12
Toleo Namba 20 Agosti 2011 Na Odhiambo Orlale W anawake wana kila sababu ya kusherehekea maadhimisho ya mwaka wa kwanza tangu kuzinduliwa rasmi kwa katiba. Milango ambayo hapo awali ilikuwa imeshika kutu nzito isiweze kufunguka imeanza kutiwa mafuta ya kuilegeza na kufunguka, yote hayo sababu yake ikiwa ni mafuta yanayojulikana kama sheria hii mpya. Mnamo siku ya kuanzishwa rasmi kwa katiba, Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mwai Kibaki, aliitia saini katiba hiyo na akawaahidi Wakenya kwamba aitailinda na kuitetea she- ria hiyo mpya. Kunako siku hii kadhalika Wakenya wa- liwashuhudia Waziri Mkuu Raila Odinga na Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka wakiahidi kuwatumikia Wakenya chini ya katiba hii mpya na kadhalika kuilinda. Watunga sheria ambao ni Wabunge pia walikula viapo vya kuitetea kat- iba huku mawaziri na majaji pia wakiapa kuit- etea katiba hiyo mpya. Hiyo ikiwa na maana ya kuheshimu kila neno lililomo ndani ya katiba hiyo yakiwemo mafanikio ambayo yanapende- lea haki za wanawake na kupewa uwezo mion- goni mwao, kupewa nafasi zaidi katika ulingo wa siasa na katika ngazi za utoaji maamuzi. Hata hivyo, uamzi wa hivi majuzi wa Bara- za la Mawaziri la kutangaza kanuni ya thuluthi moja katika katiba kuwa isiyoweza kutekelezwa ni uzandiki wazi wa ubaguzi wa kijinsia na ku- tumiwa vibaya kwa manufaa ya wanawake ka- tika sheria hiyo mpya. Hata ingawa baraza hilo la mawaziri lilipendekeza kuundwa kwa jopo kazi la ku- chunguza kanuni hiyo ambayo imezusha mgogoro, na kuwasilisha matokeo ya uchun- guzi wake kwao, wanawake wana hofu kwamba kama katika hatua hizo za awali za utekelezaji wa katiba unazusha mgogoro, haitachukua muda mrefu tena kabla ya mafanikio ya wan- awake kuondolewa kabisa. Matarajio mema Hata hivyo, Wakenya na wanawake kwa ujumla wanasubiri roho mkononi huku wa- nawake wakitazamia kwamba mzozo huo utasuluhishwa haraka iwezekanavyo na kwa manufaa yao. Tangu kuanza kutumiwa kwa katiba mpya, wanawake wamefanikiwa kupata kazi za mam- laka makubwa kwenye utekelezaji wa katiba mpya. Kwa mfano Nancy Baraza alipitia moja ya taratibu ngumu za mahojiano ya hadhara ya uteuzi wa Naibu wa Jaji Mkuu, kabla ya kuteu- liwa kwenye mamlaka hayo ili kufanyia maten- genezo idara hiyo ya mahakama. Ama kwa kweli manufaa ambayo wan- awake wamepata kuanzia wakati wa Tume ya Marekebisho ya Katiba ambayo ilijulikana kwa jina maarufu la Bomas miaka mitano ili- yopita na kushirikishwa kwenye katiba mpya, yanatekelezwa kikamilifu kwa dhati ya moyo wa katiba hiyo. Uteuzi wa aliyekuwa Mbunge Maalumu Njoki Ndung’u kama mmoja wa majaji saba wa mahakama kuu ni moja ya mafanikio ya wan- awake ingawa bado kuna kesi inayopinga urari wa kijinsia katika idadi ya majaji wa mahakama hiyo kuu. Kulingana na wengi wa viongozi wanawake, tatizo kubwa hapa ni kwamba hawako tayari kuwaruhusu viongozi wa kisiasa kuitekeleza katiba kuanza na utekelezaji usiofaa huku kuki- wa na udhaifu mkubwa katika kushughulikia maswala ya kijinsia. Jaji Mkuu, Dkt Willy Mutunga alianzisha utangulizi bora wakati alipowaambia wanasiasa kwamba wanahitajika kusikiliza kwa makini na kuelewa kwamba Kenya ina wanawake ambao wana elimu na wenye uwezo wa kufikisha idadi ya thuluthi moja ambayo katiba inapendekeza izingatiwe, wakati alipowateua wa- nawake kumi na watatu kati ya watu ishirini na wanane kuchukua nyadhi- fa za mahakimu wa mahakama kuu ambao wameteuliwa hivi punde. Lydia Achode ambaye ni msajili mkuu wa mahakama anayeondoka ni miongoni mwa majaji walioteu- liwa pamoja na Pauline Nyamweya. Wengine ni Mumbi Ngugi, Beatrice Mwaka mmoja baadaye Picha ya juu aliyekuwa Mkuu wa Sheria, Bw Amos Wako (mwenye wigi kichwani) akishuhudia Rais Mwai Kibaki akitia sahihi stakabadhi kuidhinisha rasmi katiba mpya mnamo Agosti 27, mwaka jana. Kulia, Rais Kibaki akionyesha kwa hadhara stakabadhi hiyo ya kuidhinishwa katiba mpya. Sherehe hii ilifanywa katika bustani ya Uhuru Park, Nairobi. Kutazama utekelezaji wa sheria kwa darubini ya jinsia Angalia Uk.2

Mwanamke Mkenya Toleo 20

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Mwanamke Mkenya ni toleo la African Woman and Child Feature Service. Jarida hili limechapishwa kutokana na usaidizi wa Hazina la Kidemokrasia la Umoja wa Mataifa (UNDEF)

Citation preview

Page 1: Mwanamke Mkenya Toleo 20

1 Toleo Namba 20 • Agosti 2011 Toleo Namba 20 • Agosti 2011

Na Odhiambo Orlale…

Wanawake wana kila sababu ya kusherehekea maadhimisho ya mwaka wa kwanza tangu kuzinduliwa rasmi kwa katiba.

Milango ambayo hapo awali ilikuwa imeshika kutu nzito isiweze kufunguka imeanza kutiwa mafuta ya kuilegeza na kufunguka, yote hayo sababu yake ikiwa ni mafuta yanayojulikana kama sheria hii mpya.

Mnamo siku ya kuanzishwa rasmi kwa katiba, Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mwai Kibaki, aliitia saini katiba hiyo na akawaahidi Wakenya kwamba aitailinda na kuitetea she-ria hiyo mpya.

Kunako siku hii kadhalika Wakenya wa-liwashuhudia Waziri Mkuu Raila Odinga na Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka wakiahidi kuwatumikia Wakenya chini ya katiba hii mpya na kadhalika kuilinda. Watunga sheria ambao ni Wabunge pia walikula viapo vya kuitetea kat-iba huku mawaziri na majaji pia wakiapa kuit-etea katiba hiyo mpya. Hiyo ikiwa na maana ya kuheshimu kila neno lililomo ndani ya katiba hiyo yakiwemo mafanikio ambayo yanapende-lea haki za wanawake na kupewa uwezo mion-goni mwao, kupewa nafasi zaidi katika ulingo wa siasa na katika ngazi za utoaji maamuzi.

Hata hivyo, uamzi wa hivi majuzi wa Bara-za la Mawaziri la kutangaza kanuni ya thuluthi moja katika katiba kuwa isiyoweza kutekelezwa ni uzandiki wazi wa ubaguzi wa kijinsia na ku-tumiwa vibaya kwa manufaa ya wanawake ka-tika sheria hiyo mpya.

Hata ingawa baraza hilo la mawaziri lilipendekeza kuundwa kwa jopo kazi la ku-chunguza kanuni hiyo ambayo imezusha mgogoro, na kuwasilisha matokeo ya uchun-guzi wake kwao, wanawake wana hofu kwamba kama katika hatua hizo za awali za utekelezaji wa katiba unazusha mgogoro, haitachukua muda mrefu tena kabla ya mafanikio ya wan-awake kuondolewa kabisa.

Matarajio memaHata hivyo, Wakenya na wanawake kwa

ujumla wanasubiri roho mkononi huku wa-nawake wakitazamia kwamba mzozo huo utasuluhishwa haraka iwezekanavyo na kwa manufaa yao.

Tangu kuanza kutumiwa kwa katiba mpya, wanawake wamefanikiwa kupata kazi za mam-laka makubwa kwenye utekelezaji wa katiba mpya. Kwa mfano Nancy Baraza alipitia moja ya taratibu ngumu za mahojiano ya hadhara ya uteuzi wa Naibu wa Jaji Mkuu, kabla ya kuteu-liwa kwenye mamlaka hayo ili kufanyia maten-genezo idara hiyo ya mahakama.

Ama kwa kweli manufaa ambayo wan-awake wamepata kuanzia wakati wa Tume ya Marekebisho ya Katiba ambayo ilijulikana kwa jina maarufu la Bomas miaka mitano ili-yopita na kushirikishwa kwenye katiba mpya, yanatekelezwa kikamilifu kwa dhati ya moyo wa katiba hiyo.

Uteuzi wa aliyekuwa Mbunge Maalumu Njoki Ndung’u kama mmoja wa majaji saba wa mahakama kuu ni moja ya mafanikio ya wan-awake ingawa bado kuna kesi inayopinga urari wa kijinsia katika idadi ya majaji wa mahakama hiyo kuu.

Kulingana na wengi wa viongozi wanawake, tatizo kubwa hapa ni kwamba hawako tayari

kuwaruhusu viongozi wa kisiasa kuitekeleza katiba kuanza na utekelezaji usiofaa huku kuki-wa na udhaifu mkubwa katika kushughulikia maswala ya kijinsia.

Jaji Mkuu, Dkt Willy Mutunga alianzisha utangulizi bora wakati alipowaambia wanasiasa kwamba wanahitajika kusikiliza kwa makini na kuelewa kwamba Kenya ina wanawake ambao wana elimu na wenye uwezo wa kufikisha idadi ya thuluthi moja ambayo katiba inapendekeza

izingatiwe, wakati alipowateua wa-nawake kumi na watatu kati ya watu ishirini na wanane kuchukua nyadhi-fa za mahakimu wa mahakama kuu ambao wameteuliwa hivi punde.

Lydia Achode ambaye ni msajili mkuu wa mahakama anayeondoka ni miongoni mwa majaji walioteu-liwa pamoja na Pauline Nyamweya. Wengine ni Mumbi Ngugi, Beatrice

Mwaka mmoja baadaye

Picha ya juu aliyekuwa Mkuu wa Sheria, Bw Amos Wako (mwenye wigi kichwani) akishuhudia Rais Mwai Kibaki akitia sahihi stakabadhi kuidhinisha rasmi katiba mpya mnamo Agosti 27, mwaka jana. Kulia, Rais Kibaki akionyesha kwa hadhara

stakabadhi hiyo ya kuidhinishwa katiba mpya. Sherehe hii ilifanywa katika bustani ya Uhuru Park, Nairobi.

Kutazama utekelezaji wa sheria kwa darubini ya jinsia

Angalia Uk.2

Page 2: Mwanamke Mkenya Toleo 20

2 Toleo Namba 20 • Agosti 2011

Pendekezo la Baraza la Mawaziri juu ya haja ya kutafuta njia ya kushughulikia kifungu cha 81(b) cha katiba ambacho kinasema kwamba uteuzi wa maafisa

wa kuhudumu katika nyadhifa za umma usizidi thuluthi mbili ya jinsia moja, limezusha wasiwa-si mkubwa sio tu kwa wanawake wa Kenya bali pia kwa wananchi ambao walipiga kura kuiunga mkono katiba hiyo mpya.

Kulingana na wengi wa Wakenya, hatua hiyo inaenda kinyume na misingi iliyowafanya Wak-enya kupigania katiba mpya kwa miongo miwili. Kama alivyosema mkurugenzi mkuu wa baraza la kitaifa la kupigania mageuzi, NCEC, Cyprian Nyamwamu, kwenye mkutano ulioandaliwa na wanawake kutafuta njia ya kupata kutekelezwa kwa ahadi ya kifungu hicho alifafanua kwa usta-di mkubwa.

UshirikishajiAlisema kwamba harakati za kupigania

katiba mpya zilihusu mambo matatu. “Harakati hizo zilinuiwa kupambana na urundikaji wa mamlaka katika sehemu moja na utumiaji mbaya wa mamlaka, hivyo basi kukapatikana ugavi wa mamlaka na kugawanywa kwa kazi na kuleta uwajibikaji, kukabiliana na utovu wa haki za kijinsia na kutoshirikishwa kwa makundi ya watu wanaogandamizwa na makundi ya watu wachache ambapo wanawake ni baadhi yao na kadhalika na kuratibiwa kwa haki na mipango ya utawala katika misingi ya Mswada wa Haki,” akasema Nyamwamu, huku akiongeza kwamba “hili si swala la wanawake, bali ni swala linalowa-husu Wakenya wote kwa jumla.”

Dkt Linda Musumba naye anathibitisha kwamba suluhisho la swala la thuluthi mbili linapaswa kutafutwa kwa ushirikiano wa ser-ikali na vyama vya siasa kwa kuwa vitakuwa muhimu katika kuhakikisha kwamba wanawake wanafanya idadi ya thuluthi moja ya wale wat-akaochaguliwa.

Mkurugenzi wa kongamano la wanawake viongozi wa kisiasa, Dkt Deborah Okumu ali-sisitiza kwamba suluhisho la kupatikana kwa kiwango cha thuluthi mbili halihitaji marekebi-sho ya kikatiba, bali linaweza kupatikana kupitia mswada wa uchaguzi na vyama vya siasa am-

bayo miswada hiyo iko mbele ya Bunge“Tangu kongamano za Tume ya Uchunguzi

wa Marekebisho ya Katiba ya Kenya (KCRC) hadi kwenye mkutano wa katiba wa Bomas, mkutano wa Naivasha, utaratibu wa kikatiba wa Kilifi na mwishowe Kamati ya Wataalamu, kila mtu na hasa mawakili walikuwepo na tu-kaambiwa kwamba katiba ni utaratibu wa kish-eria ambao haushirikishi mambo kwa urefu na kwamba mambo hayo yenye kueleza kwa urefu yamefanyiwa ukusuru ndani ya sheria hiyo. Kuanzia hapo wanawake wa Kenya wamesonga mbele kuweka mikakati katika miswada hiyo miwili, lakini imekataliwa,” aeleza Okumu.

Kulingana na Okumu, ni jambo la kusikit-isha kwamba wanaume wanafafanua swala hilo kumaanisha kwamba wanawake wanataka viti vya bure. “Tunahitaji kujifunza kutokana na historia kwamba kufikia kiwango cha asilimia 30 ya wanawake kwenye viti vya kiuchaguzi nchini Kenya limekuwa jambo gumu na tangu uhuru kupatikana hakujakuwa na nia njema kwa upande wa vyama vya siasa kuhusiana na uwakilishi wa wanawake,” akasisitiza.

Okumu anaongeza kwamba harakati za upiganaji maslahi ya wanawake ni za kiubaguzi kwa jinsia nyingine ili iweze kuleta ubaguzi am-bao utasababisha usawa wa kijinsia kwenye nya-dhifa za kiuchaguzi.

Huku Wakenya wakijadiliana kuhusu miun-

do mbinu ambayo itatumiwa kufanikisha hitaji la thuluthi mbili ambalo halishirikishi ufafanuzi zaidi wa kina, huko kusini mwa Afrika, viongozi wote wa nchi walitia saini maazimio ya jinsia na maendeleo ambayo yanatilia mkazo hitaji la uwakilishi wa asilimia hamsini wa wanawake katika ngazi zote za serikali kufikia mwaka 2015 na zaidi ya hayo, maazimio hayo yanayataka mataifa wanachama kutunga sheria ambazo zi-natoa hakikisho kwamba miundo ya kisiasa na ya kimaongozi inazingatia usawa wa kijinsia.

Maazimio hayo yanatayarisha mipango ya utekelezaji ambayo inaweka shabaha maalumu na wakati wa kutekelezea mipango hiyo ya ku-fanikisha usawa wa kijinsia katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya SADC pamoja na mipango stadi ya uchunguzi na ukaguzi wa mi-pango hiyo.

BeijingKatiba hiyo mpya ilichukuliwa na makundi

ya wachache miongoni mwa Wakenya kuwa chombo cha dhati cha kuimarisha ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi kuanzia ka-tika kaunti hadi katika ngazi za kitaifa. Hayo ya-naambatana na uamuzi wa kuimarisha maslahi ya wanawake katika ngazi za utoaji maamuzi kote ulimwenguni harakati ambazo zilianza ku-shika kasi mnamo miaka ya 1980 na mapema miaka ya 1990 kupitia msururu wa mikutano ya

kimataifa.Harakati hizo ziliongezewa nguvu na mku-

tano wa nne wa kimataifa uliofanywa mjini Bei-jing huko China mnamo mwaka 1995 ambao ulitoa mwito wa kuzingatiwa kwa aslimia 30 ya uwakilishi wa wanawake katika ngazi za kitaifa katika serikali za ulimwengu. Mnamo mwezi Septemba mwaka 2000 kwenye mkutano wa milenia wa Umoja wa Mataifa mjini New York, viongozi wa ulimwengu waliahidi “kuimarisha usawa wa kijinsia na wanawake kupewa uwezo kama njia mwafaka za kupambana na umaski-ni, njaa na magonjwa na kusisimua maendeleo yanayoweza kudumishwa.”

Hivyo basi, ili Kenya ichukue nafasi ya kwanza miongoni mwa nchi za Afrika, wana-siasa wanapaswa kuwajibika katika swala la ka-nuni ya thuluthi mbili na kama ilivyosemwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt Kofi Annan.”

Chunguzi baada ya chunguzi zilizofanywa zinaonyesha kwamba hakuna mbinu yoyote ya maendeleo ambayo wanawake hawatekelezi ma-jukumu makubwa na wakati ambapo wanawake hushirikishwa kikamilifu katika utekelezaji wake manufaa huonekana kwa haraka. Jamii huwa na afya bora zaidi na kulishwa vyema na mapato yao na akiba zao na uwekaji raslimali huimarika.

Dkt Annan aliongeza kwamba; “Na kilicho ni cha ukweli kwa familia ni cha ukweli kwa ja-mii nzima na hatimaye kwa nchi nzima.”

Rwanda ni mfano ambao unatumiwa katika kuonyesha athari njema za wanawake katika uongozi kwenye hatua katika masuala ya hali ya mwanamke na maendeleo kwa jumla.

Akinukuliwa katika taarifa kuhusu wan-awake, Oda Gasinzigwa ambaye ni Waziri wa Jinsia wa Rwanda anasema; “Ni vyema kutut-ambua kwamba kuna mafanikio mengi ambayo tumeyapata na utendaji stadi wa kazi unatokana na nia njema ya kisiasa.Uongozi umetuamini kushiriki katika kila ngazi ya sekta zote za ki-maendeleo.”

Ni kutokana na sababu hizo ndipo majadil-iano kuhusu kanuni ya thuluthi mbili inahitaji nia njema ya kisiasa ambayo ni serikalio pekee ndiyo inayoweza kuhakikisha.

Serikali lazima idhihirishe nia njema ya kisiasa

Thuranira, Grace Nzioka, Christine Meoli, Hedwig Ongudi, Stella Mu-tuku, Rose Ougo, Roseline Korir, Abigail Mshila na Stella Muketi.

Katiba mpya ilianzisha wadhifa mpya wa msajili mkuu kusimamia shughuli zote za mahakama na wa-dhifa huo umechukuliwa na Gladys Shollei ambaye ni msajili wa idara ya mahakama, kuchukua mahali pa Lydia Achode.

Jaji Mkuu anasema Bi Shollei aliteuliwa baada ya utaratibu thabiti wa mahojiano ya kazi ambao uliku-wa wa haki na uwazi. Kabla ya ku-teuliwa katika wadhifa huo, Gladys alihudumu kama naibu wa afisa mkuu wa usi-mamizi wa uchaguzi katika tume huru ya muda ya usimamizi wa uchaguzi (IIECC).

Umuhimu wa uteuzi huo wa mahakimu kinyume na uteuzi wa majaji wa mahakama kuu ni kwamba ulitimiza kanuni na kupitisha kiwango cha thuluthi moja ya jinsia moja kama inavyosisitiza katiba. Kanuni ya kutokuwa na zaidi ya thuluthi moja ni swala ambalo bado linazozaniwa mahakamani kuhusiana na uteuzi wa majaji wa mahakama kuu.

Kuhusiana na uteuzi wa majaji, Dkt Mu-tunga alisema: “Tumewatafuta wagombezi wa nyadhifa hizo kutoka sehemu mbali mbali kama ilivyoagiza katiba na sheria ikiwa ni pamoja na maswala ya kijinsia, asili, kaunti, vizazi watu wa makabila madogo na aina nyingine za ugan-damizaji. Huku tunapoadhimisha mwaka wa kwanza tangu kuzinduliwa rasmi kwa katiba mpya, utekelezaji wa katiba kama unavyoon-gozwa na Tume ya Usimamizi wa Utekelezaji wa Katiba umepiga hatua kubwa za manufaa, lakini bado kuna changamoto tele.

