35
TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR MAELEKEZO KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA UCHAGUZI WA RAIS WA ZANZIBAR, WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI NA MADIWANI 2015 Kimetolewa na: Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Septemba 2015

TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

  • Upload
    lenhi

  • View
    425

  • Download
    9

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR

MAELEKEZO KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA

UCHAGUZI WA RAIS WA ZANZIBAR, WAJUMBE WA BARAZA LA

WAWAKILISHI NA MADIWANI 2015

Kimetolewa na:

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar

Septemba 2015

Page 2: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

1

MAELEKEZO KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA

SALAMU ZA MKURUGENZI

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar itaendesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 siku ya

Jumapili tarehe 25 Oktoba 2015. Uchaguzi huo utatoa fursa kwa Wazanzibari kumchagua

Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani. Kwa kuwa kazi hiyo

huambatana na mambo mengi sana yanayopaswa kutekelezwa kwa uhakika na kila

atakayekabidhiwa majukumu katika uchaguzi mkuu huo, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar

imeandaa maelekezo yatakayotumiwa kama mwongozo wa kazi hiyo kwa Wasimamizi wa

vituo vya kupigia kura watakaoteuliwa kwa kazi hii.

Madhumuni ya Maelekezo haya ni kuwaongoza Wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura ili

waweze kutekeleza vizuri majukumu yao katika vituo watakavyopangiwa kufanya kazi.

Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura wanashauriwa wayasome maelekezo haya kwa

makini pamoja na Sheria ya Uchaguzi Nambari 11 ya 1984 na Kanuni za Uchaguzi, 2015.

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar itakuwa karibu sana Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura

ili kuufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

MKURUGENZI WA UCHAGUZI

TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR

ZANZIBAR

Page 3: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

2

1. UTEUZI WA WASIMAMIZI VITUO VYA KUPIGIA KURA

Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura, watateuliwa na Msimamizi wa Uchaguzi kwa

mujibu wa Sheria ya Uchaguzi Nam. 11 ya 1984, kifungu cha 63(b) na (c).

Taratibu zifuatazo zitazingatiwa katika uteuzi wa Wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura

na Wasaidizi wao:

i. Kutangaza nafasi ili wenye sifa zinazostahili waombe.

ii. Kuwafanyia usaili waombaji wote wenye sifa.

iii. Kutangaza majina ya waombaji walioteuliwa.

iv. Kutoa nafasi kwa Vyama vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi kutoa pingamizi kama

wanazo katika muda usiozidi siku nne.

v. Kufanya uteuzi rasmi, na watakaoteuliwa wajaze fomu za mkataba wa ajira. Idadi

ya walioteuliwa ilingane na mahitaji.

2. MAJUKUMU YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA

Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura wanateuliwa kwa lengo la kusimamia shughuli

mbalimbali za upigaji kura katika vituo ambavyo wanavisimamia kwa kazi hiyo. Kwa hivyo

ili kulitekeleza jukumu hilo kwa usahihi wanawajibika kufanya mambo yafuatayo katika

kazi zao:-

i. Kuhakikisha katika vituo wamepatiwa vifaa vyote vinavyohusika na upigishaji wa

kura;

ii. Kuhakikisha hali ya amani na utulivu katika kituo;

iii. Kuhakikisha kuwa zoezi la upigaji wa kura katika kituo linaendeshwa kwa kufuata

Sheria za uchaguzi, Kanuni na Sheria nyengine zinazohusiana na uchaguzi.

iv. Kuhakikisha kuwa wapiga kura walioandikishwa katika kituo anachosimamia

wanaopatiwa nafasi ya kupiga kura;

v. Kuhakikisha kwamba kura zilizopigwa katika kituo anachokisimamia zinahesabiwa

kwa njia ya uadilifu na utaratibu sahihi;

vi. Kuhakikisha kuwa anabandika fomu ya matokeo ya kituo baada ya kukamilika kazi

ya kuhesabu kura;

Page 4: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

3

vii. Kuhakikisha kuwa anawasilisha mara moja kwa Msimamizi wa Uchaguzi fomu ya

matokeo ya kura ya kituo alichokisimamia;

viii. Kuhakikisha kuwa mara baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji na kuhesabu kura

anaorodhesha vifaa vyote vilivyobakia katika kituo na kuikabidihi orodha kwa

Msimamizi wa Uchaguzi kwa uthibitisho; na

ix. Atafanya kazi yoyote inayohusiana na shughuli za uchaguzi kama atakavyopangiwa

na Msimamizi wa Uchaguzi.

3. WATENDAJI WA UCHAGUZI NDANI YA VITUO VYA KUPIGIA KURA

Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia kura kitakuwa na

watendaji wafuatao:-

i. Msimamizi wa Kituo (Presiding Officer - PO);

ii. Msimamizi Msaidizi wa Kituo Namba 1 (Polling Assistant 1 – PA1);

iii. Msimamizi Msaidizi wa Kituo Namba 2 (Polling Assistant 2 – PA2).

iv. Mwongozaji wa wapiga kura (Direction Clerk – DC)

4. MSIMAMIZI WA KITUO (PO)

Atakuwa na kazi ya kusimamia shughuli zote za uchaguzi ndani ya kituo. Atakuwa ni

dhamana wa masuala yote yatakayojitokeza na yanayohitajia kutekelezwa ndadi ya kituo

cha kupigia kura. Pamoja na majukumu hayo, Msimamizi wa Kituo atahakikisha kuwa

majina ya wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura la kituo anachokisimamia

yameorodheshwa. Atawajibika kuchunguza kwa uangalifu maelezo (taarifa za mpiga

kura) kwenye shahada yake kujiandikisha ya kujiandikisha.

Kabla ya kutoa maelekezo kwa Wasimamizi Wasaidizi, Msimamizi wa Kituo, anawajibika

kukikagua KIDOLE CHA SHAHADA cha mkono wa kushoto cha mpiga kura ili kupata

uthibitisho kuwa mpiga kura huyo anapiga kura yake mara ya kwanza. Pia atamtaka

mpiga kura huyo kuonyesha mikono yake ili kuwathibithishia mawakala na waangalizi

waliopo kama mpiga kura huyo hajapiga kura. Iwapo alama ya wino itaonesha katika

Page 5: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

4

vidole au katika sehemu nyengine ya mpiga kura huyo, Msimamizi wa Kituo atamtaka

kueleza sababu ya wino huo. Iwapo hakuridhika atampeleka kwa mpiga kura kwa

Msimamizi wa eneo la kupigia kura ambaye ataishughulikia hali hiyo.

Baada ya Msimamizi wa kituo kuridhika na taarifa za mpiga kura katika Daftari la Kudumu

la kituo anachokisimamia, atasoma kwa sauti kubwa kiasi cha kuwa mawakala walioomo

katika kituo waweze kusikia jina la mpiga kura huyo na ataweka alama ya √ (vyema au

tiki) kwenye picha ya mpiga kura ndani ya Daftari la Wapiga Kura kuashiria kuwa mpiga

kura huyo tayari amepiga kura.

