23
Yaliyomo // www.tumemadini.go.tz Profesa Kikula Atembelea Machimbo Ya Madini Pwani ... Na.05 Mtambo Wa Baruti wa Kampuni ya Nitro Explosive Kukamilika Mwishoni mwa Mwaka Huu ... Na.06 Tume ya Madini Tume ya Madini 2020 Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa Wamkosha Waziri wa Madini. . . . 07 Bilionea Laizer Awataka Watanzania Wengi Kuwekeza Kwenye Sekta ya Madini ... Na.04 Toleo Na.5 // Julai - Septemba 2020

Madini news, Toleo Na.5 LowRestumemadini.go.tz/uploads/publications/en-1602038045... · 2020. 10. 7. · 3 Tume ya Madini #5 Yaliyomo /HABARI NA MATUKIO 1 Bilione a L izer Aw atak

  • Upload
    others

  • View
    3

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

  • Yaliyomo //

    www.tumemadini.go.tz

    Profesa Kikula Atembelea Machimbo Ya MadiniPwani ... Na.05

    Mtambo Wa Baruti wa Kampuni ya Nitro Explosive Kukamilika Mwishoni mwa Mwaka Huu... Na.06

    Tume yaMadini

    Tume ya Madini 2020

    Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa Wamkosha Waziri wa Madini. . . . 07

    Bilionea Laizer Awataka Watanzania Wengi Kuwekeza Kwenye Sekta ya Madini ... Na.04

    Toleo Na.5 //

    Julai - Septemba2020

  • www.tumemadini.go.tz

  • 2 Tume ya Madini

    /TAHARIRI

    Maoni ya Mhariri

    Prof. Shukrani E. ManyaKatibu MtendajiTume ya Madini

    Moja kati ya majukumu ya Tume ya Madini ni pamoja na ukusanyaji wa maduhuli ambayo yamechangia kwa kiwango kikubwa ongezeko la ukuaji wa Sekta ya Madini.

    Ili kurahisisha ukusanyaji wa maduhuli na kusogeza huduma kwa wadau wa madini, Tume ya Madini imeanzisha Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa (RMOs) 28 na Maafisa Migodi

    Wakazi (MROs) 13 kwenye migodi mikubwa na ya kati.

    Mikakati mingine iliyowekwa na Tume ni pamoja na udhibiti wa utoroshwaji wa madini kwa uanzishwaji wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini.

    Aidha, Tume ya Madini imeweka wakaguzi kwenye mipaka ya nchi, bandarini pamoja na viwanja vya ndege ili kuhakikisha madini yote yanayosafirishwa nje ya nchi yamelipiwa kodi

    zote zinazotakiwa.

    Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019 – 2020 Tume ya Madini ilipangiwa lengo la kukusan-ya shilingi bilioni 470.3 na kufanikiwa kuvuka lengo kwa kukusanya kiasi cha

    shilingi bilioni 528.2Kwa mwaka wa fedha 2020 -2021, Tume ya Madini imepangiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 526.7. Ili kufikia lengo husika, Ofisi za Maafisa Madini Wakazi zimebuni mikakati mbal-imbali ya ukusanyaji wa maduhuli huku Ofisi ya Tume Makao Makuu ikiendelea kushughulikia

    changamoto mbalimbali.

    Katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2020 – 2021, mwezi Julai hadi Septemba, 2020 tumeshuhudia baadhi ya Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa zikivuka lengo la ukusan-yaji wa maduhuli na kuiwezesha Tume kukusanya shilingi bilioni 165.24 sawa na asilimia 31.4 ya lengo la mwaka 2020-2021. Mapato haya ni sawa na asilimia 125.5 ya lengo kwa kipindi

    husika.

    Moja ya ofisi zilizovuka malengo ni pamoja na Simiyu (asilimia 150) na Katavi (asilimia 186). Ninachukua nafasi hii kuwapongeza Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa walioweza kuvuka lengo walilopewa la ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka wa fedha 2020-2021 na kuwaelekeza Maafisa Madini Wakazi wengine kuendelea kuchapa kazi kwa ubunifu ili Tume iweze kuvuka

    lengo la ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka wa fedha 2020-2021 kwa asilimia kubwa.

    Pongezi Watumishi Tume ya Madini kwa Kuvuka Lengo la Ukusanyaji wa Maduhuli kwa Mwaka 2020-2021

    Madini Yetu, Uchumi Wetu Tuyalinde!

