MEM 106 Online.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

  • Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    Habari za nisHati &madini

    Toleo No. 106 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Februari 11 - 17, 2016

    BulletinNews

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    http://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI &MADINI

    Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

    JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

    Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

    Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

    Wabunge Soma habari Uk. 2

    Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

    WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

    Soma habari

    Uk. 3Mameneja Tanesco Kanda wasiotimiza maagizo kuondolewa

    Mgodi North Mara kuundiwa kamati

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa nne kushoto) na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (wa tatu Kulia) wakizungumza na wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara (hawapo pichani) wilayani Tarime mkoa wa Mara wakati Profesa Muhongo alipofanya ziara ya kikazi katika maeneo yanayozunguka mgodi huo wilayani Tarime. Wa Pili kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini-Leseni, Mhandisi John Nayopa, na wa Tatu kushoto ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.

  • 2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Teresia Mhagama, Tarime

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameeleza kuwa Serikali itaunda

    Kamati itakayotathmini kero zinazolalamikiwa na wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara ambapo majina ya Kamati hiyo yatawasilishwa kwake tarehe 12 Februari 2016.

    Waziri wa Nishati na Madini alitoa maamuzi hayo akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Tarime iliyolenga kutatua kero za wananchi hao ambapo kabla ya kutoa msimamo huo wa Serikali alizungumza na makundi mbalimbali ikiwemo wananchi,

    viongozi wa wananchi wakiongozwa na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo.

    Ndugu zangu, baada ya kuwasikiliza wananchi ambao walieleza kero zao na baadaye kukutana na mgodi na kuwaeleza malalamiko ya wananchi ambayo mengine wameyakubali na mengine kuyakataa. Ili kutatua suala hili kwanza lazima tuunde Kamati itakayoangalia kwa undani sehemu zinazolalamikiwa na kupata vielelezo kabla ya kufanya maamuzi yoyote, alisema Profesa Muhongo.

    Alisema Kamati hiyo itaundwa na wajumbe kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika Idara ya Madini, Mwakilishi wa Mbunge wa Tarime Vijijini, viongozi wa Vijiji na Vitongoji vinavyozunguka mgodi huo na Baraza

    la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC).

    Aliongeza kuwa Kamati hiyo pia itajumuisha Ofisa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wawakilishi wa mgodi wa Acacia North Mara, Wizara ya Uvuvi, Kilimo na Mifugo, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Ofisi ya Tarime na Ofisa kutoka Ofisi ya Madini Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi.

    Tarehe 12 Saa Nne asubuhi tunataka majina ya Kamati hii yawasilishwe ndipo tutakapopanga Kamati hii ifanye kazi kwa muda gani na watu watakaowekwa kwenye Kamati hii wasibadilike badilike ili kutopunguza ufanisi wa kazi hii, alisema Profesa Muhongo.

    Profesa Muhongo alitaja baadhi ya kero kubwa zinazolalamikiwa na wananchi na ambazo Kamati hiyo inapaswa kufanyia kazi kuwa ni suala la ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha mgodi huo wa dhahabu ambao walimweleza Waziri wa Nishati na Madini kuwa hawakuridhishwa na tathmini iliyofanywa hapo awali na Serikali na Mgodi kwani ilipelekea wananchi kulipwa fidia kidogo tofauti na matarajio yao.

    Aliongeza kuwa, Kamati hiyo pia inapaswa kufanya tathmini ya Usalama ili kubaini kama tuhuma zinazotolewa na wananchi kwa Jeshi la Polisi za kuwamwagia wananchi maji ya washawasha na watu kuuawa katika mgodi huo ni za kweli au la na kama ni za kweli Kamati iwasilishe vielelezo na idadi ya wananchi waliouawa katika mgodi huo.

    Vilevile, Kamati hiyo imetakiwa kufanya tathmini ya ajira ili kufahamu idadi na aina ya ajira zilizotolewa na Mgodi kwa wananchi wanaozunguka Mgodi, Idadi ya vijana wasiokuwa na

    ajira na jinsi Halmashauri ya Wilaya ya Tarime inavyotumia pesa zinazotolewa na mgodi za Ushuru wa huduma katika kusaidia vijana wa Tarime.

    Kamati pia iainishe fursa za kibiashara zinazopatikana katika mgodi na vigezo vyake na Mbunge awe na idadi ya Watu wanaoweza kufanya biashara na mgodi kama za usafiri, chakula na nyinginezo ili tunapotoa maagizo kwa Mgodi huu tuwe tumejiridhisha na huduma tunayotaka kutoa kwao, alisema Profesa Muhongo.

    Masuala mengine ambayo Kamati hiyo inapaswa kutathmini na kutoa mrejesho, ni madai ya athari za kiafya walizopata wananchi kutokana na shughuli za mgodi na kuwasilisha majina ya waathirika, kutambua na kuorodhesha majina ya wamiliki wa nyumba zinazodaiwa kujengwa

    ndani ya eneo la mgodi wa Acacia kwa matarajio ya kupata fidia na kuorodhesha kesi mbalimbali ambazo Mgodi husika umewashtaki wananchi kwa madai mbalimbali na kesi ambazo wananchi hao wamefungua dhidi ya mgodi huo.

    Aidha, Kamati pia imetakiwa kutoa mapendekezo ya mradi ambao utaweza kuanzishwa na Mgodi kwa ajili ya wananchi wanaozunguka Mgodi huo ili unapomaliza shughuli za uchimbaji baada ya miaka 6 ijayo wananchi wabaki na mradi ambao utawaendeleza kiuchumi na kuwapatia ajira.

    Awali, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche alimshukuru Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kulipa kipaumbele suala hilo la kutatua changamoto wanazokutana nazo wananchi wanaozunguka mgodi wa Acacia North Mara kwani Profesa Muhongo aliahidi Bungeni kuwa atafika wilayani Tarime ili kujionea athari hizo na ametimiza ahadi yake.

    Mgodi North Mara kuundiwa kamati

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akitia saini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili wilayani Tarime mkoa wa Mara kwa ziara ya kikazi katika maeneo yanayozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara wilayani humo. Kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga. Wa Kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi wa Madini-Leseni, John Nayopa, na kulia kwake ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.