5. MSIMAMIZI MSAIDIZI WA KITUO NAM. 1 (PA 1)

Msimamizi Msaidizi wa Kituo Nam. 1 atakuwa na jukumu la kutoa karatasi za kura kwa

wapiga kura waliothibitishwa na Msimamizi wa Kituo. Baada ya mpiga kura kuelekezwa

kwake atafanya mambo yafuatayo:-

i. Atakata kutoka katika kitabu karatasi ya kupigia kura;

ii. Atamuelekeza mpiga kura namna ya kukunja karatasi ya kura yaani, kwanza kwa

mapana, kisha nusu na nusu tena;

iii. Atagonga muhuri wa kituo cha kupigia kura juu ya pande zote mbili za karatasi ya

kura iliyokunjwa kwa namna ambayo muhuri utaweza kuonekana.

iv. Atampa mpiga kura karatasi ya kura na kumwelekeza:-

• Kwenda kwenye Kituturi cha kupigia kura na kuweka alama ya “√” ndani ya

chumba kilichowekwa chini ya picha ya mgombea anayemtaka;

• Baada ya kuweka alama, aikunje karatasi ya kupigia kura na kuitumbukiza

kwenye sanduku la kura ambalo mfuniko wake una rangi inayofanana na rangi

ya karatasi ya kura aliyonayo mkononi.

Endapo Msimamizi Msaidizi wa Kituo Nambari 1 anahisi kuwa mpiga kura huyo anahitaji

kusaidiwa katika kupiga kura, atawasiliana na Msimamizi wa Kituo kabla ya kumpa

karatasi ya kupigia kura.

Page 6: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

5

6. MSIMAMIZI MSAIDIZI WA KITUO NAM. 2 (PA 2)

Msimamizi Msaidizi wa Kituo Nam. 2 atakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa kila mpiga

kura anayemaliza kupiga kura amewekwa alama ya wino usiofutika katika kidole KIDOLE

CHA SHAHADA cha mkono wa kushoto cha mpiga kura. Msaidizi Msimamizi kabla ya

kumpaka wino mpiga kura atahakikisha kuwa mpiga kura huyo anafuta kidole

kinachohitajika kuwekwa wino usiofutika ili kuondoa kitu kitakachozuia wino kufika katika

sehemu za kidole zinazokusudiwa.

7. MWONGOZAJI WA WAPIGA KURA (DC)

Katika kila eneo la kupigia kura kutakuwa na waongozaji wa wapiga kura kulingana na

idadi ya vituo vya kupigia kura vilivyopo katika eneo husika. Kazi ya waongoza wapiga

kura katika eneo la kupigia kura ni kuwaelekeza wapiga kura katika vyumba ambavyo

wanastahiki kupiga kura na kujipanga katika mistari kulingana na wingi wa wapiga kura

watakaokuwepo vituoni.

Vile vile, atawajibika kuwasaidia wapiga kura ambao ni walemavu, akinamama

wajawazito, wagonjwa, wazee, ili waweze kupewa kipaumbele cha kupiga kura mapema

kama ambavyo atakuwa ameelekezwa na Tume ya Uchaguzi. Atashirikiana pia na

watendaji wa kituo na mlinzi wa kituo katika kufanikisha shughuli za upigaji kura katika

kituo alichopangiwa. Kwa kila kituo cha kupigia kura katika eneo la kupigia kura kutakuwa

na mwongozaji mistari mmoja.

8. MSIMAMIZI WA ENEO LA KUPIGIA KURA

Katika kila eneo la kupigia kura (Polling Centre) Msimamizi wa Uchaguzi atateua mtu

mmoja kuwa Msimamizi wa eneo la kupigia kura. Msimamizi wa eneo la kupigia kura,

atakuwa na kazi ya kuwasaidia Wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura vilivyomo katika

eneo kuyapatia ufumbuzi wa haraka matatizo yote ambayo yanatokea katika vituo vya

kupigia kura vya eneo analolisimamia. Msimamizi Msaidizi eneo atakuwa ni kiungo kati ya

Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura vya eneo analolisimamia na Msimamizi wa

Page 7: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

6

Uchaguzi wa Jimbo.

Katika utendaji wake wa kazi atakuwa akimpatia Msimamizi wa Jimbo taarifa zote

kuhusiana na kazi ya upigishaji kura katika eneo analolisimamia ikiwemo namna

alivyosaidiana na Msimamizi/Wasimamizi wa Vituo kusawazisha matatizo/ upungufu wa

vifaa katika vituo anavyovisimamia, hali ya upigaji wa kura, mahudhurio ya wapiga kura,

usalama na utulivu wa eneo la kupigia kura kwa ujumla wake.

9. VIFAA VYA KITUO CHA KUPIGIA KURA

Kila Msimamizi wa Kituo cha Kupigia Kura atakabidhiwa vifaa ili aweze kutekeleza

majukumu yake ya kupigisha kura katika kituo cha kupigia kura kwa ufanisi. Msimamizi

wa Kituo ni lazima ahakikishe kuwa anayaelewa na kuyazingatia maelekezo yote

atakayopewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo juu ya matumizi ya vifaa hivyo katika

kituo cha kupigia kura. Hivyo, ni jukumu lake pia kuhakikisha kuwa anapatiwa vifaa vya

kutosha vinavyohitajika katika kituo cha kupigia kura. Msimamizi wa kituo atakabidhiwa

vifaa hivyo na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo kwa maandishi. Vifaa hivyo ni

vifuatavyo:-

Vifaa vinavyohitajika kutumiwa na Wasimamizi Wasaidizi wa vituo vya kupigia kura ni:-

Nam. Vifaa Matumizi

1. Masanduku ya kupigia kura

Masanduku yenye mifuniko

myeupe

Hutumika kwa kupigia kura kwa

uchaguzi wa Rais

Masanduku yenye mifuniko myeusi Hutumika kwa kupigia kura kwa

uchaguzi wa Diwani

Masanduku yenye mifuniko ya

buluu

Hutumika kwa kupigia kura kwa

uchaguzi wa Mwakilishi

2. Vitabu vya Karatasi za kura

Page 8: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

7

Nam. Vifaa Matumizi

Vitabu vya Karatasi za Kura

ambavyo karatasi zake kwa nyuma

zitakuwa na mistari myeupe na

waridi.

Hutumika kumpigia kura Mgombea

Urais.

Vitabu vya Karatasi za Kura

ambavyo karatasi zake kwa nyuma

zitakuwa na mistari myeupe na

buluu.

Hutumika kumpigia kura Mgombea

Uwakilishi.

Vitabu vya Karatasi za Kura

ambavyo karatasi zake kwa nyuma

zitakuwa na mistari myeupe na

myeusi.

Hutumika kumpigia kura Mgombea

Udiwani.

3. Muhuri wa Kituo Hutumika kugonga nyuma ya karatasi

ya kura kabla kukabidhiwa mpiga kura.

Pia hutumika katika nyaraka nyengine

zinazotumika kituoni.

4. Wino usiofutika Hutumika kumpaka mpiga kura kwenye

kidole cha shahada cha mkono wa

kushoto baada ya kumaliza kupiga kura.

5. Daftari la Kudumu la Wapiga

Kura wa kituo cha kupigia kura

Hutumika kuthibitisha wapiga kura

wanaostahiki kupiga kura katika kituo

anachokisimamia kwa kulinganisha na

taarifa za mpiga kura zilizomo katika

shahada yake ya kupigia kura.

6. Kibati cha wino wa muhuri Hutumika kwa ajili ya muhuri wa kituo

7. Bahasha za Kituo Hutumika kuhifadhia vifaa na nyaraka

mbalimbali zinazotumika katika kituo

cha kupigia kura

Page 9: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

8

Nam. Vifaa Matumizi

8.

Vifungio vya plastiki vya kufungia masanduku

Vifungio vya Rangi Nyeupe Kufungia sanduku la Kura la Urais

Vifungio vya Rangi ya Buluu Kufungia sanduku la Kura la Uwakilishi

Vifungio vya Rangi Nyeusi Kufungia sanduku la Kura la Udiwani

Vifungio vya Rangi Nyekundu Kufungia sanduku la vifaa vya Kura

ANGALIZO

Vifungio vya plastiki vya kufungia masanduku ya kupigia kura (seals)

hutumika kufungia masanduku ya kura kabla ya kuanza kazi ya kupiga kura

na baada ya kukamilika kazi ya kuhesabu kura kituoni.

