33
  

7-Toleo la Saba.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

  • i

    Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu.

    Raudhwah Time ni Jarida maalum, linalotolewa kila mwisho wa mwezi wa muandamo na

    Raudhwah Islamic Group, kwa lengo la kumjenga Muislamu kumfahamu vilivyo Muumba wake

    na kumpelekea kutimiza majukumu yake ya kiibada na kidini kwa ujumla, ili kuweza kupata

    Radhi za Allah na kuepukana na adhabu zake.

    Katika toleo la mwezi huu, tumekuandalia mada mbali mbali katika upande wa:

    Afya. Ambayo itazungumzia maradhi ya Kipindupindu; ishara za mwenye maradhi haya,

    tiba yake, kinga yake na mengine mengi kwa kifupi.

    Jamii. Ambayo itazungumzia juu ya ujirani katika Uislamu.

    Historia ya wema waliotangulia. Hapa tutamtaja kwa uchache Tabiin maarufu

    anayejulikanwa kama Said bin Jubayr (rehma za Allah ziwe juu yake) na yaliyomfika

    kutokana na kuukataa utawala wa Hajjaj bin Yuusuf.

    Na mengine mengi yatakayokunufaisha wewe msomaji na Waislamu wote kwa ujumla.

    Ni matumaini yetu kuwa Allah atatukubalia amali yetu hii na kuleta tija katika Ummah wa

    Kiislamu, na kuwaongoza waliopotea na kuwaengezea istiqama walioongoka.

  • ii

  • 1

    Kila sifa njema zinamstahikia Allah Mola

    wa viumbe vyote. Swala na salamu

    zimuendee Mtume wetu Muhammad (swalla

    Allahu alaihi wa sallam) na ahli zake na

    maswahaba wake.

    Leo kwa Tawfiq ya Allah nimependa

    kugusia suala la ujirani katika Uislamu

    ambalo wengi wetu hulipuuzia na kuliona ni

    la kawaida, ima kwa kutambua au

    kutotambua ukubwa wa fadhila zake.

    Kama tunavyofahamu jirani ni mtu

    anayeishi karibu na wewe, ima iwe

    nyumbani kwako au kazini au popote pale

    ulipo. Na kwa vile Uislamu ni Dini

    iliyokamilika kama alivyotuambia

    mwenyewe Allah (subhanahu wa taala): ...

    Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na

    nimekutimizieni neema yangu, na

    nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo

    Dini ... [al-Maida (5): 3].

    Uislamu haukuacha jambo lolote ila

    limebainishwa na Allah (subhanah wa taala)

    pamoja na Mtume wake (Swalla Allahu

    Alayhi Wasallam). Katika kusisitiza hili

    Allah (subhanahu wa taala) hakuacha

    kulizungumzia suala la ujirani katika Qur'an

    kama alivyosema: Muabuduni Mwenyezi

    Mungu wala msimshirikishe na chochote.

    Na wafanyieni wema wazazi wawili na

    jamaa na mayatima na masikini na jirani wa

    karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa

    ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na

    mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi

    Mungu hawapendi wenye kiburi wanao

    jifakhiri. [an-Nisai (4): 36].

    Aya hii imebainisha kabisa uwajibu wa

    kuwafanyia wema majirani walio karibu na

    hata walio mbali kwa kadri tuwezavyo.

    Sasa tumuangalie Mtume (swalla Allahu

    Alayhi Wa sallam) nae anatuambia nini

    kuhusu ujirani: Hakuacha Jibril ananiusia

    kuhusu jirani mpaka nikadhania atamfanya

    kuwa ni mmoja wa warithi wangu.

    Bukhari.

    Hadithi hii inatosha kabisa kutuonyesha

    uwajibu wa kuishi kwa uzuri na jirani zetu

    kwa sababu ni jambo ambalo alikuwa

    akilitilia msisitizo Jibril (Alayhi ssalaam)

    kila anapokuja kwa Mtume (swalla Allahu

    Alayhi wa sallam).

    Aina Za Jirani na Haki walizokuwa nazo:

    1. Jirani ambaye ni ndugu yako. Huyu

    ana haki tatu juu yako:

    i. Ya Uislamu.

    ii. Ya udugu.

    iii. Ya ujirani.

    2. Jirani ambaye ni Muislamu lakini sio

    ndugu yako. Huyu ana haki mbili:

    i. Ya Uislamu.

    ii. Ya ujirani.

    3. Jirani ambae si Muislamu. Huyu ana

    haki moja kwako:

    i. Ya ujirani.

  • 2

    Hivyo ndugu zangu, lazima kila mmoja

    tumpe haki anazostahiki bila ya kupunguza

    chochote katika haki hizo.

    Ewe Ndugu yangu, jilazimishe na mambo

    matatu kuhusu jirani yako, utakua miongoni

    mwa waliofaulu.

    1. JIEPUSHE NA KUMUUDHI

    Tukizungumzia maudhi, tunajumuisha kila

    aina ya maudhi, imma ya kimaneno au

    kivitendo, kwa kudhihirisha au kujificha.

    Kwani hakika kuna makemeo makali kuhusu

    hilo, na katika ubaya wa kumuudhi jirani

    kuna khasara nyingi anazozipata mwenye

    kumuudhi jirani yake ila leo nitataja mawili

    makubwa kwa tawfiq ya Allah (Subhanahu

    Wa taala).

    a) Hawi na Imani

    Hili ni kutokana na maneno ya Mtume

    (Swalla Allahu Alayhi Wa sallam): Naapa

    kwa jina la Allah hatoamini. Naapa kwa jina

    la Allah hatoamini. Naapa kwa jina la Allah

    hatoamini. pakasemwa Ni nani huyo ewe

    Mtume wa Allah; akasema: Yule ambae

    jirani yake hapati amani (hasalimiki)

    kutokana na vitimbi vyake. Muslim.

    Kina mama wengi tumekua hatujali uwepo

    wa majirani na umuhimu wao kwetu.

    Tumekua tukiwaudhi kwa udhia mbali

    mbali. Tambua ewe ndugu yangu ya kuwa

    ukamilifu wa imani yako unachangiwa na

    kukaa kwa wema na jirani yako. Kama

    anavyotueleza Mtume (Swalla Allahu

    Alayhi Wa sallam) katika hadithi hii:

    Mwenye kumuamini Allah na siku ya

    mwisho basi na asimuudhi jirani yake.

    Bukhari.

    Hili ni himizo kwako ewe dada wa

    Kiislamu, kama tunataka tuipate pepo ya

    Allah, basi tujitahid kuishi vyema na

    majirani zetu, kama huwezi kumfanyia

    wema basi epukana na kumuudhi. Kwani

    kupitia wao ndio tutaikamilisha imani yetu

    na tutaipata pepo ya Allah (Subhanahu Wa

    taala). Kama alivyotuambia Mtume (Swalla

    Allahu Alayhi Wa sallam): Hamtoingia

    peponi mpaka muamini . Abu daud.

    b) Matendo yake hubatilika

    Jambo la kumuudhi jirani humsababishia

    mtu kuharibika matendo yake na mwishoni

    kuingizwa katika moto. Hadithi ifuatayo

    inatubainishia hilo.

    Siku moja maswahaba wa Mtume (Swalla

    Allahu Alayhi Wa sallam) walimuuliza:

    Hakika fulani anafunga mchana na

    anasimama usiku kuswali na anamuudhi

    jirani yake kwa ulimi wake. Mtume

    akawajibu: Hamna kheri kwake nae ni

    katika walio motoni wakamuuliza tena:

    Hakika fulani anaswali swala za wajibu na

    anafunga Ramadhani na anatoa sadaka

    kidogo na wala hamuudhi jirani yake.

    Mtume (Swalla Llahu Alayhi Wa sallam)

    akasema: Yeye ni katika walio peponi.

    Ahmad.

    Hii inatupa fundisho kuwa hata kama utakua

    unafanya ibada kwa wingi kiasi gani, kama

  • 3

    huishi na jirani yako kwa wema basi maishio

    yako yatakua mabaya. (Allah Atuhifadhi).

    2. MVUMILIE MAUDHI YAKE

    Hakika katika sifa za waumini wa kweli ni

    wale ambao huwa na subra katika mitihani

    aliyowapa Allah na wanatarajia malipo

    kutokana na mitihani hiyo. Allah

    (subhanahu wa taala) akikupa jirani muovu,

    basi jua amekupa mtihani ndugu yangu ni

    juu yako kufanya yafuatayo:

    a) Kuwa na Subra

    Kwani Allah (Subhanahu Wa taala)

    amesema: Na ambao husubiri kwa kutaka

    radhi ya Mola wao Mlezi, na wakashika

    Sala, na wakatoa, kwa siri na kwa uwazi,

    katika tulivyo wapa; na wakayaondoa

    maovu kwa wema. Hao ndio watakao pata

    malipo ya Nyumba ya Akhera. [ar-Raad

    (13): 22].

    b) Zuia Hasira zako na Usamehe

    Atakapokuudhi jirani yako zizuie hasira

    zako na jaribu kumsamehe. Kwani Allah

    (subhanahu wa taala) amewasifu wenye

    kufanya hivyo na amewaahidi malipo

    mazuri. Allah amesema: ... Ambao hutoa

    wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na

    dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na

    wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi

    Mungu huwapenda wafanyao wema [al-

    Imraan (3): 134].

    c) Mrekebishe na umlinganie kwa

    hekima

    Kwani majirani wengine hufanya makosa

    kwa kutojua. Hivyo inawezekana akaongoka

    kupitia wewe. Allah (Subhanahu Wa taala)

    ametuambia: Waite waelekee kwenye Njia

    ya Mola wako Mlezi kwa hikima na

    mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa

    namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi

    ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia

    yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi

    walio ongoka. [an-Nahli (16): 125].

    d) Usimlipize bali mfanyie wema kwa

    ubaya wake

    Kwani hakika katika hili kuna taathira

    kubwa kama alivyoeleza Allah (Subhanahu

    Wa taala): Mema na maovu hayalingani.

    Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule

    ambaye baina yako naye pana uadui

    atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea

    uchungu. [Fusswilat (41): 34].

    Nyoyo zikifanyiwa mema hujenga mapenzi,

    fata maneno haya ya Allah utaona maajabu

    yake.

