakati wa Mungu juu ya upandaji huo wa kanisa, hautakuwa na matokeo ya kudumu. Nashauri kuwa maombi ya kutembea katika eneo jirani au kijiji kwa weza kuwa na manufaa makubwa – kuomba kwenye eneo- na maono.

Matendo 4:23-31Hata walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha habari ya mambo yote

waliyoambiwa na wakuu wa makuhani na wazee 24 Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja wakisema, Mola wewe, ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo,25 nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha Baba yetu

Daudi mtumishi wako,“Mbona Mataifa wamefanya ghasiana makabila wametafakari ubatili?

26 Wafalme wa dunia wamejipanga na wakuu wamefanya shauri pamoja juu ya Bwana na juu ya Kristo wake”

27 Maana ni kweli, Herode na Pontia Pilato pamoja na mataifa na mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya mtumishi wako Mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta mafuta, ili

afanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee 29 Basi sasa, Bwana yaangalie matisho yao ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri

wote. 20 Ukinyoosha mkono wako kuponya, ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako Mtakatifu Yesu. 31 Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika

pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.

KUSUDI LA MAOMBI

1. Kuunyosha Mkono wa Mungu Walikuwa na mzigo na shauku kuu kwa jamii yao kuguswa na Mungu Walitambua kuwa maombi ndio ufunguo. Walihusika zaidi na mahitaji ya Kiroho ya kijamii yai kuliko usalama wao. Walikuwa ndio punde wameonywa na mamlaka husika wasihubiri Injili.

2. Uponyaji wa Jamii. Walijitambulisha na machungu ya jamii Ni dhahiri tunazungumzia juu ya machungu yote

- Kimwili- Kiroho- Kihisia

Hatuwezi kuiona jamii yetu imeokolewa mpaka machungu yao yamekuwa kuhusika kwetu, mpaka tumewahurumia.

Hatuwezi kuwa na huruma kwa jamii yetu wakati tunahangaikia nafsi zetu tu na kuzingatia machungu yetu tu.

Ni kana kwamba unapona pale unapoponya jeraha la mwingine.

30

Page 31: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

3. Kuleta Miujiza katika Jamii Jamii itaitambua nguvu ya Mungu pale kanisa litakapoidhihirisha. Hakuna furaha iliyo kuu kwa Mkristo kama kuona majibu ya maombi kwa kimiujiza. Je, waweza kuwaza utaratribu wa mipango ulivyo mbinguni kufanya maombi yako

yapate majibu Hivi karibuni tumeona nguvu ya miujiza ya Mungu katika jamii yetu pale kanisa

lilipoomba kwa ajili ya mvua.

4. Kuigundua nguvu katika Jina la Yesu. Bahati mbaya mara nyingi tunaombea nia potofu, mara nyingi maombi yetu yana

vikolezo vya kibinafsi ndani yake. Shauku yetu lazima iwe watu kumgundua Yesu. Acha kuwashawishi watu kwa hekima za kibinadamu. Waache wamjue Yesu.

KUJENGA MOYO KWA MJI WAKO.1. Bwana ana moyo si kwa mtu mmojammoja bali kwa ajili ya miji na jamii mbalimbali.2. Kabla Mungu hajatutumia kufikia miji/Jamii zetu, lazima moyo wa mahali husika.3. Nehemia 1:3-44. Mathayo 23:375. Manabii kadhaa walitumwa kuleta maneno ya kinabii kwa miji na Jamii husika.6. Uinjilisti wa kanisa la mwanzo ulianzia na mjiwao. Matendo 1:8

KUHUSIKA NA MAHITAJI NYETI YA MJI WAKO1) Isipo kuwa tumeguswa na mahitaji ya jamii yetu tutakuwa tunaomba maombi ya kidini

nay a maonyesho kuonekana na watu.2) Yatupasa kuomba tokea moyoni. Mahitaji yanayogusa watu dhidi ya mahitaji ya

kudhaniwa tu.3) Tunatambuaje mahitaji ya Jamii

Soma magazeti Uliza maswali – iwe tabia yako.Hudhuria mkutano wa taarifa wa Polisi Sikiliza kwa masikio yaliyotaswa mazungumzo ya jamii na jaribu kupima uhalali

wake.

4. Watu wanahitaji miujiza. Maombi yanawaleta kukutana na Mungu aliye hai anaye wajali. Omba pamoja na Meya wa mji juma hili.

5. Huwezi kuwahubiri mpaka umewaombea. Tunawaombea mno wala ambao yapasa wajue kuomba na kuwaombea kidogo sana wale ambao hawajui kuomba.

6. Sikia mapigo ya moyo wa Mungu kwa mji wako.

Nakushauri kwa dhati kuwa uingie katika maombi ya kutembea, kuna manufaa makubwa kwa kupanda makanisa.

31

Page 32: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

MAOMBI YA KUTEMBEA(Tafadhali tambua kuwa kitabu kiitwacho: “Praying on Site with Insight” yaani “Kuomba kwenye uwanja kwa maono” kinapatikana kutoka ofisiza DAWN Africa. Tafadhali angalia FORM YA MAELEKEZO nyuma ya jarida hili la mafunzo).

Matendo 4:29-32Sasa Bwana, yaangalie matisho yao ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri

wote, ukinyoosha mkono wako kuponya: ishara na maajabu vitafanyika kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu. Hata walipokwisha kumwomba Mungu mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu kwa ujasiri na jamii ya watu walio amini walikuwa na moyo mmoja, wala hapana aliyesema yakuwa kitu chochote alichokuwa nacho kwani nimali yake mwenyewe

bali walikuwa na vitu vyote shirika.

UTANGULIZI Maombi hutupa upenyo kufikia sehemu yoyote duniani, nyumba yoyote duniani na mtu yeyote duniani. Unaweza kuwagusa jirani zako, mji wako au hata dunia kwa maombi yako. Maombi yaliyouleta ukomunisti magotini kusalimu amri, ukuta wa Berlin kuanguka, na mabilioni ya watu kwa Kristo.

MAANANi kulichukua Kanisa nje ya kuta zake ili kuomba penye uwanja kwa maono.

Msingi Wa Kibiblia Wa Maombi Ya Kutembea

Mwanzo 13:14-17Bwana akamwambia Abrahama, alipokwisha kutengana na Lutu, “Inua sasa macho yako ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi (15) maana nchi hii yote uionayo nitakupa wewe na uzao wako hata milele. Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi, hata mtu akiweza kuya hesabu mavumbi ya nchi uzao wako nao utahesabika (17) Ondoka ukatembee katika nchi hii

katika mapana yake na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo”.

Yoshua 1:3Kila mahali zitakapokanyaga nyayo za miguu yenu nimewapa ninyi, kama nlivyomwapia

Musa.

KANUNI NI ZIPI HAPAIbrahimu Mungu alimtaka Ibrahim awe kwenye eneo la milki ili ampe kujitambulisha kwa kuona Mungu limtaka aone – ampekwa kuona .

Joshua Unaweza pia kupigana vita bila ya kuwa hasa mahali penyewe – kumtambua adui/

mamlaka za kiroho. Ahadi ya Mungu ilihusishwa na miguu ya Yoshua – kuidai nchi.

Somo la Kujifunza kwa Joshua.Hesabu 13:18 – 20

Mkaitazame nchi niya namna gani, na watu wanaokaa ndani, kwamba ni hodari au dhaifu, kwamba ni wachache au ni wengi (19) na nchi wanayoikaa kwamba ni njema mbaya,kwamba wanakaa katika matuo au ngome (20) nayo ni nchi ya namna gani,

kwamba ni nchi ya unono au ya njaa, kwamba ina misitu au sivyo. Iweni na moyo mkuu mkayalete matunda ya nchi. Basi wakati ule ulikuwa wakuiva zabibu za kwanza.

32

Page 33: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Mkakati namba #1 – Tambua nchi ikoje Tafuta mambo yatakayokuambia mengi juu ya watu wenyewe Je, wajua Wakristo wowote wakaao humo? Je, Wamejitenga au wapo wazi kuhusiana na wengine? Pata majina ya watu na umri wao kwa kukadiria

Mkakati namba #2 – Mtathmini adui

Hesabu 13:28-29“Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni

makubwa sana: na pamoja na hayo tuliwaona wana wa anaki huko 29. Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu na mhiti na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima na

Mkanaani anakaa karibu na bahari na kando ya ukingo wa Yordani”

Elewa matatizo yao ya kijamii- Wazazi wapweke?- Jamii hupendezwa na mambo gani.

Zielewe nguvu za Kiroho zitawalazo eneo hilo- Huwezi kuwa mwamuzi pekee.Lazima muwe kikundi

Usikadirie nguvu za adui kwa kiwango cha juu, usimpe ibilisi utambulisho kwa kuongelea afanyacho kila mara (Wana wa – Anaki)

Mkakati namba #3 – Yatambue Matunda ya wakati ujao.

Hesabu 13: 23 – 25Wakafika bonde la Eshkoli, na huko wakakata tawi lenye kishada kimoja cha zabibu,

wakalichukua kwa mti kati ya watu wawili wakaleta makomamanga pia na tini 24 Bonde lile lilitwa bonde la Eshkoli kwa sababu ya hicho kishada walicho kata huko wana wa

Israeli 25 wakarejea baada ya kuipeleleza nchi mwisho wa siku arobaini.

Pata maono ya eneo hilo, litakavyokuwa baadae. Mtumaini Bwana kwa ahadi zake, njozi na maono. Omba kinabii.

Maombi ya kutembea – Maandalizi ya ujio wa YesuLuka 10: 1 – 20

UMUHIMU WA KUTUMA WAMISHENARI 72. Hii huiita “Maandalizi ya kujaziliza” Vikundi vile 36 vilikwenda kufanya maandalizi kwa ajili ya ujio wa Yesu kwenye miji

hiyo. Yesu aliwapa mkakati maalum wa kuufuata. Walikwenda kama wanakondoo kati ya mbwamwitu.

- Watafurahia ulinzi wa Kimunngu- Watakuwa na ujasiri wa Kimungu

Ilionekana kama wazimu kufanya hivi- Yaonekana kama wendawazimu Mungu kututumia!

Msichukue mfuko, wala mkoba wala viatu- Hatua ya imani, weka fedha mbali na hili

Mkakati namba #1- Omba

33

Page 34: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Yesu aliwaambia nini cha kuombea.- Hawakutakiwa kuomba kwa ajili ya waongofu bali kwa waongofu ambao

watakuwa watendakazi.- Watu wengi katika jamii wamefungwa ambao bado wameweza kuwa watendakazi

katika viwanja vya mavuno ya Mungu.- Ombea wokovu wao na kufunguliwa.- Kama Joshua yapasa uone matunda ya baadae.

Mkakati namba #2 – kuwa wakala wa Amani Usijiingize katika mabishano, usipoteze muda na tunda bichi. “Mtu wa amani “ inamaana “Mtu atafutaye amani na yu radhi kuipokea”. Mtu huyu aweza kuwa ndiye ambaye kwa yeye utaifikia nyumba nzima “Oiko”

Mkakati namba #3 – Jitambulishe na Jamii Kula na kunywa kilichowekwa mbele zako, kujitambulisha.

- Katika tamaduni nyingi kula na kuywa ni ishara ya upendo kwa unao shiriki nao. Kiburi cha kiroho kitaharibu juhudi zako Usitoke kuzurura nyumba hata nyumba

- Unaweza kuangukia mtego wa kutaka raha zaidi. Ridhika.- Watu lazima wajue pa kukupata.

Mkakati namba #4 – kua wakala wa uponyaji kwa jamii yako Shetani anaangamiza watu. Hawahitaji hukumu yako Wanahitaji huruma yako.

KIELEZO CHA FADHILISteve Sjogren alichukua kutoka kitabu “Njama ya Fadhili” (Kitabu cha Vine, cha 1993 cha Ann Arbor Michigan) . Steve ni mchungaji wa Vinyard Christian Fellowship ya Cincinatti kskazini.

“Fadhili iliufungua moyo wa mtu kwa Mungu wakati tulipokuwa tukifanya huduma ya bure ya kufyeka majani. Tukibeba mashine kadhaa za kukatia majani na reki kwenye gari na tukaendesha hadi pale tulipoona nyasi ndefu. Tuliikaribia nyumba yake na kubisha mlango na kumwambia jambo gani ambalo tulitaka kulifanya. Kupitia kioo cha mlango alitoka mtu huyu na kusema “Mnataka nini?” Tulimpa maelezo mafupi bila hata kuinua kichwa kutuangalia, mwitikio wake ulikuwa “Sawa, chochote…...”

