56
Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania Taarifa ya Mwaka 2007

Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

  • Upload
    others

  • View
    8

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

TTaaaassiissii yyaa UUttaaffiittii wwaaKKaahhaawwaa TTaannzzaanniiaa

Taarifa ya Mwaka 2007

Page 2: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

2

Yaliyomo

Yaliyomo

Wajumbe wa TAP (kutoka kushoto) Dk. Francis Shao, Dk. RoshanAbdallah, Prof. Martin Kyomo (marehemu), Prof. Bruno Ndunguru, naProf. James Teri

Page

Yaliyomo 2

Risala ya Mwenyekiti 3

Risala ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji 4

Uboreshaji wa Zao 5

Uongezaji Tija na Ubora wa Zao 10

Riziki na Uhakika wa Kipato 18

Usambazaji Teknolojia na Mafunzo 20

Kituo Kidogo cha Lyamungu, Hai 24

Kituo Kidogo cha Maruku, Bukoba 27

Kituo Kidogo cha Mbimba, Mbozi 32

Kituo Kidogo cha Ugano, Mbinga 35

Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38

Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41

Fedha 45

Rasilimali Watu 46

Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi fupi & Mikutano ya Kimataifa 53

Kiambatanisho II: Vifupisho 54

Page 3: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

3

Risala ya Mwenyekiti

Risala ya MwenyekitiKwa mara nyingine tena,ninafarijika kuandika utanguliziwa hii taarifa ya TaCRI ya2007. Hii ni hatua muhimu,kwani ni miaka mitano tangutaasisi hii ilipoanza kazirasmi kisheria kama taasisiinayosimamiwa na kumilikiwana wadau. Itakumbukwakwamba kwenye taarifa yetuya kwanza ya mwaka 2003,nilieleza kwamba wadauwalikuwa na matarajiomakubwa kutoka TaCRI.

Nilikuwa na matumaini na timu tuliyoiwekakushughulikia utafiti na vipaumbele vya vikwazo vyamaendeleo ya tasnia ya kahawa kama vilivyoainishwa nawadau wa kahawa nchini. Ninajivunia mafanikioyaliyoonyeshwa na TaCRI tangu kuanzishwa kwake.

Bodi inaweza kutamka kwamba TaCRI inasimamiwa nakuongozwa vizuri kwa ufanisi, na imejijengea heshimanzuri kitaifa, kikanda na kimataifa. Taasisi imepata ujiowa baadhi ya viongozi wa juu kutokana na kazi nzuriinayofanya. Kwa mfano, Rais Jakaya Kikwete alitembeleaUgano mwezi Oktoba 2006; Makamu wa Rais, Dk.Mohammed Shein alitembelea Mbimba mwezi Novemba2006; Waziri Mkuu Edward Lowassa alitembeleaLyamungu mwezi Februari 2007 na Maruku mweziMachi 2007; na, Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya nchiniwalitembelea Lyamungu mwezi Machi 2007. Wotewalionyeshwa kuridhishwa na mafanikio ya TaCRI.

Aina mpya zilizotolewa na taasisi hii ambazo zinamuonjo mzuri, zinazaa sana na zilizo na ukinzania namagonjwa ya Chulebuni na kutu ya majani ni hatuakubwa katika kuendeleza tasnia ya kahawa. Mahitaji yamiche ya hizi aina mpya yanazidi uwezo wa TaCRI wakuizalisha, hivyo mkakati wetu ni kuwawezesha wadaukuzalisha miche yao wenyewe. Sote tunajivuniamafanikio yaliyopatikana katika kutekeleza hilo. Piatunaendelea kuchunguza uwezekano wa kuzalisha michehii kwa njia ya chupa ili kuizalisha na kuisambaza kwa wingi.

Pia katika kipindi hiki tulianza kazi ya kufanya vituo vyataasisi kuwa vya kisasa kwa kukarabati maabara namiundombinu katika makao makuu ya taasisi, Lyamunguna katika vituo vidogo vya Maruku, Mbimba na Ugano.Kazi hii ilitambuliwa kuwa ni muhimu katika kuiwezeshataasisi kufanya utafiti wa viwango bora na na matokeoyatakoyochangia katika ufufuaji wa tasnia ya kahawanchini.

Bw. Edwin Mtei, Mwenyekiti waBodi ya Wakurugenzi ya TaCRI

Uamuzi wa kihistoria katika mwaka uliopita ni ule waBodi ya Wakurugenzi kuamua kuanzisha vituo vidogoviwili vya TaCRI Mwayaya, Kasulu na Sirari, Tarime ilikuwahudumia vizuri wakulima wa kahawa kwenyemikoa ya Kigoma na Mara, maeneo ambayo yanazalishakahawa ya Arabika yenye ubora wa juu wa kipekee.Mwayaya na Sirari vitakuwa vituo vya kwanza vya utafitiwa kilimo katika mikoa hii. Hii inafanya jumla ya vituovidogo vya TaCRI kutimia sita (Lyamungu, Maruku,Mbimba, Mwayaya, Sirari na Ugano) ili kufikia maeneoyote makuu yanayolimwa kahawa nchini.

Mafanikio haya na mengine mengi yameelezwa kwakirefu katika taarifa hii, na kwa niaba ya Bodi yaWakurugezi ninaipongeza menejimenti na wafanyakaziwote wa TaCRI kwa kazi nzuri wanayofanya katikakutimiza malengo yetu.

Juhudi hizi za taasisi yetu changa zimewezekanakutokana na michango kutoka kwa wakulima wa kahawa,Serikali ya Tanzania, na Jumuiya ya Ulaya. Piatumefaidika kutokana na programu ya ushirikiano naCABI, iliyodhaminiwa na Mfuko wa wa Mazao (CFC)na mradi wa IPM/CRSP unaoshirikisha Chuo Kikuu chaOhio State na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.Ninapenda kwa mara nyingine kutoa shukrani za dhatimisaada hii iliyowezesha taasisi kufanikisha kazi zake.

Kwa masikitiko, tulimpoteza Profesa Martin Kyomo, 70,ambaye alifariki tarehe 20 Mei 2007 kutokana naugonjwa wa saratani ya kibofu. Profesa Kyomo alikuwaMwenyekiti wa kwanza wa Jopo la Ushauri wa Kitaalamu(TAP). Alikua kwenye kipindi chake cha pili kamamwenyekiti wa jopo.

Edwin MteiMwenyekiti, Bodi ya Wakurugenzi TaCRI

Wakurugenzi wa Bodi ya TaCRI wakikagua kazi za ukarabati kituoniLyamungu

Page 4: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

4

Risala ya Mkurugenzi Mkuu MtendajiHuu ni mwaka wa nne wautekelezaji wa mkakati wautekelezaji wa miaka mitano,2003-2008, na katika taarifa hiitunaeleza mafanikio muhimuya mwaka, katika jitihada zetuza kutekeleza mkakati (SAP), ilikufanikisha matokeo yafuatayo:

Matokeo 1. Tasisi ya utafitiendelevu inayoongozwa vizuri,yenye uwezo kifedha, inayojaliwadau, inayoona mbali, yenye

kuheshimika kitaifa na kimataifa inaanzishwa. Matokeo 2. Programu ya utafiti wa kuboresha zao lakahawa unatekelezwa.Matokeo 3. Programu ya utafiti wa kuongeza ubora natija ya zao unatekelezwa.Matokeo 4. Programu ya utafiti wa riziki na uhakika wakipato unatekelezwa. Matokeo 5. Teknolojia mwafaka zinainishwa nakusambazwa kwa wakulima, na zinatangazwa kupitiaugani na mafunzo kwa wakulima wa kahawa. Matokeo 6. Miundo mbinu na, vifaa vya utafiti na mfumowa utawala vinaboreshwa kuwa vya kisasa.

Katika kipindi cha mwaka uliopita tulizindua tenda zifuatazokwa ajili ya miradi ya ukarabati na uboreshaji wa vifaa vyautafiti na miundombinu kutumia fedha za STABEX:- Fungu 1 (Majengo, Lyamungu) - Fungu 2 (Barabara na maji, Lyamungu)- Fungu 3 (Majengo, barabara na maji, Mbimba)- Fungu 4 (Majengo, Maruku)- Fungu 5 (Majengo, barabara na maji , Ugano)- Ununuzi wa vifaa na chemikali za maabara

Katika mwaka unaofuata, mikataba hii itaanzakutekelezwa na hivyo taasisi itakuwa na shughuli nyingiwakati wa utekelezaji wa miradi hii.

Pia tulizindua tenda kwa ajili ya kuandika kitabu cha kahawa,ambacho kitachangia katika kutangaza kahawa ya Tanzaniandani na nje ya nchi. Kitabu hiki kitaonyesha mambo yakihistoria na umuhimu wa zao la kahawa kwa watu waTanzania, na ubora wa kipekee wa kahawa ya Tanzania.

Kwa madhumuni hayo hayo tulizindua tenda yakutayarisha filamu ya kutangaza mafanikio muhimu yaTaCRI tangu kuanzishwa kwake.

Kwa vile mkakati wa utekelezaji wa miaka mitanounakaribia kumalizika 2008, tulizindua tenda kwa ajili yaushauri wa kupitia mkakati wa utekelezaji na kuandaamkakati mwingine wa utekelezaji kwa miaka mitanoijayo, 2008-2013. Madhumuni ya ushauri huu ni:

Profesa James Teri, MkurugenziMkuu Mtendaji

Risala ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji

(i) Kuboresha mkakati wa utekelezaji wa 2003 kwakuweka mkazo katika vipaumbele vya utafiti nausambazaji wa teknolojia na kuainisha mipango ya kifedhaya muda mrefu kwa kuzingatia (i) gharama za TaCRI katikakutimiza malengo yake, na (ii) mapato kupitia michango yawadau, mchango kupitia bajeti ya serikali, utoaji wahuduma na mauzo ya vitu mbalimbali (wazo likiwauzalishaji wa miche ya aina mpya kwa wingi), uzalishaji wakahawa kibiashara na riba itakayotokana na fedhazilizowekezwa kwenye mfuko maalumu. (ii) Kuibua marekebisho ya lazima katika gharamaau mapato ili kufanya TaCRI iwe na uhakika kifedhakatika kipindi cha kati na cha muda mrefu ujao. Katikadhana hii washauri watachunguza athari zinazoendanana maamuzi tofauti na kushauri njia sahihi za uwekezaji. (iii) Kuandaa mkakati wa utekelezaji wa kibiasharana mpango mpya wa muda wa kati (miaka mitano) wamikakati ya utafiti na maendeleo ili kuimarishautekelezaji wa mkakati wa utekelezaji wa kwanza katikakufufua tasnia ya kahawa Tanzania. Kazi hii itaandaamkakati utekelezaji wa pili (SAP II) unaojitoshelezawenye kulenga matokeo ya kuonekana na unaotokana namahitaji ya wadau na pia kuandaa mipango kazi yamwaka na bajeti zake. Katika kipindi cha mwaka uliopita, tulikamilisha tathminiya mfumo wa ndani wa utawala, kwa kufanya mapitio yamifumo ya usimamizi wa fedha, utawala na rasilimali watuambayo inatumika kwa sasa. Hii ilifanywa na kampuni yaMoore Rowland Forensic Services Ltd ya Afrika Kusini,ambayo ilitoa mapendekezo kadhaa ya uboreshaji.

Mikakati ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu yaprogramu za uboreshaji wa zao inaendelea vizuri ili kutoaaina bora za Arabika zenye tija ya juu, muonjo mzuri naukinzani wa magonjwa ya chulebuni na kutu ya majani, napia aina za Robusta ambazo zina ukinzani na ugonjwahatari wa mnyauko fuzari (CWD) – magonjwa matatumakuu ambayo yanatishia tasnia ya kahawa Tanzania.

Pia tumepiga hatua katika jitihada zetu za kutafuta njiampya za kudhibiti visumbufu vya zao zinazofaa nazisizoathiri mazingira.

Ninafarijika na mahitaji makubwa ya teknolojiazilizotolewa na TaCRI mpaka sasa, hasa miche aina mpyabora za kahawa. Hii ni changamoto kubwa! Tunaendeleana kutathmini njia mpya: kupachikizaji, kuzalisha mbeguchotara, kuzalisha miche kwa njia ya chupa ilikuharakisha uzalishaji na usambazaji wa miche ya ainahizi mpya bora kahawa. Naweza kusema kwa kujiaminikwamba kuna kila dalili ya mafanikio ya kuridhishakatika kutimiza ahadi zetu kwa wadau.

Profesa James Teri,Mkurugenzi Mkuu Mtendaji

Page 5: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

5

Uboreshaji wa Zao

Uboreshaji wa Zao

Mwaka uliopita umekuwa na ongezeko la shughuli katika Idara ya Uboreshaji wazao la kahawa. Majaribio zaidi yameongezwa, mbegu chotara kuendeleza aina borazimezalishwa, na watafiti waliokuwa masomoni kwa Shahada ya Uzamiliwanakaribia kumaliza masomo yao na pia tulianza kazi ya kuzalisha miche kwa njiaya chupa. Kazi zote zilizoongezeka zimefanywa kwa kutumia wafanyakazi wachachewaliopo Idarani ambapo ongezeko la kazi lilikuwa changamoto kubwa. Hapombeleni, kuna umuhimu wa Idara kuendeleza kitaalamu Bw/Bi. Shamba waliopo nakuajiri angalau wengine watatu ili kukabiliana na ongezeko la kazi.

Mafanikio Makuu 2006-2007Mpango wa muda mfupiUUzzaalliisshhaajjii wwaa mmiicchhee yyaa aawwaammuu yyaa ppiillii yyaa aaiinnaa nnddeeffuuMoja ya vipaumbele katika msimu uliopita ilikuwa ni kutoaaina mpya nyingine moja. Mpaka sasa tumeshatoa aina mpyatisa na nyingine moja (SC 13) ilikuwa inakaribiakuidhinishwa. Hii itajumuishwa na nyinginezo katikamajaribio mtawanyiko mwaka huu. Kama ilivyoelezwakwenye taarifa ya mwaka ulitangulia, jaribio la kwanza laawamu ya pili ya aina ndefu (SGVT 1) lilipandwa kituoniLyamungu mwezi Juni 2006 na lingine lilipandwa kituoniUgano mwezi Novemba mwaka huo huo. Tayariimeshapatikana miche 5,049 kutoka shamba namba 23,ambayo inatosha kuanzisha japo majaribio matatu mwaka huu.

Uzalishaji wa aina ndefu – awamu ya pili kutoka shambanamba 27 umeshatoa miche ipatayo 341 kutoka aina 13,ambavyo vimeshapandwa kwenye bustani mama kwa ajili yakuendelea na uzalishaji. Zoezi hili litaendelea mpaka miche yakutosha itakapopatikana kwa ajili ya kuanzisha angalaumajaribio mtawanyiko 6 na mengine 10 katika mashamba yawakulima. Miche ipatavyo 35 kutoka shamba namba 27 tayariimeshapandwa kama wazazi wa kiume katika bustani ya

kuzalisha aina chotara fupi. Matarajio ni kwamba micheitakuwa tayari kwa ajili ya mashamba mtawanyiko (tathminiya kitaifa) mwaka ujao. Kikwazo kikubwa katika uzalishajikilikuwa ni badhi ya aina kutofanya vizuri zinapozalishwakwa njia ya vikonyo. Aina tisa ambazo zimeshatolewazinaendelea kuonyesha ukinzani wa magonjwa kwenyemaeneo yote; mimea haijaonyesha tofauti yoyote.

Mpango wa muda wa katiUUeennddeelleezzaajjii wwaa aaiinnaa ffuuppii cchhoottaarraa zzaa kkaahhaawwaaMpango wa kati unalenga katika upatikanaji wa njiambadala ya kufikisha aina bora za kahawa kwa wakulimana kwa ufanisi. Juhudi katika kuendeleza aina fupichotara imekuwa ndio chaguo letu. Katika msimu wa2005/06 ilipatikana miche 4,857 yenye sifa bora mabayoitatumika kuanzisha majaribio ya utafiti na kwenyemashamba ya wakulima. Kwa sasa miche ipo kwenyebustani inangojea kukamilika kwa maandalizi iliikapandwe kwenye vituo vidogo na kwa wakulimamapema mwaka ujao.

Bustani za mbegu tayari zimeshaanzishwa kwenye vituovya Lyamungu na Ugano. Katika bustani ya mbegu yaLyamungu, wazazi wa kike (na baadhi ya wakiume)wameshaanza kutoa maua. Ili kukidhi mahitaji ya mbegubora, bustani nyingine inabidi ianzishwe Mbimba.Matayarisho ya mbegu kutoka aina fupi ambazozitatumika kama wazazi wa kike PNI 086, PNI 088 &PRO 127 kwa ajili ya kupelekwa Mbimba yanaendelea.

Mwezi Juni 2007, tulipokea mashine ya kutayarishachavua, ikiwa ni tukio muhimu katika shughuli zauboreshaji wa zao la kahawa. Kifaa hiki kitatuwezeshakuvuna, kutayarisha na kuhifadhi chavua kwa kiasikikubwa, na kuwezesha shughuli za utambukishajikufanyika kwa mpangilio. Mfano ni mwaka huu, ambapomvua zilizoendelea zilisababisha maua kutoka kwanyakati tofauti kwenye miti ya kiume na kike na hivyo

Dk. Linus Masumbuko, Mkuu waIdara

Utayarishaji wa vikonyo kutoka machipukizi yaliyovunwa toka awamu yapili ya aina ndefu chotara

Page 6: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

6

kuvuruga mpango wa utambukishaji. Aina fupi zilianzakutoa maua mwezi Oktoba – Novemba; hakukuwa namaua katika wazazi wa kike wa aina fupi; na muayalikuwa yakitoka katika aina ndefu.

Kifaa cha kuhifadhi chavua kitapunguza mwingiliano na haliya hewa na kuharakisha kazi ya kufanya utambukishaji mpya.Jaribio la aina fupi chotara 1 (CVT 1) lililopandwa Lyamungumwezi Machi na lingine (CVT 2) lililopandwa mweziSeptemba 2006 yataoteshwa pia kwenye vituo vingine.

Ili kuchochea utokaji wa mua na kuzalisha chavua kwakiwango cha juu, marekebisho machache katika mfumo waumwagiliaji yatafanyika mwaka huu ambapo umwagiliaji wajuu utatumika ili kuongeza uwezo katika utambukishaji.

Mpango wa muda mrefuMpango wa muda mrefu wa kupendekeza aina za kahawandefu zitakazo zalishwa kwa njia ya mbegu, unahusishakuhamisha sifa za kipekee kutoka aina zilizopo katikamkusanyiko wa kahawa Lyamungu. Kati ya mikusanyikoitakayo tumika, kuna aina bora zilizofanyiwa utafiti wamuda mrefu toka Ethiopia na Mtafiti wa Kimataifa Dr.van der Vossen. Katika msimu wa 2006/07 utambukishajiulifanywa kutoka shamba la Ethiopia ulitoa matunda2,037.

Uendelezaji wa kahawa za aina fupi chotara ni mojawapoya malengo ya muda mrefu ya uboreshaji zao. Mara ainabora (muonjo mzuri, kuzaa sana, ukinzani wa magonjwa,nk.) zitakapochaguliwa utambukishaji wa zenyewe kwazenyewe, kwa vizazi 4-6, ili kuimarisha vinasaba nakufanya aina mpya kuwa homozygous utatoa aina bora zambegu. Kama hii ikifanikiwa, aina mpya bora zitaanzakuzalishwa kwa kutumia mbegu.

Ushirikiano wa kiutafiti unaoendelea kati ya TaCRI naCIFC katika upatikanaji wa aina za kahawa zenyeukinzani wa kudumu kwa magonjwa ya chulebuni nakutu ya majani, umewezesha watafiti wawili wa Idarakupata mafunzo ya miezi mitatu CIFC, Portugal.Mafunzo yalihusu teknolojia zinazotumika kuchambuavimelea vya chulebuni na kutu ya majani, na mihimili yaukinzani katika aina za kahawa. Nyongeza ya aina 12zinazoweza kutengua vimelea vya kutu ya majanizililetwa TaCRI Lyamungu, ambazo zitasaidia kutambuavimelea vya kutu ya majani vilivyopo nchini.

Uboreshaji wa Zao

Ukuzaji kwenye machipuzo wa machipukizi ya aina ndefu chotara tokashamba namba 27

Uboreshaji zao kwa umakini unaendelea: jaribio la aina bora ndefuchotara likiwa na miaka miwili

Uandaaji wa mchanganyiko wenye vimelea vya CBD kwa ajili kuambukizakahawa ili kuchunguza ukinzani wa magonjwa

Miche ya aina fupi chotara ikiwa kwenye bustani

Uboreshaji zao kwa umakini unaendelea: jaribio la aina bora fupichotara likiwa na miaka miwili.

Page 7: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

7

Uboreshaji wa Zao

MMkkuussaannyyiikkoo wwaa kkaahhaawwaaAina mbili za kahawa za Sarchimor kutoka CIFCzimeongezwa kwenye mkusanyiko wa kahawa mwakahuu. Aina hizi zitasaidia katika uboreshaji wa zao.

KKuuzzaalliisshhaa mmiicchhee kkwwaa nnjjiiaa yyaa cchhuuppaaAina nane ambazo zinajaribiwa kuoteshwa kwa njia yachupa zimeanza kutoa makovu (callus). Maendeleo nipolepole sana, lakini kuna matumaini ya maendeleo zaidi.

Vipaumbele Muhimu 2007-20081. Kufanya maabara ya kuzalisha miche kwa njia ya chupaiweze kufanya kazi kikamilifu kwa ajili ya jaribio lakuzalisha miche kwa njia ya chupa, na kuzalisha michekwa ajili ya majaribio mengine na kupanda kwenyebustani mama za wakulima. 2. Majaribio mtawanyiko mawili ya aina za awamu ya piliya aina ndefu na fupi (SGVT) yalianzishwa Lyamungu naUgano mwaka 2006/07; katika mwaka 2007/08 majaribiomengine yataanzishwa Mbimba na Mwayaya-Kasulu.Angalau majaribio 14 ya mashambani yanatarajiwakwenye kanda za Nyanda za juu kusini, Kaskazini naMagharibi kwenye maeneo yalimwayo kahawa. 3. Kushughulikia SC 13 ambayo ilipewa idhini ya muda(pre-release) iweze kuoteshwa kwenye mashamba yawakulima na majaribio mtawanyiko ya kitaifa ambayo

yatajumuisha pia aina za awamu ya pili ya kahawachotara. Majaribio, ya aina hizi, matatu au manne yakituoni na ya kwenye mashamba ya wakulimayatafanyika kwenye maeneo yalimwayo kahawa katikakanda ya Kaskazini. 4. Kukamilisha awamu ya kwanza ya utambukishajikwenye bustani ya kuzalisha mbegu ya Lyamungu ilikuzalisha angalau mbegu chotara 50,000 kwa ajili yamajaribio ya mashambani. 5. Kuzalisha aina 273 zenye ukinzani wa mnyauko fuzari(CWD) ili kuzalisha angalau miche 1000 kwa ajili yamajaribio mtawanyiko na ya kituoni.6. Mafunzo kwa mtafiti mmoja na wataalamu wasaidiziwawili kuhusu kuvuna, kutayarisha na kuhifadhi chavua.Mafunzo haya yatasaidia sana hasa wakati wazazi wawiliwanapokuwa na wakati tofauti wa kuchanua maua.

Muonekano wa pembeni wa bustani ya mgegu: Aina fupi chotara (mbele)na aina ndefu (nyuma)

Kahawa aina ya Robusta inachangia kwenye mipango ya baadaye yakuendeleza kahawa za Arabusta

Kahawa zilizotoka CIFC Ureno ambazo zatatumika katika utambuzi wavimelea vya kutu ya majani nchini

Mkusanyiko wa aina mbalimbali za kahawa kituoni Lyamungu

Utunzaji wa vimiche katika maabara ya kuzalisha miche kwa njia ya

Page 8: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

8

Uboreshaji wa Zao

Kuanzisha bustani za mbegu kunalenga katika kuzalishaaina fupi chotara za kahawa kwa muda mfupi hivyokusambaza aina bora kwa wakulima wengi kwa mudamfupi. Mkakati ni kutoa aina fupi chotara kwa kutumiambegu. Mpango huu una faida za ziada dhidi yakuzalisha miche kwa njia ya vikonyo, kwa kuwa marabaada ya kuainisha wazazi waliotambukishwa,kinachofuata ni uchavushaji, kuvuna mbegu, kufungashana kusambaza, ambayo ina gharama nafuu na hauhitajinguvu kubwa ya watu kuzizalisha.

Bustani zitaanzishwa na kuendelezwa Lyamungu, Uganona Mbimba katika vituo vya utafiti. Ili kuhakikisha uborawa mbegu, bustani iliyoko Lyamungu itakuwa ndiochanzo pekee cha chavua, mpaka miti itakayotumikakama wazazi wa kiume inaanzishwa kwenye vituo vidogovya utafiti na wataalamu katika vituo hivyo wamepatamafunzo.

