50
HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU 1984 – 2017

HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

  • Upload
    others

  • View
    48

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

HISTORIA YA PAROKIA

YA

MAKONGO JUU

1984 – 2017

Page 2: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

Shukurani

Katika Zaburi ya 92: 1 twaimba ‘Ni neno jema kumshukuru BWANA,

Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu’.

Kwa niaba ya Wanaparokia ya Bikira Maria Mama wa Rozari Takatifu Makongo Juu, ninapenda kutoa shukurani zangu za dhati kabisa kwa Yeye aliye juu kwa uema wake kwa Wanaparokia ya Makongo Juu ambaye “kwa imani yetu Yeye ametuleta katika hali hii ya neema ya Mungu ambamo sasa tunaishi (Rej: Rum:5:2).

Unapotaka kuzungumzia Familia ya Mungu Makongo Juu, unaanzia pale ambapo BWANA alianza taratibu kukusanya kundi dogo miaka 33 iliyopita. Katika mwaka huu wa 2017, tunaadhimisha miaka 10 ya kuwa Parokia na sio miaka ya kuwa kusanyiko la Mungu. Katika historia ya Kanisa, miaka kumi si mingi; lakini Wahenga alisema ukitaka kujua maendeleo ya mtu usiangalie alipo, bali geuka nyuma uangalie alikotoka.

Sisi tunamshukuru Mungu kwa kuwa, akiwa amelikusanya kundi lake ‘kama vile kuku akusanyavyo vifaranga chini ya mabawa yake’ (Rej Lk 13:34) alitujalia neema pia ya kukubali kukusanywa – kutoka kikundi kidogo cha Wanarozari mwaka 1984 hadi Parokia inayojitegemea na kutegemewa mwaka 2017.

Tunamshukuru Mungu pia kwa ajili ya uongozi wa wachungaji wake, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Laurian Kardinali Rugambwa na sasa Mwadhama Policarp Kardinali Pengo. Bila uchungaji wao makini ‘tungeteketea kama kichaka motoni’ (Rej Zab. 118:2).

Katika kipindi chote hicho, BWANA ametulinda na kutujalia wachungaji wenye bidii katika nafasi mbalimbali.

Shukurani pia ziende kwa waamini waliokuwa wanajitolea

i

Page 3: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

sana tangu mwanzoni mwa kusanyiko hili - katika hatua mbalimbali hadi sasa tunapotimiza miaka 10 ya kuwa Parokia.

Ninapenda pia kuwashukuru wajumbe wa Halmashauri ya Walei parokiani ambao walipata wazo la kuandika kijitabu hiki ili kiunganishe pia historia mbili zilizokuwa zimeandikwa awali pamoja na kuingiza masimulizi mapya.

Shukurani pia ziende kwa wasimulizi waliokuwa na kumbukumbu, ambazo nyingine hazikuwa zimeandikwa – kama vile Mzee Benedict Mwobhahe, Mzee Severine Gaspar Lyaruu, Mzee Timothy Kasella walioshiriki katika hatua za mwanzoni za kujikusanya na kijana Raphael Msangi ambaye alikuwa mtoto wa miaka 10 wakati BWANA anaanza kukusanya familia hii.

Mwisho, lakini sio kwa umuhimu, ninamshukuru kila mmoja wetu. Kwa hakika hakuna mmoja ambaye hana mchango wowote katika hatua hii, kama ilivyo hakuna mmoja ambaye anamiliki mafanikio haya yeye peke yake.

Kristo…Tumaini Letu

Padre Joseph Massenge

Paroko – Makongo Juu

ii

Page 4: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

Waandishi

Christopher Kidanka

Betty Jayne Humplick

Wasimulizi

Benedict Mwobhahe

Severine Gaspar Lyaruu

Timothy Kasella

Raphael Msangi

Mahojiano

Dk. Raynold Mfungahema

Wahariri

Padre Joseph Massenge

Dk. Raynold Mfungahema

Agnes Namuhisa

Msanifu wa Lugha

Theresia Mbuligwe

Mhakiki wa Herufi

Revocatus Kasikila

Msanifu wa Kusara

Christopher Kidanka

Picha

Maktaba

© Kanisa Katoliki Parokia ya Makongo Juu

iii

Page 5: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

Dibaji

Kuna sababu nyingi zinazoweza kuifanya jumuiya au jamii kutafiti, kuchunguza, kuihifadhi historia yake kulingana na malengo ya jamii hiyo.

Hata hivyo, katika malengo yoyote yale, tunaweza kusema kuna sababu kuu tatu za kufanya hivyo.

Sababu ya kwanza ni kutaka kuelewa hali ya mambo ilivyokuwa hapo zamani kwa lengo la kuelimika tu au ya kuitumia hali hiyo kama kiunzi cha maelezo ya sasa na ya baadaye, au yote mawili.

Sababu ya pili ni kutaka kuelewa sababu, namna, na hali ya tukio fulani ilivyokuwa katika kipindi fulani maalumu cha wakati uliopita. Sababu ya tatu ni kutaka kuelewa kwa nini hali ya sasa ya jambo au kitu fulani iko jinsi ilivyo, kwa kuangalia matukio ya nyuma yaliyoifanya iwe hivyo.

Uandishi wa historia ya Parokia ya Makongo Juu umetokana na kumbukumbu za nyaraka na masimulizi ya kimaandishi na ya mdomo ya matukio yaliyopita kuanzia Mwaka 1984.

Mwaka 1984, Baba Mtakatifu Yohane Paulo II, aliutangaza kuwa Mwaka wa Bikira Maria Mama wa Mungu. Familia ya Mungu duniani kote ilialikwa kumuenzi Mama wa Bwana wetu Yesu Kristu kwa kusali Rozari Takatifu katika familia na katika vikundi mbalimbali vya sala.

Hapa Tanzania, Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) lilitoa mwito wa kufanyika mafundisho mbalimbali kuhusu nafasi ya Bikira Maria katika Kanisa na hasa mafundisho ya nguzo Imani (Dogma) kuwa Maria ni Mama wa Mungu, huku wanakwaya wakitakiwa kutunga nyimbo mbalimbali za kumuenzi Mama wa Mungu.

Miaka hiyo eneo la makazi la Makongo Juu lilikuwa na idadi ndogo ya waamini Wakatoliki huku wakiwa hawana mfumo wowote rasmi wa kuwa pamoja. Baraka za Bikira Maria ziliingia na kupanda mbegu za kudumu kwa familia

iv

Page 6: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

ya Mungu. Hapo, watu wawili, Benedict Momba, wakati huo akiwa ni Katekista wa kanisa dogo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiishi Makongo Juu na Evans Nsengimana mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akitokea Burundi, walikusanya baadhi ya waamini waliokuwa wakiishi Makongo Juu na kuwahamasisha kusali Rozari katika familia zao na baadaye kuunda kikundi kilichokuwa kikikutana mara mbili kwa juma kwa ajili ya kusali rozari pamoja.

v

Page 7: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

Utangulizi

Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozari takatifu, Makongo Juu iko katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Dekania ya Mtakatifu Petro. Parokia hii iko katika Manispaa ya Kinondoni.

Kwa upande wa Kaskazini, Parokia hii inapakana na Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma, Tanki Bovu; kwa upande wa Kusini inapakana na Parokia ya Mt. Maximilian Maria Kolbe - Mwenge; kwa upande wa Mashariki inapakana na Parokia ya Mt. Mikaeli Malaika Mkuu, Kawe na upande wa Magharibi inapakana na Parokia ya Utatu Mtakatifu, Changanyikeni na Parokia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Parokia ya Makongo Juu, kulingana na makadirio ya mwaka 2017 ina waamini wapatao 4000. Aidha, Parokia ina Jumuiya Ndogondogo 42 ambazo zimegawanywa katika kanda sita ambazo ni Kanda ya Mt. Toma Mtume, Kanda ya Mt. Padre Pio, Kanda ya Mt. Maria Roza, Kanda ya Mt. Agatha, Kanda ya Mt. Yohana Mbatizaji na Kanda ya Kristu Mfalme. Jumuiya ya 42 ya Mt Yohani Bosko iliundwa Septemba 2017 na ni jumuiya ya vijana Wakatoliki wanafunzi wanaokaa bweni wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya George Washington katika Kanda ya Mt Aghata.