Alikaa kitini pake bila kujitikisa mbele ya runinga akiangalia mpira wa baseball -------tulikata nyasi kwa hamasa na bidii na kubwa, wakati mwingine ______ “Mkato wa nguvu” mizabibuni, na tukamaliza katika kipindi cha dakika thelathini, tulimwendea kumwambia tumemaliza na kumwomba iwapo twaweza kumwombea kwa ajili ya mahitaji yoyotekatika maisha yake. Akasema hana mahitaji yoyote yale, tulipoanza kuondoka na kufika hatua chache baada ya mlango, kijana mmoja kwenye kikundi alisema ana hakika alikuwa na hitaji kubwa la kihisia na yapasa tusisitize kumuombea, tuligeuka na kuomba maombi rahisi tu: Njoo Roho Mtakatifu na uguse maumivu ya mtu huyu, yawayo yote yale “Mwitikio ulikuwa wa mara moja nay a kushangaza – alitokea na machozi tele akimkamata yule aliyekuwa karibu naye katika kikundi chetu na huku akilowesha bega lake kwa machozi kwa dakika kadhaa.Kilio kilipotulia alituambia kuwa mwanawe amekamatwa usiku uliotangulia kwa kuiba gari ilikuimarisha tabia yake ya kutumia madawa ya kulevya, siku ile nguvu na uwepo wa Mungu ulipenyeza , maumivu na kutengwa kwa yule mtu katika namna dhahiri…..kwa kuwa tulikuwa radhi kukata nyasi kidogo.

Tumia nguvu aliyokupa Yesu kuleta uponyaji, ndiyo njia bora zaidi ya vita vya kiroho. Chafua mikono yako

34

Page 35: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Kumbuka1. Kuwa na subira 2. Ng’ang’ania3. Usijaribu kufanya mambo yatokee

Kutumia Kanuni Ya Yesu Katika Maombi Ya Kutembea1. MAONO YA MAVUNO

Luka 10:2Aliwaambia “Mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache: basi mwombeni Bwana

wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake”.

Unapotembea ona yale makusanyo ghalani mwa Bwana. Omba zaidi kuliko unavyodhani na kutumaini. Usimfunge Bwana kwa kutoamini kwako! Anaweza kuziangusha kuta za Yeriko, aweza kujibu maombi yako.

2. DAIMA DHIHIRISHA ROHO YA KINYUME NA DUNIA

Luka 10:3 “Enendeni , angalieni, nawatuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu.

Acha nguvu ya Mungu ionyeshe tofauti. Unyenyekevu mbele ya kiburi, fadhili mbele ya chuki na baraka mbele ya hasira. Vita isiyo ya kawaida! wewe unawaendea mbwa mwitu badala ya wao kuja kwako.

3. KARIBISHA UWEPO WA MUNGU.Luka 10:5 – 7

“Na nyumba yoyote mtakayoingia semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu 6 na akiwamo wa amani, amani yenu itamkalia, la ,hayumo amani yenu itarudi kwenu.7 Basi

kaeni katika nyumba hiyohiyo, mkila na kunywa vyakwao kwa maana mtendakazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame hame kutoka nyumba hii kwenda hii”.

Yesu ndiye mfalme wa amani Amani ndiyo iliyokuwa salamu ya baraka kwa Wakristo Yoh. 20:19. Matendo. 15:33. Matendo. 16:36.Kiyunani – “eirene”Kiebrania – “Shalom” Jifunze toka katika maombi ya Daudi kwa YerusalemuZaburi 122:6 – 9Zaburi 147:12-14

4. TOA TAMKO LA KINABIILuka 10:9 “ Wapozeni wagonjwa waliomo, waambieni , “Ufalme wa Mungu umewakaribia”. Jamii yako itapata ujuzi wa Mungu. Utangaze! Tafuta fursa.

5. TARAJIA MATOKEOLuka 10:17 – 18

35

Page 36: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

“Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakasema, Bwana hata pepo wanatutii kwa jina lako”. Akawaambia, Nilimwona shetani akianguka kutoka mbinguni kama umeme.

Luka 10:21 “saa ileile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema “Nakushukuru Baba, Bwana wa

mbingu na nchi kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili, umewafunulia watoto wachanga, Naam, Baba kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza”

Mungu anajitangaza kwa miji yote kupitia watu wa kawaida. Hili ndilo “limpendezalo” Baba.

TUNAWEZA KUTEMBEA WAPI?1. Ujiranini petu.2. Sehemu zetu za kazi3. Kanisani4. Maeneo yaliyo juu, penye miinuko.5. Maeneo yaliyo laaniwa au yenye majina mabaya.6. Maeneo ya dhambi za kale.7. Maeneo ya dhambi zinazoendelea8. Maeneo ya ngome9. Malango ya jiji10. Mahali pa juu (mahali pa tambiko)

MAONI YA KUTEMBEA UJIRANINI.

JINSI YA KUANZA

1. Pata rafiki.- Maombi ya mapatano

Mathayo 18:19“Tena nawaambieni, Yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni,

na yoyote mtakayo yafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni (19) Tena nawaambia ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote

watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.

2. Kutembea kwa familia-Kila mmoja aombe wanarika wake

3. Usiwe PekeeKama wewe sio kiongozi, hakikisha umetoa mpango wako wa kazi kwa uongozi wako.

UNAPOTEMBEA.1. Mwombe Mungu Neno kwa jiranizako2. Liombe hilo Neno kwa hao jirani

Zaburi 122:6-96. Utakieni Yerusalemu amani“Na wafanikiwe wakupendao,7.Amani na ikae ndani ya kuta zako, na kufanikiwa ndani ya majumbayako”8. Kwa ajili ya ndugu zangu, na rafiki zangu niseme sasa, Amani ikae nawe”9. Kwa ajili ya nyumba ya Bwana, Mungu wetu nikutafutie mema.

3. Muombe Bwana akuonyeshe ni ngome gani zinazotawala eneo.

36

Page 37: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

4. Unapotembea vunja vunja ngome kwa maombi.5. Omba roho ziokolewe6. Ombea milango kufunguliwa mbele zako.7. Zibariki kaya na mitaa kwa jina la Yesu.8. Sikiliza maelekezo toka kwa Roho Mtakatifu.9. Hakikisha mambo yote na kiongozi wa seli au msaidizi wake.10. Toa taarifa mara kwa mara

MAONI YA JINSI YA KUTEMBEA MAHALI PA KAZI

Usipigane na damu na nyama. Tambua ni ngome zipi zitendazo kazi kutia msukumo au mguso katika mazingira ya kazi.

1) Vunja roho ya kinyume.2) Fanya tamko la wazi mahali pale.3) Ungama dhambi za watu wale kwaniaba yao4) Ikiwezekana abudu mahali hapo.5) Endelea kuomba watu waokoke.

MAONI YA KUOMBA KATIKA MAENEO YA MAKANISA.

2 Nyakati 6: 20 – 21Ili macho yako yafumbuliwe kwa nyumba hii mchana na usiku, mahali uliponena, ndipo

utakapoliweka jina lako, usikie maombi atakayoomba mtumwa wako akikabili mahali hapa, uyasikie atakayosihi mtumwa wako, na watu wako Israeli, watakapoomba

wakikabili mahali, naam, usikie toka makaoni mwako, toka mbinguni, nawe usikiapo samehe.

Marko 11:17 Akafundisha, akasema, Je! haikuandikwa , “nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala kwa

mataifa yote? “Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.

1. Jadili jambo hili na mchungaji kwanza kupata kibali na kkuwekeana makubaliano ya mawasiliano.

2. Katika mjadala wenu na mchungaji, mwombe Bwana akuonyeshe ni ngome gani zinazotendakazi katika kanisa hilo.

3. Kama kuna kumbukumbu zozote za matamko ya kinabii dhidi ya kanisa, zitumie wakati wa maombi ya kutembea.

MAONI JUU YA KUOMBA KATIKA MAENEO YALIYO INUKA.

Maeneo yaliyoinuka na yanayotumika kutazama eneo yana umuhimu wa kipekee katika Biblia.

Mapambano makubwa kati ya Mungu na shetani yaliyotokea katika maeneo ya miinuko, Mfano Eliya katika mlima Karmeli, Yesu na shetani pale Golgotha.

Maombi ya upeo – kuomba mtazamo mpana zaidi. Mara nyingi Yesu alienda mlimani kuomba.

MAONI YA JINSI YA KUOMBA KATIKA MAENEO YALIYO LAANIWA NA YENYE MAJINA MABAYA.

37

Page 38: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Mara nyingi majina yamebadilishwa na Mungu katika maandiko. Mfano Abraham – Ibrahim; Yakobo – Israeli; Simon – Petro. Yapo maeneo ambayo yameitwa kwa majina ya miungu potofu, au waalifu sugu,

au shetani mwenyewe. Waombaji watembezi daima hupata majina kwa maombi katika kutaka kuyapa

upya majina maeneo yaliyokusudiwa kusudi la Mungu.

ONYO – Usifanye badiliko la majina mwenyewe kwanza onana na wazee wa mji.

MAONI JUU YA KUOMBEA MAENEO YA DHAMBI ZINAZOENDELEA.

Maduka ya ngono kwa watu wazima Usiende Mwenyewe asilani Usije ukawalaani watu hao Usianzishe msimamo nao

Madanguro Vilabu vya Pombe.

MAONI YA JINSI YA KUOMBA KWENYE MAENEO YA NGOME.

2 Korintho 10:4- 5Maana silaha za vita vyetu siza mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha

ngome. Tukiangusha ngome mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacha juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo.

Makao ya Freemasons Imani kengeufu – Mashahidi wa Yehova – Moronvians, Kanisa la Mitume jipya na la kale n.k.

MAONI YA JINSI YA KUOMBA KUNAKO MALANGO YA JIJI.

Katika nykati za Biblia malengo yalikuwa kama chujio, yakizuia maovu kutokuingia na kuyakaribisha yenye kustahili yaliyo na heshima, wazee wenye kuheshimiwa wa mji walitawala tokea katika malango. Hayakuwa na mfumo wa mahakma ila kulikuwa na hali ya makubaliano kijamii.

Wazee waliulinda mji kutokana na misukosuko miovu na pia hatari za kimaadili. Hivi leo panaweza kuwa mahali pa utawala – yaani kwenye baraza ambapo wazee

au Halmashauri ya mji inapokutania. Maingilio ya jiji – Barabara, Bandari, Viwanja vya ndege n.k.

38

Page 39: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

HITIMISHO Yohana 12:35 Basai Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo,

enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza, maana aendaye gizani hajui aendako.

Mika 4:5 Kwa maana Mataifa yote watakwenda, kila mmoja kwa jina la Mungu wake, na sisi tutakwenda kwa jina la Bwana, Mungu wetu milele na milele.

Yakobo 5:16…Kuomba kwake mwenyehaki kwafaa sana akiomba kwa bidii. “…Tuombeni, neno la Bwana liendelee na _________vile vile kama ilivyo kwenu,

tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya maana si wote walio na imani, lakini Bwana ni mwaminifu, atakaye wafanya imara na kuwalinda na yule mwovu. (2 Wathesalonike 3:1-3)

MAANISHA MAOMBINi wazi kutoka katika vifungu hivi kuwa wakristo wa mwanzo walikuwa na mikakati katika maombi kuieneza Injili na kinyume na misukumo ya shetani, ambayo inazua Injili isiendelee. Mahitaji haya ya maombi bado yap oleo.

Katika kuendeleza na kutekeleza mkakati wa kupandikiza kanisa, tilia maanani maombi. Usifanye lolote bila ya maombi. Huduma yako ya kupandikiza makanisa kwa kujaziliza lazima izaliwe katika maombi na iendelee kuzamishwa katika maombi daima, tokea mwanzo hadi mwisho.

39

Page 40: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

40

HATUA ZA UPANIKIZAJI

WA KANISA

3. Kupanda Mbegu

-Kupanda Kanisa-

Page 41: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

3. KUPANDA MBEGU – KUPANDA KANISABaada ya mkulima kuchimbua udongo ni wakati sasa wa kupanda mbegu. Hii inazungumzia uinjilisti na pandikizaji hasa wa kanisa – kuliunda kutaniko.Mara nyingi nimekuwa sipendelei kutoa mifano mingi juu ya jinsi makanisa yawezavyo au yanavyo anzishwa. Tuna uwepesi zaidi wa kuiga kuliko kumsikiliza Roho mtakatifu.

Katika wakati wako wa maombi Bwana atakupatia mikakati jinsi kanisa litakavyo pandikizwa, na hata mbinu ya Uinjilisti itakavyotumika. Zipo njia nyingi za kupanda kanisa lakini nitashauri Nne katika sura hii (sio katika mpangilio wa kimapendekezo);

3.1. KUANZISHAKANISA LANYUMBANI KWA WAONGOFU AMBAO UMEWAFIKIA AU WAKRISTO AMBAO HAWANA MAKANISA.

KANISA LA NYUMBANI .

Naamini kuwa muundo wa kanisa ambao unajenga viongozi bora, kwa harakana ulio na ufanisi mkubwa ni muundo wa kanisa la nyumbani – Makanisa yaliyo makubwa kulingana na kuwafikia watu nakuwafanya wanafunzi duniani pote – ni makanisa ya nyumbani.

KWANINI MAKANISA YA NYUMBANI?

Katika huduma Yesu, alianzia huduma yake katika nyumba za watu na sio kwenye majengo maalum. Mara nyingi aliwafundisha wanafunzi majumbani (Marko 2:1 7:14 – 27; 9:33; 10:2 – 12. Mathayo 13: 36). Wanafunzi wake waliishi na familia popote pale walipoenda, kuishi katika nyumba ilikuwa ni sehemu ya mpango wake wa kuwaleta watu katika ujuzi binafsi wa imani iokoayo.