Uchunguzi Kifani 1: Kuanzisha bustani za mbegu katika vituo vya utafiti

Kielelezo 1: Mpangilio wa shamba la mbegu

Aina fupi 1

Aina fupi 2

Aina fupi 3

Vizazi mbalimbali vya aina ndefu

Page 9: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

9

Uboreshaji wa Zao

Uchunguzi Kifani 2: Aina mpya za kahawa zilizoidhinishwa sio GMOs

Mchoro huu unaonyesha jinsi aina hizi chotarazilivyozalishwa:

N 39 au KP 423 x Aina zenye ukinzani wa CBD & CLR

Aina chotara zenye sifa bora za wazazi wote wawili

Kwa vile aina hizi ni chotara zinapaswa kuzalishwa kwanjia ya vikonyo ili kuendeleza sifa (uzazi).

TaCRI huwa inapata maswali kuhusu kubadilishavinasaba na maswali hayo yanauliza iwapo aina zetumpya zilizoidhinishwa rasmi zinatokana na kubadilishavinasaba (GMOs). Aina hizi mpya kutoka TaCRI siGMOs!

Mpango wa kutambukiza uzazi unaofanywa na TaCRIunahusisha kuhamisha vinasaba vyenye sifa ya ukinzanikwa chulebuni na kutu ya majani kutoka aina zenye sifaya ukinzani kwenda aina zenye sifa bora (N 39 na KP423) lakini zina upungufu wa ukinzani. Kuhamishavinasaba kunafanywa kwa mikono. Katika ua la mzazi wakike chavua huondolewa kabla ua halijafunguka(emasculation), na chavua toka ua la babu hunyunyiziwakatika sehemu ya kike.

UUttaammbbuukkiisshhaajjiiAina chotara zinazopatikana kutoka katikautambukishaji wa awali zinaendelezwa kwa kutumia njiahiyo hiyo ya kutambukisha zenyewe ili kuboresha sifazinazohitajika. Aina zilizotolewa zilifanyiwa tathmini yasifa zake kwa kupandwa kwenye maeneo yenyemagonjwa sana ili kuhakikisha kiwango cha uhimili(tathmini hii huchukua kati ya miaka 3 – 4). Pamoja natathmini ya uhimili wa magonjwa, uzaaji na ubora piavilifuatiliwa kwa karibu na kuthibitishwa.

Kuhasi maua ya wazazi wa kike kwa kuyafungua na kutoa chavua

Uhamishaji wa chavua kutoka wazazi wa kiume kwenda wazazi wa kikewakati wa kutambukisha uzazi

Page 10: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

10

Uongezaji Tija na Ubora wa Zao

Uongezaji Tija na Ubora wa Zao

Mafanikio Makuu 2006-2007Shughuli za kuongeza uboraTaarifa ya awali kuhusu utendaji wa vinu vipya vyakiikolojia vya kumenyea kahawa ilitolewa. Matokeoyameonyesha kwamba vinu hivyo vipya havitumii majikidogo kama vilivyofikiriwa, hususan wakati wa kuvioshabaada ya kazi ya siku. Vile vile, vinu hivi vipya, katikamchakato wa kuondoa utomvu kwa njia ya kukwangua(hivyo kuepusha zoezi la uvundikaji), huwa vinaharibukahawa-ngozi kwa kuzichubua au kuziminya. Matokeomengine yanahitaji uhakiki wa kina, kwani msimummoja hautoshi kutoa jibu la moja kwa moja. Majaribiohaya yameendelezwa kwa msimu mmoja tena.

Shughuli za udhibiti husishi wa visumbufuBustani ya miti ya madawa asilia ilipanuliwa zaidi nakuongezwa mimea mingine ambayo ni muratina (Aloevera), mchimba kaburi (Mammea americana) na mnyaa(Opuntia humifusa). Kuhusu mimea ya Utupa naMwarobaini, tulianzisha jaribio kutathmini ufanisi wautomvu wa majani yake dhidi ya kiuadudu cha kawaidaSelecron katika kudhibiti vidugamba na vidungata.Matokeo ya awali yanaonyesha kwamba aina hizo tatu zakiuadudu haziachani sana (Tazama Kielelezo 2).

Zoezi la kutathmini aina tofauti za vileo kama chambokwa kuwategea ruhuka liliendelea mwaka huu,kipaumbele kikiwa ni matumizi ya vileo vinavyopatikanakirahisi na vya bei nafuu. Katika jaribio hili tulihusisha“Mbege” – kinywaji maarufu miongoni mwa Wachagga,juisi ya ndizi na inayotokana na maganda ya kahawa,nazo zililinganishwa na mchanganyiko wa 1:1 wa spiritina maji ambao ulifanya vizuri zaidi katika jaribiolililopita.

Kuandaa utomvu wa miti ya madawa asilia kwa ajili ya kudhibiti wadudukwenye kahawa

Katika mwaka husika, idara imeendelea kujihusisha na majukumu yake ya msingi, mengiyakizidi kuongeza hamasa kwa wadau. Majukumu hayo ni pamoja na mafunzo juu yaudhibiti wa ubora, ufundishaji na uboreshaji wa mbinu za upachikizaji, upanuzi wa bustaniya madawa asilia na tathmini ya uwezo wa hiyo miti kama kiuadudu asilia. Kuhusu tabiaza kahawa mpya, majaribio kuhusu athari za kivuli na za matumizi kidogo ya morututuyalianzishwa Lyamungu, Ugano na Mbimba. Teknolojia komavu ya kilimo-mseto chakahawa na migomba ilikabidhiwa rasmi kwa TTD ili iweze kusambazwa kwa wakulima.

Hadithi kubwa imekuwa ni ile ya ukarabati, au tuseme ujenzi mpya wa maabara ya rutubaya udongo Lyamungu. Baada ya kusubiri kwa muda mrefu, kazi ya ujenzi wa jengoimekamilika mwaka huu. Licha ya kukamilika kwa kazi hiyo, maabara ingali na mambomengi ya kufanya kabla haijawa tayari kwa uchanganuzi. Vifaa zaidi vya kisasa vinahitajika,ikiwa ni pamoja na mfumo wa taarifa za kijiografia (GIS).

Mawasiliano na wataalam wa PUM yaliendelea kwa nia ya kuibua njia rahisi ya kimahesabu katika kudhibiti lishe yamimea, na matokeo yake ni ya kuridhisha.

Bw. Godsteven Maro, Mkuu waIdara

Kielelezo 2: Matokeo baada ya madawa asilia kupigwamara ya kwanza

Page 11: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

11

Uongezaji Tija na Ubora wa Zao

Matokeo yameonyesha kwamba mbege, na hasaikichanganywa 1:1 na spiriti, ina uwezo mkubwa zaidi,kama inavyoonyeshwa katika Kielelezo 4.

Taarifa ya kina kuhusu dodoso za IPM katika wilaya zaHai na Moshi vijijini ilikamilika na kukabidhiwa kwawatafiti wenza, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.Taarifa hiyo ilionyesha kuwa maeneo yanayohitajimsukumo wa pekee katika wilaya hizo mbili ni mafunzokuhusu utambuzi wa visumbufu na tathmini ya madharayake, mbinu salama za kuhifadhi na kutumia madawa,kuongeza kiwango cha matumizi ya IPM (ikiwa nipamoja na kuanzisha bustani ndogo za miti shambamiongoni mwa makundi ya wakulima). Kwa upande wautafiti, jitihada inahitajika kuvumbua viwatilifu,michanganyiko ifaayo, wadudu walengwa na vipimosahihi vya miti shamba husika.

Mbinu husishi za kurutubisha udongoIle kampeni kabambe ya “Lifahamu shamba lako”iliendelea, ikihusisha wakulima wengi zaidi kutokaArumeru, Rombo, Mwanga, Same, Lushoto na Kibondo.Wilaya ya Kibondo iliwakilishwa kwa nguvu zaidi mwakahuu, sio tu na wajumbe wa halmashauri ya wilaya bali piamaafisa ugani wa ngazi mbalimbali. Kama ilivyokuwamwaka jana, fundisho hili limeonekana kugusa wakulimawengi, ambao walitamani udongo wao upimwe maramoja.

Ukarabati wa maabara ya udongo, uliohusisha kuvunjajengo la mbao na kujenga la matofali katika kiwanja kilekile, ulianza Novemba, 2006. Ingawa kasi ya ujenzi nindogo kuliko tulivyotazamia, na ujenzi huuumeshapitiliza zaidi ya miezi mitano, hivi sasa jengolimekaribia kukamilika (Tazama uchunguzi kifani 3),isipokuwa ufungaji wa vifaa muhimu. Kwa ajili hiyo,muda si mrefu tutakuwa na uwezo wa kukidhi mahitajiya wadau kwa uchanganuzi wa udongo na ushauri wavirutubisho.

Mtaalam wa lishe ya mimea kutoka PUM, Uholanzi, Dk.Bert Janssen, alizuru TaCRI kwa mara ya pili kuanziatarehe 27 Mei hadi 9 Juni, 2007. Miongoni mwa mengine,alishirikiana vema na mtafiti wetu wa udongo katikakuboresha rasimu ya muundo wa SAFERNAC, namatokeo yake ni ya kuridhisha, kama yaonekanavyokatika Uchunguzi kifani 4. Vile vile aliweka msingi mzuriwa uendeshaji wa maabara hii mpya, ikihusisha ukaguziwa vifaa wa mara kwa mara (ambapo alishirikiana namtaalam wa vifaa vya maabara toka Mlingano, Tanga),kuoanisha mbinu mbalimbali za uchanganuzi na udhibitiwa ubora. Inasikitisha tu kwamba tutalazimika tenakununua mashine mpya ya “atomic absorptionspectrometer”, kwani ile ya zamani aliyotutumia haiwezikuendana na programu za siku hizi za Windows.Mwaka huu, kitengo cha lishe kiliwakilishwa kwa nguvu

Wakijadili jambo: Dk. Janssen (kulia) na Mama Faraji (wa pili kulia)kwenye shamba la Finca

Kielelezo 3: Matokeo baada ya madawa asilia kupigwa miezi miwili badaye

Kielelezo 4: Kulinganisha uwezo wa michanganyikombalimbali kwa kutega CBB

Page 12: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

12

Uongezaji Tija na Ubora wa Zao

zaidi katika maonyesho ya kilimo (Nane Nane)yaliyofanyika katika viwanja vya Themi, Arusha.Kulikuwa na maabara ndogo, ambapo wakulimawachache waliweza kunufaika na huduma rahisi yauchanganuzi wa vigezo kama uchachu (pH) nakuelekezwa juu ya aina ya mbolea iwafaayo. Hili ni tukiola kihistoria, ambalo tunatumaini litaendelezwa.

Majaribio matatu yameandaliwa, kutathmini uwezo wakilishe wa aina mbalimbali za mimea zitumikazokutengenezea mboji, badiliko la uachiaji wa virutubishokwa nyakati tofauti katika sehemu ambazo mimearutubishi imelimiwa chini, na mchanganyiko unaofaazaidi kiuchumi wa mbolea hai na za viwandani katikakahawa. Jaribio la kwanza lipo katika hatua za awaliambapo aina sita za nyasi zimekusanywa na kupandwahapa kituoni ili kuziongeza wingi.

Ukuzaji wa zaoMkazo katika ukuzaji wa kahawa umekuwa ni kuibuateknolojia mwafaka kwenda na hizi mbegu mpya. Utafitikuhusu athari za uzalishaji kwenye kivuli au bila kivulikatika uzaaji, ubora na uwepo wa wadudu waharibifuuliendelezwa mwaka huu, huku majaribio mapyayakianzishwa Lyamungu, Ugano na Mbimba. Lile jaribiola nafasi, upogoleaji na mahitaji ya virutubisho kwambegu fupi pia lilendelea kutunzwa na kukaguliwa.

Mafunzo kwa wakulima kuhusu mikakati ya kufufuamashamba, mkazo ukiwa ni upachikizaji, yaliendelea kwaufanisi mkubwa huku wakulima 516 wakifundishwa.Kiwango cha mafanikio kilifikia 85-95%. Uboreshajizaidi wa teknolojia hii unaendelea, kwa kutathmini

msimu unaofaa kwa upachikizaji na kulinganisha ukuaji,uzaaji na ubora wa mbegu mpya zikipachikizwa juu yavikonyo-shina tofauti.

Mwaka huu pia ulishuhudia tukio la kihistoria lakukabidhi teknolojia komavu na mujarabu kwa idara yaTTD, ili isambazwe kwa wakulima wa kahawa. Teknolojiahii ambayo iliibuliwa na kujengwa tangu 2003, inahusumpango mpya wa kilimo-mseto cha kahawa na migomba(mistari 3 ya kahawa kati ya mistari 2 ya migomba),pamoja na bustani ya kuvutia ya aina bora za migomba.Kwa vile ndizi zimekuwa ni zao la biashara kwa kanda yakaskazini, ilionekana ni wakati mwafaka wa kuipateknolojia hii msukumo stahili. Bibi shamba wetu waUkuzaji naye alihamishiwa TTD ili kuwezesha hilo.

Ukamilishaji na utoaji wa chapisho za kitaalamChapisho kadhaa ziliandaliwa na kukabidhiwa TTD kwauhariri na uchapishaji wa mwisho. Hizi zilijumuishakiongozi cha shambani juu ya udhibiti wa bunguamweupe (Maswali yaulizwayo mara kwa mara nawakulima), bango moja na kipeperushi kimoja juu yaumuhimu wa kupima udongo wa mashamba,vipeperushi vingine kuhusu upogoleaji, kilimo-mseto naufufuaji wa mashamba. Kijitabu cha kufundishia nampango wa ufundishaji kuhusu lishe ya zao la kahawa piavilikamilishwa na kukabidhiwa TTD.

Idara iliandaa pia mabango makubwa mapya 5 kuhusumchakato wa uchanganuzi wa udongo, utambuzi wadalili za upungufu wa virutubisho, utengenezaji bora wasamadi na mboji, utambuzi wa wadudu waharibifu naudhibiti husishi. Mabango haya yalitumika kwa mara yakwanza katika maonyesho ya Nane Nane mwaka huu.Vipeperushi viwili viko katika hatua za awali, juu yauanzishaji wa bustani ndogo za miti shamba, mbinu zautengenezaji na matumizi yake; na kingine cha mbinusalama za kutunza na kutumia madawa ya shambani.Chapisho jingine, ambamo TaCRI ilishirikiana na TCA,ni kijarida kuhusu mbinu za uendeshaji wa vinu vyashirika vya kumenyea kahawa (CPU).

Vipaumbele Muhimu 2007-2008Mchakato wa kuajiriHaja ya kuongeza watumishi, kama ilivyofafanuliwakatika taarifa ya mwaka jana, bado iko pale pale ingawamchakato huo ulicheleweshwa kutokana na ukwelikwamba tunakaribia mwisho wa mpango-mkakati wasasa (SAP I). Bado tunahitaji kuajiri watumishi wapya.Mtaalam wa ukuzaji wa mimea (Agronomist) anahitajikaili kusimamia tafiti za ukuaji, mbinu za ufufuaji wamashamba na masuala ya hali ya hewa. Tunamhitaji piamtaalam wa kuinua ubora, au mhandisi wa usindikaji,atakayehusika na utunzaji wa viwanda vya kusindika,ubunifu wa vinu mbalimbali vya nyumbani na

Mazao rutubishi: Mukuna na Lupine

Miche iliyopachikizwa kwa ufanisi ikionyesha afya na nguvu

Page 13: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

13

Uongezaji Tija na Ubora wa Zao

viwandani, uhamasishaji kuhusu amri 10 za usindikaji,angalizo kuhusu OTA na mabaki ya dawa kwenye punjeza kahawa. Hatimaye kuna haja ya dharura ya kuajirifundi mwandamizi na wachanganuzi 3 katika maabara yaudongo ambayo kwa sasa iko tayari, lakini hainawatumishi.

Tathmini ya teknolojia mbalimbali zausindikajiIdara inapanga luendelea kushirikiana na TCA na wadauwengine ili kutathmini utendaji wa mbinu mbalimbali zausindikaji. Makubaliano yamefikiwa, na TCAinawasiliana na wagavi wa vinu vya aina mbalimbali kwaajili ya tathmini. Mitambo ya kienyeji yenye ubunifu piaikipatikana itatathminiwa.

Tafiti kuhusu upachikizajiMpango hapa ni kuendeleza tathmini ya mazingirambalimbali ya upachikizaji ili ukamilike na kukubalikakirahisi na wadau (Hii ikijumuisha msimu ufaaokupachikiza miti ya zamani na kukubaliana kati yavikonyo vya mbegu mpya na vikonyo-shina vya mbegutofauti). Tumepanga pia kuwatembelea nakuwahamasisha wakulima waliokwishapokea teknolojiahii na kufundisha wakulima wapya.

Udhibiti husishi wa visumbufuTutaendelea kufanya tafiti na kukusanya taarifazinazohusu mbinu za udhibiti wa bungua mweupe,mkazo ukiwa ni IPM. Kwa mwelekeo huo huo,tutaendelea kufanya tafiti na kukusanya taarifa kuhusuudhibiti wa ruhuka kwa mitego ya vileo vinavyopatikanakirahisi, na kushauri wakulima wadogo watumie.Mikakati ya muda mrefu zaidi yaweza kuwa matumizi yamitego ya rangi kuwadhibiti uwiwi na kidomozi, pamojana kukagua uwezo na kuvumbua kemia ya miti shamba.

Ukuzaji wa zaoIdara itaendelea kufanya tafiti zake kuhusu tabia zaukuaji na mahitaji ya mbegu mpya, zile ndefu na fupi(ikihusisha nafasi, kivuli, upogoaji, kilimo hai dhidi yakile cha kawaida, mbinu husishi za kurutubisha udongo).

Huduma za UchanganuziIkiwa ujenzi wa sehemu zilizobakia za maabara yaudongo utakamilika kwa wakati, watumishi wataongezwana vifaa muhimu vitanunuliwa, tuna mpango wakuongeza ubora wa huduma za uchanganuzi, kwa

kuweka taratibu za kudhibiti ubora wa kazi, kuwa naprogramu rasmi ya ukaguzi wa vifaa, wepesi wa kutafsiritarakimu na utoaji taarifa kwa wakati. Tutaendelea piakuingiza tarakimu zitakazopatikana kwa wingiiwezekanavyo kwenye SAFERNAC ili kuendeleakuiboresha.

Utunzaji wa udongo na majiKwa ushirikiano na TTD, tunafikiria kuweka juhudikatika kuwahamasisha wakulima juu ya umuhimu nambinu za kutunza udongo na maji, ikihusisha matumiziya kivuli, matandazo, uoteshaji wa mimea yenye mizizimingi (kama Setaria splendida) kukingama mtelemko,nk. Tumepanga pia kuendelea na upandaji miti kwenyechemchemi ya Ziwani.

Usambazaji wa teknolojiaKwa ushirikiano na TTD, tumepanga kuendeleakuachilia, kuboresha, kufungasha na kusambazateknolojia zilizopo.

Page 14: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

14

Uongezaji Tija na Ubora wa Zao

Kituo cha utafiti wa kahawa Lyamungu kimekuwepotangu mwaka 1936. Kiliundwa upya kutoka ARI na kuwaTaCRI mwaka 2001 kufuatia haja ya kuwa na utafitiunaoongozwa na wadau na unaojali mahitaji yao. Suala lalishe ya mimea limekuwa ni hitaji muhimu la kimakuzitangu kituo kilipoanzishwa. Kitengo cha lishekinaendesha maabara ya upimaji wa udongo na majani,ambao una umuhimu mkubwa kwa ushauri wavirutubisho.

Kabla ya 1984, ARI ilimiliki maabara ndogo ya udongokwa matumizi ya jumla, na hususan kwa kahawa.Kutokana na udogo wake, maabara hii iliwezeshauchanganuzi kwa kiwango kidogo na ufanisi duni. Wakatihuo huo, Mradi wa ngano wa Wakanada uliokuwepohapa Tanzania ulimiliki maabara kubwa zaidi, ya udongo,iliyojengwa kwa mbao. Wakati mradi ulipohamishiwaSelian mwaka 1984, jengo la mbao la maabara liliachiwamradi wa mahindi/maharage, ila halikutumika vema.Uongozi wa maabara ya ARI waliomba na kuruhusiwakutumia jengo hilo kama maabara ya udongo mwaka1989, na kufuatia hali hiyo ufanisi uliongezeka kwa kiasikikubwa.

TaCRI ilipoingia, mkakati wake mkubwa ulikuwa nikujenga miundo-mbinu ya kisasa zaidi, na mpangokabambe wa ukarabati uliandaliwa chini ya uwezeshajiwa kifedha wa Jumuiya ya Ulaya kupitia fungu laSTABEX. Ukaguzi wa hali ya majengo ulishauri maabaraya mbao ivunjwe; na baada ya mjadala mrefu, hatimayeilikubalika kuibadilisha iwe ya kisasa na ya matofali. Kazihii ilianza rasmi mwezi Novemba, 2006; na kwa sasaimefikia kiwango cha ukamilifu cha asilimia 95%.

Kama moja ya mafanikio ya kwanza ya shughuli nzimaya ukarabati wa TaCRI, maabara hii imewavutia wageniwengi. Miongoni mwao alikuwepo Mhe. Waziri Mkuu,Bw. Edward Lowassa, aliyezuru hapa kituoni tarehe 3Februari, 2007, na kuweka jiwe la msingi la shughuli yaukarabati katika jengo hili. Wengine walikuwa mabaloziwa Jumuiya ya Ulaya hapa Tanzania, wapatao 20,waliozuru maabara hii tarehe 29 Machi, 2007. Wasilishokuhusu hali ya sasa na matarajio ya baadaye ya maabara

hii lilitolewa kwenye kongamano la wadau wauchanganuzi wa udongo hapa nchini ambalo lilifanyikakatika hoteli ya Mkonge, Tanga, tarehe 16 hadi 18 Aprili,2007, likasifiwa sana kama wasilisho bora zaidi.

Ingawa jengo limekamilika, bado yapo mengi ya kufanyaili kuiwezesha maabara hii kufanya kazi kwa ufanisi.Changamoto moja muhimu ni uhaba wa watumishi. Kwasasa tuna wachanganuzi 2 ikilinganishwa na mahitaji yawachanganuzi 6 katika maabara ya kawaida ya udongo.Tuna mpango wa kumwajiri fundi mwandamizi wamaabara na wachanganuzi 3 kwa kuanzia, na utekelezajiunaendelea vema.

Mambo Fulani yanahitajika katika maabara yenye hadhi,yakihusisha mpango endelevu wa ukaguzi namatengenezo ya vyombo vya kazi, udhibiti wa ubora wakazi, viwango vya kuaminika na vinavyoweza kurudiwa,na baadaye, kutambulika kwa maabara kimataifa.Tukifanikisha haya tutarejesha imani ya wadau wakubwa(wenye mashamba makubwa), na hii itawaondoleausumbufu wa kutuma sampuli zao nje ya nchi (Kenya auAfrika Kusini).

Tarajio la mwisho ni kujenga muundo wa kupata nakutumia tarakimu kimaeneo, yaani mfumo wa taarifa zakijiografia (GIS). Hii ni muhimu katika kuwezesha sektaya kahawa hapa Tanzania kujenga hifadhi yake yenyeweya tarakimu (database) na kuitumia kwa kilimo chakitaalam. Wakati bado tunafikiria kuagiza vifaa vya kisasavya GIS (kama vile ArcGIS), tumeanzisha ushirikiano nakituo cha huduma ya udongo cha taifa, Mlingano, juu yauwezeshaji na mafunzo yanayohitajika.

Uchunguzi Kifani 3: Maabara ya kisasa ya udongo sasa ipo tayari kuhudumia sekta ya kahawa nchini

Maabara ya zamani ilivyokuwa kabla ya ukarabati: nje (kushoto) na ndani(kulia)

Waziri Mkuu Lowassa akiweka jiwe la msingi

Maabara mpya kama inavyoonekana kwa nje (kushoto) na ndani (kulia)

Page 15: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

15

Uongezaji Tija na Ubora wa Zao

TaCRI imegundua kuwa utunzaji duni wa rutuba yaudongo ni moja ya sababu za msingi za tasnia duni yakahawa hapa Tanzania. Kufuatia kampeni ya “Lifahamushamba lako” iliyoanzishwa mwaka jana, wakulimawamehamasika sana kuleta sampuli za udongoLyamungu kwa ajili ya uchanganuzi, na kwa vile piatunatazamia kuanzisha mradi wa hifadhi-tarakimu yakitaifa ya kahawa, tunahitaji zana rahisi ya kutafsiriatarakimu. Mpango wa SAFERNAC unalenga kuibua njiakama hiyo.

SAFERNAC ni kifupi cha “Soil Analysis for FertilityEvaluation and Recommendation for NutrientApplication in Coffee”, yaani uchanganuzi wa udongokwa ajili ya tathmini ya rutuba na ushauri juu yaurutubishaji wa zao la kahawa. Huu ni muundo wakimahesabu wenye sura nyingi, uwezao kukokotoa vunotegemewa la kahawa-ngozi kwa kutumia vigezo vya kiasicha mboji (organic Carbon), fosiforasi (P-Bray-I), potashi(exchangeable K), na uchachu (pH-H2O); mwitikio wambolea za chumvi chumvi, samadi na mimea rutubishi;uchumi katika uwekaji wa virutubisho na uchanganuziwa njia mbadala za kuandaa majaribio ya mbolea zaviwandani na hai.