Dkt Mutunga alikariri kwamba utaratibu wa uteuzi ulitilia maanani pia hali ya mseto wa watu unaodhihiri katika Idara ya Mahakama kwa lengo la kushughulikia mapengo yaliyomo. Moja ya mapengo hayo ni ukosefu wa usawa wa kijinsia.

Hadi kufikia sasa, Tume ya CIC imehakiki-sha kwamba mengi ya manufaa waliyopata wan-awake kutoka kongamano la kihistoria la Bomas, yamefungamanishwa na kushirikishwa kwenye sheria ishirini na saba zilizopelekwa bungeni na Idara ya Utawala kufanywa sheria.

Utekelezaji katibaSheria tano za kwanza za kikatiba ambazo

zilijadiliwa na kupitishwa na Bunge la kumi ni sheria ya uteuzi huru wa maafisa, sheria ya tume huru ya mipaka na uchaguzi, sheria ya huduma ya Idara ya Mahakama, sheria ya huduma ya Mahakama Kuu, na sheria ya ukaguzi wa majaji na mahakimu ya mwaka 2011.

Tume ya utekelezaji wa katiba (CIC), im-etekeleza jukumu lake kama ilivyotarajiwa kwa kuhakikisha kwamba inatekeleza kazi zake

ndani ya muda iliyowekewa wa kukamilisha uchunguzi wa sheria 23 ndani ya mwaka wa kwanza tangu kuzinduliwa kwa katiba mpya.

Kati ya miswada ishirini na minne ambayo inasubiri kukamilishwa ndani ya mwaka wa kwanza wa katiba ya Kenya ya mwaka 2010, ni mswada wa Usimamizi wa Fedha za Umma ndio ambao umecheleweshwa na tofauti za kimaon-gozi kati ya pande zinazohusika bado unasubiri kukamilishwa na tume hiyo siku kumi kabla ya muda wa mwisho kufika. Jitihada zinafanywa kuhakikisha kwamba mswada huo unakamil-ishwa kabla ya muda huo kumalizika.

Huku muda ukizidi kuyoyoma kuelekea dakika za mwisho, Baraza la Mawaziri limefanya kazi ya ziada ili kuhakikisha kwamba inakamil-isha shughuli zake kuhusiana na miswada hiyo. Miswada mitatu iliyoidhinishwa na kupelekwa bungeni katikati ya mwezi Agosti ni mswada wa Kanuni na ile ya Tume ya Kupambana na ufisa-di, mswada wa Uwezo wa Imani na mswada wa Mashujaa wa Kenya.

Miswada ambayo inasubiri kushughulikiwa ni pamoja na mswada wa Uidhinishaji wa Mikataba,

mswada waUraia wa Kenya na Uhamiaji, mswada wa Uraia wa Kenya na Usimamizi wa Huduma za Raia wa Kigeni na mswada wa Miji na Vijiji, mswada wa Mazingira na Mahakama yaArdhi na mswada wa Usimamizi wa Pesa za Umma.

Pamoja na hayo yote shughuli ya utekelezaji wa katiba kwa jumla imekuwa shwari kwa wastani sio kama ilivyotarajiwa na baadhi ya watu.

Thuluthi mbiliKuna matumaini makubwa miongoni mwa

wanawake wakati huu ambao shughuli hiyo inaingia katika awamu yake ya pili ya utekelezaji wa katiba hukiu tunaposubiri uchaguzi mkuu chini ya katiba hiyo mpya.

Kwa wanawake hakuna kizuizi safari hii katika jitihada zao za kuhakikisha kwamba wanakamil-isha kanuni ya thuluthi moja katika nyadhaifa za uteuzi na za kiuchaguzi kwani elimu wanayo na uwezo wanao. Kenya ina wanawake wenye elimu na hamasa kubwa ya kisiasa kufikia shabaha yao ya kanuni ya thuluthi mbili. Wanachohitaji ni ku-pewa nafasi katika uwanja uliojaa wanaume na bila shaka watathibitisha kwamba wanaweza.

Kutazama utekelezaji wa sheria kwa darubini ya jinsiaKutoka Uk1

Na Rosemary Okello

Njoki Ndung’u Mumbi Ngugi Pauline Nyamweya Lydia Achode

“Tunapaswa kujifunza kutokana historia kwamba kupata asilimia 30 kwa vyoo vya kuchaguliwa ni ngumu sana”

— Deborah Okumu

Page 3: Mwanamke Mkenya Toleo 20

3 Toleo Namba 20 • Agosti 2011

Mfumo huu wa wanaumeNa Faith Kasiva…

Pendekezo la Baraza la Mawaziri la kutayarisha mswada wa marekebisho ya katiba kufanyia marekebisho kifun-gu cha usawa wa kijinsia katika katiba

ya Kenya (CoK) ya mwaka 2010 ni mwito wa kusisimua kwa dhati harakati za utetezi wa maslahi ya wanawake hapa nchini.

Arafa iliyotolewa na Idara ya Habari ya Rais iliyopelekwa kwenye vyombo vya habari siku ya Alhamisi Agosti 18, mwaka huu ilise-ma: Kuhusiana na hitaji la uwakilishi bungeni la thuluthi moja ya moja ya jinsia, Baraza la Mawaziri limeamua kuunda jopo kazi kuta-yarisha mswada wa marekebisho ya kikatiba kushughulikia hitaji hili muhimu ambalo lina ugumu mkubwa katika kulitekeleza chini ya kanuni zilizopo.

Hizo ni habari za kushtusha sana kwa wengi kwani hata mwaka haujamalizika tangu utekelezaji wa katiba hiyo kuanza kufanywa. Nilipochunguza kwa undani habari hizi nilifa-hamu kwamba mfumo wa wanaume kutawala mambo unajaribu kujipigania.

HistoriaHistoria ya ukombozi wa wanawake nchini

Kenya inatupeleka miaka mingi nyuma kuan-zia mapambano ya wanawake kuwa na haki ya kuchaguliwa na harakati za kuratibu mipango ya kisheria na ya kitaasisi inayowahusu wan-awake. Mnamo mwaka 1996, Charity Ngilu ambaye kwa sasa anahudumu katika wadhifa wa waziri aliwasilisha hoja bungeni kuhusi-ana na utekelezaji wa maazimio ya Beijing bila mafanikio. Kadhalika Phoebe Asiyo na Beth Mugo walijaribu bila mafanikio kuwasilisha mswada wa harakati za utetezi wa wanawake katika mwaka wa 1996 na mwaka wa 2000.

Mnamo mwaka 2007, Serikali ya Kenya kupitia aliyekuwa wakati huo Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Bi Martha Karua, wali-wasilisha bungeni mswada wa marekebisho ya katiba ya mwaka 2007 ikipendekeza kuanzish-wa viti vingine hamsini katika Bunge la kumi.

Mswada huo haukupitishwa kwa sababu Wabunge wanaume walitoka nje ya Bunge na

kuunyima mswada huo Wabunge wa kutosha wa kuujadili na kuuidhinisha.

Lakini katiba ya Kenya ya mwaka 2010, ilileta manufaa makubwa kwa wanawake kwa vile inatoa muundo wa kisheria wa usawa wa kijinsia na wanawake kupewa uwezo.

Hivyo basi utetezi wa maslahi na haki za wanawake katika katiba zinathibitishwa na ku-lindwa na vifungu vya sheria ikiwa ni pamoja na kifungu nambari 27(8) ambacho kinasema kwamba Serikali itachukua hatua za kisheria na hatua nyinginezo kutekeleza kanuni kwamba idadi isiyozidi thuluthi mbili ya maafisa katika nyadhifa za uchaguzi au za uteuzi ndio wat-akaokuwa waakilishi wa jinsi moja. Kifungu nambari 81(b) kinasema kwamba idadi isi-yozidi thuluthi mbili ya maafisa wa mashirika ya umma ambao watachaguliwa watakuwa wa jinsi moja.

Naomi ShaabanHilo ndilo tatizo linalolikanganya akili Ba-

raza la Mawaziri hadi kufikia kusema kwamba kanuni hiyo haitekelezeki, labda kwa sababu ya kesi inayoendelea mahakamani ambako shiri-ka la wanawake nchini likiongozwa na shirika la mawakili wanawake, FIDA, limepinga mu-undo wa majaji wa mahakama kuu na kuzuia utekelezaji wake hadi leo.

Pendekezo hilo la baraza la mawaziri lime-pokelewa kwa maoni tofauti. Huku mashirika ya wanawake na Wabunge wengine wanawake wakipinga kwa dhati pendekezo hilo, Waziri wa Jinsia, Dkt Naomi Shaaban kwenye mazun-gumzo na waandishi habari alionekana kuunga mkono pendekezo hilo la Baraza la Mawaziri akisema ni sehemu ya majukumu ya pamoja.

Lililoshangaza hata hivyo, ni matamshi ya Dkt Shaaban kwamba wanawake wanapaswa kupigania viti vya Bunge wakishindana na wa-naume.

Matamshi hayo yanadhihirisha kukosa fa-hamu kwa upande wa waziri huyo na hayuko sambamba na kanuni za haki na maslahi ya wanawake na usawa wa kijinsia ulimwenguni kote. Harakati za wanawake nchini zinapaswa kuhoji kutoka kwa waziri huyo kama ndiye hakika anayefaa kuongoza wizara hiyo kwa

kuwa alikuwa mmoja wa kundi la wanasiasa waliopinga kuidhinishwa kwa katiba hii.

Bi Atsango Chesoni aliyekuwa naibu mwe-nyekiti wa Tume ya Wataalamu waliotayarisha katiba ya mwaka 2010, amepinga hatua ya ku-fanyia marekebisho katiba hiyo kuhusiana na kanuni hiyo ya thuluthi moja.

Anapendekeza kwamba kama Baraza la Mawaziri linataka namna na jinsi ya kuk-abiliana na hitaji hilo, basi linapaswa kurejea kwenye kifungo cha 121 cha katiba ambacho kilipendekeza mseto wa uwakilishi wa maafi-sa ambao uliwasilishwa kwa kamati ya Bunge mnamo Januari 8, mwaka 2010.

Ubabe wa wanaumeAtsango ametaka mashauriano ya dhati

kabla ya marekebisho yoyote kufanyiwa katiba ili kuepuka kuzusha mtafaruku.

Anasema: “Swala kuu ni iwapo kuna nia njema ya kisiasa kuhusiana na kanuni za usawa na kama tunakabiliwa na wale ambao wanataka kuanzisha mzozo wa kikatiba kwa makusudio ya kuleta uchafuzi.”

Kunako maadhimisho ya mwaka wa kwan-za wa katiba mpya, manufaa waliyopata wan-awake yanakabiliwa na tishio la kuangamizwa

na kubadilishwa. Ubwana wa wanaume wa kutaka kutawala mambo yote unajitokeza upya kupigana kukomesha mafanikio ya wanawake. Maoni ya Baraza la Mawaziri kwamba kanuni ya thuluthi mbili kwa moja haiwezi kutekeleze-ka hayakubaliki.

Nchi nyingine ikiwa ni pamoja na Rwanda, Uganda, Afrika Kusini na nchi za Scandinavia zimetekeleza kanuni hiyo.

Licha ya hakikisho la Waziri Mkuu na Makamu wa Rais kwamba uamuzi huo wa Ba-raza la Mawaziri ulieleweka kimakosa, bado ni mwito wa kuwataka wanawake wawe macho.

Wanawake wa Kenya wamesubiri kwa muda mrefu kupata haki zao kwenye nyadhifa za kiuchaguzi na kiuteuzi. Majaribio yoyote ya viongozi wachache kuwanyima wanawake haki zao kama ilivyoidhinishwa na wengi wa Wakenya wakati wa kura ya maoni, wanapas-wa kupuuzwa na kutupiliwa mbali kwa njia yoyote ile.

Huu ndio wakati ambapo wanawake wa Kenya wanapaswa kuungana pamoja bila kujali kabila, asili, tofauti za kisiasa ili kulinda kwa ushupavu mafanikio ya wanawake waliyopata kupitia katiba mpya ya mwaka 2010 kwa man-ufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Enyi wanawake wa Kenya simameni kulinda haki zenu!

Wabunge wawili, Bi Joyce Laboso (kushoto) akiwa na mwenzake Mbunge Maalum Bi Rachel Shebesh wakihutubia wandishi habari kulaumu jaribio la Baraza la Mawaziri la

kutaka kubadilisha kile kifungu cha theluthi mbili kutoka kwa katiba mpya.

Rekebisho dogo katika katiba au kufutwa kwa manufaa yote?

Katika makala haya Atsango Chesoni ajibu uamuzi wa Baraza la Mawaziri wa kuifanyia katiba marekebisho dhidi ya manufaa kwa wanawake.

Kamati ya Wataalamu (CoE) kwa hakika iliweka mpan-go wa mseto wa waakili-shi kwenye mapendekezo

kadirio ya katiba yaliyowasilishwa kwa Kamati Teule ya Bunge (PSC) mnamo tarehe nane mwezi Januari

mwaka 2010.Kifungu cha 121 cha mapendek-

ezo ya katiba kinalitaka Bunge liwe na:-(a) Wabunge wachaguliwe kila eneo

mbunge mmoja kama itakavyoa-giza sheria.

(b) Wanawake wateuliwe mmoja kwa kila kaunti, kila kaunti iwe na mwakilishi wa jinsia hiyo.Kanuni hii ya kisheria ilifanyiwa

marekebisho na kamati maalum ya Bunge kuhusu uchunguzi wa kati-

ba iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Abdikadir Mohammed na naibu wake Mheshimiwa Ababu Namwamba mjini Naivasha kupanga idadi ya viti katika Bunge kuwa viti 290. Kwa kuwa idadi iliyokubaliwa ya kaunti ilikuwa ni 47, idadi ya viti vinavyopaswa kushikiliwa na wan-awake pia ni 47.

Kipengee hichoKisha waliondoa vipengee vy-

ote vinavyohusiana na uwakilishi wa mseto wa Wabunge na kuweka kipen-gee cha Wabunge 12 wa teule ambao wanawakilisha “maslahi maalum”, aina ya Wabunge ambao watu wa Kenya walielezea kwamba wana-faa kuwepo. Ijapokuwa kamati ya wataalamu ilielezea wasiwasi kuhusu marekebisho hayo, tulifahamishwa ya kwamba hicho ni kipengee ambacho hatupaswi kukigusa na kwamba ndi-cho kilichosababisha maafikiano ya Naivasha.

Kwa kuwa utayarishaji wa katiba ni shughuli ya kisiasa, tulikuwa na

wasiwasi kwamba vipengee kuhusi-ana na wanawake vingekuwa rahisi kuleta umoja kwa Bunge kufungua mapendekezo ya katiba na kuondoa mafanikio yoyote ambayo yamo ndani ya katiba hiyo. Ni muhimu pia kwam-ba kumbukumbu ya majadiliano haya zitolewe kwa vile yanaashiria ukosefu wa nia njema ya kisiasa sio tu kwa usa-wa wa kijinsia bali pia imani kwamba kwa utaratibu wa kisiasa unaotambua usawa wa kibinadamu, kwa hivyo la Profesa Ghai sio kwamba Kamati ya Wataalamu “haikujua ilichukuwa ikikifanya, tulikabiliwa na hali ngumu mno ya kisiasa kwa vile kulitolewa vit-isho kwamba wakati Wabunge wataka-posoma mapendekezo hayo manufaa ambayo wanawake walikuwa wameya-pata yangefutiliwa mbali.

Kwa vile katiba katika hali yake ya sasa haitoi utaratibu mwafaka kwa Bunge, kama kuna marekebisho ambayo yanafanywa kwa nia njema itakuwa rahisi kurekebisha kifungu kilichopo sasa nambari 97(1)(c) kure-jea katika kifungu cha asili nambari

121 kuliko kuondoa vipengee vina-vyolinda kanuni ya thuluthi moja.

Swala kuu ni iwapo kuna dhamiri ya kisiasa juu ya kanuni za usawa na kama kwa mara nyingine tena tuna-taka kuanzisha majadiliano kuhusu katiba kwa malengo mengine. La kushangaza ni kwamba swala la ku-totekelezeka kwa kanuni hiyo huzuka tu kuhusiana na usawa wa kijinsia linapowasilishwa bungeni. Swala hili liliwasilishwa mwaka 1997 wakati huo tuliambiwa tulishughulikie swala hilo kwa kushirikisha vipengee vyote kwa pamoja, kisha kwenye kongamano la kitaifa swala hilo likatupiliwa mbali.

Ni muhimu kwamba tulitafa-kari swala hili katika mtazamo wa hali yake ya kihistoria. Inashangaza kwamba hiyo ndiyo sababu inayotu-mika hasa inapokuwa ni katika shu-ghuli za kiuteuzi.

Mwandishi huyu, Astango Chesoni alikuwa Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Wataalamu wa Utayarishaji Katiba. Yeye pia ni wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya

Na Atsango Chesoni

Page 4: Mwanamke Mkenya Toleo 20

4 Toleo Namba 20 • Agosti 2011

Tume yajiandaa kwa uchaguzi wa majaribio

Na Faith Muiruri…

Muda wa mwisho wa utekelezaji katiba mpya unafikia kikomo kwa kasi sana. Ni sheria

tano pekee ambazo zimepitishwa hadi kufikia sasa kati ya sheria 26 zi-nazohitajika kufikia wakati uliokuba-liwa kwa utengenezaji wa miswada yenye umuhimu wa kwanza kwa kip-indi kinachomalizikia tarehe 30 Ago-sti, mwaka 2011.

Habari zilizopokelewa kutoka mtandao wa Tume ya Utekelezaji wa Katiba (CIC) zinaonyesha kwamba ni sheria ya kuunda Tume ya Mipaka na Uchaguzi ya mwaka 2011, Sheria ya Tume Huru ya Uteuzi wa Maafisa ya mwaka 2011, Sheria ya Mahakama Kuu ya mwaka 2011, Sheria ya Tume ya Huduma Huduma za Mahakama ya mwaka 2011 na Sheria ya Tume ya Ukaguzi wa Majaji na Mahakimu ya mwaka 2011.

Sheria ambazo utekelezaji wake umechelewa ni pamoja na Mswada wa Uchaguzi, Mswada wa Vyama vya Kisiasa na mswada wa kupambana na ufisadi. Mswada wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu, na uraia, sheria kuhusu Tume ya Kanuni na Kupam-bana na Ufisadi, kuondoka ofisini kwa Wabunge, sheria zote kuhusu ugavi wa mamlaka, na sheria kuhusu hazina maalum ya kukabiliana na mambo yasiyotarajiwa, na udhamini wa mikopo wa serikali kuu.

UboraMambo yanazidi kufanywa

magumu kutokana na kushindwa kwa watayarishaji wa sheria kuha-rakisha utaratibu huo. Kukawia huko zaidi sana kunatokana na ulimativu wa maofisa wahusika katiuka utayar-ishaji wa sheria hizo ambao unatishia kudhgoofisha ubora wa majadiliano kuhusu miswada hiyo, na uwezo wa kamati za Bunge kuichunguza kwa makini miswada hiyo. Jambo hilo matokeo yake ni kupitisha kwa haraka sheria hizo ambapo zinaweza kupitishwa zikiwa na udhaifu mkub-wa wa kisheria.

“Huenda tukaishia na sheria zili-zo dhaifu ambazo haziambatani na katiba,”akasema Hassan Omar am-baye ni Kamishna wa Tume ya Kenya ya Haki za Binadamu (KNCHR).

Hassan anasema kucheleweshwa huko kwa sheria huenda kukasaba-bisha kuundwa kwa taasisi dhaifu kutokana na kutoeleweka vizuri kwa maswala muhimu, na kadhalika mashindano ya kisiasa kati ya vyama vya ODM na PNU na jitihada za wa-pinga mabadiliko katika Bunge.

“Wapinzani wa mabadiliko wamo katika harakati za kuwaelimiswha habari za upotofu Wakenya kuhusu kile ambacho katiba inazungumzia, Dhana ya ugavi wa mamlaka kwam-ba ni majimbo huenda ikawafanya wananchi kutumiwa viubaya na vi-ongozi wa kisiasa na kuzua ghasia za kikabila,” aeleza Omar.

Anasema kwamba nyingi ya wiz-ara sasa zinajigeuza kuwa tume za kukabiliana na vipengee vya katiba vya kutokuwepo na zaidi ya wizara ishirini na mbili.

