61
ABBAS MOHAMED OMAR

Maktaba Za Skuli

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Information science, school library, information literacy, Zanzibar

Citation preview

  • ABBAS MOHAMED OMAR

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    2

    MAKTABA ZA SKULI

    HAZINA ILIYOSAHAULIWA

    School Libraries: the forgotten treasure

    ABBAS MOHAMED OMAR

  • Abbas M. Omar 2013

    3

    SHUKRANI Awali, namshukuru Allah (sw) Mjuzi wa elimu zote kwa kuniwezesha kuibua wazo na kuandika kitabu hiki. Pili, shukrani zangu za dhati ziende kwa wale wote walionisaidia kwa njia moja au nyengine kufanikisha zoezi la kuandika na kuchapisha kitabu hiki. Namshukuru bwana Hafidh Nassor Mkurugenzi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kwa kuipitia rasimu ya kazi hii. Pia, namshukuru bwana Amiir A. Mohamed mwandishi maarufu wa vitabu Zanzibar kwa kwa ushauri mzuri alionipa. Aidha, shukrani ziende kwa Bi. Saida Mahfoudh Haji wa Maktaba Kuu Zanzibar kwa kurekebisha makosa ya kiuandishi yaliyojitokeza wakati wa kuandika kazi hii. Mwisho, shukrani za pekee ziende kwa mke wangu Bi. Asha Mohamed Hassan kwa kunipa moyo katika kukamilisha kazi hii. Wote nawaambia ahsante sana!

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    4

    ZAWADI

    Kitabu hiki nawatunukia wanangu wapendwa; Juwairiya, Juhayna, Juweyda, Jumaima na Junaitha.

    Jamii ya wazanzibari, Wapenzi wa maktaba na

    Wapenda maendeleo ya elimu Zanzibar.

  • Abbas M. Omar 2013

    5

    YALIYOMO Zawadi ....................................................................................... 4

    Vifupisho.................................................................................... 7

    SURA YA KWANZA ................................................................ 11

    Utangulizi .................................................................................. 11

    Maana ya maktaba ..................................................................... 13

    Aina za maktaba ......................................................................... 14

    SURA YA PILI .......................................................................... 16

    Maktaba ya skuli ........................................................................ 16

    Malengo ya maktaba za skuli ..................................................... 18

    SURA YA TATU ...................................................................... 21

    Huduma katika maktaba ya skuli ................................................ 21

    Nafasi ya mkutubi ................................................................... 21

    Nafasi ya mwalimu ................................................................. 24

    SURA YA NNE ......................................................................... 28

    Umuhimu wa kutumia maktaba .................................................. 28

    Masuala ya Elimu ...................................................................... 31

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    6

    Masuala ya Siasa ........................................................................ 31

    Masuala ya Utamaduni ............................................................... 32

    Masuala ya Dini ......................................................................... 32

    Masuala ya Kijamii .................................................................... 33

    SURA YA TANO ...................................................................... 34

    Hali ya maktaba za skuli nchini .................................................. 34

    Mazingira ................................................................................... 35

    Vifaa .......................................................................................... 36

    Wafanyakazi wa Maktaba za Skuli ............................................. 39

    Matumizi ya maktaba za skuli .................................................... 41

    Utumiaji wa Maktaba miongoni mwa Walimu ........................... 42

    Utumiaji wa Maktaba miongoni mwa Wanafunzi ....................... 45

    Hitimisho ................................................................................... 51

    Mapendekezo ............................................................................. 53

    REJEA ....................................................................................... 58

  • Abbas M. Omar 2013

    7

    VIFUPISHO CD Compact Disc DVD Digital Versetile Disc SHM Shirika la Huduma za Maktaba UNESCO United Nations Educational Scientific

    and Cultural Organization USAID United State United States Agency for

    International Development VCD Video Compact Disc VSO Voluntery Services Overseas WEMA Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    8

    NENO LA AWALI If you have a garden and a library, you have everything you

    need. Marcus Tullius Cicero Kama unayo bustani na maktaba una kila kitu unachohitaji

    (Tafsiri yangu)

    Maneno haya machache yana ujumbe mzito na hekima yake ni pana zaidi ya upeo wa macho ya msomaji. Kalamu na kurasa nyingi zinahitajika ili kuandika uchambuzi wa maana ya maneno haya. Kwa ufupi, maktaba ni hazina pekee inayoweza kumtajirisha mtumiaji katika ulimwengu wa taaluma na taarifa. Mtumiaji wa maktaba kamwe hapitwi na wakati, huwa na mtazamo mpana na kichwa chake hujaa maarifa na taarifa muhimu juu ya mambo mbalimbali yanayohusu ulimwengu na vilivyomo. Kama zilivyo tabia nyengine, tabia ya kutumia maktaba inahitaji kukuzwa kwa mtoto mapema iwezekanavyo ili kumuwezesha kijana aweze kuendelea na tabia hii katika maisha yake yote. Kwa mtu mzima tabia hii inataka moyo, utayari na maamuzi ya dhati yatayomsukuma kutenga muda maalum kwa ajili ya

  • Abbas M. Omar 2013

    9

    kutembelea maktaba kila siku au angalau mara moja kwa wiki. Maktaba zote zina umuhimu unaolingana katika jamii, lakini wazo la kuandika kitabu hiki linajitokeza kutokana na umuhimu mkubwa uliopo katika kuzitunza na kuziendeleza maktaba za skuli ambazo ndio shina la kumuandaa na kumkuza kijana kuwa na tabia ya kujifunza kupitia maktaba. Umuhimu wa maktaba za skuli unaweza kuthibitishwa na maneno ya wahenga yasemayo mkunje samaki yungali m-bichi msemo huu unafaa kuwa dira yetu katika kuwatayarisha vijana wetu kutokea chekechea, msingi na sekondari mpaka kufikia chuo kikuu kuwa na tabia ya kutembelea na kutumia vifaa na huduma za maktaba. Abbas Mohamed Omar 2012.

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    10

  • Abbas M. Omar 2013

    11

    SURA YA KWANZA

    UTANGULIZI Maktaba ya skuli ni kiungo muhimu sana katika mpangilio wa skuli na maendeleo ya elimu kwa ujumla. Katika karne hii tuliyonayo yaani karne ya habari na taarifa information century kila skuli inapaswa kuwa na maktaba ya kisasa. Maktaba ambayo si kama itakuwa na vitabu, majarida au magazeti tu, bali iwe yenye kwenda sambamba na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Hivyo maktaba ya kileo inatarajiwa kuwa na mkusanyiko wa vifaa vya kisasa vya elektroniki vitakavyosaidia na kurahisisha upatikanaji wa taarifa. Vifaa hivyo ni kama, redio, komputa, video, televisheni, projekta, CD, VCD, DVD nakadhalika. Maktaba ya skuli yenye vifaa vya kisasa inatarajiwa kuwavutia watumiaji wake na kuwasaidia wanafunzi kuongeza upeo wao kitaaluma zaidi ya masomo wanayojifunza darasani. Endapo watumiaji hao watavutika na kuitumia maktaba hiyo hakuna shaka lengo la kuwepo kwa maktaba nalo ni kukusanya,

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    12

    kupangilia, kuhifadhi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali kwa watumiaji wake litafikiwa. Tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu wa fani ya elimu zinathibitisha kwamba endapo maktaba za skuli zitaimarishwa na kusimamiwa na wakutubi waliopata mafunzo, hakuna shaka kiwango cha elimu nchini kitapanda kwa kasi ya ajabu. Maktaba ya skuli ni sehemu muhimu sana ya kuwaunganisha walimu na wanafunzi katika kufikia lengo la elimu nalo ni kumwezesha na kumkuza msomaji kuwa na tabia ya kuendelea kujifunza mwenyewe, kuwa na uwezo wa kutafiti, kudadisi, kubuni na kuhoji pamoja na kufanya uchambuzi na kutathmini hali ya mambo na kufanya maamuzi sahihi. Kubwa zaidi ni kuwa na uwezo wa kukabiliana na matatizo mbalimbali yatayomkabili katika maisha yake ya kila siku. Hivyo, matumizi ya maktaba ni jambo lisiloepukika kwa mwanafunzi wa leo ambae kwa yakini anatambua kuwa elimu ndio hasa inayohitajika na yenye kupewa kipao mbele katika kila jambo la ulimwengu wetu wa leo. Mwanafunzi mwenye tabia ya kujifunza kupitia

  • Abbas M. Omar 2013

    13

    maktaba daima huwa na mtazamo mpana na huwa mwenye kufanya vizuri katika masomo yake. Licha ya umuhimu na mchango mkubwa unaotolewa na maktaba za skuli, taasisi hizi zinonekana kuwekwa nyuma, kudharaulika na hata kusahaulika miongoni mwa wadau wa elimu. Mwandishi wa kitabu hiki ana lengo la kuikumbusha jamii umuhimu wa kuzitunza, kuziendeleza na kuzitumia maktaba za skuli ipasavyo kwa lengo la kuwafanya walimu na wanafunzi kuendana na wakati tulionao.

