10
Bulletin News Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] http://www.mem.go.tz HABARI ZA NISHATI &MADINI Toleo No. 47 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe Desemba 19-25, 2014 Resolute wakabidhi eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma Uk7 Tanzania – Zambia - Kenya zasaini makubaliano ya Usafirishaji Umeme Habari Uk. 2 Kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Petroli wa Kenya, Davis Chirchir (katikati) na Waziri wa Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia, Christopher Yaluma. Mradi huu utaka- milika kwa awamu kati ya mwaka 2016 na 2018. Kukamilika kwa mradi huu kuta- saidia juhudi za Serikali za kuacha- na na mitambo ya dharura ambayo inauza umeme huo kwa gharama ya kati ya senti 30 na 55 za Kimarekani kwa uniti moja

JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 47

Embed Size (px)

DESCRIPTION

JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 47

Citation preview

BulletinNews

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI &MADINI

Toleo No. 47 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe Desemba 19-25, 2014

Resolute wakabidhi eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma Uk7

Tanzania – Zambia - Kenya zasaini makubaliano ya Usafirishaji Umeme Habari Uk. 2

Kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Petroli wa Kenya, Davis Chirchir (katikati) na Waziri wa Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia, Christopher Yaluma.

Mradi huu utaka-milika kwa awamu kati ya mwaka 2016 na 2018. Kukamilika kwa mradi huu kuta-saidia juhudi za Serikali za kuacha-na na mitambo ya dharura ambayo inauza umeme huo kwa gharama ya kati ya senti 30 na 55 za Kimarekani kwa uniti moja

2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI

Na Teresia Mhagama

Nchi za Tanzania, Zambia na Kenya zimetiliana saini Makubaliano ya Awali (MoU) ya

kuanza kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa miundom-binu ya kusafirisha umeme wa msongo mkubwa wa kilovolti 400.

Makubaliano hayo ya awali yamesainiwa tarehe 15 Desemba 2014, nchini Zam-bia na Mawaziri wanaosima-mia sekta ya Nishati katika nchi husika ambao ni Waziri wa Nishati na Madini Nchini, Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zam-bia, Christopher Yaluma, na Waziri wa Nishati na Petroli wa Kenya, Davis Chirchir.

Waziri wa Nishati na Ma-dini, Profesa Sospeter Muhon-go ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaziwezesha nchi hizo kuuziana umeme wa bei nafuu ambao utakuwa chi-ni ya senti 10 za Kimarekani kwa uniti moja .

“ Mradi huu utakamilika kwa awamu kati ya mwaka 2016 na 2018. Kukamilika kwa mradi huu kutasaidia juhudi

za Serikali za kuachana na mitambo ya dharura ambayo inauza umeme huo kwa ghara-ma ya kati ya senti 30 na 55 za Kimarekani kwa uniti moja,” alisema Profesa Muhongo.

Profesa Muhongo al-iongeza kuwa Tanzania ina-hitaji umeme mwingi, wa bei nafuu na wa uhakika ili kuongeza uzalishaji, uwekeza-ji, ushindani, kutengeneza ajira mpya na kukuza uchumi imara.

Alieleza kuwa madhumu-ni makuu ya muungano huo yanalenga katika kuunganisha gridi za taifa za nchi husika, kuunganisha soko la umeme la Afrika Mashariki (Eastern Africa Power Pool (EAPP)) na soko la umeme la Kusini mwa Afrika (Southern Africa Power Pool), (SAPP).

Taarifa kutoka Zambia inaeleza kuwa makubaliano hayo yaliyosainiwa na Mawa-ziri wa nchi hizo tatu yana umuhimu mkubwa kwani ndio yanayoweka misingi ita-kayotumika katika mazun-gumzo yatakayowezesha kuu-ziana umeme katika nchi hizo tatu na masoko ya SAPP na EAPP, kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa mradi kwani wadau wengi wa maendeleo sasa wanatoa kipaumbele cha

fedha kwa miradi inayoju-muisha nchi na nchi (Regional Projects) kuliko ya nchi mo-jamoja, kuwa na fursa ya soko la umeme kwa nchi zenye vyanzo vya umeme vya kuto-sha na kuwa na uhakika wa upatikanaji umeme kwa nchi zisizokuwa na vyanzo vya ku-

tosha vya nishati hiyo.Mradi huo utakuwa na

manufaa mbalimbali kwa nchi husika ikiwemo kuimarisha upatikanaji wa umeme kwa nchi hizo, kutumia rasilimali umeme kwa ufanisi zaidi, na kupanua upatikanaji wa umeme kwa wananchi husika.

Awamu ya kwanza ya mra-di ambayo itaunganisha nchi za Kenya na Tanzania itaka-milika mwezi Desemba 2016, wakati awamu ya pili itaka-milika mwaka 2018. Jumla ya gharama za mradi kwa awamu zote mbili zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni 1.2.

Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), Waziri wa Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia, Christopher Yaluma (katikati), na Waziri wa Nishati na Petroli wa Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakisaini Makubaliano ya Awali (MoU) ya mradi wa pamoja wa kujenga miundombinu ya kusafirisha umeme kati ya nchi za Zambia, Tanzania na Kenya.

Tanzania –Zambia- Kenya zasaini makubaliano ya Usafirishaji Umeme

Wakaguzi wa migodi wajengewa ujuziNa Asteria Muhozya, Mwanza

Wakaguzi wa Migodi ku-toka mikoa mbalimbali nchini wamekutana ka-tika kikao kazi kwa lengo la kuandaa miongozo

(checklist) itakayo wawezesha kutekeleza kikamilifu majukumu yao wawapo katika shughuli za ukaguzi wa migodi.

Akizungumza katika ufunguzi wa ki-kao hicho, Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje amewataka wak-aguzi hao kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kufanyika kwa ukaguzi ya-kinifu ili kuwezesha usalama migodini.

Mhandisi Samaje ameongeza kuwa, wakaguzi wa migodi wanao wajibu wa kuhakikisha usalama na afya migodini na kuongeza kuwa, masuala ya uhifadhi wa mazingira pia ni jambo la kuzingatia wakati wa kufanya ukaguzi.