Ufuatao ndio mlinganyo rahisi wa SAFERNAC:

ambapo Y1,2 huwakilisha mwitikio wa vuno kwavirutubisho 1 na 2 kutegemeana na uwepo wakirutubisho 3. Virutubisho vinavyotambuliwa namuundo huu hadi sasa ni N, P na K. Y huwakilisha vuno,D kiwango cha chini kabisa na A kiwango cha juu kabisacha kirutubisho husika. U huwakilisha kiwango cha juukabisa cha kirutubisho ambacho mmea unawezakuchukua toka ardhini. Herufi ‘a’ na ‘d’ husimama badalaya ufanisi wa kiumbile, yaani kilo ya kahawa-ngozi kwa

kila kilo ya kirutubisho kichukuliwacho toka ardhinikatika viwango vya juu na chini mtawalia. Milinganyosita ya aina hii inahitajika kwa YNP, YPN, YNK, YKN,YPK na YKP, ambapo wastani wake ndio kisio la jumla lavuno. Maelezo ya ziada kuhusu muundo huu, pamoja namawazo yaliyotumika kuujenga, vitatolewa katika andikola pekee, litakalotoka hivi karibuni.

Muundo huu ulijengwa kwanza na mtaalam wa lishekutoka PUM Uholanzi, Dk. Bert Janssen, alipozuruTaCRI mwezi Desemba, 2004. Aliujenga juu ya msingi wamuundo wake mwingine aliokuwa ameujenga awali,uitwao QUEFTS (Quantitative Evaluation of the Fertilityof Tropical Soils), au tathmini ya kimahesabu ya rutubakatika udongo wa Tropiki; akiuoanisha na mazingira yaukuaji wa zao la kahawa. Fikra maalum za kahawazilizoingizwa zilitokana na majaribio mawili ya rejea yaNPK (Kifufu, Kibo na Lyamungu C) na jaribio la mboleax idadi ya miti kwa eneo, Lyamungu.

Uchunguzi Kifani 4: Mfumo wa kimahesabu wa kutolea mapendekezo ya virutubisho kwa ajili ya kahawa hapa Tanzania.

Dr. Janssen akielezea SAFERNAC kwa mtaalamu wa udongo wa TaCRI(kushoto), na kukagua maabara mpya (kulia).

Kielelezo 5: Ufafanuzi wa matumizi yaSAFERNAC

Mavuno ( grafu ya juu) na pato halisi (grafu ya chini) kutegemeana bei ya kahawa na mbolea baada ya kuweka viwango mbalimbali vya Naitrojeni (N).

Page 16: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

16

Uongezaji Tija na Ubora wa Zao

`Soko la kahawa duniani linazidi kuwa makini kila sikukuhusu mabaki ya dawa za shambani yanayokutwakwenye punje za kahawa, na ambazo zimekuwa na atharikwa afya ya binadamu zikitumiwa mfululizo. Kamisheniya “Codex Alimentarius” ni taasisi ya kimataifainayopendekeza viwango vya juu zaidi vya mabaki navichafuzi mbalimbali kwenye chakula kinachotumiwa nabinadamu, na imeshaweka viwango vya juu vya mabakiya dawa kwenye punje za kahawa. Kwa ziada, mataifayanayoagiza vyakula toka nje huibua viwango vyaovinavyoendana na vile vya kimataifa (kama “ActiveSubstances” iliyoko Indonesia, na USEPA iliyokoMarekani). Hii ina maana kwamba mzigo wowoteuuzwao katika nchi hizo hautapokelewa ikiwahautathibitika kuendana na masharti ya viwango katikanchi inayonunua.

Mmoja wa wanunuzi wakubwa wa kahawa ya Tanzaniani Japan. Taifa hili limakuwa likifuatilia kwa makini sualala mabaki ya dawa kwa muda mrefu, na mnamo mwakajana walitoa sera ya kusimamia utaratibu uitwao “positivelist” – kanuni ya Kijapani inayodhibiti madawa yashambani yanayokutwa kwenye punje safi za kahawa.Kanuni hii inatambua makundi 2, dawa zinazohusika(positive agrochemicals) na yale yasiyohusika (exemptagrochemicals). Kundi la dawa zinazohusikalimegawanywa tena kuwa makundi madogo 3 – zilezisizotakiwa kabisa (jumla 15), nyingine ambazo kilamoja imepangiwa viwango vya juu zaidi vinavyokubalika(MRLs), (jumla 140), na zile zilizopewa kiwango sawacha ppm 0.01 – yaani zile ambazo hazipo popote katikamakundi mawili yaliyotangulia. Kupitia kampuni ya“Ueshima Coffee Company Ltd” ya Japan na chama chawauzaji wa kahawa Tanzania (TCA), habari hii ilifikaTaCRI, kama taasisi yenye dhamana ya kusimamia utafitiwa kahawa Tanzania.

TaCRI iliazimia kufanya kazi kwa ushirikiano na TPRI naTCA ili kupata taarifa juu ya madawa yaliyoandikishwana yanayotumika kwa kahawa hapa nchini. Taarifazilizokusanywa toka kwenye dodoso za IPM mwaka 2006katika wilaya za Hai na Moshi zilitumika kwa kuanzia.Dawa zinazotumika zaidi ziliibuliwa kama ionekanavyokwenye jedwali chini. Ilionekana kwamba kama MRLsziko chini mno, itakuwa vigumu kuendana nazo, hivyokiwango cha chini kabisa cha MRLs kikapendekezwakuwa ppm 0.05. Dawa zote ambazo MRLs zake ziko chiniya ppm 0.05, ni salama zaidi kutafuta dawa mbadala nakuziondoa kabisa katika matumizi ya kahawa. Dawa zotezenye asili ya morututu, kulingana na orodha ya Kijapani,zimeorodheshwa kama dawa zisizohusika, yaani zisizo namadhara dhahiri (kwa kuwa morututu nao upo kwenyekundi hili); na kwenye safu ya MRL zimeandikiwa NA(not applicable). Kwa upande mwingine, dawazilizowekewa nyota tatu kwenye jedwali ni miongonimwa zile ambazo hazikutokea kwenye orodha chanya yaKijapani, kwa hiyo zilipewa pia MRL ya ppm 0.01; hivyomatumizi yake yanahitaji uangalifu mkubwa.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi huu, TaCRIimejiridhisha kuwa kahawa inayouzwa nje ya Tanzania nisalama (na haifikii hizo MRLs zilizowekwa), ikizingatiwakuwa wakulima wadogo (wanaozalisha kahawa nyingi)wana vipato vidogo mno kuweza kununua dawa. Ingawahivyo, suala la mabaki ya dawa halipaswi kudharauliwa,hasa na wakulima wakubwa wanaomudu kuzinunua. Sighali tu bali pia ni aibu kutakiwa kurejesha mzigouliosafirishwa nje kwa kuwa tu sampuli yake imezidiviwango vya MRLs kwa bidhaa za chakula.

Shughuli hii imeweza kutoa muhtasari wa kuandikishwana matumizi shambani ya madawa ya viwandani ambayo

Uchunguzi Kifani 5: Jihadhari!: Mabaki ya dawa huweza kuchafua soko

Katika ziara yake ya pili Mei/Juni, 2007, muundo huuuliboreshwa zaidi kwa kushirikiana na mtaalam wetu waudongo, kwa kuibua milinganyo sahihi zaidi ya vuno kwamti linalotegemea wingi wa miti kwa eneo, kuingizakipengele cha mbolea hai pamoja na kile cha uchumikatika matumizi ya mbolea. Alijaribu kufanya tathminiya njia mbadala za kutekeleza majaribio ya mbolea kwakutumia SAFERNAC, na udongo wenye OC 26g/kg,2.6g/kg N, 52mg/kg P, 20mmolc/kg K na ÚH-maji ya 5.2;akatumia pia “4x3x2 factorial design” yenye kilo za N 0,50, 100 na 150 kwa ha, kilo za P 0, 40 na 80 kwa hapamoja na kilo za K 0 na 60 kwa ha, vikichanganyika natani 0, 2.5, 5, 7.5 na 10 za samadi kwa hekta.

Ilionekana kwamba ukitumia tani 10 za samadi kwahekta pamoja na kilo 80 za P na 60 za K unawezakuongeza vuno kufikia asilimia 60% kama hukuongeza

mbolea ya N, lakini tofauti hii hupungua kadiri Ninavyoongezwa. Ilionekana pia kwamba bei zikiwa juu,tuseme Tsh 2,500 kwa kilo ya kahawa-ngozi, ukitumiakilo 80 za P na 60 za K bila N, utapata hasara inayofikiaTsh 200,000. Kwa upande mwingine, shamba hilo hilolikiwekewa tani 10 za samadi litatoa faida halisi ipatayoshilingi milioni 1.6. Hii inadhihirisha umuhimu wasamadi katika kutoa virutubisho vya zao, hususannaitrojeni.

Tunaendelea kuuboresha muundo huu, ili hatimaye tuwena kipengele kinachohusisha kahawa ya kivulini na ileinayolimwa mseto, hasa kwa kuwalenga wakulimawadogo. Hatimaye, muundo huu bado unatumiaprogramu ya Excel, hivyo mkakati wa muda mrefu nikuuwezesha kuwa na “software package” yake yenyewe.

Page 17: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

17

Uongezaji Tija na Ubora wa Zao

mabaki yake yanaweza kukutwa kwenye punje kavu zakahawa, na namna madawa hayo yanavyoonekana katikaorodha ya viwango vya juu vya mabaki iliyotolewa naWajapani. Huu ni mfano mmojawapo wa kufanya kazi nawadau, had katika ngazi ya watumiaji. Kwa manenomengine, kutaka kujua mionjo yao na kurekebishamikakati yetu ipasavyo. Kwa ajili hiyo inashauriwakwamba TCA iandae shughuli kama hii katika mitiririkoya uingizaji madawa na uuzaji wa kahawa. Katikamtiririko wa kwanza, taratibu ya kuchunga biashara yamadawa chini ya kamati ya afya ya Wizara ya Kilimoinaweza kushirikishwa, kwani wamekuwa wakichungabiashara ya madawa ya shambani kwa muda sasa.

TaCRI inapendekeza, kwa kadiri iwezekanavyo, matumiziya madawa ya viwandani yaepukwe. Pale ambapo hilihaliwezekani, matumizi ya dawa zinazotembea (systemicchemicals) yapunguzwe sana na iwe ni katika kipindi chamwaka ambapo hatarisho la kutia sumu kwenye buni nila chini kabisa. Matumizi ya utomvu wa miti shambakama majani ya mwarobaini na utupa, pamoja na mbinunyingine za IPM kama utegaji wa ruhuka kwa kutumiavileo na utegaji wa kidomozi na uwiwi kwa kutumiavibao vya rangi, vitiliwe mkazo.

Jedwali 1: Viwango vya juu vya mabaki ya madawa vinavyokubalika katikamasoko ya Japan

Kundi Jina la biashara Jina la kikemia Wadudu/magonjwa MRLs (ppm) lengwa za Kijapani

Viuadudu Decis Deltamethrin Wadudu wote 2Dursban Chlorpyrifos Kimatira 0.05Selecron Profenofos Wadudu wote 0.01***Sumithion Fenitrothion + Wadudu wote 0.01***

FenvalerateThiodan Endosulfan Wadudu wote 0.1Thionex Endosulfan Kimatira 0.1

Viuakuvu Anvil Hexaconazole Kutu 0.05Banco Chlorothalonil Chulebuni, kutu 0.2Bayleton Triadimefon Kutu 0.05Blue copper Copper oxychloride Chulebuni, kutu HaihusikiCobox Copper oxychloride Kutu HaihusikiDelan Dithianon Chulebuni, kutu 0.01***Dithane Mancozeb Chulebuni 0.01***Funguran Copper hydroxide Kutu HaihusikiNordox Cuprous oxide Chulebuni, kutu HaihusikiRed copper Copper hydroxide Kutu, vidugamba HaihusikiSandoz Cuprous oxide Chulebuni, kutu Haihusiki

Chanzo: Tanzania Coffee Association (TCA)

Page 18: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

18

Riziki na Uhakika wa Kipato

Riziki na Uhakika wa Kipato Shughuli za Idara ya Riziki na Uhakika wa Kipato zinalenga kuelezea na kuelewa uanuwai wa mifumo ya ukulima na rizikikatika maeneo yalimwayo kahawa nchini na kuweka vipaumbele vya vikwazo vya tija, ubora na faida ili kuwa na tasnia yakahawa endelevu.

Inakadiriwa wakulima wadogo wapatao 420,000 na familia zao wanapata riziki kutokana na shughuli za ukulima wakahawa Tanzania. Katika baadhi ya maeneo yalimwayo kahawa nchini, kahawa ndilo zao pekee la kibiashara kwa familia.Tija na faida ya kilimo cha kahawa vimekuwa vikiporomoka kwa takribani miongo miwili iliyopita na hivyo kufanya

wakulima kupoteza matumaini na zao hili, na pia kuongezeka kwa umaskini baina yawakulima wa kahawa.

Idara hii ina majukumu yafuatayo: kuelezea na kuelewa uanuwai wa mifumo ya ukulimawa kahawa na riziki kwenye maeneo yalimwayo kahawa; kuweka vipaumbele katikavikwazo vya tija, ubora na faida na kupendekeza, kutathmini na kuendeleza suluhishozinazowezekana. Majukumu mengine ni pamoja; kuelewa na kuweka vipaumbele vya serazenye kuleta ustawi endelevu na manufaa katika tasnia ya kahawa Tanzania, kutathminimatokea ya shughuli za utafiti na usambazaji teknolojia, kushirikiana na idara nyingine zautafiti ndani ya taasisi ili kutia mkazo wa kiuchumi katika majaribio ya utafiti, nakutathmini mfumo mzima wa masoko ya kahawa yenye mahitaji maalumu (kama vilemasoko ya kahawa za kilimo hai na kahawa spesheli).

Mafanikio Makuu 2006 - 2007Kuajiri mchumiIdara imefanikiwa kuajiri mchumi kilimo mwenyeuzoefu katika tasnia ya kahawa.

Tathmini ya kiuchumi ya faida za aina mpyaza kahawaUchambuzi wa faida za kiuchumi za aina mpya zakahawa ulifanyika. Matokeo yanaonyesha kwambawakulima waliopanda aina mpya za kahawa wanapatafaida mara tatu zaidi ya wale wanaolima aina za zamani.Utofauti huu katika faida unatokana na uzalishajimkubwa na gharama ndogo za utunzaji wa aina hizimpya ikilinganishwa na aina za zamani. Uchunguzi kifaninamba 6 hapo chini unatoa maelezo ya kina kuhusu faidaza aina hizi mpya za kahawa.

Kukamilika kwa maandalizi ya tafiti zakiuchumiMaandalizi kwa ajili ya taafiti za kiuchumi kuhusuukulima wa kahawa yamekamilika. Tafiti hizo zinahusuuelewa wa uanuwai wa mifumo ya ukulima na rizikikwenye maeneo yalimwayo kahawa, na vipaumbelekatika vikwazo vya tija, ubora na faida. Tafiti hizizitafanyika mwaka ujao kwa kuanzia kwenye maeneoyalimwayo kahawa ya Arabika na baadaye kuendelezwakatika maeneo yalimwayo kahawa ya Bobusta.

Vipaumbele Muhimu 2007 - 2008 1. Kufanya tafiti za kiuchumi ili kuelewa na kuelezeamifumo ya ukulima na riziki katika maeneo yalimwayokahawa. Tafiti hizi zitafanyika katika wilaya nne zilizokwenye maeneo makuu ya kilimo cha kahawa, ambapowilaya moja itakuwa maeneo yalimwayo kahawa yaRobusta na wilaya tatu maeneo yalimwayo kahawa yaArabika.

2. Kufanya tafiti za kiuchumi zitakazo ainisha vipaumbelevya tija, ubora na faida ya kilimo cha kahawa nakupendekeza suluhisho zinazowezekana ili kufanyakilimo cha kahawa kiwe chenye manufaa na endelevu.

3. Kutathmini matokeo ya shughuli za utafiti nausambazaji teknolojia kwa wakulima. Tathmini hizizinatarajiwa kuonyesha vikwazo vya upokeaji teknolojia,mchango wa zao la kahawa kwenye kipato cha mkulima,kutoa taarifa kwa idara nyingine za utafiti kuhusuteknolojia na kuweka vipaumbele vya mahitaji yawakulima katikakuboresha teknolojia.

4. Kushiriki katika kuandaa mpango mkakati wa utendajiawamu ya pili (SAP II).

Bw. Cyril Chimilila, Mchumi Kilimo

Page 19: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

19

Riziki na Uhakika wa Kipato

Kwa miaka mingi kipato na maisha ya wakulima wakahawa vimeathirika kutokana na sababu mbalimbali nakusababisha kuongezeka kwa umasikini. Sababuzinazotajwa ni pamoja na tija ndogo ya aina za zamani zakahwa, kahawa kushambuliwa na magonjwa kama kutuya majani na chule buni, gharama kubwa za pembejeo, nakuporomoka kwa bei ya kahawa katika soko la dunia.Kuporomoka kwa bei ya kahawa kati ya mwaka 1997hadi 2002 kulifanya wakulima kuwa na hali ngumu zaidina kupoteza matumaini na zao la kahawa.

Kupitia teknolojia yake mpya ya aina za kahawa ambazozina ukinzani wa magonjwa, zinazozaa sana na zenyeradha nzuri, TaCRI inachangia katika kutatua vikwazovya kilimo cha kahawa na kuboresha hali za maisha yawakulima wa kahawa. Utafiti uliofanywa wilayaniMbinga umeonyesha kwamba wakulima ambaowamepanda aina mpya za kahawa wanapata kipato zaidiya asilimia 100 zaidi ikilinganishwa na wale wanaolimaaina za zamani. Wakulima hawa wanazalisha wastani wakilo moja ya kahawa kavu kwa mti ikilinganishwa nagramu kati ya 300 na 400 wanazopata wakulimawanaolima aina za zamani. Kwakuwa aina hizi mpyahazishambuliwi na magonjwa, gharama za uzalishajizinashuka kwa kiasi kikubwa, kwa wastani wa asilimia 30hadi 40 kwa kilo (Sh. 610 kwa kilo) ikilinganishwa naaina za zamani (Sh. 900 kwa kilo). Hii inafanya wastaniwa faida kwa hekta kwa wakulima waliopanda aina mpyaza kahawa iwe mara tatu ya ile wanayopata walewaliopanda aina za zamani.

Wakulima wanaotumia udhibiti husishi wa waduduwasumbufu wa kahawa kama vile juisi ya kahawa na vileoasilia kudhibiti ruhuka wanapunguza zaidi gharama zauzalishaji na hivyo kuongeza faida.

Teknolojia hizi ambazo zinamfanya mkulima kupunguzagharama za uzalishaji ni za muhimu katika kuhakikishakipato cha mkulima (hasa wakati wa kuporomoka kwabei), na pia kuleta ushindani wa kahawa kwenye masokona kufanya kilimo kuwa endelevu. Kwa mfano wakati wakuporomoka kwa bei ilifika wakati gharama za uzalishajizikawa juu ya bei ya kahawa na kufanya baadhi yawakulima kuacha kilimo cha kahawa.

Manufaa ya kilimo cha kahawa pia yanategemea mahitajiya masoko. Aina hizi mpya za kahawa zina muonjo mzuriwa kipekee na zinapata bei nzuri kwenye masoko. Taarifaza mauzo ya kahawa za baadhi ya wakulima wenye ainampya za kahawa (mfano kikundi cha Longa) zinaonyeshadaraja la nne na bei nzuri ya wastani wa Sh. 2,300 taslimukwa kilo.

Mahitaji ya kahawa bora yanakuwa kwa kasi na kahawabora zinapata bei nzuri zaidi wastani wa asilimia 70 juuya bei ya kahawa za madaraja ya kawaida kwenye baadhiya masoko. Hivyo kwa kupanda aina hizi mpya nakufuata taratibu za kilimo bora za kahawa wakulimawanaweza kupata kipato cha kuridhisha, kuwa na kipatocha uhakika na kuboresha maisha.

Uchunguzi Kifani 6: Kuboresha kipato cha wakulima wadogo kupitia ubunifu: faida za kuichumi zitokanazo na ainampya za kahawa na udhibiti husushi wa wadudu

Kielelezo 6: Faida kati ya aina za kahawa zazamani na aina mpya (kwa hekta)

Page 20: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

20

Usambazaji Teknolojia na Mafunzo

Usambazaji Teknolojia na Mafunzo Idara ya Usambazaji Teknolojia na Mafunzo (TTD) iliendelea na jukumu lake la kusaidiakufufua tasnia ya kahawa nchini. Hii inajumuisha kutangaza na kuzisambaza teknolojiamwafaka ili ziwafikie wadau wetu mbalimbali hususan wakulima wadogo wanaozitumia.Pia, kuimarisha mawasiliano rejea kati ya watafiti, wataalamu wa Ugani, na wakulima hasakatika kutumia mbinu shirikishi ilipewa kipaumbele.

Sambamba na utekelezaji wa mkakati kabambe (SAP 1), TTD siyo tu iliongeza nguvukuchangia katika uzalishaji na usambazaji wa miche mipya bora ya kahawa pia ilitoamafunzo kwa wakulima, wakulima wawezeshaji, maafisa ugani na wadau wengine wa sektaya kahawa.

Mafanikio Makuu 2006-2007Kutangaza matokeo ya utafiti kupitia vyombovya habariTTD ilijizatiti vilivyo kutekeleza mkakati wake wamawasiliano katika mwaka 2007. Hii ilijumuisha, pamojana mambo mengine, kutangaza na kusambaza teknolojiakwa wadau kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habarikama vile magazeti, redio na luninga. Zaidi ya matangazo350 yanayohusu teknolojia mbalimbali yalitangazwakwenye magazeti mengi tofauti na pia vipindi mbalimbali vilitangazwa kupitia redio na luninga kama TvT,Star TV na ITV.

Mafanikio makubwa kwenye mkakati wa mawasiliano niuanzishaji wa tovuti ya TaCRI ambayo imeshaanzakufanya kazi. Anwani yake ni www.tacri.org.

Uandaaji wa teknolojia mwafaka katikavijarida na mifumo tekelezi na usambazajiwake kwa wadau wetu mbalimbaliKatika mwaka husika, kwa kushirikiana na idara nyigineza utafiti, TTD ilifanikisha uchapishaji wa aina 16 zavitini vya awali vilivyohaririwa upya. Hii ilijumuishamachapisho mapya mawili na kijarida cha uundaji nauongozi bora wa vikundi vya wakulima, na pia mabangomuhimu mawili yahusuyo “Amri 8 za kuongeza tija naamri 10 za Ubora. Vitini vilivyochapishwa vinahusuteknolojia mbalimbali kama vile; Utambue ugonjwa wamnyauko fusari; Bungua mweupe, Kidomozi,Vidugamba, kimatira, Mbolea ya Minjingu, Usindikajibora wa awali, Kutu ya majani, Mbolea za Asili,Chulebuni, Uzalishaji miche kwa Vikonyo, Bustanimama, upachikizaji, Mtego wa Ruhuka na Lifahamushamba lako.

Machapisho yote yamegawanyika katika makundimakubwa manane; udhibiti wa visumbufu na vimelea,

lishe ya mmea, uzalishaji miche kwa vikonyo, ufufuajimashamba ya zamani, usindikaji wa awali, vikundi vyawakulima, na uongezaji tija na ubora.

Uzalishaji na usambazaji wa miche ya vikonyoIdara iliendelea na jukumu lake muhimu la kuwezeshauzalishaji na usambazaji wa miche ya aina mpya kwendakwa wadau. Jumla ya miti mama mipya 800,000ilisambazwa kwa wakulima kwa ajili ya kuendelezauzalishaji wa miche. Vikundi vya wakulima namashamba makubwa vilizalisha na kupanda takribanmiche 500,000 kwenye mashamba yao. Pia Idarailiendelea kutoa ushauri wa mara kwa mara kwenyebustani mama zipatazo 400 zinazomilikiwa na vikundivya wakulima, NGO, na mashamba makubwa.

Uzalishaji na usambazaji wa miche ndiyo kipaumbelechetu kwa sasa. Uanzishaji wa bustani za wilaya mwaka2007 huko Rombo, Moshi, Arumeru, Njombe, Ludewa,Rukwa na Mbozi ni moja ya juhudi za kufikia lengo hili.

Siku Kuu na Sherehe za Wakulima TaCRITaCRI na vituo vyake iliendelea kuwa kivutio cha wagenimbalimbali. Katika mwaka 2007, taasisi ilipokea jumla yawageni 5,000 ambao wanafanya jumla ya wageni 17,900waliotembelea TaCRI tangu ianze shughuli zake rasmimwaka 2001. Watu mashuhuri wakiwemo viongozi mbalimbali wa kitaifa walitembelea TaCRI: Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwetealitembelea kituo kidogo Ugano; Makamu wa Rais Mhe.Dk. Mohamed Shein alitembelea kituo kidogo Mbimba; naWaziri Mkuu Mhe. Edward Lowassa alitembelea makaomakuu Lyamungu. Viongozi wote waliridhishwa sana najuhudi za TaCRI na walitutia moyo. Wengine walikuwa niwaandishi wa habari kutoka Jumuiya ya Ulaya pamoja naViongozi wa jumuiya ya Ulaya nchini.