    Maana ya Maktaba Tafsiri ya Kumar (1987) ambayo imekusanya mawazo ya wataalamu wengi wa zama za leo katika fani ya ukutubi enaeleza kuwa maktaba ni mkusanyiko wa vitabu na rasilimali nyengine zinazotumika kutolea taarifa na elimu kama vile; majarida, magazeti, na machapisho mbalimbali, pamoja na vifaa vya kusikiliza na kuona (audio-visual) kama vile; televisheni, komputa, picha mbalimbali, ramani, kanda za redio na video, CD, VCD, DVD, nakadhalika. Vifaa hivyo hupangwa kwa mpangilio maalum na husimamiwa na

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    14

    mtu mkutubi (mtu aliyepata mafunzo maalum ya utoaji wa huduma kwa watumiaji wa maktaba) ili kusimamia na kurahisisha matumizi na upatikanaji wa taarifa zilizomo katika vifaa hivyo. Tafsiri hii inafuta mawazo ya baadhi ya watu wanaodhania kuwa maktaba ni mfano wa ghala/stoo ya vitabu ambayo vitabu na machapisho mbalimbali huwekwa ndani yake bila ya usimamizi au utaratibu wowote na hutumika pale tu haja ya kufanya hivyo inapotojitokeza.

    Aina za Maktaba Wataalamu kadhaa katika fani ya ukutubi wamezigawa aina za maktaba katika makundi mbalimbali kwa mujibu wa huduma na watumiaji wa maktaba hizo. Katika kitabu hiki hatutojadili aina za maktaba ila si vibaya kuzitaja japo kwa ufupi kama ifuatavyo; Maktaba ya Taifa na Maktaba ya Umma Maktaba hizi hutoa huduma kwa watu wote (umma) bila mipaka yoyote ya rangi, kabila, jinsia, hadhi nakadhalika.

  • Abbas M. Omar 2013

    15

    Maktaba za taaluma (maktaba za vyuo vikuu na maktaba za skuli) Maktaba hizi hutoa huduma kwa walimu, wakufunzi, wanafunzi na watafiti mbalimbali. Maktaba Maalum Hizi hujikita katika utoaji wa huduma kwa makundi maalum ya watu kama vile, wagonjwa, wafungwa, watumishi wa taasisi fulani au watu wenye aina Fulani ya ulemavu.

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    16

    SURA YA PILI

    MAKTABA YA SKULI Kama zilivyo maktaba nyengine, maktaba ya skuli huwa na vifaa mbalimbali vinavyotoa taarifa, kuelimisha na kuburudisha. Maktaba hii hutoa huduma kwa walimu na wanafunzi. Maktaba ya skuli ni kiungo muhimu katika kukamilisha malengo ya elimu ya msingi na sekondari nayo ni kumtayarisha mwanafunzi kuwa raia bora katika jamii yake na taifa kwa ujumla. Ilani ya maktaba za skuli ya UNESCO (2000) inafafanua kuwa

    Maktaba ya skuli hutoa habari na dhana za msingi kwa mafanikio ya jamii ya kisasa ambayo kimsingi inategemea zaidi habari na taarifa. Maktaba ya skuli huwapa wanafunzi mbinu za kujifunza katika maisha na kukuza ubunifu wao ili kuwawezesha kuishi kama raia wanaowajibika.

    Maktaba ya skuli inatarajiwa kuwa na mkusanyiko wa vitabu vya ziada na kiada kwa masomo yote, vitabu vya rejea, mihtasari ya masomo, atlasi, machati, vitabu vya hadithi mbalimbali, kazi zilizofanywa na wanafunzi,

  • Abbas M. Omar 2013

    17

    karatasi za mitihani iliyopita, ramani mbalimbali za nchi na dunia, nakadhalika. Jambo la kutiliwa mkazo wa kipekee ni kuweka vifaa vya kisasa vya kufundishia na kutolea taarifa katika maktaba hizo. Vifaa kama vile komputa, televisheni, projekta, redio, kanda za redio na video, CD na DVD vitasaidia sana kuamsha hamu ya wanafunzi kutembelea maktaba mara kwa mara. Maktaba ya Skuli ya Msingi Kama jina lake maktaba hii ndio msingi wa kumkuza mwanafunzi kuwa na tabia ya kupenda kujisomea vitabu. Kwa mijibu wa Baird (2004) ni vizuri kugawa machapisho katika maktaba ya skuli ya msingi kwa kuzingatia umri na ngazi zao. Kwa mfano vitabu vya hadithi za watoto, picha za watoto na vitabu kwa ajili ya wanafunzi wanaoanza kujifunza kusoma. Maktaba ya skuli ya Sekondari Ni jambo la msingi kwa maktaba hii kuendeleza hamu na shauku ya mwanafunzi ya kujisomea vitabu aliyotoka nayo katika skuli ya msingi. Ni muhimu sana kuweka machapisho mchanganyiko katika maktaba hii,

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    18

    kwa mfano vitabu vya hadithi na vitabu vya taarifa, vitabu vya kiada na ziada pamoja na machapisho mengineyo kama vile majarida na magazeti.

    Malengo ya Maktaba za Skuli Yafuatayo ni malengo ya maktaba za skuli kama yalivyoainishwa na Umoja wa Mataifa wa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO, 2000). Kusaidia na kuboresha malengo ya elimu kama

    yalivyoorodheshwa katika misheni ya skuli na mitaala.

    Tabia za wanafunzi za kupenda kusoma na

    kujifunza pamoja na kutumia maktaba ziendelezwe na kudumishwa maishani mwao.

    Kutoa fursa ya kupata ozoefu wa kuvumbua na

    kutumia habari kwa ajili ya elimu, uelewaji, ubunifu na ridhaa.

    Wanafunzi wasaidiwe katika shughuli zao za

    kujifunza na kupata umahiri katika kutathimini na kutumia habari, bila kujali taratibu/fani, muundo au njia ya upatikanaji wa habari pamoja na kiwango

  • Abbas M. Omar 2013

    19

    cha hisi katika njia za mawasiliano za jumuiya kupitia maktaba.

    Kutoa fursa kwa upatikanaji wa rasilimali za mitaa,

    mikoa, kitaifa na kimataifa na nafasi ambazo zinawawezesha wanafunzi kupata mawazo mbalimbali, uzoefu na maoni.

    Kuandaa shughuli zinazohamasisha hisia ya

    utamaduni na elimu ya jamii. Kushirikiana kikazi na wanafunzi, walimu,

    watawala na wazazi ili kufikia misheni ya skuli. Kuweka wazi dhana ya kuwa uhuru wa fikra na

    upatikanaji wa habari ni vitu muhimu kwa raia, uwajibikaji na utekelezaji wa demokrasia.

    Kukuza usomaji, rasilimali na huduma za maktaba

    ya skuli kwa jumuiya ya skuli na nje ya jumuiya.