“Naomba tuwe makini katika kutoa maoni yatakayosaidia kuandaa ‘checklist’, tumieni uzoefu mlionao tuboreshe jambo hili, ongezeni masuala mapya ambayo

yatakuwa na manufaa katika shughuli za ukaguzi wa migodi. Lazima tutofau-tishe kutembelea na kukagua migodi,” ameongeza Samaje.

Aidha, amewataka kuwa makini na kutekeleza shughuli hizo kitaalamu ku-tokana na umuhimu wake na kuongeza, “tukikutuma kufanya ukaguzi, tunataka uende kama mtaalamu kweli unayefa-hamu majukumu yako. Kwa hiyo, maoni mtakayotoa leo, yatakuwa na mchango mkubwa katika shughuli za ukaguzi,” ame-sisitiza Samaje.

Katika kikao hicho mada mbalimbali zimewasilishwa zikilenga kuwajengea uw-ezo wa namna bora ya kufanya shughuli za ukaguzi migodini.

Vilevile Mhandisi Samaje amesisitiza umuhimu wa kuwajengea uwezo wata-laamu hao katika shughuli za ukaguzi na kuongeza kuwa, “Serikali inalitambua suala hili na inalipa kipaumbele”,alisema.

Kwa mujibu wa Mhandisi Samaje, kikao kazi hicho kilichoanza tarehe 15-19 Desemba,2014, kitawawezesha wakaguzi hao kuwa na utaratibu wa pamoja unaofa-nana katika kufanya ukaguzi wa masuala ya usalama ,afya, na utunzaji wa mazingira migodini.

Baadhi ya Wakaguzi wa Madini kutoka mikoa mbalimbali nchini, wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi kuandaa miongozo (checklist) itakayosaidia kutekeleza shughuli za ukaguzi wa migodi.

Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia ukaguzi wa Migodi Mhandisi Ally Samaje (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Wakaguzi wa Migodi nchini waliohudhuria kikao kazi cha kuandaa checklist ya ukaguzi wa migodi.

Mtaalamu kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi Chagwa Marwa, (kushoto) akichangia jambo wakati wa majadiliano ya kuandaa checklist ya ukaguzi wa migodi.

3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz MAONI

TahaririMEM

Na Badra Masoud

FIVE PILLARS OF REFORMS

KWA HABARI PIGA SIMU KITENGO CHA MAWASILIANO

INCREASE EFFICIENCYQUALITY DELIVERY

OF GOODS/SERVICE

SATISFACTION OF THE CLIENT

SATISFACTION OF BUSINESS PARTNERS

SATISFACTION OF SHAREHOLDERS

TEL-2110490FAX-2110389

MOB-0732999263

Hongera Idara ya Madini kwa kuandaa miongozo (checklist)

ya Ukaguzi Migodini

TEL-2110490FAX-2110389

MOB-0732999263

Stamico yahimizwa kutumia mbinu za kisasa za ulinzi kudhibiti wizi migodini

Mnamo tarehe 15 hadi 19 Desem-ba,2014, Wizara ya Nishati na Madini kupitia Idara yake ya Madini iliandaa kikao kazi ambacho kilikuwa na lengo

la kuwawezesha wakaguzi wa migodi nchini kuwa na utaratibu wa pamoja, unaofanana katika kufan-ya shughuli za ukaguzi migodini katika masuala ya usalama ,afya, na utunzaji wa mazingira.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao kazi hi-cho, Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughu-likia Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje aliwataka wakaguzi hao wa migodi kutoa maoni na mapendekezo ambayo yatasaidia kuleta ufanisi katika utekelezaji wa shughuli hizo hasa katika uhakiki wa masuala ya usalama, afya na uhifadhi wa mazingira.

Katika kikao hicho Kamishna Msaidizi mwe-nye dhamana ya Ukaguzi Migodi kwa kutambua umuhimu wa shughuli hizo katika ustawi wa mi-godi alitoa msisitizo kwa wakaguzi hao kuwa ma-kini katika kutoa maoni ambayo ndiyo msingi wa miongozo hiyo itakayotumika katika shughuli za ukaguzi na kusisitiza kuwa lengo la serikali ni kuo-na wakaguzi hao wakifanya kazi zao kitaalam na kufahamu majukumu yao.

Kuna ujumbe mzito alioutoa Kamishna Msaid-izi, Mhandisi Samaje, kwa wakaguzi hao, nanukuu “tukikutuma kufanya ukaguzi, tunataka uende kama mtaalam kweli unayefahamu majukumu yako. Kwa hiyo, maoni mtakayotoa leo, yatakuwa na mchango mkubwa katika shughuli za ukaguzi,”

Ujumbe huu ukizingatiwa na wataalam wa migodi utasaidia kuboresha masuala ya msingi migodini ikiwemo kuepusha ajali zinazotokea mi-godini hususani kwa wachimbaji wadogo, ambazo zingeweza kuepukwa endapo kundi hilo litapatiwa miongozo ya namna bora ya kufanya shughuli za madini kwa kuzingatia masuala ya afya, usalama na kutunza mazingira katika sehemu ambazo shu-ghuli husika zinafanyika.

Pamoja na kutoa pongezi kwa Idara ya Madini kwa kuona umuhimu wa wataalam husika kutoa maoni ili kuboresha shughuli za ukaguzi wa migo-di nchini, midogo na mikubwa, tunatoa wito kwa wataalam hao kutumia miongozo hiyo ambayo tu-naamini itakuwa bora kwa vile waliohusika katika uandaaji wa miongozo hiyo tayari wana uzoefu ka-tika kazi hiyo na hivyo kikao kazi hicho wamekitu-mia pia kutatua changamoto zinazorudisha nyuma kazi hiyo muhimu kwa ukuaji wa uchumi nchini.

Tunarudia kusema kuwa hongera Idara ya Ma-dini kwa kuona umuhimu wa shughuli hizo za uk-aguzi wa madini na hivyo kuamua kuziboresha. Tu-naamini hili litasaidia kupunguza kama si kuondoa kabisa malalamiko ya wananchi wanaozunguka maeneo ambayo shughuli za migodi zinafanyika hasa katika suala la uharibifu wa mazingira.

Koleta Njelekela na Bibiana Ndumbaro –STAMICO

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limetakiwa kutumia mbinu za kisasa za Ulinzi na Usalama kudhibiti wizi, ubadhirifu na udokozi katika migodi yake ili kujiwezesha kukuza mapato

yake, kuchangia pato la Taifa na kuleta maen-deleo kwa manufaa ya Watanzania.

Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO Balozi Alexander Muganda ametoa rai hiyo mwanzoni mwa wiki kupitia kipindi cha Jambo Tanzania, kinachorushwa kwa njia ya Televisheni na Redio na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), alipokuwa akiongelea juu ya uteuzi wake na mikakati yake katika kuiende-leza STAMICO.

Balozi Muganda alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kwakumteuanakusemakuwahatamwangush-akatikautekelezajiwamajukumuyake.

Kuhusu suala la ulinzi na usalama, Ba-lozi Muganda aliendelea kusema kuwa Bodi ya STAMICO itahakikisha kuwa matumizi ya mbinu za kisasa katika ulinzi na usalama yanakwenda sambamba na udhibiti wa wachimbaji madini wasio halali wanaovamia

katika maeneo ya uchimbaji katika migodi ya STAMICO, na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kuwa na hatia.

Akiongelea kuhusu Mgodi wa Uzalishaji wa Tanzanite uliopo Mirerani, Mwenyekiti huyo wa Bodi ya STAMICO, ameishukuru Wizara ya Nishati na Madini kupitia Ofisi ya Madini ya Kanda ya Kaskazini iliyoko Arusha kwa kushirikiana na Ofisi ya OCS wa Man-yara na Kampuni ya Ulinzi ya Nguvu Moja Security Group kwa kukamilisha vyema zoezi la kuwatoa wachimbaji wasio halali, waliova-mia kitalu C katika mgodi huo.

Mgodi wa Tanzanite upo Mirerani mkoa-ni Manyara na unamilikiwa kwa ubia baina ya Tanzanite One Limited (TML) na STAMICO tangu Julai 2013 ambapo kila mbia anamiliki asilimia 50.

“Katika uendeshaji wa mgodi huu wa Mirerani, STAMICO itahakikisha kuwa timu ya watu wanne, wawili kutoka kila upande ili-youndwa kama timu ya Monitoring and Evalua-tion inafanikisha azma yake ya ufuatiliaji hatua zote za uzalishaji ikiwemo uchimbaji, udhibiti wa vitendo vya wizi na ubadhirifu, uongezaji thamani ya Tanzanite, usafirishaji na kuimari-sha uwezo wa kumudu ushindani katika soko la Kimataifa,” alifafanua Balozi Muganda.

Aidha ameongeza kuwa katika utekeleza-ji wa majukumu ya STAMICO, Bodi itajitahidi

kuboresha matumizi ya vifaa vya kisasa katika utafiti, uchimbaji na uchorongaji ili kumudu ushindani katika soko na kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia yanayoendelea kutokea duniani.

Balozi Muganda alisema hivi sasa STA-MICO inafanya vizuri katika kazi za uchoron-gaji wa kutoa sampuli za utafiti kutoka chini ya ardhi katika miamba kwa mfumo wa “Core” yaani Diamond Core Drilling, mafanikio am-bayo yametokana na uwepo wa wataalamu mahiri katika uchorongaji na wenye uwezo mkubwa wa kutumia mashine zilizopo.

“Nina imani nabodiyawakurugenzikwa-niimejipanga vizuri kusimamia matumizi ya fedha zinazopatikana na kudhibiti mapato na matumizi ya Shirika kwa manufaa ya umma jambo ambalo litasaidia pia kuongeza pato la taifa.” alisisitiza Balozi Muganda.

Mwenyekiti huyo wa Bodi ya STAMICO pia amesema licha ya kuwa na changamoto ya fedha za kuanza shughuli za uzalishaji katika miradi yake, Shirika linafanya majadil-iano na wadau katika taasisi mbalimbali za fedha ikiwemo Benki ya Maendeleo ya TIB na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) iliku-pata mkopo wa fedha za kununulia vifaa vya uzalishaji badala ya kutegemea ruzuku kutoka Serikalini.

Akihitimisha mazungumzo yake ka-tika kipindi hicho cha Jambo Tanzania, Ba-lozi Muganda ametoa wito kwa Menejimenti na wafanyakazi wa STAMICO na Kampuni Tanzu ya STAMIGOLD chini ya Uongozi wa Mhandisi Edwin Ngonyani kufanya kazi kwa ushirikiano na uadilifu mkubwa na kutam-bua kuwa STAMICO imepewa dhamana ya kuliendesha Shirika kibiashara kwa manufaa ya umma huku wakitambua Shirika hilo ni la Wananchi na Serikali ndio yenye hisa.

BODI YA UHARIRI MHARIRI MKUU: Badra Masoud

MHARIRI : Leonard Mwakalebela MSANIFU: Essy Ogunde

WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson MwaseTeresia Mhagama, Mohamed Saif na Nuru Mwasampeta

4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

Pichani ni baadhi ya Wageni mbalimbali walioudhuria hafla fupi ya makabidhiano ya eneo la Mgodi wa Resolute kwa Chuo cha Madini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Stephen Masele akizungumza jambo wakati akitoa hotuba yake katika hafla ya makabidhiano ya Mgodi wa Resolute ambao umekabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma.

Habari Ktk Picha

Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme nchini (Tanesco), (mstari wa mbele) waliohudhuria hafla iliyofanyika nchini Zambia ya kutiliana saini Makubaliano ya Awali (MoU) ya mradi wa pamoja wa kujenga miundombinu ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 400 kati ya nchi za Zambia, Tanzania na Kenya wakimsikiliza mmoja wa wazungumzaji katika hafla hiyo (haonekani pichani). Kutoka kulia ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Eng. Hosea Mbise, Decklan Mhaiki, Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Uwekezaji (Tanesco), Kasindi Malale, Injinia Mkuu (Tanesco), Mwanasheria, Abbas Kisuju (Wizara) na Leonard Masanja, Injinia Mkuu (Wizara) .

Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Bintuni Msangi, akisoma hotuba ya kufunga Mgodi wa Resolute na kukabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma. Katika hotuba yake Mkuu wa Wilaya alieleza namna Wilaya hiyo ilivyonufaika katika kipindi cha uhai wa Mgodi huo.

