JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 76

Embed Size (px)

Citation preview

  • 8/20/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 76

    1/9

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali

    kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizar a ya Nishati na MadiniWasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263

    au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    HABARI ZA

    NISHATI &MADINI

    Toleo No. 76 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Julai 17 - 23, 2015Bulletinews

     

    http://www.mem.go.tz

     

    Mradi gesi asiliawafkia asilimia 98

     S o ma hab ar i  

    U k . 2 

    Luoga aagiza miradi ya Umeme Dar ikamilike kwa wakati

    Kituo cha kupokelea gesi eneo la Somanga kikiwa kimekamilika

    Mitambo ya kupokelea gesi ya K inyerezi iliyokamilika kufungwa

    Mitambo ya kusafisha gesina nyumba za wafanyakazi

    Madimba, Mtwara

    Uk. 2

  • 8/20/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 76

    2/9

    2   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

     Asteria Muhozya naTeresia Mhagama

    Imeelezwa kuwa, utekelezaji wamiradi ya ujenzi wa mitambo yakusafisha gesi asilia ya Madimbana Songongo, Kilwa, pamoja na bomba la kusafirisha gesi hiyo

    kutoka Mtwara na Songosongo hadiDar es Salaam kupitia Somanga Funguitakamilika hivi karibuni.

    Hayo yameelezwa katika taarifa yamwezi Juni mwaka huu, iliyotolewa naKaimu Mkurugenzi wa Kampuni yaKusambaza Gesi (GASCO) ambayo niKampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleoya Petroli Tanzania (TPDC), MhandisiKapuulya Musomba

    Akielezea hatua zilizofikiwa katikamiradi hiyo, Musomba alieleza kuwa,

    kwa ujumla mradi huo umefikia asilimia

    98 za ujenzi na kukamilika kwakekutaunganisha maeneo yanayozalishagesi asilia hususan Mnazi Bay- Mtwara,Songosongo, Kiliwani, Mkuranga, Ntoryana gesi iliyogunduliwa katika eneo la bahariya kina kirefu.

    Akifafanua zaidi alisema kuwa, Bombalimekamilika kwa asilimia 99.6 kwaujumla, mitambo ya kusafisha gesi asilimia97.5. Manunuzi ya vifaa vya ujenzi wamradi yamekamilika kwa asilimia 100, namradi mzima umekamilika kwa asilimia98.

    Musomba alisema kuwa, hatua

    hiyo itaiwezesha Serikali kupitia TPDCkuhakikisha kuwa, Tanzania inazalishaumeme wa kutosha kupitia rasilimalihiyo na wananchi wake wananufaika narasilimali ya gesi asilia.

    “Serikali imedhamiria kuhakikishakuwa, gesi inatumika katika kuzalishaumeme ambao kwa sasa unazalishwakwa kutumia nishati ya mafuta ambayohuagizwa kutoka nchi za nje na hivyokuligharimu taifa kiasi kikubwa cha fedhaza kigeni,” alieleza Musomba.

    Kuhusu mitambo ya kuchakata gesi

    asilia, alisema kuwa, ujenzi wa eneo la

    kusimika mitambo, jengo la kuendeshamitambo pamoja na barabara za ndanikatika eneo la Madimba Mtwaraumekamilika kwa asilimia 98, wakati ulewa Songosongo umekamilika kwa asilimia100 na usimikaji mitambo umekamilikakwa asilimia 98.

    Akizungumzia suala la ajira katikamradi huo, alisema kuwa, kumekuwepona wafanyakazi wapatao 1,427 wenyemchanganyiko wa wageni pamoja nawatanzania kwa ngazi zote hadi taarifa hiiinatolewa.

    Aidha, kuhusu ajira kwa upande waTPDC, alieleza kuwa, shirika hilo tayarilimeajiri wafanyakazi wapya wapatao 92kwa upande wa mitambo ya kusafisha gesina 42 kwa upande wa bomba la kusafirishagesi, ambao tayari wanashiriki katika

    usimamizi wa shughuli za ujenzi.Sehemu ya taarifa hiyo inaeleza kuwa,mradi unatekelezwa kwa kutumia fedhaza mkopo wa masharti nafuu kutokaSerikali ya Jamhuri ya watu wa China.Jumla ya gharama za ujenzi wa mradihuo ni Dola za Marekani zipatazo bilioni1.255, ambapo asilimia 95 ni mkopo naasilimia 5 ni mchango wa Serikali.

    Vilevile taarifa inaeleza kuwagharama nyingine nyingi ambazo serikaliimeendelea kuzibeba nje ya asilimia 5zinazotajwa ni pamoja na gharama zaupatikanaji wa mkuza wa Bomba la gesikutoka Mtwara hadi Somanga Fungu nakuongezeka kwa upana maeneo menginemengi ya mkuza tokea Somanga Fungukuja Dar es Salaam hadi Tegeta. Hadi sasa

    zimefikia kiasi cha pesa za ki-Tanzaniazipatazo shilingi Bilioni 200.

    Katika hatua nyingine, akizungumzawakati akifunga rasmi Bunge la Jamhuriya Muungano wa Tanzania mwishonimwa wiki, Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Dkt. Jakaya MrishoKikwete alieleza kuwa, serikali imejipangakuhakikisha kuwa, hadi ifikapo mwaka2020 uzalishaji umeme unafikia kiasi chamegawati 3000 kutokana na matumizi yagesi asilia.

    Akieleza kuhusu miswada ya Sheria zaPetroli na TEITI iliyosomwa Bungeni hivikaribuni na Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene, Rais Kikwetealisema yuko tayari kuisaini miswada hiyo

    wakati wowote itakapomfikia.

    Mradi gesi asilia wakia asilimia 98

    Wakandarasiwa miradi yak u b o r e sh amiundombinuya umeme

    kwenye vituo vya kupoozeaumeme jijini Dar es Salaamwametakiwa kuhakikishawanakamilisha miradi hiyondani ya muda uliopangwa.