Vyama vya Kitume na vikundi vilivyopo katika Parokia ya Makongo Juu ni Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA), Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, Legio Mariae, Uamsho wa Roho Mtakatifu (Karismatiki Katoliki), Shirikisho la Kwaya Katoliki (SHIKWAKA) na Skauti Katoliki.

Chimbuko la Parokia ya Makongo Juu ni Kikundi kidogo cha waamini waliokuwa wanasali Rozari Takatifu katika eneo la Shule ya Msingi Makongo. Hatua kwa hatua, mwaka hadi mwaka kikundi kiliongezeka na kupata hadhi ya Kigango chini ya Parokia ya Mt. Mikaeli Malaika Mkuu - Kawe mwaka 1985. Kigango hiki kiliendlea kukua na kuongezeka idadi ya waamini, na hatimaye mwaka 2007 tarehe 7 mwezi wa Julai, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam aliitangaza rasmi kuwa Parokia ya hamsini na moja (51) katika jimbo. na hatimaye kuwa Parokia kuanzia Julai 7, 2007.

vi

Page 8: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

YALIYOMO

HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU ............................i

Dibaji ......................................................................................................iv

Utangulizi .............................................................................................vi

SURA YA KWANZA:

KIKUNDI CHA KUSALI ROZARI 1984 - 1985 .............................1

1.1 Matukio Muhimu ...................................................................1

1.2 Uongozi ..................................................................................7

SURA YA PILI:

KIGANGO CHA MAKONGO JUU 1985 – 2007 ........................5

2.1. Matukio Muhimu ..................................................................52.2. Uongozi ..................................................................................72.3. Ardhi kwa Matumizi ya Kanisa ......................................102.4. Miradi ya Ujenzi ..................................................................122.4.1 Ukumbi ...................................................................................122.4.2 Nyumba ya mapadre ........................................................142.5. Jumuiya Ndogondogo za Kikristo ..............................192.6. Mpango wa Maendeleo ...................................................22

SURA YA TATU: PAROKIA YA MAKONGO JUU ...................28

3.1 Matukio muhimu ...............................................................283.2 Uongozi ................................................................................283.3 Maandalizi ya Awali ya Ujenzi wa Kanisa ..................31 3.4 Ujenzi wa Kanisa ...............................................................33

vii

Page 9: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

SURA YA KWANZA:

KIKUNDI CHA KUSALI ROZARI 1984 - 1985

1.1 Matukio Muhimu

Mwanzo wa Parokia ya Makongo Juu ni kikundi kidogo cha waamini Wakatoliki kilichokuwa kikisali Rozari Takatifu katika eneo la Shule ya Msingi Makongo Juu kuanzia mwaka 1984. Idadi ya Wanakikundi hao iliongezeka na baadaye kuanza kuadhimisha ibada ya Misa Takatifu mara moja kila mwezi. Kikundi hiki kilikuwa kikipata huduma kutoka kwa mapadre waliokuwa wanaletwa na waamini wenyewe kutoka sehemu mbalimbali jirani na mbali kutokana na kufahamiana na baadhi ya waamini hao kwa kupangiana zamu kwa waamini waliokuwa wanamiliki magari yaliyooneka imara na kuwa na uwezo wa kuhimili njia mbovu na miinuko ya eneo la Makongo Juu.

Mwaka 1984/85 Mama Getrude Mongella aliwapa ruhusa ya kusalia kwenye jengo la Shule ya Chekechea Makongo Juu, jengo alilolifadhili kulijenga katika eneo hilo la shule.

Kikundi kiliendelea kukua ambapo waamini wengine walijiunga wakiwemo: Chrisostom Mwalongo, Deo Tungaraza, Timothy Kasella, Swithan Billa, Flora Lyaruu, Sophia Kasella na Daniel Momba ambaye alikuwa mtoto wa katekista Momba.

Kikundi hiki kiliendelea kusali Rosali mara mbili kwa wiki (Jumatano na Jumapili) baadaye wakaanza kupata huduma ya ibada ya Misa Takatifu mara moja kwa mwezi siku za Jumapili baada ya kuwapata mapadre toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na mapadre wanafunzi wa chuo kikuu hicho waliokuwa wakiishi Changanyikeni kwenye nyumba ya kupanga, Baraza la Maaskofu Tanzania au nyumba ya mapadre ya Bethania (Bethania House) au kutoka Parokia ya Kawe.

1

Page 10: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

Kutokana na hamu ya kuwa na Misa kila Jumapili waamini walipanga utaratibu wa kuwafuata na kuwarudisha mapadre kwa zamu. Waamini wafuatao walifanya kazi hiyo. Mzee Silvin Mongella, Timothy Kassella, Chris Mwalongo na Benedict Mwobhahe.

Ilipofika mwaka 1985, kikundi cha kusali Rozari kilipandishwa hadhi na kuwa sehemu ya Parokia ya Kawe kama kigango. Misa ya kwanza iliadhimishwa na Padre Apolinari Kawishe aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Mt. Mikaeli Malaika Mkuu - Kawe.

Pamoja na kukiruhusu kikundi hicho kutumia majengo ya shule kwa ibada hapo awali, mwaka 1985 Serikali ilitoa agizo kuwa maeneo ya shule yasitumike kwa ibada. Agizo hili lilichochea azma ya kutafuta eneo ili kujenga jengo la kudumu kwa ajili ya kuendeshea ibada zao.

2

Maandalizi ya Ibada ya Misa Takatifu katika moja ya darasa la Shule ya Msingi Makongo Juu

Page 11: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

Kikundi kidogo cha watu 11 kilikuwa kama ile ‘mbegu iliyoanguka katika udongo mzuri, ikamea ikazaa...’ (Mt: 13:8).

Kadiri uhamasishaji ulivyozidi kushika kasi, ndivyo kikundi hiki cha wanarozari kilivyoendelea kukua kwa kupata washiriki zaidi. Familia nyingi zaidi zilijiunga na kikundi hiki na hivyo kuleta mwamko mpya na mawazo mapya ya maendeleo kiroho. Baadhi ya mawazo mapya yaliyokuja na wanarozari hawa wapya yalikuwa ni kuwepo pia utaratibu wa kuwa na Ibada ya Misa Takatifu angalau mara moja kwa mwezi.

Wazo hili liliwavutia Wanarozari wengi hivyo Septemba 1985 ujumbe ulitumwa kwa Baba Paroko wa Parokia ya Mt. Mikaeli Malaika Mkuu, Kawe kumwomba kuangalia uwezekano wa kuwa na adhimisho la Misa Takatifu walau mara moja kwa mwezi Makongo Juu.

Baba Paroko alisita kwanza kwa sababu hakuwa na uhakika kama pangalikuwa na idadi ya kutosha ya waamini kuhalalisha uwepo wa Ibada ya Misa Takatifu kila mwezi. Baada ya kuhakikishiwa kuhusu uwepo wa waamini wa kutosha alitoa ruhusa ya kuadhimishwa kwa ibada ya misa takatifu mara moja kwa mwezi.

1.2 Uongozi

Mwaka 1984 kikundi cha rozari cha waamini 11 kilipata sura na kuwa na uongozi kama ifuatavyo:

1 Teresia Kunundu Mwenyekiti

2 Severine Lyaruu M/Mwenyekiti

3 Peter Chea Mwana Rozari

4 Ester Aloyce Mwana Rozari

5 Rozaria Nyoka Mwana Rozari

3

Page 12: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

6 Veronika Nashomba Mwana Rozari

7 Peter Mboni Mwana Rozari

8 Fidelis Samweli Mwana Rozari

9 Katekista Benedict Momba Mwana Rozari

10 Evans Nsengimana Mwana Rozari

11 Amandus Yohana Mwana Rozari

4

Page 13: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

SURA YA PILI:

KIGANGO CHA MAKONGO JUU 1985 – 2007

2.1. Matukio Muhimu

Baba Paroko Padre Apolinary Kawishe wa Shirika la Mitume wa Yesu aliadhimisha Misa Takatifu kwa mara ya kwanza hapa Makongo Juu Oktoba 3, 1985. Kwa hatua hiyo, Makongo Juu ilianza kutambuliwa kama Kigango cha Parokia ya Mt. Mikaeli Malaika Mkuu Kawe.

