Toleo Maalumu

Embed Size (px)

Citation preview

  • 7/30/2019 Toleo Maalumu

    1/10

    TOLEO MAALUM

    ZanzibarDaima

    /27AGOSTI 2013

  • 7/30/2019 Toleo Maalumu

    2/10

    MHARIRI MKUU

    Ahmed Rajab

    Email: [email protected]

    MHARIRI MSAIDIZI

    Mohammed Ghassani

    Email: [email protected]

    MHARIRI MSANIFU

    Hassan M Khamis

    Email: [email protected]

    COMMUNICATION MANAGER

    Hassan M Khamis

    WAANDISHI

    Jabir Idrissa

    Email: [email protected]

    Othman Miraji

    Email: [email protected]

    Hamza Rijal

    Email: [email protected]

    Salim Said Salim

    Email: [email protected]

    Ally Saleh

    Email: [email protected]

    WASAMBAZAJI

    mzalendo.net

    zanzibardaima.net

    zanzibardaima/facebook

    MATANGAZO

    Hassan M Khamis

    Simu: +44 7588550153

    Email: [email protected]

    WASIALIANA NASI

    [email protected]

    JARIDA HILI HUCHAPISHWA NA

    Zanzibar Daima Collective

    233 Convent Way

    Southall

    UB2 5UH

    Nonnstr. 25

    53119 Bonn

    Germany

    www.zanzibardaima.com

    Zanzibar DaimaOnl ine

    Muundo wetu

    Hii leo tumewajibika kutoa toleo maalum

    la Zanzibar Daima Online hata kabla ya

    baadhi yetu kumaliza kulisoma toleo la

    pili la hili jarida lenu lililotoka mwishoni

    mwa wiki. Tumeukata uamuzi huo kwa kauli moja

    ili tuzidi kupashana habari na kutoa maoni yetu na

    uchambuzi wetu kuhusu kadhia iliyojiri jana mcha-

    na huko Dodoma kwenye makao makuu ya Chama

    cha Mapinduzi (CCM) ya Mansoor Yussuf Himid

    kufukuzwa kutoka chama hicho.

    Hiyo si kadhia ndogo au nyepesi. Ni kubwa na nzito.

    Kwa mara nyingine tena tumemshuhudia Mzanzi-

    bari mwingine akikaangwa Dodoma kwa sababuamethubutu tu kutamka kwamba anataka Zanzibar

    irejeshewe Mamlaka yake Kamili.

    Pamoja na dai hilo Mansoor ni miongoni mwa

    walio safu ya mbele kutetea umoja wa Wazanzibari

    ambao lazima tuwe nao ikiwa tunataka kuijenga

    Zanzibar mpya, Zanzibar isiyodhalilishwa au kukali-

    wa kichwani na yoyote.

    Wengi wetu tunaamini kwamba tutaweza tu kuijen-

    ga hiyo Zanzibar mpya endapo nchi yetu itarejeshe-

    wa mamlaka yake kamili. Hapo ndipo tutapoweza

    kuijenga Zanzibar yenye amani, ufanisi na maende-

    leo kwa wote bila ya kujali rangi, kabila, dini,

    muelekeo wa kisiasa au ubaguzi wa aina yoyote

    ile.

    Mansoor ni mfano mzuri wa mwanasiasa ali-

    yeweka kando uchama na ikadi yake ya kisiasa

    kwa maslahi ya Zanzibar. Hakuna kinachotuvua

    kwake isipokuwa uzalendo wake na moyo wake

    wa kujisabilia kwa maslahi ya Zanzibar. Na hayo

    ndiyo yaliyomponza Dodoma.

    Hamna shaka yoyote kwamba kaka kipindi cha

    muda mfupi kaka siasa za nchi yake Mansoor

    ameibuka kuwa kipenzi cha Wazanzibari walio

    wanachama wa vyama vyote vya siasa nchinihumu na hata wasio wanachama wa chama cho-

    chote.

    Kama kulikuwako waliokuwa wakimlia shaka

    Mansoor basi kufumba na kufumbua wamezio-

    na shaka zao zikiyayuka kwani ameonyesha kwa

    kauli na vitendo kwamba yeye ni mwanasiasa

    mwenye dira, aliyesimama kidete kuitetea Zanzi-

    bar, tena kwa dha ya nafsi yake.

    Hii leo asubuhi maadui zake ndani ya CCM/Zan-

    zibar waliamka midomo wazi wakitabasamu kwa

    Mhariri

    Ahmed Rajabi

    vile wanakiri kuwa wameshinda. Lakini washindi

    khasa sio wao bali ni umma wa Zanzibar; ni wale

    wenye mzamo mmoja na Mansoor kuhusu nchi

    yao.

    Wengi wao wamekuwa wakifurahi na kushangi-

    ria tangu jana ili pokatwa minyonyoro iliyokuwa

    imemfunga Mansoor na CCM. Sasa ameachwa

    huru na anatoka CCM akiwa na siri nyingi ambazo

    bila ya shaka atazitumia kwa maslahi ya Zanzibar.

    Kuna wengi wengine ndani ya CCM/Zanzibar

    wenye msimamo kama wa Mansoor. Baadhi yao

    wako kaka ngazi za juu za uongozi. Wengi wao

    ni vijana wasio na nyadhifa zozote ndani ya chamahicho. Sifa yao kubwa ni kwamba wameiweka

    mbele Zanzibar badala ya chama chao.

    Toleo Maalum Zanzibar Daima Online 03

    Mansoor - Wazanzibari waponyuma yako

  • 7/30/2019 Toleo Maalumu

    3/10

    04 Zanzibar Daima OnlineToleo Maalum Toleo Maalum Zanzibar Daima Online 05

    Kitanzi cha Dodoma shingoni kwa Mansoor

    TAARIFA YA CCM KWA VYOMBO VYA HABARI

    Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) iliyomalizika leo imejadili kwa kina Masuala mbalimbali likiwemopendekezo la Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi - Zanzibar lakumvua uanachama Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Mjumbe wa Baraza laWawakilishi wa Kiembesamaki.Baadhi ya tuhuma za Ndugu Mansoor Yussuf Himid ni pamoja na:-

    1. Kushindwa kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti yauanachama.2. Kushindwa kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka Maadili yaKiongozi wa CCM.3. Kuikana Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010-2015 nakuisaliti CCM.

    Baada ya kujiridhisha vya kutosha na tuhuma dhidi ya Ndugu MansoorYussuf Himid, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) imeridhia uamuzi waHalmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar wa kumfukuzauanachama. Kwa uamuzi huo wa kumvua uanachama wa CCM Ndugu

    Mansoor Yussuf Himid, yeye kwa sasa sio Kiongozi tena wa CCM.

    Imetolewa na:

    Nape Moses Nnauye,

    KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA26/08/2013

    Historia yajirejea Dodoma yaendelea kuwa machinjio ya Wazanzibari

    CCM/Zanzibar waendelea kuchuuzana

    Na Jabir Idrissa

    Shujaa mwengine azaliwaZanzibar

    UamuziI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumfukuza uanachama Mansoor Yussuf Himid umeelezwa

    kuwa huenda usivuruge mustakbali wa kisiasa wa mwanasiasa huyo kijana hata kama ataamua kuto-

    chukua hatua ya kuupinga Mahakamani.

    Duru za siasa ndani ya jimbo la Kiembesamaki analoliwakilisha kama mjumbe wake wa Baraza la Wawakilishi,

    nafasi aliyoipata baada ya kushinda kwa kura nyingi kinyanganyiro cha ki hicho kwenye uchaguzi mkuu wa

    2010, zinasema kuwa wapigakura wake wanakiria kumuunga mkono iwapo ataamua kuhamia chama cha

    upinzani.