“Mfano ni kugawanywa katika

sehemu tatu kwa tume ambazo ziko chini ya Tume ya Kenya ya Haki za Binadamu na Tume ya Usawa, (KN-HEREC) kuanzisha ofisi ya mpokezi malalamiko ya wananchi kuhusu Serikali mswada wa mwaka 2011, mswada wa tume ya haki za bina-damu ya mwaka 2011 na mswada wa tume ya kitaifa kuhusu jinsia,” akael-eza Omar.

Omar anadai kwamba kazi ya Tume ya Haki za Binadamu (KNH-CR) na tume zilizoundwa hivi majuzi chini ya kifungu cha sheria nambari 59, huenda ikasababisha vurugu mi-ongoni mwa tume hizo.

Zaidi ya hayo, mswada wa ma-hakama ya kazi aya mwaka 2011 kad-halika unajaribu kuwasukuma majaji wa sasa kwenye nyadhifa mpya bila ya hata kuchunguzwa na vyombo vya umma na kuhakikisha kwamba wa-natimiza kanuni zinazohitajika kama ilivyoratibiwa kwenye katiba mpya.

Omar anawatahadharisha Wake-nya wawe macho kuhakikisha kwamba wapiinzani wa mabadiliko hawafani-kiwi kuvuruga utekelezaji wa katiba.

Wahusika wengine wasio wa ki-serikali kwa upande wao wanaone-lea kwamba jitihada zinazoendelea zisizokuwa na mshikamano wa moja kwa moja huenda zikazalisha sheria ambazo hazina uwiano.

Wanawataka Wakenya wasimame imara na kupinga majaribio yoyote ya kudhoofisha utekelezaji thabiti wa katiba.

“Wakenya wote wana jukumu la kuhakikisha kwamba katiba in-atekelezwa kuambatana na vifungu vya sheria vilivyomo ndani ya katiba hiyo,” wakaongeza wahusika hao kwe-nye taarifa kwa waandishi habari.

Wahusika hao ni pamoja na Taa-sisi ya Uwajibikaji wa Umma (Tisa), Kituo cha Kuimarisha Demokrasia na Utawala Bora (CEDGG), Kituo cha Haki za Binadamu na Elimu kwa Umma (CHRCE),Tume ya Kimataifa ya Waamuzi (ICJ-Kenya) na shirika la kimataifa la uwajibikaji, ambayo yanasema watu wasiotaka mabadi-liko wana dhamira kubwa ya ku-hakikisha kwamba wanajihami dhidi ya mabadiliko hayo.

Wanasema kwamba katiba in-aeleza wazi wazi kazi za ngazi mbali mbali za kiserikali. “Hata hivyo, ubidhi wa baadhi ya watu kwamba idara ya utawala wa mikoa inapaswa kudumishwa ni tukio la kusikitisha la kukataa mabadiliko kwa wale wa-naodhamiria kudumisha ofisi hiyo na katika hali hiyo kutaka kuvuruga utaratibu wa mabadiliko.

Mwito wa aina hiyo hauambatani na matakwa ya mabadiliko na un-apaswa kupuuzilowa mbali,” ika-ongeza taarifa hiyo.

KuanzishwaHuku uchaguzi mkuu wa mwaka

2012 ukiwadia, sheria tatu muhimu ni lazima zipitishwe. Sheria hizo ni mswada wa Uchaguzi, mswada wa Vyama vya Kisiasa, na mswada wa Kanuni na Harakati za Kupambana na Ufisadi. Bila ya miswada hiyo kujadi-liwa na kuidhinishwa Tume ya Uch-aguzi itakuwa haina uwezo wa kuchu-kua hatua zozote na itakuwa tepetevu.

Masuala mengine muhimu ni pamoja na mapendekezo ambayo hu-enda yakashuhudia kuanzishwa kwa taasisi nyingi ambazo huenda zika-hitaji vigezo vingine vya kuhakikisha uwajibikaji na kutoa msingi wa uen-delezaji wa uchumi thabiti.

Huku harakati za utekelezaji wa katiba zikiendelea, swala jengine muhimu ambalo linaendelea kutatiza ni ugavi wa mamlaka licha ya muda wa mwisho wa Agosti kuwadia.

Jambo lingine ambalo limejitoke-za lenye kuleta wasiwasi ni mashin-dano yasiyofaa kati ya taasisi za Ser-ikali hatua ambayo huenda ikaleta sheria zisizoambatana zenye kuenda kinyume na makusudio.

Pia kuna swala la kuzuka mgogoro katika sekta ya umma wakati huu ambapo watumishi wa Serikali wa-nahama kutoka kwenye taasisi zao za awali hadi kwenye taasisi mpya chini ya katiba mpya. Utaratibu huu unapasa kuendeshwa kwa uwazi kwa njia ya haki na kwa ustadi ku-hakikisha kwamba serikali za kaunti hazirithi wafanyi kazi wazembe wa-sioweza kufanya kazi vyema.

Mwenyekiti wa Tume ya Utekelezaji wa Katiba, Bw Charles Nyachae (kushoto) akiwa pamoja na naibu wake Bi Elizabeth Muli akihutubia mkutano wa waandishi wa habari kuhusu utaratibu ulioko.

Kucheleweshwa utekelezaji kungezusha sheria gushi

“Wakenya wote wana wajibu wa kuhakikisha kwamba Katiba imetekelwzwa kulingana na vifungu vilivyoidhinishwa ndani yake .”

Na Florence Sipalla…

Huku Kenya ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2012, Tume huru ya muda ya uchaguzi (IIEC) inata-yarisha mipango ya kufanya uch-

aguzi wa majaribio katika maeneo mawili ya Bunge kama njia ya kukadiria jinsi uchaguzi utakavyokuwa chini ya katiba mpya iliyozindu-liwa rasmi mwaka 2010.

Ni tendo bora linalokubalika kimataifa kwa mashirika ya usimamizi wa uchaguzi kufanya uchaguzi wa majaribio kabla ya uchaguzi mkuu . Kabla ya kura ya hivi majuzi ya maoni nchi-ni Sudan ambayo ilishuhudiwa kuundwa kwa taifa jipya la hamsini na nne, kuliandaliwa uch-aguzi wa majaribio kukadiria jinsi upigaji kura utakavyokuwa.

Uchaguzi huo wa majaribio utagharibu shi-lingi milioni sitini. Kwa ajili ya shughuli hiyo-muhimu tume ya uchaguzi imechagua maeneo bunge ya Kajiado na Malindi Kaskazini kama vituo vya kupigia kura.

“Hii ni kwa sababu maeneo mawili hayo ya Bunge yanawakilisha hali halisi ya kijamii ya nchi nzima kwa jumla. Ni maeneo ambayo yana watu wenye mapato ya juu na ya chini zai-di, kuwa na miji na sehemu zenye watu wengi pamoja na maeneo yenye watu wachache,” alise-ma Gladys Shollei afisa mkuu wa tume hiyo ya uchaguzi anayeondoka.

Uchaguzi huo wa majaribio utaipa nafasi tume ya uchaguzi kukadiria muda utakaochu-kuliwa kupiga kura kwa kutumia makaratasi

sita ya kupigia kura kwa uchaguzi wa Rais na Maseneta, uchaguzi wa Wabunge, Maga-vana wawakilishi wa kaunti na wa wanawake, kinyume cha makaratasi matatu ambayo yame-kuwa yakitumiwa kupigia kura kwa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

“Ni kama mtihani wa majaribio ambao un-akupa zoezi na hali ambayo mtihani wenyewe utakavyokuwa,” alieleza Shollei.

Uchaguzi huo utaipa tume ya uchaguzi na-fasi ya kuwaelimisha wapiga kura na wakati huo kufahamu changamoto ambazo itakabiliana na-vyo na kujiandaa kukabiliana nazo kwa wepesi.

MajadilianoTume hiyo itawatumia wapiga kura ambao

wamesajiliwa katika maeneo Bunge hayo mawili kama wapiga kura kwenye uchaguzi huo wa ma-jaribio. Hakutasajiliwa wapiga kura wapya kwa ajili ya uchaguzi huo. Tume hiyo huru ya muda ya uchaguzi, inafanya majadiliano ya ni akina nani watakaowatumia kama wagombea uchaguzi.

Katika jitihada za kuepuka kuwatumia wanasiasa, tume hiyo inatafakari mipango ya kuwatumia watu wasiounga mkono upande wowote . “Hawa ni Wakenya ambao hawatago-mbea uchaguzi katika viti hivyo viwili,”aliongeza kusema Shollei.

Tume hiyo itaendesha uchaguzi huo kama uchaguzi halisi na itawapa wagombezi vifaa vya kufanyia kampeini. Hiyo itakuwa sehemu ya elimu kwa wapiga kura. Kama ambavyo wata-fanya kwenye uchaguzi halisi, tume ya uchaguzi itawaajiri wafanyikazi kusaidia kwenye uch-

aguzi huo wa majaribio. Wafanyikazi hao wa-tahudumu chini ya maafisa wa usimamizi wa uchaguzi wa maeneo Bunge .

Tume hii ya uchaguzi ina hakika kwamba iko tayari kwa uchaguzi wa mwaka 2012. Uch-aguzi mkuu uliopita ulikumbwa na visa vya usa-jili mara mbili wa wapiga kura. Ili kuondoa tati-zo hilo kwenye orodha ya sajili ya wapiga kura tume hiyo ilitoa msamaha kwa wale waliokuwa wamesajiliwa mara mbili na kurejesha kadi zao.

“Tume hiyo ya uchaguzi kadhalika inafanya kazi pamoja na machifu na wasajili wa vizazi na vifo kuhakikisha kwamba wapiga kura wal-iokufa wanaondolewa kwenye orodha ya wapiga kura,” akasema Shollei.

“Katika muda wa chini ya sekunde, unaweza kuthibitisha iwapo mtu amesajiliwa hapo awali,” akizungumzia ustadi wa utendakazi wa sajili ya wapiga kura inayotumia vifaa vya kisasa.

“Tunatarajia kusambaza sajili hiyo katika kila eneo la Bunge, lakini hilo litategemea ud-hamini wa pesa,” akaeleza Shollei huku akion-geza kwamba hili ni jambo ambalo linaweza kufanikishwa pole pole.

Ingawa wanawake ndio wengi wanaopiga kura, hawawakilishwi ipasavyo kwenye nya-dhifa za uongozi. Utekelezaji wa katiba mpya unadhamiriwa kubadilisha hali hiyo kwa vile ha-kutakuwa na zaidi ya thuluthi mbili ya jinsia moja itakayoruhusiwa kuongoza katika taasisi yoyote.

Ili kuhakikisha kwamba kanuni hiyo inafani-kishwa, Shollei alivihimiza vyama vya siasa ku-wasimamisha wanawake zaidi wa kugombea viti.

Katiba kadhalika inahakikisha haki za watu

wenye ulemavu. Hayo ni kuhusiana na haki zao za kupiga kura. Katika kuhakikisha kwamba kundi hilo la watu wachache halifungiwi mlan-go kwenye utaratibu wa kuwaelimisha wapiga kura, tume ya uchaguzi inashirikiana na chama cha walemavu wa akili cha Kenya, (KSMC,) ku-hakikisha kwamba vifaa vyote vya upigaji kura vinaweza kutumiwa na watu wwenye ulemavu ikiwa ni pamoja na walemavu wasioweza ku-fikiria mambo na waliolemaa kiakili.

“Hii ni kama mtihani wa majaribio, inakupatia zoezi

na wazo kuhusu jinsi mtihani utakavyokuwa.”

— Gladys Shollei, Naibu Kinara wa IIEC aliyeondoka

Page 5: Mwanamke Mkenya Toleo 20

5 Toleo Namba 20 • Agosti 2011

Sheria yawapa wanawake nafasi ya

usimamizi wa vyama

Wabunge wamejadili na kupitisha sheria ya vyama vya siasa na kuidhinisha uwekaji

wa vyama hivyo katika mfumo wa ki-taasisi na kitaalamu katika usimamizi wa vyama hivyo vya siasa.

Sheria ya usimamizi wa vyama vya siasa ya mwaka 2011 ilitungwa kuam-batana na kanuni za kikatiba kwa mu-jibu wa vifungu nambari 91 na 92.

Sheria hiyo itakomesha mtindo wa wanasiasa kuhama kutoka chama kimoja hadi chama kingine .

Kulingana na sheria hiyo, mtu hawezi kuwa mgombeaji wa chama chochote cha siasa kama hajakuwa mwanachama kwa muda wa miezi mitatu. Hata hivyo, kulikuwa na pendekezo la hapo awali kwamba muda wa uanachama uwe miezi sita lakini wanasiasa wakapendekeza miezi mitatu ya uanachama.

Inatarajiwa kwamba sheria hiyo italeta heshima katika usimamizi wa vyama hivyo hapa nchini. Kwa mion-go mingi vyama vya siasa vimesima-miwa kama kampuni za kibinafsi na wanasiasa huku baadhi yao wakivi-tumia kama vyombo vya kupigania mamlaka ya uongozi.

KudumishaIli chama kiendelee kuwapo ni

lazima kisimamishe wagombeaji wa nyadhifa za kitaifa na za kaunti. Chama ni lazima kiwe na wanach-ama kutoka sehemu zote za nchi.

Katika kifungu nambari 91 (1) katiba inasema: “Kila chama cha sia-sa kitaimarisha na kudumisha umoja wa kitaifa.”

Sheria hiyo inapendekeza kufuti-liwa mbali kwa chama ambacho haki-tafanya uchaguzi wake kwa njia ya haki na hiari na inahimiza hatua kali kuchukuliwa dhidi ya watu wanao-hama na kaujiunga na vyama vingine. Sheria itahakikisha kwamba vyama vya siasa vina mtazamo wa ki-kanda na mseto wa kikabila usawa wa kijin-sia na uwakilishi wa makundi madogo ya watu na wanaogandamizwa.

Kwa mara ya kwanza wanawake watashirikishwa kwenye ngazi za juu za uongozi wa vyama baada ya ku-tojishirikisha kwa sababu ya kiburi cha wanaume na utumiwaji wa mbinu za kutisha na wanaume hao wakati wa kampeini za uchaguzi.

Katika kifungu cha 91 (1) (f), katiba inasema “Kila chama cha siasa kitaheshimu na kuthibiti haki za bi-nadamu na uhuru muhimu na usawa wa kijinsia kutendewa sawa”.

Kulingana Joy Othieno, wakili mwenye makao yake mjini Nairobi, alisema;“Wanawake wamejiepusha na kugombea mamlaka makuu ya vyama kwa sababu ya kuhangaishwa na wagombeaji wanaume, lakini hali hiyo sasa itabadilika wakati mswada huo utakapoanza kutumika.”

Othieno hata hivyo anafahamisha kwamba ukosefu wa pesa ndicho kikwazo kikubwa kinachowazuia wa-nawake kushiriki kikamilifu kwenye siasa za vyama.

“Imani za kitamaduni za jamii mbali mbali zinapasa kulaumiwa kwa vile jamii nyingi haziamini katika uongozi wa wanawake,” akaeleza.

Kulingana na Waziri wa Mambo ya Katiba na Fungamano la Kitaifa, Bw Mutula Kilonzo, sheria ya vyama vya siasa imeshirikisha takwa la kijin-sia na ushirikishi wa kanda ambayo

yanapaswa kutimizwa kabla ya usa-jili wa chama chochote ili kutekeleza matakwa ya katiba mpya.

Sheria hiyo inataka muundo wa maafisa wa kitaifa wa chama uwe na mtazamo wa kitaifa, hatua ambayo inataka kupiga marufuku mtazamo wa kikabila na kuleta mtazamo wa kitaifa kwa vyama..

“Sheria hiyo kadhalika inaruhusu miungano ya vyama na makubaliano ya miungano hiyo kuwasilishwa kwa msajili wa vyama katika muda wa siku ishirini na moja za muungano,” aliele-za Kilonzo. Alisema kwamba; “Sheria hiyo inawazuia watu binafsi ambao ni wanachama wa vyama vya siasa ku-tangaza mitazamo, maslahi na mao-ngozi ya chama kingine au kukifanyia kampeini chama kingine au mgom-beaji uchaguzi wa chama kingine.”

Sheria hiyo inataka kuundwe hazina ambayo itagawanyiwa vyama kuambatana na jumla ya idadi ya kura vilivyopata kwenye uchaguzi mkuu. Ili chama kifuzu kupata pesa hizo, kiasi cha asilimia 15 kwa ku-tumia kanuni sahihi, asilimia tano kwa usimamizi, asilimia themanini kwa uwakilishi wa usawa, na asili-mia arobaini kuwa chini ya misingi ya idadi ya wanawake na vijana wa-naojiunga na chama husika.

Sheria hiyo hata hivyo, inazuia vyama kupokea pesa kutoka kwa watu wasiokuwa raia na inavihitaji vyama kuchapisha orodha ya wad-hamini wa kifedha wa chama.

Waziri Msaidizi wa Elimu, Dkt Kilemi Mwiria anasema kuwa miun-gano ya vyama humu nchini inaun-dwa kwa sababu ya uzandiki kujitafu-tia mamlaka na utovu wa uaminifu.

Dkt Mwiria analaani mipangilio

ya kikabila katika uundaji wa miun-gano kama sumu kwa fungamano la kitaifa kwa sababu ni dhihirisho la ukabila. “Vikwazo vinapasa ku-wekewa vyama ambavyo vinasisitiza kwamba jamii zao zinapaswa kue-lekea njia moja au nyingine au ku-wekewa vyama vinavyounda miun-gano ya kikabila,” akashauri.

James Orengo“Twapaswa kujifunza kutokub-

aliana ndani ya vyama v ya siasa na kusuluhisha matatizo ndani ya vya-ma hivyo,” alisema waziri mwingine msaidizi, Mwangi Kiunjuri ambaye ni Mbunge wa Laikipia Mashariki.

Alitoa mwito kwa vyama kuun-da kamati za kusaidia kusuluhisha mizozo ya ndani badala ya wanao-zozana kutoa tofauti zao hadharani, mwenendo ambao husaidia kuleta chuki miongoni mwa jamii tofauti.

Waziri wa Ardhi, James Orengo ambaye aliunga mkono mswada huo, aliilaumu Serikali kwa kuchochea kuanguka kwa vyama vya siasa tangu nchi hii ijinyakulie uhuru.

Orengo anasema pia kwamba

mtindo wa vyombo vya habari wa kuwashutumu wanasiasa umesaidia kusambaza ghasia ambapo makundi ya watu wa chama kingine hufanyia kampeini wazi wazi chama kingine pinzani.

“Hizi ni imani potofu zsa kusadi-ki kwamba hakuna chochote chenye thamani au dhana mbovu ya kuwa na shaka kwa kila jambo katika siasa. Hali ambayo haina mashiko katika jamii ya kidemokrasia,” akasema.

Mwenyekiti wa kituo cha vyama cingi vya kisiasa nchini, (CMD), Jus-tin Muturi anasema kwamba nchi hii inahitaji vyama vyenye nguvu kama taasisi za usimamizi wa umma.

Vyama vinastahili kuwa na mtazamo wa kitaifa na kusimamiwa kitaalamu. Hatutaki vyama kuundwa bila misimamo ambavyo shabaha yao ni kushinda nyadhifa za mamlaka, akaeleza Muturi. “Sheria hiyo ina ad-habu kali dhidi ya wale wanaoruka kutoka chama kimoja hadi kingine kama panzi,” akakariri.

Ingawa kamati ya Bunge ya uan-galizi wa mambo ya katiba, (CIOC), iliamini kwamba marekebisho

yatakubaliwa na Bunge, kundi la Wabunge chini ya muungano wa G7 ulishinda mapendekezo ya kamati hiyo hasa kifungu nambari 10.

Walipendekeza kwamba vyama viwili au zaidi vinaweza kuunda mu-ungano kabla au baada ya uchaguzi na kuwasilisha makubaliano ya mu-ungano kwa msajili wa vyama vya siasa miezi mitatu kabla ya uchaguzi mkuu kufanywa.

Kadhalika walikubalina kwamba miungano hiyo ifanywe baada ya uchaguzi mkuu kinyume na hitaji lil-ilowekwa na katiba.

Usimamizi wa vyama vya siasa utafanywa na ofisi ya msajili wa vya-ma, ambayo itakuwa ofisi ya Serikali. Ofisi hiyo haitakuwa chini ya usima-mizi wa Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi (IEBC) iliyoundwa chini ya kifungu 8 nambari 250 ya Katiba. Kila chama ni lazima kiwe na jina to-fauti na alama yake. Haitakuwa kama mwaka 2007 wakati chama cha Or-ange Democratic Party (ODM) na chama cha Orange Democratic Party of Kenya (ODM-K)vilipongángánia alama moja ya chungwa.

Wanawake wakiimba wakiunga mkono chama cha PNU wakati wa uchaguzi mkuu wa 2007. Akina mama wanakosekana kwenye nyadhifa za juu katika vyama vikuu vya kisiasa nchini.