Kutokana na idadi ya waamini kuendelea kuongezeka, mahitaji ya kiroho pia yaliongezeka. Ilipofika 1988 iliamuliwa kwamba kuwe na ibada ya Misa Takatifu kila Dominika badala ya mara moja kwa mwezi. Uamuzi huu, pamoja na kuwafurahisha mapadre, uliwatwisha mzigo mzito zaidi kwa kuwa, kwanza, walikuwa wachache na pili walikuwa hawana usafiri wa uhakika. Hivyo, kwa kushirikiana na waamini waliokuwa wanajitolea, walilazimika kubuni mbinu za kuweza kuhakikisha kuwa Ibada ya Misa Takatifu inaadhimishwa kweli kila Dominika.

Uongozi Hairakia wa Parokia ya Kawe na ule wa Chuo Kikuu ulikubaliana kuwa mapadre wa Chuo Kikuu wawe wakiadhimisha Misa Takatifu Makongo Juu kila siku ya Dominika saa 4:00 asubuhi isipokuwa Dominika ya kwanza ya kila mwezi ambapo mapadre wa Kawe wangeadhimisha Misa hiyo. Utaratibu huu wa mapadre wa Kawe kuwa wanakuja angalau mara moja kwa mwezi ulilenga kuhakikisha kwamba waamini wa Makongo Juu wanaendelea kuwa na uhusiano wa karibu na Parokia ya Kawe kwa kuwa Makongo Juu ilikuwa sehemu ya utawala wa paroko wa Kawe.

Waamini wa Makongo Juu, kwa upande wao, walipewa jukumu la kuhakikisha kuwa mapadre wa Chuo Kikuu walipata usafiri kila walipotakiwa kuja kutoa huduma hapo kigangoni.

5

Page 14: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

Pamoja na kuwa na utaratibu huu mahsusi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kigango kilikuwa kikipata huduma kutoka kwa mapadre waliokuwa wakifanya kazi katika Sekretarieti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference - TEC) Kurasini, Kituo cha Bethania kilichopo Upanga, na Nyumba Mama ya Wamisionari wa Afrika (Atiman House) iliyopo jirani na Kanisa Kuu la Mt. Yosef wakati mapadre kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walipokosekana.

Mapadre wa Chuo Kikuu waliokuwa wakihudumia kigango hiki walikuwa ni Prof. Padre Daniel Mkude na Prof. Padre Cosmas Mogella. Kwa upande wa TEC alikuwa Padre Method Kilaini, ambaye baadaye alikuja kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Padre Paul Haule. Kutoka Nyumba Mama ya Wamisionari wa Afrika alikuwa ni Padre Wolfgang na kutoka Bethania House alikuwa ni Padre Canute Mlowe.

Mapadre hawa walihakikisha kuwa haitokei hata Dominika moja ambapo kondoo wa Bwana wa Makongo Juu walibaki bila mchungaji.

6

Mama Getrude Mongella akisoma somo katika ibada ya Komunio ya Kwanza iliyofanyika Shule ya Msingi Makongo Juu.

Page 15: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

2.2. Uongozi

1985 – 1988

Na Jina Nafasi

1 Padre Apolinary Kawishe Paroko Kawe

2 Edward Makene Mwenyekiti Kigango

3 Swithan Billa Katibu

4 Mama Mizambwa Mhazini

1988 - 1989

Na Jina Nafasi

1 Padre Ernest Ntura Paroko Kawe

2 Edward Makene Mwenyekiti Kigango

3 Swithan Billa Katibu

4 Mama Mizambwa Mhazini

1989 – 1991

Na Jina Nafasi

1 Padre Judas Shayo Paroko - Kawe

2 Chrisostom Mwalongo M/kiti Halmashauri

3 Swithan Billa Katibu

4 Martin Busanda Mhazini

1992 – 1994

Na Jina Nafasi

1 Padre Judas Shayo Paroko - Kawe

2 Benedict Mwobhahe Mwenyekiti

3 Timonthy Kasella Makamu M.kiti/Katibu

4 Martin Busanda Mhazini

7

Page 16: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

1995 -1997

Na Jina Nafasi

1 Padre Judas Shayo Paroko - Kawe

2 Benedict Mwobhahe Mwenyekiti

3 Timothy Kasella Makamu Mwenyekiti

4 Joseph Lutege Mhazini

1998 -2000

Na Jina Nafasi

1 Padre Judas Shayo Paroko - Kawe

2 Benedict Mwobhahe Mwenyekiti

3 Timothy Kasella Katibu

4 Joseph Lutege Mhazini

2001 – 2003

Na Jina Nafasi

1 Padre Judas Shayo Paroko - Kawe

2 Dk. Raynold Mfungahema Mwenyekiti

3 John Mongella Makamu Mwenyekiti

4 Peter Mutungi Katibu

5 Agnes Namuhisa Katibu Msaidizi

6 Claudio Makwinya Mhazini

2004 -2005

Na Jina Nafasi

1 Padre Martin Dominick Rutayebesibwa

Padre Mkazi, Makongo Juu

2 Dk. Raynold Mfungahema Mwenyekiti

3 John Mongella Makamu Mwenyekiti

8

Page 17: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

4 Peter Mutungi Katibu

5 Agnes Namuhisa Katibu Msaidizi

6 Claudio Makwinya Mhazini

Oktoba 22, 2005, Kamati Tendaji, chini ya uenyekiti wa Dk. Raynold Mfungahema ilijiuzulu kutokana na sababu za baadhi ya wajumbe kuhama au kuwa na majukumu mengine nje ya Kigango. Hivyo, uchaguzi mdogo ulifanyika na Padre Mkazi akateua Kamati Tendaji nyingine.

2005 – 2006

Na Jina Nafasi

1 Padre Martin Dominick Rutayebesibwa

Padre Mkazi

2 Dk. Camilus Lekule Mwenyekiti

3 Benedict Mobhahe Makamu Mwenyekiti

4 Swithan Billa Katibu

3 Edwin Nunduma Mhazini

4 Silvia Ishengoma Mhazini Msaidizi

2006 - 2006

Februari 19, 2006, uchaguzi mdogo ulifanyika ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kufuatia kujiuzulu kwa Kamati Tendaji yote. Uchaguzi huu ulifanyika chini ya usimamizi wa Balozi Nicolaus Kuhanga, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei – Jimbo Kuu la Dar es Salaam, na hivyo, uongozi ukawa kama ifuatavyo:

Na Jina Nafasi

1 Padre Martin Dominick Rutayebesibwa

Padre Mkazi

2 Dk. Mary Mboya Mwenyekiti

3 Deo Mwarabu Makamu Mwenyekiti

4 Revocatus Kasikila Katibu

9

Page 18: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

5 Agnes Namuhisa Katibu Msaidizi

6 Chesco Sapula Mhazini

7 Silvia Ishengoma Mhazini Msaidizi

Kuanzia Agosti mosi 2006, uchaguzi wa viongozi wa Halmashauri ya Walei kijimbo na kitaifa ulianza. Katika Kigango cha Makongo Juu, uchaguzi wa Kamati Tendaji ulifanyika Septemba 17, 2006 ukisimamiwa na Paulo Sangu aliyekuwa Katibu wa Hamshauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Katika uchaguzi huo, Kamati Tendaji iliyokuwepo chini ya uongozi wa Dk. Mary Mboya ilishiriki kwa kupiga kura, lakini uongozi hairakia wa kanisa ulielekeza kwamba wasipigiwe kura kwa sababu za kichungaji. Katika uchaguzi huo, wafuatao walichaguliwa:

Na Jina Nafasi

1 Dk. Camilus Lekule Mwenyekiti

2 Benedict Mwobhahe Makamu Mwenyekiti

3 Stephen Billa Katibu

4 Theresia Wandiba Katibu Msaidizi

5 Edwin Nnunduma Mhazini

6 Margaret Ngeleja Mhazini Msaidizi

Mei 13, 2007, uongozi hairakia wa Kigango uliwasimamisha uongozi Mwenyekiti na Mhazini wa Halmashauri ya Walei ya Kigango kwa sababu za kichungaji. Viongozi waliobaki walihudumia hadi Julai 15, 2007 ambapo Askofu Mkuu, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alipoteua viongozi wa mpito kabla ya kufanyika kwa uchaguzi kwa mujibu wa katiba ya walei.