    Baadhi ya Wananchi wanaozunguka mgodi wa Dhahabu wa Acacia North Mara wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani ) wakati alipofanya mazungumzo na wananchi hao wilayani Tarime, mkoa wa Mara.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (wa pili kulia) akiwa katika moja ya eneo linalozunguka mgodi wa Dhahabu wa Acacia North Mara ili kukagua athari ambazo zinadaiwa kusababishwa na mgodi katika eneo hilo. Kulia kwa Waziri ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

  • 3BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    Five Pillars oF reForms

    KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano

    Bodi ya uhariri MharIrI Mkuu: Badra Masoud

    MsaNIFu: Lucas GordonWaaNdIshI: Veronica simba, asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed saif, rhoda James ,

    Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

    increase eFFiciencyQUality delivery

    oF Goods/servicesatisFaction oF

    tHe clientsatisFaction oF

    BUsiness Partners

    satisFaction oF sHareHolders

    tel-2110490FaX-2110389

    moB-0732999263

    Hongera Profesa Muhongo kwa kujali Kero za Wananchi North Mara

    tel-2110490FaX-2110389

    moB-0732999263

    Mameneja Tanesco Kanda wasiotimiza maagizo kuondolewa Machi 1

    Hivi karibuni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alifanya ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia Mining ulioko Tarime mkoani Mara ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wananchi wanaozunguka mgodi huo.

    Lengo la ziara yake lilikuwa ni kubaini kero zinazolalamikiwa na wananchi wanaozunguka mgodi huo. Mara baada ya kuwasili katika mgodi huo, Profesa Muhongo alizungumza na makundi mbalimbali ikiwemo wananchi, viongozi wa wananchi wakiongozwa na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo.

    Kati ya kero zilizowasilishwa na makundi hayo ni pamoja na ulipwaji wa fidia ndogo kwa wananchi waliopisha mgodi huo wa dhahabu ambao walimweleza Waziri wa Nishati na Madini kuwa hawakuridhishwa na tathmini iliyofanywa hapo awali na Serikali na Mgodi kwani ilipelekea wananchi kulipwa fidia kidogo tofauti na matarajio yao, upendeleo katika ajira, unyanyasaji unaofanywa na Jeshi la Polisi pamoja na athari za kiafya na mazingira walizozipata wakati wa uendeshaji wa mgodi.

    Mara baada ya kukutana na wananchi Profesa Muhongo alikutana na uongozi wa Mgodi wa North Mara ambapo ili kubaini uhalali wa malalamiko hayo, ambapo mengine waliyakubali na mengine kuyakataa.

    Kufuatia hatua hiyo, Profesa Muhongo alielekeza kuundwa kwa Kamati itakayoangalia kwa undani sehemu zinazolalamikiwa na kupata vielelezo kabla ya kufanya maamuzi yoyote, ambapo majina ya Kamati hiyo yatawasilishwa kwake tarehe 12 Februari 2016.

    Profesa Muhongo alisema Kamati hiyo itaundwa na wajumbe kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika Idara ya Madini, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mwakilishi wa Mbunge wa Tarime Vijijini, viongozi wa Vijiji na Vitongoji vinavyozunguka mgodi huo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC).

    Aliongeza kuwa Kamati hiyo pia itajumuisha Ofisa wa Maji na Mtathmini kutoka Halmashauri ya Tarime, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wawakilishi wa Mgodi wa North Mara, Wizara ya Uvuvi, Kilimo na Mifugo, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Ofisi ya Tarime na Ofisa kutoka Ofisi ya Madini Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi.

    Aliongeza kuwa, Kamati hiyo pia inapaswa kufanya tathmini ya Usalama ili kubaini kama tuhuma zinazotolewa na wananchi kwa Jeshi la Polisi za kuwamwagia wananchi maji ya washawasha na watu kuuawa katika mgodi huo ni za kweli au la na kama ni za kweli Kamati iwasilishe vielelezo na idadi ya wananchi waliouawa katika mgodi huo.

    Vilevile, Kamati hiyo ilitakiwa kufanya tathmini ya ajira ili kufahamu idadi na aina ya ajira zilizotolewa na Mgodi kwa wananchi wanaozunguka Mgodi, Idadi ya vijana wasiokuwa na ajira na jinsi Halmashauri ya Wilaya ya Tarime inavyotumia pesa zinazotolewa na mgodi za ushuru wa huduma katika kusaidia vijana wa Tarime.

    Masuala mengine ambayo Kamati hiyo inapaswa kutathmini na kutoa mrejesho, ni madai ya athari za kiafya walizopata wananchi kutokana na shughuli za mgodi na kuwasilisha majina ya waathirika, kutambua na kuorodhesha majina ya wamiliki wa nyumba zinazodaiwa kutegwa ndani ya eneo la mgodi wa North Mara kwa matarajio ya kupata fidia na kuorodhesha kesi mbalimbali ambazo Mgodi husika umewashtaki wananchi kwa madai mbalimbali na kesi ambazo wananchi hao wamefungua dhidi ya mgodi huo.

    Aidha, Kamati hiyo ilitakiwa kutoa mapendekezo ya mradi ambao utaweza kuanzishwa na Mgodi kwa ajili ya wananchi wanaozunguka Mgodi huo ili unapomaliza shughuli za uchimbaji baada ya miaka 6 ijayo wananchi wabaki na mradi ambao utawaendeleza kiuchumi na kuwapatia ajira.

    Tunachukua fursa hii kumpongeza Profesa Muhongo kwa kulipa kipaumbele suala hilo la kutatua changamoto wanazokutana nazo wananchi wanaozunguka mgodi wa North Mara kwani Profesa Muhongo aliahidi Bungeni kuwa atafika wilayani Tarime ili kujionea athari hizo na ametimiza ahadi yake.

    Na Teresia Mhagama, Mtera

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameeleza kuwa Mameneja wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)

    wanaosimamia Kanda mbalimbali nchini wataondolewa katika vyeo hivyo iwapo hawatatimiza maagizo mbalimbali waliyopangiwa na Wizara ya Nishati na Madini ifikapo Machi 1 mwaka huu.

    Waziri wa Nishati na Madini alisema hayo wakati wa kikao chake na watendaji wa TANESCO na Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini kilichofanyika katika Kituo cha kuzalishia umeme cha Mtera.

    Profesa Muhongo alitaja maagizo hayo kuwa ni pamoja na kuunganisha umeme kwa wateja wengi, kuwa na makusanyo makubwa ya bili za umeme, kupunguza manunguniko ya wananchi katika huduma za umeme na

    uboreshaji wa mawasiliano kati ya Shirika hilo na wananchi.

    Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, ifikapo Machi Moja mwaka huu atatuthibitishia kama Mameneja hawa wataendelea na majukumu haya wanayoyasimamia ama la na hii itatokana na ufanisi wa utendaji katika majukumu tuliyowapangia, alisema Profesa Muhongo.