    Maktaba ya skuli itatekeleza shughuli hizi kwa kuanzisha sera na kanuni za utumiaji na uazimishaji wa vifaa vya maktaba, wakati wa huduma, kuchagua na

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    20

    kununua rasilimali husika, kuandaa nafasi na mazingira mazuri ya kusomea ili kutoa fursa ya kifikra itakayowawezesha watumiaji kupata vyanzo vya habari, pamoja na nyenzo na mbinu mbadala za kufundishia na vile vile kuajiri watumishi wenye taaluma. Kwa kuengezea Baird (2004) amependekeza kuundwa kwa kamati ya maktaba ya skuli ambayo itaratibu maendeleo ya maktaba hiyo. Kamati ya maktaba ya skuli itahusisha mkutubi, mwalimu mkuu, mwalimu wa somo la lugha, na wanafunzi wanne (kwa kuzingatia jinsia).

  • Abbas M. Omar 2013

    21

    SURA YA TATU

    HUDUMA KATIKA MAKTABA YA SKULI Utangulizi Huduma nzuri za maktaba zinategemeana na mazingira, vifaa vilivyomo na mtoaji wa huduma ya maktaba. Katika sura hii tutajadili nafasi ya mkutubi katika utoaji wa huduma za maktaba na nafasi ya mwalimu katika kumkuza na kumuelekeza mwanafunzi matumizi sahihi ya maktaba ya skuli. Nafasi ya Mkutubi Mkutubi ni mtu muhimu sana katika kuihuwisha maktaba, yeye ndie atakaye tengeneza au kuiharibu maktaba. Hivyo ni vyema kila skuli kuajiri mkutubi aliyepata mafunzo na kutayarishwa kwa ajili ya kuhudumia maktaba za skuli. Mkutubi wa aina hii anatarajiwa kuipenda na kuithamini kazi yake, atakuwa tayari kushirikiana na walimu katika utendaji wake wa kazi za kila siku, atakuwa mbunifu wa njia na programu mbalimbali

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    22

    zitazowashajihisha walimu na wanafunzi kutumia maktaba yake. Ili mkutubi aweze kufanya kazi zake vizuri, kwa ufanisi na kwa kujiamini, ni lazima apewe fursa sawa kama walivyo walimu wa masomo mengine. Ni lazima apate ushirikiano wa makusudi baina ya uongozi wa skuli na walimu. Endapo skuli itakuwa na mashirikiano katika utendaji wa kazi hakuna shaka mafanikio makubwa yatapatikana katika kufikia lengo la elimu nchini. Kwa ufupi huduma yanayohitaji kuzingatiwa katika utoaji wa huduma za maktaba ya skuli ni hizi zifuatazo; Kutilia mkazo katika kukamilisha malengo ya skuli

    na kukuza kiwango cha elimu nchini. Kutimiza malengo ya wizara ya elimu nayo ni

    kumtayarisha kijana aweze kutumia nafasi aliyonayo katika kuleta maendeleo ya jamii yake na taifa kwa jumla.

    Kukusanya na kupanga vifaa vilivyokuwepo

    maktaba kwa kusisitiza vifaa vyenye kukusanya

  • Abbas M. Omar 2013

    23

    picha na sauti (multimedia) ili kutimiza haja na matumizi ya walimu na wanafunzi.

    Kutoa elimu ya maktaba kwa wanafunzi ili

    kuwawezesha kuwa na ujuzi na uwezo wa kutumia maktaba kwa usahihi, wepesi na kujiamini.

    Kujenga miongoni mwa wanafunzi tabia ya

    kuendelea kujifunza kwa kutumia maktaba hata watapomaliza skuli.

    Kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji ya wanafunzi

    na walimu kwa kuzingatia vitabu na vifaa vyengine vya kisasa.

    Kushajihisha na kuwasaidia walimu kufundisha

    kwa kutumia maktaba. Kuamsha hamu ya kutumia maktaba miongoni mwa

    wanafunzi kwa kutumia njia mbadala zikiwemo programu maalum za kufanya mijadala, uandishi wa insha na nyenginezo.

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    24

    Kutoa mwongozo kwa wanafunzi juu ya mpangilio wa vitabu katika rafu, matumizi ya katalogi, na vifaa vyengine vya maktaba. Pia kuwaelekeza namna ya kutafuta taarifa muhimu kwa haraka.

    Kuchochea tabia na utamaduni wa kupenda

    kujifunza wenyewe miongoni mwa wanafunzi. Kwa hakika maktaba za skuli zina nafasi kubwa ya kupandisha kiwango cha elimu nchini endapo zitatumika ipasavyo pasi na kufumbia macho huduma ndogo inayotolewa maktaba kwa mashirikiano na maamuzi ya pamoja, basi mapinduzi makubwa ya kielimu yatatokea kuanzia mashuleni hadi vyuo vikuu. Nafasi ya Mwalimu Mwalimu ana nafasi ya pekee katika kumkuza mwanafunzi juu ya matumizi ya maktaba. Mafanikio ya maktaba ya skuli yanategemea mno mashirikiano ya walimu na mkutubi. Watu wawili hawa ni lazima washirikiane katika kazi ya kufunza. Ilani ya UNESCO (2000) inaeleza kwamba

    imedhihirika kuwa walimu na wakutubi wanapofanya kazi kwa kushirikiana, wanafunzi

  • Abbas M. Omar 2013

    25

    hupata mafanikio zaidi katika kusoma na kuandika, uwezo wa kujifunza, uwezo wa kutatua matatizo pamoja na kuwasiliana na mbinu za upashanaji habari kwa njia za teknolojia.

    Mwalimu hodari mwenye kuwajibika anatarajiwa kufanya yafuatayo katika kuhahakisha matumizi ya maktaba miongoni mwa wanafunzi; Kumuelekeza mwanafunzi hususan wa skuli za

    sekondari namna ya kutafuta taarifa na kuchukua notisi katika kitabu kuanzia katika ukurasa wa yaliyomo hadi ukurasa wa faharasa.

    Kumshajihisha mwanafunzi kutumia maktaba ya

    skuli na maktaba ya umma pia kumshawishi kununua vitabu vyake mwenyewe.

    Kutoa kazi zitakazomlazimu mwanafunzi kutafuta

    taarifa katika maktaba ya skuli au kwengineko. Mwalimu anapaswa kuandaa mada maalum na kuwataka wanafunzi kuwasilisha mada hiyo darasani.

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    26

    Mwalimu afuatilie mwenendo wa wanafunzi katika kuitembelea maktaba kwa kuchukua orodha ya wale wanahudhuria maktaba kwa kawaida.

    Mwalimu atashirikiana na mkutubi kuchagua na

    kupendekeza vitabu vya kununuliwa na kamati ya taaluma ya skuli.

    Ashirikiane na kusaidiana na mkutubi

    kuwashajihisha wanafunzi kutumia maktaba ya skuli kupitia wiki ya mwanzo ya maelekezo kwa wanafunzi wapya.

    Kuandaa kipindi maalumu kwa ajili ya kutembelea

    maktaba angalau mara moja kwa wiki. Mwalimu ataandamana na wanafunzi wake hadi maktaba na kushirikiana na mkutubi ambae atakuwa mstari wa mbele katika kuwafunza wanafunzi matumizi ya maktaba hatua baada ya hatua.

    Mwalimu mkuu ni lazima aipe maktaba ya skuli

    hadhi yake inayostahili. Azingatie matatizo yanayoikabili maktaba na mkutubi wake. Mkutubi

  • Abbas M. Omar 2013

    27

    apewe fursa sawa na mwalimu na inashauriwa mkutubi kuwemo katika kamati ya taaluma ya skuli.

    Utekelezaji wa mambo yaliyotajwa hapo juu unategemea na hamu, utayari, msimamo na usimamiaji madhubuti wa sera ya wizara ya elimu na sera ya skuli kuhusu maktaba. Kwa maoni yangu mambo haya yakifanyika katika skuli zetu sambamba na ufundishaji ulio makini darasani wenye kufuata muongozo na maadili ya ualimu utainua sana upeo wa fikra, uwezo wa kujieleza, kuhoji, kubuni pamoja na kuongeza hamu ya wanafunzi kufurahia kuendelea kubakia skuli.