    3. MFANYIE IHSANI

    Ihsani ni kila jema ambalo akifanyiwa mtu

    roho yake hufurahi sawa sawa kimaneno au

    kivitendo. Ewe Ndugu yangu jilazimishe na

    kumfanyia ihsani jirani yako, kwani hakika

    kumfanyia yeye ihsan ni miongoni mwa

    sababu zitakazokufanya uipate pepo ya

    Allah (subhanahu wa taala), pamoja na

    kukuepusha na moto wa Allah. Na miongoni

    mwa ihsan ambazo zimetajwa na Mtume

    (Swalla Allahu Alayhi Wa sallam) ni:

  • 4

    a) Kumpa chakula katika mlo

    unaoupika

    Amesema Mtume (Swalla Allaahu Alayhi

    Wa sallam): Hajaniamini mimi mwenye

    kulala hali ya kuwa ameshiba wakati jirani

    yake ana njaa pembeni yake na hali yeye

    anajua jambo jilo. Bukhari.

    Pia katika hadithi nyingine amesema Mtume

    (Swalla Allahu Alayhi wa sallam)

    kumwambia Aba Dhar: Ewe Aba Dhar!

    Ukipika mchuzi kithirisha maji yake na

    umpe jirani yako. Muslim.

    b) Pendelea kumpa zawadi

    Katika hadithi Mtume (Swalla Allahu

    Alayhi Wa sallam) aliwahimiza wanawake

    wa Kiislamu kuwapa zawadi jirani zao.

    Enyi Waislamu wa kike, asidharau jirani

    kumpa jirani yake chochote hata kama ni

    kipande kidogo cha nyama. Bukhari.

    Na Mama Aisha (radhia Allahu anha)

    alimuliza Mtume (Swalla Allahu Alayhi Wa

    sallam): Hakika yangu mimi nina jirani

    wawili jee ni yupi nimpe zawadi. Mtume

    (Swalla Allahu Alayhi Wa sallam) akasema:

    Ambae mlango wake upo karibu nawe.

    Bukhari.

    Mwisho napenda kumalizia nukta hii kwa

    hadithi ya Mtume (Swalla Llahu Alayhi wa

    sallam) aliyosema: Mwenye kumuamini

    Allah na siku ya mwisho basi na amkirimu

    jirani yake. Bukhari na Muslim.

    c) Kumtembelea mara kwa mara

    Hakika Allah huwapenda wenye

    kutembeleana kwa ajili yake na ndio maana

    akasema katika hadithi Qudsiy:

    Yamewalazimikia mapenzi yangu wenye

    kutembeleana kwa ajili yangu. Ahmad.

    Kwani hakika Mtume (Swalla Allahu Alayhi

    Wa sallam) alikuwa akipenda kuwatembelea

    majirani zake walio Waislamu na hata

    wasiokuwa Waislamu, waliokuwa

    wakimtendea wema na hata waliokuwa

    wakimuudhi.

    d) Akiumwa nenda ukamtizame

    (ukamjuulie hali)

    Kwani kufanya hivyo utapata malipo

    makubwa kama alivyotuambia Mtume

    (Swalla Allahu Alayhi Wa sallam):

    Mwenye kumtembelea Mgonjwa Hatoacha

    kuwa miongoni mwa waliomo katika

    Mabustani ya peponi. Muslim.

    HITIMISHO

    Huu ndio ufupisho wa mada ya ujirani

    katika Uislamu kama ulivyoelezewa kwenye

    Qur'an na Sunna za Mtume (Swalla Allahu

    Alayhi Wa sallam). Namuomba Allah

    atuonyeshe haki ilipo na atuwafikishe

    kuifata na atubainishie batil na atuwafikishe

    kuiacha. Amin.

  • 5

    Kipindupindu ni ugonjwa wa maambukizi

    unaosababisha kuharisha sana kinyesi

    kilicho katika mfumo wa maji maji kama

    rangi ya mchele. Maradhi haya yanaweza

    kusababisha upungufu wa maji mwilini na

    hata kifo ikiwa mgonjwa hakutibiwa

    mapema. Kipindupindu husababishwa kwa

    kula chakula au kutumia maji

    yaliyoathiriwa na vimelea vya bakteria

    ajulikanae kwa jina la kitaalamu kama

    Vibrio cholerae.

    Ugonjwa huu unatokea kwa kawaida na kwa

    kiasi kikubwa katika maeneo yaliyo katika

    hali duni ya usafi, msongamano wa watu,

    vita, na njaa. Maeneo ya kawaida ni pamoja

    na maeneo ya Afrika, Asia kusini, na

    Amerika ya kati na kusini (Latin America).

  • 6

    Sababu za kipindupindu

    Bakteria anaesababisha kipindupindu,

    kawaida hupatikana katika chakula au maji

    yaliyochafuliwa na kinyesi kutoka mtu aliye

    na maambukizi. Vyanzo vya kawaida vya

    maradhi haya ni pamoja na maji ya miji,

    barafu iliyofanywa kutokana maji ya miji,

    vyakula na vinywaji viuzwavyo na wachuuzi

    wa mitaani, mboga mboga zilizomwagiliwa

    kwa maji yaliyochafuliwa na kinyesi na

    takataka za wanaadamu, samaki wabichi na

    mazao mengine ya bahari yaliyokuwa

    hayajapikwa vizuri.

    Endapo mtu atatumia chakula au maji

    yaliyoathirika, bakteria hutoa sumu katika

    utumbo ambayo hupelekea kuharisha sana.

    Dalili za maradhi

    Dalili za ugonjwa wa kipindupindu

    zinaweza kuanza haraka sana kama saa

    chache au kwa muda mrefu kama siku tano

    baada ya kuambukizwa. Mara nyingi dalili

    huwa sio kali sana, lakini wakati mwengine

    huwa ni mbaya sana. Takriban mmoja kati

    ya watu ishirini katika watu

    walioambukizwa huonyesha dalili za

    kuharisha sana zikifuatana na kutapika,

    ambako kunaweza kusababisha upungufu

    mkubwa wa maji mwilini. Ingawa watu

    wengi walioambukizwa wanaweza kuwa na

    dalili chache au kutokuwa na dalili kabisa,

    lakini bado wanaweza kuchangia kuenea

    kwa maambukizi. Dalili na alama za

    upungufu wa maji mwilini ni pamoja na:

    i. Kuongezeka kwa kiwango cha

    mapigo ya moyo,

    ii. Kupungua kwa mkunjuko

    (elasticity),

    iii. Kukauka kwa kiwamboute (mucous

    membrane) (ikiwa ni pamoja na

    ndani ya mdomo, koo, pua, na kope),

    iv. Kupungua kwa shindikizo la damu,

    v. Kiu kali na maumivu ya misuli.

    Kama mgonjwa hakutibiwa mapema,

    upungufu wa maji mwilini unaweza

    kusababisha mshtuko (shock) na kifo ndani

    ya masaa machache.

    Kinga na tiba ya maambukizi ya

    kipindupindu

    Ingawa kuna chanjo dhidi ya kipindupindu,

    CDC na Shirika la Afya Duniani kawaida

    hawaipendekezi kutumiwa, kwa sababu

    inaweza kutowalinda nusu ya watu wenye

    kupata chanjo hiyo na huchukua muda wa

    miezi michache tu kabla kupoteza uwezo

    wake wa kufanya kazi. Hata hivyo, unaweza

    kujikinga na familia yako kwa kutumia maji

    yaliyochemshwa vizuri au maji yaliyotiwa

    dawa (chemicals) za kuua vimelea vya

    ugonjwa huo, kutumia maji ya chupa

    yaliyoandaliwa katika viwanda vyenye

    mazingira safi. Maji hayo huweza

    kutumiwa kwa madhumuni yafuatayo:

    i. Kunywa,

    ii. Maandalizi ya chakula au vinywaji,

  • 7

    iii. Kugandishia barafu,

    iv. Kusugua meno yako,

    v. Kuosha uso wako na mikono,

    vi. Kuosha sahani na vyombo ,

    vii. Matumizi ya kula au kuandaa

    chakula na kuoshea matunda na

    mboga.

    Ili kuandaa maji yako mwenyewe, chemsha

    kwa dakika zisizopungua kumi au kuyachuja

    na kuongeza matone mawili ya bleach

    (chlorine) au weka nusu kidonge cha madini

    joto aina ya IODINE kwa kila lita moja ya

    maji. Pia lazima kuepuka vyakula vibichi,

    ikiwa ni pamoja na yafuatayo:

    i. Matunda na mboga zilizokua

    hazijamenywa na kuandaliwa vizuri,

    ii. Maziwa na bidhaaa za maziwa

    ambazo hazijachemshwa au

    kuhakikishwa kuwa vimelea

    vimefariki,

    iii. Nyama iliyokua haijapikwa n.k.

    Endapo utahisi dalili za kuharisha kinyesi

    chenye rangi kama maji ya mchele mara

    kwa mara, na kutapika sana - hasa baada ya

    kula samakigamba (shellfish) wabichi au

    kusafiri kuelekea nchi ambayo kipindupindu

    ni janga tafuta msaada wa matibabu mara

    moja. Kipindupindu ni maradhi yenye

    kutibika kwa urahisi, lakini kwa sababu ya

    upungufu wa maji mwilini unaoweza

    kutokea haraka, ni muhimu kupata matibabu

    ya kipindupindu haraka sana mara tu

    unapoona dalili za maradhi hayo.

    Matibabu makuu ya ugonjwa huu ni

    kumsaidia mgonjwa kurejesha kiwango

    kikubwa cha maji ambacho amekipoteza

    kwa kuharisha sana, maji yaliyopotea

    yanaweza kuwekwa kwa njia ya drip katika

    mishipa ya damu (intravenous). Dawa za

    antibiotiki ambazo huua vimelea vya

    maradhi haya zinaweza pia kutumika katika

    kupunguza kasi na nguvu ya maradhi haya.

    Hitimisho

    Ugonjwa wa kipindupindu ni maradhi hatari

    sana kwa sababu athari zake zinajitokeza

    katika kipindi cha muda mfupi sana baada

    ya maambukizi, na vile vile huweza

    kusababisha kifo ikiwa hayajatibiwa haraka

    baada ya kuambukizwa, lakini maradhi haya

    ni yenye kutibika na kuepukika pia. Ni

    muhimu sana kutumia maji na vyakula

    vilivyo katika hali ya usafi, na wagonjwa

    wanashauriwa kuwahi kupata huduma za

    afya endapo wataona dalili za ugonjwa huu

    kwa haraka sana.

    KUMBUKA KUWA, KINGA NI BORA KULIKO TIBA!