    Aidha, Waziri wa Nishati na Madini alisema kuwa Kitengo cha Uwekezaji cha Tanesco kama hakitakuwa na miradi mipya ya umeme ifikapo tarehe 2 Aprili mwaka huu, watendaji katika Ofisi hiyo wataondolewa katika nafasi hiyo kwa kushindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo.

    Hapa hatuna mzaha kwani mahitaji ya umeme ni makubwa na tuna miradi mingi ya usambazaji umeme kwa wananchi ikiwemo miradi ya REA. Wananchi wanahitaji umeme kwa matumizi ya majumbani na kuanzisha

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (aliyesimama) akizungumza na watendaji mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zilizo chini ya Wizara wakati wa kikao chake na Watendaji hao kilichofanyika katika Kituo cha kuzalishia umeme cha Mtera. Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani na kutoka kushoto (mstari wa mbele) ni Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Norbert Kahyoza, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.

    >>Inaendelea Uk. 4

  • 4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Asteria Muhozya

    Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limesema kuwa, taratibu za kupata Kampuni ya kufanya Utafiti wa Vitalu vya mafuta na gesi

    kwa kutumia teknolojia ya Airborne Gravity Gradiometry ilifuata sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2013.

    Taarifa ya TPDC inafuatia habari ya upotoshaji iliyotolewa na Gazeti la Mtanzania la Jumapili tarehe 7 Februari, 2014 Toleo Na: 8087 lenye kichwa cha habari TPDC kwafukuta, ambapo taarifa ya gazeti hilo ilieleza kuwa, mwenendo wa upatikanaji wa kampuni ya utafiti wa mafuta na gesi ulioendeshwa na shirika hilo umeanza kulalamikiwa na baadhi ya watumishi wa TPDC.

    Aidha, taarifa ya MTANZANIA

    iliongeza kuwa, utaratibu wa kuipata kampuni ya utafiti wa vitalu vya mafuta na gesi haukuzingatia taratibu za manunuzi ya umma na kwamba uliingiliwa na viongozi wa juu wa TPDC.

    TPDC inakanusha vikali kuwepo kwa shinikizo kutoka kwa Mtu au Taasisi yoyote katika kufanikisha zoezi hili. Shirika linasisitiza kuzingatiwa kwa utaratibu wa sheria za manunuzi. Watanzania zipuuzeni taarifa hizo ni za uzushi na upotoshaji mkubwa, ilisisitiza taarifa hiyo ya TPDC.

    Ikifafanua ukweli wa jambo hilo kwa umma, taarifa ya TPDC inaeleza kuwa, zoezi zima la kutafuta mkandarasi lilikuwa la wazi na lilihusisha kampuni tatu ambazo ni Bell Geospace ya Marekani, CGG ya Ufaransa na ARKEX ya Uingereza ambazo ndizo kampuni pekee zenye uwezo wa kutumia teknolojia ya

    Airborne Gravity GradiometryAirbone Gravity Gradiometry

    ina gharama nafuu, inachukua eneo kubwa la utafutaji na kwa kipindi kifupi sana. Ni aina ya teknolojia inayotafiti maeneo mapya ya utafutaji na yale ambayo tayari yameshaonyesha dalili nzuri za utafutaji wa hapo awali, iliongeza taarifa hiyo,.

    Aidha, TPDC katika taarifa yake ilieleza kuwa, kutokana na kuwepo kwa kampuni tatu tu duniani zenye utaalamu uliohitajika, Shirika liliwasiliana na kampuni husika kwa mujibu wa kanuni ya manunuzi ya umma ya mwaka 2013 namba 152(1) (b) ili kuwasilisha taarifa za kiufundi na kifedha kwa TPDC.

    Aidha, taarifa ya TPDC iliongeza kuwa, baada ya taratibu hizo za manunuzi kufanyika na kutokana na tathmini iliyofanyika, Kampuni ya CGG ndiyo iliyopewa kazi ya

    kufanya utafiti maeneo ya Eyasi Wembere iliyopo Manyara, na Mandawa Mkoani Lindi wakati Lake Tanganyika North iliyopo Kigoma, ilifanywa na kampuni ya Bell Geospace.

    TPDC ni Shirika la Umma, linalomilikiwa kwa asilimia100 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo taratibu za kuliendesha Shirika hufuata sheria, taratibu na kanuni za nchi, iliongeza taarifa hiyo.

    Vilevile taarifa ya TPDC iliwataka wadau wote wa sekta ndogo ya mafuta kuendelea kufanya kazi za utafiti, utafutaji na uendelezaji wa sekta nzima ya gesi asilia na kuongeza kuwa, tunapenda kuutaarifu umma kuwa, taarifa iliyochapishwa katika gazeti la Mtanzania sio kweli.

    TPDC :Taratibu za Utafiti Vitalu vya Mafuta, Gesi vilifuata sheria

    viwanda vidogo vidogo, sasa bila miradi mipya ya umeme tutashindwa kusambaza umeme kwa wananchi hawa kwa kuwa kiasi cha umeme tulichonacho sasa bado hakitoshi, alisema Profesa Muhongo.

    Profesa Muhongo pia aliwaasa Mameneja wa TANESCO wa Kanda kuwakaribisha wawekezaji mbalimbali wa umeme ikiwemo miradi midogo ya uzalishaji umeme wa maji ili nchi iwe na umeme wa kutosha badala ya kuwakatisha tamaa wawekezaji hao.

    Vilevile, Profesa Muhongo alisema kuwa watumishi watakao kuwa na urasimu katika kujadili masuala ya uwekezaji wa nishati wataachia ngazi kwa kuwa ndio wanaokwamisha juhudi za serikali katika kuongeza kiasi cha umeme nchini.

    TANESCO na EWURA kuanzia sasa pale anapojitokeza mwekezaji wa miradi ya umeme lazima mjadiliane naye kwa pamoja badala ya mwekezaji husika kwenda TANESCO baadaye anaenda EWURA au TPDC hivyo mwekezaji anapokuja jadilini naye kwa pamoja ili msitumie muda mrefu katika utekelezaji wa suala moja na hivyo kuchelewesha utekelezaji wa miradi mbalimbali, alisema Profesa Muhongo.

    Vilevile Profesa Muhongo aliwaagiza watendaji wa TANESCO katika vitengo vya ukaguzi kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa ikiwemo usimamizi madhubuti wa nguzo za umeme ambazo baadhi huanguka kila inapofika msimu wa mvua na kusema kuwa suala hilo halikubaliki.