    Wito huo umetolewahivi karibuni na KamishnaMsaidizi wa Umeme, MhandisiInnocent Luoga wakati waziara yake ya ukaguzi wa

    Mradi wa Kusambaza Umemeujulikanao kwa jina la ElectricityV unaofadhiliwa na Benki yaMaendeleo ya Afrika (AfDB)ambao unahusisha ujenzi naukarabati wa vituo vya kupoozeaumeme vya Sokoine, Ilala naNjiro.

    Aidha, ziara hiyo piailihusisha ukaguzi wa Mradi waUjenzi na Ukarabati wa Vituovya Ilala na New City Centrepamoja na ujenzi wa vituovipya vya Ilala na Muhimbiliambao unafadhiliwa na Serikali

    ya Japan kupitia Shirika laMaendeleo la Japan (JICA)na vilevile Mradi wa Mfumowa Kusimamia na KudhibitiUsambazaji wa Umeme Dares Salaam ujulikanao kamaDistribution SCADA Systemuliopo Mikocheni unaofadhiliwana Serikali ya Finland.

    Mhandisi Luoga alielezealengo la ziara hiyo kuwa nikujionea hatua iliyofikiwa katikautekelezaji wa miradi hiyo

    Hatua hiyo itaiwezesha Serikali kupitia TPDCkuhakikisha kuwa, Tanzania inazalisha umeme wakutosha kupitia rasilimali hiyo na wananchi wakewananufaika na rasilimali ya gesi asilia 

    Mitambo ya kusafisha gesi ya Madimba

    Luoga aagiza miradi ya Umeme Dar ikamilike kwa wakati

    >>Inaendelea Uk. 3

    Mradi waElectricityV- Ilala:Transfomampyailiyofungwakwenye kituocha kupoozaumeme chaIlala marabaada yamajaribio yaawali.

  • 8/20/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 76

    3/9

    3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Tahariri

    MEM

      Na Badra Masoud

    FIVEPILLARS OFREFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMUKITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI

    MHARIRI MKUU: Badra MasoudMSANIFU: Essy Ogunde

    WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, GreysonMwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James

    na Nuru Mwasampeta

    INCREASE EFFICIENCY 

    QUALITY DELIVERYOF GOODS/SERVICE

    SATISFACTION OFTHE CLIENT

    SATISFACTION OFBUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OFSHAREHOLDERS

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Hongera Simbachawenekwa mkakati wa kuisuka

    Upya TIPER 

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga(wa pili kushoto) akimsikiliza Meneja Mradi wa ElectricityV, Mhandisi Florence Gwang’ombe (wa pili kulia) wakati waziara yake kwenye kituo cha kupoozea umeme cha Ilala.

    Luoga aagiza miradi ya UmemeDar ikamilike kwa wakati

    ikiwa ni pamoja na kubainichangamoto zinazokabiliutekelezaji wa miradi husika.

    Katika taarifa yake

    ya utekelezaji wa Mradiwa Electricity V, Menejawa Mradi huo, MhandisiFlorence Gwang’ombealisema kutokana na sababumbalimbali huenda mradihuo ukachelewa kukamilikatofauti na makubaliano ya awalikitendo ambacho kilimkeraMhandisi Luoga na hivyokumuagiza Meneja huyo kukaana wakandarasi wa Mradi nakurejea makubaliano ya awali.

    Mhandisi Florence alisemamoja ya sababu inayopelekea

    Mradi huo kuwa na kasi ndogoni wakandarasi kushindwakuajiri wafanyakazi wa kutosha.

    Mhandisi Luoga aliwaagizawakandarasi hao ambao nikampuni ya National ContractingCompany Ltd (NCC) ya Indiana ELTEL Group kutokaFinland kuhakikisha wanaajiriwafanyakazi wa kutosha napia kuandaa ratiba ya shughulizinazotakiwa kufanywa ilikuepuka kuchelewa kukamilikakwa miradi husika.

    Aidha, Mhandisi Luogaaliwaagiza Mameneja Miradiwa Shirika la Umeme Nchini(TANESCO) kuhakikishakunakuwepo na usimamizimadhubuti wa miradi iliyochini yao ili kuleta matokeo

    yanayotarajiwa.Alisema lengo la Serikali ni

    kuhakikisha taifa linakuwa naumeme wa uhakika kwa ajili yakukuza uchumi hivyo aliwaasamameneja hao kuhakikishaazma hiyo inatimia.

    “Ninawasisitiza muhakikishekunakuwepo na ufatiliaji makiniwa miradi mnayoisimamia na siokuwaachia wakandarasi wafanyekila kitu bila usimamizi wenu,”aliagiza Mhandisi Luoga.

    Kwa upande wake Meneja wakampuni ya NCC Ltd, SadeeshJohn alimuahidi MhandisiLuoga kuwa atahakikisha kasiya utekelezaji inaongezeka nakutimiza maagizo husika ilikuhakikisha mradi unakamilikandani ya muda uliopangwa.

    >>Inatoka Uk. 2

    Mapema wiki hii Waziri wa Nishati na

    Madini, George Simbachawene alikutana na

    Uongozi wa Shirika la kuhifadhi mafuta ya

    TIPER ambayo serikali ni mbia kwa asilimia 50.Katika kikao hicho alisisitiza kuhusu dhamira

    ya Serikali kuboresha na kulisuka upya shirika

    hilo la kuhifadhi mafuta ili liweze kutoa huduma

    ya kupokea mafuta kwa kampuni zote kwa haki

    na usawa.

    Simbachawene alisema lengo la kulisuka

    upya Shirika hilo ni kuliboresha na kuhakikisha

    kuwa linatoa huduma ya kuhifadhi na kupitisha

    mafuta yote yanayoletwa nchini, na kuhakikishagharama za kuhifadhi mafuta hapa nchini

    zinakuwa nafuu.

    Kwa mara nyingine tunapenda kupongeza

     jitihada zinazofanywa na Serikali katika

    kuhakikisha kwamba Sekta ya mafuta nchini

    inalinufaisha taifa ikiwemo kuleta unafuu wa

    nishati hiyo.