Waziri wa Nishati na Petroli wa Kenya, Davis Chirchir (aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla iliyofanyika nchini Zambia ya kutiliana saini Makubaliano ya Awali (MoU) ya mradi wa pamoja wa kujenga miundombinu ya kusafirisha umeme kati ya nchi za Zambia, Tanzania na Kenya. Wengine katika picha ni Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kushoto), Waziri wa Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia, Christopher Yaluma (wa nne kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini nchini, Eng.Ngosi Mwihava, (wa kwanza kushoto), pamoja na watendaji wengine kutoka nchini Kenya, Zambia na Umoja wa Ulaya.

u

u

5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

Resolute ilivyokabidhi eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma

Meneja Mazingira Mgodi wa Resolute Jackie Sinclair (Kulia), akimkabidhi funguo mbalimbali za majengo ya eneo la mgodi wa Resolute Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini) Stephen Masele (Kushoto) mara baada ya makabidhiano ya eneo la mgodi yalipofanyika.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Stephen Masele (aliyesimama katikati) akishuhudia utiaji saini makabidhiano ya eneo la Mgodi wa Resolute kwa Chuo cha Madini Dodoma. Wa kwanza kushoto waliokaa ni Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile, katikati ni Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje, na kulia ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Resolute Peter Beilby. Wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi (wa pili kuchoto aliyesimama),Mkurugenzi Kampuni ya Resolute Rose Aziz.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe funguo mbalimbali za majengo ya mgodi wa Resolute kwa ajili ya Chuo cha Madini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele (mwenye kofia) akiangalia chumba cha kompyuta ambacho ni miongoni mwa vifaa ambavyo Mgodi wa Resolute umekabidhi kwa ajili ya Chuo cha Madini Dodoma.

Meneja Mazingira wa mgodi wa Resolute Jackie Sinclair (mbele) akieleza jambo wakati akikabidhi baadhi ya vifaa vya maabara kwa Chuo cha Madini Dodoma. Wanaomsikiliza ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele na ujumbe alioambatana nao.

Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma wakifuatilia hotuba ya makabidhiano ya mgodi huo.

u

6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

u

Nyumba 840 zafaidika na umeme jua wa makontena

Na Teresia Mhagama

Imeelezwa kuwa jumla ya nyumba 840 katika wilaya za Kongwa, Uyui na Mlele zimefaidika na mradi wa majaribio ya umeme unaotokana na nishati ya jua unaozalishwa na

kusambazwa kutoka kwenye makontena maalum yajulikanayo kama PV generators.

Msimamizi wa Mradi huo kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila ameeleza kuwa mradi huo unahusisha uwekaji wa makontena maalum yaliyofungwa vifaa vya kuzalisha umeme unaotokana na jua ambapo kila kontena moja lina uwezo wa kuzalisha kilowatt 15 za umeme na kusambazwa ka-tika nyumba 60 na Taasisi za kijamii katika sehemu husika.

“Makontena haya pia yana sehemu za kuunganisha mitambo midogomidogo kama ya kusaga, kuchana mbao, kuchome-lea vyuma na kuendeshea pampu za maji. Hii yote ni katika kuwawezesha wananchi katika vijiji hivyo kufanya shughuli za kiuchumi na hivyo kujieletea maendeleo”, alisema Mhandisi Rwebangila.

Alisema kuwa mradi huo ambao sasa uko katika awamu ya majaribio tayari ume-shanufaisha vijiji 10 ambavyo ni, Lobilo, Ngutoto, Leganga na Silale vya wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. Vingine ni Tura, Loya na Lutende vya wilaya ya Uyui mkoani Tabora, pia vijiji vya Ilunde, Nsen-

kwa na Mapili vya wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

Alieleza kuwa umeme huo wa jua un-aozalishwa kwenye makontena haujaishia kufungwa kwenye nyumba za makazi tu, bali pia unasambazwa kwenye huduma za kijamii kama vile shule, vituo vya afya, sehemu za ibada na taa za mitaani amba-zo pia zinasaidia wananchi kwa masuala mbalimbali ikiwemo usalama.

“Ieleweke kuwa mradi huu ni tofauti na ufungaji wa mitambo ya umeme jua iliyozoeleka ambayo hufungwa sehemu ambapo mtumiaji yupo. Mradi huu una-husisha ufungaji wa mitambo mingi katika kontena moja ambalo linakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme mwingi na hatimaye kusambazwa kwa wananchi”, alisisitiza Mhandisi Rwebangila.

Alieleza kwamba kwa kuwa mitambo hiyo itakuwa ikizalisha umeme mwingi, hivyo wananchi wa eneo husika watakuwa na uwezo wa kufanya shughuli za kiuchu-mi zinazohitaji umeme mkubwa.

Aliongeza kuwa mradi huo unaotekele-zwa na serikali ya Tanzania utakuwa en-delevu na baada ya majaribio hayo, unat-egemewa kusambazwa sehemu mbalimbali nchini hasa ambazo ziko mbali na gridi ya Taifa.

Mhandisi Rwebangila ameeleza kuwa kwa sasa serikali inafanya tathmini ya utekelezaji wa mradi huo lengo likiwa ni kuleta ufanisi zaidi katika miradi kama hiyo itakayotekelezwa nchini.

Moja ya nguzo ikiwa imefungwa nyaya za kusambaza umeme unaotokana na nishati ya jua ambayo inazalishwa kutoka katika mitambo inayofungwa kwenye makontena maalum (PV generators)

Moja ya makontena ambayo yamefungwa mitambo itakayozalisha umeme unaotokana na jua ambayo wananchi katika wilaya za Uyui, Mlele na Kongwa wameanza kufaidika nayo kwa kuanza kupata nishati ya umeme.

Moja ya nyumba katika Kijiji cha Tura wilayani Uyui mkoani Tabora ikiwa imeunganishiwa umeme kutoka kwenye kontena lililofungwa mitambo ya kuzalisha umeme unaotokana na jua.

MIGODI YA STAMIGOLD NA BUZWAGI YAPONGEZWA KWA MAHUSIANO MAZURINa Elda Mahenda -Biharamulo

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya amepongeza uongozi wa Migodi ya STAMIGOLD uliopo Bi-haramulo na ACACIA-BUZWAGI wa Kahama inayojishughulisha na

uchimbaji wa madini ya dhahabu hapa nchini kwa jitihada za kudumisha mahusiano mazuri baina ya kampuni hizo.