Katika Luka sura ya 10, Yesu aliwaambia wale sabini kuingia katika nyumba, waliwatakia amani wote wakaao humo, wana pomwona “Mwana wa amani “ (Yaani atafutaye amani), basi walibaki katika nyumba hiyo, wakila na kunywa chochote kilicho wekwa mbele yao. Kwa njia hii, jamaa yote iliweza kuokolewa na kanisa la nyumbani kuanzishwa.

Kwenye kanisa lisilo na muundo, mtu mmoja anatawala wengine (hali inayoonekana katika makanisa mengi leo). Hii husuia uwezekano wa kukua kwa kanisa, hali hii haikuwezekana katika kanisa la mwanzo.

TOFAUTI KATI YA KANISA LA KIDESTURI NA KANISA LA NYUMBANI. Kanisa la kidesturi lina huduma ya kanisa la nyumbani kama moja ya shuguli zake nyingi.

Kanisa la nyumbani ni jamii ya msingi ya Kikristo.

41

Page 42: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

UWAZI JUU YA KANISA LA NYUMBANISio : Kukataa kuwepo na ratiba mbalimbali.Kanisa la Nyumbani ni : Mkakati wa kijamii ambao una msingi na lengo kwa

watu.

Sio : Kutowa na idara mbalimbali.Kanisa la Nyumbani ni : Muundo ulio na idara zenye kutegemeza

mfumo wa kanisa la

Sio : Vikundi tu.Kanisa la nyumbani ni : Mfano wa makanisa ya nyumbani, makutaniko na

mashangilio nyumbani

Sio : Kikundi cha makanisa ya nyumbani yanayojitegemea.

Kanisa la nyumbani ni : Kusudio la watu wenye kusukumwa na maono waishio katika jamii ya msingi ya Kikristo.

ASILI YA KANISA LA NYUMBANI

Kanisa la Nyumba lina sifa na Tabia zifuatazo.1) Kanisa la nyumbani halifanyi kazi jumapili tu bali pia katika siku za juma.

2) Kila linalotokea katika kanisa la nyumbani kuwepo ili ili kulitengeneza katika makanisa yenyewe ya nyumbani.

3) Kanisa la nyumbani hukua kwanza na kisha ndipo hujenga jengo.

4) Washirika hukutana katikati ya juma na wao ndio msingi wa kanisa.

5) Kanisa la nyumbani humtambua kila mshirika kama mhudumu na hiyo humpa zana kufanya kazi ya utumishi.

6) Waliopotea hufikiwa kupitia “Uinjilisti wa kirafiki wa nyumba kwa nyumba” Nyumba hukua na kuongezeka kusababisha kuzidisha kwa kanisa.

7) Washarika wanajaliana kwa kiwango cha nyumba.

8) Ibada za mashangilio, ambazo huwa jumapili, ni bubujiko la maisha mazima ya mwili, yaliyo katika kila msharika katikati ya juma.

9) Karama za rohoni kwa kujengana, kutia nguvu hutanguliwa na washirika.

10) Jamii ya washirika wa kanisa nyumbani ni mahali pa uponyaji wa mtu binafsi na hata familia.

11) Katika vikundi vidogo, washirika huweza kuondokana na vizuizi vyote na kuweza kupokea kujengwa na uponyaji.

42

Page 43: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

FAIDA ZA VIKUNDI VYA NYUMBA1 .Vyanzo Vya Utawala Wenye Ufanisi.

Nyumba inatawalika kwa kuwa inajitosheleza. Majukumu yote ya kanisa yanaweza kutekelezeka kupitia chanzo hiki kimoja nyumba ina muundo rahisi wa uongozi, ambao hujali na kuendeleza washirika wa nyumba hiyo.

2. Mfumo wenye ufanisi wa kujaliana

Muundo wa nyumba uhakikisha kuwa washirika wenye shida wanahudumiwa wakati wowote na sio jumapili tu.

3. Kukua kwa kanisa

Ufunguo wa ukuaji wa kanisa la Nyumbani na kuongezeka ni lile kanisa moja la nyumbani. Wakati washirika wanapo wafikia waliopotea, nyumbahukua na kuongezeka.

4. Kuinua Viongozi

Muundo wa kanisa la nyumbani hutoa fursa kwa washirika wenye wito katika maisha yao kutimiliza wito wao bila kuwa na umuhimu wa kuingia katika huduma ya muda wote.

5. Dunia kuweza kufikiwa.

Katika muundo wa nyumba, kila mshirika ni mtumishi, Wanagusa maisha ya wenye shida na watu waliopotea huko nje katika dunia.

6. Vipawa vya Roho hutumiwa.

Katika muundo wa nyumba, kila mtu anaaweza kutumia karama yake ya kiroho.

KUTANIKO

Mshirika wa kanisa la nyumba anahitaji wigo wa marafiki kumzunguka kwa ajili ya ushirika. Hapa ndipo ambapo shughuli za kutaniko kati ya watu 50 hadi 200 zinapoanzia kupangwa. Kuhusiana kwa kundi kubwa, shuhuda, mafundisho ya hadhara au kupashana habari hufanyika hapa, kutaniko linaweza kutenga mkesha wa usiku mmoja kuomba au wakati mwingine siku kadhaa za maombi. Mikutano ya kanda au Wilaya ni mfano wa shughuli zinazofanyika mwaka mzima.

NYUMBA NA MASHANGILIO

Kanisa la nyumba ndio mfano mwafaka kwa Mungu kuifunua asili yake, tunapokutanika jumapili kama kutaniko, tunamwabudu na kumshangilia Mundu aliye mwenyezi, mtakatifu , Mkuu, Wakufisha, Aliye juu na wa milele, kwenye mikutano ya nyumba, tunapata ujuzi wa kutukuka, au asili yake ya juu zaidi; ukaribu; undani; kuwa ndani yetu, kuhusika kwake, urafiki, Faraja, katikati na hata unyenyekevu wake.

43

Page 44: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

UINJILISTIMara nyingi makanisa yetu yana vizuizi visivyoonekana, ambavyo huwazuia watu nje. Tunazo desturi, kuna namna tunavyovaa, Tunavyofanya mambo, na hata kuwa na matarajio kadhaa kwa wale watakao kutembelewa.

Vikundi hutoa “daraja kiasili kwa wasiomini. Wakati washirika wanaposhirikiana na marafiki zao wasiomini, inakuwa ni vyepesi na jambo la kawaida kwa wao kwaalika katika mkutano wa kikundi. Ni kwa asiyeamini, kuja kwenye kutaniko dogo lisilo rasmi haiogopeshi sana kama kwenda kwenye mkutano mkubwa mahali ambapo hawajui mtu yeyote na hawana uhakika “Sheria” zikoje hapo.

Kujenga MahusianoKatika kikundi cha nyumba, washirika hutumia muda wao pamoja, wakifanya huduma pamoja, wakitiana moyo na kuomba pamoja, wakisaidiana katika mapambano na mahitaji. Panakuwa na nguvu na kina katika upendo wao na kujitoa kwao kwa Mungu na hata wao kwa wao.

Kikundi cha nyumba hutoa nafasi na mazingira muafaka kwa ajili ya kuendeleza usimamizi au utunzaji wa mahusiano, waamini waliokomaa wanaweza kuwa karibu kabisa na waamini wachanga kuwatia moyo, kuwafundisha, kufanya huduma pamoja nao. kwa kuwa moja ya malengo ni kwa nyumba kukua na kujizidisha, washirika wataendelea kupanga mikakati ya kuwafikia waliopotea wanaowazunguka.

UanafunziRumi 14: 19 inasema, “Basi kama ni hivyo, na tufuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana”.Vikundi vya nyumba hutoa nafasi ambayo waamini wanaweza wakahudumiwa nawao pia kuwahudumia wengine. Biblia inatoa majukumu dhahiri kwa waamini kuweza kuhudumiana. Yote haya hutokea kiasili kwa kawaida kabisa katika kikundi cha nyumba wakati kila mmoja anapohudumu kulingana na kipawa chake.

Karama za rohoni zilitolewa ili kuwaanda watu wa Mungu kwa kazi ya huduma, hata mwili wa Kristo ujengwe (Efeso 4: 12). Tunapaswa kutiana moyo (1 Thess. 4:18) na kuzungumza maneno yatakayowajenga wengine kulingana na mahitaji yao (Efeso 4:29).Hii ina maana kuwa tunashirikiana mzigo (Gal 6:2). Ilikwamba tuweze kusaidiana, shauku yetu kuu yapasa kuwa ni kuheshimiana kwa upendo wa kindugu (Rumi 12:10) na kupendana kwa kina toka moyoni (1Petro 1:22).

Kuendeleza Karama Za Roho.Vikundi vya nyumba ni mahali ambapo karama za Rohoni za kila mshirika zinavumbuliwa, zinatumiwa na kuendelezwa. Katika mfumo wa nyumba watu wanalelewa na kutiwa moyo kujifunza karama zao kupitia kujihusisha kwao katika huduma ya nyumba, kwa njia hii, wanakua katika imani yao na ukomavu wao na kuwa na fursa ya kujifunza toka kwa Wakristo wakomavu. Kuwafunza wenzao ambao ni wachanga kuliko nao katika kundi.

Kuendeleza ViongoziManufaa ya vikundi vya nyumba ni kwamba viongozi wanawajibika kwa maendeleo ya kiroho ya watu wachache tu na sio makumi elfu ya watu. Mfumo wa makanisa ya nyumba huhusisha watu wengi zaidi kwa kuwa huwapa viongozi wasio rasmi nafasi ya kuendeleza vipawa vyao vya kiroho vya uongozi. Badala ya kuwa na “Viongozi wenye taaluma” ambao hupewa uongozi kutokana na kile wanachojua, Viongozi wa makanisa ya nyumba wana fuzu kwa sababu ya ukomavu na uwezo ambao wameuonyesha kupitia katika huduma yao kwenye vikundi vya nyumba.

44

Page 45: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Kupanda KanisaKutumia kanisa la nyumba kwenye upandaji makanisa kuna manufaa mno. Moja ya faida kubwa ni kuwa huweza kutumiwa kwa manufaa ya mpandaji bila kujali ni muundo upi wa upandaji wa kanisa anaoutumia.

KANISA LA NYUMBA KATIKA MKAKATI WA KUPANDIKIZA MAKANISA KWA KUJAZILIZA.Katika upandikizaji makanisa kwa kujaziliza, ni shauku ya mpanda kanisa kulijaza eneo na makanisa ya kutosha yanaweza kuzaa na kuanzisha makanisa yao yenyewe.

Vikundi vya nyumba hutoa njia asili na yenye ufanisi kwa Uinjilisti, kuwafanya waongofu kuwa wanafunzi na kuendeleza Viongozi wapya. Ikiwa vikundi vinakutana katika nyumba za watu, hapatakuwa na hitaji la jengo maalim kwa ajili ya kanisa kwa kuondoa tatizo hili la gharama kuna liwezesha kanisa kuanzisha makanisa mapya wakati vikundi vya nyumba vinapokuwa tayari sio wakati fedha zinapopatikana, kwa maneno mengi kutokuwa na fedha sio kizuizi cha ukuaji wa asili wa kanisa.

Vikundi vya nyumba hutoa uwezo wa kuendeleza mkakati ambapo eneo zima la ujirani , Mji au nchi huweza kujazwa kwa ushuhudiaji wenye ufanisi wa Kristo. Bila ya vizuizi vya kidesturi vya ukuaji, makanisa ya nyumba huweza kustawi.

Kwa kauli rahisi, kuyatumia makanisa ya nyumba hurahisisha uanzishaji wa makanisa mapya.

3.2. KUFANYA KRUSEDI NA KUPANDA KANISA KWAWAONGOFU.

Kufanya mkutano wa krusedi ili tu kupata waongofu ni kutokuwajibika ipasavyo. Huna hali ya kumwongoza mtu kwa Kristo kama huna nia ya kumfanya kuwa mwanafunzi wa Kristo. Nimesikia Wainjilisti wanosema ni kazi yao kufanya waongofu na nijukumu la kanisa kuwafanya wanafunzi, Kimsingi upo ukweli kiasi fulani, lakini hii haijafanyakazi hapa Afrika. Kanisa katika Afrika halijakuwa kutokana maelfu ya Krusedi zinazofanywa. Moja ya matatizo yetu makubwa ni kuwa waongofu wengi lakini wanafunzi wachache. Ndio maana tumeweza kuwa na mauaji makubwa ya kimbari ya karne, katika Rwanda nchi yenye asilimia 80 ya wananchi ambao ni Wakristo.

Mikutano ya Krusedi ni zana njema sana ya kuanzishia kanisa kwa waongofu waliopatikana, mkiwaweka katika makanisa ya nyumbani kuwalea kuelekea ukomavu.

3.3. UINJILISTI WA NYUMBA KWANYUMBA

Bahati mbaya, hii ndio njia ambayo pia hutumiwa na watu wa imani kengeufu kama Mashahidi wa Yehova, Momons. na wengine. Hata hivyo, katika baadhi ya sehemu za Afrika bado ni njia yenye kufaa ya uinjilisti. Inajenga mazingira ya kuanzisha kanisa la nyumbani katika nyumba za waongofu.