    Hakika katika hili la kuisuka upya TIPER ni

    mikakati madhubuti ambayo inatarajia kuletamabadiliko makubwa katika Shirika hivyo,

    wadau wa TIPER na Watanzania tuunge

    mkono juhudi hizi za Serikali kwani kauli hii ya

    sasa inadhihirisha dhamira ya dhati ya Waziri

    Simbachawene juu ya kulisuka upya Shirika hilo

    ambapo alisisitiza umuhimu TIPER katika sekta

    ya mafuta nchini, na kuleza kwamba hivi sasa

    shirika hilo linahitajika kuliko wakati mwingine

    wowote.

  • 8/20/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 76

    4/9

    4   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

     

    JK ajivunia mchango Sekta ya Madini

    Na Asteria Muhozya,

    R ais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Dkt. JakayaMrisho Kikwete amesifu jitihada zilizofanywa na Serikaliya Awamu ya Nne katika

    kuimarisha Sekta ya Madini nchini nakuitaja kuwa ni ya pili kwa kuingiza fedha zakigeni baada ya Sekta ya Maliasili.

    Rais Kikwete aliyasema hayo mwishonimwa wiki wakati akihutubia wananchikupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano

    wa Tanzania, mjini Dodoma na kuyatajamafanikio kadhaa katika Sekta hiyo,ikiwemo ya migodi ya madini kuanza kulipaushuru wa huduma.

    Hotuba ya Rais Kikwete inarejeataarifa ya awali iliyotolewa na Wizara yaNishati na Madini ikieleza kuwa, mgodiwa dhahabu wa Geita unaomilikiwa nakampuni ya AngloGold Ashanti; na migodiya Bulyanhulu, Buzwagi na North Marainayomilikiwa na kampuni ya AcaciaMining, imeanza kulipa ushuru wa hudumakwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) yamapato ghafi kwa Halmashauri husika.

    “Tayari migodi inalipa kodi ambazozinachangia katika pato la Taifa. Pia tunaSheria ya Madini ya Mwaka 2010 haya yoteyamesaidi kuweza kunufaika zaidi kupitia

    rasilimali hii,” alisisitiza Rais.Aidha, Rais Kikwete alieleza mafanikio

    yaliyopatikana baada ya serikali kulifufuaupya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),ambapo alisema kuwa, mafanikio hayo

    yamechangia shirika hilo kumiliki mgodiwake wa dhahabu wa STAMIGOLDuliopo Biharamulo, ambao tayari umeanzakutoa mikuo ya dhahabu.

    Vilevile, katika hotuba yake, RaisKikwete alieleza namna Serikali ilivyofanya jitihada za kuwawezesha wachimbajiwadogo kupewa ruzuku, lengo likiwa nikuwawezesha kutoka katika uchimbajimdogo kwenda katika uchimbaji wa kati.

    Katika taarifa yake wakati akizinduaKamati inayoshughulikia maombi ya ruzukuAwamu ya Pili hivi karibuni, Kamishna waMadini Tanzania, Mhandisi Paul Masanjaalisema kuwa, kiwango cha fedha katikaawamu hii kimeongezwa kufikia Dola zaKimarekani milioni na tatu na shilingiza Kitanzania bilioni 1.7 kutoka Dola za

    Marekani Laki tano (500,000) zilizotolewaAwamu ya Kwanza.

    “Lakini pia tumetenga maeneo 8 kwaajili ya wachimbaji wadogo. Tumefanyahivi ili wasisumbuliwe na wachimbajiwakubwa,” alisema Kikwete.

    Vilevile, Rais Kikwete alisema kuwa,mikataba imerekebishwa ili kulinda nakulinufaisha taifa ambapo pia baadhiya mafanikio ya marekebisho hayoyamewezesha Kampuni za madinikuongeza huduma ya bidhaa zinatolewanchini tofauti na ilivyokuwa awali.

    Katika hotuba yake pia aliitaja migodimipya 3 ikiwemo ya Makaa ya Mawe yaNgaka na Liganga na Chuma Mkuju,ambayo ilianzishwa katika kipindi chamiaka 10 na kueleza kuwa, sekta hiyo

    imeongeza kiwango cha ajira kutoka 3,500hadi kufikia 15,000.

    >>  Aitaja ya pili kuingiza fedha za Kigeni baada ya

    Maliasili>>  Ajira zaongezeka kutoka 3,500 hadi 15,000.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete

    Ujumbe kutoka Malawi watembelea Tanzaniakujifunza sheria ya Madini, CADASTRE.Na Rhoda James

    Ujumbe kutoka Serikali ya Malawi

    umetembelea Wizara ya Nishati na Madinimwanzoni mwa wiki hii kwa lengo lakujifunza masuala mbali mbali ikiwemoSheria ya Madini ya Mwaka 2010 naMfumo mpya wa kusajili leseni za madinikwa njia ya mtandao (Online miningCadastre Transactional Portal)

    Ziara hiyo ya Malawi imekuja kufuatianchi hiyo kuwa katika mchakato wakutunga Sheria mpya ya Madini. Ujumbehuo pia umetembelea Wakala wa Ukaguziwa Madini Tanzania (TMAA),Ofisi yaMadini Kanda ya Mashariki, Kampuni yaMadini ya Acacia, pamoja na kitengo chaLeseni na TEHAMA katika Wizara yaNishati na Madini.

    Ujumbe huo kutoka Malawiumeipongeza Serikali ya Tanzania kwa

    kazi nzuri wanayoifanya katika kuendelezasekta ya Madini na kuahidi kuendelezaushirikiano uliopo kati ya Serikali hizombili.

    Ujumbe kutoka Malawi ukiwa katika Wizaraya Nishati na Madini wakati ulipofika Wizaranihapo kujifunza masuala ya Madini. Katikatini Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali WatuWizara ya Nishati, Mrimia Mchomvu na kushotokwake ni Kamishna Msaidizi wa Madini kitengocha Leseni, John Nayopa.

    Kulia ni kiongozi wa Msafara wa Ujumbekutoka Malawi Katibu Mwandamizi, Ben Botoloakielezea jambo katika kikao hicho.

