16
Bulletin News Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] http://www.mem.go.tz HABARI ZA NISHATI &MADINI Toleo No. 44 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - Novemba 28 Desemba-4, 2014 Ruzuku kwa wachimbaji wadogo sasa USD 100,000 Uk.7 ESCROW Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akitoa Maelezo ya Serikali kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Taarifa ya ukaguzi maalum kuhusiana na Miamala iliyofanyika katika akaunti ya ESCROW ya Tegeta pamoja na umiliki wa kampuni ya IPTL. n Prof. Muhongo aanika Ukweli n Soma Taarifa kamili Uk 2-5

JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

Embed Size (px)

DESCRIPTION

JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

Citation preview

Page 1: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

BulletinNews

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI &MADINI

Toleo No. 44 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - Novemba 28 Desemba-4, 2014

Ruzuku kwa wachimbaji wadogo sasa USD 100,000 Uk.7

ESCROW

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akitoa Maelezo ya Serikali kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Taarifa ya ukaguzi maalum kuhusiana na Miamala iliyofanyika katika akaunti ya ESCROW ya Tegeta pamoja na umiliki wa kampuni ya IPTL.

nProf. Muhongo aanika UkwelinSoma Taarifa kamili Uk 2-5

Page 2: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI

1. Historia ya Mradi

Mheshimiwa Spika, Katika miaka ya tisini (1990s), Tanzania ilikuwa ikikabiliwa na tatizo la uhaba wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme, hali iliyopelekea kuwepo kwa upungufu wa umeme na kuathiri shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. Ili kukabiliana na tatizo hilo, Seri-kali ilichukua hatua za dharura za kuanzisha mradi wa kufua umeme wenye uwezo wa kuzalisha Megawati (MW) 100.

2. Upatikanaji wa IPTL

Mheshimiwa Spika, Mwaka 1994 Serikali ilitoa kazi ya uwekezaji kwa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) iliyokuwa inamilikiwa na Kampuni za VIP Engineering and Mar-keting Ltd ya Tanzania iliyokuwa na Asilimia 30 na MECHMAR Corporation ya Malaysia (MECH-MAR) iliyokuwa na Asilimia 70. Kampuni ya IPTL ilipewa leseni ya kujenga, kumiliki na kuende-sha (Build-Own-Operate) Mtambo wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa MW 100 kwa kutumia mafuta mazito eneo la Tegeta-Salasala, Dar Es Salaam.

Katika Ukurasa wa 52 Aya ya 2, ya Taarifa ya PAC, Kamati imependekeza Mtambo huo utaifishwe.

Ufafanuzi:

Mheshimiwa Spika, Kulingana na Mkataba wa PPA kati ya TANESCO na IPTL, majuku-mu ya IPTL yalikuwa ni kujenga, kumiliki na kuendesha (Build, Own and Operate – BOO). Hivyo, kutaifisha Mtambo huo ni kukiuka makubaliano katika Mkataba wa PPA wa tarehe 26 Mei 1995, ukiukwaji wa aina hii ukitokea unaweza kuingiza Serikali katika mgogoro mkub-wa ikiwa ni pamoja na kushtakiwa kwenye Mahakama za kibiashara za kimataifa. Aidha utaifishaji wa miradi ya uwekezaji binafsi itakuwa ni njia ya kufukuza wawekezaji binafsi

Mheshimiwa Spika, Tarehe 26 Mei, 1995, TANESCO na IPTL walisaini Mkataba wa PPA kwa muda wa miaka ishirini (20), kwa ajili ya kununua umeme utakaozalishwa na IPTL. Kwa mujibu wa Mkataba huo, IPTL ilitakiwa kuiuzia TANESCO umeme usiopungua Asilimia 85 ya uwezo wa Mtambo (minimum off take). Hata hivyo, uzalishaji wa umeme haukuanza mara moja kutokana na mgogoro uliotokea kati ya TANESCO na IPTL kuhusu gharama halisi za uwekezaji na namna ya kukokotoa Capacity Charges. Hivyo, IPTL ilianza kuzalisha umeme tarehe 15 Januari, 2002. Kuto-kana na hali hiyo muda wa miaka 20 ya Mkataba ulianza kuhesabiwa tarehe 15 Januari, 2002 baada ya kuanza uzalishaji (Commercial Operation Date).

Mheshimiwa Spika, Pamoja na mambo mengine muhimu yaliyokuwemo katika PPA, Kifungu Na. 6 cha Mkataba huo kinaipa TANESCO wajibu wa kulipa malipo yaliyotajwa hapo juu na kwamba endapo kutakuwa na mgogoro wowote kuhusiana na malipo hayo (Disputed Amount), itafunguliwa Akaunti maalum (Escrow Account) ya kuhifadhi fedha hizo hadi pale pande mbili zitakapokubali-ana juu ya uhalali wa malipo yanayobishaniwa. Aidha, chini ya PPA, migogoro yote kuhusiana na masuala ya utekelezaji wa Mkataba huo ilitakiwa kuwasilishwa na kuamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) ya London. Hivyo, ilikuwa ni jukumu la kila mhusika katika Mkataba huu kuwasilisha malalamiko yake ICSID yanapotokea.

Katika Ukurasa wa 8 Aya ya 2 ya Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa mwaka 2004 TANESCO ilifungua shauri la ICSID 2 kupinga kiasi kikubwa cha tozo ya Capacity Charge.

Ufafanuzi

Mheshimiwa Spika, Taarifa hiyo siyo kweli. TANESCO haijawahi kufungua shauri lolote IC-SID ya London au Mahakama yo yote dhidi ya IPTL kupinga kiasi kikubwa cha Capacity Charge kama inavyoelezwa katika Taarifa ya PAC. Shauri la ICSID 2 lilifunguliwa tarehe 31 Oktoba 2010 na Standard Chatered Bank Hong Kong (SCBHK) kwa ajili ya kudai mali-po ya deni ililonunua kutokana na mkopo uliotolewa na mabenki ya ushirika ya Malaysia kwa IPTL. Wahusika katika Shauri hilo la ICSID 2 ni SCBHK na TANESCO na wala siyo TANESCO na IPTL.

Mheshimiwa Spika, tarehe 12 Februari, 2014 ICSID ilitoa uamuzi kuhusiana na Shauri la SCB-HK na TANESCO na kuwashauri wakae kukokotoa upya malipo ya Capacity Charge. Hata hivyo, ilikuwa vigumu kwa pande hizo kutekeleza uamuzi huo kutokana na pande hizo ku-tokuwa na Mkataba wa kibiashara baina yao. Vile vile, kupitia Shauri la Madai Na. 60/2014, lililofunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania na IPTL tarehe 4 Aprili, 2014 ilizuia utekelezaji wa maelekezo hayo.

3. Mgogoro kati ya IPTL na TANESCO

Mheshimiwa Spika, Migogoro kati ya TANESCO na IPTL ilianza muda mfupi baada ya PPA ku-sainiwa tarehe 26 Mei, 1995. IPTL waliitaka TANESCO wakubaliane bei za kununua umeme kwa kuzingatia gharama za uwekezaji. Pande hizo mbili zilishindwa kukubaliana gharama za Capac-ity Charge kwa vile TANESCO walidai kuwa gharama zilizoainishwa na IPTL ni kubwa kuliko gharama halisi za uwekezaji. Mwaka 1998, TANESCO iliajiri Kampuni ya Mawakili ya Mkono & Co. Advocates kutoa huduma za kisheria kwa kushirikiana na Huntons & Williams ya Marekani. Kutokana na tofauti za gharama za Uwekezaji, Mawakili hawa waliishauri TANESCO ifungue Kesi ICSID nchini Uingereza dhidi ya IPTL ili kupinga gharama hizo.

Mheshimiwa Spika, Kwa kuzingatia ushauri huo wa Mawakili, TANESCO ilifungua Kesi Na.ARB/98/8 ya Mwezi Agosti, 1998 ikidai kuwa gharama halisi za uwekezaji ni Dola za Marekani milioni 90 na siyo milioni 163.53 kama ilivyodaiwa na IPTL. Aidha, IPTL ilidai kuwa kiwango cha marejesho ya uwekezaji (Internal Rate of Return-IRR) ni Asilimia 23.10 ambacho pia kilipingwa na TANESCO.

Mheshimiwa Spika, Tarehe 12 Julai, 2001, ICSID ilitoa uamuzi wa Kesi hiyo pamoja na mambo mengine kwamba:-

i. Gharama halisi za uwekezaji zikiwemo Mtambo na nyumba za wafanyakazi wa IPTL zilizoain-ishwa katika hesabu ya IPTL zilikuwa ni Dola za Marekani milioni 163.53 lakini ICSID iliona kuwa gharama halisi ni Dola za Marekani milioni 127.20;

ii. Kiwango cha marejesho ya uwekezaji (Internal Rate of Return-IRR) ilikuwa Asilimia 22.31 badala ya Asilimia 23.10 iliyodaiwa na IPTL; naiii. TANESCO na IPTL wakubaliane mfumo wa malipo ya kununua umeme ukizingatia gharama halisi za uwekezaji na kiwango cha marejesho ya uwekezaji (IRR) cha Asilimia 22.31 kwa kutumia financial model iliyokubalika na ICSID.

Katika Ukurasa wa 11 Aya ya 2 ya Taarifa ya PAC, imeelezwa kuwa mtaji wa uwekezaji katika Mtambo wa IPTL ni Shilingi 50,000/= na kwamba huo ndio ungetumika kukokotoa Capacity Charg-es ili kulipa tozo ndogo kuliko ilivyo sasa.

Ufafanuzi

Mheshimiwa Spika, Maelezo hayo siyo sahihi. Ukweli ni kwamba kutokana na maamuzi ya ICSID 1 ya tarehe 12 Julai, 2001, gharama za ujenzi wa Mtambo wa Tegeta ni Dola za Marekani 127.20 kama ilivyoelezwa katika Ukurasa wa 47 Aya ya 4 ya Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Katika Taarifa hiyo, pia imeelezwa kuwa ilikubalika kuwa uwiano wa deni na mtaji utakuwa 70:30. Hii ikiwa na maana kwamba, deni ni Dola za Marekani milioni 89.04 na mtaji ni Dola za Marekani milioni 38.16. Uamuzi huo haujabadil-ishwa na Mahakama yo yote au mtu ye yote.

Mheshimiwa Spika, tunakubaliana kwamba fedha iliyopokelewa kutoka Mabenki ya Ushirika ya Malaysia kama mkopo ni Dola za Marekani milioni 85.86. Kati ya Dola za Marekani milioni 105 zilizokuwa zimeidhinishwa. Swali la kujiuliza, je Mtambo huo ulikamilikaje kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 85.86, huku gharama halisi ya ujenzi wa Mtambo wa Tegeta ikawa Dola za Marekani milioni 127.20?

Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kwamba kuna matumizi ya zaidi ya Dola za Marekani mil-ioni 38.16 ambazo pia zimetumika kwenye uwekezaji. Taarifa ya Kamati ya PAC haikuonesha fedha hiyo kuwa sehemu ya uwekezaji.

Mheshimiwa Spika, Tarehe 30 Juni, 2004, Kampuni ya Mawakili iliyokuwa ikiiwakilisha TANES-CO katika kesi ya kwanza ya usuluhishi, Kampuni ya Mkono & Co Advocates, iliishauri TANESCO iendelee kupinga kiwango cha malipo ya Capacity Charge kilichokuwa kimeafikiwa tarehe 12 Julai, 2001 na pande hizi mbili katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICSID) ya London. Hii ilikuwa ni miaka miwili tu baada ya usuluhishi uliochukua miaka minne kukamilika na Mtambo kuanza kuzalisha umeme tarehe 15 Januari, 2002.

Mheshimiwa Spika, Hata hivyo, baada ya ushauri huu, Mawakili hawa (Mkono & Co. Advocates) hawakuishauri TANESCO ifungue kesi katika Mahakama za Tanzania wala katika Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kimataifa (ICSID) ya London.

Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia tarehe 5 Septemba, 2013 wakati Mheshimiwa Jaji Utamwa anatoa hukumu yake juu ya mgogoro wa WanaHisa wa IPTL hapakuwepo na kesi yo yote kwenye Ma-hakama yo yote ya kupinga gharama za Capacity Charge kati ya TANESCO na IPTL, iwe katika Mahakama za ndani au za nje. Kwa kutokuwepo Msuluhishi (Broker) katika suala hili, madai yo yote ya TANESCO yanakuwa ni madai ya upande mmoja ambayo kisheria hayawezi kuchukuliwa kuwa ndiyo madai halisi. Kwa sababu hiyo haikuwepo formula rasmi ya kuutatua mgogoro huo zaidi ya majadiliano na maafikiano kati ya pande mbili (TANESCO na IPTL).

4. Uuzaji wa Hisa za VIP

Mheshimiwa Spika, Kutokana na VIP Engineering and Marketing Limited (VIP) kuona kuwa hainu-faiki na ubia wake katika IPTL, ilikusudia kuuza Hisa zake kwa MECHMAR. Hata hivyo, MECH-MAR haikuweza kununua Hisa hizo kwa sababu ilitaka thamani ya Hisa za VIP zitokane na ripoti ya ukaguzi ya mwaka (Audited Financial Report) na taratibu za kihasibu za kimataifa (International Accounting Rules), VIP haikukubaliana na utaratibu huo.