Mheshimiwa Mpesya alitoa pongezi hizo hivi ka-ribuni akiwa ni Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Siku ya familia ya Mgodi wa ACACIA-BUZWAGI ambayo iliambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo michezo ya Mpira wa Miguu na Nyavu iliyofanyika katika viwanja vya Mgodi huo wilayani Kahama.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Mgodi wa ACACIA-BUZWAGI, Mhandisi Philbert Rweyem-amu alishauri ushirikiano ulioanzishwa na Uongozi baina ya Kampuni hizo mbili uendelezwe ili kuima-risha uhusiano mzuri miongoni mwa wafanyakazi wa Migodi hiyo.

Awali, Timu za Mpira wa Miguu za STAMI-GOLD na BUZWAGI zilishiriki katika mchuano wa mechi ya kirafiki na kutoka sare ya bila kufungana. Aidha, mchezo mwingine ulishirikisha Timu za Mpira wa Nyavu kati ya Mgodi wa STAMIGOLD na Wa-nafunzi kutoka shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwendakulima ambapo shule ya Mwendakulima iliongoza kwa mabao nane (8) dhidi ya manne (4) yali-yofungwa na STAMIGOLD.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama mheshimiwa Benson Mpesya akisalimiana na wachezaji kutoka ACACIA BUZWAGI kabla ya mchuano kuanza.

Timu ya STAMIGOLD ikiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mkuu wa STAMIGOLD Mhandisi Dennis Sebugwao (mwenye shati nyeupe katikati) pamoja na Mwalimu (Kocha) wao Msema Kawewe (wa kwanza kulia), na Meneja Rasilimali Watu, Ndugu David Nyagiro katika viwanja vya Buzwagi.

7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

Resolute wakabidhi eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma

Na Asteria Muhozya, Nzega

Mgodi wa Resolute uliopo Wilayani Nzega Mkoa-ni Tabora tarehe 12 Desemba, 2014, ulik-abidhi rasmi eneo la

Mgodi huo kwa Chuo cha Madi-ni Dodoma baada ya ukarabati wa mazingira kufanywa chini ya usimamizi wa kamati ya Kitaifa ya Ufungaji Migodi.

Akihutubia katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Nishati na Ma-dini anayeshughulikia Madini, Stephen Masele alieleza kuwa, tukio la kukabidhiwa eneo la Mgodi kwa Chuo ni tukio amba-lo limefungua ukurasa mwingine kutokana na kwamba Chuo cha

Madini Dodoma kitaiwezesha Tanzania kuzalisha wataalamu zaidi waliobobea katika tasnia hiyo ambao mchango wao kwa taifa unahitajika katika kuende-leza sekta ya madini.

Aliongeza kuwa, uamuzi wa Serikali kufunga mgodi huo ni wa busara na kwamba, Tanzania inahitaji kujenga na kuimarisha sekta ya madini hususani wataal-am katika sekta hiyo kutokana na mahitaji ya soko la watalaam wa madini.

“Tunataka wanafunzi wa-some kwa vitendo, hii itawez-esha kupata wataalam waliobo-bea. Ni nafasi kwa wanafunzi na Chuo cha Madini kuitumia fursa hii vizuri. Najua kuna mawazo mchanganyiko ya kupoteza ma-pato kwa Halmashauri na men-

gine ya kupata Chuo lakini, ku-funga mgodi ni sehemu ya Sheria ya madini”, alisisitiza Masele.

Aidha, alikitaka Chuo cha Madini Dodoma kutumia fursa hiyo kuwahamasisha vijana kuona umuhimu wa kujiunga na Chuo hicho hususani kusomea masuala ya madini na kuongeza kuwa, “wazazi leteni watoto wenu wasomee madini”.

Akizungumzia upande wa Halmashauri, aliitaka Hal-mashauri ya Wilaya ya Nzega kutumia fedha zilizokusanywa kutokana na kodi zilizolipwa na mgodi huo kuchochea uchumi wilayani humo.

Akizungumzia kuhusu suala la uhifadhi wa mazingira mgo-dini hapo na ukarabati uliofany-wa, Masele alieleza kuwa, “ni-

Pichani ni eneo la mgodi wa Resolute

meridhika na hali ya mazingira, ukarabati na ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya matumi-zi ya Chuo, wanaweza kuondoka”alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi, akizungumza katika hafla hiyo, alieleza kuwa, Mgodi wa Reso-lute una historia ya kuwa mgodi wa kwan-za nchini kuzalisha madini ya dhahabu na kuongeza kuwa, ndani ya kipindi cha miaka 12 cha uhai wa mgodi huo umeweza ku-changia kiasi cha shilingi bilioni 290 za Ki-tanzania ikiwa ni kodi mbalimbali zilizotole-wa na mgodi huo kama mrabaha.

Aliongeza kuwa, Halmashauri iliweza kupata kiasi cha shilingi bilioni 6 ikiwa ni kodi na kiasi cha Tsh bilioni 6 kilitumiwa na mgodi huo kuwezesha huduma za kijamii ikiwemo ujenzi wa zahanati, shule, upati-kanaji wa huduma ya maji katika eneo lin-alozunguka mgodi huo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mgo-di huo, Mtedaji Mkuu wa Mgodi wa Reso-lute Peter Beilby alieleza kuwa, mbali na mgodi huo kuzalisha madini ya dhahabu la-kini pia uliwezesha upatikanaji wa huduma muhimu zinazozunguka eneo hilo zikiwemo zahanati,shule na huduma za maji.

Aidha, Beilby alieleza kuwa, mgodi huo umeweza kuwajengea ujuzi wataalamu wa kitanzania hususani katika masuala ya ma-dini ya dhahabu na kuongeza kuwa, “ ujuzi wa teknolojia kwa watalaamu hao utaisaidia Tanzania katika sekta ya madini. Aidha, hakusita kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini na Halmashauri ya Nzega kwa ushirikiano uliokuwepo kipindi chote cha uhai wa mgodi huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma Mhandisi Subian Chirag-wile akipokea eneo hilo, aliwataka wachim-baji wadogo kuzitumia maabara za Chuo hicho mara baada ya kuanza kazi rasmi ku-tokana na ubora wa vifaa vya upimaji ma-dini vilivyokabidhiwa na mgodi huo.