  • 3 Tume ya Madini #5

    Yaliyomo/HABARI NA MATUKIO

    1 Bilionea Laizer Awataka Watanzania Wengi Kuwekeza Kwenye Sekta ya Madini . . . . . 04

    2 Profesa Kikula Atembelea Machimbo Ya Madini Pwani . . . . 05

    3 Mtambo Wa Baruti wa Kampuni ya Nitro Explosive Kukamilika Mwishoni mwa Mwaka Huu . . . . 06

    4 Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa Wamkosha Waziri wa Madini. . . . 07

    5 Prof Msanjila: Serikali ina Matarajio Makubwa katika Sekta ya Madini . . . . 08

    6 Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Tume Ya Madini Watembelea Eneo Litakalojengwa Ofisi Mpya Za Tume . . . . 09

    7 Profesa Msanjila Akutana na Kampuni ya Madini ya Twiga. . . . 10

    9 Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Akutana na Wadau wa Madini Dodoma . . . . 12

    8 Wadau Waipongeza Wizara ya Madini, Usimamizi Sekta ya Madini. . . . 11

    10 Profesa Msanjila Afungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji Geita. . . . 13

    11 Tume ya Madini Yapongezwa kwa kutoa Elimu Bora Kwenye Maonesho ya Madini Geita. . . . 15

    /PICHA NA MATUKIO

    13 Matukio na Picha . . . . 17

    Dkt. John Pombe MagufuliRais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania

    Madini News Toleo Na.5Julai - Septemba, 2020

    HALIUZWI KUHUSU SISI

    DIRA

    Mhariri Mkuu Prof. Shukrani E. Manya

    Mhariri Msaidizi Greyson Mwase

    WajumbeWilliam MtinyaGeorge KasezaMha. Yahya SamambaDkt. Abdulrahman MwangaAsteria MuhozyaAndendekisye Mbije

    Msanifu JaridaKelvin Kanje

    Tume ya Madini imeanzishwa chini ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kama ilivyorekebishwa na Sheria (Miscellaneous Amendment) Act 2017.

    Tume ilianzishwa kupitia Gazeti la Serikali Namba 27 iliyotolewa tarehe 7 Julai, 2017.

    Tume imechukua majukumu yote ya kiutendaji ambayo yalikuwa yakifanywa na Idara ya Madini chini ya Wizara ya Nishati na Madini na kazi zote ambazo zilikuwa zikifanywa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini wa Tanzania (TMAA) na Kitengo cha Uchambuzi wa Almasi (TANSORT).

    Lengo la Tume ni kuimarisha usimamizi wa Sekta ya Madini na kuhakikisha Serikali inafaidika kutokana na mapato yanayopatika-na kwa namna endelevu.

    Kuwa Taasisi inayoongoza katika Sekta ya Madini Afrika.

    DHIMA

    Kuchochea na kurekebisha Sekta ya Uchimbaji Madini ili kuhakikisha inatoa mchango endelevu na wenye tija katika uchumi wa Taifa.

    Uzinduzi wa Hati Halisia ya Jadini ya bati... Na.1

    Uzinduzi wa Hati Halisia ya Jadini ya bati... Na.1

    Yaliyomo //

    www.tumemadini.go.tz

    Profesa Kikula Atembelea Machimbo Ya MadiniPwani ... Na.05

    Mtambo Wa Baruti wa Kampuni ya Nitro Explosive Kukamilika Mwishoni mwa Mwaka Huu... Na.06

    Tume yaMadini

    Tume ya Madini 2020

    Mwenyekiti wa Tume ya Madini Afanya Ziara Katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Simiyu ... Na.07

    Bilionea Laizer Awataka Watanzania Wengi Kuwekeza Kwenye Sekta ya Madini ... Na.04

    Toleo Na.5 //

    Septemba2020

  • /HABARI NA MATUKIO

    Bilionea Laizer Awataka Watanzania Wengi Kuwekeza Kwenye Sekta ya Madini

    Bilionea wa Tanzanite, Laizer Saniniu amewataka watanzania kushiriki katika shughuli za uchimbaji wa madini ya Tanzanite kwa kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye Sekta ya Madini.

    Bilionea Saniniu aliyasema hayo tarehe 12 Julai, 2020 mara baada ya kufanya ziara kwenye Banda la Tume ya Madini na Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

    Akielezea siri ya mafanikio kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya Tanzanite katika eneo la Mirerani lililopo Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Bilionea Saniniu alisema kuwa ni kutokana na usimamizi mzuri wa Serikali kupitia Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwenye usimamizi wa shughuli za uchimbaji na uuzaji wa madini ya Tanzanite katika eneo hilo.

    “Mara baada ya Serikali kuweka ukuta wa Mirerani, kumekuwepo na usalama wa kutosha huku wachimbaji wadogo wa madini wakiuza madini yao kwa bei inayoendana na Soko la Dunia na ya uhakika huku ulinzi ukiimarishwa katika eneo la Mirerani,” alisema Saniniu.

    Saniniu aliendelea kusema kuwa, amejipanga kuendeleza biashara ya uchimbaji wa madini ya Tanzanite kwa kununua vifaa vya kisasa na kutoa ajira zaidi kwa wananchi mbalimbali.

    Katika hatua nyingine, Saniniu alipongeza kazi kubwa inayofany-wa na Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini kwenye usimam-izi wa shughuli za uchimbaji wa madini ya Tanzanite kunapopele-kea Serikali kukusanya kodi zake za uhakika.