Na Duncan Mboyah na Jane Godia…

Je, vyama vya siasa vitaweza kuwaweka wanawake katika nyadhifa za kutoa maamuzi?Na Rosemary Okello…

Kama kuna wakati katika historia ya Kenya ambapo vyama vya siasa vitakabi-liwa na uchunguzi mkali

hasa kuhusiana na swala la uwakilishi wa wanawake katika ngazi za kitaifa na za serikali za kanda basi ni katika uch-aguzi mkuu wa mwaka 2012.

Kinyume na ilivyokuwa hapo awali, vyama vya siasa vilikuwa havichukuliwi hatua zozote kuhusiana na uwakilishaji wa wanawake chini ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2007.

Kulingana na Dinah Liech, wa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, sheria mpya ya usimamizi wa vyama vya siasa imeleta mapinduzi makubwa kwenye sheria za vyama vya kisiasa. Anaeleza kwamba sheria ya awali ya vyama vya kisiasa (sehemu ya 108), ilihusu usajili wa kila aina ya vyama. Vyama vya siasa vilisajiliwa kama vyama vingine vyovy-ote vya kawaida vikiwa na wa kisheria kama vyama vingine kama vile vilabu, vyama vya kitaalamu, vyama vya kija-mii, na makundi ya akina mama, mion-goni mwa vyama vinginevyo.

Hata ingawa sheria hiyo ya vyama sehemu ya 30 (4) inasema kwamba “Hakuna chama chochote cha siasa ambacho kitanufaika na hazina kama maafisa wake waliosajiliwa hawana mtazamo wa thuluthi moja ya kanuni ya kijinsia.”

Kulinganana Liech, “Hilo halijaku-wa na athari yoyote kwa ngazi ya utoaji maamuzi ya vyama. Uwakilishi wa wa-nawake katika ngazi za kitaifa,kanda na

maeneo ya ubunge haupo. Kwa sasa idadi rasmi ya uanachama

katika vyama vya siasa ni wanaume 82,237 ambayo inawakilisha asilimia 63 na wanawake 48,353 ambao wan-awakilisha asilimia 37. Idadi kamili ya wanaume na wanawake katika baraza kuu la vyama ni wanaume 673 wa-naowakilisha asilimia 63 na wanawake 402 wanaowakilisha asilimia 37.

Idadi kamili ya wanachama wa ka-mati ya ushirikishi wa kitaifa wa vyama vya siasa ni kama ifuatavyo: Wanaume 35 wanaowakilisha asilimiua 75 na wa-nawake kumi na wawili wanaowakilisha

asilimia 25. Kamati ya kanda ya ushiriki-shi wa vyama vya siasa kwa sasa ni kama ifuatavyo wanaume 491 wanaowak-iliswha asilimia 82, na wanawake 108 ambao inawakilisha asilimia 18. Kamati ya usimamizi wa ushirikishaji wa vyama ina jumla ya wanachama 166 ambapo 142 ni wanaume wanaowakilisha asili-mia 75, ilhali wanawake ni ni arobaini na wawili wanaowakilisha asilimia ishirini na tano.

Alisisitiza kwamba chini ya haki za kisiasa na za kiuchaguzi za wanawake katika sura ya pili ya katiba sehemu ya 4 (2), miongoni ma mambo men-gine inatilia nguvu hakika kwamba vyama vya siasa vinapasa kuongozwa na kanuni kama vile umoja wa kitaifa, usimamizi wa kisheria, demokrasia, kushiriki kwa raia, usawa, kutobagua-na, utawala mwema na uwajibikaji.

Hata ingawa wanawake wako huru sawa na wanaume wa kujiamulia kati-ka masuala ya kisiasa ikiwa ni pamoja na haki ya kuunda au kushiriki katika uundaji wa vyama vya kisiasa, Liech anasikitika kwamba kushiriki kwao kwenye masuala ya vyama vya siasa ni dhaifu sana.

Kwa mfano wanawake hawashiriki kwenye shughuli za vyama na wame-waachia wanaume kupanga mikakati katika usajili wa wanachama au katika kampeini za vyama vya kisiasa.

Hata hivyo, sehemu ya 91(1) iko wazi kuhusu jinsi vyama vya siasa vinavy-opaswa kuendesha shughuli zao. Kinavi-taka vyama hivyo kuzingatia kanuni za kidemokrasia na utawala bora, kuimar-isha na kutekeleza demokrasia kwa vi-

tendo kwa kufanya uchaguzi za mara kwa mara za haki na uwazi, kuheshimu haki za watu wote za kushiriki katika harakati zote za kisiasa, ikiwa ni pamoja na wanawake, makundi ya walio wach-ache na wanaogandamizwa.

Kwa hivyo, huku wanawake waki-tafuta mbinu za kuhakikisha kwamba kipengee cha uwakilishi wa kutozidi thuluthi mbili kwa jinsia moja inafani-kishwa, katiba chini ya sehemu ya 81, inatambua harakati za kupigania haki za wanawake kama kanuni ya utara-tibu wa uchaguzi na kanuni hiyo ni ya kurekebisha upungufu wa uwakilishi wa makundi maalum kama vile wan-awake, vijana makundi ya walio wach-ache na wanaogandamizwa.

NyadhifaKama ilivyo kwa sasa, katiba inawa-

taka wanawake na wanaume kuchagu-liwa kwenye nyadhifa zifuatazo, urais, wabunge, maseneta, waakilishi wan-awake katika kaunti na madiwani.

Vyama vya siasa kwa hivyo vita-hitajika kutayarisha orodha ya wago-mbezi yenye mseto wa kijinsia kwenye ugombezi wa viti vya kiuchaguzi na vya uteuzi kabla ya uchaguzi mkuu.

Kulingana na Kamishna Win-nie Guchu kuna haja ya kutayarisha uchambuzi hakika kuonyesha jinsi wanawake watakavyoshiriki kupitia vyama hivyo vya siasa. “Hii ni kwa sababu wanawake hujitokeza wakiwa wamechelewa hasa kwenye harakati za kisasa na siku zote huachwa nyuma wakati maamuzi makuu yanapofikiwa kwenye vyama,” akaeleza.

“Wanawake huja kama wamechelewa kwenye

utaratibu wa kisiasa hivi basi huachwa nyuma

maamuzi muhimu yanapotolewa.”

— Winnie Guchu

Page 6: Mwanamke Mkenya Toleo 20

6 Toleo Namba 20 • Agosti 2011

Na Adow Ina Kalil…

Uchaguzi wa mwanamke kwenye mamlaka dhaifu ya mwenyekiti wa kamati katika Baraza la Wilaya

lisilofanya vyema huenda lisiwe jam-bo la kusherehekea.

Hata hivyo, likitendeka katika eneo ambalo kidesturi wanawake huzuiwa kupanda ngazi za uongozi tukio hilo linaonekana kama hatua kubwa ya kubadilisha hali kwa wa-nawake kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2012.

Historia ilitendeka katika kanda ya Kaskazini Mashariki wakati wa uchaguzi unaoendelea wa udiwani baada ya wanawake watatu madiwani kuchaguliwa kuwa wenyekiti wa ka-mati za mabaraza kwenye mabaraza yanayomilikiwa na wanaume ya Wa-jir na Mandera.

Mwanamke wa kwanza kabisa kuchaguliwa diwani wa Baraza la Wilaya ya Wajir, Rukia Abdille Ab-dullah wa wadi ya Laghbokol Kaska-zini, alichaguliwa mwenyekiti wa kamati ya uhasibu naye mwenzake, Fatuma Sheikh akachaguliwa kwa urahisi kuwa mwenyekiti wa kamati ya mazingira, usafi na afya ya jamii.

UteuziKatika mpaka wa kaunti ya Man-

dera, diwani maalumu wa chama cha Safina, Maryam Dahir Hussein mwenye umri wa miaka 44, alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuongoza kamati ya mazingira na afya ya jamii, baada ya kuchaguliwa bila kupingwa kwenye uchaguzi huo un-aoamuliwa katika misingi ya mbari.

Hata hivyo, kuchaguliwa kwake kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya baraza lenye ukubwa wa kilomita 25,920 mraba hakukuwa rahisi.

Ilihitaji jitihada za madiwani wanne wanawake kupambana kufa na kupona kupata haki yao kwenye ba-raza hilo lenye kamati tisa zilizokuwa zikigombaniwa, wakingángána kupa-ta sehemu yao kwenye utekelezaji wa kanuni ya thuluthi mbili za kijinsia kama inavyokokotezwa na katiba.

Uchaguzi huo wa kihistoria uli-toa matumaini makubwa kwa wan-awake na wapiganiaji usawa wa kijin-sia, katika eneo lililofahamika hapo awali kuwa lisilowaruhusu wanawake kumiliki nyadhifa za uongozi.

Kinyume na sehemu nyingine za nchi ambako uchaguzi wa mabaraza hushindaniwa vikali huku madiwani wakipelekwa safari na madiwani wa-naopinzana kwenye ungángánizi wa viti vya uenyekiti wa kamati tofauti. Katika kanda ya kaskazini wagombea-ji hutafuta ridhaa ya wazee wa kijamii kufanya hesabu za kimbari ili kugawa-na nyadhifa zinazogombaniwa.

Kwa mfano katika kaunti ya Mandera, ilimlazimu kijana mmoja kujiondoa ili kumpisha aliyekuwa mwenyekiti hapo awali kinyume cha matakwa ya wengi wa madiwani wa mbari hiyo.

Wakati walipoachwa kungángánia nyadhifa za wenyeviti wa kamati, kwenye mkutano uliofanywa usiku uliofuatia, wazee hao wa mbari wa-liwalazimisha madiwani kumchagua aliyekuwa mwenyekiti hapo awali wa wadi ya Kutulo Kaskazini kuliongoza baraza hilo kama mwenyekiti wa kip-indi cha pili. Madiwani hao wanawake wakati wa asubuhi walifanya mapin-duzi baridi na kususia uchaguzi huo kwa muda mnamo siku ya uchaguzi hadi wasiwasi wao wa uwakilishi wao wa kijinsia ulipotiliwa maanani.

Baada ya zaidi ya saa moja ya mashauriano, madiwani hao wan-awake walifanikiwa kupata viti katika kamati muhimu ya mazingira na afya ya umma, baada ya diwani mwa-

naume kujiondoa kwa manufaa ya wanawake hao.

“Changamoto zinazowakabili wanawake kwenye nyadhifa za chini zaidi za kiuchaguzi kwenye mabaraza ya kaunti zilionekana kama kifungua macho kwa matatizo yanayowakabili katika kufanikisha kile ambacho kati-ba mpya imewatengea wanawake ka-tika kanda hiyo,” akasema Habiba Is-saq ambaye ni mtaalamu wa mambo ya kijinsia.

Issak ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Habiba Interna-tional Women and Youth Affairs, shirika lisilo la serikali lenye makao yake mjini Mandera, anasema ku-kabiliana na sheria za kienyeji am-bazo hazijaandikwa, ambazo zinali-fanya kuwa hatia kubwa tendo la kuwashirikisha wanawake kwenye mamlaka ndiyo kazi kubwa inayowa-kodolea macho wale wanaotaka kuo-na idadi ya wanawake ikiongezeka kwenye nyadhifa za kiuchaguzi.

Zainab Ithifle ambaye zamani alikuwa diwani maalumu na am-baye aligombea kiti cha Bunge cha Lagdera, alisema changamoto kubwa zaidi inayowakabili wanawake kwe-nye harakati za kuongeza idadi yao kwenye nyadhifa za kiuchaguzi iko kwenye vyama vya siasa ambavyo alivilaumu kwa kuwanyima wan-awake nafasi ya kuwa wapeperusha bendera wa vyama hivyo katika mae-neo hayo ya wafugaji.

Ithifle anaeleza: “Kwa kuimarisha elimu ya umma kuhusu maswala ya kijinsia katika kanda hiyo,mengi yanaweza kufanikishwa katika kuimarisha uwakilishi wa wanawake katika nyadhifa za kiuchaguzi na za kiuteuzi.”

“Katiba mpya inatoa kima fulani cha nyadhifa za uteuzi kwenye mam-laka makuu kwa wanawake kwa ku-toa thuluthi moja na hilo litawezeka-na wakati wanaume waliojaa uongozi wa kisiasa watabadilisha nia zao.”

Kwenye uchaguzi mkuu wa 2007, kati ya wanawake 300 walioeleza nia ya kugombea viti vya udiwani, ni wawili tu, Rukia Abdille Abdullahi wa wadi ya Laghbokol Kaskazini ka-tika Kaunti ya Wajir na Hani Has-san Hussein wa wadi ya Fino katika Kaunti ya Mandera, ndio walioch-aguliwa. Wengi wa wanawake walion-dolewa kwenye mchujo wa viongozi wa mbari wakipendelewa wagombezi wanaume licha ya kuwa maarufu mi-ongoni mwa wapiga kura.

Kaunti ya IjaraHuko Wajir kati ya madiwani 64

katika kaunti ya sehemu hiyo, kuna wa-nawake sita tu madiwani ambapo kati ya hao watano walichaguliwa kupitia vyama vyao. Katika kaunti ya Man-dera, kati ya madiwani 54 kuna wan-awake wanne pekee, watatu wakiwa ni wateule na mmoja aliyechaguliwa. Mji wa Mandera una diwani mmoja mteule kati ya madiwani kumi.

Katika kaunti ya Garissa ambayo ndiyo makao makuu ya kanda ya Kaskazini Mashariki na ambayo ina-chukuliwa kuwa iliyoendelea zaidi, kati ya madiwani 43 ni diwani mmoja pekee mwanamke, na katika baraza la mji wa Garissa hakuna mwanamke hata mmoja kati ya madiwani wanane wa baraza hilo. Katika kaunti ya Ijara, kuna diwani mmoja mwanamke kati ya madiwani kumi.

Abdullahi ambaye hali yake ni ya kipekee alipata kuchaguliwa kupi-tia kwa mbari yake na kuchaguliwa diwani kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Anasema matumaini ya wanawake katika kanda hiyo ya wafugaji kufurahia mafanikio yanay-otokana na katiba mpya ni haba kwa sababu ya uwezo mkubwa wa baraza la wazee ambalo huwaidhinisha wag-ombea uchaguzi.

“Ni vigumu siku zote kwa mwa-namke kupata mtu wa kumsikiza kwenye baraza la wazee linalotoa maamuzi kuwashawishi na kuwael-ezea ajenda yako na maono ya watu,” akasema Abdullahi. Akaongeza; “Wakati utakapopata mtu wa ku-

kusikiza kwenye baraza la wazee la mbari yako, huwa ni kibarua kigumu kwao kupendekeza jina lako kwa mbari nyingine ili kukuunga mkono, kwa sababu kupendekeza jina la mwa-namke ni sawa na kuwa na utovu wa nidhamu. Kwa hivyo, hilo linamfanya mpinzani wako wa kiume kupewa kipaumbele kwenye makabiliano ya kiuchaguzi.

Hata hivyo, Abdillahi ana matu-maini kwamba dhamira ya mabaraza hayo ya wazee kumpendekeza yeye na na mwenzake kutoka Wajir kwa nya-dhifa hizo za wenyekiti wa kamatini dalili ya kuondoka kwenye msimamo mkali wa kuwabagua wanawake.

Anasema: Ingawa bado tuko nyu-ma ya sehemu kama vile Mumias, Muranga na Bomet ambako wan-awake waliweka historia katika maba-raza yao, mwanasiasa huyo anaamini kwamba enzi zile ambapo wanawake walikuwa wakichukuliwa kuwa wa-piga kura zimekwisha, wao pia sasa wanakuwa wagombea viti.

Huko Mumias, Lillian Osundwa wa wadi ya Township, aliwabwaga wagombezi wanaume na kuchagu-liwa meya na huko Murangá, Mary Wanjiku Kimwe wa wadi ya Njogu-ini kadhalika alichaguliwa meya bila kupingwa. Huko Bomet eneo ambo wanaume wametamalaki mambo, diwani wa Songorwet Joyce Korir alishangaza kwa kuchaguliwa meya baada ya kuwabwaga wapinzani wa-naume kwenye uchaguzi wa manis-paa uliokuwa na ukinzani mkubwa.

“Hatua hiyo ni dalili wazi kwamba viongozio hao wa mbari sasa wa-naimini kwamba wanawake hufanya vyema katika “mamlaka ya uongozi kuliko wanaume,” akakariri Abdillahi.

Kuhama“Walipata kwamba huku wa-

nasiasa wengi wanaume huhamia mijini na jamaa zao baada ya kuch-aguliwa, viongozi wanawake hubaki miongoni mwao katika hali ngumu na hali nzuri,” alisema Korir kwenye mahojiano.

Abdullahi Ahmed mwenye umri wa miaka 67 ambaye ni mzee kutoka Wajir ambaye ni miongoni mwa wale waliopigania kuidhinishwa kwa wa-nawake kupewa nyadhifa kwenye mkutano wa mbari kabla ya uchaguzi wa baraza la Wajir, waliwachagua vi-ongozi wanawake kuongoza kamati za uhasibu wa ndani pamoja na maz-ingira na afya ya jamii.

“Baraza letu (Wajir) lina matatizo ya usimamizi wa pesa. Kumekuwa na malalamiko ya pesa za baraza kutumi-wa vibaya na madiwani wanaume

yaelekea hawana ustadi wa kazi au wameshirikiana na maafisa wakuu kupora pesa,” akasema Ahmed.

Alieleza kwamba; “Tuliamua kumjaribu mwanamke kulinda ma-pato ya baraza letu pamoja na maz-ingira, usafi na afya ya jamii. Tulipata ya kwamba wanaweza kufanya vye-ma zaidi kuliko madiwani wanaume. Sisi kama wazee sasa tunashauriana kuona iwapo tunaweza kuwapa wan-awake wetu nafasi katika nyadhifa za ugavana na ubunge.”

Kubadilisha fikra za kitamaduni za wanawake wenyewe, ambao ndio wengi kati ya wapiga kura ndilo tati-zo kubwa kwa mtu yeyote anayetaka kugombea viti vya kiuchaguzi.

Kulingana na Halima Osman mwenye umri wa miaka 54 wan-awake hawapaswi kupigania uongozi isipokuwa awe ni mjane, aliyepewa talaka au ambaye hataki kuwa na familia.

UsawaUongozi na kiuchunga familia ni

kazi zinazohitaji kujitolea kwa dhati na haiwezikani kwa mtu kufanya usawa katika kuhudumu kama kiongozi na wakati huo huo kutunza mume na watoto. Ni lazima ujitolee katika jambo moja na jukumu la kuangalia mume na watoto halipasi kuwekwa kando kwa sababu ya kazi,”asema Osman.

Kwa dhana hiyo, wanawake am-bao ndio wengi kati ya wapiga kura na wenye kuaminika katika sehemu ambayo viwango vya watu wasiojua kusoma na kuandika ni asilimia 80, hiyo ni changamoto kubwa inay-owakabili wanawake wanaodhamiria kugombea nyadhifa za uongozi ka-tika kanda ya Kaskazini.

Abdillahi anasema wanawake hasa katika kanda ya Kaskazini Mashariki ni lazima wawe na ujasiri wa kutosha kukabiliana na vizingiti vya kitamaduni ambavyo vinapun-guza uwezo wao wa kuchaguliwa kwenye nyadhifa za uongozi kwa kuthibitisha talanta zao za uongozi. Anasema kwamba inawalazimu kuonyesdha umahiri wao wa uongozi kwa vyama vyao kabla ya kutafuta kura kutoka kwa vyama hivyo.

Diwani huyo maalum anasema mara nyingi hafahamishwi mazung-umzo ya shughuli za baraza na katika jitihada za makusudi za kumfungia nje ya majadiliano hayo, madiwani wanaume huendesha mikutano yao wakati wa usiku na kufikia maa-muzi muhimu ya baraza, ambapo yeye kama mwananchi mwingine wa kawaida hupata habari zake wakati watu wanapoyajadili.

Wanawake watwaa viti vya manufaa vya mabaraza

“Mara nyingi imekuwa vigumu kwa mwanamke kutegewa sikio kwenye baraza

la wazee kumwezesha kuuza ajenda yake kwa

wanaanchi.” — Rukia Abdile Abdullahi

Mbunge wa Gichugu, Bi Martha Karua (wa pili kushoto) akiwa na akina mama wa mkoa wa Kaskazini Mashariki alipopeleka kampeni yake ya kujipigia debe ya uraisi katika sehemu hiyo. Kwa mara ya kwanza

Katiba mpya imewawezesha akina mama katika eneo hilo kupata nyadhifa kwenye mabaraza ya kounti. Picha na: Adow Ina Kalil.

Page 7: Mwanamke Mkenya Toleo 20

7 Toleo Namba 20 • Agosti 2011

Na Issa Haroun…

Wanawake katika kanda ya Kaskazini Mashariki wanataka kuwe na mabadiliko ya kifikra miongoni iwa jamii ya wafu-gaji wa sehemu hiyo ili kuwaunga mkono

wanawake katika jitihada zao za kupigania mamlaka ya uongozi.