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    28

    SURA YA NNE

    UMUHIMU WA KUTUMIA MAKTABA Kama tulivyotangulia kusema, maktaba ya skuli ni nyenzo muhimu sana katika kukuza kiwango cha elimu nchini. Siku moja mwalimu wangu alinisimulia hadithi ya kijana mmoja aliyezaliwa katika familia ya kimasikini kule ulaya. Kutokana na ugumu wa maisha, kijana yule alikosa fursa ya kuendelea na masomo ya sekondari baada ya kumaliza elimu yake ya msingi ambayo ilimpa uwezo wa kujua kusoma, kuandika na kuhesabu tu. Kijana yule alikuwa akiishi karibu na nyumba ya tajiri mmoja. Kwa bahati yule tajiri alikuwa akiondoka nyumbani kwake asubuhi mapema kuelekea kazini na kurudi jioni. Kwa kuwa yule kijana alikuwa na hamu ya kujifunza, alifanya kila mbinu ili aweze kuingia ndani kwa tajiri, huku akitambua kwamba ndani ya nyumba yake mlikuwa na maktaba ndogo yenye vitabu kadhaa vyenye taarifa na utajiri mkubwa wa elimu.

  • Abbas M. Omar 2013

    29

    Siku moja alifanikiwa kuingia ndani na kutimiza ndoto yake. Kumbuka kuwa ile ilikuwa nyumba ya tajiri, hivyo bila shaka mlikuwa na kila aina na vitu vya anasa. Lakini yule kijana akiwa ndani ya nyumba ile, hakuwa akifanya jambo jengine lolote zaidi ya kusoma vitabu mbalimbali vilivyozungumzia biashara (business). Kwake usomaji wa vitabu vya biashara aliupa kipaombele kwa kuwa alitamani sana kuwa mfanyabiashara. Kufumba na kufumbua kijana yule aliweza kuchota elimu kubwa iliyomo ndani ya vitabu vilivyoandikwa na waandishi mbalimbali mahiri katika fani ya biashara. Kawaida elimu yenye manufaa ni ile inayoingizwa katika matendo. Hivyo yule kijana alianza kuitumia elimu ile kwa kuanzisha biashara ndogo kulingana na mtaji alionao. Lakini kwa kuwa alifanya mambo kwa uhakika na kwa kujiamini kwa kuwa aliongozwa na elimu, kwa muda mfupi alianza kupiga hatua na kufanikiwa katika biashara yake. Amini usiasmini! Kijana yule baadae aliweza kuwa tajiri mkubwa aliyetajika katika mji wao.

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    30

    Hapo ndipo nilipoamini kuwa ukiwa na maktaba na bustani hakika una kila kitu unachohitaji katika maisha yako. Nimeamua kusimulia hadithi hii nikitarajia kuwa itachochea na kuamsha hamasa ya msomaji juu ya matumizi ya maktaba. Hadithi hii ya kijana wa kimasikini na maktaba ya tajiri, binafsi ilinishajihisha mno juu ya matumizi ya maktaba. Kumbuka tunaishi katika ulimwengu wa habari na taarifa. Taarifa zimekuwa zikichukua nafasi kubwa katika maisha ya uchumi, siasa, utamaduni, dini na mambo mbalimbali yahusuyo jamii. Katika jamii yoyote iliyostaarabika kwa maendeleo ya elimu hakuna awezae kukataa kuwa hahitaji taarifa. Hii ndio kusema watu wote katika ulimwengu wa leo wanahitaji taarifa. Raisi anahitaji taarifa, waziri anahitaji taarifa mbunge anahitaji taarifa. Mtafiti, Mwalimu, mwanafunzi, mfanyabiashara, mkulima, mvuvi, daktari na hata mama wa nyumbani anahitaji taarifa. Hivyo, hakuna taifa au mtu binafsi anaeweza kupata maendeleo ya kweli ikiwa atakosa taarifa sahihi zinazotoka katika vyanzo vya kuaminika na zinazokwenda na wakati. Maktaba imekuwa ni chombo chenye nafasi ya pekee kinachoweza kukidhi haja ya jamii ya kupata taarifa.

  • Abbas M. Omar 2013

    31

    Hebu sasa na tuangalie jinsi maktaba inavyoweza kukidhi mahitaji mbalimbali ya jamii;

    Masuala ya Elimu Elimu huzingatiwa kuwa ndio uti wa mgongo wa maendeleo ya taifa. Elimu ndio inayotengeneza heshima ya mtu na kubadilisha mtazamo na tabia yake. Maktaba za vyuo vikuu na maktaba za skuli zinatarajiwa kufanya kazi ya kutoa elimu kwa watumiaji wake. Hii ni kwa sababu maktaba hizi zinatarajiwa kuwa na mkusanyiko mkubwa wa vitabu na vifaa vyengine vya maktaba vyenye utajiri mkubwa wa elimu zilizoandikwa kwa utaalamu wa hali ya juu na wanataaluma mbalimbali. Hata maktaba za umma kwa baadhi ya wakati hufanya kazi hii kwa watumiaji wake.

    Masuala ya Siasa Mafanikio ya jamii iliyopea kisiasa yanatokana na raia wanaopata taarifa sahihi kila wakati. Kazi kubwa ya maktaba ya umma ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata taarifa na kujua haki zao za msingi kama raia wa nchi. Masuala ya demokrasia na mfumo wa serikali na taarifa za bunge, wizara na viongozi mbalimbali hupatikana katika maktaba hio.

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    32

    Masuala ya Utamaduni Utamadi wa nchi ndio kitambulisho cha raia wake. Maktaba hufanya kazi ya kuhifadhi sanaa za wasanii na simulizi asilia katika maandishi au aina nyengine za kumbukumbu. Kila mzalendo ana haki ya kujua na kudumisha mila, desturi na utamaduni wa nchi yake. Yote haya yatawezekana endapo jamii itakuwa na taarifa sahihi juu ya utamaduni wa nchi yao. Miongoni mwa huduma za maktaba ni kuburudisha watumiaji wake kwa hadithi nyingi za kila aina zilizoandikwa ndani ya vitabu vya fasihi ya sasa na ya kale.

    Masuala ya Dini Ni kawaida kwa jamii yoyote ile kuwa na mchanganyiko wa waumini na wafuasi wa dini mbalimbali. Muumini mzuri wa dini yoyote ile ni yule mwenye kusoma na kufuatilia machapisho mbalimbali yaliyoandikwa na wasomi, viongozi na waandishi mahiri wa dini yake. Maktaba ndio taasisi pekee yenye uwezo wa kuhifadhi na kutoa taarifa za dini mbalimbali zilizopo ulimwenguni. Hivyo ni kazi ya maktaba ya umma kuwahudumia waumini wenye imani tofauti na kuhakikisha kuwa kila mmoja anapata taarifa azitakazo.

  • Abbas M. Omar 2013

    33

    Masuala ya Kijamii Jamii hutengenezwa na watu. Miongoni mwa wanajamii huwemo watu wa aina mbalimbali, wenye sifa, tabia na matarajio mbalimbali. Hali hii huwafanya watu kutofautiana katika mitazamo na njia za kutafuta maisha. Ndio maana ndani ya jamii moja utakutana na watu wenye kazi tofauti. Makundi ya watu hawa yanahitaji taarifa mbalimbali kwa mujibu wa kazi zao. Maktaba za umma hutoa huduma zake bila malipo ili kumuwezesha kila mwanajamii kupata taarifa aitakayo. Taarifa kuhusu afya, maradhi, kinga na tiba, mapenzi na ndoa, michezo na mazoezi, vyakula na mapishi, biashara na kadhalika hupatikana maktaba kupitia vitabu, magazeti na majarida mbalimbali.