    “ Serikali imekuwa na msaada mkubwa kwetu, pasipo ukuta wa Mirerani ningeweza kuibiwa mawe ya Tanzanite yaliyopa-tikana, lakini nashukuru mara baada ya wataalam kutoka Tume ya Madini kuyathaminisha, nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanya biashara yenye uhakika na Serikali,” alisema Saniniu.

    Wakati huohuo akizungumza na vyombo vya habari, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya mbali na kumpongeza Bilionea Saniniu alisema kuwa lengo la Serikali kupitia Tume ya Madini ni kuhakikisha wachimbaji wadogo wa madini wanakuwa mabilionea kwa kuwapa mbinu za kisasa za uchimbaji wa madini.

    “Nitoe wito kwa wachimbaji wa madini wasio rasmi kuomba leseni za madini na kuanza kuchimba madini, na sisi kama Tume ya Madini kupitia Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa, tupo tayari kuwasaidia ili waweze kunufaika,” alisema Profesa Manya.

    Akielezea mikakati ya Serikali kwenye udhibiti wa utoroshaji wa madini nje ya nchi, Profesa Manya alieleza kuwa mbali na uanzishwaji wa masoko ya madini 37 pamoja na vituo vya ununuzi wa madini 38 nchini na ujenzi wa ukuta wa Mirerani, Serikali imeweka maafisa kwenye mipaka ya nchi pamoja na viwanja vya ndege.

    Aidha, Profesa Manya aliwataka wachimbaji wa madini nchini kufuata sheria ya madini pamoja na kanuni zake kwenye shughuli za uchimbaji wa madini.

    Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

    4Tume ya Madini

  • Mwenyekiti wa Tume ya Madini,Profesa Idris Kikula akizugumza nawamiliki wa machimbo ya madiniya mchanga (Heavy Minerals Sand-HMS)katika kijiji cha Shugubweni, Mkoa wa Pwani.

    Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akizugumza na wamiliki wa machimbo ya madini ya mchanga (Heavy Minerals Sand-HMS)katika kijiji cha Shugubweni, Mkoa wa Pwani.

    Tarehe 22 Agosti, 2020 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula alitembelea machimbo ya madini yanayopatikana katika mchanga wa baharini (Heavy Minerals Sand - HMS) yaliyopo katika Kijiji cha Shugubweni, Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya ziara yak maalum katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za madini, kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wachimbaji wa madini.

    Katika ziara hiyo, Profesa Kikula aliambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini wa Tume ya Madini, CPA. Venance Kasiki, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhandisi Ally Maganga, na wataalam wengine kutoka Tume ya Madini akiwemo Mjiolojia Lameck Masanja na Mhandisi Fadhili Kitivai.

    Katika hatua nyingine alimtaka Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Ally Maganga kuhakikisha kabla ya kutoa vibali vya usafirishaji madini hayo nje ya nchi ni lazima sampuli zipelekwe maabara ili kujiri-dhisha na kiwango cha metali zilizopo katika madini hayo na pia kujua thamani halisi za madini zitakazotumika kukokotoa tozo mbalim-bali za Serikali ikiwa ni pamoja na mrabaha na

    ada ya ukaguzi.

    Kabla ya Ziara hiyo, Mwenyekiti alifanya kikao na Watumishi wa Ofisi ya RMO Dar es salaam na kusikiliza changamoto mbalimbali wana-

    zokabiliana nazo na kuzitolea ufafanuzi.

    Wakati huohuo Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini wa Tume ya Madini, CPA Venance Kasiki alizitaka kampuni zinazo-chimba madini hayo kukamilisha mipango ya ushirikishwaji wa Watanzania kwenye Miradi ya Madini (Local Content Plans - LCPs) na kuiwasilisha Tume ya Madini mapema iweze-kanavyo ili wakidhi takwa la kisheria na kuon-doa usumbufu usio wa lazima katika shughuli

    zao za biashara ya madini.

    Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

    Profesa Kikula Atembelea Machimbo ya Madini Pwani

    5 Tume ya Madini #5

    Picha na Matukio

  • Uzalishaji kuanza mapema Januari

    Meneja Uzalishaji wa Baruti anayesimamia ujenzi wa mtambo wa kutengeneza baruti unaomilikiwa na kampuni ya Nitro Explo-sive, Biren Deusi amesema kuwa ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu hivyo uzalishaji wa baruti kuanza mapema Janu-ari, 2021.

    Deusi aliyasema hayo tarehe 21 Agosti, 2020 kwenye ziara ya Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula kwenye kiwan-da hicho Wilayani Kilwa Mkoani Lindi ikiwa ni sehemu ya ziara yake yanye lengo la kukagua shughuli za madini, kusikiliza kero mbalimbali za wachimbaji wa madini pamoja na kuzitatua katika mkoa huo.