3.4. SINEMA YA YESU

Nimeiona sinema ya Yesu kuwa moja ya zana madhubuti sana ya uinjilisti katika maeneo ya vijijini ya Afrika. Mimi mwenyewe nimepandikiza makanisa kwa njia ya krusedi kwa kuitumia sinema hiyo. Mwishoni mwa onyesho, baada ya kua tumeomba na wale waongofu wapya , tuliwa tambulisha kwa Mchungaji ambaye atakuwa nao kuanzia kanisa pamoja nao hao waongofu wasio na kanisa bado.Vilevile mtu anaweza kufanya hivyo kwa kutumia video nyumbani, huduma ya krusedi katika vyuo. (Campus Crusade for Christ) ina taarifa nyingi katika eneo hili.

45

Page 46: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

ILANI;Usithubutu kuanzisha kanisa nawatu walioghadhibika (wasio na furaha) ambao wameacha au kutukuzwa katika kanisa jingine.

Hakikisha yakuwa wameondoka kwa heshima na kuwa sio watu wa kulinenea vibaya kanisa na Mchungaji walipotoka, niamini, kama wakimfanyia hivyo Mchungaji huyo na kanisa lile, watakufanyia na wewe pia.

Misingi ya jengo ni muhimu sana kwa uimara na kudumu muda mrefu kwa jengo . Kanisa lolote ambalo limejengwa kwa kushutumu makanisa mengine litavuna hayo hayo.

3.5 MIUNDO YA UPANDAJI KANISA

Muundo “ Mpiga mbio Jamii ya mzabibu” Kwaasili mti huu jamii ya mzabibu hutoa machipukizi juu ya ardhi mbali kidogo na wenyewe ulipo. Chipukizi hili huitwa “Mpiga mbio.” Mti mpya huendelea baada ya mpiga mbio. Baada ya muda, mti huu mpya utatoa mpiga mbio wake wenyewe kuanzisha mti mwingine ili kwamba kuwe na miti mingine kadhaa yenye kujitegemea yenyewe, lakini imeunganishwa na wapiga mbio. Huu ndiyo muundo muafaka wa kuwa wapandikizaji wa makanisa. Unashauri wazo kuwa kila kanisa lazima lijizae lenyewe tena na tena. Baadhi ya makanisa hupandikiza makutaniko mapya ambayo hayakusudiwi kuwa makanisa yanayo jitegemea, bali yana kiasi tu cha kujitegemea na kiwango fulani cha kuendelea na uhusiano. Miundo hii ya uhusiano lazima ielezewe bayana.

Muundo wa” Kanisa Binti.” Wakati somo la upandikizaji kanisa unapo zungumziwa, muundo unao tujia ni muundo huu wa kanisa binti. Kwa kuwa kanisa mama hutoa hazina husika misaada na kuwajibika tokea mwanzo, aina hii ya upandikizaji wa kanisa kiujumla huwa ndiyo uliobora zaidi, udumuo, katika upandikizaji wa makanisa endelevu.

Ni mazingira gani yawezayo kuhamasisha upandikizaji wa kanisa jipya? Hebu tuangalie mazingira ya aina mbili;a. Washarika wa Kanisa hutoka eneo lingine kijiografia.Iwapo idadi fulani ya washirika katika kanisa husika husafiri toka eneo lililonje ya kanisa mama, kanisa linaweza kutambua hali hiyo kuwa kama ni fursa ya kupandikiza kanisa binti kwa kutuma kikundi toka kanisa mama kuanzisha kanisa lingine.

b. Kunapo kuwa na shauku ya kuyafikia makundi mengine ya jamii – kiuchumi.Wakati mwingine kanisa litakuwa na kuwafikia watu wengi zaidi katika eneo moja, lakini linaweza kushindwa kufikia makundi mengine ya watu katika eneo husika. Kuna nyakati watu hawajisikii huru kuabudu katika kanisa fulani kwasababu ya tofauti za rangi, tabaka, umri na kabila. Mahitaji ya makundi haya huweza kuitisha upandikizaji wa kanisa binti litakaloweza kuchukuliana na desturi zao na kuwahudumia kwa ufanisi mkubwa.

46

Page 47: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

UPANDIKIZAJI WA KANISA KWA MTU BINAFSI.a. Kupandikiza kwa mwanzilishi watu wengine kwa kipawa ni waanzilishi. Wanajisikia kuwajibika tu kupandikiza makanisa! Kwa asili wana mvuto wa watu. Watu wa jinsi hii daima huona hazina za kanisa mahali ambapo hakuna anayeweza kudhania. Waanzilishi ni watu tofauti. Wengine huweza kufanyakazi pamoja na madhehebu makubwa au mashirika ya upandikizaji makanisa. wengine wana shughuli nyingi mno na huona ni vigumu kujiingiza katika mifumo ya mashirika na hivyo hufanya kazi kwa ufanisi zaidi wao wenyewe. Waanzilishi wanaweza kuanzisha makanisa mengi katika maisha yao yote. Pidi kutaniko linapokuwa limeanzishwa, ni wakati wa waanzilishi kusonga mbele. Kukaa mahali pamoja kutadhoofishawalicho kianzisha kwa kuwa hawana kipawa za kudumisha na kuendeleza kanisa.

b. Kupandikiza kwa Mchungaji MwanzilishiBaadhi ya wapandikizaji wa makanisa hupanda kanisa na kukaa hapo kwa muda mrefu kama mchugaji kiongozi wa kanisa. Wanaweza wakaendelea kupandikiza makanisa zaidi kwa kuwafundisha wapanda makanisa na kuwatuma toka kanisa mama kupanda makanisa binti.

47

Page 48: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

48

HATUA ZA

UPANDIKIZAJI WA

KANISA

4. Kutia mbolea kwenye udongo

Page 49: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

4. KUTIA UDONGO MBOLEA.

Tunajua yakuwa ukuaji wa mbegu unategemea sana mbolea udongoni. Nilikulia katika jimbo la Free ambapo mahindi hulimwa sana. Wakati mwingine katika utiaji wa mbolea maeneo mengi husahauliwa. Hii inakuja kuonekana wakati mahindi yana urefu wa kama mita moja. Wakati mahindi yamefikia ukomavu inadhihirika jinsi yasiyo na mbolea yamenyongea.

Kadhalika kanisani, kutaniko linapolishwa vema inaonekana au pengine ni dhahiri zaidi wakati usipokuwa na lishe bora.

4.1. MAFUNDISHOWaamini wachanga na washirika yapassa waimarishwe katika Neno la Mungu, vinginevyo watanyongea kiroho na kutekwa na mafundisho potofu. Ni muhimu kwamba kila mwamini aimarishwe.

Vipo viwango viwili vya mafundisho; kiwangocha “Maziwa” na kiwango cha “Nyama ngumu”. Ni muhimu wachanga wapewe “Maziwa” mara kwa mara, lakini yapaswa wasonge kwenye “nyama” za Neno na hadtimaye.

1Korintho 3:2“Naliwanywesha maziwa, sikuwalisha chakula, kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza”.

Ebrania 5: 12 – 13“Kwa maana iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita). Mnahitaji

kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu, nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu! 13 kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui

sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga.

1Petro 2:2“Kama watoto wachanga walizaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili

kwa hayo mpata kuukulia wokovu.”

Ni mafundisho gani ya msingi yapaswayo kufundishwa? Maswala kama ubatizo, meza ya Bwana, Zaka, Mwili wa Kristo, Roho Mtakatifu, Kusikia sauti ya Mungu, Ubaba wa Mungu na nyakati za mwisho, yapasa kufundishwa tokea siku ya kwnza.

4.2. UANAFUNZIKufundisha yapasa kuzae uanafunzi. Paulo akamwambia Timotheo. “Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya wengi, hayo wakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine” (2 Timotheo 2:2)

Hapa tena ndipo makanisa ya nyumbani yanapokuwa muhimu. Yamelenga katika uanafunzi, kumbuka uanafunzi hauwezi kufanywa kwa mazingira ya darasani. Uanafunzi hufanywa kwa kuwa na mtangulizi, Hebu nikupe mfano toka kituo cha Kikristo cha Little Falls, huko Roodepoort, Afrika ya Kusini.

Pindi unapojiunga na moja ya makanisa ya nyumba unakuwa tayari unafanyika mwanafunzi, zipo hatua nne unazo pitia. Kila moja ya hatua hizi zimo katika kijitabu, kinachotumika kukuongoza.Baada ya kila kijitabu kuna mwisho wa juma(Ijumaa jioni na Jumapili)

Vijitabu hivyo vina haya yafuatayo;

49

Page 50: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Karibu kwenye familia yako mpyaSehemu ya 1……..WokovuSehemu ya 2…… Dhambi ni nini?Sehemu ya 3……Ubatizo wa maji mengiSehemu ya 4…Kuanza uhusiano na MunguSehemu ya 5…...Kujenga uhusiano na familia yako mpya.Sehemu ya 6…..Kukua katika neno la MunguSehemu ya 7…..Maombi – mawasiliano muhimu na Mungu.Sehemu ya 8….KusameheSehemu ya 9….Meza ya BwanaSehemu ya 10…..Ubwana wa KristoSehemu ya 11…..Kauli yetu ya ImaniSehemuya 12…...Tathmini ya kumaliza na hitimisho.

Kijitabu cha pili; Ushindi wa Kiroho Sehemu ya 1…….Roho, Nafsi na MwiliSehemu ya 2……...Mawazouwanja wa mapambanoSehemu ya 3…….Kuzitambua ngomeSehemu ya 4…….Nafasi ya Roho MtakatifuSehemu ya 5……Mizigo ya Kiroho(vizuizi)Sehemu ya 6…….Kutunzaviwango vya ufalmeSehemu ya 7……Nafasi yako katika familia ya MunguSehemu ya 8…...Tathmini

Kijitabu cha tatu; Kuwafikia Waliopotea Sehemu ya 1…....Hatua za uvunaji RohoSehemu ya 2………Ainaza UinjilistiSehemu ya 3……….Mahusiano ya “Oiko”Sehmu ya 4……….Ushuhudawangu BinafsiSehemu ya 5 ……..Mpango waWokovu kwa MwanadamuSehemu ya 6……..Tathmini ya kumaliza na hitimisho

Kijitabu cha Nne; Kuendeleza uwezo wako wa Uongozi. Sehemu ya 1……..Umuhimu wa UanafunziSehemu ya 2……Sifa za Timotheo/Tito.Sehemu ya 3…….Kuutikia Mwito wa MunguSehemu ya 4…….Viwango vya uongoziSehemu ya 5…….Sifa na Tabia za UongoziSehemu ya 6……..Kiongoza bora ataongoza…Sehemu ya 7……..Funguo za UongoziSehemu ya 8……..Tathmini ya kumaliza na hitimisho.

50

Page 51: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Wakristo wapya wanapitia katika masumbufu mengi kama vile wanavyoingia katika mtindo mpya wa maisha. Haya ni baadhi tu ya machache kati ya ushauri uliochukuliwa katika kozi ya Omega inayoiliyonakiliwa na Alliance for Saturation Church Planting.

MATATIZO WANAHITAJI NINI

Wanashindwa kuelewa baadhi ya funguo za Kibiblia.

Labda kama mtu atashindwa kwasababu au haelewi kusudi la Mungu kwake au haelewi kwa uhalisi kweli ninini, hajui kuishi kwa imani kwasababu hajui tumaini alilonalo kwa Kristo.

Labda haelewi msaada wa Mungu kwake kupitia Yesu, na katika mwili wa Kristo, kwasababu haelewi upendo wa kristo kwake, pia haelewi kwa uhalisi kumpenda Mungu na kuwapenda wengine au kwasababu haelewi ninini maana ya kuwa mwili wa Kristo, na kadhalika

Kusahihishwa na kufundishwa jinsi halisi ya kuwasiliana katika kweli ya kibiblia ambayo hawaielewi na jinsi ya kuitumia katika maisha yao.

Nafasi ya kusoma Biblia kwa kina zaidi.

Kuwatia moyo kuwa wanafunzi wa Neno na kuwaelekeza yawapasayo.

Kuwapa nafasi kuchunguza watu wanaoonyeshsa maana halisi ya kweli katika maisha yao.

Hawajui cha kufanya kinachohitajika.

Hawaelewi kwa uhakika wafanye nini na kwa jinsi gani. Labda inatakiwa ifanye kwa mtu binafsi kutembea na Mungu (Mfano: kuomba, kusoma Biblia, kuwa na muda wa kimya na mengine

Au, labda ni kufanya jambo la kivitendo kwa wengine (kwa mfano: kufundisha, kutia moyo, kuongoza maombi katika familia, kutoa ushuhuda, kushiriki Injili na wasioamin, na mengine).

Kuwatia moyo kutumia kile walichojifunza.

Kuwapa nafasi ya kuwachunguza watu jinsi wanavyofanya kwa yale wanayotakiwa kuyafanya.

Kuwaelekeza na mafundisho ya kivitendo kwa yale waliyojifunza.