  • 8

    SUALI

    Ninafanya kazi katika kampuni ya Aramco,

    ambayo ina program ya kustaafisha watu

    ambao wamefikia umri wa miaka khamsini

    (50), na hupata matibabu bure mpaka

    mwisho wa maisha yao. Jee inafaa

    kubadilisha umri wangu kwa kuomba katika

    idara ya kumbukumbu bila ya kulipia

    chochote au kutaja umri maalum, lakini kwa

    lengo la kupata matibabu ya bure, kwa

    sababu nikistaafu kabla ya kufikia miaka 50

    sitopata matibabu (ya bure)?

    JAWABU

    Sifa njema ni za Allah.

    Haifai mtu kudanganya kuhusu umri wake

    ili apate matibabu ya bure yanayotolewa na

    kampuni. Hii inakuwa ni kusema uongo na

    kuhadaa, na Mtume (swalla Allahu alaihi wa

    sallam) amesema: Mwenye kutuhadaa

    (kughushi/kudanganya) si katika sisi.

    Imepokewa na Muslim, 101.

    Pia amesema (swalla Allahu alaihi wa

    sallam): Hakika ukweli unamuongoza mtu

    katika wema, na wema unampeleka mtu

    Peponi. Na hakika mtu huendelea kusema

    ukweli mpaka akaitwa mkweli mbele ya

    Allaah. Na hakika uongo unampeleka mtu

    katika uchafu, na uchafu unampeleka mtu

    Motoni. Na mtu huendelea kusema uongo

    mpaka akaandikwa kuwa ni muongo mbele

    ya Allaah. Imepokewa na al-Bukhary, 6094

    na Muslim, 2607.

    Anachotakiwa Muumini kufanya ni kuwa

    mkweli katika maneno na vitendo. Allah

    (subuhanahu wataala) amesema: Enyi mlio

    amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na

    kuweni pamoja na wakweli (katika kauli zao

    na vitendo vyao). [at-Tawbah (9): 119].

    Na Allah anajua zaidi.

    CHANZO: http://islamqa.info/en/126053

  • 9

    Kila sifa njema zinamstahikia Allah

    (subhanahu wa taala), Mola wa

    walimwengu wote. Swala na salamu

    zimfikie Mtume wetu Muhammad (swalla

    Allahu alaihi wa sallam).

    Pia namshukuru Allah kwa kunipa fursa hii

    ya kuizungumzia mada hii muhimu, ambayo

    wengi katika kina mama wa Kiislamu

    tumeghafilika nalo jambo hili.

    Kama tunavyofahamu ya kuwa mara nyingi

    mtu mwenye akili timamu na aliefikia umri

    wa baleghe lazima huwa hakosi jukumu

    lolote lile ambalo humlazimu kulitekeleza.

    Lakini kwa leo nimependa khaswa,

    nimzungumzie mwanamke ambaye

    ameshaolewa na ameruzukiwa nyumba na

    watoto, kwa sababu yeye ndiye chanzo cha

    maendeleo au maharibiko ya jamii iliyopo

    na ijayo.

    Mwanamke wa Kiislamu aliyeolewa ana

    majukumu manne makubwa ambayo ni

    lazima ayatekeleze kwa ufasaha tena kwa

    mujibu wa mafundisho ya Qur'an na Sunna.

    Majukumu yenyewe ni;

    1. Majukumu juu ya Nafsi yake.

    2. Majukumu juu ya Mumewe.

    3. Majukumu juu ya nyumba yake.

    4. Majukumu juu ya jamii yake.

    1. MAJUKUMU JUU YA NAFSI

    YAKE

    Ewe dada wa Kiislamu, tambua ya kwamba

    dunia ni mapito na akhera ndio bora na

    yenye kudumu, hivyo ni lazima ujichumie

    hapa duniani kila kilicho bora kwa ajili ya

    safari ndefu uliyonayo. Na aliyebora ni yule

    aliyejitambua mapema na akaufanyia kazi

    umri wake katika yalio mema.

    Kama tunavyofahamu ya kuwa nafsi siku

    zote hutuamrisha yalio mabaya isipokua zile

    alizozirehem Allah (Subhanahu Wa taala).

    Lakini kilicho cha wajibu kwetu ni

    kuziendesha sisi katika yaliomema na sio

    kuziacha zituepeleke sisi zinavyotaka.

    Tufahamu ya kuwa nafsi ni kama mtoto,

    ukiipa kila kinachotaka mwisho hutaka hata

    chenye madhara nayo. Hivyo ni lazima

    tujifundishe kuzikatalia khaswa katika yalio

    haramishwa na Allah na Mtume (swalla

    Allahu alaihi wa sallam), kwa sababu

    Muumba wa nafsi zetu ndiye mwenye

    kuzifahamu zaidi kipi kina faida nazo na

    kipi hakifai au kipi chenye madhara.

    Dunia ni sawa na jela kwa Muumini yaani

    huwa na mipaka, nayo ni maamrisho na

    makatazo ya Allah (subhanahu wa taala)

    aliyoyaeleza kupitia katika Quraan au

    Mtume (swalla Allahu alaihi wa sallam).

    Ama kwa kafiri ni sawa na Pepo, kwani

    huwa hana mipaka hufanya anavyotaka

  • 10

    mwenyewe. Hivyo lolote ulifanyalo liwe

    jema au baya utalikuta mbele ya Allah

    (subhanahu wa taala) kwani ametueleza:

    Basi anaye tenda chembe ya wema,

    atauona! Na anaye tenda chembe ya uovu

    atauona! [az-Zilzalah (99): 7-8].

    Hivyo jukumu kubwa la nafsi yako ni

    kuifanya imuelekee mola wako katika amri

    zake na kuiepusha na makatazo yake ili siku

    hio isiwe ni yenye kujilaumu kama ambavyo

    Allah ameiapia nafsi hii ambayo itakuja

    kujuta kwa kila baya ililolitenda. Allah

    anasema: Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!

    Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu! [al-

    Qiyamah (75): 1-2].

    Jee unapenda kuwa miongoni mwa watakao

    jilaumu kesho akhera? Bila shaka hapana.

    Basi anza leo wala usingoje kesho, ambayo

    hujijui kama utafika au hutofika.

    Tujiandaeni na siku ya Qiyama ambayo

    Allah anatuambia: Siku ambayo kila nafsi

    itakuta mema iliyo yafanya

    yamehudhurishwa, na pia ubaya ilio ufanya.

    Itapenda nafsi lau kungekuwako masafa

    marefu baina ya ubaya huo na yeye. Na

    Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni naye.

    Na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja

    wake. [al-Imraan (3): 30].

    Mwisho napenda kumalizia nukta hii kwa

    kauli ya ameer wa Waislamu Umar bin

    Khattab aliyosema: "Jihisabieni nafsi zenu

    kabla hamjahisabiwa na yapimeni matendo

    yenu kabla hamjapimiwa."

    2. MAJUKUMU JUU YA MUMEWE

    Ndoa ni pingu ya maisha na ni ahadi kubwa

    ambayo huichukua mume na mke kwa kule

    kukubali kuiingia ndoa. Allah (subhanahu

    wa taala) ameiita ndani ya Qur'an kuwa ni

    "Ahadi madhubuti". Na kwa sababu hii

    tunasisitizwa sana kuijua kiundani kabla ya

    kujiingiza ndani yake, jambo ambalo wengi

    wetu hawalifatilii na ndio sababu tunaona

    machafuko makubwa yaliyopo katika ndoa

    za wakati huu kutokana na kutoijua ukweli

    wa kuijua.

    Hivyo nimependa kuyazungumzia

    majukumu ya mwanamke katika ndoa yake

    ili kuwazindua wanawake wa Kiislam

    walioolewa na ambao hawajaolewa, kwani

    huenda kwa tawfiq ya Allah ikawa ni sababu

    ya kizirekebisha ndoa zao au kuziendesha

    vizuri watakapoziingia.

    Yafuatayo ni baadhi ya majukumu ya

    mwanamke kwa mumewe:

    i. Kumtii mumewe katika yalio mema

    Kwa vile mwanamme huchukua jukumu la

    kuwa ni msimamizi kwa mkewe badala ya

    wazazi wake baada tu ya kumuoa, hivyo ni

    jukumu la mke kumsikiliza na kumtii katika

    kila analomuamrisha miongoni mwa yale

    yaliomo katika mipaka ya kisheria ya Dini

    yetu. Allah (subhanahu wa taala)

    ametuamrisha ndani ya Quraan kuwatii

    viongozi wetu pale aliposema: Enyi mlio

    amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini

  • 11

    Mtume na wenye madaraka katika nyinyi ...

    [an-Nisaa (4): 59].

    Na laiti mke angelijua umuhimu wa kumtii

    mumewe angejitahidi kumtii mumewe kadri

    awezavyo kwani Mtume (swalla Allahu

    alaihi wa sallam) amesema: Laiti

    ningekuwa ninaamrisha mtu kumsujudia

    mtu (mwengine) ningemuamrisha mke

    kumsujudia mumewe. Tirmidhiy.

    Pia katika masharti manne ambayo

    humuingiza mwanamke peponi moja wapo

    ni twaa ya mke kwa mumewe nayo imo

    katika kuonyesha fadhila na ubora wa ibada

    hii. Kama alivyotuelezea Mtume (swalla

    Allahu alaihi wa sallam): Atakapo swali

    mwanamke swala zake tano (za faradhi), na

    akamtii mumewe, na akafunga mwezi wake

    (wa Ramadhani) na akajihifadhi utupu wake

    ataambiwa siku ya Qiyama ingia peponi kwa

    mlango unaoupenda. Ahmad.

    Jee ni uzuri ulioje wa amali hii? Lakini kwa

    masikitiko makubwa wengi miongoni mwa

    walioolewa inatushinda, nayo ni kutokana

    na njama za iblis na majeshi yake kututaka

    tusiwe miongoni mwa watakaofaulu kesho

    akhera. Pamoja na kuwa mume amepewa

    amri juu ya mkewe ya kuwa ni mwenye

    kusikilizwa na kutiiwa, Uislamu umeweka

    mipaka katika hilo kwani Allah amesema:

    Na ukiwat'ii wengi katika hawa waliomo

    duniani watakupoteza na Njia ya Mwenyezi

    Mungu. Hawa hawafuati ila dhana tu, na

    hawakuwa ila ni wenye kusema uwongo tu.

    [al-An-aam (6): 116].

    Pia katika hili amesema Mtume (swalla

    Allahu alaihi wa sallam): Hakuna kumtii

    kiumbe katika kumuasi Muumbaji. Ahmad.