    Katika ziara yake Profesa Kikula aliambat-ana na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Lindi, Mhandisi Jeremiah Hango pamoja na Maafisa wengine Daudi Ntalima, Dickson Joram na Mhandisi Fadhili Kitivai.

    Akielezea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mtambo huo, Deus alifafanua kuwa, kinachosubiriwa kwa sasa ni kibali cha kuingiza mitambo hiyo kutoka Shirika la Uwekezaji Tanzania (TIC) ambapo taratibu za upatikanaji wa kibali hicho

    zinaendelea.

    Alisisitiza kuwa, mara baada ya kuka-milika kwa mtambo huo, utakuwa na uwezo wa kuzalisha baruti kiasi cha tani 28 kwa masaa 8 sawa na tani 84 kwa siku ambapo soko lake litakuwa ni wachimbaji wakubwa, wadogo na

    masoko ya nje ya nchi.

    Akielezea changamoto katika utekeleza-ji wa ujenzi wa mtambo huo, Deus alisema kuwa ni pamoja na mlipuko wa janga la virusi vya corona lililopelekea kushindwa kuingiza baadhi ya mitambo kutoka Afrika ya Kusini na Ujerumani.

    Naye Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula aliitaka kampuni hiyo kuwasiliana na Ofisi za Tume ya Madini ili kuweza kupatiwa ushauri wa kitaalamu kwa kuzingatia Sheria ya Baruti namna ya kupangilia maeneo ya uhifadhi wa baruti katika eneo la mtambo huo ili kuweka

    mazingira ya utendaji kazi kuwa salama.

    Mtambo wa Baruti wa Kampuni ya Nitro Explosive Kukamilika Mwishoni mwa Mwaka Huu

    Biren DeusiMeneja Uzalishaji

    6Tume ya Madini

    Ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu hivyo uzalishaji wa baruti

    kuanza mapema Januari, 2021.

  • 7Tume ya Madini

    Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa Wamkosha Waziri wa Madini

    Waziri wa Madini, Doto Biteko amewapongeza Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kwa utendaji mzuri uliopelekea kuvuka lengo la ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka wa fedha 2019-2020 ambapo walikusanya shilingi bilioni 528.2 ikiwa ni zaidi ya lengo la shilingi bilioni 470 lililopangwa awali.

    Waziri Biteko aliyasema hayo tarehe 25 Julai, 2020 jijini Arusha alipokuwa akifunga mkutano wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila na Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa wenye lengo la kujadili mafanikio, chan-gamoto na namna ya kuzitatua kwenye Sekta ya Madini.

    Wageni wengine waliohudhuria katika mkutano huo ni pamoja na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi David Mulabwa, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Wakuu wa Idara na Mameneja kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini.

    Naye Naibu Waziri Nyongo akizungumza kwenye mkutano huo, aliwataka Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kuendelea kushirikiana kwa karibu na Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Taasisi nyingine pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuongeza ufanisi

    kwenye utendaji kazi wao.

    Aliwataka kila mmoja kuhakikisha anatimiza lengo la makusanyo ya maduhuli kwa mwaka wa fedha 2020-2021 alilopangiwa ili Wizara iweze kuvuka

    lengo la mwaka husika.

    Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila mbali na kuwapongeza Maafisa Madini hao aliongeza kuwa, imani kwa Serikali kwa Wizara ya Madini imeongezeka mara baada ya kufani-kiwa kukusanya maduhuli zaidi ya lengo lililowekwa

    awali.

    "Mtakumbuka mwaka jana tulisaini mkataba wa shilingi bilioni 10.6 na Wizara ya Fedha kwa ajili ya kuimarisha Tume ya Madini kwa kununua vifaa mbalimbali pamoja na magari ambapo zimezaa matunda, endeleeni kuchapa kazi na tupo tayari

    kuwasaidia muda wowote."alisema Profesa Msanjila.

    Naye Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula aliishukuru Wizara ya Madini kwa ushirikiano mzuri kwa Tume ya Madini hali iliyopelekea Tume

    kufanya vizuri kwenye Sekta ya Madini.

    Alisema kuwa changamoto zilizoainishwa katika mkutano husika zitaandaliwa vyema na kuwasilishwa ngazi za juu na utekelezaji wake kufanyika mara moja.

    Alisema siri ya mafanikio makubwa katika Wizara ya Madini ni pamoja na ubunifu na uzalendo wa Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kwenye ukusanyaji wa maduhuli na kuwataka kuendelea kusimamia shughuli za uchimbaji na biashara ya madini kwa kufuata Sheria ya Madini pamoja na

    kanuni zake.

    "Nipende kueleza kuwa, ninatambua mchango wenu mkubwa sana kwenye ukuaji wa Sekta ya Madini, mmekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kodi mbalimbali zinalipwa Serikalini, hii imesaidia sana Sekta ya Madini kukua.