Kama itahitajika, kuwasaidia kuendeleza mbinu za kivitendo ambazo zinahitajika.

Kuwa na nafasi muafaka ya kufanyia mazoezi kwa yale waliyojifunza, na kwa msaada wa jinsi ilivyo.

Ushauri wa kivitendo na kuwaisia kama inavyoendeleza ujasiri na ufahamu.

51

Page 52: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

52

HATUA ZA

UPANDIKIZAJI WA

KANISA

5. Kumwagilia maji udongo

Page 53: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

5. KUUMWAGILIA MAJI UDONGO

1 Korintho 3:6 – 10“Mimi nalipanda, Apolo akatia maji bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo apandaye sikitu

wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. Basi yeye apandaye na yaya atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yke mwenyewe sawasawa na taabu yake

mwenyewe.9 Maana sisi tu wafanyakazi pamoja na Mungu ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.

“Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi kama mkuu wa wajenzi wenye hekima, naliweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie

anavyojenga juu yake”.Paulo anasema Apollo alitia maji. (Ishara mojawapo ya Roho Mtakatifu ni maji). Hii

inaniambia kuwa Paulo aliweka msingi, alilianzisha kanisa likaendelea Apollo akalilea likakuwa, kulea kundi yafuatayo yanahitajika:

5.1. KUPATA UJUZI WA ROHO MTAKATIFUWakati Apollo alipo kuwa Korintho, Paulo alichukua njia ya ndani na kuwasili Efeso. Hapo aliwakuta wanafunzi wawili na akawauliza. “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipo amini?” Wakajibu “La hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, ubatizo wa Yohana. “Paulo akasema, Yohana alibatiza ubatizo wa toba , akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake yaani Yesu. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu, “Na Paulo alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao, wakaanza kunena kwa lugha na kutabiri”. Matendo 19: 1 – 6.

Rafiki yangu mmoja alinipatia maneno haya ya hekima. “Maneno matupu bila Roho – unakauka; Roho tu bila Neno, unapasuka; Neno na Roho – unakua!”Watu hutaka kuwa na uwepo wa Mungu waingiapo katika kanisa wamechoshwa na maonyesho tu na jumbe kavu zisizo na uvuvio. Wanataka kuuhisi uwepo wa Mungu. Huwezi kuliendesha kanisa vyema kama hutampa Roho Mtakatifu nafasi yake.

5.2. KUFUNDISHA CHAKULA KIGUMU CHA NENO“Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki kwa kuwa ni mtoto

mchanga. Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima ambao akili zao kwa kutumiwa, Zimezoezwa kupambanua mema na mabaya”

Ebrania 5:13 – 14.

Yapasa tuzingatie kuwakomaza watu wa Mungu. Sababu halisi kwa nini wachungaji wengi wanawashauri watu wale wale, tena na tene ni kwasababu hawajakomaa katika Bwana.

5.3. KUWAPA ZANAKuwapa zana waamini ni zaidi tu ya kuwafundisha. Ni kuwapa “Matunzo kazini” Mafunzo mengi hutolewa darasani au kwa mawasiliano ya barua. Je, Umeshawahi kusikia mtu akipewa somo la “Jinsi ya kuogelea” kwa mawasiliano ya barua? Lakini ndivyo tufanyavyo katika mwili wa Kristo.

“Naye alitoa wengine kuwa mitume na wengine kuwa manabii na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa sudi la kuwakamilisha watakatifu, hata

kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe, hata na sisi sote tutakapo ufikia umoja wa imani na kumfahmu sana mwana wa Mungu hata kuwa mtu mkamilifu, hata

kufikia kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo” Efeso 4:11 – 13

53

Page 54: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Tunaelezea jambo toka madhabahuni na kisha kuwatarajia viongozi kulifanya kadhalika na mchungaji ambaye amekuwa na fursa ya kujitunza na kadhalika kupata ujuzi wa thamani kubwa.

5.4. MAFUNDISHO YA UONGOZIUkishindwa kufundisha – unafundisha kushindwa. Kila kitu huinuka na kuanguka kutegemea uongozi.Zipo sita na tabia nyingi za mpanda makanisa, ambazo ninazielezea kwa kina katika sura ya nane ya jarida hli. Lakini kuna “Kambi” moja maalum, ambapo viongozi wanafunzwa na kupewa zana kwa ufanisi zaidi kuliko pengine popote. Kambi ya Mungu ya mafunzo ya binafsi haiwezi kuwakilishwa na chuo chochote cha Biblia au seminary.

Hebu natuangalie baadhi ya masomo ambayo yamo katika mtaala wa mafunzo ya shule hii.

UWANJA WA MUNGU WA MAFUNZO

2 Timotheo 2: 15Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtendakazi asiye na sababu ya

kutahayari, ukitumia kua halali neno la kweli.

UTANGULIZIMungu anapoita, hutia upako na kutoa zana, Ni kama vile Daudi alivyosema “Anifundisha mikono yangu vita “ (Zab 18: 34). Kuna mambo kadhaa ambayo chuo cha Biblia hakiwezi kukupatia, wala kukufundisha.

Baada ya kufuzu toka katika chuo cha mafunzo rasmi ya theolojia. Nilijikuta kwenye shule tatu za ziada. Niligundua pia kuwa Mungu mwenyewe ndiye Profesa na anatengeneza mtaala wake.

Viongozi wote wa Kikristo yawapasa kupitia shule hizi iwapo tutataka kuligawanya neno la kweli kwa uhalali. Shule hizi ni zipi?

1. SHULE YA ROHO MTAKATIFU

Yohana 14: 26 “Lakini huyo msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote

niliyowaambia”.

Yohana 16:13 – 14 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli , atawaongoza awatie kwenye kweli yote, kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe,

lakini yote atakayoyasikia atayanena na mambo yajayo atawapasha habari 14. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha

habari.

Si kweli zote ambazo kufumbuka kutokana na kujifunza kwa makini.1 Korintho 2: 9 – 13Zipo kweli za neno la Mungu ambazo zinafumbuliwa moja kwa moja na Roho Mtakatifu pale tunapotafakari na kuliangalia neno la Mungu. Kweli hizi zina mguso wa moja kwa moja katika maisha na lazima zijaribiwe kwa Neno la Mungu ili kwamba tusichanganyike na fikra zetu wenyewe.

Na ndiyo maana ni muhimu kufundisha watu jinsi ya kuisikia sauti ya Mungu.

54

Page 55: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

KUJIFUNZA LUGHA YA ROHO MTAKATIFU Kupitia Neno la Mungu (Rhema)Rumi 10:17Kweli yote hufunuliwa katika Neno la Mungu, (Rhema). Hakuna fundisho au ufunuo ambao unafuzu kweli isipokuwa umejaribiwa kwa maandiko. Ufunuo katika maisha ya mtu binafsi ni jambi linaloendelea, Roho Mtakatifu anatumia neno la Mungu kutulisha na kupitia kulitumia neno, tunakua.

Roho Mtakatifu hutumia njoziYoeli 2:28Biblia imejaa mifano tele ambapo Mungu anazungumza na watu wake kupitia ndoto. Ndoto hizi zimejaa mafumbo ambayo yanahitaji tafsiri. Naamini tafsiri anayo mwenye kuota ndoto.

Roho Mtakatifu hutumia MaonoMatendo 9:10 – 12Maono huweza kuwa sura za kitu halisi ambacho hucheza kama sinema. Nyakati zingine ni kama picha za ghafla katika mawazo. Daima huwa kuna jumbe ndani yake.

Roho Mtakatifu hutumia watu.Matendo 21:10 – 11Watu haawa sio wachungaji tu, bali hata watu wa kawaida na hata watoto. Unamkumbuka Samweli? Mungu alimtumia kusema na Eli.

Kupitia Maneno ya Kiroho1 Korintho 2:13 – 14Kuna misisitizo ya mionekano unayoipata mawazoni mwako. Lazima ijaribiwe kwa Neno la Mungu. Kama hailingani na na Neno la Mungu basi hilo ni jaribu. Mara nyingi haya huwa mfumo wa Neno la maarifa.

Kanisa la Mwanzo liliongozwa na Roho Mtakatifu.Matendo 13:2 – 4Iwapo Roho Mtakatifu hatakuwa na nafasi yake katika kanisa, litaongozwa kwa akili za kibinadamu na mbinu za kibinadamu. Watu walioacha kanisa la namna hii na kutafuta kanisa wanaweza kukutana na Mungu.

Ni muhimu kuwa na uhusiano na Roho Mtakatifu.2 Korintho 13:14Huduma yako itakuwa na kujengeka pale unapokuwa na ushirika na Roho Mtakatifu.

2. SHULE YA MAISHA

Jifunze kwa wengieHadithi za MafanikioNapenda kusoma juu ya mafanikio ya wengine – sio kuwaiga, bali kujifunza toka kwao kanuni walizo tumia. Hadithi za KutofanikiwaKadhalika napenda kujifunza kadri niwezavyo makosa yaw engine, hakuna vitabu vingi vyenye hadithi za walioshindwa, lakini ukiangalia ulipo utaviona haraka sana. Pata TaarifaMatukio ya Dunia

55

Page 56: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Watu huona vigumu mno kuhusiana na wachungaji ambao hunena aya za maandiko tu na ambao ufahamu wao wa historia ni Agano la kale pekee. Matukio ya dunia yatakupa dokezo la jambo la kuombea.

Mwenendo wa DuniaNi muhimu kutazama dunia inavyokwenda kuhusiana na teknolojia, viwanda na biashara. Nadhani wale watakao danganywa na mpinga Kristo ni wale watu ambao hawakutupia jicho dunia inavyokwenda. Yote haya ni muhimu kwasababu watu tunaowahudumia ndio wanaopambana na maswala haya, Wanatafuta majibu. Watu waishio Sasa wanataka majibu ya Kisasa.

Yesu aliweza Kuhusiana na Yeyote.Alitumia mifano na maelezo yaliyoweza kuhusiana na WakulimaWavuviWapemdao wanyama poriWanasiasaMafarisayoMakahaba

Paulo alikuwa mtu – Msomi.II Timotheo 4:13“Lile joho nililoliacha kwa karpo huko Troa, ujapo ulilete, na vile vitabu, hasa vile vya ngozi”.

3. SHULE YA MAPITO MAGUMU

Huduma ya Kikristo ni kuhusika katika mapambano.Mapambano ya binafsiMapambano ya watendakaziMapambano katika ndoa n.k

Ushuhuda wa PauloII Korintho 4:1,8,9“Kwasababu hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei…Pande zote twadhikika, bali hatusongwi, twaona shaka, bali hatukati tama. “Twaudhiwa, bali hatuachwi; Twatupwa chini balihatuangamizwi”.

Ushauri wa Paulo kwa TimotheoII Timotheo 4:5“Bali wewe uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi mhubiri wa Injili timiliza huduma yako”.

Uwe Mwanafunzi ujisomaye mwenyewe. TambuaIshara za kuchoka kwa ndaniIshara za hisia zako n.k.

KUMBUKA.

“Kishada hupaa juu zaidi dhidi ya upepo na wala si kwa upepo”

_Winston Churchill

56

Page 57: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

57

HATUA ZA

UPANDIKIZAJI WA

KANISA

6. Kuondoa Magugu

Page 58: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

6. KUYAONDOA MAGUGU(Tafadhali elewa kuwa kiitwacho:- “Kuvielewa vita vya Kiroho na Ngome”). Kinapatikana katika ofisi za DAWN Africa. Angalia kwenye FOMU ZA MAOMBI nyuma ya kitabu hiki cha mafunzo.

Iwapo mkulima hataondoa magugu kunako konde basi magugu haya yatayazonga mazao, kwakuwa kanisa linahusisha watu na watu wanazo ngome katika maisha yao, makanisa huweza kufungwa au hata kuharibiwa kupitia ngome hizi isipokuwa zimeharibiwa. au kushuhulikiwa.

KUVIELEWA VITA VYA KIROHOVita vya Kiroho sio nini:1. Sio vita kati ya mema na mabaya2. Sio vita kati ya Mungu na shetani3. Sio kumpigaia kelele shetani na kumwita majina4. Sio vita ya waliochaguliwa au watakatifu wachache.

Vita vya Kiroho ninini:1. Ni Mapamano kati ya Ufalme wa Mungu na shetani kwa ajili ya roho za watu.2. Ni mpambano wa kila siku wa kiroho dhidi ya nguvu za giza.3. Ni kuimarisha utawala wa Kristo4. Ni mpambano wa kila Mkristo.

MAANAVita vya Kiroho ni mpambano wa ana kwa ana kati ya Ufalme wa Mungu, ukiongozwa na Bwana Yesu Kristo na nguvu za giza, zikiongozwa na shetani kwa ajili ya roho za watu.

TOKEA UUMBAJI HADI MSALABANI

SHETANI NDIYE ALIYE ANZA VITAIsaya 14:12 – 18 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni ewe nyoka ya alfajiri mwana waasubuhi. Jinsi ulivyokatwa kabisa ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ukasema moyoni mwako nitapanda mpaka mbiguni nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu, nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande za mwisho za kaskazininitapaa kupita vimo vya mawingu, nitafanana nay eye aliye juu, lakini utashushwa mpaka kuzimu mpaka pande za mwisho za shimo.