    Hivyo ewe dada wa Kiislamu pupia katika

    ibada hii kwa nia ya kuidumisha ndoa yako

    na kupata pepo, na wala usiwasikilize

    mashetani wa kijini au wa kibinaadamu pale

    watakapo kuamrisha kwenda kinyume na

    maamrisho mema ya mumeo kwani hakika

    utakapokufa hali yakuwa mumeo yupo radhi

    nawe basi pepo itakua karibu nawe in shaa

    Allah.

    ii. Kujipamba kwa ajili yake

    Hakika dini yetu ni nzuri na imesisitiza uzuri

    katika kila nyanja. Kwani hakika Mola wetu

    ni mzuri na anapenda vilivyo vizuri. Na

    uzuri kulingana na dini yetu hauangaliwi

    kwa mujibu wa sura wala maumbile, bali

    hupimwa kwa moyo na matendo yetu kwa

    ujumla. Binaadamu tumeumbwa katika

    umbile la kupenda vilivyo vizuri na ndio

    maana hata katika ibada Allah (subhanahu

    wa taala) hupenda mja wake akifanya ibada

    aifanye kwa uzuri. Katika hili la kujipamba

    Muislam amesisitiziwa kujipamba na

    kujipendezesha na ndio maana Mtume

    (swalla Allahu alaihi wa sallam) nae akiwa

    kama mfano uliobora, alikua akipenda kuvaa

    vizuri na kunukia. Hili ni msisitizo kwetu

    Waislamu wanaume kwa wanawake ya

    kuwa Muislam anatakiwa kuwa ni mtu

    mtanashati akiwa nje na ndani ya nyumba

    yake.

  • 12

    Ama tukija kwa wanawake na ndio msingi

    wa mada yetu, hutakiwa kujipamba lakini

    kwa mipaka. Nikimaanisha anatakiwa

    kujipamba mapambo yanayoendana na

    sheria na kuyadhihirisha kwa mahrim zake

    tu, nao ni wale wasiopasa kumuoa kama

    baba, kaka, babu, mjomba n.k. Ifuatayo ni

    hadithi inayomuhimiza mwanamke

    kujipendezesha kwa ajili ya mumewe.

    Amesema Mtume (swalla Allahu alaihi wa

    sallam): Mwanamke Bora ni yule ambae

    ukimtizama anakufurahisha ... Tabrani.

    Ina maana mke mbaya ni yule

    asiyejipendezesha kwa ajili ya mumewe,

    bali hujipendezesha kwa ajili ya wengine

    ambao ni haram kwake hata kuona

    mapambo yake, na jambo hili ndio miongoni

    mwa sababu zinazoporomosha ndoa nyingi

    kwani mume karibu muda wote humuona

    mkewe katika hali isiyo mvutia jambo

    ambalo huondoa mvuto na mahaba katika

    moyo wa mume na hatimae mume huenda

    nje kwenye haram kutuliza jicho lake.

    iii. Asikatae Wito wa Mumewe

    Kama tunavyofahamu kuwa mke anatakiwa

    kuwa ni tulizo la macho na moyo wa

    mumewe na pia mume. Khaswa katika dunia

    iliyojaa machafuko ya kila aina ukiachana

    na maradhi yanayozuka kila kukicha. Kwa

    kuzingatia hili mke anatakiwa ajitahidi kadri

    ya uwezo wake kumtuliza mumewe kwani

    asipofanya hivyo madhara huwaangukia

    wote.

    Uislam umekemea vikali zinaa na vile vile

    umeweka makemeo makali khaswa

    mwanamke ambaye hujizuilia na mumewe

    bila ya sababu yoyote ya msingi ya kisheria.

    Amesema Mtume (swalla Allahu alaihi wa

    sallam): Atakapomuita mume mkewe

    kwenye kitanda chake (kwa ajili ya tendo la

    ndoa) halafu asimuendee, mume akalala hali

    ya kuwa amemkasirikia malaika humlaani

    mpaka kupambazuke. Bukhari na Muslim.

    Nadhani hadithi hii inatutosha kuwa ni

    sababu ya kutokataa wito wa waume zetu

    kama kweli tunamuogopa Allah (subhanahu

    wa taala).

    iv. Asimuombe talaka

    Kwenye ndoa mke na mume lazima kila

    mmoja awe na jitihada katika kuilinda ndoa

    yake. Kwa sababu ndoa yoyote huwa haikosi

    migongano ila muhimu ni subra na hawi na

    subra ila mwanandoa alietimia sifa za

    uumini, kwani hakika Muumini huitakidi

    kuwa mwenye kupatwa na matatizo ndio

    hupandishwa darja na hulipwa malipo bila

    ya hisabu na kwa uchaMungu ndio Allah

    (subhanahu wa taala) huleta faraja.

    Kinyume na hivyo mwanandoa hushindwa

    na kudai talaka jambo ambalo ni lenye

    kuchukiza mbele ya Allah (subhanahu wa

    taala) na lenye kufurahisha sana mbele ya

    iblisi (laanatu Allahi Alayhi). Amesema

    Mtume (swalla Allahu alaihi wa sallam)

    katika kumzungumzia mwanamke mwenye

    kupenda kudai talaka bila ya sababu

    inayokubalika kisheria: Mwanamke yoyote

  • 13

    anaemuomba mumewe talaka bila ya tatizo

    lolote (la kisheria) basi ni haramu kwake

    harufu ya pepo. Ahmad.

    Ni khasara ilioje kuikosa hata harufu ya

    pepo wakati harufu yake huipata kutoka

    Masafa ya mbali kwa watakao iingia. Allah

    atujalie miongoni mwao. AMIIN.

    v. Kutunza siri za mumewe

    Mke na mume wakishaoana wanatakiwa

    kuwa kama mwili mmoja, yani kila mmoja

    aitunze aibu ya mwenziwe iwe ni kama yake

    na sio kuitangaza kwa watu wa nje sawa

    sawa ni kwa jamaa wa karibu au marafiki

    wa mbali. Dini yetu imekataza mke

    kumtolea mumewe siri zake na mume kutoa

    siri za mkewe. Amesema Mtume (swalla

    Allahu alaihi wa sallam): Hakika katika

    watu wenye nafasi mbaya siku ya Qiyama ni

    mwanamme anaemuendea mkewe au mke

    anaeendewa na mumewe halafu akaeneza

    siri za mwenziwe. Bukhary.

    Na katika Qur'an Allah (subhanahu wa

    taala) amewasifu wanawake wema kuwa ni

    wale wenye kuhifadhi siri: ... Basi

    wanawake wema ni wale wenye kut'ii na

    wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa

    Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde ...

    [an-Nisaa (4): 34].

    Tujitahidini sana kina mama wenzangu

    kuliacha hili kwa sababu kumtolea mumeo

    aibu ni sawa na kujifedhehesha mwenyewe

    na mwisho tutambue ya kuwa mwenye

    kumsitiri Muislamu mwenzake hapa duniani

    Allah humsitiri yeye duniani na kesho

    Akhera na kinyume chake ukimfedhehesha

    nduguyo duniani Allah atakufedhehesha

    duniani na kesho akhera. Jichunguze

    mwenyewe aibu zako kabla ya kuzitoa aibu

    za mwenzako kama hutaki aibu zako

    zijulikane usijaribu kuzitoa za wenzako

    kwani ni lazima na zako zitatoka kama sio

    karibu hata baadae kama hauko hai hata

    ukifa.

    Majukumu ya mke kwa mumewe yapo

    mengi hayo ni kidogo niliojaliwa

    kuyaelezea.

    Kwa taufiq ya Allah tutaendelea na mada hii

    katika toleo lijalo la jarida letu. Natarajia

    tumefaidika nayo na tutaanza kuyafanyia

    kazi in shaa Allah.

  • 14

    Alikua ni mwembamba wa mwili, mkubwa

    wa akili. Aliyejawa na imani ya kufanya

    mema na khofu ya kuingia katika maasi.

    Alikua ni katika wachaMungu na wenye

    tabia nzuri. Alikua mweusi wa sura,

    mweupe wa moyo. Alikua mweusi kutokana

    na asili yake ya uhabeshi, weusi wa rangi

    yake haukumfanya awe dhalili, kwani

    mtukufu mbele ya Allah ni yule ailyekuwa

    mchaMungu. Allah anasema: ... Hakika

    aliye mbora wenu mbele ya Allah ni yule

    anaemcha zaidi Allah miongoni mwenu ...

    [al-Hujuraati (49): 13]

    NASABA YAKE

    Anaitwa Said bin Jubayr bin Haashim Al-

    Asady, Al-Kuufy, amenasibishwa na kabila

    la bani-Asad ingawa hakuwa muarabu wala

    hakuwa katika kabila la bani-Asad, ila

    alinasibishwa nalo kwa sababu alikuwa ni

    muachwa huru wa kabila hilo, alinunuliwa

    kama mtumwa na baadae akaachwa huru.

    KUZALIWA KWAKE

    Wametofautiana wana tareikh juu ya

    kuzaliwa kwake, wako waliosema kuwa

    amezaliwa mwaka wa 45 Hijria, wengine 46

    Hijria na wengine mwaka wa 38 Hijria,

    kutokana na kifo chake kilichotokea mwaka

    wa 95 Hijria na kua alikufa akiwa na miaka

    57 au 59. Wallahu Alam. Alizaliwa katika

    mji wa Kuufah na ikapelekea kupewa laqab

    ya Al-Kuufy.

    KUSOMA KWAKE

    Said bin Jubeyr (Rahimahu Allah) alijua

    utukufu wa duniani upo kwenye kusoma, na

    utukufu wa Akhera upo kwenye ibada, hivyo

    akaamua kushikamana na vitu viwili hivi

    mpaka mwisho wa uhai wake, elimu na

    ibada. Ikawa haonekani isipokua yuko

    katika moja ya hali mbili hizi, ima anasoma

    na kusomesha au yuko katika ibada.

    Alisoma kwa wengi katika maswahaba

    akiwemo Abu-Muusa Al-Ash-ary, Abu-

    Hurayra, Abu-Said al-khudry, Abdullah bin

    Umar, Bibi Aisha na wengineo katika

    maswahaba (radhia Allahu anhum ajmain),

    lakini zaidi alishikamana na kujilazimisha na

    mwanachuoni wa umma huu na mfasiri wa

    Qur-an Abdullah bin Abbaas (Radhia Allahu

    anhu), akasoma kwake Qur-an na tafsiri, na

    pia hadithi na lugha ya Kiarabu na

    mengineyo. Mpaka akawa anamruhusu

    kutoa fatwa kwa watu na alipokua akijiwa

    na watu kutoka Kufah kutaka fatwa,

    anawauliza jee hayupo kwenu Said bin

    Jubeyr?