10. Utepe wa gundi (Cellotape) Hutumika kwa kubandikia au kufungia

vitu mbalimbali kituoni

11. Karatasi za kukaushia

(Tissues)

Hutumika kwa ajili ya kusafishia mikono

ya wapiga kura au kaushia wino.

12. Mkasi Hutumika kwa kukatia vifungio vya

masanduku (seals)

13. Karatasi za kuandikia Hutumika kwa kuandikia kumbukumbu

za matukio yanayojitokeza katika kituo

cha kupigia kura.

14. Kalamu Hutumika kwa kiandikia taarifa

mbalimbali za kituo cha kupigia kura.

Vile vile hutumika kwa kupigia kura

15.a Bango la Kituo cha Kupigia

Kura

Hutumika kutambulisha kituo cha

kupigia kura na linatakiwa libandikwe

nje ya kituo kabla ya kituo kufunguliwa

15.b Bango la Kituo cha Kuhesabia

Kura

Hutumika kutambulisha kituo cha

kuhesabia kura na linatakiwa libandikwe

nje ya kituo kabla ya kuanza kuhesabu

kura

Page 10: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

9

Nam. Vifaa Matumizi

16. Mistari (Rulers) Hutumika kwa matumizi mbalimbali ya

kituo ikiwa ni pamoja na kufuatilia kwa

usahihi majina ya wapiga kura katika

Daftari la Kudumu la wapiga kura la

kituo.

Pia hutumika kwa kuchania karatasi za

kura.

17. Karatasi za kura za mfano kwa

wagombea Urais, Uwakilishi na

Udiwani

Hutumika kuwatambulisha wagombea

kwa kuonyesha majina yao, picha na

nembo za vyama vyao.

18. Taa na Betri zake Hutumika katika kituo cha kupigia na

kuhesabia kura inapotokezea haja ya

matumizi yake.

19. “Tactile Ballot Papers

Template”

Rais, Mwakilishi na Diwani

Hutumika kuwawezesha wapiga kura

wasioona kupiga kura bila ya kusaidiwa.

20. Vituturi (Polling Booths) Hutumika kwa ajili ya kuandaa sehemu

ya faragha ili kumwezesha wapiga kura

kupiga kura zao kwa siri kituoni

21. Kitabu cha Fomu mbalimbali za Kituo cha kupigia kura ambacho

ndani yake mna fomu zifuatazo:-

i. Kumbukumbu ya mahudhurio ya

Msimamizi na Wasaidizi

Wasimamizi wa kituo cha kupigia

kura Nam. PS 2

Hutumika kwa ajili ya kuchukua taarifa

za Msimamizi na Wasaidizi Wasimamizi

wa kituo cha kupigia kura wanapowasili

kituoni na wanapoondoka kituoni baada

ya kuhesabiwa kwa kura

ii. Shahada ya kufungua kituo cha

kupigia kura Nam. PS 3

Hutumika kuthibitisha muda ambao

kituo cha kupigia kura kimefunguliwa

Page 11: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

10

Nam. Vifaa Matumizi

iii. Shahada ya kufunga kituo Nam. PS

8

Hutumika kwa uthibitisho wa kufunga

kituo cha kuhesabia kura

iv. Kumbukumbu ya Vifungio vya

masanduku na mihuri ya kituo

iliyopokelewa Nam. PS 4

Hutumika kuthibitisha idadi ya vifungio

vya masanduku ya kura vilivyopokelewa

katika kituo cha kupigia kura

v. Kumbukumbu ya vifungio

vilivyotumika (Vilivyowekwa na

kuondolewa katika sanduku la kura

la):-

o Urais Fomu Nam. PS 5A

o Uwakilishi Fomu Nam. PS 5B

o Udiwani Fomu Nam. PS 5C

Ni kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya

vifuniko vinavyotumika kwa ajili

kufunga na kufungua masanduku ya

wagombea Urais, Uwakilishi na Udiwani

katika kituo cha kupigia kura

vi. Hesabu ya Karatasi za Kura vituoni

kwa:-

o Urais Nam. PS 7A

o Uwakilishi Nam. PS 7B

o Udiwani Nam. PS 7C

Ni kwa ajili ya kuwekea kumbukumbu

ya hesabu ya karatasi za kura

zilizopokelewa na zilizotumika katika

kituo cha kupigia kura kwa Urais,

Uwakilishi na Udiwani

vii. Taarifa ya Kura za kila mgombea

baada ya hesabu ya kituo kwa:-

o Urais Fomu Nam. PS 12A

o Uwakilishi Fomu Nam. PS 22B

o Udiwani Fomu Nam. PS 32C

Hutumika kuchukulia matokeo ya kura

za wagombea ya kituo kimoja kimoja

katika jimbo kwa wagombea wa Urais,

Uwakilishi na Udiwani

viii. Orodha ya Wapiga Kura

waliosaidiwa kupiga kura Fomu

Nam. PS 6

Hutumika kuweka kumbukumbu ya

watu waliosaidiwa kupiga kura na watu

waliofuatana nao

ix. Shahada ya kufungua kituo cha

kuhesabia kura Fomu Nam. PS 9

Hutumiwa kuwekea kumbukumbu kwa

Uthibitisho wa kufungua kituo cha

kuhesabia kura

Page 12: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

11

Nam. Vifaa Matumizi

x. Shahada ya kufunga kituo cha

kuhesabia kura Fomu Nam. PS 10

Hutumiwa kuwekea kumbukumbu kwa

Uthibitisho wa kufunga kituo cha

kuhesabia kura

23. Bahasha mbali mbali za kituo cha kupigia kura

i. Bahasha Nam. 2A, 2B na 2C Hutumika kuhifadhia vishina vya vitabu

vya Karatasi za kura zilizotumika.

- 2A kwa Uchaguzi wa Rais

- 2B kwa uchaguzi wa Mwakilishi

- 2C kwa Uchaguzi wa Diwani

ii. Bahasha Nam. 3A, 3B na 3C Hutumika kuhifadhia vishina vya

Karatasi za kura ambazo hazikutumika

pamoja na zilizoharibika.

- 3A kwa Uchaguzi wa Rais

- 3B kwa uchaguzi wa Mwakilishi

- 3C kwa Uchaguzi wa Diwani

iii. Bahasha Nam. 4 Hutumika kuhifadhia Daftari la Kudumu

la Wapiga Kura, shahada za Watumishi

wa Uchaguzi na shahada maalum

iv. Bahasha Nam. 5A, 5B na 5C Hutumika kuhifadhia kura zenye

mgogoro kama zitakuwepo.

- 5A kwa Uchaguzi wa Rais

- 5B kwa uchaguzi wa Mwakilishi

- 5C kwa Uchaguzi wa Diwani

v. Bahasha Nam. 6A, 6B na 6C Hutumika kuhifadhia kura zilizokataliwa

kama zitakuwepo.

- 6A kwa Uchaguzi wa Rais

- 6B kwa uchaguzi wa Mwakilishi

- 6C kwa Uchaguzi wa Diwani

Page 13: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

12

Nam. Vifaa Matumizi

vi. Bahasha Nam. 7A, 7B na 7C Hutumika kuhifadhia Kura halali za

wagombea.