SHETANI NA THELUTHI YA MALAIKA WALITUPWA TOKA MBINGUNI.Ufunuo 12:4,9 “Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni …yule yule joka akatupwa yule mkubwa, nyoka wa zamani aitwaye Ibilisi na shetani audanganyaye ulimwengu wote, akatupwa hata nchi na malaika zake wakatupwa pamoja naye. SHETANI AKAWA MFALME WA ANGAEfeso 2:2 …”ambazo mlizitenda zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu na kwa mfalme wa uweza wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi”.

MUNGU ATANGAZA VITA BAADA YA ANGUKO LA MWANADAMUMwanzo 3:15 “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke na kati ya uzao wako na uzao wake, huo utakuponda kichwa, na wewe utauponda kisigino”.

TOKEA WAKATI HUO KUMEKUWA NA VITA VYA KIROHOTaifa (Israel) liliundwa ambalo ambalo lingemleta Masihi, Manabii walipigana vita vingi vya kiroho kwa ajili ya maandalizi na Yohana mbatizaji akawa ndiye mtangulizi mkuu.

58

Page 59: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

HATIMA KUU PALE MSALABANI

1 Yohana 3:8 “Atendaye dhambi ni wa ibilisi kwa kuwa hutenda dhambi tangu mwanzo kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibillisi”

Wakolosai 2:14 – 15 ”Akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumuzake iliyokuwa na uadui kwetu, akaiondoa isiwapo tena, akaigongomelea pale msalabani, 15. Akiisha kuzivua enzi na mamlaka na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akazishangilia katika msalaba huo”

Sehemu kubwa ya huduma ya Yesu ilikuwa kufungua watu kutokana na mapepo.

MAMLAKA YA KANISA

Marko 16:17 “…Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa jina langu watatoa pepo”

Efeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”

2 Korintho 10:4 “Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome”

YESU NA VITA VYA KIROHO

Yesu aliweka wazi kuwa anaanzisha vita vya kiroho. Angalia maandiko yafuatayo:

Luka 4:18 “Roho wa Bwana yu juu yangu kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupatakuona tena, kuwaacha huru waliosetwa….”

Mathayo 16;18 “Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitalishinda.

6.1. KUPAMBANA NA NGOME KATIKA KANISA

(2Wakorintho 10:3-5)“Maana ingawa tunaenenda katika mwili hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili maana silaha za

vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka , kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na

tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo”.

“Ngome” ni himaya ya kiroho ambapo mamlaka husika inamiliki, Himaya hizi zipo katika mfumo – wa – mawazo, fikra na dhana zinazomwongoza na kumtawala mtu, makanisa, jamii na hata mataifa. Katika Agano la kale ngome zilikuwa makaazi yaliyoimarishwa na kutumiwa kujilinda dhidi ya maadui. Haya yalikuwa majengo halisi, mara nyingi yalikuwa mapango yaliyokuwa juu ya milima, na ilikuwa vigumu kuyashambulia. Ni wazi Paulo anatumia neno “Ngome” kuelezea himaya za kiroho ambapo shetani na mapepo yake wanajificha na wako salama,

59

Page 60: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Himaya hizo zipo pia katika mfumo wa mawazo na dhana zinazomwongoza mtu binafsi, makanisa na jamii na mataifa.

Katika nyaraka kadhaa za mtume Paulo, Paulo anazungumzia ngome ambazo ziliyafunga makanisa hayo na kufanya ushuhuda wao kutokuwa na mguso wenye ufanisi, hebu tuyaangalie baadhi ya haya makanisa na ngome zinazohusika kuyafunga na pia makanisa matano katika kitabu cha ufunuo.

A. KANISA LA WAKORINTHOHili lilikuwa kanisa lenye tofauti nyingi. Lilikuwa kanisa lililokuwa tajiri na nguvu katika karama za rohoni. (1 Wakorintho 1:4 – 7). Lakini bado walikuwa wa kimwili sana katika maeneo mengi ya maisha ya kanisa. Paulo, kwa kuhatarisha sana maisha yake, haonyeshi hofu yoyote katika kuyanena haya. Japokuwa hayaiti kila mojawapo ngome, lakini yote yana maana ileile ya ngome. Yapasa tuelewe kuwa hatuwezi kushuhulikia ngome za jamii, mji au nchi, kama hatushughulikii ngome zetu wenyewe au zile za pamoja.

Ngome ya Magawanyiko…………… 1 Wakorintho 1:12-13 Ngome ya Uasherati………………… 1 Wakorintho 5:1-6, 6:15-18 Ngome ya Uhuru uliozidi…………… 1 8:9-13 Ngome ya Ibada yasanamu………….. 1Wakorintho 10:14-22 Ngome ya Kutomjua Mungu………... 1 Wakorintho 15:33-34 Ngome ya Kutokusamehe………….... II Wakorintho 2:2,5,11 Ngome ya Ubia na dunia…………….. II Wakorintho 6:14-18,17:1 Ngome ya Kupinga mamlaka………... II Wakorintho 10:8-13 Ngome ya uhaini (Mwenendo au lugha yenye kuchochea uasi dhidi ya mamlaka II Wakorintho 11:4 -15Ngome ya Kukosatoba…………………II Wakorintho 12:21

B. KANISA LA WAGALATIA Ngome ya Sheria ……………………..Wagalatia 3:1 – 5.Kuweka sheria kwa wakristo ambazo zipo nje ya maandiko, mfano nguo, kutoa meza ya Bwana n.k. Tafuta uwiano kati ya uhuru ulio zidi na sheria. Ngome ya dini………………………….wagalatia 4:8 – 10,15,21 -31Wana wa Hajiri au sara.

MAKANISA MATANO KWENYE KITABU CHA UFUNUOKANISA LA EFESO Ngome ya Upendo baridi…………………Ufunuo 2:4,7(“Yeye ashindaye…”)

2. KANISA LA PAGAMO Ngome ya mafundisho ya kishetani – Ufunuo 213 – 17(“Yeye ashindaye..)1Timotheo 4:1. Wanikolai = Uharibifu wa watu”kikundi kilicho tajwa katika ufunuo 2:6,15, ambao walishitakiwa kwakuyashika mafundisho ya Balaam, waliwawekea kwazo kanisa la Mungu kwa kuwanyima uhuru wa kutokula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu na kuwashirikisha uasherati.

3. KANISA LA THIATIRA Ngome ya Yezebeli…………………….Ufunuo 2:20- 26(“Yeye ashindaye…..”)“Roho ya Yezebeli “-Yezebeli alikuwa nani? Binti wa Ethbaali, Mfalme wa Ufoeniki. Huyu alikuwa kuhani wa kikanaani ambaye alipanda madarakani kwa hila na mabavu ni kisha kumfanya binti yake kuwa kuhani mkuu wa kike.

60

Page 61: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Maandiko yanatupa dokezo kupitia Maisha ya malkia Yezebeli.

1 Wafalme 16:31- Alimfanya mumewe na mfalme, Ahabu amtumikie Baali yaani roho ya Yezebeli inarubani viongozi wakanisa na waume na kuthubutu kuwafanya wamwache Mungu. Anatumia ngono na mabavu kufanikisha hili, kwa kupata faida yake tu.

1 Wafalme 18:19 – Aliweka manabii wake yaani aliingiza mafundisho ya uongo na mifumo ya kidini.

1 Wafalme 21:16 – Alinyakua madaraka ya kuwa kiongozi wa familia na taifa, yaani, anatafuta kuleta mageuzi ya majukumu kwenye kanisa na nyumbani katika familia. Elewa kwamba ushoga na kubadili kabisa majukumu halali na vyama vya haki za wanawake hutafuta kukomesha kubadilisha mfumo wa kibiblia wa uongozi.

2 Wafalme 9:30 – Hurubuni wanaume kujamiiana nao, yaani hujaribu kurubuni viongozi wa kanisa na waume za watu kulala nao. Tazama anguko la wainjilisti wa kwenye luninga (TV) na kiwango cha juu mno cha kutalikiana na uzinzi katika mataifa. Angalia ufunuo 2:20 kwa mafunnuo zaidi.

DALILI KUU ZA ROHO YA YEZEBELI. Ni roho ya Kumiliki; Roho hii hutumia mtu mwingine kuwamiliki viongozi na

hivyo kanisa na hata taifa. Roho hii huunda wakina “Ahab” katika viongozi. Roho ya Mabavu, Ni roho ambayo itamwangamiza yeyote ili tu kuweza kupata

matakwa yake. Ni Roho ya Uasherati,Roho hii hutumia ushoga, Usagaji, Ukahaba, Picha za

ngono na namna yoyote ya uchafu ya kujamiiana ili tu kugeuza mpango wa kibiblia wa uongozi.

Ni Roho ya Kuabudu sanamu, Roho hii huingiza mafundisho ya uongozi na mifumo ya kidini katika kuwazuia mateka wake wasipate ujuzi halisi wa Mungu kwa utimilifu wake.

Ni roho ya Ukengeufu, Roho hii ipo makusudi ili kugeuza mpango wa Mungu uliokusudiwa. Huongoza vyama vya kina mama vya madai ya usawa na kadhalika kudhoofisha jukumu la kiungu la uongozi la mume.

Roho ya Uchawi. atatumia karama za bandia kulipenyeza kanisa yaani aweza kutumia unabii (Kubashiri). Daima tii unabii binafsi kwa viongozi wako tu.

4. KANISA LA SARDII Ngome ya mauti ya kiroho – Ufunuo 3:1- 5 (“Yeye ashindaye…”)

5. KANISA LA LAODIKIA Ngome ya Uvuguvugu – Ufunuo 3:14 – 21 (“kwa Yeye ashindaye”)

Ngome zote hizi zilikuwandani ya kanisa, zilikaa ndani ya watu.

6.2. KUZISHUGHULIKIA NGOME KATIKA MAHUSIANO

61

Page 62: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Ni vema daima kuyaangalia matatizo ya mahusiano katika kanisa. Makanisa mengi hugawanyika kwa sababu ya matatizo ya mahusiano. Hii ndio maana Paulo anawaambia Waefeso.

“Kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkickuliana kwa upendo, na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungu cha amani”. Efeso 4:2 – 3.

JINSI YA KUZIVUNJA NGOME.

UTANGULIZISwali ambalo huulizwa mara kwa mara ni hili: “Je, naweza kuvunja ngome yangu mwenyewe?. Jibu ni ndiyo na hapana. Kwa maombi na kufunga waweza ukavunja ngome yako lakini ni vigumu kuchukua mamlaka dhidi ya kitu ambacho mamlaka juu yako. utahitaji mtu akusaidie, Jihadhari na majivuno.

UTAYARI WA KUTUBU. Yapasa mtu awe na utayari wa kutubu na kuona kuwa ngome yake ina dhambi. Yapasa mhusika awe na utayari wa kujisalimisha kwa Kristo. Katika hatua hii waweza kuwapoteza wengine na usiweze kuwasaidia Msamaha ni muhimu.

KUZITAMBUA NGOME Kupitia kuzitambua ishara za wazi, matendo, dhambi, na historia ya mhusika. Kupitia karama za Roho Mtakatifu. Kutambua roho – 1 Korintho 12:10

Mfano; Matendo 16::16-18 Neno la Maarifa – 1 Korintho 12:8Mfano: Matendo 5:1 – 11

KUFUNGA NA KUFUNGUA. Yesu alisema “Lakini nmimi nikitoa pepo kwaRoho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? ndipo atakapoiteka nyumba yake”. Mathayo 12:28 – 29 “Nami nakuambia wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni na lolote utakalolifungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni, na mtakalo lifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni” Mathayo 16:19-19 Ifunge roho kwa kutamka neno.

Wakati mwingine unahitaji kutumia muda kwenye kufunga na kufanya maombi.Mathayo 17:14-21 “Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti akisema 15 Bwana umrehemu mwanangu kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na maranyingi majini, 16 Nikamleta kwa wanafunzi wakko wasiweze kumponya. 17 Yesu akajibu, akasema. Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini?

Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu 18 Yesu akamkemea pepo, naye akamtoa, yule kijana akapona saa ile kisha wale wanafunzi wale wanafunzi wakamwendea yesu kwa faragha wakasema, Mbona sisi hatukuweza kumtoa?20 Yesu

62

Page 63: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

akawaambia, kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana amin nawaambia mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu ondoka hapa uende kule nao utaondoka; wala hakutakuwepo neno lisilowezekana wenu. 21 “Lakini namna hitoki il kwa kusali na kufunga”

KUAMURU Mapato yanaelewa mamlaka na yanaelewa pia usipokuwa nayo Yesu alisema

“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani”Mathayo 28:18 LAKINI baadhi ya Wayahudi wenye kutanga tanga nao ni Wapunga pepo,

wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.14Walikuwako wana saba wa mtu mmoja, Skewa, Myahudi, Kuhani mkuu, waliofanya hivyo 15 Yule pepo mchafu akawajibu akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini nyinyi ni nani? 16 Na yule mtu aliyepagawa na pepo akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa”

Matendo ya Mitume 19:13 – 16 Yapasa uwe na imani katika Jina na nguvu ya Yesu.