    Mameneja Tanesco Kanda wasiotimiza maagizo kuondolewa Machi 1>>INATOKA Uk. 3

    Watendaji mbalimbali wa Taasisi zilizo chini ya Wizara wakiwa kwenye kikao na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) kilichofanyika katika Kituo cha kuzalishia umeme cha Mtera. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mkondo wa Chini kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Dkt. Wellington Hudson, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, Mkurugenzi wa Umeme, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mhandisi Anastas Mbawala na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi.

  • 5BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Mmoja wa wazalishaji wa umeme wa maji, chini ya megawati 20, Emmanuel Shaban kutoka Misheni ya Kabanga mkoani Kigoma, akielezea mradi wa uzalishaji wa umeme wa maji wa kiasi cha kilowatt 90 unaotekelezwa na Misheni hiyo ambao unafaidisha shule ya watu wenye walemavu, Chuo na baadhi ya familia katika eneo hilo.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo katika kikao chake na wazalishaji wa umeme wa maji na wale wanaotaka kuzalisha umeme huo chini ya megawati 20 kilichofanyika katika Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Mtera. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Juliana Pallangyo.

    Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza (mwenye nguo nyekundu) akizungumza jambo wakati wa kikao na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto kwa Mkuu wa Mkoa) kilichofanyika katika kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera mkoani Dodoma ambacho kilijumuisha

    Na Teresia Mhagama, Mtera

    Imeelezwa kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ambayo wananchi wameamua kuiendeleza ikiwemo

    miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali kama maji, gesi, upepo, jua, nishati jadidifu, makaa ya mawe na mawimbi ya bahari.

    Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa kikao chake na wazalishaji wa umeme wa maji na wale wanaotaka kuzalisha umeme huo chini ya Megawati 20, kilichofanyika katika Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Mtera.

    Serikali lazima iwe ni msemaji wa wawekezaji hawa ili kuhakikisha wanapata fedha na teknolojia za kuendesha miradi yao na hii itapelekea Taifa kuwa na nishati ya kutosha kwani wawekezaji hawa sasa watakuwa na

    uwezo wa kuzalisha umeme, alisema Profesa Muhongo.

    Ili kutekeleza jambo hili kwa ufanisi, Profesa Muhongo aliwataka wadau hao wanaotaka kuzalisha umeme wa maji chini ya megawati 20 kuhakikisha kuwa wanaandika na kuwasilisha wizarani mapendekezo yanayochanganua miradi wanayotaka kuanzisha kabla ya mwisho wa mwezi Februari, 2016, ili litengenezwe kabrasha moja litakalotumika katika kutafutia fedha kwa wafadhili mbalimbali na Taasisi za Kifedha.

    Ifikapo tarehe 28 mwezi huu mchanganuo wa mapendekezo yenu yawe yamemfikia Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati ili serikali iangalie namna ya kutafuta fedha zitakazowawezesha kuendeleza miradi yenu ya umeme badala ya mtu mmoja mmoja kuanza kuzunguka na maombi yake binafsi ya kupata fedha kutoka Taasisi mbalimbali, jambo linalochelewesha upatikanaji wa fedha hizo, alisema Profesa Muhongo.

    Aidha, Profesa Muhongo alisema

    kuwa tayari serikali imeshaanza majadiliano na Taasisi za kifedha kama Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Benki ya Dunia (WB) na nchi wahisani kwa ajili ya kupata fedha za kuendeshea miradi mbalimbali ikiwemo ya Nishati ambapo alisema kuwa suala hilo litafanyika kwa ufanisi endapo miradi yote inayoombewa fedha itajumuishwa katika kabrasha moja litakaloainisha miradi yote inayohitaji kuendelezwa.

    Waziri wa Nishati na Madini alisema kuwa, hivi sasa serikali inazalisha umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwemo gesi asilia (50%), maji (35%), na mafuta mazito (15%) na kueleza kuwa Tanzania bado ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme ambavyo vinahitaji wawekezaji makini ikiwemo upepo, joto ardhi, makaa ya mawe na jua ili nchi iwe na umeme wa uhakika, unaotabirika na wa bei nafuu.

    Ndugu zangu tunapaswa kutekeleza miradi hii ya nishati kwa kasi kubwa kwani Tanzania ni nchi mwanachama wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Nishati Endelevu kwa Wote (SE4ALL) ambao unaelekeza kwamba ifikapo mwaka 2030 kila mtu anapaswa kuwa na nishati ya umeme na sisi Tanzania ndio tuliwakilisha nchi za Afrika kutengeneza Mpango huo, alisema Profesa Muhongo.

    Alisema kuwa malengo makuu ya Mpango wa SEA4ALL ni upatikanaji wa nishati kwa wote ifikapo mwaka 2030, ongezeko maradufu la utumiaji wa nishati jadidifu na matumizi bora ya

    nishati.Profesa Muhongo alisema kuwa

    tayari ameshatia saini Mpango huo ambao utaiwezesha Tanzania kufaidika na fedha zitakazotolewa ili kuendeleza miradi ya nishati na kusema kuwa tayari Tanzania iko katika nafasi nzuri ya kufaidika na Mpango huo wa SE4ALL na kutaka wawekezaji zaidi waendelee kujitokeza ili kuendeleza miradi ya umeme nchini.

    Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, alisema kuwa Shirika hilo litaendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha wawekezaji hao wa umeme wa maji na wale wanaotaka kuanzisha miradi hiyo ikiwemo kutoa msaada wa kitaalam ili kuongeza kiwango cha nishati ya umeme nchini.

    TANESCO itaendelea kutoa ushirikiano kwenu na naomba tuendelee kushirikiana ili kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika uendelezaji wa miradi hii na na ninaomba mjitokeze zaidi na kuwekeza katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kigoma, Liwale na Loliondo sehemu ambazo bado changamoto ya upatikanaji wa nishati hiyo ni kubwa, alisema Mhandisi Mramba.

    Naye, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Masoko na Teknolojia, Mhandisi Gissima Nyamohanga kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) alisema kuwa mpaka sasa Wakala huo umeshatoa Dola za Marekani milioni 3.1 kwa ajili ya upembuzi yakinifu kwa wajasiriamali wanaotaka kuwekeza katika miradi ya nishati nchini.

    Vilevile, Wakala huo umetoa Dola za Marekani milioni 5.4 kwa kampuni zilizoanza kuzalisha umeme ili ziweze kuunganisha umeme huo kwa wananchi.