    Katika hatua nyingine Waziri Biteko aliwataka Maafisa Madini Wakazi kutatua migogoro kwa kusimamia Sheria na kusisitiza kuwa wasisite kuwasilisha changamoto kwa viongozi wa Tume ya Madini pale wanapokwa-

    ma.

    Aidha, aliwataka Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kuendelea kushiriki-ana kwa kubadilishana uzoefu kwenye usimamizi wa shughuli za madini ili

    kuongeza tija kwenye utendaji kazi.

    Ni kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka 2019-2020

  • 8 Tume ya Madini #5

    Serikali imeendelea kuboresha sekta ya madini ili kuka-

    itakayosaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato nchini.

    Akizungumza hivi karibuni jijini Dodoma wakati akizin-dua Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Tume ya Madini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msan-jila alisema kuwa Serikali ina matarajio makubwa katika sekta ya madini na ndiyo maana ilirekebisha Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ili kuongeza tija.

    “Nina imani kuwa Baraza hili mtajikita kujadili namna ya kuipeleka mbele sekta ya madini kwa vile mwaka 2025 sekta hii inatarajiwa kuchangia asilimia 10 ya pato la taifa.

    Vilevile Serikali inaiwezesha Tume ya Madini kwa mategemeo kwamba makusanyo yataongezeka na wananchi watashirikishwa kikamilifu ili sekta iweze kuimarika zaidi” alisema Prof. Msanjila.

    Aliongeza kuwa, lengo la Baraza hilo la Wafanyakazi ni kutoa mchango na ushauri wa namna bora ya wafanya-kazi kushirikiana na viongozi wa Tume ya Madini katika kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya taasisi na nchi kwa ujumla.

    Naye, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula alikitaka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya

    (TUGHE) tawi la taasisi kutafuta njia muafaka za kutatua matatizo ya wafanyakazi kwa kushirikiana na

    menejimenti ya Tume ili kutunza taswira ya taasisi na kuongeza tija katika Sekta ya Madini nchini.

    Aidha, Prof. Kikula aliongeza kuwa Tume imeendelea kuimarisha sekta ya madini nchini na kuhakikisha Serikali inapata mapato endelevu na kuvuka malengo ya makusanyo

    ambayo yaliyowekwa mwaka hadi mwaka.“Mwaka 2018/2019 zilikusanywa shilingi bilioni 346.78 na kuvuka lengo la kukusanya shilingi bilioni 310.32 ambazo ni sawa na asilimia 111.59 na mwaka 2019/2020 jumla shilingi bilioni 528.24 zilikusanywa na kuvuka lengo la shilingi bilioni 470.35 ambazo ni sawa na asilimia 112” alisisitiza Prof.

    Kikula.

    Mafaniko mengine ya Tume ni uanzishwaji wa masoko 37 na vituo vya ununuzi wa madini 38 pamoja na kupungua viten-do vya utoroshwaji wa madini ambapo mwaka 2018/2019 madini yenye thamani ya dola za Marekani milioni 15.72 na shilingi bilioni 27.66 yalikamatwa kutoka maeneo mbalimba-

    li nchini yakiwa yanatoroshwa.

    Na. Immaculate Makilika – MAELEZO

    Prof Msanjila: Serikali ina Matarajio Makubwa katika Sekta ya Madini

    biliana na changamoto zinazoikabili sekta hiyo hatua

  • Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Tume Ya Madini Watembelea Eneo Litakalojengwa Ofisi Mpya Za Tume

    Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Tume ya Madini tarehe 01 Septemba, 2020 walitembelea eneo la mradi wa ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Madini jijini Dodoma.

    Akizungumza katika mahojiano maalum mmoja wa wajumbe hao ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Tume ya Madini, William Mtinya alisema kuwa wamejipanga katika kuhakikisha taratibu zote zinakamilika mapema na ujenzi kuanza mara moja.

    "Lengo letu hasa ni kuhakikisha Tume ya Madini inakuwa na ofisi zake zitakazojengwa kisasa hivyo kurahisisha utoaji wa huduma kwa wadau wa madini nchini," alisema Mtinya.

    Wajumbe wengine katika ziara hiyo walikuwa ni pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi wa Tume ya Madini, Jeremiah Mwakipesile, Mkurugenzi wa Leseni na Tehama, Mhandisi Yahya Samamba, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Dkt. Abdulrahman Mwanga, Meneja wa Biashara ya Madini, George Kaseza na Francis Fungameza

    9Tume ya Madini

    Na Greyson Mwase, Dodoma

  • 1010 Tume ya Madini #5

    Tarehe 01 Oktoba, 2020 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila alikutana na watendaji wa Kampuni ya Madini ya Twiga jijini Dodoma kwa ajili ya kupata taarifa ya utekelezaji wa kampuni hiyo pamoja na changa-moto zake kwenye shughuli za uchimbaji wa madini.