Mheshimiwa Spika, Kutokana na kutokubaliana, MECHMAR iliishauri VIP ifungue Shauri la ma-dai hayo kwenye Mahakama ya Usuluhishi ya Uingereza (LCIA) kulingana na Mkataba wa Wanahi-sa wa IPTL. Hata hivyo, VIP haikufungua Shauri katika Mahakama ya usuluhishi kama ilivyoshauri-wa na MECHMAR badala yake tarehe 25 Februari, 2002 VIP ikafungua Shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Miscellaneous Civil Application No. 49/2002) ikiomba Kampuni ya IPTL ifilisiwe ikiwa ni mwezi mmoja tangu kuanza uzalishaji.

MAELEZO YA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI MAALUM KUHUSIANA NA MIAMALA ILIYOFANYIKA KATIKA AKAUNTI YA “ESCROW” YA TEGETA PAMOJA NA UMILIKI WA KAMPUNI YA IPTL

Inaendelea Uk. 3

Page 3: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz MAONI

5. Uamuzi kuhusu Ufilisi wa IPTL

Mheshimiwa Spika, Shauri lililofunguliwa na VIP tarehe 25 Februari, 2002 liliendelea kuwa Ma-hakamani hadi ilipofika tarehe 16 Desemba, 2008. Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Jaji Oriyo, J ilitoa uamuzi wa kuiweka IPTL katika Ufilisi wa Muda (Provisional Liquidation) chini ya Kabidhi Wasii Mkuu (Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini - RITA). Mfilisi wa Muda alipewa majukumu maalum yafuatayo:

i. Kulinda mali zote za IPTL katika kipindi chote cha Ufilisi wa Muda; na

ii. Kufanya uchunguzi wa tuhuma zote zilizotolewa na VIP dhidi ya MECHMAR na kutoa ripoti za uchunguzi huo ili Mahakama iweze kutoa uamuzi.Mheshimiwa Spika, Tarehe 15 Julai, 2011, Mahakama Kuu ya Tanzania (Kaijage, J) ilitoa uamuzi kwamba, IPTL iwekwe kwenye Ufilisi Kamili (Full Liquidation) na RITA ilithibitishwa kuwa Mfilisi wa IPTL.

Mheshimiwa Spika, Kutokana na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Standard Chartered Bank Hong Kong (SCBHK) iliyokuwa imenunua deni la IPTL kutoka kwa DANHARTA, ilipinga na kuiomba Mahakama ya Rufaa ifanye mapitio ya uamuzi wa Mahakama Kuu (Application for Revision – Civil Revision No. 1/2012) ikiainisha dosari katika uamuzi wa Mahakama Kuu ulio-amuru kufilisiwa kwa IPTL. SCBHK ilibainisha dosari za maombi ya kutaka IPTL kufilisiwa kwa kuwa maombi ya SCBHK ya kutaka Mahakama iteue msimamizi (Administrator) wa kuisimamia IPTL (kwa niaba ya SCBHK) yalikuwa hayajasikilizwa.

Mheshimiwa Spika, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilikubaliana na hoja za SCBHK na hivyo kuamuru shauri hilo lirejeshwe Mahakama Kuu ili IPTL irudi mikononi mwa Mfilisi wa Muda (Provisional Liquidator) ambaye alipewa majukumu yafuatayo:-

i. Kukusanya mali na madeni yote ya IPTL; ii. Kupokea na kusajili madeni yote dhidi ya IPTL; iii. Kusuluhisha migogoro kati ya wanahisa wa IPTL; na

iv. Kusimamia na kuendesha Mtambo wa kuzalisha umeme wa IPTL kwa niaba ya IPTL.

Mheshimiwa Spika, Baada ya kuteuliwa, Mfilisi wa Muda (Provisional Liquidator) alifanya juhudi ya kumaliza mgogoro huo wa IPTL nje ya Mahakama kwa kushirikisha wadau mbalimbali (Stake-holders) wa IPTL kupitia kikao chake cha tarehe 9 Novemba, 2011. (Kiambatisho Na.1). Juhudi hizo hazikufanikiwa na ikalazimu shauri liendelee Mahakamani.

6. Uhalali wa uhamishwaji wa Asilimia 70 za Hisa zaMECHMAR kwenda PAP

Mheshimiwa Spika, Suala la uhalali wa umiliki wa Hisa katika Kampuni hizi linahusu wanahisa wa Kampuni wenyewe. Serikali haiwajibiki kuingilia mahusiano ya kibiashara ya wanahisa katika Kampuni Binafsi. Hata hivyo, kulingana na Sheria za nchi ikiwa ni pamoja na Kifungu cha 172 cha Sheria ya Makampuni (Sura 212), mauziano ya Hisa yaliyofanyika nje ya nchi yatatambuliwa tu, endapo usajili wa Hisa hizo utafanyika hapa nchini. Kwa mujibu wa taarifa za BRELA za tarehe 31 Desemba, 2013, zinaonesha kuwa uhamishaji wa Hisa 7 za MECHMAR katika IPTL kwenda PAP ulisajiliwa hapa nchini. Kwa maana hiyo, PAP ni mmiliki wa Asilimia 70 za IPTL.

Katika ukurasa wa 44 Aya ya 1 ya Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa PAP siyo mmiliki halali wa Hisa 7 za MECHMAR katika IPTL.

Ufafanuzi

Mheshimiwa Spika, katika maelezo ya Kamati ukurasa wa 30, Kamati imethibitisha kwamba nyaraka za mauziano kati ya MECHMAR na Piper Link zilipokelewa na Harbinder Singh Sethi ambaye pia ndiye mmiliki wa PAP. Kwa uthibitisho huo, Kamati inakubali kuwa Hisa za MECHMAR katika IPTL zinamilikiwa na PAP.

Katika Ukurasa wa 25 Aya ya 2 ya Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa hakuna ushahidi wa PAP kumi-liki Asilimia 70 ya Hisa zilizokuwa zikimilikiwa na MECHMAR katika IPTL.

Ufafanuzi

Mheshimiwa Spika, napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa umiliki wa Hisa 7 za IPTL unatambuliwa hata na SCBHK ambayo ilisaini makubaliano tarehe 25 Novemba, 2011 na PAP ya kulipwa deni la mkopo wa fedha za kununua deni la ujenzi wa Mtambo wa Tegeta. Kiambatisho Na 2.

7. Majadiliano ya mikopo ya IPTL na Wadai

Mheshimiwa Spika, Kutokana na Hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotolewa tarehe 5 Septemba, 2013, Kampuni ya PAP ilijadiliana na wadai halali wa mikopo ya IPTL na kuingia Mka-taba wa kuwalipa wadai wote wa IPTL. SCBHK inayodai kuidai IPTL mikopo katika ujenzi wa Mtambo wa Tegeta haikuwasilisha madai ya aina yo yote ili iweze kulipwa.

Mheshimiwa Spika, Ukweli ni kwamba, SCBHK iliyokuwa ikiidai IPTL fedha ilizotumia kununua deni lililotokana na kufilisiwa kwa MECHMAR kule Malaysia (siyo Tanzania) haijawahi kujadili-ana na IPTL kuhusu malipo ya mkopo wake kama upo. Mvutano huu unaendelea ICSID kati ya TANESCO na SCBHK, ukiitaka TANESCO ilipe gharama za kununua umeme ikijumuisha deni la IPTL. Madai ya SCBHK dhidi ya TANESCO yanatokana na madai ya kuwepo kwa Deed of Assignment ya MECHMAR kuhusiana na Mkopo wa IPTL ambapo Mtambo wa IPTL uliwekwa kama dhamana ya Mkopo.

Mheshimiwa Spika, Hata hivyo Deed of Assignment hiyo haikuwahi kusajiliwa hapa nchini kama inavyotakiwa katika Kifungu Na. 172 cha Sheria za Makampuni Sura. 212 zinavyoelekeza. Kutoka-na na kutokusajili Assignment Deed hiyo, SCBHK ilikosa sifa za kufungua madai yake hapa nchini badala yake ilifungua madai haya ICSID nchini Uingereza. Kitendo hicho kinaonesha kudharau Mahakama zetu na PAC inataka tuziamini Mahakama za nje kuliko za kwetu. 8. Jitihada za Makampuni mbali mbali kununua Hisa za VIP Mheshimiwa Spika, Kutokana na tofauti zilizokuwepo kati ya MECHMAR na VIP kuanzia mwan-zo wa mradi, VIP iliamua kuuza Hisa zake zilizoko IPTL kwa makampuni mbalimbali kwa nyakati tofauti ikiwemo MECHMAR kama mwanahisa mwenzake, NSSF, Camel Oil, Great White Shark Opportunity Fund pamoja na SYMBION lakini haikuwezekana kutokana na kutoafikiana katika bei.

Mheshimiwa Spika, Baadaye VIP chini ya usuluhishi ya RITA, iliuza Hisa zake kwa PAP kwa thamani ya Dola za Marekani milioni sabini na tano (US$ 75,000,000/=). Ununuzi wa Hisa Asilimia 30 za VIP uliofanywa na PAP ndiyo uliyomaliza mgogoro wa Wanahisa uliyokuwa Mahakamani na kuufanya Mtambo wa IPTL kumilikiwa na PAP kwa kuwa ndiyo iliyomiliki Hisa zote Asilimia 100 za IPTL.

Taarifa ya PAC: Katika ukurasa wa 58 wa Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini ndiye aliyekuwa Dalali Mkuu aliyewakutanisha Bw. Harbinder Sethi na Bw James Ruge-malira

Ufafanuzi

Mheshimiwa Spika, Taarifa hii siyo sahihi kwa kuwa tangu tarehe 9 Novemba, 2011, RITA aliitisha mkutano na kuwakutanisha wadau wote wa IPTL. Wakati huo, Waziri wa Nishati na Madini aliyeko sasa alikuwa bado hajateuliwa kwenye wadhifa huo.

9. Kufungua ESCROW Akaunti

Mheshimiwa Spika, Tarehe 30 Juni, 2004, TANESCO kwa ushauri wa Mkono & Co Advocates walitoa hoja kuwa gharama za kununua umeme zilikokotolewa kwa kutumia IRR ya Asilimia 23.10 na makadirio ya gharama za mtaji wa Asilimia 30 ambao ni Dola za Marekani milioni 38.16, wakati mtaji halisi (equity) wa IPTL ni chini ya Dola za Marekani 100. Hivyo, TANESCO walikuwa waki-toa notisi (Dispute Notice) kwa kila Ankara ya malipo kupinga gharama hiyo kulingana na Kifungu Na. 6.8 cha Mkataba wa PPA. Kifungu hicho kinaeleza kuwa ikiwa upande wote haukubaliani na usahihi wa malipo katika Ankara zilizowasilishwa kwa ajili ya malipo ya gharama za umeme wanatakiwa watoe notisi (Invoice Dispute Notice) kwa upande mwingine. Vile vile, Mawakili wa TANESCO (Mkono & Co Advocates) walishauri kwamba kutokana na pingamizi hilo, ifungu-liwe Akaunti Maalum (Escrow Account) kwa ajili ya kuhifadhi fedha ambazo zilitokana na Ankara zilizokuwa zinapingwa.

Mheshimiwa Spika, kutokana na ushauri wa Mkono Co. & Advocates tarehe 5 Julai, 2006, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilisaini Mkataba wa kufungua Akaunti Maalum (Escrow Account) kwa ajili ya kuweka fedha zote za Ankara zilizopaswa kulipwa kwa IPTL.

10. Mmiliki wa Fedha za Akaunti ya Escrow:

Mheshimiwa Spika, katika Taarifa ya Kamati ya PAC ukurasa wa 22 imeelezwa kuwa Akaunti ya Escrow ilipaswa kuwa na Shilingi bilioni 306.70 ambazo zingekuwa zimewekwa na TANESCO. Hata hivyo, katika mapendekezo ya Kamati ya PAC ukurasa wa 50, Kamati imeeleza kwamba imethibitisha bila chembe ya mashaka kwamba mchakato mzima wa kutoa fedha katika Akaunti ya Escrow umegubikwa na mchezo mchafu na kwamba Mfumo mzima wa Serikali ulipata ganzi ili kuwezesha zaidi ya Shilingi bilioni 306 kuporwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania na kutakatishwa kupitia benki mbili hapa nchini.

11. Tahadhari iliyochukuliwa na Serikali wakati wa kutoa fedha kwenye akaunti ya Escrow

Mheshimiwa Spika, kwa kuelewa kwamba kunaweza kukatokea madai kwa IPTL, na kwa kuwa Serikali ilitoa dhamana kwa TANESCO ya kununua umeme wa IPTL, Serikali ilihakikisha ina-chukua KINGA (Indemnity) kutoka IPTL katika maeneo yote muhimu. Kwa mujibu wa KINGA hiyo, kama kutajitokeza madai yo yote yale, IPTL yenyewe itawajibika. Ikumbukwe kuwa kabla ya kusaini, KINGA hiyo ilipitiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuthibitisha kwamba inaki-dhi matakwa ya kulinda maslahi ya Taifa. KINGA hii ilitolewa tarehe 27 Oktoba, 2013. Inasema, nanukuu:

“IPTL do hereby agree to INDEMNIFY and keep INDEMNIFIED the Government and the Escrow Agent (jointly and severally) against all present and future claims, actions and legal proceedings that may arise in respect of and/or all losses, charges, costs, and expenses the Government and the Escrow Agent may suffer or incur consequent upon the release and payment of the funds in the Tegeta Escrow Account or part thereof to IPTL pursuant to the Agreement for Delivery of Funds”.

KatikaUkurasa wa 48 wa Taarifa ya PAC, imeelezwa kuwa Serikali haikuchukua tahadhari ya ku-tosha dhidi ya madai mengine yanayoweza kujitokeza kabla ya kutolewa kwa fedha kutoka akaunti ya Escrow.