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    34

    SURA YA TANO

    HALI YA MAKTABA ZA SKULI NCHINI Kwa mujibu wa Shirika la Huduma za Maktaba Zanzibar (2006) takriban asilimia sitini (60%) ya skuli za msingi hazina maktaba wakati asilimia sabini (70%) ya skuli za sekondari zinaonekana kuwa na maktaba. Takwimu hizi zinaonesha kuwa suala la maktaba bado halijapewa umuhimu wake unaostahili katika skuli za msingi, skuli ambazo kama jina lake zinatarajiwa kumjengea msingi madhubuti mwanafunzi aliyepata elimu ya msingi ili aweze kuhimili vishindo vya elimu ya sekondari kama atapata fursa ya kuendelea au kumtayarisha kuwa raia mwema katika jamii yake aweze kuishi kwa matumaini na kujitegemea ikiwa atamalizia elimu ya msingi. Kwa upande mwengine skuli za sekondari kwa kiasi kikubwa huwa na maktaba. Suali la kujiuliza je, maktaba hizi zinakidhi haja za watumiaji wake? Kwa mujibu wa Shirika la Huduma za Maktaba (2006) maktaba nyingi za skuli za sekondari hazikidhi haja za

  • Abbas M. Omar 2013

    35

    watumiaji wake. Hali hii inajitokeza katika upande wa mazingira, vifaa, wafanyakazi, matumizi ya maktaba pamoja na huduma zinazotolewa katika maktaba hizo.

    Mazingira Maktaba za skuli hutofautiana katika mazingira na nafasi, Kwa upande wa mazingira, baadhi ya maktaba huonekana kuwa zimechoka na kupoteza haiba yake. Si ajabu kwa mtumiaji kukuta wadudu kama vile buibui au mende wakati anatafuta kitabu katika rafu. Vitabu hujaa mavumbi kama kwamba hakuna wa kuvishughukia. Wakati mwengine chumba kidogo cha ghala/stoo huchaguliwa na kutayarishwa kuwa maktaba, si jambo la kushangaza ndani ya maktaba hiyo kuona majembe, mipira ya kumwagilia maji na mafagio. Nafasi ya chumba kama hiki huwa ndogo mno kiasi ambacho hata madawati au meza tano haziwezi kuingizwa ndani yake. Uchache wa meza na viti vya kukalia huzifanya maktaba hizo kutumiwa na wanafunzi kidogo na wengi wao hukosa fursa ya kutumia maktaba wakati wanapohitaji kufanya hivyo. Kwa mantiki hiyo maktaba ya skuli hubaki kuhudumia wanafunzi wachache kwa muda mrefu.

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    36

    Vifaa Uhaba wa vifaa vya kusomea ni tatizo linalozungumzwa sana na waandishi pamoja na wana taaluma wengi. Skuli nyingi za binafsi na hata zile za serikali hazina maabara na maktaba zinazokidhi haja. Tatizo hili humfanya mwanafunzi ashindwe kurejea masomo yake na kupanua mawazo yake kwa kukosa vitabu na kushindwa kusoma kwa vitendo katika masomo ya sayansi kwa kuwa hakuna vifaa vya kutosha katika maabara. Maktaba yenye vifaa vya kisasa na vya kutosha huwavutia watumiaji wake. Utafiti unaonesha kuwa maktaba nyingi za skuli hazina vifaa vya kutosha. Omar (2010) ameeleza kuwa maktaba za skuli hazina vitabu vya kutosha na vitabu vilivyopo vingi vimepitwa na wakati. Tatizo la maktaba kuwa na vitabu vya kizamani linaonekana zaidi katika skuli zinazosimamiwa na serikali, kwa kuwa mara nyingi skuli hizi hupata misaada ya vitabu kutoka kwa wafadhili mbalimbali kutoka nje ya nchi. Sifa ya vitabu hivi mara nyingi huwa ni vitabu vilivyokwisha kutumika (second hand books),

  • Abbas M. Omar 2013

    37

    ambavyo mara nyingi huwa haviendani na mtaala wa Tanzania/Zanzibar lakini pia huwa ni vitabu vilivyoandaliwa kwa wanafunzi wa nchi za nje ambao lugha ya kiengereza huwa si tatizo kwao. Kubwa zaidi baadhi ya vitabu hivyo huwa na hadithi ambazo maudhui yake hayaendani na utamani wa Zanzibar. Hata hivyo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kiasi inajitahidi kwa kushirikiana na wafadhili mbalimbali kuondoa tatizo hilo. Mradi wa hivi karibuni wa Africa Education Initiative (AEI) unaosimamiwa na USAID kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Carolina, umefanikiwa kuchapisha vitabu vya masomo ya sayansi kwa ajili ya wanafunzi wa skuli za sekondari. Aidha, mradi wa maktaba za maboksi/masanduku (Book box libraries) unaofadhiliwa na Book Aid International na kusimamiwa na Shirika la Huduma za Maktaba (Zanzibar Library Services) ambao unahusisha skuli ishirini na msingi nchini (kumi Pemba na kumi Unguja) unajaribu kusaidia angalau kuibua wazo la uwepo wa aina fulani ya maktaba katika skuli za msingi. Tatizo la vitabu vya kizamani hupungua katika maktaba za skuli zinazomilikiwa na watu binafsi. Hii ni

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    38

    kwa sababu skuli hizi hujinunulia vitabu vyake wenyewe, lakini uhaba wa vitabu hivyo huwakwaza wanafunzi na walimu wanaotaka kutumia. Tatizo la uhaba wa vifaa vya maktaba haliishii katika vitabu tu, bali hata aina nyengine za rasilimali kama zilivyoainishwa katika sura ya kwanza. Uhaba wa vitabu na vifaa vyengine vya maktaba husababishwa na ukosefu au mfuko mdogo wa serikali au wa skuli binafsi unaoelekezwa katika maktaba. Maktaba za skuli zimekuwa zikipangiwa fungu dogo ambalo halitoshelezi mahitaji halisi. Utafiti wa Omar (2010) unaonesha kuwa skuli nyingi zinazosimamiwa na serikali hutenga pajeti ndogo sana kwa ajili ya maktaba. Omar anaeleza kuwa takriban shilingi laki tatu 300,000 mpaka laki nne 400,000 hutengwa kama bajeti ya maktaba ya mwaka mzima na pesa hizo wakati mwengine hutumika kwa mahitaji mengine pindi haja inapotekea. Matokeo ya hali hii ni maktaba kuendelea kutegemea misaada ya vitabu kutoka nje ya nchi. Vitabu hivi huwa vimeandikwa kwa lugha za kigeni hasa kiingereza ambayo ni tatizo sugu kwa wanafunzi wengi wa

  • Abbas M. Omar 2013

    39

    Zanzibar na Tanzania kwa jumla. Lakini pia hata mtaala na maudhui yake hayalingani na ya kwetu. Tatizo hili kwa kiasi kikubwa sana hupelekea maktaba za skuli kupoteza hadhi yake inayostahiki kama kiungo muhimu katika maendeleo ya elimu.

    Wafanyakazi wa Maktaba za Skuli Maktaba nzuri ya skuli ni ile yenye mkutubi aliyepata mafunzo maalum kwa ajili ya kuhudumia wanafunzi na walimu, yeye ndie awezae kuitengeneza au kuiharibu maktaba. Skuli nyingi hususan zinazomilikiwa na serikali hazina wafanyakazi waliopata mafunzo. Licha ya sera ya Wizara ya elimu kuhusu maktaba za skuli kueleza kuwa kila skuli itakuwa na maktaba yenye vitabu vya kutosha na mkutubi aliyepata mafunzo (Sera ya Elimu ya Zanzibar, 2006). Suala la kutokuwepo kwa wafanyakazi wa maktaba waliopata mafunzo linathibitishwa na ripoti ya Shirika la Huduma za Maktaba Zanzibar (2006) inayoeleza kwa uwazi kuwa

    jukumu la kusimamia maktaba ya skuli huachiwa mwalimu moja au wawili ambao hawawezi tena

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    40

    kufundisha kwa sababu ya maradhi au hawana muda, shauku na wala hawajapata mafunzo ya aina yoyote juu ya maktaba.