Mgodi wa Resolute umefunga rasmi shu-ghuli zake za uchimbaji madini ya dhahabu katika eneo hilo, ambapo ulianza kazi zake mwaka 1998. Kabla ya makabidhiano hayo Mgodi huo umekuwa katika hatua za ukara-bati wa mazingira kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2013 chini ya usimamizi wa kamati ya Kitaifa ya Ufungaji migodi.

Pamoja na eneo la mgodi huo kukabi-dhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma, vi-levile mgodi umekabidhi majengo, mitambo, maabara ambapo, kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile alieleza kuwa, eneo hilo litatumiwa na wanafunzi wa mwaka wa pili kwa ajili ya masomo ya vitendo.

n Masele asema tukio hilo limefungua ukurasa mpyan Aeleza kufunga mgodi ni sehemu ya Sheria ya Madini

Resolute wakabidhi eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma

8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIAMINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

Invitation for Bids for

PROPOSED REFURBISHMENT AND EXPANSION OF MTWARA MINE OFFICE BUILDING

(Bid No. .ME/008/SMMRP/W/11 1. This Invitation for Bids follows the General Procurement Notice for this Project which appeared in United Nations Development Business Issue no. 775 dated 31st May 2010.

2. The Government of the United Republic of Tanzania through the Minis try of Energy and Minerals received funds from the International Devel opment Association (IDA) towards the cost of the Sustainable Management of Minerals Resources Project (SMMRP) and it intends to apply part of the proceeds of this credit to cover eligible payments under the contract for Proposed Refurbishment and Expansion of MtwaraMineOfficeBuilding.

3. The Ministry of Energy and Minerals now invites sealed bids from eligible Building Contractors registered or capable of being registered in Class four and above for carrying out the Proposed Refurbishment and ExpansionofMtwaraMineOfficeBuilding. 4. Bidding will be conducted through the National Competitive Bidding proceduresspecifiedinthePublicProcurementAct2011(Goods,Works, NonConsultancyServiceandDisposalofPublicAssetsbyTender) Regulations, 2011 and is open to all Bidders as defined in the Regulations(2013).

5. Interested eligible Bidders may obtain further information from and inspect the Bidding Documents at the office of the Secretary, Ministerial Tender Board; Ministry of Energy and Minerals Plot No: 754/33 Samora Avenue; Tanesco Building, Wing ‘’B’’, Room No. 10, P.O.Box 2000 Dar Es Salaam Tanzania. Telephone +255-22-2121606, Facsimile No. +255-22-2123688, e-mail address: [email protected] from 0830 to 1530 Hours local time on Mondays to Fridays inclusive except on public holidays.

6. AcompletesetofBiddingDocument(s)inEnglishandadditionalsets may be purchased by interested Bidders on the submission of a written application to the address given under paragraph 5 above and upon paymentofanon-refundablefeeofTshs.150,000.00(Tanzania ShillingsOneHundredFiftyThousandOnly).Paymentshouldbeby CashorchequepayabletoPermanentSecretary,MinistryofEnergyand Minerals.

7. AllBidsmustbeaccompaniedbyaBidsecuringDeclarationinaformat provided in the bidding document.

8. Allbidsinoneoriginalplustwo(2)copies,properlyfilledin,anden closed in plain envelopes must be delivered to the address below at or before 10.00 hours local time on 12th January 2015. Bids will be opened promptly thereafter in public and in the presence of Bidders’ representatives who choose to attend in the opening at The Ministry of Energy and Minerals, 5 Samora Machel Avenue, 5th Floor in the Board Room, P.O. Box 2000, 11474 Dar es Salaam Tanzania.

9. Latebids,portionofbids,electronicbids,bidsnotreceived,bidsnot opened at the bid opening ceremony shall not be accepted for evaluation irrespective of the circumstances.

Address:Permanent Secretary,

Ministry of Energy and Minerals,5 Samora Machel Avenue;

P.O. Box 2000, 11474 Dar Es Salaam, Tanzania.Telephone: +255 – 22 – 2121 606

Facsimile No.: +255 – 22 – 212 3688email: [email protected]

KATIBU MKUU

Tangazo

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIAMINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

Invitation for Bids for

PROPOSED REFURBISHMENT OF NACHINGWEA AND TUNDURU MINE OFFICES

(Bid No. .ME/008/SMMRP/W/10 1. This Invitation for Bids follows the General Procurement Notice for this Project which appeared in United Nations Development Business Issue no. 775 dated 31st May 2010.

2. The Government of the United Republic of Tanzania through the Ministry of Energy and Minerals received funds from the International Development Association (IDA) towards the cost of the Sustainable Management of Minerals Resources Project (SMMRP) and it intends to apply part of the proceeds of this credit to cover eligible payments under the contract for Proposed Refurbishment of Nachingwea and TunduruMineOffices.

3. The Ministry of Energy and Minerals now invites sealed bids from eligible Building Contractors registered or capable of being registered inClassfiveandaboveforcarryingouttheProposedRefurbishmentof NachingweaandTunduruMineOffices.

4. Bidding will be conducted through the National Competitive Bidding proceduresspecifiedinthePublicProcurementAct2011(Goods,Works, NonConsultancyServiceandDisposalofPublicAssetsbyTender) Regulations,2011andisopentoallBiddersasdefinedintheRegulations.

5. Interested eligible Bidders may obtain further information from and inspecttheBiddingDocumentsattheofficeoftheSecretary, Ministerial Tender Board; Ministry of Energy and Minerals Plot No: 754/33 Samora Avenue; Tanesco Building, Wing ‘’B’’, Room No. 10, P.O.Box 2000 Dar Es Salaam Tanzania. Telephone +255-22-2121606, Facsimile No. +255-22-2123688, e-mail address: [email protected] from 0830 to 1530 Hours local time on Mondays to Fridays inclusive except on public holidays.

6. AcompletesetofBiddingDocument(s)inEnglishandadditionalsets may be purchased by interested Bidders on the submission of a written application to the address given under paragraph 5 above and upon paymentofanon-refundablefeeofTshs.150,000.00(Tanzania ShillingsOneHundredFiftyThousandOnly).Paymentshouldbeby CashorchequepayabletoPermanentSecretary,MinistryofEnergyand Minerals.