- 7A kwa Uchaguzi wa Rais

- 7B kwa Uchaguzi wa Mwakilishi

- 7C kwa Uchaguzi wa Diwani

Angalizo:

Vifaa vifuatavyo vitatakiwa viorodheshwe baada ya kukamilika kwa kazi ya kuhesabu kura

na akabidhiwe Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo. Hivyo ni vyema kukawa na umakini wa

hali ya juu katika utunzwaji wake. Vifaa hivyo ni vifuatavyo:-

i. Masanduku ya Kura;

ii. Karatasi za Kura;

iii. Fomu za malalamiko;

iv. Fomu za matokeo ya Uchaguzi;

v. Mihuri ya Kituo;

vi. Uniform za watendaji (Vikoti);

vii. Taa;

viii. Kitabu cha fomu mbalimbali

10. MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA SIKU YA KUPIGA KURA

Siku ya kupiga kura, kituo cha kupigia kura huwa na kazi nyingi ambazo zinahitajia

kufanywa mapema sana na kwa wakati ili kuuwezesha upigaji kura katika kituo kufanyika

kwa ufanisi. Hivyo, kabla ya siku ya kupiga kura, Msimamizi wa Kituo anawajibika

kutekeleza mambo muhimu yafuatayo:-

i. Kuhakikisha kwamba amekabidhiwa vifaa vyote vya kupigia kura vinavyohitajika kwa

kituo alichopangiwa kusimamia upigishaji wa kura na kuvihakiki kama inavyojionesha

Fomu maalum iliyowekwa katika kitabu cha Fomu mbalimbali.

ii. Kuhakikisha kuwa amepatiwa kitabu cha fomu mbalimbali za kituo cha kupigia kura.

Page 14: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

13

iii. Kuhakikisha kuwa amezipanga vizuri fomu zote zinazohitajia kujazwa na wahusika

(mawakala) kabla ya kuanza kwa kazi ya upigaji wa kura.

iv. Kuhakikisha kuwa anavitunza vifaa vyote alivyokabidhiwa katika sehemu salama hadi

siku ya upigaji wa kura.

v. Kuhakikisha kuwa amepatiwa majina ya mawakala watakaokuwemo katika kituo cha

wapiga kura kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi.

vi. Kuhakikisha kuwa kuna utaratibu utakaomwezesha kila Msimamizi Msaidizi wa Kituo

chake kufika kituoni na kuondoka kwa wakati baada ya kukamilika kwa kazi ya

kuhesabu kura.

Baada ya kuwa amepanga vizuri utaratibu mzima wa shughuli ya upigaji kura katika kituo,

Msimamizi wa kituo kabla ya kuanza upigishaji wa kura atampatia kila wakala ambaye

atakuwa kituoni Fomu Nam. PS 03 ili ajaze kuonyesha kuridhika au kutoridhika kwake na

maandalizi ya kituo cha kupigia kura. Wakala atatakiwa kutoa sababu iwapo hataridhika

na maandalizi ya kituo. Msimamizi wa kituo atapaswa kuonyesha jinsi alivyoyashughulikia

malalamiko hayo kama yapo.

Angalizo:

Kwa kuwa nafasi iliyopo katika fomu hii ni ndogo mno kutoa maelezo mengi, tumia nafasi

iliyowekwa katika kitabu cha fomu mbalimbali kujaza sababu za kutoridhika kwa wakala

na matayarisho ya kituo. Katika karatasi hiyo ya ziada ataandika jina lake, chama chake

na kuweka saini yake.

11. DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Kila kituo cha kupigia kura kitakuwa na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la kituo lenye

orodha ya wapiga kura wote wanaostahiki kupiga kura katika kituo hicho. Ni Daftari la

kudumu la wapiga kura lililotayarishwa na Tume pekee ndilo linalopaswa kutumika kwa

shughuli za upigishaji wa kura kituoni. Mawakala wa upigaji kura wameruhusika kuingia

na Daftari la wapiga kura katika kituo cha kupigia kura.

Page 15: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

14

12. UPANGAJI WA KITUO CHA KUPIGIA KURA

Vituo vya kupigia kura hupangwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kushauriana na

Msimamizi wa Uchaguzi. Katika kupanga kituo cha kupigia kura Msimamizi wa Kituo

anapaswa kuzingatia mambo yafuatayo:-

i. Kupanga meza ya Msimamizi wa Kituo kumwezesha kuangalia majina ya wapiga

kura katika Daftari la wapiga kura wakati wanapofika kituoni bila ya matatizo.

ii. Kupanga meza ya Msimamizi Msaidizi wa Kituo Nambari 1 ambaye atakuwa na

jukumu la kutoa na kupiga muhuri karatasi za kura.

iii. Kupanga meza ya Msimamizi Msaidizi wa kituo Nambari 2 ambaye atakuwa na kazi

ya kupaka wino usiofutika kwa wapiga kura wanapomaliza kutumbukiza kura

katika masanduku ya kupigia kura.

iv. Kupanga sehemu ya faragha ambayo itatumika kuweka kituturi kwa ajili ya kupiga

kura.

v. Kuandaa sehemu nzuri ya wazi ndani ya kituo kwa ajili ya kuweka sanduku la kura

na

vi. Kupanga sehemu maalum kwa ajili ya Mawakala/ Wagombea na Waangalizi wa

upigaji kura.

Page 16: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

15

Mchoro wa Kituo cha Kupigia Kura

ANGALIZO

Kumbuka kuwa mtu yeyote ambaye ameandikishwa kuwa mpiga kura katika Daftari la

Kudumu la wapiga kura, atakuwa na haki ya kupiga kura katika kituo alichopangiwa na

Tume kupiga kura yake. Aidha, mtu yeyote ambaye jina lake halimo katika Daftari la

Wapiga kura la kituo hata kama anayo shahada ya kupigia kura hataruhusiwa kupiga kura

katika kituo atakachoomba kupiga kura.

13. UTHIBITISHO WA MPIGA KURA

Kila anayefika kituoni kwa ajili ya kupiga kura, atalazimika kuonesha shahada yake ya

kupigia kura kwa Msimamizi wa Kituo. Msimamizi wa Kituo baada ya kuthibitisha kuwa

Page 17: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

16

taarifa za mpiga kura huyo zimo katika Daftari la wapiga kura na hajapiga kura,

atamruhusu mtu huyo kuendelea na taratibu za kupiga kura.

14. USAMBAZAJI ZA KARATASI ZA KURA

Tume itakabidhi karatasi zote za kura kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ambaye

kwa kusaidiana na Msimamizi wa Jimbo watazigawa kwa Wasimamizi wa Vituo Vya

Kupigia Kura katika majimbo yao. Wakati wa kupokea karatasi za kura za kituo, Msimamizi

wa Kituo atalazimika kujaza Fomu Nam. PS 7A kwa karatasi za kura za wagombea Urais,

Fomu Nam. PS 7B kwa karatasi za kura za wagombea Uwakilishi na Fomu Nam. PS 7C

kwa karatasi za kura za wagombea Udiwani. Anatakiwa kunukuu kwa usahihi nambari za

karatasi za kura katika kila hatua kama inavyoonyeshwa katika fomu hizo.

Wakati upigaji kura unaendelea, Msimamizi wa Kituo atakuwa akitoa kitabu cha karatasi

za kura kimoja baada ya chengine kulingana na mahitaji ya Msaidizi Msimamizi wa Kituo

Nambari 1 ambaye ndiye dhamana wa kutoa karatasi hizo kwa wapiga kura. Msimamizi

Msaidizi wa Kituo Nambari 1 akishatoa karatasi ya mwisho ya kura kutoka kwenye kitabu

alichopewa, atamkabidhi Msimamizi wa Kituo vishina vya kitabu kilichokwishatumika ili

akabidhiwe kitabu chengine cha karatasi za kura.Utaratibu huo utaendelea mpaka

kumalizika kwa kazi ya upigishaji wa kura.