Viongozi wa wanawake wanasema licha ya katiba mpya kuhimiza wanawake kutwaa nyadhifa za uongozi, kwenye mikutano kadha ya kisiasa iliyoandaliwa na wa-zee wa kijamii hususwan kuwaidhinisha wagombezi wa-naotaka kuwania viti vya ugavana, useneta na ubunge, wanawake hawashirikishwi kwenye majadiliano.

Rukia Abdille mwanamke wa pekee kuchaguliwa diwani kwenye uchaguzi wa madiwani wa Wajir katika wadi ya Laghbogol, aliwashauri wanawake wa Kaskazini Mashariki wajitokeze kutoka kwenye usingizi mkubwa na kupambana na wanaume kutafuta mamlaka ya uongozi.

Abdille aliweka historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa diwani kutoka Wajir. Ndiye mwanamke wa kwanza kuchaguliwa diwani katika seh-emu hiyo tangu nchi hii ilipojinyakulia uhuru.

“Ni kama kwamba nilikuwa nimeenda kinyume cha desturi na utamaduni. Tatizo kubwa lilikuwa ni ku-washawishi jamaa zangu kwamba nataka kuwania kiti cha udiwani,” akasema Rukia ambaye anajulikana kwa jina maarufu la Rainbow.

“Ili mtu atafute hatamu za uongozi katika jamii ya Wasomali, jamii ni lazima itoe pendekezo kwa mbari ambao kisha watajitwika jukumu la usimamizi na kuwas-ilisha pendekezo lao kwa mbari nzima ili kuidhinishwa,” akaeleza Rukia.

Kwa muundo huo wa kijamii Abdille akapambana na kiunzi cha kwanza. Jamaa yake haikupendelea, wakiona kuaibika kutoa jina la mwanamke kwenda kugombea mamlaka ya uongozi.

“Ilinichukua miezi miwili kuwashawishi jamii yangu na kuwasilisha pendekezo langu. Niliwatumia wanawake kadha kuzungumza na waume zao ili waniidhinishe na nikafanikiwa licha ya kukaribia kukata tamaa,” akasema.

Matajiri kadha kutoka ukoo wake walikasirishwa na hatua hiyo na wakatumia mamilioni ya pesa kufanya kampeni ya kuzuia watu kumpigia kura na badala yake kuwapigia wapinzani wake wanne, hata hivyo, yeye ndiye aliyekuwa mshindi.

Diwani huyo alianzisha kampeini ya kumsomesha mtoto wa kike na kupigania haki za wanawake huku aki-wa amekaa peke yake miongoni mwa madiwani wengi wanaume. Ni kupitia uchaguzi mdogo wa hivi majuzi ndipo alipopata mke mwenzake katika baraza hilo.

Kura za hurumaMwanamke mwengine alichaguliwa baada ya katiba

mpya kwenye uchaguzi mdogo baada ya mumewe ku-fariki dunia. Mumewe alikuwa diwani wa wadi ya Tarbaj. Kaltuma Sheikh alichaguliwa na anajiunga na wanawake walioweka historia katika kanda ya Kaskazini Mashariki.

Katika kaunti za Garissa na Mandera, kwa sasa haku-na viongozi wanawake kwenye mabaraza. Wote waliteu-liwa na vyama vikuu vya kisiasa.

Kanda ya Kaskazini Mashariki imeweka drekodi ya kuwa eneo la pekee ambalo halijawahi kumchagua mbunge mwanamke tangu nchi hii ilipojinyakulia uh-uru. Mbunge wa kwanza mwanamke kutoka Kaskazini Mashariki ni Sophia Abdi ambaye aliteuliwa na chama cha ODM.

Doris Wangeci ni miongoni mwa wanawake kadha wa-liogombea viti vya udiwani mjini Garissa bila mafanikio. Hivi majuzi alijiunga na kundi la harakati za wanawake linalopigania utekelezaji wa haraka wa katiba mpya.

Kundia la wanawake la harakati za kupigania maslahi ya wanawake mjini Garissa limeelezea wasiwasi wake kuhusu utekelezwaji pole pole wa katiba mpya.

Wakizungumza chini ya udhamini wa kundi la upi-ganaji haki za wanawake la kaunti ya Garissa, wanawake hao walisema utekelezwaji pole pole wa katiba unatia wasiwasi, huku tayari ukiwa umecheleweshwa mnio. Walitoa mwito kwa Rais na Waziri Mkuu kuingilia kati kwa dharura.

Tulipiga kura kwa kauli moja kuiunga mkono katiba hii kama wanawake kutoka Kaskazini Mashariki kwa matumaini kwamba tutashuhudia mwanamke wa kwanza kiongozi kuchaguliwa kutoka sehemu hiyo, kwa vile katika siku zilizopita wanawake walifungiwanje ya nyadhifa za uongozi na kauwaacha wanaume wakitamalaki mamlaka ya uongozi,” likasema kundi hilo la Yustur Farah.

Kundi hilo liliwahimiza wanawake kote nchini ku-ungana na kupigania utekelezaji wa haraka wa katiba, likieleza wasiwasi kwamba nchi hii huenda ikatumbukia kwenye ghasia kama tutashindwa kuharakisha utekeleza-ji wa katiba.

Wanawake wa kanda ya Kaskazini Mashariki wahimiza

mabadiliko ya kifikraNa Omwa Ombara…

Wakati Diwani Elizabeth Ow-ino mwenye umri wa miaka 50 alipojibwaga katika uwanja wa kisiasa mnamo mwaka wa

2006, alikuwa na ndoto pana kwa niaba ya akina mama wanaoishi kijijini mwake.

Kilichokuwa kikimhuzunisha ni kile alichokitaja kama kutojua miongoni mwa akina mama wanaoishi katika kaunti ya Sia-ya kwa jumla. Alijiahidi na kuapa kwamba pindi tu atakapoingia ulingoni mwa siasa, atabadilisha hali ya maisha yao kutoka kwe-nye umasikini unaothiri hadi ule wa matu-maini katika maisha yao ya baadaye. Jinsi alivyoshuhudia wanawake wakibaguliwa hali kadhalika watoto, hali hiyo ilimpa mo-tisha ya kujibidiisha zaidi kufikia malengo hayo yake.

“Niliona kwamba kulikuwa na mengi ambayo akina mama pale kijijini hawakuwa na habari kwa yale yaliyokuwa yakiendelea ama yale ambayo hayakuwa yakiwafikia kwa njia za habari. Nilianza kujiuliza, je, nitawa-hamasisha kwa njia gani? Hii hasa ni kwa sababu hawakujua haki zao. Si ajabu pale kijijini mwangu wanawake wengi walikuwa wakipigwa na waume wao, kasha asubuhi kulazimishwa kuwatayarishia waume hao hao kifungua kinywa. Yaani ukiukaji wa haki za kibinadamu kwa wanawake miongoni mwa waume katika kaunti ya Siaya, ni kama mtindo unaokubalika,” akalalamika Owino.

Kurithiwa mumeElizabeth analalamika kwamba hali

huwa ni mbaya zaidi kwa mwanamke am-baye mumewe ameaga dunia, yaani mjane. Ni jambo la kawaida kwamba mama huyo kimila ni sharti kurithiwa . “utamaduni huo kwangu mimi ni kama ulipitwa na wakati kwa sababu wanawake wengi waliofiwa na waume wao, hawapendi kabisa tendo hilo eti kwa vile wao huambiwa kwamba ili wa-jiepushe na chira waona watoto waoni sharti kurithiwa ama sivyo eti jamaa yao nzima itapata laana. Mimi kamam Elizabeth Ow-ino, siamini hayo,” alisema.

Mambo hayo yalimfikia peupe hivi majuzi wakati kundi fulani la vijana wal-imshambulia ndani ya jumba la kuhesabia kura la Baraza la Wilaya ya Siayawakisema kwamba kwa vile yeye alikataa kurithiwa, ndiyo sababu ya yeye kutoweza kupigania uongozi wa kiti cha juu cha kisiasa.

“Jamaa mmoja alinijia na kisu huku ak-ipiga makelele akisema eti kwa vile nilikataa kurithiwa wakati mume wangu alipofariki, basi ningali nimebeba ch hivyo ni sdhati eti nisafishwe kabla sijakuwa kiongozi. Wewe utawezaje kutuongoza na hali bado um-ebeba chola? Niliweza tu kujinusuru wakati nilipokimbia na kwenda kujifungia ndani ya choo kilichokuwa hapo karibu. Hata hivyo, walinifuata na hata kujaribu kuninyonga. Mwishowe walifanikiwa hata kunipiga.”

Huu ndio uhuhuda kamili ya Diwani Elizabeth Owino wa Baraza la Wilaya ya Siaya baada ya uchaguzi wa majuzi wa ua-niaji wa kiti cha mwenyekiti wa baraza hilo. Ghasia za uchaguzi ulioshuhudiwa dhidi yake ulidhihirisha wazi kwamba wanaume wengi hawako tayari kuona akina mama nao wakipigania nyadhifa za uongozi kama ilivyoratibiwa katika katiba mpya.

Yale ambayo Elizabeth aliyashuhudia kwa kweli yanaenda kinyume cha haki za kisiasa katika Katiba mpya chini ya Kifungu 38 (30 (c) kinachosema na kueleza: “ Kila mwananchi mzima ana haki, na bila kizuizi chochote kile kuzuiwa kuwa mgombezi kupigania afisi ya umma, ama hata afisi ka-tika chama cha kisiasa ambacho mwananchi kama huyo ni mwanachama na angeweza kuchaguliwa.”

Katiba hiyo hiyo inaendelea kueleza ka-tika Kifungu 28. “Kila mtu ana haki za kim-singi kuheshimiwa dhidi ya yale anayotaka kufanya bila kuingiliwa kwa njia yoyote ile pasipo na sababu maalumu ya yeye kuny-imwa haki hizo zake ambazo pia zinapaswa

kulindwa wakati wote.”Na Katiba inakairi nguvu zake zaidi kwa

kueleza chini ya Kifungu 2 (4) kwamba: “She-ria yoyote ile ikiwa ni pamoja na za kiutama-duni na ambayo huenda inahitilafiana nah ii katiba, haitatambuliwa kwa hivyo mbele ya sheria iliyopitishwa, ni sharti kuambatana na y ale yaliyopitishwa na wengi kisheria inay-opaswa kufuatwa wakati wote.”

Ukiukaji ule wa haki za kimsingi ulioshuhudiwa wilayani iaya dhidi ya Di-wani Elizabeth Owino ni dhihirisho tosha kwamba akina mama wengi bado hawa-heshimiwi kama ipasavyo kwa vile wanan-yanyaswa ili wasipiganie viti vya kisiasa ambavyo kwa kweli ni haki yao kikatiba na hasa ikitiliwa maanani kile kifungu cha theluthi tatu ya viti vya uongozi kama vile katiba mpya inavyosisitiza.

Kisa hicho cha Elizabeth Owino ni mfa-no mzuri wa kile wajane wengi watakabili-ana nao kutoka kwa wapinzani wa kiume na hasa wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 1212 ambapo porojo nyingi pia zitatukuzwa dhidi ya wanawake na hasa wale ambao kwa bahati mbaya aid-ha ni wajane ama pengine wametalakiwa. Haitakuwa ajabu kupata kwamba wapinzani wao wa kiume watafanya kila wawezalo, juu chini, kuhakikisha kwamba wanawafungia

milangona njia za kuwaelekeza kwenye viti vya uongozi.

Akihojiwa na jarida hili, Elizabeth yeye hatababaishwa kamwe wala kudhulumiwa na wapinzani licha ya kwamba alipoteza kesi dhidi ya wapinzani wake baada ya ku-washtaki kwente Mahakama Kuu ya Kisumu mnamo Agosti 9.

“Mimi ninaona mwangaza ambao ni wakwa akina mama wa Siaya ambapo nia yangu ni kuwatumuikia wanawake wa Siaya ili kwamba wakati nitakapoondoka, nitaku-wa nimewafanyia mengi kuliko nilivyopata awali,” akaahidi Elizabeth.

Yeye amekuwa diwani wa wadi ya Jera tangu mwaka 2008 aliposimama kwa kiti hicho dhidi ya waume wanane na hatimaye kuwabwaga wote. “Nilipata kura asilimia 90 ambao waume hao wanane, kura zaom ziki-wekwa pamoja, ndiyo hiyio asilimia kumi waliyopata,” akaeleza Elizabeth kwa furaha akisema wakati huo hapakuwepo na ghasia wala fujo kwani nyingi ya kura pia nilizo-pata zilitoka kwa wanaume ijapokuwa wale wapinzani wangu wa kiume walikuwa waki-niuliza ni dawa gani niliyotymia kuwavutia wapiga kura wengi wa kike.

ZilipounganishwaUshawashi wa kisiasa ulianza kwa Eliza-

beth kutoka kwa kanisa moja nyumbani Sia-ya. Hakutaka kuwa sembuje anayekaa bura asijue la kufanya baada ya mumewe kuaga dunia. Ijapokuwa hali ya umasikini iliku-wa imethiri sana mle kijijini ambapo hata kanisani waumini waliwajibika kuja na stul za kukalia wakati wa ibada, Elizabeth ali-chukulia jambo hilo kama funzo kwani baa-dhi ya waumini ambao hawakuweza kuja na stul kanisani aidha walisimama wakati wa kipindi kizima cha ibada ama sivyo kukaa sakafuni ya udongo wakati huo wote.

Wakati kaunti zilipounganishwa kutoka tarafa za Gem, Alego na Ugenya kuunda Kaunti ya Siaya, Elizabeth alijipata katika hali ya kaha li ya kuwashawihi madiwani 29 wa mabaraza hayo ya awali wamchague kama mwenyekiti.

Baadhi ya mabnadiliko ambayo Elizabeth angependa kuona yakitendeka katika baraza jipya la Kaunti ya Siaya ni utumizi wa uwazi wa pesa zinazotokana na Local Author-ity Transferr Fund (LATF) akieleza kwamba kaunti hupokea Sh700,000 mara tatu kwa mwaka kuhudumia miradi katika miezi ya Oktoba, Februari na Mei, mbali na kiasi kingine cha Sh2.1 milioni kila mwaka.

Anawashukuru akina mama wengi am-bao wamempa misaada kadha wa kadha hapo akitaja baadhi yao kama vile Kamish-na Rozah Buyu,Prof Jacquiline Oduol, Mheashimiwa Millie Odhiambon na Bi Ruth Odinga.

Juu: Hapa mmoja wa wagombezi wa kiti cha mwenyekiti wa Kaunti ya Siaya akisindikizwa na wafuasi wake wakati wa kwenda kujiandikisha kwenye uchaguzi wa hivi majuzi katika sehemu hiyo. Chini: Huyu ndiye Diwani Elizabeth Owino wa wadi ya Jera

ambaye naye alikuwa akikemezea mate kiti hicho wakati huo.

Nilipata kura asilimia 90 ambapo wapinzani

wangu wanane wanaume wakapata kura asilimia 10 kwa pamoja. Wakati

huo hapakuwepo na fujo ambapo wanaume wengi pia waliniunga mkono

— Elizabeth Owino, Diwani wa Jera kaunti ya Siaya

Katika Siaya akina mama wabaguliwa kunyakua vyeo

Page 8: Mwanamke Mkenya Toleo 20

8 Toleo Namba 20 • Agosti 2011

Mijikenda walilia haki za ardhi

Na Fibi David…

Jamii ya marehemu Mzee Nyanje Chula babu ambaye alikuwa ameoa wake wawili aliyek-ufa zaidi ya miaka kumi na mitano iliyopita, bado haijatambua uhalisi wa katiba mpya.

Kavumbi Nyanje mwenye umri wa miaka 40 ambaye ni mwana wa pili wa mke wa pili wa Mzee Chula, daima amekuwa akilalamika kwamba anabaguliwa na ndugu zake wa kiume wa mke wa kwanza kuhusiana na mali ya baba yao na hasa ardhi.

Kavumbi aliozwa mume wakati baba yake alipokuwa yungali hai na baadaye kutalikiwa lakini ilimlazimu kungángána yeye peke yake, kurejesha mahari ili apatwe sehemu ya ardhi ya baba yake.

Tangu hapo amekuwa akiishi katika ardhi hiyo ya baba yake na amekuwa akipambana kumlisha mama yake mjane ambaye pia ndiye mke aliyebaki wa baba yake kwani mke wa kwanza aliaga dunia hapo awali.

Kavumbi ndiye mtoto aliyesalia kwa upande wa mama yake baada ya kaka yake Kadhaa Chula kuua-wa na mamba katika mto miaka mitano iliyopita.

RidhaaNimepewa shilingi sabuini pekee na kaka

zangu kumsaidia mama yangu ambaye anah-angaika, tangu niliporejea nyumbani kwa baba, alalamika Kavumbi. Anaongeza; “Nilipokea pesa hizo baada ya kulalamika vikali kwa miaka kumi kwamba bado ni mmoja wa jamii hii kwa vile nililipa mahari yaliyolipwa ili niolewe.”

Akaeleza Kavumbi; “Kaka zangu wanacho-ma makaa ya thamani ya maelfu ya pesa amba-zo wanajigawia wao kwa wao wakinisahau mimi na mama yangu.”

Wazo la kurithi kipande cha ardhi kutoka shamba la wazazi wake ni ndoto isiyoweza kutimia, “sababu ni kwamba mimi ni mwana-mke na mwanamke hana haki katika jamii, ya kudai mgawo wa mali ya jamii.

“Urithi! Hilo ni jambo lisilowezekana. Nina hakika nitafukuzwa nyumbani na kaka zangu wakati nitakapoonyesha nia ya kutaka kipande cha ardhi. Ardhi ya jamii siku zote ni ardhi ya wanaume na siwezi kuzungumza juu ya swala hilo. “Hii katiba inawadanganya wanawake wawe vyombo vya kuhangaishwa na kuteswa na jamaa zao majumbani mwao,” Kavumbi asema.

Ni dhahiri kwamba katiba haijapenya mash-inani katika taifa hili. Watu bado wamekita ka-tika sharuti za kitamaduni.

Serikali ni lazima itekeleze jukumu kubwa katika kuandaa elimu ya kijamii ili kuwaelim-isha jamii juu ya hali zao za kikatiba.

Kavumbi hayuko peke yake katika swala hili. Wanawake miongoni mwa makabila ya Mijik-enda, wanaliona jambo la kurithi ardhi katika jamii hiyo kama ndoto za mchana.

Wanawake hawa wanadai kwamba hawajao-na manufaa yoyote katika haki ya kumiliki ardhi na usawa wa kijinsia kama inavyoeleza katiba mpya kwa vile utamaduni na desturi za kijamii bado zinawabagua.

Umiliki ardhi“Wanawake chipukizi ambao bado wako

chini ya umri wa miaka thelathini huenda wakabadilisha mitindo yao ya maisha na kunu-faika na katiba mpya kwa vile wanawake ambao wamekuwa watu wazima tayari wamepitwa na wakati.”alisema Naomi Cidi Kumbatha, kion-gozi mwanamke kutoka jamii ya Mijikenda.

“Wanawake wenye umri mkubwa wamekita fikra zao katika utamaduni wa kuwaachia wa-naume kufanya kila jambo,” aeleza Kumbatha huku akiongeza kwamba wanawake hao wa-naamini kwamba haki nyingi ni za wanaume.

“Wanawake watu wazima hawana uwezo kitamaduni kurejea kwa wazazi wao na kudai haki zao za umiliki wa ardhi,” akaeleza kiongozi huyo wa kutetea maslahi na matakwa za akina mama mkoani Pwani.

Kwenye mswada wa haki kifungu cha 27 juu ya usawa na kutobaguliwa (sehemu ya tatu) ya katiba inasema: “Wanawake na wanaume wana haki ya kutendewa kwa usawa, ikiwa ni pamoja na haki ya nafasi sawa katika mambo ya kisiasa, uchumi, utamaduni na sekta za kijamii.”

Kifungu cha 27 (4) kinasema: “Serikali haita-mbagua kwa njia moja au nyingine mtu yeyote katika misingi yoyote ikiwa ni pamoja na asili ya mtu, kijinsia, uja uzito, kuoa au kuolewa, hali ya afya, asili ya kijamii , rangi, umri, ulemavu, dini, imani, utamaduni, mavazi, lugha au uzazi.”

Licha ya kanuni hizo, inatia hofu kwamba watu wa umr ihuu ambayo imefungamana na tamaduni zao huenda wasinufaike na haki za kumiliki ardhi kama inavyohakikishwsa na katiba.

“Tunaitarajia katiba mpya kutoa mamlaka kikamilifu mwaka ujao baada ya uchaguzi mkuu wakati viongozi wa nchi hii watakapokuwa wakishughulika na utekelezaji thabiti wa katiba,” alitumai Kumbatha.