  • 8/20/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 76

    5/9

    5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Serikali kuisuka upya TIPERNa Mwandishi Wetu S

    erikali imedhamiria kuboresha nakulisuka upya shirika la kuhifadhimafuta TIPER ili iweze kutoahuduma ya kupokea mafuta kwakampuni zote kwa haki na usawa.

    Waziri mwenye dhama na Wizara yaNishati na Madini George Simbachaweneamebainisha hayo wiki hii alipozungumzana Uongozi wa shirika hilo huku akisisitizakwamba lengo la Serikali kuboreshashirika hilo ni kuhakikisha inatoa hudumaya kuhifadhi na kupitisha mafuta yote

    yanayoletwa nchini.Simbachewene aliongeza kusemakwamba hadi ifikapo mwishoni mwamwaka huu kampuni hiyo itakuwa nauwezo wa kuhifadhi mafuta kiasi cha lita300,000.

    “Kwa dhati kabisa tumeamuakuiboresha kampuni hiyo na tunapangaifikapo Septemba mwaka huu uwezo waTIPER wa kuhifadhi mafuta utaongezekakutoka lita 147,000 hadi kufikia 210,000 naitakapofika Desemba watakuwa na uwezowa kuhifadhi mafuta lita 300,000,” alisisitizaGeorge Simbachawene.

    Waziri Simbachawene aliongezakwamba lengo la Serikali kuchukua hatuaya kuiboresha TIPER ni kuhakikishagharama za kuhifadhi mafuta hapa nchini

    zinakuwa nafuu.

    Mkurugenzi Mtendaji waShirika la TIPER, DanielBelair ( Wa kwanza kulia)akimwongoza Waziriwa Nishati na Madini,George Simbachawene(kushoto) na ujumbewake walipotembeleashirika lake hivi karibuni.

    Mwenyekiti wa Bodi yaTIPER Prof. AbdulkarimMruma akieleza jambokatika moja ya vikao naWaziri

    Wanafunzi waliopata ufadhili wa China waaswaNa Greyson Mwase,Dar es Salaam

    Mkurugenzi wa Idara yaUtawala na Usimamizi waRasilimaliwatu, Wizara yaNishati na Madini, MrimiaMchomvu amewataka

    wanafunzi wanaosomea masuala ya gesina mafuta nchini China kutumia utaalamna uzoefu wao katika kuleta mabadilikokwenye sekta ya gesi na mafuta nchini.

    Mchomvu aliyasema hayo ofisinikwake, alipotembelewa na wanafunziwaliofadhiliwa na Wizara ya Nishati naMadini kwa ajili ya mafunzo ya Shahada yaUzamili katika masuala ya gesi na mafutakatika Chuo Kikuu cha Jiosayansi – Wuhankilichopo nchini China.

      Wanafunzi hao ambao ni miongonimwa wanafunzi nane waliofadhiliwa naWizara kusomea masuala ya gesi na mafutakwa mwaka 2013, walifanya ziara hiyo kwaengo la kuishukuru Wizara pamoja nakuelezea mikakati yao katika kutumia elimuna uzoefu walioupata kuinua sekta za gesina mafuta.

    Alisema lengo la Serikali kupitia Wizaraya Nishati na Madini la kupeleka wanafunzihao lilikuwa ni kuzalisha wataalam kwa ajiliya kufanya kazi katika Wizara, makampuniya utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi

    nchini.“ Kutokana na kukua kwa shughuli za

    utafutaji wa gesi na mafuta nchini kamaSerikali tulipanga mikakati mbalimbaliikiwa ni pamoja na kuwawezesha wazawakushiriki katika shughuli hizo kwakuwapeleka kusomea masuala ya gesi namafuta ili waweze kufanya kazi na mashirikaya umma na makampuni yaliyowekezakatika shughuli za utafutaji na uchimbaji wagesi na mafuta nchini,” alisema Mchomvu.

    Mchomvu aliendelea kusema kuwawataalam hao wanaweza kutumia elimu nauzoefu walioupata kutoka China kufanyakazi kwenye mashirika ya umma, taasisi namakampuni binafsi yanayojishughulisha nashughuli za uchimbaji na utafutaji wa gesi namafuta.

    Alisisitiza kuwa serikali pekee, haiwezikuajiri wahitimu wote wanaomalizamafunzo ya gesi na mafuta bali kazi yakekuu ni kuwapatia elimu itakayowawezeshakushiriki katika fursa mbalimbalizinazojitokeza katika setka ya gesi namafuta.

    “Sekta ya gesi na mafuta inakua kwa kasikwa sasa, fursa ni nyingi hivyo ni jukumulenu kuchangamkia fursa mbalimbali zaajira zinazojitokeza katika makampuni ya

    utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi.Kuna Shirika la Maendeleo ya PetroliNchini (TPDC) ambalo lina kampuni

    tanzu, makampuni ya utafutaji wa gesi namafuta ya Statoil na BG ambayo yanahitajiwataalam,” alisisitiza Mchomvu.

    Wakielezea uzoefu walioupata katikachuo hicho, wanafunzi hao walisemawamejifunza kwa kina hatua za utafutaji,uchimbaji na usafirishaji wa mafuta na gesikwa kutumia vifaa vya kisasa hali iliyowapauwezo wa kufanya kazi na kampuni zakimataifa.

    Bishanga Januarius ambaye ni

    mwanafunzi wa mwaka pili katika chuohicho alisema kuwa utaalam na uzoefualioupata katika chuo hicho utamwezeshakufanya kazi katika kampuni yoyote yautafiti na uchimbaji wa madini na kuwa namchango mkubwa kwa taifa.

    Alisema kuwa elimu ya vitendowaliyoipata katika makampuni ya mafutana gesi nchini China imewapa mwangamkubwa katika shughuli zote za utafiti nauchimbaji wa mafuta na gesi.

    Aliishauri Serikali kuendelea kutoaufadhili katika fani za mafuta na gesi pamojana masuala ya mazingira kwani shughuliza utafiti na uchimbaji wa gesi na mafutani lazima ziende sambamba na utunzaji wamazingira.