    Serikali kutafuta fedha za wawekezaji wa Umeme

  • 6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Na Teresia Mhagama, Mtera

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo a m e u a g i z a Wakala wa Nishati

    Vijijini (REA), kuhakikisha kuwa wakandarasi wazawa wanaotekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini wanapewa kipaumbele kwa zaidi ya asimilia 80 katika utekelezaji wa mradi wa REA wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu.

    Profesa Muhongo aliyasema hayo wakati wa kikao chake na Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini kilichofanyika katika Kituo cha kuzalishia umeme cha Mtera.

    Profesa Muhongo, alisema kuwa kampuni za wakandarasi wazawa zimefanya vizuri katika utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Awamu ya Pili hivyo ni vyema wakapewa kipaumbele katika mradi wa REA Awamu ya Tatu, na kwamba wakandarasi waliosuasua katika utekelezaji wa miradi hiyo hawatapewa nafasi katika miradi ya REA Awamu ya Tatu.

    Aidha, Profesa Muhongo aliwataka wakandarasi wote wanaosambaza umeme vijijini kuhakikisha kuwa wanafuata kanuni,

    taratibu na sheria za nchi katika utekelezaji wa miradi hiyo ikiwemo kutojihusisha na masuala ya rushwa wakati wanaposambaza nishati hiyo kwa wananchi wa vijijini na kueleza kuwa miradi ya REA Awamu ya Pili itakamilika mwezi Juni mwaka huu.

    Awali akitoa taarifa ya miradi ya usambazaji umeme vijijini, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dkt. Lutengano Mwakahesya alisema kuwa jumla ya vijiji 244 vimeunganishiwa umeme katika mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Kwanza uliokamilika mwaka 2013 kwa ufadhili na REA na kutekelezwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) .

    Dkt. Mwakahesya, alisema kuwa katika mradi huo wa REA Awamu ya Kwanza jumla ya kilometa 1,600 za njia za msongo wa kati na njia za msongo mdogo wa kilomita 970 zilijengwa, transfoma 402 zilifungwa ambapo jumla ya wateja wa awali 18,000 waliunganishwa na huduma ya umeme na wateja wapya wanaendelea kuunganishwa.

    Baada ya kukamilikwa kwa miradi ya REA Awamu ya Kwanza sasa tunaendelea na utekelezaji wa miradi hii kwa Awamu ya Pili ambapo mpaka sasa ujenzi wa vituo sita vya kuongeza nguvu ya umeme katika miji ya Kigoma, Kasulu, Kibondo, Ngara, Mbinga na Tunduru umekamilika, alisema Dkt. Mwakahesya.

    Alisema kuwa katika miradi ya REA Awamu ya Pili jumla ya Wilaya 12 kati ya 13 zimeshaunganishiwa umeme ambapo jumla ya kilometa 12,193 za msongo wa kati na kilometa 1830 za msongo mdogo wa umeme zilijengwa.

    Aidha, Dkt. Mwakahesya alisema kuwa katika mradi huo jumla ya wateja wa awali 61,023 wameshapatiwa umeme, Vijiji 1,162 vimeunganishwa na gridi ya Taifa na jumla ya Transfoma 1830 zimefungwa.

    Kwa ujumla mpaka sasa utekelezaji wa Mradi huu kabambe wa kuunganishia umeme wananchi wa vijijini umekamilika kwa asilimia 84 ambapo tunatarajia miradi hii ikamilike mwezi Juni mwaka huu, alisema Dkt. Mwakahesya.

    Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt. Lutengano Mwakahesya (mwenye shati jeupe) akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini inayofadhiliwa na Wakala huo na kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) wakati wa kikao cha Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini kilichofanyika katika Kituo cha kuzalishia umeme cha Mtera. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) na Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini kilichofanyika katika Kituo cha kuzalishia umeme cha Mtera.

    Muhongo ataka wakandarasi Wazawa kupewa kipaumbele miradi ya REA

  • 7BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Viongozi kutoka Kampuni ya kutengeneza nguzo za umeme ya TANELEC, wakiwa katika Kikao na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) hivi karibuni katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara. Kutoka Kushoto ni Peter Mwanga, Zahir Saleh na Michael Karith.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo (Kushoto) akipokea Kabrasha lenye maelezo kuhusu Wakala wa Maendeleo kutoka Ufaransa (Agence Francaise Development - afd) kutoka kwa Mwakilishi wa Wakala huo hapa nchini, Emmanuel Baulden, mara baada ya kikao kilichofanyika hivi karibuni baina ya Wakala huo na Wizara katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara jijini Dar es Salaam.

    Baadhi ya Viongozi wa Wakala wa Maendeleo kutoka Ufaransa (Agence Francaise Development - afd) wakiwa katika kikao baina yao na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) kilichofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa Wakala huo, Sehemu ya Afrika, Jean-Pierre Marcelli, Mkurugenzi wa Wakala Ofisi ya Nairobi Yves Boudot na Mwakilishi wa Wakala huo hapa nchini Emmanuel Baudran.

    Mkurugenzi wa Wakala wa Maendeleo kutoka Ufaransa, Sehemu ya Afrika Agence Francaise Development (afd), Jean-Pierre Marcelli akimweleza jambo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (Kulia), wakati wa kikao baina yao. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (Kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt Juliana Pallangyo (wa pili kutoka Kushoto), wakizungumza na Viongozi wa Kampuni ya kutengeneza nguzo za umeme ya TANELEC (Walioketi Kulia) katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hivi karibuni.

  • 8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    What is brand? A brand is what an organization means in peoples minds. So a key question, what perceptions do public sector needs to send to the general public about PPP projects? All development projects are funded by Taxi payers funds, its important for the success of the PPP projects to have support of the general public and the Parliament, support should be from both the ruling government and oppositions. The country is in transition growth period, by next ten year the country should be declared a mid-income country, and this is possible only if the public sector calls on the wider participations of the private sector in delivering public services

    through development projects programs and infrastructure development. Private sector creates employment.

    The nature of the PPP contracts usually a long term contracts and goes from 20, 25 to 30 or even 50 years, the private sector will engage and find interest in the public projects only if there are clear business projections and incentives to bid for the project. The feasibility study report of the infrastructure and other development projects is the key document that provides all the necessary and business case information for investment or the project to take off. On the other hands the public sector tend to benefit from private

    sector by demanding value for money of the total investment cost, so can public sector avoid thinking commercial when engaging private sector? Who are the right commercial focused individuals in Public side PPP teams? How much of our team understands investments and business demands? Do we have the right People, processes, and technology and innovation attitude to support commercial driven projects? That are the next right questions to be answered by public partner. Great brands start inside talks amongst other things about building internal culture including communication, dedicated great team and image makeover as the way to

    get an attentions of the interest private investments but also public support. PPP projects are characterized by huge investment funds, time, technology, legal and capacity, they are usually risker and expensive financially, legally and timely, so careful and diligence analysis and evaluations to determine its profitability and economic viability must be thoroughly done which demands high level of commitment, professionalism and corporate attitude.