15. KUFUNGUA KITUO CHA KUPIGIA KURA

Kituo cha kupigia kura ni msingi wa kazi ya uchaguzi. Ili kazi ya kupiga kura ifanyike kwa

ufanisi mkubwa ni vyema kukawa na maandalizi mazuri. Hivyo, kabla ya kufungua kituo

cha kupigia kura, Msimamizi wa Kituo atafanya mambo yafuatayo:-

i. Atahakikisha usalama wa kituo.

ii. Atatoa maelezo kwa mawakala na wapiga kura waliokuwepo kuhusu utaratibu

mzima wa upigaji wa kura kituoni.

iii. Atajaza fomu zote zinazohusiana na kufungua kituo.

iv. Atawaonyesha Mawakala na watu waliopo kituoni masanduku ya kura

Page 18: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

17

yaliyoondolewa mifuniko kuthibitisha kuwa ndani ya masanduku ya kura hamna

kitu (matupu).

v. Atalifunga sanduku la kura katika sehemu zake zote kwa kutumia vifungio vya

plastiki, isipokuwa ataacha wazi sehemu ya kuingizia kura.

vi. Ataanza upigishaji kura Saa moja kamili asubuhi.

vii. Ataifunga sehemu ya kuingizia kura kwa kifungio cha plastiki mara baada ya mtu

wa mwisho kumaliza kupiga kura yake.

Michoro iliyoainishwa chini inaonyesha hatua muhimu za kuzingatiwa wakati wa kufunga

sanduku la kura

Mchoro juu ya Ufungaji wa Sanduku la Kura

Page 19: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

18

ANGALIZO

Tahadhari LAZIMA ichukuliwe kuhakikisha kuwa vifungio vinatumika kwa uangalifu kwa

kuwa kila kituo cha kupigia kura hupewa idadi inayotosha ya vifungio kwa kazi hiyo na

ziada huwa ni kidogo sana. Sehemu ya kuingizia kura ibaki imefungwa wakati wote hata

kama vifungio vyengine vimetolewa wakati wa kuhesabu kura.

16. WATU WANAORUHUSIWA KUINGIA KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA

Watu wanaoruhusiwa kuwemo katika kituo cha kupigia kura ni hawa wafuatao:-

i. Msimamizi wa Kituo.

ii. Msimamizi Msaidizi wa kituo.

iii. Mawakala wa upigaji kura.

iv. Wagombea.

v. Wapiga kura.

Page 20: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

19

vi. Mtu anayemsaidia mpiga kura anayehitajia msaada ndani ya kituo.

vii. Mwangalizi wa Uchaguzi aliyeruhusiwa na Tume kwa maandishi.

viii. Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.

ix. Mkurugenzi wa Uchaguzi.

x. Askari Polisi na askari wa aina nyengine ikibidi kwa ajili ya kuweka usalama

katika kituo cha upigaji wa kura.

17. KUPANGA MISTARI YA WAPIGA KURA

Wapiga kura watahitajika kujipanga kwa mistari wanapoingia kituoni kupiga kura.

Kutakuwa na mistari miwili ya wapiga kura kwa kuzingatia jinsia, kwa wanawake na

wanaume. Msimamizi wa Kituo cha kupigia kura itambidi ahakikishe kuwa wapiga kura

wanaingia ndani ya kituo cha kupigia kura kwa zamu ili kusitokee mivutano isiyo ya lazima

wakati wa upigaji kura. Mwongozaji wa wapiga kura (DC) ahakikishe kuwa wapiga kura

waliojipanga katika misitari wamejipanga kulingana na vituo vyao vya kupigia kura.

Wasiohusika na kituo anachokisimamia achukue juhudi ya kuwaelekeza vituo sahihi

wanavyostahiki kupiga kura zao.

Msimamizi wa kituo kwa upande wake ahakikishe kuwa anaandaa utaratibu

utakaowawezesha wapiga kura wenye mahitaji maalum (wazee, watu wenye ulemavu,

wagonjwa, wajawazito, na wenye watoto wachanga) wanapiga kura bila ya kulazimika

kujipanga katika misitari iliyopo ili kuwaondolea usumbufu kutokana na hali zao. Tume

ya Uchaguzi imewapatia watu wenye ulemavu vitambulisho maalum kwa ajili ya

kuwasaidia kufika katika vituo vya kupigia kura bila ya kupanga mstari. Kitambulisho hicho

kinalazimika kubakia katika kituo cha kupiga kura mara baada ya Mpiga kura kumaliza

kupiga kura yake. Mtu ambaye anamsaidia mpiga kura naye anaruhusiwa kupiga kura

yake wakati huo huo ikiwa anastahiki kupiga kura katika kituo hicho.

Page 21: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

20

18. SIRI YA KURA

Sehemu ya kupigia kura lazima iwekwe kwa namna ambayo hapana mtu awezaye kuona

ndani wakati mpiga kura akiweka alama kwenye karatasi ya kupigia kura. Watu

watakaokuwemo ndani ya kituo wanakatazwa na Sheria kumshawishi mpiga kura juu ya

namna ya kupiga kura yake.

Mpiga kura asiulizwe vipi anavyotaka kupiga kura au vipi amepiga kura. Mpiga kura

anatakiwa aikunje karatasi ya kura kama alivyoelekezwa na Msaidizi Msimamizi wa Kituo

Nambari 1 kiasi cha kuwa mtu yeyote asiione alama iliyotiwa katika karatasi ya kura

wakati atakapotoka sehemu ya kupigia kura.

ANGALIZO

Msimamizi wa Kituo lazima avikague mara kwa mara vituturi vya kupigia kura ili

kuhakikisha kuwa kalamu ya kuwekea alama katika karatasi ya kura ipo mahali

inapotakiwa.

19. WAPIGA KURA WANAOHITAJI MSAADA

Mpiga kura ambaye ameondokewa na uwezo wa kuona au sababu nyengine ya

kimaumbile au asiyejua kusoma na kuandika anaweza kumuomba Msimamizi wa Kituo,

ruhusa ya kusaidiwa kupiga kura na mtu aliyefuatana naye. Mtu huyo anaweza kuwa

baba, mama, kaka, ndugu, dada, mume, mke, mtoto ambaye amefikia umri wa miaka 18

au mtu ambaye ana haki ya kupiga kura kama mpiga kura katika uchaguzi.

Msimamizi wa Kituo, atamruhusu mpiga kura huyo baada ya kuridhika kuwa ombi la

mpiga kura huyo lina uzito. Mtu anayemsaidia mpiga kura, analazimika kuweka alama

katika karatasi ya kupigia kura kulingana na matakwa ya mpiga kura.

Inapotokea mpiga kura hana jamaa, Msimamizi wa Kituo, atamtaka mpiga kura huyo

kuteua mtu wa kumsaidia ambaye anamuamini na ataandika taarifa za mpiga kura na

Page 22: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

21

msaidizi wake kwa kujaza majina yao kwenye Fomu Nam. PS 6 iliyomo katika kitabu cha

fomu mbalimbali za kituo cha kupigia kura na ataruhusu mpiga kura huyo kusaidiwa.

20. WINO USIOFUTIKA

Msimamizi wa Uchaguzi atakipatia kila kituo cha kupigia kura chupa moja ya wino

usiofutika. Kiasi hicho cha wino uliomo kwenye chupa moja kinatosha kuhudumia wapiga

kura 400. Msimamizi wa kituo atatakiwa kuwa mwangalifu katika matumizi ya wino huo

wakati mpiga kura anapopakwa kidoleni kuashiria kuwa amemaliza kupiga kura. Hadhari

lazima ichukuliwe kuhakikisha kuwa hakuna kitu kinachoweza kuzuia wino kuingia na

kuganda katika sehemu zinazohusika. Msaidizi Msimamizi wa Kituo atamtia wino mpiga

kura kwa kukichovya kidole cha shahada cha mkono wa kushoto.