    Naye Yazid Idd ambaye ni mhitimu

    katika chuo hicho aliishukuru Wizara kwaufadhili huo na kuishauri Wizara kupelekawanafunzi kwenye vyuo vingine vinavyotoa

    mafunzo ya mafuta na gesi katika nchinyingine zilizopiga hatua katika sekta hizo.

    Mkurugenzi wa Utawala naUsimamizi wa Rasilimaliwatu,Wizara ya Nishati na MadiniMrimia Mchomvu, ( wa pilikutoka kushoto) MkurugenziMsaidizi – Utumishi, Wizaraya Nishati na Madini LuciusMwenda ( wa pili kutoka kulia)wakiwa katika picha ya pamojana baadhi ya wanafunziwaliowahi kufadhiliwa naWizara kwa ajili ya kusomeaShahada ya Uzamili katikamusuala ya gesi katika vyuovya China.

  • 8/20/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 76

    6/9

    6   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Jacqueline Mattowo

    STAMIGOLD

    K ampuni ya STAMIGOLDambayo ni kampuni tanzuya Shirika la Madini la Taifa(STAMICO) imetimizamwaka mmoja wa

    uchimbaji dhahabu katika mgodi wake waBiharamulo uliopo wilayani BiharamuloMkoa wa Kagera ambapo kiasi cha wakia16,388 za dhahabu zimekwisha zalishwatangu uchimbaji dhahabu ulipoanza rasmimnamo mwezi Julai mwaka 2014 na jumla ya wakia 12,923 za dhahabu zenye

    thamani ya Dola za Kimarekani Milioni15.6 zimeuzwa kwenye soko la kimataifa.

    Kiasi hicho cha dhahabu kilipatikanakatika maeneo ya West Zone na Mojamojatakribani kilomita tatu na nusu kutoka uziowa mgodi ambapo uchimbaji wa dhahabu bado unaendelea. Maeneo hayo mapyayalikabidhiwa STAMICO kutoka mgodiwa Tulawaka uliokuwa ukimilikiwa nakampuni ya African Barrick Gold sasaACACIA mwishoni mwa mwaka 2013.

      Akizungumza katika hafla yakusherehekea mwaka mmoja tangukuanza kwa shughuli za uchimbaji wadhahabu iliyofanyika mwishoni mwa juma katika mgodi wa Biharamulo,Meneja Mkuu wa mgodi wa Biharamulo,Mhandisi Dennis Sebugwao alieleza kuwamatarajio ya mgodi ni kutafuta namna

    ya kuhakikisha uzalishaji wa dhahabuunaendelea kwa kiwango kikubwa nagharama nafuu ili kusaidia kukuza uchumiwa nchi na kuongeza nafasi za ajira kwaWatanzania kwa ajili ya maslahi ya Taifazima.

    “Siwezi kuficha furaha yangu, sikuya leo ni siku ya muhimu kwetu sotekatika historia ya Mgodi huu kwanitunathibitisha kwa Serikali na Watanzania

    wenzetu kuwa, Watanzania wasomina wenye taaluma mbalimbali katikasekta ya uchimbaji na uzalishaji wadhahabu wameendelea kuonyeshauwezo wao kwa kuhakikisha uzalishajiunaendelea kufanyika katika mgodi waSTAMIGOLD Biharamulo bila kuwepowataalam wa kigeni kama ilivyokuwaikiaminiwa.” alieleza Sebugwao.

    Mhandisi Sebugwao pia alielezeamafanikio yaliyofikiwa na mgodi ndaniya mwaka mmoja ambayo ni pamojana mgodi kuendeshwa kwa kufuatataratibu za usalama na afya kazini, ulinziimara ndani na nje ya mgodi, kupunguza

    gharama za uendeshaji wa mgodi,kulipa ushuru wa huduma wa 0.3% yamauzo kwa Halmashauri ya Wilaya yaBiharamulo kiasi cha Shillingi milioni 40.9mpaka June 2015, kuajiri wafanyakaziwa Kitanzania 340 wa fani mbalimbali zakitaalamu, ajira za muda mfupi 43 kwawakazi wa vijiji vilivyo jirani na mgodi nawakandarasi wa Kitanzania 281.

    Aliongeza kuwa mgodi umekuwaukizisaidia jamii zilizo jirani na mgodikupunguza changamoto mbalimbalizinazowakabili ikiwa ni pamoja nakugawa madawati 1500 kwa shule zenyeupungufu katika Wilaya za Biharamulo,Muleba na Ngara, ujenzi wa choo chawanafunzi Shule ya Msingi Mavota,ukamilishaji wa ujenzi wa madarasamanne Shule ya Msingi Mpago, ukarabati

    wa miundo mbinu pamoja kuwawezeshawananchi kiuchumi kupitia vikundi vitatuvya ujasiriamali kwa kununua vyakulavya asili, mbogamboga na matundawanayozalisha.

    Kwa upande mwingine, katikakusherehekea siku hiyo shamrashamrambalimbali zilifanyika ikiwemo mpira wamiguu na mpira wa kikapu ambapo timuya mgodi ya mpira wa miguu ilichezamechi ya kirafiki na timu iliyoundwa nawachezaji kutoka vijiji vya Mavota naMkunkwa na timu ya mgodi kuibukakidedea kwa bao 2-0. Baada ya michezokumalizika timu zote za mpira wa miguu

    zilikabidhiwa zawadi na Meneja Mkuu wamgodi.

    Katika kuhitimisha sherehe hizozilitolewa zawadi na vyeti kwa wafanyakazi10 ambao walifanya vizuri katika Idarazao kwa kipindi cha mwaka mmoja wauzalishaji ambao pia walipatiwa heshimaya kushiriki na Meneja Mkuu wa mgodikukata keki ya kutimiza mwaka mmojawa uzalishaji.