    Ripoti hiyo inaendelea kueleza kuwa zipo baadhi ya skuli ambazo husimamiwa na wakutubi waliopatiwa mafunzo kupitia warsha na semina mbalimbali ambazo huandaliwa na Wizara ya elimu na Mafunzo ya Amali ikishirikiana na Shirika la Huduma za maktaba na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali na wafadhili mbalimbali. Jambo linakosekana ni ufuatiliaji wa utekelezaji wa mafunzo hayo katika maktaba za skuli zinazohusika. Baadhi ya skuli za binafsi zinaonekana kuajiri wafanyakazi wa maktaba waliopata mafunzo angalau katika ngazi ya cheti lakini bado wakutubi hao hawaonekani kupewa kipao mbele katika utekelezaji wa kazi zao. Wakutubi katika maktaba hizo huhesabiwa kama kwamba ni watu wa kusubiria wanafunzi kwenda katika vyumba vyao (maktaba) na kuazima vitabu tu (Omar, 2010) hali hii labda husababishwa na uwelewa mdogo wa umuhimu wa maktaba kwa wamiliki wa skuli hizo. Ripoti ya Benki ya dunia (2008) inaeleza kuwa

  • Abbas M. Omar 2013

    41

    Ingawa maktaba iliyohai huhitajika kwa kila skuli ya binafsi inayoomba usajili, bado hitajio hilo linaonekana kukosa makali na inaripotiwa kuwa madhali skuli itakuwa na dalili ya mlango wa chumba kinachoashiria kuwa ni maktaba hakuna ufuatiliaji wowote unaendelea kufanyika.

    Kukosekana kwa wakutubi wenye sifa za kuhudumia maktaba za skuli au kuwepo kwao bila kupewa kipaombele katika utendendaji wa kazi zao za kila siku huchangia kwa kiwango kikubwa matumizi madogo au kutokutumika kabisa kwa maktaba hizo miongoni mwa walimu na wanafunzi.

    Matumizi ya Maktaba za Skuli Maktaba hupoteza hadhi yake kama haitumiki kila siku. Ushirikiano baina ya walimu na wafanyakazi wa maktaba ndio hasa unaozifanya maktaba hizo kutoa huduma zake kwa ufanisi. Baadhi ya watu wanadhani kuwa kazi ya maktaba ya skuli ni kuazimisha vitabu kwa wanafunzi, na kazi ya mkutubi ni kugonga muhuri unaonesha tarehe ya kurudishwa kwa vitabu hivyo. Huu ni mtazamo potofu dhidi ya maktaba, ukweli ni kwamba kazi ya maktaba haiishii katika uazimishaji wa

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    42

    vitabu tu, na endapo maktaba itatumika kama tulivyoona hapo kabla, basi mkutubi ni mfanyakazi wa skuli anaetarajiwa kufanya kazi na kuchoka zaidi ya mwalimu wa somo mwenye vipindi vine au sita kwa siku moja. Kwa ufupi matumizi ya maktaba za skuli miongoni mwa walimu na wanafunzi kwa kiasi kikubwa hayaridhishi katika skuli zetu. Hebu kwa pamoja na tuangalie kwa kina ni kwa kiasi gani walimu na wanafunzi hutumia maktaba za skuli.

    Utumiaji wa Maktaba miongoni mwa Walimu Baadhi ya walimu hutumia maktaba, lakini walio wengi huishia kusoma kitabu kimoja kilichopendekezwa katika muhtasari wa somo hivyo hukosa muda kabisa angalau wa kwenda kuwasalimia wafanyakazi wa maktaba seuze kuazima kitabu cha ziada. Ripoti ya (Shirika la Huduma za Maktaba, 2006). Inaeleza kuwa Walimu wengi hawatumii maktaba, hivyo huwa na nafasi ndogo sana ya kuwashajihisha vijana juu ya matumizi ya maktaba.

  • Abbas M. Omar 2013

    43

    Baadhi ya walimu hufundisha kwa kutumia notisi zilizoandaliwa miaka mitano iliyopita bila ya kuzingatia mabadiliko ya mtaala na vitabu vya rejea. Kwa upande mwengine njia za kufundishia darasani huchangia kwa kiasi kikubwa matumizi duni ya maktaba ya skuli. Ndaki (2006) anaeleza kuwa badala ya waalimu hawazingatii kuwakuza vijana kujifunza wenyewe na kutafuta taarifa kupitia maktaba, walimu wengi hutoa notisi kwa vijana na njia ya ufundishaji huwa ni ya kuzungumza na ubao. Baadhi ya walimu hawazingatii kueleweka kwa mada bali husisitiza na hufundisha kujibu maswali ya mitihani iliyopita. Hili ni tatizo kubwa linalozikabili skuli zetu za sekondari na endapo hali hii itaendelea hakuna mwalimu wala mwanafunzi atakaeona haja ya kujifunza kwa kutumia maktaba. Katika zama za leo umezuka mtindo mpya wa kufundisha masomo ya ziada pamoja na kuanzisha kambi za wanafunzi muda wa mtihani unapokaribia badala ya kumkuza mwanafunzi kujisomea mwenyewe kwa kutumia maktaba na kudurusu masomo yake tokea mwaka mpya wa masomo unapoanza.

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    44

    Hizi ni baadhi ya kasoro zinazojitokeza katika njia za ufundishaji, ambazo kwa hakika hazimsukumi mwalimu hata kidogo kujianda kwa kusoma japo vitabu viwili kabla ya kuhudhurisha mada inayohusika. Miongoni mwa walimu wanaosomesha skuli za sekondari huwapa wanafunzi mada za kuwasilisha darasani kama njia ya kuwafanya wanafunzi hao kutumia maktaba, lakini bado njia hii haihakikishi matumizi ya maktaba kwa wanafunzi, wanafunzi bado huendelea kutegemea notisi kutoka kwa wanafunzi wenzao au vitabu vya masuali na majibu. Pamoja na yote hayo, zipo hoja zinazodaiwa kuwa katika hali ya kawaida hukwamisha ufanisi wa kazi za mwalimu na kumfanya kukosa mda wa kutembelea maktaba, miongoni mwazo ni; Idadi kubwa ya wanafunzi katika darasa moja Wingi wa vipindi kwa mwalimu mmoja Kuwepo kwa vitabu vya maswali na majibu na Tatizo la walimu wanaofundisha kwa muda

    maalumu (part time teachers)

  • Abbas M. Omar 2013

    45

    Mambo yote haya kwa kiasi fulani humkosa mwalimu muda wa kuandaa somo na kupitia vitabu kadhaa, muda wa kutembelea maktaba na muda wa kuandaa vipindi vya kutembelea maktaba, kuwashajihisha na kuwasimamia wanafunzi wanapokua maktaba.

    Utumiaji wa Maktaba miongoni mwa Wanafunzi Wanafunzi wengi wa skuli za msingi na sekondari katika skuli zenye maktaba hawatumii maktaba hizo. Kama ilivyoelezwa kabla, ikiwa walimu wao hawatumii maktaba je nani atakaewashajihisha wanafunzi kutumia maktaba? Tatizo la kukosekana kwa hamu ya kusoma miangoni mwa wanafunzi wa skuli ni mada inayozungumzwa sana na waandishi wengi. Omar (2010) ameeleza kuwa kukosekana kwa hamu ya kusoma ni tatizo maarufu miongoni mwa wanafunzi wa skuli na hata wa vyuo vikuu. Hamu ya kujifunza ndio hasa inayoibua hisia za matumizi ya maktaba. Hivyo mwanafunzi asiye na hamu ya kusoma hawezi kuhangaika na kutafuta taarifa kupitia maktaba na jambo hilo kwake huwa ndoto.

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    46

    Licha ya changamoto zinazozikabili maktaba za skuli bado wapo baadhi ya wanafunzi wanaotumia maktaba hizo ingawa idadi yao ni ndogo mno na hawaitumii kila siku. Wanafunzi hao husimamiwa na mkutubi tu bila ya mashirikiano yoyote kutoka kwa mwalimu yoyote. Na endapo atatokea mwalimu wa kuwapeleka maktaba na kuwasimamia wanafunzi wake, basi hali hiyo hutokea kutokana na hamu ya mwalimu binafsi na si kwa mkakati au utaratibu ulioandaliwa na skuli husika. Hatahivyo, wanafunzi kadhaa hupendelea kutumia maktaba ya umma iliopo maiosara Zanzibar. Wanafunzi wanaotumia maktaba ya umma ni wale wanaoishi maeneo ya karibu na maktaba hiyo, tatizo huendelea kuwepo kwa wanafunzi waishio maeneo ya mbali na maktaba hiyo ukizingatia kuwa ndani ya mji wa Zanzibar maktaba ya umma ipo moja tu.