    Mansoor mwenyewe hakuzungumzia wazi hama yake baada ya uamuzi uliokatwa jana mchana wa kum-

    fukuza CCM, lakini watu walio karibu naye kutoka jimboni kwake wanasema watakufa naye na kamwe

    hawatamtelekeza.

    Toleo Maalum

  • 7/30/2019 Toleo Maalumu

    4/10

    06 Toleo Maalum Zanzibar Daima OnlineToleo Toleo Maalum Zanzibar Daima Online 07

    Baadhi ya wapigakura walioteta na mwandishi wa

    habari hizi mara baada ya uamuzi wa kikao cha Hal-

    mashauri Kuu ya Taifa (NEC-CCM) kilichokutana mjini

    Dodoma, wamesema kuwa hawako tayari kumwona

    mwakilishi wao huyo ananyanyaswa na kudhalilish-

    wa na CCM kwa sababu ya kutoa maoni yake kuhusu

    mabadiliko ya Kaba ya Jamhuri ya Muungano wa

    Tanzania.

    Kilichomponza Mansoor ni kuzingaa hali halisi ya

    mambo. Amesikia sau ya Wazanzibari walio wengiinazungumzia haja ya Zanzibar kurudishiwa hadhi yake

    kama nchi huru. Wanataka Zanzibar yenye mamlaka

    yake kamili. Wanataka Muungano wa Mkataba. Na

    haya aliamua kuyapigania. Tazo liko wapi hata wad-

    hani ametenda kosa? Alisema mpigakura wa Kembes-

    amaki bila ya kuruhusu kutajwa jina lake.

    Mpigakura huyo ambaye alimthibishia mwandi-shi kwamba anawakilisha msimamo wa mamia ya

    wapigakura wengine, alisema hawawezi kumwacha

    solemba bali watamsimamia kikamilifu kaka azma

    yake ya kupigania maslahi ya Zanzibar.Hawa wakub-

    wa wa CCM wanashangaza sana. Walitoa ruhusa kwa

    wanachama wote kuichambua rasimu ya Kaba. Sasa

    walitegemea watu wote wakiri kwa mzamo mmoja

    kama kasuku?

    Kasuku huimba kile kilichoimbwa na mfugaji wake.

    Haongezi neno lake binafsi atapayuka yaleyale ali-

    yoyasikia yakitamkwa na mtu anayemhudumia. Sasahawa CCM ndivyo wanataka iwe. Wanataka kugeuza

    wanachama wao mazuzu mfano wa kasuku pale

    mwenyeki Rais Jakaya Kikwete alipoasa wajumbe wa

    Kama Kuu kuwavumilia wanachama wenzao wenye

    mawazo yanayopingana na ya kwao aliona mbali, al-

    isema mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu kaka CCM.

    Mwenyeki wa CCM Taifa, Dk. Jakaya Kikwete ambaye

    pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

    alitoa nasaha hiyo waka akizungumza kwenye kikao

    cha Kama Kuu ya CCM mara mjadala wa rasimu ya

    Kaba ulipoanza.

    Chama hicho kilishatoa tamko kuwa kinashikilia mfu-mo uliopo wa Muungano wa serikali mbili uendelee,

    badala ya kubadilisha na kuletwa mfumo wa serikali

    tatu kama ilivyopendekezwa kaka rasimu ya awali ya

    Kaba mpya.

    Mjadala wa rasimu iliyozinduliwa Juni 3, mwaka huu

    mbele ya Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib

    Bilal, ulikuwa usiwepo baada ya mjumbe mmoja wa

    Kama Kuu kutoka Zanzibar kutaka suala hilo liachwe

    kwa madai yake kwamba si ajenda ya CCM bali ya

    wapinzani wake.

    Taarifa zilizopakana ndani ya vikao vya juu vya chama

    hicho mjini Dodoma, zimesema kuwa mjumbe huyo

    alisema ajenda hiyo iachiwe wale walioandaa ili

    kuona wataka nayo wapi, na kwamba wao CCM wajekuamua baada ya kuona wenyewe mwisho wa ajenda

    yenyewe.

    CCM haikuwa na ajenda ya kuruhusu kuandikwa kwa

    Kaba mpya. Haikuwemo kwenye Ilani ya Uchaguzi

    ya 2010, wala haikuahidiwa na mgombea wao waka

    wa kampeni ya uchaguzi huo. Hata pale Rais Kikwete

    alipokuwa ameunda Baraza la Mawaziri baada ya

    uchaguzi huo, mawaziri wawili akiwemo wa Kaba na

    Sheria, Celina Kombani, walisema suala la kaba mpya

    si sera ya CCM.

    Ajenda ya kuandaa Kaba imekuwa ni ahadi ya vyama

    vya upinzani kikiwemo Chama cha Wananchi (CUF)

    tangu mwaka 2005. Nacho Chama cha Demokrasia

    na Maendeleo (CHADEMA) kilikuwa na ajenda hiyo

    mwaka 2010 kiliposema kuwa kikiingia madarakanikitahakikisha Watanzania wanapata Kaba wanayoita-

    ka ndani ya siku 100.

    Tume ya Mabadiliko ya Kaba chini ya Mwenyeki

    wake, Jaji Joseph Warioba inatetea pendekezo lake

    huku Warioba akirudia mara kwa mara kwamba mfu-

    mo huo ndio mwafaka na kwamba mfumo wa serikali

    mbili ndio utakaosababisha Muungano kuvunjika.

    CCM nayo imekuwa ikisema kuwa mfumo wa serikali

    tatu utaongeza gharama za uendeshaji, madai yan-

    ayopingwa na Tume ambayo imesema kupia wataa-

    lamu wake iligundua kuwa kwa mwaka 2010/11, kwa

    mambo yanayohusu Muungano pekee, gharama za

    kuendesha serikali mbili ni chini ya Sh. trilioni mojakupia mapato yatokanayo na ushuru wa bidhaa.

    Kwa sababu ya hali hiyo, Tume inashikilia kuwa ghara-

    ma za kuendesha Muungano kwa mfumo wa serikali

    tatu hazitakuwa kubwa kama inavyodaiwa na CCM na

    wengine.

    Toleo MaalumToleo Maalum

    Sifikirii kama kufukuzwa kwa Mansoorni kwa sababu ya msimamo wake wakudai Zanzibar irejeshewe MamlakaKamili. Naona ajenda imewekwa kwa

    Mansoor kwa vile ni mwepesi mno kumdhuruna kisingizio kimepatikana. Wako waliochangiazaidi ya yeye kwenye Baraza la Wawakilishi -Mheshimiwa Mohammed Raza, Hamza Has-san, Bi Asha Bakari, na orodha inaendelea.

    Kwa nini nguvu kubwa ya kupita kiasi itumikekwake pekee? Angalia maoni ya Bara: wakuuwametaka serikali moja hadharani, wenginetatu na wengine huku wakiibeza Zanzibarndani ya bunge wote hao ni CCM pia. Sasakulikoni kwa Mansoor? Hizi ni siasa za visasi

    baina ya wahafidhina na wapenda mageuzindani ya CCM Zanzibar.

    Tazama 2010 na namna gani Dk. Ali MohamedShein alichaguliwa huku akiwa hata katikaDaftari la Kura hayumo visiwani na mchakatomzima ulivyokuwa mpaka akapita kwa tiketi yaCCM.

    Hiki ndicho kisasi chao kwa wana-CCM wana-openda mabadiliko. Isitoshe makubaliano yakuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ile asilimia33 ya waliokataa kwenye kura ya maoni inaju-likana.