ANGALIZO

Mtu yeyote aliyemsaidia mpiga kura atatakiwa kutiwa wino kidole cha kati cha mkono wa

kushoto ili kuthibitisha kwamba ameshamsaidia mpiga kura. Mtu mmoja anaruhusiwa

kumsaidia mpiga kura mmoja tu.

21. YANAYOKATAZWA SIKU YA UPIGAJI WA KURA

Zoezi la kupiga kura kufanikiwa kwake kunategemea hali ya utulivu kutoka kwa jamii.

Kuhakikisha utulivu unapatikana katika maeneo ya vituo vya kupigia. Wapiga kura

wanakatazwa na Kanuni kufanya mambo yafuatayo wakati wa kupiga kura:-

i. Kupiga kampeni.

ii. Kufanya au kusababisha vurugu.

iii. Kutoa maneno ya uchochezi.

iv. Kubeba silaha ya aina yoyote kwa siri au dhahiri katika maeneo ya kupigia kura.

v. Kuvaa nguo yoyote yenye rangi inayoashiria alama au rangi za chama cha siasa.

vi. Kukaa kituoni bila ya kazi maalum baada ya kumaliza kupiga kura yake.

Page 23: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

22

22. KUAHIRISHA UPIGAJI KURA

Upigaji kura katika kituo unaweza kuahirishwa iwapo umeingiliwa na ghasia au kutokea

kwa maafa ya kimaumbile. Msimamizi wa Kituo cha kupigia kura, anaweza kuahirisha

upigaji kura kwa muda kituoni mpaka hali ya utulivu itakaporejea. Msimamizi wa kituo

atalazimika kumjulisha Msimamizi wa Jimbo haraka juu ya uamuzi huo kwa ajili ya kupata

maelekezo juu ya hatua nyengine madhubuti za kuchukuliwa kukabiliana na hali

iliyotokezea kituoni.

Endapo sababu zilizopelekea kuahirishwa zimechukuwa muda mrefu, Msimamizi wa Kituo

ataahirisha upigaji kura mpaka siku inayofuata na haraka atatoa taarifa hiyo kwa

Msimamizi wa Jimbo. Sababu za uahirishaji lazima ziandikwe kwenye Daftari la

kumbukumbu la kituo cha kupigia kura.

23. MAWASILIANO

Mawasiliano kati ya watendaji wa kituo cha kupigia kura, Msimamizi wa Jimbo na

Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya yana umuhimu mkubwa sana. Kwa hivyo ni vyema

Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya kupatiwa taarifa mara kwa mara kutoka kwa

Msimamizi wa Jimbo. Vile vile Msimamizi wa Jimbo atahitajika kupatiwa taarifa za mara

kwa mara kutoka kwa Msimamizi wa Kituo kupitia kwa Msimamizi wa Eneo la kupigia

kura. Msimamizi wa Eneo la kupigia kura atakuwa akipatiwa taarifa na Msimamizi wa

Kituo cha kupigia kura kila linapotokezea tatizo linalohitajia ufumbuzi kituoni. Msimamizi

wa Kituo kwa upande wake atawasilisha taarifa juu ya tatizo hilo kwa Msimamizi wa Jimbo

ambaye pia atawasilisha taarifa hiyo kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya.

24. KUFUNGA UPIGAJI WA KURA

Kituo cha kupigia kura kitafungwa saa 10.00 za jioni. Hata hivyo, kabla ya muda halisi

wa kufunga kituo, Msimamizi wa Kituo cha kupigia kura itampasa amwamuru Askari Polisi

au Msimamizi Msaidizi wa Kituo, kusimama nyuma ya mtu wa mwisho katika msitari wa

wapiga kura ifikapo saa 10.00 jioni. Upigaji kura kituoni utaendelea mpaka mpiga kura

Page 24: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

23

wa mwisho kutoka kwenye msitari atakapopiga kura yake.

25. UTARATIBU WA KUFUNGA KITUO

Baada ya mpiga kura wa mwisho kupiga kura yake katika kituo, Msimamizi wa Kituo,

atamtaka kila wakala aliyekuwepo katika kituo cha kupigia kura kuweka maelezo katika

Fomu Nam. PS 8 akionyesha kuridhika au kutoridhika na mwenendo wa upigaji wa kura,

iwapo hakuridhika, aelezee sababu za kutoridhika kwake. Msimamizi wa Kituo anatakiwa

kukiri kupokea malalamiko hayo kwa kuweka jina lake na saini yake na wakati wa kupokea

malalamiko hayo. Kukataa kwa wakala kujaza fomu hizo hakutamzuia Msimamizi wa kituo

kuendelea na majukumu mengine.

Baada ya mawakala kukamilisha kujaza Fomu Nam. PS 8, Msimamizi wa kituo atawajibika

kutoa maelezo juu ya mambo mengine ambayo yanafanyika kituoni kabla ya kuhesabiwa

kwa kura. Baada ya taarifa hiyo atafanya mambo yafuatayo:-

i. Ataufunga upenyo wa juu wa sanduku la kura uliokuwa ukitumika kwa kupenyezea

karatasi za kura kwa kutumia vifungio vya sanduku la kura ili mtu yoyote asiweze

kutumbukiza karatasi nyengine ya kura ama kitu chochote kile.

ii. Atamaliza kuandika hesabu ya karatasi za kura kwa kutumia Fomu Nam. 7A, 7B

na 7C alizopatiwa kwa uchaguzi wa Rais, Wawakilishi na Madiwani ambazo zimo

ndani ya kitabu cha fomu mbalimbali za kituo. Ni muhimu sana kujaza hesabu hizi

sawa sawa bila ya kufanya makosa.

iii. Ataviweka vishina vya karatasi za kura zilizotumika ndani ya bahasha zinazohusika

(ambazo ni 2A kwa karatasi za kura za Urais, 2B kwa karatasi za kura za Uwakilishi

na 2C kwa karatasi za kura za Udiwani). Endapo itatokezea kuwa kuna kitabu cha

karatasi za kura ambacho hakikumalizika chote, itabidi avitenganishe vishina vya

karatasi zilizotumika kutoka kwenye kitabu hicho na kuviweka pamoja na vile

vinavyotokana na vitabu vilivyomalizika vyote na kuviweka ndani ya bahasha

kulingana na uchaguzi na baadae kuzifunga.

iv. Ataziweka pamoja karatasi za kura ambazo hazikutumika na zile zilizoharibika na

sehemu ya karatasi zilizokuwa hazikutumika ndani ya bahasha zinazohusika

Page 25: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

24

(bahasha 3A kwa karatasi za kura za Urais, bahasha 3B kwa karatasi za kura za

Uwakilishi na bahasha 3C kwa karatasi za kura za Udiwani.

v. Ataweka ndani ya bahasha Namba 4, Daftari la Kudumu la wapiga kura.

vi. Kwa kila bahasha ya kituo aandike nambari ya sanduku la kura husika. Bahasha

zinazohusika ni kama zifuatazo:-

• Bahasha Nam. 2A, 2B na 2C – Vishina vya Karatasi za Kura zilizotumika

• Bahasha Nam. 3A, 3B na3C – Karatasi za kura ambazo hazikutumika

• Bahasha Nam. 5A, 5B na 5C – Kura zenye mgogoro

• Bahasha Nam. 6A, 6B na 6C – Kura zilizokataliwa

• Bahasha Nam. 7A, 7B na 7C – Kura halali

vii. Avikusanye vifaa vyengine vyote vilivyokuwa vikitumika katika kituo na aviweke

ndani ya bahasha ya kituo (isifungwe) mpaka baada ya kuhesabu kura. Taa na

kichupa cha wino visiwekwe ndani ya bahasha. Bahasha ya kituo isiwekwe ndani

ya sanduku la kura.