Utamaduni wa Kimijikenda siku zote um-ewazuia sana wanawake kuchukua nyadhifa za

utoaji maamuzi miongoni mwa jamii hiyo.Mzee mmoja wa Kayafungo katika eneo la

Kaloleni kaunti ya Kilifi na mshauri wa jamii ya Mijikenda, Babu Katana Kalulu, mwenye umri wa miaka 80 anaipinga katiba mpya akisema in-avunja haki za kitamaduni za jamii hiyo. Mzee Kalulu anadai kwamba katiba imeenda kinyume na utamaduni wa Kimijikenda.

“Mabinti zangu hawana wawe wameolewa au la, hawawezi kuwa na haki ya kurithi ardhi yangu. Hafai kugawanyiwa ardhi hiyo hata ki-dogo. Kama kiongozi katika jamii hii, huenda nikaishia kulaaniwa na miungu yetu wakati nitakapotoa ardhi kwa mtoto wa kike,” akalala-mika Kalulu..

Akiwa mzee maarufu wa Kigiriama na ki-ongozi wa kiimani, Mzee Kalulu ana wajibu wa kuongoza ibada katika sherehe zozote za kita-maduni wanazoandaa wana Mijikenda.

Mzee Kalulu ni mwanachama wa chama cha

kitamaduni kinachojulikana kama Malindi Dis-trict Cultural Association (MADICA).

Chama cha MADICA kimekuwa kikiongoza katika kupigania utamaduni wa Kimijikenda na kudumisha kitambulishi cha kitamaduni cha jamii hiyo hapa nchini na katika nchi za nje kupitia Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu (KNCHR).

Katiba imeweka wazi usawa wa kijinsia na umilikaji kuwe na utamaduni au usiwepo.

Wanaume sasa waweka vizingiti kwa ugawaji ardhi kwa wanawakeNa Omwa Ombara…

Ramadhan Ibrahim Onguto mwenye umri wa miaka 69 ni mwenye hasira. Ingawa alipiga kura kuiunga mkono

katiba, anaapa kwamba hakuipigia kura katiba hiyo ili wanawake wapewe ardhi.

Jambo linalozidi kuudhi kulin-gana na Onguto ni kwamba Serikali inathubutu “kunichukulia mimi kuwa sawa na wanawake hasa kuhusiana na masuala ya ardhi”.

Kulishughulikia“Tangu ulimwengu ulipoanza, jam-

bo hili halijatokea na nakuhakikishia ya kwamba halitatokea. Kwa kusema kweli sintawapa watoto wangu wa kike haki sawa ya ardhi na wale wa kiume. Serika-li haiwezi kunilazimisha kufanya jambo kama hilo, isipokuwa iwe inataka vita. Hili ni swala hatari ambalo linaweza kusababisha maafa na hata vifo. Serikai inafaa kulishughulikia jambo hili kwa makini,” alisema Onguto.

Onguto ni msemaji wa kijiji na mzee wa kijiji anayeheshimika katika kijii cha Nyakoko huko Kano Kaska-zini katika kaunti ya Kisumu.

Ana hasira ka sababu Serikali haiheshimu desturi za kitamaduni ambazo tulizipokea kutoka kwa wazee wetu wa zamani. Anasema katiba mpya inawapa wanawake haki kwa mkono wa kulia na kuwanyang’anya wanaume haki zao kwa mkono wa pili.

Onguto tayari ameigawanya ardhi yake ya ukubwa wa ekari moja kwa wa-toto wake wa kiume na anasubiri hati yake ya kumiliki ardhi iwasili kutoka makao makuu ya Wizara ya Ardhi.

Akihojiwa na jarida hili kuhusu watoto alio nao, Onguto aliwataja wa-toto wake watatu wa kiume na hataji chochote kuhusu watoto wa kike.

“Ni jambo la kusikitisha kwamba mabinti zetu ambao tayari wame-olewa wanataka keki yao waile. Tayari wana ardhi ya kujenga , kulima na kuvuna . Kwa nini wapate ardhi ny-ingine kutoka kwa baba zao? Kwa nini warejee kutoka kule waliokoole-wa na kuja kung’ang’ania ardhi na ndugu zao wa kiume ambao pia wana wake zao na watoto?” akauliza Ong-uto. Aliongeza; “Hakuna mtu yeyote katika kijiji hicho ambaye ataruhusu jambo hilo lifanyike. Tutawapeleka mahakamani.”

Onguto hata hivyo, anakubali kwamba hatika hali ya matatizo am-bapo mabinti zake watafukuzwa na waume zao, hatawaacha wahangaike.

“NItawapa mabinti zangu wanao-pata taabu kipande kidogo cha ardhi wajenge hapo kwa sababu ya uhusiano wetu wa damu. Ninawapenda sana laki-ni kuwapa ardhi ni jambo tofauti. Siwezi kuwapa watoto wa kike ardhi yoyote. “

Kulingana na Onguto wanawake katika mpangilio wa kitamaduni hu-chukuliwa kama paka mwitu kwa sa-babu ya tabia zao zisizobashirika za ku-pata mimba wakiwa shule na kuvunjilia mbali matumaini ya wazazi wao baada ya kuweka raslimali katika elimu yao.

Jamii inaweza kuuza kipande cha ardhi ilicho nacho ili kupata karo za shule kuwasomesha kisha baadaye wanagundua kwamba binti yao si mja mzito pekee bali ametoroka na mwanaume ambaye hana msingi wowote wa kimaisha. Kwa kawaida mwanamume kama huyo hata kulipa mahari hawezi na wazazi huona ni kama kwamba wamedanganywa. Visa hivyo vimevuruga sana jamii nyingi na kupunguza thamani na heshima aliyokuwa akipewa mtoto wa kike.

“Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba binti aliyeolewa ambaye atarithi ardhi huenda akarithiwa au akaolewa upya na mtu asiyejulikana na mtu huyo akaishia kurithi aridhi yangu. Urithi wa wake bado unaende-lea na umekita mizizi katika jamii yetu na hii ndiyo sababu haikubaliki kwa wanaume wengi kuacha ardhi yao ku-rithiwa na wageni,” akasema Onguto.

Kwa katiba mpya aina ya vizuizi na hasira zinazotoka kwa Ongoto na wa-naume wengine wenye ardhi vitakuwa visa vitakavyosahauliwa. Katiba itaku-wa juu ya sheria zote za kitamaduni na imewapa wanawake uwezo na chombo cha kupigania haki zao za kumiliki ar-dhi. Si wanawake ambao wanalindwa na kuwa salama bali watoto pia.

Sehemu ya 27 na ya 60 ya katiba mpya iko wazi kwani inasema sasa ni kinyume cha sheria kumnyima ardhi mwanamke katika misingi ya kijinsia. Hakika haijalishi kama mwanamke ameolewa au la. Sheria inayosima-mia masuala ya kijamii inatilia nguvu msimamo huo wa kisheria ambapo inasema watoto wote watarithi ardhi kwa usawa bila ya kubagua iwapo mtoto ni wa kike au wa kiume.

Hiki ni kipande cha ardhi katika eneo la uwakilishi bungeni la Magarini mkoani Pwani na ambacho kama sehemu nyingine yoyote ile nchini Kenya, hata wasichana na wanawake wana haki a kupewa ardhi na wazazi wao.

Picha: Fibi David

“Bila shaka sitampa binti yangu yeyote kipande cha ardhi

yangu. Serikali haiwezi kunilazimisha kufanya hivyo, ila kama wako

tayari kwa vita.” — Ramadhan Ibrahim Onguto

“Kama mzee wa jamii ya Mijikenda, huenda

nikalaaniwa na miungu yetu iwapo nitatoa ardhi kwa

msichana.” — Mzee Katana Kalulu

Page 9: Mwanamke Mkenya Toleo 20

9 Toleo Namba 20 • Agosti 2011

Na Ben Oroko…

Wakati Mary Orwe-nyo alipostaafu kama mwalimu wa shule za msingi mnamo mwa-

ka 2008, ili kujiingiza katika ndoto yake ya kuongoza na kuwapa uwezo wanawake wa kundi la akina mama la Ritii katika kata ya Kiabonyoru ya kaunti ya Nyamira, haikumthubu-tukia kwamba alikuwa anajitupa kati-ka ulingo mpana wa mambo makub-wa katika majukumu ya uongozi wa wanawake na jamii.

Tangu kuchaguliwa kwake katika wadhifa wa mwandishi wa tawi la wilaya la Chama cha Maendeleo ya Wanawake (MWYO) mnamo mwaka 1991, matumaini yake ya uongozi yameimarika, na kwa sasa ni mwe-nyekiti wa chama hicho tawi la kaunti ya Nyamira. Kuimarika kwake katika sekta ya uongozi kunampa nafasi ya kuwa mmoja wa wanawake viongozi ambao wamo katika nafasi nzuri ya kutwaa nyadhifa zilizotolewa na kat-iba mpya.

Akihimizwa na maarifa yake ya uongozi, Orwenyo ametangaza nia yake ya kugombea kiti cha mwakilishi wa wanawake katika kiti katika kaunti ya Nyamira kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2012.

Mary alizaliwa mwaka 1953 katika kijiji cha Monga , Bomagacho katika eneo Bunge la Mugirango Magharibi katika kaunti ya Nyamira, akiwa ni mtoto wa saba wa Mzee Michael Kim-wei na Mama Susan Kwamboka. Ali-somea shule ya msingi ya Gekomoni huko Mugirango Magharibi kuanzia

mwaka 1962 hadi 1966 kabla ya ku-jiunga na shule ya msingi ya Rigena klatika sehemu iliyokuwa ikijulikana kama Wanjare Mugirango Kusini ka-tika kaunti ya Kisii kuanzia mwaka 1967 hadi mwaka 1969 ambako ali-fanya mtihani wa CPE.

Alijiunga na shule ya sekondari ya Nyanchwa Mixed High School mjini Kisii ambako alifanya mtihani wa kidato cha nne na kuibuka na hati ya daraja ya tatu yaani Div .III kabla ya kujiunga na chuo cha mafunzo ya ualimu cha Shanzu kwa mafunzo ya ualimu ya P1 kuanzia mwaka 1977 hadi 1979.

Baada ya masomo yake ya P1, Orwenyo alipelekwa katika shule ya msingi ya Nyangoge katika sehemu ya Mugirango-Borabu Kaskazini am-bako alisomesha katika shule kadha katika sehemu hiyo hadi alipostaafu mwaka 2008.

HarakatiKufuatia kushughulika kwake

kwenye harakati nyingi za wanawake nyanjani, aliongoza makundi ya akina mama ya jkijamii na makundi ya kujisaidia wenyewe ambako ali-panda mamlaka na kuhudumu katika Chama cha Maendeleo ya Wanawake katika nyadhifa mbali mbali kabla ya kupanda na hatimaye kuwa mwe-nyekiti wa tawi la kaunti ya Nyamira wa shirika hilo.

Mary anawataka wanawake wa-jinasue kutoka kwenye tamaduni za Kikisii ambazo kwa miaka mingi zimewanyima nafasi ya kuchukua nyadhifa za uongozi.

“Nimejiandaa kupigania wadhifa

wa mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Nyamira kwenye uchaguzi wa mwaka 2012 kwa vie ninaamini kwamba wanawake wana imani na uongozi wangu kwa vile imekuwa nikiwahudumia kuanzia mashinani hadi kwenye chama cha Maendeleo ya Wanawake,” akasema kinara huyo.

Nikichaguliwa kwenye mamlaka hayo, Orwenyo anasema, ataendelea kufuatilia kutimiza ndoto yake ya ku-hakikisha kwamba wanawake wana-kaa mahali wanapostahili katika jamii.

Kwenye mahijiano ya pekee na Mwanamke Mkenya, Orwenyo anasema ana imani na wanawake wa sehemu hiyo akisema wana vipaji vya uongozi na kama watapewa nafasi wanaweza kuleta mabadiliko ya kisia-sa na kiuchumi miongoni mwa jamiii na nchi nzima kwa jumla.

“Nilizaliwa na kulelewa katika vijiji, nikifahamu kwamba mahali pa mwanamke ni jikoni na kuwatunza watoto nyumbani,” akumbuka Bi Orwenyo.

Anaeleza; “Tangu wakati huo mengi yamepeperushwa na upepo na ulimwengu umepitia mabadiliko makubwa na kubadiisha jinsi mambo yalivyokuwa yakifanyika wakati wa uhai wa nyanya yangu.”

Anasema wakati umefika ambapo kila mwanamke anapasa kutumia na-fasi inayotolewa katika katiba mpya kuwapa amii zao uongozi wa kisiasa na uchumi wa kijamii na kuwapa uw-ezo wanawake na vijana ambao ndio walio aslimali kubwa zaidi ya kibina-damu nchini.

Orwenyo aliamua kujitupa ka-tika uongozi wa wanawake baada

ya kustaafu kazi ya ualimu baada ya kutambua kwamba akiwa darasani hawezi kupata nafasi ya kutangamana na kubadiishana maoni na marika yake ambao walihitaji uongozi wake katika ngazi za kijamii na majumbani.

Anasikitika kwamba wanasiasa wamekuwa wakitumia umaskini wa wanawake kwa miongo mingi na ku-tumiwa vibaya kwenye kampeini za kisiasa na kwenye uchaguzi.

Wanasiasa“Huwa naungulika moyo wakati

ninapowaona wanawake katika jamii wakiwa wamebeba watoto wadogo migongoni wakicheza mbele ya wa-nasiasa siku nzima wakati wa kam-peini za uchaguzi, kasha baadaye wanasiasa hao huwapa akina mama hao shilingi hamsini tu,” Orwenyo akalalamika. Akauliza; “Je, shilingi hamsini ni kitu gani kwa mwana-mke mwenye watoto wa kuwalisha kuwanunulia nguo na kuwapeleka shule?”

Aliwahimiza wanaume kutoka sehemu hiyo waonyeshe mwelek-ezo wa uongozi na kuwakataza wake zao kutumiwa vibaya na wanasiasa wakati wa kampeini za uchaguzi na badala yake, watafute mbinu za ku-wapa uwezo wanawake na wao we-nyewe kiuchumi majumbani mwao ili kuziba mapengo ambayo yatawafanya washawishike kwenda kutumiwa vibaya na wanasiasa.

“Ili nchi hii ifanikishe ruwaza ya mwaka 2030 na kufanikisha shabaha za millennia, wanawake wanapaswa kupewa uwezokatika sekta zote, “ akaeleza Bi Mary Orwenyo.

Harakati za ukombozi wa wanawake wa Gusii kwenye kifungo cha kisiasa

“Ili taifa hili liweze kufikia malengo

ya ruwaza ya 2030 na lengo la ustawi wa milinia, akina

mama sharti wapewe motisha kwa yote

wafanyayo .” — Mary Orwenyo

Shujaa mwenye azma ya kuingia katika BungeNa George Omonso…

Hebu fikira haya: Wewe ni mwanamke chipukizi na mwanasiasa, hujati-miza miaka 35, una jamii

changa. Uligombea uteuzi wa chama fulani cha kisiasa na kushinda lakini ukatolewa kwa hila kwa sababu wewe ni mwanamke.

Matokeo ya uchaguzi yanafutiliwa mbali na hati ya chama cha uakilishi anapewa mwanaume ambaye ulim-shinda kwenye uteuzi. Unapeleka malalamiko mahakamani. Rais mwe-nyewe anaingilia kati na anakwambia ujiondoe akisema; “Wewe bado mtoto mdogo.” kisha akwambie atakupa kazi.

Anang’ang’aniaJe, ungetetemeka na kutupilia

mbali jitihada zako za kutafuta haki? Je, ungekubali kupewa kazi nzuri , ukifikiria kwamba ulikuwa mfanyi bi-ashara ambaye awali ulikuwa umejiu-zulu kazi?

Hayo ndiyo masaibu yaliyompata Jeniffer Chekwemoi Masis miaka kumi iliyopita. Leo bado anang’ang’ania kutimiza ndoto yake ya kuwa Mbunge na sasa ameonyesha hamu ya kupiga-nia kiti cha Endebess kilichoanzishwa hivi majuzi.

Masis alikuwa ameshinda uteuzi wa chama cha Kanu na alikuwa anaji-andaa kupambana na wagombezi wen-gine katika kiti cha Bunge cha Kwanza. Alikuwa amewabwaga wanaume 14, wawili wakiwa ni wanasiasa shupavu, Michael Kitiyo na Mbunge Maalumu wa zamani, Samwel Moiben.

Hati ya chama ilikabiliwa Moi-ben kwa njia ya udanganyifu baada

ya madai na propaganda kwamba ja-mii hiyo bado haijakuwa tayari kuwa na kiongozi mwanamke hasa katika mamlaka ya Ubunge.

“Liliniuma moyo jambo hili la kunizuia kuwa mpeperusha bendera, katika misingi hiyo,” akasema Masis huku akibubujikwa na machozi.

Anakumbuka: “Nilipiga hatua kubwa mwaka 2007 wakati nilipogom-bea uchaguzi wa kiti cha bunge cha Kwanza ambacho sasa kimegawanywa mara mbii huku sehemu moja ikiwa ni eneo bunge la Endebess.”

Masis alikuwa amechapishwa kati-ka gazeti kuwa mgombezi wa ubunge

wa chama cha ODM Kenya. Wakati wa uchaguzi mkuu, Masis alipata kura elfu tisa na kushikilia nafasi ya pili.

“Haikuwa rahisi hasa ukifikiria kwamba mpinzani wangu mkuu ali-kuwa Dkt Noah Wekesa mtu ambaye ana raslimali na kisha ni waziri.”

Baada ya uchaguzi, mgombezi huyo ambaye alipata masomo katika shule ya Kibuk Girls kwenye miterem-ko ya Mlima Elgon, alirejea kwenye kazi yake ya huduma za jamii.

KuwakilishaKwa kuwa ajenda yake kubwa

ni kuwapa wanawake uwezo., Masis ambaye ni mwanaharakati wa kupi-gania haki za wanawake amesafiri na wanawake kupitia shirika la kibinafsi la Tears of Women, yaani Machozi ya Wanawake.

Si mshirikishi tu wa kongamano la wanawake katika uongozi katika kaun-ti ya Nzoia, bali pia naibu mwenyekiti wa Agenda ya Kitaifa ya Wanawake.

Masis anasema kundi la wazee wa Kisabaot kutoka eneo la Kwanza wali-iendea jamii yake kuiomba imruhusu kuwawakilisha. Kwanza alisita lakini wa-zee hao wakasisitiza, wakisema kwamba wamemjua kwa muda mrefu na wame-ona utenda kazi wake. Waliamini wazee hao kwamba Masis angekuwa kiongozi bora kwa jamii hiyo.

“Nilishangaa na nikaomba nipewe wakati wa kufikiria jambo hilo na ku-toa uamuzi na kisha kushauriana na jamii yangu na jamaa zetu kwa jumla,” akasema.

Maoni ya jamaa zake hayakuwa na msimamo mmoja isipokuwa kwa dada zake wawili, mumewe, baba yake na ndugu zake ambao walimuunga mkono kwa dhati.

“Iliniuma roho sana niliponyimwa fursa ya

kuwa mgombezi wa chama changu kwenye uchaguzi mkuu uliopita

wa 2007.” — Jennifer Chekwemoi Masis

Omanyo aazimia kuiamsha NambaleNa Frank Ouma…

Ruwaza yake ni kuwatia mo-tisha akina mama, vijana na hata wanaume kiuchumi, kija-mii na kisiasa ili kuwawezesha

kujiamulia hali yao kwa siku za usoni.Tunataka hali ambapo wakazi wa

Nambale wataweza kuamka kutoka kwenye usingizi pono na waweze kum-chagua kiongozi kutokana na manifesto yake na ajenda ya kuleta mabadiliko kwenye nyanja za kimaendeleo na wala si kwa sababu mtu kama huyo anach-aguliwa kwa sababu alihongana na ndipo akafanikiwa kunyakua kiti cha uongozi, akaeleza Catherine Nakhaabi Omanyo.

Chris OkemoHapo mwakani 1212, Catherine

mwenye umri wa miaka 33, atajib-waga tena uwanjani kwa mara ya pili kugombea kiti cha ubunge cha nam-bale. Mnamo Mwaka wa 2007 kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Catherine am-baye alikuwa mojawapo wa wale wa-liokigombea kiti hicho, alinyakua na-fasi ya tatu nyuma ya mbunge wa sasa, Chris Okemo wa chama cha Orange Democratic Party aliyefuatwa na John Bunyasi wa chama cha Narc.

Omanyo ambaye alisimama na tiki-ti ya chama cha Kenya African Demo-cratic Development Union, hajatangaza ni chama kipi ambacho Mwaka ujao ataomba tikiti yake.