    Public Institutions working on PPP projects, should think branding, thinking branding is thinking business, building culture, communication, equipping and empowering staffs, aligning stakeholders and extending brand building externally will stir the growth and success on the PPP investment in long run, and will empower private sector while delivering public services and building the economy.

    BUSINESS PERSPECTIVESalum Mnuna is MBA, Certified PPP specialist based in Dar es Salaam

    Can be reached via email [email protected] or WhatsApp 0767457817The views in the article are solely based on the knowledge of the author and should

    not be associated with his employer.

    Email: [email protected]

    Branding Public Private Partnership projects for Investment and Economy:

    Like what Denise Lee Yohn mentioned in her book great brands start inside as one of the principles of worlds top brands consistently live out,

    some other six principals are mentioned out in the book but for the interest of this discussions starting inside principle attracts interest to my opinions about branding public-private partnership projects for investments. In her book she argued by mentioning spotting an

    exceptional brand is easy, but building an exceptional brand is one of the most overwhelming and elusive challenges organizations face. I could not agree less especially when am looking at a snail speed business growth in this part of the world. This piece of work is motivated and referenced from her book titled what great brand do. This article addresses branding of PPP projects from inside that goes beyond thinking

    of Logos, fonts and other elements of brand expressions which remains to be important part of branding but excluded from my personal opinion on branding PPP projects for investment.

    Branding PPP projects from inside calls for Peoples ownership, attitude shaping operations Excellency and improvement on the PPP institutions arrangements, that will provides and build confidence amongst interest PPP investors and stakeholders. Currently Tanzania and most African countries are missing on development targets due to financial, capacity and technology constraints and at the moment PPP

    discipline arrangements addresses the above challenges to certain degree. Competent business minded public official will be key drivers of the success of the projects and value for money (VfM).The public sector has the choice on the solicited proposal likewise the unsolicited proposal from the private sector to push for PPP branding internally. Like in the cooperate world if the government wants to succeed in attracting serious PPP investment, we have no choice but to think business and branding PPP projects is inevitable for healthy bidders, competition and overall return on the investment from both partners.

    Public private partnership branding

    By Salum Mnuna

  • 9BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    MAKALA

    Nuru Mwasampeta na Latifah Boma

    Imeelezwa kuwa Wizara ya Nishati na Madini itaendelea kuboresha mazingira ya wachimbaji wadogo ili wawe na mchango mkubwa na hivyo kuinua pato la taifa.

    Hayo yalisemwa Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Dkt. Juliana Palangyo hivi karibuni katika mkutano wa tano uliokutanisha wadau wa madini nchini, lengo lake likiwa ni kujadili mchango wa wachimbaji wadogo katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

    Dkt. Palangyo alisema kutokana na mchango mkubwa wa wachimbaji wadogo wa madini nchini, serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuwasaidia ili waweze kufanya kazi katika mazingira mazuri zaidi.

    Alieleza kuwa mikakati hiyo ni pamoja na kutoa ruzuku na kuwatengea maeneo yaliyofanyiwa utafiti ili waweze kufanya shughuli zao za uchimbaji.

    Alisisitiza kuwa Wizara imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali kwa wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na sheria na kanuni za uchimbaji bora wa madini na huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal; OMCTP)

    Naye Kamishna wa Madini

    Nchini Mhandisi Ally Samaje alisema kuwa serikali inaendelea kuhakikisha inawainua wachimbaji wadogo ili watoke katika uzalishaji holela na hivyo kuwa na utaratibu maalumu wa kutunza kumbukumbu zitakazoiwezesha Serikali kukusanya mapato lakini pia kuwasaidia wao kufahamu kiasi wanachokizalisha pamoja na kiasi kinachotumika.

    Alisema, sera ya madini ya mwaka 2009 na ile ya mwaka 2010 imelenga zaidi katika kuwawezesha wachimbaji wadogo kukua kiuchumi na hivyo kuwapatia kipaumbele kikubwa ili kuwawezesha kufanya kazi zao kiurahisi.

    Akielezea changamoto wanazokumbana wachimbaji wadogo wa madini nchini mwezeshaji wa

    mkutano huo kutoka kampuni MTL Dkt. Wilson Mutagwaba alisema mgawanyo wa kipato baina ya mmiliki wa ardhi, mwekezaji na mchimbaji hauko sawa na hivyo kuwafanya wachimbaji wadogo kuhamahama kutoka eneo moja kwenda jingine ili kujipatia kipato kinachokidhi mahitaji yao.

    Wachimbaji wadogo wamekuwa wakihamahama na kuvamia maeneo ya wachimbaji wakubwa wa madini kutokana na kutokuwa na uwezo wa kununua vifaa vitakavyowasaidia kupasua miamba hivyo uvamizi huo unawarahisishia kupata mawe yenye madini yaliyoachwa na wawekezaji wakubwa kiurahisi aliongeza.

    Na Asteria Muhozya

    Imeelezwa kuwa, ukaguzi wa mgodi wa TanzaniteOne uliofanywa tarehe 2 Februari, 2016 ili kuangalia usalama wake, ulikuwa na uwazi na

    uliwashirikisha Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Migodini (TAMICO) Tawi la Merelani, Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).

    Hayo yalielezwa na Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Ally Samaje kufuatia shutuma zilizotolewa na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo kuwa, Kamishna huyo hakutoa taarifa sahihi kuhusu usalama wa mgodi huo.

    Akizungumza na MEM Bulletin kuhusu suala hilo, Mhandisi Samaje aliongeza kuwa, baada ya ukaguzi wa tarehe 2 Februari, kikao cha majumuisho pia kilimshirikisha Mwenyekiti wa Tawi hilo.

    Alisema kuwa, ukaguzi huo ulibaini kuwa hakuna tena uchimbaji wa kuchokonoa pembeni ya mgodi na maeneo backfilling ilikuwa imefanywa kuimarisha usalama wa mgodi na kuongeza mgodi uliokaguliwa ni Main shaft katika levels 73, 75 na 77, maeneo ambayo yalikaguliwa hapo awali, na hivyo hakukuwa na tatizo la usalama wa mgodi maeneo hayo, alisema Samaje.