2.3. Ardhi kwa Matumizi ya Kanisa

Juhudi za mwanzo za kupata eneo kwa ajili ya matumizi ya kanisa zilifanywa na Mzee Severin Gaspar Lyaruu aliyemwomba Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa wakati huo, Mzee Mtumwa Mwinyimbegu sehemu ya kujenga

10

Page 19: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

nyumba ya ibada baada ya kutolewa agizo la Serikali kuwa shule zisitumike kama sehemu za kufanyia ibada.

Mwenyekiti Mwinyimbegu alitoa eneo dogo kama hatua 15 kwa 20 kwa maandishi kwenye njia ya ng’ombe ambapo kwa sasa ni eneo la Makaravati. Hata hivyo eneo hilo halikuendelezwa kwa vile lilionekana kuwa dogo mno kwa ajili ya matumizi ya kikundi na Kanisa.

Mzee Lyaruu aliendelea na kazi ya kutafuta eneo na kukutana na Mzee Mwanamalongo ambaye alikubali kuliuzia kanisa kiwanja kikubwa kidogo katika eneo ambalo parokia ipo kwa sasa, kwa Sh 70,000.00 baada ya ushawishi mkubwa uliofanywa na Mzee Teophil Nshiku.

Mzee Mwanamalongo aliliuza eneo kwa masharti kuwa asomeshewe watoto wake wawili msichana na mvulana; ambao walisomeshwa na Mzee Busanda kwa niaba ya kanisa hadi walipomaliza darasa la saba ambapo waliishia kwa kuwa hawakuweza kuendelea na masomo.

Mnamo Julai 10, 1988 waamini wa Makongo Juu walinunua kiwanja chenye ukubwa wa hekta kama mbili hivi kutoka kwa muumini mmoja, Mzee Yohana Ngoya Mwanamalongo, kwa kiasi cha Sh300,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa na matumizi mengine. Fedha hii ililipwa kwa awamu tatu. Muumini huyo pia alitoa bure ardhi ya ukubwa wa kama nusu ekari kwa ajili makaburi ya wakristo wakatoliki.

Katika kiwanja hiki, waamini walianza kwa kujenga kanisa dogo katika eneo ambalo kwa sasa inajengwa nyumba ya masista kwa sasa (2017). Mjenzi alikuwa ndugu Edward Mhagama lakini mpango huo uliachwa kutokana na waamini kutoafikiana.

Eneo la kanisa liendelea kuongezeka kwa kununua maeneo yaliyoko jirani na eneo la awali. Kwa mfano, mwaka 2004, lilinunuliwa eneo lenye ukubwa wa robo tatu eka kwa Sh7,0000,000 kutoka kwa mmliki wa awali Mama Miti. Fedha hiyo ilikopwa na Parokia kutoka kwa Askofu Mkuu,

11

Page 20: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam na ilifanikiwa kuzirejesha kidogo kidogo hadi deni lilipoisha.

Aidha, muumini mwingine, Timothy Nkondola alitoa eneo lake kwa ajili ya makaburi ya Wakatoliki, ambalo kinatumika hadi sasa kwa ajili hiyo.

Aidha, kazi ya kuongeza ardhi kwa ajili ya matumizi ya kanisa ilikuwa ikiendelea kwa kununua nyumba zilizo pembeni mwa eneo la kanisa. Mwaka 2013 ilinunuliwa nyumba kutoka kwa bibi aliyekuwa jirani na eneo la kanisa kwa makubaliano ya parokia kumtafutia kiwanja na kumjengea nyumba katika eneo jingine. Parokia ilinunua kiwanja huko Goba na kumjengea nyumba . Mwaka 2016 ilinunuliwa nyumba kutoka kwa Bwana na Bibi Shedrack kwa Sh80,000,000. Nyumba hiyo ilianza kutumika Septemba 2017 kama duka la WAWATA kwa ajili ya kuuza vikuza imani na mahitaji mengine.

2.4. Miradi ya Ujenzi

12

Ukumbi wa shughuli mbalimbali ambao umekuwa ukitumika kama kanisa kabla ya kumalizika kwa ujenzi wa kanisa la Parokia.

Page 21: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

2.4.1 Ukumbi

Ujenzi wa mwanzo katika kiwanja kilichonunuliwa mwaka 1988 ulianza mwezi Septemba 13, 1989, chini ya usimamizi wa ndugu Edward Mhagama; ukitarajiwa kuwa ukumbi wa shughuli mbalimbali (Multipurpose Hall). Ujenzi huuuliokuwa ukiendelea kwa kasi ndogo sana huku jengo likiwa linajengwa katikati kabisa ya kiwanja, kinyume na maelekezo ya uongozi wa kigango, ulikumbwa na matatizo mengi ya kiufundi, ukasitishwa.

Tarehe 21 Septemba 1992, awamu ya pili ya ujenzi wa ukumbi ilianza chini ya usimamizi wa kamati iliyokuwa na wajumbe wafuatao:

1 Benedict Mwobahe Mwenyekiti

2 L. M. Kiswaga Mjumbe

3 Severine Lyaruu Mjumbe

4 Simon Billa Katibu

Kamati hii ilipewa hadidu za rejea zifuatazo:

(a) Ukumbi huo ujengwe pembeni kabisa mwa kiwanja ili kutoa nafasi ya ujenzi wa kanisa, nyumba ya mapadre, nyumba ya masista, shule ya awali na zahanati hapo baadaye.

(b) Ujenzi uzingatie kwamba jengo hilo litatumika kama kanisa kwa muda mrefu hivyo liwe na altare na sakrastia.

Mnamo Agosti 20 mwaka 1994, ujenzi wa ukumbi ulikamilika na kufunguliwa rasmi na Mheshimiwa Padre Hermenegild Muba ambaye wakati huo alikuwa ni Makamu wa Askofu (Vicar General) wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Aidha, hiyo ndiyo siku ambayo Misa Takatifu iliadhimishwa katika jengo hilo kwa mara ya kwanza. Sakramenti za ubatizo, Komunio ya Kwanza na Kipaimara zilitolewa.

13

Page 22: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

Februari 18, 1995, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, alikuja kuadhimisha Misa Takatifu katika Parokia ya Makongo Juu. Madhumuni ya ziara hiyo yalikuwa ni kujionea hatua ambayo waamini walikuwa wamefikia katika kukiendeleza kiwanja cha Kanisa.

Tarehe 30 Agosti 1997, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alikuja kutoa Sakramenti ya Kipaimara hapa kigangoni Makongo Juu. Pamoja na kazi hii ya kiuchungaji, Mwadhama alitoa agizo kuwa ilikuwa ni vema iwapo Kigango kingejiwekea mkakati wa kukiandaa kuwa parokia ifikapo mwaka 2002.

Mnamo Septemba 24, 1998, mpango mkuu wa matumizi ya ardhi (master plan) wa Kigango ambao ulijumuisha ujenzi wa kanisa, nyumba ya mapadre, nyumba ya masista, shule ya awali, zahanati, pamoja na michoro sanifu ya nyumba ya mapadre na shule ya awali uliidhinishwa rasmi na Mwadhama Kardinali Pengo.

Mwezi tarehe moja Juni mwaka 1999, Mpango wa Maendeleo ya Kiroho na Kimwili wa Miaka Mitatu 1999/00 – 2001/02 wa Kigango cha Makongo Juu ulizinduliwa rasmi na kuanza kutekelezwa. Dhamira kuu ya mpango huo ilikuwa kukiandaa kigango kuwa parokia ifikapo 2002 na ulikuwa na sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza ilianisha miundombinu ambayo ilitakiwa kuwapo kabla ya kigango kuwa parokia na mikakati ya namna ya kujenga miundo mbinu hiyo. Sehemu ya pili iliainisha shughuli za kiroho ambazo zilitakiwa kufanywa ili kuwandaa waamini kiroho, kifikra na kisaikolojia ili wamudu kubeba majukumu ya kuwa Parokia.

2.4.2 Nyumba ya Mapadre

Katika kujiandaa kuwa kigango na kupata wachungaji watakaoweza kuishi kati ya waumini, kulionekana umuhimu wa kuwepo na makazi rasmi ya mapadre ambapo Agosti

14

Page 23: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

1999, ujenzi wa nyumba ya mapadre ulianza chini ya Kamati ya Ujenzi ikiongozwa na Evaristo Liwa kama mwenyekiti na E. Mhango (sasa marehemu) na Severine Lyaruu kama wajumbe. Kamati hii baadaye iliongozwa na Rogart Kisanga. Baada ya Kisanga kwenda Swaziland, Deo Mugishagwe aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo.