    Wakati huo huo, Mkurugenzi waRasilimali Watu na Utawala kutokaSTAMICO Deusdedith Magala,aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji waShirika hilo Mhandisi Edwin Ngonyani,aliupongeza uongozi na wafanyakazi wamgodi kwa kazi nzuri ambayo inaendelea

    kufanyika na kusema kuwa mafanikioyanayopatikana ni sifa kwa Shirika naTaifa kwa ujumla kwani tayari mgodiumethibitisha uwezo wa Watanzaniakuzalisha dhahabu bila kuongozwa nawataalam wa kigeni.

    “ Nimefurahishwa sana na mafanikiomliyofikia pamoja na namna wafanyakaziwanavyojituma baada ya kutembeleamaeneo mbalimbali hapa mgodini nakujionea kazi zinavyofanyika naombamuendelee na bidii hiyo na vile vile mjitahidikuongeza zaidi njia za mawasiliano zakutangaza mafanikio ya mgodi huu mfanomisaada inayotolewa katika jamii ili duniana taifa kwa ujumla kufahamu kuwaipo kampuni ya Kitanzania inayochimbadhahabu kwa manufaa ya Taifa zima laTanzania” alifafanua Magala.

    Mbali na mafanikio hayo mgodiwa STAMIGOLD Biharamulo badounakabiliwa na changamoto mbalimbaliambazo ni pamoja na kuyumba kwa bei yadhahabu katika soko la dunia, ufinyu wamtaji wa kuendesha shughuli mbalimbaliza mgodi pamoja na uhaba wa majikutokana na vyanzo vilivyopo kutegemeamsimu wa mvua.

    Kampuni ya STAMIGOLDBiharamulo ilizalisha dhahabu yake yakwanza mnamo mwezi Agosti 2014 nampaka sasa imeendelea kuweka historiakwa kuwa kampuni pekee hapa nchiniinayozalisha dhahabu kwa kusimamiwana kuendeshwa na wataalam waKitanzania pekee.

    Stamigold yatimiza mwaka

    mmoja wa uchimbaji dhahabu.

    Mratibu wa kitengo cha Tehama na Mawasiliano, Belatrix Kasuga akipokea cheti chamfanyakazi bora kutoka kwa Meneja mkuu wa mgodi Mhandisi Dennis Sebugwao (kulia)wakati wa maadhimisho ya mgodi kutimiza mwaka mmoja wa uzalishaji. Pembeni niMeneja Uchimbaji, Mhandisi Abdallah Kwassa aliyeshikilia zawadi tayari kwa kumkabidhi.

    Pichani Keki ya mfanowa mawe ya dhahabuiliyoandaliwa katika haflaya mgodi wa STAMIGOLDBiharamulo kutimiza mwakammoja wa uzalishaji.

  • 8/20/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 76

    7/9

    7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Veronica Simba

    Wakala wa JiolojiaTanzania (GST)imetoa taarifa yake yautendaji kwa kipindicha Serikali ya Awamu

    ya Nne (2005-2015), ambayo pamoja namambo mengine imeainisha mafanikioyaliyopatikana katika nyanja mbalimbali.

    Taarifa hiyo iliyotolewa hivi karibuni,imeainisha mafanikio ya Wakala huokwa kipindi husika katika makundimatatu ambayo ni utekelezaji wa kaziza jiosayansi, kuboresha rasilimaliwatu, vitendea kazi, miundombinuna mazingira yake pamoja na kazi natafiti zilizokamilika na zinazoendeleakutekelezwa.

    Kwa upande wa utekelezaji wa kaziza jiosayansi, Taarifa ya GST imeelezakuwa Ramani mpya 60 za jiolojiazimekamilika na kuchapishwa. Ramanihizi ni muhimu kwani huwezeshakubainisha uwepo wa madini katikaeneo husika.

    Pia, taarifa ilibainisha kuwaukusanyaji wa takwimu za jiofizikiakwa kutumia ndege umefanyika katikaWilaya 35 ambayo ni asilimia 15 yaeneo la nchi. Wilaya hizo ni Dodoma,Bahi, Kongwa, Mpwapwa, Nchemba,Kondoa, Chamwino, Iramba, Manyoni,Ikungi, Mkarama na Singida.

    Wilaya nyingine ni pamoja naIgunga, Babati, Kiteto, Hanang,

    Simanjiro, Mbulu, Moshi, Same,Monduli, Korogwe, Handeni, Kilindi,Bagamoyo, Mvomero, Kilosa, Gairo,

    Mbarali, Chunya, Bukombe, Kahama,Ushirombo, Biharamulo na Mpanda.

    “Takwimu hizi zimeainisha maeneoyenye viashiria mbalimbali vya uwepowa madini, kwa mfano eneo la Misaki,Mpambaa, Sambaru na Londoniambapo ufahamu wa uwepo wa madiniya dhahabu umeongezeka,” taarifaimeeleza na kuongeza kuwa, takwimuhizi zimeonesha ongezeko la uwepowa madini ya graphite huko Merelanimkoani Manyara na katika wilaya zaKilindi na Handeni.

    Imeelezwa kuwa, pamoja nakubaini ongezeko la madini mbalimbali,pia taarifa hizi hubaini mipasukokwenye ardhi hivyo kusaidia kuratibumatetemeko na majanga mengine yaasili.

    Vilevile, uchunguzi wa sampulikwenye maabara umeongezeka kutokasampuli 650 (mwaka 2005) kwamwaka na kufikia jumla ya sampuli4500 hadi 5600 kwa mwaka kwa hivisasa. Imeelezwa kuwa ongezeko hilila sampuli limetokana na kuboreshwakwa vitendea kazi, majibu sahihi yauchunguzi na wafanyakazi kupatiwaelimu na motisha.

    Kuhusu kuboresha rasilimaliwatu, vitendea kazi, miundombinuna mazingira yake, taarifa ya GSTinaonyesha kwamba watumishi wapyawapatao 100 wameajiriwa na mafunzombalimbali ya muda mfupi na mrefuyameendelea kutolewa ndani na njeya nchi. Vilevile, Wakala umeboresha

    vitendea kazi vya maabara, ugani, jiofizikia, uchoraji ramani, ofisi nasamani.