Bw. Twahir Nzallawahe, Mkuu waIdara

Page 21: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

21

Usambazaji Teknolojia na Mafunzo

TaCRI iliendelea kushiriki katika maonyesho ya kilimoya kikanda na kitaifa. Takriban watu zaidi ya 1,600walitembeelea banda la Mbimba Mbeya kikanda na 3,700viwanja vya Themi Arusha kitaifa.

Ziara maalaumu na mawasiliano thabiti kwawadau nchi nzimaZiara mbalimbali zenye lengo la kujibu matakwa yawadau wetu ziliimarishwa kwenye wilaya zote 27zilimazo kahawa. Hususan vikundi vya wakulima 159kanda ya kaskazini, 145 kanda ya kusini, 40 nyanda za juukusini, 25 kanda ya magharibi Maruku, 7 Kigoma na 5Tarime. Kadhalika, Mashamba makubwa ya APK, KaratuCoffee Estates, Ngorongoro Coffee Estates, BlackburnEstate, Manyata, Finca, Levy Farm, Finagro Plantations,Eldeweisse Estates, Burka Estates, Tanzania Episcopal ofConference (TEC), Vasso, Tudley na Shiwandayalitembelewa pia.

Kuimarisha ushirikiano kati ya utafiti, uganina wadauJumla ya maafisa ugani wa vijiji pamoja na maafisa uganiwa wilaya 12 kutoka wilaya 12 muhimu kwa kahawawalipata mafunzo juu ya uimarishaji mawasiliano kati yautafiti, ugani na wakulima. Hii ni muhimu hasa katikakutumia mkakati wetu wa mbinu shirikishi kuwafikiawadau wetu ili watumie teknolojia zetu kwa usahihi.

Vipaumbele Muhimu 2007-20081. Kuendelea kushirikiana na idara za utafiti za TaCRI ilikusambaza teknolojia za udhibiti wadudu waharibifu,urutubishaji na usimamizi wa udongo, usindikaji waawali na utunzaji wa kahawa kwa ujumla2. Kuendelea na uandaaji wa matokeo na mapendekezoya ya teknolojia muhimu kama udhibiti Husishi, Udhibitiwa magonjwa muhimu, Usindikaji wa awali, Kukatamatawi, kilimo bora mseto na Lishe bora ya kahawa 3. Kuandaa na kushiriki kwenye maonyesho mbalimbaliya wakulima kwenye wilaya zote 12 muhimu 4. Kuandaa mashamba 50 ya mfano kuonyesha matumizimazuri kilimo bora mseto kahawa na migomba,matumizi ya mbolea mabalimbali, ukataji matawi n.k 5. Kuendelea kujenge na kuimarisha uhusiano nawatumishi wa ugani katika wilaya 25, vikundi vyawakulima wadogo na mashamba makubwa 6. Kutoa mafunzo kwa Afisa Ugani 250 wanaofanya kazina TaCRI kwa kutumia mbinu shirikishi7. Kutoa mafunzo kwa wakulima 1,500 kwenye vituovyote vya Mafunzo TaCRI 8. Kuanzisha na kuimarisha mafunzo vijijini kwa vikundi200 kati ya 400 vinavyofanya kazi na TaCRI9. Kuanzisha bustani za miti mama katika wilaya 10 10. Kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa bustani za michetakriban wasiopungua 25011. Kuendesha kampeni za “Kahawa bora - Usindikajimakini wa awali” kwenye wilaya zote muhimu 12 nanyingine mpya (Lushoto, Same, Kasulu, Kibondo,Njombe, Iringa, Rukwa, Mpanda, Tarime and Kigoma)12. Kuunganisha na Kuwezesha vikundi vya wakulimakutoka Mbinga, Mbozi, Arumeru, Moshi, Rombo na Haiwaweze kusindika kahawa yao kutumia CPU ilikuboresha ubora uliofanana13. Kushiriki na kuhamasisha juhudi za kuongezaunywaji kahawa wa ndani kwa Watanzania wote.

Page 22: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

22

Usambazaji Teknolojia na Mafunzo

Katika kipindi cha mwaka uliopita TaCRI ilipata ujio waviongozi wa juu kutoka serikalini na umoja wa nchi zaulaya nchini Tanzania, ambao walikuwa na shahukukuona jinsi taasisi hii inavyotimiza malengo.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. JakayaKikwete alitembelea kituo kidogo cha Ugano kilichopowilayani Mbinga tarehe 9 Oktoba 2006. Rais Kikwetealifurahishwa sana na shughuli za TaCRI wilayaniMbinga na hasa jinsi taasisi hii inavyojizatiti kufufuatasnia ya kahawa na kuboresha maisha ya wakulima wakahawa. Alivutiwa sana na njia ya uzalishaji wa michekwa njia ya vikonyo amabyo inatumiwa na TaCRI katikakuzalisha miche ya kahawa. “Sikuwahi kutambuakwamba mche unaweza kuzalishwa kutoka katikakipande cha tawi” alisema wakati akiangalia mche wakahawa.

Ujio wa Rais ulifuatiwa na ujio wa viongozi wenginekadhaa wa juu wa serikali: Makamu wa Rais, Mhe. Dk.Ally Mohamed Shein alitembelea kituo kidogo chaMbimba kilichopo Mbozi tarehe 24 Novemba 2006;Waziri Mkuu, Mhe. Edward Lowassa alitembelea makaomakuu ya TaCRI yaliyopo Lyamungu wilayani Haimnamo tarehe 3 Februari 2007 na baadaye kituo kidogocha Maruku kilichopo Bukoba tarehe 12 Machi 2007;Mawaziri, Mhe. Dk. Juma Ngasongwa na Mhe. JosephMungai, walitembelea taasisi hii tarehe 28 Agosti 2006, naMhe. Steven Wasira alitembelea tarehe 3 Machi 2007.

Ujio wa viongoi wengi wa juu serikalini katika kipindikisichozidi miezi sita inaashiria thamani na sifa nzuri yataasisi, na pia utayari wa serikali katika kuchangiakufufua tasnia ya kahawa.

TaCRI pia inajivunia ujio wa wakuu wa umoja wa ulayanchini ambao walitembelea Tarehe 29 Machi 2007.Jumuiya ya ulaya inasaidia shughuli za TaCRI kupitiamfuko wa Stabex na hivyo viongozi hawa alitembeleaTaCRI ili kujionea jinsi shughuli zinavyofanyika. Ujiohuu ulikuwa ni mkubwa wa aina yake kwa wawakilishikutoka umoja wa ulaya kuwahi kutembelea TaCRI, nawalifurahishwa sana na jinsi TaCRI inavyotekelezamiradi inayodhaminiwa na Stabex.

Wageni wote hawa waligushwa na changamoto iliyombele ya TaCRI kutimiza mahitaji makubwa ya miche yakahawa aina mpya nchini. Akijibu hili, Mkurugenzimkuu mtendaji wa TaCRI Profesa James Teri alielezakwamba taasisi inafanya kazi kwa jitihada kubwakuhakikisha mahitaji yanatimizwa, kwa kuimarishauwezo wa vituo vyote vidogo kuzalisha miche zaidi, nakufungua vituo vingine vidogo viwili huko Kigoma naTarime. Jitihada nyingine ni pamoja na kufanya kazi navikundi vya wakulima, wakulima binafsi na Halmashauriza wilaya ili kuanzisha bustani mama zao wenyewe kwaajili ya kuzalisha na kusambaza miche.

Profesa Teri aliongeza kwamba ni muhimu kuwa namazingira mazuri ya sera hasa mkakati wa kitaifa watasnia ya kahawa, na pia kuongezeka kwa michango yawadau, masoko bora, upatikanaji wa pembejeo, nakuboresha miundombinu kama barabara na maji katikamaeneo yalimwayo kahawa, ili kuharakisha ukuaji nauendelevu wa tasnia ya kahawa nchini.

Uchunguzi Kifani 7: TaCRI inajivunia kupata ujio wa viongozi wa juu wa serikali na umoja wa nchi za ulaya

Wakuu wa Jumuiya ya Ulaya nchini walipotembelea Makao Makuu ya TaCRILyamungu

Mhe. Rais Jakaya Kikwete (wa mbele kushoto) alipotembelea kituo kidogo chaUgano

Page 23: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

23

Usambazaji Teknolojia na Mafunzo

Mwaka uliopita, Bodi ya Wakurugenzi ilifanya uamuziwa kuanzishwa kwa kituo kidogo cha TaCRI mkoaniKigoma kufuatia mahitaji ya wadau kuwa na msaada wakaribu katika maendeleo ya kahawa mkoani humo.Kigoma ina ekari 280,000 za kahawa zilizopo wilaya zaKigoma kaskazini, Kasulu na Kibondo, huku wilayanyingine kama Kigoma zikiwa na uwezo wa kuendelezwakuwa maeneo ya kahawa.

Changamoto zinazokabili wakulima wa kahawa katikamkoa huu ni pamoja na uhaba wa huduma za uganikwenye kahawa hasa kuhusu matumizi ya mbolea,samadi, udhibiti wa visumbufu na magonjwa, upogoaji,na usindikaji, na pia ukosefu wa taarifa za masoko yamazao yao.

La zaidi, aina za kahawa zilimwazo kwa sasa ni zile za KP423 na N 39, ambazo zinashambuliwa na magonjwa yachulebuni na kutu ya majani.

TaCRI imeshatoa aina za kahawa chotara ambazo zinaukinzani na magonjwa ya chule buni na kutu ya majanina pia zinazaa sana hadi kilo 2,300 kwa hekta. MpakaJuni 2007, tayari miche 10,000 ilikuwa imeshasambazwakwenye vijiji vinane mkoani humu ambapo vijiji vitanowilayani Kigoma vimeshapata miche hii: Mkigo, 1300;Nyarubanda, 1448; Kalinzi, 1465; Matyazo, 1200; naMukabugo, 1205). Katika wilaya ya Kasulu vijiji vitatuvimeshapata miche hii: Kitambuka, 1148; Mkatanga,1130; na Rusaba, 1130. Katika siku za mwanzo micheilikuwa inakufa sana kutokana na kukosekana kwausimamizi wa mara kwa mara, hali ambayo ililazimukuwepo kwa kituo cha TaCRI mkoani Kigoma.

Mamlaka za mkoa wa Kigoma na wilaya ya Kasuluzimetenga hekta 78.5 kwa TaCRI katika eneo yaMwayaya ambalo litajengwa kituo kidogo cha TaCRI kwamsaada wa umoja wa ulaya kupitia mfuko wa Stabex.

Mkuu wa wawakilishi wa Umoja wa Ulaya, Balozi FransBaan alitembelea Kigoma mwezi Septemba 2006 naalifurahishwa na ubora wa kahawa ya Kigoma na nia yawakulima wadogo wa mkoani humo kuongeza uzalishajina ubora wa kahawa.

Tarime iliyopo mkoani Mara inazalisha kahawa yaArabica yenye ubora wa juu wa kipekee duniani. Ingawa,kama vile Kigoma, wilaya ya tarime pia ipo mbali navituo vidogo vya TaCRI vilivyopo hivyo kufanya wilayahizi kutopata huduma ya uhakika. Ili kukabiliana na hayaBodi ya Wakurugenzi iliidhinisha nafasi ya Afisa Uganikwenda Tarime ili kusaidia maendeleo ya kahawawilayani humo. Hivi punde bustani mama ya wilayaitaanzishwa huko Sirari ili kuharakisha upatikanaji wamiche ya aina mpya za kahawa kwa wakulima wa Tarime.

Uchunguzi Kifani 8: TaCRI imepanua mbawa zake hadi mikoa ya Kigoma na Mara

Page 24: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

24

Kituo Kidogo cha Lyamungu, Hai

Kituo Kidogo cha Lyamungu, Hai Mafanikio Makuu 2006 - 2007

Tangu kuanza kwautekelezaji wa SAP 1,majukumu makuu mawiliyamekuwa yakitekelezwa:Mawasiliano, naUzalishaji na usambazajiwa miche bora ya kahawa.

Mafunzo kituoniLyamunguJumla ya wakulima watu340 walipata mafunzombalimbali kituoniLyamungu katika mwaka

husika, ambapo kati yao 320 walikuwa ni wawakilishi wavikundi vya wakulima na 20 maafisa ugani wa vijiji.Msisitizo uliwekwa kwenye mbinu za kuzalisha miche kwanja ya vikonyo, mbinu shirikishi za kufikisha teknolojia kwawadau, mbinu za kukarabati mashamba ya zamani, Amri8 za kuongeza tija na Amri 10 za kusindika kahawa bora.

Juhudi binafsi za kujizalishia miche bora yavikonyoJuhudi za kuwezesha wakulima wazalishe michewenyewe zimeendelea kupewa kipaumbele cha pakee naTaCRI. Kwa kutumia mbinu shirikishi zilizo imarishwazaidi, TaCRI iliwezesha vikundi 51 vya wakulimaambavyo vimejizalishia miche zaidi ya 400,000. Kati yahiyo, miche 380,000 ilipandwa shambani (wastani waeneo la hekta 200) na 45,000 iliuzwa na vikundi husikakuimarisha kipato. Bei ya mche ilikuwa wastani wa Tsh300 na kuleta mapato ya Tsh 13.5 milioni. Kwa sasa tunazaidi ya vikundi 150 vinavyojizalishia miche vyenyewe.

Mafunzo ya vijijiniJumla ya wakulima 1,200 (320 wanawake & 1,170wanaume) walifaidika na mafunzo vijijini yaliyofanyikakatika wilaya ya Hai, na pia wakulima 60 (10 wanawake &50 wanaume) katika wilaya ya Moshi, 34 (10 wanawake &

24 wanaume) katika wilaya ya Mwanga, na 55 (15wanawake & 40 wanaume) katika wilaya ya Rombo.

Kuimarisha ushirikiano kati ya utafiti na uganiKituo kidogo cha Lyamungu kiliendesha warsha 3 ilikuimarisha ushirikiano katika utafiti kwa wakulimawawezeshaji (FPs) 140 kutoka vikundi 70 vya wakulimawilayani Rombo (20) na Moshi (50). Maudhui yamafunzo yalisisitiza majukumu ya FPs na mbinushirikishi za ugani. Mengine yalihusu utunzaji wakahawa, usindikaji wa awali, uanzishaji wa vikundi nauongozi. Hawa sasa wamekuwa wawezeshaji wetukwenye wilaya hizi mbili wakifanya kazi mkono kwamkono na TaCRI.

Siku Kuu za Wakulima na TaCRIMfululizo wa pili wa Siku Kuu za wakulimazilizoandaliwa kwa ushirikiano wa vikundi vya wakulimana TaCRI zilifanyika kwa ufanisi mkubwa mwaka huukatika sehemu zifuatazo: Ledea-Lekura, Undugu-Mkomomgo vyote vya wilaya ya Moshi; Lambo wilaya yaMwanga, Mti Mama – Mshewa Wilaya ya Same naNronga A – Machame Hai.

Vikundi vitatu kutoka wilaya ya Siha – Rafiki, Ngaronyina Wandri kwa pamoja viliandaa siku ya wakulimaambapo Mhe. Mohamed Babu, Mkuu wa mkoa waKilimanjaro, alikuwa mgeni rasmi. Inakadiriwa watuwapatao 4,200 walihudhuria sherehe hiyo.

Uanzishaji wa bustani za miti mama za wilayaKatika maandalizi ya kampeni ya kupanda kahawamwaka 2007, uanzishwaji wa bustani za wilayaulizinduliwa katika wilaya za Rombo, Moshi na Arumerukila moja ikiwa na miti mama 2,000. Ili kuongeza tija yauzalishaji, bustani zote hizi zimewekewa mifumo yakumwagilia maji kwa matone. Mategemeo ni uzalishajiwa miche 50 kwa mti mama kwa mwaka badala ya miche

Bw. Msanjo Temu, Afisa Ugani,Lyamungu

Bw. Nkya akifundisha wakulima upachikizaji wa miti ya kahawa

Jedwali 2: Juhudi binafsi za wakulimakuzalisha miche bora Mwaka Idadi ya Idadi ya miche

vikundi Iliyozalishwa Iliyopandwa Iliyouzwavilivyoundwa

2003 5 --- --- ---2004 15 5,000 2,600 9502005 30 27,400 15,900 2,7002006 41 43,500 35,115 3,3002007 58 424,000 386,385 45,500Jumla 150 500,000 440,000 52,500

Page 25: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

25

Kituo Kidogo cha Lyamungu, Hai

10 ya sasa bila mfumo wa umwagiliaji. Upanuzi wabustani ya Arumeru unafanyika ili kuwa na uwezo wamiti mama 3,000.

Vipaumbele Muhimu 2007 - 2008Kutoa teknolojia mpyaKituo kidogo cha Lyamungu kitaendelea kushirikiana naidara za utafiti kufungasha teknolojia kwenye muundosahihi na kupelekwa kwa wakulima.

Siku za wakulimaKuandaa siku za wakulima zitakazofanyika katikavikundi vifuatavyo – 1 Singisi Arumeru, 1 MamseraRombo, 1 Msindo Same, na 1 Narumu Hai.

Mashamba ya mfano Kuanzisha mashamba ya mfano katika maeneo mbalimbali - 3 Machame Hai, 2 Uru, 2 Old Moshi, 1 Kilema, 2Marangu Moshi, 1 in Monduli, 2 Mwanga, 2 Lushoto, na2 Same.

Kutangaza teknolojiaKuendelea kutumia vyombo vya habari kufikishateknolojia mbalimbali kwa wadau wetu: Lengo ni walaukipindi kimoja cha dakika 30 kwenye luninga kuelezeautunzaji kahawa na usindikaji wa awali mara 1 kwa wiki2; na kipindi cha radio cha dakika 30 mara 1 kwa wiki.

Maonyesho ya wakulimaTutaendelea kushiriki katika maonyesho yote makubwa yawakulima, ikijumuisha nane nane Arusha na ngazi ya taifa.

Ushirikino kati wa utafiti na uganiIli kuimarisha mawasiliano kati ya ugani, utafiti na

wakulima tutaendeleza mahusiano na maafisa uganikatika wilaya 10 zilimazo kahawa.

Mafunzo kwa wakulima wawezeshajiKuwezesha wakulima katika kueneza teknolojia nikuhimu. Ili kutimiza lengo hili, wakulima wawezeshajiwapatao 300 watapatiwa mafunzo.

Mafunzo vijijini (VBT)Juhudi za kuwezesha wakulima zitaendelezwa kwa kutoamafunzo vijijni kwa vikundi 100 vya wakulima.

Kuunganisha wakulima na sokoni Ili vikundi vuya wakulima wapate bei nzuri kwa uborawa kahawa yao, tutasaidia kuunganisha vikundi 4 vyawakulima na masoko ya kahawa.

Kupanua uzalishaji wa miche Kuongeza uwezo wa kuzalihs miche kwa kupanua bustanimama ya kituoni kwa kuongeza miche 3,000 na machipuzo48. Ikiwa na miti mama 25,000 inakadiriwa kuzalishamiche 1.5 milioni kwa mwaka (miche 60 kwa mti).

Wasimamizi wa bustani mama Kuboresha ufanisi katika usimamizi wa bustani mamakatika bustani za vikundi na za wilaya kwa kutoamafunzo kwa wasimamizi wa bustani mama 300.

Kupanua eneo la uzalishaji miche Kuanzisha bustani mama mpya : 1 Same, 1 Lushoto, na 1Mwanga

Kuwezesha mashamba makubwa Kuwezesha Mashamba makubwa 3 kuanzisha bustanimama na machipuzo: Usa Ltd, Nkwasira na Kararagua.

Kupanua vyanzo vya riziki na kipatoKuwezesha na kuimarisha vikundi 100 vya wakulimakuanzisha bustani za miti bora ya kivuli na kuipanda iliitumike pia kwa shughuli nyingine za kuimarisha uchumina mazingira, hasa ufugaji nyuki na matumizi yanyumbani.

Kushirikiana na idara za utafiti katikamajaribio Kushiriki katika kuanzisha na kutunza majaribio yakituoni na mtawanyiko.

Kusaidia teknolojia ya umwagiliaji wa matoneUmwagiliaji wa matone tayari upo kwenye bustani kuu yaLyamungu, na bustani nne za wilaya za Rombo, Marangu,Arumeru, Same, Lushoto, na bustani mbili za kata(Mwanga na Monduli) pamoja na vikundi 10 vyawakulima. Jukumu letu la mbeleni ni kuendelea kusaidiajitiada hizi za kisasa.

Siku ya wakulima Lekura iliyoandaliwa na kikundi cha LEDEA

Siku ya wakulima Wandri iliyoandaliwa na wakulima

Page 26: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

26

Kituo Kidogo cha Lyamungu, Hai

Kuna mtazamo kwamba jukumu la kanisa kwenye jamiizote ni kushughulika na mambo ya kidini tu. Ingawa,Kanisa la Kiinjili la Kiruteri Dayosisi ya Kaskazini naParokia ya Rombo limedhihirisha vinginevyo kwambawaumini wataongeza imani ya dini endapo watakuwa nahali nzuri kiuchumi. Kwani, mtu mwenye hali mbayakiuchumi hawezi kujikita kwenye mambo ya kuabudu aukuchangia sadaka kwa maendeleo ya kanisa.

Kwa kutambua uhusiano huu, KKKTDY na KKTRwalianza mapema kuhamasisha waumini wao kuungamkono na kushiriki kikamilifu katika mchakato wakufufua zao la kahawa ambalo limekuwa ni mhimilimkuu wa maisha ya familia nyingi kwa miaka mingi.

Mchango wa KKKTDY ulianza mwaka wa 2005 wakatiLEDEA (Jumuiya ya Maendeleo – Lekura) walipotualikakushiriki kwenye semina iliyoitishwa mahususi kujadilimikakati tekelezi ya jinsi waumuni wake wanavyowezakujikomboa kiuchumi kwa kujishughulisha na shughulimbalimbali kama kilimo bora mseto cha kahawa namigomba, ufugaji bora wa kuku na ngo’mbe wa kisasa nauanzishaji wa SACCOS. Kutokana na semina hii, vikundivitatu shirikishi (Masia A & B na Kiwako Kotela)viliundwa. Tangu hapo vikundi hivi vimekuwa niwashirika wetu katika kufufua zao la kahawa kwakujijengea uwezo wa kuzalisha jumla ya miche yavikonyo 43,000 kwa mwaka. Pia, kupitia mafunzo vijijini,wakulima wawezeshaji kutoka vikundi hiviwameshasaidia wakulima wenzao matumizi bora yateknolojia ya kilimo bora mseto cha kahawa na migombapamoja na amri kumi za usindikaji wa kahawa bora naamri nane za tija.

Mwaka 2005 na 2006 TaCRI ilialikwa kwenye MkutanoMkuu wa Dayosisi uliofanyika Chuo cha Uongozi

Masoka na kujumuisha zaidi ya Wachungaji Viongozi waSharika 250 na viongozi wengine wa Sharika. TaCRIilitoa mada kuhusu mchakato wa ufufuaji kahawa navipaumbele muhimu na matokeo yake vikundi vitatushirikishi vya wakulima na bustani mama vikaanzishwa:Nronga B, Wakabosu- Sonu; Kiukabosa – Sawe; Ukaki –Uswaa and Wakabongi – Ngira. Bustani hizi ni kati yabustani nzuri sana chache wilayani Hai zenye tija kubwaya uzalishaji miche takriban 160,000 kwa mwaka. Lamuhimu zaidi ni kwamba wakulima wawezeshajiwamefanya kazi kubwa sana ya kuwawezesha wakulimawenzao matumizi bora ya teknolojia mbalimbali hasa zaamri 8 na kumi za kuongeza tija na ubora wa kahawa.

Tukio muhimu katika mchango wa KKKTDY ni hatua yaujasiri ya Baba Askofu Dr. Martin F. Shao kwa kuonyeshamfano wa kuongoza kwa vitendo alipoamua kubadilishashamba lake lililoko Lole Mwika na kuwa la kilimo boramseto.

Kwa sehemu yake, KKTR limeshiriki katika kufufuakahawa ulichukua mwelekeo wa kuwezesha Parokia zake15 kuanzisha bustani mama za kuzalisha miche borazikijumuisha jumuia zake wilayani Rombo. Hatua hizi nimuhimu kwani zitaharakisha uzalishaji miche mipya nakuwezesha waumini kubadilisha mashamba yao kwa kwamiche aina mpya.

Mtazamo huu wa mbali wa kanisa utatoa mchangomuhimu katika kusaidia kubadilisha maisha ya waumuniwengi wenye uchumi duni ambao baadaye watatumiwana kanisa katika kujenga miradi ya kijamii kama shule,zahanati na mengineyo. Huu ni ushindi mkubwa, na nikazi ya kiungwana.