    KISA CHAKE NA HAJJAJ BIN YUUSUF

    Jina la Hajjaaj si jina geni katika historia ya

    Kiislamu baada ya Mtume (swalla Allahu

    alayhi wassalam), amefanya aliyoyafanya na

    si mada yetu ya leo kumhusu Hajjaaj. Ila

    tutatizama miongoni mwa aliyoyafanya

    ambayo yanamgusa Said Bin Jubeyr ambae

  • 15

    ndiye mlengwa wa mada yetu ya leo. Hajjaj

    alikua ni mtawala wa Iraq, uongozi aliopewa

    na Bani-Umayyah ambao ndio walikua

    wanashikilia hatamu za uongozi kwa wakati

    huo. Kutokana na fitna iliyokuweko wakati

    huo kwa Waislamu, baadhi ya Waislamu

    wakaupinga utawala wa Bani-Umayyah na

    Hajjaaj akapigana na kila anayeupinga

    utawala wa Bani Umayyah au kumpinga

    yeye. Aliuwa wengi na kuwahiarisha baina

    ya kujiita makafiri, kutokana na kitendo

    chao cha kumpinga khalifa au wauwawe.

    Wapo walouwawa na wapo walokubali

    kuitwa makafiri hivyo wakasilimu upya, na

    kumuunga mkono khalifa ili kujinusuru

    maisha yao kutokana na kiongozi huyu

    muuwaji. Baada ya kuona hayo Said bin

    Jubeyr ambae alikua yuko Kuufah, sehemu

    ambayo ndio aliyokuweko Hajjaaj akaamua

    kuelekea Makka, kunusuru maisha yake

    kwani alikua hana njia zaidi ya kuuwawa au

    kuukubali utawala wa dhulma. Said bin

    Jubeyr aliishi muda mrefu Makka kwa

    kujificha ficha, huku akiendelea na darsa

    zake, hadi Makka ilipopata mtawala mpya

    wa Bani-Ummayyah ambae alikua dhalimu

    akijulikana kwa jina la Khalid bin Abdallah

    Al-Qusry. Alipoingia madarakani alimtafuta

    Said bin Jubeyr, na alipomuona, aliamrisha

    wanajeshi wampeleke kwa Hajjaj bin

    Yuusuf. Wakati yuko njiani kupelekwa kwa

    Hajjaaj (machinjioni) alisikika akiwaambia

    wanafunzi wake, tulikaa usiku mmoja mimi

    na marafiki zangu wawili tukamuomba

    Allah tuliyomuomba, na tukamuomba

    atuandikie shahada, wenzangu tayari

    wameshaipata na mimi ndio naelekea.

    Alipelekwa kwa Hajjaaj hali ya kua mtulivu

    wa nafsi na mwenye shauku ya kukutana na

    Mola wake.

    KUULIWA KWAKE

    Aliingia Said bin Jubeyr kwa Hajjaaj huku

    akijua kua damu yake iko ukingoni

    kunywiwa na Hajjaj. Alipoingia Hajjaaj

    alimuuliza maswali mengi na mazungumzo

    yao yalikua kama ifuatavyo:

    Hajjaaj: Jina lako nani?

    Said : Jina langu ni Said Bin Jubeyr (lenye

    maana mwema, alieungwa).

    Hajjaaj: Bali wewe ni muovu uliyevunjika

    vunjika.

    Said: Mama yangu alikua akinijua zaidi

    kuliko wewe ndio maana akanipa jina hilo.

    Hajjaaj: Unamzungumziaje Muhammad?

    Said: Unamkusudia Muhammad bin

    Abdillah Mtume wa Allah (rehma na amani

    ziwe juu yake)?

    Hajjaaj: Ndio.

    Said: Ni bwana wa watoto wa Adam, mbora

    wa viumbe, mbashiriaji na muonyaji,

    amebeba ujumbe na akafikisha amana na

    akaunasihi Umma.

    Hajjaaj: Unamzungumziaje Abubakar?

    Said: Yeye ni Swiddyq, khalifa wa Mtume

    (swalla Allahu alayhi wassallam),

  • 16

    ameondoka akiwa mwenye kushukuriwa, na

    ameishi akiwa mwenye kufurahiwa, amepita

    katika muongozo wa Mtume (swalla Allahu

    alayhi wasallam), hakubadilisha wala

    kugeuza chochote.

    Hajjaaj: Unamzungumziaje Umar?

    Said: Yeye ni Faaruq, ambae Allah

    ametofautisha Haki na Baatil kupitia kwake,

    alikuwa ni katika vipenzi vya Allah na

    Mtume wake, na amepita katika muongozo

    wa waliomtangulia, akaishi akiwa mwenye

    kushukuriwa na akafa akiwa mwenye

    kuuliwa (shahidi).

    Hajjaaj: Unamzungumziaje Uthmaan?

    Said: Alikua muandaaji wa vita vilivyokuwa

    vigumu (taabuk), aliyechimba kisima cha

    Ruumah, aliyejinunulia nyumba peponi.

    Mkwe wa Mtume (swalla Allahu alayhi

    wasallam). Na ameuliwa kwa dhulma.

    Hajjaaj: Unamzungumziaje Aliy?

    Said: Ni mtoto wa Ami yake Mtume, wa

    mwanzo kusilimu akiwa na umri mdogo,

    amemuoa bibi Faatimaah na ni baba wa

    Hassan na Hussein, mabwana wa vijana wa

    peponi.

    Hajjaaj: Ni nani katika makhlifa wa Bani-

    Umayyah aliyekupendezesha zaidi?

    Said: Aliemridhisha zaidi Mola wake.

    Hajjaaj: Ni nani aliyemridhisha zaidi Mola

    wake?

    Said: Anaeyajua hayo ni yule anaejua siri

    zao na minongono yao.

    Hajjaaj: Basi unanizungumziaje mimi?

    Said: Unajijua zaidi nafsi yako kuliko

    ninavyokujua.

    Hajjaaj: Nataka unavyonijua wewe?

    Said: Mimi ninavyokujua wewe ni kuwa

    unaenda kinyume na kitabu cha Allah,

    unafanya lile unalolipenda kwa matamanio

    yako, na hayo yatakuangamiza na

    kukupeleka motoni.

    Hajjaj: Nitakuua.

    Said: Itakua umenifisidia dunia yangu na

    mimi nimekufisidia Akhera yako.

    Hajjaaj: Chagua namna gani nikuue.

    Said: Chagua wewe kifo cha nafsi yako,

    kwani hutoniua kifo chochote isipokua nawe

    Allah atakuua kifo hicho hicho Akhera.

    Hajjaaj: Hutaki msamaha?

    Said : Ikiwa kutoka kwa Allah basi nautaka,

    na kama kutoka kwako basi siutaki.

    Akakasirika Hajjaaj na akaamrisha kukatwa

    kichwa chake, na akamuona Said bin Jubeyr

    anacheka, (Hajjaaj) akamuuliza kipi

    kinachokuchekesha? Akasema (Said bin

    Jubair): Unanishangaza ujeuri wako kwa

    Allah na upole wake kwako. Akaelekezwa

    kibla ili auwawe, akasoma aya ya Allah

    Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu

    sawa sawa kwa aliye ziumba mbingu na

  • 17

    ardhi, wala mimi si miongoni mwa

    washirikina. [al-An-aam (6): 79].

    Hajjaaj: Mgeuzeni kutoka kiblani.

    Said: Akasoma: ... Na popote

    mtakapoelekea mtamkuta Allah ... [al-

    Baqarah (2): 115].

    Hajjaaj: Muekeni kufudifudi.

    Said: Kutoka na udongo tumekuumbeni, na

    huko tutakurejesheni na humo tutakutoeni

    kwa mara ya pili. [Twaha (20): 55].

    Hajjaaj : Mchinjeni uyo adui wa Allah

    anayejidai kusoma aya za Qur-an.

    Said: Ewe Mola usimsalitishe mtu yoyote

    baada yangu kwa Hajjaaj. Na akauwawa hali

    ya kuwa ulimi wake unamtaja Allaah.

    Subhanallah ni wema gani aliouonyesha

    Said bin Jubeyr, kiasi ambacho unawaombea

    wenzako wasiuliwe tena na Hajjaj na yeye

    ndiye awe mtu wa mwisho kuuwawa. Na

    Allah aliijibu dua yake kwani haukupita

    muda ila Hajjaj alisumbuliwa na maradhi na

    alikua hawezi kulala kwani kila anapolala

    anaota anajiwa na Said Bin Jubeyr, hadi kifo

    kilipomkuta. Walimuota watu Hajjaaj

    wakamuuliza, nini alichokulipa Allah

    kutokana na nafsi ulizoziua? Akajibu: Kwa

    kila nafsi moja ameniua mara moja, lakini

    kwa nafsi ya Said bin Jubeyr ameniua mara

    70.

    Amekufa Said Bin Jubeyr mwezi 11

    Ramadhan mwaka wa 95 Hijria sawa na

    mwaka 714 Miladiyya na wako waliosema

    amekufa Shaaban (Wallahu Alam).

    Amekufa akiwa na umri wa miaka 59, na

    kama alivyosema Imam Ahmad amekufa na

    hakuna mtu katika ardhi isipokua alikua

    akiihitaaji elimu yake (Rahimahu Allahu).

    Allah atujaalie tuwe ni wenye kujifunza

    mazuri kutoka kwa hawa wema

    waliotangulia. Aamin.

  • 18

    Kila sifa njema zinamstahikia Allah

    (subhanahu wa taala) Muumba wa kila

    kilichomo katika ulimwengu huu. Swala na

    salamu zimuendee Mtume wetu Muhammad

    (swalla Allahu alaihi wa sallam).

    Katika ulimwengu wetu wa sasa, ulimwengu

    ambao unaitwa wa Sayansi na Teknolojia,

    kwa hakika kuna kila sababu ya kumfanya

    Muislamu alisahau lengo la kuumbwa

    kwake hapa duniani. Hatuwezi kuzuia

    mabadiliko haya yasitokee. Ila lililokuwa la

    wajibu kwetu ni kuhimizana na

    kukumbushana juu ya sharia za Allah

    (subhanahu wa taala) na vipi mja akae

    katika njia iliyosalimika. Akiwa katika njia

    hiyo kiukweli kabisa, basi Allah (subhanahu

    wa taala) atamridhia mja wake duniani na

    kesho akhera.