    Wengine waliohudhuria katika kikao hicho ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Kamishna wa Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki, Katibu Mtend-aji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya, Kamishna Msaidizi- Ushirikishwaji wa Watan-zania kwenye Sekta ya Madini kutoka Wizara ya Madini, Terence Ngole na watendaji wengine kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini.

    Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utendaji wa kampuni hiyo, Profesa Msanjila aliitaka kampuni ya Twiga kuhakikisha inatoa kipaumbele cha ajira kwa watanzania wenye sifa kama Miongozo ya Ushirikishwaji wa Watanzania kwenye Sekta ya Madini inavyotaka.

    “Ni vyema mkahakikisha ajira ambazo watanzania wenye sifa wanaweza kupata zinatolewa, badala ya kutoa ajira kwa wageni

    pekee,” alisema Profesa Msanjila.

    Katika hatua nyingine, Profesa Msanjila aliitaka kampuni ya Twiga kuhakikisha inatangaza mpango wa manunuzi wa mwaka katika vyombo vya habari kama vile magazeti na tovuti mbalim-bali ili kutoa fursa kwa watanzania wengi kujipanga na kuomba

    zabuni za kutoa huduma kwenye kampuni hiyo.

    Aidha, Profesa Msanjila aliitaka kampuni hiyo kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa viwango vya mishahara kulingana na sifa na uzoefu wa wataalam wa Tanzania na wa kutoka nje badala

    ya kuwepo na utofauti kulingana na uraia.

    Akielezea utendaji wa kampuni hiyo Meneja wake, Benedict Busunzu alieleza kuwa katika shughuli zake za kila siku kampuni imekuwa ikishirikisha jamii inayozunguka mgodi wake fursa za biashara na kununua bidhaa mbalimbali kutoka katika jamii

    husika.

    Aliongeza kuwa, kampuni inaendelea kubuni teknolojia mbalim-bali ili kuhakikisha shughuli za uchimbaji wa madini zinaleta tija

    huku wakizingatia usalama wa afya na mazingira.

    Profesa Msanjila Akutana na Kampuni ya Madini ya Twiga

  • 11Tume ya Madini

    Na Greyson Mwase, Simiyu

    Wadau wa madini nchini wameipongeza Wizara ya Madini pamoja na Taasisi zake kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini, uliopelekea Sekta hiyo kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi.

    Wakizungumza katika nyakati tofauti walipotembelea katika banda la Tume ya Madini kwenye Maonesho ya Kitaifa ya Nane Nane yaliyofanyika kuanzia tarehe 01 hadi 10 Agosti,2020 katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu walisema kuwa, mabadiliko ya Sheria ya Madini yaliyopelekea uanzishwaji wa Tume ya Madini yameboresha huduma zinazotole-wa na Serikali kwa wachimbaji wa madini.

    Akizungumza kwa niaba ya wadau wengine wa madini, Ngumila Mangu, mchimbaji wa madini kutoka Wilayani Maswa alisema kuwa, kufunguliwa kwa Ofisi za Maafisa Madini Wakazi Mikoani kumeboresha huduma za upatikanaji wa leseni za madini tofauti na zamani walipokuwa wanafuata huduma mbali.

    Katika hatua nyingine, alimpongeza Waziri wa Madini, Doto Biteko, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya na watendaji wa Tume ya

    Madini.

    Aliongeza kuwa, pia kuanzishwa kwa masoko ya madini nchini kumewasaidia kupata masoko ya biashara ya madini na kuuza kulin-gana na bei elekezi zinazotolewa kila siku

    kulingana na soko la dunia.

    Nao wadau wengine walipongeza kazi kubwa inayofanywa na Vitengo vya Mawasiliano Serikalini vya Wizara ya Madini na Tume ya Madini katika kuelimisha umma na kutangaza

    mafanikio ya Sekta ya Madini.

    "Kila mara tunapata taarifa mbalimbali kuhusu mafanikio ya Sekta ya Madini, shuhuda mbalimbali za wachimbaji wadogo waliofanikiwa kama Laizer Sanin-iu wa Mirerani, jana tumeshuhudia akika-bidhi jiwe kubwa lenye takribani kilo sita, pongezi kubwa tunatoa kwa Meneja Habari wa Tume ya Madini na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Madini, alisema John Damas kutoka

    Wilayani Maswa.

    Aliongeza kuwa, wamekuwa wakipata majarida na vipeperushi mbalimbali kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini ambavyo vinakuwepo kwenye tovuti na mitandao ya kijamii hivyo kuwa

    na uelewa mpana wa Sekta ya Madini.

    Wadau Waipongeza Wizara ya Madini, Usimamizi Sekta ya Madini

    Mtaalam kutoka Tume ya Madini, Kasmil Daudi akitoa elimu kuhusu ushirikishwaji wa wazawa kwenye utoaji wa huduma

    katika Sekta ya Madini kwa wanafunzi wa shule mbalimbali waliotembelea banda la Tume ya

    Madini kwenye Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani

    Simiyu tarehe 05 Agosti, 2020

  • 12 Tume ya Madini #5

    Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Akutana na Wadau wa Madini Dodoma

    Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya tarehe 10 Septemba, 2020 alikutana na wadau wa madini jijini Dodoma kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali.