    Hebu rudia nyuma katika ule mkutano wa CCMKisonge, ambapo Katibu wa UVCCM alipowaitaMansoor na Edi Riyami Waarabu na ha-waaminiki na alipomuonya Rais Shein. Jungulilikuwa linapikwa.

    Haiendani kabisa na ukweli wa mambo. Ubayawa uhafidhina ni kuwa hata kama una upeo waelimu wa aina gani lazima uwe ni mfuasi wasiasa za chuki, choyo na ugomvi.

    Majeruhi ya wahafidhina ni makubwa mnombele ya wananchi kuanzia kuw aangamizaUamsho, Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na sasawana-CCM wanaotaka mabadiliko ambaohawakuwapa nafasi ya kufurukuta wakawa

    katika ile zoni yao ya kujilabu ya siasa chafuambayo ndiyo iliyowekea shina la tukio la jana.

    Ushauri wangu kwa Mansoor ni kubaki katikaKamati ya Maridhiano ya Watu sita na kuende-lea na msukumo mpya wa amani unaowalengawananchi zaidi kupeleka hoja mbadala dhidi yamfumo wa sasa au wowote unaoelekea katikaSerikali Moja.

    Vile vile, asiwape nafasi ya kuliacha jimbo laKiembesamaki. Lazima sauti mbadala zipaezaidi ndani ya Baraza la Wawakilishi mpaka2015.

    Mansoor kaangushwa kwa visasi vyawanamageuzi

    Na Farrel Foum

    Dk. Ali M Shein na Vua A Vuai

  • 7/30/2019 Toleo Maalumu

    5/10

    Toleo Maalum Toleo Maalum

    08 Zanzibar Daima onlinetoleo maalum toleo maalum Zanzibar Daima online 09

    Waswahili wanayo ada ya kila baada yamuda kuwa na tambiko. Imani iliopo nikuwa tambiko ni kinga dhidi ya mabaya.Imani hiyo iliwapeleka Rais wa Tangan-

    yika, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na Rais waJamhuri ya Watu wa Zanzibar, Sheikh Abeid AmaniKarume, hadi kijiji cha Kibada, nje kidogo ya jiji la Dares Salaam.

    Marais hao walikwenda huko kufanya tambiko sikumbili kabla hawajaziunganisha nchi hizi mbili, bila ya

    ridhaa ya watu wao 24 Aprili, 1964.Tambiko hilo lilifanywa nyumbani kwa mzee mmojawa Kinyamwezi (kutoka Tabora), Athumani RamadhaniMatulanga ambaye sasa ni marehemu.

    Kwa mujibu wa maelezo ya mjukuu wake ambaye piaanaitwa Athumani Ramadhani Matulanga, aliyehu-dumia shughuli hio kilichotumika ni sarafu ya senti10 iliyokuwa na maandishi ya 1922, mwaka alozaliwaNyerere.

    Sarafu hiyo anayo Mzee Ramadhani hadi leo.

    Hapo tena, kutokana na na alivyonieleza mzeeRamadhani Mwalimu alipewa kipande cha kijitikilichokatwa katika pori la kijiji cha Kibada nakukisaga kwenye jiwe kwa mate yake Nyerere.

    Baada ya hapo Nyerere akachanjwa marambili; mara moja chini ya kidevu na maranyingine usoni.

    Hilo ndilo tambiko alilofanyiwa Nyerere nabaada ya kufanyiwa tambiko hilo aliambiwakuwa upo umuhimu wa kuwa na tambikobaada ya kila kipindi ili kujikinga na maadui.

    Inavyoonyesha ni kwamba chama kinacho-tawala cha CCM kinaendeleza matambikoaliyokuwa akifanya kiongozi wao, lakinikwa aina mbili tofauti, moja ikifuatiwa nanyingine na kurudiana.

    MansoorYussuf

    Sasa Zanzibar kumekucha

    Na Salim Said Salim

    Hili tambiko la kufukuzana sio la leo walala jana. Miongoni mwa viongozi mashuhuriwaliotimuliwa, ijapokuwa wenginehawakufukuzwa moja kwa moja ni pamoja na

    Rais wa Pili wa Zanzibar, Sheikh Aboud JumbeMwinyi..

    Tambiko moja ni la kuwafukuza katika chamaviongozi wenye kutoa mawazo yanayokiudhichama na ambao huitwa waasi.

    Tambiko la pili ni la kuwatangaza viongozi auwatu wanaoikosoa vikali CCM kuwa sio raia.

    Tambiko la kuwatangaza kuwa si raia watuwalioshika nafasi mbali mbali za uongozilimewakumba wengi wakiwa pamoja na wazi-

    ri wa zamani Austin Shaba, wabunge, maofisakatika balozi za Tanzania na viongozi walioshi-ka nafasi za juu ndani ya CCM katika nyakatitafauti.

    Hili tambiko la kufukuzana sio la leo wala lajana. Miongoni mwa viongozi mashuhuri wal-iotimuliwa, ijapokuwa wengine hawakufukuz-wa moja kwa moja ni pamoja na Rais wa piliwa Zanzibar, Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi.

    Wengine ni pamoja Maalim Seif Sharif Hama-di aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar naMkuu wa Idara ya Uchumi na Mipango ya CCMna ambaye sasa ni Makamu wa Kwanza waRais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa chamacha CUF.

    Katika kundi hili alikuwemo Shaaban Mlooaliyewahi kuwa Katibu Mkuu na baadayeMakamu Mwenyekiti wa CUF na wenginewengi,baadhi yao sasa ni wabunge.

    Wapo pia waliotolewa mhanga kama aliyeku-wa Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba.Yeye kosa lake lilikuwa kueleza kwamba CCMimepoteza mwelekeo.

    Sasa tambiko limemuangukia Mansoor YusufHimid. Kosa lake ni kutoa maoni yake ya kuta-

    ka Tanzania iwe na serikali tatu.

    Hili lilitarajiwa kwani ni kawaida kwa viongoziwa CCM kuwatimua watu wanaojiamini kuwawako huru kutoa mawazo yao na wanaou-kataa utamaduni wa kuitika hewalla Bwanaau hewalla Bibi.

    Lakini kama CCM imamua kuwafukuza katikachama watu wanaotaka serikali tatu basi ita-

    poteza maelfu ya wanachama Bara na Visi-wani. Miongoni mwoa ni viongozi wastaafu waZanzibar na Wajumbe wa CCM katika Baraza laWawakilishi.

    Mansoor ametolewa muhanga na sifikiriujabari wa kuendelea kuwatimua wanaodaiserikali tatu haupo. Kilichofanyika ni kuendele-za ada ya kutambika kwa kwa imani kwambaada hiyo itakisaidia chama hicho ambacho kilakukicha kinadhoofika na kusambaratika.

    Tusibiri tuone kama tambiko hili litawagusawengine. Lakini kwa vyovyote vile Mansoor, vi-ongozi na wanachama wengine wa CCM, kamawalivyotamka Watazania wengi, wanatakaserikali tatu.

    Hatua iliyochukuliwa ya kumfukuza Mansoorni sawa na kutaka kuzuia maji kujaa au kuk-wepa. Liliotota limetota na ukiliota linazorota.Na ujue kwenda mrama ndio dalili ya kuzama.

    Hali ya CCM sasa ni kama ya mnyama ana-vyokata roho, kama anavyofanya farasi, kwamfano. Hurusha mateke yenye nguvu na hikindicho kinachoonekana ndani ya CCM hivisasa.

    Sasa unaweza kusema kumekucha Zanzibar.