7. AllBidsmustbeaccompaniedbyaBidsecuringDeclarationinaformat provided in the bidding document.

8. Allbidsinoneoriginalplustwo(2)copies,properlyfilledin,and enclosed in plain envelopes must be delivered to the address below at or before 10.00 hours local time on 12th January 2015. Bids will be opened promptly thereafter in public and in the presence of Bidders’ representatives who choose to attend in the opening at The Ministry of Energy and Minerals, 5 Samora Machel Avenue, 5th Floor in the Board Room, P.O. Box 2000, 11474 Dar es Salaam Tanzania.

9. Latebids,portionofbids,electronicbids,bidsnotreceived,bidsnot opened at the bid opening ceremony shall not be accepted for evaluation irrespective of the circumstances.

Address:Permanent Secretary,

Ministry of Energy and Minerals,5 Samora Machel Avenue;

P.O. Box 2000, 11474 Dar Es Salaam, Tanzania.Telephone: +255 – 22 – 2121 606

Facsimile No.: +255 – 22 – 212 3688email: [email protected]

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

Invitation for Bids for

PROPOSED REFURBISHMENT OF NACHINGWEA AND TUNDURU MINE

OFFICES

(Bid No. .ME/008/SMMRP/W/10

1. This Invitation for Bids follows the General Procurement Notice for this Project which appeared in United Nations Development Business Issue no. 775 dated 31st May 2010.

2. The Government of the United Republic of Tanzania through the Ministry of Energy and Minerals received funds from the International Development Association (IDA) towards the cost of the Sustainable Management of Minerals Resources Project (SMMRP) and it intends to apply part of the proceeds of this credit to cover eligible payments under the contract for Proposed Refurbishment of Nachingwea and Tunduru Mine Offices.

3. The Ministry of Energy and Minerals now invites sealed bids from eligible Building Contractors registered or capable of being registered in Class five and above for carrying out the Proposed Refurbishment of Nachingwea and Tunduru Mine Offices.

LOT DESCRIPTION QTY 1 Refurbishment of Nachingwea Mine Office 1 2 Refurbishment of Tunduru Mine Office 1

Bidder may bid for one or all two lots, but in each case the responsive bidders will be awarded one lot.

4. Bidding will be conducted through the National Competitive Bidding

procedures specified in the Public Procurement Act 2011 (Goods, Works,

9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

Mkuu wa Wilaya ya Butiama Bi Angelina Mabula (wa pili kutoka kushoto) akitoa mwongozo wa mjadala wa zoezi la kubainisha mahitaji ya jamii kwa wananchi wa Buhemba. Wa kwanza Ku-shoto ni Meneja wa Masoko na Uhusiano kwa Umma (STAMIC0, Koleta Njelekela na kulia pichani ni baadhi ya wananchi wa Buhemba wakimsikiliza.

STAMICO yatathmini mahitaji ya jamii Na Bibiana Ndumbaro, STAMICO

Shirika la Madini la Taifa (STA-MICO) limeanza mchakato wa kubaini mahitaji ya jamii (Com-munity Needs Assessment) ili kukamilisha mpango wa Shirika

wa miaka mitano wa kuchangia Huduma za Jamii katika maeneo yanayozunguka miradi yake.

Akizungumzia kuhusu hatua hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi Edwin Ngonyani amesema zoezi hilo litafanyika katika maeneo yote yanayozunguka migodi ya STAMICO ya uzalishaji ikiwemo Mradi wa Uzalishaji Dhahabu wa Buhemba; na Mradi wa kuchimba Makaa ya Mawe na Uzalishaji Umeme wa Kiwira uliopo wilayani Ileje mkoa wa Mbeya;

Aidha, aliyataja maeneo mengine kuwa ni pamoja na Mradi wa Un-unuzi wa Madini ya Bati uliopo wilayani Kyerwa; mkoani Kagera; Mradi wa uzalishaji dhahabu wa Buckreef uliopo wilayani Geita, mkoani Geita na Mradi wa uzalishaji Tanzanite ulipo Mirerani mkoani Manyara na kuongeza kuwa, hivi sasa zoezi hilo limeanza katika eneo linalozunguka Mgodi wa Buhemba.

“STAMICO kama ilivyo kwa ma-shirika mengine nchini inaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za ku-leta maendeleo ya jamii kupitia migodi ya uzalishaji kulingana na uwezo wa Shirika kifedha” alifafanua Mhandisi Ngonyani.

Akizungumza hivi karibuni katika

Kijiji cha Biatika, kata ya Buhemba, kuhusu umuhimu wa zoezi hilo kwa wa-nanchi, Mkuu wa Wilaya ya Butiama Bi Angelina Mabula aliipongeza STAMICO kwa kutambua umuhimu wa kujenga mazingira rafiki katika eneo la uwekezaji. Aliwataka wananchi kuwa wawazi na kushiriki kikamilifu katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya jamii katika vijiji vyao. “Suala la msingi ni kutathmini kwa upeo mkubwa ili kukubaliana vitu ambavyo vitaweza kutekelezeka na kuu-fanya mradi kuwa wa mrejesho na wenye faida kwa wananchi na STAMICO kwa ujumla” alisisitiza Bi Mabula.

Aidha, Bi Mabula amesema ana imani kubwa na STAMICO, na kwamba zoezi la kutathmini mahitaji ya jamii ka-tika miradi yake itaiwezesha STAMICO kuongeza kasi ya kuchangia maendeleo ya jamii kulingana na uwezo wake wa kifedha na hivyo kuwa mfano wa kuigwa kwa wawekezaji wengine nchini katika uchangiaji wa huduma za maendeleo ya jamii.