    Aidha, taarifa imeeleza kuwa kwaupande wa kazi zilizofanyika ni pamojana kukamilika kwa jumla ya tafiti 27.Tafiti hizo zilihusu utafutaji wa madini yametali/vito, madini ya viwanda, nishati

    ya jotoardhi, matetemeko ya ardhi,milipuko ya volkano, mmomonyoko waardhi, upatikanaji wa magadi, uchenjuaji

    wa madini, ushauri wa namna bora yautafutaji na uchimbaji wa madini kwawachimbaji wadogo na uhifadhi wamazingira.

    Wakala wa Jiolojia Tanzaniaulianzishwa kama Wakala waSerikali chini ya Wizara ya Nishatina Madini mwaka 2005 na kupewa jukumu la kubainisha maeneo yenyekupatikana madini mbalimbali nchini ilikuhamasisha uwekezaji katika sekta yamadini kwa lengo la kukuza uchumi waTaifa.

    Pia, GST imepewa jukumu la kuratibumajanga asili ya jiolojia (matetemeko yaardhi, milipuko ya volkano, mionzi yaasili kutoka kwenye miamba, kemikaliza sumu zitokazo kwenye miamba na

    udongo, maporomoko ya ardhi) nakutoa ushauri wa namna ya kujikinga nakupunguza athari za majanga hayo.

    Dhima ya GST ni kutoa takwimuna taarifa za jiosayansi za kiwango bora kwa gharama stahiki kwa wadauili kuongeza ufahamu wa rasilimali zamadini, hivyo kuchangia katika lengo laTaifa la kupunguza umaskini, kuongezaufahamu wa majanga ya asili na jinsiya kupunguza athari zake, utunzaji wamazingira, kuboresha usalama wa watuna mali zao.

     

    GST yaeleza mafanikio katika Serikali ya Awamu ya Nne

    Takwimu hizi zimeainisha maeneo yenye viashiriambalimbali vya uwepo wa madini, kwa mfano eneola Misaki, Mpambaa, Sambaru na Londoni ambapo ufahamu wa uwepo wa madini ya dhahabu umeongezeka 

    Watalaam wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) wakifanya utafiti wa Jiolojia katika ukanda waDhahabu wa Lupa(Lupa Gold Field), wilayani Chunya mkoani Mbeya

  • 8/20/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 76

    8/9

    8   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Elimu ya OMCTP kuanza kutolewakwa kutumia gari la matangazo

    Na Zuena Msuya

    Wizara ya Nishati naMadini imeanzishamfumo mpya wausajili wa watejakwa kutumia

    njia ya mtandao ijulikanayo kamaOnline Mining Cadastre TransactinalPortal( OMCTP) utakaowawezeshawaombaji na wamiliki wa leseni zamadini kujisajili kwa njia ya mtandaoili kufahamu na kuhakiki taarifa zaokwa urahisi.

    Kamishna Msaidizi wa Madinianayeshughulikia leseni, John Nayopaamesema utaratibu huo umeanzishwaili kutekeleza agizo la Serikali la kutakaWizara na Taasisi za Serikali kurahishaupatikanaji wa huduma bora karibu na

    wananchi, kupokea malipo ya Serikalikwa njia za kielektroniki ili kudhibitimapato tofauti na ilivyokuwa hapo

    awali.“Mwaka 2000, kitengo cha utoaji

    leseni kilikuwa Dodoma Wakati huomamlaka ya utoaji leseni ilikuwa

    Dar-es-Salaam hali iliyosababishaucheleweshaji wa kutolewa leseni napia mfumo wa utoaji na kuchambua

    leseni ilifanyika kwa mkono”, alisemaNayopa.

    Aliongeza kuwa mfumo huounafanana na ule unaotumiwa naMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)katika malipo ya leseni za magari aumfumo wa kununua luku ambaoutawapunguzia wananchi ugumu wakupata huduma.

    Nayopa alisema mfumo waOMCTP utaongeza uwazi na kasiya utoaji wa leseni za madini,watejawataingiza maombi ya leseni waowenyewe, hivyo kupunguza tatizo lamlundikano wa maombi katika ofisiza madini.

    Vile vile alisema kuwa watejawatapata taarifa za leseni zao kilawakati na kujua wanapotakiwa kufanyamalipo ya leseni au watakapotakiwa

    kutuma taarifa za utendaji kazi piakurahisisha mawasiliano kati yaWizara na wamiliki wa leseni.

    “Awali waombaji wa leseniwalilazimika kwenda katika ofisi zamadini kujaza fomu za maombi,kufyeka mipaka ya eneo wanaloombana kuweka vibao; kisha kumleta Afisamadini ili kukagua eneo linaloombwana hatimaye kwenda kufanya malipoya maombi hayo kwenye ofisi yaMadini,”alisema Nayopa

    Aliongeza kuwa wateja na Serikaliwatakuwa na uhakika na maombiyote yatakayowasilishwa (yakiwamomaombi ya sihia (transfer), kuhuishaleseni n.k.); na pia kuwa na uhakika namalipo yote yatakayofanywa kupitiamfumo wa OMCTP

    Aidha aliongeza kuwa ili kutoaelimu kwa wadau wote wa madiniWizara itatoa mafunzo kuanzia tarehe19 Julai hadi pale itakapomaliza wadau

    wote kwa kuanzia mikoa ya Kanda yaMashariki, Kanda ya Kati,Magharibina Kanda ya Kusini.

  • 8/20/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 76

    9/9

    9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    STAMIGOLD YATIMIZA MWAKAMMOJA WA UCHIMBAJI DHAHABU

    Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandaoya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya ‘Nishati na Madini’ Karibu tuhabarishane na

    tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

    Kampuni ya STAMIGOLD ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imetimiza mwaka mmoja wa uchimbaji dhahabu

    katika mgodi wake wa Biharamulo uliopo wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera ambapo uchimbaji ulianza rasmi mnamo mwezi Julai, 2014. Ndani yakipindi cha mwaka mmoja wa uchimbaji (Julai 2014 – Juni 2015), kiasi cha wakia 16,388 za dhahabu zimekwishazalishwa na jumla ya wakia 12,923 zadhahabu zenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 15.6 zimekwishauzwa kwenye soko la kimataifa.