  • Abbas M. Omar 2013

    47

    Wanafunzi wakijisomea katika maktaba kuu Zanzibar

    Idadi kubwa ya wanafunzi wanaotumia maktaba ya umma bado wanakabiliwa na tatizo la kutojua matumizi sahihi ya maktaba. Ngozani (1998) ameeleza kuwa ni dhahiri kuwa wengi miongoni mwa watumiaji wa maktaba ya umma hawana elimu ya matumizi ya maktaba kiasi kwamba baadhi yao hawajui hata maana ya katalogi ya maktaba seuze matumizi yake. Si katalogi tu, bali hata matumizi sahihi ya

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    48

    teknolojia ya kisasa ya mawasiliano kama vile intaneti yamekuwa ni kitendawili kigumu kwa wanafunzi kadhaa wa vyuo vikuu usizungumze kuhusu wanafunzi wa sekondari. Baadhi ya wanafunzi hutembelea maktaba kwa ajili ya kufanya mjadala (discussion) hali ya kuwa maktaba ni sehemu ya mtu kujisomea mwenyewe katika hali ya ukimya, ndio maana hakuna maktaba utayoingia usikutane na maandishi makubwa yanayokutaka kudumisha ukimya (silence please). Baadhi ya wanafunzi hutumia muda wao wa maktaba kwa kudurusu muhtasari (notes) waliopewa na mwalimu wao wa masomo. Na wengi wao huenda kuazima vitabu vya fasihi ya Kiswahili au ya kiengereza ambavyo hulazimika kuvisoma kwa ajili ya kujibia mtihani. Ununuzi wa vitabu si jambo rahisi miongoni mwa wanafunzi wengi wa Zanzibar kutokana na hali ya maisha, ingawa wapo baadhi yao hununua vitabu na kujisomea nyumbani. Hali hii huwafanya wanafunzi wengi kuendelea kutegemea muhtasari wa mwalimu au utoaji fotokopi/vivuli kwa baadhi ya kurasa za vitabu. Wanafunzi wengi hupendelea kujadili maswali ya

  • Abbas M. Omar 2013

    49

    mitihani ya taifa iliyopita na kubeza ufuatiliaji wa masomo yao wanayofundishwa darasani. Wanafunzi wengi hawapendi kujisumbua katika kusoma, akili zao mara nyingi huwaza mtihani kuliko kufahamu masomo, hivyo hata kama mwalimu atawashajihisha kutumia maktaba bado huwa ni jambo zito kwao, vyenginevyo alama maalum zitolewe kwa wale wataotumia maktaba. Kwa upande mwengine yapo mambo yanayorudisha nyuma utumiaji wa maktaba za skuli miongoni mwa wanafunzi. Kama vile; Uchakavu wa maktaba za skuli Upungufu wa vitabu na vilivyopo kupitwa na

    wakati Uchache wa vitabu katika lugha ya Kiswahili Uwepo wa vitabu kadhaa katika lugha ya

    kiengereza ambayo yenyewe ni tatizo kwa wanafunzi na

    Kukosekana kwa elimu ya maktaba Hutajwa kama sababu zinazowafanya wanafunzi kutokutumia maktaba za skuli. Kubwa zaidi jamii zetu hazikupata fursa ya kutosha kujenga utamaduni wa kujisomea tokea utotoni.

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    50

    Jukumu la kumkuza mwanafunzi kuwa na tabia ya kujisomea mwenyewe linabaki kwa wazazi na walimu. Lakini kwa bahati mbaya wazazi wengi hawana tabia na muamko wa kujisomea hivyo huwa na nafasi ndogo mno ya kukaa na watoto wao angalau kuwasomea hadithi katika vitabu. Kwa hivyo, wakati umefika kwa wazazi kubadilika na kuwahimiza watoto kudurusu na kujisomea masomo yao kupitia maktaba.

  • Abbas M. Omar 2013

    51

    HITIMISHO Kumkuza mwamafunzi katika tabia ya kujisomea na kujifunza mwenyewe ni zana muhimu sana katika kufikia mafanikio ya kitaaluma. Maktaba za skuli ni kiungo muhimu mno katika kuleta mabadiliko na maendeleo ya elimu nchini. Ndio msingi wa kuwatayarisha wanafunzi wanaopenda kujisomea na kutafuta taarifa mbalimbali zinazohusu maendeleo ya mwanadamu na dunia kwa jumla. Umuhimu wa maktaba za skuli huonekana pale tu endapo maktaba hizo zitakuwa na vitabu vya kutosha ambavyo vinaendana na haja ya watumiaji wake. Si vitabu tu, bali hata vifaa vyengine vya kisasa vitumikavyo katika zoezi zima la kujifunza na kufundisha. Maktaba nzuri husifika kutokana na huduma zake. Huduma hizo ni kuazimisha vitabu, kutoa taarifa na ushauri, kukuza tabia ya kujisomea nakadhalika. Huduma hizo hutegemea sana mhudumu anaehudumia maktaba hiyo. Mkutubi mzuri ni yule aliyepata mafunzo ya kusimamia na kuendeleza maktaba. Kutokana na taaluma aliyonayo hushirikiana na walimu

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    52

    na uongozi wa skuli katika kuleta ufanisi na maendeleo ya huduma za maktaba. Katika hali kama hii ndipo tunapoweza kuona matunda halisi ya maktaba za skuli. Hali haiko hivi katika skuli zetu, mazingira yasiyoridhisha, uhaba wa vitabu na vifaa vyengine vya maktaba, kukosekana kwa wafanyakazi wa maktaba waliopata mafunzo na kutokuwepo kwa mashirikiano baina ya wakutubi, walimu na mamlaka husika na hatimaye kutokutumika ipasavyo kwa maktaba hizo, huzifanya maktaba za skuli kupoteza haiba, sifa na hadhi yake katika kuleta mabadiliko na maendeleo katika sekta ya elimu. Hali hii hupelekea kukosekana kwa msingi madhubuti wa elimu na tabia ya kutumia maktaba kwa wanafunzi wamalizao elimu ya sekondari ambao wanatarajia kuendelea na elimu ya juu katika vyuo vikuu na hatimaye kuwa wasomi wanaotegemewa katika kuleta maendeleo ya kweli nchini. Omar (2010) anaeleza kuwa wanafunzi wengi humaliza skuli katika ngazi ya sekondari wakiwa hawana hata taaluma ya msingi juu ya matumizi ya maktaba, hali hii huwafanya kushindwa

  • Abbas M. Omar 2013

    53

    kuitumia maktaba endapo wapatapo fursa ya kuendelea na masomo ya chuo kikuu. Ikiwa hali halisi iko hivyo suali moja tunaweza kujiuliza je, ni wasomi wa aina gani tunaotarajia ambao hata matumizi ya katalogi ya maktaba ni tatizo kwao usizungumzie kutahmini, kuchambua, kunukuu mawazo ya wataalamu na hata kuandika rejea ya kitabu (reference).