Wakati huu, akasema, nimejitokeza kimatso matso kukinyakua kiti cho kwa upale na ulimbe kwani naamini wakazi wengi wa Nambale wameji-pata wameachwa nyuma kimaendeleo kulinganishwa na sehemu nyinginezo za wilaya ya Busia. Tunataka uongozi ambao unatilia maanani mahitaji ya wananchi ili nao waweze kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Catherine alikubaliana na dhana kwamba si rahisi kwa mwanamke ku-pambana vilivyo uwanjani na kundi la wapinzani wa kiume. Hata hivyo, anaamini kwmba kilicho muhimu kwa mwanasiasa ye yote Yule jinsi atakavy-ouza sera zake kwa wapiga kura kabla ya uchaguzi, jambo ambalo anaamini limempa motisha ya kutosha.

Ametoa wito kwa wagombezi wa kike kwa viti mbalimbali mwaka ujao, wasilegeza kamba wala kufa moyo ku-tokana na propaganda chungu nzima ambazo hupenda kupeperushwa na wa-nasiasa wengi pamoja na wafuasi wao dhidi ya wagombezi wa kike. Alisema kilicho muhimu ni kuanza kujipanga mapema ili wakati filimbi itakapopigwa ya kuingia uwanjani, akina mama wana-siasa wasipatikane kama wameduwaa.

Omanyo alisikitika kuona kwamba si wanawake wengi hutangamana na wanasiasa wenzao wa kiume kama ita-kikanavyo. Alieleza kwamba kufanya hivyo hakumaanishi kwamba ushiriki-ano kama huo una dhana ama nia ya mambo ya mapenzi, la, kwani hayo yote ni mapenzi ya mtu binafsi na zaidi ya yot hayo, si kila mwanamke huwa yuko tayari kujihusisha na mambo kama hayo eti ndipo aweze kufanikiwa kisiasa.

Alilaani mila Fulani za kiutamadu-ni ambazo zinapinga kuona msichana akigombea kiti cha udiwani ama hata ubunge katika eneo alikozaliwa akise-ma kwamba mawazo kama hayo yalip-itwa na wakati hwa sababu msichana kuolewa kwingineko, huwa ni hiari ya mtu binafsi.

Catherine alieleza kwamba kwa sa-babu tarafa zote za Busia sasa zitakuwa chii ya kaunti moja, nia yake iatakuwa ni kuhakikisha kwamba akichaguliwa, atasukuma gurudumu la maendeleo vilivyo kwa manufaa ya wakazi wote wa Busia kwa jumla.

Page 10: Mwanamke Mkenya Toleo 20

10 Toleo Namba 20 • Agosti 2011

Ardhi: Wanubi sasa wana matumaini makubwaNa Odhiambo Orlale…

Swala la ardhi katika mtaa wa Kibera mjini Nairobi ni swala zito ambalo ni sawa na bomu iliyotegwa ambayo inaweza

kulipuka wakati wowote , hasa kwa wanawake wa Kinubi wenye ardhi.

Jamii ya Wanubi inadai kwamba ardhi hiyo ni yao na ambayo wa-naiita Kibra, na wametumia kila na-fasi kupitia kwa baraza la wazee wao kuwakumbusha wakuu wa Serikali kuhusu maovu ya kihistoria kuhusi-ana na haki yao ya kisheria na umi-likaji wa mali.

Wanashikilia kwamba eneo hilo la ardhi lilinyakuliwa na Serikali na watu kutoka nje kujenga majumba ya kifahari bila ya kuwajali.

Maafa ya wanawake wenye ar-dhi katika mtaa huo mkubwa wa mabanda yameongezewa ubaya na kuingizwa kwa siasa kwenye swala la kodi ya nyumba katika siku zilizopita na kukataa kwa baadhi ya wapangaji wanaume kuheshimu makubaliano ya upangaji nyumba za mtaa huo.

MiziziWanubi ambao wazee wao wa kale

walitoka Sudan Kusini wanasema na kushikilia kwamba walipewa ardhi hiyo na serikali ya mkoloni kwa ku-tambua jukumu walilotekeleza kwenye vita vya kwanza na vya pili vya dunia. Ardhi hiyo inaanzia sehemu inayoju-likana kama Dagoretti Corner karibu na njia panda kwenye duka la Naku-matt katika barabara ya Ngong, hadi kwenye makaburi ya Langata na hadi uwanja wa ndege wa Wilson kwenye barabara hiyo hiyo ya Langata.

Kulingana na kumbukumbu za Serikali, eneo hilo la hekta 225 ni mali ya Serikali na asilimia 95 ya wakazi wa sehemu hiyo ni wapangaji.

Hivi leo wengi wa Wanubi wa-naishi katika maeneo mawili ya vijiji kumi ambapo viwili hivyo ni Maki-

na na Lindi ambako wana moja wa misikiti mikubwa.

Kwa upande wao wanawake wa Kinubi hawajaachwa nyuma na siku zote wamekuwa wakipigania haki zao hasa kwa wale ambao wana ardhi.

Swala hilo ni gumu mno hivi kwamba wanawake wote waliohojiwa kwa ajili ya taarifa hii wameomba wa-sitajwe wakihofia kufanyiwa dhuluma . Pia walisema kwamba wamo katika mwezi wa saumu wa Ramadhan am-bayo iliangukia katika mwezi wa Ago-sti katika kalenda ya kimataifa.

Mama Amina (silo jina lake hal-isi) anasema kwamba yeye ni mama wa watoto saba na ni mwenye maban-da kumi katika mitaa ya Makina na Lindi katika mtaa huo wa Kibera ulio katika eneo Bunge la Langata. Alirithi majengo hayo kutoka kwa mumewe ambaye alifariki miaka kumi iliyopita. Wapangaji wake wanamlipa kiasi cha shilingi elfu moja kila mwezi , ambazo si pamoja na malipo mengine kama vile umeme na maji. Wapangaji hao wanatumia choo kimoja pamoja na wapangaji wa nyumba nyingine ka-tika sehemu hizo.

Mama Rukia (sio jina lake halisi) ni mama wa watoto watano na anaishi katika mtaa wa Olympic. Ana maban-da ishirini ya kukodisha katika mi-taa ya Gatwikira na Kianda ambako analipwa kiasi cha shilingi elfu moja na mia tano kwa mwezi kwa nyumba zake zilizoezekwa kwa mabati ingawa ni za udongo.

Rukia ambaye pia ni mjane ilim-lazimu kujitetea vikali yeye na wa-nawe, baada ya mumewe kufariki dunia miaka mitano iliyopita ili ku-linda mali yao.

Tatizo lingine lilikuwa wapan-gaji ambao walikuwa ‘kichwa ngumu’ dhidi yake, lakini aliwatumia maajenti na idara ya utawala kumsaidia kuku-sanya kodi yake kama kawaida.

Kwa upande wao, Amina na Rukia ni mifano wazi ya matatizo

makubwa ambayo yanawakabili wan-awake Wanubi wenye nyumba.

Niwahasiriwa wa tamaduni za Ki-afrika katika upande mmoja na siasa za Kibera katika upande mwingine na eneo Bunge la Langata kwa upande mwingine.

Kupigania hakiKatika siku ziizopita, wamekuwa

wakibaguliwa kwa sababu ya jinsia yao. Ndugu zao wa kiume huingilia wakati kuna swala la mirathi wakitoa mifano ya haki za Kiafrika na Kiis-lamu kuhusu ardhi.

Kulingana na Amina ilikuwa vigumu hapo mwanzo. Ilimlazimu kusimama kidete kupigania haki yake kutoka kwa wapangaji wake ambao wengi wao waliwadharau wanawake na kuitumia sababu hiyo kuchelewe-sha malipo ya kodi ya nyumba.

Amina anasema: “Tulilazimika

kutumia idara ya utawala katika visa mbali mbali hasa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 kulipozuka ghasia za baada ya uchaguzi , ili idara hiyo iingilie kati kuwataka wapangaji walipe kodi ya nyumba.”

Kwa hakika wengi wa wenye nyum-ba katika mtaa huo wa Kibera wameku-wa na historia ya chuki kati yao na wa-pangaji juu ya swala la kodi ya nyumba, ambalo wakati mmoja lililipuka na kusababisha ghasia kubwa na kuwalazi-misha polisi kuingilia kati.

Visa vibaya zaidi vilitokea baada ya uchaguzi mkuu wa miaka ya 1997 na 2007 wakati nyumba nyingi zilipo-chomwa na wenye nyumba kulazimika kukimbilia usalama baada ya swala la kodi za nyumba kuingizwa siasa.

Anasema Amina; “Katiba hii mpya inawapa wanawake wenye nyumba kaka mimi, matumaini kwamba haki zetu na haki ya kumiliki mali zita-

heshimiwa na kulindwa. Hofu yetu ni kwamba imehukuwa muda mrefu kutekeleza sura muhimu zinazoathiri maisha yetu ya kila siku, lakini bado tuna matumaini.”

Hata hivyo, baadhi ya Wanubi am-bao wana uhusiano mzuri na wakuu, wamehamia kwenye mitaa ya kisasa iliyojengwa na shirika la taifa la nyum-ba, yaani National Housing Corpora-tion, shirika la Serikali linalomilikiwa na Wizara ya Nyumba. Mitaa hiyo ni pamoja na mradi wa pamoja kati ya Serikali ya Kenya na shirika la Habitat la Umoja wa Mataifa wa kustawisha mitaa ya mabanda.

Baraza lenye uwezo mkubwa la wazee wa Kinubi, limeasilisha taarifa kwa njia ya barua na kwa kusema kwa tume , majopo kazi na tume ya uchunguzi wa marekebisho ya katiba ambako waliwasilisha malalamiko thabiti kwa madai yao.

Jamii ya Wanubi kutoka mtaa wa Kibera (ama Kibra) wakiandamana nje ya Mahakama Kuu mjini Nairobi wakilalamikia unyakuzi wa ardhi yao. Akina mama wa Kinubi wenye mabanda ya kuishi katika Kibera sasa wana matumaini kwamba katiba mpya itawawawezesha kurejeshewa ardhi yao iliyokuwa

imenyakuliwa. Picha: Odhiambo Orlale

Na Hussein Dido…

Huku Tume Huru ya Mipa-ka na Uchaguzi, (IEBC), ikianza shughuli zake chi-ni ya katiba mpya, hakika

inakabiliwa na kibaru kigumu mion-goni mwa maswala mengine kama vile dhuluma za ardhi zilizofanywa na tawala zilizopita na kunako mwanzo wa kupatikana kwa uhuru.

Mji wa Isiolo ni moja ya miji am-bayo imekalia bomu kubwa linalo-subiri kulipuka ambalo linaingojea tume hiyo ya mipaka na uchaguzi kuanza kazi yake.

Uzito wa kikatibaMji wa Isiolo unakabiliwa na

matatizo makubwa baada ya majirani Nyambene kujiamulia kujiwekea mi-paka pasi na kufanya mashauriano na wahusika wengine huku kukiwa na mapendekezo ya miradi mipya am-bayo ni pamoja na mji wa kisasa we-nye barabara za kimataifa na barabara za reli zikikingama mjini humo.

Jamii za wafugaji kutoka sehemu iliyojulikana kama wilaya ya mpaka wa kaskazini yaani Northern Fron-tier District (NFD)walikabiliwa na mizozo ya kisiasa ya uzito wa kikatiba katika siku zilizopita kukiweko na kikundi kilichokuwa kikutaka ku-jitenga, na kutokana na hayo serikali

ikaanzisha harakati za kupambana na kikundi hicho cha mashifta.

Wakati wa kipindi cha machafuko hayo baadhi ya watu waliokuwa na uwe-zo mkubwa serikalini walichukua nafasi hiyo na kubadilisha mipaka na kuiingiza Isiolo katika wilaya kubwa ya Meru.

Chama cha wakfu wa ardhi ya Waso ambacho kinatetea maswala ya ardhi katika sehemu hiyo kilimlaumu Jackson Angaine sasa marehemu, am-baye wakati huo alikuwa Waziri wa Ardhi kwa kufanya mageuzi kadha wa kadha ya mipaka na taratibu za ugavi wa ardhi ambazo zilibadilisha mipaka ya Isiolo huku akipanua wila-ya ya Meru.

Barua nyingi ziliandikwa kati ya lililokuwa Baraza la Wilaya ya Isiolo, Idara ya Utawala wilayani, Baraza la Wilaya ya Meru na Wizara ya Ardhi mapema miaka ya 1970 ambazo zi-naashiria msururu wa harakati zili-zofanywa kutokana na umaarufu wa waziri huyo katika kubadilisha mipaka hiyo na kuipendelea wilaya ya Meru.

Mshirikishi wa wakfu huo wa ar-dhi, Hassan Shano anasema kuzindu-liwa kwa katiba mpya ni afueni kwa sehemu hiyo na kesi za mipaka na dhuluma za awali zitashughulikiwa chini ya sheria hii mpya.

Akiwasilisha taarifa ya kumbuku-mnbu kwa maafisa wa tume ya TJRC katika kituo cha Mafunzo cha Rural

Training Centre, Shano alisema kwamba Serikali ya Kenya ili-yokuwa ndio mwanzo imepata uhuru, ilibadilisha mipaka ya wilaya ya Isiolo bila ya ku-jali kwa manufaa ya wilaya ya Meru kwa kuchukua maeneo yaliyokuwa ya Isiolo ya mal-isho, na sehemu nyingine ya rehani na nyingine zenye rasli-mali za kimazingira zinazofaa kwa malisho zinazopakana na wilaya kubwa ya Meru.

Kulinganana taarifa yake, sehemu ambazo zimetwaliwa na kuingizwa katika wilaya ya Meru na ambazo zinazozaniwa ni pamoja na Boqe, Magaado, Daka Borr, Roqa (hadi kuvuka mpaka wa mbuga un-aopakana na Tharaka), Kambi Roqa, Qubi Chafesa, Kubi Sera, Hamares, (Kachuru) Baricha Boru , Jaro, Yaqa Bute na kuvuka sehemu za Maili Nane.

Sehemu nyingine zilizoathiriwa vibaya na mabadiliko ya mipaka hiyo ni sehemu ambazo ni pamoja na eneo la shamba la ufugaji la Livestock Marketing Holding Group Complex ambalo liko chini ya vyama kadha ambapo hapo awali maeneo hayo ya-likuwa yanakaliwa na mbari za Kiso-mali za Harti na Issak na wafugaji wa Waso Borana.

Ingawa kuna kesi mahakamani

inayopinga baadhi ya madai na licha ya rufaa kadha zilizowasilishwa na baraza lililokuwa la wilaya ya Isiolo, Serikali haishughuliki katika kusu-luhisha tatizo hili ambalo limekuwa likizusha migogoro katika miaka ya hivi karibuni.

Hali hiyo bado inaendelea huku Nyambene na majirani wengine wakijiongezea maeneo ya kaunti zao kutoka kaunti ya Isiolo. Tunatumai kwamba katiba mpya itatuokoa kuto-kana na unyanyasaji huo wa kikoloni, äsema Shano.

Mshirikishi huyo anasema ka-tika siku za hivi karibuni, sehemu za Kaskazini na Mashariki mwa Isiolo zimekuwa zikimenywa na Nyambene kwa usaidizi wa watu wenye uwezo mkubwa serikalini. Isiolo imepoteza sehemu nyingi za malisho na sehemu

kuhifadhi maji kama vile tarafa ya Kina (Bisan Adi) iliyochukuliwa na wilaya kubwa ya Meru.

Kwa upande mwingine jamii za Kisomali ziliingia katika maeneo ya Isiolo na sehemu zilizonyaku-liwa ni pamoja na Hadado, Arb Ja-han, Banane, Irres Wachile, Guchi Chachafa, Dusot, Basir, Gofo, katika wilaya jirani ya Wajir.

Kubadilishwa kwa mipaka na dhuluma nyingine za ardhi yaseme-kana zilitokea baada ya mwaka 1963 wakati Serikali ya Kenya ilipotangaza hali ya hatari katika sehemu za Kaska-zini na kuzitumia sehemu za mkoa wa Kaskazini Mashariki na wilaya jirani zilizowekwa chini ya usimam-izi mmoja ili kutekeleza mpango wa kiusalama uliosababisha mauaji ya halaiki na kupotea kwa mali za raia.

Mng’ang’anio wa ardhi mpakani watishia kulipuka

Sehemu ya mji wa Isiolo. Kwa sasa kuna ung’ang’aniaji wa ardhi kwenye Kaunti ya Isiolo sawa na tangu Kenya haijajitawala. Wakazi wa sehemu hii wana matumaini kwamba katiba mpya itasuluhisha mizozo hiyo yote. Picha:

Hussein Dido

Page 11: Mwanamke Mkenya Toleo 20

11 Toleo Namba 20 • Agosti 2011

Kushinikiza haki za wanawake za kumili kimali

Na Ruth Omukhango…

Wakati ambapo wa-nawake wanapigia tarumbetamsfanikio ambayo wamepata

kwenye katiba kuhusiana na haki ya umilikaji wa ardhi na mali huku kukitiliwa mkazo mali ya pamoja ya mke na mume waliooana, na urithi wa ardhi, changamoto kubwa itakuwa ni kupatikana kwa haki hizo pale am-bapo sheria za tamaduni na sheria za nchi zinagongana.

Kidesturi katika jamii nyingi nchi-ni wanawake hawakuruhusiwa kurithi ardhi na mali kwa kuwa baadhi yao walichukuliwa kuwa mali ya waume zao. Wakati inapotokea kwamba ndoa hizo zivunjike kufuatia kifo cha mume, wanawake hao hupoteza mali yake na ardhi ya mumewe kwa sa-babu mali hiyo hurejea kwa jamaa wa kiume wa mumewe ambao huenda wakawa ndugu za mumewe au watoto wao wa kiume.

UbaguziKwa wengi, wale ambao tamaduni

za aina hiyo zimedumisha ubaguzi kwa wanawake kwa kuwazuia kurithi ardhi na mali, sheria mpya imeibuka kama tukio la ajabu na la kushanga-za. Imezua maoni tofauti. Ni dhahiri kwamba kwa usaidizi wa sheria hiyo mpya iliyoko ndani ya katiba na mao-ngozi ya kitaifa ya ardhi, kumekuwa na mwelekeo mpya katika kanuni am-bazo zimebadilishwa ili kumnufaisha mwanamke ambaye ndiye anayegan-damizwa katika jamii.

Mfumo huu mpya wa kisheria

inahitaji kuwe na mbinu mpya za utekelezaji kati ya wapiganaji wa haki za wanawake na jamii zinazohusika ili kupatikane mabadiliko ya kinadharia na kifikra.

“Kuna haja ya kuchunguza kwa undani na kuelewa tamaduni za ja-mii hizo ambako tunahudumu kama wapiganaji wa haki za wanawake, kwa lengo la kutekeleza kanuni za katiba mpya na sheria nyingine ambazo zi-nalinda haki za wanawake za kumi-liki mali ili kushughulika kwa njia ya hakika itakayoleta mabadiliko yanay-okusudiwa,” asema Priscilla Nyokabi ambaye ni mkurugenzi mkuu wa Ki-tuo cha Sheria .

Wamilikaji ardhiHadi kuzinduliwa rasmi kwa kati-

ba mpya mnamo mwezi Agosti 2010, haki za wanawake za kumiliki ardhi na mali nyinginezo nchini zilisima-miwa na sheria za kijamii na sheria ya Uingereza ya umiliki wa mali kwa wa-nawake walioolewa ya mwaka 1882 ambayo ilishirikisha tofauti kadha kuhusu maswala ya mirathi, ubadil-ishaji wa wamilikaji wa ardhi hauku-washirikisha wanawake katika utoaji maamuzi kuhusu ardhi.

Ingawa sheria ya mirathi ilip-itishwa mwaka 1991, kulikuwa na migongano kati ya vifungu vya katiba na usawa wa kijinsia na desturi za ki-tamaduni ambazo ziliwabagua wan-awake katika utekelezaji wake. Baadhi ya hitilafu hizo ni kwamba sheria hiyo haishughulikii maswala ya wajane kwenye ndoa za mume mmoja wake wengi na mume mmoja mke mmoja. Kadhalika sheria hiyo inawapa nguvu

zaidi waume kuliko wake zao katika urithi. Zaidi ya hayo ni kwamba she-ria hiyo haikutoa ulinzi wa kutosha kwa watoto wanaozaliwa nje ya ndoa.

Sehemu ya arobaini ya katiba inasema kwamba kila mtu ana haki ya kumiliki ardhi awe mtu binafsi au kwa kushirikiana na wengine. Haki za wanawake zinatambuliwa zaidi katika kifungu cha 60 (1) (f) ambacho ki-naondoa ubaguzi wa kijinsia kwenye umiliki wa ardhi na mali nyingine hapa Kenya.