    Aliekuwa Mwakilishi wa Kiembesamaki,Mheshimiwa Mansoor Yussuf Himid

    Mzee Hassan Nassor Moyo, Mmoja wa waasisi wa

    Afro Shirazi Party

  • 7/30/2019 Toleo Maalumu

    6/10

    Toleo Maalum Toleo Maalum

    10 Zanzibar Daima onlinetoleo maalum toleo maalum Zanzibar Daima online 11

    Mzee Moyo: Laiti CCMingemsikilizaMansoor

    Kwa maana hiyo ni sawa kwamba ni kwelikenda kinyume na chama, lakini yeye pia ni raia.Amekuwa akizungumza kama raia wa Zanzibar.

    Sasa unamzuia raia kwa sababu ni mwanachamawako?

    Kuna hoja kwamba hatua yaCCM ya kumfukuza Mansoorsio tu kumwadhibu yeye Man-soor kwa kwenda kinyume nasera ya chama hicho ya Mu-ungano wa Serikali Mbili, balipia kuijeruhi Serikali ya Umojawa Kitaifa na dhana nzima yaMaridhiano. Endelea....

    ZDOnline: Ulihisi vipi ulipo-pokea taarifa hizi za kuvuliwauanachama Mansoor YussufHimid?

    Mzee Moyo: Kusema kweli,msimamo wangu kwenyesuala hili nimekiwachiawenyewe Chama (cha Mapin-duzi, CCM). Uamuzi wa chama

    ni huo, lakini bado mimi nina-maintain (ninashikilia) kwam-ba Mansoor ataendelea kuwa mjumbe wa Kamati yetu hii yaMaridhiano na tutaendelea kueleza msimamo wetu juu ya ma-suala ya mchakato huu wa Katiba Mpya na sisi tunaamini sanakwamba lazima katika Muungano wetu papatikane mabadilikoambayo yatakuwa na faida kwa pande zote mbili. Sisi tunaami-ni hivyo.

    ZDOnline: Lakini umejihisije wewe binafsi kwa tukio hili?Umeshtuka? Umefadhaika? Umevunjika moyo?

    Mzee Moyo: Siwezi kuvunjika moyo, lakini sikupendezewa. Huondio ukweli. Sikupendezewa kwa sababu tumeruhusiwa kishe-ria, kama wanachama wa CCM, wanachama wa vyama, raia tumeruhusiwa kwa mujibu wa sheria tutoe maoni yetu, na ali-chofanya Mansoor kilikuwa ni kutoa maoni yake. Sasa, bila yashaka, kama maoni yake yanatafautiana na viongozi wa chamachake, hilo ni suala jenginelo. Lakini la kumfukuza kwa sababuanatafautiana na msimamo wa chama chake, sidhani kwam-ba ilikuwa fair (haki). Na vile vile, sera ya CCM kuwa na serikali

    mbili kuelekea moja. Mbonahili la moja hawalisemi? Wa-namalizia hapo hapo tu penyeserikali mbili, basi? Kwa nini,wakati sera inasema serikalimbili kuelekea moja. Wat-wambie hivyo, mbona hawat-wambii?

    ZDOnline: Kwa hivyo, un-asema ruhusa ilitolewa naviongozi wa juu wa chamachako cha Mapinduzi ya watukuzungumza wanavyoamini

    juu ya Muungano. Ruhusahii ilipotumiwa na Mansoor,ameadhibiwa. Je, unaonakuwa amesalitiwa?

    Mzee Moyo: Ruhu-sa ilitolewa nasharia ya nchina sio Cha-ma. Msi-

    mamo waChamani huo,

    kwam-ba waowana-aminikatikaMuungano waserikali mbili.Raia wengine nawanachama wenginehatuamini kwamba nilazima iwe hivyo. Tunaaminilazima kupatikane mabadilikokwenye hili jambo. Hili jambolimekuja kufuatana na sharia

    iliyotokana na tamko la Rais kwamba Rais (Jakaya Kikwete)aliona bora watu watoe maoni yao juu ya masuala haya yamabadiliko ya Katiba na ikatungwa sharia. Kwa hivyo shariainatwambia tutoe maoni yetu raia, mwanachama, aliyekuwasi mwanachama atoe maoni yake. Sasa Mansoor alikuwa aki-toa maoni yake kama raia na kama mwanachama wa CCM vilevile. Sasa kutafautiana msimamo kupelekee kumfukuza, mimisidhani kama ilikuwa ni sawasawa.

    ZDOnline: Wengine wanasema kwamba Mansoor Yusuf Himid,kama mwanachama wa CCM, si mwanachama pekee ambayeamekuwa na msimamo wa kuwa na aina tafauti ya Muungano.Imepigwa mifano kwamba ndani ya T anzania Bara, Naibu SpikaJob Ndugai na hata baadhi ya mawaziri wa serikali ya RaisKiwete ya sasa, na hata kwa hakika wajumbe waliomo kwenye

    Tume ya Katiba na ambao ni wana-CCM kama vile Joseph Bu-tiku, Salim Ahmed Salim na Mwenyekiti wa

    Tume hiyo, Joseph Warioba. Hawawote hawajaitwa kuhojiwa wala

    kufukuzwa na Chama. Je,katika muktadha kama

    huo, unaweza kuuitajeuamuzi huu wa kum-

    wadhibu Mansoor

    peke yake?

    Mzee Moyo:Mimi nasema niuamuzi ambaoumetolewa bilakumpa Man-soor nafasiya kujieleza.Kwanza yeyehakuitwa navikao vya juu

    vya Chama. Kwautaratibu wa

    Chama chetu am-bao sisi tunaujua,

    likitokea jambo kamahilo au mengine kama

    hayo, huwa anapewafursa mwanachama ku-

    jieleza kwenye vikao vya juu.Mansoor hakupata nafasi hiyo.

    Imechukuliwa ripoti tu ya vikao vyachini, vya mikoani na jimbo lake huko na

    kamati maalum, basi. Majungu yametumika. Mimi sina wasi-wasi kwamba majungu yametumika ya kama kumpa adabu.

    ZDOnline: Kumpa adabu kwa lipi tena?

    K

    ufuatia uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana mjiniDodoma wa kumvua uanachama wa chama hicho mjumbe wa jimbo la Kiembesamakikwenye Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mansoor Yussuf Himid, Zanzibar Daima Online

    imezungumza na Mzee Hassan Nassor Moyo, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhianoya Wazanzibari, chimbuko la Serikali ya Umoj a wa Kitaifa visiwani Zanzibar, na ambayo Man-soor mwenyewe ni mjumbe wake.

    Kuna hoja kwamba hatua ya CCM ya kumfukuza Mansoor sio tu kumwadhibu yeye Mansoorkwa kwenda kinyume na sera ya chama hicho ya Muungano wa Serikali Mbili, bali pia kuijeruhiSerikali ya Umoja wa Kitaifa na dhana nzima ya Maridhiano. Endelea....

  • 7/30/2019 Toleo Maalumu

    7/10

    Toleo Maalum Toleo Maalum

    12 Zanzibar Daima OnlineToleo Maalum Toleo Maalum Zanzibar Daima Online 13

    Mzee Moyo: Si hilo la kum-fukuza kwenye chama.

    ZDOnline: Kwa nini apikiwemajungu wakati ni kweli niwazi kabisa kakiuka sera yaChama katetea muundowa Muungano ambao hau-mo kwenye chama chake,

    na amelisema hilo hadha-rani akilirejea hata baada yakuonywa na wenzake chama-ni?

    Mzee Moyo: Kwa maana hiyoni sawa kwamba ni kweli ken-da kinyume na chama, lakiniyeye pia ni raia. Amekuwaakizungumza kama ni raia waZanzibar. Sasa unamzuia raiakwa sababu ni mwanachamawako?