    Aliongeza kuwa, Novemba 4, 2015, alifanya ukaguzi na kubaini kuwa, kulikuwa na vitendo vya kuchimba pembeni kwenye ukuta wa mgodi katika baadhi ya maeneo yaliyohisiwa kuwa na madini, ambayo ni maeneo yaliyochimbwa nyuma, ambapo alizuia vitendo hivyo visiendelee kwa kuwaandikia barua rasmi 8 Disemba, 2015.

    Samaje aliongeza kuwa, kilichobainika ni kukosekana vikao vya usalama vya wafanyakazi na viongozi

    wao ili kujadili masuala ya usalama na utendaji kazi kwenye mgodi pamoja na kuhakikisha kuwa kuna Mpango wa uchimbaji (Mine Plan) ambao uko wazi kwa kila mfanyakazi kuujua na aelewe uchimbaji unavyoendeshwa.

    Akizungumzia alizungumzia kuhusu mahusiano baina ya wafanyakazi na menejimenti alisema kuwa, hakukuwa na mahusiano na mawasiliano mazuri na kuagiza kuboreshwa kwa mahusiano baina ya pande mbili, jambo ambalo pia

    lilionekana katika kikao cha tarehe 1 Februari, 2016, ambapo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha ilibaini suala hilo na kuagiza kuimarishwa kwa mahusiano ili kuwezesha shughuli za mgodi kuendelea.

    Akizungumzia mgomo uliotokea baada ya ule wa tarehe 1 Februari, 2016 kumalizwa, Kamishna Samaje alisema kuwa ulitokana na mgodi kuchelewa kuwalipa mishahara wafanyakazi na

    hivyo fedha kuchelewa kuingia katika baadhi ya akaunti za wafanyakazi.

    Awali wafanyakazi walipokutana na viongozi wa wizara pamoja na Kamati za ulinzi na usalama za mikoa mitatu, waliahidiwa mishahara kulipwa ndani ya siku mbili au tatu kuanzia tarehe 1 Februari 2016. Hata hivyo, Uongozi wa Wilaya ya Simanjiro unashughulikia suala la mgomo huo, alisisitiza Samaje.

    Akizungumzia suala la wafanyakazi 201 kwa mgodi huo kufukuzwa kazi, Mhandisi Samaje alieleza kuwa, Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro alifanya mazungumzo na mgodi kuhusu kurudishwa kazini kwa watumishi hao badala yake, Menejimenti ilitenda kinyume na hivyo, kuamuru meneja wa mgodi akamatwe.

    Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje akifafanua jambo wakati wa kikao kati ya amati ya Ulinzi na Usalama ya Mikoa Mitatu Kilimanjaro, Manyara na Arusha inayoratibu Uthibiti na Utoroshaji wa Madini ya Tanzanite, Menejimenti ya mgodi na wawakilishi wa Chama cha Wafanyakazi Mgodini Tawi la TanzaniteOne (TAMICO).

    Ukaguzi TanzaniteOne ulifanywa kwa uwazi- Kamishna Samaje

    Wizara kuboresha mazingira ya wachimbaji wadogo

  • 10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Jengo la hosteli Chuo cha Madini lakamilikaNa Mohamed Saif- Dodoma

    Wizara ya Nishati na Madini imepokea jengo la hosteli ya wasichana ya Chuo cha Madini cha

    Dodoma (MRI) kutoka kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Chichi Engineering Construction Limited katika makabidhiano yaliyofanywa hivi karibuni, mkoani Dodoma mara baada ya ujenzi kukamilika.

    Akizungumza kwa niaba ya Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), Mhandisi Idrisa Yahya, wakati wa makabidhiano hayo Msanifu Majengo (Architect) wa SMMRP, Joseph Ringo alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutapunguza uhaba wa nafasi za malazi kwa wanafunzi hususan wa kike katika

    chuo hichoAidha, alisema kulingana na takwimu

    za MRI inaonyesha kila mwaka usaili wa wanafunzi unaongezeka na kwa kuwa chuo hicho hakina hosteli za kutosha, inawalazimu wanafunzi wengi kupanga vyumba nje ya chuo jambo ambalo alisema si jema kwa wanafunzi hao.

    Kila mwaka wanafunzi wanaongezeka, kwahiyo kupitia jengo hili jipya la hosteli ya wasichana nina imani changamoto ya malazi kwao itakuwa imetatuliwa, alisema.

    Katika makabidhiano hayo, ilielezwa kuwa jengo hilo la hosteli linao uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 88.

    Aidha, mbali na jengo hilo la hosteli, makabidhiano hayo pia yalihusisha bwalo la wanafunzi ambalo likikuwa limekarabatiwa kwa kupanulia pamoja na ofisi ya Mkuu wa Chuo.

    Ringo alieleza kuwa, makabidhiano hayo yanakamilisha Awamu ya Kwanza

    ya Mradi wa SMMRP kwa chuo hicho na kuongeza kuwa matarajio ya baadaye ni kujenga miundombinu zaidi ili kukidhi mahitaji ya chuo hicho.

    Mahitaji ya chuo kuhusiana na majengo ni makubwa kuliko haya yaliyojengwa, alisema.

    Akizungumzia mikakati ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya mradi wa SMMRP (Additional Financing), Msanifu Ringo alisema hatua zote za kuanza utekelezaji zimeanza.

    Matarajio yetu ni kuwa malengo yaliyopangwa yatafikiwa kwa muda uliopangwa. Mradi huu umebeba dhima kubwa ya kuhakikisha Watanzania wananufaika zaidi na sekta ya Madini, alisema.

    Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho cha Madini, Mhandisi Oforo Ngowi, alisema mradi huo wa ukarabati na ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Chuo, bwalo la wanafunzi na hosteli unao

    umuhimu wa kipekee katika kuboresha miundombinu pamoja na kuleta maendeleo endelevu ya chuo hicho.

    Huu ni ukombozi mkubwa sana kwa wanafunzi waliokuwa wanahangaika kutafuta malazi nje ya chuo. Kilichobaki hapa ni kusoma tu, alisema.

    Mradi huo wa Chuo cha Madini uliokabidhiwa umefadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya usimamizi wa SMMRP na ulianza Julai, 2014 na kukamilika mwaka huu 2016 na ilielezwa kwamba umegharimu takriban milioni 997.