Katiba ambayo ndiyo sheria kuu, inawalinda wanawake na makundi ya watu wanaogandamizwa katika jamii kama inavyosema Sura ya kwanza kifungu 2(4) “Sheria yoyote ikiwa ni pamoja na sheria ya kitamaduni ambayo inaenda kinyume na katiba haifai na kutofaa kwake katika ulin-ganifu, na sheria yoyote kinyume cha katiba si halali.

Kifungu hicho kinawalinda wan-awake ambao ndio kundi linalofanya kazi nyingi kwenye ardhi kuliko kun-di lolote la watu katika jamii kuanzia asilimia 80 hadi asilimia 90 ya wafanyi kazi katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na zaidi ya asilimia 70 ya uzal-ishaji wa mazao ya kibiashara, lakini wanabaguliwa katika masuala yote yanayohusu umilikaji wa ardhi.

Haki za wanawake za kumiliki ar-dhi na mali nyingine ndizo ufunguo wa uendelezaji wa ustawi na usalama wa chakula nchini. Ni muhimu hivyo basi kwamba, kila jitihada zifanywe katika kuhakikisha kwamba haki ya wanawake ya kumiliki ardhi na mali mengine zinalindwa kwa njia ya hala-li, kiuchumi, kijamii na kitamaduni.

Kulingana na Nyokabi, wapi-ganaji wa haki za wanawake bado wana nafasi ya kutoa michango yao na kushiriki katika utungaji wa she-ria mpya kuhakikisha kuwa sheria hizo zinafungamanisha mambo yote

na kuwahami wanawake dhidi ya vipengee vilivyo na mianya ambayo inaweza kutumiwa kuwabagua katika masuala ya haki za umilikaji wa ardhi na mali nyinginezo.

Hayo kulingana na kifungu cha 68 cha Sura ya tano (iii) ya katiba, inalipa bunge jukumu la kuchunguza, kuzi-fanya thabiti na kuziimarisha sheria zilizopo na kutunga sheria kusima-mia kutambuliwa na kulindwa kwa mali ya watu waliooana hasa nyumba ya wahusika hao wakati na baada ya ndoa kuvunjika.

Mbinu zinazofaaKulingana na Rebecca Wangui,

mshirikishi wa mambo ya haki za ar-dhi katika shirika la Kenya Land Al-liance, wapiganiaji haki za wanawake wanapaswa kujitokeza na mbinu zina-zofaa ili kufanikisha malengo yao ya kupata haki kamili za kumiliki ardhi na mali nyinginezo, kupitia mbinu mbali mbali.

“Wanawake ni lazima wapate changamoto za kuwahimiza kupata haki za umilikaji wa ardhi na mali ny-ingine iwe ni katika njia za kibinafsi au kwa ushirikiano na kupata hati ya pamoja ya umilikaji ardhi na waume zao ili kuhami na kulinda maslahi yao katika maswala ya ardhi na mali ny-inginezo,” akasema Wangui.

Mbali na kutoa ufahamu kuhusu desturi za kitamaduni zenye madhara, kubadilisha dhana na misimamo, kuna haja ya kuwaleta wanaume kwe-nye harakati za kuwaelimisha kuhusu haja ya kuimarisha usawa wa kijinsia kuanzia kwa kijamii.

Kulingana na Wangui ili kuimar-isha manufaa yaliyopatikana, wan-awake ni lazima wawe walinzi wa sheria za usimamizi wa mambo ya kijinsia katika taasisi za usimamizi kuhakikisha urari wa kijinsia na mao-ngozi na sheria.

Changamoto ni utekelezaji kwa katiba kwa ukamilifu

“Kuna umuhimu wa kuchunguza na

kuelewa tamaduni ili kuwezaesha maongozi yaliyomo katika katiba

mpya yanayolinda haki za wanawake

kimali yaweze kuwa ya manufaa kwao .”

— Priscilla Nyokabi, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Sheria

Shaibu wa zaidi ya umri wa miaka 85 apigania ardhi yake iliyonyakuliwaNa Emeldah Rutendo…

Fatuma wa Mzee Bonaya ana miaka the-manini na mitano. Katika umri huo wakati ambapo anapaswa kupumzika kusubiri siku zake za kuiahiri dunia,

kikongwe huyo kila mara anahangaishwa na ukosefu wa usalama na mahali atakapolala usi-ku utakaofuata k wa sababu wastawishaji miradi wanachukua ardhi yake.

Macho yake yaliyochujuka yamezama ndani ya kikombe cha macho na kuonekana kama ma-tundu, lakini ukimtazama kwa makini, utaona ameyaelekeza kwenye ukuta wa matofali hata kupesa ni vigumu. Ukuta huo umezungukwa na huzuni nyingi.

“Ükuta ule ambao umenizuia kufikia ardhi yangu ya ekari nne umekuwa jinamizi katika maisha yangu. Mnamo mwisho wa mwaka jana ardhi yangu ilitwaliwa kinyume cha sheria na msitawishaji miradi wa kibinafsi ambaye aliva-mia ardhi bila ya idhini yangu,” akaeleza Fatuma.

Kujenga nyumba“Nilitupwa nje ya nyumba yangu wakati wa-

lipokuwa wakiweka sengenge kuzunguka ardhi hiyo ambayo sasa wanadai wanaimiliki. Sikupe-wa nafasi yoyote ya kutoa kitu chochote kutoka kwenye nyumba yangu,”akaongeza.

Kulingana na Fatuma ardhi inayohusika ilikuwa ya baba yake miaka mingi kabla Kenya kupata uhuru. Baada ya wazazi wake kufariki dunia, aliendelea kuishi katika shamba hilo akil-inda raslimali iliyoko ndani ya shamba hilo am-balo limejaa minazi na miembe katika sehemu ya Bichanga tarafa ya Kisauni, Mombasa.

“Mzozo huo wa ardhi ulisababisha kufuku-liwa kwa maiti ya baba na wastawishaji miradi hao,”akalalama Fatuma huku akiongeza kwamba mstawishaji miradi huyo alifanya hivyo ili apate

kujenga nyumba kwenye sehemu hiyo ya kaburi.“Mnyakuzi huyo wa ardhi alitaka kunipa

shilingi elfu hamsini kwa sehemu hiyo ya ardhi ya ekari nne akiniambia niende kununua ardhi mahali pengine, lakini nikakataa,” akasema Fa-tuma, huku akichungulia ndani ya shamba hilo kwenye tundu la ukuta wa matofali.

Kama baba yangu na ndugu yangu wan-galikuwa wako hai leo, nisingepitia masaibu haya . Nilikuwa nikilima mazao kama vile mi-hogo, mahindi, viazi tamu, na mboga , lakini sasa sina chakula wala nguo za kuvaa . Katika umri wangu siwezi kupigana kupata ardhi yangu,”akalalamika.

Dhuluma za ardhiKisa cha Fatuma ni mfano mzuri wa dhu-

luma wanazopitia wanawake mikononi mwa wanaume ambao hudai ndio wamiliki halali wa ardhi.

Wanawake wengi katika Mkoa wa Pwani wamejipata wakihamishwa kutoka makazi yao ya asili ya ardhi zao za jadi kwa madai kwamba hawana haki ya kumiliki ardhi na mali. Wakati mwingine hata hawafahamu kwamba wana haki ya kumiliki ardhi na kuwa na mali.

Wakili mmoja wa Pwani, Samuel Ouma anasema katiba mpya haijafanikisha mengi kwa

sababu bado inategemea utekelezaji wa maon-gozi ya kitaifa ya ardhi.

“Sheria inayosimamia maongozi mapya ya ardhi haijatayarishwa vilivyo, lakini nina hakika kwamba wakati itakapotekelezwa tutapiga hatua kubwa katika kulinda haki za umilikaji wa ar-dhi,” akasema wakili huyo.

Ouma anasema ni jambo jema kwamba wan-awake wana haki sawa na wanaume na sasa wanawe-za kumiliki ardhi kinyume cha katiba ya zamani.

“Wanawake hawapaswi kunyimwa nafasi ya

kumiliki ardhi, kama watadhulumiwa na msi-tawishaji miradi yeyote, wana haki ya kushtaki hasa wakiwa na stakabadhi zifaazo kama ushahi-di ya umilikaji wa ardhi,” akaeleza Wakili Ouma.

Kimsingi ni kwamba hali halisi ya mambo ni tofauti kabisa kwani wanawake wengi wana uw-ezo haba katika kutoa maamuzi juu ya maswala ya ardhi na umilikaji wa mali nyinginezo.

Fatuma sasa anatoa mwito kwa Serikali ku-ingilia kati na kumsaidia kupata ardhi ambayo ilikuwa mali yake.

“Nilitupwa nje nyumba yangu wakati walipokuja kuweka ua kwenye ardhi yangu na

ambayo kwa sasa wanadai ni mali yao.”

— Fatuma wa Mzee Bonaya

Ajuza Fatuma wa Mzee Bonaya akichungulia ukutani sehemu ya ardhi iliyokuwa awali mali yake lakini kwa

sasa imenyakuliwa na mstawishaji fulani. Kulia, ajuza huyo amejishika tama asijue

lakufanya. Picha: Emelda Rutendo

Page 12: Mwanamke Mkenya Toleo 20

12 Toleo Namba 20 • Agosti 2011

Mwanamke Mkenya ni toleo la African Woman and Child Feature Service

Email: [email protected]

Jarida hili limechapishwa kutokana na usaidizi wa Hazina la Kidemokrasia la Umoja wa Mataifa (UNDEF)

Mkurugenzi Mkuu: Rosemary Okello-Orlale

Mhariri Mkurugenzi: Arthur Okwemba

Mhariri Msimamizi: Jane Godia

Wahariri Wasaidizi: Bob Okoth, Gunga Chea

Waandishi: Joyce Chimbi, Faith Muiruri, Duncan Mboyah, Omwa Ombara, Florence Sipalla, Ben Oroko, Ruth Omukhango, Adow Ina Kalil, Issa Haroun, Odhiambo Orlale, Fibi David, George Omonso, Emeldah Rutendo

Wapambe: Bernadette Muliru na Noel Lumbama, (Noel Creative

Media Ltd)

Vijana watafuta kuleta mapinduzi katika utaratibu wa uongozi

Na Ruth Omukhango…

Kwa miaka mingi vijana wa-megandamizwa kwenye sekta za kisiasa na utoaji wa maamuzi licha ya kuwa

sehemu muhimu katika sekta ya ki-uchaguzi. Licha ya kuchukuliwa kuwa mhimili wa jamii na tumaini na kien-delezi cha tamaduni na thamani za kijamii hadi kwenye vizazi vijavyo, wamekuwa wakiishi katika dhana po-tofu ya kuwa viongozi wa kesho.

Hata hivyo, kupitia katiba mpya vijana hawatafunikwa tena na msemo huo wa kale na badala yake watakuwa sehemu ya sekta ya kisiasa na ya utoaji maamuzi kama inavyohakikishwa kwenye vifungu tofauti vya katiba.

Sehemu ya tisiniKwa vifungu hivyo vya katiba hu-

enda kukatokea mapinduzi makubwa kuhusiana na jinsi vijana wanavyochu-kuliwa. Viongozi hawataweza tena ku-watumia vijana hao kama magenge ya kuwashambulia wapinzani wa kisiasa na badala yake watawachukulia kuwa washirika katika jukwaa moja.

Kwa mfano katika kifungu cha 97 (1) (b) katiba inasema hivi: “Bunge litakuwa na Wabunge kumi na wawili maalumu ambao watachaguliwa na vyama vya siasa bungeni kulingana na idadi ya Wabunge kila chama kilionao, kuambatana na sehemu ya 90 kuwak-ilisha makundi ya maslahi maalumu ikiwa ni pamoja na vijana, watu wenye ulemavu na wafanya kazi.

Katika kifungu cha 98 (1) ( c) katiba inaeleza: “Baraza la Senate lita-kuwa na Wabunge wawili ambao wat-akuwa mwanamume mmoja na mwa-namke moja, ambao watawawakilisha vijana.”

Vijana ambao ni kundi la watu wa kuanzia umri wa miaka kumi na mi-nane hadi miaka thelathini na mitano lenye kuwakilisha asilimia 75 ya idadi ya watu nchini ambao wanajipanga vilivyo kupitia miungano ya kimbinu ili kuun-da mshikamano thabiti na kuleta athari kubwa zaidi kupitia uwakilishi wao ka-tika uwanja wa kisiasa na kijamii.

Moja ya makundi hayo ni kundi linalojulikana kama Langata Youth Network, kundi la kijamii la vijana wa kujitolea ambalo linawaleta pamoja vijana thelathini na watano viongozi wa makundi kumi ya kijamii kutoka eneo zima la kaunti ya Langata am-bayo inachanganya maeneo ya Bunge ya Langata na Dagoretti.

Likijulikana kwa jina maarufu la “Kisima cha akili na vipawa” wana-chama cha kundi hilo, walikusanyika pamoja tangu kuzinduliwa rasmi kwa katiba mpya kutumia kwa ustadi manufaa ambayo yanapatikana ndani ya katiba mpya kuleta muungano mi-ongoni mwa vijana kuwahimiza juu ya haki zao za kuanzia, kutekeleza, kuimarisha na kuendeleza maendeleo yao huko Kibera.

Moja ya shabaha za kikundi hicho ni kuvunjilia mbali mpango wa

kutegemea michango ya usaidizi ku-toka nje katika mtaa huo wa vibanda kwa kuhimiza na kuimarisha moyo wa kufanya kazi kwa bidii, uaminifu, uthabiti ambao utahakikisha hali bora ya uchumi wa kijamii kwao bi-nafsi na kwa taifa zima na hali ya ki-siasa kwa jumla.

Wanadhamiria kupeperusha bendera ya uongozi kwa kuonye-sha kwamba wanaweza kama vijana kupitia kuwahimiza vijana kujiunga na vyama vya kisiasa na kugombea viti vya kiuchaguzi katika ngazi zote. Vijana hao wanazidi kuungwa mkono kwa wanachama ambao wana maono ya kiuongozi na maarifa ili kugombea nyadhifa muhimu kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2012 .

Wanachama wa kundi hilo kadha-lika ni wawakilishi wa makundi mbali mbali ya vijana na ambao wamehitimu katika vyuo tofauti ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu. Wana hamu na ustadi ambao umekitwa katika dhamira ya kuona jamii ambayo iko huru yenye kutoa nafasi sawa kwa wote na maen-deleo kwa vijana wote.

“Tunayo katiba sasa na kazi yetu ni kujitendea kazi, na kupitia hali hii tungependa kuona jamii ambayo haitegemei Serikali kutoa kila kitu ku-wakimu na kuilaumu wakati mambo yanaposhindikana,” alisema Daniel Orogo, mwenyekiti wa kundi hilo.

Alisema kwamba ingawa wingi wa uanachama wa chama hicho uko wazi kwa vijana wenye elimu ya taasisi na vyuo, kundi hilo linaendesha miradi ya ushauri kwa vijana walio katika shule za sekondari pamoja na warsha za kielimu katika baadhi ya shule.

Kwa sababu ya shughuli nyingi za wanachama, mikutano ya viongozi hao wa makundi ya vijana ya Langata (LYN) hufanywa siku za Jumamosi mchana kuanzia saa nane kwenye ofi-si zao zilizoko katika shule ya St Ce-cilia Academy katika kijiji cha Kianda mtaa wa Kibera.

Ada ya uanachama hi shilingi 250 ambazo hulipwa mara moja na ada ya shilingi 100 ambayo hulipwa kila mwezi. Faini ya shilingi 50 hutozwa wale ambao hukosa kufika mikutano-ni au kwenda mikutanoni wakiwa wamechelewa.

MwanzilishiPesa hizo husaidia kugharamia

shughuli za chama kama vile kulipa madeni kama vile kodi ya ofisi am-bayo huilipa shule.

Shughuli za kundi hilo zimekitwa katika vifungu vya katiba ikiwa ni pamoja na mswada wa haki na uon-gozi na uthabiti. Kulinganana kundi hilo katiba inawapa haki ya kudai kile kilicho chao kama raia, lakini pia wa-natambua ya kwamba wanahitajika kuchukua jukumu wenyewe jambo ambalo linaanza na wao wenyewe.

Kulinganana Winnie Obure, am-baye ni mwanachama mwanzilishi wa kundi hilo, na mwanzilishi wa kundi la Sebuleni katika mtaa wa Kibera, uon-gozi na uthabiti huanza na wanach-ama. Kundi hilo linadhamiria kuweka viwango ambavyo vitazalisha matun-da, kwa kujenga na kuwafungulia mil-ango vijana wa vizazi vipya ambavyo vitawajibika kwa vitendo vyao.

Kundi hilo limechukua mfano wa kanuni za uongozi na uthabiti

kama inavyokokotezwa na katiba na kushirikisha misingi ya uteuzi wa uthabiti wa kibinafsi, uwezo na kufaa au uchaguzi wa haki na huru.

Kwa kutambua manufaa kwa wa-nawake ndani ya katiba hasa kuhusu harakati za maslahi ya wanawake, kundi hilo linaandaa mikutano maalumu kwa wanawake kuwapa changamoto ya kutilia umuhimu kipengee cha thuluthi moja, lakini wangángánie viti vya mamlaka zaidi ili kuimarisha uwakilishi wao.

“Tunapinga propaganda kwamba wanawake watosheke na thuluthi moja kwa sababu tunataka kuona wa-nawake zaidi wakiwakilisha sekta zote za utoaji maamuzi ili wawe na nguvu za kutosha,”akasema Winnie.

“Kulingana na kifungo cha 55 cha Mswada wa Haki, Serikali itachukua hatua, ikiwa ni harakati za maslahi ya wanawake kuhakikisha kwamba vijana wanapata elimu inayofaa na mafunzo, kuwa na nafasi ya tangama-no, wawakilishwe na kushiriki katika sekta za siasa,uchumi wa kijamii na sekta nyinginezo za kimaisha, kupata nafasi za kazi, na kulindwa dhidi ya vitendo vya kitamaduni vyenye kuleta madhara na kunyanyaswa.”

Shughuli za kundi hilo ni pamoja na kauandaa mikutano kwa vijana kuwaelimisha kuhusu haki zao za kikatiba, kupewa uwezo kiuchumi kupata mikopo kupitia ushirikiano katika Benki ya Equity.

Tangu kuanzishwa kwake wanach-ama wanaweza kushuhudia kwamba baada ya mwaka mmoja jitihada zao zimezaa matunda na kuwapa matu-maini ya maisha ya siku za usoni.

Chama cha LYN kimeshirikiana na mashirika maarufu nje na ndani ya eneo bunge la Langata kama vile Kituo cha Sheria, Youth Platform for Change, Youth for Kenya, Proj-ect Amani, CREAW na Inuka Trust. Kundi hilo limeandaa mikutano ya kuwaelimisha jamii kuhusu haki zao za uchumi wa kijamii kama ina-vyosema katiba. Baadhi ya haki hizo ni kupata huduma za kijamii ambazo ni pamoja na huduma za afya, elimu, haki ya wanawake ya kumiliki mali na kurithi pamoja na usalama wa kijamii kwa watu wazima katika jamii.

Kutokana na kushirikiana na mashirika mengine kama vile Inu-ka Trust, kundi hilo limefanikiwa kushirikiana na Kliniki ya Bomu katika mtaa wa Changamwe mjini Mombasa kuanzisha kituo cha mati-babu katika mtaa wa Soweto, ambao ni moja ya vijiji vya Kibera ambacho wanatumai kitaanza kazi mwakani.

Vyombo vya habariKwa chama cha LYN ushirikiano

na vyombo vya hanbari ni muhimu. Kundi hilo limetumia vituo vya ma-tangazo vya hapa nchini ambavyo ni pamoja na Pamoja FM kutangaza vip-indi vyake ambavyo vinawahamasisha vijana kuhusu majukumu na haki zao katika jamii.

“Tunaendesha vipindi hivi kila wiki katika radio ya Pamoja FM ku-wahamasisha vijana kuhusu maswala mbali mbali ya leo huku uzito ukiti-liwa katika swala la uthabiti na kut-waa nyadhifa za uongozi katika ngazi zote,” akakariri.

Chama hicho kadhalika kime-husika kwenye harakati za kuleta amani huku wakitilia mkazo vijana kudumisha amani kwa sababu pasi na utulivu hakuwezi kuwa na uongozi.

Wanatumia kila nafasi inayopati-kana kama vile kufanya usafi na shu-ghuli za michezo.

“Huwa tunaendesha vipindi vitatu kila wiki katika kituo chetu cha Pamoja FM ili kuhamasisha vijana kuhusu mambo kadha wa kadha na hasa lengo pia likiwa

ni kuwataka kuchukua uongozi siku za usoni.” — Daniel Orogo

Hawa ni baadhi ya wanachama wa kundi la Lang’ata Youth Network wakitafakari juu ya jambo fulani linalowahusu. Vijana kwa sasa wanawahamasisha wenzao kuhusu manufaa ya katiba mpya. Picha: George Ngesa