    Kiasi hicho cha dhahabu kilipatikana katika maeneo ya West Zone na Mojamoja takribani kilomita tatu na nusu kutoka uzio wa mgodi ambapo uchimbajiwa dhahabu bado unaendelea. Maeneo hayo mapya yalikabidhiwa STAMICO kutoka mgodi wa Tulawaka uliokuwa ukimilikiwa na kampuni ya AfricanBarrick Gold sasa ACACIA mwishoni mwa mwaka 2013.

     Akizungumza katika hafla ya kusherehekea mwaka mmoja tangu kuanza kwa shughuli za uchimbaji wa dhahabu iliyofanyika katika mgodi waBiharamulo, Meneja Mkuu wa mgodi wa Biharamulo, Mhandisi Dennis Sebugwao alieleza kuwa matarajio ya mgodi ni kutafuta namna ya kuhakikishauzalishaji wa dhahabu unaendelea kwa kiwango kikubwa na gharama nafuu ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuongeza nafasi za ajira kwa Watanzaniakwa ajili ya maslahi ya Taifa zima.

      “Siwezi kuficha furaha yangu, siku ya leo ni siku ya muhimu kwetu sote katika historia ya Mgodi huu kwani tunathibitisha kwa Serikali na Watanzaniawenzetu kuwa, Watanzania wasomi na wenye taaluma mbalimbali katika sekta ya uchimbaji na uzalishaji wa dhahabu wameendelea kuonyesha uwezowao kwa kuhakikisha uzalishaji unaendelea kufanyika katika mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo bila kuwepo wataalam wa kigeni kama ilivyokuwaikiaminiwa.” alieleza Sebugwao.

    Mhandisi Sebugwao pia alielezea mafanikio yaliyofikiwa na mgodi ndani ya mwaka mmoja ambayo ni pamoja na mgodi kuendeshwa kwa kufuatataratibu za usalama na afya kazini, ulinzi imara ndani na nje ya mgodi, kupunguza gharama za uendeshaji wa mgodi, kulipa ushuru wa huduma wa 0.3%ya mauzo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kiasi cha Shillingi milioni 40.9 mpaka June 2015, kuajiri wafanyakazi wa Kitanzania 340 wa fanimbalimbali za kitaalamu, ajira za muda mfupi 43 kwa wakazi wa vijiji vilivyo jirani na mgodi na wakandarasi wa Kitanzania 281.

    Aliongeza kuwa mgodi umekuwa ukizisaidia jamii zilizo jirani na mgodi kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kugawamadawati 1500 kwa shule zenye upungufu katika Wilaya za Biharamulo, Muleba na Ngara, ujenzi wa choo cha wanafunzi Shule ya Msingi Mavota,ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa manne Shule ya Msingi Mpago, ukarabati wa miundo mbinu pamoja kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia vikundivitatu vya ujasiriamali kwa kununua vyakula vya asili, mbogamboga na matunda wanayozalisha.

    Kwa upande mwingine, katika kusherekea siku hiyo shamrashamra mbalimbali zilifanyika ikiwemo mechi ya mpira wa miguu ambapo timu ya mgodiilicheza mechi ya kirafiki na timu iliyoundwa na wachezaji kutoka vijiji vya Mavota na Mkunkwa na timu ya mgodi kuibuka kidedea kwa bao 2-0. Baada yamichezo kumalizika timu zote za mpira wa miguu zilikabidhiwa zawadi na Meneja Mkuu wa mgodi.

    Katika kuhitimisha sherehe hizo zilitolewa zawadi na vyeti kwa wafanyakazi 10 ambao walifanya vizuri katika Idara zao kwa kipindi cha mwaka mmojawa uzalishaji ambao pia walipatiwa heshima ya kushiriki na Meneja Mkuu wa mgodi kukata keki ya kutimiza mwaka mmoja wa uzalishaji.

    Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka STAMICO Deusdedith Magala, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikahilo Mhandisi Edwin Ngonyani, aliupongeza uongozi na wafanyakazi wa mgodi kwa kazi nzuri ambayo inaendelea kufanyika na kusema kuwa mafanikioyanayopatikana ni sifa kwa Shirika na Taifa kwa ujumla kwani tayari mgodi umethibitisha uwezo wa Watanzania kuzalisha dhahabu bila kuongozwa nawataalam wa kigeni.

    “ Nimefurahishwa sana na mafanikio mliyofikia pamoja na namna wafanyakazi wanavyojituma baada ya kutembelea maeneo mbalimbali hapa mgodinina kujionea kazi zinavyofanyika. Naomba muendelee na bidii hiyo na vile vile mjitahidi kuongeza zaidi njia za mawasiliano za kutangaza mafanikio ya mgodihuu mfano misaada inayotolewa katika jamii ili dunia na taifa kwa ujumla kufahamu kuwa ipo kampuni ya Kitanzania inayochimba dhahabu kwa manufaaya Taifa zima la Tanzania” alifafanua Magala.

    Mbali na mafanikio hayo mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na kuyumba kwa

     bei ya dhahabu katika soko la dunia, ufinyu wa mtaji wa kuendesha shughuli mbalimbali za mgodi pamoja na uhaba wa maji kutokana na vyanzo vilivyopokutegemea msimu wa mvua.

    Kampuni ya STAMIGOLD Biharamulo ilizalisha dhahabu yake ya kwanza mnamo mwezi Agosti 2014 na mpaka sasa imeendelea kuweka historia kwakuwa kampuni pekee hapa nchini inayozalisha dhahabu kwa kusimamiwa na kuendeshwa na wataalam wa Kitanzania pekee.

    Imetolewa na:Kitengo cha Mawasiliano

    STAMIGOLD BiharamuloPlot. No. 417/418

    UN RoadS.L.P 78508

    Dar es Salaam.Email: [email protected] Website: www.staigold.co.tz

    KAMPUNI YA STAMIGOLDMGODI WA BIHARAMULO

    TAARIFA KWA UMMA