Katika kuhakikisha Shirika linaji-wekea mpango endelevu wa kuchangia huduma za maendeleo ya jamii, hivi karibuni STAMICO ilituma timu ya wataalamu huko Buhemba wilayani Butiama, kutathmini mahitaji halisi ya Huduma za Jamii kwa vijiji vinavyozun-guka mradi wa Uchenjuaji Dhahabu wa Buhemba. Hatua hiyo itasaidia Shirika kukamilisha Mpango Mkakati wa miaka mitano wa kuchangia Huduma za Jamii (CSRP) katika kuleta maendeleo.

http://www.mem.go.tz

n Ni katika maeneo yanayozunguka miradi yake

Na Asteria Muhozya, Mwanza

Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshu-ghulikia Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi, Ally Samaje, amesifu zoezi

la kuandaa miongozo (checklist) ya Ukaguzi wa Migodi na kueleza kuwa, litaleta matokeo bora ku-tokana na kwamba shughuli hiyo imekuwa shirikishi.

Kamishna Samaje ameyasema hayo katika kikao kazi kilichofanyika Jijini Mwanza na kuwashirikisha Wakaguzi wa migodi kutoka mae-neo mbalimbali nchini kwa lengo la kuandaa miongozo itakayokuwa nyenzo muhimu kwa shughuli za ukaguzi wa migodi nchini.

“ Kimekuwa ni kikao kizuri, kila mmoja ameshiriki kikamilifu jambo ambalo linaashiria kuwa, tuta-toka hapa tukiwa na kitu ambacho kitawezesha shughuli za ukaguzi migodini kufanyika kwa utaalam,” amesema Samaje.

Ameongeza kuwa, miongozo hiyo inatarajiwa kuleta mabadiliko katika shughuli za ukaguzi wa migo-di. Vilevile shughuli nzima itafanyika katika muonekano unaofafana ku-tokana na kwamba, miongozo hiyo inaandaliwa kwa ajili ya ukaguzi wa

migodi yote nchini , ikiwemo migodi mikubwa na midogo.

“Tutatoka hapa na miongozo mi-zuri, nina imani kwamba tutakuwa tofauti na miaka mingine. Tutaon-gea lugha moja katika shughuli za ukaguzi, lakini zaidi tutajenga kikosi bora kwa ajili ya shughuli za ukaguzi”, amesisitiza Samaje.

Aidha, ameongeza kuwa, uwepo wa miongozo hiyo, utawezesha shughuli za ukaguzi migodi ku-fanyika kitaalamu zaidi na kuongeza kuwa, “suala jingine la kuzingatia ni kwamba uandaaji wa miongozo hii unazingatia hali halisi ya mazingira yetu, huku masuala ya afya,usalama na uhifadhi wa mazingira yakizin-gatiwa,” .

Kwa upande wake, mwezeshaji katika kikao hicho, Mtaalam ku-toka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi, Laurian Rwebembera , akifafanua masuala kadhaa katika ki-kao hicho, ameeleza kuwa, miongo-zo hiyo inatarajiwa kuwa, shirikishi kutokana na kwamba washiriki wote wameshiriki kikamilifu katika zoezi zima la uandaaji miongozo hiyo.

“Kila mmoja ameshiriki kuonesha uzoefu na namna bora ya kufanya kazi ili kufikia lengo. Miongozo hii itakuwa nyenzo bora za kufanyia kazi, amesema Mhandisi Rwebembera.

Miongozo ya ukaguzi kuleta mabadiliko migodini- kamishna

Mmoja wa washiriki wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi akiwasilisha kazi ya vikundi wakati wa kikao cha kuandaa miongozo ya Ukaguzi wa Migodi

10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII UJUMBE WA WAZIRI WIKI HIIWAFANYAKAZI WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI, KAMPUNI NA

TAASISI ZETU TUENDELEE KUCHAPA KAZI KWA UMAKINI, UADILIFU NA UBUNIFU MKUBWA SANA KWA KUSUDIO LA KUFUTA UMASIKINI NCHINI

MWETU. TUTASHINDA, TUSIKATISHWE TAMAA.

Washiriki wa kikao kazi cha kuandaa miongozo (checklist) ya ukaguzi wa migodi wakiwa katika makundi kujadiliana namna ya kuandaa miongozo hiyo.

Wakaguzi wa migodi waelezwa umuhimu wa checklist katika ukaguzi

Na Asteria Muhozya, Mwanza

Imeelezwa kuwa, wakaguzi wa migodi wanao mchango mkubwa katika kuepusha ajali zinazotokea migodini hususani kwa wachimbaji

wadogo endapo watatoa mapende-kezo na maoni yatakayowezesha kuandaa miongozo (checklist) itakayotumika katika ukaguzi wa migodi.

Hayo yameelezwa na Mtaal-amu kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini , Mhandisi Noel Baraka wakati akitoa mada katika kikao kazi cha wakaguzi wa migodi wanaokutana kwa lengo la kuandaa miongozo itakayotumika kwa ajili ya shughuli za ukaguzi wa migodi.

Akizungumzia hali halisi ya watalaam hao, alieleza kuwa, bado kuna upungufu wa wakaguzi wa migodi huku idadi kubwa ikiwa ni watalaam wachanga ambao bado hawana uzoefu wa kutosha katika shughuli hizo. “Pamoja na upun-gufu huu lakini endapo tutaandaa miongozo mizuri, itasaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha ajali migo-dini,” ,alisisitiza Mhandisi Baraka.

Wakati huo huo, akitoa mada katika kikao hicho, Mhandisi Assa Mwakilembe amewataka wakaguzi hao kuzingatia maeneo muhimu ambayo yameainishwa katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010 yakiwemo masuala ya uhifadhi wa mazingira, usalama na afya na kuwataka wataalam hao kutoa kipaumbele katika maeneo hayo wakati wa shughuli za ukaguzi wa migodi nchini.

Vilevile, akitoa mada ya namna ya kuandaa miongozo ya ukaguzi, Kamishna Msaidizi anayeshughu-likia Ukaguzi wa Migodi Mhandisi Ally Samaje ameeleza umuhimu wa kuwa na miongozo katika shu-ghuli za migodi kwamba, zitaweze-sha kufahamu mapungufu yaliyoko migodini na hivyo kujua namna bora ya kutoa ushauri wafanyapo ukaguzi katika migodi ya wachim-baji wakubwa na wadogo.

Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha kuandaa checklist ya wakaguzi wa migodi wakiwa katika kazi za vikundi kuandaa miongozo hiyo.

u

u

Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Madini, Mhandisi Noel Baraka akiongea jambo wakati akitoa mada kuhusu Ukaguzi wa Madini wakati wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi nchini.