ANGALIZO

Msimamizi wa kituo anawajibika kufanya shughuli zote hizo kwa kushuhudiwa na

mawakala wa upigaji kura ama wagombea. Kutokuwepo kwa watu hao hakuzuii shughuli

hiyo kufanyika kwa utaratibu ulioelezwa hapo juu. Aidha, ahakikishe kuwa fomu za

matokeo na kura zenye mgogoro haziingizi ndani ya sanduku la kura.

26. KUHESABU KURA

Kura kwa kawaida zinahesabiwa katika vituo vya kupigia kura. Hivyo, mara baada ya

kukamilika kwa kazi ya upigaji kura na kituo hicho kufungwa rasmi kwa kazi hiyo, kituo

hicho kinabadilika na kuwa kituo cha kuhesabia kura. Msimamizi wa Kituo, atawatangazia

watu wanaoruhusiwa kuwemo ndani ya kituo juu ya mabadiliko ya kituo (kutoka Kituo

cha Kupigia Kura na kuwa Kituo cha Kuhesabia Kura); na kuwaeleza utaratibu

utakaotumika katika kuhesabu kura.

Page 26: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

25

27. WANAORUHUSIWA KUWEMO WAKATI WA KUHESABU KURA

Watu wanaoruhusiwa kuwemo katika kituo cha kuhesabu kura ni hawa wafuatao:-

i. Msimamizi wa kituo

ii. Msimamizi Msaidizi wa kituo

iii. Wakala wa kupiga kura au kuhesabu kura

iv. Mgombea

v. Mjumbe wa Tume

vi. Msimamizi wa Uchaguzi

vii. Afisa wa Uchaguzi

viii. Mwangalizi aliyeruhusiwa na Tume kwa maandishi na

ix. Afisa wa Polisi au mtu mwengine mwenye dhamana ya ulinzi katika sehemu

ambayo kura zinahesabiwa

28. MAMBO YA KUZINGATIWA WAKATI WA KUHESABU KURA

Msimamizi wa Kituo na wasaidizi wake ndio watakaohesabu kura mbele ya watu wote

walioruhusiwa kisheria kuwepo kituoni wakati wa kuhesabu kura. Katika kuifanya kazi

hiyo, Msimamizi wa Kituo anawajibika na mambo yafuatayo:-

i. Kuhakikisha kuwa baada ya kazi ya upigishaji kura kukamilika na kufungwa kituo

wanafanya maandalizi kwa ajili ya kuhesabu kura.

ii. Kuhakikisha kuwa kabla ya kuhesabu kura wagombea au mawakala wa kuhesabu

wa kura wanaeleza kuridhika au kutoridhika na maandalizi ya kituo cha kuhesabu

kura kwa kujaza maelezo yao katika Fomu Nam. PS 9. Msimamizi wa kituo

ataelezea kwa maandishi malamiko yaliyotolewa na jinsi alivyoyashughulikia.

29. UTARATIBU WA KUHESABU KURA

Kazi ya kuhesabu kura itafanywa kwa mpangilio ufuatao:-

i. Atakata vifungio vya masanduku ya kura akianzia na sanduku la kura la wagombea

Urais, baadae zitafuata kura za wagombea Uwakilishi na hatimaye kura za

Page 27: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

26

wagombea Udiwani.

ii. Atamimina kura zote juu ya meza ama katika sehemu maalum iliyoandaliwa kwa

ajili ya kazi ya kuhesabu kura.

iii. Atahesabu kura moja baada ya nyengine kwa sauti ili kujua idadi ya kura zilizomo

katika sanduku la kupigia kura.

iv. Atandaka katika buku la kumbukumbu (Note book) idadi ya kura zote zilizopatikana

katika kila sanduku la kura.

v. Atahakikisha kuwa idadi ya kura katika sanduku la kura inalingana na idadi ya watu

wote waliopiga kura kituoni hapo.

vi. Baada ya idadi ya kura zote katika sanduku kujulikana, Msimamizi wa kituo

atakunjua kura moja baada ya nyengine kwa kuonyesha upande wenye picha za

wagombea na atatangaza kwa sauti kubwa

• Mgombea aliyepigiwa kura au

• Karatasi ya kura haina alama yoyote au

• Kura imeharibika

Alama inayokubalika katika chumba kinachokuwa chini ya picha ya mgombea ni

alama ya “√”. Endapo mpiga kura atashindwa kuweka alama katika chumba

kilichopo chini ya picha ya mgombea lakini ameweka alama hiyo katika picha ya

mgombea au katika alama ya chama chake, alama hiyo itakubaliwa na ni kura

halali.

vii. Atazipanga kura kwa mafungu tofauti kwa kila mgombea na upande wa picha za

wagombea uelekezwe juu. Kura zitakazokataliwa na zile zenye mgogoro zipangwe

sehemu tofauti.

viii. Baada ya kukamilisha hatua hiyo, Msimamizi wa kituo atahesabu kwa sauti kubwa

hesabu ya kura kwa kila fungu na baadae ataandika idadi ya kura zilizopatikana

kwa kila fungu.

ix. Atalinganisha idadi ya kura alizopata kwa kila mgombea, kura zilizokataliwa na

kura zenye mgogoro na idadi ya kura zilizopatikana katika sanduku la kura

zilizopigwa katika kituo.

Page 28: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

27

x. Baada ya kumaliza kuhesabu kura, Msimamizi wa kituo atazifunga kura hizo na

kuziweka kwenye bahasha tofauti kama ifuatavyo:-

• Kura zenye mgogoro- Bahasha Nam. 5A – Urais, 5B- Uwakilishi na 5C-

Udiwani.

• Kura zilizokataliwa- Bahasha Nam. 6A – Urais, 6B –Uwakilishi na 6C –

Udiwani.

• Kura halali –Bahasha Nam. 7A – Urais, 7B – Uwakilishi na 7C – Udiwani.

xi. Msimamizi wa kituo baada ya hatua zote hizo atajaza matokeo ya Uchaguzi wa

Rais, Uwakilishi na Udiwani katika kituo chake kwa kujaza Fomu Nam. 12A kwa

Urais, Fomu Namba 22A kwa Uwakilishi na Fomu Namba 32A kwa Udiwani ambazo

zinauwezo wa kutoa kopi.

xii. Baada ya kuhesabu kura mawakala wajaze Fomu Nam. PS 10 kuthibitisha kwamba

wanaridhika au hawakuridhika na namna kura zilivyohesabiwa na iwapo wana

malalamiko yoyote.

xiii. Mawakala ama wagombea katika kituo cha kuhesabia kura ambao wameshuhudia

kazi za kuhesabu kura wataandikwa majina katika fomu hizo na watatia saini katika

fomu ya matokeo ya kituo kuthibitisha kuwa wameshuhudia matokeo ya

wagombea katika kura zilizohesabiwa kituoni.

xiv. Msimamizi wa Kituo atapeleka ukurasa wa kwanza wa fomu ya matokeo kwa kila

uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo wakati wa majumuisho ya jimbo.

xv. Atabandika nakala moja ya fomu ya matokeo nje ya kituo cha kuhesabia kura na

nakala nyengine za matokeo atawakabidhi mawakala walioshuhudia kazi ya

kuhesabu kura kituoni.

xvi. Msimamizi wa Kituo ataziweka bahasha za kura halali na kura zilizokataliwa kwenye

masanduku ya kupigia kura kulingana na uchaguzi husika. Bahasha ya kituo cha

kupigia kura na fomu zote za matokeo zisiwekwe ndani ya sanduku.

Page 29: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

28

ANGALIZO

1. Vifungio vinavyokatwa ni vya pembeni tu. Kifungio kilichozuia sehemu ya kuingizia

kura visikatwe.