Uchunguzi Kifani 9: Jukumu la Kanisa katika kufufua sekta ndogo ya kahawa: Mchango wa Kanisa la Kiinjili la KilutheriTanzania – Dayosisi ya Kaskazini (KKKTDY) na Kanisa la Katoliki Tanzania – Rombo (KKTR)

Shamba la Askofu Dk. Martin Shao kabla ya ukarabati Baada ya ukarabati

Page 27: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

27

Kituo Kidogo cha Maruku, BukobaKituo Kidogo cha Maruku kiliendeleza jitihada zake za kuendeleza zao la kahawa aina yarobusta katika mkoa wa Kagera mkazo ukiwa katika wilaya za Bukoba, Karagwe, Misenyina Muleba ambako mazao ya kahawa na migombo yanalimwa. Kituo kilishughulika nausambazaji wa teknolojia mwafaka kwa wakulima na maafisa ugani kwa kutoa mafunzombalimbali kuhusu matumizi ya samadi, mbolea za chumvi chumvi aina za CAN na NPK,kulengeta mibuni iliyozeeka, kuweka matandazo, kupalilia kwa wakati, kutoa machipukizi,kuvuna kahawa iliyoiva, uanikaji wa kahawa, kukoboa kahawa katika ngazi ya kaya nautaratibu wa kuuza kahawa. Kituo pia kwa kushirikiana na serikali ya mkoa na wadauwengine kilishiriki katika mchakato wa kuhakikisha kuwa uzalishaji wa zao la kahawaunaongezeka kutoka wastani wa tani 21,000 za sasa (au gramu 320 za kahawa safi kwa mtiwa kahawa) kufikia tani 68,000 (au kilo 1 ya kahawa safi kwa mti), kwa lengo la kuboreshamaisha ya kaya 250,000 zinazotegemea zao la kahawa kwa mapato.

Katika msimu uliopita, Maruku ilifanikiwa kuhamasisha watunga sera katika ngazi za wilaya, mkoa na taifa kuhusuugonjwa wa mnyauko fuzari wa kahawa unaotishia uhai wa kahawa ya robusta mkoani Kagera. Mfano, wakati wa warshaya kutengeneza mkakati wa uboreshaji wa kilimo na mifugo ulioandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, mtumishi wa TaCRIkutoka kituo cha Maruku aliwasilisha mada kuhusu mkakati wa kuboresha tasnia ya kahawa katika mkoa na mkazo ukiwakatika mikakati ya kampeni za kutokomeza mnyauko fuzari na kukagua mashamba ya kahawa yaliyotelekezwa. Washirikiwa warsha hii walitoka katika viwanda vya kusindika kahawa, taasisi za kifedha, watunga sera, mashirika yasiyokuwa yakiserikali, vyama vikuu vya ushirika na vyama vya siasa. Katika maazimio yaliyofikiwa iliamriwa kila wilaya kutengenezamkakati wa kuboresha zao la kahawa na kutokomeza ugonjwa wa mnyauko fuzari wa kahawa katika mipango yao yakilimo.

Mafanikio Makuu 2006 - 2007 Uzalishaji wa miche ya Robusta kwa njia ya vikonyoMaruku iliendelea na uzalishaji wa miche ya vikonyo yakahawa ya Robusta ili kutosheleza mahitajiyanayoongezeka ya miche ya kahawa kwa wakulimamkoani Kagera. Katika msimu wa 2006/2007, jumla yamiche 110,076 ya vikonyo ilizalishwa na kati ya hiyo miche52,000 ilisambazwa kwa wakulima. Pia miche 42,000kutokana na mbegu zilizoombwa na Chama kikuu chaUshirika cha KCU ilizalishwa katika bustani ya Ibwera.

Uanzishaji wa bustani mama za kahawa ya ArabikaKituo kidogo Maruku ilifanikiwa kuanzisha bustanimama tatu za kahawa chotara aina ya Arabika zenyeukinzani wa magonjwa ya chulebuni na kutu ya majanikama ifuatavyo: Maruku (miche 194), Ibwera (miche200) and Biirabo (miche 200). Kituo pia kwa mafanikiokilisambaza miche 400 iliyo kwenye viriba kwa wakulimawilayani Muleba, miche 2,000 itagawiwa kwa wakulimabinafsi, na miche 1600 itapelekwa kuanzisha bustanimama za Biirabo na Ibwera.

Mafunzo kwa wakulimaVikundi thelathini na moja vya wakulima vimenufaika namafunzo katika ngazi ya vijiji kupitia mfumo wa mafunzoshirikishi ambapo jumla ya wakulima 930 walifunndishwambinu mbalimbali kuhusu kanuni za kilimo bora cha zaola kahawa. Mkazo wa mafunzo ulikuwa katika matumizi

ya mbolea za samadi, CAN na NPK, kulengeta miti yakahawa iliyozeeka, kuondoa machipukizi, kupalilia kwamuda mwafaka, uvunaji na uanika mwafaka, utunzaji wakahawa kwenye stoo na masoko.

Mashamba darasa (Mashamba darasayaliyoboreshwaMashamba darasa ni njia mwafaka ya kuwafundishawakulima teknolojia sahihi za kuongeza uzalishaji naubora wa zao la kahawa. Katika kipindi hiki jumla yawakulima 630 na wataalamu 15 wa ugani walishirikikujifunza kupitia mashamba darasa, na kutokana namafanikio yaliyopatikana msimu huu mashamba darasazaidi yataanzishwa katika maeneo mengine.

Bw. Nyabisi Nghoma, Afisa Ugani,Maruku

Moja ya bustani mama mpya za vikundi vya wakulima kwa ajili yakuzalisha na kusambaza miche bora kwa wakulima wa kahawa

Kituo Kidogo cha Maruku, Bukoba

Page 28: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

28

Ufuatiliaji wa Mnyauko Fuzari wa KahawaUgonjwa wa mnyauko fuzari bado ni tishio kwauzalishaji wa kahawa ya Robusta mkoani hapa na ripotiza hivi karibuni zinaonyesha kuwa wilaya za Bukoba naMisenyi zimeathiriwa zaidi. Utafiti wa kina uliofanywa nakikundi cha Manyafubu na vikundi vingine katika tarafaza Bugabo, Kyamutwara, Katerero na Kiziba katika wilayaza Bukoba na Misenyi matokeo yake ni kamayanavyooneshwa kwenye Jedwali hapo chini.

Mafunzo kuhusu udhibiti wa mnyauko fuzariwa kahawaTaasisi iliendesha mafunzo kwa watalaamu wa uganikuhusu kuutambua na kuudhibiti ugonjwa wa mnyaukofuzari wa kahawa. Katika msimu huu, Mabwana shamba95 kutoka wilaya tatu (32 Bukoba, 26 Muleba na 37Karagwe) walipatiwa mafunzo. Wakulima wa kahawamkoani Kagera wamehamashishwa kuhusu madhara yaugonjwa wa mnyauko fuzari wa kahawa katika maishayao na kutokana na hali hiyo wakulima wamekuwa nashauku kubwa kupata habari na mbinu za kuutambua nakuudhibiti ugonjwa huu. Kutokana na mafunzowaliyopatiwa maafisa ugani wana uwezo wakuwaelimisha wakulima wa mkoa huu namna yakuutambua na kuudhibiti ugonjwa huu.

Mafunzo ya mkulima na mkulimaKituo cha Maruku kimekiwezesha kikundi chaManyafubu kuendesha mafunzo kwa wakulima katikakata za Rubafu, Kishanje, Kaagya, Buhendangabo,Nyakato na Buhembe wilayani Bukoba kuhusu namna yakuutambua na kuudhibiti ugonjwa wa mnyauko fuzariwa kahawa. Jumla ya wakulima 2,000 wamepatiwamafunzo. Moja ya malengo ya TaCRI ni kuharakishausambazaji teknolojia nchi nzima kwa kutumia njia yavikundi vya wakulima kufundisha wakulima wengine.Kwahiyo kazi ya kikundi cha Manyafubu ni mafanikiomakubwa katika kufikia lengo.

Siku za maonyesho Kituo cha Maruku kiliendesha siku ya maonyesho katikakijiji cha Bugombe kata ya Kanyigo kuhamasishawakulima, wanasiasa na viongozi wengine wa katakuhusu umuhimu na mbinu mwafaka ya kuudhibitimnyauko fuzari wa kahawa. Jumla ya washiriki 213walihudhuria siku ya maonyesho.

Ziara za kimafunzo kwa wakulimaKituo cha Maruku pia kiliwawezesha wakulima kufanyaziara za mafunzo katika vikundi vya wakulima kwenyewilaya za Bukoba, Karagwe, Missenyi na Muleba. Lengola ziara lilikuwa kuwawezesha wakulima kuona jinsiuzalishaji wa zao la kahawa unavyoweza kuongezeka kwakufuata kanuni bora za kilimo cha kahawa. Ziarazilitumika kama majukwaa ya kuhamasisha wakulima nawadau kuhusu mnyauko fuzari wa kahawa unaoathirikahawa ya robusta Mkoani Kagera. Ziara hizi zilifanyikakatika vijiji vya Bwizandulu, Bulinda, Bushumba, Rubya,Kamachumu, Muhurile, Rukuraijo, Kayungu, naChabuhora ambapo jumla ya wakulima 577 walishiriki.

Kutangaza matokeo ya utafiti kupitia vyombovya habariKituo kiliendelea kuzitangaza na kuzisambaza teknolojiamwafaka za kilimo cha kahawa kwa wadau kupitiavyombo vya habari ikiwa ni pamoja na redio, luninga, namagazeti. Zaidi ya mada nne ziliandikwa kwenyemagazeti mbalimbali ya hapa nchini na progamu kuhusukanuni za kilimo bora cha kahawa na mbinu mwafaka zakuudhibiti mnyuko fuzari wa kahawa zilitangazwa katikavyombo vya habari vya Redio Free Afrika (RFA) RedioTanzania, Televisheni ya Taifa (TVT) na Star TV.

Kuanzisha mashamba ya mfano kwawakulimaKwa kushirikiana na vikundi vya wakulima, kituokimetumia mashamba 43 ya mfano ambamo ukarabatiwa miti ya kahawa iliyozeeka, kuonyesha matumizi sahihiya mbolea za samadi, CAN na NPK, na njia mwafaka yakuudhibiti mnyauko fuzari wa kahawa vilifanyika.Matokeo kutoka katika mashamba haya yalikuwa mazurina ya kuvutia. Matokeo yake yatatumika kusambateknolojia mwafaka mkoani pote.

Upanuzi wa shamba la mkusanyiko wakahawa ya RobustaKituo kiliendelea kutunza aina 216 za mkusanyiko wakahawa ya robusta kwa kupalilia, kuweka mbolea,kupunguzia machipukizi na kujaziliza micheiliyoharibika. Juhudi zimefanyika kupanua shamba lamkusanyiko wa kahawa kwa kukusanya aina 396 zakahawa ya robusta kutoka mashamba ya wakulima katikawilaya za Bukoba, Karagwe, Missenyi and Muleba. Mpakasasa kituo cha Maruku kimekusanya aina 300 za kahawaya robusta ambazo zitapandwa mwezi Aprili 2008.

Kituo Kidogo cha Maruku, Bukoba

Jedwali 3: Ufuatiliaji wa ugonjwa wa mnyaukofuzari katika wilaya za Bukoba na Misenyi

Wilaya Kata Idadi ya Idadi ya Asilimia yamibuni mibuni mibuniiliyoathiriwa iliyong'olewa iliyong'olewa

Bukoba Rubafu 1,318 727 55.1Kishanje 3,878 2,958 76.3Kaagya 6,350 4,184 65.9Buhendangabo 3,332 2,577 77.4Nyakato 2,714 1,565 57.7Buhembe (Bukoba mjini) 101 0 0Maruku 235 235 100Kanyangereko 45 45 100Ibwera 60 60 100

Misenyi Kanyigo 11,411 2,809 24.6

Page 29: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

29

Utafiti wa aina za Robusta zenye ukinzani wamnyauko fuzari wa kahawaKwa kushirikana na idara ya uboreshaji zao kutokaLyamungu, kituo kiliendelea kutunza bustani mama yakorona za kahawa ya robusta zenye ukinzani wa mnyaukofuzari wa kahawa iliyoanzishwa Maruku kati ya miezi yaFebruari na Juni 2006. Bustani hii ina aina mbalimbali 201za kahawa ya robusta. Miche hii inatunzwa kwa kuwekewambolea za samadi na chumvi chumvi na kupaliliwa kwamuda mwafaka na kudhibiti visumbufu vya mimea kwakutumia viua visumbufu vya mimea. Inategemewa kuwakuanzia 2008, bustani itakuwa na uwezo wa kuzalisha zaidiya miche 2000 kwa mwaka. Miche itakayozalishwaitatumika kuanzisha mashamba ya majaribio kwawakulima na mashamba ya majaribio mtawanyiko.

Vipaumbele Muhimu 2007- 2008Programu ya mafunzoKituo kimepanga kuendesha mafunzo kituoni na kwawakulima yatakayolenga katika ukarabati wa mashambana mibuni ya robusta iliyozeeka, matumizi sahihi yapembejeo na ubora wa kahawa. Lengo ni kufundishawakulima 4,680, kuendesha mafunzo kwenye vikundi120 na vyama vya msingi 185 ifikapo 2010.

Kufanya siku za maonyesho na ziara za mafunzoKituo kimepanga kufanya siku za maonyesho ambapowakulima 1,000 watashiriki. Pia kituo kimepangakuwezesha ziara za mafunzo kwa wakulima 300 namaafisa ugani 20.

Uzalishaji wa miche bora ya kahawa ya robustaKituo kitaendelea na uzalishaji wa miche bora ya kahawaza arabika na robusta kwenye bustani za Ibwera, Biirabona Maruku ili kukidhi mahitaji ya wadau hapa mkoani.Kuna mpango wa kupanua bustani mama za kahawa yaarabika kutoka 594 kufikia 2194 kwenye bustani zaMaruku, Biirabo na Ibwera ili kukidhi mahitaji ya michekwa wadau hapa mkoani, na kuzalisha miche ya robusta640,000 ifikapo mwezi Juni 2008.

Kituo Kidogo cha Maruku, Bukoba

Utunzaji na uanzishaji wa shamba la ainambali mbali za kahawa ya RobustaMaruku itaendelea kutunza mashamba ya majaribioyaliyopo kituoni kwa kuweka mbolea za samadi, chumvichumvi, kupalilia, kuondoa machipukizi, kuvuna,kuanika na kukoboa kahawa. Kituo pia kitaendeleakukusanya takwimu za mavuno, kutathmini uwezo wauzaaji na ubora wa kahawa ya robusta kwa kufuatavigezo vifuatavyo: uwezo wa kuzaa, uzito wa punje,uwiano wa kahawa safi na maganda, na muonjo. Pia kituokitaanzisha shamba jipya la aina mbalimbali za kahawaya robusta hapa kituoni. Majaribio hayo ni pamoja na:• Kutathmini uwezo/matokeo ya aina 5 za kahawa yarobusta zilizochanguliwa kutokana na aina zilizopoMaruku,• Kutathmini uwezo/ matokeo ya aina 24 nzuri za kahawaya robusta zilizochagualiwa kutokana na aina 136zilizokusanywa kutoka mashamba ya wakulima mkoaniKagera • Kutathmini uwezo wa aina 136 za kahawa ya robustazilizokusanywa kutoka kwenye mashamba ya wakulimakatika mkoa wa Kagera

Pamoja na majaribio hayo, taasisi itaendelea na mpangowake wa kuanzisha shamba la mkusanyiko wa kahawambalimbali kutoka kwenye mashamba ya wakulimakatika wilaya za Bukoba, Karagwe, Misenyi na Muleba nakuziotesha kituoni Maruku.

Pia, jaribio la kutathmini athari za mahusiano yamazingira na kiinitete katika ubora / muonjo wa kahawaya robusta litaanzishwa kwa kukusanya zaidi ya sampuli100 za kahawa ya vikonyo na kahawa ya asili kutokamashamba mbalimbali ya wakulima katika wilaya zaBukoba, Karagwe, Misenyi na Muleba.

Programu ya kuchunguza aina za kahawa yaRobusta yenye ukinzani na mnyauko fuzari Kwa kushirikiana na idara ya uboreshaji wa zao, kituokitaendelea na uchunguzi na uzalishaji wa aina 201 zakahawa ya robusta zenye ukinzani kwa ugonjwa wamnyauko fuzari wa kahawa kwa ajili ya majaribiomtawanyiko katika maeneo yaliyoathiriwa na mnyaukofuzari wa kahawa katika wilaya za Bukoba, Karagwe,Misenyi na Muleba. Pia kituo kitaendelea na kampeni yakeya kutokomeza ugonjwa wa mnyauko fuzari wa kahawa.

Majaribio ya kilimo mseto na ufugaji nyuki Mwaka ujao, kituo kitaanzisha programu ya kilimo msetowa kahawa na miti; na ufugaji wa nyuki katika kijiji chaByamutemba ili kuwaongezea kipato wakulima wakahawa. Jaribio la kutathmini kilimo mseto cha kahawana migomba lililoko Maruku litaimarika mwaka kesho.

Wakulima wakivutiwa na uzalishaji wa miche wakati wa ziara za mafunzo

Page 30: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

30

Kituo Kidogo cha Maruku, Bukoba

TaCRI inaviwezesha vikundi vya wakulima kupitiampango wake wa mafunzo shirikishi (PTA) ambaokimsingi ni kuwatumia wakulima wenyewe kusaidiakusambaza teknolojia mwafaka za kilimo bora chakahawa kwenda kwa wakulima wengine wa kahawa.Dhana ya kuwawezesha wakulima kuendesha mafunzoimekuwa na mafanikio makubwa katika kusaidiakufikisha taarifa kwa watu wanaozihitaji

Juhudi ni kikundi cha wakulima kilichopo katika kijijicha Chabuhora wilayani Karagwe na kina zaidi yawanakikundi 30. Kikundi kilianzishwa ili kuwawezeshawakulima ambao walitelekeza mashamba yao, kwasababu ya bei ya kahawa kuwa chini, kufanya kazi pamojana kuanza kufufua mashamba yao.

Kwa kushirikiana na idara ya kilimo ya halmashauri yawilaya ya Karagwe, Kituo kidogo cha TaCRI Marukukilikuwa kinafanya kazi karibu sana na kikundi hiki kwakuwapatia mafunzo, miche ya kupanda na taarifa zamasoko ili kuwapatia wakulima hali ya kujiamini na vifaawanavyohitaji ili kuanza programu ya uboreshaji. Kwakipindi cha miaka michache iliyopita kikundi kilishirikikatika mafunzo yaliyoratibiwa na TaCRI Maruku kwakushirikiana na ofisi ya kilimo wilayani Karagwe.Kikundi kilianzisha mashamba ya mfano/ majaribiokuonyesha njia ya kulengeta mibuni iliyozeeka, kuondoa

machipukizi, kutengeneza makinga maji, matumizi yambolea ya samadi na njia sahihi ya kutengeneza mboleavunde. Matokeo ya kazi hii yaliivutia TaCRI, na kituocha Maruku kilikiomba kikundi kufanya siku yamaonyesho mwezi Juni 2006, ambapo zaidi ya watu 2,500walihudhuria.

Mwezi Novemba 2006, Bodi ya wakurugenzi ya TaCRIilikitembelea kikundi hiki na iliridhishwa na mashambayalivyokuwa yametunzwa na kila mwanakikundi alikuwatayari kuhakikisha kuwa kila mwanakikundi mwenzakeana shamba la kahawa lililotunzwa vizuri.

Kikundi cha Juhudi -TaCRI tayari kimewahamashishawanakijiji wengine kujiunga na utaratibu huu wamafunzo na matokeo yake wakulima kutoka vijiji jiraniwaliunda vikundi vyao. Vikundi vilivyofauluvimeendelea kuvutia wakulima wengine kuunda vikundivyao, kuboresha mashamba yao na maisha yao na kishakuvutia wakulima wengine zaidi.

Uchunguzi Kifani 10: Vikundi vya wakulima kuendesha mafunzo shirikishi kwa vikundi vya wakulima: Uchunguzikifani kutoka Kikundi cha Juhudi wilaya ya Karagwe

Page 31: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

31

Manyafubu ni kikundi cha wakulima kilichoko katikakijiji cha Bushasha, tarafa ya Bugabo katika wilaya yaBukoba. Kikundi kina wanakikundi 25 (13 wanaume na12 wanawake) na kilianzishwa mwezi Machi 2004 kwalengo la kuwaunganisha wakulima kushirikiana katikakupambana na mnyauko fuzari wa kahawa kwenyewilaya.

Tangu kikundi kianzishwe, zaidi ya wakulima 1,800wameshapatiwa mafunzo katika vijiji 18 vya tarafa yaBugabo. Katika mwaka wa 2006/2007, mashamba 1513yalitembelewa kati yake mashamba 508 yalikutwayameathiriwa na mnyauko fuzari. Jumla ya miti yakahawa 17,693 ilikuwa imeathiriwa na ugonjwa na miti12,658 imeng’olewa.

Hadi sasa, kikundi cha Manyafubu pia kimeanzishamashamba darasa 7, vikundi 10 na vituo vya mafunzo 20.Ili kutekeleza kazi vizuri, kikundi kimewesheshwakifedha na utaalamu kutoka TaCRI. Tayari kukundikimeshapokea jumla ya Shilingi milioni moja kutokaTaCRI, kiasi ambacho kilitumika kwa usafiri wawakufunzi waliokuwa wakisafiri ndani ya tarafa.Wanakikundi walichangia zaidi ya shilingi laki sabaambazo ni mchango wao unaoonyesha utayari waokatika kuleta mabadiliko.

Muundo wa kikundiIli kusambaza teknolojia kwa ufanisi kikundi chaManyafubu kina muundo wa kamati mbalimbali zenyekazi tofauti. Kamati na kazi zake ni kama zinazoanishwahapo chini:-

11.. KKaammaattii kkuuuu yyaa uutteennddaajjiiKamati hii ina wajumbe wane; mwenyekiti wa kikundi,katibu (mwezeshaji), mweka hazina na mtunza nidhamu.Kazi za kamati hii ni kuhakikisha kuwa mikutano yakikundi inafanyika kama ilivyopangwa, kusaidiakuendesha mashamba darasa kila Jumamosi ya mwishowa mwezi, kufuatilia na kutoa misaada katika maswala yakijamii kama vile ugonjwa, misiba na harusi, kuwesheshamikutano na majadiliano wakati wa vipindi vya shambadarasa, kusaidia kutatua matatizo ndani ya kikundi nakuratibu utoaji wa ripoti kuhusu hali ya ugonjwa wamnyauko fuzari wa kahawa na maendeleo ya mafunzo naprogramu ya kutokomeza ugonjwa wa mnyauko fuzarikutoka katika vijiji 18 vya tarafa ya Bugabo.

22.. KKaammaattii yyaa mmiippaannggoo // mmaaffuunnzzooWajumbe wa kamati hii ni mwenyekiti (mwezeshaji) nakatibu (mwenyekiti wa nidhamu) na mlezi ambao kaziyao ni kutayarisha mpamgo wa mafunzo, kuunda kwayana kutunga nyimbo, kutayarisha mikakati ya mafunzo nakusimamia chama cha akiba na kukopa (SACCOS)kinachomilikiwa na kikundi.

33.. KKaammaattii yyaa NNiiddhhaammuuWajumbe wa kamati hii ni mwenyekiti wa kamati yanidhamu na mlezi wa kikundi. Kazi za kamati ni kutunzanidhamu ya kikundi wakati wa mikutano, kuhakikishakuwa wanakikundi wanakuwa na maadili mema katikajamii, kufuatilia kung’oa na kuchoma miti yote ya mibuniiliyoathiriwa na ugonjwa katika mashamba yao, kutunzasiri za kikundi na kuhakikisha kuwa vifaa ya kufanyiakazi vinatunzwa kwenye ofisi ya kikundi.

44.. KKaammaattii yyaa uukkaagguuzziiWajumbe wa kamati ni pamoja na mwezeshaji(Mwenyekiti), Mwenyekiti wa kikundi and mtunzamidhamu wa kikundi. Kamati hii huhoji uhalali wataarifa za mnyauko fuzari kutoka vijiji mbali mbali vyatarafa ya Bugabo na kusimamia ratiba ya mafunzo yakikundi.

55.. KKaammaattii yyaa ffeeddhhaa nnaa mmiippaannggooKamati hii ina wajumbe wanne; Mwenyekiti, Katibu,Mlezi wa kikundi na mjumbe mmoja kutokawanakikundi. Kazi za kamati hii ni kuhakikisha kuwamapato yote yameingizwa kwenye akaunti ya SACCOS,kuhakikisha kuwa fedha yote iliyopangwa imetumikakwa kazi zilizokusudiwa, kuhakikisha kuwa matumizi yapesa yanafuata utaratibu unaofaa na kutoa huduma zaharaka na kwa ufanisi kwa wanakikundi.

66.. MMlleezzii wwaa kkiikkuunnddiiKazi ya mlezi ni kuhakikisha kuwa ada za wanakikundizinakusanywa, kusaidia kutatua matatizo ya wanakikundina kutunza vifaa vya kikundi.

77.. BBooddii yyaa wwaaddhhaammiinniiWajumbe wa bodi ya wadhamini ni: Mwenyekiti wa bodi(Diwani), Mwenyekiti wa kijiji (Mjumbe) na Mwezeshaji(Katibu). Kazi za bodi ni kuangaliza kazi za kikundi kwamtazamo wa kuona mbali.

Uchunguzi Kifani 11: Uchunguzi wa kikundi cha Manyafubu-matumizi ya vikundi vilivyofanikiwa katika kusambazateknolojia

Kituo Kidogo cha Maruku, Bukoba

Page 32: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

32

Kituo Kidogo cha Mbimba, Mbozi

Kituo Kidogo cha Mbimba, MboziKituo kidogo cha Mbimba kinaendelea kujiimarisha katika jukumu lake kuu la kuboreshamaisha ya wakulima wa kahawa katika mikoa ya Mbeya na Rukwa.