    MAPENDEKEZO Mambo kadhaa yametajwa katika kitabu hiki kama ni vikwazo vya maendeleo ya maktaba za skuli nchini. Ikiwa vikazo hivyo havitatauliwa, matumizi na maendeleo ya maktaba za skuli yatabaki kuwa ndoto. Yafuatayo ni maeneo muhimu yanayohitaji kushughulikiwa ili kusawazisha hali iliyopo sasa katika maktaba za skuli. Moja, nguvu za ziada zielekezwe katika maendeleo ya vifaa vya skuli na msisitizo uwekwe katika vifaa vya kisasa vya kufundushia kama vile redio, CD, DVD, televisheni, video na komputa ikiwezekana hata huduma za intaneti ziwepo katika maktaba za skuli. Hii

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    54

    itasaidia kuziba pengo la uchache wa vitabu na tatizo la vitabu vilivyopitwa na wakati. Pia matumizi ya intaneti yatasaidia kuwatayarisha wanafunzi katika matumizi ya teknologia ya kisasa ya habari na taarifa. Pili, Wizara ya Elimu Mafunzo ya Amali ikishirikiana na Shirika la Huduma za Maktaba iandae waraka maalumu utakaoonesha thamani na umuhimu wa matumizi ya maktaba katika kufundisha na kujifunza. Waraka huo utaeleze kwa uwazi mpangilio mzima wa uendeshaji, usimamiaji na utoaji wa huduma za maktaba kwa wanafunzi. Hii itasaidia utekelezaji wa sera ya elimu kuhusu maktaba. Tatu, Shirika la Huduma za Maktaba kwa usaidizi wa Wizara ya Elimu Mafunzo ya Amali ziandae mafunzo maalumu kwa ajili ya wafanyakazi wa maktaba za skuli ili kuongeza uwezo wa wahudumu wa maktaba na kushajihisha matumizi ya maktaba kwa walimu na wanafunzi. Kwa maana hiyo, Wizara ya Elimu Mafunzo ya Amali iajiri wakutubi waliopata mafunzo maalum ya kusimamia maktaba za skuli. Katika miaka michache iliyopita haikua jambo rahisi kuwapata watu wa aina hii kutokana na uchache wao na pengine kutotiliwa

  • Abbas M. Omar 2013

    55

    maanani fani ya ukutubi. Lakini katika wakati tulionao Zanzibar pekee ina wakutubi kadhaa waliopata mafunzo katika ngazi ya cheti, diploma, shahada ya kwanza hata shahada ya pili na jambo la kutia moyo zaidi, taaluma hii inatolewa hapahapa katika vyuo vikuu vya nyumbani. Nne, ipo haja ya kujengwa maktaba za umma katika kila mkoa miongoni mwa mikoa ya Zanzibar ili kurahisisha na kutoa fursa kwa kila mwanafunzi na mwanajamii kutumia na kufaidika na huduma za maktaba. Tano, skuli ziandae programu na ratiba maalumu zitakazohusisha vipindi vya masomo kupitia matumizi ya maktaba na kila mwalimu atalazimika kuwapeleka wanafunzi wake maktaba wakiwa chini ya uangalizi wake na kwa msaada wa mkutubi, utaratibu huu utasaidia sana kujenga tabia ya matumizi ya maktaba kwa wanafunzi. Sita, mashindano ya uandishi wa insha na mijadala juu ya umuhimu wa maktaba baina ya wanafunzi wa skuli moja na nyengine yaandaliwe. Hii itapelekea utambuzi

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    56

    wa uwepo, huduma zake na umuhimu wa matumizi ya maktaba kwa wanafunzi. Saba, skuli ziandae utaratibu wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wanaotumia maktaba kikawaida. Hii itasaidia kuhuisha na kuamsha hamu, shauku na ari ya wanafunzi juu ya matumizi ya maktaba. Nane, mashirikiano baina ya walimu, wafanyakazi wa maktaba ya skuli na uongozi wa juu wa skuli yaimarishwe. Kama ilivyoelezwa hapo kabla kuwa kila skuli inapaswa kuwa na kamati ya maendeleo ya maktaba. Mashirikiano haya yatasaidia kurahisisha utendaji wa kazi kwa wafanyakazi wa maktaba na hatimaye kila mmoja atapata hisia kuwa ana dhima kubwa ya kuendeleza maktaba ya skuli na kumkuza mwanafunzi kujisomea kwa kutumia maktaba hiyo. Mwisho, wanafunzi walioko vyuo vikuu wanaochukua stashahada, diploma na shahada katika fani ya ualimu, wapatiwe mafunzo ya maktaba na wafunzwe jinsi ya kuwafundisha na kuwahamasisha wanafunzi kujisomea kupitia maktaba. Utaratibu huu utasaidia sana katika kuwafanya walimu watarajiwa kujua umuhimu na kazi

  • Abbas M. Omar 2013

    57

    za maktaba, hivyo utaamsha hamasa kwa walimu hawa juu ya kuwakuza wanafunzi katika matamumizi ya maktaba na tabia ya kuendelea kujifunza wenyewe.

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    58

    REJEA Ali, Z. M. (2004). An Evaluation of the Capacity of Secondary School Library in Providing Services to Teachers and Students. Unpublished Research Paper of Nkrumah Teachers training College. Baird, N. (1994) Setting Up and Running a School Library. Heinemann Education, Ibadan Chowdhury, D. D. et al (2008) Librarianship: an introduction. Facet Publishing. London. Felix K. T. na P.A. L. (2005). Tafsiri ya Kiswahili ya Ilani ya Maktaba za Skuli iliyotolewa na IFLA/UNESCO. Imepatikana tarehe 20 Juni, 2010 katika tovuti; http://ifla.queenslibrary.org/VII/s11/pubs/manifesto-sw.html Kumar, K. (1987). Library Organization. Vikas Publication. New Delhi. Kumar, S. (1997). Problems of School Libraries in Present Day Education: some Observation and

  • Abbas M. Omar 2013

    59

    Solutions. Annals of Library Science and Documentation, Vol 44, No4, pp. 140-152. Ndaki, J. M. (2006). Factors Contributing to Poor Reading Habits and Ineffective Use of Library Services Among Secondary School Students. A case study of secondary school students in Tabora Municipality. Unpublished dissertation of the University of Dar es Salaam. Tanzania Ngozani, A. N. (1998). The Provision of Urban Library Services: Case Study of Zanzibar Central Library. Unpublished Research Report of the School of Library, Archives and Documentation Studies. Tanzania Omar, A. M. (2010). The Role Of Teachers Infostering Students Independent Learning Through School Library Use. A Case Of Selected High Schools In Zanzibar. Unpublished Dissertation of the University of Dar es Salaam. Tanzania Revolutionary Government of Zanzibar. Ministry of Education and Vocational Training (2006). Zanzibar Education Policy

  • Maktaba za skuli hazina iliyosahauliwa

    60

    World Bank (2008). Text books and School Library Provision in Secondary Education in Sub-Saharan Africa. Africa Human Development Series. World Bank Working Paper No. 126. pp. 71- 80. Imepatikana tarehe 15 May, 2010 katika tovuti; http://siteresources.worldbank.org/INTAFRREGTOPSEIA/Resources/OtherTextbooks.pdf

  • Abbas M. Omar 2013

    61

    Abbas Mohamed Omar alipitia mfumo rasmi wa elimu ya Tanzania kuanzia skuli ya msingi hadi sekondari. Mnamo mwaka 2005 alijiunga na Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro na kufanya shahada ya kwanza katika fani ya Ualimu. Mwaka 2008 aliendelea na masomo katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuchukua shahada ya pili

    katika fani ya ukutubi. Kwa sasa ni mkutubi katika Maktaba ya Chuo Kikuu cha Zanzibar. Maktaba za skuli ni kiongo muhimu sana katika kuleta mabadiliko na maendeleo ya elimu nchini. Umuhimu wa maktaba hizo huonekana pale tu endapo maktaba hizo zitakuwa na vifaa vya kutosha ambavyo vitaendana na haja ya watumiaji wake. Sifa ya maktaba iliyo hai ni kutumika kila wakati. Na maktaba nzuri husifika kutokana na huduma bora zitolewazo na wakutubi waliopata mafunzo maalum. Katika hali kama hii ndipo tunapoweza kuona matunda halisi ya maktaba za skuli. Hali haiko hivi katika skuli zetu, mazingira yasiyoridhisha, uhaba wa vitabu na vifaa vyengine vya maktaba, kukosekana kwa wafanyakazi waliopata mafunzo ya kuhudumia maktaba na mashirikiano hafifu baina ya wakutubi, walimu na uongozi hupelekea kutokutumika ipasavyo kwa maktaba hizo. Hali hii, huzifanya maktaba za skuli kupoteza haiba, sifa na hadhi yake katika kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu nchini.