Ufafanuzi

Mheshimiwa Spika, KINGA iliyochukuliwa inakidhi matakwa ya kisheria na imezingatia athari yo yote ambayo ingeweza kutokea baadaye kutokana na kutolewa kwa fedha katika Akaunti ya Escrow. Kwa hiyo siyo kweli kwamba Serikali haikuchukua tahadhari kama ili-vyodaiwa na PAC.

Inaendelea Uk. 4

Inatoka Uk.2

Page 4: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

12. Dhana ya Madai ya Shilingi Bilioni 321

Mheshimiwa Spika, Madai ya kwamba TANESCO inaidai IPTL Shilingi bilioni 321 msingi wake ni dhana kwamba mtaji wa IPTL ni Dola za Marekani 100, sawa na Shilingi za Tanzania 50,000/- kwa wakati huo. Dhana hii ilipuuza ukweli kwamba Dola za Marekani milion 38.16 zili-wekezwa kwenye mradi wa Tegeta. Aidha, Bodi ya TANESCO imekana kuyatambua madai hayo ya Shilingi bilioni 321. Kimsingi hata Vitabu vya Hesabu vya TANESCO ambavyo vimekuwa viki-kaguliwa na CAG, havioneshi kuwepo kwa deni hilo.

Mheshimiwa Spika, Madai ya Shilingi bilioni 321 yaliyowasilishwa kwa Mfilisi na Mwanasheria wa TANESCO (Mkono & Co. Advocates) ulihitaji kuhakikiwa kabla ya kukubaliwa na Mfilisi kama madai halali. Hata hivyo, uhakiki huo haukufanyika kwa sababu ya Hukumu ya Mahakama ya Ru-faa katika Civil Revision No. 1 ya Mwaka 2012, ambayo ilifuta maamuzi ya Mahakama Kuu ya kuiweka IPTL katika Ufilisi na kuirudisha kwenye Ufilisi wa Muda. Hivyo, madai hayo ya Shilingi bilioni 321 na kiapo chake ambacho hakitambuliwi na Bodi ya TANESCO hayakuwa tena na uhalali wo wote.

Kamati ya PAC: Katika ukurasa wa 47 Aya ya 2 Kamati imejiridhisha kuwa madai ya TANESCO ya Shilingi Billioni 321 yana uhalali japo usahihi wake utapatikana baada ya kutekelezwa kwa uamuzi wa ICSID 2 na TANESCO na IPTL kukubaliana kiwango sahihi cha Capacity Charge.

Ufafanuzi

Mheshimiwa Spika, Madai ya kwamba TANESCO inaidai IPTL Shilingi bilioni 321 msingi wake ni dhana kwamba mtaji wa IPTL ni Dola za Marekani 100, sawa na Shilingi za Tanzania 50,000/- kwa wakati huo. Dhana hii ilipuuza ukweli kwamba Dola za Marekani milion 38.16 ziliwekezwa kwenye mradi wa Tegeta. Aidha, Bodi ya TANESCO imekana kuyatambua ma-dai hayo ya Shilingi bilioni 321. Kimsingi hata Vitabu vya Hesabu vya TANESCO ambavyo vimekuwa vikikaguliwa na CAG, havioneshi kuwepo kwa deni hilo.

13. TANESCO na IPTL kufanya Reconcillation ya fedha iliyokuwa kwenye Akaunti ya Escrow

Mheshimiwa Spika, TANESCO kwa kushirikiana na IPTL ilifanya uhakiki (reconciliation) tarehe 9 Oktoba, 2013 ili kujua madai halali ya IPTL kabla ya kufanya malipo. Takwimu za Mfilisi wa Muda wa IPTL (RITA) wakati akikabidhi mali na madeni ya IPTL, ilionesha kwamba deni lote alilokuwa akidaiwa TANESCO na IPTL kama Capacity Charges ni Shilingi bilioni 370.70, sawa na Dola za Marekani milioni 224.30. Katika majadiliano kati ya TANESCO na IPTL, gharama zilizokubaliwa kama Capacity Charges zilizokuwa zinadaiwa ni Shilingi bilioni 275.20. Fedha hizi ni pungufu kwa Shilingi bilioni 95.50 ya madai ya IPTL. Hadi kufikia tarehe 25 Novemba, 2013, fedha iliyokuwa katika Akaunti ya Escrow ilikuwa jumla ya Dola za Marekani milioni 22.20, sawa na Shilingi bil-ioni 36.72 na Shilingi bilioni 161.39.

Mheshimiwa Spika, ukaguzi maalum umeonesha pia kuwa fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow wakati wa kuifunga ni Shilingi bilioni 182.77 na kuwa na upungufu wa Shilingi bilioni 123.90 wa madai ya IPTL.

14. Iwapo Serikali ilistahili kutoa fedha katika Akaunti ya Escrow wakati Shauri la ICSID, London inaendelea.

Mheshimiwa Spika, Kesi iliyopo ICSID, London ilihusu madai ya Benki ya Standard Chatered ya Hong Kong yaliyotokana na kununua deni lililotokana na uwekezaji katika Mtambo wa IPTL wa Tegeta. Katika Mkopo huo, Mkataba wa kuuziana umeme (PPA) na Mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta viliwekwa kama dhamana.

Mheshimiwa Spika, TANESCO haikuhusishwa kwenye majadiliano ya dhamana hiyo. IPTL ilishindwa kumaliza marejesho ya Mkopo huo na hivyo Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong kuanza kuidai TANESCO madeni yaliyotokana na Mkopo huo. Hata hivyo, fedha katika Akaunti ya Escrow ilitokana na Ankara za Capacity Charges zilizokuwa zikibishaniwa kati ya TANESCO na IPTL kuhusu viwango vilivyotumika kukokotoa malipo hayo na siyo mikopo ya IPTL.

Mheshimiwa Spika, Hata hivyo, Standard Chartered Bank Hong Kong siyo mhusika (not a party) katika Mkataba wa tarehe 26 Mei, 1995 wa PPA kati ya TANESCO na IPTL. Kwa mujibu wa She-ria za Tanzania, madai yo yote yaliyotokea nje ya nchi yakihusu uwekezaji ulioko nchini ni lazima yasajiliwe hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, Kwa mantiki hiyo, Shauri lililoko ICSID, London halihusiani na fedha za Akaunti ya Escrow bali mikopo ya IPTL. Hata hivyo, wadai wa IPTL waliamriwa na Mahakama Kuu ya Tanzania tarehe 5 Septemba, 2013 kuwasilisha madai yao kwa PAP. Benki ya Standard Chatered ya Hong Kong haijafanya hivyo.

15. Ulipwaji wa Madai na Madeni

Mheshimiwa Spika, Kuhusu madai na madeni dhidi ya IPTL ikiwemo VAT, Serikali na BOT zilii-taka IPTL iweke KINGA (Indemnity) ili kuihakikishia Serikali kuwa endapo kutakuwa na madai au madeni ya aina yo yote, IPTL itawajibika kuyalipa. Tarehe 27 Oktoba, 2013, IPTL ilitoa KINGA hiyo, nanukuu:

“IPTL do hereby agree to INDEMNIFY and keep INDEMNIFIED the Government and the Escrow Agent (jointly and severally) against all present and future claims, actions and legal proceedings that may arise in respect of and/or all losses, charges, costs, and expenses the Government and the Escrow Agent may suffer or incur consequent upon the release and payment of the funds in the Tegeta Escrow Account or part thereof to IPTL pursuant to the Agreement for Delivery of Funds”.

16. Gharama za Mawakili (Mkono & Co. Advocates naHunton & Williams ya Marekani) Katika Kuendesha Kesi za IPTL

Mheshimiwa Spika, Hadi Hukumu ya Mheshimiwa Jaji Utamwa inatolewa tarehe 5 Septemba mwaka 2013, TANESCO na Serikali zilikuwa zimewalipa Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) jumla ya Shilingi za Tanzania bilioni 62.90 na bado Mawakili hawa (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) wanaidai TANESCO Dola za Marekani milioni 4.50. Ka-tika ushauri wao walikuwa wamependekeza kwa Serikali wapewe kazi nyingine ya kwenda kutetea Guarantee ya Serikali pamoja na kupinga Hukumu ya tarehe 12 Februari, 2014 ili-yotolewa katika uamuzi wa ICSID-2. Ushauri wao upo katika Memorandum ya tarehe 9 Oktoba, 2013 waliyowasilisha TANESCO.

Mheshimiwa Spika, Wakati ambapo hatukujua ni kiasi gani Serikali na TANESCO ingeweza ku-pata kwa kuendelea kupinga Capacity Charges za IPTL, tunajua fika ni hasara gani tumepata kupitia malipo ya Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) yaani ya Shilingi bilioni 62.9 na bado wanadai Dola za Marekani milioni 4.5.

Mheshimiwa Spika, kumalizika kwa mgogoro huu wa IPTL si tu kwamba kumetuondoa kwe-nye hatari ya kuendelea kukamuliwa na Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) hawa bali pia katika mazungumzo yaliyofanywa kati ya TANESCO na IPTL tu-meweza kuokoa takribani Shilingi bilioni 95 katika madai ya awali ya IPTL.

17. Ushauri wa Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) wa TANESCO wa Tarehe 4 Oktoba, 2012

Mheshimiwa Spika, Mawakili wa TANESCO na Serikali yaani Kampuni za Mkono & Co Ad-vocates na Hunton & Williams waliandika ushauri wa pamoja wa tarehe 4 Oktoba, 2012 ambapo walifafanua kwa kina juu ya Shauri lililokuwa likiendelea katika Mahakama ya Kimataifa ya Usu-luhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICSID) ya London. Katika Ushauri wao walionyesha wazi kwamba TANESCO ilikuwa na nafasi finyu mno ya kushinda katika Kesi iliyokuwa ikiendelea kati ya TANESCO na SCBHK.

Mheshimiwa Spika, katika ushauri wao walieleza mambo muhimu ambayo ni vema Bunge lako Tukufu likayaelewa hasa kwa ajili ya watu wanaodhani kwamba ilikuwa ni makosa kwa TANESCO kukaa na IPTL baada ya Hukumu ya Mahakama Kuu ya tarehe 5 Septemba, 2013. Baadhi ya mae-neo walioshauri TANESCO ikae na IPTL kujadiliana kwa kile kilichoelezwa na Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) kuwa uwezekano wa kushinda kesi ni mdogo ni pamoja na:-

18. Ushauri wa Mawakili unaokinzana

Mheshimiwa Spika, tarehe 4 Oktoba, 2012, Mawakili wetu (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) walitoa ushauri kwamba, kwa kuzingatia utetezi walioutoa kwa TANESCO kwenye kesi hii kule ICSID, London kiasi cha chini kabisa kinachoweza kuidhinishwa na Mahakama ya ICSID, London kama malipo ya Capacity Charges kwa IPTL ni kati ya Dola za Marekani milioni 85 hadi 90 na Mawakili wetu (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) wakasema, nanukuu, “This could be considered TANESCO’s Best Case Scenario”. Hata hivyo waliendelea kusema “This best Case Scenario is overly optimistic”

Mheshimiwa Spika, katika maelezo yao mengine ya tarehe 4 Oktoba, 2012, Mawakili hawa (Mko-no & Co. Advocates na Hunton & Williams) wanasema, “In these circumstances, SCBHK may recover 100% of its claimed damages of USD 130 milion even if substantially TANESCO prevails on a portion of its equity defense”.

Kwa lugha nyingine Mheshimiwa Spika Mawakili hawa (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) wanasema kiasi cha chini kabisa ambacho TANESCO ingedaiwa na SCBHK kingekuwa Dola za Marekani milioni 130 bila kujumuisha gharama nyingine za moja kwa moja kwa IPTL.

Mheshimiwa Spika, Katika majumuisho yao ya tarehe 4 Oktoba, 2012, Mawakili (Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams) waliishauri TANESCO ikae na SCBHK na kukubaliana nje ya Mahakama na kumlipa Dola za Marekani kati ya milioni 75 na milioni 90 na kiasi kitakachobaki kikidaiwa kilipwe kwa wadai wengine, wakiwemo IPTL, Law Associates na Kampuni ya Mafuta ya TOTAL.

Mheshimiwa Spika, Kufikia tarehe 5 Septemba, 2013 kwa mujibu wa Taarifa ya Mfilisi (RITA), ilionesha kuwa Kampuni ya IPTL ilikuwa ikiidai TANESCO zaidi ya Dola za Marekani milioni 224.30, sawa na Shilingi bilioni 370.70. Majadiliano yaliyofanyika kati ya TANESCO na IPTL tarehe 9 Oktoba, 2013 yaliwezesha kukubaliana kuwa malipo stahiki kwa IPTL ni jumla ya Dola za Marekani milioni 166, sawa na Shilingi bilioni 274.56. Kati ya hizo, Dola za Marekani milioni 121, sawa na Shilingi bilioni 220.13 zilikuwa kwenye Akaunti ya ESCROW na Dola za Marekani milioni 45, sawa na Shilingi bilioni 74.43 zitalipwa kwa kipindi cha muda mrefu usiozidi miaka mitano.

19. Kama fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ni za Umma Katika ukurasa wa 58 wa Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa fedha zilizokuwa katika Akaunti ya Escrow zilikuwa za Serikali.

Ufafanuzi:

Mheshimiwa Spika, Huu si ukweli zipo sababu kuu zinazothibitisha kuwa fedha hizo hazikuwa za Serikali.