    ZDOnline: Hii si mara yamwanzo kwa wanacha-

    ma na viongozi wa Chamacha Mapinduzi wa Zanzibarkuadhibiwa Dodoma kwakwenda kinyume na sera yaChama juu ya Muungano.Huko nyuma inakumbuk-wa historia ya Mzee AboudJumbe Mwinyi, aliyekuwaRais wa Zanzibar, Makamuwa Kwanza wa Rais wa Mu-ungano, Makamu Mwenyekitiwa CCM kwa wakati huo.Zinakumbukwa pia hadithi zaMaalim Seif Sharif Hamad nawenzake saba waliofukuzwa

    pia Dodoma. Je, unadhanikwamba katika suala hilihistoria imejirejea, kwambawakati wowote Wazanzibariwanapotumia haki yao kuu-kosoa mfumo wa Muunga-no, wanavyosema wenyewewanachinjiwa Dodoma? Je,haya yamekuwa machinjiomengine?

    Mzee Moyo: (Anacheka) Mimi

    nafikiri, sitaki niamini hivyo, lakini nataka niamini kwamba ki-tendo ambacho kafanyiwa Mansoor si sahihi. Hakupewa nafasiya kwenda kujieleza kwenye vikao vya juu. Mimi ningesemahivyo.

    ZDOnline: Kwa hivyo, unadhani kama angelipewa nafasi yakwenda kujieleza mbele ya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu yaCCM, maamuzi yangelikuwa tafauti na haya yaliyofikiwa?

    Mzee Moyo: Pengine yangelikuwa tafauti, kwa sababu siwatu wangelipata nafasi ya kumsikia anasema nini? Hatakama wangelimpa adhabu, lakini ni baada ya kupata nafasiya kujieleza. Muhimu sana ni kupata nafasi, maana huyu nimwanachama, anatakiwa apatiwe fursa ya kujieleza kwa lilekosa analoambiwa kalifanya. Lakini nafasi haikupatikana.

    ZDOnline:Tunaambiwa kwamba katika barua ambayo alim-wandikia Katibu Mkuu wa CCM, Bwana Abdulrahman Kinana,Mansoor alielezea msimamo wake akisema kwamba yukotayari kwa lolote lile lakini sio kubadilisha msimamo wake.Ikiwa hivyo ni sahihi, basi utetezi wake ulifika kwenye vikao vya

    juu hata kama yeye mwenyewe hakuitwa. Je, hiyo haikutoshakuwa sababu ya kumwadhibu?

    Mzee Moyo: Mimi hilo silijuwi, na kwa hivyo siwezi kulijibu hilo.

    ZDOnline: Sasa tuelekee mustakabali wa Zanzibar baada ya tu-kio hili. Katika moja ya mahojiano aliyofanyiwa Mansoor katikasiku za karibuni, aliashiria kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifaya Zanzibar ambayo chimbuko lake ni Kamati yenu ya Maridh-iano ambayo yeye Mansoor ni mjumbe wake, inaandamwa. Je,ni sawa kusema sasa kwamba kwa uamuzi huu wa kumfukuzaMansoor, inayoandamwa hasa ni Kamati yako ya Maridhianona Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa ujumla?

    Mzee Moyo: Aaah, mimi nasema bwana, sisi Kamati yetu ipo naitaendelea kuwepo na hatuna khofu yoyote kuyaelezea mamboambayo tunayaamini na tutaendelea kuyaamini kwa sababutunaamini kazi ambayo Kamati yetu ilipewa na Rais Amani (Ka-rume) na Katibu Mkuu wa CUF (Chama cha Wananchi, MaalimSeif Sharif Hamad), ilikuwa ni kazi ya kheri kwa ajili ya watu wa

    Zanzibar na tuliitumikia kwa moyo mmoja na tuliifanikisha. Nampaka sasa hivi, hakuna ambaye anaweza kusema kwambaKamati yetu ilifanya uovu. Wale ambao walikuwa wamepinga,kwa sababu walikuwa na sababu zao za kupinga tusiwe naserikali ya pamoja na ndio hao hao ambao wanaendelea kutu-minyaminya ionekane Kamati yetu ni ya ovyo na hivi na vile.Lakini sisi tunajua kuwa tunafanya kazi kubwa na nzuri kabisana nadhani wote ambao wanapenda hali ya usalama na utulivukatika nchi, wanafurahi kwamba tulifanya kazi ya ukweli, yakizalendo katika nchi yetu.

    CCM inaenda kinyume na MapinduziNa Salim Abdullah

    Machinjio ya Wazanzibari yameende-lea kuwachinja Wazanzibari, marahii wamemchinja Mtoto wa Mwana-Mapinduzi, Mansour Yussuf Himid,

    Mzanzibari Kindakindaki, Mwakilishi wa Jimbola Kiembe Samaki ambako mimi ni mkaazi.

    Sababu kuu ya kumchinja Mansour ni ile kauliyake ya kuunga mkono Muungano wa Mkata-ba ambao utarudisha Mamlaka Kamili Zanzi-bar katika mfumo wa Muungano.

    Sisi wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki tu-mefadhaika, tumeduwaa, tumeachwa mdomowazi, huku tukisubiri kauli ya Mwakilishi wetuili tuifanyie kazi.

    Sio sisi wananchi wa Kiembesamaki peke yetutulioduwaa na kufadhaishwa na wanaoisubirikauli ya Mansoor ili waifanyie kazi, ni wana-nchi wote Wazanzibari, Unguja na Pemba,mashamba na Mjini.

    Watu wamekata tamaa na CCM na wengiwana CCM wametamka hadharani watarudi-sha kadi CCM. Wazanzibari wamechoshwa naMachinjio ya Dodoma, leo ni Mansour, keshoMwana CCM Zanzibari mwengine.

    Swali lipo hapa, kwa nini ni Wazanzibari pekeyetu tunaochinjwa Dodoma? Hatujapatakusikia chinjio hili likimchinja Mtanganyika.

    Huenda labda kwa Watanganyika chinjio hiloni butu.

    Tumeyashuhudia ya Aboud Jumbe, ya MaalimSeif na wenzake, ya Salmin Amour kutakiwaaitoe Zanzibar kutoka Jumuiya ya Organizationof Islamic Conference na leo kufukuzwa Man-soor Yussuf Himid.

    Tayari pia kuna wito wa kudai MwanasheriaMkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman,afukuzwe Serikalini kwa kuunga mkono Ra-simu ya Katiba yenye mfumo wa Muunganowa Serikali Tatu.

    Maneno yanafika mbali zaidi kuwa hata Maa-lim Seif, Makamu wa Kwanza wa Rais, ambayeameekwa Serikalini na Katiba ya Zanzibar piaafukuzwe kazi.

    Kikubwa zaidi wenye kuchongea mambo yotehayo wanatamani Umoja wa Kitaifa Zanzibaruvunjike ili turudi nyuma tulipotoka ambapo

    kila mwananchi wa Zanzibar hataki turudihuko.

    Na kuibadili Katiba ya Zanzibar hawawezi.Kwanza hawana thuluthi mbili ndani ya Bara-za la Wawakilishi lakini pia ni lazima waitishe

    Kura ya Maoni kuiondoa Serikali ya Umoja waKitaifa, hakuna mwananchi hata mmoja waZanzibar atakaye sema Ndio Serikali ya Umo-

    ja wa Kitaifa iondoke, isipokuwa labda wao,nao ni wachache.