    Wadau waliohudhuria kikao chake ni pamoja na wawakilishi kutoka Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Benki na Wizara ya Madini.

    Akizungumza kupita mahojiano maalum Profesa Manya alisema kuwa, kikao hicho kiliipa Tume ya Madini picha ya changamoto zilizopo katika Sekta ya Madini kwenye usimamizi na ukusanyaji wa kodi mbal-imbali ili Sekta ya Madini iwe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa Uchumi wa Nchi.

    "Kama Tume ya Madini tumejipanga katika kuhakikisha Sekta ya Madini inaongeza mchango wake kwenye ukuaji wa uchumi wa

    nchi" alisema Profesa Manya.

    Akielezea mikakati ya kuwawezesha wachim-baji wadogo alisema kuwa Serikali inahamasi-sha wachimbaji wadogo kuunda vikundi ili kupatiwa leseni za madini na kuomba mikopo

    kwenye benki mbalimbali nchini.

    Aidha, Profesa Manya aliwataka wachimbaji wa madini nchini kuendesha shughuli zao kwa kufuata Sheria ya Madini pamoja na kanuni

    zake.

  • 13Tume ya Madini

    Tarehe 23 Septemba, 2020 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila alifungua kongama-no la biashara na uwekezaji katika Maonesho ya Tatu ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yaliyokuwa yanaendelea katika Uwanja wa Kituo

    Kongamano hilo lilikutanisha wadau wa madini kwa lengo la kujadili na kujenga uelewa wa pamoja wa fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini ndani ya mkoa wa Geita.

    Wadau walioshiriki katika kongamano hilo ni pamoja na wawakilishi kutoka Wizara ya Madini na Taasisi zake, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Kampuni za Uchimbaji wa Madini, Wawakilishi kutoka Chama cha Wachimbaji wa Madini wa Mkoa wa Geita (GEREMA) Benki Mbalim-bali na Taasisi nyingine za Serikali.

    Kupitia hotuba yake Profesa Msanjila aliwataka wananchi wa mkoa wa Geita kuchangamkia fursa za uwekezaji kwenye Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja na kutoa huduma mbalimbali kwenye kampuni zinazoji-husisha na uchimbaji wa madini ikiwa ni pamoja na ulinzi, vyakula n.k.

    Akielezea mafanikio katika Wizara ya Madini, Profesa Msanjila alieleza kuwa ni pamoja na ukusanyaji wa maduhuli kutoka shilingi bilioni 160 hadi shilingi bilioni 528 ndani ya kipindi cha miaka mitano, ongezeko la kasi ya utoaji wa leseni za madini, kutengwa maeneo zaidi kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini pamoja

    na uanzishwaji wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini.Katika hatua nyingine Profesa Msanjila aliziomba taasisi za kifedha kutokusita kutoa mikopo kwa wachimbaji wa madini na wajasiriamali wanaotoa huduma

    kwenye kampuni za uchimbaji wa madini.

    Aidha, Profesa Msanjila aliwataka wananchi kuzalisha bidhaa bora ili kupata soko la uhakika kwenye kampuni zinazochimba madini.

    “Nia yetu kama Serikali ni kuhakikisha Sekta ya Madini inawezesha ukuaji wa sekta nyingine kama vile kilimo na uvuvi, tunatamani kuona hata madini yakiisha, kunakuwepo na ukuaji wa sekta nyingine zitakazowezesha uchumi wa nchi kupaa.Aidha, Profesa Msanjila aliipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Wizara ya Madini na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa maan-

    dalizi mazuri ya maonesho hayo.

    Taasisi zilizopo chini ya Wizara zilizoshiriki katika maonesho hayo ni pamoja na Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), Taasisi ya Uhama-sishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia

    (TEITI), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Mgodi wa STAMIGOLD.

    Profesa Msanjila Afungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji Geita

    cha Uwekezaji Bomba Mbili Mjini Geita.

  • ya bati... Na.1

    www.tumemadini.go.tz

  • 15 Tume ya Madini

    Na Greyson Mwase, Geita

    Tume ya Madini Yapongezwa kwa kutoa Elimu Bora Kwenye Maonesho

    ya Madini Geita

    Wadau wa madini nchini wameipongeza Tume ya Madini kwa elimu bora kuhusu shughuli za utafiti, uchimbaji na biashara ya madini na kuongeza kuwa elimu hiyo itawasaidia sana kuboresha ushiriki wao kwenye Sekta ya Madini.

    Wadau hao walitoa pongezi hizo tarehe 19 Septemba, 2020 katika Maonesho ya Tatu Ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yaliyokua yanaende-lea katika Uwanja wa Kituo cha Uwekezaji cha Bombam-bili Mkoani Geita.