    Wanaiita mitandao ya kijamii, ila mimi

    nitasema mitandao inayoharibu Jamii

    ikiwemo facebook, tweeter, instagram,

    whatsapp na mengineyo. Faida imekuwa

    kwa wachache wenye kumuogopa Allah na

    khasara ni kubwa mno. Jee unajua kuwa

    mitandao hii ishasababisha ndoa za watu

    kuvunjika? Jee unajua ndoa zinakosa utulivu

    kwa sababu ya mambo haya? Jee ni yepi

    yanayofanywa kwenye mitandao ya kijamii?

    Namuomba Allah anijaalie tawfiq na iwe ni

    sababu kwa kila atakayesoma makala hii

    aweze kujirekebisha pale alipokosea na

    kumuomba msamaha Allah (subhanahu wa

    taala).

    Kushughulishwa na mitandao hii na

    kumdharau mke au mume au kusahau

    majukumu ya lazima

    Katika jambo muhimu analolihitaji mke au

    mume ni kujaliwa na mwenzake. Endapo

    ataoona mwenzake hamjali huwa hana

    furaha ndani ya ndoa yake na lazima

    itasababisha ugomvi mara kwa mara.

    Tuchukulie mfano mume ametoka tokea

    asubuhi kutafuta rizki. Anarudi usiku hana

    jambo la lazima bali anakaa kwenye

    mitandao hii na kuanza kuchat. Mwenzake

    amemsubiri kwa hamu ila yeye amekuwa na

    hamu na marafiki wake wa mitandaoni na

    kumdharau mke wake. Jee hivi ni kweli

    ndoa hii itakuwa na furaha? Kama kuna la

    lazima basi mwambie mwenzako na ufanye

    haraka kumaliza ili umpatie fursa mke wako

    nae mufurahi wote.

    Hebu tumuangalie mke nae. Mumewe

    ametoka anaanza kuchat kutwa nzima.

  • 19

    Anayozungumza na wenzake anayajua

    mwenyewe iwe ya kweli, ya uongo, ya

    kuzua au ya fitina. Ushakaribia wakati wa

    kuandaa chakula anaingia jikoni na kuripua

    kupika. Akimaliza anarudi kwenye simu

    yake. Au atasafisha nyumba yake haraka

    haraka ili awahi kurudi kwenye simu yake

    aendelee kuchat. Ewe dada wa Kiislamu jee

    hujui kuwa mume anahitaji aone

    anathaminiwa? Kwa nini usitumie muda

    wako kumpikia chakula kizuri na kitamu?

    Chakula kizuri na kitamu kitamsahaulisha

    machofu ya kazi. Kwa nini wakati wa kula

    usile nae wewe umeshika simu yako? Jee

    huoni aibu nyumba yako kutokuwa safi kwa

    sababu ya simu yako?

    Enyi wanandoa ikiwa kukesha kwenye

    mitandao ya kijamii ndio ibada kwenu hivi

    hamuwaonei huruma watoto wenu? Wakati

    wa kuzungumza nao na kucheza nao hamna

    ila wakati wa kuchat yasiyokuwa na maana

    mnao? Tujirekebisheni tabia hizi kwani

    zitaharibu ndoa zetu.

    Mazungumzo ya kimapenzi na watu

    wengine

    Tembelea inbox za facebook na whatsapp za

    wanandoa jee kweli zitasalimika na ujumbe

    wa kimapenzi? Ujumbe ambao mtu

    hajatumiwa na mke wake au mume wake.

    Tena huwa ni ujumbe wa mapenzi

    unaoashiria kuwa mke au mume ni mwenye

    kutoka nje ya ndoa yake. Mume au mke

    akiwa anazungumza na mtu husema hajaoa

    au hajaolewa lengo atimize lile analolitaka.

    Jee kweli utulivu ndani ya ndoa utapatikana?

    Inapotokea kufumwa na ujumbe huo wa

    kimapenzi kwa wanandoa, wako wengine

    hujifanya mafundi wa kusema uongo na

    wengine huishia kutoa maneno na kukosa

    jibu. Au mwanamme kujifanya yeye ndio

    bwana hatakiwi kuhojiwa. Na hata wengine

    huishia kupiga wake zao kwa sababu tu

    atamwambia amemchunguza na kumzulia.

    Hivi mke asiwe na wivu na mume wake?

    Kwa nini mtu ukose uaminifu kwa

    mwanandoa mwenzako? Kwa nini

    mutumiane ujumbe wa kimapenzi na mtu

    asiyekuwa mume wako au mke wako? Hivi

    unadhani hesabu yako hutaikuta kwa Allah?

    Tunakwenda wapi enyi umma wa Kiislamu?

    Kwa nini tunazifisidi ndoa zetu kwa kufuata

    matamanio ya nafsi zetu tu?

    Ewe uliyeoa au kuolewa acha tabia za

    kutoka nje ya ndoa yako. Acha tabia za

    kuchat mambo ya kimapenzi na asiyekuwa

    halali kwako. Umeaminiwa basi na wewe

    jiaminishe. Kwani hakika ni mnafik yule

    anayeaminiwa akavunja uaminifu. Tambua

    kuwa Allah (subhanahu wa taala) anakuona

    na tambua ya kuwa hakuna la siri kwake na

    ipo siku siri hiyo itatoka tena itakuwa ni siku

    ya majuto makubwa na fedheha. Na mwisho

  • 20

    wake kuingia katika moto. Allah atuhifadhi.

    Allah (subhanahu wa taala) anasema: Siku

    zitakapo dhihirishwa siri. [at-Twaariq (86):

    9].

    Pia napenda kutoa nasaha kwa wanandoa

    kuwa, unapokuta ujumbe ambao unaashiria

    machafu kwa mume wako au mke wako,

    basi usikimbilie kutoa maneno au kufanya

    yasiyostahiki kwani huweza kuwa ni jambo

    lililopangwa na kuzuliwa. Kwanza uliza kwa

    hekima na uwe na subra, yawezekana ni

    fitna tu imeundwa ili kukuharibieni ndoa

    yenu. Na haya yapo tayari yameshavunja

    ndoa za watu wengi. Allah (subhanahu wa

    taala) anasema Enyi mlio amini! Akikujieni

    mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni,

    msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na

    mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo

    yatenda. [al-Hujuraat (49): 6].

    Chunguza kwanza ili baadae usije kujuta

    kwa kumuingiza mwenzako kwenye makosa

    yasiyokuwa yake.

    Kusambaza picha zao wakati wakiwa

    chumbani kwenye mitandao hii

    Inawezekana ukashangaa na kujiuliza kweli

    suala hili lipo? Kwanza nielezee mtindo

    uliojitokeza siku hizi wa watu kujirikodi

    video wakati wakifanya zinaa. Au kupigana

    picha za mmoja akiwa hana nguo iwe kwa

    ridhaa au bila ya ridhaa. Na kwa masikitiko

    makubwa, wanandoa nao wameingia katika

    tabia hizi chafu.

    Achiliambali kusambaza, kwa nini ujirikodi

    video zako za ndani? Kwa nini uzisambaze

    picha zako za ndani? Munapata faida gani?

    Kubwa ni kudhalilishana na kuvuana nguo

    mbele za watu. Na lililokuwa baya zaidi ni

    kumkera Allah (subhanahu wa taala).

    Amesema Rasoul (swalla Allahu alayhi wa

    sallam) katika hadithi aliyoisimulia Said

    Khudry kwamba: Hakika katika watu

    wenye nafasi mbaya siku ya Qiyama ni

    mwanamme anaemuendea mkewe au mke

    anaeendewa na mumewe halafu akazieneza

    siri za mwenziwe. Bukhary.

    Jua ewe ndugu yagu Muislamu,

    unapojirikodi video au picha huwa unatoa

    siri zako na kuelezea ni yepi unayoyafanya

    ndani. Jua makaazi yako ni mabaya siku ya

    Qiyama ikiwa hutotubia kwa Allah

    (subhanahu wa taala) tawba ya kweli.

    Mke au mume anayesambaza video au picha

    za haramu na huku anacheka akiona

    anawafurahisha wenzake na kujisifia, jee

    amesahau kauli ya Allah (subhanahu wa

    taala) isemayo: Kwa hakika wale wanao

    penda uenee uchafu kwa walio amini,

    watapata adhabu chungu katika dunia na

    Akhera. Na Mwenyezi Mungu anajua na

    nyinyi hamjui. [an-Nnuur (24): 19].

    Jee hajiulizi akifa leo watu wataangalia

    video ile au picha ile kwa miaka mingapi na

    ni wangapi wataangalia? Jee anajua na yeye

    anapata dhambi kwani alichangia

    kusambaza uchafu? Allah (subhanahu wa

    taala) anasema: "Na hapana shaka wataibeba

  • 21

    mizigo yao na mizigo mingine pamoja na

    mizigo yao. Na kwa yakini wataulizwa Siku

    ya Qiyama juu ya waliyo kuwa wakiyazua."

    [al-Ankabut (29): 13].

    Usiri wa kuficha password ya kwenye

    mitandao na simu

    Katika hali ya kustajaabisha mke na mume

    kila mmoja simu yake ina password na

    mwenzake haijui na hataki aijue.

    Inawezekana mtu akasema kuna mambo

    mengine ya siri zaidi sitaki ajue. Leo

    nakujibu hakuna siri katika mitandao wala

    katika simu. Jee unajua kuwa kuna program

    tu zinawekwa kwenye simu na kila

    unachokipata kwenye simu yako yule

    alokuwekea anakipata? Jee mtu akiulizia

    kwa watu wa mitandao ataweza kupata

    ukweli? Jee hujui mazungumzo ya simu ya

    marais na viongozi yanavujishwa? Nakupa

    mifano kukwambia tu hakuna siri katika

    mitandao.

    Ili usimtie shaka mwanandoa mwenzako na

    ujiamini katika ndoa yako basi usiogope

    kutoa password yako. Hii itamtuliza

    mwenzako moyo wake na kuondosha shaka

    juu yako. Ila ikiwa simu ina password,

    facebook yako password, ukiingia ndani

    simu unazima, sio kwa sababu ya kutaka

    kupumzika bali kwa kukimbia fedheha. Vipi

    utaitunza ndoa yako?

    Kuweka picha zao binafsi zisizofaa katika

    mitandao

    Mwanamme nae anaamua kupiga picha

    akiwa amevaa bukta tu au yuko tumbo wazi

    anaweka katika mitandao. Jua unaleta fitna

    kwa wanawake wengine. Kutamani ni

    maumbile ya wanaadamu wote. Jua sehemu

    hizo hazidhihirishwi ila kwa mke wako tu na

    sio wengine wasiokuwa halali kwako.