1. TANESCO ilikuwa inapata huduma ya umeme bila kulipa moja kwa moja IPTL, lakini ikawa inapeleka fedha hizo katika Akaunti ya Escrow.

Inaendelea Uk. 5

Inatoka Uk.3

Page 5: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

2. TANESCO ilisimamisha kupeleka malipo kwenye Akaunti ya Escrow na wala kulipa IPTL kuan-zia tarehe 30 Oktoba, 2010.

Pamoja na kutokulipa, TANESCO iliendelea kupata huduma ya umeme kwa kadri ilivyohitaji kutoka IPTL.

Mheshimiwa Spika, katika Ukurasa wa 36 hadi 42 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambayo tumekabidhiwa inaonesha kiasi ambacho TANESCO inadaiwa na IPTL.

Mheshimiwa Spika, Kulingana na Taarifa hiyo ukurasa wa 36 hadi 42 imeonesha kuwa kiasi ambacho kilipaswa kuwekwa kwenye Escrow Account kwa mujibu wa Ankara za IPTL ni Shilingi bilioni 306.68. hata hivyo, kwa mujibu wa Ukaguzi huo fedha zilizokuwa kwenye Akaunti wakati wa kuifunga ni Shilingi bilioni 182.77 na kuwa na upungufu wa Shilingi bilioni 123.90 ikiwa ni deni ambalo TANESCO bado wanadaiwa na IPTL.

Mheshimiwa Spika, Kwa msingi huo fedha zote zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ni mali ya IPTL na IPTL kama Wakala wa Kodi anastahili kudaiwa na mwisho kulipa kodi yo yote ambayo hajalipa.

Kwa msingi huo, Taarifa ya PAC haisemi ukweli kuhusu fedha zilizowekwa katika Akaunti ya Escrow kuwa ni fedha za umma.

Mheshimiwa spika, ili kuthibitisha kwamba fedha hizi siyo za Umma, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ukaguzi wake wa Hesabu za TANESCO wa tarehe 31 Desem-ba, 2012 alielekeza kutoa fedha za Escrow kwenye Vitabu vya Hesabu vya TANESCO na kupunguza deni kwa kiasi hicho hicho kwa maelezo yafuatayo:

“As a result, the deposit balance in Escrow account does not meets the definition of an asset of the Company and therefore an adjustment has been made to de-recognize the asset and related liability to the tune of the amounts available in the Escrow account”.

20. Iwapo kwa mujibu wa Mkataba wa PPA TANESCO na IPTL walilazimika kutumia Mta-alamu wa Upatanishi (Mediation Expert) katika utatuzi wa mgogoro kabla ya kutolewa fedha zilizopo kwenye Akaunti ya Escrow.

Mheshimiwa Spika, Taarifa ya Kamati ya PAC ukurasa wa 9, imeeleza kuwa kwa mujibu wa Mka-taba wa PPA, TANESCO na IPTL walipaswa kutumia Mtaalam wa Upatanishi katika mgogoro wa Capacity Charge.

Mheshimiwa Spika, tunapenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 18.1 ya Mkataba wa PPA, wahusika wa Mkataba huo ambao ni TANESCO na IPTL wanatakiwa kwanza kumaliza mgogoro baina yao kwa njia ya upatanishi (amicable settlement). Iwapo watashindwa kufikia makubaliano ndipo watalazimika kutumia Mtaalam wa Upatanishi kutatua mgogoro huo. TANESCO na IPTL walimaliza mgogoro baina yao kwa njia upatanishi kwa kufanya uhakiki wa kiasi ambacho kila upande ulikuwa unastahili kulipwa katika Akaunti ya ESCROW kabla ya akaunti hiyo kufungwa. Kwa msingi huo, hapakuwa na sababu ya kutumia Mtaalam wa Usuluhishi kama ilivyoelezwa katika Taarifa ya PAC.

21. Kama muda wote wa Mkataba wa TANESCO na IPTL hapakuwahi kuwa na Kamati ya Uendeshaji

Mheshimiwa Spika, taarifa ya PAC inaeleza kuwa hapakuwahi kuwa na Kamati ya Uendeshaji kwa kipindi chote cha Mkataba wa PPA. Ukweli ni kwamba, Kamati ya Uendeshaji iliundwa kabla ya kuanza uzalishaji wa Mtambo hapo 2002 na imeendelea kuwepo hadi leo. Kamati hiyo ina wajumbe sita. Wajumbe watatu kati ya hao wanatoka TANESCO. Wajumbe watatu waliobakia wanatoka IPTL. Wajumbe wa TANESCO walikuwa ni kama ifuatavyo:

1. Mhandisi Masanyiwa Malale;2. Mhandisi Christian Msyani; na3. Mhandisi James Mtei.

Mheshimiwa Spika, kwa msingi huo si kweli kwamba Kamati ya Uendeshaji haikuundwa kama ilivyoelezwa na Kamati ya PAC katika ukurasa wa 10.

22. Wizara kutambua Hati za Hisa za Makampuni

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 27 wa Taarifa ya Kamati ya PAC, Kamati hiyo imeitaka Wizara ya Nishati na Madini kutambua usajili wa Hati za Hisa za Makampuni. Tunaomba ieleweke kuwa siyo majukumu ya Wizara kutambua na wala kujishughulisha na Hati za Hisa za Makampuni Binafsi. Aidha, katika ukurasa wa 45, imeelezwa kwamba “Waziri wa Nishati na Madini ndiyo Mamlaka ya kuthibitisha uhamishaji wa umiliki wa Kampuni katika sekta yake”. Ningependa kulijulisha Bunge lako Tukufu kwamba jukumu hilo pia siyo la Wizara ya Nishati na Madini ni vizuri majukumu ya Wizara yakaangaliwa vizuri na kutoleta mkanganyiko na kuwadanganya wananchi wetu. Hii inaonesha kuwa kamati haikupitia vizuri majukumu ya Wizara.

Mheshimiwa Spika, katika Taarifa ya PAC, ukurasa wa 30 Aya ya 2, imeelezwa nanukuu “nili-shuhudia nyaraka kwamba Piper Link ilinunua Hisa za MECHMAR na katika mauziano hayo Kam-puni hiyo iliwakilishwa na Bw. Harbinder Singh Sethi hivyo huyu bwana ndiye Piper Link na ndiye PAP”. Kwa maneno haya ya Kamati ya PAC, aliyekuwa na hati za Piper Link ni Bw. Sethi na aliy-

enunua Piper Link ni Bw. Sethi anayemiliki PAP. Kwa kuzingatia maelezo haya ya kamati ya PAC, inaonesha kwamba hakuna tatizo la uhamishaji wa Hisa Asilimia 70 kwenda kwa PAP.

Mheshimiwa Spika, pamoja na maelezo ya Aya iliyotangulia, bado Kamati ya PAC ukurasa 44 wa taarifa yake, inaonesha kuwa Hisa hizo zinashikiwa na Martha Renju huko BVI lakini Martha Renju amefungua kesi mara mbili Mahakama Kuu ya Tanzania kwa kutumiwa na SCBHK akiwa na lengo la kutaka kujipatia fedha za Escrow bila uhalali. Hata hivyo, amekuwa akiziondoa kesi hizo mahakamani.

23. Mikutano ya Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 29 wa Taarifa ya PAC, inasema kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO ilifanya mikutano miwili mfulilizo kati ya tarehe 16 na tarehe 19 Septemba, 2013 na kwamba uharaka huo unatia mashaka kwamba kulikuwa na njama.

Mheshimiwa Spika, muda wa siku 3 kwa Bodi kukutana si jambo la kutiliwa mashaka kwani Bodi haikutani kwa ajenda moja tu. Napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa tarehe 16 Septemba, 2013 hapakuwa na kikao cha Bodi isipokuwa kikao cha Bodi kilifanyika tarehe 19 Septemba, 2013. Hivyo si sahihi kusema kuwa Bodi ya TANESCO ilikuwa ina njama katika kushughulikia na kuli-tolea maamuzi suala la Akaunti ya Escrow na kwamba ilikutana ndani ya siku tatu.

24. Hoja ya Mwanasheria wa TANESCO Kufukuzwa Kazi

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 30 wa Taarifa ya PAC kuna hoja kuwa Mwanasheria wa TANESCO kwa wakati huo Bw. Godwin Ngwilimi aliagizwa na TANESCO kwenda Malaysia ku-fanya Due Diligence ya Kampuni ya MECHMAR Corporation na kwamba taarifa hiyo ya Due Dili-gence ilifikishwa katika Bodi na Bodi iliipuuza na kinyume chake Mwanasheria huyo aliachishwa kazi.

Mheshimiwa Spika, Taarifa hizi si za kweli na ni uongo uliokithiri kwa aliyekuwa Mtumishi wa Umma kuudanganya umma wa Watanzania kwa kiasi cha kutisha na Kamati inatoa taarifa ya uongo ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Spika, ukweli wa jambo hili ni kama ifuatavyo:

1. Mwanasheria huyo Bw. Ngwilimi alileta ombi la kusafiri kwenda Malaysia kwa kumdanganya Mwajiri wake kwa kudai kuwa alipewa ushauri wa kwenda Malaysia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Katika barua ya kuomba ruhusa alisema kuwa alikuwa aende na Mwanasheria Mwandamizi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliruhusiwa. Hata hivyo, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali haikutoa Ofisa huyo na hivyo kuamua kwenda peke yake.

2. Bw. Ngwilimi hakufukuzwa kazi na Bodi kama ilivyodaiwa katika Taarifa ya kamati ya PAC katika ukurasa wa 30, bali aliomba kuacha kazi mwenyewe kwa kutoa taarifa kwa Mkurugenzi Mtendaji kwa barua ya yenye Kumb na. SEC.215/Conf/2/2014 ya tarehe 27 Februari, 2014 iliyoku-wa inasomeka “Notice to Terminate my Service with TANESCO” akitoa notisi ya siku 90 kwa mu-jibu wa Mkataba wake wa kazi.

3. Katika ombi lake alidai kuwa anaacha kazi kwa hiari yake mwenyewe kwa kuwa anahitaji kufanya shughuli nyingine na akaushukuru uongozi wa TANESCO kwa ushirikiano kwa kipindi chote ali-chofanyakazi. Machi 10, 2014 Shirika lilimjibu Bw. Ngwilimi kwa barua yenye Kumb. Na. N.837 kuwa Uongozi na Bodi ya TANESCO wamekubali ombi lake la kuacha kazi.

Mheshimiwa Spika, kwa maelezo hayo ni wazi kuwa Bodi haikuwahi kumfukuza na Bodi haiku-kataa utoaji wa fedha za IPTL katika Akaunti ya Escrow. Badala yake Bodi ilielekeza IPTL ipewe fedha zilizopo kwenye Akaunti ya Escrow tu na kwamba usuluhisho uliyofanyika unakubalika. Aidha, Bwana Ngwilimi aliamua kuacha kazi mwenyewe na kukimbia baada ya kuelewa kuwa angechukuliwa hatua kutokana kumsingizia Mtumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa walitumwa wote na kusafiri wote kwenda kufanya kile alichodai due diligence.

Page 6: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wenzake.

Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Arusha siku ya mahafali ya kuhitimu Shahada ya uzamili (Masters) ya Business Adminstration katika Viwanja vya ESAMI.

Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud (Watatu kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (wa pili kushoto) pamoja na wahitimu wengine wakati wa mahafali ya kuhitimu Shahada ya Uzamili ya Business Adminstration katika Chuo Kikuu cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) kilichopo Mkoani Arusha.

Graduation

u

uMsemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud, (wa pili kulia) akielekea katika viwanja vya ESAMI kwa ajili ya mahafali ya Chuo ambapo alipokea shahada ya uzamili.

Page 7: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

FIVE PILLARS OF

KWA HABARI PIGA SIMU KITENGO CHA MAWASILIANO

INCREASE EFFICIENCYQUALITY DELIVERY

OF GOODS/SERVICE

SATISFACTION OF THE CLIENT

SATISFACTION OF BUSINESS PARTNERS

SATISFACTION OF SHAREHOLDERS

TEL-2110490FAX-2110389

MOB-0732999263

TEL-2110490FAX-2110389

MOB-0732999263

Ruzuku kwa wachimbaji wadogo Na Asteria Muho-

zya, Dar es Salaam

Awamu ya pili ya utoaji ruzuku kwa wachimbaji wadogo wa ma-dini nchini kwa

mwaka 2014/15 imepanda kutoka kiasi cha dola za Ki-marekani 50,000 hadi dola 100,000 kikiwa ni kiwango cha juu cha ruzuku, jambo ambalo linalenga kuongeza kiwango cha uzalishaji wa madini mbalimbali yanayo-patikana nchini ikiwemo ku-waendeleza wachimbaji hao.

Hayo yaliaelezwa na Kam-ishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia wachimbaji wadogo Julius Sarota wakati akitoa mada kuhusu Ruzuku na mikopo kwa maendeleo ya wchimbaji madini katika mkutano wa wadau wa ma-dini ya Shaba uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25- 26 Novemba, 2014.

Sarota aliongeza kuwa, ruzuku hiyo imejaribu kuan-galia masuala mbalimbali ambayo Serikali imedhamiria kuwawezesha wachimbaji wa-dogo nchini kunufaika kupitia tasnia hiyo, ikiwemo kuwa-saidia wachimbaji wadogo kuongeza uwezo wa uzalishaji wa madini, kuongeza thamani ya madini hayo jambo ambalo litawawezesha wachimbaji na Serikali kunufaika zaidi kuto-kana na rasilimali hiyo.