Yapasa uwe salama katika mamlaka aliyokupa Yesu.

Usitoshwe na ukaidi wao, lazima watoke.

Wakumbushe alichofanya Yesu pale msalabani

UPONYAJI WA NDANI Mara nyingi watu watahitaji uponyaji wa kumbukumbu (matukio ya siku za nyuma

kama picha) katika matukio kama ubakaji wa watoto. Hatua za uponyaji wa ndani Uponyaji wa Agape.

Nilijifunza maelekezo haya toka kwa Marko vilevileNO HATUA MFANO WA BIBLIA

(Petro: Math 26:69-75; Yoh. 21:2-17)1 Kutumia Maono, rudi nyuma

liguse upya jerahaMoto, mapambazuko, Ungamo mara tatu

2 Kutumia Maono, nilete Yesu dimbani

“Yesu alisimama pwani…….”

3 Kutumia Maono, mwache Yesu atembee akiponya majeraha kwa uwepo wake wa upendo

Kauli ya Yesu kuthibitisha Upendo “Lisha kondoo wangu” “Chunga kondoo wangu” “Lisha wana kondoo wangu”

HUU UWE UJUZI HAISIO ZOEZI LA TAALUMA TU

MAMBO MUHIMU YA KUKUMBUKA Biblia sio jarida juu ya Ukombozi Mengi hufahamika kwa kujaribu na kukosea Linalofanya kazi kwangu sio lazima lifanye kwako pia Tahadhari kadhaa

TAHADHARI Usiwe peke yako na mtu wa jinsia tofauti isipokuwa katika mazingira ya fani

maalum

63

Page 64: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Usiwe na haraka wakati wa huduma Usibabaike uonapo hakuna kinachotokea Usipige kelele na kumtikisa mtu Usitumie nguvu Usipoteze ujasiri Usiogope kuomba msaada

JINSI YA KUJIWEKA HURU NA NGOME

Iwapo umewekwa huru toka katika ngome (2Korintho 10:3-5), sio mwisho wa vita vyako bali ni mwanzo. Ni jambo la kwawaida kwamba shetani atafaribu kila awezalo kuitwaa upya himaya aliyoipoteza.

2 Korintho 2:11 “ …….. Shetani asije akapata kutushinda kwa maana hatukosi kuzijua fikra zake”

Efeso 6:11 “Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani”

Napenda nikushirikishe kanuni kadhaa ambazo zitakusaidia kukaa huru. Kumbuka tu kwamba, unayo fursa kubwa kwa kuwa “ ………….yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia” (1Yohana 4:4b)

Vaa silaha zote za Mungu (Efeso 6:11-18)Silaha hizi ulizipewa kwa ajili ya kujilinda na kumshambulia ibilisi. Watu wengi hipigana na shetani anaposhambulia tu. Si dhani kuwa hiyo ni mbinu bora. Hakuna mtu anayejilinda tu anayetegemea kushinda. Sio shetani aliyetangaza vita dhidi yetu. ni ufalme wetu ambao umetangaza vita dhidi yake. 1Yohana 3:8. “Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi.”

Mtii MunguYakobo 4;7 “Basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani, naye atawakimbia”Ninapo mtii Mungu, ninajiweka chini ya mwambuli wa ulinzi wake Hapa basi ninakuwa wazi kwa sauti yake na amri zake. Utii wangu kwake unanipa uhakika wa uhuru dhidi ya ngome.

Mpinge Shetani“…Mpingeni Shetani, naye atawakimbia”Huwezi kumpinga shetani kikamilifu iwapo hujajitiisha kwa Mungu. Lakini unapomtiiMungu unaweza kumpinga shetani kakamilifu. Tutakuwa wazi kwa majaribu maisha yetu yote lakini si zaidi ya yale tuwezayo kuyamudu. (1Koritho 10:13). Kuyapinga kwako majaribu kutakusaidia kuzivunja tabia mbaya ulizojijengea.

Ungama dhambi UpesiUkitenda dhambi usiiache bila ya kushughulikia adui asije akaitumia kujengea ngome. Uwe mwaminifu na wale uliowakosea litakusaidia kuwa huru na ngome. 1Yohana 1:9 “Tukiziungama dhambi zetu. Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote”

64

Page 65: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

“Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana mpate kuponywa” Yakobo 5:16

Fanya haraka, kwa kuwa kadiri unavyongojea ndivyo inavyokuwa vigumu zaidi.

Linda Moyo wako na Mawazo Kutokusamehe, Uchungu an Kinyongo ni ngome kuu katika maisha ya watu. Watu wa jinsi hii hawana amani mioyoni mwao na mawazoni mwao kwa sababu ya mapambano wanayobeba. (arko 11:25-26) Jifnze kusamehe kama Yes alivyotusamehe. Ufanyapo hivyo amani ya Mungu itakulinda. (Wafilipi 4:6-8)

JiimarisheKwanza, ni muhimu mno kutumia muda wa kutosha na Mungu katika kusoma na maombi. Soma vifungu vifuatavyo:2Timotheo 2:15; Matendo 17:11; Mathayo 4:4; 1Petro 2:2; Efeso 4:12; Yakobo 1:22-25;Zaburi 119:105; 1Wakoritho 14:14-15; Yuda 20; 1 Thesalonike 5:17; Yakobo 5:16;

HITIMISHOKanisa lazima liwe na vita dhidi ya ngome badala ya wenyewe kuwa wenyewe. Tatupigani dhidi ya damu na nyama.

65

Page 66: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

66

HATUA ZA

UPANDIKIZAJI WA

KANISA

7. Kujiandaa kwa Mavuno

Page 67: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

7. KUVUNA

Kusudi zima la kupanda zao ni kupata mavuno. Kanisa lazima lipandwe kwa mtizamo kwamba litajizidisha lenyewe kuwa makutaniko mengi zaidi vinginevyo tunapandikiza makanisa tasa. Waongofu lazima wajifunze kuwa yawapasa kujizidisha wenyewe kwa kuwa wavuna roho wao wenyewe.

7.1 MRABA WA KUJIZATITI

Napenda ule mraba wa kujizatiti ambao Larry Stockstill anautumia katika kanisa lake. Unaonekana namna hii.

Yawapasa waongofu waelewe kuwa wapo safarini. Kwamba hakuokolewa ili kwenda mbinguni tu bali wana lengo katika maisha yao ya hapa duniani. Mungu anao mpango wa kuwatumia katika ufalme wake. Ndio mana kuna ukuhani wa waamini.

Kuzatiti ni zaidi ya kufundisha. Kunahusisha. Kuwa mtangulizi mafunzo-kazini-kuonyesha jinsi inavyofanyika. Ndio maana mfumo wa makanisa ya nyumbani unazalisha viongozi wengi zaidi ya mfumo wowote ule wa kanisa. Bahati mbaya makanisa mengi hupoteza viongozi wao katika huduma saidizi za kanisa na taasisi nyinginezo kwa kuwa hakuna fursa kwa wao kukua kama huduma inayojitegemea katika kanisa. Kawaida siku hizi imekuwa na wachungaji waliolelewa na kanisa.

7.2 WEKA MAONO YA UPANDIKIZAJI WA KANISA WAZI KUTANIKOkama kuzidishwa kwa kanisa kiwango kilichowekwa, maono hayo yatafifia kama si kupotea. Hebu nielezee kwa kukuuliza swali. Kwanini unapiga meno yako mswaki? Hapana shaka ni kuwa na meno yenye afya! Lakini ulianzia wapi? Ilianzia kwa wazazi ambao walikuambia upige mswaki kila siku na wakakuwajibisha kufanya hivyo kila siku. Sasa, unafanya hivyo kwa kuwa ni kiwango cha thamani.

7.3 KUZIDISHAFanya kuzidisha kanisa kuwa ni kiwango, katika kanisa lako. Pindi tu unapopanda kanisa lingine hakikisha unawawajibisha jukumu la kuzaliana kumbuka kuwa mavuno huleta mbegu kwaajili ya ukuaji.

67

Wavune Wahusishe

WatumeWafundishe

1

3 4

2

Page 68: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Ellis na Mitchell wanasema “Kama lipo kanisa ambalo haliwazi juu ya kujizalia lenyewe.. wala halitarajii au kutegemea kuwa hii ndio njia ya kiasili ya kukua, basi kanisa hilo ni tasa.”

“Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha ……( Mwanzo 1:28)

“Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa Bwana, kama maji yaifunikavyo bahari” (Habakuki 2:14)

7.4 KUWA SEHEMU YA MWENDOFikiria jinsi ya ukoo wako, uko katika familia ambayo ina vizazi vingi vya jina moja. Una vizazi ambavyo huvijui vilikotoka. Inaanzia na mume na mke ambao inazalisha watoto, ambao unazidi kuzalisha watoto hadi tunafikia tulipo. Huku ni kuongezeka kivizazi. Madhehebu yameanza kama hivi. Unaweza kuona mfano huu kwa kwa uamsho wa Wesleyan kupitia kwa John Wesley. Alianza na mwendo uliowagusa karibia ulimwengu wote na ukazidi hadi sasa.

Muhimu katika maongezeko ya Upandikizaji wa Makanisa Maono

Mara nyingi wachungaji wanaona wale kondoo wadogo walionao na kama “huduma” maana wanaangalia roho hizi. Hili ni muhimu lakini sio kimaono. Tunawahitaji watu kama John knox ambaye aliomba “Bwana, nipe Scotland au nife!” Tunawahitaji watu wenye maono wanaoweza wakaleta changamoto ya Matendo 1:8 – Yerusalemu, Yudea, Samaria na mwisho wan chi. Tunahitaji wanachangamoto ambao hawatakata tamaa mpaka kuna kanisa katika kila mahali katika jamii. Tunawahitaji wenye maono ambao wataona makanisa ambapo hamna makanisa. Ijapokuwa sio vizuri kwa viongozi kutokuwa na maono. Mwenendo mzima lazima usukumwe na Maono.

MbinuKila mkulima ana Mbinu. Kila Kamanda ana mbinu za kivita. Kila mfanyabiashara mzuri ana mbinu nzuri. Kila mtu anayetaka kuwa mpanda kanisa mzuri anahitaji mbinu kutoka Juu. Bila maombi mazuri yenye mipango ya utendaji ya kimaono yaliyo na thamani, hayatafanikiwa. Kila mmoja katika timu ya Wapanda Makanisa lazima wajue mbinu ninini na kufuata kwa ujumla.

UongoziKila Mpanda Kanisa ambaye hajafundishwa, Wapanda makanisa wengine wana maono madogo, hawawezi kuongoza mwendelezo wa Upandaji kanisa. Katika 1994 Mungu alimleta Mchungaji wa Kimalawi katika njia yangu. Henry Mkhomanya alikuwa mchungaji ambaye alisumbuka na kusanyiko lilikutana katika mkusanyiko mdogo. Akafikiri kuwa ameitwa kuwa ni Mpanda Kanisa. Nikamchukua katika mbawa zangu, na kumfunika kwa vazi langu. Henry ilibidi achangue kama atataka kukua kwa kanisa lake au kuwa Kiongozi wa mkusanyiko. Akachagua baadaye.

Leo Henry anaongoza huduma ya Antioch “Antioch Ministry”. Kila mwaka anafundisha kiasi cha Wapanda makanisa kwa muda wa miezi tisa. Wanahusika sana na kabila la Yao katika Malawi ambao kiasi cha 95% ni waislamu. Sababu za kukua huko ni kwasababu aliutoa moyo wake na ufahamu wake katika watu. Makanisa yanapandwa sasa yamezalisha makanisa mengine ambayo yanazaa makanisa mengine tena.

68

Page 69: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Viongozi lazima watoe viongozi wengine. Lazima watengeneze njia kwa ajili ya mtu aliye na vipaji katika huduma ambao watakuja kupitia yeye. Hata Yesu alifanya nafasi kwa ajili ya wengine ili wengine pia waje wafanye makuu zaidi ya yale aliyofanya.

DhabihuMungu hawezi kukupa taifa. Kama hujajiandaa kujitoa kwa taifa. Kupandwa kanisa si katika moyo wa kuzimia. Inachukua imani na dhabihu. Ni kazi nzito.

Katika Afrika nimeona Wachungaji wengi wanatoa sababu za kukosa fedha. Wanangoja kwa ajili ya Mmarekani mmoja aliye tajiri ili aje na kuwapa pesa ambayo itafanya miujiza. Kwa kufikiria huko, hautafanikiwa. Mungu atakutana nawe katika kiwango cha Imani.

Mpanda Kanisa anachukua muda mrefu na nguvu. Mtu anayeongoza mkusanyiko lazima awe tayari kujidhabihu mwenyewe kuona maono yanatimia. Kufundisha kila mmoja katika mkusanyiko lazima awe katika maono. Lakini asiishie hapo. Lazima ajihusishe na hayo.

Heshima kwa Mwili mzima wa KristoNimeona makusanyiko yanakuwa kibinafsi kwa sababu wanafikiri kuwa wanajihusisha kikamilifu katika Ufalme wa Mungu. Kiongozi mzuri wa kusanyiko ataona mbinu za wenzake. Hauwezi kufikia nchi nzima peke yako. Jifunze kubariki huduma nyingine na Mungu atabariki huduma yako. Usiwaone Wapanda Makanisa wengine kama waasi lakini kama watenda kazi wa pamoja.