Novemba 14, 1999, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliweka jiwe la msingi la nyumba hiyo ya Mapadre na akapanda mti wa WAWATA na Mti wa Milenia mahali ambapo pango la Mama Bikira Maria lingejegwa.

Mnamo Juni tarehe moja mwaka 1999, mpango wa maendeleo ya kiroho na kimwili wa miaka mitatu 1999/01 – 2001/02 wa Kigango cha Makongo Juu ulizinduliwa rasmi na kuanza kutekelezwa. Dhamira kuu ya mpango

15

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Methodius Kilaini akisindikizwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei Kigango cha Makongo Juu, Benedict Mwobhahe kukagua ujenzi wa nyumba ya Mapadre

Page 24: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

huo ilikuwa ni kukiandaa kigango kuwa Parokia ifikapo 2002 na ulikuwa na sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza ilianisha miundombinu ambayo ilitakiwa kuwapo kabla ya kigango kuwa Parokia na mikakati ya namna ya kujenga miundo mbinu hiyo. Sehemu ya pili ilianisha shughuli za kiroho ambazo zilitakiwa kufanywa ili kuwaandaa waamini kiroho, kifikra na kisaikolojia ili wamudu kubeba majukumu ya kuwa Parokia.

Tarehe 13 Februari, 2000, Askofu Mteule Padre Method Kilaini, kwa ombi maalum la waamini wa Kigango cha Makongo Juu, alikuja kigangoni na kuadhimisha Misa Takatifu ya shukurani, na kumpongeza kwa kuteuliwa kwake kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Waamini walimpa zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na nguo za Misa. Akajibu risala ya waamini, Askofu Mteule Method Kilaini alikiri kuwa tangu uteuzi wake waamini wa Parokia ya Makongo Juu walikuwa wa kwanza kumpongeza, hivyo akaahidi kutowasahau kamwe katika sala zake.

Mnamo Novemba 23, 2000, Msalaba wa Milenia ulipokelewa kwa shangwe na nderemo na waamini wa Kigango na kuzungushwa katika Jumuiya 14 za Kigango. Kila ulipofika msalaba katika Jumuiya, wanajumuiya walisali vituo cha njia ya msalaba.

Mnamo mwezi Machi 2001, Halmashauri ya Kigango, kupitia kamati yake ya ujenzi iliandaa tamasha la kwaya ili kuchangisha fedha ya kununua mabati ya kuezekea nyumba ya mapadre.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa Mheshimiwa Askofu Kilaini. Kiasi cha Sh. 8,000,000 zilipatikana. Desemba 13, 2002 nyumba ya Mapadre ilikamilika kuezekwa.

Mnamo Juni mosi, 2003, Halmashauri kupitia kamati yake ya michango iliandaa harambee ili kutafuta fedha za kuwezesha kupiga lipu nyumba ya Mapadre. Mgeni rasmi alikuwa mheshimiwa Yusufu Makamba, Mkuu wa Mkoa wa

16

Page 25: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

Dar es Salaam; na Mheshimiwa Padre Pius Rutechura, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, aliongoza Misa Takatifu siku hiyo. Shilingi milioni 22 zilipatikana. Fedha hii ilitumika kwa ajili ya kuweka fremu za milango na madirisha, mabomba ya maji na umeme, kupiga lipu ndani na nje na kuweka sakafu. Kazi hii ilikamilika Oktoba 25, 2003.

Julai 18, 2004 Mhashamu Askofu Method Kilaini, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam alikuja kigangoni kutoa Sakramenti ya Kipaimara na kuzindua harambee ya kukamilisha ujenzi wa nyumba ya Mapadre. Akizindua harambee hiyo, Mhashamu alitoa changamoto kwa waamini kuwa iwapo wangefanikiwa kukamilisha angalao upande mmoja wa jengo hilo, Baba Askofu angekuja kulala hapa kigangoni na kusherehekea sikukuu ya Noeli kwa kuadhimisha misa ya usiku na mchana. Ahadi hii ilikuwa ni changamoto kubwa katika kukamilisha ujenzi wa nyumba hii.

Desemba 23, 2004, ujenzi wa upande mmoja (Wing A) wa nyumba ya mapadre ulikamilika. Shukurani za pekee zinastahili kutolewa kwa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) wa Kigango cha Makongo Juu, ambao, pamoja na kushiriki katika michango ya kufanikisha ujenzi huu uliokuwa unawakabili waamini wote wa Kigango kwa ujumla, walijiwekea utaratibu wa kuchangia ununuzi wa vyombo vyote vya ndani ya nyumba hiyo ikiwa ni pamoja na vyombo vya jikoni, vitanda, mapazia, samani, n.k. Utaratibu huu ambao waliuita “Mchango wa Kapu la Mama kwa ajili ya Nyumba ya Mapadre” ulikusanya kiasi cha Sh. 1,900,000 na hivyo kuifanya nyumba hiyo iweze kufunguliwa rasmi kwa ibada na Mhashamu Askofu Method Kilaini Desemba 24, 2004. Askofu Kilaini alifuatana na Mheshimiwa Padre Martin Dominick Rutayebesibwa na Frt. Gallen Mvungi na hawa ndiyo walikuwa watu wa kwanza kulala katika nyumba siku hiyo, kama alivyoahidi Baba Askofu Julai 18, 2004.

17

Page 26: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

Baada ya nyumba ya mapadre kukamilika, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Policarp Kardinali Pengo alimtuma Padre Martin Dominick Rutayebesibwa kuwa Padre Mkazi katika Kigango cha Makongo Juu tarehe 2 Machi, 2005.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Method Kilaini alikabidhiwa funguo za nyumba ya Mapadre baada ya kutoa Sakramenti ya Kipaimara. Aliwaambia waamini kuwa kuwepo kwa nyumba ya mapadre lilikuwa ni jambo jema na ili nyumba isikaliwe na popo atamwacha Padre Martin Dominick Rutayebesibwa kama Padre Mkazi na Frt. Gallen Mvungi. Waamini walipewa jukumu la kuwatunza na kushirikiana nao katika kuendeleza kazi za Kanisa.

Akizungumza na waamini wa Kigango cha Makongo Juu wakati wa ibada ya Mkesha wa Noeli, Baba Askofu Kilaini aliwapongeza kwa kazi nzuri waliyofanya ya kukamilisha sehemu hiyo kwa kiwango cha hali ya juu kabisa. Hivyo akasema isingalikuwa vema kufunga nyumba hiyo mara atakapoondoka. Kwa hali hiyo aliamua kumwacha Kigangoni Padre Martin Dominick Rutayebesibwa kama Padre Mkazi ili huduma zote za kiroho ziweze kupatikana hapa hapa. Ili Padre Martin asijisikie mpweke mno, alitangaza pia kuwa Frt. Mvungi angebaki Makongo Juu hadi mwisho wa kipindi chake cha uchungaji.

Uamuzi huu wa Mhashamu Askofu ulipokelewa kwa shangwe, nderemo na vifijo na waamini wa Makongo na kuhitimishwa kwa wimbo wa ‘Ni Neno Jema Kumshukuru Bwana’ uliotungwa na Ansbert Ngurumo.

2.5. Jumuiya Ndogondogo za Kikristo

Ilipofika Mei 1991, Kigango kilianzisha mfumo wa Jumuiya Ndogondogo (JNNK)za Kikristo, Jumuiya sita ziliundwa kama ifuatavyo:

18

Page 27: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

1. Jumuiya ya Mt. Cesilia

2. Jumuiya ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu

3. Jumuiya ya Mt. Thomas

4. Jumuiya ya Mt. Francis

5. Jumuiya ya Mt. Yuda Tadei

6. Jumuiya ya Mt. Agatha

Jumuiya hizi zilizinduliwa rasmi na Mhashamu Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo mnamo Septemba 28, 1991 alipotembelea Kigango cha Makongo kwa mara ya kwanza. Pamoja na kuunda Jumuiya Ndogondogo za Kikristo, mwaka huo pia ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi. Hivyo tarehe

19

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuph Makamba akichangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mapadre

Page 28: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

21 Aprili 1991, wajumbe wa Halmashauri ya Walei Kigango walichaguliwa kama ifuatavyo:

Na. Jina Nafasi

1 Chris Mwalongo Mwenyekiti

2 David Makene Makamu Mwenyekiti

3 Swithan Billa Katibu

4 Martin Busanda Mhazina

5 Benedict

Mwobhahe

Mjumbe na Mwenyekiti wa

Liturjia

6 Silvin Mongella Mjumbe

7 Ritha Mbotto Mjumbe

8 L. Kiswaga Mjumbe

9 Severine Lyaruu Mjumbe

Kufuatia kifo cha Mwenyekiti Chrisostom Mwalongo Aprili mosi, 1994, na kujiuzulu uongozi kwa Makamu Mwenyekiti David Makene kwa sababu ya kujiunga na Wanamaombi, Halmashauri ilimchagua Benedict Mwombahe kukaimu uenyekiti hadi uchaguzi ulipofanyika.