    Lakini yote haya yanatokea wakati BungeMaalum la Katiba linakaribia kuundwa. Nidhahiri kwamba lengo ni kuwatisha Wawakili-shi na Wabunge watakaoteuliwa katika Bungehilo wasende kusimamia hoja ya MamlakaKamili Zanzibar. Wahafidhina wa CCM/Zan-zibar wanajidanganya; hakuna atakayetishikakuhusu hili.

    Kufanya hivi wanadhani watawanyamazi-sha Wazanzibari; kufanya hivi wanadhaniwatairudisha haki nyuma; haki haijawahi ku-rudi nyuma. Siku zote haki huenda mbele hataukiichelewesha kwa miaka mia.

    Wazanzibari tulifanya Mapinduzi ili tuwe Huru.Wazanzibari hatukufanya Mapinduzi ili tuun-gane na Tanganyika. Tulifanya Mapinduzi ilitujitawale na lengo kuu ili tuwe Huru, kukataaZanzibar yenye Mamlaka Kamili ni kuyapingaMapinduzi ya Zanzibar.

    Mansoor na wenzake wanayalinda Mapinduziya Zanzibar kwani wanaujua msingi, malengona sababu ya kufanyika kwake.

    Suala la kutoa maoni ni haki ya kila mmojawetu. Ni haki yetu ya kimaumbile na ni haki yaKikatiba.

    Wakati mchakato wa Katiba mpya ulipoanzaviongozi wetu walituhimiza tusema chochotetunachokitaka. Rais Dk. Ali Mohamed Sheinaliyasema hayo sehemu tafauti. Mara mbili al-itwambia hayo uwanja wa Aman na wakati wakuizindua Tume ya Katiba, Rais Jakaya Kikwetenaye kayasema hayo mara kadhaa na hataalipokuwa analifungua Baraza la Katiba la CCMalisema wastahamiliwe wenye maoni tofautina Chama. Nashangaa leo kumwona mwenyemaoni tofauti na wao wamemfukuza CCM.

  • 7/30/2019 Toleo Maalumu

    8/10

    Toleo Maalum Toleo Maalum

    14 Zanzibar Daima OnlineToleo Maalum Toleo Maalum Zanzibar Daima Online 15

    Vereje kama Mwanakindakindaki

    angekuwa wa Bara?

    Siku zote nikiamini kuwa fujo na ghasiaza kila aina hutuama na kutia mizizikwenye vyama vya upinzani. Nikiaminihivyo kwa sababu kila kukicha nikisikia

    mwanachama Fulani katimuliwa kutoka chamahichi au chengine. Baada ya kutimuliwa wengiwao huamini kuwa walikua kweli waasi na kwahivyo hurudi kwenye Chama cha Mapinduzi(CCM) chenye uzoefu wa kutawala kwa kuwa nikizazi cha vyama vya Tanganyika African Nation-al Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP).

    Nikirudi nyuma nitasema kuwa TANU haikuwaikiwatimua wanachama ila wanachama waowalikihama TANU kuanzia kina Kasela Bantu, AlHaj Zuberi Mwinshehe Mtemvu, Al Haj AbdullahSaid Fundikira, Christopher Kasanga Tumbo na

    wengineo. TANU haikuwa inawafukuza watubali ilikuwa ikiwapiga watu pande kama paleMujahid Suleiman Takadiri alivyoanza kumwonaMwalimu Julius Nyerere kuwa ni mdini na baadaya Mwalimu kushauriana na wazee Mujahid

    Suleiman Takadiri ndiye aloiyeonekana kuwa nimdini.

    Mujahid Takadiri, aliyepewa jina la Makarios,hakufukuzwa bali alipigwa pande na aliishi katikahali ya upweke hadi alipofariki.

    Historia ni kioo kinachokuelekeza kama unata-ka uwe makini wapi pakwenda na kutoyarejeleamakosa ya waliopita. Historia kama ni somohalijawekwa kama ni pumbazo bali ni sehemu ya

    kuwaongoza watu, ndipo namkumbuka MarcusGarvey aliposema : Every man has a right to hisown opinion. Every race has a right t o its ownaction; therefore let no man persuade you againstyour will, let no other race influence you againstyour own.

    Tafsiri ya juu juu ya maneno hayo ni kuwa kilammoja anayo haki ya kuwa na fikra zake, na kilakabila lina haki ya kuchukua hatua yake; kwa hiyomsiwaache wengine kukulazimisheni kutendakinyume na mnachokiamini, msiliachie kabila

    jengine kukulazimishena kuchukua hatua dhidi yakabila lenu.

    Marcus Garvey mzalendo ambaye labda angeku-weko hai hii leo tungesema alijipenyeza Dodomana kuchungulia na kuwaambia wajumbe wa CCmaneno hayo kisha akatoka mbio.

    Kwa nini CCM/Zanzibar ilingangania MheshimiwaMansoor afukuzwe chamani na Rais wa Jamhuri yaMuungano Jakaya Kikwete akawa anasitasita nakutaka watu wavumiliane?

    Jawabu wanayo wao hao walioshikilia hilo laki-

    ni miye naona hayo yanatokana na viwango vyausomi, yaani tafauti ya usomi, kati ya pande hizombili. Huku Zanzibar na huko Bara kwenye CCMyananijia yale aliyoyasema Rais Idi Amin wa Ugan-da kumwambia Nyerere kuwa atapigana naye nahuku aekewe chuma cha ratili 100 ni sawa sawana chuma cha kilo 50 mkono mmoja kisha apiganenaye. Amin alijitapa kuwa atashinda, kwa kuwaaliamini ana maguvu kumshinda Mwalimu na ata-mtwanga tena kwenda dafaa (knockout).

    Wenzetu wa Bara ukweli ni kuwa kielimu wao ndiokwenye mizani wenye uzito na wapo makini nawanajua wanayoyapanga. Ndio maana hadi leo

    kina Andrew Chenge, Basil Mramba, Nazir Karamagi naRostam Aziz hawajafukuzwa kutoka CCM licha ya shtu-ma wanazoshtumiwa.

    Kwenye CCM/Zanzibar mambo ni kinyume. Viongoziwake bado kama wamo kati enzi za Ministerium frStaatssicherheit, kwa ufupi Stasi (Idara ya Polisi wa Siriwa Usalama wa iliyokuwa Ujerumani ya Mashariki chama ni chama ukenda kinyume nacho utafyekwa. Juuya yote nawapa heko wana-CCM kwa kufukuza pasinakuua, kwani lau Mansoor angekuwa kwenye chama chaBaath cha Iraq zama za Saddam Hussein basi angefye-kwa kinamna, ima ajali ya gari ingemmaliza au angekuti-kana kanywa sumu.

    CCM/Bara wapo makini. Wanaliona wimbi la upinzanililivyo na wanaona kuwa sio vyema kuchukua mchi kut-wanga sahani iliyojaa ufa na mapengo. Wanaona borawatafute gundi ya aina ya super glue wagandishe, lakiniCCM/Zanzibar wao juu ya nyufa zilitopea kwenye sahaniyao wao wameamua kuchukua mchi na kutwanga. Sasavigae vishatawanyika na ukitembea miguu chini utate-gemea nini? Kule Bara wao sahani wameziziba.

    Mheshimiwa Mansoor sasa ataanza kuitwa msaliti kwalugha ya CCM/Zanzibar lakini angekuwa ametoka Baraataendelea kuitwa Mheshimiwa.

    Ndipo wengine wakasema ije Tanganyika, iweko Jamhu-ri yake ili Zanzibar ipate akili iache kuendesha mambokidarmadaru.