    Mwanamke amepiga picha yake akiwa

    amejipamba vizuri. Anachukua picha ile na

    kuiweka katika facebook au whatsapp ili

    awaonyeshe watu wengine. Tena picha

    nyengine huonyesha ni jinsi gani

    alivyoumbwa na Allah (subhanahu wa taala)

    kwa sababu amevaa nguo yenye kubana. Jee

    unajua ewe dada wa Kiislamu kuwa uzuri

    huo hutakiwi kuudhihirisha isipokuwa kwa

    mume wako tu? Halafu unalaumu watu

    hawana adabu wanakutongoza na wewe ni

    mke wa mtu. Sasa kwa nini umeiweka? Yote

    hayo yatakukuta kwa sababu umevunja

    sheria Allah (subhanahu wa taala). Allah

    anasema: "Ewe Nabii! Waambie wake zako,

    na binti zako, na wake za Waumini

    wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu

    zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe.

    Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye

    kusamehe, Mwenye kurehemu." [al-Ahzaab

    (33): 59].

    Allah (subhanahu wa taala) ameshasema

    lengo la hijaab ni mtu asiudhiwe.

    Ukiondosha sheria hii basi jua tayari

    unakaribisha madhambi na maudhi kutoka

    kwa watu. Ama hukmu ya kuweka picha

    hiyo tayari ilishaelezwa katika toleo la

    kwanza kabisa la jarida letu hili

  • 22

    (https://www.dropbox.com/s/kc7uyruai1wn7

    91/TOLEO%20LA%20KWANZA.pdf?dl=0

    ).

    Kwa hakika mada hii ni refu na ina mifano

    mingi sana. Naomba niishie hapa na nitoe

    nasaha zifuatazo: Matamanio ya nafsi zetu

    yasituhadae hadi tukawa tayari kumuasi

    Allah (subhanahu wa taala) na kuvunja ndoa

    zetu, na tusipochunga matamanio yetu

    yatatupeleka pabaya siku ya Qiyama.

    Tumuogopeni Allah (subhanahu wa taala).

    Hebu kaa na utafakari ni muda gani

    unautupa katika mitandao hii kwa kuchat?

    Jee muda huo ungeweka maalum kwa ajili

    ya mola wako na mume wako au mke wako

    na hata watoto wako ungepata faida kiasi

    gani? Tambua unatumia neema ya wakati.

    Allah (subhanahu wa taala) atakuja

    kukuuliza juu ya neema hiyo.

    Ewe mwanandoa muogope mola wako na

    itunze ndoa yako. Usiwe tayari kuiharibu

    kwa sababu ya mitandao hii michafu. Dunia

    ni hadaa na hesabu zetu zote tutazikuta

    mbele ya Allah (subhanahu wa taala).

    Na tuikumbuke aya ya Allah (subhanahu wa

    taala) isemayo: Na iogopeni Siku ambayo

    mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha

    kila nafsi italipwa ilicho chuma. Nao

    hawatadhulumiwa. [al-Baqara (2) : 281].

  • 23

    Kila sifa njema zinamstahikia Allah

    (subhanahu wa taala), Mola wa

    walimwengu wote. Swala na salamu

    zimfikie Mtume wetu Muhammad (swalla

    Allahu alaihi wa sallam).

    Ndugu wa Kiislamu, Allah (subhanahu wa

    taala) ametuwekea sherehe maalum za Eid

    kila baada ya kumalizika kwa ibada ya

    mfungo wa Ramadhaan na ibada ya Hijjah.

    Watu wa Madina walikuwa wakisherehekea

    Eid zao, lakini Mtume (swalla Allahu alaihi

    wa sallam) aliwataka waachane nazo na

    badala yake washerehekee Eid mbili tu

    ambazo ni Eid al-Adhwha na Eid al-Fitri.

    Kama kawaida ya sherehe yoyote ile huwa

    kuna furaha na watu hujiburudisha kwa vitu

    mbali mbali ikiwemo vyakula na vinywaji.

    Ni wajibu wa kila Muislamu kujichunga

    kwanza juu ya suala zima la kutofanya israfu

    katika kusherehekea Eid hizi. Pia ni sunnah

    kufanya yafuatayo katika siku ya Eid ili

    kuzidi kupata faida ya ibada tulizozifanya

    ima katika mfungo wa Ramadhaan au

    Hijjah.

    Kukoga kabla ya kwenda kuswali swala ya

    Eid

    Ni mustahab (inapendeza) kukoga kabla ya

    kwenda kuswali swala ya Eid na kujitia

    manukato mazuri kwa wanaume, kwani hivi

    ndivyo walivyokuwa wakifanya watu wema

    waliotangulia. Imesimuliwa hadithi sahihi

    katika Al-Muwatta na kwengineko kuwa

    Abd-Allah ibn Omar alikuwa akikoga

    asubuhi ya Fitri kabla ya kwenda sehemu ya

    kuswali.

    Kula kabla ya kwenda kuswali katika Eid

    al-Fitri na baada ya kuswali katika Eid al-

    Adhwha

    Ni katika sunnah kula tende kwa idadi ya

    witri kabla ya kwenda kuswali Eid al-Fitri

    au chochote kile cha halali ikiwa

    itakosekana tende, kwani huo ndio ulikuwa

    utaratibu wa Mtume wetu (swalla Allahu

    alaihi wa sallam) kama ilivyoripotiwa na

    Imam Bukhari kutoka kwa Anass ibn Malik

    ambae amesema kuwa Mtume wa Allah

    (swalla Allahu alaihi wa sallam) alikuwa

    hatoki asubuhi kwenda kuswali Eid al-Fitri

    mpaka ale tende ... ambazo alizila kwa idadi

    ya witri.

    Ama katika Eid al-Adhwha ni vyema mtu

    kutokula mpaka baada ya kuswali, ili aje ale

    katika kichinjo alichokichinja kwa ajili ya

  • 24

    Allah, lakini kwa asiyechinja hakuna ubaya

    kwake kula kabla ya kwenda kuswali.

    Kuleta takbira

    Hii ni katika sunnah kubwa za siku ya Eid

    kwani Allah (subhanahu wa taala) anasema:

    ... Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo

    mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na

    mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze

    Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni

    ili mpate kushukuru. [al-Baqara (2): 185].

    Takbira huanza kutolewa pale tu mtu

    anapotoka nyumbani kwake kuelekea

    sehemu ya kuswalia. Na ni sunnah kwa

    wanaume kuileta kwa sauti kubwa na kwa

    wanawake kwa sauti ndogo isiyosikika.

    Imesimuliwa kwamba al-Walid ibn Muslim

    alisema: Nilimuuliza al-Awzaai na Malik

    ibn Anas kuhusiana na kuleta takbira kwa

    sauti kubwa katika Eid mbili. Wakasema;

    Ndio, Abd-Allah ibn Omar alikuwa

    akiisema kwa sauti kubwa katika Eid al-Fitri

    mpaka anapokuja Imam (kuswalisha).

    Katika Eid al-Fitri takbira huanza baada ya

    kuonekanwa mwezi muandamo na humaliza

    baada kumalizika kwa swala ya Eid, ama

    katika Eid al-Adhwha takbira huanza mwezi

    tisa Dhulhijjah mpaka laasiri ya siku ya

    mwisho ya Tashriq.

    Na maneno ya takbira ni:

    , , ,

    .

    Kama ilivyosimuliwa katika Musannaf wa

    Ibn Abi Shaibah kwa sanadi sahihi kutoka

    kwa Ibn Masoud (radhi za Allah ziwe juu

    yake) kwamba alikuwa akisoma takbira

    katika siku za Tashriq: Allaahu akbar,

    Allaahu akbar, laa ilaaha ill-Allaah, wa

    Allaahu akbar, Allaah akbar, wa Lillaah il-

    hamd (Allaah ni Mkubwa, Allaah ni

    Mkubwa, Hapana Mola anayepasa

    kuabudiwa kwa Haki Ila Allaah, Allaah ni

    Mkubwa, Allaah ni Mkubwa Na Shukrani

    Zote ni za Allaah).

    Imesimuliwa pia na Abi Shaibah katika

    sehemu nyengine kwa sanad sawa ila tamko

    la Allaahu akbar limejirejea mara tatu

    (badala ya mara mbili).

    Ama ile takbira refu tuliyoizoea wengi:

    , , , ,

    ,

    , ,

    , ,

    ,

  • 25

    Kwa vile haijathibiti namna maalum

    aliyoifundisha Mtume (swalla Allahu alaihi

    wa sallam), ni rai yetu kuwa hakuna tatizo

    kuisoma takbira hii, na Allah Anajua zaidi.

    Kupongezana

    Pia ni katika sunnah kupongezana katika

    siku za Eid kwa kusema Taqabbala Allaah

    minna wa minkum (Allah azikubali (amali

    nzuri) kutoka kwetu na kwako) au Eid

    mubaarak au kwa namna nyenginezo

    zinazokubalika.

    Imesimuliwa kwamba Jubayr ibn Nufayr

    amesema: Wakati maswahaba wa Mtume

    (swalla Allahu alaihi wa sallam)

    wanapokutana katika siku ya Eid, walikuwa

    wakisema kuambiana, Allah azikubali

    (amali nzuri) kutoka kwetu na kwako.

    Amesema Ibn Hajar sanad yake ni hasan.

    Kuvaa mavazi mazuri

    Ni sunnah kuvaa mavazi mazuri na

    kujipamba kwa wanaume wanapokwenda

    kuswali Eid. Ama kwa wanawake

    watakaokwenda kuswali Eid hawatakiwi

    kujipamba wala kujitia mafuta mazuri kwani

    hawatakiwi kuyafanya hayo kwa wasiokuwa

    maharimu wao. Imesimuliwa na Jabir (radhi

    za Allah ziwe juu yake) kwamba: Mtume

    (swalla Allahu alaihi wa sallam) alikuwa na

    jubba ambalo alilivaa katika Eid mbili na

    siku ya Ijumaa. Sahih Ibn Khuzayma.

    Pia Abd-Allaah bin Omar (radhi za Allah

    ziwe juu yake) amesema: Omar alichagua

    jubbah (nguo refu inayovaliwa juu ya kanzu)

    ambayo ilitengenezwa kwa hariri na ilikuwa

    ikiuzwa kwa bei ya takhfifu sokoni, aliileta

    kwa Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa

    aalihi wa sallam) na akasema: "Ewe Mtume

    nunua hii na uvae kwa ajili ya Eid na

    watakapokuja wageni" Mtume (Swalla

    Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam)

    akasema: "Hizi ni nguo za yule ambaye hana

    sehemu akhera. Al-Bukhaariy.