Ilipofika mwaka 1998, baada ya kuwa na ongezeko kubwa la waamini, Kigango kiligawanywa upya katika mitaa minne,.

Mnamo Septemba 28, 1991, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Polycarp Kardinali Pengo, kwa mara ya kwanza alitembelea Kigango cha Makongo Juu na kuadhimisha Misa Takatifu katika viwanja vya Shule ya Msingi Makongo.

Katika ibada hiyo, wakatekumeni wanane walibatizwa, waamini 21 walipata Sakramenti ya Kipaimara na watatu walibariki ndoa zao. Hawa walikuwa malimbuko ya kusanyiko la Mungu Makongo Juu.

Akijibu risala ya waamini wa Makongo Juu, Mhashamu Askofu Pengo aliwapongeza waamini kwa kupata ardhi

20

Page 29: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

kwa ajili ya kujenga nyumba ya Mungu akawahimiza kuharakisha ujenzi wa kanisa ili waweze kuondokana na adha ya kuendelea kutumia majengo ya Shule ya Msingi kwa ibada.

Mwaka 1987 ulikuwa ni mwaka wa Uchaguzi wa viongozi wa Halmashauri ya Walei katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Kigango cha Makongo Juu kilishiriki kwa mara ya kwanza katika uchaguzi huu. Ili kuweza kuchagua viongozi, kigango kiligawanyika katika Kanda tatu kama ifuatavyo.

1. Kanda ya Makongo Chini

2. Kanda ya Makongo Juu

3. Kanda ya Makongo Mbezi/Changanyikeni

Waamini wa kila kanda walichagua viongozi wawili ambao

21

Nyumba ya Mapadre ikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi

Page 30: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

walijulikana kama walezi wa Kanda Kama ifuatavyo:

(a) Kanda ya Makongo Chini

Teophil Nshiku

David Makene

(b) Kanda ya Makongo Juu

Silvin Mongella

Severin Lyaruu

(c) Kanda ya Makongo Mbezi/Changanyikeni

Martin Busanda

Timothy Kasella

Walezi hawa wa kanda ndiyo waliofanya uchaguzi wa viongozi Agosti 2, 1987 na wafuatao walichaguliwa:

Na. Jina Nafasi

1 Timothy Kasella Mwenyekiti

2 Severin Lyaruu Makamu Mwenyekiti

3 D. Mizambwa Katibu

2.6. Mpango wa Maendeleo

Kufuatia ziara ya kufahamiana iliyofanywa na Padre Mkazi wa Kigango cha Makongo Juu, Padre Martin Dominick Rutayebesibwa katika mitaa na JNNK za Kigango miezi minne ya kwanza ya ujio wake Januari - Aprili 2005, umuhimu wa Kigango kuwa na mpango wa maendeleo wa maisha ya kiroho na kimwili wa muda mrefu ambao dira/dhamira ya Kigango ingetamkwa ulidhihirika wazi. Hivyo, Kamati ya watu wanne ya kuandaa mpango huo iliteuliwa na mkutano wa pamoja na Kamati Tendaji; na Kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi ya Halmashauri kama ifuatavyo:

22

Page 31: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

Timothy Kasella Mwenyekiti

Benedict Mwobhahe Katibu

Padre Martin Dominick

Rutayebesibwa

Mjumbe

Frt. Gallen Mvungi Mjumbe

Rasimu ya mpango huu wa maendeleo ya maisha ya kiroho na mwili wa miaka kumi (Julai 2005 – Juni 2015) iliidhinishwa na Kamati Tendaji na Halmashauri ya Kigango na hatimaye kuzinduliwa rasmi na Mhashamu Askofu Msaidizi Method Kilaini tarehe 31 Julai 2005 alipokuja kigangoni kutoa Sakramenti ya Kipaimara. Mpango huu ndio uliokuwa unaongoza shughuli zote za kiroho na kimwili za kigango na sasa parokia.

Baada ya muumini mmoja kujitolea kununua Tabernakulo kwa gharama ya Sh. 1,000,000 kutoka Peramiho na kujengewa kanisani na Bruda Polycarp, umuhimu wa kulikarabati kanisa ili kuimarisha usalama na kuboresha unadhifu wa madhabahu ulidhihirika. Mheshimiwa Padre Martin Dominick Rutayebesibwa, Padre Mkazi, alihimiza kwa namna ya pekee ukarabati huo mpaka akalazimika kumtoa Yesu Kristo ndani ya Tabernakulo hiyo hadi ukarabati ulipokamilika. Hatua hii iliwashtua na kuwaamsha waamini, na hivyo Jumapili za tarehe 5 na 12 Juni 2005 waamini walichanga jumla ya shilingi milioni tano, laki tano na elfu sitini na sita na arobaini (5,566,040) ambazo zilitumika kwa ajili ya kukamilisha kazi za ukarabati zifuatazo:

(i) Kutengeneza na kuweka madirisha na milango mipya, magrili ya madirisha na milango ya kanisa.

(ii) Kukarabati sakafu ya kanisa na kuweka marumaru madhabahuni na njia zote kuelekea madhabahuni kutoka milango midogo na mikubwa ya kanisani.

(iii) Kutengeneza altare na mimbari mpya kwa mbao za

mninga.

23

Page 32: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

Kazi zote hizi zilikamilika Julai 29, 2005 na hivyo kumwezesha Padre Mkazi kumrejesha Yesu Kristo ndani ya Tabernakulo tarehe 20 Julai 2005 tayari kwa ujio wa Mhashamu Askofu Method Kilaini Julai 31, 2005 kuja kutoa Sakramenti ya Kipaimara.

Padre Martin Dominick Rutayebesibwa alipoteuliwa kuwa Padre Mkazi wa Kigango cha Makongo Juu Desemba 24, 2004, kigango kilikuwa na vyama/vikundi vya kitume sita tu vifuatavyo:

(i) WAWATA

(ii) VIWAWA

(iii) Utoto Mtakatifu

(iv) Ministranti

(v) Kwaya ya Mtakatifu Bikira Maria Mama wa Rozari

Takatifu

(vi) Kwaya ya Mt. Felista

Moja ya mambo yaliyojitokeza wakati wa ziara aliyofanya padre kkazi katika kanda na JNNK mwezi Januari hadi Aprili, 2005 ni haja ya kuamsha miongoni mwa waumini moyo wa ibada kupitia vyama vya kitume. Hivyo, hatua zilichukuliwa na padre mkazi ikiwa ni pamoja na kuwaalika viongozi mbalimbali wa vyama vya kitume ngazi za jimbo kuja kuhamasisha na matunda ya juhudi hizi yalianza kuonekana mwezi Aprili 2006 kwa kuanzishwa kwa vyama vifuatavyo:

(i) Neokatekumenato

(ii) Moyo Mtakatifu wa Yesu

(iii) Chama cha Miito

24

Page 33: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

(iv) UWAKA (Utume wa Wanaume Katoliki)

(v) Chama cha Wasoma Masomo

(vi) VIWAWA

Vyama hivi vilisaidia kwa kiasi kuamsha moyo wa ibada na uchaji wa moyo miongoni mwa waumini wa kigangoni.