Vilevile, alieleza kuwa, awamu ya pili ya utoaji ru-zuku inalenga kuwahamasi-sha akina mama wanaofanya shughuli za uchimbaji madini lakini wanataka kuongeza kipato kwa kujihusisha na shughuli nyingine za kiu-chumi, hususan kilimo au biashara nyingine. Kiwango cha juu cha ruzuku hii ni dola za Marekani 30,000. “Kina mama angalieni fursa hii na itumieni vizuri pindi matan-gazo rasmi ya utoaji ruzuku hizi yatakapotolewa,” alisisiti-za Sarota.

Akizungumzia mchakato wa kuwapata washindi, Sa-rota alieleza kuwa, mchakato mzima utahusisha taasisi kadhaa za Serikali. Kutaku-wa na Kamati ya Utendaji itakayokuwa chini ya Ue-nyekiti wa Kamishna wa Ma-dini. Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) watafanyakazi

ya kutoa ushauri wa kitalaam katika utoaji ruzuku hiyo na Benki ya Maendeleo ya TIB watahusika na utoaji wa fedha ya ruzuku baada ya washindi kupatikana.

“Serikali inawajali wachimbaji ndio maana tunaweka mazingira rafiki katika zoezi zima, taratibu za ruzuku zimewekwa kwa urahisi. Lakini mzingatie, tut-aingia mkataba na ninyi pindi mtakapopata fedha hizi tuna-taka kujua namna mtakavyoz-itumia fedha hizi”, alisisitiza Sarota.

Aliongeza kuwa, kuongezeka kwa taasisi zi-takazo ratibu zoezi zima la utoaji ruzuku kunatarajiwa kuwa na mafanikio mazuri na hivyo kuwataka wadau katika sekta ya madini, kuunga mko-no juhudi za Wizara katika kuwawezesha wachimbaji wa-dogo nchini.

Akizungumzia historia ya namna juhudi mbalimbali zi-lizofanywa na serikali katika kuwezesha wachimbaji wa-dogo nchini, Sarota alieleza kuwa, juhudi hizo zilianza tangu miaka ya 1960 kuto-kana na changamoto kadhaa katika sekta hiyo na kuyataja baadhi kuwa ni pamoja na wachimbaji kufanya shughuli zao katika mfumo usio rasmi, matatizo ya masoko, miun-dombinu duni katika maeneo ya machimbo na wachimbaji kufanya shughuli hizo bila kuyafanyia utafiti maeneo yao.

Wakati huo huo, ak-ichangia katika mada hiyo, Kamishna Msaidizi wa Madi-ni anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje, aliwataka wachimbaji watakaopata ruzuku hizo wa-zitumie vizuri kama yalivyo malengo ya Serikali katika ku-wapatia ruzuku hizo.

Akizungumzia taratibu za utoaji fomu mara baada taarifa ya utoaji rasmi wa ru-zuku alieleza kuwa, “fomu zitaletwa karibu na ninyi kwa kupitia ofisi zetu za ma-dini, watawasaidia namna ya kuzijaza,kwasababu dhami-ra yetu ni kuwawezesha ninyi,”aliongeza Mhandisi Samaje.

“Msituangushe, tunataka kuona matokeo bora yatakay-otokana na ruzuku hizo”, ali-malizia Samaje.

BODI YA UHARIRI MHARIRI MKUU: Badra Masoud

MHARIRI : Leonard Mwakalebela MSANIFU: Essy Ogunde

WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson MwaseTeresia Mhagama, Mohamed Saif na Nuru Mwasampeta

nSasa ni USD 100,000

Page 8: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

Tanzania kushirikisha Interpol udhibiti magendo ya vito Na Teresia Mhagama

Serikali imeeleza kuwa iko kwenye mpango wa kuanza kushirikiana na Polisi wa Ki-mataifa (Interpol) ili kuimarisha mtandao wa kutokomeza biashara ya magendo ya madini ya vito hasa Tanzanite.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini nchini, Richard Kasesera wakati akifunga rasmi Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yaliyofanyika jijini humo kuanzia tarehe 18 hadi 20 Novemba 2014.

Kasesera alieleza kuwa serikali imeona umuhimu wa kushirikiana na Polisi hao wa Kimataifa hasa ka-tika udhibiti wa madini ya Tanzanite ili kuweza ku-wakamata wafanyabiashara wanaosafirisha madini hayo nje ya nchi bila kuwa na cheti cha uhalisia (cer-tificate of origin) kinachoonesha kuwa Madini husika yametoka Tanzania.

“Tutazungumza na Interpol sio tu katika kukama-ta wafanyabiashara wasiokuwa na cheti cha uhalisia kinachoonesha kuwa madini ya Tanzanite yanatoka nchini, bali pia ukisafirisha madini ghafi zaidi ya ki-wango ulichoruhusiwa. Yeyote atakayebainika ita-bidi arudishwe nchini ili taratibu za kisheria zichukue

mkondo wake, hivyo tukiwa na mkataba wa kubadil-ishana watuhumiwa na nchi uliyokamatiwa, wataku-rudisha hapa hapa nchini”, alisisitiza Kasesera.

Kasesera alieleza kuwa, serikali haifanyi utani ka-tika suala la kuwakamata wale watakaotorosha madi-ni ya Tanzanite na madini mengine ya thamani nje ya nchi hasa kuelekea katika nchi zinazoingiza madini hayo kwa wingi kama Kenya na India.

“Pia Afrika Mashariki na Afrika yote kwa ujumla tunajua kuwa Zambia inakuwa maarufu kwa madini ya Tanzanite, kama ilivyo kwa Kenya na Uganda. Tutazungumza na Mamlaka za nchi hizo ili kutaifi-sha madini yote ya vito yasiyo na vibali yanayoingia katika nchi hizo”, alieleza Kasesera.

Aidha alieleza kuwa, kwa vile Tanzanite inapati-kana Tanzania pekee, hivi sasa Serikali na wadau wa madini nchini wanahamasisha Maonesho mbalim-bali ya madini ya Vito duniani kuhakikisha kwamba hawapokei madini ya Tanzanite yasiyokuwa na cheti cha uhalisia (certificate of origin) au Tanzanite ghafi katika maonesho hayo.

Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito yaliyo-fanyika katika hoteli ya Mount Meru jiijini Arusha yalishirikisha waoneshaji (exhibitors) kutoka nchi za Afrika Mashariki, kati na Kusini ambapo makampu-ni 69 na washiriki zaidi ya 500 walihudhuria.

Wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini nchini, Richard Kasesera wakati akifunga rasmi Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha kwa mwaka 2014. Maonesho hayo yalifanyika tarehe 18 hadi 20 Novemba.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini nchini, Richard Kasesera akifunga rasmi Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha kwa mwaka 2014.Maonesho hayo yalifanyika tarehe 18 hadi 20 Novemba, 2014.

Uongezaji Thamani madini kuimarisha pato la Taifa-Masanja

Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam

Kamishna wa Madini Tanza-nia, Mhandisi Paul Masan-ja amesisitiza umuhimu wa wachimbaji na wadau wa sekta ya madini ya

shaba nchini kuhakikisha wanaongeza thamani ya madini kupitia viwanda vya uchenjuaji vya ndani kwa kuwa, uongezaji huo una mchango kiuchumi, katika kuongeza pato la Taifa mtu mmo-ja mmoja na katika kukuza soko la ajira.

Kamishna Masanja aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wa madini ya Shaba uliofanyika tarehe 25-26 Novemba, 2014 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyabiashara wa

madini hayo, wachimbaji wadogo, vi-wanda vya kuyeyusha madini ya Shaba, Makamishana Wasaidizi wa Madini ku-toka Kanda mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya Maafisa Madini Wakaazi.

Aliongeza kuwa, uwezo wa vi-wanda kuzalisha shaba nchini bado ni mdogo hivyo kuwataka washiriki hao kutoa mapendekezo yatakayosaidia kui-marisha na kuchochea ukuaji wa viwan-da vya uchenjuaji na uyeyushaji madini hayo badala ya kusafirisha madini ghafi ya Shaba nje ya nchi kwa kuwa, madini hayo yanakuwa na mchanganyiko wa madini mengine zaidi ya Shaba .

Vilevile, Kamishna Masanja alieleza kuwa, Serikali itaendelea kuzuia usa-firishaji madini ghafi ya Shaba na kue-leza kuwa, “Haturuhusu madini ghafi ya shaba kutoka nje, tunataka yatoke yaki-

wa tayari ni madini, kwasababu kuna zaidi ya shaba hivyo tunapoteza, tuna-taka kuyaongeza thamani madini yetu hapa hapa nchini. Lazima tulisimamie hili,” alisisitiza Masanja.

Kutokana na kupoteza kiasi kikub-wa cha madini yanayokuwa pamoja na madini ghafi hayo, Kamishna Masanja alitumia fursa hiyo, kuwataka wachim-baji na wafanyabiashara wa madini ya Shaba kuacha kufanya biashara kiny-ume na sheria na taratibu kwa kuwa jambo hilo linaikosesha Serikali mapato ikiwemo kuchangia madini hayo ku-tokupata thamani halisi.

Aliongeza kuwa, dhamira ya Seri-kali kupiga marufuku usafirishaji wa ma-dini ghafi ya Shaba unalenga kuhama-sisha ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani madini hayo nchini, hivyo ku-

wataka wadau wa tasnia hiyo kujipanga kufanikisha jambo hilo.

“Tunachotaka ni Serikali na wadau kunufaika na rasilimali zetu, tukilisima-mia vizuri jambo hili tutanufaika sana. Zuio la mwaka 2010-211 kusafirisha madini ghafi nje ilikuwa kuhamasisha ujenzi wa viwanda,” aliongeza masanja.

Akizungumzia suala la ruzuku kwa wachimbaji alieleza kuwa, serikali itatoa ruzuku badala ya mikopo kwa wachim-baji wadogo lengo likiwa kuongeza tija na mafanikio.

Kamishna Masanja alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wachimbaji wado-go kutumia fursa zinazotolewa na Wiz-ara kupitia ruzuku katika kuendeleza shughuli zao za uchimbaji.

“Kwa namna tulivyojipanga, na kufuatia juhudi zinazofanywa na Wa-ziri wa Nishati na Madini, Profesa

Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu Eliakim Maswi, mchimbaji kupata ru-zuku haitazidi kipindi cha miezi mitatu. Naamini kufikia mwezi Mei, 2015 wengi watakuwa wamenufaika,” alisisitiza Masanja.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Ma-dini Tanzania, uchimbaji wa madini ya Shaba nchini ulianza mwaka 2006 ambapo kiasi cha takribani tani 3000 za Shaba kilizalishwa. Aidha, alieleza kuwa kipindi cha mwaka 2009 hadi 2013 lakiri (pound) 52,453,886 za Shaba za Dola za marekani 178,347,072 zilizalishwa na migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi.

Vilevile Kamishna Masanja al-iongeza kuwa, katika kipindi cha kuan-zia mwaka 2009 hadi 2013 jumla ya tani 1,147,882 za Shaba ghafi zenye thamani ya Dola za Marekani 5,594,810 zilizal-ishwa na wachimbaji wadogo.

n Asema kupata ruzuku haitazidi miezi mitatu

Page 9: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz TANGAZO

Mtendaji TMAA ahimiza ujenzi viwanda uchenjuaji Shaba

Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam

Mtendaji Mkuu wa Waka-la wa Ukaguzi wa Ma-dini Tanzania (TMAA), Mhandisi Dominick Rwekaza, ameeleza

kuwa, usafirishaji shaba ghafi nje ya nchi unapoteza madini mengi na kuwataka wachimbaji wadogo na wafanyabiashara kuhakikisha wanajenga viwanda vya ndani vya kuyeyusha madini hayo ili kuyaongezea thamani.

Mhandisi Rwekaza aliyasema hayo wakati akifunga mkutano wa siku mbili wa wadau wa madini ya Shaba uliofanyi-ka tarehe 25-26 Novemba, 2014 ulilenga kujadili masuala mbalimbali kuhusu sek-ta ndogo ya madini ya shaba pamoja na uongezaji thamani madini hayo.

Aliongeza kuwa, mkutano huo ulien-ga kuboresha sekta ya madini hususani kuongeza thamani madini ya shaba na kuongeza kuwa, kutokana na umuhimu wa sekta ya madini katika ukuaji uchu-mi, wadau hao wanalo jukumu katika

kuchangia uongezaji thamani madini husika kutokana na kwamba, jambo hilo linawezekana kufanyika nchini kupitia viwanda vya ndani.

“Uwezo wa kuongeza thamani ma-dini haya upo. Jukumu letu ni kuhakiki-sha tunakuwa na viwanda vya ndani kwa kiasi kikubwa, jambo hili linawezekana, serikali tutatimiza majukumu yetu ku-hakikisha tunaweka mazingira bora ya kuendeleza sekta hii kwa maendeleo ya Taifa, na ninyi mnalo jukumu la ku-hakikisha tunakuwa na viwanda hivi”, alisisitiza Rwekaza.