    Wakizungumza katika nyakati tofauti wadau hao walisema kuwa walikuwa na uelewa mdogo juu ya namna ya kuomba na kupata leseni za madini pamoja na namna bora ya uendeshaji wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini lakini kupitia maonesho husika wamepata elimu ya namna ya kupata leseni, namna bora ya uendeshaji wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini.

    Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wasio rasmi wanaoendesha shughuli zao katika eneo la Mwakitolyo Mkoani Shinyanga Mohamed Ramadhan alisema kuwa mara baada ya kupata elimu husika, wataunda kikundi na kuomba leseni ili waanze kuchimba na kupata faida huku wakilipa kodi mbalimbali Serikalini.

    Naye Lazaro Paul ambaye ni mchimbaji mdogo anaye-chimba madini ya dhahabu katika eneo la Kakola mkoani Shinyanga alisema kuwa, kabla ya kupewa elimu na wataalam wa Tume ya Madini alikuwa hafahamu tarati-bu za uchimbaji wa madini na kuongeza kuwa kuanzia sasa ataomba leseni na kuanza kuchimba madini rasmi.

    “Baada ya kupata elimu safi kutoka kwa wataalam nitaomba leseni ya kuchimba madini ya dhahabu mkoani Morogoro maana ninatambua kuwa sasa ninaweza kumi-liki leseni ya madini kwa kufuata taratibu,” alisema Paul.

    Aidha, Edward Makanza ambaye ni mchimbaji mdogo katika Mgodi wa Buckreef uliopo mkoani Geita aliongeza kuwa kupitia maonesho hayo amepata uelewa wa namna ya kuendesha shughuli za uchimbaji wa madini kwa kuzingatia usalama wa

    mazingira.

    Naye Mhandisi Uchenjuaji wa Madini kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Cosmas Festo aliipongeza Tume ya Madini kwa elimu inayotolewa mara kwa mara kwa wadau wa madini nchini.

    Akielezea lengo la ushiriki wa Tume ya Madini kwenye maonesho hayo, Mtakwimu wa Tume ya Madini, Azihar Kashakara alisema kuwa ni pamoja na kuelimisha wadau wa madini hususan wachimbaji wadogo kuhusu namna ya kuomba leseni za madini, namna bora ya uendeshaji wa shughuli za uchimbaji na biashara

    ya madini.

    Alisema kuwa kumekuwepo na changamoto ya wananchi wengi kutokuwa na uelewa wa namna ya kuomba leseni za madini,

    uchimbaji salama na biashara ya madini.

    #5

  • 16 Tume ya Madini

  • 17 Tume ya Madini #5

    /PICHA NA MATUKIO

    ZIARA YA KATIBU MTENDAJI WA TUME YA MADINI KATIKA BANDA LA TUME KWENYE

    MAONESHO YA SABASABA

    Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (kushoto) akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kikundi cha MIVA kinachohusika na uongezaji wa thamani wa madini.

    Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Profesa Shukrani Manya (aliyekaa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki kutoka Tume ya Madini.

  • BALOZI WA UJERUMANI NCHINI ATEMBELEA BANDA

    LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA SABASABA

    Balozi wa Ujerumani Nchini, Regine Hess tarehe 10 Julai, 2020 alifanya ziara kwenye Banda la Tume ya Madini na Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyi-ka katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

    Mara baada ya kupokewa na kutembezwa kwenye mabanda Balozi Hess alipongeza kazi nzuri inayofanywa na Wizara ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini. Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali kwenye ziara hiyo.

    18 Tume ya Madini #5

  • 19 Tume ya Madini #5

    MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA – USHIRIKI WA TUME YA MADINI KATIKA MAONESHO

    YA SABASABA JULAI 1- 13, 2020

  • 20 Tume ya Madini #5

    ZIARA YA WAZIRI WA MADINI DOTO BITEKO KWENYE BANDA LA TUME YA MADINI

    KATIKA MAONESHO YA MADINI GEITA TAREHE21 SEPTEMBA 2020.

  • VIONGOZI WA TUME YA MADINI WATEMBELEA BANDA LA TUME KWENYE MAONESHO YA

    MADINI GEITA 26 SEPTEMBA 2020

    21 Tume ya Madini #5

    Viongozi wa Tume ya Madini wakiongozwa na Kamishna wa Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki tarehe 26 Septemba 2020, walitembelea Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yaliyofanyika katika

    Uwanja wa Kituo cha Bombambili Mjini Geita.

  • www.tumemadini.go.tz

    Tume ya Madini

    MAWASILIANO Telegramu "MADINI" Simu: + 255-26 2320051 Nukushi: +255 26 2322282Barua pepe: [email protected]. L. P 2292 , DODOMA.

    Jarida la Mtandaoni

    Tume ya Madini 2020 | Toleo Na.5