    Je, huku ni kuwaziba midomo wanachama wa CCMwenye mawazo mbadala? Nitamalizia makala haya kwamaneno mengine ya Marcus Garvey: We have a beau-tiful history, and we shall create another in the futurethat will astonish the world. Tunayo tarekhe iliyo bulbulna tutatengeneza nyingine katika siku zijazo ambayoitaushtua ulimwengu. Dunia ni mdawari hayo tuyajueameyaeleza mweledi malenga Abdilatif Abdalla, Duniainabadilika haibaki tuli ikawa siku zote vilevile.

    Na Mwandishi Maalum

    Mansoor Y Himid

    Mbunge Ester Bulaya

    M/M Kiti Phillip MangulaSerikali Moja

    Naibu Speaker JobNdugaiSerikali Tatu

    Mbunge Beatrice ShelukindoSerikali Tatu

    Serikali tatu

  • 7/30/2019 Toleo Maalumu

    9/10

    Toleo Maalum Toleo Maalum

    16 Zanzibar Daima OnlineToleo Maalum

    Lengo si kummaliza Mansoor tubali Maridhiano pia

    Tangu hapo vijana wengi wa CCM/Zanzibarwa kizazi kipya walishaonesha mwelekeowa kupoteza imani na chama chao

    kutokana na ukakasi wa viongozi wake muflisikushindwa kusimamia matakwa na maslahi yaWazanzibari na badala yake kuonekana kamani mawakala wa ukoloni wa Tanganyika dhidiya Zanzibar.

    Rais Ali Mohamed Shein, Balozi Seif Ali Iddi,Vuai Ali Vuai na Sekretarieti ya akina HajiMkema, Hamad Masauni na Waride BakariJabu hawaonekani kuwakilisha hisia za

    Wazanzibari.

    Kielelezo thabiti cha hali hiyo kilionekanapale mamia ya vijana wa CCM walipoonekanakupanga misururu mirefu huko Matemwe naKitope kurejesha kadi za kijani kwa kiongoziwaliyempa matumaini yao Maalim Seif SharifHamad.

    Hali kama hiyo ikajitokeza kwa wazee waCCM wa maeneo yenye ngome zao Pembakama Kangagani ambao nao walirudisha kadihuku wakiomba msamaha kwa kuchelewakufahamu kuwa kumbe CCM hakipo kwa

    maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari.

    Katika hali kama hiyo ungetegemea chamamakini na kinachojikosoa kingejirudi nakujitazama upya. Lakini wapi? Wahengawalisema: La kuvunda halina ubani.

    Ni juzi tu nilipokuwa nikihutubia mkutano wahadhara hapo katika viwanja vya Komba Wapyaniliwaambia wanachama wa CCM na hususanvijana kwamba mpaka lini wataendeleakukubali Dodoma kuwa machinjio ya kisiasa yaviongozi wa Zanzibar?

    Alianza Aboud Jumbe mwaka 1984, akafuataMaalim Seif Sharif Hamad na wenzakesita mwaka 1988, akaja Dk. Salmin Amouralipojiunga na OIC mwaka 1993 na sasatena mwaka 2013 anadhalilishwa MansoorYussuf Himid kwa sababu tu amethubutukukhitilafiana na watawala wa Dodoma kwakusimamia kidete hoja ya Mamlaka Kamili.

    Nikasema umefika wakati wana-CCM waZanzibar na hasa vijana kujiuliza hichi kwelini chama chao na kipo kwa maslahi yao? Hichikweli ndicho mzawa na mrithi wa kisiasa wa

    Mansoor Yussuf Himid. Jina hili sasa huwezikulitenganisha na matakwa halali yaWazanzibari walio wengi wanaotaka Zanzibarirejeshe hadhi yake kama nchi yenye MAMLAKA KAMILIkitaifa na kimataifa.

    Kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumfutiauanachama wake jana ni kitendo cha kujiangamizachenyewe katika siasa za sasa za Zanzibar ambazozimetawaliwa na hoja moja kuu ambayo ni MamlakaKamili.

    Afro-Shirazi Party (ASP)?

    Uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCMwa kumfuta uanachama Mansoor ni ujumbe toshakwamba yeyote atakayesimamia maslahi yaZanzibar hana nafasi kwenye chamahicho. Kwa lugha nyingine, Zanzibar naCCM ni Lila na Fila, hazitangamani.

    Na tazama hata majibu ya Katibu Mweneziwa CCM wa upande wa Tanganyika, NapeNnauye, alipoulizwa autaje usaliti waMansoor anaodaiwa kuufanya dhidi

    ya Chama. Alisema ni pale Mansooraliposimama ndani ya Baraza laWawakilishi mwaka 2009 na kusemaSerikali ya Muungano ni wizi wa mchanakweupe wa rasilimali za Zanzibar. Swalila kumuuliza Nape ni kwamba je, madaihayo ni uongo?

    Lakini hebu tuje kwenye hilo la kuteteamsimamo wa muundo wa Muungano waMkataba unaokwenda kinyume na seraya CCM ya Serikali Mbili. Kama hilo ni kosambona aliyeadhibiwa ni Mansoor pekeyake?

    Wajumbe vigogo wa Tume ya Mabadilikoya Katiba ambayo ndiyo iliyokuja na

    pendekezo la muundo wa Shirikishola Serikali Tatu, wakiwemo Jaji JosephWarioba, Salim Ahmed Salim na JosephButiku, ni wanachama wa CCM mbonahawakufukuzwa?

    Mwaka 1994 Kundi la Wabunge55 maarufu kama G-55 walipelekahoja Bungeni na hoja ikapitishwa naBunge zima ya kuanzisha Serikali ya

    Tanganyika kinyume na sera ya CCM.Mbona hawakufukuzwa?

    Katika huu mjadala unaoendelea

    Na Ismail Jussa

    Mwandishi wa makala haya, Ismail Jussa [kushoto] naMansoor Yussuf

  • 7/30/2019 Toleo Maalumu

    10/10

    Toleo Maalum

    18 Zanzibar Daima OnlineToleo Maalum Toleo MaalumZanzibar Daima Online 19

    wamejitokeza wabunge kama Esther Bulayana Beatrice Shelukindo na hivi karibuni NaibuSpika Job Ndugai kutetea mfumo wa Shirikishola Serikali Tatu. Mbona hawakufukuzwa?

    Achilia mbali hao, hata Makamu Mwenyekitiwa CCM (Bara), Philip Mangula alisema yeyemsimamo wake ni kutaka mfumo wa SerikaliMoja tu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

    jambo ambalo ni kinyume na sera ya Chamachao mbona hakufukuzwa?

    Kwa nini Mansoor Yussuf Himid pekeyake? Kwa mtazamo wangu mimi Mansoorameadhibiwa kwa sababu ya msimamowake aliouchukua katika kuleta amanikupitia Maridhiano ya Wazanzibari ambayowahafidhina wa CCM/Zanzibar na walewenye kujali matumbo yao tu hawakuyatakana mpaka leo hawajayaridhia na wakipatanafasi wanayamezea mate wayavuruge.

    Wanaona Maridhiano na Serikali ya Umojawa Kitaifa iliyopatikana kupitia Maridhianohayo yamewatiribulia nafasi za kuwaMawaziri au Manaibu Waziri na pia kufanya

    watakavyo kujinufaisha wao na aila zao hukuwatoto wa wanyonge, wakwezi na wakulimawakiendelea kusaga meno.

    Na la pili ndilo hili la kusimama bila yakuyumba kwenye hoja ya MAMLAKA KAMILIkwa Zanzibar, msimamo ambao unakwendakinyume na misingi ya CCM iliyoachwa namwasisi wake Julius Nyerere.

    Ala kulli hali, hukumu imeshapitishwana Mansoor Yussuf Himid siyo tenamwanachama wa CCM.