Katika jitihada za kuhakikisha kuwa uchaguzi mdogo wa Kamati Tendaji unafanyika baada ya kamati iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Dk. Raynold Mfungahema kujiuzulu na unakuwa na wigo mpana wa wajumbe, Padre Mkazi alitumia fursa hiyo kuzigawa JNNK upya ili kuhakikisha kuwa ukubwa wa jumuiya unakuwa na familia zisizopungua saba na zisizozidi 15. Ili kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi, Novemba 30, 2005, Padre Mkazi aliteua kamati maalum ya kuratibu ugawanywaji wa jumuiya hizo pamoja na mchakato mzima wa uchaguzi huo mdogo kuanzia JNNK mpya ambazo zingeanzishwa hadi uchaguzi wa Kamati Tendaji, na wafuatao waliteuliwa kuwa wajumbe wa kamati hiyo:

Benedict Mwobhahe Mwenyekiti

Mary Ngole Katibu

Timothy Nkondola Mjumbe

Damian Meella Mjumbe

Mtaita Mjumbe

A. Ndibalema Mjumbe

Frt. Denis Wigira Mjumbe

Zoezi hili lilipokamilika, JNNK ziliongezeka kutoka 16 na kanda nne hadi kufikia 32 na kanda kutoka nne hadi sita. Mgawanyo huu mpya wa jumuiya si tu ulifanikisha uchaguzi huo mdogo bali pia uliboresha kwa kiasi kikubwa uendeshaji wake. Wanajumuiya, kwa sababu ya udogo wa jumuiya hizo, waliweza kufahamiana kwa urahisi na kushirikiana katika shida na raha.

25

Page 34: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

Mwezi Mei wa kila mwaka ni mwezi wa Mama Bikira Maria. Aprili 30, 2006 jioni saa 11:30 kuliadhimishwa Misa Takatifu ya uzinduzi wa mwezi wa Bikira Maria. Kwa kuwa Bikira Maria wa Rozari Takatifu alikuwa somo wa kigango, siku hiyo ilienziwa kwa matukio yafuatayo:

(i) Sanamu kubwa ya Bikira Maria Mama wa Rozari Takatifu ikiwa juu ya mwimo maridadi wa mbao za mninga ilibarikiwa na kusimikwa rasmi kanisani.

(ii) Sanamu ndogo ya Mama Maria pia ilibarikiwa na utaratibu wa kumuenzi Mama Maria kwa kuitembeza katika jumuiya, na familia hadi familia kwa kipindi chote cha Mei wa kila mwaka ulifanyika.

Mwezi Oktoba ni mwezi wa Rozari Takatifu. Hivyo, waamini hukumbushwa kusali rozari katika familia zao, jumuiya, hadi ngazi ya kigango. Mnamo Oktoba mosi, 2006, rozari maalumu ilibarikiwa wakati wa ibada ya misa takatifu, na utaratibu wa kuizungusha rozari hiyo katika jumuiya zote, kutoka familia moja hadi nyingine ulifanyika kwa kipindi chote cha mwezi Oktoba, 2006 ili kuhamasisha waumini kusali rozari siku zote.

Aidha enzi za kigango na baadaye parokia, katika vipindi tofauti, kulikuwa na bahati ya kuwa na mapadre wageni kutoka majimbo mbalimbali walioishi hapo kigangoni huku wakisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Chuo Kikuu cha Ardhi ambavyo viko jirani; na wengine walifika kwa shughuli mbalimbali za kikazi. Padre Damas Mahali aliyekuwa masomoni katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Jimbo la Njombe); Padre Camilius Nyandwi aliyekuja kwa matibabu (Jimbo la Mwanza); Padre Moses Dimoso (Jimbo la Morogoro); Padre GaudenceTalemwa aliyekuwa akisoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Jimbo la Rulenge; Padre Charles Kasuku wa Jimbo la Sumbawanga na Padre Emmanuel Meza wa Jimbo la Mbeya waliokuwa wakisoma katika Shule Kuu ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Jimbo la Sumbawanga), na Padre Eusebus

26

Page 35: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

Nzigilwa na Padre Aidan Mubezi waliokuwa wakisoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Jimbo Kuu la Dar es Salaam). Aidha, mapadre Eusebius Nzigilwa na Aidan Mubezi walipewa majukumu ya kuwa maparoko wasaidizi. Padre Nicholaus Masamba alikaimu nafasi ya Paroko mwaka 2014, wakati Baba Paroko Padre Joseph Massenge aliposafiri kwenda Ujerumani kwa majuma mawili,.

Mnamo mwaka 2010, Padre Eusebius Nzigilwa aliteuliwa na Baba Mtakatifu Benedicto XVI kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Dar es Salaam, na Padre Aidan Mubezi alikuja kuwa Katibu wa Askofu.

Kikao cha dharura cha Halmashauri ya Walei Kigango cha Makongo kiliitishwa mahsusi kutoa fursa kwa wajumbe wa Halmashauri kukutana rasmi na Padre Mkazi. Moja ya maazimio ya kihistoria yaliyofanywa na Halmashauri katika kikao hicho yalihusu umuhimu wa kuweka katika maandishi, historia Kigango.

Kazi ya kuandika historia hiyo ilipewa kipaumbele cha hali ya juu, na hivyo ilipofika Agosti 2005 toleo la kwanza la historia ya Kigango chetu kwa kipindi cha 1984 hadi 2004 lilichapwa na kuzinduliwa rasmi katika katika ibada ya misa takatifu, siku ya sikukuu ya somo wa Kigango mnamo Oktoba 7, 2006.

27

Page 36: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

SURA YA TATU:

PAROKIA YA MAKONGO JUU

3.1 Matukio muhimu

Tarehe 7 Julai 2017 ndio siku ambayo Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozari Takatifu, Makongo Juu ilizaliwa. Tangazo lililotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. Pamoja na kuitangaza Makongo Juu kuwa Parokia, alimteua Padre Mkazi wa Makongo Juu Padre Martin Dominick Rutayebesibwa kwenda kuwa Paroko wa Parokia ya Mlandizi na Padre Maximilian Wambura aliyekuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Familia Takatifu Mburahati kuwa Paroko wa kwanza wa Parokia ya Makongo Juu. Aidha alimteua padre mpya Gaston Mkude aliyepewa daraja la Upadre siku hiyo kuwa Paroko Msaidizi wa Parokia mpya ya Makongo Juu.

3.2 Uongozi

Kufuatia kigango cha Makongo Juu kutamkwa kuwa parokia, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbu Kuu Katoliki la Dar es Salaam aliwateua Padre Maximillian Wambura kuwa paroko na Padre Gaston Mkude kuwa Paroko Msaidizi wa kwanza. Aidha, mnamo Julai 15, alitengua Kamati tendaji iliyokuwepo chini ya uenyekiti wa Dk. Camillus Lekule na kuteua Kamati Tendaji ya mpito ambayo ingefanya kazi hadi hapo ambapo uchaguzi ungefanyika. Kama ifuatavyo:

2007 – 2009

Na Jina Nafasi

1 Padre Maximillian Wambura Paroko

2 Padre Gaston Mkude Paroko Msaidizi

3 Prof. Athanas Kauzeni Mwenyekiti

28

Page 37: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

4 Revocatus Kasikila Makamu Mwenyekiti

5 Simon Billa Katibu

6 Theresia Wandibha Katibu Msaidizi

7 Joseph Lutege Mhazini

8 Deo Mwarabu Mjumbe

9 Menedora Liwa Mjumbe

Mwaka 2009, ulifanyika uchaguzi kwa mujibu wa katiba ya Halmashauri ya Walei ambapo wajumbe waliochaguliwa, walikuwa kama wafuatao:

Na Jina Nafasi

1 Dk. Raynold Mfungahema

Mwenyekiti

2 Revocatus Kasikila Makamu Mwenyekiti

3 Theresia Wandibha Katibu

4 Agnes Namuhisa Katibu Msaidizi

5 Victoria Samkyi Mhazini

Aidha, mhazini na katibu hawakuweza kuendelea na nafasi zao kutokana na majukumu binafsi, na hivyo kujiuzulu mwaka 2010. Uchaguzi mdogo uliofanyika mwaka huo uliwachagua Christopher Kidanka kuziba nafasi ya katibu na Chesco Sapula kuziba nafasi ya mhazini.