69

Page 70: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

70

SIFA ZA MPANDIKIZAJI

MAKANISA

Page 71: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

Sifa za Kanisa Mpandikizaji1. SHAUKU KWA WALIOPOTEA

Ni ukweli usiofichika kuwa, isipokuwa mpanda makanisa ana shauku kwa waliopotea, atapanda kanisa linalotokana na kukamilisha washarika toka makanisa mengine. Mchungaji wa namna hiyo atazingatia kuwa na vipndi vya kuwabutia watu na huduma yake madhabahuni. Itakuwa zaidi “Mahubiri ya Mada” ambayo inaburudisha kudni. Wakristo wasioridhishwa na makanisa yao mara nyingi na kwa urahisi zaidi huvutiwa na kanisa hilo. Ijapokuwa kanisa hili linakuwa lakini ufalme hauongezeki.

Aina ya wapanda makanisa tunaowahitaji ni wale ambao wana roho ya Paulo ndani yao. Alisema “.. Kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.” (Warumi 15:20). Tunahitaji wachungaji wenye shauku kali kwa waliopotea ambao watawalenga kwa uwezo wao wote wale ambao wamepofushwa wasioone Injili/

1Timotheo 2:3-4“Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu ambaye watu wote waokolewe na kupata kujua yaliyo kweli.

2. MAWAZO YA UFALMENimesikia watu wakisema kuwa “madhehebu yametoka kwa shetani” inasikitisha sana! Ujinga ulioje! Mungu alipoumba ua, Hakuumba ua moja jeupe lenye harufu moja. Aliumba maelfu ya maua tofautu tofauti yenye harufu tofauti tofauti na hata maumbile yasiyofanana. Ni ua gani lililosahihi? Ni ua lipi ambalo ni ua zaidi kuliko mengine? Yanapokuwa yamefungwa pamoja kama shada, yanasaidiana, pasi na kunyimana kuwepo kwa mojawapo.

Efeso 4:3“Nakujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani” Tueitiwa umoja na si kufanana. Kuna tofauti kubwa sana kati ya haya mawili.Mpanda makanisa anayeheshimiwa na Mungu ni yule ambaye hatamuumiza mwili wa Kristo. Watembelee wachungaji wengine pale mjini na uwaambie ukusudiayo kuyafanya.

3. MWENYE MAONO

Mithali 29:18 “Pasipo Maono watu huacha kujizuia…..”Mpanda Makanisa yampasa awe na maono kwa maana kwamba anapata maono toka kwa Bwana.Ni muhimu kumngojea Bwana kwa Maono. Haipasi kuwa ni wazo la haraka alilolipokea akilini. Mchukue Habakuki kama mfano.

Habakuki 2:1-3“Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara nitaagalia ili nione atakaloniambia na jinsi nitakavyomjibu katika habari ya kulalamika kwangu. Bwana akanijibu akasema. Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa inafanya haraka ili kuifikilia mwisho wake. Wala haitasema uongo. Ijapokawia ingojee kwa kuwa haina budi kuja haitakawia.

71

Page 72: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

4. KUWAPENDA WATU

Hili halina haja kusemwa. Hakuna mpanda makanisa ambaye atakuwa na ufanisi iwapo hana upendo kwa watu. Kwanini kupanda kanisa kama hukuhamasishwa na upendo wa Kristo. Paulo alisema “kwa maana upendo wa Kristo watubiidiisha. Maana tumehukumu hivi ya kwamba mmoja alikufa alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote. (2Korintho 5:14) Kwa EWathesalonike alisema: “Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili ya nyote, tukiwataja katika maombi yetu” (1Wathesalonike1:2)

5. RADHI KUJITOA

Kujitoa ni sehemu ya maisha yam panda makanisa. Kuanzisha ni kazi ngumu zaidi kuliko kudumisha. Mara nyingi mpanda kanisa imepasa kujitoa na kuachana na faraja ya kanisa lililoimarika ili kwenda kuanzisha kanisa jipya au huduma mpya tokea mwanzoni kabisa. Sikiliza asemacho Paulo Mpanda makanisa.

2Wakorintho 4:7-12“Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu. Pande zote twadhikika bali hatusongwi., twaona shaka bali hatukati tama, twaudhiwa, bali hatuachwi, twatupwa chini bali hatuangamizwi. Siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti. Basi hapo mauti hufanya kazi ndani yetu, bali uzima ndani yenu”. Andiko hili ndio kauli mbiu yam panda Makanisa.

6. KUUNGWA MKONO NA FAMILIA

Ni muhimu sana kwamba mpanda kanisa aungwe mkono na familia yake. Iwapo shetani atakwenda kumvamia mpanda makanisa, itakuwa ni katika familia yake. Ni mbinu yake ya siku nyingi. Ndio maana Paulo anatoa maagizo haya kwa Timotheo.

1Timotheo 3:1-7“Ni Neno la kuaminiwa mtu akitaka kazi ya askofu, anatamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, makaribishaji, ajuaye kufundisha, si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu, bali awe mpole, si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha. Mwenye kusimamina nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu, yaani mtu asiyejua kusimamia nyumba yake mwenyewe atalitunzaje kanisa la Mungu? Wala asiwe mtu aliyeongoka karibuni, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya ibilisi. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.

7. MTUMWA

Moja ya matatizo makubwa katika huduma ya kikristo ni “kutafuta vyeo”. Hata Yesu alikumbana na tatizo hili katika huduma yake

Marko 10:35-45“ Na Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo wakamwendea, wakamwambia, Mwalimu , twataka utufanyie lolote tutakalokuomba 36 Akawaambia mwataka niwafanyie nini? 37 Wakamwambia, utujalie sisi tuketi, mmoja mkono wako wa kuume na mmoja mkono wako wa kushoto katika utukufu wako. 38 Yesu akawaambia, hamjui mnaloliomba.

Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi? 39 Wakamwambia, twaweza. Yesu akawaambia, kikombe ninyweacho mimi mtakinywea

na ubatizo nibatizwao mimi mtabatizwa. 40 Lakini habari ya kuketi mkono wangu wa

72

Page 73: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

kuume au mkono wangu wa kushoto si langu kuwapa, ila wao watapewa waliowekewa tayari. 41 Hata wale kumi waliposikia wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana. 42 Yesu akawaita akawaambia, mwajua yakuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa

mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha 43 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu atakuwa mtumishi wenu 44 na

mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu atakuwa mtumwa wa wote. 45 Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.”

Utumishi ndiyo ngazi ya juu katika kanisa. Mchungaji aweza kuliongoza kanisa kibinafsi kwa kuwatumikisha watu.

1Petro 5:2-4“Lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo, si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. 3 Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, ali kwa kujifanya kielelezo kwa lile kundi. 4 Na Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa mtaipokea taji ya utukufu ile isiyokauka”

8. BIDII YA KAZI

Mpanda makanisa lazima mtu aliyetiwa mafuta, lakini nimegundua ya kwamba upako haupaswi kuwa sababu ya uvivu. Upako huingia wakati kazi ngumu imefanyika. Lakini huwezi vilevile kubadili upako kwa kazi ngumuk. Vyote vinakwenda pamoja. Ni rahisi mno kuwa mvivu katika huduma lakini niamini, hatimaye inaonekana wazi.

9 UTIMILIFU/UNYOOFU

Watu hupata viongozi watimilifu, wanyoofu. Iwapo mpanda kanisa anataka jamii imkubali na kumheshimu, itakuwa ni kwa sababu ya utimilifu anaoudhihirisha katika kupandikiza kanisa na jinsi anavyoliongoza kanisa. Kama ukiwarubuni washirika kutoka makanisa mengine hiyo italichafua jina la kanisa na utimilifu wako. Kwanini hawakuweza kumyooshea Yesu vidole na kumkamata na hatia ya lolote lile? Ni sababu ya utimilifu wake.

10. UNYENYEKEVU

Mpanda makanisa yapasa awe na mtizamo wa Yesu. (Wafilipi 2:5-11)Yesu alijinyenyekeza. Isipokuwa tumejinyenyekeza wenyewe itabidi Mungu atumie hatua za kuumba unyenyekevu ndani yetu. Hii huweza kuwa hali ya kuumiza sana na wakati mwingine hughadhibisha. Vema ujinyenyekeze mwenyewe kuliko unyenyekezwe na Mungu.

73

Page 74: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

74

VIKWAZO VYA

KUEPUKA

Page 75: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

VIKWAZO VYA KUEPUKA

Wakati mwingine tunajikwaa kwenye vikwazo, ambavyo kutegemeana na sababu mbalimbali, vinaweza kutufanya tukose msimamo kwa muda au daima. Ni muhimu kuwa macho na makini juu ya vikwazo vilivyo njiani ili kwamba tuweze kuviepuka. Baadhi ya vikwazo hivyo ni hivi hapa.

MPANDA MAKANISA ANACHUKULIA MAOMBI NI VITA VYA KIROHO KIRAHISI

Iwapo maombi yatapuuzwa matokeo yake yatakuwa maamuzi mengi kufanywa kwa ufahamu tu wa kibinadamu na hata kuondoa uwezekano wa miujiza na matokeo ya kiungu. Kumbuka daima Mungu hulipa maono yake.

Iwapo mpanda makanisa atadharau vita vya kiroho atakaa na kanisa lililojaa ngome na anakuwa ni mlengwa wazi wa shetani. Lazima kuleta silaha za kimungu katika vita.

MPANDA MAKANISA ANAJARIBU KUPANDA KANISA LA KUMFIKIA KILA MTU BADALA YA WALENGWA MAALUM.

Kanisa lako halitaweza kumfikia kila mtu, bila kujali mila, mifumo ya kijamii na jumuiya husika. Watu matajiri hawatakuja mahali walipojaa watu maskini mno. Tunaweza kuwa wa kiroho mno na kusema ni kiburi, lakini ukweliunabakia “ndege walofanana manyoya hukaa pamoja” kwa watu kuwa na uhusiano wa karibu. Lazima wawe na mambo yanayofanana. Hii huitwa “umoja was are” (“homogenous units”}

Lenga jamii fulani ya watu ambao wanajisikia kuwa pamoja na ambao waweza kushirikishana mengi..

HUANZISHA KANISA MAPEMA MNOWakati upande makanisa anapokosa subira na kukata njia za mkato kwene kupandikiza kanisayaweza kuleta maafa hatimaye Mungu kufanya kazi kwa majira na nyakati. Usidharau hilo.

KANISA KUWA TUKIO LA JUMAPILIKama Mpanda kanisa anajenga mila ya kanisa jumapili. Kanisa lake litaishia kwenye kujitoa kwa “Ukristo wa siku moja kwa juma” Sasa linakuwa swala la kwenda kanisani badala ya kuwa kanisa – kwenda kusikiliza ujumbe badala ya kuwa jumbe zilizo kutubiwa.

HOFU YA KUONGELEA JUU YA FEDHA HADI KUNAPOKUWA NA DHARURANdiyo, wakristo wametumiwa nwa watumishi waombao fedha. Lakini, hatuwezi kumtupamwana na mbeleko. Kuna maandiko mengi yanayohamasisha utoaji kwa mwamini. Zipo ahadi ziwezazo kuwa halisi pale tunapotoa.Kutoa zaka na sadaka ni sehemu ya ujuzi wa kikristo kama yalivyo maombi! Tunahitaji kuwaambia watu mambo haya, sio kupata fedha kwa njia hiyo, bali kwamba waweze kubarikiwa.

75

Page 76: Agiza toka: - Judea Harvest · Web viewHii inahusisha kuweka ufahamu wetu wa nguvu za Kiroho na matukio katika ulimwengu wa Kiroho katika maeneo na mazingira kwenye dunia halisi ya

KUWEKA WATU KWENYE UONGOZI MAPEMA

Paulo anasema kiongozi asiwe mtu aliyeongoka karibuni asije akajivuna. (1Timotheo 3:6). Ni rahisi kumchagua mtu kuliko kumwondoa. Usimchague mtu kwa sababu ya cheo katika jamii. Usimchague mtu kwa uwezo wake wa kifedha.

KUFANYA JAMBO SAHIHI WAKATI USIO SAHIHI

Usifanye jambo mpaka kila mtu ameelewa kwa nini naye atakufuata. Kiongozi mwema atawachukua watu wake pamoja naye.

KUSHINDWA KULIKUMBUSHA KANISA KUWA WATAONGEZEKA

Maono lazima yawekwe wazi na mapya mbele za watu vinginevyo wanaweza kusahau. Maono yawe na msingi wa viwango. Tokea mwanzo lazima watu wajue kuwa kuzaliana ni kiwango kisicho na mjadala toka katika Neno la Mungu. Panga kanisa lako inavyostahili.Vipo vikwazo utakavyo vigundua utakapoanza kupandikiza makanisa. Lakini kaza macho yako kwa Yesu, kuwa msikivu kwa sauti ya Yako, hutaangushwa na vikwazo hivyo.

“Maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari”

(Isaya 11:9)

76