    Kwa jinsi nimjuavyo Mansoor hakuyumbishwana uamuzi huu na kwa hakika akiutarajia.Natambua jinsi alivyo jasiri, shupavu, mkwelina mzalendo na hivyo najua hatoteterekakatika kuendeleza msimamo wake nakuendeleza harakati za Mamlaka Kamili kwaZanzibar.

    Nilikuwa namheshimu sana na kwa kulekuonesha kwake mfano katika kusimamiaanachokiamini. Sasa namheshimu zaidi.

    Sina shaka kwamba huu si mwisho waMansoor kisiasa bali naamini kwa dhatikuwa hatua ya leo ndiyo mwanzo wa kupaakisiasa Mansoor Yussuf Himid. Nilicho nauhakika nacho ni kwamba huu ni mwanzowa mwisho wa CCM katika medani za siasaza Zanzibar. Kwa sababu ya chuki, choyo navisasi wamechukua maamuzi ya hasira yakujipiga wenyewe risasi mguuni.

    Mwaka 1988, CCM iliwatengenezeaWazanzibari shujaa Maalim Seif Sharif Hamad.

    Tuna furaha kuwa sasa 2013 imetutengenezea

    shujaa mwingine wa Zanzibar, MansoorYussuf Himid. Wazanzibari tumempokea kwamikono miwili. Wakiungana mashujaa wawilihawa hakuna wa kuzuia wimbi kubwa lamabadiliko linalokuja. Aluta Continua!

    Ismail Jussa ni mwakilishi wa Jimbo la MjiMkongwe. Naye, kama alivyo Mansoor YussufHimid, ni mjumbe wa Kamati ya Maridhianoinayoongozwa na mwanaCCM Hassan NassorMoyo.

    Kamati iliopelekea kupatikana kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ZanzibarKing KijokiMansoor tuko pamo-

    ja na uchaguzi ujao jimbo lake ni

    Mtambile Pemba na nafasi ya uwa-

    ziri kama kawaida kwa hiyo asiwe na

    joto mapambano kama kawaida.

    Rashid Mohammed Wazanzibari,CCM sio chama chetu wabunge wa-

    metoa maoni yao ya Serikali Tatu la-

    kini wao ni Watanganyika hawavunji

    ilani ya chama.

    Nevline KiwiaNimefurahi sana kwa

    hili la Mansoor. Anatakiwa kuhamiaupinzani kisha awe sambamba na

    Hamad. Pia wanatakiwa waongeze-

    ke wengine kutoka CCM ili hiki

    chama kife kabisa na Zanzibar huruipakane.

    Fahim SeifKaribu Zanzibar baba. Siwaka wa kuamuliwa, ni waka wa

    kujiamulia wenyewe.

    Haji Al HarthyMimi kama mimi sim-

    shauri Mhe. Mansour kukata rufaa

    kwani atakuwa anapoteza muda

    wake bure. Cha msingi aangalie

    mwenyewe chama gani ataingia aukama ataamua kuunda chama chake

    au kukaa kimya bila ya kuwa na cha-ma kama nilivyo mimi hapa. Maana

    tokea nilipo pingwa kaka kujiand-

    ikisha 2005 basi hadi leo nimeamua

    kutulia tu siko chama chochote.

    Dr-Abdul AE CCM imewadhalilishaWazanzibari kwa mara nyingine

    tena. Juzi juzi tu wao wenyewe CCM

    walisema maamuzi ya Wazanzibari

    yaamuliwe na ZNZ leo hii imekuaje?Aibu na imetudhalilisha Wazanzibari

    sote. Ole wao wakifanya uchaguzi

    ndio wameumia.

    Juma K. HamadWacha yatokee.Tuliyatarajia. Tutamuunga mkono

    na tuko pamoja naye kwa lolote lile.Kamwe hawatutoi kaka mstari

    madai yetu Zanzibar yenye mamlaka

    kamili. Huu ndio msimamo wetu

    Wazanzibari na hatutorudi nyuma

    kamwe. Na Mansoor tunampenda,

    tunamthamini, tunamjali na tunam-

    heshimu. Wazanzibari tuko pamoja

    naye.

    Abdalla Sleiman Ni kweli kabisamaana hawa kina (Arcado) Ntag-

    azwa na wenzake walikuwa G55

    lakini wapo mpaka leo na wengine

    nadhani wamekuwa maraisi kwa

    maslahi ya nchi yao. Je, mimi na

    wewe tupo kwa ajili ya maslahi ya

    nini?

    Omar HusseinMimi naaminiWazanzibari kwa sasa hawana

    utashi wa vyama bali wanataka

    maslahi ya nchi kwanza. Kwa hiyo

    chama chochote ambacho atajiun-

    ga Jemedari Mansoor, wananchi

    wataangalia mambo gani mazuriameyafanya kwao na hawataangalia

    ni chama gani kimemsimamisha.

    Mansoor kanyongwa kwa haki

    ambayo alikua akiisimamia. Allah

    ampe nguvu zaidi ya kusimamia lile

    lililomlisha kitanzi.

    Shamis Alkhatry Ndiyo, vyamavipo vingi, kuna CUF na JAHAZIAsilia, ajiunge tu arudishe kiti

    chake au asubiri 2015 ikiwakuna mgombea huru kwenyeKatiba mpya. Bali ushauri wan-gu kwake ni kusonga mbelekwa makosa yao yaliogeukakiwembe cha upande mmojakudai maslahi ya Zanzibar. Asi-mame hapo alipofika ni sautiisiyoweza kuzimika.

    Mzalendo MtanzaniaSim-shauri Mansoor kujiunga CUF,

    ila anaweza kufanya kamaalichofanya Hamad Rashidkufungua kesi MahakamaKuu ya Tanzania kwa kuwauamuzi umetolewa Dodomawa kumfukuza na kuitakaCCM Mkoa wa Mjini Zanzibarkuthibitisha mbele ya Ma-hakama kwa Mansoor kusemaanawafiki Serikali Tatu anaku-wa amevunja Katiba wakatiwapo viongozi wa CCM/Barawaliotoa kauli zinazofanana naza Mansoor na hawakufukuz-wa uanachama. Ni mapema

    mno kwenda vyama vyengine.Apiganie haki yake ndani yaCCM na sheria zilizopo. Ananafasi kubwa ya kushindadhidi ya ushawishi wa BorafyaSilima. Tuna sheria nchini Tan-zania, na sasa hakuna kikomo

    ila mbingu tu.

    Wasemavyo wanaFacebook juu yakufukuzwa Mansoor CCM

    https://www.facebook.com/king.kijokihttps://www.facebook.com/Rakamo25https://www.facebook.com/nevline.kiwiahttps://www.facebook.com/fahim.seifhttps://www.facebook.com/haji.kombo.96https://www.facebook.com/drabdul.emilyhttps://www.facebook.com/profile.php?id=100003339276722https://www.facebook.com/abdalla.sleiman.52https://www.facebook.com/Ommykisshttps://www.facebook.com/shamis.alkhatryhttps://www.facebook.com/mzalendo.mtanzaniahttps://www.facebook.com/mzalendo.mtanzaniahttps://www.facebook.com/shamis.alkhatryhttps://www.facebook.com/Ommykisshttps://www.facebook.com/abdalla.sleiman.52https://www.facebook.com/profile.php?id=100003339276722https://www.facebook.com/drabdul.emilyhttps://www.facebook.com/haji.kombo.96https://www.facebook.com/fahim.seifhttps://www.facebook.com/nevline.kiwiahttps://www.facebook.com/Rakamo25https://www.facebook.com/king.kijoki