Ili kufikia malengo hayo kituo cha Mbimba kimeongeza jitihada zake kwa kuunda vikundivya wakulima wadogo wadogo vyenye wakulima kati ya 25-30. Jumla ya vikundi vipatavyo80 vimekwishaundwa na vimefaidika na elimu ya uzalishaji na uboreshaji wa kahawa ilikuongeza tija. Katika mwaka husika mafunzo yaliendelea kutolewa kwa wadau wa kahawa,mahusiano kati ya watafiti, wataalamu wa ugani na wakulima yameimarishwa, nauzalishaji wa miche bora chotara ya kahawa ambayo haishambuliwi na chulebuni na kutuya majani kwa ajili ya kubadili mashamba na upanuzi.

Mafanikio Makuu 2006 - 2007Mnamo tarehe 24/11/2006, Makamu wa Rais Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na ujumbe uliojumuishaMkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi naviongizi wengine wa Serikali walitembelea kituo chaMbimba. Makamu wa Rais pamoja na ujumbe wakewalivutiwa sana na shughuli za utafiti zinazofanywa nakituo pamoja na mbinu zinazotumika katika kusambazateknologia husika kwa wadau. Makamu wa Raisalitembelea na kuona bustani mama ya kahawa,inayotumika kuzalisha miche ya kahawa kwa kutumiavikonyo.

Katika jitihada za kukidhi ongezeko la mahitaji yateknolojia kwa wakulima mkoani hapa, kituo kidogo chaMbimba kimefanya kazi zifuatazo katika mwaka uliopita:

Kuboresha Mawasiliano Miongoni mwaWadauKituo kidogo cha Mbimba kinaendelea kusambazamatokeo ya utafiti kwa wadau kwa kutumia vipeperushi,mabango, kalenda na vyombo vya habari. Zaidi ya seti2000 za vipeperushi vyenye ujumbe mbalimbalivimesambazwa kwa wataalamu wa ugani, vikundi vyawakulima, mashamba makubwa ya kahawa na kwawadau wengine. Vipeperushi na mabango vinaelezeateknologia zifuatazo; Uzalishaji wa miche bora kwa njiaya vikonyo, Teknologia ya upachikizaji, udhibiti wawadudu na magonjwa ya kahawa, na usindikaji wakahawa.

Matumizi ya vyombo vya habariMbimba imeendelea kutangazwa kazi zake kwa wigompana. Kituo kimetangazwa kupitia TVT, ITV, StarTV,RTD na RFA, na Magazeti mbali mbali kama Majira,Mwananchi na Daily News.

Ziara za MafunzoTaCRI imegharamia ziara ya mafunzo kwa wakulima 20kutoka Wilaya ya Rungwe na Mbozi, Maafisa Ugani

wanne, viongozi wanne wa ngazi ya wilaya na mjumbemmoja wa Bodi ya TaCRI Bw. Godfrey Makonganyakutembelea wakulima wa kahawa wa wilaya ya Mbinga.Malengo ya ziara hii ilikuwa ni kuwapa fursa wakulimana viongozi kuona, kujifunza na kubadilishana uzoefu wauzalishaji na uboreshaji wa kahawa, pia uundaji nauendeshaji wa vikundi vya uzalishaji na uboreshaji wakahawa na uzalishaji wa miche bora kwa njia ya vikonyo.Ziara hii imekuwa na mafanikio makubwa kwa wajumbekwani wamekuwa waalimu bora kwa wakulima wenginekatika maeneo yao. Ziara kama hizi pia ziliendeshwandani ya wilaya kwa wakulima wa vikundi vya wakulimakutembeleana.

MafunzoMafunzo ya mbinu za uzalishaji na uboreshaji wakahawa pamoja na utaalamu wa uzalishaji wa miche kwanjia ya vikonyo na upachikizaji yaliendelea kutolewa kwawadau mbalimbali hapa kituoni Mbimba. Wadauwaliofaidika na mafunzo haya ni; Wakulima 80 naMaafisa ugani 40 toka Wilaya za Mbozi na Rungwe,wanafunzi 53 wa Shule za Sekondari, na wanafunzi 10toka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA).

Mafunzo yalifanyika kwa wakulima vijijini kupitiavikundi. Jumla ya wakulima 520 toka Wilaya za Mbozi(wakulima 369), Rungwe (wakulima 120) na Mbeya(wakulima 38) walipata mafunzo. Mafunzo hayo yawakulima na wadau wengineo yamesaidia wakulimakuboresha kahawa yao kutoka daraja la 9 mpaka daraja la6 na 5. Haya ni mafanikio makubwa na ya wazi katikangazi ya wakulima.

Mafunzo Kwa Wahudumu wa BustaniMafunzo ya kina ya nadharia na vitendo ya usimamizi wabustani mama za uzalishaji wa miche vijijini yalifanywakwa wahudumu 24 kutoka wilaya Mbozi.

Uzalishaji na Usambazaji wa Miche ChotaraIli kukidhi mahitaji ya miche chotara kwa wadau, TaCRIMbimba ikishirikiana na Halmashauri za Wilaya husika

Bw. Issac Mushi, Afisa Ugani,Mbimba

Page 33: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

33

Kituo Kidogo cha Mbimba, Mbozi

wamehamasisha na kuviwezesha vikundi vya wakulimakuanzisha na kutunza bustani ili kujizalishia miche yaowenyewe. Ifuatayo ni orodha ya bustani zilizoanzishwakatika maeneo mbalimbali. Mbozi bustani 12 zenyemiche mama 4,200; Ileje bustani 2 zenye miche mama1,040; Mbeya bustani moja yenye miche mama 650; naRungwe bustani 4 zenye miche mama 1,600.

Uanzishaji wa machipuzo kwa wakulimaMachipuzo kwa ajili ya kuchipuza vikonyoyanayomilikiwa na vikundi vya wakulima wadogowadogo yameanzishwa katika maeneo yale yenyeupungufu wa maji kwa ajili ya kuanzisha bustani mama.Vikonyo vya kupanda kwenye machipuzo vinatokakatika bustani mama ya kituoni Mbimba. Kikundi chawakulima cha Hiyari ya Moyo na Masangula vimepandajumla ya vikonyo 1500 na 3000 kwenye machipuzo yao.

UpachikizajiUpachizakaji wa vikonyo kutoka katika miti bora ya kahawachotara umefanywa katika miti ya zamani. Jumla ya miti 670ya zamani imepachikizwa na inaendelea vizuri.

Jumla ya miche 2,000 ilioteshwa kwenye bustani yakituoni ambayo itapachikizwa na aina mpya za kahawa.Zoezi hili litafanywa kwenye bustani za wakulima zenyemiche ya zamani karibu 40,000.

Ukarabati wa majengo na miundombinuKazi ya ukarabati kituoni Mbimba ilianza mwezi Oktoba2006 na ilienda kwa haraka. Ukarabati ulijumuisha: a) Majengo manne ya kuishi pamoja na nyumba moja yawageni, madarasa na mabweni, jingo la ofisi, paa lamagari, na paa la pampu ya maji.b) Kingo za bwawa, kufunga tenki la maji, miundombinuya umwagiliaji kwenye mashamba ya kahawa na bustani,ukarabati wa machipuzo na ujenzi wa machipuzo mapya.

Vipaumbele Muhimu 2007 - 20081. Kuendelea na usambazaji wa teknolojia na matokeo yautafiti kwa wadau lengo likiwa ni wakulima 40,000ifikapo mwezi Juni 2008.2. Kutembelea na kuhamasisha wadau wa kahawa katikawilaya tano; Mbozi, Rungwe, Ileje, Mbeya na Mpandawalau mara moja kila miezi mitatu.3. Kuendeleza ziara za mafunzo kwa wakulima ndani nanje ya mkoa.4. Kuwezesha vikundi vya wakulima kufanya maonyeshokatika vijiji husika.5. Kushiriki katika maonyesho ya kilimo (Nane Nane) yakanda yatakayofanyika Jijini Mbeya.6. Kuendeleza vishamba vya maonyesho vyenye teknolijiampya kwa wadau katika wilaya tano (5).7. Kuendesha warsha ili kuimarisha ushirikiano kwamaafisa ugani katika Wilaya tano kwa kulenga angalaumaafisa ugani 75.8. Kuendesha mafunzo ya teknolojia mpya katika juhudizinazo endelea ili kuongeza tija na ubora wa kahawa kwavikundi visivyopungua 80 vya wakulima katika wilaya 5pamoja na wakulima 40,000 na maafisa ugani 75.9. Kuhamasisha wakulima kumenya kahawa kwa pamojakatika vituo vya kati vya kumenyea kahawa ili kuongezaubora na kufaidi bei nzuri.10. Kupanua bustani mama ya hapa kituoni kutoka miche10,000 hadi 12,000.11. Kuhamasisha na kuwezesha Halmashauri za wilaya zaRungwe na Ileje kuanzisha na kuendesha bustani zenyemiche mama 2,000 kila moja.12. Kuwezesha uanzishaji wa Bustani mbili za michemama katika shamba la Itende N.S and Shiwanda.

Wakulima wakimsikiliza Bw. Charles Mwingira kwa makini wakati wamavunzo ya wakulima vijijini

Uanzishaji wa bustani mama mpya za wakuilima ili kuharakisha uzalishajiwa aina mpya bora za kahawa: Upandaji bustani mama (kushoto) nabutani mama mpya inayotunzwa vizuri (kulia)

Page 34: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

34

Kituo Kidogo cha Mbimba, Mbozi

Vidugamba vya kahawa (Coccus viridis) ni wadudusumbufu katika nchi nyingi zinazolima kahawa.Vidugamba wamekuwa tishio la uzalishaji wa kahawakatika Nyanda za Juu Kusini pamoja na wilaya ya Mbozi.Katika maeneo ambayo wadudu hawa hawakudhibitiwa,inakadiriwa kusababisha upotevu wa mazao kwa asilimia60. Uthibiti wa vidugamba unaonekana kuwa mgumukwa sababu wakulima wengi bado hawana elimu kuhusuvitu vinavyosabisha vidugamba, na uhusiano kati yavidugamba na sisimizi. Kwa kukosea zaidi, kuna baadhiya wakulima wanaamini kuwa husababishwa na sisimizi.

UfafanuziVidugamba ni wadudu wa kijani, wenye umbo bapa,umbo la yai na rangi ya kijani ana madoa meusi sehemuya katikati mgongoni. Vidugamba ni mdudu mdogo sanamwenye urefu kati ya milimita 2.5 hadi 3.25.na upanakati ya milimita 1.5 hadi 2. Kidugamba aliyekomaa huishimaisha yake yote sehemu moja ya jani bila ya kuhamaiwapo kwenye jani alilopo halitakufa. Vidugambawalioanguliwa ni wachangamfu na huweza kutembeamwendo wa kasi wa mita moja kwa saa. Kwa kawaidahuishi upande wa chini wa jani karibu na mshipa wa katiya jani au karibu na ncha ya chipukizi la kijani.

Vidugamba na SisimiziVidugamba huzalisha kiasi kikubwa cha uchafu chenyeasili ya utamu kama asali, ambao huvutia sisimizi najamii nyingine za Sisimizi. Muungano wa sisimizi navidugamba ni visumbufu katika mmea wa kahawa.Inafikiriwa kuwa kuna uhusiano wa kutegemeana kati yaVidugamba na sisimizi ya kwamba Sisimizi wanafaidikakwa kula asali, ambapo Sisimizi wanaposafiri kwenyemmea, husafirisha vidugamba kuzunguka mti wakahawa, hivyo kuongeza uwezo wa vidugamba kufanyauharibifu zaidi.

Hata hivyo, tafiti nyingi zimeonyesha kutokuwepo kwamahusiano ya kutegemeana katika maisha. Kwa mfanoVan der Goot, kwenye utafiti wake aligundua kuwaSisimizi wanavutiwa na vidugamba, lakini hawasafirishividugamba. Vilevile mtafiti Keuchinius aligundua kuwahakuna uhusiano uliopo katika kuenea kwa Vidugambana sisimizi unaohusisha kuenea kwa Vidugamba kwanihuwezi kukuta vidugamba kwenye kiota cha sisimizilakini pia siyo kawaida kukuta mti wa kahawaulioshambuliwa na vudugamba na hauna sisimizi kabisaambao husababisha ungozeko la uzalianaji wavidugamba na hivyo kuongeza uharibifu. Kwa hiyokutokana na vithibitisho vingi kuhusu uhusiano wakaribu baina ya sisimizi na vidugamba, ni faida kudhibitisisimizi ili kutokomeza vidugamba.

Historia ya MaishaVidugamba hutaga mayai ambayo huanguliwa kwaharaka sana kiasi kwamba wadudu wachangawachangamfu huonekana chini ya vidugambawanaoendelea kutaga mayai. Kuna hatua tatu za waduduwachanga mithili umbile la yai na bapa, wanao ongezekaumbile kwa kila hatua. Mdudu huendelea kutembeatembea hadi ukomavu wake unapofikia ambapo hutagamayai kiasi cha 50 na huweza kufikia hadi mayai 600.Kuzaliana kwa weza kuanza mdudu anapotimiza umriwa wiki 6. Kidugamba ana uwezo wa kuendelea kutagamayai kwa muda wa siku 21 hadi siku 111. Muda wakewa kuishi ni kati ya siku 89 hadi 214. Vidugamba hujilishakatika sehemu za bapa za chini ya jani lililonawiri namara chache katika sehemu ya juu. Pia huweza kulasehemu teketeke kwenye shina nchani na kwenye punjechanga.

Madhara katika MmeaVidugamba hufyonza majimaji na virutubisho kutokakwenye mmea, hatimaye husababisha mmea kufa hasakwa mimea iliyo kwenye kitalu. Sukari na virutubishovinginevyo vya chakula vinavyochukuliwa kutokakwenye mmea wa kahawa hutolewa na vidugamba kwanjia ya kinyesi ambacho husababisha utando mweusi wamasizi kwenye majani na matawi ambapo hupunguzaeneo la mmea la kutengeneza chakula. Nta huendeleakuwepo kwa kiasi kikubwa iwapo hapatakuwepo nasisimizi, hatimaye husababisha majani kukauka na mmeakufa.

Udhibiti wa VidugambaKwa kufahamu uhusiano uliopo kati ya sisimizi navidugamba njia dhabiti ya kupunguza mashambulizi aukuzuia maambukizi ni kutoruhusu Sisimizi kupandakwenye miti ya kahawa kwa kutumia mbinu zifuatazo;kukata matawi yote ya mikahawa yanayogusana na ardhi,kupulizia dawa kwa kuelekeza kwenye shina ambapokuna uwezekano wa kuwa na kiota cha Sisimizi, kufungakipande cha kitambaa cha nguo kilichochovywa kwenyesumu ya kuulia wadudu kwenye shina chini kidogo yamatawi ya mwanzo, kunyunyuzia madawa ya sumuyanayoshauriwa na wataalamu. (dawa aina ya Selecron720EC (profenophos) inashauriwa kunyunyuziwakiwango cha lita moja kwa hekta moja na unyunyuziajiurudiwe kila baada wiki mbili mara tatu kiwango hikikitaangamiza vidugamba pamoja na Sisimizi).

Uchunguzi Kifani 12:Vidugamba: Tishio katika Uzalishaji wa Kahawa Kanda za Juu Kusini

Page 35: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

35

Kituo Kidogo cha Ugano, MbingaKituo kidogo cha Mbinga kimeendelea kusaidia ufufuaji wa kilimo cha kahawa mkoaniRuvuma (Mbinga na Songea) na kupanua shughuli zake kwa mafanikio kwenye mkoa waIringa mbao ni mkoa mwingine unaolima kahawa. Mkazo umekuwa katika kutangaza nakusambaza teknolojia mwafaka kwa wadau, na kuhamasisha wakulima kujiunga kwenyevikundi kwa kutumia mbinu shirikishi.

Kituo kiliendelea kusaidia maendeleo ya bustani mpya ili kuzalisha miche kwa ajili yaupandaji upya, na pia kuandaa na kutoa mafunzo kwa wakulima na maafisa ugani. Piakulikuwa na shughuli maalum zilizolenga kuhamasisha wakulima kukarabati mashambayao ya zamani kwa kulengeta na kupachikiza aina mpya za kahawa. Kampeni yakuhamasisha unywaji wa ndani wa kahawa ilifanyika ndani ya mkoa ili kusaidia juhudi zakupanua masoko na kuongeza mahitaji.

Mafanikio Makuu 2006-2007Kituoni Ugano, azima ya kufanya kazi na vikundi vyawakulima iliendelea kwa kupeleka teknolojia sahihi kwawakulima. Uanzishaji wa vikundi vya wakulimauliendelea na matokeo yake ni kwamba vikundi 92 vyawakulima vilianzishwa. Kituo pia kiliendelea kutangazashughuli za utafiti kwa kupitia mikutano mbali mbaliiliyofanyika katika wilaya za Ludewa, Njombe, na Kilolozilizopo mkoa wa Iringa na wilaya za Songea vijijini naMbinga zilizopo mkoa wa Ruvuma.

Mafunzo kwa WakulimaWakulima walifundishwa mbinu bora za kilimo chakahawa na uzalishaji wa miche wa aina mpya hususanjinsi ya kuanzisha bustani mama, utayarishaji wa sehemuza kuweka bustani mama, umbali kati ya miche, namnaya kupanda, jinsi ya kuvuna machipukizi, jinsi yakupanda kwenye viriba, utunzaji wa bustani mama nambinu zote zinazotumika. Vikundi 84 vya wakulimakutoka kata mbalimbali wilayani Mbinga na wilaya za njeya Mbinga zilinufaika na mafunzo hayo zikiwemo kata 9toka Mbinga, 8 Njombe, 4 Ludewa, 2 Songea vijijini na 4Kilolo.

Matumizi ya vyombo vya habari katikakutangaza matokeo ya utafitiShughuli za Ugano ziliendelea kutangazwa vizuri. Kituokilitangazwa kupitia ITV, TBC1, Star TV, Channel 10,TBC FM, Radio Free Afrika na Radio Maria. Vipindivilivyotangazwa vilihusu uzalishaji na usambazaji waaina mpya za kahawa, mafunzo kwa wakulima nauboreshaji wa zao la kahawa. Makala mpya zipatazo nanezilichapishwa katika magazeti mbalimbali ya hapanchini.

Kubadilishana ziara za mafunzo kwawakulimaWakulima 147 wakifuatana na maafisa ugani tokavikundi 18 vya wakulima wilayani Mbinga na wakulima135 na maafisa ugani toka wilaya za Njombe, Ludewa naKilolo Mkoani Iringa walitembelea Ugano katika kipindicha mwaka uliopita.

Mafunzo kwa wakufunziKituo kiliendesha programu ya mafunzo kwa wakulima175 na maafisa ugani toka vikundi mbali mbali vyawakulima vya mikoa ya Ruvuma na Iringa. Mafunzoyaliweka mkazo kwenye usimamizi wa bustani, uzalishajiwa aina mpya ya kahawa na uendelezaji wa bustanimama.

Upachikizaji Upachikizaji wa aina mpya ya kahawa juu ya mashina yazamani, ni njia mojawapo inayotumika kubadilishamashamba ya zamani. Katika mwaka husika, mashamba45 yalilengetwa na kupachikizwa kama inavyoonyeshwakwenye mabano: Mbinga (18), Njombe (18), Kilolo (5),na Songea (4). Jumla ya miti 210 ilipachikizwa.

Bw. Felician Swai, Afisa Ugani,Ugano

Bw. Felician Swai (aliyesimama kushoto) akiongea kwenye moja yamikutano ya kufufua kahawa wilayani Kilolo

Kituo Kidogo cha Ugano, Mbinga

Page 36: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

36

Kituo Kidogo cha Ugano, Mbinga

Ushirikiano kati ya utafiti, ugani nawakulimaKituo cha Ugano kiliendelea kushirikiana na maafisaugani na kiliendesha warsha nne. Warsha mbiliziliendeshwa Mbinga, ambapo maafisa ugani 45 tokasehemu zinazolima kahawa walishiriki. Nyingineilifanyika Ludewa, Iringa na kuvutia maafisa ugani 6, naya nne ilifanyika wilayani Njombe ambapo maafisa uganiwanane walishiriki.

Kuandaa wakulima kwa ajili ya kutumiaviwanda vya kati kusindika kahawa pamojaJuhudi kubwa imefanyika kuwaandaa wakulima katikavikundi na kutumia kwa pamoja teknolojia sanifu yakumenya kahawa ambapo vikundi 127 toka Mbinga,Njombe, Kilolo, Ludewa na Songea vijijini vilinufaika namafunzo hayo. Baada ya mafunzo hayo, ubora wa kahawauliongezeka toka daraja 7-9 mpaka daraja 5-7. Hayo nimafanikio makubwa kwa wakulima wadogo na ni faidainayoonekana kwao kwamba juhudi zao zinalipakutokana na ukweli kwamba uongezekaji wa ubora wakahawa hupandisha bei na kuongeza kipato chamkulima.

Kusambaza miche ya vikonyoZaidi ya miche 22,700 ya kahawa ya vikonyo ilisambazwakwa wakulima. Jumla ya miti mama 1,800 ilisambazwakwa vikundi kila kimoja kikipatiwa miche 100 wilayaniMbinga na miche zaidi ya 3,950 ilitolewa kwa wakulimana vikundi na kupandwa mashambani katika wilaya zaLudewa, Njombe, Kilolo na Songea vijijini.

Katika kipindi cha mwaka uliopita, Wakurugenzi wote waHalmashauri za wilaya husika walitoa ushirikiano wa haliya juu na kuwezesha kuanzishwa kwa bustani za kahawaya vikonyo za ngazi ya wilaya, kata na vijiji. Kwa maranyingine tena kituo cha TaCRI Ugano kinashukuru kwadhati kwa mshikamano ulioonyeshwa katika kulengakuwaboresha wakulima wadogo katika maeneo yao.Vikundi vya wakulima na mkulima mmoja mmoja wenyevitalu walipatiwa miche 11,000 yenye mizizi kwa ajili yakuikomaza, na baadaye kuipanda kwenye mashamba yao.La ziada, miche 3,000 ilisambazwa kwa vikundi vyawakulima vyenye machipuzo.

Uanzishwaji wa bustani za WilayaTaCRI inaongeza msukumo mkubwa wa kuanzishabustani zaidi katika wilaya zote zinazolima kahawa ndaniya Mikoa husika. Mwaka 2007, bustani mbili kila mojaikiwa na miche 2,000 zilianzishwa wilayani Ludewa naMadaba Songea.

Uzalishaji wa miche ya vikonyo kwa wakulimaWakulima binafsi na vikundi vya wakulima vyenyebustani mama walifanikisha kuzalisha miche 31,000

ambayo walipanda mashambani mwao. Katika wilaya yaMbinga wakulima waliendelea kujenga jumla yamachipuzo mapya 82 kwa ajili ya kuendeleza uzalishajiwa miche. Hayo ni mafanikio yenye kuonekana.

Ushirikiano na Idara za utafiti TaCRIKituo kilifanya kazi vizuri na Idara ya Uboreshaji zaokwa kuanzisha shamba la mbegu kwa kupanda miche4,700 majike na shamba mtawanyiko la miti ya kahawafupi chotara. Kwa kushirikiana na idara ya kuongeza tijana ubora wa zao, kituo kilitathimini mbinu za usindikajiwa awali wa kahawa kwa mihula miwili mfululizo nakuanzisha jaribio kuhusu athari za miti ya kivuli kwenyekahawa, na athari za kutopiga morututu ili kupima kamakuna haja ya kutumia morututu kwenye hizi aina mpya.

Warsha za kimataifa, mikutano namaonyeshoKituo cha Ugano kiliendelea kushiriki katika shughulimbalimbali ngazi ya kanda, kitaifa na kimataifa. Bw.Feliciani Swai, Afisa Ugani, alishiriki katika Kongamanola wakulima wa Afrika Mashariki Novemba 2006,lililofanyika Buhuri Tanga, mwezi November 2006, nakuwasilisha mada ya “Kuboresha Maisha ya mkulima waKahawa, kusini Tanzania”. Vile vile alihudhuria mkutanowa kimataifa na maonyesho ya Shirikisho mahususi lakahawa la Amerika uliofanyika mwezi Mei 2007 hukoLong Beach, California nchini Marekani.

Kampeni ya unywaji wa kahawa hapa nchiniKatika kipindi cha mwaka uliopita, Kituo cha Ugano kwamara ya kwanza kilihamasisha unywaji wa kahawa. Kituokiliweka banda katika kituo cha magari ya abiria, Mbingamjini kilichotumika kufanya kampeni ya kunywa kahawana kiliwavutia watu zaidi ya 500. Mhe. Amina JumaMasenza, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga alishiriki kwakufungua kampeni hiyo.

Ufugaji nyuki – chanzo cha mapato mbadalaUfugaji nyuki ni chanzo cha pato mbadala kwa mkulimawa kahawa, na TaCRI iliwahamasisha wakulima kuhusuufugaji wa nyuki. Kituo kilitoa mizinga 8 kwa wakulimawa kahawa wa Madaba Songea, na kina mizinga 6 kituoniambayo hutumika kwa mafunzo.