2009 - 2011

Na Jina Nafasi

1 Padre Maximillian Wambura Paroko

2 Padre Eusebius Nzigilwa Paroko Msaidizi

3 Dk. Raynold Mfungahema Mwenyekiti

4 Revocatus Kasikila Makamu Mwenyekiti

5 Theresia Wandibha/Christopher Kidanka

Katibu

29

Page 38: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

6 Agnes Namuhisa Katibu Msaidizi

7 Victoria Samkyi/Chesco Sapula Mhazini

Mwaka 2012 ulifanyika uchaguzi wa kawaida ambapo viongozi walichaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Tendaji. Aidha, Baba Paroko aliteua wajumbe wengine wawili kwenye Kamati Tendaji kwa kazi maalum kama ifuatavyo:

2012- 2014

Na Jina Nafasi

1 Padre Maximillian Wambura

Paroko

2 Padre Eusebius Nzigilwa Paroko Msaidizi

3 Dk. Raynold Mfungahema Mwenyekiti

4 Revocatus Kasikila Makamu Mwenyekiti

5 Theresia Wandibha/Christopher Kidanka

Katibu

6 Agnes Namuhisa Katibu Msaidizi

7 Victoria Samkyi/Chesco Sapula

Mhazini

8 Agnes Namuhisa Uratibu wa Chama cha Akiba na Mikopo (SACCOS)

9 Harold Matemu Uratibu Masuala ya Liturjia

10 Salome Mwero Kuimarisha Kamati ya Fedha

Wajumbe watano walichaguliwa tena katika uchaguzi wa mwaka 2016 na Baba Paroko aliwateua Deo Macha, Harold Matemu na Cecilia Kassonga kuwa wajumbe wa kuteuliwa kusaidia kazi maalum.

30

Page 39: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

2016 – 2017

Na. Jina Nafasi

1 Padre Joseph Massenge Paroko

2 Padre Aidan Mubezi Paroko Msaidizi

3 Dkt. Raynold Mfungahe-ma

Mwenyekiti

4 Revocatus Kasikila Makamu Mwenyekiti

5 Christopher Kidanka Katibu

6 Betty Jayne Humplick Katibu Msaidizi

7 Chesco Sapula Mhazini

8 Dkt. Deo macha Kamati ya fedha

9 Harold Matemu Mjumbe Kamati ya Liturjia

10 Cecilia Kasonga/Victo-ria Yongolo

WAWATA

Wachungaji waliolichunga Kondoo wa Bwana wakiwa Maparoko tangu Makongo Juu ilipotamkwa rasmi kuwa parokia kamili hadi sasa ni:

1. Padre Maxmillian Wambura (2007 – 2011)

2. Padre Gallen Mvungi (2011 – 2012)

3. Padre Joseph Massenge (2013 hadi sasa)

3.3 Maandalizi ya Awali ya Ujenzi wa Kanisa

Parokia ilirithi ndoto ya ujenzi wa kanisa kutoka enzi za kigango na pia kutokana na kuwepo kwa Mpango Mkakati wa Kigango. Aidha, kulikuwa na ndoto ya kujenga nyumba ya masista katika eneo lililotengwa.

Ndoto ya kuwa na Parokia yenye miundombinu inayotosheleza mahitaji ilianza kujidhihirisha mapema sana. Tayari kulikuwa na ukumbi uliokuwa ukitumika kama kanisa,

31

Page 40: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

na nyumba ya mapadre. Jengo moja muhimu lilikuwa bado nalo ni kanisa.

Baada ya kushinda zabuni mwaka 2008, kampuni ya Afri Arch Associates ilipewa kazi ya kusanifu jengo la kanisa.

Mnamo Mei 10, 2010, Maaskofu wasaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa na Salutaris Libena, walikuja parokiani kwa ajili ya kutoa Sakramenti ya Kipaimara na kuzindua rasmi mkakati wa ujenzi wa kanisa jipya.

Ujenzi huo uliazimiwa kufanyika kwa awamu, ili kukabiliana na changamoto ya rasilimali fedha. Awamu ya kwanza ilihusisha kuweka jiwe la msingi na kuchimba na kujenga msingi, pamoja na kuweka jamvi. Awamu ya pili ilihusisha kusimika nguzo; awamu ya tatu ilikuwa ni kuezeka na

Maaskofu wasaidizi, Eusebius Nzigilwa (kushoto) na Salutaris Libena wakikata keki baada ya uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa

32

Page 41: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

awamu ya nne kumalizia. Wakati huu ambapo parokia inaadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, ujenzi wa kanisa upo katika awamu ya nne ya umaliziaji.

Sambamba na ujenzi wa kanisa, juhudi zilifanyika kujenga nyumba ya Katekista katika kiwanja kilichopo pembeni mwa eneo la kanisa. Ujenzi huo ulikamilika kwa kutumia baadhi ya vifaa vilivyokuwa vinabaki katika ujenzi wa kanisa. Nyumba hii ilizinduliwa na Askofu msaidizi Titus Mdoe alipofika kutoa sakramenti ya Kipaimara.

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, katika ziara yake mwaka 2015, aliiagiza parokia kuanza ujenzi wa nyumba ya masista ili waweze kusaidia utume katika Parokia. Pamoja na kuwepo kwa ujenzi wa kanisa uliokuwa ukiendelea, wanaparokia walipokea agizo hilo kwa moyo wa utii, na maandalizi yake yakaanza mara moja.

Baada ya kukamilika kwa mchoro wa nyumba hiyo na kukaguliwa na Mwadhama Kardinali, ujenzi rasmi ulianza Septemba 2017 na jiwe la msingi kuwekwa na Mwadhama Oktoba mwaka huo.

Aidha, Kamati ya Ujenzi iliundwa ikiwa na wajumbe wafuatao.

Na Jina Nafasi

1 Raymond Mushi Mwenyekiti

2 Geraldine Kikwasi Katibu

3 Boniface Bulamile Mjumbe

4 Geofrey John Mjumbe

5 Gabriel Mwero Mjumbe

3.4 Ujenzi wa Kanisa

Mchakato wa kutafuta mchoro wa kanisa unaofaa ulianza na wachoraji wakashindanishwa. Mchakato wa ujenzi

33

Page 42: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

34

ulianza mwaka 2010. Hata hivyo, Jiwe la Msingi la kanisa jipya liliwekwa Septemba 22, 2012 na Mwadhama Kardinali na ujenzi ukaanza hatua kwa hatua.

Baada ya Mwenyekiti Raymond Moshi kufariki dunia, nafasi yake ilichukuliwa na Thomas Samkyi.

Katika kuimarisha utafutaji fedha kwa ajili ya ujenzi, iliundwa Timu ya Uhamasishaji iliyokuwa ikifanya kazi chini ya Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango. Timu hiyo, ikiongozwa na Dr. Fratern Mboya iliandaa harambee mwaka 2013 na kufanikisha kupata fedha kwa ajili ya hatua za mwanzo za ujenzi.

Mmoja wa Waamini wa mwanzo wa Makongo Juu, Benedict Mwobhahe (kushoto) na Paroko Padre Joseph Massenge wakimkabidhi Prof. Anna Tibaijuka picha aliyoinunua ili kuchangia ujenzi wa kanisa

Page 43: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

35

Dk Fratern Mboya aliitwa na Mungu tarehe 25 Julai 2013 na hivyo nafasi yake ikachukuliwa na Dk. Deoscorus Ndoloi aliyeendeleza gurudumu la umahasishaji na utafutaji fedha kwa njia mbalimbali. Mwaka 2016, timu hii iliandaa harambee nyingine na kisha mwaka 2017 iliandaliwa harambee nyingine tena ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya Parokia.Hatua ya kwanza ya ujenzi ilihusisha uchimbaji wa visima viwili vya maji, kuhamisha barabara iliyokuwa ikipita katikati ya kiwanja cha kanisa na kutengeneza barabara mbadala inayozunguka kiwanja; kujenga uzio na kuchimba msingi mpaka kufunika jamvi.

Hatua ya pili ilihusisha kujenga nguzo, mihimili (beams) na bamba (slab), kusanifu paa na kuezeka.

Hatua ya tatu inahusisha kuweka milango na madirisha; vigae vya sakafu, altare, mimbari za masomo na matangazo, kisima cha ubatizo na shughuli za ukamilishaji wa ujenzi.

Mhandisi Deo Mugishagwe (kushoto) akisaidiana na Paroko Gallene Mvungi (kulia) kumuelekeza fundi wakati wa kuweka msingi wa kanisa

UJENZI WA KANISA KATIKA HATUA MBALIMBALI

Page 44: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

36

Page 45: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo

37

Page 46: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo
Page 47: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo
Page 48: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo
Page 49: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo
Page 50: HISTORIA YA PAROKIA YA MAKONGO JUU · Utume wa Wanaume Katoliki (UWAKA), Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA), Ministranti, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, Ushirika wa Moyo