    Hadithi hii inaonyesha kuwa, katika kuvaa

    vizuri huko ni lazima pia kuchunga mipaka

    ya mavazi, yaani wanaume wasivae mavazi

    ya kike na wanawake wasivae mavazi ya

    kiume wala kusivaliwe mavazi ambayo

    yanayoshabihiana na ya makafiri. Na kwa

    vile wanaume wamekatazwa kuvaa hariri

    ndio maana Mtume (swalla Allahu alaihi wa

    sallam) akalikataa vazi lile aliloletewa.

    Kuswali swala ya Eid

    Swala ya Eid ni katika sunnah muakkadah

    (zilizokokotezwa), hivyo ni wajibu wa kila

    Muislamu kuihuwisha sunnah hii na sio

    kukimbilia kwenye kula tu asubuhi ya siku

    ya Eid.

  • 26

    Na ni juu ya kila Muislamu kuhakikisha

    kuwa ameshatoa zakatul Fitri kabla ya

    kwenda kuswali Eid kwani anayetoa baada

    ya swala huwa ametoa sadaka tu na sio

    zakatul Fitri tena.

    Kubadilisha njia ya sehemu ya kuswalia

    Ni sunnah vile vile kuenda kwenye sehemu

    ya kuswalia Eid kwa njia moja na kurudi

    kwa kutumia njia nyengine. Jaabir bin Abd-

    Allaah (radhi za Allah ziwe juu yake)

    ameripoti kuwa: Mtume (Swalla Allaahu

    alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa

    akibadilisha njia siku ya Eid. al-Bukhari.

    Ndugu wa Kiislamu hayo ni katika ya

    sunnah tunayotakiwa kujihimu kuyafanya

    katika siku ya Eid. Lakini kwa vile katika

    jamii zetu kuna mambo mengi ambayo

    hufanyika katika siku za sherehe hizi, ni

    vyema kuwanasihi ndugu zetu khasa wazee

    na walezi wa familia kuwa, wazingatie sana

    nyenendo za vijana wao, kwani wengi katika

    vijana huzigeuza sherehe hizi kuwa ni siku

    walizoachiwa huru kufanya kila aina ya

    maasi wayatakayo.

    Pia ni vyema Waislamu wote tukajichunga

    na kutofanya yafuatayo, ili kutoharibu ibada

    yetu ya mwezi mzima wa Ramadhaan.

    Kuzuru makaburi

    Kuzuru makaburi katika siku ya Eid ni

    kitendo kinachokwenda kinyume na lengo

    zima la kusherehekea Eid, kwani siku ya Eid

    ni siku ya furaha, kutembeleana,

    kupongezana na kupeana zawadi. Kuzuru

    makaburi kutaibadilisha furaha hii na

    kuifanya kuwa huzuni na huu si katika

    utaratibu wa Mtume wetu Muhammad

    (swalla Allahu alaihi wa sallam).

    Kuacha swala za jamaa

    Wengi wetu katika kutekeleza sunnah ya

    kutembeleana hujisahau na kuwacha wajibu,

    kwani hufikia baadhi ya watu kukosa nafasi

    ya kwenda kuswali jamaa na wengine

    hufikia hata kuacha kuswali katika siku ya

    Eid. Hili si jambo zuri hata kidogo kwani

    swala ni nguzo ya Dini na lengo la funga ni

    kutufanya kuwa wachaMungu. Sasa

    tutalifikiaje lengo hili ikiwa tutaiacha swala

    siku ya kwanza mara tu baada ya kuisha

    Ramadhaan? Mtume (swallah Allahu alaihi

    wa sallam) amesema: Tofauti iliyopo baina

    yetu na wao (makafiri) ni swala, mwenye

    kuiacha basi amekufuru. Tirmidhy na An-

    Nasai.

    Kuchanginyika wanawake na wanaume

    sehemu moja

  • 27

    Hili tunalishuhudia sana katika viwanja vya

    Eid, na watu huliona kama ni jambo la

    kawaida, matokeo yake huamsha hisia

    mbaya kwa vijana wabaya na kupelekea

    kuwabaka wasichana wadogo,

    kuwanyanganya vitu vyao vya dhahabu na

    hata kuwavunjia heshima wazee wa kike.

    Pia michanganyiko hii huzaa fitna nyingi na

    huengeza vishawishi vya kufanyika zinaa.

    Hivyo ni bora kuliepuka hili na

    alhamdulillah baadhi ya misikiti

    wameanzisha viwanja vyao vya

    kusherehekea Eid katika mazingira ya

    Kiislamu, kwa hivyo tunawashauri wazazi

    na walezi kuwapeleka watoto wao katika

    viwanja vyenye kuendeshwa kwa maadili ya

    Dini yetu tukufu.

    Kutoka pasi na kutimiza hijab kwa

    wanawake

    Imekuwa ni kawaida ya wanawake wengi

    kuhisi kuwa siku ya Eid ni siku ambayo

    wameruhusiwa kutoka bila ya kuchunga

    sheria ya hijab. Hili ni kosa na haifai kwa

    mwanamke yeyote yule kutoka nje ya

    nyumba yake hali ya kudhihirisha mapambo

    yake kwa wasiokuwa maharim wake. Allah

    anasema: Na waambie Waumini wanawake

    wainamishe macho yao, na wazilinde tupu

    zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa

    unao dhihirika. Na waangushe shungi zao

    juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri

    wao ila kwa waume zao, au baba zao ...

    [an-Nur (24): 31].

    Pia katika kutilia mkazo namna ya uvaaji wa

    shungi, ni kama tunavyoona katika aya kuwa

    shungi inatakiwa ishuke hadi chini ya kifua

    na sio kujizonga kichwa tu na kifua chote

    kikawa wazi (style ya kiandazi) kama

    wafanyavyo wengi katika dada zetu siku

    hizi.

    Hivyo ni juu ya waume na wazee kwa

    ujumla kuwachunga na kuwasimamia wake

    na mabinti zao, kwani hilo ni jukumu lao

    kama Allah anavyosema: Wanaume ni

    wasimamizi wa wanawake ... [an-Nisaa (4):

    34].

    Kusikiliza na kupiga miziki pamoja na

    kuenda madisko

    Ni uwazi usio na shaka yoyote ile kuwa

    miziki na madisko ni jambo lilio haramu

    katika Dini yetu. Kuiaga Ramadhaan kwa

    mambo kama haya itathibitisha kuwa

    mfanyaji hakuwa akifunga kwa ajili ya

    Allah na kulipata lengo la kufunga ambalo

    ni uchaMungu. Pia tunashuhudia kuwa

    wengi hudhurika kwa kuenda kwenye

    madisko, kwani baadhi yao huibiwa vitu

    vyao na wasichana wengine hufikia mpaka

    kubakwa kutokana na shari ipatikanayo

    humo. Ni vyema kwa ndugu zetu wa

    Kiislamu kujiepusha na mambo kama haya

    ili kupata radhi za Allah (subhanahu wa

    taala).

    Kucheza kamari na mambo mengine ya

    bahati nasibu

  • 28

    Kamari na vyenye kufanana nayo ni haramu

    katika Uislamu kwa kauli ya Allah

    (subhanahu wa taala) isemayo: Enyi mlio

    amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na

    kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni

    uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi

    jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa. [al-

    Maida (5): 90].

    Michezo ya kamari hushamiri sana katika

    viwanja vya Eid, ni jukumu la kila

    Muislamu kumkataza na kumnasihi

    mwenziwe kujiepusha na mambo kama hayo

    ili kuepukana na adhabu za Allah

    (subhanahu wa taala) kwani hakuna

    anayeweza kustahamili adhabu hizo.

    Ndugu wa Kiislamu, yafaa kujiuliza jee

    tumejifunza nini katika mwezi wa

    Ramadhaan? Jee kuisha kwa Ramadhaan

    ndio kuachwa wazi kwa mlango wa kufanya

    maasi? Jee kuisha kwa Ramadhaan ndio

    turudie katika maasi tuliyokuwa

    tukiyafanya?

    Bila ya shaka jawabu ni hapana, hivyo ni

    vyema tukajihimu kuyaendeleza yale yote ya

    kheri tuliyokuwa tukiyafanya katika mwezi

    wa Ramadhaan kama kusimama usiku kwa

    swala na ibada nyengi, kuwa wakarimu kwa

    majirani na ndungu zetu, kuwa na huruma

    na kuwasaidia mayatima, wajane, wagonjwa

    na masikini. Pia kujihimu katika kuendelea

    kuswali jamaa misikitini, kwani ni jambo

    lenye kusikitisha kuona kuwa Ramadhaan

    inapoisha, misikiti hupwaya kutokana na

    vijana wengi kutoendeleza kuswali jamaa.

    Tunamuomba Allah Mtukufu azikubali

    funga zetu na amali zetu nyengine

    tulizozifanya katika mwezi mzima wa

    Ramadhaan na atuwafiqishe kuziendeleza

    katika miezi mingine na atuwezeshe kuingia

    katika Pepo yake katika mlango wa Rayaan.

    Amin.

  • 29

    Twakuomba Mtukufu - Aso kijana na kufu

    Mola wetu maarufu - Allahu ulo Karima

    Mikono tumeinuwa - Mola wetu watujuwa

    Taqabali zetu dua - Utupe lilo na wema

    Mola machozi yatoka - Hakika yabugujika

    Tumetubu kwa hakika - Waja wako tumekoma

    Ya Rabbi tupe elimu - Utupe njema fahamu

    Ya kutambua vigumu - Vya Dini yako Karima

    Utupe matunda yake - Tuisome tusichoke

    Mola elimu iweke - Moyoni mahala pema

    Rabbi ijapo hukumu - Isiwe kwetu ni ngumu

    Tusiweze kudhulumu - Tukuche wewe Karima

    Utupe na kupendana - Sisi na wetu vijana

    Mapenzi yaso khiana - Yalo mazuri daima

    Tutuze mijini mwetu - Tuqidhie deni zetu

    Kabla ya kuja kwetu - Mjumbe wa mauti mwema

    Kila ajae na shari - Waijua yake siri

    Ivunde yake dhamiri - Asiweze kusimama

    Rabbi sala na salamu - Zimfikie Hashimu

    Na swahabaze kiramu - Na aali na kila mwema

    Amina Rabbi amina - Amina Rabbi amina

    Amina Rabbi amina - Ya Rabbi watusikia