Bustani mama ya kituo cha Ugano

Page 37: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

37

Kituo Kidogo cha Ugano, Mbinga

Vipaumbele Muhimu 2007- 20081. Kuzalisha miche 2.7 milioni kukidhi kampeni yaupandaji wa kahawa mikoa ya Ruvuma na Iringa.2. Kuendelea kutoa mafunzo vijijini ndani ya Wilaya zaMbinga (walau 25), Songea (10), Njombe (10), Ludewa(10), Kilolo (5), Mufindi (5) na Makete (5).3. Kuandaa na kuendesha sikukuu za wakulima mkoaniIringa (2 Ludewa, 2 Njombe) na Ruvuma (5 Mbinga).4. Kuendelea kutoa mafunzo kwa Maafisa ugani kuhusumbinu bora za kilimo cha kahawa mkoani Iringa(maafisa ugani wa vijiji 20) na Ruvuma (38).5. Kuanzisha bustani mama za wilaya katika wilaya zaNjombe, Ludewa na Kilolo mkoani Iringa na wilaya yaMbinga.6. Kuendelea na ziara za mafunzo kwa wakulima namaafisa ugani mkoani Iringa (vikundi 20) na Ruvuma(vikundi 40).7. Kutoa mafunzo ya mbinu bora za kilimo cha kahawakwa wakulima mkoani Iringa (vikundi 20) na Ruvuma(vikundi 30).8. Kuendelea na juhudi za kuwaunganisha wakulimakatika vikundi ili kuwawezesha kuuza kahawa yao mojakwa moja mnadani.9. Kuhamasisha wakulima zaidi kujiunga katika vikundi(walau vikundi 50) kutumia teknolojia ya umenyaji wakahawa katika mitambo ya pamoja kwa lengo la

Ufugaji nyuki ni chanzo cha mapato ya ziada kwa wakulima wa kahawa

kuboresha zaidi ubora wa kahawa.10. Kuhamasisha kulengeta na kupachikiza kahawabora kwa wakulima wapatao 100 ndani ya mikoa yaRuvuma na Iringa.11. Kuendeleza kampeni ya unywaji wa kahawamkoani Ruvuma.12. Kuwapatia wakulima wa Iringa miti mama zaidi(Kilolo 4,000, Njombe 5,000, Ludewa 4,000, naMufindi 2,000) na mkoani Ruvuma (Mbinga 8,000na Songea 5,000)13. Jumla ya wakufunzi 150 watapata mafunzo yakufundisha wenzao, washauri 8 wa ubora ngazi yaWilaya na maafisa ugani 60 ambao watafundishwauzalishaji bora wa kahawa, soko a kahawa,upachikizaji na upangaji wa mapato na matumizi.14. Kuongeza mashamba ya maonyesho wilayaniNjombe (3), Ludewa (3), Mbinga (3) na Songea (1).

Page 38: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

38

Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime

Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime

Kituo hiki kidogo cha Sirari ni kipya, kilianzishwa katika kipindi hiki cha utoaji taarifa kwaajili ya kusaidia kuendeleza na kupanua uzalishaji wa zao la kahawa katika Mkoa wa Marana Wilaya jirani. Kwa sasa kuna hekta 2,900 tu zilizolimwa na kupandwa kahawa katikaMkoa huu ambazo huzalisha karibu tani 2,300 za kahawa kwa mwaka, lakini inakadiriwakuwa na karibu hekta 35,000 zinazofaa kwa kilimo cha kahawa, kwa makisio haya zaidi yaasilimia 90 ya eneo linalofaa kilimo cha kahawa halilimwi zao hilo.

Kahawa aina ya Robusta na Arabica inaweza kulimwa na kustawi katika mkoa wa Mara,Nyanda za juu zikifaa kwa uzalishaji wa kahawa aina ya Arabica na Nyanda za chini kwakahawa aina ya Robusta. Hivi sasa kuna wakulima wapatao 8,000 tu katika mkoawanaotegemea kuendeleza maisha yao kutokana na kipato cha zao la kahawa. Kwa wakatihuu, lengo kubwa ni kusaidia wakulima wa kahawa waliopo kwa sasa. Kwa hali hiyo katikakipindi hiki cha utekelezaji vikundi 6 vya wakulima vilipewa mafunzo juu ya uzalishaji wa

kahawa ya vikonyo na kupewa miche mama 1,490 ya kahawa ya vikonyo. Miche 4,000, 000 ya kahawa ya vikonyoinahitajika kwa ajili ya kutosheleza hekta 2850 zinazolimwa kahawa aina ya Arabica kwa sasa.

Mafanikio Makuu 2006 - 2007 Kazi ya kwanza ya Afisa Ugani ilikuwa ni kupata majengoya Ofisi na vifaa vya kufanyia kazi pamoja na kujengauhusiano na watumishi wa Ofisi zingine katika wilaya yaTarime. Mara baada ya kunzishwa kituo kilifanyayafuatayo:

Mafunzo ya wakulima vijijiniShughuli muhimu ya kwanza ilikuwa ni kuendeshamafunzo ya wakulima vijiji kuhusu uzalishaji wa miche yakahawa ya vikonyo na uboreshaji wa miti ya zamani yakahawa.

Kilimo mseto Wakulima wengi katika eneo linalolimwa kahawa ulimakilimo mseto, huchanganya kahawa na mazao menginekama mahindi, viazi vitamu, mihogo, urezi, mtama, viazivikuu, ndizi, maparachichi na miti ya vivuli ya aina mbalimbali. Vikundi 5 vya wakulimwa vyenye jumla yawanachama 222 walishiriki katika mafunzo hayo yaushauri juu ya njia bora za kilimo mseto, nafasi nzuri zaupandaji pamoja na mbinu zingine za uzalishaji.

Uanzishaji wa bustani za miche ya kahawa yavikonyoJumla ya vikundi 8 vya wakulima vimeanzishwa katikakipindi cha mwaka uliopita na pia bustani mama za kahawaya vikonyo zinaendelea vizuri, vikundi vya wakulimaviliendelea kupewa mafunzo juu ya upandaji na utunzajiwa miche ya kahawa ya vikonyo, kwa kuwajengea uwezo namaarifa muhimu ya utunzaji sahihi wa bustani.

Vipaumbele Muhimu 2007 - 2008Uanzishaji wa bustani ya miche ya kahawa yavikonyo ya WilayaBustani ya wilaya ya miche ya kahawa ya vikonyoitaanzishwa Sirari, eneo lenye ukubwa la ekari 14.5 ambalolimetolewa na Wilaya. Mpango uliopo ni kuanzisha bustanimama ya miche ya kahawa ya vikonyo yenye miti 3,000ambayo itaongezwa hadi kufikia 10,000. Bustani hiyoitaongeza uwezo wa kuzalisha na kusambaza miche mipyaya kahawa ya vikonyo kwa wakulima wengi kwa ajili yakupanda.

Bi. Sheila Mdemu, Afisa Ugani, Sirari

Mafunzo ya kulengeta miti mizee ya kahawa

Page 39: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

39

Uanzishaji wa vikundi zaidi vya wakulima Katika kipindi hicho lengo ni kuanzisha vikundi vingine 8vya wakulima, ili kufikia idadi ya vikundi 16 ifikapomwishoni wa mwaka 2008.

Mafunzo kwa wakulimaKatika kipindi hicho lengo ni kuvipatia vikundi vyote vyawakulima mafunzo juu ya kanuni bora za utunzaji wa zaola kahawa pamoja na uzalishaji wa miche ya kahawa yavikonyo. Mafunzo ya darasani yatatolewa kwa vikindihivyo na wawezeshaji wakulima kwa muda wa siku tatukwa kila kikundi.

Mafunzo kwa wakufunzi yataendelea kupata kipaumbelekwa kutumia mafunzo ya wakulima vijijini ili kuimarishamafunzo hayo.

Ushirikiano na Halmashauri za Wilaya.Ushirikiano na Halmashauri za Wilaya utaimirishwa katikamaeneo ya ugani ili kusaidia na kuhimiza wakulimakuanzisha bustani za miche ya kahawa ya vikonyo.

Upanuzi wa huduma katika Wilaya zinazolimakahawaImepangwa kuwa huduma zitapanuliwa katika wilayanyingine zinazolima zao la kahawa. Wilaya zilizolengwakwa ajili ya kupanua huduma ni Serengeti na Ukereweambako vikundi vya wakulima pamoja na bustani za micheya kahawa ya vikonyo vitaanzishwa na mafunzo kwavikundi vya wakulima yatatolewa.

Maonesho ya wakulimaItakuwepo siku moja ya maonesho ya wakulima wa kahawakatika kikundi kimoja cha wakulima. Siku ambayo utunzajiwa zao la kahawa na mbinu za uzalishaji wa miche bora yakahawa kwa njia ya vikonyo vitaoneshwa kwa vitendo.Inakadiriwa kuwa wakulima 3,000 au zaidi watahudhuriasiku hiyo.

Uanzishaji wa mashamba darasaKatika kipindi hicho kituo kidogo kimepanga kuanzishamashamba darasa katika kila kikundi cha wakulima wakahawa, kuonyesha kwa vitendo njia bora za kilimo chakahawa pamoja na kuonyesha maendeleo ya uzalishaji wakahawa ya vikonyo.

Uzalishaji wa miche kwa njia ya vikonyo kwenye kikundi cha wakulima

Mandhari ya Tarime

Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime

Page 40: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

40

Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime

TaCRI inatumia mbinu shirikishi katika kufanya kazipamoja na wakulima. Mkakati ambao wakulimahujifunza kutoka kwa wakulima wenzao unasaidiakubadilishana maarifa, kukutana mara kwa mara kwaajili ya kujadili changamoto mbalimbali na kupata uzoefuwa pamoja kwa ajili ya kuboresha mashamba yao yakahawa pamoja na mazao mengine.

Kikundi cha Taswira ni kikundi cha mfano katika wilayaya Tarime. Kikundi kilianzishwa mwaka 2004 kwa lengomaalum la kuanzisha uzalishaji wa kahawa bora yavikonyo. Wawakilishi wa kikundi walifundishwa juu yauzalishaji wa miche ya kahawa kwa njia ya vikonyo nawalipewa miti mama ya kahawa kwa ajili ya uzalishaji.Kikundi kilianza na miti mama 250, lakini mingineilikufa na kubaki miti mama iliyokomaa na yenye afyanzuri ipatayo 236.

Mwanzoni kikundi kilianza shighuli zake vibaya nakilifanya vibaya kati ya vikundi vyote 6 vilivyokuwavimeanzisha bustani mama kwa ajili ya uzalishaji michekwa njia ya vikonyo. Lakini, kama methali ya kishwahiliisemavyo “Penye nia pana njia”, kikundi kilibadilika nahivi sasa kuwa kikundi shujaa. Kikundi kwa sasakimejizalishia zaidi ya miche 1,000 kwa wana kikundiwake, lakini kikundi hiki kimejitofautisha na vingine kwa

wanakikundi wake kuwa wahamasishaji hai wa wakulimawengine, wana nia thabiti na wanajituma kufundisha nakuvipatia vikundi vingine pamoja na wakulima binafsimaarifa waliyonayo. Kwa matokeo haya, vikundi vingine4 vipya vya wakulima vimeanzishwa katika kipindi hikicha utoaji taarifa.

Vikundi hivyo vipya hivi sasa vimeanza kuzalishakahawa mpya kwa njia ya vikonyo na kikundi chaTaswira kikiwapatia vikonyo na utaalam. Huu ndiotunaouita mfano wa kusambaza maarifa mara dufu,mfano ambao unawawezesha wakulima kusaidiana waokwa wao.

Uchunguzi Kifani 13: Ugani wa mkulima kwa mkulima – Kikundi cha Taswira – Gwitiryo

Wakulima wakishiriki kupanda vikonyo kwenye machipuzo wakati waziara za kimafunzo

Page 41: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

41

Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu

Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu Kituo kidogo cha Mwayaya katika wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma, ni cha pili kuanzishwana TaCRI katika mwaka uliopita.

Kituo kidogo cha Mwayaya ni cha pekee katika utafiti wa kilimo katika mkoa wa Kigoma naukanda mzima wa Ziwa Tanganyika kinachoshughulikia zao la kahawa. Kituo hiki kinapangakuhudumia takribani familia 4,000 zinazojishughulisha na kilimo cha kahawa katika mkoa waKigoma na wilaya jirani ya Ngara katika Mkoa wa Kagera.

Mkoa wa Kigoma ni maarufu kwa kuzalisha kahawa nzuri, yenye muonjo na harufu nzuri yau-asali na machungwa, ikiwa imekaangwa kwa wastani. Kituo kidogo cha Mwayaya kinanuiakukuza uzalishaji endeleu wa kahawa yenye ubora kwa kuwapa wakulima teknolojia mwafaka.

Afisa ugani wa Kituo kidogo cha Mwayaya aliwasili kituoni hapo mwezi Mei 2007 katika maandalizi ya awali katikakuwahudumia wadau wetu katika mkoa wa Kigoma.

Mafanikio Makuu 2006-2007Mawasiliano TaCRI Mwayaya ilihudhuria mkutano mkuu wa mwakawa chama cha ushirika cha RUMAKO ambapo wajumbezaidi ya 300 walihudhuria. Wajumbe walifarijika kuonaTaCRI ipo sasa kuwasaidia, nao walikuwa na maombimakuu matatu kwa TaCRI: TaCRI iwe mstari wa mbelekatika juhudi za kuwaelimisha wakulima katika njia boraza kilimo bora cha kahawa; taasisi ishirikiane na ushirikakatika kuitangaza kahawa ya Kigoma na taasisi iwapashewakulima habari za mara kwa mara kuhusu bei zakahawa katika soko la dunia.

Uhamasihaji wa usindikaji bora wa awali wakahawaWakulima waliendelea kufundishwa mbinu bora kuhusuusindikaji wa awali ili kuongeza ubora wa kahawa yao.Jumla ya wakulima 97 kutoka vikundi vya wakulima wavijiji vya Matiazo na Mukigo walipata mafunzo. Katikakijiji cha Mukigo, kikundi cha wakulima kilipatiwa vifaamuhimu ili kuwasaidia katika kukausha kahawa yao kwajinsi invyostahili, ikiwemo wavu (mabunda 2) misumali(kilo 10) na mbao (vipande 16).

MafunzoMafunzo yaliyofunguliwa na mkuu wa wilaya ya KigomaNdugu John Mongella yalihusisha wakulima 30 kutokakatika vijiji vitano vya Kalinzi, Mukigo, Matiazo,Mukabogo na Nyarubanda. Washiriki walipewa mafunzokatika uzalishaji wa miche ya kahawa bora kwa njia yavikonyo.

Katika kijiji cha Muhange, mafunzo kwa wakulimayaliendeshwa hususan katika nyanja za ukarabati wamashamba, udhibiti wa visumbufu vya zao na utunzaji

wa mashamba ya kahawa. Jumula ya wakulima 30wakiwemo wanawake 7 walishiriki katika mafunzo hayo.

Ziara za nje/vijijiniKatika kipindi cha mwaka 2006/07, wakulimawalitembelewa katika maeneo yanayolima kahawa katikamkoa wa Kigoma, miongoni mwa malengo ya ziara hizoikiwa ni kufahamu maswala mbalimbali wanayokabiliananayo katika uzalishaji wa kahawa. Ingawaje wengi wawakulima wanashgulikia vema mashamba yao, baadhiwameacha kabisa na miti ya kahawa katika mashambayao iko katika hali mbaya wakidai kukosa utaalam,pembejeo, bei ndogo ya kahawa na umri mkubwa wabaadhi ya wakulima.

Vipaumbele Muhimu 2007 - 2008Uzalishaji wa miche bora ya kahawaKuzalisha miche mingi ya kahawa kwa kutumia njia yambegu na pia kwa njia ya vikonyo, na kupachikiza micheya zamani kwa kutumia vikonyo vya kahawa bora. Lengoni kuwa na jumla ya miche 200,000 ya kahwa kwa mwakaujao.

Bw. Sixbert Mourice, Afisa Ugani,Mwayaya

Mfumo wa ukulima wa kahawa Kigoma

Page 42: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

42

Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu

Usambazaji na mawasilianoKuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na vikundi vyawakulima, lengo likiwa ni kuongeza vikundi 9 kutoka 11vilivyopo sasa.

Vikundi hivi vitaundwa katika wilaya zifuatazo: Kigoma(Mkongoro 1, Rusaba 1 and Mukigo 1), Kasulu (Mubanga1, Muhinda 1 and Kibwigwa 1), Kibondo (Muhange Juu1, Gwarama 1 na Kabale 1), na Ngara (Rulenge 1). Piakushiriki katika maonesho ya wakulima kama vile nanenane na siku za wakulima.

Mashamba ya maonyeshoJumla ya mashamba 7 ya maonesho yanatarajiwakuanzishwa katika wilaya zote na inatarajiwa kila shambala maonyesho litakuwa na miche ya kahawa bora 200.Mgawanyo wa mashamba haya utakuwa kama ifuatavyo.Kigoma (Mikabogo 1, Nyarubanda 1) Kasulu (Mwayaya1, Rusaba 1) Kibondo (Mabamba 1, Muhange 1), naNgara (Rulenge 1).

MafunzoMafunzo kwa wakufunzi yatafanyika kwa washiriki 300,ikiwemo wawakilishi wa wakulima na maafisa ughani,msisitizo ukiwa ni katika kuzalisha miche bora yakahawa na kukarabati mashamba.

Mafunzo vijijiniJumla ya wakulima 600 inalengwa kupatiwa mafunzovijijini katika wilaya zote nne, kwa kuwafikia angalauwakulima 150 kwa kila robo mwaka.

Mahusiano baina ya Utafiti na Ugani Mahusiano baina ya ofisi za ughani za wilaya yatazidikuboreshwa kwa kutumia maafisa ughani wa vijijikufikisha utaalam wa kilimo cha kahawa kwa wakulima.

Kutumia vyombo vya habariKuendelea kuwafikia wakulima kwa njia ya vyombo vyahabari mbalimbali vikiwemo magazeti, radio natelevisheni.

Siku za wakulimaJumla ya siku za wakulima 8 zinapangwa kufanyikakatika wilaya zote 4 na lengo ni kuwafikia angalauwakulima 5,000.

MachapishoKalenda ya zao la kahawa kwa ukanda wa Kigomaitaandaliwa na kuchapishwa. Pia andiko kuhusu kahawaya Kigoma kwa ajili ya ASIC 2008 litaandaliwa.

Kuimarisha vikundiBustani mama yenye miche 10,000 itaanzishwa katikakituo cha Mwayaya ili kuzalisha miche ya kutosha ilikupanua mashamba mama ya vikundi 9 vya wakulimavilivyopo hivi sasa. Lengo ni kuhakikisha kuwa kilakikundi cha wakulima kinakuwa na shamba mama lenyemiche 1, 000. Wakati huo huo, machipuzo 40 yatajengwakituoni Mwayaya huku machipuzo 36 yatajengwa katikavikundi vya wakulima.

Shughuli nyingineKituo kidogo kina mpango wa kutengeneza mizinga yanyuki wa asli, kama njia ya uzalishaji mali, ambapo piawakulima watahamasishwa kufanya hivyo ili kuborehsana kuongeza kipato chao.

Page 43: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

43

Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu

Kuna utamaduni wa kunywa kahawa iliyotengenezwakienyeji katika mkoa wa Kigoma, hususan miongonimwa jamii za kiislam, na kwa watengenezaji wa kahawa,inaweza kuwa ni biashara nzuri sana, kuweza kujipatiakiasi cha Sh. 18,000 kwa siku.

Bw. Idrisa ni mfano mzuri. Akiwa ni mkazi wa Kalinzimwenye umri wa miaka 36 alianza kutengeneza kahawamnamo mwaka 1991. kwa maneno yake mwenyewe,hawezi kuthubutu kuacha biashara yake hii kwani huuzakahawa yake kwa wing kwa wateja wake na hujipatiakipato kizuri. Kwa wanywaji wa kahawa katika kijiji chaKalinzi, Idrisa anasifika kwa kutengeneza kahawa nzuriwakati wote.

Je anafanyaje? Bw. Idrisa mara nyingi hununua kahawa ghafi au kahawaya ubora cha chini popote anapoweza kuipata kwa kulipakiasi cha Sh. 3,500 kwa bakuli moja linalokadiriwakubeba kiasi cha kilo moja na nusu.

Kwa kutumia kinu na mchi, buni hutwangwa ili kuondoamaganda ambayo hutenganishwa na punje kwa kupetwa.Punje hukaangwa kwa takribani dakika 45 kwenye jiko lakuni hadi punje zinapobadilika na kuwa na rangi nyeusiangavu.

Baada ya kukaangwa, kahawa sasa hutwangwa maranyingi iwezekanavyo huku ikichekechwa ambapohutokeza unga wa kahawa.

Katika kutengeneza kinywaji hiki, Ndugu Idrisahuchemsha katika maji unga wa kahawa kwa muda wadakika kumi ambapo hutokeza kahawa yenye ranginyeusi, pia yenye ladha chungu, lakini yenye kunukiavema. Humimina kinywaji chake katika birika nakuwauzia wateja wake katika vikombe vidogo. Wanywajiwa kahawa ya aina hii hutumia pia kashata ili kuongezautamu.

Biashara yenyeweKwa upande wa kipato, birika moja laweza kutokezavikombe vidogo vya kahawa 64 ambapo kila kimojahuuzwa kwa Sh. 50. Katika siku nzuri (siku ya sokokatika kituo cha Kalinzi) huweza kuuza wastani wabirika 12 za kahawa ambazo ni sawa na vikombe 760,ambavyo humpatia kiasi cha Sh. 38,400. Kwa siku zakawaida (hakuna soko) huuza wastani wa birika 9 sawana vikombe 570 na kumpatia kiasi cha Sh. 28,800.

Uchunguzi Kifani 14: Unywaji wa kahawa

Kahawa iliyokaushwa, mali ghafi ya kutengeneza kinywaji!

Kahawa iliyokobolewa na kupetwa

Ukaangaji wa kahawa

Page 44: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

44

Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu

Kwa upande wa gharama Bw. Idrisa hutumia Sh. 14,000kwa siku katika unnuuzi wa kahawa ghafi na shilingi4,000 kwa kununulia kuni na maji, na shilingi nyingine1,500 kwa kumlipa msaidizi.

Kuna Faida yoyote?Katika siku nzuri, ndugu Idrisa hupata hadi Sh. 18,000wakati kati siku siku za kawaida, hupata Sh. 8,000,kiwango ambacho ni kizuri, na cha juu zaidi ya kipato chataifa cha mtu mmoja mmoja kwa siku. Ni biashara nzurikwa kweli.

WatejaBw. Idrisa ana wateja wengi ambao kila siku huhudhuria.Mzee Ashel Katamba kwa mfano, hunywa wastani wavikombe 8 vya kahawa kwa siku, ambavyo, kwa manenoyake humfanya ajisikie vizuri.

Kahawa iliyokaangwa ikimwagwa kwenye kinu kwa ajiri ya kusaga

HitimishoKatika uchunguzi kifani kuhusu biashara hii ya Bw.Idrisa, ni dhahiri kuwa kutengeneza na kuuza kahawainaweza kuwa biashara nzuri, na kuna uwezekanomkubwa wa kuongeza kiasi cha unywaji wa kahawa.Kituo kidogo cha Mwayaya kinafikiria kusaidia kukuzaunywaji wa ndani wa kahawa kupitia mikakati ifuatayo. • Kuanzisha na kukuza mashindano ya unywaji nauonjaji wa kahawa• Kutoa mafunzo kwa watengenezaji wa kahawa jinsi yakuwahudumia vema wateja wao kwa kuboresha ubora nakuwasaidia wawe na mtazamo wa kijasiriamali• Kudahmini/kufadhili vilabu vya kahawa ambapo watuwengi wataweza kunywa kahawa iliyotengenezwa nakuandaliwa kienyeji.

Kwa sasa, wauza kahawa wengi wanatumia kahawa zaubora wa chini ambazo kimsingi sio nafuu kamawanavyofikiria. Kwa bei ya sasa ya kahawa ghafi, badowanaweza kununua kahawa iliyosafishwa kutokakiwandani, ambacho kipo karibu kabisa na watengenezajikahawa. Idrisa pekee hutumia kahawa inayofikia aukukaribia tani 1.5 kwa mwaka. Wauza kahawa kama yeyewapo wengi katika mkoa wa Kigoma. Ikiwawatengenezaji/wauzaji kahawa wanaweza kununuakahawa safi toka kiwandani Matiazo, ina maana soko landani litaweza kukua na kuongeza thamani ya kahawainayozalishwa mkoani hapa.

Kuchekecha (kushoto) na kuandaa kinywaji (kulia)

Unywaji! Wateja wakipata kahawa kwenye kidanda cha kahawa cha Bw.Idrisa

Page 45: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

45

Fedha

FedhaKatika kipindi cha mwakauliopita TaCRI iliendeleakupokea misaada yakifedha kutoka EUkupitia programu yaEDF/Stabex, wadau wakahawa kupitia tozo lahiari la mauzo ya kahawa,serikali kupitia mchangowa bajeti ya kusaidia utafitina uzalishaji wa miche, nakutoka CFC kupitia CABIchini ya programu yakutokomeza ugonjwa wamnyauko fuzari.