Vilevile, Rwekaza aliongeza kuwa, maazimizo yaliyotolewa katika mku-tano huo kwa kushirikiana pamoja yanaweza kuchangia kuboresha sekta hiyo ikiwemo kuliwezesha Shirika la Madini la taifa (STAMICO) liwezeshwe kujenga kiwanda cha kuchenjua madini ya shaba chenye uwezo wa kuchen-jua madini mengine kwa kushirikiana na sekta binafsi (PPP) na kuwataka wadau wote katika tasnia hiyo kutimiza wajibu wao kikamilifu. Vilevile,mkutano huo uliazimia kuwa, usafirishaji mbale ghafi nje ya nchi usiruhusiwe baada ya tarehe

31 Disemba, 2014.Aidha, aliwataka wadau hao ku-

tumia ofisi za madini za Kanda na ofisi

za Maafisa Madini Wakaazi kupata taarifa mbalimbali kuhusu sekta hiyo ikiwemo kupata ushauri wa kitaalamu.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi Dominick Rwekaza, akiongea jambo wakati akifunga mkutano wa wadau wa madini ya Shaba. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje, na kulia ni Kaimu Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Uongezaji Thamani Madini, Latifa Mtoro

Ngonyani ang’aka Mirerani

Na: Issa Mtuwa – Aliyekuwa Mirerani

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STA-MICO) Mhandisi Edwin Ngonyani amefanya zi-

ara ya kushtukiza katika mgodi wa TanzaniteOne ulioko Mirerani wilay-ani Simanjiro na kufanya vikao vitatu mfululizo kwa nyakati tofauti kwa lengo la kuona ufanisi wa utendaji kazi mgodini hapo.

Mhandisi Ngonyani alitembelea mgodini hapo na kuitisha kikao cha kwanza na menejimenti ya mgodi huo iliyohusisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzan-

iteOne, Meneja wa Ulinzi, Meneja Uhusiano wa Jamii, Meneja wa Fedha na wawakilishi watatu kutoka STA-MICO mgodini hapo. Kikao kingine kilimkutanisha na Idara ya Jiolojia ikiongozwa na Mjiolojia Mkuu Bw. Amosi Chakupewa na pia alikutana na Idara ya Rasilimali watu ikiongo-zwa na Meneja Jonson Mwani.

Katika vikao hivyo, Mhandisi Ngonyani alilenga katika kufahamu

hali ya uzalishaji wa Tanzanite, hali ya ulinzi na usalama, uvamizi wa maeneo ya uchimbaji, na mahusiano kazini la-kini kubwa akisisitiza kuwa kinachohi-tajika ni kuongezeka kwa uzalishaji wa Tanzanite hivyo kuchangia katika ukuaji wa sekta ya madini.

Aidha, aliomba kupatiwa taar-ifa ya mapato na matumizi ili kuona mwenendo mzima wa uendeshaji wa mgodi. Mhandisi Ngonyani alisema kuwa Watanzania na Serikali ha-watamwelewa endapo Tanzanite hai-tozalishwa ya kutosha katika kipindi hiki ambacho Serikali kupitia STA-MICO imeingia ubia wa kugawana hisa asilimia 50 kwa 50 na Kampuni ya TanzaniteOne.

“Sitokubali kabisa, tena naomba mnielewe, asiyeweza si vibaya aka-omba kuondoka, pamoja na yote nili-yoyasema ninachotaka hapa ni taarifa za uzalishaji wa Tanzanite, umizeni vichwa vyenu na kuona ni kwa nam-na gani hili litafanikiwa na si vingi-nevyo, hiyo ndiyo rai yangu kwenu”, alisema Mhandisi Ngonyani

’’Ninyi ni wataalamu tunaowat-egemea katika Idara ya Jiolojia hivyo ninategemea muwaelekeze watu taarifa za kijiolojia kwani wachim-baji wanategemea taarifa zenu katika uchimbaji madini”, alisisitiza Mhandi-

si NgonyaniAkiongea na Meneja rasilimali

watu Mhandisi Ngonyani alisisitiza suala la kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za kazi na mahusiano kazini, na kwamba kitu pekee ni kutenda haki kwa wafanyakazi na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa kusikiliza majungu.

Aidha, aliwataka kuchukua hatua za kinidhamu kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria na kuongeza kuwa njia hiyo itasaidia kuepusha hasara pindi watumishi wanaporudishwa ka-zini kwa amri ya mahakama.

Naye Mjiolijia Mkuu, Amosi Chakupewa akiongea katika kikao hicho alimhakikishia Kaimu Mku-rugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi Ngonyani kuwa watafikia malengo waliyojiwekea katika ku-hakikisha Tanzanite inanchangia katika ukuaji wa sekta ya madini na kuongeza kuwa taarifa za kijiolojia za mwaka 2011 ambazo bado zinatumi-wa na mgodi zinaonesha kuwa mgodi bado una uhai wa kuchimbwa Tan-zanite kwa kipindi cha miaka thelathi-ni (30) ijayo hivyo, kinachohitajika ni kujipanga na kuweka mikakati na ku-dhibiti uvamizi na uchimbaji haramu.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi Edwin Ngonyani katikati akiwa kwenye kikao na viongozi wa Kampuni ya TanzaniteOne na wafanyakazi wa STAMICO walioko mgodini hapo wakijadili masuala mbalimbali yanayohusu uzalishaji wa Tanzanite, utawala, ulinzi, uwajibikaji na haki za watumishi.

n Lengo ni kuongeza thamani

n Asema hatoeleweka na hatokubali ikiwa Tanzanite haitazalishwa

Page 10: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

Na LEONARD MWAKALEBELA, Norway

Viongozi wa dini nchini wameishauri serikali kuziongezea nguvu za kisheria mamlaka za udhibiti nchini ili ku-

dhibiti kampuni hewa, kuongeza makusanyo ya mapato na ku-punguza rushwa, ubabaishaji na udanganyifu.

Viongozi hao wametoa ushau-ri huo nchini Norway wakati wakichangia mada zilizokuwa zikitolewa kwa nyakati tofauti na watendaji wa Taasisi za Nor-way akiwemo Meneja Miradi wa Kurugenzi ya Mafuta ya Nor-way (NPD) Bw. Gunnar Soiland, Mshauri Mwandamizi wa Mam-laka ya Usalama wa Petroli (PSA)

Bw. Paul Bang na Mkurugenzi wa Kazi Maalum wa Wizara ya Nishati na Petroli(MPE) Bw. Helge Westborg, wakati viongozi hao wa dini na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini walipotembelea Taasisi hizo.

Watoa mada hao, walionye-sha jinsi taasisi zao zinavyodhibiti sekta hiyo kuanzia utoaji leseni, utendaji wa kampuni husika baada ya kupata leseni, ulipaji kodi, gharama za uendeshaji za kampuni husika na mwingilio wa wanasiasa.

Kwa mujibu wao,kampuni haipewi leseni kabla ya kuchun-guzwa na jopo la wataaalam na leseni itakayopewa inakuwa na masharti ambayo ndio mkataba wenyewe kati ya serikali na kam-puni hiyo.

Hivyo serikali ndio inay-otengeneza mkataba( leseni) na

kampuni husika lazima ifuate masharti ya leseni hiyo (mkataba) au isichukue leseni hiyo.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dk. Stephen Munga aliishauri serikali kudhibiti utoaji leseni na kuachana na mfumo wa mika-taba ambao unalitia hasara Taifa.

Dk Munga aliongeza kuwa ni muhimu kukawa na uchunguzi wa kina kwa kampuni zinazoom-ba leseni ili kudhibiti kampuni za kitapeli, hewa na ambazo hazina uwezo kabisa.

Kwa upande wake, Mkuru-genzi wa Utawala wa Jumuiya ya Kikristo (CCT) Bw. John Mapesa alisema kuwa kamwe Tanzania haitanufaika na mafuta na gesi endapo haitatengeneza mfumo madhubuti wa udhibiti kama ili-vyo kwa nchi ya Norway.

“Hili eneo (udhibiti) ni lazima tufanye kama Norway maana wanadhibiti sana ulipaji wa kodi wa kampuni hizi halafu wa-nafuatilia kwa kina gharama za uwekezaji na uendeshaji wa kampuni hizi ili kudhibiti udanganyifu na hivyo kuongeza mapato”, al-iongeza Mapesa.

Ustaadhi Lolila na Mhasibu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato (SDA), Kanda ya Kaskazini, Mchungaji Dickson Matiko wal-izipongeza taasisi hizo za Norway kwa ku-wadhibiti wanasiasa kutoingilia kazi zao au kuingiza siasa kwenye sekta ndogo ya mafuta na gesi.

Viongozi hao wa dini wapo mjini Sta-vanger kwa ziara ya mafunzo juu ya sekta ndogo ya mafuta na gesi, ziara iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini, Ubalozi wa Norway nchini na Taasisi ya Petrad ya Nor-way.

Takwimu za 2012 zinaonyesha kuwa Norway ilikuwa nchi ya tatu duniani kwa uu-zaji wa gesi nje ya nchi na nchi ya 10 duniani kwa uuzaji wa mafuta nje ya nchi. Uuzaji wa mafuta na gesi ulifikia Krooner ya Norway bilioni 564 (Dola moja ya Marekani sawa na Krooner 6.6) mwaka 2013, ambazo ni sawa na asilimia 49 ya mauzo yote ya nje ya nchi hiyo.

Waandishi wa habari watakiwa kuzingatia maadili ya taaluma yao

Na Mohamed Saif- Kilwa

Waandishi wa habari wame-sisitizwa kuacha-na na uandishi wa kishabiki

badala yake wajikite katika kuan-dika habari ambazo ni za kweli bila kuegemea upande wowote.

Rai hiyo ilitolewa hivi karibu-ni katika mji wa Kilwa Masoko na mwandishi wa habari mwan-damizi na mkongwe ambaye pia ni mshauri wa masuala ya habari nchini, Ndimara Tegambwage alipokuwa akizungumza ka-tika mafunzo ya gesi asilia kwa waandishi wa habari kutoka Lindi na Mtwara ambayo yalilenga ku-wajengea uwezo wa kutambua fursa zinazotokana na gesi asilia.

Tegambwage alisema kwam-ba mwandishi wa habari kabla hajasambaza habari aliyoipata na kuiandaa, anapaswa kufanya tathmini ili kubaini athari ya taar-ifa husika kwa jamii na kwa taifa kwa ujumla. Alieleza kuwa, bila kufanyika kwa tathmini, huenda

habari hiyo ikaleta mkanganyiko kwa jamii. “Bila utafiti, jamii itakuwa inachanganywa na kama huna hoja, ushahidi ni vyema ukaachana na kazi ya uandishi wa habari na ukafanya kazi nyingine,” alieleza.

Alisema endapo waandishi wa habari watatumia vizuri taalu-ma yao ya uandishi, watakuwa na nafasi kubwa ya kusukuma mbele maendeleo na kuepusha migogoro inayotokana na jamii kuwa na ma-tarajio makubwa yasiyolingana na hali halisi ya rasilimali iliyogun-duliwa.

Tegambwage alifafanua kwamba jamii kutokana na kutozi-tambua fursa kutokana na kukose-kana kwa elimu, imejikuta ikijenga matarajio makubwa na yakutaka mabadiliko ya haraka ya kimaen-deleo bila kujiandaa kupokea na kuzitumia fursa husika.

Aliwasisitiza waandishi hao kujenga mazoea ya kusoma masu-ala mbalimbali yanayohusu gesi asilia ambayo yamefanyika katika nchi nyingine ili kuweza kuishauri serikali namna ya kuboresha sekta hiyo kama nchi zingine walivyo-fanya. “Twende tukaandike ukwe-

li na usahihi. Hii ifanyike kwa ku-fanya uchunguzi. Tusome mambo yaliyotokea nchi zingine ili nasisi tuandike kwa kuishauri serikali,” alieleza.

Alibainisha kuwa, licha ya vy-ombo vya habari kuwa na wajibu wa kuelimisha umma, lakini pia hata waandishi wenyewe wataka-poandika taarifa kwa ukweli na usahihi na pia kwa takwimu zi-nazokubalika, watakuwa ni watu wenye hadhi na pia watajijengea heshima katika jamii na huku wak-ilisaidia taifa.

Tegambwage aliongeza kuwa ili mwandishi aweze kuandika habari zilizo na maudhui yaliyo sahihi na yenye maslahi kwa taifa lazima awe na ufahamu wa kuto-sha wa kile anachotaka kukiandi-ka badala ya kukimbilia kuandika wakati hafahamu chochote.

Alieleza kwamba miongoni mwa sifa za uzalendo ni kuan-dika habari zinazoelimisha umma na huku zikichochea maendeleo badala ya vurugu ambazo ghara-ma ya kuzimaliza ni kubwa na zenye athari mbaya kwa jamii na kwa taifa kwa ujumla.

Wekeni mfumo madhubuti udhibiti sekta ndogo mafuta na gesi, n Viongozi wa Dini wanena, Norway

Mwandishi Mwandamizi na Mshauri wa masuala ya habari Tanzania, Ndimara Tegambwage akizungumza na waandishi wa habari

Page 11: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

Utafiti wa Jiolojia na Jiokemia wafanyika Lindi Na Priscus Benard

Dodoma

Jumla ya eneo la ukubwa wa kilometa za mraba 17,496 katika wilaya za Lindi na Liwale mkoani Lindi zimefanyiwa utafiti wa jiolo-jia na jiokemia na wataalam wa

Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST). Mkurugenzi wa Huduma za Jiolojia,

Bw. Fadhil Mosses amesema kuwa utafiti huo wa jiokemia ulihusisha ukusanyaji wa sampuli za miamba na mchanga wa vijito (stream sediments) ambazo zina-fanyiwa uchunguzi wa kimaabara kwa ajili ya kutambua aina ya elementi na ma-dini yaliyomo kwenye eneo husika.

Bw. Mosses alifafanua kuwa eneo hilo lililofanyiwa utafiti ni sawa na QDS sita (six Quarter Degree Sheets) ambapo QDS nne zilifanyiwa utafiti wa jiolojia na QDS mbili zilifanyiwa utafiti wa jiokemia.