    Aidha jengo hilo la hosteli limebuniwa na kampuni ya ubunifu Majengo ya PSM Architects Ltd kwa kushirikiana na Howard Humphreys (T) Ltd na Mas-Q Associates Ltd.

    Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotekeleza miradi mbalimbali ya sekta ya madini chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.

    Msanifu Majengo wa SMMRP, Joseph Ringo (mwenye shati jeupe) akifafanua jambo katika kikao na Mkuu wa Chuo cha Madini cha Dodoma, Mhandisi Oforo Ngowi (mbele katikati) mara baada ya kuwasili chuoni hapo. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Wizara ya Nishati na Madini, Francis Fungameza na kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Nishati na Madini, Caroline Musika.

    Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika akikabidhiwa funguo za jengo la hosteli la Chuo cha MRI na Mkandarasi aliyejenga jengo hilo kutoka kampuni ya Chichi Engineering Construction Ltd, Shaibu Katindi. Wanaoshuhudia ni Msanifu Majengo wa SMMRP, Arch. Joseph Ringo (kulia), Mkuu wa Chuo cha MRI, Mhandisi Oforo Ngowi (kushoto kwa Mkandarasi), Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini na washauri waliosimamia ujenzi wa jengo hilo

    Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika (kushoto) akiendelea na ukaguzi katika moja ya chumba katika jengo la hosteli. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Wizara ya Nishati na Madini, Francis Fungameza.

    Jengo jipya la hosteli ya wasichana la Chuo cha Madini Dodoma (MRI) ambalo ujenzi wake umekamilika hivi karibuni.

  • 11BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MKUTANO NA WAWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA NISHATI TAREHE 15 18 FEBRUARI, 2016

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINI

    Itakumbukwa kuwa tarehe 20 Desemba, 2015, Wizara ya Nishati na Madini ilitoa Mwaliko kwa Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwasiliana na Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya kuwekeza katika uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia, maporomoko ya maji, makaa ya mawe na nishati jadidifu (jotoardhi, upepo, nguvu ya jua, tungamotaka, mawimbi (tides & waves)). Lengo la kuhamasisha uwekezaji kwenye vyanzo hivyo ni kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wa kutosha, wenye uhakika na wa bei nafuu.

    Wizara inapenda kuzitaarifu Kampuni zilizoonesha nia ya kuwekeza nchini pamoja

    na wananchi kuwa, hadi tarehe 26 Januari, 2016 jumla ya Kampuni 100 zimeonesha nia ya kuwekeza katika Sekta ndogo ya Umeme. Kabla ya kuanza utaratibu rasmi wa kupata Wawekezaji wenye uwezo wa rasilimali fedha, teknolojia na kutoa huduma husika ndani ya kipindi kifupi, Wizara imeandaa Mkutano wa Wawekezaji kuanzia tarehe 15 hadi 18 Februari, 2016. Wawekezaji wote wa ndani walioomba wametakiwa kuja na wabia wao katika Wizara ya Nishati na Madini.

    Lengo la Mkutano huo ni kuwawezesha Wawekezaji kupata maelezo ya kina kuhusu fursa zilizopo nchini na pia kuiwezesha Wizara kupata maelezo kutoka kwa Wawekezaji

    kuhusu uwezo wao wa kutekeleza miradi wanayokusudia. Ili kutimiza lengo hilo, kila Mwekezaji amepangiwa tarehe na muda wa kukutana na Viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Taasisi zake chini ya uenyekiti wa Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo.

    Washirika wote wanaombwa kuhudhuria Mkutano huo bila kukosa na kama walivyopangiwa kupitia barua za mialiko.

    Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    Jengo la hosteli Chuo cha Madini lakamilika

    Msanifu Majengo wa SMMRP, Msanifu Joseph Ringo (kulia) akiweka saini Hati ya Makabidhiano mara baada ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika.

    Bwalo la wanafunzi wa Chuo cha Madini Dodoma baada ya kukarabatiwa na kupanuliwa.

  • 12 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

    Maonesho ya 5 ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yenye aina mbalimbali za vito zikiwemo

    Tanzanite , Ruby, Sapphire , Tsavori te , Rhodol i te , Spessart i te , Tourmaline,

    Chrysobery l na Almasi yanatarajiwa kuvutia

    Zaidi ya kampuni 100 za wafanyabiashara na wachimbaji madini ya Vito kutoka Tanzania na

    nchi zingine za Afrika Mashariki, Kati na Kusini; na zaidi ya wanunuzi 500 kutoka zaidi ya nchi 25

    ulimwenguni

    Jisajili na Ushiriki Sasa!!!

    Wasiliana na: Kamati ya Maandalizi AGF Simu: +255 784352299 or +255 767106773

    Barua pepe: [email protected]

    :ama Ofisi za Madini za Kanda

    Yameandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini

    kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA)

    NAFASI ZA MAFUNZO YA UKATAJI VITO KWA WANAWAKE

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINI

    Kamati ndogo ya kusimamia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (Women Foundation Fund) iliyo chini ya Kamati ya Maandalizi ya Arusha Gem Fair (AGF) inatangaza nafasi 18 za mafunzo ya muda mfupi katika fani ya ukataji na usanifu wa madini ya vito (lapidary training course). Mafunzo hayo yatatolewa katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kilicho chini ya Wizara ya Nishati na Madini, kilichoko eneo la Themi, Jijini Arusha kuanzia mwezi Machi, 2016. Atakayechaguliwa kujiunga atalipiwa ada na posho ya kujikimu kumuwezesha kuhudhuria mafunzo kila siku. Hata hivyo, atajitegemea malazi kwa muda wote.

    Lengo la Mafunzo

    Lengo la mafunzo haya ni kuwawezesha wanawake kujiajiri au kuajiriwa katika fani ya ukataji na usanifu madini ya vito ili kuongeza thamani ya madini hayo.

    Muda wa Mafunzo

    Muda wa mafunzo ya cheti cha Lapidary Technology utakuwa miezi sita (6).

    Sifa za Mwombaji- Awe mwanamke Mtanzania mwenye

    umri usiozidi miaka 30; na- Awe na elimu ya kidato cha nne na

    kuendelea mwenye kufaulu Kingereza na Hisabati.

    Barua za maombi, CV na vyeti vitumwe kwa: - Mwenyekiti, Kamati ya AGF Women Foundation Fund, S. L. P. 641, Arusha; au yaletwe kwa mkono katika ofisi za Madini Kanda ya Kaskazini zilizopo Themi, Njiro. Kwa maelekezo zaidi piga simu Namba 027 254 4079. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 22/02/2016.