2. Wakati wa kuhesabu kura, karatasi za kura zitakazoonekana katika sanduku

lisilohusika zitahesabiwa katika sanduku linalohusika.

3. Kuhesabu kura upya kutafanyika endapo mgombea au wakala wa mgombea wa

kuhesabu kura ataomba kura zihesabiwe tena. Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi

ombi la kwanza lazima kura zihesabiwe. Ombi la pili lazima kura zihesabiwe na ombi

la tatu, Msimamizi wa kituo anaweza kukataa endapo matokeo ya hesabu ya ombi la

kwanza na la pili ni yale yale.

4. Wakala wa kuhesabu kura haruhusiwi kuhesabu kura wala kushika karatasi za kura

wakati wa zoezi la kuhesabu kura.

30. KURA AMBAZO HAZITAHESABIWA KUWA NI KURA HALALI

Uamuzi wa kura halali na isiyo halali

Wakati wa kuhesabu kura, uamuzi wa mwisho juu ya uhalali wa kura itakayohesabiwa ni

wa Msimamizi wa Kituo. Kwa hiyo, iwapo Msimamizi wa Kituo ataridhika kuwa kura

imeharibika ataikataa na haitahesabiwa na ataandika nyuma ya karatasi hiyo ya kura

maneno yanayosomeka ”IMEKATALIWA”. Iwapo uamuzi huo wa Msimamizi wa Kituo

utapingwa na wakala, Msimamizi wa Kituo ataandika nyuma ya karatasi hiyo maneno

yanayosomeka ”UAMUZI UMEPINGWA NA”......... (Ataandika jina na chama cha

anaepinga). Kura ambayo imepingwa itachukuliwa kuwa ni kura yenye mgogoro.

Kura zilizoharibika

Kura itahesabiwa kuwa imeharibika iwapo:-

• Haina muhuri wa Kituo.

• Ina alama ya maandishi yanayoweza kumtambulisha mtu aliyepiga kura hiyo na.

• Aliyopigiwa zaidi ya mgombea mmoja.

Page 30: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

29

31. KURA ZENYE MGOGORO

Kura zenye mgogoro zitaamuliwa na Msimamizi wa Uchaguzi wakati wa kujumlisha kura.

Msimamizi wa Uchaguzi baada ya kufanya uamuzi wa kura zenye mgogoro atajaza

matokeo husika kwenye fomu ya majumuisho ya jimbo Namba. 12B kwa Urais, Namba

22B kwa Uwakilishi na Namba 32B kwa Udiwani.

32. MAKABIDHIANO YA VIFAA

Baada ya kumaliza shughuli zote za kuhesabu kura kama zilivyoainishwa katika maelekezo

haya, Msimamizi wa Kituo atawajibika kufanya yafuatayo:-

i. Atamkabidhi Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo masanduku yote ya kura, bahasha

pamoja na vifaa vyote alivyokabidhiwa.

ii. Baada ya makabidhiano hayo ahakikishe kuwa amepewa uthibitisho kuwa vitu vyote

ni sawa na salama na kazi ya Msimamizi wa Kituo itakuwa imemalizika.

33. TAHADHARI KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA

Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo

wanatahadharishwa wasitumie vibaya nafasi wanazokabidhiwa. Ni makosa kutumia nafasi

hizo kwa lengo la kumtia adabu mpiga kura asipige kura. Wasimamizi wa Vituo vya

kupigia kura na Wasaidizi wao pia wanatahadharishwa kujiepusha na mambo yafuatayo:-

i. Kutoa au kutumia karatasi za kura kinyume na maelekezo.

ii. Kufanya makosa ya kuwapa karatasi za kura watu wasiostahiki.

iii. Kujaribu kufungua masanduku ya kura au bahasha zilizofungwa.

iv. Kuacha kupiga muhuri wa Kituo katika karatasi ya kura kwa makusudi au kwa

uzembe.

v. Kuficha karatasi za kura ili wananchi wenye haki wasiweze kupiga kura zao

kutokana na hila hiyo.

Page 31: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

30

34. MAKOSA KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA

Ifahamike kuwa ni makosa kufanya jambo lolote ambalo litaingilia, litatatiza au litaleta

ucheleweshaji wa mwenendo wa upigaji kura.

Makosa hayo ni:-

i. Kutaka kupiga kura kabla ya kituo hakijafunguliwa au baada ya kufungwa.

ii. Kupiga kura au kukusudia kupiga kura ikiwa mtu hana haki ya kufanya hivyo.

iii. Kupiga kura au kukusudia kupiga kura zaidi ya mara moja.

iv. Kupiga kura kwa jina la mtu mwengine.

v. Kutia ndani ya sanduku la kura kitu chengine chochote zaidi ya kura.

vi. Kubandua katika eneo la kituo cha kupigia kura karatasi yoyote ya matangazo

halali kuhusu upigaji kura.

vii. Kuingiza au kuharibu karatasi ya kura au shahada ya matokeo au fomu yoyote

inayohusiana na kupiga kura.

viii. Kuchapisha au kuwa na au kumpa mtu yeyote karatasi ya kura bila ya kuwa na

mamlaka ya kisheria.

ix. Kuwa na sanduku la kura bila ya kuwa na mamlaka hayo.

x. Kuzuia au kuingilia kazi za Msaidizi Msimamizi wa kituo.

xi. Kumlazimisha mpiga kura kupiga kura.

xii. Kumzuia au kumkinga mpiga kura kupiga kura yake katika hali ya faragha.

xiii. Kutoa taarifa juu ya namna alivyopiga kura.

xiv. Kuonesha jinsi alivyopiga kura yake.

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imewateuwa nyinyi kutokana na maombi mengi

yaliyowasilishwa kwetu. Tunawaomba mfanye kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.

Ahsanteni

TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR INAWATAKIA KAZI NJEMA

Page 32: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

31

MIFANO YA KURA ZINAZOKUBALIKA NA ZISIZOKUBALIKA

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

///

Chama Chama Chama

Alama iliyowekwa kwenye picha ya mgombea kinyume na maelekezo

(uso wa mgombea): nia ya mpiga kura inaeleweka

Picha ya Mgombea

Picha ya mgombea

Picha ya Mgombea

Chama Chama √ Chama

Alama ya √ (vyema) imewekwa katika alama ya chama (logo) nia ya mpiga kura

inaeleweka, kura hiyo itahesabiwa.

Page 33: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

32

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Chama Chama Chama

Ni alama sahihi inayoruhusiwa moja kwa moja na sheria.

MFANO WA KURA ZISIZOKUBALIKA

Kuweka alama √ (vyema) katika chumba kinachokubalika na alama ya X katika sura au

picha ya mgombea. Kura hii haikubaliki kwa sababu nia ya mpiga kura haiko wazi.

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

X

CHAMA CHAMA CHAMA

Page 34: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

33

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Chama Chama Chama

Alama ya √ (Vyema) imewekwa nje ya eneo lote la kupigia kura

(iko nje chumba kinachopendekezwa); haitahesabiwa

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Chama Chama Chama

Alama za VYEMA (√) ziko kama ilivyoelekezwa chini ya picha za wagombea wote, kura

hiyo haikubaliki kwani mpiga kura hakumpigia mgombea moja kama anavyotakiwa na

Sheria.

Page 35: TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - zec.go.tzzec.go.tz/elections/wp-content/uploads/2015/10/Presiding-Officer... · Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia

34

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Chama Chama Chama

Karatasi ya kura ambayo haikupigwa muhuri wa kituo sehemu ya nyuma kama

inavyoelekezwa na Sheria, karatasi hiyo haifunguliwi na haihesabiwi.