Akitoa sababu za kufanya utafiti ka-tika eneo hili, Bw. Mosses alisema kuwa eneo hilo lilifanyiwa utafiti kwa sababu halijawahi kufanyiwa utafiti wa aina hiyo.

“GST ina taratibu zake za kufanya hizi tafiti, kila mwaka wa fedha tunafanya tafiti kwenye QDS sita yaani QDS nne za jiolojia na QDS mbili za jiokemia katika maeneo ambayo hayajafikiwa na tafiti hizi na tafiti hizi zinalenga kubaini rasili-mali madini zilizopo katika eneo husika,” alifafanua Bw. Mosses.

Alieleza kuwa licha ya utafiti huo kusaidia nchi kufahamu uwezekano wa

uwepo wa mashapo ya madini lakini pia unapelekea kuvutia uwekezaji na kura-hisiha shughuli za uchimbaji madini kwa wachimbaji wadogo na wakubwa.

Takwimu na taarifa zinaonesha kuwa asilimia 92 ya eneo lote la Tanzania Bara limefanyiwa utafiti wa jiolojia na asilimia 18 ya eneo lote la nchi limeshafanyiwa utafiti wa Jiokemia na Jiofizikia kwa ku-tumia ndege (High Resolution Airborne Geophysical Survey). Aidha asilimia 100 ya eneo lote la nchi limefanyiwa utafiti wa Jiofizikia kwa kutumia ndege (Low Reso-lution Airborne Geophysical Survey)

GST imekuwa ikikusanya taarifa za jiosayansi tokea mwaka 1925 ikiwa kama kitengo cha upimaji wa kijiolojia (Geological Survey Department - GSD)

kilichoanzishwa mwaka 1925 na Mam-laka ya Utawala wa Makoloni ya Nje ya serikali ya kikoloni ya Kiingereza (Brit-ish Overseas Management Authority - BOMA).

Wakala huo una majukumu mbal-imbali ikiwemo kukusanya, kucham-bua, kutafasiri na kutunza takwimu na taarifa za kijiosayansi (jiolojia, jiokemia, na jiofizikia) ambazo ni muhimu katika ufahamu wa kuwepo kwa madini mbal-imbali yaliyopo nchini na kutoa maele-kezo ya njia/namna bora za kutafuta na kuchenjua madini.

Utafiti wa Jiolojia na Jiokemia ka-tika wilaya za Lindi na Liwale ulihusisha wajiolojia kumi na tano (15) na mafundi sanifu kumi na mbili(12) kutoka Wakala huo.

Wataalam kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania wakifanya utafiti wa jiolojia katika hifadhi ya wanyamapori ya Selous mkoani Lindi wakiambatana na maafisa wanyama pori kwa ajili ya usalama wao.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Prof. Abdukarim Mruma (wa pili kulia) akiwa katika eneo la utafiti kwa ajili ya kuongoza timu ya wataalam wa GST.

Mtendaji Mkuu wa GST Prof. A. Mruma (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa wataalam wakati wakiwa katika utafiti wa jiolojia huko mkoani Lindi.

Mtaalam kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (kulia) akiwa katika hifadhi ya wanyamapori ya Selous mkoani Lindi akiambatana afisa wanyama pori kwa ajili ya usalama wake

Page 12: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

12 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

Matukio Pichani

Makamishna Wasaidizi wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini,wakifuatilia majadiliano kuhusu uendelezaji endelevu wa madini ya Tanzanite nchini yaliyofanyika sambamba na Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha (AGF). Kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini-Leseni, John Nayopa, Kamishna Msadizi wa Madini-Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane, na Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Salim Salim.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava, (wa kwanza kulia) akizungumza na mfanyabiashara wa madini nchini, Peter Pereirra mara alipotembelea banda la mfanyabiashara huyo katika Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha. Kulia kwa Naibu Katibu Mkuu ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja

Mtaalamu kutoka Wakala wa Jilojia Tanzania (GST), Mhandisi Heri Issa, akitoa mada wakati wa mkutano wa wadau wa madini ya Shaba.

u

Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja (katikati) katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa wadau wa madini ya Shaba ambao umewajumuisha wafanyabiashara wa madini ya Shaba, wachimbaji wadogo, viwanda vya kuyeyusha madini ya Shaba, Makamishna Wasaidizi wa Madini kutoka Kanda mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya Maafisa Madini Wakaazi.

Mmoja wa washiriki wa mkutano wa Madini ya Shaba, akiongea jambo wakati akichangia mada kuhusu madini ya Shaba.

Mfanyabiashara wa madini ya Shaba kutoka Kanda ya Kati Doreen Kisia, akisistiza jambo wakati akichangia hoja katika mkutano mkutano wa Madini ya Shaba.

Page 13: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

13BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eng.Ngosi Mwihava (wa sita kulia), Kamishna wa Madini nchini, Eng Paul Masanja (wa tano kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini nchini, Richard Kasesera (wa pili kulia), na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabishara wa Madini (TAMIDA) Sammy Mollel (wa nne kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Shirikisho la Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), Chama cha Wachimba Madini Wanawake (TAWOMA), Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) walioshiriki Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito, Arusha (AGF).

Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Paul Masanja (kulia) akitoa Tuzo kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini nchini (TAMIDA), Sammy Mollel, kutambua mchango wa Chama hicho katika kufanikisha Maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha tangu kuanza kwake mwaka 2012.

Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi. Paul Masanja (kulia) akitoa Tuzo kwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA), Bruno Mteta kutambua mchango wa Wakala huo katika kufanikisha Maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha 2014.

Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Paul Masanja (kulia) akitoa Tuzo kwa Idara ya Uhamiaji nchini, kutambua mchango wao katika kufanikisha Maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha 2014, anayepokea kwa niaba ya Idara hiyo ni Sophia Gunda .

Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Madini ya Vito na Usonara, nchini Thailand, Tony Brooks akionesha machapisho mbalimbali kuhusu madini ya Vito kwa mgeni rasmi wa maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa pili kutoka kushoto), wengine ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja(wa kwanza kutoka kushoto). Nchi ya Thailand ina uzoefu mkubwa katika uandaaji wa maonesho ya Vito ambapo wameshafanya maonesho zaidi ya 50 na wafanyabiashara wa madini ya Vito kutoka Tanzania wamekuwa wakishiriki Maonesho hayo.

Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja (kulia) akitoa Tuzo kwa Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kusini, Benjamin Mchwampaka ambaye ametoa mchango mkubwa katika kufanikisha Maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha tangu kuanza kwake mwaka 2012.

u

Page 14: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

14 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

Kamishna wa Madini, afungua mafunzo ya uongezaji thamani madini kwa wanawake.

Na Teresia Mhagama

Kamishna wa madini nchini, Mhandisi Paul Masanja amefungua rasmi mafunzo ya uongezaji thamani madini kwa wanawake 15 wa ki-

tanzania waliopata ufadhili wa masomo hayo ambayo ni matunda ya harambee iliyoanzishwa na Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha mwaka 2012.

Mafunzo hayo ya ukataji madini yatakayowawezesha wanafunzi husika kukata madini na kuyachonga katika maumbile ya kuvutia yatakuwa yakitole-wa kwa muda wa miezi Sita katika Kituo cha Jimolojia (TGC) kilichopo jijini Arusha ambacho kipo chini ya Wizara ya Nishati na Madini.

Akiongea katika hafla ya ufun-guzi wa masomo hayo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini nchini (TAMIDA) ambaye pia ni mjumbe

wa Kamati ya Maandalizi iliyoanzisha Harambee ya ufadhili wa masomo hayo, Sammy Mollel, alisema kuwa kuendesh-wa kwa mafunzo hayo ni utekelezaji wa Sera ya Madini ya mwaka 2009 ambayo imeweka mkazo katika suala la uongeza-ji thamani madini yanayozalishwa nchini kwa lengo la kuwapatia mapato watan-zania na shughuli hizo kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini.

“Kituo hiki kimeanzishwa ili kupata wataalam watakaofanya shughuli za uongezaji thamani madini ikiwemo ukataji, uchongaji na kunakshi madini ya aina mbalimbali hivyo kupitia wataalam hawa tutaweza kupata faida mbalimbali ikiwemo kuongeza thamani ya madini yanayozalishwa Tanzania, kuhamishia teknolojia hiyo nchini na kukuza ajira kwa watanzania”, alisema Mollel.

Alieleza kuwa, kwa sasa Tanzania haina wataalam wa kutosha wa kufanya shughuli hizo za uongezaji thamani

madini hivyo kituo hicho kitatoa jawabu hilo kwa kuwa kitazalisha wataalam watakaofanya kazi hiyo kwa ubora wa hali ya juu na kuweza kuingiza madini hayo katika soko la kimataifa .Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa TAMIDA aliiomba serikali kuendelea na juhudi za kukien-deleza Kituo hicho ili kizalishe wataalam wengi zaidi.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushau-ri wa Madini nchini, Richard Kasesera alisema kuwa serikali na wadau wa ma-dini ndani na nje ya nchi wanaendelea na juhudi za kutafuta fedha ili kukiendeleza kituo hicho, ikiwemo kutafuta wataalam waliobobea katika masuala ya ukataji na kuchonga madini kutoka nchi mbalim-bali duniani ikiwemo Sri Lanka.

Kasesera pia alieleza kuwa Wizara itaendelea kuwezesha mafunzo hayo, pia alitumia fursa hiyo kuiasa TAMIDA na wadau wengine kuendelea kuchangisha fedha zaidi ili mafunzo husika yawe endelevu .

Aidha, alimshukuru Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Paul Masanja kwa kutoa chumba cha darasa la kue-ndeshea mafunzo hayo katika Kituo cha Jimolojia (TGC) Arusha.

Kwa Upande wake Kamishna wa Madini, Mhandisi Paul Masanja amesema kuwa Sekta ya Madini inaen-delea kukua kwa kasi kubwa na hivi sasa serikali imeanza kutilia mkazo zaidi masuala ya uongezaji thamani madini hivyo eneo la vito litapewa mkazo kama ilivyokuwa kwa madini ya dhahabu.

“Nimefurahia sana suala la wanawake hawa 15 wa kitanzania kujifunza utaalam huu adimu sana duniani unaobadilisha maisha ya mtu binafsi, pamoja na nchi wanazofanyia kazi. Ukifikia hatua ya ule ukataji unaotakiwa, wewe utakuwa ni mtu wa mafanikio makubwa, mfano unaweza kuchukua jiwe la thamani ya Dola za Marekani 20,000 lakini kwa mikono yako ukaligeuza likawa na thamani ya Dola 2,000,000 hivyo inabidi mtambue jinsi mtakavyokuwa na utaalam huu muhimu sana”,alisisitiza Masanja.

Kamishna wa Madini aliwataka wa-nafunzi hao kujifunza utaalam huo kwa umakini mkubwa ili kuibadilisha tasnia ya vito nchini na kuahidi kuwa serikali itaendelea kuwapa ushirikiano hadi hapo watakapofikia hatua inayotakiwa. Pia aliipongeza Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha mwaka 2012 ambayo ilianzisha harambee ya kufadhili mafunzo hayo.

Kamishna wa Madini pia alim-pongeza Mratibu wa kituo cha Jimolojia Arusha, Mussa Shanyangi kwa usi-mamizi mzuri wa kituo hicho kinacho-ratibu mafunzo hayo ambapo alieleza kuwa ujenzi wa kituo hicho kitakachotoa mafunzo mbalimbali ya uongezaji tham-ani madini utakapokamilika, utawezesha sekta ya vito nchini kubadilika kwa kiasi kikubwa na kuliletea Taifa faida kubwa.

Mafunzo hayo ya uongezaji thamani madini yalianza rasmi tarehe 10 Novemba, 2014 ambapo wanafunzi 15 waliopata ufadhili wa masomo hayo watafundishwa kwa kutumia mtaala wa masomo ulioandaliwa na wataalam wa Kituo cha Jimolojia nchini kwa ushiriki-ano na wataalam kutoka Taasisi ya Vito na Usonara ya nchini Sri Lanka.

Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja (wa tatu kutoka kulia) akizungumza na mmoja wa wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo ya uongezaji thamani madini yanayoendeshwa katika Kituo cha Jimolojia (TGC) jijini Arusha, wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini nchini, Richard Kasesera (wa nne kutoka kulia), Meneja wa Uthaminishaji Ma-dini kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA), George Kaseza (wa pili kutoka kulia) na Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud (wa kwanza kulia).

Mmoja wa wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo ya uongezaji thamani madini akijifunza kuchon-ga madini ya vito ili yawe katika umbo la kuvutia kabla ya kumfikia mtumiaji.

http://www.mem.go.tz

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza na Balozi wa Uje-rumani nchini, Bw. Egon Kochanke.

Kamishna wa Madini nchini, Mhan-dis Paul Masanja (wa nne kutoka kushoto mstari wa pili) akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi 15 waliopata ufadhili wa masomo ya uongezaji thamani madini yanay-oendeshwa katika Kituo cha Ji-molojia (TGC) jijini Arusha. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini nchini, Rich-ard Kasesera (wa pili kushoto mstari wa pili),Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini nchini (TAMIDA), Sammy Mollel (wa tatu kushoto mstari wa pili),Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maone-sho ya Kimataifa ya Vito Arusha, (AGF), Peter Pereirra(wa tatu kulia mstari wa pili) Mwalimu anayefundi-sha masomo hayo kutoka nchini Sri Lanka, Pathmasiri Alwis (wa kwanza kushoto mstari wa pili) pamoja na watendaji Kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Kituo cha Jimolojia (TGC)

Page 15: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

15BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

http://www.mem.go.tz

TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE.