Mfuko wa akiba iliyowekezwa ulioanzishwa ilikuimarisha uwezo wa taasisi kifedha kwa siku za baadayeumeendelea kuonyesha mafanikio. TaCRI inatarajiakutumia mapato ya mfuko huu kwa siku za baadaye haliitakapolazimu hasa baada ya ukomo wa vyanzo vinginevya mapato. TaCRI ina vyanzo vingine kadhaa vyamapato, kujumuisha mauzo ya miche ya kahawa namazao kutoka mashamba ya utafiti (hasa ndizi nakahawa), na riba kutokana na fedha kwenye akaunti zamuda mrefu. Muhtasari wa vyanzo vya fedha unaoelezwa

hapa chini, umethibitishwa na wakaguzi wa mahesabu yafedha kuwa ni sahihi.

Mapato na matumiziTaarifa za mapato na matumizi ya TaCRI katika mwakawa mapitio wa fedha wa 2006/2007 zinaonyesha ziada yaSh. 703.46 milioni ikilinganishwa na ziada ya Sh. 853.09milioni katika mwaka uliotangulia; kushuka kwa ziadahii kunatokana na kuongezeka kwa idadi ya wafanyakazi,utawala na gharama za usambazaji teknolojia kwa wadaukutokana na kuajiri watumishi wapya, mabadiliko yamishahara na mabadiliko ya bei katika gharama zauendeshaji.

Gharama za watumishi zimeshuka kutoka 44% hadi 31%katika mwaka 2006/2007, pamoja na uwiano wa gharamaza utawala kushuka kutoka 43% hadi 30% ndani yamwaka huo. Ingawa kuongezeka kwa gharamakumetokea kwenye shughuli za utafiti kwa 22% nausambazaji teknolojia kwa 17% kutoka 15% na 2% kwakila moja ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Hiiinaonyesha ongezeko la gharama za uendeshaji katikamaeneo yote mawili. Kwa ujumla, uwiano wa gharama zautawala na watumishi zipo katika viwangovinavyokubalika, ingawa tunaweka tahadhari katikaubanaji wa matumizi.

Bw. Hubert Lema, Mhasibu

TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI (Isiyokaguliwa) Tsh 000

2007 2006 2005 2004 Baki ya Mwaka uliopita 983,877 589,424 183,711 140,311

MAPATOMichango ya wadau 169,748 501,019 536,801 408,763Mfuko wa EDF 800,184 733,857 497,681 1,159,555Mchango wa serikali 257,062 - 77,744 - Mapato mengine 7,503 85,123 55,376 11,344

1,234,497 1,320,000 1,167,603 1,579,663Jumla ya mapato 2,218,374 1,909,424 1,351,314 1,719,974

MATUMIZIGharama za watumishi 449,301 385,149 271,895 441,877Gharama za utawala 428,975 407,201 227,106 382,447Gharama za kusaidia utafiti 311,384 148,372 96,644 221,653Gharama za usambazaji teknolojia 270,162 19,783 3,494 1,080Ukarabati na matunzo 2,186 124 4,251 167Matumizi ya mtaji na mikataba 52,907 95,709 - 232,208Jumla ya Matumim 1,514,915 1,056,338 603,391 1,279,432Ziada 703,460 853,086 747,924 440,542

AKIBA WASILISHIAkiba: Akaunti za Benki 340,177 853,086 747,924 440,542 Akiba: Muda Mfupi/Kati 363,283 - - -

Jumla 703,460 853,086 747,924 440,542

Page 46: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

46

Rasilimali Watu

Rasilimali Watuwanaofanya shughuli za usambazaji teknolojia kwawadau.

Utawala na seraKatika mwaka uliopita Bodi ya Wakurugenzi ya TaCRIilikutana na kuidhinisha kitabu cha mwongozo chawafanyakazi ambacho kinatoa mwongozo katikamaswala yote yanayohusu taratibu za kazi kujumuishauajiri, nidhamu kazini, ustawi, na kanuni za nidhamu nauongozi kulingana na sheria.

Kujenga timu na kujiendelezaKatika mwaka uliopita, shughuli za kujenga timu nakujiendeleza ziliendelea kama ifuatavyo.

Kwa ujumla mazingira ya kazi yaliendelea kuwa mazuri,ambapo marupurupu yaliendelea kuwa yenye motisha,na uboreshaji wa vitendea kazi ili kuweka mazingira yakazi mazuri zaidi.

Sera ya rasilimali watu yaTaCRI ni kuwa na timu yawafanyakazi mahirikwenye fani zao ambaowanafanya kazi kwaubora wa juu nakitaalamu. Inatia moyokwamba katika kipindikilichopita, TaCRI iliwezakubaki na wafanyakaziwake muhimu.

KuajiriKatika kipindi cha mwaka uliopita, timu ya wafanyakaziwa TaCRI iliendelea kuimarika kufuatia kuongezeka kwawafanyakazi wapya wafuatao: Bw. Cyril Ignas Chimilila(Mchumi Kilimo) na Bw. Epafra Mosi (Mtaalamu wamaabara). Wengine ni Bw. Godlisten Mphuru na DavidMjaila (Madereva). Ushirikiano katika shughuli za uganipia ziliimarika kwa TaCRI kuleta pamoja wenza

Dk. Omar Kizango, Meneja Utawala

Jedwali 4: Semina na kozi zilizoudhuriwa 2006 - 2007

Semina, Kozi fupi, Warsha Washiriki Idara Tarehena Kujiendeleza

Mkutano kuhusu tathmini ya utendaji ya Wafanyakazi wote Idara zote Januari 2007mwaka na ujenzi wa timu

Ziara ya kimafunzo katika kituo cha CIFC Bw. D.L. Kilambo CID Machi- Mei 2007kama sehemu ya masomo ya shahada ya Bw. D.J. Mtenga CIDuzamili wanayotarajia kuhitimu Septemba 2007 Dk. L.I. Masumbuko CID

Wafanyakazi 9 walihudhuria kongamano la Dk. J.M. Haki Bodi Septemba 200621 la ASIC liliofanyika Montpellier, Ufaransa, Prof. J. M Teri Utawalamwezi Septemba 2006 Bw. D.L. Kilambo CPQI

Bw. D.J. Mtenga CIDBw. N.M Ngh’oma CIDBw. F.L Magina CPQIBw. T.S Nzallawahe TTTDBw. M.H. Temu TTTDDk. L.I. Masumbuko CID

Makongamano mawili, la kwanza kuhusu Sheria Dk. O.S Kizango Utawala Desemba 2006mpya makumpuni na tathmini ya utendaji wa Mr. H.N Lema Februari 2007makumpuni, na la pili kuhusu viwango vya kumataifa vya utoaji taarifa za kifedha yaliyoandaliwa na Bodi ya Taifa a wahasibu nawakaguzi wa fedha

Semina kuhusu maendeleo ya maktaba za mfumo Bi. A. P. Kimaro Utawala Februari 2007wa kitarakimu nchini, changamoto, matarajio na mikakati

Page 47: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

47

Rasilimali Watu

Jedwali 4: inaendelea

Semina, Kozi fupi, Warsha Washiriki Idara Tarehena Kujiendeleza

Semina kuhusu uchunguzi wa magonjwa ya mimea Bi. J. Meli Urassa CID Machi 2007iliyofanyika Nairobi Kenya.

Semina kuhusu maendeleo ya maktaba za mfumo Bi. A. P. Kimaro Utawala Februari 2007wa kitarakimu nchini, changamoto, matarajio na mikakati.

Semina kuhusu uchunguzi wa magonjwa ya mimea Bi. J. Meli Urassa CID Machi 2007iliyofanyika Nairobi Kenya.

Mkutano wa kujadili mambo mbalimbali Bw. Felician B. Swai TTTD Novemba 2006 yanayohusu wakulima wa Afrika ya Mashariki Bw. Isaac K. Mushiuliofanyika Buhuri, Tanga.

Warsha ya uendelezaji wa zao la kahawa mkoani Bw. N.M. Ng'homa TTTD Februari 2007Kagera & mkutano wa nne na maonyesho ya Chama cha kahawa cha Afrika mashariki (EAFCA) uliofanyika Addis Ababa-Ethiopia.

Semina kuhusu taratibu nzuri za kilimo iliyofanyika Bw. F.L. Magina CPQI Februari 2007Ngurdoto Hotel, Arusha Bi. S. Malinga CPQI

Masomo ya shahada ya uzamili-SUA Bw. F.L. Magina CPQI Septemba 2006

Warsha kuhusu usimamizi wa miradi ya kilimo Bw. G. P. Maro CPQIkatika utafiti na maendeleo iliyofanyika Dk. O.S. Kizango Utawala Desemba 2006Mombasa Kenya

Warsha ya wadau wa sayansi ya udingo-ARI Tanga Bw. G. P. Maro CPQI April 2007

Page 48: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

Uchambuzi Kifani 15:Kustaafu kwa heshima

Bw. Abbas (kulia) na Profesa Teri (kushoto)

Katika mwaka uliopita mmoja wa wafanyakazi waliowahikufanya kazi kwa kipindi kirefu zaidi katika taasisi hii,Bw. Abbas Adam Mushi alistaafu baada ya kutumikiaserikali kwa kipindi cha miaka 36.

Alipoulizwa kuhusu siri ya mafanikio yake katika kazi,Bw. Mushi alieleza “Ni matokeo ya kutimiza wajibu,nidhamu, na kudumisha heshima na wafanyakaziwenzake, pamoja na kujituma”.

Kauli yake ni ya kweli, kwani wakati akiwa kwenye ajira,Bw. Mushi amewahi kutunukiwa “Ufanyakazi bora” marakadhaa wakati wa sherehe za kitaifa za wafanyakazi.

Bw. Mushi alifurahishwa na tafrija nzuri ya kumuaga naakasema amefurahi kuondoka katika utumishi akiwa namarafiki, uongozi na pia wafanyakazi wenzake ambaoataendela kuwakumbuka.

Tunamtakia maisha mema baada ya kustaafu.

TanziaMwenyekiti wa Bodi yawakurugenzi ya TaCRIanasikitika kutangaza kifocha Profesa MartinLuther Kyomo (70)ambaye alifariki tarehe 20Mei 2007 mkoaniMorogoro kutokana nakansa ya kibofu. Kama

mshauri, Profesa Kyomo alitoa mchango mkubwa katikakutengeneza mikakati ya taasisi ili kukidhi mahitaji yawadau wa kahawa nchini. Mnamo mwaka 2001, Bodi yawakurugenzi ya TaCRI ilimchagua Profesa Kyomo kuwammoja wa Jopo la Ushauri wa Kitaalamu kwa kipindi chamiaka minne ambapo alichaguliwa kuwa mwenyekiti wajopo hilo. Mwaka 2007 kutokana na mchango wake kwataasisi alichaguliwa kuwa mwenyekiti kwa kipindikingine cha miaka miwili, kazi ambayo kwa bahati mbayakahuweza kuikamilisha. Tunaungana na familia, nduguna jamaa wa marehemu katika kuomboleza.

Marehemu Profesa Martin L. Kyomo

Rasilimali Watu

48

Page 49: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

49

Maafisa na wafanyakazi wa TaCRIBODI YA WAKURUGENZIBw. Edwin I. M. Mtei MwenyekitiDk. Jeremiah M. Haki Makamu MwenyekitiBw. Vedastus I. Ngaiza MkurugenziBw. Geoffrey Makonganya MkurugenziBw. Ernest J. Komba MkurugenziBw. Bill Harris MkurugenziBw. Tobias I. Masaki MkurugenziBw. Leslie D. Omari MkurugenziProf. James M. Teri Katibu

JOPO LA WASHAURI WA KITAALAMUProf. Martin Kyomo Mwenyekiti (amefariki)Prof. Bruno Ngunguru Makamu MwenyekitiDk. Roshan Abdallah MjumbeProf. Emmanuel Mbiha MjumbeDk. Francis Shao MjumbeProf. James M. Teri Katibu

UTAWALAProf. James M. Teri Mkurugenzi Mtendaji MkuuB.Sc. Agric. (Makerere)M.Sc., PhD (Cornell)

Dk. Omar S. K. Kizango Meneja Utawala na Rasilimali WatuFInst.CM (Bournemouth),FCIM (Bournemouth),CMA (Karachi), FCHAD (Hong Kong),D.Lit. (Prospect Australia)

Bw. Hubert N. Lema MhasibuCert. Acc. (Tanzania Inst. of Acc.), Dip. Bus. Adm. (CBE), Dip. Fin. Mgt. (Inst. Comm. Mgt.)

Bw. Geoffrey N. Mtei Meneja MilikiDip. Agric. Eng. (Egerton), Adv. Dip. Ind. Mgt. (Krans College)

Bi. Salama A. Kozi Katibu MuhtasiSecretarial Cert. (Modern College)Comp. Appl. Certificate (KIT)Off. Mgt. Certificate (NIP)

Bi. Amelda P. Kimaro MkutubiNational Librarian Certificate (TLS)Higher Librarian Certificate (Mantep)

Bi. Restituta A. Mallya Msaidizi wa Ofisi ya UhasibuNational Bus. Exam. Cert. (NABE)Secretarial Certificate (MCC)Comp. Appl. Certificate (MCC)

Bw. Haruna S.Msangi Mtunza StooCertificate (NABE)

Rasilimali Watu

Page 50: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

50

Rasilimali Watu

Bw. Hassan O. Kimathi Fundi UmemeElect. Tech. Cert. (NVTC)

Bw. Ismail S. Msuya Fundi BombaBw. Abbas A. Mushi* Mtunza OfisiBw. Joseph D. Kweka Mkuu wa WalinziBw. Bertini C. Kweka MlinziBi. Isdora C. Mankya MlinziBw. Ludovick B.Kweka MlinziBw. Nuru J. Ilala DerevaBw. Aloyce Koinange DerevaBw. Ally R. Chakasambi DerevaBw. Geoffrey E. Nkilosibi DerevaBw. Godsteven Mphuru DerevaBw. David Mjaila DerevaBw. Fidelis E. Soka DerevaBw. Robson I. Mushi Dereva

IDARA YA UBORESHAJI WA ZAODk. Linus I. Masumbuko Mkuu wa IdaraB.Sc. Agric. (SUA)M.Phil. (Birmigham)PhD (Swed. Univ. of Agric. Sciences)

Bw. Deusdedit L.Kilambo Afisa Utafiti*Dip. Crop Prod. (Ukiriguru), B.Sc. Agric. (SUA), M.Sc. Crop Science (SUA)**

Bw. Damian J. Mtenga Afisa Utafiti*Dip. Irrig. (Nyegezi),B.Sc. Agric. (SUA),M.Sc. Crop Science (SUA)**

Bw. Faustin L. Mtuy Bwana ShambaCert. Agric. (Nyegezi),Dip. Hort. (Tengeru)

Bi. Josephine M. Urassa Bibi ShambaDip. Crop Prod. (Uyole)

Bi. Eliansoe E. Mosha Bibi ShambaCert. Agric. (Ukiriguru)

Bi. Grace K. Monyo Bibi ShambaCert. Agric. (Ukiriguru),Dip. Crop Prod. (Uyole)

Bw. William N. Kimaro Bwana ShambaCert. Animal Prod. (Mpwapwa) Dip. Animal Prod. (Tengeru)

IDARA YA UONGEZAJI TIJA NA UBORA WA ZAOBw. Godsteven P. Maro Mkuu wa IdaraB.Sc. Agric. (SUA),M.Sc. Physical Land Resources (Ghent)

Page 51: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

51

Bw. Fredrick L. Magina Afisa Utafiti*Dip. Land Use Plann. (Nyegezi)B.Sc. Agric. (SUA),M.Sc. Crop Science (SUA)***

Bw. Emanuel O. Nkya Bwana ShambaDip. Crop Prod. (Uyole)

Bw. Harrisson E. Monyo Bwana ShambaDip. Crop Prod. (Uyole)

Bi. Donatha F. Mbowe Bibi ShambaDip. Crop Prod. (Uyole)

Bw. Leonard N. Mushi Bwana Shamba MsaidiziBw. Focas M. Ritte Bwana Shamba MsaidiziBw. Hassan H. Kisere Bwana Shamba MsaidiziBi. Paulina P. Salla Bibi Shamba Msaidizi

IDARA YA RIZIKI NA UHAKIKA WA KIPATOBw. Cyril I. Chimilila Afisa UtafitiB.Sc. Agric. Econ. & Bus. (SUA)M.Sc. Agric. Econ. (SUA)

IDARA YA USAMBAZAJI TEKNOLOJIA NA MAFUNZOMAKAO MAKUU NA KITUO KIDOGO CHA LYAMUNGUBw. Twahir S. Nzallawahe (Resigned) Mkuu wa Idara*B.Sc. Agric. (SUA)M.Sc. Rural Dev. (Irish Inst. Mgt.)

Bw. Msanjo H. Temu Afisa UganiB.Sc. Agric. (UDSM)Post. Grad. Rural Dev. (ITC)M.Sc. Rural Dev. (ITC, Netherlands).

Bw. Aligaesha B. Aminieli Afisa UtafitiAdv. Dip. Journalism (St. Aug. Univ.) M.A. Rural Dev. (SUA)

Bi. Sophia E. Malinga Bibi ShambaDip. Crop Prod. (Uyole)

Bi. Margret E. Koinange Bibi ShambaCert. Agric. (Ukiriguru)Dip. Agric. (Tengeru)

Bi. Aisha L. Kimambo Mpiga ChapaSecretarial Certificate (AETC, Arusha)

Bw. Mohammed A. Munisi Bwana Shamba MsaidiziBi. Catherine B. Ritte Bibi Shamba MsaidiziBi. Lydia S. Lema Mtunza BweniBw. Melkior B. Ngowi Mpishi

Rasilimali Watu

Page 52: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

52

Rasilimali Watu

KITUO KIDOGO CHA MARUKUBw. Nyabisi M. Ng’homa Afisa UganiDip. Crop. Prod. (Ukiriguru)B.Sc. Agric. (SUA)M.Sc. Agric. (SUA)

Bw. Laurean P. Kaiza Bwana ShambaDip. Agric. (Uyole)

KITUO KIDOGO CHA UGANOBw. Felician B. Swai Afisa UganiDip. Crop Prod. (Ukiriguru)B.Sc. Agric. (SUA)

Bw. Victor C. Akulumuka Bwana ShambaDip. Agric. (Ukiriguru)

KITUO KIDOGO CHA MBIMBABw. Isaac K. Mushi Afisa UganiB.Sc. Agric. Ext. (UDSM),M.Sc. Agric. Ext. (Reading)

Bw. Charles J. Mwingira Bwana ShambaDip. Crop Prod. (Uyole)

KITUO KIDOGO CHA SIRARIBi. Sheila Mdemu Afisa UganiDip. Crop Prod. (Uyole),B.Sc. Agric. (SUA),M.Sc. Agric. Ed. & Ext. (SUA)

KITUO KIDOGO CHA MWAYAYABw. Sixbert K. Mourice Afisa UganiB.Sc. Agric. (SUA),M.Sc. Agric. (SUA)

** Anatarajia kukamilisha masomo ya Shahada ya Uzamili Septemba 2007.*** Anaendelea na Utafiti kwa ajili ya Shahada ya Uzamili

Page 53: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

53

Viambatanisho

Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi fupi & Mikutano ya Kimataida

Ripoti za Kitaalamu 2006 - 2007

1. Maro, G.P (2007). Maabara ya uchunguzi wa udongo ya TaCRI: Hali yake na matarajio. Madailiyowakilishwa kwenye Warsha ya wadau wa PADEP iliyofanyika Mkonge Hotel, Tanga, 16-18 April 2007

2. Mtenga, D.J; Kilambo, D.L; Teri, J.M; Masumbuko, L.I. (2006) Mafanikio katika kuendeleza aina fupi zakahawa ya Arabika ambazo hazishambuliwi na ugonjwa wa chule buni.

3. Swai, F & Mushi, I (2006) Maendeleo ya wakulima wadogo wa kahawa katika Nyanda za juu kusini. Madailiyowakilishwa kwenye Kongamano la wakulima lililofanyika Buhuri, Tanga, 5-10 Novemba 2006

Kozi fupi na mikutano ya kimataifa

1. Kizango, O.S.K & Maro, G.P, Warsha kuhusu uanzishaji na uendeshaji wa miradi (Iliandaliwa naASARECA kushirikiana na CORNET) iliyofanyika Sarova Whitesands Hotel, Mombasa, Kenya, 3-7Desemba 2006.

2. Aminiel, A; Mdemu, Y.S; Teri, J.M, Mkutano na maonyesho ya nne ya chama cha kahawa cha AfrikaMashariki, uliofanyika kwenye ukumbi wa Umoja wa Mataifa, Addis Ababa, Ethiopia, 15 -17 Februari 2007.

3. Urassa J, Mkutano wa wadau kuhusu tathmini ya uwezo wa kuchunguza magonjwa ya kahawa katikaAfrika Mashariki, iliyofanyika Nairobi, Kenya, 5 – 9 Machi 2007.

4. Aminiel A, and S. Mdemu, Warsha kuhusu ukuzaji wa soko la ndani la kahawa na maendeleo ya masoko(iliandaliwa na EAFCA kushirikiana na Swedish Chambers), iliyofanyika Kilimanjaro Crane Hotel, Moshi,Tanzania, 4th April 2007.

5. Swai, F and Teri, J.M, Mkutano wa kimataifa na maonyesho ya kahawa ya chama cha kahawa cha Amerikauliofanyika Long Beach, California, USA, 4-9 Mei 2007.

Page 54: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

54

Viambatanisho

Kiambatanisho II: VifupishoASIC Shirikisho la Kimataifa la Sayansi ya KahawaASARECA Shirikisho la Kuimarisha Utafiti wa Kilimo katika Afrika ya Mashariki na KatiCABI Kituo cha Kimataifa cha Kilimo na Sayansi ya ViumbeCBB Ugonjwa wa kahawa wa chule buniCED Mkurugenzi Mkuu MtendajiCFC Mfuko wa Kuendeleza Mazao ya BiasharaCID Idara ya Uboreshaji wa ZaoCIFC Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya KahawaCLR Ugonjwa wa kahawa wa kutu ya majaniCORNET Mtandao wa Vituo vya Utafiti wa KahawaCPU Kiwanda cha kati cha kumenya kahawaCPQI Idara ya Uongezaji Tija na Ubora wa ZaoCRSP Mradi wa kusaidia ushirikiano katika utafitiCVT Majaribio ya kahawa chotara aina fupiCWD Ugonjwa wa kahawa wa mnyauko fuzariDCSMS Mtaalamu wa Kahawa wa WilayaEAFCA Shirikisho la kahawa bora la Afrika MasharikiEDF Mfuko wa Maendeleo wa Nchi za UlayaEU Umoja wa Nchi za UlayaFFS Mafunzo kwa wakulima mashambaniFPs Mkulima MwezeshajiFYM Mbolea ya SamadiGIS Mfumo wa Taarifa za KijiografiaGMO Viumbe vilivyobadirishwa vinasabaIPM Udhibiti husishi wa wadudu na magonjwaNABE Mitihani ya Biashara ya TaifaNGO Shirika lisilo la kiserikaliNVTC Chuo cha Taifa cha Mafunzo ya UfundiPUM Taasisi ya ushauri wa kitaalamu ya UholanziSACCOS Chama cha Ushirika wa kuweka na kukopaSAFERNAC Uchunguzi wa Udongo kwa ajili ya tathmini ya rutuba na ushauri kuhusu matumizi ya mbolea kwenye kahawaSAP Mpango mkakatiSGVT Jaribio la Kizazi cha Pili cha Mmea SUA Chuo Kikuu cha Kilimo cha SokoineTaCRI Taasisi ya Utafiti wa Kahawa TanzaniaTAP Jopo la Washauri wa KitaalamuTCA Chama cha wauzaji wa Kahawa TanzaniaToT Mafunzo kwa WafundishajiTPRI Taasisi ya Utafiti wa Viuadudu ya KitropikiTTTD Idara ya Usambazaji Teknolojia na MafunzoTZS Shilingi ya KitanzaniaUDSM Chuo Kikuu cha Dar es SalaamUSEPA Taasisi ya Udhibiti wa Mazingira ya MarekaniVBT Mafunzo ya VijijiniVPU Sehemu ya Kuchipuzia Miche kwa Vikonyo

Page 55: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

55

Page 56: Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania...Kituo Kidogo cha Sirari, Tarime 38 Kituo Kidogo cha Mwayaya, Kasulu 41 Fedha 45 Rasilimali Watu 46 Kiambatanisho I: Ripoti za Kitaalamu, Kozi

Mwanza

Dodoma

Iringa

Mbeya

Songea Mtwara

Tanga

Dar es Salaam

ArushaMoshi

Musoma

Bukoba

Maruku Sub-Station

SirariSub-Station

MwayayaSub-Station

MbimbaSub-Station

UganoSub-Station

LyamunguTaCRI

Headquarters

Key:

Major CoffeeGrowing Areas

Kigoma

MMaaeenneeoo MMaakkuuuu YYaannaayyoolliimmaa KKaahhaawwaa TTaannzzaanniiaa nnaa VViittuuoo VViiddooggoo vvyyaa TTaaCCRRII

TTaaaassiissii yyaa UUttaaffiittii wwaa KKaahhaawwaa TTaannzzaanniiaaOfisi Kuu, Lyamungu

SLP 3004, Moshi, TanzaniaSimu: + 255 27 275 6868

Simu Nukshi: + 255 27 275 6773Barua pepe: [email protected]

www.tacri.org