YAH: UTEUZI WA WAKURUGENZI NA MENEJA KATIKA WAKALA WA JIOLOJIA TANZANIA.

TheNinapenda kuwa taarifu kuwa kwa kuzingatia kifungu Na. 10(1) na (2) cha Sheria ya Waka-la wa Serikali Na. 30 ya Mwaka 1997 (kama ilivyorekebishwa) Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wawili (2) na Meneja sita (6) kama ifuatavyo:-

1. Fadhili M. Moses – Mkurugenzi wa Huduma za Jiolojia.2. Bi. Yorkbeth F. Myumbilwa – Mkurugenzi wa Kanzidata na Mifumo ya habari.3. Bw. Petro Faustine Nyanda – Meneja Mapping and Economic Geology.4. Bw. Maruvuko E. Msechu – Meneja Applied Geology.5. Bw. Momburi Philip Bazili – Meneja Mawe na Miamba.6. Bw. Mohamed Z. Makongoro – Meneja Kemia7. Terence T. Ngole – Meneja Uchoraji ramani na uchakataji wa taarifa za Kijiosayansi8. Massota M. Magigita – Meneja Makumbusho na Maktaba

Aidha, uteuzi huu umeanza rasmi tarehe 01/11/2014

Hivyo, tunaomba wapewe ushirikiano wa kutosha ili waweze kutekeleza majukumu yao ipas-avyo.

UTAWALA

Matangazo

 

Na Samwel Mtuwa - Dodoma

Wakala wa Jiolo-jia Tanzania (GST) umean-daa mafunzo elekezi na up-

ekuzi kwa waajiriwa wapya na baadhi ya watumishi wa zamani juu ya Sheria , Maadili , Kanuni na taratibu za kazi za Wakala wa Jiolojia Tanzania na Utumishi wa Umma kwa ujumla wake .

Kwa mujibu wa Meneja Ra-silimali Watu na Maendeleo Bw. Gabriel Kasase , alisema kuwa ni sheria na utaratibu kwa taasisi ya Umma kufanya mafunzo ya awali na upekuzi pindi inapoajiri mtumishi mpya wa umma kwa sababu inamsaidia mtumishi ku-jua taratibu , sheria , Kanuni na stahiki zake za kazi katika sehe-mu yake ya kazi..

“Ni utaratibu wa kisheria kwa mtumishi wa umma kufany-iwa mafunzo ya awali na upekuzi pindi anapoingia katika ajira ya utumishi wa umma, mafunzo haya yatamsaidia kujua sheria , taratibu , kanuni na haki zake katika sehemu ya kazi,” alisema

Kasase Bw. Kasase alieleza kuwa,

mafunzo hayo yana lengo la kumjulisha mtumishi juu ya kuz-ingatia Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8/2002 ( na Mareke-bisho yake),Kanuni za Utumishi 2003 na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma(Standing Orders ) za Mwaka 2009 .

Aidha, aliongeza kuwa wa-shiriki wamepitia nyaraka mbal-imbali za Utumishi Umma kama vile Waraka Na.1 wa mwaka 2000 kuhusu Maadili ya Mtumi-shi wa Umma katika Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa na Wara-ka Na.2 wa mwaka 2014 kuhusu kudhibiti virusi vya Ukimwi na Magonjwa sugu yasiyoambuki-zwa mahali pa kazi na Na.3 wa mwaka 2007 kuhusu mavazi kwa mtumishi wa umma.

Naye Rodney Matalis, mwezeshaji wa mafunzo hayo alisema sambamba na Sheria za zinazosimamia utumishi wa umma na nyaraka mbalimbali mtumishi wa umma pia ana wa-jibu wa kujua sheria nyinginezo zinazosimamia ajira kwa ujumla wake mfano Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Na. 6/2004 na Sheria ya Taasisi za Kazi ya Na. 7/2004 .

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST Bi. Augustine Rutaihwa wakati wa kufunga mafunzo hayo alisema kuwa ni vyema watumishi wazin-

gatie Sheria na kanuni husika ili kuleta tija na kuondoa migogoro katika eneo la kazi.

Mafunzo haya ya siku mbili yalianza Novemba 25 na 26,

2014 na kufunguliwa na kaimu Mtendaji Mkuu wa GST Bi. Au-gustine Rutaihwa ambaye pamo-ja na baadhi ya maafisa wa GST walihudhuria ufunguzi huo.

GST YATOA MAFUNZO ELEKEZI KWA WAAJIRIWA WAPYA

Fundi Sanifu wa Mifumo ya Habari na Mawasiliano (ICT), Clement Mwasamila , akimuelezea Afisa Habari wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) hayupo pichani juu ya mageuzi ya mfumo wa utunzaji taarifa za Jiosayansi katika kifaa maalum kilichopo katika Wakala huo.

Pichani waliokaa ni kaimu Mtendaji Mkuu wa GST, Bi . Augustine Rutaihwa,(katikati waliokaa) Wengine ni Meneja Rasilimali watu na Maendeleo wa GST, Bw. Gabriel Kasase (wa kwanza kulia) na Bw. Rodney Matalis (wa kwanza ku-shoto waliokaa) ambaye ni mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA) katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wapya wa Wakala wa Jiolojia Tanzania.

Page 16: JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 44

16 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Tangulizeni Uzalendo, Waandishi waelezwaNa Mohamed Saif-

Kilwa

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuwa wazalendo na kushirikiana na serikali

katika kufikisha elimu na taarifa sa-hihi kwa wananchi.

Wito huo umetolewa wilayani Kilwa na Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Badra Masoud alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili ya gesi asilia na mafuta kwa waandishi wa habari kutoka mkoa wa Lindi na Mtwara.

Masoud aliwataka waandishi hao kutanguliza uzalendo mbele na kufanya kazi kwa weledi ili kuepuka

kuliingiza taifa katika migogoro. “Waandishi wenzangu tufanye kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yetu, wananchi wanatuamini sana na wana imani na habari ambazo tunatoa. Si busara hata kidogo kupoteza uaminifu tulionao kwa wananchi. Tufanye kazi zetu kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari huku tukitanguliza uzalendo mbele,” alisisitiza Badra.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari katika kufikisha elimu na taarifa kwa umma, Wizara ya Nishati na Ma-dini imeandaa mkakati maalumu wa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini ili kuwajengea uwezo wa ku-toa taarifa iliyo sahihi katika jamii na taifa kwa ujumla.

Alieleza kuwa, wizara in-atekeleza shughuli zake kwa uwazi ili

kila mwananchi aweze kuelewa mi-kakati na shughuli mbalimbali zina-zofanywa na wizara. “Ili kila mwa-nanchi aweze kufahamu shughuli zinazofanywa na wizara pamoja na kuelewa mikakati ambayo wizara imejipangia tumeona njia nzuri ni kuwaelimisha waandishi wa habari ili waweze kutoa taarifa sahihi,” al-iongeza Masoud.

Aidha, Msemaji huyo aliwa-tahadharisha waandishi wa habari kuepuka kuandika habari zenye mu-elekeo wa kuleta mtafaruku katika jamii. “Ninawasihi muandike habari ambazo zinalenga kuliendeleza taifa letu na sio habari zenye muelekeo wa kupotosha jamii. Tukumbuke ya kwamba Tanzania ni yetu sote hivyo wizara ipo tayari kushirikiana nanyi ili sote kwa pamoja tuhakikishe tu-naliletea taifa letu maendeleo thabi-ti,” alisisitiza msemaji huyo.

Masoud aliwasisitiza waandishi waliohudhuria mafunzo hayo ku-hakikisha wanazingatia yale ambayo yatafundishwa ili baada ya mafunzo hayo wanaporejea katika sehemu zao za kazi wawe katika nafasi nzuri zaidi ya kuelimisha jamii. “Zinga-tieni yale ambayo mnafundishwa na mtakaporejea kwenye jamii muo-nyeshe mabadiliko, habari zenu kwa umma ziwe ni za ukweli na sahihi,” alieleza Masoud.

Msemaji huyo alieleza kuwa mbali na kutumia vyombo vya habari katika kuelimisha umma, wizara im-ejipanga kutumia njia mbalimbali za kutoa elimu kwa umma kwa nyakati tofauti. “Si kila mwananchi ana uw-ezo wa kununua gazeti ama kumiliki luninga ama redio. Hivyo sisi kama wizara tumeandaa njia mbadala ny-ingi ili kuhakikisha tunafikisha elimu kwa umma. Tumejiandaa kuzun-

guka nchi nzima tukitoa elimu kwa umma,” alieleza.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoani Lindi, Abdulaziz Ahmad aliishuku-ru Wizara ya Nishati na Madini kwa kuandaa mafunzo hayo waandishi wa habari na pia aliwataka waandi-shi waliohudhuria mafunzo hayo ku-fanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya taaluma ya uandishi wa habari na siyo kufanya kazi kwa mazoea.

“Waandishi mara nyingi tume-kuwa tukiandika habari zetu kwa mazoea na pia kwa kufurahisha baadhi ya watu wachache wenye maslahi binafsi kitu ambacho ni ha-tari kwa mustakabali wa taifa letu. Ni vyema sasa tukabadilika, bado hatu-jachelewa, tukiamua tunaweza, na ninaamini kwa dhati kabisa kwamba tunaweza,” alisisitiza Ahmad.

UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII UJUMBE WA WAZIRI WIKI HIIWAFANYAKAZI WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI, KAMPUNI NA

TAASISI ZETU TUENDELEE KUCHAPA KAZI KWA UMAKINI, UADILIFU NA UBUNIFU MKUBWA SANA KWA KUSUDIO LA KUFUTA UMASIKINI NCHINI

MWETU. TUTASHINDA, TUSIKATISHWE TAMAA.

Wanahabari watakiwa kuandika habari za ukweli na uhakika Na Mohamed Saif-

Kilwa

Waandishi wa habari wa mikoa ya Lindi na Mt-wara wametakiwa kuji-tambua kwa kuandika

habari za kweli na uhakika kuhusu masuala mbalimbali yanayohu-su sekta ya gesi asilia.

Wito huo ulitolewa hivi karibuni wilayani Kilwa na mwandishi wa habari mwan-damizi kutoka gazeti la The East African, Joseph Mwamun-yange alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo ya siku mbili ya gesi

asilia yaliyoandaliwa na Wiz-ara ya Nishati na Madini kwa waandishi wa habari kutoka ka-tika mikoa hiyo.

Mwamunyange aliwasisiti-za waandishi hao kuhakikisha wanajenga mazoea ya kuji-somea na kufanya tafiti kabla ya kuchukua uamuzi wa kuandika habari kwani kwa kufanya hivyo kutawasaidia kuwa na uelewa mpana wa masuala ambayo wa-nataka kuuhabarisha umma na hivyo kutoa taarifa sahihi.

Alisema waandishi wa habari wanapaswa kuwa na uelewa mkubwa wa masu-ala ya gesi asilia ili kuepuka kutoa habari za uchochezi au

za upande mmoja na hivyo ku-sababisha mazingira ambayo yatasababisha wananchi kukosa imani na serikali yao.

“Mwandishi mzuri ni yule ambaye hupendelea kusoma na pia mwenye udadisi wa mam-bo mbalimbali. Ili Mwandishi aweze kutoa habari kwa usahihi na ukweli kuhusu sekta ya gesi asilia, ni muhimu akaifahamu sekta hii kwa undani zaidi. Tusi-we wanahabari wa kuandika matukio tu, na hii itawezekana kwa kuwa wadadisi na kusoma sana,” alisisitiza Mwamun-yange. Aidha, Mwamunyange aliwashauri waandishi hao kuhakikisha wanapima kauli

na taarifa za wanasiasa na wa-naharakati kabla taarifa hizo hazijatumika kuandikia habari. Alisema ni vyema waandishi wa habari wakatafakari kuhusu taarifa hizo ikiwa ni pamoja na kuzifanyia uchunguzi wa kina ili kuepuka upotoshaji.

“Waandishi daima tuna-paswa kuwa waangalifu sana, unaweza ukajikuta unatumiwa na wanasiasa bila hata wewe kujua, hivyo ni vyema tukawa tunafanya utafiti wa kina kabla hatujaamua kuandika chochote. Tusaidie kupandisha uelewa wa wananchi na baadhi ya wabunge kuhusu hii sekta kwa kutoa taarifa zilizo fanyiwa

utafiti wa kutosha,” alisisitiza Mwamunyange.

Alisisitiza kuwa ni jukumu la waandishi wa habari kufanya utafiti wa fursa ambazo zinapa-tikana kutokana na ugunduzi wa gesi asilia nchini ili kuifa-hamisha jamii namna ambavyo zinaweza kuchangamkia fursa hizo na kujiletea maendeleo.

“Kuna fursa nyingi sana ambazo jamii inaweza kuzitu-mia kujiletea maendeleo, sasa sisi waandishi ndio inapasa tuzitambue fursa hizo na baada ya hapo tutazame ni namna gani jamii inaweza kuzitumia fursa hizo kujiletea maendeleo,” alieleza Mwamunyange.

Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo ya gesi asilia yaliyofanyikia mjini Kilwa.

Baadhi ya waandishi wa habari wa Lindi na Mtwara wakifuatilia mafunzo ya gesi asilia yaliyofanyikia mjini Kilwa, Mkoani Lindi.